Search This Blog

Friday, 20 May 2022

DUKA LA ROHO - 4

 







    Simulizi : Duka La Roho

    Sehemu Ya Nne (4)



    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Yaani mimi hiki nikikipuliza tu! Kitayumba yumba kama kimelewa. Embu kione." Mlinzi wa tatu aliongea kwa mara ya kwanza huku anamsonda Masai kwa bunduki. Muda wote Masai alikuwa akiwatazama huku akihesabu pumzi zao kwa chati.

    Katika hali ambayo hakuna mlinzi aliyetegemea, walijikuta hawana bunduki zao na wakati huo ile suti ya Masai ilishatengeneza maski usoni kwa kwake. Ilikuwa ni kasi ambayo hakuna aliyeidhania kwani wakati wao wakicheka hadi wanafumba macho yao, Masai alikuwa akibofya saa maalumu ya kuendesha suti yake.

    "Haya sasa. Naanza na wewe ambaye hata bila binduki unanipiga." Masai akaongea huku akimfuata yule mlinzi aliyetupa bunduki pembeni. Ngumi mbili za kifua, na nne za tumboni kisha mbili za shingoni, zilotosha kumuondoa maisha yake yule mlinzi kwa sekunde kadhaa tu.

    "Nakuja kwa wewe ambaye ukinipuliza naanguka. Haya nipulize." Yule mlinzi alikuwa akitetemeka kama vile kaona jini. Hawezi kufanya chochote na hapohapo haja ndogo ikawa inamchuruzika toka juu na kushukia kwenye mabuti aliyovaa. "Oooh! Hapo ndio unanipuliza?" Masai akauliza na wala hakupoteza muda wa kusikia jibu.

    Akamshika yule bwana mkono wake na kwa nguvu akapiga ngumi mbili za kwapani zilizovunja mkono wa yule bwana. Kabla hajapiga kelele za maumivu, Masai akamalizia pigo la mwisho la kichwa cha mdomo. Jamaa alipopiga kelele, mdomo wake ulionekana wenye mapengo.

    "Aaah! Nilitaka kukusahau. Umesema mimi sitishi? Na hapa je?" Baada ya maneno hayo, Masai akaitanua ile maski sehemu ya macho na kuonekana kama alien. Halafu kwa mdomo wake akapiga kelele zilizomfanya yule jamaa kuinama huku kaziba masikio yake kwa viganja vya mkono. Aliposimama, Masai akamtisha kama anamkimbiza. Jamaa akaona isiwe tabu, njia rahisi ni kukimbia tu. Jamaa akamuacha yule jamaa mwenye mapengo akiwa hana la kufanya.

    "Siku nyingine muwe na heshima." Masai aliongea huku akimsukuma kichwa yule bwana na kumfanya ajigonge vibaya kwenye mti. Jamaa akazimia.

    "Upo vizuri kaka." Sauti ya mtaalamu wa Malocha ilisikika ikimpongeza Masai kwenye mawasiliano aliyovaa sikioni kama kifungo cha shati.

    "Usijali mtaalamu. Utajifunza mengi." Masai akajibu huku sura yake ikifunguka na muda huohuo, akarukia ukuta na kutokomea mbali na eneo lile.

    ****

    " Boss. Masai alikuwepo hapa dakika kumi zilizopita na alionekana akigusa mtambo wa SGT ambao sasa haufanyi kazi." Boyka alimpa taarifa Gunner kwenye simu wakati jamaa yule akirudi na Lobo katika makao yao.

    "Unasemaje Boyka?" Kwa mshangao Gunner akauliza.

    "Na kaua walinzi wawili na mwingine yupo hapa hajitambui wala kuwa na meno." Boyka akazidi kumchanganya Gunner. Maongezi hayo Lobo alikuwa anayapata moja kwa moja wakati yanaendelea.

    "Katega bomu kwenye SGT. Waambie hao jamaa waondoke haraka eneo hilo." Lobo akamwambia Gunner ambaye alitimiza suala hilo haraka.

    "Boyka, ng'oa vitu vyote muhimu na kisha nenda kwenye ile nyumba yetu ya pili. Fanya haraka, kuna hatari hapo." Hakusubiri jibu Gunner, akakata simu na kuongeza kasi ya gari lake kupitia barabara ya Tazara kabla hajapindia Buguruni na kunyoosha kama anaelekea Ubungo.

    ****

    "Wajinga naona wanakimbia nyumba." Mtaalamu wa mitambo upande wa Malocha aliongea baada ya kumuona Masai akiingia katika kile chumba chao cha kazi.

    Tayari Lisa, Mubah na Malocha walisharudi na kuoneshwa kazi ambayo Masai kaifanya.

    "Lazima wakimbie hapo. Kimbembe kitabaki kwa wale wajinga wanaojiita FBI. Lazma walie." Frank aliongea huku akivua koti la suti yake na kuliweka juu ya kiti kimoja mle ndani.

    "Man'Sai nimeizimia hiyo suti yako." Malocha alimwambia Masai.

    "Usijali Kamanda. Hii yako tu. Ngoja nimalize kazi yangu." Masai akajibu na kumfanya Malocha atabasamu kwani atakuwa kapata vazi ghali kuliko vazi lolote analolimiliki. Maongezi ya hapa na pale yaliendelea lakini yalikatishwa tena na mtaalamu.

    "Hey. Naona kuna wazungu wamezunguka lile eneo la Gunner." Jamaa akatoa taarifa ambayo ilifanya kila mmoja kusogea karibu na skrini za mle ndani.

    "Washenzi sana hawa. Sasa ngoja niwaoneshe kazi." Baada ya wapelelezi wale kulizunguka eneo zima la Gunner, wakaanza kuingia ndani mmoja mmoja na mwisho wake, wote walikuwa wamejaa ndani.

    "Frank akabonyeza kitufe cha Enter kwenye kompyuta ambayo hakuna hata mmoja aliyewaza kuitumia. Mlipuko mkubwa ukaikumba ardhi ya pale na maeneo ya karibu. Ardhi ikatitia na kujifukia. FBI wote wakateketea palepale.

    "Nawachukia sana hawa washenzi." Frank alitamka na kutoka katika kile chumba cha mitambo akiwaacha wakina Malocha wametumbua macho.

    "Masai ni kichaa." Malocha aliongea huku akitikisa kichwa kushoto na kulia.

    "Ila nampenda akifanyacho. Huwa hakosei, yupo sahihi." Mubah aliongea hayo na yule mtaalam alimpa 'tano' kuonesha kakubaliana na maneno yale ya Mubah.

    ***** CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika kitongoji kilichopo nje kidogo mwa jiji la Dar es Salaam, wanapaita Mbezi Beach. John Lobo, Gunner na kundi lake la watu watatu waliobaki walikuwa wanajaribu kuunda mitambo yao tena kwa ajili ya mawasiliano.

    Wakati hayo yakiendelea, simu ya Gunner iliita, na alipoiangalia aliona namba ngeni na 'code' namba yake si ya Tanzania. Kwa uoga na kujishuku, akaipokea na kuiweka sikioni.

    "Nini kimetokea?" Swali la kwanza kulisikia Gunner baada ya simu ile kuipokea. Ilikuwa ni sauti nzito na inafanana na sauti ya redio iliyokwisha betri.

    "Ni Masai." Gunner akajibu huku akitetema.

    "Masai ndiye nani?" Sauti ile ikauliza kwa ukali na kumfanya Gunner kutojibu chochote. "Acha ujinga we mpumbavu. Nitakuua mimi. Umefanya ujinga ambao hutakiwi kusamehewa kosa lako." Ile sauti ilizidi kufoka.

    "Hapana The Shadow. Tunaomba msamaha. Tupe nafasi nyingine tutafanya vema." Gunner alijitetea huku kijasho chembamba kikimtoka.



    "Hakuna kitu kama hicho Gunner. Wote mtakufa kwa sababu ya huu ujinga." Mtu aliyeitwa The Shadow, aliongea na kumfanya Gunner kutulia bila kusema chochote. "Natuma watu wangu wawili hatari kuja huko kumuangamiza huyo kinyago wenu. Baada ya hapo, watakuja kuwamaliza nyie. Sitaki muingilie chochote wakati hawa watu wanafanya kazi yao." The Shadow alimaliza na Gunner akajibu sawa. Simu ikakatwa.



    GENIVA, USWISI.



    Jamaa wawili walikuwa wamesimama nyuma ya kiti kimoja ambacho kilikuwa kimewapa mgongo na sigara kubwa (cigar) ilionekana ikivutwa na moshi wake ukipulizwa juu.

    Watu hawa hawakuweza kuona sura ya mtu huyo bali kuisikia sauti yake wakati inaongea na Gunner aliye nchini Tanzania.

    "Pinto na Trina." The Shadow aliwaita wale watu bila kugeuka.

    "Ndio The Shadow." Waliitika kwa sauti ya pamoja.

    "Nawatuma Tanzania kwa kazi moja tu! Ya kuua. Kauweni kundi la mtu anayeitwa Masai." Alipoongea hayo, akarusha bahasha mezani lakini hakugeuka nyuma.

    Msichana mmoja anayejulikana kwa jina la Trina, akasogea na kuichukua ile bahasha. Akaifungua na hapo akakuta picha kadhaa za Frank Masai na kundi lake lote.

    "Hao wote wanatakiwa kufa. Lakini wa kwanza awe ni Masai. Kichwa chake nikione hapa." The Shadow akapiga pafu nzito kwa kuivuta cigar yake, kisha akapuliza moshi mzito angani.

    "Baada ya kumaliza hawa wajinga wa Masai, malizeni na haya majinga mengine." Akatupa bahasha tena mezani na jamaa wa kiume kwa jina la Pinto, aliisogelea na kuifungua bahasha hiyo. Sura za wakina Gunner na Lobo zikaonekana katika picha zilizomo kwenye bahasha ile.

    "Yametimia haya Boss." Sauti nzito ya Pinto ilijibu wote wawili, yaani Pinto na Trina, wakatoka kwenye ofisi ile ambayo ilikuwa inawaka mwanga wa bluu.



    PINTO NA TRINA.



    Pinto au alivyopenda kujiita El Pinto, alizaliwa nchini Mexico. Ana miaka ishirini na nne pekee (24) lakini amekwishaua watu thelathini wakiwemo viongozi wakubwa kumi na mbili. Hajawahi kushindwa kazi ambayo kapewa. Mataifa makubwa yote yamewahi kumtumia huyu kijana na mafanikio yake yalikuwa makubwa kuliko walivyotaraji.

    Mwili mdogo kama kawaida ya Wamexico wengi, uliwafanya wale wanaowindwa kudharau kazi ya yule bwana.

    Ni mkali wa kutumia silaha za moto. Mwili wake wote hujaza silaha hizo jambo linalofanya asishindwe mpambano wowote. Licha ya kuwa mkali wa silaha hizo za moto (mfano bunduki), pia hakuwa nyuma katika mapambano ya uso kwa uso. Ana mapigo ambayo yanaweza kumfanya adui akimbie bila kupenda.

    Historia ya wazazi wake, iliishia pale alipowaua wote kwa sababu ya wao kukubuhu katika kuvuta madawa ya kulevya na kusahau kabisa mahitaji mengine ya familia. Hasira ambazo alikuwanazo Pinto, aliweza kumng'ata baba yake kwenye koo hadi akanyofoa koromeo lake.

    Mama yake ambaye alikuwa kalewa madawa, alimchinja kwa kisu kikali kinachotumika jikoni kwa ajili ya kukatia nyama. Baada ya mauaji hayo, Pinto akachukuliwa na kundi la wahuni wa Mexico ambao walimfumdisha njia mbalimbali za kuishi kama muhuni. Katika njia hizo, kamwe hakuwahi kujihusisha na uvutaji wa madawa wala bangi. Kilevi chake kikubwa kilikuwa ni Trina.

    Trina yeye katokea nchi ya Italia. Anamiaka ishirini na mbili (22). Kishatekeza roho zipatazo arobaini na tano za watu wakubwa kwa wadogo, matajiri kwa masikini. Yeye yupo kimaslahi zaidi. Ukitaka kazi yako.ifanyike bila kero, mlipe pesa zake zote, majibu utayapata baada ya masaa ishirini na nne.

    Yeye kaua watu wengi kuliko Pinto kwa sababu ya uzuri wake ambao uliwafanya mabosi wanaomtuma waamini kuwa unaweza kuwateketeza maadui zao bila shida. Trina alisifika zaidi katika kucheza na silaha zenye ncha kali kama visu, mapanga na silaha za kininja. Pia hakuwa nyuma katika mapigano ya viungo na kutumia sumu. Trina alikuwa vema sana katika kazi yake.

    Wazazi wa Trina waliuawa huko Italia na kundi la Mafia baada ya baba yake nna Trina kukutaa kujichinja kwa kosa la kutosambaza madawa ya kulevya katika kituo cha watoto yatima. Hali hiyo ndio ikawapa hasira Mafia na wakaamua kuiteketeza familia nzima ya Trina akiwepo Dada yake aliyekuwa na umri wa miaka sita kipindi hicho. Trina akiwa na miaka mitatu, aliweza kuona mauaji hayo akiwa kwenye kabati alipofichwa na baba yake.

    Trina akaishi kwa upweke muda mrefu baada ya familia yake kuuawa. Akawa mtoto wa mitaani huku akiwa na boksi dogo aliloweka baadhi ya picha za wazazi wake na zawadi mbalimbali alizowahi kupewa. Alipotimiza miaka saba, akawa si Trina tena bali Trina wa hatari. Aliweza kuishi katika mtaa wowote kwa amani au kwa vurugu. Japo hakuwa mkali sana katika mapambano ya viungo, lakini aliposhika silaha kali, aliweza kunyamazisha kila ambaye alitaka kuingia anga zake. Aliwahi kumchana mgongo kwa kiwembe mkuu wake anayempa madawa ya kulevya akauze kisa hakukamilisha malipo sahihi ya kazi aliyopewa. Pia aliwahi kukata nyeti za bwana mmoja mtu mzima aliyekuwa akitaka kumuingilia kinguvu mwilini. Na baada ya kukata nyeti hizo kwa kisu kikali, akakinga damu ya baba lile jitu zima na kuinywa.

    Sifa hizo na nyingine nyingi, ndizo ziliwafikia Mafia na kuamua kumchukua yule mtoto pasipokujua wamemchukua mtoto wa nyoka waliyemuua.

    Baada ya Mafia kumfunza na kumuivisha kwa kila kitu, ndipo Trina akatoa picha fulani ambayo kwa nyuma iliandikwa "Hawa ndiyo adui zako, wauwe ukipata nafasi."

    Mwandiko huo wa baba yake, ndiyo ulikuwa muda wa kuufanyia kazi. Akaingia hadi kule anapotaka na kisha akaua maadui zake wote. Baada ya hapo, akapotea kabisa nchini Italia.

    Ilikuja kuonekana akiwa na miaka kumi na minane nchini Japan. Alikuwa binti tajiri kuliko binti yeyote pale Japan. Alimiliki miradi mbalimbali iliwemo vituo vya matangazo na viwanda kadhaa vya magari. Mali zote zilikuwa za baba yake na yeye aliziongeza kwa kazi yake ya kuua.

    Alipotumwa nchini Hispania kwenda kumuua mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa, ndipo alipokutana na Pinto ambaye yeye alikuwa na jukumu la kuiba siri za usalama wa taifa. Wakiwa hawajuani, wote wakaajiriwa kama wapelelezi katika nchi ile. Kilichokuja kuwaunga, ni pale Trina alipomkamata Pinto anaiba siri nzito za Hispania. Na wakati anamkamata, yeye tayari alikuwa amekwishamuua mkuu wa upelelezi kama alivyoagizwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walichofanya hawa watu ni kutoroka kwa pamoja na baadaye wakaungana na kuwa marafiki wakubwa hadi kufikia kuitwa wapenzi.

    Sasa The Shadow kawatuma wapenzi hawa waje Tanzania kummaliza Frank Masai na kundi lake. Masai hajui kama kuna mpango wa yeye kuangamizwa na wakati huo taarifa zinazagaa kuwa kafika Tanzania na anaendesha ugaidi kama kulipua ndege kwenye Bahari ya Hindi na kulipua jengo la usalama wa taifa na kuua wapelelezi kumi na mbili wakuokuwepo katika jengo hilo. Tanzania yote ikabandikwa matangazo na picha za Masai kama " The Most Wanted".

    Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vikatapakaa picha nne zikiwatuhumu watu hao kuwa ni magaidi wa kutisha. Picha ziliwaonesha Mubah, Malocha, Lisa na Masai kama ndio tatizo la nchi ya Tanzania.

    Rais alishasema mengi kuhusu hawa watu na akaweka vizuizi kadhaa juu ya watu hawa. Lakini tatizo ambalo walikuwa nalo wengi wa wapelelezi, ni kutojua watawapatia wapi watuhumiwa hawa. Ni vigumu kuwapata kwa sababu wanavifaa vingi vya kuzuia mawasiliano yao yasifike sehemu nyingine na zaidi, kabla hujawafikia, tayari wanakuwa wamekwishajua hilo.

    "Masai. Ndio kama hivyo kaka, tunasakwa kwa ugaidi. Tuwe makini tu." Mubah aliongea baada ya kuzima runinga iliyokuwa ikionesha taarifa zao.

    "Usijali Mubah. Hapa hamna atakayekamatwa. Cha msingi ni kuondoka hii sehemu." Masai alitoa ushauri.

    "Twende wapi sasa." Malocha aliuliza.

    "Kuna nyumba ya Lisa kule Sinza, nadhani ni sehemu nzuri ya sisi kujificha." Frank akatoa wazo.

    "Haa! Yaani twende kule katikati ya jiji tena? Masai unatafuta kukamatwa." Mubah aliongea kama anapinga kauli ile.

    "Siku zote penye watu ndipo pa kujificha. Usitegemee simba kutafutwa mjini, anatafutwa porini Mubah. Sisi tunawindwa, lazima watuwindie nje ya mji. Sasa kama hamuamini, subirini siku mbili tu. Mtasikia tumevamiwa, na huyo Rais wa Urusi kaondoka kachukia balaa, lazima alete watu wake watusake."

    "Okay. Upo sawa Masai. Ngoja Lisa atoke tuongee naye." Malocha alimaliza maongezi ya asubuhi ile kwa kumsubiri Lisa ambaye bado alikuwa chumbani kalala na mwanaye.

    ****

    "Lobo. Unajua The Shadow kawatuma Pinto na Trina." Gunner alikuwa akimpa taarifa mtu wake wa kazi.

    "Kwa hiyo." Lobo akauliza huku akinoa kisu chake chenye meno upande mwingine.

    "Wakiwamaliza wakina Masai, ni zamu yetu. Na unawajua wale, hawajawahi kushindwa vita."

    "Umewahi kumsikia Masai kashindwa vita? Hata ya makundi ya kigaidi na kipelelezi. Kawahi kushindwa?"

    "Sawa, hajawahi kushindwa lakini angalia na uwezo wa wakina Pinto. Angalia watu waliwaondoa, ni tofauti na aliowaua Masai."

    "Trina na Pinto, walipata kazi gani katika mauaji yao? Wao ni watu wa kumendea tu! Hata mimi hawaniwezi. Wale ni watu wa kusubiri mtuhumiwa wao atoke sehemu ndio wamvamie. Lakini mimi, nakupa taarifa kuwa ndani ya masaa ishirini na nne au siku kadhaa, uwe umefanya hivi au vile, usipofanya naku kraa." Lobo akaweka ishara ya kuchinja shingoni kwa kutumia kisu chake.

    "Kwa hiyo wewe hawakutishi hata kidogo?" Gunner akamuuliza Lobo.

    "Watanitisha nikikutana nao uso kwa uso. Lakini tukiwindana, watakufa wao mapema tu."

    "Unadhani Masai atafanikiwa kuwazima hawa?"

    "Uzuri wa Masai anavitu vingi anavyowazidi wale. Wale wanatumia silaha za moto na vitu vyenye ncha kali, Masai ni mkali wa vyote hivyo. Pia Masai anaweza mapigano ya ana kwa ana na anaweza kuwinda pia, vitu ambavyo hao Pinto na Trina wanavyo kwa mmoja mmoja. Lakini tatizo la hao watu wa The Shadow, hawana mbinu za kisheria, Masai akisema nitakuwa hapo dakika moja ijayo, basi jiandae kumpokea. Hawa hawana sumu hizo. Akikutana na Pinto, atacheza naye kwa visu na mapanga. Pinto hawezi hiyo. Akikutana na Trina, atacheza naye kwa bunduki na bastola, unadhani nani atashindwa?" Lobo akampa ufafanuzi yakinifu Gunner.

    "Ndio maana The Shadow kawatuma wote wawili. Unadhani Masai atapona?"

    "Masai hajui kama hawa watu wanakuja, hilo ni tatizo kubwa sana na atapata shida kuwazuia. Lakini angekuwa anajua kuwa wanakuja, angewamalizia hukohuko kwao."

    "Kwa hiyo tumwambie au? Unajua wakifa wale na sisi tutapona."

    "Gunner. Acha uoga. Ile si vita yetu, subiri wamalizane na Masai ije zamu yetu. Tutacheza na sheria tu. Watoto wadogo wale, wala hawana tatizo. Na Masai namjua tangu zamani sana, nimesoma naye na kupambana naye. Acha uoga tu!" Lobo aliongea kwa kujiamini.

    "Okay. Ila Masai asipouawa na hawa, nitamuua mwenyewe, naapa kwa MUNGU. Bahati yake tumesimamishwa." Lobo akawa mtu wa kutabasamu kwa maneno yale ya Gunner, hadithi zao zikaishia hapo. Gunner akatoka kwenda kuvuta sigara, Lobo akabaki kitini anaendelea kunoa kisu chake.

    ****

    WIKI MOJA MBELE. UWANJA WA NDEGE WA DAR ES SALAAM.



    Ndege binafsi lakini kubwa kiasi, ikatua katika uwanja ule kwa mbwembwe zake zote. Pembeni iliandikwa PITRI yaani Pinto na Trina, na kulembwa na rangi za kijani na nyekundu, rangi ambazo zinapatikana kwenye bendera za Italia na Mexico.

    Hakuna aliyejua maana ya neno lile la PITRI kwa hapa Tanzania. Hivyo waliiacha ndege ile itulie ndipo wawaangalie wageni wake.

    Baada ya dakika tano za ndege ile kutua, wakashuka vijana wa kizungu wawili wakiwa wamevalia suti nyeusi na makoti makubwa juu yake.

    Yule wa mbele alitazama huku na huko kabla hajatoka pale mlangoni na kumpisha wa nyuma yake ambaye naye macho yake yakaitazama nchi ya Tanzania vema. Akavaa mawani yake nyeusi na kisha akaanza kushuka katika ngazi za ndege ile ghali.

    Wakiwa na mabegi yao kila upande, wakafika sehemu ya ukaguzi na kuyatupia mabegi hayo kwenye vifaa maalum vya kukagulia na wao wakapita kwenye mlango wa ukaguzi bila wasiwasi.

    Mabegi yalipita salama, ila wao walivyopita taa nyekundu iliyoambatana na mlio wa hatari, kwa pamoja vilitoa ishara kuwa watu wale wamebeba vitu vya vyuma.

    "It's my belt. (Ni mkanda wangu)" Pinto aliongea huku akivua mkanda wenye bakoni kubwa kama wapendavyo kuvaa wamexico wengi. Akauweka juu ya meza ya idara ile na kupita tena lakini bado sauti na taa ile vilitoa ishara tena.



    Pinto akamuangalia Trina kwa macho ya kumpa taarifa ya jambo fulani. Wale wana idara ya uhamiaji, wakaweka mikono yao kiunoni kwa kuzikamata bastola zao tayari kwa kuwaweka chini ya Ulinzi.

    "Ooooh! PITRI. Welcome in Tanzania." Sauti kutoka kwenye mlango wa kuingilia uwanja wa ndege ilisikika na mara polisi na wanaidara wote walisimama wima kama wapo kwenye gwaride la jeshi.

    Alikuwa ni Mheshimiwa Rais wa nchi ya Tanzania akiwa kanyoosha mikono yake na kuwakumbatia Pinto na Trina mmoja baada ya mwingine.

    "Hawa ni wageni wangu jamani, hamkuona taarifa zao kuwa nitakuja kuwapokea?" Rais akawauliza wana idara ya uhamiaji na wote wakatulia tuli huku vichwa vikiwa chini.

    "Okay Guys, lets pass in VIP doors. (Sawa vijana, twendeni tukapite kwenye milango maalumu)" Rais akawachukua Pinto na Trina na kuanza kwenda nao kwenye mlango wa watu maalumu huku nyuma, mabegi yao yakiwa yamebebwa na wafanyakazi wanne waliokuja na Rais.

    "Ilibakia sekunde chache tuangamize watu wako." Pinto alimwambia Rais kwa kiingereza cha shida wakiwa ndani ya gari maalumu walilopanda watu watatu tu. Rais akiwa ndiye dereva.

    "Nilichelewa kidogo tu. Samahanini sana." Rais aliomba msamaha na wote wakaupokea. Macho yao, Pinto na Trina, yakawa kwenye vioo vya gari walilopanda wakishangaa jiji la Dar es Salaam.

    Baada ya saa moja, Rais alikuwa anawakaribisha Pinto na Trina katika Ikulu na moja kwa moja akawaongoza hadi chumba maalumu kwa ajili ya maongezi.

    "Kwa taarifa nilizozipata, Masai anaonekana sana mida ya usiku katika maduka ya Mlimani City. Sasa mkianzia pale, nadhani mtapata nyama yenu bila wasiwasi. Si mnamtaka mzima tu! Nadhani atawasaidia sana kwenye upelelezi wenu." Rais aliongea kwa tabasamu pana akidhani watu wale wapo kwa ajili ya kumkamata Masai, kumbe kumuangamiza.

    "Mlimani City ipo wapi." Trina aliuliza huku akitoa mawani yake na kumuangalia Rais kwa macho yake ya kahawia na ya kung'aa kama ya paka.

    "Nitawapa dereva awatembeze ili mpajue kote huku." Rais aliongea huku akijichekesha chekesha.

    "Fanya sasa hivi." Trina akaongea na kuvaa mawani yake tena kisha akaegemea kochi. Rais akanyanyua simu yake na kuipiga. Akaongea kwa Kiswahili kumpa maelekezo mtu aliyempigia.

    Baada ya dakika mbili, akaingia jamaa kalivalia suti ya kupendeza. Akapewa ugeni alioitiwa na kuondoka nao.

    Trina na Pinto walilitazama eneo zima la Mlimani City. Wakalichora sehemu zote muhimu na baada ya kumaliza, wakamuomba mwenyeji wao awatafutie hotel yenye hadhi maeneo yale.

    Ndipo wakapelekwa kwenye hotel ambayo walipoiona, wakaikubali bila neno. Wakalipia kwa pesa za Marekani na kuchukua chumba cha juu ambacho waliweza kuona mengi ya chini kwa kutumia vifaa vyao. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    ****

    Kundi la Malocha walishahamia kwenye nyumba ya Lisa na baada ya kuhamia, siku mbili mbele, nyumba yao ya Kivule ikivamiwa na wapelelezi walioagizwa kuwasaka. Lakini kwa bahati mbaya wakawakosa.

    Bado waliendelea kucheza na mitambo yao na kamwe hawakuwa lelemama katika kusaka kinachoendelea. Kitu ambacho walikikosa, ni ujio wa Pinto na Trina ambao walishajua kuwa Masai anapenda sana kwenda Mlimani City usiku kwa ajili ya kununua mahitaji ya nyumbani lakini pia zawadi kwa Martina ambaye bado alikuwa hamtaki baba yake.

    "Lisa." Masai alimuita mpenzi wake mida ya saa mbili usiku. Hiyo ni baada ya siku nne za Trina na Pinto kufika Tanzania.

    "Abee switie." Lisa aliitika huku anakimbilia alipo Masai.

    "Naenda Mlimani mara moja kuchukua mazaga ya hapa."

    "Okay baby. Lakini na hiyo suti yako, harahara wasinipokonye huko." Lisa alitania kwa ile suti ya Masai ambayo alitoka nayo Italia. Hakuivaa tangu kipindi alipoharibu mipango ya Gunner.

    "Hahahaaa. Hamna kitu kama hicho."Masai akamuhakikishia mpenzi wake na kumpa busu dogo la shavuni.

    "Okay. Bye sweetie." Lisa alimuaga Masai aliyetoka katika chumba kile na kupita sebuleni ambapo pia aliwaaga rafiki zake kama alivomwambia Lisa.

    ****

    Saa tatu, Masai alikuwa ameegesha gari lake nje ya maduka ya Mlimani City na kisha akavaa kofia yake ambayo haikuendana na suti. Alifanya hivyo ili asijulikane na watu hasa ukizingatia Masai anatafutwa kwa udi na uvumba.

    Akiwa ameanza kuchagua hiki na kile mle dukani, wazungu wawili ambao walionekana ni wapenzi, waliingia na kuweka mabegi makubwa sehemu ya mapokezi na kisha kuchukua vitoroli maalumu vya kubebea bidhaa na kuanza kwenda kuchagua wavitakavyo.

    Wakasogea hadi karibu na Masai, kisha wakawa wanacheka na saa nyingine wananyonyana ndimi zao. Masai hakuwatambua na wala hakuwafatilia, akawa anaendelea kuchagua bidhaa zake.

    Wazungu wale wakaanza kuchagua bidhaa upande wa kushoto na Masai upande wa kulia, hivyo wakawa wamepeana migongo. Masai akasogea mbele kidogo na kisha akachagua kioo cha kujiangalia. Akakitazama na kukijaribu kwa kujiangalia. Akajiona ndevu zake alivozifuga ili asijulikane, akatabasamu na kuanza kukirudisha kioo kile.

    Lakini kabla hajakishusha, alimuona yule mwanamke wa kizungu nyuma yake akiwa kakamata panga fulani lenye makali pande zote na alikuwa kalinyanyua juu tayari kwa kulishusha katika kichwa cha Masai.

    Masai aliruka kwa pembeni na panga lile likamkosa na kukata kabati lililokuwa limebeba bidhaa. Alikuwa ni Trina ambaye kamkosa kwa panga Masai.

    Masai akakaa mkao wa kupigana na wakati huo watu walikuwa wameanza kusogea kujionea kinachoendelea. Asivyotegemea Masai labda Trina atasogea yeye kupambana, akatokea mpenzi wake, Pinto ambaye aliruka sarakasi na kutua mbele ya Masai huku kakamata bunduki fupi (short gun) iliyokuwa na matundu mawili lakini imepunguzwa bomba za mbele na kuwa fupi zaidi kiasi kwamba wakaguzi wa duka lile hawakuiona. Pinto alikuwa kaielekeza kifuani kwa Masai na hakusita kuifyatua.

    Ikamrusha Masai hatua sita nyuma lakini haikumuua wala kumdhuru kwa sababu ya suti aliyovaa.

    Mlio wa short gun ile, ukawafanya wananchi kukimbia hovyo kwenda nje. Masai akanyanyuka haraka na kutaka kikimbia lakini mara viatu vyake vikachomwa na visu na kuvishikilia hapohapo chini. Ikabidi avivue na kubaki peku. Hadi anamaliza kuvivua, tayari Trina alishasogea na kurusha visu vidogo vinne. Masai akavizuia kwa mkono wa kushoto na kudunda juu ya suti yake matata.

    Mambo yakawa mazito kwa Masai, alichofanya ni kubonyeza saa yake haraka na suti yake ikajifunga miguuni, kwenye viganja vya mikono na usoni.

    Ile anageuka aangalie maadui zake, anakutana tena na midomo ya short gun iliyokuwa imelenga kichwani. Ngoma ikaachiwa tena na kumpaisha Masai mbali na pale aliposimama.

    Akili ikamvurugika na maumivu aliyahisi. Akataka kunyanyuka akajikuta anadondokea makabati yenye bidhaa mle Mlimani City. Wakati anahaha na hayo, Trina alikuwa anakuja kwa kasi na kuruka teke lililomkuta kifuani Masai. Masai hoi mbele ya ile miili ya vijana wawili wanaopiga kwa mtindo wa ‘one by one’, yaani wanapigana kwa kuachiana.

    Mwanaume akawa anagaa kwa maumivu tele, na sasa ilikuwa zamu ya Pinto kumshambulia. Katika hali ambayo haikutegemewa na kila mtu ambaye alikuwa anashuhudia mpambano ule, Pinto alikimbilia kwenye moja ya mabegi makubwa alilyokuja nayo. Akaingiza mkono wake ndani ya begi lake, na mara akachomoa bunduki nzito inayomwaga risasi karibu mia moja kwa dakika. Wanaiita Min Machine Gun. Ina mkanda wenye risasi zenye idadi kubwa.

    Pinto akaikoki vema mbele ya Masai, na bila huruma alianza kumimina risasi zisizo na idadi. Ilitisha na kusikitisha hasa risasi zile zilivyokuwa zinajaribu kutoboa suti maridhawa ya Masai.

    Baada ya dakika mbili, Pinto alitulia na kutazama hali ya windo lake. Masai akawa anagaa-gaa chini anashindwa kunyanyuka pale kwa sababu ya kuelemewa na anachofanyiwa.

    Akiwa kama mtoto, akawa anatambaa kwa tumbo kuufuata mlango wa kutokea. Masai anajaribu kuokoa nafsi yake, anasikia nyuma yake sauti ya kitu kama injini ya gari dogo la kuchezea watoto. Kugeuka angalie japo kwa shida, anaona viatu vya Trina kwa mbele kuna visu ambavyo vinazunguka kwa kasi miguuni kwake.

    Masai akaongeza kasi ya kutambaa kwa tumbo kwenda nje, lakini Trina akamuwahi kukandamiza usoni visu vile na kuvizungushia hapohapo bila huruma. Ni cheche tu ndizo ambazo zilikuwa zinamwagika. Haileweki ni vipi angekuwa huyu Masai kama asingekuwa na ile suti. Amshukuru aliyeitengeneza.

    Hali ikazidi kuwa mbaya. Kizunguzungu kikamkumba yule mwanaume na taratibu akaanza kukubali kuwa anashindwa.

    "Suti hii pia inaweza kutoa shoti ya umeme mikononi." Maneno ya Alejandro, aliyeitengeneza ile suti yakajirudia kichwani kwa Masai. "Kivipi sasa? Inatoaje hiyo shoti?" Masai akajiuliza bila kupata jibu. "Ngoja nijaribu." Masai akajishauri na kwa kuwa ndio uokozi pekee uliyokuwa umebaki, akajaribu kwa kuukamata mguu wa Trina. Lakini hakuna kilichotokea zaidi ya kazi ya vile visu vya miguuni kuendelea kuchimbua maski iliyoziba uso wake.

    Ikabidi Masai aruke pembeni na kumuacha Trina akimfuta kwa kasi. Akaangalia saa yake na kuona kuna kitufe ambacho huwa hakitumii sana, kwa chini kimechorwa alama ya radi. Akakibonyeza na wakati huo Trina alikuwa kafika na viatu vyake.

    Mtoto yule wa kike akarusha teke ambalo lilimkuta Masai kifuani. Masai akazidi kuvuruga bidhaa za duka lile kubwa kwa kuzipamia. Trina akaruka sarakasi na kutua juu ya kifua cha Masai, akawa kamkalia kifuani.

    Akanyoosha mikono yake juu, na hapo vikachomoza visu virefu kiasi toka kwenye koti la mterezo alilolivaa. Akaanza kuvishusha kwa kasi kuelekea kifuani, hapo ndipo Masai akajaribu bahati yake kwa kunyoosha mikono yake miwili na kugusa kifua cha Trina. Bila kutegemea, Trina akarushwa na umeme mkali toka katika mikono ya Masai. Akarushwa hatua kumi nyuma na kilichomzuia ni ukuta wa uliozunguka mle ndani.

    Pinto akashtuka hasa pale alipomuona mpenzi wake anakukuruka kama mtu mwenye degedege au kifafa.

    "Shit." Pinto akatukana na kulivua koti lake. Sasa silaha zake baadhi zilizomzunguka mwili mzima, zikaonekana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akachomoa bunduki nyingine ya hatari toka mgongoni kwake. M16 naizungumzia. Akaikoki na kuanza kumwaga njugu kwa fujo kumuelekea Masai aliyekuwa bado hajarudisha nguvu ipasavyo. Baadhi ya risasi zilimpata lakini hazikumdhuru sana kwa sababu ya suti yake.

    Risasi zikaisha kwenye M16. Pinto akatupa bunduki ile pembeni na kisha katika kifua chake, akanyofoa mabomu mawili yaliyokuwa yananing'inia. Akayarusha sehemu ambayo Masai alikuwa kalala. Pinto akaruka pembeni na Masai alisikia vyuma vikidunda chini ya sakafu ile ya Mlimani City, kutazama anaona mabomu yanakuja kwa haraka.

    Mtoto wa kiume akapata nguvu za kunyanyuka na kwa kasi ya ajabu, akajirusha kwenye mlango wa kutokea ambao ni kioo tupu. Kikavunjika na Masai akawa nje wakati huo mabomu yakawa yanalipuka na kuzidi kuleta tatizo katika mtaa ule.

    Baada ya mabomu yale kutulia, Pinto alinyanyuka na kuangalia kama kafanikiwa zoezi lake. Akatazama katika mlango wa kutokea, akaona gari likiondoka kwa kasi toka katika uzio wa duka lile. Alijua kuwa ni la Masai kwa sababu katika kumfuatilia, aliliona mara kwa mara Masai analiendesha.

    "Bastardo (Mpumbavu)" Pinto akatema tusi dogo kwa lugha ya Kiitaliano. Akakimbilia pale alipo mpenzi wake na kumkuta kazimia. Akampiga makofi kadhaa na Trina akafungua macho yake na kumuangalia Pinto.

    "Kakimbia yule mbwa?" Trina akamuuliza Pinto.

    "Ndio. Tuondoke hapa haraka." Pinto alijibu na kumnyanyua Trina tayari kwa kuondoka eneo lile ambalo taratibu lilianza kunyemelewa na wanausalama.

    ****

    Masai akiwa hana nguvu za kutosha, akawa anakimbiza gari lake kuelekea maeneo ya Sinza, makao mapya waliyohamia na washirika wake. Kwa bahati nzuri alifika salama na kushuka garini.

    Aligonga mlango na Lisa ndiye aliyeufungua. Lisa akakutana na mwili wa Masai ambao hauna nguvu. Ukamdondokea taratibu lakini mtoto wa kike akamdaka na kuanza kuwaita wenzake.





    Malocha na Mubah wakatoka na kumsaidia Lisa kumuingiza Masai ndani.

    "Nini kimetokea Masai?" Malocha aliuliza kwa kitetemeshi.

    "Wamenivamia." Masai alijibu kwa shida huku bado maski yake hajaifungua usoni.

    "Embu mvue hiyo saa. Malocha alimuamuru Mubah aliyekuwa upande wa mkono uliyovishwa saa. Alipomvua, maski nayo ikajifungua. Uso wa Frank ukaonekana wazi.

    Damu zilikuwa zinamtoka puani na masikioni. Kila alipojaribu kuongea, alitokwa na damu sehemu hizo zote hadi mdomoni.

    "Kalete vifaa ya huduma ya kwanza." Lisa akatoka haraka na kutekeleza alichoambiwa na Malocha. Vifaa vikaja na Malocha akaanza kuvitumia kumhudumia Masai.

    "Mwambie Ndita aende duka lolote la Madawa na kuleta dripu za maji." Malocha akatoa ujumbe huo na mara moja Mubah akatoka kupeleka ujumbe kwa Ndita, mmoja wa wataalam wao.

    Ndita akatoka pale nyumbani haraka na kwenda alipoagizwa. Lakini kwa bahati mbaya akakosa dripu. Ikabidi aende hospitali ya Mwananyamala ambako alutumia pesa kiasi na kupata dripu pamoja na damu pakiti mbili. Safari ya kurudi nyumbani anapoishi ikachukua nafasi yake tena.

    "Na wewe umechelewa sana. Ila umefanya la maana kuleta na damu." Malocha aliongea huku akipiga piga mkono wa Masai aliyekuwa hajitambui lakini macho yake yakiangaza huku na huko kama mlevi ambaye pombe zimemzidi kichwani. Misuli ilipopatikana, Malocha akatundika pakiti ya dripu ya maji kwanza juu, na kisha kuingiza sindano ndogo iliyoanza kusafirisha maji hayo katika mwili wa Masai.

    "Hii damu tutaweka baadae kama itahitajika, ngoja kwanza apate nguvu na haya maji kwanza." Alifuta jasho Malocha baada ya kazi hiyo nzito ya kidaktari.

    "Atapona kweli Malocha." Lisa aliuliza kwa mashaka.

    "Ondoa shaka Lisa. Hii ni kianzio tu. Nampigia daktari bingwa aje hapa amuangalie zaidi hadi ndani. Usitie shaka." Lisa akapewa moyo. Kwa unyonge akatoka katika chumba kile na kwenda chumbani kwake ambapo alimkuta Martina kakaa juu ya kitanda.

    "Mbona hujalala Swetie." Lisa alimuuliza mwanaye huku akichongesha tabasamu.

    "Yule atapona." Martina akauliza kwa sauti ya unyonge.

    "Atapona. Usijali eeh." Lisa akamjibu na kumkumbatia mwanaye kisha kwa uchungu akaanza kulia kwa ndanindani ili mwanaye asisikie.

    Hali ya Masai ilikuwa siyo ile aliyoondoka nayo. Mwili ulikuwa umechoka kwa sababu ya kipigo alichokipata kwa wale wauaji wa Kimataifa. Damu nyingi zilimtoka mwanaume yule, masikioni, puani na mdomoni zilikuwa hazizuiliki wala kukatishwa kirahisi.

    Malocha alijaribu kumfunga vitambaa lakini kiukweli hali ilikuwa mbaya kwa Masai ambaye alikuwa anajikaza ili asipoteze fahamu.

    Saa nane usiku, Lisa alisikia hodi ikigongwa kwa kengere maalumu na baada ya mlango kufunguliwa, Malocha akasikika akiongea na mtu. Lisa akashuka kitandani na kwenda hadi sebuleni ambapo alikuta Malocha kasimama na mzee mwenye miwani huku kabeba mkoba fulani wenye ukubwa kiasi chake.

    "Lisa. Huyu ndiye dokta niliyemuita. Anaitwa Dokta Zabron, ni muaminifu, usitie shaka." Malocha alimtambulisha Daktari kwa Lisa na bila kuchelewa, tabibu yule akapelekwa chumba ambacho Masai kalazwa.

    Mzee yule kwa haraka akaanza kazi yake aliyoisomea huku akifungua begi lake na kutoa kamera ndogo na kuanza kuupiga mwili wa Masai hasa ubavuni na sehemu zinazopita mifupa.

    "Chukua funguo ya gari langu hii, nenda kafungue kwa nyuma, utakuta begi moja kubwa na mkoba wa kompyuta, vilete haraka." Dokta Zabron aliongea hayo huku akimkabidhi ufunguo wa gari Malocha. Wakati huo Mubah na wengine walikuwa wamezama katika usingizi mzito katika chumba walichoweka mitambo yao.

    Baada ya dakika zipatazo tatu, Malocha akawa karudi na vitu alivyoagizwa. Mzee Zabron akatoa kompyuta yake mpakato na kuiwasha. Wakati anasubiria ilete mawasiliano, akaiweka pembeni na kisha akafungua begi kubwa aliloletewa na Malocha, akatoa vyuma fulani virefu ambavyo alivibana katika mbavu za Masai kisha akafanya kama anavijaza. Masai akawa anapanda juu.

    "Binti, mshike kichwani na Malocha mshike miguuni ili asipinde." Bila kuchelewa, alolisema Daktari likatekelezwa na yeye akazidi kujaza vile vyuma hadi Masai akafika kiwango fulani pale juu. Wakati huo mwanaume yule alikuwa hajitambui hata chembe. Fahamu alizokuwa akijitahidi zisimuondoke, alishindwa kuzuia zisifanye hivyo. Alikuwa kapoteza fahamu kwa kipigo kikali cha Pinto na Trina.

    Haraka Mzee Zabron alichukua kamera yake na kuingiza waya fulani (USB) na kuunga kwenye kompyuta yake. Akafungua programu moja iliyomo katika kompyuta yake na baadaye programu hiyo ikazichuja zile picha na kuonekana kwa mtindo wa picha za x rays.

    "Hajavunjika kiungo chochote, sema kidogo kwenye kifua damu imegandia sana ndio maana haikatiki. Hapo nimemnyanyua ili damu iwe inatambaa mwilini kwake kwa kasi na hiyo itasaidia hata huo mgando wa damu kufagiwa taratibu." Mzee Zabron aliongea alichokiona. "Ngoja nimuwekee na hivi ili msipate shida ya kumkamata." Zabron akachukua vyuma vingine na kuviweka kichwani kwa Masai na miguuni. Mwanaume akawa kama anaelea angani.

    "Na hii sindano itasaidia kulainisha damu iliyoganda." Mzee yule alizidi kufafanua huku anavuta dawa hiyo na kisha akaidunga kwenye kifua kipana cha Masai. Masai akatoa pumzi ndefu kama mwanariadha aliyetoka kukimbia mbio ndefu. "Kila baada ya masaa manne uwe unamchoma kifuani kwa kiasi kilichoandikwa hapo. Hiyo pia ni busta nzuri ya moyo kama utakuwa unafeli kupeleka damu na hewa." Mzee Zabron alimaliza maongezi yake na kuanza kukusanya vifaa baadhi alivyovitoa kwenyw mkoba wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Asante sana Dokta." Malocha alishukuru wakati daktari yule akifungia vifaa vyake.

    "Usijali. Hizo dripu zikiisha, basi. Msimuwekee tena. Kuweni waangalifu sana. Kifuani yaonekana kapigwa sana na vitu kama risasi hivi. Sasa damu imegandia hapo. Ni damu kubwa ambayo mkizembea kumchoma hizo sindano kumi, mtampoteza mtu wenu." Mzee Zabron aliwapa onyo mapema.

    "Usijali Mzee wangu. Tumekuelewa." Malocha akaongea.

    "Oooh! Halafu nilitaka kusahau." Mzee yule aliongea na kufungua mkoba wake mwingine na kutoa mashine fulani wanayoitumia sana hospitali kwa wagonjwa wasiojitambua. Akamvisha kiduwasha fulani Masai kwenye kidole chake na katika kidubuwasha hicho kuna waya ambao unaenda moja kwa moja katika mashine ile iliyoungwa katika umeme.

    "Hii inasoma mapigo yake ya moyo. Sasa hivi yapo sitini na tano, yanatakiwa yapande hadi mia moja hasa hapo mnapomchoma sindano. Akiwa mzima, yacheze kwenye sabini hadi themanini. Sawa?" Mzee Zabron akazidi kutoa maelekezo mbalimbali hadi pale alipoona watu wake wameelewa. Akatoka nje ya nyumba ile saa kumi na yeye akaelekea kwake.

    ****

    "Pumbavu tumemkosa yule." Pinto aliongea kwa lugha zao za huko akiwa na Trina aliyekuwa kaweka barafu kisogoni.

    "Itakuwa ngumu sana kumpata sasa hivi na kumuua. Kishajua kuwa tunamuwinda." Trina akaongea.

    "Inabidi twende naye hivyohivyo, hakuna kumkawiza tukimpata."

    "Ndiyo hivyo. Sema na ile suti sijui kaitoa wapi. Anabahati sana yule mjinga."

    "Sijawahi kuona vazi la namna ile duniani. Wote tuliowaua wangejua kuwa kuna vazi lile, tungepata shida sana. Lakini huyu tutamuua tu. Ngoja tufanye mkakati mwingine. Huyo Rais wao tusionekane tena kwake na wala kugusa katika ile hoteli." Pinto alishauri na kunyanyuka kwenda kwenye friji lililokuwepo katika chumba chao kipya. Akafungua na kutoa juisi ambayo alianza kuigida kwa fujo kama mwenye kiu.

    ****

    "Hawa ni Pinto na Trina kumbe?" Sauti ya Malocha ilisikika katika mshangao mkubwa. Ilikuwa ni asubuhi na kituo fulani cha Runinga kilikuwa kinaonesha taarifa ya habari zilizowafikia asubuhi ile.

    Ilikuwa ni taarifa ambayo ilieleza tukio zima lililotokea usiku wa jana yake. Kamera zilizopo maduka ya Mlimani City, zilinasa tukio na picha za watuhumiwa wakiwa katika mpambano. Wazungu wawili ambao ni Pinto na Trina, walionekana sura zao lakini mmoja ambaye ni Masai, hakuweza kutambulika haraka kwa sababu ya mavazi aliyokuwa kayavaa.

    "Unawajua hawa watu Malocha?" Lisa alimuuliza Malocha ambaye alimuangalia usoni kidogo na kisha kufungua mdomo wake kuongea akijuacho.

    "Hawa ni wauaji wa kimataifa. Hutumwa kuua tu! Hawana kazi nyingine zaidi ya hiyo. Na hulipwa mabilioni ya fedha kwa wakifanyacho."

    "Kwa hiyo wametumwa kumuua Masai?" Mubah aliuliza.

    "Nadhani. Lakini tushukuru MUNGU hawajafanikiwa. Hawa hufanya kazi yao mara moja tu. Masai ndio wa kwanza kutoroka kifo."

    "Nani atakuwa kawatuma?" Lisa akatupa swali.

    "Itakuwa wanetumwa baada ya yale aliyoyasimamisha. Mtu wa kwanza kumuhisi kafanya haya ni The Shadow. Kama si huyu basi Lobo na Gunner."

    "Mmmh! Hii sasa ni hatari hadi wanawatuma Pro Killers? Duh!" Mubah akaonesha mshangao wake waziwazi.

    "Hawa ni hatari kuliko simba mwenye njaa. Wamezungukwa na silaha katika miili yao yote." Malocha akaongeza sukari katika chai ya maongezi yale.

    "Mmh! Sasa wakijua kuwa tupo hapa kabla Masai hajapona, si watakuja kummaliza?" Lisa wasiwasi wake ukawa juu baada ya maneno ya Malocha.

    "Hapana. Hawawezi kujua japo wakijua itakuwa ni tatizo kubwa." Malocha akajibu.

    "Itabidi tuwe makini sana. Kaanza Masai, tunaofatia ni sisi. Haya mambo ya kutoka toka hovyo, yatatufanya tuvamiwe hapa. Tujaribu kujificha kwa muda huu hadi Masai apone ndipo tujue jinsi ya kuwakabiri hawa watu." Mubah akatoa pendekezo zuri kabisa.

    "Umeeleweka kijana. Ushauri mzuri sana." Malocha alimuunga mkono Mubah.

    ****

    Wiki ilikata huku Masai akiwa kitandani lakini akiwa kashushwa chini alipokuwa kanyanyuliwa na vyuma maalumu kwa ajili hiyo. Alikuwa anapumua vema kabisa lakini bado fahamu zilikuwa hazijarudi.

    "Martina. Njoo umuone baba." Lisa alimuita mwanaye ambaye hakuwahi.kuingia chumba alichokuwepo baba yake bali kuishia mlangoni na kuchungulia tu. Aliposikia mama yake anamuita, akabaki kasimama asijue anataka kwenda au kuondoka. "Martina." Lisa akamuita tena mwanaye.

    Martina kwa hatua za woga akasogea kwa kusita kama gari linaloendeshwa na mtu anayejifunza. "Njoo." Lisa akamuita zaidi Martina.

    Mtoto akajivuta hadi pale alipomama yake lakini hakumsogelea baba yake aliyekuwa kitandani anapumua taratibu bila mashine.

    "Kamguse baba pale." Lisa akamuonesha Martina sehemu ya shavu ili Martina akaguse. Mtoto yule akafikiria kwa muda kabla hajafanya maamuzi.

    Akakumbuka zawadi za midoli aliyokuwa analetewa na mtu yule. Akakumbuka jinsi anavyofurahi akiwa na mama yake na jinsi anavyojaribu kumvutia ili amkubali. Akaenda mbali zaidi na kumkumbuka Gunner ambaye mara nyingi ni mtu wa kumfundisha mambo ya kigaidi tu. Akafananisha uso wa mama yake awapo na Gunner na awapo na Masai. Akagundua kuwa mama yake kawa na furaha zaidi kuliko kipindi cha nyuma alipokuwa na Gunner.

    Hakuishia hapo pekee. Akawaangalia watu aliowazoea mle ndani, wote walikuwa wanaamani wawapo na Masai kasoro yeye tu! Akajiona kama mwenye makosa kukaa mbali na mtu yule.

    Taratibu akapiga hatua moja kwenda kitandani alipolala Masai. Baada ya hatua hiyo, akageuka nyuma na kumuaangalia mama yake.

    "Nenda." Lisa akamsukuma kwa ishara. Martina akazidi kusogea hadi pale alipo Masai na kisha kwa kutetemeka, akanyoosha mkono wake na kumshika Masai shavuni.

    "Mshike kwa mikono miwili." Lisa akampa maelekezo tena mwanaye ambaye naye alifanya hivyo kwa kushika mashavu ya Masai yaloliyokuwa yamejaa ndevu laini.

    Mara Masai akapumua pumzi ndefu iliyomfanya Martina arudi nyuma haraka kwa uoga.

    "Usikimbie Martina. Ataamka kama ukiwa hapohapo." Lisa akamwambia mwanaye kwa furaha huku naye akinyanyuka na kusomsogeza mwanaye zaidi. "Mshike tena." Lisa akamuongoza mwanaye. Martina akafanya kama alivyofanya mwanzo kwa sekunde kadhaa.

    "Mbona haamki?" Martina aliuliza kwa upole wa kitoto.

    "Mlalie kifuani na kumkumbatia, utaona anaamka." Martina akamuangalia mama yake kabla hajafanya hivyo lakini kwa kuwa alikusudia kumuamsha baba yake, akaamua kufanya hivyo kwa dakika moja.

    Akiwa kamkumbatia na kufumba macho, mara Martina alihisi mkono ukizipapasa nywele zake. Akaamka haraka na kutazama anayefanya hayo, uso kwa uso na sura ya Masai iliyokuwa inatabasamu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Asante Martina." Masai akashukuru na wakati huo Lisa alikuwa haamini akionacho. Tabasamu lililoambatana na machozi ya furaha, vyote vilijitokeza.

    "Kaamka huyu mama." Martina aliongea huku naye anaonesha furaha yake.

    "Ni baba yako Martina." Lisa alijaribu kumuelekeza Martina ambaye alimgeukia Masai na kumuangalia tena.



    "Siyo baba yangu huyu. Namjua baba aliyenilea." Martina aliongea kwa sauti ya ukali na kumfanya mama yake atake kujibu kwa ukali pia lakini Masai akamuwahi.

    "Yupo sahihi Lisa. Martina yupo sahihi sana." Masai aliongea kwa sauti ya chini na kukohoa kidogo.

    "Yupo sahihi kumkana baba yake." Lisa akamuuliza huku macho yake ya hasira kamuelekezea Martina.

    "Lisa. Nimefanya nini cha maana kwa huyu mtoto hadi astahili kuniita baba? Mi' ni baba kibailojia tu! Ila kiuhalisia Martina hastahili kuniita hata mjomba. Sijui alikuwaje wala sijui ni mangapi aliyapitia. Nachojua ni kwamba nilijificha miaka mitano pasipo wasiliana na wewe wala kutaka kumjua Martina. Hata wewe, ni roho yako njema ndio umenipokea mimi tena, lakini mimi si wa kuwa na wewe Lisa. I don't deserve you, Lisa." Masai aliongea kwa uchungu na kujikuta akitoa machozi.

    "Samahani Frank. Labda Martina yupo sawa." Lisa aliongea huku akimkumbatia mpenzi wake pale kitandani.

    "Martina. Usijali mama eeh." Lisa alijaribu kumfariji na Martina pia aliyekuwa kakasirika.

    "Martina. Mi ni Anko Masai, sawa eeh." Martina akaitikia kwa kichwa kukubali.

    "At least naweza kuwa naye karibu. Atabadilika na kunitambua. Usimfanye anichukie Lisa." Masai akatamka hayo baada ya Martina kutoka mle chumbani kwenda kuwaita wakina Malocha waje kumuona Masai.

    ****

    Baada ya siku tano, Masai alikuwa anaweza kutembea na hali yake ilikuwa inarudi taratibu japo bado alikuwa analalamika sana kifua kuwa kinamuuma. Alikuwa anafanya mazoezi ya mwili kwa dakika kadhaa na kukaa kwa sababu ya kifua hicho.

    "Bado sijakaa sawa kabisa. Dakika tatu tu! Tayari maumivu yananiganda." Masai alikuwa anampa taarifa Malocha.

    "Usijali Kamanda, utakuwa sawa tu." Malocha akamfariji.

    "Mmefikia wapi katika kuwasaka hawa wajinga." Masai akauliza kuhusu mkakati wa wakina Malocha katika kuwasaka Pinto na Trina.

    "Wajinga bado wapo nchini sema mafichoni sana. Hapa kuna jamaa yupo FISSA mle, ndio anatusaidia sana kutupa taarifa za hawa jamaa." Malocha akajibu.

    "Nitawapata tu. Ngoja nitengamae. Na bahati yao hawatumii mawasaliano yanatumia satellite." Masai akaongea huku akichukua taulo na kujifuta jasho.

    Baada ya wiki mbili, Masai alikuwa katengamaa na sasa hali yake ilikuwa safi zaidi. Alikuwa tayari kwa lolote japo katika upande wa suti yake, ile maski ya kichwani ilikuwa haifanyi kazi tena na upande wa kushoto wa kifua wa ile suti, kulitengeneza mchakao ambao ungefanya suti ile kuharibika baada ya kupigwa kidogo tu. Lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kumshukuru MUNGU kwa pale alipofikia.

    Ukaribu wake na Martina ulianza kuwa mzuri na mtoto yule alikuwa hamuogopi sana Masai kama zamani. Alikuwa akicheza naye hadi usiku ambapo alikuwa analala usingizi mnono kama Masai atamuimbia. Martina akawa mwenye furaha lakini hakumzidi Masai furaha hiyo japo aliitwa Anko na mtoto wake wa damu.

    "Hey Masai. Kuna mawasiliano yamenaswa na FISSA kati ya Pinto na mtu ambaye hajulikani yupo huko Hispania." Mtaalamu wa mitambo wa Malocha alimpa taarifa Masai zilizoletwa na mtu anayewasiliana na Malocha ndani ya FISSA. Masai akasogea hadi pale zilipotumwa taarifa zile na kuzisoma vema.

    "Okay. Weka hiyo namba kwenye tracer yetu. Tuone inapatikana wapi." Masai akashauri na baada ya muda namba ile ikajieleza imepigwa wapi.

    Ilikuwa ni Buza Kanisani na Frank kwa umakini mkubwa, akafunga safari hadi huko kwa kufuata ramani iliyotoka wakati wa kuitafuta namba hiyo.

    "Oya." Masai akatoa uso nje ya kioo cha gari na kumuita dereva mmoja wa bajaji aliyekuwepo karibu na pale.

    "Sema Bro." Jamaa akasalimia kwa mahashamu.

    "Fresh. Najua we' mwenyeji hapa. Naomba kukuulizia kama umewahi kuwaona wazungu wawili, wa kike na wa kiume wakilanda mitaa hii." Masai akauliza na kumfanya yule jamaa asimamishe kichwa angani kama mwenye kufikiria jambo.

    "Ahaaa. Wale watasha wawili wanaopiga bendi? Wanakaa pale Buza Tanesco, kama si pale, basi Kipera." Jamaa akajibu kwa furaha huku akitaja mitaa kadhaa ya Buza ambayo Masai anaweza kuwapata wale wazungu.

    "Kumbe wasanii?" Masai akajidai kuuliza kwa hamaki.

    "Weee. Wale acha kabisa. Wanapiga magitaa kama hawana akili nzuri. Kila Jumamosi wanapiga Toxido hapo." Jamaa yule aliongea na kunyoshea katika kilabu cha pombe za kisasa kiitwacho Toxido.

    "Daaah. Nawatafuta sana maana walinipa mawasiliano yao lakini hawapatikani. Waliniambia kuwa wanataka kutafuta wacheza filamu wa kitanzania, sasa hapa kati nikaumwa ndio nikasimama hata kuwasaka." Masai akadanganya ili asishtukiwe.

    "Aah! Kumbe wanaigiza. Basi kaka ukitaka kupata waigizaji, mimi tayari nimooo. Yaani napiga mateke kama Damme." Jamaa akajinadi.

    "Nittakutafuta jembe langu. Kamata hii, halafu Jumamosi mbili zijazo, njoo hapo Toxido ujionee." Masai akaongea huku akimpa noti ya elfu kumi yule bwana.

    "Ohooo. Rangi ya mende hii kaka mkubwa. Asante sana, mmmhmwaaa." Jamaa alishukuru na kuibusu ile elfu kumi. Masai akatabasamu na kuondoka eneo lile akiwa na wazo la kurudi Jumamosi mbili zijazo.

    Alinyoosha barabara moja kwa moja kutoka Buza Kanisani na kupita Buza Tanesco. Akatazama mazingira ya pale kidogo, kisha akanyoosha gari lake kuelekea Machimbo Mwisho wa Rami ambapo napo alichora alama za kutosha zitakazo msaidia kufanya mambo yake. Baada ya hapo, akakanyaga mafuta na kutitia mahali pale kwa kurudi nyumbani.

    "Nimekwishawapata wale wajinga." Masai aliongea akiwa na Malocha.

    "Kazi nzuri Kamanda. Hawa lazima tuwaue." Malocha akajibu huku akivuta glasi yake yenye juisi ya mapera na kunywa.

    "Hii kazi nitaitimiza mwenyewe Maloo. Niachie tu! Nyie tulieni."

    "Aah! Masai acha zako kaka. Hawa si watu wa kuwapiga peke yako."

    "Nimekwishapanga jinsi ya kuwadhibiti. Naomba nijaribu peke yangu. Kama ikitokea nimeshindwa, nitaomba msaada."

    "Hapana Masai. Afadhali hata uwe na msaada na mtu mwingine. Hapo sawa."

    "Okay. Nimekuelewa. Tutakuwa wote siku hiyo. Lakini naomba Lisa asijue hili. Tutafanya haya chinichini, yeye asikie tu! Tumewaadabisha."

    "Hilo si tatizo kaka. Watakaa tu wajinga hao." Malocha alifurahi baada ya kualikwa kwenye vita ile ngumu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Jumamosi tutaenda kuwaona wakipiga muziki kule Buza. Halafu Jumamosi itakayofuata tutakuwa tumekwisha wasoma vema na kuelewa njia baadhi za kuwaangamiza bila kujulikana." Masai akaongea huku anamtazama Malocha.

    "Hamna tatizo. We' ndiye kiongozi." Baada ya maongezi hayo, wakaanza habari nyingine ambazo zilikuwa zinawatoa mawazo mengine ya ajabu.

    ****

    Siku zikapita na kwenda na hatimaye ikafika Jumamosi ambayo si Malocha au Masai ambao walikuwa hawana hamu ya kuiona. Walihisi kama usiku haufiki na hata pale usiku ulipofika, waliona kama gari lao haliendi haraka kule wanapotaka. Lakini hatimaye walifika katika baa ya Toxido ambayo ilijaa walevi wengi Jumamosi ile kwa sababu ya mwezi kuwa mwisho na hata watumbuizaji waliokuwepo siku hiyo.

    "Kwa sasa Manguli Band ndio watapanda na kuanza kutumbuiza kabla ya wale watasha wetu hawajamaliza kazi yao kwa mziki mzito na wa kijanja." Mtangazaji mmoja alitangaza na wakati huo Manguli Band walikuwa wanajaribu vyombo vyao.

    Malocha na Masai waliingia katika baa ile wakiwa wamependezea sana kwa suti zao za gharama. Masai kama kawaida hakuiacha suti yake japo ilikuwa haina sumu kama ya zamani. Wakaenda katika nafasi za nyuma na gizani, kisha wakajibweteka na kuagiza vinywaji vinavyowafaa.

    "Sehemu nzuri sana hii. Inanikumbusha kipindi kile tupo sekondari." Malocha aliongea huku akifungua bia aina ya Castle na kuipitisha kinywani mwake. Masai naye hakuwa nyuma, dawa alizokuwa anameza, tayari zilikuwa zimekwisha mwilini, bia aina ya Tusker ikawa kama maji katika kinywa chake.

    "Hahaaa. Ilikuwa hatari sana. Watu tulienjoy sana." Masai akaungana na Malocha huku akigida Tusker yake.

    Manguli Band walishaanza kutumbuiza kwa nyimbo mbalimbali zilizoimbwa na magwiji wa muziki wa Tanzania wa kipindi hicho. Zilibadilishwa nyimbo mbalimbali za kuvutia na kupendeza na kila mtu aliyekuwepo pale alikuwa akitikisa kichwa kuonesha muziki ulikuwa unazama ndani ya medula zao.

    "Hao ndio Manguli Band. Wametisha sanaa." Mtangazaji aliongea kwa mbwembwe baada ya Manguli kumaliza kazi yao waliyotumia masaa mawili. Ilikuwa ni raha kwa kila mtu aliyehudhuria hasa pale wale jamaa walipoleta wanawake waliovalia vimini vya kuwavutia wanaume. Baada ya kupanda watoto hao wa kike, walianza kujimenya na kujimenyua na kufanya watu waburudike mara mia zaidi.

    Bia zilikuwa zikipita kwenda meza mbalimbali ikiwemo na ya wakina Malocha ambao tayari walishadondosha chupa sita kila mmoja.

    "Na sasa ni ule muda ambao tulikuwa tunausubiri kwa muda mrefu. Wale tunaowaita Watasha, sasa wanapanda jukwaani kwa ajili ya kuleta burudani maridadi kutoka kwenye magita yao. Tuwapigie makofi jamani." Mtangazaji alizogoa hayo na kushuka katika kile kisehemu kidogo cha kutolea burudani. Wageni waliokuja kupata burudani hiyo walikuwa wakipiga makofi kwa pamoja lakini mioyo ya Malocha na Masai ilikuwa ikiwadunda huku wakiwa kama hawaamini kile wanachokifikiria.

    "Yawezekana si PITRI hawa. Ni vipi waamue kupiga muziki kwenye mabaa? Ni kufulia au?" Malocha alionesha wasiwasi wake kuhusu Pinto na Trina.

    "Ni wenyewe Maloo. Wanafanya hivi kuvuta muda tu. Na nahisi kuna kitu hiku Buza wanakifatilia. Tutakijua tu." Masai aliongea kwa makini huku akitazama huku na huko kuona kama watu wao wataingia.

    Wakati macho ya wengi yakiwa yanajiandaa na kwa ajili ya sura za Wazungu wale, mara walisikia mlipuko mmoja mdogo wa fataki zilizopaa juu na kulipuka tena huko. Watu wakatazama juu kushuhudia mambo mazuri wanayopewa hasa kwa sababu baa ile ilikuwa haina uzio wa juu ambao utawafanya wasione mazuri hayo. Baada ya fataki, moshi mdogo ukaanza kutokea katika jukwaa ambalo wazungu wale walikuwa wanapanga kuingilia.

    Ndani ya moshi ule kwa mbali wakaanza kuonekana watu wawili wakiwa wameshika magitaa makubwa. Sekunde kadhaa, moshi ule ulititia na wazungu wawili wenye miili midogo wakaonekana mbele ya macho ya watazamaji. Shangwe la nguvu likapigwa na watu karibu wote kasoro Malocha na Masai ambao walikuwa wanazitathimini kwa kina sura zile.

    "Mbona kama si wale?" Malocha alianza kuuliza.

    "Ni wenyewe. Angalia nywele na miili yao. Ni uso tu ndio wamebadili ili wasijulikane na watu au usalama." Masai alijibu huku akiwakazia macho wale wazungu.

    "Waone walivyo. Kama watu wema, kumbe ni majoka makubwa yanayobugia na kutafuna kabla hayajameza." Malocha aliongea na kupeleka maongezi yake na mfyonzo mrefu.

    Pinto na Trina walianza kupiga magitaa yao kwa utaalam na kufanya wapenzi wa burudani wanyanyuke na kuwatuza pesa mbalimbali kutokana na shughuli yao. Walikuwa wanafanya muziki wa Rock ambao kwa Tanzania hakuna anayediriki hata kuugusa kwa sababu ya sifa zake, hasa uvutaji madawa ya kulevya na kuabudu ushetani.

    Baada ya magitaa kupigwa kwa dakika zipatazo kumi na tano, Pinto alishusha gitaa na kwenda kwenye ngoma zilizoandaliwa kwa ajili yao. Kilichofuata hapo ni muziki uliorusha nyoyo za wananchi wengi waliofika pale.

    Pinto akipiga ngoma, Trina akilikamua gitaa na kuimba kwa fujo, ni nani ambaye angekaa? Ilikuwa ni mshikemshike.

    ****

    Nusu saa mbele, Trina akabaki mbele ya wahuzuriaji akiburudisha kwa gitaa taratibu na kuimba nyimbo zinazogusa hisia. Pinto akamuacha mchumba wake na kwenda katika chumba kimoja kwa ajili ya kujisaidia.

    "Malocha." Masai akaita kwa ulevi.

    "Sema Kamanda langu." Malocha akaitika huku kalegea asijue hata ni nini kinaendelea. Pombe zilishamkamata kichwa.

    "Naenda msalani Kamanda. Nisubiri." Masai akampa taarifa Malocha ambaye alimruhusu bila shida.

    Kwa kupepesuka, Masai akanyoosha hadi kwenye chumba ambacho hutumika kama choo pale baa. Na ndipo huko Pinto alipoelekea.

    Masai alipofika katika mlango wa choo kile, aliangalia huku na huko kisha akaufungua kwa kitasa chake na kuingia ndani huku sura yake ikibadilika na kuwa sura yenye uchu na kitu na si tena ya kilevi. Akafunga mlango wa choo kile, kisha akatoa funguo malaya iwezayo kufunga na kufungua vitasa na makufuri karibu yote ya duniani. Akaufunga mlango ule kwa ndani na kisha akaangaza huku na huko kuona kama kuna watu. Hakuona chochote zaidi ya maji yaliyokuwa yanamwagika mlango fulani uliomo mle uwani.

    Masai akaupita ule mlango bila sauti yake ya viatu kutoka, akaenda sehemu ambayo wanaume hujisaidia kwa pamoja. Akaanza kufanya yake.

    Wakati anajisaidia, alisikia ule mlango wa kile choo cha ndani ukifunguliwa. Akafunga zipu yake na kunawa mikono kisha akaenda ulipo mlango wa kutokea. Hapo alimkuta Pinto akihangaika kuufungua ule mlango na kutokana na kelele zilizokuwa zinaendelea nje, hakusikika purukushani zake za kuufungua.

    "Can I help you? (Nikusaidie?)" Masai akimuuliza Pinto akiwa nyuma yake. Pinto akageuka haraka na kumuangalia aliyeongea hayo. Macho yakamtoka kama kakabwa na kiazi kitamu au anapoteza hewa ya OksijeniCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Can I help you Pinto." Masai akamuuliza tena huku akimtaja jina lake.

    Katika hali ya kushtukiza, kwenye mkono wa koti la Pinto, ikachomoka bastola ndefu sababu ya kufungwa kiwambo cha sauti. Mtoto wa kiume akaifyatua haraka, lakini Masai alikwishasoma kila mchezo. Alijibiringa kiustadi kweye sakafu ile na wakati huo Pinto alikuwa anahaha kumshambulia na bastola yake.

    Masai akawa mtu wa kwenda kulia na kushoto na mwisho wake ulikuwa mtama mzito aliomlisha Pinto na kumbwaga. Bastola ya kijana yule ikadondoka na Masai akaimalizia kwa kuipigia mbali na pale. Wote wakiwa chini wakaangaliana kwa macho ya kutamaniana.

    Pinto akawa wa kwanza kumvamia Masai kwa kurusha teke la chini kwa chini ambalo Masai alilikwepa na kwa ustadi akarusha lake lililompata Pinto kifuani na kumsogeza hadi kwenye mlango wa kutokea. Pinto akafunua suruali yake kwenye mguu wa kulia, akachomoa bastola nyingine fupi lakini Masai alishawahi kufika na wakati Pinto ananyoosha mkono wake kumlenga mwanaume yule, alikutana na teke lililopiga mkono wake na kuifanya bastola ile nayo kudondokea mbali kabisa ba yeye.

    Akiwa haamini kama yale anafanyiwa yeye tena na ngozi nyeusi, akajikuta akipokea teke lingine zito la shavu na kumfanya atokwe na damu mdomoni.

    Ulikuwa ni mpambano wa kimyakimya na wakati huo shangwe ziliendelea kuongezeka nje ya maliwato ile ambayo kulikuwa hakuna wateja walishughulika kuingia.

    Pinto akamtazama Masai kwa jicho la kithirani hasa kwa anachofanyiwa. Lakini jicho hilo halikumaanisha ndio aogopwe na adui yake bali kuendelea kuvamiwa. Masai akasogea na kurusha teke lingine kama anaye piga mpira, hapo Pinto akadaka teke hilo na kujizungusha chinichini na kuukata mguu wa Masai uliokuwa umesimama.

    Frank Masai akadondokea mgongo na kwa wepesi wa hali ya juu, Pinto akaruka kama mwenye kuogolea baharini, kichwa kizito kikatua kwenye kidevu cha Masai. Pinto akazidi kumchanganya adui yake. Akarusha ngumi kwa mkono wa kulia, ikakita kwenye shavu la Masai. Akatupa ngumi nyingine ya kushoto, ikatua pia kwenye shavu. Ngumi ya mwisho akaitupa na kutua kwenye paji la uso wa Masai. Mtoto wa kiume akakubali ngumi hizo zititie mwilini bila shida.

    Pinto akajibetua kwenda mbele na kusimama wima wakati Masai akiwa anasikilizia maumivu wa ngumi zilizorushwa na Pinto.

    Kwa kasi, Pinto akamfata adui yake na kutupa teke ambalo Masai alilizuia kwa kuweka mikono miwili usoni kwake. Alipohakikisha kuwa kazuia, akajiachia kwa nguvu toka pale chini na kumkumba Pinto maeneo ya tumboni kwa kutumia bega lake.

    Mkumbo huo ukamfanya amsukume kijana yule na kuuvunja mlango wa choo kimojawapo kati ya vinne vilivyomo mle. Pinto akalegea kwa pigo lile na Masai akaamua kuukamata mchezo. Akashika nywele laini za boya yule na kusukuma kichwa chake hadi.kwenye ukuta wa marumaru na kukigosha hapo mara tatu.

    Alipomgeuza Pinto, alikuwa anavuja damu puani na mdomoni. Masai akakwida koti la Pinto na kuubamiza mgongo wake ukutani na kijana yule alikubali yote bila kubisha.

    Baada ya kumgonga mara kadhaa ukutani, Masai akaanza kukandamiza ngumi nzito katika tumbo la Pinto na mwisho akapiga ngumi ya nguvu kwenye koo la kijana yule na kulivunja hapohapo. Pinto akawa anashuka chini huku macho yako kayatoa pima kama mgonjwa wa Pumu. Masai akawa kammaliza muuaji wa kimataifa ambaye hajawahi kushindwa vita na mapambano dhidi ya adui yake.

    Akamvuta Pinto hadi choo kingine na kumtupia huko kisha akaufunga mlango ule kwa funguo yake malaya. Akaenda kwenye sinki la maji, akanawa damu zilizokuwepo mikononi kwake na zile zinazomtoka puani. Akatoa kitambaa mfukoni na kujifuta, kisha akauendea mlango wa kutokea.

    "Nyie mnajifungia humu mnadhani choo chenu hichi." Jamaa mmoja mlevi alilalama huku anaingia msalani akionesha wazi haja ilimbana. Masai hakutaka maneno naye, akaenda hadi alipo Malocha.

    "Oyaa. Utaibwa wewe." Masai aliongea kilevi huku anamtikisa Malocha aliyekuwa kalalia meza na kubebwa na usingizi.

    "Aaah! Upo Kamanda. Naona mabwege wanaendelea kuburudisha." Malocha aliongea huku akitazama mbele bila kuangalia uso wa Masai ambao ulikuwa umevimba kiasi.

    "Ndiyo maana yake. Naona binti anafanya makubwa pale." Masai akajibu huku naye akimtazama Trina kwa makini. Tayari zilikwisha katika dakika ishirini bila Trina kumuona Pinto, macho yake yakawa yanaangaza huku na huko bila mafanikio ya kumuona mpenzi wake. Masai aliona hali ambayo Trina anayo, akatabasamu baada ya kugundua kuwa atakamilisha lengo lake muda si mrefu.

    "Ila naona kimpenzi chake kimechepuka, hakirudi." Malocha aliongea na kumfanya Masai kutabasamu bila kujibu chochote.

    "Asanteni sana jamani. Na usiku mwema kwenu." Trina alisikika kwenye kipaza sauti akiongea Kiswahili kwa shida. Akakamata gitaa lake na la mpenzi wake na kuingia chumba walichotokea mwanzo.

    "Kaka. Ngoja nikachukue vinywaji tena. Hapa hakuna kulala." Masai alimwambia Malocha na bila kupinga, Malocha akamuacha rafiki yake afanye anachokifanya. Masai kwa kuyumbayumba, akajidai mwenye kukosea njia na moja kwa moja akanyoosha kwenye kile chumba alichoingia Trina.

    Akamkuta Trina ambaye kampa mgongo anapanga gitaa lake kwenye begi maalumu la kubebea kifaa kile. Masai hakumshtua bali kumpita na kwenda sehemu moja alipovuta kiti na kwenda nacho hadi mbele ya Trina.

    "Hey beautiful. (Halo Mrembo)" Masai akamsalimia Trina ambaye aliinua kichwa chake na kumtazama yule aliyemsalimia. Macho ya Trina yakawa kama yale ya Pinto alipomuona Masai kule msalani.

    "Pinto hatunaye duniani. Ukifanikiwa kuniua, utasikia kifo chake redioni na utaona kwenye matv. Usiponiua, basi utakutana naye jehanamu." Masai akaongea huku hamtizami adui yake. Ni kama alikuwa anamdharau kwa jinsi alivyokuwa analeta mbwembwe.

    Trina akiwa kapagawa kwa taarifa zile, akafungua gitaa lake lililofunguka kama yale mabegi ya chuma ya wanafunzi wa bweni. Ndani ya gitaa, Trina akachomoka na mapanga mawili ambayo alimfata nayo Masai na kuanza kujaribu kumkata.

    Masai akawa mwepesi wa kuruka na kukwepa hatari ile. Mwanamke wa shoka hakuchoka katika kujaribu kumsambaratisha adui yake. Akawa anajaribu kumfyeka Masai kichwa chake lakini anaambulia patupu.

    Masai akatulia na kuangalia mwendo wa Trina jinsi anavyotupa mapanga yake, ndipo na yeye akasubiri mtupo fulani wa msichana yule, alipouona unakuja akakwepa tena kidogo na kisha akarusha ngumi iliyopita katikati ya mikono ya Trina na kutua puani. Kwa haraka, akapiga teke panga la kwanza na kudondoka. Trina katika mshangao, akajikuta akipoteza panga lingine lililoporwa kwa ustadi na Masai.

    Mwanaume akatupa pembeni panga lile na sasa uso wa Trina ulikuwa katika mapambano ya ana kwa ana.

    Mwanamke yule akaruka teke, na wakati yupo angani, kisu fulani kikachomoka kwenye kiatu chake na kwa ghafla, akakirusha na kutua kifuani kwa Masai tena upande ule wa suti uliokwisha. Kisu kile kikachana suti ya Masai lakini hakikumdhuru.

    Wakati Masai anashangaa uwezo wa ajabu wa yule dada, akajisahau kuwa alikuwa karukiwa teke. Akakutwa na teke hilo palepale ambapo kisu kimechana. Endapo kama kisu kingezama pale, basi teke lile lingezamisha zaidi. Masai akadondoka chini na sura yake ikakumbwa na hamaniko kubwa kwa pigo lile la kijinga.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Trina akaikuna miguu yake, na viatu vyake vikatengeneza nyayo zenye vyuma vyenye ncha kali. Akamfata Masai ambaye alikuwa chini na hatambui kama viatu vya adui yake vimebadilika. Teke likatoka kwenye mguu wa Trina, Masai akajaribu kulizuia kwa mkono, matokeo yake ilikuwa suti yake kuchanwa katika mkono huo na ngozi yake ya mwili kiasi ikakwanguliwa.

    "Hapa umekutana na nyoka, mbwa wee." Trina aliongea kiitaliano na kumfuata adui yake na kutaka kumkanyaga mkono wake, lakini akakosa mkanyago huo baada ya Masai kuutoa haraka pale sakafuni.

    Trina akageuza kibao kwa kurusha teke la mguu mwingine ambalo nalo Masai alilikwepa kwa kujivilinga sarakasi ya kinyume huku akiwa bado chini. Haraka Trina, akachomoka na kuruka juu tayari kwa kumkanyaga Masai kwa viatu vyake vyenye vyuma. Kidume akabiringita tena upande wa kushoto na kisha akasimama na kumtazama Trina aliyegeuza shingo yake na kukutana na uso wa mwanaume wa shoka ukitabasamu tabasamu la mauaji.

    "You are going down, you Monkey. (Unadondoka/ Nakudondosha nyani wewe)" Trina akamkashifu Masai kwa kumuita nyani kwa sababu ya rangi yake nyeusi.

    "Monkey’s fighting with pig. Guess what? ( Nyani anapigana na nguruwe. Otea nini)" Masai naye akajibu kashfa huku akitabasamu tabasamu la upande mmoja wa mdomo wake.

    Trina akaacha maongezi na kujitoma kwenye mpambano kwa kasi ya ajabu. Mateke aliyokuwa anayaruka, hayakuwa ya kitoto. Alijizungusha na kumpiga Masai mateke karibu matano bila majibu. Mtoto wa kike akisimama wima na kumuangalia mtu anayepigana naye kama anaweza kunyanyuka kwa kichapo kile.

    Masai akapiga ngumi sakafu kuonesha kachukia kile kitendo cha Trina kumgonga vile. Akainuka haraka na kwenda alipo Trina aliyezidi kumuadabisha yule mwanaume kwa kumtuliza kwa teke la kifua na baada ya hapo akamaliza kwa teke lingine lililomsababishia Masai kuchubuka kifuani sababu ya vile viatu vyenye ncha kali chini yake.

    Trina akatabasamu baada ya kuona mtoto wa kiume anatiririka damu. Akamfuata Masai pale chini alipokuwa kapiga goti moja, akarusha teke ambalo alilenga kumpiga kidevuni, lakini Masai tayari alikuwa amesoma mwenendo mzima wa pigo lile. Akakwepa kwa kurudisha kichwa chake nyuma na teke lile likapiga hewa.

    Katika hali ambayo Trina hakuitegemea, akajikuta tayari imemkumba kwa yeye kudondoka. chini baada ya mtama mzito toka kwa mwanaume wa shoka, Frank Masai. Akiwa katika taharuki ya mtama mzito wa Masai, Trina anapokea teke lingine la mdomo akiwa bado palepale chini.

    Masai anajibetua kwenda mbele na kusimama wima na wakati huo muziki wa kawaida toka kwa DJ wa kilabu kile, ulikuwa unazidi kupamba moto huko nje hata wasisikie purupushani kati ya Trina na Masai.

    Trina anapitisha kidole kwenye mdomo wake, anachota damu inayomtoka. Anaiangalia kwa macho makali, kisha anamtazama Masai aliyesimama wima huku kakunja ngumi tayari kwa kumngoja yule mwanamke asimame. Trina analamba ile damu, huku anamtazama Masai kwa macho ya shari pekee. Baada ya kuonja utamu wa damu yake, sasa anakuwa kama kapagawa. Anaruka sarakasi ya chinichini hadi karibu na Masai. Anataka kumkata mtama, lakini kidume anakwepa kwa kuruka kidogo juu. Akiwa juu, Trina anajibetua kwa makini na kumtandandika teke la tumbo mwanaume. Masai anasogezwa nyuma kidogo lakini hadhuriki na teke lile japo limesheheni vyuma vya hatari chini yake.

    Trina hamuachi Masai, anaruka mtupu na kusogea alipo adui yake na kuanza kurusha ngumi kadha wa kadha zilizokuwa zinamsambaratisha Masai ambaye alishachoka kwa sababu ya mapigano yake na Pinto pamoja na kuchanwa kifuani. Trina anamiliki mpambano na hali ya ushindi inaanza kunukia hasa pale Masai alipokuwa hafanyi lolote kuzuia mapigo ya Trina.

    Ngumi kali ya kummaliza Masai, Trina anaivutia toka mbali na kuipeleka kwa kasi kwenda kwenye uso wa Masai. Lakini bahati inakuwa si yake baada ya Masai kukwepa na ngumi ile kugonga ukuta mgumu uliyojengwa kwa theruji bora ya twiga.

    Trina anajikuta akiumia mkono wake wa mapambano na Masai halazi damu baada ya kuona hayo. Anamtandika ngumi ya shavu binti yule, kabla hajafikiria kujibu mapigo, kidume anarusha ngumi nyingine kali inayokita puani kwa mtoto mzuri Trina na kumsogeza mbali na pale. Trina anahisi hali kuwa mbaya, anajaribu kutupa ngumi yake ambayo haijaumia, Masai anaidaka vema, kisha anaunyonga mkono ule kwa nguvu zake zote na kuuvunja. Trina analia kama mtoto wa kitanzania kanyimwa titi. Au kama mbwa kapigwa kwa jiwe la mbavu.

    Masai anamgeuza Trina na kuzidi kuunyonga mkono ule nyuma ya mgongo wake na kusababisha maumivu kwa Trina.

    Kwa kasi, anamsukumia Trina ukutani, mtoto wa kike anajigonga paji la uso na kifua chake. Anaachiwa mkono wake, na Masai anaanza kumpiga ngumi nzito ubavu kwa ubavu. Trina analegea kama denda la tahira akiwa bado anautazama ukuta.



    Baada ya ngumi nyingi, Masai anampiga binti yule nyuma ya magoti, Trina anasaliti amri mwenyewe na kujikuta anapiga magoti huku bado anatazama ukuta na akiwa kalegea kwa kichapo kikali. Masai anamuacha Trina pale alipopiga magoti ya kwenda kwenye gitaa la binti yule alilolikuta wazi. Akapekuwa na kutoa kisu aina ya mundu. Kisu hicho ni sawa na kile kinachotumika kukatia majani ya mifugo sema alichokamata Masai ni kikali na kinatisha hata kwa kukitazama.

    "Auae kwa upanga, hufa kwa upanga." Masai aliongea maneno hayo kwa lugha ya Kiitaliano ambayo Trina ilimuingia vema ubongoni. Masai akamgeuza Trina, na wakawa wanatazamana.

    "Umeshinda mbwa wewe." Trina aliongea kwa shida huku damu zikimtoka puani na mdomoni.

    "Sijawahi kushindwa hata mara moja." Masai akamjibu Trina.

    "Utashindwa tu! Siku moja." Trina alitoa maneno ambayo yalimfanya Masai acheke kidogo.

    "If I will loose, I will die trying. Just like what I did to you suckers. (Kama nitashindwa, nitajaribu hadi nife. Kama nilivyofanya kwa nyie wajinga)" Masai aliongea huku akipita nyuma ya Trina na kusimama mgongoni kwake.

    "One day we will meet again Masai (Siku moja tutakutana tena Masai)" Trina aliongea akiwa tayari kukipokea kifo chake. Masai akamziba Trina mdomo kwa mkono na kuweka ile mundu shingoni kwa binti yule.

    "Sehemu yako ni kuzimu baada ya hapa, na mimi ni paradiso. Vipi tutakutana? Msalimie Lusifa. Mwambie kuna zaidi yake huku duniani lakini hayupo upande wake. Nendeni mkazae muongezeke huko kuzimu, wewe na Pinto." Masai akapitisha mundu ile kwenye shingo ya Trina na damu zikaruka na kuchafua ukuta. Trina akaachiwa mwili wake na kudondoka mzima mzima kama kigunia cha mapera.

    Mwanaume akawa kamaliza kazi nzito iliyotaka kugharimu maisha yake. Akatoka mle ndani kwa makini, kisha akapitiliza hadi maliwato ambapo alinawa mikono yake vema na kwenda kwenye meza aliyomuacha Malocha.

    "Oya kaka. Duuuh! Umezima." Masai aliongea huku akimtikisa rafiki yake. Alichukua dakika kama kumi na nane kupambana na Trina, lakini kwa Malocha aliona kama dakika tatu tu sababu ya pombe ambazo alibwia siku hiyo.

    "Aaagh. Umeleta nyingine tayari." Malocha aliongea huku akitikisa chupa za pombe zilizopo mezani.

    "Twende nyumbani kaka. Umekunywa sana." Masai alimwambia Malocha huku akijaribu kumnyanyua pale alipokuwa kakaa. Malocha akanyanyuka huku akibeua beua hovyo kama mbuzi aliyeshiba majani na maji. Masai akaweka mkono wa Malocha begani kwake na kuanza kutoka naye kwenye kile kilabu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Aaah! Kaka. Umekuja kuwaona wale Watasha." Jamaa wa bodaboda alitokea mbele ya Masai na kwa furaha akamuuliza.

    "Nimeonana nao wote. Kesho utapata taarifa njema sana." Masai akajibu huku katabasamu.

    "Naisubiri hiyo asubuhi maana si kesho tena, hii tayari ni siku mpya." Jamaa yule aliongea huku akijitahidi kuelewesha majira na mabadiliko yake. Ilikuwa ni saa nane usiku muda huo walipokutana.

    "Okay. Asubuhi njoo hapa utakuta taarifa njema." Masai aliongea na kumkokota Malocha hadi lilipo gari lao. Akampandisha rafiki yake na kuondoka eneo lile huku huko ndani ya kilabu kukiendelea kuwashwa moto wa burudani.

    ****



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog