Search This Blog

Friday, 20 May 2022

FARIDA - 5

 







    Simulizi : Farida

    Sehemu Ya Tano (5)



    Saa tano na dakika hamsini usiku ilinikuta nikiwa nje ya nyumba ya kulala wageni ya Machenza, Machenza Guest House. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kwa mwendo wa taratibu, kama nilikuwa nalazimishwa nilienda hadi mapokezi. Nilikutana na Dada mmoja akimhudumia mteja. Nilisimama wima nikisubiri zamu yangu. Baada ya kuyaandika maelezo ya yule jamaa kwenye kitabu cha wateja. Alimuelekeza chumba yule mteja, hapo nami nililisogelea dirisha. Baada ya salamu nilimueleza chumba maelezo aliyonipa mwenyeji yangu niyaseme kwake. Na nilimtajia hadi namba ya chumba alichokuwemo mwenyeji wangu.

    Chumba namba nane.

    Chumba alichokuwa amepanga kijana niliyekuwa namfahamu kwa jina moja tu, Bizzo. Mhudumu alinielewa, aliniamini, aliniruhusu niende chumba namba nane huku akinionesha mahali kilipo kwa mkono. Bila shaka Bizzo aliacha salamu kwamba atakuwa na mgeni kama alivyoniambia.



    Nilitembea taratibu sana kuelekea chumba namba nane. Nilitembea huku mawazo lukuki yakija kichwani mwangu.



    "Pole sana kwa yote yaliyokukuta Nassib. Na nakwambia hauwezi kuishi kwa raha Bongo kwa hiko kisanga kilichokukuta mshkaji wangu. Cha msingi na cha sekondari hapo ni kusepa nje. Kajichimbie Bondeni huko ama hata Malawi na huyo mtoto, haya mambo yakipoa utarejea tena Bongo.." Niliikumbuka sauti ya Bizzo ikivyonambia ndani ya gari. Wakati huo Farida akiwa kajilaza magotini kwangu.



    Nakumbuka nilimuuliza "Sasa mimi nitapata wapi pesa za kuweza kunifikisha South Africa au Malawi Bizzo? Yatakiwa niwe na pesa za kutosha ili nisiende kugeuka ombaomba katika nchi za watu"



    " We mwanaume man. Ukifanya mishe utapata mpunga wa kukufikisha huko. Sasa sikia mshkaji wangu, njoo Machenza Guest house saa sita kamili usiku. Usiongeze hata sekunde moja, ni saa sita kamili usiku, ila waweza kuja kabla ya muda huo. Nitakupa mchongo, kesho asubuhi utaamka na zaidi ya milioni ishirini mkononi, utaenda nje ukiwa na pesa nzuri ya kuanzia maisha" Bizzo alisema kwa kujiamini sana.



    Kwa upande wangu, sikuwa na shida ya kwenda Bondeni au Malawi. Nilikuwa na shida ya kitu kimoja tu. Pesa.

    Nilikuwa nahitaji pesa kuliko kitu chochote kile kwa wakati ule. Sikuwa na akiba yoyote ile benki. Mkopo niliouchukua benki kwa kwaajili ya kujengea nyumba yangu uliuteketeza vilivyo mshahara wangu. Sikuwa na njia nyingine ya kupata pesa. Na sasa Bizzo ananiambia habari ya kumiliki milioni ishirini kwa mkupuo.



    "Nitakuja Bizzo. Nakuahidi nitakuja. Hebu nielekeze hiyo Machenza Guest House ilipo?"



    Bizzo alijibu akiwa na furaha sana moyoni mwake "Huwezi kupotea man, ukifika Ilulu stadium muulize msela yoyote yule, atakuelekeza mahali ilipo hiyo guest. Ni guest maarufu sana"



    Na sasa ndio nilikuwa naelekea chumba namba nane ndani ya guest ya Machenza. Chumba cha Bizzo ili kupewa huo mchongo utakaoniwezesha kupata shilingi milioni ishirini.



    Niligonga mlango mara sita. Kama Bizzo alivyonambia garini.



    "Sukuma tu uko wazi" Nilisikia sauti kutoka ndani ya chumba namba nane.



    Nilisukuma mlango kwa woga. Niliuona jinsi mkono wangu mwenyewe ulivyokuwa unatetemeka. Nikajitosa ndani. Kulikuwa na giza totoro. Sikuweza kumuona mtu yeyote yule, bila kuisikia ile sauti ya awali nisingeamini kama mle kulikuwa na kiumbe chenye uhai.

    Woga ulinizidi maradufu. Jasho la kwapa lilikuwa linanitoka mfululizo. Mikono yanitetemeka vibaya sana. Nilihisi nimeingia katika hatari. Hatari kubwa sana. Hatari ya kujitakia. Picha jinsi nilivyoagana na mpenzi wangu Farida ilinijia kichwani kwangu. Moyo wangu uliingia unabaridi, ubaridi wa majuto.



    Mara taa ikawashwa. Ndani kukawa na mwanga hafifu ulioletwa na taa ya bluu. Kwa harakaharaka niliwaona watu watatu. Mmoja alikuwa amekaa juu ya kiti cha mbao, wengine wawili walikuwa wamekaa juu ya kitanda. Cha ajabu, kati ya watu hao sikumuona mtu niliyemtarajia, Bizzo.

    Woga ulinizidi.



    "Karibu kamanda, umekuja on time" Yule jamaa aliyekuwa amekaa katika kiti cha mbao alisema.



    Sikuitikia. Sikujibu. Nilibaki kimya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jamaa mmoja aliyekuwa amekaa kitandani alianza kuongea "Umekuja muda mzuri sana mshkaji. Tumepewa sifa zako na Bizzo, na nina uhakika kwa umahiri uliouonesha huko ulikotoka waweza kuifanya kazi yetu kwa ufanisi mkubwa" jamaa aliacha kuongea. Alitoa sigara mfukoni, kisha alichukua kiberiti juu ya meza ndogo iliyokuwepo mle chumbani. Aliwasha ile sigara. Akaivuta funda refu. Aliruhusu moshi mwingi usambae mle chumbani. Akacheka kicheko cha majivuno.



    Aliendelea kuongea " Saa sita na robo itabidi uwe nje ya geti ya shule ya msingi Stadium. Ukiwa na mzigo ule" Alisema huku akiionesha 'briefcase' nyeusi iliyokuwa imewekwa chini sakafuni.



    "Saa sita na dakika kumi na sita itasimama gari mbele ya miguu yako. Itakuwa ni Toyota Prado ya rangi ya maziwa. Atatoka mtu upande wa kushoto, sio upande wa dereva, atakuwa amevaa suti nyeusi na miwani ndogo nyeupe, miguuni atakuwa pekupeku, hajavaa viatu. Utamkabidhi mzigo huo hapo uliolala sakafuni. Hatoongea neno lolote. Nawe usiongee neno lolote. Ukishampa ataondoka, nawe utarejea hapa. Nitakukabidhi milioni hamsini baada ya kufanya hiyo kazi kama nilivyokuelekeza"



    Mwengine alidakia " Sasa hivi ni saa sita kamili"



    Mwengine alimalizia " Chukua mzigo peleka, una dakika kumi na tano za kufika shule ya msingi stadium"



    Nilibaki nimesimama wima. Nikiwa sielewi. Nikiwa nimechanganyikiwa. Niifanye ile kazi ama la. Na dau lilikuwa limepanda, milioni thelathini zaidi juu ya zile ishirini alizonambia Bizzo.



    "Hapa nishaingia choo cha kike. Nilikuwa na uwezo wa kumkatalia Bizzo kabla, lakini sio watu hawa wasioeleweka" Niliwaza kimoyomoyo.



    Nikajipa moyo " Nayafanya haya yote kwa ajili ya maisha yangu na Farida. Mwanamke ninayempenda kuliko kitu chochote kile. Wacha niende niko tayari kwa lolote, na hii ni kwaajili ya Farida.."



    Niliinama na kuichukua ile 'brief case' nyeusi. Nilisikia majamaa wote watatu wakipiga magoti ya kunipongeza.



    Nilitoka nje ya chumba namba nane ndani ya nyumba ya kulala wageni ya Machenza na kuelekea shule ya msingi Stadium, nikiwa na begi langu mkononi, nilipita katika kichochoro kirefu ili kutokea katika njia itakayonipeleka moja kwa moja katika barabara itakayoweza kunifikisha shule ya msingi Stadium.



    Niliumaliza uchochoro. Nilipofika tu barabarani. Mbele ya miguu yangu lilikuwa limesimama gari ndogo ya Polisi huku ikipiga ving'ora kwa fujo. Harakaharaka walishuka askari wanne wakiwa na bunduki mkononi. Zote zilielekezwa kwangu. Nilisimama wima nikiwa na 'brief case' yangu mkononi. Nilichanganyikiwa sana...



    Ulikuwa wakati wa mashaka kuliko wakati wowote katika maisha yangu. Ulikuwa wakati wa uwoga kuliko wakati wowote katika maisha yangu. Uwoga wa kiwango cha juu. Nilitetemeka haijawahi kutokea hapa duniani. Nilitetemeka vibaya mno.



    Sikuwa na kosa lolote. Lakini sikujua ni kitu gani kilichokuwemo katika 'brief case' iliyokuwepo mikononi mwangu.



    Polisi walianza kunisogelea kwa hatua za taratibu. Midomo ya bunduki zao zote zikielekezwa katikati ya kifua changu. Sikuweza kuvumilia, sikuweza katu...Niliyahisi majimaji mepesi ya moto yakitiririka mapajani mwangu, mkojo ulinitoka bila kupenda.

    Nilijikojolea.



    Askari mmoja alinizunguka kwa nyuma. Mkono wa kulia akiwa kashika bunduki kubwa, kwa kutumia mkono wa kushoto alinikwida suruali yangu na kuninyanyua juujuu. Nilikuwa natembelea vidole. Nilitembezwa kuelekea garini, nilipokaribia gari alinibeba msobemsobe na kuniingiza garini. Nilitaka kupiga kelele, vibao viwili vya nguvu vya kiume vilitua mashavuni mwangu, vibao ambavyo vilinifanya nigugumie kama nguruwe.



    Gari lilikata kona kwa nguvu. Safari ya kuelekea kituo cha Polisi ilianza.



    Tulivyopita usawa wa shule ya msingi Stadium tulipishana na Toyote Prado nyeupe. Nilipata nafasi ya kuangalia saa yangu, ilikuwa ni saa sita na dakika kumi na sita.

    Nilifumba macho kwa hasira. Machozi yalikuwa yananitoka huku nimefumba macho, nililia kama mtoto mdogo. Kichwani mwangu nilifikiri kwamba ....nilikuwa napishana na milioni hamsini. Nilikuwa natenganishwa na Farida milele. Nilikuwa naongeza idadi ya maadui hapa duniani.... We unafikiri wakina Bizzo wangenielewa kwa kupoteza mzigo wao?



    Tulifika kituoni. Niliandikisha maelezo yangu. Huku nikiambiwa nimekamatwa kwa kosa la uzururaji. Niliandikisha kila kitu nilichokuwa nacho. Ndipo ilipobidi ifunguliwe ile 'brief case' nyeusi. Wajue kulikuwa na nini?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hofu ilinikimbilia kwa kasi na kuuvaa moyo wangu.

    Maana hata mimi mwenyewe sikuwa najua ndani ya 'brief case' kuna nini.



    Askari mmoja wa kiume aliichukua ile 'brief case'. Akaiweka mezani. Alijaribu kuifingua. Hakuweza. 'Brief case' ilihitaji kuwekwa namba za siri ili ifunguke.



    "Njoo uandike namba za siri hapa tuipekue na hii!" Yule askari Polisi alisema kwa ukali.



    Nilibabaika sana.



    Sikuwa nazijua namba za siri za kuifungua ile 'brief case' nyeusi.

    "Namba za siri za kufungulia nimezisahau" Nilisema kwa sauti iliyojaa uwoga.



    Kofi moja la nguvu lilinishukia usoni. Niliona nyotanyota nyingi sana.



    "Usilete utani hapa" Askari aliyenipiga alisema.



    "Asituangaishe hebu tuivunje tu!" Askari mwengine alisema akiwa na hasira.



    "Kachukue nyundo stoo"



    Askari mmoja alitoka nje kwenda kuchukua nyundo. Dakika mbili baadae alirejea na nyundo mkononi.

    Alianza kuigonga kwa nguvu ile 'brief case' yenye mzigo nisioujua.



    Wakati yule askari polisi akiigonga ile 'brief case' nilikuwa nimekalishwa chini, sakafuni. Nikiwa sina viatu, nikiwa sina mkanda. Nikiwa sina Farida. Nilikuwa mimi peke yangu. Mimi na woga wangu. Maana jasho la woga lilikuwa lanitiririka. Hisia zangu zilikuwa zinaniambia mle ndani ya 'brief case' hakuna jambo la heri.



    "Vunja hilo dude haraka" Askari mmoja alisema kwa sauti kubwa.



    Askari alipiga nyundo nyingine ya nguvu. Nyundo ilitua vizuri. Kila kitu kilikuwa kwake.

    'Brief case' ilianguka chini toka pale mezani kutokana na uzito wa nyundo.

    Niliona.

    Kumbe ndani ya 'brief case' kulikuwa na unga mwingi mweupe ndani ya vipakti vidogovidogo. Vipakti zaidi ya mia vikikuwa vimesambaa sakafuni.

    Ilikuwa ni Kasheshe.



    "Kumbe huyu jamaa ni Zungu la unga" Yule askari aliyeamrisha ile 'brief case' ivunjwe alisema kwa nguvu huku akinipiga bonge kofi la uso. Niliziona nyotanyota zisizo na idadi. Machozi yalinitoka vibaya sana. Nililia sana.



    "Mimi sijui kitu jamaani" Nilitoa utetezi ambao hata mimi mwenyewe sikuukubali.



    "Kelele!" Askari mwengine alinipiga teke la shingo huku akininyamazisha.



    "Mnanionea tu" Nilisema kwa uchungu huku nikiwa nimelala kifudifudi kutokana na uzito wa lile teke.



    "Unaambiwa nyamaza!" Kirungu cha kichwa kilitua kisogoni mwangu.



    Damu zilianza kunibubujika. Hakuna aliyenionea huruma. Wote walikuwa mbogo kwangu. Walikuwa wananichukia vibaya sana.



    "Umeutoa wapi huu mzigo?" Askari mmoja aliniuliza.



    "Mi sifahamu" Nilijibu nikiwa na hofu.



    "Acha ujinga wewe. Ukileta ujuaji utakufa hapahapa kaunta!" Askari mwengine alitahadharisha.



    "Umeyatoa wapi haya madawa ya kulevya" Aliniuliza tena.



    "Kwa Bizzo" Nilijibu kwa kifupi.



    "Bizzo ndio nini?" Askari mwengine alidakia.



    Niliwaeleza Polisi namna nilivyokutana na Bizzo ndani ya gari usiku wa manane. Ingawa sikuwaeleza ni kitu gani kilichonikimbiza huko Kilwa kwa sababu nilizozijua mimi.



    Baada ya maalezo yangu, na wao kuandika kila nilichoongea waliniingiza katika selo harakaharaka.

    Muda uleule gari ya polisi iliwashwa. Bila shaka kwenda kuvamia nyumba ya kulala wageni ya Machenza, kuwakamata wakina Bizzo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndani ya selo ya Polisi niliwakuta watuhumiwa saba. Wote wakiwa wamekamatwa usiku uleule niliokamatwa mimi, tena kwa kosa lilelile la uzururaji. Harufu ya oombe za kienyeji ilikuwa imetapakaa ndani ya selo. Nilichagua sehemu niliyoiona inafaa. Nilisimama nikiwa nimeuegemea ukuta.



    Nilianza kuwaza. Ingawa nilipanga kuwaza mambo mengine juu ya mustakabari wa maisha yangu, lakini mawazo hayakutaka kabisa, mawazo yangu yote yalienda kwa Farida. Niliwaza sana.

    Nilifikiria Farida atakuwa katika hali gani usiku ule kule stendi. Nilimuacha peke yake. Niliwaza sana atanifikiriaje Farida. Si atadhani labda nimemkimbia? Nimemkimbia kutokana na matatizo, roho yangu iliniuma sana.



    Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu. Sikuwahi kuingia selo katika maisha yangu tangu nizaliwe. Leo hii nilikuwa selo tena kwa kosa baya sana. Kosa la kukamatwa na madawa ya haramu, madawa ya kulevya.



    Sasa nilikuwa na msala mzito sana. Nilikuwa na msala Kilwa. Nilikuwa na msala Lindi. Nilijiona mpweke sana. Maana mimi nilikuwa ndani na rafiki yangu pekee hapa duniani, mpenzi wangu Farida, nilikuwa nimemuacha peke yake stendi.



    Baada ya saa kama mbili nilitolewa nje ya selo. Nilikutana na askari walewale niliokuwa nao mwanzo. Walikuwa wamerudi na mfanyakazi wa kike wa nyumba ya kulala wageni ya Machenza. Nilipofika tu nilikaribishwa na maswali.



    "Unatudanganya sisi?" Askari mmoja aliniuliza.



    "Nawadanganya nini jamani?" Niliuliza kwa sauti yenye uwoga.



    "Chumba ulichosema walikuwepo watu waliokupa mzigo hakijapangishwa tangu juzi. Iweje wewe unasema ulikuwepo chumba hiko usiku huu?" Askari aliniuliza.



    Macho yalinitoka pima!



    Sikuamini.



    Nilimwangalia yule mhudumu, nilikuwa namkumbuka vizuri sana, ni yeye ndiye niliyemkuta kaunta na kunielekeza chumba namba nane. Ni yeye aliyenielekeza chumba walichokuwa wageni wangu. Lakini hivi sasa naye aliniangalia kwa jicho la hajawahi kuniona hata siku moja.



    "Huyu dada unamkumbuka?" Askari mmoja aliniuliza.



    "Ndio namfahamu sana, na ndiye aliyenielekeza chumbani kwa hao jamaa...wakina Bizo" Nilijibu kwa kujiamini huku nikimwangalia yule dada, niliamini yeye ndiye alikuwa mkombozi wangu pekee kwa wakati ule mgumu.



    "We baba vipi. Una kichaaa? Sijawahi kukuona tangu nizaliwe. Ndo nakuona hapa leo. Lini ulikuja guest kwetu. Na hiko chumba unachokizungumzia akijapangishwa tangu juzi, kipo katika matengenezo" Dada aliongea katika ule mtindo wa kunisuta.



    "Sio kweli kabisa...." Nilibisha.



    "Twende nae akatuoneshe hiko chumba anachokisema nilimuelekeza" Yule dada alishauri.



    Tulikubaliana.



    Niliingizwa kwenye gari la polisi nikiwa chini ya ulinzi, nalindwa na mitutu ya bunduki kama gaidi vile. Safari kwenda katika nyumba ya kulala wageni ya Machenza.



    Tulifika.



    Mimi ndiye nilikuwa nawaongoza kuwapeleka katika chumba namba nane, chumba nilichokabidhiwa ule mzigo. Nilipokaribia nilistuka sana. Chumba hakikuwa na mlango wa kuingilia. Wakati nakumbuka ule usiku niliugonga mlango kabla ya kuingia.



    Nilifika hadi pale mlangoni. Nilisimama wima. Macho yalinitoka vibaya sana!

    Chumba hakikuwa na kitu hata kimoja. Huku sakafu ikiwa imetibuliwa.

    Nilihemwa.

    Nilianza kulia kwa nguvu mithili ya mtoto mdogo. Niliona kwamba jumba bovu lilikuwa limenidondokea na udongo wake kunifukia, hakukuwa na mtu wa kunitoa katika kifusi, wote waliniacha nife.



    "Ndio hiki chumba ulichokutana na hao jamaa" Askari mmoja aliniuliza.



    Sikujibu.



    "Hatuongei na bubu hapa!" Alisema kwa ukali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndio hiki" Nilijibu nikiwa nimekata tamaa.



    "Mlikutana katika chumba hiki kweli. Hebu kuwa serious" Yule askari aliuliza tena. Maana haikumuingia akilini hata kidogo.



    "Kweli afande nilikuwa hapa na wale washenzi" Nilikuwa najibu huku nalia.



    "Chumba kilikuwa katika hali hii?" Aliniuliza tena.



    "Hapana"



    "Chumba kipo kwenye matengenezo hiki. Njooni kesho muwaulize mafundi walianza kujenga lini hiki chumba?" Yule mhudumu alidakia.



    Sikuwa na jinsi.



    Nilibebwa msobwemsobwe na kupelekwa ndani ya gari la Polisi. Moja kwa moja katika kituo cha Polisi.

    Nilikuwa nimekaa nyuma ya gari huku nikiamini ule ulikuwa ni mwisho wa uhuru wangu. Mwisho wa ndoto zangu na Farida...Mwisho wa kila kitu katika maisha yangu ...



    Ndani ya gari, Polisi walikuwa hawaongei. Walitulia tuli ndani ya gari. Kila mmoja akiniangalia mimi kwa jicho la hasira. Walihisi nimewadanganya, walihisi nimewasumbua kuwapeleka kule katika nyumba ya kulala wageni ya Machenza.



    Tulifika kituoni.



    Safari hii hawakujishughulisha kabisa na mimi. Nilishuka mwenyewe garini. Niliingia ndani, wakanipa kiti cha kukalia. Moyoni nilishangaa sana iweje Polisi wamekuwa wema sana kwangu ghafla.



    Baada ya muda kidogo alikuja askari wa kike, akaniongoza hadi katika chumba kingine kabisa ndani ya lile jengo la Polisi.



    Kilikuwa chumba kikubwa. Kilichokuwa na vitu vichache sana. Kulikuwa na meza moja iliyozungukwa na viti vinne. Na pembeni, konani kulikuwa na kabati kubwa la chuma. Nilipepesa macho harakaharaka toka kona moja hadi nyingine, toka chini hadi juu. Hakukuwa na kitu chochote cha ajabu. Vyote vilikuwa katika hali ya kawaida.



    Yule dada aliniacha mle ndani. Alitoka nje huku mlango akiuacha wazi. Nilijikuta moja kwa moja macho yangu yanatazama dirishani. Lilikuwa dirisha la kioo lililoniwezesha kumuona mtu hata kwa nje. Niliweza kuwaona watu waliokuwa wanakuja. Alikuwa yule dada askari pamoja na watu wawili. Yule askari wa kike alikuwa katikati, pembeni yake kushoto na kulia kulikuwa na wanaume. Nikajua bila shaka watu wale wanakuja mle ndani. Bila shaka wanakuja kunihoji mimi.



    Nilikuwa nimeupa mgongo mlango. Hadi wale watu wanaingia mle ndani sikuwa nawajua. Walipofika mbele yangu, kila mmoja alisogeza kiti ili akae ndipo niliponyanyua sura yangu kuwaangalia.



    Moyo wangu ulinipiga vibaya sana!



    Nilikuwa natizamana macho kwa macho na Bizzo. Kijana niliyekutana nae ndani ya lori wakati nakimbia Kilwa. Ni sura tu ndio ilinijulisha kama yule ni Bizzo. Lakini hakuwa katika mavazi ya Bizzo. Hakuwa katika haiba ya Bizzo. Nilimuangalia huku nikiwa siamini macho yangu. Bizzo alikuwa amevaa suti safi nyeusi. Suti ya gharama sana. Kifuani, nilikuwa naliona shati safi jeupe na tai nyeupe ikining'inia.

    Nilimuangalia usoni. Hakika alikuwa Bizzo yuleyule. Mtu aliyeniambia kwamba kuna dili la kupata pesa usiku wa saa sits katika nyumba ya kulala wageni ya Machenza.



    Niliwaza peke yangu " Sasa Bizzo anahusikaje na Polisi? Amefata nini? anataka nini hapa?"



    Nilimwangalia Bizzo, alikuwa anatabasamu.



    Macho yangu yalitembea. Yakatua kwa yule askari mwingine.

    Nilimtambua.

    Ni mmoja ya watu walionipa brief case yenye madawa ya kulevya katika nyumba ya kulala wageni ya Machenza.



    Sasa tumaini langu pekee mle ndani lilikuwa yule askari wa kike, ambaye alikuwa amesimama wima nyuma yangu. Ilikuwa nipo hatarini. Nilijua tumaini langu pekee ni yule msichana wa kike. Nikajua yule askari pekee ndiye anaweza kunipokea mle ndani. Niligeuka nyuma, ili kumtazama nyuma yule askari kwa jicho la huruma, na nimueleze kwamba wale watu walikuwa watu wabaya sana. Ndio watu walionipa brief case yenye madawa ya kulevya.



    Nilimtambua nae!



    Alikuwa ni Vampire. Askari Polisi wa kike kumbe alikuwa ni Vampire!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilistuka sana. Nilijiona nipo katika mdomo, mdomo wa mamba. Sikuelewa kabisa watu wale wanahusikaje na Polisi. Niligeuka mbele. Macho yangu yalikuwa kwa Bizzo, ambaye yeye alikuwa anakuna pua yake kwa mkono wa kushoto.



    "Huyu ni Bizzo, hata ndani ya gari nilimuona akikuna pua yake kwa mkono wa kushoto"



    Yule jamaa mwengine alimuonesha Vampire ishara. Vampire aliielewa, akatembea taratibu na kwenda kufunga mlango.

    Ndani tukabaki watu watatu, mimi, Vampire, na yule jamaa wa Machenza Guest house.



    Ulikuwa ni miongoni mwa vipindi vibaya sana kwangu. Nilikuwa katikati ya maadui. Maadui hatari. Nilijawa na hofu. Hofu ya kuuwawa. Nilijawa na uwoga, uwoga mkubwa sana. Nilikuwa kikaangoni, nikisubiri hatma ya maisha yangu...





    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog