Simulizi : C.O.D.EX. 3 (The Real Me)
Sehemu Ya Pili (2)
Alifika mlangoni na kukuta moto umeshatanda, bila kusita alielekea uoande wenye dirisha na kulivunja kisha akanisukuma nje na yeye akafuata. Alipotua tu alitoa simu yake na kupiga "baba naomba helicopter yangu sasa hivi ije huku kwenye sherehe kuna mgonjwa amezidiwa" nilimsikia akiogea maneni hayo kwa masikio yangu, nilianza kuona kiza kinatanda machoni mwangu, na kabla sijafunga macho nilivua cheni yangu yenye kopa la dogo na kumkabidhi mkononi. Hakuijali aliitia mfukoni mwake na kwa mbali nikaanza kusikia mlio wa helicopter ila kabla haijafika nilipoteza fahamu kabisa. Sikujua nini kiliendelea, mawazo yagu ya mwisho kabla ya kufunga macho nilidhani kuwa ndio siku yangu yamwisho duniani.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikuja kushtuka, na kitu cha kwanza macho alikutana na mwangaza mkali sana na baada kuangaza kulia na kshoyo nikagundua niko hospitali. Nilijivuta vuta ili nikae lakini nesi aliniwahi na kunirudisha kitandani na kunambia sijaruhusiwa kukaa. Baada ya dakika kumi alikuja daktari na kuchukua vipimo kisha akatoka na baada ya nusu saa alirudi tena na kuchukua kiti kisha akakaa pembeni na kuanza kuniuliza maswali. Mengi yalikuwa ni kunijaribu kama kumbukumbu zangu ziko sawa, na baada kurdhika na majibu alioyapata alinikabidhi bahasha nyekundu. Niliifungua ndani na kukuta kuna barua, niliitoa na kuanza kuisoma. "najivunia kuwa na rafiki kama wewe, umenitoa upweke ambao ulikuwa umejizika ndani ya moyo wangu. Kitu ambacho sikuwahi kukwambia ni kwamba mimi nilikuwa mpweke kama wewe baada ya kumpoteza mama yangu mzazi pamoja na pacha wangu wa kike Adriana na kaka zangu wengine wawili na dada mmoja. Lakini baada ya kukutana na wewe upweke huo wote ulinitoka na kujikuta nikiwa huru kabisa, nakushukuru kwa hilo. Pia asante kwa zawadi yako nzuri ulionipa lakini nasikitika kuwa kwa sasa hatutaweza kuonana tena mimi na wewe mpaka pale Mungu atakapo tukutanisha tena kwa mara ya pili lakini kaa ukijua nakupenda sana. Nilipanga nikwambie siku ile ya sherehe na niliweka pete ya uchumba katika chupa yenye kinywaji lakini mambo yakaenda bila kutegemea. Nakuahidi kuwa nitakuhifadhia penzi lako ikibidi hata nizikwe nalo lakini nitakutafuta kwa ajili ukurasa mpya wa maisha yetu. NAKUPENDA SANA ARIELLA......WAKO ADRIAN" barua ilishia hapo na bila kutegemea nikajikuta nanyong'ojea na macho yangu yalishindwa kuhimili hali hio na kuanza kutoa machozi. Nililia kwa muda mrefu lakini jibu nililolipata ni kuwa yote ilikuwa ni mipango ya Mungu na kama amepanga mimi na Adrian tuoanane tena basi hakuna atakaeweza kuzia na kama amepanga vingine basi hakuna atakaeweza kubadilisha.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya baada ya siku mbili niliruhusiwa na kurudi nyumbani, daktari alinipa dawa fulani hivi ya kuondoa kovu japo alinambia kuwa kovo hilo haliwezi kuondoka lote kutokana na kuwa limekwenda ndani sana ya sura yangu. Hivyo dawa ingesaidia kuondoa ule uvimbe na kuirudisha sura yangu kuwa laini huku ikiacha alama ya weusi wa kimtindo. Nilirudi katika kituo nlichokuwa nakaa na kuanza maisha upya huku nikiwa nimepata funzo kuwa "ukijiona uko mpweke basi jua kuna ambae ni mpweke zaidi kuliko wewe" maisha yaliendelea na baada ya mwaka mmoja alikuja mzee mmoja na mkewe kwa lengo la kutaka mtoto wa kulea. Hivyo tuliitwa wote na kuelezwa kuwa mmoja kati yetu amgepata bahati ya kupata wazazi siku hiyo, hivyo tusiache nafasi hiyo ipite bila kutoka. Baada ya nusu saa alianza kuingia mmoja katika chumba maalum ambcho walikuwepo wanafamilia hiyo. Zamu yangu ilifika na kuingia, nilisalimia kwanza kisha nikakaa kwenye kiti. Yule mzee aliniangalia kisha akatabasamu na kunambia kuwa alikuwa na maswali machache anataka kuniuliza. Nilitikisa kichwa kuashiria nimemuelewa, "unaitwa nani" ndio swali la kwanza kuniuliza. "jina langu ni Scarlette Mark Anderson" nilimjibu jina kamili. "hivi una ndoto ya kuwa nani na kwanini" likuwa swali lake la pili na la mwisho, "nataka kuwa mtu ambae ataitumikia jamii bila kujali rika wala kabila kwa sababu furaha yangu ni kuona watu wakiwa na furaha" nilijibu huku nikimuangalia usoni. Yule mzee alitabasamu na kumuangalia mkewe, yule mama alinigeukia na kuniuliza "usoni umefanya nini". Nilimueleza kila kitu na swali jingine aliloniuliza lilikuwa "hujisikii vibaya au aibu kutembea na njiani na sura kama hiyo". Kwa upande fulani nilihisi kama amenidhalilisha lakini sikutaka kuonesha wazi. "hapana sijiskii aibu kabisa tena nahisi faraja kutembea kama nilivo bila kuificha sura kwa sababu hivi ndivyo nilivo na hata kama nitiaficha siwezi kubadilika....THIS IS THE REAL ME" hivyo ndivyo nilivojibu na kumwanagalia mama yule usoni kwa mbali nikamuona akitabasamu na kumgeukia mumewe kisha akatingiha kichwa. Baada ya hapo waliniruhusu nitoke ili waendelee kuongea na wengine. Baada ya muda kidogo kupita wote tulikuwa vyumbani mwetu. Aliingia msimamizi wetu na kuniita, aliongoza njia na mimi nikafata nyuma mpaka katika chumba kingine. Huku nilimkuta yule mzee na mkewe wakiwa wanaongea, walipotuon waligeuka na kuniangalia huku wakitabasamu. "hongera Scarlette umepata wazazi wa kukulea sasa" aliongea yule msimamizi wetu. Nilifurahi sana japo sikuonesha wazi kiasi nimefurahi, basi taratibu zote zilifuatwa ikiwemo kubadilishwa jina la baba na kuitwa Scarlette G. Jackson ambalo ni jina la mzee huyo.
Niliwaaga wenzangu na kuwaahidi kuwa nikipata nafasi nitawatembelea, tuliondoka hapo kituoni na siku hiyo hiyo tulioanda ndege na kuja America. Tokea siku hiyo maisha yangu yalibadilika kabisa, wazazi hao walinipenda sana kama mtoto wao wa kuzaa. Nikiwa na miaka ishirini Baba alikuja akiwa na karatasi mkononi na kunikabidhi kisha akakaa pembeni kwenye kochi na kuongea "ulisema unataka kuitumikia jamii ili iwe na furaha, basi nafasi hiyo imetoka kujiunga na kitengo cha polisi" aliongea maneno hayo huku akitabasamu. Nilisogea pale alipo na kupiga magoti mbele yake na kwa mara ya kwanza sikumuangalia kama baba bali nilimwangalia katika cheo chake, combat aliokuwa ameivaa ilikuwa imechafuka na vyeo vya kutosha vilivomtanabahisha mbele ya wengine na kuitwa General Griffin Jackson. "hii ndio kazi niliokuwa naitaka ila nilikuwa nashindwa niaizie wapi" niliongea na kuinuka kwa nguvu kisha nikamkumbatia "najua unataka kulinda heshima ya familia yako basi usijali hapa heshima na thamani ya familia hii itadumishwa mpaka mwisho wa dunia" nilimnong'oneza hilo wakati nimemkubatia. kwakweli sikuwahi kuona sikua liofurahi mzee huyo kama siku hiyo tokea nianze kukaa nae. Mama alikuja na kumwambia taarifa hizo nae alionekana kufutahi sana, walianda kijisherehe kidogo kwa ajili yangu. Na baada ya hapo niliijazo fomu ya kujiunga na mafunzo ya polisi, baba aliipeleka inapostahiki.
Alirudi nyumbani na fomu nyingine na kunikabidhi na kunambia kuwa natakiwa niripoti kituo kikubwa siku ya pili.Basi siku ya pili ilifika mapema na baba alinikabidhi suti nzuri sana na kunambia nivae. Baada hapo tuliungana na mama sebleni tukapata chai ya asubuhi kisha mimi na baba tukatoka kuelekea kituo kikuu. Tulifika na baba akaniacha hapo kisha yeye akaelekea makao makuu ya jeshi ambako alikuwa ameitwa. Niliingia ndani na kukuta atu wengine washafika, kuna baadhi waliponiona walianza kucheka lakini wala sikuwajali kabisa. Niliwachukulia kama wapuuzi tu, baada muda kidogo alikuja mkuu wa kituo hicho na kuanza kutueleza mambo kadhaa. Baada ya hapo wanawake tulielekezwa katika chumba maalum kwaajili ya kuchukuliwa vipimo mbali vikiwemo vya magonjwa. Baada kumaliza mchakato huo tuliambiwa tufike katika kambi maalum kwa ajili ya mafunzo kuanza.
Basi nilirudi nyumbani nikiwa na furaha sana, nilimueleza mama kila kitu na alionekana mwenye kufurahi sana. Baada ya hapo kila mtu aliendelea na majukumu yake na jiobi ilipofika baba alirudi lakini alikuwa tofauti na alivyoondoka asubuhi. Alionekana mwenye huzuni sana, mama alijaribu kumdadisi lakini hakuongea kitu bali alimpatia karatasi. Mama nae baada ya kuisoma alianza kunyong'onyea, ilibidi niichukue na mimi niisome na hapo ndio nikagndua kwanini wote wamenyong'onyea. ilikuwa ni barua ilioandikwa na kusainiwa na raisi wa nchi hii ikimueleza baba kuwa amelitumikia taifa sana hivyo alitakiwa kustaafu na kupumzika ili awaachie wengine waendelee kupeperusha bendera.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kitu hicho kilmuuma sana baba hata mama pia, basi nilimsogolea na kumwambia kuwa kila kitu kinachofanyika ni mipango ya Mungu. Labda kwa wakati ule alikuwa anatakiwa akae nyumbani aendeshe maisha ya kawaida ili alipe ule muda wote aliokuwa mbali na mama. Niliongea nae sana mpaka mwisho akaelewa na kuchangamka tena, mama aliandaa chakula cha usiku tukala na kila mtu akaelekea chumbani kwake kupumzika. Siku ya pili mapema baba aliamka na kupeleka barua ya kukubali kustaafu, alirudi nyumbani akiwa mchangamfu kama kawaida na kuungana na mimi pamoja na mama. Siku chache mbele iliandaliwa sherehe ya kuagwa na mheshimiwa raisi, na hapi alikabidhiwa medani ya dhahabu ya General bora katika kulitumikia taifa lake.
Siku ya kuripoti mafunzoni ilifika na mapema niliwasili katika kambi tulioambiwa, tulipewa maelekezo yote yaliokuwa yanatuhusu na baada hapo tukaanza mazoezi. Kwakweli yalikuwa mazoezi magumu sana kuliko nilivofikiria, ulifika wakati nilifikiria hata kutoroka lakini kila nilipokumbuka hadi niliompa baba nilipata ujasiri na kuendelea na mazoezi. Nilichunika chunika vya kutosha mpaka basi. Ila mwisho nilizoea maumivu na kuendelea na mazoezi bila shida yoyote ile. Muda wa mazoezi ulimaliza na tulikabidhiwa vyeti vyetu pamoja na nguo za kazi, siku hiyi ilikuwa ni ya furaha sana kwa kila mtu ambae alishieiki katika mazoezi yale magumu. Baada ya sherehe fupi tulipew ruhusa ya kurudi nyumbani huku tukisubiri kupangiwa vituo vya kufanyia kazi. Baba alionesha furaha ya hali ya juu sana, alinifanyia kasherehe kadogo hivi. "mwanangu jukumu ulilobeba sio dogo na sio kila mtu atakua na furaha na wewe, kwa hiyo ujiandae vilivo" maneno yalitoka kinywani mwa baba akinihusia. Nilitikisa kichwa kuashiria nimemuelewa, baada ya siku ya mbili nilipokea simu kuwa nimepangiwa kituo kikuu. Hiyo ilikuwa furaha nyingine kwa sababu sikupangiwa mbali na nnapo kaa. Siku ya pili niliwasili kituoni na kutambulishwa kituoni pamoja na kutambulishwa kwa mtu ambae nitakuwa nashirikiana nae. Alikuwa anaitwa Mike, alikuwa mtu mcheshi sana na alikuwa mchangamfu na mchapa kazi. Mike alikuwa mzoefu katika kazi hio, alikuwa na zaidi ya miaka mitatu. Mwanzo kila mtu alinisangaa kituoni kutokana na kovu langu usoni lakini kadiri siku zilivyokwenda walinizoea na kutokana na kujichanganya kwangu nao basi ilikuwa rahisi sana kupata marafiki wengi. Baada ya wiki moja nilipangiwa kazi ya kwanza nje ya kituo, na ilikuwa ni kuongoza msafara wa waziri mkuu katika eneo karibu na kituo chetu. Haikuwa kazi ngumu kabisa hasa ukizingatia ilikuwa ni kufunga njia tu wakati msafara unapita. Nilimaliza na kuripotu kituonim, Maisha kama askari wa kawaida yaliendelea kuwa mazuri huku kila siku sifa zangu zikizidi kutapakaa kutokana na uchangamfu wangu.
Siku moja nikiwa na Mike katika mgahawa mmoja hivi nikipata chai, ghafla tulisikia mlio wa risasi na bila kuchelewa tulitoka huku mikono ikiwa viunoni ambako kulikuwa na bastola zetu ndogo. Tulishuhudia gari moja likitupita kwa kasi huku mtu mmoja akiwa ametoa kichwa nje na kushambulia, tuliingia kwenye gari yetu na kuanza kuwafukuza. Ukweli Mike alikuwa dereva mzuri sana maana aliweza kumudu gari na kukwepa gari nyingi akiwa katika mwendo kasi. Nilitoa kichwa nje na kuipiga gari tuliokuwa tunaifukuza risasi katika tairi ya nyuma na kusababisha ipoteze muelekeo na kugonga nguzo pembeni. Walishuka watu watatu na kuanza kutushambulia, kwa bahati mbaya risasi moja ilimpata Mike begani. Sikuhitaji kufikiria mara mbili, niliteremka kwenye gari na kujificha pembeni kwenye mlango kisha nikatoa radio call na kuomba msaada. Wakati nasubiri msaada mashambulizi yalizidi kuwa makali kawa sababu wale majambazi walikuwa wanatumia silaha nzito sana. Wakati nikiendelea kushambuliana nao nilishutuka mlango ukifunguliwa na Mike akajiangusha chini kisha akanipa ishara niende nyuma kwenye buti. Nilifanya hivo bila kuchelewa, nilifika nyuma na kukuta buti limeshafunguliwa, nilikuta bastola aina ya shotgun na SMG. Nilibeba zote mbili na kurudi mbele ambako Mike alikuwa akiendelea kupambana nao. Nilimkabidhi SMG lakini akanambia nitumie mimi yeye akachukua shotgun. Hapo sasa moto ulizidi kuwa mkali maana sasa uwezo wa silaha ulikuwa unafanana. Baada ya dakika chache msaada ulifika na hapo tukafaikiwa kuwakamata, gari ya wagonjwa ilifika na Mike pamoja na raia kadhaa waliojeruhiwa katika pambano hilo waliwahishwa hospitali punde baada ya kupatiwa huduma ya kwanza. Niliporudi kituoni, mkuu wa kituo aliniita ndani moja kwa moja nikajua kuwa hizo ni lawama. Lakini haikuwa hivo, mkuu wa kituo alinisifu kutokana na ujasiri wangu hasa ukizingatia bado nilikuwa mgeni kati anga hizo. "karibu katika matatizo" mkuu wangu aliongea maneno hayo ambayo kwa haraka sikuweza kuifahamu maana yake, Baada ya hapo niliruhusiwa kurudi nyumbani kupumzika. Lakini nilipofika nyumbani nilimkuta mzee akiwa amevimba kwa hasira, nilipojaribu kumuuliza kuna tatizo gani hakunijibu kitu na kuinuka akaingia zake ndani. Hapo kichwa kilijaa mawazo, basi niliingia chumbani kwangu na kujifanyia usafi kisha nikatoka. Nilipofika ukumbini nilimkuta mzee akiwa anaangalia taarifa ya habari, nilimsalimia kisha nikakaa pembeni yake. "jemedari mzuri anazuia uhalifu na wakati huo huo ana hakikisha mtu asiehusika hapati jeraha lolote, na pia jemedari mzuri ni yule anaehakikisha mwenzake hajeruhiwi" alianza kuongea maneno hayo kisha akaniangalia na kunambia "umefanya vizuri lakini unatakia ujitahidi na kuhakikisha usalama wa raia". Baada kuongea maneno hayo alinikabidhi karatasi nyeupe ambayo haikuandikwa kitu, kisha akanipa ishara nisiongee kitu na niihifadhi ile karatasi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada maongezi mafupi na baba chakula kilikuwa tayari, wote tulisogea mezani na kupata chakula cha usiku. Tulipomaliza niliaga na kuingia chumbani kwangu kulala, na kutokana na uchovo wa mchana, usingizi ulinizoa nilipogusa tu kitanda. Nilikuja kushtuka baada kuota ndoto mbaya sana, nilipoangalia saa nikagundua ilikuwa saa kum na moja usiku. Niliamka na kujiandaa, niliingia jikoni na kuandaa chai na vitafunuwa vya asubuhi. Nilipomaliza niliandika ujumbe na kuuacha mezani kisha nikatoka. Kitu cha kwanza nilichokifanya, nilielekea hospitali kwenda kumuangalia Mike ambae alikuwa anendelea na matibabu. Baada ya hapo nilielekea kituoni kwa ajili ya kuanza majukumu yangu ya kila siku. Kila mtu kituoni alikuwa akinisifu, na magazeti hayakuwa nyuma nayo. Kila gazeti liliandika linavojisikia "tunahitaji polisi kama huyu", "Waabudu matatizo kaeni pembei, simba jike kaingia mtaani". "mamilioni ya pesa yaoolewa". Hivyo ni baadhi ya vuchwa vya habari vya magazeti machache, niljifanya kama siyashughulikii lakini moyoni nilikuwa nnafuraha na kichwa kilikuwa kikubwa kama dunia kwa sifa. Niliendelea na majukumu yangu ya kila siku kama polisi, baada ya mwezi mmoja Mike alirudi kazini na kuendelea kama kawaida. Wakati huo jina langu lilikuwa lishasambaa na kila mtu alikuwa anataka kunijaribu na kila aliefanya hivo alikutana na kisiki. Baada ya Mike kurudi alianza kunipa mazoezi mengine ya kupigana, kila siku baada ya kazi tulikutana Gym na kuoata mazoezi kadhaa ya kujiweka powa. Maana alinambia kuwa niko hatarini sana kutokana na sifa zangu, mpaka majambazi sugu na wale wanasiasa watakuwa wananiwinda hivyo ni lazima niwe fiti, nisiwe nategemea silaha tu. Na pia alinishauri nihame nyumbani ili familia yangu iwe salama kutokana na mikono ya wabaya. Nililiwasilisha wazo hilo kwa mzee nae hakupinga alikubali na taratibu za kutafuta nyumba zikaanza, haukipita muda nilikuwa na kwangu. Kumbuka hapo nilikuwa na miaka ishirini tu na tayari nilishakutana na vikwazo vingi sana katika kazi yangu.Niliendelea na majukumu yangu huku nikiendelea kupokea mafunzo ya ngumi kutoka kwa Mike, ambae alionekana kama komando. Maana mazoezi aliyokuwa ananipa hayakuwa na tofauti na yale nliokuwa nayaona katika TV na movie mbalimbali wakifanya makomando. Miaka miwili ilipita huku nikiwa nimepandishwa cheo mara mbili, siku hiyo baada ya kumaliza mazoezi. Mike aliniita na kunambia kuwa anataka kuanambia kitu. Mapigo ya moyo yalianza kudunda na kihasho chembamba kikaanza kunitoka. "nimemaliza kazi niliopewa na General, natumai umeiva vya kutosha sasa" aliogea maneno hayo na kuniacha njia panda na kumuomba anielezee. Na hapo ndio akafunguka kuwa yeye ni Leutenant General Mike Kings, na alipewa kazi ya kuhakikisha kuwa naiva vya kutosha katika mafunzo ya kijeshi hasa kwenye mkono.
Na hapo akanitonya kitu kuwa kuwa polisi ni maandalizi ya kuelekea katika jeshi la nchi hiyo. Baada ya mazungumzo hayo aliniaga na kunambia kuwa tutakuja kuonana tena labda jeshini katika mafunzo maalum. Kisha akaondoka, nilikaa kitako kwanza huku nikijiambia mwenyewe kuwa naota na nikiamka kila kitu kitakuwa sawa. Lakini ukweli ulibaki kuwa ukweli tu, maana siku ya pili nilipofika kazini nikakabidhiwa msaidizi mwengine na nilipouliza kuhusu Mike nikaambiwa kuwa amehamishwa kituo. Hapo sasa nikaamini kuwa ndio ulikuwa mwisho wa kuonana na Mike.
Baada ya miezi sita tokea Mike nilipokea barua kuwa nimeitwa katika makao makuu ya jeshi, na bila kuchelewa nilielekea huko. Nilishanga kumkuta baba akiwa katika Gwanda zake za Kijenerali huku pembei akiwa amesimama Mike katika combat takatifu ya Lt. General. Baada ya robo saa waliingia watu wengine sita wakiwa wameongozana na vijana ambao walikuwa mapolisi kama mimi kisha tukaelekezwa katika chumba maalumu cha vikao. Hapo alisimama baba na kutoa salamu kisha akaanza kuonge "najua wengi mtajiuliza kwanini mumeitwa hapa, ila ukweli ni kuwa toke mwanzo nyinyi mlichaguliwa kujiunga na kikosi maalum cha kupambana wahalifu sugu. Natumai wote mumewahi kusikia kikosi kinachoitwa "THE PIRATES". Na wengi mlikuwa mnadhani ni stori lakini kikosi hichi kipo na ndio kinachopambana na wahalifu sugu hapa nchini na je ya nchi. Na sheria, ili ujiunge na kikosi hichi ni lazima uanze katika ngazi za askari wa kawaida. Hivyo basi hongereni na karibuni katika anga za majanga".
Kuna kitu sikukielewa na nlipotaka kuongea kitu, mzee alinipa ishara kuwa ninyamaze. Baada ya kikao kile kifupi cha utambulisho tulipelekwa katika chumba maalum na kupigwa picha kisha tukaruhusiwa turudi katika maeneo yetu ya kazi na kuambiwa kuwa hiyo ni siri na hakutakiwa mtu mwengine zaidi yetu kujua. Nilirudi kituoni kwangu nikiwa na maswali kadhaa lakini wa kuyajibu alikuwa ni mzee tu. Hivyo nilisubiria mpaka zamu yangu ilipokwisha na kuondoka kituoni lakini sikwenda nyumbani kwangu. Moja kwa moja nilielekea nyumbani kwa wazazi wangu na nilipofika tu baba alitabasamu na kunipa ishara nikae. Na kwa sababu mama alikuwa hayupo nikaona huo ndio mwanya pekee wa kumuuliza maswali yangu. Swali la kwanza lilikuwa ni ilikuwaje hasa akarudia gwanda wakati yeye alishastaafu. Nae akanijibu kuwa kustaafishwa kwake ilikuwa ni moja kati ya mipango ya raisi ili amkabidhi majukumu mengine ambayo yalikuwa ni siri. Akasema kuwa ile siku alipokwenda kukabidhi barua ya kukubali kustaafu, mheshimiwa raisi alimwambia kuwa hajastaafishwa bali alipewa majukumu mengine makubwa zaidi ya kuendesha kikosi maalum cha THE PIRATES.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Yeye mwenyewe alishangaa baada kusikia jina hilo kwani alikuwa akidhani uwepo wa kikosi kile maalum ni maneno tu ya watu. Lakini mhshimiwa raisi alitaka baba akiongoze kikosi hicho ambacho alikuwa akikiongoza mwenyewe kwa muda mrefu, kutokana na majukumukuwa mengi aliamua kukibadhi kikosi hicho kwa mtu ambae ni mzalendo sana na hakuwa mwengine isipokuwa baba. Baada ya hapo ndio akapewa maelekezo yote yanayostahiki, baada kunieleza hivo kidogo roho yangu ilitulia. Basi tuliendelea na mazungumzo mengine mpaka mama aliporudi nikamsalimia na baada dakika kidogo niliaga na kuondoka. Nilirudi nyumbani nikiwa mwepesi kabisa baada ya maswali yangu yote kujibiwa, nilipumzika kwa amani kabisa usiku huo.
Siku iliofuata mapema niliamka na kufanya mazoezi kisha niakaoga na kupata kifungua kinywa, nilipomaliza kila kitu nilitoka na kuelekea kazini. Nilipofika niliambiwa nahitajika na bosi ofisini, na nilipoingia tu alinikabidhi karatasi ya uhamisho wangu. Nilijua tu mambo yashaiva, niliichukua karatasi ile na kurudi nayo ofisini kwangu. Niliifungua na kuanza kuiosoma mwisho iliandikwa "ukiupata ujumbe huu, mara moja fika makao makuu ya jeshi ukiwa na hii karatasi". Nilitoka ofisini kwangu mbio za ajabu na moja kwa moja hadi kwenye gari yangu na safari ikaanza. Nilikanyaga mafuta kisawa kwa mara ya kwanza sikuheshimu hata sheria za barabara. Baada ya dakika kumi nilifika makao makuu na kuwaonyesha ile karatasi wanajeshi waliokuwa getini. Walinipa maelekezo ni wapi natakiwa nifike, bila asante niliondoa gari na kuelekea sehemu ya megesho. Nilishuka na kuanza kukimbia, nilifika katika koridoo ambayo ndio nilipoelekzwa nikakuta karatasi imeandikwa "una sekunde sitini tu kufika juu kabisa ya jengo hili, ukichelewa helicopter ina kuacha" nilihisi kuchanganyikiwa hasa ukizingatia katika koridoo ile kulikua na watu wengi kweli. Nilianza kukimbia huku nikipigana vikumbo na watu wengine lakini wala sikujali, na nilipoona nazidi kuchelewa ilibidi nitumie mafunzo ya ziada ili kuwapita watu hao. Nilivua viatu huku nakimbia, hapo sasa nilianza kuwaruka kwa kukanyaga kuta za koridoo hio. Wengine niliwasukuma kwa nguvu na kuwatupa pembeni, niliongeza mwendo huku akili yangu ikiwa inafanya kazi kama computer. Nilifika juu ya jengo hilo lakini sikuikuta helicopter, nilianza kujilaumu lakini ghafla alitokea mtu kwa pembeni na kunipa ishara nimfate kisha yeye akaongoza njia. Tulifika katika chumba kimoja hivi na kuwakuta wengine wakiwa wananiangalia, mara walianza kupiga makofi. "umetumia sekunde hamsini na tatu" aliongea Mike huku akitbasamu. Baada ya nusu saa tulipewa mabegi na kuambiwa tuongozane na Mike mpaka juu kule, tulipofika tulikuta helicopter ikitusubiri. Tulipanda na safari ikaanza, tukiwa ndani ya chombo hicho tulipewa maziwa kuambiwa tujwe kwa sababu safari ni ndefu sana. Cha ajabu baada ya kunywa tu maziwa hayo macho yalianza kuwa mazito na mwisho wote tukapitia na usingizi mzito. Mimi nikuja kushtuka baada kuhisi hewa nzito, na nilipofungua macho nilishtuka baada kuona chombo tulichopanda kinawaka moto, niliwaangalia marubani wote walikuwa wakivuja damu. Nilianza kuwaamsha wenzangu wengine ambao kwa ujumla wetu tulikuwa saba, wote tulitoa nje ya chombo hicho. Baada kuridhika kuwa hakuna hata mmoja wetu alieumia sana, tulikaa kwanza huku kila mtu akitafakari kuwa ni jambo gani lililotokea. Kutokana na kiza tulishindwa kugundua tuko wapi, na ilibidi tulale hapo hapo. Siku ya pili mapema tuliamka na kila mtu alichukua begi lake alilopewa na kufungua, ndani ya mabegi hayo kulikuwa na combat pamoja na silaha nyepesi na vifaa vya mawasiliano.
Kila mtu alitoa nguo na kubadili kisha akachukua na vile vifaa maalum vya mawasiliano na kuweka sikioni. "jamani ndio tumepata ajali hivi, tunatakiwa tutafute njia ya kutokea" aliongea mwanaume mmoja kati yetu. Na wote tulikubaliana nae na pia tukakubaliana kuwa tutakaa pamoja hata litokee jambo gani. Kila mtu alijipanga vilivyo na wakati naendelea kukagua begi langu nikakuta ramani, niliitoa na kuitandika chini kisha kwa pamoja tukaanza kuiangalia kwa makini. Mschana mmoja alitoa kampas na kuweka juu ya ramani hio, wakati tunendele kukagua ramani hio tukaona alama ya fuvu. Tukakualiana kuwa tunaelekea hapo kweye hiyo alama, baada hapo tulisimama na safari ikaanza huku tukiwa tunapiga stori mbili tatu ili kupunguza safari. Baada ya masaa sita mfululizo ya kutembea tulifika pahali tukakuta makazi yaliokimbiwa na watu kabisa. Majumba ya eneo hilo yalikuwa yamevunjika na kubomoka, sehemu hiyo ilitawaliwa na vumbi na moshi. "jamani hapa tunatakiwa tuwe makini sana" niliongea huku nikitoa bastola yangu ndogo na kuishika vizuri mkononu. Na wengine wote waliniunga mkono nao wakatoa za kwao na tukaaanza kutembea taratibu kwa umakini wa hali ya juu kabisa. Tulitembea huku macho yetu yakiwa wazi na kuangaza pande zote, ghafla tulianza kusikia milio ya risasi. Ilibidi tujibanze pembeni na hapo sasa kila mtu akawa muoga kukaa mbele, ilibidi nijitolee kuwa kiti moto. Nilishika bastola yangu kisawa na kucungulia, kwa mbali nilimuona mtu akiwa amejibanza sehemu huku akiwa na bastola. Niliwageukia wenzangu na kuwaambia nilichokiona, baada kushauriana tukaaanza kukimbia ukuta baada ya ukuta. Cha ajabu yule mtu alikuwa hashambulii lakini tulipomkaribia zilirindima risasi kama mvua, ilibidi tugawanyike makundi mawili ili kumchanganya. Tukawa tunasogea taratibu, na alipowashambulia wenzangu kundi jingine. Nilichomoka sehemu nilio kwa kasi kubwa na kubirngitia kabla hata hajageuka nilipo nilifyetu risasi iliompata kifuani na kumfanya aanguke kama mzigo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulimsogelea na kumuangalia, baada kuhakikishakuwa ameshakufa tayari. Nilirudisha bastola yangu ndogo kiunoni na kubeba ile AK47 aliokuwa anatumia adui yetu. Safari iliendelea kwa umakini wa hali ya juu huku mara kadhaa tukishambuliana na watu. Kadri muda ulivyokwenda walizidi kuwa wengi lakini tulifanikiwa kupita eneo hilo bila hata mmoja kupata majeraha makubwa zaidi ya michubuko tu. Baada ya kutoka eneo hilo tuliingia porini na kwa vile tulitembea muda mrefu bila kupumzika na hasa baada ya kupata ule mshikemshike tulijikuta tukiwa tumechoka sana na kuamua kupiga kambi ndani ya msitu huo ili siku ya pili. Tuligawana majukumu, wengine walitengeneza mahema na wengine tuliinia vichakani kutafuta kuni za kuwashia moto. Baada ya kazi zote kukamilika, tuligawana majukumu ya ulinzi usiku huo. Wawili walilinda na wengine walila, baada ya masaa matatu wale walikuwa wanalinda walikuja kuniamsha mimi na mwenzangu mmoja tukaendelee na zoezi lile wakati wao wanapumzika. Baada ya masaa matatu mengine tuliwaamsha wengine waendelee na kazi ya ulinzi lakini mimi sikurudi ndani kulala.
Niliendelea na wale wengine mpaka asubuhi, palikucha na kila mtu alijiandaa kuendelea na safari. Kwa kweli njaa ilikuwa inauma sana, siku nzima tulikuwa hatujala baada ya kunywa ya maziwa yaliotulaza. Wenzetu wawili walikuwa wameshaanza kulegea, lakini ilibidi wajikaze tu maana safari haikuwa ndefu tena. Baada ya masaa mawili tulifika katika geti kubwa. Tulishangaa kweli baada kwaona wale marubani ambao tuliamini walikuwa wamekufa katika ajali ya ndege wakiwa wanatusubiri getini. "hongereni kwa kumaliza mafunzo ya awali" waliongea wanajeshi hao na kutukabidhi kila mmoja wetu chupa ya maji. Baada ya hapo tuliingia ndani ya kambi hiyo kubwa na kupelekwa katika sehemu ya kula na kupata chakula. Kila mtu alikula kama chakula kinataka kukimbia, chezea njaa wewe.
Baada ya kumaliza kula tulipelekwa katika vyumba vyetu vya kupmzikia na kuambiwa tupumzike mpaka pale tutakapoitwa. Niliingia chumbani kwangu na kujilaza na viatu vyangu, na kutokana na uchovu wa hali ya juu usingizi ulinichukua gubigubi. Nilikuja kushtuka baada ya kusikia mlango ukigongwa kwa nguvu. Niliufungua na kukutana na Mike ambae alinipa ishara nimfuate, tulitembea kama dakika tano kisha tukaingia katika chumba maalum. Mike alwasha TV kubwa, macho yalinitoka baada kuona matukio yote tulioyafanya katika mafunzo ya awali. Kumbe tukio zima lilikuwa linarikodiwa, pia alinionyesha makosa tuliyatenda wakati wa kozi nzima. Baada ya kumaliza aliinuka na kunipa ishara niondoke.
Nilirudi chumbani kwangu na kuendelea kupumzika, huku nikiwaza kama nitaweza kumaliza kozi nyingine maana ni balaa. Jioni tuliitwa na kupata chakula cha jioni kisha tukapelekwa kwenye chumba kingine na tukaambiwa tusubri humo. Baada ya dakika mbili hivi aliingia mtu mmoja na kutukabidhi funguo za gari kila na kila mmoja wetu alipewa funguo ya kwake. Baada ya kukabidhiwa fungo hizo tuliambiwa turudi vyumbani mwetu ili kuchukua mabegi yetu na kisha tukutane katika uwanja wa maegesho ya gari. Tulifanya hivo na kufika eneo husika, tulipewa maelezo kuwa tunatakiwa tufike katika bandari fulani hivi. Na safari hio kwa kawaida ilichukua siku tatu lakini tuliambiwa tufike katika bandari hiyo ndani ya masaa arobaini na nane. Hapo nadhani utaelewa kuwa tulitakiwa tundeshe vipi, basi baada ya maelezo hayo tulipewa ruhusa na kila mmoja aliwkenda kwenye gari yenye namba iliofanana na namba ya funguo alipewa. Tuliwasha gari na safaro ikaanza, safaru hio ilianza karibu na kiza kungia, tuliendesha kwa umakini wa hali ya juu japo mwendo ulikuwa mkubwa sana. Safari hio iliendelea usiku kucha bila kupumzika, tayari mpaka asubuhi tulishatumia zaidi ya masaa kumi na mbili na tulikuwa hatujamega hata robo ya safari. Hapo mimi binafsi nikaona kuna dalili za kuchelewa. Kwa kupitia kifaa maalum cha mawasiliano niliwaambia wenzangu kuwa tumechelewa hivo tunatakiwa tuongeze mwendo zaidi. Mwanzo walinipinga kutokana na kuhofia kupata ajali, na nlipoona hawataki kukubaliana na mimi nikajisemea isiwe tabu kwa sababu kila atakula alichokivuna. Niliweka gia na kuamua kukanyaga mafuta kisawasawa, na gari nayo ilitii kwa kutimua vumbi la kutosha katika barabara hiyo ya vumbi. Nlikuwa makini sana huku mikono ikiwa metulia katika usukani, nilitembea kwa mwendo kasi huo kwa muda mrefu sana. Wenzangu nilikuwa nimewaacha umbali mkubwa sana, kuna wakati nilianza kuhisi uchovu na ikabidi nisimamishe gari. Nikatoa dumu moja la maji na kuanza kujimwagia ili niondoe uchovu kisha nikarudi kwenye gari na kuendelea na safari.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tayari masaa ishirini na kadhaa yalishapotea na kiza kilianza kuingia tena, lakini gari ilikuwa na taa zenye mwanga za mkali sana. Hivyo haikuwa shida kutembea mwendo ule ule wa kibabe. Nilzidi kukanyaga mafuta huku nikiwa na lengo niimalize safari hiyo chini ya masaa arobaii na nane. Ghafla mvua kubwa ilianza kunyesha na kutoka na njia ile kuwa ya vumbi, ilipolowa iligeuka na kuwa tope. Ilibidi sasa nipunguze mwendo ili kuepuka kuteleza, mara kadhaa gari ilitaka kukwamba lakini asante kwa alietengeneza ile gari na kuiweka mashine yenye nguvu sana huku ikiwa inasukumwa na matairi yote manne. Nilitembea hivo kwa muda kidogo kabla kuamua kutembea tena kwa mwendo kasi japo ilikuwa hatari lakini bado nilikuwa nataka niweke rikodi mpya ya kutembea masaa machache zaidi. Ilkuwa hatari lakini sikujali kabisa, baada ya masaa kadhaaa mvua ilikata na cha ajabu zaidi baada mwendo wa dakika kama tano hivi nilikuta njia yenye vumbi kama ile mwanzo utadhani mvua haikunyesha kabisa. Niliangalia computer yangu ili kujua wenzangu nimewaacha kilometa ngapi, baada kuona kuwa nimewaacha kilometea zaidi ya kumi nilitabsamu na kuuendelea na safari kwa mwendo uleule. Niliangalia saa yangu na kugundua kuwa nilishatumia masaa thalathini, niliongeza mwendo tena na kufikia wakati nikamaliza kisahani chote. Mshale wa kuonyeshea spidi iliogonga mwisho kabisa, laiti kama gari ingepanda jiwe dogo tu basi leo ingekuwa stori nyingine kabisa. Baada ya mwendo wa masaa manne hatiamae niliikuta barabara ya lami na kwa mbali niliana kuona makazi ya watu japo walikuwa si wengi sana. Nilipunguza mwendo kwa sababu tayari nilishaingi mjini, lakini cha ajabu hakuna mtu alieshughulika kila mtu aliendelea na shughuli zake kama kawaida. NIliumaliza mji na kuanza tena kazi ya mwanzo, kwa sababu barabara ilikuwa ya lami sikupata shida sana kwenda kasi. Kwa mbali niliaza kuona bahari, nilipata matumaini kuwa huenda nikawa nishafika lakini wapi, nilitembea kwa masaa matano mpaka nipoaza kuona bandari na tayari nilishatumia masaa arobaini na na tatu na baada saa moja nilikuwa tayari nimeshafika sehemu tuliotakiwa kufika. Mtu aliekuja kunipokea hakuwa mwengine bali alikuwa ni baba, nilifurahi sana maana nilikuwa na siku kama mbili hvi sijamuona. Alinionyesha ishara ya dole gumba kama kunisifia na baada ya masaa manne waliingia wenzangu, wakati huo tayari mimi nilishaoga na kujipumzisha. Siku ya pili mapema tuliitwa na kuanza kukabdhiwa nafasi, mimi nilichaguliwa kuwa kiongozi na jina nililopewa likuwa ni RED BUTTERFLY (kipepeo mwekundu).
Kila mtu alifurahi kutokana na cheo alichopewa, baada ya hapo tuliruhusiwa kuzunguka ndani ya meli hiyo kubwa ilikouwa ikakata mawimbi kuelekea nisipopajua. Baada ya safari ndefu hatimae meli ilitia nanga katika kisiwa kimoja hivo, tulishuka na kuzama ndani ya msitu wa kisiwa hicho. Tulikuja kutokea mbele ya ukuta mkubwa sana ukiwa umechorwa alama ya fuvu. Wakati nikiendelea kushangaa ghafla ukuta huo ulianza kufunguka na kisha tukaingie ndani. "karibuni nyumbani" aliongea Lt general Mike, kwa kweli ukisikia watu wanamaficho basi haya yalikuwa balaa maana hiyo mitambo ilikuwa inalinda eneo hilo si mchezo kabisa. Tuliingia mpaka ndani na kupelekwa katika vyumba vyetu kisha tukaambiwa tukutane uwanjani baada ya nusu saa. Nilijilaza kitandani huku nikiwaza juu ya mazoezi yote niliopitia maana kama mtu ungekuwa na moyo laini basi kama sikuacha ungekuwa ushakufa maana acha kabisa. Muda ulipotoka nilivaa gwanda na kutoka nje, huko tulikutana na Mike akiwa kama msimamizi wetu. Kuanzia siku hiyo tulianza kufanya mazoezi yenyewe sasa, na yalikuwa magumu kupita maelezo. Kutegua viuongo katika mazoezi hayo ilikuwa ni jambo la kawaida sana, mazoezi hayo yaliendelea kwa muda wa mwaka mzima. Na baada ya safri ndefu hatimae mazoezi yaliisha na hapo sasa tukaapishwa rasmi kuwa PIRATES, ikiwa ni pamoja na kuchorwa tatu ya fuvu kwenye mkono wa kulia" Scarlette alipofika hapo alinyamaza na kumuangalia Alex usoni, alikuwa ameacha mdomo wazi huku akimshanga mwanamke huyo ambae kwa kumuona nje hivi utadhani ni mlaini sana kumbe ni moto wa kuotea mbali. "sasa ikawaje baada ya kumaliza mazoezi" Alex aliuliza huku akionekana kunogewa na simulizi ya maisha ya bidada Scarlette.
Scarlette alikaa sawa na kuendelea "baada ya kumaliza mazoezi hayo tulipewa ruhusa ya kurudi majumbani kwetu, huku tukiambiwa tutakapohitajika basi tutaambiwa. Nilifurahi sana kwa sababu ni muda mrefu sana sijamuona mama, tulikunja kunja na siku ya pili mapema tulipanda helicopter na kurudi majumbani. Lakini taarifa niliokutana nayo nyumbani ilikuwa si nzuri, mama alikua hospitali kalazwa baada kuzidiwa. Haraka niliacha vitu vyangu na kubadili nguo kisha nikachukua gari na kuelekea hospitali, aliponiona aliyabasamu na kuniita. Nilisogea na kukaa pembeni yake kisha akafunua shuka na aliokuwa amefunikwa na kunionesha tatoo ya fuvu mgongoni kwake. Macho yalinitoka baada kugundua kuwa hata mama pia alikuwa ni mmoja kati ya wanajeshi wa kikosi cha siri na pia kilichonichosha zaid ni pale aliponambia kuwa alikuwa akiniftilia kila siku katika mazoezi. Kwa maana nyingine na yeye alikuwepo katika sehemu zote nilizopita. Baada ya hapo ndio akanieleza kuwa hata baba pia alikuwa ni mmoja kati yao na huko ndipo walipokutana na pia huko ndio chanzo kikubwa cha wao kupoteza uwezo wa kuzaa baada kupigwa na mionzi mikali sana ya bomu. Tuliongea mengi sana na alionekana kuchangamka sana, muda wa kutizama wagonjwa uliisha.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment