Simulizi : C.O.D.EX. 2 (The Dirty Game)
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**************
"Tumepoteza mawasiliano na project 78" Ms Helen aliongea huku akivua kifaa maalum cha mawasiliano, "shit" Mr Clinton alifoka. "Huu ni mwanzo tu, hali ikiendelea hivi sisi wote vibarua vyetu viko mashakani kuota nyasi" aliendelea kuongea. "Tupunguze jazba kwanza halafu tukae kitako tupange mipango mengine maana huu ndio umefeli" Rodriguez aliongea huku akiweka tai yake vizuri. "Yeah hilo ndio la kufanya sasa" Martin alichangia. "Mkuu kuna simu kutoka ikulu" aliingia Maggy ambae alikuwa secretary mpya baada aliekuwa secretary wa zamani kufa.
Mr Clinton alikwenda ofisini kwa ajili ya kuongea "hali ni tete mpaka sasa, tumeshapoteza watatu kati ya project wetu bora kabisa" Aliongea kwa unyonge. Baada ya maongezi ya muda mrefu alikata simu na kurudi alipokuwa mwanzo. "Kuna mpya gani huko" Ms Helen alimuuliza punde tu baada ya kufika, "hakuna mpya" Alijibu kwa mkato akionekana kuwa na mawazo mengi sana.
"Inabidi ufike Durban kwanza kisha nitakupa maelekezo zaidi" ilikuwa ni sauti kwenye simu, baada maongezi hayo alirudi mpaka kwenye gari. "Inabidi tuelelekee Durban kwanza " aliongea na kuingia kwenye gari, Leonard aliingia na safari ikaanza. Njia nzima walikuwa kimya huku kila mmoja akiwaza la kwake. Safari ilikuwa ndefu lakini walifanikiwa kufika salama bila matatizo yoyote, na kwa sababu waliingia usiku hivyo walitafuta hoteli na kupumzika.
Asubuhi mapema uliingia ujumbe kweny simu ya Alex ukimwambia mahali na saa, aliamka bila kumshtua Leonard na kutoka alikwenda mpaka sehemu ambayo aliambiwa kwenye ujumbe na kusubiri. Ulipofia ule muda alioambiwa alikuja mtu na kumkabidi bahasha kisha akaondoka. Alex baada kupokea bahasha ile alirudi hotelini kisha akaifungua, alikuta passport pamoja na vitambulisho kadhaa tiket ya ndege pamoja na kikaratasi kidogo kilichoandikwa Rio De Janeiro Brazil.
Baada ya hapo aliingia chooni na kujimwagia maji na kuvaa kwa ajili ya safari. "Leonard , mimi inabidi niondoke mtu wangu" aliongea, "wapi tena" aliuliza Leonard. "Naelekea Brazil" Alijibu, "dah haina noma kaka, mi nashukuru kwa msaada wako katika kulipiza kisasi cha wadogo zangu" Alijibu huku akitabasamu. "Sasa ni hivi katika gari kuna pesa nyingi tu na zinaweza kukusaidia, zichukue na uanze maisha upya" Alex aliongea. "Hakuna shida nimekuelewa" alijibu Leonard na kisha akajiandaa na kumsindikiza rafiki yake uwanja wa ndege. "ipo siku nitakulipa wema wako" Leonard aliongea maneno hayo wakati akimuaga Alex, "sawa" Alex alijibu na kuingia ndani ya uwanja huo.
******************
Maisha ya Allen James yalikuwa ya amani kabisa, jioni hiyo alikuwa na familia yake katika fukwe moja hivi mjini Florida. Kwa kweli alikuwa amesahau kabisa machungu alioyapata kipindi cha nyuma, " Mume wangu unawaza nini" Aliuliza mkewe Tania. Mwanamke ambae uzuri wake haujapingua hata kidogo machoni mwa Allen James. "Siwazi kitu" alijibu huku akitabasamu na kumuangaliwa mkewe ambae nae pia alikuwa akitabsamu. "Baba inuka" aliongea Christina ambae muonekano wake haukuwa tofauti n alivyokuwa mama yake Melinda. "Unataka nini" aliuliza baba ake, "halafu unajua siku hizi umekuwa mvivu sana" Christina alijibu huku akimsukuma mgongoni, "we mtoto wee kuwa na adabu, babaako huyu" Tania aliingilia kati. "Mama mimi si mtoto tena nina miaka ishirini na tano sasa" Christina alijibu.
Wakati akiendelea kubishana na wazazi wake simu yake iliita "Agent Darling unahitajika ikulu, kaa tayari helicopter inakuja kukuchukua hapo hapo ulipo". "Hii mijitu hainipi hata nafasi ya kukaa na familia yangu" aliongea kwa hasira kidogo. "Kazi au" Babaake alimuuliza, "hata sijui wamesema nahitajika tu ikulu" alijibu na kwa mbali alisikia mlio wa helicopter na sekunde kadhaa mbele ilifika eneo hilo na kutua. Alishuka kijana mmoja na kuelekea alipo Christina au Agent Darling kama anavojulikana akiwa kazini.
Alitoa heshima na kisha akamuambia amfuate "nahisi piknik yangu itakuwa imeishia hapa" aliongea Christina huku akiondoka taratibu. "Kama ni kazi ya kwenda kumchapa mtu hakikisha unamfundisha heshima kisawasawa" Allen James aliongea kwa nguvu mpaka watu waliokuwa pembeni walishangaa. "Duh mi wazazi wengine hasa makatili" alisikika mtu mmoja akiongea pembeni yao. "Na wewe unataka kuchapwa" Allen James aliongea na kumuangalia.
Ndege ilikanyaga ardhi ya Brazil mjini Rio de Janeiro, "hewa safi kabisa" aliongea Alex wakati anashuka ndege akiongozana na abiria wengine. Alitoka mpaka nje ya uwanja na kukuta watu na mabango ya fukwe tofauti tofauti. Ujumbe uliingia kwenye simu yake ukiwa umeandikwa Copacabana, aliinua macho na kutafuta bango lililoandikwa hivyo. Alipoliona alinyoosha mkono na dereva alipouona mkono, haraka bila kuchelewa alimfata na kumsaidia mabegi mpaka kwenye gari. Safari ilianza "karibu Rio" aliongea yule dereva, "asante" alijibu Alex. Safari haikuwa fupi na dereva alionekana kuwa mcheshi sana jambo ambalo lilimfurahisha Alex.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walifika mpaka katika pwani hiyo iliyozungukwa na mahoteli makubwa makubwa na yenye mvuto wa aina yake. Alex alimlipa dereva kiasi cha fedha alichohitaji na kuingia katika hoteli moja hivi na kuchukua chumba. Kutokana na uchovu wa safari alioga na kujitupa kitandani, usingizi nao haukucheza mbali ulimchukua ghafla na kuanza kumuhamisha katika maeneo tofauti kabisa. "Baba Alex si nilikwambia usiwaite watoto wote wawili Alex, ona sasa hata wakifanya kosa kila mmoja anasema yeye ndie amehusika", "mke wangu hiyo sio shida, sasa hao si watoto tu wakikuwa wataaacha". "Mpige risasi mdogo wako", "hapana siwezi kumuua mdogo wangu". Ghafla Alex alishtuka kutoka usingizini huku jasho jingi likimtoka, ni ndoto hiyo ambayo inajirudia kila siku lakini kutokana na kuwa alifutwa kumbukumbu huwa anahisi ni kitu ambacho hakijawahi kutokea.
Alipoangalia saa yake ilikuwa ni saa kumi na moja jioni, aliamka na kuvaa mavazi ya kutembelea baharini na kutoka hotelini.Kwa kweli fukwe hiyo ilipendeza sana, na watu wengi walionekana kufurahia upepo wake. Alex alitembea tembea katika ufukwe huo huku akiwa ameshika dafu na kufurahia maji yake. Alifika sehemu na kuamua kupumzika, wakati akiwa amekaa alikuja mtu pembeni yake na kukaa.
"Habari yako Alex Junior" aliongea yule mtu, Alex alishangaa kulisikia jina hilo. "Najua utakuwa unajiuliza nimelijuaje jina hilo" alizidi kuongea yule mtu, "wewe utakuwa hunijui ila mimi nakufahamu kinaga ubaga". Alex aligeuka na kumuangalia anaeongea na kugundua alikuwa mtu mmoja mzee sana lakini alivomuona tu alihisi kama kumfahamu. "Hivi tumewahi kuonana mimi na wewe" aliuliza Alex akiwa na wasiwasi, "ndio lakini miaka mingi sana" alijibu huku akitabasamu. "Alex, Alex, Alex" yule mzee aliita jina hilo mara tatu ghafla Alex akaanza kuhisi kichwa kinamuuma, vitu kama kumbkumbu vilianza kugongana kwa kasi ndani ya kichwa chake na kujikuta akiishiwa nguvu na mwisho akaanguka na kupoteza fahamu kabisa.
Alikuja kushtuka akiwa chumbani kwake na yule mzee akiwa pembeni yake, "unafanya nini chumbani kwangu" aliuliza akijaribu kukaa lakini bado kichwa kilikuwa kinamuuma. "Unajua tatizo lako unajaribu kuzipinga kumbukumbu zako" aliongea yule mzee, "unamaanisha nini kusema hivyo" Alex aliuliza kwa mshangao. "Si unakuwa unaota ndoto za ajabu ajabu" aliongea yule mzee, "ndio" Al alijibu Alex. "Sasa ni hivi, hizo unazoota si ndoto ni kumbukumbu zako mwenyewe zinarudi lakini wewe unapingana nazo na ndio maana mara nyingien zinakuangusha" aliongea yule mzee.
"Acha kunizungusha we mzee, nambie ukweli kuhusu mimi" alifoka Alex. "sasa umeona bado una hasira zako za ajabu" aliongea yule mzee kisha akaendelea "umeletwa huku ili kuja kuujua ukweli kuhusu maisha kabla ya kufika hapo ulipo leo, Alex Alex Alex. Babaako ndie alikuwa akiwaita hivo baada kufanya makosa, ukweli ni kwamba wewe ni wa pili katika familia yenu. Wa kwanza alikuwa anaitwa Alex Seniour na wewe ni Alex Juniour, mlikuwa watundu kupindukia na siku zote mukifanya makosa munasingiziana. Wewe na kaka yako mumepishana mwaka mmoja tu na mlikuwa mukipendana sana na ndio maana mukifanya kosa aidha mupigwe wote au muachiwe wote. Mimi nilikuwa mlinzi wa babaako wakati huo na nlikuwa naelewa mambo mengi sana pamoja na siri nzito ambazo hata mamaako hakuzijua.
Siku moja wakati tupo safarini babaako alipokea simu ya vitosho kutoka makao makuu ya kipelelezi nchini, baada kupokea taarifa hizo haraka tuligeuza na kurudi nyumbani. Lakini bahati haikuwa upande wetu,tulifika nyumbani lakini tulikuta nyumba inamalizika tena kwa moto. Baba ako alipata mshtuko mkubwa na kupelekea kupoteza maisha lakini akiwa katika hali aliniachia kazi moja kama ikiwa kuna hata mmoja kati ya wanafamilia atakuwa amepona basi niondoke nae mimi. Lakini baada moto kuzimwa mifupa iliokutwa ni ya mtu mmoja tu ambae ni mama ako, kuanzia hapo nikaanza kufanya uchunguzi wa siri na nikafanikiwa kugundua kuwa nyote wawili mumechukuliwa na serekali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi maalum wa kemikali inayojulikana kama CODE X. Hapo sasa ikabidi nirudi tena kwenye gwanda ili niweze kuingia katika kambi ambazo zinasadikika kuwa watoto wengi mayatima wanapelekwa huko. Na kutokana na kazi nilioifanya kuitumikia nchi kipindi niko jeshini haikuwa tabu kuaminiwa lakini siku niliofika ndio siku niliokuta wewe na kaka yako mnapewa jaribio la kuuwana lakini kaka ako alishindwa na wewe ulipokabidhiwa bastola ilikuwa haina risasi hata moja. Kuna mtu alikuwa nyuma yako na ndie aliepiga risasi na kumuua kakaako huku ukidhani wewe ndie uliemuuwa. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada kushuhudia tukio hilo nilitupilia mbali wazo la kukuokoa bali niliamua nikupe mafunzo kama kawaida na uendelee kuwa chini ya uchunguzi maalum. Na ndio maana ulivyotoroka wakati ukiwa na miaka kumi na mbili nilikuachia uishi nje kwa muda wa mwaka mzima, nilifanya hivo ili kukujenga kiakili kuwa kuna maisha nje ya kambi. Na ulivyotoroka mwezi uliopita unadhani nini kilitokea, ulitoroka baada kuona moto umezuka. Moto niliuwasha mimi mwenyewe ili kukupa nafasi hiyo na yote hio ni kukutaka ulipe kisasi cha familia yako" Alimaliza kuongea na kumuangalia Alex usoni.
"Kwa we nani" Alex aliuliza, "we kweli kilaza kama mpaka saa hivi umeshindwa kunitambua, mimi ni General David kiongozi Marine Base 71" alijibu na kucheka kidogo. Alex alitoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango maana katika watu ambao alikuwa anawachukia wakati akiwa kambini. "Ina maana mara zote wakati natoroka wewe ndio ulikuwa chanzo" Alex aliuliza kwa mshangao kisha akaendelea "na kule kambini umetokaje sasa".
"Sasa ikiwa nimeweza kukutorosha wewe, iweje mimi nishindwe kutoroka" aliongea General David, "baada ya kupata taarifa za kuthibitika kuwa umefanikiwa kukimbia nilitega bomu ofisini kwangu na kutoroka kabla ya kulipuka na kwasababu lilikuwa kali sana halikuacha ushahidi wowote ule hivyo wanaamini mimi nimekufa" alijibu.
*************************
"Tumepokea taarifa kutoka kwa watu wetu ambao wapo nchini Brazil kuwa Project 75 ameonekana Rio De Janeiro" aliingia Martin ofisini kwa bosi wake na kutoa taarifa. "Vipi umeshatuma vijana huko" aliuliza Mr Clinton, "ndio nimemtuma Project O" alijibu Martin. "Ataweza kutekeleza kazi huyo" aliuliza, "katika wote huyu ndie ana uwezo unaolingana na project 75 kwa hiyo usijali mkuu, mara hii mambo yatakuwa sawa kabisa" Martin alijibu huku akitabasamu. "Tuone wakati huu utatotokea wapi" Mr Clinton alijisemea moyoni. Baada kuwasilisha ripoti hiyo Martin alitoka ofisini, Mr Clinton alinyanyua simu na kumpigia secretary wake. Maggy alifika ofisini mara moja baada kukata simu, Mr Clinton alianza mambo yake yake yakipuuzi lakini alikutana na kibao kizito kilichomuangusha chini. Aliinuka kwa hasira na kutoa bastola lakini alikuwa kashachelewa maana alihisi kitu cha baridi kikigusa katika paji la uso, "ukileta ujinga nakufumua ubongo, kawafanyia malaya wenzako upuuzi kama huu mimi sie tumeelewana" alifoka kwa hasira Maggy. "Sawa nimekuelewa" Mr Clinton alijibu huku akimeza funda kubwa la mate maana alihisi kama kifo chake kina karibia. Baada hapo Maggy alirudisha bastola yake na kuondoka, Mr Clinton aliishia kula kwa macho tu huku akijilaumu kwanini amemuachia kirahisi namna ile.
Beach ya Copacabana ilikuwa imechangamka siku hiyo kuliko siku nyingine nyingi, kwa mbali alionekana kijana mmoja akiwa anatembea taratiu huku mkononi akiwa amebeba boksi dogo. Alionekana hayuko sehemu hiyo kupata upepo bali alikuwepo eneo hilo kikazi zaidi. Alikuwa akielekea sehemu aliokuwa amelala Alex ambae alikuwa akiota jua, alikuwa bize akisikiliza mziki lakini alianza kuhisi hali ambayo si ya kawaida. Mshale wa hatari uligonga kichwani mwake, alitoa earphone masikioni na kuanza kuangaza pande zote za pwani hiyo na ndipo akamuona yule mtu aliekuwa akija upande wake. Yule jamaa alifungua lile boksi na kutoa bastola ndogo iliofungwa kiwambo cha kuzuia sauti na kuanza kumshambulia Alex.
Kwa kasi ya ajabu Alex alifanikiwa kuondoka kwenye kitanda alichokuwa amelala na kuruka pembeni, uwezo wa kujitetea wakatai huo uikuwa mdogo sana kwa sababu hakuwa na silaha yoyote ile. Yule jamaa hakuwa mwengine isipokuwa project 0, huyo ndie anaefuata kwa hatari baada Alex. Yeye hakujali watu aliendelea kumwaga risasi tu na kila aliepita mbele yake alikwenda na maji, "simama na weka silaha chini" iliskika sauti ikitokea nyuma ya Alex. "Inspecta usisogee huyo jamaa atakuua" Alex aliongea lakini alikuwa kashachelewa, yule askari alichezea risasi ya kichwa na kudondoka kama mzigo. Alex hakulaza damu alirukia bastola ya yule asakari, alipoinuka tu alianza kushambulia. Alifanya kama njia ya kujinunulia muda wa kutoroka eneo hilo maana ilikuwa pazito. Na kweli mbinu yake ilifanikiwa na hapo hapo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Alifika chumbani kwake na kufungua begi lake, alitoa vipande vipande vya chuma na kuanza kuviunga. Dakika tano baadae akawa amemaliza kuviunga na kupata batola kamili, alitoa magazine za kutosha kisha akavaa nguo zake za kazi na kuziweka magazine hizo. Alichukua simu yake na kukuta ujumbe uliomwambia ujio wa Project 0, "ahaa kumbe wewe ndio project zero, basi wacha nikuonyeshe kama ziro haina thamani ikiwa mwanzo" alijisemea moyoni na kutoka chumbani kwake. Uko chini katika hoteli hiyo palikuwa pamevurugwa na project 0, "project 75 jitokeze upambane na mwanaume mwenzio" alifoka kwa hasira na kumfumua ubongo dada wa mapokezi kisha akaendelea kuongea "kama ukiendelea kujificha nitauwa mtu mmoja mmoja mpaka waishe".
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Umesema nitoke nipambane na mwanaume mwenzangu sasa mbona unauwa wanawake au ndio wenzako" Alex aliongea huku akitoka katika lifti na kujibanza pembeni kwenye ukuta. "Waache hao, hii vita ni kati yangu mimi na wewe" Alex aliongea na kutabasamu, na kweli project 0 aliwaachia watu wote aliokuwa amewakamata. Alex alitoa bastola yake na kuanza mashambulizi ya kasi, project 0 nae alijibu mashambulizi hayo. ulikuwa ni mwendo wa kujibizana kwa risasi tu, mashambulizi yalendela kuwa ya na namna hiyo kwa muda mrefu huku wakitupiana maneno ya kejeli. "mi nahisi wewe ni mjinga, yaani umetumwa kuja kukinunua kifo chako au sio" Alex aliongea akiwa amejificha sehemu, "hahaha,.. mimi nimekuja hapa kuchukua roho yako" Project o alijibu.
"hivi wewe unalijua hata jina lako" Alex aliuliza, "project o ndio jina langu" alijibu. "mi nlijua tu utakuwa zezeta, hata jina lako hulikumbuki" Alex aliendelea kujibu majibu ya hovyo. "kama vipi tuoneshana ni nani mwanaume halisi kati yetu" Alex aliongea na kusimama kisha akaweka bastola pembeni, "nilikuwa nataka sana tuchapane kwa mkono na sio msaada wa bastola" project 0 aliongea huku akisimama na kuweka bastola pembeni. " sawa tuoneshane" Alex alijibu na kuchomoka sehemu aliokuwa amesimama kama mshale na kumvaa project 0. Mkono si wa kitoto ulianza kutembea huku kila mmoja akionyesha uwezo wake. Kila mmoja alipokea masumbwi kadha kutoka kwa mwenzake lakini upande project 0 hali ilikuwa mbaya sana mwisho akaona bora akimbiie bastola yake. Na Alex kama alimsoma hivi na yeye akaruka pembeni na kuokota bastola yake na kuanza kutupiana risasi tena.
Risasi zilizidi kumiminwa, huku kila upande ukijitahidi kumshambulia mwenzake. Alex alichomoka sehemu aliokuwa amejificha na kwa kasi na wepesi aliokuwa nao. Alijirusha upande mwengine huku akishambulia, alipokaa sawa alitoa magazine katika bastola yake ndogo na kuangalia imebakiwa na risasi ngapi. "risasi sita, zinatosha kunitoa hapa" alijesemea moyoni na kuirudisha magazine katika bastola yake. Aliokota chuma kidogo pembeni na kukirusha, ghafla uliskika mlio wa bastola. Ulipokata tu aliinuka na kupiga risasi moja tu iliokwenda moja kwa moja mpaka kwenye goti la project 0 ambae alipiga kelele za maumivu. Na bila kuchelewa alikimbilia sehemu aliokuwepo na kumnyang'anya bastola. "najua umeahidiwa zawadi nono ukiniuwa lakini kaa ukijua kuwa wameshindwa wenye uwezo kuliko wewe" Alex aliongea na kumuekea bastola katika paji la uso, "hahaha... hata ukiniuwa mimi ujue kuna wengine watakuja kuendelea nilipopaacha" aliongea kijana huyo ambae alionekana kutokukiogopa hasa kifo. "sawa waache waje tu, na mimi nitakuwa nawauwa mpaka pale watakapoacha kunifatilia maisha yangu" Alex aliongea na kufyetua risasi kisha akachukua kile kifaa cha kuwasiliana "nawatangazia vita rasmi, mtalipa kwa mlioiendea familia yangu na kama mlikuwa mnadhani sijitambui mmekosea naitwa Alex Juniour" aliongea na kukikata kile kifaa.
*******************
"Kosa kubwa tunalolifanya ni kwamba tunajaribu kumuwinda simba kwa kutumia nyati, hatuwezi kumnasa hata siku moja, simba anawindwa na simba mwenzie" aliongea Mr Robert katika kikao cha siri kilichokuwa kikiendelea katika moja kati ya ofisi kubwa za kipelelezi mjini New york nchini Marekani. "Unamaanisha kwamba wanajeshi wetu wote hawana maana si ndio" alifoka mwengine, "tuseme hivyo ni sahihi kabisa, wanajeshi wetu wote hawawezi na hawatoweza kumtia mbaroni huyu kijana" alijibu. "sasa wewe kuna mtu unamfahamu ambae anaweza kuifanya kazi hii" aliongea mkuu wa kikao hicho, "ndio namfahamu na ndio mtu pekee anaeweza kumtia kizuizini huyu kijana" alijibu. "na mtu huyo ni nani" aliuliza tena mkuu wao kwa shauku. "mtu mwenyewe ni Project X" alijibu Mr Robert.
"Robert hebu tuambie huyo mtu ana kipi hasa ambaco wanajeshi wetu hawana" aliongea Mr Clinton, "project X ndio mtu wa kwanza kufanikiwa wakati wa uhunguzi wa mwanzo wa CODE X, analingana kila kitu na Alex. Kwa maana nyingine yuko rank moja na Alex na hivyo ndio maana anakuwa mtu wa pekee ambae atafanikisha kumtia Alex mbaroni" Robert alijibu kwa kujiamini sana huku akitabasamu. "kwa sasa unajua yuko wapi" Aliuliza Mr Clinton, "nipeni siku tatu tu nitawaletea hapahapa ofisini" Robert aliongea na wote wakatikisa vichwa kuanshiria kuwa wamekubaliana nae. "jamani acheni masihara mujue huyu kijana ni hatari" aliongea Helen, "na kawaida yao wakiweka ahadi lazima waitimize kwa hiyo tusijiachie tu kutegemea mia mia kama atatiwa mbaroni, tuwe tayari kwa lolote litakalotokea" aliendelea kuongea.
*****************************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Habari yako Mr Allen" Robert aliongea na kuka katika kiti cha pembeni katika mgahawa mmoja mjini Florida nchini Marekani. "safi, unataka nini na kama ni lile swala tuliloongea mwanzo acha tu niondoke" Alijibu lakini alionekana kukerwa. "hamna shida we ondoka tu lakini ntakufungulia kesi ambayo najua utashindwa kuiepuka" alitisha Robert, ilibidi Mr Allen atulie ili kumsikiliza. "hapa sis tunaongelea maisha kwa ujumla, wewe nisaidie kumtia mkononi Alex mimi ntakusaidia kukufuta katika ubao wa blacklist" aliongea Robert. "wewe ndio unaongelea maisha na unataka kunituma kwenye kifo changu, kijana umri umekwenda tayari nini kinachokufanya ujiamini kama nitaweza kumkamata Alex" alijaribu kujitetea Mr Allen.
"unajua Alex hahitaji mtu mwenye nguvu ili kukamatwa bali anahitaji mwenye uwezo wa kufikiri kama yeye ili aweze kugundua mbinu na mipango yake kabla hajafanya chochote, na kwa sasa hakuna mtu mwenye uwezo wa kufikiria kama Alex isipokuwa wewe" Robert aliongea. "mimi nawafahamu sana nyinyi mkitaka lenu mpaka liwe, iwe kwa njia ya kawaida au yoyote ile" Mr Allen aliongea na kukunja uso. "nashkuru umelifahamu hilo, nakupa siku mbili unipe jibu" Robert alimaliza kuongea na kuondoka, alimuachia bahasha ndogo mezani. Allen James aliichukua na kuondoka lakini kichwani alikuwa na mwazo kibao, maana alielewa hatari iliokuwa mbele yake ikiwa atakubali au atakataa.
Alirudi nyumabani kwake akiwa na sura ya huzuni, "mume kuna tatizo gani" mkewe aliuliza. "we acha tu, twende chumbani nikakueleze kila kitu" alijibu na kuongoza njia. Walipofika chumbani alimueleza kila bila kumifcha chochote kile. "si ukatae tu" mkewe aliongea, "kukata sio tatizo, litakalotokea baada ya kukataa ndio tatizo" Alijibu Mr Allen. "we unadhani serekali ya nchi hii inakuacha tu huru hasa baada kufanya matukio makubwa, wakikuacha ujue wanakuacha kwa sababu zao maalum" alimfafanulia mkewe. "sasa tunafanyaje" aliuliza mkewe, "sikia usiku ntaongea na watoto, wakati huo we fanya mpango wa kuelekea Qatar, na usinipigie simu mpaka nitakapokupigia mimi" aliongea kwa masikitiko, mkewe mwanzo alikataa lakini alijaribu kumuelewesaha mpaka akaelewa. Usiku aliwaita watoto wake wote na kuwaeleza hali halisi, wote walikubaliana nae na kukubali kuondoka na mama yao siku ya pili. Christina hakuwepo kwenye kikao hicho, alikuwa mbali sana katika mafunzo maalum ya kikomando.
Siku ya pili mapema familia yake yote iliondoka na kumuacha peke yake, alifungua kabati lake na kuangalia vifaa vyake vya kazi. Alitoa suti moja kali sana na kuvaa ikiambatana na viatu vyeusi vilivyong'aa, shingoni alining'iniza tai maridadi kabisa. katika sehemu ya nyuma ya kabati hilo aliiondoa nguo na kubonyeza kitufe, sehemu hio ilifunguka na kisha akaingia. Hicho kilikuwa ni chumba maalum cha siri na ndipo alipokuwa ameweka silaha zake zote pamoja na passport zake. Alichagua vifaa ambavyo vingemsaidia kufanikisha kazi hiyo ngumu, alipordhika na maandalizi hayo alitoka na kurudisha kila kitu kama kilivokuwa. Alitoa simu yake na kumpigia Robert "tukutane wapi" aliongea Mr Allen, "subiri hapo hapo kwako, natuma helicopter sasa hivi" Robert alijibu na kukata simu.
Nusu saa baadae helicopter ilitua mbele ya nyumba ya Mr Allen na bila kuchelewa alipanda na safari ikaanza. Helicopter hiyo ilitua makao makuu ya kitengo cha upelelezi mjini Washington DC, Robert alikuwa akimsubiri kwa hamu "karibu Washington" aliongea baada Mr Allen kushuka. Kisha akamfanyia ishara amfata, walitembea mpaka walipofika katika chumba maalum ambacho wengine wote walikuwa wakimsubiria mbabe wa Alex kwa hamu. Ila alipoingia tu Mr Clinton alicheka "ina maana huyo mzee ndio atakaeweza kumkamata Alex".
Maneno hayo yalimkera sana Mr Allen na bila kuchelewa aliingiza mkono nyuma ya koti lake na kutoa kisu kidogo. Kwa nguvu alikirusha kikaenda kuchoma pembeni ya kichwa cha Mr Clinton katika kiti, Mr Clinton alimeza funda kubwa la mate kisha akasema kwa nguvu "makamateni". Walinzi kama sita hivi waliokuwemo katika chumba hicho walisogea mpaka alipo Allen na kutaka kumshika lakini walichokutana nacho wanakijiua wenyewe. Mmoja alirusha kirungu kwa nguvu lakini Allen alikiona na kukikwepa kisha akamzadiwa ngumi nzito ya shingo na kumfanya aanguke kama mzigo, na hapo akaanza kuwachakaza wengine. Dakika tatu baadae wote walikuwa chini hoi "usihukumu kitabu kwa gamba lake la nje" aliongea maneno hayo huku akiweka tai yake vizuri.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wote waliokuwepo katika chumba kile walibakia mdomo wazi kwani hawakutegemea kabisa kama mzee kama yule ambae kwa haraka utafikiri ana miaka kati ya hamsini na hamsini na tano atakuwa na uwezo kiasi kile. "Jamani huyu ndie project X au unaweza kumita Allen James lakini jina lake halisi ni David Robert Mc cannon" Aliongea Robert na hapo sasa ndio wengi wakamtambua, "karibu Project X" aliongea Helen, "samahani niite Allen, Project X halina tofauti na ukiniita mbwa" alijibu huku akiwa amekunja sura kuashiria kama hapendi kuitwa vile. "hakuna shida Mr Allen" Helen alijibu huku akijibabaisha, "Sawa kwanza nina masharti yangu" aliongea Allen.
"Yapi hayo" Mr Clinton aliuliza, "la kwanza sitaki familia yangu ihusishwe na kitu chochote, pili sitapokea amri ya yoyote kati yenu isipokuwa Robert na tatu nataka kazi niifanye peke yangu sihitaji msaada wowote kutoka kwenu" alimaliza. "hakuna shida yoyote" Mr Clinton alijibu, "tuongee sasa" Allen aliongea na kuvuta kiti na kukaa. Kikao kilifanyika kwa muda wa robo saa mpaka wakafikia makubaliano, "Kwa taarifa tulizozipata Alex ameonakana Hongkong jana" Robert aliongea.
************************
Baada mshikemshike wa Brasil Alex aliondoka na kuelekea Hongkong, hii ilikuwa ni mbinu ya kuwapoteza ili wasijue anaelekea wapi. Usiku alitoka katika hoteli aliofikia kwa ajili ya kunyoosha miguu, alifika katika bar moja hivi na kuingia ili apate kinywaji. Alikaa kwenye meza moja na mrembo fulani hivi lakini Alex alipomuangalia tu aligundua kuwa hakuwa mtu wa kawaida na alionekana pale kikazi zaidi. Muhudumu alifika kusikiliza oda ya Alex, aliagiza alichotaka na muhudumu akondoka. "habari yako mrembo" alivunja ukimya, "safi mambo vipi" alijibu. "powa, mimi naitwa Alex" Alex alijitambulisha, "nashkuru kukufaham" alijibu kisha akatulia.
"Wewe unaitwa nani" ilibidi amuulize, "kulijua jina langu ni kujitia matatizoni tu" yule msichana alijibu na kutoa sigara. Wakati wote huo alikuwa akiangalia meza fulani hivi, walikuwa wamekaa watu wanne waloonekana kama wakifanya biashara. Alex aliwaangalia watu wale na kugundua kuwa walikuwa ni wafanya biashara za madawa ya kulevya. Aliingia mtu mwengie na kwenda mpaka kwenye ile meza na kumnong'oneza mmoja, ghafla baada kumnong'oneza yule jamaa aliinuka na kutoa bastola na kuielekeza katika meza aliokaa Alex na yule mschana. Kwa kasi ya ajabu yule mschana aliruka pembeni na kutoa bastola katika pochi yake, Alex nae hakulaza damu aliruka pembeni na kupiga teke ile meza waliokaa kisha akajificha nyuma. Vurugu lilianza ndani ya bar hiyo huku watu wakikimbia ovyo, yule mschana aliendelea kuwashambulia wale watu. Alex nae akaona si vibaya kama angemsaidia, alitoa bastola yake na kuanza kushambulia.
Ghafla alisikia ukwenzi mkali wa maumivu, alipogeuka alimuona yule mschana akigaragara chini huku akitoka damu mkononi, alipoona hivo aliisogeza meza upande wa yule mschana kisha yeye akabetuka kwa nguvu kutoka chini na kuanza kuwafata wale watu huku akijitahdi kukwepa risasi zao. Alipowafikia tu aliwachakaza ile mbaya, walipoona hali imekuwa ngumu waliamua kukimbia. Alex alitaka kuwafukuza lakini alikumbuka kuwa yule mschana ameumia. Alirudi sehemu aliyomuacha lakini hakumkuta, ilibidi atoke nje na kuanza kumatafuta na baada kumtafuta sana alifanikiwa kumuona akiwa anajikokota.
"Wewe huoni kama umeumia sana" aliropoka alipomfikia, "kwanini unanifata huoni kama unahatarisha maisha yako" aliongea yule mschana kwa tabu kidogo. "sasa kati yangu na wewe nani yupo katika hatari" aliongea Alex na kujaribu kumshika bega kisha akaendelea "mi najua kama wewe ulikuwa unapeleleza". Yule mschana aliposikia maneno hayo aliruka pembeni na kutoa bastola "wewe ni nani" aliuliza. "weka bastola pembeni mimi siko hapa kukudhuru" Alex alijibu huku akitabasamu. "nambie wewe ni nani" alifoka sasa yule mschana, "si nimekwambia naitwa Alex au ushasahau" Alex alijibu.
"Najua kama jina lako ni Alex" Alifoka yule mschana akionekana kuzidiwa na maumivu. Bastola ilimdondoka na hapohapo akaanguka chini na kupoteza fahamu. "nilijua tu hutoweza kusatahamili maumivu lakini kwa kweli sijawahi ona mwanamke mkakamavu kama wewe" Alex alijisemea moyoni huku akihisi mwili wake wote umekuwa baridi. Alimbeba na kurudi nae hotelini, alipoingia chumbani kwake alimuweka juu ya meza na kisha akatoa vifaa vyake vya huduma ya kwanza. Kitu cha kwanza alichikifanya ni kuitoa risasi mkononi mwa mschana huyo kisha akamsafisha kidonda hicho na kumfunga bendeg.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada hapo alimbeba na kumlaza kitandani, lakini alishidwa kuyatoa macho yake katika sura ya mschana huyo mrembo kupitiliza. "hivi mtoto mzuri kama wewe, kwa nini unachagua kazi ngumu kama zetu wakati kazi nyingine za hadhi yenu zipo" alijisemea moyoni Alex. Alijitahidi kuyaonda macho yake katika sura ya binti huyo lakini alishindwa kabisa, "we Alex unafikiria nini hebu tafuta njia uende huko acha kushangaa kazi ya Mungu" alijisemea mwenyewe na kuelekea sebeleni kwa ajili ya kuupitisha usiku ambao ulikuwa mrefu sana kwake.
Alikuja kushtuka jua lishatoka, alisimama na kuanza kunyoosha viungo kama kawaida yake kisha akaelekea chooni kupiga mswaki. Alipotoka alielekea chumbani na alipofungua tuu mlango yule mschana alikurupika huku akihema. "niko wapi hapa" aliuliza kwa wasiwasi, "usijali uko sehemu salama kabisa" Alex alijibu huku akifungua kabati. Yule mwanamke alihisi kitu tafauti mwilini mwake alifunuwa shuka na kuchungulia akajikuta akitoa macho baada kugundua kuwa amebadilishwa na nguo. "umenifanya nini" aliuliza huku akitoa macho, "we unahisi nemekufanya nini" Alex alijibu bila kumuangalia.
Yule mschana alichomoka kwa kasi na kumvaa Alex na kuanza kumshushia makonde ya haja, Alex alijaribu kuyakwepa lakini baadhi yalimuingia. Alifanikiwa kumtoka mikononi "duh wewe mbona mkorofi kiasi hicho, we unadhani nimekufanya kitu kibaya. Mimi nimekutoa tu risasi iliganda mkononi na kukubadilisha nguo, sijafanya kingine" Alex aliongea huku akihema. Hapo alijiangalia mkononi na kukuta bendeg, "oh samahani si unajua watu wengi wanajichukulia point ikiwa mwanamake hajielewi" Alibadilika ghafla na kuwa mpole. "bila samahani hata ingekuwa ni mimi nisingekuelewa kwanza" Alex alijibu huku akijishangaa na kujiuliza mbona mwepes sana kwa binti huyo. Alex alitoa suruali yake moja na kumrushia, baada kuvaa walitoka wakaelekea sebeleni.
"sorry kwa lililotokea jana" alianza kuongea yule mschana "jina langu Scarlet" alijitambulisha. "jina zuri" Alex alijibu, "we umesema unaitwa Alex si ndio" aliendelea kuongea Scarlet, "yeah" Alex alijibu. "imekuaje ukajua kama mimi ni mpelelezi" Aliuliza kwa shauku, "kwa sababu mimi mwenyewe ni kama wewe tu" Alex alijibu. "na wewe pia mpelelezi" aliuliza kwa mshangao, "si mpelelezi kama unavofikiria, mimi ni muuaji wa kimataifa" Alex alijibu na kuzidi kumshangaza binti huyo. Waliendelea kuongea mambo mengi sana kama kwamba walikuwa ni marafiki wa muda mrefu. Wakati wanaendelea na maongezi simu ya Alex iliita "kuna nini" alipokea na kuongea kwa hasira, alisikiliza simu kwa makini na baada kukata mudi yake ilibadilika ghafla. "wewe unaelekea wapi ukitoka hapa" Alex aliuliza, "kuna pahali nakwenda ambapo itakuja helicopter kunichukua" Scarlet alijibu. Alex aliinuka na kuelekea chumbani kwake na kungia bafuni, alioga na alipomaliza alirudi sebeleni kashabadilisha nguo. "hii sehemu haifai tena tuondoke" Aliongea a Scarlet alimuelewa anamaanisha nini. Walitoka hotelini na kuelekea sehemu ambayo scarlet anakuja kuchukuliwa na wenzake.
**********************************
Ndege inakanyaga ardhi ya Hongkong na anaonekana mzee mmoja wa makamo akishuka akiwa na briefcase ndogo. Hakuwa mwengine isipokuwa Allen James ambae ndie rasmi aliekabidhiwa kazi ya kumtia Alex nguvuni. Alitoka mpaka nje ya uwanja na kuangaza huku na kule mpaka alipoona gari nyweusi aina ya mercides benzi. Kwa mwendo wa taratibu alitembea mpaka ilipo na kuingia, aliwsha gari na kwenye kioo ikatokea ramani inayomuonyesha hoteli anayokaa Alex ilipo. Aliondoa gari hiyo kwa mwendo mdogo na kuelekea inapomuelekeza ramani. Alifika nje ya hoteli hiyo na kushuka, aliingia ndani na hakuuliza chochote mapokezi. Moja kwa moja mpaka kwenye lifti na kuelekea gorfa ambayo chumba cha Alex kilikuwepo, kwa umakini wa hali ya juu alifungua mlango na kuingia. Alitembeza macho chumba kizima na kuyaangalia madirisha yote. Alipofika kweny dirisha moja alisimama na kuangalia nje, aliangalia kwa umakini wa hali ya juu na bila kusita alitoa bastola yake kiunoni na kufyatua risasi iliopasua kioo na kuelekea gorofa jirani. "mbinu hizi ni za kitoto sana" alijisemea na kujibanza ukutani.
Kumbe Alex alikuwa ametega gorofa jirani na hilo akiwa na bunduki yake ya kudungulia, lakini Allen alishtuka na kumtungua yeye kwanza bahati nzuri Alex aliwahi kuinama hivyo risasi iliopita kwenye darubini ya bunduki yake ilimkosa na kama angechelewa kidogo tu basi risasi ile ingeingia jichoni. "si nilikwambia alitumwa wakati huu kukukamata, unatakiwa ukajipange upya kabla ya kumvaa" . Alikuwa akiwasiliana na mtu kupitia kifaa maalum alichokiweka sikioni. "huyi ndio Allen James" aliongea kwa taharuki, "kabisa ndio mwenyewe huyo, au wanamuita Project x. Huyo ndugu ni balaa na usipokuwa makini huenda akakuzidi katika mchezo huu ambao umeuanzisha wewe mweyewe".
"Sasa nifanye nini kwa maana tayari kashaiharibu bunduki yangu" Alex aliuliza na kwa maara ya kwanza anajikuta akiingiwa na hofu na mwili wake kuwa wa baridi. "cha kufanya toroka na uje Russia, muda wa kuonana mimi na wewe umefika" , "hakuna shida, wacha nitafute mbinu mbadala ya kuchomoka hapa bila kushtukiwa"Alex aliongea na kuipangua bunduki yake aina ya M21 na kuirudisha katika begi lake. Alishuka gorofa hilo kwa umakini na alippfika chini aliingia kweye gari aliokuja nayo na kutoweka eneo hilo.
***********************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kufika sehemu ambayo Scarlet anakuja kuchukuliwa, Scarlet alitoa kifaa maalum kidogo na kukibonyeza. Dakika kumi baadae ilifika helicopter "kwa heri Alex na nashkuru kwa msaada wako, na kuhusu tabia yangu usijali kwa sababu THIS IS THE REAL ME, ipo siku nitakulipa wema wako" Alipanda kwenye helicopter na kuondoka. "dah kwa hiyo ndio wananiletea kizee wakati huu, ama kweli wamechoka. Alitoa kifaa maalum cha mawasilino na kukiweka masikioni kisha akakiwasha "naomba unielekeze sehemu ambayo nitapata vifaa vya kazi" aliongea Alex, "Alex huyo jamaa ni balaa, kila uanchokifanya wewe yeye tayari alishakifnya. wewe leo unatafutwa watu wachache tu, yeye alikuwa akitautwa na serekali America na bado amewauwa mpaka viongozi wakubwa wenye ulinzi mkali sana".
"Lakini kipindi hicho sio saa hivi eti" Alex aliongea kwa dharau, " mi nakushauri tulia kwanza ujipange ndio umkabili laa sivyo atakushinda tu". "nimekwambia unielekeze duka la silaha na siyo kuanza kunipa mawaidha" Alex alifoka kwa hasira. "sawa nenda mpaka kwenye hoteli uliofikia katila maegesho ya magari kuna toyota nyeupe chukua na kila kitu utakuta humo". Baada maongezi hayo Alex alirudi katika ile hoteli na kuchukua gari alioelekezwa. Alikuta ramani ya maduka yote yanayouzwa silaha a bila kuchelelewa aliwasha gari na kuondoka.Alinunua kila alichotaka na kuondoka, alirudi kule kule hotelini lakini hakuingia katika hoteli aliyofikia badala yake alipada katika gorofa la pembeni yake na kwenda kujitega sehemu aliokuwa na uhakika hatoonekana. Alipanga sniper yake na kuweka kila kitu tayari kwa ajili ya kazi "we mzee umechoka na maisha subiri nikusaidie kukupeleka kwa muumba" aliongea na kutabasamu.
*****************************
Baada kutoka gorofa lile aliingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi bila kujua kama Allen alikuwa tayari chini akimsubiri, baada Alex kuondoa gari tu Allen nae aliwasha na kuanza kumafatilia. "doh hiki kizee balaa" Alex alijisemea moyoni lakini alipoangalia kwenye kioo cha pembeni akagundua kama kuna gari inamfatilia. "ntumie ramanai ya jiji zima hili"Alibonyeza kile kifaa cha mawasiliano na kuongea na muda si mrefu katika omputer ya gari yake ilitokea ramani ya Hongkong yote. Aliongeza mwendo wa gari na Allen nae hakuwa nyuma ila yeye hakuhitaji ramano mji mzima alikuwa anaujua kama kiganja chake cha mkono. Sasa ilikuwa ni fast and furious maana wote wawili walikuwa mafunfi katika kumudu gari. Alex alijitahidi kumtoroka mzee huyo lakini wapi ngoma ilikuwa nzito, wakati Allen akiendelea kumfukuza Alex aliangalia kwenye kioo cha pemebeni na kugundua kuwa kuna gari zinamfatilia. Alichikifanya aliacha kumfukuza Alex na kubadilisha njia ili awatoroke na hiyo ndio ikawa nafuu kwa Alex.
Allen alizidi kukanyaga mafuta na alifka katika kona na kuserereka, gari yake iligeuka ilipotoka hivo akawa yuko uso kwa uso na gari ya waliokuwa wanamfatilia. Alitoa bastola yake na kutoa mkono nje kisha akaanza kuishambulia ile na kuisababishia kugongana na gari nyingine. Alivuta handbreak na gari yake ikaserereka tena na kugeuka ilipokuwa ianaelekea kisha akakanyga mafuta na kutoweka. "ndio umefanya nini vile sasa" Robert alilalamika wakati anangea na Allen kupitia kifaa maalum, "umesahau kama tulikubaliana kazi hii nitaifanya peke yangu bila kufuatwa fuatwa" Alijibu Allen akionekana kukerwa na kitendo kile. "sasa kama leo nimeshambulia gari mara nyingine nitawauwa kabisa muje kubeba mizoga, na mukiendelea kunifatilia nitawafanya kitu ambacho hata Alex hatokufikia kwa ubaya" Aliongea Allen na kukata simu, "Allen, Allen" Robert aliita lakini wapi. "mi niliwaambia musifanye mukajifanya hamuelewi sasa mnaona, huyu ni hatari zaidi kuliko Alex. Hivi hamjui kama yupo namba mbili kwenye Blacklist" Alifoka Robert kuwaambia kina Mr Clinton na wengine waliojifanya kukiuka masharti ya Allen James.
Alex alifika uwanja wa ndege na kukata ticket ya kuelekea Urusi, "hivi huyu Allen ndio mbabe sana ama vipi, haiwezekani kizee kinishinde. Kwani ana nini hasa kinachomfanya awe special kuliko mimi" hayo yalikuwa ni baadhi ya maneno aliokuwa akijisemea moyoni baada kupata pigo kubwa kutoka kwa Allen James. Muda wa kupanda ndege ulfika na abiria wote waliingia kwenye ndege na safari ikaanza, safari yote Alex hakupata usingizi hata kidogo alikuwa akiwaza na kuwazua mbinu za kumchapa Allen.
Allen baada kukata mawasiliano na makao makuu ya upelelezi alitafuta mgahawa na kikata akaaanza kuwaza ni sehemu gani aliokwenda Alex. "kama natafautwa na Marekani, nitakwenda nhi gani ambayo nitakuwa salama" alikuwa akijiuliza swali hilo kichwani mwake. "kwa vyovyote vile nitakwenda nchi ambayo ina mkwaruzano mzito na Marekani na hiyo itakuwa ni Urusi tu" alipata jibu na kunuka sehemu aliokaa moja kwa moja mpaka kwenye gari yake na safari ya kwenda uwanja wa ndege ilianza. Njiani aliwasiliana na Robert aone kama atapata majina ya abiria walioondoka siku hiyo, majina yalipatikana lakini la Alex halikuwemo. Hata hivyo alikuwa na uhakika kama Alex atakuwa ameelekea urusi. Alifika uwanja wa ndege na kukata tiket, muda ulifika na safari ikaanza.
*********************************
Ndege ilituwa mjini Moscow majira ya saa saba usiku, kijana Alex alishuka na kuelekea njea ya uwanja. Ujumbe uliingia kwenye simu yake na kumpa maelekezo, alifata maelekezo hayo. "karibu Moscow" Nicolay aliongea na kumpa mkono Alex, "asante" Alex alijibu. Nicolay alimwabia, amfuate na kuongoza njia. Walifika mpaka kwenye gari na safari ya kuelekea asipopajua Alex ikaanza, ilkuwa ni safari ndefu na hatimae walifika. Alex alishuka na Nicolay akaoandoka, mlango ulifunguliwa "karibu nani Mr Alex" Christine aliongea. Alex aliingia bila kuuliza hata swali moja, alipelekwa mpaka katika chumba ambacho angelala kwa usiku huo. "Saa hivi pumzika, tutaongea kesho" Christine aliongea na kuaga. Alex aliingia bafuni na kujimwagia maji kisha alirudi chumbani na kujilaza kitandani na kutokana na uchovu wa safari usingizi ulimchukua ghafla.
Siku ya pili mapema asubuhi Alex aliamka na kama kawaida yake kufanya mazoezi kwa ajili ya kuweka mwili sawa. Aliingia chooni na kujifanyia usafi, baada kumaliza kila kitu ndani ndipo akaamua kutoka nje. Alikuta chakula mezani, "habari zaasubuhi" Christine alimuuliza. "nzuri tu" Alex alijibu na kukaa kwenye kochi. "kariu mezani tupate kifunguwa kinywa halafu tuingie kazini kuna mambo mengi sana unatakiwa uyajue" alisemea Christine huku akisimama na kuelekea mezani Alex nae hakuwa nyuma hasa ukizingatia jana yote baada kula asubuhi hakula tena mpaka wakati huo. Wakati wanakula "hivi umenijuaje" Alex alivunja ukimya, "nilijua tu utaniuliza swali hilo" Christine alijibu kisha akaendelea.
"Mimi nakujua kuliko unavojifahamu wewe mwenyewe, ila kiufupi nilikuwa nikifanya kazi kama secretary katika kitengo cha upelelezi nchini Marekani lakini kutokana na mambo ambayo bosi wangu alikuwa akinifanyia ilibidi niache kazi kwa kufeki kifo, mpaka muda huu tunaoongea wanaamini nimekufa. Na nilijipa ahadi moyoni kama lazima nitalipa kisasi" Aliongea Christine huku macho yake yakionesha ishara ya kujaa maji. "dah pole sana lakini kwanini ukanisaidia" Alex aliuliza, "ni kutokana na kuwa na ugumu kulipa kisasi mimi kama mimi ndio maana nikaamua kukusaidia kwa sababu mimi na wewe tunashare adui mmoja" Alijibu. Maongezi yalienedelea mpaka walipomaliza kula. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Christine aliinuka na kumwambia Alex amfuate, moja kwa moja walielekea katika chumba maalum ambacho kilikuwa kimepambwa na computer nyingi sana. "karibu humu ndio ofisini kwangu" aliongea Christine na kukaa kwenye kiti, "unafanya kazi peke yako humu" aliuliza kwa mshangao Alex. "ndio, ila nina wasaidizi wangu ambao ndio wale waliokuletea bahasha na yule alikuja kukupokea uwanja wa ndege. "si mchezo" Alex alijikuta akisema tu maneno hayo, "ok hatuna muda wakupoteza muda si mrefu Allen James atajua uko wapi, inabidi tufanya haraka na tuondoke eneo hili" Christine aliongea.
"hivi imekuaje huyu Allen akawa hatari kiasi hichi" Aliuliza Alex, "huyo mzee ni miongoni mwa watu wa mwanzo kujaribiwa na kemikali ya CODE X, mwanzo kemikali hiyo ilikuwa kali sana na wenzake wote walikufa wakati wa mchakato. hata hivyo mkewe ndie mtu ambae aliivumbua kemikali hiyo, na baada kugundua madhara yake ikiwa itaangukia mikononi mwa wa baya. Aliiharibu na kupoteza ushahidi wote, na pia aliitengeza keikali nyingine kwa ajili ya kuizimuwa lakini matokeo yake ndio akatengeza kiumbe kama huyo" Christine alimueleza, Alex alikuwa hoi baada kusikia hivo "sasa huyu jamaa nitapamabana nae vipi unadhani". "hatuna haja ya kupamabana nae, tunachotakiwa kufanya ni kumkwepa tu mpaka tuhakikishe tunamaliza kazi yetu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment