Search This Blog

Friday, 20 May 2022

KIKOSI CHA PILI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : BAHATI MWAMBA (NDIMI KUDO )



    *********************************************************************************



    Simulizi : Kikosi Cha Pili

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali ya hewa ilikuwa metulia,si ndege wa usiku au wadudu waliokuwa wakisikika,haijulikani kwanini kulikuwa na hali Kama hiyo usiku mnene namna ile ambao ni lazima kuzisikia sauti zao hasa kwenye msitu mkubwa kama ule,.

    Utulivu ule uliondoshwa muda mfupi baadae pale ambapo ilitokea helkopita ya kijeshi na kuganda juu ya anga la eneo hili la Monigi pembeni kidogo ya mji wa Goba,.



    Helkopita ile ilikuwa imebeba wanajeshi wapatao watano,huku mmoja miongoni mwao alieonekana kuwa kiongozi aliwasihi vijana wake washuke kwa kutumia kamba.



    Alianza wa kwanza,wa pili...walipendeza katika ushukaji wao,ilionesha ni wazoefu katika fani hiyo,na haikuwa na Shaka wote walikuwa ni makomando katika kikosi flani cha jeshi,



    Wapili alivyofika chini tayari watatu na wanne nao walikuwa wapo kwenye kamba wanateremka huku silaha zao za kivita zikiwa tayari mikononi mwao,kwa lolote huku wale waliotangulia kushuka wakihakikisha usalama wa wenzao washukao,.Walitua chini kwa kishindo kidogo kisha mmoja akatikisa kamba kuashiria tayari wametua salama,.



    Kapten Shayo aliona mtikisiko ule wa kamba alijua ni nini maana yake nae akaamuru rubani wa helkopta ile ya kijeshi iuache salama msitu wa Monig,wakati rubani akiigeuza helkpita ile,kepten Shayo yeye alikuwa anatafuta mawasiliano na upande mwingine anaojua kisha bila kusikiwa na rubani yule alisema maneno machache tu kwa upande wa pili "Wameshuka salama" kisha bila kungoja akaweka pembeni kifaa kile na kutulia kimya.



    Msitu ule uliwalaki kwa utulivu wa hali ya juu,hakuna walichosikia zaidi ya hatua zao wenyew,huku kwa mbali wakisikia sauti za vibuyu vyao vya maji walivyufunga viunoni mwao,.hawakutaka kuhadaika na ukimya ule wa msitu,walitembea kiuangalifu huku wakiwekeana ulinzi wao kwa wao,

    Mmoja akiwa mbele alitoa ishara kwa wenzie kwa kukunja ngumi kisha kunyoosha mkono juu,wenzie walipoona hivyo wakajiweka tayari maana hiyo ilikuwa ni ishara ya kuwataarifu kuwa kuna jambo mbele yao na wanapaswa kutulia kimya nao wakatii na kusimama,.



    Kama ungeliwaona katikati ya kiza kile ungelidhani ni kichaka kidogo kilichokatikati ya miti mirefu iliotosha kutengeneza msitu ule mkubwa,



    Wakiwa katika utulivu wao walihisi kama mvumo wa kitu mita kadhaa mbele yao,na hapo tena yule aliekuwa mbele akatoa ishara ya kusambaza vidole vyake viwili mara tatu kisha bila kusubiri na kwa wepesi wa karatasi akaruka upande wa pili kuliko kuwa na majani marefu,wakati yeye akifanya hivyo wenzie nao wakachumpa na kuangukia upande tofauti kila mmoja huku wakiiacha njia ikiwa nyeupe kama vile hakukua na watu waliokuwa wakiipita dakika kadhaa nyuma.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakiwa wapo makini kufuatilia mvumo ule wa sauti nao ukakaribia zaidi punde ikatokea gari aina ya jeep yenye kubeba watu wawili ndani na dereva,iliwapita wanajeshi wale wakiwa wametulia kwenye maficho yao,.



    Wakiwa bado wametulia ili kuthibitisha usalama kabla ya kuendelea na safari,wakasikia tena sauti zikijia njia hiyo hiyo ilikotokea ile jeep, Mara hii haikuwa gari ila ilikuwa ni watu waliokuwa wakipita pale kwa miguu,miongoni mwa watu wale ambao kwa idadi walikuwa saba wawili walikuwa wamefungwa kamba miguuni na mikononi huku waliosalia walikuwa wamebeba bunduki mikononi mwao na walionesha wako makini kwa kila hatua waliopiga mateka wao,haikueleweka watu wale walitekwa kwanini na kwanini walikuwa wakisafirishwa usiku ule na walikuwa wakipelekwa wapi nao ni kinanini? Ni maswali ambayo walijiuliza wanajeshi wale bila majibu.



    Baada ya dakika zipatazo kama kumi hivi masikio ya makomando wale yalipata uhai na hii ni kulingana na vifaa vya mawasiliano vilivyofungwa masikioni mwao ili waweze kuwasiliana bila kutoa sauti ilianza kwa mmoja kusikia akiitwa,

    Code 01" mwenye utambulisho wa namba hiyo akaitika "clear"

    "Z4"

    "clear"

    G2"

    "clear"

    Basi alipokwisha kuwaita wenzie akatoa kauli moja kwa wote "let's go" nao pale walipokuwa wakanyanyuka na kurudi njiani huku usimamji wao ukiwa ni wa tahadhari zaidi kila mmoja akijaribi kutazama ndani ya kiza kile,kuhakikisha usalama wake na wawenzie.



    Walipokwisha kuungana wote wakaanza tena Safari yao huku wakiwa kimya kila mmoja,mitutu ya bunduki ikitizama mbele na mitutu mingine ikitizama nyuma,kisha yule kiongozi wao akanyoosha mkono juu wote wakasimama napo akawaelekeza kwa ishara ya kidole kimoja kuelekea mbele na hapo wakaihama njia na kuanza kutembea msituni.Ilikuwa ni mwendo wa nusu saa hadi kufika kwenye eneo la Rukoko mji ambao wakazi wake walishahama,hapo makomando wale wanne wakapokewa na utulivu wa kutisha,hawakujali na hapo wakajadili jambo kidogo kisha alieitika kwa codename Z4 akatoa ramani na kwa kusaidiwa penlight akawaonesha wenzie ni wapi walipo na hapo ikasikika sauti kutoka kwa G2 sauti ilioongea kiswahili safi kabisa akawashauri wenzie "badala ya kwenda na njia hii itakayo tufikisha Kibati,sisi tupite upande huu wa magharibi ili tutokee kwenye eneo husika,kisha tukifanikiwa hapo tutatokea huku na kwenda kutokea buhimba."



    Hakukua na maelezo zaidi ya kutekeleza wazo na hapo wakaamua kuanza safari ya kukatiza katikati ya msitu wa Rukoko ili wawahi kufika nyiragongo sehemu watakayoenda kukamilisha mpango wao,



    Iliwachukua dakika araobaino na tano kuikaribia ngome hiyo ya waasi wa AGFT(Against Government we make Future Tommorow),walizidi kuikaribia ngome ile inayolindwa na waasi wenye mafunzo ya hali ya juu,makomando wale walisimama baada ya kufika karibu kabisa na eneo hilo la kambi ya Nyiragongo,Z4 na G2 wakachukua jukumu la kubaki nyuma ya wenzao wawili ambao wao waliamua kuingia kambini humo kwa kupitia nyuma ambako kwa uelewa wao huko ndiko hakukua na ulinzi mkali,

    01 na yule kiongozi ambae namba yake ya utambulisho ni K3 walisonga kwenda kulifuata lango la nyuma ya kambi ile,iliwabidi watambae ili kukwepa taa za ulinzi zisiwamulike,Z4 na G2 wao walikuwa wakifuata kila hatu ya 01 na K3 kwa kutumia lens za sniper rifle walizokuwa wamebeba mikononi mwao ili kuhakikisha mpango wao unakamilika kabla ya saa kumi usiku....





    DAR ES LAAM saa nane na nusu usiku.



    Kikao kiliendelea huku kila aliehudhuria kikao kile akiwa amekwisha kuchangia hoja yake,huku sasa ikiwa imebaki hitimisho la kiongozi wa kikao kile macho ya wanakikao kile yakiwa kwake alitingishika kidogo kisha akajikohoza na hatua kwa hatua aliwatupia jicho wajumbe wake na hapo sauti ikamtoka

    "hakuna namna kepten shayo lazima afe na rubani wake leutanant Koba,maana hawa hawajui chochote kinachoendelea,ila inaweza kuja kuleta shida wakibaki hai na wakajua walitumika kinyume cha kazi yao" hapo akanyamaza kisha kama mwanzo aliendelea kuwatizama wajumbe wake,aliporidhika na utulivu wao akaendelea

    "vijana hao walioenda Goba na imani watakamilisha huo mpango ila kabla ya kesho jioni nao wawe wamekwisha kuondolewa duniani na atakae waondoa taarifa anayo tayari"

    Wajumbe wengine wakasimama na na kupiga salute kwa kiongozi huyo kisha wakaanza kutoka chumbani humo na kila mmoja alkielekea anakokujua..



    Helkopita iliombeba kepten Shayo na Lieutenant Koba iliendelea kuyakata mawimbi na sasa ilikuwa inaikaribia kambi yao kijeshi ilioko mkoani humo na kwa maelezo ya wakuu wao ilipaswa helkopita hiyo kutua hapo,Kisha wao watapewa usafiri wa gari ili kuwarudisha morogoro ilipo kambi yao ya kuripoti kazini,



    Walitua salama na bila kuchelewa wakapikiwa ndani ya gari Safari ya kutoka Kigoma kwenda morogoro ikaanza,ndani ya gari hakuna aliemsemesha mwenzie huku kichwa cha Kepten Shayo kikiwa na mawazo lukuki kuhusu mpango huo asioulewa na vijana wake kawaacha huko Goba,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kukiwa kunakaribia kukuchwa tayari wao walikuwa wamekwisha iacha tabora wameikanyaga singida,na walikuwa katikati ya pori la Chaya kilometa chache kabla hujaifikia Manyoni na hapo si dereva au leutanant,aliegundua kitu isipokuwa kepten Shayo alieona mtu alievalia kijeshi huku akiwa na kiona mbali,akiwatizama wakati bado akifikiria hilo dereva wa gari lao akapiga ukulele mdogo na kisha kuulalia usukani huku gari likikosa mwelekeo na likiongeza kasi,

    Si leutanant Koba au Kepten Shayo aliefanikiwa kutoka ndani yake gari likapaa juu na kushuka chini kwa kasi kisha kujipigiza chini huku moto ukiwaka juu yake na injini ya gari lile aina ya Ashok ikizimika,akiwa anaona kwa mbali kepten Shayo aliona wanajeshi wawili wakiwa na silaha wakilifuata gari lao na hapo hakushuhudia tena zaidi ya kusikia milio ya risasi ikiliendea gari lao linaloteketea kwa moto huku Leutaenant Koba akiwa mbali na dunia hii...



    Z4 alikuwa makini kufuatilia hatua za 01 lengo ni kuhakikisha usalama wake,G2 nae alikuwa makini sana kufuatilia hatua za K3.

    Hawakutaka kupoteza muda walipolifikia lango la kuingilia ndani ya ngome ya waasi wale wa AGFT 01 alisimama kisha akatoa kalamu ndogo mfukoni mwake na kumulika eneo alilokuwepo,aliporidhika kutazama amitakacho akainama tena na hapo akatumia Nguvu zake zote kufunua mfuniko uliokuwa umeziba chemba moja ya kinyesi,alipofanikiwa kufungua chemba hiyo bila kusita akazama ndani,K3 nae bila kuchelewa akazama ndani,huko ndani walikutana na harufu kali ya kinyesi ila hawakujali taratibu walianza kusonga mbele kuufuata mkondo ule unaotiririsha kinyesi kuelekea mto Kali.



    Walikuwa wakitembea huku wakihesabu hatua zao,hatua zao zilipofika ishirini ikabidi wasimame na kwa uangalifu wa hali ya juu,walianza kuangalia juu ya chemba ile ya maji machafu yaliochanganyika na kinyesi,kwa macho ya paka walifanikiwa kuona bamba la kuzibia chemba likiwa juu ya vichwa vyao,.



    K3 akazama mfukoni na kutoka na kichupa kidogo mfano wa zile chupa zinazohifadhi manukato,akakibinya kwa juu na kikatoa mlio wa kuruhusu kilichomo kutoka na kwa uangalifu sana akazungusha eneo lote aliloamini ndio ukubwa wa bampa lile,alipokwisha maliza akasogea pembeni kidogo,punde eneo lote lililoguswa na kimiminika kile,likaanza kumeguka,01,K3 kwa pamoja wakahesabu ilipofika tatu walikinga mikono juu punde lile bamba likashuka na bila kutoa kelele likatua mikononi mwa makomando wale,ukabaki uwazi hapo juu nao ukatumika kama njia ya kuzamia ndani ya ngome ile ya waasi wale,



    Bunduki mikononi tayari kwa lolote,wakajikuta katikati ya banda lenye watu waliokondeana,na pembeni kukiwa na maiti za watu waliokufa muda mchache uliopita,ilitisha kuwatizama ni watu walikula mateso ya haja,.



    Taratibu na kwa umakini makomando wale wawili walianza kuwagua baadhi ya watu pale ndani,haikuwachukua muda mrefu wakampata mtu waliemtaka,kwa mwonekano alikuwa ni mwanaume mrefu kiasi,mweusi kiasi na macho yake yaliingia ndani,inaonekana kabla ya mateso alikuwa ni mtu mwenye mwonekano kimazoezi,



    Alipokwisha kunyanyuliwa K3 akataka kumbeba ila alikataa na akaomba apewe silaha ndogo,01 akampa kisha kwa kusaidiana waliweza kutoka ndani ya banda lile na kurudi ndani ya chemba ile kisha wakaianza safari us kutoka ndani ya ngome ile ya AGFT.



    Z4 alianza kuona kichwa kisha kiwiliwili kikitua nje,hakuwa peke yake alifuatia mtu wa pili kisha mtu wa tatu kisha kwa mwendo nyoka kibisa walianza kutambaa kuifuata njia waliotokea,.



    Ni maiti pekee ndio isingeliweza kuhisi harufu kali ya kitu uvundo au kinyesi ila si kwa binadamu aliehai.

    Harufu ya maji machafu yenye kinyesi ikamfikia mlinzi mmoja wapo kwenye ile kambi,akashawishika kuifuatilia harufu ile kwa mujibu wa pua yake.



    Ni wakati mlinzi yule akiukaribia mlango wa nyuma wa ngome yao kulipokuwa na chemba ya maji machafu,hapo akagundua kitu,

    Mburuzo wa kitu akachukua kurunzi yake ili amulike hakuifikia ile kurunzi aliokuwa ameifunga kiunoni akapigwa risasi ya kichwa hakuomba hata maji akaiga dunia lakini wakati akipaa juu na kudondoka mlinzi aliekuwa kwenye taa za ulinzi aliona kitu,akamulika tena eneo lile hapo kwa mbali akaona sare kama yake imelala chini,hakuwa na chaguo zaidi ya kupiga filimbi ya hatari na Wendie wote wakanyuka walikolala na kushika bunduki,kisha wakapelekwa eneo la tukio,



    Haikuchukua muda kugundulika uvamizi ule na mmoja wa mateka wao muhimu ametoroshwa,msako ukaanza mara moja kuuzunguka msitu ule wa nyarugongo na kuhakikisha wavamizi wale hawatoki salama.



    ***********

    Vifo vya wanejeshi wale watatu,vilizua gumzo nchini Tanzania,kikubwa vile vifo vyao vilivyotokea gari lao kulipuliwa na bomu,

    Kulingana na taarifa hiyo vikosi vya jeshi kushirikiana na polisi vilielekea eneo la tukio,watalaamu wa milipuko haikuwachukua muda kubaini aina ya kombora lililotumika,lakini kikubwa zaidi ni vile risasi zilivyoriharibu gari ikimaanisha kuwa walishambuliwa kwa risasi baada au kabla ya gari lao kulipuliwa.



    Wengi waliowafahamu kepten Shayo na leutanant Koba walishindwa kujua sababu za vifo vyao ilihali jioni ya siku hiyo walionekana kambi ya ngerengere Morogoro,ilikuwaje walifika kigoma na ilionekana ndiko walikotokea? CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Upelelezi wa mwanzo ulizidiha utata hawakuonekana kambi ya Tabora na hata Kambi ya kigoma swali likaja walikuwa wapi na walitoka wapi? Hakuna aliejua zaidi ya marehemu wenyewe.



    Miongoni mwa watu walioumizwa na jambo hili ni Meja Salimu Komba,alimjua vizuri Shayo,na pia alikuwa rafiki yake,hakukubali jambo hili lipite kimya,alichukua usafiri wake hadi kambi ya Ngerengere morogoro,alipokwisha kufika akapokelewa na moja kwa moja akaenda kuonana na Meja kizurungu,mkuu wa kikosi cha hapo ngerengere,walikaa ofisini kisha meja Salimu Komba akauliza mwelekeo wa upelelezi wa tukio lile hapo napo akakutana na jibu gumu kidogo kwamba,lolote lile linalohusu kesi hiyo lilipotiwe makao makuu,.



    Akiwa anatoka Morogoro,kwenda Msata akapiga simu makao makuu na hapo akakutana na jibu liliobua hisia mbovu kichwani pake,alikutana na jibu moja tu faili la vifo hivyo lipo kwa Afisa mwandamizi wa jeshi la wananchi na taarifa zote zipo kwake.



    Swali lilibaki kwake kwanini hadi sasa hajapewa mtu wa kufuatilia tukio hilo kubwa,na kwanini basi wasiachie usalama wa taifa au jeshi la polisi kama wao hawahitaji kuingilia jambo hilo?



    Akaona kuna tatizo,akachukua simu akapiga,punde simu ikapokelewa upande wa pili

    "Nambie mkuu"

    "upo wapi "

    "kwangu"

    "Tukutane Chalinze bar"

    "Nimefika mkuu"



    *****************



    Makomano wale wanne walijitahidi kukimbia ili kuacha msitu wa Nyarugongo wawahi kufika upande wa msitu mwingine ambao kwa ungelikuwa salama zaidi,ila kadri walivyokwenda ndivyo walivozidi kusikia Milio ya mbwa ikiwakaribia

    Hawakuwa na namna zaidi ya kujificha mstuni humo waweze kutumia ujuzi wao,



    Wakati walipokuwa wakiiacha kibati na kuikaribia Buhimba,wakasikia tena mbele yao kundi lingine tena likiwafuata,walikuwa wamezingirwa tayari,punde milio ya risasi ikaanza kusikika,kwa wepesi wa hali ya juu,makomando wale waliendelea kuwadondosha waasi kama mchezo hivi,



    Wakati mapambano yakiendelea yule mtu alieokolewa na makomando wale akawapa ishara wamfuate nao bila kuuliza wakaanza kumfuata hatua chache wakajikuta wapo kwenye kingo za mto Rwerwe na bila kujiuliza wakazamia ndani na kuvuka upande mwingine,huko nyuma waasi waliachwa solemba hawakujua adui kaelekea wapi kizani mule.



    Walizidi kulikata pori lile nene huku sasa kukikaribia kukuchwa hawakuwa wamepewa uelekeo wa kukutana na kikosi cha msaada wapi au upande gani zaidi walihitajika kufuata maelekezo ya mtu watakae mwokoa na kweli ndie walifuata maelekezo yake,waliukata msitu ule mnene punde wakafika kwenye kichaka kidogo,yule mwanaume waliemuokoa akatangulia kukifikia kile kichaka,akapekenyua kidogo akatoa ficho lile liliokuwa kama kichaka,hawakuamini macho yao kulikuwa na helkopita ndogo ya kisasa ilikuwa imehifadhiwa pale,GR Chinook iliotengenezwa urusi,wakiwa bado wanashangaa mwanaume yule akadandia juu yake na kuingia ndani,wakati G2 anataka kuingia ndani akapigwa kikumbo na K3 wakati 01 akistaajabu kitendo kile risasi ikalia alipo 01, G2 akaelekeza macho kule alipokuwa 01 akashuhudia akidondoka chini alipongalia akipokuwa Z4 akamshudia akihepa na kudondoka upande mwingne mtutu wa bunduki ukawa usawa wa kichwa cha G2



    Kisha mwanaume yule akajitambulisha kwake

    "Naitwa Ibrahim Mbaya ila wengi huniita Ibra Mbaya" hakumaliza kauli yake G2 akaruka upande ule alioangukia Z4,nyuma zikafuata risasi nyingi kutoka kwenye bunduki ya K3. Kisha kihelkopita kile kikaicha ardhi ile ya DRc Congo..



    Meja Salim Komba aliegesha gari kwenye eneo la maegesho ndani ya Chalinze bar,akatazama kulia na kushoto hakupata tabu kuliona gari la mgeni wake likiwa limeegeshwa pale,akashuka na kwa hatua za ukakamavu akaliendea lango la baa ile,

    Akazama ndani,haikumchukua muda kuona pahali alipokaa mgeni wake akiendelea kuburudika na maji baridi kutoka kampuni ya jambo.



    "Zedi Mbiwa"Meja Salim Komba hakungoja mgeni wake aitike aliendelea kuzungumza baada ukimya kutoka kwa Zedi kuashiria alikuwa tayari kuyasikia mazungumzo yale alioitiwa na Meja Salim Komba,

    " Bila Shaka unazotaarifa za anguko la pacha wako,japo mlitengana miaka michache hapo nyuma,hii haimanishi kwamba undugu wenu umekwisha".

    Zedi mbiwa akadakia...

    "Nimesikia kifo chake kimeniuma lakini kinahusiana nini wito wako hapa?"

    '"camoon Zedi hujawa mtoto kiasi hicho,lile ni tukio zaidi ya tukio,yeye na Leutenant Koba hadi jana jioni walikuwa wapo kambini haieweki kwanini wamekutwa kwenye mapori ya Singida,risasi zaidi ya kumi mwilini mwake huku bomu likihitimisha safari ya uhai wake,"

    "ok nimekuelewa ripoti inasemaje"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hakuna ripoti yoyote hadi sasa inayoeleweka zaidi kila hatua ya tukio inatakiwa kuripotiwa kwa mnadhimu mkuu wa jeshi,polisi na usalama wote wamezuiwa kufuatilia kesi hii, lakini kubwa zaidi vyombo vyote vya habari vimezuiwa kutangaza tukio hilo kwa vyovyote vile"

    Zedi alivuta pumzi ndefu kisha akazishusha kisha kwa upole akamtazama Meja na kusema

    " Mbona bado mapema sana kushuku chochote mkuu"

    Meja Salim komba ikawa zamu yake kumtazama tena Zedi Mbiwa kisha kwa upole akasema

    "Sijazeeka kiasi hicho Zedi naujua upupu na mapupu vilivyotofauti,pia kumbuka kabla ya kuwa ulivyo nilikuwa mwalimu wako so tambua sijashindwa kutambua utata wowote ingali ukiwa mbichi kabisa"

    "sawa mkuu hakuna shaka nipe siku kadhaa na kumbuka hatujawahi kuonana"

    "hayo ndo maneno sasa angalau nitaenda kwenye mazishi nikiwa sawa kimwili na kiakili na sitoogopa kuitizama maiti ya Shayo.



    Watu wengi walihudhuria mazishi ya kepteni Shayo na leutenant Koba,ambapo maiti zao ziliagwa kwenye viwanja vya kambi ya ngerengere Mkoani Morogoro,

    Viongozi wengi wa kijeshi walikuwa pale wakiaga miili ya vijana wao ambapo kimsingi haikufahamika chanzo cha vifo vyao,.



    Miongoni mwa waombolezaji wale alikuwepo Zedi Wimba,alivaa tisheti ya rangi ya kijivu na suruali ya jeans,usoni alijipamba na miwani yake safi ya rangi ya gold mfifio,aliwatizama watu wote pale na nyendo zao,ila miongoni mwa watu wote alistukia nyendo za mtu mmoja aliekuwa kavaa suti nyeusi,mtu yule mara kwa mara alikuwa akitoka na kujitenga pembeni kisha kuongea na simu huku mara kwa mara akitizama kwa mashaka kama kuna mtu anafuatilia nyedo zake,

    Uvaaji wake na nyendo zake vilizidi kumtia mashaka bwana Zedi,na akashawishika kumfuata bwana yule pindi alipoelekea kuliko paki magari ya watu binafsi.

    Zedi hakuacha alama ya mashaka kwa waliomuona wakati akijaribu kufuata nyendo za bwana yule,

    Safari yake ilimfikisha hadi usawa wa maegesho ya magari na hapo akaliona windo lake,na kwa utaratibu sana pale alipokuwa yeye na yule mtu aliona ili amuone kwa uzuri zaidi yahitajika apande ndani ya gari,akaangaza gari lake akaona lipo mahali pazuri zaidi,

    Wakati Zedi akifunga mlango wa gari lake alipata kuona kitu kilichomsitua,yule bwana alikuwa amesimama pembeni kidogo ya gari moja jeusi na ndani ya gari kulionekana kuna mtu ambae yule mtu alikua akizungumza nae,hapo akaamini yupo sahihi kwa hisia zake.



    Baada ya dakika kadhaa za mazungumzo baina ya watu wale kwenye maegesho yale ya jeshi yule mtu aliekuwa akifuatiliwa na Zedi aliondoka na kurudi kule kuliko na shughuli za kuiaga miili ya wanajeshi wale.

    Wakati akidhani yupo salama alikosea sana jicho la Zedi lilikuwa nae hatua kwa hatua,na halikumwacha na hata wakati akiweka kifaa cha kunasia sauti kwenye kombati ya kanali Magati,Zedi aliona hicho kitendo na hapo akili yake ikafanya kazi haraka alipaswa nae kufanya kitu ili apige hatua katika utata wa matukio yale,akajipapasa hapo nae akatoka na kifaa kidogo mithili ya betri ya saa akajipitisha alipo kanali Magati kisha akaondoka na kuelekea kwenye gari lake na kutokomea anakokujua.



    *************

    G2 alidondoka kwa wepesi wa hali ya juu na kwa kuwa alijua risasi zitafuata alimuona Z4 akiwa kajificha sehemu akamparamia wakadondoka upande wa pili kisha kwa kunong'ona akamwambia Z4

    "Tumegeukwa kwenye nchi ya watu"

    Nae Z4 akamwambia

    " Cool down solder sio muda wake bado tupo kwenye mdomo wa mbwa mwitu"

    "R.I.P 01"

    kisha bila kusubiri kwa pamoja wakasimama na kuishuhudia helkopita ile ya wasaliti ikipotelea angani,Z4 akamtazama G2 kisha akamuuliza

    "Tutafanya nini na mapambazuko tayari"

    "hakuna namna tupo karibu Sana na mji wa goma tatizo haya mavazi "

    Hawakuwa na budi kuanza Safari ya uangalifu ili kuutafta mji wa Goma ili iwe rahisi kwao kuingia Rwanda.kwa mbali walizisikia sauti za mbwa zikiwaandama.



    Zeso Nigamba alikuwa ni kiongozi wa waasi AGFT,aliwaongoza vijana wake hadi eneo ilipokuwa helkopita ile ya Ibra Mbaya,kisha kama ambae hataki akainama chini aliponyanyuka alikuwa na beji ya yenye nembo ya bendera ya nchi ya Tanzania,kisha kwa mguu wake uliovaa kiatu kigumu akausukuma mwili wa 01 uliokuwa umelala chini, akautazama tena kwa macho yake mekundu,pasi kusema neno Zeso akageuza shingo yake,punde tendo hilo likapokelewa na mpiganaji wake,akainama na kuweka sikio lake upande wa kushoto wa kifua cha komando yule wa kitanzania,kisha bila kumwemwesa akasema

    "He is alive"

    01 akachukuliwa haraka na kupelekwa wanakojua wao,



    Z4 alisimama kwenye kilima kidogo na kutizama mbele waelekeapo akamwitaG2 aliekuwa akisubara eneo flani kilimani pale,Kisha bila kuhakikisha kama aliemwita yupo au la akamwambia hatuna budi kukivamia kiijiji kile kwa njia ya amani ili tupate mavazi"



    Tayari walikuwa wapo ndani ya kijiji cha Kisagenyi,wananchi waliwatizama kwa viulizo maana hawakujua ile kombati mpya machoni mwao illikuwa na lengo gani,ila waliendelea kuonesha wao wamezoea kuona bunduki,hawakutetereka kuwaona makomando wale,waliendelea na shughuli zao,.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    G2 akamwita kijana mmoja aliemuona wanaendana maumbo,alipokwisha mfikia akaomba apatiwe mavazi yeye na mwenzie,kijana yule nae kwa kiswahili kibovu akawajibu wazunguke upande wa pili kulikokuwa na karo la maji huko watapata nguo zilizochakaa zitawafaa ila ni kwa kuwa hawakujua lengo la yule kijana,.



    Kulingana na kuzoea vita yule kijana alipowaona watanzania wale alijua wako matatani hivyo alipowaelekeza kule nyuma alitaka wapate sehemu ya kutorokea iwapo waasi watatokea eneo lile,.



    Ni muda ambao G2 alikuwa akimalizia kuvaa nguo,Z4 alikuwa ameshuhudia gari nne za maaskari wa AGFT wakiruka kutoka kwenye magari hayo huku bunduki zao zikiwa mkononi,G2 aliona tukio lile aliwahi kuikamata SMG yake,Z4 nae akajiweka tayari kwa lolote,

    Kupitia uwazi mdogo ndani ya lile karo walishuhudia askari kama sita wakija kwa kasi kwenye karo lile huku wengine wakikusanya wanakikiji Wa kijiji kile.....



    Waasi waliendelea kuwakusanya wanakijiji wale,huku baadhi yao wakiingia nyumba hadi nyumba kukagua,



    Palepale walipokuwa makomando wale,walishuhudia wale askari wa waasi wakikaribia eneo walilokuwa,haikuwachukua muda kugundua ndani ya Karo mule kunasehemu yenye upenyo wa kupita mtu,



    Z4 akaigusa sehemu ile akagundua inawatosha kupita na bila kusubiri akamkonyeza G2 na kwa pamoja wakazama kwenye upenyo ule kisha wakaparudishia vile palivyokuwa,



    Tofauti ya matarajio yao kwenye upenyo ule ndani walikutana na uwazi wa kutosha mtu kupita,na ilionekana huwa ni sehemu ya watu kupita,wakaifuata hiyo njia iliokuwa chini ya ardhi huku wakiwa makini na kila hatua wanayoipiga,bunduki mkononi,macho mbele.



    Zeso na wanajeshi wenzie wakawaita wanakijiji kadhaa mbele, na kwa kutumia lugha ya kimaghibeni akawauliza kama wameona wageni kijijini pale,jibu alilolipata hakulifurahia,na ili kuwatisha wawili kati ya watu waliopitishwa mbele akawamiminia risasi vichwani mwao.

    Pengine hiyo ingelikuwa ni njia rahisi ya kuwatisha ila si kwa wamanghibeni wale waliozoea misukosuko ya kivita kila uchwao huku wakiamini hata wakisema ukweli bado wangeliuwa tu.



    Askari wake Zeso walifika hadi usawa wa lile karo haikuwachukua muda mrefu kuyaona mavazi ya makomando wale wawili,na bila kujiuliza mmoja kati ya waasi wale akayabeba na kuyapaleka kwa Zeso,Zeso aliyatizama kisha bila kujiuliza akanyanyuka na kufuata usawa alikotokea mleta taarifa yule, Askari wake wakafuata nyuma na hapo ukafuata msako mkali ndani ya kijiji kile,wanawake na watoto walisikika wakilia vilio vya woga ila waasi wale hawakujali lolote walizidi kutafuta kila walipoamini adui yao kajificha hapo.



    Walizidi kutembea kwa tahadhari sana maana hawakujua kijia kile kingeliwapeleka wapi,punde wakaona mwanga,hapo G2 aliekuwa ametangulia akaonyesha ishara kwa mwenzie,kwa uangalifu wa hali ya juu wakaanza kuufuata mwanga ule,punde walijikuta wapo nje ila kama walidhani wapo salama walikosea sana,wakati wakimalizia kutoka wakajikuta wakizingirwa na kikundi cha watu zaidi ya sita walioshika silaha kuwaelekeza wao,na mmoja kati ya watu wale akawaamuru watupe silaha chini nao wakatii huku hofu ya kuuwawa ikiwa wazi nyusoni mwao.

    ************



    Zedi Wimba alikuwa njiani kurudi yalipo makazi yake ndani ya mji wa chalinze,ni wakati akiwa njiani akagundua nyuma ya gari lake kulikuwa na gari nyeusi ikimfuata taratibu ili isigundulike,akatabasamu kisha akajiambia "inaonekana wapo makini sana kweli Shayo umehijumiwa."



    Kitendo bila kusubiri akatizama mbele hakuona gari akaamua kukunja gari arudi alipotoka ina maana morogoro,waliokuwa ndani ya gari ya nyuma hawakutarajia tukio lile na wakashindwa kugeuza na wao ili kumuondolea mashaka mtu waliekuwa wakimfuata,wao wakaamua kusonga na mbele wakiwa wamekosa namna ya kufanya.



    Zedi alikuwa na wazo moja kurudi hospital ya mkoa wa morogoro kulikofanyika uchunguzi wa kidakitari juu wanajeshi wale,aliamini hapo anaweza kupata taarifa muhimu juu ya mkasa ule,.



    Gari lake alilizima punde tu alipoingia sehemu ya kuegesha magari ndani ya hospital ya mkoa wa Morogoro,kisha kama vile hataki akazivuta hatua zake hadi ndani ya wodi za watu mahututi,huko akakutana na nesi mmoja akamuuliza wapi zilipo ofisi za dr Pius,alipokwisha kuelekezwa akazipiga hatua kuiendea ofisi ile,.



    Dr Pius alisikia mtu akigonga nae akamruhusu aingie,hakuyaamini macho yake mbele yake alisimama Zedi mtu waliepotezana miaka mingi,mwanafunzi mwenzie katika chuo cha utabibu muhimbili leo wanaonana hakuficha furaha yake si yeye tu hata Zedi alifurahi kumuona bwana huyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *********

    Ndani ya chumba kimoja walisimama mabwana wawili huku mtu mmoja akiwa kakaa na hivyo kupelekea kuwa na idadi ya watu watatu mle chumbani,



    Yule bwana aliekaa aliwatizama vijana wale waliosimama kisha kwa upole kidogo akawaambia "mlipaswa kuhakikisha kama koplo Ziga na Koplo makame wamekufa,kufa kwa Koplo Shija sio mwisho wa hao makoplo kama watakuwa hai wanaeza leta taabu baadae"

    Lakini sio mbaya Ibra Mbaya pole kwa matatizo nawe Luteni Zegera hongera kwa kutuletea Simba"



    Luteni Zegera na Ibra Mbaya wakaombwa wapumzike ili wapewe majukumu mengine baadae,ili kuhakikisha mpango wanaouandaa nchini Tanzania unakamilika kwa muda husika.



    Luteni Zegera yeye alienda moja kwa moja hadi nyumbani kwake huko hakukaa sana ujumbe ukaingia kwenye simu yake anahitajika kuoanana na mtu stendi ya mabasi ubungo kuna kazi ya kufanya huko,alipofika akakutana na kijana wa makamo akampa karatasi yenye maneno machache "Waziri wa Afya"

    Alipokwisha kusoma akakitia mdomoni kikaratasi kile kisha akakwea gari na kuitafuta zahanati ya Mbezi kulikokuwa na ufunguzi wa zahanati hiyo....





    Baada ya kusalimiana na kukumbushana ya nyuma,Zedi akaamua kuuvunja ukimya kwa kusema nini hasa lengo la yeye kufika pale,.



    Dr Pius akamtazama Zedi kisha akajikuna kidevu chake kilichogoma kuotesha ndevu japo umri umekwenda makumi,kisha akazishusha pumzi zake taratibu na akazungumza kwa upole kuwa wao kama wauguzi na matabibu wa hospital ile kweli walipokea miili hiyo mitatu lakini waliitwa madaktari wachache tu kuchunguza miili ile,na miongoni mwa madaktari wale alikuwamo Dr Kije anaehusika na uchunguzi kama huo.



    Zedi akatafakari kidogo kisha kama alieridhika na maelezo yale akauliza yalipo makazi ya Dr Kije akaelekezwa si mbali hospital ile.



    Makazi ya Dr Kije yalikuwa mita chache kutoka shule ya morogoro sekondari,haikuchukua muda kufika yalipo makazi ya Dr Kije,

    Zedi aliitazama nyumba ile iliokuwa imezungushiwa uzio mfupi wa tofali za kuchomwa,alitizama mazingira yale yalivyokuwa yametulia,hapakuwa na pilika za watu is isipokuwa ni kelele za wanafunzi zilisikika kwa mbali,

    Aliegesha gari lake kisha akatembea taratibu kufuata kijia ambacho kingemfikisha getini mwa nyumba ya Dr kije.



    Aligonga mara kadhaa bila kuitikiwa hapo akaingiwa na mashaka kidogo,akatoa kisu kidogo kwenye mguu wake akakishika mkononi mwake,ilihitaji macho ya paka kuona silaha iliokuwa mikononi mwake,kisha kama alieogopa kuligusa lile geti akalisukuma ajabu likafunguka nae kwa haraka akazama ndani huku macho yake yakizunguka kila pande ya uwanja wa nyumba ile,akashuhudia utulivu ulivyo ndani ya nyumba ile,akavuta hatua zake hadi mlangoni napo akakuta mlango upo wazi ila akasita kuingia,



    Wakati akijiuliza aingie au afanye nini akasikia sauti ya mtu kukohoa,alipoidadisi akagundua ni ya mtu alikabwa kwa nguvu zote na anapigania pumzi ya uhai wake,akajua lazima Dr atakua matatizoni,kwa kasi ya 4g akaukumba mlango kisha akahepa kuliendea jokofu lililokuwa karibu na mlango ule na hapo akapishana na risasi kadhaa kutoka kwenye silaha iliokuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti,akatulia kimya na muda huo risasi zilikuwa zishakoma na kutoka pale alipokuwa Zedi aliona kivuli cha mtu kikisogea kwenye eneo lile,hakutaka kusubiri akasimama gafla na kujitokeza ila ni kama hesabu zake zilistukiwa akajikuta akikutana na mtutu wa bastola aina coltrevover huku mshikaji akiwa makini na ukamataji wake,

    Zedi alijikuta bila kushurutishwa ananyanyua mikono ishara ya mateka,na hapo macho yake yakagongana na sura ya mtu katili kupindukia,kwa macho inaonesha ni mtu aliepitia hekaheka nyingi hadi kufikia hapo alipo,Zedi alishuhudia kovu kubwa lililoanzia upande wa kulia wa jicho hadi usawa wa kidevu huku jicho hilo likiingia ndani na kumfanya mtu huyo aongeze ubaya wa sura yake,

    Zedi alitupia pembeni macho yake hapo akashuhudia mtu mwingine mrefu akiivunja shingo ya Dr Kije kama kijiti kisha kutupwa pembeni kama mzigo akiachwa hana uhai tena.

    Zedi aliona kakutana na watu wa sayari ya fitina na mauaji ya wazi bila kuogopa,kisha akamshudia mtu yule akijongea pale alipo huku akiwa amekwisha kutoa bastola yake,hakutaka kusubiri kuona mwisho wake,mikono yake ikiwa juu akahamisha uso wake pembeni kidogo napo yule aliekuwa amemnyooshea bastola usoni mwake akahadaika kutaka kushuhudia huko mateka wake atazamapo,lilikuwa kosa ambalo pengine hatolisahau kamwe mtekaji yule.



    Kwa kutumia uzoefu wa kurusha visu alipinda kidogo mkono wake ukiwa juu kisha akaachia kisu kidogo kilichokwenda kutua shingoni mwa yule bwana alimvunja Dr kije shingo,alipiga ukelele kidogo kisha akatua chini kama mzigo,.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati akifanya lile tukio mikono yake imara ikaipangusa bastola ya mtekaji usoni mwake na mkono uliotupa kisu ukashuka kwa kasi hadi utosini kwa mtekaji,lilikuwa pigo baya ambalo aliwahi kupigwa katika maisha yake yote,



    Baada ya kupigwa wote wawili yule sura mbaya hakuwa na namna zaidi ya kufanya hila ili aweze kutoroka,licha ya kupigwa vile alihimili kusimama kisha kupanga mapigo yake aliofundishwa mwalimu wake,alitia mbwembwe nyingi huku akorudi nyuma hadi usawa wa dirisha pana la nyumba ile,



    Ni wakati Zedi akipanga na yeye mapigo yake,akashangaa yule bwana akipaa hewani kisha bila kutarajia akajiachia na kutua chini kisha kwa wepesi wa tawi akaliparamia dirisha lile la vioo na kutua nje na kutokomea,.



    Katika vitu asivyohitaji Zedi ni haraka katika mambo yake hakujihangaisha kumfuata akapiga hatua kumwendea Dr aliekuwa amelala chini akamtikisa kidogo na kubaini hana tena uhai,akasimama na kuendea mwili wa muuaji yule kisha bila papara akaanza kumpekuwa hakukuta kitu cha maana zaidi ya msokoto wa bangi,akaachana nae na kujipa utulivu kuikagua nyumba ile,haikuchukua muda kugundua upekuzi uliofanywa mule ndani,

    Hata yeye hakutaka kujihangaisha kukagua tena akaanza kupiga hatua kutoka nje ila kabla hajaufikia mlango akakumbuka kitu na akarudi haraka alipolala Dr Kije akampekua na yeye punde akatoka kijitabu kidogo kilichokuwa mifukoni kwa suruali ya Dr.



    Ni wakati akipiga hatua kuuendea mlango aliposikia king'ora cha gari la maaskari kikija upande bila kujiuliza akachumpa na kudondoka nje kupitia uwazi wa dirisha lililopasuliwa na mtekaji yule ambae alimpachika jina la Deepaklipa kwa ufanano wa sura na mhusika wa kula watu kwenye filamu hiyo ya Deepaklpa.



    *********

    Wakiwa wamefungwa kichwa chini miguu juu G2 alimuuliza Z4

    "Mimi na wewe hatujuani mkuu"

    "Naitwa koplo makame wa kikosi cha jeshi 820 Unguja"

    G2 nae akajitambulisha "naitwa koplo Ziga 882kj Makutupora."



    Hawakwendelea na maongezi yao punde walisikia nyayo za mtu akijongea kuja kwenye kile chumba walichofungiwa,

    Akaingia mtu mmoja mrefu na mweusi,alikuwa ameshika kisu kikali,aliwatizama makomando wale kisha kwa lugha ya lingala akawaamuru wafuasi wake wawafungue makondo wale,



    Kitendo bila kuchelewa wakashushwa chini huku mitutu ya bunduki ikiwaelekea.Mtu yule alieaamuru wafufunguliwe akawatazama kwa tuo makomando wale ambao hawakuonesha wasiwasi wowote kwa watekaji wao,



    "Mbona mmemwacha mwenzenu mikononi mwa agft au mlidhani kafa!?"

    Koplo Makame akashangaa si yeye tu hata koplo Ziga inamaana 01 mzima?

    Swali vichwani mwao halikuwa hilo tu ikiwa wale waliokuwa wanawakimbiza ni AGFT na hawa waliotukamata ni kinanani na wanalengo gani?

    Yakabaki ni maswali bila majibu mbele ya watekaji wao.........



    "Hampaswi kujiuliza mara nyingi,labda niwaambie hatupendezwi na unyanyasaji wa watu eneo hili,tunautaka uhuru wetu,dakika chache zilizopita nadhani mmeona vifo vya wakazi wa kijiji kile,wale ni waasi lakini hawapiganii haki ya raia,wanapigana kwa kutumika tu na faida ya matumbo yao,sisi ndio tunapigana kwa haki za wanyonge hapa Goma.Lakini hatuna silaha na hatuna ujuzi wa kutosha kutoka kwa maaskari wetu,pia ni wachache sisi, basi kama hamtojali tunaomba muungane na sisi katika ukombozi wa watu wetu,"

    Kiongozi yule akawatazama tena mateka wake,kisha bila kusema neno akasimama na kutaka kuondoka,Koplo Makame akamzuia kisha akamuuliza alijuaje kuwa mwenzao bado yu hai ilihali wao waliona kifo chake machoni mwao,"



    Kiongozi yule akageuka na kuwatazama makomando wale kisha akawaambia,yeye anaitwa Kimbu alikuwa ni mpiganaji wa kikundi cha AGFT,lakini hakupendezwa na yanayoendelea kule,kuua watu badala ya kutetea,pia wamekuwa ni watekaji wa migodi mikubwa na kisafarisha madini wanayoyapata kwa watu wa magharibi,hapo ndipo aliamua kuwa muasi ndani ya jeshi la waasi,Kimbu akaamua kutengeneza kikosi chake cha La people Front(LPF),ila muda wote hajawahi kupigana na was so wale AGFT kwa sababu ya nguvu ndogo walizonazo,pia akawaambia wakubaliane nae yeah yeye atajua jinsi ya kuwasafirisha kurudi Tanzania,pia aliwaahidi kuwapa siri nzito kuhusu matukio yalionyuma ya mpango wa kumkomboa Ibra Mbaya aliekuwa mpiganji wa Loraa Nkunda huku akiwa ndie mlinzi mkuu wa muasi yule alieigana na kujipatia umaarufu miaka ya tisini kwenye mipaka ya Kongo,Rwanda,Burundi hadi uganda.

    Na hapo makoplo wale ndipo waliona walivyokuwa gizani kwenda kumkomboa muasi yule kumpeleka nchini mwao,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakaona kuna tatizo Tanzania,wanapaswa kufanya wawezalo kukomesha yajayo wasio yajua,na watazuia vipi ikiwa wako nchi ya watu,lakini swali kubwa lilibaki kwanini wakubwa wao waliwatuma kumkomboa Ibrahim Mbaya,na kwanini waliopelekwa kwenye mpango huo walitolewa sehemu tofauti tofauti huku wakipewa oda Hakuna kutambuana majina wala vikosi walivyotoka,si Koplo Ziga au Koplo Makame aliekuwa na imani na jeshi la nchini Tanzania,japo waliamini mpango si wa wote,ni wachache miongoni mwao,hawakuwa na namna ilibidi wakubali kutumika ili wajue watatokaje nchini Congo ili waje kukabiliana na Ibrahim Mbaya.



    *********



    Alipotoka nyumbani kwa Dr kije alikata shauri kwenda mkoani singida,eneo yalipotokea mauji ya kepteni Shayo na Luteni Koba,alipita Gapco petro station akajaza mafuta gari lake,kisha akaianza safari huku akiamini adui zake walioanza kuihisi harufu yake wametega njia ya Dar es laam ili wamnase,hapo akaikumbuka sura ya Deepaklpa akatabasamu huku akijiambia Duniani kuna watu wabaya hata Harmorapa yuko sura nzuri,akakoleza mafuta wakati akizidi kuuacha mji kasoro bahari ukiomboleza kifo cha Dr Kije.



    Wakati Zedi akitimka kuelekea Singida Deepaklipa yeye alikuwa kawekwa kitimoto na kundi la watu zaidi ya sita wakiwa wanamlaum uzembe aliofanya kumwacha adui yake akiwa hai,.



    Kiongozi wa lawama zile hakuwa mwingine zaidi ya Ibra Mbaya,hakuishia tu kulaumu isipokuwa kutoa onyo kwa vijana wote aliokabidhiwa katika mpango huo uliopewa jina mpango Tikisa.

    Hakuna kurudi nyuma ukifeli ni bora ufe kuliko kurudi kwenye timu Tikisa,.



    Baada ya kupeana vitisho vya hapa na pale Ibra akatoa majina ya watu watatu wanao stahili kufa maana wao ndio kikwazo,iwapo wasipowazima mapema,walikuwa wanne ila tayari mmoja tayari ashauwawa kisomi na Zegera,.

    Vijana walisamabaratika huku wakielekeza nguvu kumtafuta Zedi ambae waliamini ashanusa harufu ya yajayo,.



    ********

    Nchi nzima ilizizima kwa kifo cha waziri wa Afya bwana Makaya Changulu alieuwa kwa kupigwa risasi ya kichwa,akiwa katikati ya mkutano wa ufunguzi wa Zahanati ya Mbezi,vyombo vya usalama viliahidi kufuatilia hatua kwa hatua juu ya hilo na wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria,



    Taarifa hii Zedi aliisikia akiwa anaukaribia mji wa Dodoma,kilichomvutia katika taarifa hii ni kule kusikia alishambuliwa na mtu inaesadikika ni mdunguaji,hakutaka kujipa maswali,akatia gari moto na kuinusa Dodoma.



    Alipofika Dodoma,akaamua kuvuta muda kwa kupita kwenye mgahawa wa Chef Asili ili kujipatia staftahi.

    Mgahawa huu ulijaa watu jioni hiyo,nae akajiunga nao akatafuta meza iliokuwa haina watu akakaa hapo punde mhudumu alievalia nadhifu akajongea mahali pale na kumsikiliza,alipokwisha kusikilizwa akaona huu ndio wasaa wa kukipitia kitabu kile cha Dr Kije,.

    Alioyakuta humo yakampa mwanga angalau wa kilichotokea siku hiyo.....



    Alisoma tena maelezo ya kitabibu yaliokuwa yameandikwa kwenye kijitabu kile cha Dr Kije,ambapo yalieleza ugunduzi katika miili ile,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alifunua kurasa kadhaa kwenye kijitabu kile,akavutiwa na kurasa moja iliokuwa imeandikwa kwa kirefu zaidi,ilijiieleza kuwa,dereva wa gari lile la kijeshi alishambuliwa na mtu aliekuwa amesimama mbele au alijibanza mahali ambapo ilikuwa rahisi kuwaona wakati wakija.

    Kwenye mabano paliwekwa neno(mdunguaji).

    Kijitabu kile kiliaendelea kueleza kuwa,kulingana na vipimo kutoka kwenye mwili wa dereva yule,risasi ilitoka kwenye bunduki iliokuwa umbali wa mita sabini au sitini ndio maana mgandamizo ulikuwa mkubwa wakati risasi ikitokea upande wa nyuma,pia Kepteni shayo kifo kimemkuta akiwa nje ya gari maana hakuwa na majeraha makubwa ya kuunguzwa na moto uliolipuwa lile gari lao,lakini hata risasi zilizompata zilipigwa na mtu aliekuwa hatua mbili au moja kutoka usawa wa mwili wake.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog