Search This Blog

Friday, 20 May 2022

C.O.D.EX. 3 (THE REAL ME) - 1







    IMEANDIKWA NA : TARIQ HAJI



    *********************************************************************************





    Simulizi : C.O.D.EX. 3 (The Real Me)

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Niko wapi, niko mbinguni au" aliongea Alex baada kufumbua macho kutoka katka usingizi wa kifo, "tulia kijana, utafikaje mbinguni wakati hujafa" aliongea mzee mmoja wa makamo huku akitabasamu na kumuekea Alex mkono begani "uko mahali salama kabisa" aliendelea kuongea mzee huyo. Alex alijaribu kuzivuta kumbukumbu zake za mara ya mwisho. Na ndipo akakumbuka kuwa alipigwa risasi na Agent Darling, akaanza kuwaza ikiwa risasi ile hajapigwa yeye , je aliepigwa ni nani?. Swali hilo lilizuka ghafla kichwani mwake, "isije ikawa wamemuuwa hawa". "Alex karibu tena duniani" aliingia mwanamke mmoja aliekuwa amevaa kinyago nusu katika uso wake. "unanikumbuka" aliobgea mwanamke na kukaa pembeni kwenye kiti. "hapana sikukumbuki" alijibu Alex huku akijaribu kukaa, "hahaha kweli Alex umenisahau?" aliuliza tena huku akicheka. "subiri hiyo sauti kama naijua" Alex aliongea huku akivuta kumbkumbu zake vizuri ghafla akaruka "Scarlet ni wewe au". "kumbe bado kichwa chako kipo vizuri" alijibu Scarlet, "wema haupotei" aliendelea kuongea mwanamke huyo mwenye tabasamu lenye kumuweka simba kichaa chini. Alionekana kuwa mchangamfu kupita maelezo lakini kwa mtu ambe na uwezo wa kusoma sura vizuri basi angegundua kuwa uchamgamfu wake pamoja na tabsamu vilikuwa ni danganya toto tu. Mtu pekee alielielewa hilo ni General Griffin, ambae ni baba mlezi wa Scarlet. "Hebu nambie nimeokokaje" aliongea Alex, "usijali nitakwambia kila" alijibu Scarlet na kumuangalia Alex.

    "Ni hivi, nilisikia kinachoendelea kupitia vyanzo vyangu vya habari na uchunguzi. Taarifa nilizipata wakati natoka Mexico katika kazi maalum niliyopewa na serekali, ndipo nikaskia kuwa kua mtu anaitwa Alex na ni muuaji mkubwa sana. Nikaanza kufatilia na ndipo nikagundua kuwa Alex mwenyewe ni wewe, na pia nilianza kufatilia kwanini ulikuwa unatekeleza mauji hayo. Sasa siku moja nilifika katika ofisi za kitengo maalum cha upelelezi kama mwandishi wa habari. Wakati nashuka gari niliona vikosi vingi sana vya kuimarisha ulinzi wakati nataka kudadisi ghafla nilipitwa na gari ndogo nyeusi ikielekea upande waliopo wanajeshi na ilipofka ikaripuka. Kwa mbali nikauona ukianza kugawa dozi, bila kuchelewa nilipiga simu makao makuu waniletee chopa niondoke. ilichukua muda kufika, wakati naondoka sasa ndipo nikakuona juu ya jengo ukiwa umepiga magoti na mbele alikuwepo mwanamke aliekuwa ameshikilia bastola. Nilichukua sniper na kabla hajakupiga wewe nikamuwahi yeye, sijui hata nilimpiga wapi maana sikulenga kwa makini. Baada hapo nilikuchukua na kukuleta huku" Alimaliza kuongea Scarlet na kumuangalia Alex ambae macho yalikuwa yamemtoka kam mjusi aliebanwa na Mlango.

    *******************************

    "mkuu, Christina amemka" aliigia mwanamke mmoja aliejiulikana kwa jina la Martina, jeff aliinuka alipokaa na kuelekea chumba alichokuwa amelazwa Christina. "vipi hali yako" Swali a kwanza kuuliza alipofika ndani ya chumba hicho, "Jeff nimefikaje hapa?" aliuliza Christina. "tulia utajua kila kitu lakini kwanza unajiskiaje" Jeff alimtuliza na kumuuliza tena swali la kwanza. "vizuri kiasi na maumivu kwa mbali katika bega la mkono wa kushoto" alijibu Christina huku akijiangalia mkono ambao ulikuwa umefungwa bendeg. "usijali unahitaji siku chache tu, mkono utapona kabisa" alijibu Jeff huku akimshika mkono, "nilikukuta juu ya gorofa ukiwa unavuja damu huku ukiwa umepoteza fahamu,ndipo nikakuchukua na kukuleta huku katika kambi maalum, na wala usijali hakuna mtu anaejua kama uko hai ama umekufa" aliongea Jeff huku akimuangalia kwa makini, kwa vipi atazipokea taarifa hizo. "na kwanini wasijue kama niko hai ama nimekufa" aliuliza kwa mshangao, "nilikuwa nategemea swali hilo kutoka kwako" alijibu Jeff na kuinuka, alisogea mpaka ukutani na kubonyeza pahali. Ukuta ulifunguka na kulikuwa na TV, "naomba usikilize mwenyewe kabla sijakueleza chochote" aliongea Jeff na kuwasha Tv hiyo kubwa kisha akarudi alipokuwa amekaa wali na kukaa.

    "mpendwa mwanangu Christina" iliskika sauti ya Allen James, "wakati utakapoupokea ujumbe huu uenda nikawa sipo tena duniani, nakuomba sikiliza kwa makini na uwatabue marafiki zako na maadui zako usije ukatumika kama nilivyotumika mimi" baada hapo sauti ya Allen ilikata na kuanza kusikika sauti nyingine "ndio baada Allen James kukamilisha kazi inabidi na yey afe, si mnaelwa kuwa kazi hii ni siri ya hali ya juu na hatakiwi mtu mwengien asiehusika afahamu, na kama Allen atashidwa kumuua Alex basi itabidi sisi tumuue yeye halafu kesi hii tunambambikizia Alex. Akirudi Christina na kufahamu kuwa babaake ameuwawa na Alex, nina uhakika hatopumzika mpaka atakapohakikisha Aex amekufa na baada ya hapo na yeye pia tunamuua ili kupoteza ushahidi kabisa. Mapinduzi hayawezi kuzuilika, na mtu na mwanae wote watatumika kama mbwa wa kuwindia"baada ya sauti hiyo kukata ilirudi tena sauti ya Allen "natumai utakuwa umefahamu nani mbaya wako na nani rafiki yako, atakae kuletea ujumbe ni Alex na ni mmoja kati ya watu ambao watakuwa msaada mkubwa kwako katika kukamilisha kazi ntakayokupa kama babaako. Nataka uwasambaratishe kama vumbi wale wote wanaotaka kuitndea nchi yetu mabaya, na kunitenda mimi babaako. Ni matumaini yangu kwamba utafanikisha zoezi hili kwa hali na mali, kama ikibidi ufe ili likamilike basi fanya hivo. Nakupenda sana mwanangu...mimi babaako Allen James" hapo ndio ulikuwa mwisho wa rikodi hiyo na katika kioo cha TV hio kutaoke maandishi mekundu yaliosemeka "THE END IS THE BEGINNING".CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Christina alijikuta machozi yakimtoka bila mategemeo na kujisemea kwa sauti ya kinyonge "kwanini hukunipa mapema taarifa hii Alex", "Christina punguza jazba" aliongea Jeff. "najaribu ila nshindwa, kwakweli mtu niliokuwa nataka kumuua ndie mtu aliekuwa bega kwa bega na babangu katika mapambano, unafikiri ningemuua ningeenda kuiweka sura yangu siku ambayo ningekutana na babaangu" alianza kujilaumu sasa. "lakini jambo zuri ni kwamba hujamuua" aliongea Jeff akijaribu kumpa moyo. "una uhakika gani, mi sidhani kama atakuwa amepona baada majeraha yale niliompa" alizidi kujilaumu huku moyoni akijiapiza kulipiza kisasi hata kama itabidi damu yake imwagike. Jeff baada kusikia hivo, ikabidi anyamaze kwanza na kisha akainuka na kutoka na kutoka nje huku akimuacha Christina akiendelea kulia. "mbona umemuacha peke yake" aliuliza Talbot, "ndio inavotakiwa, kwa sasa anajaribu kukabiliana na uhalisia kwamba aliekuwa anamuwinda sie aliemuaa baba ake. Na tujiandae kwa mechi ngumu mbele kwasababu lazima atahitaji msaada wetu kukamilisha kazi yake" Jeff alijibu na kuelekea chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika.

    Christina aliendelea kulia huku akiwa mwekundu kwa hasira ambayo ilianza kukikitesa kichwa chake, mara kadhaa alipiga kelele na kuangusa vitu chini. Lakini hakuna mtu alieingia katika chumba chake, "hahaha....Christina wewe ni mjinga sana tena mjinga wa mwisho, hukuona muda wote kama Alex alikuwa kiajribu kukufikishia ujumbe". "hahaha... lakini amefanya uzembe mwenyewe kwa kutokupa ujumbe mapema", "General David mpumbavu mkubwa wee, utalipa huu unyama kwa damu yako mjinga mkubwa wewe. Ulidhani mimi ni babaangu, umekosea sana kucheza na baba angu kwani umesaini mkataba wa kifo na mimi...hahaha mshenzi wee". Alikuwa akiongea mwenyewe na kujijibu huku akicheka na baadhi ya wakati alikuwa analia, alionekana kama mtu aliechanganyikiwa tena si kidogo maana chumba kizima alikichafua chafua, alikuwa mevunja kila kitu kilichokuwemo katika chumba hicho kuanzia vitu viukubwa mpaka vidogo vidogo. "THE END IS THE BEGINNING....NDIO KWANZA SAFARI IMEANZA" alisema kwa nguvu huku machozi yakimtoka. "furahia siku zako za mwisho na kila anaehusika na wewe,nitauwa kuanzia sisimizi na kila kitu ambacho kimo katika himaya yako na yoyote atakaekaa mbele yangu na yeye pia atakufa...General David" alijisemea na kusimama kwenye kiti alichokuwa amekaa baada ya kushuka kitandani.

    CODE X 3: THE REAL ME 2

    ***************************

    "nimekwambia nenda nyumbani ukanyonye. leo ni siku mbya sana" Alex aliikumbuka sentensi aliomwambia Allen Jr kabla ya kumpa kichapo cha fisi mwizi. "natumai kwa sasa utakuwa ushaujua ukweli" alijisemea huku akijisifu kwa kufikisha ujumbe wa mwalimu wake Allen. Siku ile baada ya kumpiga mpaka kumzimisha, alitoa ile recorder alioambiwa kuwa ni kwa ajili ya Christina na kumtilia katika mfuko wa suruali yake kisha yeye akaondoka na kuendelea na pambano lake. "hivi kwanini hukuniacha nife tu maana tayari nilishapanga kwena kukutana na familia yangu mzima" Alex alimuuliza Scarlet aliekuwa pembeni bize akicheza game ya kivita. "unadhani kila mtu ambae anapata mikosi angetaka kufa, unadhani kungekuwa nawatu amabao wangekuwa tayari kupigania haki ya mtu" Scarlet alijibu na kuacha kucheza game, alionekana kukerwa na swali hilo la Alex. " ni bora ushukuru ulikuwa sehemu ambayo ulikuwa na marafiki na walikuwa wakikujali japo mlikuwa kambini" Scarlet aliongea huku akikaa mbele ya Alex na kumuangalia usoni. "mimi nimeishi maisha ya manyanyaso sana tokea nilipozaliwa" Scarlet aliendelea kuongea huku akionekana wazi kuumizwa na anachokiongea. "hebu nielezee maisha yako" Alex aliomba na kukaa mkao wa kula kusuburi binti huo aanze kumporomoshea mkasa wa maisha yake.

    ********************

    Scarlet alianza kuelezea hadithi ya maisha yake "Jina langu halisi sio Scarlet kama wanavolifahamu wengi, ila jina langu ni Ariella Mark. Ni mtoto wa pekee katika familia yangu, na babaangu alinipa jina hilo kwa sababu mama angu alijifungua katika wakati mgumu sana wa maisha yao. Japo hali ilikuwa duni lakini niliweza kukuwa vizuri tu bila kusumbuliwa na magonjwa kama wengi walivyodhani. Ukweli wazazi wangu walinipenda sana, tena sana kupita maelezo. Nilipata kila kitu nilicholikitaka, taratibu maisha yalianza kunyooka na kuwa mazuri huku kubadilika huko kwa maisha kukiwachukiza ndugu wa karibu wa wazazi wangu. Nikiwa na miaka minne tulihama tulipokuwa tunakaa na kuhamia mjini kabisa ambako baba alikuwa amejenga nyumba mpya na ya kisasa kwa wakti huo. Nilianza shule japo nilikuwa nimechelewa lakini wazazi wangu hawakumsikliza mtu, nilianza shule ya awali na baada ya miaka mitatu niliingia darasa la kwanza. Wakati huo nilikuwa na miaka saba lakini kutokana na mwili wangu kuwa mdogo sana hakuna alieamini kuwa nina miaka hiyo. Lakini nashukuru Mungu kwa kunipa wazazi wenye hekima na busara kama wale, lakini kama tunavojua kuwa duniani tunapita hakuna kiumbe kitakachoishi milele. Basi hivyo ndivyo ilivokuwa kwa babaangu ambae nikiwa na kumi alpoteza ajali katika ajali ya ndege nikabaki na mama yangu tu.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Maisha yalizidi kusonga mbele huku ndugu zake baba wakizidi kuleta vita juu ya mali alioacha baba, na taratibu walianza kutupora. Na walipoona mama ameleta ubishi sana wa kuzikabodhi mali, Baba mkubwa alituma vijana wakaja kuchoma nyumba yetu moto. Moto huo ulianzishwa usiku wa manane, na ulitanda kwa kasi ya ajabu. Nilikuja kushtuka baada kuhisi maumivu makali usoni na kugundua kuwa chumba changu kina moshi mwingi sana. Na haukupita muda mama alifika chumbani na kunibeba huku nikilia kwa nguvu. Kwakweli siwezi kuyasahau maumivu nilioyapata usiku ule, na kwa sababu moti ulikuwa umeshaienea sana ilikuwa hakuna jinsi ya kutoka ndani ya nyumba hiyo. Mama alichokifanya alinitia kwenye friza, nikiwa humo ndani nilihisi friza hilo likisogea kwa nguvu huku nikisikia kelele za mama kutoka na maumivu anayoyapata baada moto huo kuanza kumuunguza. Aliendelea kulisukuma friza hilo lakini ghafla nilihisi kama likianguka na kweli kwasababu lilipiga chini kwa nguvu na kunifanya niumie. Baada hapo nilisikia mlipuko mkubwa sana, kutokana na baridi kuwa kali katika friza hilo nilipoteza fahamu. Nilikuja kushtuka niko hospitali, na swali la kwanza lilikuwa ni kumuulizia mamaangu lakini majibu niliokutana nayo yalikuwa ni ya kutisha sana. Huwezi amini ndani ya miezi minne baada kifo cha babaangu, nilimpoteza mamaangu tena kwa kifo cha mateso. Na taarifa nyingine mbaya ambao niliipokea baada kuamka ni kuwa upande wa kushoto wa uso wangu wote ulikuwa umeungua, na kutokana na umri wangu kuwa mdogo sana ilikuwa ni vigumu kufanyiwa plastic surgery. Nilikaa kwa sikukadha hospitali bila hata ndugu yangu mmoja kuja kunitembelea.

    Baada wiki kupita huku kukiwa hakuna dalili ya mtu yoyote anaenifahamu kuja kuniona, daktari mkuu wa hospitali hiyo alichukuwa uamuazi wa kunipeleka katika kituo cha kulelea watoto yatima. Na kwasababu alikuwa hanijui jina na mimi sikutaka kumwambia mtu jina kutokana na kutonesha kidonda kibichi kwa sababu kila nnapolitaja jina hilo nawakumbuka wazazi na kuanza kumlaumu Mungu kwa kunitenda. Sasa sikutaka kumkosoa na kuingilia majukumu ya muumba wangu na hivyo ndivyo nilivyofundisha na wazazi wangu kuwa kila linalotokea basi limepangwa na Mungu litokee. Basi aliniandikisha kwa jina la Scarlette. Maisha mapya yalianza baada tu daktari huyo kuondoka, yule mama nilomkuta katika zamu siku niliofika alikuwa na roho nzuri. na alinieleza kuwa nijiandae kwa maisha magumu sana kutokana na tabia za watoto waliekuwepo katika kituo hicho na baadhi ya wasimamizi. Alinipelaka mpaka katiak chumba ambacho ndio nilitakiwa kulala na kunikabidhi kwa kiongozi wa chumba hicho. Yule msichana alikuwa anaitwa Harleen, alikua ni binti mwenye asili ya kihindi aliyechanganyika na muingereza. Yeye pia alikuwa na roho nzuri na alikuwa mchangamfu, alinipeleka mpaka kwenye kitanda ambacho kilikuwa pembeni ya kitanda chake. Alinikabdihi shuka kadhaa pamoja na nguo za kubadilisha, kwakweli nilimshkuru sana. Siku hiyo ilipita huku usiku kucha nikiwa macho bila kupata hata lepe la usingizi na usiku mzima nilikuwa nikilia huku nikijaumu kwa nini sikufa pamoja na mama ili tukaenda kuonana na baba tukiwa pamoja na kuungana tena kwa mara ya pili kama familia nzima. Hapo awali maisha katika kituo hicho yalikuwa magumu kutokana na kuwa mgen wa mazingira hayo, pia waschna wengine walinitenga kutokana na kovu langu usoni. Walinipa majina tofauti tofauti, wapo walioniita laana wakimaanisha kuwa nimelaaniwa. Kuna wengine waliniita jini, wengine waliniita mdudu. Yote kwa yote kila mtu aliniita alivojisikia, kwa kweli nilikuwa najiskia vibaya sana hasa nnapo kumbukua uzuri wangu ulioteketezwa na moto na kuuzika pamoja na jina langu.

    Lakini kadiri siku zilivyokwenda nilizoea hali hiyo, baada wiki moja katika kituo hicho. Nilipelekwa shule kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo. Nilifurahi sana na wakati huo huo nilikuwa na hofu, kwasababu ya sura yangu ambayo ilikuwa nyeusi upande mmoja na nyeupe uoande mwengine. Siku ya kwanza shuleni watu wengi walinicheka hasa wanaume, hakuna hata mwanafunzi mmoja aliekuwa akiniongelesha darasani. Wote walinitenga na wengine walikimbia mbio waliponiona, kuna baadhi waliziba pua wakati napita. Hali hizo zilinitesa sana lakini ningefanyaje na yote ni mipango ya muumba. Mwaka uliisha na hatimae tukafanya mitihani ya kuingia darasa la nne, nilipasi vizuri tu lakini sikuwa na furaha kabisa kwa sababu hakuna mtu alionekana kuthamini matokeo yangu. Baada likizo kuisha tulirudi shule kwa ajili ya mwaka mpaya wa masomo, niliamua kufanya mabadiliko kwa kuzichukulia changa moto zote zilizonikuta mwaka uliopita kama sehemu yangu ya maisha ya kila siku. Hivyo basi niliondoa wasiwasi kabisa na kuyavaa maisha yangu kwa sura ya kipekee, nilifanya hivo baada kugundua maana ya jina langu halisi kuwa ni SIMBA JIKE LA MIUNGU YA KIGIRIKI.



    Niliamua kuwapuuzia wote wanaonikejeli na kuendelea na maisha yangu mweyewe mimi kama mimi bila kuendeshwa na woga uliokithiri. Hali hiyo ilipelekea hata hali yangu ya kimwili kutengemaa kutokana na kudhoofika na mawazo ya mwanzo kuhusu watu wanavonichukulia. "atakae nikimbia na akimbie, atakaeziba pua na azibe nnapo pita, mimi ni mimi na siwezi kubadilika hata kama ntacukia.....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    THIS IS THE REAL ME"



    Hiyo ndio ilikuwa kauli mbiu yangu.

    Basi jitihada zangu zote nilizielekeza kwenye masomo sasa, sikujali tena waliokuwa wakinikera. Japo nikuwa mzito kidogo darasani sikuwa tayari kukubali kufeli, hivyo niliongeza bidii mara dufu katika masomo. Siku moja nikiwa peke yangu nikipata chakula wakati wa mapumziko, nilisikia mtu akiniita. Nilipogeuka nikakutana na kijana mmoja mzuri sana, "samahani wewe ndio Scarlet" aliniuliza. Nikamjibu ndio, wakati huo upande ambao nilikuwa nimeungua na moto ulikuwa umefunikwa kwa nywele. Alitabasamu kidogo kisha akajitambulisha "mimi naitwa Adrian", pia alinambia kuwa yeye ni mwanafunzi mgeni pale shuleni hivyo wakati anaulizia sehemu akaelekezwa aje kwangu. Maskini hakujua kama aliambiwa aje pale ili anicheke kutokana na kovu langu kubwa usoni. "kwangu hukuambiwa uje nikuelekeze, umeambiwa uje kuniangalia usoni, nina kovu kubwa la moto" nilimwambia huku nikimkazia macho lakini cha kushangaza alikuwa kaitabasamu tu kisha akanijibu "unajua kuwa na kasoro si jambo la kujitenga na wengine, we huoni kama Mungu amekupendelea kukufanya hivo. Huoni kama kuna mantiki ya wewe kuwa hivyo labda ungekuwa kama wengine huwezi jua mangapi yangekuwa yamekufika mpaka sasa. Mimi naelewa ni kiasi gani upweke unanyonya na kumiza, muda wowote ukitaka mtu wa kuongea nae usisite kunitafuta rafiki yangu Scarlet" maneno alioongea yalikuwa na busara kubwa ndani yake hasa ukizingatia umri wake na darasa. Adrian ndio mwanaume wa kwanza kujenga nae urafiki, na kila wakati tuliokuwa tunaonana, nilikuwa nasahau kabisa karaha zangu.

    Alikuwa mcheshi na muelwa, alifahamu wakati nilokuwa niko sawa na wakati ambao niliko sawa. Na alikuwepo nyakati zote nilizomuhitaji, ukaribu wangu kwake uliendelea kukuwa kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele. Tulimaliza elimu ya msingi na kuanz elimu ya sekondary na kwa bahati nzuri tulipata shule moja hivyo urafiki wetu uliendelea. Wakati tunaingia sekondary mimi nilikuwa na miaka kumi na sita na Adrian alikuwa na miaka kumi na saba, hapo nilianza kuhisi kitu tofauti kwangu lakini nilikipotezea. Urafiki wetu waliwakera sana wanawake wanaotaka sifa kutoka na wanaume tofauti hasa wa kitajiri kama Adrian. Nilianza kupokea vitisho kuwa niache kujipendekeza kwa Adrian. Ukweli maneno hayo yaliniumiza sana na kuamua kumuita Adrian na kumueleza lakini kabla sijamaliza kuongea Adrian alinivuta karibu na kunikumbatia kisha akanambia "mimi na wewe tumetoka mbali sana, hakuna mtu anaekujua vizuri zaidi yangu. Wewe ni rafiki wangu wa damu, wa kufa na kuzikana na wala yasikutishe maneno ya wajinga wewe wa puuze tu" maneno yake yalinipa faraja kubwa sana, ukiunganishe na mkubatio ndio kabisa. Basi maisha yaliendelea hivo hivo huku wenye wivu wakizidi kuumia, siku moja uongozi wa shule ukatangaza sherehe ndogo ya msimu wa joto. Ilikuwa ni sherehe ya kucheza maarufu kama "dancing ball", nikiwa sina hili wala lile Adrian alinifuata na kuniomba niwe mweza wake katika usiku wa sherehe. Nilikataa kwa kisngizio cha kutokujua kucheza lakini akanambia hilo si tatizo na kwa sababu kulikuwa na wiki nzima kabla ya sherehe basi angenufundisha kucheza. Nilijaribu kutoa sababu nyingi ili mradi tu nisiende kwenye sherehe lakini alinizidi ujanja na mwisho nikakubali, basi kunzia siku hiyo tulikuwa tunakutana sehemu na akawa ananifundisha kucheza mchezo aina ya blues. Nilishangaa kuona kwa jinsi nilivyokuwa mwepesi katika mchezi huo wakati darasani nilikuwa mzito sana kupita maelezo kuelewa. Siku moja kabla ya sherehe alikuja na box la wastani na kunikabidhi kisha akanambia natakiwa kilichokuwa humo wakati wa sherehe. Sikulifunua hapo tuliendelea kufanya mazoezi mpaka tukamaliza na kuondoka tukikubaliana nimsubiri nje ya kituo nnacho kaa siku ya pili kwa ajili ya kwenda huko kwenye hiyo sherehe. Nilirudi nyumbani na kukaa kitandani kisha nikalifungua box, macho yalinitoka kama mjusi aliebanwa na mlango baada kukuta gauni kubwa lenye rangi ya dhahabu, lilikuwa zuri kupita kiasi. Pia nilikuta kinyago cha dhahabu kikiwa kiana ujumbe juu "kama unaona aibu kutokana na sura yako, vaa hichi". Nilitabasamu kidogo na kulifunga box hilo kisha nikaliweka pembeni ya kitanda changu.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya pili jioni nilianza maandalizi na kwa msaada wa Harleen nilimaliza mapema, nilipotoka ndani kila mtu alitoa macho huku wakionesha kutoamini wanachokiona mbele yao. Kila mtu aliongea neno lake, yote kwa yote walinisifu kwa kuniambia "umependeza kama sio wewe vile rangi mbili usoni". Tulicheka wote kutokana na kuwa nilishazoea kuitwa majina kama hayo, na huo ulikuwa ni utani tu. Nilitoka mpaka nje ya kituo na wala sikukaa sana, nilishangaa kuona garo aina Rolls Royce nyeusi ikisamama mbele yangu. Mlango ulifunguka na Adrian akashuka, alikuja upande wa pili na kunifungulia mlango. Wakati naingia kwenye gari alininong'neza "umependeza sana", sikuwa na cha kusema zaidi ya kujichekesha tu kama mjinga. Safari ilianza huku kila mmoja akiwa kimya mpaka sehemu ya sherehe, baada ya kushuka nilimsikia akiongea na dereva wakem "Simon unaweza kwenda kujirusha au sio, nikikuhitaji nitakushtua", "sawa mkuu" yule dereva alijibu kwa furaha na kuondoka. Adrian alikuja nilipokuwa nimesimama na kunishika mkono kisha tukaanza kutembea kuingia ndani ya ukumbi, kila tuliepishana nae hakuacha kutushangaa na kutusifu. Kutokana na kinyang'o usoni hakuna alienitambua. Kinyang'o hicho kilikuwa kimeifunika sehemu yangu nlioungua yote, kiufupi kiliugawa uso wangu katika nusu mbili. Baada kuingia humo ndani nilishangaa kuona tunaelekea upande wa V.I.P, nilisita lakini Adrian aliminya kidogo. Tulifika kwenye meza moja iliopambwa vizuri sana na juu ilikuwa ilikuwa imeandikwa "THE GOLD PARTNERS" (marafiki wa dhahabu). Sherehe ilifunguliwa rasmi na ratiba ikawa inaendelea vizuri, Adrian aliniomba tukacheze na mimi nikakubali. Siku hiyo ilikuwa ni miongoni mwa siku nilizokuwa na furaha katika maisha yangu na pia ni miongoni mwa siku nilizopata huzuni kubwa pia. Tuliendelea kucheza kwa kuburudika na baada ya muda kidogo kukatangazwa mashindano ya kucheza wawili wawili. Adrian aliinua mkono na kunionyesha ishara na mimi niinue. Baada ya kupatikana washindani wa kutosha, mashindano yalianza na kuendelea mpaka mwisho. Mshindi alitangazwa kuwa ni "THE GOLD PARTNERS", ambao ni mimi na Adrian. Tulikabidhiwa tuzo na kurudi katika meza yetu kwa ajili ya kupata chakula.

    Wakti tunaendelea kula nilianza kuhisi harufu flani hivi ambayo nilishwahi kuihis huko nyuma, moyo ulianza kwenda mbio huku kinyasho chembamba kikinitoka. Adrian alinishika mkono baada kugundua hilo, nilimuangalia na kumwambia kuwa nahisi harufu ya kitu kuungua. Na kweli kabla hata hajanijibu ghfla moto mkubwa ulirupuka na kila akaanza kukimbia upande wake. ukweli mimi na moto ni vitu viwili tafauti kabisha, nguvu ziliniishia na taswira ya uso wangu kuungua ikaanza kunirudia. "Scarlet tuondoke" nilisikia kwa mbali Adrian akinambia lakini hata hivo nilishindwa kinua hata kidole nikamjibu "wewe nenda tu mimi siwezi hata kuinuka hapa". Moto ulizidi kuwa mkali huku mimi na Adrian tukizidi kubishana juu ya swala zima la kuondoka. Adrian alipoona nmekuwa mbishi alininyanyua kwa nguvu na kunibeba kisha akaanza kukimbia, kwa muonekano wake sikutegemea kama angekuwa na nguvu kiasi kile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog