Simulizi : Duka La Roho
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Masai, Masai,
Masai." Sauti ya Mubah iliita nje ya chumba cha Malocha aliyelala na Masai siku
hiyo. Masai na Malocha wote wakaamka na kutazama saa. Ilikuwa ni saa nne
asubuhi. Sauti ya Mubah iliendelea kuita pale mlangoni.
"Nini wewe."
Malocha aling'aka kwa hasira.
"Pinto na Trina." Mubah akajibu na
kufanya kimya kitawale baina yake na Malocha.
"Wamefanyaje?" Malocha
ikabidi aulize kile ambacho Mubah alipaswa kukimalizia.
"Wamekutwa
wameuawa Toxido Bar." Baada ya maneno hayo ya Mubah, Malocha akamuangalia Masai.
Masai akaangalia pembeni na kujifanya anapiga mhayo mrefu.
Malocha
akampiga kofi zito la kisogoni rafiki yake. "Wewe ndio umewaua?" Swali la ukali
likatoka kwa sauti toka kinywani kwa Malocha.
"Si mimi mkuu.
Wametangaza kuwa kuna alama za vidole vya Masai ndivyo walivyovikuta katika kila
mwili." Mubah alijibu kana kwamba yeye ndiye aliyeulizwa.
"Sikuulizi
wewe pumbavu. Embu toka hapo mlangoni." Malocha akafoka na kumfanya Mubah
aondoke.
"Sasa kwa nini hukunishirikisha?" Malocha akamuuliza
Masai.
"Ungeweza na pombe zako ulizokuwa umezimimina?" Masai akamjibu
kwa swali huku akivua nguo alizokuwa nazo na mara kifuani Malocha akaona kidonda
alichojeruhiwa rafiki yake. Akayafikiria maneno yale ya Masai, akaona yana
ukweli ndani yake hasa kwa jinsi Masai alivyokuwa. Kavimba na kuchoka japo si
kawaida yake hata anywe pombe chupa mia.
"Lakini si ulisema tutafanya
Jumamosi ijayo?"
"Zege halilali bro. Sina muda wa kuwaremba maadui."
Masai akajibu huku anavaa singlendi fulani yenye rangi nyekundu. "Pia sikutaka
kukuingiza matatizoni hadi alama zako zionekane kwenye miili ya wale wajinga."
Masai akamaliza.
"Daaah! Sasa uliwezaje kuwaua?" Malocha akauliza na
Masai akampa hadithi nzima ilivyokuwa. "Mmmh! Naishi na gaidi bila kujua."
Malocha akaongea kwa utani na kunyanyuka pale kitandani. Wakavaa nguo za mazoezi
na kutoka chumbani.
"Baby." Lisa alimkimbilia Masai na
kumkumbatia.
"Wenye baby wao hao." Malocha akatania huku akiwapita
Masai na Lisa waliokumbatiana.
"Jibebe au jikumbatie mwenyewe." Mubah
hakuwa nyuma kumshushua bosi wake.
"Umeona eeh Mubah." Lisa akaongea
huku akitoka mwilini kwa Masai.
"Halafu mnatakiwa kuwa na wapenzi nyie
wajinga. Mmekaa humu kama mazuzu. Hasa we' Malocha." Masai alitania na wote
wakacheka.
"Pole sana." Lisa alimpa pole mpenzi wake na kisha kwenda
kuchukua vifaa vya huduma ya kwanza na mara moja huduma
ikaanza.
****
"Mjinga kawamaliza wale wajinga." Gunner
aliongea huku akiwa na kundi lake.
"Walikosea mara ya kwanza
walipomkosa. Hawakumjua Masai, walidhani wanapambana na kibabu kizee." Lobo
aliongea huku safari hii akiifuta bastola yake nyeusi kwa kitambaa chenye mafuta
ya breki.
"Mmh! We Lobo mbona unamsifia sana Masai." Ikabidi Gunner
aulize maana alishachoshwa na ile hali ya Lobo kumsifia Masai.
"Kwa
sababu anajua anachokifanya. Ni mimi pekee ndiye naweza kupambana naye na si
wale wajinga wa kumendea." Lobo alisindikiza maneno hayo kwa kuikoki bastola
yake.
"Mmh! Alishakuua yule, leo unajidai
mjanja."
"Hakuniua. Alifanya vile sababu sikuwa namjua vema. Sasa hivi
namjua vizuri. Nimeshamsoma adui yangu, sasa ajiandae tu." Lobo aliongea kwa
kujiamini.
"Tutaona." Gunner akaongea na kukaa sawa kochini
kwake.
"Shadow akipiga simu, mwambie tunahitaji ile bidhaa ya
Malaysia." Lobo akatoa ombi kwenda kwa Gunner. Akiwa anajiandaa kujibu, simu
yake ikaita kwa namba nyingine tofauti kabisa na zile ambazo alizoea kupigiwa
nazo. Kifupi hakuwahi kuziona namba zile. Akajua huyo ni The Shadow lakini yupo
nchi nyingine tofauti na ile aliyompigia hapo nyuma.
"Haloo." Gunner
akapokea na kuita.
"Nadhani mmepata taarifa za Pinto na Trina." Sauti
nyembamba ilisikika. Ni tofauti na ile ambayo aliongea nayo mara ya mwisho
ambayo ilikuwa nene kama kanda ya redio inayoliwa.
"Ndiyo mkuu."
Gunner akajibu kwa heshima zote.
"Sasa nalaumiwa huku na baadhi ya
wajinga kwa kitendo cha huyo mbwa mmoja. Nataka ndani ya wiki mbili kuanzia
sasa, muue wote hao. Mkianza na Masai." The Shadow akatoa majukumu mengine kwa
kundi la Gunner. Gunner akatabasamu na kumuangalia Lobo.
"Usijali
mkuu."
"Mnataka nini niwaongezee." The Shadow akauliza.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Malaysia na
wanawake wa Iran watano." Gunner akajibu.
"Imepita. Kesho kawapokee
burundi. Huko mtapata magari yatakayowarudisha Tanzania." Maneno hayo yakawa ya
mwisho kwa The Shadow. Simu ikakatwa.
"Back in business. (Tunarudi
biasharani)" Gunner aliongea kwa tabasamu huku akimuangalia Lobo, na Lobo naye
akakita risasi kwenye bastola yake na kuifanya ilie mlio wa kuwa tayari kwa
kazi.
****
Kesho yake Gunner na Lobo walichukua ndege ya
kukodi ambayo iliwapeleka hadi uwanja fulani wa vumbi uliopo
Burundi.
Baada ya kushuka toka kwenye ndege hiyo, gari ya kizamani
kabisa ilitokea nyuma ya ndege ile. Ilikuwa Land Rover One Ten toleo la kwanza
la Muingereza.
"Naitwa Buyangi Mukundilii. Mimi ndiye nitawafikisha
mpatakapo." Dereva wa gari aliongea huku akiwapokea mizigo Lobo na Gunner na
kuitupa siti za nyuma ambazo zilikuwa hazina makwisheni. "Mtakaa huku nyie."
Buyangi aliongea harakaharaka na kuwafungulia mlango ambao aliung'oa tu na
wakina Lobo wakaingia kisha jamaa yule msanii, akaupachika tena mlango wake na
safari ndefu ikaanza.
"Hapo ndipo nilipoambiwa niwalete." Buyangi
aliwapa taarifa wageni wake huku akiwaonesha kiwanda ambacho hakitumiwi.
Kilijengwa kwa mabati kwa asilimia zote.
Buyangi, akatoka nje ya gari
lake na kufungua mlango kwa njia ileile ya mwanzo. Lobo na Gunner wakatoka na
kupewa mikoba yao.
"Asante Mkuu." Gunner akashukuru na Buyangi
akaondoka eneo lile.
Wakapiga hatua zipatazo kumi kwenda kwenye jengo
lile lakini walipotaka kusogea mbele zaidi, risasi kadhaa zikapigwa chini, mbele
ya miguu yao na kuwafanya wasimame.
"Nyie ni nini na mwataka nani."
Sauti ya kike iliuliza lakini hakuoneka ni wapi alipo.
"Gunner, Lobo.
Toka kwa The Shadow." Baada ya maneno hayo ya Lobo, kwenye kichaka kimoja
akatokea kwanamke mrefu na mwembaba huku begani kabeba SMG akawafuata wageni
wale waliposimama.
Akawatazama usoni kwa sekunde, kisha akapiga makofi
matatu. Hapo akashuka mwanamke mmoja toka mtini ambaye kavaa kajani na kumfanya
aonekane naye kama mti. Mkononi alikuwa kakamata sniper rifle, bunduki maalumu
kwa wadunguaji.
Mwanamke mwingine akatokea nyuma ya wakina Gunner naye
kabeba SMG. Lakini wote walikuwa Warundi.
"Twendeni huku." Yule wa
kwanza kujitokeza akawa mbele yao kuwaongoza wote. Gunner akatazama makalio ya
yule mwanamke na kumbonyeza Lobo ambaye alitabasamu bila kusema
chochote.
"Mkiendelesa huo upumbafu wenu, natwanga mashine zenu
bullet." Mwanamke yule alichimba mkwara ambao ulifanya Gunner atengeneze picha
wakati anapigwa risasi nyeti zake. Akajikuta anazikamata.
Ndani ya
jengo lile, walikuta wanawake watano wamevalia majuba meusi na kuvaa shungi
zilizozunguka nyuso zao vema. Walikuwa ni warembo kwa kuwaangalia, ila
walichotumwa kukifanya, urembo wao usingeuona.
Gunner na Lobo
wakasimama upande wa meza moja ndefu na hapo mwanamke mmoja wa Kiiran, akasukuma
mkoba (briefcase) ikawaendea wale jamaa wawili, yaani Lobo na
Gunner.
Wakafungua ule mkoba kwa namba maalumu ambazo walikuwa nazo
toka Tanzania. Mkoba ukafunguka na macho yao yakatua kwenye vibanio kumi. Ni
sawa na kibanio alichopewa Martina katika siku yake ya kuzaliwa, na ni kilekile
kilichotema sumu kwa Mubah.
Gunner akatabasamu na Lobo akakenua kwa
kazi ambayo waliitazama mbele yao. Kumuangamiza Masai tu.
"Good Job
(kazi nzuri)" Lobo akatamka na wanawake wote wakatabasamu.
Mlango
walioingilia, ukafungwa na kufunguka mlango mwingine ambao waliambiwa waende
huko pamoja na wasichana wao waliowaomba kwa The Shadow. Huko wakakuta gari sita
za kifahari zikiwasubiri. Lobo na Gunner wakapanda gari moja, na wale wanawake
wa Iran, wakapanda kila mmoja ya kwake lakini wakaiweka katikati gari
walilopanda wakina Gunner. Safari ya kwenda Tanzania, ikachukua nafasi
yake.
Ni kama msafara wa matajiri wa mafuta wakikatisha jangwani kwa
jinsi vumbi lilivyokuwa linatimka kutokana na gari zile za bei mbaya kwenda
mwendo wa kasi kupindukia.
Zilipita katika barabara ya vumbi ambayo
haina watu wengi na baadaye gari zile zikaingia kwenye mpaka wa Uganda ambapo
ndipo walipopanga kuingilia kwa sababu ya kufupisha safari yao ya kuja
Tanzania.
Mpakani hawakukukaa sana kwa sababu wale wa mpakani
walikwishapata taarifa za ujio ule. Wakawapa na msaada hadi kwenye mpaka wa
kuingilia Tanzania uliopo Kagera. Huko pia hawakupata shida ya kuvuka mpakani,
wakachukuliwa tena hadi Bukoba ambapo walipata meli kubwa iliyobeba na magari
yao. Meli hiyo ikawasukuma hadi Mwanza kupitia Ziwa Victoria. Ziwa linalosifika
kutoa samaki watamu wa Sato.
"Ni Mwanza hii Lobo. Tuanzie kazi hapa au
twende tukaanzie Dar es Salaam." Gunner alimuuliza John Lobo ambaye muda mwingi
alikuwa akiutumia kutazama maajabu ya jiji lile tajiri kwa
mawe.
"Hapahapa ndipo pa kuwapa taarifa wale wajinga. Lazima wajue
kuwa Duka La Roho limerudi kuuza na kununua tu!" Lobo alijibu huku uso wake
ukionesha chuki isiyo na kifani.
"Watakaa tu." Gunner akampa tano Lobo
na wote wakashuka toka katika gari lao na kuwaamuru na wale wanawake washuke kwa
sababu walikuwa wamefika katika hoteli moja kubwa na ya kisasa iliyopo Jijini
Mwanza.
"Tuna vitendea kazi vyetu." Mrembo mmoja
kati ya wale watano aliongea kwa shida lugha ya Kiingereza.
"Njoeni
navyo vyote huku ndani." Gunner akawajibu na yeye akiwa na Lobo wakaenda
mapokezi ya hoteli ile.
"Vyumba vitatu vinavyokaribiana na viwe vya
juu." Gunner aliongea na mhudumu wa mapokezi baada ya kuulizwa aina ya vyumba
anavyovihitaji.
"Hizi hapa funguo kaka." Mhudumu akampa kadi maalumu
ambazo zinafungua milango waliyokuwa wamepangiwa. Baada ya kukabidhiwa funguo,
Gunner na Lobo wakalipia vyumba vyote kwa siku tatu.
Baada ya malipo,
wanawake wale watano waliingia wakiwa na mabegi makubwa mawili kila mmoja.
Muhudumu alishikwa na butwaa lakini hakuuliza kwa sababu wateja wake tayari
walishafanya malipo muhimu.
Gunner na Lobo wakasaidia mabegi baadhi na
kuelekea ilipo lift ya kuwapeleka juu ya hoteli ambako kulikuwa na vyumba
vyao.
"Wawili ufunguo huu, na watatu ufunguo huu. Mkisha jipanga,
njoeni chumba hichi. Kuna kazi ya kufanya kesho asubuhi." Gunner alitoa maelezo
huku akiwakabidhi wanawake wale funguo maalumu za kufungulia milango yao.
Wakaingia vyumbani na kujifungia huko kwa muda mrefu wakipanga kwa hili na
lile.
*****
KITUO KIKUU CHA POLISI
MWANZA.
Wanawake watano waliyovalia suruali za jinzi pamoja na fulana
nyekundu na nyeusi zilizoandikwa DUKA LA ROHO halafu kwa chini kuna mchoro wa
mzani. Upande mmoja wa mzani kuna bunduki kubwa, na upande mwingine kuna mkono
umekamata moyo na kuutumbukiza kwenye sahani ya maalumu ya mzani ule. Yaani
bunduki, inapimana uzito na moyo wa binadamu, sijui kipi kitashinda mwenzake
uzito.
Wanawake wale hawakuziba nyuso zao na watatu kati yao, mikononi
mwao walikamata bunduki hatari za kivita. Huku wawili wakiwa wameshikilia kamera
za kuchukulia stili picha (video) na wakionesha wapo makini na kazi yao.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tanzania."
Mwanadada mmoja aliita kwa sauti ya kithilani baada ya kamera kuelekezewa kwake.
"You have two days to give us Frank Masai and his crew. Only two days you got.
If nothing happen, Duka La Roho is comes to take what's mine.(Mna siku mbili za
kutupa Frank Masai na kundi lake. Siku mbili tu! Kama hamna kitakachotokea, Duka
La Roho litachukua kilicho chake)" Maneno hayo yakaongozwa na risasi tatu
zilizowapata askari polisi wawili na kuwamaliza palepale.
"Tick Tock."
Dada mwingine alimaliza maongezi yale na mjadala ukafungwa hapo. Wakatoka nje
ambapo walichukua gari fulani walilolikodi pale hotelini, na kwa fujo wakaondoka
kuelekea walipopanga kukutana na wakina Gunner.
****
"Sasa
hao askari wamefanya nini?" Lilikuwa ni swali la Masai baada ya kuangalia tukio
zima lililotokea Mwanza asubuhi ile.
"Nadhani ni ujumbe tu kwenda kwa
wanausalama." Malocha akamjibu wakati huo watu wote kasoro Martina aliyekuwa
kalala, walikuwa sebuleni wakitazama taarifa hiyo iliyozagaa mtandaoni na katika
vyombo vya habari.
"Siku mbili wametoa. Ngoja tuone baada ya siku hizo
nini kitatokea." Masai aliongea huku akinyanyuka toka.kwenye kochi alilokuwa
amekalia na kuelekea chumbani alipokuwa kalala Martina. Mubah akakamata rimoti
na kubadili stesheni ya runinga ile kwa kuweka stesheni ya
miziki.
BAADA YA SIKU MBILI
Dar es Salaam ilikuwa imepamba
moto kwa mauaji ya polisi na wanausalama wa taifa ambao walikuwa wanajulikana
mtaani na sehemu wanazoishi. Polisi wa barabarani walikutwa wamejifia na katika
mavazi yao kuliandikwa Duka La Roho. Gari za jeshi zilizokuwa zinawarudisha watu
hawa majumbani mwao, zilitekwa na wanajeshi walipata shida na mateso hadi kufa.
Ilikuwa ni mshikemshike ndani ya Tanzania.
Ndani ya siku nne,
kulikuwa hakuna askari anayeonekana hovyo jijini. Wananchi wenye hila na mioyo
isiyopenda amani, ndio ukawa muda wao wa kujidai. Sheria wakazivunja na
kijichukulia majukumu hata ambayo hayawahusu. Hapo ndipo wananchi walielewa nini
maana ya kuanzishwa vyombo vya ulinzi na usalama.
Machozi yaliwatoka
wale wasiyo na nguvu kwani walishindwa kwenda kudai haki zao sehemu husika.
Ubakaji, wizi, uzinzi, unyanyasaji, ukakua na kutanuka kwa kasi ya ajabu ndani
ya siku chache tu. Ilikuwa inatisha Dar es Salaam.
Tambua kazi za
vyombo vya usalama hasa majeshi yetu ya polisi. Usidharau wakifanyacho kwani wao
ndio amani muhimu ya hii nchi.
Hakuna askari, basi amani nayo huwa
sifuri na huwa hivyo daima. Kila chozi la mnyonge hutegemea vyombo hivi muhimu.
Hata wanasheria, hawawezi kufanya chochote bila jeshi la polisi. Tuheshimu
vyombo hivi kama tunavyoheshimu kazi zetu za mikono au tunavyoheshimu chakula.
Tuwape heshima yao wanausalama wote. Dharau, kejeli, chuki na hila baina ya
vyombo hivi, havijengi nchi bali kuibomoa.
****
"Naona
majamaa wamechachamaa jijini." Malocha aliongea huku anamtazama
Masai.
"Wamekuwa moto sana na wakifanyacho, nadhani kitakuwa kina
madhara makubwa katika mambo yetu." Masai aliongea kwa
utaratibu.
"Tunaweza kufanya nini ili kukomboa amani ya nchi
hii."
"Hakuna kingine zaidi ya kumpigia simu Rais." Masai akajibu.
Malocha akashusha pumzi ndefu kisha akawaita wenzake wote ili wajadiliane suala
lile.
"Martina naomba nimpeleke kwa rafiki yangu. Huko nadhani atakuwa
salama." Lisa alitoa pendekezo baada ya kukubaliana na mawazo yao ya kumpigia
simu rais. Masai alikubaliana na Lisa kuhusu Martina kwa sababu ni ngumu sana
kumuhusisha mtoto kwenye matatizo makubwa kama yale.
"Hallow." Malocha
aliita baada ya kusikia upande wa pili wa simu aliyoipiga ikiita. "Malocha
hapa." Akajitambulisha.
"Afadhali nimekupata kijana, nakuomba urudi
FISSA. Ni kweli nina makosa na nilikuwa siyajui ndio maana nikakutoa bila
kufikiria. Mambo yamekuwa magumu toka uondoke. Nimenusurika kuuawa mara mbili."
Rais alikuwa mpole wakati anaongea hayo na hakutoa nafasi ya Malocha kuongea
hadi alipomaliza.
"Yawezekana hujui kama pia ulitakiwa kuuawa siku
Rais wa Urusi alipokuja." Malocha akaongeza habari iliyomfanya Rais ashikwe na
kigugumizi.
"Mbona huongei mkuu." Malocha akamuuliza Rais wake baada
ya kutosikia sauti yake.
"Mambo makubwa haya. Au ndio ule mlipuko
uliyotokea siku ile?" Rais akauliza.
"Hata PITRI walikuja kuuteketeza
uma. Na hiyo tunakulaumu wewe kwa sababu yasemekana
uliwalea."
"Tuyaache hayo Malocha. Nakuhitaji wewe na kundi lako,
FISSA inateketea kwa sababu ya upofu wangu. Wale wema wote, wameuawa na Lobo.
Kifupi FISSA imekuwa ya magaidi inayoongozwa na Gunner." Rais alionesha wazi
kuwa sasa maji yapo shingoni.
"Nipo na Masai hapa." Malocha aliongea
huku akimkabidhi simu Masai.
"Ndio mkuu." Masai
akaita.
"Kwako sina la kusema kwa sababu unatafutwa sana. Cha msingi,
leo tukutane kisiri siri ili tupange mpango utakao tutoa katika hili sakata
zito." Rais akashauri.
"Hayo ndio tunataka kuyasikia. Ni sisi na wewe
tu. Hatuhitaji mtu mwingine."
"Limepita." Rais akapitisha ombi ambalo
wote walinufaika. Wakapanga pa kukutana na kila kitu cha
muhimu.
*****
Hali bado ilikuwa mbaya katika jiji la Dar
es Salaam. Hakuna watu kuzurula usiku kwa sababu ya kundi lililojiita Duka La
Roho kutishia amani ya kila mwananchi. Polisi hawakuenda makazini kwa sababu ya
kitete cha kuuawa. Kifupi maisha ya kila mmoja yalikuwa rehani.
Wakati
hayo yanaendelea, kundi lililorudi kwa kasi kwa ajili ya kulipa kisasi cha
mauaji ya Pinto na Trina, kulipuliwa kwa ndege yao muhimu ambayo ingesababisha
Rais wa Urusi kufa na kuharibiwa mtambo wa SGT, lilikuwa linazidi kupanga
mipango kabambe ya kufanya ili kuwachimbua Masai na kundi lake kule
walipo.
"Dar es Salaam sasa ipo kimya. Wamefumba midomo yao. Mkoa
unaofuata ni Arusha. Kama kawaida yetu, ni tifu hadi wamfukue huyo boya wao
wanaomuita Masai." Gunner aliongea kwa lugha ambayo kila aliyemsikia pale
walipokuwepo, alimuelewa.
"Hapa kazi kwa vitendo. Siku mbili za
kuwapa. Hawamfukui mbwa wao, basi kitakachofuata ni mauaji tu." Lobo akachangia
mawazo ambayo kila mmoja alitikisa kichwa kukubaliana naye.
"Tomorrow.
(Kesho)" Gunner akatabasamu baada ya maneno hayo kumtoka kinywani. Ni kama
walikuwa wanafanya jambo la sahihi sana, kumbe walikuwa wanazidi kuhangamia
nafsi zao.
*****
"Tuachie kazi sisi mkuu. Hawa tutawazima
tu." Malocha alikuwa anampa moyo Rais baada ya kukutana naye katika daraja moja
kubwa lililopo nje ya Jiji la Dar es Salaam.
"Niwafanyie nini jamani."
Rais aliwauliza Masai na Malocha ambao ndio walikuwa wameenda kukutana
naye.
"Tunahitaji silaha nzito. Wale watu tunaopigana nao wamekula
kiapo cha damu. Wamezaliwa kufanya yale, hivyo tunaomba silaha ambazo zinaweza
kudumu katika mapambano haya." Masai akajibu.
"Okay. Kesho mida kama
hii, nitakuwa na mzigo mzima muutakao. Kumbukeni nafanya haya kwa mapenzi ya
nchi hii. Ni kweli nimekosea, lakini sasa nataka kurekebisha hali hii. Baada ya
kuwamaliza wale wajinga, mtarudi kwenye viti vyenu, ila Masai kuna kazi ngumu
unayo ili kuepuka mikono ya wapelelezi wanaokutafuta."
"Usijali
kuhusu mimi. Nitakuwa salama baada ya kumaliza haya."
"Huwezi kuwa
salama kamwe. Utajificha hadi lini na taifa linahitaji msaada wako? Unatakiwa
kuwa huru kijana." Masai akafikiria maneno ya Rais mara kadhaa hasa kuhusu mtoto
wake Martina. Akaona wazi anahitaji ukaribu na Martina. CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Fanya uonalo
sahihi." Masai akajibu na kuingia kwenye gari walilokuja nalo yeye na Malocha.
Rais akakubali kwa kichwa naye akaingia kwenye gari lake na kuondoka. ****
Katika jiji kubwa la Arusha, anaonekana mwanaume mmoja akiwa barabarani kavaa
sare za jeshi.
Basi kubwa lililosheheni wanajeshi, linafika
aliposimama yule bwana na kusimama. Jamaa anaingia ndani ya basi na kusimama
katikati ya gari lile kwa sababu sehemu za kukaa zilikuwa
zimekwisha.
Alikuwa ni Gunner ndani ya basi la jeshi. Akachomoa
kibanio kimoja toka kwenye mifuko yake ya kombati alilovaa, kisha akajidai
anajifunga kamba za viatu. Akakiweka kibanio chake chini bila mtu kumuona.
Alipomaliza kufunga kamba za viatu, akasimama huku banio lile akiliacha palepale
chini. Akasukuma kwa mguu wake banio lile chini ya kiti kimoja mle ndani ya
basi.
Akatoka pale aliposimama na kwenda mbele karibu na dereva.
Dakika tatu mbele, vikohozi kwa baadhi ya wanajeshi vilianza kusikika. Gunner
akatoa kitambaa cha kujifutia jasho na kuziba pua zake huku akijitahidi kutovuta
hewa mara nyingi. Mbele kidogo alimuona dereva anaanza kulegea, akawahi
'sterling' ya basi lile na kuanza kuliongoza kwa mkono mmoja na mkono mwingine
ukiwa puani umekamata kitambaa.
Dereva yule akadondoka kabisa na
kumpa fursa Gunner kukaa na kulisimamisha gari lile lilklokuwa na wanajeshi
karibu sitini.
Baada ya kusimama, zikatokea gari mbili za kifahari
mbele yake. Ni zilezile walizotoka nazo Burundi. Zikasimama na wanawake wanne
wakashuka pamoja na vifaa vya kuchukulia video na mara moja wakaanza kazi
yao.
****
Usiku wa saa mbili, Rais alikuwa amekuja na
silaha nzito za maangamizi kwa ajili ya kuwawapa watu wake. Licha ya silaha
hizo, pia Rais alikuwa katika majonzi hasa baada ya kupokea mkanda uliokuwa
unaonesha wanajeshi wakipukutika miili yao na kubaki mafuvu yaliyokuwa yamevalia
gwanda maalumu za jeshi.
"Jamani naombeni watu hawa mpambane nao. Mimi
nashindwa cha kufanya." Rais aliongea kwa majonzi.
"Usijali mkuu.
Maadam umetualika kwenye kalamu yako, basi kila kitu kitatulia." Malocha alimpa
moyo Rais huku akitazama bunduki zilizoletwa na Rais kisha kumpasia Masai naye
azitazame.
"Leo hii usiku, safari ya Arusha inaanza." Masai akaongea
maneno baada ya kulidhika na silaha zilizoletwa. Na hakika zilikuwa silaha
nzito.
"Safi sana. Nitawashukuru mkiwanyamazisha hawa
washenzi."
"Shaka ondoa." Malocha akamaliza huku anafungia silaha zile
kwenye begi kubwa lililokuja nazo.
Wakabeba silaha zile na kuzipakiza
kwenye gari lao. Wakaondoka eneo lile kurudi nyumbani kwao kwa matumaini
mapya.
Walipofika, wakawapa ujumbe wakundi wao, na kila mmoja alikuwa
tayari kwa mapigano dhidi ya kundi la Gunner. Lisa akamchukua Martina aliyekuwa
kalala na kumpandisha kwenye gari walilopanga kwenda nalo
Arusha.
Kabla ya safari hiyo haijaanza, Martina
akapitishwa kwa rafiki kipenzi wa Lisa aitwaye Salome Makala. Martina akaamshwa
na kupewa maelekezo kadhaa ambayo hakuwa mbishi katika kuyakubali. Baada ya
hapo, gari ikaingia barabarani kwenda Arusha.
****
Likiwa
limebaki saa moja ili kauli ya Gunner kwenye ile video itimie kwenda kwa vyombo
vya usalama. Askari na wanausalama wa aina zote walijipanga barabarani na
mabango wakiandamana ili Masai atoke. Waliimba nyimbo za ukombozi huku wakiwa na
silaha za moto mikononi mwao. Lengo la kufanya hivyo ni katika kufikisha ujumbe
kwa wale wanaomficha Masai. Hakuna aliyekuwa tayari kuona jeshi lao linaendelea
kuhangamia pasi na sababu ya msingi. Waliandamana huku wakishinikiza kuwa Masai
asipoonekana, basi vita dhidi ya serikali itaanza mara moja.
Wakati
hayo yanaendelea, nyuso za Gunner na Lobo ziliambatana na tabasamu zito kwani ni
wazi vita yao ilianza kuzaa matunda. Wakiwa ndani ya gari lao mwanana,
walitabasamu na kugonga tano kwa mchanganyo wanaoufanya
Tanzania.
Upande mwingine wa shilingi, Malocha, Masai, Lisa, Mubah,
na wataalam wa mitambo yao, walikuwa wapo ndani ya gari linalokimbia kwa kasi
kwenda Arusha kuwahi muda wa Duka La Roho. Masai akiwa nyuma ya usukani, kavalia
kaptula ya kombati na juu kaushi nyekundu, alikuwa kama mwehu aliyeanza kuwehuka
zaidi kwa jinsi alivyokuwa analiendesha gari lililobeba roho za wenzake. Licha
ya hayo yote, hakuna aliyebisha kwani roho ya vita iliwaingia katika viini vyao
vya nafsi na kuwaza vita tu.
Saa mbili asubuhi, kundi la Masai
lilikuwa limefunga breki mbele ya hotel moja kubwa iliyopo katika jiji la
Arusha. Wanaume wakashuka na mabegi yao yenye silaha, kisha akafuata Lisa ambaye
yeye alikuwa kabeba begi la kawaida la nguo.
Moja kwa moja wakaenda
mapokezi na kutoa kibali ambacho Rais kawapa kwa ajili ya utambulisho wakifika
sehemu ile. Hoteli hiyo inamilikiwa na Rais. Mwanamke aliyekuwa pale mapokezi,
baada ya kuona kile kibali, haraka akapiga simu kwa tajiri wake na dakika mbili
mbele, meneja wa hoteli ile alikuwa anaongea na Malocha jambo
fulani.
"Twendeni wazee wa kazi." Malocha aliwaambia wenzake baada ya
kumaliza kuongea na Meneja.
Moja kwa moja wakaongozwa hadi chumba
kimoja ambacho mlangoni kiliandikwa 'Conference Room' yaani chumba cha mikutano.
Meneja akaondoka ndani ya chumba kile baada ya kuwakabidhi wale watu, na kitendo
bila kuchelewa, mabegi ya wale watu yakafunguliwa na kila mmoja akatoa kompyuta
yake tayari kwa kuanza kazi ya kumsaka Gunner na washirika wake kwa kutumia
kifaa alichokuja nacho Masai toka Italia.
Baada ya dakika kumi, kila
mmoja akaanza kutoa mafanikio yake kwa kile alichokuwa
anakitafuta.
"Nimepata namba zake alizowasiliana nusu saa iliyopita."
Mtaalam wao aliitoa taarifa na kuzitaja namba hizo na Lisa akazinakiri
mahala.
"Nimepata maongezi yao waliyoyaongea kwa nusu saa iliyopita."
Mtaalamu mwingine alitoa taarifa na kucheza yale maongezi ambayo Gunner alikuwa
anawasiliana na wenzake na kuwaelekeza cha kufanya. Masai akatikisa kichwa
kukubali kazi ya vijana wake.
"Kuna namba nyingine zimeonekana kabla
ya nusu saa ya maongezi ya Gunner. Ni namba ya nchi za mbali na sauti yake hii
hapa." Lisa naye akatoa alolichokinasa kwenye kazi aliyopewa.
"Ni The
Shadow huyo. Naona anafurahi sana wajinga wanachokifanya. Mshenzi mkubwa." Masai
aliongea kwa hasira kuliko siku zote ambazo kawahi kuishi katika dunia
hii.
"Na hapa mimi nimepata ramani ambayo walikuwepo nusu saa
iliyopita. Yaonekana baada ya mawasiliano haya, wameelekea upande wa Kaskazini
lakini sisi tukipita barabara nyingine, tutakutana nao mbele japo wametuwahi."
Malocha alitoa taarifa.
"Upande wa Kaskazini kuna nini?" Masai
akauliza.
"Hapa Kaka. Kuna kambi ya jeshi ambayo ndio ngome kuu ya
Tanzania kwenye upande wa Silaha. Wakifanikiwa kuteka eneo hili, basi Tanzania
tutakwisha. Silaha zote watakuwa nazo wao." Malocha alitoa maelezo ambayo
yakamfanya Masai apumue pumzi ndefu iliyo na mashaka.
"Naona wamepania
sana. Ngoja nijaribu kuwatafuta maana majibu yenu ndio mwongozo wangu." Masai
baada ya kuongea hayo, akaanza kubonyeza kompyuta yake harakaharaka na kufanya
mle ndani kulie kiparaza kile cha kompyuta.
"Masai. Kuna mawasiliano
yanafanyika sasa hivi hapa. Namba ya Gunner na hii namba." Mubah aliongea hayo
huku anamgeuzia kompyuta yake Masai.
"Angalia hiyo namba nyingine ni
ya nani." Malocha alitoa wazo haraka na Masai akaingiza namba hizo kwenye
mtandao wake wa kutafuta mahali inapotokea.
"Shit. Ni ya hotel hii.
Wajinga wanataka kutuchoma." Masai aliongea huku macho yake kayakodoa kwa
hamaki.
"Ni yule mbwa wa mapokezi ndio katoa taarifa." Mtaalamu mmoja
aliongea na kucheza sauti ambayo ilisikika ikiongea na Gunner. CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wamefanya vizuri
sana ili kusimamisha zoezi la kwenda kambini. Tuna dakika kumi za kufanya mambo
yetu. Wao baada ya nusu saa watakuwa hapa." Masai aliongea huku akiendelea
kutafuta mahali ambapo ataweza kuwaona Gunner na kundi lake kwa kutumia
Satellite Trace.
"Okay." Baada ya dakika tano, Masai akatoa sauti yake
na wote wakatega sikio. "Kuna makundi matatu ya hawa wajinga. Kuna la wanawake
ambalo hili linaendelea kusonga Kaskazini lakini kwa taratibu kwa lengo
kuwangoja wakina Gunner, kuna lingine la watu watatu ambao nadhani ni wale
wataalamu wao, hili naona lipo katikati ya jiji na karibu sana na AICC. Nadhani
wanataka kufanya kitu pale. Na kundi la tatu, ni Lobo na Gunner, hawa wapo
njiani wanakuja kwetu." Masai alitoa maelezo hayo lakini kabla hajaendelea, Lisa
akaingilia maongezi hayo.
"Naona wanawasiliana na kundi lililo jijini.
Wanasema wakutane hapa." Lisa akatoa taarifa.
"Safi wife." Masai
akampongeza mchumba wake. Lisa akatabasamu tu.
"Wanadakika ngapi
kufika hapa." Malocha akauliza na Masai akabonyeza vitufe fulani kwenye kompyuta
yake. Kompyuta ikaonesha gari walilopanda wakina Gunner na umbali lilipo toka
pale walipo. Kisha akabadili ule umbali ukawa katika muda. Hapo akapata majibu
ya kumjibu Malocha.
"Dakika kumi na tano tu."
"Tufunge vitu
tuondoke." Malocha akashauri na kila mmoja akaanza kupakia vitu vyake haraka,
lakini Masai akawa anaendelea kubonyeza kiparaza cha kompyuta mpakato yake. Hadi
wenzake wanaliza kufunga, na yeye ndio alikuwa anamaliza kazi
yake.
Bila kuifunga kompyuta yake, akaiweka mezani na kutoka na
wenzake ndani ya chumba kile cha mikutano.
"Kwa nini umeacha mashine."
Mubah akamuuliza Masai.
"Kuna meseji ya Gunner na Lobo, wanatakiwa
waipate." Masai akajibu huku wakizishuka ngazi baadhi zilizopo katika hoteli
ile.
"Huyo dada wa mapokezi msiongee naye chochote. Tupite tu."
Malocha akatoa ushauri baada ya kuanza kukaribia mapokezi.
"Heee!
Mnaondoka? Mbona mlisema hadi jioni mtakuwepo." Yule mwanamke aliyekuwa na weupe
wa 'kosmatiksi' alijibalaguza lakini watu wa kazi walikuwa hawana muda naye
zaidi ya kupita pale alipo na kutoka zao nje.
Kwa umbea zaidi, yule
dada alikimbia hadi mlangoni na kuwatazama wakina Lisa wanavyoingia katika gari
lao. Kwa bahati mbaya Masai akageuka na uso kwa uso wakakutanisha macho. Masai
akapinda vidole vyake na kuwa mfano wa bastola, akamuelekezea na kufanya kama
anashuti. Yule dada akashtuka na kijasho kikamtoka ghafla, akakimbia hadi katika
ofisi yake na kukaa huku akitetemeka kama mgonjwa mwenye
kifadulu.
Dakika mbili mbele, ndipo akapata wazo na kunyanyua simu
ambayo alipiga namba za wakina Gunner.
"Haloo. Wameondoka wale watu."
Dada wa mapokezi aliongea kwa kitete.
"Usijali tumeshaona
wanapoelekea." Sauti ya upande wa pili ilijibu.
"Haya. Mkija, njoeni
na dau langu." Dada yule akawakumbusha watu anaongea nao kuhusu
aluchoahidiwa.
"Usijali." Simu ikakatwa na ahueni ya yule dada
ikarudi.
****
Baada ya gari walilopanda wakina Masai
kuondoka, zikapita dakika kumi ndipo magari mawili, moja la Gunner na Lobo na
lingine la wale wataalam wao akiwemo yule mwenye mapengo, lilifunga breki kwenye
hoteli ambayo wakina Masai walishaiacha muda mrefu.
Gunner na Lobo
wakashuka na kufuatiwa na wenzao. Wakanyoosha hadi mapokezi walipomkuta yule
dada akajipaka 'angel face' na kutengeneza muonekano wa maiti.
"Wapo
wapi wale wajinga." Gunner alimuuliza na dada yule akashtuka hasa kwa sababu
alikuwa hajawaona wale watu kama wamekuja.
"E.... e..... e....
e......" Yule dada alikuwa anakitete na macho kayatoa.
"Wapo wapi?
Hatujifunzi kusoma hapa." Gunner akafoka na kumfanya yule dada arudi nyuma kwa
uoga.
"Nili.... nili.... niliwa...pigia nyie ....si... si...si....
simu na kuwaambia wameooondo.... ka. Sasa sijui hamkunielewa." Maneno ya mwisho
yakamtoka vema yule mwanamke baada ya yale ya mwanzo kutoka kwa
kukatakata.
"Ulimpigia simu nani? We' mbwa nini. Embu usituletee
uchuro hapa. Chumba walichokuepo kipo wapi?" Gunner alibwata na dada yule akatoa
ufunguo uliobaki na kuanza kuwaelekeza chumba kile kilipo.
"Twende
wote." Lobo kwa mara ya kwanza aliongea kwa sauti nzito na kumchomoa yule dada
kwenye kitalu chake cha kupokelea wageni. Akamkamata mkono kwa nguvu na kwenda
naye hadi chumba cha mikutano. Hata mlango haukufungwa, wakaingia na moja kwa
moja macho yao yakatua mezani na kuona kompyuta aliyoiacha Masai ikiwa inapumua
kutokana na AC yake kuwa nzima.
Gunner akaifata ile kompyuta na
kubonyeza kitufe kimoja. Kioo kikaonesha maneno yasemayo 'Press Enter', Gunner
akabonyeza kama alivyoelekezwa. Mara kompyuta ile ikaanza kuonesha gari la wale
wanawake linapoelekea kwa kasi. Baada ya kulionesha gari hilo, kamera
inayoendeshwa na satellite, ikaonesha gari la wakina Malocha ambalo lilikuwa
kasi zaidi ya lile la wale Wairan wa kike. Ikaonesha umbali wa gari zile jinsi
zilivyoachana. Kisha ule umbali ukabadilika na kuwa muda. Kutoka umbali wa gari
analoendesha Masai hadi kwenye gari la wale wanawake, ni masaa mawili hadi
kufikiana kwa mwendo waendao.
Gunner akatabasamu hasa alipoona kuwa
ule muda ni mkubwa sana kwa wale wanawake kufanya anachotaka. Lakini wakati
anatabasamu, mara kompyuta ile ikaonesha neno 'Plan B'.
Picha
waliyokuwa wanaiangalia wakina Gunner, ikavutwa kwa mbali zaidi. Gari zikawa
zinaonekana ndogo kiasi lakini zote zilionekana vema vilivyo.
Katika
gari walilokuwa wakina Masai, kukaonekana mstari mwekundu, mstari huo ukaanza
kuchora gari la Masai litakapopita.
Ni wazi plan B ilikuwa inaonesha
njia ya mkato ambayo Masai angepitisha gari lake.
Gunner akawa kakodoa
macho asiamini akionacho. Mchoro ule ukazidi kutembea hadi kwenye barabara
ambayo itakutana na ile inayopita gari la wale Wairan. Baada ya kukutana
ikaonesha muda ambao watakuwa wamezidiana, ni dakika tano tu.
Kompyuta
ikazidi kudadavua na sasa ikaonesha baada ya dakika tano kitakachotokea. Neno
lililoandikwa kwa herufi kubwa likatokea kwenye kompyuta. "WAR (VITA)" Baada ya
neno hilo, kikatokea kibozo kikubwa na kuanza kucheka kwa nguvu. Kikacheka na
kucheka lakini kilikuja kunyamaza baada ya Lobo kupiga risasi kioo cha kompyuta
ile.
Gunner akiwa anatokwa na jasho la mgongoni, akachomoa simu yake
haraka na kuanza kubofya namba za wale wanawake, kisha akaweka
sikioni.
"Haloo Gunner. Umeona hiyo?" Badala ya sauti ya mwanamke
mmojawapo kuitikia simu ile, akaitikia Frank Masai. Gunner akabaki kinywa
wazi.
"Tatizo mnakurupuka nyie. Huyo muhudumu wenu katupa taarifa zote
na tumemlipa pesa nyingi kuliko zenu." Masai akamchongea yule dada wa mapokezi.
Gunner akamgeukia yule mwanamke aliyejikubua hadi kuwa mwekundu, akamuangalia
kwa jicho baya.
"Nitakupata tu Masai. Huwezi kushinda vita vyetu hata
siku moja. Wewe ni koko kama yalivyo mambwa koko mengine." Gunner alijibu mapigo
kwa chuki nyingi.
"Haijalishi. Baadaye mje kuchukua maiti zenu." Masai
akamjibu kwa nyodo.
"Okay. Na wewe baadae tutakupa
taarifa njema ambayo itakulazimu tukutane tu." Gunner akajibu naye
mapigo.
"Ni muda tu! Nasubiri." Simu ikakatwa baada ya maneno hayo ya
Masai. Gunner akamsogelea yule muhudumu na kumkaba kwa mkono wake
mmoja.
"Nani kakwambia uwaambie wale wajinga kuwa tunakuja hapa?"
Hasira zilizojikita moyoni mwa Gunner ilijionesha wazi.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sijathemaaa." Dada
yule aliongea kwa shida kwa sababu ya kabali aliyopigwa.
"Unasemaje?"
Akaulizwa tena baada ya kuachiwa shingo yake. Akakohoa huku kainama kitu
kilichomfanya Gunner ampige kofi la mgongoni. Dada yule akasimama huku
anajikuna.
"Sijawaambia." Sauti iliyoambatana na kilio ilimtoka yule
mwanamke.
"Lobo." Gunner akampa rungu John Lobo, mtu ambaye hana
maongezi mengi bali vitendo. Mlango ukafunguliwa, na Gunner akiwa na wenzake
wakatoka na kumuacha Lobo na yule dada.
"Huwa sipendi wambea, hilo
moja. Pili wanawake wanaotumia muda mwingi kwenye kioo hata kazini, sitaki hata
kuwaona. Na tatu, wanawake wanaojitoa rangi walizoumbwa nazo, nawafananisha na
shetani mtoa roho. Hakuna anayempenda shetani huyu. Nikibahatika kukutana na
huyu shetani, nitamuua. Leo nimekutana na mfano wake, unajua nini kitatokea?"
Maneno ya Lobo yaliambatana na tabasamu la kuchonga na wakati huo anatoa bastola
yake na kuanza kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti. Mwanadada yule akaanza kurudi
nyuma huku akionesha hali ya kuomba msamaha na uoga ndani yake.
"Una
sekunde ishirini za kutubu dhambi zako. Chagua kutubu, au kutotubu." Lobo
aliongea baada ya kumaliza kufunga kile kiwambo cha kuzuia
sauti.
"Jamani Kaka Jambazi nisamehee." Maneno yalimtoka yule dada na
machozi kedekede, lakini Lobo hakujibu kitu.
"Zimebaki sekunde kumi.
Kulia hakusaidii." Lobo akampa taarifa yule mwanamke huku akimuangalia usoni kwa
macho ya vitisho.
"Naomba unisamehe MUNGU." Dada yule aliongea maneno
hayo na muda huohuo Lobo akampiga risasi moja ya kichwa na dada yule
hakufurukuta tena bali kudondoka na kupoteza uhai wake.
"Umbea
umekuponza." Lobo akamtemea mate yule mwanamke na kutoka katika chumba
kile.
****
Katika utaalamu wa kompyuta aliosomea Masai huko
China, aliweza kujifunza mambo mengi sana yakiwemo kuunga namba fulani ya simu
na kuwa simu zote zinaingia kwake tu. Na hicho ndicho ambacho alikifanya
mwanaume yule. Akaunga namba anayowasiliana nayo Gunner na simu zote ambazo
angepiga au kupigiwa Gunner, zingeingia kwake. Hata yule dada marehemu wa
mapokezi, alikuwa anadhani anaongea na Gunner, alifanyiwa kitu hichohicho na
kikamponza mbele ya mkono wa Lobo.
Gunner baada ya kutoka mle ndani,
akaenda hadi kwenye kibanda cha simu na kupiga simu kwa wale wanawake. Ubaya
wanawake wale walikuwa wana simu moja na simu hiyo pia Masai aliiunga kwake.
Hata Gunner alipojaribu kupiga namba zile, alikutana na sauti ya Masai
ikimcheka.
"Utahangaika sana mbwa wewe. Halafu hata wakitushinda, pale
ni karibu na jeshini, tutasaidiwa na wanajeshi tu." Hayo ndio majibu ya dharau
aliyoyapata Gunner baada ya.Masai kupokea simu.
Akaikata simu ile na
mara hiyohiyo akaipiga Dar es Salaam.
"Andaa kile kitu na kukipeleka
lile gholofa kubwa la Posta. Tunakuja usiku huu kumaliza kazi ya hawa wajinga.
Tutawapata na kuwaua." Gunner akakata ile simu baada ya maneno hayo kisha
akarudi katika gari lao na kumkuta Lobo akiwa katulia anasikiliza nyimbo za
Eminem.
"Naweza kuondoka?" Gunner akamuuliza Lobo na Lobo akamuonesha
kwa ishara mshirika wake aliyeliwasha gari na kuondoka eneo lile kuelekea
barabara itakayowapeleka Dar es Salaam.
****
Masai akiwa
makini katika usukani wa gari lao, alipita njia za mkato ili wawawahi wale
Wairan na kuwasimamisha kwa kile walichopanga kukifanya. Gari lilikuwa lipo
katika mwendo wa kasi kuliko kawaida.
"Tunakaribia kuwafikia wajinga
hawa." Masai alitamka hayo huku akizidi kushindilia mafuta na
kuyachoma.
Baada ya dakika kumi, wakaingia barabara ya rami na mbele
yao kwa mbali walishuhudia gari aina ya Ford ikichanganya mbariga zake kwa kasi
ya ajabu. Masai akazidisha kasi na punde wale waliomo kwenye ile Ford ya kisasa,
waliliona gari la wakina Masai likiwafukuzia lakini hawakuwa na uhakika kama
wanafukuzwa wao.
Masai akiwa makini na barabara, simu yake ikaita na
sauti ya kike ikasikika kwa lugha ya kiingereza.
"Gunner. Mpo wapi?"
Ilisikika sauti ikiuliza.
"Tupo nyuma yenu kuja kuwaangamiza." Masai
akajibu na kukata simu kwa sababu alikuwa anapoteza umakini wa kuendesha gari
lake.
Katika hali isiyo ya kawaida, wale wanawake wakaanza kurusha
risasi kwenye gari ka Masai. Ilikuwa ni mshikemshike lakini Kamanda Masai
alikuwa makini kukwepa hali ile kwa kupunguza mwendo na muda mwingine kwenda
huku na huko.
"Malocha. Fanya yako." Kusikia hivyo, Malocha akakoki
gobole lake na kutoa kichwa chake kupitia kioo cha pembeni. Akafyatua ule
mzinga, risasi zikakita nyuma ya taa za gari lile. Akarudisha kichwa chake ndani
na kukoki tena dude lake. Alipomaliza akatoa kichwa tena lakini wanawake
wakaanza kutupa mvua ya risasi na kumfanya Malocha arudi ndani
haraka.
"Mubah. Sehemu yako hiyo." Mubah aliyekuwa nyuma ya gari lile,
akaruka nyuma zaidi na kufungua mlango wa nyuma ya V8 ile na kwa ustadi mkubwa,
akachungulia kulia lilipo gari la maadui kuona kama anaweza kupata muonekano
mzuri wa gari bila kudhulika na risasi zao. Alipoona hamna tatizo kubwa, akatoa
mabomu mawili yaliyo kama viazi mviringo, akatupa moja baada ya jingine kwa
nguvu. Mabomu yake yakalipukia pembeni na katikati hali iliyosababisha gari la
wale wanawake kuyumba huku na huko.
"Safi jamaa." Malocha alimpongeza
Mubah baada ya kurudi ndani.
"Wife." Masai akaita na kumpa ishara Lisa
ambaye alitabasamu kabla hajafanya alichopangiwa.
Mtoto wa kike
akasimama na kufungua paa la gari lile kisha akatoa bunduki ya kudungulia.
Akaweka jicho lake kwenye lenzi na wakati huo gari analoendesha Masai lilitulia
na lilikuwa haliendi kasi kama mwanzo.
Gari la maadui wao lilikuwa
limetulia na kuendelea na safari kwa kasi ya ajabu.
Lisa akafyatua
risasi ya kwanza, ikakosa lengo alilolenga. Akakoki na ganda la risasi
likadondokea ndani, akaweka tena jicho lake kwenye lenzi na kufyatua bunduki
yake. Risasi akanyooka na kutua katika tairi la wapinzani wao. Gari ya
wakinadada wale inapoteza mwelekeo na kujikuta ikiyumba na baadae kugeuka na
mbele kukawa nyuma huku nyuma kukiwa mbele.
"Malochaa." Masai akaita
kwa sauti na Malocha akatoa uso wake tena akiwa kakamata gobole lake, akafyatua
na risasi zikatua kwenye boneti la gari lile na kuifunua kabisa.
Masai
akapiga breki ya gari lake na kushuka haraka pamoja na RPG 4. Akaiweka begani na
kulenga gari ile ambayo ilikuwa imepoteza dira. Akafyatua mashine ile na bomu la
mashine ile likachomoka na kutua kwenye gari lile. Mlipuko mkubwa ikatokea eneo
lile ukiambatana na moto mkali. Wale wanawake wakawa hawana chao mbele ya
Watanzania watata.
Kundi zima la Malocha likatoka na kwenda
kushangilia ushindi wa kuliteketeza kundi lile la kishenzi. Wakashangilia na
kucheza kwa furaha katika pori lile kubwa lakini limepitiwa na
barabara.
"Mikono juu." Sauti kali ya amri iliwaamrisha wakina Masai
waliokuwa wanashangilia kwa furaha.
"Tupa silaha zote." Sauti nyingine
ilitoka nyuma yao. Wakatii kwa kufanya wakitakacho.
"Haya geuka." Amri
nyingine ikatoka. Walipogeuka walikutana na sura za wanajeshi nane wakiwa na M16
silaha hatari kabisa kwenye mapambano.
"Naitwa Malocha Malingumu."
Malocha alijaribu kujitetea kwa kujitambulisha.
"Mnafanya nini katika
eneo la jeshi tena na silaha za kivita?" Aliyeonekana kiongozi wa kikosi kile
aliuliza kwa sauti ya juu.
"Tumekuja kuwamaliza magaidi waliokuwa
wanakuja kuteketeza kambi yenu." Sauti hiyo ya Malocha iliwafanya wale wanajeshi
kunyamaza kidogo na kisha kuwaamuru Malocha na wenzake kusogea walipo
wao.
Wakasogea huku mikono yao ikiwa juu kama mateka wa Kimarekani
mbele ya Wavietnam.
"We ndiye Masai. Shenzi, unasakwa." Maneno
yakamtoka yule mkuu na kumlenga Masai jambo lililofanya kila mwanajeshi kufanya
hivyo.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tumetumwa na Rais
kazi hii. Msijidai mnajua sana, mtapotea wote." Malocha ikabidi atumie sauti
yake ya kiume.
"Rais hawezi kuwatuma magaidi mahiri kama nyie."
Kiongozi wa jeshi lile akazidi kuzogoa.
"Mpigie simu na muulize."
Malocha aliongea huku akiingiza mkono wake mfukoni bila uoga na kutoa simu
ambayo alimrushia yule mkuu.
Simu ikadakwa na mwanajeshi aliyeonekana
mjuzi wa mambo mengi, akapiga namba za Ikulu tukufu ya Tanzania. Na sekunde
kadhaa, akawa anaongea na mtu wa mapokezi aliyemuunga moja kwa moja hadi kwa
Rais baada ya kujitambulisha kwa jina la Meja Jenerali Kiroboo
Mapombe.
"Watu wangu hao. We hujui Dar imekuwa vurugu huku? Nimewatuma
waje kuwamaliza hao wajinga. Waachieni wafanye kazi yao." Sauti ya Rais iliongea
na Meja Kiroboo alisaliti amri kwa heshima kubwa.
"Sawa mkuu." Akakata
simu baada ya maneno ya Rais. "Okay. Shusheni silaha zenu wazee." Kiroboo
aliwaamuru wenzake na wao wakatii. "Shusheni mikono nanyi." Akatoa ombi kwa
wakina Masai ambao walikuwa bado wamenyoosha mikono juu kasoro
Malocha.
Baada ya hayo, wanajeshi wale waliwasogelea wazee wa kazi na
kuwasalimia kiheshima kama wafanyavyo kwa wakuu wao.
"Kwa hiyo hawa ni
wale wanawake magaidi?" Kiroboo aliwauliza wakina Masai baada ya kupata mkasa
mzima uliyotokea.
"Ndio hao aisee. Walijidai maninja sana." Mubah
aliwajibu baada ya kuona swali lile hakuna aliyelitilia maanani kwa sababu
tayari kila kitu kilishawekwa hadharani.
"Okay. Basi twendeni hapo
mbele tuwape gari lingine maana hili sidhani kama mtafika nalo
mpatakapo."
"Sawa kabisa. Ila kuna vitu vyetu, naomba wazee mvitoe na
silaha zetu tuokoteeni." Malocha aliongea huku wenzake wakiwa kimya wakimfatilia
kwa makini.
Kiroboo akawatuma vijana wanne na kwenda kulipekua gari
lile na kuchukua kila kitu ambacho kilikuwemo ndani yake. Baada ya kumaliza,
wakaokota silaha ambazo walizitupa wakina Malocha na kisha wakaelekea ambako
wenzao wameelekea.
Lilikuwa ni gari pana la jeshi aina ya Hummer, gari
zinazotengenezwa Marekani. Ilikuwa ina matairi mapana na imara kitu
kinachoyafanya magari haya iwe ngumu kupinduka au kukwama kwenye tope au
kushindwa kupita sehemu zenye kutitia.
"Okay wakuu. Gari lenu ndilo
hili. Kuna msaada mwingine mnaoutaka?" Kiroboo akauliza.
"Ndio Meja."
Kwa mara ya kwanza Masai akaongea.
"Sema mheshimiwa." Kiroboo akatoa
ruhusa.
"Nguo zangu zimechafuka. Naweza kupata kama zenu
hizo."
"Hamna tatizo Kamanda." Kiroboo wala hakuwa na pingamizi kuhusu
hilo. Akachukua simu ya sauti ya upepo na kuwasiliana na mwanaugavi wa kambi yao
na kumuomba aje na mzigo alioutaja kwa namba wazijuazo wao.
Simu ya
upepo ikakatwa na wazee wa kazi wakaanza kupanga vitu vyao kwenye gari lao jipya
ambalo kwa mbele ya kioo kulikuwa kuna nyavu maalumu ya kuzuia majani na
uwezekano wa kioo kuvunjika.
Baada ya dakika kumi na tano, ikaja Jeep
ya jeshi na wanajeshi wawili walishuka wakiwa na mabegi mawili makubwa kiasi.
Wakamkabidhi Kiroboo na kupiga saluti. Kiroboo akawapa yale mabegi wakina
Masai.
Masai akawa wa kwanza kufungua. Akapekua na kukuta kombati
zikiwa 'full'. Palepale akavua nguo za juu na kuvaa kombati zile. Baada ya hapo,
akavua na kaptula yake kisha akapachika mwilini suruali ya jeshi la
Tanzania.
Kwa kumuona tu! Huwezi kukataa kuwa jamaa ni mwanajeshi hai
wa jeshi la wananchi wa Tanzania. Urefu, rangi na muonekano wake, wala huulizi
kama ni mwanajeshi.
Wote walitabasamu na kila mmoja akapendezwa na
muonekano wa Masai. Wakapekua nao kwenye mabegi na kwenda vichakani kuzivaa
kombati walizoletewa. Baada ya kuvaa, wakarudi na kukwea gari walilopewa na
kuanza kurudi mjini ikiwa tayari muda umeenda.
****
John
Lobo, Gunner Samuel Bokwa, Boyka na wataalamu wenzake wawili, walikuwa wanachoma
mafuta mida ya saa kumi na mbili jioni kuelekea Dar es Salaam kutoka Arusha
walipotoka mida ya saa saba mchana. Gunner akiwa nyuma ya usukani, injini ya
gari lao ilikuwa inakoroma kwa sauti kali kutokana na kukanyagwa mafuta kwa
wingi.
"Saa mbili usiku tutakuwa Jijini." Gunner Bokwa akatamka hayo
huku gari yake akizidi kuichochea kwenye rami mtelezo ya
Tanzania.
"Nadhani wakina Hulyaman wamekwishapotea katika uso wa
dunia hii." Mlinzi yule aliyepigwa kichwa na Masai hadi meno yakang'ooka,
aliongea kuhusu wale wanawake na kumfanya Gunner amtazame kwa jicho la ubaya.
Baada ya jicho hilo, akamgeuka Lobo na kumpa ishara fulani. Lobo wala
hakufikiria jambo, akachomoa bastola yake na kumpiga risasi ya kichwa yule
bwana.
Gunner akakanyaga breki kali na kusimama, kisha akawaambia wale
wataalamu wa kompyuta waitoe ile maiti na kuitupia porini. Baada ya kumaliza,
wale majamaa, wakarudi garini ambapo waliwakuta Lobo na Gunner wakiwasubiri kwa
kuliacha gari likinguruma.
"The most died man in this world, is a
coward. (Mtu anayekufa sana dunia hii, ni muoga)" Gunner aliongea msemo ambao
ulimuingia kila mmoja kichwani. "A coward never lives long but died so simple,
just like this bastard. (Muoga haishi muda mrefu lakini hufa kifo rahisi sana,
ni kama huyu mpumhavu)" Gunner akazidi kutiririka. "It's better dies like a man,
than a coward. Am I clear? (Ni bora kufa kama mwanaume kuliko kama muoga.
Nimeeleweka?"
"Ndio mkuu." Wakajibu wale mabwana kwa
heshima.
"Pandeni ndani ya gari. Bado wale
wanawake wapo hai. Hakuna atakayekufa." Gunner akaongea na wale jamaa wakakwea
ndani ya gari lililowashwa na kuondoka kwa kasi ileile waliyokuwa nayo kabla
hawajasimama.
Saa tatu usiku, gari linaloendeshwa na Gunner lilikuwa
nje ya nyumba moja kubwa kiasi. Ilikuwa ni nyumba nzuri na ya kisasa lakini
huwezi kuamini ukiambiwa anayeimiliki ni msichana mdogo tu! Ambaye hajulikani
anafanya kazi gani, na mbaya zaidi hajawahi kuonekana na mwanaume yeyote huyu
dada.
Gunner na kundi lake wakashuka ndani ya gari lao na kupakua
mizigo kadhaa ikiwemo mtambo mdogo ambao walikuja nao wale wanawake kwa ajili ya
kuchapa fulana walizokuwa wanazivaa. Wakaingia ndani wakiwa wapo kamili kwa
lolote. Hiyo ni baada ya yule msichana kufungua mlango.
"Yule kuku
unaye au ulimpeleka kule gholofani nilipokwambia." Gunner akamuuliza yule
msichana.
"Sikupata mtu wa kumuachia kule. Hivyo ninaye bado hapa."
Yule dada alijibu kwa ujasiri.
"Okay. Good. Yupo macho?" Gunner
akatupa swali lingine wakati huo Lobo alikuwa kajiegesha kwenye kochi moja na
kukunja nne.
"Ndio bado hajalala. Kutwa nzima anawaulizia watu
aliowazoea."
"Embu mlete hapa." Yule dada akatoka eneo lile na kwenda
chumba cha pili baada ya sebule lake. Baada ya dakika moja, alitoka na mtoto wa
kike.
"Babaaaaa." Sauti ya mtoto mdogo iliita na kwenda kumkumbatia
Gunner.
"Hayaa Martina. Hujambo katoto kangu." Gunner alimuuliza
mtoto yule ambaye ni Martina, mtoto wa Lisa na Masai. Yule rafiki ambaye Lisa
alimuona kama mwokozi wake, sasa kamsaliti na kumuuza mwanaye kwa wakina
Gunner.
"Sijambo. Mbona hukunitafuta tena?" Martina aliuliza kwa
unyonge.
"Ndio nimekuja hivyo. Umemuona anko?" Gunner akamuonesha
Martina alipo Lobo. Kwa furaha Martina alienda na kumsabahi John
Lobo.
"Shikamoo anko." CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Marahabaa Tina.
Hujambo." Gunner akaonesha upendo wa usoni na kumfanya Martina kucheka hadi
mapengo yake ya pembeni yakaonekana. Mtoto akawa na faraja baada ya kukutana na
timu ambayo yeye alidhani ni familia yake na kumbe ni chui ndani ya ngozi ya
kondoo.
"Mama yupo wapi baba?" Martina alimuuliza Gunner baada ya
kupiga story hizi na zile.
"Oooh! Unataka uongee na mama eeh." Martina
akaitikia kwa kichwa. Gunner akatoa simu yake na kupiga namba za wale wanawake
ambapo kwa uhakika alijua ni lazima itaita kwa Masai.
"Haloo Gunner."
Sauti ya Masai ilitikia.
"Mpe mke wangu aongee na mwanaye." Gunner
akaongea huku katabasamu. Masai akashtuka na kujihisi kutaka kudondoka na wakati
huo walikuwa pembeni ya jiji la Arusha wakijiandaa kwa ajili ya safari ya kesho
kurudi Dar Es Salaam.
"Hey. Mpe mke wangu simu." Gunner akarudia kauli
yake tena.
"Haloo." Sauti ya Lisa ikasikika.
"Haloo wife.
Ongea na Martina." Gunner akampa simu Martina.
"Hey mamy. I miss
you." Martina aliongea kwa furaha baada ya kupewa simu. Lisa akawa kama mtu
aliyepigwa ganzi la mwili kwa kitendo kile alichokifanya
Gunner.
"Martina. Anti Salome yupo." Lisa aliuliza kwa
taratibu.
"Yupo. Nachezaga naye."
"Nipe niongee naye
kidogo.",
"Haya." Martina akakubali na kumwambia Gunner kuwa mama yake
anataka kuongea na Salome, yule mwanamke aliyemkabidhi mwanaye.
"Haloo
Lisa. Mambo vipi shosti." Salome aliongea kwa madaha.
"Mbona
nilikuamini sana Salome? Why?" Lisa aliongea kwa uchungu.
"Never trust
a woman. A woman is like a coin, have two sides. Don't you remember this quote
from our teacher? (Usimuamini mwanamke. Mwanamke ni kama sarafu, ana pande
mbili. Hukumbuki hii kauli kutoka kwa mwalimu wetu?)"
"Nimekuelewa
Salome. Nakuja kukuangamiza kwa mikono yangu. Msaliti mkubwa
wee."
"Trust No One. Ongea na mumeooo." Salome alimpa simu Gunner kwa
kujiamini na bila kuogopa ile kauli ya Lisa.
"Okay Lisa. Hayo ni yenu
na 'best' wako, siingilii."
"Unataka nini Gunner." Lisa akauliza kwa
hasira.
"Hujui nikitakacho?"
"Ndio
sifahamu."
"Mpe simu Masai. Atakuambia tukitakacho."
"Ipo
'Loud Speaker' simu yetu, ongea tu." Malocha akadakia kwa
nguvu.
"Oooh! Malocha. Mambo vipi jamaa." Gunner akasalimia huku
akimpa ishara Salome amwondoe Martina pale sebuleni.
"Ongea shida
yako." Malocha alifoka wakati huo Masai alikuwa kimya ndani ya kombati zake
akitafakari hili na lile hasa kutekwa kwa mwanaye.
"Sina jipya miye.
Ongeeni na Lobo." Gunner akampelekea simu Lobo wakati huo Martina alikuwa
amekwishaondolewa pale.
"Nahitaji kumsikia Masai tu. Nyie wengine
kaeni mbali au kimya. Atakayeongea neno moja, ni sawa na kidole kimoja cha
Martina. Sheria nitaifata na nitatimiza hilo." Kihere here kikawaisha waropokaji
wote hasa kwa sababu walimfahamu Lobo maneno yake.
"Ongea shida yako."
Masai akaanzisha maongezi.
"Kitambo sana sijaongea na wewe
Masai."
"Na mimi ni kitambo sijakuvunja pua yako." Masai
akajibu.
"Siku nyingine nitakuvunja yako." Lobo akajibu
mapigo.
"Shida yako nini?"
"Roho ya Martina ipo dukani.
Nunua au uza, chaguo ni lako. Ukitaka kununua, njoo haraka Dar es Salaam na
tukutane katika gholofa lile la Posta. Ukitaka ninunue mimi roho ya Martina,
basi usije. Nakupa masaa arobaini na nane kuanzia sasa. Tick Tock." Lobo
akamaliza kwa sauti yake nzito.
"Nakupa masaa arobaini. Usipomuachia
Martina, roho yako naiuza kwa Mubah. Niamini nikwambiacho. Kabla ya masaa
arobaini na nane, tayari roho yako itakuwa mikoni mwa Mubah." Masai naye akatoa
sheria yake.
"And let the game begins. Tick Tock." Lobo aliongea na
kumpa simu Gunner. "Hakuna sheria katika huu mchezo. Ruksa kuja kundi lenu lote.
Tick Tock." Gunner hakusubiri majibu ya upande wa pili, akakata simu
yake.
*****
Pumzi ndefu ya uoga ikamtoka Lisa. Mawazo
yakawa tele juu ya mwanaye. Akatoka mle ndani alipokuwa na wenzake na kwenda nje
ya hoteli ile. Masai naye akatoka na kumkuta mpenzi wake akiangalia angani kama
mwenye kuhesabu nyota za usiku ule.
Masai akamkamata kiuno na
kumkumbatia kwa nyuma mwanamke wake.
"Usijali Lisa. Mambo yote
yatakuwa sawa." Maneno hayo toka kwa Masai ni kama ndio yakamwambia Lisa alie.
Mtoto wa kike akaanza kulia kwa kwikwi na kuanza kumpa wakati mgumu Masai ambaye
alokuwa anajitahidi kumbembeleza.
"Frank. Naomba tuondoke sasa hivi
kwenda Dar." Lisa alitoa ombi baada ya kulia kwa muda mrefu.
"Hapana
Lisa. Tupumzike kwanza. Kesho asubuhi, tutakuwa barabarani." Masai alimuomba
Lisa ombi ambalo Lisa hakupinga japo moyoni alitamani waondoke muda
ule.
Akamchukua mpenzi wake na kumpeleka chumba ambacho wangelala
usiku ule.
"Nakuja Lisa. Naenda kuongea na Malocha." Masai alimuaga
Lisa ambaye alikuwa kajikunyata kitandani huku akajifunika blanketi zito sababu
ya kuzuia baridi kali iliyokuwa inaendelea katika Jiji la
Arusha.
"Mubah. Malocha yupo wapi?" Masai akamuuliza Mubah ambaye
alikuwa katika chumba alichotakiwa kulala na Malocha.
"Katoka mara
moja." Akajibu Mubah kwa upole.
"Okay. Usiku mwema." Masai akataka
kutoka baada ya kuaga lakini Mubah alimuita na kumuomba aongee naye. Masai
akarudi chumbani na kwenda kukaa kitandani kwa Mubah.
"Kaka. Nakuita
kaka kwa sababu umenizidi mambo mengi sana." Mubah alianza kuongea. "Katika
maisha yangu, sijawahi kupitia nyakati ngumu kama hizi. Naishi kama njiwa
aliyeachwa na wazazi wake ili akajitegemee. Nimepoteza familia yangu yote
akiwemo mjomba wangu kipenzi." Chozi likamtoka Mubah wakati anatabainisha maneno
yale.
Masai akamshika bega na kumgonga gonga kama kumpa faraja. Mubah
akafuta machozi na kuendelea.
"Mpenzi wangu niliyedhani ni mpenzi,
akanisaliti na kuuza familia yangu kama rafiki wa Lisa alivyofanya. Mwanamke
niliyempenda kuliko kitu chochote, kumbe ni joka lenye mapembe. Shetani mkubwa
kabisa kuliko shetani mwenyewe. Akaisababishia familia yangu iteketee. Inauma
sana Kaka Masai. Inauma vibaya sana.
Lakini nimekuwa jasiri kama
ambaye sijakutwa na mkasa. Ninejitahidi kulia ndani ya maji ili machozi yangu
yasiwe.kikwazo cha kazi yangu, na nimefanikiwa.
Leo hii nasikia mtu
yuleyule aliyeondoa roho za familia yangu, anataka kuondoa roho ya mtoto
anayelingana na mjomba wangu. Haiwezekani Masai, nipo tayari kufa mimi na si
Martina. Nitapigana hadi kufa." Mubah akafuta chozi lililokuwa linatiririka na
kuapa kiapo cha nguvu.
"Hakuna atakayekufa Mubah. Niamini mimi. Hakuna
kifo tena kati yetu." Masai aliongea kwa kujiamini.
"Nitakufa kwa hili
Masai. Lakini kabla sijafa, Lobo atakufa kwa risasi zangu." Mubah akaapa
tena.
"Huwezi kufa. Lobo ni mali yako." Masai aliongea huku
ananyanyuka na kutoka chumbani kwa Mubah.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa kumi na mbili
alfajiri, kundi la Malocha lilikuwa limekwishaanza safari ndefu ya kutoka Arusha
kuelekea Dar Es Salaam. Wakiwa katika mavazi yao ya jeshi la wananchi pamoja na
gari pana ya Jeshi hilo hilo, hakuna hata mmoja ambaye akikuwa anawaza jema
nafsini mwake. Akili yao ilikuwa imetapakaa kisasi pamoja na vita kati yao na
kundi hatari la Gunner.
Kila Malocha alipojaribu kukanyaga mafuta ya
gari lile, aliona kama hayakanyagiki bali kupungua mwendo japo gari lilikuwa
katika kasi isiyo ya kawaida.
"Malocha slow down." Ndita, mtaalam wa
kompyuta alimuonya Malocha juu ya kasi anayoendeshea gari. Malocha hakuwa hata
na wazo la kujibu chochote bali kuendeleza kazi yake ya kulikimbiza gari
lile.
"Yupo kazini, muache." Masai akamtaarifu
Ndita.
****
Upande wa Gunner na Lobo, hali yao ilikuwa ni
imara kimawazo na kimwili. Walikuwa hawana wasiwasi hata kidogo kuhusu maisha
yao. Kila muda walitazama saa zao na kuangalia kama muda
umefika.
"Masaa ishirini na mbili yamebaki."
Gunner aliongea huku akienda huku na huko ndani ya nyumba ya
Salome.
"Muda wa kushinda vita unawadia." Lobo akajibu mapigo huku
tabasamu la kikatili likichanua katika uso wake.
"Kila kitu kipo
tayari. Tutahakikisha mbwa wote wanakufa wale." Gunner
akajitapa.
"Nakuamini kamanda. Ungekuwa hivi tangu mwanzo, maboya
wangekuwa kaburini."
"Muda wao ndio huu sasa." Maongezi hayo
yalichukua nafasi mida ya saa sita usiku wakati huo Masai na wenzake tayari
walikwishafika jijini Dar es Salaam na kwenda katika nyumba ya Lisa tayari kwa
mtanange wao na kundi la Gunner.
"Kesho ni siku ambayo itakuwa
tofauti sana kwetu. Ni kati ya kifo na kuishi, damu na machozi, kilio na
maumivu, na zaidi ni siku ya uhuru wangu na wenu. Hii ni siku ambayo hatutakiwi
kuikosa katika maisha yetu kwani MUNGU pamoja na SHETANI, wanaingia vitani
kugombea kondoo wema. Ni kazi kwetu, eidha kwenda kuwa kondoo wema au kuwa
kondoo wa SHETANI. Naamini sote ni binadamu ambao miili yetu inaendeshwa na damu
pamoja na moyo. Tunahisi na kuyapokea maumivu sawa na mnyama yeyote
anayejeruhiwa. Hakuna cha kupoteza kama maumivu hayo utayapokea kwenye kuutafuta
uhuru wako." Maneno ya Masai katika kuwahamasisha kundi lake kwenda kupambana na
kundi la Gunner wajiitao Duka La Roho.
"Mimi napenda kuita siku hii
kuwa ni SIKU YA MPAMBANO KWA TUWAPENDAO. Tunapigana kwa sababu tunapendana na
tunapenda kile tukifanyacho. Tunawapenda Watanzania na hatupendi kuwaona
wakiingia kwenye migogoro na nchi nyingine. Tunampenda Lisa na Martina,
tunampenda Mubah na Ndita, Masai na Yogo na ndio maana tunaingia na mioyo ya
kupambana. Tupambane kwa umoja na tufe kwa pamoja kama wenzetu wanavyofanya.
Tupambane kwa kile tunachokipenda. Nani yupo pamoja katika hili?" Malocha
aliongea huku akinyoosha mkono wake mbele ya duara waliweka katikati ya sebule
lao.
"Kwa Watanzania." Yogo, mmoja wa wataalamu wa kompyuta aliunga
mkono wake kwa Malocha na kuwa kama anatoa tano.
"Kwa Martina." Mubah
aliongeza naye mkono wake.
"Kwa familia ya Mubah na Baba yangu. Na
wote waliotutoka sababu ya mapambano haya." Lisa aliunga.
"Kwa FISSA."
Ndita, au rafiki wa Martina, hakuwa nyuma. Macho yakabaki kwa Frank Masai. Jamaa
akatabasamu kisha akasogea mbele ya wenzake na kuunga ngumi.
"Kwa
Manchester United." Watu wote wakamshangaa Masai. "Nini sasa." Masai aliwauliza
huku anatabasamu.
"Hao Manchester, wanahusika nini hapa." Lisa
akauliza kwa hasira.
"Basi wife kha! Hutaniwi?" Masai aliongea huku
akishika kidevu cha Lisa. "Kwa Martina, nakuja kukuchukua muda si mrefu." Masai
akaongea huku uso wake ukipotea lile tabasamu alilokuwa nalo
kabla.
"Kwa upendo." Malocha akafunga
kazi.
****
Ilikuwa ni saa tatu usiku katika ghorofa moja
refu na ambalo liliandaliwa mahususi kwa ajili ya kazi ya makundi mawili
mahasimu katika mapambano.
Masai akiwa na kundi lake zima waliobeba
mfuko wenye silaha, walienda hadi ghorofa ya kumi na kumkuta John Lobo akiwa
kamkamata Martina aliyevaa begi dogo kama la shule.
"Mama." Martina
aliita na kutaka kumkimbilia mama yake lakini Lobo alimzuia na kumfanya Martina
aanze kujipapatua kutoka. Kwa ghadhabu, Lobo alimtandika kofi yule mtoto na
kuweka kidole cha shahada mdomoni kwa akimaanisha Martina
atulie.
"Unarisasi yangu moja kwa sababu ya hilo kofi." Masai
akamwambia Lobo huku macho yake yakiwa mekundu kama nyanya sababu ya
hasira.
"Ooooh. Masai the Soldier. Karibu Bro." Sauti ya Gunner
ilitoka huku akitoka katika chumba kimoja kilichokuwa kama
ofisi.
"Mmekuja kabla ya muda. Yaonekana mna usongo sana." Gunner
alizidi kuzogoa huku nyuma akiwa kafuatana na wale wataalamu wake wenye
miili.
"Nilimuahidi Lobo kuwa saa la arobaini, moja kutoka sasa,
atakuwa hana uhai wake." Masai akajibu kwa kujiamini.
"Kwa hiyo
umekuja na hawa wote wa nini?" Gunner akauliza.
"Kwa sababu ya upendo.
Tunapigana kwa upendo." Malocha akasogea mbele na kujibu.
"Oooh! Kwa
hiyo upendo umewavuta hapa. Haya bwana. Karibuni wazee wa upendo." Gunner
akajibu huku akisogea hadi kwa Lobo na kumkamata Martina.
"Mbona
unalia." Gunner akamuuliza.
"Anko huyu kanipiga." Mtoto
akajibu.
"Usimsumbue tena. Atakuumiza kabla ya muda." Gunner akamuonya
huku akionesha kutokujali hali ya Martina.
"Tubadilishe sheria." Lobo
alifungua mdomo wake na kuongea jambo hilo.
"Unatakaje Kamanda."
Gunner akataka kumsikiliza mshirika wake.
"Masai apambane na mimi.
Ndani ya saa limoja ambalo limebaki. Akifanikiwa kunizimisha, tunampa kimdoli
chao. Asipofanikiwa, utamuua huyu mdoli mbele ya macho yake." Lobo alitoa
pendekezo.
"Masai unaafiki hili swala." Gunner akamuuliza
Masai.
"Nipo kupambana. Na lazima afe bwege huyu. Am in." Masai
akaongea huku akivua koti lake la jeshi na kulitupia pembeni.
"Sheria
imepita." Gunner akawa kama refa.
"Sitaki kupigana mbele ya Martina."
Masai akapendekeza.
"Oooh! Hiyo hamna. Ataona yote unayofanya na
kufanywa. Hamna kumtoa." Gunner aliongea na kumfanya Masai ajute kukubali ule
mpambano.
"Anko usipigane." Martina aliongea wakati Lobo
anamkabidhisha kwa Gunner.
"Hee! Anakuita Anko? Mi nilidhani
kishakujua. Kumbe huna tofauti na Lobo. Mi ndiye Baba hapa." Gunner alijitapa
baada ya Martina kumuita Masai, Anko. Masai akazidi kunyong'onyea kwa maneno ya
Martina kumkataza asipigane lakini alishaamua, na kama walivyo Makamanda wengi,
wakiamua kufanya jambo, hufanya hata kama yanawagalimu damu na maisha
yao.
Masai na Lobo wakaingia katikati na kwa kasi ya ajabu, Lobo
aliruka teke na kulituliza kifuani kwa Masai na kumrusha mbali.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Anko John muache
Ankoo." Martina alilia kwa uchungu kwa lile tendo lakini Lobo hakusikia, akaruka
sarakasi haraka na kutua karibu na Masai aliyekuwa anagalagala chini na kumpa
teke aina ya dochi kwenye tumbo.
Maumivu yakamzidi Masai kwa kile
kitendo lakini alikuwa hana jinsi kwa sababu mwanaye alikuwa anaona na yeye
alikuwa hataki Martina aone kitu chochote cha kikatili atakachokifanya. Uwanja
ukawa wa John Lobo. Masai alikuwa anachambuliwa kama karanga mbele ya
Lobo.
"Mmeona? Hamna kitu hapa." Lobo aliongea huku kamkanyaga Masai
aliyeelemewa kwa kipigo kikali ndani ya dakika kumi tu.
"Safi sana
kamanda." Gunner akamsifu Lobo. Hapo hapo Lobo akamtandika teke lingine zito
Masai lililotua kidevuni na kufanya damu zilizochanganyikana na mate kuruka kama
bata kachinjwa.
"Sema Loboo." John Lobo aliwaambia wenzake na wote
wakaitikia kama sauti za jeshini.
"Loboo." Akatupa teke lingine la
tumbo. Baada ya hapo akamkalia Masai kifuani na kuanza kumchapa ngumi za uso.
Masai akawa kachanika katika paji la uso na juu ya jicho. Kipigo kikaendelea kwa
dakika ishirini huku Lisa, Martina wakiwa wanalia kwa.kuomba
msaada.
"Baba mpige huyo." Martina akatamka hasira baada ya kuona baba
yake kaelemewa.
"Umeniitaje Martina." Masai akawa kama haamini
anachokisikia toka kwa Martina.
"Mpige baba. Mpige na muue." Martina
akajibu swali la baba yake wakati huo Lobo alikuwa kifuani
kwake.
"Zamu yangu." Masai akamwambia Lobo na kisha akambetua haraka
na kumbwaga chini. Yeye akawa juu sasa. Ngumi zisizo na idadi zikaanza kushuka
usoni kwa Lobo. Zikamchana na kumfumua yule jamaa aliyekuwa kamiliki mchezo muda
mchache uliyopita.
Masai akakamata kichwa cha Lobo na kuanza
kukibamiza kwenye sakafu nzito ya pale ndani. Lobo akawa hoi, ndipo Masai
akashuka toka juu yake.
"Unakufa kilaini sana Lobo. Sababu ya ujinga
wako. Ulimpiga kofi moja mwanangu, nikakuahidi ni sawa na risasi moja." Masai
alimwambia Lobo ambaye alijiinua na kupiga magoti mbele ya Masai. Masai
akamuonesha ishara Mubah ampe kitu. Mubah akachomoa bastola yake iliyofungwa
kiwambo cha kuzuia sauti toka kiunoni kwake na kumrushia Masai.
"Kwa
ajili ya kofi." Masai akafyatua risasi iliyomkuta begani Lobo.
"Na pia
nilikwambia roho yako namnunulia Mubah. Natimiza ahadi." Masai akatembea hadi
kwa Mubah na kumpa bastola yake. "Kazi kwako." Masai akamwambia.
Mubah
akamsogelea Lobo na mara akaanza kuvuta picha ya familia yake. Akavuta picha ya
mjomba wake ambaye alikuwa anapenda sana kucheka akiwa na Mubah. Hasira
zikampanda na kujikuta machozi yakimtoka bila kupenda.
"Kuniua si
suluhisho. Huwezi kuwarudisha mbwa zako bwege wewe." Lobo aliongea kwa kejeli.
Mubah akampiga risasi kwenye bega lilelile alilompiga Masai.
"Hiyo kwa
kuwaita niwapendao mbwa." Mubah akaongea baada ya ile risasi.
"Kwa
mama." Akafyatua nyingine na kutua kwenye bega lingine
"Na hii ni kwa
mama pia." Akampiga kwenye paja la kulia. Akaelekeza kwenye paja la kushoto na
kufyatua risasi nyingine.
"Kwa dada." Akadedicate risasi
nyingine.
"Na hii ni kwa mjomba wangu." Chozi likamtoka Mubah baada ya
maneno hayo na bastola yake kailekezea kichwani kwa Lobo. Akafyatua lakini
risasi zikawa zimekwisha.
"Hahahaa. Mjomba wako hataki nife." Lobo
aliongea huku akilazimisha cheko palipo na maumivu.
"Hapana. Hataki
ufe na bastola hii, bali hii." Malocha aliongea na kumrushia Mubah bunduki aina
ya SMG. Mubah akampiga risasi za magotini yule bwana na kumfanya alie huku
katanua mdomo, akaingiza ncha ya bunduki kwenye kinywa kile kilichowazi na
kumimina risasi zisizo na idadi. Hadi anamaliza, kichwa cha Lobo kilikuwa
kimepukutika.
"Kwa mjomba." Mubah akaongea kupeleka salamu za risasi
zile lakini ghafla ukasikika mlio wa risasi na wakati huohuo Mubah akarushwa
mbali.
"Safi Salome." Gunner alionga na simu ya sauti ya upepo
kumpongeza Salome aliyefyatua risasi iliyomkuta Mubah upande wa kulia wa kifua
chake. Mubah akawa kama amekufa, na kuacha macho ya wenzake yameshikwa na
butwaa. Ndipo kwa ghafla, wakavamiana na kila mtu akagawana
wake.
Malocha akapambana na Gunner, wale wataalamu wa kompyuta,
wakapambana wao kwa wao na wakati huo Lisa na Masai wakaenda kumuangalia
Mubah.
Lisa akakimbia kwenye begi lao la silaha na kutoa bunduki ya
udunguliaji (sniper rifle) na kwenda hadi sehemu ambapo risasi ile ilipita.
Akaweka lensi yenye uwezo wa kuona usiku na kuanza kumtafuta Salome. Akamuaona
mwanamke yule akivuta sigara wala hana mpango na kazi yake.
Akamlenga
kichwani na kufyatua bunduki yake. Mlio mkali ukasikika na kuwashtua wengi mle
ndani.
"Nimemuondoa Salome." Lisa akaongea huku katabasamu. Wakati
Martina alikuwa kajibanza kwenye pembe ya chumba kile na kuziba masikio yake
asisikie kitu.
Gunner aliposikia kuwa Lisa kaumuua Salome, akapata
hasira na kumuacha Malocha aliyekuwa kalegea kwa kipigo na kwenda kwa kasi mbele
ya Lisa. Lakini akakutana na upinzani mzito kwa teke la Masai. Gunner hakujilaza
chini muda mrefu, akajibetua haraka na kumpiga teke la kuzunguka
Masai.
Hajakaa sawa Masai, akapokea teke lingine lililompeleka hadi
chini. Lisa akajitoma kwenye mpambano lakini kofi alilokutana nalo, hakuwa na
budi kujitupa pembeni.
Malocha kuona hivyo, naye akajiachia na kuruka
teke la kutanguliza mguu, lakini Gunner akajizungusha kwa nguvu na kumzuia
Malocha akiwa angani kwa teke la korodani. Malocha akatua chini na kuanza
kugalagala.
Masai akanyanyuka na wakati huo wale wataalamu wao nao
walikuwa wanazidiwa ufundi wa ngumi za kundi la Gunner.
Masai
akamfuata Gunner na kuanza kurusha ngumi ambazo Gunner alikuwa anazipangua kwa
ustadi na pale aliporusha yake, ikatua puani kwa Masai. Masai akarudi nyuma
kidogo lakini akarudishwa nyuma zaidi kwa teke lililotua usoni.
Lisa
haraka naye akanyanyuka na kwenda kumdandia Gunner mgongoni na kumkaba kwa
nguvu, lakini bahati.mbaya alikutana na mtu makini aliyeinama kidogo kisha
akamtupia mwanamke yule kwa mbele. Akamuongezea na dochi zito la tumbo
lililomsogeza hadi kwa Masai. Mpambano akawa kaumiliki Gunner.
"Hamna
kitu nyie. Napiga wote." Gunner akajitapa. "Na bado dakika ishirini masaa
arobaini na nane yatimie. Kwenye begi la Martina kuna zawadi ya bomu kama masaa
arobaini na nane yatatimia. Sheria ilibadilika lakini bomu hatukubadili sheria
zake, bado dakika ishirini. Na rimoti hii hapa, nikishinda tu! Nakibomoa kijitu
chenu." Gunner alimaliza na kunyoosha rimoti ya kulipulia bomu kisha akaiweka
mfukoni.
Lisa na Masai wakaangaliana, kisha wakakumbuka kipindi cha
nyuma walivyowahi kupambana katika umoja. Hapo wakapata nguvu mpya na kuanza
kunyanyuka.
Lisa alikuwa wa kwanza kumvamia Gunner kwa kuruka teke la
mguu mmoja, Gunner akamkwepa na Lisa akapitiliza lakini bahati mbaya Gunner
alikuwa kampa mgongo Masai baada ya kumkwepa Lisa. Masai akatumia fursa hiyo kwa
kumpiga teke la kisogo jamaa yule. Gunner alipojaribu kugeuka apambane na Masai,
Lisa akajitupa naye kumpiga teke la mgongo lililomsukuma Gunner hadi kwa Masai
ambaye naye akarusha ngumi kali na kutua kifuani kwa Gunner.
Malocha
alinyanyuka na kwenda kuongeza nguvu kwa wale wataalamu ambao baada ya hapo,
wakaanza kuumiliki mchezo kama Masai na Lisa kwa Gunner.
Gunner akawa
kalegea na wenzake pia baada ya dakika kumi. Kwa mbali Gunner akamuona Mubah
akihangaika kumvua begi Martina.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Muache huyo we
bwege." Gunner alifoka huku kalala chini baada ya kipigo kikali toka kwa Masai
na Lisa. "Navunja sheria tuliyoweka." Gunner akaanza kujipapasa atoe rimoti
yake.
Hadi anaipata, Mubah alishavua begi lenye bomu na kwa
kujitutumua, akanyanyuka na kukimbia kwa kasi kwenda kwenye dirisha la kioo cha
ghorofa lile la kumi, akapita na kujitupa nje na wakati huo Gunner akabonyeza
kitufe cha kutegulia bomu. Mlipuko mkubwa na mwanga mkali wa bomu lile aliloruka
nalo Mubah ukatokea nje. Macho yakawatoka Lisa na wenzake kwa kitendo kile.
Masai aakashindwa kuvumilia na kujikuta akipiga kelele za
uchungu.
Kelele hizo zilikuwa za hasira kali zilizomkumba moyoni mwake
kwa kile kilichotokea kwa Mubah. Alipomtazama Gunner, alishuhudia tabasamu la
kero usoni pake.
Masai akanyanyuka na kumfuata kwa kasi pale alipo
yule mtu. Alipofika karibu yake, Gunner akataka kumkata mtama lakini kijana yule
ni kama alikuwa kauona, akaruka juu kidogo na kumtandika ngumi ya utosi adui
yake. Maumivu yakakikumba kichwa cha Gunner, lakini haikutosha kumnyamazisha
Masai asiendelee kutupa makonde yake ya nguvu kwenda kwenye uso wa
wake.
Gunner akawa kahelemewa na mapigo mazito ya Masai. Makonde
aliyokuwa anayatupa kijana ni kama ya Tyson au Frank Bruno. Hadi anamaliza
kumtupia zile ngumi, Gunner alikuwa kachakaa kwa vidonda na damu hasa upande wa
usoni.
Akadondoka chini yule mwanaume na kuwa kama mwenye kupiga
magoti.
"Lisa. Huyu ni wako." Masai akasogea pembeni na kwenda alipo
Martina ili amfiche asione ambacho mama yake anakifanya.
"Ulifanya
kosa kubwa sana kuniambia kuwa ulimuua baba yangu. Lakini nilikusamehe kwa
sababu nilijua ni kosa letu. Ukamteka mwanangu na kabla ya hapo ukataka
kumfundisha ugaidi, ukaona haitoshi ukamfunga bomu ili umuue. Bahati mbaya,
kaenda mwenye roho nzuri. Siwezi kukusamehe mume wangu wa zamani." Lisa
akachomoa bastola yake na kumpiga risasi moja ya kichwa iliyoacha tobo katika
paji la uso wa Gunner.
Mwanaume Gunner akaiacha dunia kwa mtindo wa
kipekee. Lisa akapiga magoti na kulia hasa kwa sababu yule alikwishakuwa ubavu
wake, alijaribu kumpenda kwa moyo wake lakini mwanaume huyu hakuona thamani ya
upendo wake na kuamua kubadilisha moyo wake kuwa wa kishetani. Mwisho wa yote,
Lisa anamuua mumewe kama mumewe alivyomuua mkwewe.
"Kwa nini Gunner,
kwa nini." Lisa alilia kwa uchungu na kwa sauti kuu.
"Oya kama
mmemmaliza huyo boya njooni mnivute bwana. Mi' naning'inia tu huku." Sauti
ilisikika toka katika dirisha ambalo Mubah alipita na kujitupa pamoja na bomu.
Malocha na Masai wakajikuta wakikimbilia kule inapotokea sauti. Wakati huo wale
jamaa wa Malocha walikuwa wamewaweka chini ya ulinzi washirika wa Gunner na John
Lobo.
Lisa naye akanyanyuka haraka na kwenda katika dirisha lile kubwa
lililokuwa wazi. Wakachungulia kwenda chini na kumkuta Mubah kanasa shati lake
kwenye bomba dogo la chuma linalotumiaka kupitishia maji ya mvua pale
itakaponyesha.
"Mnaangalia nini badala ya kunivuta, nyie wajinga
nini?" Mubah akalalamika na kuwafanya washirika wake watabasamu na kuanza
kuhangaika kumrudisha juu. Wakafanikiwa na kumwingiza ndani.
"Imekuaje
wewe? Si' umepigwa risasi wewe?" Malocha alimuuliza Mubah. Mubah kwa mbwembwe
akafungua vishikizo vya shati lake na wote wakashuhudia vazi la kuzuia risasi
likiwa mwilini kwa Mubah.
"Mlidhani siogopi kufa? Nani afe kibwege.
Mngekufa nyie mi' mngeniacha."
"Kumbe boya ulivaa bullet proof."
Malocha aliongea huku akianza kumsogelea tayari kwa kumuadhibu kijana
wake.
"Na hii ndio imenisaidia asee. Ningelipuka mimi leo hii. Mwee.
Yaani nilivyojitupa tu, shati likaingia kwenye lile bomba. Lakini shati pekee
halikutosha kunishikilia hadi mwisho, hii nayo ilinisaidia sana. Wakati huo
namsikia huyu boya anawaambia anabonyeza kidude, nikalitupa lile begi
likalipukia huko chini. Na bahati nzuri hakuna watu usiku huu." Mubah aliongea
na kuwaacha wenzake wakiwa katika taharuki wakati huo Malocha akawa kasimama tu,
hajui amfanye nini Mubah.
"Una MUNGU mkubwa Mubah. Karibu tena." Masai
aliongea na kwenda kumpa mkono Mubah pale alipokuwa kakaa. Mubah akampa mkono,
Masai akamvuta juu na kumsimamisha kisha akamkumbatia kijana yule. Lisa na
Malocha nao wakajiunga katika upendo ule.
"Martina njoo." Martina
kusikia anaitwa na Mama yake, naye akanyanyuka haraka na kukimbia hadi pale
walipofamilia yake inayompenda. Wakacheka na kufurahi hasa baada ya Martina
kumkubali Masai kama baba yake.
Wataalamu wa Gunner wakapigwa pingu na
baada ya hapo, wakaanza kushuka ghorofa lile taratibu ikiwa tayari ni saa kumi
alfajiri.
Baada ya kufika chini, wakaenda hadi kwenye mlango wa
kutokea. Wakafungua na wote kwa pamoja wakatoka nje.
"Mpo chini ya
ulinzi." Sauti kali kutoka kwenye kipaza sauti ilisikika ikiwaamrisha Malocha na
kundi lake.
Mbele yao kulikuwa na magari ya polisi karibu ishirini na
taa zake za bluu na nyekundu zikilanda juu ya magari hayo. Polisi wapatao
thelathini wakiwa wakamata bastola na mitutu, walielekeza dhana zote hizo katika
mlango wa kutokea.
"Tayari hapa. Hamna ujanja tena." Masai aliongea
huku akimshusha Martina na kunyoosha mikono yake juu sambamba na
wenzake.
Askari kadhaa wakafika eneo lile na kuwapora silaha zao kisha
wakawafunga pingu kasoro Martina. Baada ya tendo hilo, wakawachukua na
kuwapeleka kwenye magari yao tayari kwa safari kuwafikisha
kituoni.
Asubuhi ya saa moja, vituo mbalimbali duniani vilikuwa
vinatangaza habari za vifo vya Gunner na Lobo pamoja na kukamatwa kwa watu
wanaotafutwa kwa muda mrefu na mashirika mbalimbali ya kipelelezi. Picha za
wakina Malocha zilionyeshwa kwenye vituo vingi vya runinga na kuwafanya watu
wale kuonekana katika vituo vingi vya runinga kuliko mtu mwingine yeyote
duniani.
Rais wa Tanzania akatoa tamko lake rasmi kuhusu watu wale.
Japo hapo mwanzo walishukiwa kuwa ni magaidi, lakini Rais aliwatunuku cheo cha
mashujaa. Na kwa furaha, akawarudisha Malocha na kundi lake FISSA. Akatimua wale
waliokuwepo kwenye viti vya watu hawa.
Kwa Frank Masai, alikuwa kapata
ugumu sana kutoka katika msala wake hasa kwa sababu alikuwa anakesi nzito ya
mauaji aliyoyafanya huko nyuma (SIMULIZI NYINGINE HII. UTAPATA MKASA HUU KWA
UNDANI).
Rais alionesha ukali wake kwa alichokifanya Masai huko nyuma
na hakuthubutu kutoa maneno ya kumtetea kwa sababu karibu mataifa makubwa yote
yalikuwa yanamshutumu kijana huyu kwa mambo aliyokuwa kayafanya.
"Kwa
Masai. Naiachia mahakama ya makosa ya jinai imuhukumu, sina mamlaka naye hata
chembe. Na siwezi kumtetea hata kidogo sababu ya ushenzi ambao kaufanya." Sauti
ya Rais ilitangaza baada ya kuwarudisha wakina Malocha ndani ya FISSA. Watu
walilalamika na kuishutumu serikali kwa kushindwa kutetea mashujaa wake lakini
maneno hayo hayakumaanisha kauli ya Rais itenguke japo moyoni alikuwa anajiona
kama mwenye kusaliti wananchi wake.
Hatimaye ikafika siku ambayo Masai
alipaswa kupewa hukumu yake na mahakama ya makosa ya jinai kutokana na kosa la
mauaji alilolifanya miaka kadhaa iliyopita. Waaandishi wa habari waliruhusiwa
kutangaza kesi ile mwanzo hadi mwisho. Hivyo hukumu yake ilipatwa kuhudhuriwa na
watu wengi na pia kusikilizwa na kutazamwa kwa wingi uleule.
"Frank
Brown Masai. Hutakiwi kujibu chochote katika hukumu hii. Vithibitisho vyote vipo
kwa uliyoyafanya. Maneno na matendo yako yapo yote, hamna haja kujibu kesi hii."
Ni hakimu wa kesi ya Masai akiwa katika ubora wake.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wanasheria
mbalimbali walijaribu kumtetea Masai lakini hawakufanikiwa kupunguza ukali wa
kesi ile na mwisho wake ulikuwa ni hukumu nzito kwenda kwa Masai.
"Kwa
makosa aliyoyafanya Frank Masai, anahukumiwa kifungo cha maisha katika jela ya
L.O.R.D. Atafanya kazi ngumu na kukutana na vikwazo vingi sana. Hiyo ndio hukumu
yake." Watu wote waliokuwa wanafuatilia ile kesi wakashikwa na butwaa na macho
yakawatoka baada ya hukumu ambayo kwao waliona ni nzito kuliko hukumu zote.
Waliona ni kheri kuhukumiwa kinyongo kuliko kupelekwa ile jela ambayo hakuna
anayejua ipo sehemu gani katika nchi ile ya Cambodia.
Hakimu wa
mahakama ile ya juu duniani, akagonga nyundo yake kumaliza kesi ile. Masai akawa
kahukumiwa na kuwaacha Lisa na Martina katika simanzi, lakini alipewa ruhusa ya
kuwaaga na kuwaahidi ataishi licha ya vikwazo
vitakavyomkuta.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment