Simulizi : C.O.D.EX. 1
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mpendwa mume wangu najua utadhani nilikuwa nakasirika kwa jinsi ulivyobadilika, laa sikuwahi hata siku moja kufikiria hivo. Matatizo yote uliokumbana nayo chanzo ni mimi na timu yangu yenye wanasayansi ishirini, tulipewa tenda ya kutengeneza kemikali ambayo itamfanya mtu atii chochote atakachoambiwa bila kuuliza sikujua kama na wewe utakuwa ni mmoja wapo naomba unisamehe kwa hilo. Siku ile uliorudi kutoka safarini baada mwaka mzima kupita, niligundua kuwa huko sawa hivyo usiku nilikutilia dawa ya usingizi ili niweze kuchukuwa damu yako na kuipima nilichogundua kilinitisha sana hivyo niliandika ripoti na kuiwasilisha ikulu kwa lengo la kupewa kibali cha kuteneza dawa yake. Lakini raisi alikataa kuniruhusu kufanya hivyo kwa ajili ya maslahi yake mwenyewe, Kwa kweli niliumia sana na nikaamua kufanya kazi hio bia ruhusa. Pia nilichogundua kuwa ni kwamba hakukuwa na dawa yoyote inayoweza kuizimua kemikali hiyo hivyo nikaamua kutengeza tena kemikali kama hiyo ila hii ilikuwa tofauti kidogo kwa maana iliweza kumpa uwezo mtu uwezo wa kujenga hoja. Kwa muda wa miaka mitatu nimekuwa niifanyia uchunguzi wa kina kemikali hiyo nilioipa jina la CINDREX OLTIVIASO DECA ENDROLINE X (C.O.D.E.X). Baada kuridhika na majibu hayo ndio niliamua kuja Miami ambapo ndipo zilipo maabara zangu. Lakini kuna mmoja kati ya wenzangu kwa tamaa ya fedha alivujisha siri hii kwa raisi hivyo amri ya kuuwawa wewe pamoaja na familia yako yote ikatolewa. Na ulivyoomba likizo tu wamekupa bila maswali hiyo ni kwa sababu walitaka wafanye tukio hilo liwe kama ajali ya moto. Siku uliofika tu usiku wakati umelela nilikuingiza maabara kwa siri na kukufanyia operesheni ndogo ya jicho la kushoto na kukuingiza kifaa kidogo ambacho kilikuwa na kemikali hiyo. Na niliiset computer ikiwa nitakufa basi, kemikali hiyo iachiwe kidogo ili kuzifuta kumbukumbu zako na uanze maisha mapya kama Allen James. Na kuhusu mtoto wetu usijali yuko hai na yupo na wazazi wangu Califonia. Ile miili mitatu ilikuwa ni ya kutengeneza tu ila mimi nimeona bora nife kwa sababu mimi pekee ndie ninae jua kitu gani nimekiongeza katika kemikali ile na kuifanya iweze kumpa mtu uwezo wa kuhoji tafauti na awali. WAKO MPENDWA MELINDA"
Nilijikuta nikitokwa na machozi baada kuisoma barua hiyo, huku nikijiuliza kwanini watake kuniuwa wakati nilifanya kila walichotaka. Au kwasababu mke wangu ametaka kunipa uhuru tu "nakuahidi Melinda muhanga wako hautoenda bure, lazima watalipa kwa kila walichotutendea, nitauwa mmoja badala ya mwengine mpaka niwamalize wote waliohusika na kifo chako na mateso yangu" nilijikuta nikiongea kwa hasira kisha nikaipiga meza ngumi na kuivunja. Mi mwenyewe nilishangaa kisha nikasema "pia asante kwa zawadi ulionipatia", "sasa Mr David ingia store kwa ajili ya kuchukua silaha kisha utoke kabisa katika nyumba hii maana muda si mrefu italipuka, na pia fuata akili yako itakapokuelekeza" iliongea ile comuter na ghafala taa nyekundu zikaanza kuwaka, bila kuchelewa niliingia store na kukusanya kila kitu ambacho nilihisi kingenisaidia katika kazi yangu kisa nikatoka nje na kuelekea gereji na kuchukua gari aina ya Jeep, niliiwasha na kuondoka. Sikufika hata mbali niliskia mlipuko mkubwa na nilipangalia ile nyumba yote ilikuwa inatekeketea kwa moto. Nilitafuta nyumba nyingine hukohuko Miami na kuhifandhi silaha zangu kisha nikaelekea uwanja wa ndege na kukata tiket ya kueleke Califonia kwa ajili ya kumuona mwanangu.
Muda wa safari ulifika na ndege ikaondoka, safari nzima kwangu ilikuwa ya unyonge na hatimae ndege ilitua Califonia na kwa msaada wa kitabu nilichokicukua niliweza kufika kwa wakwe zangu lakini sikutaka wajue kama niko hai mpaka nitakapomaliza kazi yangu. Kwa mbali nilimuona binyi mdogo kati ya miaka nane na kumi, kwa kweli alikuwa kafanana na mama yake kama katolewa photocopy. Nilitamani kwenda kumkumbatia lakini haikuwezekana kabisa hivo nilimuangalia kwa mbali huku nikibubujikwa na machozi kisha nikajisemea "nisubiri mwanangu muda si mrefu tutaungana tena" kisha nikageuza na kurudi uwanja wa ndege na kurudi Miami. Nikiwa Miami nilianza kufuatilia nyenendo za kila aliehusika na yalionikuta, na kwa kweli kemikali iliyokuwemo kwenye mwiliwalngu ilinisaidia sana maana iliugeza ubongo wangu na kuwa unafanya kazi kama computer. Baada mwezi mmoja nilipata majina thalathini jina la aliekuwa raisi likiwemo, nilianza kujipanga sasa kwa ajili ya ukatili wa hali ya juu. Nilikusudia niwamalize wote ndani ya muda mfupi sana ili nikaungane na mwanangu pamoja na mke wangu mtarajiwa Tania. Niliondoka Miami siku ya pilia asubuhi na kuelekea mjia wa macasio yaani Las Vegas, huko kulikuwa na watu sita katika list yangu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilifika nikakodi nyumba na kuanza mikakati yangu, usiku nilipumzika na asubuhi mapema nikatoka na kuelekea maabara anayofanya kazi yule mwanasayansi aliemuuza mke wangu wangu kwa rais. Nilivomuona tu hasira zikaanza kunipanda, nilitamani nimfate nikamkate vipandevipande halafu nimlee kwa wali mchana. Lakini nilijizuia, kwa vile niliiona gari yake nilisubiri aingiendani nikamuwekee ujumbe mdogo tu. Baada kungia ndani nilifanya hivo kisha nikakaa kwenye mgahawa pembeni, hakupita muda alitoka na kuingia kwenye gari yake huku akitabasamu. Nikajisemea
"laiti ungejua kama leo unakufa wala usingetabasamu", aliondoa gari kwa mwendi mdogo na mimi niliingia kwenye gari yangu na kumfata kwa yuma. Nilipohakikisha amefika mbali kiogo nilitoa simu yangu na kumpigia kwa simu ambayo nilimuekea kama zawadi kwenye gari yake, ilichukua muda kupokewa na alipoipokea alianza hivi
" vipi kuna tenda nyingine nini maana nyinyi kwa kuniwekea simu hamchoki",
"ndio dokta kuna tenda nyingine" nilimjibu.
"ok nambie nikufanyie kitu gani",
"unamjua David Robert Mccanoo" nilimuuliza,
"ndio si yule mpumbavu" alijibu huku akicheka.
"sasa tumepokea taarifa kuwa hakufa siku ile na hivi sasa yupo nyuma anakufatilia" niliongea hivo ili kumtia hofu, nilimuona akianza kuongeza mwendo.
"huna haja ya kuongeza mwendo bwana mkubwa kwa sababu hivi sasa unaongea na David".
"natumai mungu atakulaza mahali panapostahiki" nilongea kisha nikakata simu na hapohapo gari yake ikalipuka na huo ndio ukawa mwisho wake. Watu wengi walikusanyika katika ajali hiyo mimi nilipita na kueleke nyumba niliokodi, niliinfia ndani na kuipiga yake mstari mwekundu nikiimanisha kuwa kazi yake imekwisha.
Usiku nilitoka na kuelekea katika Casino, kama kawaida huwa siendi pahali kama hakuna kitu nnachohitaji. Niliingia ndani kuanza kuangaza huku na kule na hatimae nikamuona mlengwa mmoja, nilisogea mpaka katika eza aliokaa na kukaa meza ya pembeni yake. Kwa sababu nilijua nimtu wa madawa hivo nilitoa kipakti kidogo chenye unga mwupe mezani, alipokiona tu alinipa ishara nimafate bila kuchelewa aliinuka na mimi nikamfata. Alielekea chooni na kwa furaha kubwa nikmfata, nilipofika nilimkuta akinisubiri, nilimpa kile kijipakti nae alikipokea kwa shange na kuchana kisha akalamba ule unga kidogo, "kiasi gani" alinuliza, " nilimuangalia kisha nikamjibu "bei yake ni maisha yako" hapohapo akaaza kutoka damu maskioni,puani,mdomoni na kuanza kukakamaa. nilitoka chooni na kutoka nje kabisa ya casino na kuenda zangu nyumbani kupimzika nikiwa nimebakiza watu wanne tu katika orodha waliokuwepo Las Vegas.
Asubuhi ilifika na bila kuchelewa nilitoka kuelekea kukamilisha kazi yangu maana nilitaka siku hiyo hiyo nisafiri kuelekea Moscow Russia. Na kwa bahati nzuri nilwafumania watatu wakiwa pamoja, katika mgahawa fulani hivi, nilikwenda kukaa pembeni yao na kuagiza kifungua kinywa huku nikiwaangalia kwa makini wanavyofurahia chai yao ya mwisho. Walimaliza na kuinuka kisha wakaondoka, bila kuchelewa niliinuka na kuanza kuwafata mpaka walipoicha njia kubwa na kupita vichochoroni. Kwa vile nyuma sikuwa peke yangu hawakunishtukia, walitokea barabara nyingine kubwa na kuza kwenye kundi la watu na hapo nikaona muda muafaka wakutekeleza mauji ya kisayansi. Kwa mweno wa haraka nilikatiza kati yao na kuwachoma vishindano vidogo nyuma kweye shingo zao. Vishindano hivyo vilikuwa na sumu kali sana inayosababisha mwili kupoteza mawasilia na akili kukosa damu safi, vinauwa kwa sekunde thalathini tu. Ghafla wote walianguka chini na kuanza kupaparika kama samaki waliotolewa majini, nilitabasamu na kabla askari hawajafika katika eneo hilo nilitoweka kama vumbi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilirudi katika nyumba niliokodi na kupanga kila kitu changu kwaajili ya safai ya Moscow, baada kuridhika na kila kitu niliekea uwanja wa ndege na kukata tiket ya usiku kuelekea Moscow. Nilirudi na kuchukua sniper kisha nikaelekea mahala ambapo ningemkuta mtu huyo. Nilifka eneo hilo na kumsaka, kwa mbali nilimuona akitoka katika jengo moja hivi. Nilitafuta gorofa la karibu na kuipanga sniper yangu. Lakini hii ilikuwa tafauti na zile za kawaida, hii ilikuwa ikiendesha kwa computer, baada kumaliza kazi hiyo nilitoa simu yangu na kuiconnect na GPS ya sniper hiyo kisha nikashuka chini na kuelekea alipokwa amesimama. Nilimpa salamu na kumuomba tuongee kidogo, alikubali na tukasogea pembeni. "unajua Mr Hudson upo katika hatari" nilimwambia huku nikijifanya nina wasiwasi, "we nani" aliuliza kwa sintofahamu. "kweli umeenisahau mr" nilimuuliza huku nikimakzia macho, aliniangalia kwa makini kisha akshtuka kidogo na kusema "haiwezekani, wewe ulishakufa siku nyingi" alongea kwa kitete. "vipi kwani unasema nimekufa mbona niko mbele yako" niliongea huku nikisogea pembeni na kumuweka usawa wa sniper ambalo nilikuwa nalicontrol kwa kutumia siku yanugu ambayo nilikuwa nimeshika mkononi na nilipoitazama ilinambia "target locked" kisha nikabonyeza kitufe cha kupiga simu na hapohapo ukaskika mlio wa bunduk, Mr Hudson alianguka vhini huku akiwa na tundu la risasi katika paji la uso kisha nikabonyeza kitufe cha kukata na ghafla sehemu iliokuwepo sniper uliskika mlipuko mkubwa. Kisha nikaungana na watu waliokuwa akikimbia hovyo na kutokomea.
nilirudi katika nyumba niliopanga na kuchukua mabegi yangu, nilirudisha funguo na kuaga kisha nikaondoka. Nilifika uwanja wa ndege na kupanda, hatukukaa sanaa ndege iliacha ardhi na kuwa angani kueleke Russia. Moyoni nilikuwa na furaha sana na pia nilikuwa na majonzi makubwa juu ya mke wangu, usingizi ulinichukua na kulala fofofofooooo. Nilishtushwa na mtingisiko uliotokana na ndege niliopanda kwenda chini kwa kasi sana, nilishtuka baada kusikia kelele za watu wakisali kwa lugha wanazozojua wao wenyewe. Mimi sikuwa mgeni kwenye matukio hayo kwa sababua si mara ya kwanza kupata majanga ya ndege. Kwa mbali nilimsikia rubani akisema tutulie kwenye siti zetu, ndege inatua kwenye maji. Bila kujishauri niliukaza mkanda wangu na kuinama kama maelekezo yanavyosema wakati wa dharura kama hiyo unatakiwa kuegemeza kifua chako kwenye magoti ili kuepuka mgandamizo na mara ndege iligota kwa nguvu juu ya maji na kwa umakini marubani wa ndege hiyo waliweza kuituliza isibiringitie na hatimae tuligota ufukweni. Mlango ulifyetuka na wote tukaabiwa tutoke haraka na bila kuchelewa watu walianza kukimbilia mlangoni, mimi nilitenbea taratibu mpaka nilipofika na kuruka kwa msaada kifaa maalum cha dharura niliteleza mpaka chini.
Hata tulikuwa hatujui tuko wapi maana sehemu ndege ilionguka ilikuwa ni kisiwa tu, baadhi ya abiria walipata majeraha makubwa na kwa wakati huo walikuwa wakipewa huduma ya kwanza. Mimi binafsi sikuumia sana zaidi ya michubuko midogo midogo tu, wakati nikiendelea kutafakari wapi tulipo niliskia kelele kutoka kwenye ndege. Kulikuwa na mtu akiomba msaada ilibidi nisikilize kwa makini sana ili kujua sauti hiyo ilikuwa ikitokea upande gani. Ghafla nilijuta nikitimka tu bila kutarajia kueleleka kwenye ndege, niliparamia lile dude la kuteleza kwa kasi ya ajabu sana japo kuna wakati niliteleza lakini sikukata tamaa. Niliingia ndani ya ndege moja kwa moja na kugundua kuwa sauti ilikuwa inatokea chumba cha rubani, kwa haraka niliusigelea mlango na kuupiga push mara kadha kabla ya kufunguka. Niliingia na kuwakuta marubani watatu wakiwa tayari washaaga dunia na mmoja alionekana ni mweny maumivu makali sana, nilitumia nguvu zangu zote kumtoa katika kiti na kufanikiwa. Baada ya hapo nilimsaidia kwa kumshika begani na kutoka nae nje kisha tukateleza mpaka chini, watu walimpokea na haraka akaanza kupatiwa huduma ya kwanza.
Kwa vile ndege ilianguaka usiku, tulisubiri mpaka asubuhi ili kujua tuko wapi. Kulipambazuka bila kupata hata lepe la i usingizi maana mipango yote nilihisis huenda ikaharibika. Kwa msaada wa black box ambayo inapitikana kwenye ndege tuliona meli na helicopter zikija kwa ajili ya uokozi. Baada ya kutua tu jambo la kwanza nilimbebba rubani ambae hali yake ilikuwa mbaya sana na kumpeleka kwenya helicopter na hiyo pia iliniaptia njia ya rahisi kuingia keny helicopter hiyo na punde ikaruka. Ilielekea moja kwa moja mpaka hospitali ya Saint Petersburg, alishushwa na kuwahishwa chumba cha wagonjwa mahututi huku mimi nikipelekwa kwa ajili ya kupata matibabu madogomadogo. Ukweli sikutaka kukaa hapo hospitali maana nilikuwa na haraka sana, niliwaambia mimi ni mzima na nina uhakika ndugu zangu watakuwa wananisubiria Moscow. Walinielewa na kwa msaada wa helicopter nilipelekwa mpaka uwanja wa ndege na kupandishwa ndege ya mmuda ule kuelekea Mjini Moscow. Masaa machache baadae tulituwa Moscow na moja kwa moja nikaelekea hoteli na kuchukua chumba, nilioga na kubadili nguo kisha nikapumzika. Jioni nilitoka kama kawaida kuelekea mawindoni.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipita duka la silaha na kununua silaha ambazo zingetosha kukimu haja zangu ikiwemo shot gun pamoja na AK47 na sniper pamoja na bastola ndogo mbili. Kisha niliondoka hapo na kuelekea internate cafe, niliwasachi watu nnao wataaka nikagundua kuwa wapo wawili tu. NIlirudi hotelini na kujipanga vizuri kwaajili ya kazi siku ya pili, nilila mapema usiku huo. Mapema siku ya pilia asubuhi nilielekea ubalozi wa marekani uliokuwepo Moscow kwa sababu mmoja alikuwa anafanya kazi hapo. niliziweka silaha zangu sehemu nzuri na kuingia ndani, nilimtafuta pande zote lakini sikumuona. Baada kugundua hayupo nilitoka nje kwaajili ya kujipanga upya, bahati alikuwa ndio kwanza anashuka gari bila kuchelewa nilielekea upande alipo na kumpiga kikumbo kisha nikamuomba samahni. Alikubali na kuelekea zake ndani, lakini kikumbo kilie hakikuwa cha bure. Katika simu yangu kuna programa inayoniruhusu kuiconnect na simu nyingine pindi zinapo gongana tu. Na kwa vilie alikuwa anaongea na simu wakati tunagongana, simu yake ilianguka na kwa kasi ya ajabu niliitoa simu yangu na kuikutanisha na yake hapo ikawa tayari nishaivamia sim yake.
Nilielekea sehemu nilioficha silaha zangu na kuzichukua kisha nikapanda katika gorofa lililokaribu na ubalozi huo. Nilipofika juu nilianza kuipanga sniper yangu na kama kawaida huwa naweka risasi moja tu katika mtutu huo, kisha nikaangalia simu yangu nikagundua sehemu alipo basi na mimi nikabadilisha upande na kuelekea kule ambapo ntampta vizuri kabisa. Baada kuridhika na nafasi niliokaa nilianza kumlenga kwa kutumia darubini ya sniper mpaka pale nilipohakikisha yupo katika kumi na nane zangu. Nilifyatua risasi na kukisambaratisha kichwa huku nikitabasamu kwa kazi nzuri.
Nilirudi hoteli niliopanga na kupumzika huku nikitafakari jinsi ya kummaliza aliebakia, usingizi ulinichukua na ndoto zangu zilikuwa ni za kumwaga damu tu. Asubuhi nilirauka mapema na kupata kifungua kinywa na kutoka kuelekea kwenye kazi ilionipeleka nchini humo. Najua mtajiuliza pesa napata wapi lakini ukweli ni kwamba kutokana na asili ya kazi yangu mimi nina uraia wa nchi nyingi sana takriban nchi zote za zinazounda bara Europe.
Nina uraia wa England, France, Italy, spain na nyingine nyingi tu, na pia nina account nyingi tu ambazo zinapesa za kuniendesha kwa muda wa miaka zaidi ya thalathini mbele kwa sababu kila kazi nilipewa nililipwa mpunga mrefu sana kiasi kwamba hata kama ningesema niache kazi ile basi nigeweza kuishi kwa muda mrefu bila kupata tatizo la pesa. Basi nilianzakuzunguka huku na huko kutafuta kitu ambacho kitanipa muelekeo nianze wapi katika kumsaka huyo mpuuzi. Baada kuzunguka muda mrefu bila mafanikio yeyote yale hatimae nilikutana na gazeti lilisoma kuwa bado the BERGS ni tatizo uturuki, habari hyo ilinivutia na kulinunua gazeti lile. Habari ya ndani katika gazeti hilo imesema kuwa
"bado kikundi cha THE BERGS kinachoongozwa na Louise Millano ni tatizo kwa nchi ya urusi, wamefanya uhalifu katika kampuni kubwa ya vifaa vya umeme na magari" niliishia hapo kusoma maana mtu niliekuwa namtafuta ndie mkuu wa kikundi hicho cha majambzi. Na moja kati ya sera za kikundi hicho ni kwamba ukimapiga mmoja wanakuwinda na hawapumziki mpaka wahakikishe na wewe umekufa.
Akili ilinichemka huku nikiwaza ni mbinu gani nitumie ili kumfikia na kutenda nnachotaka kutenda. Nilianza kufwatilia nyendi zao kwa uakribu zaidi na mwisho nikafikia maamuzi ya kujiunga nao ili niweze kutekeleza kazi yangu. Basi niliendelea kuwafatilia chini kwa chini na siku moja nilikuwa nje ya bank moja hivi, ghafla ilisimama gari moja hivi aina mercedes banz nyeusi na kushuka watu watatu na kuingia bank. Baada dakika kama mbili hivi walitoka na kuingia kwenye gari yao na kuondoka kwa kasi ya ajabu bila kuchelewa niliingia kwenye gari yangu na kuanza kuwafata kwa nyuma. Loooo hawakufika mbali wakagongwa pembeni na gari ya askari, walitoka kwenye gari huku wakimimina risasi na kuwaua maaskari waliokuwepo kwnye gari ile. Bila kuchlelewa nilipita mbele yao na kusimamisha gari na kuwaambia waingie kisha nikaondoa gari kwa kasi huku nikifwata na gari kadhaa za polisi. Lakini kutokana na ufundi wangu mkubwa katika usukani nilifanikiwa kuwatoroka polisi na kufika sehemu salama kisha nikasimama na kuwaambia washuke niondoke. Basi hapo hapo mmoja akatoa bastola na kuniekea kichwani kisha akanambia niendeshe gari, sikubisha kwa sababu hicho ndio nilichokitaka na mimi ndio niliowapigia polisi simu na kuwapa maelekezo njia waliopita. Basi bila kuuliza huku nikionyesha kutetemeka niliondoa gari huku nikifata maelekezo wallionipa mpaka tukafika katika jengo moja kubwa hivi. Hapo walinambia nisimame na nishuke kwenye gari, bila kuhoji nilifanya hivyo. Mmoja wao alinishika na kunivuta akielekea ndani, sikuonesha ugumu wowote ule. Tuliingia ndani huku wakiongea kwa sauti ya chini chini, nilipigwa na bumbuwazi baada kuingia ndani na kuona umati wa watu ambao ni wanachama wa kikundi hicho. Kwa mbali nilimuona mtu aliekaa kwenye kiti na kwa haraka sana niligundua kuwa ni Mr Louise Millano. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuja mpaka walipo wale wawili pamoja na mie, walimkabidhi pesa walizoiba na kila mmoja akapewa bunda moja nono la pesa. Aliniangalia sana na kuwauliza wale wawili "huyu ni nani na inakuwaje yuko hapa" kwa hasira. "ah bosi huyu ametusaidia baada gari yetu kugongwa na polisi" mmoja aliongea kwa kigugumizi, aliangalia tena kisha akaniuliza "kijana unaitwa nani", "naitwa Hilarove Gregovic" nilidanganya jina langu. "IMekuaje ukatoa msaaada wakati unaju kabisa kama ungekamatwa ungehukumiwa kifo" aliendelea kunuliza, "ah mi nimechoka kuishi maisha ya kudhalilika". "kivipi"alihoji tena "mimi ni dereva wa taxi tu hapa Moscow lakini nimechoka kuishi maisha ya utumwa na leo wakati nasubiria abiria ndio nikaona gari ikigongwa na polisi ndipo nilipowaona hawa wakitoka na kuanza kuwashambulia polisi, nikaona bora niwasaidie kwa sababu hata wao ni kama mimi wanatafuta riziki japo njia yao ni ngumu, ukweli nilishindwa kuvumilia kuona vijana wenzangu wadogo wakiingia mikononi mwa polisi hivyo nikawapa msaada kwa kuwatorosha pale" nilijibu kwa kujiamini sana. Basi alianza kupiga makofi na wengine wakafuata, kisha aliwatuliza na kuongea "karibu kwenye kikosi, karibu THE BERGS". Nilifurahi sana na kujisemea moyoni laiti kama angejua anakikaribisha kifo wala asingenipongeza, maana alikuwa anamkaribisha izraieli katika maisha yake.
Kuanzia siku hiyo nilianza kufanya nao kazi na kwa muda mfupi nilijizolea mapenzi ya kutosha kutoka kwa bosi wangu ambae pia ni adui yangu mkubwa. Hayo yote yamewezekana kutokana na kuwa mimi nilikuwa si mgeni kwenye mchezo huo. Kuna mara moja tulipewa mchongo wa kwenda kuiba mabilioni ya mapesa katika bank moja hivi, hapo nilitaka kuonyesha uwezo wangu katika kuendesha gari. Niliomba kitengo cha kutoroka na pesa hizo nae akanikabidhi kwa roho safi, mapema siku iliofuata tulitoka kambini na kuelekea kwenye bank hio. Mimi nilibaki nje nikisubiri mzigo uletewe na mara walitoka na mifuko kadhaa mikononi huku wakiongozwa na Mr louise Millano. Waliingiza mifuko ya pesa kwenye gari yangu na Mr Louise aliingia siti ya mbele na kunambia niondoe gari.
Kwa kasi ya ajabu niliondoka huku nyuma nikifatwa na wenzangu,na haukupita muda polisi walikuwa nyuma yetu wakitufukuza. Nilimgeukia Mr Louise na kumambia afunge mkanda maana sasa itakuwa pata shika nguo kuchanika. Alifanya hivo na hapo sasa nikakanyaga mafuta na kuanza kuzungushana na maskari lakini nia yangu ilikuwa ni kupotezana na wengine ili nikamalize kazi yangu. Mara kadhaa nilishuhudia gari za wenzangu zikipata ajali, lakini niliendelea kusepa zangu huku askari wakiona kutokata tamaa. Nilindelea kucheza na usukani kwa uzoefu wa hali ya juu huku nikijitahidi kuwakwepa askari pamoja na kukwepa miba wanayo weka njiani. Nilizungushana na polisi kwa muda wa dakika thalathini na nilipohakikisha nimepotezana na wenzangu wote ndipo nikaamua kuwatoroka askari, na Kwa sababu nilizijua njia za vichochoroni nyingi haikuwa shida sana. Nilifika katika jengo moja na kuingia ndani kisha nikasimama, "hapa ni wapi" aliuliza Mr Louise. "tulia bosi subiri joto la polisi liishe halafu tutaondoka" nilimjibu huku nikimuangalia kwa makini usoni. "kama unata maji angalia siti ya nyuma" nilongea na kushuka, na kwa kweli baada mshike mshike ule lazima uhisi kiu. Basi aligeuka nyuma na kuchukua chupa ya maji na kunywa, kisha alishuka kwenye gari na kuanza kuelekea nipokuwa nimesimama. Hatua ya kwanza, ya pili , ya tatu akaanguka chini na kupoteza fahamu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuja kuzinduka baada kumwagia maji ya baridi usoni, "we ni nani na yuko wapi Hilarove" hilo ndio swali la kwanza alilouliza, nilicheka kidogo na kuongea " Jina langu ni David Robert Mccanoon au ukipenda pia unaweza kuniita Hilarove". Alishtuka baada kusikia kauli ile, najua utajiuliza kwanini kanisahahau lakini baada kuamua kujiunga nao nilianza kufuga ndevu nyingi na nywele ili kuficha sura yangu halisi. Jasho lilianza kumtoka huku akioneka akijibizana na akili yake kuhusu jambo fulani, nilitoa bastola ndogo na kuifunga kiwambo cha kuzui sauti kisha nikamwambia "ukifika huko kwa mungu nisalimie na wenzako saba kisha waambie wasijali kwani waliobaki wote wataungana nanyi muda si mrefu. Nilipomaliza nilimtandika risasi kadhaa za kifua mpaka nilipohakikisha hapumui tena, ndipo nikambeba na kumuingiza kwenye gari iliokuwa na pesa. Nilikamata usukani na kuondoka mpak karibu na kitu cha polisi kisha nikapiga simu na kuwapa taarifa juu ya gari hilo. Mimi mdogomdogo nikasepa na kwasababu nilishaanyowa nywele hakuna alienijua. Huyo ndo mimi bwana mzee wa kumwaga damu na kuuwa ndio starehe yangu.
Nilirudi hotelini na kupimzika, usiku uliingia na taarifa iliopamba moto ni kuuwa kwa kiongozi wa kikundi hatari cha THE BERGS. Serekali ilitoa sana shukrani za dhati kwa aliemuuwa mtu huyo, nilitabasamu kidogo kisha nikatoa simu yangu ambayo ni satellite phone. Nikisema hivi namaanisha kuwa simu hiyo ni aina ya simu ambayo haiwezi kugundulika kwa kutrack. Niliandika ujumbe mdogo wa maneno uliambatana na ramani kisha nikautuma makao makuu ya jeshi la polisi la urusi. Baada hapo nilala usingizi mwanana kabisa , nilikuja kushtuka asubuhi baada simu yangu muita, nilipoiangalia niligundua aliekuwa anapiga ni Tania kipenzi cha roho yangu na asali wa moyo wangu. Niliipokea kwa tabasamu kisha tukaongea machache, baada ya kumaliza mazungumzo niliingia chooni na kujimwagia maji. Nilimaliza nikajiandaa na kutoka, nilirudisha funguo mapokezi na kuaga kisha nikatoka hotelini hapo na kuingia katika mgahawa wa karibu na kupata chai nzuri ya asubuhi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment