IMEANDIKWA NA : HASSAN O MAMBOSASA
*********************************************************************************
Simulizi : Wakala Wa Giza
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
(MFUNIKO)
Mlio wa saa ya mezani ndiyo ulisikika ukileta bugudha katika kitanda walicholala wapendanao majira ya asubuhi ikiashiria muda waliokuwa wanahitaji kuwa macho wakati bado usingizi unawazonga ndiyo huo umewadia, wa kwanza kushtuka alikuwa mwenye jinsia ya kiume ambaye baada ya kushtuka tu alinyanyua mikono juu kisha akaipeleka kushoto na kulia ili kunyoosha baadhi ya viungo halafu akamuangalia mpenzi wake aliyekuwa amelala usingizi. Alimuamsha taratibu sana kwa namna isiyoleta karaha kwa mpenzi wake halafu akampiga busu baada tu ya mpenzi wake kuamka, alinyanyuka kitandani akaelekea sehemu kilipo kioo cha kabati dogo la kuwekea vipodozi na uturi wa aina mbalimbali wanaoutumia, mwanaume huyo alipofika hapo kwenye kioo alijiangalia kwa muda akakagua uso wake na aliporidhika akageuka upande wa kitandani akamuona mpenzi akiwa amekaa kitako huku sehemu kubwa ya mapaja yake ikiwa ipo wazi kutokana na kuvaa gauni fupi la kulalia. Mwanaume huyo alibaki akimtazama mpenzi kwa muda mrefu hadi mwanamke huyo akajua kwamba anatazamwa na mpenzi wake tena kwa mshangao.
"Mbona unaniangalia hivyo jamani?" Mwanamke aliuliza huku akiangalia chini.
"Yaani mke wangu kama ndiyo kwanza nakuona, kila siku wewe ni mpya ndani ya macho yangu kuanzia urembo wako hadi...dah! Ngoja niache" Mwanaume huyo huyo aliongea huku akiachia tabasamu lililomfanya aonekane na mvuto zaidi kuliko hata ilivyokuwa awali.
"Hata wewe nakuona ni mwanaume mpya kila saa ndiyo maana hata ukiwa unaendesha gari kuelekea kazini huwa siishi kukutazama machoni huku nikiwa nina tabasamu usoni mwangu mume wangu, Moses nakupenda sana mume wangu" Maneno hayo yalimtoka mwanamke huyo akiwa amesimama na kulifanya umbo lake tata na mapaja yaliyo jaa vionekane dhahiri ambapo laiti kama vikionekana mbele ya mwanaume mkamilifu yoyote basi lazima aingiwe na matamanio papo hapo, kifua chake kichanga kisichofunikwa na kitu kingine chochote zaidi ya gauni laini la kulalia ndiyo kilionekana na kilimfanya aonekane mrembo zaidi kwa Moses.
"Hata mimi nakupenda pia Beatrice na sitaacha kukuonesha nakupenda na hata ikibidi nitumie misamiati mbalimbali ila ibebe ujumbe huo wa kuonesha jinsi gani ninavyokupenda mke wangu" Moses aliongea kisha akamkumbatia mke wake kwa mapenzi ya dhati.
"Nafurahi sana kusikia unanipenda kama ninavyokupenda mimi mume wangu, nina suprise yako muda huu jana sikukuambia" Beatrice aliongea baada tu ya kuachiana na Moses huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu halafu akageuka akampa mgongo Moses, hiyo ilikuwa ishara tosha kwa Moses ambapo na yeye alimkumbatia mke wake kwa nyuma halafu akampiga busu sehemu ya juu ya sikio na kupelekea Beatrice asisimkwe mwili mzima.
"My queen tell me( malkia wangu miambie)" Moses alimuambia Beatrice jirani kabisa na sikio lake tena kwa sauti ya chini huku akitoa muhemo hafifu, Beatrice aliposikia hiyo kauli ya Moses aliuchukua mkono wa kuume wa Moses akauweka tumboni mwake halafu akasema, "You guess what? (we unadhani nini?)"
"Wooow! Don't tell me, I'll be crazy more than now(Wooow! Usiniambie, nitakuwa kichaa zaidi ya sasa)" Moses aliongea huku akiwa amepigwa na mshangao pamoja na tabasamu kubwa usoni mwake.
"Nimenasa Moses na nimejua jana tu na leo asubuhi ndiyo nilitaka ujue kama ulivyojua sasa hivi" Beatrice aliongea huku akimuegemea Moses kwa nyuma, kauli hiyo ilimfanya Mosea ambusu mara nyingi sehemu za shingoni, kwenye mashavu na mdomoni hadi Beatrice akaanza kupata msisimko mwili mzima.
"Moses hapana siyo sasa hivi mume wangu, tutachelewa kazini twende tukaoge bwana" Beatrice alimuambia Moses ambaye alimuonesha kumuelewa na wote wakatoka wakaelekea bafuni.
Baada ya nusu saa wapendanao hao walitoka pamoja wakiwa wanatumia gari moja wakaelekea kazini kama ilivyo kawaida yao katika siku za kazi, Beatrice alipelekwa mpaka kazini kwake posta kwenye jengo la Benjamin william mkapa ambalo ni makao makuu ya shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Moses kumshusha mke wake katika jengo analofanyia kazi aliimgiza gari barabarani akiwa na tabasamu kubwa usoni mwake kutokana na taarifa aliyoambiwa pindi alipoamka, baada ya dakika kumi na tano alikuwa tayari ameshafika katika jengo la maabara kubwa ya umoja wa mataifa iliyojengwa maeneo ya Magogoni jijini Dar es salaam katika wilaya ya Ilala. Ilikuwa ndiyo eneo lake analofanyia kaziili kuweza kuficha utambulisho wake wa pili kama mkurugenzi wa idara ya usalama aliyeteuliwa na Rais Zuber Ameir baada tu ya kuingia toka apinduliwe rais muovu Filbert Ole aliyetaka kuuza rasilimali za nchi kwa wahalifu wa kimataifa waliokuwa chini Hilton maarufu kama eagle the don ambye kwa muda huo tayari alikuwa ni marehemu baada ya kuangamizwa katika OPERESHENI FAGIO LA CHUMA iliyokuwa ikifagia viongozi wote waovu ndani ya jamhuri ya muungano pamoja na vibaraka wao wote. Ulikuwa ni mwaka wa tatu umepita tangu operesheni hiyo imefanyika na kuleta mapinduzi makubwa kwa watanzania baada ya kuondoshwa uongozi usiofaa kwa wananchi.
Moses akiwa na furaha kubwa usoni alitembea huku akitabasamu na alikuwa akisalimiana na wanafanyakazi wenzake kama ilivyo kawaida ingawa siku hiyo uchamgamfu wake tofauti na ilivyo siku nyingine, ujauzito wa mkewe Beatrice ndiyo ulimfanya afurahi kuliko kitu chochote kwani alijua baada ya miezi kadhaa angeitwa baba baada ya Beatrice kujifungua mtoto aliyekuwa amembeba katika tumbo lake. Kawaida ya wanaume wote walioko kwenye ndoa ambao huwa na ndoto za kuwa familia wakipata habari kama hiyo ni lazima wawe na furaha, ndiyo maana hata Moses alikuwa nafuraha vilevile baada ya kupata habari hiyo kutoka kwa mkewe.
Aliingia ofisini kwake akiwa na furaha vilevile na aliketi kwenye kiti chake cha kuzunguka ambacho kilikuwa kimevishwa koti jeupe kwa nyuma ambalo hutumiwa sana na matabibu au watu wa maabara, sekunde kadhaa toka aketi kwenye kiti mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na akaingia mtu aliyevaa mavazi ya kanisa la kiluteri akiwa na tabasamu pana sana usoni ambaye alipoonekana mbele ya macho ya Moses naye alijikuta akitabasamu baada ya kumbaini mtu huyo aliyehusika katika kuwaunganisha wawe mwili mmoja yeye na Beatrice. Alikuwa ni askofu wa kanisa la kiluteri dayosisi ya mashariki na pwani Dkt Edson David ambaye ni mtu aliyemheshimu sana kutokana na busara alizonazo pamoja na hekima katika kuongoza ibada mbalimbali katika kanisa lake, Moses alisimama kwenye kiti kwa heshima aliyonayo kwa askofu huyo na alimfuata akiwa na uso uliojawa furaha sana hadi akasababisha Askofu naye atabasasmu zaidi kama anaelekea kucheka kutokana na kuridhishwa na uchangamfu aliyooneshwa na Moses ambaye ni kijana aliyejizolea umaarufu nchini kutona na kazi yake ya sayansi.
"Bwana yesu asifiwe baba askofu" Moses alioongea kwa uchangamfu huku akimpatia mkono Askofu Edson
"Ameen Bwama yesu asifiwe Professa" Askofu Edson alijibu kwa uchngamfu huku akitumia jina la cheo alichotunukiwa Moses baada ya kufanya mapinduzi makubwa katika sayansi nchini Tanzania kwa kuweza kugundua vitu mbalimbali ambavyo havikuwahi kugunduliwa na wanasayansi waliopita baada ya kufariki kwa Professa Lawrence Gawaza ambaye alikuwa ni baba yake mzazi.
"Karibu sana baba" Moses alimkaribisha Askofu Edison akitumia jina la baba alilozoea kumuita kutokana na kumheshimu sana.
"Asante mwanangu vipi mkeo hajambo?" Askofu Edson alishukuru kwa ukaribisho huo kisha akauliza hali ya mke wake Moses.
"hajambo baba tunamshukuru Mungu miezi tisa baadaye tunatarajia na sisi kuongeza familia yetu" Moses alimuambia hali ya mkewe Askofu Edson kisha akamfunulia habari za ujauzito aliokuwa nao Beatrice, askofu aliposikia taarifa hiyo alitoa tabasamu kubwa kama ilivyo kawaida ambalo halitofautiani na kicheko.
"hongera sana mwanangu hakika Yehova ametenda kazi yake ndoa yenu, apewe sifa kwa hilo. Bwana wa mabwana amewapa baraka itokaye kwake atukuzwe kwa hilo kama ilivyobainishwa na waraka wa pili wa Wakorinto 9:8 ambayo inasema,'na Mungu anaweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili kila wakati muwe na kila kitu kwa kiasi cha kutosha na ziada kwa ajili ya kazi njema'.
Bwana asifiwe katika hilo mwanangu kwani amewapatia kila kitu katika maisha yenu kwa kwa ajili ya kazi njema iliyowaleta hapa duniani, ameweza kuwapa maisha mazuri mliyokuwa mkiyahitaji, ameweza kuwapa upendo katika mioyo yenu mliokuwa mnauhitaji kwenye ndoa yenu, ameweza kuwapa maisha yenya amani na upendo katika ndoa yenu, ameweza kuwapatia kile mnachokitafuta kutokana na jasho lenu, pia ameweza kuwajalia afya njema mliyokuwa mkiihityaji katika ndoa, pia ameweza kuwajalia kuongeza mwanakondoo mmoja kutokana na ndoa yenu ili akikua aweze kumsifu bwana kama mnavyomsifu nyinyi na pia amewajalia elimu na heshima ndani jamii yenu ambayo ndiyo mliyokuwa mkiihitaji. Hakika bwana ni muweza wa yote mwanangu, bwana asifiwe" Askofu Edson alihubiri neno baada ya kuambiwa habari njema ya ujuzito wa Beatrice na alizidi kumfungulia Moses juu ya neema za muweza yote kwa kuwajalia mambo mbalimbali katika maisha yao, mahubiri hayo yaliingia sawasawa katika moyo wa Moses ambaye alikuwa akinyoosha mikono kila pale mchungaji alipokuwa akihubiri na alitamka amen kwa kila uwezo wa muweza uliotajwa na Askofu Edson.
"Amen" Moses alisema tena neno hilo baada ya mchungaji kufikia kituo cha mahubiri yake aliyoyahubiri kwa hisia huku akitetemeka.
"Baada ya kumshukuru kwa kila jambo alilolitenda katika maisha yenu pia na mimi kumshukuru bwana kwa kila jambo alilolitenda kwa maisha yangu hadi kuniwezesha mimi kufika eneo hili nikiwa na uzima pia nina afya njema, napenda niongee kile kilichonileta hapa mwanangu kwa uwezo wa mkuu wa majeshi na mwenye uweza kuliko majeshi yote ndani ya ulimwengu huu" Askofu Edsona alileta utangulizi wa maneno kabla hajanena kile kilichomleta katika ofisi ya Moses asubuhi ya siku hiyo, aliingiza mkono wake katika kanzu yake ya kiaskofu akatoa karatasi zilizokunjwa vizuri akampatia Moses huku akiwa na tabasamu usoni mwake kama ilivyo kawaida yake.
Moses alizipokea karatasi hizo akazipitia kisha akamtazama Askofu Edfson akioneshwa hajaelewa juu ya kile kilichoandikwa katika karatasdi zile, aliamua kuzipitia kwa mara ya pili karatasi hizo kisha akaziweka juu ya meza akamtazama Askofu Edson kwa macho yanayoasharia anataka ufafanuzi juu ya kile akilichoandikwa katika katika karatasi zile.
"Mwanangu kanisa kuu la kiluteri la nchini Ujerumani limetambua sana mchango wako kitaifa na hata kimataifa katika medani ya sayansi ndiyo maana ikakuteua wewe ushiriki katika mchango wa kiroho katika kulisaidia kanisa hili kwa jina la bwana kwani amekusaidia katika mambo mengi hivyo inabidi na wewe usaidie katika kutoa amchango wako katika asasi zinazoendeshwa na wanakondoo wa bwana. Hakika bwana amejitolea katika maisha yako basi nawe unatakiwa ujitolee katika kuendeleza asasi za wanakondoo wa bwana walau kwa mchango mdogo uwezao kuutoa katika hili mwanangu, yapasa uwe na fadhila kwa kila wema alokutendea bwana katika maisha yako ya kila siku. Mwanangu wanakondoo wa nchini ujerumani kwenye kubwa ya kanisa la kiruteri duniani wamekumbwa na na balaa kubwa la kufiwa kwa mazao yao mizabibu katika mashmba yao yaliyopo nchini Italia ambayo yamekuwa yakiendeshwa na asasi yao kubwa ya kidini nchini humo, kutokana na kutambua mchango wako wa kisayansi kimataifa na hata kitaifa wameamua kukuletea ujumbe huo waliokuomba ili wapate dawa ya quantanise ambayo uliigundua mwezi uliopita ili iwe sulushisho kwa uharibifu wa zao linaloingizia asasi hii kubwa ya kanisa la kileteri kubwa sana duniani. Mwanangu kanisa hili la Evangelical lutheran la Ujerumani linaomba msaada katika hili uwakomboe na janga hili kwa kuwatumia sehemu ya dawa yako" Askofu Edson alieleza kiini cha safari yake ilyomleta ofisini kwa Norbert ili aeleze shida inayo wasumbua kanisa kubwa la kiluteri duniani ambalo, maelezo hayo yalimfanya Moses ajifikirie kwa muda wa dakika kadhaa kisha akashusha pumzi ndefu akayachukua makratasi yale akayasoma kwa mara ya pili. Hakika maneno ya Askofu Edson yalimuingia barabara katika mtima wake kwani alikuwa muumini mzuri wa kanisa la kiluteri, uhudhuriaji wake wa misa katika siku ya jumapili ulimfanya awe na moyo wa kuwasaidia waumini wenzake wa kanisa la kiruteri kwani walikuwa wamoja hivyo kusaidiana ni jambo muhimu.
Alipomaliza kusoma karatasi zile alinyanyua macho akamtazamat Askofu Edson kisha akamwambia,"nipo tayari baba katika kuwasaidia wanakondoo wa bwana"
Maneno yake yalimfanya Askofu Edson aachie tabsamu lake linalofanana na kicheko kwa mara pili ambalo sasa hivi lilikuwa pana kulikuwa awali hadi mapengo yake ya sehemu za magego yakaonekana, kauli ya Mosaes ilimfanya atamke."Ubarikiwe mwangu kwa jina baba ubarikiwe ,ubarikiwe mwanangu kwa jina mwana na ubarikiwe mwanagu kwa jina la roho mtakatifu".
"Amin" Moses aliitikia huku akiachia tabasamu kutokana na kunogewa sana na neno la uzima alilokuwa anapewa na Askofu Edson.
"Mwanangu haina budi nikuache uendelee kuutafuta mkate wa kila siku ambao amekuwekea bwana wa mabwana uutafute kwa njia nhii, amani ya bwana iwe nawe" Askofu Edson aliaga baada ya ujumbe aliouleta kupokelewa kwa mikono miwili na Moses ambaye alikuwa ni professa mwenye umri mdogo kabisa katika nchi ya Tanzania na akiwa amefanya maajabu mengi sana katika medani ya sayansi kama alivyofanya baba yake katika kipindi ch maisha yake ingawa aliitumia kinyume muda mwingine.
Dakika kumi kupita tangu aondoke Askofu Edson, Moses alikuwa akipitia baadhi ya mafaili yaliyopo mezani iliaangalie kazi zilizokuwa zimeachwa kiporo aweze kuzimalizia, alipitia faili moja moja hadi akamaliza kisha kanyanyua mkonga wa simu ya mezani akbonyeza namba moja tu kisha kaweka sikioni akasikiliza milo wa simu ukiita hadi ikapokelewa.
'Dokta Roshan namuhitaji ofisini kwangu mara moja' Aliongea maneno hayo kisha akakata simu akaurudisha mkonga mahala pake, alisubiri baada ya dakika moja na mlango wake ukafunguliwa akaingia kijana wa kihindi aliyepishana naye kiumri akiwa amevaa koti la kitabibu na miwani ikiwa ipo chini kidogo ya macho yake ikiwa imejenga mpaka kati ya pua na macho yake. Kijana huyo wa kihindi aliashiriwa na Moses aketi kwenye kiti naye akataii halafu akasema,"Yes Professor(ndiyo professa)"
"Doctor two cointainer of Quantanise must remain here for community needs(Daktari vyombo viwili vya Quantanise vinatakiwa vibaki hapa kwa matumizi ya jamii" Moses aliongea huku akimtazama Dokta Roshan kwa umakini.
"Ok Professor(sawa Professa)" Dokta Roshan alitii amri ya Moses kwa heshima na utiifu.
"you may go(unaweza kwenda)" Moses alisema na Dokta Roshan alinyanyuka kwenye kiti akatoka nje ya ofisi hiyo, Moses alichukua koti la kikazi akalivaa na akabeba mafaili yaliyopo mezani kwake akatoka nje ya ofisi yake na akaufunga mlango akenda kuendelea na kazi kama ilivyo kawaida yake akiwa yupo ndani ya maabara hiyo ya Umoja wa mataifa
****
YOMBO
WILAYANI TEMEKE
DAR ES SALAAM
Upande huu jijini Dar es salaam kulikuwa kuna hali shwari sana ndani yake na watu walikuwa wakiendelea na shughuli zao kama kawaida, ilikuwa ni katika mtaa unaoitwa Bakwata jirani kabisa kabisa na makutano ya reli mbili za Tazara ambapo moja ilikuwa ikitokea bandarini na nyingine ikitokea katika kituo cha treni za abiria cha Tazara kilichopo mkabala na kiwanda cha kutengeneza mikate kinachokuwa kikimilikiwa na mfanyabiashara maarufu sana jijini Dar es salaam.
Eneo hili la Yombo mtaa wa Bakwata jirani kabisa mwembe ambao hutumiwa na watu katika kucheza bao pamoja na kunywa kahawa kulikuwa na hali ya utulivu huku baadhi ya vijana wakiwa wapo na shughuli zao na wazee pia walikuwa wapo katika mizunguko takribani mitano wakiangalia wazee wenzao waliokuwa wanacheza bao. Kulikuwa na hali ya amani ambapo amani hiyo iliingia dosari katika namna isiyotarajiwa baada ya kupita mzee wa kanisa moja mgeni maarufu sana maeneo hayo akiwa kaongozana na vijana wake wawili pamoja na mlinzi huku mbele yao kukiwa na kijana anayesukuma toroli kubwa lililosheheni nyama mbichi ambayo hupendwa kuitwa na vijana kwa jina la mbuzi katoliki na wengine wanaiita kitimoto. Kijana huyo alionekama akiendesha mkokoteni huo kwa kasi bila ya kujali uwepo watu njiani na uzito wa mzigo wa mzee wa kanisa huyo mwenye lafudhi ya kichaga naye hakuisha katika kumuhimiza yule kijana afanye haraka, mkokoteni huo pamoja na msafara wa mzee wa kanisa huyo ulikuwa ukitokea upande lilipo daraja la tingatinga na ulikuwa ukielekea upande uliopo miembe hiyo ambapo yule kijana mwenye mkokoteni alionekana kutaka kupitiliza eneo hilo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Aisee bwashee nimekuambia kata kona hapo kwenye huo muembe uingie ndani ndipo ilipo njia ya kuelekea nyumbani kwangu" Mzee wa Kanisa huyo ambaye anatambulika kwa kutozungumza na watu maeneo hayo alimkumbusha yule kijana baada ya kuonekana alitaka kupitiliza njia anayoelekzwa. yule kijana ilimbidi akate kwa upesi kwani angepitiliza ingekuwa ngumu kurudi nyuma kutokana na wingi wa mchanga uliopo eneo hilo na hapo ndipo alipotibua amani ya eneo hilo baada ya kusababisha kile kilichowaudhi wazee waliokuwa wmacheza bao. Alikuwa amefanya kosa kubwa sana kwa kona yake aliyoikata kwa nguvu katika eneo hilo kutokana na kushurutishwa na aliyempa ajira ya kubeba mzigo wake ili aweze kupata ujira.
Kijana huyo alikuwa amezua makuu ambayo laiti angelijua yangelitokea wala asingelikubali kubeba mizigo za mzee huyo wa kanisa maarufu sana maeneo hayo kutokana na kuwa jeuri na kutozungumza na watu sana hasa waliokuwa wapo imani tofauti sana na yeye kutokana tofuti za kiimani.
Kona kali aliyoikata yule kijana ilisababisha majimaji yaliyokuwa yapo ndani ya nyama hiyo ambayo ilikuwa haijafunikwa vizuri kuwamwagikia wazee waliokuwa wamekaa makundi mawili wakiwa wanacheza mchezo wa bao huku wengi wakiwa wanakunywa kahawa wakibadilisha mawazo tofauti, wazee hao walimtazama kwa hamaki yule kijana kisha wakamuangalia yule mzee wa Kanisa ambaye alionesha kutojali kabisa juu ya suala hilo na ndiyo kwanza alimuhimiza yule kijana aendelee na safari baada ya kumuona yule kijana akiwa ameduwaa akiweka mikono ishara ya kuomba kwa wale wazee.
"Aisee bwashee huu siyo mwisho wa safari mama Minaeli yupo nyumbani anasubiri mzigo kwa sjili ya Kipaimara cha mtoto wetu anayekuja kesho!! Twende mbele wewe" Mzee wa kanisa huyo aliongea kwa kufoka akimuhimiza yule kijana asonge.
"We Kimaro ina maana huoni huyo kijan alichokifanya, katumwagia najisi ambayo na wewe una upuuzi tu" Mzee mmoja alilalamika huku akikunja uso kutokana na majimaji yaliyopo kwenye nyama hiyo kumwagikia.
"mabwashee kwani akiwamwagia ndiyo mnakufa mpaka malalmike hivyo' Mzee wa Kanisa aliongea kwa dharau huku wale vijana aliokuwa nao wawili wakiwa wapo pembeni yake wakitazama tu.
'Yaani wewe kimaro pamoja na hao wanao ni mna mwezi tu tangu mhamie naona sasa mwataka kutupanda kichwani sisi wenyeji wako uliotukuta" Mzee alimaka kwa sauti kisha kasimama juu akafunua shati lake akatoa msime halafu akasema,"hizi ni dharau kabisa yaani wewe mchaga kuja mwezi tu unatuletea jeuri hivi kiasi cha kudhalilika hivi tukajikoshe makosho saba".
Mzee huyu aliwavamia Kimaro na wenzake na kusababohsa kutokea kwa vurugu kubwa sana, ambyo iliwafanya baadhi ya waumini wa dini kiislamu kulivalia njuga suala hilo.
****
GEREZA LA UKONGA
PUGU
Mlango wa chuma wa gereza ulifunguliwa kwa nguvu na askari aliyeonekana alikuwa hajapenda kwenda kumtoa mfungwa aliyekuwa ndani ya gereza ambaye kwa muda huo alikuwa tayari ameota ndevu nyingi sana kutokana kukaa gerezani kwa muda wa miaka kadhaa tu tangu ahukumiwe kifungo cha maisha, alikuwa ni adui mkubwa wa nchi ya Tanzania kutokana na maovu aliyoyafanya ambayo yalimstahiki hata apewe adhabu ya kifo kwa sheria kali za nchi nyingine tofauti na Tanzania. Mzee huyu ulipofunguliwa mlango alionesha kutojali ndiyo alijigeuza upande wa ukutani wa godoro alilolalia akionesha ni kiburi sana. Jambo hilo lilimuudhi sana askari aliyefungua mlango hadi akmfuata akampiga rungu la kwenye paja lilomfanya mzee huyo augulie maumivu kisha akamvuta kwa nguvu.
"Pumbavu wewe unadhani hapa ni ikulu ulipoingia kwa kumwaga damu ya wenzako" Askari alimfokea huku akimsukuma nje mzee huyo ambaye alikuwa ameshika sehemu ya paja liyopigwa runmgu.
"tena ongoza njia kabla sijakuongeza rungu la pili fisadi wa nchi wewe" Askari alimuambia kwaukali huku akimsukuma atangulie mbele.
Mzee huyo aliongoza njia huku akiwa anatembea kwa kuchechemea kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kupigwa rungu la paja, maumivu yalizidi kuongezeka zaidi baada ya hofu kubwa kuugubika moyo wake alipofikiria jambo aliloitiwa na askari wa gereza hilo kutokana na kuchukiwa sana. Jambo hilo hakuhitaji litokee ndani ya muda huo kwani hakuna kiumbe anayevuta pumzi atakuwa tayari kuona jambo hilo likitokea kwake hasa mwenye ndoto zake ambazo zinaishi ndani ya halmashauri ya kichwa chake, upande wa pili alijipa moyo kwani alidhani huenda kuna ugeni ulikuwa umekuja kumtembelea baada ya kupita mwezi mmoja hakutembelewa na mtu yoyote yule.
Wasiwasi wa kutokea kwa jambo asilolitaka litokee akiwa ana malengo yake ambayo yanaishi ulizidi ndani ya ubongo wake kiasi cha kuzidi uzito upande wa matumaini yake, kwa wasiwasi aliokuwa nao alijikuta akigeuka nyuma kumtazama yule askari anayemsindikiza na hapo ndipo akaibua jambo jingine kabisa.
Macho yake yalipotazama uso wa askari yule yalizidisha chuki aliyonayo askari yule kwake na hapo ndipo akaibua jambo jingine likatokea baada ya kurudisha shingo yake kutazama mbele, lilikuwa ni kofi zito la mkono mgumu na wenye sugu wa askari huyo ambalo lilimfanya hadi ahisi kiwewe kilichomyumbisha na alipokaa sawa alisonga mbele na hakuthubutu kutazama tena nyuma.
"Ukigeuza shingo yake nakuongeza rungu la kichogoni kenge wee! Unafikiri kuna mtu anayetaka atazamwe humu na macho yako ya kishetani hayo, tena ongeza mwendo tusikupunguzie muda sisi" Yule askari alifoka huku akizidi kumsogelea karibu zaidi kwa mwendo wa kasi na kusababisha mzee huyo atembee kwa haraka zaidi, hakika aliogopa kupigwa kofi la pli na yule askari kutokana na kofi la kwanza kumletea maumivu makubwa.
Ujasiri wote aliokuwa kipindi yupo uraiani ulikuwa umemuisha kabisa na hapo uoga ndiyo ulitawala moyo wake kwani hakuwa na ujanja, ama kweli yamemfika asiyoyatarajia kama yatamfika katika maisha yake.
Aliongozwa na yule askari anayeongozwa naye kwa chuki hadi katika eneo maalum la kuonana na wageni katika gereza hilo na hapo ndipp nafsi yake ikapata ahueni baada ya kumuona ndugu yake akiwa yupo upande wa pili akimsubiria na simu ya mkonga ilikuwa ipo sikioni mwake. Naye aliweka mkonga wa simu sikioni mwake kisha akasema, "mdogo wangu vipi mradi unaenda sawa?".
"unaenda sawa kaka sasa hivi umefikia pazuri na ndugu zako uliotuachia tutanufaika nao, hatua ya kwanza ya ukuaji imeanza tunatarajia hatua ya pili itafuatia mpaka zitimie hatua zote tano ndiyo matunda ya mradi tuyaone" Ndugu yake aliongea akiachia tabasamu pana na kusababisha mzee yule naye aachie tabasamu kisha akaongea neno la lugha ya kimasai lililomfanya ndugu yake atoe hofu naye akamjibu kwa kimasai mzee yule naye akarudisha tabasamu kwa ndugu yake.
"Sasa hakikisha mradi unafikia malengo mdogo wangu si unajua familia inanitegemea kwa sasa sina njia ya kutimiza mahitaji yao ila hiyo ndiyo njia pekee" Yule mzee aliongea kisha akaweka mkonga wa simu chini halafu akamtazama ndugu yake kwa tabasamu ambapo naye aliridisha tabasamu lile, alimuonesha ndugu ya ishara ya kumuaga akawa amesimama palepale.
Ndugu yake alianza kuondoka taratibu sana akiwa aanatazamwa na mzee huyo hadi alipopotea katika upeo wa macho ya mzee huyo akiwa hamuoni tena katika eneo alllokuwa amekaa ndugu yake akiposimama hapo awali, mzee huyo alibaki papo hapo akimtazama upande wa pili wa kioo kwenye eneo maalum ambalo wageni wakija kuwatembelea wafungwa husimama akiwa anawaza kitu ndani ya kichwa chake hadi muda waliopewa uliopoisha akawa bado amesimama pale mpaka alipokuja kukumbushwa na askari aliyomleta kwa namna asiyoipendelea kabisa kukumbushwa nayo. Kofi la kisogoni na kuvutwa kwa ukosi wa vazi lake la kifungwa ndiyonamna aliyokumbushwa na askari huyo wa gereza na akajikuta akiingia tena kwenye maumivu aliyokuwa akiyakwepa awali alipokuwa akihusiwa kazane na askari yule wakatia kimleta eneo hilo. Alitolea eneo hilo na kupelekwa ndani ya chumba chake cha gerezani humo kwa namna ambayo ilitumiwa wakati analetwa katika chumba cha kuzungumzwa na mgeni.
****
YOMBO
DAR ES SALAAM
Amani ya eneo la Yombo tayari ilisjakuwa imepotea kwa tukio lililofanywa na mzee wa kqnisa ambaye ni mgeni katika mtaa huo, amani ya eneo hilo ilibidi irudi kwa kutumia nguvu ya polisi kwani mapigano yalishazuka baada ya tukio hilo, upande wa dini zote ulikuwa ukiwatetea wenzao na hapo ndipo baadhi ya raia wa eneo wakijikuta wakikatishwa maisha yao kutokana ugomvi huo.
Hali ilipozidi kuwa tete mabomu ya machozi yalihusika katika kuwatawanya wanadini hao walioingia dosari katika kutetea waumini wenzao katika kila dini, askari wakutuliza ghasia walikuwa wameenea katika eneo hilo wakiwa na kazi ya kutuliza ugomvi huo kwa kutumia kila mbinu ikiwemo kupiga raia wabishi na hata kurusha mabomu ya machozi. Juhudi za askari hao ziligonga mwamba na hapo magari yenye maji yanayowasha yakaingia eneo hilo na kuanza kumwaga maji hayo kwa wananchi ambalo walikuwa wakipigana wenyewe, ahueni ya vurugu hizo zilionekana ingawa kuna baadhi ya raia bado walikuwa wabishi kuacha kupigana hata kwa maji hayo na ikawabidi askari wakutuliza ghasia wabadili mbinu ili kumaliza tatizo hilo.
Risasi za mpira ndiyo mbinu iliyofuata baada ya mbinu ya awali kushindikana walifyatua risasi hizo kwa raia waliopo mbele yao ambayo iliwafanya raia hao wache ugomvi mara moja baada ya kuona wenzao wakirushwa na bunduki hizo baada ya kuwapata, dhana ya kwamba wenzao walikuwa wamepigwa risasi za moto ndiyo iliowajia raia katika vichwa na kukimbia ili kuokoa masiha yao mkutokana risasi hizo walizodhani za moto ndiyo jambo waliloliona linafaa kuliko kukaa katika eneo hilo.
Ndani ya dakika tano tayari eneo hilo lilikuwa tulivu baada ya kutumika kwa risasi za mpira katika kutawanya watu na wale walioangushwa na risasi za mpira waliiingia katika mikono ya askari baada ya kuwahiwa na kutiwa nguvuni, ndani ya dakika nyingine tano tayari magari ya wagonjwa yalifika eneo hilo na mengine ya kubeba miili yalikuwa tayari yamefika katika eneo. Waandishi wa habari kutoka vituo mbalimbali vya habari nao tayari walikuwa wamefika eneo hilo wakitafuta habari ili waweze kuwafikishia hadhira ya watanzania waliookuwa nje ya eneo hilo.
Upelelezi wa kiini cha tukio nao ulianza mara moja ili kubaini chanzo chake kupitis kuwahoji wale watu waliokuwa wametiwa nguvuni na maaskari, chanzo kilipobainiwa maaskari hao waliingia kazini katika kumtafuta aliyesababisha tukio zima hilo na hapo ndipo wakabaki na mshtuko baaada ya kubaini jambo jingine lililo zidi kuwashangaza wale maaskari kuhusu mtu kiiini cha tukio hilo. Mzee wa kanisa ambaye ndiye kiini cha tukio hilo hakupatikana yeye wala familia yake na hata alipoulizwa mwenye nyumba ambayo mzee huyo wa kanisa alipangisha mwezi mmoja uliopita tangu ahamie mtaa huo alitoa jibu ambalo lilizidi kuwashngaza sana maaskari hao.
Mvurugo, mkanganyhiko, machanganyo ndiyo ulikuwa umevamia vichwa vya maaskari waliokuwa na ari ya kufanya kazi tangu alipoingia rais mpya anayewajali ndiyo ulikuwa umevamia vichwa vyao na kuwafanya wabaki wakikuna bongo zao watafute mahali pa kuanzia kwa upande mwingine kutokana na kukosekana kile walichokuwa wakikihitaji kutokana na majibu waliyopewa na mwenye nyumba iliyokuwa anatumia na mzee wa kanisa huyo. Maaskari hao waliafikiana waende kwenye kanisa ambalo lilikuwa likiomgozwa na Mzee Kimaro kama mzee wa kanisa ili kupata walau kitu kitakachowapa mwanga katika jambo wanalolitafuta, walifanya upesi na wakaenda kanisani hapo lakini napo waliambulia patupu wakabaki wakikuna bongo zao kwa mara nyingine juu ya tukio hilo linalowachanganya vichwa vyao hadi muda huo. Akili zao walizifikirisha kinyume na kufikiria kwa kawaida juu ya tukio hilo lakini napo ilikuwa ni kazi bure kwani haikuleta matunda ya kuvuta fikra zao zaidi, walitumia mbinu mbalimbali za kiaskari lakini mwisho wake ikawabidi waliweke hilo suala kiporo walianze baadaye kidogo kwa kutumia mbinu nyingine tofauti naya awali waliyokuwa wanaitumia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
Jioni ilipofika vituo mbalimbali vya habari vilikuwa vinarusha taarifa ya tukio zima lilotokea Yombo na ikawa ndiyo habari kuu kwa baadhi ya vituo vya televisheni nchini, saa mbili usiku ilipowadia vituo vikubwa vya habari navyo vilirusha juu ya tukio hilo kutokana na kuchukua sura mpya ndani ya nchi yenye amani Tanzania.
Taarifa hiyo ya habari ilikuwa ikiangaliwa na Moses pamoja na mkewe Beatrice wakiwa wameegemeana subeleni katika nyumba ya Moses Mikocheni ambapo Beatrice alikuwa amelaza kichwa chake kwenye mapaja ya Moses huku akuelekeza macho kwenye luninga, taarifa hiyo pamoja na umwagaji damu wa eneo uliotokea ulionekana kumsikitisha sana Moses na Beatrice wakiwa wameelekza macho yao kwenye luninga iliyopo sebuleni hapo. Zilipoonekna damu zilizokuwa zimemwagika eneo hilo Beatrice alijikuta akigeuza uso pembeni na hakutaka hata kuangalia hadi pale habari hiyo ilipoisha na ikafuata habri nyingine ndiyo akarudisha macho yake yatazame kioo cha luninga kwa mara nyingine. Moyo mwepesi alionao Beatrice ndiyo ulimfanya Beatrice aangalie pembeni na hakutaka kulitazama tukio hilo hata kidogo, kwa Moses aliona kawaida kutazama habari hiyo hadi inaisha.
"Loh! Yaani nchi hii sijui inaelekea wapi kwa kweli" Beatrice aliongea baada ya habari hiyo kuisha.
"usiseme nchi hii sema raia wa nchii hii because nchi haina kosa mke wangu" Moses alimrekebisha Bratrice kauli yake.
"mmh haya vyovyote" Beatrice aliongea huku akijiweka vizuri kwenye mapaja ya Moses, muda huo Moses alitaka kuongea neno lakini alisitisha baada ya simu yake ya kiganjani iliyopo kwenye kochi kuita. Aliitupia macho yake yote mawili simu ile ambayo hakuweza kuifuta bila ya kumnyanyua Beatrice katika mapaja yake alipokuwa amegemeza kichwa chake, kikwazo chake cha kutoweza kuifuata simu hiyo kiligunduliwa mapema na Beatrice ambaye aliisogeza simu kwa mguu wake hadi ilipofika usawa wqa mikono yake kisha akainyanyua ile simu akaitazama kwenye kioo kuona jina la mpigaji na alipoliona alisema,"Honey askofu Edson huyo anakupigia"
Moses aliposikia hivyo aliichukua simu kwa haraka kisha akaipokea na kuiweka sikioni akasikiliza upande wa pili wa simu hiyo halfu akasema,"amen Bwana Yesu asifiwe baba.....si mgekuja kesho asubuhi kuufuata tu huo mzigo baba....sawa hamna tabu ngoja niwataarifu vijana waliopo shift ya usiku kazini wawapatie huo mzigo..amen asante baba".
Simu ilikatwa kisha akabonyeza namba kadhaa kwenye simu yake akaiweka sikioni akaongea,"Benson askofu Edson anakuja hapo kazini mpatie ule mzigo uliotengwa wa chupa za dawa Quntanise kwani zintakiwa zisafirishwe usiku huu kwa boti hadi Zanzibar walipo wawakilishi waliozihitaji ili ziweze kuondoka Italy siku inayofuata". Alipomaliza alikata simu kisha akarudisha macho yake kwenye kioo cha televisheni akagundua ulikuwa ni muda wa matangazo baada ya habari za kitaifa kuisha, aliipoona hivyo aliinamisha kichwa chake na akambusu mke wake mdomoni kwa ghafla na kusababisha mke wake aachie tabasamu.
"Honey time ya kula hii" Moses alimuambia Beatrice baada ya kuangalia katika meza ya chakula chakula kilikuwa kikimaliziwa kutengwa na msichana wa kazi, Beatrice aliposikia alijifanya kusononeka akionekana hataki kutoa kichwa chake katika m iguu ya Moses. Alibaki vile vile akiwa anatabasamu usoni huku akimuangalia Moses ambaye alibaki akimtazama tu baada ya kumuambia kuhusu muda wa kula, Moses alipoona kimya aliamua kupenyeza mkono wake mmoja kwenye uvungu wa mapaja ya Beatrice kisha mkono mwingine akashika kwenye shingo.
Alimyanyua kwa kushtukiza na kusababisha acheke kwa furaha huku mikono akiwa ameizungusha shingoni mwa Moses, alibebwa hivyo hadi mezani kisha wote kwa pamoja wakakutanisha ndimi zao halafu Beatrice akashushwa jirani na kiti kimojawapo kilichopo kwenye meza ya chakula akakaa. Walianza muda wa kuweka matumbo yao sawa kwa pamoja huku wakilishana kama ilivyo kawaida yao kutokana na jinsi walivyo na furaha wakiwa pamoja, Beatrice aliendelea na mtindo wake wa kudeka kila mahali ambapo Moses yupo karibu.
Baada ya chakula wote kwa pamoja walirudi kwenyye luninga kisha baadaye walielekea chumbani kwao.
ASUBUHI ILIYOFUATA
Simu ya Moses iliita kwa fujo majira ya ssa kumi na mbili asubuhi muda mchache kabla ya kengele ya kumuamsha kulia, simu hiyo ilimfanya usingizi wake ausitishe kisha akaipokea kwa haraka hiyo simu na kuiweka.
"What(nini)?" Aliongea kwa nguvu baada ya kupokea taarifa kwa njia ya simu ambayo ilimfanya atoke kitandani hapohapo kwa haraka hadi Beatrice naye akaamka kutokana na papara aliyokuwa nayo mumewe.
"Mume wangu kuna nini mbona mapema hivyo?" Beatrice aliuliza huku akifikicha macho yake kutokana na usingizi alionao, alipokaa kitandani alimuona Moses akiwa anavaa mavazi maalum anayoyatumia kwenda nayo bafuni kuoga.
"kuna dharura imetokea inabidi niwahi sasa hivi nyumbani kwa Askofu Edson nimepigiwa simu na Kaila yupo huko ananisubiri ili nikafanye uchunguzi wa kina wa tatizo lililotokea" Moses aliongea akionekana anawahi bafuni.
"Baby mbona sikuelewi kuna nini?" Beatrice aliuliza wakati Moses akiwa ameshaingia kwenye kizingiti cha bafuni,Moses aliposikia swali la mke wake alirudisha kichwa chake nyuma akawa anachungulia mahali alipo Beatrice akasema,"Bishop Edson is dead(Askofu Edson amefariki)".
"What?" Beatrice aliuliza kwa mshngao lakini swali lilkosa kujibiwa kwani Moses tayari alikuwa ameshaingia kwenye mlango wa bafuni kwa haraka sana, Beatrice naye taarifa hiyo ikamtoa uchovu wote kwani alijua kuwa kazi aliyoitiwa mume wake akiwa kama mwanasaynsi pia ni hufanya uchunguzi wa vipimo mbalimbali vya miili ya watu waliyokufa kwa utata. Aliamka kitandani akatoa nguo za mume wake kwa ajili ya kutumia siku hiyo pamoja na viatu ambavyo tayari vilikuwa vimeng'arishwa na dawa, baada ya dakika tano Moses alitoka akiwa tayari ameshajifuta maji na taulo lililopo bafuni na alijiandaa haraka sana na baada ya kuwa tayari Beatrice alimkabidhi mkoba wake wa muhimu wa kiofisi kisha alimbusu mke wake na akamkumbatia akachukua funguo ya gari.
"My love utatumia gari nyingine kwenda kazini acha niwahi" Moses alimuambia Beatrice akatoka upesi sana akawa anaelekea mlangoni.
"Take care(kuwa mwangalifu)" Beatrice alimuambiwa kwa sauti na kusababisha Moses ageuke amtazame akiwa na tabasamu kisha akasema,"I will".
Alifunga mlango akatoka nje akimuacha Beatrice akiwa amerudi kitandani akakaa kitako, baada dakika takribani mbili mlio wa gari analolitumia Moses ulisikika kuashiria kuwa ndiyo alikuwa anatoka
****
NUSU SAA BAADAYE
MBEZI BEACH
Gari aian ya Bmw yenye rangi nyekundu ilionekana ikiingia ndani ya nyumba moja yenye geti kubwa baada geti kufunguliwa, gari hiyo ilipitiliza moja kwa moja hadi sehemu ya maegesho ambapo kulikuwa kuna gari tatu za polisi na mbili za kiraia. Moses alionekana akishuka ndani ya gari hiyo aina ya BMW baada tu ya gari hiyo kuegeshwa. Alipokelewa na msaidizi wa hapo ndani ambaye alimpeleka hadi mlangoni ambapo alikuta utepe umezungushwa eneo hilo, alivuka utepe akaingia ndani akakutana na baadhi ya maaskari,Norbert pamoja Dokta Hilary kutoka hospitali ya taifa .
Ilikuwa ni ndani ya eneo la sebule ambako mwili ulionekana kufunikwa shuka jeupe, maasakri walipomuona Moses ambaye wanamtambua kama mwansayansi mashuhuri tu walimkaribisha kisha wakamsimulia kila kitu na ripoti yao ilivyo.
"mwili vipi mmeshaanza kuchunguza?" Moses aliuliza baada ya kupewa taarifa hiyo
"hapana bado ndiyo Dokta Hilary alikuwa anakusubiri wewe kwani kuna kitu amekibaini" Askari mmoja alijibu
"vizuri' Moses alipongeza kisha kamfuata Dokta Hilary akasalimiana kwani ni rafiki yake wa siku nyingi tangu kipindi yupo shuleni.
"vipi Bite hajambo?" Dokta Hilary aliuliza
"Ndiyo hajambo, vipi Irene naye?" Moses alimuleleza kuhusu hali ya Irene kisha kamuulizia kuhusu hali ya Beatrice
"hajambo,afadhali umefika njoo uone nilichokibaini katika mwili huu" Hilary alimuambia Moses huku akimpatia mipira ya kuuvaa mikononi, Moses alivaa mipira hiyo na kwa pamoja wakuendea mwili uliokuwa umefunika shuka wakaufunua. Ulikuwa ni mwili wa Askofu Edson ambao tayari ulikuwa kuwa mwekundu tofauti na miili mingine inavyokuwa baada ya kuondokwa na uhai.
"Shit! Waambie wauguziaskari waupeleke hospitali tukachukue vipimo" Moses alisema huku akisimama akawa anavua mipira ya mkononi aliyovaa halafu akampa ishara Norbert kisha akasogea mahali ambapo hapakuwa na mtu, Norbert alimfuata hadi mahala hapo akawa anamtazama kumuashiria aongee.
'Quantanise ipo ndani ya mwili wake na ndiyo chanzo cha kumuua, hivyo kauawa hisia zangu zinanipa jibu hilo na nitakupa jibu sahihi zaidi" Moses aliongea pasipo kujali kama Norbert kamsikiliza au hakumsiliza na aliondoka eneo hilo akatoka hadi nje akarudi kwenye gari lake akaingia ndani, alitoa simu yake ya mkononi akabonyeza baadhi ya namba halafu akaiweka sikioni
"Moses Gawaza mkurugenzi mkuu TISS,naomba alama za vidole zitakazochukuliwa katika eneo la tukio la kifo cha Askofu ziletwe ofisini kwangu haraka sana" Aliomgea baada ya simu kupokelewa kisha akakata akashuka kwenye gari lake.
****
Upande mwingine wa jiji la Dar es salaam katika nyumba iliyopo maeneo ya Ilala, kulikuwa kuna kikao cha watu watano ambao walionekana kufurahi sana kwani mpango wao ulikuwa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuufanya. Watu hao walikuwa wameweka duara na mbele yao kulikuwa na boksi kubwa lenye alama ya nembo ya maabara ya umoja wa mataifa ambayo alikuwa akifanya kazi Moses. Wawili kati ya hao watu walikuwa ni viongozi wakubwa wa kiimani nchini, wawili walikuwa ni vijana wa makamo wanaokaribia utuzima ambao walikuwa mapacha na mmoja alikuwa kijana anayekaribia utuzima mwenye muonekano wa kitanshati sana.
"Yaani nyinyi Panthers nimeamini kuwa sikuwaleta hapa kwa kazi bure kwani umuhimu wenu tumeuona jana maana Edson angetuchomesha yule" Yule kijana aliongea huku akitabasamu tu akiwaambia wale mapacha wanaokaribia utuzima.
"unajua uliposema kwamba Askofu Edson ameenda huku akiwa kavaa lile vazi la kiaskofi kupeleka ile barua nilijua tu tayari alikuwa amekosea na uliponieleza kuwa yule jamaa ni mkurugenzi wa usalama wa taifa basi nilijua inabidi tupoteze ushahidi kabisa ili mambo yasiwe mabaya. Kumbuka haitakiwi kuvaa vazi lile nje ya kanisa angevaa suti yake na shati lake la zambarau linalomtambulisha kama askofu' Mmoja wa wale mapacha alisema.
"hata mimi nilikuwa nina wasiwasi maana nilimsisitiza asivae ila yeye kavaa halafu anakuja kutuambia alitaka kumteka akili zaidi" Kiongozi wa dini ya kikristo aliongea.
"Ok siyo ishu tena hiyo sasa tuanze na mkakati mwingine nafikiri ni zamu ya Young Panther utekeleza" Yule kijana aliwaambia kisha wakaanza kupanga mikakati mipya ya mpango wao ambao laiti ingejulikana mapema basi serikali pamoja na wanachi wangeweza kuondokwa mabalaa ambayo yalikuwa yankuja kuikumba nchi yenye amani na upendo Tanzania, usiri wa mpango wao ndiyo umefanya jamii isitambue azma ya watu hawa.
****
Baada ya masaa kadhaa mpango mwingine usukwe tayari majibu ya uchunguzi wa Mwili wa Askofu Edson yalikuwa yameshatoka na nakala moja ilikuwa imeshawasilishwa polisi na nakala nyingine ilikuwa ipo mikononi mwa Moses ambaye muda huo alikuwa akiijadili na Norbert katika ofisi ya wahanga iliyopo katikati ya jiji la Dar es salaam. Kile alichokifikiria Moses juu ya kilichosababisha kifo cha Askofu Edson ndiyo hicho hicho kilikuwa kwenye majibu hayo, mwili wa Askofu Edson ulikutwa na kiwango kidogo cha dawa ya Qyantanise ambayo hutumika kuua wadudu kwenye mimea pia alama za vidole zilikuwa zimekutwa katika eneo hilo tayri zilikuwepo hapo mbele yao ambayo bado haikujikana muhusika ni yupi hadi muda huo.
"Dogo aliyefanya haya mauaji si mtanzania kabisa" Norbert baada ya kuyapitia majibu hayo kwa mara ya aliongea .CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"hata mimi hilo nimelibaini mapema tu kwani kila mtanzania mwenye umri kuanzia miaka kumi na nane alama yake ya mkono ipo kwenye kitambulisho cha kupiga kura au kitambulisho cha taifa, hivyo kila mtanzania fingerprint yake imeingia kwenye database ya serikali. Kutokana na serikali kuvitilia mkazo vitambulisho hivi kila mtu amejisajili sasa kama angekuwa mtanzania angekuwa kashajulikana sura hadi picha kwani vipo kwenye mitambo ya serikali" Moses alikubaliana na maneno ya Norbert kisha akatoa ufafanuzi zaidi.
"wajibu wa kumjua mhusika wa hili suala ni wetu, inabidi ajulikane tulinde heshima ya nchi na rais wetu' Norbert aliongea
"nafikiri tu..." Moses aliongea lakini alishindwa kumalizia kauli yake baada ya simu ya Norbert kuita, Norbert alizuia Moses asiongee kisha akapokea simu akasikiliza bila kusema kitu hadi ikakatwa.
Aliirudisha aliweka simu yake kisha katikitisa kichwa chake halafu akavuta pumzi kwa nguvu akaiachia akmtazma Moses.
"kuna nini?" Moses aliuliza
"Mufti mkuu wa Dar es salaam amekutwa amefariki ofisini kwake na mwili ni kama wa Askofu Edson" Norbert aliongea kisha akanyanyua macho juu kutazama dari la ofisi.
"Shit!" Moses alisema huku akipiga ngumi mezani kwa nguvu
****
Kwa mara ya kwanza alianza kuufikiria uamuzi wake wa kutoa dawa ya Quantanise hapo ndipo akabaini kwamba alifanya kosa, ilikuwa imeshatokea na hana muda wa kurekebisha ili isitokee na alitamani hata muda urudi nyuma aweze kurekebisha pale alipokosea. Kumpa Askofu Edson zile kemikali lilikuwa ni kosa kubwa ambalo anaona amelifanya na alizidi kujuta zaidi kwa kumpatia kemikali, kwani isingetokea yeye kumpatia hiyo dawa hayo yasingetokea. Hakuhisi kabisa kama mtumishi yule wa mungu angeweza kuwa na uhusika na watu wanaofanya mauaji hayo kwa kutumia kemikali hizo, kilichomjia ndani ya fikra zake ni kwamba Askofu Edson alifanyiwa mchezo mchafu wa kunyang'anywa kemikali hizo na watu hao wanaofanya mauaji kisha akauawa kwa kutumia kemikali hizo ambazo zilikuwa katika mikono yake. Majuto yake yalikuwa zaidi katika kumpatia kemikali hizo usiku kwani alibaini ndiyo kosa pekee aliloweza kulifanya, alitamamni muda urudi nyuma ili amzuie afuate asubuhi kwani aliamini angekuwa ameweza kumuokoa na mambo mengi na hata kuokoa balaa ililokuwa lipo mbioni kumkaribia la kutumika kitu kilivumbuliwa na mikono yake kwa kupoteza uhai wa watu wengine wasio na hatia kabisa. Moses aliwaza sana na kuwazua juu ya suiala hilo kwani lilikuwa likiekea kumchafulia jina lake na heshima yake ambayo amejijengea Tanzania kutokana na kazi zake ambazo anazifanya kwa ajili ya Taifa lake, aliona kuna jambo la hatari ambalo lilikuwa likimjia kwa muda huo yey na familia yake ijayo hivyo alihitaji kufanya kitu kwa manufaa ya familia pia aepushe balaa ambalo lionaelekea kumkumba ndani ya muda huo.
Alipozidi kulifikiria suala hilo alijikuta akiinuka kwenye kiti alichokuwa ameketi akaelekea dirishani ambapo aliangaza macho nje huku mikono akiwa akiwa ameshika kiuno chake, hali aliyokuwa nayo Moses kwa muda huo ilimfanya hata Norbert amtazame sana kwani alihisi kuna jambo zaidi linamtatiza ukiachana na hilo la vifo vinavyotokea.
"Dogo vipi mbona una mawazo sana au hii ishu imekutachi sana?" Norbert alimuuliza Moses kutokana na hali aliyokuwa nayo baada ya kupokea taarifa hiyo ya kufa kiongozi wa dini ya kiislamu.
"hii ishu itachukua sura mpya zaidi tofauti hata unavyoifikiria kaka, nahisi itamletea matatizo hata mke wangu kwani ni mjamzito sasa hivi" Moes alimuambia Norbert huku akitazama dirishani na hakujighulisha kumtazama kwani mawazo aliyokuwa nayo ndiyo yalimfanya ashindwe hata kuangalia nyuma alipo Norbert.
"Dogo nafikiri tuingie kazini tuweze kuwapata hawa wahusika tu haina haja ya kuhofia namalna hiyo" Norbert alimuambia Moses.
"Hapana broda ujue hii kitu inalenga kunichafua mimi ndani ya jamii hii ninayoheshimika, hebu fikiria mauaji hayo yanayotokea kutoka kwa viongozi wa dini tofauti kwa kutumia kemikali ambayo ni sumu niliyoitengeneza mwenyewe kwa mikono yangu ikijulikana na wanachi itakuwa vipi? Kama si kudhani mimi ndiyo nahusika na mpango huu wote na hapo hasira zote za waumini wa dini zote zitanigeukia mimi, fikiria mke wangu atakuwa kwenye hali gani kaka na watu watatuchukulia hatua gani?" Moses aliongea kwa hisia sana huku akigeuka akimtazama Norbert machozi yakiwa yanaanza kumlenga katika macho yake lakini hayakutiririka kudhihirika wazi ionekane kama ni yupo ndani ya kilio kutokana na suala hilo.
"mojawapo ya sheria ya kijasusi inasema, usiruhusu hisia za moyo wako zikutawale katika mambo kama haya Moses. Kumbuka wewe intelligence hivyo akili zinatakiwa ziwe nyingi kuliko hisia za moyu mdogo wangu. ukifuatisha hisia ni mwanzo wa kuharibu na pia kujiharibia na hata kuhatarisha maisha ya wengine na maisha ya Beatrice. Unatakiwa umlinde kwa akili zako za kijasusi na siyo ufuate hisia mdogo, wewe ni mtu mwenye akili sana na ndiyo maana ulistahiki kuitwa shujaa ulipoharibu mipango ya Browan Stockman alipotaka kuiletea maafa Tanzania na sifa hiyo imekufanya uwe ndani ya kazi hii" Norbert alimsihi Moses kutokana na kutaka kutenda kosa ambalo ni kinyume cha kanuni za kijasusi, ushauri huo ulimrudisha Moses kwenye hali yake ya kiwaida kabisa baada ya kushusha pumzi ndefu akionesha kuwa ushauri ule ameuafiki.
"Asante, nafikiri ni muda wa kucheza na akili zaidi" Moses aliongea.
"Tuanze kupunguza hofu zako kwanza then, mengine yatafuata dogo" Norbert aliongea.
"hilo nalo ni la muhimu ngoja nifanye mpango wa ghafla wa kupunguza hofu yangu tukitoka hapa, halafu kuna kingine cha ziada inabidi tukijue" Moses aliongea huku akikuna kichwa kama ilivyo kawaida yake akifikiria mawazo chanya.
"sema tuanze kazi mara moja, ari ishanijia " Norbert alimuambia huku akitabasamu.
"cha kwanza kabisa inabidi twende kwenye bandari ndogo ya boti zinazoenda Zanzibar kuna kitu kimenijia kichwani" Moses alisema kisha akamuashiria Norbert waondoke.
"Ok twende na wazo lako halafu nitakuambia wazo langu nadhani linaweza kuwa endelezo la wazo kama likiwa chanya na pia linaweza kuwa ni jipya kabisa kama wazo lako lisipokuwa chanya, uaminifu kwa mwingine hakuna" Norbert alisema huku akielekea mlangoni.
"hakika" Moses aliafikiana na maelezo yake hukui akimfuata nyuma.
****
BANDARINI
DAR ES SALAAM
Robo saa tangu Norbert na Moses watoke kwenye ofisi ya Norbert maeneo ya bandarini upande wenye boti ziendazo Zanzibar walionekana watu wawili wenye asili ya kisomali wakiwa wamevaa kinadhifu wakiingia mahala hapo, walielekea hadi wenye uongozi wa bandari hapo wakajitambulisha kam maofisa wa Interpol(INTERNATIONAL POLICE) waliopo hapo kwa kazi maalum. Maofisa hao walijitambulisha pia kwa kiongozi husika waliomkuta kisha wakaeleza shida yao iliyowapeleka hapo, walieleza umuhimu wa kitu wanachokitafuta ndiyo maana wakafika hapo kwa ajili ya usalama wa Taifa hili kwani limevamiwa tayari.
"Kusema kweli jana usiku kuanzia saa mbili hakukuwa na boti ya kampuni yoyote iliyotoka hapa bandarini na wala hakukuwa na boti yoyote iliyoingia muda huo hapa bandarini, siku ya jana boti zote zilifanya safari mapema tu tofauti na siku nyingine kwa hofu ya machafuko ya bahari wakati wa usiku kama ilivyotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa. Uongozio wa bandari ulichukua tahadhari mapema sana kwa kuzuia makampuni yote yenye kumiliki Boti za safari kwa bahari ya hindi zisifanye safari zake kuepusha ajali zenye kuweza kuepukika" Kiongozi husika waliyemkuta hapo kwenye uongozi wa bandari aliwapa maelezo.
"Ok, je tunaweza kuziona rekodi zinazoonesha juu ya suala hilo" Mmoja wa maofisa wa Interpol aliuliza
"bila shaka mnaweza kuziona ngoja niagize kitabu chenye rekodi hizo kiletwe" Kiongozi huyo aliongea kisha akanyanyua mkonga wa simu uliopo mezani kwakole akabonyeza tarakimu mbili kwenye simu hiyo akaongea,"leta record book ya safari za jana"
Alirudisha simu mahala pake na muda huohuo aliingia binti mrembo ofisini humo akakabidhi kitabu hicho kwa huyo kiongozi husika halafu akatoka nje huku akisindikizwa kwa macho na mmoja w maofisa wa Interpol ambaye alionesha kumuangalia sana huyo binti hasa umbo lake la kuvutia. Afisa huyo aliacha kusindikiza binti huyo pale tu alipopotea katika upeo wa macho yake baada ya mlango kufungwa.
"nadhani mjionee mwenyewe" Yule kiongozi alisema kisha akawasogezea kitabu hicho ambapo kilitazamwa na maofisa hao kwa umakini mkubwa sana halafu wakakirudisha kwa kiongozi huyo.
"sawa tunashukuru kwa ushirikiano wako, tukikuhitaji hatutasita kukutafuta tena. Nafikiri utatupa msaada zaidi kama huuu ulitupatia leo' Mmoja wa maofisa wa Interpol alisema
"Hofu ondoeni kuhusu hilo, karibuni tena" kiongoiz huyo aliwaaga kwa ukarimu na maofisa hao walitoka katika ofisi hizo za uongozi wakelekea walipoacha gari lao, waliondoa gari lao wakawa wanelekea usawa wa posta ya zamani na walipofika aktika jengo la benki ya taifa ya biashara(NBC0 wakaingia kwenye barabara iendayo Posta mpya. Walienda kwa mwendo wa wastani kutokana na wingi wa magri hadi kwenye mzunguko wa barabarani wenye sanamu la askari waliuzunguka mzunguko huo wakaingia upande wa kushoto wakafuata barabara ya Samora ambayo iliwapeleka hadi kwenye mtaa wa Ohio ambapo waloinyoosha barabara hadi mtaa wa Mirambo jirani na ubalozi wa Finland na Sweden kisha wakaingia kushoto kushoto. Safari yao iliendelea akwa kuizunguka mitaa ya eneo hilo wakiwa hawana uelekeo maaalum na hatimaye wakaeleka ilipo maabara ya umoja wa mataifa. Waloshuka hapo wakaingia ndani ya ofisi za maabara hiyo wakajitambulisha wakaeleza shida yao iliyowaleta hapo, walipelekwa kwa kiongozi wa ulinzi wa maabara hiyo wakapewa kile walichokuwa wakikihitaji na hapo ndipo alama ya taa ndani ya vichwa vyao iliwajia kutokana na mwangaza walioupata kutokana na kile walichokuwa wakikitafuta.
Baada ya kukamilisha kila kitu walichokuwa wakikihitaji walichukua sehemu ya ushahidi wakaondoka nayo humo baada ya kutoa shukrani kwa wenyeji wao, walitoka hadi kwenye maegesho ya magari hapo kwenye eneo la maabara hiyo na wakaingia ndani ya gari walilokuja wakaondoka eneo hilo wakiwa na mwaqngaza wa kile walichojkuwa wakikitafuta.
Jambo ambalo halikujulikana na maofisa hao wa Interpol ni kwamba walikuwa wakicheza na mtu anayejua kucheza mchezo waliokuwa wakiucheza, walipokuwa wanaingia Bandarini na kujitambulisha hakika hawakuwa wamebaini pale kulikuwa na sehemu ya mkono wa mtu wanayecheza naye huo mchezo, hadi wanatoka pale wanaelekea ilipo Maabara ya umoja wa mataifa kwa kuzunguka kwenye mitaa ili wapoteze lengo hawakujua kama walikuwa wnafuatiliwa baada ya sehemu ya mkono wa mhusika wanaomtafuta kutoa taarifa kwenye mwili kupitia mshipa wa fahamu uliounganisha sehemu ya hiyo ya mkono wake iliyopo kwenye ofisi za Bandari na mwili mzima uliopo mahala pasipojulikana. Walipoingia ndani ya maabara hiyo ndipo waliokuwa wanawafuatlia waliwafanyia kitu kingine kwa kupitia kutegeshea vitu kwenye gari lao.
Maofisa hao walipotoka ndani ya maabara hiyo tayari walikuwa wanafuatwa na kivuli kisichoonekana bila ya wao kujua, gari ya maofisa hao ilienda barabarani kwa mwendo mzuri hadi ilipofika katika mtaa wa Shaaban Robert ndipo mambo yalipobadilika kwani ilianza kuyumba na hatimaye ikagonga sehemu ya uzio wa chuo cha IFM ikatoa Moshi mbele na hakukuonekana dalili ya mtu kutoka ndanio yake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda huohuo gari aina ford ilifika kwa kasi eneo kisha watu wawili wenye miili iliyojengeka kimazoezi wakashuka haraka sna, walienda kwenye milango ya gari ya maofisa wa Interpol wakafungua milango wakiwa na uhakika wa kile wanachokifanya na walijua mpango wao. Kila mmoja alizunguka mlango wa upande wake kuifungua kwa upesi na hapo ndipo walipokutana na kisanga kingine kilichotoka ndani ya gari hiyo, kitendo cha kuifungua milango ya gari hiyo kila mmoja alisalimiana na soli ya kiatu ya pua iliyowayumbisha hadi wakakaribia kuanguka.
Walipokaa sawa waliwaoana wale maoofisa wawili wa Interpol wenye asili ya kisomali ambao walitofautiana kwa vimo tu wakiwa wamesimama huku wakiwatazama, kitendo cha kuwaona maafisa hao wakiwa na fahamu zao ilikuwa ni jambo la ajabu sana kwao na hapo ndipo walipobaioni kuwa sehemu ya mpango wao haikuwa imefanikiwa.
Wale maafisa wawili wa Interpol walitaka kuwavamia wote kwa pamoja wawapige lakini walipowatazma wapinzani wao walitambua fika hawakuwa na upinzani wa kutisha kwao hivyo afisa mmoja ambaye alikuwa amezidiwa urefu na mwenzake ndiyo aliwasogelea wale watu waliokuja na gari aina ya Ford akiwa hata hajakaa kimapigano, wale watu walimvamia kwa pamoja afisa huyo lakini walijikuta wakisalimiana na ardhi baada kupigwa mateke mawili ya karate yaliyopigwa kwa mpigo kutoka kwa Afisa huyo. Walijiinua kwa haraka baada ya kubaini wananchi walishaanza kujaa na kama wangepigwa ingekuwa ni aibu, wqalimfuata kwa pamoja kwa mapigo ya karate ili waende nae sambamba lakini waligonga mwamba tena baada ya afisa yule kuja na mapigo ya kininja tofauti na mapigo ya awali. Mapigo hayo yalimvunja mmoja mguu papo hapo akawa hawezi tena kupigana na mwingine aliyebakia akajipa ujasiri akaja kwa kasi bila hata ya kuwa na tahadhari, alipopiga hatua kumfikia yule Afisa alipewa pigo la karate lililompata kwenye pua yake ambalo lilimchanganya hadi akawa hamuoni adui yake na hapo ndiyo ikawa nafasi nzuri kwa yule Afisa kuachia teke liitwalo YOKO GERI KEKOMI(teke hili hupigwa kwa sehemu ya pembeni ya mguu kwa kutumia nguvu nyingikatika kupiga), teke hilo lilitua katika mbavu na hapo ndiyo ikawa mwisho wa yule mtu kupigana na afisa Interpol.
Muda huohuo ving'ora vya gari la polisi vilisikika na hapo maafisa hao wote kwa pmoja walipiga sarakasi kuruka uzio wa Chuo cha IFM wakazunguka nyuma ya jengo lilloandikwa BLOCK A.
Baada ya dakika moja tangu maafisa wale waingie ndani ya uzio nyuma ya jengo lile Norbert na Moses walionekana na wakitoka katika lango kuu la chuo wakipishana na maaskari waliokuwa wakiingia ndani ya chuo hicho kwa kasi sana, Norbert na Moses walitoka nje wakajichanganya na raia ambao walikuwa wameshajaa eneo hilo wakaondoka bila kujulikana.
MUDA MFUPI KALA
Baada ya Norbert na Moses kutoka katika ofisi za WAHANGA walikuwa wamevaa sura za bandia kisomali pamoja suti nadhifu zenye vitambulisho feki vya Interpol , walielekea hadi bandarini ambapo walikuwa wakifuatilia juu ya suala la linalotaka kumkumba Moses. Walipopata taarifa muhimu wote kwa pamoja walielekea katika maabara ya Umoja wa mataifa anayofanya kazi Moses huko walichukua mkanda uliorekodi tukio zima la usiku uliopita wakati Askofu Edson anakuja kuchukua huo mzigo wa kemikali zenye sumu, walipopata mkanda huo waliondoka wakarudi maegesho kwenye gari yao ambapo wakati wqnaingia ndani ya gari Norbert aliuipindisha mguu chini ya kiti cha dereva wakati anaketi na akahisi kugusa kitu. Aliingiza mkono chini ya kiti hicho akatoa chupa ndogo kama ya manukato ikwa imebandikwa kitu mfano wa saa kilichokuwa kikihesabu dakika.
"Klorofomu hii, ndani ya gari letu kulitembelewa na wajinga wanojifanya wajanja ngoja na sisi tuwaoneshe ujanja, fungua hapo utoe kitamba viwili kimoja nipatie kingine chukua" Norbert aliongea na Moses akafanya kama alivyoambiwa. Walichuua na chupa ya maji enye maji iliyopo ndani ya gari yao wakaifungua wakaiacha wazi makusudi.
"sasa tuone kama klorofomu inaweza kufanya kazi mbele ya maji na hapo ndiyo wageni wetu watakapokujua nina imani wanafutuatilia" Norbert alisema huku akiwasha gari, kauli hiyo ilimfanya Moses atabasamu tu.
Walizunguka kwa gari makusudi ili kusubiri dakika za kile kifaa mfano wa saa ziishe, walipokuwa wamefika usawa wa chuo cha Maliasili na utalii ndiyo dakika ziliisha na ile chupa ikapasuka hewa nzito ikatanda ndani ya gari. Norbert na Moses waliweka vitamba midomoni mwao ili hewa ile isiwadhuru, Norbert aliligongesha gari makusudi alipofika kwenye ukuta wa IFM na hapo ndipo wapinzani wao wakjua wamefanikiwa kumbe ulikuwa ni mtego kwao baada ya mtego wao kubainika.
****
JENGO LA PENSHENI LA BENJAMINI MKAPA
MTAA WA AZIKIWE
Ndani ya idara ya sheria ya jengo hili iliyopo ghhorofa ya kumi na tano Beatrice ambaye alikuwa ni wakili wa shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii alikuwa akifanya kazi zake za ofisini kama kawaida baada ya kutoka mahakamani kwenda kufuatilia kesi ya shirika lake lililoishtaki shirika jingine kwa kushindwa kuleta michango kama waliyoandikishiana mikataba. Akiwa hana wala lile simu ya mezani iliyopo katika meza yake iliita, aliipokea simu hiyo akaiweka sikioni kisha akaisikiliza akasema, "ndiyo bosi....ok nakuja".
Alieleka moja kwa moja kwa mkuu wa idara ya sheria ambaye ndiye bosi aliyempigia simu, aliruhusiwa kuingia na aliijgia ndani akamkuta mkuu wa idara ya sheria akiwa katika kusubiri ujio wake.
"ndiyo bosi" Beatrice aliongea baada ya kuketi kwenye kiti kilichotenganisha kiti cha mkuu wa idara na kiti chake.
"Mrs Gawaza nimekuita hapa, nimepokea simu kwa mkurugenzi mkuu kuwa unahitajika uende kwenye semina ya sheria Uingereza itakayoanza kesho kutwa hivyo kesho inabidi ujiandae kusafiri" Mkuu wa idara ya sheria alimueleza.
"lakini bosi mbona ghafla hivyo?" Beatrice aliuliza akiwa anashangazwa na jinsi safari hiyo alivyoshtukizwa.
"hata mimi nimeletewa ghafla na mkurugenzi ambaye naye ameletewa ghafla na ngazi za juu" Mkuu wa idara ya sheria alieleza, Beatrice aliposikia maneno hayo alishusha pumzi tu kwani hakutarajia na hakuwa na uwezo wa kupinga safari hiyo pasipo kupoteza kibarua chake jambo ambalo hakutaka litokee ingawa mumewe alikuwa na pesa nyingi.
"Sawa bosi nimekuelewa" Beatrice alikubali
"vizuri Mrs Gawaza, kila kitu kipo tayari kilichobaki ni wewe kujiandaa tu. Unaachiwa muda huu mpaka kesho ukapumzike kwa ajili ya safari hiyo" Mkuu wa idara alimueleza
"sawa bosi nashukuru" Beatrice alikubali hilo suala ingawa moyoni mwake alikuwa na simanzi kubwa ya kumuacha mume wake kipenzi kwa ghafla.
"vizuri, tiketi hii hapa ya ndege na taratibu nyingine zote zipo tayari, nakutakia safari njema ukatuwakilishe vizuri huko Ulaya zaidi hata ya unavyotuwakilisha hapa nchini sehemu mbalimbali" Mkuu wa idaraya sheria aliongea huku akimpatia mkono wa kumuaga Beatrice, mkono huo ulipokelewa na Beatrice kisha akatoka ofisini kwake na hapo sura isiyo na furaha ikauvaa moyo wake kwani hakutaka hata kidogo kukaa mbali na mumewe. Alienda kuwaaga wafanyakazi wenzake akiwa na furaha ya bandia ambayo aliiweka usoni mwake lakini moyoni alikuwa na huzuni kuu ambayo ilibaki ikimtafuna ndani kwa ndani, kila alipolifikiria suala la kukaa mbali na Moses kiasi cha bara tofauti ambayo haijawahi kutokea tangu walipoanza mahusiano aliona ni suala ambalo ni gumu sana kukubaliana nalo kwani moyo ulikuwa unauma sana akifikiria suala hilo. Mapenzi mazito aliyonayo kwa mume wake ndiyo yalimfanya awe na hali hiyo ambayo ilimbidi apigane nayo ili aweze kuizoea ikiwa tu mume wake ataridhia kuondoka kwake kwenda nje ya nchi akiwa na kiumbe tumboni mwake. Aliondoka kazini kwake baada ya kumuaga kila mtu anayefahamiana naye hapo ofisini kisha akaelekea nyumbani kwake akisubiri ujio wa mume wake jioni ya siku hiyo aweze kumpa taarifa hiyo yenye simanzi ambayo kwake ni zaidi ya msiba.
****
MAKAO MAKUU
USALAMA WA TAIFA
DAR ES SALAAM
Wakati Beatrice akipokea taarifa ya safari mume wake alikuwa katika ofisi yake ya usalama wa taifa baada kuaagana na Norbert tangu walipoanza hatua ya awali katika kazi yao ya kutegua kitendawili ambacho kilikuwa kipo katika anga zao, mbele ya ofisi yake iliyojaa samani za kisasa kulikuwa kuna mwanaume anayekaribia kuitwa mtu mzima ambaye kium,ri alikuwa analingana na marehemu Kennedy aliyekuwa mjomba wake Moses ingawa kicheo ndani ya usalama wa taifa alikuwa yupo chini ya Moses hivyo alikuwa akimheshimu sana. Mwanume huyo alikuwa ni msaidizi wa Moses katika idara ya usalama wa taifa pia ni mkurugenzi wa shirirka la mfuko wa hifahdi ya jamii ambalo ndilo sjirika analofanyi kazi mke wa Moses.
"Ndiyo Mr Mabina niambie kazi niliyokupatia imeendaje?" Moses alimuuliza msaidizi wake huyo akiwa sura isiyo na mzaha hata kidogo.
"Imefanikiwa mkuu kwa asilimia zote kwani nimeweza kumchomeka katika safari ya kwenda Uingereza ambayo ilikuwa ikihusisha mawakili wanne wa shirika la mfuko wahifadhi ya jamii" Mabina alijibu akiwa ana sura ya umakini kama ilivyo mkuu wake.
"vizuri sana na umefanya kazi nzuri kwani hofu yangu ipo kwake tu, sasa inabidi uwe makini wasikujue kama wewe ni msaidizi wangu kwani itakucost Mr Mabina. Waache wanaojulikana wansongoza idara hii ndiyo hao hao wajulikane lakini si uongozi halisi wa Idara hii kwani hiyo itakuwa ni hatari sana kwako pia......Unaeza ukaenda" Moses aliongea kisha akamruhusu msaidizi wake aonde akaendelee na kazi nyingine, kisha yeye akamalizia kazi muhimu katika ofisi yake akaondoka kuelekea nyumbnai.
****
Wakati Moses akiwa anaongea na msaidizi ilikuwa tayari ni mida ya saa tisa na nusu ambao ni muda kutoka kazini kwa baadhi ya wafanyakzi wa mashirika mbalimbali, Norbert muda huo alikuwa yupo ndani ya gari yake aina ya suzuki Escudo akiwa ameegesha kando ya barabara akionekana alikuwa navuta subira ya jambo ambalo lilimfanya awepo hapo. Alikuwa yupo jirani na bandari inayotumiwa na na boti ndogo zinazosafiri kwenda zanzibar, baada ya dakika takribani kumi yule binti aliyeleta kitabu cha rekodi walipokuja hapo kuulizia kuhusu boti zilizoondoka jana alionekana akitoka ndani ya geti, alikuwa akielekea barabarani akitembea kwa mwendo wa uchovu sana ingawa mapambo yake aliyojaliwa yalikuwa yakitikisiika na kuzidi kumchanganya Norbhert.
"Moyo wee! Usikome mjini hamna mwenye chake" Moyo aliongea kwa sauti ya chini huku akiachia breki ya gari akimfuata binti huyo.
****
Yule binti alikuwa akitembea kivivu sana pembezoni mwa barabara ya Sokoine bila ya kujua kama alikuwa akifuatiliwa na Nobert kwa nyuma yake akiwa na anamtazama kwa uchu sana, alikuja kumuona Norbert baada ya gari ya Norbert kumfikia ikiwa inaenda kwa mwendo wa wastani huku Norbert akimuangalia akiwa anatabasamu usoni. Tabasamu lake ambalo ndiyo sumu kubwa sana kwa mabinti lilionekana kwa binti huyu mrembo ambaye alimtambua Norbert kutokana na umaarufu alionao kama mwandishi wa habri wakujitegemea nchini. Alimtazma Norbert kwa tabasamu aliloliachia na akajikuta akiona aibu sana akatazama pembeni.
"uchovu ni kitu cha kawaida kinachomkuta mtu yoyote akiwa anatoka kwenye mihangaiko mrembo" Norbert aliongea huku akiwa analiachia gari katika mwendo wa taratibu huku akiwa anaenda sambamba na yule binti akionekana kuwa ni msindikizaji wake, maneno yake yalinyamaziwa kimya na binti huyo ambaye alizidi kuongeza mwendo ndipo Norbert akaegesha gari pembeni akamfuata akamshika mkono ili kumzuia asiende.
"We kaka nini jamani?" yule binti alilalamika baada ya Norbert kumvuta mkono na kumzuia asiende mbali zaidi.
"ukiona nakuzuia hivi ujue nakuzuia na mengi binti kukubali kuzuiwa na mimi utakuwa umeepuka mjengi bibie" Norbert aliongea huku akimtazama yule binti usoni.
"mbona sikuelewi unaongea nini?" Yule binti aliuliza baada ya kuona haelewi Norbert anachoongea.
"utaelewa tu ikiwa ukinipa wasaa wa kukuelewesha haya ninayoyaongea" Norbert aliongea huku akimtazam yule binti usoni akionesha anamaanisha kile anachokiongea, binti yule alimtazma Norbert kwa sekunde kadhaa kisha akashusha pumzi halafu akaangalia chini kukwepesha macho yake yasikutane na macho ya Norbert.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kiufupi we nione kama mwokozi niliyetumwa kuja kukukomboa na kadhua iliyopo mbele yako bibie ikiwa tu utanipa wasaa wa kuyasikiliza maneno yangu ya uokovu" Norbert aliongea huku akiachia tabsamu hafifu usoni akiwa anamtazama sana yule binti.
"kaka yangu ongea nakusikiliza nataka niwahi daladala" Yule binti alimuambia.
"kwanza wokovu wa kwanza wa kuokoka na kadhia ya daladala ushaupata bibie nafikiri uokovu kamili unafuata hivyo vuta subira hutachelewa kufika kwako" Norbert aliongea
"Ayiii! Jamani si useme tu nitachelewa mwenzako daladala za Tandika zinazopita Keko ni chache sana kaka yangu, hebu ongea basi niwahi kabla usafiri haujawa wa tabu zaidi" Yule binti aliongea
"Ndiyo maana nikakuambia hata uokovu wa kupanda daladala umeupata kwani usafiri wangu unapita hapo unapoelekea hivyo ondoa wasi kabisa leo hutapata tabu ya kutumia nguvu katika kupata usafiri" Norbert aliongea huku akimtazma yule binti ambaye aliona ni bahati kutopanda daladala kwa siku hiyo kutokana na kubainishiwa juu ya usafiri wa Norbert ulikuwa ukipita maeneo hayo. Alishukuru kimoyomoyo kwa kupata bahati ya kubana bajeti yake asipande daladala .
"Nafikri leo ni siku nzuri ya kuwahi kupumzika mapema nyumbani kwako kwa uokovu huu wa awali naweza nikakusogeza hapo unapoelekea bibie" Norbert aliongea huku akiachia tabasamu lake ambalo ni ugonjwa tosha kwa mabinti, tabasamu hilo lilimfanya yule binri ashindwe kumtazama machoni kwani alihisi hali ya tofauti alipomtazama Norbert usoni.
"Nitashukuru" Hatimaye yule binti alikubali kupanda katika usafiri wa Norbert.
"Ni vyema, Norbert naitwa wewe je?" norbert alijitambulisha huku akimpa mkono akihitaji kuju jina ya yule binti.
"nakujua vema,Josephine" Yule binti alimpa mkono Norbert huku akitaja jina lake.
"ok unaweza kuingia kwenye uokovu wako wa awali" Norbert alimuambia Josephine huku akimuonesha mahala gari lilipo, Josephine hukujibu kitu zaidi ya kumtazama Norbert kwa jicho linaloashiria yupo tayri kuingia kwenye gari la Norbert. Jicho hilo lilimfanya Norbert atembee hadi ulipo mlango wa pili wa abiria kwenye gari lake akamfungulia Josephine ambaye alimfuata Norbert kwa nyuma na akaingia ndani ya gari baada ya mlango huo kufunguliwa, ilikuwa ni hatua ya awali ya mafanikio aliyoipata mzee wa mabinti baada ya kuweza kumshawishi yule binti aingie ndani ya gari yake. Furaha iliyojificha ndani ya moyo iliendelea kuwepo na aliona ameanza kupata ushindi katika hatua yake ya awali kumfuata Josephine, alizunguka upande wa dereva akaingia akaliongoza gari kuingia barabarani akafuata barabara ya Sokoine hadi stesheni akaingia upande wa kushoto kuifuata barabara iendayo katika mzunguko wa clock tower. Njiani Norbert aliendelea kuongea maongezi ya kawaida yenye kufurahisha ambayo yalimfanya yule binti atabasamu muda wote, alikuwa akiongea huku akiwa hajsahau dhumuni lake liliolomfanya amfuate bunti huyo kule kazini kwake.
Walipofika eneo la karibu na kwenye mataa ya Kariakoo mtaa wa Gerezani walikuta foleni kubwa ambapo ndiyo Norbert alitumia muda huo kuanza kutimiza kile kilichomfanya apoteze muda wake kumsubiri binti tangu alipomuona alipokuja kiupelelzi zaidi.
"Josephine umeona sasa umepata uokovu mdogo hadi sasa nafikiri bado uokovu mkubwa haujaupata" Norbert aliongea wakati wakisubirio magari yaweze kuruhusiwa.
"upi huo Norbert?" Josephine aliuliza
"Huo uokovu mkubwa zaidi kupita yote unatakiwa uwe nayo katika maisha yako na mimi ndiyo nimetumwa kuja kukupati uokovu huo" Norbert aliongea huku akitabasmau na kusababisha Josephine aone aibu na kuishia kucheka akaangalia pembeni.
"Mh1 Nawe nawe unataka kuanza vituko vyako nicheke tu maana hapa mbavu zinaniuma kwa jinsi ulivyokuwa ukinichekesha" Josephine aliongea huku akicheka kutokana na kufurahishwa na vituko vya Norbert alivyokuwa akivionesha ndani ya gari hilo kabla hajafika hapo kwenye mataa.
"Huu wakovu nafikri utakuwa ni tulizo kwa hizo mabvu zinazouma kwa ajili ya kucheka bibie, utegee sikio wala hutapata maumivu ya kuumia mbavu kama mwanzo" Norbert aliongea huku akimtazama Josephine kwa umakini sana.
"Mh! Haya" Josephine aliguna akionekana yupo tayri kuusikiliza wokovu huo anaoambiwa na Norbert ingawa hakutambua ni wokovu wa aina gani, alimtazama Norbert akionesha nataka kusikiliza kile anchotka kuambiwa na tabasamu la Norbert ndiyo lilizidi kumpa ari ya kutaka kusikiliza kile anachotaka kuambiwa na Norbert. Hakujua kama yupo anaongea na bwana wa mitego ambaye ni nadra sana mtego wake kukosa malengo akiutega, hakujua kama naongea na bingwa kudungua ambaye ni nadra sana kukosa shabaha na anapodungua mioyo ya kina dada warembo. Hakujua anaongea na simba dume mwenye njaa ambaye hana jike wa kuweza kumletea chakula hivyo huwinda mwenyewe kutafuta chakula, utanashati wa Norbert alionao na mavazi anayovaa ambayo yanaonekana kumkaa sana ndiyo vilizidi kumpa hamasa zaidi Josephine ya kumsikiliza Norbert kile anachokisema. Uzuri wa sura alionao Norbert nao ulizidi kumpa hamsa huyo binti ya kumsikiliza Norbert na uchangamfu pamoja na sifa nyingine alizonazo zilizidi kumvutia.
"kwa muda wa siku nne nimeagizwa nije kukuletea uokovu katika moyo wako ambao ulikuwa ni muhimu sana kuwa nao, siku zote hizo nilikuwa nikija eneo la jirani na kazini kwenu nikiwa ninavuta subira zaidi ili nikupatie wokovu huo lakini aliyenituma alizidi kunihimiza nifanye hima nikukomboe kutokana na balaa ambalo lingekufika ndiyo maana leo nikakusubiri hadi unatoka nikaweza kukupa uokovu wa awali kabla ya kukupa uokovu kamili" Norbert aliongea huku akimtazama kwa umakini yule binti tena aliongea kwa hisia aonekane kile anachoongea ndiyo anahokimaanisha.
"Norbert wait umesema umetumwa uwahi ili balaa lisije likanifika. Nani aliyekutuma na balaa gani linataka kunifika" Josephine aliuliza akiwa hajaelewa kauli alizozitumia Norbert.
"Aliyenituma hayupo mbali na hapa bali yumo amejificha ndani ya ya sehemu ya kifua changu na si mwingine bali ni moyo wangu tangu kwa mara ya kwanza nilipokuona alinihimiza nikuokoe na balaa la kutekwa na wale wasio na upendo kwako na nikupe sehemu ya hifadhi katika chumba cha upendo wangu upate uokovu wa kudumu Josephine,ndiyo umenifanya nifunge safari hadi hapa nikakupa wokovu wa kukuokoa usipate na kadhia ya kugombania daladala ambayo huleta maafa mengi kwa watumiaji ikiwemo kuibiwa vitu muhimu" Norbert alitiririka maana ya maneno aliyokuwa anampa Josephine ambayo yalimfanya Josephine aangalie pemebni kwa iabu. Norbert alitaka kuongeza neno jingine baada ya kuona aibu iliyomuingia Josephine lakii sauti ya honi ya gari iliyopo nyuma ilimshtua na ikamfanya aangalie mbele kwa haraka baada ya kushtuliwa na honi hiyo, alipotazma mbele aliona magari yameanza kuondoka ndipo akabaini kuwa Askari wa usalama barabarani alikuwa ameruhusu magari tayari na hapo akaachia breki ya gari akaliondoa kwa kasi ili asizidi kukera watu waliopo nyuma yake kwenye foleni hiyo. Ndani ya nafsi yake aliachia tusi zito kwa yule Askari wa usalama barabarani kwa kuruhusu magari kwani ulikuwa ndiyo muda muafaka wa kuweza kumchombeza Josephine, aliweka umakini mbele akiwa anawahi foleni nyingine iliyopo katika makutano ya barabara yaliyopo Keko. Muda huo akiweka yupo makini kwa kucheza na usukani hakuwa akitambua kuwa Josephine alikuwa akimtazama na alipokaribia kwenye makutano ya barabara yaliyopo keko kwenye foleni ndipo alipobaini kuwa alikuwa akitazamwa.
Alipogeuza jicho kumtazama Josephine baada ya kumbaini alikuwa akimtazama alimfanya Josephine aingiwe na aibu ambapo alitazma kando kutokana na kutostahimili kuweza kutazmana na macho ya Norbert.
"Bibie nadhani umenisikia juu ya wokovu niliyokuwa nahitajika kukupatia na ndiyo huo, sasa nafikiri upo tayari kuupokea' Norbert alimuambia Josephine huku akimtazama kwa jicho lenye ujumbe mzito sana.
"Norbert" Josephine aliita akiwa ameangalia pembeni baada ya kusikia maneno ya Norbert.
"Naam nakusikiliza" Norbert aliitikia
"Aaah! Hamna" Josephine alijikuta akibabaika baada ya kuita jina la Norbert.
****
HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
UPANGA
DAR ES SALAAM
Wakati Norbert akiwa yupo na harakati za kufuata mrembo Josephine upande mwingine katika hospitali ya taifa Muhimbili katika wodi mojawapo ya wagonjwa kulikuwa kuna watu wawili tu walikuwa wamelazwa huku wakiwa na pingu mguuni kila mmoja, muonekano wa watu hao walikuwa ni watuhumiwa kabisa kwani watuhumiwa ndiyo hulazwa wakiwa na pingu ili kuwazuia wasitoroke. Walikuwa ni watu wenye miili mikubwa ya kimazoezi ambao mmoja alikuwa amefungwa bendeji ngumu mguuni na mwingine alikuwa amelazwa huku ubavu mmoja ukiwa juu akiwa amefunikwwa shuka,pembeni yao kulikuwa kuna askari mwenye silaha akiwa anaonekana yupo makini kulinda kuhakikisha watuhumiwa hao hawatoroki. Ulinzi wao waliekewa ulikuwa ni ulinzi dhabiti sana kimuonekano kutokana na aina ya ya tuhuma waliokutwa nayo, askari polisi wengine wanaolinda eneo hilo walionekana kuwa ni makini sana kiasi kwamba eneo la wodi hiyo likawa linawatisha hata wauguzi waliokuwa wakiwahudumia watuhumiwa hao
Upeo wa macho na akili za maaskari hao katika kuimarisha ulinzi katika eneo hilo ulikuwa umezidiwa na upeo na akili za mtu mwingine tofauti ambaye ana ujuzi kuliko wao, waliendelea kufanya ulinzi wao uliozidiwa daraja na umakini wa mtu mwingine tofauti ambaye alikuwa anawatazama umakini wao ulivyo. Hakika akili kila mtu anazo sawa na mwingine ila hutofautiana katika kuzitumia hizo akili ndiyo maana tunaonekana hatupo sawa kiakili kabisa, hata hawa maaskari walikuwa na akili sawa na mtu anayewatazama umakini wao ila walizidiwa jinsi ya kuzitumia hizo akili.
Nusu saa baadaye muuguzi wa kiume alifika katika eneo la wodi hiyo akiwa amebeba kisahani chenye dawa pamoja na mipira ya mikononi, maaskari walipomuona muuguzi huyo waliangalia saa zao wakampekua ili kuhakikisha hana chochote cha hatari wakamruhusu aingie ndani ya wodi hiyo. Muuguzi huyo aliingia ndani ya wodi hiyo akakutana na askari mwingine aliyepo hapo ndani ambaye alimpekua kisha akakaa kwenye kiti akimuacha ahudumie wagonjwa, askari huyo alimuangalia Muuguzi huyo kwa umakini akiwa anaanza kuhudumia wagonjwa huku mikono yake ikiwa inachezea bunduki uake aina ya SMG. Kutazamwa huko na askari kulimfanya yule mhudumu asite kufanya kazi yake akabaki anamtazama Askari huyo kwa macho yaliyojaa uoga.
"Aisee we vipi hebu fanya kazi yako uende" Askari huyo aliongea kwa ukali.
"samahani afande sauti ya juu hairuhusiwi eneo kama hili pia mimi ni raia wa kawaida tu ninayeuguza wagonjwa tu sasa kitendo cha kunisimamia na bunduki eneo hili jua unanifanya nisiweze kufanya kazi yangu kwa ufanisi unaotakiwa. Kwa uoga niliokuwa nao nikiona hiyo silaha na magwanda yako na jinsi unavyonitazama jua utanifanya hata nizidishe kiwango cha dawa kwa mgonjwa akapoteza maisha wakati ni muhimu kwenu kuwa hai, afande kama hutojali naomba unisubiri nje ya mlango niwahudumie hawa wagonjwa kwa ufanisi" Yule Muuguzi aliongea akionesha wazi kuwa ana hofu sana, maneno yake yalimuingia yule askari aliyekuwa ana jukumu la kulinda wagonjwa hao ndani ya wodi hadi akanyanyuka akaelekea nje akimuacha Mhudumu afanye kazi yake. Maneno yaliyomlainisha askari yule yalikuwa ni wasaa mkubwa kwa Mhudumu yule kufanya kazi iliyomleta hapo ndani ya wodi hiyo, aliwaamsha wagonjwa hao ambao walishtuka sana baada ya kumuona aliwa eneo hilo.
"Panther" kwa pamoja walitamka kwa sauti ya tabu sana.
"Shiiiii! Mbona wajinga sana nyinyi niliwaambiaje?" Yule mhudumu aliuliza kisha akaendelea kuongea, "yaani mnaenda kutumia Klorofomu katika kuwanasa wale watu kwanini msitumie sumu kabisa muwaue, klorofomu si nusu kaputi ya kufanyia upasuaji kama wana maji si mnatambua haifanyi kazi sehemu yenye maji"
"Mkuu sisi tulitaka tuwatie nguvuni kwanza halafu ndiyo tuwamalize, sumu ya gesi tuliyokuwa nayo ni hatsri sana ingesambaa eneo zima na hatukuwa na vifaa vya kujizuia" Mmojawapo aliyevunjika mguu aliongea mbele ya Panther.
"Ok my boys siyo neno tena nafikiri nitafute njia ya kuwakomboa eneo hili" Panther aliongea huku akitabsamu na kusababisha vijana wake nao watabsamu pia, alikuwa tayari ameshavaa mipira ya mikononi.
"sawa bosi tunakutegemea kwa hilo sana maana tukiingia rumande hatutatoka,gari yetu imekutwa na MP5 mbili" Yule mwingine aliyevunjika mbavu alioongea kwa tabu sana huku akisikia maumivu kwa kila anavyoongea.
"Worry out my boys, give me your hands tupo pamoja" Panther aliongea huku akimyooshea mkono kila kijana wake akitaka wampe mikono yao kuashiria kuwa wapo pamoja katika hili. Vijana wale walimpa mikono yao wote kwa pamoja ambapo mmoja alishikana naye kwa mkono wa kushoto na mwingine kwa mkono wa kulia wakiwa na tabasamu pana ambalo halikudumu hata ndani ya nusu dakika kwani wote waliohisi kutobolewa na vitu kwenye viganja vyao. Walikuwa wamekamatwa kwa nguvu sana na mikono ya Panther iliyojaa nguvu nyingi sana, Panther alipoachia mikono yao kila mmoja alikuwa na damu kwenye kiganja chake huku akiugulia maumivu kwani walihisi maumivu makali sana baada ya kutobolewa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Stupid! Mnadhani mtapona mbele ya uzembe wenu kwenye kazi ya Panthers. Yaani mnabeba MP5 silaha ya kivita katika mission ndogo hivyo, sasa onjeni uchungu wa sumu ya Quantanise ikitembea kwenye miili yenu kuwamaliza, mna dakika moja tu ya kupumua" Panther aliongea kwa sauti ya chini ambyo ilikuwa imejaa ukali sana.
Miili ya wale vijana wake taratibu ilianza kubadilika rangi na kuwa ya rangi nyekundu kuanzia walipotobolewa na sindano za mipira ya mkononi aliyovaa Panther, rangi nyekundu hiyo kwenye ngozi yao ilikuwa ikisambaa kwa kasi sana mithili ya moto wa nyikani unavyosambaa kwenye nyasi na ndani ya sekunde kadhaa ilikuwa imeshasambaa mwili mzima na huo ndiyo ukawa mwisho wa maisha yao na Panther alitoweka eneo hilo kwa nja nyingine tofauti na mlangoni.
***
Askari aliyekuwa anawalinda wale vijana alikuwa amekaa nje ya wodi hiyo pamoja na maaskari wenzake na hapo ndipo akakumbuka alisahau simu yake katika meza ndogo iliyopo humo ndani na ikamlazimu aingie ndani kwenda kuifuata kwa haraka ili ampishe mhudumu aendele kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi, alifungua mlango na akaingia ndani akakutana na hali ambayo hakutarajia kama atakutana nayo kwa muda huo. Muguzi aliyekuwa akifanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa hao hakumkuta na badala yake alikuta kisahani tu cha dawa alichokuwa amekibeba kikiwa kipo juu ya meza ndogo inayotenganisha vitanda vya wagonjwa hao, miili ya wagonjwa aliiona ikiwa ina dalili ya kutokuwa na uhai kabisa na ilikuwa imebadilika rangi na kuwa ya rangi nyekundu ambayo inaonesha kabisa kuwa damu imeviria juu ya ngozi mwili mzima.
Askari huyo kwa haraka alichukiua silaha yake akaitoa usalama akawa anasogea upande waliokuwa wagonjwa akiangaliwa kila pande na hapo ndipo akashududia sehemu ya mfuniko wa dari ikiwa haijafungwa vizuri, hali hiyo ilimpa uhakika kwamba aliyeingia ndani ya wodi hiyo hakuwa Muuguzi bali ni mhalifu mwingine aliyekuja kupoteza ushahidi wa uwepo wa watu hao. Askari huyo kwa haraka zaidi aliwataarifu wenzake juu ya kile alichokiona mule ndani kupitia simu ya upepo. Msako mkali ulianza mara moja ndani ya wodi za jirani ambazo dari hilo lilikuwa na mifuniko wa kutokea ambayo ingeweza kumpa nafasi mtuhumiwa kutoka ndani ya dari na kushuka chini, waliingia ndani ya wodi zote lakini waliambulia patupu kwani hapakuwa na dalili za uwepo wa mtuhumiwa waliyekuwa wanamtafuta. Mwisho kabisa walieleka katika Maliwato ambayo ipo mbali kidogo kutoka kwenye wodi waliyokuwa wamelazwa watuhumiwa waliokuwa wanawalinda ili waweze kukagua napo, kwa kasi walifika kwenye Maliwato hiyo ambapo walimkuba kikumbo mzee mmoja aliyezeeka aliyekuwa anatoka huko chooni alimanusura aanguke chini.
"Samahani mzee wangu" Askari mmoja aliomba radhi kwa haraka kisha akaingia pamoja na wenzake humo ndani ya Maliwato na wakaanza kukagua chumba kimoja baada ya kingine vya vyoo ili wahakikishe wanamtia mtuhumiwa nguvuni, ukaguzi wao uliendela kwa kasi ya ajabu hadi walipofikia kwenye mabafu ambapo ndipo walipopigwa na butwaa baada ya kuona zile nguo alizovaa yule mhudumu pamoja na viatu vyake vikiwa vipo katika chuma la kuwekea nguo bafuni na sehemu ya dari ikiwa ipo wazi.
"Wait" Alisema askari mmoja kisha akafikiria na hatimaye akasema,"jamani ni yule mzee tuliyempush mlangoni maana hakuna mtu mwingine humu mwingine humu na yeye ndiye aliyetoka humu".
Kauli hiyo iliwazindua wote kwa pamoja wakatoka nje wote wakakimbilia nje kumtafuta yule mzee huku wakiuliza baadhi ya watu juu ya yule mzee alipoeleka na walitaja muonekano wa huyo pamoja na jinsi alivyovaa. Majibu ya kila waliyemuuliza yalikuwa ni kutomuona mzee huyo na hapo maaskari hao wakazidi kupagawa na jinsi ambavyo mtuhumiwa wanyemtafuta alivyowapiga chenga ya kuwatoroka katika mazingira ambayo hawakuyaeleweka.
Hawakutambua kwamba mtu waliyekuwa wanamtafuta alitumia akili zaidi yao ndiyo maana akawaacha kwenye mataa wakiwa wanashangaa zaidi, hakika walizidiwa ujanja wa kila namna na mtuhumiwa wao aliyekuwa amefanya tukio ndani ya wodi waliyokuwa wanailinda kutokana na uwepo wa watuhumiwa waliokuwa na shaka nao.
****
Muda ambao askari wakiwa wanachezeshwa kandanda la kutumia ubongo na mtuhumiwa aliyekuwa amewaachia maafa ya kuwaua watu waliopewa jukumu la kuwalinda, Norbert tayari alikuwa ameshafika Keko na alikuwa ameegesha gari pembeni akiwa yupo anaongea na Josephine ambaye alikuwa ameshafika mwisho wa safari yake. Alikuwa tayari ameshafanya kazi nzito ya kumvua pweza mkorofi katika kina kirefu cha bahari na alikuwa na anapima kama pweza yule alikuwa na dalili ya uzima ili asije akamletea athari yoyote ile, alikuwa tayari ameshalainisha ugumu wa moyo wa Josephine kwa mbinu zote za hali ya juu alizonazo katika kulainisha mioyo ya kinadada.
"Norbert bwana mbona mapema sana kuhusu hili suala?" Josephine aliongea huku mikono yake ikiwa inachezea kucha zake nadhifu zilizo na matunzo ya hali ya juu sana.
"Hayana wakati wala ratiba useme yamewahi sana cha msingi ni kufungua mlango wa moyo wako uruhusu yaingie ndani yako" Norbert aliongea huku akipeleka mkono wake kushika viganja vya Josephine,alipogusa alikutana na ulaini wa ngozi ya Josephine ambao ulikuwa usio wa kawaida ambao ulizidi kumfanya aone hakukosea kuja kuleta maombi kwa binti huyo ili aweze kuijaribu ladha iliyokuwepo kwa binti huyo.
"Basi tufanye kesho Norbert leo muda tayri umeenda jamani" Josephine aliongea.
'Ok, no problem nakupa muda wa kulifikiria zaidi suala hili ila nilikuwa nina obmi jingine" Norbert aliongea aliongea kisha akaendelea,"nikiwa kama muokozi naomba unipatie simu yakko mara moja kama hutojali".
Ombi hilo lilimfanya Josephine amuangalie Norbert kwa sekunde kadhaa kisha akamptia simu yake ya kiganjani,Norbert aliichukua simu hiyo akaandika namba zake za simu kisha akapiga ambapo simu yake ilianza kuita. Alikata simu kisha akaihifadhi namba hiyo kwenye simu ya Josephine akamrudishia huku akiwa anatabasamu.
"sijui nimefanya vibaya?" Alimuuiza Josephine huku akimpatia simu yake.
"No hujafanya vibaya jamani" Josephine alijibu.
"Ok nadhani tomorrow tutaonana" Norbert aliongea huku akimpatia Josephine ili waagane, Josephine alipompatia mkono aliuvuta karibu akaubusu halafu akamtazama usoni.
Ilikuwa ni tendo ambalo halikutarajiwa na Josephine na alibaki akimtazama Norbert kwa mshangao kisha akatabasamu akaangalia pembeni kwa aibu.
****
Josephine alishuka ndani ya gari ya Norbert kisha akampungia mkono akaingia mtaani huku akitembea kwa madaha sana, miondoko yake na jinsi mapambo aliyojaaliwa yalikuwa yakileta ugomvi kwa kila hatua aliyokuwa anaipiga wakati akiingia mitaani. Norbert alibaki akimtazama kwa muda wa dakika takribani moja kisha akatingisha kichwa kuashiria anasikitika, Josephine alipoingia kwenye mitaa ya ndani sehemu za Keko ndiyo ukawa mwisho wa Norbert kumuona na pia kufaidi uhondo aliouona sehemu ya burudani kila akiuona na macho yake.
"Aisee kama kashushwa vile" Norbert aliongea huku akiweka gia ya gari lake akaachia breki gari likaingia barabarani, alikuwa akiwaza sana juu ya uzuri wa Josephine na jinsi itakavyokuwa siku akiwa naye mahali palipo na uhuru zaidi.
"bahati naishi Temeke hivyo sijapoteza mafuta sana, ningekuwa naishi mahali kama Tegeta mama angu ningekuja hadi huku nirudi tena Tegeta. Mtoto mkali balaa" Norbert aliongea mwenyewe akiwa anakata kona kushoto alipofika Tameko jirani kabisa na maghorofa ya shirika la nyumba la taifa NHC, aliingia kwenye barabara ya Chang'ombe akawa anaongeza mwendo wa gari kutokana na uchache wa magari katika barabara hiyo. Alienda hadi kwenye mataa ya Chang'ombe akasubiri baada ya taa kuwaka nyekundu katika upande wake, kwa mara nyingine mataa hayo yalimfanya arudi kwenye mawazo juu ya mwanamke yule kutokana na kuweka subira yaweze kuruhusu apite. Uzuri wa Josephine kwa mara nyingine ulijirudia ndani ya kichwa chake na kumfanya atikise kichwa kila akikumbuka umbo lake aliloliona kwa mara ya kwanza, hamasa ya kuwa naye tayari ilishaamka katika mwili wake lakini hakuwa katika moyo wake kabisa. Alikuwa hana tofauti na muonjaji karanga bila ya kununua ili ajue karanga hizo zina ladha gani tu, pia alikuwa na muuza karanga maalum ambaye karanga zake hakuchoka kuzila kwa muda wowote ule autakao ule na ndiyo huyo aliyekuwa yupo moyoni mwake siku zote. Kwa huyo ambaye yupo moyoni mwake laiti Norbert angekuwa ni treni basi huyo angekuwa ni mwisho wa reli haendi popote pale, hakika alikuwa hasikii wala haoni kwa huyo aliyekuwa moyoni mwake ingawa hakuacha tabia yake ya kuonja kila kinachopita mbele yake. Nusura za Mungu muweza katika uonjaji wake ndiyo zilimfanya aweze kuwa mzima mpaka muda huo kwani katika uonjaji wake huo hakuwahi kuonja sumu hata siku moja, hakika muweza bado alikuwa akimpenda sana mja wake huyu na bado alikuwa anahitaji kumuona akipumua katika mgongo wa ardhi ndiyo maana yupo salama mpaka muda huo.
Mataa yaliporuhusu Norbert alinyoosha moja kwa moja barabara ambayo ilimpeleka hadi jirani kwenye kituo cha polisi cha Chang'ombe maarufu kama Usalama, alikata kona upande wa kushoto akaingia katika barabara ya Temeke ambapo alitembea kwa umbali mdogo tu halafu akakata kona akaingia upande wa kulia kwenye barabara ya vumbi inayopita jirani na mtaa wa Maneno kitongoji cha Temeke. Alienda na barabara hiyo hadi alipoipita shule ya msingi ya Muungano akakata kona akaingia upande wa kushoto, alienda kwa mwendo mfupi kisha akasimama kwenye geti la nyumba yenye uzio mkubwa sana. Hapo alipiga honi mara moja geti likafunguliwa akaingiza gari ndani akalipeleka hadi sehemu maalum ya kulaza gari akalizima akashuka, alitembea kuelekea ndani ya nyumba yake akiwa hana habari juu ya mabadiliko yaliyopo ndani nyumba hiyo. Hakuwa na habari kama palikuwa na ongezeko la watu ndani ya nyumba hiyo na alikuja kujua baada ya kumuona mmojawapo ambaye alikuwa akimpenda sana, huyo ndiyo alimfanya abaini kwamba kulikuwa na mwingine ndani ya nyumba hiyo kwani hawezi kuja peke yake hata siku moja.
Jerry ndiye alikuwepo mbele ya macho yake kwa muda huo akamfanya abaini kwamba hakuwa amekuja peke yake kabisa kwani hakuwa na uwezo wa kuja peke yake, mtoto huyo hakuwa na uwezo wa kuja peke yake bila uwepo wa mama yake na hapo ndipo akabaini kwamba Jerry alikuwa amekuja na mama yake hapo nyumbani. Jerry alikuwa ni mtoto aliyefanana na Norbert kwa sura hadi mwendo wake anaotembea na bila shaka haikuwa na haja ya kuhitaji vipimo vya vinasaba katika kujua kama ni mtoto wake kwani alikuwa na kila ushahidi wa kumuonesha ni damu yake. Jerry alipomuona Norbert alimkimbilia kwa haraka sana akamkumbatia huku akionesha furaha aliyonayo kwa kumuona baba yake kwa muda huo, Norbert alimnyanyua kwa furaha mtoto wake huku akifarijika sana na kumuona eneo hilo.
"Oooh! Son, mummy yupo wapi?" Norbert alimuuliza Jerry akiwa amembeba kwa furaha.
"Inside, I miss you daddy" Jerry aliongea huku akimkumbatia baba yake kwa upendo na alionesha alikuwa akitaka kumuona baba yake kwamuda mrefu sana.
"me more my son, masomo vipi?" Norbert alimuuliza Jerry huku akifanya matani naye ambayo yalizidi kumfurahisha sana Jerry, aliingia ndani akiwa amembeba Jerry na alienda sebuleni ambapo alipokelewa na mama yake Jerry kwa mapokezi tofauti na yale aliyompokea Jerry.
Alimkuta Norene akiwa amekaa kwenye kochi akiwa amenuna sana na alipomuona aligeuza sura pembeni kabisa, Norbert hapo alibaini kwamba Norene hakuwa amependezwa na kitu ambacho hakukifahamu na hata alipomfuata akamshika mkono Norebe aliupiga kibao mkono wake.
"Nor ulikuwa wapi muda wote huo?" Norene aliuliza akiwa amenuna.
"Norene nilikuwa nina kazi ya kiofisi kidogo" Norbert alijitetea.
"Muongo wewe haukuwa ofisini kwako nimepiga simu yako ya mezani hukupokea, hivi unajua nimekuja muda mrefu sana nakusubiri wewe" Norene aliongea akuoneshwa kutopendezwa kabisa na kutopokelewa kwa simu yake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Siyo ofisi ya mazugio bali ni ofisi halisi, nilikuwa na Gawaza tukipiga kazi muhimu" Norbert alijitetea.
"una uhakika ulikuwa na Moses? Nimpigie simu nimuulize?" Norene aliuliza akiwa amekaza macho yake
"unaweza ukampigia simu hiyo hapo mezani" Norbert alimuambia Norene huku akijiamini na hakuonesha chembe yoyote ya wasiwasi kwani alijua yupo anajibu maswali ya jasusi mwenzake, kauli hiyo ilimfanya Norene asimame wima amkumbatie Norbert.
"Nakupenda sana Norbert tambua ukiwa mbali nami na usipopokea simu unanipa wasiwasi mpenzi" Norene aliongea kwa hisia akiwa amemkumbatia Norbert.
"Nakupenda pia mama yake, kuwa na amani tu" Norbert aliongea.
"amani nitakuwa nayo wapi mpenzi wakati wewe kazi yako ni ya hatari na muda mwingine inakuhitaji uwe karibu na wanawake" Norene aliongea kwa kulalamika akiwa bado amemkumbatia Norbert.
"wewe ndiyo mwisho wa vituo vyote sina pa kwenda zaidi mpenzi wangu" Norbert aliongea huku akimtoa Norene mwilini mwake akamshika kiuno akawa anaelekea naye chumbani huku wakiwa na Jerry.
****
Wakati Norbert akiwa yupo na Norene wanaelekea chumbani muda huo ndiyo muda ambao Moses alikuwa akirejea nyumbani kwake kutoka kwenye mihangaiko yake, aliingiza gari yake sehemu maalum ya kulaza magari na akaingia ndani ya nyumba. Sura isiyo na furaha ya mke wake ndiyo ilimpokea kuashiria hakukuwa na taarifa nzuri usoni mwa mke wake ingawa yeye aliijua taarifa hiyo tangu hata mke wake hajapatiwa, alimkuta Beatrice akiwa amekaa kwenye kochi akiwa ni mwingi wa mawazo huku mkono wake akiwa ameweka shavuni kuonesha alikuwa na huzuni sana. Moses alipoona yupo katika hali hiyo alimsogelea akapiga magoti mbele halafu akaweka mikono kwenye mapaja yake akambusu mdomoni akionesha mwingi wa furaha kama ilivyo kawaida yake lakini Beatrice alionesha kutokuwa na hali ya furaha hata kidogo. Chozi lilianza kumdondoka taratibu kwenye macho yake akabaki akimtazama Moses kisha mvua isiyosababishwa na mawingu kwenye macho ya Beatrice ilianza kwa manyunyu taratibu na hatimaye ikawa mvua kubwa sana iliyoanza hata kumtia simanzi hata Moses mwenyewe, Beatrice alikuwa akilia kilio cha uchungu na alimkumbatia Moses kwa nguvu wakati akilia na machozi yake yakachukua nafasi nyingine ya kulowanisha kifua cha Moses.
"Mume wangu nakupenda sana na sipendi kuwa mbali nawe ila.." Beatrice aliongea huku akilia kwa uchungu sna kwa taarifa aliyopewa mchana ambayo kwake ilikuwa ni zaidi ya simanzi kabisa
"No no usilie mke wangu tell me tatizo nini?" Moses aliuliza huku akianza kuumika moyoni kwa kusikia kilio cha mke wake,alimtoa Beatrice kifunai mwake na akamfuta machozi yaliyokuwa yakimtoka na akambembeleza hadi alipotulia kisha akamuambia "nieleze my queen tatizo nini hujui sipendi kukuona ukihuzunika".
Beatrice alichukua nafasi hiyo kumueleza Moses kila kitu juu ya taarifa aliyopewa mchana wa siku hiyo alipokuwa kazini kisha akabaki akimtazama Moses aone taarifa hiyo ataipokea vipi,haikuwa taarifa ngeni katika masikio ya Moses kwani yeye ndiye aliyetuma hicho kitu kifanyike kwa ajili ya usalama wa mke wake. Taarifa hiyo ilipopenya kwa mara ya pili kwenye masikio yake alisimama pale alipokuwa amepiga magoti mbele ya mke halafu akageuka nyuma akampa mgongo akawa anapiga mkono kichwani kwake akionesha taarifa ile ilikuwa ni taarifa ambayo hakutarajia kuisikia hata kidogo, alipogeuka kwa mara ya pili kumtazama mke wake tayari uso wake ulikuwa umebadilika na kuwa usio na furaha hata kidogo hadi akaanza kumpa Beatrice hofu. Alishusha pumzi kwa nguvu kisha uso wake ukarudi katika hali ya kawaida kama awali akataka kufungua mdomo kutamka kitu ila akasita akahema kwa nguvu halafu akainamisha uso wake chini. Alipoinua uso wake alionesha kuwa na hali siyo na furaha kabisa na alibaki akimtazama Beatrice kusema chochote, alifumbata mikono yake kifuani mwake halafu akawa anatafuta neno la kuongea.
"Mke wangu" Hatimaye alitamka akamfanya Beatrice amtazame asikie kauli itakayotoka kwenye kinywa chake kwani alihisi asipomtazama usoni atakuwa haisikii vizuri kauli ya mumewe.
Moses aliendelea,"wewe ni mke wa professa tena tajiri mwenye utajiri binafsi na pia amerithi kutoka kwa mzazi professa aliyekuwa tajiri, wanawake wenzao wanataka uwaoneshe mfano ulivyo ingawa mume wako ni tajiri. Ukaamua kuchapa kazi kama wewe ukionesha mwanamke hutakiwi kubweteka ukitosheka na utajiri wa mumeo, ukiwa mke wa mtu maarufu umeweza kuwahamasisha wenzako pongezi kwa hilo na najivunia kuwa na mke kama wewe nakupenda sana. Sasa basi hiyo ni sehemu ya kazi mke wangu unatakiwa uwaoneshe upo mchapakazi kiasi gani,naumia sana kwa wewe kwenda mbali na mimi lakini yote ni maisha mke wangu hicho kitu ni cha muda mfupi" Moses aliongea
"No Moses" Beatrice alisema huku akisimama akamkikmbilia Moses akamkumbatia halafu akatamka kwa uchungu, "sitaki kuwa mbali na wewe". Kilio cha uchungu kutoka kwa Beatrice ndiyo kilifuata akabaki akimkumbatia Moses Moses kwa nguvu, Moses alimpokea mke wake na akawa ana kazi ya kumbembeleza tu.
"Najua nina mwanamke shupavu na mchapakazi sasa show how strong you are,upo mbali nami ila umebeba kiumbe changu mke wangu huo ni wajibu usilie baby" Moses alimuambia Beatrice huku akichezea nywele zake, Beatrice alitingisha kichwa kukubaliana na Moses halafu akasogeza mdomo wake jirani na mdomo wa Moses kuashiria alikuwa na hitaji jingine alilokuwa analihitaji tofauti na hiyo taarifa aliyompa mume wake.
Moses alitambua hitaji la mke na alimtimizia papo hapo kisha akamuinua kwa ghafla na kusababisha Beatrice arudiwe na furaha kisha akacheka kwa nguvu sana kuonesha alikuwa na furaha sana kila anapokuwa karibu na Moses. Aliingia naye ndani na siku hiyo wakaimaliza wakiwa na furaha akama ilivyo kawaida yao kuwa na furaha kila siku,walipopanda kitandani kupumzika napurukushani za aina zote za siku nzima bado walikuwa na furaha vilevile.
Asubuhi ya siku iliyofuata Beatrice alijiandaa na Moses pia akajiaandaa kwa kama ilivyo kawaida yake, wote kwa pamoja walitoka na gari moja na safari ya kuelekea Uwanja wa ndege ilianza kwani ndani ya saa moja na nusu lijalo ndege ya shirika la ndege la Uswisi ilikuwa ikisafiri kuelekea Uingereza ikipitia nchi tofauti. Ilikuwa ni siku inayowatenganisha wapendanao ambao hawakuhitaji kutenganishwa lakini kutokana na sababu isiyoepukika ilibidi watengane tu. Baada ya saa moja tayari walikuwa wameshafika katika maeneo ya maegesho ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, wote kwa pamoja walishuka na Moses akamsaidia mke wake kukokota sanduku la vitu vyake muhimu ambavyo angevitumia akiwa safarini. Waliingia ndani kwani muda wa abiria kuingia kwenye ndege ulikuwa umeshawadia,kwa pamoja waliachana eneo maalum ambalo msindikizaji hutakiwa kuishia hapo ndipo ikachukua huzuni ikazidi mahala pake. Waliagana kwa kukumbatiana kisha Beatrice akaelekea sehemu maalum ya ukaguzi na hatimaye akaingia ndani ya ndege, Moses aliendelea kusubiri eneo hilo hadi ndege ilipoacha ardhi ya Tanzania ndiyo na yeye akaondoka eneo hilo akiwa yupo huru ndani ya nafsi yake na hana wasiwasi wowote ule kwani udhaifu wake tayari ulikuwa umeshaondoka ndani ya eneo hilo sasa ilikuwa ni muda mzuri kwa yeye kuanza kufanya kazi kwa ufasaha kabisa.
****
IKULU
MAGOGONI
DAR ES SALAAM
Taarifa za kuuawa kwa viongozi mbalimbali wa kidini tayari zilikuwa zishafika kwenye ofisi ya rais Zuber Ameir na kutokana na upeo wake mkubwa kufikiria aliamua awaite viongozi wakubwa wa polisi wakiongozwa na IGP Rashid Chulanga, katika chumba cha mkutano ndani ya ikulu hiyo rais alionekana kutokuwa na mzaha kabisa na suala la linalotaka kuchangia kuvurugika kwa amani nchini. Baada ya kuhakikisha viongozi wote aliowaita wametimia wakiwemo makamishna mbalimbali wakiongozwa na IGP mkutano ulianza rasmi.
"Hali ya amani kwa sasa naona itaelekea mahali pasipohitajika nchi iwe, mauaji haya viongozi wakubwa wa kidini siyo suala la kulifumbia macho hata kidogo kwani naona litaelekea mahali ambapo si pazuri. Nimeamua kuwaita hapa ili niwaambie kuhusu hili suala ambalo litaweza kuchukua sura nyingine ndani ya nchi yetu iliyo na amani, yametokea mauaji ya kwanza ya askofu wa KKKT dayosisi ya Mashariki tukajua ni moja ya njama ya wahalifu hivyo uchnguzi ufanyike ili watiwe mbaroni wahukumiwe lakini yalipotokea haya mauaji ya Mufti wa jiji jili nimeona kama kuna kitu kinataka kupandikizwa katika vichwa vya waumini sasa inabidi nyinyi kama viongozi wa jeshi la polisi mhakikishe suala hili halitokei. Amani ndani ya nchi yote ni suala la muhimu kudumishwa sasa nataka suala la kuvurugika kwa amani lisiwepo ndani ya nchi hii, nimemaliza ningehitaji kusikiliza maoni yenu juu ya suala hili" Rais Zuber aliongea, baada ya kumaliza kuongea Kamishna wa kanda maalum alinyoosha mkono akiashiria ana wazo.
"Ndiyo kamishna Wilfred" Rais Zuber alimruhusu aongee, Kamishna Wilfred alisimama akatoa saluti kwa watu waliomo humo ndani kuonesha heshima kisha akajikohoza ili kuweka sawa njia yake ipitayo shingo apate kuongea kwa ufasaha
"Mheshimiwa rais pamoja na wakuu mbalimbali mliopo humu napenda nitoe maelezo ytafuatayo, undani wa matukio haya ni malipizo ya kisasi baada ya kutokea matatizo mbalimbali ya kidini ndani ya jiji hili ambayo yalianzia Yombo kwa kusababisha mauaji ya watu kadhaa. Kimtazamo wangu naona baadhi ya watu walikuwa hawajiridhika na sabau hiyo ndiyo maana wakaanza kumuua askofu wa kanisa la KKKT kwani chanzo cha ugomvi kule Yombo ilikuwa ni mzee wa kanisa la KKKT, hivyo basi kutokana na kuuawa kwa askofu huyo waumini wachache waliokuwa na hasira naona ndiyo wakafanya mauaji kwa mufti wa jiji hili. Mheshimiwa rais suala hili litafikia tamati na amani itarudi ikiwa tu tutawaita viongozi wa dini zote na kukaa nao meza moja kisha tusuluhishe suala hili na si vinginevyo, wao ndiyo wana uwezo wa kuwatuliza waumini wao tu. Ni hayo tu mheshimiwa" Kamishna Wilfred aliongea
"Asante kamishna, naam ACP John ongea" Rais Zuber alishukuru mchango wa Kamishna Wilfred kisha akamruhusu kamishna msaidizi wa polisi ACP John Faustin aongee, ACP John alisimama akapiga saluti kwa wote kisha akawatazama kila mmoja aliyekuwemo humo ndani halafu akarudisha macho yake kwa rais Zuber Ameir.
"Mheshimiwa rais mimi sikubaliani kabisa na mawazo ya kamishna Wilfred kwa kwasababu" ACP John aliongea kisha akaweka kituo halafu akaendelea, "hii ni mbinu ambayo inatumiwa na kikundi fulani cha watu katika kuhakikisha amani inatoweka ndani ya Tanzania na wao waweze kufanya kazi yao wanayoijua wao, hivyo basi tusihadaike na mpango wa watu wachache tu inabidi tutumie mbinu za ziada katika kuhakikisha hawa watu wanatiwa nguvuni halafu ndiyo hao viongozi hao wa dini waitwe waeleweshwe na pia wawaeleweshe watu wao tutakuwa tumefanikiwa vinginevyo nchi itavurugika".
Makamishana wote pamoja na IGP waliposikia kauli hiyo waliinga mkono kwa pamoja ingawa mmoja alikuwa akiiunga mkono kwa shingo upande, walipoulizwa wengine kama walikuwa na la zida bgaada ya kauli hiyo wote kwa pamoja walikataa kuwa hakuyna mwenye la ziada.
"Nafikiri ACP John amemaliza kila kitu sasa kilichobaki ni utekelezaji tu, naomba timu nzima ya CID iiingie kazini kuanzi muda huu tuokoe janga amblo litaikumba nchi yetu, kazi ianze mara moja na kabla mwezi huu haujaisha watuhumiwa wote wawe mikononi mwa vyombo vya dola,uzembe wowote mtawajibishwa. Sina la ziada" Rais Zuber alitoa amri kisha akaondoka eneo hilo bila hata kuongeza neno jingine la ziada.
Alitoka katika chumba cha mkutano ndani ya ikulu akaingia katika ofisi yake ya ambapo akakutana na ugeni wa ghafla sana ndani ya ofisi hiyo, katika kiti cha upande wa pili wanachokaa waqeni alimkuta Moses akiwa amekaa akimsubiri na hakuelewa alikuwa kaingia muda gani humo ofisini.
"Moses vipi mbona ghafla?" Rais Zuber aliuliza
"kwasababu nimekumbwa na ughafla" Moses alijibu.
"ongea nikuelewe basi" Rais Zuber alimuambia
"Mkuu tambua kuna mbwa mwitu kati ya kondoo wote uliokuwa nao sasa jambo hili usimuamini mtu" Moses aliongea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"unasema?!" Rais Zuber aliuliza kwa mshangao sana.
"Ni mapema sana kujua ya jioni wakati ndiyo kwanza jua linachomoza, subiri hiyo jioni ifike ndiyo ya jioni utayajua. Suala lipo mkononi mwangu utalielewa zaidi" Moses aliopngea kisha akatoka ndani ya ofisi hiyo ya rais, rais Zuber hakutaka kumuuliza neno kwani alimtambua fika katika hatua kama hiyo Moses huwa hafafanui jambo hadi likamilike ndiyo hutoi ufanunuzi wote.
****
Majira ya saa nne asubuhi ofisi ya Norbert anayoitumia kama muandishi wa habari ilipata ugeni ambao ulikuwa wa ghafla sana ambao hakuutarajia kabisa,majira hayo ilikuwa ni muda ambao katibu mkhtasi wake alikuwa ameenda kupata kifungua kinywa akamuacha Norbert akiwa ofisini akimalizia kazi ambazo hakuwa amezimalizia siku iliyopita. Mlango wa ofisi yake uligongwa mara mbili kisha mgongaji akatulia, Norbert alimruhusu mgongaji huyo huku macho yake yakiwa yapo makini kwenye tarakilishi yake akiwa hajamjua aliyekuwa anangonga mlango huo alikuwa nani. Alipoinua macho yake alikutana uso kwa uso na mzee wa takribani miaka hamsini akiwa amevaa suti nadhifu sana na akiwa amebeba mkongoja mrefu ambao hupendwa sana kubebwa na matajiri, mkono mwingine mzee huyo alikuwa na mkoba wa kufungwa kwa namba.
"Karibu mzee wangu" Norbert alimkaribisha mzee huyo huku akimsanifu mwili wake na muonekano wake jinsi ulivyo na hapo akabaini alikuwa na alama atofauti na watu wengine wa kawaida ambayo wanayo.
"Asante kijana mimi si mkaaji ila nimekuja kukupa ujumbe tu ambao utapata bahati tu ya kuuona" Mzee huyo aliongea kisha akawa anaunyanyua mkongoja wake juu kidogo, Norbert alikuwa akimtazama huku akijizungusha kwenye kiti chake cha matairi alichokuwa amekikalia.
"ndiyo mzee wangu nakusikiliza" Norbert aliongea huku akili ikiwa imeweka utulivu wa hali ya juu na macho yake yote yakiwa yapo katika mkono wa mzee huyo.
Kwa wepesi wa hali ya juu yule mzee alipigiza sehemu ya chini ya mkongojo wake katika marumaru zilizopo ofisini hapo, fito za fimbo hiyo ziligawanyika zikaanguka na ndani yake kikaonekana kisu kikali sana. Mzee huyo alifanya wepesi mwingine katika kukipeleka kile kisu usawa wa eneo alilokaa Norbert lakini aliambulia patupu baada ya Norbert kujisukuma na kiti cha matairi akaeleka pembeni kisha akapiga sakarakasi akatua upande aliokuwa amesimama yule mzee. Yule mzee naye hakubaki nyuma aliendela kumletea mashambhulizi ya panga Norbert kila upande anaoenda na ikawa ni kazi ya ziada kwa Norbert kuanza kukwepa mapanga hayo kwa umakini wa hali ya juu na alipoona mzee huyo kazidi kushambulia aliruka sarakasi nyingine akarudi kule alipokuwa kisha akalegeza vigungo vya shati lake akasimama kimakabiliano.
"Ninja" Yule mzee alisema na Norbert akamtazama kwa tabsamu lisiloonesha furaha, yule mzee aliiruka meza kwa sarakasi akapambane na Norbert ana kwa ana lakini Sarakasi aliyoipiga alipotua mitaa kadhaa toka Norbert alipo alijikuta akianguka chini moja kwa moja baada ya kuhisi kitu kikitoboa kifua chake, alipoangalia eneo alilotobolewa alikuta kitu chenye rangi ya dhahabu ambacho kinafanana kwa kila kitu na vifungo vya Norbert.
"Ulidhani sina silaha siyo,sasa pata dose ya kifungo changu hicho" Norbert aliongea huku akimuonesha yule mzee sehemu ya shati ambacho kifungo hamna,alikuwa ametobolewa na moja ya silaha hatari ambazo hukaa kama kifungo katika mashati ya majasusi kwa ajili ya tahadhari. Yule mzee alikichomoa kile kifungo ambacho kilikuwa na ncha kali sana, ukungu ulitanda kwenye macho ya mzee huyo na hatimaye kiza kikatanda kabisa.
"Pongezi sana kwako nafikiri umejileta unieleze kile nilichokuwa sikijui" Norbert alimuambia yule mzee kwa dharau na hakujali kuwa yule mzee tayari alikuwa ameshatokwa na fahamu kutokana na kuchomwa na kile kifungo ambacho ni silaha ya kijasusi, sumu kali iliyokuwa ipo ndani ya kifungo hicho ilitosha kabisa kumpa usingizi mzee huyo ambao ndiyo sasa ameuanza. Norbert alimtazama mzee huyo kwa mara nyingine kisha akamsonya halafu akamsogelea hadi pale alipo akampekua kila mahali katika nguo alizovaa na sehemu mbalimbali za mwili wake, aliitoa simu ya mkononi ya yule mzee na hakuwa na kingine cha ziada zaidi ya hiko.
Aliamua kuufuata ule mkoba aliokuja nao yule mzee akautazama sehemu ya kufunga kwa namba halafu akajaribu kuingiza namba za kuufungua ule mkoba lakini ikashindikana, alisonya kwa nguvu kisha akasogeza meza yake anayotumia ofisini humo na akafungua sehemu ya marumaru ambayo ilikuwa ina sehemu ya kubonyeza ambayo aliibonyeza mara moja kisha akasubiri. Eneo la marumaru liliachana na kupelekea kuonekana na shimo lenye ngazi zinazoenda chini ya ardhi, Norbert alimbeba yule mzee akaingia naye humo ndani ya shimo akaenda kumfunga kwenye kiti cha chuma kilichopo humo ndani ya shimo halafu akarudi akafunga ule mfuniko akarudisha meza mahali ilipokuwa awali.
Alirudi akaketi kwenye kiti kisha akauchukua ule mkoba wa yule mzee kwa mara nyingine ili aufungue kwa njia isiyo rasmi baada ya ile rasmi kutofanya juhudi zozote, alichukua chuma akaupinda mkoba huo ili aufungue lakini alikutana na kitu tofauti na alivyotarajia baada ya ule mkoba kufunguka kwa uwazi mdogo tu. Gesi nzito ilitoka ndaniya mkoba ule kwa ghafla ambayo ilivamia pua zake papo hapo na kumfanya akohoe autupe ule mkobe pembeni, alikohoa kwa nguvu na kisha nguvu taratibu zikaanza kumuishia na mwisho wake na yeye akaanguka chini.
Ukungu mzito taratibu ulianza kutanda kwenye macho yake na alipolazimisha kufungua haikuwezekana kwa yeye kuweza kuona kama alivyokuwa anaona hapo awali, alijaribhu kusimama lakini ikashindikana na akaanguka chini mwili mzima ukaanza kuishiwa nguvu zaidi na akawa hawezi hata kunyanyua mkono wake. Muda huo aliweza kusikia mlango wa ofisi yake unafunguliwa kisha sauti za viatu vikikanyaga chini zikasikika kwa mbali lakini muda huo hakuweza tena kufanya chochote, giza zito lilianza kutanda kwenye macho yake kwa taratibu na hakusikia kitu kinmgine chochote kilichoendelea baada ya hapo.
Kulowana kwa uso wake ndiyo kuliweza kumuamsha kwa nyingine na akajikuta kwenye mazingira tofauti na aliyokuwa awali wakati anapambana na mzee,alikuwa amemwagiwa maji na mtu ambaye hakumuona. Mazingira ya eneo alilokuwepo baada ya kuamka yalizidi kumshangaza sana, yalikuwa ni mazingira yaliyojaa giza nene sana ambayo hakuweza kuyatambua kwa mara moja yalikuwa ni ndani ya eneo gani. Maumivu ya sehemu ya mwanzo wa viganja vyake kwa kila mkono ndiyo aliyoanza kuyasikia yakimletea fujo sana.
Alifumbua macho akaangaza sehemu ya mkono wake ambayo inatoka maumivu hayo akabaini alikuwa amefungwa kamba ngumu ambayo ilikuwa imefungwa katika vyuma viwili vilivyopo kila upande ndani ya eneo alilopo, alipoangalia chini kwenye miguu yake alibaini napo alikuwa amefungwa kamba ngumu ambazo zilikuwa zimefungwa kwenye vyuma upande wa kushoto na kulia kama ilivyo mikono yake. Kwa mara nyingine alimwagiwa maji kisha mjeledi mzito ukatua mgongoni mwake ambao ulimletea maumivu sana baada ya kuichana ngozi yake, hakuweza kumuona aliyekuwa anamfanyia hivyo kutokana na uwepo wa taa moja tu iliyokuwa ikimmulika zaidi usoni mwake kwa muda huo.
"Norbert Kaila karibu kwenye himaya ya Panthers" Sauti kutoka kwenye spika iliyopo mahali hapo ilisikika vyema ikapenya vizuri kwenye masikio yake kisha taa yenye mwanga mkali ikawaka papo ikamulika uso wa Norbert, taa hiyo yenye kuumiza macho ilimfanya Norbert afumbe macho papo hapo na akainamisha macho yake chini lakini alijikuta akiinua macho yake juu baada ya mjeledi mwingine kutua kwenye mgongo wake.
"Huwezi kutoka kutoka nje ya mawindo ya Panthers hata siku moja Kaila, jicho la Panther lilikuwa lipo karibu na wewe katika kila hatua yako. Ha! Ha! Ha! Ha! Finaly upo ndani ya mikono ya Panthers, you know what ulitakiwa ufe mapema kwa sumu ya Quantanise kama alivyokufa Bishop Edson na Muft Abdullatwiif lakini kwakuwa una jambo tunalolihitaji inabidi sasa ulieleze kabla ya kufa kwako. Ha! Ha! Ha! Ha! Welcome in the Cats kingdom feel at home Norbert" Sauti iliyosikika kutoka ndani ya spika ambazo Norbert hakujua ni eneo gani zilipo ilizidi kumkebehi na alipogeuza shingo kutazama kila upande ajue ni wapi inapotokea hakuambulia chochote zaidi ya giza tu na taa kubwa ilikuwa ikimulika eneo lile alilokuwepo yeye tu.
"Who are you? kama ni mwanaume kweli jitokeze, wanawake ndiyo wanajificha kutokana n auoga na aibu lakini mwanaume kamili anajitokeza wewe" Norbert aliongea kwa jazba yenye lengo maalum baada ya kusikia sauti ya aliyekuwa anamkera huku akiwa hamuoni mhusika, baada ya kuongea maneno hayo taa zote ziliwaka katika eneo hilo na kulifanya eneo zima lionekane vizuri kwa Norbert.
Alijiona yupo ndani ya ghala kubwa la kuhifadhia bidhaa ambalo hakujua ni ghala gani, sehemu ya ghala hiyo ilikuwa ipo chini na iliyojichimbiwa ikiwa na ngazi maalum zilizoenda juu ambapo kulikuwa kuna korido ndefu kama ya kibarza cha ghorofa ikiwa imeznguka eneo lote alilokuwepo hapo chini. Juu kwenye hicho kibaraza ndiyo kulikuwa na milango sita ya kuingilia humo ndani ya ghala kabla hujashuka ngazi kwenda chini, vile vyuma viwili vilivyoifungwa kamba ambayo ilienda kufungwa kwenye mikono na miguu yake alibaini ni greda ndogo mbili ambazo hutumika sana kwenda kubeba mizigo midogo bandarini ambazo mbele huwa na vyuma vidogo vilivyopangana kama chaga.
Alipogeuza macho upande wa mbele yake aliona kundi la watu sita wakiwa wamevaa mavazi na vinyago usoni kama wanyama, wawili kati yao walikuwa wamevaa vinyago vinavyofanana na vya chui mweusi anayeitwa Panther kwa kingereza na wanne waliosalia walikuwa wamevaa vinyago vinavyofanana na chui wa kawaida ambavyo viliwakaa vyema katika nyuso zao. Mmoja kati ya wale waliovaa vinyago vya chui wa kawaida alikuwa ni mwanamke ambaye aliweza kumtambua kutokana na umbile la kike alilonalo tena lenye mvuto ambalo lilionekana baada ya kuwa amevaa suruali iliyombana yenye rangi ya madoa kama chui.
"Tumejitokeza sasa shida yako si kutuona tu haya sasa tupo hapa, we are Cats kingdom na wewe ni windo letu. You know what is next Kaila ukikamatwa na wanyama jamii ya paka kama sisi, ni kugeuzwa chakula chao tu. Au Panther nimekosea" Mmoja kati ya wale waliovaa vinyago vya chui mweusi aliongea kisha akamtazama mwenzake akamuuliza juu ya kauli yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Uko sahihi Panther mwenzangu lakini kabla ya kumgeuza chakula chetu inabidi atuambie ni wapi alipompeleka Lion tuliyemtuma aje kutembelea ofisi yake" Mwenzake alimjibu kisha wote kwa pamoja wakamsogelea Norbert karibu zaidi wakiwaacha wale waliovaa vinyago vya chui wa kawaida nyuma, walipomfikia walimtazama kwa muda wa sekunde kadhaa kisha wakatazamana wao wenyewe wakapeana ishara. Mmoja aliongea,"Kaila you know what kifo ni haki yako mbele ya Panthers hakuna anayeweza kupona kabisa but you have option, kufa kwa kistarabu au upasuliwe kwa hizo greda ulizofungiwa zikikuvuta mikono na miguu kwa kila upande zikuchane kabisa. Pia utakufa kisrtarabu tu ikiwa utaweza kutuambia ni wapi ulipomuweka Lion alipovamia ofisi yako, nina uhakika ulimtia mikononi ukambana kabla hawa Leopards hawajafika ofisini kwako na kukuokota. So tell me where is he?".
Maneno hayo Norbert aliyasikia vizuri yakipenya katika masikio lakini alikaa kimya makusudi kutokana na jeuri aliyonayo kisha akasonya huku akiwatazama wale Panthers, jambo hilo lilionekana kuwakera sana wale Panthers ingawa walicheka kwa nguvu sana kisha wakamtazama Norbert halafu wakisikitika.
"Nafikri hujajua kwamba sisi huwa hatutanii tukiongea jambo, ngoja tukuoneshe demo kidogo I hope utasema mwenyewe" Panther mmoja aliongea kisha akawaonesha ishara wale wengine wanne waliovaa mavazi yanayowafananisha na chui wa kawaida, wawili kati yao waliingia kwenye magreda ambayo Norbert alikuwa amefungiwa kisha wakayawasha. Kuwashwa kwa magreda hayo hakukumtisha Norbertna ndiyo kwanza aliwatukana matusi makubwa kwa jeuri, kitendo hicho kiliwakera sana Panthers na waliwaamuru wale wayarudishe magreda hayo nyuma wammalize Norbert moja kwa moja.
Magreda yaliaanza kutembea kwa taratibu yakivuta miguu na mikono ya Norbert kwa upande wa kulia na kushoto hadi Norbert akaanza kufumba macho kwa maumivu, maumivu yalipozidi Noebert alipiga kelele kwa maumivu na hapo ndipo hali ya usalama kwa watu waliomshikilia Norbert ikabadilika papo hapo na ikawafanya wote waruke pembeni kujificha kwa kila mtu upande wake.
Mlipuko mzito ulitokea upande wa juu sehemu yenye milango ya kuingilia humo ndani na milango yote sita ilirushwa kwa ndani ikaaanguka hapo walipo, moshi mzito ulitanda eneo hilo hilo huku milio ya bunduki ikaanza kusikika ikivuma humo. Si Panthers wala Leopards aliyeweza kusalia eneo hilo wote kwa pamoja walijibana katika sehemu wanazohisi ni salama kwao ili waweze kujilinda, milio ya risasi ilirindima karibia dakika tatu na ilipokoma kurindima ilisikika sauti ya bunduki isiyo na risasi ikilia baada ya kubonyezwa sehemu ya kupiga risasi.
Taratibu moshi mzito uliokuwa umetanda eneo hilo ulianza kupungua na hatimaye ukaondoka kabisa, eneo alilofungwa Norbert hakuwepo zaidi ya kuwepo kamba ngumu alizokuwa amefungwa. Wale Leopards wawili waliokuwa wanayaongozwa magreda ili yamuue Norbert wote pamoja walionekana wakiwa wamechomwa visu shingoni mwao, Panthers na Leopards walipotazama juu kwenye milango ya kuingilia ndiyo walichoka zaidi kwani hawakuona dalili yoyote ya uwepo wa watu waliokuwa wanapiga risasi zaidi tu ya kuona milango ikiwa imevunjwa kwa mlipuko.
Eneo walilosimama halikuwa na hata ganda moja la risasi kuashiria kwamba kulikuwa kunatupwa risasi, haikuwezekana kwa milio ya bunduki za kivita isikikike halafu kusiwe na dalili ya uwepo wa maganda ya risasi eneo.
"Damn! Tumezidiwa akili sasa hebu Leopards nendeni juu mkaangalie zaidi" Panther mmoja aliongea kea hasira huku akirusha ngumi hewani kutokana na kuzidiwa ujanja na mtu ambaye hakujulikana alifika eneo hilo saa ngapi, Leopards walipanda juu haraka na walirejea wakiwa wameshika bunduki nne ambazo mbili zilikuwa AK47 na mbili nyingine zilikuwa ni SMG T-56.
"Boss zilikuwa zimefungwa kamba kwenye trigger zake kwa kila bunduki na hazina dalili ya uwepo wa risasi zaidi ya magazine zake kuwa na dalili ya uwepo wa baruti tu" Leopard mmoja aliongea.
"Oooh! Shit" Panthers kwa pamoja walisema kwa hasira baada ya kubaini walikuwa wamezidiwa akili na mtu ambaye hawakumjua ni nani.
ILIVYOKUWA
Kutokana na mapenzi mazito aliyonayo Norene kwa Norbert na kukaa siku nyingi bila kumuona na hata akafaidi siku moja tu akiwa naye, moyo wake haukuridhia kabisa na akatamani kukaa naye kwa siku ya pili lakini majukumu yalikuwa yamemzonga Norbert hivyo akaondoka asubuhi kwenda kwenye mihangaiko.Hamu ya Norene ya kukaa naye siku nzima ilipozidi aliona hamna jinsi, aliamua kumfuata kazini kwake ili walau akakae naye kidogo kutokana na kuwa na hamu naye sana.
Alitoka asubuhi akimpeleka Jerry kwa dada yake halafu akaelekea ofisini kwa Norbert akitumia usafiri wake binafsi.
Alipofika jirani kabisa na ofisi ya Norbert tayari ilikuwa ni saa nne na aliamua apate kifungua kinywa kwenye mgahawa uliopo jirani na ofisi ya Norbert kwanza halafu akimaliza ndiyo aingie kwenye ofisi ya Norbert, eneo alilokaa kwenye mgahawa huo lilikuwa likitazamana na ofisi ya Norbert kwa upande wa pili wa barabara. Wakati anaingia yule mzee ofisini kwa Norbert tayari alikuwa ameshamuona na kilipopita kipindi kifupi cha muda toyota hiace inayotumika kubeba wagonjwa ilikuja kuegeshwa jirani na mlango ya ofisi ya Norbert, Norene tayari alikuwa ameiona kila kitu.
Norene hapo alihisi kuna kitu kisicho cha kawaida kinachotaka kutendeka baada ya kuiona hiyo gari, kifungua kinywa chote hakikuwa na maana kwake na alikiacha hapohapo akaanza kutembea kwa umakini huku macho yakiwa makini sana kuangalia pale kwenye lango la ofisi ya Norbert. Wasiwasi ulimzidi zaidi alipishuhudia Norbert akitolewa ndani akiwa amelazwa kwenye kitanda cha Magurudumu akiwa amefungiwa dripu kwenye mkono wake, moyo wake ulipiga kwa nguvu kwa kitendo hicho lakini nafsi yake ikamsihi atulie aangalie kila kitu. Norbert aliingizwa kwenye gari ile na milango ya gari ile na milango ikafungwa hapohapo, ving'ora vya gari hilo la wagonjwa vilianza kusikika na gari hiyo ikaanza kuingia barabarani kwa kasi.
Kusikika kwa ving'ora hivyo kulimpa utambuzi mwingine Norene kuhusu gari hilo, alijiuliza kwanini gari hilo la wagonjwa lisije likiwa linapiga king'ora mahali hapo na lije kimyakimya tu tena kwa mwendo wa kawaida. Kwanini halikuonesha dalili yoyote ya kuwahi kumchukua mgonjwa wakati linakuja, maswali hayo yaliamsha akili ya Norene kwa ghafla na hisia juu ya uwepo jambo jingine tofauti.
Hakutaka kupoteza kwa haraka sana alikimbia eneo aliloegesha gari lake akaingia akaliwasha na akaingia barabarani akawa anaenda kwa mwendo wa kasi aliwahi lile gari la wagonjwa, alikuja kulikuta gari hilo la wagonjwa katika barabara ya Bibi titi likijiandaa kuingia kwenye barabara ya Morogoro. Gari hilo lilipoingia kwenye barabara ya Morogoro bado alikuwa nalo yupo kwa nyuma na alikuwa anaenda nalo kwa kasi sambamba akionekana alitumia njia hiyo ili awahi aepuke foleni ya barabarani, gari hilo la wagonjwa lilipofika makutano ya barabara ya Fire lilinyoosha moja kwa moja likiwa na mwendo ule ule.
Norene alilifuatilia lile gari hadi linapita Magomeni, Manzese, Ubungo, Kimara na hadi linafika Mbezi bila kujulikana kama analifuatilia, gari hilo lilipofika Mbezi Kibanda cha Mkaa kweye kituo cha daladala lilizima king'ora likakata kona kuingia kona kushoto likawa linaelekea barabara ipitayo jirani na kanisa la kiluteri la Mbezi Louis. Aliendelea kulifuatilia gari hilo hadi linafika tasisi ya Agape ambapo liliendelea mbele kwa mwendo mfupi kisha likatakata kuingia kulia mahali kwenye geti kubwa liloandikwa Northern brothers warehouse, Norene alipofikia eneo hilo alisimamisha gari kwa mbali kidogo ambapo aliliona hilo gari likiingia ndani ya ghala hiyo baada ya lango kufunguliwa.
Baada ya kuona mahali ambapo gari hilo lilikuwa limeingia Norene alitoa simu akampigia Moses lakini simu iliita bila kupokelewa, alipiga usukani wa gari kwa hasira kisha akageuza gari akaondoka.
Alirejea majira ya jioni akiwa amevaa nguo za kimazoezi na mgongoni akiwa na begi kubwa sana, aliegesha gari lake mbali na eneo la ghala hilo kisha akashuka akapita njia za mkato akatokea mahali ulipo uzio wa nyuma wa ghala hilo. Norene alitazama pande zote za uzio wa ghala hiyo kisha akafungua begi kubwa alilokuja nalo akatoa vitu viwili mithili ya soksi nzito ambavyo aliviva mikononi akaanza kupanda ukutani akiwa amelivaa begi lake mgongoni, alipofika juu kabisa ya uzio huo aliangalia pande zote alipojihakikishia usalama alishuka taratibu kuingia ndani akatokea sehemu yenye magari makubwa mengi.
Alitembea kwa kunyata hadi kilipo chumba cha walinzi wa ghala hiyo ambapo kulijaa kila aina ya kelele kutoka kwa walinzi hao wakionesha walikuwa wakifurahia jambo, Norene hapo aliamua kufungua begi lake akatoa chupa inayofanana na ya manukato ambayo ni sumu inayolaza mtu kwa masaa mengi akaifungua huku akiwa amejiziba mdomo na pua halafu akaitupa ndani ya chumba hicho kwa kupitia upenyo wa dirishani.
Ndani ya sekunde kadhaa watu hao walikuwa kimya kabisa, alipomaliza sehemu hiyo ya walinzi ndipo akaingia ndani akashuka hadi chini sehemu aliyofungwa Norbert. Alishuhudia kila kitu akiwa amejibana sehemu yenye dirisha dogo na akaona uwezekano wa kumuokoa Norbert upo ikiwa atatumia akili nyingi kuliko nguvu, alifikiria kwa sekunde kadhaa ndipo akapata mbinu ya kwenda kumkomboa mwanaume anayempenda.
Alifungua begi lake akachukua mabomu madogo yenye rimoti ambayo aliyatega kwenye kila mlango wa kuingilia eneo alilofungwa Norbert halafu akachukua bunduki nne zenye baruti ndani akazielekeza kwenye milango hiyo zikiwa kwa umbali wa mitaa kadhaa akiwa amezifunga kamba moja sehemu yenye kifyatulio cha risasi, alichukua visu viwili akavichomeka kiunoni pamoja na mabomu mawili ya machozi akayashika mkononi.
Panther alipoamuru magreda yamchane Norbert na ukelele wa mamumivu uliotoka kwa Norbert ambao ulimfanya Norene na yeye aumie kwa jinsi anavyompenda Norbert, hapo ndipo alipominya rimoti mabomu yote aliyoyatega kwenye milango hiyo yakalipuka yakalipuka yakavunja milango. Norene aliyatoa mabomu ya machozi ufunguo wake kisha akayatupa kule chini walipo, Moshi mzito ulitanda ambao uliwafanya Panthers na wenzao waamini kwamba walivamiwa na hivyo wakajibana pembeni kujilinda, Norene alivuta ile kamba aliyoipitisha kwenye vifyatulio vya risasi na kupelekea Panthers na wenzao wazidi kujibana kwani waliamini wamevamiwa na hawakuwa na silaha yoyote ya kujihami kwa muda huo baada ya kusikika milio ya risasi ikirindima.
Norene alivaa kinyago cha kuzuia gesi na aliutumia muda huo kuvamia eneo la chini kwa kasi ajabu akaanza kwa kurusha visu kwa utaalamu wa hali ya juu na kila kisu kilitua katika shingo ya Leopards waliokuwa wakiendesha magreda. Alimfungua Norbert sehemu aliyofungwa kisha kwa kasi ya ajabu akapanda juu ilipo milango, aliondoka na Norbert akiacha zile bunduki zikiendelea kulia na hata mlio ulipoisha tayari alikuwa ameshatoweka eneo hilo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
Panthers walipandwa na hasira wakazidi kulaani mioyo yao kwa kutaka kujihami badala ya kushambulia pale walipowekewa shambulizi hewa lililowafanya wahisi kwamba wamevamiwa kikosi kizito kumbe ilikuwa ni mchezo mdogo wa kiakili uliochezeka hapo ambao uliwazidi kiakili zaidi, laiti kama wangelitumia akili bado muda huo Norbert angekuwa yupo katika mikono yao na Norene aliyekuwa akiwachezea akili kiasi cha kumtorosha Norbert basi angekuwa yupo katika mikono yao hadi muda huo.
Walijiona walikuwa wamefanya uzembe mkubwa sana kwa kuendekeza kujilinda zaidi badala ya kufuata akili zao zilizowafanya wapewe jukumu maalum ambalo linawapa ulaji katika maisha yao, muda huo ndipo fikira za juu ya uhalisia wa Norbert zilikuja ndani ya vichwa vyao hawakuelewa alikuwa ni nani mpaka akombolewe na mtu mwenye ujuzi wa kijasusi zaidi. Walipozidi kufikiria zaidi kuhusu Norbert waliona kama vinyago walivyovivaa usoni vinavyoonesha sura ya chui mweusi vilikuwa vikiwaletea usumbufu katika fikra zao, walivivua wote kwa pamoja kisha wakatazamana bila ya kuambiana kitu chochote kwa sekunde kadhaa halafu wakawatazama Leopards waliobaki wawili ambao nao walivua vinyago vyao na sura zikaonekana.
Hakika mapacha hawa wanaojiita jina la chui mweusi kutokana na kuwa na sifa za huyo chui mweusi wote kwa pamoja waliona kama wametukanwa tusi kubwa sana kwa jinsi walivyochezewa akili, kitendo hicho waliona kama walikuwa wamevuliwa nguo mbele ya hadhara kwa jinsi walivyokuwa na mbinu za hali ya ju hawakufaa kupumbazwa kirahisi namna ile.
"brother we have to find out huyu Norbert ni nani na kamfanya kitu gani Lion, aaaaaargh!" Panther mmoja aliongea huku akimtazama Pacha wake usoni akionekana kuwa na hasira sana.
"Brother poa kidogo tusitumie hasira katika hili kwani tutazidi kuvuliwa nguo zaidi ya hivi tulivyovuliwa,sasa hivi najiona tumebaki na underwear pekee kwa jinsi tulivyofanywa wajinga. Sasa unafikiri tukivuliwa zaidi si itakuwa ni aibu sasa,akili zetu zifanye kazi" Panther wa pili alimtuliza mwenzake kwani hasira zilikuwa zimezidi uwezo wake wa kufikiri, maneno hayo hatimaye yaliweza kuishusha hasira yake na akahema kwa nguvu zaidi.
"Ok brother,plan inayofuata ni ipi?" Panther wa kwanza alimuuliza pacha wake baada ya hasira kumshuka.
"Brother kumbuka samaki hutegwa kwa chambo wala hawezi kutegwa kwa ulimbo, so we have the trap. Leopard Queen atakuambia vizuri, Panther wa pili aliongea kisha akawatazama Leopards waliobaki ambaye mmoja alikuwa ni mwanamke mrembo sana akiwa amesimama kikakamavu akamwambia,"Leopard Queen unaweza ukatuambia ndoano ipo tayari maana samaki yupo karibu sana na chambo asije akala chambo wakati ndoano hamna".
"Ndoano ipo tayari kilichobaki ni kumnasa tu samaki aliyeifuata chambo akitaka kuila tu akijua ndoano hamna" Leopard Queen aliongea na kuwafanya Panthers watabasamu wakiona hawakuwa na haja ya kutia nguvu zaidi. Hawakuwa na zaidi katika mpango huo na kilichobaki ni kuendelea na kazi ile iliyowafanya wapate ulaji wa awali, hasira zao za kuchezewa akili ziliisha papo baada ya kuhakikishiwa mpango namba mbili ulikuwa ukifanya kazi.
Norene baada ya kumkomboa Norbert alitumia usafiri wake kutoweka eneo hilo kwa kasi sana, alienda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Norbert akiwa hana amani ndani ya moyo wake kutokana na hali ya Norbert ilivyokuwa mbaya sana. Alifika nyumbani akiwa salama pasipo kufuatiliwa na mtu yoyote akamuingiza Norbert ndani ya nyumba akaanza kumpa huduma ya kwanza kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kunusurika kupasuliwa na magreda ya kubebea mizigo.
Baada ya kumuhudumia hadi akamaliza ndipo Norene alipokumbuka kwa mara nyingine kumpigia simu Moses kwa mara nyingine baada ya simu yake kutopokelewa kwa mara ya kwanza alipompigia, mara ya pili simu ilipokelewa na Moses mwenyewe na Norene akampa taarifa juu ya hali ya Norbert na kilichompata. Taarifa hiyo ilizimwa na taarifa nyingine kutoka kwa Moses ambayo ilikuwa ni zaidi ya hiyo taarifa aliyoipata, taarifa hiyo ilimfanya Norene aropoke kwa fadhaa sana kutokana na uzito wa taarifa yenyewe ambayo haikuwa ya kawaida kwa Moses.
"sasa sikia wewe upo wapi sasa hizi?......ok njoo Temeke kwa Nor kama umefanikiwa kuwapumbaza kabisa" Norene alimuambia Mosea akionekana kuwa na wahka sana kwani mambo yalikuwa yameanza kuwa mabaya kwa upande wao, alipoikata simu yake ya mkononi aligeuza shingo kumtazama Norbert ambaye alikuwa amezama kwa usingizi mzito muda huo. Norene alimshukuru Mungu sana kwakuweza kufanikisha kumkomboa Norbert, alinyanyua mikono yake pamoja na uso wake juu kama anaomba dua kisha akafanya alama msalaba.
Aliachia tabasamu hafifu akamsogelea Norbert pale alipolala akambusu kwnye paji la uso kwa upendo mkubwa sana halafu akatoka akaelekea sebuleni ili akamsubiri Moses
Baada ya nusu saa Moses alifika nyumbani hapo akiwa anatumia pikipiki, aliiingia ndani akamkuta Norene akiwa amekaa sebuleni akiwa ameshika tamaa la kuvuta fikra akionekana anawaza kitu kingine cha kufanya. Aliketi kwenye kochi kisha akamtazama Norene kwa muda mfupi akaachia tabasamu hafifu sana lililotoka sambamba na kushusha pumzi mithili ya mtu aliyepata faraja hafifu.
"Mchana au usiku upande wenu?" Moses aliuliza
"naona ni alasiri sijui kwako" Norene alijibu kwa kimafumbo kama swali lilivyoulizwa na Moses, mchana uliokuwa unamaanishwa ni mambo yapo vizuri na usiku uliokuwa unamanishwa ni mambo yameharibika. Alipojibu alasiri alimaanisha yanaelekea kuwa mabaya kabisa.
"kwangu yalikuwa jioni ikielekea usiku ila nimepata nusu ya ghafla imekuwa alasiri, vipi jamaa huko wamemkaliaje?" Moses aliongea huku akitabasamu.
"we acha tu yaani tena ni watu wanaojua kazi zao waliomfanyia hivyo, vipi wewe imekuaje" Norene aliongea kisha akamuuliza Moses.
"Dah! Nafikiri mizimu ya babu zangu iliniotesha niwe makini nyumbani kwangu maana special force imeingia na sijui aliiagiza nani maana hata IGP Chulanga amekana hakuagiza kikosi" Moses aliongea halafu akasikitika akaendelea, "yaani nimetumia ujanja wa panya kuwakwepa wale".
"Ila ujanja wa Panya mbaya ikiwa utakutakana na mwenye ujanja wa paka" Norene alisema huku akitabasamu halafu akanyanyuka kwenye kochi akaenda kwenye jokofu akachukua chupa moja ya mvinyo usio na kilevi, akauweka kwenye meza ya inayotumika kula chakula ambayo ipo jirani na jokofu, alienda kwenye kabati la vyombo akarudi na bilauri mbili ambazo alizimimininia mvinyo halafu akarudi sebuleni akiwa amebeba bilauri hizo.
"Kidume mwenzio kapewa kifinyo kidogo na hao Cats kalala" Norene aliongea huku akimpa Mosea bilauri ya mvinyo, Moses aliipokea bilauri hiyo na hakuinywa na badala yake alimnyooshea Norene ambaye alisogeza mdomo wake akapiga funda moja akaachia tabasamu.
"uaminifu hakuna kwa yoyote" Moses alisema huku akitabasamu baada ya Norene kuonja mvinyo aliomletea.
"ni sehemu ya kazi yetu" Norene alisema kisha akaketi kwenye kochi kisha akaendelea kunena, "special forces huwa wanapewa mamlaka na IGP na makamishna na huwa hawaonekani kwa sababu ndogondogo isipokuwa kwa sababu maalum sasa tambua hao kuna kamishna mmojawapo ndiyo katoa mamlaka".
"Hiyo fact kabisa, sasa suala kujiuliza ni wamepewa mamlaka kwa lengo gani?" Moses aliongea
"huenda ile sumu imekuwa matatani" Norene alikisia.
"hiyo sababu nafikiri hawa watu walitaka kuniangamiza mimi wakanikosa au walitaka kumtia nguvuni mke wangu vilevile. Kosa nimempa sumu mwenye kushawishi umuamini kumbe hafai kumuamini, bishop Edson ndiyo chanzo" Moses aliongea.
"ni vyema kwa kulitambua hilo" Sauti ya Norbert ilisikika ikitokea kwenye korido ndefu inayotenganisha vyumba, Norene na Moses walipotazama upande huo walimuona Norbert akija kwa kujikongoja huku akiwa ameachia tabasamu usoni mwake.
Norene aliweka bilauri ya mvinyo haraka akamkimbilia Norbert ili amsaidie katika kutembea lakini Norbert alimzuia na akajikongoja hadi sebuleni akakaa kwenye kochi lililopo mkabala na kochi alilokaa Moses.
"Naona dogo umeanza wizi yaani unakaa unaongea na mali za watu wakati wenyewe tupo vyumbani" Norbert alitumbukiza utani huku akitabasamu na kusababisha wote wacheke.
"akaa babu wee hujanimiliki mpaka uniite mali yako" Norene alibatilisha maneno ya Norbert.
"Alaaa sasa naenda kumiliki nyingine kama ndiyo hivyo" Norbert aliongea akionesha kususa baada ya kusikia hayo maneno ya Norene, maneno hayo yalimfanya Norene anyanyuke sehemu aliyokaa aje kukaa pembeni ya Norbert akionesha hajafurahishwa na maneno hayo na alianza kudeka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Loh! Kumbe unakashifu zimamoto na nyumba inaungua muone vile" Moses alimuumbua Norene baada ya kubatilisha maneno ya Norbert ilihali hajiwezi katika penzi.
"Haya tuachaneni na hayo, Mose kule ofisini kwangu kwenye basement yenye emergence exit nimemuhifadhi kunguru mmoja aliyetumwa kuja kuniua mimi kipanga!" Norbert alimuambia Moses kisha akameza mate kidogo akaendelea, "inabidi ukamchukue upitie mlango wa nyuma na umlete hapa yeye ndiyo atakayetuambia kuhusu wenzake nafikiri umenipata".
Moses alitikisa kichwa kuashiria amekubali kisha akanyanyuka kwa haraka ili akatekeleze kazi aliyopewa, alionekana ni mwenye papara na Norbert alimzuia kwa papara hizo ili asije akaingia kichwakichwa.
"Hey siyo ngumi zako na marehemu Andrew Kabaita unazoenda kuzifuata, jiandae wewe" Norbert alimuambia Moses ambaye alisitisha kuondoka kisha akauliza, "mapambo yapo ya kujiandaa?"
"Kila kitu wewe nenda ukajipambe kwanza" Norbert alimjibu, Moses alipojibiwa hivyo aliifuata korido ndefu iliyompeleka hadi kwenye mlango wa chumba ambacho kilikuwa hakitumiki kabisa.
Alifungua mlango wa chumba hicho akaingia akaenda hadi lilipo kabati la nguo nalo akalifunga ajakutana na mlango mwingine, aliufungua mlango huo akakutana na ngazi ambazo alizifuata akashuka hadi chini akatokea sehemu yenye silaha za kila aina za kijasusi na za wanausalama wa kawaida.
Hakika alikuwa ameingia kwenye chumba chenye mapambo ambayo ndiyo hayo yalikuwa yanazungumziwa na Norbert, alikuwa akimaanisha silaha za kijasusi na hakutaka kuongea kwa uwazi kwani hakuwa na imani na eneo lolote alilopo hata iwe ndani ya nyumba yake. Lugha hiyo ilikuwa ikieleweka kwa wapelelezi wenzake lakini si kwa mtu wa kawaida na ilikuwa ikitumiwa kuficha mtu memwingine yeyote atakayekuwa anasikiliza asijue wanamaanisha nini, ilikuwa ni bora mpango ujulikane kuliko kujulika eneo la siri la silaha ndiyo maana hawakuwa tayari kutoa taarifa za wazi ili wamchanganye mtu.
Moses alipomaliza kujiandaa alitoka humo ndani akiwa amevaa mavazi ya aina nyingine na viatu vya aina nyingine pamoja na kofia aina ya hat nyeusi, urembo wote unaozungumziwa na Norbert tayari ulikuwa ndani ya mwili wake kwa ajili ya usalama.
****
SINZA
Majira ya saa tano za usiku ndiyo muda aliokuwa anatoka Moses nyumbani kwa Norbert ambao kwa upande wa pili ulikuwa ni muda wa kulala kwa walio na uchovu wa kutwa nzima, ilikuwa ni ndani ya mtaa wa Megasiti maeneo ya Sinza katika nyumba ambayo ilikuwa kubwa na ya kifahari ambayo ilitambulika kama nyumba ya mkuu wa majeshi ya anga na nchi kavu nchini Tanzania. Utulivu ndani ya nyumba hiyo ulikuwa upo kama ulivyozoeleka kutokana na kuheshimika sana mwenye nyumba hiyo ambaye anaogopeka sana kutokana na cheo alichonacho halafu yupo katika umri mdogo sana, hakuna mkazi wa Sinza asiyemjua Meja jenerali huyu ambaye amesaidia katika kuufanya mtaa unaoishi uwe na utulivu kupitiliza.
Nyumba hiyo yenye utulivu iliingiwa na dosari ambayo iliufanya utulivu wake uwe katika hali tata baada ya ugeni usio rasmi kuingia katika nyumba hiyo namna isiyo rasmi, ugeni huu wa usiku wenye mambo yanayofanana na rangi ya usiku uliingia katika namna isiyokuwa ya kawaida.
Lilikuwa ni kundi la watu sita wenye mavazi meusi yaliyoandikwa SPECISL FORCE ndiyo lilikuwa limeizuru nyumba ya Meja Jenerali wakiwa na bunduki aina ya UZI zenye kiwambo cha kuzuia pamoja na silaha mbalimbali za hatari, ujio wao ulitanguliwa na umwagaji wa hewa ya sumu iliyowalaza walinzi kisha wote kwa pamoja wakauruka uzio wa nyumba hiyo kwa utaalamu wa juu.
Waliingia kwa kupitia mlango wa nyuma wa nyumba hiyo huku wakinekana kuitambua vilivyo nyumba hiyo kwani wote walielekea kwenye mlango wa chumba kimoja, walifungua mlango wa chumba hicho wakaingia ndani wakakuta kitanda ambacho kilikuwa kimebeba umbile la mtu aliyeonekana amelala kwenye kitanda chake akiwa hana hili wala lile. Watu hao walielekeza silaha zao alipolala huyo mtu, kisha wakamsogelea aliyelala kitandani hapo wakamzunguka kwa ukaribu.
Mmojawao alishusha silaha yake kisha akatoa sindano yenye kimiminika chekundu, aliitoa sindano hiyo kifuniko chake akachoma sehemu ya begani kwa nguvu. Alipotaka kuingiza dawa iliyokuwa kwenye bomba la sindano umeme wa nyumba nzima ulizimika kwa ghafla na kukawa na giza, taa za nje zilizowapa mwangaza watu hao wa kuona ndani sasa ziliwanyima uhuru wote wa kuona vizuri.
Umeme wa humo ndani uliwaka na hadi taa ya humo chumbani iliyokuwa imezimwa iliwaka na hapo kile kikosi kilishangaa kuona walikuwa wameizunguka mito iliwekwa kama mtu kitandani, walibaki wakiwa wameduwaa na hata kabla hawajazinduka kwenye mshangao wao umeme ukazimika tena kisha sauti ya kila mmoja akitoa maumivu ikasikika. Ulipokuja kuwaka kwa mara nyingine kila mmoja alikuwa akishikilia kiganja chake kinachovuja damu kwa maumivu huku silaha zao zikiwa chini, walipotaka kuinama waziokote walishindwa papo hapo kwani walikuwa wameshawahiwa tayari.
"inamisha mgongo tu nimwage ubongo wako" Ilisikika sauti ya kike ikitoka ndani ya kabati huku mkono wenye bastola yenye kiwambo cha kuzuia ikitoka ndani ya kabati, walipoangalia upande inapotoka sauti walimuona Meja Jenerali Belinda aliwa na mavazi ya kulalia yaliyo katika mfumo wa suruali na shati refu mithili ya nusu kanzu akiwa kawanyooshea bunduki.
"nani kawatuma? , sirudii swali mara mbili" Meja Jenerali Belinda aliuliza, swali hilo liliwafanya wote wanyamaze wakawa wanababaika. M.J Belinda hakuuliza lile swali tena na badala yake alimtandika mmoja risasi ya goti akatoa ukelele wa maumivu akawa anataka kukaa chini.
"Weee! Kimya mbona hukupiga kelele wakati unaingia, tena hakuna kukaa simama hivyo hivyo na goti lako" M.J Belinda aliongea kwa sauti ya chini ya ukali baada ya mpinzani wake, mwingine alipuuza agizo la M.J Belinda akainama kwa upesi akijua ataiwahi silaha yake. Alitumia wepesi wake wa kimazoezi katika kuinama akajua ataiwahi bila hata kufikiria kwamba alikuwa akishindana kasi na komandoo ambaye mkononi ana chombo cha moto, kuinama kwake mkono wake ukiwa haujafika hata kwa sentimita kumi kutoka ilipo silaha tayari bastola ya M.J Belinda ilikuwa imeshakohoa tena ikafumua kichwa chake.
"mwingine nani anataka kuiokota silaha yake amfuate mwenzake kuzimu?" M.J Belinda aliuliza kisha akasema, "nimesema sirudii swali nataka jibu sasa hivi, kimya chenu navunja goti la mwingine. Kwanza pigeni mateke silaha zenu mbele".
Hawakuwa na ujanja wote kwa pamoja walizipiga teke silaha zao mbele wakawa wanamtazama M.J Belinda kwa wasiwasi.
Swali hilo walikaa kimya kwa mara ya pili ili wasitoe siri ingawa walikuwa mbele ya mdomo wa bastola, kimya chao kilisababisha bastola ya M.J Belinda ikohoe mara mbili mfululizo akiwa ameielekeza kwenye magoti ya wawili wengine ambao walishindwa kustahimili wakaenda chini moja kwa moja wakabaki wawili waliokuwa hawajajeruhiwa.
Kikosi hicho kilidhamiria kutotoa chochote juu ya mpango huo uliowaleta nyumbani kwa M.J Belinda, kubaki wawili nao walikuwa wajeuri hawakutaka kitu chochote ambacho kingezidi kuwaweka pabaya waliowatuma. Wawili waliobaki nao walionja risasi za goti moja kila mmoja kama ilivyo wenzao lakini hakuna yoyote aliyejaribu kuufungua mdomo, walikuwa wameweka kiburi chao cha kukaa kimya kuliko kuongea kile walichoulizwa. Jeuri ya kufunzwa katika sehemu za hatari ndiyo iliwafanya wasinyanyue midomo yao katika kuongea, M.J Belinda aliwataza tu jinsi wanavyougulia maumivu ya magoti akiwa na tabasamu lisilotangaza furaha yoyote katika uso wake.
"Kwangu mtasema tu si viburi nyinyi mmejileta wenyewe wavamizi" M.J Belinda aliongea kwa hasira sana huku tukio lililomkuta miaka kadhaa iliyopita likirudi ndani ya kichwa na kuzidi kumchanganya kabisa, alipowaona kikosi hicho kinachofanya uvamizi alikumbuka mengi ya miaka iliyopita hasa mauaji ya Simion aliyekuwa mpenzi wake na pia rafiki mkubwa wa Norbert. Tangu afariki huyo mpenzi wake Belinda hakuhitaji kuwa na mwanaume yoyote na alijiapiza hadi anakufa hatakuwa kimahusiano na mwanaume yeyote, macho yake yalipowatazama kwa makini wale vijana ndipo akakumbuka kile kisa cha Unyayo wa simba ambacho Simion alipoteza uhai kwa kumkingia kifua jasusi mwenzake Norbert asipigwe risasi na gaidi Elius katika mpambano wa kumtia nguvuni gaidi huyo.
Hasira za kuuawa kwa mpenzi wake zilimjia kichwani kwa kasi ya ajabu na akajikuta akinyanyua risasi kwa mara nyingine ili awamalize wavamizi waliomkumbusha kifo cha mpenzi wake, alianza kumuelekezea mmoja risasi akaminya sehemu ya kufyatulia risasi lakini bastola ilitoa mlio wa vyuma vyake vinavyosukuma risasi tu kuashiria ilikuwa imeisha risasi. Hasira zake zikazidi zaidi baada ya bastola kuisha risasi ikasaliti adhama yake ya kuwamaliza hao wavamizi, aliitazama bastola yake akiona imemfanyia usaliti mkubwa sana kwa mgomo joto iliyomuwekea. Suala la kuisha risasi halikuwepo ndani ya kichwa zaidi ya kuona amesalitiwa na bastola, hasira za kuwamaliza zilimfanya hata asahau kabisa kama alikuwa ameweka risasi sita tu katika bastola yake baada ya wavamizi kuwa sita ambao aliwaona kipindi wanaingia nyumbani kwake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hasira zake zilikuwa zimeonwa kama ni njia pekee kwa wale wavamizi wake waweze kupambana naye, wavamizi wawili kwa kasi ya ajabu walisimama kwa mguu mmoja wakiwa na wazo tu la kujirusha mahali zilipo silaha zao baada ya kuzipiga mateke kutokana na kuamriwa na M.J Belinda wafanye hivyo.
Fikra zao zilizotoka katika halmashauri ya ubongo ziliona ni jambo la zuri kufanya hivyo ili wapambane, lilikuwa ni jambo ambalo lilikuwa ni kosa kubwa kulifanya kwani lilirudisha mahala pake kile kilichokuwa kimetoka.
Kitendo cha wao kusimama kwa ghafla tayari walikuwa wameshaurudisha umakini wa M.J Belinda uliokuwa umetoweka hapo awali kutokana na kutawaliwa na hasira kupitiliza, walipojirusha kufuata silaha zao M.J Belinda tayari alishajua lengo lao naye alijirusha kwa mateke mawili ambayo yaliwapata wavamizi wake kutoka Special force kwenye vifua vyao wakarudi walipotoka.
M.J Belinda hakuishia hapo aliendelea kuwapa kipigo kizito wale wavamizi mmoja baada ya mmoja hadi wakapoteza fahamu wote wakiwa na majeraha mbalimbali katika miili yao.
"mkiamka mtasema wenyewe" M.J Belinda aliongea huku akihema kwa nguvu baada ya kumaliza kugawa kipigo.
****
Muda ambao vijana wavamizi wa special force wanaingia matatani nyumbani kwa M.J Belinda ndiyo muda ambao Moses aliwasili ofisini kwa Norbert akiwa na mapambo yake aliyojipamba katika nguo alizovaa, alitumia mlango wa nyuma ambao ulimpeleka moja kwa moja hadi kwenye chumba kilichokuwa kikifungwa kwa namba maalum. Moses aliingiza namba hizo za kufungua huo mlango ambao ulifunguka na akaingia ndani ya chumba chenye giza nene ambapo aliwasha taa kisha akabonyeza kitufe kilichopo ukutani mlango alioingia nao ukajifunga.
Chumba chenye ukubwa wa wastani ndiyo kilionekana mbele ya macho yake kikiwa kina kabati moja pamoja na kiti ambacho hutumika katika kutesa watu. Kiti hicho kilikuwa kimefungwa yule mzee maarufu kama Lion aliyekuwa akipigana na Norbert ambaye muda huo tayari alikuwa amerudiwa na fahamu akiwa hana nguvu kutokana na sumu hatari iliyomuingia mwilini baada ya kuchomwa na kifungo chaa Norbert, Moses alisimama kwa muda akawa anamtazama Lion halafu akamsogelea karibu zaidi jirani kabisa na kiti alichofungwa.
Muda huo Lion alikuwa ameinamisha kichwa chini kutokana na sumu ya Norbert kumlevya na kumfanya hata ashindwe kuwa na nguvu ya kuinua kichwa chake, Moses alimtazama kisha akampiga kibao cha shavu kilichomfanya ajaribu kuinua kichwa lakini akashindwa kutokana na kuzidiwa sana. Lion alibaki akihena kwa nguvu sana kisha akatukana tusi zito lililosikika kwa sauti ya chini sana ambayo ilieleweka kwa Moses, kibao kingine kilitoka kwenye mikono ya Moses ndiyo kilifuata ambacho kiliacha alama katika shavu la Lion.
"Uzee huo bado unaleta jeuri tu, basi utakuwa mpole tu kwanza pokea hii zawadi yako" Moses aliongea huku akitabasamu akatoa kitambaa cheupe ambacho alimbandika Lion kwenye pua na mdomo wake, alimshikilia kwa nguvu na kitambaa hicho na hatimaye Lion nguvu zikamuishia kabisa akaondokwa na fahamu kwa mara nyingine.
Moses alimfungua kwenye kiti kisha akamshusha chini akajiandaa kumbeba atoke naye humo ndani akijua ilikuwa ni kazi rahisi tofauti alivyodhani kumbe ilikuwa ni kazi ngumu sana. Ugumu uliopo kwenye kazi hiyo hakuwa ameuona na hadi muda huo na alikuja kuuona baada ya kuhisi vumbi likimuangukia kwenye suti aliyovaa. Moses alitazama juu usawa mahali lilipotoka vumbi hilo akahisi kulikuwa kuna kitu kikiendelea huko juu ambapo ndiyo kuna ofisi ya Norbert, kishindo kikubwa kilifuata kikazidi kumfanya Moses akae kwa tahadhari humo ndani kwani hali ya usalama ilishaanza kuwa mbaya.
Aliamua kujibana kwenye pembe ya chumba hicho kisha akazima taa kukawa na giza zito, kwa mara nyingine aliona mfuniko wa chuma unaotokea ofisini kwa Notbert ukiwa mwekundu kisha moto ukaonekana ukiwa unatoboa mfuniko kuuzunguka. Tobo kubwa lilitokea baada ya moto huo wa gesi ya kutoboa vyuma kutoboa mfuniko huo ambao ulimfanya Moses azidi kukaa kwa tahadhari, kurunzi yenye mwanga mkali ikamulika katika eneo alilokuwa amelazwa Lion baada ya Moses kumuacha akabana pembeni kwa tahadhari.
"Yupo humo ndani, mmoja ashuke amfuate aje naye juu wengine tulinde usalama" Ilisikika sauti ya chini ikiongea baada ya Kurunzi kumulika kuonesha kuwa kuna mtu waliyekuwa wanamfuata, sauti hiyo ilikuwa imesikika sawia kwenye masikio ya Moses na hapo akabaini tayari kuna ugeni umekuja kumfuata yule aliyemfuata. Ambao wangeweza hata kumuharibia kazi iliyomleta humo ndani, hakuwa tayari kuona jambo hilo linatokea kwani wangekuwa wamerudi nyuma hatua mbili nyuma badala ya kupiga hatua moja mbele katika kazi yao. Wale watu waliokuwa juu nao walikuwa wameshaanza kumtanguliza mwenzao ili akamchukue Lion, muda huo huo Moses alikuwa akiyakagua mapambo yake aliyojipamba kama yapo sawa ili aweze kuyatumia.
Mtu mwenye mavazi meusi alionekana akishuka kwenye ngazi zilizopo kwenye mfuniko huo na hatimaye akafika hadi chini, alianza kuangaza kwa kutumia kurunzi yake aone mandhari ya humo ndani na hatimaye miale ya kurunzi hiyo ikamulika katika sura ya Moses. Lilikuwa ni jambo asilolitarajia kama humo ndani kutakuwa na mtu mwingine tofauti na yeye, pia lilikuwa ni jambo ambalo hakulitarajia kama humo ndani kutakuwa na mtu mwingine ambaye ni kikwazo katika kazi yao waliyotumwa hapo.
Mshtuko wa ghafla ndiyo ulimkumba papo hapo kutokana na jambo lenyewe kuwa la ghafla, nywele na vinyweleo vyake zilimsisimka baada ya kumuona Moses akiwa eneo hilo tena muda ambao ameiweka silaha yake kwenye kipochi maalum cha kuweka silaha kilichokuwa kipo begani na silaha yake ikiwa inaning'inia kwapani ambapo ni gumu kuitoa bila Moses kumuwahi. Mshutuko aliyoupata ulikuwa siyo wa kawaida kutokana na mavazi nadhifu meusi aliyovaa Moses na utulivu aliokuwa nao Moses baada ya kumuona adui yake ambaye akipatwa na mshtuko mkubwa sana ambao ulimfanya huyo mvamizi aone kuwa alikuwa akitazamana na kiumbe asiyekuwa wa kawaida ambaye muda huo alikuwa anatabasamu tu baada ya miale ya kurunzi kutua katika uso wake.
"hey" Alijikuta akiropoka basda ya kumuona Moses.
Mzubao alioupata ulimfanya hata asahau mbinu nyingine zitakazomuwezesha kutoa silaha kwenye mkoba uliopo kwapani, sauti yake ya kuropoka nayo ilizidi kuufanya moyo wake upige kwa nguvu na kumfanya abaki anaduwaa zaidi.
Hiyo ilikuwa ni hatua pekee kwa Moses katika kumtangulia mpinzani wake huyo kimbinu, hakutaka kuitumia nafsi hiyo vibaya kwani hakuwa na uhakika kama angelipata nafasi nyingine adimu kama hiyo. Kwa wepesi wa ajabu alitoka mahali alipokuwa amejibana akaruka juu akiwa ametanguliza mguu mmoja mbele, mguu huo ulitua sawia kwenye kifua cha mpinzani ambaye alienda chini moja na kurunzi yake ikaruka huku ikiwa inazunguka inapiga miale hovyo ambayo ilimulika juu sehemu yenye mfuniko kulipokuwa na wavamizi wengine.
Muale wa tochi uliomulika juu ulikuwa ni alama tosha kwa wavamizi wengine kujua kwamba mwenzao amekumbwa na kitu cha hatari, tochi ilivyomulika moja kwa moja fikra zao zikajua dhahiri kwamba wenzao amekimbwa na balaa hivyo alihitaji kusaidiwa. Kwa upesi nao wakajiachia ndani ya mfuniko huo kwa umakini sana lakini walikuwa wamefanya kosa moja kubwa sana, hawakutambua kwamba walikuwa wanaingia kwenda kukabiliana na kiumbe asiyekuwa wa kawaida ambaye alikuwa anatumia udhaifu mdogo katika kuwamaliza wapinzani wake.
Pia hawakutambua kuwa udhaifu mdogo ambao adui wao wanayemfuata anaweza kutumia kuwamaliza tayari walikuwa wameuonesha dhahiri walipoingia humo ndani, mbinu kali ya kuingia kwa ghafla katika eneo hilo tayari ilikuwa imemezwa na udhaifu waliokuwa wameingia nao humo ndani ambao haukufaa kuwepo kabisa wakati wanaingia kupambana na adui yao.
Kurunzi walizoingia nazo ndiyo ilikuwa ni udhaifu tosha ambao haikutakiwa kuwepo muda wanaenda kupambana na adui mwepesi sana katika mapigano ambaye yupo humo ndani ya shimo, walipotua tu humo ndani mmoja wao alitoa ukelele wa maumivu kisha akaanguka chini na wote wakaelekeza bsstola zao upande ambao mwenzao alishambuliwa wakapiga risasi lakini waliambulia patupu hawakuona mtu yoyote hsta walipomulika na kurunzi zao.
"Aaaaargh!" Mwenzao mwingine alitoa ukelele wa maumivu akaanguka chini akawa anatupatupa miguu mwisho akatulia, walimulika upande mwingine ambao wanahisi mwenzao alishambuliwa kisha wakapiga risasi lakini napo waliambulia patupu.
Kuchanganyikiwa ndiyo kulivamia vichwa vyao hadi fikra zao zikaenda mbali sana zikawaza mawazo yaliyokuwa potofu kabisa juu ya mtu waliyekuwa wanaapambana naye, hakika waliona walikuwa wakipambana na mzimu ambaye alikuwa haonekani ni wapi alipo. Walikuwa wamebaki wawili tu humo ndani na muda huo walikuwa wanatembea kwa uoga sana, wakijua wamepatikana na wameingia katika himaya ya mzimu.
Mvurugano wa fikra juu ya tukio hilo ulivamia vichwa vyao wakachanganyikiwa hadi wakaharibu kazi iliyowaleta humo ndani bila hata kutarajia kama wangeweza kuiharibu, mmojawapo katika harakati za kutembea alijikuta akimkanyaga Lion akashtuka akamimina risasi katika mwili wa Lion kisha akamulika na kutunzi aone kama kama mpinzani eake tayari risasi zimempata.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ooooh! Damn" Alisema kwa fadhaa baada ya kubaini alikuwa amempiga risasi mtu waliyetumwa waje kumkomboa, alishusha hata silaha yake chini akionekana amekata tamaa kabisa kwa jambo hilo alilolitenda.
Mfadhao uliyompata ulikuwa ni uzembe ambao ulimuweka kwenye hatua nyingine kabisa ambayo hakutakiwa kuwemo kirahisi namna hiyo, kitu chenye ncha kali kilipenya kwenye mkono wake ulioshika silaha na silaha ikaenda chini kisha muda huo huo taa zikawaka kwa ghafla sana. Walichanganyikuwa zaidi baada kuona mwangaza kwa mara ya pili kisha kicheko cha kejeli kikafuata, walipotazama upande ulipo mlango wa kutokea humo ndani walimuona Moses akiwa amesimama amewanyooshea bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti.
"Weka bastola chini na uisukume mbele nilipo" Moses alimuambia yule aliyekuwa bado ana silaha ambaye alikuwa ameishusha baada ya kuchanganywa na jinsi taa zilivyowaka humo ndani, hakuwa na ujanja zaidi ya kutii amri aliyopewa na Moses akaitupa silaha chini kisha akapiga teke.
"nafikiri mmekuja muda muafaka kabisa niliokuwa nawahitaji muje sasa ngoja niwape uturi kidogo muendane na hadhi ya ukaribisho wenu" Moses aliongea kisha akaingiza mkono mfukoni akatoa chupa inayofanana na ya uturi akawarushia kisha akaipiga risasi na hewa ya gesi ikatoka ndani ya chupa hiyo ambayo waliivuta bila kupenda na wakaanza kuishiwa nguvu wakaanguka chini.
Alibaki akitazama kwa dharau jinsi walivyopitiwa na usingizi mzito baada ya kuivuta hewa iliyotoka ndani ya uturi yenye sumu ya kulaza, hewa hiyo kwake haikuwa imemdhuru chochote kutokana na kuwa amepaka dawa inayozuia hewa hiyp isiingie ndani ya mwili wake kupitia puani.
****
Mawasiliano baina ya vikosi vya specilal force na watu waliowatuma yalikuwa yamekatika kwa ghafla, katika chumba cha mawasiliano ndani ya eneo lililotangaza usiri wake kutokana na mandhari yake jinsi ilivyo. Panthers na Leopard pamoja na kijana mwingine wa makamo anayelekea utuzima ndiyo walikuwa wapo kwenye mitambo hiyo wakiwasiliana na vikosi vya special force vilivyopo chini ya amri yao, baada ya kuita kwa muda mrefu wakiwa wameshikilia vifaa vya mawasiliano hatimaye walikata tamaa wakabaki wanatazamana.
"Something is wrong, si kawaida hii" Panther mmoja aliongea.
"ni kweli brother but hatuwezi kuacha kazi yetu iharibike hivihivi tena zaidi ya mara moja kwa siku moja" Panther mwingine aliongea kisha akamtazama yule kijana anayeelekea utuzima akamuuliza,"Kamishna tutumie njia nyingine au tuache?".
"Tumieni tu ila hawa walioshiriki operesheni fagio la chuma iliyomuua binamu yangu na mkuu wetu wasibaki hai, Gawaza,Kaila,Belinda, Kulika hawatakiwi kubaki hai ni sehemu ya hatua ya awali kabla mkubwa zaidi hajingia nchini" Kamishna aliongea kutoa amri ya kutumia njia nyingine kabisa ili wakamilishe mpango wao
"Ok we must kill General Kulika, yeye ndiye kiongozi wa operesheni fagio la chuma kama file lililotupa kazi linavyosema" Panther aliongea kisha akamtazama Kamishna ambaye alitikisa kichwa kukubali, alimgeukia pacha wake kisha akamuambia "Brother no time to waste lets go" Kauli ilimtoka Panther mmoja ambaye kiswahili kilikuwa tabu na huwa anapenda kuchanganya kiswahili na lugha ya wenye ngozi nyeupe waliopata kuitumia ardhi ya bara la mtu mweusi waitakavyo, Panthers hawa walikuwa wanafanana kila kitu ila walitofautiana huo mtindo wa kuomgea ambapo mmoja alikuwa ni mwenye ujuzi katika kiswahili na mwingine alikuwa anakielewa kiswahili lakini si mjuzi katika kukiongea.
"Kamishna nafikiri leo ndiyo siku ya mwisho ya kupumua kwa general Kulika, ufagio wa tindikali sasa unampitia kufagia ufagio wake wa chuma" Panther mwenye uelewa wa kiswahili aliongea.
"nawaamini sana nafikiri kazi yenu itakuwa na mafanikio" Kamishna aliwaambia huku akitabasamu kutokana na uwezo walionao Panthers katika kazi yao, matunda mazuri ya kazi ya Panthers alianza kuisikia harufu yake kwani dalili za kuiva kwa matunda hayo tayari zilianza kuonekana.
Adhma iliyowekwa na wakubwa zake katika umoja wao iliyoonekana kuanza kwenda kombo sasa ilianza kurejea baada ya kuwagiza watu hao wenye uwezo wa hali ya juu ulioendana na sifa ya mnyama waliyejipatia jina lake. Chui mweusi ambaye ni hatari kwa mawindo ya usiku kutokana na rangi yake kumfanya asionekana hata kwenye mwanga hafifu ndiyo sifa kuu hawa mapacha waliojiita jina hilo, Panthers walikuwa ni wapiganaji hatari wakiwa katika maeneo yenye giza ndiyo maana wakapewa jina hilo.
Walijua kulitumia giza vyema katika mapambano tofauti na wapambanaji wa kawaida, tumaini la mafanikio katika kazi yao tayari alikuwa ameshalinusa katika pua yake kutokana na sifa hiyo waliyonayo Panthers. Hadi anabaki na Leopard katika chumba chenye mitambo ya kuongezea mawasiliano, bado tumaini hilo liliendelea kuwa ndani ya kichwa chake baada ya kuona Panthers tayari walikuwa wameondoka.
****
"griiii! Griiii! Griiii!" Mlio wa simu ya mkononi ya kisasa ulisikika ukileta bugudha kwa mpumzikaji aliyekuwa na mwenza wake wakiwa wamejifunika shuka mwili mzima, karaha za mlio wa simu hiyo zilipozidi mkono wa mwanaume ulionekana ukitoka ndani ya shuka hiyo iliyofunika mwili ukaishika simu hiyo simu kisha mkono wa pili ukaonekana ukiifunua shuka hiyo kwa sehemu ya usoni.
Mwanaume huyo aliitazama kioo hicho cha simu kisha akawasha taa ndogo za umeme zilizo katika mfumo wa kandili ambazo huwekwa pembezoni mwa vitanda katika nyumba zilizojengwa kisasa, mwangaza wa taa hiyo uliifanya sura ya mwanaume huyo ionekane dhahiri akiwa yupo kifua wazi.
Mkuu wa majeshi Jenerali Augustin Kulika ndiyo alionekana sura yake kwa dhahiri baada ya mwangaza wa taa hiyo ndogo kufukuza giza lililokuwa likificha sura yake, pembezoni mwake alionekana mke wake ambaye tayari alikuwa ameshaamka baada ya mume wake kuwasha taa.
Jenerali Kulika aliipokea simu hiyo iliyomkatishia starehe zake na akaongea, "Jambooo!...Unasemaa! Ok subiri". Alinyanyuka kitandani hivyo hivyo simu yake ikiwa katika sikio lake la kushoto akawa anauendea mlango, alikuwa akitoka kimya kimya bila hata kumsemesha mke wake jambo lilimfanya mke wake ahisi kulikuwa kuna jambo lisilo la kawaida ambalo lilikuwa limekatisha kupumzika kwake kwa raha na starehe akiwa amelala juu ya kifua cha mume wake.
Aliona ameondolewa raha ya kupumzika na mume wake ambaye ndiyo amerejea kutoka safari ya kikazi nje ya nchi, kitu alichokuwa akikihitaji kwa mume wake alikuwa tayari amekipata lakini muda wa kujilaza na mume wake ndiyo nao aliokuwa anauhitaji ambao umevurugwa na mlio wa simu hiyo iliyoita usiku wa manane akiwa yupo katika usingizi wa raha uliongezwa raha kwa kulala na mume wake kitandani.
"Baba Dorry kuna nini mbona.." Alimuuliza mume wake kwani haikuwa jambo la kawaida kabisa kuongea na simu mbali na yeye katika kipindi cha usiku kama hicho, kuuliza kwake juu ya hali hiyo kulikatishwa na Jenerali Kulika akichelea sauti ya mke isikike kwa mtu aliyekuwa akiongea.
Jenerali Kulika alimuashiria mke wake amsubiri kisha akatoka ndani ya chumba cheke cha kulala mkono wake bado ukiwa umeshikilia simu sikioni mwake, alitembea kwa haraka akifuata korido ndefu hadi zilipo ngazi kisha akawasha taa akateremka ngazi hizo hadi sebuleni kwake akaketi kwenye kochi linalotazamana na mlango wa kuingia sebuleni kutokea nje.
"ndiyo Belinda umesema special forces kutoka police force wamekuvamia nyumbani kwako wakiwa na lengo la kukumaliza...aisee kuna mtu nyuma ya tukio hilo aliyewaagiza hao.....ok ok asubuhi waletwe kambini kwa mahojiano maalum watutajie wahusika wa mchezo kabla hatujawauliza viongozi wa juu wa polisi. Halafu nita" Jenerali Kulika kaa sauti ya chini wakati akimpa maelekezo mwanajeshi wake wa kuaminika aliyepo chini yake kwa vyeo viwili, alipotaka kutoa maelekezo zaidi umeme ulizimika humo ndani.na ukamfanya aseme, "nina wageni tayari nitakupigia simu nikimaliza kikao na wageni wangu wasio na taarifa".
Ukweli wa msemo huo wa mwisho haukumaanisha wageni hata kidogo bali ulimaanisha kuvamiwa, umeme kuzimika ndani ya nyumba haikuwa jambo la kawaida kwani alikuwa akitumia umeme wa mionzi ya jua kwa muda wa usiku na si kutumia umeme wa shirika la umeme ambao muda mwingine hukumbwa na hitilafu na vitu kama hivyo hutokea.
Dalili ya kuvamiwa ndiyo ilikuwa ipo ndani ya kichwa chake, wavamizi wenye uwezo wa hali ya juu ndiyo aliwawaza katika fikra zake kutokana na uwepo wanajeshi wa private wenye jukumu la kulinda nje ya nyumba yake. Kengele ya hatari ndani ya kichwa chake tayari ilikuwa imelia na akajionya nafsini mwake awe makini zaidi kwani hali ya hatari ilielekea kuikumba familia yake, Jenerali Kulika hakutambua kabisa kama kufika kwenye sebule ya nyumba yake tayari alikuwa amefanya kosa kubwa pindi alipokuwa alijiandaa kushusha ngazi za kuja hapo.
Utambuzi wa kosa alilolifanya haukuwepo ndani ya kamati kuu ya fikra katika mwili wake kutokana kuwa na sifa ya wanadamu wa kawaida kutojua lijalo mbele, akili yake ilimtuma apande juu ghorofani kwa tahadhari aende chumbani kwake akachukuae silaha yake aihami familia yake ambayo ilikuwepo huko ghorofani.
Alijiinua kwenye kochi kwa umakini wa hali ya juu akiyalazimisha macho yake kuzoea hilo giza ghafla kisha akawa anaelekea upande ilipo ngazi ya kuelekea ghorofani kwa tahadhari iliyokuwa ikitazamwa na wenye hadhari zaidi, hakuwahi kuzikifikia ngazi za kuelekea ghorofani tayari ngumi nzito ya ilitua kwenye taya lake ikamyumbisha na kumuachia maumivu ambayo aliyapuuzia ili asipoteze umakini katika kupambana Teke zito la kuzunguka lilifuata ambalo halikumpata baada ya kuinama aliposikia mlio wa suruali ya mpigaji teke hilo, teke jingine la mgongo kilifuata alipokuwa yupo kwenye hali ya kuinama ambalo lilitokea upande wa nyuma yake ambalo lilimpeleka chini moja kwa moja.
Jenerali Kulika alibiringita pale chini alipo akasogea kwa umbali wa mitaa takribani mbili kisha akajiinua kwa kufyatuka akakaa sawa akaangalia upande yalipotokea mapigo hayo ambayo tayari yalimpa tangazo kwenye ubongo wake juu ya uwepo wa wapinzani wawili wanaomshambulia, ngumi nyingine ilifuata ambayo aliikwepa aliposikia mlio wa nguo aliyovaa mpigaji na teke jingine likatua juu ya kifua chake likamsukuma nyuma akaanguka kwenye kochi la kukaa watu watatu sebuleni hapo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Pigo jingine la kutumia goti lilikuwa lilifuata ambalo lililengwa kumpata kifuani kwake lakini Jenerali Kulika alijibiringisha kwa upesi akasogea pembeni, mpigaji wa pigo hilo alitua na pigo lake kwenye mito ya kochi na Jenerali Kulika akaachia teke liitwalo ushiro geri kekomi (teke linalopigwa kwa kutumia kisigino) ambalo lililompata kwenye mbavu hadi mguno wa kubana pumzi ukasikika na hapo Jenerali Kulika akabaini mpinzani wake huyo alibana pumzi kwa nguvu ili kuzuia teke hilo lisimvunje mbavu.
Jenerali Kulika alisimama wima kwa mara nyingine akatuliza masikio yake ambayo ndiyo kiungo peke kitakachomsaidia katika kujihami na mapigo ya wapinzani wake, kwa mara nyingine alisikia mapigo ya mateke mawili yakija upande wa kushoto akayumba kimapigano zaidi yakamkosa. Alijirudisha sawa baada ya kuyumba kuyakwepa mateke ya mpinzani wake wa pili na hapo ndipo ikawa nafasi kwa mpinzani aliyempiga teke kwenye kochi kutimiza azma iliyowafanya wawepo humo ndani, kofi zito lilitua kwenye shingo ya Jenerali Kulika ambalo liliambatana kutobolewa kitu ambacho hakukitambua.
Maumivu makali ndiyo yalifuata baada ya kutobolewa huko kisha misuli ya shingo ikaanza kumkamaa na nguvu zikaanza kumuishia muda huo, nguvu yote ya kupigana ilimuishia papo hapo kisha alajikuta akipiga magoti baada ya kuanza kuishiwa nguvu.
"You are dead General" Sauti ya mpinzani wake mmoja ilisikika ilimuambia kisha teke zito la kifuani ndiyo lilifuata hadi likaenda kumtupa kwenye kochi, taratibu Jenerali Kulika alikunja miguu yake kisha akainyoosha kwa nguvu akatulia hapohapo.
****
ASUBUHI ILIYOFUATA
Taarifa ya kifo cha mkuu wa majeshi nchini ndiyo habari iliyoteka vyombo vya habari, ilikuwa ni taarifa yenye kuhuzunisha kwa watu waliomtaka awepo kwenye orodha ya viumbe hai na pia yenye kufurahisha kwa watu wasiomtaka awepo kwenye orodha ya viumbe hai. Hali ya huzuni ilikuwa imetawala miongoni mwa wanajeshi pamoja na raia waliokuwa wakimpenda sana Jenerali Kulika kutokana na mchango wake kwa taifa, majira ya saa nne asubuhi mkuu wa majeshi ya majini Luteni Jenerali Ibrahim Salim alithibitisha juu kifo hicho.
Taarifa hiyo ya kifo cha mkuu wa majeshi kilitolewa mbele ya vyombo vya habari, mzizimo wa nchi juu ya kifo cha komandoo hatari na kiongozi wa makomandoo ndiyo ulifuata huku uchunguzi wa kifo chake ukiwa unaendelea. Nyumbani kwa Jenerali Kulika tayari kulishaanza kujaa watu asubuhi hiyo na ilipofika saa tano asubuhi viongozi mbambali wa kijeshi na wa kitaifa walianza kumiminika nyumbani hapo kwa utaratibu maalum, waandishi wa habari nao hawakuwepo nyuma katika suala hilo tayari walikuwa wameshaweka kambi nyumbani kwa Komandoo wa kutegemewa wakiwa wanarusha habari za matukio yanayoendelea humo kwa wasioweza kushuhudia kile kinachoendelea.
Ulinzi dhabiti ulikuwa umeimarishwa ndani ya eneo hilo kutokana na uwepo wa viongozi wazito ndani ya serikali, askari wenye nguo rasmi , wasio nguo pamoja na wsnajeshi walikuwa wapo ndani ya mazingira ya nyumba ya Jenerali Kulika maeneo ya Oysterbay.
Moses akiwa kama kiongozi wa usalama wa taifa naye alikuwepo ndani ya eneo hilo, upande wa kulia kwake alikuwa amekaa M.J Belinda na upande wa kushoto kwake aliuwa amekaa Norbert Kaila ambaye tayari alikuwa amepata ahueni baada ya kuokoka siku iliyopita kwa msaada wa Norene. Walikuwa wametulia katika viti vyao wakiwa wamezama kwenye fikra nzito juu ya tukio hilo, mkombozi mwenzao aliyeikomboa nchi pamoja nao kabla rais mzalendo hajapata wasaa wa kuiongoza nchi.
Ilikuwa ni simanzi kwao pamoja na hasira za kuuawa kwa kiongozi wa operesheni fagio la chuma lililoacha historia kwa watanzania, kadri muda ulivyozidi kwenda ndiyo walivyozidi kuzama kwenye fikra zao katika kuliangalia hilo suala hilo kwa upana zaidi. Akili zao za kijasusi tayari ziliamka na zikaanza kulichekecha hilo suala, Moses na Norbert kwa pamoja baada ya kuwaza kwa muda mrefu walijikuta wakiangukia kwenye wazo la aina moja ambalo lilisababisha wamuite M.J Belinda kwa pamoja kwa sauti ya chini kisha kila mmoja akawa na wahka wa kuongea kumuambia lile wazo lilipo ndani ya kichwa chake.
"aongee mmoja basi" M.J Belinda aliwaambia baada ya kuona wote waliingiwa na wahka wa ghafla wa kutaka kuongea juu ya suala hilo.
"Unaweza ukaanza" Norbert alimuambia Moses kisha akatega masikio asikilize kile kitakachotoka kwenye kinywa cha Moses.
"ninahitaji kuonana na Mke wa General nafikiri ataweza kutupa mwangaza wa kutegua hichi kitendawili kinachonikabili ndani ya kichwa changu" Moses aliongea kisha akakaa kimya akamtazama Norbert akimuashiria aseme naye.
"wazo ndiyo hilohilo nililolifikiri" Norbert aliongea halafu akatazama kulia na kushoto kisha akasema, "tunahitaji msaada wako juu ya hili".
M.J Belinda aliwatazama wote kwa pamoja baada ya kusikia maneno hayo kisha akawa anajiandaa kutamka kitu lakini alisita baada ya kuona mkubwa wake kicheo akija eneo hilo akiwa ameongozana na mwanaume wa makamo aliyevalia kinadhifu. Alisimama kwa haraka akatoa saluti kisha akaganda kumsikiliza kutokana na kutambua ujio wa huo ulimlenga yeye, Luteni Jenerali Ibrahim Salim ndiyo alikuwa mbele yake akiwa na huyo mtu aliyeonekana ni mgeni kwake.
"Benson, kutana na Major general Belinda. Major General Belinda kutana na Benson afisa aliyepo hapa kwa kazi maalum" Luteni Jenerali Ibeshim aliongea kutoa utambulisho, M.J Belinda na Benson walishikana mikono huku wakitoleana tabasamu hafifu la kuridhika na utambulisho huo.
"Major General Belinda nafikiri utakuwa msaada kwake katika kazi iliyomleta, ni hayo tu" Luteni Jenerali Ibrahim aliongea kisha akaondoka akiwa na Benson.
Belinda aliwageukia Norbert na Moses kisha akawapa ishara wamfuate, alitembea kutoka katika eneo hilo la kupumzika wageni akiwa pamoja na Norbert na Moses. Walipanda ngazi ndogo za kibsrazani wakiekea katika mlango wa mbele wa kuingia humo ndani ambapo walimkuta mwanajeshi mwenye cheo cha koplo aliyetoa saluti akafungua mlango wakaingia ndani, walipita sebuleni hapo ambapo kulikuwa na kundi kubwa la kinamama wakapanda ngazi kuelekea juu. Walifika juu kwenye ghorofa wakatembea kwenye korido ndefu iliyowapeleka hadi kwenye mlango wa chumba ambao waliufungua wakaingia, walikutana na mwanajeshi wa kike ambaye alitoa saluti baada ya kumuona M.J Belinda.
"Huyu ni Moses Gawaza kutoka UN laboratory na huyu ni Norbert Kaila mwandishi wa habari wa kujitegemea, wana maongezi maalum na mfiwa hivyo unahitajika usubiri nje ya mlango wa chumba Koplo usu" M.J Belinda alimuambia mwanajeshi wa kike aliyekuwemo humo ndani na alimuita kuendana na cheo cha V moja iliyopo begani ambayo huitwa Koplo Usu.
"Afande" Aliitikia kwa ukakamavu akatoka nje mara moja.
Koplo usu wa kike alipofunga mlango baada ya kutoka nje, Moses na Norbert walibaki wakimtazama mke wa Jenerali Kulika kwa huruma sana kisha wakamtazama M.J Belinda kwa sekunde kadhaa. Waliyarudisha macho yao kwa mke wa Jenerali Kulika wakamtazama sana mama yule ambaye kiumri alikuwa sawa mama yao akiwa amekuwa mwekundu baada ya kulia sana, nywele zilizovurugika zilionekana kichwani mwake na macho yalikuwa yameuka rangi na kuwa yanafanana nyanya mbivu.
"Mama" Moses aliita kisha akaendelea kuonges, "pole sana mama yangu".
Maneno hayo yalimfanya mke wa Jenerali Kulika aanze kulia kwa uchungu huku akitamka maneno yenye kumlaumu muumba kwa kumchukua mume wake kipenzi, wote kwa pamoja walimuacha alie mpaka akanyamaza akawa kainamisha uso wake kwa majonzi.
"Mama naamini Jenerali hakufa hivihivi tu bali kuna mtu ndiyo chanzo naamini hivyo, imani yangu inaweza ikapata uhalisia kuwa ni kweli ikiwa tu nitasikia kidogo kutoka kwako na nikakusanya na kile nilichokipata kwingine kibaini ukweli" Norbert aliongea kisha akatoa simu yake ya mkononi akabonyeza kitufe cha kurekodi.
Mke wa Jenerali Kulika alipoambiwa kuhusu hilo alianza kulia upya tena zaidi ya mwanzo Mke wa Jenerali Kulika alianza kuvuta picha tukio aliloliona usiku uliopita na akajikuta hata akishindwa jinsi ya kulielezea na akazidi kulia. Iliwabidi wambembeleze kwa muda mrefu na wakisitisha kumhoji mwanamke ambaye weupe wake tayari ulikuwa ushajenga rangi nyekundu juu ya ngozi kwa kulia, alipobembelezwa na kunyamaza Mke wa Jenerali Kulika ndipo alipopata wasaa wa kuweza kuongea kile ambacho Norbert na Moses walihitaji kukijua kwa muda huo.
“Mume wangu nakumbuka vizuri ni jana tu ametoka safari ya nje ya nchi na alikuwa ameenda kiofisi zadi, nilikuwa na hamu sana na mume wangu kutokana siku zote hizo kutomuona akiwa nje ya nchi kwa ajili ya safari hiyo ya kikazi. Usiku wa jana tulilala pamoja vizuri hadi muda ambao simu yake ilipoita ndiyo alipotoka kwenda kuzungumza nayo, muda mfupi baadaye baada ya kutoka kwenda kuzngumza nayo nilishuhudia mlango wa chumbani ukifunguliwa na kisha mkono wa mtu ambaye niliamini ni mume wangu ulichomoa funguo kwenye kitasa kwa ndani. Kutokana na usingizi niliokuwa nao niliamini kabisa alikuwa ni mume wangu anachukua funguo hiyo kwani ilikuwa si mara ya kwanza kwa yeye kuchukua ufunguo akiwa ameamka usiku ili aende kufungua chumba chake cha vitabu na nyaraka zingine muhimu sana” Mke wa Jenerali Kuiika aliongea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwanini unasema mwanzoni uliamini je hivi sasa huamini kama alikuwa ni mume wako?" Moses aliuliza.
"Ndiyo hakuwa na sikuweza kumtilia maanani kutokana na usingizi nilionao na pia mume wangu hana mchoro wa kipepeo mkononi" Alijibu.
"Je baada ya kuchukua ufunguo wa mlnago alifanyaeje?"Moses aliuliza tena
"Baada ya kuchukua ufnguo wa mlangoni nilisikia mlio wa ufunguo ukichomekwa kwenye kitasa cha nje kisha ukafungwa kabisa, sikuwa na wasiwasi nilijua kwa muda huo huenda ni yeye lakini asubuhi hii ndipo nilikumbuka kuhusu ule mchoro nikajua kabisa hakuwa mume wangu yule aliyefungua mlango ule" Alijibu
"Baada ya kukumbuka mama ulichukua hatua gani?" Norbert aliuliza.
"Niliamka kitandani baada ya kukumbuka suala hilo mume wangu hakuwepo na sikuwa na imani nalo kabisa niliamini ulikuwa ni wasiwasi wangu tu. Nilipoenda mlangoni kwenda kuufungua nilibaini ulikuwa umefungwa kwa nje" Alieleza
"Enhe ikawaje baada ya hapo?" Norbert aliuliza
"Nilimuita kwa nguvu Baba Dorry nikimuambia anifungulie mlango nikiamini alikuwa amefunga kwa kujisahahu lakini sikuitikiwa, muda huo nikasiikia sauti ya Dorry na wadogo zake wakimuambia baba yao pia awafungulie mlango hapo ndipo nikahisi kulikuwa na hali tofauti ndani ya nyumba" Alieleza.
"ulikuja kujua vipi kama kumetokea tukio ndani ya nyumba yako?" Norbert aliuliza.
"Nilikuja kujua kama kumtokea tukio ndani ya nyumba yangu baada ya kutoitikia na mume wangu kwa mara zote nilizokuwa nikigonga mlango na kumuita jina lake na kumuhimiza afungue mlango,nilienda dirishani na kuchungulia eneo la getini labda vijana wake watanisikia hapo niliwaona wote wakiwa wamelala chini kila mmoja wakiwa hawajitambui kuashiria kulikuwa najmbo lisilo la kawaida. Sikuweza kuvumilia nilipoona hali hiyo niliamua kupiga kelele kwa nguvu sana hadi majirani wakanisikia nidyo waliyokuja kutoka msaada wa kunifungulia mimi na wanangu" Alieleza
"Je watumishi wa ndani wa nyumba hii nao hawakuwepo siku iliyopita?" Moses aliuliza
"Wote walikuwepo baba yangu ila walikuwa wamefungiwa kama nilivyofungiwa mimi na wanangu isipokuwa hawakuwa na fahamu hadi muda huo ambao tunafunguliwa na majirani" Alijibu, baada ya kujibu swali hilo Moses na Norbert walitazamana kwa muda wa sekunde kadhaa katika nyuso zao kisha wakaafikiana jambo kwa ishara.
"Ok mama yetu asante kwa maelezo yako tukikuhitaji tutakuja kwa mara nyingine ilimradi tu mhalifu afikishwe katika chombo cha sheria,sote tuna uchungu hapa kwa kumpoteza kamanda mwenye msimamo ndani ya nchi hii. Tupo pamoja na wewe hadi tunampata huyo mhusika aliyesababisha haya" Norbert aliongea huku akimpatia mkono mke wa Jenerali na Moses naye akampatia hivyo, wote kwa pamoja walitoka humo chumbani wakiwa pamoja na M.J Belinda.
Walipofungua mlango wa kutoka nje walimuona Benson ambaye awali walikuwa wamemuacha nje akiwa anaongea na Koplo usu ambaye alikuwa yupo mlangoni mwa chumba hicho, alipowaona alitoa tabasamu huku akimuangalia kila mmoja wao na akawa amesitisha kuongea na Koplo Usu huyo wa kike aliyekuwa akiongea naye kwa muda huo. Koplo Usu huyo naye alishtuka alipomuona mkuu wake akiwa amemkuta anaongea na Benson katika eneo hilo, wote wAlibaki wakiwatazama kina Norbet baada ya kutoka humo ndani ya chumba cha mke wa Jenerali Kulika.
"Lance koplo" M.J Belinda alimuita yule Koplo usu
"Afande" Koplo usu aliitika huku akitoa heshima.
"Kaendelee na kazi yako ndani" M.J Belinda alitoa amri huku akimtazama Benson kwa umakini, Benson alirudishha tabasamu kwa kutazamwa huko na macho ya kirembo ya M.J Belinda ambaye hakutabsamu badala yake alikwepesha macho kisha akawatazama Norbert na Moses.
"Tunaweza tukaenda" Aliwaambia huku akitembea kuufuata ukumbi huo mwemba hadi mwisho kabisa ambapo kulikuwa na chumba kingine, walipofika kwenye chumba hiko M.J Belinda alifungua mlango akaingia ndani akiwaacha Moses na Norbert nje wakiwa wanamsubiria yeye kama alivyowasihi wamsubiri. Alitumia muda mfupi humo ndani ya chumba ambapo alirejea akiwa ameongozana na askari mwingine wa kike aliyekuwa amevaa sare za JWTZ za ofisini akiwa na cheo cha sajini(V tatu).
"Kutana na Norbert Kaila mwandishi wa habari maarufu wa makala za kufichua maovu" M.J Belinda alimwambia Sajini huyo wa kike ambaye alitoa tabasamu kisha akampatia mkono Norbert ambaye aliupokea mkono huo akamtekenya kwenye kiganja cha mkono kisha akambania jicho wakati anasalimiana naye.a
"Pia kutana na Professa Moses Lawrence Gawaza kutoka UN laboratory, wote kwa pamoja wanataka kufanya mahojiano na Dorry hivyo naomba usubiri hapa mlangoni na uhakikishe mtu haingii ndani wala kusogelea huu lango hadi sisi tutoke. Tunaelewana!" M.J Belinda aliongea kumtambulisha Moses ambaye pia alipeana mkono na Sajini huyo wa kike ila hakufanya kituko kama alichofanya Norbert baada ya kupewa mkono na Sajini huyo, M.J Belinda pia alimpa maelekezo mapya Sajini huyo pindi atapokuwa yupo ndani kutokana na kutokuwa na imani na watu wote waliokuwa wapo humo ndani ya nyumba hiyo hadi huo ambao wanaingia.
Wasiwasi wa kuwepo msaliti ndani ya eneo hilo ndiyo ulikuwa umemtawala ndani ya moyo wake muda huo baada tu ya kungia ndani ya eneo hilo kutokana na kushuhudia kitu ambacho hakuwa anakielewa kabisa tangu aingie ndani ya ukumbi huo ambao ulikuwa na vyumba vya wanafamilia wa Kamanda wake mkuu, hivyo maelekezo juu ya kutoruhusu mtu kusogea katika eneo hilo yalikuwa ni muhimu sana kwa Sajini aliyekuwa na jukumu la kulinda chumba cha watoto wa Jenerali Kulika katika kipindi hiko ambacho walikuwa na wasiwasi muuaji hakuwa mbali na maeneo na huenda hata kwenye msiba huo alikuwa amekuja kutokana umaarufu alionao Jenerali Kulika.
M.J Belinda pamoja na kina Norbert waliingia ndani ya chumba hicho ambapo ndani kulikuwa na binti wa takribani miaka ishirini na ushee kidogo aliyekuwa amekumbatiwa na wadogo zake ambao wote walikuwa wakilia tu muda wote. Binti huyo ndiye aliyekuwa mtoto mkubwa wa Jenerali Kulika,macho ya binti huyo tayari yalikuwa yamebadilika rangi kwa kulia muda mrefu kutoka na uchungu alionao kwa kufiwa na baba yake
"Dorry antii" M.J Belinda alimuita biti huyo huku akiketi kitandani jirani naye, Dorrry aliposikia kuitwa huko na M.J Belinda alimkumbatia kwa haraka sana huku akilia kwa uchungu sana akimtaja baba yake akilalamika kwanini alikuwa amemuacha mwenyewe. Ilimchukua muda wa ziada kuanza kumbembeleza hadi aliponyamaza ndipo alipoambiwa lengo la uwepo wa Norbert na Moses ndani ya eneo hilo kwa muda huo ambao alikuwa na majonzi ju ya kifo cha baba yake, Dorry kwa kuwa alikiuwa na uchungu na mapenzi makubwa sana kwa baba yake alikubali kutoa ushirikiano huo kwa watu hao ambao walikuwa wamekuja katika eneo hilo kumhoji kama walivyomuhoji watu wengine waliokuwa wametangulia kabla yao.
"Binti unaweza ukatuambia jana usiku mlipolala hadi inafika muda wa asubuhi ilikuwaje"" Moses aliuliza.
"jana usiku baba yatu alikuwa amerudi kutoka safari na tulikuwa tumemkumbuka sana hivyo tulikaa naye kwa muda mrefu hadi ulipofika muda wa kulala ndiyo akaenda kulala chumbani kwake pamoja na mama" Dorry alieleza
"Enhe ikawaje?" Moses aliuliza tena.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nasi tulikuja kulala chumbani kwetu hadi kama kawaida, sisi tulikuwa na kawaida ya kusahau kuzima taa ambapo Baba yetu huwa anakuja kuizimma tukiwa tumelala. Usiku muda ambao nilishtuka kutoka usingizini nilisikia mlango wa chumbani kwa baba ukifunguliwa nikajua kabisa ni yeye maana huwa ana kawaida kutoka usiku na kuelekea sebuleni au makataba yake akiwa anaongea na simu muhimu au ana kazi ambayo imemjia kwa ghfla usiku huo. Nilisikia mtu akiwa anashuka ngazi za kuelekea sebuleni na kisha baada ya muda mfupi nilisikia sauti ya kufunguliwa mlango wa chumbani kwa baba nikajua ni mama alikuwa natoka hivyo sikuwa na wasiwasi kabisa,mlango huo ulifungwa tena na hapo baada ya muda mfupi nikashuhudia mlango wa chumbani kwetu ukifunguliwa. Muda huo mama alikuwa hapendi sana kutuona watoto wake tukiwa macho hivyo ili asijue niko macho niliamua kujifunika shuka hadi usoni nikiamini alikuwa ni yeye anafungua mlango huo" Dorry alisita kueleza na akapandisha takamwili za ndani ya pua huku akivuta pumzi kwa kasi sana.
"Haikuwa kama mawazo yangu yalivyokuwa yanadhania kuwa huwa huyo alikuwa ni mama, kwani mama hakuwa na kawaida ya kupapasa kujua taa ilipo ili aizime kutokana kuijuan nyumba hii na mfumo wa swichi ulivyo. Nilisikia huyu aliyefungua mlango akiwa anapapasa ukutani kwa sekunde kadhaa hapo ilinibidi nifungue shuka niweze kumuona alikuwa ni nani. Nilivyofungua shuka tu mkono huo tayari ulikuwa umeshaifikia swichi na ulikuwa umezima taa na kuiichukua funguo mlangoni lakini niliweza kuuona ule mkono" Aliendelea kueleza.
"Je huo mkono ulikuwa ni wa nani hasa?" Norbert aliuliza.
"ulikuwa ni mkono wa mwanaume ambao ulikuwa na kovu la mshono" Dorry alijibu.
"Je ulipouona huo mkono hukuweza kupiga kelele?" Norbert aliuliza
"Sikuweza kwakweli kutokana na uoga na pia nilijua nilikuwa nimeona vibaya labda kwani kufunguliwa kwa mlango wa chumbani kwa mama kulinipa uhakika huo" Alijibu.
"Ok Baada ya hapo ilikuwa vipi?" Moses aliuliza kwa mara nyingine.
"Baada ya hapo nilipitiwa na usingizi hadi nilipokuja kusikia makelele ya wadogo zangu wakimuita baba afungue mlango, mlango ulikuwa kufunguliwa na ndiyo hapo nilikuja kujua baba hatupo naye" Dorry aliongea na alipofikia hapo alianza kulia tena, M.J Belind alichukua wasaa mwingine wa kumbembeleza hadi pale alipotulia.
Moses na Norbert walipomaliza kuuliza maswali hayo walitazamana na wakapeana ishara kama walivyokuwa wamemaliza kumuhoji mke wa Jenerali Kulika, walimtazama na M.J Belinda kisha wakampa ishara ileile waliyokuwa wamepeana ambapo M.J Belinda naye alitikisa kichwa kukubaliana nayo.
"Dorry asante sana kwa ushirikiano wako nakuahidi kukusaidieni katika hali hii,tukikuhitaji tutarejea tena" Moses aliongea hukua akimpa mkono na Norbert akafanya hivyohivyo, wote kwa pamoja walitoka humo ndani baada ya kuridhishwa na maelezo ya Dorry ambayo yalikuwa yapo kwenye kifaa chao cha kunasia sauti.
Sajini aliyekuwa yupo mlangoni alirudi ndani muda huohuo baada ya wao kutoka nje ambapo bado walimshuhudia Benson akiwa yupo kwenye eneo la hapo kwenye ukumbi ambao unatenganisha vyumba hivyo, muda huo alikuwa yupo kwenye eneo la mwanzo ambapo ngazi za kupanda huko juu kutoka sebuleni zilikuwepo. Wote walipomuona walitazamana kisha wakawa wamemetilia shaka juu ya uwepo wake mahala hapo lakini hawakutaka kuzionesha shaka zao juu yake, walikuwa bado wamesimama kwenye ukumbi huo mbele ya mlango wa chumbani kwa Dorry wakiwa wanamtazama Benson ambaye alikuwa amewapa mgongo.
"Huyu jamaa sina imani naye kabisa" Moses aliongea kwa sauti ya chini sana.
"Hata mimi sikuwa na imani naye kabisa nilipomuona yupo mlangoni mwa chumba cha mjane nilijiuliza kafuata nini maana huku maofisa wa jeshi wenye kazi maalum na ndugu tu ndiyo wapo" M.J Belinda alisema
"Ok hebu muweke jicho la umakini naye kabisa, halafu Belinda kuna jambo nilisahau kukuuliza" Norbert aliongea
"Yap lipi hilo umesahau?" Belinda alimuuliza naye.
"Hivi hawa majirani waliokuja kuwafungulia walikuta kuna athari yoyote zaidi ya kuukuta mwili wa marehamu?" Norbert aliuliza.
"Hakukuwa na athari yoyote zadi ya kuukuta huo mwili wa marehemu ukiwa upo sebuleni na walinzi wake wa jeshi wakiwa wapo jirani na geti ambao sasa hivi wapo Muhimbili walipowahishwa kwa ajili ya matibabu" M.J Belinda alijibu.
"Nahitaji kuwahoji na hao walinzi pia nahisi watakuwa na jingine, Moses safari moja Muhimbili" Norbert alimuambia Moses na wote kwa pamoja wakatoka kwenye eneo hilo hadi kwenye ngazi na kumpita Benson akiwa amesimama kwenye eneo hilo.
Walishuka ngazi hadi sebuleni ambapo walitoka nje moja kwa moja hadi barazani mwa nyumba hiyo. M.J Belinda alibaki katika eneo hilo Moses na Norbert walitoka hadi nje kwenye eneo la maegesho ya dharura kwa ajili ya msiba huo. Waliingia ndani ya gari walilokuwa wamekuja nalo eneo hilo na wakatoweka kuelekea Muhimbili, walikuwa wakitaka kwenda kumalizia sehemu ya kujua kile ambacho walikuwa nacho wanajeshi waliokuwa wakilinda nyumba ya Jenerali Kulika kwa siku hiyo iliyopita.
Moses ndiye alikuwa dereva wa gari hilo katika safari hiyo ya kuelekea Muhimbili, alikuwa yupo makini sana gari na kuangalia usalama wao katika muda huo ambao walikuwa wakielekea katika hospitali ya Muhimbili. Hadi wanaingia barabara ya Ally Hassan Mwinyi bado hali ilikuwa ipo shwari isipokuwa waliona baadhi ya magari yakiwa yapo nyuma yao na hawakuwa na wasiwasi nao kabisa,Moses aliendelea kuendelea kuendesha hadi walipovuka kwenye kituo cha polisi cha Daraja la Salenda ambapo gari aina ya Toyota altezza nyeusi ndiyo pekee ilikuwa ipo nyuma yao.
Walipoyafikia makutano ya barabara ya umoja wa mataifa gari hiyo ilikata kona kuingia upande wa kulia kwenye barabara ya Umoja wa mataifa. Moses alipoiona gari hiyo imeingia upande huo alishusha pumzi kisha akaongeza mwendo kuendelea na barabara ya Ally Hassan Mwinyi hadi kwenye kituo cha daladala cha Palm Beach, hapo alikata kona kuingia kwenye barabara ya lami iliyokuwa ikielekea ulipo ubalozi wa Burundi. Walienda nayo nayo barabara hiyo na wapofika kwenye ubalozi wa Burundi walipita moja kwa moja hadi kwenye makutano ya barabara hiyo na barabara ipitayo mtaa wa Lugalo.
Hapo kwa mara nyingine waliishuhudia ile gari aina ya Toyota altezza nyeusi ikiwa ipo upande wa barabara hiyo wanayotaka kuingia katika upande ambao ilikuwa ikielekea kukutana na barabara ya Umoja wa mataifa, gari hiyo ilipowaona walikuwa wanataka kuingia katika barabara hiyo ilisimama na ikawawashia taa za mbele mara moja na kuwaaashiria waingie kwenye barabra hiyo. Moses hakutaka kusita yeye alikata kona kuingia upande wa kushoto na akaingia rasmi kwenye barabara hiyo inayopita mtaa wa Lugalo, aliongeza mwendo huku ile gari ikiwa ipo nyuma yake.
Walienda na barabara hiyo huku ile gari ikiwa bado ipo nyuma yao hadi walipofika makutano ya Mtaa wa Kitonga na mtaa wa Lugalo, hapo Moses aliingia kwenye barabara iliyokuwa ikipita mtaa wa Kitonga akiiacha ile gari ikinyoosha barabara ya Mtaa wa Lugalo. Moses alienda na barabara hiyo hadi alipofika kwenye makutano ya barabara hiyo na barabara ya Malik iliyokuwa ikielekea kwenye makutano ya barabara ya Mtaa wa Magore na kuendelea hadi Muhimbili, alipofika kwenye makutano ya barabaara hiyo na barabara ya Malik alikata kona kuingia kulia mwa barabara ya Malik kisha akaaangalia nyuma kupitia vioo vya pembeni hakuweza kuliona tena gari hilo.
Alinyoosha na barabara hiyo na alipokuwa akikaribia kwenye makutano ya barabara ya Magore aliiona ile gari ikiwa inakuja kwa mwendo wa wastani sana jambo ambalo lilimfanya aingie kwenye barabara inayopita mtaa wa Magore jirani kabisa na shule ya sekondari ya Shaaban Robert akiacha ile inayopita kati ya makao mkuu ya jeshi na ukumbi wa Aga Khan Diamond jubilee na kwenda moja kwa moja Muhimbili. Aliongeza mwendo akiwa kwenye njia hiyo hadi alipoivuka njia shule hiyo na akaingia upande wa kushoto kwenye barabara ya mtaa Undali kwa kasi. Safari yake ya kasi iliishia kwenye hoteli ya Kangaroo akaingiza gari ndani kwa kasi,alienda hadi kwenye maegesho ya ndani ya hotel akasimamisha gari halafu akalizima.
"Nawatakia ufutiliaji mwema, si wanajua kufuatilia magari ya watu" Moses alisema huku akinyoosha kiti cha dereva akajilaza
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"na inaonekana wanajua tunaelekea Muhimbili walipolazwa wanajedhi waliokuwa wanalinda kwa Jenerali waliyokutwa hawajitambui" Norbert aliongea.
"ndiyo maana yake" Moses alidakia.
Moses na Norbert walikaa hapo kwenye maegesho ya hoteli kwa dakika kadhaa kisha wakashuka kwenye gari yao wakiwa na wazo jipya litakalozidi kumchanganya aliyekuwa akiwafuatilia, waliamua kuingia ndani ya hotel hiyo iliyo chini ya Gawaza&Son company ambayo ipo chini ya Moses baada ya kuachiwa urithi na baba yake.
Baada ya muda wa dakika takribani kumi na tano tayari Norbert na Moses walikuwa wameshabadili mavazi waliyokuwa wameyavaa hapo awali, ubadilisho wa kiutambuzi tayari ulikuwa katika miili yao ambapo ingekuwa ngumu kwa mtu wa kawaida kuwatambua. Kofia maarufu kama kapelo ndiyo zilikuwa zimefunika vichwa vyao vikawafanya wasijulikane kwa urahisi kabisa, walitumia gari nyingine tofauri na ile waliyoingia nayo hapo hotelini ambayo iliwafikisha hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Walienda hadi kwa Dokta Hilary wakiwa na wahka wa kutaka kuwahoji wale wanajeshi kwani waliamini wakifanya hivyo watakuwa wameweza kusaidia kwa kiasi fulani katika kufanikisha jambo, walipofika ofisini kwa Dokta Hilary walipokewa na simanzi nzito iliyokuwa imetanda katika uso wa daktari huyo. Dokta Hilary alikuwa ameweka mikono shavuni tangu kina Moses wanaingia ofisini na hakuwa ameitoa mikono hiyo shavuni hadi wanaketi kwenye viti, alionekana kuzama ndani ya majuto zaidi.
Moses na Norbert walipoketi kwenye viti vyao hakuwa amenyanyua kauli kuwakaribisha kama ilivyozoeleka, utofauti wa hali hiyo uliwapa mshangao nao wakataka kujua kipi kilichomsibu rafiki na pia mtu wao wa karibu kwa baadhi ya vitu. Ukimya wa Dokta Hilary ulipozidi Norbert aliamua kupiga meza na kumshtua kisha akamuuliza, "whats the problem(nini tatizo)?".
"Hii sasa ni uzembe wa hali ya juu najuta hata kwanini nilikuja humu nisibaki kule" Dokta Hilary aliongea huku akijipiga kichwa chake kwa nguvu mithili ya mtu anayeelekea kupatwa na wazimu, alikiona kichwa chake hicho ndiyo kilisababisha afanye huo aliuona uzembe ndani ya nafsi yake ambao hakutakiwa kuufanya kabisa.
"aaaaargh! My head!(Kichwa changu) My brain(ubongo wangu), ndiyo chanzo cha yote haya natamani hata ningefuata ile sauti iliyonisihi nisiende ofisini kuliko kulusikuliza. Huenda haya yote yasingetokea huenda huyu mdondosha kadhia asingeweza, ila hili bichwa na bongo iliyomo ndani yake ndiyo chanzo" Dokta Hilary alizidi kulalamika kwa hasira sana zilizosababishwa na majuto ndani ya nafsi yake, alipiga ngumi kwa nguvu kwenye meza yake ya kitabibu kwa mara tatu mfululizo kisha akapiga ukelele wa jazba.
Alipotaka kuongeza ngumi nyingine kwenye meza hiyo isiyokuwa na hatia juu ya hilo linalomfanya ajute ndani ya kichwa Norber aliudaka mkono ili asizidi kuiadhibu meza hiyo isiyokuwa na hatia wala kuhusika na hicho alichokuwa akilalamikia.
"Hey hebu punguza hasira na utuambie nini tatizo basi" Norbert aliongea huku akimkamata mkono kwa nguvu Hilary ili asizidi kuiadhibu hiyo meza ambayo haina hatia yoyote wala haikustahiki adhabu hiyo aliyokuwa akiipa, pia alimzuia ili apate kumtuliza ili ajue kile kilichomsibu Hilary ndani ya kichwa chake hadi akawa na jazba hiyo.
"Aaaargh! Hichi kichwa hiki ndiyo chanzo kimenishawishi niondoke, ngoja nikitie adabu kwanza. Haiwezekani kabisa" Dokta Hilary aliongea kisha akachukua mashine ya kutobolea karatasi ili zibanwe katika mafaili iliyopo mezani, aliinyanyua mashine hiyo kwa mkono mwingine tofauti na ule wa awali aliokuwa anautumia kuiadhibu meza ambao sasa hivi ulikwa umekamatwa barabara na Norbert.
Aliiituliza mashine hiyo katikati ya utosi wake hadi sehemu ya nyuma ya mashine hiyo yenye plastiki maalum kwa kuhifadhi vipande vinavyotobolewa ikavunjika, hakuridhika kabisa na wala hakuhisi kama kichwa chake kitakuwa kimepata adhabu kwa kujipiga na plastiki hilo hivyo hamu ya kuendelea kukiadhibu kichwa chake ikamjia. Aliinyanyua mashine hiyo ambayo kwa sasa imebaki chuma kitupu akiazimia kuituliza katika utosi kwa mara nyingine ikiwa imebaki chuma kitupu tu, hakujali kujeruhiwa na mashine hiyo zaidi ya kutaka kukipa adhabu kichwa chake alichokiona kina hatia sana.
Alinyanyua mashine hiyo kwa mara nyingine tena kwa kutumia nguvu kuliko awali akilenga kuituliza kwenye kichwa chake ili akipe adhabu tena, mashine hiyo ya chuma nayo ilikuwa imetulia kimya sana na ilikuwa ikitii amri wa mikono ya Hilary na jinsi alivyokuwa akiiiamrisha. Mashine hiyo ilipotaka kutua kwenye kichwa cha Dokta Hilary kwa mara nyingine Norbert aliipangua kwa karate moja matata kabisa ikaenda chini moja kwa moja ikakutana na sakafu, mlio wa chuma cha mashine ndiyo ulifuata ambao ulimrudisha Hilary sawasawa akawa na hali ya kawaida.
Alibaki akihema kwa nguvu huku akishikilia kifua chake kisha akaketi kwenye kiti chake akawa ameinamisha uso wake chini, muda wote huo Moses alikuwa akimtazama rafiki yake akiwa amezama ndani ya tafakuri nzito juu ya kile anachokifanya.
"Hilary tuambie kuna nini" Moses alimuambia Dokta Hilary kwa sauti ya upole huku akimtazama usoni.
"wanajeshi walioletwa hapa baada ya kuwa hawajitambui tayari ni marehemu kwa sasa na mmoja hajulikani halipo, chanzo cha kifo ni kimoja na kile cha Bishop Edson, Mufti na General" Dokta Hilary alimuambia Moses akiwa ameingiwa na unyonge baada ya hasira yake kumshuka.
"Nesi mmoja amemuona mwanamke aliyevaa mavazi ya wauguzi akitoka katika wodi hiyo" Dokta Hilary aliwaambia, Moses na Norbert kwa pamoja walibaki wamegwaya kwa taarifa hiyo. Akili zao tayari zilikuwa zimezidiwa na mtu aliyekuwa akijua kwa kina juu ya mipango yao, tegemezi la mwangaza mwingine wa jinsi ya kuanza kazi zao tayari lilikuwa limemalizwa na adui yao wasiomtambua.
"Hili ni tatizo Moses try to think chanzo cha kifo cha General, wanajeshi hawa ikifika makao makuu jeshini nini kitafuata unafikiri? Moses kumbuka hii sumu uliitengeneza wewe itumiwe kwa ajili ya kuua wadudu waharibifu wa mazao lakini sasa inatumuea kuua watu, Luteni Jenerali Ibrahim Salim ndiyo mwenye cheo kikubwa aliyebakia katika majeshi ya hapa. Jaribu kufikiria akiipata taarifa hiyo atakuchukulia hatua gani? Hapa utakamatwa wewe tu na heshima yako kwa taifa itaingia doa Moses, wewe ni professa na ni mtoto wa professa hebu fikiria hilo" Dokta Hilary aliongea kwa hisia sana kisha akanyanyuka kwenye kiti chake kwa mara nyingine akapiga hatua akaelekea dirishani, alisimama dirishani akawa anaangalia nje kwa dakika kadhaa kisha akageuka akawatazama Moses.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"You know what(unajua nini)? Mimi ni daktari wa kuaminika na hawa wanajeshi hawa nimeletewa mimi niwape huduma kwa kuaminika kwangu kwani kutoka Oysterbay hadi Lugalo hospital ni mbali sana na Muhinbili ni karibu. Wameamua wawalete hapa kwani wakicheleweshwa wangekuwa na hali mbaya sana na hata kupoteza maisha kabisa, wameniletea hapa nimewahudumia wakawa na hali nzuri kabisa hadi mmoja amerudiwa na fahamu kabisa. Lakini hichi kichwa kilichobeba uso wangu kimesababisha nichukue uamuzi wa kwenda ofisi ya manesi kumuita nesi aje kuwahudumia na hatimaye nikaja ofisi kuendelea na kazi zingine, matokeo yake ni nesi huyo kupishana na mwanamke aliyemuona mlangoni akiwa ana sare za manesi akitoka humo ndani. Yaani wagonjwa niliokabidhiwa niwatibu kwa kuaminiwa na L.J Ibrahim tayari wameuawa, ni aibu kwangu pia ni balaa kwetu hebu fikiria aliyenipa jukumu hili atanionaje mimi na atakufikiria vipi Moses ikiwa anatagundua sumu iliyowaua watu wake na mkuu wake inatoka kwako" Dokta Hilary aliongea kwa kulalamika sana, aliwatazama Moses na Norbert akaona ukimya ulikuwa umetanda kwao. Ilichukua muda wa dakika nzima ndipo Moses akanyanyua kinywa chake akasema, "Hilary wasiwasi juu ya hili suala haupo kwako bali upo kwangu kwani hawa wamefariki na kuna baadhi ya watu wamejua nimekuja hapa Muhimbili ndiyo watu hao wakafariki, nimeshaanza kuharibikiwa ila nitaomba msaada wako kwa mara nyingine ili unisaidie".
"No Moses siwezi kukusaidia tena utaniweka matatizoni zaidi kumbuka urafiki wetu unajulikana" Dokta Hilary alikataa kumsaidia rafiki yake kutokana na tatizo alilonalo, kauli hiyo ya rafiki yake kipenzi ilimfanya Moses aheme kwa nguvu kisha akamtazama Norbert ambaye alimpa ishara ya kificho sana. Aliporudisha uso wake kwa Hilary tayari ulikuwa umebadilika usio na hata na chembe ya mzaha, alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akazamisha mkono wake mfukoni akatoa kitu cha rangi ya kahawia mfano wa kitabu cha kutunza namba za simu chenye nembo ya rauda pembeni akamkabidhi Dokta Hilary.
"Sipo kiurafiki tena na inabidi ufanye ninachokuambia Hilary nipo kwa ajili ya kutetea taifa" Moses aliongea huku akimpatia Moses kitu hicho akichokitia katika mfuko wake, Dokta Hilary alikipokea kisha akakifungua aone kilichomo ndani yake.
Macho ya Dokta Hilary yalitua juu ya kitambulisho adimu kuviona vya usalama wa taifa ambacho kulikuwa kikimtambulisha vizuri Moses kuwa ni mmoja wa wanausalama hao, mshtuko wa ghafla ndiyo ulimpata Hilary baada ya kubaini kuwa alikuwa na urafiki na mwanausalama wa siri kwa muda mrefu sana.
"Inabidi utusaidie katika kazi yetu Hilary na huu utambulisho wangu ubaki siri yako umeelewa?!" Moses aliongra kwa msisitizo huku akipuuzia mshangao uliomkumba Dokta Hilary halafu akachukua kitambulisho chake.
"namuhitaji huyo nesi aliyemuona huyo mwanamke na pia nahitaji nijue ni dawa gani iliyowalaza hao wanajeshi hadi wakawa na hali mbaya hivyo" Moses aliendelea kuongea
.
"OK, wagonjwa hawa wamevuta dawa ya gesi ambayo hutumika katika upasuaji tu na hairuhusiwi kuuzwa kwa maduka mengine ya dawa isipokuwa hupatikana bohari kuu ya dawa tu tena kwa kibali maalum tu" Dk Hillary aliongea.
"unaweza ukanionesha ripoti kamili?" Moses aliuliza
"Bila shaka" Dk Hilary alijibu kisha akafungua mtoto wa meza akatoa makaratasi ambayo alimkabidhi Moses, Moses aliyapitia makaratasi hayo kisha akamkabidhi Norbert ambaye naye aliyapitia hadi mwisho.
"Lexone hutoka kwa madaktari maalum tu kule bohari kuu ya dawa kwa ajili ya kuzuia damu isitoke nyingi katika upasuaji mkubwa tu na mara nyingi hutolewa kwa taasisi ya moyo katika kufanya upasuaji tu" Moses aliongea huku akimtazama Norbert halafu akamgeukia Dk Hilary akamuambia, "muite huyo nesi ninuhitaji nataka atusaidie katika jambo hili pia".
Dk Hilary aliafiki maneno hayo ya Moses na akanyanyua mkonga wa simu ya mezani abonyeza kitufe cha tarakimu moja akaweka sikioni, alisubiri kwa muda wa sekunde kadhaa simu ilipopokelewa akaongea, "namuhitaji Phina ofisini kwangu haraka sana".
Aliweka mkonga wa simu mahala pake kisha akawaashiria kina Moses wasubiri baada ya simu hiyo kutoa ujumbe kwa mhusika, muda huo wakisubiri mlango wa ofisi ya Dk Hilary ulifunguliwa kwa taratibu akaingia muuguzi wa kiume ambaye alishtuka baada ya kuona ugeni uliopo humo ndani.
"We Japhet ndiyo adabu gani kuingia bila hodi ofisini kwangu?" Dk Hillary aliongea kwa ukali.
"samahani Dokta" Muuguzi huyo wa kiume aliomba radhi kisha akatoka nje mara moja akiwa na wasiwasi sana, Dokta Hilary alimpuuzia huyo muuguzi sambamba na Moses na Norbert.
Baada ya dakika mbili mlango wa ofisi ya Dk Hilary uligongwa mara mbili, Dk Hilary alimuamrisha anayegonga hodi aingie na hapo akaingia muuguzi wa kike aliyevaa gauni la rangi ya kijani iliyopauka ambalo lilimuishia juu kidogo ya magoti na kuifanya miguu iliyojaa vyema ionekane kwa wote. Alikuwa amesuka nywele kwa mtindo uliompendeza, alikuwa ni mwenye mwili wa wastani wa wastani sura pana mwenye pua iliyo na umbo dogo pamoja midomo mipana iliyopakwa rangi ya mdomo iliyoendana na rangi ya ngozi yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Abee Dokta" Muuguzi huyo aliitikia.
"Phina kuna wageni hawa walihitaji msaada wako kidogo" Dk Hilary aliongea huku akimuonesha Phina wageni hao ambao hawakuwa wageni katika macho yake, kisha akaendelea kusema, "Nafikiri wewe ndiyo uliyemuona yule mwanamke ambaye umesema hujawahi kumuona nesi kama huyo hapa hospitali".
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment