Simulizi : C.O.D.EX. 1
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimaliza na kuchukua taxi na kuelekea uwanja wa ndege, nilikata ticket ya kuelekea mjini Hong kong kwa ajili ya kufa kama nilivyofanya urusi na kwengineko ambako nimepita. Ndege ilitua mjini Hongkong, nilishuka na kuelekea nje ya uwanja huo. Nikavhukua taxi mpaka hotelini na kuchukuwa chumba, kitu cha kwanzo baada kuingia chumbani humo niliwasha tv na kuangulia BBC. Habari iliokuwa imepamba moto ni ya kukamatwa kwa kikosi kizima cha BERGS, na serekali ilikuwa ikitoa shukrani kwa msamaria mwema alietoa ramani ya kufika katika kambi yao lakini kilichonishtua ni baada kuona taarifa ikisema kuwa bado mmoja hajakamatwa na anaitwa Hilarove Gregovic na picha iliowekwa ni ile nlokuwa na madevu. Sikuitilia maanani japo ilinishtua, niliingia chooni na kujisafisha then nikavaa nguo nzuri na kutoka kuelekea katika harkati zangu za kawaida. Kupitia msaada wa google nilifanikiwa kuwapata watu niliokuwa na haja nao, lakini kilichimiweka njia panda ni kwamba watu hao takriban ishirini kati ya ishirini na mbili wameuwawa. Sasa walibakia wawili tu nilamuwa kuwasaka kwa udi na uvumba ili niwafikie mimi mwanzo, nilifanikiwa kupata anuani ya mmoja wao na bila kupoteza muda nilianza safari ya kuelekea kwake. Nilipofika nilijitanbulisha kama mwandishi wa kujitegemea na nlikuwa nahitaji kuongea nae mawili matatu. Alikubali bila kipingamizi, tuliingia ofisini kwake kwa ajili mahojiano hayo.
Nilimuuliza kuhusu kuuwawa kwa wenzake, alichonijibu kilinifanya nikae vizuri ili nisikose kitu. Japo tulikubaliana nisiirekodi kitu lakini ukweli ni kwamba katika shati langu kulikuwa na kamera ndogo mithili ya kifungo na wala hakikuwa tofauti na vifungo vingine katika shati hilo. "Najua hata mimi mua wangu wa kufa ushakaribia sina budi kukwambia ukweli kuhusu mauaji ya wenzangu ishirini, ukweli ni kwamba miaka takribani kumi iliopita tulishiriki kitendo kibaya sana kwa kumtumia kijana aliekuwa ni agent wa siri wa marekani na sniper mzuri sana. Kwa sababu ya tamaa zetu tulimfanya auwe watoto zaidi ya mia moja ili kuzitia matatizoni nchi mbili amabazo kwa muda mrefu zimekuwa na ugomvi lakini mwishoni walitaka kumaliza ugomvi wao kwa kukaa na kuzimaliza tafauti zao. Lakini sisi kama mataifa makubwa tulijua kabisa ikiwa watakubaliana kuishi kwa amani kati yao basi tungekosa sehemu za kuuza silaha na kuiba rasilimali nyingi sana ambazo tilikuwa tukizifaidi kipindi chote cha mapigano yao ambayo pia chanzo kilikuwa ni amtaifa mkubwa. Basi tulitowa tenda kwa madaktari bingwa ili watengeze kemikali ambayo ingeweza kumfanya mtu aweze kutii bila kuuliza maswali yeyote yale, na tulifanikiwa.
Baada ya hapo tuliwarubuni vijana watano ambao tulitaka kuwafanya kama majaribio ya kemikali hiyo ambayo haikuwahi kutumika katika mwili wa binaadamu. Tulikwenda nao mpaka karibu na nchi moja kati ya zile mbili na kufanya majaribio lakini matokeo yalikuwa mabaya kati ya wale watano mmoja tu ndie aliepona na kemikali ile ikafanya kazi yake, nakumbuka yule kijana aliitwa David Robert Mccanoon na ndie alietumika kufanya mauaji yale ya kinyama huku akijifanya ni mwananjeshi wa nchi zile kwa nyakati mbili tafauti." mpaka hapo mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio na kijasho chembamba kilianza kunitoka japo chumba hicho kilikuwa na ac.
"nikiongea hivyo namaanisha kuwa kuna baadhi ya wakati alivaa kama askari wa nchi moja na kuuwa watoto wa nchi jirani na wakati mwengine alivaa kama asakari wa nchi waliouwawa watoto na kuuwa wale wa nchi nyingine. Kazi iliendelea kuwa hiyo mpka tulipohakikisha ugomvi umeanza upya ndipo tuliamua kurudi kila mtu nchini kwake. Miaka mingi imepita mpaka havi karibuni kukatokea mtafaruku kati yetu na hapo ndipo mauwaji yalipoanza na anaetoa amri hizo ni....." kabla hajamaliza alidondoka chini huku kukiwa na tobo kubwa la risasi iliopenya sawa sawia usoni katila paji la uso. Kwa upigaji ule ilikuwa niwazi kabisa muuaji ni mzoefu nabila kupoteza muda nilichomoka kutoka kweny kiti nikaruka kupitia dirishani na kuanza kukimbia upande uliotoka risasi na kwa mbali niliweza kumuona mtu akiwa katika mavazi meusi.
Moja kwa moja nilijua ndio mwenyewe na kuanza kumuungia, kutokana na kemikali niliokuwa nayo mwilini ilinisaidia na kunipa uwezo mkubwa wa kukimbia bila kuchi mapema. Nilipomkaribia nilimchota mtamaa na kumfanya aanguke kama mzigo, nilimshindilia ngumi za kutosha baada ya kufika huku nkimhoji nani aliemtuma kufanya kazi hiyo. Hakujibu chiochote zaidi ya kuniangalia tu usoni, nikaona isiwe tabu nilimgonga kweny mshipa wa fahamu na kumkata network kisha nikaondoka nae. Nilikwenda nae hadi sehemu moja ya siri na kumuseka hapo kisha nikaelekea hotelini kuchukua zana zangu za mateso. Nilifika sehemu niliomuacha na kujianda vizuri maana lazima ukweli niupate hata kama kwa kutoa tone mojamoja la damu katika mwili wake. Nilimgusa tena sehemu ileile na ghafla akazinduka "kijana naomba unieleze kishkaji tu nani aliekutuma, mimi sina haja ya kukuuwa" niliongea uku nikivaa gloves, "hahahahahahaha" alicheka kwa nguvu "hivi we unajua kama unadili na muuaji wa kimataifa" aliongea kwa kujiamini. Nilimwangalia kisha nikaachia tabasamu zito "dah nilikuwa sijui lakini na wewe unajua unaongea na mtu ambae dunia nzima inamtafuta", alishtuka kidogo "muda wa kujigamba umekwisha,sasa utasema au nikufanye useme" niliendelea kuongoea lakini wakati huu nilivaa sura ya kikatili "kama unaweza nifanye niseme" alijibu kwa kejeli.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilifungua begi yangu ndogo na kutoa nguo iliozungusha kisha nikaitandaza kwenye meza, alivoona vitu vilivyokuwa ndani alianza kucheka "ndio utanifanya niseme kwa kutumia sindano". "ndio na utasema tu" nilimjibu kiulaini kisha nikatoa koleo ndogo, nilimsogelea na kumbana kucha kwa koleo "nambie umetumwa na nani". Akanitemea mate usoni, bila kuchelewa niliivuta kucha ya kidole gumba na kuinyofoa, alipiga kelele za maumivu lakini wala sikushtuka.Nilisogea mkono mwengine na kuibana kucha ya kidole gumba cha mkono huo kisha nikamuuliza tena, muda huu alinitukana basi nikarudia tena zoezi lile nikaing'oa kucha ile kisha nikarudisha koleo kwenye ile nguo na kucgukua kisu kidogo cha kufanyia operesheni na kumsogelea. "bado tu hutaki kusema" nilimuuliza tena, "nimeshakwambia kuwa utaambulia patupu hapa" alijibu jabo kwa tabu. "ulishawahi kumuona mnyama akichunwa ngozi, basi na mimi ntakuchuna ngozi tena bila ganzi" nilongea nikiwaserios kabisa. Nilimshika mkono wa kulia na kuanza na kwa kutumia kisu kile kidogo, nlikiingiza katika ngozi na kuanza kazi ya kuibandua ngozi kutoka katika mwili. Alipiga kelele mpaka lakini wala hazikunshtua "nitasem,nitasema nakuomba acha kufanya hivyo" aliongea kwa kwikwi. "ah sasa ungesema mapema yasingekukuta haya yote" niliongea huku nikirudisha kile kisu. "ok ongea sasa" nilivuta kiti na kukaa, huku nikimuangalia usoni maana nilielewa katika hali ile akiongea uongo tu nitajua.
"mimi ni mwanajeshi wa U.S.A na niwasiri kutoka katika kitengo cha CIA , nimepewa kazi hii ya kuwaua wote waliohusika katika Project code x na alienipa kazi hii ni raisi mstaafu" alimaliza, "sasa ungesema mapema yote haya yasingekukuta" nilongea huku nikiinuka na kuelekea kwenye ile nguo na kutoa pini mbili ndogo. "hivi vipini vitakusaidia kupunguza maumivu, lakini vitakupa usingizi kwanza na utakaposhtuka nenda kamwambia aliekutuma kuwa David Robert Mccanoon anakuja" aliposkia jina langu alishtuka bila kumruhusu kuhoji zaidi nilimchoma vile visindano na hapo hapo usingizi ukamchukua.Na kwa sababu sikuwa na nia ya kumuua basi nilimpatia huduma ya kwanza na kumueka GPS tracker katika sehemu ambayo nilijua haitoshtukiwa,kisha nilimfngua kamba. Bila kuchelewa nkasepa zangu. Nilirudi hotelini na kupanga kila kit changu kwaajili ya kumafatilia kila atakapo kwenda. Masaa mawili baadae GPS tracker iliwaka kwenye simu yangu na hapo hapo nikatoka na kuelekea kwenye gari yangu. Bila kuchelewa niliiwasha na kuanza kuelekea kule iliponionyesha simu yangu, niliendelea kufwatilia mpaka nilipofika nje ya nyumba alioingua yule kijana. NIliipaki gari pembeni na kusubiria atoke, masaa mawili baadae alitoka na kuingia kwenye gari yake na kuondoka na mimi bila kuchelewa nilimfata. Alielekea uwanja wa ndege, "hapa leo mpaka kieleweka,utakapoelekea mi ntakua nyuma yako kasoro kaburini tu" nilijisemea moyoni na mwisho nikajifanyia utani.
Alishuka na kuingia ndani ya uwanja huo, nilisubiri mpaka kashapita mlangoni na mimi nikashuka kweya gari na kuchukua begi langu kisha nikavaa kapelo na kuilekea ndani ya uwanja wa ndege. Kwa msaada wa kile kifaa nilichomuekea niliweza kugundua yuko wapi, nilishtuka baada kuona tiket aliokata ni ya kuelekea nchi za Africa. Na mimi nilikwenda kukata tiket na kwa sababu tulipishana kwa karibu niliona kuwa amekata tiket ya kuelekea nchi moja miongoni mwanchi zilizojaa amani duniani japo ilikuwa na maisha duni. Nchi hiyo ni inajulikana kwa jina la Tanzania. Machale yalianza kunicheza kwa nilivyosoma Tanzania ni miongonimwa nchi zenye vito vingi sana yakiwemo madini yaliobeba jina la nchi hiyo maarufu kama tanzanite na pia kunapatikana madini hatari aina Uranium yanayotumika kutengeneza mabomu ya nyuklia. Basi muda ulifika tukapanda ndege na safari ikaanza, safari yote sikupata usingizi kwani niliwaza itakuwaje ikiwa nchi kama ile ikiingia matatizoni na amani walioilinda kwa miaka mingi ikitoweka itakuwaje, maana ni wazi kama yule mshenzi atakuwa Tanzania basi ni lazima atakuwa anataka kufany mchezo mchafu. "kweli katika maisha yangu sijafanya hata moja zuri lakini nitahakikisha nchi ya watu haingii matatizoni kwa sabau ya tamaa za huyu fisi" nilijisemea moyoni huku mwili ukinitetemeka kwa hasira.
Ndege ilikanyaga ardhi ya Tanzania na abiria wote waliokuwa wakishuka hapo wakashuka, nilitoka huku nimevaa kapelo yangu hivyo kunifnya nisitambulike. Nilimfata mpaka nje ya uwanja huo huo wa DIA, aliingia kwenye gari na kuondoka mimi nilichukua taxi na kumwambia awafuate lakini kwa umbali kidogo. Safari ilikuwa ndefu kutokana na foleni kubwa iliokuepo katika jiji maarufu la Daressalaam, walifika sehemu ya kuvuka na kulikuwa boti ndogo za mwendo kasi mbili zikiwasubiri. Nilishuka na kumlipa derva pesa yake kisha taratibu nikasogea maeneo ya ambayo niliamini ndio mlango wa kuingilia katika pantoni. Mbele ya watanzania waliokuwa katika eneo hilo nilikuwa kama mtalii na hata mimi nilitaka iwe hivyo na mara kadhaa niliwahoji vijana ambao nillikuwa nao karibu kuhusu utamaduni wa nchi yao na kwa hali gani wanapambana na maisha ya kupigwa na jua tokea wanapoamka mpaka wanapokwenda kuupitisha usiku. Kwa kweli nilishangazwa na baadhi ya majibu ya baadhi yao, na nilistaajabu sana inakuaje mtu anaweza kuishi na kiwango kidogo cha fedha chini ya dola moja ya kimarekani. Katika ongea ongea yangu nilikutana na kijana mmoja ambae alinifurahishwa kwa uchangamfu wake. Alionekana ni msomi kidogo maana hata kujibu kwake maswali alikuwa akijibu vizuri sana. Tuliongea mengi mpaka pantoni lilipofika upande wa pili ambapo kwa jina paliitwa kigamboni. Nilimuomba anitafutie nyumba nitakayokaa kwa muda wote nitakaokuwa nchini humu, hakuwa nyuma tulihangaika kwa pamoja mpaka tukapata nyumba. Yeye alinisaidia katika kuwasiliana maana kiswahili nilikuwa sikijui hata kidogo. Nilimlipa kiasi kadha cha fedha na kumwambia kuwa makutano yetu mimi na yeye yawe ni siri.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya hapo tuliagana na yeye akaondoka zake, niliingia ndani na kujiweka sawa kabla kuanza kazi ya kuwasaka maadui zangu. Kutokana na joto kali nilioga na kuvaa nguo nyepesi kama hali ya hewa ya nchi hio inavotaka. Nilipomaliza nilitoa computer yangu na kuiunga na internate kupitia satellite ya CIA na kwasababu nilikuwa hacker mzuri nilifanikiwa kuifunga kabisa ili wasijue nani aliehaki satellite yao. kisha nilitoa simu yangu na kuiconnect na computer yangu, nikaanza kutumia elimu yangu mpaka nikajua walipowweka kambi yao. Nilifanikiwa kuhack system yao nakuchunguza kila kitu kunaziz njia mpaka kila mtu aliehusika na kambi hiyo. Baada ya kuridhikka na taarifa nlokuwa nilizozipata,niliamua kupumzika ili siku ya pili niangalie uwezekano wa kupata silaha nzito kwaajili ya kazi hiyo. Huku nikisindikizwa na kiyoyozi usingizi ulinichukua ghafla tu, nilikua kushtuka baada kupiagwa na miale ya jua usoni. Kwa kujikongoja niliamka na kuelekea chooni kwaa ajili ya kujisafisha, dakika kumi baadae nilitoka na kubadili nguo kisha nikavaa ndevu za bandi pamoja nasharubu ambazo zilinibadilisha na knifanya kama mkoloni. Bila kuchelewa nilitoka na kuelekea katika maeneo kambi hiyo ilipo, nilijifanya nazunguka tu huku nikiangaza sehemu mbali mbali. Nilijua kabisa itakua shida kupenya katika kambi hasa ukiziningatia katika nchi ile kupata silaha itakuwa ngumu. Lakini ilikuwa ni lazima nipenye tu kwa gharama yoyote ile, niliumiza sana kichwa nikifikiria njia ambayo nitaingia bila kuonekana.
Katika kufikiria sana nikagundua ipo njia ila ni lazika nipate gwanda za mmoja kati ya wanajeshi wanaolinda kambi ile. Nilisubiri hadi usiku ulipoingia nikavaa nguo nyeusi na kufunika uso wangu kama ninja kisha nikatoka kimykimy bila hata kushtukiwa. Nilijibanza pahali kwa umakiniwa hali ya juu sana ili ikitokea akapita mwaajeshi yeyote yule basi atakuwa mali yangu. Baasa kama nusu saa hivi alipita mmoja akiwa anaongozana na mwanamke na nilipowatazama vizuri niligundua kuwa alikuwa amelewa tilalila. Hiyo ndio ilikuwa nafasi pekee nilinza kumfatilia kwa taratibu na kwa umakini wa hali yajuu sana. Nilipofika sehemu nikaona muda wa kuchukua gwanda zangu umefika, nilimvamia kwa nguvu na kumgonga shingoni kitendo kilicomfanya apoteze fahamu kabisa, na yule mwanamke nimminya kwenye sehemu ambayo nilijua akiamka hatokumbuka chochote kilichotokea usiku ule. Baada hapo nilimbeba na kurudi nae nyumbani kwangu, nilimuingiza katika chumba kimoja na kumfungia humo lakini kabla ya kutoka humo nilichukua finger print zake na kwenda nazo kuzifanyia uchunguzi, hiyo ilikuwa ni kwaajili ya kusoma tabia zake. Na kwa utaalamu wangu nilitengeza kifaa kidogo ambacho nilikiweka shingoni kwa ajili ya kuiga sauti yake. Nilirudi yena kule ndani na kumpiga picha kisha nikaitia kwenye computer, nilifanya nnavo jua mwenyewe na kuchukua kifaa ambacho nilikuwa nacho muda mrefu, kifaa hicho kilikuwa maalum kwa kubadlisha sura. Nilikivaa nyuma ya sikio na kukiactivate, papo hapo sura yangu ilibadilika na kuwa kama ya yule mwanajeshi. Niliporidhika na maandalizi hayo nilisubiri mpka asubuhi nakavaa gwanda za yule mwanajeshi na kuelekea kambini.
Nilipofika getini nilionesha kitambulisho changu na kuruhusiwa kupita,nilitabasamu kama ishara ya kushukuru na kwa vile nilizisoma tabia zake zote hivo kwa msaada wa kifaa maalumu nilliweza kuzivaa tabia hizo jambo ambalo lilinifanya niwe kama yeye tu kwa kila kitu. Nilielekea mpaka kwanye chumbaa alichokuwa anakaa na kuvua gwanda zile kisha nikavaa nyingine. Nikiwa chumbani humo aliingia mwanajeshi mwengine na kuongea "sergnt Jones unaitwa na bosi", bila kuchelewa nilitoka na kuelekea ofisini nikakuta kikao cha dharura, nilisalimia na kuungana nao na aliekuwa anaongwa hakuwa mwengine bali ni raisi mstaafu "hapa mambo mawili makubwa, la kwanza ni kwamba tumetumia mbinu zote kutaka kuanzisha vurugu lakini inaonekana kama ilivyosifa ya watu hawa kuwa vurugu kwao ni mwiko lakini la pili ambalo huenda likawa kikwazo kikubwa ni kwamba yule kijana tulimtuma Hongkong ameleta salamu kuwa David Robert Mccanoon yuko hai na kama hivo nikweli basi nilazima atakuja tu huku. Na shughuli ya huyu mpuuzi si ndogo maana kuuwa kwake ni jambo dogo sana na wala halimuumizi kichwa. Ili kuepuka yote haya sasa inabidi tuje na mbinu mpya ili tufanya kazi mapema na kila mtu arudi kwao. Mbinu yenyewe ni kwamba, tufanye matukio ya kigaidi kisha lawama tuzipeleka kwa kikundi maarufu cha kigaidi cha Al-shabaab". "una maanisha nini bosi" niliuliza kwa kujiamini, aliniangalia kisha akatabasamu na kuongea "ninachomaanisha ni kuwa, tutatega mabomu na kuripuwa na target ya kwanza ni mji huu wa Daresalaam. huu ni mji wa kibiashara na umejaa watu wa aina mbalimbali hivyo na ikisadikika kuwa ni kitendo cha kigaidi basi watalii wataanza kurudishwa katika nchi zao kisha tufanya tena hivo katika visiwa vya Zanzibar, Arusha, Dodoma pamoja na morogoro. Matukio haya yatasababisha nchi kuingia machafuko na hapo ndio tutakapoingia sisi kwaajili ya kuwapa msaada na masharti tutakayowapa ni kutuurusu kuchimba madini ya Tanzanite pamoja na Uranium" alimaliza kuongea wote tukapiga makofi, "kazi itaanza lini" aliuliza mmoja kati ya watu waliokuepo katika kikao hicho. "mabomu yatawasili mwishoni mwa wiki hii na punde yatakapofika basi kazi itaanza, kwa heri amani ya Tanznia kwa heri furaha" aliongea maneno hayo watu wote wakayarudia nikiwemo na mimi na kikao kiliishia hapo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilirudi chumbani kule nikiwa na mawazo kibao maana nilijua nikifanya mchezo kweli watafanikiwa mipango yao hivyo nilitakiwa kuisambaratisha kambi hiyo ndani ya siku tatu kwa sababu ndizo zilizokuwa zimebaki mpaka kuwasili kwa mabomu hayo ya kuangamiza amani ya nchi ile. Maongezi yote niliyarikodi bila mtu kujua, usiku ulifika na kama kawaida yake sergent Jones huwa anatoka kwenda kunya kidogo na kulala na wanawake wa kiswahili. Basi na mimi nilitoka na kuelekea nyumbani kwangu, niliingia katika kile chumba nilichomuweka na kumkuta akiwa macho. "habari yako pacha wangu" nilimtania "we nani" aliuliza kwa hasira, "mimi ni kifo chako" nilimjibu na kutabasamu kisha nikatoka ndani ya chumba hicho.
Siku ya pili mapema nilirudi kule kambini kwaajili ya kuanza mipango ya kuisambaratisha, na kutikana na cheo basi sikusachiwa hata kidogo. niliitumia nafasa hiyo kuingia na nyaya kadha pamoja na vitu muhimu vya kutengenezea mabomu. Kutengeneza mabomu nimejua kwa sababu ni moja kati ya kozi nilizopewa kipindi nataka kuwa sniper. Nilifanya kila kitu changu nikijuwa zimebakia siku mbili tu mpaka mabomu yafike nchini humo. Usiku siku hiyo sikutoka kama ilivyo kawaida, na pia sikulalala nilizunguka zunguka na kujichanganya na wenngine lengo na madhumuni ilikuwa ni kukagua eneo zima ili kwanza nijue wapi kunakaa silaha maana naelewa kuwa ili kumpunguza nguvu adui yako ni lazima umnyang'anye silaha kwanza. Na kweli nilifika kwenye ghala la silaha na kushangazwa na silaha nzito zilizokuwemo katika ghala hilo vikiwemo vifaru ambavyo tayari vimesachorwa bendera ya Al-shabaab, niilkuta na nguo ambazo wanazivaa Al-shabaab katika kutekeleza mashambulizi. Niliangalia kushoto na kulia na nilipoona hakuna mtu mwengine kwenye ghala, nilitoa vitu kama vigololi viwili na kuviingiza kwenye boxi la mabomu aina ya grenade. Vigololi hivo ni mabomu madogo sana lakini ya uwezo wake wa kuripuwa ni mkubwa sana, baada kuviseti niliondoka na kurudi chumbani kwangu. Nilipofika nilianza kutengeza mabomu mengine aina ya C4, natumai wengi mtakua mnaelewa kasheshe ya bomu hili. usiku mzima sikulala, nilihakikisha paki pambazuka niwe tayari nishaakamilisha kazi ile maana siku zilikuwa hamna tena. Ilibakika siku moja tu kabla ya ndege inayokuja na mabomu kufika. Siku nilipanga nikitoka kambini hapo natoka kama sergent Jones lakini nikirudi narudi kama David Robert Mccanon. Asubuhi mapema niliamka na kuungana na wengine katika mazoezi na kwa sababu hata mimi mwenyewe nilitrainiwa na jeshi la marekani hivyo niliafahamu mazoezi yote vzuri sana.
Baada ya mazoezi nilirudi chumbani na kujimwagia maji, baada ya hapo nilikula gwanda safi na wakati nasachisachi nikafungua box fukani hivi na kukuta yale mambo nnayoyapenda. Kulikuwa na pistol semi-auto, revolver, shotgun, mashine gun six rounds, AK47 pamoja na mwana nimpendae kuliko wote sniper.
Nilijkuta nikitabasamu bila kutaka lakini swali likawa ni jinsi ya kutoka nazo humo kambini maana huruhusiwi kutoka na silaha. Niliumiza sana akili maana kwa wakati nilizihitaji kuliko kitu kingine chochote "nitatoka nazo tu" nilijisemea na kutafuta begi la kutilia silaha nikaanz kuziweka humo, ilibidi nizipangue ili kuepuka kushtukiwa. Kazi hiyo niliifanya kwa nusu saa, mara mlango ukagongwa. Nilipofungua nikakutana na kijana
“sergent unahitajika chamber kuu" aliongea na kuondoka, nilijiandaa na kuelekea huko, nilipofika nilikutana na raisi mstaafu akanipa karatasi na kunambia nchukue vijana wengine watatu tuelekee baharini sehemu ambayo ndege ndio ingetua kwaajili ya kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kufika kwa ndege hiyo ambayo itatua baharini.
Niliitika na kutoka na kuelekea sehemu ya mazoezi, niliwakuta wanajeshiwengine wakiwa wapiga story. Bila kuchelewa niliwaita wanne na kuwaambia wajiandae, waliitika na kuelekea vyumbani mwao na mimi nilikwenda chumbani kwangu na kubeba lile begi. Mpaka hapo niliona Mungu yuko karibu nami, nilitoka na kuelekea sehemu ya magari na kuwakuta wakinisubiri. Naam na kila mmoja alitoka kamili gado maana ilikuwa ni kuweka ulinzi. Tuliingia kwenye gari na kutoka kambini kwa mwendo mdogo, haikuwa ngumu kufika sehemu ile. Tulipofika nikatoa ile barua na kusoma
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" hakikisha vijana ulowachukua ndio wanaobeba mabomu na kujitoa muhanga, tumia jina la nchi yetu kuhakikisha wanakubali na wakikataa wauwe wote" nilishtuka sana baada kusoma ile barua mpaka wale vijana wakaniuliza imeandikwa nini.
"mnajua tunalotaka kulifanya ni hatari sana" niliwauliza,
"ndio lakini tunafanya kwa ajili ya nchi yetu" mmoja wao alijibu.
"Ukishafanya kwa ajili ya nchi yako wewe unalipwa nini" nilimuuliza kwa hasira kidogo, alikaa kimya.
"Nikikwambieni kuwa mimi sio sergent Jones mtaamini" niliwauliza tena, walicheka kidogo wakizani nafanya utani.
"najua mtakuwa mshawahi kusikia kuhusu mtu anaeitwa David Robert Mccannon" niliwauliza tena "dah! naskia huyo jamaa ni hatari hata awepo mita miatano hakukosi na sniper yake" mmoja alijibu
"halafu naskia anachapa mbaya yaani ni hatari kuliko ukoma" mwengine alidakia,
"halafu naskia ni mtaalamu sana na anaweza kujibadilisha kuwa mtu yeyote yule" mwengine aliongea na ghafla wote wakanyamaza na kuniangalia. Baada kuona wakiwa na waswas na hapo ndio nikavua kile kinyago kisha nikwapa ishara wasijaribu kuto kunyanyua silaha zao "huyo David ndio mimi, lakini kawaida yang huwa siuwi mtu ambae sijakusdia" niliwaambia na kidogo wakapumua maana waliona hali ilishakuwa mbaya. Kisha nikawarushia ile karatasi, baada ya kuisoma walitumbua macho kama mijusi waliobanwa na milango.
"hiyo ndio faida mnayoipata kwa ajili ya kuitumikia nchi yenu, nyie mnakufa huku wenzenu wakirudi nyumbanii wanapandishwa vyeo na nyie picha zenu zinavalishwa maua na kuwashiwa mishumaa halafu wanasema hawa wameuza maisha yao kwa ajili ya nchi hii halafu mnasahaulika kabisa" niliwaambia na kuonekana maneno hayo yamewaingia kisawasawa vichwani. Baada ya hapo niliwasimulia mkasa wangu wote na kuwashishi kuungana na mimi ili tufanye kazi ya kuikimbo nchi isio na hatia kuingia matatani.
Walikubali kwa moyo mmoja, tulikubaliana kuwa ikifika ndege tunawateka marubani kisha wao wanne wanaondoka na ndege ile kurudi nayo marekani hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya usalama wao. Baada ya maongezi mawili matatu nilichukua lile begi na kumwaga silaha zote lakini zilikuwa zimepanguliwa, walishangaa kuoa vile.
"nani anaweza kuzipanga hizi bila kukosea" niliwauliza lakini hakuna hata mmoja aliejibu hiyo ilimaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambae anaweza. Basi niyaka kuwaonyesha kama mimi ni moto wa kuotea mbali, nilitoa kitambaa cheusi na kujifunga machoni kisha nikakaa chini na kuanza kuzipanga. Nilianza na sniper, nilweza kufanya hivo kwa sababu kila kipande nilichokishika nilijua ni cha bastola gani. Kipindi nikiwa training, nilifundiswa kuunga silaha katika kiza kizito na kunawakati niliunga silaha wakati nakimbi kwenye mabonde na milima. Siku nyingine ilikuwa hatari zaidi, niliunga wakati nashambuliwa japo hazikuwa risasi za kwenli lakini usiombe zikakupata uanweza kupoteza fahamu. Nusu saa baadae nilikuwa nimeshamaliza kuunga zote, nilipofungua macho niliwakuta wote wakiwa hawaamini nilichokuwa nakifanya. Nikawaambia kuwa hayo ni mambo ya kawaida hasa unapopewa mafunzo ya kuwa muuaji. tulipiga stori nyingi sana huku tukujaribu kuzoeana, kiza kiliingia nikawaambia wafungue mahema na wapumzikie. Mimi nikatoka kidog na kurudi kule nyumbani kwangu, nilipofika niliingia moja kwa moja katika kile chumba cha serjent Jones. Nilimkuta akiwa kalegea kwa njaa, nikamwambia asihofu mimi sitamuua ila nilihitaji akae pale kwa muda kidogo ili niweze kumaliza kazi zangu. Japo alikuwa lakini hakuacha kunyesha kama anachuki juu yangu. Basi nkamchoma sindano yenye Glucose ndani yake ili kunfanya aweze kuendelea kuishi. Nilichukua baadhi ya vitu muhimu na kuvificha sehemy nje ya nyuma hiyo, nilipohakikisha hakuna ushaahidi kama nilikuwa pale nilimchoma sindano ya usingizi kisha nikamfungua na kumuacha ili akiamka arudi kambini. Baada hapo niliondoka na kurudi kule baharini kwaajili ya kuipokea ndege ambayo ilikuwa inaingia asubuhi. Nilipofika niliwakuta wale wanajeshi wakiwa makini sana maana nilipotokeza tu mmoja wao aliinua mtutu wake na kuelekeza kwangu. Nikamuonesha ishara ambayo tulikubaliana na hapo akanitambua, usiku huo mimi sikulala japo wao wote walila. mapema alfajiri niliwaamsha na kuwaambia wajiandae kwani muda si mrefu ndeg itatu, kisha nikatoa karatasi ndogo pamoja na flash nikamkabidhi mmoja wao na kumwambia wakifika tu amkabidhi karatasi ile pamoja na flash muheshimiwa raisi. Waliponiuliza vipi kuhusu mimi, nikawajibu tutakutana makao makuu nyumbani huko. Wakati tukiendelea kuongea kwa mbali niliiona ndege ikitua katika maji na taratibu tukasogea mpaka karibu na maji hasaa, ilisimama na rubani akashuka nilimpa ishara kuwa sisi ndo tulokuja kumpokea lakini alionesha kuwa na wasiwasi maana alijua sergent ndio mpokeaji, nililishtukia hilo na kabla hajafanya chochote nilimpasua kichwa. Nikawapa ishara haraka waingie kenye ndege na waondoke,na wao bila kuchelewa walfanya hivo. Kwa mbali nilianza kusimia milio ya gari ikija upande wetu, hivyo nikawapa ishara waondoke haraka. Na mimi nikatafuta sehemu nikajificha maana eneo loe hilo nilikuwa nimetega mabomu, kwa mbali ni niliiona ndge ikizama kwenye mawingu. Nilitabasamu kidogo nikajua ule muda wa kuwamaliza umefika.
Nilitulia sehemu niliojificha mpaka walipoingia katika eneo lenye mabomu na hapo hapo gari zao kadhaa ziliripuka na kuwafanya wasimame. Njia pekee ya kupanda nao ilikuwa ni kwa mfumo kombolela, sikutaka kutumia silaha zang kwanza maan nilijuwa nikizimaliza wataniua. Nilichokuwa nakifanya ni kuwavizia na kuwaua pasi na wengine kujua, kwa kweli mchezo huo ulinifurahisha sana hata sijui kwanini. Walipoona hali imekuwa mbaya waligeuza na kukimblia kambini kwao,ila kabla hawajaondoka niliwahi kuingia chini ya mvungu wa gar moja na kukamata ipasavyo nisije nikaanguka. Malengo yangu ilikuwa nijitahidi kuwa hai mpaka siku ya pili msaada kutoka marekani utakapofika lakini raisi mstaafu ilikuwa ni lazima afe tena kwa mikono yangu. Waliingia kambini na moja kwa moja kuelekea ofisini kwa bosi wao, na haukupita muda ilipigwa honi ya hatari na wote walikusanyika na mimi nikiwemo lakini kwa vile mavazi yangu yalifanana na yao hawakunijua. Mbele alisimama sergent Jones "tumepata tatizo kubwa sana, na tunatakiwa kuanzia sasa tuwe makini sana maana kuna mtu anaitwa David Robert Mccannon. Huyu mtu ni hatari sana kuliko mnavofikiria na anawezakuwa yoyote miongoni mwetu, sasa baada kutano huu tuelekee kwenye ghala la silaha. Hii ni vita na vita hii tunapambana na mtu mmoja tu". Alimaliza kuongea na hapo walianza kuelekea katika ghala lakini kabla wahajafikia, nilitoa remote ndogo na kubonyeza kitufe papo hapo ghala liakaripuka wote wakabaki wameshangaa tu. Nilirudi chini ya mvungu wa ile gari na kutoa silaha zangu kisha nikaingia ndani bila kutambulikana kwa sababu kila mtu alikuwa akijaribu kuokoa maisha yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"simama" niliskia sauti ikitokea nyuma yangu, nilisimama ila sikugeuka maana sauti ile niliijuwa kama Serjent Jones, alikuja kunishika bega ili nigeuke na mimi sikusita niligeuka ila iliyangulia ngumi nzito iliogota usoni mwa serjent Jones. Alishtuka sana baada kuniona "afadhali tumekutana ili tumalize deni kati yetu" aliongea huku akisimama, "hakuna kutumia silaha wala kuita mtu, hapa ni mimi na wewe na mmoja tu kati yetu ndie atakaetoka mzima" aliendelea kuongea na kunifanya nitabsamu. nilivua silaha zote nkaweka pembeni na yeye akatoa bastola ndogo na kuitupa chini. Alinifwata kwa kasi huku akirusha ngumi kadhaa ambazo nilifanikiwa kuzikwepa bila shida, alipoona vile aligeuka na kuja tena lakini safari hii alikuwa makini zaidi. Alirusha ngumi kadhaa ambazo ziliishia mikononi mwangu kwa kuzipangua na kumtandika ngumi nzito ya tumbo. Alitoa sauti ya maumivu japo hakutaka nijue kama imemuingia, kwa kasi ya ajabu nilimfata na kurusha ngumi kadhaa ambazo chache alifanikiwa kuzipangua lakini nyingine ziliingia sawa sawia katika mwili wake. Kinachonisaidia mimi ni kwamba situmii aina moja ya ngumi katika kupanda,huwa nachangaya. Kama hapo nilitumia aina ya mchezo unaitwa tai boxing, baada kumuona ana mawenge nikabadilisha kukaa katika mkao unaojulikana kama nekoashidat, huo ni mkao wa saba katika karati. Nilimdanganya kwa mguu wa mbele na bila mategemeo alijikuta akiambulia teke zito la shingo na kumtupa huko. Ila alikuwa mbishi kwelikweli alisimama ila kabla hajakaa sawa, niliinama na kurudi juu na mfumo wa ngumu wa boxer, nilimtandika ngumi ya kidevu maarufu kama uppercut na kumrusha juu kabla hajatua nikamsindikiza na teke la tumbo na moja kwa moja alienda mpaka kweny chuma kilichoingia mgongoni na kutoke tumboni.
Baada hapo niliokota silaha zangu na kuondoka, nilianza kumsaka raisi mstaafu bila mafanikio yoyote. NIliingia katika chumba kimoja na kabla hata sijaangaza vizuri nilihisi kitu kizito kikinipiga kichwa na kupoteza fahamu. Nikuja kushtuka baada kumwagiwa maji ya uso, na nilipofungua macho nilimuona raisi mstaafu akiniangalia huku akicheka kwa dharau."unajua mi nilidhani mtu anakufa mara moja tu lakini kwa wewe imekuwa tofauti, mara hii nakuahidi utakufa kweli na hutaonekana tena duniani" aliongea huku akichezea bastola yake ndogo. "labda katika ndoto zako ndio nitakufa lakini kaa ukijua wewe utakufa mwanzo kabla yangu" niliongea kwa hasira. "hahaha... sasa hebu jiangalia wewe ndie uliefungwa kwenye kiti halafu chini ya kiti hicho kuna bomu, unasema nitakufa mimi mwanzo" alijibu huku akicheka. Nikajisemea kasahau huyu kama katika kichwa changu kuna GPS tracker, na ninauwezo kuhack kitu chochote ambacho kina mfumo wa mawasilino. basi bila kuchelewa nikaanza kuihack remote ya bomu ambalo lipo chini kwenye kiti nilichokaa. wakati huo yeye alikuwa akiongea tu bila kujua kuwa wala nilikuwa sijui anaongea nini. Nilipohakikisha nishaivuruga remoti ile nilianza kuzungusha viganja vyangu ili nione kama kuna uwezekano wa kuvitoa katika pingu alionifunga. Ila sikufanikiwa, "muda wako wa kuishi duniani umwekwisha, kwa heri maana naskia jeshi la nyumbani lishafika kuja kuniokoa" alisema huku akiondoka. Hiyo ndio ikawa nafasi pekee ya mimi kutoka katika kiti hicho, kwa nguvu zangu zote nilijirusha na kuanguka, kiti kilivunjika na mimi bila kuchelewa nikasimama, nilikiteuwa kiganja changu kimoja ili nitoe pingu na nikafanikia japo maumivu yalikuwa makali lakini sikujali. NIlitoka chumbani humo huku nakimbia kumfata, kisha nikatuma kodi kupitia kichwa changu na lile bomu likaripuka. Nilimkuta akiwa kasima huku anacheka, nilimvizia na kumtia kabali kisha nikamvuta ndani na kuingia nae katika chumba kimoja hivi. "leo nataka nikuonyeshe maumivu ya kuungua na moto" nilimwambia huku nikimwagia mafuta ya taa, "tafadhali usinichome,nina familia inanitegemea" alijaribu kujitetea. "unajua saa hivi kama una familia, lakini kipindi ukinitenganisha na familia yangu hukujali kama ningeteseka kiasi hichi" nilijibu huku machozi yakinitoka. "Mungu akuingize katika moto mkali kuliko yote huko unakokwenda, nakutakia safari ya misukosuko iliojaa mateso, manyanyaso na fedheha" niliongea maneno hayo kuwasha kibiriti na kukiangusha kwenye mafuta. Alipiga kelele lakini wala sikujali nilitoka nje na kukuta kumeshaanza kupambazuka, sikutaka kusubiri niliondoka eneo hilo na kutafuta pahali nikajisafisha, mwili wangu niliuhisi umekuwa mwepesi. Nilivaa mavazi ya kiraia kisha nikatoa simu na kumpigia yule kijana aniletee taxi.
Hakukaa sana alifika na taxi, niliingia na kumwambia amwambie dereva anipeleke auwanja wa ndege. Muda huo mawazo yangu yote yalikuwa kwa mwanangu Christina na mke wangu mtarajiwa Tania. Nilifika uwanja wa ndege na kumlipa yule dereva, kisha nikatoa mfuko mdogo nikamkabidhi yule kijana na kumwambia "hizo ni dola elfu tano, anza maisha yako upya na ujiajiri mwenyewe" alifurahi sana. tuliagan na mimi nikaingia ndani na kukata ticket ya kuelekea marekani, masaa kadhaa baadae ndege ilitua. Nilishangaa sana nilipotoka nje baada kuona gari za serekali zikiwa zinanisubiri, ukweli nilijua tayari naenda kuozea jela lakini kabla sijaamua la kufanya nilimuona kija mmoja kati ya wale wanne akija. KIdogo nilikaa sawa, alipofika aliniambia kuwa nahitajika white house. Tuliingia kwenye gari na kuelekea huko, nilikutana na raisi na kuongea mambo mengi lakini nikamwambia siko tayari kufanya kazi ile tena na sasa nataka kuanzisha maisha yangu ili niwe na familia yangu. Alinielewa na kuaguza nipewe ulinzi mpaka Califonia ambako ndipo alipokuwa mwangu Christina. Japo mwanzo hakunijua lakini kwa msaada wa baba mkwe wangu mambo yalikuwa mazuri. Nilitoa simu yangu na kumpigia Tania na kumuuliza yupo nchi gani, alinijibu kuwa yupo London. NIkamwambia apnde ndege aje Califonia nae hakupinga, siku ya pili mapema nilikwenda kuompokea na kumpeleka nyumbani. kwa vile mi sikuwa na wazazi,niliwafanya wake zangu kama wazazi wangu na kuwaeleza kila kitu. Walikubali na baada miezi miwili Tania aliacha kazi ya ndege na tukafunga ndoa. Na mpaka sasa tunaishi pamoja na tuna watoto wanne,Christina ambae anamiaka 22 na ni personal secretary wa rais, Jeff ambae ana miaka 18 na yuko high school, Edward ambae ana 12 na yuko junior school na wa mwisho ni Tatiana ambae ana mika 3 na yuko baby class.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
NA MIMI SIE DAVID ROBERT MCCANNON KWA SABABU ALIKUFA SIKU ILE NILOMUUA ADUI YANGU MKUBWA.
JINA LANGU NI JAMES ALLEN
MWISHO.
HUU NI MWISHO WA C.O.D.E.X season one.
Kwa Season two, kaa hapahapa.
Tariq Haji anawapa shukrani wote mliokuwa mnamsapoti katika kazi hii kwa hali na mali na kumkosoa kwa makosa ambayo mliyaona.
Bado anajifunza kupitia waandishi wengine, hivyo anaomba zaidi muwe mnamfunza hasa pale mnapoona makosa ambayo yanajitokeza kwake mara kwa mara, yaani yale ambayo yanaonekana kwake ni ubovu na si yale ya bahati mbaya.
Kaa tayari kwa Season Two.
0 comments:
Post a Comment