Simulizi : C.O.D.EX. 1
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
NIlitulia nikiitafakari ile ndoto kwa muda bila kupata jibu lolote basi nikaamua kuachana nayo. Kwa vile nilitoka kulala basi sikuwa na usigizi hata kidogo mpaka ndege ilipogusa ardhi ya korea. Nilishuka na wakati naelekea mlango wa kutokea uliingia ujumbe mwengine " kata ticket ya kuelekeea Doha Qatar" ,nilifanya hivyo na baada masaa matatu niliingia kwenye ndege na safar ya Qatar ikaanza, kutokana na uchovu wa safar ya mwnzo usingizi mzito ulinichukua na haukupita muda mrefu nilianza kuota tena ndoto ile ile lakini wakati huu yule mtot alikuwa anaungua moto. Nilishtuka kutoka usingizini baada ya kuguswa bega na mhudumu mmoja wa ndege mwenye asili ya kiarabu akaniuliza kuna tatizo gani, nilimjibu kuwa ni ndoto tu alitabasamua na kuurudi katika siti yake.
Na mimi nikaamua kubadilisha upande, ili niendelee kulala na kile kitendo cha kufunga macho tu basi ile ndoto ikajirudia tena, nilishtuka tena baada ya kuguswa tena kwenye bega na yule yule mhudumu akaniambia nimfuate. Mtu hakatai wito niliinuka na kumfata nyuma kabisa kwenye kama kijichumba kidogo, akaniuliza tena kama nina tatizo, nikaona bora nimwambie tu basi nikamuelekza kila kitu kuhusu ile ndoto na kuwa ni mara ya tatu naiota. Akanambia mara nyingi hizo huwa si ndoto bali nikumbukumbu kisha akaniuliza kama nishawahi kupata amnesia, Nilimjibu kuwa sikuwahi kupata ugonjwa huo, basi alinipa kikombe cha kahawa. Nilikunywa huku nikiutathminia uzuri wake, nilimaliza kumshukuru na kurudi kwenye siti yangu. Kwa vile nilikunywa kahawa basi usingizi uliruka wote na macho yalikuwa makavu. Hatimae ndege iligusa ardhi ya Doha.
Nilishuka kwa lengo la kutoka nje, nilihisi kama mtu ananiita na nilipogeuka nilimuona yule mhdumu akija upande wangu. Nilisimama mpaka alipofika pale na kuniuliza kuwa kama ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika katika jiji hilo. Nilimjibu ndio basi akaomba kuwa mwenyeji wangu, nilikubali lakini pia nilihofia yasije yakawa kama yalonikuta mjini Shanghai, lakini nikajisema mazari kama haya huwa yanakuja mara chache sana hivyo nisiache amba chao kwa msala upitao. Tulitoka uwanja wa ndege na kuelekea hotelini, haikuwa mbali na uwanja wa ndege. Kila mtu alichukua chumba chake na tukakubaliana tukutane mapokezi baada ya saa moja.
Nilipoingia chumbani, nilifanya mambo yangu yote na nlipomaliza nilishuka chini kama tulivyokubaliana ila mimi niliwahi dakika tano nyuma kabla ya muda wa ahadi. Kwa mbali nilimuona mschana akiteremka kwenye ngazi, macho yalinitoka na kujikuta mapigo ya moyo yanakwenda mbio baada kugundua kuwa ni yule mhudumu wa ndege. Mpaka ananikaribia sikushtuka kabisa, alinigusa mkono ndipo akili ilirudi. Nilijikuta nikisema tu umependeza sana alijibu asante na kunambia nimfate, tulitoka nje na kuchukua taxi. Mimi nilikuwa kama bendera nafuata upepo hasa ukizingatia mji wenyewe nlikuwa siujui. Tulifika kwenye mgahawa mmoja ulotulia sana na kuchukua meza, alikuja mhudumu nikamuachia yeye aagize chakula. Baada mhudumu kuondoka "mimi naitwa Tania" alijitambulisha, "Allen James ndio jina langu" nilimjibu. "nashkuru kukufahamu" aliongea huku akitabasamu na kunifanya nijiulize " hivi Mungu alimuumba huyu mschana akamchivya kwenye maji ya uzuri na kumwabia nenda duniani ukawachanganye wanaume au". Maana kwa kweli sijawahi kuona mschana mrembo kama huyo. Basi tuliongea mengi pale mpaka chakula kilipo kuja na kula, baada ya hapo tulizunguka sehemu mbalimbali za starehe na kujikuta nasahau hasaa kama nawindwa kama pesa. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni kwa mara ya kwanza nilikunywa pombe mpaka nikahisi mawenge, baada ya kuzunguka sana mrembo huyo tulirudi hotelini lakini akaniambia nimpe kampany chumbani kwake maana alikuwa hana usingizi pamoja na kuwa amelewa. Basi niliingia katika chumba chake kilichofukizwa kisawa sawiya, harufu nzuri nilioikuta humo ilikuwa balaa. Tuliongea sana na kucheka utasema ni watu ambao tulikuwa tukijuana muda mrefu sana. ila mwishio nilikaa kimya huku nikumuangalia tu na kujikuta tunaangaliana tu bila kuongea kitu.
Kwa kweli nilijikuta nikimsogelea bila kutaka, akili yangu kwa wakati huo ilikuwa kama imezima haifanyi kazi kabisa. Basi kwa vile kila mmoja alijikuta akimtani mwenzake, bila kuulizana chochoe tulijikuta tukizama katika ulimwengu wa huba wenye bahari tulivu isio na mawimbi hata kidogo ikisindikizwa na raha zote za dunia. Nilikuja kushtuka asubuhi baada Tania kunishtua, alikuwa ni mwenye aibu kutokana na kitendo tulichokifanya usiku wake akisingizia ni pombe ndio iliomsikuma. Lakini mimi nikamwambia wala sijutii kilichotokea usiku kwani hakuna hata mmoja kati alielewa kiasi cha kutojitambua. Tuliongea mawili matatu huku tukijaribu kuekana sawa mwisho kabisa akanieleza hisia zake juu yangu.
NIlipomuuliza kwa muda mfupi tu tuliokutana imekuwaje akanipenda, alichonijibu kilinishtua. Alisema si mara ya kwanza kuniona kwani miaka mitatu nyuma aliniona White house U.S.A, na tokea hapo alianza kunifatilia lakini Ghafla baada miezi sita tokea anione nilitoweka katika mazingira ya kutatanisha. kwa kweli hata mwenyewe sikumbuki kama nishawahi kufanya kazi White house, lakini nilijifanya kama najua ili asihtukie kama sina kumbukumbu.
Baada maongezi hayo nilirudi chumbani kwangu huku kichwani nikiwa na mwazo mengi sana kiasi cha kunikosesha amani. Lakini nilijatahidi kuyapotezea ili nisiharibu mudi, niliingia chooni na kujimwagia maji na nlipotoka nilikuta nguo kwenye kitanda na kikaratasi kidogo kilichoandikwa "tukutane kwenye mgahawa wa hoteli hiyo"nilivaa haraka haraka na kushuka chini kuelekea kwenye mgahawa. Nilimkuta akiwa ananisubiri, tulikunywa chai huku tukipiga story mbili tatu, "unategemea kukaa siku ngapi Doha" aliniuliza swali wakati tukiendelea kupata kifungua kinywa. Nilimjibu kuwa nakaa wiki moja kisha naelekea London. Akasema mara hii bahati iko kwake maana na yeye wiki hiyo yote alikuwa off na wiki itakayofuata ndege yake inaenda London. Nikajisemea kwa kweli Mungu ananipenda, tulimaliza kunywa chai na kurudi vyumbani mwetu. Baada ya dakika kadhaa niliskia mlango wangu ukigongwa, nilifungua na kumkuta Tania. Aliingia ndani akionekana kuwa ana jambo anataka kusema lakini alikuwa anashindwa.
Alikaa kimya kwa muda kisha akasema "unaonaje Allen tukabadilisha hoteli", Nikamuuliza kwanini, akasema ni maamuzi tu. Kwa vile alikuwa mwenyeji wangu sikuwa na haja ya kukataa, basi tulipaga kila kitu chetu na kuondoka hotelini, tulielekea nje ya mji kidogo na kukodi nyumba kwa muda huo ulobakia. Ilikuwa nzuri sana na ilikuwa mbali na makazi ya watu, ilikuwa ni ya kisasa na kila kitu ndani ikiwemo sweemingpool. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huko kwa kweli tulipotea hasa katika ulimwengu wa maraha ya kila aina, maana tulikaa kama mtu na mke wake. Wiki hiyo moja naweza nikasema ilikuwa kama pepo kwangu maana nilisahau kabisa kuhusu ulimwengu wangu wa vita na mawindo. Wiki moja ilitosha kukita mizizi migumu ya mapenzi katika mioyo yetu, nilitamani isiishe au kama ingekuwa ndoto basi nisiamk abadan. Lakini kama tunavyojua kuwa siku hazigandi, muda ulikwisha na safari ya kuelekea London iliwadia na kwa vile yeye mwenyewe alikuwa anaelekea huko huko nilipanda ndege anayofanya kazi. Mara nyingi alikuwa akija nilipokaa na kuongea mawili matatu mpaka ndege inatua. Wakati wa kuagana nilimuahidi kuwa tutakuwa pamoja katika maisha yetu yaliobakia lakini kuna mambo nilikuwa nahitaji kuyaweka sawa kwanza. Alifurahi sana kusikia hivo na kunikumatia kwa nguvu huku machozi yakimtoka.
Nilipotoka tu, uliingia ujumbe "kuna gari tatu aina ya macedes benz nyeusi upande wangu wa kushoto, hizo gari ni za CIA wa Marekani na wako hapo kukukamata. Sasa wewe elekea kulia kuna Audi nyeupe, chukua hiyo na uwatoreke tafuta sehemu ujifiche ukisubiria maelezo zaidi" niligeuka na kuiona gari niloambiwa na kwa mwendo wa haraka niliekea ilipo na kuingia. Kwa kupitia side mirrors niliziona zile gari zikija upande wangu, nilitabasamu kidogo kisha nikaondoka kwa kasi ya hali ya juu sana. Kwa vile sikuwa mgeni sana katika mji huo haikuwa tabu kuwatoroka na nikafanikiwa kupata sehemu ya kujificha. Baada ya nusu saa uliingia ujumbe mwengine " sasa umefika muda wa sisi kuonana lakini kwanza kuna watu wawili wanatakiwa watoke katika mchezo huu" ziliingia picha zao kwenye simu yangu, lakini nilihisi kama nawakumbuka japo si sana. Nilotafuta hoteli na kukaa huku nikifwatilia mienendo yao. Niliporidhika na taarifa nilizo zipata nilitafuta mtu na kumuagiza silaha zote ninazo taka, siku ya pili mapema aliniletea na kumlipa.
Mr Peterson ndie alikuwa mtu wa kwanza katika list ya hao wawili, na huwa anapenda kuenda Casino fulani hivi. Mchana nilikwenda kwenye Casino hilo na kuzificha silaha zangu kwa sababu hawaruhusu kuingia na silaha.
Usiku uliwadia na huo ndio ulikuwa muda wa kuingia kazini, nilivaa vizuri na kuelekea zangu huko kwenye casino. Niliangaza humo ndani nikitafuta sehemu aliokaa, baada kujiridhisha naweza kupata shabaha nzuri, nilichukua kahaba mmoja na kuelekea nae katika chumba ambacho katika mfumo wake wa kupitishia hewa ndippo zilipo silaha zangu. Kwa sababu hakuwa kwenye mipango yangu nilimwacha acheze na alipomaliza nilimlipa na kumwambia atoke ili nipate uwanja mzuri wa kufanya kazi yangu. Baada ya kutoka tu nilivuta stuli na kupanda nikashusha mzigo wangu, nilinza kuupanga taratibu huku nikisubiria muda kutenda ufike.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipohakikisha mashine imekamilika, niliiweka kwenye meza na kupata kinywaji kidogo. Kisha nikatoa simu na kumpigia Mr Peterson "habari yako Bwana Peterson, unanikumbuka". Hayo ni maneno yalionitoka bila kutegemea baada simu kupokewa, "we nani, subiri....haiwezekani wewe si ushakufa" aliongea kwa kigugumizi, "ndio nimekufa na ndio maana nimekaa karibu na wewe" nilimjibu nikitabasamu. Kwa kupitia darubini ya sniper nilimuona akiwaambia walinzi wake wanitafute "usipate shida mzee kwa sababu mzimu hauonekani" niliendellea kumtia mshikemshike.
"Sema unataka nini au unataka maisha yangu na kama ni hivo tafadhali usiniue nina familia inanitegemea na ntakupa chochote unachotaka" aliropokwa mzee wa watu, kauli hiyo ilinitia hasira sana na sijui kwa nini.
"Umemuona huyo malaya pembeni yako kwenye kiti, muondoe hapo kuna mzigo nimekuekea" niliongea kwa hasira sasa, na kweli alisogea mpaka pale alipo yule malaya na kumuondoa.
"Mbona siuoni huo mzigo" aliongea huku akigeukia dirishani,”
“Ni kwa sababu mzigo uko hapo dirishani na unaitwa kifo" kabla hajajibu chochote nilifyetua risasi iliopenya katikati ya paji la uso na kumfumua kichwa.
Puuu kama mzigo alianguka chini na kwa mbali nikaanza kusikia makelele, haraka niliipangua ile sniper na nlikuwa na kibomu kidogo cha dakika, basi nilikitega na mimi nikatoka huku nakimbia kama walivokuwa wakifanya watu wengine waliokuwepo katika casno hilo. Baada kufika nje kwa mbali nikiaskia mlipuko, nilitabasamu na kuondoka.
Siku ya pili asubuhi vituo vingi vya televisheni vilikuwa vinatangaza mauwaji ya aliekuwa katibu mkuu wa kitengo cha usalama marekani Mr Peterson. Sikuwa nikishughulika sana lakini kuna sauti niliiskia ikabidi nitazame tu, "wewe muuaji tunakuahidi tutakamat tu na utalipa kwa ulichokifanya" hayo yalikuwa ni maneno aliyoyasema Mr Jones ambae muda mfupi na yeye atamfuata rafiki yake kuzimu. Baada kunywa chai nilitoka kwa ajili ya kupanga mauaji ya kuhitimisha kazi yangu, lakini kuna kitu kilikuwa kinanitattiza sana tokea Mr Peterson alipoongea kama mimi nimekufa. Nikaona njia pekee ya kupata jibu ni kupitia Jones.
Usiku nilielekea katika ofisi yake na kuingia kwa siri kisha nikaweka vinasa sauti vyangu na kuondoka. Asubuhi nilibeba nguvu kazi yangu nyingine na kuelekea katika jengo ambalo lilikuwa jirani na ofisi hiyo kubwa, na kama kawaida nilianza kumpanga mwanangu kisha nikaweka earphone sikioni kusikiliza majadiliano yao. " hii ndio simu ya mwisho aliopigiwa kabla ya kuuwawa" aliongea mtu mmoja kisha akaiwasha recorder na wote wakakaa kimya kuisikiliza. " dah huu ni msala, aina hii ya mauaji ilikuwa inafanywa na mtu mmoja, mnajua kwanini alimlaghai asoge dirishani kisha akamsubiri mpaka ageuke ndio akamchapa risasi" aliongea Jones na kuuliza "hatujui mkuu"walijibu kwa pamoja. "kwa sababu huyu muuaji hawezi kukuuwa ukiwa umempa mgongo, ni lazima akuone unavotoa macho wakati wa kufa" aliongea Jones na kunifanya nitabasamu kidogo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"David Robert Mc'canoon ndio jina la huyo muuaji na hivi tunavyoongea anatusikia, na tayari mimi niko chini ya jicho lake lakini kwa sababu nimempa mgongo hawezi kuniuwa" aliongea Jones na kunifanya nishtuke. Nilitamani sana kufyatua risasi lakini nlihisi sitamtendea haki nikimuua bila kumuona sura yake na anavokodoa macho wakati wa kufa. Hivyo niliipangua sniper yangu haraka kuirudisha kwenye begi na kuanza kuondoka, nilipofika tu chini uso kwa uso na Jones. "huyo hapo muueni" aliropokwa huku akijificha nyuma ya walinzi wake, na wao bila kupoteza muda walianza kufyatua risasi. Nilibana ukutani na kutoa bastola mbili ndogo na kuanza kujibu mashambulizi hayo, wakati huo Jones aliingia kwenye gari na kuondoka. Kwa kweli niliingia hasira sana maana nilipanga nimmalize pale pale lakini walinzi wake wameleta shobo, nilichomoka nilipo kwa kasi ya hali ya juu sana huku nikifyatua risasi lakini kwa vile wale walinzi hawakuwa miongoni mwa nnaotaka kuwaua basi niliwapiga risasi za miguu tu na kukimbilia ilipo gari yangu na kuondoka kwa kasi.
Niliwasha computer na kuitrack gari ya Jones kwa sababu nilikuwa nimeiwekea GPS tracker hivyo nilijua imeelekea wapi na mimi bila kupoteza muda niliifata, kwa mwendo wa kasi nilifanikiwa kuwa fikia karibu. Nilishusha kioo na kulipiga tairi la gari ya Jones risasi hivyo likapoteza muelekeo na kupinduka, nilishuka kwenye gari yangu na kuelekea ilipo gari hiyo na kumtoa Jones kwa bahati nzuri alikuwa hai. Nimuingiza kwenye gari yangu naa kuondoka nae, nilitafuta sehemu nzuri ya kujificha ili nipate muda mzuri wa kupata majibu yangu. "David hivi imekuaje ukawa hai leo" aliuliza baada kuzinduka, "Jina langu ni Allen James" nilongea kwa hasira, "ah kumbe wewe mwenyewe hukumbuki kitu" aliongea huku akitabasamu, "na ndio maana uko hai mpaka sasa kwa sababu nataka kujua ukweli kwanini mnasema nimekufa" nilimjibu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment