Simulizi : Kikosi Cha Pili
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alifika hadi karibu na makazi ya waziri yule,makazi yake yalikuwa kwenye maeneo ya watu wanaojiweza na makazi haya yalikuwa Masaki,akayapita huku akijaribu kuyasomna maeneo yale na ulinzi wake,akaona kitumia njia za panya hatofanikiwa kuingia ndani ilihitjika akili ya ziada ili fanikiwe kuingia ndani pale,akapaki gari lake hatua kadhaa kutoka langoni kwa waziri.
Taratibu kabisa kafika hadi getini na katumia kengele kuwajulisha wa ndani kuna mtu yupo nje,akasubiri kidogo kwa dakika kadhaa punde aksikia hatua za mtu akija na kwa haraka kajua ni askari polisi mwenye dhamana ya kuweksa ulinzi nyumbani kwa waziri yule.
Mlango ukafunguliwa na akatokeza askari polisi akiwa ndani yasare zake safi kabisa huku mkononi akiwa ameshikilia SMG,akamtazama Zedi kisha akamuuliza shida yake.
Zedi hakujibu ila akatopa kitambulisho chake feki na kumunesha askari yule na kwa uongo wa kubuni akasema amemfuata mtoto wa waziri ili ampeleke kwenye fukwe za bahari,hilo likakubaliwa bila kipangamizi na Zedi akazama ndani.
Alikaribishwa ndani na mama wa makamo aliekuwa amejiachia kwenye sofa ndani ya sebule ile ya kuvutia,Zedi akamtazama mama yule akajaribu kuvuta fikira za namna ya kumuanza mwanamke yule alieonekana na dharau na kiburi cha madaraka ya muwewe na hatimae Zedi akaamua kuuvunja ukimya ule uliokuwa umejiweka ndani ya sebule ile.
“aah nimeagizwa kumchukua binti yenu nimsindikize ufukweni’
Kusikia hivyo mama yule akanyanyuka kisha akaanza kulaumu ya kuwa mwanae tangu ahsubuhi alikuwa akilia na alitaka kwenda huko ufukweni lakini mjomba wake amempeleka na akaenda mbali kwa kusema kama yeye (Zedi) ametumwa basi aende kuwapa ulinzi huko koko walikoelekea .
Zedi akaanza kupiga hesabu zake ili afanikiwe kubaki pale ndani.
Wakati akijifikiria mara yule mwanamke akasimama na kumuaga zedi ya kuwa amsubiri nayeye ajiandae waelekee huko huko hata yeye anatamani kufika fukweni na yuko mpweke tangu mume wake aende ziarani,Zedi akaona hiyo ndio nafasi pekee ya kutumiaujuzi wake wote kufanya ajuacho ndani pale.
Kwa alivyomtazama mwanamke yule alijua kabisa lazima nagelienda kuoga na huko c atatumia si chini ya dakika tano,hizo zilimtosha kabisa kufanya akitakacho.
Akasimama na kukiendea chumba cha mwanamke yule,kisha akausukuma mlango uliokuwa umeachwa wazi,akaingia ndani kwa hatua za kunyata na kwa haraka akakitupia macho chumba kile,akaona kimepambwa vizuri na kinanukia pesa,mbali na kitanda cha garama kilichokuwa mle ndani lakini pia kulikuwa na kabarti kubwa la nguo,na seti moja ya sofa zakukalia,pia palikuwa na tv na raedio kubwa ya son.
Akapiga hatua na kulifikia kabati la nguo na juu ya kabati lile kulikua na begi dogo au kwa luga ya wengi briefcase.akalifikai na kulitwaaa kisha kwa haraka akataka kulifungua lakini akakutana na ugumu kidogo maana ilihitajika kulifungua kwa namba akagwaya kidogo,akaachana nalo na kumbilia kwenye faili chache zilizokuwa chini ya meza ya kuwekea tv kazipekua harakaharaka nako hakuona kinachomfaa,akarudi tena kwenye kabati lile akalifungua akaaishia tu kuona nguo nyingi zilizopangwa katika mtindo wa kuvutia akaachana nalo na macho yake akayatupia chini alipoliacha begi lile la kuhifadhia nyaraka.
Akageuka ili aliendee begi lile na hapo akajikuta hayuko peke yake ndani ya chumba kile,nyuma yake alikuwepo mwanamke amesimama huku akiwa ememkodolea macho kwa woga,na alipomtizama akamwona alikuwa umejifunga taulo tu tena upande mmoja huku upande mwingine ukiwa wazi na ulikuwa wazi kabisa na hapo akafanikiwa kukiona kibokisi manyoya cha mwanamke yule.
Ilikuwa rahisi kwa Zedi kuona kibongonyoleo cha mke wa waziri maana alikuwa ameushika upande mmoja wa taulo na kuuweka usawa wa mdomo hii ilimpa ishara kuwa mwanamke yule alikuwa katilka harakati za kujifuta maji.
Zedi akataka kupiga hatua za kumfuata lakini mwanamke yule akawahi kuruka pembeni kwa woga nahapo Zedi akashuhudia taulo lililokuwa limmestiri mwanamke yule likiwa mbali na mwili wake na hapo akakiona bila chenga kiboksi manyoya na mwili mzima kiujumla.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Zedi akapiga hatua kumfuata mwanamke yule aliekuwa amegota ukutani huku akitweta,akili ya jasusi huyu ilikuwa ikipiga hesabu za manufaa kwake,akamfikia mwana,ke yule kisha bila kumsemesha akaanza kuvua nguo zake na yeye na punde akawa uchi wa mnyama huku maewneo yake nyeti yakiwa yametutumuka tayari kwa tendo.
Tofauti na mawazo ya mke wa waziri aliekuwa ameloa kwa jasho la uoga,Zedi akainama kuchukua simu iliokuwa mfukoni mwa suruali yake na akaanza kujipiga yeye akiwa uchi vilevile,kisha akaanza kumpiga mke wa waziri akiwa uchi na akamfikia na kuanza kupiga picha za pamoja wakiwa uchi hivyohivyo kisha bila kusema kitu akavaa nguo zake na kumtupia taulo mwanamke yule na ili aone kama hesabu zake ziko sawa akapiga hatua kuuendea mlango wala hakuufikia…
“wewe kaka!” zedi akasikia akiitwa nae akageuka
“Tafadhali naomba usimpe mume wangu hizo picha nitakupa ukitakacho kaka aangulakini usiniadhiri..”
Zedi akamtazama mwanamke yule na hapo akajiridhisha na akili yake ya kufikiri
“nitaacha kuzisambaza ukinipa namba ya siri ya begi la nyaraka la mumeo” akasema Zedi
“Tafadhali kaka angu sizifahamu namba hizo na mara zote hatakagi kunambia” aliongea mwanamke yule kwa kubebembeleza
“Sawa mimi naondoka’” aliongea zedi na kuanza kupiga hatua za kuondoka ila kabla hajaufikia mlango akadakwa mkono na mwanamke yule ambae tayari alikuwa ameshajifunga taulo
“Sizijui kaka lakini yaeza kuwa 333 ambazo ni tarehe za kuzaliwa mwanae yaani tarehe 03/03/2003 na..” Zedi hakutaka kungoja zaidi akapiga hatua kubwa na kulifikia begi lile akalifungua kwa kutumia namba hizo na kweli likafungunguka,harakaharaka kapekua na hukukuta cha maana zaidi bahasgha ndogo iliokuwa imeandikwa kwa juu “TAFITI” akataka kuiacha lakini akaona sio busara mawazo yake hayatakuwa sawa kama ataiacha.
Akaichukua na kabla hajaondoka akacelekea ilipomeza ya kuweka tv akaokota bahasha ndogo ya aina ileile na akachukua kalamu kutoka mfukoni kwake nakuandika juu maandishimkama yale ‘TAFITI’ kisha akaiweka ndani ya begi la nyaraka nakuifunga hukuile alioichukua kwenye lile begi akiiweka mfukoni kwake na akamgeukia mwanamke yule
“usisahau mimi na wewe ni wapenzi tena tulikuwa chumbani kwa waziri na ukithubutu kusema nitazisambaza picha zetu tukiwa uchi” Zedi alisema huku akiundea mlango na kabla hajafungua mlango ule akageuka tena
“si vibaya ukinipa namba ya simu yako nitakuhitaji baadae”
Bila kujiuliza mwanake yule akaanza kutaja namba na alipomaliza aliendelea kumsihi asifanye lolote kwa ke lakini zedi hakumjibu na haraka akaondoka chumbanimle huku akimwavcha mwanamke yule kiwa kazama kwenye lindi la mawazo bila kujua hatim ya picha alizopigwa na mgeni wa ajabu yule lakini pia alijilaumu kwa kumuonesha utupu wake mwanaume asie mume wake lakini nafsii mwake akajiambia hiyo ni uoga alionao katika maisha yake.
Wakati mwanamke yule akiwa mbali kimawazo huku nje Zedi alikuwa anampita mlinzi huku akimwaga kwa bashasha na mlinzi hakutiamshaka mana zilikuwa zimeppita dakika kama kumi tu tangu aingie ndani na hakutoia shaka zaidi maana alijua muda ule binti aliefatwa hakuwepo kwa hiyo alimruhusu kuingia kwa sababu alijua askari mwenzie alikuwa kazini na ili kutimiza wajibu hakuwa na budi kumruhusu tu aende akutane na jibu la wahusika wa mtoto ila ni kwa kuwa hakujua mtu yule ni nani na hata huko ndani kumefanyika nini lakini hata angejua isinelimsaidia maana Zedi hakuwa saizi yake na ni heri hakujua maana ugali bado ataufaidi.
**********************************
Ndege ya Ethiopia airlines iilikuwa inasugua tairi zake ndani ya uwanja wa kimataifa wa mwalimu Julius kambarage nyerere jijini Dar es laam.
Ilipokwisha kusimama abiria walianza kushuka mmoja baada ya mwingine na miongoni mwa abiria hao alikuwemo waziri wa michezo bwana Muruga Wesa.
Macho ya Zedi hayakumwacha waziri yule kila hatua aliopiga uwanjani pale.
Zedi alikuwa katika hatua za mwisho kabisa za kutaka kumfkia waziri yule lakini alisita baada ya kuona wazri hakuwa peke yake na pale alipo kuna ulinzi mkali sana hilo likamshangaza Zedi.
“Iweje waziri awe na ulinzi mkali kiasi hiki tena ulinzi kama Rais mmh”alijiuliza na hakupata jibu akazidi kutazama kinachoendelea uwanjani pale.
Akiwa katulia kimya tub ado jicho lake halikumwacha waziri na pia hakukawia tena kumuona Deepaklipa akiwa miongoni mwa walinzi waliokuwa nje ya uwanja wakijaribu kufuata nyendo za waziri hapo roho yake ikapata mashaka na kashindwa kuelewa ni nini kinaendelea.
Waziri wakati anaikaribia gariyake akawapungia mkono watu waliokuwa pembeni wakimtizama na miongoni mwao alikuwemo Deepklipa kisha yeye akaenda kupanda gari la serikali lililokuwa linamsubiri.
Zedi alikuwa akiwaona kila hatua waliopiga na hata wakati wanaondoka akapata kushuhudia gari la Deepklipa likiunga tela kufuata nyuma ya gari la waziri.Zedi akatuklia kidogo ili kuona kama kuna gari linguine litakua katika msafara ule na kweli kulikuwa na gari lingine likifuata na yeye kaunga tela sasa kukawa na magari matatu yakifuata nyuma yagari la waziri.
Deepaklipa hakukawia kujua nyuma ya gari la Zegera kulikuwa na gari ikiwafuata,na bila kujiuliza akabonyeza sikio lake na sauti ikatoka
“kuna tela nyuma yako” kisha akatuylia na punde akasikia sauti sikioni pake
“Nilishamsoma na utapata majibu wewe endelea kuweka jicho kwa kiumbe” kisha mawasiliano yakakata na kila mmoja ndani ya gari zile akawa makini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Zedi hakuwa mjinga alijua kabisa watu wale wameshajua yupo nyuma yao na hiyo ni baada ya kufika tazara akaona gari ya waziri ikielekea kushoto na gari moja nyuma huku gari moja ikiendelea mbele na yeye akakunja kushoto na kwa kuwa kulikuwa na msururu wa magari nyuma yake alijuakabisa akipaki karibu na lango la bakhresa basi ile gari itaenda kugeuza zilipo ofisi za Azam hivyo yeye bado atakuwa nahesabu zake za kukaa nyuma yake kama ataamua kurudi .
Na kweli ile gari haikukawia kurudi naikapita kwa kasi ikijaribu kuziweka pembeni gari kadhaa mbele yake na yeye akaamua kuunga nyuma na akawa nyuma yake huku akiacha waziri aende zake yeye akaamua kudili kwanza na hawa walioko kwenye gari hiyo na aliamini ni watu wenye ujuzi ndio maana wakataka wamweke katikati.
Akaendesha gari huku akihakikisha hawamwachi lakini hakuiona tena gari ya waziri mbele yake ,hilo hakujali akaamua kufunga kamba nyuma ya gari ile ambayo hadi wakati huo hakujua ina watu wangapi ndani yake.
Bada ya kutembea mwendo wa dakika kadhaa wakwa wameifikia ile barabara ya uhuru hapo Zedi akaona gari la mbele yake likikunja kuelekeakuifuata barabara hiyo nay eye akaamua kuifuta huku akijua tena watu wale wanajua uwepo wake nyuma yao.
Gari ile iliokuwa mbele yake ikaendelea kukata mbuga na hawakukawia kufika Bungoni na hapo ikachepuka na kuingia mtaa huo wa Bungoni kisha ika simama baada ya kufika katikati ya vichochoro na wakateremka watu wawili huku mmoja akiwa na begi mgogngoni alikuwa ni Dulla na mwingine alikuwa ni Zegera wakaamua kulitelekeza gari lile na wao waktembea mbele kidogo na kukunja kushoto kisha wakatokea mtaa wa Tunduru na wakarudi tena uhuru road.
Zedi alishuka na akaanza kuwafuata kwa miguu,hatua chache mbele akaliona lile gari lliw limepaki na ka mwendo wa kuibia akalisogelea na alipotizama ndani hakuona mtu akajua wahusika wamemchezea shere,akaona isiwe tabu hakuhangaikanalo lile gari akarudi ilipo gari yake na kabla hajaipanda kuna mdada alitokea na kumzuia
“usipande hilo gari kaka yangu” alisema yule dada huku akianza kukimbia kwa kasi na kumwacha Zedi akiwa amepigwa na butwaa lakini hakutaka kuzubaa na yeye akaanza kukimbia kumfuata na alipomfikia alimkunja na kabla hajamuuliza chochote akasikia mlpuko mkubwa nyuma yake akachana na yule dada akakimbia kurudi ilipokuwa gari yake na huko hakuona kitu zaidi ya kulio0na likiwa linateketea kwa moto akaiwakama kachanganyikiwa hivi akakimbia kulekea kule Bungoni street ilipokuwa gari ya mahasimu wake na hakulikuta lile gari akaishia tu kutoa tusi kali la nguoni huku akiwsa mbali kimawzo akarudi tena ilipo gari yake inayoumgua moto,hata hakuikaribia maana tayari polisi walikuwa wameshafika na ulinzi likuwa imara sana.
Zedi aliamua kuchukua boadaboda iliompeleka hadi ubungo na huko akawasiliana na wadada wa kazina wakapanga kukutana mwenge yalipo makazi ya Sajini Mina.
*********
Tayari walkuwa wameenea watu watatu huku Zedi akiwa kimya kabisa akiwatizama wadada wale waliokuwa nao wamekaa kimya tu.
Afsa ndie alienza kuvunja ukimya
“Hakuna haja ya kusikitika kikubwa nbi kufanya kama vile hakujatokeakitu hivi”
“Ni kweli hatupaswi kusikitika tunawapa uhuru zaidi adui zetu” alisema Sajini Mina
“sawa upande wangu ni kama mlivyosikia vipi upande wenu nyinyi” aliuliza Zedi
“ndugu wa waziri wa Afya hawajasema la maana na zaidi hawajui ni kwa ninindugu yao aliuwa na polisi hadi sasa hawajarudisha majibu yoyote kwao na kilka sdiku wanadai upelelezi unaendelea. Si hivyo tu hta waziriwa viwanda hajui kwa nini walitaka kuhatarisha maisha yake japo anahisi ni mambo ya kisiasa na tulipojaribu kumuuliza hajasema la maana japo tunaamini kuna kitu alikuwa anajaribu kutuficha na haihitaji elimu kulijua hilo na sisis tumeamua kumweka kipolo kwanza ili twende nae sawa.” Alimaliza kusema Afsa na Sajini mina akatikisa kichwa kukubaliana na maelezo yake.
Zedi alionekana kuzama katika tafakuri na kama aliekumbuka kitu aakijipapasa katika mfuko wake na akatoka bahasha ndogo na kwa pupa aakifungua na kuanza kuisoma taratibu kana kwamba hana haraka nayo,na kadri alivyoisoma alizidi kutokwa jasho na hapo wenzake wakapata shauku ya kutaka kujua kulikoni na bila kuulizwa akasema
“hii ni ripoti kutoka kwa dokta Manoni ambae ni mtaalamu wa tafiti kuhusu madini na huu ni utafiti unaonesha katika mkoa wa Ruvuma kuna madini mapya katika dunia hii na yana thamani kuliko dhahabu na madini haya yanaitwa URANO. Ni madini yanayopatikana kwa wingi sana katika mkoa huo hii ina maana kwamba ili serikali ifaidi haya madini inapaswa kuwekeza yenyewe la sivyo kampuni kutoka nje zikija kuwekeza hapo itabidi zigawane na serikali katika ailimia zinazoendana na kwa a hilo hakuna namna labda ndio maana Rais ameamua kuweka pembeni suala hilo,lakini la kujiuliza tafiti hii imemfikiaje huyu baradhuli?” alimaliza kusema Zedi
Sajini mina akavuta pumzi ndefu na kuzishusha kisha akasema
“mtu wa kwanza kuuwawa alikuwa ni huyu mtaalamu na hapa nimepata pich kwa nini laiwawa hii ina maana kna sababu nyuma ya kifo chake”
Wakaafikiana katika hilo na hapo Zedi akamkumbuka Meja Salim Komba akanyanyua simu na kupiga akassikiliza kidogo kisha akawageukia wenzie na kuwambia
“Anadai amepata ujumbe kutoka huko kongo na vijana wapo mbiuoni kumkomboa kijana mwenzao hivyo basi kikubwa yatupasa kufanyaliwezekanalo ili tuone namna bora ya kuwapa usafiri wafike hapa tufanye kla nia ya kuzima huu mpango tikisa nilioambiwa mna ibra mbaya”
Bila kusubiri zaidi wakapanga kuondoka ili wafike kwa Meja wapate utaritibu zaidi na wao wafanye mawasiliano na Ikulu wajue namna ya kusaidia katika hilo.
*************CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
NCHINI KONGO
Kitu pekee qwalichokihitaji wakati ule ilikuwa ni kuwaweka sawa vijana ili wawe katika mpango thabiti wa kumkomboa 01 ambae alikuwa anasafirishwa usiku huo,lakini kikubwa walikuwa wameshapata habari walizozihitaji kutoka mateka wao na aliwapa mango kamili wa makabidhiano ya mtu kutoka katika idara ya jeshi alie katika mikono ya waasi wa AGFT.
Makame alikuwa na kazi moja tu kuhakikisha vijana wanajipanga katika kzi itakayokuwa mbele yao muda mfupi ujao na koplo Ziga yeye alikuwa makini kuhakikisha vijana wnkuwa fiti hasa wale wa mapambano ya ana kwa ana.
*****
Usiku uliingia na tayari vijana wa kambi ya LPF chini ya uongozi wa makomando wa kitanzania walikuwa wako tyari kwa lolote na kila mmoja alikuwa makini mahali alipo
Nyiragongo iliuwa inaenda kuwaka moto wa mauaji usiku huo.
Usiku wa deni haukawii kukucha ndivyo ilivyokuwa wakati huo,koplo makame akiwa makini na vijana wake alisikia gari ikija na haraka katoa taarifa kwa koplo Ziga na kKimbu waliokuwa umbali tofauti tofauti na mawasiliano yalifanyika kwa kutumia vinasa sauti vilivyopachikwa masikioni mwao na kila mmoja baada ya taarifa ilre alikuwa makini kujua kinachofuata.
Kamanda lubengo alikuwa tena anaungoza msafara wa makabidhiano yale leo tena alikuwa mbele huku akiwa makini na bado kumbukumbu ya nyuma ilikuwa haijatoka kichwani pake hivyo alikuwa makini sana na ndio maana hata wkati juo alikuwa na jeshi kubwa nyuma yake na gari alilopanda ndilo alilkuwemo 01.
Baada ya mwendo wa dakika chache gari la kamanda lubengo lilisimama na haukupita muda murefu gari la kijeshi lilifika pale likiwa na wanajeshi kama kumi hivi wakiwa wamejizatiti nasilaha za kivita za AK47.
Lubengo akiwa maiini kabisa alitoa salamu kwa watu wale nao wakajibu na punde akamuru katika ishara Fulani na vijana wake wakamtoa mtu aliekua amefungwa kwa kamba ngumu na kumfikisha mbele yake na punde wanajeshi wale nao wakatoa begi dogo ambalo bila shaka lilikuwa na pesa na wkamkabidhi kamanda lubengo.
Lakini si wao wala wale wanajeshi alietambua kuwa tayari baadhi ya vijana walikuwa wameanza kudodosha kimya kimya na kuja kutahamaki jeshi la kamanda lubengo lilbaki na wtu kama thelethini badala ya sitini na hata wakati wanatambua tayrai walikuwa wemzungukwa na vijana imara wa kamanda Makame na wanajeshi wale wale walipotaka kuleta upinzani waliambulia risasi zisizo na idadi.
Baada ya kuwa yupo mateka lubengo alishuhudia watu wengine wakiongezeka alikuwa ni yule aliemkimbia siku chache nyuma mwanaume wa shoka koplo Ziga akiwa na vijana na hakupita muda akashuhudia vijana wakianza kutandaza ngumi safi kabisa kwa viujana wake na hawakutumia silaha walikuwa wanatumia mikono tu.
Kamanda lubengo alikuwa anapiga hesabu za kujiodoa pale lakini hakuona pa kutokea na akafanya kosa dogo tu akaenda kwa mateka wake 01 ambae alikuwa katulia tu huku akiwa hajui kipi kinaendelea,alipomfikia akamfanya ngao yake na hapo akashuhudia mbabe wake kjoplo Ziga akiwa kaganda.
“@$%^&**(!@#” ilikuwa ni lugha iliomwingia vizuri kabisa 01 ni lugha ya kikomando inayotaarifu usalama na hapo 01 akajipindua katika mtindo safi kabisa na kupiga tejke la kutoka mbele na likamfikia lubenngo katika uso wake,likamzubaisha na kwa kuwa 01 alikuwa amefungwa mikono na kuzibwa uso akatumia masikio yake kuweka sawa hisia zake na akausikia mguno wa uchungu kutoka kwa mtesi wake na hapo akageuka na kuruka kwa miguu yote miwil na kumpiga kamanda lubengo kifuani na kumtupa upande wa pili na bila kujiuliza 01 akafuata kishindo cha mtesi wake na kwa haraka akaruka juu na kushuka kwa magoti na kumfikia kifuani kamanda lubengo na kuishia kutema damu huku roho yake ikianza kuwa mbali mwili nah ii baaa ya goti kugota usawa wa moyo na kumuathiri kamanda lubengo.
Watu wote walimtazama 01 ambae alikuwa amesimama na kila mtu akaukubali uwezo binafsi wa mtu yule inaghli akiwa kafungwa mikono na kazibwa macho lakini ameweza kumdhibiti adui ndani ya dakika chache na watu kuhesabu maiti.
Wakiwa katika mzubao ule wakamwona 01 akdondoka chini na hapo ndipo wakaweka umakini kisha bila kujiuliza vijana wawili wakamfikia na kumwinua na hapo wakagundua anavuja damu mwilini mwake haraka wakamyanyua na kumfungua kamba na 01 akawa huru na wakambeba haraka ili wawahi kumpa huduma na wakatokomea huku wakiacha kilio kwa kambi ya ZESO NIGAMBA na vijana wake wa AGFT ambao walibaki kambini na hawakujua kilichowapata wenzao huko njiani.
Kolpo ziga akachukua begi lile la pesa na wakatoka eneo lile huku wakitumia msitu mnene kurudi kambini kwao na wakiacha nyuma maiti ziwe chakula cha fisi usiku ule.
***
Walipofika kambini kwao haraka wakaanza kumpa tiba 01 huku Makame akiwa nafanya jitihada za kuwasiliana na meja salimu komba ili wapate msaada wa dharura na walikuwa wakiwasiliana kwa njia ya email.
Haikuchukua muda wakapata taarifa kuna ndege ndogo itakayo wafuata baada ya siku mbili na hilo liwe siri yao wasimwambie mtu yeyote,hiyo ikawa furaha upande wa makomando wale.
Taarifa ikamfikia koplo ziga laiekuwa anahakikisha anamtibu 01 na ilipomfikia hakuona sababu ya wao kukaa ilihitajika warudi tena hadi kwa papaa deo mukamba.
***
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Usiku huo uliwakuta makomando wa kitanzania wakiwa wanauruka ukuta iliwapate kuingia hadi ndani ya nyumba ile na bila ajizi hilo lwakafinikiwa na kukuitana na ulinzi ukiwa umeimarishwa vya kutosha lakini hilo halikuwa la kuwazubaisha na hapo Ziga akabinya sikio lake na kkusema maneno kadhaa na punde mtu aliekuwa mbele yake akadondoka,hii ilimanisha hawkuwa peke yao walikuwa pamoja na mdunguaji na hakuwa mwingine alikuwa ni Kimbu aliekuwwa juu ya mti mrefu uliomwezesha klu9ona ndani vizuri na alikuwa ameshikilia sniper rifle ya kisasa kabisa ikiwa ni miongoni mwa silaha zilizoporwa kutoka mikononi mwa waasi wa AGFT.
Ziga akaendelea kwenda mbele huku akishuhudia maiiti kadhaa mbele yake zilizodondoshwa na KImbu na alikuwa na uhuriu zaidi maana hata alipoingia langoni alikutana na Makame alikuwa kapita upande wa pili na tayari alishaangusha walinzi kadhaa kwa mapigo mujarabu kazi ikabaki wao kuingia ndani na hilo walkalifanya katika mtindo safi kabisa na wakaingia bila kutoa kelele silaha zao mkononi,na huko ndani wakakutana na watu wane ambao hawakuwa tayari kwa ugeni ule na walipokuwa tayri wakawa mewshasalimiana na kaburi isipokuwa mmoja tu aliejifanya nae ni mjuzi katika medamni hiyoakaruka na kudondokea upande wa pili wa sebule ile lakini alikuwa ameshachelewa na akakutana na Makame akiwa imara kabisa na akamtandika teke safi lakifua liliomyupa mbali na ukuta huku lilimwacha akigugumia kwa maumivu yasio kifani,lakini mtu yule kabla hajafanya maamuzi akakutana na mateke mengine kutoka kwa makame na yakamnyanyua kutoka chini na kumrusha juu kisha akajikuta akirudi chini kama mzigo bila mtu aliempiga kufanya jitihada za kumzuia asianguke.
Koplo makame alimtazma Ziga aliekuwa akimpa kichapo mtu mwningine aliekutwa akijaribu kutoroka kwa kutumia dirisha lililo katika vyumba vya juu vya nyumba ile na aliposhuka chini wakiajikuta wanatazama wote huku wakiwa na maumivu lukuki mwilini mwao .
Koplo ziga akwanyanyua watu wale na qkatumia kichwa chake kikgumu kumtandika mmoja wapo na kumwacha akijibwaga chini akiwa hana uhai na akabaki mmoja akiwa kashikwa imara kabisa na mono wa mazoezi wa koplo Ziga.
Makame nae alisogea na kuuliza maswali kadhaa na yulke mtu aliekuwa hoi kwa kipigo alisema yote na hapo makomando wale wakabaki wakitazmana na walipouliza mmliki wa nyumba ile wakaambiwa kaenda ufaransa na akitoka huko ataelekea Tanzania,hapo wakaona ni muda muafaka wa wao kurudi huku wakiwa nataarifa muhimu kabisa na ilihitajika wazipeleke kwa vyombo husika,lakini lililowatisah zaidi ni kusikia kuna mpango wa kumuua Rais siku ya uhuru na kisha waasi kuchukua nchi na hadi muda huo tayari vijana wap[o msituni wakijifua na hapo wanasubiri kazi tu.
Walifika salama kambini na tayari kulikuwa kunaelekea kupambazuka lakini wao hawakuwa na muda wa kupumzika walikuwa wanahkikisha 01 anapata nafuu kabisa.
****
Ilikuwa yapata saa nne na nusu usiku ambap[o makomando watatuwalikuwa tayari kwa safri yakurudi kwao salama,wal;iwatazma vujana waliwafunza wakiwa katika huzuni lakini hilo halikuwapa shida japo hata wao walikuwa katika majonzi ila hawakuwa nama zaidi ya kuodoka tu.
Kwa mbali ilisikika sauti ya helkopita ya kivita ikisogea mahali walipokuwa wao wakajiweka mbali naeneo lile huku wakijaribu kuwasha penlight mara kadhaa kama ishara ya kuonesha mahali walipo kwa rubani helkopita ile na kweli ika shuka hadi usawa wa ardhi na punde rubani wa helkopita ile akasemma katika kwa sauti kwa luga ya kikomando na iukawafikia walengwa na wao wakajongea hadi ilipo na kupanda na muda mfupi ilikuwa hewani ikikata mawimbi na ikipitia anga ya Burundi.
Kimbu aliwatizama makomando wale kisha akapunga mkono mmoja hewni ishara ya kuwaaga amakomando wale na hapo akatoa amri vijana wote warudi msituni kujiweka sawa ili wamalize kikundi cha waasi wenzao na wao wabaki kuwapa uhuru raia wema wanaoteseka ndani ya mji wao wenyewe.
****
“Naitwa Zedi” alivunja ukimya Zedi aliekuwa ndie rubani wa helkopita ile iiowabeba makomando wa kitanzania.
Wakamtazama pasi na kusema neon kisha wakendelea kukaa kimya bila kusema kitu.
“Tunashukia Ikulu vijana msiwe na shaka” alisema tena Zedi
Hawakumjibu kitu vijana wale nae akaendelea
“nani koplo Makame na nai koplo Ziga”
Ikabidi kila mmoja ajitambulishe kivyake lakini muda wote 01 alikuwa kimya na hapo vijana wenzie wakahamishia macho kwake.
“Naitwa koplo Mwita Chacha 863kj Arusha” hapo wote wakafanya tabasmu mbele ya koplo mwita na safari ikaendelea.
****
Helkpoita ikatua salama ndani ya viunga vya ikulu ya Tanzania na ilikuwa yapta saa kumi na moja alfajiri.
Rais wa jamhuri alikuwa tayari yuko macho na walinzi wake huku pembeni akiwepo Afsa na sajini Mina pamoja na Meja salim komba.
Vijana wakashuka na kupokelewa kishujaa na baadhi ya wanajeshi waliowakuta pale huku rais akionyesha tabasamu lawazi kwa vijana wake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rais aliwangoza makomanedo wale huku nyuma akifuatiwa na walizi wake,safari yao iliwafikisha hadi chumba cha mikutanio na huko kikao kisicho rasimi kikaanza
“Poleni sana vijana wangu na mnastahili heshima hadi kuf8kamlipo”alisema Rais na kisha akendelea tena
“kila kinachoendelea katika nchi hii ninakifahamu na hata mapinduzi yanayotakiwa kufanyika sik tatu zijazo ninayajua,lakini mimi ninawategemea nyinyi katika kila hatua na tayarui mmezidi kuongezeka na sasa mtakuwa watu sita huku mkiongozwa na Meja Salim Komba..hawa wajinga nitawaumbua tu na nyinyi nitawapa jina la KIKOSI CHA PILI,mtakuwa nje mkisafisha vibaraka wa wawazungu waliopandikizwa hapa eti kisa wanyataka madidini ya URANO.na taarifa isio rasimi tayari kuna watu wachache wameenda mjini Tunduru kumwaga sumu ya die soft kuttutetemesha lakini nimeagiza vijana wangu wa kazi wameenda kuzuia hiyo njama…..”
Rais alizungumza mengi na hatimae aaksitisha kikao na kuwapa vijana wake wote vibali maalumu vya kuingia kila sehemu lakini pia alitoa amri kwa jeshi la polisi kuacha kumtafuta Zedi ama Meja na waache wafanye kazi.
***
Baada ya kutoka pale walijipanga katika makundi mawili huku kila kundi likiwa na mwanamke mmoja,japo Mwita laikuwa bado hajapona lakini hakukubali kukaa alipanga kufanya jambo gumu kwa yeyote aliehusika katikanjama za kutaka kumuangamiza yeye nataifa lake.
Koplo ziga na makme wao wakawa na kazi moja tu kuhakikisha wanamfikia Zegera siku hiyo nahuko atakipata cha moto huku wakiwa sambamba na sajini Mina. Na Zedi yeye alikuwa na kazi ya kumfimia mnadhimu wa jeshi la wananchi huku akiwa sambamba na koplo mwita na AFsa.
*****
Safari ya koplo ziga na koplo makame pamoja na Mina iliwafikisha mabibo yalipo makazi ya Zegera na baada ya kupaki gari yao ikawa zamu ya kila mmoja kushuka huku wakiwa wamejipanga kuingiandani kwa namna yoyote, kuvamia au wa kukaribishwa hawakuogopa kitu.
Koplo ziga alilifikia geti na kuligonga na punde akatokea kijana mdogo kama miaka ishiri hivi akiwa na bunduki kubwa mkononi,kijana yule hakukumbuuka kuuliza chochote akapokeam pigo tata katikati ya shingo yake na kupasua koo kisha taratibu komando yule akaingia kwa ndani ya geti huku nyuma wakifuatia wababe wengine katika vita ya silaha au mkono.
Wakati wao wanaingia ndio wakti ambao Deepaklipa alikuwa anjiandaa kutoka ndani ya uzio ule na nyuma alikuwa na vijana wengine kama sita hivi.
Deepa alipiga ukulele mmoja tu wa kutoa tahadhari kwa wengine lakini alikuwa kachelewa mbele yake alikuwa kasimama Ziga na hta kumtazma tu uliapaswa ufe kabla hajakufikia lakini Depaklipa alifanya kosa kudhani bado anaubavu wa kupambana na askari yule aliejeruhiwa.
Sidhani kama aliona au kuhisi alifikaje chini ila alichishuhudia ni kuwa yupo chini na Ziga yupo kasimamana bastola mkononi na laipotaka kuinuka alishindwa na hapo alikumbuka teke moja tu alilopigwa nyuma ya uti wa mgongo na hiyop akajua hawezi kusimama katika maisha yake yote,deepklipa alilia na hapo akadhihirisha ana sura mbaya kuliko hata hamorapa nba alipotizamza pembeni akaona vijana wake wote wamewshalala na hiyo ilimanisha hawakuweza japo kupambana na wale wawili na huku mmoja akiwa kasimama mbele yake nakukamilisha idadi ya watu watatu.
“Zegera yuko wapi” swali hilo liliambatana na kofi kali lilompa nyotanyota usoni.,hakuwa na namna zaidi ya kueleza maana hata agekificha bado isingelisaidia akaona mawage mchekle kwa kuku wengi akasema
“yupo kempisk hotel kuna wageni kutoka ufaransa’ baada ya kusema hivyo ni kama vile hawakuwas wakijua ya kuwa amevunjika kiuno wakmbeba mzegamzega na kwenda kumtupa ndani ya buti ya gari kisha safari ya kempisk ikaanza.
Zedi alimpa taarifa Ziga ya kuwa hata wao wamekosa walichokuwa wanakitafuta na safari yao ipo kwelekea kwa mdhimu wa jeshi huku waziri wa michezo wakimweka kiporo na tayari taarifa ilishasambazwa kote ya kuwa viwanja vya ndege havitaruhusu kurusha ndege ya aina yoyote ile hadi hapo taarifa rasimi mitakapotoka ikulu.
K
Hakuna raia aliejua kunanini hadi wakti huo ila kila mmoja alijua tu labda kuna tatizo palhali ila hakuna liekuwa akijua tatizo ni nini.
***
maana watu watatu walishuka na bila kuuliza wakelekea hadi ilipo ofisi ya mapokezi na huko wakuliza chumba namba 50c na wakaelekezwa na bila kuulizwa wakapanda kuelea huko huku sajini mina akiwa makini kuwasindikiza baada ya katika nchi ya ufaransa ulinzi wa dharura.
Aliekuwa wa kwanza kuvamia chumba kile alikuwa ni koplo makame na kwa mtindo wa kujirusha akatangulia kuingia na huko akakutana na wazungu wawili wakiwa wamekaa peke yao na wao walipoona vile hawakukawia kujua hali imechafuka,wakajirusha pembeni huku kila mmoja kaijipanga kivyake,walikuwa wazoefu p[ia katika medani hiyo.
Ziga aliekuwa nyuma ya makame akjipindua kama ninja na kumfikia mmoja wapo na kwa wepesi wa karatsi akamsushia mashambulizi matatu ya nguvu ila mawili yalipanguliwa kiufundi na moja lilimpata mfaransa yule.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Haikuwa kutulia ili amsome yeye akabadili mtindio haraka n akumcharaza ngumi safi usawa wa tumbo na bila kiuliza akamchapa tena teke safi usawa wa mbavu za kulia na kumwacha akigugumia mzungu yule huku akitukana katika lugha isioeleqweka.
Koplo makame nae hakuwa haba akendeleza ubabe kwa baradhuli yule aliejifanya anajua kutandaza mkono lakini hqakujua anacheza na watu wanaopenda kifo na ndani ya dakika ya pili tu tayari alikuwa anaienda kuikata roho baada ya kupigwa numi yenye uzito wa kilo saba hivi kwenye chembe ya moyo na kumpa shida kupumua kisha ikamaliziwa nyinginew ilituia kisogoni na kuharibu mfumo wa ubongo akwa maiti huku akimwacha makame akimgeukia Ziga amabe nae alikua akienda kuua lakini akwahi kumzuia.
“Zegera yuko wapi’ aliuliza makame
“%%@$^” alijibu kilinggala na hapo make akatambua kuwa wapo na kikako huko Malaika hoteli akampasha habari hiyo Ziga na ziga akatoa pigo la mwisho lililoondoka nauhai wa bazazi yule
Zedi alikuwa anaingia lugalo na akaonesha kitambulisho chake kutoka ikulu na hapo hakutaka maelezo mengi akamtafuta Meja jenero kisha akampasha habari na ruhusa ikatolewa ya kumkamata mnadhimuwa jeshi laini ajabu walipofika katika makazi yake hawakumkuta na hapo ikawa ni kasheshe jeshi zima likaagizwa kumtafuta msaliti yule.
Zedi akiwa na Mwita wakapata taarifa kuwa kuna ndege itaingia dakika chache ikiwa imebeba Papaa deo Mukamba na hiyo ikawa ni fahari kwao,wakaacha wanajshi wanamtafuta msaliti wao wakelekea uwanja wa ndege kumpokea shetani wa kikongo.
****
Ndege ilitua salama na abiria wakaanza kushuka na haikuchukua muda waliemhitaji wakamwona,alikuwa ni papaa Deo Mukamba.
Zedi alijipamnga kuwakabili walinzi wake huku Mwita akijaribu kuwafuata watu walionda kumpokea bazazi yule.
Ilianza kama mzaha gari jesi likagongwa kioo cha mbele waliomo wakatahamaki wakashuka kwa gadhabu kumkabili mpuuzi wao aliekuwa kafungwa bandeji upande wa kichwa ila hawakujua kwanini Mwita alienda cuba kujifunza ukomando.
Aliekuwa upande wa kulia akawahi kumkwida shati lakini dahmira yake haikufanikiwa akijikuta akichezea ngumi zisizo na idadi na kumwacha akitepeta kama mlenda.
Mwita alimwona yule aliekuwa upnde wakushoto akijaribu kuchomoa bastola na huku akipiga hatua kumfikia yeye akaamua kumrahisishia safari akaruka upande wa mbele wa gari na katua mbele yake na bila kuuliza akanza kumwangushia mvua ya makofi ya miguu na dakika iliofuata tayari alikuwa maiti.
Kile kitendo cha haraka vile kilichukua dakika moja hivi na kilimwacha Afsa akiwa hajui ampe nani hongera kati ya Zedi na mwita maana wote walikuwa wamefanya matukio ndani ya dakika moja na tayri papaa deo mukamba alikuwa mikononi mwao na niyeye tu alipaswa kuwasha gari wapate kuondoka.
*****
Papaa Deo mukamba alikuwa katikati ya watu saba na alitakiwa kusemayote katika mpango tikisa unaoendelea nchini Tanzania.
Aliamua tu kusema ukweli maanahakuwa nanamna na hta shehena ya silaha iliokuwa bandarini alisema pia na alisema muda huo kuna watu wmenda kuzitoa laini pia alisema kuhusu kambi ya mafuzo ya kijehi ilioko kitunda na alisema pia ufadhili wao unafanywa na wafaransa na wanataka kuchimba madini ya Urano na dhahabu huku wakifadhili vita mabayo itakuwa haikomi kama nchini Kongo.laiki pia alisma kuna kikao kinendelea huko kitunda cha mwakilishi wa wafaransa na mabazazi walioko hapa ncini.
Taarifa yake ilifanyiwa kazi haraka na askari jeshi wapatao mia moja walitumwa kwenda bandarini kuzuia shehena ya silaha lakini pia kikosi cha watu saba kiliondoka kwenda kukabiliana na wanajeshi wanafundishwa huko kitunda ambao hawakuzidi miamoja wakiongozwa na Ibra mbaya.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
Taarifa yake ilifanyiwa kazi haraka na askari jeshi wapatao mia moja walitumwa kwenda bandarini kuzuia shehena ya silaha lakini pia kikosi cha watu saba kiliondoka kwenda kukabiliana na wanajeshi wanafundishwa huko kitunda ambao hawakuzidi miamoja wakiongozwa na Ibra mbaya.
*****
Kitu pekee walichokuwa nacho mikononi kmwao ilikuwa ni ramani ya eneo husika na wakapanda gari kuelekea huko,hwakuhitaji kupata masaada wa jeshiwao walitosha.
Wlibakiza hatua kadhaa iliwaweze kufika katika kambi ya waasi uchwara na hapo wakagawanyika watatu watatu kuizunguka kambi ile.
Ilikuwa kama mzaha walianza kuwaangusha vijana wa Ibra mbaya walikuwa wamewekwa kuizunguka kambi ile kwa ajili ya ulinzi.
Uwepo wa adui ukawa umegundulika na kilichofuta hapo ni risasi za moto kurindima kila kona lakini wangeliweza wapi ikiwa waliovamia ni makomndo wa kiwango cha juu kabisa wakiongozwa na Meja salim komba.
Ndani ya nusu saa mambo yalikuwa yamekwisha kuwaenda murama vijana wa Ibra mbaya.
*****
Huko ndani hali ilikuwa tete kwa waziri mkuu na waziri wa michezo walitamani kujiharishia kila wakijaribu kusema wakimbie hawakuwa na pa kutokea kabisa na msaada pekee ukabaki kwa Zegera,Seko,Niyankuru, na Ibra Mbaya.
Ibra mbaya na Zegera wakachukua jukumu la kuwalinda mabwanyenye wale huku wakitafuta eneo lillokuwa na nafuu waweze kutoka lakini hawwakujua huko nje hakukuwa na kijana yeyote aliekuwa hai na watui pekee walikuwa hai ni wao tu na walipojaribu kutokeza walikutana na mitutu saba ikiwatizama lakini mtu aliegwaya zaidi ni Zegera baada ya kuwaona vijana aliwasaliti wakiwa mbele yake akajaribu kukimbia na hapo akakutana namtumbaya kuliko alivyodhani a MWITA CHACHA.
Alipigwa bila kujua kapigwaje alikni si yeye tu msala ulikuwa umemwangukia Ibra mbaya liangukia mikononi mwa ziga yaani ni bora nagelipigwana zedi lakini si ziga.
Seko alikutana na Mina huku niyankuru akikutana AFSA zedi alibaki akiwatizama tu huku ulinzi ukiwa umewekwa kwa viongozi wale wasio wazalendo na nchi yao.
Dakika mbili mbele wajinga wale walikuwa metepeta laini Ibra mbaya alikuwa mbali na dunia au tuseme alikuwa ni marehemu baada ya kupokea kipigo safi kutoka kwa Ziga na zegera alikuwa hoi akitema damu tu bada ya kunyukwa na Mwita makame yeye alikutana na Dula na hakumwacha hai huku Deko akiwa amepigwa risasi ya mguu na meja baada ya kutaka kutoroka.
Zegera haustahili kuwa hai vijana wale watatu walimyewshea mvua ya risasi huku wakimwacha akiwa kama tenga kwa wingi wa tundu za risasi.
Mgeni wa kifaransa alikuwa amejikojolea baada ya kuona hana ujnja wa kutoroka.
Ving’ora vya jeshi vilikua vinasikika kwa mbali na punde kundi kubwa la wanajeshi lilifika pale na mtu wa kwanza kutiwa pingu alikuwa ni mnadhimu wa jeshi n a kisha mawziri wale wlifuata,waandishi wqa habari walikuwa tayari wamefika na walianza kupiga picha zisizo na idadi.
******
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliutangazia uma kuhusu majaribio ya kuipindua serikali huku akiweka wazi ubora wa kikosi cha pili mbali na kile cha jeshi kilivyofanya kazi hadi kuwaumbua watu wale,mbali ya kutaka kuipindua serikali lakini walimuua waziri wa afya na kujaribu kumuua waziri wa viwanda baada ya kuona hawasapoti ujinga huo,laini pia aliwataja watu waliokuwa nyuma ya mpango huo kama wabunge na badhi ya wakuu wa mikoa.
Mbali ya yote rais alisitihsa mahusiano na nchi ya ufaransa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dunia nzima ilizizima kwa taarifa hiyo hukumataifa makubwa yakiinyoshea serikali ya ufarnsa kushiriki njama hizo.
MWISHO WA SEASON ONE YA KIKOSI CHA PILI HIVI KARIBUNI UTAIPATA SEASON TWO
0 comments:
Post a Comment