Search This Blog

Friday, 20 May 2022

KIKOSI CHA PILI - 3

 







    Simulizi : Kikosi Cha Pili

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akasita kujibu koplo Ziga,akamtazama koplo makame,Koplo Makame akampa ishara ambayo haikuonwa na sajenti yule kutoka jeshi la Kongo.



    'Ndio sisi sio wakongo"



    "passport?!"



    "Aah tumezisahau kwa mwenyeji wetu"



    Sajenti akawatazama kwa muda kisha akatoa ishara kwenda kwa watu wake,punde lile gari likawa limezingukwa na wanajeshi wale huku waliondani wakiamuliwa washuke.



    Makoplo wale wakateremka,baada ya kuteremka askari mmoja akawakagua kisha akarudi kwa mkuu wake na kutoa taarifa hajapata kitu toka kwao na hata gari yao haikuwa na kitu pia.



    Sajenti yule akawafuata tena makoplo wale kisha kwa upole akawaambia



    "Samahani kwa usumbufu ila ni mambo ya kiusalama tu maana silaha zinapita hapa kila siku,kifupi tu karibuni Kongo,naitwa Sajenti Zebyirimana"



    Akageuka na kwenda zake huku makomando wale wakiondoka eneo lile kwenda wanakokujua.

    ****

    Papaa Deo Mukamba aligurugwa na taarifa alioipata ya kuwa vijana wake wawili wameuwa na mtu waliemtilia shaka baada ya kuonekana akiikagua nyumba yake.

    Hakuwa anajua huyo mtu katokea wapi na kwanini anaichunguza nyumba yake,na kama anaichunguza inamaana anamjua yeye.

    Akanyanyua simu na kupiga simu mahali fulani huko akatoa maagizo mji mzima wa Goma upekuliwe na kila mgeni anaeingia na kutoka apate taarifa zao,ila hakujua wageni wake hawakuwa na urafiki na makazi ya watu wa mjini.

    ****

    Kilikuwa kama kichaka kikihama upande mmoja kwenda mwingine huku nyuma kikifuata kichaka kingine kikipita kwa hatua zile zile za kile cha kwanza.

    Alikuwa ni Komando Makame na Komando Ziga na hapa ni baada ya kutoka goma kufanya harakati za kujua ni wapi wataanzia ili waeze pata taarifa muhimu walizozihitaji,na sasa walikuwa karibu na Kambi ya AGFT na silaha pekee ni visu vya kikomando vilivyokuwa mikononi mwao na bastola mbili kila mmoja walizokuwa wamezipachika viunoni mwao

    Nia ni kuitafuta ramani halisi ya kambi ile yote na wajue jinsi ya kumwokoa 01 ambae hawakuwa na hakika kama yuko hai hadi muda huo.

    ........



    Zedi alipokea taarifa kutoka kwa Meja Salim komba ya kuwa hizo code ni utambulisho wa makomando wanne wanaotoka vikosi tofauti vya jeshi kuna anaetoka Makutopora Dodoma,unguja,Msata na orojolo Arusha.



    Ila katika hao wote taarifa zinasema walichukua likizo tarehe 30 ina maana wote walichukua likizo siku moja japo wanatoka vikosi tofauti isipokua huyo kepten Zegera yeye alipewa ruhusa ya dharura tarehe hiyo hiyo ila hadi sasa anaripoti kazini hapo hapo msata.



    Meja Salim aliendelea kueleza kuwa siku ya tarehe hiyo hiyo alifuatwa na kepteni Zegera akiwa na barua ya kuomba dharura ana shida nyumbani kwake mabibo dar es laam.

    Baada ya siku mbili alirudi na kimsingi ndo dharura yake ilikuwa inaisha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zedi akahitimisha maelezo yake mbele ya wenzie Afsa na Mina.wakapanga mkakati pangua maana waliiuta pangua kwa sababu waliamini wenzao watakua wanapanga jambo wasilolijua na wao hapo walipo wanapanga kupangua wasichokijua.



    Zedi alijipa jukumu la kumtafuta Zegera kwa kuamini kuna jambo analijua katika mpango wa mauji ya wanajeshi na kukosekana kwa baadhi ya makomando na taarifa zilizokinyume cha utaratibu na kutia mashaka.



    Sajini Mina alijipa jukumu la kufuatilia kifo cha waziri wa afya bwana Makaya Changulu.Ambapo kimsingi kifo chake kuwa na taarifa ya kudunguliwa kwa bunduki ya kudungulia au sniper rifle.



    Afsa yeye akajipa jukuma la kutoa Msaada wa dharura kila panapohitajika.



    ****

    Kepteni Zegera alitoka mapema kazini kwake kwa sababu alikuwa na jukumu moja tu kuhakikisha silaha zilizoagizwa zinaingia bandarini na kutolewa salama bila kuwa na kizuizi na kwa kuwa silaha zile zilikuwa zinaingia nchini kwa kibali cha serikali hakuwa na shaka kuwa atapata usumbufu wowote kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha silaha zile zinatua mikononi mwa Mbaya ili ziwafikie vijana waliokuwa kambini wakijiandaa kwa ajili ya mpango Tikisa.



    Alifika mabibo akiwa amepoteza saa mbili za kuwa safarini kwa kutumia gari yake ndogo.

    Alipofika nyumbani kwake akapokelewa na vijana watatu waliotoka kwa Ibra Mbaya akiwemo Deepaklipa.

    Ukafanyika mgawanyo wa kazi,Deepaklipa yeye alipangiwa kuhudhuria mkutano wa waziri wa viwanda bwana Zakayo kuzigwa lengo ni kummaliza akiwa mkutanoni na waandishi wa habari.

    Zegera alikuwa na jukumu la kukutana mkurugenzi wa bandari ili kuhakikisha kunakuwepo na uangalizi siku ya kufika mzigo wa silaha ambazo mkurugenzi yule alijua kazi yake.



    Kepteni Zegera hakuwa sawa kifikira kuna kitu kilimsumbua ila hakujua kinachosumbua akili yake.Baada ya kufikiria kidogo akachukua simu na kupiga na punde ikapokelewa upande wa pili



    "Zagamba hapa"



    "Naomba ufike kwangu na mbwa wako natoka"



    "Nimekupata"



    Akakata simu na kujipaki kisha akaondoka eneo lile yeye wenzie wakipanga kukutana tena baada ya saa kadhaa na hiyo ilikuwa ni saa kumi na moja jioni.

    *****

    Zedi alikuwa kavaa nguo nyeusi juu mpaka chini alitembea kwa mguu kutoka KKT Mabibo alipokuwa kaipaki gari yake,akaifikia paraise bar napo akapapita,kisha akafika zilipo ofisi za Ale kampani hapo akasimama na kuangalia mbele hatua kadhaa kabla hajaifikia nyumba ya kepteni zegera,akajipa utulivu katika akili yake,akazidi kusogea na kuipita nyumba ile akakunja kushoto na kuiacha nyumba ile ikiwa nyuma yake,hakufika mbali akageuza na kuambaa na vivuli vya mti kisha kwa wepesi usioufikiria akadandia ukuta mmoja na kudondokea ndani bila kutoa kishindo.

    Haikuwa tageti yake nyumba ile ila aliruka kuingia pale maana ukuta wa nyumba zile ulikuwa umeungana kwa hiyo ili uingie nyumbani kwa zegera kwa njia za panya ilikupasa upitie ukuta ule na ndivyo alivyofanya.

    Akatazama kushoto na kulia hakuona wenyeji wa nyumba ile hapo akapiga hatua kadhaa na kuutathimini ukuta ule akauparamia akadondokea kwenye uwanja mpana wa nyumba ya kepteni Zegera ila hakujua kuna macho ya mtu yalikuwa yakimtazama kila alichofanya ikabaki ni mwindano pale ndani.





    Zagamba huwa haamini sana ulinzi wa kukaa ndani,anaamini zaidi kuzitafuta harakati za mtuhumiwa wake ukiwa hatua kadhaa kutoka eneo husika.

    Usiku huu alikuwa mbali na kidogo na nyumba ya Kepteni zegera aliokuwa na jukumu la kuhakikisha inakuwa salama hadi kepteni arudi.



    Zagamba alikuwa ni miongoni mwa vijana waishio Dar wenye magenge ya kihalifu,nae alikuwa na genge lake,na usiku huu alikuwa anatimiza wajibu ulinzi kwa mtu wake wa karibu.



    Alikuwa ametulia mahali akamwona mtu ambae alimtilia Shaka kulingana na utembeaji wake,ilikuwa ni rahisi kwake kutilia shaka nyendo kwa sababu hajawahi kuwa mgeni na watu wa aina hiyo,hivyo hata Zedi aliporuka ukuta macho ya Zagamba hayakumwacha na kitendo kile kililipua hisia tofauti mwilini mwake,hapo kwa haraka akavuka barabara na kukimbia kidogo na kuingia ndani haraka huko akawakuta vijana wake wawili akawapasha habari za kuhisi wanavamiwa wakajipanga kumpokea mgeni wao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zedi alinyata haraka na kukifikia kichaka kilichotengenezwa na kwa maua ya kisasa,hapo akatulia kidogo na kutazama lango la kuingilia ndani ya nyumba ile akaona mlango mdogo getini upo wazi na kutokana hakukua na upepo ila mlango ule ulikuwa unacheza,hii ilimaanisha kuna mtu kaingia au katoka kwa haraka ndio maana alisahau kuufunga,aliwaza hivyo maana alipopita kwa mbele mlango ule haukuwa wazi.



    Alijipa tahadhari akanyata tena kwa kutumia vidole vya miguu yake na kuikaribia korido ya nyumba ile,akajipa tena utulivu akatazama mlangoni akauona upo wazi,akajua ni mtego nae akapanga kupangua,kushoto kulia akaona kigogo kidogo kilichokuwa pembeni ya maua akakifuata na kukishika kisha akachomoa bastola yake na kuilenga taa iliokuwa inampa mwangaza pale nje afu akatulia.



    Zilibaki taa za ndani peke yake zilizokuwa zikitoa mwanga hafifu kuja nje.Zedi akasogea hadi ilipo nguzo kubwa iliokuwa imetumika kuipamba korido ile,akautazama mlango kwa mara nyingine tena na kwa kutumia kigogo alichokiokota akarusha kwenda mlangoni,punde ukasikika mlio mkubwa kukifuatiwa na risasi zilisovurumishwa kutokea ndani.



    Risasi zilipokoma tu Zedi akateleza na kama washingiliavyo wachezaji uwanjani na kudondokea kujikuta yupo ndani kwenye sebule pana huku watu watatu wakiwa wamesimama na bastola mkononi wakiwa wanashangaa kigogo walichokishambulia kwa risasi.

    Bila hata kuomba msamaha wakajikuta wakidondoka chini kama mzaha hivi kumbe ndo uhai unawatoroka hivyo.



    Zagamba aliona kama kivuli kikija kwa kasi hakuwa mjinga akaruka pembeni haraka na kuwashuhudia wenzie wakiwa wanadondoka chini,na alipotaka kunyanyuka afanye shambulizi kwa adui akashangaa akikutana na mtutu wa bunduki ukimtazama.Zagamba akacheka mwenyewe akiwa chini,sio kama alicheka jeuri,alicheka kwa sababu hakupata kuona mtu akifanya kazi kwa wepesi wa kiasi kile tena kwa ufanisi kabisa.



    Zedi akamwamuru zagamba atupe silaha yake chini nae akatii huku akiamini kaingia choo cha mzungu.

    *****

    Deepaklipa alikuwa ni miongoni mwa waandishi waliohudhuria mkutano wa waziri wa viwanda uliokuwa ukifanyika kwenye ukumbi wa Legancy Hotel.

    Alivalia suti nzuri rangi ya kijivu,machoni alivalia mawani pana ya jua,mikononi alijipamba kwa pete kubwa za rangi ya silva zinazotolewa na waganga wa kienyeji eti huziita pete za bahati.



    Sajini Mina alikuwa ni miongoni mwa wahudhuriaji wa mkutano uleza, alihudhuria kwa kuwa alidhani atapata chochote kitu kwa msemo wa wahenga penye wengi kuna mengi.



    Japo aliona ni mwanaume aliependeza lakini hakutaka kushawishika kirahisi ya kuwa siku hizi kuna wandishi wa habari wenye sura Mbaya kama aliemuona pale sio sura tu hata mwonekano wake ulikaa kishari sana lakini pia hakuwa mtu wa kutulia muda mongol alikuwa anazungusha macho yake kutazama kitu upande flani wa ukumbi ule,jambo lile likampa mashaka sajini Mina na hakutulia akala na mjinga Deepaklipa sahani moja.



    Kama ungeliingia ukumbi ule wa mkutano usingelichelea kuona milango ya kuingilia vyooni upande wa kulia wa mlango wa kuingilia ukumbini pale,na kama ungeliingia moja kwa moja vyooni kule ungekutana na sehemu ya kutenganisha korido mbili ya kike na kiume,lakini katika uwazi huo wa kutenganisha kulikuwa na mlango upande wa pembeni kidogo sehemu ya kuingilia wanawake,mlango ule ulikuwa ni mlango wa dharura ndogondogo kwa jinsia zote,moja ikiwa ni kupata hewa safi,kuzungumza na simu,n.k.



    Sajini Mina aliona toafauti kwa mtu aliekuwa anafuatilia nyendo zake,mtu yule alievaa suti hakuwa mwingine ni Deepaklipa.



    Sajini Mina alifuata kila hatua anayopiga Deepaklipa ukumbini pale,hata wakati Deepaklipa alipokuwa akiingia chooni yeye aliona na kuvuta subira.



    Waziri wa viwanda aliingia ukumbini na kukaribishwa na msoma ratiba,ni wakati alipokuwa akisimama kuiendea kinasa sauti au maiki,ndipo Koplo Mina akaona jambo upande wa pembeni kidogo kulipokuwa na mapazia mapana ya kuziba madirisha,mapazia kadhaa yalikuwa yamekunjwa hivyo kuruhusu vioo vya madirisha yale kuonekana hivyo alipotizama kwenye moja ya vioo vile akaona kitu mfano mdomo wa bastola,akafikiria vioo vile vingeweza kuakisi kitu kutoka wapi,hakukawia kugundua ni nyuma ya ukumbi usawa wa mlango wa vyoo alipotizama hakuona kitu,akatulia na kujipa umakini akamtazama Deepaklipa napo akagundua jipya,sikioni alikuwa na kicheep kidogo na alikuwa akimwemwesa midomo na mkononi alishika kamera kubwa,

    Mina akaona hakuna mawasiliano ya kamera ile na chip ile kuna jambo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akasimama akapiga hatua kuvifuata vyoo vile.

    Akafika mlangoni akatazama usawa aliohis kumetokea mtutu ule hapo akaona uwazi wa kioo kilichomwezesha mtumiaji wa vyumba vile kuona upande wa ukumbi,akafanya hima kuingia kule vyooni,akazama ndani hapo akaona upande wa vyoo vya kike milango ile ya vyumba vya dharura ila akakutana na neno closed,ikimaanisha hapatumiki kwanini wakati ukumbi ulikuwa unafanya kazi,akachomoa bastola yake akasogea hadi ulipo mlango ule akaujaribu nao ukaitikia kwa utaratibu sana wa hatua za kutokupiga kelele,akaingia ndani ila akakuta kuko kimya akatazamana na viti kadhaa,hapo akachukua jukumu la kutazama alipohisi aliona kitu.

    Ilikuwa ni sniper rifle Gt 91 new model ilikuwa imesimama mdomo wake ukichungulia dirishani,ajabu mmliki wake hakuwepo Mina akageuka ili atazame ni wapi mmliki alikuwa hapo akakutana na kitu ambacho hakukitarajia mtutu wa bastola ukimtizama.



    Sajini Mina akapokonywa silaha yake,na akaaamuliwa kugeuka nyuma,punde mlango ukasukumwa alikuwa ni Deepaklipa aliengia baada ya kuambiwa kuna tatizo upande wa ndani,akaingia akiwa amefura kwa hasira maana muda ulizidi kwenda na hajafanya lilowapeleka,akamtazama Mina akamchapa kofi lililopelekea aone nyotanyota,kisha wakashauriana kumfunga kamba koplo Mina.

    Deepaklipa akaangaza mle akaikosa kamba akainama kufungua kamba ya kiatu chake.



    Sajini Mina alikuwa akipiga hesabu zake namna ya kufanya ili ajiokoe lakini hakuona upenyo maana jamaa aliemshikia bastola hakumpa hata dakika ya kupepesa macho,hata wakati Deepa akiinama kufungua kamba bwana yule hakutikisika alijua anachokifanya.



    Afsa pia alikuwa ni miongoni mwa wahudhuriaji wa mkutano ule,alikua akiona kila kitu alichokuwa anakifanya Sajini Mina,hata alipoingia kule vyooni aliona,na alipoingia Deepaklipa aliona pia hapo akapata Shaka nae bila kujiuliza akapiga hatua kadhaa kuingia kule,alipoingia akakutana na watu kadhaa wakiwa wanaingia na kutoka macho yake yakatua mlango wa vyumba vya dharura akakutana na neno Closed.

    Akasogea mlangoni pale baada ya watu kupungua mle vyooni,akatazma kushoto na kulia hakuona mtu,akapanga kuingia mle ndani kwa njia ya kustukiza,ila kabla ya kuingia akachungulia kupitia upenyo wa maandishi yale hapo akafanikiwa kuona Mina alivyotaitiwa na alikuwa anafungwa kamba,akapiga hesabu,

    Vile walivyokuwa wamesimama aliamini kama akiwastua kwa kufanya lolote Mina atajinasua hapo akanyanyua bastola yake akapiga kioo cha mlango ule nao ukagawanyika na kwa kasi ya ajabu mwanamke yule wa shoka akazama ndani,na kama alivyotarajia akamkuta Mina ameshaingia mchezoni nae hakuwa na budi kujiunga.



    Deepaklipa alikuwa na Safari mgumu wa kuyapangua mapigo maridadi yaliotoka kwa koplo Mina huku Afsa yeye akiwa anajitahidi kumkwepa msaidizi wa Deepaklipa,



    Afsa alimtazama adui yake vile alivyokuwa akitumia nguvu nyingi na hii ilimpa picha Afsa ya kuwa adui yake alikuwa na plani za kumshambulia haraka ili amalize mchezo,hivyo yeye akataka kwenda kinyume awe na kazi ya kupangua tu bila shambulizi.

    Haukupita muda adui wa Afsa akaanza kuhema baada kutumia nguvu nyingi na hapa ndipo alipopahitaji Afsa kwa weledi wa hali ya juu akaanza kutupia mapigo ya kuvunja,akatupa ngumi ya kike yenye ujazo wa lita tano za mafuta ya taa,ngumi ile ikaondoka na mbavu za mtu,akatupa teke la uzani wa Kilo nne likampata adui kwenye shingo,akaenda chini na hakunyuka tena.



    Sajini Mina akawa anapata tabu kidogo kushambulia hasa alipogundua uwezo wa Deepaklipa akaona kosa moja litamgarimu akawa anavizia,punde akapata usaidizi wa Afsa wakawa wawili kwa mmoja.



    Katika wakati mgumu katika maisha yake,huu ni wakati ambao Deepaklipa alikiri amepigika vibaya na hadi muda huo alikuwa hoi kwa kichapo cha madada wawili wanaujua kupiga kwa mitindo ya ajabu kabisa,hapo akakumbuka mbinu zake za kujiokoa hasa kwa kukimbia na pia alikiri yeye hajawahi kufaulu mara nyingi huwa anachezea kichapo hevi.



    Bila kutarajia akajikuta akipokea teke maridhawa kutoka kwa Sajini Mina,teke lile likampeleka hadi mlangoni,akaona mungu ampe nini zaidi ya kuokoa kiroho chake,akajizoa zoa ili anyanyuke akamshudia Afsa akiwa katika ubora wake akimfuata kwa kasi ya kimbunga,Deepa klipa akaona usinitanie wewe kwa upenyo wa mpasuko wa vioo mlangoni akajitupa nje na kuanza kutimka huko akakutana na kundi kubwa la watu waliokuwa wameanza kujisogeza kule vyooni baada ya mmoja wa walioenda kujisaidia kusikia mtafaruku akarudi kutoa taarifa,waandishi wa habari na kamera zao wakaanza kwenda kule.



    Afsa na sajini Mina baada ya kukimbiwa na mtu yule mbaya wa sura wakaona wasiuze nyago magazetini wakatumia milango ya dharura walioikuta kule wakatokomea zao huku wakiiacha maiti na mtutu wa bunduki dirishani,waziri wa viwanda nae akiwa mbali eneo lile kwa ulinzi wa maaskari...



    *******

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hata ungelibahatika kumuona ungelijua kabisa anapata tabu kufikiria namna ya kuukwea ukuta ule mrefu wa jumba la Papaa Deo Mukamba.

    Koplo makame akasema na peke yake.

    "Tutumie mbinu nyingine"

    Akasikiliza kidogo kisha akahama eneo alilokuwa akaambaa na ukuta mrefu akafika nyuma ya kasiri lile,huko akakutana na koplo Ziga wakateta kidogo kisha kwa wepesi wa kustukiza Ziga akawa mabegani mwa Makame,na kitendo kilichofuatia ni koplo Ziga kutua taratibu ndani ya jumba lile la kifahari,akajipa utulivu wa kuyasoma mazingira.

    Akakutana na miti mizuri ya maua iliokuwa imesimama mithili ya miti ya Azuni,akautazama mlango wa mbele wa jumba lile,hapo akaona walinzi wawili wakiwa wamesimama wima,upande wa kushoto mwake kulikuwa na magari kadhaa ya kifahari,akatazama kuuzunguka ukuta ule hapo akakutana na taa kali zilizokuwa zikimulika uwanja mzima,ina maana hakuna kitu ambacho kingekakatiza mbele bila kuonekana na walinzi,lakini pia nyuma ya kila taa kulikuwa na kamera ndogo.

    Akajivuta kwa hatua za mtu anaeogopa kukanyaga moto.

    Hatua ya kwanza,ya pili,akajikuta akitoa tusi kubwa la nguoni huku mguu mmoja ukiwa umebaki hewani bila kutua kumalizia hatua ya tatu,akaurudisha mguu ule hivyo akawa amebaki na hatua zilezile mbili.

    Zilikuwa ni nyaya ndogo zilizokuwa zimetawanywa chini, nyaya hizi zilitumika kutoa tahadhari ndani kama zingeguswa na kiumbe yoyote.

    Akaangaza kwa macho ya paka hapo akaona upande mwingine kukiwa na mitego kadhaa ya kunasia miguu au kiumbe ambae angeligusa pale,akatabasamu kisha akatoa vibati kadhaa kutoka mifukoni kwake,akatupia kimoja kwenye mtego ukafyatuka nae akarukia hapo hapo.



    Akafika hadi karibu na dirisha kubwa akatazama ndani akaona watu watatu wakiwa wamezunguka meza wakizungumza,akafungua kioo kile polepole akawa anapiga hesabu za kuingia ndani kabla hakafanya hivyo akamwona mtu aliemfahamu.

    Akaduwaa kwa sekunde kadhaa na akapoteza umakini kwa kumshangaa mtu yule,akiwa hivyo ametulia akawashuhudia watu wale wakisimama na kuondoka mle ndani akanong'ona kidogo kisha akatumia utalamu mdogo kioo kile kikaachia akazama ndani ya jumba lile huku kwa nje akisikia miungurumo ya gari kuashiria gari zilikuwa zikiondoka eneo lile.



    Koplo Makame alipokea taarifa kutoka kwa koplo Ziga,punde akaona gari mbili za kifahari zikitoka pale,akapiga hesabu za kijeshi akaona umbali uliopo kati yake na usafiri wao uliowaleta Goma upo mbali,hivyo asingeliweza kuwahi gari zile akajipapasa akatoa kidude kidogo mfano wa betri ya saa kwa wepesi wa ajabu akakirusha kikaenda kukita nyuma ya gari moja wapo,kisha akageuka na kurudi kuendelea na harakati zake.



    Ziga alinyata hadi karibu na korido ya kulia chakula,hapo akatulia kuyasoma mazingira ya nyumba ile,hakukawia kuziona ngazi zilizokuwa zikipandisha juu,pia upande wake wa mbele akaiona sebule pana iliopambwa kwa samani za kisasa,akajivuta baada ya kuhakikisha hakuna mtu kwenye sebule ile.



    Wakati akikaribia kuifikia sebule ile akazisikia hatua za mtu akija kwa kasi akiwa anatokea kwenye vyumba vilivyojuu,akasimama punde akamwona mwanajeshi wa wa jeshi la Kongo akiifikia sebule ile na kuchukua kitu kwa haraka na kurudi juu haraka,hapo akagundua kuna watu upande huo.



    Akaifikia sebule ile na kunyata akaziendea ngazi kwa hatua za haraka na bila kelele,akajikuta akikutana na uwazi mpana huku mbele yake kukiwa na milango mitatu iliopangana,akaisogelea milango ile ni wakati akitaka kujipa umakini wa kama wa popo akasikia nyuma yake.

    "freezee"

    Hakutaka kusubiri akaruka pembeni ni kama alijua alipotoka tu zikafuatia risasi tatu na zilipomkosa zikapiga mlango na mmoja wapo na kuwastua waliomo.



    Ziga kwa wepesi ule ule akarusha kisu chake kikatua kichwani kwa mtu yule alietoka nyuma yake,alipogeuka nyuma akaona mlango ukifunguliwa na kutoka wanajeshi watatu wakiwa na silaha zao mikononi.

    Akabiringita chini na kuzikwepa risasi kadhaa zilizovurumishwa na wanajeshi wale hakutaka kuwa mzembe akawahi kuipiga taa iliokuwa ikitoa mwanga ikazima kukabaki kiza ndani ya korido ile,na kwa kutumia tumbo akaanza kutambaa kisogea pembeni kulikokuwa na milango mingine.

    Akiwa katika harakati hizo koplo ziga akajikuta akiguswa na kitu cha baridi upande wake wa kulia kisha akaamuliwa kusimama,ni wakati akisimama kukawaka taa za dharura mle ndani hapo akakutana na midomo minne ya bastola ikimtazama





    Ziga akanyang'anywa silaha aliokuwa nayo na mmoja kati ya wale wanajeshi wanne,akaamuliwa kutangulia mbele huku akiwa kanyoosha mikono juu nae akatii.

    Kwa mwendo wa mateka akaanza kupiga hatua kuzifuata ngazi zilizokuwa zikiteremka chini kwenye sebule ya nyumba ile.



    Koplo Ziga maisha yake yote furaha yake ni kuona akiingia mikononi mwa adui kisha atumie maarifa kuwatoka huku akiamini zaidi mikono na miguu yake katika mapambano.

    Kadri alivyokuwa akipiga hatua kuzishuka ngazi alikuwa anapiga hesabu za kufanya lolote.Aliamini adui yake hawezi kumuua kwa sababu watataka kujua yeye ni nani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alibakisha ngazi tatu kuikanyaga sebule pana iliozungukwa na samani za kisasa huku kukiwa na utulivu wa hali ya juu,ukimya ule aliutumia vyema koplo Ziga akatega sikio na kizisikia hatua za watu walioko nyuma katika utembeaji wao.

    Akakanyaga hatua kama anasita akaweka utulivu kichwani pake akazisikia hatua za walioko nyuma yake zikakanyaga kwa pupa hapo akapata jawabu ya kuwa watu hao hawako katika umakini ila wanawahi kufamfanyia jambo.



    Wakati akitafakari kwa muda huo akasukumwa na mtu aliekuwa karibu yake,alilitegemea hilo akajirusha kutoka pale alipokuwa akadondokea kwenye zulia na kwa haraka akasimama na kunyoosha mikono juu huku akiwatizama watekaji wake wakiwa wamesimama imara na mitutu mikononi.



    Mmoja kati ya watekaji wale akapiga hatua na kumfuata akamtazama machoni kisha akamuuliza kwa lugha ya kingereza cha kuhangaika



    "Who are you"

    Ziga hakujibu nae akauliza



    "Who is Papaa "



    Wanajeshi wale wakatazamana kisha wakasemezana kwa lugha ya kilingala punde wakamzunguka wote na kuendelea kumuuliza mwaswali ambayo hayakujibiwa na koplo Ziga.

    Kuona vile wakasemezana tena kwa kilingala,hapo Ziga akajua wanataka kuumaliza mchezo na yeye hapaswi kupoteza Muda,

    Akakohoa kidogo na kikohozi chake hakikwenda bure akaona alie nyuma yake ndie hatari zaidi kuliko walioko mbele alipokohoa tu kikafuata kitendo cha kuruka sarakasi ya nyuma huku mikono ikifanya egemeo kwenye mabega ya mwanajeshi alienyuma yake,alipotua chini mwanajeshi yule tayari alikuwa ngao yake na kitendo bila kuchelewa akampiga pigo dhaifu kwa kutumia ubapa wa kiganja chake nyuma ya shingo lengo ni kumzimisha kwa muda kidogo kitendo hiki hakikuchukua hata dakika moja.

    Wale watatu wakashindwa cha kufanya wakipiga risasi watamuua mwenzao wakaanza kucheza pata potea nae Ziga akaliona hilo kwa kutumia mtu aliemweka mbele akataka kumfanya silaha yake akampiga nyuma ya magoti bwana yule akawa kama anataka kujiandaa kukimbia,Ziga akaruka na kumpita juu kisha akiwa hewani akatawanya miguu yake teke moja likampata mmoja na kumdondosha chini na teke lingine likamkosa mmoja wake na kumfanya akose mhimili wa kusimama baada ya kulikwepa teke la Ziga.



    Ziga hakutaka kupoteza muda akatumia uzoefu wake katika medani za kivita na ndani ya dakika tatu akawa anamalizia kuivunja shingo ya mmoja wa wanajeshi wale kisha akasimama na kuwatazama akajisemea





    "sory soldier!"kisha akaweka kidole sikioni pake akasema tena



    "All clear" bila kusubiri jibu akanwendea yule mtu aliemzimisha akampigapiga usoni akaona itamchukua muda kuamuka akajipapasa akatoka na kichupa kidogo mithili ya dawa ya mafua au vikiskingo kabla hajakifungua akasikia mlango wa hapo sebuleni ukifunguka akaruka pembeni kutazama vizuri alikuwa ni koplo Makame,Ziga akasimama akajitokeza akampa koplo makame kile kichupa kisha akanena,



    "Napanda juu mtemeshe huyo bwege"



    "Copied"

    Ndani ya muda mfupi Ziga alikuwa akipotelea juu ya ngazi za nyumba ile,huko hakukaa sana punde akatoka na mikaratasi kadhaa mkononi mwake akamfikia Makame wakateta.



    "Lolote?"



    "Nimemhoji kanambia Papaa Deo Mukamba anakikao Ashton Hotel usiku huu,zaidi ya hapo inaonekana hajui lolote na hapa anadai walikuwepo kwa ulinzi wa nyumba hii"



    "OK soldier hana thamani huyu kuku"

    Ziga akanyanyau bastola yake na kumwagia risasi kadhaa bwana yule na wakaanza safari huku wakipanga kwenda kumtafuta yule mtu kutoka tanzania alieonekana usiku ule kwa kufuata maelekezo ya saa ya Makame iliokuwa ikisoma mwenendo wa kifaa alichokirusha kwenye magari yaliokuwa na mtu yule.



    ****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zagamba akaona bora afe kuliko kusubiri kuuawa na mtu kama kepteni Zegera,alimjua nje ndani bwana yule alivyokatili akaona hana la kujitetea mbele yake,atamwambia nini ikiwa mvamizi mwenyewe alikuwa ni mmoja tu na wao walikuwa watatu fadhaa ikamkumba.



    Alimtazama Zedi anavyoondoka katika nyumba ile,akaonelea bora afanye kitu ili amshawishi mwamaume mwenzake amtoe uhai katika utaritibu pasipo maumivu kuliko kutolewa uhai kwa maumivu makubwa.

    Kwa taabu akaipata sauti yake nayo ikamfikia Zedi,Zedi akageuka.



    "umenipiga nakubali,ukaona haitoshi ukanivunja uti wa mgongo,hata nisipokwambia ninachokijua itakuwa kazi bure maana sintoweza kujitetea kwa lolote"



    Zedi akamtazama akavutiwa na maneno ya Zagamba,jambazi maarufu katika vyombo vya dola,anatafutwa kwa garama kama shilingi ya kale.

    Zedi akaacha hatua zake zimfikie mhalifu yule pale chini,alipomfikia akamwinamia nae akaipata sauti yake katika utulivu wa mume kuomba unyumba kwa mkewe.



    "waeza zungumza sasa nami nitakusaidia!"



    "Namfahamu Zegera ni mtu anaetumia vibaya vazi lake la taifa,amekuwa akinitumia katika matukio mengi ya uhalifu,anahusika na Ibrahim wa dawa za kulevya,lakini kubwa zaidi hivi sasa anampango tikisa na kuna mtu alinikutanisha nae anaitwa Ibra Mbaya....."



    "Hebu ngoja we unamjua vizuri Ibra au umetamka tu hilo jina!"



    "Namfahamu nimekutana nae juzi na kesho alinambia atanipangia kazi ambayo sikuijua.

    Mwonekano wake ni mrefu sawa na wewe ni mpole anapozungumza ila ni hatari na maamuzi magumu,jana to ameua mtu mbele yangu baada ya kukosea mpango fulani na hivi sasa yupo mahali anafanya jambo pamoja Zegera".



    "unahisi wanafanya nini huko waliko?"



    "Siwezi jua ila nahisi wapo bandarini na...... "



    Zagamba hakumaliza kauli yake risasi ikatua kichwani pake na kuutawanya ubongo wake huku na huko na mwingine ukamrukia Zedi mwilini kwake.

    Zedi hakuwa amempiga risasi Zagamba alishangaa risasi ilipotokea nae hakungoja akaruka upande mwingine na kuiweka sawa silaha yake lakini wakati akiijaribu bahati yake akashangaa risasi nyingine ikizipasua taa zilizokuwa zikiwaka subuleni pale.



    Zedi akiwa anapambana na giza akasikia mdondoko wa kitu kama paka,wakati akijiuliza na kupambana na kulizoe giza la gafla kutoka pale alipo kwa mbali aliona kama mtu akinyata na kusogea mahali kulipokuwa na meza kisha akaruka na kulikumba dirisha la kioo na kutokomea kusiko julikana.



    Zedi akaliona tukio lile akajiuliza pale mtu yule alifuata nini,hapo akakumbuka hata yeye aliona kitu pale ila hakukitilia maanani Sana,hapo akajikuta akitukana tusi zito la nguoni na kunyanyuka alipokuwa baada ya kuhisi usalama eneo lile na lengo lake ni kuwahi huko bandarini usiku huo.



    Nusu saa nyuma...



    Zegera alikuwa kimya ndani ya gari lake alikuwa akiiacha moroko ili aikamate kawe,huko alikuwa na miadi ya kukutana na mkurugenzai wa bandari ambapo angemchukua na kufanya nae mazungumzo kisha yeye angelienda bandarini ili kufanya hila mizigo yao iwahi kutoka lakini alikumbuka jambo.

    Katika mpango tikisa huwa anahifadhi kila kitu kwenye kihifadhi kumbukumbu au kwa lugha rahisi kwa wengi Flash,na hata wakati huo alipaswa kuwa nayo ili achukue baadhi ya mambo ya muhimu kwa mkurugenzi wa bandari,akajipapasa hakuwa nayo,akapaki pembeni na kukagua gari ila hakuambulia kitu.



    Kumbukumbu zake zikamwambia aliiaahau nyumbani kwake mezani na alipaswa kuifuata,ila muda haukuwa rafiki,hapo akaamua jambo,akanyanyua simu yake na kupiga



    "Yes!!"



    "Nenda kwangu kunamzigo upo mezani niletee kawe"



    "sawa mkuu"



    "ila yupo Zagamba"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    '"Hapana Shaka mkuu"



    "Dula fanya chapu"



    "ok"



    Dula hakutaka kuchelewa akajipaki ajuavyo na begi lake mgongoni akachukua pikipiki yake na kuingia barabarani.

    Haikuchukua muda akawa yupo nje ya geti la nyumba ya Zegera,akataka kupiga honi afunguliwe,akasita baada ya kuona mlango mdogo ukiwa wazi,akajua kuna la zaidi hapo ndani.

    Aliingiwa na hisia za jambo baya maana hakuwa mgeni katika kazi ya ushushushu,akaona asijipe tabu,anajua njia mbadala ya kuingilia pale ndani akazunguka nyuma ya nyumba ile akaangaza kushoto na kulia hakuona kitu akasimama katikati ya barabara hapo akatazamana na bampa la kuzibia mifereji ya maji machafu,akatumia nguvu kidogo akabetua bampa lile kisha akazama ndani.

    Haikuwa njia ya maji machafu ila ni njia ya kuingilia au kutokea ndani ya nyumba ya kepteni zegera.

    Ndani ya dakika chache akatokezea kwene chumba cha bwana zegera.

    Wakati akipiga hatua ili afungue mlango akasikia miguno ya mtu aliekatika mateso,akaweka umakini zaidi na kwa kutumia utalaamu wa kijasusi akafungua mlango bila mtu kusikia hata yeye aliefungua hakusikia sauti yoyote kisha taratibu mwendo wa teja akasogea kutazama ilipo sebule,hakuamini macho yake akamwona mwanaume mrefu akiwa ameikamata vyema bastola yake huku akisikiliza maongezi flani kutoka kwa zagamba.



    Alifikia maamuzi ya kumuua zagamba baada ya kuona Zagamba hana nguvu za kujiokoa hata kama yeye atakuwa kamsaidia kufanya hivyo,pia aliiona Flash ikiwa bado mezani hivyo hakuwa na namna ya kuichukua isipokuwa kucheza pata potea,akanyoosha mkono na kidole kikacheza risasi ikampata Zagamba na hapo akaona wepesi wa mtesaji yule alivyoruka kuikwepa risasi iliomlenga baada ya ile ya kwanza kumpata mhusika,l.

    Dula akaona sio muda wa kujipima ubavu na kiumbe yule ila ni kuichukua flash na atamtafuta wakati mwingine kwa mchezo kama ule,na bila kupoteza muda akapiga taa ikazima kisha kwa wepesi wa moshi wa sigara akaruka na kutua kama paka na kupiga hesabu za kichwa namna ilivyokaa ile Flash mezani akaikwapua ilipojaa mkononi akatumia begi lake kulikumba dirisha la vioo na sekunde chache alikuwa nje ya nyumba ile akiipeleka flash kwa mwenyewe huku nyuma akimwacha Zedi akiwasha usafiri wake kuwahi bandarini ila ni kwa kuwa hakujua huko anapoteza atakutana na nini heri angelibakia kumtafuta Dula kwanza.





    ******



    Zedi alikuwa akitembea kwa mguu kuikaribia bandari kuu ya Tanzania,alitazama upande wa kuingilia bandarini pale,akastaajabu kwa alichokiona.



    Dakika kumi nyuma....



    Dula baada ya kumtoroka Zedi,akaamua kumpigia simu kepten Zegera,akampasha habari ya uvamizi nyumbani kwake,kisha akakata simu na kuendelea na safari kumfuata Zegera Kawe ili ampe mzigo wake.



    Kuvamiwa nyumbani kwake kisha kuelekezwa mwonekano wa mvamizi yule,hakuwa na mashaka kabisa ya mtu aliefanya vile zaidi ya Zedi Wimba.

    Alimjua Zagamba nje ndani ila alipofikiria uwezo wa Zedi akatoa mawazo ya kumlaumu Zagamba kutepeta mbele ya kiumbe yule.



    Alijua kama Zagamba alitamka neno bandari basi muda huo Zedi atakuwa njiani kuelekea bandarini,akaona maongezi yake na mkurugenzi hayafai kwa muda huo,akatoka nje akapiga simu mahali na kutoa maelekezo flani kisha akapanda gari na kuondoka mahali pale huku akimwelekeza Dula mahali pa kukutana na si kawe tena.

    ****

    Wakati Zedi akizidi kulisogelea eneo la bandari,akashuhudia gari za jeshi zaidi ya kumi zikiingia pale kwa fujo,huku wanajeshi wakiruka kwa weledi wa hali ya juu kabla gari hazijasimama.



    Zedi akashangaa inakwaje wanajeshi wavamie eneo lile kuna nini,hakupata majibu,si yeye tu aliejiuliza hata baadhi ya walinzi wanaolinda bandari ile hawakujua nini kinaendelea,punde akasikika sauti kutoka kwenye kipaza sauti ilioamuru walinzi wote wajisalimishe kutoka kwenye maeneo yao ni amri si ombi.



    Walinzi wote wakasogea na silaha zao kisha wakaamriwa kila alipo mlinzi mmoja awepo na askari mmoja wa jeshi la wananchi,amri ikatekelezwa bila kupoteza Wakati.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zedi akiwa kajibana pahali aliyashuhudia yote yale lakini aligundua kitu kwa kiongozi wa msafara ule,hakuwa kiongozi aliestahili kuongoza kundi lile la wanajeshi wengi vile,lakini pia hakuwa akitoa amri katika weledi wa kijeshi,kikubwa zaidi alikuwa na bastola ya rangi nyeupe,ambapo katika majeshi yote nchini hakuna silaha yenye mwonekano ule,akapiga hesabu za kiutu uzima na mwongozo wa sheria za kivita.



    Pale alipokuwa kulikuwa na kontena kadhaa upande wake wa kulia na kiongozi yule alikuwa upande wa mbele wa kontena zile na kabla hujamfikia ilibidi uwapite askari watatu waliokuwa wakilinda upande ule.



    Akanyata na kuvuka kipenyo flani akalifikia moja ya kontena zile,kama paka akadandia na kutua juu yake kisha akaanza kutambaa kama mamba,akafika hadi usawa wa mwisho wa kontena lile,na kwa wepesi wa mwewe kwa kifaranga cha kuku Zedi akatua kwenye gari moja wapo kisha akaruka na kutua chini bila kujiuliza akafyatuka kama mpira na kumzoa kiongozi yule na hakusubiri aanguke akamdaka na kumkaba kabari ya ngao kisha yeye akajiegemeza kwenye gari ili alienyuma yake asimfanyie shambulizi kisha akatulia kujipa ujatulivu namna ya kuwatoka wanajeshi wengi walioanza kujaa pale huku silaha zao zikiwa tayari kwa lolote.



    Palepale alipokuwa akatoa mkono mmoja na kufungua mlango wa gari ya kijeshi kisha akatangulia kuingia ndani huku akimburuza bwana yule katika namna ya Simba aburuzavyo windo lake alipokwisha kujaa ndani ya gari ile akaitia moto,lakini akagundua jambo.

    Mateka wake hakuwa na uhai akapigwa na mzubao si yeye alieshambulia wala kabali yake haikuwa ya kuua.

    Akiwa katika tafakuri akasikia amri kutoka kwa mtu ambae hakumuona,punde zikafuatia risasi za moto kuliendea gari lile nae zedi akainama kidogo na kuliondoa kwa kasi akiwa na maiti na alipotazama vizuri mateka wake alikuwa na tundu la risasi kwenye paji la uso

    Akajisemea

    "Mdunguaji".....



    Moja ya taarifa mbaya kwa Ibra ni hii aliopokea akiwa kakaa kwenye kiti cha mbao huku akiwatizama vijana zaidi ya themanini wakicheza michezo ya judo chini ya usimamizi wake.



    Hakupenda kuwa mbali na hekaheka katika maisha yake yote,na hapo akamtazama Deepaklipa akiwa pembeni akimtizama kwa woga.



    Ibra Mbaya alimtazama juu mpaka chini Deepaklipa,akamtathomini katika umbo lake na uwezo wake anashindwaje kumaliza kazi katika muda muafaka.



    Aliwaza kushindwa kwao kukamilisha mipango kunawarudisha nyuma kila siku,akaona hana sababu ya kuendelea kuwa mkufunzi katika kambi ya maficho huku harakati zikiwa zipo mikononi mwa wavivu.



    Akasimama na kumwita kijana mmoja wapo katika wale anawaamini,kisha akamkabidhi madaraka ya kuisimamia kambi ile haramu.



    Na bila kusema neno akamgeukia Deepaklipa na kumpa ishara amfuate na hilo likatekelezwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alinyanyua simu yake na kupiga mahali kisha akasikiliza kidogo na kumpa Deepaklipa,nae akasikiliza kidogo na kumrudishia Ibra Mbaya.

    Na baada ya kujiandaa wajuavyo wakapanda gari na kutokomea kuitafuta mjini Dar iliokuwa kilomita kumi tu kutoka walipokuwa kwa muda huo.



    ****



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog