Search This Blog

Friday, 20 May 2022

MKAKATI WA KUELEKEA IKULU - 1

 

    .





    IMEANDIKWA NA : HUSSEIN WAMAYYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Mkakati Wa Kuelekea Ikulu

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Utangulizi



    Wakati Baba wa Taifa anamlea Masurufu Hussein Masurufu hakuwa anajua kuwa analea mtu ambaye alikuwa amechoshwa na udhalili wanaoishi wapigania uhuru.



    Hakujua pia kuwa mzazi mwingine wa Masurufu alikuwa mstaafu wa uliokuwa Muungano wa Afrika Mashariki na ambaye licha ya kuutumikia Muungano huo kwa nguvu na uwezo wake wote, bado ameishia kudhalilika wakati akidai mafao yake kiasi cha kufikia kuvua nguo hadharani.



    Hakujua pia kuwa hizo ni sababu chache miongoni mwa nyingi zilizomfanya Masurufu huyu aanze kuhubiri utakatifu huku akifanya uhalifu baada ya kupata nafasi na kuzitumia vyema fursa za Vita vya Kagera, Uhujumu uchumi, Ubunge, Uwaziri na baadae ubalozi wa Tanzania nje ya nchi.



    Na sasa akishirikiana na Christopher MacDonald Beberu wa G-8 Original, Masurufu anajiandaa vyema kwenda Ikulu kwa lengo moja tu, kuzinyonya rasilimali za Tanzania mpaka tone la mwisho…!



    Ikoje hiyo safari yake?



    SURA YA KWANZA

    UHOLANZI - JANUARI 2005



    Zilishapita siku za kutosha toka Dr. Masurufu na watumushi wenzie katika Ubalozi wao kule Uholanzi wafanye mkutano. Na ilishapita miaka tisa toka Dr. Masurufu alipoteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi hiyo. Asubuhi hii akiwa ndiyo kwanza ametoka kuoga, mkewe akaingia ndani na kumuuliza.

    “Habari za Asubuhi Baba Rose!”

    “Nzuri tu, sijui za kwako” Anajibu hali akijifuta maji kwa taulo. Mkewe anafungua kabati na kumtolea suti safi.

    “Zangu pia njema!”

    “Ulikuwa wapi?”

    “Nilikuwa namuhimiza Rose awahi shule. Mwenzie Dan keshaondoka saa nyingi!”

    “Oh!Vizuri!” Masurufu akaanza kuvaa nguo.

    “Una habari mume wangu?”

    “Habari gani?”

    “Rais wa nchi yetu ya Tanzania anamaliza muda wake mwaka huu. Nasikia chama tawala kitaanza kugawa fomu mwezi ujao!”

    “Sema haki ya Mungu!”

    “Haki ya nani tena!”

    “We habari hizi umezipata wapi?” Sasa Dr. Masurufu alikuwa akivaa viatu.

    “Redioni. Idhaa ya kiswahili ya BBC. Zimetangazwa asubuhi wakati ulipokwenda kuoga!”

    “Enhe!” Dr. Masurufu akaacha kufunga kamba za viatu na kumtazama mkewe kwa mshangao. “Wamesemaje?”

    “Katibu Mkuu amesema fomu zitaanza kutolewa mwezi ujao kwa watanzania wenye sifa. Gharama yake itakuwa shilingi milioni mbili kwa kila fomu. Kutoka hapo itakubidi uzunguke nchi nzima kutafuta wadhamini kabla ya kurudisha fomu mwezi unaofuata ambapo chama kitayapitia majina ya wagombea safi na kuyapeleka kwa wajumbe wa Kamati kuu kwa uamuzi wa mwisho!”

    Masurufu akamaliza kuvaa viatu, mkewe akamuongoza mpaka eneo la kupatia chakula ambako kulikuwa na chai ya nguvu. Akasema.

    “Kikao kilichopita nilitoa onyo kali kwa wale watumishi wenzangu ambao walidhani wanaweza kuniendesha kama yule Balozi aliyepelekwa Singapore. Hiki ni chuma cha pua bwana hawataniweza katu ha…ha….haaah!” Akacheka. Mkewe akatabasamu tu. Dakika chache baadae tabasamu lilizimika akarudi ndani ya tafakuri tena.

    “Mpenzi mke wangu!” Dr. Masurufu akamwita “Kwa nini una majonzi mpenzi? Huonekani kuwa mke wangu niliyekuzoea. Kulikoni?”

    “Huu Uchaguzi laaziz!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Uchaguzi?!”

    “Ndiyo!”

    “Una nini ?”

    “Huujali kabisa!”

    “Siujali ndiyo!”

    “Kwa nini huujali?”

    “Unatuhusu nini? Ingawa sisi ni watanzania, tuko maili nyingi nje ya Tanzania. Sidhani kama una athari kwetu!”

    Kicheko cha uchungu kikamponyoka Glady mkewe! Akamwambia “Kwa taarifa yako, uchaguzi huu unatuhusu sisi zaidi, kuliko unavyowahusu watanzania wengine!”

    “Kwa namna gani dia?”

    “Swali zuri, sisi tunaitegemea Serikali iliyopo madarakani kutuweka huku Ubalozini. Ikimaliza muda wake na kuondoka hatutaipata tena fursa ya kuishi kivulini hapa Uholanzi. Hatutaipata nafasi ya kuishi katika kasri hili wala hatutapata wasaa wa kutembelea magari haya ya kifahari. Hii ni pamoja na watoto wetu kuacha kusoma shule za kimataifa na kwenda kubanana na akina kajamba nani huko uswahilini. Bado tu hujali?”

    Yakamuingia Dr. Masurufu. Akavua miwani na kuisafisha “Unajua kwa nini sijali?” Akairudisha miwani usoni.

    “Sijui!”

    “Yupo mtu anayenifanya nisijali. Mtu ambaye amechangia kwa asilimia kubwa mimi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi. Mtu huyu ni Profesa Zonga!”

    “We’ ndiyo uko nyuma kweli kweli. Huyo Profesa Zonga ndio atasababisha uteuliwe tena?”

    “Ndiyo! Hata akiingia nani pale Ikulu, sisi tutaendelea kuula tu. Watake tutaula, wasitake tutaula!”

    “Yaelekea unajiamini kupita kiasi baba Rose?!”

    “Kwa nini nisijiamini mama watoto?! Dawa zake ninatumia vizuri, masharti yake ninatimiza. Gari nimemuachia. Nyumba nimemjengea. Kwa nini nisijiamini?! Kwa nini?”

    Mkewe akashusha pumzi za kukata tamaa.

    “Lakini mume wangu, utakuwa Balozi mpaka lini? Lini na sisi tutakuwa viongozi wa juu kabisa wa Taifa letu la Tanzania, tukiandikwa na vyombo vya habari kila tunapokohoa, tukilindwa kama miungu wadogo, tukimiliki uchumi wote wa nchi?

    Saini yako ikiamua juu ya kuishi au kufa kwa mtu yeyote. Ukiwa Amiri Jeshi Mkuu unayeheshimika, zulia jekundu likikulaki kila unapokuwa ziarani! Kwa nini hutaki neema hii mume wangu?”

    Dr. Masurufu akavuta tafakuri kwa muda. Akasema, “Tatizo ni watu laaziz, watanikubali kweli? Watu watanipa nafasi?!”

    “Watu ndio kitu gani?”

    “Una maana gani?”

    “Labda ungezungumzia fedha. Kama huna fedha kabisa, labda hicho kinaweza kuwa kikwazo. Lakini watu?! Mbona ukiwa na fedha ni rahisi kupata chochote unachotaka. Seuze watu! Na wewe fedha unazo!”

    “Lakini hazitoshi kufanya kampeni katika chama na nchi nzima.”

    “Zinatosha mume wangu. Zinatosha kabisa Dr. Masurufu! Jiulize una rasilimali kiasi gani, una marafiki wangapi wanaokuunga mkono ndani na nje ya nchi. Hapa hapa Uholanzi wapo zaidi ya kumi. Hao ni wale uliopata kunitambulisha na kuwaleta nyumbani ambao kwa kinywa chako umekiri kwamba ni wafanyabiashara wakubwa ambao hawazungumzii milioni bali bilioni!”

    “Hilo ni kweli!” Masurufu akaafiki.

    “Bado hujanitambulisha wa nje ya hapo. Ambao sina shaka unao wa kutosha!”

    “Ni kweli ninao wa kutosha!”

    “Unataka kuniambia wote hawa ukiwaendea kuwaomba msaada na sio msaada hasa bali wakuazime na ukishaukwaa urais tu utawarudishia. Unataka kuniambia watakataa wote?”

    “Glady, unafahamu vizuri sana kama kitu hicho hakiwezekani!”

    “Kumbe kinachokufanya uhofie ni nini?”

    “Hofu yangu iko kwenye kuanguka. Watu wanaweza kula fedha zako halafu wakakunyima kura!”

    “Mawazo kama hayo mtafutaji hatakiwi kuwa nayo, lakini pia huwajui watanzania vizuri. Watanzania wana ukarimu uliopatiliza. Wanakumbuka hisani kama sio fadhila hata katika hali inayokatisha tamaa kabisa. Wakishakula fedha zako hawatakuwa na zaidi ila kukupigia kura wakifika katika sanduku la kura.

    Kwa sasa ukiwazungukia marafiki zako wa ndani na nje wakatupa walau bilioni mbili tu, hesabu utakuwa umeshinda tayari. Niulize kwa nini!”

    “Kwa nini?”

    “Ukiwa na fedha hizo, ukaongezea na zako haidhuru hata zikafikia bilioni nne au tano. Unaweza kuanzisha gazeti lako ambalo si tu litakuwa likikupigia debe kama mgombea safi, mgombea chaguo, mgombea unayefaa na kupendwa na wengi, usiye na kashfa na kadhalika na kadhalika. Lakini pia, gazeti lako hilo litashiriki kwa siri kuwachafua na kuwapaka matope wagombea wengine kwa hila , wagombea ambao watakuwa tishio kwako!”

    “Enhe, nikingali nakusikiliza!” Dr. Masurufu alianza kusisimkwa.

    “Huo hautakuwa mwisho, utawanunua wahariri na wamiliki wa vyombo vingine vya habari pamwe na waandishi wao, ambao kazi yao itakuwa ni kukufagilia mpaka chama kitakapokupitisha ambapo hutalazimika kutumia nguvu katika Uchaguzi Mkuu kwa vile chama na Serikali yake vitakusaidia kwa nguvu zote, mpaka unaingia Ikulu!” Masurufu akakenua

    “Je,” Mkewe akahitimisha kwa swali akitabasamu “Bado tu una hofu?”

    “Hapana, sina hofu kabisa!” Alijibu Masurufu kwa moyo mweupe kabisa.

    “Kwa hiyo tunakwenda kupigana siyo? Kupigana kwa ajili ya maslahi yetu, kupigana kwa ajili ya urais wetu, kwa ajili ya kuiweka Tanzania ya sasa na ijayo mikononi mwetu siyo!”

    “Ndiyo mke wangu!”

    “Ahadi?!”

    “Ahadi!”

    “Good!” Glady akafurahi akitabasamu. Alikuwa amefaulu kumfanya mumewe arudi katika reli. Arudi kuyatazama maisha katka mwanga bora. Mwanga ambao kama utawamulika vizuri utawafanya waingie katika historia ya nchi na kuishi kama sio kukumbukwa milele. Heshima iliyo



    SURA YA PILI

    KIGOMA - 1952

    Wakati Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961, Masurufu Hussein Masurufu alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili akiwa darasa la pili katika shule ya Mkoloni. Alikuwa kijana shababi na umbile lake liliashiria kuwa atakuja kuwa jitu la miraba mine baadae. Alijaaliwa sura jamali iliyowavutia wengi ingawa mwenyewe hakulijua hilo kwa wakati huo.

    Baba yake Kepteni Hussein Masurufu alikuwa katibu Mkuu wa TANU kanda ya magharibi kanda iliyojumuisha mikoa ya Kigoma, Tabora na Rukwa. Yeye akiishi Kigoma Mjini.

    Akiwa miongoni mwa wazee wa awali wa Tanganyika walioianzisha TAA na baadae kumkaribisha Nyerere kabla hawajamchagua kuwa Mwenyekiti wake, Hussein alikuwa ameshiriki kwa kina katika harakati za kuisambaza TAA na baadae TANU, na kupigania Uhuru mpaka hapo ulipopatikana

    Kuipenda kwake TAA hakukuja bure, alijikuta akiipenda TAA kupita kiasi baada ya kuchoshwa na utawala wa kibabe na wa kidhalimu wa wakoloni wa Ujerumani na baadae Waingereza.

    Awali alikuwa chini ya wajerumani Kapteni wa meli, akiendesha meli za MV Lyemba na MV Mwongozo zilizokuwa zikitoa huduma katika ziwa Tanganyika kwenda katika nchi za Zambia, Burundi na Zaire (sasa Congo), kupitia katika vijiji vilivyopo katika mwambao wa Ziwa hilo lenye kina kirefu kuliko yote Afrika. Katika Dunia likishika nafasi ya pili baada ya lile la Bekari lililopo Urusi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa akilipwa mshahara mzuri wa wastani uliomfanya awe na maisha mazuri tofauti na wananchi wengi ambao walikuwa hawaishi kuwatupia lawama wakoloni kuwa hawafai hawafai.

    Yeye akiwa na kisomo cha darasa la nane, kilichomuwezesha kuzijua lugha za kingereza, kijerumani, kigiriki na kiitaliano sawasawa, mke mzuri, nyumba bora, mshahara wa kutakata na mengine mengi, kamwe hakuona ubaya wa wakoloni mpaka ilipofika siku ile.

    Siku ambayo alikuwa anakabiliwa na safari ya kwenda Zambia na baadae Zaire. Kama kawaida alijilawa asubuhi na mapema na kuelekea bafuni. Aliporudi mswaki ukingali mdomoni na taulo likiwa mkononi ndipo mambo yalipoanza kuwa mambo.

    Mkewe ambaye alikuwa mjamzito mwenye mimba ya miezi nane na ushei alikuwa akigaa gaa huku na huko kitandani mdomoni akiachia mayowe yaliyoashiria kuwa alikuwa ndani ya Uchungu uliopatiliza

    Taulo likatupwa kushoto mswaki ukindondoka mdomoni bila yeye kuwa na habari akakimbia kimbia hovyo mle ndani akishika hiki na kile bila uelekeo maalumu baadae akili zikamrejea, akamjongelea mkewe na kumuuliza

    “Fatuma…. Fatuma, vipi mpenzi?!”

    “Na… na…. nahisi siku zimefika!” Akasema kwa taabu akishusha pumzi kwa nguvu. Maumivu yakamzidi katika nyonga.

    “Kwani hujaenda kliniki tena?”

    “Nilienda! Niitie gari Hussein”

    “Madaktari walisemaje?”

    “Gari Pliz, gari tafadhali”

    “Bila kujua tatizo ita…!

    “Hussein!” Fatuma akabweka kwa nguvu machozi yakimtoka kwa wingi. Hussein Masurufu akashtuka, “Naam!” Akaitika kwa woga!

    “Unataka nife?”

    “Oooh! No hapana…. Hapana mahabuba wangu nakupenda sana!”

    “Basi ita gari Upesi!”

    Wakati anainuka akayaona majimaji mazito yakichuruzika katika miguu ya mkewe. Akaogopa zaidi umakini ukimpotea akaondoka upesi akielekea sebuleni akajigonga katika mlango na kuanguka chini.

    “Shit!” Akaguta akiinuka na kuingia sebuleni.

    Akaifikia simu ya mezani na kupiga hospitali kuomba aletewe gari la wagonjwa. Baada ya kuelekeza vya kutosha, alirudi tena sebuleni kwa mkewe, akawa akiugulia pamoja nae. Ingawa huu ulikuwa uzazi wake wa kwanza, na uchungu ulikuwa ukimsumbua bado, lakini mafundisho aliyoyapata kabla hajaolewa na Hussein Masurufu yalikuwa yakingali mabichi kichwani mwa Fatuma.

    Alimuagiza mumewe amuandalie kanga na pamba za kutosha katika mkoba. Alimwambia pia amchukulie kadi ya kliniki chupa la chai na vingine vingi.

    Kutahamaki gari lilishafika

    Fatuma alichukuliwa mpaka katika hospitali ya Maweni akapokelewa na kupewa kitanda. Manesi wakimuakikishia Hussein kwamba mgonjwa wake angejifungua baada ya muda mfupi.

    Dakika kumi baadae akawa ndani ya Teksi no. 7 Peugeot 404 mali ya mzee Shaka wakieleka Kasingirima Ujiji aliko mama mzazi wa Fatuma Malilo. Ambako alifika anamzoa na kuja nae hospitali.

    Kichwa chake kikiwa hakitulii, Hussein Masurufu alirandaranda hospitali nzima bila uelekeo maalumu mpaka zilipokuja zile taarifa za faraja masaa sita baadae, kwamba mkewe alikuwa amejifungua mtoto wa kiume kwa operesheni ndogo.

    Furaha zilizomvaa hazikuwa na mfano, “Nami nitaitwa baba! Nimemzaa baba yangu! Mzee Masurufu Laiti angelikuwepo!” Aliendelea kufurahi nusunusu mpaka waliporuhusiwa kuingia wodini na yeye kukabidhiwa mtoto ambebe! Akambeba kwa furaha na bashasha, tabasamu likiupamba uso wake. Walifanana kama reale kwa ya pili

    Waliporuhusiwa na kurejea nyumbani, ndipo akili zilipomrejea Hussein kwamba alitakuwa kuwa ndani ya meli ya Liemba muda huu akiwapeleka abiria Zambia, Zaire na baadae Burundi. Ukweli huu ukafanya akiliye iingiwe na ganzi.

    Aliwafamu waajiri wake vizuri sana kosa dogo tu la kutosafisha sakafu vizuri lingeweza kukugharimu kibarua. Au wizi wa mali ya shirika wakati chombo kikiwa safarini, hukumu yake ilikuwa kutoswa baharini na kupoteza maisha yako.

    Akajifikiria yeye!

    Meli ilitakiwa kuondoa saa mbili kamili asubuhi. Inapeleka abiria. Abiria waliolipa pesa zao, pesa ambazo zinampa yeye mshahara. Mpaka muda huu saa nane mchana yeye alikuwa hajatokea bandarini

    Masaa sita mbele!

    Akajipeleka ofisini kama ambavyo mbwa hujipeleka mbele ya chatu tayari kuliwa! Yeye akiamini kwamba alikuwa na sababu ya msingi. Sababu ya kuokoa maisha ya mkewe na maisha ya mwanae.



    * * *

    waajiri wake vizuri sana kosa dogo tu la kutosafisha sakafu vizuri lingeweza kukugharimu kibarua. Au wizi wa mali ya shirika wakati chombo kikiwa safarini, hukumu yake ilikuwa kutoswa baharini na kupoteza maisha yako.

    Akajifikiria yeye!

    Meli ilitakiwa kuondoa saa mbili kamili asubuhi. Inapeleka abiria. Abiria waliolipa pesa zao, pesa ambazo zinampa yeye mshahara. Mpaka muda huu saa nane mchana yeye alikuwa hajatokea bandarini

    Masaa sita mbele!

    Akajipeleka ofisini kama ambavyo mbwa hujipeleka mbele ya chatu tayari kuliwa! Yeye akiamini kwamba alikuwa na sababu ya msingi. Sababu ya kuokoa maisha ya mkewe na maisha ya mwanae.



    * * *

    Hussein hatakaa aisahau siku ile. Maana alimkuta mwenyeji wake Meneja uajiri akiwa mwekundu amefura kwa hasira. Hakupewa hata nafasi ya kusikilizwa, alitupiwa barua ya kufukuzwa kazi akingali mbali wa hatua tano hivi toka ilipo ofisi ya Meneja.

    Maneno ya kashfa kejeli na dharau yakimfuta huku akimtimua na kumfukuza ki-mbwa kinguruwe!

    Katika mambo yote hili Hussein hakulitarajia. Kufukuzwa kazi?! Kwa staili hii? Hata kama alikuwa na makosa bado alikuwa na haki ya kusikilizwa, haki ya kuachishwa kistaarabu na mengine mengi. Ni hili lililomfanya asiondoke licha ya matusi na kashfa alizopewa.

    “Tokah!” Von Duzy Meneja uajiri akaunguruma “Toka unasuburi nini? Sitaki uingie ofisini kwangu wala sitaki kukuona hapa teena. Tokah!”

    “Ungenisikiliza kwanza lakini!”

    “Eti nini?” Kicheko cha Uchungu kikamtoka Von. “Sikiliza wewe Sokwe mweusi usiye na mkia. Baada ya hasara yote uliyotutia bado unataka tukusikilize? Umefanya tuingie gharama ya kumkodia mtu ndege kutoka Zambia aje apeleke meli? Tumekupigia simu hupatikani tumekuja nyumbani kwako haupo, la hapana wako wengine wa kuvumilia sio sisi. Tokaah!”

    “Ndio, ungenisikiliza sasa!”

    “Sitaki, tokaah!”

    “Nilikuwa na matatizo…!”

    “Tokaah!”

    “Mke wangu ame…!”

    “Tokaah!”

    “Lakini…!”

    “Tokaah!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hasira zikaanza kumpanda Hussein. Mikono ikanza kumchezacheza hali akili yake akishindwa kuidhibiti sawaswa. Naye akabweka!

    “Sitoki! Sitoki sasa!”

    Von akageuka na kumtazama vizuri, zaidi akimshangaa. Hussein akaendelea

    “Kama mnadhani kunifukuza ndio tumemalizana mnakosea. Nimekuwa mfanyakazi wenu kwa karibuni miaka 10 sasa. Bado nina wadai haki zangu nyingi tu, tena za msingi kabisa.”

    “ Haki?” Von akauliza kama ambaye hakulisikia vizuri neno lile.

    “Ndiyo haki!” Hussein akaunguruma tena.

    “Haki gani?”

    “Kwanza mafao, nataka nipewe pesa zangu za kiinua mgongo!”

    “Oooh!” Alikuwa Von kwa dharau, kumbe unataka haki; ngoja nikuletee. Von akavuta hatua ndefu ndefu mpaka pale aliposimama Hussein. Alimpofikia tu bila kuchelewa akaupeleka mkono wake kushoto na kuurudisha kwa nguvu, ukatua vizuri sana katika shavu la kulia la Hussein na kulia Paah! “Ukiambiwa uwe unaelewa kenge we!” Ikawa kauli iliyosindikiza kofi.

    Kofi kali la Kelbu.

    Hussein akayumba mara mbili kwa nguvu na kwenda chini sikio lake la kulia likipiga mbinja ya kukata na shoka. Alikuwa amepigwa na kitu kama ubao vile. Shavu lote lilikuwa linawaka moto vibaya sana.

    Kupigwa?! Hussein akashangaa zaidi ya alivoumia. Hakuwa na kumbukumbu kama aliwahi kupigwa toka kule shule ya msingi ambapo alichapwa fimbo mbili tu kutokana na mwenendo wake mzuri.

    Hasira sasa zikauvaa mwili katika namna ambayo hakuweza kuihimili. Akaimuka kama zombie, akamkamata Von na kumkunja kunja huku akimsuka suka kwa nguvu kabla hajampigiza chini mara mbili.

    Pamoja na Von kujitahidi kupambana na Hussein bado alijikuta chini mara kadhaa mpaka nguvu zilipomuishia ambapo aliamua kupiga filimbi ya hatari iliyofika inatuama kunako masikio ya walinzi wake vibaraka.Wakaja mbio na kumdhibiti Hussein.

    Hapo ndipo Von aliposimama akaanza kumtandika Hussein makonde mazito mazito katika katika tumbo, mbavuni, usoni na pengine popote alipoweza kupiga. Alimtandika hasa, alimtandika kweli kweli. Kutoka hapo mashataka yakaandaliwa ombi likapelekwa kwa DC na baadae mahakamani. Kesi ikapelekwa haraka haraka, hatimaye Hussein akafungwa jela miezi tisa na kazi ngumu.

    Hakuna cha mafao, hakuna haki, hakuna kusikilizwa, hakuna kila kitu na kifungo juu.

    Alipotoka kifungoni, kila kitu kilikuwa kimebadilika! Kila kitu. Alikuwa amepoteza kazi, wamefukuzwa katika nyumba ya Shirika mwanae alikuwa na afya mbaya huku akiwa hana uhakikia wa chakula; Hali wajerumani wakiwa wameondoka tayari na nafasi yao kuchukuliwa na Waingereza. Ni hili lililomfanya awachukie wakoloni.

    Akaapa kupambana nao.

    Kupambana kwa hali na mali. “Ni aibu kutawaliwa!” Aliropoka mara kwa mara akiwahamasisha wenzake kuungana pamoja ili kumtia adabu Mjerumani, “Umoja ndiyo nguvu yetu. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu!” Aliendelea kuhamasisha. Watu wakaendelea kumuunga mkono.

    Halafu akasikia kitu

    Kwamba akina Abdulwahid Sykes, Dossa Aziz Dossa na Tewa Said Tewa walikuwa wameanzisha chama, Tanganyika African Association TAA. Chama cha kudai na kupigania uhuru. Zilikuwa zaidi ya habari njema. Haraka akaruka hadi Pwani akaeleza dhamira yake na kupokelewa kwa mikono miwili akapewa kanda nzima ya magharibi ahangaike nayo.

    Akarejea nyumbani na kuhangaika nayo.

    Hata Nyerere alipojiunga na TAA baada ya juhudi zake na wenzake za kuanzisha chama cha kupigania Uhuru wa Tanganyika yeye na wenzake kule Makerere kukwama, alikuta wakina Hussein wameshafanya kazi kubwa hasa. Kazi ya kutosha kama sio kujivunia.

    Kwa sababu ya usomi na uwezo wake wa kujenga hoja, kushawishi wachilia mbali Busara na hekima alizokuwa nazo, Nyerere akapewa Uongozi mara moja katika mkutano uliofanyika Tarehe 17 April 1953 katika ukumbi wa Arnatouglo; huku waanzilishi wakikaa pembeni kwa hiyari yao. Wakibakia kuwa washauri. Na hatimaye ikaundwa TANU badala ya TAA chini ya Nyerere.

    Na matunda yakaonekana. Ghafla TANU ilivuma na kupaa kama dege la kivita. Kila mmoja aliisikia. Kila mmoja akaipenda kuitamani, kuikubali na kuihubiri. Nchi ikawa haitawaliki kwa raha. Kila mara, kila mahali ikawa ni kelele za Tunataka Uhuru! Tumechoka kutawaliwa!

    Wakati huu akiwa anatawala Muingereza hali ilikuwa mbaya zaidi, watu walipigwa na wengine kuuawa wakidai na kuulilia Uhuru, wakiupigania ujamaa na kujitegemea wakiuhami umoja na mshikamano hadi ilipofika ile siku.

    Siku ambayo Nyerere alisimamama katika baraza la Udhamini la la Umoja wa Mataifa pale New York Marekani na kuuhutubia Ulimwengu. Akawaambia Waingereza sasa inatosha! Mmeshatutawala kiasi cha kutosha, Tunataka nchi yetu, Tunataka Uhuru!

    Kama mnadhani kwamba hatuna uwezo wa kujitawala mmekosea sana. Tupeni nchi yetu kisha mje kuitazama tena baada ya miaka kumi tu. Mtaona jinsi tutakavyokuwa tumeboresha huduma, mtaona tutakavyokuwa tunaishi kwa upendo, amani na mshikamano, mtayaona matunda matunda ya uhuru wetu, mtaona… mtaona!

    Nyerere akasema mengi na vingi. Hotuba yake ikamvutia na kumsisimua kila mmoja. Mmoja wapo akiwa Malkia wa Uingereza. Huyu aliamua kumtembelea Nyerere jioni yake Akamsaili hili na kumuuliza lile. Akapokea maelezo timilifu yaliyomtosheleza. Mpaka anaondoka, moyo wake ulikuwa safi na usio na chembe cha shaka juu ya Tanganyika.

    Hatima ya mkutano huo ikawa ni Nyerere kurejea tena Uingereza kwa mara kadhaa na aliporudi kwa mara mwisho, Uhuru wa Tanganyika ukawa umepatikana.

    Kila mmoja hakuamini. Kila mmoja alifurahi kupita kiasi. “Hatimaye!” watu walinong’ona baada ya kuona bendera ya Mwingereza ikishushwa na kupandishwa ya Tanganyika “Mwingereza amesalimu amri! Shenzi taip!” walihitimisha.

    Miongoni mwa watu ambao hawakujiweza kwa furaha alikuwa Kepteni Hussein Masurufu. Yeye alicheka mpaka nguvu zikamuishia. Akacheka mpaka machozi yakamtoka.

    Aliitamani alie, apae juu hadi juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro akaitangazie dunia kuwa wamefaulu kuirudisha nchi mikononi mwa watanganyika, akatamani laiti angeweza kufyatuka atoke mbio aende mpaka kule bandarini ili akampashe yule bwege, gabachori wa kijerumani Von. Kwamba nchi imerudi mikononi mwa wenye nayo, wananchi! Na kwamba afungashe kila kilicho chake arudi kwako.

    Hakuweza kufanya lolote kati ya hayo, na hii ilikuwa ni baada ya kujikumbusha kuwa Wajerumani walishaondoka kitambo. Akaishia kucheka tu. Alicheka na kucheka na kucheka. Watu walipomuulizia jibu lake lilikuwa moja tu “Yako wapi?

    Wangemuulizia zaidi angeanza kuimba ule wimbo maarufu wa uhamasishaji “Wako wapi waliowakijigamba sasa twawataka! Tumekwisha kuwakanyagaa..!”

    “Huu Uhuru unatufanya tuwehuke sasa!” Mmoja alihitimisha wakiondoka.



    * * *

    Akiwa amekwishakuwa mwanasiasa mzoefu, Kepteni Hussein Masurufu alikataa tena kurudi kuendesha meli, kazi aliyokuwa akiifanya awali. Hili lilijiri wakati kamati kuu ya TANU, ilipoketi chini ya Uenyekiti wa Rais Nyerere na kuamua kipi kiende wapi baada ya Uhuru.

    Kwa kuzingatia historia yake na mchango wake katika chama, Hussein alikuwa amepewa kuisimamia Bandari ya ziwa Tanganyika. Akawashangaza watu pale alipokataa jukumu hilo. Alipotakiwa kutoa sababu zilikuwa tele, kwamba ameshazoea harakati, kwamba umri ulikuwa unaanza kumtupa mkono na hadhani kama angeweza kuhimili mikikimikiki ya Bandari. Akataka aendelee kuwa Mwanasiasa.

    Ni hapo alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa TANU kanda ya magharibi ili aendelee na siasa. Aendelee kufanya ile kitu roho yake inapenda. Aliifanya kazi hiyo kwa miaka michache kabla hajateuliwa kuwa Katibu Tawala wa kanda ya magharibi, wadhifa aliondelea nao hadi alipostaafu miaka mingi baadae.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Masurufu angali anakumbuka vizuri sana.

    Kwamba kitendo cha baba yake kustaafu kilikuwa kama kukata mzizi wa mwisho wa mawasiliano baina yake na TANU na viongozi wa Serikali.

    Vile alikuwa kiongozi bora na siyo mtawala, vile alikuwa mkweli wa maneno na vitendo, vile ambavyo alichukia ubepari na kukataa kujilimbikizia mali kama walivyo Nyerere, Kawawa na wengineo, Kapteni Hussein Masurufu alijikuta hana pa kushika.

    Hakuwa amejilimbikizia mali, rasilimali pekee aliyokuwa nayo lilikuwa shamba la michikichi la ekari tano ambalo ndani yake kulikuwa na kibanda cha kuishi kilichokandikwa tope na kuezekwa Bati huko katika mashamba ya Ruwanda kando kando ya mto Luiche.

    Baada ya kustaafu na kutoka katika nyumba za shirika la nyumba la Taifa pale Mwembetogwaalikokuwa amepangiwa, Hussein Masurufu alikwenda kuishi katika kibanda hicho yeye na familia yake. Wakati huu mwanae Masurufu alishakuwa mkubwa akielekea kunako balehe, sasa akiwa anasoma middle school.

    Maisha mapya baada ya kustaafu katika viunga hivi vya mto Luiche yalikuwa mabaya na yaliyoumiza sana waliishi kwa kutegemea kilimo ambacho nacho hakikuwa msaada wa kujivunia.

    Hali ikiwa hivi kwa upande mmoja upande, upande wa pili mafuriko hayakuwaonea huruma hata kidogo, yaliwajia mara kwa mara na kusomba mazao kama sio mifugo yao. Yalisomba hata akiba ya chakula walikuwa wamehifadhi ghalani kwa ajili ya baadae.

    Nguvu zikiwa zimeanza kumtupa mkono, Hussein kwa msaada wa mwanae Masurufu alifanya kila alichoweza kutaka kuonana na viongozi wa TANU ili wafikishe kilio chake makao makuu ambako wangeweza kumsaidia.

    Jibu alilopewa mara zote lilimtia matumaini

    “Suala lako linajulikana na linashughulikiwa njoo mwezi ujao, kila kitu kitakuwa sawa!” Sekretari angemjibu lakini angekuja tena huo mwezi ujao jibu hili hili lingekuwa linamsubiri tena. Mara hii alipojibiwa tena hivi mwanae Masurufu hakukubali “Lakini mwezi uliopita ulituambia hivyo hivyo” akakumbusha kwa hasira.

    “Mimi nakueleza nilichoambiwa!” Alikuwa Sekretari wa Mwenyekiti kijeuri kabisa.

    “Ndio maana nimekwambia leo tunahitaji kumuona. Vyovyote iwavyo lazima tumuone. Hatutaondoka hapa hadi tumemuona!”

    “We bwana ni kiziwi, hayawani au kitu gani?” Sekretari akauliza kwa karaha akiacha kujipodoa kwa muda na kumtazama Masurufu kwa jicho kali. Akaendelea, “Nimekwambia Mwenyekiti hayupo mwezi wa pili huu. Anahudhuria semina za Utawala bora kule Ngurdolo! Semina zitachukua mwezi mzima!”

    “Basi tumuone Katibu mkuu!”

    “Hayupo pia! Wameondoka pamoja!”

    Kitu fulani kikamfanya Masurufu ashindwe kuondoka hapo, akimtazama baba yake, akifikiria shida walizonazo kule shamba na yale mafuriko ya wiki iliyopita ambayo yaliwachukulia akiba yote na kuwaachia roho zao katika tundu la sindano baada ya wao kuparamia paa la nyumba, akaona leo hawezi kuondoka mpaka kimeeleweka.

    “Kwa hiyo?” Akauliza tena. “Shughuli za hapa kwa wakati huu anazifanya nani? Au wameondoka na ofisi yao?”

    Jicho alilotazamwa lilitosha kuwa jibu.

    “Si nimekuuliza dada yangu!”Akakazania.

    “Anakaimu Mapunda! Program 0fficer!”

    “Tunaomba tumuone huyo huyo, pengine hujui tu. Lakini wenzio tuna tatizo na kuendelea kwenu kutupiga kalenda kunatuumiza zaidi.”

    “Naye hayupo! Msubiri pale katika benchi la ofisi yake.”

    Alipomaliza kuwaambia hivyo akageukia kioo chake na kuendelea kujipodoa! Hussein na mwanae wakaenda na kuketi.

    Mapunda aliingia ofisini saa tisa mchana. Alikuwa na haraka mno. Akawasikiliza kidogo na kuwaambia, “Suala lenu linashughulikiwa! Njooni wiki ijayo!”

    Hussein ambaye wakati huu hakuwa muongeaji sana alimtuliza mwanae na wakaondoka na kurejea shambani kwao. Njiani alisononeka sana kutosikilizwa, thamani yake kutoonekana na vibinti vidogo vidogo kutomtambua na kumdharau kana kwamba alikuwa si lolote si chochote.

    Masononeko hayo na hali halisi ya maisha waliyoishi vilimchosha, kumuudhi na kumuumiza sana mwanae Masurufu. Akajikuta anaanza kukichukia chama, Serikali na viongozi wake.

    Binafsi hakuona ni vipi chama kilishindwa kutengeneza mifumo ya kuwasaidia watu waliojitolea jasho na damu katika kupigania kufikisha chama hapo kilipofika. Hakuona ni vipi walishindwa kumjengea mzee wake nyumba ya kisasa, kumpa gari ya kutembelea na nyenzo zingine za kuboreshea maisha katika wakati huu ambapo nguvu zilikuwa zimemtupa ukweli wa kumtupa.

    “Bahati yake!” Hussein alimsikia mwanae akiropoka kwa bahati mbaya, mara tu walipomaliza kujenga zizi jingine. Akamsaili kwa macho na kugundua kwamba ingawa Masurufu alikuwa jirani yake pale alipoketi juu ya mtumbwi; lakini alikuwa maili nyingi nje ya pale kifikra.

    Ilikuwa ni katika wakati huu Hussein alipopata fursa nyingine ya kumwangalia mwanae vizuri. Alikuwa kijana barobaro hasa, videvu vikianza kuchomoza kidevuni misuli iliyokaidi kukaa vizuri katika mikono yake ilikuwa imevimba na kutokeza hapa na pale katika mikono yake na kuashiria kitu kimoja tu, kuwa itakuwa mikono yenye nguvu.

    Ile sura ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imeanza kuachana na ujamali, sasa ilikuwa imerandana na ya kwake ikiashiria upole na utulivu siku zote. Kifua kipana na mwili wa wastani, upole, utaratibu, busara na hekima vilimfanya Hussein atabasamu tena. Alikuwa amejizaa “Bila shaka litakuwa jitu la miraba minne”





    ni katika wakati huu Hussein alipopata fursa nyingine ya kumwangalia mwanae vizuri. Alikuwa kijana barobaro hasa, videvu vikianza kuchomoza kidevuni misuli iliyokaidi kukaa vizuri katika mikono yake ilikuwa imevimba na kutokeza hapa na pale katika mikono yake na kuashiria kitu kimoja tu, kuwa itakuwa mikono yenye nguvu.

    Ile sura ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imeanza kuachana na ujamali, sasa ilikuwa imerandana na ya kwake ikiashiria upole na utulivu siku zote. Kifua kipana na mwili wa wastani, upole, utaratibu, busara na hekima vilimfanya Hussein atabasamu tena. Alikuwa amejizaa “Bila shaka litakuwa jitu la miraba minne”

    Akanong’ona, akiendelea kumuangalia mithili ya msanii anayeangaliwa kazi bora kabisa aliyoifanya kwa mikono yake.

    Halafu wazo likampata. Itakuwaje mwanae akiwa mwanasiasa, kama yeye? “Bila shaka na yeye ataishia katika maisha haya!” Akawaza kwa uoga akijitahidi kuyafukuza mawazo haya.

    Lakini ikamshangaza mawazo haya yalipoonyesha ukaidi, yakarudi kumtembelea tena tena. Katika mawazo haya alimuona mwanae katika picha na vyeo vya kisiasa. Ubunge, Uwaziri na kadhalika, akipitia huku na huko akifanya mambo makubwa kama akina Nyeree, Kawawa, Sokoine, Karume na wengine.

    Vyombo vya habari vikimsimulia kama kiongozi wa mfano, mtu wa watu kama baba yake, akialikwa huku na huko kufanya shughuli za kijamii zenye tija. Akiwa havumilii uozo wa aina yoyote, hana tamaa ya utajiri, muadilifu, mwenye kukubali matakwa ya jamii, mtu wa watu n.k.

    Huku yeye Kapteni Masurufu wakati huo licha pengine ya umri wake kuwa umeenda sana akisimama kidete kumshauri kufanya haya na yale, historia yake ikiendelea kudumu masikioni mwa watu kupitia kwa mwanae Neema iliyoje! Fahari iliyoje? Akawaza tena tabasamu lake likikomaa zaidi.

    Bila shaka, akaendelea kuwaza kwa furaha hali tabasamu likiwa bado limeupamba uso wake. Nchi itakimbia vibaya sana. Utendaji wake utawaambukiza vijana wengi kama sisi tulivyoambukizwa uadilifu na Nyerere, na hapo Tanzania itaelekea moja kwa moja katika nchi ya maziwa na asali bila wasiwasi wowote tena…CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Bahati yake!” Sauti ya mwanae ikatoka tena kwa ukali ikayakata mawazo yake. Akaacha kuwaza na kumtazama Masurufu kwa mara nyingine tena. Bado Masurufu alikuwa mbali kifikra. Akamsogelea taratibu na kuketi jirani yake. Akamtikisa mwanae taratibu, akimuuliza.

    “Bahati yake nani?”

    Mwanae akashtuka na kutaharuki “Hapana!” Akasema kwa hofu na kuongeza “Hakuna kitu!”. Hussein akamkazia macho na kumsaili tena

    “Kwani nani amesema kuna kitu?”

    Masurufu akababaika asijue mzee wake amekusudia nini hasa Akajikusuru “Si wewe umeniuliza?”

    “Ndiyo nimekuuliza, Bahati yake nani? Sijakuuliza kama kuna kitu!”

    Masurufu akashindwa kujibu. Mzee Hussein akaendelea “Mara mbili nimekusikia ukitamka kwa dhati bahati yake! Tena ukiwa hatua nyingi nje ya hapa kifikra. Ndio maana nikaona nikurudishe tusadiane kufikiri usiumize kichwa peka yako mwanangu!”

    Masurufu akatahayari.

    Akashangaa jinsi alivyokosa umakini hata akaruhusu maneno kutoka nje ya kinywa pasipo ridhaa yake. Hakujua ametamka mangapi akiwa katika hali hiyo. Hata hivyo akajikakamua na kusema “Leave it baba, yaache tu. Hayawezi kukusaidia!”

    “Kwa nini?”

    Akashusha pumzi. “Nahisi kama ni ya kijinga. No! yaache kama yalivyo baba!”

    “Masurufu!” Hussein akaita kwa upendo. Mwanae akaitika “Naam!”

    “Umeanza lini tabia hii?”

    Masurufu akatatanishwa, akainua uso na kumtazama baba yake. Akajikuta akitazamwa mfano wa fundi aingaliavyo saa ya thamani kutafuta tatizo liisumbuavyo. Akashindwa kuyakabili macho ya baba yake na kuangalia chini haraka.

    “Tabia gani?” Akauliza kwa sauti isiyo yake!

    “Ya kunificha mambo yako?”

    “Kukuficha mambo yangu? Mambo gani baba?”

    “Mambo yako ndiyo!! Mara hii umesahau kwamba mimi ndimi baba yako, rafiki yako mpendwa na mwandani wako pekee. Ambaye daima nimeondokea kuwa mshauri, kiongozi na msiri wako mkuu. Ulidiriki kuniambia hata habari za Glady msichana ambaye ungependa awe mkeo baadae! Mbona hayo hukutaka niyaache yalivyo?! Halafu ujinga unaoweza kukutoa mbele yangu na kukupeleka maili nyingi nje ya hapa, ni ujinga ambao kila mzazi mwenye mwanae angependa kuusikiliza. Au ndio umekuwa sana siku hizi?”

    Masurufu akajiona mwenye hatia.

    “Mimi najua!”Aliendela kushutumu mzee Hussein “Najua lipo jambo. Tena jambo kubwa, jambo linaloitafuna akili yako kiasi hata cha kuondoa kama sio kuathiri umakini wako. Na kwa taarifa yako mimi ninamjua sana Mwanangu Masurufu. Huwa hapotezi umakini kizembe.

    Toka ulivyomaliza kazi niliyokutuma na wewe kuketi juu ya mtumbwi huo, nimekuwa jirani yako nikikuangalia na kufuatisha kila akitendo chako, ambapo nimegundua mengi tu! Ndio maana nakuuliza umeanza lini tabia hiyo?” Akahitimisha Hussein.

    Hatia zikamuelemea Masurufu, machozi yakamtoka. Akainuka na kwenda kupiga magoti mbele ya baba yake. Huku machozi yakiendelea kumtoka akamwambia kwa majuto.

    “Samahani baba, nimekosa!”

    Baba yake akamuinua pale chini na kumketisha jirani yake kwa upendo uliotukuka. akamfuta machozi huku akinong’ona “Haina haja ya kulia! Usilie kijana wangu. Kulia ni tukio la mwisho unaloweza kufanya baada ya kutokea kitu ambacho hukipendi na jitihada zako zote zimeshindwa kukizuia.

    Mimi na wewe hatujafika huko bado tukingali tuna nguvu nyingi uwezo mzuri wa kufikiri na njia nyingine mbadala. Tafadhali yahifadhi machozi yako leo, ili siku utakapoyahitaji uweze kuyatumia kikamilifu sawa?” Akatua na kumeza mate

    Masurufu akaafiki kwa kutikisa kichwa

    “Good!” Baba yake akasema kwa furaha “Sasa niambie huyo unayemwambia bahati yake ni nani?”

    “Nyerere!” Masurufu akajibu pasipo kutafuna maneno

    Ilikuwa sawa na nyundo iliyogongwa katika kichwa cha Kapteni kwa nguvu, Akahisi akipepesuka mithili ya bondia aliyepigwa konde la maana jukwaani. Akauliza kwa mshtuko.

    “Umesema nani?”

    “Nyerere! Julius Kambarage. Baba wa Taifa la Tanzania!” Masurufu alirejea jibule kwa sauti thabiti. Safari hii akimtazama baba yake usoni, kuashiria kwamba alikuwa na uhakika na anachokinena.

    “Kwa nini?” Mzee Hussein akasaili kwa macho.

    Jibu la Masurufu kwa baba yake likawa kuyasaili mazingira wanayoishi kwa macho. Ile nyumba ya tope ya vyumba vinne na sebule mbili ambayo iliezekwa bati ndiyo kilikuwa kitu pekee cha thamani.

    Vingine viivyofuatia vilichusha na kuudhi. Zizi bovu la ngo’mbe na mbuzi ambalo halikuwa na mifugo ya kujivunia, mabanda ya kuku ambayo nayo yalikuwa matupu baada ya mafuriko kuwachukua. Ghala lisilo na kitu, Mashine ya kukamulia mafuta, michikichi michache isiyo na afya na pengine siha ya kuridhisha pamoja na kutokuwa na uhakika vilikwisha baadhi ya vitu vilivyoyafanya mazingira yao kuwa duni hasa, duni kwa maana halisi.

    Kamwe maisha haya hayakumstahili mtu aliyepigania uhuru kwa jasho na damu yake. Hayakumfaa hata kidogo mtu aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama na katibu Tawala wa Kanda ya magharibi katika Serikali ya wamu ya kwanza. Hayakumstahili hata kidogo.

    Ilikuwa ni baadae sana Masurufu alipoanza kueleza

    “Chama kimekutelekeza baba, Serikali hali kadhalika. Jinsi ulivyokitumikia na kukitendea sivyo kinavyokutendea wewe. Nimefikiria sana baba, halafu nikajaribu kubashiri mwisho wa maisha yetu nikagundua utakuwa mbaya na unaodhalilisha kama sio wa kuabisha.

    Ni haya yanayoyonifanya nikione chama na Serikali katika jicho hasi, ambalo daima dawamu huwa halivutii hata kidogo. Na bahati yake alivyoufuta upinzani na vyama vyake. La sivyo mimi ningejiunga na upinzani, nikashirikiana na akina Kasangatumbo, Kasela Bantu, Kambona na wenzao kuwaeleza wanachi ukweli hata wakauona ubaya wa chama na Serikali yake. Ningekuwa na mifano hai Mingi wewe ukiwa mmoja wao!”

    Hussein akatabasamu

    Mwanae alikuwa anaanza kuiva kisiasa. Uwezo wa kuunganisha mambo na mazingira, na kisha kuufanyia uchambuzi mzito, ulikuwa unalithibitisha hilo vizuri kabisa. Kwa upande mmoja akauhusudu upande huu, lakini kwa upande mwingine hakuvutiwa na njia aliyotaka kupita mwanae. Njia ya chuki dhidi ya Nyerere na Serikali yake. Chuki dhidi ya chama tawala.

    Hapana ninahitaji kufanya kitu. Akajiambia akimwambia mwanae.

    “Penginse uko sahihi mwanangu, pengine hauko sahihi. Ninachotaka kukwambia ni hiki, humjui Nyerere mwanangu. Humjui baba wa Taifa na katika hili kumlaumu au kumchukia ni kumuonea bure.

    Mimi nimefanya kazi na Yule mtu. Ni mtu muadilifu mfano hakuna, msikivu, mtulivu na mwaminifu hujapata kuona. Mtu anayewatazama wenzake kwanza. Anayeitazama nchi yake kwanza! Sisi ametulea hivyo na ndio maana unaona hatukujilimbikizia mali japo uwezo huo tulikuwa nao.

    Mali hizo tuliwawekea ninyi, nanyi mnatakiwa kuzitunza kwa manufaa ya vizazi vyenu. Unachosahau ni kwamba, Nyerere sasa ni kiongozi wa juu kabisa nchini. Ana watu na matatizo mengine mengi ya msingi. Na tena usisahau kuwa mimi ni mwakilishi wa kanda moja tu ya magharibi.

    Wapo wa kanda ya mashariki, kanda ya kati, kanda ya Nyanda za juu kusini, kanda ya Kaskazini na kanda ya pwani. Na kote kuna watu zaidi ya mmoja, ukisema aboreshe mazingira ataboresha mazingira ya wangapi? Na rasilimali za kufanya hivyo ziko wapi hali unajua kuwa nchi yetu ni miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani?

    Mbona mie tayari nimepewa kiinua mgongo? Nimejenga na kufuga ingawa Mungu hakupenda. Nadhani kutokuwa na uhakika wa maisha ya kesho kunatokana na sisi kutokuwa na kazi. Unaonaje nikikutafutia kazi mwanangu?” Akahitimsha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hakuna taabu!” Masurufu akakubali akitafakari maelezo ya baba yake. Alikuwa na hoja, ingawa haikuwa na nguvu kiasi kile. Kama Serikali inaweza kuwahudumia makatibu Kata, Tarafa, Wakuu wa wilaya, Mikoa, Wabunge, Mawaziri, Waalimu, Wanajeshi na wengineo, inashindwaje kuwaangalia hawa wapigania Uhuru? Ambao idadi yao haifiki hata mia mbili?

    Eti kiinua mgongo! Akawaza kwa hasira. Kiinua mgongo gani ambacho kimeshindwa hata kuigharamia elimu yangu hapa hapa nchini? Hivi wabunge na mawaziri nao wanalipwa kiinua mgongo kama hiki. Kama sio ugawaji wa rasilimali za taifa usiozingatia jinsia ni nini? Katika hali hii unawezaje kukiita kiinua mgongo?! Hapana hiki ni kiua mgongo kabisa.

    Na je, hivi yeye Nyerere anaishi maisha kama haya ya Hussein Masurufu kule Ikulu? Mjadala ulikuwa mkali sana kichwani mwake. Na aliufanyika kichwani mwake kwa vile alimjua vizuri baba yake, kwamba Demokrasia ilikuwa imemuingia hadi katika mishipa ya damu yake na kuweka hifadhi ya kudumu ndani ya mifupa na chini kabisa ya moyo wake.

    Kubishana na huyu ni kujisumbua. Akaamua kukubaliana nae kwa nje huku ndani akimpinga vibaya sana. Bahati yake hakuna upinzani! Masurufu akarudia kuwaza tena, baada ya kukubaliana na mzee wake, na mzee huyo kuondoka. Kungekuwa na upinzani imara ningejiunga na kumuondolea mbali! Akahitimisha.



    * * *

    Wiki iliyofuata walirudi tena ofisi za chama pale mkoani Mapunda akawapokea na kuipeleka shida yao kwa Mwenyekiti. Mwenyekiti naye akuwazungusha kwa siku kadhaa mpaka Masurufu alipomlilia machozi ofisini. Ambapo alisutwa na dhamira akajikuta akimshughlikia kikamilifu, wakapata fedha za kutosha kiasi.

    Pesa ambazo, Hussein alizitumia pia kama nauli kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kwenda kuonana na Nyerere!

    Walipokelewa vizuri sana, na kupelekwa nyumbani ambako waliandaliwa chakula cha maana. Chakula maalumu wakala na kusaza kama vile haitoshi wakaletewa hiki na kile na mradi tu wajisikie wako nyumbani.

    Jioni Nyerere alirudi, akaketi na kuzungumza pamoja nao. Kapteni Hussein alimueleza maisha anayoishi sasa na jinsi alivyo na taabu. Machozi ya uchungu yakamtoka Nyerere.

    “Pole sana!” Akamwambia kwa upendo “Kwanini hukwenda pale makao Makuu na ukawaeleza yako?”

    “Nilikwenda lakini sikupolewa vizuri. Nimezungushwa karibuni miezi sita!”

    “Kitu gani?” Nyerere akaghadhibika

    Hussein Masurufu akamueleza kila kitu tokea walivyoanza kufuatilia, dharau walizoonyeshwa, ahadi za njoo kesho na mengine kadha wa kadha hadi pale walipompigia magoti na kumlilia Mwenyekiti ofisini kwake ambapo aliidhinisha pesa kidogo walizopewa.

    Kilichofuatia hakuna aliyekitarajia.

    Kwa kutumia simu,Nyerere alimuauru Katibu Mkuu wa TANU Taifa kuushughulikia Uongozi wa mkoa Kigoma kwa vitendo walivyomfanyika Kapteni Hussein na familia yake, akaomba kupewa taarifa zake ndani ya wiki moja

    “Mie sitapenda uwafukuze kazi?” Hussein alimwambia baadae Hasira zilipotulia. Nyerere akamtazama kwa mshangano, kabla hajamuuliza baadae.

    “Kwa nini?”

    “Ningependa waonywe tu, ili kama watarudia tena, ndippo hatua hizo zichukuliwe maana wana familia zinazowategemea! Kuwaondoa pale itawafanya wao na hasa familia zao kuishi katika wakati mgumu na m’baya zaidi!”

    Nyerere akatafakari tena akishangazwa na moyo wa mtu huyu.

    Hata hivyo alitabasamu alipoona kuwa falsafa yake ya Ujamaa na lile azimio la Arusha vilikuwa vimewakaa watu wake katika namna iliyomfanya hata wakati mwingine awaogope. Walikuwa na huruma mno! Wakawa na upendo uliopitiliza huku wakiiweka nchi na raia wao mbele.

    Pamoja na ukweli kwamba wao walikuwa washika wadau wakuu, walihakikisha washikiwa dau wengine hasa jamii wamenufaika vya kutosha ndipo na wao walipofikiria kunufaika. Bahati mbaya washikiwa dau hao walikuwa wengi mno, wengi hasa! Kuwanufaisha wote ingekuwa shughuli pevu kweli kweli, pevu haswa! Kwa maana hiyo wao waliendelea kusubiri mpaka mdau wa mwisho afikiwe…, ndipo wajifikirie na wao!

    “Any way!” Akasema baadae. “Tuache hayo, tuzungumze yetu, nimemleta kijana! Nataka umsaidie kupata kazi ili naye anisaidie kuishi. Pamoja na kazi nataka pia umfundishe siasa!”

    Nyerere akamtazama Masurufu kwa muda na kutikisa kichwa. Alikuwa kama anayemuangualia Kapteni Hussein enzi za ujana wake. Akaulizia elimu yake na kuambia darasa la sita.



    Nyerere akamtazama Masurufu kwa muda na kutikisa kichwa. Alikuwa kama anayemuangualia Kapteni Hussein enzi za ujana wake. Akaulizia elimu yake na kuambia darasa la sita.

    Alipouliza sababu ya kutohitimu, jibu lilikuwa lile lile, umaskini ulioikumba ghafla baada ya yale mafuriko. Nyerere akasikitika tena.

    “Itabidi asome kwanza!”

    “Hilo silikatai, lakini kwa sasa huyu ndio mboni yangu. Namtegemea kwa kila kitu. Nilitegema mshahara atakaopewa…!”

    “Usijali!” Akamkata kalima na kuendelea “Tutafanya utaratibu uwe unapata senti za kujikimu, huyu mwache asome. Akifanya siasa huku ana kisomo atakuwa msaada mkubwa kwa taifa sawa?

    “Sawa” Alikuwa Kapteni kwa shingo upande. Hakutaka kuendelea kuwa tegemezi kwa chama na Serikali lakini alipojitahidi alisemee hili, akawa anazidiwa hoja.

    Ndivyo ilivyokuwa.

    Masurufu akarudi shule, akawa pia miongozi mwa watoto kadhaa waliokuwa wakilelewa na mwalimu. Kapteni Hussein alikaa pale kwa wiki chache kabla hajaomba ruhusa na kurejea nyumbani kwa mkewe. Juhudi za kumtaka abakie hapo ikibidi ailete familia yake zikashindikana.

    Kitu kimoja kilikuwa dhahiri kwa Masurufu.

    Kwamba mafahali wa uadilifu walikuwa wamekutana! Mazungumzo yao na mapendekezo yao kuhusu maisha na familia zao yakawa yamemfanya ajifunze kitu kikubwa maishani. Kwamba ni muhimu kuishi kwa ajili ya watu, kwa ajili ya makundi yaliyo pembezoni. Ili utakapoondoka duniani uwe umetimiza wajibu wako wa kuletwa hapa duniani. Jamii ikukumbuke na uendelee kuishi milele.

    Pia akagungua kuwa kumbe Nyerere hakuwa mtu mbaya. Alikuwa mtu mzuri kwa maneno na vitendo, akifurahia kuona mabadiliko na maendelo ya kweli ya watu wake. Lakin ah! Laiti angeliweka utaratibu wa kuonana na watu wake mara kwa mara na kusikiliza shida zao…

    Akaendelea kusoma akiongeza bidii na juhudi katika masomo.



    * * *



    Ki’ uhakika kabisa, Masurufu aliacha kabisa kumchukia Nyerere na CCM. Badala yake akampenda na kumthamini. Akawa jirani nae akimuomba ushauri huu na ule pamoja na kumsaidia kazi hizi na zile. Ni katika wakati huu Nyerere alipogundua akili na Busara za kijana huyu. Naye akajikuta akimpenda na kumuamini.

    Shule alihitimu vizuri akajiunga jeshi la kujenga Taifa baadae akaenda Chuo kikuu kuchukua Digrii ya Sayansi na utawala wa jamii miaka mitatu baadae akarudi na kuwekwa Makao Makuu ya chama ofisi ndogo pale Lumumba, akisaidia hiki na kile pamoja na kuisaidia ofisi ya umoja wa vijana.

    Hakudumu sana, akapelekwa Kigamboni kuongeza ujuzi wa kisiasa na kupelekwa nje ya nchi mara kadhaa. Aliporejea akapewa kazi ya kuwaandaa vijana kuwa wanasiasa bora, kupenda siasa ya nchi yao na kupenda kujitolea kwa ajili ya nchi yao.

    Kazi alizozifanya kwa moyo mmoja.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Matokeo yake yalishangaza kama sio kustaajabisha. Vijana wakatokea kuwa wazalendo wa kweli , wakiijenga nchi yao kwa kasi ya aina yake.

    Hali ikiwa hivi, akili ya Masurufu ilikuwa haitulii kila kukicha yeye alikuwa akitafuta mwanya wa kujilimbikizia mali, kuchuma zaidi. Hakutaka kuja kuishi kama babaye yake.

    Katika Upenzi huo baina yake na Nyerere, alikuwa amefaulu kutembelea mikoa mingi na akawa amejionea kwa macho yake namna wastaafu wengi wakiwemo mawaziri jinsi wanavyoishi maisha duni kwa kutegemea kilimo na mifugo, huku jamii ikiwacheka na kuwaona mabwege. Wakitolewa mfano usiofaa na kususuikwa hata na watoto wadogo.

    Hapana! Haya siyo maisha!! Masurufu akaamua kwa dhati. Leo Nyerere yupo, kesho atakuwa hayupo. Nisipogangamala na kuuanika katika kijua hiki, ntautwanga mbichi.

    Kweli akagangamala

    Alihubiri na kufundisha uadilifu huku yeye akifanya uhalifu. Kila ulipotokea mwanya aliutumia kikamilifu kwa maslahi yake binafsi kwa manufaa ya baadae. Kila alipotumwa mahala, hakusita kujipa majukumu ya ziada.

    Majukumu ambayo yalimkutanisha na wafanyabiashara wa magendo, wakwepa kodi, majambazi wa kalamu na wengineo. Ambapo aliwatisha na kuwaambia ametumwa na Nyerere awashughulikie. Kitambulisho chake halisi na kile cha bandia vikimtisha yeyote aliyeonyesha ukaidi.

    Naam! Alifanikiwa, akaunti na miradi yake ambavyo alivifungua kwa majina bandia na mikoa tofauti zikinenepa taratibu. Alipohisi uwepo wa msako wa wahujumu uchumi waliopenya kwenye chujio la azimio la Arusha, Upesi akazihamisha pesa zake nchini na kuzifungulia akaunti nje ya nchi.

    Bahati ikawa yake, yeye akapewa ukuu wa kuendesha msako huo. Ilikuwa neema nyingine. Waliokamatwa na kufikishwa mbele ya sheria ni wale tu ambao yeye hakuafikiana nao, au walileta ujuaji na kujifanya wajuzi.

    Nduli alipotuchokoza na mwalimu kutangaza vita, baada ya TANU kuungana na Afro-Shiraz Party na kuzaa CCM; Masurufu naye hakuwa nyuma. Alishirikiana vilivyo kumchapa nduli Amin ambaye alikimbia na kuacha vitu vingi vya thamani katika Ikulu yake.

    Yeye akiwa miongoni mwa askari wachache waliongia katika Ikulu ya Uganda na kukuta amana hizo madini yakiwemo, akajikuta akipagawa huku akiomba kimoyomoyo wagawane. Hawakugawana! Badala yake vito hivyo walimpa Masurufu avifikishe kwa Nyerere kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

    Hakufikisha.

    Waliporejea kutoka Uganda na yeye kuzifanyia utaratibu wa kuzificha na kuziingiza mali alizochuma katika mkondo halali; akawa amemkabili Nyerere na kumuomba ruhusa aende kwao akagombee Ubunge. Nyerere akamshangaa kwa uamuzi huu, akamuuliza.

    “Kwanini umefikiria uamuzi huu Dokta?”

    Aseme nini? Akawaza kwa haraka. Ndiyo kwanza akagundua kuwa hakuwa amejipanga kama angeulizwa hivi. Sababu ya kutaka kupata mshahara mnono, saluti, gari la mamilioni, posho hata ukisinzia, lita elfu moja za mafuta kila mwezi, na marupurupu mengine, hazikuwa sababu ambazo zingemvutia Nyerere.

    “Nataka kuwa karibu na baba yangu!” Akatamka baada ya kufikiri kwa muda “Nataka kuwa jirani nae. Nataka kuwapigania watu wa jimbo langu, kusaidiana nao kuboresha maisha na miundombinu yetu! Nataka… Nataka..”

    Alisema vingi na mengi! Nyerere alimsaili zaidi na zaidi kabla ya kuridhika na kumpa ridhaa. Akamuuliza tena, “Vipi vijana wako pale Umoja wa vijana?”

    “Hakutaribika kitu!” Akamjibu kwa unyenyekevu. “Nimeacha kila kitu katika mstari. Boniface ataendelea pale nilipoishia. Ni mmoja kati vijana wangu ninaowaamini. Na Kigoma sio kuzimu mwalimu nitakuwa nikirudi mara kwa mara kuangalia maendelo ya pale nilipoishia. Isitoshe kuna simu, naweza kupigiwa na kuambiwa hivi au vile nami nikatoa ushirikiano wangu!” Akamalizia.

    Ilitosha.

    Mwalimu akainama kutafakari. Masurufu ambaye sasa alikuwa Daktari wa filosofia alikuwa na sababu za msingi. Vile alikuwa kijana mwenye busara na hekima huku akifanya kazi kwa nguvu zake zote, Nyerere akajaribu kuuhisi upweke ambao ungemtawala baada ya Masurufu kuondoka.

    Hata hivyo akajirudi pale alipogundua kuwa Dokta Masurufu sasa sio mtoto tena ingawa angali alikuwa akihitaji ushauri wa hapa na pale. Ushauri utakaomfanya aendelee kuwa Masurufu halisi liwazo na chaguo la watu.

    “Dokta” Nyerere akasema akingali ameinama kwa tafakari “Sio uamuzi mbaya! Sio uamuzi mbaya hata kidogo. Bahati mbaya na mimi nang’atuka, Uchaguzi ujao sitagombea Urais wa nchi hii tena, miaka ishirini na mitano niliyokaa Ikulu ni mingi sana, inatosha. Nastaafu! Nawapa nafasi wengine.

    “Kitu gani?” Dokta akashtuka. Zilikuwa habari mpya kwake.

    “Umesikia vizuri. Ukigombea Ubunge na kushinda kisha Rais atakayeteuliwa akakuwekea katika Baraza la mawaziri, nchini itakimbia vibaya sana.

    Ni hili linalonifanya nikuruhusu kwa moyo mkunjufu. Maana hata nikiendelea kukuzuia bado unatakiwa uwatumikie watanzania wote ambao ni muhimu kuliko mimi mmoja, watanzania ambao kwa hakika wanahitaji mchango wako ili kufanikiwa. Nenda baba, nenda ukatimize wajibu wako wa kuletwa hapa duniani! Nenda!”

    Nyerere alisema mengi kumuasa Masurufu. Haikuhitaji digirii kujua kuwa Nyerere alikuwa anaumizwa na kutengana na kijana huyo. Lakini angefanya nini? Akamruhusu.

    Labda ambacho hakukijua na ambacho kilikuwa chini kabisa ya moyo wa Dokta Masurufu ni ule ukweli uliotisha. Kwamba Masurufu huyu, hakuwa yule Masurufu anayeonekana mitaani kila siku akihubiri na kutenda upendo, midomo yake imejaa maadili na macho kubeba utakatifu.

    Huyu alikuwa Masurufu mwingine chui katika ngozi ya kondoo. Masurufu mwenye pipi mdomoni hali mikono yake ikichuruzika damu. Masurufu mwenye hofu ya umaskini unaochusha na kuudhi baada ya kustaafu.

    Ilikuwa vigumu kwa Nyerere kujua. Kwani Masurufu aliyafanya haya kwa hila sana, wakati mwingine katikakati ya usiku mnene huku akiwa kilometa nyingi nje ya macho na upeo wa Nyerere. Wakati huo huo akimpeleka kuzimu yeyote aliyeonyesha kumjua na kutaka kutia mchanga kitumbua chake.

    Akaruhusiwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akijua anakwenda kuingia katika siasa rasmi, sasa Masurufu aliweza kuandaa washenga waliopeleka posa kwa mpenzi wake Glady. Majibu yalipokuja mazuri na taratibu zingine kufanyika, ndipo Masurufu Hussein Masurufu alipofunga pingu za maisha na Glady Stevenson Ombwe. Ndoa yao ilifanyikia bomani kwa Mkuu wa wilaya.



    Akijua anakwenda kuingia katika siasa rasmi, sasa Masurufu aliweza kuandaa washenga waliopeleka posa kwa mpenzi wake Glady. Majibu yalipokuja mazuri na taratibu zingine kufanyika, ndipo Masurufu Hussein Masurufu alipofunga pingu za maisha na Glady Stevenson Ombwe. Ndoa yao ilifanyikia bomani kwa Mkuu wa wilaya.



    * * *

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog