Search This Blog

Friday, 20 May 2022

C.O.D.EX. 3 (THE REAL ME) - 3

 







    Simulizi : C.O.D.EX. 3 (The Real Me)

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilimuaga na kuondoka huku nikiahidi kurejea siku ya pili, nilirudi nyumbai kwangu na kujipumzisha kitandani na kutokana na kuwa ni muda mrefu sikupata kulala vizuri basi usingizi ulinichukua na kutokomea katika ulimwengu wa ndoto za kivita tu. Nilikuja kushtuka baada ya alarm ya saa kulia, nilishuka kitandani na kupasha mwili kidogo kisha nikaingia chooni na kujisafisha. Nilipata kifungua kinywa na baada ya hapo nilingia kwenye gari na kuelekea hospitali, lakini nilipofika katika kile chumba alichokuwa amelazwa sikumkuta. Wakati natoka nilikutana na baba ambae alionekana kuwa na majonzi huku akijikaza asitoe machozi. Nilimsogelea na kumshika mkono kisha nikamwambia anipeleke alipo mama. Na hapo ndio akaniambia tayari alishatangulia mbele za haki, nilijikaza sana nisilie lakini nilishindwa na kujikuta nikitoa machozi kwa kilio cha kimya kimya. Nilimuomba baba turudi nyumbani kwenda kuanda taratibu za mazishi, alikubali na tukarudi nyumbani. Lakini nilichogundua kua baba alikuwa akijizuia kulia, nilimshika mkono na kumwambia kulia sio ishara ya udhaifu. Ni kama nilifungua bomba la maji maana alianza kulia kama mtoto mdogo, lakini wala sikumnyamzisha nilimuacha aendelee kulia mpaka atakaporidhika. Baada masaa kadhaa alikuwa kashatulia na hapo tukapanga taratibu za mazishi na siku ya pili mapema tulimzika na kutokana na heshima yake mpaka raisi alihudhuria mazishi yake. Baada kumaliza kila mtu alitawanyika na kurudi nyumbai kwake, pale makabrini nilibaki mimi na baba tu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Baada ya dakika chache tuliondoka na kurudi nyumbani, siku za mwanzo zilikuwa ni miongoni mwa siku ngumu sana kwa baba kutokana na mazoea na mapenzi aliyokuwa nayo juu ya mke wake. Lakini hakukuwa na jinsi kwani kazi ya Mungu haina makosa, kwani binaadamu wote safari yetu ndio hiyo moja. Baada ya mwezi kupita mzee alikaa sawa na kuendelea na majukumu yake kama kawaida. Siku hiyo tukiwa nyumbani ghafla ilituwa Helicopter na bila kuchelewa mzee alinipa ishara tuingie na safari ya kuelekea kambini ikaanza. Tulifika huko na kukaribishwa na barua maalum iliyotoka kwa mheshimiwa raisi. Mzee aliisoma kwa makini kisha akaichana na kuichoma moto, baada ya hapo alituambia baada ya nusu saa tukutane katika chumba cha mikutano. Kila mmoja wetu aliingia chumbani kwake na kuvaa combat ya kazi na baada nusu wote kwa pamoja tulifika katika chumba cha mikutano. Baba alisimama na kuanza kuongea "nimepokea ujumbe kutoka ngazi ya juu kabisa katika nchi hii, ujumbe huu umeandikwa kwa mikono ya raisi pamoja na kuweka saini yake. Kuna mtu mmoja ametekwa na watu wasiojulikana, lakini kupitia vyombo vya kiintelijensia wameweza kugundua alipopelekwa. Mtu huyo ni muhimu sana na tunatakiwa tumrudishe nyumbani na kama itashindikana basi auwawe ili kulinda siri aliokuwa nayo". Wote tulishangaa na mimi nilijiuliza ni kitu gani hasa alichokuwa amekificha mpaka raisi afanye maamuzi magumu kiasi kile. Chini ya uongozi wa Lt general Mike pamoja kikosi kichanga chetu tulipewa masaa sabini na mbili tuwe tumekamilisha kazi hiyo. Baada mzee kutoa amri hiyo, Lt general Mike alituomba tumfate mpaka katika chumba cha kupanga mikakati.

    Tuliingia ndani ya chumba hicho na kukuta silaha kadhaa ambazo ndizo zingetumika katika kufanikisha kazi hiyo, tuliambiwa tukae kwenye viti kisha taa zilizimwa na kuwashwa projector kubwa. Lt genaral Mike aliinuka na kuanza kutueleza "hizo picha mnazo ziona katika runinga hii, zimepigwa muda si mrefu kwa kutumia ndege aina ya drone, picha hizo ni za kambi anashikiliwa huyo mlengwa wetu. Kambi hii ipo katikati ya msitu mmoja mkubwa sana, upande mmoja wa msitu huo kuna bahari na hiyo ndio njia tutakayoingilia katika kambi hiyo. Kutoka eneo la bahari mpaka ilipo kambi hiyo ni mwendo wa masa matano ya kukimbia bila kusimama. Na ijulikane kuwa tukiondoka hapa tuna masaa sabini na mbili tu mpaka kurudi hivyo umakini wa hali ya juu unatakiwa uzingatiwe katika kufanikisha kazi hii, tumeelewana", sote kwa pamoja tuliitika kuwa tumeelewa. Basi baada ya hapo tuliondoka na kuelekea sehemu ambayo kulikuwa ndege ikitusubiri. Tulipanda na safari ikaanza huku kila mmoja akionekana kuwa wababridi kutokana na kuwa hio ndio ilikuwa kazi yetu ya kwanza tena ilikuwa ni hatari sana. Tulikaa angani kwa muda wa masaa zaidi ya matano huku kila mmoja akiomba mungu wake kazi ile iende vizuri. na kumbuka tulikuwa kiloketa kadhaa kutoka kwenye kisiwa amabcho tulitakiwa kufika. Ndege ilishuka mpaka usawa wa bahari na hapo tukapewa ishara ya kuruka, haikuwa ngumu kwa sababu mazoezi kama hayo tulishafanya kipindi cha nyuma. Tulikuwa watu nane tu, na baada kuingia ndani ya maji ndipo kasheshe ikaanza tulitakiwa kuogelea mpaka nchi. Lt general Mike alikuwa sawa kupita maelezo, aliogelea kwa kasi ya ajabu huku sisi tukimfata kwa nyuma mpaka tukafika kisiwani. Tulitoka kwenye maji na kupumzika kwa nusu saa kabla ya kuendelea na safari, mapumziko yalipokwisha Lt general Mike alitupa amri ya kusimama na kuendelea na safari.

    Safari ilikuwa ni mchakachaka tu huku kila mtu akiwa makini, tulitembea kwa muda wa masaa zaidi ya matatu mpaka tukawa tumebakiza kilometa nne mpaka kufika kweye kambi ile. Hapo ndio tukaambiwa tuweke kambi kwaajili ya kuendelea na operesheni siku ya pili. Mpaka wakati huo tulikuwa tumeshatumia masaa kama tisa hivi kati ya masaa sabini na mbili tuliopewa. Kila alifuahi sana aliposikia kupumzika, tuliweka vitu chini lakini wakati tunataka kutandika vitambaa maalum vya kulalia chini. Lt G Mike alituambia kuwa kulala ni juu ya miti na si chini, baada ya hapo kwa kasi ya ajabu alikimbia na kukanyaga mti kisha akashika tawi na kupotelea kwenye miti. Hatukuwa na budu kumuiga, tulipanda kila mtu na mti aliochagua. Kufika kwenye tawi kila mtu allitoa kamba yake na kujifunga vizuri kisha tukalala, nilikuja kushtuka baada kitu kunipiga kichwani na nilipoangalia chini nilimuona LTG Mike akiwa anawashtua wengine. Nilishuka kwenye mti na kunawa uso kisha LTG Mike akatowa karatasi yenye ramani na kuitandika chini kisha akaanza kutupangia majukumu. Sara pamoja Alfred wakapangiwa utunguaji(sniper). James, Kyle na mimi tukapangiwa kazi ya kuzama ndani ya kambi na kutoka na mlengwa. LTG Mike na wawili waliobaki ambao ni Lameck na Rosequeen walikuwa ni wakuwapoteza maadui zetu. Baada kila mtu kukabidhiwa majukumu yake tuliagana na kukubaliana tukutane ufukweni baada ya kazi hiyo kuisha. Kila kikundi kilishika njia yake na kutokomea upande wake, tuliwasiliana kupitia vifaa maalum vya mawasiliano. Mimi na wenzangu watatu tulisogea mpaka karibu na fensi kubwa ya kambai na kujificha. Kwa mbali tulishuhudia wale walinzi wanaokaa juu kama masniper, wakianguka mmoja baada ya mwengine mpka waote wanne wakaisha. Baada ya hapo tulimuona LTG Mike na kikosi chake wakiingia kambini na kuuwasha moto. Wakati huo huo na sisi tukapenya bila kuonekana katika kambi hiyo. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na kwa sababu tulikuwa tunajua hasa target wetu yuko wapi, hatukupata shida sana kumtafuta. Shida ilikuwa ni kukabiliana na wale wanajeshi wa kambi hio. Tulifanikiwa kufika ndani kabisa na kukumta target akiwa hoi, nilikimbia mbio mpaka alipo na kumfungua kamba kisha nikaampa maji yeye chemichal maalum yenye kuzalisha nguvu kwa wakati mfupi. Kisha nikamkabidhi bastola moja kisha safari ya kutoka ikaanza. Huku nje milio iliokuwa inasikika ilikuwa ni hatari tupu, risasi zilikuwa zinarindima si masihara. Tulifanikiwe kutoka nje ya kambi hiyo bila shida yoyote na kuanza safari ya kuelekea ufukwenu ambapo tulikubaliana tukutane. Huyo jamaa tuliomuokoa alikuwa balaa, alikuwa hapigi risasi zaidi ya moja kwa kila aliepita mbele yake. Alihakikisha hakosei, tulitembea kwa kasi bila kupumzika mpaka tulipohakikisha tumefika mbali na kambi. Tuliwasiliana na wengien ili kujua mambo yakoje upnde wao, na wao walitujibu kuwa wako njiani wanaelekea ufukweni. Baada ya kupokea taarifa hizo tulianztena safari huku tukiwa makini tusije kamatwa. Baada ya masaa mawili na kidogo hivi tulifika ufukweni na kujifcha sehemu. Nusu saa baadae wenzetu wengine waliingia na hapo sisi tuakatoka tulitoka na kuelekea walipo wenzetu. Yule jamaa tuliemuokoa alipofika tu alipiga salute na kumpa heshima LTG Mike, tulikaa hapo ufukweni kwa robo saa tu kisha zikapita ndege mbli za kivita na kuelekea kule kwenye kambi na hazikupita hata sekunde chache tuliskika milio ya mabomu. "mission accompilished", LTG Mike aliongea maneno hayo kisha akaongea na code maalumu na baada ya nusu saa ilitua ndege katika maji na safari ya kuelekea kambini ikaanza.

    Tulipokewa kwa furaha kubwa sana, na nilishangaa pale nilipomuona raisi mwenyewe akiwa ni miongoni mwa watu walikuja kutupokea. Tulishuka kwenye ndege na kuelekea mpaka alipo raisi na kutoa heshima. Raisi alitabasamu na kutupongeza kwa kazi nzuri tulioifanya. Baada ya mapokezi hayo tulikea katika ukumbi wa vikao na raisi akaongea maneno mawili matatu hasa upande wa uaminifu. Na alituasa kuwa bora mtu afe kuliko kutoa siri ya nchi, baada kikao kifupi raisi aliondoka pamoja na yule jamaa tuliekwenda kumuokoa.



    Kila mmoja wetu alitawanyika na kurudi chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika maana shughuli tuliokwenda kuifanya haikuwa ndogo. Kutokana na uchovu niliokuwa nao usingizi mzito ulinichukuwa na kuanza kuota ndoto kuwa niko kule katika kituo cha kulelea watoto yatima. Katika ndoto hiyo alikuja mtu kunitembelea lakini hakuruhusiwa kuniona na kuondoka. Nilishtuka kutoka usingizini baada ya kuota ndoto hiyo ambayo sikujua maana yake hasa ni nini. Ah kwa sababu ilikuwa ni ndoto tu niligeuka upande wa pili na kuendelea kulala.

    Niikuja kushtuka tena baada kusikia mlango wanu ukigongwa, nilikurupuka kitandani na kwenda kuufungua na kumkuta anae gonga ni baba. Aliingia ndani na kuketi kwenye kiti kidogo, tuliongea mambo mawili matatu kuhisiana na kazi ile. Baada ya maopngezi hayo nilimuuliza kama naweza kupata likizo fupi nataka niende nikatembee kule kwenye kituo cha kulelea watot yatima. Alinijibu kuwa inawezakana lakini nisikae sana maana ndio kwanza kazi ilikuwa imeanza.

    Nilimshukuru na kuanza kupanga mipango ya safari, siku ya pili niliondoka kambini kwa ndege maalim na kupelekwa hadi kwenye kambi ya kawaida ya jeshi na hapo nikapewa ari ya kuelekea uwanja wa ndege. safari haikuwa kubwa sana nilifika uwanja wa ndege na kukata ticket tayari kwa safari. Muda wa safari uliwadia na kuodoka, safari yote sikupata usingizi hata kidogo kwani nilikuwa na shauku ya kutaka kufika tu. Baada ya masaa kadha kuwa angani hatimae ndege ilikanyaga ardhi na abiria wote tukashuka. Kwangu kufika huko tu ilikuwa ni furaha tosha na mtu hakuhitaji kuuliza kwani hata sura yangu pekee ilinekana kuwa na furaha sana.



    Nilitoka nje ya uwanja na kupanda taxi na kumpa maelekezo nnapowenda, baada ya hapo safari ilianza huku njia nzima nikiwa nimetabasamu. Alinifikisha mpaka nje ya geti la kituo kile, nilimlipa na kushuka. Kwa mwendo wa taratibu nilijongea getini ambako nilikutana na mlinzi, nilimuomba kuingia ila alikataa kutokana na kile alichoamini kuwa siku hiyo haikuwa siku ya kuwatembelea mayatima.

    nilijaribu kuongea nae lakini alikataa kata kata kunikubalia, nilimuelewa na kuamua kukaa pmbeni ya kituo hicho nikiwa natumaini labda huenda akatokea mtu ambae ananifahamu. Nilikaaa zaidi ya masaa mawili bila kutokea mtu yoyote, mwisho nilikata tamaa. Ila wakati nataka kuondoka nilimuona mwanamke kwa mbali akiwa anakuja maeneo ya getini. Nilipomuangalia kwa makini nikagundua kuwa alikuwa Harleen, bila kutaka nilijikuta namkimbilia na nilipomfikia nilimrukia na kumkumbatia. Lakini nilipomuacha niligundua kuwa amenikodolea macho.

    Nilitabasamu kuzitoa nywele zangu upande wa uso ambao nilikuwa na kovu, hapo sasa nilimuona akianza kutabasamu na kunikumbatia tena kwa nguvu. Kwa pamoja tuliongozana na kuingia ndani, nilishangaa kukuta kumebadilika sana. Harleen alinambia kuwa yeye amekuwa matron wa kituo baada ya yule aliekuwepo mwanzo kufariki.

    Tuliongea mambo mengi sana na hapo ndio nikagundua kuwa nilikuwa nimepitwa sana na maisha ya kawaida kutokana na muda mwingi kuwa kambini. Baada ya maongezi marefu alinionesha chumba ambacho ningelala, yeye alielekea jikoni kuanda chakula wakati mimi nikiingia ndani kwa ajili ya kuoga.

    Baada ya saa na nusu alikuja kunigongea na kwenda kupata chakula, wakati tunakula alinambia kuwa Adrian alirudi kuja kunitembelea lakini nilikuwa nishaondoka. Hivyo aliacha barua kutokana na kuwa wakati huo nilikuwa sina hata simu. Tulipomaliza kula Harleen aliingia chumbani na kurudi na barua mkononi na kunikabidhi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliifungua na kusioma mpaka mwisho kisha nikatabasamu na kuendelea na maongezi menine na Harleen pamoja na waschana wengine. Niliendelea kufurahia maisha hayo ya uraiani kwa siku tatu. Siku ya nne nilipokea simu inayo nitaka niripoti kambini kambini haraka iwezekanavyo. Bila kuchelewa niliwaaga wenyeji wangu na kuondoka kituoni hapo.

    Nilichukua gari mpaka nje mji kidogo kisha nikashuka na hapo nikapiga simu maalum na kuongea code za sehemu niliopo. Nusu saa baadae ilifika chopa ya jeshi nikapanda na safari ikaanza, baada ya masaa kadhaa chopa ile ilitua kambini na bila kusubiria niliruka na kukimbilia kwenye ukumbi wa vikao kwa ajili ya kuripoti.

    Baada ya kuripoti nilikabidhiwa bahasha ndogo na kuifungua, kama kiongozi wa kikosi changu niliifunua bahasha ile na kusoma maelezo. Baada ya kujiridhisha na maelezo yaliokuwemo humo niliaga na kuondoka kwenye ukumbi huo. Nilitoa kifaa maalum kama simu kilichoitwa Jet telecommunicator (J.T.C). Nilibonyeza mara kadhaa kisha nikatuma ujumbe kwa wenzengu wote.

    Baada ya dakika tano wote tulikuwa katika chumba maalum, niliwaeleza kila kitu. Mission yetu ilikuwa ya kuokoa watoto ambao wanatekwa nchi mbali mbali na kuuzwa nchi nyingine. Baada ya maelezo hayo tulikubaliana tukutane baada ya nusu saa kwa ajili ya kuelekea eneo la tukio ili kukamilisha kazi hiyo muhimu sana.

    Tulikutana tena na moja kwa moja tukaelekea kweny ndege na safari ikaanza, njia nzima tulikuwa tunaongea mambo ya kawaida kama watu ambao tunakwenda kwenye sherehe. Rubani alituambia tukae tayari kwa ajili ya kuruka maana uokozi huo ulikuwa unafanyika baharini katika meli kubwa ambayo ndio ilikuwa inasafirisha watoto hao.

    Na kwa sababu ilikuwa ni usiku, maadui zetu hawakufanikiwa kutuona wakatu tunatoka katika ndge. Bahati nzuri sana sisi hatutumii maparashuti kwa misheni za baharini labda chombo kiwe kinatembea. Tulipiga mbizi kwenye maji na kuogelea mpaka ilipo meli hiyo, kwa umakini wa hali ya juu tulipanda minyororo ya nanga na kufanikiwa kuingia ndani bila kushtukiwa.

    Niliwakabidhi wenzangu majukumu kisha tukatawanyika huku tukikubaliana tuifanye kazi hiyo kwa siri kubwa sana ili kuwapunguza maadui zetu. tulijigawa katika timu za watu wawili wawili isipokuwa mmoja wetu tu, yeye alikuwa ni sniper hivyo alitafuta sehemu ya juu kabisa katika meli hityo na kujitega huko.

    Kwa umakini wa hali ya juu tulianza kazi huku tukiwasiliana kwa vifaa maalum, kazi ilikwenda kama yulivyoipanga huku maadui zetu wakiwa hawajui nini kinaendelea. Tuliendelea na kazi ya kuwapunguza taratibu mpakatuliporidika ndio tukaanza kuwashambulia bila siri tena. Moto uliowaka ulikuwa si mdogo maana hata hao tuliokuwa tunapamabana nao walikuwa wanajihami kwa silaha nzito sana.

    Baada mpambano wa takriban saa nzima tulifanikiwa kuiteka meli na kuwakamata wote waliohusika. Baada ya hapo tulikwenda moja kwa moja katika vyumba ambavyo walikuwa wamefungiwa watoto hao. Kwa kweli machozi yalinitoka baada kukuta watoto wengi sana ambao kwa muda ule walitakiwa wawe nyumbani kwa wazazi wao lakini wamejikuta wakichukuliwa kwaajili ya biashara.

    Tulipohakikisha tumeidhibiti vilivyo meli hiyo, nilipiga simu makao makuu na kutoa taarifa kuwa kazi imekamilika. Tulikaa mpaka asubuhi ambapo zilifika meli kadhaa za serekali ya eneo la bahari tuliopo. Tuliwakabidhi watoto hao na sisi tukasubiria ndege helicopta ambayo ilifika na safari ya kurudi kambini ikaanza.



    Njia nzima kila mtu alikuwa akijisifi kwa jinsi alivyo wachakaza maadui zetu, basi zilikuwa ni stori za damu tu. Tulifika kambini na kupokielea kwa shangwe kubwa. Baada ya siku hiyo sasa ikawa ni vita kati yetu na wanaojifanya wapindishaji sheria. Japo kikosi kilikuwa ni siri lakini kilikuwa tishio kwa kila mtu ambae anajua kabisa ni mkiukaji wa sheria.

    Baada muda wote tulipandishwa vyeo na kuwa makando sasa, na mpaka tunafikia cheo hicho kuuwa kwetu ilikuwa jambo dogo sana. Yaani akili zetu ailijenga mazingira ya kuwa haziwezi kutulia ikiwa utapita muda mrefu bila kuingia kazini. Na kila mtu alifurahia kazi hii, ni kwa kazi hii tumetembea nchi nyingi sana na kujifunza tamaduni za watu mbali mbali.

    Siku moja niliitwa na wakuu wangu na kukabidhiwa bahasha, niliifungua na kuisoma na kujikuta nikishangaa. Maana mission hiyo nilitakiwa kuwa mpelelezi na nitakiwa kuifanya peke yangu pasi na wenzangu kujua chochote. Nilikubali na nilianza maandalizi ya kuondoka kambini hapo kwa kisingizio cha kuumwa. Na wenzangu wote waliniamini na kunisindikiza katika ndege kwa majonzi makubwa sana.

    Ndege hiyo iliondoka kambini hapo na moja kwa moja kuelekea mjini New York, ndege ilituwa katika uwanja wa jeshi na baada ya hapo nikapelekwa hadi ikulu kwa raisi na kukabidhiwa mafaili maalum. Niliyapititia kwa umakini wa hali ya juu sana na baada kuridhika niliruyarudisha kisha nikapewa passport mpya pamoja na kila kilichohitajika kwaajili ya kazi hiyo muhimu sana.

    Baada ya hapo nilielekea nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya safari hiyo, kwa wakati huo jina lilikuwa ni Judith. Nilipohakikisha kila kitu kipo sawa, niliamua kungia chooni na kuanza kujibadilisha muonekano maana niliambiwa kuwa kuna watu wakubwa wa nchi yetu wanashirikiana na hao nnao kwenda kuwachunguza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipomaliza kila kitu nilitoka na kupanda kitandani kwa ajili ya kupumzika, siku ya pili mapema nilitoka nyumbani na kuelekea uwanja wa ndege bila mtu yoyote kujua. Hilo nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya kuzipunguza nywele zangu na kuwa ndogo kiasi. Dakika kumi baadae nilikuwa uwanja wa ndege tayari, na wala sikupata shida yoyote ile kwa sababu taarifa zangu zote zilikuwa tayari zipo kwenye mitandao ya nchi.

    Muda wa kupanda ndege ulifika na abiria wote tuliokuwa tunalekea Hongkong tulipanda ndege na safari ikaanza. Njia nzima nilikuwa nawaza jinsi ya kuweza kuingia katika himaya ya ninaekweda kumchunguza. Kwa sababu nilielewa kabisa ni kiasi gani mtu huyo ni hatari, nikiwa naendelea kuwaza njia mbadala ghafla usngizi ulinichukua. Nilikuja kushtuka baada mtikisiko mdogo uliosababishwa na magurudumu ya ndege hiyo wakati yanakanyaga uwanja barabara za uwanja wa ndege wa Hongkong.

    Tukiongozana na abiria wengine, tulishuka ndege na kuelekea sehemu ya ukaguzi. Baada ya kumaliza taratibu zote tuliruhusiwa kutoka nje ya uwanja, huko nilikutwa mji ukiwa umechangamka kweli kweli. Nilichukua Taxi na kumpa kikaratasi kidogo kilichoandikwa jina la hoteli, yule dereva alitabasamu na safari ikaanza. Aliendesha kwa muda wa nusu saa kabla ya kusimama mbele ya hoteli kubwa, nilimlipa kiasi cha fedha anachotaka na kushuka.

    Nilisimama hapo nje nikaiangalia hoteli hiyo kwa makini kisha kwa mwendo wa haraka nikaanza kutembea mpaka mapokezi. Nilikamilsha taratubu zote na kuchukua funguo ya chumba changu na kuondoka. Nilipofika chumbani nilijibwaga na kutoakana na uchovu wa safari nilipitiwa na usingizi mzito. Nilikuja kushtuka baada ya simu yangu kuita, niliipokea na kuongea kwa dakika kama tano hivi. Nilipokata uliingi ujumbe ukinieleza sehemu ambayo nitapata kila ninachokitk kukamilisha kazi hiyo.

    Niliweka simu pembeni na kuingia bafuni kwa ajili ya usafi wa mwili, nilimaliza na kujianda vya kutosha niliangalia saa yangu ya mkononi ilionambia kuwa ni majira ya saa moja usiku. Nilitoka chumbani kwangu na kuelekea chini ambapo niliacha funguo mapokezi kama desturi ya hoteli hiyo. Baada y kuikbidhi nilitok nje kabisa na kuanza kuangaza huku na kule nikitafuta sehmu ya kuanzia kazi yangu.

    Kutokana na kuwafahamu kwa sura watu ambao natakiwa kuwachunguza, sikutaka kujipa shida sana. Niliulizia Casino ambalo ndilo vibosile hao hukuta kwa ajili ya kupanga mipango yao, haikuwa shida sana kuweza kujua lilipo casino hilo hasa ukizingatia nilitumia uschana zaidi. Niliweza kufika katika casino hilo, kufanya utaratibu wa kuingia ndani



    Naam wala sikubahatisha niliwakuta wanne kati ya nane walikuwepo sehemu hio, lakini kwasababu nilikuwa natafuta njia ya kwa karibu ili nipate taarifa zao, basi sikuwa na haraka kabisa. Nilitembea mpaka counter na kuagiza kinywaji na kuanza kunywa taratibu. Ila kwa kweli hakuna kilevi kilichokuwa kinanipangua akili, huwa nalewa lakini kila nnalofanya nilikuwa nalielewa kabisa.

    Niliendelea kupata mvinyo wa kirusi huku nikisindikizwa na muziki laini wa kiingerea, muda wote huo wakati naendelea kunywa nikuwa namuangalia mmoja wao na kumkonyeza. Ah kam ilivyokawaida yenu wanaume, mschana akikuangalia sana eti amekupenda. Basi jamaa alijikusanya taratibu na kusogea sehemu nilipo.

    Alipofika tu kwanza alinilipia kinywaji na kunambia kama nataka kuongeza, basi tukaanza kuongea mawili matatu huku ukiendelea kupata maji ya dhahabu. Na nilichagua pombe kali makusudu kumuangalia kama anamoto au nguvu ya gesi tu. Tuliendelea kunywa pale mpaka nilipomuona jamaa ameanza kurembuwa, ndipo nikamwambia tuondoke. Nae alikubali bila kinyongo, tuliongozana huku tumeshikana viuno. Wenzake walipomuona anatoka walimpigia makofii kama kushangilia ushindi wake. Moja kwa moja mpaka katika hoteli ambyo haikua mbali na casino lile.

    Tulichukua chumba hapo na nikaagiza mtungi mwengine wa Red wine uletwe chumbani. Tulipoingia chumbani hata hatujakaa sana mlango uligongwa na nilipofunga nilimkuta muhudumu akiwa na chupa nilioagiza. Nilimshukuru na kuingia ndani, hapo sasa tulianza mashindano ya kunywa. Siku hiyo ni miongoni mwa siku ambazo nimewahi kunywa pombe nyingi kweli, shindano liliendelea mpaka jamaa akanoki na kuangakia kitandani.

    Baada kuhakikisha kuwa amelala fofofo, nilitoa kisindano chenye dawa kidogo na kumdunga shingoni. Dawa iliokuwemo katika sindano ile inamfanya ahisi anafanya mapenzi kumbe anaota. Hapo sasa nikaanza kazi yangu ya kupekuwa, nilianza simu yake na nikanyonyo kila taarifa nilioikuta. Niliendelea na kazi hio mpaka niliporidhika, nikamvua nguo zote na kumfunika shuka halafu namimi nikalala pembeni yake.

    Asubuhi mapema niliwahi kuamka na kuagiza kifungua kinywa, kilipofika ndipo nikamuamsha yule jamaa. Basi alipofungua tu macho alianza kutabasamu na kunushukuru kwa penzi zito nililompatia usiku. Aliingia bafuni na kuoga, alipotoka tulikunywa chai na baadae tukatoka hotelini hapo na kila mtu akachukua mia zake huku jamaa akiniachia namba yake ya simu,

    Nilirudi hoyeli niliofikia na nilipoingia tu chumbani nilifungua begi langu na kutoa Laptop na kuchomeka microchip ndogo ambayo ilikuwa na taarifa zote nilizochukua kutoka kwenye ile simu. Baada ya kuzikagua vizuri na kuridhika, niliingiza code maalum kwenye computer yangu na kuzituma.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitoa simu yangu na kuingiza namba fulani hivi ambazo pia niliziingiza katik simu ya yule jamaa jana yake. Hapo nikawa nimeunganisha simu yangu na yake bila yeye kujua.

    Baada ya hapo niliingia bafuni, nilipotoka nilika kitandani na kuanza kuwafatilia kinaga ubaga. Usiku wa siku hiyo nilitoka kivingine zaidi nikiwa nimevalia wigi jeupe lililonibadilisha kabisa. Nilikwenda mpaka sehemu niliombiwa nitakuta kila nnacho kitaka kwa ajili ya kazi yangu. Baada ya kuhakikisha nimechukua kila ninachotaka, nilifunga safari ya kuelekea sehemu moja hivi ambako siku walikuwa na kikao.

    Kwa msaada wa simu yangu niliweza kufika eneo la tukio bila shida, nilitoa kinyago cha dhahabu na kukivaa. Kinyago hicho kiliniziba sehemu yenye kovu la moto, kwa kutumia mbinu ninazo jua mwenyewe nilifanikiwa kuingia katika ukumbi huo na kujificha sehemu. Nilitoa kifaa maalum kidogo kinachoitwa microcamera na kuanza kurikodi mkutano mzima.

    Kila kitu kilikwenda kama nilivotaka mpaka kikao hicho kinaisha, kasheshe lilikuwa kwenye kutoka eneo hilo. Maana ulinzi uliongezeka nje ile mbaya utasema alikuwa anakuja raisi, na kwa bahati mbaya wakati natafuta njia ya kutokea ghafla mlinzi mmoja aliniona na kuanza kunifukuza. Sikutaka kupambana sehemu ile kwa maana wao walikuwa wengi kweli kweli.

    Nilikimbia kadiri miguu yangu ilivyonibeba na nilipoangalia nyuma walikuwa wameshaingezeka. Nilifika sehemu na kujibanza kwanza ili nivute pumzi, nilitoa bastola yangu ndogo na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti. Taratibu na kwa umakini mkubwa sana nilianza kuwapunguza mmoja baada ya mwengine, na hapo sijisifii lakini kilichowakuta nahisi waliopona walikwenda kusimulia wenzao.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog