Simulizi : C.O.D.EX. 2 (The Dirty Game)
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Allen James anatoka nje ya uwanja wa ndege mjini Moscow, "Alex utakuwa umejificha wapi" Aliongea na kutafuta mgahawa wa karibu na kuingia. Alitoa laptop yake na kuanza kuhack computer za uwanja ndege kwa ajili ya kuangalia kama atapata chochote cha kuanzia. Lakini bahati mbaya sana hakukuta hata video moja iliomuonyesha Alex, tayari Christine alishafuta picha na video zote zilizomuonyehsa Alex. "vizuri sana lakini hapa umegonga mwamba ulioizamisha titanic" Allen alijisemea moyoni na kuatabasamu, kisha akaanza kuhack katika mafaili yaliofutwa. "bingo" Alijisemea baada kuzipata video zilizofutwa na zilimuonyesha Alex akitoka uwanjani. Video zilionyesha kila kitu mpaka alivopokewa na Nicolay, alifanikiwa kupata namba za gari ya Nicolay. "wacha mchezo uendelee" aliongea na kufunga laptop yake kisha akaondoka kwenye mgahawa huo. Alikodi taxi na kuelekea mpaka anapokaa Nicolay, aligonga mlango "nani wewe na unataka nini" alitoka mwanamke mmoja wa makamo hivi. "naomba kuonana na Nicolay" aliongea kwa upole, "Nicolay ndio nani" aliongea na kutaka kufunga mlango. Allen aliweka mguu na kutoa bastola yake na kumuwekea katika paji la uso, yule mwanamke alianza kutetemeka huku kijashi chembamba kikimtoka. "hakuna haja ya kuekeana bastola" ilisikika sauti ikitokea nyuma, "karibu" Nicolay aliongea kwa tabasamu. Allen aliingia na kumshukuru. Nicolay aliumuonyesha ishara yule mwanamke na kuondoka, "mimi nataka kujua tu kuhusu sehemu alipo Alex" Aliongea Allen. "na nisipokwambia je utanifanya nini" Nicolay aliongea kwa kujiamini, "utaniambia tu hata kama itabidi nijue kwa kutoa tone moja moja la damu katika mwili wako basi nitafanya hivo" Alijibu Allen akionekana kuwa hana masihara hata kidogo na jambo aliloongea.
NIcolay alikaa kimya akiwaza kitu, "akikuuliza chochoe wewe mwambie tu maana hatoondoka mpaka apate jibu analoliyaka" aliakumbuka maneno ya Alex. Ndio wakati Allen alivyokuwa anabasihana na yule mwanamke, Nicolay alimpigia simu Christine na kumwambia kuwa Allen yupo nyumbani kwake, Christine alishindw ajibu nini na ndipo akampa Alex simu. Alex baada kupewa simu alimwambia kuwa amwambie anachotaka kujua jwa sababu pangechimbika kama asingemwambia ukweli. "sawa unataka kujua alipo Alex" aliuliza Nicolay, "ndio we nambie tu yuko wapi na wala sitokugusa" Allen alijibu. Basi Nicolay hakuwa mbishi tena alimwabia sehemu alipo Alex, na Allen aliondoka bila hata kumgusa unywele. "doh kiasi Alex amuogope huyu mtu" Nicolay alisijisemea moyoni huku akijifuta kihasho kilichokuwa kikimtoka japo kulikuwa na naridi kali wakati huo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa tunafanyaje" Christine alimuuliza Alex baada kumsikia akimwambia Nicolay amwambie Allen anachotaka. "ikiwa Nicolay atamwambia ukweli nina uhakika Allen hatomdhuru so sisi tutafute makazi mengine maana hapa hapafai tena" Alex alijibu. Bila kuchelewa walianza kufungasha mizigo yao na walipohakikisha wamechukua vitu muhimu Alex akasema "we tangulia katafute pakukaa, niache hapa ili tusije tukamponza Nicolay, akifika Allen hapa nitajaribu kumpotezea muda halafu nitamtoroka". "acha na hilo wazo lako, unadhani utaweza kumtoroka kirahisi rahisi hivyo" Christine aliongea huku akionyesha wasiwasi. "we nenda haraka mi najua nitamtokaje huyu kiumbe" Alex aliongea kwa ukakamavu na Christine alikubali na kuondoka. Alex alijipanga ikiwemo na kukagua silaha zake ambazo angezitumia kukabialiana na Allen.
Dakika kumi tu baada kuondoka Christine, Allen alitia timu eneo hilo na kuanza kulikagua kabla hajaingia ndani. Alifika mlangoni na kutoa bastola yake ndogo kisha akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti. Aliribu kuufungua mlango ukafungunguka bila shida yoyote, ile kuingia tu Alex alianza kumimina risasi lakini kutokana na wepesi wa Allen alifanikiwa kuruka pembeni na kujibanza kwenye kipembe. "mi nilijua tu huwezi kukimbia kwa sababu unataka kujua kitu gani hasa nnacho ambacho wewe huna" Allen aliongea, "humu ndani ni mimi au wewe lakini wote wawili hatutoki" Alex alijibu kwa hasira. "punguza hasira kijana"Allen aliongea na kutoka sehemu alipokuwa amejificha huku akishamblia kwa risasi. "hivi huoni kama unatumika tu, baada kukaa kwako na familia yako" Alex aliongea kujaribu kumvuruga. "sasa wewe ungetulia kwenye kambi yako, uandhani mimi ningekuwa hapa kukuwinda" Allen alijibu akionekana ana wasiwasi hata kidogo. Alex alichungulia ili aone Allen uko wapi, alipotoa tu kichwa alikoswakoswa na risasi.
"Sijakukosa hiyo ujue, nimefanya makusudi ili ujisalimishe na kila mtu akaendelea na maisha yake" Allen aliongea huku akicheka. "kama unahisi wewe unajiweza kwanini tusichapane mkono" Alex aliongea huku akitoka sehemu aliokuwa amejificha. "halafu mimi pia nlikuwa nataka iwe hivo maana nina miaka mingi sana, sijapigana na mikono yangu inawasha sana" Allen alijibu na yeye akatoka sehemu aliyojibanza. Ni kwa mara ya kwanza Alex anamuona kwa ukaribu zaidi, alishangaa kuona mtu anaemuita mzee kumbe ni kijana kabisa. "ulidhani nitakuwa kikongwe, asante kwa dawa alionipa mke wangu umri unakwenda lakini kasi ya kuzeeka ni ndogo" Allen aliongea baada kugundua mshangao wa Alex. "natumai hutoniangusha, isije ikawa ni mpambano wa sekunde kadhaa tu" Alex aliongea na kunja ngumi kisha akamfata Allen kwa kasi, Allen alimkwepa na kumzawadia ngumu tatu nzito za mbavu na moja ya kifua. "acha kuja kama nguruwe kijana utaumia" Allen aliongea baada kuhisi ngumi zake zimegonga ndipo.
Alex alikohoa kidogo na alihisi kitu kama maji kikimtoka mdomoni, na alipojigusa akagundua kuwa alikuwa akitoka damu. Lakini hakulijali hilo, alijiweka sawa na kumfata tena. Wakati huu alikuwa makini sana, alisukuma masumbwi kadhaa lakini Allen aliyakwepa yote na kumtadika teke zito la kifua lakini Alex aliliona na kurudi nyuma na kabla Allen hajakaa sawa, Alex alirudi mbele kwa kasi na kurusha ngumi nzito ilipenya sawasawa kwenye kifua cha Allen. Allen alipoona kashachelwa kuizuia ngumi hiyo alipiga hatua moja nyuma na kukaza misuli ya kifua, ngumi hiyo ilimpata lakini haikuwa kali kama alivyotegemea Alex. "so mbaya kumbe ukitulia unaweza kupambana vizuri tu" Allen aliongea na kutabasamu.
Mpambano uliendelea huku Alex akionekana kuzidiwa na Allen, Allen alirudi hatua kadha nyuma ili kumpa Alex uwanja wa kupumua maana alielewa shughuli imemuelemea, Alex alipoona hali mbaya alikimbilia bastola yake lakini alipogeuka Allen alikuwa kashatoweka tayari. Alimtafuta nyumba nzima bila mafanikio yoyote, wakati akiendelea kufanya hivo simu yake iliita na alipoipokea "leo si siku ya kukumata nilikuwa nakupima uwezo tu lakini nasikitika umeniangusha sikutegemea kama anaesifiwa kuwa yuko rank moja na mimi ni mwepesi kiasi hicho, kajipange upya lakini kaa ukijua nitaendelea kukufatilia" simu ilikatika, Allen James ndie aliepiga simu hiyo. Alex alijikuta akiumuka kwa hasira maana yale maneno yalikuwa yamejaa dharau, siku hiyo ndio siku ambayo alihisi amedhalilika vibaya. Alikaa kwenye kochi na kumpigia Christine simu, baada kupewa malezo alipo mwanamke huyo. Alex alitoka na kuelekea huko lakini alikuwa amekasirika vibaya.
******************************
Mafunzo makali yaliendelea katika kambi moja hivi iliokuwepo jangwani, "ukiendelea hivo hutomaliza mafunzo" aliongea mtu ambae alikuwa akisimamia mafunzi hayo. "nani kasema mimi sitamaliza haya mafunzo" Agent Darling ama Christina au mtoto wa Allen James alijibu. "wengi walisema hivo lakini wakaachia mafunzo njiani" alijibu mwanaume huyo huku akitabasamu. "hata mimi nina imani utamaliza ikiwa utajitahidi sana maana mafunzo haya kila siku yanazidi kuwa magumu" alienedelea kuongea mwanaume huyo. Baada mazoezi Christina alimtafuta mwalimu wake huyo, "hivi mbona unaoenekana mdogo kuliko cheo ulichokuwa nacho" alimuuliza.
"Mimi nilinngia jeshini nikiwa mdogo sana" alijibu kisha akaendelea "si uliwahi kusikia kuna mtu anatumia jina la Ghost kama jina lake la kazi". "ndio" Christina alijibu, "sasa huyo mtu ndio mimi" Alijibu na kumuangalia Christina usoni, "wewe ndie Supreme commando Jeff the Ghost" aliuliza kwa mshangao. "ndio ni mimi" Jeff alijibu, Christina alibaki ametoa macho tu kwa sababu katika watu ambao alikuwa akiwakubali mmoja ni Jeff. "mafunzo haya ni magumu sana lakini matunda yake acha kabisa, ukisikia mtu anacheo cha THE ONE AND THE ONLY, ujue ni mtu wa kuogopwa sana ni zaidi ya commando" Jeff aliongea maneno hayo na kuona uso wa Christina ukichanua kwa tabasamu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"haya nambie imekuaje" Christine alimuuliza Alex alipofika hoteli aliyopanga, "acha tu kweli yule jamaa ni kiboko, kwa kweli amenitimba kisawasawa" Alex alijibu huku akishika upande wa mbavu za kulia. "mi nilikwambia Allen ni hatari sana" Chrstine aliongea, "lakini cha ajabu ameniachia wakati alikuwa na uwezo wa kuniua" Alex aliongea kwa sintofahamu. "achana na mambo hayo kwanza hebu badilisha nguo tuende hospitali kwanza maana naona hali yako si nzuri. Alex alikubali lakini aliposimama miguu ilikataa kumuonyesha ushrikiano kabisa alijikuta anaanguka na macho yake yakaanza kutandwa na ukungu na kwa mbali akaanza kuona kiza. Alijitahidi kupambana na hali hiyo lakini wapi kila sekunde kiza kiliongezeka na hatimae akapoteza fahamu kabisa, Christine alijaribu kumuamsha lakini wapi. Alitoa simu na kupiga namba za dharura, haukupita muda gari ya kubebea wagonjwa ilifika na Alex akawahishwa hospitali.
Alipofika alipelekwa moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha matibabu ya dharura kwanza ili kupewa hatua ya kwanza ya matibabu. Baada hapo alipelekwa chumba cha wagonjwa mahututi na kianza kupewa matibabu. Christine alibakia nje akingojea majibu kutoka kwa daktari ambae alikuwa anamshughulikia Alex. "wewe ndie ndugu wa mgonjwa" alitoka datkri mmoja na kuuliza "ndio" Christine alijibu. "Sawa sasa ni hivi, tumefanikiwa kumstablize mgonjwa lakini hatujui lini ataamka kutoka a kuumia sana hasa sehemu za ndani" Daktari aliongea. "kwani kitu gani alichoumia sana" aliuliza kwa shauku Christine. "amevunjika mbavu mbili za kulia, na nyingine mbili zina ufa, pamoja na kuchanika baadhi ya mishipa mikubwa ya damu" alijibu daktari.
"Sasa anaweza kuchukua siku ngapi mpaka kupata fahamu zake" aliuliza tena. "hatujui kwa kweli, inategemea na nguvu ya mgonjwa wako" alijibu daktari. "asante kwa taarifa zako" aliongea Christine na kukaa kwenye kiti akiwa anamawazo kibao kichwani. Siku mbili zilipita na bado Alex alikuwa chini ya uangalizi maalum wa madaktari, japo hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri lakini bado hakuamka. Alionekana mtu mmoja ndani ya mavazi ya kidaktari, alielekea kwenye ngazi na kupanda taratibu bila wasiwasi. na alipofika gorofa ya tano alikata kulia na kuelekea chumba ambacho alikuwa amelazwa Alex.
Aliingia ndani na kufunga mlango kisha akakaa pembeni ya kutanda. "kijana ndio unataka kulipa kisasi ukiwa katika hali hiyo, dhaifu namna hiyo" aliongea daktari ambae hakuwa mwengine ila ni Allen James, "huwezi kuondoka mapema kiasi hicho, ni lazima uamke ili na mimi nikamilishe kazi yangu" aliendelea kuongea Allen James akionekana kusikitishwa na udhaifu wa Alex katika kuhimili kishindo kidogo tu. Mapigo ya yaliokuwa yakisomwa katika computer maalum yalianza kuongezeka huku upumuaji wa Alex ukianza kubadilika. "hivo ndivo ninavotaka lazima uamke" aliongea Allen huku akitabasamu, hali ilizidi kubadilika. "amka ili tuendelee kucheza kamchezo ketu, lazima uamke commando hawezi kukaa kitandani siku zaidi ya tatu" Aliendelea kuongea huku akicheka.
Kwa mbali Alex alianza kusiki mawimbi ya sauti na alihisi kama anaifahamu vile, alijaribu kupambana na usingizi wake wa kifo ili kurudi hewani. "ndio, hivo ndio commando anatakiwa awe" Allen aliendelea kuongea manen ambayo yalitikisa ngoma za masikio za Alex na kuufanya ubongo wake ambao ulikuwa umelala kurudiwa na maisha huku akiitambua sauti hio kuwa ni ya mtu aliepeleka kwenye ulimwengu wa kiza. Ghafla Alex alifungua macho na ana kwa ana akakutana na sura ya Allen James aliekuwa akitabasamu. Alex alitaka kuinuka lakini Allen alimzuia na kumwambia"bado acha haraka subiri kwanza wala usiwe na wasiwasi mimi nimekuja kama rafiki kuja kukuona tu na wala sina nia ya kukudhuru" aliongea Allen na kumrudisha Alex kitandani.
"Natumai karibuni tutaonana tena vitani Alex Jr" aliongea Allen na kuinuka kisha akaminyia jicho na kuweka kidole mdomoni kama ishara ya kumwambia asije akaongea kitu kisha alifungua mlango na kuondoka. Dakika mbili baadae daktari alifika huku akihema, "viipi kijana unajisikiaje" Aliuliza. "niko powa" Alex alijibu , doctor alizikagua computer zote na kufanya tathimini ya haraka mpaka aliporidhika. Aliwaita wasaidizi wake na kuzifungua mashine zote ailizokuwa zikimsaidia Alex na baada ya hapo walimuhamisha chumba na kumpeleka katika wodi za wagonjwa wa kawaida.
Baada hapo doctor alimpigia simu Christine na kumueleza hali halisi kama ilivyo, haukupita muda mrefu Christine alifika hospitali na moja kwa moja alikwenda katika chumba alicholazwa Alex baada kuamishwa ICU. "unajisikiaje" swali la kwanza alilomuuliza, "ah najiskia fresh tu" Alex alijibu huku akitabasamu. Taratibu za kutoka hospitali zikafanyika na akaruhusiwa kuondoka aende kumalizia kujiuguza nyumbani. Alipewa baadhi ya dawa za kumsaidia, walitoka Hospitali na kuanza safari ya kurudi bila kujua kama kulikuwa kuna mtu ana wafatilia katika gari nyingine. Lakini ghafala kioo cha mbele cha gari iliokuwa ikiwafatilia kipasuka na damu nyingi ikaruka. "nimesema sitaki kuingiliwa katika kazi yangu" Allen aliongea huku akiliangalia bomba la sniper yake likitoa moshi baada kufyatua risasi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********************************
"Bosi mtu wetu aliekuwa akimfatilia Alex ameuwawa" Aliingia Martin ofisini kwa Mr Clinton na kutoa taarifa hizo, "unasemaje wewe" aliongea huku akisimama. "ndio amepigwa risasi lakini mpaka sasa hatujajua aliempiga ni nani" alijibu na kuongezea. "we unadhani atakuwa nani kama si Allen James" aliongea kwa hasira Mr Clinton, "niitie Robert" alitoa agizo na bila kuchelewa Martin alitoka na kuelekea ofisini kwa Robert na kumpa taarifa ya wito huo. "naam bosi" alifikia na kuongea, "umemuona mbwa wako alichokifanya" alifoka Mr Clinton,"mi mbona sina mbwa" alijibu Robert. "unajifanya humjui mbwa wako Allen James" aliongea kwa sauti kubwa, hapo hapo Robert alivua kitambulisho chake na kuchomoa bastola yake kiunoni pamoja na funguo za ofisi na kuziweka mezani.
"Una maana gani kufanya hivi" alifoka Mr Clinton, "kwani hujui maana yake au vipi" sasa na Robert alipandisha kifua. "nimeacha kazi rasmi leo, siwezi kuvumilia ushenzi wako. we utamuitaje binaadamu mwenzio mbwa wakati unajua ameacha familia yake nyumbani kuja kukuasaidia wewe wakati anajua kabisa huenda matokeo ya kazi hiyo yakamgharimu maisha yake. Kwani Allen alisemaje kuhusu kazi hii, ataifanya peke yake bila msaada wenu sasa kilichokutuma upeleke watu wako ni kitu gani.
"Na kama hujui mimi ndie niliemwambia kama bado unamfatilia na ndie nliempa ruhusa ya kumuua mtu wako" Robert alimaliza kuongea na kuondoka. Mr Clinton alinyanyua mkonga wa simu na kutoa amri akamatwe na bila kuchelewa wanajeshi wakaingia ndani yamjengo na kuanza kumuwinda Robert. Ambalo hawakuliju kuhusu Robert ni kwamba alikuwa mmoja kati ya watu watano wa mwanzo pamoja na Allen waliofanyiwa jaribio la CODE X. Ila yeye alipewa jina la HUMAN KILLING MACHINE (H.K.M), mashine ya kibinaadamu ya kuuwa. Alipogundua kama imetolewa amri akamatwe alijibanza pahali, na mwanajeshi wa kwanza kupita alimkamata na kumvunja shingo. Kisha akahukua bastola na kuanza kukimbia, kila mwanajeshi aliepeita mbele yake alichezea risasi.
Risasi kwenye bastola aliokuwa anatumia zilikwisha, hivyo aliitupa na kuendelea kukimbia. Kwenye kona ghafla alitokea mwanajeshi, Robert alidunda na kupiga sarakasi ya mbele na alipotuwa tu alibiringitia chini na kufika alipo mwanajehi huyo. Hakuchelewa alibetuka kutoka chini na kumtandika teke zito la kidevu lililomrusha mwanajeshi huyo na kumbamiza ukutani. baada hapo alichungulia kwenye ngazi na kuona kundi la wanajeshi likipanda juu, alirudi kwenye koridoo na kuangalia disrisha moja la upande wa kulia ambalo lilikuwepo mita kadhaa kutoka alipo. Na kwa sababu alilielewa jengo hilo vizuri hakusita alifyetuka kama risasi na kwa kasi ya ajabu alikwenda moja kwa moja kuruka.
Alipasua dirisha katika gorofa ya thalathini na kutoka, kutokana na kasi aliokuwa nayo alifanikiwa kupenya katika kioo cha gorofa jirani na kuangukia kitandani. Aliinuka na kuweka suti yake sawa kisha akatoa check ya bank na kumkabidhi mwanaume aliemkuta katika chumba hicho. "wakitaka uwalipe utawapa hio sawa" aliongea na yule mwanaume alingisha kichwa kuashiria amekubali. Baada hapa Robert alifungua mlango na kutoka, alifika chini na kukuta mtu anashuka kwenye pikipiki, "niazime usafiri wako" aliongea huku akimnyang'anya funguo kijana huyo na alipoleta ubishi alichezea ngumi ya kifua na kuanguka chini kama mzigo.
Aliwasha na kutoweka eneo hilo kama vumbi, "ametutoroka" aliripoti mwanajeshi mmoja. "nyie ama kweli hamuna faida" alifoka Mr Clinton, "mkuu kuna tatizo" aliingia Martin huku akihema. "nini tena" Mr Clinton aliuliza, "njoo mwenyewe ujionee" aliongea Martin na kutoka ofisini, Mr Clinton alifata nyuma. Alifika katika chumba ambacho alipelekwa na Martin. Macho yalimtoka baada kukuta miili ya wanajeshi zaidi ya thalathini ikiwa imelazwa. "nani aliefanya hivo" aliuliza, "Robert mkuu" Alijibu Martin. "haiwezekani na alivyo boya vile" aliongea kwa dharau. Maggy aliingia na laptop ndogo mkononi ikionyesha video kwa jinsi Robert alivyokuwa akitekeleza mauaji, Mr Clinton alipoiona tu hiyo video alipata mshtuko wa ghafla na kuanguka chini na kupoteza fahamu.
**********************************
"Nipe ripoti"aliongea mtu mmoja, "kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa" alijibu Robert. "kazi nzuri sana" alipongeza yule mtu. "ikiwa mambo yatakwenda hivi mpaka mwisho basi itakuwa vizuri sana" aliongea yule mtu. "unaweza kwenda kupumzika" Robert alipewa ruhusa na kutoka, "mkuu, kazi inakwenda kama ulivyopanga" yule mtu alinyanyua simu na kupiga. "usijali hakuna hata mmoja atakaeshtukia mchezo mzima, lets them play the dirty game" aliongea kwa majigambo huku akicheka.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alex na Christine wala hawakushtuka kama wanafatiliwa, waliekea mpaka katika hoteli waliopanga. Lakini Alex alikuwa na mawazo sana kuhusu Allen kuja kumtembelea hospitali na alitaka kumwambia Christine lakini akakumbuka ishara aliopewa na Allen wakati anaondoka. Kwa jinsi alivyokiweka kidole mdomoni ni dhahiri hakutakuwa kumwambia mtu yoyote ujio wake. "karibu tena" Christine aliongea, "asante" Alex alijibu na kuelekea chumbani kwake. Na kwavile walikodi apartment kila mtu alilala katika chumba chake. Alipofika chumbani kwake aliingia bafuni na kujimwagia maji japo bado alihisi maumuvi makali lakini alijikaza kiume.
Alirudi ndani na kukaa kitandani huku akiendelea kuwaza, ghafla uliingia ujumbe kwenye simu yake "kuanzia sasa usimuamini mtu yoyote hata huyo mschana unaekaa nae..... Allen James". "kwanini" Alex alijibu ujumbe huo, "ukifika muda nitakwambia lakini nahisi kuna kamchezo kachafu unachezewa" Allen alijibu. "unasemaje wewe unataka kunitenganisha na mtu anaenisaidia si ndio" Alex alindika ujumbe na kutuma. "Kesho tukutane 18''20 saa A6:3M" Allen alituma ujumbe huo kwa njia ya kodi maalum ambazo watu wa aina yao tu ndio walizielewa. "sawa" Alex alijibu na kuweka simu pembeni kisha akajilaza kitandani.
Siku iliofuata Alex alitoka mapema asubuhi, "unaenda wapi" Christine alimuuliza. "ah naenda kutafuta dhana za kazi" Alex alijibu, "nikusindikize" Christine aliongea. "hapana na nashkuru ila ntakuwa sawa tu" Alex alijibu na kutoka. "mhh mbona kabadilika ghafla"Christine alijisemea moyoni, baada Alex kutoka tu Christine alifungua begi lake na kutoa simu nyingine. "habari yako mkuu" aliongea baada simu kpokewa, "ndio ila nahisi Alex kashaanza kushtuka" "ok hamna shida". Alimaliza kuongea na kukata simu "yatukuke mapinduzi" Christine alijisemea na kukunja ngumi kisha akaiweka kifuani kama ishara ya kutoa heshima.
Alex alitembea kwa umakini wa hali ya juu huku akihakikisha hakuna anaemfuatilia, alifika mpaka katika jengo aliloambiwa afike na kupanda lifti kuelekea juu kabisa. "unakwenda na muda kijana" Allen aliongea punde tu baada Alex kufika, "usiwe na wasiwasi kuanzia sasa mimi sio adui yako kabisa lakini nataka kukusaidia" Allen aliongea na kumshangaza Alex. "unataka kunisaidia kivipi" aliuliza ka mshangao, "kijana mimi pia niliwahi kuwa katika hali kama yako wakati fulani kwa hiyo naelewa ni kiasi gani unateseka kutaka kujikomboa na utumwa wa akili" aliongea Allen na kutoa kitu mfukoni kisha akakirusha kwa nguvu lakini Alex alikiona na kukidaka na alipoangalia vizuri aligundua kama kilikuwa kisu kidogo.
"Umeniita uje kuniuwa" aliongea kwa hasira Alex, "hapana siwezi kumuua mgonjwa kisha nikajisifu nimefanya kazi" Aliongea Allen na kutabasamu. "akili yako ni kama yangu tu, lakini wewe bado hujajizoesha kuitumia inavotakiwa" Aliongea Allen kisha akaendelea "we unadhani kwanini mara zote mbili nilizokutana na wewe nimekushinda, ni kwasababu nilikuwa nafikiria hatua moja au mbili mbele yako". "sijakufahamu" Alex aliongea "sisi ni watu amabao tuna uwezo mkubwa sana wa kufikiria, kama saa hivi najua kama unataka kutoa bastola ili uniue" Aliongea huku akicheka na kweli Alex alikuwa na bastola ndogo mfukoni ambayo ilikuwa tayari imeshakokiwa vizuri tu.
"Umejuaje" Alex aliuliza huku akitoa macho, "mi si nimekwambia nafikiria hatua moja au mbili mbele yako" Allen alijibu."usijali utajua jinsi ya kusoma mchezo wa aina yoyote ile" aliendelea kuongea Allen kisha akampa ishara amfuate na Alex nae alifanya hivo bili kusita mpaka alipofika mwisho wa jengo hilo kabisa. "we unadhani kwa nini Rose anakusaidia" aliongea Allen, "Rose ndio nani" Alex aliuliza, "ah nimesahau kumbe anatumia jina la Christine" alijibu huku akitabasamu. "ananisaidia kwa sababu anataka na mimi nimsaidie kulipa fedheha alioipata kutoka kwa bosi wake" Alex alijibu kwa kujiamini kwasababu ndivyo alvyoamini.
"Umechezwa akili kiajana" aliongea Allen na kumshika bega Alex, "una maanisha nini" Aliuliza. "we unadhani ni rahisi sana mtu kufanya hivo, hapana kijana. Kuna mchezo unachezewa hapa, kwanza wewe ni miongoni mwa watu wanotafutwa kwa udi na uvumba Marekani yote. Sasa basi Christine au Rose jina lake halisi anakutumia kuondoa vikwazo vyote katika njia ya mkuu wake kuelekea utawalani. Wewe ndie unaekwenda kufanya mashambulizi ikiwa utakamatwa basi yeye atakuacha ufe mikononi mwa serekali. Au pili ikiwa utafanikisha kazi ya kuwauwa watu wote ambao wapo katika list yake basi kuna vijana wake ambao huwa wanakufatilia kwa siri watakuuwa ili kupoteza ushahidi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo huo nimetumwa mimi kuja kukumata nikurudishe mikononi mwa serekali, lakini nilichogundua ni kwamba wamenituma makusidi wakielewa kuwa sitakuuwa wala kukukamata bali utajifunza mbinu zaidi kupitia mimi. Hapa sasa ndipo unapokuja mchezo mchafu na kaa tayari na kuumia kwa ntakachokwambia, kuna kikundi maalum cha watu wamejipanga kuiingiza dunia katika machafuko. Hicho kikundi kinaitwa "THE REVOLUTIONARIES" (WANA MAPINDUZI), kiongozi wao bado sijamjua ila Christine, Mr Clinton, Robert na wengine wengi wanamtumikia bila kujua kama wanawindana wenyewe kwa wenyewe"Alimaliza kuongea na kumtazama Alex amabe alikuwa haamini anachokisikia.
"Huo upuuzi umetoa wapi" Alex aliongea, "kijana huu si upuuzi bali nakutahadharisha tu ujiandae kiakili kwa chochote kila kitakachokukuta" Allen alijibu na kumwagalia kwa makini. "ukitaka kuugundua ukweli fanya hivi, kwa sababu wao wanatuchezea mchezo mchafu na sisi tuwaingizie mchezo ndani ya mchezo wao ili tujue nani kiongozi wao na hapo ndio tutaweza kuokoa maisha yetu na ya wale tunaowapenda pamoja na dunia kwa ujumla. Kitendo cha kuondoka hapa mimi na wewe si marafiki bali ni maadui kama mwanzo tu na kaa ukijua nikikutana na wewe kwenye anga zangu nakuchapa kama kawaida lakini ukiwa makini utajifunza mengi"Allen aliongea na kumpa mkono Alex kama ishara ya urafiki. Alex aliupokea na kutabasamu, "acha tuwaoneshe kama sisi si panya wa maabara kututumia wanavotaka" Alex alionea na kumfanya Allen atabasamu "that is the spirit boy" Allen aliongea huku akiondoka.
****************************
Kikao cha siri kilikuwa kikiendelea katika makao makuu ya THE REVOLUTIONARIES, ajenda ya kikao hicho ilikuwa ni kukusanya ripoti kuhusu mienendo yao. Ripoti zote zilikuwa zinaridhisha "vizuri sana wanangu, mnanipa furaha sana" Aliongea mtu alievalia gwanda jeshi, alikuwa anafanana na Hitler katika ubora wake. "hatua ya kwanza imekwisha, sasa tunaelekea hatua ya pili ya kuwaondoa viongozi wote ambao wamekataa kuungana nasi" aliendelea kuongea, "hatua hii ni muhimu sana na hakutakiwi kutendeke makosa yoyote yale na ikiwa itafeli mujue hatutafika pale tunapopataka"."tumekuelewa mkuu na tunakuahidi kuwa hakutatendeka makosa yoyote yale na kazi itakwenda kama ulivyopanga" walijibu wote kwa pamoja na kusimama. Na tena kwa pamoja wakakunja ngumi na kusema YATUKUKE MAPINDUZI.
Alex alirudi katika hoteli waliopanga lakini cha ajabu hakumkuta Christine, wakati anazungukuzunguka alikuta karatasi mezani iliokuwa na ujmbe "kuna kitu nafatilia nitarudi jioni". Baada kuisoma alitabasamu kidogo kisha akaelekea chumbani akiwa na begi alilorudi nalo, alipofika kitandani alilifungua na kumwaga silaha kuanzia ndogondogo mpaka kubwa. Alipanga vizuri na kuhakikisha kuwa zote zina risasi na ziko sawa. Baada hapo aliingia bafuni na kuoga, aliva suti nzuri na iliotulia kisha akarudi sebleni na kukaa.
Christine aliporudi na kumkuta Alex sebleni, ilibidi ashangae kwanza kwa jinsi alivyokuwa amependeza. "wapi tena mbona umevaa suti" aliuliza kwa mashangao, "ah nimeamua tu kutoka kiofisi zaidi" Alex alijibu huku akitabasamu. "sasa mipango tunaanza lini" aliuliza Alex, " we si bado hujapona" Christine aliuliza na yeye. "mi mbona mzima kabisa, nashkuru kwa kemikali walioingiza mwilini mwangu" Alex alijibu huku akitabasamu. "kama ni hivo itakuwa vizuri sana, maana nilijua ungekaa sana" Christine alijibu na kuelekea chumbani kwake. Baada kama dakika mbili hivi alirudi akiwa na bahasaha ya wastani mkononi na kuiweka mezani, kwa muonekano tu Alex aligundua ile bahasha ilikuwa imeletwa kama amri kutoka sehemu fulani "acha tu nicheze kwa sheria " Alijisemea moyoni.
Christine aliifungua ile bahsasha na kutoa picha kadhaa. "huyo kwenye picha anaitwa Marko, yupo hapa Urusi na mmoja kati watu waliohusika na vifo vya familia yako" Christine aliongea huku akimuangalia Alex kwa makini usoni. Sura ya Alex ghafla ilibadilika na kuoneha wazi kuwa alikuwa na hasira. Aliichukua ile picha na kuiangalia kwa umakini sana kisha akairudisha mezani na kuicora alama ya X kwa kalamu nyekundu. "lini anatakiwa aondoke duniani" Aliuliza akionesha kabisa hasira zake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndani ya masaa arobaini na nane awe tayari ameshatangulia mbele za haki" Aliongea Christine na kuichukua ile picha na kuirudisha katika bahasha, baada hapo alimpa Alex maelezo ya anaweza kumpata mtu huyo. Baada ya maongezi hayo Alex alikwenda chumbani kwake na kubadilisha nguo na kuvaa zile nguo zake maalum za kazi. Alitoa begi la silaha na kuchagua silaha lakini wakati anafanya hivo uliingia ujumbe katika simu yake ukisema "chukua M23...Allen James". Alitabasamu kidogo na kuujibu "asante mkuu". Alitoa begi jingine dogo na kuiweka sniper yake kisha aktoka na kumuaga Christine, alitoka nje na kuchukua gari na kuondoka.
Akiwa kwenye gari uliingia ujumbe mwengine "kuwa makini unafatiliwa", alizdi kukanyaga mafuta na kufanikiwa kuwatoroka walikuwa wanamfatilia. Alifika mpaka kwenye sehemu alioambiwa atamkuta huyo mtu, alipanda gorfa jirani na kwenda juu kabisa. "umechelewa dakika moja" Allen aliongea baada Alex kufika, "duh unafanya nini hapa" Alex aliuliza kwa mshangao. "niko hapa kukupa mafunzo ambayo hujawahi kupewa ukiwa kambini" Allen alijibu bila kumuangalia Alex. "mtu uanetakiwa kumuua bado hajafika, na ni mtu ambae anaheshimika sana katika nchi hii hivyo basi kaa ukijua kuwa ukifanya kosa tu umekwisha naa natumai unalielewa jeshi la nchi hii katika usakaji wake" Allen alimueleza kisha akendelea "risasi inayo takiwa kutumika ni moja tu na hakuna kurudia, ukikosea unatakiwa kukimbia haraka iwezekanavyo. Jingine hutakiwi kutumia darubini kwa sababu wanavifaa maalum vya kisasa ambavyo vinasensa moja matata sana, unatakiwa kutumia macho tu.
Na umbali kutoka hapa mpaka atakapokaa ni makadirio ya mita 60. Dakika yoyote kutoka sasa ataingia nakutakia jaribio jema"Allen alimaliza kuongea na kuondoka bila kusubir Alex aongee chochote. Alex alibaki ameshangaa tu huku akijiuliza atawezaje kulenga mita 60 bila kutumia darubini, aliona huo ni mtihani mkubwa sana lakini alijipa moyo kupitia jina la familia yake ilioteketea bila hatia kuwa ataweza kumtungua. Alifungua begi lake kuanza kuipanga sniper yake na kama alivyoambiwa na Allen aliweka risasi moja tu kakaa sehemu ambayo angeweza kumpata vizuri.
Gari sita zilifika nje ya hiteli na Marko akashuka na vijana wake na kuingia ndani, moja kwa moja alielekea mpaka katika meza maalum ambayo huwa anakaa akifika katika hoteli hiyo na kukaa. Ukaguzi ulifanyika na baada hapo walinzi wake walisogea mita kama tano hivi kutoka alipo kwasababu alikuwa akikutana na mtu kuongea kitu ambacho ni siri. Alex alikuwa makini juu huku akipata tabu sana kumlenga kutokana na umbali, wakati akiwa katika hali hiyo uliingia ujumbe kwenye simu yake "tuliza akili yako na fanya kama hakuna kitu kingine mbele yako zaidi ya Marko na pumua taratibu sana hakikisha husikii chochote zaidi ya pumzi yako.... Allen James".
Alifanya hivo na taratibu akili yake ikatulia, baada hapo alifuta kila kitu mbele yake isipokuwa Marko peke yake. Kisha akaanza kupumua taratibu huku akiisikilizia pumzi yake. Mapigo yake ya moyo yalirudi kati hali ya kawaida na alishanga kuona kama hata macho yake yana uwezo kuvuta. Hakupoteza tena muda aliweka kidole kwenye trigger na kufyatua risasi iliosafiri moja kwa kwa moja mpaka kwenye kichwa cha Marko na kuweka saini kama imefika. Marko alianguaka chini kama mzigo na kukata upepo. Bila kuchelewa alirudisha sniper yake kwenye begi na kuanza kuondoka lakini uliingia ujumbe ukimwambia "kwenye mlango wa kutokea juu hapo kuna begi la parachute, chukua na uruke upande wapili wa gorofa na ukatue 18:71 nitakuwa nakusuburi". Alikwenda mpaka kwenye mlango na kuchukua begi na kulivaa, alianza kukimbia na kuruka.
Alifika sehemu alioelekezwa na kumkuta Allen akimsubiri "kazi nzuri, umefaulu jaribio la kwanza" Allen aliongea na kumpa mkono Alex ambae alionekana kuwa na furaha sana. "lakini kitu kimoja, kumbuka ukishafanya kazi ni mwiko kurudia njia uliopita mwanzo, kwa hiyo kabla ya kutekeleza kazi yoyote ile unatakiwa kutengeza mbinu za kuitekeleza kazi hiyo bila kusahau kutengeza mbinu ya kujiokoa (back up plan) ikiwa itatokea utafeli. "nimekuelwa na nashkuru kwa msaada wako" Alex aliongea "tukutane tena katika kazi yako ya pili, na nina uhakika itakuwa ni moja kati ya nchi hizi mbili Uingereza ama Marekani" Allen aliongea na kungia kwenye gari yake kuondoka "dah huyu mzee kumbe ni balaa yaani angekuwa ni adui yangu nina uhakika saa hivi ningekuwa jela au marehemu" alijisemea moyoni huku akicheka na kuondoka eneo hilo. Alirudi mpaka katika ile hoteli alipoacha gari yake na kupanda kisha akaondoka eneo hilo.
"Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Don Marko ameuwawa kwa kupigwa risasi ya kichwa" hiyo ilikuwa ni taarifaa ya habari ikitangazwa na kituo kimoja cha taifa nchini urusi, habari hiyo iliwaumiza wengi ambao walikuwa wakimtegemea Don Marko. Lakini haikuwa hivyo kwa wale wanaoishi mitaani walionekana kufurahi sana. "afadhali amekufa maana tulikuwa hatuna amani, mtu anajiona kama mungu bwana" alisikika mtu mmoja akiongea. Mfarakano ulitokea katika kikao cha dharura kilichowahusisha watu wakubwa, "hebu tulieni kwanza sasa mukibishana atarudi duniani au vipi" aliongea mmija mabe alionekana kuwa kiongozi wao. "baada kubishana ujinga tutafute nani aliehusika na kifo chake na lazima alipe kwa maisha yake" aliongea kwa hasira sana mpaka akwa natetemeka. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati kikao kikiendelea aliingia mschana mmoja kumkabidhi mkuu wake bahasha, alipoifungua alikuta picha ya Marko ikiwa na alama ya X na alipoigeuza nyuma akakuta ujumbe "anaefuata atakuwa nani". Aliishiwa nguvu na kukaa kwenye kiti huku akiiweka ile bahasha mezani, wengine waliichukua na kuangalia kilichokuwemo ndani. walishangaa kukuta picha zao zote ambazo zimepigwa wakati huo wakiwa kwenye kikao. Vurugu lilizuka tena huku kila mmoja akianza kumuhisi mwenzake kuwa ndie ambae anahusika na mauaji ya Marko. Kutokana na vurugu kuwa kubwa kikao kilivunjika na kila mmoja akaondoka akiwa kachukia sana
**************************
"hahahahaha ukitaka kuwaongoza watu vizuri wagawe makundi" aliongea mtu mmoja ambae alikuwa amevaa gwanda za jeshi na kucheka kwa nguvu huku akiwa anaangalia video zilizowaonyesha wale wenzake na marehemu Marko wakigombana.
"Unahis vipi baada kumuondoa Marko katika uso wa dunia" swali la kwanza alilokutana nalo kutoka kwa Christine baada kufika tu hoteli. "ah kawaida tu, mbona kuuwa kwangu ni jambo dogo sana" alijibu Alex na kuelekea chumbani kwake, alijitupa kitandani huku akiwaza na kuwazua inakuaje Allen James anakuwa hatari kiasi kile. Maana zile mbinu nazotumia si mchezo, kuweza kulenga mita zaidi ya 70 bila kutumia darubini. Mwisho aliona atapasuka kichwa tu ikiwa ataendelea kuwaza, aliamua kuinuka na uingia chooni kwa ajili ya kujifanyia usafi. Alimaliza na kurudi chumbani, alivaa nguo za kawaida na kutoka.
Chakula kilikuwa kimeshaletwa walikaa pamoja na kuanza kula huku wakiongea mambo mengi. "kesho tutaelekea Uingereza na tutaondoka hapa asubuhi" Aliongea christine, "sawa hakuna shida" Alex alijibu kwa sababu alishajua mapema kuwa wangeondoka Urusi. Baada ya kula kila mtu alikwenda chumbani kwake na kuupitisha usiku ambao kwa Alex ulikuwa ni mzuri sana hasa ukizingatia kuwa kuna mtu ambae anamthamini kama mtu na sio mashine tu ya kufanyia mauaji.
Siku ya pili mapema waliondoka na kuelekea uingereza, katila ndege walipata viti vya mbali mbali. Alex alikaa na mtu mmoaja ambae alikuwa akisoma gazeti hivo hakufanikiwa kumuona sura. "naona tunakwenda Uingereza" Aliongea yule mzee na kumafanya Alex kushtuka kwa maana sauti hiyo aliifahamu kama ilikuwa ya Allen. "Allen unafanya nini humu" Alex aliuliza kwa sauti ya chini, "si nasafri kama abiria wengine" Allen alijibu huku akiondoa gazeti. Alex karibu acheke kwa nguvu maana kwa jinsi alivyokuwa Allen ni shida, alikuwa amebandika ndevu nyngi pamoja na sharubu kitu ambacho kama hujawaho kukutana nae lazima usingemjua.
"sasa sikia tupange mikakati, kwanza walioiteketeza familia yako ndio waanze kuangamia halafu ao wengine watafuata" aliongea Allen, "ah sasa si nimeshaanza kuwaondoa" Alex alijibu kwa kujiamini. "acha ujinga wewe yule uliemuua jana hahusiki na vifo vya familia yako" Allen aliongea na ghafla sura ya Alex ilibadilika na kuwa kama ameanza kukasirika. "mi nimekwambia unatumiwa kufanikisha kazi za watu" Allen aliendelea kusukuma msumari wa moto katika kifua cha Alex. "mbona sielewe elewi" Alex aliongea huku akionekana kuwa amechanganyikiwa, "ndio lazima usielewe kwa sababu unachezewa mchezo mchafu" Allen alijibu.
"Sasa nisikilize kwa makini, huko tunapokwenda yupo mtu mmoja ambae alihusika moja kwa moja katika utekelezaji wa mauaji ya familia yako. Huyo mtu ni mjapan mwenye uraia wa uingereza na anaitwa Masaya Okinamoto. Ni mtu hatari na ili umfikie karibu lazima upitie mashindano maalum ya ngumi za haram, mchezo huo unaendeshwa na matajiri wengi sana pasi na serekali kushtukia. Na kwa sababu Masaya hajawahi kushindwa, hivyo fainali lazima utapambana nae na hapo ndio muda ambao nitaingilia kati na kumteka. Lakini hakikisha unamchakaza vya kutosha lakini usimuue" Allen alimaliza kuongea na kumuangalia Alex aliekuwa ametoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango.
"Hivi kwanini umeamua kunisaidia" Alex aliuliza swali ambalo lilimshtua kidogo Allen, "kijana mimi ni mtu mzima sana, na katika maisha yangu sikuwahi kufanya jambo zuri kama hili. Nimekuwa katika mazingira mazuri sana na sikutegemea hata siku moja kama saahivi ningekuwa katika hali hiii. Nimeona nikusaidia kwa sababu kiupande fulani najiona mwenyewe nikikuangalia kwa jinsi maisha yalivyokufanyia na watu waliokutenda ubaya. Wao saa hivi wanaishi vizuri na familia zao hali ya kuwa wewe maisha yako yamejaa misukosuko kama nilioipata mimi" Allen aliongea huku akionekana kama kutonesha kidonda ambacho kilikuwa kimepona juu lakini ndani bado kilikuwa kibichi. Na hapo ndipo akaanza kumuelezea historia yake na mambo yote yaliomkuta kipindi hicho akiwatumika watu wasio na shukrani hata kiodogo. "kwakweli sikujua kama ulipitia mambo yote hayo na nisamehe kwa kuktonesha kidonda ambacho kilikuwa kimeshaanza kupona" Alex aliongea baada kugundua kuwa macho ya Allen James yalikuwa yashaanza kuja maji na hapo ndio akaona kwa nini mzee huyo amekubali kumsaidia wakati akijua kabisa mwisho wke hautokuwa mzuri. "kijana katika haya maisha kuna mambo mawili ya kuchagua aidha uishi kama mtu huru au usishi kama mtumwa lakini huwezi kuishi katikati ya mambo hayo mawili. Namaanisha ukubali kuendelea kutumika au uutafute uhuru wako na uendeshe maisha yako kama watu wengine na hakuna kitu kizuri kama kusihi ukiwa na amani" Allen alimsihi Alex achague njia ambayo itampa faida katika masiha yake yote.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alex alikuwa kimya kwa muda akitafakari maneno ya mzee huyo ambe kwa nje alinekana mzee lakini ndani alikua ni kijana kabisa. "nimekuelewa, na usijali nitachagua njia nzuri tu ambayo hata wewe utaipenda" Alex aliongea huku akitabasamu, "na kitu kimoja pia ukae ukikijua kuwa kisasi si kizuri kabisa hata ukiwauwa watu wote waliokutendea ubaya lakini familia yako haitorudi tena duniani, pia kisasi ni kizuri ikiwa utafanikisha malengo yako kwa sababu utakuwa umeutuwa mzigo mzito uliokuwa umeubeba moyoni mwako" Allen alizidi kumpanga Alex kisaikolojia bila Alex kutambuwa hilo, "sawa nimekuelewa lakini kwangu mimi kisasi ni kizuri sana hapa ni mwendo kutengua viungo mpaka kieleweke" Alex aliongea na kumwangalia Allen ambae alionekana kutabasamu. Waliendelea kuongea mambo mengi tu huku wakipanga mikakati ya kuwakomesha wale wote wanaowachukua vijana na kuwafanya panya wa lab kwa kuwafanyia manyaribio mbali mbali. Hatimae ndege ilikanyaga ardhi ya uingereza mjini London, kila mmoja alishuka na kuelekea njia yake kama hawajuani kabisa. Na mbaya zaidi hata Christine hakushtuka kama ndan ya ndege hio hio moja kachezwa akili, akiongozna na Alex walitoka mpaka nje ya uwanja na kuchukua taxi kisha safari ikaanza. "tunakwenda wapi" Alex aliuliza, "we utapaona tu"Christine alijibu basi na Alex alijifanya mjinga bila kuuliza swali jingine lolote lile. Walitembea kwa muda wa nusu saa mpaka nje mji kidogo, Taxi ilisimama nje ya jengo kubwa sana na wakashuka. Christine aliomgoza njia huku Alex akimfata kwa nyuma, walifika mlangoni na Christine akatoa funguo na kufungua. Waliingia ndani na hapo ndipo Alex alishangaa maana jumba hilo lilikuwa nasafi ndani na haliakuwa lilikuwa halina mtu. Sasa aliamini mia kwa mia maneno ya Allen kama kuna kamchezo cha harufu mbaya kanachezwa. Hata hivyo hakuuliza chochote, Christine alimwangalia Alex kwa makini usoni na kugundua kitu kisicho kawaida lakini aliamua kufunga mdomo wake na kukaa kimya. "mmh kashaanza kushtuka nini" Alijiuliza moyoni, "na kama ni hivo basi utakuwa msala mkubwa sana" aliendelea kujisemea moyoni. Wakati huo hakushtka kama alikuwa akiitwa mpaka alipoguswa bega ndipo akshtuka kutoka katika mawazo yake.
"unavoonekana ulikwa mbali sana" Alex aliongea huku akimuangalia kwa makini usoni, "unajua nilikuwa sitaki kurudi kwenye nyumba hii" Christine aliongea huku akilisogelea kochi na kukaa. "kwanini sasa" Alex aliuliza huku akitafuta kochi la kukaa, "hapa ndio nyumbani kwetu nilipozaliwa na nilipokulia kabla ya wazazi wangu kuuwawa kikatili mbele ya macho yangu. na mimi nikafanyiwa unyama mkubwa sana, kwa umri niliokuwa nao lilikuwa pigo ambalo sikuwahi kufikiria kama lingewahi kutokea" Christine alishindwa kuendelea kuongea na kuanza kulia huku akikumbuke usiku wa matukio yote hayo yaliomkuta akiwa binti mdogo sana. Alex aljitahidi kumnyamazisha lakini wapi ilikuwa ni kutwanga maji kwenye kinu, kumbukumbu za Christine kubakwa na wanaume sita walioshiba zilizidi kumrudia kichwani mwake na kujikuta akiabana miguu yake kwa nguvu na kukunja ngumi. Alex alipoona hivyo alielewa nini kilimtokea binti huyo. Baada robo saa alinyamaza kimya na kumuangalia Alex ambae alikuwa ametulia akisubiria kitu anachoaka kukiongea . "kama sio yule mzee aliekuja kuniokoa leo hii ningekua marehemu" Christine aliongea, "Mzee gani huyo" Alex aljikuta akiuliza. "Alinambia anaitwa Jason CJ" Christine alilisema jina na ghafla Alex alijikuta kinyong'onyea. "nini sasa" aliuliza Christine, "wewe ndio Ms Rose" Alex aliuliza kwa mshangao. Christine alishtuka baada kusikia jina hilo kwani ni watu wachache tu waliokuwa wakilifahamu jina baada ya familia yake.
Kabla Alex hajajibu, Christne aliruka nyuma na kutoa bastola yake kiunoni "nambie umelijuaje hilo jina" alifoka huku akiikoki bastola yake. "duh" Alex alishangaa kwanza kwa maana hakutegemea kabisa kama mwanamke huyo angekuwa mwepesi kiasi hicho. "Jason CJ ni babaangu mzazi" ilibidi ajibu kwa maana alishaona hali ya hewa humo ndani ilikuwa imeshaanza kuchafuka, "kama unakumbuka siku ulioletwa uliokuja nyumbani na baba, mimi ndo nilikuwa wa kwanza kukupokea" Alex aliongea huku akiilia taiming ile bastola kwa maana alielewa ikiendelea kuwa mikononi mwa mwanamke huyo basi maisha yake talikuwa hatarini. Christine alijaribu kuvuta kumbukumbu zake na kukumbuka siku ile baada kuokolewa na Mr Jason CJ alielekea marekani na mzee huyo. Wakati akiwa katika mawzo hayo Alex hakuchezea nafasi alifyetuka alipokuwa amekaa na kuikwapua mikononi mwa mschana huyo. Christine alishtuka na kuwa mnyonge, huku akijikunyata taratibu kwa sababu alielewa sababu ya kutekea kwa familia nzima ya Alex ni yeye. Ilibidi arudi kwenye kochi akae maana alihisi kuanguka na kweli haukupita muda alipiga ukwenzi mmoja tu na kupoteza fahamu. Alex alijaribu kumuamsha lakini wapi Christine alikuwa amepoteza fahamu kabisa, Alex alimbeba na kumpeleka chumbani kisha yeye akarudi ukumbini huku kichwani akiwa na maswali mengi yaliokosa majibu. Alihisi mishipa ya kichwa ikianza kutanuka kutokana na kuwaza mambo mengi ambayoa alijaribu kutafuta majibu ambayo yalikuwa hayapo kabisa kichwani mwake. Alipoona hali inazidi kuwa mbaya alitoa simu na kumuandikia ujumbe Allen, na haukupita muda Allen alifika katika jengi na kuingia ndani. "sikiliza kijana maswali yako yote yatapata majibu lakini si kutoka kwangu, unachotakiwa ni kutuliza kichwa na upumzike, kesho asubuhi akiamka Christine utamuuliza" Allen aliongea huku akijaribu kumtuliza Alex ambae alionekana kuelemewa na msongo wa mawazo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alex alkubaliana nae na kuelekea katika chumba kingine ambacho alioga na kubadilisha nguo, lakini aliporudi sebeleni hakumkuta Allen badala yake alikuta karatasi ndogo yenye ujumbe "kesho nitakuja". Aliichana na kurudi zake chumbani baada kuhakikisha kila kitu kipo sawa, usiku huo kwake haukuwa rahisi kukatika kutokana na msongo wa mawazo uliokuwa ukimuandama. Alikuja kushtuka asubuhi baada kupigw na mwanga wa jua usoni, kwa kujizoazoa alishuka kitandani. Alielekea bafuni na kujifanyia usafi, baada hapo alitoka na kuelekea sebleni ambaoko alimkuta Christine akiwa amekaa kimyaa na alipomuona tu Alex alishtuka na kuangaliapembeni. "habari za asubuhi" Alex alisalimia, "n..zu..zuri" Christine alijibu kwa woga. Hakuongea neno jingine, aliekea jikoni na kuandaa kifungua kinywa. Alirudi akiwa na vikombe viwili vya kahawa na kimoja akampa Chrsitine, "leo kuna mtu nataka uonane nae" Alex aliongea baada ukimya wa muda mdupi kutawala. "umeshatafuta mtu wa kuniua" Christine aliongea huku akitabasamu. "hapana anakuja kutusaidia mawazo tu" Alex aliongea na alipomaliza tu mlango uligongwa. "ndo huyo atakuwa kashafika" Alex aliongea na kuinuka akaenda kuufungua, Allen aliingia na Christine alivomuona tu alikiachia kikombe cha kahawa na kuanza kutetemeka. Kiufupi Christine alikuwa amechanganyikiwa kiupande fulani, "karibu Allen" Alex aliongea na kumpa mkono kama ishara ya salamu. Walielekea ukumbini ambako walimkuta Christine akiwa anatiririka jasho kama, "Habari yako Rose" Allen alimpa salamu na kumuita jina lake halisi. Christine au Rose alikuwa kimya tu huku akiwa amekodoa macho kama mtu alikabwa na tonge la ugali wa moto kooni. "binti sikia, mimi siko hapa kwaajili ya kukudhuru bali nataka kukusaidia" Allen aliongea maneno hayo kumuhakikishia mschana huyo usalama, "ah nani asie kujua wewe" Christine aliongea huku akijifuta jasho, "najua nina historia mbaya sana huko nyuma lakini amini kwa wakati huu sina nia ya kukudhuru kabisa. Unadhani ningetaka kukudhuru ungekuwa hai muda, ungekuwa ushakufa muda mrefu tu" Allen alijibu na kumsogelea Christine ambae alikua bado anatetemeka kwa woga. Alianza kuongea nae katika mfumo ambao hata Alex alishindwa kufahamu alikuwa anamaanisha nini japo maneno aliyasikia vizuri tu. baada ya dakika tano Christine alirudi katika hali yake ya kawaida kabisa. "ok muda hakuna tuanze mazungumzo" Allen aliongea, "Christine unajua chochote kuhusu vifo vya familia yangu" Alex aliuliza.
"ndio najua kila kitu na watu wote waliohusika" alijibu Christine, "ok, hebu nieleze maana nna hamu kweli ya kujua" Alex aliongea tena. "ni hivi siku alioniokoa ndio siku ambayo alinunua matatizo kwa huruma yake, kwasababu ilipangwa katika familia yangu asibakie hata mtu mmoja hai.Nilikuja kugundua kuwa vifo vya wazazi wangu vilitokana na mikono ya watu wakubwa katika matiafa kadhaa, watu hao walikuwa wakiendesha kampeni za chini kwa chini kuwashishi watu wajiunge na kikundi ambacho kilijiita WANAMAPINDUZI. Na kila aliyekataa yalimkuta kama yalioikuta familia yangu na yako, wazazi waliuwawa pamoja na watoto wa kike. Watoto wa kiume walichukuliwa na kupelekwa katika makambi mbali mbali ya siri kwa ajili ya kufanyiwa majaribio ya kutengenezwa jeshi ambalo ni tiifu. Moja kati ya watoto hao ni wewe japo mwanzo nilidhani umekufa pamoja na kakaako katika moto ule uliowashwa nyumbani kwenu. Wewe ulikuwa katika kambai ilokuwepo bahari ya pacific marine base71, lakini kaa ukijua kuwa kuna makambi mengine kama hayo zaidi ya mia. Watu waliokuwepo huko ni watoto yatima, wahanga wa vita hasa kutoka nchi za mashariki ya kati na mbali pamoja na Africa. Ukweli kwa sasa hicho kikundi kina jeshi kubwa sana ambalo likipewa tu amri basi dunia nzima inatumbukia katika majanga na mito ya damu. Watu wanaohusika na matukio yote haya ni watu wa kitengo cha upelelezi nchini Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na kadhalika. Lakini mkuu wa kikundi nimemjua hivi karibu anajiita THE GREAT GENERAL au GENEARAL DAVID. Ndie huyohuyo unaemfikiria saa hivi, mtu ambae wewe unamuona kama Godfather wako ndie mtu alieingamiza familia yako. Najua atakuwa amekwambia babaako amekufa kwa mshtuko baada kuona nyumba yake ikitetekea kwa moto, si kweli huo ni uongo mkubwa kwa sababu yeye ndie aliemuua.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Babaako alikuwa ni simba, sio mtu wa kutetemeshwa na vifo vya familia yake. Katika maisha yake amepoteza watu muhimu sana lakini bado alisimama kwa miguu yake miwili na kusonga mbele, unajua babaako alimpoteza rafiki wa pekee ambae walijuana tokea wadogo sana. Huyo mtu aliuwawa mbele ya macho yake na wala hakutoa chozi, lakini upendo wake kwa mtu huyo ulikuwa hauna mfano kabisa. Huyo aliitwa Mr Robert Mc cannon ambae ni baba wa Allen James au David Robert kwa jina lake halisi" alimaliza kuongea na kuwaangalia wote wawili usoni, Alex alionekana kuvimba kwa hasira lakini Allen alikuwa kimya huku akitabasamu, tabasamu ambalo lilifuatwa na micheirizi ya machozi yalioshindwa kujizuia ndani ya macho yake.
"yaani sikupata hata kumzika babaangu, halafu leo ndio nagundua kuwa watu niliowatumikia kwa moyo wa kizalendo ndio waliouchukua uhai babaangu, ni aibu gani hii" Allen aliongea huku akikunja ngumi kwa nguvu, vidole vilisikika vikidata na mishipa ilivimba usoni. "haki ya Mungu watalipa kwa walichomtendea marehemu babaangu" alisema kwa nguvu na ghafla damu za pua zilianza kumtoka na wala hakushtuka kabisa. Upande wa Alex yeye ndo alikuwa ameishiwa nguvu kabisa maana alikuwa hoi hasa alipofikiria kuwa mtu aliekua akimuamini sana ndio chanzo cha matatizo yake yote. Christine aliendelea "ukweli wote huu niliusoma katika kitabu cha kumbukumbu cha babaako ambacho nilikiba siku alionipeleka katika nyumba za kulelea watoto yatima, na nilikifanya ndio muongozo wangu wa maisha na humo ndio nikakuta siri nyingi kuhusu hicho kikundi cha wanamapinduzi na ndipo nikaweka azma kuwa lazima nitajiunga kwenye hicho kikundi ili nikisambaratishe ndani kwa ndani" alimaliza na kukaa kimya. "unaweza ukanionesha hich kitabu chake cha kumbukumbu" Alex aliuliza kinyonge huku machozi yakimtoka.
Cheistine aliinuka na kuelekea chumbani, alirudi akiwa na kitabu mkononi na kumkabidhi Alex. Alikipokea ka mikono miwili na kukifungua nakweli muandiko aliokuta ulifanana kabisa na a babaake, alikuta pia picha moja amayo ilikua ni ya familia nzima. Machozi hayakuacha kutiririrka machoni mwake na uchungu pamoja na hasira vilizidi kila alipokuwa akikisoma kitabu hicho cha kumbukumbu za babaake. Allen aliliona na kujua abisa huko wanapoelekea si pazuri hata kidogo hivyo aliinuka na kumsogelea Alex. "kijana okoa nguvu zako, acha kulia mi naelewa uchungu wa kupoteza familia kuliko unavoulewa wewe. Futa machozi na usimame na kitu kimoja tu kichwani nacho ni kisasi, mimi nitakua na wewe mpaka mwisho a mpambano huu" Allen aliongo huku akimpiga piga Alex begani. Alex alifuta machozi kama alivomabiwa na kuinuka kisha akaelekea chumbani kwake, baada dakika kumi alirudi akiwa kashabadilisha nguo. Christine na Allen walimshangaa maana alikuwa amebadilika kabisa na kiunoni alipambwa na mkanda flani hivi ulikua umejaa magazine za bastola yake ndogo. "tunaanza wapi" Alex aliuliza, "hapa inabidi tuanze na mtu mmoja anaitwa William maarufu kama Willy" Christine alianza kuongea. Alitoa picha ya Willy na kumuonyesha Alex na kumpa maelezo yote kama yalivyotakiwa. Baada hapo Alex na Allen waliinuka na kutoka nje huku Christine akiwa na jukumu la kuhakikisha matukio yote yatakayofanyika hayarikodiwi na kamera zozote zile. "twende kwangu kwanz halafu tutaelekea huko wa hicho kitoweo" Allen aliongea na kumfanya Alex acheke kidogo baada kusikia neno kitoweo. Alikubali ba safari ya kuelekea kwa Allen ikaanza, walitumia dakika kumi na tano mpaka kufika huko. Waliingia ndani na Allen akamwambia Alex amsubiri sebleni na yeye akaelekea chumbani kae baada dakika kumi alirudi akiwa katika mavazi yake ya kazi huku akiwa amebeba mashine kuba mgongni iliotembea kwa jina la AK 47. Kiunono alikuwa na bastola ndogo nne semmiauto. Pia alibeba begi dogo lililokuwa na vipande vya sniper yake.
**************************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment