Search This Blog

Friday, 20 May 2022

C.O.D.EX. 1 - 1

 






    IMEANDIKWA NA : TARIQ HAJI



    ************************************************************************************





    Simulizi : C.O.D.EX. 1

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Allen James ni jina langu, ni dereva wa taxi katika jiji moja maarufu sana duniani Los Angels maarufu kama LA. Kama kawaida mapema vijana tunaingia kazini kutafuta mapeni. Nikiwa nasubiria abiria ghafla aliingia mtu na kunambia niondoe gari. Nami nikifanya hivyo lakini nlipoangalia nyuma niligundua jamaa alikuwa akitoka damu na nlipojaribu kumwambia nimpeleke hospital alikataa na kunambia nimpeleke sehemu ambayo atakua salama. Nilijaribu kufikiria ni sehemu gani hiyo jibu lililokuja kichwani mwangu ilikuwa ni nyumbani kwangu.

    Bila kuchelewa niliekea nnapo ishi, nilijaribu kumpatia huduma ya kwanza lakini alikuwa tayari kashapoteza damu nyingi sana hivyo uwezekano wa kuishi ulikuwa mdogo sana. Mwisho kabisa aliniita na kuninong'oneza CODE X, kisha akanipa kitu kama kitambulisho na picha, akanambia nisimtajie mtu yeyote neno lile hadi nitakapomuona mtu alienipa kwenye picha kisha hapo nae akaaga dunia. Nilibakia mdomo wazi nisijue nini cha kufanya kabisa.

    Wakati nikiendelea kuwaza hivyo ghafla nikaskia gari zikifunga breki nje ya nyumba yangu. Nilipoangalia kupitia dirisha sikuamini macho yangu baada kuona watu waliovalia suti nyeusi huku wakiwa na silaha nzito. Mshale wa hatari uligonga kichwani mwangu na bila kufikiria nikajikuta nimenyanyuka na kuelekea ulipo mwili wa yule mtu. Nilichomoa bastola yake kwa ajili ya kujihami na haraka haraka nikapitia mlango wa nyuma.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hata sijui ni kitu gani kilinipata lakini akili yangu iliniambia nielekee moja kwa moja New York City. Na bila kuchelewa niliingia kwenye gari yangu na safari ikaanza. Kwa bahati mbaya sana mmoja wao aliiona gari yangu na kuwashtua wenzake. Kivumbi kakaanza hapo, nilijitahidi kuwakimbia lakini wapi gari zao aina AUDI zilikuwa na uwezo mkubwa sana, hivyo walinifikia na kuanza kunigonga. Nlipoona mambo yanazidi kuwa magumu niliamua kuwapatisha ajali tu, nilifanikiw kwa gari kadhaa lakini bila mategemeo nilipgwa mzinga na gari yangu ikapinduka.

    Niliwahi kutoka kabla hawajanifikia na nikaanza kujibizana nao kwa risasi. Mwenyewe nilikuwa najishangaa maana sijawahi kuenda hata polisi lakini kwa jinsi nilivyokuwa nashambuliana nao ni kama nilikuwa nimebobea kwenye utumiaji wa silaha. Nilipohakikisha nimewamaliza nilichukua gari yao moja na safari ya kuekea New York ikaanza.

    Safari ya kuelekea New York ikaanza, huku njia nzima nlikuwa nawaza uwezo ule wa kupigana nimetoa wapi maana tokea nipate fahamu zangu sikuwahi kujifunza ngumi. Lakini niliona bora niachane na mawazo hayo. Usiku ulinikuta njiani hivyo nikaona bora nitafute Motel nilale. Siku ya pili mapema niliendelea na safari yangu yenye sintofahamu nyingi, niliwasili New York mnamo saa nne na kidogo. Niliacha gari sehemu ya maegesho na kuanza kutembea kwa miguu lakini kwa umakini sana. Nilitembea mpaka kwenye hotel moja hivi na kuingia, maajabu nilioyakuta mapokezi yalizidi kunichanganya maana yule mschana aliekuwepo pale alinichamgamkia utasema labda tunajuana kwa muda mrefu sana. Bila hata kuongea kitu alinipa funguo ya chumba. Nilimshukuru na kuondoka huku moyoni nikijaimbia lazima nitafute muda niongee nae kwani anaonekana kujua mengi kuhusu mimi.

    Nilifika chumbani kwangu kitu cha kwanza niliingia bafuni nikaoga maana uchovu ulikuwa ukinitafuna. Nilirudi ndani na kufungua kabati, macho yangu yalikutana na suti za bei mbaya tu. Nilichagua moja na kuvaa baada kuona nishapendeza nilikaa kitandani nikifiria mambo mengi yaliotokea siku ya nyuma. Wakati nikiwa mbali kwenye mawazo ghafla niliskia simu ikiita, niliangaza wapi ilipo na kwenda kuichukua. Nilipoipokea ukaingia ujumbe uliosema "kaa tayari ukisubiria maelekezo mengine". Ukaingia ujumbe mwengine "katika kabati kuna begi, litoe na fuata maelekezo utakayoyakuta".

    Nilifungua kabati na kutoa begi nikalifungua, nilikuta picha ya mzee mmoja nyuma ikiwa na ujumbe "chukua sniper iliokuwepo humu na uhakikishe huyu mtu anakwenda kuzimu". Niliiangalia ile sniper nikajikuta natabasamu, nilibeba lile begi na kuchukua ile simu kisha nikatoka. Nilipofika nje uliingia ujumbe mwengine "huyo mtu anapatiakana mji wa Alexandria na kazi ikamilike ndani ya masaa kumi na sita, chukua hiyo gari nyekundu mbele yako". Niliingia kwenye ile gari na safari ya kuelekea Alexandria ikaanza. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipofika tu uliingia ujumbe ulionielekeza alipo, nilifika sehemu ya tukio na kupanda katika jengo moja refu kidogo lilikuwepo pembeni ya jumba alilokuepo huyo mlengwa. Nilipofika juu nilitoa sniper na kuiunga baada kukamilisha zoezi hilo nilijweka sehemu nzuri na kuanza kumtunga. Kwa msaada darubini ya sniper nilimuona vizuri na hapo nikafyetua risasi ilioingia kichwani na kusambaratisha ubongo. Sikuwa na haja ya kuichukua ile sniper, nilitoa bomu dogo na kulitega pale kisha nikaondoka. Iliripuka na Ushahidi ukapotea, nilipofika tu chini nilikaribishwa na risasi kadhaa hapo nikajuwa nimeshtukiwa.

    Nilitoa bastola mbili ndogo na kuanza kujibu mashambulizi huku nikikoswa na risasi kadhaa. Kutoka kwa mlango huo ilikuwa haiwezekani nilirudi ndani na kuanza kutafuta mbinu za kutoka humo maana hata risasi zilikuwa zimeniishia. Mara walianza kuingia ndani,nilijibanza sehemu nikajisemea atakaepita kwanza ni halali yangu. Mara mmoja akapita nilimvuta ndani na kumvunja shingo, nikachukua bastola yake na kukimbia. Wakati nikiwa katika mapambano hayo uliingia ujumbe mwengine ukinitaka niondoke nchini marekani nielekee shanghai china. Nilifanikiwa kutoka nje na kuelekea ilipogari yangu na kutokomea, nilifanikiwa kuwatoroka. Moja kwa moja nilielekea uwanja wa ndege na kukata tiket ya ndege inayofuata kuelekea zangu Shanghai China. Muda wa kupanda ulifika na safari ya Shanghai ilianza na kwa jinsi nilivyokuwa nimechoka usungizi ulinichukua, usingizi uliombatana na ndoto mbaya za mateso ya hali ya juu sana.

    *****

    "jina lako nani" aliendelea kuniuliza uku akinipiga mgumi kadhaa za tumbo "Allen James" nilijibu lakini bado hakukubali. Mara nikamsikia akisema leteni mashine ya shot, haukupita muda ililetwa mashine hiyo. Aliiwasha na kutaka kunipiga shoti, ghafla nilishtuka kutoka usingizini huku jasho likinitoka, nilimuita muhudumu nikamwambia anipe kinywaji cha baridi baada hapo nilitulia nikiwaza ile ndoto. Kwa sababu ilikuwa ni ndoto tu nikaona bora niipoteze.

    Ndege iligusa ardhi ya Shanghai, nilishuka na kuelekea nje na nlipofika tu nje uliingia ujumbe "kuna macedes benz nyeupe kwenye maegesho, chukua hiyo gari na fuata maelekezo utakayoyakuta" niliangaza huku na huko mpaka nilipoiona na kuifuata. Niliingia kwenye gari hiyo, nilipowasha tu nikaskia sauti ya kike "karibu Shanghai Allen, fuata raman katika computer ya gari hii kufika katika hoteli uliopangiwa" baada hapo ile computer iliionyesha ramani na bila kupoteza muda nilianza safari ya kuelekea katika hiyo hoteli, ilinichukua dakika kumi kufika huko hotelini. Nilifika mapokezi nikataja jina, nikipewa funguo na kuelekezwa kilipokuwa chumba changu. Nilipofika chumbani niliingia chooni nikajimwagia maji na kubadilisha nguo. Wakati nikiwa nimepumzika ukaingia ujumbe "kwenye meza kuna picha na kisu, muue huyo mtu kwenye picha" nilsogea mezani na kuichukua picha. Dah macho yalinitoka kwasababu mlengwa wakati huu ni mwanamke. Nikajisemea moyono huyu mschana anabahati mbaya kweli na uzuri wote huu alokuwa nao leo anakwenda kuzimu. Nilishtuka kidogo na kujishangaa roho ile ya kikatili nimeitoa wapi. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilisubiri hadi usiku nikatoka kuelekea alipo huyo mschana na kwa msaada computer sikupata tabu sana kuijua nyumba yake. Basi nilifika lakini yeye hakuwepo hivyo niliingia ndani na kumsubiria, nusu saa baadae mlango ulifunguliwa, nilijibanza ukutani ili asije akaniona. "umekuja kuniua" aliongea yule mwanamke, nilijikuta nikimuuliza amejuaje kama nipo alkanijibu kuwa mambo yote ninayo yafanya yeye anajua. Nikamuuliza sasa alikuwa anajua kwanini aliamua kurudi, akaniambia kuwa anataka kunisaidia tu ili nitoke kwenye kifungo hicho cha utumwa.

    Kidogo nilipowa baada kumsikia anataka kunisaidia maana hata mimi Mwenyewe nilikuwa sijijui tena. Aliniambia kuna kifaa nimewekewa kinachonindesha katika kufanya maamuzi na ndio maana kuuwa naona ni jambo sahihi kwangu. Nilimuuliza kama anaweza kukitoa akanijibu ndio lakini si wakati huo kwa sababu muda si mrefu tutavamiwa. Na kweli hatujakaa sawa tukaskia gari zikifunga breki. Aliniambia nimfate nami nikafanya hivyo, tulifanikiwa kutoka nje bila tabu na kwa kutumia usafiri wake tuliweza kuwaponyoka maadui zetu.

    Kwa sababu yeye alikuwa mwenyeji nilimuachia awe kiongozi. Aliendesha gari kwa muda wa saa nzima, tulitoka nje ya mji wa Shanghai. Tulifika katika nyumba moja, hapo ndio ikawa mwisho wa safari yetu. Tulingia ndani, akasema tutapumzika usiku huo na siku itakayo fuata atanitoa hicho kitu.

    Mapema siku iliyofuata alinifanyia operesheni ndogo na kukitoa. Alipokitoa tu nikapoteza fahamu. Nilikuja kushtuka nimo ndani ya chumba chenye kiza sana nilipojaribu kuinuka nilishindwa na nilipoangalia vizuri mikono yangu pamoja na miguu ilikuwa imefumgwa na ghafla taa zikawaka.

    Dah nilijiona bwege kweli kudanganyika kirahisi kiasi kile, kwa mbali niliona watu wakija na nilipoangaza vizuri miongoni mwao ni yule mwanamke. Alipofika akaniuliza kama nimefurahia usingizi mzito, "kwani nimelala kwa muda gani?" nilimuuliza kwa shauku, akanijibu kuwa nimelala kwa muda wa masaa 72 kwa maneno mwengine nimelala kwa siku tatu. Baada maongezi hayo aliingia mtu wa makamo hivi, kwa kumkadiria ni kati ya miaka sabini au sabini na tano.

    "kijana mimi sitak tusumbuwane" aliongea, "tusisumbuwane kivipi" ,nilihoji kwa sauti iliojaa hasira. Akanambia kuwa anahitaji password ya kufungua computer yenye siri za Project CODE X. Nikamwambia kuwa mimi sifahamu chochote kuhusu jambo analoliongea, ghafla nilishtukia konde zito la tumbo lililonifanya nikohoe damu. Akarudia tena kuniambia jambo lile lile na mimi jibu langu lilikuwa lile kuwa sifaamu kitu chichite anachokiongea.

    "inavoonekana kupata ukweli nitahitaji nitumie nguvu kidogo" aliongea yule mzee na kutoa ishara. Hapo waliingia jamaa watatu miraba minne na walionekana wapo kikazi zaidi. "Pigeni mpaka atakapo tupa kodi" aliongea yule mzee na kutoka. Basi wale washkaji walinisogelea na kunipa kipondo, nilijiapiza nikifanikiwa kutoka hai basi kila mmoja ataambulia kifo kibaya sana ambacho hajawahi kufikiria. Sikumbuki hata muda gani waliacha kunipiga lakini nilikuja kushtuka nimefungiwa chumbani. Kosa walilofanya ni kuamini kuwa mlango utanizuia kutoka na ndio maana hawakunifunga kama mwanzo.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikagua mule chumbani nikaona kuna kamera, nikajisemea subiri niwaonyeshe mwanaume wa kweli anavofanya maamuzi magumu. Haraka haraka nilichukua shuka na kulichana, nilifanya nikijuwa kabisa watakuwa wananiona. Kwa ufahamu niliokuwa nao binadamu anaweza kubana pumzi kwa dakika tano bila kupata madhara yoyote yale. Kwa kasi ya ajabu nililifunga lileshuka kwenye dari na kujinyonga, kama hesabu zangu zilivokwenda. Walinzi walikuja mbio kuniokoa, nilitulia vilevile mpaka waliponivua kile kitanzi ndipo nilipoamuwa kuwatenda.

    Nilimpiga ngumi ya koromeo yule aliekuwa ameinama na kulivunja na kabla yule mwengine hajafkiria nini cha kufanya nilimpiga teke zito kwenye goti na kumfanya aanguke kama mzigo. Hapo nilikimbilia shingo na kuivunja, kisha nikachukua redio call moja pamoja na bastola zao na kutoka kwenye chumba hicho.

    Tayaria wengine walishashituka na kubonyeza alarm, wala sikujali hilo nilitoka humo chumbani na kitu cha kwanza kufanya ni kuzipasua kamera ili tucheze kombolela bila wizi. Nilfanya hivo kila nilipokutana na kamera huku nikiwapunguza mmoja mmoja, wakati nikiendelea na zoezi hilo si nikakutana na mmoja kati ya wale washkaji walonipa kipigo cha mbwa mwizi. Ila alikuwa bastola basi nikatumia tu akili ya kisungura na kumwabia kuwa wanaume hawaneshani kwa silaha kama vipi tuweke moto chini twende mtu kavu tu, nae akakubali bila kinyongo. Nikajisemea unadhani kuwa utaokota hata moja, basi jamaa akaja kichwa kichwa nilimkwepa na kumtegeshea mguu, basi nalo likaanguka kama ngurue alopigwa gongo la kichwa.

    Wakati wa kuinuka si ainuke hovyo, hapo sikuchelewa nilimpiga ngumi nzito ya uso na kumfanya aweweseke kama mlevi na kabla hajakaa sawa nilimsindikiza na teke la kifua na kumpeleka chini. Tayari mchuzi ulikuwa ushaachemka na kumwagika. Nikamwambia nitamvunja kiungo kimoja kimoja mpaka vimalizike mwili mzima, aliinuka na kurusha ngumi wala sikuikwepa bali niliidaka na kuviminya vidole katika shemu inayojulikana kama pressure point na kuvivunja. Sikumuwacha augulie vizuri, nilimvuta na kumkandamiza teke kwenye goti na kulivunja, niliendelea na shughuli hio mpaka nilipohaikisha hakuna cha kuvunja tena zaidi ya shingo. Nikaona haina haja ya kumvunja shingo kwani angekufa mapema, nilichokifanya nilitafuta msumari na kusindika kwenye chemba ya kifua kisha nikamuacha na kuendelea na safari. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifanikiwa kuwapunguza kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa nilijuwa kila kitu kilichoendelea kupitia redio call niliochokuwa. Nilifanikiwa kufika mpaka katika mlango uloandikwa EXIT, niliufunguwa kwa furaha lakini nilipigwa na bumbuwazi na pia nilichoka na kukosa la kuongea wala kufanya nikabaki nashangaa tu.

    Nilihisi kuishiwa nguvu maana sikutegemea kama nitakutana hali hiyo kabisa maana baada ya kufungua mlango niligundua kuwa nipo jangwani. Nikajisemea ina maana juhudi zangu za kujiokoa ndio ziishie hapa, hata haiwezekani lazima nitafute njia ya kutoroka tu katika jangwa hili. Nilijua ikiwa nitaamua kuingia jangwani basi kuna mawili aidha ningekufa au ningepona lakini la asilimia kubwa ilikuwa ni kufa maana hata hilo jangwa lenyewe nilikua sijui ni la wapi.

    Wakati nikiendelea kuwaza nifanye nini lilinijia wazo la kuirudia ile simu yangu labda yule mtu aliekuwa ananitumia ujumbe angenisaidia kutoroka. Lakini pia niliwaza eti nirudi ndani kisa simu, dah lakini kuna wakati inabidi mtu ufanye maamuzi magumu sana.

    Basi mwisho niliamua kurudi ndani, huku nikiwaza njia ya kuipata simu hiyo ambayo hata sikujua iko wapi. Lakini nikaona njia pekee ya kujua ilipo ni kujikamatisha kwa sababu katika wakati kama huo hata maadui zangu wakinikamata watanipeleka kwa mkubwa wao. Basi nilirudi kizembembe makusudi, na mpango wangu ulifanikiwa. Walinikamata na kunipeleka kwa mkubwa wao, na kwa kweli bahati ilikuwa kwangu maana vitu vyangu vyote ikiwemo ile simu vilikuwa katika meza ile aliokaa yule kiongozi wao. Alitabasamu kwa kejeli baada ya kuniona, kisha akasema kuwa ndege mjanja hunaswa na tundu bovu. "hivi ulidhani utaweza kutoroka humu" aliuliza kwa hasira, wala sikumjibu kitu maana akili yangu yote ilikuwa ni kwenye ile simu tu. Nilikuwa nikipiga hesabu nitaipaje na kuwatoroka.

    Kwa hesabu za haraka niligundua kuwa walikuwepo watu kama kumi ndani ya chumba kile, kwa kujiamini nilisimama kwa kasi ya hali ya juu na kujirusha kwenye ile meza na niakfanikiwa kuichukua simu pamoja funguo mbili za gari na passport yangu. Na pia nilifanikiwa kuwapeleka chini watu watatu na kufanikiwa kufika mlangoni lakini kabla sijatoka nilihisi kitu cha moto kikipenya kwenye mguu wangu wa kulia. Lakini kama unavyojua wakati wa hatari binadamu anaweza kufanya jambo lolote lile, sikuyajali maumivu niliendelea kukimbia mpaka nje na kutoa zile funguo kisha nikabonyeza funguo moja, kwa mbali nikaskia gari ikilia. Nilielekea kule ilipo na kuingia kisha safari ikaanza nikiwa hata sijui naelekea wapi maana sikuweza kuona hata mji. Wakati huo naendesha nilitoa ile simu na kuiwasha, na papo hapo ukaingia ujumbe uliosema ni bonyeze nyota kwenye simu kisha nipige. Nilifanya hivyo kisha nikapiga, ilipokea upande wa pili na kunambia kuwa nisiiache hewani kwani walikuwa wanataka kuitrack ili wajue niko wapi. Dakika mbili baadae computer iliokuwepo kwenye gari hiyo iliwaka na kuingia ujmbe, nilipoufungua ilikuwa ni ramani.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kisha ukaingia ujumbe kwenye simu ukinambia kuwa nipo katika jangwa moja lilokuwepo nchini Afghanisatan, na kutoka nilipo mpaka kwenye makazi ya watu ni kama kilometa 300. Dah ukizingatia na jeraha la mguu nililopata nilijua uwezo wa kutoboa ni mdogo sana, kwasababu nilishapoteza damu nyingi sana. Nilisimamisha gari baada kukumbuka kuwa gari nnayo endesha ni Jeep ya kijeshi na mara nyingi huwa zina kuwa kile kibox cha huduma ya kwanza.

    Basi nilishuka na kuikagua na kwa bahati nzuri nilikiona, wala sikutaka kuitoa risasi bai nilichoma sindano ya ganzi ili kupunguza maumivi na kupaka dawa ya kuzuia kutoka damu baada ya hapo nilijifunga bendeg na kurudi siti ya dereva na safari ikaendelea. Nilihakikisha nakwenda kasi kadri gari hyo ilivokubali, na kweli gari hizo maalum kwa kutembelea jangwani na misituni basi haikufanya ajizi kila nilikanyaga mafuta iliitika na kutimua vumbi kiasi kwamba mpaka nikahisi kama nikikanyaga kijwe au kigogo basi itakuwa ndio mwisho wa safari yamgu.

    Masaa mawili baadae nilifika mjini na moja kwa moja nilikwenda hospitali iliokuwa karibu kwa ajili ya matibabu zaidi. Walifanikiwa kuitoa risasi na kunambia kuwa haikupiga katika mfupa zilizoathirika zilikuwa ni nyama tu za paja. Baada kutoka hospitali nilirudi kwenye gari na kuifungua ile simu na kupiga nyota. ILipokewa upande wa pili, "hebu nambieni mimi hasa ni nani" hilo niswali la kwanza kuuliza punde ilipopokewa, maana mnajua maisha yanavokuwa magumu kujikuta unawindwa na kila mtu bila kutambua hasa wanachokitak nini. "tukionana utajua kila kitu lakini kwa sasa unatakiwa ufanye haraka uondoke nchini Afghanistan, maana tayari CIA ya Marekani imeshatoa picha zako kuwa unatafutwa iwe umekufa au mzima" upande wa pili ulinijibu kisha ukaendelea "na kwa sasa hatuwezi kukutrack maana GPS device tuliokuekea imetolewa na wale wakidhani ndio protocol CODE X, lakini ukweli wewe unayo hio katika jicho lako la kushoto na itabidi tuiwashe hio ili tuweze kuwasiliana kirahisi zaidi. Dah nilichoka kabisa " wangeipata hiyo ingekuwa balaa na ndio maana sisi tukawa tunakupa kazi ya kuuwa kwa sababu ikiwa hao watu wataendelea kuwa hai basi hawataacha kukufatilia", "sasa cha kufanya nenda bank iliokaribu nawe na onyesha passport yako" alimaliza kuongea na simu ikakatika.

    Nilifanya kama alivonambia, niliielekea bank na kuwaonyesha passport yangu. Basi aliitwa mtu na kunipeleka katika makabati fulani hivi na kunambia ningize neno la siri nami ikafanya hivo. Lilifunguka na kuchuka begi na kurudi kwenye gari, kisha nikapiga tena simu " sasa tafuta sehemu ambayo unahisi utakaa kwa masaa matatu bila kusumbuliwa kwaajili ya kuiwasha protocol CODE X" nilingalia ramani yangu kwenye gari na kutafuta hoteli moja ya kisasa sana baada kuridhika na maelezo nilioyapata kupitia computer ile nilielekea kwenye hiyo hoteli na kuchukua chumba. Niliingia chooni kwa ajili ya kujisafaisha, nlipotoka nikapiga simu mapokezi kwa ajili ya kunitafutia suti na niipate baada masaa matatu.

    Niliekea kitandani na ile simu kisha nikapiga tena, "uko tayari" nilijibu ndio, "tutakapoiwasha tu, utapoteza fahamu maana itaachia kemikal inayoitwa CINDREX OLTIVIASO DECA ENDROLINE X (C.O.D.E.X), na ili iweze kuenea vizuri katika mwili ni lazima uwe umerelax na njiapekee ya kuhaikikisha hilo ni kulala usingizi wa kifo maana maumivu yake huwezi kusatahamili". nilikubali tu maana sasa sikuwa na jinsi kwa sababu kila mtu alikuwa anataka kunikamata au kuniua na sasa nishakuwa WANTED serekali ya Marekani. Baada kukata simu niliwasha AC na kujifunika shuka. Sekunde kadhaa tu nilipoteza fahamu.

    ****CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Baba umeniletea zawadi yangu" mtoto mdogo wa kike aliniuliza, "ndio nimekuletea princess wangu" nilimjibu huku nikimbeba. "Pole kwa kazi mume wangu" aliingia mwanamke na kunambia maneno hayo. Nilibaki nimeshangaa maana mimi nilikuwa hata siwajui lakini yule mtoto kaniita baba na yule mwanamke kaniita mumewe. "baba zawadi yangu iko wapi, nataka zawadi yangu, baba zawadi zawad izawadi. nilikurupika kutoka usingizini huku kijasho chembachemba kikinitoka kumbe nilikuwa naota tu, nilipoangalia saa yangu niligumdua tayar masaa matatu yashatimia na mara nikaskia mlango unagongwa. Nilikwenda kufungua nikamkuta muhudumu akiwa na suti, niliichukua na kurudi ndani, nilivaa vizuri kabisa na kuwa kama mtu wa ofisini, simu yangu iliita ,nilipoipokea tu " Habari yako na unajiskiaje, tulia hivo hivo tunakukagua kama hujapata madhara yoyote yale, kila kitu kipo sawa na baada kukata, simu hii itaungua na kuanzia sasa tutakuwa tunakutumia ujumbe moja kwa moja kwenye ubongo wako na chukua tahadhari" ilikatika na hapo ikaanza kutoa moshi kumaanisha kuwa ilikuwa inaungua.

    " kuna ndege inaondoka masaa mawili kutoka sasa, inaelekea Korea ya kusini panda hiyo ndege" uliingia ujumbe huo kama mawazo kichwani mwangu na bila kuchelewa niliishuka chini na kuchukua taxi kuelekea uwanja wa ndege. Nilipofika nilikata ticket na kukamilisha tarabi zote na muda ulifika tulipanda abiria wote na safari ikaanza.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog