Search This Blog

Friday, 20 May 2022

KIKOSI CHA PILI - 2

 







    Simulizi : Kikosi Cha Pili

    Sehemu Ya Pili (2)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zedi alikifunga kijitabu kile,kisha akasimama na kuondoka eneo lile la Chefu Asili na kuikamata barabara ya Singida.



    Mida ya saa kumi na mbili jioni ilimkuta eneo la pori yalipotokea mauji yale ya wanajeshi,kisha kama yeye ndie mlengwa akageuza gari likawa kama linatoka Tabora kwenda Manyoni akasimama eneo lililoonesha ulipo mchoro wa polisi kuonesha ndipo tukio lilipotokea,kisha akatazama mbele hatua hamsini akauona mti mrefu kiasi,akapitisha shauri ndo mti alipokaa mdunguaji,

    Akajiuliza kwanini alitumika mdunguaji,ilihali walikuwa na RPG?

    Akafikiri kidogo kisha jibu likaja ilikuwa ni kurahisisha kazi ili dereva asiweze ona aliposimama mtu alilipuwa lile gari,kwa kuwa ni mwanajeshi kama Angeliona alikuwa na uwezo wa kutumia maarifa kukwepa na hapo walengwa wangejiokoa.



    Akiwa bado ndani ya gari akatafakari kama aliepigwa risasi ni dereva gali lilikosa uelekeo,nae akawasha gari na kuyumbisha kidogo kisha akasimama,hapo akatazama mbele,kushoto akakadiria alipokuwa kasimama alieshika RPG,



    Akashuka akapiga hatua Hulu akizihesabu,akafika hadi eneo lenye makisio,akatazama juu akaona uwezekano wa mtu kukaa hapo,akalikagua eneo hilo vizuri kabisa,kwa mbali akaona ganda la risasi,akaliokota na kulitia mfukoni,akaangaza angaza tena eneo hilo,hakuona cha maana akapiga hatua kwenda eneo lile alilohisi mshika RPG alikuwa amesimama,alipofika hapo akapachunguza kwa makini akauona mburuzo kama kumepitika na watu,akaufuata mburuzo ule.



    Mburuzo ukampeleka hadi eneo kulikokuwa na makazi ya watu,nyumba nzuri japo zilionesha zimekosa matunzo kwa muda mrefu,.Haikumchukua muda kugundua yalikuwa ni makazi ya wachina wakati wa ukarabati barabara ile,huku macho yake yakiangaza kama paka mwizi hakukawia kuona kivuli cha mtu kikijaribu kumtazama kutoka moja ya nyumba zile,hapo Mwili wake ukasisimka,akahisi kuna jambo hapo,akazidi kujongea kwenye nyumba zile,punde akajikuta akitazamana na milango kadhaa huku hali ikionesha ni makazi yalioachwa muda mrefu bila wakazi,.



    Aliuendea mlango mmoja na kuusukuma kisha akaingia ndani ajabu alikutana mandhari safi kuashiria kunaishi watu au mtu,na chini palikuwa na vipisi vya sigara kuashiria palikaliwa na mtu anaependa kuvuta sigara.



    Akageuka ili atoke akakutana na mitutu miwili ya bastola ikimtazama huku walioshika wakionekana hawana masihara Kia ujanja wowote ambao angelijaribu kuufanya.



    Mmoja kati ya watu wale alimuamuru Zedi atoke nje nae akafuata kabla hata hajapiga hatua tatu akajikuta yuko chini na kiza kikitanda usoni pake......

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ilikuwa ni siku ya tatu tangu waanze mazoezi na vijana wake Kimbu,

    Kama ungeliwatizama ungehisi ni zaidi ya miezi wamekuwa wakijifunza msituni mle,vijana walikuwa na ari ya kupokea mafunzo kutoka kwa makomando wa kitanzania waliokubuhu katika fani hiyo,



    Vijana yapata thelathini walikuwa wako makini kuipanda milima na kushuka huku wakifanya kila alichokifanya koplo Makame,walibeba vitu vizito na kupanda navyo milimani,kisha walishuka navyo,ilipendeza kuwatizama,



    Walipokwisha maliza mazoezi ya ukakamavu wakapokelewa na koplo Ziga aliewapa mazoezi ya kukabiliana na adui bila silaha,.



    Ilikuwa ni heka heka ndani ya misitu ya Goma,hakuna kulala ni kupumzika masaa machache na kuendelea na mazoezi,.



    Wakati Koplo Ziga na Koplo Makame wakiwafunza weledi waasi wa kikosi cha La People Front upande wa pili koplo Mwita au 01 kama alivyotambulika alikuwa katikati ya mateso makali hii ni baada ya kutibiwa majeraha ya risasi kisha akapata nafuu kidogo,

    Vipigo viliendelea bila huruma,kwa muda alikuwa hoi damu zilimtapakaa kila mahali.



    Haya yote yalikuwa yakitazamwa na Zeso muasi asiekuwa na huruma hata kidogo,lengo lake alitaka aambiwe ni nani aliwatuma kumkomboa Ibra Mbaya mshirika wa Loraa Nkunda,.



    Kila alipoulizwa hakuwa na jibu la kuwapa,alikuwa ni kama bubu,ila kiukweli komando huyu mbali ya mafunzo ya kuhimili mateso ya kila aina kuwa nayo lakini hakuwa anajua hadi muda huo Ibra mbaya na K3 au luteni Zegera wako wapi na kwanini walimsaliti pia hakujua wenzie walipo,.

    Hata angeliteswa vipi hakuwa na ukweli wowote zaidi ya kujua walitumwa na serikali ya Tanzania kumkomboa Ibra Mbaya.



    Baada ya kuona mbinu zake hazizai matunda,Zeso aliamuru wasitishe mateso kwa koplo Mwita na arudishwe kwenye mahabusu yao ndani ya ngome ya waasi hao wa AGFT.



    Kumfundisha muasi mbinu za mapigano za hali ya juu ni sawa na mtu anae beti,kuna kukosa na kupata na mtu anaebeti anauwezekano mkubwa wa kukosa kuliko kupata kwa hiyo wao wakati huo walikuwa wanabeti kwa waasi wale ambao kiuhalisia hawajui upande halisi waliopo ni upi,



    Waliendelea kushauriana wakati wakipata chakula cha usiku pembeni kidogo ya kambi yao,alikuwa ni koplo Ziga aliefikisha wazo hilo kwa koplo Makame.

    Koplo Makame nae akaunga mkono kisha wakashauriana kufanya jambo moja nalo ni kuwafundisha waasi wale hadi ngazi ya kuwa kama askari wa jeshi la wananchi na si kufikia kiwango cha ukomando.



    Wakamaliza kula chakula wakamwita Kimbu mkuu wa LPF, wakamweleza wanahitaji kujua japo kidogo kuhusu kusalitiwa kwao na ilikuwaje waasi wale wa AGFT waliweza kukaa na Ibra Mbaya nae alijuaje watakuja kumwokoa ilihali wao walikuwa hawajui wanakuja kumwokoa nani.



    Akawatazama kisha akawaambia yeye hana taarifa nzuri za kuwahusu isipokuwa taarifa zao atakuwa nazo mtu mmoja maarufu sana kwa jina la Papaa Deo Mukamba nae anaishi katikati ya Goma mjini karibu kabisa na kituo cha kuoshea magari ya wafaransa,Mtaa wa Haidu nyumba namba 24 kushoto mwa barabara ya Nyerere.



    Baada ya taarifa hizo wakaahidi kumfikia huyo mtu wapatapo nafasi ila ni kwa kuwa hawakumjua Papaa Deo Mukamba ni nani.



    ***************

    Alistuka dakika chache baada ya kupoteza fahamu,na ni baada ya kumwagiwa maji ya baridi,alijikuta kafungwa kwenye kiti na kamba ngumu ya katani,akapepesa macho pembeni yake kulikuwa na mtu mwingine nae alikuwa amefungwa kamba kama yeye tofauti yao ni kuwa yule mtu alionekana kupitia mateso makali ndani ya muda mfupi uliopita.



    Alipokwisha kumtathimini yule mateka mwenzie akahamishia macho kwa mabwana wawili waliokuwa wamesimama mbele yake huku mmoja akiwa ameshika fimbo kama zile zitumikazo kwenye mchezo wa gofu,na mmoja alikua imara na bastola mkononi huku akimtizama Zedi kwa uchu wa kufanya lolote.



    Yule alieshika fimbo alimsogelea Zedi kisha akamuuliza

    " wewe ni nani na unafanya nini hapa"

    Zedi akamtazama kisha akamjibu

    "labda nikuulize wewe na kwanini umeniteka raia kama mimi"

    Mtu yule aliekuwa amejazia vizuri kimazoezi kama wacheza rugby alimtizama kwa jicho la hasira na kumzaba kofi kali usoni lililompelekea Zedi kuziona nyota za anga zipo ardhini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati bwana yule akishika fimbo yake vizuri kwa ajili ya kumuadhibu Zedi simu yake ikaita,akaitoa mfukoni na kupokea kisha kusikiliza maongezi upande wa pili,.

    Alipokwisha kusikiliza akageuka upande wa pili alipo mwenzie na kuteta nae jambo na kisha wakaanza kumwendea Zedi,Ila hawakumfikia lilitokea tukio ambalo hawakulitegemea na wakabaki vinywa wazi kila mmoja akishangaa.......





    Kosa moja walilolifanya watekaji wale,nikumwacha Zedi na nguo zake,na mara nyingi alipenda kuvaa shati la mikono mirefu ambalo hutumia kuhifadhi visu vyake vidogo,ni wakati alipokuwa akimtizama yule mtu aliepokea simu nae akafanya hila kwenye mikono iliofungwa kisu kidogo kikateleza kutoka kwenye shati lile kikadondoka kwenye kiganja moja wapo,haikuwa ngumu kukata kamba ya katani na alipokwisha kumaliza ndipo wale mabwana wakawa wakimfuata kwa gadhabu nao wakashuhidia mateka wao akisimima wima kitendo bila kusubiri akatawanya miguu yake hewani na kuwapata watekaji wale,wakati wakidondoka kila mmoja kivyake,yeye akawahi kuikota bastola iliokuwa imedondoka upande mwingine na kitendo bila kusubiri akaachia risasi mbili zilizoenda kumtupa yule mtu alimpiga kofi kisha akamwelekezea yule aliekuwa ameishika hiyo bastola ilioko mikononi mwake nae akagwaya akabaki anamtizama mwanaume Zedi.



    Zedi kwa mbwembwe akamsogelea yule mtu kisha akaishusha bastola na kuitupa pembeni akamwonyesha ishara yule mtu anahitaji mapambano ya mkono kwa mkono,yule bwana nae akaafiki akajipanga katika mtindo uliovutia akimaanisha na yeye si haba katika fani hiyo,akamtazama Zedi aliekuwa amesimama hatua kadhaa kutoka kwake,akamwendea kwa pupa akakutana na hewa kwa wepesi wa mbinyo wa jicho akageuka na kurusha teke lenye uzani wa kilo kumi ila lilipangulia kiustadi na Zedi,kisha bila kusubiri akauvuta ule mguu kumfuata alipo kisha yeye zedi akawa kama anapishana nao akarudi kumkumba yule bwana kwa kutumia kiwiko,yule bwana akajaribu kukika lile pigo likawa kosa akakutana na mapigo mengine ya haraka yaliompeleka chini,huku yakimwacha Zedi akiwa amesimama imara akimngojea asimame,kwa maumivu makali na kwa kujizoa zoa alisimama akajipanga ila hakumaliza kujipanga mateke matatu ya uzani wa kilogram kadhaa yakatua katika mwili wake akayumba na kuanguka chini kisha akajikuta akikabwa na mikono imara ya mwanaume anaekula dona au ugali wa mtama Zedi.



    Zedi akamtandika makofi mawili kisha akamuuliza wako pale kwa nini,yule bwana hakujibu zaidi ya kutabasamu tabasamu la kukera machoni kwa Zedi.

    Zedi hakutaka kupoteza akampa kipigo cha sema unalolijua, nae yule bwana akazungumza kiswahili cha Kiha,kwamba yeye hajui la kichwa wala miguu zaidi alitumwa tu kulinda yeyote atakae fika hapo ni halali yake,na aliempa hiyo tenda akamtaja kwa jina la Masunga,.



    Zedi aliipoona yule bwana hana analolijua akaamua kumpeleka kwa mungu akajibu tuhuma zake za kufanya uhalifu,kisha akasimama na kumwendea mateka yule alikuwa bado kafungwa kwenye kiti huku akiwa anatizama yote yale,akamfuata na kumfungua kisha akamkokota na kwenda nae sehemu alioacha gari lake,akamsaidia kumwingiza ndani ya gari kisha akamuuliza

    " Hujabakwa na wale vilaza?" yule binti aliekuwa ametekwa akatikisa kichwa kukataa na bila maelezo mengi Zedi akalitia moto gari likaanza kulikata pori la Chaya kuitafuta Manyoni.



    Masunga alipagaishwa na taarifa za kuonekana mwanaume amefika kwenye eneo lile huku tayari akiwa na taarifa za kutekwa kwa mwanamke ambae alikuwa eneo lile mwanamke yule baada ya kufuatilia habari zake hawakukawia kujua ni kutoka katika idara ya usalama Ikulu,aliekwenda kwa jina la Sajini Mina,mwanamke mwenye weledi katika ushushu,kilichompagawisha zaidi ni baada ya kupokea taarifa kuwa vijana waliwekwa pale wamepoteza uhai huku si Sajini Mina au mwanaume yule alifahamika aliko,kibaya zaidi mwanaume yule kimwonekano ni sawa na yule alieoonekana Morogoro,

    Hakukubali kulifumbia macho akatoa taarifa kwa kiongozi wake Ibra Mbaya,Ibra nae akafikisha taarifa anakokujua punde taarifa zakamrudia Masunga,yule mwanaume ni komando Zedi Wimba aliekataa jeshi na kuamua kuishi kitaa,kisha akapewa mikakati ya kumpata Zedi akaingia kazini kwa miguu yote.



    ******

    Kufikishiwa taarifa ya kuwa Zedi yupo mtaani kutafuta ukweli kukampa mashaka Luteni Zegera,akaona hila zao hazitazaa matunda wala wayatarajiayo yanaeza yasifanikiwe hapo akaomba kukutana na wakuu wa mpango Tikisa,akiwemo mnadhimu mkuu wa jeshi,kikao kikakaliwa huku hoja ni vipi wataeza zimisha juhudi za Zedi Wimba,kibaya zaidi itakuwa Ikulu imeshanusa ubaya ndio maana alitumwa Sajini Mina,ila Zegera akatoa wazo na hilo wazo likatekelezwa kwa kuwa mmoja ya vinara wa mpango Tikisa alikuwepo pia,



    Ilikuwa kama utani ila ndivyo ilikuwa usiku huo ambao Zedi na Mina wako njiani kurudi Dar,tayari Dar kulishasambaa taarifa ya kutajwa kwa mhusika wa mauji yale ya wanajeshi watatu,vyombo vyote vya ulinzi na usalama vikawa chonjo usiku huo na taarifa ikafika ya kuwa mlengwa yupo njiani kufika Dar,wakatumwa wanajeshi kikosi kazi kuweka kizuizi njiani si jeshi tu hata polisi nao walikuwa kwenye magari yao wakiweka ulinzi kwenye kila uchochoro wa kupita gari,usiku huo ukageuka kuwa usiku Tikisa mikoa mitatu morogoro,dodoma na Dar,huku madereva taxi wakipata adha ya kupekuliwa kila dakika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****.......



    Akiwa anaiacha manyoni anaitafuta Bahi,ndipo simu yake ilipoita,akaitoa kisha akaiweka sikioni na kusikiliza maelezo ya mtu upande wa pili,kisha alipokwisha kusikia ya mpigaji akairudisha simu mfukoni mwake kisha akamgeukia mwanadada aleikuwa amekaa upande wa pili wa dereva.



    Hawakuwa wamezungumza chochote tangu walipotoka Chaya,sasa ni wakati Zedi alioamua kumuuliza mwanamke aliemuokoa yeye ni nani na kwanini alitekwa,.Mwanamke yule hakumjibu Zedi alikaa kimya,Zedi akaamua kukaa kimya na yeye pasipo kuongea.Japo alihisi yule mdada aeza kuwa askari ila akaamua kukaa kimya tu pasipo kusema kitu huku akili yake ikifanya kazi mara mbili zaidi ya uwezo wake,kikubwa aliwaza taarifa aliopokea ya kuwa msako umeanza wa kumtafuta kama mtuhumiwa wa kwanza wa mauji yanayoendelea.



    Waliipita Bahi,hatua kadhaa mbele Zedi akakiona kituo cha kujazia mafuta cha princess Muro na Mabasi kadhaa yakiwa yamepaki huku watu wakijipatia chakula kwenye mgahawa ulioko hapo.

    Nae akakunja gari na kwenda hapo kituoni akajaza mafuta kisha akamwambia yule mwanadada ni wakati wa kusambaratika,hataki kuzungumza basi itambidi ampandishe kwenye basi mojawapo ili waachane salama.

    Yule mwanamke akamtazama Zedi kisha akamwambia yeye anaitwa Sajini Mina,mengine watatambuana wakija kukutana huko mbele ya safari maana anaona wanatembelea mbuga moja,kisha pasipo kusubiri akateremka na kufuata moja ya mabasi yale,ila kabla hajafika mbali Zedi akamwita nae akarudi Zedi akatoa noti kadhaa za kitanzania na kumkabidhi kama nauli ndani ya basi.



    Alifanya hivi kwa kuwa Meja Salim Komba alimpigia simu na kumueleza yanayoendelea juu yake,hivyo hakuona sababu ya kuhatarisha maisha ya mrembo yule.

    Akalitia gari mafuta na kuitafuta Dodoma.



    Ni wakati akiwa kilomita tano kabla hajaufikia mzani wa Nala,akaona mbele kuna magari machache yameweka foleni njiani,hakukawia kujua sasa amekamatika,punde na yeye akajikuta yupo kwenye foleni ile.huku kwa kutumia mwanga wa taa za magari ya mbele akaona maaskari polisi wakikagua gari moja baada ya jingine.



    Akateremka ndani ya gari lake,kisha kama anaeenda haja akachepuka upande wa pili kulikokuwa na kipori,akaambaa nacho hadi sehemu kulipokuwa na kimlima kidogo na hapo akapata kuona magari kama matatu ya askari polisi,akafikiria cha kufanya akajipekuwa mfukoni akakutana kifaa kidogo cha kuhifadhia milipuko ya dharura ambayo lengo ni kumpoteza adui uelekeo,akainama kidogo chini akakutana na jiwe,akapiga hesabu zake pale gizani,lengo ni kuwachanganya maaskari wale ili apate njia rahisi ya kuchomoka pale,akachimba kidogo chini ya jiwe na kukitega kibomu kile akiamini ndani ya dakika mbili kitatoa mlipuko mkubwa kutokana na mkandamizo ule wa jiwe,.



    Ili kuwavuruga zaidi ikabidi atoe bastola yake akaondoa kiwambo cha kuzuia sauti kisha akapiga risasi kule walipo maaskari wale,na kwa kasi ya mionzi akapotea eneo lile huku akiwaacha maaskari polisi wale wakihaha kujua risasi imetoka kwa nani na ememdhuru nani. Wakati wao wakiwaza vita ukatokea mlipuko mkubwa eneo lile polisi baadhi wakaanza kupiga hovyo risasi huku wengine wakikimbia hovyo eneo lile,si polisi tu hata madereva wa malori waliokuwa wametii kukaguliwa hawakupenda kifo aliekuwa mbele akaanzisha safari kwa kiroho,wa nyuma nae akafuata,ikawa ni mtibuano barabarani.



    Zedi nae akaunga pale pale nyuma ya yale magari,polisi hawakuwa na kuzuia magari ikiwa wao hawajui hatima ya uhai wao,.



    Zedi ilikuwa ni lazima afanye jambo kuwakwepa polisi au wanajeshi ambao ni lazima wangelikuwa na taarifa ya kilichotokea,kwa hiyo umakini ungehitajika kwenye upekuzi wao akaona isiwe tabu akachukua simu yake na kuwasha data kisha akaingia ilipo ramani ya kimtandao akaona eneo alipo ila upande wa magaribi yake hatua chache kuna njia inayochomoza kupita kipori flani cha makutupora,kisha atatokea mundemu na hapo atapata barabara itakayomfikisha mzakwe,kisha ataipita kambi ya jeshi makutopora inamaana atarudi Dodoma mjini na hapo atajua cha kufanya,hakutaka kungoja safari ikaanza.

    ***********

    Katikati ya misitu ya Goma,mazoezi yaliendelea kwa weledi wa hali ya juu,vijana wapatao arobaini walikuwa wanazidi kuiva ndani ya muda mfupi,koplo Makame na Koplo Ziga walikuwa wamesaidia kuwapa ujasiri vijana wale wa kikongo,kilichokuwa kimebaki ni kutumia uchache wao kuleta mapinduzi kwa kundi lingine la waasi wa AGFT,lakini tatizo likawa silaha walikuwa nazo tano tu na hazikuwa na ubora wowote,pia walikuwa na nguvu kidogo.



    Kimbu kiongozi wa LPF akatoa wazo la kuongeza nguvu kutoka kwa vijana walio kijiji cha jirani na wao,hilo likatekelezwa na vijana yapata mia moja wakaletwa mbele ya Koplo Makame na Koplo Ziga mazoezi yakaendelea,.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waasi wa AGFT kila ilipokuwa ikifika mwisho wa mwezi ni lazima silaha ziletwe kutoka sehemu wanayoijua wao na kwa kuwa kutoka goma kwenda goba hamna barabara iliwalazimu kupokea silaha katikakati ya mji wa Goma kisha kuzisafirisha kupitia misitu ya Goma wakitumia mto Kivu kuvuka kwenda Goba ilipo kambi yao,hayo yalisemwa na Kimbu kiongozi wa Lpf.Kisha ikawekwa ramani mbele ya makomando wa kitanzania wakaisoma na wakaona mahali pa kuzichukulia silaha zile ni mto kivu kwa weledi wa mapigano ya kuvizia napo wakachagua vijana kama kumi akiwemo na Kimbu wakaanza kupewa mazoezi ya kikomando ili iwe rahisi kuwavamia waasi wake Zeso.



    Papaa Deo Mukamba alikuwa na kikao na watu watatu ila mmoja kati yao alikuwa ni mzungu,kikao chao kilikaliwa nyumbani kwake Papaa.

    "Tunajaribu Tanzania maana wao wanamali nyingi Sana ila hazifaidishi watu isipokuwa zinafaidisha serikali tena kwa kiasi kidogo,mipango inakwenda sawa na tayari mbabe wa mafunzo na mapambano Ibra Mbaya yupo huko na anapata sapoti kubwa kutoka kwa maafisa wa jeshi ambao wao watautumia mpango huu kumpindua rais kisha wajimilikishe wao madaraka na faida tugawane"

    Hiyo ilikuwa ni hoja ya mmoja wa wajumbe katika kikao kile,akadakia mwingine

    "japo tunamatumaini na kuitikisa Tanzania lakini hata majaribio ya ile sumu yafanyike huko huko ili kuwavuruga zaidi"

    Hapo akadakia mzungu yule

    "Silaha tayari zipo njiani kufika Tanzania zinapotia Zanzibar kisha zinatua mikononi mwa mbwa mwitu"

    Papaa nae akazungumza

    "yote yanafanyika lakini kuna baadhi ya vijana wao wawili wamepotelea hapa na haijulikani walipo na mmoja yupo mikononi kwa Zeso,Zeso anapenda pesa akigundua mpango wetu basi atatutisha ili apate pesa lakini kikubwa huyo komando aliemikononi mwa Zeso pia si kuamini sana anaeza..."



    Papaa hakumaliza kauli yake kikao kikapata ugeni,ugeni wa dharura ugeni ambao hawakuutarajia...



    Ni mbalamwezi tu iliokuwa inatoa mwanga katika eneo hilo,na kwa mbali sauti za ndege na wadudu wausiku walikuwa wanapiga kelele,.

    Milio yao haikuwa kikwazo kwa watu kumi na mbili kuzunguka pembe tofauti za mto kivu huku ishara yao pekee ikiwa ni mluzi hafafifu kutoka kwa viongozi walioongoza kikundi hicho cha kiasi.

    Waligawanya makundi matatu ya watu wanne wanne.

    Kimbu alikaa upande wa mashariki mwa mto ule ili yeye ashambulie watakao kuwa wakitoka upande huo ambapo kimsingi ndipo yalikuwa mavukio ya waasi wa AGFT,.

    Koplo Makame alikaa magharibi mwa mto kivu hii ikimaanisha hakuna waasi kutorokea upande wowote huku koplo Ziga yeye alikaa nyuma kabisa ya njia waliongilia wao kulinda endapo kungekuwa na mashambulizi kutoka upande wa goma,kifupi kama watalaamu wa Geospitial wangelifanya kazi yao basi wangebaini watu wale walikuwa wametengeneza pembe tatu huku eye point yao ikiwa utofauti wa nyuzi thelathini na mbili kwa kila moja ili kuifikia misheni hivyo kitalaamu kungekuwa na hatua si chini ya hamsini ili kuifikia tageti yao.



    Kamanda Lubengo alikuwa na vijana kama ishirini na tano waliokuwa wamebeba silaha walizotoka kuzipokea katikati ya mji wa Goba usiku ule,ni silaha nzuri za kivita huku kukiwa na makombora ya kutupa kwa mkono na shehena ya risasi za smg.



    Ulinzi wa mali ile uliimarishwa na vijana watano,wawili walikaa nyuma ya gari la mwisho huku mitutu yao ikielekea nyuma kuhakikisha hakuna atakae sogea au kuhatarisha usalama wa mali yao,mbele kulikuwa na gari pia iliokuwa imebebelea askari watatu wa kihasi waliokuwa wameshika silaha nzito aina ya LMG(light machine gun)au watalaamu katika medani za kivita huita silaha ya msaada.

    Katikakati ya hizo gari mbili kulikuwa na lori kubwa lililo kuwa limefunikwa kwa juu huku upande mbele kushoto mwa dereva alikaa kamanda Lubengo na nyuma kulikokuwa na shehena ya silaha walikaa vijana yapata kumi na Saba kulinda silaha zao na wakiwa tayari kwa lolote.



    Walizidi kulikaribia eneo la kivuko cha mto kivu.Na walipofika gari ya mbele ikawasha taa mara mbili kisha magari yote ya kazimwa taa injini zake kukawa kimya kabisa hakuna mwanajeshi wa AGFT alieshuka wala kuongea.



    Ishara ya taa kuwaka na kuzimwa kisha kufuatiwa na ukimya ilikuwa ni ishara ya kwa pande mbili tofauti.

    Upande wa koplo makame na wenzie ilikuwa ni ishara ya kuendelea jambo jingine ambalo wao walipaswa kuwa na subira kulisubiri.

    Lakini upande wa AGFT kuona taa zile kuliashiria mambo ni shwari kunapaswa kuvusha mitumbwi kupokea mizigo pamoja na kuvusha wapiganaji wenzao.

    Mitumbwi mitatu ikiwa na askari watatu watatu ikaanza kujongea eneo lile zilikopaki gari,.

    Waliokwenye gari nao walipoona mitumbwi ile ikisogea wakashuka na kuwapa ishara vijana walioko kwenye lori nao wakashuka.



    Yote yale yalionwa na macho ya watu kumi na mbili ambao kila kikosi kilikuwa na bunduki mbili tu kiujumla zinakuwa sita pekee,huku tumaini lao likiwa ni mikono na visu vyao ilihitajika akili na weledi wa hali ya juu kuwavamia waasi wale wenye silaha kali za kila aina.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kilianza kikosi cha Koplo makame kwa kujiamini kabisa akaanza kutambaa kama nyoka huku nyuma akifuatiwa na vijana watatu waliokuwa wakimfuata kwa nyuma,akaambaaambaa na ukingo wa mto hadi alipofika ilipokuwa mitumbwi ya waasi wale,akaachana nayo hadi usawa wa liliposimama gari la waasi wale likiwa kijana mmoja tu aliekuwa kaishika LMG,akiwa hana tahadhari yoyote na kwa wepesi wa karatasi koplo makame akakitupa kisu chake kwa ustadi wa hali ya juu kikaenda kukita mgongoni mwa muhasi yule ambae hakuomba hata maji akadondoka chini huku silaha yake ikidondokea mikononi mwa Koplo makame,.



    Ilikuwa kama utani ila ndivyo ilikuwa,kamanda Lubenga alishuhudia kikosi cha watu wanne wakichomoza kutoka kwenye vichaka vilivyo karibu na mto ule,ni wakati akipiga kelele ya tahadhari akashuhidia jambo asilolisahau

    Bunduki iliokuwa mikononi mwa kijana wake inatua mikononi kwa mtu asiemjua na kwa wepesi wa hali ya juu risasi zikaanza kutoka kwa mpangilio safi kabisa huku ikienda na mpiganaji wake mmoja mmoja bila hata kuagwa na vijana hao,.

    Hakuwa tu yule fundi wa kutumia bunduki ile kubwa inayohitaji kishikizio na Msaada wa mtu pembeni ili ifanye kazi sasa aliiona ikiwa imeshikwa na mtu mmoja tu tena kwa mkono mmoja huku mwingine ukiwa umeshika mkanda wa risasi,lakini pia aliona vijana watatu nyuma yake wakirusha ngumi na mateke huku wakikwepa risasi kwa weledi wa hali ya juu na kuwanyofoa shingo vijana wake walio mtii.



    Kamanda Lubenga akashuka haraka ndani ya gari ili akimbilie nyuma ya lori lile alikoamini atakuta vijana wengine wajipange kulipa mashambulizi huko mbele,hakuamini macho yake pale alipoona kundi lingine la watu wanne likiwachakaza kwa mapigo ya ajabu kabisa vijana wake waliokuwa wakilinda nyuma,huku mmoja wa watu wale akipiga mapigo ya kushangaza ulimwengu na kwa wepesi wa hali ya juu.

    Alikuwa ni koplo Ziga mbabe katika mapigano ya ana kwa ana akiwa na vijana watatu walikuwa wakifanya yao.

    Kamanda Lubenga alikuwa fundi wa ngumi ila kwa mtazamo tu aliona mwanaume yule sio saizi yake,akaona akizubaa atazikwa kwa wepesi wa nzi kukimbia kidonda akachumpa na kudondokea kichakani na kutokomea.

    Kukimbia kwake Ziga aliona ila hakuwa na muda wa kumfuata akaachana nae.



    Ilikuwa ni ndani ya dakika tatu tu kazi ikawa imeisha vijana wote walikuwa salama,ni maumivu ya hapa na pale kwa vijana wale.

    koplo Makame alipoona kuko shwari akapiga mluzi kama ishara kwa Kimbu na vijana wake watatu kuwa muda wa kuondoka umefika kama wako salama na upande wao kuko shwari.



    Kimbu ndie alikuwa dereva sasa wa lori lile ikiwa ni mali yake huku nyuma kwenye gari dogo alikuwapo mtalaam wa bunduki koplo Makame,na mbele alikuwepo koplo Ziga wakirudisha ushindi kwao huku majonzi yakienda kwa Zeso mnyama wa msitu....



    Wakati vikosi vya askari polisi vikizidi kuweka ulinzi sehemu mbalimbali ili kuhakikisha Zedi Wimba anaingia mikononi mwao,ni wakati huhuo Zedi alikuwa kawapiga chenga ya akili na mwili,.



    Baada ya kuchepuka na kuwatoroka askari lengo lake lilifanikiwa na akajikuta yupo Dodoma mjini,pasipo kusubiri akapaki gari lake kwenye gereji ya champion kisha akachukua daladala hadi uwanja wa ndege wa Dodoma,hapo akajitbulisha kwa jina la Zamoyoni akaomba ndege binafsi,akalipia pesa iliohitajika na baada ya utaratibu kukamilika akapaa mwewe kwenda Dar kufanya alioyajua.

    *****

    Kikao kilikaliwa eneo tofauti na lile la mwanzo,huku mwenyekiti wa kikao kile akiwa mwingi wa wasiwasi na sura ya kupungua morali,akawatazama tena kisha akanena.

    "Zedi kaingia zoezini"akaiacha kauli yake ikiambaa kwa wajumbe wake kisha akaendelea

    "Zedi hayuko peke yake,na kuna mtu atakuwa kamtuma kufanya jambo hili na bila Shaka ni mwalimu wake kijeshi"

    Mjumbe mwingine akadakia

    "Meja Salim Komba? inawezekanaje hii? Akatoa swali kwenda kwa wenzie na bila kumwemwesa mkuu wa kikao kile akatoa ufafanuzi,



    "kepteni Shayo alikuwa ni mtu wa karibu na Meja Salim,mbali ya kuwa rafiki yake pia alikua ni mwanafunzi wake katika medani ya vita,kubwa zaidi Zedi ni ni rafiki wa wote japo Zedi aliasi jeshi lakini bado anatumia taaluma yake kwa malipo sehemu mbalimbali za Dunia hii."

    Akaendela baada ya kupisha ukimya ndani ya dakika moja.



    "kilichonifanya niwaite hapa ni kwa sababu mwakilishi wetu Ikulu amenipa taarifa ya kuwa hata Rais anahisi hili jambo la kuuawa wanajeshi wake lina jambo nyuma yake,na ndo maana akatumwa Sajini Mina kuanza upelelezi,sasa sijui tufanyeje ili mambo yaende sawa." akamaliza kuongea bwana yule.



    Baada ya ukimya mfupi akakohoa mjumbe mmoja na macho yote yakaelekezwa kwake kumsikiliza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mpango Tikisa lazima uitikise Tanzania kisha baada ya raia kutikiswa bungeni nitapeleka hoja ya kumpinga rais ikishindikana nyinyi mtapindua nchi,Ibra mbaya anaendelea kuwafua vijana msituni,lakini hatutaweza kufanya yote hayo kama Zedi atakuwa duniani na Meja Salum ashughulikiwe....



    ****

    Wakati kikao kikiendelea Zedi Wimba alikuwa anatoka maabara ya silaha ya usalama wa taifa Mbezi mwisho.

    Huko alikutana na mpenzi wake ambae kimsingi ndie alikuwa mtalam wa silaha.

    Alikuwa na jibu la ganda la risasi alilolichukua kutoka Chaya alikofia kepten Shayo.

    Jambo moja lilimchanganya ile risasi ilikuwa ina kipenyo cha 18mm na hii ni risasi kubwa sana na inauwezo wa kutembea nusu kilomita au mita hamsini kwa sekunde moja,na inatumika na bunduki ya kudungulia aina ya magnum rifle slig hii ilikuwa ni silaha mpya na hapa kwetu hatukua nayo na wagunduzi wa silaha hii ni wafaransa.

    Zedi akaihisi hatari katika nchi hii,.

    Wakati akitafakari hayo alikuwa anaikaribia ubungo stendi ya mabasi lengo lake ni kwenda kitunda kulikokuwa na msiba wa kepteni shayo,alipanga kwenda kule akiamini atapata jambo la kumtatulia kitendawili cha matukio haya.



    Ni wakati alipokuwa akikunja kona kuifuata barabara ya Tazara,akakumbuka kitu siku anamwokoa Mina alimwibia kijitabu kidogo kilichokuwa kipo kwenye kifua cha mwanadada yule.

    Akatafuta maegesho akasimamisha gari aliloazima kwa mpenzi wake.



    Akakitafuta kijitabu kile katika mfuko mdogo wa kuhifadhia vitu vyake muhimu,

    Hakukawia akakipata,alipokitoa tu kwenye mfuko,akakutana na damu iliokuwa imeganda juu kwenye kijitabu kile cha kumbukumbu,hapo akatafakari kidogo yawezekana hiki kijitabu kilipokonywa mikononi mwa mtu aliekuwa yupo hoi akipigania uhai wake.



    Akakifunua na neno la kwanza kukutana nalo juu kabisa ya kijitabu kile ni "MEGA 09" akajua hiyo ilikuwa ni namba ya utambulisho ya kepteni Shayo katika medani za kimkakati vitani.



    Akazidi kukifunua akakutana na mambo mengi ya kumbukumbu za maisha ya kepteni shayo.

    Punde akakutana na ukurasa mmoja uliokuwa umeandikwa lugha ya fumbo

    "Usimwambie mtu kifo"

    Kisha akakuta jingine

    "Kivu kongo (Goba)"

    "saa tatu usiku ngerengere"

    "Fire team"



    Kisha kukafuatia orodha ya namba zikianza na neno Mega,hii ikimaanisha zilikuwa ni namba utambulisho wa makomando

    "Mega 01,G2,Z4,K3"

    Kisha kukafuatia na alama ya kuuliza na hakukua na neno lingine zaidi ikabaki ni tafakuri ya nini alichomaanisha kepteni Shayo,hakuona kama ni wakati sahihi wa kutafakari jambo hilo akawahi kwenda Kitunda kwenye mazishi ya rafiki yake Shayo.



    Watu wengi walihudhuria msiba ule, Zedi akiwa yupo tofauti kimwenekano alikuwa ni mmoja ya watu waliohudhuria msiba ule.

    Alikuwa makini na kila hatua ya mtu msibani pale lengo lilikuwa ni kumtafuta mtu aliemwona kwenye viwanja vya jeshi kambi ya ngerengere siku ya kuaga mwili wa Kepteni Shayo na luteni Koba na dereva private Zedekiah.



    Katika pitapita za macho yake akakutanisha macho na mwanamke mmoja aliekuwa kavalia hijabu,walipokutanisha macho Zedi akagundua kariba ya mwanamke yule akatabasamu maana alijua kapata msindikizaji wa nyendo zake.



    Baada ya kuuzika mwili wa kepteni shayo kukafuatia heshima ya kijeshi kupiga saluti na mizinga.

    Kisha Zedi hakutaka kusubiri zaidi akaenda ilipo gari yake na kuitafuta barabara.

    Ni wakati akiwa anaikaribia ukonga akagundua nyuma kuna gari inayomfuata akatabasamu kisha akapanga la kufanya ili akutane na msindikizaji wake...



    Manchester Pub ilikuwa mbele ya gari la Zedi,hakuwa na namna zaidi ya kuifuata pub na kupaki pembeni zilipokuwa gari nyingine,akatulia kidogo na kutazama pembeni kwenye kioo,akaliona gari la lilokuwa linamfuata likipaki pembeni kidogo ya Pub ile,akashuka haraka na kwa mwendo wa kuwahi foleni ya mshahara akaufikia mlango wa kuingilia Pub.Hakuingia akasimama kidogo na kuinama akafunga kamba za viatu vyake,lengo halikuwa hilo alihitaji kuona kama aliekwenye gari lile atashuka ilikuwa hivyo alimuona mtu akishuka na alikuwa ni mwanamke,yeye akazama Pub.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alienda kaunta na kuagiza maji,wakati alipotaka kulipa yule mwanamke alikuwa kafika na kutoa noti ya elfu tano na kumlipia kisha wakatazamana alikuwa ni koplo Mina mwanamke mzuri ajabu,.Zedi akatabasamu akashuka kitini akamwomba koplo Mina amfuate.



    Waliingia ndani ya gari ya Zedi,wakaanza mazungumzo



    "Ulinitambuaje wakati nimejitahidi kubadili mwelekeo?"



    Koplo Mina hakujibu nae akauliza



    "wew ulitambuaje nakuafuata anyway nimefuata kitabu changu"



    "kipi"



    "Ulichonipokonya kule porini afu huna aibu unaingizaje mikono kifuani kwa mwanamke mwizi wewe"



    Zedi akamtazama kwa jicho la kwanini umeniita mwizi,kisha pasipo kumuuliza Mina akawasha gari na kuindoa kwa kasi,koplo Mina akamtazama Zedi kisha pasipo kuongea jambo akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu akaweka sikioni akatoa maagizo upande wa pili.

    "T685 DLK ipo Manchester pub"kisha akashusha mkono chini na kuitia mfukoni simu yake na kukaa kimya ila Zedi akauvunja ukimya ule

    "unaniamini kiasi gani"



    "Asilimia sifuri"



    "sasa mbona umekubali tuandamane"



    "Nataka kitabu ni changu nilikitolea damu kwa wanaharamu wale"



    "Nisipo kupa?"



    "Itafahamika"



    "OK tuachane na hayo hatuna muda wa marumbano,mimi na wewe namba moja tuyajenge mahali flani hapo mbele kisha tusaidiane ila Mimi nikupe wewe ripoti"



    Mina hakujibu akakaa kimya na Safari ikaendelea kimya.



    ****

    Ilikuwa ni mida ya jua kuifikia magaribi na mida ni saa kumi na mbili kasoro jioni,ni muda Zedi na Mina walikuwa Mabibo nyumbani kwa mpenzi wake Zedi aliitwa Afsa wakijadili taarifa iliokutwa kwenye kitabu cha kepteni Shayo.



    "09 hii ni namba ya Shayo naijua ila hizi code zingine ni ngeni kidogo na hii K3 ni namba ya Luteni Zegera huyu namfahamu hadi kwake tuliwahi kuwa kombania moja ila hawa wengine ni ngumu"



    Akadakia Mina

    "kinachoniumiza alikuwa anamaanisha nini kuhusu Goba Kivu na kwanini iwe Kongo"



    Afsa akadakia

    "Hapa jibu laeza kuwa Shayo alikufa akitoka kongo na alishukia kigoma..."

    Akaingilia Zedi



    "Ok ndoo maana aliandika hapa muda wa kuondoka saa tatu,pia hii ilikuwa ni siri lakini kwanini walikufa watatu na wengine wako wapi,na huyu luteni Koba ni rubani wa jeshi,hii inamaana walikuwa na Safari ya kongo lakini walifuata nini ?"

    Hakuna aliejibu Zedi akachukua simu na kumpigia Meja Salimu komba akamweleza alipofikia kisha akampa code za wanajeshi anaohisi walikuwa pamoja na kepten Shayo.

    ****

    Koplo Makame alikuwa katikati ya mji wa Goma alikuwa anaukata mtaa wa Angani akanyoosha na barabara hadi alipofika ilipo kanisa ya waromani akakunja kushoto hadi mtaa wa Lucy lameki hapo akawa anaambaa na mtaa huo hadi akaifikia nyumba kubwa na ya kisasa kuliko zote katika mtaa ule,hapo akapunguza hatua za miguu yake na kwa chati akawa anaitazama nyumba ile mandhari yake kwa nje,akaipita nyumba ile iliokuwa imezungushwa kwa ukuta mrefu na nyaya za umeme,jumba lilikuwa tulivu kama vile halikaliwi na mtu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Koplo makame alikuwa ameiacha nyumba ile hatua kadhaa ila akagundua hakuwa peke yake kulikuwa na watu wawili nyuma yake,hakuwajali akazidi kusonga mbele akaifikia barabara ya Nyerere,hapo akakunja na kuingia mtaa wa magzabe huko hakwenda kibahati mbaya alienda maeneo yale kwa sababu kulikuwa na utulivu na vichaka vidogo vidogo,japo ni mchana ila hakukua na pilika za watu hivyo akajibanza kwenye moja ya vichaka hivyo kitalaam kabisa.

    Punde wakafika watu wawili eneo lile waliongea kiringala huku wakihangaika kuangaza macho yao huku na huko,punde akatokea koplo Makame mbele yao,kwanza mabwana wale walizubaa bila kufanya jambo makame hakuwasemesha akabaki akiwatizama mmoja kati yao akamuuliza kwa kifaransa lugha ambayo haikueleweka mbele ya koplo Makame.

    Waliona kama wanadharauliwa kwa kitojibiwa maswali yao na koplo makame kwa wepesi wa ajabu wakamvamia koplo Makame kwa pupa,walikosea Sana hakuwa mzembe kiasi hicho kwa wepesi ule ule akawakwepa watu wale,mmoja kati yao akayumba kisha akajipanga katika mtindo wa kupendeza,Makame akatabasamu nae akajiweka tayari kwa lolote,.

    Akamfuata mmoja aliekuwa kasimama kushoto kwake akampiga usawa wa maungio ya goti na kwa kasi ileile akatupia ngumi mparazo iliompata mtu yule kisha akasimama hakutaka kuuweka usiku akapanga kuumaliza mchezo akajiweka mkao wa nyani au monkey style,akateleza chini akakutana na ubavu wa mmoja kati yao aliponyanyuka bwana yule alikuwa mbali na dunia hii akabaki na mmoja aliekuwa anatapatapa kutaka kukimbia akamwahi na kumvunja shingo kisha akatoka pale kama sie yeye aliefanya vile akarudi hadi mtaa wa Angani hapo akasubiri kidogo punde ikaja gari ndogo ya kizamani ikapaki pembeni akadandia ndani akamkuta koplo Ziga bila kusema neno safari ikaanza ila hawakufika mbali mbele yao wakakutana na kizuizi cha gari la kijeshi walikuwa wanajeshi wa kongo wakiwa wamewaelekezea mitutu ya bunduki.



    Koplo Ziga aliekuwa dereva wa gari lile aina ya pijot toleo la zamani la mwaka 1992,akasimama kisha kama aliesubiri neno toka kwa koplo Makame akaweka usikivu na macho mbele akilitazama gari lile la wanajeshi wa Demokrasia ya Kongo.



    Akamtazama koplo Makame aliekuwa tayari kwa lolote na kwa utulivu kabisa akamuuliza Koplo Makame...



    "Tunafanyaje soldier!"



    "wapo wangapi kwani"



    "Hawafiki saba"



    "Ila tusiwatege isije kuwa ni trap hii"



    "upo sahihi soldier ngoja waje"



    Wakati wakijadili wakaona lile gari likisogea karibu yao na askari waliokuwa kwenye lile gari wakaweka silaha zao tayari kwa lolote.



    Akashuka mwanajeshi mmoja aliekuwa na cheo cha sajenti akionekana ndie kiongozi wa kikundi kile,akalifuata gari la lile la Pijot lililobeba makomando wawili wa kitanzania.



    Kwa lugha ya kifaransa akamwongelesha koplo Ziga ambae nae alikuwa anaielewa lugha ile japo kwa mbali na mazungumzo yao yakawa,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nani mmliki wa gari hili"



    "Kimbu Zibora"



    "Nani kimbu kati yenu"



    "Hakuna kati yetu"



    "Afu nyinyi sio wakongo!"



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog