Simulizi : Pigo La Mwisho
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
KAMA siyo vicheko vya askari waliopita nje ya ofisi yake koridoni, huenda Inspekta Maliyatabu angetekwa na usingizi ulioanza kumnyemelea. Alishtuka na kujishangaa. Ninaanza kuzeeka? alijiuliza huku akitwaa simu yake na kuitazama kwenye kioo.
Akaguna baada ya kugundua kuwa ilitimu saa tano! Tano usiku bado yuko ofisini na mambo yanakwenda mrama! Muuaji aliyelitikisa jiji tangu asubuhi bado hajapatikana na mbaya zaidi hakimu maarufu ameuawa usiku huu huku askari wa kitengo cha upelelezi akiwa amepigwa na huyohuyo Kamba na hali yake haijulikani inaendelea vipi.
Akakurupuka na kuirejesha ile laini ya simu ambayo aliitoa. Kisha akabonyeza tarakimu kadhaa na kuitega sikioni. Punde akasikia sauti kutoka upande wa pili, “Halloo afande?”
“Sajenti, vipi kuhusu Makella?”
“Bado hali yake siyo nzuri, afande,” alikuwa ni Sajini Kitowela.
Inspekta Maliyatabu alihema kwa nguvu na kuona jahazi likizidi kuzama. “Dokta anasemaje?”
“Inaonekana kaumia sana kwa ndani,” Sajini Kitowela alijibu. “Anapumua kwa shida sana. Itabidi afanyiwe vipimo zaidi hasa vya X-ray.”
“Panga watu wawili watakaokuwa wanafuatilia hali yake huko hospitali. Mimi na wewe sasa inabidi tuipindue Dar juu, chini ili tupate kitu kinachoeleweka. Kamba asipopatikana, ujue tutakuwa pabaya. Kwani uko wapi saa hizi?”
“Natokea Muhimbili, afande.”
“Njoo ofisini mara moja.”
**********
KAMA kuna usiku uliokuwa mbaya kwa Sajini Kitowela na Inspekta Maliyatabu katika maisha yao ya uaskari basi ni huu. Walipokutana ofisini saa 6 usiku walizungumza hili na lile wakijaribu kupambanua jambo moja hadi jingine lakini bado hawakupata njia ya kuweza kuamka asubuhi huku taifa likitangaziwa kuwa mhusika wa mauaji ya kikatili yaliyotokea jana amekamatwa.
Ndipo Inspekta Maliyatabu alipodiriki kumwambia Kitowela, “Unasikia sajenti, kesho asubuhi nitatoa taarifa ya kuacha kazi!”
Sajni Kitowela alishtuka na kumtazama Inspekta Maliyatabu kwa macho ya kutomwamini. “Kwa nini?” hatimaye alimuuliza huku akiendelea kumwangalia kwa mshangao. “ Umekosa ujasiri wa kuweza kukabiliana na wakuu na kuwaeleza chochote watakachokubaliana nawe?”
Akatulia kidogo kisha akaongeza, “Waeleze ukweli, uone watafanya nini au watasema nini! Siyo kuchukua uamuzi wa kuacha kazi! Itakuwa ni kushindwa na kuuaibisha wadhifa wa U-inspekta, afande!”
“Lakini sajenti, unadhani nani atanielewa nitakaposema chochote tofauti na kuutaarifu umma kuwa mhusika ametiwa mbaroni?”
“Waelewe, wasielewe, wewe usijali! Waeleze ugumu wa kazi ulivyo na hatua tuliyofikia. Kama mpaka sasa kuna ukaguzi mkubwa kwa njia zote kuu za kutoka nje ya jiji, mimi na wewe tutafanya nini kwa saa hizi chache za zahama iliyotokea? Na sisi ni binadamu! IGP, RPC na hata OCD wanapaswa kutambua hivyo. Hata waziri anapaswa kutambua hilo.
“Afande,” Sajini Kitowela aliendelea, “Kumsaka mtu ambaye hatujui kaelekea wapi, siyo kitu cha kawaida na cha kimchezo-mchezo. Cha muhimu kwa sasa ni kwenda zetu nyumbani, vinginevyo kama tutakesha tukivisumbua vichwa vyetu kwa kuliwazia tukio hili, matokeo yake tutajikuta tumekuwa vichaa kutakapopambazuka.
“Tukapumzike na kuiweka akili sawa kwa ajili ya kesho. Naamini kuwa doria yetu ni kubwa na ya uhakika kwa njia zote kuu za kutoka nje ya jiji.”
Inspekta Maliyatabu alifarijika kwa maneno hayo ya askari wa chini yake kicheo. Wakaondoka kila mmoja akielekea nyumbani kwake.
**********
TANGANYIKA Hotel ni jengo la ghorofa tatu ambalo liko kando ya Barabara ya Morogoro eneo la Manzese. Kamba alipofika hapo alikabidhiwa chumba namba 20 kilichokuwa ghorofa ya kwanza. Kwa usiku huo hakuoga wala kula. Alimwagiza mhudumu bia tatu na chupa ndogo ya Konyagi, akaamua kunywa huku akijaribu kuwaza hatima ya hali iliyomkabili.
Usingizi haukumjia. Ataupataje usingizi ilhali anatambua fika kuwa jicho la serikali linamsaka kwa nguvu zote? Kawaua Wahindi wawili na mfanyakazi wao! Kamuua Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay! Kamuua Hakimu wa Mahakama ya Kisutu!
Ni matukio makubwa yatakayolifanya Jeshi la Polisi lisimamishe baadhi ya majukumu yake na kuamua kumsaka. Atasakwa kama haini au gaidi na isitoshe, magazeti ya kesho yatazisahau habari zinazoongoza kila siku kwenye kurasa za mbele, habari za siasa za uchaguzi mkuu. Ni yeye ndiye atakayekuwa habari kuu.
Ndiyo, atayatawala magazeti hayo makubwa japo hana uhakika kama wahariri wana uthibitisho kuwa ni yeye ndiye mhusika mkuu.
Zaidi, atanukuliwa na kamanda wa polisi wa kanda maalum akizungumzia vifo vya hao aliowashughulikia, ndipo waandishi wataandika, wahariri watahariri na wahakiki watahakiki. Hatimaye wasanifu kurasa watazisanifu kurasa kisha, kwa njia ya mtandao, gazeti litatumwa kiwandani. Karatasi zitajichanganya kwenye mashine za uchapaji na usiku wa manane gazeti litakuwa limekamilika. Kesho Watanzania watanunua.
Hakuwa amefuatilia taarifa za redio na televisheni kwa siku nzima hii inayoisha, lakini alihisi kuwa lazima taarifa hizo zitakuwa zimeshawafikia waandishi wa vyombo hivyo na huenda zimeshatangazwa. Alijua kuwa ameibadili taswira ya jiji, ameziduwaza akili za Watanzania na amewachanganya wakuu wa vyombo vya dola. Dar es Salaam imesukwasukwa, Tanzania imetikisika.
Akiwa ameketi kwenye sofa na chupa ya bia pembeni, alifungua begi na kutoa fedha zilizokuwamo. Akazihesabu taratibu na kukuta ana shilingi milioni tatu na laki mbili. Akazirejesha ndani ya begi huku akimlaumu Jitu kimoyomoyo kwa kutokuwa tayari kuchukua dhamana ya nyumba na kumpatia pesa zaidi ili aweze kutorokea nje ya nchi.
Atakaa hapo hotelini mpaka lini? Gharama ya chumba ni shilingi elfu thelathini kwa siku. Hakuwa tayari kutumia bila kuzalisha. Ni woga wa kitoto, alijisemea kimoyomoyo. Ni lazima nifanye kila liwezekanalo, niondoke zangu. Najua baada ya muda mambo yatapoa na nitarudi.
Bastola aliyompora Makela na ile aliyopewa na Jitu, kwake zilikuwa ni nyenzo madhubuti katika kufanikisha lolote lile atakalotaka kulitekeleza. Sasa akaamua kuwa, ndani ya siku tatu atakazokaa hapo awe ameshapata ufumbuzi na kama itawezekana, siku ya nne asilale hapo.
Bia ya tatu hakuinywa. Ilikuwa ni saa nane usiku huo, ndipo alipokumbwa na usingizi kutokana na uchovu na kiwango kikubwa cha ulevi. Akasinzia akiwa palepale sofani, nusu kaketi, nusu kalala.
Labda angeendelea kulala kama asingegongewa mlango saa mbili asubuhi na mhudumu aliyemuuliza atapata stafutahi gani.
“Supu ya samaki ipo?” alimuuliza mhudumu huyo huku akimtazama kichovu.
“Ipo kaka.”
“Samaki gani?”
“Sato.”
“Hapo sawa. Leta.”
Wakati mhudumu akiondoka, Kamba alijiandaa kuingia bafuni.
*****
Haikuwa asubuhi njema kama zilivyokuwa asubuhi nyingine kwa Inspekta Maliyatabu. Hakuweza hata kunywa chai. Mara tu alipooga na kuvaa, aliondoka. Saa moja u nusu alikuwa ofisini ambako alikaa kwa takriban nusu saa akiyapitia magazeti mbalimbali yaliyosheheni habari za mauaji yaliyotokea jana.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Gazeti moja lilikuwa na picha ya Mheshimiwa Hakimu John Mwakipesile na habari kuhusu kifo cha mfanyabiashara mzee Ladhu, mwanaye Hassanali na mfanyakazi wao, Juma. Pia lilikuwa na taarifa kuhusu mauaji ya mkuu wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
Gazeti lingine pamoja na taarifa iliyonukuliwa kutoka kwa kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, hata hivyo katika tahariri yake lililishambulia Jeshi la Polisi kwa uzembe, likidiriki kudai kuwa imekuwa ni kawaida kwa jeshi hilo kutoa taarifa kuwa msako mkali unaendelea na matokeo yake itapita miaka kadhaa bila ya mhusika kupatikana. Hatimaye suala hilo litapotea kama lilivyoibuka.
Tahariri hiyo ilimkera sana Inspekta Maliyatabu. Akasonya na kulitupa pembeni gazeti hilo huku akinong’ona, “Waandishi wengine wapo, mradi wapo. Ni waandishi kwa sababu wanajua ‘a’ na ‘be’.”
Akiwa hajui aanze kufanya nini kuhusu sakata hilo lililomuumiza kichwa, mara mlango wa ofisi yake ukafunguliwa. Sajini Kitowela na Tina wakaingia.
Tina ni askari wa Kitengo cha Uchunguzi, ambaye jeshi hilo lilimtumia kikamilifu katika kuwakamata wahalifu ambao walijihusisha na biashara za dawa za kulevya na matukio mengine makubwa. Uzuri wa sura na umbo lake vilikuwa vivutio na ulimbo thabiti pale alipotaka kumnasa mtu aliyemhitaji.
Kazi kubwa ya mwisho ambayo aliifanya kwa ufanisi wa hali ya juu kiasi cha jeshi hilo kukaribia kumsujudia ni siku alipouibua mpango hatari kutoka katika kundi la watu watatu walioasi katika Jeshi la Wananchi. Waasi hao walikuwa wamepanga kuyalipua majengo kadhaa yenye ofisi mbalimbali jijini Dar es Salaam pamoja na msikiti na kanisa.
Kabla ya hapo, Tina alikuwa amefanya kazi nyingine kubwa. Alimkamata mfanyabiashara wa dawa za kulevya ambaye alikuwa akiishi katika hoteli moja kubwa jijini Dar. Mfanyabiashara huyo alijiingiza kichwa-kichwa kwa Tina, ambaye alikuwa amekwishapata tetesi kuhusu nyendo za mfanyabiashara huyo.
Akamwomba penzi, Tina naye akakubali japo kwa dhamira maalum. Akampa ahadi ya kumtimizia matakwa yake siku inayofuata. Hata hivyo, kilichotokea siku hiyo ya ahadi ni mfanyabiashara huyo kujikuta akivishwa pingu mikononi, kesi kubwa ikimkaabili.
Inspekta Maliyatabu aliamua kumwita Tina asubuhi hii katika kupata msaada zaidi kutokana na sakata hili la mauaji. Alishaona maji ni marefu kwake hivyo aliamini kuwa vichwa vitatu vitakapokaa na kujadiliana, huenda vikapata namna na kumnasa mlengwa.
“Tina, kazi iliyo mbele yetu ni kubwa,” Maliyatabu alimwambia huku akimtazama, muda mfupi baada ya wote watatu kukutana humo ofisini kwa Maliyatabu. “Najua muda mrefu ujao nitaitwa ili kutoa taarifa ya wapi tulipofikia katika suala hili. Sijui nitasema kipi kitakachokubalika kwa wakubwa.
“Ukweli ni kwamba mpaka sasa tuko ndani ya kiza kinene. Kamba kaua na kapotea. Tangu jana usiku picha yake imesambazwa kwa njia ya mtandao na vikosi vyote vinavyofanya ukaguzi makini mipakani mwa njia kuu za kutoka nje ya jiji.
“Lakini kama mnavyojua,” aliendelea, “ Tunadili na mtu mwenye akili timamu, anayejua nini anafanya na vipi ajilinde. Anatambua fika kuwa tunamsaka kwa hiyo atakuwa makini zaidi na ninahisi atakuwa hapahapa Dar kajichimbia sehemu fulani akisikilizia. Jiji lina watu zaidi ya milioni kumi. Utaanzia wapi kumsaka?”
“Vipi kuhusu vyombo vya habari?” Tina alihoji.
“Ki-vipi?” Inspekta hakumwelewa.
“Nina maana kutumia televisheni na magazeti kutangaza picha yake,” Tina alifafanua.
“Haitasaidia, tutakuwa tumemzindua zaidi na kumfanya awe makini zaidi,” Inspekta Maliyatabu alisema. “Na huenda ndiyo tunaweza kumpoteza kabisa. Mimi nina wazo moja.”
“Lipi?” Kitowela aliuliza huku akimtazama kwa makini.
“Kampuni za simu zinaweza kutusaidia sana.”
Tina na Kitowela walitikisa vichwa wakiashiria kukubali. Na wote wakaonekana kutulia wakisubiri Inspekta aendelee.
“Tina, uende kwenye ofisi za KINTEL uwaambie unataka kupata data za jana kuhusu simu ya mheshimiwa hakimu na marehemu James,” alisema huku kamkazia macho Tina. Akaendelea, “Ujue kwa jana tu wameongea na simu zipi, kama ni wao waliopiga au walipigiwa. Ninajua kuwa marehemu hakimu na hata James walikuwa wakitumia namba za mtandao wa KINTEL. Kama walikuwa pia na namba za mitandao mingine hapo sijui, ila nakumbuka kama mara mbili tatu niliwahi kuwasiliana na marehemu Mwakipesile kwa namba yake ya KINTEL. Na marehemu James, yeye mara nyingi alikuwa anawasiliana nami kwa namba moja tu ya KINTEL.
“Kwa hali hiyo, kichwani mwangu naona ni vizuri kama tutaanzia kwenye kampuni hiyo. Bado tuko gizani, tunajaribu huku na huko, hivyo ninaamini huko ndiko tunakoweza kupata mwanga wa kuanzia kazi yetu. Tina, wewe wameshakuzoea, watakusaidia na hasa kwa kuwa tukio lenyewe bado moto.”
Sajini Kitowela naye aliafiki na kusema, “Nadhani kwa hapo tunaweza kupata mwanga na kupiga hatua kubwa.”
“Tina,” Maliyatabu alisema akiwa bado anaonekana kusawijika usoni. Macho yake yalionekana kuchoka na kwa siku hiyo alionekana kuzeeka ghafla. Akaendelea, “Kumbuka ulivyowatia mikononi wale watu wa ‘unga’ kirahisi kwa kutumia msaada wa kampuni za simu. Nimeona hata kwa huyu tunaweza kumpata kwa njia hiyohiyo. Nakutegemea.”
Haukuwa mtihani mgumu kwa Tina. Nusu saa baadaye alikuwa katika ofisi za Kampuni ya Mawasiliano ya KINTEL ambako alizungumza na Joshua, ambaye walifahamiana kwa muda mrefu na baada ya dakika zisizozidi kumi, akapata kile alichokihitaji.
Ilibainika kuwa siku iliyopita, Mheshimiwa Hakimu John Mwakipesile alizungumza na simu tofauti kumi na nane kati ya saa moja asubuhi na saa kumi na mbili jioni. Namba kumi na mbili kati ya hizo zilikuwa ni za mtandao wa kampuni hiyo na namba sita zilikuwa ni za Kampuni ya ZCC. Kulingana na mfumo wa utendaji wa kampuni hiyo, majina ya hizo namba kumi na mbili yalipatikana kwa kuwa yalisajiliwa hapo. Tina aliyachukua majina hayo ili akayafanyie kazi lakini moyoni aliamini kuwa bado hajapiga hatua nzuri kwa kuwa hajalipata jina alilolihitaji. Au atakuwa anatumia jina lingine? Alijiuliza kwa hasira. Kama angepata namba ambayo inaonekana ni usajili wa mtu aitwaye Kamba Kiroboto ni hapo angekuwa amepiga hatua kubwa zaidi.
Kuhusu marehemu James Ntilampa, Tina aliambulia namba nyingi za simu alizozungumza nazo na majina tofauti mengi lakini hakukuwa na jina ambalo alilitilia shaka. Jina la Kamba Kiroboto ambaye tayari jeshi zima limeamua kumsaka kwa tuhuma za mauaji hayo, halikuwa katika orodha ya watu ambao walizungumza na mkuu huyo wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
Saa sita mchana Tina alikuwa amesharudi ofisini na akawa na kikao na Inspekta Maliyatabu na Sajini Kitowela. Akawaeleza hatua aliyofikia.
“Naamini tumeanza kupata picha fulani japo tuko nyuma,” Inspekta Maliyatabu alisema. “Tina, nakutegemea. Inatupasa tuipindue Dar es Salaam juu, chini hadi tupate kitu cha kuifanya jamii ituelewe. Tufanye kitu kitakachowapunguzia wanahabari cha kuandika magazetini na kutangaza redioni na kuonyesha kwenye televisheni.”
Tina aliinamisha uso kidogo, kisha akaunyanyua tena na kutabasamu kwa mbali. Akasema, “Afande, hapa tuna namba sita ambazo ni za usajili wa ZCC. Na mimi ninatumia pia mtandao wa ZCC. Siwezi kushindwa kuyajua majina ya wamiliki wa namba hizi.”
“Utazijuaje, Tina?”
“Naingia kwenye programu ya kuwatumia pesa,” Tina alisema kwa kujiamini. “Itakapofikia kuwa nataka kutuma, mtandao utaniambia kuwa natuma pesa kwa Fulani na kwamba niweke namba zangu za siri. Mtandao huu unatoa jina na ubini wa mwenye namba. Ngoja nicheze bahati nasibu.”
Haikuwa kazi ya bure kwake. Namba ya nne ilikata mzizi wa fitina. Jina la KAMBA KIROBOTO lilijitokeza.
“Yap…tunaye mshenzi huyu,” Tina alisema kwa majidai.
Kitowela na Maliyatabu walishtuka na kumsogelea Tina ili kuangalia kama anachosema ni kweli. Wakashuhudia mfumo wa ZCC-Pesa ulivyotegua kitendawili hicho.
Sasa Tina akamtazama Inspekta Maliyatabu kwa sura isiyo na amani. Kisha: “Afande, nataka nimpandie hewani huyu mshenzi,” Tina alisema. “Nitampigia, akipokea tu ameumia. Labda mie sio Tina. Si mnanijua?”
“Nakuamini, Tina,” Maliyatabu alisema akimtazama Tina kwa namna ya mtu aombaye msaada.
“Tumtangulize Mungu katika suala hili zito,” Tina alisema huku akinyanyuka kitini na kupachika mkoba wake begani. Akaongeza,
“Nipeni saa moja hivi halafu nitawaambia kitu.”
“Tunakuruhusu, Tina,” Maliyatabu alisema huku akiuegemeza mgongo kitini, akashusha pumzi ndefu huku akimwangalia Tina kwa macho ambayo ni kama yalikuwa yakimwambia, wewe ndiye umebeba dhamana ya Jeshi la Polisi.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Robo saa baadaye Tina alikuwa Riki Hotel, Kariakoo akinywa chai. Wakati huo mawazo yake yalikuwa ni kuhusu Inspekta Maliyatabu na Sajini Kitowela walivyomtupia mzigo huo. Na alitambua kuwa huenda wakati wowote kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam pamoja na wakuu wengine watakuwa wameshataka maelezo kuhusu hatua ambayo jeshi hili limefikia katika kumsaka mhusika wa mauaji hayo.
Namna Inspekta Maliyatabu atakavyojieleza huko kwa wakuu, Tina hakutaka kulifikiria, lakini aliamini kuwa atawapa maelezo ya kuwaridhisha na kuwatia matumaini ya mafanikio. Yeye akaendelea kunywa chai kabla ya kufanya kile ambacho aliamini kuwa kitatoa picha halisi ya kufanikiwa au kutofanikiwa katika jukumu lililo mbele yake.
Dakika kumi baadaye alitoka hotelini hapo. Akaingia garini lakini hakuondoka, akaamua kumpigia huyo Kamba Kiroboto. Alitambua fika kuwa huenda simu yake ikapokewa kwa namna tofauti na mpokeaji akiwa mjanja na makini, akihakikisha halaghaiki kibwege. Huenda Kamba siyo limbukeni wa wanawake, kama ataikata simu mara tu atakapohisi kuwa mpigaji ni changudoa, kitakachofuata ni nini?
Alishawaahidi Maliyatabu na Kitowela kuwa atahakikisha anafikia hatua nzuri katika kumsaka Kamba. Ikitokea akashindwa, itakuwa ni aibu iliyoje kwake? “Nishindwe?” alijiuliza kwa mnong’ono uliofurika hasira. “Nampigia na akipokea ndipo nitakapojua kinachoendelea.”
*****
Kamba alipokwishaoga alibadili nguo na kuketi kwenye sofa huku akiwaza ni kipi alistahili kukifanya katika kutafuta ufumbuzi wa hali iliyopo. Hata hivyo, kabla akili haijatulia mara yule mhudumu alirejea na supu ya samaki sanjari na vikorombwezo vingine vinavyostahili kwenye stafutahi.
Mhudumu alipokwishaondoka Kamba alianza kuishambulia supu hiyo, akiamini kuwa kama asipolishindilia tumbo kwa wakati huo, basi huenda akajikuta akikosa wasaa wa kutia chochote tumboni kutwa nzima.
Wakati akiendelea kupata stafutahi mara simu yake ikaita. Ilikuwa kitandani, mbali na pale sofani. Akawaza, ni nani huyo atakayekuwa akimpigia? Ni Jitu? Labda ni Jitu kwa sababu hakukuwa na mtu ambaye alijua kuwa ana simu zaidi ya Jitu. Na kama ni Jitu anataka nini asubuhi hii? Kuna tatizo kubwa?
Akaduwaa kwa muda kipande cha chapati kikiwa mkononi. Akabaki akiiangalia simu hiyo bila ya kunyanyuka na kwenda kuitwaa. Simu ikaita hatimaye ikakata. Punde ikaanza kuita tena. Sasa Kamba hakutulia, akanyanyuka na kuifuata simu hiyo. Kabla ya kuitwaa akakitazama kiganja cha mkono wa kushoto na kukiona kina mafuta yaliyotokana na kipande cha samaki alichokuwa akikila.
Hakuwa na muda wa kunawa wala kutafuta kitambaa. Alijifuta kwenye shuka kitandani kisha haraka akaitwaa simu na kuiangalia. Akakunja uso huku akiendelea kukitazama kioo ambako kulikuwa na tarakimu kadhaa zikielea wakati simu ikiita.
Zilikuwa ni namba ambazo ni ngeni na zilimshangaza kwa kuwa alikuwa na hakika kuwa tangu alipoinunua simu hiyo, zaidi ya kuzungumza na Jitu jana, alizungumza na Hassanali muda mfupi kabla ya kwenda dukani kumuua, kisha akazungumza na hakimu ambaye tayari naye kishakufa.
Ni nani huyu anayepiga? Kaipata wapi namba yangu? Je, ni kweli mpigaji amedhamiria kunipigia au kakosea namba?
Ni hapo pia ndipo Kamba alipojiuliza, kama ilimstahili kuipokea simu hiyo au aachane nayo. Aliwahi kusikia kuwa watu wengi maarufu mathalan matajiri au viongozi wa ngazi za juu serikalini au katika taasisi mbalimbali kubwa huwa na kawaida ya kutopokea simu kama hawaijui namba ya mpigaji.
Je, na mimi nifanye hivyo? alijiuliza kwa kuwa pia alitambua fika alipaswa kuwa makini sana na kuchukua hadhari kubwa akizingatia tayari kishafanya matukio yaliyolitikisa Jiji la Dar es Salaam na hata nchi nzima.
Lakini hatimaye alipiga moyo konde na kuamua kuipokea. Akabonyeza kitufe cha kupokelea na kuitega sikioni.
“Haloo,” akasema kwa sauti nzito na ya chini, akiwa ameibadili kabisa sauti yake halisi kwa makusudi.
“Helloo baby..” sauti nyororo ikapenya masikioni mwake. Akaguna na kushangaa. Hakuwa na uhusiano na mwanamke yeyote zaidi ya mkewe, Mama Safi. Ni nani huyu anayemwita baby?
Akatulia bila ya kuitika.
“Haloo,” kwa mara nyingine sauti ile ilipenya masikioni mwake, safari hii ikiwa tofauti na awali, ikionyesha umakini.
“Sema,” Kamba alisema kwa sauti yake ileile nzito na ya chini.
“Vipi mbona mnyonge?”
“Nazungumza na nani?” Kamba alimbana mpigaji.
“Kha! yaani haunijui tena baby?”
“Nadhani umekosea namba.”
“Mmmh, jamaaani, Kamba...Catherine hapa, kwani ulishaifuta namba yangu kwa kutowasiliana wiki moja tu? Si nilikwambia kuwa simu yangu iliibwa? Hivi ndo nimetoka kununua simu nyingine Sapna,” sauti ya upande wa pili ilipenya masikioni mwa Kamba kwa namna ya kipekee, ikiwa kama ibembelezayo na kunung’unika.
Ukimya wa sekunde kadhaa ukapita. Kisha tena sauti ikapenya sikioni mwa Kamba: “ Baby, leo nataka uje nikiuondolee upweke…nina siku nyingi wangu…niko tayari kwa ajili yako. Pesa ninayo. Njoo tunywe kisha tuonyeshane umwamba baby…aaaah…”
Sekunde kadhaa ambazo sikio la Kamba lilikuwa likipokea ‘shairi kutoka simuni, alihisi msisimko fulani maungoni mwake. Hata hivyo, alikuwa makini, hivyo hakubabaishwa na sauti hiyo. Badala yake sasa zikamjia hisia nyingine, kwamba huyo ni mmoja wa wanawake wanaopiga simu ovyo na kujilengesha kwa wanaume. Aliwahi kusikia kuwa kinadada wanaoiuza miili yao wamezua mtindo mpya wa kuwanasa wanaume.
Inavyofanyika ni kwamba, mwanamke anaperuzi kwenye kurasa za magazeti na kuibua namba za simu za waandishi au wale wanaotafuta marafiki na kuanza kupiga. Simu ikipokewa, na hasa ikitokea sauti ya kiume hapo mwanadada huona kuwa dili limekwenda vizuri, hivyo hujitia kuita jina lolote la kiume na mwenye simu akikana jina hilo haitasaidia, bado mpigaji atajitia kuzungumza hili na lile kwa mbwembwe za kike kiasi cha mwanamume kuamua kurusha ndoana. Mpigaji akibaini kuwa mwanamume huyo kamshtukia, atakimbilia kudai kuwa kakosea namba.
Pia alisikia kuwa hata wanaume wana tabia hiyo, wakitumia zaidi mitandao ya kijamii kwa kuunda uhusiano wa mapenzi na wanawake. Lakini tabia ya kuunda uhusiano kwa kutumia simu Kamba aliijua sana kwani ilishamtokea hata kabla hajaikwaa miaka saba gerezani.
Ni kwamba mawasiliano kupitia simu au mitandao ya kijamii yatakapofanyika kikamilifu, ndipo hutokea kupeana miadi ya kukutana. Wapenzi hao watakapokutana, kama mwanamume atavutiwa na mwanamke, basi biashara hufanyika. Ni hilo ambalo Kamba alihisi ndilo analotaka kufanya huyu mpigaji.
“Kwangu hanipati, malaya mkubwa,” alinong’ona huku akikata simu na kuitupa kitandani.
Akalitwaa bakuli la mchuzi wa supu na kulipeleka mdomoni. Akanywa mchuzi huo kwa nguvu na alipomaliza akaenda tena bafuni ambako alinawa kisha akarudi sofani, akajilaza, akiamua kuutumia muda huo kujipumzisha kabla ya kufikiria hatua nyingine ya kuchukua.
AKIWAamejilaza hapo sofani, usingizi ulianza kumnyemela na dakika chache baadaye alipitiwa na usingizi huo kutokana na shibe ya supu nzito. Alizinduliwa na mhudumu aliyeingia taratibu na kutwaa vyombo kisha akamwambia, “Kaka, usingizi ulikuteka tena asubuhi hii! Au ulikesha na wifi?”
Kamba alililazimisha tabasamu usoni na kumjibu, “ Wifi yako atoke wapi, we’ mtoto mzuri? Nipo tu kiupweke-upweke.”
“Mmmh, basi umeyataka mwenyewe,” mhudumu huyo alisema kwa sauti ya kudekadeka huku akimtazama Kamba kwa namna fulani ya kushawishi.
Kamba akamtazama vizuri na kuyagundua hayo macho yakizungumza zaidi ya kutazama. Akakumbuka maneno ya mtu mmoja ambaye aliwahi kumwambia kuwa ukiwa na msongo wa mawazo jitahidi kusahau kwa kuiburudisha nafsi yako kwa kufanya chochote kile ukipendacho au unachokitamani.Kwa muda huu aliona kuwa alipaswa kuufuata usemi huo hivyo akaamua kutupa karata yake mapema kwa mhudumu huyo. Akamwambia,“Peleka vyombo halafu urudi mtoto mzuri. Sawa?”
Tabasamu la mhudumu huyo likakua. Akaendelea kumtazama Kamba kwa namna ileile ya kipekee, tazama yenye kitu fulani kilichojificha katikati ya mtima wake. Kisha, kabla hajageuka na kutoka akamuuliza Kamba, “Nitapata bia moja?”
Kamba akashangaa. “Asubuhi yote hii mtoto mzuri?”
“Siyo ajabu. Naweka akili sawa. Jana kazi zilikuwa nyingi na nikachelewa kulala.”
“Ulikesha na mzee?”
"Akha…basi tu mikazi mingi.”
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kamba akacheka kidogo kisha akasema, “Poa, wewe nitakupa bia mbili, na mimi utapata nini?”
“Tutajua nitakaporudi.”
**********
“SHIT!” Tina alisonya baada ya kugundua simu imekatwa. Papohapo akalisaka jina lingine. Ni Martha, mfanyakazi wa kampuni nyingine ya simu ya ZCC. Alipolipata, akapiga.
“Tina, nambie,” Martha alimpokea.
“Martha, nina shida ya kikazi,” Tina alimwambia kwa sauti thabiti.
“Nakusikiliza.”
“Dakika mbili zilizopita nilikuwa naongea na mtu anayetumia mtandao wa kampuni yenu,” Tina alianza kuongea. “Tafadhali nahitaji kujua alikuwa akiongea na mimi akiwa eneo gani.”
“Ok, nipe dakika tano.”
“Poa.”
Dakika chache baadaye Tina alipata taarifa kutoka kwa Martha kuwa mtu aliyekuwa akizungumza naye alikuwa eneo la Manzese Tip Top jijini Dar es Salaam. Ilikuwa ni taarifa njema kiasi kwa Tina lakini bado hakuwa na matumaini ya mafanikio.
Kwamba Kamba bado yuko Dar es Salaam ilikuwa ni habari njema. Hata hivyo, kujua kuwa yuko Manzese siyo ufumbuzi wa kumtia mbaroni. Manzese ni kubwa sana. Ni kitongoji chenye mrundikano wa nyumba na wakazi. Ataanzia kumtafutia mtaa gani na nyumba gani ilhali hata simu kakata na huenda asipokee tena simu yoyote asiyoijua?
Anajua kuwa anasakwa ni lazima awe mwangalifu, Tina alijiambia. Hata hivyo, bado hakutaka kukata tamaa. Wazo moja likamjia na akajipa matumaini kuwa huenda wazo hilo likamsaidia zaidi. Haraka akatia moto gari na kurudi kule kwenye ofisi za kampuni ya KINTEL ambako alikwenda moja kwa moja hadi kwa Joshua, mtu ambaye amekuwa akimpa kipaumbele katika kushughulikia masuala yake.
“Nimerudi Joshua,” ndivyo alivyomwingia mara tu alipoingia ofisini mwake.
“Vipi tena, Tina?” Joshua alimtolea macho.
“Ripoti yenu inaonyesha kuwa huyo Kamba aliongea na mtu mmoja anayeitwa Jitu Kobelo, jana saa moja na kitu usiku, na Jitu Kobelo anatumia namba za mtandao wenu. Ninamhitaji huyo Jitu. Kwa kuwa namba yake ni ya mtandao wenu mkimpa wito kwa kutumia sababu za kitaalamu, atakuja. Ni muhimu sana! Naamini unaiweza kazi hiyo Joshua.”
Joshua aliguna na kukunja uso, kisha akasema, “Nimekuelewa. Nitakusaidia lakini utafanikiwa endapo huyo mtu atakuwa hapa Dar. Ni hapo atakaposema yuko nje ya Dar, tutakuwa tumepiga chini Tina.”
“Ondoa uchuro katika ulimi wako Joshua!” Tina alisema. “Mcheki kwanza tujue kama maharage ni mbegu au mboga. Naamini Mungu yuko upande wangu. Naomba awe hapa Dar. Na kama kweli yuko hapa Dar hachomoki kudadek!”
Ok, subiri,” Joshua alisema huku akinyanyuka na kwenda kwenye kijimeza kilichokuwa kando ya dirisha ambako kulikuwa na kompyuta ndogo. Akaiwasha na kuanza kuchakurachakura huku akionekana kuwa makini. Kisha akamgeukia Tina na kumwambia, “Jitu Kobelo alizungumza na Kamba Kiroboto akiwa eneo la Mikocheni saa moja na nusu usiku. Na alizungumza tena na Kamba Kiroboto saa moja na dakika hamsini akiwa Mwenge.”
“Joshua, ninachotaka ni kumleta hapa!” Tina alijikuta akizungumza kiaskari zaidi, tayari ni kama alishachanganyikiwa.
Joshua alibonyeza tarakimu kadhaa kwenye simu iliyokuwa kando yake na kuitega sikioni. Ukimya ukatawala kwa muda, Tina akiwa amemkodolea macho Joshua akisubiri kusikia ni vipi atazungumza na Jitu.
“Haloo Mista Jitu,” hatimaye Joshua alianza kuzungumza. “Unaongea na Kevin kutoka kampuni ya simu ya KINTEL…Tafadhali tunakuomba ufike hapa makao makuu ya ofisi zetu ili kufanya marekebisho fulani ya kitaalamu kulingana na data zako tulizonazo…yeah…Uko hapahapa city centre? Ok, kama unaweza njoo mara moja, ni suala la muda mfupi tu katika kuweka kumbukumbu zetu vizuri. Asante kwa ushirikiano wako.”
Joshua aliporudisha simu mahala pake, alimgeukia Tina na kumwambia, “Yuko hapa mjini, Peack Cock Hotel anapata stafutahi. Anasema tano na robo atakuwa hapa.”
Tina alitabasamu kidogo, tabasamu lisilokuwa hata na chembe ya furaha. Akaitazama saa iliyokuwa ukutani na kusema, “Nne na dakika kumi. Muda unatosha.” Papohapo akabonyeza tarakimu kadhaa katika simu yake kisha akaitega sikioni.
*********
INSPEKTA Maliyatabu alikuwa akinywa soda wakati simu yake ya mkononi ilipoita. Akashtuka na kuitazama. Alikuwa ni Tina!
Soda haikunyweka tena. Akaitua chupa mezani na kuita, “Haloo Tina!”
Kikafuata kipindi kifupi cha ukimya, Inspekta Maliyatabu akisikiliza kwa makini na wakati mwingine akikunja uso. Kisha akasema, “Kamba hawezi kuwa na rafiki wa maana, kwa vyovyote ni mhalifu kama yeye. Huyo aliyekuwa akizungumza naye, kwa vyovyote vile naye ni kama yeye, hawezi kuwa mtu mzuri. Sasa hivi sajenti Kitowela atakuja na watu wengine watatu. Ni huyo ndiye atakayetuambia jamaa yuko wapi. Kama atashindwa kusema kweli, basi atalazimishwa autapike huo ukweli wenyewe.”
Dakika iliyofuata Inspekta Maliyatabu alikuwa akipiga simu mbili, tatu na kuzungumza kwa msisitizo lakini kwa sauti ya wastani. Ndipo alipoirudia soda yake na kuigugumia. Kisha akanyanyuka na kunyoosha viungo. Akajitoa nyuma ya meza na kwenda kwenye sofa ambako alijipweteka na kushusha pumzi ndefu.
Hadi wakati huo hakuwa amepata wito wowote kutoka kwa wakuu wake, hivyo na yeye hakutaka kuwa na pupa ya kuwaeleza chochote kwa kuwa aliona bado hajawa na chochote cha maana cha kuwaambia.
Hazikutimu hata dakika tano mara mlango ukafunguliwa. Sajini Kitowela na askari wengine wanne wakaingia. Wote walikuwa wamevaa kiraia. Tofauti na Sajini Kitowela aliyekuwa ametinga shati la rangi ya maziwa na suruali nyeusi akiwa amechomekea, askari hao wengine walikuwa wamevaa suruali za jeans na fulana ambazo ziliwabana na hivyo kuiweka bayana taswira ya miili yao iliyojengeka kimazoezi.
“Tina amefikia pazuri,” Inspekta Maliyatabu aliwaambia huku naye akiwa amesimama, akiwatazama kwa zamu, macho yake makali yakiwa hayapepesi. “Jamaa aliyewasiliana na Kamba mara mbili jana, atakuja pale KINTEL kama bwege f’lani hivi kwa sababu staff wa KINTEL ndiye kampigia na kumpa wito wa kiofisi. Kwa umbulula wake kakubali kufika pale saa tano na robo. Cha kufanya sasa ni kuwahi pale ili akifika tu tumdake, atueleze Kamba yuko wapi.”
Dakika chache baadaye Inspekta Maliyatabu alikuwa ndani ya Land Rover 110 defender jeupe pamoja na Sajini Kitowela na askari wengine watatu wakielekea Mtaa wa Mansfield yaliko makao makuu ya Kampuni ya KINTEL.
Ni kama walikuwa wakienda kulitia mbaroni kundi la wahalifu kumi wenye silaha! Inspekta Maliyatabu alikuwa na bastola yenye risasi sita, Sajini Kitowela hali kadhalika huku wale askari wanne waliovaa ‘kisela’ na ambao hawakuwa na kumbukumbu mara ya mwisho walitabasamu lini, wao walikuwa na bunduki fupi kila mmoja, wakiwa wamesimama eneo la nyuma, mikono yao mikakamavu ikiwa imeshikilia mabomba.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Gari halikwenda moja kwa moja hadi kwenye ofisi za KINTEL bali lilisimama Mtaa wa Samora, jirani na PPF House. Maliyatabu na Kitowela wakateremka na kuvuka barabara wakielekea Mtaa wa Mansfield, tembea yao ikiwa ni ile isiyowatia shaka watu wengine waliokuwa katika eneo hilo. Wale askari wengine wanne, walibaki garini wakisubiri maagizo mengine kutoka kwa Inspekta Maliyatabu.
Wakati Inspekta Maliyatabu na Kitowela wakienda kwenye ofisi za KINTEL, Maliyatabu alitoa simu mfukoni na kumpigia Tina.
“Tuko hapa jirani,” Maliyatabu alisema mara tu Tina alipopokea simu.
“Ok, Niko ndani,” Tina alijibu na kuongeza. “Nisubirini hapo nje dakika moja tu.”
Papohapo Tina akamwambia Joshua, “Si mimi wala wenzangu tunaomjua huyo Jitu. Kwa hiyo, waambie watu wa mapokezi kuwa akifika mtu atakayejitambulisha kwa jina hilo, aje huku ofisini kwako na wewe utatutaarifu. Sisi tutakuwa pale nje. Umenisoma?”
“Nimekusoma, Tina,” Joshua alijibu.
Tina alitoka humo ofisini haraka, alipofika mapokezi akawakuta wateja zaidi ya kumi, baadhi wakihudumiwa na wengine wakiwa wamekaa wakisubiri zamu zao. Miongoni mwa walioketi ni Inspekta Maliyatabu na Sajini Kitowela ambao walionekana kuwa katika mtazamo wa kawaida kama hao wateja wengine.
Tina alipowafikia aliwakonyeza na wote wakatoka, wakaenda nje kwenye kijikorido ambako walijikuta wakiwa peke yao.
“Nimemwambia Joshua, awaambie watu wa reception, mshenzi akifika wamwelekeze ofisini kwake,” Tina alianza kuzungumza. “Na atakapofika huko tu Joshua atatuambia. Bado dakika chache. Cha muhimu ni kuomba Mungu aje, lakini machale yakimcheza akaghairi, tumeumia.”
Tofauti na Tina alivyokuwa akionyesha kujiamini na ujasiri mkubwa katika kuongea, Maliyatabu yeye alionekana kutokuwa na utulivu. Uso wake ulikuwa umekunjamana na kuwa kama mtu asiyejiamini. Kila wakati alikuwa akitupa macho huku na kule kwa chati kama vile alitazamia kumwona huyo waliyekuwa wakimsubiri. Na mara kwa mara akawa anaangalia saa.
Saa tano ilipotimu askari hao walikuwa makini zaidi, wakawa wakimtazama kila mteja aliyeingia humo ndani, huku wao wakionekana kama watu wa kawaida hususan Kitowela na Tina ambao walizua mazungumzo ya hapa na pale huku wakitembea-tembea kwenye korido hiyo.
Ni katika muda huo ndipo macho yao yalipowaona watu wawili waliokuja kwa magari. Mmoja aliegesha gari jeusi aina ya Land Cruiser GX na kuteremka. Akaingia ndani ya ofisi hizo na kufikia mapokezi ambako alizungumza kidogo na mhudumu kisha akajiunga na wateja wengine waliokuwa wamekaa wakisubiri kuhudumiwa.
Mwingine aliteremka kwenye gari dogo la kifahari, Honda Civic na kutembea kwa hatua za kikakamavu, akiingia ndani ya ofisi hizo za KINTEL.
Tina, Sajini Kitowela na Inspekta Maliyatabu walitazamana, macho ya kila mmoja yakiwa kama yanayosema, tuwe tayari…huenda kati ya hao yupo mtu wetu…
Hata hivyo, askari hao waliendelea kuwa makini wakihakikisha hakuna yeyote asiyewahusu ambaye anaweza kuwatilia shaka. Ni Inspekta Maliyatabu pekee ambaye bado moyo wake ulikuwa katika mapigo yasiyokuwa ya kawaida na hasa kwa kuzingatia kuwa muda wowote anaweza kupigiwa simu na wakubwa wake akitakiwa kutoa maelezo kuhusu hatua iliyofikiwa katika operesheni ya kumsaka muuaji aliyelitikisa jiji siku iliyopita.
Moyoni aliomba kwanza wampate huyo aliyezungumza na Kamba jana na hapo atakuwa na jibu la kuwapa wakubwa wake wa kazi endapo watamuuliza chochote.
**********
SUPU aliyokunywa Kamba ilimpa shibe ya kutosha na hivyo kuudhihirisha ule usemi wa shibe mwana malevya na njaa mwana malegeza. Ndiyo, viungo vililegea na alipojilaza kitandani akahisi usingizi ukimnyemelea. Hata hivyo, hakuwa tayari kutekwa na hali hiyo. Huu haukuwa wakati wa kuuendekeza usingizi. Bado alikuwa na jukumu kubwa mbele yake, jukumu la kuondoka jijini Dar es Salaam na kutokomea mbali.
Hivyo alijitutumua, akajitoa kitandani na kuifuata chupa ya Konyagi ambayo ilikuwa nusu, akaifungua na kunywa funda kubwa la pombe hiyo. Akaitazama tena chupa na kubaini kiwango cha kinywaji kilichobaki ni kidogo, akagugumia yote! Kisha akaiweka chupa juu ya kistuli kilichokuwa kando yake.
Mara akashtuka. Alisikia mlango ukigongwa. Akakodoa macho mlangoni na kusikiliza vizuri. Hakutaka kujipa imani kuwa masikio yake yalikuwa sahihi. Baada ya muda mfupi tena mlango ukagongwa. Akanyanyuka na kwenda kufungua. Mbele yake alikuwa ni yule mhudumu, safari hii akiwa amebadili mavazi na kuvutia kwa suruali nyeusi iliyolichora umbo lake kwa uwazi zaidi.
Blauzi nyepesi aliyovaa nayo ilimkubali japo kama ilivyokuwa suruali, hayakuwa mavazi ambayo mtu unaweza kuyaweka kwenye thamani ya juu, lakini yalimpendeza.
Kamba alijua kuwa sasa mhudumu huyu kaja rasmi. Macho yao yalipokutana, msichana aliinamisha uso, akiyaepuka macho ya Kamba. Kamba akampisha huku akimwambia kimasihara, “Nina bahati ya mtende leo…kutembelewa na toto zuri kiasi hiki!”
“Nyoo…wazuri hujawaona wewe?” mhudumu huyo alisema huku akipenyeza chumbani.
Alionekana kutokuwa na aibu au woga mara tu alipokwishaingia chumbani humo. Akajitupa sofani na kumtazama Kamba sawia. Kisha akamwambia, “Wewe umeshaanza kushtua…mimi je?”
“Sema wewe.”
“Nipe pesa nikachukue Castle Lite yangu,” msichana alisema.
Kamba alilifuata begi na kulifungua kisha akazamisha mkono na baada ya muda mfupi akautoa ukiwa umeshika noti ya shilingi 10,000. Akampatia.
“Na wewe nikuletee kinywaji gani?” Zinduna akamuuliza.
“Unaona ile?” Kamba akamwonesha chupa ya bia ambayo aliiacha usiku. “Itanitosha kwa asubuhi hii. Wewe kachukue hizo tatu uje tupige stori, au una haraka?”
“Sina haraka. Nd’o nimetoka night. Na leo nd’o naanza off. Wewe tu.”
Kamba akajisikia huru na akamwona huyu mrembo kama dawa ya kumwondolea msongo wa mawazo na kumpotezea kwa muda kumbukumbu ya yale aliyoyafanya jana.
Mrembo huyo alipoondoka, Kamba aliifungua ile chupa ya bia na kunywa mafunda kadhaa kwa nguvu kisha akairejesha mezani. Kama jana leo tena akili ikaruka hadi kwa mkewe, Mama Safi. Akajisikia uchungu kuwa mbali naye ilhali ni majuzi tu amerudi kutoka jela. Akamkumbuka mwanaye Safi.
Moyo ukamuuma kwa kutojua wako wapi na wanajisikia vipi huko waliko. Alijisikia kuwa na hatia zaidi muda huu kwa kuwa anamsubiri huyu mhudumu na kitakachofuata hakutaka kujidanganya kuwa itakuwa ni kuchukua Msahafu au Biblia na kuanza kusoma. Ni mapenzi.
Hata hivyo, aliwaza haraka kuwa huo haukuwa muda mwafaka wa kumfikiria mkewe au mwanaye ilhali anatambua kuwa Jeshi la Polisi litakuwa linamsaka kwa nguvu kubwa. Alipaswa kujali namna ya kujiokoa ndipo mambo mengine yatafuata. Akaitwaa tena bia na kunywa funda zito.
Dakika chache baadaye mrembo huyo akarejea na chupa mbili za bia aina ya Castle Lite. Akaziweka kwenye kijimeza kilichokuwa mbele ya sofa alilokuwa kaketi Kamba, naye akaketi sofani hapo kiasi cha kugusana mabega na Kamba.
Uchokozi dhahiri, Kamba alijisemea huku akiutupa mkono kwenye paja la mhudumu huyo na kujibu huo aliona kuwa ni uchokozi. Akalitomasa kidogo. Kisha akanong’ona, “Karibu baby…”
“Hee! yamekuwa hayo tena ya kuitana baby mapema hivi?” mhudumu huyo ambaye kwa umri alikuwa na miaka kumi na tisa aliuliza huku akiuzuia mkono wa Kamba kwa mfumo wa sitaki-nataka.
“Kwani ni kosa?” Kamba aliuliza huku sasa akiutupa mkono begani na kumpigapiga. “Hujaniambia unaitwa nani…nadhani si vibaya nikikuita baby kulingana na mazingira tuliyomo.”
Mhudumu huyu akacheka huku akifungua chupa na kuanza kunywa bia yake. “Naitwa Zinduna,” alisema huku akishusha funda la pili.
“Zinduna,” Kamba naye alisema kwa sauti ya chini. “Asante. Mi’ ni Gogo.”
“Gogo?!” Zinduna aliuliza kama asiyemwamini Kamba. “Kabila gani?”
Kamba akacheka na badala ya kujibu naye akauliza, “Yamekuwa hayo tena ya kuulizana kabila? Kwani unataka kutambika?”
Kwa mara nyingine Zinduna akacheka huku akimwegemea-egemea Kamba. Hatimaye akasema, “Sina maana hiyo. Jina lako nd’o limenifanya niulize. Sijawahi kumsikia mtu akiitwa Gogo.”
“Yeah, hujawahi kumsikia. Hilo siyo kosa na sasa ndiyo umelisikia kwa mara ya kwanza. Huyu ndiye Gogo.”
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Poa.”
Kichwa cha Kamba kilikuwa kimeanza kuchangamka kutokana na mchanganyiko wa vinywaji alivyokunywa. Na sasa alijisikia kuwa huru zaidi. Akajisikia pia kuhitaji kunywa tena na tena huku akiwa na huyu mrembo.
Saa nzima baadaye Zinduna naye alikuwa amekwishakunywa chupa nne na Kamba alikuwa ameongeza moja. Kikafikia kipindi ambacho hawakuzungumza kwa maneno bali vinywa na mikono ndivyo vilivyokuwa kazini, ndimi zikisumbuana na mikono ikitaabika kugusa hapa na kutomasa pale.
“Zinduna…” kuna wakati Kamba aliita, sauti yake ikiwa ni kama anayeilazimisha.
Zinduna hakuitika. Aliendelea kufanya kile alichojua kuwa kitamchanganya zaidi Kamba. Akamsukuma chali pale sofani na kumpambua bukta, vazi pekee lililokuwa limeusitiri mwili wa Kamba kwa wakati huo. Kisha akanong’ona, “Tulia…tulia baby…sipendi upate tabu wakati nipo kwa ajili yako…tulia…” wakati huo akiutembeza ulimi kutoka kwenye chuchu hii hadi ile na kisha taratibu ulimi huo wa moto ukateleza hadi kitovuni ambako uliganda kwa muda mfupi sana na kushuka chini zaidi.
Sasa ulimi huo ukawa umefika pale ambako Zinduna alipahitaji. Akatulia na kuendelea kumnyanyasa Kamba kwa utaalamu wa kipekee. Kamba akawa anatapatapa.
**********
JITU alipokwishapata stafutahi alitia moto gari moja kwa moja akielekea katika ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya Simu ya KINTEL. Dakika kama kumi tu zilitosha kumfikisha katika ofisi hizo, akateremka na kuwahi kuingia, tembea yake ikiwa ya kikakamavu.
Alikwenda moja kwa moja hadi kwa mhudumu wa mapokezi na kumwambia, “Samahani dada, nimepata simu kutoka hapa kwenu kuwa ninahitajika kwa suala la kiofisi.”
YULE mhudumu alimtazama kidogo na kumuuliza, “Aliyekupigia hakukupa maelezo zaidi?”
“Hapana. Lakini alijitambulisha kwa jina la Joshua.”
Mhudumu huyo akatikisa kichwa na kutwaa simu lakini kabla hajafanya kitu kingine, akamtupia tena swali Jitu, “Jina lako?”
“Jitu Kobelo.”
Mhudumu huyo akabonyeza tarakimu kadhaa kwenye simu hiyo ya mezani kisha akatega sikioni. “Kuna mgeni hapa anaitwa Jitu Kobelo. Anasema amepokea wito kutoka hapa ofisini kuwa aje.”
Ukimya mfupi ukatawala mhudumu huyo akionekana kusikiliza kisha akairudisha simu mahali pake na kumtazama Jitu usoni sawia. “Panda ghorofa ya kwanza, chumba namba mbili.”
Jitu akaitika kwa kutikisa kichwa kisha akazifuata ngazi za kuelekea ghorofani, akitembea kimadaha, funguo za gari zikichezeshwa mkono wa kulia na mluzi wa majidai ukipulizwa mdomoni.
Muda mfupi baadaye alikuwa nje ya ofisi namba 2. Akagonga kistaarabu.
**********
MARA tu Joshua alipopigiwa simu na mhudumu kuwa kuna mgeni aitwaye Jitu Kobelo, mapigo ya moyo wake yakaongeza kasi. Akawa na hofu ya kutokea vurugu kubwa hapo ofisini. Akajikuta akiduwaa, macho amekodoa kwenye ‘skrini’ ya kompyuta ilhali hayaoni.
Punde akasikia mlango ukigongwa kwa utulivu. Akashtuka zaidi na kujiweka sawa. Kisha akaipata sauti yake, “Ingia.”
Mlango ukafunguliwa taratibu na mtu, mwanamume pandikizi akiwa ndani ya suti maridadi, uso mng’aavu akaingia kwa hatua za asteaste macho yake makali yaliyotangaza ukwasi yakimtazama Joshua sawia huku tabasamu la pesa likichanua usoni pake.
Mwonekano wa mtu huyu ulimwondolea ujasiri na kujiamini Joshua. Alikuwa ni mgeni ambaye Joshua aliamini kuwa hadhi yake haifai kufuatwa na mtu wa aina ya Tina, askari wa kawaida. Hapana. Huyu alistahili kufuatwa na wakubwa zaidi wa Jeshi la Polisi.
Kwa kutojiamini huko Joshua akasimama na kujitia kutabasamu huku wasiwasi ukiwa bado umetawala moyo wake. “Karibu…karibu sana…mista…” akaiacha sentensi hiyo ikielea.
“Jitu Kobelo,” Jitu alimalizia kwa sauti ya kujiamini zaidi, sauti ya kimadaraka, akiwa kama yeye ndiye bosi wa Joshua.
“Ok, mista Jitu, karibu sana.”
Wakapeana mikono kisha Joshua akamwonesha sofa kubwa lililokuwa humo ofisini na Jitu akajitupa kimajidaidai, funguo za gari zikiendelea kuchezeshwa mkononi na zaidi, sasa aliuweka mguu mmoja juu ya mwingine kama vile akitaka Joshua akishuhudie kiatu hiki cha bei ya kutisha kilichong’ara mguuni.
“Ndiye, mista Joshua?” Jitu alimuuliza huku akimtazama kwa makini, mikunjo ya mbali ikijitokeza usoni pake.
“Yeah, ndiye mimi.”
‘Ok, nimeitika wito Nadhani sijachelewa sana.”
“Hujachelewa, mista Jitu,” Joshua alijibu akiyaepuka macho ya Jitu ambayo aliona kuwa hayatofautiani na macho ya paka. Akaongeza, “Subiri nimwite mtaalamu aje ashughulikie suala la laini yako. Ni suala la dakika mbili, tatu tu.”
Joshua alitwaa simu yake ya mkononi na kubonyeza jina la Tina kisha akatega sikioni.
*********
SIMU YA Tina ilipoita, aliitoa haraka na papohapo Inspekta Maliyatabu naye akamsogelea. “N’ambie, dude limeshaingia?”
“Tayari,” alijibiwa.
Akamgeukia Inspekta Maliyatabu na Kitowela. “Kumekucha, afande. Nadhani uwaite na kina Salum garini waje haraka. Huyu mtu sio wa kumwamini.”
Wakati Inspekta Maliyatabu akiwasiliana na wale askari kule garini, Tina alianza kuvuta hatua akizifuata ngazi za kwenda ghorofa ya kwanza, Kitowela akimfuata
Walipofika kwenye mlango wa chumba namba 2 walitulia kidogo, wakatazamana kisha Inspekta Maliyatabu akakikamata kitasa na kukizungusha. Mlango ukaitika, wakaingia taratibu, mmoja baada ya mwingine. Moja kwa moja macho yao yakatua kwenye sofa kubwa ambako Jitu alikuwa kaketi.
Inspekta Maliyatabu akatoa kitambulisho na kumwonesha kwa mbali, Tina naye akafanya hivyo isipokuwa Kitowela. “Askari polisi!” Maliyatabu akatamka kwa sauti ya kiaskari zaidi, macho yake makali yakimtazama Jitu kwa namna ya usharishari.
Akaongeza, “Kuanzia sasa uko chini ya ulinzi. Tuko hapa kwa jambo moja tu ambalo kama utatupa ushirikiano wa kutosha, tutaachana na wewe muda huu-huu.”
Lilikuwa ni tukio ambalo Jitu hakulitarajia. Ikawa ni aina fulani ya tamthilia isiyopendeza akilini na machoni mwake. Akakunja uso na kuwatazama kwa zamu askari hao. Akautoa mguu uliokuwa umewekwa juu ya mwingine, akakaa vizuri na kuhoji, “Vipi, mbona siwaelewi? Kuna nini?”
Inspekta Maliyatabu alisogea upande wa meza ya Joshua na sasa wakawa wamesimama mbalimbali, wakiwa katika tahadhari ya hatari yoyote ile.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Jitu,” Inspekta Maliyatabu aliita. “Tuambie Kamba yuko wapi?”
Jitu alikunja uso zaidi na kumtazama Maliyatabu kwa makini, kisha akayahamishia macho kwa Joshua. “Joshua, ni kipi kinachoendelea hapa?”
“Mr. Kisu, tafadhali msikilize afande,” Joshua alijibu kwa upole.
“Nimsikilize afande?” Jitu aliwaka, macho yakiwa bado kwa Joshua. “Umeniita wewe, hawa maafande wanahusikaje na wito wako kwangu? Na mbona wananiuliza maswali ya ajabu yasiyo na kichwa wala miguu? Unajua sikuelewi Joshua!”
“Taratibu mista Jitu,” Maliyatabu alisema kwa upole kidogo. “Tunajitahidi kuwa wastaarabu ili tupate mwafaka. Tuambie, Kamba yuko wapi?”
Sasa macho ya Jitu yalirudi kwa Inspekta Maliyatabu. “Sikuelewi!” akatamka kwa uthabiti, akionekana kuwa jasiri, macho yake makali yakimtazama Maliyatabu bila ya kupepesa.
“ Nakuuliza kwa mara ya mwisho, Kamba Kiroboto yuko wapi?”
“Simjui huyo mtu unayeniuliza!” Jitu alijibu kwa kujiamini vilevile.
“Jana,” Inspekta alimwambia Jitu. “Ulikuwa ukiwasiliana na Kamba Kiroboto kwa njia ya simu saa moja jioni. Bisha!”
Jitu hakujibu. Akabaki akimtazama Maliyatabu huku akihisi hatari mbele yake. Hata hivyo, hakutaka kukiri mapema kiasi hicho japo ni kweli jana usiku alikuwa akiongea na Kamba kwa simu na baadaye wakaonana kule Mwenge.
“Sema Jitu,” Kitowela alisema huku akimsogelea.
Kitowela na Maliyatabu walitazamana kidogo kisha Maliyatabu akamgeukia Joshua na kumwambia, “Samahani Joshua, tutalazimika kuondoka na mgeni wako. Nadhani hapendi kurahisisha mambo na hapendi tumalize maongezi yetu kwa ustaarabu wa Kitanzania. Samahani sana.”
“Hakuna tabu, afande, “ Joshua alijibu huku akiyanyanyua na kuyashusha mabega na pia akinyoosha mikono akionesha ishara ya kuafiki. “Kama ni masuala ya kikazi endeleeni tu, sina pingamizi.”
Inspekta Maliyatabu akamgeukia tena Jitu na kumwamuru kwa sauti kali, “Simama!”
“Lakini kuna tatizo gani?!” Jitu hakusimama. “Nina kosa gani mimi?”
“Unapenda tukuvunjie heshima?” Kitowela aliingilia kati.
Bado Jitu alikuwa ngangari. Mara mlango ukafunguliwa. Wale askari watatu waliokuwa wamevaa fulana zisizokuwa na mikono, suruali za jeans na raba miguuni wakaingia.
“Anajitia kujua, mpelekeni kwenye gari. Amekataa kuzungumza, sasa twende naye central na huko atautapika ukweli!” Inspekta Maliyatabu aliwaambia.
Wale askari ni kama vile walikuwa na njaa ya kazi iliyokuwa mbele yao. Mmoja alimfuata Jitu na kuupenyeza mkono kwenye kwapa la kulia la Jitu kisha akamnyanyua kimsobemsobe. Wakati huohuo, askari mwingine akaja nyuma ya Jitu na kumshika kwenye pindo la suruali kisha akamnyanyua na kumfanya Jitu ajikute akisimamia vidole.
Jitu hakukubaliana na hali hiyo. Kwa kasi ya ajabu alimpiga kwa kiwiko huyu askari aliyemshika kwa nyuma, likawa ni pigo zito lililomfanya askari huyo agune kwa maumivu, akajikunja na kulazimika kumwachia Jitu.
Kitendo hicho kiliwashtua wote na wakati Jitu akijiandaa kumvurumishia konde huyu askari aliyeupenyeza mkono kwapani mwake, teke zito, teke la kiufundi lenye kilo nyingi nyuma yake kutoka kwa askari wa tatu lilitua kifuani kwa Jitu na kumtia maumivu makali!
Kilichofuata ni mvua ya vipigo mwilini mwa Jitu kiasi cha kumwacha hoi na walipobaini kuwa katepeta wakamtupa sakafuni na kumtazama kama watazamao mzoga unaotoa uvundo mkali.
“Bado unajitia umwamba?” Inspekta Maliyatabu alimuuliza huku akimwinamia.
Jitu alihema kwa nguvu na kumtazama kidogo Inspekta Maliyatabu kisha akafumba macho. Alionesha kuwa vipigo vimwemwathiri kwa kiasi kikubwa. Akawa akikunja na kukunjua uso kwa maumivu.
“Jitu, Kamba yuko wapi?” Inspekta Maliyatabu alimuuliza tena, safari hii akiwa amemkanyaga kifuani. Kisha akaongeza, “Sikia we bwege! Tunaweza kukumaliza kwa hasira kama utajitia kujua. Hatutajali! Kuua ni sehemu ya kazi yetu hasa kuwamaliza watu wa aina yako!”
Jitu aliiona dunia chungu. Akajiona kama achunguliaye kaburi! Aliwahi kusikia tetesi kuwa askari polisi wanapompata mhalifu mkubwa hususan jambazi, humuua na kisha hutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa mtuhumiwa aliuawa wakati wa majibizano ya risasi na askari au alikuwa akijaribu kutoroka chini ya ulinzi.
Na akitambua fika kuwa Jeshi la Polisi lina hasira kali kuhusu Kamba, hakutaka kujidanganya kuwa huenda hawa askari wakamwonea huruma, wakamwinua pale chini kistaarabu na kumpeleka hospitali.
Alitambua kuwa kutokana na hasira zilizofura ndani ya vichwa vyao, wanaweza wakatumia utaratibu uleule wa kumshindilia risasi kama ataendelea kuwawekea ngumu kuhusu Kamba.
Hata hivyo, hakutaka kujidanganya kuwa kitendo cha kuwaambia ukweli kinaweza kumsalimisha na mkono huo wa dola. Hapana. Wataondoka naye hadi watakapompata Kamba na huenda hata hivyo na yeye akajumuishwa kama jambazi sugu na muuaji mkubwa.
Kwa hali hiyo, akaamua kupasua jipu. “Yuko Manzese wazee wangu,” alisema kwa tabu.
“Manzese ipi?” Kitowela alimuuliza haraka.
“Sijui, labda niongee naye.”
“Sasa unaanza kuwa na akili,” Inspekta alimwambia huku akiutoa mguu uliokuwa umekita kifuani. Papohapo akampekua na kutoa simu mfukoni na alifanya hivyo kwa kuwa hakuamini kuwa hana silaha.
Unaweza kumwachia atoe simu na badala yake isitolewe simu ikatolewa bastola. Kitakachofuata ni nini?
Inspekta alipoitoa simu alimwambia, “Umesevu kwa jina gani?”
“Kamba.”
Inspekta akacheza na vidubwasha vya simu hiyo kisha akaitega sikioni na kusikia ikinguruma. Haraka akaunganisha ‘loud speaker’ kisha akampa Jitu huku akimwamuru, “Ongea naye. Muulize kuwa yuko wapi na unataka kuonana naye. Zungumza katika sauti ya kawaida. Usiseme kuwa uko chini ya ulinzi! Vinginevyo…”
Huku akihema kwa shida, Jitu alitwaa simu hiyo na kuitega katika sikio la kulia.
Zinduna aliendelea kumwadhibu Kamba kwa namna ya kipekee, akiutumia huu ulimi wake kitaalamu kiasi cha Kamba kujiona akipaa hadi katika sayari nyingine. Na hawakuhitaji kulihama sofa hilo kubwa, bali kilipofika kipindi ambacho Zinduna aliona kuwa ni mwafaka kwa utekelezaji wa hatua nyingine, alichojoa nguo na kumfuata Kamba palepale.
Ikafuata hatua nyingine ambayo kwa kiasi kikubwa ilimsahaulisha Kamba na mawazo kuhusu mambo yaliyotokea jana na hatua inayopaswa kuchukuliwa leo katika kuendelea kujilinda. Zinduna alijua kumsahaulisha, akivitumia viungo vyake kwa umahiri mkubwa huku kinywa chake sasa kikiropoka yale aliyoamini huwa ni burudani zaidi masikioni mwa mwanamume hususan katika kipindi kama hicho.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Labda wangeendelea na kuendelea kama simu hii ya Kamba iliyokuwa katika sofa lingine isingeanza kuita bila kukoma. Iliita hadi ikakatika na ikaanza kuita tena. Ni hapo ndipo akili ya Kamba ilipozinduka.
“Subiri kidogo…” alitamka kwa shida akijaribu kumsogeza taratibu Zinduna aliyekuwa amemdhibiti kwa namna yake, akiwa amesimika mguu huu huku na huu kule, halikadhalika mikono, huku matiti yake yenye uhai yakichezacheza kadiri alivyokuwa akijituma, akiwa hatofautiani na mwanariadha anayesubiri kuambiwa on your marks.
Zinduna hakuonekana kukubali, zaidi aliongeza kasi. Hata hivyo, sasa Kamba alihisi jambo zaidi ya jambo katika simu hiyo. Alikumbuka kuwa hakuna mtu yeyote mwenye namba yake ya simu zaidi ya Jitu. Hata yule mwanamke aliyepiga muda fulani asubuhi hii, aliamini kuwa ni kati ya wale malaya wanaobahatisha namba ili wawanase wanaume wakware.
“Subiri…” Kamba alisema tena, na safari hii kilichomfanya Zinduna atii kauli hiyo ni baada ya kugundua kuwa Kamba hakuwa na msisimko tena maungoni mwake. Hakuwa yule Kamba wa dakika chache zilizopita, akiwa timilifu katika idara zote. Taratibu mtoto wa kike akajing’atua na kujitupa pembeni.
Kamba akanyanyuka na kuifuata simu. Alipoiangalia kwenye kioo akashtuka; jina la JITU lilielea. Haraka, bila ya kufikiri zaidi akabonyeza kitufe cha kupokelea na kuitega sikioni. “Haloo!” akasema huku akihema kwa nguvu, kwa mbali wasiwasi ukimwingia.
“Kamba vipi?” ilikuwa ni sauti ya Jitu.
“Poa tu. Vipi msh’kaji?”
“Uko wapi?”
Bado niponipo…sijasepa, labda kesho. Kwani vipi?”
“Nilitaka tuonane mara moja.”
“Njoo Manzese.”
“Manzese ipi?”
“Unaijua Tanganyika Hotel?”
“Siijui. Iko Manzese gani?”
“Ukifika Manzese Darajani utaiona. Iko kulia kama unatoka Magomeni. Ghorofa tatu.”
“Poa, nakuja. Please, usitoke.”
“Poa. Lakini kwani vipi, kimenuka?”
Simu ilikatwa.
*****
Mazungumzo yote kati ya Kamba na Jitu yaliwafikia Inspekta Maliyatabu na wenzake kwa usahihi. Kwa hali hiyo, wakati Kamba alipouliza lile swali, vipi kimenuka? Maliyatabu hakumwachia Jitu ajibu chochote, alimnyang’anya simu hiyo na kuikata kisha akaizima!
Jitu akapigwa pingu na kuamriwa kutangulia kutoka humo ofisini. Kundi zima hilo lilipofika nje, Inspekta Maliyatabu akamwamuru Jitu aingie ndani ya ile Land Rover Defender na akaketi chini huku wale askari wengine wakiwa wamesimama.
Gari likaondoka kwa kasi likielekea Manzese. Jitu akiwa ameketi huku pingu zikiwa zimemzingira mikono, alijihisi kuwa yuko katika dunia mpya, dunia isiyoelezeka kwa urahisi. Aliyaona maisha yake yako ukingoni. Akamkumbuka mkewe aliyemwacha nyumbani. Akawakumbuka wanaye! Ndoto za kunusurika katika mkono wa sheria zikamtoka. Kwa kiasi fulani akajilaumu kwa kuchukua hatua ya kumfuata Kamba siku alipotoka gerezani na kumpa pesa za pole. Kwani angeachana naye kungetokea nini? Kamba angejua chochote?
Amempa pesa, shilingi milioni tano, lakini sasa Kamba kishatibua mambo na matokeo yake ndiyo haya! Jitu alijuta, akakiona kiza kinene mbele yake!
Hatimaye gari lilikuwa likivuka eneo la Mwembechai. Maliyatabu akakumbuka kuwa wakati Jitu akizungumza na Kamba kwa simu maneno yote waliyasikia. Akakumbuka pia kuwa alimsikia Kamba akisema yuko Tanganyika Hotel.
Tabasamu la mbali likamtoka Inspekta Maliyatabu kwa kuwa aliijua hiyo hoteli. Mara mbili aliwahi kufika hapo kwa sababu zake binafsi akiwa na rafiki yake wa kike na kuchukua saa kadhaa wakistarehe.
Walipofika Darajani, gari likaegeshwa na Maliyatabu akaitwaa tena simu ya Jitu. Akabonyeza jina la Kamba kisha akamsogezea mdomoni Jitu huku akimwambia kwa ukali lakini kwa sauti ya chini sana, “Mwambie neno moja tu, kwamba umefika! Basi!”
Huku simu ikiwa imetegwa loud speaker ili sauti iwafikie wote, Jitu alisubiri wakati simu ikiita upande wa pili. Hatimaye sauti nzito ikasikika: “Haloo, u’shafika?”
“Nipo Darajani,” Jitu alijibu kwa taharuki.
“Ok, njoo moja kwa moja ghorofa ya kwanza chumba namba ishirini.”
“Poa.”
Maliyatabu akaikata simu papohapo. “Twendeni!” akawaambia askari wote huku Jitu naye akishurutishwa kuteremka na kwenda nao, pingu mikononi mwake vilevile!
“Hapa ni kujitoa mhanga!” Maliyatabu alimwambia Kitowela kwa sauti ya chini, macho yake mekundu yakimtazama kwa chati, uso ukionekana kutawaliwa na hasira zilizochanganyika na taharuki. Akaongeza, “Hii ni hatua ya mwisho kwetu Kito! Fanya chochote bila kujali matokeo, mradi tumalize mchezo!”
Kisha akawageukia wale askari na kuwaambia, “Mtafikia pale reception na huyu bwege. Sisi tutakwenda moja kwa moja kwenye room aliyotaja. Ole wake tusimkute! Kichwa cha huyu bwege kitakuwa halali yetu!” Mara akamtazama Jitu usoni sawia na kumbwatukia, “Ole wako tusimkute, nitakuua kwa risasi zote zilizomo humu!”
Walitembea kwa hatua za kikakamavu, hadi mapokezi ambako Inspekta Maliyatabu alimfuata mhudumu aliyekuwa ndani ya chumba maalumu na kumtolea kitambulisho huku akimwambia kwa sauti ya chini, “Tunakwenda chumba namba ishirini.”
Hakusubiri ruhusa wala kauli yoyote kutoka kwa huyo mhudumu wa kike ambaye tayari macho yake yalionesha bayana woga uliomkumba. Maliyatabu na Kitowela wakazikwaa ngazi harakaharaka wakielekea ghorofa ya kwanza.
Walipoifikia korido ya ghorofa hiyo, wakatazamana kisha wakazisoma namba katika vyumba vitatu na kutambua kuwa uelekeo wao ungekuwa upi. Kiaskari zaidi wakavuta hatua na kukifuata chumba husika. Punde wakawa kando ya chumba namba 20.
Wakatazamana tena kisha Kitowela akagonga mlango mara mbili. Wakatulia wakisubiri kuona kitakachotokea. Mara kitasa kikazungushwa na mlango ukafunguliwa.
amba Kiroboto alikuwa mbele yao!
SURA YA ISHIRINI
MARA tu Kamba alipomaliza kuongea na Jitu alimgeukia Zinduna na kumwambia, “Kuna jamaa yangu anakuja kwa maongezi. Sipendi akukute. Kanisubiri kidogo nje kama dakika tano hivi.”
Zinduna alivaa harakaharaka na kumwambia Kamba, “Lakini mida hii mimi siko kazini. Wenzangu wakiniona nazagaazagaa hapa watanishangaa. Nataka n’ende zangu home.”
Kamba alimwelewa. Huku akiwa amevaa boksa pekee, alilifuata begi na kulifungua kisha akachomoa noti mbili za shilingi elfu kumi, kumi na kumpatia huku akiongezea, “Tuonane jioni. Mi’ nipo mpaka keshokutwa.”
“Poa,” Zinduna alijibu huku akipokea noti zile na kuondoka.
Kamba akarudi sofani na kujitupa kivivuvivu, akivitafakari vituko alivyofanyiwa na Zinduna muda mfupi uliopita na kujikuta akimpongeza kimoyomoyo kuwa ni miongoni mwa wanawake wanaoijua kazi yao pale wakutanapo na wanaume wenye ‘njaa.’
Aliendelea kujilaza akimsubiri Jitu, akiamini kuwa atakuwa jirani kwani hoteli hiyo iko kando tu ya Barabara ya Morogoro na ingawa hakujua kuwa wakati Jitu anampigia alikuwa wapi, hata hivyo kwa jinsi miundombinu ya sasa ya Jiji la Dar ilivyo na kwa muda huo wa mchana, na akitambua kuwa Jitu ana gari, haikumwingia akilini kuwa inaweza kufika saa nzima hajafika.
Mara akajikuta akijiwa na wazo jipya. Akajiuliza, ni kipi kilichomfanya Jitu aamue kuja kuonana naye kwa mfumo huo? Wakati wakiongea sauti yake haikuwa ya kawaida. Alikuwa kama mwenye taharuki hivi. Alizungumza kwa sauti isiyokuwa ya kawaida. Na kuna wakati, kabla ya kutamka neno alihema kwanza, kwa nguvu.
Kuna nini? Kimenuka? Akilini alijenga hisia kuwa huenda Jitu amepata taarifa mbaya na hivyo ameona kuwa si vizuri kuongea kwenye simu, akaamua kuja kumwona na kuzungumza kinagaubaga.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jana waliagana vizuri, Jitu akimtaka atulie kidogo na kama mambo yataharibika ndipo aondoke Dar. Hazijapita hata saa ishirini na nne tangu waachane, Jitu anampigia na kumtaka waonane! Hapana, hapa kuna kitu, aliwaza. Na papohapo akaamua kuichukua hadhari. Haraka akavaa na kuwa tayari kama hata itamlazimu kuondoka muda wowote kuanzia dakika hiyo. Kisha akalifungua begi na kuziangalia pesa zake. Alipohakikisha kuwa ziko salama, akaitoa bastola aliyompora Makela, akaitia mfukoni kisha akalifunga begi hilo na kulipachika mgongoni, mikanda miwili iliyozunguka mabegani ikiwa ni nyenzo madhubuti.
Akaitazama saa na kujenga hisia kuwa huenda Jitu hayuko mbali, lakini ni jambo gani lililomfanya aje kuonana naye ghafla hivyo? Na kwa nini hakumjibu kitu alipomuuliza kama mambo yameharibika? Kwa nini alikata simu haraka? Kuna nini?
Kitu fulani akilini mwake kikamwambia, uwe makini. Usijione uko salama kwa asilimia mia moja. Sasa hakuketi sofani tena, badala yake akawa akizungukazunguka humo chumbani, chupa ya bia mkononi, akinywa funda hadi funda taratibu, lakini bado akihisi kuna jambo zaidi ya jambo mbele yake.
Kwa muda wa dakika tano akiwa anazungukazunguka humo chumbani, akaamua kutwaa simu na kumpigia Jitu ili amuulize kafika wapi. Kilichotokea kikamshangaza; jibu lililomjia ni namba unayopiga kwa sasa haipatikani. Hakukubali, akatulia kwa dakika mbili, tatu kisha akapiga tena kwa kuamini kuwa mara nyingi mitandao ya simu hupoteza mawasiliano kutokana na sababu za kiufundi. Jibu likawa lilelile. Mara ya tatu, tatizo lilelile!
Akaguna na kuirejesha simu mfukoni. Akaenda dirishani kuchungulia. Papohapo akasonya baada ya kugundua kuwa dirisha hilo haliwezi kumsaidia kuiona Barabara ya Morogoro ambako alijua kuwa ndiko atakakotokea Jitu. Chumba hiki kilikuwa upanda wa nyuma wa hoteli hiyo, hivyo alichoambulia ni nyumba nyingi za wakazi zilizosongamana katika eneo hilo.
Ni wakati alipogeuka kutoka kuziangalia nyumba za wakazi ndipo aliposikia mlango ukigongwa mara mbili kistaarabu. Hakuwa na fikra za kujiwa na mhudumu wa hoteli, zaidi alimfikiria Jitu ambaye wamezungumza naye muda mfupi uliopita.
Akanyanyuka na kwenda mlangoni. Kitasa kilipomtii, kisha akaufungua mlango, ndipo macho yake yakashindwa kuamini yakionacho! Wanaume wawili wenye miili ya kikakamavu, macho makali, walikuwa mbele yake na kabla hajajua ni kipi kinachoendelea, akasukumwa na kono la mmojawao huku mwingine akitoa bastola na kumwelekezea kisha akamwambia kwa ukali, “Uko chini ya ulinzi! Kaa chini!”
Kilikuwa ni kipindi kibaya sana kwa Kamba. Tayari akajua kuwa Jitu ndiye kasababisha yote haya. Kitu kimoja kikawa kikimtahadharisha kichwani, ‘usiwe bwege…hii ni nafasi yako ya mwisho…cheza karata yako kwa umakini wa hali ya juu…vinginevyo sasa jela inakuita na kitanzi kitakupokea….’
“Kaa chini!” Kitowela aliyekuwa ameishika bastola ile akairudia kauli yake safari hii kwa msisitizo mkali zaidi.
Haikuwa amri ambayo Kamba aliiheshimu au kuiogopa. Na hakuwa mtu wa kukiogopa kifo lakini hakupenda kiingilie ratiba zake. Alishaamua kuwa lazima atekeleze malengo yake, na ameyatekeleza. Kufyatua risasi kwa usahihi mkubwa dhidi ya Mwasia Ladhu Hassanali Ladhu na mwanaye, Hassanali kisha akamshindilia kisu mfanyakazi wao, Juma katika muda wa dakika kumi tu, tena ndani ya jengo moja, ulikuwa ni mwanzo mzuri katika utekelezaji wa maazimio yake.
Kumfuata Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay, James Ntilampa nyumbani kwake na kumvunja shingo mbele ya mkewe aliichukulia kama hatua nyingine muhimu kwake katika operesheni maalum aliyoianza. Isitoshe, kitendo cha kuinua bastola na kufyatua risasi kwa shabaha kali pale Machopi Bar, risasi iliyozama kifuani mwa Hakimu John Mwakipesile na kuikata pumzi yake ya uhai, lilikuwa ni pigo la mwisho alilodhamiria kulitoa kwa wote walioshiriki katika kumsotesha jela kwa miaka saba.
Kwa hali hiyo, sasa alikuwa tayari kwa lolote. Hii bastola iliyoshikwa kwa uthabiti na kono la Sajini Kitowela, ikimtazama, alijua wakati wowote inaweza kutema risasi na hapo ukawa ni mwisho jina la Kamba Kiroboto aliye hai. Na kama alivyokwishaweka nadhiri, hakuhofia kufa bali alihofia kufa kabla hajayatimiza malengo yake. Hivyo hata muda huu alijua kuwa anaweza kufa kwa kuwa alizijua hasira za askari polisi kutokana na matukio aliyoyafanya ndani ya saa ishirini na nne tu!
Niko tayari kufa lakini siyo kufa kikondoo, alijiapiza. Ndipo, kwa kasi isiyo ya kawaida na kwa shabaha isiyo ya kawaida, alirusha teke kwa guu la kulia, teke lililogota sawia kwenye mkono wa Kitowela ulioishika bastola! Bastola hiyo ikapaa hewani na kuligonga dari kisha ikarudi sakafuni.
Alikuwa amechokoza nyuki! Mateke mawili, mazito kutoka kwa Sajini Kitowela, yalimjia kwa wepesi uliodhihirisha uwezo na utaalamu wa askari huyo katika taaluma yake, moja likampata mbavuni kwa usahihi ilhali akifanikiwa kuzuia la pili kwa kono lake la kulia. Naye akachukua uamuzi wa haraka, papohapo akamsukumizia Kitowela konde zito ambalo halikukosa shabaha, likakifikia kidevu cha Kitowela na kumsukuma nyuma kiasi cha kumgonga Inspekta Maliyatabu. Askari hao wakapepesuka na kujikuta wakiacha mwanya mdogo mlangoni.
Kamba akazidi kutekeleza kile alichoamua; akakaza misuli ya tumbo na kunyanyua guu la kulia, teke la kukandamiza likamtoka, teke lililokuwa na uzito wa kilo nyingi nyuma yake, likatua chini kidogo ya tumbo la Inspekta Maliyatabu. Inspekta akajikuta akijikunja kwa maumivu, tendo lililokuwa kosa kubwa, sekunde ya pili Kamba alikuwa ameshampiga kumbo la haja na kupenya mlangoni kwa kasi.
Wakati huo Maliyatabu naye alikuwa amekwishaweka bastola mkononi na alikuwa ameamua kummaliza Kamba, lakini kitendo cha kupigwa kumbo kikawa kimemzuia asitekeleze jukumu hilo kwa ufanisi. Akajikuta akipoteza mwelekeo na hivyo kusita kufyatua risasi kwa kuhofia kumjeruhi au kumuua mwenzake bila ya kudhamiria.
Wepesi wa Kamba haukuwa wa kawaida, alipokwishapenya nje ya chumba alikimbia kwa kasi koridoni na alipozifikia ngazi alishuka kwa kuruka mbili, mbiIi kama kichaa bastola ikiwa mkono wa kulia! Muda mfupi baadaye alikuwa amefika chini. Akamwona Jitu ametiwa pingu, wale askari wengine wakiwa kando yake. Akajua kuwa tayari mambo si mambo. Hakuhitaji kujiuliza imekuwaje askari wakayang’amua hayo maficho yake. Jitu ndiye aliyekuwa jibu halisi.
Hata hivyo, hakuwa na muda wa kushughulika na Jitu kwa kuwa aliijua hatari iliyomkabili, akiamini kuwa askari aliowakimbia huko juu watakuwa wakimwandama, hivyo alihitaji kuwa katika mazingira yenye usalama zaidi kabla ya kutokomea au kupambana nao. Kuna hawa askari waliomweka chini ya ulinzi Jitu na kuna wale aliowakimbia kule ghorofani. Ni idadi kubwa, hivyo alihitaji kuwa makini sana na kutumia akili zaidi kama kweli anataka kusalimika.
Alipita kasi akikimbilia nje na kabla hajavuka mlango akakumbana na mhudumu mwenye sinia lenye chupa ya chai, kikombe cha kauri na sahani yenye mayai ya kukaanga huenda akimpelekea mteja. Kamba hakuwa na muda wa kumkwepa, alimpamia na kumwacha akianguka huku, sinia la stafutahi kule!
Wale askari waliokuwa na Jitu walishtuka lakini wakashindwa kuchukua hatua yoyote kwa kuwa kati yao hakuna aliyekuwa na silaha. Na muda huohuo wakawaona Inspekta Maliyatabu na Kitowela wakishuka mbiombio huku Kitowela akitokwa damu mdomoni. Walipofika nje Inspekta Maliyatabu alimwona Kamba akivuka barabara kuu, akikimbia. Inspekta akafyatua risasi mbili ambazo zote zilipita patupu, moja ikalivaa bodi la lori lililokuwa katika uelekeo wa Magomeni na nyingine ikazama kando ya barabara.
Kamba hakusimama, akaendelea kukimbia. Mara akaliona lori la kubeba mchanga lililokuwa likielekea upande wa Ubungo. Akazidisha kasi kulikimbilia huku akiyakwepa magari mengine. Huku nyuma, Inspekta Maliyatabu na Kitowela na askari mwingine walikuwa wakimwandama huku mara chache na kwa hadhari wakimrushia risasi ambazo ziliambulia patupu.
Mbio zake zikazaa matunda pale alipofanikiwa kulifikia lile lori na kulidandia kisha akajirusha ndani. Akaanguka kama gunia kwa kuwa hakukuwa na chochote huko ndani. Huyu hakuwa Kamba wa kuhisi maumivu, alikuwa Kamba mwingine aliyejali usalama wake. Hivyo hata hakujua hata kaanguka vipi. Sekunde ya kwanza alikuwa kalala katika sakafu ya lori na sekunde ya tatu alikuwa kaka.
Hata hivyo, kwa hasira ambazo hakujua ni kwa vipi zilimjia kwa nguvu kubwa, akaamua kutokeza kichwa juu na kuchungulia nje huku sasa gari hilo likienda taratibu kutokana na msongamano wa magari kwenye njiapanda ya kuelekea Mabibo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akawaona Inspekta Maliyatabu na Kitowela wakikimbia kwa nguvu wakilifuata lori hilo na sasa walikuwa wamelikaribia kwa umbali wa hatua kama kumi tu! Kamba aliyajua matokeo ya kukamatwa na askari hao; kifo au mateso makali yanayoweza kumtia kilema na hata kusababisha kifo.
Hivyo, akiwa na nadhiri yake ileile ya kutoogopa kufa bali afe baada ya kutimiza malengo yake, aliinyanyua bastola na kulenga kwa shabaha kali kisha akafyatua risasi moja kumwelekea Inspekta Maliyatabu. Hakuwa na uhakika kama risasi aliyofyatua imefanya kazi kwa usahihi, lakini muda wa kuthibitisha hilo hakuwa nao, hivyo papohapo, kwa kasi ya ajabu akaielekeza bastola usawa wa paji la Sajini Kitowela.
Risasi ya pili ikamtoka!
Sasa alikuwa kama kichaa, akafyatua tena risasi moja kwa yule askari mwingine!
*****
Ilikuwa ni kama sinema ya kutisha machoni mwa yeyote aliyekuwa katika eneo hilo na kushuhudia kwa usahihi. Risasi iliyotoka kwenye bastola ya Kamba ilipenya kwenye paji la uso wa Inspekta Maliyatabu na kuacha taswira ya kutisha kisogoni. Inspekta aliruka juu na kuanguka chali barabarani! Bastola yake ikaserereka kwenye lami kwa zaidi ya hatua kumi kutoka pale alipoangukia.
Daladala lililotokea Kimara lilikuwa katika mwendo mkali na dereva hakuwa na uwezo kumkwepa Maliyatabu, tairi la kulia likapanda juu ya kichwa chake na kutoa kishindo kama mlipuko wa baruti ndogo! Dereva akataharuki na kuongeza mwendo zaidi!
Katika sekunde hizohizo, Kitowela naye alikuwa akitapatapa baada ya risasi iliyodhamiriwa kutua kwenye paji lake kukosa shabaha na kupenya shingoni kisha kutokeza upande wa pili.
Wakati akiipigania roho yake bila mafanikio, askari mwingine, huyu akiwa ni kati ya wale watatu waliokuwa wakimchunga Jitu, yeye alishtukia kitu chenye joto kali kikipenya katika bega la kushoto na kumzulia maumivu makali! Hakuhitaji kujiuliza ni kipi kilichompata. Tangu pale Kamba alipoibuka na kulenga bastola kwa Maliyatabu alimwona lakini hakuwa na uwezo wa kumzuia asifanye kile alichokidhamiria.
Maumivu ya risasi hiyo yalimfanya askari huyo asitishe kufanya chochote kile na badala yake akainama na kulishika bega huku akigugumia kwa maumivu.
Kukawa na vurugu kubwa katika eneo hilo. Watu wakawa wakikimbia huku na kule katika kuzisalimisha roho zao. Ni wengi waliokimbia, siyo wote. Baadhi, wale wenye ‘mioyo ya mawe’ walikimbilia pale ulipokuwa mwili wa Inspekta Maliyatabu na kushuhudia kichwa kikiwa kimesagwa huku damu imetapakaa barabarani na kutoa taswira ya kutisha machoni mwa yeyote aliyeshuhudia.
Hali hiyo iliyozuka ndani ya dakika zisizotimu tano iliwafanya wale askari wawili waliobaki wakiwa wamemweka chini ya ulinzi Jitu kule Tanganyika Hotel, wajikute wakishindwa kupata uamuzi wa haraka na sahihi nini wafanye. Punde askari mmoja akatoka nje na kwenda kushuhudia kule barabarani ambako watu walikuwa wameuzunguka mwili wa Inspekta Maliyatabu. Haikutimu hata dakika moja akawa amerudi macho yamemtoka pima!
“Simon piga simu central! Wameuawa na mhalifu anazidi kutokomea!” alimwambia mwenzake.
Simon akatwaa simu na kupiga Kituo Kikuu cha Polisi.
*****
Wakati Inspekta Maliyatabu na wenzake wakiondoka na Jitu katika ofisi za KINTEL kuelekea Manzese, Tina hakuandamana nao. Yeye alirudi ofisini kutekeleza majukumu mengine. Wakati akiendelea na kazi ndipo simu ilipomjia, simu iliyomshtua na kumsononesha.
“Afande Maliyatabu, Kitowela na Mahfudh wameuawa na mtuhumiwa…!”
“Nini!” Tina alibwata simuni. “Wameuawa! Mbona sikuelewi?”
“Wameuawa! Hapa nimebaki mimi na Kasha tukiwa na mtuhumiwa Jitu! Kamba kakimbilia lori lakini ana silaha!”
“Mmh! My God…!” Tina alibwata.
“ Tuma askari wenye silaha…tunashindwa kumwacha huyu mtuhumiwa Jitu peke yake! Hatuna silaha! Tuko Tanganyika Hotel! Haraka sana afande!”
Dakika tano baadaye Land Rover nyingine ikiwa na askari watatu wenye silaha nzito ilikuwa ikiondoka kwa kasi ya kutisha katika Kituo Kikuu cha Polisi, taa kubwa zikiwa zimewashwa na king’ora kikipigwa njia nzima!
Dakika chache baadaye walikuwa Barabara ya Morogoro ambako dereva alikanyaga moto zaidi, Land Rover ikawa kama vile inataka kupaa! Askari wa Usalama Barabarani wakiwa wameshataarifiwa juu ya mkasa huo, walihakikisha njia ya kwenda Manzese inakuwa nyeupe, kuipisha hiyo Land Rover iliyokuwa ikinguruma kama vile injini inataka kupasuka!
*****
Kusuasua kwa lile lori pale njiapanda ya kwenda Mabibo kulimtia shaka Kamba kuhusu usalama wake. Bastola ikiwa bado inang’aa mkononi, alirukia nje, kushoto mwa gari kisha akakimbia huku akipunga mkono juu, bastola ikiwa imemtangulia, akiashiria kumlipua yeyote ambaye angemtilia kikwazo.
Hata hivyo, katika kujihakikishia usalama zaidi, alipiga risasi moja angani, tendo lililozidi kuwatia taharuki waliokuwa katika eneo hilo. Papohapo akamvaa dereva wa bodaboda aliyekuwa ameegesha kando ya barabara hiyo. Akamlenga bastola usoni na kumwamuru, “Haraka sana shika njia ya Ubungo!” tusi zito la nguoni likafuata, tusi liwezalo kumtia mtu kiza machoni na kuzipasua ngoma za masikio japo lilitoka kwa sauti ya kawaida.
Kijana yule alitetemeka na kuiwasha pikipiki kwa wasiwasi lakini akafanikiwa kuiondoa. Muda mfupi baadaye walikuwa wakivuka njiapanda ya Barabara ya Shekilango, kama vile Mungu alikuwa upande wao, taa za Usalama Barabarani kwenye makutano ya barabara hiyo ya Morogoro, Sam Nujoma na Mandela zilikuwa zikitoa nuru ya kijani.
Magari yalikuwa yakienda kasi hivyo hata huyu kijana wa bodaboda naye alikanyaga moto zaidi na pikipiki yake aina ya Boxer.
“Kanyaga moto!” Kamba alimhimiza wakati walipokuwa wakiianza Kimara.
Walipofika Kimara Resort, Kamba akafoka, “Chepuka katika barabara yoyote ya uchochoroni kisha usimame!”
Dereva alitii. Mbele kidogo akapunguza mwendo na kuingia katika barabara ya vumbi, akaendelea kukanyaga moto japo sasa hakuwa katika mwendo mkali. Akaendesha akifuata tu njia ilhali hajui anakokwenda.
Kisha: “Simama!” Kamba alimwamuru.
Dereva akatii kwa mara nyingine.
“Nipe pesa!” amri nyingine.
Huku akitetemeka, dereva huyo aliingiza mkono mfukoni na kutoa pesa zote. Shilingi 70,000. Kamba akazinyakua haraka na kuongeza kwa ukali uleule: “Potea machoni mwangu haraka sana…potea!”
Dakika iliyofuata Kamba alikuwa kando ya duka moja ambako alifanikiwa kununua shati na akalivaa hapohapo, akanunua kofia pana, ikatinga kichwani na koti lenye shingo ndefu likavaliwa juu likifunika kuanzia kichwani na kuacha sehemu ya uso pekee.
Wakati huo akawa akiwaza kutumia usafiri mwingine wowote utakaomfikisha Morogoro na kutoka hapo atatumia usafiri mwingine hadi Kigoma. Wakati Jeshi la Polisi litakapokuwa likihaha katika msako mkali zaidi dhidi yake, yeye atakuwa ndani ya meli ya Mwongozo akienda Burundi!
Pesa ninazo, kipi kitashindikana? Kwa Tanzania ya leo kuna lisilowezekana mbele ya pesa? alijiuliza huku akitabasamu.
Akajitazama kutoka juu mpaka chini. Akaridhika kuwa sasa alikuwa tofauti. Akatokeza barabarani na baada ya muda mfupi akaiona Coaster ikija kasi. Akapunga mkono, ikasimama.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Morogoro mjomba!” kondakta alimwambia.
Kamba ndani! Coaster ikasaga lami kwa kasi ya kutisha!
Walipovuka Chalinze, Kamba akashusha pumzi na kutabasamu!
HITIMISHO
Askari waliotoka Kituo Kikuu walifika Manzese na kujikuta wakiduwaa baada ya kusikia kuwa mtu waliyemfuata ametokomea na pikipiki… Mpaka leo Jeshi la Polisi halijafanikiwa kujua Kamba ametokomea wapi, tume zinaundwa, tume zinavunjwa bado ni kiza kinene.
0 comments:
Post a Comment