Simulizi : Duka La Roho
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwa hiyo unaondoka lini." Padri alimuuliza Pirlo baada ya kusikiliza yote yaliyotokea.
"Leoleo. Natakiwa kufika kule kabla ya saa nne." Pirlo akajibu na yule Padri akamwambia aende chumba fulani kwa ajili ya kukutana naye uso kwa uso na kujadili suala hilo. Pirlo akapiga ishara ya msalaba na kwenda kwenye viti ambapo alitumia dakika kama tano kujifanya anasali. Akatoka hapo na kuelekea nje kwenye chumba alichoelekezwa na yule Padri.
Huko akakutana na Mzee mmoja mwenye mvi nyingi kichwani kwake na walipoonana wakakumbatiana na mzee yule akampeleka kwenye chumba kingine cha siri zaidi.
Chumba kilijaa vifaa vingi vya mapigano hadi kijana Pirlo alikuwa haamini kama huko nje kuna kanisa. Mapanga ya kininja, bunduki na silaha zote aliziona hapo.
"Huku ndipo kwenye nyanja yetu ya upelelezi Pirlo." Mzee yule alimwambia Pirlo huku akicheka na macho ya Pirlo yalikuwa yanalanda huku na huko akishangaa wafanyakazi wenye mavazi ya Kitawa wanavyochalaza kiparaza cha kompyuta. "Ulichagua jina zuri sana kijana. Eti Pirlo, ukajidai yule mchezaji wetu wa Italia. Kwa nini usingejiita Balloteli, Muafrika mwenzako?" Mzee yule alikuwa akiongea kwa utani na kuchechemea kutokana na uzee wake.
Akafika sehemu moja ambayo ndio ilikuwa mwisho wa safari yake. Akagota na kumuita jamaa mmoja aliyekuwa anahusika na sehemu ile.
"Alejandro." Mzee yule aliita kwa sauti kutokana na mtu aliyekuwa anamuita kutokuwepo. Mara akiwa anamtafuta huku na huko, akashangaa kitu kinapita mbele yake kwa kasi halafu kikasimama mbele yake na kuanza kuongea.
"Hellow Mr. Alexander." Kitu hicho kilikuwa kimevaa suti lakini baada ya sauti hiyo, hali fulani ya umeme ikatokea kwenye suti hiyo na sura ya Muitaliano ikaonekana ikiwa inatabasamu.
"Alejandro. Kila wakati we' ni mtu wa kubuni ujinga tu!" Mzee Alexander alilalamika huku akimuangalia yule mtaalamu.
"Hii ni suti ambayo unaweza ukakimbia kwa kasi yoyote bila kuonekana. Na pia haingizi risasi hata kidogo. Mbali na hapo, ukivaa suti hii, na hii saa unaweza kuwa unatoa umeme mwilini mwako." Yule bwana aliyefahamika kwa jina Alejandro alitoa sifa baadhi ya vazi alilovaa na kumfanya Pirlo kuitamani suti ile.
"Achana na mambo yako. Huyu ni yule kijana wetu wa SGT, anasema mtambo umefunguliwa huko na anataka akauteketeze. Nimemleta kwako ili umpe vifaa maalumu." Mzee Alexander alieleza yote kuhusu Pirlo.
"Oooh! Mr. Hyung. Hii suti nakupa wewe Kamanda. Nenda nayo." Alejandro akiongea huku akiivua ile suti na yeye kubaki na boxer. Sekunde kadhaa akachukua rimoti fulani akaibonyeza vitufe fulani na ghafla likasogea begi fulani na kufunguka. Baada ya kufunguka, zikatokea nguo nyingine na mara zikaanza kujivalisha zenyewe mwilini.
"Haya twende." Alejandro alimwambia Pirlo baada mbwembwe nyingi. Pirlo akacheka na kisha akamfuata kijana yule mtukutu sehemu anayotaka waende.
Huko Alejandro akamtengenezea kitambulisho kingine atakachoingilia Tanzania na kisha akampa vifaa maalumu kwa ajili ya mapambano.
Pirlo akalidhika na kazi ya Mzee Alexander na Alejandro.
Akaaga na kuelekea uwanja wa ndege ambapo alikuta ndege maalumu kwa ajili ya kumpeleka Dar es Salaam, Tanzania.
****
Saa mbili usiku, yakiwa yamebaki masaa manne ya Lobo kutimiza adhma yake, Lisa alikuwa kwenye chumba cha mawasiliano akisubiri simu maalumu kutoka kwa Gunner.
Hali ya mawingu ilikuwa imetanda nje na Dar es Salaam nzima. Ilionesha wazi muda wowote mvua itakunya katika Jiji lile.
Saa tatu, simu ya Malocha iliita na hapohapo ikaungwa na mtaalamu wao na maongezi yao yakaanza kusikika bila chenga.
"Haloo FISSA. Lisa kabakiza masaa matatu. Naomba mfuate haya maelezo machache ambayo nitawapa. Mtoto yupo sehemu nyingine ambapo ni huko Gongo La Mboto kwa mbele na Lisa naomba aje huku Kibaha. Najua ndani ya masaa mawili atakuwa amefika. Hamna foleni usiku huu. Kama mnampenda Martina, naomba Lisa aje peke yake. Sitaki mchezo kuhusu hilo. Nawatazama kwa ukaribu, mkijaribu kuleta ukanjanja wowote, Martina mtaletewa mzoga hapo kesho. Zingatieni hilo, nawaoneni. Umebakiza masaa matatu, Lisa. Fanya maamuzi.TICK TOCK." Sauti ya Lobo ilisikika na wala hakuwa na muda wa kusikiliza upande wa pili, akakata simu.
"Mambo yatakuwa magumu hapa. Kama wamefanikiwa kujua mawasiliano yangu, nauhakika wanajua pia kuwa tupo wapi." Malocha aliongea kwa kukata tamaa mbele ya wafanyakazi wake.
"Usijali Malocha, mmefanya kazi kubwa sana hadi hapa. Naomba mwanangu mnilelee vizuri. Mkimpata Frank, muonesheni mwanaye, msimfiche na mwambieni nampenda sana." Lisa alimaliza kuongea maneno machache na kisha akatoka nje tayari kwa safari ya kibaha.
Hakusahau simu ambayo atakuwa anawasiliana na wakina Lobo kama hatowaona. Akawaacha wakina Malocha wakiwa katika masikitiko makubwa mioyoni mwao.
"Hamna jinsi. Tunakupenda Lisa." Malocha alinong'ona maneno ambayo Lisa hakuyasikia. Mtoto wa kike akakwea gari tayari kwa kwenda alipoelekezwa.
****
"Oooh! Lisa. Karibu tena katika mikono yangu." Ni sauti ya Gunner ambayo iliongea baada ya Lisa kusimamishwa kwenye barabara ya rami iliyopo eneo la Kibaha na kutoka nje ya gari lake.
"Muachie mwanangu Gunner." Lisa akafoka kwa hasira.
"Usijali. Tayari nimekwishawaambia mbwa wako mwanao alipo. Wapo njiani wanaelekea huko." Gunner akaongea na wakati huo mvua ya manyunyu ilikuwa imeanza kushika namba eneo hilo. "Zimebaki dakika kumi za Lobo kichukua roho yako. Umefanya maamuzi sahihi sana kwa kununua roho ya Martina." Lobo akazidi kutiririka.
"Fanyeni haraka. Sina muda wa kukaa na hii roho, ni yenu." Lisa akafoka tena.
"Hapana mke wangu, sheria zinasema masaa ishirini na nne. Bado dakika saba tu, utakuwa kuzimu. Lobo yumo mle, anasubiri kazi yake." Gunner alipoonesha sehemu Lobo alipo, taa za gari zikawashwa mara moja na kuzimwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mi' si mke wako pia." Lisa aliongea kwa kujiamini mbele ya Gunner ambaye alimpiga kofi zito lililompeleka Lisa chini ya rami. Mara baada ya kofi hilo, akaanza kumpiga mateke mazito binti yule kana kwamba hamjui.
"Mjinga wewe. Nitakuua mimi." Gunner aliongea kwa hasira huku akimtemea maji ya mvua Lisa. Radi nazo zilikuwa zinawaka huku na huko na kuonesha vazi la suti nyeusi aliyovaa Gunner. "Muda wa Lobo umewadia, kwa heri Lisa." Gunner alimuaga mkewe na kwenda kwenye gari alilopo Lobo. Wakati anaingia, John Lobo akawa anatoka upande mwingine.
Koti lake jeusi na refu linalochagizwa na kung'aa kama la majambazi, lilimfanya kumchora Lobo kama katili la hatari sana. Kila radi zilivyocharaza anga, uso wa Lobo ulionekana na mkononi kwake akiwa kakamata bastola iliyofungwa kiwambo cha sauti.
"Muda wa kufa Lisa. Imebaki dakika moja." Alipoongea hayo, radi ikapiga tena na uso wake mweupe kiasi huku kichwani akiwa hana nywele, zikamfanya Lisa aamini kuwa muda wake kweli umeisha.
Akanyanyuka pale alipokuwa kalala baada ya kupigwa na Gunner, akapiga magoti tayari kwa kukipokea kifo chake.
"Kumi, Tisa, Nane, Saba, Sita, Tano ......" Lobo akawa anahesabu sekunde ambazo zilikuwa zimebaki. Lisa akafumba macho yake baada ya sekunde kufikia nne.
Akiwa kajiandaa kufa mtoto wa kike, na wakati huo kifyatulio cha risasi kikiwa tayari kufyatuliwa na Lobo, muujiza wa ajabu ukatokea. Hakika ulikuwa muujiza wa aina yake.
Lobo akiwa anaanza kufyatua kifyatulio cha bastola yake, mara mkono wake wa kushoto ukachomwa na vitu kama nyota zenye ncha kali. Maumivu aliyoyapata dakika hiyo, yalikuwa hayaelezeki. Akiwa katika hali hiyo akajikuta akidondosha bastola yake na kuanza kutazama ni wapi vitu vile vimetokea. Wakati anatazama huku na huko, radi ikapiga na hapo akaona kitu mfano wa mtu aliyevaa nguo nyeusi anakuja kwa kasi ya popo mbele yake. Nasema ni mfano wa mtu kwa sababu kilikuwa kina kasi ambayo mtu wa kawaida hana hata kidogo lakini umbile hilo la mtu lilikuwa limetunukiwa kasi hiyo.
Kuja kutahamaki, kitu hicho kikampiga mateke mawili mazito John Lobo. La kwanza lilimkuta kifuani, kitu hicho kikiwa bado kipo angani, kikammalizia teke la pili la hatari shingoni. Lobo akapaishwa hadi kwenye boneti ya gari walilokuja nalo.
Radi nyingine ikapiga, hapo kile kitu kikaonekana kimesimama wima kwa mtindo wa kupigana. Lobo akagonga boneti la gari ile, na Gunner akawasha taa. Sasa alionekana mtu ambaye kafunikwa sura lakini kavaa suti ya gharama.
Kwa kasi, Lobo akashuka toka kwenye boneti na kumfuata yule mtu asiye na sura na kuanza kupambana naye wakati huo Lisa maswali kibao yaliendelea kutiririka katika kichwa chake asijue kile ni kitu gani au ni mtu gani na kaja sehemu ile kufanya nini.
Lobo akarusha teke, lakini cha kushangaza mtu yule alilidaka teke hilo kwa mguu wake wa kushoto na kulibana nyuma ya goti. Lobo akawa hana ujanja wa kutumia miguu yake. Akaanza kurusha ngumi ambapo yule mtu asiye na sura alikuwa akizitoa nje bila hata kurusha zake.
Ngumi ambayo Lobo aliivuta kwa nguvu zake zote, mtu yule aliidaka na sasa akawa kakamata mkono na mguu wa Lobo. Lobo akawa kakamatika hana la kufanya. Mara yule mtu alirudisha kichwa chake nyuma na kukipeleka mbele kwa kasi, kikatua kwenye pua ya Lobo. Damu zikamchuruzika Lobo lakini hakuenda popote kwa sababu alikuwa kabanwa ipasavyo na mtu yule.
Wakati damu zinaendelea kumtoka, Lobo akajikuta akipokea kichwa kingine palepale alipopigwa mwanzo. Maumivu yaliyompata, hakusita kupiga kelele na nadhani angesimulia hadi kwa wajukuu zake.
Hapo yule mtu alimuachia mkono na kisha akaanza kutandaza ngumi zisizo na idadi kwenye kifua cha Lobo. Ngumi ya mwisho ilitua tena kwenye pua, na hapohapo mtu yule akamuachia Lobo mguu wake na kuruka teke zito la kuzunguka. Lobo akapaa juu na kisha akatua chini kama mzigo akiwa kachafuka kwa damu na hali yake ikiwa wazi ni mbaya.
Yule bwana akawa bado kasimama palepale akiwa kakunja ngumi na sura yake iliyofungwa na sijui nini, ikiwa imeinama kwa kusubiri jambo lingine.
Mvua sasa ilikuwa hainyeshi tena bali kubaki miungurumo ya hapa na pale. Gunner akafungua mlango wa gari yake na kwa madaha akachomoka toka mle ndani na kisha akaenda kwa Lobo na kumuingiza ndani ya gari.
"Safi sana. Yaonekana una uwezo mkubwa wa kupigana. Haijalishi, lakini sasa unapambana na mzimu." Gunner aliongea na muda huohuo akachomoka kwa kasi na alipofika mbele ya yule mtu, alisimama ghafla na kuanza kurusha ngumi nyingi zisizo na idadi. Zilikuwa zinarushwa kuelekea kichwani, kifuani na kila mahali ambapo Gunner aliona patamsaidia kumnyamazisha mpinzani wake aliyekuwa anakazi ya kuzitoa na kuzikwepa.
Kuna ngumi moja ya hatari Gunner aliirusha na jamaa yule aliikwepa kwa kuinama kidogo, lakini kwa bahati mbaya alipoinama, Gunner akaachia ngumi ya mkono mwingine ambayo ilimkuta jamaa yule kidevuni na kumrusha hadi alipo Lisa. Alipotua chini, tayari Gunner alikwishafika, akamkalia kwa juu na kuanza kumtwanga ngumi za usoni.
Ilikuwa ni 'kimuhemuhe' au patashika kwa shimo kuchimbika. Mtu yule ambaye alikuwa kazibwa na mask, ni wazi alikuwa taabani hasa pale mwanaume wa shoka Gunner aliposhika ile mask iliyoungana na suti yake na kutaka kuiondoa.
Alipoishika, ndipo alipogundua inaseli za umeme ambazo ni hadi ubonyeze kitu fulani ndizo nazo zijifungue. Gunner akajaribu kuzamisha vidole vyake kwenye ile mask kwa kutaka kuirarua lakini kwa bahati mbaya alipokea pigo hafifu toka kwa Lisa lililopigwa kwa teke baada ya Lisa kuona mtu anayemsaidia kuzidiwa maarifa. Ni pigo hafifu kwa sababu si lile ambalo ungepigwa nalo na Lisa wakati yu mzima.
Gunner akajikuta akimuachia yule mtu na kumfuata Lisa ambaye alikuwa kasimama pembeni kidogo na pale. Kwa hasira nyingi, Gunner alimpiga kofi zito Lisa na lile kofi yule mtu aliyechini aliliona na likamshtua vilivyo. Mwanamke kupigwa kama mwanaume, yule mtu alistaajabu ya Filauni sasa baada ya kuyashuhudia ya Mussa.
Gunner hakuishia kwenye kofi pekee, Lisa alipoyumba baada ya kofi lile, Gunner akaruka teke la kutanguliza mguu mbele na likakita nyuma ya kiuno cha Lisa. Lisa masikini ya MUNGU akadondoka chini na kugaa gaa kwa maumivu.
Gunner akazidi kuonesha ukatili wake dhidi ya wanawake. Na hakika alikuwa katili. Mateke mazito kwenda tumboni, kifuani na saa nyingine kumkanyaga Lisa kichwani kama mwenye kuua nyoka kwa kumkanyaga na kiatu, usingeweza kusema huyu jamaa ana roho ya utu hata kidogo.
"Heeeey." Sauti kali ilisikika nyuma ya Gunner aliyekuwa anamsulubu Lisa. Akiwa anapumua haraka, Gunner akageuka nyuma kumuangalia anayemuita huku bado mguu wake upo juu ya mwili wa Lisa.
Akamtazama Lisa aliyekuwa anagaragara kwa maumivu, kisha Gunner akampiga teke dogo kama anatoa pasi ya mpira. Akamuacha na taratibu akaanza kwenda alipo yule mtu aliyekuwa kasimama na kuweka mguu mmoja mbele kama wafanyavyo wacheza mapigano ya miguu na mikono (karate).
"Hivyo ndivyo mama yako alivyokufundisha kucheza na mwanamke?" Yule bwana kwa mara ya kwanza aliongea baada ya kufoka.
"Oooh! Mama? Namchukia mama yangu kwa sababu alinitelekeza nilipozaliwa tu. Nampenda sana baba." Gunner alijibu huku akivaa vizuri groves zake nyeusi.
"Kwa hiyo baba yako ndio kakufundisha kuwapiga wanawake? Eti we' tasa." Yule jamaa aliongea maneno ya kukarahisha na Gunner yakamuuma.
"Usiniite hivyo."
"Tayari nimekwisha kuita sasa." Jamaa yule safari hii alikuwa anaongea huku akizunguka kwa hatua ndogondogo akimtazama Gunner kwa makini. "We' ni mgumba tu, hahahaaa." Jamaa akacheka kwa dharau.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mmmh! Yaonekana mswahili sana kijana. Lakini mbona hauvui hicho kiuchafu kichwani? Unaogopa nini?" Gunner aliuliza na wakati huo Lobo alikuwa ndani ya gari akifatilia ule mpambano kwa makini japo alikuwa katika maumivu makali ya kuvunjwa mfupa wa pua.
"Ooooh! Nimesahau kuwa ulikuwa unataka kuvua hii sura. Usijali Mgumba, ngoja nitimize." Jamaa yule aliongea na kufunua koti lake la suti sehemu ya mkononi, akaanza kuiobonyeza saa yake na sekunde kadhaa, ile mask ikaanza kutoa sauti za shoti ya umeme na baadaye ikapotea kabisa na kubaki sura ya yule bwana akiwa katika suti mwanana na ya kumpendeza pia.
Ni yuleyule Pirlo wa Italia na Hyung wa China, ndiye sasa alioneokana vema kwenye uso wa Gunner aliyebaki katabasamu tu bila kusema chochote.
"A coward's back. (Muoga karudi)" Gunner aliongea huku bado katabasamu.
"Karudi kuangamiza zao la wagumba na matasa." Pirlo au Hyung akajibu.
"Huwezi kunisimamisha Man'Sai, tayari nina kila kitu." Gunner akaongea akilitaja jina la Man'Sai ambalo ni jina alilojipa Frank Masai. Lisa kusikia jina hilo, akajikuta akipata hata nguvu na kutazama kule Frank Masai alipo.
Tabasamu la shida likamtoka mwanamke yule alipothibitisha sura ya Frank Masai.
"Oooh! Kumbe wanijua eeh. Sasa ndio nimerudi hivyo. Naanza na SGT kisha namalizia na Jet P112. Zote naziharibu." Frank aliongea kwa utulivu na sasa alikuwa kasimama akimuangalia adui yake.
"Hahahaaa. Wameshindwa makundi kama FBI, we bwege utaweza." Gunner akaongea kwa dharau.
"Hizo ni akili za Wagumba wengi wa dunia hii. Wanadhani kufanya kazi katika makundi ndio kufanikiwa. Njia ya kufanikiwa ni kuwa peke yako na kufanya kila kitu peke yako. Sihitaji msaada kutimiza nilichokitaka. Msaada wangu ni MUNGU tu." Masai aliongea kwa utulivu na Gunner akacheka tena.
"Okay Man'Sai. Lisa huyo hapo, nimekulindia sana. Ni mtamu mnooo, hahahaaa." Gunner akajidai anatoa maneno ya kejeli.
"Hahahaa. Usemayo ni ya kweli, ila unapewa utamu unashindwa kuleta matunda ya utamu huo. Mwanaume suruali wewe. Hahahaaa." Masai akakejeli naye jambo lililomfanya Gunner apandwe na hasira na kujikuta akikimbia kwa haraka kwenda kwa Masai ambaye safari hii alimuonesha huyu bwana kwa nini anatafutwa kwa udi na uvumba kwenye hii dunia na hapatikani.
Gunner akiwa katika kasi hiyo, akamfikia Frank Masai na kuanza kurusha ngumi nzito kama kawaida yake, lakini ubaya alimkuta hata Masai akiwa katika hasira za kumuona akimpiga Lisa kama mwanaume mwenzake.
Ngumi nyingi alizorusha Gunner, Masai alizipangua na yeye akawa anarusha zake kwa chati, yaani kwa kumendea. Gunner akajichanganya kidogo kwenye kurusha ngumi hizo, Masai akapangua na kutupa yake ambayo ilimkuta jamaa kwenye pua. Gunner akashika pua yake na kujisahau kuwa yupo mpambanoni. Frank akatupa ngumi nyingine ambayo hiyo ikatua kwenye shavu la kushoto na kumfanya Gunner aegemee upande wa kulia. Kosa kubwa kwa Gunner kwani wakati anaegemea upande huo, tayari Man'Sai alikuwa katupa ngumi nyingine nzito zaidi na kupiga shavu la kulia ambapo alikuwa anaegemea Gunner.
Damu kiasi zikamtoka Gunner lakini haikumaanisha ndio mpambano umeisha. Man'Sai akaruka teke zito lililompeleka Gunner hadi kwenye gari la Lisa.
Frank akiwa katika ubora wake wa kwenye riwaya ya Jina na Ukurasa wa Hamsini, akamuonesha Gunner kuwa yeye si wale aliowategemea katika maisha yake, bali yeye ni yule ambaye hakupaswa hata kumuota ujio wake.
Gunner alisikia sauti ya maji na sauti kama ya karatasi inayopepea ikija nyuma yake. Alipogeuka, kwa msaada wa taa za gari alizoziwasha wakati Lobo anasulubishwa, aliona viatu vya gharama alivyovaa Frank vikichapua katikati ya maji ya mvua iliyokata muda mchache uliopita. Maji hayo kila Frank alipotua mguu wake huku akikimbia, basi yaliruka kwa pembeni kuonesha kuwa zile mbio zilikuwa ni nzito. Sauti kama karatasi inayopepea, ilikuwa ni suti mwanana aliyotinga Man'Sai, ilikuwa inatoa sauti hiyo wakati anakimbia kwa hatua ndogondogo kumfuata Gunner aliyekaribu na gari la Lisa.
Gunner kugeuka tu! Anakutana na mzigo mzito wa ngumi ya paji la uso toka kwa Man'Sai, na wala hakupewa muda wa kujitetea au kuuliza kapigwa na nini, maana ngumi nyingine ni kama umegongwa na treni ya umeme. Ngwara au mtama mkali ulipigwa na Masai kwenda kwa Gunner. Jamaa akaruka kimo cha nyani mrukia miti na kutulia mgongo ambapo Frank naye aliruka mtupumtupu na kutuliza mgongo wake juu ya tumbo pa Gunner. Katili yule akawa hoi bin taabani ndani ya dakika mbili tu.
"Siwezi kukuua kwa sasa we' tasa. Nitamkabidhi Lisa roho yako alipe ulichomfanyia baba yake. Na mwambie Lobo, Roho yake nitampa Mubah. Mimi naishia hapa maana naona kama nakuonea tu." Masai aliongea wakati kanyanyuka na kumfuata Lisa pale alipokuwa kalala kwa maumivu ya kipigo cha Gunner.
"Tutakutana tena Masai. Karibu sana. Unamtihani mkubwa wa kununua roho za uwapendao au usiowapenda. Tutakutana tu!" Gunner aliongea hayo huku akienda garini kwake kainama na kushikilia tumbo kama mama mjamzito anayetaka kujifungua.
"Kuuza na kununua roho, ni mchezo wa kufuata sheria pekee. Mmeuziwa roho ya Lisa na Martina, mmeshindwa kuzinunua bali mimi ndiye nimezinunua. Sasa sijui kama mtaweza kununua zenu pale nitakapo wakabidhi roho hizo Lisa na Mubah." Frank naye alijibu huku akimkokota Lisa kumuingiza kwenye gari.
"Ni sheria tu ndizo zitakazofuatwa. Kama leo umefanikiwa, jipange zaidi." Gunner akamaliza na kuingia ndani ya gari lake na kuliwasha kisha akaondoka eneo lile akiwa na Lobo ambaye alikuwa taabani sababu ya kuendelea kuvuja damu.
Masai alipoona watu wale wameondoka, naye akapanda gari la Lisa na kisha akaliingiza barabarani tayari kwa kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
"Lisa. Twende hospitali kwanza." Masai alimwambia Lisa wakati anaendesha gari kutoka pale Kibaha.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Asante Frank. Ila sijajua kama mwanangu yupo salama kweli." Lisa aliongea kwa sauti ya chini.
"Yupo salama kwa Malocha. Usijali."
"Asante sana. Usitie shaka kuhusu hospitali, nitakuwa sawa ukinipeleka kwenye nyumba yangu ya Sinza." Lisa alimwambia Frank wakati huo ilikuwa yapata saa nane za usiku. Frank akabonyeza vitufe kadhaa kwenye kompyuta ya gari lile, kisha akamwambia Lisa ampe namba za nyumba yake. Alipompa, akaziingiza mahala husika na ramani ambayo itampeleka katika nyumba hiyo ikaonekana.
Lisa akawa anapitiwa na usingizi na Frank akawa anaendesha gari kuelekea Sinza. Macho ya Frank yakatua kwenye maungo ya Lisa aliyekuwa kasinzia. Sketi fupi aliyokuwa kaivaa, ikaonesha mapaja ya kuvutia ya Lisa. Blazia ya mtelezo aliyoivaa bila kitu ndani yake, ikiwa imelowana sababu ya mvua, ikaonesha matiti madogo yaliyojaa na kusimama na ambayo hayakunyonywa sana na Martina.
Frank akameza mate ya uchu wa ngono hasa alipokumbuka kwa mara ya kwanza alipomvua Lisa nguo zake. Ilikuwa ni kipindi wanasoma shule ya sekondari. Baada ya kupata chakula kwa pamoja kantini mida ya usiku, wakaamua kwenda darasani usiku huohuo kujisomea. Wakati wanajadili hili na lile kwenye masomo yao, mguu wa Lisa kwa bahati mbaya ukamkanyaga Frank. Lisa alijaribu kumuomba msamaha Frank lakini jamaa alikataa katukatu na kutaka na yeye alipize. Hatimaye Frank akalipiza kwa kumkanyaga Lisa.
Lisa aliumia moyoni lakini Frank yeye alijua kafanya utani tu. Hamu ya kuendelea kusoma, ikamtoka Lisa. Akamuomba Frank watoke darasani na warudi vyumbani mwao. Frank alikubali na kuinuka kitini kwake tayari kwa kuondoka bila kung'amua kuwa mwenzake kachukia.
Lisa akiponyanyuka na kuanza kutembea, akaonekana akiwa anachechemea kidogo. Hali hiyo ikampa mashaka Frank na kumuuliza kwa nini anachechemea wakati walipoingia darasani hakuwa hivyo. Ndipo Lisa akaanza kulia na kumjibu Frank kuwa kamuumiza baada ya kulipizia akivyomkanyaga.
Frank kwa haraka, akamrudisha kwenye kiti Lisa na kwa kuwa darasani mle kulikuwa hamna watu zaidi yao, na darasa lipo mbali na ofisi za walimu, Frank akamvua kiatu cha mguu aliomkanyaga Lisa. Hapo akaona wekundu uliotokana na kulipa kisasi chake. Moyo ukamuuma Frank na kujiona mkosaji. Akamtazama Lisa usoni na macho yao yakagongana lakini ya Lisa yakiwa yanatiririka machozi na ya Frank yakiwa na huruma.
"Samahani Lisa." Maneno yalimtoka Frank. Lisa akafuta machozi na kutulia asijue ajibu nini baada ya ile samahani ya mwanaume ampendaye kuliko chochote. "So sorry Lisa." Akasisitiza kauli yake Frank na kuinuka akipokuwa kachutama wakati anamvua kiatu Lisa. Akamshika mikononi na kumnyanyua mwanadada yule, naye akasimama. Frank akamkumbatia Lisa huku samahani na machozi ya uchungu yakimtiririka mwanaume yule.
"Nimekusamehe Masai. Nakupenda sana." Lisa alimwambia Frank kwa sauti yake laini na yeye akijifunga kwenye kumbate hilo kama Frank alivyofanya.
Sekunde kadhaa za kukumbatiana, wakaanza kuachiana na baada ya hapo, wakajikuta wanaangaliana usoni huku mikono ya Frank ikipita kiunoni kwa Lisa na mikono ya Lisa ikipita mabegani kwa Frank. Macho yao yakiwa yanatazamana, yakawa yanaongea lugha moja pekee, wataalamu tunaiitia lugha ya mapenzi.
Frank ndiye aliyekuwa wa kwanza kusogeza kichwa chake kwenda kwenye kichwa cha Lisa. Lisa akasogeza kidogo lakini kama akasita, na kumfanya Frank pia kusita. Lakini baadaye akasogeza zaidi na midomo yake kugusa midomo ya Lisa.
Lisa ni kama alikuwa akisubiri jambo fulani litokee ndio na yeye aingie. Frank alipoutoa ulimi wake na kujaribu kuuingiza kwenye kinywa cha Lisa kilichokuwa kimefumbwa, Lisa ndipo alipofungua kinywa chake na kuruhusu ulimi ule kupenya na kinywa chake kikaudaka na kuanza kuunyonya ulimi ule kwa chati.
Likawa tendo lenye raha sana hasa ukizingatia ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kupeana busu la namna ile. Frank akamsukumia Lisa katika ukuta mmojawapo wa darasa lile na kuzidi kunyonya ulimi wake.
Mikono yake haikuishia kiunoni pekee, safari hii akapeleka hadi kifuani na kuanza kutomasa matiti ya Lisa. Lisa naye hakuwa nyuma, akapitisha mikono yake kwenye shati la Frank na kuanza kupapasa kifua cha kijana yule na kufanya maruhani ya mapenzi kutapakaa kila sehemu ya miili ya wawili wale.
Frank akaenda mbali zaidi kwa kuitoa blazia wanayoiita kitopu, na Lisa akabaki kifua wazi. Frank akashambulia kifua kile kwa ulimi na kumfanya Lisa awe taabani na mwenye uhitaji wa tendo.
Frank akashusha suruali yake kidogo, kisha akashusha na nguo ya ndani ya Lisa bila kuondoa sketi yake ya shule. Akakamata mguu wa Lisa na kuubana vema kwa mkono wake. Akazidi kumsukumia ukutani ambapo Lisa naye aliruhusu maungo ya Frank kuingia mwilini mwake kwani alimkumbatia ipasavyo mwanaume yule wakati anajaribu kuingia zaidi.
Frank akatabasamu baada ya kukumbuka jambo lile na akili yake kujikuta ikicheka tu. Akawaza endapo angekamatwa siku ile na mwalimu wa nidhamu au mnoko yeyote. Akacheka na kuzidi kuingia Jijini kwa gari la Lisa.
****
Saa kumi kasoro, Frank akawa kasimamisha gari lake kwenye nyumba ambayo Lisa alisema ni yake. Akapitisha gari hilo getini lililokuwa linajifungua lenyewe unapoingiza namba zake kwenye kibonyezeo fulani kilichopo getini hapo. Frank alibonyeza namba hizo kwa sababu tayari Lisa alimwambia.
Alipoingiza gari, akafungua milango ya nyumba ambayo yote inafunguka kwa kadi maalumu inayotumika kama ufunguo. Frank akarudi kwenye gari na kumnyanyua Lisa asiyejitambua kwa sababu ya usingizi na maumivu ya kipigo. Akampeleka ndani na kumlaza kisha akaanza kumpa huduma ya kwanza bila kumuondoa nguo zake. Vifaa vya huduma hiyo vilikuwepo mlemle ndani hivyo hakuhangaika katika hilo. Baada ya kumaliza, naye akachukua barafu na kuweka katika sehemu ambazo aliona kaumia. Kisha akatoka kwenye chumba alicholala Lisa na kwenda sebuleni ambapo yeye alikamatiwa na usingizi hapohapo.
****
Saa nne, Frank alikuja kuamshwa na Lisa ambaye alikuwa anaonekana kama mpya kwa jinsi alivyokuwa mchangamfu.
"Wewe. Hujaacha tu kulala mdomo wazi." Lisa akamtania Frank baada ya kumuamsha.
"Acha zako wewe. We jana ulikuwa unakoroma kwenye gari."
"Kwenda huko. Lione kwanza." Lisa aliongea huku kachanua tabasamu. "Kaoge, maji yapo tayari bafuni." Lisa akamwambia Frank na kumpa mgongo kwa yeye kuelekea chumbani kwake. Huku nyuma Frank alibaki akitabasamu hasa kwa kuona umbo adimu la Lisa pamoja na uchangamfu wake.
Frank akanyanyuka na kuelekea bafuni ambalo lilikuwepo mlemle ndani. Akaoga na kutoka ambapo alielekezwa aende chumba kingine alichokuta vitu kadhaa vya kupaka mwili wake.
Akiwa na taulo pekee chumbani mle, akaingia Lisa huku kashika nguo fulani za kiume. Frank akazipokea na kumuangalia Lisa aliyekuwa naye kavaa taulo kubwa lililo kama gauni.
Frank akaweka nguo zile kitandani na alipogeuka, akamuona Lisa anaelekea mlangoni tayari kwa kutoka.
"Lisa." Frank aliita na Lisa akageuka na kumuangalia Frank ambaye alijongea karibu yake na kumshika mabega.
"I miss you. (Nimekukumbuka)" Frank akaongea maneno hayo na kusogeza.kichwa chake na midomo yake akaikutanisha na midomo ya Lisa. Akaibusu, lakini Lisa akataka zaidi ya pale, akaingiza ulimi wake kwenye kinywa cha Frank na Frank akaupokea kwa furaha. Ndimi zao zikawa zinatimiza kila kitu walichokipanga.
Punde, kila mmoja alikuwa kama alivyozaliwa na mataulo yao yakiwa chini huku kitanda kikilalamika kwa shughuli nzito ya mapenzi. Hakika walikuwa wanafaidi hawa watu.
****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Bado huu mzuri Lisa. Kamwe hupotezi uzuri wako. You still the same, my wife." Sauti ya Masai ilikuwa inamsifia Lisa aliyekuwa kalala kwenye kifua chake kwa deko.
"Asante. U bado handsome pia Man'Sai. Haubadiliki mambo yako ambayo kamwe hayajawahi kunitoka kichwani." Lisa aliongea kwa sauti ya mahaba huku akizidi kupapasa kifua kilichopasuka katikati sababu ya mazoezi ayafanyayo Frank.
"Asante Lisa. Tuamke sasa twende kwa Malocha maana kuna kazi nyingi za kufanya kule." Frank aliongea lakini Lisa alipandisha mabega juu na kuyashusha kuonesha kuwa hataki. "Acha bwana Lisa. Twende sasa hivi halafu si wajua tunatafutwa kama magaidi. Muda wowote wajinga wanaweza kuwa hapa." Frank alikazia mada yake lakini Lisa hakuelewa na badala yake akapanda juu ya kifua cha Frank na kuchukua ulimi wa Masai kwa kutumia kinywa chake na kuanza kuumumusa kwa raha na burudani.
Baada ya dakika kadhaa za kuchezeana hapa na pale, wakajikuta wapo katika dunia ya mapenzi tena. Kilichoendelea hapo, muamuzi alikuwa ni kitanda na mashuka yaliyokuwa yametandikwa juu yake.
****
Muda wa saa nane mchana, kundi la watu wanne walikuwa wamekaa sebuleni katika nyumba ya Kivule wakijadili hili na lile kuhusu Lisa. Hakuna aliyekuwa na uhakika kama Lisa kapona au hajapona. Simu waliyompa ilikuwa haipatikani na wala yeye mwenyewe hakuwataarifu kama amefika sehemu aliyohitajika.
Hawakuishia hapo pekee. Walikumbuka picha mbaya za usiku wa jana walipoenda kumchukua Martina. Walikuta maiti kadhaa zikiwa hazina uhai kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali kwenye mishipa yao mikuu iliyopita shingoni. Walipomuuliza
Martina ni nani aliyefanya yale, mtoto yule naye aliwauliza kufanya nini? Martina hakubahatika kuona maiti za wale watu kwa sababu wakati analetwa eneo lile, alikuwa kalala.
"Hatufahamu sasa. Sijui wamemuua au katoka mzima." Malocha aliongea kwa sauti ya chini huku kajiinamia.
"Watakuwa wametimiza adhma yao. Lobo huwa hana utani." Mubah aliongea naye kwa sauti ya kukata tamaa.
"Lakini kama wamemuua, wangetupa taarifa twende kumchukua. Yawezekana wamemteka au kimetokea kilichotokea kwa Martina." Malocha alichangia mada tena na kutulia. Wakakaa kimya kwa dakika tano kila mmoja akiwaza jambo lake. Wakiwa katika mawazo hayo, mara mlango wao uligongwa na jamaa mmoja alienda kuufungua.
"Lisaa!!" Jamaa yule alipiga kelele ya mshangao akiwa haamini kilichokuwa mlangoni kwake kwa wakati ule. Wengine waliobaki pale sebuleni, nao walinyanyuka na kusimama wima, macho yakiwa pima katika mlango ambao wanaingilia wageni wote.
Mara Lisa akaingia huku akiwa na tabasamu la bashasha katika uso wake. Wote waliokuwa pale wakasimama kama askari wa gwaride la jeshi wanamsikiliza mkuu wao. Hawakuamini kama kwa muda ule wanaweza kumuona Lisa aliyemzima wa afya na mwenye kila hali ya furaha.
Lisa akaingia lakini akawa kasimama mahala ambapo anaweza kumuona mtu wa nje kupitia ule mlango wa sebuleni. Kwa kidole cha shahada, akaita kwa kuonesha mkono kule mlangoni. Hapo Frank Masai akaingia akiwa kavaa suti maridadi ya kijivu na viatu vya damu ya mzee huku ndani ya suti hiyo akiwa kavalia shati la matirio ya kung'aa rangi nyekundu.
"You son of the bitch Man'Sai." Malocha alisikika akitukana huku akiwa kachanua tabasamu la haja usoni kwake. Akamfuata Masai na kumkumbatia kwa nguvu huku akicheka kwa furaha.
"Nimerudi sasa. Nimekuja kununua roho." Masai aliongea baada ya kuachiana na Malocha ambaye alikuwa haamini kama mtu aliyedhani hatotokea, atatokea.
"Karibu Jambazi langu. Nilikusubiri kwa muda mrefu sana. Hadi nikaamua kuingia kazini mwenyewe." Malocha alitamka hayo huku akimuangalia Frank usoni.
"Usijali. Subira yavuta heri." Naye akampa msemo wa Kihenga rafiki yake kipenzi Malocha.
"Jamani. Mlikuwa mkisikia nikiongea kuhusu Frank Masai au Man'Sai kila mara. Huyu ndiye yeye sasa." Malocha.alimtambulisha Masai mbele ya kikundi kazi chake cha watu watatu.
"Nilikuwa natamani sana kukuona. Hatimaye leo nimekutana na 'legend' wa nchi hii." Mubah aliongea hayo huku akimpa Masai mkono. "Naitwa Prince Mubarak au Mubah." Akajitambulisha Mubah.
"Nakufahamu Mubah. Pole sana kwa yaliyokukuta." Maneno hayo yalienda sambamba na mkono mwingine wa Masai kuogonga gonga begani Mubah.
Baada ya maneno machache na kutambuana, moja kwa moja hadithi mbalimbali zikapamba moto baina ya wale watu.
"Kwa hiyo mlipo mkamata Lobo, alisema anatumwa na nani na kwa nini?" Masai aliwauliza wale wapelelezi swali hilo.
"Aaagh. Boya tu yule. Hakujibu jibu sahihi bali kusema kuwa katumwa na uchafu kuja kusafisha pasafi kwa kuweka uchafu." Malocha alijibu kwa sauti ya kukereka.
"Kwa hiyo hilo jibu nyie hamkulifanyia kazi?" Masai akauliza tena na kuwafanya wale wana FISSA kengere ya kitu kugongwa vichwani mwao.
"Hapana. Hatukufanyia kazi chochote. Kwani kuna jambo hapo kati Man'Sai?" Malocha alijibu na kuuliza akiwa na shahuku ya kujua alichong'amua Masai.
"Ndio. Lipo jambo ambalo mlipaswa kulifanya. Kusafisha pasafi kwa kuweka uchafu. Kauli hii haiwagongi vichwani hata kidogo?" Wote wakanyanyua vichwa juu kama wenye kufikiria jambo lakini wasipate mawazo sahihi.
"Mmmh! Masai, haya mambo mengine yapaswa kuwa na watu kama wewe, wenye kutambua jambo mapema kwa mara moja pale walisikiapo tu." Ni sauti ya Lisa ilichombeza katika mjadala ule.
"Kweli kabisa Man'Sai. Lisa yupo sahihi." Malocha akashabikia huku akisogeza mgongo wake kwenda mbele kusikiliza maneno ya Masai atakayoyaongea.
"Kuna viongozi wangapi ambao John Lobo kawaua?" Masai akauliza huku akimuangalia Malocha usoni. Malocha akatulia na kufanya hesabu za watu ambao Lobo alifanikiwa kuwaua.
"Saba. Nakumbuka wakuu saba Lobo aliwamaliza. Akiwemo waziri wa Wanawake na watoto." Malocha akajibu.
"Baada ya kuwaua, ni wakina nani waliowekwa madarakani?" Masai akatupa swali lingine.
"Damn you Man'Sai. You're crazy son of the bitch."Malocha akarudisha mgongo wake kwenye kochi huku kachanua tabasamu baada ya kupata maana ya maneno ya John Lobo.
"Nadhani umekwishanielewa nachomaanisha na alichojaribu kuwaambia Lobo." Masai akaingia kwenye vichwa vya wale watu.
"Kusafisha pasafi kwa kuweka uchafu. Yaani kuondoa watu wasafi sehemu fulani kwa kuwaweka wachafu. Kwa hiyo njia aliyokuwa anaitumia ni kwa kuua au kuwalazimisha waachie madaraka." Malocha aliongea peke yake na kuwafungua hata wale ambao hawakuelewa. "Upo sahihi Man' Sai. Natazama watu waliowekwa hizo nafasi, ni wazi hawana usafi bali uchafu tu. Tazama baada ya kifo cha Kamanda wa Polisi kanda ya kati, limewekwa lile pumbavu, mikoa imezidi kuongezeka maovu." Malocha alizidi kutiririka anachokijua.
"Upo sahihi kabisa Man'Sai. Hata uongozi uliowekwa FISSA baada ya sisi kuondolewa, ni wa ajabu." Mubah akachangia.
"Nadhani sasa tumekwishajua nini kipo katikati ya haya mambo kwa kutumia kauli ya Lobo. Sasa kama tumejua, tuangalie chanzo chake. Nani anayewateua hawa?" Masai akauliza tena.
"Ni Rais yule kidomo domo." Mubah akadakia hata bila kujiuliza mara kadhaa.
"Ni kweli, Rais wa nchi anahusika sana na haya mambo, lakini na yeye roho yake ipo dukani na ndio maana anafanya haya yote." Malocha akajibu na kuwashangaza wote waliokuwepo katika mjadala ule kasoro Masai.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nani yupo katikati ya haya mambo sasa?" Masai akamuuliza Malocha.
"Chris Shadow au The Shadow ndiye kila kitu." Jibu hilo likamnyong'onyeza kabisa Frank Masai. Hakutegemea kabisa jibu lile kwa wakati ule.
"Kwa hiyo wote wanafanya kazi chini ya The Shadow. Nitamtafuta huyu mbwa kwa gharama yoyote ile, na nitamuua." Frank alijikuta akijiapiza.
"The Shadow ndiye nani jamani." Mubah aliomba kutolewa gizani kuhusu mtu aitwaye The Shadow.
"Alipojiita The Shadow, hakukosea hata kidogo. Jamaa ni kama kivuli. Hutembea kutokana na kubadilika kwa majira. Hukufuata popote uendapo kama akiamua kufanya hivyo. Na mbaya zaidi, hata wafanyakazi wake hawajawahi kumuona. Hao wakina Gunner, wanasikiaga sauti ya mgurumo tu wakati wanaambiwa waongee na bosi wao. Huyo ndiye aliyewaunda wale watoto wa mauaji miaka ishirini iliyopita, wale watoto waliojiita Panya Roads, na mimi nilikuwepo. Aliua wazazi wangu wote kabla ya kuniunganisha kwenye lile kundi la wachafu. Na ndiye aliyepachika viongozi kwenye kila nchi akiwatumia viongozi hao kunyonya wananchi. Namsaka kwa mwaka wa saba sasa. Kwenye ile ishu ya Jina, alihusika kwa asilimia tisini. Kwenye ukurasa wa hamsini, jina lake lilikuwa la mwisho, lakini nilimkosa. Ni mtu hatari, usiombe aweke mkono wake kwenye ukifanyacho, utajuta." Masai akamaliza kumuelezea The Shadow kwa kifupi.
Sura za wapelelezi zilikuwa kimya zikichambua neno hadi neno kutoka kinywani mwa Masai. Kimya kikatanda huku sura ya kila mmoja aliyekuwamo mle ndani zikitafakari jambo lake.
"Mamaa." Sauti ya Martina ilisikika na kila mmoja aligeuka kumtazama. Alikuwa katoka katika usingizi mzito wakati anamuita mama yake.
Akaanza kusogea taratibu kwenda kwa mama yake huku akifikicha macho yake. Lakini alipomuona Masai, akasita kidogo na kurudi nyuma kwa uoga.
"Martina. Njoo umsalimu baba eeh." Lisa liongea huku akiinuka pale kochini alipokuwa amekaa na Frank.
"Huyo ni adui. Baba aliniambia." Martina aliongea hayo huku akizidi kurudi nyuma kwa uoga.
"Hapana Martina. Huyu ndiye baba yako, siyo adui." Lisa alijaribu kumuelekeza mwanaye ambaye hakusikia ushauri huo na badala yake alikimbilia chumbani alipotoka huku mama yake akimfuata kwa nyuma.
"Unakazi hapo baba mtu. Na sura lako la kijambazi hilo. Hahahaaa, mtoto lazima azogoe." Malocha alimtania Frank ambaye macho yake yalikuwa kule walipokimbilia familia yake.
"Nakwambia. Hapo ni tatizo. Noma na soo kilo kumi. Sijui kama ataelewa." Frank aliongea huku akitabasamu kana kwamba hajashtuka sana kwa kilichotokea. Lakini kiundani, alikuwa kaumia sana hasa alipogundua mtoto wake anafundishwa ugaidi.
"Na wewe umezidi. Hata kuja kumtembelea shem ukawa unaona tatizo. Kujificha gani huko. Acha mtoto akuoneshe." Malocha alizidi kumkandamiza Masai.
"Aaaagh. Sasa unadhani nisipojificha nitaishije. Mi ni kama embe, naonekana msimu hadi msimu. Kama hapa ni msimu wa kazi, na mimi ndio naibuka toka chimbo na 'full materials'." Wale jamaa ambao walikuwa hawamjui Frank Masai, walikuwa ni wa kutabasamu tu wakati wawili wale wakitaniana.
Hakuna aliyeamini na atakayeamini pale atakapokutana na Masai na kuambiwa huyu ndiye yeye. Kijana mtukutu na mjanja mdomoni. Anajua lugha zipatazo tano, tena zote zinatumika Kimataifa. Lakini ni kama muhuni wa jijini asiye na faida yoyote.
"Hahahaaa. Kwa hiyo sasa hivi ni msimu wa maembe." Malocha akauliza na kuzidi kucheka.
"Haaa! Huyu kiongozi wenu vipi? Hajui maembe yapo sokoni sasa hivi yanauza roho zao. Hapa nimepewa hela na Lisa, naenda kununua roho ya embe liitwalo Gunner. Na wewe Mubah, nipe changu mapema nikununulie embe Lobo." Masai akaongea na kuwaacha wale jamaa kutabasamu wasijue cha kujibu. "Huyu jambazi, nilimnunulia roho ya Lobo, lakini upimbi wake akamkwangua na kisu, matokeo yake, leo anapasua watu vichwa hadimu kama hivi." Wakazidi kutaniana wale watu hadi Lisa aliporudi.
"Kakataa katakata kuja kukusalimia." Lisa akamwambia Masai.
"Hamna tatizo, punde atanielewa tu." Frank hakutaka kumkatisha tamaa Lisa wala nafsi yake.
"Okay. Hamna tatizo. Naona kalala tena." Lisa aliongeza maneno.
"Okay. Nasikia kesho Rais wa Urusi anakuja. Mnajua mikakati ya hawa jamaa?" Frank aliwauliza wale wapelelezi.
"Aagh. Sisi hatuhusiki tena. Kazi ya FISSA hiyo." Malocha akajibu kwa kukereka.
"Hapana Malocha. Wajua kuwa wamechukua ndege ya P.112 toka kwako? Halafu pia wanamtambo wa kuzima satellites zote uzijuazo. Mtambo huo waliuiba China. Na mimi nilishiriki kuutengeneza na ni mimi pekee ndiye mwenye kifaa cha kuufatilia. Hata mawasiliano yenu niliyanasa kupitia kifaa changu hicho.
Namba zako walizipata kwa kutumia huo mtambo. Wajua nia yao?" Masai akaacha swali likielea angani na hakuna aliyelijibu. "Basi ipo hivi, ndege waliyoichukua, kumbuka ni mali ya Marekani na Urusi hawajui kuwa Tanzania kapewa ndege hiyo. Kitakachofanyika hiyo kesho wakati Rais wa Urusi anakuja, ni kushambulia ndege yake kwa kutumia Jet P.112 na hali hiyo itafanya Urusi kuamini kuwa Wamarekani wamewaulia Rais wao. Unajua Urus anashirikiana na nani?" Swali lingine likabaki linaelea hewani na Frank hakutaka kuwakosesha majibu. "China, Cuba, Korea Kaskazini na Japan ambao hawa Wajapan, pia wapo pamoja na Ujerumani, Italia na Bulgaria.
Hawa Wamarekani, mabest wao ni Ufaransa, Uingereza, Hispania, America yote ile, Poland na nchi nyingi za 'Capitalism'. Sasa nini kitakachotokea baada ya mauaji ya Rais wa Urusi?" Masai akauliza tena.
"World War Three ( Vita ya Tatu ya Dunia)" Mubah akajibu swali hilo.
"Exactly Mubah (Upo sawa Mubah). Dunia itaingia vitani na wakati sisi weusi tukibebwa na kupelekwa kupigana vita vyao. Ndicho mkitakacho?" Wote wakatikisa vichwa vyao kushoto kulia kuonesha kuwa hawataki. " Sasa The Shadow, anataka iwe hivyo. Ili kumdhibiti isitokee, yapasa kuzuia huu ujinga. Tukizuia hii, roho ya Lobo na mwenzake, ni yetu." Masai akamaliza huku akiwapa hamasa wenzake walioukubali ukweli kwa kila neno.
"Sasa tunafanyaje kuwazuia hawa washenzi?" Malocha akauliza swali ambalo Frank alilipokea kwa tabasamu pana.
"So easy my friend. Nimekuja kusimamisha kila ujinga hapa. Niachieni mimi haya mambo. Mtaona wenyewe mabadiliko. Lakini wakati mimi najiandaa kuzima ujinga wa hawa watu, nyie nendeni mkamchukue yule mkuu wa polisi kanda ya kati, atatusaidia sana." Masai akatoa maelekezo mengine ambayo yaliitikiwa kwa ari ya hali ya juu. " Na huyu Rais wenu anapelekwapelekwa tu, kesho naye anauawa ili kisingizio kiwe kikubwa. Sasa hapo ndipo patakuwa pabaya. Tunatakiwa kufahamu sisi ni wakina nani? Nchi yetu inamarafiki wangapi? Hawa wanaotengenezwa kuwa maadui, wote tuna urafiki nao. Sasa nini kitatokea baada ya kundi la Gunner kufanya upuuzi wake? Jibu nawaachia vichwani mwenu. Mubah na jamaa hapo, kamleteni Kamanda Kondo, yupo Dar hapahapa kwa ajili ya shughuli ya kesho. Mimi naelekea mahala kuchukua vifaa vyangu, baada ya saa moja, nitakuwepo hapa. Naomba na nyie muwepo." Frank akamaliza kikao kile na kila mmoja akaenda kwenye majukumu yake.
****
IJUMAA SAA SABA MCHANA.
Wakati Masai na Lisa wakiitaabisha miili yao kabla hawajaenda kwa Malocha, kundi zima linaloongozwa na Gunner Samuel Bokwa lilikuwa linajadili mambo yatakayofanyika kesho yake, yaani katika ujio wa Rais wa Urusi. Waliona wazi kuwa vita vya tatu vya dunia vilikuwa vimewadia, ama la! Basi lazima kutatokea vita kubwa baina ya mataifa yale makubwa duniani.
"Kesho ndiyo kesho jamani. Kama ni siku ya kuzaliwa, basi ni krisimasi, Yesu anazaliwa. Lakini si Krisimasi bali 'Armageddon' ." Gunner aliongea huku akienda huko na huku kwa tambo na mbwembwe akijaribu kufananisha siku ya kesho na siku kuzaliwa Yesu au mwisho wa dunia. (Armageddon)CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kweli boss. Na tayari dereva maalumu wa kuendesha Jet P.112 amekwishapatikana. Hiyo ni fursa pekee ya sisi kuitawala dunia. Vita wapigane wao, sisi tuwe watu wa kuuza silaha tu! Mwisho wa siku vita vikiisha, tunachukua uongozi wa kidunia kwa ubabe." Yule Mrusi mmoja anayeendesha mitambo ya mle ndani aliongea kuunga mkono kauli ya mkuu wake, Gunner.
"Upo sahihi Boyka. Na kwa ushindi huo, hata The Shadow atatutunuku nishani ya pekee." Gunner alizidi kutamba.
"Lakini mkuu." Sauti nzito iliita. Gunner akamuangalia yule aliyemuita. Alikuwa kabandikwa bandeji puani na kwenye paji lake la uso. Alikuwa ni John Lobo.
"Sema Lobo." Gunner akampa nafasi ya kuongea mshirika wake.
"Kuna mtu katika maongezi haya tunamsahau wakati tunafikiria kusheherekea." Akameza mate kidogo kisha akasongesha maongezi yake. " Frank Masai. Atakuwa tatizo kubwa sana katika mpango wetu. Unamjua yule alivyoking'ang'anizi." Akatulia kusikia upande wa pili utajibu nini.
"Masai ni kama sisimizi ambaye hana miguu. Hana teknolojia ya kutuzuia sisi hata kidogo. Yule ni kama samaki ndani ya maji ya moto, humo haogelei bali kupikwa." Gunner akatamba kwa maneno bila kujua ni nini akizungumziacho.
"Gunner. Masai si hivyo umdhaniavyo. Yule ni kikwazo kuliko kikwazo chenyewe. Embu fikiria ni vipi kajua kuwa tupo Kibaha na Lisa? Fikiria katumia muda gani kuwauwa wale walinzi tuliowapa Martina halafu katokea tena Kibaha. Unadhani ni mtu wa aina gani yule?" Lobo akaonesha wasiwasi wake wazi kabisa.
"Hahahaa. Lobo my friend. Hilo lisikuumize kichwa hata chembe. Yule ni sisimizi, as I told you. Don't worry man, hana madhara yule." Gunner akajihakikishia kuwa yupo salama bila kujua upande wa shilingi wa sisimizi huyo ambaye hana miguu. Yawezekana ndiye mfalme wa sisimizi wote duniani, hakujua hilo.
"Tatizo lako Gunner hujui na hutaki kuumiza kichwa chako kujua. Sasa mimi nakufungua kichwa chako. Subiri hapo." Lobo akanyanyuka na kuwaacha wenzake pale katika chumba cha mkutano na kwenda chumba fulani ambapo alitoka na bahasha fulani kuu kuu. " Angalia kilichomo humo." Lobo akamkabidhi Gunner bahasha ile.
"Hizi ni picha za wale waliotengeneza mtambo wa SGT." Gunner akaongea baada ya kutoa kilichomo ndani ya bahasha.
"Hujang'amua chochote kwenye hiyo picha?" Lobo akatupa swali kwa kiongozi wake.
"Nachojua hawa jamaa walikuwa ni hatari katika sayansi hasa kwenye mitambo itumiayo kompyuta, lakini wote tuliwaua." Gunner akajibu alichokijua kwenye ile picha.
"Hahahahaaaa. Ndio maana nilikwambia hutaki kushughulisha akili yako kufikiria. Embu muangalie huyo Muafrika aliyevaa miwani ya macho." Gunner akasogeza ile picha karibu zaidi na macho yake. Akaona haitoshi, akaanza kuangalia picha hadi picha kwa sababu ya yule Muafrika.
"Shit. Ina maana Masai alikuwa mmoja wa hawa wanasayansi? Halafu hawakumuua wale wajinga licha ya kuwalipa mabilioni ya dollars." Macho ya Gunner ni wazi yalikumbwa na mshtuko baada ya kujua ni nini Lobo anajaribu kumuelekeza.
"Na japo walishindwa kumuua, huyo jamaa pia The Shadow alimuhitaji akiwa hai ili awe mfanyakazi wake. Huyo ndiye alikuwa tegemeo la Wanasayansi wote katika kile chuo ambacho ndicho chuo bora duniani kwa Sayansi. Sasa vuta picha hapa unapambana na nani." Lobo akamtazama usoni Gunner kabla hajaendelea. " Anajua Sayansi kuliko sisi, mjanja kuliko sisi. Kajificha miaka mitano bila kuonekana nchini kwake. Anapiga mkono kuliko sisi na mbaya zaidi, anawashirika makini kuliko sisi, kuna kichwa Gunner." Lobo akamaliza kwa tabasamu pana kutokana na maelezo yake.
"Hizo dharau sasa Lobo. Yule ni mbwa tu. Hana sifa uzitajazo." Gunner akawa kapandisha hasira kwa maneno kuntu ya Lobo.
"Huo ndio ukweli Gunner. Man'Sai ni mbwa haswa, tena mbwa wa mtaa. Anajua shida za mtaa wake na anajua njia zote za mtaani. We can't stop him by ourselves." Lobo akazidi kuropoka lakini maneno yake, yakachukuliwa tofauti na Gunner.
"Wewe ni muoga Lobo. Wewe ni kunguru mla sabuni ambaye muosha vyombo akija, huchapa mbawa zake kwa uoga wa kumwagiwa ukoko." Gunner aliongea shombo ambazo ziliwafanya wale washirika wengine waanze kucheka.
"Tatizo lako Gunner ni kichwa kokoto. Mgumu kuelewa nachomaanisha. Hapa mimi namaanisha, tuombe msaada zaidi kuhusu hili. Peke yetu hatuwezi nakwambia. Hatujui ni nini anacho Masai na hatujui atatumiaje alichonacho. Hivi kwa akili yako, unadhani nani anajua kuwa tuna mtambo wa SGT zaidi ya sisi wenyewe?" Lobo akauliza na kuwaangalia wenzake, alipoona hamna jibu, akatupa jiwe la msingi kwenye uelewesho wake. "Masai anajua kuwa tuna mtambo wa SGT. Kajuaje? Hilo nalo bado unataka kuelekezwa kuwa ni la hatari katika mpango wetu? Don't be stupid. Na nyie wote mnaochekacheka kama Malaya kaona pochi ya mwanaume inafunguliwa, acheni ujinga." Hasira tayari zilikuwa zimempanda Lobo.
"Okay Lobo. Nini unachoshauri sasa. Tugandishe mpango wetu? Huo ni ujinga kuliko ujinga wenyewe. Au tuongeze jeshi? Huo pia ni ujinga zaidi hata ya kusitisha mpango wetu. Tumeteketeza nusu ng'ombe, sembuse haka kamkia Masai?" Hali ya kujiamini ilikuwa katika mwili wa Gunner na kufanya asisikie la mtu wa.karibu katika kazi zake.
"Okay. Kwa kuwa wewe ndiye kiongozi kipofu unayeongoza baadhi ya vipofu, hamna tatizo kuhusu ulichoamua. Ila kwa kukupa taarifa tu! Kama mpango utabumba, basi ujue mkono wa The Shadow utatuchezea sana. Hatutosalimika hata kwa ukubwa wa punje moja ya mchanga. Katupa kila kitu tulichokihitaji tena kwa gharama kubwa, sasa ngoja mpango uende kinyume, na kauli zako chafu za kibishi, zitakutokea puani." Lobo akasimama na kukusanya picha zake na kuanza kuondoka mle ndani. Licha ya Gunner kuwa kiongozi mkuu wa mapambano yale, lakini anapofika kwa Lobo, huwa kama wanalingana na anashindwa kuonesha cheche zake za uongozi.
"A coward (Muoga)" Gunner alitamka hayo wakati Lobo anaelekea kwenye mlango wa kutokea mle ndani.
"We'll see what's next. (Tutaona kitakachofuata)"Lobo akatoka nje ya chumba kile baada ya maneno hayo.
"Mpango utakamilika tu. Msijali wandugu, maadam tuna kila kitu cha muhimu, hakuna kitakachotusimamisha." Gunner akawatoa hofu washirika waliobaki kabla na yeye hajatoka katika chumba kile.
****
Saa kumi na dakika kadhaa, kundi lililotumwa kwenda kumkamata Kamanda Kondo lilikuwa limerudi na Masai naye alikuwa katika chumba maalumu kwa ajili ya mahojiano ya mtu yule ambaye alipewa ukuu wa polisi kanda ya kati baada ya kifo cha kutatanisha cha Mzee Ismail Ambazeki ambaye alikuwa anaendeshwa kwenda na kurudi na askari mwenye cheo kidogo wa kipindi hicho, Bwana Prince Mubarak.
"Kwa nini ulimuua Mzee Ismail?" Sauti ya Mubah ilimuuliza Kondo.
"Hapana. Mimi mbona sijamuua? Mimi niponipo tu, wala sikumuua." Kamanda yule alijibu huku akitetemeka kama si polisi mkuu tena wa mikoa kama mitatu ya kati.
"Kwa hiyo nani alimuua." Mubah akamuuliza huku akiweka mikono yake miwili kwenye magoti ya yule mzee ambaye alizidi kuchanganyikiwa licha ya Mubah kuwa katika hali ya kawaida.
"Mimi niliwekwa na Rais. Lakini kuna mtu huwa naongea naye simjui anasema nikileta ujinga na mimi nitakufa kama Mzee Ismail. Hivyo kama kuna jambo la maovu linataka kufanyika kanda ya kati, wananipa taarifa nisilifatilie." Huku akitetemeka, yule mzee akawa anaropoka kila anachokijua hadi wakina Mubah wakalidhika.
"Sasa sisi tunakuachia, nenda kaendelee na majukumu yako ila fumba domo lako na kamwe usije ukasema kuwa umekutana na sisi. Kesho wanataka kumuua Rais wa Urusi, ni sisi pekee wa kuzuia jambo hili, lakini na wewe tunaomba uwe makini sana. Macho yako yawe yanatembea huku na huko kama nyuki yatima." Mubah aliongea maneno ambayo yaliitikiwa kwa kichwa na Mzee yule.
Akatolewa katika chumba kile na kupelekwa sebuleni kisha akavishwa mzula mweusi na kutolewa katika nyumba ile tayari kwa kupelekwa katika hoteli aliyofikia.
"Upo vizuri kijana. Nimependa sana unavyofanya kazi zako. Hongera." Frank akamsifia Mubah.
"Kawaida kaka. Kazi ya Lisa hii, ndiye ticha wangu." Mubah aliongea na wote wakacheka kwa maneno hayo. Wakati huo, mtoto Martina alikuwa anacheza uwani na jamaa ambaye alizoeana naye.
*****
JUMAMOSI, SIKU YA RAIS WA URUSI KUJA.
Gunner na kundi lake waliiita siku hii ni mwisho wa dunia. Lakini kundi la Malocha waliita siku hii ya ukombozi wa dunia. Sayansi na akili nyingi ndivyo ambavyo vilikuwa vinatawala siku hii ya aina yake. Mitambo kama SGT na ndege aina ya Jet P.112, ndivyo hasa viliwapa vichwa mtuno Gunner na wenzake.
Wakati huo Masai naye alikuwa anacheza na akili zao. Alishajua kila kitu kuhusu mpango wao. Alichofanya yeye ni kuunga mitambo kadhaa kwenye chumba cha mitambo ya Malocha.
Hakuna aliyejua anachokifanya Masai hadi pale waliposhuhudia kwenye skrini zao wanaiona Dar es Salaam nzima bila kokoro wala papara. Hapo ndipo walipoamini kuwa mtu waliyenaye siyo 'size' yao hata kidogo.
"Hapa ndipo kambi ya Gunner na wenzake ilipo." Masai alionesha kwa kidole sehemu ambayo alitaka wenzake waone.
"Ukifanya hivi, utaona kila kitu." Akavuta lile eneo na mara pakaoneka vizuri kabisa na kila kitu kinachoendelea eneo lile kilionekana safi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mmmh! Kaka upo vizuri. Hapo tunafatilia kila kitu bila tatizo." Mubah alimpongeza Masai.
"Hichi nilichoweka humu, hata satellites zote zikizimwa na mtambo wao, sisi tutaendelea kuona mambo yote. Cha msingi ni sisi kuwa macho zaidi ya kila kitu. Picha ya kile tendo inakuja baada ya dakika moja. Na ndege yenu ipo mlee." Akaonesha tena kwa kidole Masai..
"Mmmmh! Aisee hawa jamaa ni hatari sana. Sasa wameichimbia au?" Mubah akauliza na wakati huo wenzake wote walikuwa kimya wakisubiri muda ufike wa kuanza kazi.
"Pale pana kitu kama handaki. Pakifunguka ujue ndio muda wa dege lile kutoka. Tupaangalie sana pale." Akaongeza jambo la muhimu Masai.
"Sasa mbona kuna miti? Wamewezaje kuchimba na wakati kuna miti mikubwa kama ile." Mubah aliuliza kwa mshangao.
"Mzungu anaakili ndogo sana ya kuteka hata akili ya kuku. Hapo ndipo katuzidi huyu mtu." Frank aliongea bila kujibu swali la Mubah. "Kwa hiyo tunawasimamishia tukiwa hapahapa?" Lisa akauliza.
"Hapana. Nyie mtaenda na hivi hapa vidude. Mi' nitabaki na huyu fundi hapa, rafiki wa Martina. Tutawasiliana na mtapata matokeo yote ya kinachoendelea. Mtaona tu wenyewe." Masai akamaliza maelezo mafupi aliyoyatoa na kila mmoja alikubaliana na mpango ule.
****
Wakati huku wengine wakipanga kuukaribisha mwisho wa dunia na wengine kuikomboa, kuna wale wananchi ambao walikuwa hawana A wala E. Hawa ndio wale waliokuwa wamejipanga kandokando ya barabara ambazo zilikuwa safi siku ile kuliko siku zote za maisha yao. Zilipigwa maji na kung'aa kama zimesafishwa kwa mafuta ya kupikia. Walishangilia na kutandika khanga zao kama vile sikukuu ya matawi, hakika walikuwa katika furaha.
Mbali na hao wa kujipanga barabarani, kule uwanja wa ndege kulikuwa na vikundi mbalimbali vya jadi. Waliimba na kucheza ngoma za jadi. Wakaonesha uwezo wao wa kuvaa mavazi ya asili na mbwembwe mbalimbali za kijadi, yote ilimradi kuionesha dunia kuwa Tanzania bado inadumisha mila na wakati teknolojia imevamia mila hizo na sasa utandawazi ndio neno linalochukua nafasi kubwa kuliko jadi.
Vifijo na nderemo viliendelea kuchukua nafasi yake na kila aliyebahatika kuona hali ile, hakusita kutabasamu kwa kutoa meno yake yote nje. Hakuna aliyejua kuwa mwisho wa dunia unaanzia pale. Hakuna aliyejua na kamwe wasingeweza kujua hilo.
Ndani ya ndege ya Rais wa Urusi, kulikuwa kuna marubani kadha wa kadha wakiingoza ndege ile kwa utaratibu na kwa heshima kubwa bila kuwa na papara kwa sababu wamembeba mtu mkubwa labda kushinda hata Rais wa Marekani, Warusi wote wanaamini hilo.
Rais wa Urusi, Bwana Ragio Pendrovic alikuwa akiangalia huku na huko wakati akipewa makaratasi kadhaa ya kupitia ambayo yangehusika katika kutoa hotuba afikapo nchini Tanzania. Hakuwa na wasiwasi hasa pale alipowaza kichwani mwake kuwa ndege yake inaulinzi wa kipekee ambao hakuna kitakachotokea kama ikivamiwa. Na wakati huohuo, moyo wake uliiamini Tanzania kama nchi ya amani hivyo hamna ambacho kitamdhulu pindi atakapokanyaga ardhi yenye utajiri kuliko ardhi yoyote Afrika lakini wananchi wake ni masikini labda kuliko nchi yoyote ukanda wa Afrika Kusini.
Hiyo ni kwa sababu viongozi wa nchi hiyo wanajali zaidi kujaza matumbo yao yasiyotosheka hata kwa sinia zima la pilau.
Viongozi hawa naweza kuwafananisha na fisi ambaye hata kama kashiba, bado atafatilia hata kile kidogo ambacho kimebebwa na kunguru mroho. Wapo tayari kuchukua chochote ambacho masikini kajitafutia au kajivumbulia na kukifanya kuwa chao.
Kamwe hawataifanya nchi hiyo kuwa na matajiri kama watajali matumbo yao yajae na wakati huo wanayaminya ya wengine chakula wakilacho, na wanaenda mbali zaidi kwa kuyatapisha chakula hicho wanachojitafutia.
Naweza sema ni upuuzi kwa mtu kusema nchi hiyo ni ya demokrasia. Demokrasia ipo wapi?
Au labda sisi wananchi akili zetu zimeingiliwa na mafuta ya taa. Ila tukirudi nyuma miaka ya 1861 hadi 1865, kuna Rais mmoja wa Marekani anaitwa Abraham Lincoln, alikuwa ni Rais wa Kumi na Sita na ndiye aliyepigana zaidi kuondoa ubaguzi wa rangi Marekani. Yeye alisema kuwa "Democracy is a government "of the people, by the people, and for the people." (Demokrasia ni serikali ya watu, kwa watu na kwa ajili ya watu). Je, serikali yetu ipo hivyo, au ndio tunakunwa vichwa na wakati hata sisi tuna kucha? Ukisema sana wanakuzima, je hiyo ni demokrasia? Mimi sijui na sitaki kuongelea sana huko.
****
Wakati tendo la kumpokea Rais wa Urusi likizidi kuchukua nafasi yake katika ardhi ya Demokrasia ya Tanzania, Gunner Bokwa alikuwa anafatilia kila kitu kwa makini kwenye kamera kadhaa ambazo waliweza kuona eneo zima atakalopita Rais na mazingira yake.
"Pale ndipo tulipoweka bomu la masaa, na kule nyuma yapo mawili. Na pale ndipo Jet P.112 itakapoharibu mambo yote. Na wakati huo, sisi tutakuwa hapo kwenye huo mnara tunashuhudia tukio zima. Itakuwa sherehe leo." Gunner aliongea huku akiwaonesha wenzake kazi nzima waliyoifanya.
"Kwa hiyo hayo mabomu ya masaa yanalinalipuka saa ngapi?" Lobo akamuuliza Gunner.
"Ni dakika tano. Hapa nikibonyeza hii saa, mabomu yanaanza kijihesabu. Nataka huyo rais kabla hajatoka nje ya uwanja, kuwe tayari kuna mlipuko huko nje." Gunner alizidi kutabainisha alochokipanga.
"Okay. Sasa tungeenda maana kuna masaa mawili ili Rais afike. Tungeenda hilo eneo tulilolipanga." Lobo alitoa ushauri na Gunner akaanza kuwapa majukumu ya kufanya watu wake hasa yule mtaalamu wa TEHAMA.
"Nitakupigia simu baada ya kuona mambo yapo sawa. Hapo ndipo utawasha SGT ili kuwazingua wale wanaotufatilia. Baada ya hapo, ni tifu tu!" Gunner akampa muongozo yule bwana kwa jina la Boyka. Akakubali kila mpango na muda huohuo, Gunner akaenda kwenye Jet P.112 na kuwakuta madereva watatu wakijaribu hili na lile.
"Baada ya mlipuko, kazi itakuwa kwenu. Ni kuteketeza kila kitu hadi ndege yao wanayojidai nayo. Hamna kuacha na wakati huo sisi tutakuwa tunachukua video zetu za kuchonganisha." Muongozo ukazidi kitolewa toka kwenye kinywa cha Gunner.
"Usijali bosi." Wale jamaa wakajibu kwa lugha sijui ya wapi.
Gunner akatoka ndani ya ndege na kwenda lilipo gari lake ambapo alipanda na John Lobo na kijana mwingine machachari kwa muonekano tu.
****
"Bosi." Mtaalamu wa TEHAMA upande wa akina Malocha aliita. "Naona gari hili hapa la wakina Gunner linaondoka pale kwao." Akatoa taarifa mbele ya Malocha na Masai.
"Vema. Sasa Malocha, Lisa na Ndita rafiki wa Martina, mtaenda sehemu ambayo nitawaelekeza." Masai akagawa majukumu na hakuna aliyepinga hilo.
Kama walivyochaguliwa, wakatoka nje ya nyumba ile na kwenda kukwea gari lao ambalo nalo liliwashwa na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.
NUSU SAA KABLA YA RAIS WA URUSI HAJAFIKA.
Mioyo ya wengi ilikuwa inapwita kwa kihoro hasa kutokana na ujio ule wa Rais mkubwa katika dunia hii. Kila moyo ulidunda kwa njia yake. Lakini kuna mioyo ya makundi mawili, yenyewe ilikuwa inadunda kimapinduzi pekee.
"Naona kama muda hauendi kabisa." Gunner aliongea na Lobo akatabasamu na kutikisa kichwa chake kama kusikitika. Wote walikuwamo ndani ya gari lao aina ya VX8. Gunner akashusha punzi ndefu na kisha katwaa simu yake maalumu kwa ajili ya kuwasiliana na wataalamu wake kule nyumbani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Boyka. Anza kufungua mtambo wa SGT na waambie wale wa ndege nao wafanye yao kabisa. Waanze kuipasha moto hiyo ndege, muda wa mapinduzi umewadia." Gunner akatoa taarifa na kukata simu yake hiyo. "Lobo. Tunamaliza mchezo leo hii." Kwa furaha ya hali ya juu alimgeukia rafiki yake na kumshika mkono wa heri.
Kwa upande wa akina Malocha na Lisa, bado walikuwa wanafuata maelekezo ya Masai na gari lao lilikuwa limeegeshwa mbali kabisa na eneo la uwanja wa ndege. Waliwaona wapelelezi mbalimbali wakiwepo wale wa FISSA na binafsi. Wote walikuwa wanavifaa maalumu ambavyo waliweza kuwasiliana na kundi zima ambalo lilikuwa linalanda huku na huko katika kudumisha usalama wa eneo lile.
Zikiwa zimebaki dakika kumi, gari zipatazo kumi na mbili zote zikiwa zinafanana kwa rangi zake nyeusi, na aina ya Mercedes Benz zilifika pale uwanjani kwa msururu mrefu ambao uliwafanya wananchi kusogezwa pembeni na wengine kuamriwa waache kupita pale.
Naam baada ya vuguvugu hilo kutulia, Rais wa Nchi ya Tanzania alishuka toka katika gari ya pili akiwa na mkewe aliyevalia mavazi ya kitenge. Gari ya nyuma yake, alitoka waziri mkuu na mkewe pia aliyevaa vazi la badhee, vazi maarufu sana nchini Nigeria. Wanaume hawa wakubwa wa nchi, waliyaweka makoti yao ya suti nyeusi vema kabla hawajaanza kupiga hatua kwa hatua kuingia uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.
Wakaingia uwanjani na moja kwa moja wakaenda kwenye sehemu fulani iliyoezekwa turubai ili jua lisiwapate. Wakawa wanaburudika na ngoma za asili.
****
"Muda umefika." Gunner aliongea na kutoa rimoti ndogo ambayo aliibonyeza na mara ikaanza kuhesabau dakika. Tayari alikuwa ameyafungulia mabomu matatu ambayo yalitegwa kuzunguka ule uwanja wa ndege.
Yalikuwa ni mabomu magumu kutambulika na wanausalama kwa sababu yalikuwa yameezekwa au kujengwa kwa plastiki kwenye lile kava lake la nje. Hakuna aliyejua kuwa yapo maeneo yale na yanaendeshwa kwa rimoti maalumu.
Wakati hayo yanaendelea huko nje, kwa mbali angani, ndege ya Rais wa Urusi ilionekana na kwa mbwembwe nyingi, Tanzania nao walirusha ndege tatu za kivita na kuikaribisha ndege ya rais huyo kwa kuisindikiza kwa nyuma. Baada ya ndege ya Rais wa Urusi kutua, zikiwa zimebaki dakika mbili mabomu kulipuka, ndege zile za jeshi zikapaa juu kwa pamoja na kisha zikapinda bawa moja mbele ya Rais wa nchi yao, hiyo ni ishara ya heshima kwa Kamanda wao wa Majeshi.
Dakika moja mbele, Rais wa Urusi alikuwa anashuka toka kwenye ndege yake na kama shamra shamra ndipo zilipozidi maradufu ya pale. Wacheza ngoma walizidi kukata viuno na wakati huo wanaume wakiruka sarakasi za hapa na pale kwa madaha na kwa kupendeza.
"Hey. Mawasiliano kwangu yamekatika." Jamaa mmoja ambaye ni mpelelezi, alimfuata mwenzake na kumpa taarifa hiyo.
"Hata mimi aisee." Jamaa mmoja alijibu.
"Kutakuwa na hatari, haraka twende kwa Rais kabla mambo hayajawa mambo." Jamaa yule aliyempa taarifa mwenzake na kisha wakaanza kukimbilia ndani ya uwanja wa ndege.
"Vipi. Mbona mambo hayajipi?" Lobo akamgeukia Gunner na kumuuliza. Gunner akawa anabonyeza kitufe cha rimoti yake lakini hakuna jipya. "Dakika ya saba hii. Hadi wanaanza kuimba wimbo wa taifa, naona kimya tu." Lobo akazidi kupambanisha maongezi yake.
"Shit. Wajinga wametegua nini mabomu?" Gunner akaongea huku kijasho chembamba kikimtiririka. Wakati hajui la kifanya, mara simu yake ikaita.
Akatazama kioo cha simu hiyo, hakuona hata namba ya mpigaji. Lakini haikuwa sababu ya yeye kutoipokea.
Baada ya kuipokea tu! Ndani ya gari alilopanda pakakumbwa na giza kiasi kisha kioo cha mbele cha gari yake, kikaanza kama kuchorwa chorwa na umeme mwekundu na hali hiyo ilipotulia, akaona sura ambayo kamwe hakuitegemea kwa wakati ule. Alikuwa ni Frank Masai akicheka kwa nyodo nyingi.
"Tatizo lako Gunner huna akili. Mi nadhani unajua kabisa kuwa mimi ni mmoja wa walioshiriki kutengeneza SGT. Sasa kwa mawazo yako ya uozo, unadhani baada ya kutengeneza huo mtambo, hatukutengeneza ant-SGT?" Masai akakaa kimya kidogo na kuendelea. "Ant-SGT, ninayo mimi peke yangu. Wale wengine wametengeneza lakini hadi sasa bado hawajang'amua mtambo huu upo wapi." Masai akamaliza na Gunner ni wazi alikuwa hoi kwa kile akionacho.
"Okay. Sipo huko Gunner. Naona jinsi unavyohangaika na mabomu yako. Hayo ni sisi ndio tuliyabuni, tunajua njia zote za kuyategua hata bila kuyashika. Nilichofanya kikubwa ni kuyazima tu kwa kutumia kompyuta. Usihangaike kuyategua. Na ndege ambayo unaitegemea kama pigo la mwisho, bora uwaambie jamaa zako waache tu. Mambo yatakuwa magumu endapo watajitokeza." Frank akachimba mkwara wakati huo Lobo alikuwa kimya akifatilia kila neno la Masai.
"Hakisimami kitu Masai. Tutamaliza kila kitu hapahapa." Gunner akaleta upinzani wa maneno.
"Oooh! Na wewe nawe mbishi hivyo? Labda tufanye hivi." Masai alipoongea hayo, Gunner alihisi kitu kikali kikipita katika bega lake. Maumivu aliyoyapata, yalikuwa hayasimuliki, lakini pia alipomuangalia dereva wake, alikuwa tayari ni maiti kwa risasi ile kupita shingoni kwake.
"Hiyo risasi hatujakukosa bahati mbaya. Ilipangwa ipite hapohapo kwenye bega lako. Huyo bwege tumemuua makusudi tu." Sauti ya Masai ilisikika tena baada ya Gunner kushika bega lake kwa sababu ya maumivu. Gunner akatazama huku na huko kuona ile risasi imetokea wapi lakini hakuona dalili yoyote ya risasi hiyo ilipotokea. Vioo vya gari vilivyofungwa hadi juu, vilikuwa salama kabisa.
"Unataka nini Masai?" Gunner aliuliza kwa hasira.
"Nachotaka ni wewe kusimamisha mpango wako haraka kabla sijafanya chochote cha ajabu." Masai akajibu jibu ambalo Gunner alikataa katukatu kulitimiza.
"Bora nife Masai. Bora nife kuliko kupindua mpango wangu." Sauti kavu na yenye kujiamini ilijibu.
"Okay. Kama umechagua kufa, ngoja nikupeleke huko unapopataka." Masai akiwa na sauti ya umakini, alikubaliana na Gunner na mara gari la watu wale likawaka bila wao kuligusa. Wote wawili waliokuwamo mle ndani walishangaa mambo yaliyokuwa yanatukia. Wakadhani labda ni ndoto lakini ilikuwa kweli hiyo.
Wakajaribu kufungua milango ya gari lile, haikufunguka wala kuwa dalili ya.kufunguka.
"Gunner, chini ya kiti chako kuna zawadi yako maalumu, naomba uitazame."Sauti ya Masai iliwatoa mawazoni wale jamaa wawili na wakati huo gari lao lilikuwa linabadili gia. Gunner akapinda mgongo na kuingiza mkono chini ya kiti na kuvuta begi fulani lililokuwepo huko.
Akaliweka mapajani na kisha akalifungua zipu. Macho yakamtoka pima kama jusi lililobanwa na mlango.
"Mabomu yako hayo. Zilibaki dakika mbili ili yawalipukie, lakini nikagandisha yasifanye hivyo. Sasa chagua, kuuza au kununua roho zenu. Mkitaka kununua, waambie wajinga wenu wa ndege ambao naweza kuwasimamisha hata mimi, lakini nataka Gunner ndio asimamishe. Waambie hao wajinga, waachane na mpango huo. Au kama hautaki, mi sina tatizo. Nakuachia mabomu yako. Chaguo ni lako, TICK TOCK." Mara baada ya maneno hayo, mabomu yale yakaanza kuhesabau dakika zilizobaki na gari lao hawa mabwana, likazidi kutembea lenyewe toka pale lilipo kwa kwenda sehemu nyingine ambayo haina watu wengi.
Lobo alikuwa kimya akimuangalia mkuu wake alivyopagawa na wakati huo, kile kioo chenye picha ya Frank Masai kilikuwa kinaendelea kuonesha picha hiyo kwa kumuona Masai akipiga mluzi na kucheza kwa furaha.
"Umeshinda Masai. Nawaambia waache." Hata Lobo aliyepembeni alishusha pumzi ndefu baada ya maneno yale. Na hapo mabomu yake yakasimama zikiwa zikebaki sekunde tisa yalipuke.
"Wasiliana nao sasa hivi, ukileta ubwege, ngoma inasoma hadi sifuri hiyo." Masai akatoa onyo na simu yake akaikata lakini kwenye kioo cha gari ile bado alionekana akiwaangalia Lobo na Gunner wanachokifanya.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hallow Morgan. Abort the mission now. (Holoo Morgan. Achana na huo mpango sasa hivi)" Gunner alimwambia mmoja wa marubani wa ndege ile.
"Kwa nini Gunner?" Swali likatoka kwa mtu ambaye anawasiliana naye.
"Nimekwishasema. Fanya nilichokwambia." Baada ya maneno hayo ya hasira, Gunner akakata simu yake.
"Safi Gunner. Safi sana. We ni mwanaume sasa kwa kuwa umesikiliza mwanaume mwenzako anataka nini." Mbele ya kile kioo cha gari yao, sauti ilisikika na kumfanya Lobo atabasamu na kutokea kumpenda sana Masai kwa mambo anayoyafanya.
"Nikikukamata Masai. Utajuta." Gunner alifoka kwa hasira na wakati anafanya hayo, mara simu yake ikaita. Alipoangalia alikuta ni yule rubani aliyetoka kuwasiliana naye punde. Gunner akapokea ile simu.
"Tumeambiwa hakuna kuabort mission." Yule rubani aliongea kwa wahka.
"Nani kasema?" Gunner aliuliza kwa sauti yenye kitetemeshi na hasira juu yake.
"The Shadow." Rubani yule alijibu na kukata simu haraka. Gunner akabaki kinywa wazi asijue Masai atachukua maamuzi gani.
"Usiwe na wasiwasi Gunner. Nilijua haya yatatokea tu. Nimekuja kuteketeza matkenolojia yenu yote mliyopewa, sihitaji kuona haya mauchafu. Angalia ubishi wa huyo mbwa wenu mnayemuabudu." Frank Masai aliongea hayo na kisha akabonyeza vitu fulani fulani alipokuwa kasimama, na picha kwenye kile kioo cha gari la Gunner,ikabadilika na kuanza kuonesha ndege aina ya Jet P.112.
Ndege ilikuwa inatoka angani kwa kasi ya ajabu tayari kwa kudondoka uwanja wa ndege ambapo Rais wa Urusi na Tanzania tayari walishamaliza mambo mengi na sasa walikuwa wanasalimia wacheza ngoma za jadi.
Ndege ile ikiwa inashuka, mara ikaanza kukata kona kuelekea kushoto. Marubani wa mle ndani wakaanza kuhaha kuirudisha katika uelekeo wake lakini wakawa wanashindwa. Ikawa hali tete kwao hasa pale ndege ilipoacha muelekeo wa kwenda kudondoka uwanjani na kuanza kwenda kwa kasi eneo ilipo bahari ya Hindi.
P.112 ilipofika katikati ya bahari ya Hindi, ikiwa bado ipo juu, ikalipuka na mshindo mkubwa ukaikumba Dar es Salaam.
"Yuhuuuuu." Sauti ya Man'Sai ilisikika ikishangilia kama mchezaji aliyefunga goli. Wakati huo Gunner alikuwa katoa macho kama kaona maiti inayotembea.
"Man'Sai The Great." Lobo alijikuta akitamka maneno hayo na kumfanya Gunner amwangalie kwa jicho la hasira.
"Umeona hiyo Gunner?" Masai alimuuliza Gunner wakati vipande vya ndege ile vikidondokea baharini. "Bado SGT, hiyo rahisi tu. Sasa hivi FBI wamekwishajua upo wapi huo mtambo. Kabla hawajaufikia, nitakuwa nimekwisha umaliza." Masai alimaliza na mawasiliano kukata. Hali ya gari ikarudi palepale. Kioo kikawa safi na kuonesha ya nje kama mwanzo.
Gunner akatupa macho labda ataona risasi aliyopigwa ilipopita, hakuona chochote zaidi ya kumuona Lisa akimpigia saluti na kuingia kwenye gari fulani ambalo namba zake zilikuwa hazieleweki. Yaani zinabadilika kila dakika.
"Mmh! Ulisema Lobo. Katuzidi ujanja huyu bwege. Sasa ni muda wa kulipa kisasi, atatutambua huyu bwege." Gunner aliongea hayo kwa hasira huku akifungua vishikizo vya koti lake na kuangalia pale alipopigwa risasi na wakati huo, Lobo anamsukuma yule dereva mfu siti ya nyuma.
"Nilikwambia lakini. Namjua Masai kuliko unavyodhani. Ni msumbufu na ni mtu wa neno lake. Hukunielewa. Pale mpango ulipopanguka, kungekuwa na watu wengine wa kujitoa muhanga, wangemaliza yote haya. Wewe hukunielewa nilipokwambia tuongeze watu. Now what? Japo Masai hayupo upande wangu, lakini huyo jamaa mi namkubali kuliko wewe. Yaani angekuwa ndiye Gunner yule, sasa hivi tungekuwa tunatangaza vita vya dunia." Lobo aliongea huku akifoka.
"Sasa huko unanilaumu Lobo." Gunner aliongea kwa sauti ya kinyonge.
"Hapana. Ulipaswa kusikiliza pande zote na si kufanya maamuzi ya peke yako." Lobo alizidi kumpa maneno ya kweli patina wake.
"Okay Lobo, next tutapiga kazi kwa umoja." Gunner aliongea na kumruhusu Lobo kuwasha gari lake tayari kwa kuondoka eneo lile.
****
Masai baada ya kumaliza alichokifanya, akavaa suti aliyopewa ja Alejandro na kutoka nje ambapo alichukua usafiri wa pikipiki na kuanza kuelekea pori moja lililopo barabara ya kwenda Kibaha.
Kasi ya pikipiki aliyokuwa anaiendesha, kila mmoja pale Kivule alikuwa haamini kama ni mtu ndiye anaendesha. Pikipiki bora kabisa kupata kutokea duniani, ndiyo ambayo ilikuwa inatitia mtaa hadi mtaa hadi kufanikiwa kutoka Jiji la Dar es Salaam.
Alifika eneo analolitaka mapema kabisa na kukuta kupo kimya.
"Nenda kulia Masai." Alisikia sauti ikimuakuru kwenye kishikizo alichokibandika sikioni. Naye akaenda na kujificha pembezoni kidogo mwa ukuta mzito uliojengwa eneo lile.
Mara akatokea mlinzi mmoja ambaye alikuwa anakimbia na kama kangaroo, yaani akirukaruka. Akasimama mbele ya kichaka fulani na kupekua kwenye zipu yake. Akatoa sijui kinini na kuanza kujisaidia haja ndogo.
Kwa jinsi ilivyokuwa inatoka ile haja, mlinzi yule alijikuta akifumba macho yake na kuburudika ipasavyo na lile tendo.
Frank akiwa nyuma yake, akatoa nyota mbili na kuzirusha kiustadi kama ninja. Zikamkuta yule bwana shingoni upande wa nyuma. Akadondoka kama mzigo wa kuni. Umauti ukamkumba.
"Okay Masai. Hakuna kizuizi tena. Endelea." Mtaalamu aliyemuacha Kivule aliongea na Frank akapanda ukuta mkubwa uliokuwepo pale. Akajitoma ndani kwa kutulia miguu na kisha akaweka goti lake moja chini na kutazama huku na huko.
Akakimbia kwa kasi ya ajabu kutokana na suti aliyoivaa. Akafika eneo moja ambalo ndipo anaamini mtambo wa SGT upo.
"Fungua kidogo mtaalamu wangu." Masai aliongea huku kashika kishikizo chake kilichopo sikioni. Mara sehemu ile ilifunguka kwa ukimya mkubwa ambao si kawaida yake kuwa hivyo. Ukapatikana upenyo ambao Frank Masai atapita. Kijana wa watu akarusha kamba ambayo ilinasa mahala kwenye mti na kujikaza hapohapo.
Akiwa na begi lenye vifaa fulani humo, akarushia kamba iliyobaki ndani ya shimo lile na yeye akaanza kushuka hadi chini yake palipo mtambo wa SGT.
"Okay Mtaalamu. Nimeshakanyaga chini." Frank alimpa taarifa jamaa ambaye alikuwa anaendesha mitambo kule Kivule.
"Naona kila kitu Kamanda. Kazi nzuri sana." Mtaalamu akajibu kwa furaha. Frank akawasha taa ambayo aliigonga mkononi na kutoa mwanga wa buluu. Akaitupa taa ile sehemu fulani, na shimo lile refu likatapakaa ule mwanga. Sasa akaweza kuuona mtambo wa SGT ukiwa umetulia kando kando ya shimo lile.
Masai akasogea kwa uangalifu ili asilete kelele mle ndani. Akaufikia mtambo ule kisha akatoa vifaa fulani kwenye begi lake, na kwa taratibu, akaanza kufungua mfuniko uliokazwa vema kwa nati za China.
Kifaa alichotumia, kilikuwa kinatumia umeme hivyo ndani ya dakika mbili, mfuniko mdogo wa mtambo ule ulifunguka na Masai akaingiza mkono wake ndani ya mtambo na kushika kitu fulani ambacho kilikuwa kimeungwa na nyaya nyingi za mtambo ule.
Akazikata nyaya zile kwa uangalifu na pale alipomaliza, akaweka kile kitu kwenye begi lake.
Baada ya hapo. Akatoa bomu moja la kubandika ukutani na kufanya kama bomu linavyotaka. Baada ya kulibandika, akaliwasha liwe tayari kulipuka atakapo bonyeza rimoti yake. Akawa kamaliza kazi iliyompeleka. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akashika kamba yake na kuanza kutoka nje. Dakika mbili mbele, akawa kashikilia uzio wa shimo lile na kichwa kimetoka nje. Akatoka kwa uangalifu mkubwa ili asidondokee ndani.
"Holoo." Masai akasikia sauti hiyo ikimshtua na alipotazama ni nani, akakutana na walinzi watatu huku wote wameshikilia mitutu yao ya bunduki.
"Ulipogusa mtambo, ukapeleka taarifa hadi ndani. Huku kwangu mawasiliano yalikatia." Masai alisikia sauti hiyo ikimuambia kwenye kile kishikizo chake cha sikioni.
"Karibu kwetu. Wewe ndiye Masai." Mlinzi mmoja aliuliza huku akicheka kwa dharau.
"Mbona chembamba halafu huna sura ya kutisha kama wanavyosema wakina Lobo." Mlinzi mwingine aliuliza huku akiwa hana mbavu kwa kicheko.
"Yaani hichi hata nikitupa bunduki... ." Mlinzi yule wa kwanza aliongea huku akitupa bunduki yake upande wa kushoto. "Hakinigusi hata ngumi moja." Akamaliza kwa kujigamba na kusogea mbele ya Masai
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment