Simulizi : Duka La Roho
Sehemu Ya Pili (2)
"Kile kibanio umempa wewe kweli?" Mubah akamuuliza swali Lisa.
"Hapana. Kapewa zawadi na baba yake. Lakini aliambiwa mimi ndiye niliyempa kwa sababu sikuwa na zawadi hii leo. Kwani vipi Mubah?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hamna tatizo. Ila ni kibanio ghali sana kile, hadi nimeshtuka." Mubah alidanganya lakini ukweli ni kwamba kile kibanio alichokuwa nacho Martina, ndicho ambacho mjomba wake alipewa na Lobo. Yaani vinafanana.
Ndicho kile kilichotoa sumu hatari kutoka kwenye Yellowstone.
Wakarudi kwenye gari baada ya maongezi machache na kisha gari likakaza mwendo kuelekea Kivule.
Kichwa cha Mubah hakikutulia hata kidogo kimawazo. Akiwa katika mawazo hayo, ndipo akakumbuka sura ile iliyompita kwenye gari wakati yeye anazimia.
Akakurupuka tena na kumuangalia Lisa kwa macho ya kushuku kitu. Lisa akabaki mwenye mshangao wa hali ya juu kwa matendo nadra ayafanyayo Mubah.
"Yule ni Gunner, mume wa Lisa. Mshenzi anashirikiana na Lobo. Mungu wangu." Mubah akajisemea mwenyewe moyoni huku akimkodolea macho makali Lisa.
"We' Mubah unamatatizo gani!? Hiyo tabia umeitoa wapi." Ikabidi Lisa amuulize Muhah jambo linalomsibu hasa baada ya kuona macho ya Mubah hayakauki usoni pake.
"Hakuna Madam. Basi tu!" Mubah alijichekesha huku akijaribu kuumba tabasamu la mbao usoni pake.
"Usinifanye mimi mtoto Mubah. Mi' ni Jasusi na pia ni mpelelezi kuliko wewe. Najua unafahamu kitu, haya haraka eleza nini kipo nyuma ya pazia." Lisa akauliza tena akiwa katika uso usio na masikhara. Wakati huo, gari lao lilikuwa likizidi kusonga mbele na Martina akionekana kufurahia mwenendo mzima wa safari ile.
"Hamna kitu madam Lisa. Nitakwambia tukifika kwani kwa sasa kidogo, itafanya kazi yetu kugoma." Mubah alijitetea huku akijing'ata ng'ata bila kujua sababu ya kufanya hivyo.
"Basi sitaki unitazame tena usoni. Acha kabisa." Lisa alifoka na kumuangalia mtoto wake ambaye alikuwa anacheza kwa kumrusha mdoli fulani aliyenunuliwa na mama yake.
Mubah akaamua kutulia kama si yule wa mwanzo. Na kwa bahati mbaya au nzuri, alikuwa anajali kazi zaidi kuliko matukio yaliyompata. Akili yake yote ilijaa kisasi kuliko jambo lolote lile.
Gari ikazidi kutitia kwa mwendo wa madaha hasa kwa sababu ya barabara mbovu ya kuelekea Kivule.
"Mama, baba ananifundishaga kupiga kwa kutumia hiyo." Martina alimwambia mama yake huku akisonta kidole kwenye kiuno cha dereva wa gari lile.
Alikuwa kapachika bastola yake ambayo ilionekana vema baada ya shati lake kujivuta na hiyo ndio ikampa wasaa Martina kuongea hayo.
"Anakulengeshaga nini?" Mubah alimuuliza Martina kwa hamasa huku Lisa akiwa kama haamini kile ambacho anakisikia.
"Anakunywagwa bia, halafu ananiwekea chupa nilenge. Siku nyingine ananipeleka porini na kuniwekea mbao zikizochongwa kama watu, ananiambia niwe nawapiga kichwani au kifuani. Hao ni maadui." Mtoto Martina alizidi kutiririka bila uoga.
"Na kingine anachokufanyiaga." Mubah akatupa swali lingine.
"Ananipaga picha na kuniambia huyo ni adui yetu, nikimuona kama nina bunduki nimpige kichwani."
"Picha hiyo yupo nani?"
"Mubah muache mwanangu. Nitashuka sasa hivi. Sitaki huo ujinga kuusikia ukimuuliza mwanangu." Ikabidi Lisa amfokee Mubah kwa sababu ya maswali makavu amuulizayo mtoto wake wa pekee.
Mubah akameza mate ya hasira lakini akakaa kimya kwa sababu angeendelea, angemkosa Lisa katika mipango yao.
Kimya kikachukua nafasi yake na safari ya kwenda Kivule ndio ilikuwa inaendelea kwa wakati huo.
****
Malocha alikuwa hajui cha kufanya baada ya kuisubiri simu ya jamaa aliyemtegemea labda atapiga baada ya kusikia kuwa hata Lisa atakuwa matatizoni. Akawa amechoka kuisubiri kwa sababu jamaa hakupiga wala kubipu au kutuma meseji.
Usiku wa manane Malocha akawa analanda landa ndani ya FISSA bila kujua ni nini anatafuta au nini anataka kufanya. Mara anaenda huku mara huko ili mradi awe anatembea tu.
Mwisho wake ulikuwa ni ofisini kwake na mawazo tele yakimwandama hasa kwa sababu ya mtu wake kutopiga wala kuitikia anachokitaka.
"Ina maana Masai amekwisha sahau ahadi yetu? Kasahau kabisa kuwa nitakapomuhitaji nitamtaarifu? Lakini hilo si kitu, inamaana pia kamsahau Lisa? Kamsahau kabisa mtu aliyesema anampenda kila mara. Frank atakuwa anamatatizo huyu mtu." Malocha alijisemea peke yake muda wa saa kumi usiku.
Ama kwa hakika alikuwa kapagawa hasa kwa matendo kama kuwafukuza wafanyakazi wake wote usiku huo.
Asubuhi ya saa moja, akiwa kidogo kapitiwa na usingizi, simu ya ofisini kwake ililia kwa nguvu na kumfanya akurupuke kama mwenye kuwehuka. Alipoangalia kioo kodogo cha simu ile ya mezani, aliona ni namba ya Ikulu ndio yenye kupiga.
"It's over now. (Yameisha sasa)" Malocha aliongea hayo wakati akiiangalia simu hiyo ikiita.
"Hallow mkuu." Malocha aliita kwa sauti ya taratibu.
"Sijawahi kuona mtu mpumbavu kama wewe. Jinga la kutupwa kama mbwa lililokosa matunzo. Yaani unadiriki kufukuza wafanyakazi wote usiku kama vile shirika ni lako. Unavunja sheria za shirika kama vile umelianzisha wewe." Rais alikuwa anaongea kwa sauti ya juu kana kwamba alikuwa anaongea na mtu wa maili kadhaa mbali.
"Kwa hiyo unataka nini mkuu. Nimeshafanya." Malocha akamuuliza mkuu wake kwa nyodo.
"Unasemaje we mbwa? Dharau umezianza lini? Sasa kwa taarifa yako, nimekwisha andaa uongozi mpya. Wewe, na mbwa wenzako hao wawili, Mubarak na Lisa, wote mtakuwa nje ya FISSA. Katafuteni pa kufanyia kazi, si hapo. Sihitaji washenzi tena." Maneno hayo yakaenda sanjari na kukata simu.
Malocha akatabasamu kisha akaanza kukusanya kilicho chake kabla ya huo uongozi mpya haujafika.
****
"Usafiri uwatoao nje wafanyakazi wa FISSA ni usafiri ambao si rahisi kwa mtu wa ndani kuona nje. Na hata Malocha alipoamua kwenda kuupanda, ilikuwa ni vivyo hivyo.
Usafiri huu hutambua sauti za wafanyakazi wote wa shirika lile la siri. Na pindi wapandapo, basi hutoa sindano ndogo ambazo zinachomwa mikononi na usingizi mzito huwachukua waliopanda usafiri huu. Pia hujiendesha wenyewe kwa kuwa umetengenezwa maalumu kuwafikisha wafanyakazi wake sehemu husika.
Muda wa saa sita, Malocha tayari alikuwa amekwishakwea kwenye usafiri mwingine ambao huo ulikuwa ni wa wananchi wa kawaida. Wale wazoefu wa jiji na miji wanauita usafiri huu ni tax, na ndio Malocha alikuwa kaupanda.
"Mkuu tunaelekea wapi." Dereva mmoja mchangamfu alimuuliza mteja wake ambaye alikuwa kama katoka kulewa pombe kali usiku wa jana.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nipeleke Kivule Kamanda." Malocha alijibu na dereva yule hakujali gharama ambayo itatokea kwa sababu muonekano wa Malocha, haukuwa wa kukosa fedha ambazo atamtajia.
"Hallow Mubah." Malocha alisikika kwenye simu.
"Ndio mkuu."
"Hatuna chetu FISSA. Fanya hima tukutane Kivule ukiwa na ripoti nzima ya Lobo."
"Sawa mkuu. Rais ndio katutoa au?"
"Yaap. Ni mkuu."
"Na nani mwingine kamtoa."
"Lisa naye katolewa."
"Okay. Basi na mimi nakuja huko Kivule sasa hivi." Mubah aliongea kwa shahuku kubwa.
"Na mimi ndio nipo Posta hapa, nakuja taratibu." Malocha akamalizia kabla ya kuanza maongezi mengine ya kijamii na maisha na Mubah kupitia simu.
****
"Najua umeona hilo bomu lilivoenda na kulipua nyumba yako. Lakini sasa unatakiwa kuangalia mazingira ambayo bomu hilo limetokea. Rudisha huo mkanda nyuma na kuanza kuchunguza kimoja baada ya kingine." Sauti ya Malocha ilikuwa ikimuelekeza mtaalamu wa mmoja wa kompyuta aliyekuwa anacheza mkanda mzima ambao ulionesha tukio zima lililotokea nyumbani kwa Mubah.
Nyumba hiyo ya Kivule, ilikuwa ni nyumba moja kubwa kiasi na huwezi kujua ndani kunafanyika nini kama hujaingia na kuchunguza.
Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa kumetapakaa dhana mbalimbali za Kijasusi na kipelelezi. Bunduki za kila aina na vifaa vya kipelelezi, vilipendezesha chumba ambacho Mubah na Malocha walisimama wakiwaangalia wale jamaa wanaocheza video nzima ya tukio la Mubah.
"Hapo hapo Banchi. Umeona hilo gari jeusi?" Mubah alimsimamisha jamaa mmojawapo wa kompyuta na kumuonesha gari ambalo alilishuku vibaya.
"Hilo ndilo nililiona wakati nazimia. Naomba ulichunguze."
"Kama ndio hilo, basi tutaanzia kazi zetu hapo. Cha msingi tupate namba za usajili za gari hili (plate number)." Malocha aliongea huku kafumbata mikono yake kifuani.
"Namba hizi hapa mkuu. Ni T 900 QJG." Opareta wa kompyuta zile, alitoa taarifa hizo na kuwafanya Mubah na Malocha kusogea kwa karibu na kuzitazma.
"Okay. Safi Banchi. Sasa Mubah, hapa tunamuhitaji sana Lisa kwa sababu yeye ni mwanamke awezaye kuwavuta watu wowote na wakafungua vinywa vyao kusema siri. Cha msingi, mpigie simu sasa hivi mwambie muonane Kitunda. Halafu mkikutana, mpe hii hapa simu halafu ndio mje huku." Malocha alimpa maelekezo ambayo Mubah alikuwa anatikisa kichwa kukubaliana nayo.
"Sasa kwa nini unampa simu hii?" Mubah akamuuliza Malocha.
"Lisa yupo hatarini bila yeye kujitambua. Mume wake si mtu kama anavyodhani, muda wowote anamgeuka. Huyo ndio sababu ya Lobo kujua njia nyingi za FISSA kwa sababu anamuwekea GPS kila anapojua zimetolewa. Nakwambia haya lakini usimwambie chochote kile. Atakuja kuju a ya kumaliza mambo haya." Malocha alimuelekeza Mubah mambo kadhaa, kisha kuanza kumpa siri za Lisa ambaye alikuwa anacheza na mwanaye anayesheherekea siku yake ya kuzaliwa.
"Kwa hiyo mume wa Lisa anashirikiana na Lobo."
"Hilo ndilo jibu." Malocha akamjibu kifupi na kumuacha Mubah bila swali na badala yake akatwaa simu yake na kubofya namba kadhaa ambazo alimpigia simu Lisa.
****
Ukimya ulitawala ndani ya gari alilochukua Mubah kwenda Kivule yalipo makao mapya ya FISSA ndogo ikiongozwa na Malocha. Ukimya huo ni kwa sababu Lisa alichimba mkwara ambao Mubah alikubali yaishe kuliko kuzidi kuchongoa mdomo wake.
Baada ya dakika kadhaa, walikuwa wamekwishafika kwenye nyumba hiyo ambayo wanaitumia kama makazi yao.
"Heee! Malocha leo upo huku." Lisa akamuita mkuu wake jina ambalo walishazoeana kuitana shuleni.
"Leo nimekuja kuwatembelea aisee." Malocha akajibu huku anatabasamu.
"Mmmh! Haya karibu." Lisa aliongea kwa sauti ya furaha huku akisogea kwenye kochi lililo sebuleni pale walipofikia.
"Hey. Martina, hujambo mama." Malocha akamsalimia Martina mtoto wa Lisa.
"Sijambo shikamoo."
"Marahabaa. Mimi ni Anko Malocha."
"Shikamoo Anko Malocha."
"Leo sherehe yako ya kuzaliwa. Nikupe zawadi nisikupeee." Malocha alimuuliza kwa furaha Martina.
"Nipee Ankoo." Martina naye akajibu huku mikono yake akiipunga kama vile kaungua. Malocha akatabasamu baada ya kumuona mtoto mwenye furaha kiasi kile.
Akaenda chumba fulani kisha akatoka na baiskeli moja ya rangi ya pinki, rangi ambayo hakuna watoto wa kike wasiyoipenda.
"Asante Anko." Martina alimshukuru Malocha na kumkumbatia kwa nguvu.
"Haya Martina. Nenda na yule pale mkaendeshe baiskeli huko." Malocha alimkabidhi Martina kwa jamaa mmoja ambaye alimchukua Martina na kumpeleka uwani mwa nyumba ile walipoanza kufurahia zawadi hiyo.
"Okay Lisa. Nimekuita hapa kukwambia kuwa FISSA tumefukuzwa kazi lakini tutarudi baada ya mambo fulani kukamilika. FISSA sasa hivi wameingia watu wapya lakini ni watu ambao kwangu mimi siwapi sana nafasi." Malocha akaweka tuo kabla ya kuzidi kutiririka.
"Sasa kwa kuanzia, tuanze na kazi ya kuutafuta ukweli kuhusu Lobo. Ila kwanza nataka kusikia kama upo tayari kufanya kazi na sisi." Malocha akatupa swali kabla hajaendelea na mengine.
"Nimezaliwa kufanya hayo. Siwezi kukataa na wakati huyo ndiye mimi." Lisa akajibu kwa kujiamini na Malocha akamchukua mwanadada huyu jasiri na kwenda naye kwenye chumba maalumu kwa ajili ya upelelezi. Wakati huo Mubah alikuwa kimya akiwafuata wafanyakazi wenzake kwa nyuma.
"Kazi yetu inaanzia hapa." Malocha akamuonesha gari ambalo waliling'amua namba zake.
Maelezo kadhaa yakaanza baada ya kumuonesha gari lile. Hiyo yote ni katika kumuelekeza Lisa ili aelewe nini sababu ya kuoneshwa picha hiyo.
"Sasa tumekwisha fatilia gari hili ni la nani na ninataka wewe na Mubah muongozane hadi kwa huyu bwana kisha mumuhoji maswali kadhaa. Kama hatojibu, basi tumieni mbinu za kumchukua na kumleta huku. Atajibu tu." Malocha akamaliza maongezi yale na kuwatazama watu wale.
"Hamna tatizo. Ila naomba mkae na Martina vizuri." Lisa akatoa ombi na.kuchukua dhana kadhaa kwa ajili ya kujilinda na kujijulisha (vitambulisho).
Baada ya hapo akatoka nje na kuwaacha Mubah na Malocha wakiwa na opareta wao wakijadiliana.
"Mkuu. Wakati nazimia nilikwambia nimemuona mtu kwenye hii gari. Mtu huyo ni Gunner, mume wa Lisa. Kitu kilichonifanya nijue ni kibanio cha Martina ambacho ni sawa na kile ambacho kilimwaga sumu kule nyumbani. Na mbaya zaidi, huyu mtoto anafundishwa ujasusi na baba yake." Mubah akatoa taarifa kadha wa kadha hadi pale aliporidhika ndipo alipoamua kutoka nje akiongozana na Malocha.
"Hicho kibanio lazima kibaki ili nacho tujue ni wapi kimetoka." Malocha aliongea huku wakiendelea kwenda sehemu nyingine.
"Sawa mkuu. Ngoja sisi twende." Mubah alikubali wakati alipofika sebuleni na kumuona Lisa akiwa anawasubiri.
"Umemuaga kijana wetu." Malocha alimuiliza Lisa kama kamuaga Martina.
"Ndio. Naona hana tatizo. Yupo na furaha." Lisa akajibu huku akinyanyuka ambapo alitoka nje na kukwea gari ambalo wameandaliwa kwa ajili ya kwenda walipopanga.
****
Majira ya saa moja jioni, Mubah, Lisa wakiwa na dereva wao, walifika eneo la Sinza na moja kwa moja wakaenda nyumba ambayo walipata maelezo kuwa mtuhumiwa wao anapatikana. Lakini cha kushangaza walipofika, walikuta watu wamefurika na vilio vikisikika huku na kule.
Walisogea na kuuliza kuna nini, wakajibiwa kuwa Mzee Mofo, ambaye ndiye walimfuata amefariki dunia kwa kuchinjwa kama kuku.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa ni hadithi ya kusikitisha kwenye kila kichwa cha aliyeisikia, lakini hakuna ambaye alikuwa tayari kuingilia hayo maswala kwa kuwashuku watu fulani.
"Lisa tunafanyaje sasa. Doa limeshaingia kwenye nguo nyeupe kama uonavyo." Mubah alimuuliza Lisa baada ya kufuata watu kadhaa na watu hao kutotoa ushirikiano wowote katika kujibu.
"Mambo magumu hapa Mubah. Ila tujitahidi tuonane na mke wake kabla hawajaenda mazikoni hiyo kesho." Lisa alishauri huku macho yakiwa yametua mbele ya mwanamke mmoja, mnene kiasi na mwenye weupe wa asili.
Alikuwa katika majonzi mazito na baadhi ya wanawake wenzake walikuwa pembeni yake wakimpooza kwa kila neno zuri.
Mara kwa mara alijigonga kifua na kuwa mtu wa kulalamika kwa lugha ya Kidigo.
"Sawa sawa. Yaonekana kuna jambo analalamika kwa sababu ya kifo cha mumewe. Ikibidi tumtoe pale sasa hivi tukamuhoji pembeni." Mubah alishauri kitu ambacho Lisa hakukawia kukifanya.
Akasonga hadi pale ambapo yule mwanamke anapolia, na kisha kwa chati akamuomba watoke eneo lile mara moja wakazungumze.
Ilikuwa ngumu kwa mwanadada yule kukubali, lakini baada ya Lisa kujitambulisha vema, hatimaye mwanamke yule alikubali na kwenda naye katika chumba ambacho aliona ni sawa kwa kumpasha yote yaliyojiri.
"Sijui dada yangu. Roho inaniuma sana kumpoteza mume wangu. Ila yote hiyo ni kwa sababu ya upinzani wa kibiashara tu. Wameniulia mume wangu ofisini kwake, na kisha kwenye ukuta ule wameandika Duka La Roho." Ni maneno ya yule mwanamke akijaribu kuelezea kilichokuwa kinaendelea mbele ya Lisa, wakati huo Mubah alikuwa nje.
"Ofisi yake ipo wapi."
"Zipo Ukonga, Madafu."
"Okay. Ngoja twende huko tukaangalie taarifa yoyote. Naomba funguo za huko na kibali pia." Lisa aliongea na yule dada, kisha akamuacha atafute alichokihitaji.
Baada ya sekunde kadhaa, mke wa Mofo alikuwa amekamata funguo za ofisi zile za akiba na karatasi moja ambayo itasimama kama kibali.
Lisa akapokea vitu hivyo na kisha akataka kutoka mle ndani. Lakini ni kama Mke wa Mofo alikuwa kasahau jambo, akamuita huku akiwa na uoga mkubwa machoni pake.
"Dada. Maisha yangu pia yapo matatani kwa sababu ya mume wangu. Roho yangu pia ipo dukani. Njia ya kuinunua ni kutosema ukweli juu ya hili jambo. Lakini siwezi nikakaa na siri hii kwa sababu tayari mume wangu si naye tena. Naomba nikwambie wewe." Mke wa Mofo alikuwa akiangalia huku na huko wakati akitamka haya.
"Eheee! Niambie dada yangu." Lisa akasogea karibu na kumshika mkono na kumkalisha kwenye kitanda cha chumba kile.
"Mume wangu alikuwa anauza madawa ya kulevya na ni mshirika mkubwa wa makundi haya makubwa ya kuuza madawa. Watu kama Mafia, Yakuza nakadhalika, alishirikiana nao sana. Baada ya kuona kapata mafanikio, akaomba kujitoa kundini ili aendeshe maisha yake kiuhalali. Kitendo hicho kilimpa machaguo mawili. Kama anataka kujitoa basi auze roho yake au anunue. Yaani angetaka kununua roho yake, akubali kufirisiwa. Angetaka kuuza, basi afe lakini mali zitabaki chini ya familia yako. Wakampa siku mbili ya kununua au kuuza.
Mume wangu akadhani ni utani na hakuna ambaye ataweza kumuua. Akajidhatiti na kuweka walinzi nyumbani na popote alipokuwapo. Siku ya pili inatimia tu! Mume wangu akauawa na maiti kukutwa ofisini huku mwili umekaa kwenye kochi na kichwa kimewekwa juu ya meza." Mke wa Mofo alimaliza maelezo kadhaa anayoyajua.
"Hiyo kampuni ni yake kweli?" Lisa akatupa swali lingine na kumfanya yule dada kuzidi kuwa na mashaka. Ila kwa kuwa aliyavulia maji nguo, basi kuyaoga ni njia inayofuata.
"Si ya kwake. Na ndio ofisi kubwa ya kusambaza madawa nchini Tanzania." Akajibu dada wa watu.
"Sasa ipo chini ya nani?" Mke wa Mofo akaangalia tena pande kadha wa kadha ijapokuwa chumba kile walikuwamo wawili tu.
Akasogea karibu zaidi kwa Lisa na kwa sauti ya chini akaanza kujibu.
"Ipo chini ya tajiri mmoja Mkam......" Kimya kikamkumba dada yule. Hakumaliza sentensi yake. Lisa alipomuangalia mwanamke mwenzake, alimshuhudia akidondoka kitandani kama mzigo huku damu zikimvuja kichwani palipokuwa pana tobo la risasi. Ukuta nao ulikuwa umechafuka kwa damu hizo.
Yote hayo yalitokea saa mbili usiku. Kwa bastola ambayo imefungwa kifaa cha kuzuia mlio wa risasi, ikamtoa uhai mke wa Mofo.
Lisa akatazama huku na huko lakini hakuona chanzo cha risasi ile.
Akajaribu kwenda dirishani, ndipo alipoona dirisha limefunguliwa kidogo. Yeye akafungua lote na kisha akapita hapo kwa sababu kulikuwa hakuna kizuizi kikubwa cha yeye kutopita.
Alipotoka alikutana na teke zito la uso. Hajakaa sawa kiakili, akakutana tena na ngumi ya uso iliyomrudisha nyuma zaidi kimawazo. Hadi anakuja kutulia na kukaa sawa, tayari alishapokea kipigo cha maana toka kwa mtu ambaye hakumuona.
Alisikia vishindo vya kukimbia ndipo naye akajaribu kukimbia wakati huo lile eneo la nyuma kulikuwa hamna watu.
Katika kukimbia, alimuona mtu yule akimalizia kuruka geti kubwa la nyumba ile. Hapo Lisa ndipo alipoamini kuwa alikuwa hapamabani na 'kinyangala mafuta' bali chatu mwenyewe.
Naye akajitahidi kuruka na kutua nje. Akakuta mtu wake anahangaika kuwasha pikipiki aliyokuja nayo, huo ndio ukawa upenyo pekee wa Lisa kujitambulisha katika nyanja za mapigano.
Teke zito la kifuani likamkuta yule mtu na kumrusha nyuma ya pikipiki ile. Kabla hajanyanyuka, Lisa akateleza chinichini na kumkung'uta teke lingine la uso. Adui wa Lisa akadhani yataishia hapo, kumbe mwenzake ndio kwanza anayaanza.
Sarakasi mbili za kujibetua kwenda nyuma, zikapigwa na Lisa, kisha akamaliza kwa kujitupa kwenye tumbo la adui yule. Hapo akasikia sauti kali ikitoka kwenye kinywa cha mtu yule.
"Kumbe ni mwanamke." Lisa akajikuta akiropoka baada ya sauti ile. Kwa mavazi ya kininja aliyovaa mtu yule, ni ngumu kujua anajinsia gani. Baada ya kipigo akajitambulisha kwa mlio huo wa kike.
Lisa akajisahau kidogo na huo ndio uliokuwa wasaa wa yule adui kupitisha miguu yake shingoni kwa Lisa na kisha kumkaba kwa nguvu bila kumuachia. Kila Lisa alipojaribu kufurukuta, hakuchomoka na badala yake, roba ikawa inazidi kumbana hadi akasaliti amri kwa kuzimia palepale.
Hapo yule Mwanamke ninja, akawahi pikipiki yake na kuipa kiki ya nguvu, nayo ikakubali sheria. Mwendo wa ajabu ukachukua nafasi yake baada ya kuwaka. Akaondoka eneo hilo huku akimuacha Lisa hana fahamu.
****
"Lisa, Lisa, Lisa." Sauti ya mwangwi ilisikika kwenye kichwa cha Lisa. Akajaribu kufumbua macho na kuona nani anamuita.
Ilikuwa ngumu kwake kurudiwa na fikra zake lakini alijitahidi na kufanikiwa kufungua milango yake ya fahamu.
Sura za rafiki au wafanyakazi wenzake aliziona zikiwa zinamtazama. Akatulia dakika kama tatu kisha akafyonza baada ya kukumbuka tukio zima lililotokea nyumbani kwa Mzee Rofo.
"Mbwa yule ni kweli hayupo peke yake. Leo nimepambana na mwanamke mwingine." Lisa aliongea huku akinyanyuka kwenye kitanda ambacho alikuwa kalazwa.
Ni katika nyumba ileile ya Kivule ndipo aliporudishwa tena.
"Vipi hali yako lakini?" Malocha alimuuliza Lisa.
"Nitakuwa vizuri. Martina yupo wapi?" Lisa akamkumbuka mwanaye.
"Yupo chumba cha mapumziko kalala." Akajibiwa.
"Kwani sasa hivi saa ngapi?"
"Ni saa nne hii."
"Oooh! Mungu wangu. Sijui mume wangu atakuaje."
"Usijali tumempa taarifa kuwa upo kwetu na utarudi kesho."
Lisa akapumua pumzi ya ahueni kisha akatulia kitandani na kuanza kusimulia mkasa mzima ambao ulimtokea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Daah! Hawa watu si wa kuchezea kabisa. Wapo vema kila idara. Hapa cha msingi ni kujitahidi kucheza na silaha." Mubah alitoa ushauri kabla hawajamuacha Lisa peke yake mle chumbani.
"Sasa kama ulivyoona, tumepoteza chanzo kingine. Hapa tumebaki na hicho kibanio tu! Tumejaribu kufuatilia vinapotoka, tumegundua ni Malyasia. Huko itabidi uende peke yako Mubah." Malocha alikuwa akimpa mchakato mwingine wa kufanya Mubah.
"Mmmh! Mkuu, kwa nini tusimwambie ukweli Lisa ili tushirikiane naye kupambana? Wajua siwezi peke yangu. Tumwambie tu ukweli." Mubah alitoa ushauri ambao Malocha aliinamisha kichwa chake chini kabla hajatoa maamuzi.
"Wajua ni ngumu sana. Halafu maisha ya Lisa tutayaweka matatani zaidi." Malocha akatoa jibu.
"Lakini hata hivyo siku akijua tayari maisha yake yatakuwa hatarini." Mubah aliweka neno ambalo nalo halikuwa baya.
"Okay. Tutamwambia. Lakini siyo leo wala kesho. Hiyo ni kwa usalama wa.mwanaye zaidi." Malocha aliongea.
"Kwani mtoto naye ana nini. Mtoto wao halafu wamdhuru?" Mubah akapatwa na mshangao.
Malocha akamsogelea Mubah pale alipo kisha akaanza kwa kumgonga gonga bega.
"Jambo usilolijua, ni sawa na usiku wa kiza. Tuyaache hayo, nishatoa neno na litimizwe. Utaenda Malyasia." Malocha akamaliza.
"Sitaenda kama huwezi kumwambia ukweli Lisa. Lisa yapaswa aambiwe ukweli." Mubah alimfata mkuu wake na kumwambia maneno hayo kwa msisitizo.
"Mnataka kunificha nini?" Lisa akatokea na kuwauliza Malocha na Mubah huku akiwaangalia kwa zamu.
"Mnataka kunifanya na mimi ni mtoto mdogo? Niambieni mlicho kificha. Yawezekana hata yule mtu aliyemuua mke wa Rofo mlinitegea nyie. Tangu natoka pale Kitunda, huyu alikuwa ananiangalia kwa mashaka. Sasa nataka mniambie ukweli sasa hivi." Lisa akaweka mkazo kwenye akitakacho huku sauti yake ikiwa katika hasira.
"Lisa tulia. Kila kitu kitakuwa sawa. Na kila....." Hakumaliza kauli Malocha, ikawa imekatwa na Lisa.
"Sitaki maelezo ya kipumbavu kama hayo. Nataka muwe straight katika majibu nayoyataka. Nini mnanificha?"
"Mume wako anashirikiana na Lobo." Malocha akamwambia Lisa na kuondoka lile eneo huku akiwa kakunja sura yake.
Akabaki Mubah ambaye alikuwa akimtazama Lisa aliyekuwa katika mkanganyiko wa hali ya juu baada ya maneno yale.
"Haiwezekani." Lisa akatamka hayo huku taratibu akishuka na kujikuta akikaa chini.
"Ni kweli Lisa. Na ndiye niliyemuona mara ya mwisho kabla sijazimia ile juzi wakati nyumba yangu inalipuliwa." Mubah alichomelea ukweli ambao anaujua.
"Na hata hicho kibanio cha mwanao, kinafanana na kile ambacho kilitema sumu na kuua wenzetu kule nyumbani. Na yewezekana yule mtu uliyepambana naye, kakuacha sababu ya ukaribu wako na Gunner." Mubah akamaliza huku naye akienda na kukaa pale alipokaa Lisa.
"Yawezekana ile picha ya Martina aliyonionesha Lobo wakati tumemkamata, kampa yeye Gunner. Kama kampa yeye, basi tayari anajua siri nyingi sana zituhusuzo." Lisa akaamua kufunguka.
"Ni kweli. Kakuwekea GPS katika mifuko yako mingi unayokuja nayo kazini. GPS hizo ni ngumu kujulikana pale unapokaguliwa na vifaa vya FISSA kwani GPS hizo ni za plastiki na hazitumii aina yoyote ya umeme." Mubah akamtobolea ukweli uliokuwa mgumu kuamini kwa yeyote mwenye mapenzi.
"Okay. Sasa naanza kupata picha kwa nini anamfundisha Martina kutumia silaha. Mjinga sana yule, kesho naenda
kumuua." Lisa aliongea kwa kiapo na kunyanyua uso wake ambapo alikutana na uso wa Malocha ukiwa unamtazama kwa makini.
"Lisa. Hata ukipewa miaka ishirini ya kumuua Gunner, hutoweza. Yule umuonavyo, sivyo alivyo. Ni heri ukutane na treni ya umeme relini, kuliko kukutana na uso halisi wa yule mtu. Tutakupoteza dakika sifuri tu." Malocha alimtahadharisha Lisa kwa maneno machache.
"Sasa nifanyaje?" Lisa alimuuliza Malocha.
"Cha msingi ni wewe kutulia hapa. Hatofika mtu hapa. Au kama waweza, rudi kwako na kujifanya hujui lolote. Na kingine, mtoto wako anafundishwa kulenga huku akioneshwa picha ya Frank." Malocha akamaliza na kuelekea chumba kilichokuwa na mitambo ya kipelelezi.
Akamuacha Lisa akiwa kakodoa macho asijue ni nini afanye kwa wakati ule. Mubah naye akanyanyuka na kuondoka eneo lile akiwa na amani kiasi baada ya Lisa kuugundua ukweli.
****
Kesho yake asubuhi, Lisa alikuwa wa kwanza kuamka na kumtazama mwanaye kama kaamka. Alipomuona hajaamka, akatwaa simu yake ambayo alibadilishiwa na wakina Mubah, kisha akampigia mumewe.
"Nakuja asubuhi hii Gunner. Naomba nikukute." Lisa aliongea na upande wa pili ukamjibu.
Akamuamsha mtoto wake na kumuuliza maswali ambayo alikuwa anayauliza Mubah kwenye gari.
"Hiyo picha ambayo anakuonesha, yupoje huyo mtu." Swali mojawapo la Lisa kwenda kwa Martina.
"Mweusi hivi, mrefu kiasi halafu ananywele za kung'aa na nyeusi." Martina alimjibu Lisa majibu ambayo yalimfanya apumue kwa shida.
"Okay. Basi twende nyumbani kwa baba eeeh. Leo tutamuaga na kuja kukaa huku. Si ndio eeh." Lisa akamwambia mwanaye huku akijitahidi kuchongesha tabasamu.
"Haya mama." Martina alijibu kwa furaha hasa kwa sababu atakuwa karibu na mama yake kuliko kipindi chochote cha maisha yake.
****
"Nitakuwa nyumbani tu leo, sitaondoka kabisa." Lisa alikuwa anamwambia Gunner huku akiwa katabasamu kana kwamba hajui kitu.
Alishaondoka Kivule na sasa alikuwa uso kwa uso akitazamana na Gunner.
"Okay. Basi mimi naelekea ofisini. Nitarudi usiku leo." Gunner aliongea na kumpa busu dogo mke wake. Akatoka nje na kuondoka.
BAADA YA SAA MOJA.
Lisa alikuwa akitupia nguo zake haraka haraka kwenye begi lake kwa lengo la kuondoka katika nyumba ile. Akafanikiwa hilo na hata kuandika ujumbe ambao atauacha mezani baada ya kuondoka.
Akanyanyua begi lake tayari kwa kutoka nje ya chumba chake. Akatoka na kuanza kuelekea sebuleni huku akiita jina la Martina.
"Una safari mke wangu." Macho ya Lisa hayakuamini pale alipomkuta Gunner kakaa sebuleni na Martina ambaye alikuwa hana habari wala kuhisi kitu kibaya.
Lisa akashindwa kujitetea na badala yake akawa anatetemeka huku akimuangalia mwanaye ambaye Gunner alikuwa akizilaza nywele zake kwa taratibu.
Gunner akanyanyuka pale kochini na kumfuata Lisa kisha akampora karatasi aliyokuwa kaikamata. Ni ujumbe ambao alikuwa kauandika Lisa na alitaka kuuacha mezani kabla hajaondoka.
"Kwa hiyo umekwisha nifahamu. Safi sana. Ndivyo mpelelezi unavotakiwa kuwa." Gunner aliongea hayo baada ya kuusoma ule ujumbe.
Hakuishia hapo yule mwanaume, akaongea kwenye kinasa sauti alichokuwa kakivaa na baada ya dakika mbili akaingia msichana ambaye Martina alipomuona alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha akimuita mama mdogo.
Lisa alikuwa katoa macho asiamini kile anachokiona mbele yake. Ni mzimu au nini?
"Huyu ndiye ulikuwa ukipambana naye jana Lisa." Gunner aliongea kwa utaratibu kama kawaida yake.
"Zakia!?" Lisa akaita kwa mshangao asiamini kile akionacho.
"Ndiye mimi Lisa. Mchumba wa Mubarak. Prince Mubarak au Mubah." Mtu aliyeitwa Zakia alijibu kwa nyodo nyingi huku akimpapasa Martina kwa upendo.
"Kweli jambo usilolijua, ni sawa na usiku wa kiza. Malocha aliongea haya hapo jana." Lisa akajikuta akiropoka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kuna muda unatakiwa kutambua kuwa hakuna siri inayodumu katika moyo wa mtu. Ukikuta siri imedumu baina yenu wawili, basi ujue ipo karibuni kuvunjika.
Umenificha jambo dogo sana Lisa. Na kila siku nilikuwa nasubiri ulitamke, lakini ulishindwa kuniambia. Sijui ni mke wa aina gani wewe." Gunner alikuwa anaongea kwa makini hasa akitaka Martina asiyasikie yale maongezi."Baada ya kujua kuwa sina uwezo wa kuzalisha, nikatafuta ukweli juu ya hiki kijimtu nachokilea. Kishetani kipya, kidogo-dogo." Gunner alinyoosha kidole kwa Martina wakati anaropoka maneno haya.
"Usimuite mwanangu hayo majina we' mshenzi mkubwa." Lisa naye kwa umakini alijikuta akimkaripia Gunner.
"Nikafatilia kwa makini sana kuhusu hiki kishetani, ni cha nani? Ndipo nikapekua vitu vyako na kukuta ile picha aliyokuonesha Kamanda Lobo. Hapo ndipo nikajua kishetani baba yake ni yule mbwa muoga. Mbwa anayeogopa kurudi nchini kwao na kulowea nchi za watu. A coward." Lisa alijikuta akijawa na hasira na kurusha mkono wake lakini Gunner aliudaka vema na kumkamata Lisa kiuno wakawa kama wachezao nyimbo za taratibu.
"Baada ya kugundua kuwa ni mtoto wa yule muoga au mzamiaji, nikaamua kuutafuta ukweli zaidi. Nikamfuata baba yako na kumuuliza kuhusu hali ile." Gunner alikuwa akiongea taratibu huku bado kamkamata Lisa kiuno na kucheza naye blues.
"Jinsi baba yako alivyokuwa mjinga, akaanza kuniomba msamaha kama vile mimi ni MUNGU. Lakini kwa bahati mbaya, alinikuta si mimi yule niwezaye kucheka kama katuni. Akanikuta ni Gunner mwingine kabisa. Kwa hii mikono yangu." Gunner akamuachia Lisa na kukunja mikono yake hadi misuli kadhaa ikatutumka na kumuonesha ukubwa wa mwili wake."Nikamnyonga baba yako hadi akafa hapo hapo. Hiyo ndiyo ikawa ahueni kwangu Lisa, nikapunguza hasira zangu kihivyo." Gunner alimaliza akiwa na tabasamu pana kana kwamba kile akiongeacho ni kitamu sana kukimeza.
"Martina. Nenda na mama mdogo kule nyumba nyingine, mimi nitakuja na mama eeh."Gunner alimwambia Martina ambaye hakupinga lolote bali kujawa na furaha hasa kwa kuwa huko kuna raha na starehe za kila aina kwa watoto.
"Bayi mama." Martina alimuaga mama yake huku akiwa na furaha tele.
"Muage mtoto wako Lisa." Gunner akamnong'oneza Lisa lakini Lisa hakufanya chochote zaidi ya kupumua kwa kasi kutokana na hasira zilizojishindilia akilini mwake.
"Kama hutaki, basi. Muache aende." Lisa akashuhudia mwanaye anaondoka bila kuaga.
"We mshenzi kumbe ndiye uliyemuua baba yangu." Lisa akamsukuma Gunner aliyekuwa akicheka kwa nyodo kutokana na hali ambayo Lisa alikuwa nayo.
"Tena baada ya kumuua, tukavumisha kiharusi ndicho kilichombeba yule Mmarekani. Pesa tu." Gunner akazidi kumjaza hasira Lisa.
Lisa akaanza kumpiga ngumi nyingi kila mahali mwanaume yule lakini ngumi zile zilikuwa kama kumpiga mwizi kwa ndala, hazimuumizi.
Lisa akajikuta akiishiwa nguvu sababu ya hasira na hizo ngumi alizokuwa anazitupa.
"Umemaliza wife?" Gunner aliuliza huku akiwa anatabasamu pana usoni pake. "Okay. Sasa ni muda wa wewe kwenda kumsalimu baba yako huko kuzimu. Nadhani kakumiss sana." Gunner akaongeza huku akianza kumufata taratibu Lisa ambaye naye alianza kusogea nyuma huku akitetemeka na maneno ya Malocha yakamrudia kichwani kuwa ni heri akutane na treni ya umeme relini kuliko kukutana na sura halisi ya Gunner.
Mwisho wa safari ya Lisa ilikuwa ni kugota ukutani ambapo alishindwa kwenda zaidi nyuma.
"Midomo yako, ni midomo ambayo nilienjoy sana pale nilipokuwa nainyonya. Ni milaini na inatoa sauti mororo pale inapokutana na kitu kitamu. Mmmh! You're so sweet my sweet Lisa." Maneno hayo yaliongozana na mkono wa kuume wa Gunner kushika midomo hiyo mwanana ya kiumbe Lisa.
Hakuishia hapo, akashuka hadi kifuani na kuanza kuminya matiti murua na yenye mvuto aliyobarikiwa kuumbwa nayo Lisa.
"Hapa ndipo ubovu wangu ulipo, always nilijihisi mwenye bahati kula mbivu kama hizi. Hakika zilinipeleka katika sayari nyingine ya mahaba. Kama usingekuwa na kosa hili ulilolifanya, ningeendelea kula kifua hiki mwanana." Akatoka kifuani Gunner na kuhamia katika kiuno chembamba na kilichojichimbia ndani kiasi na kisha kuibuka tena kwa chini kwa shepu matata.
"Oooh Lisa. Unanichanganya na hichi kiuno chako hasa pale kinapozunguka katika maumbile yangu. Ulinichanganya kwa kila hila we' mwanamke. Kiuno chako hakifiki kwa yule Waziri malaya wa Wanawake. Alikuwa anajitahidi sana kukilandisha, lakini ni kama kabanwa na plaizi ya kiuno. Kiuno kigumu kama kinu." Gunner akacheka sana kutokana na maneno hayo. Akaendelea,
"Najua utashangaa, lakini ndivyo ilivyo. Nilikuwa nachepuka naye mara kwa mara kwa sababu ya miradi anayomiliki. Lakini alifanya kosa moja tu! Ndilo lilimpeleka kaburini mpumbavu yule.
Sijui alitumwa na nani kunichunguza. Akakosea akagusa pasipogusika. Nikampa roho yake Lobo. Na Lobo hafanyi makosa, akampa masaa. Akashindwa kutimiza kuachia madaraka na kuondoka nchini. Roho yake ikawa yetu baada ya kushindwa kuinunua." Gunner alizidi kumtisha Lisa ambaye alikuwa anatetemeka kama mwenye ugonjwa wa tetenasi.
Gunner akazidi kushuka chini ya mwili wa Lisa. Akafika kwenye kitovu chake na kuanza kukifikicha kwa chati na kumfanya Lisa azidi kutetemeka lakini kwa kujisikilizia.
Gunner akaenda mbali zaidi na kuingiza mkono wake ndani ya sketi matata aliyovaa Lisa. Akaanza kuukita mkono wake ndani zaidi.
Kwa mwanamke anayejiheshimu na kujitambua, hiyo ni dharau isiyo na kifani. Na Lisa alitambua hilo. Kwa nguvu zake zote, akazitumia kumsukuma Gunner kutoka kwenye maungo yake.
Gunner kweli aliyumba na ilikuwa kidogo adondoke.
Wakati Gunner akitafuta balansi kutokana na ule msukumo, Lisa tayari alishajiachia kwa kuruka juu kidogo akiwa tayari kwa kumpa pigo la teke Gunner. Lakini bahati haikuwa yake, Gunner tayari alishamuona na teke la Lisa lilidakwa kiustadi na kisha akamrusha juu mwanamke yule ambaye naye alikubali hali ile. Mwisho wake ulikuwa ni kutua kwenye meza ya kioo iliyokuwapo sebuleni mle, ikavunjika vipande vipande.
Gunner tayari alikuwa kajaa gesi ya hasira. Akamfuata Lisa pale chini na kuanza kumpa kipigo cha haja. Ngumi zisizo na idadi zilipigwa katika uso wa Lisa. Gunner hakuishia hapo, akazidi kumsulubu yule mtoto wa kike.
Akamuinua na kumkwida blazia yake aliyokuwa kaivaa.
Ngumi nyingi za tumbo zikaanza kupigwa kwenda kwa Lisa. Mtoto wa kike akawa anakohoa pumzi nyingi zisizo na idadi. Akalegea na kuwa tayari kwa kifo au kwa lolote toka kwa Gunner.
"Nilikuwa naisubiri siku hii kwa hamu. Sasa imetimia. Nakuua kama nilivyomuua baba yako." Gunner aliongea hayo huku kamsukuma Lisa ukutani na kumkabia hapohapo hadi macho ya Lisa yakawa yanageuka na kuwa meupe. Hakika mwisho wa Lisa ulikuwa umewadia.
Ilikuwa ni kama ndoto ambayo Lisa alikuwa anaiota kila wakati ili itokee. Kama ni sala, basi yawezekana MUNGU aliijibu haraka kuliko sala zake zote ambazo kawahi kuzisali.
Gunner akiwa katika hatua za mwisho kummaliza Lisa kwa roba nzito aliyokuwa kamkaba, alishituka mlango wake ukifunguliwa na kabla hajakaa sawa alikutana na teke zito la kuzunguka kutoka kwa mvamizi huyo. Akiwa anayumbayumba kama mlevi, wakati huo kamuachia Lisa aliyekuwa anagaa gaa chini akikohoa kutokana na roba ya mumewe, akapokea teke lingine la kifuani na kumrusha hadi kwenye kochi lake. Akili ilikuwa haijakaa sawa kabisa kichwani kwa Gunner. Akijitahidi kuiweka sawa, anakutana na makonde mazito toka kwa mvamizi wake. Gunner ikabidi asaliti amri na kutulia pale kwenye kochi.
Na hiyo ndiyo ilikuwa pona yake. Yule mvamizi akaenda hadi kwa Lisa na kumuinua kwa kumkalisha katika sakafu ya sebule lao.
"Hahahaaa. Malocha Malingumu. Naona unajitahidi kuwalinda watu wako. Safi sana tena sana. Lakini kuna jambo moja ambalo hauwezi kutuzuia, Jumamosi hii, Rais wa Urusi tunamuangamiza. Itakuwa raha sana." Gunner aliongea huku meno yake yakiwa yamejaa damu
"Hayo hayatuhusu tena. Ni kazi ya watu wengine. Go to hell Gunner." Malocha akampiga teke la kisogoni Gunner na hapohapo fahamu za yule bwana zikamtoka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Malocha haraka akamnyanyua Lisa na kuanza kutoka naye nje. Akaenda upande mwingine wa gari lake na kumpakiza Lisa aliyekuwa bado hajarudiwa na nguvu zake kama kawaida. Akampakiza nafasi ya mbele karibu na dereva kisha yeye akazunguka upande wa dereva na kutaka kuingia kwa ajili ya kuondoka. Lakini ni kama aliyekuwa kasahau kitu, akatoka haraka garini na kutaka kwenda ndani kwa Gunner ili amchukue.
Lakini kabla hajafanya hayo, yaani hata hajafunga mlango wa gari lake, ilitokea pikipiki moja kubwa kiasi na mtu ambaye alikuwa kavalia kofia maalumu ya kuendeshea pikipiki, alitoa bunduki aina ya SMG na kuanza 'kumwaga njugu' kwenda kwenye gari la Malocha. Zaidi alikuwa anavamia upande wa Lisa ambaye aliingia chini ya uvungu baada ya kuona hali ile.
Malocha naye alichutama huku akiwa makini kutokana na risasi ambazo zilikuwa zinamwagwa bila mpangilio.
Baada ya sekunde kadhaa ya patashika kutoka kwa yule mtu mwenye pikipiki, risasi zikamuishia na alikuwa anaikoki tena kwa ajili ya kuendeleza 'tifu' alilolianza. Lakini kitendo cha kumaliza risasi, kikawa ni nafasi kubwa kwa Malocha ambaye alitoka eneo alilokuwa kajificha na kwa haraka akapanda juu ya boneti ya gari lake, na kwa ustaha wa ajabu, akaruka huku katanguliza mguu. Na mguu huo ukamkuta yule mwenye pikipiki na kumrusha pembeni ya pikipiki yake huku bunduki yake akiitupa pembeni kabisa na yeye.
Wakati anajiuliza akiwa chini, Malocha alishafika na kumtwanga teke zito la kidevuni kama vile mpira na kuifanya kofia ya pikipiki kumvuka.
Nywele ndefu zikavurugika na kupepea hewani baada ya kofia lile kuvuuka.
"Ooh! Ni Zakia. Nadhani mwisho wako unaishia hapa leo. Umekutana na Israel mtoa roho,mbwa jike wee." Malocha hakuwa na maneno mengi mdomoni mwake, akakimbia kwa mwendo wa hatua za karibu~karibu lakini za haraka na Zakia bila kutambua, alikuta mtoto wa kiume yupo naye uso kwa uso.
Ngumi za haraka toka kwa Malocha zilitiririka kwenda usoni kwa Zakia kabla hajamalizia kwa ngumi nyingine nzito ya kidevu iliyomrusha yule mwanamke hadi karibu na bunduki yake. Zakia kwa haraka akaishika bunduki yake tayari kwa kuinyanyua, lakini haraka yake haikuwa kitu mbele ya kasi ya Malocha.
Tayari mwanaume alikuwa kafika na kuikanyaga ile bunduki. Zakia akashangaa kuona kiatu kizuri cha harusi kikiwa kimekanyaga bunduki yake. Akaangalia juu na kumshuhudia dume la mbegu likiwa ndani ya suti mwanana kana kwamba yupo harusini, na kumbe mapambanoni.
Teke lingine la kidevu likatua kwa Zakia na kumsukuma hadi kwenye gari la Malocha ambalo alikuwa kaliharibu kwa risasi zake.
Zakia akasimama tayari kwa mpambano wa ana kwa ana maana mbinu za kuchukua silaha yake zilishindikana. Akawa kakunja ngumi tayari kwa mpambano mkali. Lakini kwa bahati mbaya alikuwa kasimama karibu na mlango wa gari la Malocha ambapo Lisa alikuwa sehemu hiyo.
Na Lisa hakufanya kosa la kipumbavu kama wengi wanavyodhani. Kwa nguvu zake za kike, akausukuma ule mlango na kumkumba Zakia ambaye alipiga yowe la maumivu na kusukumika mbele ambapo Malocha alikuwepo. Hapo naye Malocha aliruka teke zito likamkuta yule mwanamke kwenye shingo na kumgongesha tena kwenye mlango wa gari. Zakia akiwa kakubali yaishe, Malocha ndio kwanza alikuwa kafunguliiwa.
Akamfata palepale na kuanza kumpa ngumi nyingi zilizoanzia kwenye tumbo zikafata kifuani, shingoni na kumalizikia kwenye paji la uso ambapo ngumi ile ilimfanya Zakia ajigonge kisogo kwenye gari la Malocha.
Damu zikaruka kama kuku aliyechinjwa, lakini Malocha hakuona kama inatosha, akamdaka na kumkaba vilivyo Zakia na kilichofuata ni kumvunja shingo mwanamke yule.
"Shit." Malocha aliongea neno hilo huku akitema mate pembeni baada ya kuuacha mwili wa Zakia ukiwa hauna uhai tena.
"R. I. P Zakia." Sauti ya Lisa ilisikika nayo, huku akifungua mlango wa gari yao iliyoshambuliwa.
"Tuondoke hapa haraka Lisa." Malocha aliongea hayo huku akiifuata ile pikipiki ya Zakia na kuiwasha. Lisa ambaye alikuwa karudiwa na nguvu, naye akaenda na kukwea nyuma ya pikipiki hiyo.
Lisa akaangalia maskani yake kwa mara ya mwisho, hapo akamuona Gunner akitoka nje ya nyumba yao na macho yake yakaenda kwenye gari la Malocha. Akakimbia na ghafla alikuwa kama kaishiwa nguvu baada ya kuuona mwili wa Zakia ukiwa hauna uhai.
Gunner akaufuata ule mwili na kisha kwa uchungu akaupakata na kulia kwa sauti ya juu. Wakati huo pikipiki inayoendeshwa na Malocha, ilishatimua vumbi na kuacha tafulani pale mtaani.
Gunner akaangalia pikipiki aliyokuwa anaendesha Malocha ambayo sasa ilikuwa inakata kona kuingia mtaa mwingine mbali na pale. Gunner akauma meno kwa hasira kisha akaanza kupiga ngumi chini. Akaona hiyo haitoshi, akaifata ile bunduki ya Zakia na kuijaza risasi, kisha kwa fujo akaanza kumwaga risasi hizo angani. Ni kama alikuwa kachanganyikiwa kwa sababu ya kifo cha Zakia.
Baada ya risasi kuisha, akausogelea mwili wa Zakia na kuutazama tena huku machozi yakimtoka zaidi ya pale. Lakini kulia siyo suluhisho la tatizo kwa mwanaume yeyote. Na yeye alijua hilo, akatwaa simu ya Zakia aliyokuwanayo mfukoni na kisha akabofya namba kadhaa na kuweka sikioni.
"Haloo Lobo. Wamemuua Zakia." Gunner akaongea na kutulia kusikiliza upande wa pili.
"Ni Malocha na Lisa ndio wamefanya hivi." Gunner akajibu tena na kumsikiliza Lobo.
"Okay. Nataka umuue Lisa. Huyu Malocha nitamuua mimi. Nenda kule nyumba ya shambani, Zakia kampeleka Martina kule. Kichukue hicho kifisadi na kukileta hapo kambini, mimi nipo njiani naanza kuja huko ili tupange." Gunner aliongea kwa hasira huku akianza kuondoka eneo lile akimuacha Zakia palepale alipofia.
Akaenda kwenye gari lake ambalo lilikuwa mbali na nyumbani kwake kwa sababu angeliweka karibu, basi mkewe angelisikia pale wakati anataka kutoroka. Gunner akawasha gari lile na kutitia sehemu nyingine.
****
Majira ya saa mbili usiku, vyombo vya habari hasa vya matangazo ya runinga, vilikuwa vikionesha taarifa ya masamaria mwema kuuawa na magaidi hatari waliokuwa hawajulikani kama magaidi bali wananchi wa kawaida.
Picha ya Zakia kama msamaria huyo, ilioneshwa kwenye runinga na baadaye zikapita picha za Malocha na Lisa kama magaidi hatari yaliyoondoa roho ya Zakia.
"Nasema hivii. Watu hawa hatari, watakamatwa na watahukumiwa hadharani adhabu ya kinyongo. Tunatoa taarifa kwa wananchi wote, kama utawaona watu hawa, toa taarifa kituo cha usalama chochote, nasi tutakuzawadia zawadi nono ya pesa taslimu. Usikose zawadi hii kwa kuyaficha haya ........." Runinga ikazimwa na Malocha baada ya kuitathmini ile taarifa iliyokuwa unasomwa na Kamanda wa Polisi Kanda ya Mashariki.
"Wapumbavu hawa. Wamekwisha wekwa dukani na roho zao. Uoga umekithiri katika nafsi zao. Shenzi kabisa." Malocha aliongea na kuendelea kutakana matusi mbalimbali mbele ya Lisa aliyekuwa kakaa kwenye kitanda na mawazo tele yakimzonga.
Walishafika nyumba ya Kivule na sasa walikuwa wametulia wakitafakari ili na lile hasa kwa kilichotokea muda uliopita.
"Malocha. Martina wangu. Sijui nitampataje mwanangu. Naomba mnisaidie jamani." Lisa aliongea kwa uchungu na chozi la uchungu wa mwana likamtiririka mwanamke huyu.
"Usijali Lisa. Hawawezi kumfanya chochote na tutampata tu. Najua tumekwisha wachokoza, sasa hivi wanapanga cha kufanya ili watuvute twende. Huo ndio utakuwa wakati wa kumwokoa Martina. Hawawezi kumdhulu." Malocha aliongea kwa kumsugua sugua bega binti yule na kwa faraja hiyo, alijikuta akimkumbatia Malocha.
"Usijali Lisa. Everything will be alright." Malocha kwa kunong'ona akambembeleza Lisa ambaye kama mama wengine ambavyo wangekuwa na wasiwasi kuhusu watoto wao, basi na yeye yupo vivyo hivyo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya dakika kumi na tano, usingizi wa mchoko na maumivu ambayo yalitokana na kipigo toka kwa Gunner, ukamkamata Lisa na bila hiyana akaruhusu usingizi huo uwe kulala.
Malocha akamfunika vema Lisa na kisha akatoka nje ya chumba kile na kuelekea sebuleni ambapo alimkuta Mubah katika hamasa kubwa ya kutaka kujua nini kilitokea hadi mchumba wake akawa hai na kuwa anashirikiana na wakina Lobo.
"Niambie Malocha. Nini kipo katikati hadi tunaanzisha mahusiano na magaidi halafu hata hamtumbii." Mubah alikuwa anaongea kwa kufoka.
"Ulisahau jana wakati unataka kumuambia Lisa habari za Gunner, nami nilikuambia, jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza." Malocha kwa makini akamwambia Mubah na kisha akaenda kwenye kochi moja na kukaa kisha akakunja nne kabla hajaanza kuutikisa mguu wake uliojuu ya mwingine kwa chati.
"Kwa hiyo ulikuwa unajua kuwa Zakia ni mbwa wa wakina Lobo." Mubah alimuuliza Malocha kwa kumtolea macho haswa.
"Ndio. Na si wewe tu. Karibu kila mfanyakazi mle FISSA, anamahusiano na gaidi. Lakini magaidi hawa si kama wanashirikiana na wakina Lobo, sema wapo kwa ajili ya dharula tu. Kama hivyo Zakia amekufa, basi anachukuliwa mwingine." Malocha akamjibu Mubah ambaye kwa hasira akaupiga kofi ule mguu wa Malocha uliokuwa unatingishika. Akaona haitoshi, akaushusha kwa nguvu mguu ule chini na kumfanya Malocha atabasamu tu.
"Hakuna GPS iliyotumika kuifata familia yako. Ni Zakia ndiye aliyetoa taarifa kwa Lobo ni wapi walipopelekwa. Na wakati huo mimi nilikuwa sijui kama Zakia pia anamahusiano na Lobo. Nilijua baada ya kufuatilia mawasiliano yote ambayo Lobo alikuwa akiyafanya. Na baadaye nikafuatilia ya Zakia na hadi hapa jana, nilikuwa nayafatilia.
Hakuna mwanamke ambaye alikuwa anapendana na Gunner kama Zakia. Gunner alikuwa anampenda huyu mwanamke mpaka kero na ndio maana nikamuua ili kumpandisha mori yule mbwa." Malocha alizidi kutiririka ukweli wakati huo Mubah alikuwa anamuangalia kwa macho ya hasira.
"Kwa hiyo wajua mengi tu. Mbona hukutuambia wewe mtu. Unakuwa mchoyo wa taarifa za muhimu kama hizi? We ni mtu gani Malocha." Mubah alibwata kama mbwa aliyeona sura asiyoifahamu.
"Mapenzi upofu, Mubah. Ulikuwa kipofu kipindi kile. Ningekwambia kuwa Gunner anatoka na mchumba wako, usingeamini na zaidi ungeniona mchonganishi. Hiyo yote ni kwa sababu ulikuwa umependa. Na isingetokea kwako tu, hata kwa Lisa." Mubah akatafakari na kuyachambua maneno hayo na kuona undani wenye ukweli kuhusu hilo.
Akapunguza jazba na kukaa kwenye kochi huku kajiinamia.
"Lakini Mkuu, ungeniambia tu! Ningekuwa makini japo ni kweli nilikuwa nampenda huyu mshenzi."
"Ukishakuwa ndani ya mapenzi, ni sawa na kuwepo ndani ya pango lenye giza na hujui wapi pa kutokea wala wapi pa kushika. Unaweza kuisikia sauti inaita, lakini hujui pa kuanzia ili uiombe msaada.
Ungesikia nilichokwambia, lakini ungekuwa huna uwezo wa kuamini." Malocha akazidi kuufunua ukweli ambao ulikuwa ni kiza kinene mbele ya macho ya Mubah.
"Nimekuelewa sana Mkuu. Lakini naomba safari hii, aliyeshiriki kuangamiza familia yangu, huyu Lobo, msimuue. Nahitaji kumuua mimi mwenyewe kwa risasi zenye idadi ya familia yangu." Mubah aliongea kwa hamasa na kumfanya Malocha akubaliane na ombi hilo. Swali likabaki, wataweza?
****
Mida ya saa nne usiku, ndani ya kambi kubwa ya Gunner iliyopo katika pori moja huko nje kidogo ya Jiji Dar es Salaam, watu kadhaa walikuwa kwenye chumba cha kompyuta wakijaribu kutafuta mawasiliano ya Malocha. Ilikuwa ngumu sana kwani safari hii Malocha hakuwa tayari kufuatiliwa kama wakati yupo ndani ya FISSA. Lobo alijaribu kumbembeleza Martina ili aseme ni wapi wapo wakina Malocha, lakini mtoto yule alikuwa hana uhakika wa akisemacho. Mara tulienda sokoni, mara barabara inamaji, mara tukapanda na kushuka daraja, haeleweki. Huko ndio kuelekeza alikokuwa anaelekeza Martina.
"Boss." Sauti nzito na yenye ukatili ndani yake ilimuita mkuu wake.
Alikuwa ni kijana mrefu na mwenye misuli na asili ya Kirusi ilikuwa imemtapakaa kila sehemu ya mwili wake.
Gunner akasogea pale alipoitwa na mtaalamu yule aloyekuwa nguli wa kompyuta katika kambi ile.
"Tumekosa mawasiliano ya hawa watu kwa njia hii." Jamaa yule alijibu kwa uhakika na kumfanya Gunner kutulia kwa sekunde kadhaa akitafakari jambo huku akikuna kidevu chake chenye ndevu za kiasi na zimechongwa kwa ufahamu na mtaalamu sijui kutoka wapi.
Macho ya Gunner yalikuwa hayatulii katika anga la jumba lile lililokuwa limetapakaa nyaya za umeme mkali ambao waliutengeneza wenyewe kwa kutumia madini hatari ya sumu ya Yellowstone. Haijulikani madini hayo ya njano yanachimbwa wapi, lakini ni madini yanayoweza kuwa hatari kuliko hata Uranium.
"Fungua SGT." Maneno hayo yakamfanya yule mtaalam wa TEHAMA kubaki akimshangaa mkuu wake kwa maamuzi mazito kama hayo.
"Mkuu. Lakini ni mapema sana kufungua SGT. Tutakamatwa mapema sana kabla ya mpango wetu kukamilika." Yule mtaalam akatoa wazo lake.
"Nimeshasema Boyka. Just Do It." Yule bwana aliyejulikana kwa jina Boyka akaamua kufanya alichoambiwa.
Akafungua mtambo ghali kabisa duniani ambao uliibwa toka mikononi mwa Wachina na watu wasiojulikana na ulikuwa unaogopwa na yeyote ambaye anahusika uhalifu, uliweza kunasa wahalifu karibu sitini baada ya kuindwa.
SGT (Satellite GPS and Traces). Ni mtambo ambao unaweza kuzima Satellites zote duniani na vifaa vyote vinavyoweza kufuatwa kama vina GPS. Hapa nazungumzia simu, kompyuta na vifaa vyote viwezavyo kutumia Internets.
Mtambo huu, Gunner akishirikiana na wenzake baadhi kuuiba. Waliuiba kwenye Chuo cha Sayansi kilichopo nchini China baada ya kukamilika kufanyiwa majaribio na kuwa tayari kutumika kwa ajili ya kuiba siri mbalimbali hasa za kipelelezi.
Marekani walipopata sifa za mtambo huo, udenda ukawatoka na kutaka kuumiliki. Wakatengeneza mtambo wao mdogo kutokana na wazo walilopewa na Wanasayansi wao wakuu. Mtambo walioutengeneza waliuita Ant-SGT. Yaani hata wakiwasha STG mtambo huo hauwezi kuzima na unaweza kuungwa kwenye kompyuta zaidi ya trilioni duniani. Lakini kwa kuwa Marekani ni wa binafsi na wanataka SGT uwe wao, wakaamua kuwapa FBI ili wautafute mtambo ulioibwa na Gunner.
Sifa nyingine ya hatari kuhusu SGT, unaweza kuangamiza eneo ambalo wanalishuku linawaharifu. Inamvuto wa hatari ambao umetengezwa kwa madini ya Uranium. Mvuto huo upo kama sumaku au nguvu ya ukinzani, ukichomoka, huwa kama upepo na sifa yake huaribu kwa kulipua eneo zima lililotakiwa kuharibiwa.
Sifa mbaya ya Ant-SGT, mtambo uwezao kuufatilia SGT mahala ulipo, wenyewe huweza kung'amua SGT upo wapi baada ya dakika tatu za mtambo huo kuwaka.
Tatizo hilo, kundi la Gunner ulilitambua na ndio maana hakuwa na shaka sana kuhusu akifanyacho.
Boyka akaanza kubofya vitufe vingi vilivyo kwenye kiparaza (keyboard) cha kompyuta yake anayoitumia.
Mara eneo la nje ya jumba lile kukasikika mtikisiko mkubwa ambao unafanana na tetemeko la ardhi.
Baada ya mtikisiko huo, ardhi ya eneo lile ilifunguka na mwanga mkali ukaangaza eneo lile na kuonekana kama mchana na kumbe ni usiku wa saa tano kasoro.
Baada ya hali hiyo kutulia, ikasikika sauti nyingine kama ya ndege kubwa ya Rais wa Marekani ikipaa au kutua. Sekunde kadhaa ya karaha hiyo ya sauti kubwa, kikachomoka kitu toka katika mlango ule uliofunguka na kwenda angani ambapo kilitawanyika na kutoa vitu kama kambakamba za umeme ambazo zilitengeneza duara na kufunika eneo zima ambalo Gunner alikuwa kaliwekea makazi.
Hiyo yote ilikuwa ni katika kulinda mtambo huo wa SGT na eneo zima ili wanaoutafuta wasiweze kuupata. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Una dakika mbili za kutafuta nachokitaka." Gunner alimwambia Boyka ambaye naye kwa haraka akaanza kubonyeza kiparaza cha kompyuta yake kwa haraka kuliko kawaida. Hata dakika mbili hazikuisha, tayari alikuwa kamaliza kazi aliyoambiwa lakini alipata mawasiliano ya simu ambayo alikuwa anaitumia Malocha. Aliipata kwa sababu simu ilikuwa wazi na alipoitazama vizuri simu hiyo aligundua kuwa inakifaa ambacho ni kazi kufuatilia mawasiliano yake kikawaida. Hivyo mtambo wa SGT ulikuwa umefaulu vema mtihani wake.
"Safi Boyka. Funga mtambo haraka." Gunner akampongeza mtaalam wake na kubofya vitufe kadhaa na kile kitu kilichoruka angani, kikarudi mahala pake na lango lile la ardhini likajifunga kwa njia ileile ya kelele na tetemeko.
****
NCHINI VATICAN, ITALIA.
Upande wa Dar es Salaam, masaa yalisomeka ni saa nne au saa tano kasoro usiku wakati mtambo wa SGT unafunguliwa lakini kwa upande wa Jiji la Vatican lililopo nchini Italia, ilikuwa ni saa Tatu au saa nne kasoro usiku kwa sababu Tanzania imepishana na Vatican masaa mawili nyuma.
Chumba kimoja cha hoteli iitwayo Aspereado kulikuwa na miili miwili yenye jinsia tofauti ikiendelea kupalangana katika kitanda cha hoteli hiyo. Mwanaume mwenye rangi nyeusi alikuwa anataabisha maungio yake ya kiume katika kiuno chembamba lakini kilichobeba mwili wenye mvuto. Ni miguno ya mapenzi ndio iloyokuwa inaendelea wakati hayo yote yakijiri.
Wakati wakiendelea kupeta katika dunia ya mapenzi kwenye Jiji lenye ulinzi mkali kuliko yote ya dunia hii, mara sauti kali ilianza kulia kutoka kwenye droo ya kitanda wanachokitumia. Yule bwana mweusi kwa haraka akaacha shughuli yake ya uzinzi na kufungua droo hiyo ambayo alitoa saa ikiwa inalia mlio huo. Akaibofya bofya kwa pembeni na ghafla macho yake yakajawa na mshangao mkubwa kwa alichokiona.
"They're opening SGT. (Wamefungua SGT)" Jamaa yule alijisemea huku akitabasamu.
"Quello che hai fatto? (Umesemaje?)" Yule mwanamke akamuuliza yule jamaa kwa lugha ya Kiitaliano.
"Lo sposerò, Veronica. (Nitakuoa, Veronica)" Jamaa yule alijibu huku akimuangalia Veronica, binti wa Kiitalia asiyeelewa Kiingereza. Binti ambaye anasoma Chuo cha Utawa cha pale Vatican, lakini kadondoka kwenye penzi zito la kijana yule mweusi, na sasa hataki tena Utawa bali kuolewa na yule mweusi, japo rangi hiyo inadharirika sana nchini humo.
"Ma stai scherzando, Pirlo? (Unanitania, Pirlo?)" Binti yule alikuwa haamini yale aliyoyasikia na kujikuta akimuuliza swali hilo Bwana Pirlo.
"Sicuro che dico, Veronica. (Ukweli nakwambia Veronica)" Pirlo alimjibu Veronica na kumfanya binti yule amrukie kifuani Pirlo na kisha kwa mbwembwe akaanza kumlamba Pirlo huku na huko na kilichoendelea hapo ni mapenzi tu.
****
"Pirlo, Pirlo svegliati (Pirlo, Pirlo, amka)" Veronica alikuwa akimuamsha kwa sauti ya chini Pirlo ikiwa ni asubuhi matata ya saa moja. "Mio Papà è qui, in cerca di mi. (Baba yangu yupo hapa, ananitafuta mimi)" Pirlo kusikia hivyo, akakurupuka haraka na kuvaa suruali yake. Wakati anaanza kuvaa shati lake mara mlango wa chumba walichopanga ukaanza kugongwa kwa nguvu.
"Aprire la porta bastardo (Fungua mlango we' mpumbavu)" Sauti ilisikika ikifoka kwa hasira mlangoni na wakati huo Pirlo aliinama uvunguni na kuchukua viatu vyake aina ya raba na kuviweka mguuni kabla hajachukua saa yake na kuivaa mkononi.
Pirlo alipomaliza, akamfata Veronica na kisha akaanza kunyonya ulimi wake kwa hamasa.
"Mi mancherai tanto, Veronica (Nitakukumbuka sana, Veronica)" Pirlo alimwambia Veronica.
"Anch'io, Pirlo. (Nami pia, Pirlo)" Wakanyonyana tena ndimi zao na mara mlango ukaanza kufunguliwa kwa kusukumwa kama unataka kuvunjwa.
"Andare veloce, vai Pirlo. ( Ondoka haraka, nenda Pirlo)" Veronica alimwambia Pirlo na Pirlo kwa haraka akakimbilia katika dirisha la chumba kile na kuanza kutoka. Alipofika dirishani, akabusu mkono wake na kupuliza busu lile kwenda kwa Veronica aliyekuwa kavaa gauni laini la kulalia hadi matiti yake machanga yakawa yameinua gauni hiyo na kuleta hamasa kwa kila jicho la mwanaume.
Pirlo akaruka kwa ustadi na kutua dirisha la chini yake kwa sababu walikuwa katika ghorofa ya saba, yeye na Veronica.
Akaruka tena kwenda chini na kutulia kwenye chumba kilichopo katika ghorofa ya tano. Hapo akafungua dirisha la chumba hicho na kuingia ambapo waenyeji waliokuwa katika kustarehesha miili yao walishtuka na kujikunyata pembezoni mwa kitanda chao.
"Scusate.( Samahani)" Pirlo aliongea hayo huku akiwa na tabasamu pana na kuwapita wale vijana kisha kwenda katika mlango wa chumba kile na kutoka. Akaenda kupanda lift ambayo ilimshusha hadi chini na kisha akatoka nje ya hoteli na kuchukua gari yake aina ya Ferrari Gt rangi nyekundu, na kupotea eneo lile.
Kule juu alipomuacha Veronica, mlango ulivunjwa na kuingia Mzee mmoja aliyekuwa kavalia suti ya kijivu na nywele zake za kichwani zikiwa nyeupe huku ndevu zake kaweka brichi ya kijivu upande mmoja, na mwingine kaziacha na weusi wake. Aliingia kakamata bastola yake aina ya revolva pamoja na vijana wawili ambao nao walikuwa na silaha nzito. Walimkuta Veronica akiwa kakaa dirishani akimpungia Pirlo mkono baada ya kufanikiwa kufika chini.
"Dov'è questo bastardo? (Yupo wapi huyu mpumbavu)" Yule mzee aliuliza huku akianza kufunua kitanda cha kile chumba wakati huo Veronica akionekana mwenye kununa kama kakosewa sana.
"Papà, perché stai facendo questo? (Baba, kwa nini unafanya hivi?)" Veronica alimuuliza baba yake na mzee yule akamuangalia na kumuona yupo katika vazi ambalo si sahihi kwa.watu kumuona vile hasa wale alioingia nao.
Akawaangalia wale vibaraka wake, wote wakaonekana wenye kutazama maungio mwanana ya Veronica. Hasira zikamshika yule mzee na kujikuta akiwafukuza wale jamaa wote mle ndani.
"Samahani mwanangu, nilipata taarifa.kuwa upo na mwanaume humu ndio maana nikaja kuhakikisha." Mzee yule alimuomba msamaha mwanaye huku kaangalia pembeni. Veronica akawa anamzomea kwa nyuma kana kwamba yule si baba yake, hakika ilikuwa kituko hasa kwa sababu mtu mwenye hela na msomi kama baba wa Veronica anasumbuliwa na muhuni kama Pirlo.
"Nenda nje. Nashuka baada ya kuvaa." Veronica alimuamuru baba yake ambaye haraka alitoka nje ja kwenda sehemu ya kusubiria wageni.
Veronica akatoka akiwa kavalia mavazi ya Kitawa kama wavaavyo wanachuo wa chuo chao na kisha akachukuliwa na baba yake huku akijiona bora sana kwa kuushinda mpango ule.
*****
DAR ES SALAAM SAA SITA USIKU.
Simu ya Malocha iliita na haraka akaipokea kwa sababu ilikuwa ni namba binafsi imepiga (Private Number). Akamwambia yule opareta wao aiunge ili kila mmoja aliyekuwamo mle ofisini aisikie. Kama alivyotegemea alikuwa ni Gunner na kwa makini akaanza kuongea.
"Hey Malocha." Alisalimia.
"Pole kwa msiba Gunner." Malocha alikejeli.
"Naomba niongee na mke wangu."
Hapohapo Malocha akamtuma Mubah akamuite Lisa.
Lisa alipokuja, Gunner akaanza kuongea kilichompigisha simu.
"Nadhani sasa umekwishajua mimi ni nani. Lakini kosa kubwa ambalo utalijutia, ni kumuua mwanamke nimpendaye kuliko wewe malaya mkubwa. Sasa nitakachokifanya, ni kumuachia Lobo kazi ya kufanya." Gunner akamaliza na kisha akamkabidhi simu John Lobo, mtu ambaye hajui kuhusu huruma, ukisikia hadithi azisimuliazo, utamkimbia. Zote uhusu kuua na mauaji pekee. Sasa simu kakibidhiwa yeye.
"Lisa, kuna machaguo mawili pekee katika haya. Kuuza au Kununua roho ya Martina. Ukitaka kununua roho ya mwanao, njoo mwenyewe tutakapokwambia. Ukitaka kuuza roho ya mwanao, usije tutakapokwambia. Roho yake itakuwa halali yangu.
Una masaa ishirini na nne Lisa kuanzia sasa. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHAGUO NI LAKO, TICK TOCK." Simu ikakatwa baada ya maneno na sura ya Lisa ilikuwa katika kijasho chembamba.
Ni kumbate dogo kutoka kwa Malocha ndilo lilimtoa katika mateso ya fikra Lisa ambaye kichwa chake chote kilijawa na woga kuhusu kifo cha mwanaye. Alikuwa haelewi ni vipi atamuokoa mtoto wake toka mikononi mwa mikono ya Gunner na alikuwa hajui ni wapi ataanzia kuongea ili sauti yake ipokelewe katika masikio ya mwenye uweza wa yote.
"Ee MUNGU, naomba uniondolee kikombe hiki kizito kilichokuwa mbele yangu. Wajua siwezi bila wewe na siwezi kufanya chochote bila ya uweza wako. Kama malipo ya dhambi ni haya, basi naomba niyalipie mimi lakini si roho ya mwanangu. Nipo tayari kufa lakini naomba roho ya mwanangu uiokoe baba." Lisa aliongea hayo kwa uchungu na kuwafanya wanaume wote mle ndani kukabwa na donge la uchungu kwenye makoo yao.
"Lisa." Malocha aliita huku akiwa kumkumbatia. "Ni kheri nife mimi kuliko wewe au Martina. Nipo tayari kuitoa roho yangu ili ninyi nyote mpone. Hakuna ambaye atakufa baada ya masaa ishirini na nne."
"Nimempoteza Mjomba wangu kipenzi kwa mkono Lobo. Nimuonapo Martina nahisi kama namuona Mjomba wangu. Sitakuwa tayari kumpoteza Martina kama nilivyompoteza Mjomba wangu. Nitakuwa nawe Lisa." Mubah aliongea kwa sauti ya hamasa na kuonekana mwenye utayari kwa lolote lile.
"Sijawahi kuingia mapambanoni. Huu ndio muda wangu wa kufanya hivyo. Nitakuwa nyuma yako Lisa." Opareta wa mitambo wa Malocha alisimama na kuungana na wakina Lisa waliokuwa wanafarijiana.
"Mimi pia. Naingia katika mpambano." Jamaa mwingine akakamilisha kundi la watu watano ambao waliweka mikono yao katika umoja na kisha kwa pamoja wakatamka. "Kwa Martina na Lisa." Sauti hizo zikawapa amsha katika mioyo yao na mpango kabambe wa kumuokoa Martina ukaanza papo hapo.
****
TURIN, ITALIA.
Pirlo baada ya kutoroka salama kule Vatican, alichukua ndege binafsi na kwenda moja kwa moja katika Jiji lingine la marah, Jiji la Turin. Si kama alienda huko kwa ajili ya raha, bali alienda kwa ajili ya taarifa maalumu ya alichokipata usiku wa kuamkia siku hiyo.
Akaingia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro lililopo hapo Turin na kisha akakaa kwenye viti vya kanisa hivyo na kupiga ishara ya msalaba kwa kutazama sanamu ya Bikira la Maria iliyokuwa imembeba mtoto mdogo na shingo yake ikiwa imepindia kushoto kuonesha huruma ya Mama huyo.
Ndani ya kanisa kulikuwepo na watu sita pekee wakionekana wenye kufanya sala za toba baada ya maungamo yao. Pirlo alikuwa katika sala fupi za kujiandaa kabla hajaenda kwenye maungamo.
Ilikuwa ni kawaida yake kufanya maungamo kila Alhamisi, na alikuwa anafanya maungamo hayo katika kanisa moja tu! Ambalo alikuwepo muda huo. Japo pia alikuwa anafanya maungamo hayo katika kanisa hilo, pia alikuwa anafanyia kwenye kijumba kilekile kila akienda. Na muda wa saa saba ndio ulikuwa muda wake wa kufanya maungamo hayo.
Ilipotimu saa saba kamili, akaenda kwenye kijumba hicho maalumu na kupiga magoti tayari kwa maungamo.
"Father. I need to go back in Tanzania. (Baba. Nahitaji kurudi Tanzania)" Pirlo aliongea hayo baada ya kupiga ishara ya msalaba.
"Why? (Kwa nini?)" Yule Padri akamuuliza swali Pirlo. Pirlo akaanza kumuhadithia kila kitu alichokisikia na kukiona.
Wakati yupo kwenye ndege binafsi akielekea Turin, Pirlo alitoa kompyuta yake mpakato na kisha akavua saa yake ambayo ilikuwa inagonga kengere usiku wa jana yake. Kwenye saa hiyo, akachomoa kitu kidogo kama memori kadi lakini hakikuwa memori kadi kwa sababu chenyewe waweza kukiwasha na kukizima.
Akakiwasha na kisha akakichoneka katika kifaa maalumu ambacho hutumika kuchomekea memori kadi. Akaingiza kifaa hicho kwenye kompyuta yake mpakato na kuperuzi kila kitu kilichoonekana mle kwenye kile kifaa alichokitoa kwenye saa. Hapo akaanza kuona tukio zima ambalo limefanyika nchini Tanzania hasa baada ya ule mtambo wa SGT kufunguka. Akaona eneo zima ambapo mtambo ule ulikuwepo na akaona ni nani anamiliki mtambo huo.
Pia akaona kazi uliyoifanya ya kutafuta namba fulani ambayo ni za Malocha na kisha baada ya kuipata, mtambo ule ulifungwa.
Pirlo hakuishia hapo, katika kile kifaa, pia akafanikiwa kudaka maongezi yaliyofanyika katika namba ile iliyochukuliwa na SGT. Pirlo akapumua pumzi ndefu na akawa hana raha baada ya kugundua nia ya wale watu.
Akafunga kompyuta yake mpakato na kutulia. Kisha akili yake akaihamishia China alipowahi kusomea Sayansi.
SHANGHAI, CHINA.
Kulikuwa kuna jopo la wanafunzi wapatao kumi katika chumba kimoja cha kufanya majaribio ya Kisayansi. Katika wanafunzi hao kumi ambao walionekana akili yao wameegemeza kwenye kutengeneza kitu fulani, kulikuwa kuna mweusi mmoja tu!
Mweusi huyo alijiita Hyung Sheing. Wenzake walijuwa historia yake kuwa alikuwa anaasili mbili, ya Kichina na Kimarekani. Hyung aliwaambia kuwa baba yake ni Mchina lakini Mama yake ni Mmarekani mweusi ambaye alifariki pindi anamleta yeye duniani. Pia akawaambia wenzake kuwa baba yake aliondoka duniani wakati yeye anamiaka kumi tu! Aliishi katika uyatima hadi alipopata mfadhili akiwa na miaka kumi na mitano, na ndiye anayemsomesha hadi muda huo akiwa na miaka ishirini na saba.
Historia hiyo ikawafanya wenzake na wanafunzi wote kumuona wa kipekee na kuwa naye bega kwa bega ili atimize ndoto zake za kuwa mwanasayansi mkubwa duniani.
Na ndoto hiyo ndiyo alikuwa anaifanyia kazi siku hiyo ambapo jopo la wanafunzi wenzake lilikuwa likitengeneza mtambo uliyoitwa Satellite GPS Traces (SGT). Baada ya kuumaliza mtambo huo, waliujaribu na kuona unafaa sana kwa ajili ya kufanya kazi za kipelelezi na nyingine nyingi zenye manufaa na zisizo na manufaa.
Lakini japo pia walifanikiwa kuutengeneza mtambo ule, Hyung akatoa wazo kuwa watengeneze kitu ambacho kitaweza kuufatilia mtambo huo kwa chochote utakachofanya. Wengi walikataa wazo hilo kwa sababu kazi waliyopewa na shirika la kipelelezi la China, walikwisha imaliza. Lakini hawakumkatisha tamaa, wakampa formula zote ambazo wameutengenezea mtambo ule, kisha wakamuacha peke yake katika maabara ile.
Hyung akaanza kuunda kitu ambacho kitaufatilia mtambo ule. Tangu saa sita mchana hadi saa nane za usiku, Hyung alikuwa bado anatengeneza kifaa hicho ambacho hakutaka kiwe kikubwa sana. Ndipo mida ya saa kumi usiku, akafanikiwa kumaliza kazi yake na kuijaribu. Kweli kifaa chake kikakubali punde tu, mtambo wa SGT ulipofunguliwa. Akaenda mbali zaidi kwa kuchunguza mambo mbalimbali ya duniani na kwa kile kifaa alichokitengeneza, kikadaka yote hayo. Na ndiyo hiyo saa ambayo sasa anaimiliki Pirlo aliyekuwapo Italia.
Ni kwa nini saa anayo Pirlo? Hili ndilo jibu.
Baada ya kuumaliza ule mtambo na wanafunzi waliofanikisha suala hilo kutunukiwa vyeti maalumu kabisa akiwemo Hyung, mtambo huo ukachukuliwa na kuanza kupelekwa katika shirika la kipelelezi huku Hyung akiwa hajawaambia wenzake wala mtu yeyote kuwa kafanikiwa kutengeneza kifaa kitakachoufatilia mtambo ule.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kukiwa na ulinzi hafifu wakati mtambo huo mkubwa unapelekwa kwenye idara ya upelelezi China, mbele ya gari lililoubeba mtambo huo, ilitokea gari nyingine kubwa zaidi na kuanza kuishambulia gari yenye mtambo. Haikupita muda, gari hilo likawa kimya na walinzi wote wakiwa maiti.
Kundi la watu wasiojulikana, wakashuka toka garini na kufungua gari lile kubwa lililobeba mtambo. Walipohakiki kuwa kuna mali yao, wakaita helkopta waliyoiandaa na kushusha sumaku kubwa ambayo ilinasa kwenye mtambo ule wenye ukubwa wa duara lile la katikati kwenye uwanja wa mpira lakini kwenda juu mtambo ule ni mrefu zaidi. Helkopta ikauchukua mtambo huo na kutitia nao pasipojulikana.
Baada ya patashika hiyo, ndipo kundi hilohilo, likapewa amri nyingine ya kwenda kuwaangamiza wanafunzi wote walioshiriki kuutengeneza mtambo ule. Wanafunzi karibu wote walipoteza maisha yao kasoro Hyung ambaye alichezwa na chale mapema na kuamua kukimbilia Italia ambapo huko alibadili jina na kujiita Pirlo.
****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment