Search This Blog

Friday, 20 May 2022

C.O.D.EX. 3 (THE REAL ME) - 5

 







    Simulizi : C.O.D.EX. 3 (The Real Me)

    Sehemu Ya Tano (5)





    Kamanda Willy aliondoka na kuelekea katika chumba cha mawasiliano, alifanya kama alivyoambiwa na General David. Masaa matano baadae watu walianza kufurika katika kambi hiyo, wengine walionekana kukerwa na wito huo kutokana na sura kujiknja sana. "ndugu zangu nashukuru kwa kuitika wito huu wa ghafla tu" General David alianza kuongea, "wacha nielekee moja kwa moja katika jambo ambalo nataka kusema. Mpaka jana mambo yalikuwa yanakwenda kama tulivyopnga lakini taarifa nilizozipokea leo ndizo zilizonifanya niwaite ili tujadili na kuona tutafanya nini. Natumai wote mtakuwa mnajua kuwa Alex alifariki" aliongea mpaka hapo na kuangalia umati utaitikaje.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nilitegemea sura zenu ziwe hivyo, sasa naomba muelewe kuwa Alex yuko hai na ndie alietuvurugia mipango yetu. Ila kwa sasa hatuwezi kukabiliana nae kirahisi kwa sababu kuna kikosi kikubwa na hatari sana THE PIRATES kinashirikiana nae. Nimewaita hapa kutak maoni yenu tunafanya kitu ili kuondoa kizuizi hichi" alimaliza kuongea General na kuwaangalia wenzake.

    "mimi naona bora tutume vijana wetu wakawaangamize huko huko kambini kwao" alisimama mzee mmoja na kuonge, "kuwashambulia kambini kwao itakuwa vigumu, mimi naona tucheze kamchezo fulani kitakachomtoa kambini halafu tunamalizana nae kiume zaidi" alisimama mtu mwengine na kutoa wazo lake. Hilo lilionekana kuungwa mkono na wengi, "hilo wazo ni zuri sana ila na mimi nina wazo langu" aliongea General David. "mimi nahisi ule mpango wa kufanya mapinduzi uanze tu" aliendelea kuongea na kutoa wazo lake.

    "lakini bado maandalizi hayajakamilika mkuu, tutaanza vipi" aliongea mtu mmoja, "hakuna haja ya kuchelewesha kwa sababu maandalizi yote yamekamilika na hizo taarifa alizokuwa nazo yule rubani si muhimu sana. Mi nawaambia tukichelewa basi Alex atatukaa kooni, huyu kijana mimi namjua vizuri sana. Ni hatari kuliko yoyote yule ambae amepitia Project CODE X" alijibu General na kuwafafanulia vizuri. Ukimya ulipita kidogo huku kila mmoja akionyesha kuyatafakri maneno alioyasema general, "mi nahisi wazo la genera lina mashiko, kwanini tusubirie wakati maandalizi yote yalishakamilika" alisimama mwanaume mmoja lafudhi kirusi na kuongea.

    Kuliibuka mzozo mkubwa na watu wakawanyika pande mbili, kuna wale waliokubaliana na general na wale waliopingana nae. Mzozo huo ulidumu kwa muda mrefu na mwisho wote walikubaliana na general katika wazo lake. Kikao hicho cha dharura kilimaliza huku viongozi wote wakikubaliana kukutana baada siku tatu kwa ajili ya mcahakato mzima wa kuanza mapinduzi, kila mtu alitwanyika na kurudi alipotoka.

    **************************

    "mkuu tumepata taarifa nzuri na mbaya kwa wakati mmoja" aliingia kijana mmoja ndani ya ofisi ya Jeff, "haya anza na mbaya halafu utafata nzuri" Jeff alimjibu huku akimuagalia Aget Darling ambae alikuwa akifanya mambo yake. "taarifa nzuri ni kwamba siku tatu kutoka leo kile kikundi cha wana mapinduzi kitaanza kufanya ushenzi wake, na taarifa nzuru ni kwamba ule muda wa kunyoosha viongo umefika" alimaliza kijana huyo aliejulikana kwa jila La Talbot.

    "mwisho kabisa, General David unatoka kuja kujibu mashtaka yako" Agent Darling aliongea huku akianza kuvimba kwa hasira. "Ok, sasa anzeni maandalizi ili wao wakianza sisi tunamaliza" Jeff alijibu na Talbot akatoka. "mpenzi kwa hasira hizo General David atakuuwa" Jeff aliinuka huku akiongea na kumsogelea Agent Darling au Christine jina lake halisi na kumkumbatia kwa nyuma. Wakati huo tayari machozi yalisharowanisha mashavu yake.

    Alex akiwa usingizini alishtuka ghafla na kuinuka, moja kwa moja hadi cumba cha rubani. Alipofungua mlango alipigwa na bumbuwazi baada ya kukuta wawili hao wakiwa wamekumbatiana. "samahanini kwa kuingilia kati starehe zenu" aliongea, "hapana tena bora ulivyokuja maana huyu bibie hataki kuniacha" alijibu Adrian na kujaribu kumtoa Scarlet KIfuani. "Ariella tafadhali punguza basi, najua ni muda mrefu lakini wacha tumalize ili kwanza halafu nitakuacha unikumbatie mpaka uridhike" Adrian aliongea kwa sauti ya chini lakini Alex alifanikiwa kusikia jina la Ariella. "Adrian" aliita Alex, "ndio mimi" Adrian alijibu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Ni hivi kwa sasa hatuwezi kuelekea kambini, si kwetu wala si kwako. Hii ni kwasababu katika kambi zote mbili kuna kunguni wamepandikizwa na waasi" aliongea Alex, "unasemaje?" Scarlet aliropokwa kwa nguvu. "natumai umenisikia bila shaka, kuna vikunguni vimepandikizwa na ile kambi kwa sasa sio siri tena kwasababu waasi wanajua ilipo na kila kinachofanyika humo" alijibu Alex na kufafanua. "Adrian sasa hivi tuko wapi" aliuliza Alex, Adrian alisoma rada "tunakaribia New York".

    "hii ndege inabidi tuiangushe majini ili tusijulikane tulipo, Scarlet kawaambie wavae makamanda wavae parashute kabisa" Alex aliongea na Scarlet alitoka katika chumba hicho na kuelekea walipo wengine na kuwapa taarifa. Bila kuchelewa walianza kujiandaa, "Adrian igeuze ndege na uielekeze chini" Alex aliongea na kutoka chumbani humo. Adrian aliigeuza na ufanya kama alivyoelekezwa. Kisha alitoka humo nakwenda kuungana na wengine.

    Walipohakikisha kila mtu amejiandaa, walifungua mlango wa nyuma wa ndege hiyo na wote wakaruka na kuiacha ndege ikielekea baharini na kulipuka. Alex akiwa kama kiongozi kwa sasa, aliongoza msafara huo unaoelea angani kuelekea mjini New York. Baada kama dakika ishirni hivi walifungua maparachute na kushuka nje ya mji kidogo. Walipohakikisha wote wakosalama, Alex aliwapa ishara wamfuate. Walitembea kwa nusu saa mpaka walipofika katika nyumba moja ambayo ilikuwa imejitenga sana na nyingine.

    Alex alisogea mlangoni na kubonyeza sehemu, kilitoka kitu kama keyboard ndogo. alibonyeza bonyeza na mlango ukafunguka, "karibuni nyumbani" Alex aliongea na kuingia ndani huku nyuma akiafatiwa na makamanda wengine. "Alex hii nyumba ni ya nani?" aliuliza Scarlet, "ni ya mwalimu wangu Allen James" Alex alijibu na kukaa kwenye kochi. Kila mtu alionekana kuchoka kivyake vyake, baada muda kidogo kupita Alex aliinuka na kuelekea katika chumba chake. Alikaa kwa muda kabla ya kusikikia vitu vikivunjika. Wote walikimbilia chamba ambcho alikwenda Alex, walimkuta akimeshika picha mschana huku akilia kwa majonzi ya hali ya juu. "najua bado amani hujaipata lakini nakuahidi kuwa muda si mrefu utaipata" Alex aliongea huku akifuta machozi.

    Scarlet alipoona vile aliwaambia wenzake watoke na wamuache peke yake, afanye analotaka. Dakika ya saa kupita Alex alirudi ukumbini akiwa anatabasamu sana, "Scarlet wasialiana na general mwambie aondoke kambini hapafai tena" aliongea Alex na kumkabidhi simu maalum lakini kila Scarlet alipojaribu namba ya General haikupatikan kabisa. Alijaribu zaidi ya mara kumi lakini hali ilikuwa ndio ile ile. Alijikuta akiingiwa na baridi ghafla, wenzake walijaribu kumtuliza na kumwambia kuwa atakua salama. "labda amezima simu kwa sababu za kiusalama zaidi" aliongea Adrian.

    "jamani leo pumzikeni maana kuanzia kesho kutakuwa na kazi kubwa sana ya kufanya" Alex aliongea na kuwaomba wamfuate, aliwaonyesha vyumba vya kulala na mwisho alibaki yeye, Scarlet na Adrian. "nyinyi chumba chenu kile pale, maana hueda baada ya leo msipate tena usiku wa kuwa pamoja" Alex aliongea na kuwafanya wote wacheke. Waliagana na kuelekea vyumbani mwao, huko chumbani kwa Scarlet na Adrian kulikuwa ni peponi kwa usiku huo.

    Baada ya kuingia chumbani kwake Alex alitoa computer ndogo inayojulikana kama master computer. Aliichezea na kuingiza code anazojua yeye mwenyewe na akili yake kisha akatuma ujumbe "Allen Jr za siku nyingi" ndivyo ulivyosomeka ujumbe huo. "Christine kuna ujumbe wako huku" Martina alimuita Christine, macho yalimtoka baada kugundua kama ujumbe huo umetoka kwa Alex. Na hilo halikumpa tabu kutokana na kuwa ni Alex pekee ndie anaemuita Allen Jr. "unataka nini?" alijibu, "wakati huu ni wakati wa kueka tafauti zetu pembeni" Alex alijibu. "unamaanisha nini?" Christine alihoji.

    "wewe unataka kulipa kisasi cha babaako na mimi nataka kulipa cha mwalimu wangu, sasa kwanini mimi na wew tuwe maadui?" alex alijibu na kuuliza swali. "sihitaji msaada wako" Christine alijibu kuonesha jeuri, "bado hujakua kumbe, au unaringa kwasababu uko na Jeff" alijibu pigo na kuwafanya wote washtuke. "musishituke sana na wala musihangaike kutafuta ni wapi ninapo waonea" Alex alijibu. "sasa ni hivi mimi najua ulipo nakupa nafasi ya mwisho, aidha tueke tafauti pembeni au tuendelee kuwa maadui" Alex alituma tena ujumbe.

    "na kama nikikata kushirikiana na wewe" Christine alijibu, hapo hapo computer zao zilizima na zilipo waka tu ilionekana picha ya Alex akicheka. "naona kukuandikia kwa ujumbe hutaki kunielewa na natumai sasa tutaelewana vzuri" aliongea kisha akaendelea "ukikataa, hao wote waliouwa pembeni yako watakufa mmoja baada ya mwengine". "Christine hebu kaa pembeni kwanza" aliongea Jeff, "Alex tuongee kiume maana huyu mtoto wa kike anaonekana hajakua bado" Jeff aliongea jambo lilimkera sana Christine. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mambo si hayo sasa, Allen Jr kaa pembeni kaka zako tuongee" aliongea Alex na kucheka kidogo. "Sasa ni hivi hawa jamaa wanakambi nyingi sana na ili kuwapunguza makali tuanze kuteketeza kambi moja moja mpaka zibakie chache ambazo tutaweza kuzimudu" Aliongea Alex. "kwa makadirio zinafika kambi ngapi" Jeff aliuliza, "mia moja na hamisini na kidogo hivi lakini hazifiki mia mbili" Alex alijibu. "hizo nyingi kweli" Jeff alijibu na kuendelea "sasa una mpango gani?" aliuliza, "hizo kambi zimegawanyika sehemu tatu, kuna za baharini, za msituni na za jangwani. Nyingi ziko jangwani na baharini na hizo ndio rahisi kuziangamiza" alifafanua Alex na kuendelea "kwa vile sisi tuko makundi mawili, inabidi tugawane kundi moja lichukue kamba za baharini na kundi la pili lichukue za jangwani. Tukizimaliza hizo tushirikiane kuzimalizia za msituni maana hizo ndio kambi kubwa kuliko zote".

    "sawa hakuna shida mimi na timu yangu tutachukua za jangwani, kesho usiku tutahakikisha zimekweisha zote" Jeff aliongea na kutabasamu. "ok sis huku tutachukua za baharini, tukutane tena kesho usiku kwa ajili ya mipango mengine" Alex alimaliza kuongea na kukata mawasiliano. Sekunde chache tu baada ya kukata mawasiliano hayo, uliingia ujumbe kambini kwa Jeff. Ilikuwa ni ramani ya kambi za janngwani, "kwa nini unataka kushirikiana nae?" Christine alifoka. "tatizo lako wewe hutaki kuwa muelewa, unadhani pekeetu tungewezaje kupata taarifa zote hizi. Kuna baadhi ya wakati inabidi ukubali tu kama umeshindwa, na kuanzia sasa jina langu ni Ghost na sio Jeff" Jeff aliongea huku akikunja sura. Christine alitaka kumjibu lakini Talbot alimuwahi na kumziba mdomo kisha akamwambia "kumjibu ni wazo baya sana na utalijutia, ni bora unyamze tu maana ushamvuruga. Akibadilisha jina na kujiita Ghost ujue tayari yupo katika maandalizi ya kuuwa au kutoa dozi isio na kipimo maalum"

    Christine alipoambiwa hivo alinyamaza kimya, Jeff alielekea chumbani kwake na kujichimbia. Alianza kupanga na kupangua mipango yake, mpaka muda huo alishaelewa kusudio la Alex. "kwanini yule mwanamke anakuwa kichwa ngumu" alijiuliza swali hilo, wakati akiendelea kuwaza mlango ulifunguliwa na alieingia alikuwa ni Christine. "Jeff nimekukwaza?"aliuliza, "hivi kwanini unaweka sana vinyongo, we hujaona maana ya Alex kukutafuta" aliongea Jeff au Ghost kama anavyojulikana na wakiuka sheria wengi.

    "kinachoniuma ni babaangu kufa kwaajili ya mtu mwengine" Christine alitoa donge hilo moyoni, "wewe kwani leo unavyopambana na majambazi sugu, unapigania maisha ya familia yako au?" alifoka Jeff. "hapana napigania maisha ya watu wa nchi yangu" alijibu huku akiona aibu, "sasa babaako kufa kwa ajili ya mtu mwengine huoni kama alikuwa akitimiza wajibu wake" Jeff aliongea. "basi yaishe nimejifunza" ilibidi Christine akubali sasa, "sio kujifunza unatakiwa kuwa mwanajeshia aliekomaa, yaani pamoja na kuwa na cheo kikubwa kama cha THE ONE AND THE ONLY. Unashindwa na mtu mwenye cheo cha ukomando tu kweli mpenzi wangu" Jeff alionekana kukereka sana na tabisa alioinesha Christine mbele ya Alex na mbele ya kikosi chake chote.



    Ilibidi Christine atumie nguvu ya ziada kuomba msamaha, kwasababu alielewa ni kiasi gani amekidhalilisha cheo chake. Baada kuomba msamaha muda mrefu, Jeff alisamehe na kumona ikiwa atarudia tena basi atamvua cheo. Hilo lilikuwa onyo kali sana ambalo Christine tokea anze kulitumikia jeshi hakuwahi kupewa. Jeff alirudi ukumbini na kukiita kikosi chake chote "kesho kutakuwa na kazi ngumu sana ya kufanya, na kazi hiyo ndio itatupa muelekeo wa nchi zetu. Tukae tukijua kuwa tukiharibu basi tumeziumiza nchi zetu. Kufa vitani ni ushujaa kuliko kurudi nyumbani na mkia katikati ya mapaja eti tumeshindwa. Tunasimama pamoja hadi mwisho, hadi tujue mbivu na mbichi" Jeff alimaliza kuongea na kuweka mkono kati, ilifata mikono mingine juu na kwa pamoja wakasema "pamoja hadi mwisho".

    Upande wa Alex huko nako mambo yalikuwa yameiva sana, "sisi tuko tisa na ndege zipo tano, sasa ni hivi kila ndege itakuwa na watu wawili kasoro moja. Hiyo moja ntakuwa pekeangu, kumbukeni kuwa kuifanikisha kazi hii ni muhimu sana hata kama itatugharimu maisha yetu" aliongea Alex na alionekana kuwa makini sana na anacho kiongea. "nifateni" aliwaambia na kuanza kuongoza njia, aliingia katika chumba chake na kufungua kabati ambako kulikuwa na mlango wa siri. Waliingia wote, mlango ulifungwa na lift ikaanza kushka chini. Kumbe ilie ni lifti, iliposimama na mlango kufuguka wote walipgwa na bumbuwazi baada kkutana na ndege za kipekee za kivita.

    "sijawahi kuona ndege kama hizi zaidi ya kwenye filamu" aliogea Adrian, "basi leo utarusha kabisa" Alex alijibu na kutabasamu. walichagua wawili wawili na kila kikundi kikaelekea kwenye ndege moja, "kabla ya kuondoka, kila mtu aombe mungu wake kutokana na imani yake. Maana huenda tusionane tena baada ya leo" alimaliza kuongea Alex na kila mtu akasali anavojua yeye. Waliingia kwenye ndege zao, mlango mkubwa ulifunguka na kuonesha njia ndege kwa uzuri zaidi. Zilianza kutoka moja moja, Alex ndie aliekuwa wa mwisho. Zilifuatana kwa dakika tano kisha kila ndege ikashika njia yake, haikuwa shida kwa sababu ramani walikua nazo wote.Wakati huo huo upande wa kina Christine walitoka na ndege zao, na kuelekea katika kambi zilizokuwa jangwani.

    ***********************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Mkuu kambi zetu zaidi ya hamsini zimesharipuliwa" aliingia kamanda Willy na kutoa taarifa ofisini kwa general David. "unasemaje wewe, mbona sikuelewi" aliuliza huku akisimama, "kambi zetu zaid ya hamsini zimesharipuliwa na hakuna hata mwanajeshi mmoja aliepona" alifafanua kamanda Willy. "zimeshambuliwa kwa kitu gani" aliuliza General, "ndege za kivita lakini hazijulikani ni za kikosi gani" alijibu kamanda Willy. "Alex" general David aliita kwa nguvu, "tuma ndege miamoja zikakabiliane nao kabla hawajatumalizia kambi zetu" General David alitoa amri hiyo iliotekelezwa punde tu baada kamanda Willy kuondoka.

    Ndege mia moja za kikosi cha waasi ziliingia angani, wakati huo Alex na kikosi chake walikuwa wanakaibia kuzimaliza kambi za waasi zilizokuwepo baharini. "makamanda hakikisheni tunazimaliza kambi zote, zimebakia kumi tu. Halafu kwa kasi ya ajabu elekeeni upande wa kambi ya The pirates, msishuke piteni maana muda si mrefu tutapata marafiki kutoka kwa waasi" aliongea Alex kupitia kifaa maalum kilichowaunganisha kikosi chote. "umesomeka mkuu" walijibu kwa pamoja na kila mmoja akaendelea na kazi ya kuziteketeza kambi zilizosalia. Baada kuhakikisha zimekwisha walianza kugeuza na kuelekea upabde wa kambi ya the pirates.

    "general Griffin unanisoma" Alex aliongea, "unasomeka over" General alijibu. "nakuletea tunakuletea sherehe upande wako" Aleo aliongea, "muziki uko tayari over". "rodger" Alex aliongea na kuanza kuongeza mwendo wa ndege yake. Wakati huo tayari ndege kadhaa za waasi ailikuwa nyuma yao zinawafukuza huku zikijaribu kuwashambulia. Lakini kutokana na teknolojia ya ndege wanazo endesha, mabomu ya ndege hizo yalijkuta yakipoteza muelekeo na kugongana yenyewe.

    Kwa mbali Alex aliona ndege wenzake zikielekea kule aliposema, "hapo kwenye sehemu yenye vitufe, kuna kitufe kimoja kimeandikwa HS. Hiyo inamaanisha hypersonic speed, bonyezeni hicho kitufe na mufurahie mwendo kasi usio wa kawaida" aliongea kupitia kifaa maalum. "umesomeke" walijibu kwa pamoja na kila akabonyeza. Ndege hizo ziliongezeka kasi na kuanza kutoweka hasa katika upeo wa ndege za waasi. Masiki waasi bila kujua kama walikuwa wanaingizwa megoni, waliendelea kuwafukuza. Ndge za kina Alex zilipita juu ya kambi ya the pirates, na zilipoanza tu kupita za waasi, zilianza kutunguliwa na bunduki maalum zinazoitwa Anti-aircraft.

    Ndege zote za waasi zilizokuwa zinawafukuza zilitunguliwa na bastola hizo, baada ya hapo Alex alitoa amri wageuze na kutua katika kambi yao hiyo ya the pirates. Dakika chache baada ndege zilitua lakini zilikuwa nne tu moja haikuwepo, walishuka wote ila kabla hawajafanya lolote Alex aliwaita "tufungeni macho ili tuwaombee wenzetu wawili waliopoteza maisha vitani". Walishtuka kidogo lakini walifunga macho na Adrian akaongoza sala. "karibuni nyumbani mashujaa" General Griffin alongea huku akija upande wao akiwa anaongozana na raisi.

    Adrian alipomuona tu raisi alimsogelea na kutoa heshima kisha akatoa kisu kidogo na kujichana sehemu ya nyuma katika paja la kulia. Wote walimshangaa, alitoa kitu kilizunusha katika mfuko maalum. Aliufungua na kutoa chip ndogo, "muheshimiwa nawasilisha taarifa ulizoziagiza" aliongea Adrian na kumkabidhi raisi ile chip. "asante na pole kwa yaliokukuta" raisi aliongea na kutoa amri madaktari wamshughulikie Adrian. Waliingia ndani na kila akaelekea chumbani kwake kwa ajili kuoga na kupumzika.

    Baada ya nusu saa wote waliitwa katika ukumbi maalum wa vikao, "Alex umekuja na ule mzigo" aliuliza general. "ndio mkuu" Alex alijibu, "mleteni huyo kunguni huku" General aliongea na hapo wakaingia wanajeshi wawili wakiwa na mtu mmoja aliefungwa pingu. "makamanda huyu ndie kunguni aliepandikizwa na waasi. "umemjuaje?" Scarlet aliuliza akionekana wazi kutokubaliana na aliloliongea Alex. "siku ile niliokuwa nikonyesha uwezo wangu, si nilisema achaguliwe sniper bora" Scarlet alikisa kichwa kuashiria anakumbuka. "huyu alijikosesha makusudi, kwa sababu aliogopa nitamgindua. Kwa hiyo baada ya kupiga kifuniko akapiga chini kidogo katika shingo ya ile chupa, sio hilo tu. mgongoni ana mchoro unaotukuza mapinduzi" Allex aliongea hivo na kuinuka.

    Alisogea mpaka alipo yule muasi na kuwaambia wale waliomshika wamlaze chini, "someni hayo maneno kinyumenyume" aliwaamba wengine. Hapo kila mmoja alishangaa kuona maneno hayo yakisomeka "yametukuka mapinduzi", lakini katika hali ya kawaida huwezi yagundua kabisa. Baada hapo Alex alimsimamisha na kusogea nae kwenye meza, alimfungua pingu na kuwambia aeke mikoni kwenye meza. Aliifunga mikono hiyo na vyuma maalum vilivyokuwa katika meza hiyo na kuacha vodole vikiwa vimenyooka. "sasa ni hivi kijana, naomba unambie kambi yenu kubwa iko wapi na nakutahadharisha kama hutotoa ushurikiano basi nitahakikisha naukamua ukweli hata kama itabidi nikukaushe damu" Alex aliongea akionekana hatani hata kidogo.

    Upande wa Agent Darling na Jeff mambo pia yalikuwa mazuri, walimaliza kambi zote jangwani pamoja na ndege zilizotumwa kwenda kupambana nao. Walipohakikisha hawafauatiliwi tena, walirudi kambini kwao, "hongereni sana" Jeff aliongea kuwapongeza majenedari wake. "huu ndio kwanza mwanzo kwa hiyo tusudhani tumeshinda" aliendelea kuongea na alipomaliza kila mtu alitawanyika na kuelekea sehemu yake ya kupumzika.

    "inavyoonekana hutaki kutoa ushirikiano kwa njia ya amani" Alex aliongea baada yule kijana kuleta ubishi. "basi hakuna shida" alitoa sindao ndogo yenye dawa kiasi na kumchoma, "hii ni sindano ya ganzi" aliongea baada kumchoma na kusubiri dakika kadhaa. Wakati huo mpaka raisi alikuwa akishuhudia mateso anayotoa Alex. Alifungua pochi maalum na kutoa sindano ndefu jma sentimita tani na kuanza kumchom chini ya kucha kwenye vidole vya mkono. Aliingiza urefu wote hadi mwisho mpaka alipohakikisha amevichoma vidle vyote kumi.



    "saa hivi huhisi kitu lakini niamimi hiyo ganzi ikiisha utajuta kwanini hukutoa ushrikiano mapema" Alex aliongea na kukaa tena kwenye kiti akisuiri ganzi iishe. Baada kama dakika sita jamaa alianza kukunja uso, na kwa mbali macho yake yalianza kurowa maji. "muda umefika, sasa nambie kambi yenu kuu iko wapi?" Alex aliongea, lakin bado jamaa alikuwa mbishi. Alex alianza kuchomoa sindano ya kidole kimoja na kuirudisha kama vile anachokonoa kitu.

    Jamaa alipiga sana kelele, "yaani nimekwambia hata ikibidi nikukaushe damu niupate ukweli basi nitafabya hivo kwa maana huu ni mwanzo tu" Alex aliongea kwa hasira huku akiedelea kufanya kazi yake. "nitasema tafadhali usifanye tena hivo" maumivu yalipozidi jamaa aliamua kutoa ushirikiano, "mambo si hayo sasa, ungekubali mapema tusingefika hapa" Alex aliongea na kukaa kwenye kiti. Basi jamaa hakuwa na jinsi aliongea kila kitu bila kuficha hata kidogo, "tafadhali naomba unichome tena ganzi ili nipunguze maumivu" aliomba baada kumaliza kuongea.

    "usijali yatakwisha sasa hivi" alijibiwa lakini si na Alex bali ilikuwa nisauti ya raisi, alisogea mpaka alipo Alex na kuchomoa bastola ndogo. Alimuekea kichwani na kumpasua kichwa, "tunajitahidi kuleta amani nyinyi mnaleta upumbavu, eti mapinduzi" aliongea raisi baada kumchapa risasi. Wote walipigwa na bumbuwazi na wasiamini kitendo alichokifanya raisi, "muheshimiwa bado kitu kimoja" Alex aliongea na kuunganisha computer yake na rubinga kubwa iliokuwepo hapo ukumbini.

    "Jeff mambo yameendaje" Alex aliongea baada kioo cha runinga kuonesha picha ya Jeff akiwa na majemedari wake. "umekwenda vizuri sana na hakuna hata kambi moja iliosalia jangwani" alijibu, "safi sana, sasa tunaelekea hatua ya mwisho. Zimebaki kambi kadhaa pamoja na kambi yao kubwa" Alex alimueleza Jeff kila kitu na wakakubaliana wakutane sehemu karibu na kambi hizo ambazo ziko porini. Baada ya maongezi ya dakika kadhaa alimpisha raisi nae aongea kijana Jeff ambae cheo chake ni zaidi ya kamanda.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **************************************************

    Katika ndege mia zilizotoka ilirudi moja tu, ilipotua tu alishuka rubani wa ndege hiyo na kukimbilia ofisini kwa general David. "mkuu tupo matatani" aliongea baada kuingia katika ofiso hiyo, "kivipi" aliuliza kamanda Willy ambae alikuwa akiongea na general wakati rubani huyo ameigia ofisini. "ndege zote zimeripuliwa, mimi nimeokoka ki bahati bahati tu. Pia sijawahi kuona ndege zenye uwezo kama tulizokutana nazo huko, na mbaya zaidi kambia zetu za jangwani na baharini zimeripuliwa zote na sidhani kama kuna mtu aliepona. Na kama wapo basi sijui hata kama mia wanafika" alieleza kijana huyo.

    "hii kasheshe nyingine" kamanda Willy aliongea huku akitikisa kichwa, "hizi ni alama za majanga" aliongea General David. "master mind wa mchezo huu ni Alex, na ili kujihakikishia ushindi lazima tumuue" aliendelea kuongea. "kamanda Willy tuma ujumbe kwa wakuu wote tukutane leo hii kabla jua halijazama", kamanda Willy aliinuka na kuondoka. "hivi kwanini ulizaliwa we mwanaharamu Alex, ah lakini kosa ni langu kudhani utanifaa" alijisemea mwenyewe general

    "majemedari wote tusikilizane, leo hii ndio itaamua hatma ya nchi yetu. Tuwaonyeshe wale wanaidhani wanaweza kuchwza na amani yetu. Vita ya leo ni ua ama uawa lakini mpaka kieleweke" hayo yalikuwa ni maneno General Griffin kwa vijana wake. "tumekusoma mkuu" walijibu kwa pamoja, "Alex utaendelea na kikosi hicho kidogo, na kazi yako ni kutufngula njia tu. Mimi nitakuja na kikosi kikubwa halafu tutaongana katika mapambano" General aliongea na Alex alitikisa kichwa kukubali. "mimi je" ilikuwa sauti ya raisi, "mkuu usalama wako ni muhimu" alijibu General Griffin.

    "Muheshimwa raisi tutahitaji msaada wako" Alex aliongea na kumsogelea kisha akamnong'oneza kitu sikioni. Raisi alitabasamu na kuashiria amemuelewa, "basi hakuna shida wacha mimi niondoke niwaache muendelee na majukumu mengine" Raisi aliongea na kusimama kisha akaondoka. Waliendelea kupanda mipango yao kwa makini sana, walifanya hivo kuhakikisha hatoki mtu hata mmoja kati ya waasi.



    Mipango ilipokamilika Alex aliondoka na kikosi chake, walikuwa wamejipanga kisawa sawa. kila mtu alibeba ile silaha ambayo aliamini ni rafiki yake mkubwa. Walipanda ndege na safari ikaanza, kila mtu kwenye ndege alisali anavyojua yeye. "baada ya vita hii,kutakuwa na mambo mazuri sana" aliongea Alex huku akicheka na kuwafanya wenzake wote kumuangalia kwa sintofahamu.

    Ndege ilifika karibu na eneo la waasi kushuka usawa wa bahari, Alex na kikosi chake waliruka na kuingia kwenye maji. Waliogelea mpaka nchi kavu, "tutasubiri kikosi cha Jeff na Darling kifike" aliongea Alex na kila mmoja akatafuta kicha cha kujificha. Nusu saa baadae waliibuka watu kadhaa kutoka maji, walianza kutembea taratibu mpka juu kabisa kwenye mchanga. Mmoja wao aliweka silha chini na kuinyanyua mara tatu, Alex alitoka na kikosi chake. "nimefurahi kukuona tena Allen jr" Alex aliongea baada kumuona Christine, "Jeff nashkuru kwa kufika" aliongea tena na kumpa mkono Jeff ambae aliupokea kwa tabasamu.

    "tunaanzia wapi?" aliuliza Jeff, "tusubiri kama dakika kumi hivi" tutapata pa kuanzia. Alex aliongea na wote wakatoa ishara ya kuelewa. Walianza kuongea utasema hawako hatarini, baada ya dakika kumi zilipita ndege kadhaa zinazojulikana kwa jina la DRONE au ndege isio na rubani. Zilianza kushambulia kambi ndogo ndogo zote ambazo zimezunguka kambi kubwa. "natumai tushapata pakuanzia" Alex aliongea na kushika mtutu wake vizuri.

    Kazi ilianza huku wakijitahidi kuwaondoa wale walibahatika kupona mavamizi ya ndege zile zisizo na rubani. Walipohakikisha wamesafisha njia, Alex alitoa radio na kuongea "miba yote imeendoka", "rodger" alijibiwa upande wa pili. Vilianza kutoka vifaru kwenye maji pamoja na jambizi amabzp zilishusha magari na vifa vingine vya kivita. Walifika mpaka walipo kina Alex na Jeff, "kazi nzuri kijana" aliongea general Griffin. Waliingia kwenye gari na safari ikaanza, sasa walikuwa wamebakiwa na kambi kubwa tu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "mkuu kitumbua kimeingia mchanga" Kamanda Willy alirpoti, wakati huo kulikuwa na kikao kinaendelea. "inavyoonekana Alex amekucheza akili mkuu" aliendelea kuongea Willy, "kivipi" aliuliza General David. "alijua akishambulia kambi ndogo ungeita wakuu wote ili kujadili mstakbali wa dhamira yenu na inaonekana amelenga ndipo" alifafanua Kamanda Willy. "ndio yuko sahihi kabisa" walisikia sauti, "msishtuke sana, kwasababu hivi punde tu tutakutana. Na nasikitika sana kukwambia General David, kosa lako kubwa ulolifanya ni kucheza na familia yangu. Kosa hilo litakugharimu vile inavyostahiki" aliongea Aex kwa sauti nzito na kukata mawasiliano.

    "mkuu tumevamiwa" aliingia mwanajeshi mwengine na kuongea, sasa wale wote waiokuwepo katika kikao hicho walianza kuhisi tumbo la kuharisha. "sasa tnafanyaje" aliuliza mzee mmoja alieonekana muoga kidogo. "hapa hakuna la kufanya tumezungukwa na mjeshi ya serekali, mimi niliwaambia tufanye mapema mukaniona mjinga" aliongea General David. "sasa kila mtu hapa atatoka kwa nguvu zake" aliendelea kuongea na alipomaliza aliinuka na kuondoka.

    Huko nje moto ulikuwa si wa kitoto, mkali Alex na Jeff na vikosi vyao walikuwa wakitembeza dozi. "Scarlet achana nae huyo kashakufa" Adrian alimwambia Scarlet baada kumuona akimuamsha mwenzake mmoja ambae amepigwa risasi. Mpambano ulizidi kuwa mkali, maana hiyo kambi haikuwa na wanajeshi kidogo. Wakati mpambano unaendelea Scarlet alizembea kidogo na kuna mtu alikuwa kashamlenga mlenga, ghafla General Griffin alipita mbele yake na kukinga kifua. Risasi iliopigwa kwa lengo la kumuua Scarlet ilipenya kifuani mwa General na kuanguka chini. Alipotaka kuongea nae alimpa ishara aendelee kupambanaa.



    Huko ufukweni ziliibuka nyambizi nyinngine zikiongozwa na raisi mwenyewe, mambo sasa yalizidi kunoga maana waasi hawakutegemea kama jeshi kubwa kama vile lingekwenda kupambana nao. Jeshi hilo lilokuwa chini ya raisi liliekea uwanjani na kuendeleza mapigano, general David alifanikiwa kufika mpaka kwenye helicopter. "tuondoke haraka" aliongea na hapo aliongezeka mwanajeshi mmoja kwa ajili ya ulinzi na helicopter ikaondoka. Ilipofika kwenye ufukwe ilianza kushuka, "mbona unaishusha hapa" aliuliza. "ulidhani unaweza kututoroka" sauti ya Alex ilisikika kutoka mbele, "general mzima unaacha wanajeshi wako wanakufa wewe unakimbia" sauti ya kike ilisikika pembeni yake na ilikuwa ni ya Agent Darling.

    Helicopter ilikanyaga fukwe na papo hapo ikazungukwa na wanajeshi, "wekeni silaha chini" ilikuwa sauti ya raisi. "mheshimiwa raisi mkuu wa waasi huyu hapa" Alex aliongea huku akimshusha general David kwa nguvu. "kazi nzuri kijana" raisi alimpongeza, "Agent Darling nahisi mimi nikuachie wewe huyo mpuuzi, mfanye unavotaka na hakuna atakae kuuliza" Raisi aliongea na kurudi nyuma. Masikini General David alichokutana nacho nahisi atamsimulia Allen huko kwa alipokwenda. Agent Darling alipohakikisha General David hajiwezi tena, alimchapa risasi ya kichwa na kummaliza kabisa.

    Vita hiyo ilikwisha na waasi wote waliokamatwa waliuliwa huko huko, lakini hali ya general Griffin ilikuwa mbaya mno. Aliwaita Scarlet na Adrian na kuongea nao kitu kidogo, baada ya hapo raisi alifika "mheshimiwa nasikitika sitokuwepo karibu yako tena na kukusaidia katika kufanikisha malengo yako" aliongea japo kwa tabu kidog. "siku zote utakuwa karibu yangu, najivunia kuwa na General kama wewe katika nchi yangu" aliongea raisi na kumshika General mkono. "una ombi lolote la mwisho kabla hujasafiri safari ya milele" raisi alimuuliza.

    "ndio mkuu, naomba Alex aongoze kikosi cha THE PIRATES. Ana mbinu nyingi sana za kivita na uwezo wa kipekee, atasaidia katika kiwango kikubwa sana katika kuimarisha ulinzi wa nchi yetu" aliongea General na kukohoa damu. "kwa mamlaka niliokuwa nayo kama raisi wa nchi hii, Bwana Alex Jr umepandishwa cheo na kuwa General wa nchii hii. Kuanzia sasa utakuwa mkuu wa kikosi cha The Pirates" raisi alimuapisha Alex mbele ya General Griffin ambae alikata roho huku ametabasamu.

    Maiti yake ilibebwa a safari ya kurudi ufukweni ikaanza, lakini kabla hajaingia kwenye nyambizi Alex alimnongoneza kitu raisi nae akaonesha kama kukumbuka kitu. "Adrian, Ariella, Jeff na Christine nomba musogee hapa" alitoa amri rais, nao walisogea lakini walikuwa hawajui kitu gani kinaendelea. Ghafla kwenye nyambizi alishuka mchungaji akiwa amembatana na watu kadhaa. Walifungishwa ndoa hapo hapo katika uwanja wa vita, "Alex asante na naomba unisamehe" aliongea Christine na kumkumbatia. "usijali mdogo wangu, Allen alinambia nikulinde mpaka pale utakapopata wa kukulinda mwengine" Alex alimjibu huku akicheka.

    Waliigia kwenye nyambizi na safari ya kurudi ikaanza, siku hiyo iliwekwa katika kumbukmbu za nchi hiyo kama siku ya mashujaa. Mazishi yalikamilika huko Adrian na Scarlet wakianza maisha yao nje ya jeshi, Jeff na Christine walielekea Qatar kwa ajili ya kuwasalimu ndugu wa Christine. Alex alirudi katika kambi ya the pirates kwa lengo la kukikuza kikosi hicho na kuwa hatari kuliko wanajeshi wa Project CODE X. Amani ilirejea nchini na hofu ilipotea, na kila mwaka waliadhimisha siku ya mashuja katika nchi hiyo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    UZALENDO NI NGAO PEKEE YA KUIKOMBOA NCHI KUTOKA KATIKA MAJANGA, JIVUNIE KUWA RAIA WA NCHI YAKO MAANA KUWEPO KWA NCHI NDIO KUNATAFSIRI UTAIFA WAKO.

    IN GOD WE TRUST



    MWISHO.







0 comments:

Post a Comment

Blog