Search This Blog

Friday, 20 May 2022

WITO WA KUZIMU - 5

 







    Simulizi : Wito Wa Kuzimu

    Sehemu Ya Tano (5)



    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    OFISI YA KATIBU MKUU

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda huo ambao waki na Kamishna walikuwa wamekaa kikao cha dharura, Norbert alikuwa ameshatia mguu kwenye ofisi ya wizara ya nishati na madini. Huko alipanga kwenda kuonana na Mhusika mwingine ambaye alikuwa yupo kwenye mzunguko wa pili ndani ya orodha hiyo, alikaribishwa kama alivyokaribishwa alipoenda hukoh awali na Katibu mkuu wa wizara hiyo ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka. Uzito wake pamoja na kazi zake ndani ya jamii ndiyo vilimfanya Katibu mkuu huyo asitishe kuondoka na abaki akimsikiliza yeye kwanza kabla hajaianza safari ya kuondoka hapo ofisini, Kijana huyu machachari alipoketi kwenye kiti tu aliachia tabasamu pana na kisha akamtazama Mwenyeji wake.



    "Ndiyo Bwana Kaila ni adimu wewe sana kuja sehemu kama hizi na ukija basi kuna jambo" Aliambiwa maneno ambayo yalimfanya azidi kutabasamu.



    "Na uadimu wangu ukipungua ujue kuna jambo zito sana" Aliongea akiwa ni mwenye tabasamu.



    "Ndiyo ndiyo leta habari"



    "Mzee wangu nimekuja kukumbusha tu ile kazi uliyoifanya ambayo hukupata malipo sasa ndani ya siku ya Ijumaa utayapata tu"



    "Kazi ipi Kaila mbona sikuelewi unachoongelea, hebu funguka Bwana hatupo kwenye vitadawili hapa"



    "Ile kazi ya kuwasaliti watanzania na kutumia mapato ya wizara hii vibaya pamoja na kumfanya mkuu wako wa kazi aingie rumande basi malipo yake yamefika usubiri ujira wako akija Mheshimiwa Rais"



    "Ndiyo hilo tu Norbert sasa nikuambie hivi wewe bado ni kijana mdogo sana, hayo mambo acha nayo huwezi kufikia malengo yako ya maisha ukijifanya unayafuatilia Kaila. Tutakuzika mapema sana" Katibu mkuu aliongea huku akiminya kitufe kilichopo mezani kwake



    "Kufa ni bora kuliko kuishi na viwavi wanaofuja nchi"



    "Ok sasa subiri utajua kwanini nilikuambia hivi" Alipoongea hivyo Kaitbu mkuu wa wizara aliingiza mkono kwenye meza yake na kisha akaibuka na silaha ya moto.



    "Sasa Mzee wangu bastola kama hiyo ukinifyatulia hapa si itatoa sauti na wewe uje kushikwa"



    "Sijali kuhusu hilo sitofungwa Pesa inaongea" Maneno hayo yalipotoka bastola yake tayari ilikuwa imeelekea kwa Norbert ambaye alikuwa nayo kwa umbali wa mita moja, Katibu mkuu walikuwa amenyoosha mkono wenye bastola kumuelekezea akijua kuwa ndiyo alikuwa amemaliza kazi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitendo cha kuwekewa bastola namna hiyo akiwa amekaa kwenye kiti aliamua kuchekecha akili kwa haraka sana, alimtazama mwenyeji wake huyo akiwa amefikia hatua hiyo ambayo alikuwa hakuitarajia kabisa. Alitarajia angemuona akichachawa kwa taarifa hiyo na badala yake aliwekewa bastola kuelekea lilipo paji lake la uso, mweyeji wake alikuwa ni mwenye uso usio na mzaha hata kidogo alipokuwa amemuwekea bastola hiyo.



    "Kwahiyo pesa ndiyo itakuweka wewe huru siyo?" Aliuliza akiwa na lengo la kutafuta nafasi ya kujiokoa kwani Mwenyeji hakuwa ametambua kama yeye ni kiumbe mmoja hatari sana



    "Wewe kajamba nani unaetupekenyua ili upate cha kujaza kwenye jarida lako tuone huo uzalnedo wako utakusaidia nini" Katibu Mkuu aliongea akiwa ni mwenye kuweka jeuri mbele kutokana na cheo alichokuwa nacho.



    "Tatizo unajidai una jeuri hata unajisahau kama kuna watu wamekuweka kinasa sauti hapo kwenye mfuko wa shati kinarekodi yote" Norbert alitamka kauli hiyo ilimfanya mwenyeji wake atazame mahali ulipo mfuko wa shati lake nadhifu, hiyo ilikuwa ni hila kwani alipotazama eneo hilo alisahau kabisa kuwa alikuwa amefanya kosa ambalo lilikuwa likingojewa kwa hamu san. Kitendo cha kuhamisha macho kuelekea ulipo mfuko wa shati ni jambo ambalo halifai kabisa kwa mtu kama huyo aliyekuwa naye ofisini huyo, mtu ambaye alikuwa na kasi zaidi yake.



    Kitendo cha Katibu mkuu kuhamisha macho hadi kwenye mfuko wa shati lake tayari alikuwa ameweka balaa jingine kabisa, Norbert kwa kasi ya ajabu kabisa aliunyanyua mguu wake mmojwapo akiwa amekaa hapohapo kwenye kiti. Aliupiga mkono wa Mwenyeji wake uliokuwa umeshikilia bastola na kupelekea bastola hiyo ianguke pembeni mbali na hapo. Hakukaa tena kwenye kiti yeye ajifyatua kwa haraka sana na akaruka saraksi moja maridadi sana, baada ya kutua kwenye upande wa pembeni kwa kasi ya ajabu sana alipiga saraksi ya 'roll akaifikia bastola hiyo ambayo aliitwaa na mikono yake.



    Kilikuwa ni kitendo ambacho alikifanya hakikuzidi nusu dakika baada ya mwenyeji wake kufanya kosa la kitoto sana, mwenyeji alipopigwa teke hilo alikuwa akiangalia ilipokuwa ikienda kuangukia bastola yake. Alipokuja kurudisha macho kwenye eneo ambalo alikuwa yupo Norbert hapo, hakumuona kabisa kutokana na wepesi alioufanya. Aliporudisha macho kule ambapo ilikuwa imeanguka bastola yake alimuona akiwa amesimama ameishikilia. Loh! Aliona ni kama alikuwa amefanya uchawi kuweza kutoka pale alipokuwa kusogea pembeni, hakika hakuwahi kumuona kiumbe wa aina hiyo. Alibaki akiingiwa na uoga akiamini kuwa Norbert alikuwa ni mshirikina ndiyo maana alikuwa amefanya hayo ya ajabu ya kupoteza na kutokea pembeni. Alishindwa kuongea kitu chochhote zaidi ya kubaki na uoga wake, alikutana na uso wenye tabasamu pana sana kutoka kwa huyo aliyekuwa amefanya jambo la ajabu hadi akamuweka kwenye hali ya uoga namna hiyo.



    Norbert hakujishughulisha na kuongea kitu chochote alipoona Mwenyeji wake akiwa amekumbwa na uoga, yeye alitoa Kirekodi sauti kama ilivyo kawaida yake na akasitisha kurekodi. Baada ya hapo kama kawaida aliicheza sehemu aliyokuwa ameirekodi na kisha akatulia, mazungumzo yote yaliyokuwa yakiongelewa ndani yaofisi hiyo yaliweza kusikika. Hapo Mwenyeji wake aliingiwa na kihoro sana kwa jinsi alivyokuwa ameingizwa kwenye mtego , alibaki akiwa ameganda asiongee chochote hadi pale Norbert alipositisha kuicheza sauti hiyo kwenye kifaa chake. Akiwa ameganda hivyohvyo asijue la kufanya, alimtazama Mgeni akitoa kibebea risasi cha bastola yake kisha akazitoa risasi zote. Alirushiwa bastola yake ambayo alikurupuka kuidaka huku akimtazama Norbert kwa uso uliojaa huruma sana, huruma hiyo haikubadilisha kitu chochote kwa mgeni wake huyo aliyekuja kumtia homa ya matumbo. Alimshuhudia akigeuka na kuanza kupiga hatua kuelekea mahali ulipo mlango, alipofika mlangoni alimshuhudia akizitia risasi zake zote kwenye chombo cha kuwekea takataka na kisha alitoka nje. Alibaki akimsindikiza kwa macho na si kuongea chochote kwani hakuwa hata na ujasiri wa kuongea, pindi alipotoka tu ndipo alipokimbia hadi kwenye chombo kile cha uchafu akachukua risasi zake na kuzirudisha ndani ya bastola na kisha akarudi kitini. Alitambua kabisa hakuwa na uwezo wa kumfanya kitu chochote Norbert ikiwa atauvuka mlango wa ofisi yake, tayari ameuvuka na kaondoka kwa kutumia ujanja wake.



    ****



    JIONI

    Baada ya kutoka kazini kwake kituo cha kwanza ilikuwa nikwenda hadi eneo ambalo alikuwa ameweka chambo, ni katika eneo ambalo wale vijana wake wote waliokuwa wakimfanyia kazi walikuwa wakikaa na pia kuweka mikakati yao mingine. Kamishna alikuwa akielekea huko akiwa ni mwenye furaha sana kwani alikuwa ameshapata habari nzuri ya kukamatwa kwa mpenzi wa Norbert ambaye alikuwa akijifanya ni jeuri sana. Alipofika kwenye mlango la makao hayo ambayo ilikuwa ni sehemu ya kutengeneza magari iliyojengwa kisasa iliyokuwa haitumiki, aliamua kutoa simu yake mfukoni na kuzitafuta namba za Norbert. Alikuwa yupo jirani na vijana wake ambao walikuwa wakimsubiria kwa hamu sana wakiwa na imani zote kiongozi wao atafurahia kazi waliyokuwa wameifanya, muda si mrefu simu yake ilipokelewa na mtu huyo aliyekuwa anampigia.



    "Kaila kijana wangu hivi una jeuri gani wewe? Tukimchinja huyu hawara yako unafikiri utakuwa kwenye hali gani? Hebu fikiria kuhusu hilo siyo kuzidi kutuletea wazimu wako. Sasa ni hivi nakuomba ujisalimishe mwenye kama unampenda huyu mwanamke la si hivyo utakuta maiti yake....siyo nisifanye hivyo nakupa saa moja tu uonekane eneo la Yombo daraja la Tingatinga uletwe huku la si hivyo utaiokota maiti ya huu hawara wako kesho hapohapo....good boy uende na muda" Alipomaliza kuongea na simu alikatana kisha akawatzama vijana wake akawaambia,"Twendeni mkanioneshe huyo malaya wake".



    Kauli hiyo iliwafanya vijana wake hao wageuke na kuelekea huko walipomueka Happy, waliingia ndani ya eneo hilo hadi kwenye sehemu ambayo ilikuwa na magari mabovu mwengi sana. Walitembea hadi mwisho kabisa wa eneo ambapo kulikuwa na mashine ngumu sana ya gari ambayo ndiyo Happy alikuwa amefungiwa hapo. Muda huo alikuwa akijitikisa sana lakini hakuweza kabisa kutoka, alikuwa amevishwa kofia nzito sana usoni ambayo ilifunika uso wake hadi shingoni. Hakika alimuona ni Mwanamke aliyekuwa na umbo la haja ambalo hata yeye lilimtamanisha sana, kwa umbile hilo aliona kabisa Norbert angejileta mwenyewe.



    Alisubiri kwa muda ambao alikuwa amemwambia Norbert lakini hakutokea kabisa, hilo lilimuudhi na akaamua kumpigia simu kwa mara ya pili tena na muda huo aliweka spika kubwa kabisa. Mlio wa kuita kwa simu ulisikika na muda huo tayari alikuwa amekasirika kwa kutofika kwa Norbert ndani ya eneo hilo, simu ilipopokelewa alikuwa tayari ameshapandwa na jazba kwa kufanyiwa uhuni namna hiyo.



    "Kijana hujui kutunza ahadi zako siyo sasa namkata kichwa huyu malaya wako" Aliongea kwa hasira



    "No! No! No! Kamishna ninakaribia kufika sasa hivi nipo njiani, muweke kwanza nimsikie yeye mwenyewe" Sauti ya Norbert ilisikika, hapo Kamishna alisoge hadi karibu ya Mwanamke huyo aliyekuwa na mvuto ingawa alikuwa na mwili mkubwa kisha akaamrisha vijana wamtoe kitambaa kile kilichoficha uso wake.



    Kitendo cha kutolewa kitambaa kwa Happy ilikuwa ni mshangao mkubwa sana kwa Kamishana, hakika hakutarajia kabisa kuwa angekuwa ni huyo mwanamke ambaye alikuwa ni mtu wake wa karibu sana. Alipotolewa gundi iliyokuwa imeweka mdomoni, bado Kamishna alikuwa amepigwa na bumbuwazi la mwaka.



    "Shemeji wewe ndiyo wa kunifanyia hivi kweli?" Happy aliuliza akiwa haamini kabisa



    "Haaa! Kamishna hongera kwa kutumia nguvu zako nyingi na kumteka shemeji yako, ninataka utambue kuwa mimi sipo njiani wala nini. Nipo kitandani nimepumzika kesho naendelea na kazi yangu ya kuwatia matumbo ya kuhara" Sauti ya Norbert iliyokuwa imejaa kejeli ilisikika.





    Upande wa pili wa maisha yake alikuwa ni mwanaume ambaye alikuwa ni mwenye tamaa sana, fedha alikuwa nazo lakini bado hakuwa akiishiwa na tamaa ya kuztika za ziada. Mke alikuwa anye bado alikuwa haishi kutamani wanwake wengine kila anayekuwa ni mwenye kupendeza macho yake, hilo lilimfanya hadi afikie hatua ya kumtongoza shemeji yake ambaye alikuwa ni mdogo wa mke wake. Kamishna alikuwa akimtamani sana Shemeji yake kwa kipindi cha muda mrefu lakini alikuwa ameishiwa mbinu zote za kumuweka ndani ya umiliki wake, alikuwa hawezi kabisa kutumia jeuri ya fedha kwani huyo Shemeji yake naye alikuwa anazo na hakubabaika kabisa. Kila alipojaribu kuachia chombezo mnaso aweze kumpata aliishia kukataliwa kabisa, alipozidi kumsumbua aliwekewa kitisho cha kusemewa kwa mkewe. Hapo jeuri yoe iliisha na hakuwa na ubavu tena wa kuendelea kumsumbua, umbile la Shemeji yake halikuisha kabisa kumtesa na akatamani kabisa kuwa naye. Alikuwa ameshapuuzia kabisa naye alikuwa ameoa mwanmke mrembo sana ambaye alikuwa na kila kitu ambacho alikuwa akikitamani, sasa tamaa ndiyo ilikuwa ikimuongoza ya kuonja asali ya njiani wakati alikuwa nayo Kibuyu kizima ndani ya nyumba yake. Hadi inafika siku hiyo tayari ilikuwa imepita muda mrefu sana tangu akataliwe na Shemeji yake huyo ambaye alianza kujengea chuki dhidi yake, sasa amemteka bila ya kujua kuwa aliyekuwa akimteka alikuwa ni huyo Shemeji yake ambaye alikuwa amemuonesha ya kila namna ili aweze kumshawishi kuwa naye lakini aligonga mwamba.



    Happy naye alipoona uso wa Shemeji yake mahala hapo alitambua kabisa kuwa ndiyo alikuwa akihusika na mchezo mzima uliokuwa umetokea, aliamini kabisa kwani alikuwa amewekewa chuki naye baada ya kukataa kuwa na mahusiano naye kutokana na kumuheshimu sana Dada yake. Alibaki akimtazama kwa mshngao sans na muda huo uso wa Kamishna ulikuwa umeingiwa unyonge wa hali ya juu,na moyoni alibaki akimtusi Norbert kwa mchezo aliokuwa amemfanyia.



    "Shemeji kisa kukukataa ndiyo unadiriki kuniteka kweli" Happy aliongea akiwa hajui kabisa chanzo cha yeye kuwa hapo, muda huo Kamishna hakujibu kitu chochote aligeuka nyuma na kuwatazama vijana wake. Aliwaashiria kuwaita na wote walisogea karibu yake wakiwa wamekaa kiutiifu sana, uso wake ulikuwa tayari umebadilika kwani aliona vijana hao walikuwa wamefanya uzembe mkubwa sana kwa kumteka yule ambaye hakustahiki kutekwa kabisa.



    "Nyinyi ndiyo niliyowatuma hii kazi, mpenzi wa Kaila ni Shemeji yangu toka lini? Si nawauliza?" Aliongea wa ukali huku akiwatazama wote kwenye nyuso zao.



    "Mimi ndiyo mpenzi wa Norbert Kaila kweli tangu nipo chuo" Happy aliongea na kumfanya Kamishna ageuke na kumtazama usoni mwake, jeuri yote ilikuwa imemuisha kwa kusikia jibu hilo na kisha na alimsogelea karibu Shemeji yake kwani roho yote ya ukatili ilikuwa imemtoka.



    "Samahani sana Shemeji, sikukujua kama wewe ndiyo mpenzi wa yule Mhalifu. Unaowaona hao ni maaskari wote na Kaila amefanya kosa kubwa ndiyo tukatumia njia kwani ametukimbia" Alidanganya maneno ambayo yalimfanya Shemeji yake amuamini, aliamua kumfungulia hapo alipokuwa amemfunga baada ya uongo wake kumkolea kisawasawa Happy na kisha akaondoka naye.



    "Hadi kesho mchana namtaka Norbert Kaila awepo kwenye mikono yenu" Aliongea kwa amri huku akimshikilia Shemeji yake ambaye alikuwa hatembei vizuri kutokana na kufungwa sehemu moja kwa muda mrefu sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****



    Ahueni ya ubavu wake alianza kuiona yalipoingia majira ya usiku kwenye nyumba ya kulala wageni aliyokuwa wamejihifadhi, Askofu Valdermar ndipo alipotoka nje ya eneo hilo akiwa amejikaza kisabuni katika kutembea sawasawa ingawa bado alikuwa yu mgonjwa. Pigo alilokuwa amepigwa na Norbert lilikuwa ni zito sana na laiti kama angekuwa hajabana pumzi wakati anapigwa, yanmgekuwa ni mengine kabisa kwani angekuwa amevunjwa mbavu yake na Komandoo huyo mwenye mchanganyiko wa Ninja. Hakika alikuwa amewezwa sana na hata mawasiliano alikuwa amekata ndani ya siku nzima akiuguza maumivu yake hayo, alikuwa ni mwenye kuletewa vyakula kule chumbani na kuvila tu na hakuwa maetoka nje tangu alipoingia hapo.



    Dawa alizokuwa akizitumia tayari zilikuwa zimempa ahueni ambayo ilimfanya atoke hadi nje kwenda kupunga hewa kidogo, alipokuwa nje huko ndipo alipokumbuka kuwapigia simu watu ambao alikuwa na ushirika nao ili kuwaaambia kila kitu ya kilichotokea kwani aliamini kabisa walikuwa wakimtafuta sana yeye. Hapo alitoa simu yake na kumpigia Meshimiwa Roho kwani alikuwa akitambua kabisa kuwa Mheshimiwa moyo alikuwa hajiwezi na yu kitandani mgonjwa. Simu yake ilipopokelewa tu aliamua kueleza ukweli wa kile ambacho kilikuwa kimetokea hadi akawa yupo kimya namna hiyo, simu yake hiyo aliyokuwa ameitoa taarifa ilikatika ghafla mawasiliano jabmo mbalo lilimfanya aingiwe na shaka kubwa sana.



    "Norbert siku nikikushika nakugeuza supu, umemuua Scrpio na Spider vijana wangu tegemeo. Josephine pia sidhani kama ni mzima" Alijisemea mwenyewe akiwa ameuma meno kwa hasira sana kwani hadi muda huo alikuwa ameshatambua kabisa kuwa vijana wake wote walikuwa wameteketea, hakika hakutegema kabisa kuwa atakuja kuchezewa namna hiyo na kijana mwenye ngozi nyeusi katika nchi ambayo alikuwa akiidharau kila siku kutokana na hali yake ilivyo. Aliona ni kama alikuwa ameanikwa mbele ya hadhira kwa kitendo chake cha kuolewa na mwanaume mwenzie, akiwa amekaa kwenye eneo hilo aliamua kuzitafuta namba za mtu mwingine ambazo alizipiga mara moja na kisha akamueleza juu ya eneo ambalo alikuwepo. Aliahidiwa kuwa angefuatwa mara moja na mtu huyo kwani hakuwa na mwingine angeweza kumuhifadhi kwa muda huo kwa haraka zaidi baada ya kukatika kwa mawasiliano na Mheshimiwa Roho.



    Haikupita hata dakika thelathini gari laki fahari ambalo lilikuwa limeagizwa kuja kumfuata liliwasili, Askofu kwakuwa hakuwa na kitu cha muhimu ndani ya Nyumba hiyo ya kulala wageni aliyomua kulala aliamua kujichukua yeye kama yeye na kuingia ndani ya gari hilo na kuondoka. Safari yake ilikuja kuishia kwenye nyumba ya kisasa kabisa iliyokuwa ipo Tabata Kinyerezi. Hapo gari hilo lilingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo baada lango kubwa lililokuwa likiendeshwa kwa mtambo maalum kufunguliwa. Gari hilo lilienda hadi eneo la maegesho ambako alikuta kulikuwa na mwenyeji wake akiwa anamsubiri, Mwenyeji wake hakuwa mwingine ila ni Askofu mkuu wa kanisa katoliki Kardinali Michael Severine ambaye alikuwa yupo ndani ya mavazi ya kiraia.



    Hapo wote wawili walikumbatiana kwani walikuwa wapo kwenye mnyororo mmoja wa uhaini wa nchi hii, huyu ndiye Askofu ambaye alikuwa yupo pamoja na Askofu Edson kwenye kisa cha WAKALA WA GIZA. Ndiye ambaye alimlaumu Askofu mwenzake kwa kufanya uzembe hadi akauawa kwa uzembe wake, ndiye huyuhuyu aliyeitwa ofisini mwa aliyekuwa Mnadhimu mkuu wa jeshi kupewa kazi maalum akiwa pamoja na Mufti. Walikuwa wapate ujira mkubwa sana kama nchi hii itakuwa imepinduliwa na kisha wao wawafanye raia wakubali mapinduzi haramu waliyokuwa wameyasuka.



    Mambo yalipozidi kombo aliamua kujifanya kinyonga na kisha akalaumu sana kiongozi wa dini ya upande wa pili kwa kushiriki usaliti wa imani yake. Baada ya Rais Zuber kurudi tena kuendela na shughuli zake yeye alimpa baraka zake zote, hii ilisababisha aongezekewe na heshima kwa kitu hicho ambacho haikustahiki apewe heshima hiyo.



    Mpango wa pili wa kuifuja nchi ya Tanzania baada ya ule wa awali kushindikana yeye alikuwepo yupo ndani yake kama kawada, alikuwa bado yupo nao kwani kazi yake ilikuwa haijafikia kwa yeye kuweza kuifanya. Mambo yalipoharibika na kuelezwa kila kitu alituma gari kwa ajili ya kumleta Akosfu ndani ya nyumba yake hiyo ya siri, muda huo alikuwa naye wakiwa wapo hapo sebuleni kwa pamoja.



    "Ndiyo Askofu nipe habari nzima yote" Kardinali Michael aliongea



    "Mambo si mazuri kabisa huko Kadrino, Scorpio na Spider wameuawa na Joesphine katiwa nguvuni" Askofu Valdrmar alieleza



    "Ni nani huyu anafanya haya au kuna mwingine?"



    "Yuleyule kirusi hatari sana ambaye hajazuilika mpaka sasa ndiyo mfanyaji wa yote haya"



    "Inamaana pamoja na kuongeza nguvu bado huyu kiumbe anafanya haya kweli"



    "Huyo ni hatari sana na nilikuwa sijui kama ni hatari namna hii, hadi nilipopamnana naye. Tazama mwenyewe" Askofu Valderma ra alipoongea hivyo alifungua sehemu ya ubavu wake ambako kulionekana ni penye rangi nyekundu kutokana na weupe wake"



    "Huyu ni Norbert?"



    "Ni kiumbe hatari sana na wala sikuwahi kufikiria kuwa kutatokea kiumbe mweusi akanifanya kama hivi, nilikuwa napambana naye kinguvu sana hasa baada ya kujua uhatari wake lakini kutokana na kumuwekea dharau mwanzo haya ndiyo yaliyonikuta"



    "Pole sana Askofu, sasa inabidi upumzike hapa nitakuletea mtu akutibu mimi wacha nikimbie nyumbani kwangu kwani sikuiaga famili huko" Kardinali Michael alipoongea maneno hayo alisimama na kisha akatoka ndani ya nyumba hiyo akimuacha kiongozi wa dini wa kigiza mwenzake akiwa amepumzika sebuleni.



    ****

    [4]

    ASUBUHI ILIYOFUATA



    Siku zinayoyoma nazo na hatimaye zimebaki siku nne tu kati ya siku ambazo alikuwa amepewa Norbert kazi hii iwe kamili, asubuhi ya siku hii alitoka kwenye nyumba yake akiwa anatumia usafiri wake ule ule aliokuwa amepatiwa ofisini. Alivuta mafuta akiwa anaelekea katikati ya jiji la Dar es salaam, safari yake ilikuja kuishia kwenye jengo la Tancot 2 lililopo makutano ya barabara ya Sokoine na barabara ya Pamba katikati ya jiji a Dar es salaam. Ilikuwa ni kwenye makao ya wizara ya uchukuzi nchini, hapo ndipo alipokuwa amepanga kuingia kwa siku hiyo kuendeleza kazi yake iliyokuwa imeunyima kabisa muda wa kuwa karibu na famili yake. Hapo aliegesha pikipiki yake na kuizima na kisha akaweka ulinzi wa pikipiki yake kama ilivyo kawaida yake, alipiga hatua kuingia ndani ya jengo hilo ambalo lilikuwa lina Mlengwa wake ndani ya siku hiyo.



    Tayari Kirekod sauti kilikuwa kipo ndani ya mfuko wake wa suruali, alifika hadi mapokezi kwenye ofisi ya Katibu mkuu wa wizara hiyo aliyekuwa ana uhakika asilimia zote yupo ofisni kwake.

    "Samahani dada habari yako" Alimsabahi Msichana ambaye alimkuta kwenye dawati la Kaitbu Mukhtasi katika ofisi hiyo



    "Safi kaka yangu nikusaidie nini?" Aliitikiwa salamu yake na kisha akaulizwa shoda yake ambayo ilikuwa imemfanya kuja eneo hilo.



    "Ninahitaji kuonana na Mheshimiwa nina mahojiano naye muhimu sana"



    "Nimuambie nani upo hapa?"



    "Mwambie Norbert Kaila yupo hapa" Norbeert alipojibu hivyo yule Msichana ambaye tayari alikuwa ameshanyanyua mkonga wa simu aliushusha mara moja akiwa ameingiwa na mshangao baada ya kusikia jina.



    "Kumbe ni wewe jinsi ulivyo nilikuwa sijakujua, nice smile kama ulivyo uzuri wako" Aliongea huku akimtazama Norbert usoni, alipopewa tabasamu naye alilisifia tabasamu hilo.



    "Uzuri lakini sikuzidi wewe kabisa, ukiongea unabaki kuwa mzuri, ukitabsamu unabaki kuwa mzuri, kila ukifanya unabaki kuwa mzuri. Nahisi ukilia pia unabaki kuwa mzuri vilevile" Maneno hayo yalimfanya atabasmau nusura atake kucheka lakini alijizuia kutokana na simu aliyokuwa ameirudisha sikioni kwa mara ya pili kupokelewa.



    "Haloo! Bosi, Mwandishi Norbert Kaila anakusubiri hapa ana maongezi muhimu sana na wewe........Sawa" Aliweka mkonga wa simu mahala pake na kisha akamtazama Norbert akamuambia, "Kasema usubiri kidogo atakuita uingie."



    Alipoambiwa maneno hayo wala hakuwa na ubishi kabisa yeye alienda kukaa kwenye kiti cha kusubiri, alikaa hapo kwa takribani dakika tano ambapo alimuona Mtu ambaye alikuwa amevaa nguo za Mafundi akisogelea eneo la Katibu Mukhtasi



    "Dada Mzee kaniita huko ndani nikatengeneze koki ya sinki la kunawia" Aliongea fundi huyo



    "Ok ngoja nimpe taarifa" Katibu Mukhtasi aliongea na kisha akanyanyua simu yake na kupiga kwa mara nyingine tena, alisikiliza simu hiyo kwa dakika kadhaa na kisha alikubali amari aliyokuwa amepewa.



    "Unaweze ukaenda.....Norbert pia amekuruhusu uingie ndani anakusubiri huko" Alimuambia pia na Norbert ambaye alijinyanyua kwa taratibu sana,muda huo tayari yule Fundi ambaye alionekana alikuw ni mwenye haraka alikuwa ameshazama ndani ya ofisi ya Katibu wa Wizara hiyo.



    Alijiinua kwenye kiti hicho baada ya kuruhusiwa kuingia humo ndani, alitembea kwa mwendo wa taratibu sana na huku akiwa ameingiza mkono wake mfukoni. Alikiwasha kile kifaa chake alipokuwa ameingiza mkono huo mfukoni na kisha akausogelea mlango wa ofisi ya Mlengwa wake, alipiga hatua kuingia ndani ambapo alitokea kwenye ofisi ya kisasa sana iliyokuwa ina kiyoyozi ndani yake. Ubaridi wa kiyoyozi ndiyo ulimkaribisha kabla hata mwenye ofisi hiyo hajanyanyua mdomo wake kumkaribisha, alikutana na manadhari iliyokuwa imejaa usafi ulipitiliza ambapo mbele yake kulikuwa na Mzee wa makamo aliyekuwa ni mwembamba. Kichwani Mzee huyo alionekana ni mwenye kupungukiwa nywele sehemu ya utosini, alibakiwa na nywele zilizopo juu ya paji la uso pamoja na nyingine zilizoanzia kwenye sehemu ya nyuma baada ya utosi huo. Alikuwa amevaa miwani ya macho ya bei ghali sana ambayo ilimkaa vyema, alikuwa amefuga sharubu za watani .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huyo ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa wizara ya uchukuzi ambaye alikuwa akimlenga ndani ya siku hiyo, alipomuona tu alitabasamu na kisha akapiga hatua kusoge zaidi karibu aweze kumtia homa ya kuhara kama alivyowatia wengine aliowapitia kabla yake. Tabasamu la mwenyeji wake lilimfanya azidi kuwa na hari ya kuweza kumtia homa ya kuhara kwani alikuwa ni mmoja kayi ya waliokuweo kwenye orodha ile, alipopiga hatua hata hakufika hatua mbili. Alisikia kitu kizito sana kikitua kwenye eneo la chini kidogo ya kisogo chake.



    Taratibu alianza kujisikia hali ya kupungua uwezo wake wa kuona na huku kizunguzungu kikali kikimkumba, alipomtazama Mwenyeji wake alimuona akiwa na tabasamu lilelile. Norbert aliishiwa nguu kabisa na alianza kwenda chini kwa taratibu huku akisikia kicheko cha kejeli kutoka kwa Mmiliki wa ofisi hiyo.



    "Kailaa umepata ulichoki.." Maneno ya mwisho kuyasikia ndani ya masikio yake yalikuwa ni hayo, tena hayakumalizika kabisa kwani fahamu zilikuwa zimeshamtoka tayari. Hakika alikuwa amepatikana kabisa kutokana na kuzidiwa mbinu, sasa hana uwezo kabisa wa kufanya kingine chochote.



    Mwenyeji wake pamoja na yule Fundi ambaye alikuwa yupo ndani ya ofisi hiyo ambaye mwanzo hakumtilia maanani, walipeana ishara ya dole gumba. Kitendo hicho ilikuwa ni mpango kabambe uliokuwa umesukwa na ukasukika, wote walibaki wakitabasamu kwa kuweza kumtia nguvuni kwani tayari sifa zake walikuwa wameshazisikia kama alikuwa ni mjanja sana. Mwenyeji wake alinyanyuka pale kitini alipokuwa amekaa na alijongea hadi eneo ambalo Norbert alikuwa ameangukia, alimpiga teke la kumsukuma na kupelekea ageuke chali kwani alikuwa yupo kifudifudi.



    "Simba hachezewi sharubu hata siku moja, sasa kakuparua na kucha" ALiongea huku akimtazama mateka wake kwa dharau kuu.



    ILIVYOKUWA

    Homa ya matumbo ya kuhara aliyokuwa ameachia baadhi ya wale waliokuwa kwenye mtandao wa ufisadi katika siku iliyopita, ndiyo ilifanya Kamishna aweze kukutana na wenzao ambao walikuwa mtandao mmoja aliokuwa akiwajua. Walikuwa wamebaki wawili tu ambapo mmoja alikuwa ni huyo Katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi na mwingine alikuwa ni Kardinali Michael, wote waliambiwa ikiwa ataingia kwenye eneo lao lazima wamuweke kwenye mtego akamatwe. Hilo ndiyo lilikuwa limefanyika bila ya Norbert mwenyewe kujua wala Waheshimiwa kuambiwa kwani haikuwa na umuhimu wa kuwaambia mtu huyo awe amewekwa nguvuni, Norbert alipoingia kwenye eneo la ofisi ambayo ilikuwa na mtego uliomnasa. Hakujua kabisa kuwa tayari kulikuwa na mpango ambao ulikuwa umeundwa, alichojua ni lazima wale waliokuwa amewapitia jana watakuwa wamechnganyikiwa sana kiasi cha kushindwa kufukiria jambo jingine lolote. Hakujua mmmoja wao kati ya aliokuwa amewatembelea jana bado akili yake ilikuwa ipo sawa, ndiyo huyo aliyefanya mipango ya kila namna afute aibu aliyokuwa nayo.



    Alipofika kwnye ofisi ya Katibu Mukhtasi na kumuambia kuwa alikuwa akitaka kuonana na Katibu mkuu, hakujua kabisa kuwa kupewa taarifa Mhusika juu ya kuonana naye ilikuwa ni kama alikuwaa amempa muda wa kusuka mpango. Muda aliokuwa ameambiwa asubiri hapo nje, Mhusika mkuu huko ndani alikuwa akiwasiliana na mmoja wa kijana wao kuja kutekeleza kazi, Kijana huyo alikuwa ni yule Fundi aliyekuwa ameingia ofisini humo. Norbert bila ya kujua aliingia na hapo Fundi huyo aliyekuwa amejibana kwenye mlango alichukua kifaa muhimu sana miongoni mwa vifaa alivyokuwa amekuja navyo. Ilikuwa ni spana kubwa sana itumikayo kufungua koki za maji ndiyo alikuwa ameishika, windo lao lilipoingia kwenye anga zao kilichofuata ni ile spana ambayo ilishuka kwenye kisogo chake na kumpoteza fahamu zote.



    ****



    Haikupia muda mrefu tangu Norbert aanguke, Katibu Mukhatsi aliagizwa na bosi wake mahali na hapo akawa ametoka kwenye eneo lake la kazi. Yule Fundi aliitumia nafasi hiyo iliyokuwa imepangwa na Katibu mkuu kumchukua Teka lao na kisha akaondoka nalo katika eneo hilo, ilikuwa ni hila iliyokuwa imepangwa ya kumtoa yule binti mahali alipokuwa ili waweze kumtoa Norbert ofisini humo na ilifanikiwa. Yule Fundi mhalifu alimshusha Norbert kwenye ngazi za dharura za ghorofa hiyo hadi chini, alimpakia kwenye gari lake alilokuja nalo hapo akiwa na mwenzake humo ndani.



    Baada ya kuingizwa tu humo ndani ya gari alifungwa kamba na kisha, akashikliwa barabara. Safari ya kuondoka hapo wizarani ndiyo ilianza baada ya kazi hiyo kukamilika, ilikuwa ni kitendo ambacho kilikuwa kimefanywa kwa kimyakimya na hakikujulikana na mtu yeyote hyule adi wanaondoka kwenye eneo hilo baada ya kukamilisha kazi yao iliyokuwa imewaleta hapo.



    *****



    Fahamu zilikuja kumrudia Norbert akajikuta yupo ndani ya chumba ambacho kilikuwa na giza sana, alikuwa kafungwa kwenye nguzo moja ndefu sana mithili ya mtu aliyekuwa amesulubiwa msalabani. Mkononi ma miguuni kwenye nguzo hiyo alikuwa amefungwa kamba ngumu sana ambayo ilimuumiza mikono kutokana na kukazwa sana, alipoangaza ndani ya chumba hiko bado hakuwa ameujua alikuwa yupo wapi. Akili ilipokuja kumkaa vizuri alikuja kujua kuwa alikuwa yupo ndani ya chumba ambacho kilikuwa na giza sana, alijua kabisa kuwa alikuwa aameingia mtegoni katika siku ambayo hakutarajia kabisa kuwa angeweza kuingia mtegoni kinamna ile.



    Moyoni alijilaumu sana kwa kufanya kosa la kujiamini kupita kiasi alipoingia ndani ya ofisi hiyo, aliona laiti asingejiamini namna ile basi hayo yasingemkuta kabisa na angeweza hata kujikomboa kutoka kwenye balaa ambalo limempata tayari. Alikuwa yupo ndani ya chumba hicho ambacho kilikuwa hakina dirisha hata moja na kufanya humo ndani kuwe na joto kali sana, giza la humo ndani alipolizoea alikuwa kujua kuwa ilikuwa ni sehemu ya ghala au chumba kimojawao ndani ya kiwanda ambako hakukijua ni kipi. Alikaa ndani ya chumba hicho kwa muda ambao hakuujua kabisa, alikuja kujua kuwa muda ulikuwa umekwenda sana baada ya njaa kuanza kumsumbua kwenye tumbo lake lakini hakujali kabisa. Aliendelea kukaa kwenye mazingira hayo huku nguvu tayari zikiwa zimeanza kumuishia, ulikuja kufunguliwa mlango katika muda ambao hakuujua na hapo alibaini kuwa giza lilikuwa tayari limeingia kutokana na kuonekana hakukuwa na dalili ya mwanga huko nje. Alijua kabisa kuwa chumba hiko alichokuwa amefungiwa kuwa mlango wake haukuwa ndani ya kabisa baada kusikia mlio wa magari ukisikika nje, mlango huo ulipofunguliwa aliona kundi la watu wale waliokuwa wamepatwa na homa ya kuhara aliyokuwa ameisambaza wakiingia humo ndani wakiwa wameongozana na Kamishna. Bi Kishimba,Kaitbu Mkuu waizara ya nishati na madini, Bwana Mushi na yule Katibu mkuu wa wazara ya uchukuzi walipomuona tu walitoa matabasamu yao tu.



    "Kaila umeona matokeo ya ukaidi wako sasa, siku nzima upo humu ndani na hujala chochote" Kamishana aliongea huku akimsogolea karibu.



    "Na hutokula humu ndani uishiwe nguvu na ufe hapohapo, hatutaki kukuua na mikono yetu sisi, yote kwa ubishi wako tu yaani ungekubali hata upokee hongo yetu na uachane na huo upuuzi wako ungekuwa upo mtaani sasa hivi unadunda" Bwana Mushi naye alimsema



    "Sawasawa handsome mwenye mvuto, dawa ya mabinti leo hii utaishia hapo kwenye nguzo kwa ukaidi wako wa kijinga tu. Eti unakataa hela kisa uzalendo wewe, wazalndo na walikuwa kina Hayati Sokoine kijana wangu na nataka ufe huku ukijifunza kuwa upekuzi si mzuri" Mrs Kishimba aliongea



    "Yaani wewe hujui kitu wewe kuhusu hii nchi unajifanya wewe mjuaji sana yaani, tumesoma kwa shida kwenye udogo wetu huku tukishuhudia ulanguzi uliotupa tabu sisi wa chini. Sasa tumeipata nafasi kwanini tusijivunie wewe, nataka ujue uzalendo hakuna sasa hii nipesa tu" Katibu Mkuu wa wizara ya uchukuzi aliongea, muda huohuo yule Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini aliyetaka kumpiga risasi alisogelea karibu huku akicheka sana.



    "Niambie Jet li wangu, si wewe jana uliyeipiga bastola yangu teke na kisha ukaruka pembeni kama unacheza The bodyguaard. Kiko wapi sasa, unaishia kufa kwa upumbavu wako tu. Yaani wenzako waliokuwa wakikaa kimya ulikuwa unawaona wajinga siyo sasa huo upelelezi wako na uandishi wakowa habari ni kwishinei" Katibu wa wizara ya nishati na madini aliongea kwa kejeli.



    "Sijakataa nitakufa ndiyo ila inabidi mfikirie kwa umakini sana juu yenu, nani atapona hapo mnafikiri kuwa ndiyo mtapona hapo. Laptop zote tano zipo mikononi mwa Jama wa Majama. Mtu pkee aliyebakia kati ya watu waliofanya utafiti wakajua kuhusu ufisadi wenu, na anayo ile yenye ripoti kamili. Mkumbuke ni yeye tu anayeweza kuchambua lile neno siri sasa kazi kwenu" Norbert alionge maneno ambayo yaliwafanya wote waliokuwa humo ndani wakae kimya ghafla na wakaanza kutazamana kila mmoja kutokana na habari hiyo iliyiwaletea homa tena.



    "Mimi na wenzangu tulipoitwa Wahanga hamkuwa mkijua maana yake sasa ndiyo hii, sisi ni waandishi tulio tayari kufa na kwajili ya kuongea ukweli tu. Najua nitakufa tu hapa nikifika kesho kwa vidonda vya tumbo na njaa hii ila hilo mkubali kabisa mmekwisha nyinyi, ule ushahidi wenu mkiniomba rushwa upo kamili kwa wenzangu" Norbert aliongea huku akitia chumvi katika maneno yake, hakuwa ni mgonjwa ila aliamua awahadae kwani wangekuwa wapo makini na yeye na hapo ndipo angeweza kuwazidi akili wote.



    "Tunaondoka Kaila ila tutarudi na dawa yako" Kamishna alisema akiwa ameanza kubabaika na kisha alitoka ndani ya chumnba hicho, alifuatiwa na wenzake wote waliokuwa wameanza kuingiwa na unyonge kutokana na maneno ahyo waliyokuwa wameambiwa na Norbert aliyekuwa yupo tayari kwa loloteCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ****



    Ziliopita siku mbili hakuwa amepata chakula na alikuwa akilalamika sana kuwa tuombo likimuuma, hakuwa aliyemsikiliza humo ndani. Baada ya kupiga kelele kwa muda mrefu sana hatimaye majira ya alasiri Norbert alionekana akiwa ametulia tu, walinzi waliokuw wapo eneo hilo walikuja kumuangalia na kuangalia pumzi zake hawakuona dalili ya kupumua kwake. Hilo lilifanya wote kwa pamoja wamshushe hapo alipokuwa amefungwa, walikuwa wakidhani kuwa alikuwa ameaga dunia tayari kumbe ilikuwa ni hila tu. Hakuwa na vidonda vya tumbo wala vya utumbo, walipomuweka chini alianza kizaazaa ingawa hakuwa na nguvu vizuri kutokana na kutokula kwa siku mbili. Alianza kuwachota wote wawili kwa miguu yake aliyozingusha kama feni, walipanguka aliwawahi kila mmoja katika shingo zao.



    Mmoja alimbana na miguu na mwingine alimkamata na mikono yake, ingawa hakuwa kabisa na nguvu hakutaka kabisa kuachia shingo zao hao watu hadi pale walipotulia kuashiria hawakuwa na uhai. Hapo alijinua huku akimpekua mmoja na kuchukua funguo za humo, alifanikiwa kutoka nje ambapo alijikuta akiwa yupo ndani ya ghala ambayo alikuwa akiijua vymea. Ilikuwa ni ghala ambayo ilikuwa ipo maeneo ya Mwembeyanga, kule ambako Josephine alijaribu kumtia nguvuni kwenye kisa cha WAKALA WA GIZA akashindwa. Norbert alipotoka nje tu ya ghala hiyo kwenye sehemu ambayo alikuwa amefungiwa aliuendea uzio wa nyumba hiyo kwenye upande ambao ulikuwa upo karibu na paa la kibanda kidogo kilichokuwa kipo nyuma ya Ghala hiyo. Alipanda hicho kibanda na kisha akashika ukuta na kutoka nje akiwa yupo na uchafu mwingi sana, hapo alijikongoja kwa taratibu sana kwani hakukuwa na umbali mkubwa kutoka pale alipokuwa akiishi ingawa hakuwa akijulikana kama alikuwa na nyumba maeneo hayo. Alifanikiwa kufika Temeke alipokuwa akiishi na aliingia ndani ya nyumba yake, baada ya kuingia ndani kwake alishusha pumzi kwa kuweza kutoroka kule ambako alikuwa amewekwa mateka.



    ****



    Ndani ya siku ilikuwa ni siku ya jumatano ambapo siku mbili tu zilikuwa zimebaki katika muda aliokuwa amepewa Norbert, pia ilikuwa ni siku ambayo Rais Zuber kwa mara ya mwsiho atalala nje ya Tanzania kabla hajarejea nchini siku inyofuata. Ndani ya siku hii agizo jingine lilitoka kwa Rais akiwa yupo nje kabla hajarudi nchini. Agiza hilo lilikuwa ni kuzuia hati zote za kusafiria wa watumishi wa umma mpaka atakaporudi, agiza hilo lilitangazwa kwenye vyombo vya habari jambo ambalo lilizdi kuwashangaza wengi hasa wale waliokuwa watumishi wa umma.



    Kikundi cha watu ambao walikuwa wamejiandaa waondoke nje ya chi mambo yakiwa mabay ilishindikana kabisa, siku ya Jumamosi kulitarajiwa kulikuwa na ziara ya Rais wa marekani nchini hivyo hiyo ilikuwa imewekwa kuwa sababu kuu ya kuweza kuzuia. Watumishi wote wa umma walitakiwa waanze maandalizi mapema sana ya kuampokeaa Rais huyo ambaye mwenyeji wake alikuwa akitangulia siku inayofuata.



    Hilo lilikuwa ni suala ambalo lilipokewa vizuri kwa wafujaji uchumi ndani ya nchi hii, waliamini kabisa kuwa bajeti maalum ingetengwa kwa ajili ya ziara hiyo jambo ambalo walikuwa wakilisubiria kwa hamu sana waweze kuzifuja pesa kwa mara nyingine kabisa. Wengine wale waliokuwa wakihusika walikuwa wameshateuliwa haraka sana na Makamu wa rais, hao waliambiwa kabisa kuwa Rais Zuber akifika tu mapema asubuhi ya siku inayofuata alikuwa akitaka sana kuongea nao baada ya kupumzika na uchovu wa safari.



    Ilikuwa ni neema kabisa kwa wafujaji hao kwani waliona walikuwa wakifuja kwa mara ya mwisho kabla ya kutoroka, waliamini kabisa siku yeyote bomu walilokuwa wakilizuia lisilipuke lingelipuka kutoka na kuwa lilikuwa lipo mikononi mwa watu mwingine kabisa. Walikuwa wakikaa na furaha wakiingojea kwa hamu sana hiyo siku ya kuja huyo kiongozi mwenye jina kubwa duniani ili waweze kujichumia kupitia ujio wake. Waliamini kabisa kuwa serikali ingetenga bajeti kubwa sana kwa ujio wake huyo kwa shughuli mbalimbali na kwakuwa walikuwa wameaminiwa wao waliona ni nafasi yao.



    ****



    Majira ya jioni Norbert alikuwa amesharudiwa na nguvu zake ambazo hazikuwepo hapo awali kutokana na kukosa mlo, alikuwa ameshapata mlo stahiki ambao ulirudisha nguvu zake zilizokuwa zimepotea. Alikuwa pia amehsajisafisha mwili wake kutokana na kuka siku mbili bila kujisafisha, baada ya hapo alitoka na kwenda kule ambako alikuwa amemuacha Jama Wa Majama akiwa amejificha kuwa muda huo ambao hali ya hewa ya usalama wake ilikuwa imetibuka. Alimkuta akiwa yupo kama alivyomuacha, walipoonana kitu cha kwanza kuulizwa iikuwa ni kutoonekana kwake. Jambo hilon diyo alikimbilia kuulizwa kutokana na kuadimika sana, Norbert ilimbidi atumie wasaa huo kumueleza kila kitu ambacho kilikuwa kimemkuta hadi akawa namna hiyo.



    "Ule ni mtandao mpana Kaila uujue hivyo na hawaingiliwi tu" Jama alimueleza



    "Kujiamini sana huondoa umakini naamini sitolifanya kosa hili tena" Norbert aliongea



    "Sasa mpango upo vipi maana Mheshimiwa anateseka tu bila ya hatia yeyote ile"



    "Kuwa na subira Jama mpango kila kitu ni kesho kutwa leo hii wewe pumzika mimi ninaenda kuimaliza kazi"



    "Ok ila majamaa hawajakufinya wale"



    "Hawajanigusa hata eti walitaka nife kwaa njaa nikawa natafuta golden ndiyo hiyo nimeipata"



    "Uwe makini sana"



    "Hilo usihofu kabisa ndugu nipo makini sana" Baada ya kuongea maneno hayo Norbert alinyanyuka na kisha akasema, "nina kiporo cha kuifanya hapa, baadaye panapo majaliwa ndugu"



    "Hamna shida ndugu"



    Baada ya kuagana hapo alitoka hadi nje ya nyumba hiyo akiwa hajatumia usaifri wowote ule, hesabu yake yote ilikuwa ni kwenda kuichukua ile Pikipiki yake ambayo alikuwa ameiacha kule wizarani katika muda huo kwani aliamini kabisa haitokuwa imeondolewa eneo lile kutokana na ulinzi ambao inao.



    ****



    "Jamani mambo magumu huko" Kamishna aliongea majira ya jioni kwenye kikao walichokuwa wameitana kwenye chumba cha hoteli



    "Kuna nini Kamishna?" Bi Kishimba aliuliza akiwa hajaelewa kabisa, swali hilo lilifanya wengine nao waulize kwani alionekana kuwa na uso ambao umechachawa kabisa.



    "Kaila ametoroka kule na kaua walinzi wawili" Aliwajibu wote huku akionekana kachanganyikiwa sana



    "Ooooh! Sasa atatuvua nguo huyu jamani" Bwana Msuhi aliongea akionekan kuchoka kabla hajachoshwa kwaa taarifa hiyo aliyopewa hapo



    "Mushi come down bado muda upo, tujue jinsi gani tunaweza tukaokoka hapa na pia tumnyamazishe huyu" Katibu wa wizara ya uchukuzi aliongea



    "Enhee Shija umeongea hapo si muda wakukata tamaa huu, bado tuna nafasi ya kumshikisha adabu huyu mtoto tusimuhofie kisa yeye ni Mpelelezi wa daraja la juu. Tunaye Askofu naye ni dawa tosha kwake" Kamishna aliongea



    Mida michache baadaye Norbert alifika hadi kwenye jengo la Wizara ya uchukuzi, aliingia ndani ya uzuo wa jngo hilo pasipo kuwa na hofu ya kitu chochote. Alienda hadi ilipo Pikiiki ambayo aliikuta ikiwa ipo palepale ena pembeni kukiwa nagari lililokuwa limeegeshwa. Hakulijali kabisa gari hilo yeye alifika kwenye pikipiki hiyo akatoa ulinzi wake na kisha akipanda. Aliiwasha na kisha akaitoa hadi eneo zuri kabisa kwa yeye kuendesha, hapo aliweka gia na kutoka nayo nje. Aliweka giza nzuri ambayo ilimuwezesha kuondoka kwa kasi hadi alipokuja maeneo ya Kariakoo kulipokuwa na makutano ya barabara ambapo Taa zilikuwa zimewea nyekundu upande wake, upande wa barabra ambayo magari yalikuwa yakielekea barabara ya Kilwa magari yalikuwa yameruhusiwa mengi sana hivyo hakuwa na uwezo hata kujipenyeza avuke maeneo hayo.



    Alipofika eneo hilo ndipo alipoweza kuiona gari iliyo kuwa pale kwenye maegesho ikija hapo, aliamua kujipenyeza katikati ya magari mengine akaenda mbele na kuifanya gari hiyo ibaki nyuma. Alihisi alikuwa anafuatiliwa kutokana na gari hiyo kuwa ipo kwenye mazingira ambayo ni eneo alikuwa amekumbwa na balaa, mataa yaliporuhusu tu alizungusha mafuta kwa nguvu sana kuelekea moja kwa moja ambapo alikuja kuingia kwenye barabara iliyokuwa ikienda mtaa wa Shaurimoyo baada ya kuivuka Shoprite kwenye eneo ambalo Mabasi ya Rahaleo yalikuwa yakianza safari. Alipoingua njia hiyo aliendesha mwendo wa wastani sana kutokana na uwepo reli zilizokuwa zikipita eneo hilo, alipozivuke reli hizo ndiyo alikuja hadi eneo ambalo lilikuwa na sehemu za maduka ya kupangisha baada ya kuvuka makao ya mabasi ya Rahaleo yaendayo jijini Tanga.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapo kulikuwa na kuna sehemu nyingi za fundi wa magari ambapo kulikuwa na sehemu moja ya duka ilikuwa wazi, Norbert alichomeka pikipiki yake ndani ya sehemu hiyo ya kupangisha duka ambayo haikuwa na milango na kisha aliizima na kutulia eneo kama hakuwa ni yeye. Alikaa kwenye eneo ambalo lilikuwa na giza huku akiwa anasubiria kwa hamu sanauyo aliyekuwa akimfuata aweze kufika enep hilo. Haikupita muda kama hisia zake zilipokuwa zinamuambia, kweli gari ile ilionekana na ilikuja kwa kasi sana na kisha ilisimama kwenye tawi la benki ya NB. Aliona mtu akishuka ndani ya gari hilo akiwa ni mwenye kushangaa sana eneo hilo kwani alitambua kabisa angeweza kushuka hapo na asingeweza kuendelea mbele hakumuona alikuwa ameelekea wapi, uwepo wa njia panda mele lazima kungemtatiza na asijue alikuwa ameelekea wapi wapi. Kulikuwa na njia iliyokuwa ikielekea Jengo la Machinga Karume, kulikuwa na njia iliyokuwa ikielea Soko kuu la mitumba la Mchikichini. Pia kulikuwa na njia iliyokuwa ikielea ikielekea mahali ambapo ipo Shule ya Msingi Uhuru, ukiachana na njia ile ambayo alikuwa amepotea mwenye hivyo ni lazima asingejua kabisa alikuwa akieleka upande gani. Alimuona huyo mtu akiuliza sana kwa watu waliokuwa wapo eneo hilo na kisha alipanda ndani ya gari na kuondoka, hapo Norbert alisubiri kwa dakika karibani kumi tangu ilipooondoka ndipo alipoiendea pikipiki yake. Aiipanda pikipiki hiyona kuiwasha kisha akaitoa ndani ya eneo hilo la duka la kupangisha ambalo halikuwa limemaliziwa, aliingia barabbrani na kurudi kule ambako alikuwa ametoka.



    ****



    [1]

    ASUBUHI



    Ndani ya siku hii majira ya asubuhi ilimkuta Norbert skiwa yupo ndani ya jengola wizara ya mambo ya ndani akiwa ameitwa, ulikuwa ni wito wa mkuu wa jeshi la polisi nchini aliyekuwa akiihusudu sana kazi yake kama mwanahabari. Norbert alitikia wito wa IGP Mbwambo ndani ya siku hiyo kwani ndiye aliyekuwa akifanya kazi yake kizalendo miongoni mwa maofisa wachache ndani ya jeshi hilo waliokuwa wakifanya hivyo, muda huo alikuwa yupo ndani ya ofisi hiyo. Alikuwa akitazamana na mandhari ya ofisi huku pia akitazamana na mwenyeji wake ambaye ndiye alikuwa ameuita asubuhi hiyo, siku hiyo Norbert alikuwa yupo ndani ya vazi nadhifu la suti yenye nyeusi iliyokuwa imemkaa vyema na usoni alikuwa na miwani ya giza ambayo ilizidi kufanya muonekano wake uwe wa kipekee.



    "Ndiyo IGP" Alimuambia mwenyeji wake baada ya kufika kukaa hapo kwenye kiti ikiwa zimepita sekunde kadhaa tangu wasalimiane.



    "Norbert natambua wewe ni mwandishi mmojawapo kati ya waandishi wenye kuaminika ndani ya nchi hii" IGP Mbwambo aliongea huku Norbert akitikisa kichwa kuashiria alikuwa anamuelewa. Aliendelea kusema, "siku mbili zijazo ijayo yaani siku ya Jumamosi ndani ya nchi hii Rais wa Marekani anatarajia kuwasili hapa nchini kwa ziara maalum, hivyo katika kikao hicho cha kupanga maandalizi ya mwishoni unaombwa wewe kuwepo kwani Mheshimiwa atakayeongoza kikao hicho atawasili leo hii muda wowote kuanzia hivi sasa akitoka ziarani. Leo atapumzika na kisha kesho ndiyo siku maalum ten asubuhi"



    "Sawa nimekuelewa, lakini kwanini hamkuteua Mwandishi mwingine wa habari mpaka mkaniteua mimi tu?"



    "Usiri wa kikao hicho ndiyo umefanya wewe uteuliwe kwani tunatambua kabisa hakuna awezaye kukaa na mambo nyeti kama haya miongoni mwa wanahabari isipokuwa wewe tu. Wengi wa wanahabari wanfanyakazi kimaslahi zaidi hivyo wewe ndiyo mtu pekee ambaye unafanyakazi kizalendo na unweza kukaa na jambo ambalo halitakiwi kusemwa ingawa ukilisema linakuingizia pesa sana"



    "Sawa nimekuelewa utaratibu ni upi?"



    "Kwanza shika hii kadi ni maalum kesho kwa ajili ya kikao hicho Ikulu, ukifika langoni utaonesha na wewe utaruhusiwa kuingia" IGP Mbwambo aliongea huku akichukua kadi maalium iliyo na mfumo wa kitambulisho cha kuvaa shingoni akampatia.



    "Sawa nimekuelewa hamna tatizo"



    "Kikao hicho kinahusu jinsi ambavyo mtajipanga kwenye kuwasili kwa Raisi huyo mgeni wetu hakuna kingine, kamera na vinasa sauti ni marufuku kabisa usije ukasema sikukuambiwa yakikukuta ya kukuta"



    "Worryout IGP natambua nini nachofanya"



    "Ok sina la ziada unaweza kwenda, tutakutana kesho Ikulu kwenye kikao hicho"



    "Nashukuru sana" Norbert alisimama bada ya kutoa shukrani hiyo na kisha alipeana mkono na IGP MBwambo, baada ya hapo alitoka nje ya ofisi ya IGP.



    ****



    SAA NNE ASUBUHI



    Ndege ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzani maarufu kama 5H-ONE ilionekana ikishuka taratibu kwenye eneo maaluum ambalo ndege hushuka, ilikuwa ipo kwa kasi sana muda huo ilipokuwa inatua. Ilikuja kushuka chini kabisa na kisha matairi yake yalitoka, taratibu iligusa ardhi ya Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kisha ikakimbia juu ya uwanja huo kwa kasi sana hadi eneo maalum la kutua ambapo kulikuwa kumewekwa zulia jekundu juu yake. Hapo ndipo iliweka kituo chake baada ya kupunguza mwendo, wanausalama mbalimbali walikuwa wamejipanga kenye uwanja huo katika muda ambao mlaago wa ndege hiyo ulifunguliwa. Alionekana Rasi Zuber akiwa ni mwenye tabasmau kubwa akishuka kwenye ndege hiyo kwa mwendo wa taratibu sana, heshima juu yake zilitoka kwenye muda huo aliokuwa akishuka ndani ya ndege hiyo akiwa yupo ADCwake kwa nyuma aliyekuwa amebeba vitu vyake muhimu.



    Baada ya kupokea hesima zote muhimu aliongozwa na walinzi wake ambao walikuwa wakitoa ulinzi wake wa hali ya juu, walienda hadi sehemu maalum amapo kulikuwa na msururu wa magari yaliyokuwa yakitumika kwenye msafara wake yakiwa yamejipangwa vilivyo. Aliingia ndani ya gari ambalo alitakiwa awepo ndani yake katika muda ambao alikuwa akielekea Ikulu, baada ya muda mfupi msafara huo ulianza kutoka hapo uwanja wa ndege kwa mwendo wa wastani hadi ilipo Barabara ya Mwalimu Nyerere. Uliingia barabara ya Mwalimu Nyerere kwa mwendo wa kasi kutokana na barabara kuwa imeondoloewa magari yote kwa muda huo, ving'ora vya Pikipiki kadhaa zilizokuwa zipo mbele ya safara huo vilisikika kwa nguvu sana katika muda ambao Maaskari wa usalama barabarani ambao ndiyo walikuwa madereva wa pikipiki hizo walikuwa wakivuta mafuta kwa nguvu sana kuendana na kasi ya msafara huo ilivyo.



    Baada ya dakika takribani kumi na tano msafara huo ulikuja kuingia ndani ya eneo la Magogoni na kisha ukaelekea moja kwa moja hadi Ikulu iliyokuwa ipo ndani ya kata hiyo. Ulifikia mlangoni kwenye mlango ambao ulikuwa na nembo ya taifa katikati, ulikuwa ni mlango wenye kuongozwa na mitambo maalum ya umeme ambapo ulijifungua wenyewe huku ile nembo ya Taifa iliyokuwa ipo katikati yake ikigawanyika.Uliingia ndani kabisa hadi kwenye eneo maalum ambalo Rais Zuber alishuka huku akipata mapokezi mazuri ya kurudi safari kutoka kwa Mke wake pamoja na vijana wake waliokuwa wakimsbiria kwa hamu sana aweze kufika hapo ndani ya siku hiyo. Rais Zuber aliingia ndani ya Ikulu ambapo aliendea kukaa na familia yake moja kwa moja baada tu ya kukaa nje kwa muda wa siku kadhaa bila kuonana nayo.



    ****



    Huo ulikuwa ni muda ambao wale waliokuwa wakihitajika kwa ajili ya kikao iku inayofuata walikuwa wakiandaa maandalizi ya kuelekea huko, karibu kila ambayo alikuwa na jeuri ya pesa alikuwa akifanya kufuru ya maandalizi hayo kutokana na siku ambayo walikuwa wakienda kuonana na Rais Zuber. Ilipofikia majira ya mchana tu tayari walikuwa wameshayanufaisha maduka mengi yaliyokuwa yakiuza vitu vya bei ghali san, karibu kila aliyekuwa kihitajika kwenye kikao hicho alikuwa amenunua kitu kipya atakachokitumia kwa ajili ya kikao hicho na pia kwa ajili ya siku moja mbele baada ya kikao ambayo walikuwa wamepewa taarifa ya uwepo wa ugeni mkubwa sana nchni ambao haukuwa ukijulikana na vyombo vya habari vya Ughaibuni, ugeni huo ulikuwa una sababu maalum na ungeweza kuwasili hapo ndani ya muda wowote.



    Hivyo walifanya maandalizi hayo ya kuongeza vitu ambavyo vingine walikuwa navyo hadi wakawa hawawezi kuvirudia, walikuwa wakizitumia kwa nguvu sana fedha zilizopatikana baada ya kubanwa kina Baba Kabwela huku wale ambao walitakiwa kuingizia serikali wakiwa wanawakingia ngao lilipokuja suala la kulipa kodi ili nchi inufaike na kodi zao. Hakika hawakujali kabisa kuwa hizo fedha zilikuwa zikihitajika kwa ajili ya kuendesha maendeleo ndani ya nchi hii wao walichojali ilikuwa ni kuzitumia tu, walikuwa wakilipwa kiasi kikubwa sana cha pesa kama mshahara pamoja na marupurupu meingine lakini wao walikuwa wasioridhika kabisa. Muda huo walikuwa wakichukua mavazi hayo ili waende kula pesa za wananchi vizuri baada ya kusikia kulikuwa na ziara kubwa iliyokuwa ikiingia hapo nchini kutoka nje ya nchi. Waliona hiyo ndiyo ilikuwa ni nafasi pekee ya kuweza kuzitumia tu pesa za wananchi kwa ajili ya ziara hiyo, kwani ilikuwa ni lazima itengwe bajeti kwa ajili yake



    Magari mbalimbali ya kianasa waliyokuwa wakiyatumia yalikuwa yakiranda kwenye maeneo mbalimbali yaliyokuwa yakiuzwa bidhaa mbalimbali ghali kwa ajili ya wao kununua vitu hivyo. Walikuwa wameacha sehemu zao kazi zikiwahitaji sana kwa ajili ya kuzidi kuleta maendeleo wakaja huko ambapo walikuwa wamejali maslahi yao binafsi tu, hawakujali kabisa kama kuondoka kwao ndani ya ofisi walikuwa wa ilikuwa ni pigo kubwa sana kwa maendeleo ya taifa hili ambalo bado lilikuwa halijafikia hadhi ya kuitwa taifa lililoendelea. Ujenzi wa taifa muda huo ulikuwa unafanyika wajenzi hawa walikuwa wakitega kujenga huku wengine wakiwa wanafuja vifaa ambavyo vingetumika kwa ajili ya ujenzi wake. Hawakujali hiyo ilikuwa ikirudisha nyuma muda uliokuwa umepangwa kwa ajili ya kufikia maendeleo wao waliendelea kufuja tu hizo mali.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ilipotimia saa nane kamili Mheshimiwa Mahujuraja ambaye alikuwa ametoka hospitalini siku iliypita alienda moja kwa moja hadi kwenye gereza la Ukonga, huko aliomba kuonana na waziri mwenzake ambaye alikuwa na tuhuma nzito sana. Kutokana na uzito wake alikubaliwa mara moja na akapelekwa kwenye chumba maalum ambacho alikuwa akitakiwa kuonana naye, hakupelekwa kwenye eneo ambalo lilikuwa likitumika na wale wote waliokuwa wakifika hapo gerezani kuwaona watu wao wa karibu. Alipelekwa huko kutokana na wadhifa wake na hakutaka aonekane kama alikuja kumtembelea huyo anayechukiwa na watanzania, walipoketi kwenye kiti wote wawili walikuwa wakitazamana kwa muda wa sekunde kadhaa hadi pale mmojawapo akanyanyua mdomo na kuongea.



    "Umefuata nini Mahujuraja?" Mheshimiwa Kabinuki alimuuliza



    "Kabinuki come on kwani nikija kukuona wewe mwanachama mwenzangu na pia uliyekuwa nami Bungeni ni kosa?" Mahujuraja liongea



    "Ok, nakusikiliza maana wewe katika watu waliokuwa wamenihukumu ulikuwepo ukionesha hukunidhania. Sema kilichokuleta fisadi mkubwa wewe"



    "Kabinuki sasa huko kuvunjiana heshima mimi fisadi wewe"



    "Asiyekujua nani wewe na kwa taarifa yako jua mwisho wako umefika" Mheshimiwa Kabinuki alipotoa kauli hiyo mwenzake alianza kucheka kwa nguvu sana huku akimtazama kwa dharau.



    "Sasa wewe uliye siye fisadi mbona upo humu ndani?"



    "Nawaambia ipo siku ukweli utajulikana tu mafisadi nyinyi"



    "Hiyo siku ni lini tena huoni kama jumatatu unapandishwa mahakamani kule Mahakama kuu, unavyojua kabisa kuwa kesi yako Mhshimiwa alitoa amri iendeshwe haraka. Utaendelea kuisubiri hiyo siku hadi unaingia gerezani"



    "Mungu hamtupi mja wake"



    "Kama hakutupi mbona kakuacha huku nyuma ya nondo ukilia kama mtoto wa kike aliyepewa talaka, Kabinuki umekwisha wewe si ulijifanya una mdomo sana. Sasa kaa hapo ukisubiri Mheshimiwa aje kujua ukweli ndiyo akutoe, subiri tu huenda taoteshwa"



    "Nitukane unavyoweza ila jua nikitoka hapa nitakuja kuwarudisha haya yote uliyoniambia wewe na Liwale mkiwa mpo nyuma ya nondo"



    "Hizo ni ndoto za alinacha tu, subiri hivyohivyo hadi jua lizame sisi tunakula maisha mtaani wewe ukiendelea kula dona la humu maana Mheshimiwa kasema hakuna mlo maalum kwa ajili yako humu. Kwaheri ndugu" Mheshimiwa Mahujuraja alipoongea maneno hayo aliondoka ndani ya chumba hiko huku akicheka kwa nguvu sana, alikuwa akimkejeli waziri mwenzake aliyekuwa amewekwa hatiani nyuma ya nondo.



    Mheshimiwa Kabinuki alibaki akiwa na uchungu mkubwa sana baada ya Mheshimiwa mwenzake aliyekuwa na uhuru kuondoka, alijua kabisa kuwa aliyekuwa akistahiki kuwepo ndani ya eneo hio alikuwa ni yeye lakini kutokana na mchezo mchafu aliochezewa yeye ndiyo aliingia ndani ya gereza hilo. Ushahidi ambao ungeweza kumuweka huyo aliyekuwa akimkejeli nyuma ya nondo haukuwepo kabisa ndiyo maana alikuwa akitaabika yeye baada ya kukutwa na vidhibiti vyote vilivyokuwa ni muhimu san kwa ajili ya kesi hiyo. Hakika alikuwa amepewa kesi ya kuiba Ng'ombe kwa kuwekewa mifupa ndani ya eneo lake, huo ulikuwa ni ushahidi tosha wa tuhuma hiyo ya kuiba Ng'ombe ambayo ilikua ikimkabili hakukuwa na ushahidi mwingine ambao ungeweza kumnusuru.





    ****



    Muda ambao alikuwa akiondoka Mheshimiwa Mahujuraja ndiyo muda ambao Norbert alikuwa akiingia kwenye nyumba moja ya kifahari sana iliyopo maeneo ya Mbezi. Alikuta mwanamke mtu mzima aliyekuwa amevaa kiheshima sana, alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa ni mchangamfu sana alidhihirsha uchanganmfu wake. Norbert alikaribishwa hadi ndani ya nyma hiyo kwa uchangamfua mkubwa sana kutokana na heshima aliyokuwa ameionesha kwa mwanamke huyo. Ndiyo matokeo ya uchangamfu huo aliokuwa ameupata hapo nyumbani, alikaribishwa hadi ndani ya nyumba hiyo ambapo alikaa kwenye kochi akiwa yupo sambamba na Mwenyeji wake.



    "Karibu san mwanangu" Alizidi kukaribishwa na mama huyo



    "Asante sana mama, Baba Askofu nimemkuta?" Norbert aliitikia ukaribihso huo kisha akauliza.



    "Kabisa mwanangu umemkuta tena alikuwa akijiandaa kutoka ungechelewa kidogo usingemkuta"



    "Sawa mama huu mguu ulikuwa wake"



    "Haya ngoja nikamuite sasa hivi" Mama huyo aliongea na kisha alielekea kwenye upande mwingine wa vyumba hivyo kwenye eneo ambalo lilikuwa na ukumbi mwembamba , zilipopita dakika takribani tano tangu aondoke aliingia Kardinali Michael akiwa ni mwenye usio na furaha kabisa kutokana na ujio huo wa adui yake



    Alibaki akimtazama tu akiwa hata hajaketi kwenye kiti, Norbert alipomsalimia kwa uchngamfu yeye alikaa kimya tu na wala hakujibu salamu hiyo kutokana na kutofurahia ujio wake. Hilo halikumzuia kabisa Norbert asiendelee kutabsamu kwani alitambua Kardinali Michael hakuwa na ujanja kabisa baada ya kuwa yupo ndani ya nyumba ambayo kulikuwa na familia yake na si nyumba ile ambayo ingekuwa yupo yeye na wenzake.



    "Baba Askofu wa nchi hii si nakusalimia jamani" Askofu alimuambia



    "Kaila najua hukuja kwa heri hapa nyumbani kwangu naomba useme kilichokuleta na kisha uondoke upesi" Aliongea kwa sauti ya chini iliyojaa ukali



    "Baba wewe si mtumishi wa Mungu jamani au biblia inakutuma ndiyo utuambie namna hiyo wanakondoo wako, mgeni kwako ni kiumbe kingine kichopaswa kupokewa kwa namna ya kipekee kabisa jamani si namna hiyo baba yangu" Maneno hayo yalipomalizwa yakiongelewa muda huonuo Kardinali Michael alijibandika tabasamu usoni mwake la ghafla sana, akiwa kwenye tabasamu hilo alionekana mtumishi wa ndani wa nyumba hiyo akileta vinywaji ambavyo aliviweka mezani kwenye eneo ambalo halikuwa mbali sana na alipokuwa Norbert akiwa amevamia ndani ya himaya ya adui yake.



    "Karibuni" Mtumishi wa nyumba hiyo aliwakaribisha akiwa na tabasamu pana huku akimtazama bosi wake, ilimbidi Kardinali Michale ajongee hadi kwenye meza hiyo na akatwaa bilauri mojawapo ya kinywaji hicho. Mtumishi huyo alipomuona bvosi wake amechukua kinywaji, alitoka kwenye eneo hilo kwani alitambua kabisa alikuwa hahusiki na maongezi yaliyokuwa yanaendelea hapo.



    "Haya sema kilichokuleta hapa" Kardinali Michael aliongea kwa suati ya chini



    "Baba Askofu ndiyo namna ya kumpa ukarimu mgeni hiyo uliyojifunza kupitia sheria za dini, ok tuachane na hayo nimekuja kukupa ujumbe murua sana" Norbert aliongea



    "Usizunguke Kaila sitaki mchezo kwenye masuala kama haya hadi familia yangu wajue"



    "Ok nimekuja kukuambiwa hivi kesho ni arobaini yenu"



    "Unaongea nini wewe?"



    "Naongea habari iliyotokana na sentesi, ambayo ilitokana na vichazi ambavyo vilitokana na kuundwa kwa maneno hadi yakaleta maana. Kesho ndiyo mwisho wenu"



    "Kama umemaliza toka nje ya nyumba yangu haraka sana"



    "Natoka ndiyo ngoja nimalize hii juice maana nimeandaliwa mimi, ni wasifu wafanyakazi wako kwa kujua kutengeneza Juice namna hii Bba Askofu" Alipoongea hivyo alikutana na uso ambao uliojaa chuki sana kutoka kwa Askofu ambaye alikuwa amekerwa sana na ujio wake, hilo hakulijali kabisa yeye aliachia tabasamu pana. Alimuambia kwa mara nyingine, "Hivi umejiandaa vipi kuingia ndani ya gereza lile lilichongwa katikati ya Mlima kule Iringa maarufu kama Nyumba ya giza, utaiacha vipi familia yako na utaficha wapi uso wako na aibu hii"



    "Kaila nakuambia kama huna la maana uondoke"



    "Tulia basi hebu fikiri kwanza nikiondoka muda huu utamjibu nini mke wako kwani atahisi kuna namna"



    "Sijali hilo mimi"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Ok kama hujali ila ni hayo nilikuja kukuambia si unajua kama mwenye kujua kila kitu kuhusu ripoti amepatikana sasa ujiandae. Jama Wa Majama yupo uraiani" Norbert alipoongea maneno hayo alimaliza Shurubati iliyokuwa ipo kwenye bilauri yake na kisha alisimama juu.



    "Muite mama nimuage basi huoni itakuwa ni vibaya kuondoka wakati kanikaribisha kwa heshima sana" Aliongea huku akimtazama Kardinali Michael usoni, yeye hakuwa na ujanja kabisa kutokana maneno ahyo aliyokua akiambiwa. Ilibidi tu amuite mke wake ambaye alitoka hadi hapo alipo, aliagana na Norbert akiwa na uchangamfu uleule huku Mumewe naye akivaa tabsamu la bandia kutokana na kutokuwa na furaha muda mchache uliopita tangu alipotembelewa na huyo Adui aliyeigiza kama rafiki mbele ya mke wake.



    Norbert naye alipomaliza kumuaga mke Kardinali Michael hakutaka kabisa kuendelea kubaki kwenye eneo hilo, aliondoka kwa mwendo wa taratibu huku akisindikizwa na wenyeji wake hadi nje alipoegesha Pikipiki yake. Aliipanda kisha akaiwsha na kuvaa kofia la kichwani, aliwapungia mkono wenyeji wake na kisha aliweka gia kuiruhusu pikipiki hiyo ianze kuondoka. Alitoka hadi nje ya nyumba hiyo na aliendesha pikipiki hiyo hadi kwenye eneo ambalo lilikuwa na kituo cha kujaza mafuta, hapo aliegesha kando akiwa si mwenye hitaji la kwenda kujaza mafuta kwani Pikipiki ilikuwa mafuta ya kutosha ya kuzunguka hadi anamaliza kazi yake. Hapo alitoa simu yake ya mkononi nyingine kabisa tofauti na aliyokuwa nayo awali ambayo iliishia mikononi mwa maadui zake baada ya kumteka, aligusa mara kadhaa kwenye kioo hicho cha simu yake na kisha akaiweka sikioni baada ya kupata kile ambacho alikuwa anakitafuta



    "Nahitaji sasa hivi uje Nyumbani kwa Kardinali, ufuatilie nyendo zake zote uje kunipa taarifa baadaye" Baada ya hapo alikata simu kisha akaiweka mfukoni na aliondoa Pikipiki kwa kasi kubwa sana, hakuwa na muda wa kupoteza yeye alikuwa ameamua kumaliza kazi kwani alikuwa amebakiwa na siku moja tu ambayo ilikuwa ni inayofuata baada ya hapo atakuwa ameenda nje ya maagizo.



    ****



    GEREZA LA NYUMBA YA GIZA

    KATIKATI YA MILIMA

    IRINGA



    Helikopta ya kampuni ya EASA ilionekana ikishuka kwa taratibu san katika eneo la ndani ya gereza hilo ambalo lilikuwa limenjenga katikati ya milima iliyokuwa mkonai Iringa ambayo ilikuwa imetobolewa kwa katikati. Helikopta hiyo ilikuwa ikishuka kwa taratibu sana kwenye eneo ambalo ndani yake kulikuwa na gereza jipya ambalo lilikuwa limejengwa kwa waliokuwa wakifanya matukio makubwa ndani ya Tanzania. Ujenzi wa gereza hili ulikuwa umelifanya liwe gereza kubwa nchi nzima na hakukuwa na gereza ambalo lilikuwa kubwa kushinda hili, lilikuwa limejengwa kwa taaluma ya juu wahandisi waliokuwa wameagizwa kutoka China ambao walipasua milima hiyo kati na kupelekea uwazi mkubwa sana ndiyo wakalijenga hilo Gereza. Eneo la katikati kulikuwa na shimo refu sana ambalo lingegharimu karibia ghorofa tisa kiurefu kuweza kufika juu mtu akitokea chini, hii ilifanya iwe ngumu sana kwa mtu yeyote kutoroka ndani yake kwani hakukuwa na njia ya kutokea nje. Wafungwa waliokuwa wakiletwa ndani ya Gereza hilo walikuwa wakiletwa kwa kutumia Helikopta na hakukuwa na usafiri mwingine wowote wa kuwaleta kwenye neo hilo, ndiyo maana ikaitwa Nyumba ya giza ,asilimia kubwa ya eneo la ndani ya gereza hilo kulikuwa ukiongozwa na mataa maalum kwani mwangaza uliokuwa ukiingizwa ndani ya gereza hilo ulikuwa ni mdogo sana



    Helikopta hiyo ilipofika chini tu tayari maaskari wa jeshi la Magereza walikuwa wameshafika jirani nayo wakiwa na silaha nzito, ilikuwa imetua kwenye eneo maalum lililokuwa limejengewa kwa ajili ya kutua. Maaskari hao walikuwa tayari wameizunguka Helikopta hiyo wakiwa na silaha kwani walikuwa wakijua kabisa walikuwa wanakuja kupokea Mhalifu mwingine mkubwa, wahalifu wa eneo hilo wote walikuwa ni tishio hivyo ulikuwa ni muhimu katika kipindi chote wanaletwa kwani uzembe mmoja tu wangeweza kufanya maafa makubwa sana. Kila Mhalifu aliyekuwa akiletwa humo ndani alikuwa na utukutu wake, hakuna ambaye aliyekuwa humo ndani hakuwahi kabisa kukutwa na tuhuma ya kuua au kufanya balaa zito. Asilimia kubwa waliokuwa wakiletwa humo walikuwa ni wale Magaidi na waliokuwa na makosa mazito sana.



    Helikopta ilipositisha kuzungusha upanga wake mlango mmoja ulifunguliwa, na kisha mwanamke ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kawaida alishushwa akiwa amefungwa pingu kwenye mikono yake yote pamoja na miguuni. Mwanamke huyo alikuwa amefunikwa uso wake na aliposhuwa tu alikuwa ameshikiliwa mikononi na maofisa wawili waliokuwa wamevaa nguo nyeusi zilizo katika mfumo wa gwanda ambazo hutumiwa sana na wanausalama wa EASA wale waliokuwa kitengo kingine ambacho kilikuwa na sare kama jeshi. Maafisa haoo waliposhuka tu heshima za kutoka kwa wanajeshi wa jesi la Magereza ilitoka na kisha wakasogela karibu, walipeana mikono wanausalama hao na yule Mwanamke alichukuliwa na kuwekwa kwenye mikono ya jeshi la Magereza.



    "Mzigo wenu huo, huyo ni hatari sana zaidi ya hao wanawake wote walokuwa wapo ndani ya gereza hili. Mchungeni sana atakaa humu hadi pale atakapohukumiwa na akihukumiwa atarudi tena humuhumu haya ndiyo maisha yake" Mmoja wa maofisa wa EASA ambaye alikuwa mkubwa kuliko wengine aliongea.



    "Usijali Kamnda amefika huyu hatoweza kutoroka" Afisa mmoja wa jeshi la magereza aliongea na kisha aliitoa kofia iliyokuwa imefunika uso akakutana na sura ya Josephine Msichna mrembo sana. Afisa huyo alimtazama Josephine usoni kisha akasema, "honekani kabisa kuwa ni mahlifu huyu ila hawa ndiyo zaidi ya hatari kabisa"



    "Ana kesi ya kuua maelfu ya watu jijini Dar huyu, hivyo ujue nii zaidi ya hatari, chungeni sana huu urembo wake usije ukawahadaa mkautaka huo mwili ulio na umbo lenye kuvutia mtajuta sana na atatoroka huyu" Aifa wa EASA aliongea



    "Ha! Ha! Ha! Ha! Hakuna jambo kama hilo litakalotokea sisi tunajali kazi yetu siyo kuendekeza tamaa"



    "Msione nawadhania dhana mbaya natambua kabisa maisha ya humu kukaa muda mrefu wanaume nyinyi mnazidiwa hapo muweke makini sana sisi tumemaliza wajibu wetu. Akitoroka huyo ndani ya gereza hili lililoshindikana kupatania ya kufanya hivyo mkuu N001 atajua ni nyinyi sasa mjichunge sana nafikiri huyo mkuuwetumnamjua sana"



    "Usihofu kabisa halitatokea hilo ndani ya gereza hili"



    "Haya sisi hatuna la ziada tunaondoka" Baada ya hapo wote waliagana kwa namna ya kipekee sana, maofisa wa EASA wote walipanda helikopta yao n kuondoka katika eneo hilo. Maofisa wa jeshi la magereza waliokuwa wamempokea Josephine waliingia naye hadi ndani ya gereza hilo ambako kulikuwa na vyumba vyenye taa tupu, walitembea kwa mwendo mrefu sana wakashuka ngazi mbalimbali ambapo walikuwa wakielekea chini zaidi ya gereza hilo ambalo lipo katikati ya Mlima. Walifika kwenye ofisi maalum baada ya kutembea kwa mda mrefu kisha wakamkabidhi kwa Maaskari wa magereza wa kike na wakaondoka, alipokabidhiwa tu aliingizwa moja kwa moja kwenye chumba maalum ambapo alitolewa nguo zote.



    Zoezi la ukaguzi lilianza kwani walikuwa wakihofia huenda akawa ameingia na silaha humo ndani, baada yakuridhika kuwa hakuwa na silaha walimpatia nguo nyingine ambazo ni sare ya wafungwa gereza zenye rangi ya machungwa. Hapo walimpelekea hadi chumba kingine aliandikishwa kisha akatolewa, alikuwa akipelekwa kwa mkukuu sana kuelekea huko kulipokuwa na chumba cha kufungiwa. Mwendo huo aliokuwa akipelekwa ulikuwa ni kukera sana na ambapo alifikia muda akaamua kuwekwa mgomo kwani alikuwa hapendi kuonewa namna hiyo.



    Joephine hakutambua kabisa kuwa humo ndani kulikuwa na wajeuri watupu hata hao maaskari wenyewe walikuwa ni wajeuri pia ingawa walikuwa wamejipamba na kuonakana walikuwa warembo sana. Kugoma huko kwenda akiwa hajakaa sawa bada ya kugoma alichotwa mtama ambao ulipeleka chini mzima kutokana na pingu alizokuwa amefungwa. Akiwa hajaka swaa huko chini alipoanguka alipigwa virungu ambavyo havikuwa na idadi kabisa na hapo alijuta kabisa kugoma, alpokuwa akitoa ukelele wa maumivu wala hakujaliwa kabisa na Maaskari hao wanawake walio jeuri kupitiliza. Alipozidi kelele aliongezewa mabuti kabisa ya sehemu mbalimbali za mwili wake, alitulia mwenyewe huku akigulia maumivu kwani hakuona faida yeyote ya kupiga kelele.



    Wale Maaskari wanawake walipoacha kumpiga walimuinua juu kinguvu na kisha wakamtazama jinsi alivyo, Josephine alikuwa na manundu katika sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na kipigo hiko alichokuwa amepewa na watukutu.



    "Leta ubishi tena tunakuvunja miguu, ukijifanya umepinda jua sisi tumenyongorota ndiyo maana tukatolewa magereza ya kawaida tukaleta humu" Askari mmoja wa kike aliongea na kisha akampiga kofi la kisogo la nguvu ambalo lilimfanya Josephine aone uchungu wa kupigwa na mkono uliokuwa umekomaa sana



    "Ongoza njia kenge wewe" Kofi hilo liliambatana na kuambiwa maneno hayo, hakuwa na ujanja mwenyewe alikuwa mtiifu na aliongoza njia kuelekea huko alipotakiwa kwenda kwani alihofia angeweza kupigwa zaidi. Hadi hapo alikuwa hatamaniki kwa manundu katika sehemu mbalimbali za mwili wake, kuanzia usoni mkononi na sehemu zingine ambazo zilikuwa zikionekana ukiachilia mbali manundu mawili ya asili.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Alipelekwa hadi ene ambalo lilikuwa na ngazi ambapo alisukumwa akiambiwa ashuke kwa haraka sana, Jopsehine alishuka kwa haraka akiwa anahofia kuongezwa tena kipigo kingine. Walikuja kutokea kwenye eneo ambalo lilikuwa na vymba vingi vya gereza vilivyojengwa kisasa zaidi tofauti na magereza mengine ya ndani ya Tanzania, alipokuwa akitembea kupita kwenye njia ambayo ilikuwa ikitenganisha vyumba hivyo baadhi ya wanawake wengine wataukutu walikuwa wakimnyooshea mikono kutamani sana angewekwa ndani ya chumba chake chao. Wao hawakusimama naye waliongoza naye hivyo hadi kwenye chumba kimojawapo ambacho watu wake walikuwa wametulia, hapo Askari mmoja wa kike alifungua mlango na kisha akamsukuma kwenye usawa wa mlango wa chumba hicho kilichokuwa kimejengwa kwa ukubwa wa wastani kikiwa na kila kitu ndani. Kilikuwa ni chumba ambcho kilikuwa na mwangaza kila muda huku ndani yake kukiwa na vitanda vitatu vya kubebana. Ndani ya chumba hicho alishuhudia wasichana watatu wakiwa wamekaa wanacheza karata,alisimama mlangoni hapo akiyathaminisha mazingira ya humo. Kabla hata hajamaliza kuyathaminisha alifunguliwa pingu zote alizofungwa na kisha alisukumwa ndani kwa nguvu.





    Aligeuka kuwatazama mabinti watatu waliokuwa wamevaa sare kama zake wakiwa wanacheza karata, alibaki akishangaa wasichana hao ambao walimtazama kwa nyodo kila mmoja na kisha waliendelea kucheza karata kama kawaida. Josephine hakuwajali kabisa alienda hadi kwenye eneo ambalo kitanda kimojawapo kilikuwa kitupu kisha akajilaza akiwa anasikilizia maumivu. Alipojilaza tu kwenye kitanda hiko wale wasichna waliweka karata zao chini na kisha wakaenda hadi hapo walipo, bila kuuliza mmojawapo alimvuta mguu kamuangusha chini kisha akampiga teke la ubavu.



    "Kenge umeingia umetukuta humu ndani hivyo ni wakubwa salimia wewe" Aliongea mmojawapo ambaye alikuwa amenyoa upara huku akiwa amekunja uso kihasira zaidi, mwingine alikuwa akimnyaga na hapo walikuwa wamemkasirisha zaidi sana. Hakuwa akitaka kuonewa zaidi kwani kile kipigo alichokuwa amepewa na maaskari wajeuri kilikuwa kikimtosha hivyo hawa aliona hawana sababu ya kumuonea. Alipowatazama watu wenyewe waliomuonea walikuwa ni wadogo zake kabisa, hivyo aliona hiyo ilikuwa ni dharau kubwa sanakwa hao watu kumuonea. Hakutaka kabisa kuruhusu mwingine ampige teka kwani aliona watakuwa amemdhalilisha sana, wa tatu wake aliponyoosha mguu ampige teke aliudaka na kisha alimrudisha nyuma, alijifyatua akasimama na kisha alimpiga teka zito yule msichana ambaye alikuwa ana sura ya kitoto zaidi akiwa amenyoa kipara. Mwingine alipotaka kuingilia alimrudisha na teke kali sana hadi akaenda kujipigiza kwenye kitanda, yule mwenye upara aliona alikuwa amefanyiwa kitu ambacho hakutakiwa kabisa kufanyiwa na mtu kama huyo ambaye anaingia muda huo gerezani wakati wao walikuwa na miaka wakitumikia kifungo ingawa walikuwa wana muda mfupi ndani ya gereza hilo.



    Alimjia kwa kasi sana kumfuata Josephine na akiwa ana lengo la kumzoa aanguke naye chini, kuja huko kwa kasi alipitliza baada ya Josephine kumkwepa na kisha akamuongezea teke la kisigino lililompata kiunoni. Yule msichana mwenye upara alienda moja kwa moja kujigonga kwenye nondo ngumu za gereza na kupelekea kishindo kikubwa kisikike, wafungwa wote wa kike waliokuwa wapo gereza mkabala na hilo walishangilia kwa nguvu sana. Baada ya hapo Josepine alipiga sarakasi moja maridadi a akatua kitanda cha juu akajilaza, wale wafungwa wengine watatu walipoona vitendo alivyokuwa akivifanya walinywea wote wakaona walikuwa wamepata mbabe zaidi yao. Baada ya hapo wote walijikusanya sehemu moja na kisha wakamsogelea karibu, Josephine aliwatazama kwa macho makali lakini alikutana na matabasamu kwenye nyuso zao.



    "Getu" Aliongea yule mwenye upara kisha akanyoosha mkono kumpatia akiwa na tabasamu, Josephine naye alionesha tabasamu kisha akampa mkono



    "Frida" Mwingine alifuata ambaye alikuwa amesuka mabutu kujitmbulisha na kisha akampa mkono



    "Stella" Alimalizia wa mwisho ambaye alikuwa amesuka minyoosho kumpa mkono na kisha wote kwa pamoja wakamtazama kwa tabasamu wakisubiria jina lake.



    "Josephine" Alijitambulisha



    "Karibu" Walimkaribisha huyo mwenzao mpya ambaye alikuwa ameletwa humo ndani, hao wasichana watatu walikuwa ni wale waliokuwa marafiki zake Marehemu Annie waliokamatwa kwenye kisa cha SHUJAA sasa walikuwa wapo pamoja na humo ndani na walifurahia sana kupata rafiki mpya ambaye aliwapa kipigo muda mfupi walipomchokoza.



    ****



    USIKU

    Majira ya usiku huo tayari mtu ambaye alikuwa ametumwa na Norbert kwenda kumfuatilia Kardinali Michael alikuwa amesharudisha majibu, alikuwa ametaja kila kitu juu ya mahali ambapo alikuwa akienda Kardinali katika kipindi ambacho haendi ofisini. Norbert alikuwa amemuagiza huyo kijana ili aweze kupapata hapo kwani aliamini kabisa kuwa kama Askofu Valdremar akiwa yupo hapa nchini basi mtu ambaye alikuwa amemficha alikuwa ni huyohuyo na hakukuwa na mwingine ambaye angemficha yule Askfu kabisa.



    Vyeo vya kidini walivyonavyo vilimfanya kabisa aamini kuwa alikuwa amefichwa hapo tu, alikuwa akitambua kabisa kuwa huyo Kardinali hakuwa mtu wa ziara majira ya siku sasa alipopata habari muda mfupi ulipita alikuwa akitoka kwenye nyumba yake ambayo ilikuwa ipo Tabata Kinyerezi ikiwa na ulinzi mkali ambao aliuona baada ya lango kuachwa wazi. Muda huo Norbert alikuwa tayri ameshawasili kwenye eneo la nyumba hiyo baada ya kupokea taarifa hizo. Alikuwa amevaa mavazi ya kininja ambayo yalikuwa na rangi nyeusi kipindi anaufikia ukuta wa nyumba hiyo, akitumia ufundi wake wa kininja aliupanda ukuta huo hadi ndani ambapo ajiachia na kutua chini chini kisha akajibiringita kuepusha asitoe kishindo.



    Baada ya hapo alijosogeza hadi eneo la jirani nakwenye maua kisha akajibana kwa muda mfupi akisubiri, muda huohuo alipita mlinzi ambaye alikuwa na silaha. Mlinzi huyo alipofika usawa wake alimrukia shingoni na kisha akamuwekea kitambaa mdomoni, alimshikilia kwa nguvu sana hadi alipotulia ndiyo alimsogeza pembeni na kumuweka kwenye maua ya nyumba hiyo. Alinyata hadi upande mwingine kabisa ambao alimfanyia Mlinzi mwingine namna hiyo kisha akamficha, alifanya namna hiyo akizunguka nyumba nzima akitumia kitambaa ambacho kilikuwa na dawa ya nusu kaputi.



    Dakika nne baadaye eneo zima la ndani ya nyumba hiyo lilikuwa ni tupu kabisa, hakukuwa na Mlinzi aliyekuwa anazunguka humo ndani. Baada ya kufanya hivyo Norber alikwea hadi juu ya bati ya nyumba hiyo, alienda hadi sehemu ambayo kulikuwa na tundu kubwa sana ambalo angeweza kupita hata yeye. Tundu hili lilikuwa ni kutokana na kuwepo sehemu ya moto ndani ya sebule hiyo ambayo wazungu hupenda kujenga wakiota moto, nyumba hii ilijengwa kwa mtindo huo ingawa ulikuwa ukijulikana kabisa kuwa mtindo huo ulikuwa ukijengwa kwenye nyumba ambazo zilikuwa zipo maneno ya baridi sana. Norbert aliingia ndani ya tundu hilo na kisha alishuka taratibu hadi chini, alikuja kutokea kwenye uwazi mkubwa sana. Eneo hilo alipochunguliwa tu alikutana na teke kali ambalo lilimfanya aanguke mita moja mbele, alipokuwa yupo hapo chini alimuona Askofu Valdermar akimjia huku akiwa ametanguliza goti mbele kupiga pigo la kummaliza moja kwa moja. Hakutaka kabisa kuona akipigwa pigo hilo kizembe sana aliamua kujibiringisha kwa upesi sana akaenda pembeni kisha akasimama wima kukabiliana na adui yake



    "Niliuhisi ujio wako ninja mwenzangu" Askofu Valdermar aliongea na kisha akatoa ishara ya kininja, wote wawili walikaa mkao moja chini ya sakafu ya nyumba hiyo. Walianza kuweka ishara mbalimbali ambazo maninja huweka kabla ya kupambana, baada ya hapo walinyanyuka taratibu na kisha walikaa mkao wa kupambana.



    Mpambano ulianza kwa Askofu kurusha mateke mawili akiwa juu mfululizo na yote yalikosa lengo kutokana wepesi aliokuwa nao Norbert katika kukwepa. Naye alikuja ana ngumi mfululizo na kisha akarusha teka, mapigo yake nayo yalionwa na Askofu ambaye aliyapangua kisha akarudha teke la miguu miwili la kifua. Teke hilo lilipita nalo kwani Norbert aliyumba pembeni kiufundi na kisha akamsukuma na mguu wake aangukia kando akiwa bado yupo juu, Askofu alipoanguka chini alijifyatua akasimama na kisha akakunja ngumi kwa namna ya kuvizia akimtazama ninja mwenzake ambaye alikuwa amefunika uso wake. Pigo hilo aliopigwa muda huo alijua kabisa mpigaji alikuwa ni Norbert kwani alishawahi kumuotea hapo awali walipokuwa wakipigana, sasa akaweka akili sawa aweze kukabiliana na Norbert akiwa anakumbuka mitindo yote ya kupigana aliyoitumia.



    Hapo alikumbuka kabisa kuwa hizo zilikuwa ni mojawapo ya mbinu ambazo Norbert alizitumia wakati anapambana naye, alijiweka sawa na kisha akaingia tena uwanjani kwenda kupambana naye. muda huo alionekana kuyamudu mapigo yote aliyokuwa akiletewa kutokana na kukumbuka mitindo yote pindi alipokuwa akipigana naye, alifanikiwa kumuotea Norbert pigo la mgongo ambalo lilimpelekea hadi chini. Alitaka kufuata amuongezee lakini Norbert alibinuka kwa saraksi akiwa hapo chini akatua kando, hapo alijipanga upya kumfuata mpinzani akijua atakuwa na mtindo uleule. Alipojaribu kutia ngumi alijikuta yupo chini kwani tayari mpinzani alikuwa amebadili mtindo, sasa likuwa akitumia judo huku akichanganya na mapigo ya Ninjutsu alimaarufu kama ninja. Mapigo hayo yalimfanya Askofu aingie kwenye wakati mgumu kwani alikuwa akiionja sakafu ya nyumba kwa mara nyingi sana kila alipopiga pigo moja, hakukata tamaa aliendelea kumfuata tu Norbert.



    Mapigo hayo ya judo yaliyotumika ndiyo ambayo mapigo yalilainisha kila kitu kwa Norbert, ndani ya muda mfupi Akofu alikuja na pigo la kutumia ngumi yake. Mzee wa kazi alikwepa pigo hilo kwa kuyumba pembeni kisha alimrusha kwa mtindo wa judo Askofu akaenda kuangukia ule ubavu ambao alimuumiza, maumivu yalianza upya na hata aliposimama hakusimama sawasawa. Alizidi kujiongezea hatari kwani mpinzani alikuwa ameshajua tayari alikuwa ameumia, alichofanya ni kuja na mtindo mwingine wa kupigana. Huu ulikuwa ni mtindo wa sarakasi kisha anaachia pigo moja, hiyo ilimchangnya sana Askofu na alijikuta akipigwa sehemu ileile aliyokuwa ameumia kwani alikuwa amemuonesha ameumia. Jambo la hatari kuliko yote ni kumuonesha mpinzani kuwa umeumia na Askofu alikuwa tayari amelifanya, haikupita hata dakika za kukadiria ziwe zimefika tano. Askofu alishavunjwa mbavu zake kwa mapigo ya mchanganyiko, hakuwa tena na ujanja na Norbert muda huohuo alimvunja mkono kwa kuzungusha kijudo alijaribu kurusha ngumi. Alipiga makelele kwa kuvunjwa mkono huo lakini hakukubali kushindwa kabisa, alirusha teke ambalo lilikosa lengo baada ya mpinzani kubonyea chini. Akiwa amebonyea huku chini alipiga teke la pembeni maarufu kama 'Yoko geri kekome" ambalo lilitua kwenye maungio na akamvunja kabisa, Askofu alianguka chini akawa hana ujanja tena. Akiwa yupo hapo chini Norbert alimjia na alipomsogelea alichomoa upanga wake ambao alikuwa amueweka nyuma, Askofu alijua kabisa kuwa ulikuwa ni mwisho wake na alikuwa yupo tayari kwa kufa kifo cha kukatwa kichwa. Alijiweka tayari kukatwa kichwa lakini panga hilo lilienda kutua kifuani mwake likaingia kwenye sehemu ambayo moyo upo, alitoa macho nje kwa nguvu sana baada ya kuchomwa eneo hilo kisha akatanu kinywa kinywa. Huo ndiyo ukawa mwisho wake wa kucheza na wanausalama makini sana ndani ya Afrika ya mashariki, sasa si kiumbe hai bali ni aliyeporwa uhai'

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hustahiki kufa kifo cha kiheshima cha kininja wewe" Alimuambia kisha akaliachia panga na Askofu alidondoka kama gunia, Nobert alipokamilisha kazi hiyo alitoka nje ya nyumba hiyo kwa kupitia njia aliyokuja nayo na kisha aliruka uzio na kutokomea mbali na eneo hilo.



    ****



    [0]

    MAPEMA ASUBUHI

    IKULU



    Muda ule wa kikao ambacho kilikuwa kimeandaliwa ulikuwa ukikaribia, wahusika wote waliokuwa wakitakiwa kwenye kikao hicho walikuwepo hapo. Mawaziri wawii ambao ni Mheshimiwa Liwale nai Mheshimiwa Mahujuraja walikuwepo, upande mwingine walikuwa Katbu wa wizara ya nishati na madini pamoja na Katibu Mkuu wa wizara ya uchukuzi.Humo ndani pia Mhasibu wa bandari Bwana Mushi alikuwepo, Afisa wa juu kabisa wa mamlaka ya mapato Bibi Mushi alikuwepo. Upande wa jeshi la wananchi wa Tanzania Luteni jenerali Belinda ambaye alikuwa ni mnadhimu mkuu wa jeshi alikuwepo, upande wa jeshi la polisi kulikuwa kuna Kamishna fisadi pamoja na IGP Mbwambo ambao walikuwepo wamekaa hapo. Muda hawakuonekana Norbert wala mtu mngine yeyote, kiusalama tu alikuwa ameonekana kwenye meza hiyo Moses Gawaza.



    Wote walikuwa wamepambwa na tabasamu kwenye nyuso kwani waliona ulaji ndiyo huo ulikuwa ukijileta, nyuma ya kiti cha kila mmoja alikuwepo yupo mwanajeshi aliyekuwa amesimama kiukakamavu. Hiyo waliambiwa kuwa ilikuwa ni kwa ajili ya ulinzi wa mahala hapo kutokana na unyeti wa jambo walilokuwa wakiongea, waliliamini moja kwa moja kwani kila alikuwa amesima akiwa na mlinzi wa aina hiyo nyuma yake. Ulipotimia muda walimuona Rais Zuber akiingia humo ndani akiwa ameongozana na watu wawili, mmoja alikuwa hajajulikana kwani alikuwa na ndevu nyingi sana na mwngine alikuwa ni Norbert.



    Wote humo ndani walisimama na maofisa wale ambao walikuwa na vyeo vya juu kabisa walitoa saluti huku ale waliokuwa wadogo wakikakamaa kiheshima. Rais Zuber pamoja na wote waliokuwa wameingia naye walichukua nafasi wakakaa, hapo kikao kilifunguliwa ulipofikia muda na Rais Zuber.



    "Natumai wote ni wazima kabisa wa afya hilo tumshukuru Mungu na pia niwapongeze kwa kuja hapa ndani ya eneo hili, ningependa kuchukua nafasi hii kumtamblisha huyu mmojawapo ambaye mlikuwa hamumjui kabisa hapa. Anaitwa Jama Wa Majama" Rais Zuber alianza utangulizi kisha akatoa utambulisho kwa Jama ambaye alitoa ndevu alizokuwa amezibandika kisha akasimama juu, watu wote waliokuwa kwenye mtandao walipomuona mioyo yao ilipigwa kwa nguvu sana.



    "Niliwahi kusema kuwa nitapambana na ufisadi na kila aliyeshikwa na tuhuma hizi alihukumiwa, huu mwendo unaendelea. Sasa naomba kila mtu atulie humu ndani Jama Wa Majama asome ripoti nzima ambayo haikufika kwenye mikono yetu. Hakuna ziara ya Rais wa Marekani bali mliloitiwa ni hili " Muda huohuo ilipotoka amri hiyo taa za humo ndani zilipunguzwa mwanga na kisha Kirusha picha ukutani(projector) iliwashwa na pembeni kulikuwa na ubao mdogo wa kuandika na kalamu ya kuweka alama, Jama alitoa tarakilishi alizokuwa amekuja nazo zote tano akaziweka kwenye meza maalum na kisha aziwasha.



    "Hadi siku tunaumaliza uchunguzi huu mimi na wenzangu tulipanga kabisa kuwa ripoti hii ya akiba tuifiche kinamna ya kipekee bila ya mtu kujua. Tulitia password kwenye laptop nne tofauti ambazo ni hizi hapa zenye ukubwa mdogo na kisha hii kubwa tukaweka ripoti hiyo, maneno yaliyokuwa kwenye laptop hizi nne ukiyaunganisha unapata neno 'BARA JANGWA NA USTARABU BARABARA LIWE NA MAHUJAJI ALEKUWA UMRA AU HIJA'" Aliweka kituo kisha akatazama kama alikuwa akisikilizwa.



    "Ni neno lisilokuwa na maana kwa mtazamo wa kawaida ila ni neno lenye maana kubwa sana, hili ni neno ambalo ndiyo neno siri la kufungua faili lote lenye ripoti. Lakini lote ni nenosiri bado ulichambue, wazungu wanasema 'transdescribe" ndiyo utapata nno siri ya laptop yenye ripoti kamili. Aliweka kituo kwa mara nyingine, muda huo Mheshimiwa Liwale alinyanyuka kwenye kiti chake.



    "Mheshimiwa kumradhi kidogo naenda msalani" Alisema



    "Kaa kwenye kiti Liwale mpaka Laptop ifunguliwe ndiyo utarauhusiwa" Rais Zuber alizuia na hakuwa na kupinga alikaa chini.



    "BARA JANGWA NA USTARABU NA USTARABU BARABRA tukilichambua tutapata ufupisho BAR JAN NA NSTU BA, sasa tuyabadili hizi silabi na irabu tulizozipata. Kifungu cha kwanza nakiunga na kifungu na tatu na kisha nakiunga tena na kifungu cha tano, ianakuwa BAR-NA-BA na hapa unapata jina la mtu BARNABA. Kifungu cha pili ukikiunganisha na cha nne yaani JAN-STU unapata jina JANSTU" Jama aliweka kituoniten hapo na muda huohuo Mheshimiwa Liwale na Mheshimiwa Mahujuraja walikuwa tumbo joto.



    "Tuje kifungu LIWE NA MAHUJALI ALEKUWA UMRA AU HIJA, tunachukua LIW MAHUJ ALE URAJA. Ufupisho tunachukua hicho kifungu cha kwanza na cha tatu tunaunganisha yaani LIW na ALE tunapata jina la mtu LIWALE, tukichukua kifungu cha pili na kuunga na cha nne yaani MAHUJ na URAJA unapata jina la mtu MAHUJURAJA. Sasa hapa password yetu imekamilika tuunganishe vifungu vya kwanza pamoja katika kile upande na vya pili pamoja, BARNABA LIWALE na JANSTU MAHUJURAJA ndiyo unapata sasa tuingize sehemu ya neno siri kwenye faili ya hii laptop kubwa itadai mara mbili na uzingiza maneno kwa wakati tofauti tukianza na la kwanza" Jama alipoonge hivyo alihamia kwenye tarakilishi ambayo picha kubwa ilikuwa ikionekana juu yake, aliingiza maneno yake kama alivyosema na hapo faili hilo likafunguka na kila kitu kikawa wazi.



    "Hatua imekamilika sasa kabla hatujaendelea napenda niwambie kuwa wahusika ambayo majina yao ni password ndiyo wahusika wakuu wa uhaini huu wakiwa wanatumia jina Roho kwa Mheshimiwa Liwale na Moyo kwa Mheshimiwa Mahujuraja" Alizidi kuweka mambo wazi na ilipofika hatu hiyo Mheshimiwa Mahujuraja alizidiwa na shinikizo la damu akaanguka chini na kupoteza fahamu



    "Askari toa huyo upige pingu huku unampa huduma ya kwanza,weka pingu na Liwale pia" Rais Zuber alitoa amri hiyo na kisha wote walifungwa pingu na wale wanajeshi wakatolewa nje, baada ya hapo Jama alianza kuichambua ripoti nzima hadi ilipofikia mwisho. Alipoifika mwisho alikuwa ametumia saa takribani mbili, muda huo wale wote waliokuwa wapo kwenye mtandaao walikuwa na pingu tayari huku wengine machozi yakiwatoka. Waliobaki humo ndani walikuwa ni Rais Zuber, Jama, L.J Belinda, Norbert, Moses, IGP Mbwambo pamoja na maasakri wote wa jeshi la wananchi.



    ****



    Mwisho wa mafisadi wote ulijulikana na hapo ndiyo ikawa nafasi nzuri kwa Mheshimiwa Kabinuki kuachiwa huru siku iliyofuata tu baada ya kujulikana hakuwa na hatia, ilijulikana wazi wale waliokuwa wakihusika kwa yote hayo walikuwa ndiyo hao waliokuwa wamekamatwa. Agiza lilitolewa kwa Rais Zuber wote walichukuliwa pesa zao benki, wakafilisiwa mali na kisha wakashtakiwa. Walianza kuwa ni wenye kwenda mahakamani kuhudhuria kesi zao kila muda, juma chache zijazo wote walihukumiwa vifungo vya maisha kutokana na mauaji waliyokuwa wameyasuka na walitupwa kwenye shimo la giza kule ambapo walikuwa watu wenye makosa kama yao. Huo ndiyo ukawa mwisho wale wote waliosuka mabomu ya barua wakiyaita wito wa kuzimu ili wapoteze ushahidi wa ufisadi wao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ulikuwa ni muda ambao Norbert aliongezewa likizo akawa yupo na familia yake akifurahia, alimkumbuka sana mtoto wake katika muda huo na aliutumia kushinda naye ndani baada ya kumaliza hiyo kazi ambayo ilikatisha raha ya kukaa na mtoto wake. Alifurahia kukaa na mwanamke anayempenda katika muda huo wa likizo aliyokuwa amepewa na ofisi kupumzika, alibaki akiwa yupo Norene pamoja na mwanae katika kipindi chote cha likizo yake.



    MWISHO!!

0 comments:

Post a Comment

Blog