Search This Blog

Friday, 20 May 2022

C.O.D.EX. 3 (THE REAL ME) - 4

 







    Simulizi : C.O.D.EX. 3 (The Real Me)

    Sehemu Ya Nne (4)





    Baada ya kusafisha njia yangu, niliondoka eneo hilo na kurudi hotelini nilipofikia. Nilichomeka ile micro camera kweny computer na kuanza kuangalia tena kikao kile, halafu kama kawaida nikaingiza code maalum na kuituma video ile.

    Kazi niliiendeleza kwa umakini wa hali ya juu huku nikijitahidi nisijulikane mapema, maana niliielewa hatari ya kazi hiyo. Siku moja nilikuwa katika mawindo yangu kama kawaida lakini kikao cha siku hiyo kilihudhuriwa na watu wengi sana na kutoka mataifa mbai mbali. Jambo kubwa lilikuwa linaongelewa hapo lilikuwa ni PROJECT CODE X, mwanzo sikulifahamu vizuri lakini baadae kijasho kilianza kunitoka baada kusikia wingi wa jeshi linalohusiana na project ile.

    Niliendelea kusikiliza wakati huo nikirudi mkutano mzima bila kushtukiwa na yoyote, ila wakati natoka kuna mzee mmoja alikuwa na combat flani hivi ya kipekee. Kwa haraka niligundua kuwa gwanda ile ilikuwa na ya nchi hii. Tulipishana mlangoni lakini aliniangalia sana kisha akatabasamu na kuendelea na mia zake. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilirudi hotelini na kuituma ile video pamoja na picha ambazo nilizipiga kwenye kikao kile,baada ya nusu saa uliingia ujumbe ukinataka nifanye haraka nirudi kambini. Nilituma ujumbe kutaka kujua kwanini nirudi muda huo wakati nilikuwa naelekea mwisho kabisa wa upelelezi wangu. Nilijibiwa kuwa kuna mtu hatari sana, anaitwa General David. Huyo akikuangalia tu anajua kama wewe ni mpelelezi, hapo sasa nikarudisha kumbukumbu zangu nyuma na kumkumbuka mtu alieniangalia kisha akatabasamu.

    Nilituma tena ujumbe mwingine ili nitumiwe picha, na haikupita hata dakika iliingia picha ya General David. Hapo sasa nikaona hali ya hatari iko mbele yangu, bila kupoteza muda nilichukua Cd maalum na kuitia katika computer. Cd hiyo ilikuwa ni virus maalum ya kuharibu computer ili kufuta ushahidi wowote ule. Baada kuhakikisha data zote zimeliwa kweye computer hiyo, niliingia nayo chooni na kutia kwenye jakuzi lililojaa maji na kuiharibu kabisa.

    Nilirudi chumbani na kuchukua bastola zang ndogo nne na kuziweka kiunoni, pia nilikusanya makaratasi yote na kuyachoma moto. Nilipohakikisha nimeteketeza ushahidi wote, nilitoka chumbani na kuelekea kwenye lift. Taratibu lift ilianza kushuka huku mikono yangu ikiwa nyumakaribu na bastola zangu. Iliposimama tu nilizishika vizuri kwa ajili ya usalama zaidi, lakini nashkuru kulikuwa salama kabisa.

    Nilitoka katika lift na kuelekea mapokezi ambapo nilikabidhi funguo na kuaga kisha nikatoka nje ya hoteli hiyo kwa tahadhari kubwa sana. Nilikodi taxi na kutafuta sehemu ili kutafuta sehemu salama kwa ajili ya kupitisha usiku ili siku ya pili nifanye utaratibu wa kurudi kambini. Lakini wakati naingia kwenye taxi hiyo nilimuona mtu ambae nilimfananisha akiingia kwenye gari nyingine. Hivyo basi nikamwambia dereva wa taxi aifaute ile gari.

    Aliifata mpaka nje ya bar moja hivi, nilishuka na kumlipa kisha taratibu nikaanza kusoge kwenye bar hiyo. Lakini nikakumbuka kuwa nguo nilizofaa zilikuwa ni za kazi zaidi. ilibidi niingie katika duka la nguo la nguo la karibu na kubadilisha kwanza halafu nikaelekea bar. Nilifika na kutafuta sehemu na kukaa, dakika kumi baadae uliingia wewe (Alex) na kuanza kuniletea fujo. Natumai kilichotokea pale una kikumbuka vuzuri" Scarlet aliongea maneno hayo na kumuangalia Alex usoni.

    Alex alikisa kichwa kuashiria kuwa anakumbuka vizuri sana, "duh pole kwa mkasa yote iliyokukuta" Alex alijikuta akimpa pole huku akitabsamu. Wakati akiendelea kuongea aliingia mtu mmoja na kuwapa taarifa kuwa chakula kipo tayari. "nina njaa kweli" Alex aliongea na kusimama jambo ambalo lilimuwacha Scarlet mdomo wazi. "ongoza njia basai bibie" Alex aliongea tena baada kumuona Scarlet amekodoa macho.

    Alisimama na taratibu wakaanza kutembea kuelekea sehemu ya kupata chakula, watu wote waliokuwepo huko walimkaribisha Alex kwa tabasamu. Walikaa kwenye meza na kuanza kupata kula, wakati wakiendelea kula General Griffin alimuuliza Alex "hivi Alex unafahamu nini kuhusu C.O.D.E X". "mnata kufahamu kuhusu CODE X, nipeni wiki moja tu nifanye mazoezi halafu nitawaonyesha hilo ni balaa gani" Alex alijibu huku akitabsamu na kumuangalia General ambae alikubaliana nae.

    Siku zilikatika na hatiame wiki ikatimia, siku hiyo asubuhi mapema Alex alitoka akiwa amevaa nguo za mazoezi. "General, habari za asubuhi" Alex aliongea alipofika sehemu alipokuwa amesimama mtu huyo. "leo ndio umesema utanieleza kuhusu CODE X", "ndio lakini nitakueleza kwa vitendo kwa maana nikikueleza kwa maneno tutakesha hapa" alijibu Alex huku akinyoosha nyoosha viungo kisha akaendelea "Mimi napasha lakini naomba uandae vijana kumi ambao unaamini wana uwezo wa hali ya juu katika kupambana bila silha, uniandalie mtunguaji mmoja mkali sana na mtu mmoja ambae unaamini kwenye kucheza na silaha ni hatari sana"

    General aliwaita wanajeshi wote katika kambi hiyo na kuchagua wale wakali zaid kuliko wote katika kupamabana bila silaha akiwemo Scarlet. Alichagua na wengine kama alivyotaka Alex, "vipi wako tayari" Alex aliuliza baada ya kumaliza mzunguko wa hamsini katika kiwanja hicho. "ndio" General alijibu na kuwapa amri vijana wake waingie uwanjani nao wakatii. Kwa kwel kila mu alikuwa na hamu ya kutaka kujua Alex anataka kuwaonyesha nini. Wapo waliosema anataka umaarufu na wengine walisema amechanganyikiwa.

    Basi Alex alikaa katikati ya duara la watu kumi na kutabasamu kisha akajisemea "like old days". kipenga kilipulizwa na wote kumi kwa wakati mmoja walimvamia, Alex hakuwa na papara kabisa kwani alikuwa akijiamini vya kutosha. Taratibu alianza kupambana nao na kadiri muda ulivyokwenda ndio mpambano ulizidi kupamba moto. Alipigana nao kwa muda wa dakika kumi na tano tu na wote kumi walikuwa chini hoi bi taabani.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mpambano huo alikwenda mpaka kwenye meza maalum ya maji na kuchukua chupa mbili za maji na kurudi nazo mpaka walipo wengine. Alimkabidhi mwanajeshi mmoja na kumwambia azipeleke umbali wa mita mia mbili kisha azifukie nusu. Baada alimuomba mtunguaji (sniper) aliechaguliwa, "umeziona zile chupa mbili, moja ni yako na moja ni yangu na unatakiwa upige sehemu ya kifuniko" Alex aliongea na kuchukua bastola aina ya Riffle huku yule kijana akichukua bastola maalum ya masniper.

    Kila mmoja alitafuta sehemu yake na kulala chini, kumbuka bastola ya Alex haikuwa hata na darubini na kuvutia kitu na kukiona kwa ukaribu zaidi. Kipenga kilipulizwa na wote kwa pamoja wakafyetua risasi, "kijana hujapiga kifuniko, umepiga kwenye shingo ya chupa" Alex aliongea huku akiikabidhi bastola yake kwa mwanajeshi mwengine. Yule aliepeleka zile chupa alirudi huku akiwa haamini kabisa kilichotokea.

    Alizikabidhi zote mbili kwa generel na hapo sasa wote walitoa macho, chupa iliopigwa na Alex ilikuwa umetawanyika sehemu ya kifunikio tu na ile nyingine ilikuwa imetawanyika katika shingo. Baada ya hapo Alex alimuomba mtu aliechaguliwa upande wa utmiaji silaha, Scarlet aliingia uwanjani akiwa na bastola maalum zenye risasi za mpira wenye rangi. Alex alichuku bastolo yenye vigololi maalum ambavo hata vikimpat mtu hawezi kuumia sana. Kwa pamoja waliingiwa uwanjani kwa ajili ya kuonyeshana nani ni mkali zaid.

    Kama kawaida yake General lipuliza penga na mmpambano ukaanza, na mpaka unaisha nguo za Alex zilikuwa kama wa walivyoanza ila nguo za Scarlet zikuwa zimejaa madoa ya risasi. "natumai general utakuwa umpeta jibu lako"Alex aliongea baada kuikabidhi bastola yake. "kijana hivi wewe ni mtu au mashine" General aliuliza kwa sintofahamu. "hahaha, mimi ni mtu wa kawaida mbona" Alex alijibu. "hapana wewe huwezi kuwa mtu wa kawaida kwa mambo ulioyafanya hapa leo hakuna atakae amini kama wewe ni mtu wa kawaida" General alijibu huku akionekana kutoamini kilichoyokea muda mfupi ulipita.

    "Sasa subiri niwaeleza maana ya CODE X" Alex aliongea na wote walisogea karibu kusikiliza kwa umakini wa hali ya juu. "kirefu cha CODE X ni CINDREX OLTIVIASO DECA ENDROLINE X, hii chemical maalumu imetengenezwa kwa ajili kuwafanya wanajeshi kuwa hatari zaid. Ni project ambayo ni hatari sana kuliko watu wengi wanavyoifikiria, na mtu wa kwanza ambae ilitumika kimikali hii na kufanikiwa alikuwa naitwa Alen James. Huyo ndie aliekuw hatari zaidi lakinu ameshafariki tayari, mtu wa kwa hatari ni mimi Alex Jr au Project 75".

    Alex alinyamaza kidogo na kuwaangalia kisha akaendelea "Mimi nina uwezo wa kupiga risasi mita mia mbili bila kutumia darubini, pia nina uwezo wa kukwepa risasi na natumai mumeona baada ya pamabano na Scarlet. Na katika ubora wangu nina uwezo wa kupambana na makomando zaidi ya kumi na tano, sasa jiulizeni kambi ya kawaida ya vibaka naifanyaje. Na kwa wakati huu siko peke yangu, kuna wanajeshi wengine wengi wanaandaliwa na kikundi kinachojulikana kama WANAMAPINDUZI. Na harakati zote zile za kusakwa ilikuwa ni kuhakikisha wananizuia siingilia kati katika kufanikisha hilo" Alex alimaliza kuwaeleza kwa ufupi kuhusiana na Project CODE X.

    Alex aliwaangalia wote kwa umakini wa hali ya juu sanana kugundua wasiwasi waliokuwa nao. "Kijana asante kwa kutifmbua macho maana ni muda mrefu sasa tumadili na kikosi fulani xha watu ambao hatuwajui" general aliongea huku akimshika bega Alex. "chochote kwa taifa langu" Alex alijibu kisha akapia salute kama ishara ya heshim. Walirudi ndani na kila mtu akaelekea upande wake, general alielekea katika chumba cha mawasiliani kwa ajili ya kuzifikisha taarifa hizo kwa raisi.

    "habari yako muheshimiwa" General aliongea baada kuunganishwa ikulu na rais, "nzuri tu, pole na majukumu" Raisi alijibu. "asante mkuu, kuna video nitakutumia naomba uiyangalie kwa makini kisha tujadii kitu mkuu"."ok, hakun shida", General akampa ishara mtalamu wa computer na hapo akaituma video ambayo ilirikodiwa wakati Alex anaonyesha uwezo wake. Raisi aliiangalia mpaka mwisho, "naam general unataka tujadili kitu" Raisi aliongea baada kumaliza kuangalia video hiyo.

    "Mi nashauri huyu kijana tumuunge na kikosi hichi kwa sababu atakuwa ni msaada mkubwa sana kwetu", "wewe umeamuamini?". "ndio mkuu, huyu ni mzalendo na haina haja ya kumtilia mshaka kabisa", "basi hakuna shida juu ya hilo, andaa taratibu zote zinazohitajika kuapishwa kwa kijana huyo. Mimi kesho asubuhi nitakuwa hapo kwaajili ya kumkabidhi gwanda zake". Walimaliza kuongea na kuagana, General alitoka katika chumba hicho na kumuita mtu maalum wa kuchora tattoo na kuongozana nae mpaka katika ukumbi maalum. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliamuru wanajeshi wote waitwe, haukupita muda mrefu wote walikuwa katika eneo hilo. "msishangae kwanini nimewaita wakati sio muda mkusanyiko, lakini ni hivi nimeongea na raisi muda si mrefu na kumtumia video ambayo ilirikodiwa wakati wa mazoezi ya Alex. Hivyo basi ametoa agizo kuwa Alex awe miongoni mwetu katika kulitumikia taifa" General aliongea na uwanja mzima ulilipuka kwa sauti za kushangilia.

    Alex alipewa amri atoke mbele kwaajili ya kuchorwa tattoo la kikosi hicho, bila kupinga alivua fulana yake na kusogea. Mchoraji alianza kazi yake huku watu wakishuhudia tukio hilo, "ebwana unajua huyu ndugu habari nyingine". "huyu jamaa ana hatari kwakweli, sasa ikiwa huyu mmoja tu yuko hivi hao wengie sijui wakoje". "lakini si mbaya, tunae mmoja wao kati yetu hivyo tutajifunza kupitia yeye jinsi ya kukabiliana nao katika mpambano" hayo ni baadhi ya yaliokuwa yakiongelewa na baadhi ya wanajeshi wakati zoezi la uchoraji likiendelea.

    **************

    "may day, may day mimi ni rubani wa kikosi cha KING's SQUAD (K.S)" Alisikika kijana mmoja akiongea kupitia kifaa maalum, "rodger, tunaomba nambari yako tuhakikishe" upande wa pili ulimjibu. "Nambari yangu KS099" alijibu rubani huyo, "tueleze kuna nini". "nimefanikiwa kuupata mzigo lakini sidhani kama nitafika nao, kuna ndege nyingine nne za waasi zinani fukuza na mpaka muda huu tunaongea wenzangu wawili wameshatung....." kabla hajamaliza mawasilino yalikata na kila control tower ilivojaribu hakupatina.

    Ripoti ya kutunguliwa ndege hiyo ilifikishwa kwa raisi, wakati huo alikuwa anajianda kuelekea katika kambi ya THE PIRATES kwaajili kumuapisha kijana Alex. Baada ya kupewa taarifa hiyo alitoa amri kuwa iandikwe haraka na apewe hiyo document aondokea nayo. Hazikupita hata dakika kumi ilikuwa imeshakamilika na raisi aliichukua na kuondoka nayo. Safari ilianza huku raisi akiwa na wasiwasi sana kutokana na tarofa muhimu alizokuwa nazo rubani aliepotea.

    Baada ya masaa kadhaa hatimae ndege ilikanyaga uwanja wa PIRATES, raisi alishuka na kuelekea ndani. Haikuchukua muda mrefu kumuapisha kutokana na maandalizi yalikuwa yamekamilika. Baada shughuli hiyo fupi, Alex alikabidiwa gwanda zake rasmi na kupewa amri akazivae muda huo huo. Raisi alimwita General na kumkabidhi ile bahasha yenye ile document, kisha yeye akaaga na kuondoka. General aliifungua bahasha ile na kusoma kilichokuwemo ndani na aliporidhika alibofya kitufe fulani hivi ikaanza kusikika honi ya dharura.



    Muda huo huo kikosi chote kikasanyika katika ukumbu wa vikao, Scarlet na timu yake akaambiwa ajiandae. Alex pia alijumuishwa katika kikosi hicho chenye jumla ya wati saba hivyo na yeye akawa mtu wa nane. Baada kukamilisha maandalizi walirudi katika ukumb huo na kupewa maelekezo "kuna rubani mmoja ametunguliwa na alikuwa amebeba taarifa muhimu sana, tunaamini ametunguliwa maeneo hayo" General aliongea na kuonyesha sehemu katika ramani.

    Alex alishtuka kidogo baada general kuonesha hio sehemu, ni kama kwamba anaifahamu. "samahani general, hiyo kambi ni kambi ya watu gani?" aliuliza. "mpaka sasa hatujahakikisha ni kambi ya wtu lakini nahisi ni kambi ya ncho amabazo hatupatani nazo General alijibu kisha akauliza "kwani vipi". Alex alikaa kimya kwa muda kama mtu amabe alikua anajaribu kukumbuka kitu, alishtuka tena na hapo akijipa uhakika kuwa hajakosea. "hiyo ni kambi nambari ishirini ya jangwani, ni moja kati ya kambi kubwa sana Project CODE X" Alex alijibu kwa uhakika.

    Wote waliokuwepo pale walishtuka baada ya kusikia hivo, "basi vizuri kwasababu sasa tumeshaifahamu, basi hakuna shida" General alijibu na kuendelea kutoa maelezo. Kikosi cha Scarlet kiliingia katika chumba maalum cha kuchukua silaha na hapo ndipo alipozidi kuonyesha maajabu. "hivi katika kikosi hichi kuna sniper wangapi?" aliuliza Alex, "wawili tu" alijibu Scarlet. "ok, sasa inatakiwa kuwe na wanne" Alex aliongea na kuwafanya wote wamuangalie.

    " Na wote hao wanatakiwa wakae masafa yenye umbali zaidi ya mita mia mbili, na bastola ziwe zile ambazo ni nzito sana" Alex aliongea na wote wakakubaliana nae. Walimaliza maandalizi na kuondoka kambini hapo kwa chopa maalum amabyo iliandaliwa kwa kazi hiyo tu.

    "kijana unaleta jeuri sio" aliongea mtu mmoja kwa hasira sana, "narudia tena kwa mara ya mwisho, jina lako nani na ni nani aliekutmuma". "huna haki ya kujibiwa na mimi, mimi najibu wakubwa zangu tu" aliongea kijana huyo ambae alikuwa amerowa damu baada ya kuchezea kichapo kikali sana. "naona wewe hujafunzawa kwenu"aliogea tena kwa hasira yule mtu na kumtandika ngumi ya tumbo. "P102 (project 102) unaitwa na mkuu" aliingia kijana mwengine na kutoa taarifa.

    P102 aliondoka na kuelekea ofisini kwa mkuu wake "umepata chochote kutoka kwa yule rubani?" aliuliza mkuu wake, "hapana anaonekana amekaza kweli kweli" P102 alijibu. "sawa muache apumzike kwanza utaendelea kumhoji baadae maana huyo mtu ni muhimu sana" aliongea mkuu huyo na kumpa ishara aondoke. P102 alifunga mguu na kuondoka huku akiwa mechukiwa kwa kitendo cha kuambiwa amuache.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wakati huo tayari kikosi cha PIRATES killishakanyaga ardhi ya eneo la jangwa, walikuwa umbali wa kilometer kama nne hivi kutoka katika kambi hiyo. Taratibu walianza kusogea huku macho yao yakiwa wazi sana. Ilikuwa ni vigumu kujulikana kutokaana na kiza kilichokuwepo kwa wakati hu, wao waliweza kuona vizuri kutokan na kuvaa miwani maalum za kwenye kiza. Walitembea mchaka mchaka mpaka walipoikaribia kambi hiyo. Kama walivyokubaliana, masniper wanne walikaa umbali wa mita miatatu kutoka katika kambi hiyo huku kila mmoja akitafuta sehemu nzuri ya kufanya kazi yake.

    Uzuri eneo hilo lilikuwa na vyuma chakavu vingi sana, na hiyo iliwapa urahisi masniper hao kwa kupata sehemu za juu kidogo. Alex akiongozana na Scarlet na wengine wawili waliendelea na safari huku wakikubaliana na wale wengine kuwa wasishambulie mpaka watakapopewa ishara. Walitembea mpaka karibu na kambi hiyo kabisa, hapo Alex alichukua begi dogo lenye mabomu aina ya C4 na kuondoka eneo hilo.

    Kwa mbinu anazozijua yeye mwenyewe alizunguka kambi nzima na kutega mabomu hayo yalipokwisha na kurudi walipo wenzake. "sasa hapa mchezo unacheza hivi, nitakwenda kufunga kifaa maalum kwenye ile sehemu ya kuzalishia umeme. Umeme ukikata tu tutakuwa na nusu saa kabla ya kurudi na huo muda tunatakiwa tuwe tumeshamaliza kazi ikwezekana na kutokomea" Alex aliongea hivo na wote watatu walioko pale pamoja na wale wanne ambao ni masniper walikubaliana nae.

    "Mimi nitakuwa nawasumbua huku nje Scarlet na wenzako mutaingia ndani kwaajili ya kumuokoa rubani, na kumbukeni risasi pigeni za vichwa tu" Alex alimaliza kuongea kuondoka. Moja kwa moja mpaka kwenye mtambo wa kuzalishia umeme na kuweka kile kifaa kinachojulikana kama Electromagnetic pulse (EMP). Kifaa hichi kinatoa mionzi ya sumaku na kupelekea kukatika kwa umeme. Bila kuchelewa alibonyeza kitufe katika rimoti yake na papo hapo umeme ukakata.

    Kila mtu aliweka miwani yake sawa na kuanza kazi, Alex aliingia katika kambi hiyo bil kujifich ili wale wanajeshi wamfate yeye na Scarlet na kikosi chake waingie ndani. Na kweli mbinu hiyo ilifanya kazi, Alex alianza kupambana akisaidiwa na wale masniper wanne. Scarlet na wenzake wawili waliingia ndani ya kambi hiyo na kufanya kama walivyoelekezwa na Alex. Mpambano ulizidi kuwa mkali huku kila upande ukijitahidi kujilinda.

    Scarlet na kikosi chake walifanikiwa kufika katika chumba ambacho alikuwepa rubani baada ya kukagua vyumba vingi sana. walimfungu kamba na kumuinuia, kisha wakampa vidonge maalum atafune kwa ajili ya kurudisha nguvu. Baada hapo Scarlet alitoa bastola moja na kumkabidhi "tunakwenda nyumbani" Scarlet aliongea huku akiwa ameshika kifaa sikioni "ok tokeeni upande wa kusini wa kambi" Alex alijibu wakati akiendelea kupambana na wale waliokuwa nje na kusahau kama wana mateka ndani.

    Walifanya kama walivyopokea maelezo kutoka kwa Alex na kufanikiwa kutok nje ya kambi lakini kwa bahati mwenzao mmoja alipigwa risasi ya mgongo kabla ya aliempiga kutunguliwa na sniper. "wape mtoto" Scarlet aliongea na hapo Alex akatafuta upenyo na kutoroka. Alipotoka tu nje ya kambi hiyo alitoa rimoti ndogo na kuongea kabala ya kukibonyeza "ungizi mwema mtoto" na kukibonyeza.Ndani ya sekunde kadhaa kulikuwa na moto tu eneo hilo, kambi nzima iliangamizwa na kuwa majivu kama ya kuni. Na hiyo ndio kazi kubwa ya bomu aina ya C4, wenyewe wanaliit kumuta kunguni kwenye kitanda.

    Walimbeba yule mwenzao aliepigwa risasi na kuelekea sehemu waliokubaliana wakutane baada ya kufanya tukio. "vipi kafanyaje tena huyo?" Alex aliuliza walipofika, "kapigwa risasi ya mgongo" Scarlet alijibu. Alex akampa ishara amlaze kifudi fudi kisha akato kisu kidogo pamoja na spirit. Alikimwagia kisu kile na kisha akaanza kazi ya kuitoa risasi hiyo mgongoni, alifanya hivo akielewa kuwa ingebakia kwa muda mrefu basi ingekuwa hatari zaidi.

    "vipi rubani unajisikiaje" Alex aliuliza, "ah kawaida tu nimeshazoea mambo ya aina hii" alijibu rubani huyo. Kwa vile kulikuwa na kiza hawakufanikiwa kuonana vizuri na hawakutaka kuwasha kitu chochote kile ambacho kingewakamatisha kama ingekuwa wanatafutwa. Scarlet alitoa kifaa maalum na kuanza kuongea, alitoa code zote sehemu walipo na kisha akarudisha kifaa hichi na kukaa pembeni ya wenzake. "tunakuja kuchukuliwa saa ngapi?" aliuliza yule rubani, "baada ya masaa matatu watakuwa washafika" Scarlet alijibu.

    "mh masaa matatu ni mengi sana kwa kweli" Alex alijibu huku akisimama, ni kama mtu aliehisi kitu. "samahani rubani, hivi ulikuwa ukifatana ndege ngapi" aliuliza Alex, "tulikuwa watatu" alijibu kijana huyo. "kuna kitu hakipo sawa hapa" Alex machale yalimcheza na kuanza kupiga hesabu anazozijua yeye mwenye kichwani mwake. "kwani vipi Alex" ilibidi Scarlet aulize, "kwa haraka ndege yake huyu haikutunguliwa na ndege ya maadui kama ilivyosema ripoti" Alex alijibu huku akiwa anawaza kitu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hivi Scarlet wamekuuliza jina lako la kazi wakati unawapa maelezo ya sehemu tulipo" Alex aliuliza tena wakati huu alikuwa kashabadilika. "ha..p..ana, damn wanevamia mawasiliano yetu" Scarlet alijibu baada ya kushtuka. "hii sehemu sio salama kabisa" aliongea kijana mwengine, "inabidi tuondoke hapa haraka iwezekanavyo" aliongezea mwengine. Bila kupoteza muda walimbeba yule aliepigwa risasi na kuanza safari, "jamani mimi niacheni nitawachelewesha bure, hiyo taarifa aliokuwa nayo huyo rubani ni muhimu zaidi" aliongea kijana yule aliekuwa amepigwa risasi.

    "marafiki hawaachani nyuma" Alex alijibu huku wakizidi kukaza mwendo, "subirini" Alex aliongea na kuwafanya wenzake wote wasimame. "kama hapa kuna kambi basi lazima kutakuwa na kambi nyingine ndogo ya kuwekea silaha za dharura ikiwa kambi kubwa itavamiwa" Alex aliongea kwa sauti ndogo kama mtu alikuwa anajisimulia kitu mwenyewe. "Alex unawaza nini, muda hakuna ni lazima tuondoke" Scarlet aliongea kwa hasira kidogo.

    "hivi hatutafika, tutakamatwa tu" aliongea Alex na kuzidi kuwachanganya wengine. "hapa tutafute sehemu ya kujificha kwanza halafu tutapanga tunaondokaje maana hatuwezi kuwasiliana na makao makuu kwa muda huu" Alex aliongea huku akiangaza angaza sehemu tofauti. "Nifateni" aliongea na kuanza kuelekea mashariki mwa jangwa hilo. Walitembea kwa nusu saa na hatiamae walifikia sehemu zenye mawe makubwa sana. "sasa hapa ndio mtakapo jificha, ingieni kwenye hilo pango na msije mkajaribu kuwasiliana na mtu yoyote yule" Alex aliongea huku akionysha kidole sehemu kwenye uchochoro flani hivi.

    "wewe huingii" alihoji Scarlet, "hapana mimi nakwenda kutafuta usafiri, kawaida huwa kuna kambi kubwa na kambi ndogo ya dharura na huko lazima nitakut gari japo moja" Alex aliongea akionekana kuwa na uhakika kabisa. "Nipeni masaa mawili kama sijarudi ondokeni eneo hili" Alex aliongea na wote wakatisa vichwa kuashiria kuwa wamemuelewa. Ilibidi wafanye vile alivyowaambia kwa sababu na yeye lishawahi kupitia katika kambi kama hiyo.

    Alex alichukua bunduki ndogo ana kuondoka eneo hilo, alipofika mita kadhaa kutoka kwenye yale mawe alianza kukimbia. Alikimbia kwa nusu saa mpaka alipofika katika kambi ile aliyoiripuwa na kuanza kutafuta kitu. Alizunguka eneo hilo kwa dakika kadhaa kabla kusimama na kuangalia chini, kulikuwa na shimo flani hivi lilionekana ni lakutengeneza. Bila kupoteza muda alianza kushuka ndani ya shimo hilo huku akiwa bastola yake mkononi.

    Alikuwa akishuka kwa umakini wa hali ya juu sana kutokana na kuwa alikuwa hajui kama kuko salama au laa ndani ya shimo hilo. Alifika mpaka chini na kuanza kuifata njia iliokuwa mbele yake, alitembea dakika kama kumi na tano hivi mpaka alipofika mwisho wa njia hio. Aliangaza huku na kule na kuona ngazi, alianza kupanda taratibu mpaka alipofika juu na kufungua mfuniko uliokuwa umefunika shimo hilo. Alitoka na kujibanza sehemu kwa ajili ya kulichunguza vizuri eneo alilotokea.

    Baada kuridhika aliondoka sehemu aliojibanza na tarattibu alianza kuelekea katika mlango mkubwa ambao ulikuwa umeandikwa control room. Aliufungua taratibu n kuoenya pasi kujulikana na mtu yoyote aliekuwemo ndani ya chumba hicho. Hata hivyo kulikuw na watu watatu tu ndani ya chumba hicho ambao walikuwa wakijaribu kuwasiliana na makao makuu yao kwa ajili ya msaada.

    "nimekwambi wawili kati yenu watangulie ili kufanya uchunguzi kama kuna aliepona kambini" ilisikika sauti ya mtu kwenye spika maalum. "mkuu ni vigumu sana kuenda huko kwa sababu hatujui wako wanagapi" alijibu mtu mmoja. "ni kikosi cha watu nane tu, hizo ni taarifa za uhakika nilizozipata kutoka kwa mpelelezi wangu aliekuwemo katika kambi ya THE PIRATES" alijibu. Alex alisikiliza kwa makini na simu ilipokatwa tu aliwavamia na kuwaua wote.

    "zimebaki dakika kumi na tano tu, kama hajarudi tunaondoka" aliongea Scarlet, "hapana kama yatatimia masaa mawili hajarudi inabidi tuumpe nusu saa nyingine baada ya hapo kama hajarudi ndio tuondoke" alishauri yule rubani. Wakati wakiendelea kubishana ghafla waliona mwanga wa taa ukija upande wao. Kila mmoja alitoa bunduki yake na kujiweka sawa kwaajili ya chochote.

    Gari ile ilisimama mbele ya mawe hayo na mtu akashuka kuelekea ndani, "taratibuni mimi ni Alex" Alex aliongea huku akiingia ndani katika mawe hayo. "tufanyeni haraka, tuondoke eneo hili maana kuna hatari kubwa inakuja mbele yetu" Alex aliongea na kugeuza. Alitoka nje na wengine wakafuata nyuma, waliingia kwenye gari na safari ikaanza. "tubaelekea wapi" Scarlet aliuliza, "kilometer kama hamsini hivi kutoka hapa kuna kambi nyingine na katika kambi hiyo kuna uwanja wa ndege na ndipo tunapoelekea" Alex alijibu huku akiongeza mwendo wa gari hiyo.

    "sasa tukishafika tunaingiaje katika kambi hiyo bila kujulikana" aliuliza mwenzao mmoja, "musijali kila kiti nishapanga ninacho waomba kuwa mufate vile ntakavowaambia" Alex alijibu swali hilo huku akipunguza mwendo wa gari na kupunguza mwanga wa taa kwa sababu tayari walikuwa washakaribia kambini. Tartibu alisogea mpaka katika geti la kambi hiyo, Mlinzi alinyoosha mkono kusimamisha gari hiyo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Yametukuka mapinduzi" Alex aliongea huku akipiga ngumi kifuani mara tatu kisha akanyoosha mkono juu. Yule mwanajeshi nae akafanya vile vile "hawa ni wale wanajeshi tuliopewa taarifa tuwakamate" Alex aliongea na kumpiga Scarlet kibao. Jambo lilimuudhi Scarlet na kujikuta akifoka, "umeona wana hatari sana, huyo nyau nimemgusa kakasirika" aliendelea kuongea Alex. "vipi usafiri ulioandaliwa kuwabeba upo tayari?" aliuliza swali, "ndio nyoosha mpaka katika barabara nambari ishirini kuna ndege hapo inawasubiri" alijibu yule mlinzi bila kujua kuwa nachezwa akili.

    Alex alimshukuru na kuondoka, muda wote Scarlet alikuwa amevimba kwa hasira lakini Alex hakumuuliza kitu wa kumsemesha. Walifika mpaka walipoelekezwa na kukuta ndege ikiwa inawasubiri. Alisimama nyuma ya ndege hiyo na kushukua kisha akawafokea washuke, nao walitii na kushuka. Alex aliwaongoza mpaka mlangoni na kutoa taarifa kwa wale wanajeshi waliokuwa wakisubiri. Wakawashika na kuwapandisha kwa nguvu huku wakiwapiga vibao na ngumi, Alex nae alifuata nyuma huku akitamani kucheka.

    Walipoingia kwenye ndege yule mlinzi aligeuka na kukutana na ngumi nzito ya shingo ilimpeleka hadi chini na kukata mawasiliano. Alex aligeuka na kufunga mlango, baada ya hapo alielekea chumba cha marubani huku akiwa amembeba yule mwanajeshi aliempiga. Alibonyeza kitufe maalum na kumuelekeza yule mwanajeshi kwenye camera maalum. Mlango wa marubani ulifunguliwa na hapo aliingia ndani ndani ya chumba hicho kwa kasi ya juu sana na kuwachapa marubani wote wawili.

    Alipohakikisha wote wapo chini, aliwaburuza mpaka nje ya chumba na kurudi walipo wenzake. Alimpa rubani ishara amfate nae aliinuka moja moja kwa moja mpaka katika kile chumba cha marubani. Alex alikaa upande mmoja na yule rubani akakaa upande mwengine, "ndugu zangu, makamanda wenzangu katika kuimarisha ulinzi tunawaomba mukae kwenye viti na mufunge mikana. Muda wowote kuanzia sasa tutaanza safari" Alex alionge kupitia kipaza sauti na wote walifanya hivo.

    "ok, rubani hii ndio nafasi pekee ya kuokoka" Alex aliongea huku akibonyeza vitufe vidogo vidogo. Yule rubani nae hakuwa nyuma, alibonyeza vitufe vingine na mashine za ndege hiyo ziliamka na kuanza kufanya kazi yake. Taratibu ndege ilinza kutembea mpaka ilipofika kwenye njia inayotumika kwa ndege kupaa na kutua. Baada kukamilisha taratibu zote za awali walipata ruhusa kutoka kitengo kinachoongoza ndege (contrilling tower). Rubani alianza taratibu nyingine na taratibu ndge ilianza kushika kasi na hatimae iliacha ardhi.



    Wote kwa pamoja walifurahi kwa nguvu, ndege ilizidi kutokomea angani mpaka pale ilipofika umbali unaotakiwa na kukaa sawa. Baada kuhakikisha hakuna shida yoyote Alex alitoka katika chumba cha rubani na kuelekea walipo wengine. Kitu cha kwanza alichokutana nacho ni ngumi ya tumbo kutok kwa Scarlet "hiyo ni malipo ya kunipiga kibao" Scarlet aliongea huku akitabasamu. "sawa hakuna shida" Alex alijibu na kucheka kidogo.

    Safari iliendelea huku wote wakiwa wamepitiwa na usingizi kutokana na uchovu kasoro Scarlet peke yake. Alivoona hakuna wa kuongea nae aliamua kwenda chumba cha rubani labda huenda akapata mawili matatu. "Vipi naona kimya huko" aliongea yule rubani, "ah wote wamelala" Scarlet alijibu huku akikaa kwenye kiti. "mbona umeshika huo mkufu mkononi" Scarlet aliuliza, "ah huu mkufu ndio unaonifanya niendelee kuishi hata kama nitakutana na balaa la aina gani" aliongea rubani.

    "inavyoonekana una maana sana kwako", "ndio tena sana" alijibu yule rubani. Lakini Scarlet alipouangalia vizuri aligundua kuwa ulikuwa na kopa. "Adrian" Scarlet alijesemea kwa sauti ya chini huku akijikunyata, "umeita jina gani?" aliuliza rubani. "a..h hamna sijaita jina lolote" Scarlet alibabaika kifogo kabl kujibu swali hilo, "unajua nimesikia kama umetaja Adrian" aliongea yule rubani na wakati aligeuka ili amuone vizuri Scarlet. Alikuta akitoa macho huku kama akifikiria kitu, "haiwezekani nimemfananisha tu" aliongea yule rubani huku akigeuza uso wake mbele.

    Alikaa kwa muda huku akionekana kuwaza mambo mengi sana,"litakalokuwa na liwe tu" alijisemea yule rubani kisha akabonyeza kitufe kilichoandikwa autopilot. Kitufe hicho huifanya ndege ijiongoze yenyewe, kisha alimgeukia Scarlet ambae muda wote alikuwa kimya na mwenye kujikunyata. "Ariella" aliita kwa sauti ya chini, Scarlet alishtuka baada kusikia jina hilo. "hivi ni kweli au naona miujiza tu" alizidi kuongea yule rubani na kupeleka mkono kwaajili ya kuziondoa nywele usoni mwa Scarlet.

    "Ariella ni wewe kweli" aliongea huku akisimama na kutok kwenye kiti alichokuw amekaa, alifungua mkufu mkononi na kumkabidhi Scarlet. Yeye alisimama bila kumwambia kitu, Scarlet alifungua lile kopa na kukuta picha mbili, moja yake moja ya Adrian kipindi walichokuwa wadogo. Aliinuka kwa nguvu na kumrukia Adrian ambae alikuwa akitokwa na machozi ya furaha. walikumbatiana kwa nguvu huku wote wawili wakitokwa na machozi, "nilidhani sitokuona tena" aliongea Scarlet. "shhshh usiongee kitu tafadhali" Adrian alimnyamazisha.

    **************************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "mnasemaje nini wewe" alifoka general David baada ya kupoekea taarifa mbaya, "ndio mkuu, yule rubani mwenye taarifa ametoroshwa" alijibu aliekwenda kuripoti. "hilo sasa tatizo kwa kweli" aliongea General David na kuka kwenye kiti kama mtu aliotoka safari ndefu yenye kuchosha. Wakati wakiendelea kuongea, ghafla aliingia mwanajeshi mwengine huku akiwa na bahasha mkononi na kumkabidhi general. Alifungua na kuangalia kilicho ndani, alishtuka kidogo na kujikuta akiishiwa nguvu kabisa.

    "sasa kazi yetu itazidi kuwa ngumu" aliongea na kutoa kitambaa cha kujifuta jasho, "kivipi mkuu" aliuliza kamanda Willy ambae ndie alieleta ile bahasha. "mtu ambae nilidhani ameshakufa yuko hai kumbe" alijibu, "ni nani kwani huyo". "Alex, Alex, Alex" aliongea General David huku akikuna kichwa, "na kama Alex hajafa maana yake Agent Darling atakuwa kashaujua ukweli, hili ni tatizo kubwa sana" alijoiongelesha mwenyewe General David. "Kamanda Willy sambaza ujumbe kwa wakuu wote wa kambi zote, waambie tukutane ndani ya masaa ishirini na nne" alitoa amri hiyo general David kisha aliinuka na kuondoka.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog