Search This Blog

Friday, 20 May 2022

KIKOSI CHA PILI - 4

 







    Simulizi : Kikosi Cha Pili

    Sehemu Ya Nne (4)



    Kapteni Zegera alikuwa amekaa akitazamana na Ibra Mbaya na pembeni yake alikaa Dula na Deepaklipa,huku kulia kwake wakikaa watu wengine watatu ambao walikuwa ni wageni machoni kwa wengine isipokuwa kapteni Zegera.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Macho ya watu wote yalimtazama Zegera,Zegera nae akaelewa nini maana ya kutazamwa kule na hapo akanena ili kuwaweka sawa wageni wake.



    "Tunapokea lawama nyingi kutoka kwa bwana mkubwa,na kwa hili hata mimi naona wanastahili kutulaumu.

    Tumeshindwa kumuua Zedi na anazidi kutuumbua na kwa hili limedhihirika usiku huu,ametuzidi akili bandarini na hivyo silaha zetu hazitatoka maana vyombo vya habari visharipoti na watu watataka kujua kinachoendelea.

    Lakini tumeshindwa pia kummliza waziri wa viwanda na taarifa nilionayo ni kuonekana kwa watu wawili wakike eneo lile.

    Kia kuuona ugumu wa katika harakati hizi tumepokea usaidizi kutoka kwa wenzetu Kongo wametuletea watu hawa waliokaa hapa,huyu wa kwanza anaitwa Sanko,anaefuatia anaitwa Niyankuru na yule anaitwa Bedo.

    Kwa taarifa nilizonazo hawa watu ni wazuri kila idara ila hilo litathibitika katika kazi,lakini kabla hatujasambaratika Ibra naomba mikakati yako"



    Akasimama Ibra Mbaya,akawatizama watu wote kisha akasema mipango yote mezani.



    "Zedi hayuko peke yake kuna mtu nyuma yake, na taarifa za awali zinatwambia hakuna mtu alienyuma yake anaejulikana ila Mimi nasema yupo na si mwingine ni Meja Salim komba.

    Na ili tumtoe katika ubora wake lazima tumtoe kafara Meja Salim Komba hatuna namna.

    Pia kuna huyu malaya wa kike Sajini Mina asiachwe hata kidogo na tukiondoka hapa kila mtu ajue jukumu lake"



    Akamaliza tena kusema na kukaa na kilichofuatia ni vijana kusambaratika katika makundi matatu

    Kundi la kwanza liliongozwa na Zegera na vijana wawili akiwepo Bedo.

    Kundi la pili liliongozwa na Deepaklipa na vijana wengine wawili akiwemo Sanko na kundi la tatu liliongozwa na Ibra Mbaya na kundi hili lilimjumisha Niyankuru na ndilo lilikuwa na kazi ya kumuua meja Salim komba.

    ****

    Meja Salimu komba aliisikia muito mdogo katika kompyuta yake iliokuwa wazi na alijisahau kuizima akapitiwa na usingizi.



    Alistuka kutoka alipokuwa amekaa na kusonya kisha akajinyoosha viuongo vyake na kujisemea

    '"Dah uzee huu kazi yaani nalala bila kujijua"alipiga mwayo na kujongea kwenye kioo cha kompyuta yake na kutazama upande wa jumbe zilizoingia kwenye email yake na hakukagua sana akapigwa na butwaa kwa alichokiona kwenye ujumbe ule na kwa wahaka mkubwa akasogeza macho asiamini anachokiona ila ndicho alichokiona.



    Ulikuwa ni ujumbe wa kimafumbo kutoka kwa moja ya vijana wake katika kazi alitambua ujumbe ule uliotumwa katika lugha ya mafumbo ukiambatana na utambulisho wa mtumaji.



    Kufupi ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Ziga na Makame,makomando waliofuzu katika medani zote za kivita,walimtaarifu kwa kifupi uwepo wao nchini Kongo.

    Hilo lilimshangaza hakuwa na taarifa hiyo lakini kilichomshangaza zaidi ni picha zilizombatanishwa katika ujumbe ule akapagawa kupita maelezo,akachukua simu ili apige ikulu kutoa taarifa ila akasita kufanya hivyo na njia pekee ilikuwa ni kumtafuta Zedi usiku huo,na kweli akapiga namba ya zedi ikapokelewa akasema kidogo kisha akaitupa mezani na kubeba kilichomfaa usiku ule na kutokomea na gari akiitafuta chalinze.



    Kitu kimoja hakujua aendako kuna zahama inamnyemelea na angejua ni bora safari yake angeipeleka kwenye kikosi chake anachokisimamia angalau angelipata msaada lakini hakujua,hakujua

    ****

    ***



    Meja Salim komba aliwasha gari yake na kuingia barabarani,alitaka kukutana na Zedi chalinze bar kama kawaida yao ili amshirikishe katika jambo alilodokezwa na makomando walioko nchini Kongo kinyume cha taratibu.



    Akakanyaga mafuta na kuzidi kuiacha Msata,lakini kitu ambacho hakujua ni kuwa wakati anaondoka nyumbani kwake kuna mtu alikuwa akimtizama,na kuondoka kwake machoni mwa mtu yule nae akapiga simu anakokujua kutoa taarifa ya kuonekana kwa meja kuifunga safari kusiko julikana.

    ****

    Ibra mbaya ndie aliepokea simu yenye taarifa za nyendo za Meja Salim komba,akatabasamu kidogo na kujipa tafakari kidogo



    "Baada ya miaka mingi hatimae leo naenda kukutana na mbaya wangu,atashangaa kuniona mbwa yule,na kama alidhani nimekufa au kuzeeka basi leo nitamwonesha mimi huwa sifi kizembe na..."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ibra hakumalizia kauli yake akasikia tusi zito likimtoka dereva wa gari lao aliekuwa akijaribu kuliweka sawa gari baada ya kupitwa na gari flani kwa kasi ya ajabu.



    Ibra mbaya alipojua kisa cha dereva wao kutukana akaamuru dereva alifukuze gari lile na alipite au amsimashe wazungumze kwanini anaendesha usiku kwa mwendo ule,dereva nae akatii ukawa mfukuzano wa magari mawili ya mahisimu ambao hawakujuana wakati huo.



    Meja Salim komba ndie alikuwa wa kwanza kufika pale bar,akapaki gari lake na kushuka kisha akaangaza kushoto na kulia hakuona mtu akachepuka kidogo na kulisogelea gari lingine na kufungua mlango kisha kukaa ndani ya gari lile huku mawazo yakipita kichwani pake.

    ***

    Zedi alipolipita gari lile hakuwa na Shaka nalo,lakini kadri muda ulivyokuwa unazidi kusogea ndivyo alivyohisi tofauti hasa pale gari lile lilipoanza kumfuata nyuma kwa kasi mara kwa mara dereva wa gari lile akimulika taa kumpa ishara zedi asimame.



    Ili kujiridhisha na hisia zake akapunguza mwendo wa gari lake na kuwa kama anaetaka kusimama,na kabla hajatimiza azma yake akavaa mawani zilizomsaidia kuona kizani hata nyuma ya kioo kisha akasimama.



    Wakati gari lile lilipokuwa likimpita kwa mbele ili lisimame alipata kuona watu watatu wakiwa wamekaa viti vya nyuma huku mmoja Kati yao akiwa na bastola mkononi na hapo akajiwa na hisia mbaya zaidi.



    Baada ya gari lile kusimama,tofauti na matarajio yao Zedi yeye akiingia barabarani na kukanya mafuta hadi mwisho na kufanya kina Ibra wasipate tena kumuona japo walijitahidi kumfukuzia lengo wamtie adabu mtu yule,ila ni kwa kuwa hawakujua adui yao ndie walie mwacha awatangulie kufika kwa Meja Salim komba.



    Meja Salim komba alimwona zedi wakati akipaki,akampa ishara ya kijasusi,nae akapaki pembeni na kuchepuka kuingia ndani ya gari lile alilokuwako Meja.



    ***

    Walitazamana kisha Meja akasema

    "wako wapi wageni wangu uliosema upo nao?"

    Zedi hakujibu kitu akageuka na kutizama nyuma,jambo lile likamfanya Meja nae ageuke na hapo akashuhudia wanaume wanne wakiteremka haraka haraka ndani ya gari lao na kuliendea gari la Zedi na kuanza kulilagua.



    Meja Salim hakuwa anawajua watu wale ila alijua ni watu wa kazi,pia hakujua kwanini wanajiamini vile lakini majibu aliyapata baada ya mmoja wa watu wale kuvua kofia kwa minajili ya kujikuna kichwa.

    Alimanusura Meja salimu komba augue kifafa baada ya kumtambua mtu yule kwa msaada wa taa za nje ya bar ile na akajikuta akitamka taratibu kwa mzubao

    "Ibra Mbaya"

    Baada ya kutajwa jina hilo tu Zedi nae akageuka kutazama nae mwili ukamfa ganzi kwa sekunde kadhaa..

    ***



    REJEA NCHINI KONGO



    Baada ya koplo Makame na Koplo Ziga kutoka nyumbani kwa papaa Deo Mukamba,safari yao ilikuwa ni kuifuata gari iliokuwa imetegeshwa kifaa cha kusoma eneo au GPS katika lugha ya watalamu.



    Safari yao iliwafikisha hadi Shelaton Hotel, wakatafuta maegesho ya gari yao hotelin pale,kisha akaanza kushuka Koplo Makame na kutangulia kuingia ndani.



    Alikuta ndani kumefurika watu wa aina mbalimbali,wazungu wachache na waafrika wengi wakiwa wamekaa kwenye viti huku kila mmoja akiburudika na akipendacho.



    Koplo Makame akachagua eneo zuri la kukaa huku akitizama eneo la mlango wa kuingilia ndani ya hotel ile.



    Mhudumu alimfikia na kumuuliza atakacho,yeye Kwa makusudi akaagiza supu ya pweza huku akijua nchini Kongo ni nadra sana kukutana na chakula kile.



    Mhudumu aliaga baada ya kushindwa kukidhi matakwa mteja wake.



    Akiwa palepale kakaa akamwona msaidizi wa mtu waliemfuata akiwa anatoka ndani ya Hotel ile kisha alipofika nje kidogo ya mlango akatokea mtu mwingine na akawaona wakiteta jambo kwa muda mfupi kisha msaidizi yule akarudi ndani.



    Koplo Ziga na yeye akatokea,ila yeye hakwenda kukaa akapitiliza Mika kwa moja hadi ulipo mlango wa kuingilia ndani ya Hotel akiwa kama mteja anaetafuta chumba cha kulala.



    Alipofika ndani na yeye akapata kushuhudia msaidizi yule akiishilizia kuzipanda ngazi kwelekea vyumba vya juu.



    Alimfuata binti aliekuwa mapokezi kisha yeye akajitambulisha kwa jina la Msuke Paul ni mjumbe kutoka Afrika ya kusini na anahitaji kuonana na Waziri wa Michezo kutoka Tanzania.



    Mhudumu yule akawa mgumu kutoa ushirikiano ila kwa hila za komando yule mbobezi akadanganywa kwa cheki bandia kama hongo na mhudumu akakubali kuonesha kilipo chumba cha Waziri wa michezo Tanzania bwana Muruga Wesa.



    Koplo Ziga akazipanda ngazi na kutokea juu kulipokuwa na korido pana huku kukiwa na vyumba kadhaa kushoto na kulia kwake.



    Akazidi kujongea huku macho yake yakiwa makini kutazama kushoto na kulia kutafuta chumba namba 15C.



    Haikumchukua muda akakiona,kwa tahadhari kabisa akakisogelea chumba kile na kutega sikio ili kusikia chochote mle ndani na hakusikia akitakacho.



    Akasukuma mlango kuujaribu kama upo wazi nao ukasukumika ishara ya kuwa upo wazi.



    Kwa hila kabisa akausukuma ukabaki wazi huku yeye akiwa hajaingia bado.



    Akasikilizia kwa sekunde kadhaa kisha bila kujishauri akadunda na kudondondokea ndani bila kutoa kishindo huku bastola yake ikiwa mkononi kwa lolote.



    Ajabu chumba kilikuwa kitupu na kwa mbali alisikia maji yakimwagika upande kulipokuwa na chumba cha maliwato,hapo akajua mlengwa wao yupo huko.



    Akatazama kushoto na kulia ndani ya chumba kile hakuona cha maana akataka kumfuata mheshimiwa hukohuko maliwato ila akasita baada ya kuona kumpyuta mpakato ikiwa kitandani na ipo wazi ikimaanisha ilikuwa ikitumiwa muda mfupi uliopita.



    Kwa haraka akaipekuwa na kukutana na mafaili kadhaa ila faili moja ndani ya kompyuta ile lilimsutua lilikuwa limeandikwa "TIKISA".



    akalitazama kisha akataka kulifungua akakutana na neno lilohitaji aweke nywila au neno la siri katika lugha rahisi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kichwa kikamgonga kwa wahka,akafikiri kidogo kisha akabinya sikio lake yakatoka maneno machache kumfikia Koplo Makame aliekuwa nje nae akaelekeza machache yakamrudia koplo Ziga.



    Koplo Ziga akajaribu alichoambiwa na kweli kikazaa matunda na alichokikuta ndicho kilichomshawishi awasiliane nchini Tanzania kwa njia ya email na Meja Salim Komba alie amini anaweza kumpa utatuzi japo kwa hapo walipofikia walikuwa hawamwini mtu na alituma kucheza pata potea.



    Akiwa anatafakari cha kufanya mlango wa kuingilia ukagongwa kwa nguvu roho yake ikaruka sarakasi za vandame,.



    Maliwatoni kuna mtu na mlangoni kuna mtu hadi hapo papara isingemsaidia.....



    ****



    koplo Ziga alikaa mkao wa mwizi wa maziwa kwenye susu,huku mawazo yake yakifanya kazi kama mpiga hesabu za Mada ngumu kabisa ya kidato cha pili,ya tafuta thamani ya X huku x unaiyona haina thamani imekaa tu.



    Mlango ukagongwa tena kwa nguvu zaidi ya mwanzo na hapo koplo Ziga,akasikia michakacho ya mtu kule maliwato ikipanda na kushuka chini hii ilimpa ishara kuwa mtu yule alikuwa anavaa.



    Upepo uliopiga kutokea nyuma ya mwili wa Ziga ndio uliomkurupua katika hesabu za pata potea alizokuwa akizipiga komando Ziga.



    Akageuka kama mwehu na kutizama nyuma hapo ubongo wake ukajenga tabasamu kama mtu aliebeti na kushinda pesa.



    Bila kujiuliza akalivamia dirisha liliokuwa nyuma yake tena likiwa wazi,akatoa kidogo pazia akapata upenyo wa kuchomoka mle ndani na dakika hiyo hiyo akasikia kishindo cha mtu aliusukuma mlango kwa nguvu na kuingia ndani,ila yeye hakujali na alikuwa tayari akifanya jitihada za kulifikia bomba la maji machafu lililokuwa limeanzia juu kushuka chini na yeye akalitumia kama usafiri wa kuondoka katika vyumba vile vya juu hotelini pale.



    Alipofika chini akabinya tena sikio na kusema maneno machache ya kijasusi kisha akafanya jitihada za kuuruka ukuta wa hoteli ile ili atoke nje maana alikuwa kadondokea nyuma kabisa.



    Dakika moja mbele alikuwa ndani ya gari ya kizamani pamoja na koplo Makame wakijaribu kuiacha Goma iliokuwa imejaa taharuki visivyokifani.



    ***

    Papaa Deo Mukamba,baada ya kutoka kumsindikiza mshirika wake kutoka Tanzania waziri wa Michezo bwana Muruga wesa,alikuwa akiingia ndani kwake huku walinzi kama sita wakiwa nyuma yake.



    Mlinzi wa mmoja wakati akizungusha macho yake alipata kuona mlinzi waliemwacha akiwa kadondoka chini na kwa haraka akatoa ishara kwa wenzie ambao bila kufikiri wakamzunguka mkubwa wao ili kumkinga na hatari yoyote.



    Papaa Deo Mukamba akiwa na uoga ndani yake,akaamuru mlinzi mmoja aende kushuhudia ni nini kilichomkuta mwenzao.



    Kwa hatua za tahadhari mlinzi yule alikuwa akimsogelea mlinzi yule,ni wakati akikaribia akaona hakuwa peke yake,walikuwa walinzi wote wa mbele walikuwa chini tayari ni maiti akarudisha taarifa kwa mkubwa Papaa.



    Mlinzi mwingine akatumwa ndani,nae hakukaa sana akarudi na taarifa kuwa ndani nako kuna maiti za walinzi.



    Katika siku za uchungu na woga ilikuwa siku hiyo.Papaa Deo Mukamba alijiuliza bila majibu ni nani wa kuingia katika ngome yake na kufanya mauaji kiasi kile kisha akatoka salama?



    Moyoni mwake alikiri watu au mtu huyo alikuwa fundi katika medani ya kivita.



    Alijaribu kufika katika kila maeneo yake muhimu,akakuta kuko salama lakini baadhi ya bahasha za muhimu pia hakuzikuta hapo akachanganyikiwa, haraka akakimbia chumba cha ulinzi huko akakuta askari aliemwacha akiwa maiti na alipotizama kamera zilirekodi nini akaambulia kuona mgongo wa kidume Ukitoka na nyaraka mkononi.



    Hakuwa na namna akaamua kuwapigia wafadhili wake huko ufaransa kisha akapiga simu Tanzania kutoa taarifa ya nyaraka kadhaa kutua mikononi mwa asie hitajika.



    ***



    Kimbu kiongozi wa LPFaliwapokea makomando wale wakitanzania katika kambi yao ilioko mafichoni katikati ya misitu ya Goba.



    Baada ya maelekezo machache ya usalama wa kambi yao ulikuwa ni muda wa kupumzika baada ya hekaheka za siku nzima.



    Ni kawaida kwa komando yeyote kutokupata usingizi mzuri ndani ya masaa mawili hasa wanapoukuwa katika hekaheka zozote,na ndivyo ilikuwa usiku alfajiri ile.



    Koplo Ziga alikuwa akiwaza stakabali ya maisha yao ndani ya mji ule wa Goba katika nchi ya kidemokrasia ya Kongo.



    Aliwaza usaliti aliofanyiwa na viongozi wake yeye na wenzie,lakini kubwa alikuwa na hofu ya jambo flani linalotaka kutokea katika nchi yake.



    Si yeye tu hata koplo Makame alikuwa katika mawazo hayohayo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Koplo Ziga hakuona umuhimu wa kulala akanyanyuka kisha kukaa punde Koplo Makame nae akanyanyuka na kukaa huku kila mmoja akiwa kimya akitafakari yake.



    Wakiwa vilevile wakasikia hatua za mtu zikijongea kikakamavu kulifuata hema lao.



    Alikuwa ni Kimbu.Alipofika akakohoa kama ishara ya kuweka amani katika vichwa vya makomando wale ambao aliamini walikuwa tayari kwa lolote muda huo,kisha akasukuma kimlango cha miti kilichokuwa kimeegeshwa pale mlangoni mwa hema lile.



    Alipoingia akakutana na makomando wakiwa katika mkao wa lolote,nae bila salamu akaweka yaliompeleka mule ahsubuh ile.



    "Kama mjuavyo mwenzenu yupo bado kwa waasi,basi nami nimekuwa nikifanya jitihada za kujua anaendeleaje huko.Lakini kwa taarifa nilizozipata muda mfupi uliopita 01 leo jioni anasafirihswa kwenda Goma na kuna Makubaliano flani kati ya Papaa Deo Mukamba na Kiongozi wa waasi,hivyo basi nasubiri mawazo yenu nini kifanyike"



    Walitazamana Makomando wale,kisha Makame akasema



    "Hatutaweza kuruhusu hili litokee na kuanzia sasa inabidi atumwe kijana hodari aanze kufuatilia nyendo za waasi wale,na..."



    Hakumaliza kauli yake kikasikika kipenga cha hatari pale kambini na kwa haraka wakatoka nje na kukutana na vijana wengi wakiwa wamekamata silaha kumwelekezea mtu mmoja aliekuwa kaloa damu kuashiria kapigika muda mfupi uliopita.



    Wakasogea hadi kwa mtu yule na hapo wakapokea taarifa kutoka kwa kiongozi wa vijana wale shupavu.



    "Amekuwa hapa usiku kucha akipiga picha na kuchora,nasi tumekuwa nae kila hatua bila yeye kujua na wakati akijiandaa kutoka tukamweka kati alijaribu kujitetea lakini tumefanikiwa kumdhibiti"



    Kimbu akatabasamu na hakuwa na shaka yule alikuwa ni mpelelezi kutoka mahali fulani,akaagiza vijana wamfunge asubiri hukumu yake na hilo likatekelezwa mbele ya macho ya Koplo Makame na koplo Ziga.



    *****



    CHALINZE USIKU





    wakiwa wametulia ndani ya gari,walizidi kuwatizama wale watu wanne walivyokuwa wakihaha kumtafuta mmliki wa gari ile iliowapa usumbufu njiani.



    "Unaonaje tuwasombe au!" aliuliza Meja Salimu Komba



    "Ngoja tuone nia yao ni nini,ni kulifuata gari na mmliki wake au walikuwa wanajua wanaemfuata"akajibu Zedi.



    ***

    Ibra Mbaya hakuona umuhimu wa kuendelea kuizunguka gari ile,japo kumkosa mhusika lilikuwa ni kosa walilolifanya na hawakuwa na namna ya kuliacha lipite.



    Akawaamuru vijana wake waendelee na safari ili wawahi kuikamilisha hatua yao wanayoitarajia kuipiga kwa kumwondoa Meja Salimu Komba.



    Ibra na vijana wake wakati wakiondoka waliacha mjadala nyuma yao,mjadala wa Meja na Zedi.



    "Hii ni hatari sana kuonekana kwa mwanaharamu yule" aliongea Meja



    "Nashangaa hata Mimi amewezaje kuwepo wakati niliona kabisa mwisho wake kule Uganda,na aliendelea vipi kuwasiliana na watu wa hapa?" aliongea Zedi kwa kuuliza



    "Hata Mimi sina jibu kama wewe ila ni hatari sana na naona nchi inaenda kuingia kwenye machafuko muda wa usoni" alisema Meja



    "Sasa na huko wanaenda kufanya nini ?" aliuliza Zedi kana kwamba anaemuuliza anajibu



    "Sijui Zedi lakini nadhani..." Meja Salim Komba hakumalizia kauli yake Zedi akadakia



    "Watakuwa wamegundua uhusika wako na mimi na wanaenda kukupa salamu za mauti"



    Kauli ile ikamtetemesha kwa hasira Meja Salim komba na bila kujiuliza akapiga ngumi hewani kwa kukabwa koo la uchungu na kisha akasema



    "Hawajui kuteleza kwa nyoka ni ishara ya kulipa windo uzubaifu,wasidhani mimi ni nge asimamishae mkia huku akijua hana mfupa wa kuzuia kuvunjika kwa mgongo wake,washa gari tuwafuate sijazeeka bado"



    Zedi akamtazama mzee yule aliepata kuelekea miaka hamsini na mitatu hivi kisha pasipo kutia neno akawasha ile gari na ukawa ni mtafutano kwenye barabara usiku ule.



    ***

    Ibra alikuwa na taarifa za Meja Salim komba kuwepo njiani lakini hadi muda huo hakuona dalili za kukutana nae ama kuliona gari lake.



    Akawaamuru wapunguze mwendo huku akijaribu kutafakari afanye nini usiku huo maana kulikuwa na mawili yawezekana alipotoka alielekea morogoro ama alikuwa akielekea chalinze.



    Akapiga chapuo la kinywa akawatazama vijana wake anaowafahamu kiundani kisha akamtazama mgeni katika wao Niyankuru aliekuwa kimya muda wote wa safari.



    Ibra Mbaya akamtazama tena kijana yule wa Kikongo,akatabasamu maana mara nyingi alipenda vijana watulivu na wanaofanya mambo yao kwa weledi japo alikuwa hajamshudia katika hilo.



    "Kuna gari nyuma yetu,tangu muda sasa haitaki kutupita" Alisema dereva wa gari la Ibra.



    Ibra nae akageuka nyuma na kweli akaliona gari nyuma yao japo hakuwa na hakika ni dogo au kubwa kulingana na usiku kuwa wa kiza na alienyuma aliwasha taa kali.



    Akaamuru dereva aendeshe kwa kasi, alichokifikiria ndicho kilitokea gari nyuma yao nayo ikaongeza mwendo,Ibra akatabasamu kisha akawaamuru vijana wakae tayari na hapo zikavutwa mashine za vita kutoka chini ya viti vya gari kisha zikakokiwa na kukaa tayari.



    Dereva akapunguza mwendo makusudi na kwa kasi ya ajabu vijana wakafungua milango na kujitupa nje katika mtindo wa kuvutia kisha wakachukua nafasi kungojea kifuatacho.



    Ibra alisalia katika gari lakini hakudumu nae akachumpa na kukita mguu kwenye rami kisha akahepa katika majani mafupi yaliokuwa pembezoni mwa barabara na kuicha gari ikienda kusimama hatua kadhaa mbele yao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***

    Matukio yote yalifanyika mbele ya macho ya Zedi na Meja Salim Komba.



    Meja akiwa ndani ya bukta fupi akachukua bastola yake ya 45H&K USP yenye bulge kubwa na uwezo wa kumdondosha adui dakika sifuri,.



    Zedi yeye alichukua M42 double colt kisha kwa usanii mkubwa akaipunguza mwendo na kuruka nje huku Meja tayari akiwa nje na yeye.



    Jambo ambalo Ibrahim Mbaya hakujua ni kuwa gari liliachwa makusudi na wababe wale wa Vita.



    Wakati likienda bila dereva lilikuwa likiyumba kushoto kulia na kwa kuwa lilikuwa linawaka taa basi liliwamulika vizuri maadui walipochutama na walionekana kirahisi kwa kuwa hakukua na majani marefu ya kujificha likawa kosa upande wa Ibra na kuwagarimu vijana wake wawili katika muda mfupi.



    ***

    Pale alipodondokea Meja Salim alipata kuwaona vizuri kabisa adui wawili wakiwa wanajaribu kuotea kujificha nae pasipo ajizi akaachia risasi mbili zilizowapata wale vijana na kuanguka papo hapo.



    Akatumia nafasi hiyo kusonga mbele huku akijitahidi kuchutama ili akingwe na majani.Na katika jitihada zake akawafikia wale vijana akawakagua mifukoni mwao hakukuta chochote na wakati huo akasikia ukimya wa ajabu katika eneo lile.



    Akatambaa kama mamba kuufuata mti mmoja uliokuwa kando ya barabara ile ili apate kusimama na kutizama eneo lile kwa uzuri kabisa.



    Kitu ambacho hakujua Meja Salim Komba ni kuwa kwenye mti ule alikuwepo Niyankuru na alikuwa akimtizama kila hatua yake,.



    Niyankuru kule juu ya mti alipojaribu kupiga kwa kutumia bunduki,hakuona kama ni busara huwa anaamini zaidi mikono kuliko silaha.



    Kulekule juu ya mti ajigeuza kama nyoka na akaanza kushuka kwa kasi bila kutoa sauti huku pigo lake likiwa limemlenga vizuri Meja Salim Komba aliekuwa akifanya jitihada za kujinyanyua ili aegemee ule mti.



    Meja Salim Komba kwa mbali alihisi mjongeo wa kitu kichwani pake ni kama aliotea hivi akahepa kidogo na akalikwepa pigo la kifo la Niyankuru.



    Japo alikwepa lakini hadi muda huo hakujua bastola yake ilikuwa wapi na tayari ilikuwa mbali na mikono yake,na bila kutegemea alijikuta akiwa chini na maumivu makali katikati ya kifua huku adui yake akiwa kasimama kimya bila kusema.



    Meja alijiinua kivivu,kisha akasimama akamtazama adui na akafanya pata potea akarusha ngumi ikapita bila kitu,akatulia kidogo lakini kwa uwezo wa ajabu akashangaa akitandikwa makonde mazito na sehemu nyeti kabisa akaona akizubaa atakufa kwa nguvu zake zote akajirusha nyuma ili awe mbali na kijana yule alionekana fiti katika medani za mapigano ya ana kwa ana.



    Akatua pembeni lakini hakuwa na nguvu hata kidogo,alikuwa ameotewa kupigwa maeneo ya kunyongonyesha, na akawa hajiwezi kwa lolote hadi wakati huo.



    Niyankuru hakuona sababu ya kumchelewesha adui akanyanyua bunduki yake iliokuwa ikining'inia mgongoni na kwa hasira akamimina risasi kuelekea alipodondokea Meja.



    Niyankuru hakutaka kuhakikisha shabaha yake akaweka silaha yake na kupepea.



    ***



    Zedi aliendelea kutambaa kuelekea kule alikoona kadondokea Ibra Mbaya.



    Katika harakati hizo za kutambaa kama Mamba akajikuta akitazamana na domo la bastola alikuwa ni Ibra Mbaya aliekuwa na yeye akitambaa akajikuta akikutana na Zedi.



    Wote bastola mbele huku wakiwa wamelala chini ni vichwa tu vikitazamana kizani.



    "Karibu tena kwenye mpango Tikisa"alisema Ibra Mbaya.



    "Naona umeubadili kutoka ule wa Agano hadi Tikisa" alijibu Zedi



    "Sikuwa na hakika kama ni wewe Zedi Wimba umenijibu nimekwel..."



    Ibra hakumaliza kauli yake akajikuta akimshudia Zedi akiwa kasimama kwa mtindo wa Japan Kicks na miguu yake kaitanua hewani kwa shambulizi.



    Ibra hakuwa mjinda na yeye pale alipo akaanza kwa kunyanyua miguu na kama ungelimtizama kwa mbali basi ungeamini ni wale aina ya nge wanyanyuao mikia(tandu),kisha akaifanya itangulie chini na kifua kikafuata lakini akaambulia teke maridhawa kutoka kwa Zedi ambae alikuwa amempa mgongo.



    Katika dakika tatu Zedi aliutawala mchezo alimpiga atakavyo Ibra Mbaya lakini hazikufika dakika nne Ibra Mbaya Mwanaharamu akarudi katika ubora wake akaanza kumpelekea za nguvu Zedi sasa ikawa ni patashika nguo kuchanika.



    Wahenga walisema ivumayo haidumu licha ya Ibra kufurukuta lakini uwezo wa Zedi ukawa bado upo imara na ilihitaji mbinu mbadala kumdhibiti.



    Ibra Mbaya akiwa anapiga hesabu za kuijinasua mara ukatokea usadizi alikuwa ni Niyankuru aliengia kusaidia pambano na kwa kutaka sifa akaanza mbwembwe za kurusha ngumi mfululizo ila zote zikatua kwa mikono imara ya Zedi.



    Zedi alijiweka kimkakati maana alikuwa anapambana na watu wawili hatari hivyo kosa moja lingempa tiketi ya kifo.



    Akaanza kupambana na wale wababe,lakini hakufua dafu akajikuta akipokea kipigo kila dakika inavyosogea.



    Akajipanga upya lakini hakufanikiwa hila zake,ukatokea mvumo wa risasi na akajitupa pembeni kisha kujivuruta kuelekea pahali salama.



    Mvumo ulipokoma akaisimama akaishudia gari ya akina Ibra ikiyoyoma kwenda Morogoro na yeye alipotizama kule risasi zilipotokea alimwona Meja akiwa kasimama.



    Kwa haraka akamfikia Meja na hakukawia kujua Meja alikuwa na jeraha mkono wa kushoto na alihitaji Msaada akaliendea gari lao lililokuwa limeacha barabara kidogo akamweka ndani na wakageuza kurudi Dar huku akipiga simu kwa Sajini Mina na Afsa kuomba msaada wa dharura.



    *****



    Sajini Mina na Afsa walikuwa katikati ya barabara huku wakijaribu kuwahi walikoelekezwa kufika ili kutoa Msaada.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haikuwa taabu maana usiku huu mnene palikuwa hapana magari mengi njiani na kazi yao ilikuwa ni moja tu kuongeza kasi ya mwendo wa gari kila ilipobidi.



    Wakati wakiikaribia mto Ruvuma kwa mbele wakaona gari dogo likija kwa kasi.



    Sajini Mina akanyanyua simu na kupiga kwa Zedi,punde ikapokelewa na akasikiliza kidogo kisha akashusha chini na kumwambia Afsa aliekuwa dereva.



    "Punguza mwendo ndo wenyewe"



    Afsa akapinguza mwendo huku akiruhusu gari lao litoe ishara kwa gari inayokuja mbele yao ipate kusimama huku wao nao wakisimama kando ya barabara.



    Zedi ndie alikuwa wa kwanza kushuka na haraka akawaomba wamsaidie kuweka viti vya nyuma katika mkao unaotakiwa ili aweze kumlaza Meja Salim Komba aliekuwa hoi kwa kuvuja damu nyingi kwenye jeraha lake.



    Haraka akapakiwa kwenye gari la akina Afsa huku Zedi akiingia ndani yake na kuacha sauti yake nje ikimfikia sajini Mina aliekuwa kasimama ikimwomba aendeshe gari la Meja Salim Komba,hilo likatekelezeka.



    ***



    Kwa kutumia vifaa vichache vya kitabibu vilivyokuwa ndani ya gari ya Afsa,Zedi alifanikiwa kumweka sawa japo kidogo Meja Salim Komba na akarudi katika hali yake japo si sana na tayari walikuwa wanaingia Mbezi Mwisho yalipo makazi ya Afsa.



    Geti lilifunguliwa na gari mbili zikazama ndani.



    Haraka wakasaidiana kumshusha Meja na kumwingiza ndani,kisha wakampeleka kwene chumba kidogo kilichokuwa kama Zahanati ndogo japo kilikuwa na vifaa vya kisasa kabisa na huko Zedi akajitoa damu na ikatumika kumwongeza Meja Salim Komba.



    ***

    Deepaklipa alijitahidi kila namna kutafuta makazi ya sajini Mina na hakufanikiwa hata kidogo japo kunusa tu aliishi wapi.



    Kitu ambacho hakujua ni kuwa Sajini Mina alikuwa ni miongoni mwa askari tegemezi kutoka kitengo maalumu ndani ya Ikulu na hata Makazi yake yalikuwa ndani ya Ikulu na kipindi hiki alitoka nje ni baada ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kazuzu Manumbu kuona kuna yofauti katika majeshi yake na akihitaji taarifa ili ajue pa kuanzia.



    Deepaklipa akaona isiwe tabu akanyanyua simu na kumpigia Zegera akampasha habari ya kukosa taarifa za makazi ya Mina.



    "Tumeambiwa turudi kambini tukapumzike"Deepaklipa aliwambia wenzie



    ***

    Wakati Deepaklipa akienda kulala huku kwa akina Zedi tayari walikuwa wameweka taarifa za Makomando walioko Kongo Mezani wakijaribu kuzipembua.



    "wanataka msaada pia lakini sioni njia ya kuwasaidia vijana hawa" alisema Zedi.



    "Kwani wapo wangapi" akauliza Afsa



    "wapo watatu lakini walioko huru ni wawili na mmoja yupo mateka kwenye kambi ya AGFT" alisema Zedi



    "Shida sio kuwafuata shida ni namna gani tutawsiliana nao tena ili tujue tutawapataje" Alisema Sajini Mina



    "Tunawafuata vipi kwa Mfano" Aliuliza Zedi



    "Nitawasiliana na Rais tutapata usafiri" alijibu Sajini Mina



    Zedi akamtazama kisha pasipo kusema neno akanyanyuka na kuelekea chumbani huku sebuleni wakabaki Afsa na Mina nao wakatazamana kisha Afsa akasimama na kumwelekeza chumba cha kulala Sajini Mina huku yeye akienda chumba alichoingia Zedi.



    Ulikuwa ni wakati wa mapumziko baada ya hekeheka za siku nzima.



    ****



    Ahsubuhi ilikuwa tulivu ndani ya jiji la Dar es laam, kila mtu alikuwa na shuguli zake ili kuhakikisha mambo yanamwendea sawa.

    Ibra Mbaya aliuwa kainama akiwa amezama kwenye tafakuri nzito huku pembeni kukiwa na watu zaidi ya kumi wakimtazama.

    Mionngoni mwao watu hao alikuwepo Zegera akiwa anamtzama Ibra mbaya alivyogwaya baada ya kukosea kufankisha kile walichokipanga ndani ya muda sahihi.

    Zegera aliwatazima wote ,le chumbani huku akijaribu kufikiri ni kipi anaweza kufanya ili mpango TIKISA uweze kuwa imara zaidi,akiwa vilevile kaka alimgeukia Deepaklipa kasha akasema

    “tunawzaje kufeli kizembe hivi?”

    Ikawa zamu ya Ibra Mbaya kumtazama Zegera kasha akama asietaka akasem kwa upole kabisa

    “Hatujashindwqa ila ni kwa kuwa bado hatujataka kutumia akili zaidi na tuynatumia nguvu nyingi bila sababu za msingi lakini pia hesabu zetu hazipo sahihi na ZEDI anazidi kutuzidi kumbuka na sasa tumeshaharibu kabisa Meja Salim Komba ameshajua kinachoendelea”

    Ikawa zamu ya Deepaklpa kusema

    “Hatujashindwa ila naoana tujaribu kuweka mambo sawa kwanza hasa ilintufanikiwe yatupasa kumziba mdomo Meja Sali komba na…..” hakumalizia kauli yake tsysri Zegera alishasimama na akatoa tabasamu la ushindi ni kama alikumbuka kitu na akarudia kuwatazama vijana wote walikuwa nao wakati huo na akasema kwa satio iliotia matumaini

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yatupasa tufanye jambo jambo litakalomwacha mdomo wazi Meja,nitasema na mkurugenzi wa SOTE MEDIA ili angalau ajue atezaje kuyapamba magazeti yake hapo kesho.Hakuna mtu ambae atakataa kuwa Meja Salim komba hakumuua Kepten Shayo.”



    Ikawa zamu ya Ibra Mbaya kuwatazama watu wote mle kasha akahamishia macho yake kwa Zegera na kwa upole kama mtu aliekatika hatari ya kifo akasema

    “nadhani ni njia rahisi ya kumrudisha nyuma yeye na kundi lake na….” hakumalizia kauli yake simu yake ikaanza kuita akawatazama wenzie na akapokea bila kusema neon akawa anasikikiliza maelezp kutoka upande wa pili.

    Baada ya dakika chache za kuisikiliza simu yake akashusha ile simu kutoka sikioni kwake na akawatazama wenzie waliokuwa wakimtazama katika namna ya kuuliza yaliosemwa na mpiga simu.

    “wiki ijayo tunapokea wafadhili kutoka Kongo,lakini pia tumeombwa tufanye jitihada za kumzuia Zedi,na pia ulinzi uwekwe sawa maana wanakuja na sumu ya kumaliza fitina ya mpango Tikisa”alimaliza kuzungumza Ibra Mbaya na baada ya hapoa yakaanza mazungumzo ya kuweka sawa mpango huo wa kuwazima kina Zedi ila ni kwa kuwa hawakujua yajayo na l;aiti wangejua basi kila jambo walipangalo wangeliahirisha kuanzia siku hiyo.



    ******************



    Zedi alikuwa wa kwanza kuamka akatazama pembeni akamwona bado Afsa akiwa kalala na kitu pekee mwilini mwake kilikuwa ni shuka lilkikouwa limekatisha kiunoni mwake huku kifuani kwake kukiwa wazi kabisa.

    Zedi alimtazama kwa matamanio mpenzi wake yule ila akajiambia nafsini mwake haukuwa muda sahihi way eye kufanya akiwazacho.



    Akasimama kasha akavaa nguo bila kuoga akatoka na kwenda chumba cha pili alipokuwa amehifadhiwa Meja salim Komba.



    Akafungua mlango na hapo akaliona tabasamu kwa mbali kutoka kwa meja Salim Komba aliekuwa anajaribu kujiinua kutoka kitandani huku akionekana wazi kupitia mateso makubwa ya maumivu ya jeraha la risasi.



    “Hababri yako chief” alianza kusabahi Zedi



    “afadhali leo kuliko jana kijana wangu yule mshenzi angeniua jana’’ alijiibu Meja.



    Walitazamana kasha Zedi akamsogelea Meja na kumsaidia kumuinua kutoka kitandani alipokuwa amelala,na alipokwiosha kumkalisha ,wakasikia miguu ikijongea kuja kule chumbani alikuwa ni Sajini Mina.



    Akawasahbahi wote kasha akaomba kujua kinachoendelea ila kabla yeyote kuzungumza aliingia Afsa akiwa amevaa taulo pekee na mswaki ukiwa mdomomoni na hakusema kitu akakaa karibu na aliposimama Sajini Mina.



    “wamejipanga wale watu lakini tusiseme kuwahusu wao hebu tumfikirie kwanza huyu waziri wa michezo na kwa taarifa zilizopo leo anaingia kutokea huko kopngo japo wengi wanajua alikuwa ziara kikazi nchini Burundi” alizungumza Zedi



    “Naona ujaribu kumweka kitimoto ili aseme kinachoendelea na kikubwa tupate kile anachokihifadhi ndani kwake maana naamini atakuwa na taarifa muhimu sana kwetu huyu mtu’ alizungumza Meja.



    Kwa pamoja waliafiki lile wazo na wakapanga kufanya hujuma ili wafanikiwe katika mpango wao wa kumteka waziri awape kile walichohitaji makamanda wale.



    Waligawana majukumu na AFsa alipangwa kuongozana na sajini mina ili kwenda nyumbani kwa waziri wa afya kuwahoji ndugu waziri na wajue kile kilichokuwa kianaendelea wakati wa uhai wake,lakini pia walikuwa na jukumu nla kufika ofisini kwa waziri wa viwanda ili angalau awambie kwanini yeye aliokuwa anawindwa auwawe.



    Zedi yeye alipangiwa kuwapo uwanja wa ndege kusubiri mwanaharamu wa kisiasa waziri wa afya bwana MURUGA WESA.



    Meja Salim komba aliachwa nyumbani kwa ajili ya kupata taarifa kutoka kwa yeyote kati yao au hata taarifa kutoka kwa makomando walioko kongo ila ni kwa kuwa hawakujua huko nje tayari jiji lilikuwa katika mzizimo wa kuwatafuta wauaji sugu wa wanajeshi nchini.



    ************



    Zedi alikuwa anatoka nyumbani kwa AFSA akiwa na gari dogo linalomilikiwa na mpenzi wake huyo,ni wakati akichomoza nje alipoona kibanda cha magazeti pembeni akaamua kwenda kupaki pembeni ya eneo lile kasha akashuka na kupiga hatua kufika kilipo kibanda kile cha magazeti.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ukurasa wa mbele wa gazeti la SOTE lilipambwa na picha mbili za wauaji wa kepteni Shayo,wauaji wale hawakuwa na kipingamizi asiwajue alikuwa ni yeye na Meja salim komba.



    Swali lilibaki ni kwanini mina hajawekwa kwenye orojha ile jibu likaja ni kuwa yeye ni mtu kutoksa ikulu na aliweka jambo lile anawafahamu wote nje ndani.akatabasmu kisha hakuhangaika kununua akajongea na kupanda gari lake na kutokomea huku akiwa na mawazo lukuki juu ya sakata hilo liliombele yao na wakati akiwa na mawazo hayo akapata wazo la kwenda nyumbani kwa waziri wa michezo huku akijaribu kuvuta muda hadi wakati atakaokuwa akifika uwanjani.



    **************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog