Search This Blog

Friday, 20 May 2022

C.O.D.EX. 1 - 3

 







    Simulizi : C.O.D.EX. 1

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Na unadhani nitakwambia chochote" alinijbu na kunitemea mate usoni, "nadhani unafahamu kuwa ninapo taka kujua kitu chochote kutoka kwa mtu ni lazima nikijua kwa hali yeyote ile" niliongea huku nikijifuta yale mate. Nilifungua begi langu na kutoa kisu chembamba kisha nikavuta kiti na kuka mbele yake. "naona kwa njia ya kiungwana umeshindwa kutoa ushirikiano sasa itabidi niukwangue ukweli kupitia maumivu" niliongeaa hilo na kwa nguvu zote nilimkita kisu cha paja na kufanya kama nachokonowa hivi. Alipiga kelele lakini ni kama alikuwa ananihamasisha niendelee kumtoboa toboa."nambie ukweli", "sahau" alinijibu, nilitoa pini ngumu na nyemba zenye urefu sentimita saba. "sawa basi tuendelee na mchezo wetu, mimi ntaendelea kukutesa na wewe goma hivo mpaka mmoja wetu atakaposarenda amri". Nilitoa sindano ya ganzi na kumchoma ili asisikie maumivu wakati naziiningiza pini hizo kwenye mwili wake.

    Taratibu nilianza kuingiza pini kwenye kidole cha kati cha mkono wa kulia, niliendelea na zoezi hilo mpaka nilipohakikisha hakuna kidole nilicho sahau kunazia vya mikono mpaka vya miguu. "najua saa hivi huhisi kitu lakini baada ya dakika mbili hivi utaona kilichomtoa nyoka pangoni kama ni sauti nzuri ya mrembo au maji ya moto" niliongea kisha nikakaa kimya nikisubiria kazi iyanze. Naam baada dakika mbili alianza kukunja uso na machozi yalianza kumtoka bila kupenda, alianza kutetemeka na kijasho chembamba kilianza kumchuruzika katika paji la uso. Alianza kupiga kelele, "hazitakusaidia hizo" nilimjibu huku nikicheka. Hata sikujua ukatili ule na adhabu za aina ile nimejifunza wapi. "sawa nitatoa ushirikiano, naapa naomba unitoe hizi pini" alilalamika kwa nguvu, "namna hiyo ungekubali mapema yasingekufika haya" nilimchoma tena sindano ya ganzi kukata maumivu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alianza kuongea kwa kusema "wewe ulikuwa ni mmoja kati ya watu hatari sana ambao walipata mafunzo kupitia serekali ya USA, katika kitengo cha siri ndani ya C.I.A. Lengo la kupewa mafunzo hayo ilikuwa ni kuwaondoa katika ramani wale ambao walioonekana kumuandama raisi na hiyo ndio ilikuwa kazi yako. Ulifika wakati mpaka raisi akawa anakuogopa kutokana kujua mambo mengi ya siri hivyo akatoa amri na wewe pia upotezwe katika ramani. Mimi ndie niliepewa jukumu hilo na nilihakikisha natimiza wajibu wangu kama mtumishi wa serekali kwa kukuuwa na nilifankiwa lakini nashangaa leo kuona uko hai" alimalza kuongea na kuniangalia. Wakati huo nilikuwa nimevimba kama mbogo aliejeruhiwa, nilisimama "asante kwa ushirikiano wako" nilitowa bastola ndogo na kuweka saini katika paji lake la uso kisha nikatokomea zangu.

    Nikiwa natembea uliingia ujumbe "tunajua kwa sasa una maswali mengi hayana majibu, lakini kila kitu kitu kitakaa sawa baada kupata kumbukumbu zako zote, Panda ndege uje Miami". Bila kupoteza muda nilielekea uwanja wa ndege na kukata ticket ya miami, baada masaa mawili niliingia kwenye ndege na safari ya kuelekea Miami ikaanza. Baada muda mrefu wa kukaa angani hatimae ndege ilitua mjini Miami na nilipotoka tu uwanja wa ndege ukaingia ujumbe. "Katika maegesho ya gari kuna gari aina ya Macerati nyekundu, chukua na ufate ramani" nilekea kwenye maegesho na kuchukua gari hiyo na kuondoka, Nilifata ramani mpaka nilipofika kwenye nyumba ambapo ndipo ilipokoma ramani hiyo. Mlango ulikuwa umefungwa lakini haukutiwa loki, niliingia ndani na kushangaa maana kulikuwa hakuna kitu. Uliingia ujumbe mwengine "sogea mpaka ilipo alama nyekudu kweny ukuta na uweke kiganya chako" nilisogea kama nilivoelekezwa na kuweka kiganja katika alama hio. Ghafla ukuta ulisogea na lifti ikafunguka, niliingia na lifti ikajifunga na kuanza kuteremka chini kwa kasi ya hali ya hali ya juu sana.

    Ghafla ilisimama na mlango ukafunguka, mwangaza mkali uliokuwemo ndani ya chumba hicho uliniumiza macho kwa dakika kadhaa kabla kuzoea hali ile. "karibu Mr Allen James" niliskia sauti ikinikaribisha, "jina langu ni Albiana Master Computer" iliendelea, nilijiuliza sauti hiyo inatokea wapi maana sijaona mtu humo ndani. "mimi ni compter na ndie niliekuwa nawasiliana na wewe muda wote" nilichoka baada kusikia hivo. "sawa mimi nimeshafika na nataka unieleze kila kitu kinacho nihusu" niliongea kwa kujiamini. "sina haja ya kukuelelza kwani muda mfupi tu utajua kila kitu" ilinijibu computer hiyo, "hatua kadhaa mbele yako kuna mlango umeandikwa PROJECT CODE X, ingia ndani ya chumba hicho". Nilisogea mpaka kwenye mlango huo na kuufungua kisha nikaingia. "vua nguo zako zote na ulale kwenye hicho kitanda" iliniabia na mimi nikafanya hivo. Baada ya kulala tu taa zote humo ndani zikazimika na ghafla ikatoka mikanda na kunizunguka kuotoka upande wa kulia wa kitanda kuelekea kushoto na kisha kitanda kikaingia kwenye mashine fulani hivi. Baada ya hapo mashine ilijifunga na kuwaka taa nyekundu ndani ya mashine hiyo. "nakutakia usingizi mwema" iliongea ile computer na ghafla usingizi mzito ukanichukua.

    *****CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "We David si unakwenda kwenye interview leo" baba alifungua mlango wa chumba changu na kunishtua, nilikurupuka kutoka kitandani na kuangalia saa yangu ya mezani. Iliniambia saa moja kamili asubuhi, na natakiwa niripoti white house saa moja na nusu kwaajili ya hiyo interview.Hapo nilikuwa na miaka ishirirni na ndio kwanza nilikuwa nimaliza chuo kikuu katika cozi ya IT. Niliingia chooni haraka na kujisafisha kisha nilirudi chumbani kwangu na kuvaa suti aliyoninunulia baba. Hata chai sikunnwa nilitoka nduki mpaka kwenye gari yangu na kuelekea ikulu.

    Dakika ishirini na nane nilikuwa mapokezi na kuelekezwa sehemu nnayo takiwa kuwepo, nilipofika nilishangaa kuona msururu wa vijana wakisubiri na wengine walikuwa wakitoka katika chumba cha interview huku machozi yakiwatoka, hiyo ilikuwa ni dhahiri kuwa walikosa kazi hiyo. NIkiwa katika hali hiyo niliskia jina langu likiitwa. Niliitika na kuelekea mlangoni, mlango ulifunguliwa nikaingia. Alinihoji maswali ya kawaida kwanza kisha wakanisogezea computer na kunambia nihack system ya white house, nilitabasamu kidogo kwa sababu kuhack ndio kitu nnachokipenda katika maisha yangu. Wakaniekea saa mbele na kunambia nina dakika tano tu za kufanya hivo.





    Saa ilipobonyezwa tu na mimi nikaanza maujuzi yangu, kila nilivojaribu nilifika pahali nikakwama lakini baadae nilishtuka kama kuna mtu mwengine pia anahack computer ninayo tumia. kwanza lazima nimzuie halafu ndio niendelea na kuhack. Nilipoangalia saa niligundua kuwa dakika mbili na nusu zishateketea, niliongeza kasi na kufanikiwa kumzuia anaehack compuetr niliopewa ndani ya sekunde arobaini tu. Hapo niliongeza kasi mara dufu huku nikitumia ufundi wa hali ya juu kufanya kazi hiyo ngumu, dakika nne na sekunde hamsini na sita ndio muda niliomaliza kuhack na kufanikiwa. Kisha nikiwapa computer yao. Hawakushangaa sana, mmoja aliondoka nayo na baada dakika kadhaa alirudi huku akionyesha uso wa simanzi, mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio na kijasho chembamba kikaanza kunitoka. "samahani umejitahid sana lakini hujafikia kiwango tulichokitaka" aliongea na kunionyesha mlango uliokua na alama ya kutokea. Kiunyonge niliiuka na kuelekea kwenye mlango huo, lakini nilipoufungua nilishangaa kuona hakuna hata mtu mmoja aliekuwa akisubiria kuingia kwenye chumba hicho. Lakini sikutilia maanani kwani mawazo yote yalikuwa mbali sana nikikumbuka jinsi nilivyokuwa natamani sana kulitumikia taifa langu.

    Ghafla nikiwa katika dimbwi hilo la mawazo kengele zinazoashiria hatari zilianza kulia, na kwa mbali niliona kikundi cha watu kikija upande wangu wakiona kama kuna mtu wanamlinda. Na kila walivyosogea niligundua kuwa alikuwa ni raisi, nilianza kuetetemeka huku nikishangaa, waliponikaribia mmoaja wao alinivuta na kunambia "mlinde raisi" nilitaka kumwambia kuwa mimi sio mlinzi lakini nilichelewa kwani risasi zilianza kurindika na kunibakisha nisiwe na chaguo zaidi ya kumlinda raisi lakin Ukweli hata kukamata silaha nilikuwa sijui. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mambo yalikuwa magumu sana kwangu maana nilikuwa sijui nifanye nini kumuokoa raisi, japo mkono nlikuwa nauweza kidogo lakini sikuwa na moyo wa kupambana na watu wenye silaha kali. Ila nilielewa kitu kimoja kama sasa maisha ya raisi yapo miokononi mwangu, basi nilimshika na kuanza kutmimia nae lakini ajabu nilipoangalia nyuma wlinzi wote walikuwa chini, na sasa nilikuwa nafuatwa mimi na raisi. Nilifika pahali nikajibanza na kumvizia anaekuja, kwa kasi ya ajabu nilichomoka na kumpiga kikumbo kilichomfanya aangushe silaha. Hapo sasa ilikuwa ni mkono kwa mkono, nilichezea ngumi kadhaa nilifanikwa kumpiga katika sehemu ambazoni pressure point na kumzidi lakini sikumuuwa. Wakati nageuka tu nilimuona mtu akiwa na bastola na amemlenga raisi bala kuchelewa nilimuwahi raisi na kukinga mgongo. Niliskia tu mlio wa risasi lakini sikujua nini kimeendelea.



    Nilikuja kushtuka nipo katika chumba kidogo hivi, na nilipoangalia pembeni nilishangaa kuwaona wale walinzi wote ambao nilidhani wamekufa. Hapo nikajua bila shaka niko kuzimu, "hongera kijana umechagulia kujiunga na kikosi maalum cha siri cha kumtumikia raisi wa nchi hii". Aliongeamzee mmoja aliekua pembeni ya kitanda hicho. Kisha akanipa mkono kuashiria nikae, "kesho fika ikulu saa mbili asubuhi na chunga kila kilichoanyika kiwe siri kisitoke nje ya chumba hichi" aliniambia na kunionya "yoyote atakae kuuliza unafanya kazi gani,mwambie kuwa wewe ni mlinzi tu wa ikulu" aiendelea kuongea. Baada hapo alikuja mtu mwengine na kunambia nimfuate nami nikafanya hivo bila kuuliza, alinipeleka mpaka nje na kunambia tukutane kesho.



    Nilienda kwenye gari yangu na kurudi zangu nyumbani, nilipofika tu baba aliniuliza kama nimefanikiwa nikamjibu ndio. Basi akanipa hongera na kunambia sasa maisha yangu yameanza hapo, baada maongezi mawili matatu nilielekea chumbani kwangu kwa ajili ya mapumziko. siku ya pili mapema niliamka na kujiandaa, nilifika sebleni na kumsalimia baba maana ndie mzazi pekee nlokuwa naishi nae, mamaangu alishatangulia mbeleza haki siku nyingi sana. Baada kunywa chai niliaga na kuondoka kuelekea ikulu, huko nilipewa maelekezo yoote na kuambiwa kuwa nijiandae na safari ya kuelekea mafunzoni. Jioni nilirudi nyumbani na kumueleza mzee, alifurahi sana na kunipa baraka zote. Siku ya safari ilifika, sikuwa peke yangu nlikuwa na wenzangu wanne ambao pia walipata nafasi hiyo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kwa muda wa miezi sita tulikuwa mafunzoni na kwa kweli mafunzo yalikuwa magmu sana kiasi kwamba kuna wakati nilijuta kukubali kazi hiyo. Wote watano tulipewa mafunzo ya sniper na kiukundi chetu kikapewa jina la "suicide squad" (kikosi cha mauaji). tulipikwa tukapikika mpaka tukaiva. Nikiwa nimebakiza mwezi mmoja tu kumaliza nikapokea habari mbaya sana, baba yangu alipata mshtuko wa ghafla nakupoteza maisha. Nililia lakini mwiso nikakumbuka msemo mmoja ambao mzee alipenda kuutumia "Maisha ni safari na wote tunapita, kama ilivyo hatuwezi kuchagua tuzaliwe na nani na siku gani ndio hivyo hivyo hatuwezi kuchagua tufe vipi na kwa muda upi". Maneno hayo yaliibadilisha hali yangu kunipa moyo wa chuma. Hatimae tulimaliza mazoezi na kutambuliwa rasmi na raisi wa nchi hiyo.



    Mwisho niliitwa katika chumba fulani hivi na kupewa picha, ilikuwa na maelezo nyuma. Nilitakiwa kumuua huyo mtu kwenye picha, nilipewa sniper na risasi moja tu. Jaribio hilo ni la kufa au kupona maana nikimkosa atanishambulia mimi. Nilijiandaa na mapema siku ya pili nikapanda ndege kuelekea Moscow Russia, kama kawaida nilimfuatilia mpaka niliporidhika na taarifa nilizochuma ndio nikaamua kumtenda. Nilitafuta jengo moja refu jirani sehemu anayopenda kukaa usiku, niliiunnga mtambo na kuingiza risasi ile kisha nikaikoki na kuanza kumlenga, sikutka kupoteza muda nilfyatua risasi na iliopita sawa sawia katika paji la uso. Kisha haraka nikakunja sniper yangu na kusepa.

    Nilirudi na kupokewa kwa shangwe na kuanzia siku hiyo ikawa ndio kazi yangu, kuuwa kwa sababu ya raisi. Ukweli niliingia katika mapenzi mazito na kazi hiyo, maana mwisho nilikuwa naona kuuwa kwangu ni kitu cha kawaida sana. Lakini tulivyo binaadamu tumeumbwa na moyo wenye kupenda, miaka mitatu ilipita na ndipo nilipokutana na mwanadada mmoja alieitwa Melinda. Nilitokea kumpenda sana, na nilimueleza hisia zangu juu yake. Mwanadada huyo mmarekani mwenye asili Yahudi, mrefu wa wastani, macho yenye kiini cha buluu kilichokoza na mcheshi kupita maelezo alinikubalia ombi langu na muda si mrefu tukafunga ndoa japo kuwa shirika langu walikubali shingo upande lakini ndio hivyo moyo ulishapenda.

    Ndoa hiyo ndio ilionifanya nigundue kuwa kazi nnayofanya si nzuri hata kidogo lakini kuiacha ilikuwa siwezi kwa muda huo. Mke wangu alipo niuliza kazi nnayo fanya nilimdanganya na kumwambia kuwa nafanya kazi kama mtu computer tu. Na hakuwahi kuinyesha kama nlikuwa namdanganya, alikubali bila kpingamizi. Maisha yaliendelea kuwa mazuri na yenye fuaraha na amani tele ndani ya nyumba yangu, hatimae mwaka mmoja ulikata tukafanikiwa kupata mtoto wa kike, tulimwita Christina. Kwa kweli furaha yangu ilikuwa sio ya kitoto maana dah hata kueleza nashindwa, nikiwa katika furaha hiyo nilipigiwa simu kuwa raisi anataka kusafiri kuelekea Syria kwa ajili ya mazungumzo hivyo nikuwa nahitajika kwenye msafara huo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimueleza mke wangu, alikubali japo hakupendezwa na mimi kuondoka siku muhimu kama ile. Nilimbusu yeye pamoja na mwanangu na kuondoka kuelekea ikulu kwa ajili ya safari, kumbuka huu ni mwaka wa nne tokea niwe sniper. Muda wa safari ulifika tukapanda ndege na safari ikaanza, kilichonishangaza ni kwamba inakuaje masniper wote watano tumechukuliwa na hiyo sio utaratibu wa kawaida. Lakini hakuna alioongea, nakumbuka tulipewa kikombe cha chai kwa ajili ya kupasha tumbo, ila baada ya kunywa funda moja tu nilianza kuona mawenge na hatimae nikapoteza majira. Sikujua chochote kilichoendelea, nilikuja kushtuka nipo kwenye jengo moja refu sana huku nikiwa tayari jicho langu lipo kwenye daubini ya sniper yangu. Pembeni kulikuwa na simu ghafla ikaingia sms ikinambia kwa kuna watu wamevaa nguo sare na wapo wanne niwauwe wote. Bila kuchelewa niliwatafuta lakini kilichonishtua baada kuwaona ni watoto wadogo umri kati ya miaka kumi hadi kumi na tano. Sikuwahi kuuwa mtoto na kila nilivojaribu kujiizia akili yangu haikuwa tayari kukubaliana na mimi na bila kuchelewa niliafyatua risasi tano tena kwa kasi ya hali ya juu na kuwauwa wote lakini baada kufanya hilo machozi yalianza kunitoka.

    Nilikunja kila kitu changu na kuondoka eneo hilo, maswali mengi yalinijia kichwani na kukosa majibu. Kilichonishtua zaidi nilikuwa hata sijui niko wapi lakini nilikuwa nikitembea tu mpaka kwenye gari na kuingia kisha nikaondoka zangu. Kwa kweli nilianza kuhisi kama naendeshwa sasa maana mambo yote hayo sijui yalikuwa yanatokea vipi. Nilifika kambini na kuwataarifu kuwa kazi imefanyika na kukamilika, lakini nilipotaka kuuliza imekuwaje nikauwa watoto mdomo ulikuwa mzito na hivyo kushindwa kuuliza. Tuliambiwa tukunje kila kitu safari ya kurudi nyumabni ilikuwa imewadia, kwa furaha nilokuwa nayo nilijianda huku lengo langu ni kuwa kuonana na mke wangu na mtoto wangu ambae amezaliwa siku chache zilizopita.



    Jambo la kwanza baada kutua marekani niliaga na kuelekea nyumbanni, lakini nilishanga kuona mazingira yamebadilika sana kilichonifanya nishtuke sana. Niligonga mlango, mke wangu alifungua lakini hakuonesha furaha hata kidogo badala ya kunipa salamu alitandika kibao kizito shavuni jambo lilinishangaza sana. Kisha akaongea "sasa ndio nini kuniacha peke katika kipindi ambacho nilikuwa nakuhitaji zaidi", "sasa mi si nimeondoka juzi tu" nilimjibu kwa mshangao, "juzi gani inamaana hata hujui leo ni siku gani" aliniuliza kwa mshangao pia. Na kwa kweli nilikuwa sijui "tokea uondoke siku ile niliojifungua mpaka leo ni mwaka mzima umepita" aliongea na kunifanya nitoe macho kama mjusi aliebanwa na mlango.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwakweli nilihisi kuchanganyikiwa maana sikutegemea kama muda ambao nilikuwa nje ni mkubwa hivo. Lakini ni kweli hata mwanangu christina alikuwa tayari anaweza kukaa, hasira ilianza kunipanda na ile furaha yangu yote ya kukutana na familia yangu ilitoeka. Siku hiyo ilipita kwa mtindo wa kulazimisha tabasamu, siku ya pili kama kawaida nilienda kazini lakini nilikwenda kiugomvi ugomvi tu. Sikumpa hata mtu mmoja salamu wala kumuuliza hali na wote walioniongelesha niliwalia bati tu, wakubwa wangu waligundua kuwa mda wowote ule mtu atakaonizingua basi atakiona cha mtema kuni. Wakati nikiwa katika ofisi yangu alipita mtu mmoja na kuniangalia sana kisha akaondoka na alipofika mbele nilimsikia akimwambia mtu "jamaa kawa kama mbwa sasa maana akiambiwa uwa basi haulizi, anafanya tu" maneno yalinitia hasira na kujikuta nikiinuka na kumfata na nilipomkaribia nilimsalimia kwa ngumi mbili nzito za uso zilizomtia mawenge na kumtupa chini.







    Niliendelea kumshushia kipondo, kwa mbali nikamsikia mtu akiniambia "acha" kwa ukali, nikshangaa kuona mwili wangu unatii amri hiyo. Kisha akanambia "Njoo" basi nami nikafanya hivo na nilipofika alipo akaniambia "kaa" nami nikakaa, yote hayo niliyafanya bili akili yangu kufanya maamuzi yoyote yale. Nilihisi kweli sasa nimekuwa mbwa maana siwezi kukataa amri yoyote ntakayopewa, nilitamani kulia lakini mbele za watu ingekuwa aibu. Hali hiyo ya kuendeshwa kama mbwa iliendelea kwa muda mrefu takriban miaka mitatu, kuna wakati nilitumiwa sms usiku nikiwa faragha na mke wangu. Nilijikuta naacha kila kitu na kuelekea kazini. Hali hiyo iliitia dosari familia yangu na furaha ilitoweka, siku moja mke wangu akaniambia kuwa anahitaji kwenda kuwaona wazazi wake Miami. Na kwa hali ilivokuwa ikiendelea ndani ya nyumba yangu nilihisi nisipomruhusu basi ndoa yangu ingevunjika, nilikubali na siku ya pili mapema akaondoka pamoja na mwanangu.

    Ukweli niliwalaumu sana kitengo changu kwa kuniharibia maisha yangu, maana nilikuwa sina maamuzi tena juu ya maisha yangu. Siku zilipita, na wiki zikakata na hatimae mwezi bila kuiona familia yangu, niliomba ruhusa na kuelekea miami kwaajili ya kuungana na familia yangu. Nilikubaliwa nasiku ya pili mapema nilifunga safari ya kuelekea huko, nilifurahisi sana kuonana na mke wangu, wakwe zangu pamoja na mtotot wangu ambae alishkilia kusema "baba umeniletea pipi". Nilimkabidhi mfuko mzima wa pipi kutokana na uchovu wa safari nilitaka kupumzika, mke wangu akanipeleka kwenye nyumba nyingine. Aliniandalia maji na kuniogesha kisha akaniandalia chakula na pia alinilisha, kwa kweli nilishangaa sana alifanya yote hayo utadhani mtu aliekuwa anakaribia kuiga dunia. Kisha alinisindikiza kitandani na yeye akiwa pembeni yangu na bila kuchelewa tukajikuta tupo katika huba za dunia. Baada jambo hilo nilipata usingizi mzito sana uliojaa ndoto nzuri, nilikuja kushtuka asubuhi baada kusikia kelele za watu na kwa mbali kupitia dirisha langu nikawa naona moshi mzito sana. Nilivaa nguo haraka na kutoka nje ili kama kunahitajika msaada nitoe. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikuamini kama ilokuwa inangua ni nyumba ya wazazi wa mke wangu, nilijikutanikienda mbio na kuingia ndani bila kujali kama ningeungua au laa. Nilichokutana nacho ndani ndo kilonifanya nikaishiwa nguvu, miili minne ilikuwa chini, na kwa haraka niliitambua yote kuwa ni ya wakwe zangu,mke wangu pamoja na mtoto wangu. Nilipoangalia vizuri niligundua kuwa bado mke wangu alikuwa hai, nilimfata nimbebe lakin akanishika mkono na kutaka kunambia kitu "CODE....." hakuwahi kumalizia alikata roho. Machozi ya lianza kunitoka na kujikuta napoteza fahamu."

    Nilizinduka kutoka katika usingizi huo huku jasho likinitoka kama maji, "karibu tena duniani MR Allen James" niliiskia ile computer ikiongea, "ile ni ndoto au" niliuliza kwa mshangao. "hapana yale ni maisha yako kabla ya kuitwa Allen James, zote ni kumbukumbu za maisha yako ya nyuma". Nilishindwa kujizuia na kuanza kulia kama mtoto mdogo, lakini swali lilikuwa ni nani alieiteketeza familia yangu yote. NIkiwa katika dimbwi hilo la mawazo nikaskia "na kuna ujumbe wa mwisho aliuwacha mke wako". Nilishuka kitandani na kuelekea kwenye meza ilioluwa na computer na punde ulifunguka ujumbe kwenye computer hiyo uliosema hivi.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog