Search This Blog

Friday, 20 May 2022

C.O.D.EX. 2 (THE DIRTY GAME) - 5

 







    Simulizi : C.O.D.EX. 2 (The Dirty Game)

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "tembea 220 km/saa" Alex aliongea huku akizidi kukanyaga mafuta na Rose nae hakuwa nyuma. "namuona mlengwa" Rose aliongea alipoiona gari ya Masaya mbele yake, "mpite na umzingue" Alex aliongea na Rose alifanya hivo. Aliipita gari ya Masaya na kuanza kupunguza mwendo huku akijitahidi kuibania isipite, dereva wa Masaya alipoona hivo aliamua kuingia njia za ndani kwa ndani na hilo ndio kosa alilofanya. Alex alishatangulia mbele na kufunga njia kwa gari kubwa ambalo alikuwa ameliandaa. "mkuu hakuna tena njia huku" Aliongea yule dereva, "rudi nyuma" aliongea Masaya lakini dereva alipoangalia kwenye kioo cha pembeni alishtuka "mkuu kuna gari mbili nyum zimefunga njia" aliongea dereva. Alex na Rose walishukwa kwenye gari huku mkononi wakiwa na SMG na kuanza kuishambulia gari ya Masaya. Walimimina risasi za kutosha mpaka gari ikawa haitamaniki, waliporidhika taratibu waliisogelea gari hiyo na kufungua mlango. Walimkuta Masaya akihema juujuu huku akiwa na majeraha kadhaa. "nyie ni kina nani na mnatakat nini" Aliuliza kwa tabu, Alex wala hakumjibu alimsachi na kuchukua flash ndogo pamoja na pete. "Rose, halali yako huyo" aliongea Alex na kurudi nyuma, Rose alitabasamu na kumyandika Masaya ngumi ya koo. Masaya wala hakufurukuta alitulia tuli na kutoa upepo wa mwisho na kuaga dunia, walirudi kwenye gari na kuondoka eneo hilo. Wakati wanatoka katika kichochoro hicho uso kwa uso na Agent Darling, Alex alishusha kioo wakatia anapishana nae na kusema "Allen Jr umechelewa tena, unamuangasha babaako" kisha akapandisha kioo na kukanyaga mafuta. Agent Darling alikanyaga breki na kuserereka, alianza kumfukuza huku akiwa na hasira ile mbaya. Alex alipoona Gari ya Agent Darling inakuja akaongea "Juliet tukutane nyumbani", "umesomeka Romeo" Rose alijinbu na kupumguza mwendo. Gari ya Agent Darling ilimpita kwa kasi sana, alitabsamu kidogo na kubadilisha njia. Mtanange ulianza kati ya Alex na Agent Darling, "kama ulivyosema mkuu mwanao ni mbishi sana" aliongea Alex akimaanisha Allen. "leo haki ya nani sikuachi labda gari yangu ipinduke" Agent Darling aliongea huku akizidi kukanyaga mafuta na gari yake aina ya lambogini Galado ilitii amri na kuteleza barabarani kwa mwendo kasi wa hali ya juu sana.

    Manguli hao wawili walizidi kuonyesha uwezo wao katika fani hio ya kuchoma matairi, Agent Darling alishusha kioo na kujaribu kuishambulia gari ya Alex lakini kutokana na mwendo kuwa wa kasi sana ilikuwa ni vigumu kuipata. Hivyo basi kwa sababu gari yake ilikuwa ni yenye kufunguka paa, alibonyeza kitufe na lile paa la gari likafunguka na alipoona linachelewa alilipiga ngumi na kuling'oa. Wakati wote Alex alikuwa akumuangalia kupitia kioo cha pembeni na kutabasamu "ni kweli ulioyasema Allen, binti yako ni mbishi sana" Alex aliongea maneno hayo huku macho yake yakianza kujaa maji. Agent Darling aliwasha computer ya gari yake na kuweka tracking mode, mfumo huo uliiwezesha gari yake kuikariri gari ya Alex. Kisha akabonyeza kitufe kingine kilichoandikwa auto drive, na baada hapo aliachia msukani na kusimama kwenye siti yake. Gari yake ilizidi kusonga mbele na wakati huo ilikuwa ikijiendesha wenyewe, alichukua bastola kubwa aina AK47 na kuanza kuishambulia gari ya Alex. Bastola hio ilikuwa ina nguvu sana kiasi cha kutengeza nyufa wakati risasi yake ilipopiga katika kioo cha gari ya Alex japo ilikuwa ni bullet proof. "mbili nyingine navunja kioo cha nyuma" Agent Darling alijisemea moyoni, alifyetua risasi ya pili ikaende kupiga pale pale ilipopiga ya kwanza na bila kuchelewa alifyetua ya tatu na hatimae kioo cha nyuma cha gari ya Alex kikavunjika.





    Alex alishtuka baada kioo hicho kuvunja na ndipo akakanyaga breki na kuizungusha gari na ikaelekeana uso kwa uso na gari ya Agent Darling. Aliweka gia ya kurudi nyuma kuanza kurudi nyuma kwa kasi kubwa sana kisha alishusha kioo cha na kutoa bastola yake ndogo na kuanza kujibu mashambulizi. Lakini wala hayakumtisha Agent Daeling badala yake alitabasamu na kutoa bastola ndogo na kuanza kumimina risasi. Alex aliangalia saa yake ya na kugundua kuwa muda umekwenda sana, "siku nyingine tutamalizia mpambano wetu" Aliongea na kutabasamu kidogo kisha akalenga tairi la upande wa kulia la gari ya Agent Darling na kulichapa risasi. Tairi hilo lilipasuka na kutokana na mwendo mkubwa wa gari ile ilianza kuyumbayumba na kupoteza muelekeo. Lakini kabla gari hiyo haijapinduka Agent Darling aliruka na kupiga sarakasi nyuma, alitua barabarani na kubiringitia kwa ufundu wa hali ya juu sana. Alex alishuhudia tukio hilo zima na kujikuta akikodoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango na ilibidi asimamishe ari kwanza. Agent Darling alisimama na kuiangalia gari ya Alex kwa hasira "bahati yako mpumbavu wewe" alijisemea na kusonya kwa nguvu kisha akatoa simu yake na kupiga. Alex aligeuza gari yake na kuondoka eneo hilo.

    Baada ya dakika tano ilifika ndege moja ambayo watu wengi hawakuwahi kuiona, ilitua alipokuwa Agent Darling na kushuka mtu mmoja ambae kwa mbali ni mtu aliejengeka vizuri kimaumbile. "pole kwa kazi ngumu" aliongea Jeff baada kufika alipokuwa amesimama mwanamke huyo, "ah pole ya kazi gani sasa wakati sijafanikiwa kumchuna japo kidogo" Aliongea kwa masikitiko makubwa sana. "usijali huo ni mwanzo tu, mbona muda si mrefu utamuingiza mkononi" Jeff alimjibu huku akimsogelea na kumkumbatia, kwa jinsi alivyomkumbatia ilionyesha wazi kuwa hao walikuwa ni mtu na mpenzi wake. Agent Darling alikuwa akilia sio kwamba ameumia au kwa sababu kuna mtu anamjali sana bali alikuwa akilia akijilaumua kwa nini amemuacha Alex amemtoroka mikononi mwake. Jeff alimshika mkono na kurudi katika ndege na ndege hiyo ikaondoka na kupotelea angani. Alex alifika nyumbani kwake na kuingiza gari ndani, lakini mpaka wakati huo bado ile picha ya Agent Darling namna alivyochomoka kwenye ile gari ilikuwa ikimrudia kichwani mwake. "inawezekanaje mtu kuweza kutoka katika gari inayokwenda karibu kilometa 180 kwa saa kisha atue bila hata kuumia au kuvunjika" hilo ndio lilikuwa swali alilokuwa akijiuliza. "mbona umechelewa" Rose aliuliza baada Alex kuingia ndani, "ah we acha tu nilichokiona huko ni balaa, na inabidi tuwe makini sana na huyu mtoto wa Allen maana huyu mtoto ni balaa" Alex alijibu huku akijitupa kwenye kochi.

    CODE X 2: THE DIRTY GAME 25

    Muda wote alikuwa hajamuangalia vizuri Rose, baada kukaa kwenye kochi ndipo akamuangalia. Alishtuka baada kuona nguo aliovaa inaonyesha vizuri na kumchora umbile lake lenye asili ya kilatini. Aljitahidi kupotezea lakini wapi, mwanaume ni mwanaume tu hata awe kauzu vipi. Rose alilishtukia hilo na kuinuka, moja kwa moja alikwenda na kukaa juu ya mapaja ya Alex na wakawa wanaangaliana uso kwa uso. "hivi Alex mpaka lini tutakuwa tunalala vyumba tofauti" Rose aliuliza kwa sauto ya kike zaidi, "Rose vipi umechanganyikiwa nini" Alex alijibu huku akijitahidi kuyaondoa macho yake katika kifua cha binti kilichochorwa na matiti ya wastani na yaliojaa. "Alex mimi sijanganyikiwa ila nimejitahidi sana kuzuia hisia zangu juu yako lakini kwakweli nimeshindwa" Rose alijibu huku akisogeza kichwa chake karibu zaidi na cha Alex mpaka kikafika sehemu wakawa kila mmoja anahisi mvuke wa pumzi ya mwenzake.

    *****************************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "huyu Alex anazidi kutuyia heka heka kwa kweli" Helen alioongea wakati wakiwa kwenye kikao, "unajua vitu alivyochukua kwa Masaya vina siri kubwa na nzito sana" Martin aliongea huku akikuna kichwa. "sasa tunafanyaje kumpunguza makali" Helen aliuliza, "nimewasiliana na mtu mmoja hatari sana na amekubali kutusaidia ikiwa tutamlipa hela ya kutosha" Jafar alijibu. "ni nani huyo mtu mwenyewe"aliuliza Martin."Huyo anaitwa Shadow jina lake la kazi na anamiliki kikundi kinachoitwa COBRA, ni kikundi hatari sana cha majambazi ya kimataifa" alieleza Jafar. "hivi wewe una akili timamu kweli" alifoka mtu mwengine aliekuwepo kwenye kikao hicho kisha akaendelea "kwanini tusitumie tu wanajeshi wa kawaida, hivi unadhani...."kabla hajamaliza ulisikika mlio wa risasi na yule jamaa akaanguka chini huku akiwa na tundu linalotoa damu kichwani. "kwenye vita hakuna sahihi wala kosa, yote ni sawa" Helen aliongea maneno hayo wakati anairudisha bastola yake mezani. "Jafar mpe kazi huyo jamaa na kuhusu malipo tutamlipa kiasi anachotaka" Helen aliongea na kusimama akimaanisha kikao kimefungwa. Kila mtu aliondoka na kurudi sehemu yake ya kazi, ule mzoga ulibebwa na kupelekwa sehemu ya kuchomea maiti. "Shadow, kazi kwako sasa" Jafar aliongea maneno hayo baada simu yake kupokelewa upande wa pili kisha akakata. "vijana ule muda tuliokuwa tunausubiri umefika sasa, maana mikono ilikuwa inawasha kweli. Hivi ni muda gani hatujamwaga damu ya mtu" aliongea Shadow na mwisho akauliza. "ni wiki sasa mkuu" alijibu kijana mmoja ambe alioenekana mkorofi sana maana baada kuambiwa tu kuna kazi alinza kuweka silaha zake vizuri. "huyu kwenye picha ni Alex na ndie tunaetakiwa kumuondoa duniani, inavyosemekana eti ni mtu hatari sana. Sasa sijui ni hatari kuliko sisi lakini hakuna mtu hatari kama sisi katika dunia hii" aliongea na kucheka kwa kejeli. "wale vijana wa kupeleleza naomba muingie kazini hakikisheni ndani ya siku mbili mnajua tunampata wapi" alitoa amri hiyo na vijana kumi wakaondoka kambini kwa ajili ya kusaka taarifa za Alex na wapi anapatikana.

    Kabla hajakutanisha mdomo wake na wa Alex, Alex alimzuia na kumshusha mapajani mwake kisha yeye akainuka na kuelekea chumbani kwake. "huyu nae kama karogwa" aljisemea moyoni wakati anaingia chumbani kwake. Alivua nguo na kuingia chooni kwaajili ya kuoga, wakati anaendelea kuoga ghafla alihisi mikono laini ikitambaa mgongoni kwake na alipogeuka alishangaa kumuona Rose akiwa mtupu na hapo ndio akakumbuka kama alisahau kufunga mlango kwa ufunguo. Lakini mpaka hapo alipofikia tayari alishainua mikono na kumpokea mschana huyo kwa moyo mkunjufu kabisa na kujikuta wakitokomea katika ulimwengu furaha zisizo na mwisho. Walikuja kushtuka asubuhi kumeshakucha, "Alex mbona mpema hivo" Rose aliongea baada Alex kumtingisha. "nenda kamalizie usingizi chumbani kwako" Alex alimjibu, "chumbani ni humu humu siendi kokote" Rose alijibu. "wee kuanzia lini" Alex aliuliza kwa mshangao, "kuanzia jana usiku" Rose alijibu na kugeuka upande wapili kisha akaendelea kulala. Alex alishuka kitandani lakini alishangaa kwa jinsi alivyokuwa mwepesi asubuhi hiyo, "duh nimepungua uzito nini" alijisemea na kujicheka mwenyewe kisha akatoka chumbani na kuelekea jikoni. Alitengeza kahawa na kunywa kisha akenda kuchukua ile flash na kuichomeka katika laptop yake, mambo alioyakuta humo yalianza kumfanya atoke jasho. "lazima watu zaidi ya milion 100 wafe, ili wafahamu kuwa mapinduzi lazima" hayo ni miongoni mwa maneno yaliosikika katika video aliokuwa anaangalia. "karibu tena duniani" Jeff aliongea baada Christina kufungua macho, "hapa ni wapi" Christina aliuliza. "karibu katika GHOST CHAMBER" Jeff alimjibu huku akitabasamu, "nimelala kwa muda gani" Christina aliuliza tena. "ah ni usiku mmoja tu" Jeff alimjibu na kuinuka, alikwenda mezani na kurudi na vikombe viwili vya kahawa. Kimoja alimpa kimoja Christina na kimoja alikunywa yeye. "nahitaji kurudi ofisini" Christina aliongea huku akisimama, "kwa leo huwahi tena, subiri mpaka kesho nitakupeleka" Jeff aliongea huku akimrudisha kwenye kitanda. "sawa" Christina alikubali na kukaa, "dah gari yangu hata sijui iko katika hali gani" aliongea Christina huku akionekana kama mwenye majonzi. "usijali, ile ilikuwa ya mpito tu. kuna gari yako ya aina yake peke yake iko katika hatua za mwisho kukamilika, inaitwa DARLING" Jeff alijibu huku akimuangalia Christina usoni.

    ********************************

    "Masaya tumeshampoteza tayari halafu munanambia nikae chini nitulie, hivi nyie mnaaakili au mumechanganyikiwa" General David alifoka katika kilichokuwa kinaendelea kwa siri. "mkuu usijali kila ktu kitakuwa sawa muda si mrefu" mtu mmoj aliongea ili kumtia moyo bosi wao ambae alienekana kukasirishwa n avifo vya watu wake hasa wale wenye umuhimu mkubwa. "sasa nawapa wiki moja tu ikiwa hamujanileteza Alex hapa naingia mwenyewe kazini" alifoka na kusimama, "sawa mkuu na tunakuahidi kuwa ndani ya wiki moja tutamleta Alex kwako akiwa hai ama amaekufa" walijibu kwa pamoja na kikao hicho kikafungwa. "huyu Alex huyu ni maumivu shingoni", "lakini ilikuaje kuaje mpaka tukafikia hapa". "unamaanisha nini kusema hivyo", "yaani namaanisha kwanini tumeingia katika mkumbo huu wakati tuna vyeo vikubwa tu katika nchi zetu na watu walikuwa wakituheshimu na kututumikia sisi". Hayo yalikuwa ni mazungumzo kati ya viongozi wawili wa nchi fulani. "Alex, Alex, Alex kosa langu kubwa n kukuacha hai" General David aliongea mwenyewe huku akionyesha ni mwenye hasira sana, "lakini nakuahidi utakufa tu kama walivyokufa wengine" aliongea tena kucheka kicheko kilichojaa uasi, chuki na hasira.





    "Christina nifuate" Jeff aliingia katika chumba alichokuwa amepumzika Christina na kuongea, Christina alinyanyuka na kumafata bila kumuuliza swali. Walietembea mpaka kwenye chumba kimoja kikubwa sana, kwa mbali kulikuwa na kitu kimefunikwa na turubai nyeupe. "nenda ukafunue" Jeff alimwambia na yeye akakaa pembeni, Chritina alitembea kwa mwendo wa haraka mpaka alipofika alipoambiwa afunue. Mapigo ya moyo wake yaliongezeka kasi mpaka akawa anayasikia masikioni mwake, taratibu alianza kufunua turubai hilo mpaka anamaliza alikuwa haamini macho yake kabisa na alijaribu kuyafikicha ili kama yupo kwenye ndoto basi aamke. "happy birthday Darling" Jeff aliongea huku akimkumbatia kwa nyuma, christina alifurahi sana maana hata yeye mwenyewe alikuwa amesahau siku hiyo muhimu kwake. "hiyi ndio zawadi yako ya siku ya kuzaliwa" Jeff aliongea na kumkabidhi funguo za gari yake mpya inayokwenda kwa jina la darling. "unaweza ukatest, gari hii ni ya kisasa na iko hii hakuna nyingine. Ni bullet proof na mifumo ya silaha na kila kitu huna haja ya kushusha kioo na kushambulia wakati unamkimbiza mtu. Unabonyeza tu ndani na mbele zitatoka bunduki na utashambulia ukiwa ndani ya gari hii" Jeff aliendelea kumpa maelezo juu ya gari hiyo mpya kabisa hata katika ulimwengu haijawahi kuonekana.

    Alex alimaliza kuikagua flash ile na kugundua siri nyingi sana na kwa msaada wa Rose walifanikiwa kugundua mpaka makao makuu ya kikundi hichi haramu. "sasa kilichobaki itabidi tuongeze kasi ya mauaji ili tuikamilishe kazi hii kabla ile siku waliopanga haijafika" Alex aliongea na Rose alikubali. Wakati wao wakipanga mikakati hiyo, vijana wa Shadow waliripoti kambini na kutoa taarifa zote walizozipata. "kazi nzuri vijana wangu" Shadow aliwasifu kwa kazi nzueri waliofanya, alitoa amri maandalizi ya mavamizi yaanze. Kikosi hicho kilikuwa na vijana thalathini waliobobea katika mbinu za kivita chini ya Shadow kiongozi asie na huruma hata kidogo.

    "ah nimesahau kukuambia kitu" Jeff aliongea wakati Christina anajiandaa kuondoka, "kitu gani tena2 Christina aliuliza. "chukua hii flash itakupa maelezo mazuri tu" Jeff aliongea na kumkabidhi flash hiyo. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Waliagana na Christina akaondoka na kurudi zake ofisini, kila alippita watu waliishangaa gari yake wapo waliomsimamisha ili wapige picha na gari hiyo. Alifika Ofisini na moja kwa moja mpaka katika ofisi yake na kuwasha computer, alichomeka ile flash ili ajue ndani kuna nini. Macho yalimtoka baada kuona taarifa zote za Alex na mwenzake, alitabasamu kidogo na kujisemea "leo ndio leo asemae kesho muongo". Aliichomoa flash na kuivunja, "bosi ulikuwa wapi siku hizi mbili" aliingia Joe na kuuliza swali. "nilikuwa undercover kidogo, kulikuwa na kazi na fanya" Christina alijibu na jibu hilo lilionekana kumridhisha Joe ambae baada maongezi hayo alimkabidhi mafaili mawili kisha yeye akatoka. Christina aliayafungua mafaili hayo na kuyasoma baada hapo aliyafunga na kuyaweka katika droo. Alikaa ofisini akiisbiri jioni ifike kwa hamu ili aingie kazini, wakati yeye anawaza hivyo Shadow na vijana wake pia walikuwa wamepanga usiku huo wakamavamie Alex kwa sababu walishapajua anapokaa.

    ******************************

    Alex alikuwa ametulia ukumbini lakini moyo wake ulikuwa hauna amani kabisa, mwisho aliamua kuinuka na kuelekea chumbani alipokuwa akilala Allen. Alianza kukagua kagua vitu mbali mbali mpaka alipofika kwenye kabati la nguo. Alilifungua na kukuta kijikaratasi chenye ujumbe "ukishaanza kazi nyumba hii haitokufaa tena, utabidi uondoke lakini kwenye kabati hili nyuma kuna mlango wa siri. Na kuna usafiri maalum utakaokupeleka mpaka katika nyumba yangu nyingine hapa hapa New York...Allen James" Alex alitabasamu na kurudi sebleni. Wakati anafika alioma vivuli kwa nje vikitembea tembea, bila kusita alielekea jikoni ambako Rose alikuwa anaandaa chakula cha usiku. "tumevamiwa" Alex alimnong'oneza masikioni na taratibu wote wawili wakatoka jikoni na kuelekea chumba cha silaha. Kila mmoja alichukua dhana zake za kazi na kukaa tayari kwa yoyote atakae imgia, Rose alipanda sehemu ya juu kabisa ya jumba hilo na kujibanza pahali akiwa na sniper.Alex alijibana ukutani na kusikilizia, ghafla kilipasuka na kitu kama chuma kikasikika kikilia wakati kina gusa ardhi na kuanza kutoa moshi mzito. Mlango ulivunjwa na vijana wa Shadow wakaanza kuingia kwa fujo, masikini watatu wa mwanzo wote walianguka chuni wakiwa na matundu ya risasi kichwani. "haka kamchezo katakuwa kazuri kweli leo" Rose alijisemea baada ya kuwachapa watati wa mwanzo. Alex alichomoka alipojibanza kwa kasi ya hali ya juu huku mkononi akiwa na bastola ndogo mbili, alianza kufyatua risasi bila mpango ili ajipe mwanya wa kuingia sehemu nyingine. Vijana wa Shadow walijibanza mpaka Alex alipoacha kupiga risasi. Ndipo walipojitkeza na kuanza kujibu mashambulizi, walilimimina risasi lakini walishangaa sana maana wao ndio waliokuwa wakishambulia lakini wao ndio waliokuwa wananguka chini wakivuja damu. "kuna mtu mwengine amejificha humu na anatumia sniper" Aliongea mmoja wao na wote wakarudi kujibanza ukutani. Mwengine alitoa bomu dogo na kulirusha upande ambao waliamini ndipo alipokuwa amejificha huyo anaeshambulia, bomu hilo lilitua pembeni kidogo na alipokuwa Rose lakini aliwahi kuondoka kabla halijalipuka.

    Wakati mpambano ndani ya nyumba hiyo kubwa ukindelea Agent Darling ndio alikuwa anafika, lakini alishangaa baada kuona moto ukirindima ndani ya jengo hilo. "mshenzi gani huyo anaeingilia kitoweo changu" Alijiesemea huku akiuma meno kwa hasira, "Alex atakufa kwa mikono yangu tu" alijisemea kwa mara nyingine na kutchukua bastola yake kisha kshika gari na kuelekea katika jengo hilo. "Juliet uko sawa" Alex aliongea baada kusikia mlio wa bomu, "ndio usijali kuhusu mimi" Rose alijibu. Agent Darling alipitia dirishani na kuanza kushambulia, Alex alipoona hivyo alijitokeza na kuendelea na mashambulizi. Na risasi zilipomuishia alianza kutumia kisu chake, hapo ndio walipoisoma namba. Alex alikuwa mtaalum sana hasa katika kombat ya kujihami mwenyewe, kila aliekutana nae alikwenda chini akiwa na alama kisu mwilini mwake. Ghafla wakati anaendea na mpambano aligongana mgogo na mtu mwengine na alipogeuka ni ana kwa ana na Agent Darling. "nimefutahi kukuona tena Allen Jr" Alex aliongea na kurusha kisu kilichokwenda moja kwa moja mpaka katika paji la uso la kijana mmoja wa Shadow. "mshenzi we tukiwamaliza hawa, nakuungia na wewe" Agent Darling aliongea huku akiendeleza mshambulizi. Kila mmoja aliendelea kupambana na wengine kwanza, "Juliet elekea chumbani kwa Allen nikukute huko"Alex aliongea na Rose akaitika na kuelekea huko. Vijana wa shadow walipoona hali imezidi kuwa mbaya waliamua kuchapa ndala, na wakati huo Alex alikimbilia chumbani kwa Allen ambalo alimkuta Rose na bila kuchelewa alielekea kwenye kabati na kulifungua kisha akampa ishara amfate, waliingia na kulifunga kwa ndani kisha akafungua mlango wa siri wa kabati hilo na na kuingia, Kumbe io ilikuwa ni lifti na ghafla ilianza kushuka kwa kasi kuelekea chini. Ilisimama na kufunguka, walitoka na kuelekea katika kitu kama treni lakini ilikuwa ndogo. Waliingia ndani ya chombo hicho na safari ikaanza. Agent Darling baada kuwaaliza wale walioshindwa kutoroka alianza kumtafuta Alex bila mafanikio. Wakati anaendelea na zoezi hilo ghafla simu ya mezani ikaita, aliipokea "asante kwa msaada wako, lakini nasikitika kuwa ungwe yetu mimi na wewe bado muda. Ukifika muda wa kuonyeshana usije ukaniangusha na nimependa ushujaa wako" Alex aliongea upande wa pili na bila kusikiliza kitu alikata simu na kuivunja kabisa huku akitabasamu. "nataka uone sababu ya yote hayo" alijisemea moyoni na kumkubatia Rose ambae alikuwa ameumia kidogo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Treni hio ilisimama na mlango ukafunguka, Alex alimbeba Rose na kushuka. Mbele yake kulikuwa na mlango, alitebea mpaka katika malango huo na kuufungua. Alishangaa kuona nyumba ile ilivyokuwa imefanana na ile waliokuwepo manzo kila. Kutokana na ufanano huo hakupata shiada kujua maabara iko wapi. Alielekea katika Maabara na kumlaza Rose kisha akachukua vifaa na kuanza kumchunuza, baada kumpatai huduma ya kwanza alimuacha apumzike yeye akatoka na kuelekea katika chumba kimoja ambacho aliamini ndio kama chumba alichokiacha kule alipotoka. Aliingia na kuelekea chooni na kujimwagia maji, alipomaliza alielekea jikoni na kujiandalia chakula. Alipomaliza alipata maakuli kisha akaelekea maabara kumuangalia Rose ambae alikuwa amelala hajitambui. Alikaa pembeni ya kitanda hicho na kujipumzisha. kutokana na uchovu na kuchoka sana usingizi ulimchukua gubigubi. Alikuja kushtuka baada kuhis kama akiguswa na mtu, alipofumbua macho alikutana natabasamu zuri usoni mwa rose. Lakini alishangaa kumuona akiwa ameshabadilisha nguo, hata hivyo alipojaribu kumuongelesha hakumjibu kitu badala yake alikuwa akitabasamu tu ila ghafla alianza kutoka damu nyingi mdomoni. Alex alikurupuka kutoka usingizini huku akihema kama mtu aliekuwa akifukuzwa. Alimuangalia Rose ambae alikuwa bado amelala hajitambui, alianza kuziangalia mashine ambazo zilikuwa zikifuatilia maendeleo yake lakini aligundua mapigo ya moyo yalikuwa yanasomwa katika kiwango cha chini kabisa. Hofu ilianza kumtanda, alitoka maabara na kuelekea gereji. Alitoa gari na kuipeleka mbele ya nyumba, alirudi ndani na kumbeba na kumpeleka kwenye gari kisha safari ya hospitali ikaanza. Aliendesha mwendo wa kiasi mpaka akiafika, alishuka na ufungua mlango wa nyuma. alimbeba na kukimbia nae ndani ya hosipitali. Wahudumu walipomuona walichukua kitanda cha matairi na kumfata. Alex alimlaza kwenye kitanda na hapo alikimbizwa katika chumba cha matibabu ya dharura, na baada kufanyiwa uchunguzi wa awali ikagundulika kuwa yupo katika hali mbaya. Hivyo dakatari mkuu anaemsimamia alitoa amri ahamishiwe chumba cha wagonjwa mahututi na ikafanywa hivo. "kijana nakuomba utulie utuache tufanye kazi yetu" Daktari huyo aliongea na kuzama katika chumba hicho cha wagonjwa mahututi.





    Agent Darling alipiga simu kituo cha polisi cha karibu na nyumba aliokuwa anakaa Alex, dakika tano baadae kilifika kikosi cha askari kikiambatana na gari la zima moto pamoja na gari ya kubebea wagonjwa. Alitoa maelezo yote hayo lakini hakuomtaja Alex. Baada ya hapo aliacha polisi wafanye kazi yao, yeye akarudi kwenye gari yake na kuondoka. Kwa sabau ulikuwa ni usiku alirudi nyumbani kwake na kupumzika lakini mawazo yake yote yalikuwa ni kutaka kuua wale waliomvamia Alex walikuwa wanahusika nae vipi. usiingizi ulimchukua bila hata kutegemea, alikuja kushtuka asubuhi baada ya saa yake kupiga kelele. Alipoangalia aligundua kuwa siku hiyo amechelewa kuamka, alikurupuka kiatanani na kuingia chooni. Alioga haraka na kutoka, alivaa nguo za kazi na kutoka bila hata kunywa chai. Aliingia kwenye gari na kuondoka, siku hiyo kamera za barabarani zilipiga picha za kutosha za gari hio kutokana na mwendo kasi. Alifika ofisini na kukuta wenzake wote wakimshangaa, "hebu acheni kunitolea mimacho" aliongea na kuingia katika ofisi yake.



    *************************************

    Daktari alotoka katika chumba hicho huku akionekana ni mwenye huruma "nambie mpenzi wangu anaendeleaje" alijikuta akimuita hivo wakati anauliza. "kijana nakuomba utulie kwanza kisha ndio nikueleze" Daktari aliongea huku akimuweka kitako Alex ambae aliokana kama kuchanganyikiwa. "pole kwanza kwa kilichowakuta, na kwa upande wa mgonjwa sisi tumejitahidi kadri ya uwezo wetu lakini uwezo wake wa kuishi ni mdogo sana". "unasemaje" Alex alipanik kusikia hivo, "tulia sasa, kwa nje anaonekana hakuumia sana lakini ameumia sana ndani, tumetoa vipande sita vidogo vidogo vya vyuma. Vilikuwa vimeganda katia moyo wake na kupelekea moyo kuoteza nguvu ya kusukuma damu hivo kupeleka sehemu nyingi katika mwili wake kukosa damu ya kutosha. Hiyo imepelekea kupata tatizo la ubongo na pia kibaya zaidi utapoteza watu wawili, tumemkuta na uja uzito siku chache. Mpaka sasa kiumbe kilichokuwepo tumboni mwake kimeshakufa. Na tunahitaji kauli yako ili tuziondoe mashine zinazomuweka hai, hakuna uwezekano wa kupona kutokana na kua karibu nusu na robo ya seli zake za ubongo zimeshakufa. Usifanye maamuzi ya haraka, fikiria kwa umakini mkubwa hili swala kwa sabau ni swala la kifo na uhai" Daktari alimaliza kuongea na kumpa pole Alex kisha akainuka na kuondoka. Machozi yalianza kumtoka japo alijitahidi kuyazuia, "kwa nini mimi kila siku" alijisemea moyoni. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliinuka na kuelekea katika chumba alichwekwa Rose na kuomba kumuona, manesi walimruhusu na kuingia. Alikwenda pembeni na kumuangalia mwanamke huyo ambae alionekana kupauka, alikaa pembeni na kuanza kuongea "hivi hata wewe unaondoka unaniacha peke yangu, kwanini lakini wote mumeamua kuondoka mapema kiasi hichi. Basi ungesubiri japo nikupe zawadi yako" Alex alizidi kulalamika, wakati anendelea kuongea alihisi kama mkono ukimgusa. Aliinua macho na kumuangalia Rose ambae alionekana kutabasamu. Akampa ishara amuondole kifaa kilichokuwa mdomo ili aongee na Alex alifanya hivo "mbona bado sijafa, unaweza kunipa hata saa hivi hiyo zawadi yangu" Rose aliongea japo kwa shida kidogo, Alex alitabasamu huku akitokwa na machozi kisha akamuonyesha ishara kuwa amsubiri anakuja. Alimrudishia kile kifaa cha kupumulia na kutoka kisha yeye akatoka na kuomba kuonana na daktari. Alielekezwa ofisi kwa daktari na kuongea nae,baada dakika tano alitoka na kutoka kabisa hospitali hapo. Nusu saa baadae alirudi na boxi kubwa na kuwakabidhi manesi, na kwa sababu walikuwa washaambiwa na mkuu wao jambo litakalo kwenda kufanyika. waliingia katika chumba alichokuwa amelazwa Rose na kufanya kama walivyoelekezwa. Alex aliekezwa katika chumba kingine na kubadilisha nguo. Alivaa suti moja safi sana na kutoka "maandalizi yamekamilika" Daktari aliongea, na kuongoza njia mpaka katika chumba alichokuwa Rose. Waliingia ndani na kumkuta padri akiwa tayari ameshafika. "karibu kijana" aliongea mzee huyo, "asante" Alex alijibu kukaa pembeni ya Rose. "unajua kama unachotaka kukifaya ni kitu kikubwa sana" aliongea tena mzee huyo. "naelewa" Alex alijibu, taratibu zilifanyika na muda wa ndoa ukafika. "bwana Alex Jr Jason umekubali kumchukua bi Rose kuwa mke wako halali wa ndoa kuanzia leo hadi mwisho wa uhai wako", "nimekubali" Alex alijibu bila kusita. "bi Rose umekubali kumchukuwa bwana Alex kuwa mume wako halali wa ndoa kuanzia leo hadi mwisho wa maisha yako", "nimekubali" Rose alijibu. Basi Padri aliwatangaza wawili hao kuwa mume na mke rasmi kuanzia muda huo. Wote waliokuwa wakishuhudia tikio hilo walikuwa wakitokwa na machozi kwa sababu walielewa kuwa mwanamke huyo asingeweza kutoboa hata masaa matatu yajayo. "Rose hii ndio zawadi yako" Alex alijibu na kumkumbatia" walipigwa pica kadhaa kama kumbukumbu za tukio hilo.

    Baada hapo Alex aliwaomba wote watoke ili abaki na mke wake, na wote wakatoka. Baada nusu saa Alex alitoka huku analia na kumwambia daktari kuwa tayari. Gakatari alielewa nini amemaanisha na kumsogolea Alex ambae alikuwa anashindwa kuyazuia machozi "pole kwa kumpoteza mtu unaempeda" aliongea huku akimpiga piga begani. Maiti ya Rose ilitolewa na kuplekwa kwa ajili ya maandalizi ya safari ya mwisho. Baada hapo taratibu za mazishi zilifanyika na waliohudhuria wengi walikuwa ni miongoni mwa wale wauguzi wa hospitali, baada ya kuzika watu wote walioondoka kasoro Alex alibakia pale pale na mvua ilianza kunyesha lakini wala hakujali hilo. "nisalimie Allen huko unakokwenda na usijali ombi nitalishughulikia kama ulivosema na nakuhakikishia hatobaki mtu hata kama itabidi nipambane na duni nzima nitafanya hivo" Aliongea kisha akondoka eneo hilo la makaburi na kurudi nyumbani kwake, nyumba hiyo aliiona kubwa sana.

    *************************************

    "Alex niahidi kuwa kifo changu hakitokwenda bila kulipwa", "nakuahid na wala usijali wote waliohusika na kifo chako na cha Allen watalipa kwa maisha yao, hatobakia hata mmoja". "nafurahi kusikia hivo" Rose aliongea huku akianza kukosa pumzi, "vipi unaumia" Alex aliuliza huku akimsogeza karibu, "hapana siumii kabisa, nitaumiaje wakati naondoka katika mikono ya mwanaume nnaempemda" Rose alijibu huku akimuangalia Alex usoni. Kadri muda ulivyokwenda ndivo hali yake ilivyozidi kuwa mbaya. "Alex muda wangu umefika" Rose aliongea huku akimgusa Alex usoni kwa mikono yake ambayo ilikuwa ishapoa tayari na haikupita hat sekunde tano ilianguka na hapo alitoa pumzi ya mwisho na kuaga dunia. Alex alilia kwa nguvu mpaka waliokuwepo nje ya chumba hicho walisikia na wao wakakijukuta wakitokwa na machozi lakini wangefanyaje na kazi ya Mungu haina makosa.

    "umetumwa na nani" Agent Darling alikomaa na swali hilo, "unadhani nitakwambia" alijibu kijana mmoja miongoni mwa vijana wa Shadow alikamtwa wakati wakijaribu kutoroka. "narudia kwa mara ya mwisho, ni nani aliekutuma" alifoka sasa, "kama nilivokwambia mwanzo, huwezi kuoata chochite kutoka kwangu ni bora uniue tu" aliibu kijana huyo. Ilibidi kwanza Agent Darling atoke katika chumba hicho maalum cha mahojiano. "huyu jamaa amepewa mafunzo ya kuhimili maumivu ya aina yoyote ile" aliongea Agent Darling huku akiwa amekunja sura. "kuna taarifa zozote kuhusu Alex" alimuuliza Joe ambae alikuwa akindela kutafuta kitu atika computer yake. "hapana mkuu sijapata chochote mpaka sasa" Alijibu Joe, "dah ni wiki nzima sasa huyu kiumbe hajapnekana atakuwa amejificha wapi" alijisemea Agent Darling. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande wa pili kulikuwa kuna kikao cha siri kinaendelea "usijali mkuu yule kijana hatosema chochote kwa sababu katiba yao inasema hatoweza kutaja jina la alie muajiri katika mazingira yoyote yale" Aliongea Jafar kumpoza Helen ambae alionekana kuchanganyikiwa. "sawa, lakini huyu Agent Darling ni tatizo kwa kweli" aliendelea kuongea "hasa akija akigundua kuwa babaake hakuuliwa na Alex yaani hapo ndio patakuwa hapatoshi". "na haitotokea siku akajua" alijibu Hansen ambae amerudi muda si mrefu kutoka mishen ya siri nchini Somalia, "una uhakika gani" aliuliza Martin. "ni kwa sababu wakati atakaopambana na Alex atakuwa anapambana kihisia zaidi na hatokuwa tayari kusikiliza chochote kutoka kwa hasimu wake huyo" alifafanua Hansen. "basi sawa lakini hakikisheni wote wawili wanakufa" aliongea Helen na kufunga kikao. Kila mmoja aliyawanyika na urudi anapofanya kazi zake.

    "eti nini" alifoka Shadow baada vijana wake wa taarifa kumfikishia taarifa kuwa hawajapata taarifa yoyote juu ya Alex. "mnajua amewauwa ndugu zetu wangapi" aliuliza na kukunja ndita usoni, "tunafahamu mkuu lakini tumesachi kila kona ya nchi hatujapata chochote" alijibu mmoja wao. "sawa na vipi kuhusu yule mwenzetu aliekamatwa" alihoji kijana mwengine, "nimeongea na mtu mmoja kati ya wale waliotupa kazi hii na amesema kuwa kesho atakuwa anapelekwa jela na hapo ndio utakuwa muda wetu wa kwenda kumuokoa" alijibu Shadow. "sawa mkuu" walijibu kwa pamoja na kutawanyika, "Alex hivi umejificha wapi mtoto wa mama" Shadow alijiemea moyoni na kukunja ngumi.

    Siku ya pili mapema asubuhi kijana wa Shadowa alikuwa anapelekwa gerezani baada kukataa kabisa kutoa ushirikiano. Alisindikizwa na gari sita za kikosi maalum, tatu zikiwa mbele na tatu zikiwa nyuma. Safari hiyo ilianza bila kujua kuwa Vijana wengine wa Shadow walikuwa wanaifatilia kwa nyuma, na kwa sababu gereza hilo lilikuwa nje mji kidogo waliusubiri msafara huo utoke nje ya mji ndio waanze mashambulizi. Lakini kabla hawajafanya chochote walipitwa na gari ndogo aina ya ferarri nyeusi kwa kasi kubwa sana. Haikuishia hapo tu iliupita mpak msafara huo na kutokomea mbele, baada mwendo wa sejunde kumi msafara ulisimama ghafla kutokana na njia kublokiwa na mti ulioanguka.



    Polisi walishuka kwa ajili ya kwenda kuondoa, walikuwa sita ghafla wote walianguka chini huku wakitoka damu shingoni baada visu vidogo kupenya. Mnyama Alex Jr alichomoka kuotoka kwenye kichaka na kuivamia gari ya mbele kabisa na kumuua dereva wake, aliendeleza mashambulizi hayo ya kinyama. Maana alikuwa hachagui ukipita mbele yake umekwisa, baada dakika tano kikosi kizima kilichokuwa kinamsindikiza kijana huyo kilikuwa chini. Alex alikwenda nyuma na kufungua gari hilo la wafungwa na kumshusha kijana huyo. Na hapo ndio vijana wa shadow walipojitokeza lakini walichokutana nacho wanajuwa wenyewe. Alex hakuwa yule wa kawaida, alikuwa amebadilika kabisa. Roho ya kikatili ndio iliotawala mwili wake hivyo alikuwa akiua tu bila kujali kabisa. Vijana wa Shadow walipoona moto umezidi kuwa mkali, walikimbia bila mafanikio yoyote yale ya kumuokoa mwenzao. Alex alimgonga kijana huyo shingoni na kumfanya amepoteze fahamu kabisa. Alimuingiza kwenye gari na kuondoka nae

    Taarifa za msafara kuvamiwa zilimfikia Agent Darling na kitengo kizima, bila kuchelewa walitoka na kuelekea eneo la tukio. "haya mauaji ni ya kikatili sana" aliongea mtu mmoja baada kumuangalia polisi mmoja ambae alitobolwa macho yote mawili. "mh huyu aliefanya mauaji haya ni katili kupita maelezo"aliongea mwengine, "huyu aliefanya mauaji haya ni simba mwenye jeraha" Agent Darling aliongea huku akizichunguza maiti hizo, "nadhani namfahamu aliefanya mauai haya" Joe aliongea baada kukagua mwili mmoja, "huyu ni Alex" alijibu hivo na kuwafanya wote wageuke na kumuangalia. "umejuaje" aliuliza mtu mmoja, "kila mtu huwa anaacha alama za mauaji yake na Alex huwa anafanya mauaji ya aina hii" aliongea hivo na kuonnyesha maiti moja, "maiti zote hizi zina matundu ya risasi zilizopita mbele na kutokea nyuma, Alex hakushambulii akiwa nyuma yako bali anakuuwa wakati unamuona kabisa" alindelea kufafanua.

    "kijana kiupole kabisa nambie ni wapi kwenye kambi yenu" Alex aliongea kiunyonge kabisa, "halafu nyinyi wote hamnielewi nimekwambia huwezi ambulia kitu kutoka kwangu" Alijibu kijana huyo kwa jeuri. "mara ya mwisho nambie kikundi chenu kipo wapi" Alex aliongea tena lakani wakati huu sauti yake ilikuwa na mikwaruzo. "mtu mzima hatishiwi nyau" aliongea kijana huyo na kucheka kwa dharau, "huwa ninapotaka kujua kitu basi huwa nakijua kwa gharama yoyote ile" Alex aliongea na kuinuka alipokuwa amekaa. Alimsogelea kijana huyo na kumuangalia usoni, kwa kweli alikuwa anatisha sana. Macho yake yalikuwa mekundu kama mtu aliekuwa amevuta bangi, alitoa kifaa kidogo kama kiwembe cha kukatia kucha. Alimshka mkono kwa nguvu na kumuuliza "utasema ama hutosema", "sise...." hajamalizia alipiga kelele baada Alex kumgoa kucha ya kidole gumba. "utasema au husemi", "sise.." hakumaliza tena akagolewa kucha ya kidole kingine. "unajua kama itabdi nikchune ngozi ndio nipate nnachokitaka nitafanya hivo" Alex aliongea kwa upole. "fanya unavotaka" Alijibu kijana huyo huku akilia kutokana na maumivu anayoyapata. Alex aliondoka na kurudi akiwa na pochi ndogo yenye vifaa kadhaa. Alibeba koleo na kumsogelea "we nambie tu wala sitakuuwa" Alex alimbembeleza, "nimesema hupati kitu kutoka kwangu" alijbu kijana huyo. Alex alimshika mdomo na kuufungua kwa nguvu kisha akakamata jino moja la chini kwa koleo na kuling'oa.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Masikini kijana wa watu alipiga kelele za maumivu lakini ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gita maana Alex wala hakushtuka kabisa na kelele hizo, alikamata jino la pili kwa koleo na kuling'oa. Kijana huyo alizidi kupiga kelele mpaka akapoteza fahamu. Alex aliinuka na kwenda kuchukua ndo ya maji ya baridi, alimwagia na kijana huyo akazinduka, "sema tu maana ndio wanza nimeanza" Alex aliongea huku akitoa kisu kidogo cha kukatia ngozi na nyama wakati wa opereshen. Yule kijana alicheka "sisemi" alijibu. "basi sawa" Alex aliongea na kumsogelea kisha akamshika mkono na kupitisha kisu, taratibu alianza kumchuna ngozi. Maumivu alioyapata hayakuelezeka "ntasema basi usiendelee nitasema" aliongea kijana huyo kwa nguvu baada kuzidiwa na maumivu. "mambo si hayo sasa, kama ungekubali mapema labda saa hivi tungekuwa mezani tunapata chakula" aliongea Alex na kuacha kumchuna ngozi. Yule kijana alianza kuongea kila bila hata kuficha chochote mpaka mwisho "nakuomba uniue tu" aliongea hivo baada kumaliza kuongea. "bado kufa muda wako ukifika utakufa tu" Alex alimjibu na kutoka katika chumba hicho. Alielekea chumba cha silha na kubeba za kutosha, alirudi kule alipomfunga yule kijana na kumfungua. Alimuingiza kwenye gari na safari ikaanza, kwa vile ulikuwa ni usiku hakukuwa na shida polisi.

    "oya sio Jimmy yule" mmoja kati ya vijana walikuwa doria aliuliza, "ndio mwenyewe yule" mwenzake alimjibu. Lakini alikuwa akiwafanyia ishara wasimsogelee, masikini wee walishindwa kumuelewa na walipomfikia aliripuka na kufa nao wote wawili. "Rules have change (sheria zimebadilika)" aliongea na Alex na kuzama kambini, alianza kuuwasha moto sio wa kitoto "mkuu Alex ametufuata huku huku" aliingia kijana mmoja na kutoa taarifa "anaonekana kama mtu aliechanganyikwa kabisa. Shadow aliinuka na kutoa bastola yake kisha akatoka nje, macho yalimtoka baada kukutana na maiti za vijana wake zikiwa zimatapakaa kila kona. Wakati akiwa katika mshangao huo alishtuliwa na kelele za kijana wake aliesimama pembeni yake baada kucheze risasi kadhaa za kifua. Na alipotoka kushambulia alicheze risasi ya mkono na kuingusha bastola chini. "kama ungekuwa hujanifata kwangu, yasingekufika haya lakini kwa sababu ya pesa na tamaa zako umeuvamia moto wa volacano" Aliongea alex huku akipandisha ngazi kueleke alipokuwa Shadow. "wewe hukujiuliza kwanini serekali imekupa kazi hii wakati yenyewe ina vikosi vingi tu vya kupambana na mimi" Alex aliongea tena kwa hasira kisha akaendelea "sasa subiri nikuonyeshe kwanini serekali yenyewe imeshindwa kunitia mikononi".

    Alex alikuwa amezama katika dibwi la kisasi, hakusikiliza chochote alimvaa Shadow kama mbogo na kuanza kumchakaza. Japo Shadow alikuwa ni mpambanaji mzuri lakini alijikuta katika wakati mgumu sana maana kila alipojaribu kujitetea alishindwa. Alex aliendelea kumpa kichapo mpaka Shadow akalegea kabisa, "muda wako wa kuga bado, kwanza huwezi kufa kirahisi rahisi hivo. Umemuona huyu kwenye hii picha ni mke wangu na wewe ndio sababu ya kumpoteza pamoja na mwanangu aliekuwa tumboni kwake" Alex aliongea huku akimuonyesha picha ya Rose katika siku zake za mwisho. Shadow alikuwa ametulia kama maji mtungini maana alielewa hasira ya Alex haijaisha bado maana macho yake tu yalitosha kuongea. Alex alianza kumburuza Shadow mpaka nje na kumuingiza kwenye gari, kisha alimgonga shingoni na kumfanya alale fofofo. Alirudi ndani ya kambi hiyo na uanza kutega mabomu na kutoka aliondoa kwa gari kwa mwendo kasi sana na baada ya dakika tano kambi nzima iliripuka na kuteketea kabisa. Siku ya pili taarifa ya kuripuliwa kambi maarufu ya majambazi sugu ilienea kama moto wa gesi huku watu wakionekana kufurahishwa na tukio hilo.

    Helicopter ya binafsi ilitua juu kabisa ya jengo hilo la kitengo maalum cha upelelezi, General David alitoka na kuelekea mlangoni ambapo watu wengi walikuwa wakimsubiri. "karibu mkuu" Helen aliongea "asante, kila kitu kipo tayari?" alishukuru na kuuliza, "vijana wote na wawakilishi pamoja na wakuu wa nchi mbali mbali wameshafika" Helen alijibu huku akiongoza njia kuelekea katika chumba maalum ambacho ndipo mkutano huo wa siri ulipokuwa unafanyika. Watu wote waliokuwemo katika chumba hicho walisimama baada ya General David kuingia, aliwaangalia wote na kutabasamu isha akanyoosha mkono juu kama ishara ya kutoa salamu. Wote waliinamisha vichwa chini na kujibu salamu hio kwa kukunja ngumi ya mkono wa kulia na kuweka kwenye moyo pande wa kushoto. "Yatukuke mapinduzi" kwa pamoja bila kupishana walisema. General David alitikisha kichwa na kuelekea kwenye kiti chake na kufubgua kikao rasmi. "mkuu kambi zote zipo tayari na tunasubiria amri yako tu" aliongea mtu mmoja mwenye lafudhi ya kichina, "vizuri sana" General David aliitika kwa kutabasamu. "kwa jumla tuna kambi Mia moja za baharini, sabiini za jangwani na hamsini za mwituni na kila kambi ina wanajeshi Mia moja ambao kwa ujumla wao tuna wanajeshi maalum wa CODE X elfu ishirini na mbili" aliendelea kufafanua mtu huyo. Wote walipiga makofi kuashiria wamefurahishwa na idadi ya wanajeshi hao wenye uwezo mara dufu kuliko wanajeshi wa kawaida. "idadi hiyo inatosha kufanya mapinduzi, maana ikiwa mwanajeshi mmoja anauwezo wa kupambana na makomando watano peke yake, jee hao wote inakuaje" aliongea mtu mwengine na wote wakacheka. Wakati kikao kinaendelea ndani Agent Darling ndie alikabidhiwa jukumu la kuimarisha ulinzi maana tokea Alex ajitokeze kwa sura mpya watu wote waliiniwa na wasiwasi na kupelekea hata ulinzi kuimarishwa katika eneo hilo. "vipi hujahisi kitu chochote kisicho kawaida" Agent Darling alimuuliza mmoja kati ya watunguaji (sniper) kupitia kifaa cha mawasiliano. "negative" alijibu sniper huyo.



    Agent Darling alienedelea kuwauluza wote waliokuwa wamejificha katika majengo hayo wakiwa wamejiandaa vya kutosha. "habari yako Allen Jr" alishtuka aliposikia sauti hiyo maana aliitabua kama ilikuwa ni ya Alex, "we mshenzi uko wapi" alifoka kwa hasira Agent Darling.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ah mbona hivo sasa, mimi ninachokitaka ni uondoe vijana wako hao watunguaji kabla sijaanza kuwapeleka kuzimu mmoja baada ya mwengine kwa sababu sina uhasama nao" Alex aliongea na suati yake ilitosha kumueleza Aent Darling kuwa alikuwa hatanii hata kidogo. "kama kweli wewe mwanume uanejiamini jitokeze" Agent Darling alimjaribu, "yaani leo usijali, tutacheza mpaka utachoka lakini sitaki mtu asie na hatia afe kwa kumlinda mkosaji" alijibu Alex taratibu na kumfanya Agent Darling aingiwe na wasiwasi. "vikosi vyote kaeni tayari" alitoa amri hiyo na vikosi vyote vikajipanga, "naona umeamua kuwatoa kafara binaadamu wenzako" Alex aliongea na kukata mawasiliano na ghafla ikasikika milio sita ya bastola, Agent Darling alijaribu kuwasiliana na watunguaji wake lakini wapi alikuwa hajibiwi kitu na hiyo ilitosa kumueleza kuwa tayari walishaaga dunia. Kwa mbali aliona gari nyeusi ikija upande wake, "shambulieni hiyo gari" alito amri na bila kusita wanajeshi wakaanza kushambulia lakini gari hiyo ilikuwa ni bullet proof hivyo hakupenya hata risasi moja. Agent Darling aliingia ndani na kutoa taarifa kuwa Alex ameshafika, ile gari ilipofika karibu na wanajeshi iliripuka na wengi walijeruhiwa.Hapo ndio Alex akajitokeza akiwa katika mavazi yake ya kikomando, alianza mashambulizi ya kasi huku kila aliepita mbele yake alikwenda na maji. Alex Jr aliendelea na kazi yake ya mauaji bila kujali kuwa aliokuwa anapambana nao walikuwa wakitekeleza majukumu yao tu. "mkuu kuna tatizo unatakiwa kuondoka" Aliingia mlinzi wa General David na kutoa taarifa "tatizo gani wewe huoni kama tupo kati kati ya kikao" alifoka General David. "mkuu niamini nusu na robo ya vikosi vinavyohakikisha usalama vimeshateketea katika mikono ya Alex. Alipolitaja jina hilo tu ukumbu mzima ulizuka na tafrani. "nini, Helen nieleze kwa kina" aliongea General David, "nu...ku...ku..eleze nini mkuu, wakati hali ndio ushaiona hivi" Helen aliongea kwa kigugumizi cha ghafla. Wakati wakiendelea na majibizano Alex tayari alikuwa kashaingia mjengoni tena bila hata kuguswa huko nje, alianza kuwachakaza waliokuwemo ndani sasa. Yaani Alex alikuwa kavurugwa kisawasawa maana alikuwa akitowa dozi bila kipimo maalum.

    "Finally, tumekutana uso uso kwa uso tena" Aliongea Agent Darling baada kuonana ana kwa ana na Alex, "nenda nyumbani ukanyonye leo ni siku mbaya sana" Alex aliogea huku akivua miwani yake nyeusi iliokuwa umeficha macho mekundu mithili ya mtu alievuta bangi. "hahaha...eti nini" Agent Darling aliongea kwa kejeli, "nasema nenda nyumbani ukanywe maziwa, siku ya leo hutakaa uisahau maishani mwako hivyo ni bora tu ufanye nnavyo kwambia" Alex alifoka sasa alipoona hawaelewani. "itabidi unipeleke" Agent Darling aliongea na kwa kasi ya ajabu alifyetuka alipokuwa na kumvaa Alex. Bila mategemeo alirudishwa alipotoka baada kutandikwa ngumi nzito ya kifua iliomfanya akohoe kidogo. "hivi wewe hunielewi nnapo kwambi siku ya leo ni mbaya sana" Alex alifoka tena na safari hii hakusimama alimfata kwa nguvu na kumtandika makonde sita ya nguvu ya kifua na uso mpaka Agent Darling akaanguka na kupoteza fahamu. "vizuri, watoto wazuri huwa wanalala mapema ili kuepuka kuingizwa katika ugomvi wa wazazi wao" Alex aliongea na kuondoka eneo hilo, aliingia kwenye lifti na kuelekea ghorofa ya juu kabisa ambapo ndio kikao kilikuwa kinafanyika. General David alionekana kuwa mbishi kuondoka, "mkuu huyu mtu si wa kawaida hebu angalia anavyopiga tena hatumii hata bastola lakini ngumu yake moja tu inatosha kuwa risasi tena ya Shotgun" alizidi kuongea mlinzi wake, "sasa nitamkimbia mpaka lini" General David aliongea. "mkuu tufanye leo humkimbii bali unakwenda kujipanga upya ili kukabiliana nae" alisisitiza mlizi. Helen na baadhi ya viongozi na wawakilishi wengine walitoka wakiwa na bastola mkononi. "shoot on site" Helen alitoa maelekezohayo akimaanisha kuwa yoyote atakae muona Alex amuue. "sawa" wote walijibu na kujibanza wakisubiri lifti ifunguke lakini ilipofunguka kulikuwa hakuna mtu ndani. "habari yako Helen, umenimiss eeh" Helen alisikia sauti hiyo ikitokea nyuma yake na alipogeuka alikutana na mdomo wa bastola ndogo na bila kuchelewa Alex aliyetua risasi na kumwaga ubongo. Wale wengine wote walivyoona vile walianza kupoteana huku kila mmoja akitafua njia ya kutorokea. Alex wala hakuwajali kwa sababu yeye aliekuwa anamtaka ni General David, aliingia katika chumba cha mikutano lakini kwa mbali aliona mlango ukifungwa hakufikiria mara mbili alianza kukimbia kuelekea ulipo mlango huo. General David na mlinzi wake walikuwa wanakaribia juu, "washa helicopter" mlinzi aliongea kupitia radio call. Walifika juu huku mlinzi akiwa nyuma akiimarisha ulinzi, lakini hatua chache kabla ya kufika kwenye helicopter mlinzi alianguka chini na kupoteza maisha baada kupigwa risasi ya kifua. "simama na geuka taratibu" Alex aliongea na General David alisimama na kuanza kugeuka huku akichomoa bastola yake, lakini kabla hajashambulia alipigwa risasi ya mkono na kuingusha bastola. "Alex, Alex, Alex kwanini tusikae kitako tukayamaliza" General David aliongea huku akiugulia maumivu mkononi, "hivi wewe kitu gani ulikikosa mpaka ukaamua kuingamiza familia yangu" Alex aliuliza kwa hasira. "unajua Alex sisi ni binaadamu na kila binaadamu huwa amepangiwa siku zake za kuishi duniani, hivyo basi iliandikwa na Mungu kuwa familia yako yote ife kwa mikono yangu na wewe ubakie. Sasa mimi nina kosa gani kutekeleza kilichopangwa na Mungu" aliongea General David. "yaanu huoni hata aibu kumsingizia Mungu upuuzi wako" aliongea Alex na kubadilisha magazine ya bastola yake kisha akakoki. Wakati anafanya hivo, alisikia mlio na ghafla kitu cha moto kilipenya mgongoni. "ukithubutu kufanya chochote nakumaliza" Agent Darling aliongea, Alex aligeuka kwa nguvu na kumnyooshea bastola lakini Agent Darling alifyetua tena risasi iliopenya kifuani mwa Alex na kumfanya apige magoti. General David aliona huo ndio muda muafaka wa kutoroka, alikimbia na kungia kwenye helicopter na rubani akaiondoa.

    Alex alijitahidi kusimama huku akijishika sehemu alipigwa risasi na Agent Darling, kutokana na hasira alizokuwa nazo Agent darling alifyetua risasi nyingine na kumpata Alex kifuani tena. "imebakia moja tu ambayo ntaisukuma kichwani mwako na kukuvuruga hicho kichwa" aliongea Agent Darling huku machozi yakimtoka. "kwanini umemuaa babaangu" aliuliza, "ama kweli kama baba kama mwana" Alex aliongea huku akikohoa na kutema damu. "babaako alikuwa ni mtu shujaa sana sijui kwanini mambo yalikwenda vile" Alex aliongea na kumuangalia Agent darling, "hivi unadhani nilishindwa kukuua mwanzo, hapana nilikuwa na asilimia mia moja ya kukuuwa lakini sikufanya vile kwa sababu nilidhani ni mwerevu sana kuujua ukweli wa mchezo huu ambao umechezewa bila kujitambua. Kama uliwahi kusikia DIRTY GAME basi ujue wewe umekuwa jokeri na kicheko cha kila mtu" Alex alizidi kuongea maneno kunya bila kujali kuwa anaeongea nae ni mtu ambae yuko hapo kumuua. "acha kuongea upuuzi, sali sala yako ya mwisho kabla hujafa" alifoka Agent Darling, "hivi kweli maiti nakufa tena, maana mimi nilishakufa siku aliokufa mke wangu kipenzi pamoja na mtoto wangu aliekuwa tumboni. Kuanzia siku hiyo nilipoteza kabisa dira ya maisha na kama kuniuwa utarudhika na kuweza kumuona babaako siki ya mwisho basi fanya hivo maana utakuwa umenisaidia na mimi kwenda kumuona mke wangu na mwanangu mbinguni" Alex aliongea maneno hayo na kuiangusha bastola yake chini kisha akainua mikono na kuangalia juu. "muda kidogo tu nitaungana na wewe mpenzi wangu na mwanangu ili nitimize ombi la mwisho la Allen James la kuwa na familia yangu" aliongea tena kufunga macho. Mlio wa risasi ulisikika "PAA".

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    MWISHO.





0 comments:

Post a Comment

Blog