Search This Blog

Friday, 20 May 2022

C.O.D.EX. 2 (THE DIRTY GAME) - 1

 







    IMEANDIKWA NA : TARIQ HAJI



    *********************************************************************************



    Simulizi : C.O.D.EX. 2 (The Dirty Game)

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    "Mkuu Marine base 71 imepata tatizo" aliigia Hansen huku akihema katika ofisi kubwa za CIA Marekani, "unasemaje wewe?" aliinuka huku akifoka Ms Helen. "Ndio taarifa tulizozipata muda huu na inasemekana mmoja kati ya wale vijana ambao wapo katika project inayoendelea ametoroka" Hansen aliongea huku akijiweka sawa. "Shit bila shaka huyo atakuwa Project 75" aliongea Ms Helen aliongea huku akijishika kiuno, "hebu waambia wawakague halafu watuambie ni yupi ambae ametoroka" alimaliza kuongea na Hansen akatoka.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ms Helen alikaa kwenye kiti chake na kushusha pumzi kwa nguvu, maana aliwaza awaambie nini wakubwa wake. Robo saa Hansen alirudi tena huku akiwa na huzuni, "wala hujakosea, alietoroka ni project 75" aliongea Hansen. "Hapo ndio kwenye tatizo kubwa maana unafahamu mara ya mwisho alivotoroka ilituchukua mwaka mzima mpaka kumkamata" Ms Helen aliongea huku akikuna kichwa, alionesha kuchanganyikiwa. "Na kipindi kile alikuwa na miaka kumi na tatu tu, sasa saa hivi ana miaka kumi na nane unadhani tutafanyaje na ikiwa ataendelea kukaa uraiani itakuwa hatari kwetu sisi" aliendelea kuongea Ms Helen huku akionyesha kukata tamaa. "Sasa tunafanyaje mkuu" Hansen aliuliza, "wewe nenda kaendelee na mambo mengine" Ms Helen alijibu na Hansen akaondoka.

    "Habari bosi kuna tatizo huku limetokea, naomba kesho asubuhi nije kuonana na wewe" Ms Helen alitoa simu yake na kupiga. Baada kukata simu alibeba begi yake na kutoka ofisini, siku hiyo ilikuwa imeharibika kabisa hata hamu ya kufanya kazi iliondoka kabisa.

    **********************************

    Jitihda za kuzima moto ambao ulikuwa ukiendelea kuitekeketeza Marine Base 71 ziliendelea huku wakijitahidi kuuzuia moto huo usisambae sehemu nyingine. "Mkuu tuna tatizo kubwa, project 75 ametoroka" sajenti Louise aliongea, "ah huyo dogo anatabu sana, tuma boti sita ndogo zifanye msako atakua hajafika mbali" General David alijibu na kutoa amri ziachie boti kadhaa kwa ajili ya kumtafuta project 75. Sajent Louise aliondoka na kuelekea kwenye vikosi maalum vya msako, alitoa amri hio boti sita ziliingiz kazini kumsaka kijana machachari na hatari kuliko wote na hakuwa mwengine bali ni project 75.

    Muda uliyoyoyoma lakini haikurudi hata moja, muda ulizidi kukatika bila kuwepo kwa mawasiliano kati ya wale walikwenda kumtafuta na kambi yao. "Vipi kuna majibu yoyote" aliuliza General David wakati akiingia ofisini kwa na kumkuta sajent Louise huku akiwa amejiinamia. "Habari ni mbaya tu mkuu, nimefanya vile ulivonambia lakini, umepita muda mrefu bila mawasiliano na wale waliokwenda, ndio nikaamua kutuma kikosi kingine kwenda kuangalia lakini wamerudi na boti tano zikiwa na miili iliotapakaa damu halafu mafuta ya boti hizo zote yalikuwa yamekwisha" alijibu sajent Louise.

    "Dah huyu kijana ana balaa kwa kweli," sawa wacha niwasiliane na makao makuu niwape taarifa za kutoweka kwa Project 75" aliongea General David na kwenda moja kwa moja kwenye mkonga wa simu ambao ulikuwa umewekwa pembeni. "Hali ni mbaya kwa kweli, na alietoroka ni Project 75" aliongea kwenye mkonga huo na baada mangezi machache alikata simu na kukaa kwenye kiti chake huku akiwa ameshika kichwa asijue nini la kufanya. Jitihada za kuuzima moto huo zilifanikiwa lakini ulichukua muda mrefu sana hivyo vitu vingi viliteketea. Wanajeshi kwa pamoja walisaidiana kutoa mabaki ya vitu vilivyoungua.

    Marine Base 71 ni moja kati ya kambi kubwa za siri ambazo hazijulikani na raia wa kawaida, ni miongoni mwa kambi ambazo kunafanyika uchunguzi juu ya swala zima la kuweza kuzalisha wanajeshi ambao watakuwa na uwezo kuliko kawaida. Kambi hii ipo katika kina kirefu sana cha maji katika kisiwa kimoja miongoni mwa visiwa vinavyopatikana katika bahari ya Pacific. Kwa jumla kambi kama hiyo zipo zaidi ya kumi lakini hii ndio ilikuwa kubwa kuliko zote. Na serekali imeamua kufungua kambi hizo kwa siri baada ile kemikali aina ya Cindrex ootliviaso deca endroline X (CODE X) kugundilika baada ya aliekuwa mtu wa kwanza kuitengeza kupoteza ushahidi kabisa ili isiendelee kutumika.

    Mwanasayansi huyo aliejulikana kwa jina la Melinda alipoteza ushahidi juu ya kemikali hiyo baada kugundua madhara itakayosababisha ikiwa itaingia mikononi mwa watu wabaya. Lakini kama ilivyoada ya wanasayansi kutokubali kushindwa jambo, walianza kufanya uchunguzi tena kupitia nakala maalum waliopewa na mwanasayansi ambae alimsaliti Melinda na kuuza uchunguzi huo. Kazi haikuwa rahisi katika kufanikisha hilo lakini walijitahdi kadiri ya uwezo huku wakiahidiwa donge nono ikiwa wataitengeza tena. Na ndipo mwanasayansi mmoja anejulikana kwa jina la Dr Hudson alipofanikiwa kuitengeza tena kwa mara nyingine.

    (siku tatu baadae)

    Watu wengi walionekana kukusanyika katika eneo moja kweny fukwe za bahari, walionekana kushangaa kitu fulani na minong'ono ya hapa na pale iliskika. "Hebu mguse labda ni mzima", "hapana usimguse sasa hivi gari ya wagonjwa itafika kumchukua", walisikika watu wakiongea huku kila mmoja akiongea la kwake. Dakika moja mbele gari ya wagonjwa ilifika na bila kuchelewa walishuka na machela kwenda mpaka alipo mlengwa. Kwa uangalifu na tahadhari ya hali ya juu walimnyanyua na kumuweka kwenye machela kisha wakaelekea kwenye gari na safari ya hospitali ikaanza.

    Kutokana na sheria zinavosema kuwa gari ya wagonjwa ikiwa inapita gari nyingine zote zinatakiwa kukaa pembeni kuipisha. Robo saa walikua washafika hospitali, kitanda kilishushwa kwenye gari na kukimbizwa wodi ya wagonjwa mahututi. Madaktari walifika na kuanza kutoa huduma, kutokana na chumvi shati ilikuwa imegandana na mwili hivyo ilibidi ichanwe lakini kwa umakini wa hali ya juu. "Bado moyo wake unapidunda lakini katika kasi ndogo sana" daktari mmoja aliongea, walimpatia huduma za haraka ili kuhakikisha wanaokoa maisha yake. "Doh sijawahi ona binaadamu mwenye roho ngumu kama huyu" aliongea daktari mmoja huku akiwapongeza wenzake kwa kazi nzuri waloifanya, "wakushukuriwa ni Mungu kwa kweli" alijibu daktari mmoja wa kike.

    ****************************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Je kuna taarifa zozote za kuonekana pahali Project 75" Mr Clinton aliuliza, "mpaka sasa hatujapokea taarifa zozote, huenda akawa amezama baharini labda" alijibu Rodriguez, "hahaha unadhani atakufa kirahisi kiais hicho, sisi tusubiri tu maana hata bila kumtafuta atakuja mwenyewe kwetu" alijibu Ms Helen. "Acheni kubishana ujinga nyinyi, mnadhani ni jambo la kukaa tukabishana wakati tunaelewa wazi kuwa akirudi huyu kijana basi maisha yetu yatakuwa hatarini" alifoka Mr Clinton, na wote wakanyamaza kimya. "kesho kutakuwa na kikao cha dharura kuhusu huyu Project 75, wote mnatakiwa mufike, haya tawanyikeni" aliendelea Kufoka Mr Clinton.

    Wajumbe wote wakatawanyika na kurudi katika sehemu zao za kazi. "hallow muheshimiwa raisi, ndio naelewa na tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha tunamtia mbaroni. Sawa mkuu nimekuelewa hakuna shida, nakutakia jioni njema" Mr Clinton alimaliza kuongea na simu kisha akaipiga na chini kwa hasira "naapa ukikamatwa utajuta kuzaliwa mshenzi mkubwa wee" alijisemea huku akitetemeka kwa hasira. "Rose niletee simu nyingine" Mr Clinton aliitwa kwa nguvu na kutoa agizo, papo hapo mlango ulifunguliwa akaingia binti mmoja mrembo sana mwenye asili ya kivenezuela akiwa na boxi jeupe mkononi. Alilifingua na kutoa simu mpaya kisha akaiokota ile ilovonjwa na kutoa sim card kisha akaitia kwenye ile simu mpya. "Bosi tayari simu yako" aliongea kwa taratibu huku akimkabidhi ile simu, "unahitaji kingine chochote" aliuliza. "Nihitaji nitakwambia hebu nitolee sura yako hapa nisije nikakupiga risasi bure" alijibu kwa hasira na Rose bila kuuliza jambo alitoka nje na kurudi katika sehemu yake ya kazi.

    "Dokta yule kijana ameamka" aliingia nesi mmoja ofisini na kusema, bila kupoteza muda dokta aliinuka na kuelekea katika wodi aliokuwa amelazwa Project 75. "Habari yako kijana, mimi naitwa dr Jacob sijui wewe mwenzangu unaitwa nani" alijitambulisha dr Jacob. "Jina langu ni Alex Jr" alijibu Project 75, "hapa niko wapi" kisha akauliza, "uko hospitali" alijibu Dr Jacob. "Najua kama niko hospitali ninachotaka kujua niko nchi gani" alianza kuongea kwa hasira. "Punguza jazba kijana, uko South Africa" Dr Jacob alijibu, Alex Jr alishtuka aliposikia kama yuko South Africa na swali lilomjia ni kuwa amefikaje nchini humo.

    "Hebu tueleze imekuwaje ukakutwa ufukweni" aliuliza Dr Jacob, swali lilikuwa gumu sana hasa ukizingatia hataki kusema ukweli kabisa kuhusu alipotoka "Amm meli nliokuwa nafanya kazi imekutana na dhoruba na kuzama, mimi peke yangu ndio nimefanikiwa kuokoka kwa sababu nilikuwa katika chumba maalum cha kuhifadhia data, chumba hicho huwa kinachelewa kuingia maji na kina mlango wa dharura ambao moja kwa moja unakwenda mpaka zilipo boti za uokozi" kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa akili Alex alifanikiwa kutnga uongo huo na kufanikiwa kuwafanya wote waamini kuwa meli yao imezama. "Basi kwa sasa kuwa na amani kabisa mpaka afya yako itakapokaa sawa ndio tutaanza mchakato wa kuwatafuta ndugu zako" aliongea Dr Jacob. "Nashkuru kwa ukarimu wako" alijibu Alex na kujilaza kitandani huku akipanga nakupangua jinsi ya kutoroka hospitali hapo maana alielewa akiendelea kukaa hapo kutawatia matatizoni wote waliohusika na kumuhudumia.

    "Kuna taarifa yoyote kuhusu project 75" aliuliza Mr Clinton, "hakuna mkuu" Ms Helen alijibu. "Hebu nambieni nyie wote kuwepo hapa halafu mkashindwa kugundua ni wapi alipo huyu mwehu, hivi muna faida gani". "Usijali mkuu tumeshatuma taarifa kwa maagent wetu waliokuwepo pande zote za dunia, tunaamini kuwa atapatikana" aliongea Rodriguez. "Bosi mheshimiwa raisi kashafika" aliingia Rose na kutoa taarifa. "Sawa, jamani tuelekee ukumbi wa kikao".





    "Mr Clinton nategemea kupata majibu ya kuridhisha kutoka kwako" Raisi aliongea na kudhihirisha kuwa amechukizwa na utendaji mbovu wa kazi wa watu hao aliokuwa akiwaamini sana. "Ah kwa kweli mkuu mpaka sasa hakuna taarifa nzuri hata moja" alijibu kiunyonge Mr Clinton. "Shit, siku hizi umekuwa mvivu sana Mr Clinton" alifoka Raisi. "Lakini usijali mkuu tumeshasambaza taarifa kwa maagent wetu wote na tunaamini muda si mrefu tutapata majibu" alijaribu kujitetea Mr Clinton. "Nakupa wiki moja tu, huyo mpuuzi apatikane akiwa hai au amekufa" alifoka Raisi na kisha akainuka na kuondoka. "Dah, yaani huyu bwana mdogo ananitesa kiasi hichi" alijisemea moyoni akiumia kupita maelezo.

    Kikao kiliendelea baada raisi kuondoka, walijadiliana nini cha kufanya wakimpata Project 75. Ndipo wakafikia muafaka kuwa wakigundua sehemu alipo basi watume wauwaji nguli kwenda kummaliza na kurudisha mzoga huo Marekani. Kikao kilimalizika na watu wote wakatawanyika na kurudi majumbani kwao.

    *******************

    "Eti nesi hii ni hospitali gani" aliuliza Alex wakati Nesi akimpa dawa za kupunguza maumivu, "hii ni Cecilia Makiwane Hospital" alijibu yule Nesi, "ah sawa" aliitika na kuchukua vidonge kisha akameza. "Usiku wa leo lazima niondoke hapa" alijisemea moyoni na kuanza kupanga mchakato wa kutoroka, wakati akiendele kupanga alichkuliwa na usingizi mzito kutokana na dawa alizokula.

    "Nimesema muue", "siwezi kufanya hivo, siwezi kumuaa mdogo wangu", "sawa kama huwezi", "wewe shika bastol, haya muue yeye sasa". "hapana siwezi kumuaa kakaangu", "sikiliza mwanangu hii bastola haina risasi, kwa hiyo hapa tunajifunza kutumia tu sawa, sasa ielekeze mbele halafu bonyeza hicho kidude" alianza kubembelezwa, na kwa sababu ya akili ya utoto alifanya hivyo lakini, Ghafla Alex alishtuka kutoka usingizini huku jasho likimtoka. Alipoangalia nje mvua ilikuwa inanyesha ikiambatana na upepo mkali.

    Alianza kuchomoa mashine zote zilizokuwa mwilini mwake na kushuka kitandani. Alipokanyaga tu chini alianguka kutokana na kukosa nguvu kabisa, kwa msaada wa kitanda alisimama na kuangaza pande zote za chumba hicho ndipo akaona kabati. Alisogea mpaka kwenye kabati hilo na kulifungua, alikuta vichupa vingi vya dawa lakini alichukua kimoja tu chenye vidonge vyenye glucose ya kutosha kuzalisha nguvu kwa muda mfupi. Alimeza viwili na kisha akachukua na vidonge vya kukata maumivu, dakika kumi baadae alianza kuchangamka na hapo kazi ikawa imeanza.

    Alisogea mpaka dirishani na kwa bahati nzuri lilikuwa dirisha la kuburizika hivyo kulikuwa nanafasi kubwa ya yeye kupenya. Alipenya nakutoka nje kabisa kwenye varanda, akaanza kutemebea taratibu huku akijitahidi asiteleze. Alifanikiwa kutoka nje kabisa ya Hospitali bila kugundulika, tatizo lilikuwa hajui aende wapi maana alikuwa mgeni katika eneo hilo. "Oya wewe simama" alisikia sauti kwa nyuma, alipogeuka akakutana na sura nyeusi inayotisha "toa kila kitu ulichokuwa nacho" alifoka yule mtu huku akitoa kisu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sina kitu labda nikupe hii gauni la hospitali na vidonge" alijibu Alex, "unasemaje bwana mdogo" alinguruma yule mtu. "Hujasikia au vipi" Alex alijibu kwa dharau. "Unaleta jeuri sio" alifoka yule na kusogea kwa kasi sehemu alipo Alex, Alex alimkwepa na kumsindikiza na teke zito la mgongo. "bwana mdogo hapa sipo bora uondoke tu" aliongea Alex huku akiwa anaondoka, yule mtu alirudi tena lakini wakati Alex hakumkwepa, alimtandika ngumi nzito ya kuromeo na kulivunja. Yule jamaa alianguka chini kama mzigo na kukata moto. Alex hakuchelewa alimvua nguo na kuzivaa kisha akatafuata njia na kuondoka eneo hilo.

    "Dr yule kijana ametoroka" Nesi aliwasilisha taarifa hizo punde tu baada Dr Jacob kufika ofisini, "eti nini" Dr Jacob aliuliza kwa mshangao. "Duh ngoja niwasiliana na polisi kwanza" aliongea kisha akatoa simu na kupiga polisi, muda si mrefu walifika hospitalini hapo na kupewa taarifa zote pamoja na picha alipigwa wakati hajitambui. Baada hapo polisi walipiga simu katika vituo mbali mbali kuwapa taarifa pamoja na kutuma picha za Alex.

    "Mkuu kijana yuko South Africa" ujumbe uliingia katika simu ya Mr Clinton, na bila kuchelewa akampigia simu Helen na kumueleza. Baada ya mazungumzo hayo, Helen alitoa simu nyingine na kupiga, "halo, Gerald kuna kazi, kuna kiti moto huko South Africa tunataka ukichinje" alimaliza kuongea na kukata simu. Baada kupokea agizo hilo Gerald ambae yuko Durban South Africa alichukua vifaa vya kazi na safari ya kuelekea alipoelekezwa ikaanza. "Halo Dr Jacob, mimi ni Alex na naomba unisikilize kwa makini. Jambo ulilolifanya linahatarisha maisha yako hivyo fanya kama nitakavo kwambia. Akija mtu yoyote kukuuliza kuhusu mimi mwambie kila kitu usimfiche hata kimoja maana hiyo ndio njia pekee ya wewe kuokoa maisha yako" simu ilikatika bila Dr Jacob kuongea chochote.

    "Asante kwa msaada wako" Alex aliongea wakati akimrudishia simu dada mmoja ambae alimuomba kisha akaondoka. Kwa sababu alikuwa na vidonge vya glucose hakupata tabu ya kutafuta chakula.

    "Habari za kazi dada" Gerald alimsabahi, "nzuri nikusaidie nini" alijibu. "naomba kuonana na Dr Jacob" aliongea, "leo hana appointment na mtu" alijibu dada huyo lakini alihisi kitu kama cha baridi kikimgusa mkononi. "Na wewe leo huna appointment na Mungu lakini nitakupeleka hivyo hivyo ukamuone" Gerald aliongea huku akimgusa mkono kwa bastola yake. "nenda chumba upande wa kushoto" yule mschana alijibu huku akitetemeka, "mtoto mzuri hawi mbishi na ole wako useme kitu" Gerald aliongea na kuirudisha bastola yake kweye koti kisha akaondoka na moja kwa moja mpaka ofisini kwa Dr Jacob.

    "Habari za saa hizi Dr" aliongea wakati akifunga mlango. "sina ahadi ya kukutana na yoyote yule" alijibu bila kuangalia. "mimi pia huwa sina ahadi ya kukutana na mtu siku zote lakini nikitaka tu huwa nakutana nae" Gerald aliongea kisha akatoa bastola na kuiweka kwenye meza. Dr Jacob alishtuka baada kuiona na kukumbuka maneno ya Alex. "naomba unieleze kila kitu unachojua kuhusu kijana uliemtibu hapa" aliongea Gerald. "Mimi natibu watu wengi hapa siwezi kuwakumbuka wote" Dr Jacob alijaribu kucheza na nyoka. "Narudia kwa mara ya mwisho la sivyo ntakufanya kitu ambacho utajuta maisha yako yote" Gerald alifoka kwa hasira.

    Dr alipoona hali sio akakubali kutoa ushirikiano, alimueleza kila kitu bila kumficha hadi mwisho. "Dr asante kwa ushirikiano wako na nakutakia kazi njema" Baada kuridhika na maelezo hayo Gerald alishukuru na kuondoka. "Duh binaadamu wengine hawana hata chembe ya huruma" Dr Jacob alijisemea moyoni na kutoa kitambaa kwa ajili ya kujifuta jasho lilirowanisha koti lake japo ndani ya ofisi yake kulikuwa na AC.

    "Halow mkuu, ndio nimeshamaliza hatua ya kwanza, sasa naingia mitaani kumtafuta. Usijali mkuu kazi itakwisha tena kwa haraka tu" Gerald alipiga simu na kutoa taarifa hizo, alimaliza kuongea na kurudi kwenye gari yake na kuondoka eneo la hospitali. Alex akiwa mitaani anazurura kama mtu ambae anatafuta kitu, ghafla anashangaa watu wanaanza kutimua ovyo, wenye maduka wanafunga, wenye migahawa wanafunga na kila mtu anatafuta pa kujificha.

    Alijikuta amebakia peke yake ambae amesimama barabarani, "wewe ndio unajifanya nunda eenh" alisikia sauti nzito ikitokea nyuma. "Halafu anaonekana kama nguruwe hivi" aliongea mwengine lakini kwa lugha ya kimila, "nguruwe ni wewe mweneyewe" Alex alijibu kwa kimila hivohivo na kuwashangaza wale waliovamia. "Huyu dogo anataka kufundshwa adabu kidogo" aliongea jamaa mmoja ambae alionekana kama ni mkuu wa kikosi hicho.

    "Amose hebu mtengeze huyu dogo" yule kiongozi aliongea, lilitoka jitu moja kubwa sana na jeusi lenye kutisha ile mbaya. Alex alirudi nyuma kidogo kwa ajili kupata nafasi ya kumsoma mpinzani wake. Alimuangalia kwa makini wakati anakuja mbio upande wake, alipomkaribia tu, Alex alimkwepa na kusogea pembeni. Lile jiti likageuza na kumfata kichwa kichwa, Alex alikunja ngumi na kukaza miguu, lilipomfikia tu alivurumisha masumbwi manne ya nguvu iliompata kwenye sehemu ya maungio ya bega na kufanikiwa kumtegua mikono yote miwili.

    Alex alirudi nyuma ili amalize kazi lakini kabla hajafanya hivo alisikia mlio wa risasi na alipoangalia vizuri alimuona yule kiongozi wa kundi hilo akianguka chini huku akiwa na tobo katika paji la uso. Kwa kasi ya ajabu alimsogelea yule aliekuwa kipigana nae na kumgonga shingoni katika mshipa wa fahamu na kumfanya azimie.

    Moto ulianza kuwaka kati ya wale majambazi na mtu aliempiga risasi kiongozi wao, lakini mtu huyo alikuwemo ndani ya gari na alifanya mashambulizi yote akiwa ndani ya gari. Alex aliangalia mpambano huo kwa umakini na akagundua kuwa wanaepambana nae ni mtu aliyebobea. "hamuwezi kushindana nae huyo, atawamaliza wote bora mukimbie" Aliongea kwa nguvu kisha akachomoka mpaka walipo wale majambazi, "nipeni silaha, huyo hamumuwezi na ananitaka mimi" aliongea Alex na kuwashangaza wote pale, "okoeni maisha yenu, huyo niachieni mimi" aliendelea kusisitiza Alex.

    Walikubali na kumpatia bunduki moja kubwa aina ya AK 47 na bastola mbili ndogo, "sasa pambana na mbabe mwenzio" Alex aliongea na kulenga tayri ya mbele ya gari ya anaewashambulia, alifyetua risasi na kuipasua tairi hiyo. Gari ilisimama na yule mtu aliekuwa ndani akashuka, naam hakuwa mwengine isipokuwa Gerald. "Project 75 bora ukubali yaishe, maana nimeambiwa nipeleka mzoga wako" aliongea huku akicheka, "mi nahisi wamekutoa kafara tu maana wao wenyewe wananitambua mimi nani" Alex alijibu, "tutaona" Gerald alijibu na kuanza kumimina risasi.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Alex alitulia na kumuacha japo azifaidi risasi zake ili atakapomuua asije akalalamika hajazitendea haki risasi zake. "acha kujificha kama mtoto wa kike" Gerald aliropoka, "unajua ningekuwa mimi ndio wewe ningekimbia tu tena kama mbwa koko na mkia wangu katikati ya miguu" Alex alimjibu kwa kumkejeli. Maneno hayo yalimkera sana Gerald, na kujikuta akitoka kichwa kichwa sehemu amabayo alikuwa amejificha ila kitu ambacho hakukitambua ni kuwa tayari alikuwa kashalalengwa na Alex. Kitendo cha kutoa sura tu Alex alimchapa risasi ya uso, "nilikwambia mimi ukadhani nakutania, nenda kwa amani na Mungu akulaze mahali panapostahiki amen" Alex aliongea huku akisimama na kuelekea ulipo mwili wa Gerald, alimsachi na kuchukua simu kisha akapiga. "ehe kazi imekwendaje" Mr Clinton alipokea kwa shauku ya kutaka kujua, "kazi imekwenda vizuri sana,nimeshamuua Gerald na sasa nasubiri mwengine chambo mwengine mtakaemtuma, lakini kaeni mkao wa kula nikishawamaliza nyungunyungu wenu nawafuata nyinyi" Alex aliongea na alipoaliza akavunja simu.

    Alikwenda mpaka walipojificha wale majambazi na kuwakabidhi silaha zao, "unakwenda wapi" aliuliza mmoja wao. "naenda zangu" alijibu kimkato, "umetusaidia leo tunaomba uje na sisi" aliongea yule mmoja wao. Alex alikubali na kwa pamoja walisaidiana kumbeba Amose na kumuingiza kwenye gari na safari ikaanza.

    *****************

    "ah, fuck" Mr Clintona aliropoka kwa nguvu na kutoa bastola kisha akavunja vioo na tv katika ofisi yake, "bosi punguza hasira" Rose aliingia ndani na kumuomba. "huy Alex huyu mwanaharamu mkubwa, hebu ita kikao cha dharura" aliongea na kutoa amri.Dakika kumi walikuwa kwenye kikao. "jamani taarifa ni mbaya, Gerald ameuwawa" aliongea Mr Clinton, "mi niliwaambia Project 75 ni namba nyingine" Alijibu Helen. "mimi nahisi nina wazo" Rodriguez alisimama na kuongea, "haya tuambie wazo lako" Mr Clintom alijibu. "kwa nini tusiwatumie wengine ambao ni kama yeye" Aliongea lakini kwa kusitasita, "unamaanisha tuwatumie Project waengine" Aliongea Mr Clinton. "ndio, labda tutaweza kufanikiwa kumkamata" alijibu Rodriguez. "wazo zuri lakini sidhani maana Project 75 ndie pekee ambae amemaliza mchakato wote wa CODE X" Helen aliongea. "nafahamu hilo lakini huyu kwa kuwatuma wauwaji wa kawaida kamwe hatutaweza kumkamata" Aliongea Rodriguez. "sawa nimelisikia wazo lako na nitalifanyia kazi" Aliitika Mr Clinton, kila mtu alitoa wazo lake na mwisho walikubaliana wakutane baada siku tatu kwa ajili ya majibu na kikao kikavunjwa. Mr Clinton alirudi ofisini kwake akiwa hana hata hamu ya kufanya kazi, "Rose njoo mara moja" alinyanyua mkonga wa simu na kumuita secretary wake. Baada ya kukata tu simu Rose aliingia "nikusaidie nini mkuu" aliongea, "njoo karibu" Aliongea kiupole Mr Clinton. Rose baada kusikia hivo alijua ni kitu gani amekusudia bosi wake, kila Mr Clinton alipokuwa anahasira alimuita Rose na kufanya ne mapenzi kama sehemu ya kupunguza hasira na kujiliwaza. Japo Rose alikichikia sanakitendo hicho lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali maana Mr Clinton ndie aliemfanyia mchono mpaka akafikia pale alipo.

    Basi mwanadada huyo alifunga mlango na kusogea mpaka katika meza ya bosi wake, na bila kuchelewa Mr Clinton alimvamia na kutekeleza haja yake mpaka aliporidhika. Rose alivaa nguo zake na kutoka ofisini, "Afadhali sasa" Mr Clinton alijisemea moyoni. Rose alielekea mpaka chooni na kuanza kulia maana tabia hiyo ya bosi wake ilimkera sana, yeye kufanywa kama chombo cha kujiliwazia "ipo siku utalipa kwa unacho nifanyia" Rose alijesemea moyoni na kujiweka sawa kisha akarudi katika sehemu yake ya kazi. Siku hiyo ilimuendea vibaya sana maana mpaka muda wa kutoka ofisini unafika tayari alikuwa kashafanya mapenzi na bosi wake mara nne. Na wakati anatoka Mr Clinton alimuita tena na kupata cha kuondokea. Kwa kweli hakuna siku aliodhalilika binti huyo kama siku hiyo. "kila kitu kina mwanzo na mwisho wake" alijisemea moyoni akiwa kwenye gari yake kuelekea nyumbani kwake, "na leo ndio mwisho wa manyanyaso haya" aliongea na kuzidisha mwendo wa gari lake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Siku ya pili mapema katika taarifa za habari kulikuwa na habari moja iliosema" ajali mbaya imetokea na gari hiyo inasadikika kuwa ni ya dada mmoja anaejulikana kwa jina la Rose, chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa akiendesha mschana huyo".

    "Kweli ni yeye au wamekosea" aliongea Mr Clinton baada kusikia taarifa hiyo, "ndio mkuu na ushahidi tushaupata" alijibu Martin. "Ah sawa kazi ya Mungu haina makosa" alijibu huku akioenakana mwenye hzuni sana. Na kwa vile hakuwa na ndugu karibu serekali ilisimamia maziko yake, na yalipokamilika waliomboleza kwa siku kadhaa na kila mtu kurudi kazini kuendelea na kazi yake.

    "Karibu Alex hapa ndio nyumbani" aliongea mmoja kati ya wale vijana walioondoka na Alex, "mimi naitwa Leonard" alijitambulisha, "yuko wapi yule mwenzenu niliepambana nae" Alex aliuliza. "tumemlaza ndani" Leonard alijibu na Alex akaomba aonyeshwe chumba alicholazwa. Aliingia na kuanza kumnyoosha zile sehemu alizomtegua, wengine walikaa kimya wakimuangalia anachokifanya. Amose alipiga kelele za maumivu makali sana aliyoyapata wakati Alex anayarudisha mabega sehemu yake.

    "Tayari, pumzika kwa sasa baada masaa mawili utakuwa sawa" Alex aliongea na kusimama. "Hivi wewe ni mtu wa aina gani" aliuliza kijana mmoja, "ah mimi ni mtu wa kawaida tu" Alex alijibu huku akimshika kichwa kijana huyo ambae alionekana kufurahia kitu hicho. "Hivi kwanini mumeamua kufanya hivi, kwanini mnakuwa waharibifu" Alex aliuliza wakati akikaa kwenye kigogo cha mti. "inabidi tufanye hivi ili tule, maisha yetu ni magumu sana" Leonard alijibu, kwa sasa alionekana kama kiongozi baada kiongozi wao kupigwa risasi na Gerald.

    "Sio lazima muibe ili mule, nyie kama mimi bado ni vijana mna nguvu za kutosha kufanya kazi na kujikomboa kimaisha kuwa vibaka sio suala jema kabisa" Alex aliongea kama mshauri sasa, "na wewe kama nani unatuambia hivo" jamaa mmoja aliongea kwa hasira. "mimi, mimi ni mtu mmoja mbaya na hatari sana, na hapa nilipo natafutwa na jeshi la America" Aliwavunjia dafu kisha akaendelea "mimi najaribu kutafuta maisha ya kawaida nimechoka maisha ya kuwa mtumwa wa ujinga, sasa nawashangaa nyie mna ardhi nzuri hapa, mnaweza hata mkalima na kupanda miti ambayo inazaa mapema, mkauza mkapata pesa japo za kula".

    "Laiti mimi ningekuwa katika nafasi yenu wala nisinge hangaika kutafuta silaha na kukaba watu, rafiki zangu bado mnayo nafasi ya kurekebisha makosa yenu" Alex alisisitiza. "Kwani we huna fursa hiyo" Leonard alimuuliza, "sina kabisa, muda wowote ntakamatwa na adhabu yangu itakuwa ni kifo tu" Alex alijibu. "Kwa sasa kaa na sisi hapa" Leonard aliongea na Alex akakubali.

    ************************************

    "Karibu Russia madam, mimi naitwa Nikolay" aliongea mwanaume wakati akimpokea mwanadada mmoja mrembo sana. "Asante mimi naitwa Christine" alijibu mwanamke huyo na kuingia kwenye gari, Nikolay aliweka mizigo kwenye buti na yeye akaingia kisha akampa dereva ishara waondoke. "kila kitu nilichoagiza kipo tayari" Christine aliuliza, "ndio madam kila ulichosema kipo" Nikolay alijibu. Safari iliendelea kwa muda mrefu sana mpaka walipofika katika nyumba fulani nje kidogo ya mji wa Moscow.

    "Hii ndio nyumba ulioagiza" Nikolay aliongea kisha Christine alishuka kwenye gari na kuingia kwenye nyumba hio. "Ni nzuri sana na inanifaa" Aliongea baada kuridhika na ukaguzi mfupi aliofanya, baada ya hapo Nikolay alirudi kwenye gari na kushusha mizigo yote na kuingiza ndani. Alipomaliza Christine alimlipa kiasi alichokihitaji cha feha na kumuongeza kidogo ili kumfunga mdomo. Nikolay aliaga na kuondoka, "sasa subiri niwaoneshe mimi ni nani" aliongea Christine huku macho yake yakirowa machozi. Christine hakuwa mwanamke mwengine bali alikuwa ni Rose ambae inasadikika amekufa mwezi mmoja nyuma.

    Katika ajali ambayo inasadikika kuwa amekufa hakuwa yeye bali ilikuwa ni mtu ambae ametengenezwa na kufanana na yeye kabisa kila kitu, hiyo ni kazi malum aliokuwa akiisimamia yeye mwenyewe kama njia moja wapo ya kufanikisha lengo lake la kutoroka kwa kufeki kifo. kabla ya ajali ile alipita katika sehemu ambayo kazi ile ilikuwa ianendelea, aliwauwa wote waliohsika na kutengeneza sanamu hilo ili kujihakakikishia usalama. Baada hapo aliliingia kwenye gari na kuondoka.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipofika karibu na daraja moja hivi, alishuka kwenye gari na kulihamishia lile sanamu ubande wa dereva kisha akachukua kibao kizito na kukiweka kwenye sehemu ya kukanyagia mafuta na kuliacha gari likaenda kugonga kwa nguvu kwenye vyuma vya dara hilo. Baada hapo alikwenda mpaka ilipo gari kisha akatoa mfuko wa kihifadhia damu ambapo ndani ya mfuko huo kulikuwa na damu yake mwenyewe na kulimwagia sanamu hilo na nyingine akamwaga katika kioo cha mbele na nyengine akaeneza kwenye dashboard. Kisha akaliwasha moto na kuhakikisha linateketea lote.

    "Kazi nzuri" Alex aliongea baada kutoka shambani na wenzake ambao aliwachukulia kama ndugu zake, ni mwezi mzima umepita sasa tokea Alex awe nao. "Leonard nahisi muda wangu wa kuondoka umefika" alimwita rafiki yake kipenzi pembeni na kumueleza. "Mbona mapema sana, tumeshakuzoea" Leonard alijibu kwa masikitiko, "nikiendelea kukaa hapa nyinyi nyote mtakuwa hatarini sana, hivyo kuwaokowa nyinyi inabidi niondoke" alijaribu kumueleza uhalisia wa mambo.



    "Siwezi kukaa sehemu moja zaidi mwezi, ni lazima nibadilishe makazi mara kwa mara" alizdi kumuelewesha mpaka mwisho akaelewa. "Lakini ongeza japo wiki moja tu" Leonard alimuomba na Alex akakubali japo shingo upande maana machale ya hatari yalishamcheza. Walirudi na kuungana na wengine kwa ajili ya kupata chakula cha jioni.

    "Taarifa zozote juu ya Project 75" aliuliza Mr Clintona wakati wakiwa kwenye kikao, "ndio tumefanikiwa kugundua sehemu alipo ila bado tunataka tupate uhakika" alijibu Martin. "Vizuri sana kijana" Mr Clinton aliongea huku akitabasamu. Kikao kiliendelea mpaka kilipofikia tamati na kila akatawanyika. Mr Clinton alirudi ofisini kwake huku moyo wake ukiwa umejawa na furah baada kusikia kuwa sehemu aliokuwepo Project 75. "ngoja uone nitakachokufanya mpuuzi mkubwa wewe" alisema kwa nguvu mpaka akajishtukia.

    "Leonard usigeuke na nisikilize kwa makini, kuna mtu anatuftilia na bila shaka atakuwa mpelelezi. Sasa fanya hivi wewe pita njia yako na mimi nipite yangu tukutane nyumbani" Alex aliongea baada kushtuka kama wanafatiliwa. Leonard alikubali na kila mtu akaelekea njia yake, yule aliekuwa akiwafatilia alielekea upande aliokwenda Alex. Alex alitembea mpaka sehemu yenye viti vya kupumzikia na yule mtu alifika pale akakaa pembeni yake na kuweka bahasha kisha akainuka na kuondoka.

    Alex aliichukua bahasha hio na kuondoka eneo hilo, alitembea mpaka alipofika sehemu ambayo alihisi ni salama na kuifungua. Alikuta vipande vya simu, alivitoa na kuiunga simu kisha akaiwasha, muda mfupi baada kuwaka simu ilianza kuita. "we nani" aliuliza baada kupokea, "punguza jazba kijana" upande wa pili wa simu ulimjibu, "najua hunijui lakini mimi nakujua na niko tayari kukusaidia kama utataka".

    "Sitaki msaada wako" Alex alijibu kwa hasira mpaka wapita njia wakamuangalia, "ni sahihi kabisa kutomuamini mtu, lakini niamini nataka kukusadia tu". "utanisaidiaje, jisaidie mwenyewe kwanza", "kwa sasa wewe huko hatarini ila rafiki zako wako hatarini kwani tayari wanaokusaka washajua uko wapi, na wala usihangaike kurudi kwani utakutana na miili tu ya marafiki zako"

    ********************

    "Sisi tunataka mtueleze tu Project 75 yuko wapi" Project 52 aliuliza kwa mara nyingine tena, "sisi hatumjui huyo project 75" Amose alijibu. "Naona hawa madogo wanajifanya manunda" Project 66 aliongea huku akikoki bastola yake. "Basi kama hawajui, wacha tuache salamu tu akija atatutafuta" Project 78 aliongea na kuwamiminia risasi wote. Yote hayo yanafanyika Leonard akiwa anashuhudia kwa mbali, alipotaka kwenda alizuia na mtu, alipogeuka alikutana na Alex. "Usiende watakuuwa na wewe, tuondoke eneo hili" Alex alimnong'oneza, "wamewauwa ndugu zangu na wao lazima wafe" Leonard aliongea kwa hasira huku machozi yakimtoka.

    "Leonard kuwa mwanaume shupavu, kubali leo ipite ili ujipange na kesho" Alex alizidi kumsihi rafiki yake huyo. Leonard alikubali na kuondoka eneo hilo, wakiwa njiani simu iliita tena. "unataka nini" Alex aliongea kwa gadhabu, "nenda mpaka pale ulipopewa bahasha kuna gari aina ya jeep, chukua hio gari na angalia tv yake utakuta ramani itakayokuelekeza katika hoteli" kisha simu ikakatika. "Leonard tukazane wasije wakatukuta njiani, hao jamaa hawajui utani hata kidogo" Alex aliongea huku akizidi kukazana nae Leonard alifanya hivo. Walifkika mpaka sehemu aliyopewa bahasha Alex na kukuta Jeep kama alivyoelekezwa.

    Alifungua mlango na kuingia kisha akamfungulia Leonard nae akaingia, alipowasha tu ikatokea ramani kwenye kitv cha gari hio. Aliweka gia na kuondoka, njia nzima Leonard alikuwa akilia mpaka walipofika katika hoteli ilioonyeshwa kwenye ramani. "Leonard futa machozi mtu wangu, ukiendelea kulia haitakusaidia chochote kile" Alex aliongea akijaribu kumnyamazisha. Leonard alifuta machozi na wote wakashuka kweny gari na kuelekea mapokezi, "jina tafadhali" mtu wa mapokezi aliuliza baada salamu, Alex alishindwa aseme jina gani na ghafla ukaingia ujumbe kweny simu yake na alipoangalia akakuta ni jina lake. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Jina ni Alex Jr" alijibu, "karibu sana Mr Alex jisikie uko nyumbani" alijibu yule mtu wa mapokezi na kumkabidhi funguo Alex. "Asante" Alex alijibu na kuondoka, moja kwa moja alielekea mpaka chumba chenye namba iliokuwepo kwenye ufunguo. Alifungua na wote wakaingia ndani, Leonard alikaa chini na kuendelea kuomboleza. "lia mpaka uridhike" Alex aliongea na kuingia chooni kwa ajili ya kuoga, alimaliza na kurudi ndani. Alifungua kabati na kutoa suti moja kali na kuvaa. "Leonard kaoge tuje kupanga mpango wa kulipa kisasi" Alex alimwambia, hiyo ilikuwa kama shoti kwa Leonard maana alisimama na bila kupoteza muda aliingia chooni na kuoga. Alipotoka alikuta suti kwenye kitanda ikiwa na kikaratasi "pendeza kwanza". Alivaa suti hiyo na kuonekana kama inamusha hivi kwa sababu ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuvaa suti tokea azaliwe.

    Dakika kumi Alex alirudi na chakula na wote wakala na kunywa hadi wakashiba, "sasa kichaa wangu nambie wapi nitapata silaha nzito nzito" Alex alimuuliza Leonard. "Yako machimbo mengi tu kama uko tayari tuende" Leonard alijibu akionekana mwenye furaha. "Sasa mbona unaendelea kukaa" Alex aliongea akiwa kashasimama, Leonard aliinuka na kwa pamoja wakatoka mpaka nje ya hoteli hiyo. Walielekea mpaka kwenye maegesho ya gari na kuingia kisha Alex akalitoa gari hilo kwa fujo mpaka walinzi wakashanga. Kwa uenyeji wa Leonard katika mji huo mashariki mwa South Africa walifanikiwa kufika eneo husika bila shida yoyote ile.

    Walishuka kwenye gari na kuingia ndani wakifuata vichochoro kadhaa mpaka walipofika katika nyumba moja hivi ambayo kwa nje tu unakaribishwa na moshi wa bangi. "nisubiri hapa nikaongee nao" Leonard aliongea na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Baada dakika tano alirudi na kumfanyia ishara Alex amfate, "karibu ndugu tumesikia unataka vitu vizuri basi hapa ndio kwao. Tuna kuanzia bastola ndogo ndogo mpaka makombora, wewe tu mkwanja wako" aliongea mtu mmoja mwenye rasta chafu hivi huku mkononi akiwa na kipande cha bangi.

    "Asante hebu kwanza nipatie hicho kipisi cha bangi kilichobakia nishtue ili nipate mzuka wa kuchagua" Alex aliongea huku akinyoosha mkono, kama ilivo ada ya rasta ni watu ambao wako na amani sana, alimpa kipande na Alex akapiga mafunda ya fasta huku akitoa moshi kama jiko la kuni zilizorowa maji.

    Baada kupata pafu kadhaa, alisogea mpaka ilipo mitutu na kuanza kuchagua, aliendelea na zoezi hilo mpaka aliporidhika "hizi kwa sasa zitafanya kazi yangu" Aliongea Alex huku akiweka mitutu kadhaa kwenye meza. Yule jamaa aliziangalia kwa makini kisha akamuangalia Alex, "unavoonekana umebobea kwenye kuchagua silaha nzuri na makini" aliongea kisha akamtajia bei. "Leonard nenda kwenye gari kuna begi jeusi njoo nalo" Alex aliongea na Leonard bila kuchelewa aliondoka na haukupita muda alirudi akiwa na begi jeusi mkononi.

    "Kuna pesa kwenye begi hili, angalia kama zitakutosha au nikuongeze" Alex alilisogeza lile begi karibu na muuzaji. Alilifungua na kuziangalia kisha akatabasamu, "usiwe na wasi wasi zinatosha hizi" alijibu na kusimama. "Nimefarijika kufanya biashara na wewe Mr Alex" Aliongea na kumpa mkono, "hata mimi nimefarijika, ni mategemeo yangu tutaendelea kufanya biashara vizuri zaidi huko mbeleni" alijibu Alex huku akitabasam.

    Baada ya hapo walibeba dhana zao za kazi na kuondoka, "tunarudi hotelini au vipi" Leonard aliuliza. "Hapana kurudi kule ni kujipeleka katika mdomo wa mamba, wale jamaa watakuwa washaajua kama tuko pale hivyo watakwenda kututafuta. Ila kwa sababu saa hivi ni usiku sana watafika pale mapema asubuhi na wataelekea chumbani kama wahudumu wa hoteli" Alex alimjibu huku akizidi kukanyaga mafuta. "Sasa tunakwenda wapi" Leonard aliuliza tena, "tunaelekea kule kule hotelini lakini tutakaa kwenye gari" Alex alijibu huku akizidisha umakini kweny usukani.

    Walifika mpaka karibu na hoteli waliofikia mwanzo lakini walikaa mbali kidogo na kupaki gari katika maegesho ya barabarani na kupumzika. Kutokana na uchovu usingizi mzito ulimchukua Leonard, Alex hakulala kabisa usiku huo alikuwa akiandaa silaha ambazo atazitumia asubuhi kutuma salamu kwa wanaomfatilia maisha yake. Kulipambazuka "oya umelala sana kumekucha kaka" Alex alikuwa akimuamsha Leonard ambae alionekana kuwa na usingizi mzito.

    "Ah mapema kaka wacha nipatilize kidogo" Alijibu kivivu, "oya acha zako wewe, amka upashe mwili kuna kibarua kizito" Alex alizidi kumkera mpaka Leo akaamka na kushuka kwenye gari kwa ajili ya kupasha. Wakati Alex akiendelea na maandalizi yake, alichungulia nje na kwa mbali aliwaona maadui zake wakiingia katika ile hoteli. "Leonard ingia kwenye gari haraka" Alex aliongea kwa sauti kubwa na Leonard akaingia. "unaweza kazi ya utunguaji (sniper)" alimuuliza, "ndio ila si sana" Leonard alijibu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa chukua hili begi na panda juu kabisa ya gorofa hili, ukifika kaa usawa na dirisha la pili kutoka kushoto halafu jipange" Alex aliongea na kumkabidhi begi Leonard. "chukua na hiki kifaa, kitatusaidia katika mawasilino" Alex aliendelea kuongea na kumkabidhi kidude fulani hivi. Leonard alikipokea na kukiweka sikio la kushoto kisha akashuka kwenye gari na kuelekea alipoambiwa.

    Alex alichukua kila alichohisi kitamsaidia na yeye pia akashuka kwenye gari na kuelekea hotelini, moja kwa moja alielekea mpaka gorofa ambayo chumba chake kilikuwepo. Alitembea kwa umakini mpaka katika mlango wa chumba chake, na kwa umakini wa hali ya juu aliuchunguza mlango huo ili ahakikishe kama walishafika chumbani kwake au laa. Aliporidhika kuwa hawajaingia alifungua na kuingia kisha akaufunga na kusimama mbele, "unaniona nilipo" aliongea, "nakuona kaka" Leonard alijibu. "Basi wa kwanza akiingia atasimama hapa, atakuwa anaangalia dirisha. Usimruhusu akainua kichwa, akisimama tu mpasue kichwa au mchimbe moyo" Alex alimueleza Leonard kwa umakini.





    "Nimekusoma mkubwa" Leonard alijibu huku akiikoki bunduki yake. Baada kama dakika tano hivi mlango uligongwa lakini Alex hakujibu "jiandae" aliongea kwa sauti ya chini, "on position" Leonard alijibu. Baada kuona kimya mlango ulifunguliwa taratibu na project 52 akawa wa kwanza kuingia. kama alivyotegemea Alex, baada kuingia tu alisimama mbele ya mlango na Leonard hakufanya makosa alimchapa risasi ya kichwa. "vizuri sana kijana" Alex aliongea, "sasa we tulia hapo na usome mchezo kupitia darubini yako, kuwa makini ntakuuliza baadae" Alex aliongea na kucheka kwa sauti ya chini. "umesomeka mkuu" Leonard alijibu huku akicheka kwa nguvu kidogo.

    Alex alikuwa amejifcha ndani ya kabati la nguo, akiwa na mitutu mkononi. Baada Project 52 kutandikwa risasi, waliokuwa nyuma yake walisita kuingia kwa sekunde kadhaa. Mlango ulisukumwa taratibu na kwa umakini wa hali ya juu, alitangulia project 66 ambae ni mwanamke na kufuatiwa na project 78. "atakuwa kajificha wapi huyu mwehu" aliongea Project 66, "kwa akili zake huyu atakuwa amejificha nje katika varanda" Alijibu project 78 na wote wakaelekea varanda.

    Muda wote Alex alikuwa akiwasikia na alitamani kucheka "wapumbavu sana hawa, ina maana hawakucheza hata kombolela walivokuwa wadogo. Ah lakini sishangai sana kwa sababu haya ndio madhara ya kulelelewa kama makuku ya nyama hata yakitolewa nje ya banda yanashindwa hata kutafuta chakula" aliongea hayo moyoni huku akitabasamu. Walipofika mmoja aifungua dirisha na kuchungulia lakini hakuona mtu, hapo Alex alitoka kwenye kabati na kumimina risasi huku akitafua sehemu ya kujifcha.

    "Aghh" ulisikika ukwenzi wa maumivu na ghafla project 66 alianguka chini na kusogea pemebeni kwa ajili ya kujificha. Kisha aliangalia sehemu aliopigwa risasi na kusema "unadhani utatoka leo", "swali hilo ujiulize mwenyewe" Alex aljibu huku akibadilsha magazine na kuweka ambayo imejaa risasi. "Project 75 kubali kama umeshindwa na hatutakuuwa" project 78 aliongea huku akijaribu kuchungulia, lakini mara alikoswa na risasi. "Duh huyu jamaa ni balaa" alijisemea moyoni, "project 66 vipi unaweza kuendelea na mpambano" aliuliza project 78.

    "Mimi mbona niko sawa" alijibu huku akijiweka sawa, baada kuongea hivo aliinuka na kuanza kushambulia hovyo n Alex aliitumia nafasi hiyo kumueka matobo kadhaa upande wa moyo. "Project 66 amepigwa risasi" Project 78 aliongea, "fanya lolote utoke humo ndani" upande wa pili ulijibu. "Sawa mkuu" Project 78 alijibu, alichomoka alipokuwa amejificha huku akipiga risasi bila mpango lakini Alex alitulia akisikiliza sauti ya bastola inaeleka upande gani.

    Project 78 alifanikiwa kufika mlangoni, aliurukia na kuanguka nao nje kisha akainuka na kuanza kukimbia. Alex hakuchelewa aliinuka na kuanza kumkimbiza, Project 78 alikimbilia mpaka kwenye ngazi na kuanza kushuka. Alex alikuwa nyuma nae akimfukuza bila kupiga risasi akiepuka asije akapiga mtu asie na hatia. Watu wote waliokuwa wakitumia ngazi walikaa pembeni baada kuona wawili hao wakikimbizana na bastola mikononi. Project 78 alifanikiwa kufika chini kabisa lakini bahati ikawa mbaya kwake alijikwaa na kuanguka, bastola yake ikaangukia mbali kidogo na alipodondoka.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipojaribu kuinuka aifate alijikuta akichezea teke zito la tumbo. "Mimi nilidhani una ubavu wa kupambana na mimi kumbe ni mbwa koko tu" Alex aliongea kwa kejeli, aliirudisha bastola yake kiunoni na kumuinua. Alianza kumtembeza kichapo,kila Project 78 alivojitahidi kuzuia mashambulizi hayo alijikuta akichezea ngumi zisizi na idadi. Bahati nzuri alifanikiwa kuponyoka mikononi mwa Alex na kumkimbilia mschana na kumuweka kama ngao "ukinisogelea namuua huyu" aliongea kwa tabu kidogo.

    Wakati Alex anafikiria nini cha kufanya ghafla project 78 alianguka chini huku akiwa na tobo katika paji la uso. "usiwaze sana kaka, kazi imekwisha" Leonard aliongea huku akiiangalia bomba ya bunduki iliyokuwa inatoka moshi. "Kazi nzuri, sasa tukutane kwenye gari haraka" Alex aliongea na kuanza kukimbia, alifika kwenye gari na sekunde kadhaa mbele Leonard alifika na kuingia. Alex aliiondoa gari kwa kasi ya ajabu sana, "ni lazima tutoke nje ya mji kwanza" aliongea huku akiwa makini na barabara. "Hakuna shida we nyoosha tu hiyo njia" Leonard alijibu, Alex aliongeza mwendo na kufungulia mziki kabisa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog