Simulizi : C.O.D.EX. 2 (The Dirty Game)
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ni miezi minne sasa bado hatujui Alex na huyo Allen wako wapi" Mr Clinton alifoka kwa hasira, "mkuu tunaendelea kuwasaka na pia tumeshatoa taarifa katika nchi rafiki zote ikiwa wataonekana basi tutajua tu" Helen aliongea kujaribu kumtuliza mkuu wake. "Mkuu tuna tatizo kubwa sana" Martin aliingia huku akihema kama mtu aliekuwa akifukuzwa na jini, "kuna nini tena" Mr Clinton aliuliza kwa sintofahamu. "Agent William ameuwawa" Martin aliongea huku akihitahid kuhemama sawasawa, "tobaa" Mr Clinton alishtuka ile mbaya. "hii ina maanisha nini" Aliuliza, "hii inamaanisha kuwa kama ni Alex basi tayari ameanza safari ya kutuwinda" Aliongea Helen huku akionekana kama alikuwa kitetemeka. "kuna ushahidi wowote juu ya mauaji hayo" Helen alihoji, "kwa bahati mabya sana hata kamera za ofisini kwake hazijarikodo tukio zima" Martin aliongea kwa masikitiko makubwa sana. "hebu niunganishe na ofisi zetu nchini uingereza" Alitoa amri Mr Clinton na bila kuchelewa Martin aliondoka na kwaajili kazi hiyo. Alrudi baada dakika tano " mkuu tayari" alitoa majibu, Mr Clinton alinyanyua mkonga wa simu "hebu nielezeni kwa kina nini hasa kimeetokea" aliongea lakini majibu aliyoyapata upande apili yalikua hayana tafauti na yale allioletewa na Martin.
Baada maandalizi kukamilika majemedari wawili waliondoka kuelekea sehemu ambayo ndio chakula chao kwa siku hiyo kilikuwa kinapatikana. " Alex wewe utaingia katika ofisi zao, mimi nitakaa katika jengo moja hapa nje kwa ajili ya usalama, hakikisha unafanya kazi haraka iwezekanvyo" Aliongea Allen na Alex alikubali. Walifika nje ya ofisi na hapo wakatengana na kila mtu akaelekea upande wake. Christine alicheza na mitambo ya ofisi hiyo na kufanikiwa kuzihack computer zote huku akimpa Alex njia rahisi ya kufika katika chumba ambacho ndo William alikuwepo, na kutokana na mavazi aliovaa yalitosha kueleza kuwa alikuwa na Agent kama alivyo William na kwa sababu mitambo yao ilikuwa imevamiwa walishindwa kumgundua kabisa kama ni mtu amnae muda si mrefu wametumiwa picha yake kuwa ni wanted. "karibu" William alimpokea akiamini ni miongoni mwa wenzake maana maagent kujuana ilikua ni kitu kigumu sana kutokana na protokoli haiwaruhusu kujitambulisha ka majina yao isipokuwa kwa wakubwa zao tu. Allen tayari alishafika katika sehemu amabayo aliweza kuwaona wawili hao wakiongea.
"nipe ripoti kamili kuhusu mauaji ya familia ya Jason CJ" Alex aliongea akiwa serious, kwa mtazamo wa haraka William aligundua kuwa ujio huo haukuwa wa amani kabisa, alijaribu kupeleka mkono kwenye droo ili atoe bastola lakoni wapi Allen alipiga shaba pemebeni kidogo na ilipokuwepo bastola hiyo. "Unadhani nitakwambia kitu sahau" William alijibu kwa kujiamini huku akibonyeza kitufe cha siri ambacho kinatumika nyakati kama hizo za hatari. Lakini hakuna kilichotokea, "Alex umeona hiyo pete mkononi, muue huyo mjinga na uchukue hiyo pete" Allen aliongea kupitia kifaa maalum cha mawasiliano. Alex aliinuka na kumfumua William risasi ya kichwa kisha akamvua pete na kutoka zake bila mtu yoyote kushtukiwa na yoyote yule, wote aliopishana nao alimpa ishara ya heshma.
Allen alifunga vifaa vyake na kushuka, moja kwa moja mpaka kwenye gari na kusoge eneo ambalo walikubaliana wakutane baada ya kazi. Dakika moja baadae Alex alifika eneo hilo na kuingiakwenye gari na safari ya kurudi ikaanza. Walifika nyumbani kwa CHristine na kumkabodhi ile pete, na kwa sababu Christine alifanya kazi nao alijua kabisa kama hiyo pete ni kifaa maalum cha kuhifadhia mambo ambayo ni siri kubwa sana. Alichukua kifaa maalum na kuiweka kisha akaanza utundu wake wa computer, baada nusu saa alifanikiwa kuhack pete hiyo na hapo sasa mafaili yote yalifunguka na kuzianika siri zote hewani. Walianza kukutana na mambo ambayo kwa kweli yalitisha sana, mauaji yasio ya kitoto yalirikodiwa wakati yanafanyika. Yaani hapo ubaya wa kitengo cha upelelezi ulimwagika, mauaji yaliopita na yanayofanyika kwa wakati huo na yatakayofanyika baadae yote yalikuwa yameandikwa humo. Yaani kwa siku moja waliua zaidi ya watu 20, Alex, Allen na Christine walibaki mdomo wazi wakionyesha kutoamini baada kila mmoja kushuhudia vifo vya familia yake bila chenga. "washenzi sana hawa na sasa watakoma" Allen aliongea na kukunja sura kama mtu alilamba ukwaju. Ghafla ile pete ilianza kuwaka rangi nyekundu, "Alex mchukue Christine na tukutane 73:56, FBI hawako mbali na hapa na wanakuja pamoja na S.W.A.T" Allen aliongea na kutoa bastol mbli kisha akaelekea dirishani na kuchungulia na kweli hakukosea kwa mabli alisikia ving'ora. Alex alichukua vitu muhimu na kutoka mlango wa nyuma akiongozana na Christine. Allen alitoa mabomu madogo mawili na kuayaset dakika moja na nusu. Alichungulia tena na tayari nyumba upande wa mbele ilikuwa imeshazingirwa, alifumua risasi kadhaa ili kuwashtua kisha akakimbilia mlango wa nyuma na kutoka. Baada sekunde kidogo tu mabomu yaliripuka a kuusambaratisha mjengo mzima, mabomu hayo yalikuwa madogo lakini shughuli yake ilikuwa kubwa si mchezo.
Christine kwa mbali alishuhudia nyumba yake ikiwaka moto "bora uende zako maana kila siku unanitonesha kidonda ambacho huwa kishanza kupona" alijisemea. dakika chache baadae Allen alifika na kuingia kwenye gari na safari ikaanza, "wapi sasa" Alex aliuliza. "tunaelekea Amrica lakini kwa njia za panya, hatutaki washtukie ujio wetu" Allen aliongea na kuwasha computer katika gari hiyo, alitafuta kitu kama ramani hivi na kumwambia Alex ambae ndo alikua dereva kwa wakati huo "fuata hiyo ramani". Alex alitikisa kichwa na kukanyaga mafuta na kuzdi kutokomea nje jiji la London, huko nyuma yalikuwa majanga matupu maana askari wengi waliofika kwaajili ya msako walijeruhiwa vibaya sana na wachache walipoteza maisha.
********************
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"mkuu kuna jambo nahitaji kukwambia" aliingia Robert katika ofisi ya boss wake ndani ya kambi ya kikundi cha wanamapinduzi, "habari njema au mbaya" aliuliza General David ambae ndie mkuu wa kikosi hicho hatari. "mbaya tena sana" alijibu Robert, "mh nambie" aliongea tena. "kwanza tumempoteza Agent William lakini kibaya zaidi kuhusu mtu aliemuuwa ni yule kijana Alex akisaidia na Allen James" aliongea Robert huku akimuangalia bosi wake ambae tayari sura yake ilishaingia makunyanzi ikiashiria kuwa amekasirika. "huyo kijana hana kosa, mwenye kosa hapo ni huyo Allen James. Unajua familia yake iko wapi" aliongea na kutwanga swali. "hapana mpaka sasa hatujafamikiwa kujua familia yake iko wapi lakini ninachojua tu ni kwamba mtoto wake mmoja yupo mafunzoni katika kambi maalum" alijibu Robert. "sasa cha kufanya ni kumuua Allen halafu kesi ya mauaji yake tumatupia Alex, baada hapo tunamuingiza mchezoni mtoto wa Allen. Unajua tukimuingiza huyo mschana kutakuwa na asilimia kubwa ya kumkamata Alex kwa sababu atachanganya hisia na kazi na hapo itakuwa ni vigumu kushindwa kazi hii kwa sababu ata fanya chochote ikiwezeakana hata kuvunja sheria ilimradi tu na yeye amuue Alex kama sehemu ya kulipa kisasi cha babaake. Na hapo tutakuwa tumeuwa ndege wawili kwa jiwe moja, maana atakapo kamilisha kazi hiyo na yeye tutamuua" Aliongea General David na kuachia tabasamu la kinafiki lililojaa ubaya.
Alex alizidi kukanyaga mafuta mpaka walipofika katika sehemu ambayo ramani ilimuelekeza, alisimamisha gari na wote wakashuka. Alipigwa na butwa baada kuona sehemu hiyo imejaa vyuma chakavu yakiwemo mabaki ya ndege, na vifaa vingine vya kivita. Allen aloingoza njia na wengine wakafuata mpaka alipofika sehemu na mumanyaga. GHaflaardhi ilianza kutikisika na ukafunguka mlango mkubwa katika ardhi, Allen aliingia na kuwafanyia ishara wengine wamfuate. Baada kuingia wote mlango ulijifunga na kukarudo kama mwanzo. Aliwasha taa na hapo sasa Alex alikaa kitako kwa mshangao maana chumba hicho kilikuwa kimejaa silaha za aina zote. "tutapumzika hapa kwa siku moja na kesho usiku tutasafiri kueleke mjini New York" Allen aliongea na kuwaonesha bafu lilipo kwa ajili ya kuoga. Walijisafisha na kubadili nguo lakini Christine alishangaa kupewa nguo za kike "hizi nguo ni za nani" aliuliza kwa mshangao. "ni za marehemu mke wangu" Allen alijibu huku akionekana kutotaka endelea kuongea chochote juu ya mwanamke huyo. Christine aliligundua hilo hivo na yeye hakuuliza tena swali, waliandaa chakula na kula kisha wakapumzika. Siku ya pili maandalizi ya safari yalianza, "sasa tunatumia usafiri gani" Alex aliuliza. "tutatumia usafiri wa pipe inayotembea chini ya bahari mpaka katika kambi yangu nyingine mjini Florida, baada hapo tutakodi ndege mpaka New York" Alifafanua Allen. Alex hakuwa na swali jingine alikaa kimya kumuachiwa nguli huyo wa vita afanye kazi yake. Usiku ulipowadia walikwenda mpaka sehemu kilipochombo cha kusafiria na wote wakapanda. Safari ikaanza kwa mwendo mdogo lakini kadri muda ulivyokwenda chombo hicho kiliongezeka kasi, na baada ya dakika tano kilikuwa katika kasi kubwa sana kiasi ya kwamba kama ingekuwa ni ndege basi hata rada zingeshindwa kusoma. Baada ya nusu saa kilianza kipinguza mwendo na hatimae kilisimama, "karibuni Florida" Allen aliongea. Alex alikuwa haamini kabisa kama ndani ya muda mdogo kiasi hicho wameshafika Florida.
"acha utani we mzee" Alex aliongea akidhania ni utani, "kweli tumeshafika" Allen alisistiza. Alex bado hakumini kabisa lakini ilibidi ashuke ili ajiamishe kuwa kweli wako Florida au laa, Allen aliongoza njia mpka kwenye mlango na kuufungua. Kwa vile ulikuwa ni usiku hata watu wengi hawakuwa njiani, Alex alitoka nje na hapo sasa aliamini kama kweli wako Florida. Bila kuchelewa usiku huo walifika katika kiwanja kimoja cha ndege za kukodi. Walikodi ndege lakini hawakukodi rubani, "rubani nitakuwa mimi mwenyew" Aliongea Allen na kuingia ndani ya ndege. Baada maandalizi yote kukamilika safari ya kuelekea New York ikaanza, Allen alikuwa ni bingwa katika urushaji wa ndege. "mh kiasi wamuogope huyu mtu" Alex alijisemea moyoni, walifika katika uwanja wa ndege wa kampuni ile ile waliokodi. "karibuni New York ni matumaini yangu kuwa ndege yetu haijawaletea tatizo lolote" aliongea mzee mmoja. "tunashkuru sana kwa kuwa na huduma nzuri" Allen alijibu na kumkabdhi mzee huyo pesa taslim kwa ajili ya kumalizia deni lake.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walitoka nje ya uwanja huo na kuchuku taxi, walielekea mpaka katika nyumba moja hivi ya wastani. "karibuni hapa ni nyumbani kwangu" Allen aliongea huku akitabasamu, waliingia ndani na kuweka kila kitu sawa. Kutokana na uchovu wa safari wote walikuwa hoi na baada ya kula tu kila mmoja liingia ndani na kulala japo ilikuwa tayari ishakaribia asubuhi.
Mafunzo makali yaliendelea katika kambi ambayo Christina au Agent Darling alipelekwa kuongeza ujuzi. Wengi aliokuwa nao waliishia njiani na wachache waliaga dunia kabisa, lakini ilikuwa tofauti wa mwanamke huyo ambe tayari mwili wake ulishaweza kumudu mazoezi ya aina hiyo. "unajua umenakiza kiezi mingapi" Jeff alimuuliza Christina, "dah hata sijui kabisa maana ni balaa, hata tarehe ya leo siijui" Christina alijibu huku akiendelea kupasha. "umebakisha miezi minne tu, halafu utapewa mtihani maalum wa kukabidhia medali yako ya THE ONE AND THE ONLY" Jeff aliongea huku akitabasamu lakini ndani ya tabasamu hilo kulikuwa na sura ya wasiwasi maana alieulewa vizuri mtihani huo ambao una matokea mawili tu, aidha ushinde ama ufe. Lakini kwa Christina alikuwa ni mwenye furaha sana, na alichowaza ni kurudi nyumbani na kumuonesha babaake medali yake ambayo ingempa cheo kuliko mwanajeshi yoyote yule katika nchi yake. Upande wa wanamapinduzi kulikuwa na kikao kikiendelea, na agenda ya kikao hicho ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Allen James anakufa na kesi anabambikiwa Alex. "usijali mkuu mimi kama raisi wa nchi hii, nitahakikisha kuwa Agent Darling anaingia kichwa kichwa katika mchezi huu" Aliongea mtu mmoja wa makamo amabe kwa cheo alikuwa ni raisi wa nchi hiyo, "nitakushkuru sana Mr Jackson" aliongea General David na kucheka kidogo.
Wakati wao wakiendelea na kikao, upande wa kina Alex nao pia walikuwa wanapanga mikakati ya kuwaondoa mmoja mmoja duniani. "sasa leo tunaanza na Mr Clinton, na kazi hii ataifanya Christine" aliongea Allen. "kwanini nisiifanye mimi" Alex alihoji, "Alex niachie huyo mbwa nikammalize mwenyewe, maana alichokuwa akinifanyia acha kabisa" Christine alijibu swali la Alex. "wakati Christine anatekeleza kazi hiyo Alex utakua nje unafatilia tukio zima, na ikiwa ksaada utahiajika basi fanya hivo" Allen aliendela kuongea, huyu mzee alikuwa ni master mind si mchezo. "wakati nyinyi mukiendelea na hilo, mimi nitakwenda kudili na mjinga mwengine ili kupata taarifa zote juu ya vikao vinavyoendelea katika kambi za hao wanaojiita wanamapinduzi" Allen aliendelea kuonesha yake katika kupanga mikakati. "tukifanya hivo tutazidi kuwachanganya, maana kupoteza watu wawili ndani ya siSilaha zote mtakazo zitumia zipo humu ndani" aliongea n kuinuka, alisogea mpaka katika ukuta na kuweka kiganja. Ukuta ulifunguka na kisha akaingia huku nyuma akifatwa na Alex na Christine, "ninapoongea kuhusu silaha namaanisha hizi" aliongea huku akiikamata bunduki moja mfano wa sniper lakini hii ilikuwa tafauti kidogo. "silaha hizi hata jeshi la nchi halimiliki" aliongea na kuwafanyia ishara kila mmoja ajisevia mashine amabazo angehisi zingemfaa katika kukamilisha kazi yake. walipordhika walitoka katika chumba hicho na kurudi sebleni, "tukutane hapa jioni baada kukamilisha kazi zetu" Allen aliongea na kutoa fungu ya gari mfukoni na kumrushia Alex. "katika gereji kuna gari aina GT harness bullet proof, mutatumia hiyo. Maisha yenu ni muhimu kwa hiyo msife huko hata kama itabidi uuwe wengine ili uokoeke basi usisite" Alimaliza kuongea na kuwahusia kisha yeye akatoka zake bila kuongea neno jingine lolete.
Alex aliinuka na kuingia ndani kwake na alipotoka alikuwa tayari katika commbat ya kazi, Christine hakuwa nyuma nae alivaa nguo zake za kazi na kubeba kila kitu ambacho angehisi kingemsaidia. Walitoka na kuelekea gereji ambapo walichukuwa gari na safari ikaanza, kwasababu kwa Christine ilikuwa ni mara ya kwanza kuingia uwanjani kutoa uhai wa mtu basi moyo wake ulikuwa ukinda mbio kupita maelezo. Alex aliligundua hilo na kummuwekea mkono juu ya mkono wake kisha akamawambia "usijali wala usiwe na wasi wasi kabisa, una mimi na Allen tunakuahidi kuwa hakuna jambo litakalo kutokea". Hapo kidogo mapigo ya moyo yalipungua kasi na kurudi katika hali yake ya kawaida, Alex alikanyaga mafuta na kuwa makini na kamera za barabarani. Walifika mpka nje jengo ambalo kwa nje linaaminika ni sehemu ya kufanyia biashara, Christine alishuka na kuvaa beji yake kifuani na kuweka miwai ake vizuri. Alikuwa amevaa kiofisi zaidi na beji alioweka ilimzuia yoyote kumuuliza swali isipokuwa bosi tu wa ofisi hio ambae ni Mr Clinton. Aliingia kwenye lifti na kuanza kupandisha juu, lifti ilisimama na mwanadada huyo akatoka na kila aliepishana nae alimpa heshima yake. Alifika mpaka kwenye meza ya secretary, "nataka kuongea na bosi wako" alitoa amri. Maggy alinyanyua simu na kupiga, "unaweza kupita" alijibu baada ya kukata simu hio. Christine alishukuru na kuingia ndani katika ofisi hiyo, kwa umakini wa hali ya juu aliweka kifaa maalum kwenye mlango kilichokuwa na sumaku na mlango huo ukajitia loki wenyewe. "karibu Agent" aliongea Mr Clinto huku akiuthaminsha mwili wa Christine, na aliganda pale alipofika kifuani na kukuta dodo zikiwa zimebustiwa vizuri. Hakuishia hapo aliendelea kushuka chini mpaka kiunoni na kuanza kukagua hips sasa. Hili jinga muda wote lilikuwa linawaza ngono, "eh Mungu wee tokea alivyokufa Rose nimekosa kabisa mambo mazito kama haya" alijisemea moyoni huku ute wa hamu ya ngono ukimjaa mdomoni. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"nitasimama mpaka saa ngapi" aliongea Christine na Mr Clintone alishuka kutoka katika ndoto yake ya mchana. "ah karibu ukae" alijibu huku akijiuma meno, Christine alisogea na kukaa kwenye kiti huku ndani kwa ndani hasira zikizidi kumjaa. Alex alikuwa kwenye garia akifatilia kila kitu kilichokuwa kinaendelea katika jengo hilo, "ok nini hasa kilichokuleta hapa" aliuliza Mr Clintone baada utambuliso wa muda mfupi. "tumesikia unashirikiana na kikundi cha wanamapinduzi kutaka kuanzaisha vita" aliongea Christine huku akimkazia macho, kijasho chembamba kilianza kumtoka Mr Clintone huku akitfuta neno la kujibu. "ha...hap..hapana mkuu" alijibu kwa kudodosa, "lakini unawafahamu wanaofanya kazi hio si ndio" Christine aliongea tena na wakati huu alizidi kumkazia. "hapana mimk sijui chochote, hata hicho kikundi sijawahi kukisikia" alijibu kwa kujiamini sasa. Christine alifungua koti lake na kutoa bastola ndogo mbili na kuziweka mezani, "sasa utanambia ukweli au nitafanya nilichoagizwa nikifanye" aliongea huku akimuangalia Mr Clintone ambae alikuwa hajui afanye nini maana alielewa agizo likitoka katika kitengo hicho cha Christine lina uwezo wa kumuua mpaka raisi. Baada kuona hakuna jinsi ilibidi acheuke ukweli wote bila kujua kuwa alikuwa kashaachezwa akili. "hivo nilivoeleza ndivo nnavo jua mimi" alijitetea baada kumaliza kuongea, "nashkuru kwa ushirikiano wako lakini kuna jambo la mwisho nataka kukuuliza" aliongea Christine. "hivi unamjua Rose" aliuliza swali hilo huku akikunja ngumi lakini kwa vile mikono yake ilikuwa chini ya meza Mr Clintone hakufanikiwa kuiona ngumi hio. "ndio namjua, alikuwa secretary wangu lakini alishakufa muda mrefu mbona" alijibu Mr Clintone, hapo Christine alisimama na kuvua wigi alilokuwa amelivaa. Mr Clintone alitokwa na macho baada kugundua kuwa mwanamke huyo ndie Rose, "leo nimekuja kuweka mambo sawa kati yetu" aliongea kwa hasira na kunyanyua bastola zale kisha akafyetua risasi kadhaa, lakini Mr Clintone alikuwa mwepesi sana hivyo alifanikiwa kuruak pembeni. Kabla hajatoa bastola yake Christine alimuwahi na kumpiga teke zitola uso na kwa kasi ya ajabu akamuwekea bomba mbili za bastola katika macho yote mawili na hakuuliza hata shikamoo akafyetua risasi zilizoteokea nyuma ya kichwa cha Mr Clintone. Mr Clintone alianguka chini kama mzigo, wakati akiwa anamuangalia mzee huyo alielala katika dimbwi la damu ghafla alisikia mlango ukisukumwa kwa nguvu. Hakutaka kulaza damu alishika kitu kwenye sikio lake na kuongea "64:90" kisha akavua ile sketi na kushusha surualia aliokuwa maevaa ndani hapo sasa alionekana kama Angelina Jolie katika Tomb Rider. Miongoni wa mwa vifungo vya shati lake kulikuwa kuna bomu dogo la kuvunjia kioo. Alikitoa kifungo hicho na kukiweka kwenye kioo na haiukupita hata dakika kioo kikavunjika, wala hakufikiria mara mbili alikimbia na kuruka kutoka gorofa ya thalathini na moja. Aligungua parachute na kuelekea sehemu walioubalina wakutane na Alex, mpaka wanafanikiwa kuvunja mlango waliambulia peupe.
"kwanini umeamua kutufanyia hivo lakini, nani mwingine atatupa muongozo pale tutakapo kwama" Alex alilalamika huku akizidi kulia, alijiona ni mkosa mbele ya muumba wake kwa kumuacha mtu mwenye mke na watoto kufa. Christine alijitahidi kumtuliza Alex japo yeye mwenyewe alikuwa hoi kwa kulia, Alex hakuonge kitu tena alisimama na kuelekea chumbani kwa Allen, Alitafuta droo aliloambiwa na kulifungua, alivichukua vichupa na kurudi navo ukumbini. "nifate" aliongea na Christine aliinuka na kumfata, alielekea pale alipoweka mkono Allen na yeye akaweka wa kwake. Mlango ulifunguka na wote wakaingia, alielekea mpaka alipoanmbiwa kuna mlango mwengine wa siri. Aliugusa mlango huo nao ukafunguka, huku ukisindikizwa na taa zenye mwanga mkali. Walishangaa kukuta macomputer mengi sana, alisogea mpaka kwenye meza moja ambayo alikuta karatasi yenye maelekezo jinsi ya kutumia kemikali hiyo hatari. Kila mmoja aliingia chooni na kuoga, walipomaliza walivaa yale magauni ya hospitali kisha Alex akamchoma ile kemikali Christine na yeye pia akajichoma. Kila mmoja alipanda kitandani na kujiwekea vifaa maalum ambavo vimeunganishwa na computer ambayo itakuwa inafuatilia mifumo yote ya mwili. Pia walichoma drip ambayo ilikuwa na maji yenye virutubisho vya aina zote. "nakutakia usngizi mwema na tukutane baada miezi mitano" Alex aliongea huku akimuangalia Christine. "nawe pia" Christine alijibu huku akitabasamu, na ghafla wote wawili walianza kuona kiza na haukupita muda wote wakachukuliwa na usingizi mzito.
*********************************
(baada ya miezi mitano)
Bado Christina hakuamini kama babaake ameuwawa, maana alihisi kama anaota vile. Ni mwezi mmoja sasa tokea Chritina Allen atoke katika kozi maalum ya THE ONE AND THE ONLY. Alikuwa ni mwenye furaha sana lakini furaha hio yote ilitoweka baada kupokea taarifa za kifo cha babaake kipenzi. Taarifa hizo zilimuumiza sana na kujikuta akiapa kumuua Alex kwa mikono yake miwili, "kuna taarifa zozote kuhusu Alex" Christina aliingia ofisini kwake huku akiuliza. "bado mkuu,hatujafanikiwa kujua yuko wapi" alijibu Joe. "endeleeni kusachi hakikisheni hamuachi jiwe halijafunuliwa" Aliongea mwanamke huyo ambae kwa muonekano tuu ilitoosha kuonyesha kama alikuwa hatari kupita maelezo.
"Alex, Alex" Christine alikuwa wa kwanza kuamka na kuanza kumuamsha Alex ambae alikuwa kiweweseka kama mtu aliekuwa akiota ndoto mabaya. "Allen" Alishtuka huku akiita jina hilo, "karibu tena duniani" Christine aliongea kwa uchangamfu sana. "Christine ni wewe au" Alex ilibidi aulize kwanza maana alikuwa amebadilika kidogo, "yeah ni mim na kuanzia leo usiniite Christine, niite jina langu halisi ...ROSE" aliongea Rose, Alex alishuka kitandani mara akakosea kuanguka kutokana na kuwa alikuwa amelala muda mrefu sana. Alitembe mpaka kwenye kioo na kujiangalia, macho yalimtoka baaada kujiona alivokuwa amevimba misuli na pia kidevu chake kilikuwa kimechafuka ndevu ambao ziliota kwa wingi wakati akiwa usingizini.
Alikitoa kifungo hicho na kukiweka kwenye kioo na haiukupita hata dakika kioo kikavunjika, wala hakufikiria mara mbili alikimbia na kuruka kutoka gorofa ya thalathini na moja. Aligungua parachute na kuelekea sehemu walioubalina wakutane na Alex, mpaka wanafanikiwa kuvunja mlango waliambulia peupe.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati Alex na Christine wakikamilisha kazi yao, Allen huku aliekea katika sehemu ambayo ndio alikuwa na ahadi ya kukutana na huyo mtu mwingine. Alipofika kwenye jengo hilo alitoa bastola zake na kujiweka sawa kisha akaingia kwa umakini wa hali ya juu sana. "Naona umekuja kufuata kifo chako si ndio" ilisikika sauti ikitokea kwenye ambacho alikuwa amekaa mtu mmoja lievalia suti matata sana. "Mimi nimekuja kuhukua uhai wako tu" alijbu Allen huku na yeye akivuta kiti na kukaa, "hivi kweli unadhani utanishinda" aliuliza Robert kwa kejeli. "Mbona unauliza jibu" Allen nae alijibu kwa swali, jibu hilo lilipelekea kutokea kwa makunyanzi usoni mwa Robert.
"Mimi naona hakuna haja ya kupoteza muda zaidi, na napenda twende kiuwanaume zaidi hakuna kutumia silaha" aliongea Robert kwa kujiamini sana. "Itakuwa vizuri sana maana nina muda kweli sijapata mtu mwenye uwezo kama wangu katika ulingo. Ni matumaini yangu mpambano huu hautaisha mapema" alijibu Allen na kuweka bastola zake kwenye meza pamoja na kisu kidogo. Robert hakutaka kupoteza muda tena, alifyetuka kutoka katika kiti kwa kasi ya ajabu kusukuma masumbiw kadhaa ambayo mtaalamu Allen aliyatoka na kumzawadia ngumi nzito ya uso. "Uzembe ndio unao waua wengi" aliongea huku akikaa sawa.
"Acha kuongea wewe" alijibu Robert na kumvaa tena, safari hii alikuwa makini sana, Allen alijitahidi sana kuyatoka bila kushambulia. Na alifanya hivyo kuusoma mchezo wa adui yake huyo, kwa bahati mbaya aliteleza na kujikuta akichezea ngumi tatu kali sana za kifua. Alirudi nyuma na kukohoa kidogo, kikohozi hicho kiliambatana na mchirizi wa damu kutoak mdomoni. "Wewe ndio wanakuita Project x, sasa mimi ni Human killing machine (HKM)" Robert alijitamba kidogo. "Sasa ndio nimepasha na kama hujui kwa nini wameniita Project X. Ni kwa sababu utakavyoigeza X itabakia kuwa X tu" aliongea Allen na bila kusubiri jibu alifyetuka kutoka alipo na kumvaa Robert.
Robert kabla hajafikiri afanye nini alijikuta yuko hewani na kujibamiza ukutani, Allen hakumuachia hata asimame. Alimsogelea pale pale chini na kuanza kumshishia kipigo kitkatifu, Robert alijitahidi alijiyahidi kuzuia makonde ya kiumbe huyo lakini alishindwa kutokana na kasi ya makonde hayo. Allen baada kuona mpinzani wake amechapika, alimshika kooni na kumuinua mpaka akasimama sawa kisha akamuegemeza ukutani. "Unajua baada kukuondoa wewe duniani, Alex atakuwa amepata njia nyeupe kuelekea ushindi" aliongea Allen akisogea kwenye meza ambako alikuwa ameweka kisu chake. Alimgeukia Robert na kasi kubwa akaanza kumfata lakini kabla hajafika, alihisi kitu kikipenya mgongoni na kutokea mbele huku kikifuatiwa na mlio wa risasi iliofyetuliwa kutoka nyuma. Hata hivyo risasi hiyo haikumzuia kutimiza kil alichokusudia. Alijirusha kwa nguvu zake zote zilizobakia na kutua katika koromeo la Robert huku kisu alichokishika kikitengeza njia kubwa katika shingo ya Robert.
Wote wawili walianguka chini huku kila mmoja akijaribu kutetea uhai wake lakini wapi. General David alisogea walipo wote wawili huku akiwa haamini kilichotokea mbele yake na yeye ndie aliempiga risasi Allen. "Alex kazi kwako sasa, nitimizie kisasi ambacho sijakifanikisha" Allen aliongea maneno hayo na kuachia pini ya Grenade alilokuwa amebeba. General David kuona alikimbia na kutoka nje ya jengo hilo ambalo sekunde chache tu baada ya kutoka jengo zima likaripuka. Alikuta machozi yakimtoka na kuongea "nenda kwa amani mwanangu Robert na nasikitika mpaka unaaga dunia hujajua kama ni babaako mzazi" kisha akaondoka eneo hilo.
Alex na Christine walifanikiwa kutoroka na kurudi nyumbani, lakini mpaka usiku unaingia Allen hakuonekana. Hapo ndio Alex akaanza kupata wasiwasi, aliinuka alipokaana na kuanza kutembea tembea sebuleni. Bado haikutosha akaelekea chumbani kwa Allen, alikuta flash mbili nyeusu juu ya kitanda moja ikiwa imeandikwa jina lake na nyingine imeandikwa Christina pamoja na karatasi yenye ujumbe, aliichukua na kuanza kuisoma. "hicho kimoja ni cha kwako na kimoja cha mwanangu Christina au Agent Darling. Fungua chako tu na kimoja mkabidhi mwanangu".
Alex alitoka na flash hizo na kuelekea ukumbini ambako aliunganisha flash hiyo kwenye computer na kuifungua, Christine alikuja kuungana nae kuangalia ni kitu gani hicho. "Alex ninakwenda lakini sijui kama nitarudi, maana ninaekwenda kupambana nae ni hatari sana. Na uwepo wake tu kuna hatarisha kazi yako. Si mwingine bali ni Robert, ni hatari sana hivyo basi mimi nakwenda kukusafisha njia kuelekea ushindi. Kama nitakufa basi kifo changu utapachikiwa wewe kuwa ndio muuaji na watamtumia mwanagu Christina au Agent Darling kukukamata. Hivi sasa yuko mafunzoni katika kambi maalum anchukua mafunzo ya hali ya juu kabisa kuliko hata makombando wa nchi hii. Hivyo kaa ukijua atakuwa kikwazo kikubwa sana katika kufanisha kazi yako lakini naomba mmchukulie kama mdogo wako anaetenda asilolijua. Ukipata nafasi nzuri mkabidi hiyo flash na fanya hivyo bila kuchelewa. Mwisho kabisa chumbani kwangu katika droo kuna vichup viwili vya kemikali iliozimuliwa ya CODE X. Tumia kimoja wewe na kingine atumie Rose maana muna kazi kubwa sana mbele, kumalizia ikiwa sitarudi nakuomba unitimizie kisasi changu kwa walionitenda. Familia ni kitu muhimu sana basi fanya ufanyalo lakini baadae uwe na familia. Alex wewe ni kama mwanangu na kaa ukijua kuwa nilikuwa nakupenda sana na sitakuacha peke yako katika hii kazi. Nitakuwa nawe hata kama nitakuwa mbiguni" mpaka ujumbe huo unaisha Alex alijkuta akimwagikwa na machozi kama mtoto mdogo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kwanini umeamua kutufanyia hivo lakini, nani mwingine atatupa muongozo pale tutakapo kwama" Alex alilalamika huku akizidi kulia, alijiona ni mkosa mbele ya muumba wake kwa kumuacha mtu mwenye mke na watoto kufa. Christine alijitahidi kumtuliza Alex japo yeye mwenyewe alikuwa hoi kwa kulia, Alex hakuonge kitu tena alisimama na kuelekea chumbani kwa Allen, Alitafuta droo aliloambiwa na kulifungua, alivichukua vichupa na kurudi navo ukumbini.
Mabega yake yalizidi kuwa makubwa, misuli ya kifua ilikuwa pia imeongezeka kutanuka. Six packs tumboni zilizidi kukamaa kama matofali ya kuchoma. "we Alex huoni kama uko uchi" Alshtuka baada kuguswa mgongoni na Rose, "damn" aliliweka guo lake vizuri kisha akaelekea sehemu ya kutokea. Aliweka mkono na mlango ukafunguka . Alipofika sebeleni alishangaa kukuta nyumba ikikwa haina hata vumbi utadhani kulikuwa kuna mtu anaishi. Lakini wala hakulijali hilo alielekea chooni na kuanza kujifanyija usafi, Rose nae alifanya hivo. Baada ya nusu saa wote walikuwa wameshamaliza, walirudi ukumbini huku kila mmoja akiwa na nguo za kawaida. Walirudi tena katika kile chumba chenye silaha na kuanza kutafuta silaha za kufanyia kazi, wakati wanaendelea kutafuta walikuwa mfuko mweusi na walipoufungua ulikuwa nguo nzuri za kazi. Hapo walitabasamu na kila mmoja kuchukua na kwenda kubadilisha, hapo sasa ndio wakawa wamekamilika. Kila mmoja alichukua silaha zitakazomfaa na kutoka katika chumba hicho. "tunaanza wapi" Aliuliza Alex, "inabidi tutoke tukachunguze kwanza" ROse alimjibu na wakakubaliana hivo. Waliingia gereji na kutoka na gari moja kwa moja mpaka katika makao makuu ya kitengo cha upelelezi. Walifika na kuweka fgari pembeni, "tusishuke" Alex aliongea kwa sababu alishaanza kuhisi kitu tofauti, aliliangalia eneo hilo kwa makini sana na kugundua kuwa lina kamera nyingi sana zimefichwa. "fikiria hatua moja mbele" alihisi kama sauti ikimwambia, alitabasamu kidogo na kujua japo Allen ameaga dunia lakini bad yupo pamja nae. Aliangalia kiti cha nyuma na kuchukua laptop kisha akaanza kufanya yake, alifanikiwa kuzihack kamera zote za eneo hilo na kuziunganisha katika laptop hiyo. Baada hapo waliondoka na kurudi nyumbani kwao, "sasa hatuna haja ya kwenda tena kule kila kitu tutaona huku huku" Alex alijisemea na kukaa kwenye kochi na kutoa pumzi ndefu.
"mkuu, njoo uangalie" Joe aliingia ofisini kwa Christina na kuongea, Christina bila kuchelewa aliinuka na kumfata mtaalamu huyo wa IT. "umeona ile gari" Joe aliongea, "ina sadikika ilionkena eneo hili siku aliokufa Mr Clinton" Joe alizidi kufafanua. "ok nipatie kila kinachohusika na gari hio" Christina aliongea na kuondoka. Joe alianza mandingo yake lakini cha ajabu hakukuta hata rikodi moja ya gari hio, ni wapi ilipopita baada kuondoka hapo. Kiufupi kamera zote za barabarani zilikuwa haziioneshi gari hio, "duh huyu jamaa anaenekana mtaalamu sana wa computer" Joe alijisemea na kuinuka kisha akaelekea ofisini kwa Christina. "mkuu inavyoonekana tunapambana na mtu amabe si wa kawaida kwa sababu amefanikiwa kufuta video zilizorikodiwa na kamera za barabarani" Aliongea Joe, "usiniambie anakushinda wewe" Christina aliongea kwa hasira. "ah sijasema kama ananishinda mimi ila kwa Computer zetu za kawaida hatuwezi kujua chochote kwa sababu huyu jamaa anatumia Master Computer" Alijitetea Joe. "sasa nikupatie hiyo Computer" Aliuliza Christina. "we nipe pesa tu kwa sababu hiyo computer huwezi kuipata bali unatengenezesha sehemu maalum" Joe aliongea na hapo hapo Christina alito kadi yake ya bank na kumkabidhi Joe "1313" aliongea na Joe akaondoka. "hahaha hatua moja mbele" Alex alikua akicheka baada kumzidi akili mtu amabe ndie atakaemuwinda, "Rose unataka kujifunza shabaha"Alex aliuliza. "natamani sana hasa kwa sniper" Rose alijibu huku akitabasamu, "jiandae basi nishampata mtu amabe utaanza kujifunzia shabaha kichwa chake" Alex aliongea na kuinuka, Rose nae alikwenda ndani aliporudi alikuwa na sniper mkononi na kwa pamoja walitoka na safari ikaanza. Walifika mpaka kwenye jengo fulani na kupanda mpaka juu, "kuna mtu mmoja atakuja katika ofisi hio hapo mbele na atakaa kwenye kiti kile pale" Alex aliongea, Rose alianza kuipanga sniper yake kwa ajili ya kazi "weka risasi moja tu inatosha" Alex aliongea tena Rose nae akafanya hivo. Baada dakika kumi Rodriguez alifika katika ofisi hio na kukaa pale pale Alex aliposema atakaa. Alex alikuwa na darubini hivyo alimuoma vizuri, "haya kazi kwako, pumua taratibu na usipige risasi mpaka pale utakapohisi mapigo yako ya moyo yamerudi katika hali yake ya kawaida" alimpa maelekezo hayo kama alivyopewa na Allen. Rose alitulia huku akijitahidi kupumua taratibu mpaka mwisho mapigo yakakaa sawa, akaweka jicho kwenye darubini ya sniper na kuanza kulenga. "sehemu nzuri ya kupiga ni kichwani" Alex alimpa maelkezo tena, "Rodriguez, Mungu akakubanika" Rose aliongea na kufyetua risasi ilioingia katika paji la uso la mzee huyo. "kazi nzuri" Alex alimpongeza na kukunja vitu vyao na kutokomea eneo hilo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taarifa hizo za kifo cha Rodriguez ziliwafikia wengine na kujikuta katika wakati mgumu sana, bila kuchelwa waliitisha kikao kilichoongozwa na Hellen. "nahisi sasa ule muda wa kuishi kwa amani umeisha" Aliongea baada kufungua kikao, "una maanisha Alex kasharudi" Martin aliuliza. "ndio na inaonekana sasa amejipanga kisawasawa" Hellen alijibu. "inabidi tumwage vikosi vianze kazi ya kumsaka" Mtu mwengine aliongea."acha ujinga wewe kwani hujui kama ule muda wa kufanya mapinduzi umefika" alifoka mwanamke huyo kwa hasira. "sasa unataka tuendelee kufa au vipi" aliuliza tena yule mtu, swali hilo lilimkera sana Hellen na kujikuta akichomoa bastola yake ndogo na kumchapa risasi kadhaa za kifua. "kuna bweha mwingine yoyote bado anaogopa" Aliongea Hellen na wote wa kutingisha vichwa kuashiria kuwa hakuna aliekuwa anaogopa. Acha kabisa kifo bwana, waliendelea na kikao chao na mwisho walikubaliana kuwa kila mtu afanye lolote lile linalowezekana amtoroke Alex hata kama itabidi kukodi bodigadi wake binafsi. Upande wa Christina alivimba kwa hasira baada kusikiwa kuwa Alex kashaanza kazi halafu yeye amekaa anasubiria master computer. "una mikono yenye nguvu sana, sikutegemea kama ungefanikiwa kumpata kichwani" Alex alimwabia Rose wakati wanapata chakula cha usiku. "ah nimebahatisha tu" Rose aliongea huku akitabasamu, "hapana hujabahatisha, ile ni kutokana na kuzidisha umakini kwa sababu ulikuwa ukitambua kuwa kwenye sniper ulikuwa na risasi moja tu hivyo kama ungemkosa ilikuwa ni vigumu kuweza kuweka risasi nyingine" Alex alifafanua. Basi walimaliza kula na kila mtu alielekea chumbani kwake na kupumzika. Siku ya pili mapema waliamka na kufanya mazoezi yakiwemo ya ngumi kwa sababu walielewa kuwa kazi hiyo itazidi kuwa ngumu kadri siku zinavyokwenda.
Wiki sasa ilikuwa imekatika bila matukio yoyote yale na master cimputer ilikuwa imeshakamilika, "sasa tuone nani kama Joe kwenye computer" alijisemea moyoni na kukaa kwenye kiti kisha akaanza mautundu yake na baada dakika tano aliweza kuziunga camera zote za barabarani na kila kona katika computer yake alioipa jina la Samurai. "bingo" alipiga kelela na kuinuka kiksha akenda kumuita Christina, "hii ni video ya kifo cha Rodriguez" aliongea Joe na kuanza kuirusiha nyuma taratibu ili kutafuta risasi imetoka wapi na alifanikiwa. "kuna vivuli vya watu wawili mmoja amesimama na mwengine amelala" alifafanua Joe. Baada hapo alianza kusafisha picha mpaka kufanikiwa kuwaona watu hao vizuri sana, "washenzi mumekwisha" Christina aliongea huku akitabasamu, tabasamu amabalo lilikuwa na maumivu tele. "halafu inaonekana aliepiga si nguli sana" Alizidi kufafanua Joe baada kuchunguza kwa jinsi alivyolala mpigaji huyo. "na hawa wanawalenga wakuu wa kitengo cha upelelezi" Christina aliongea na kuweka alama ya kuuliza kichwani. Wakati wakiendelea kuchambua video hiyo, simu ya Christina iliita "hallo" aliipokea. "naona unahangaika, kuchambua video si ndio" Aliongea Alex upande wa pili. Christina hapo alimpa ishara Joe aitrack simu hiyo, "usipate shida ya kuitrack maana utajiudhi tu" Alex aliongea tena na kuachia kicheko cha chini kwa chini. "nilijuwa tu utafanya juu chini kujua taarifa zangu na ndio maana nikafanya makusudi mauajia ya Rodriguez na hio na kukupa taarifa kuwa hata ukusanye jeshi lote la nchi hii basi hamtaweza kunizuia nisifanye nilichokusudia kwa sababu nimempa mtu ahadi na kama unavojua ahadi ni deni basi na mimi sitokaa mpaka niitimize" Alex alimaliza kuongea na kukata simu bila kusubiri Christina ajibu chochote. "mkuu hii simu imepigwa humu humu ofisini" Joe alitoa majibu baada kuitrack simu hio. "eti nini" Christina alimaka kwa mshangao. "WELCOME TO THE DIRTY GAME" Alex aliongea baada kukata simu hiyo na kutabsamu kwa hasira na machungu ya hali ya juu.
Christina alijikuta akifura kwa hasira na kila alipojitahidi kuzituliza ilikuwa kazi bure, mwisho aliona bora aondoke kabisa ofisini. Moja kwa moja lienda mpaka nyumbani kwake na kujitupa kitandani huku akiwa na mwazo kibao. Na yote ilikuwa ni kivipi atamkamata Alex na kulipa kisasi kama alivyoamini kuwa Alex ndie aliemuuwa babaake. "Lakini kwa nini aseme hata nikikusanya jeshi zima siwezi kumzuia asitekeleze ahadi aliomuahidi mtu" swali hilo liliibuka tu kichwani mwake. "ana uhusiano gani na viongozi wa kitengo cha upelelezi" swali jingine liliibuka, "mh kuna kitu kinanuka vumba lakini hio sio kazi yangu kabisa, maisha yake ni halali yangu kuyatoa" alijisemea huku akitokwa na machozi.
Na maumivu yalizidi pale alipokumbuka kipindi akicheza na babaake wakati ni mdogo sana. "Hivi unataka kuwa nani ukiwa mkubwa" aliuliza babaake, "nataka kuwa kama wewe baba" Christina alijibu kwa sauti ya kitoto huku akicheka na kumkumbatia babaake. Mapenzi aliokuwa nayo binti huyo kwa babaake yalikuwa makubwa sana hasa ukizingatia mamaake alikufa wakati yeye ni mdogo hivyo basu mapenzi yote aliyahamishia kwa babaake. "kwanini lakini ulirudi katika mazingira ya vita tena wakati uliniahidi kuwa wewe na silha basi tena" Christina alijisemea mwenyewe huku akimlaumu babaake kwak kuto timiza ahadi yake. "kila kitu nilichokifanya nilikifanya kukupa tabasamu usoni, sasa hizi medani zote nilizozipapta nani nitamuonyesha na nani atakae ziona za thamani sana" alizidi kulalamika. Wakati akiendelea kulia alihisi kitu kama kikimgusa begani na aliogeuka alishangaa kumuona babaake akitabasamu huku akimuonyesha ishara kuwa anyamaze na kuwa mkakamavu. Alitaka kumkumbatia kwa furaha lakini alijikuta akikumbatia hewa, kumbe yale yalikuwa ni mawazo yake tu. Na hiyo ilikuwa ni kawaida ya babaake kumgusa begani wakati anapokuwa na wakati mgumu sana na kushundwa kupata majibu.
Alex akijishangaa mwenyewe ni kwa jinsi hata uwezo wake wa kupanga matukio ulivokuwa mkubwa sana. "kweli hii kemikali ni balaa" alijisemea moyoni wakati akiendelea kupanga mikakati kuanza kuwaondoa maadui zake kwa kasi ya kubwa. Rose alikuwa katika chumba maalum akifanya mazoezi ya kujiweka sawa maana alielewa shughuli iliokuwa mbele yake ilikuwa si ya kitoto. Alex alikamilisha mipango na kuelekea chumba cha mazoezi, "naona umeiva sasa" aliongea huku akivua shati lake. "unataka spaling nini" Rose aliongea huku akitabasamu, "ah huniwezi wewe" Alex alijibu na kuvaa vigloves maalum vya spaling. "ntatumi mkono mmoja tu" Alex aliongea na kuweka mkono wake wa kulia nyuma, Rose alijiweka sawa na mpambano ukaanza. Uwezo wa Alex uliongezeka mara dufu kuliko mwanzo maana alivyokuwa akizitoka ngumi ilikuwa ni kama mtu anaepelekwa na mashine. Rose alijitahidi kupeleka masumbwi mazito lakini wapi Alex alikuwa level nyingine kabisa na kuna wakati alitabiri kabisa atapiga wapi. Baada dakika kumi Rose alikuwa hoi na hapo alikuwa anashambulia tu, Alex wala hakurusha ngumi hata moja. "kweli umeiva sana" Alex alimsifia baada zoezi hilo fupi, "ah wapi sijakupata hata ngumi moja" Rose aliongea huku akicheka. "usijali kuna watu kibao mikono yako tu, hadi utachoka mwenyewe kwani ndi kwanza safari imeanza" Alex aliongea na kutoka na kuelekea chumbani kwake kwa ajili ya kujifanyia usafi. Baada saa moja walirudi sebleni na kupata chakula cha usiku kisha wakaanza kuoanga mipango ya usiku huo. "kuna huyu jamaa anaingia leo kutoka Uingereza, anaitwa Masaya. Ni mjapani mwenye asili ya kiingereza na ni miongoni mwa watu waliotumika katika kuhakikisha familia zetu znatetekea" Alex aliongea na kuendelea "huyu jamaa ana ulinzi wa hali ya juu sana lakini tukimuondoa mchezoni huyu tutakuwa tumejisafishia njia kuelekea ushindi maana baada Robert kwa hatari anafata huyu".
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"so tunampelekaje kuzimu" Aliuliza Rose huku akiwa amevaa sura ya kazi. "kwa karibu hatuwezi kumpata lakini itabidi tuwapunguze walinzi wake, ili yeye afanikiwa kutoroka na baada hapo tutamsubiri 98:11, hapo tunaishambulia gari yake na kuhakikisha hatoki mtu. Kwa hiyo leo tutabeba bastola tatu sniper, smg na ndogo ya dharura" Alimaliza kuongea na kila mmoja akachukua silaha zake na kutoka nje. "mbona kuna gari mbili" Rose aliuliza kwa mshangao baada kukuta ferari nyeusi nje, "ndio, nimesahau kukwambi kuwa kuanzia sasa kila mtu atakuwa na usafiri wake. Hii itatupa urahisi kusaidiana ikiwa mmoja wetu atakamtwa" aliongea Alex na kumkabidhi Rose fungo ya ferari na safari ikaanza. kila mmoja alionesha ufundi wake katika kumudi gari hizo ndogo zenye mashine kubwa sana, walipofika sehemu walipeana ishara na kila mmoja alichukua njia yake.
Katikati ya usiku, ndege binafsi ilituwa katika moja kati ya viwanja vyake nchini marekani. "karibu marekani mkuu" aliongea mtu mmoja wakati anamkaribisha, "asante" Masaya alijibu huku akishusha pumzi kwa kasi. "tafadhali nifate" aliongea yule mtu na Masaya aliimfata huku akizungukwa na walinzi wake, "Juliet, uko katika nafasi yako" Alex aliongea katika kifaa maalum cha mawasiliano. "ndio Romeo, Roger that" Rose alijibu huku akijiweka sawa. "Mlengwa anaelekea saa 7:00" Alex aliongea, "nimekusoma Romeo" Rose alijibu. "usishambulie mpaka nitakapokwambia, over and out" Alex aliongea. "mkuu kuna mtu mmoja anaengia leo kutoka uingereza, na nina wasiwasi Alex atakuwa anamfatilia maana nimefanikiwa kuvamia computer yake" Joe aliingia Ofisini na kutoa taarifa, "nindalie gari yangu" alitoa amri huku akianza kutoa mashine za kazi. "tunaanza kushambulia ndani ya tatu, mbili na moja" Alex alimaliza kuongea na hapo sasa walinzi wa Masaya walianza kuenda chini mmoja baada ya mwengine. "mkuu tafuta sehemu ujifiche kuna masniper hapa" aliongea mlinzi mmoja kabla ya kupasuliwa kichwa na risasi iliyotoka kwa Rose. Masaya alikimbia na kufanikiwa kuingia katika gari na kumwambia dereva wake aondoe gari. "Juliet Kimbiza" Alex aliongea na hapo hapo waliacha kushambulia na kushuka chini, kila mmoja aliingia kwenye gari yake na safari ikaanza.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment