Search This Blog

Friday, 20 May 2022

WITO WA KUZIMU - 4

 







    Simulizi : Wito Wa Kuzimu

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ALASIRI

    Ilikuwa ni kawaida yake kila akitoka kwenye ofisi zile kuja kupata kinywaji ili kuweka akili sawa, hakuna mtu ambaye alikuwa hamfahamu kabisa ndani klabu moja maeneo ya Ilala ambayo muda wa mchana huwa ni sehemu ya kunywea vinywaji na usiku huwa ni sehemu ya muziki. Siku hiyo aliingia ndani ya Klabu hiyo kama ilivyo kawaida yake akiwa ni mwenye mawazo tele kwani alikuwa ameshapewa taarifa ya kuuawa kwa rafiki yake kipenzi ndani ya nyumba yao huko Kibada. Scorpio aliagiza pombe akiwa kwenye meza kuu ndani ya Klabu hiyo, alionekana kunywa pombe hiyo kwa pupa sana. Pombe ilipoisha aliongeza nyingine na kisha akaendelea kunywa kama kawaida huku akitikisa kichwa kuendana na mdundo wa muziki ambao ulikuwa ukiendelea humo ndani, haikupita muda mrefu kwenye eneo alilokaa alikuja kukaa Msichana mwenye urembo wa kuvutia akiwa amevaaa kaptula fupi ambayo iliacha mapaja yake nje. Msichana huyo alipokaa tu hakujishughulisha kabisa kumuangalia Scorpio yeye alipaza sauti kuagiza kinywaji na kupelekea Scorpio amuone ambapo alibaki akimtazama kwa sekunde kadhaa huku akiutazama mwili wake ambao ulikuwa una mvuto kuliko kawaida, ALijikuta akipiga uruzi baada ya kuuona mwili wa mrembo huyo ukiwa na unavuti sana na kisha alimbania jicho baada ya Mlimbwende huyo alipomtazama kwenye uso wake.



    "Hellow" Alimsabahi



    "Hi" Alijibiwa na kisha mrembo huyo akaweka umakini wake kwenye kinywaji hiko alichokuwa ameagiza, hilo halimkutia karaha kabisa aliona ilikuwa ni jambo la kawaida sana.



    "My I Know your name(naweza kukujua jina lako)?"



    "Hey do not about the bush, say how much do you have(Hey usizunguke sana sema una kiasi gani)" Kauli hiyo ilimfanya Scorpio atabasamu kwani alikuwa ameingia mulemule alipokuwa akipataka, alikuwa amemtamani sana huyo mwanamke lakini alipotajiwa kuhusu hilo la bei alitambu wazi alikuwa ni kahaba hivyo halikuwa tatizo.



    "Its Full time baby, are you ready?(Ni muda wote mpenzi upo tayari?)"



    "Its you(ni wewe)" Alipopewa jibu hilo alimpa ishara huyo msichana ambaye alichukua kinywaji chake na kisha akaongozana naye, kwakuwa Makahaba wengi walikuwa wakijiandaa kwa kila kitu yeye alikuwa hana wasiwasi wowote kwani alijua kabisa huyo msichana alikuwa akielekea mahali ambapo alipazoea kwa ajili ya kufanyia kazi. Moyoni alijipa ushindi kwa kujifanya hajui kiswahili kwani hilo limemfanya aweze kuwapata wasichana wa namna hiyo wengi sana, huyo aliona ilikuwa ni kawaida kumpata ikiwa ni Kahaba sasa alikuwa akielekea kutimiza hitaji lake la kimwili na huyo msichana huyo mrembo sana mwenye umbile la kibantu ambalo lilikuwa ni ugonjwa sana kwake.



    Walitoka kwenye eneo hilo hadi mtaa wa pili ambako kulikuwa na nyumba ya kulala wageni ya kisasa sana, hapo walikuta funguo ilikuwa tayari kabisa na ikamfanya ajue kabisa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa eneo ambalo Mrembo huyo alikuwa akilitumia kujipatia kipato chake kwa kutegema viungo vyake alivyoumbwa navyo. Waliingia ndani ya chumba hiko ambacho kilikuwa na kila kitu ndani, Scorpio baada ya kuingia ndani ya chumba hiko alianza papara yake ya kuuparamia mwili wa msichana huyo kwani ulikuwa ni ugonjwa wake mkubwa sana tangu alipoingia ndani ya nchi hii.



    Alitokea kuvutika sana na wasichana wa kibantu tangu alipoonja ladha zao ndiyo maana hakung'atuka kabisa, ilikuwa ni kawaida sana kila msichana aliyekuwa kinavutia kumfuata na kisha kumtongoza akiwa namna hiyo ilikuwa ni kawaida yake kujitolea pesa yoyote ilimradi aonje asali iliyopo. Hakika alikuwa ni Simba ambaye alikuwa ameonja nyama ya binadamu hivyo kuiacha kula nyama hiyo ilikuwa ni ngumu sana, alikutana na ladha mpya kabisa tofauti ya ladha ya mawindo yale aliyokuwa ameyazoea huko alipotoka. Kitu kipya na mazoea yake kulimfanya awe namna hii na si kama alivyokuwa akivila huko alipotoka, hakika alikuwa mgonjwa wa hicho kitu kuliko kawaida.



    Alianza kuutomasa mwili wa binti huyo akakutana na laini ambayo ilikuwa ikimpa hamasa ya kutaka kuendelea kufanya kile ambacho alikuwa akikifanya, alipotaka kupunguza vizuizi vya mrembo huyo alikutana pingamizi ambalo hakuwahi kukutana nalo kutoka kwa warembo wote ambao aliwahi kukutana nao tangu aanze kuonja asali mpya mali ya bara adimu sana.



    "What?!" Aliuliza kwa mshangao akionekna alikuwa hajapenda kabisa kuzuiwa huko kwani alikuwa akilipia kila kitu.



    "The door please close it(Mlango tafadhali ufunge" Hakubisha kabisa aliuachi mwili wa Msichana huyo na kisha alienda kuufunga, muda huo msichana huyo alichukua taulo lililokuwa limetundikwa humo ndani na kisha akawa anaingia mahali ilipo choo na bafu ndani ya chumba hiko. Hiyo ilimfanya Scorpio akereke lakini alipewa tulizo muhimu na akaombwa asubiri kwani alikuwa yupo naye kwa siku nzima, Msichana huyo alizama bafuni muda huo akimuacha Scorpio akitoa mavazi yake na kisha akabakiwa na kaptula tu ambayo ilikuwa imeishia mapajani. Alifika hapo kitandani akiwa na hamu sana na muda huo tayari 'Ali haji bin Kofia' alikuwa ameamka kutoka kwenye usingizi wake lakini amekaa mguu sawa, alikuwa akizidi kumsumbua Scorpio katika muda huo ambao alikuwa akimsburia huyo mrembo aliyekuwa amezama ndani ya maliwato kwa ajili ya kubadili nguo.



    Hakuchukua muda mrefu sauti ya hatua zilisikika ambazo hazikumfanya ashtuke hata kidogo, kutawaliwa na mawazo ya jimai yalikuwa yamemsahaulisha kabisa Mrembo aliyekuwa ameingia huko ndani alikuwa amevua viatu kabisa na alichukua viatu vya wazi viliwekwa maalum kwa ajili ya kuuingia huko. Alizidi kutabasamu aliposikia mlio wa viatu ivyo kutokana na tamaa kuizidi akili yake ya kufikiri, alipokuja kutahamaki aliona bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti ikitokea kwenye mlango wa huko Maliwatoni. Mshongo wote uliokuwa umekuja ndani ya mwili wake ulimtoka muda huohuo akiwa ameitazama Bastola hiyo akijua tayari alikuwa amekwisha, alinyanyuka hapo ktandani lakini bastola ile ilichezeshwa kumpa ishara akae hapohapo. Mwenye bastola hiyo alipojitokeza alimuona hakuwa mwingine ila ni Norbert ambaye walitaka kuyatoa maisha yake siku chache zilizopita, alishtuka sana kwani alikuwa amekuja kwenye muda ambao hakutaraji kabisa. Sasa alianza kuulaumu mshongo wake ambao alikuwa akiuendekeza kila akiona msichana mrembo wa kibantu ambaye alikuwa ana umbo tata, alijilaumu katika muda ambao alikuwa ameshachelewa kabisa kwani kila kitu kilikuwa kimeharibika. Norbert alipiga hatua kuingia ndani ya chumba hicho akiwa anatabasamu tu huku akimtazama adui yake ambaye alikuwa ameingiwa na uoga ingawa bado alikuwa akijifanya yupo sawa.



    "Scorpio hatimaye tumeonana ten kwa mara ya pili tangu siku ile tulivyokuwa pamoja kule Singita na bosi wenu shoga pamoja na mume wake" Norbert aliongea maneno ambayo yalimshtua sana adui yake ambaye hakujua kabisa kuwa alikuwa akifuatilia hivyo.



    "Unashangaa nini? Kutana na yule Mtumishi wa Mungu mliyefikiri mlimuua kule Mbugani na bomu sasa nimerejea tena sifi kijinga namna ile" Norbert alizidi kumuandama Scorpio kwa maneno ambayo yalikuwa yakimfanya azidi kuchanganyikiwa na hakujua ndani ya nchi hii kulikuwa na watu wajanja zaidi hadi kufikia hatua hiyo aliyokuwa ameifanya.



    Muda huohuo yule Kahaba ambaye alikuwa amemchukua kule Klabu alijitokeza akiwa amebadili mavazi, alikuwa amebadili pia mtindo wa nywele ambao ulikuwa umemfanya aonekane ni mtu tofauti kabisa. Alisogea hadi akaja kusimama kwenye eneo ambalo lilikuwa lipo jirani kabisa na eneo alilokuwa yupo Norbert,yule naye aliachia tabasamu huku akimtazama Scorpio ambaye alionekana kutoamini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Huyu ndiye ulikuwa ukidhania kuwa ni Kahaba, muite NORMAL SERVICE TZ 97 au jina halisi ni Eva" Alimtambulisha hapo, Msichana huyu alikuwa ni mpelelezi wa EASA liyekuwa yupo chini ya Norbert. Huyu ndiye alshiriki katika kumuwekea mtego Thomas hotelini katika siku ile ambayo aliuawa kwa bomu, amerudi tena baada ya kuitwa na mkuu wake wa kazi ambaye alimpa kazi ya kumnasa huyo Mzungu mpenda wasichana.



    "We mzungu koko karibu sana kwenye anga ya EASA nafikiri ulikuwa hujui kama ukanda huu sasa hivi unatisha kwa ujasusi sasa jionee mwenyewe" Eva aliogea huku akimuegemea Norbert began



    "Eti jana walikuwa wamekaa wanapanga kabisa kuwa waninase kupitia mwanamke akiwa hajafikiria kabisa nilikuwa nimeshamjua kuwa yeye ana udhaifu uleule, sasa bwana Scorpio eleza mwenyewe mkuu wake ni kina nani la hivyo nakuua taratibu na si kistarabu kama nilivyomuua Spider" Aliambiwa lakini kutokana na jeuri yake aligoma kueleza na alikaa kimya tu huku akitazama suruali yake ambayo ilikuwa ipo mbali na hapo, kutazama huko Norbert alikuwa ameshamuona muda mrefu sana na alimpa ishara Eva akaenda kuichukua suruali hiyo. Scorpio aligoma kueleza na hapo risasi ile yenye kiwambo cha zuia sauti ikatoa kikohozi hafifu sana, bastola hiyo ilitua kwenye mfupa wa paja na kumfanya ashikilie eneo hilo ndani ya sekunde chache tu baada ya maumivu kusambaa. Norbert alimtolea tabasamu tu na kisha alimuongeza risasi nyingine kwenye paja la upande mwingine.



    "Yaani mpaka uongee leo ndiyo nitaacha kuvifyatua hivyo viungo vyako" Aliongea na kisha akikoholesha tena bastola na safari hii ilienda kuvua kwenye kifuniko cha goti, maumivu yalimzidia na hata alitamani kupiga kelele lakini alijizuia kutokana na uwepo wa mwanamke humo ndani. Alibaki akigaragara hapo kitandani huku damu ikimvuja, bado hakutaka kusema kuonesha ni jinsi gani alivyokuwa jeuri. Alipoongezewa risasi nyingine aliona kabisa kuwa angeweza kuongea hilo suala hakutaka kabisa, kwa kasi ya ajabu akichoamua kukifanya iikuwa ni kuuweka mkufu ambao alikuwa amevaa shingoni ambao ulikuwa na msalaba wenye mapambo ya ajabu. Alifumba mdomo wake kwa nguvu alipouweka mkufu huo kwa muda wa dakika kadhaa, alipokuja kufungua mdomo alikuwa hana uhai tena. Hapo wanausalama hao wa EASA wakajua kabisa kuwa huyo alikuwa amejiua kwa kutumia sumu na hawakutaka kuendelea kubaki humo kwani walikuwa wakipoteza muda.



    Norbert alitoka hadi zilipo nguo za Scorpio na akazipekua, hakuona cha maana kabisa kwenye nguo hizo na aliamua kuziacha na kisha akafuta kwenye sehemu zote alizokuwa amegusa na kiganja cha mkono wake na kisha wote kwa pamoja walitoka hadi nje ya chumba hicho na wakaufunga mlango kwa ufunguo na kisha funguo hiyo wakitua ndani ya chumba hicho kwa kupitia uwazi wa chini ya mlango, Baada ya hapo Norbert aliuzungusha mkono kwenye kiuno ch Eva na kisha akaanza kupiga hatua kuelekea naye nje kupitia eneo la mapokezi. Walipofika eneo la mapokezi Norbert aliingiza mkono mfukoni na akatoa funguo nyingine kabisa ambayo alimpatia Mhuhumu huyo, baada ya hapo waliaga na kisha wakatoka nje yNyumba hiyo hadi kwenye gari na kisha wakatokomea kwenye eneo hilo baada ya kuwa walikuwa wameshawapunguza nguvu maadui zao kwa mara nyingine ndani ya siku moja. Walikuwa wamecheza mchezo mmoja hatari sana ambao haukufahamika hata na Mhudumu mmoja wa ndani ya nyumba hiyo ya kulala wa geni ya kisasa zaidi, mchezo huo ndiyo maana walifanikiwa kutoka bila hata ya kubakisha maswali kwenye vichwa cha Wahudumu hao juu ya yule MZungu ambaye alikuwa ameingia na Eva mahala hapo. Muda huo hesabu ya haraka iliyokuwa imebaki upande wa maadui ulikuwa umebakia na watu wawili tu ambao ndiyo walikuwa na upinzani mkubwa sana, watu hao nao walikuwa wakihitajika kumalizwa ndani ya muda wowote kwani mzee wa kazi alikuwa amedhamiria kumaliza kazi yake kabla ya muda aliokuwa amepewa.





    ILIVYOKUWA

    Norbert kwenda kumalizia kazi yake ilikuwa alikuwa akielekea kwenda kumpunguza nguvu adui yake, tayari alikuwa ameshaujua udhaifu wa mmojawapo ambao alikuwa ameambiwa na msichana ambaye alikuwa amelala naye. Kitendo cha Cellina kuropoka tu bila ya kujifikiria alijikuta kiwa ameuza ramani ya vita kwa adui, sasa adui huyo alikuwa akiitumia ramani hiyo katika kumshbulia bosi wake.



    Norbert alikuwa amelala naye kwa lengo hilo tu na pia aweze kupata habari nyingine alizokuwa akizitaka, sasa alikuwa amepata hicho na alikuwa anaingia kazini. Ilikuwani hatua moja kubwa sana kuujua udhifu wa adui yako kabla yeye hajujua wa kwako, muda ambao walikuwa wakikaribia kuujua udhaifu wake tayari alikuwa ameshaujua udhaifu wa adui na tayari mbinu dhidi yake ilikuwa imeshagunduliwa.



    Kitendo cha kupenda wasichana ilihali alikuwa akifanya kazi hiyo ilikuwa ni alama nyingine kwa Norbert, kwani alikuwa akitambua kabisa kuwa wazungu wengi hataa wale ambao walikuwa kwenye kazi nzito kama hizi ni watu wasio makini kabisa wakiziona ngozi nyeusi. Dharau waliyokuwa wameijenga juu ya ngozi nyeusi kwamba hawakuwa na uhatari wowote hasa wanawake ilikuwa ikielekea kumgharimu yeye mwenyewe kwani muda huo tayari ilikuwa ikitumika kama silaha, dharau hii ilikuja kutumika kwa kumchukua Eva ambaye alikuwa ni msichana mrembo sana. Hakuwa na umbile la kimazoezi hivyo uwezekano wa kumuweka matatani ilikuwa ni rahisi kwani alikuwa ana mwili ambao kudhania kama alikuwa ni mwanausalama ni ngumu sana. Siku hiyo walikuwa Salim ambaye walikuwa wameshirikiana naye kwenye kisa cha WAKALA WA GIZA, yeye alikaa ndani ya Klabu kwani ilikuwa ni utaratibu uliozoeleka kwa Scorpio kutia mguu ndani yake.



    Mchezo ulipangwa kwa Eva siku hiyo kuingia na Norbert ndani ya nyumba ya wageni akiwa na mavazi ya heshima sana, alikuwa ameingia wakiwa wamekumbatiana na Norbert hadi eneo la mapokezi ambako walichukua chumba kingine kabisa si kile ambacho walikuwa wamechukua hapo awali. Baada ya hapo waliingia ndani ya chumba hicho wakiwa wamekumbatiana namana hiyo, walikuwa na mkoba mwingine ambao ulikuwa na nguo kama zile alizoingia nazo Eva pamoja na wigi alilokuwa amelivaa kichwani. Kitendo cha kuingia ndani ya chumba hiko walipanga mpango mwingine na kisha walikaa ndani ya chumba hiko kwa muda mrefu sana, muda wa kutoka Scorpio kule kwenye ile ofisi ulipokaribia Eva alitoka kwa kupita hapo kimaficho katika muda ambao Mhudumu yule hakuwepo kabisa.



    Alienda hadi kwenye eneo jingine walilokuwa wamelitenga na huko aliingia ndani, alizitoa nguo pamoja na wigi na kisha akavaa nguo zile alizotumia kumnasa Mzungu mwenye uchu. Baada ya hapo alitoka na akarudi hadi kwenye ile nyumba ya wageni, alienda kuchukua chumba kingine kabisa na alipelekwa hadi kwenye chumba hicho na akaachwa mwenyewe. Mhudumu alipoondoka tu kwenye chumba hiko tayari ilikuwa ni nafasi nyingne kwani Norbert aliingia ndani akiwa na mkoba wenye nguo nyingine za msaidizi wake akamkuta Eva akiwa amekaa kwenye kitanda akiwa anamsubiri, mpango uliokuwepo ulikuwa ni Eva kumuacha Norbert ndani ya chumba hiko na kisha kwenda huko lilipokuwa lipo windo lao. Hilo lilifanikiwa na Norbert alienda moja kwa moja kukaa ndani ya maliwato ya chumba hiko na mlango ulifungwa kwa nje na kisha Eva alirudisha funguo mapokezi akitoa ahadi angerejea tena muda mfupi ujao.



    Ulikuwa ni muda ambao Scorpio alikuwa amefika kwenye Klabu ile na kisha akakaa kwenye meza kuu, akiwa anazifakamia pombe ndipo Eva alipojipeleka pale kwenye kiti na akakaa kama vile alikuwa hana habari. Tamaa za mzungu mwenye uchu muda huo ndiyo zilimponza kwani aliingia kwenye mtego, alipoona binti huyo wa kijasusi ambaye alikuwa yupo mbele yake akijifanya ni changudoa aliingia kwenye mtego kweli ndani ya siku hiyo. Walipofikia makubaliano na kisha wote wakatoka, Eva alimpeleka kwenye hoteli bubu ileile na kisha alipofika hapo mapokezi hakuandikisha kwakuwa tayari alikuwa ameshachukua chumba. Alichokifanya ni kuomba tu ufunguo wa chumba chake na kisha akaingia ndani na mzungu huyo baada ya kupewa funguo hiyo, hiyo ilifanya Mzungu mwenye uchu ajenge picha kichwani mwake kuwa alikuwa amebeba kahaba kweli ambaye hadi nyumba hiyo ya kulala wageni walikuwa wamemzoea kiasi cha kumtengea chumba chake cha kufanyia mambo yake.



    Hivyo ndivyo alivyowekewa mtego na akaingia kichwakichwa bila ya yeye kujua kuwa huo ni mtego, Eva aliposema anaelekea bafuni lengo lilikuwa ni kwenda kumshtua Norbert kuwa mpango ulikuwa umekamilika. Norbert alipokuwa akitoka Eva alikuwa yupo ndani ya bafu hilo akibadili nguo zile alizowekea windo kisha akavaa nuo nyingine zilizokuwa zikifanana na nguo ambazo aliingia nazo akiwa ameshikana na Norbert. Kichwani alivaa wigi pia kama la mwanzo na kisha akatoka, walipofanya tukio na kutokomea ndani ya eneo hilo walimfungia na kutupa funguo chini ya mlango ili akija Mhudumu ajue mlango huo ulikuwa umefungwa kwa ndani. Mapokezi waliweka funguo ya kile chumba ambacho alichukua akiwa na Norbert huku akiwa na mkoba kama alioutumia kuingia ndani hapo ambao ulikuwa na nguo ambazo alizivaa kwa ajili ya mtego.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    BAADA YA KUTOKA HAPO

    Norbert akiwa yupo kwenye usukani walielekea moja kwa moja kwenye Klabu ile ambapo walipofika nje tu, walimkuta Salum akiwa yupo nje akiwasubiri. Aliingia ndani ya gari hilo na kisha wote kwa pamoja waliondoka katika eneo hilo wakiwa wameshaacha maafa kwa madui zao, safari yao iliishia Bunju kwenye eneo ambalo kulikuwa na nyumba ya Brian aliyeuawa kwenye kisa cha SHUJAA. Huko Salum na Eva walishuka kwani ndiyo lilikuwa eneo la kazi. Nyumba hiyo kutokana na muundo wake uliojengwa ilikuwa tayari imeshafanywa ofisi za shirika hilo na wafanyakazi walikuwa ni wengi sana wakiendelea na kazi zao, hapo aliwaacha na kisha alirejea katikati ya jiji kuendeleana harakati zingine.



    ****





    Majira hayo Mheshimiwa Roho alikuwa yupo kwenye jengo jingine na vijana wake baada ya kufika kwa taarifa mpya. ilikuwa ni taarifa ya kifo cha Spider aliyekutwa na Askofu nyumbani walipokuwa wakiishi. Hilo lilikuwa ni pigo sana kwa Mheshimiwa huyo kwani hakuwa akidhani kuwa mambo yatakuwa mabaya namna hii katika kipindi kifupi ambacho hata juma moja lilikuwa halijafika, tangu aanze kushirikiana nao kina Askofu na tangu Mzee Ole yupo hai. Hakuwa akiwaza kama mambo yatakuja kuwa mabaya namna hii kiasi cha kuzidi kumuweka mashakani, huyu ndiye alikuwa waziri yule ambaye alitoa agizo Mufti auawe alipotaka kumuweka pabaya. Sasa alikuwa akiendea na ujahili wake katika uchumi wa Tanzania, mambo yalipoharibika ni yeye ambaye alitoa gizo la kufuta ushaidi na pia kuchukua ushahidi mpya ambao ulikuwa umekusanywa. Kuibiwa kwa Tarakilisjhi zile mbili alijikuta akiwa hana amani na mapigo yake ya moyo yakiwa yanamuenda mbio kwani ilikuwa ni pigo kubwa sana kwake na hakuwa akiwaza kama lingekuja kutokea, aliona ushahidi ulikuwa upo mikono salama lakini kuibiwa kwake aliona hakukuwa na usalama kabisa,



    Yaani muda huo alikuwa amekuwa mmoja wa wanasiasa matajiri sana ambaye mali zake alikuwa amewaweka watu wengine ili asizue kitendawili zaidi juu ya alipozipata. Kampuni ya mafuta yote ilikuwa ni ya kwake ingawa alikuwa amemuweka Khemiri kama mmiliki wake. Bado alikuwa na vitega uchumi vingi sana, vyote alivipata kwa namna ya kiharamu. Magari yote ya mafuta yaliyokuwa yapo ndani ya kampuni yake yalikuwa yakisafirisha mafuta na hata mizogo mingine ambayo haikuwa ikitozwa kodi kutokana kuwepo waziri Mwenzake waliyempa jina la Moyo kwani hiyo ndiyo kazi yake. Rekodi za mapato ya TRA mzigo yote ilikuwa imelipiwa kodi lakini haikuwa hivyo, yote ilikuwa ni sehemu ya mchezo mchafu waliokuwa wakiucheza. Yeye ndiye alikuwa akivizima vyombo vya dola ikiwa pakaonekana hakuna sehemu yeyote ile ambayo ilikuwa na usalama, alikuwa akiweka wanausalama wale waliokuwa vibaraka wake katika siku ambayo mizigo yake haramu ilikuwa ikitoka. Pia maafisa wa kodi ambao walikuwa ni haramu alikuwa akiwaweka kwenye siku hizo, yote hiyo ilifnya awe akikwepa ukaguzi wa kila namna kwenye hiyo kampuni yake huku uraiani akisifika ni mmoja kati ya viongozi waliokuwa wakiaminika sana.



    Kutokana na kazi zake haramu alijikuta akiingiwa na joto katika tumbo lake kwa ghafla sana baada ya kusikia kuwa tarakilishi zile zenye nenosiri zilikuwa zimechukuliwa,muda huo alikuwa amejiinamia akiwa ameshika kifaa cha gesi ambacho hutumiwa na wagonjwa wa pumu. Alikuwa akihema sana baada ya pumu yake kumpanda kwa ghafla sana, mafeni yaliyokuwa eneo hilo yote yalikuwa yamezimwa kwani ilikuwa nu hatari sana kwake. Alitulia baada ya kipindi cha muda ndipo aliweza kuwa katika hali ya kawaida kidogo, aliinua kichwa chake na kisha akamtazama Askofu ambaye alikuwa ameleta taarifa hiyo akiwa na Josephine aliyetoka kufanya mauaji.



    "Hii ni mbaya sana jamani hebu fikirieni mara mbili ikija kujulikana je? Pesa zetu zote zimekombwa na huyu kiumbe na isitoshe amechukua ushahidi uliokuwa ni muhimu sana kwetu. Nimejitahidi kupoteza kushahidi kwa kuwauzia habari juu ya uwepo wanausalama waliotumwa kufatilia kifo cha Bai kule Dodoma ili tu tusiwe pabaya lakini mambo ndiyo haya yanazidi kuwa mabaya zaidi sijui hata tufanyeje" Aliongea kwa sauti ya chini yenye kulalamika



    "Mheshimiwa hapa tusiwe namna hiyo ni ishara tosha ya kukubali kushindwa, hapa ni kama tunacheza masumbwi. Jua upande mmoja umetuelemea" Askofu aliongea



    "Sasa tufanyeje maana Moyo hajajua chochote kile kuhusu hili tujadilini na kisha tumjulishe kuhusu hili jamani" Aliongea



    "Hakuna jambo litakaloharibika Mheshimiwa sisi tuo makini bado na muda huu tunamfuatilia Jama, na imani ipo siku atatoa atarifa idara yake na hapo tutampata vizuri kwani mawasilinao yao yote tunayasikiliza kwa sasa" Josephine aliongea



    "Unasema nini wewe Josephine? Hamna lililoharibika na haya yanayotokeni nini? Khemiri mtu wetu lakini tumemuua kwa mikono yetu kwani yeye ndiye angetuweka pabaya zaidi kwani nyendo zake zilikuwa zipo machoni mwa huyu mtu kutokana na kuharibika mambo ili tujiokoe. Bado mwenzatu ameauwa na pia laptop zote mbili zimeibiwa unasema hakuna lililoharibika hebu chekecha akili yako binti" Alimuambia kisha akaanza kuhema tena kwa nguvu sana na kupelekea aipeleke mashine yake mdomoni kwa mara nyingine na kisha akaiminya na kuvuta hewa iliyokuwa ikitoka ndani yake, baada ya hapo alijiinamia chini.



    "Mheshimiwa cool down bado tupo kazini na sasa hivi nitaingia Jack Shaw mwenyewe kazini" Askofu aliongea huku akimshika bega kutokana na hali aliyokuwa nayo hasa akifikiria kuja kujulikana hadharani.



    "Siwezi nikawa kwenye hali ya kawaida mpaka haya mambo yawe sawa jamani si kazi ndogo kujenga heshima ambayo ninayo kwa sasa jamani ni kazi nzito sana ina inagharimua hata miaka kumi kwa mtu mwenye kutumia njia za kiuhalali" Aliongea kwa tabu sana



    "Mheshimiwa sisi tupo makini na tupo pamoja na wewe usihofu kabisa kuhusu hilo" Josehine alimuambiwa kwa namna ya kupole sana na kupelekea anyanyue kichwa kuashiria kuwa alikuwa amekubali kabisa.



    "Ok mpigieni na Scorpio aje hapa na awepo wakati tunapanga mipango mipya" Aliongea pindi aliponyanyua kichwa chake kwa mara ya pili, muda huohuo Josephine alichukua simu na kumpigia Scorpio lakini simu iliita tu bila ya kupokelewa.



    "Hapokei simu huyu" Josephine alisema baada ya simu kutopokelewa.



    "Pumbavu huyu yupo kwenye umalaya wake, yaani tangu aingie Tanzania hiyo imekuwa kazi yake. Inaonekana wasichana wa kitazania wamemtia wazimu" Askofu aliongea kwa hasira sana



    "Yaani mkuu hata mimi nimeshamsema sana kuhusu hilo lakini kila nikimuambia tunakuwa hatupatani kabisa yaani" Josephine aliongea



    "Jamani hapa ni kumtafuta tu huyu hatuwezi kuweka mpango akiwa hayupo tutakuwa tunacheza tu kwani yeye ni muhimu pia ndiyo maana tukalipa pesa ya nauli yake kutoka Ujarumani hadi hapa Tanzania" Mheshimiwa naye aliingilia



    ****



    Muda huo Moses alkuwa akijiandaa kutoka ofisni kwake kwenye idara ya usalama wa taifa, alikuwa akiweka mizigo yake muhimu kwenye mkoba kwa ajili ya kuondoka nyumbani kwake. Alipomaliza kuweka vitu muhimu kabisa kwenye mkoba wake simu ya mezani ya hapo ofisni iliita, muda huo haukuwa muda ambo alikuwa akipokea simu za kikazi kwani alikuwa umeisha muda ilimbidi ainyanyue simu hiyo na kuipoke an hakuwa na namna.



    "Mkurugenzi hapa ongea........Jama wa Majama ni wewe kweli.....Oooh! Thank god tunakutafuta zaidi hata ya pumzi zetu nakuomba sana tuonane au uje ofisni kwangu....ok nitawasiliana na wewe zaidi" Baada ya hapo alikata simu na kisha alitoka kwenye ofisi hiyo akiwa na tabasamu kwani kazi aliyokua ameambiwa na Mzee Kabaita alianza kuona urahisi wake, kumbe hakujua kabisa kuwa mambo hayo yalikuwa ni magumu sana tofauti na alivyokuwa akifikiria kwani tayari yalikuwa yametupiwa jicho na aliyekuwa yupo upande wa kushoto kwake. Ingawa kulikuwa na mwingine ambaye alikuwa yupo kulia kwake bado jambo hilo lilikuwa na ugumu sana tofauti na alivyofikiria, hakika hakujua kabisa kuwa walikuwepo waliokuwa wakihaha kuzima hicho alichokuwa akikitafuta.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Muda huohuo simu ya Askofu iliita ikabidi wote wakae kimya ili aweze kupokea, aliipokea simu hiyo na kisha akaongea na huyo mtu ambaye alikuwa amempigia simu muda huo. Ilikuwa ni taarifa ambayo ilikuwa ni njema kabisa kwa upande wao na alipomaliza kuongea na simu alijikuta akitabasamu na kisha akawaangaliz wenzake, wenzake walibaki wanashangaa kwani hawakujua kabisa alikuwa akitabasamu kitu gani hadi muda huo aliokuwa amemaliza kuongea na simu hiyo. Aliwatazama wenzake kwa sekunde kadhaa akiwa yupo kimya kabisa kama vile alikuwa amekumbwa na mshangao wa ghafla sana, baada ya hapo alisimama akiwa bado ni mwenye tabasamu na kisha akaendelea kuwatazama.



    "Shaw kuna kitu gani?" Mheshimiwa Roho aliuliza lakini Askofu hakujibu bali alitulia tu huku akiwatazama kwa tabasamu pana usoni mwake



    "Mkuu nini kipya?" Josephine naye aliuliza



    "Jama Wa Majam hatimaye yupo jijini, amepiga simu kwa bosi wake sasa hivi. Vijan wamenasa location yake tayari" Aliongea na kuwafanya wenzake nao watabasamu.



    "Yes! Leo hii tunamfuata hatusubiri zaidi tukitoka hapa tu jioni hii" Josephine aiongea



    "Mfuateni pia msiende kichwakichwa tena inabidi muwe wawili maana yule mtu naye ana akili kama mchawi" Mheshimiwa aliwambia



    "worry out Jack Shaw nipo kazini sasa hivi na tunaenda sasa hivi" Askofu alimtoa hofu



    "Yaani tukiipata tu ile paltop yake tutamuachie huyo N001 hayo malaptop yote manne halafu ile tunaiharibu hakuna namna sitaki kwenda Segerea" Mheshimiwa aliongea.





    USIKU

    Majira hayo Jama Wa Majama alikuwa ameketi kwenye kiti ndani ya moja ya chumba ndani ya nyumba yake, akili iikuwa ipo katika kutafakari kitukile ambacho kilikuwa kimemfanya hadi akatoa mguu kutoka kijijini hadi akafika mjini hapo. Akili ilikuwa ipo makini tu katika kupanga mkakakti wake maalum wa kuweza kufanya kile akilichokuwa kimemleta hapo, huruma aliyokuwa nayo kwa mtu asiye na hatia kupewa kesi ndiyo ilimfanya hadi awe hapo. Alikuwa amekuja kwa siri sana na alijua kuwa uwepo wake ndani ya eneo hilo utaendelea kuwa siri, hakujua kabisa kuwa alikuwa ameshauza siri yake ya kuwepo ndani ya eneo hilo kwa watu waliokuwa wakimsaka kwa udi na uvumba.



    Alichojua kuchikicha ubongo wake ambao ulikuwa umegeuka chekecheo la mawazo, ilikuwa ni jinsi ya kuweza kumfanya Mheshimiwa Kabinuki atoke nje ya nondo na heshima yake irudi kama ilivyokuwa hapo awali. Uzalendo aliokuwa nao Mheshimiwa yule, aliona haikufaa kabisa kuweza kuwekwa nyuma ya nondo kwani ilikuwa ni sawa na kumkosea heshiam sana na kumtusi. Muonekano wake wa kuvaa nguo ambazo zilikuwa zikiunadi umasikini asiokuwa nao, alikuwa ameshauodoa na muda huo alikuwa amevaa suruali nyeusi ya kitambaa pamoja na shati jeusi ambalo lilikuwa limempendeza sana. Bado hakuwa ameutoa ule muonekano wake wa kizee aliendelea kuwa nao kama kawaida, hakutaka kuutoa katika muda huo aliokuwa akitafutwa kwa udi na uvumba. Hata msiba wa mke we kipenzi hakuwa amehudhuria kutokana na kuwa na kitu kile ambacho kilikuwa na manufaa kwa taifa lake, aliona ni bora aonekne ni nuksi kwa familia na ndugu wa mke wake kuliko kupoteza kitu muhimu sana kwa taifa zima.



    Muda akiwa anachekecha mawazo kwenye ubongo wake alianza kusikia sauti ya mbwa waliokuwa wakifanya ulinzi nje ya nyumba hiyo wakibweka kwa nguvu sana, kubweka huko kuliashiria kuwa kulikuwa na ugeni ambao haukuwa wa kawaida kabisa. Aliposikia sauti hizo alinyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekiwekea kalisho lake, alisogea hadi dirishani na kisha akachungulia nje. Aliwaona mbwa wake wakiwa wanabweka kwenye eneo ambalo taa za nyumba hiyo zilikuwa zimefika kikomo, ilikuwa ni ndani ya eneo lenye giza ndiyo Mbwa hao walikuwa wakibweka kwa nguvu sana jambo ambalo lilimfanya asiwe hata na hamu ya kuendelea kukaa ndani ya chumba hiko. Alichoamua kukifanya ilikuwa ni kuinua silaha yake na kisha kuipachika kunoni na akatoka nje ya nyumba hiyo, akiwa ni mwenye hadhari kwa akili na hata mwili. Alitembea hadi kunako mlango wa kutokea nje, alipokuwa yupo njiani katika kutembea huko ghafla mbwa wote walinyamaza kimya ghafla na hwakuendelea kubweka. Hilo lilimfanya asikubali kabisa kuwa hao mbwa alikuwa wakibweka tu kwakuwa nje ya eneo hilo amepita mpita njia nje ya uzio, alitoka nje kwa mlango mwingine kabisa na akasogea hadi eneo ambalo walikuwa wapo mbwa wake akiwa ni mwenye kuhadhari mazingira hayo yaliyokuwa yapo karibu.



    Aliwakuta mbwa wake wakiwa wamelala chini kama vile walikuwa na usingizi, alipoona hali hiyo alijua kabisa kuwa kwenye himaya yake hiyo kulikuwa na ugeni ambao haukuwa rasmi wala taarifa. Hilo lilimfanya aaangalie eneo lote kwa tahadhari na kisha asogee jirani kabisa na eneo hilo, alipowagusa mbwa wake hao kuwatazama hali zao aliona hawakuwa wameondokwa na uhai zaidi ya kuingiwa na usingizi usio na ratiba. Jama Ma Majama vinyweleo vyote vya mwilini mwake vilimsisimka alipogundua hilo, alikuwa ni kama alikuwa amekumbwa na msisimkoo wa ghafla kutokana na kufanyiwa kile ambacho husisimua mwili. Hali kama hiyo alikuwa akijua kabisa kuwa utokeaji wake ulikuwa ukiambatanishwa na kuwepo kwa hali isiyo ya kawaida, akiwa kwenye msisimko huo hata haikupita dakika alihisi kitu kikitua kwenye kiuno chake kwa nyuma na kumfanya aende chini. Akiwa anaanguka kwenda huko chini alijiwahi kwa kupiga sarakasi maridadi sana, alibiringika mtindo wa 'roll' ili asije akaumia. Alipokaa sawa aligeuka nyuma kwa namna ya kipekee kwani alikuwa ameshatambuwa kuwa ndani ya nyumba hiyo alikuwa amevamiwa, alikutana na mwanadada aliyekuwa amevaa nguo ya mazoezi akija kwa teke la kasi sana. Jama hapo alidunda kamz mcheza masumbwi na kisha akasoge kando kwa kasi ya ajabu, yule Mwanadada alipitiliza na teke lake na kisha aliongezewa na teke jingine ambalo lilimyumbisha nusura limuangushe.



    Mwanadada huyo alipokaa sawaa kugeuka nyuma kupambana ma Mamba aliyekuwa kitetea himaya yake, alimkuta akiwa tayari ameshajiweka sawa. Alichokifanya baada ya hapo ni kukunja mikono ya shati lake alilokuwa ameliva kwani alishatambua kabisa huyo Mwanadada hakuwa kiumbe cha kawaida , teke ambalo ilitua kiunoni uzito wake tayari ulikuwa umeshatangaza kuwa alikuwa amevamiwa na kiumbe ambaye alikuwa na uwezo naye sawa. Baada ya kukunja shati hilo alianza kunesa huku akimsogelea huyo Mwanadada, naye hakuwa nyuma alipoona anasogelewa na mtu ambaye alikuwa na muonekano wa kizee aliona ulikuwa si muda wa yeye kumtuliza kwani aliamini kabisa hakuwa huyo waliyekuwa wakimtafuta. Aliingia kwa ngumi ya kikarate akilenga sehemu mbalimbali za mwili wa Jama, ngumi hizo zilitoka nje ya lengo kabisa kwani alikutana na mpanguaji mzuri sana wa mapigo kama hayo ambayo yote yaliishia nje. Aliletewa mapigo naye aliyapangua kwa ustadi hapo na hapo ndipo na yeye akatambua kuwa alikuwa akipambana na kiumbe kama yeye, aliongeza mashambaulizi hayo kwa kiumbe huyo lakini hayakufikia lengo. Alipobadili mtindo wa upiganaji alikutana na kiumbe huyo alikuwa akiujua mtindo huo, alipigana kwa muda na hatimaye Mwanadada huyo alianza kuishiwa pumzi na hapo ndiyo ikawa nafasi nzuri kwa Jama.



    Hakuwataka kuipoteza nafasi hiyo kabisa yeye alianza kushambulisha kwa nguvu zake zote huku akiwa karibu ya mwanadada huyo, kuishiwa na pumzi pamoja na kuwa karibu na adui yake ambaye alikuwa amemzidi ghafla mwendo wa upiganaji. Lilikuwa ni suala ambalo lilimchnganya sana Mwanadada huyo aliyekuwa akimudu mwanzo kusimama na mpinzani wake katika pambano hilo, alijaribu kuzuia lakini alijikuta akipatwa na baadhi ya mapigo ambayo yalizidi kumpunguza nguvu kabisa. Alipozidi kupungua zaidi Jama Wa Majama alifanya kitu cha haraka ambacho kilikuwa ni kama kumlevya huyo Mwanadada asizidi kuleta upingamizi, aliachia ngumi mfululizo ambazo chache zilikosa lengo kutokana na kubahatishwa kukwepa. Hakusubiri zaidi alijirusha juu akijiandaa kutoa teke la kuzunguka maarufu kama 'round kick', akiwa yupo juu kabla hajatoa teka hilo alijikuta akisukumwa na kitu kigumu sana kwenye bega na alienda kusalimiana na ardhi ya eneo hilo. Lilikuwa ni teke ambalo lilitoka kwa haraka kwa Kiumbe mwingine aliyekuwa amevamia eneo hilo kuja kupambana nao, teke hilo lilikuwa ni zito kuliko lile la kwanza. Alipoanguka chini alibiringita hakutaka kukaa sehemu moja hiyo aliyoangukia kwa hofu ya kuongezewa pigo jingine la kushushwa, alipobiringita na kukaa katika ambalo ulimuwezesha kujiinua. Aliweza kumuona Mwanaume wa kizungu ambaye uso wake ulikuwa hauonekani vizuri, hakutaka kujiuliza mara mbili kuwa huyo mtu alikuwa ni kiumbe wa hatari kiasi gani. Alijifyatua kutoka hapo chini na akasimama wima na kisha alibadili mtindo wa upiganaji Wa kumfuata Mzungu huyo, kitendo cha uvamizi wa mzungu huyo alijua kabisa kuwa alikuwa akitazama mtindo wa upiganaji aliokuwa akiutumia. Hivyo kutumia mtindo ule ilikuwa ni hatari nyingine kabisa kwake, kwani angepigwa vibaya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuja na mtindo wa kombati katika kupigana na huyo Mzungu lakini hakufua dafu kwani mapigo yote yalizuiwa na Mzungu huyo alionekana alikuwa ni kiumbe mwenye kazi zaidi kuliko kawaida. Alianza kupewa mapigo ya ajabu kutoka kwa yule Mzungu ambaye yalimrudisha chini tena katika upande ule aliokuwa ameangukia, hapo alijua alikuwa akipambana na Jinamizi na si kiumbe kama yule aliyekuwa akipambana naye mwanzo. Jinamizi hili hakuwa na uwezo wa kupambana nalo kwani lilikuwa limemzidi ujuzi, pamoja na kukiri hayo bado alisimama tena wima kupambana.



    "Komando" Aljisemea moyoni hukua akiwa amekunja ngumi kumuagalia Mzungu yule ambaye alikuwa amekaa kwenye mkao wa kimadharau kabisa. Alimfuata kwa mtindo wa aina nyingine wa kupigana kwani alitambua kabisa alikuwa akipigana na mtu ambaye alikuwa na uwezo sawa na idadi ya wanajeshi mia moja wa kawaida, yeye hakuwa amefikia ngazi hiyo.



    Alipigwa sana kutokana na Mzungu huyo kubadili mapigo na kutumia yaliyokuwa yakimchosha zaidi, alipigwa hadi kaanguka chini na kushindwa kuinuka. Muda huo Yule Mzungu alimsogelea karibu yake akiwa amenyoosha mkono wake akitaka kumaliza pigo la mwisho, kabla hajapiga pigo hilo alisikia upepo ukivuma kwa nguvu sana kuelekea kichwani mwake. Mzungu huyu alitambua kabisa huo upepo haukuwa upepo wa kawaida kabisa bali lilikuwa ni pigo la nguvu sana, alipiga saraksi moja matata kulikwepa pigo hilo na kisha akaosogea ambali na eneo hilo.



    "Norbert" Mzungu huyo aliita huku akimtazama huyo aliyemletea pigo hilo.



    "Askofu Valdermar hatimaye tunaonana tena, sasa hivi ni kimakabiliano zaidi" Norbert aliongea huku akimsogelea Askofu kwenye eneo ambalo alikuwa amesogea baada ya kukwepa pigo lake.



    Majinamizi mawili yaliyokuwa yakikaribiana kiuwezo kwa mara ya kwanza yalikuwa yamekutana ndani ya mpambano, wale waliokuwa wamjeruhiwa walikuwa wamekaa kando huku wakiangalia mpambano huo uliokuwa ukiwahusu wale waliokuwa na maajabu kuliko wao. Mpambano ulianza kwa kila mtu kuonesha ujuzi wake katika kupigana, wote walipigana kwa uwezo wao na ikafika muda hakuna aliyekuwa amefanikiwa kutia pigo kwa mwenzake. Hiyo ilisababisha wote kwa pamoja watie mbinu za kininja kwenye mpambano huo, hapo ndipo aliyekuwa na ujuzi kushinda mwenzake aliweza kujulikana walipotia mbinu hizo. Haikufika hata muda wa dakika tano tayari Askofu alikuwa amesharuhusu mapigo matano tofauti kuingia kwenye mwili wake kutokana na kuzidiwa uwezo, mtindo wa sarakasi pamoja kukwepa vitu kwa ufundi wa hali ya juu ndiyo vilifuata kwa muda huo waliokuwa wakipambana. Norbert alidhihirisha wepesi wake na Askofu vilevile alidhihirisha ingawa alikuwa akipatwa na baadhi ya mapigo, ujuzi wa kininja wa hali ya hai ya juu alionao Mzee wa kazi ulisababisha aweze kumtawala Askofu ndani ya pambano hilo. Muda mfupi baadaye aliachia pigo ambalo lilimpata Askofu kwenye mbavu hadi akaenda chini, pigo hilo halikuleta athari kubwaa nyingine kwenye mbavu zake zaidi ya kuzijeruhi. Askofu hapo aliona alikuwa amezidiwa hatua kubwa sana na laiti kama angeendelea kupambana angekuwa ameshajiweka kwenye hali mbaya sana kutokana na kujeruhiwa huko, ingawa alikuwa amejua hilo alijaribu kupambana kwa mara ya mwisho na alipoona alikuwa amezidiwa aliamua kuuruka uzio wa nyumba hiyo na hakujali kabisa Josephine aliyekuwa amenguka chini akiwa hajiwezi. Aliona alikuwa na mzigo tayari kwa kujaeruhiwa na laiti kama angemchukua Josephinea angekuwa amejiongezea mzigo, alimuacha hapo kwenye mikono isiyo salama kabisa ndani ya nyumba ya adui waliyewakuwa wamemvamia.



    Hilo lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa Josephine na muda huo ndipo alipijuta kuingia kwenye kundi hilo, alimlaani sana Askofu kwa kukimbia na kumuacha eneo hilo wakati walikuwa wapo apmoja. Umoja waliokuwa nao katia mambo mbalimbali hasa wakiwa mtuna Bosi wake aliuona ulikuwa wa kinafiki ikiwa ameshindwa kumsaidia akiwa yupo kwenye eneo hilo, akiwa amelala chini alimshuhudia Norbert akimuinua Jama wa Majama na kisha akajongea naye kwa taratibu hadi eneo ambalo alikuwepo muda huo alikuwa amekaa kitako.



    "Nafikiri ushaiona faida ya kuwa Mhalifu ukiwa kwenye shida hukumbukwi" Alimuambia na kisha alimuongeza teka la mdomo hadi akatema damu mdomoni kutokana na uzito wa teka hilo.



    "Hii ni trela tu,ulinikimbia na kisha unakuja kuua Watanzani leo utaniambia mwenyewe anayewatuma" Norbert alimuambia na kisha alimuachia Jama mara moja ambaye alijiegemeza kwenye ukuta, alimpiga teka la tumbo Josephine na wala hakujali kabisa jinsi alivyokuwa akitoa miguno ya maumivu.



    "Ni bora ningemsikiliza Eva nikakuua na bomu pamoja na Thomas kumbe kukudharau ndiyo ukaota mapembe na kurudi tena" Aliongea huku akisitisha kumpiga na kisha akamnyanyua na kuingia ndani ya nyumba ya mwenyeji wake, mwenyeji wake alifuatia kwa nyuma akiwa anajikongoja akiushikilia ukuta wa nyumba hiyo.



    ****



    Taarifa iliyokuwa imepamba vyombo vya habari kwa muda huo ilikuwa ni kuzidiwa ghafla kwa waziri wa fedha Mheshimiwa Janstu Mahujuraja, ilikuwani shinikizo la damu ambalo lilikuwa limemkamata Mheshimiwa huyu aliyekuwa akiheshimiwa sana ndani ya nchi kutokana na sifa zake alizokuwa amejijengea akiwa yupo chini ya Rais Zuber. Kuzidiwa kwake na hadi kukimbizwa kwenye hospitali ya Regency maeneo ya Upanga, ilikuwa ni jambo la kusikitisha sana kwa watanzania. Ilikuwa ni shinikizo la damu la kupanda ndiyo lilikuwa limemkumba kwa ghafla sana akiwa yu ndani ya nyumba yake, kuanguka huko kwa shinikizo hilo kulipelekea hata simu yake ya kisasa aliyokuwa akiitumia nayo isalimiane na sakafu ya nyumbani kwake. Alikuwa amepokea taarifa ambayo ilimfanya aanguke huko hadi apoteze fahamu kutokana na shinikizo la damu, pamoja na kuanguka huko hadi akafikia hatuz ya kupoteza fahamu bado jambo hilo lililosababisha hadi akaanguka halikujulikana kabisa na familia yake haikuwa imefungua mdomo kuzungumza kwa kile kilichokuwa kimemfanya aanguke.



    Uzushi wa vyombo vya habari ndiyo suala ambalo walikuwa wakilihofia sana famiia hiyo, hakutaka kabisa kusema kuwa chanzo ilikuwa ni simu. Waandishi wa habari wapekuzi walikuwa wamefika kwenye neo hilo la hospitali ambako kulikuwa kumewekwa ungalizi mkubwa kwenye chumba alichokuwa amelazwa. Walianza kufanya mahojiano na wanafamilia hao lakini hawakuambulia kitu chochote, walipozidisha maswali yenyee kuudhi na kukera walijikuta wakafukuzwa kama Mbwa aliyekuwa ameingia nyumba ambayo haikuwa ya kwao. Bado waandishi hawa hawakukoma kabisa waliendela kubaki nje ya hospitali hiyo kwani walijikua kabisa kulikuwa na ulaji ndani ya eneo hilo, tabia ya mamba akikosa windo kubaki kwenye eneo ambalo kulikuwa na nafasi ya kupata windo ndiyo walikuwa nayo. Hata imani za kuwa windo hilo litaurdi tena ilikuwa imejengeka kwenye vichwa vyao, hawakuwa tayari kunyanyuka eneo hilo hasa waandishi wa habari wa magazeti.



    Waliendelea kukaa kwenye eneo ilo hata walipoanza kuingia mawaziri wengine waliokuja kumuona mwenzao, wao walijaribu hata kuwahoji hao kutokana na kuisaka habari kwa nmna yeyote ile huku wakiwapiga picha mbalimbali walipokuwa wakiingia eneo hilo. Waandishi wa hxbari hao walibaki midomo wazi baada ndani ya eneo hilo kuingia waziri mbaye alikuwa ni chui na paka na Mheshimiwa Mahujuraja, huyu hakuwa mwingine ila ni Mheshimiwa Barnaba Liwale aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani. Yeye alikutana na maswali ya waandishi wa habari kuhusu ugomvi wao waliokuwa nao ingawa walikuwa ni wanachama wa chama kimoja, maswali hayo yalikuwa ni yenye kuudhi lakini Meshimiwa Liwale aliweka uvumilivu.



    Aliyajibu maswali yote kwanamna ya kistarabu sana huku akiwaumbua badhi ya waandishi waliokuwa wakiuliza maswali ambayo yalikuwa hayana maana, Mheshimiwa liwale aliutumia muda huo aliokuwa yupo hapo kujibu maswali yote ya waandishi hadi pale waliporidhika ndipo akingia ndani ya jengo la hospitali akiwa ameongozana na kundi la watu. Hata yeye mmwenyewe hakuwa kwenye hali nzuri kabisa ila kutokana na kuwa mawenzake alikuwa amezidiwa kuliko yeye ilimbidi aje kumuona kwani ilikuwa ni muhimu. Muda huo alikuwa akiongea kwa kupooza sana ambako haikuwa kawaida yake kabisa. Ule uchangamfu wake aliokuwa nao ulikuwa umefifia ikiwa siku hiyo ni mara ya pili kumuona, mara ya kwanza kuonekana akiwa kwenye hali kama hiyo ilikuwa ni katika mwaka uliopita ambapo alifikia hatua ya kulazwa kwenye hospitali hali ilipokuwa mbaya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa na tatizo moja kubwa kama alivyokuwa Mheshimiwa Mahujuraja, matatizo yao wote yalikuwa hayaponi kabisa katika hospitali yoyote jambo lililopelekea awe nimtumiaji wa dawa kwa ajili ya tulizo ya tatizo hilo. Sasa dalili za kuonekana kwa tatizo hilo lililokuwa nalo lilikuwa limeshamuanza lakini alivumilia na kuja kumuona huyo mwenzaekambaye alikuwa amezidiwa.



    Kitendo cha kuwaaacha wanahabari hapo nje ilikuwa ni kama amewapa habari , haikupita muda wale waliokuwa wana tovuti mitandaoni walianza kuiripoti habari hiyo huku wakimwagia sifa kedekede. Kitendo cha yeye kuja kumuona hasimu wake kwenye mambo mbalimbali wawapo kwenye Bunge ndiyo kilifanya apewe sifa hizo ambazo alikuwa amejichukulia muda huo aliokuwa ameingia humo ndani. Huko ndani alikutana na familia ya kiongozi mwenzake ambayo ilimpokea kwa ukarimu mkubwa sana. Wao kwa mara ya kwanza ndiyo walimpa kisa kizima cha kupatwa kwa hali hiyo, Mheeshimiwa Liwale alisikitishwa sana na hali hiyo ilikuwa imemkumba kiongozi mwenzake kisha akakaa na familia yake kwenye eneo la kusubiri wagonjwa.



    Akiwa amekaa eneo hilo alikuwa akifanya kazi kubwa ya kuifariji familia hiyo juu ya hali ya Mheshimiwa mwenzake, maneno yake anayoyatumia kwenye siasa aliyatumia hapo alipokuwa amekaa na familia hiyo. Haikuwa mara ya kwanza kwa familia hiyo kumuona Mheshimiwa Liwale hivyo walikuwa wamemzoea sana, walikuwa wameshazoea ukorofi wao waliokuwa wakiuweka ndani ya bunge na hata kwenye mitandao ya kijamii. Haikuwa kutokea ukorofi huo ukawa umewekwa uraiani, ndiyo maana walikuwa ano katika eneo hilo kwani walikuwa hawana ukorofi uliokuwa umewekwa sehemu kama hizo Hakika ya siasa ni mchezo wa kuigiza mtupu na wote waliokuwa wapo ndani yake ndiyo yalivyokuwa maisha yao, ndiyo maana hata hawa wenye kauli wawili walikuwa na maelewano geresha wakiwa wapo ndani ya ulingo wao mwingine ambao adhira ilikuwa ikiona kama walikuwa wakishindan kihoja.



    ****



    Joephine akiwa hana nguvu aliburuzwa hadi sehemu ya ndani ya nyumba ya Jama Wa Majama, alipelekwa hadi eneo ambalo kulikuwa na chumba kimoja kikiwa na bomba la chuma refu sana lililotokeza juu ya dari ya chumba hicho. Hapo alifungiwa kwenye bomba hilo imara kwa pingu kuanzi mikono hadi miguu. Ilikuwa ni mara ya kwanza kuanza kujuta kwenye maisha yake tangu ajiunge na upande huo haramu, sasa alikuwa ameishia kwenye eneo ambalo ilikuwa ni ngumu sana kupona au kutoka. Alikuwa ameingia kwa mara ya pili kwa mtu ambaye alinusurika kuuawa naye, aliona kupona ilikuwa ni ngumu sana kwani mtu huyo alikuwa najuta sana kwa kuendelea kwake kuwa hai juu ya mgongo wa radhi.



    Mbele yake Jama Wa Majama ambaye tayari alikuwa ameshapatiwa huduma muhimu baada ya kupatwa na baala la kipigo, alikuwa yupo yupo kwnye kiti huku Norbert ambaye hakuwa na mzaha hata kidogo akiwa yupo amesimama. Wote wawili macho yao yalikuwa yapo kwa binti huyo aliyekuwa amefanya matukio mazito sana ndani ya nchi hii, matukio hayo ambayo yalikuwa ni muhimu sana kwa wakubwa zake ambao walikuwa wamempa ulaji ndani ya nchi hii.



    "Haya sasa jiangalie upo wapi kwa huo ujinga wako" Norbert alimuambia huku akimtazama usoni, maneno hayo yalimfanya awe ni mwenye kujuta sana.



    "sasa jiulize ni nani atakayekusaidia hapa zaidi ya sisi kukupa huruma hii tunayotaka kukupa, tunahitaji ukweli wako tujue ambao wapo nyuma ya masuala haya na kwa ajili gani wapo yake" mzee wa waotot warrembo wapendezesha macho aliongea.



    "Nor please nipo tayari kukuambia ile niahidi kitu kimoja tu nitakuwa huru" Aliongea



    "Yaani pamoja na kutuletea maafa yote hayo bado unatuletea masharti huna akili wewe" Norbeet aliongea na akamfuata kwa kasi hadi karibu yake na kuanza kumpiga kipigo kizito kama alikuwa akipigana na mwanaume mwenzake, kipigo hicho kilimchosha tu Josephine ndani ya muda mfupi na alikubali mwenyewe kuongea.



    "Ukweli wako ndiyo utakaotufanya tukuonee huruma haya ongea kwa sasa, ukichelewesha dakika moja tu utakuwa upo kwenye kipigo kingine. Sitaki zaha na watu kama nyinyi kwenye kazi yangu kabisa" Alipewa kitisho kizito ambacho kilikuwa kikienda kumpata kweli ikiwa ataenndelea na ukaidi wake alikuwa ameuonesha, Josephine hakuwa na namna mwenyewe aliutapika ukweli ambao ulikuwa unashabihiana kila kitu na ukweli ambao alikuwa nao Jama. Mwenye ukweli huo mwenyewe aliafiki kuwa alikuwa akiongea ukweli mtupu na hakukuwa na uongo ndani yake.



    "Baada ya kueleza ukweli una machaguo mawili tu kuanzia sasa, chaguo la kwanza ni kwenda kwenye gereza la magaidi lililokuwa lipo Iringa huko porini ukutane na wenzako waliokuwa wapo kwenye kazi kma hizi au uuawe hapo" Norbeert alimuambiwa pasipo kumjonea huruma yeyote kutokana na mabalaa aliyokuwa ameyaleta, Josephine alibaki akiwa ni mwenye kuumia sana kutokana machaguo hayo aliyokuwa amepewa. Mwenyewe alichagua kwenda kupelkewa huko gerezani, lilikuwa ni gereza jipya lililokuwa mbali sana ambako hakukuwa na njia yoyote ya gari ingeweza kufika huko. Kamishna Wilfred na wale wote waliokamatwa kwa matukio ndani ya nchi ya Tanzania walitupwa huko ambako kulikuwa na mateso sana kuliko kawaida kwa wenye ujeuri.



    Wapo ambao gereza hilo walilifananisha na gereza la Guantanamo la ndani ya bara la Amerika, yote ilikuwa ni kutokana na jinsi lilivyo. Gereza hilo lililogharimu mabilioni ya shilingi katika kukamilika kwake na waliokuwa wamekamatwa kwenye kisa cha WAKALA WA GIZA na wale wote aliokuwa wamekamatwa kwenye matukio makubwa nchini walipelekwa huko kuanza maisha yao huku Magereza ya kawaida yakiendelea kuwa na wafungwa wa kawaida. Matukio ya kuawa pamoja na kufanyiwa vitu vibaya baadhi ya wafungwa wa kawaida waliokuwa wamechanganywa na wale wa matukio ndiyo yalipelekea kujengwa kwa gereza hilo. Sasa Josephine alikuwa akitaka kupelekwa huko ambako kulikuwa na wanwake wajeuri zaidi yake, lililokuwa na utukutu zaidi yake.



    "Mama eh! Huruma yako ni kwenda Nyumba ya giza huko na si vinginevyo hivyo jiandae tu wewe ni wa kutupwa huko" Norbert alimuambia kisha akatoka kwenye eneo hilo akiwa ameongozana Jama Wa Majama ambaye alikuwa akimtegema yeye kuweza kutembea vizuri.



    ****



    Baada ya kuweza kutoroka mkono wa kifo kutoka kwa Norbert alipoona amezidiwa nguvu, muda ambao Josephine alikuwa akimaliza kuutapika ukweli yeye alikuwa yupo ndani ya nyumba ya wageni kwani alikuwa yupo kwenye wakati mgumu sana kwenda kwenye makazi ambayo tayari yalikuwa yamegunduliwa na Norbert. Askofu muda huo alichukua simu na kumpigia Scorpio akijua bado yupo hai lakini simu yake iliita tu bia ya kupokelewa, aliipiga mara nyingi zaidi lakini jibu ilikuwa ni kazi bure kwani simu hiyo haikuwa ikipokelewa kabisa na huyo aliyekuwa akimpigia simu. Jambo hilo lilimuudhi sana akaona kuwa alikuwa akidharauliwa na huyo kijana wake, alijua kuwa alikuwa yupo kwenye umalaya kumbe hakuwa si miongoni mwa waliokuwa wakivuta pumzi ndani ya dunia hii. Hasira zilimpanda hasa na ziliongezewa na maumivu yaliyokuwa yakimsumbua, ubavu ulikuwa ukimsumbua sana na kuchnganya na kutojibiwa kwa simu yake ilikuwa ni hasira kabisa.



    Ubavu uliokuwa umechezea dhahama nao ulikuwa ukimjua kumtesa sana, alishindwa hata kuulalia na akajikuta akiuweka juu. Hakika ubavu huo ulijua kumpa masharti kama vile alikuwa yupo kwa Mganga wa kienyeji aliyekuwa akimtengezea dawa. Jeuri zote na ukaidi wote aliokuwa nao mbele ya ubavu huo , hakuwa mjanja kabisa kwani jinsi ulivyokuwa ukimuuma. Haukuwa umevunjika ila cha moto alikuwa amekionja na muda huo kinachoma ulimi wake, hakika maumivu yalijua kumkata hata uwezo wake wote wa kumudu kimapigano ukawa hauna msaada kwake. Alishikwa akashikika, alipatwa na akapatikanika kutokana namaumivu hayo yaliyokuwa yakimsumbua kwenye sehemu hiyo ya ubavu, kunnyanyuka ilikuwa ni mthili ya gari bovu kuupanda mlima kutokana na maumivu hayo aliyokuwa kiyasikia. Yaliyokuwa yamezidi kabisa tofauti na muda ule almabo alikuwa amemkimbia adui yake, siku hiyo alikiri kabisa kuwa alikuwa amepigana na kiumbe mwenye uwezo kama yeye aliyekuwa amemzidi ujanja katika mapigano.



    "Mara nyingine sitokubali, nishajua mbinu zake za kupigana sasa tutapambana vizuri sana" Aljisemea huku akiwa ameulalia ubavu usio a maumivu.



    ****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    [5]

    ASUBUHI ILIYOFUATA



    Hadi mwangaza wa siku mpya unaingia Norbert alikuwa yupo ndani ya nyumba ya Jama wa Majama ambaye alikuwa na nafuu muda huo hadi kuweza kutembea mwenyewe, ukweli wote uliokuwa ukiwahusu walikuwa wanao kwenye tarakilishi hizo na ilikuwa ikisubiriwa muda muafaka wa kuweza kuwasilishwa kwa Mheshimiwa ili kuweza kumuokoa yule ambaye alikuwa hana hatia kabisa. Yale manenosiri ambayo yalikuwa kwenye tarakilishi tofauti yalikuwa tayai yameshawekwa bayana , Jama alitumia muda huo kumuelekeza kila kitu Norbert juu ya uchambuzi wa maneno hayo. Siku hiyo Norbert alikiri kabisa wale waliokuwa wameanda utafiti huo walikuwa wametumia akili sana katika kuyaficha maneno hayo kwani pamoja na ujuzi kwa wote wa kujua maneno ya kimafumbo alishindwa kuyabaini maneno hayo yaliyokuwa yana maana kubwa.



    Alikubali kabisa kuwa Jama na kundi lote waliokuwa wamendaa utafiti huo walikuwa ni watu ambao walikuwa na akili ambazo waliziunda kwa pamoja wakapata kile ambacho kilikuwa kikihitsjika. Aliwapa pongezi kwa kazi hiyo nzuri waliyokuwa m

    wameifanya na hawakukaa kabisa ndani ya nyumba hiyo, ilipofika majira ya saa nne asubuhi wote kwa pamoja walitoka na kuelekea zilipo ofisi za Moses ambaye alikuwa akimtafuta mfanyazi huyo aliyekuwa yupo chini yake kwa siku kadhaa alizokuwa ametoweka kwenye upeo wa macho yake.



    Safari yao ilifikia kwenye ofisi za za maabara ya Umoja wa mataifa huko hawakumkuta kabisa, hawakuwa na changuo jingine iliwabidi watoke na kwenda zilipo ofisi za Idara ya usalama wa taifa kwani walijua kabisa takuwa yupo huko na alikuwa na kazi muhimu sana. Safari yao ilifikia kwenye ofisi hizo na waliingia hadi ndani, wote walisema shida ya kutaka kumuona Moses ambaye alipopewa taarifa ya uwepo wao eneo hilo aliridhia moja kwa moja waingie ndani. Norbert na Jama waliingia ndani ya ofisi ya Moses ambako alimkuta akiwa amekaa kwenye kiti chake akijizungusha, aliwakaribisha kwenye viti akiwa hajamjua kabisa huyo mwingine aliyekuwa na Norbert alikuwa ni nani.



    "Mkuu nafikiri muda wako wa kuniona ndiyo huu umewadia" Jama aliongea kwa sauti yake ambayo ilikuwa imezoeleka na Moses na kupelekea mkuu wake huyo wa kazi ashangae sana kwani hakutarajia kabisa.



    "Jama is tha you?" Moses aliuliza



    "Ys its me, nimekuja kwa ajili ya kumkomboa yule asiye na hatia ambaye alikuwa yupo mbioni kutumikia hukumu isiyo yake" Jam aliongea.



    "Aisee ni bora umeonekana yaani wewe ni mtu muhimu sana kuweza kuwasilisha ushahidi ulionao kwa Mheshimiwa kwani nao ulikuwa ukihitajika kwenye kesi ya Mheshimiwa Kabinuki. Huo ndiyo ungeweza kuamua kila kitu ila kwa ushahidi wa sasa umemuweka ndani" Moses aliongea, muda huohuo Jama alifungua tarakilishi yake ambayo alikuwa kaitunza kama mboni ya macho na kumpatia Moses hukua akiwa tayari ameshaingiza neno siri. Ilikuwa ni ndani ya siku ambayo Mkurugenzi huyu wa idara hii nyeti aliweza kabisa kukubaliana na maneno ya Norbert na kumjuona waziri huyo aliyekuwa amewekwa ndani hakuwa na hatia kabisa, alisoma ushahidi wote muhimu na kisha akairudisha Tarakilishi ile kwa mwenyewe kwani hakuwa na mamlaka ya kukaa nayo kutokana na masharti liyokuwa ameyatoa Rais Zuber wakati akitoa kazi hiyo kwa watu wake.



    "Nikweli kabisa hapa Mheshimiwa ha hatia na wale wawili ndiyo wenye hatia" Moses aliongea



    "Ndiyo hivyo nilitaka ujue tu hilo kwani sikuona hatia aliyokuwa nayo hasa nikijiuliza jinsi alivyoshikwa kwa haraka sana na vidhibiti vilijulikana. Huu ushahidi unatakiwa ufike kwa Mheshimiwa mwenyewe ndiyo aamue" Norbert aliongea



    "Kibaya zaidi Mheshimiwa kasafiri kikazi mara moja na anaingia nchini Alhamisi" Moses aliwaambia huku akiona taarifa hiyo ilikuwa ikichelewa kabisa kufika kwani ndiyo kwanza ilikuwa ni jumapili



    "Thats another issue, huyu jamaa inabidi alindwe kama mboni ya macho hadi inafika siku hiyo" Norbert aliongea kisha akamtazama Jama usoni halafu akamwambia, "Inabidi ukakae kwenye ofisi zetu hadi siku itakapofika kwa usalama wako yule Askofu ni mtu mmoja hatari sana"



    "Hilo la muhimu awe chini ya uangalizi wako wakati unamalizia kazi yako" Moses alisisitiza



    "Kingine kabisa dogo langu napenda nikuambie kuwa hapa ofisni kwako kuna msaliti ambaye ndiye anayeuza taarifa kwa maadui wa nchi hii. Mwanzo kabisa nilijua kabisa kuwa huyu jamaa kirudi jijini hatokutafuta kwa simu yako ya mkononi kamwe bali atatumia ya ofisini humu akijua ni salama zaidi kwani ya mkononi kunaswa mawasiliano ni kitu rahisi sana. Na kweli alitumia simu hiyo na hatimaye akakuambia yupo jijini, nilipokuwa nimesikia hicho ulichooongea kutokana na kukupa taarifa ya kufuatilia simu zako kuna mtu ambaye alikuwa tayari ameshanasa mawasiliano hayo sasa mjiulize vizuri alikuwa ni nani. Unasaji wa simu za humu mnaujua wenyewe hakuna wa nje anayeujua, jiuize ni nani huyo?" Norbert alieleza kwa kirefu, maelezo ambao yaliamsha kabisa akili ya Moses na kuwafikiria wafanyakazi ambao walikuwa wapo chini yake.



    "Hii inaonesha hii simu ninayotumia imewekwa hardware inayofanya haya na sijui ni nani huyu" Moses aliongea na kisha aliichukua simu yake ya mezani na kuigeuza,aliifungua simu hiyo bila ya kifaa chochote kwani ilikuwa imefungwa kwa mtindo kama wa tarakilishi zisizo na nati. Aliipekua ndani ambako alitoka akiwa na kifa kidogo klichokuwa kikiwa taa ya rangi ya bluu na akamuonesha Norbert ambaye alisikitika tu.



    "Huyu ndiye mchawi ndani ya ofisi hii ananasa mawasiliano na pia simu zinazoingia na eneo zinapotoka" Norbert aliongea na kisha alimpa ishara Moses jun ya cha kufanya kwani walikuwa wametambua wazi kuwa walikuwa wakisilikizwa na msaliti huyo ambaye yupo humo ofisini.



    Hawakutaka kuongea suala jingine lolote la siri baada ya kujua kuwa walikuwa wakifuatiliwa na mtu mwingine, ambaye alikuwa yupo upande wa maadui zao akwa anavujisha taarifa Mtu ambaye alikuwa amevunja kiapo cha utii alichokiwek kipindi anajiunga na ofisi hiyo, Moses aliipokea tu ishara hiyo kisha akamuonesha Norbeert alama ya dole gumba kuashiri amemuelewa. Kilichofuata hapo ilikuwa ni Norbert kuaga kuwa anaondoka humo ofisini, alifuatiwa na Jama ambaye naye aliaga vilevile kuwa alikuwa akiondoka baada ya kuweza kufika kuonana na mkuu wake wa kazi.



    Wawili hawa walioingia pamoja ndani ya ofisi hiyo walitoka kwa pamoja wakiwa ni wenye macho ya tahadhari katika kila eneo walilokuwa wakipita ndani ya ofisi hizo zilizokuwa zimesheheni vitengo tofauti vilivyokuwa vimejitosheleza. Walifika hadi nje kabisa ya jengo la ofisi hizo na kisha wote kwa pamoja walipanda pikipiki aliyokuwa akiitumia Norbert kwani hawakuwa mwaekuja mahala hapo na gari.



    Waliondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana na walizunguka kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Dar, hawakutka kunyooka moja kwa moja kuelekea walipokuwa wakitaka kuelekea kwa hofu ya kufuatiliwa baada ya kubainika kuwa walikuwa wametoka ofisini kwa mtu ambaye alikuwa nao kwenye harakati moja za kuwaumbua wale waliokuwa wanaifuja Tanzania kwa manufaa yao binafsi. Baada ya kuzunguka mitaa mbalimbali huku wakipita njia ambazo hazikuwa na umuhimu wowote hatimaye walifika Kurasini na si Pugu tena, Norbert aliingiza Pikipiki ndani ambako alipokewa na mmoja wa vijana wa EASA ambaye yupo humo ndani ya hiyo nyumba kama sehemu muhimu ya kufanyia kazi. Muda huo walipofika tu Tarakilishi ile ambayo ilikuwa na siri zote pamoja na majina wahusika kuanzia ngazi za chini hadi za ju, ilifunguliwa kwa mara nyingine ambapo Norbert aliyakariri majina yote yaliyokuwa yapo kwenye tarakilishi hiyo ya watumishi wote wa serikali wa ngazi za chini kisha alimuaga Jama Wa Majama na kuingia kazini kwa mara nyingine.



    ****



    Baada ya wenzake waliokuwa naye kwenye mbio moja kutoka ofisini kwake, aliona huo ndiyo ulikuwa muda muafaka wa yeye kuchunguza kile ambacho kilikuwa kimetokea. Moses aliamua kutoka ofisini kwake akiwa amekitoa kile kifaa kwenye simu yake na sasa alikuwa nacho mkononi, alitokea kwenye eneo ambalo lilikuwa na dawati la Katibu Mukhtasi na kisha kukifuatiwa na madawati mengi sana ya wafanyazi waliokuwa wapo chini yake kwenye idara hiyo wakiwa wanaendelea na kazi zao kama kawaida.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Alianza kuwatazama mmoja baada ya mmoja huku akiwa ni mwenye jicho la umakini sana, akili yake ile iliyofanya aajiriwe kwenye idara nyeti kama hiyo ndiyo iliamka katika kuwatazama wafanyakazi hao. Hakuwa akimmini kabisa kuwa msaliti ndani ya idara hiyo alikuwa akitoka mbali na ofisi yake kutokana na mfumo wa kifaa kilichowekwa, alitambua kabisa mtu huyo alikuwa yupo karibu kabisa na ofisi yake kwani kile kifaa kilikuwa kikiendesha nao kuwa kina mionzi ambacho kilikuwa kikichukua taarifa kwenye kifaa kile kilichokuwa kipo ndani kilikuwa hapohapo alitambua kingine kilichokuwa kikichukua mionzi kwenye kifaa kile. Hakutaka kukubali kabisa kuwa kifaa kile kilikuwa kipo umbali hata wa mita kumi kutoka mahali ilipo ofisi yake



    Macho yake yalipokuwa yapo eneo hilo kila mmoja alikuwa akizidisha umakini wake wa kazi, hilo suala halikumuhadaa kabisa hadi apunguze kuwatazama kwani alishajua kabisa kuwa mbaya wake yupo ndani ya eneo hilo. Baada ya kuwatazama kwa umakini mkubwa sana hatimaye macho yake yoe yalikuwa yametua mahali ambapo alikuwa amekaa Mfanyakazi mmoja mabye alikuwa amevaa spika za masikioni, mfanyakazi huyu alikuwa akihusika na kunasa njia zote za mawasiliano ndani ya ofisi hiyo ambazo hazikuwa salama hata kugundua wale wote waliokuwa wakifanya mchezo wa kufuatili mawasiliano na kuwaharibia. Moses hakutaka kupoteza muda kabisa aliamua kupiga hatua na kumsogelea karibu zaidi na kisha akabaki akimtazama yule Mfanyakazi ambaye alikuwa yupo makini sana katika kufuatili kitu kwenye tarakilishi akiwa hajatilia maanani uwepo wa mkuu wake mahala hapo. Aliweka mikono kwenye meza yake akawa anamtazam kwa umakini sana kisha akageuka kwenye dawati ambalo lilikuwa lipo pembeni ya huyo mfanyakazi, Hapo alikutana na Mfanyakzi mwngine akiwa anaendelea na kazikama kawaida akionekana naye yupo makini katika kufanya kazi.



    Macho yake yalivutika kabisa na Mfanyakazi huyo na akapelekea azidi kumwangalia zaidi, alijikuta akitabasamu kila akimuangalia Mfanyakazi huyo ambaye alikuwa akionekana yupo makini sana kwenye ofisi hiyo kila siku akiingia hata kama alikuwa ameingia kw ghfla. Macho yake yaliaanza kumuangalia mfanyakazi huyo kisha yakashuka kwenye kioo bapa ambacho kilikuwa kimeungwa na sehemu ya mfumo wa tarakilishi, mashine nzima ya kicho hicho ilikuwa ikijulikna zaidi ilikuwa ipo chini ya meza yake iliyokuwa imewekewa juu kwani ndiyo ilikuwa utaribu wa kila siku. Moses alijikuta akifuatilia waya uliokuwa ukitoka kwenye mashine hiyo ambayo ulikuwa ukiunganisha na mashine ya chini maarufu kama 'VGA(Video graphic arrays) cable'.



    Waya huo aliukuta ukiwa haujaelekea katika eneo ambalo mashine ipo bali ulikuwa umeelekea kwenye uwazi uliokuwa upo meza yake iliyokuwa na mitoto mingi sana, kuuona huo waya alijikuta akiingwa na wasiwasi kkwani haikuwa utaritibu wa ofisi hapo kwa nyaya kuwa namna hiyo. Hapo Moses alijiua moja kwa moja kuwa huyo ndiye alikuwa msaliti wake haiwezekani kabisa kuwa waya huo uliochukua taarifa kwnye mashine usiende kwenye mashine na badala yake uingie kwenye upenyo uliokuwa ukielekea eneo lenye mitoto mingi sana, alijua wazi kuwa kulikuwa na mashine nyingine iliyokuwa imefichwa huko ulipoelekea huo waya. Mashine nyingine ya Tarakilishi iliyokuwa haijaunganishwa na mashine na mfumo wa mawasiliano wa humo kama ilivyo mashine zote za kuweka chini zilizopo humo ofisini. Hakutaka kujiuliza swali mara mbaioli alipiga hatua kwenye hadi kwenye dawati hilo huku akiweka kifaa kile mfukoni, alipofika alianza kutazama kama alivyokuwa akiwatazama wengine na kisha alitoa bastola yake kwa ghafla sana na kumuwekea kichwani.



    "Inuka hapo kama ulivyo" Alimuambia huyo Mfanyakazi ambaye alishtuka sana, wafanyakzi wote waligeuza macho kumtazama huyo mwenzao ambaye alikuwa amewekewa bastola kichwani.



    "Wewe mfunge pingu huyu na umshikilie" Alimpa amri mfanyakazi mwingine kabisa ambaye alitoa pingu kwani hazikuwa mbali nao, alimfunga yule mfanyakazi na kisha akamshikilia barabara.



    Moses alipopata uhakika kuwa Mfanyakazi huyo hawezi kutoroka aliingia hadi kwenye eneo lake la kufanyia kazi kisha mkono wake akaupeleka chini ya meza hiyo, alikuta na kitu ambacho kilimpa uhakika kabisa wa jinsi mawazo yake yalivyokuwa. Huko alipeleka mkono hadi kagusa sehemu ambayo waya wa kioo cha tarakilishi ile ulikuwa umeingia, alifungua nati za waya huo. Baada ya hapo aliingia chini ya meza ile vizuri ambapoa aliweza kuona waya mwingine uliokuwa ukitoka kwenye mashine ya awali na kuingia kwenye mashine kwenye mashine hiyo isiyo rasmi ambayo ilikuwa ikitumika kwa kazi haramu hapo ofisini kwake. Moses alipoona hicho hicho kitu aliamua kuichukua ile mashine haramu ha kuiweka juu ya mashine ya ofisini na kisha vyote akavisukuma kuelekea nje ya meza hiyo kwa upande wa mbele, wafanyazi wote walishuhudia mashine hizo mbili zikitolewa ambapo moja ilikuwa ikitegmea nyingine ili iweze kupata umeme wake wa kuongoza mfumo mzima uliokuwa upo ndani. Ilikuwa ni mashine ndogo sana kuliko hata zile ambazo huwekwa nyuma ya kioo cha Tarakilishi, wote waliipoona mfumo wa nyaya za mashine hiyo ndogo ikiingia kwenye mashine kubwa. Walijua kabisa kuwa mwenzao alikuwa akifanya jambo la haramu humo ofisini, walijua pia ndiyo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea kubaki humo na badala yake kifo au gereza lilikuwa likimuita.



    "Unaweza kuniambia hii Kompyuta ya pili inafanya nini humu?" Alimuuliza kwa ukali, lakini hakupata jibu. Alipoona amekaa kimya alienda hadi kwenye Tarakilishi ile haramu ambayo ilikuwa ni ndogo akaifungua mfuniko wa juu na kuanza kuangalia vifaa vya ndani, alikuta kifaa kama kile kilichokuwa kimewekwa kwenye simu yake ambacho alikichomoa na kisha akamuonesha yule msaliti.



    "Sound detecter plus phone track and locator(Kinasa sauti jumlisha kinasaji na kionesha uelekeo wa simu) Vinafanya nini humu? Kwanini usitumie tarakilishi ya ofisi kama ulikuwa ukitumia kazi za humu mpaka ulete nyingine ya haramu na uifunge kienyeji."Alipoongea kwa mara nyingine alitumbukiza mkono kwenye mfuko wake wa suruali akatoa kile kifaa kilichokuwa kipo kwenye simu yake ya ofisini.



    "Si ndiyo ukaniweka hiki ili uweze kunasa simu zangu na kuwauzia taarifa maadui wa taifa, hebu pelekeni chumba cha adhabu huyo akapate malipo ya usaliti wake mjinga sana" Aliongea akiwa mwenye hasira na mwisho wake alitoa amri juu ya huyo msaliti wake na kisha aliingia ofisini kwake.



    ****



    BANDARINI



    Alipoondoka kwenye nyumba ya shirika lake kituo cha kwanza ilikuwa ni ndani ya ofisi za Bandari jijini Dar es salaam, alikuwa amepanga kabisa kuonana na Mhasibu mkuu wa bandarini hapo kwani kutoa mguu kutoka kule muda huo wa asubuhi majira ya saa tano. Ilikuwa ni kuja kuonana na huyo Mhasibu mkuu wa bandari, alikuta Mlengwa wake akiwa ni mwenye wageni wengi sana jambo lililomfanya asubirie kwenye viti vilivyopo jirani na mapokezi. Zamu yake ilipofika tu aliingia ndani ya ofisi hiyo, alimkuta Mzee wa makamo aliyekuwa hana nywele hata moja kichwani akiwa amevaa suti nadhifu sana. Alipomtupia jicho Mzee huyo aliona kabisa alikuwa akitangaza ukwasi aliokuwa nao kwa jinsi ambavyo muonekano wake ulivyo, alienda kukaa kwenye kiti kilichopo mkabala na yeye na kisha akatoa salamu ambayo iliitikiwa kwani huyo Mhasibu mkuu alikuwa akimjua vyema Norbert kuwa ni mwandishi wa habari hivyo hakupata tabu ya kuhoji sana ujio wake.



    "Ndiyo Bwana Kaila nikusaidie nini?" Alimuuliza



    "NImekuja kukumbusha unatakiwa ulipedeni ulilokuwa ukidaiwa haraka iwezekanavyo" Norbert alimuambia na kupelekea atokwe na mshangao sana.



    "Kijana ujue sikuelewi kabisa"



    "Utanielewa tu Mzee tulia nikueleweshe, ni hivi mwenzako Khemiri ambaye mlikuwa mkishirikiana naye katika kupitisha bidhaa bila kodi na hata kuingiza Magendo kinyelemela yasikaguliwe amefariki nafikiri hili unalijua. Sasa ukwepaji kodi wote ni deni kwako unatakiwa ukalipe sasa hivi ninavyokuambia, watazania wanakudai wewe uliyewaweka kwenye shida ukakaa hapo ukitumbua jasho lao"



    "Kijana usiniletee mchezo toka nje ya ofisi yangu kabla sijakuitia polisi"



    "Sasa sitoki ita hao polisi ukanyee debe vizuri, Ushahidi wote ninao na nitautoa kwenye gazeti hivi punde tu" Maneno ahyo yalimfanya Mhasibu huyo aanza kutokwa na jasho ingawa kulikuwa na kiyoyozi kilichokuwa kikifanya kazi humo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Vipi Mzee nikuwashie feni naona hali ya hewa ya Dar inakusumbua sana hadi kiyoyozi hakina nafasi" Norbert aliongea kwa kejeli



    "Norbeet tafadhali sana naomba hili suala lisifike huko, tuongee kiutuzima na mimi mzee wako"



    "Kwani hapa tunaongee kitoto, au maneno yetu ya awali yalikuwa yakinuka maziwa"



    "Nooo! Najua na wewe unataka kusogeza life yako, sema unataka kiasi gani nikupe ili usilitoe kwenye magazine yako hili"



    "Khaa! Kwahiyo unataka kunipa rushwa siyo" Norbeet aliongea aliongea huku akichomoa kanda ya kurekodi iliyokuwa ipo mfukoni na akaisitisha kurekodi, baada ya hapo aliicheza na maongezi yote yaliyokuwa yakiongelewa hapo yakisikika vyema na aliamua kuisitisha tena na akaitia mfukoni.



    "Norbert usiniadhirishe kumbuka mimi ni sawa na Mzee wake please tulimaliza hili suala"



    "Sina la ziada ndugu kizito kwaheri" Alimuaga na kisha akatoka nje ya ofisi hiyo akimuacha Mhasibu huyo akiwa amesimama wima asijue cha kufanya kwa jinsi alivyokuwa amezidiwa ujanja.



    Norbert alipotoka hapo alienda hadi kwenye makao makuu ya mapato(TRA) kwenye ofisi ya mtu mwingine ambaye alikuwa yupo kwenye orodha ile, huko aliomba kuonana na Mhusika mwingine aliyekuwa amemkusudia kuendana na orodha ile ilivyo. Kutokana na kuwa mwandishi wa habari na kuhofiwa kuweza kuipa sifa mbaya ofisi hiyo, aliambiwa subiri hadi pale atakapotoka mtu aliyekuwa yupo ndani ya ofisi hiyo ndiyo aingie. Aliporuhusiwa muda wa kuingia kutokana na zamu yake kufika, hakutaka kupoteza muda hadi yule Kizito wa bandari aje kukawa na akili sawa ampe taarifa huyu. Aliingia ndani moja kwa moja akakutana na Mwanamke wa makamo ambaye alikuwa ni umri wa kuweza kumzaa yeye, Norbert alipomuona tu huyo mwanamke alitoa tabasamu usoni mwake na kisha na kisha akaketi kwenye kiti kilichokuwa kikitazamna naye. Alipokewa na tabasamu kutoka kwa Mwenyeji wake ambaye alikuwa mtu mzima ingawa si haba sana, kwani pesa ilikuwa haizeeshi sana kaisi cha kumfanya aonekane amechoka. Tabasamu lake la usoni lilimfanya mwanamke huyo aonekane na mvuto wa sura aliokuwa nao mgeni wake huyo aliyekuwa ni kijana matanashati, alijua ulikuwa ni ugeni uliokuwa hauna shari ndani yake kupitia tabasamu hilo ambalo lilikuwa likimpa matumaini hayo kabisa.



    "Ndiyo Kaila nikusaidie nini?" Alimuuliza



    "Mama yangu ujio huu ni wako na nimekuja kukumbusha tu kuwa unatakiwa ulipe madeni unayodaiwa na watanzania" Norbert aliongea na kupelekea huyo Mwanamke amtazame kwa jicho akionesha kutomuelewa.



    "Sijakuelewa kabisa Norbert go straight to the point" Aliongea Mwanamke huyo



    "Ok ni hivi zile pesa ulizokuwa ukila kwa kufanya uhaini ndani ya mamlaka hii ikiwemo kuonesha rekodi feki za kuwa kodi yote iliyokuwa ikidaiwa kampuni ya Khemiri imelipa, sasa ni hilo ni deni kubwa sana kwa Watanzania wanaolia njaa kwasababu yako"



    "Eeeeh!"



    "Sijakuita nimekukumbusha tu huo ni wajibu wako kwani ulikuwa ukijaza tumbo lako kwa kuwa mmoja aliyekuwa akifanya mizgo haramu iingie. Mama ulipe deni la watu kabla serikali haijakulipisha"



    "Norbert out of my office"



    "Kabla sijatoka mama napenda ujue kuwa haya yanatoka kwenye jarida langu la mwezi huu"



    "Nooo please isiwe usitoke kwanza tulimalize hilo kumbuka mimi ni sawa na mama yako, sema kiasi gani nikupe si rushwa hii bali nasogeza maisha yako mbele kidogo tu"



    "Kwahiyo unanipa hongo siyo"



    "Hapana"



    "Natoka mama maana ulishaniambia ila ukumbuke kabisa haya niliyokwambia kwani mwenzenu Khemiri ni marehemu sasa mzigo wake mtaubeba nyinyi" Norbert alingea na kisha alitoa Kirekodi sauti kingine ambacho klikuwa tofauti na kile cha awali, alikisitisha kurekodi na kisha akacheza sehemu ile ambayo alikuwa amerokodi . Sauti ya maongezi yao ndani ya ofisi hiyo yalisikika wazi ambapo Mwanamama huyo alizidi kuchanganyikiwa.





    Alipotoka ndani ya ofisi hiyo akiwa amemuachia mlengwa kivumbi cha roho, aliamua kwenda eneo la maegesho na kupanda pikipiki yake. Aliondoka moja na safari ya kwenda kwingine alikuwa imeanza kwani orodha kamili aliyokuwa nayo, ilikuwa bado haijaisha kabisa na ilimbidi akakutane na wahusika wengine waliokuwa kwenye mnyonyoro mmoja. Safari yake iliishia kwenye makao ya jeshi la polisi nchini, hapo aliweka pikipiki kwenye eneo la maegesho na kisha akafungua sehemu maalum ya kuweka mizigo midogo akatoka Kirekodi sauti kingine. Kama kawaida yake aliomba kuonana na mlengwa mwingine kabisa aliyekuwa akimlenga. Kitendo cha kuwa mtu ambaye alikuwa ni mzalendo katika mambo mbalimbali, aliruhusiwa kuingia ndani ya ofisi ya Mlengwa baada ya kutoka ruhusa lwa Mlengwa akijua kuwa ulikuwa ni ujio ambao ulikuwa wa kawaida sana. Mlengwa wa ofisi yake alijua wazi huenda alikuwa akija kuulizwa mambo yanayohusu taratibu za jeshi la polisi kabla ya Mwandishi huyo hajaandaa jarida lake lenye mashiko sana kwa jamii, alikaa ndani ya ofisi yake akiwa amevaa vazi la jeshi la polisi ambalo lilikuwa likionesha ni jinsi gani alivyokuwa na cheo kikubwa sana ndani ya jeshi hilo.



    Aliweza kumshuhudia Norbert akiwa na tabasamu lake lile sliingia humo ofisini, alimkaribisha kwenye kiti akiwa na tabasamu vilevile kutokana na ujio wa mwandishi wa habari huyo. Alimuacha hadi akaketi kisha akamtazama kwa mtazamo uliokuwa ukionesha alikuwa tayari kumsikiliza, mtazamo huo ulimfanya mgeni wake kuamua kuongea kile kilichokuwa kimemleta eneo hilo.



    "Kamishna nimekuja kukumbusha tu" Norbert alisema



    "Ndiyo Kaila kunikumbusha nini?" Aliuliza akiwa ni mwenye shauku ya kutaka kujua hicho kitu.



    "Mzee lile deni lako la kuamrisha vijana wako wahakikishe wanapitisha mizigo yenu haramu kule Bandarini na ile isiyo na kodi, sasa ni muda wa kuilipa kwani waliyokuwa wamekupa nafasi hii wanahitaji ulilipe"



    "Kijana sikuelewi"



    "Utanielewa tu Mzee wangu,sasa huvi nimetoka Bandari kwa Mr Mushi kisha nikapitia TRA kwa Mrs Kishimba. Wote hao ni wenzako na nafikiri mnajuana, sasa ni hivi napenda ujue kuwa muda wenu wa kulipa lile deni lenu la kupewa madaraka na kuyatumia vibaya umefika. Ujitahidi kulilipa"



    "Kaila! Naona umekuja kunitukana ofisini kwangu sasa naomba utoke kabla sijakutupa ndani ukanyee debe, sishindwi kukupa kesi usionekane kwenye uso wa dunia ukaenda Nyumba ya giza wewe"



    "Ohoo! Bado upo kwenye deni la kukitumia cheo chako vibaya na sasa unataka kujiongezea deni jingine siyo, Mzee wangu utaishia pabaya haya yote ninayaandika kwenye jarida"



    "Naona hunijui vizuri wewe ngoja nikuonesha mimi ni nani, sasa tuone na hicho unachokiandika utapata faida wakati ni wa kuozea jela wewe" Aliongea huku akinyanyua mkonga wa simu yake akianza akjiandaa kubonyeza badhi ya tarakimu, kitando hicho kilimfanya Norbert aingize mkono mfukoni mwake na kutoa Kirekodi sauti ambacho kilikuwa ikirekodi, alikisimamisha na kisha akaicheza nafasi ile ambayo aliitumia kwenye mazungumzo. Maneno ambayo yalikuwa yakiwatoka kipindi chote cha mazungumzo yalikuwa yakisikika vyema kwenye Kirekodi sauti hicho, mkonga wa simu aliokuwa ameushika akiwa anajivunia jeuri ya kuwa na cheo kikubwa. Alijikuta akiuachia bila ya kupenda na akabaki akimtazama Norbert kwa jicho la huruma kwani alishajua kuwa alikuwa ameshika makali na mgeni wake ameshika mpini, baada ya kusikika kwa sauti hiyo Norbert alisimama akabaki akitabasamu tu na kisha akakisitisha kile Kirekodi na kukitia mfukoni mwake.



    "Kwaheri Mzee wangu tutakutana siku ambayo uso wako utakuwa na aibu kama umefumaniwa na Mama mkwe wako" Norbert alimuaga akiwa anamtazam kwa tabasamu la kejeli Kamishna yule ambaye alikuwa ameingia na unyonge wa ghafla



    "Kaila kijana wangu subiri tuzungumze" Alimzuia na kupelekea aliyemvurga kichwa chake ageuke na kumtazama akiwa na macho ya kumsikiliza kile atakachokisema, muda huo hakujua kabisa kuwa kile Kirekodi sauti kilikuwa na uwezo wa kurekodi sauti zaidi ya mara moja. Kitendo cha kumsimamisha tu Mtibuaji huyu wa usalama wake alikibonyeza tena kitufe cha kurekodi, Kamishna aliona ilikuwa ni nafasi nzuri sana ya kuweza kumshawishi Norbert aweze kuachana na hilo wazo. Aliona kuwa alikuwa ni mwandioshi mwenye kukimbiza pesa, hivyo ilikuwa alidhani ni nafsi nzuri sana ya kuweza kumuhadaa. Aliamini kabisa kuwa hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akikataa pesa kwenye kizazi cha sasa, hivyo aliamua kuitumianafasi hiyo kulimaliza hilo.



    "Wanadammu tunasaidiana Kaila ni kawaida, mimi na hao watu tulikuwa tukitegemeana kwenye mambo mbalimbali ndiyo maana tu popamoja kama unavyotuona. Hata wewe unaweza ukawa na msaada kwetu na sisi tukakusaidia"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Sijakuelewa hapo Kamishna point ni ipi?"



    "Utanielewa tu Kaila kwanza nipe namba yako ya benki nikusogeze kiasi kidogo tu, si unajua Mheshimiwa alisema atafuta rushwa serikalini sasa ishafutwa na hii si rushwa bali ni kukusaidia tu kimaisha"



    "Ohoo! Unataka kunihadaa na hongo siyo, aibu kubwa mvaaji wa vazi la heshima la jeshila polisi unafanya mambo kinyume cha kiapo chako. Anyway asante kwa kuniongezea ushahidi" Norbert alipoongea maneno hayo alibonyeza kitufe cha kucheza sehemu ya aliyoirekodi kwa mara nyingine, maongezi hayo ya kuomba hongo yalisikika vilivyo kwa Mhusika. Baada ya hapo hakuongea neno jingine lolote lile, alitoka nje ya ofisi hiyo na kisha akauendea usafiri wake na kuondoka upesi akiwa amewaachia hewa chafu walengwa wake ambao muda huo walikuwa hawajatimia kabisa.



    ****



    Alipotoka nje ya ofisi tu yule Kamishna ambaye alikuwa yupo kwenye mnyororo ule, alichukua simu yake ya mkononi na kuwapigia vijana wake wamfuatilie. Amri hiyo aliyokuwa ameitoa ilichukuliwa hatua mara moja, Norbert alipoingia barabarani vijan waliokuwa wamepigiwa simu walikuwa wameshafika mara moja, walimuona na walianza kumfuatilia wakiwa kwenye pikipiki kama alivyokuwa yeye. Safari ya kumfuatilia ilikuwa ni ndefu sana lakini hawakukata tamaa waliendelea kumfuatilia, safari hiyo ilienda kuishia Kimara ambapo kwa macho yao walimshuhudia Norbert akisimama kwenye lango la nyumba moja ambalo aligonga hapo. Haukupita muda alikuja mwanamke ambaye alikuwa ambaye ni binti aliyekuwa na mwili uliojaa, mwanamke huyo alipomuona Norbert alimfuata hadi hapo kwenye pikipiki akamkumbatia akionekana alikuwa na hamu naye sana. Alimbusu Norbert akiwa yupo hapo na kupelekea wale waliokuwa wakimfuatilia waone kila kitu.



    Hiyo ilikuwa ni nafasi adimu sana kwa hao watu kwani walitambua kabisa kuwa huyo alikuwa ni mpenzi wake, hapo walipatwa na na wazo ambalo kabla hawajalifanya iliwabidi wampigie simu Kamishna na kumueleza. Wazo hilo lilikuwa ni lenye kufurahisha sana kwa Kamishna, aliwaruhusu vijana hao walitekeleze upesi sana baada ya Norbert kutoka ndani ya nyuumba hiyo. Muda huo walikuwa wakitazama na kuomuona Nobeet akiingiza pikipiki yake ndani ya nyumba hiyo, walipohakikisha alikuwa ameingiza pikipiki ndani kabisa. Waliamua wawapigie simu wenzao ambao walikuwa na usafari mwingine waweze kufika eneo hilo, watu hao walikuwa wameshadhamiria kabisa kumteka huyo mwanamke kwani waliona ndiyo utakuwa mwanzo mzuri wa kuweza kumfanya Norbert awe mpole mwenyewe. Waliamini kabisa hakukuwa na mwanaume aliyekuwa na ujanja mbele ya udhaifu wake ukiwa matatani hivyo ilikuwa ni nafasi ya dhahabu, waliendelea kusubiri katika eneo hilo ambalo lilikuwa limejibana kwa muda wote ambao yule waliyekuwa wakimfuatilia alikuwa ameingia ndani ya nyumba hiyo.



    ****



    Baada ya kutoka kuwatia homa maadui wa taifa na maendeleo yake, aliamua kwenda moja kwa moja hadi Kimara. Huko kulikuwa na Mpenzi wake ambaye walikuwa wamepotezana kwa muda mrefu sana, mpenzi huyo ambaye alikuwa yupo kwenye mnyororo mrefu wa wapenzi waliokuwa wakimuhusudu ndiyo aliamua kumuona. Ilikuwa ni akili ya ajabu aliyonayo ilikuwa imemjia ndiyo ilipelekea hadi afunge safari kuelekea huko, alifika na alipokewa na mabusu na mwanmke huyo ambaye hakuwa ameolewa ingawa umri wake ulikuwa umeenda sana. Norbert alifunguliwa lango kubwa na aliingiza Pikipiki yake ndani baada ya lango kufungwa, kilichofuata hapo ilikuwa ni michezo ya kitoto ambayo watu wazima walikuwa wakishriki kwenye eneo hilo ambalo alikuwa ameegsha pikipiki yake. Mwanamke huyo aliyeonesha kuwa alikuwa na hamu naye sana hakujali kuanza kucheza michezo eneo hilo la ndani ya uzio wa nyumba yake,alichojali yeye ilikuwa ni kufanya kile ambacho alikuwa ameshurutishwa na mwili wake. Unene wa mwili wake hakuujali kabisa ,muda huo alikuwa amekaa sehemu ya mbele ya Pikipiki ya Norbert akiwa amemkumbatia huku miguu yake akiwa ameizungusha kiunoni mwa Norbert ambaye alikuwa ameukamata usukuani barabara na kuweka miguu chini azuie Pikipiki isianguke kwa uzito alionao mwanmke huyo.



    Ulimwengu ule usiojaa viumbe wengi sana ndiyo waliokuwa wapo ndani yake, mandhari yale yaliyokuwa yakileta mchanganyo ndani ya damu zao ndiyo walikuwa nayo kwa muda huo ingawa mmoja bado akili yake ilikuwa ipo kwenye mandhari ya kawaida ikiwa na tahadhari sana. Waliendelea na mchezo ule hadi pale Norbert alipukatisha kwa ghafla sana kitendo hicho bado kilimfanya Mwanamke huyo awe ni mwenye kukazania waendelee kwani alipokuwa amefikia hapakuwa pazuri kiupande wake.



    "Nor ndiyo nini hivyo?" Aliuliza baada ya starehe kukatikia katikati.



    "Happy nipo kwenye kazi mpenzi wangu, hapa nilipita mara moja nilikuwa naenda mtaa wa pili kwenye mahojiano na mtu muhimu. Naomba uvumilie kidogo nikamalize mahojiano halafu tutakuja kufurahi hadi asubuhi umesikia kipenzi" Alimuambia



    "Nor nimekumis ujue, sasa huko utachukua muda gani?" Happy aliuliza



    "Yaani ndiyo kwanza hata saa sita bado sasa fikiria nikirudi mchana wote nipo hapa hadi kesho, utaridhka mwenyewe"



    "Kweli?"



    "Tangu lini kinywa hiki kikatamka uongo kwako jamani"



    "Hay basi Mpenzi we nenda ukirudi utanikuta nimejaa tele hapa kama pishi ya mchele



    "Na nilivyokuhamu tutakesha hapa"



    "Nor nenda basi unazidi kunitia hamu ukiniambia hayo maneno"



    "Sawa basi nipe busu la mara ya mwisho nikitoka nikirudi nakupatia langu refu la hadi kunakucha" Hapo Happy aliachia tabasamu na kisha alienda kumbusu kimahaba zaidi Mpenzi wake huyo , baada ya hapo Norbert aliwasha pikipiki yake na kisha alienda kufungua Lango. Pikipiki ilitoka hapo kwake akabaki akiisindikiza hadi ilipoishia ndipo aliporudi ndani ya nyumba yake akafunga lango hilo, alibaki akitabasamu baada ya kufunga lango hilo kutokana na kutembelewa na huyo mwanaume aliyekuwa akimuhusudu sana.



    ****



    Muda mfupi tangu Norbert aondoke pale kwenye nyumba hiyo ya Happy, gari aina ya Toyota Noah yenye rangi ya zambarau pamoja na vioo vya giza ilifika hapo. Kijana aliyekuwa na mwili uliojaa kimazoezi alishuka ndani ya gari hilo, aliposhuka tu alitazama katika upande ambao walikuwa wamekaa vijana wenzake waliokuwa wamekuja na pikipiki kwenye eneo hilo. Aliwapa ishara mojawapo ya ishara zao na kisha akasogea hadi kwenye lango la nyumba hiyo, aligonga mlango huku akizngalia kulia na kushoto na muda huo wale vijana waliokuwa wapo pamoja naye waliwasili kwenye eneo la langoni hapo wakajibana pembeni.



    Mlango ulifunguliwa na Happy yule ambaye hakuwa akijua chochote kilichokuwa kikiendelea, alipofungua na kukutana mtu huyo ambaye alikuwa amejengeka kimazoezi alibaki akimtazama kwa mshangao. Muoneano mtu yule na jinsi alivyokuwa amekomaa alibaki akiwa ameganda akimtazama sana.



    "Habari yako" Yule Mtu alimsabahi



    "Safi tu za kwako?" Alijibu na kisha akauliza kuhusu hali yake huyo mgeni.



    "Salama... kuna mzigo wako huu" Yule Mtu alijibu na kisha akaingiza mkono kwenye mfuko wa ndani wa kotilake alilolivaa, alipotoa mkono huo ulikuwa na bastola ambayo ilikuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti na alimuelekezea huku akimuwekea kidole cha shahada mdomoni. Alimuashiria arudi ndani ya nyumba hiyo na yeye alitii huku akitetemeka, wale vijana waliokuwa wamejibana pembeni ya gati nao waliingia ndani kwa haraka sana nakisha wakamshikilia kwa nguvu na kwenda kubana naye kwenye eneo ambalo lilikuwa limejificha hata lango likifunguliwa wasionekne kama wamemshikilia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wachache kati yao walifungua lango kubwa la nyumba hiyo, gari lile ambalo lilikuwa limekuja hapo lilikuwa na mtu ndani yake. Gari hilo liliwashwa na taratibu likaingia ndani ya nyumba hiyo hadi kwenye eneo la maegesho. Lango la nyuma la gari hilo lilifunguliwa, Happy aliingizwa ndani na kisha akafungwa miguu na mikono pamoja na kuwekwa gundi nzito mdomoni. Baada ya hapo lango hilo lilifunguliwa kwa mara nyingne tena, gari hilo lilitoka na kuondoka kwa mwendo wa kasi eneo hilo huku wale vijana wakifunga lango hilo na kwenda eneo lenye pikipiki zao wakaondoka nao kwani kazi yao ya utekaji nyara ilikuwa imekamilika tayari. Hawakujua kuwa hilo walilokuwa wamefanya lilikuwa ni kosa kubwa ambalo lingeweza kuwagharimu sana, kosa mbalo lingeweza hata kusababisha wakose ulaji wao kwa kazi hiyo waliyokuwa wameifanya. Wote waliona ilikuwa ni haki yao kutimiza wajibu wa mkuu wao aliyekuwa amewatuma, walikuwa na faraja sana kwa kuweza kuikamilisha kazi kirahisi sana.



    ****



    Walipokuwa wakitekeleza amrikubwa waliyokuwa wamepewana mkubwa, Norbert alikuwa yupo njiani akikata mitaa na muda huo alikuwa ameshafika Ubungo. Alikuwa akijua wazi kitu ambacho kilikuwa kikikaribia kutokea ndiyo maana alielekea eneo lile, aliamini kabisa majuto yatawarudia wale ambao walitekeleza utekaji nyara huo. Muda huo alikuwa akivuta mafuta zaidi kwenye Pikipiki akiimaliza mitaa, alikuwa yupo ndani ya Barabara ya Mandela baada ya kuimaliza Ubungo. Kutokana na mwendo kasi aliokuw akiutumia, baada ya dakika kumi tu alikuwa tayari yupo Buguruni. Aliendela na safari yake hadi akafika Temeke panapo nyumbaye yake ambapo aliingia ndani moja kwa moja, aliegesha Pikipiki hiyo kwenye eneo la maegesho na kisha akazama ndani na aliishia kwenye sebule ya nyumba hiyo aliyokuwa ameikacha kwa siku nyingi akiwa anaishi kule ambapo yupo Mpenzi wake na mtoto wake. Hapo alikaa kwenye kochi mojawapo la sebuleni hapo baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya kuwatia wazimu wale waliokuwa maadui wa taifa, alibaki akishusha pumzi kwa hatua hiyo aliyofikia kwani alikuwa akicheza kamari ya kifo. Kuwafuata wale ambao walikuwa wao mnyororo hatari ilikuwa ni kamari ya kifo lakini alikuwa akijiamini sana, pamoja na hayo alipokuwa kwenye eneo hilo alikumbuka kumshukuru Mungu kwa hatua hiyo aliyokuwa amefikia. Pamoja na kuwa ni mtu ambaye alikuwa haishi kubadili wasichana bado alikuwa akimkumbuka Mumba kwani imani ilikuwa ipo ndani yake, ndiyo maana alimshukuru ingawa alikuwa akimuasi sana muda mwingine aliokuwa yupo kwenye kazi yake.



    Akiwa yupo kwenye kutoa shukrani hizo kwa aliyemjalia pumzi, simu yake ya mkononi iliita, alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Kamishna ambaye alikuwa ametoka kumtia homa isiyohitaji tiba muda mfupi uliopita.



    Aliamua kuipokea hiyo simu ambayo ilikuwa imeingia kisha akaongea,"Yes Hellow.....nani.....No! No! No! Kafanya nini huyo tena hana kosa ni mimi mwenye makosa....sawa nitakuja"



    Baada ya hao simu ilikatika ambapo ilimfanya Norbert abaki akitabasamu kwani alikisia kile ambacho kilikuwa kimetokea, safari yake ya kuelekea huko alipoelekea ilikuwa ni kutoka na kukisia kitu na ndiyo hicho kimetokea. Alijua mmojawapo kati ya wale wahalifu atampigia simu na ndiyo huyo kapiga, kikubwa kilichokuwa ndani ya simu hiyo ilikuwa ni kutiwa nguvuni kwa Happy ambapo aliambiwa ajisalimishe ili ampate. Hilo lilikuwa ni jambo ambalo sawa na kitendawili kwa Norbert kwani hakuwa tayari kabisa kujisalimisha kisa Mwanamke, ambaye alikuwa amemfanya makusudi akijua kabisa maadui zake walikuwa wakijiwashia moto wenyewe. Hakutaka kabisa kwenda huko alipokuwa ameambiwa aende ili akampate akiwa na ushahidi wote alikuwa ameukusanya, alimua kubaki hapohapo ndani ya nyumba yake.



    ****



    ALASIRI



    "Jamani hebu fikirieni vizuri Mheshimiwa Rais akijua tutakuwa vipi?" Bi Kishimba aliuliza



    "yaani ni tabu tupu hapa jamani fikireni sura zetu tutaziweka wapi?" Bawana Mushi naye aliongea akionekan kuchanganyikiwa kabisa kwa homa aliyokuwa amepewa na Norbert ambaye alikuja kuvamia ofisi yake mara moja, wote walikuwa wamechangayikiwa ila Kamishna pekee ndiyo alikuwa ana afadhali.



    "Jamani huyu mtu kashakuwa mnyonge uoga wa nini sasa?" Kamishna aliuliza



    "Mnyonge! Hivi unafikiri yule kijana ni yupo namna hiyo nakuambia hapa akiliona jua huyu hadi Mheshimiwa Rais anarudi safari yake jua tumekwisha" Bwana Mushi aliingilia huku akimshangaa Kamishna.



    "Hata mimi namshangaa huyu jamani hivi anamjua huyo kijana kweli" Bi Kashimba naye alionesha kumshangaa Kamishna



    "Alivyotoka tu ofisini kwangu niliwapa amri vijana wangu wamfuatilie,kaja kuishia Kimara kwenye nyumba ya Hawara wake na vijana wameshuhudia akipigana mabusu na huyo mwanamke. Sasa nimemteka muda mrefu namsubiri ikifika jioni tu ajilete atoe ushahidi wote na kisha nimuue tu akinipa huku hawara wake akiona hamna namna hapa" Kamishna alieleza na kupelekea wote watabsamu kwani ilikuwa ni mbinu nzuri sana.



    "Hapo Kamishna nakubaliana na wewe, amani itakuwpo namna hiyo. Umeweza sana kufanya hivyo. Mwanamke ni udhaifu mkubwa sana" Bi Kishimba aliongea huku akishusha pumzi



    "Ndiyo mpunguze presha nyinyi mtakufa bure, huyu kijana hiyo JKT aliyoenda inamdanganya sasa nafikiri nimuambie na Mheshimiwa kuhusu hilo ili aje kumshuhudia" Kamishna alipoongea hivyo alitoa simu na kutafuta namba ya Mheshimiwa wa upande wao, aliipiga kisha akaweka sikioni baada ya simu kupokelewa.



    "Haloo Mheshimiwa......si kwema Norbert Kaila kaja ofisinni kwangu, kwa Mushi na Bi Kishimba pia katuambia kuhusu mishe zetu na kasema anatoa kwenye gazeti........nimeamua kumshika malaya wake nimuambie aje kujisalimisha maana ni mtu mdogo sana.......nini? Unasem kweli Mheshimiwa basi nitakuwa makini sana naye kuanzia hivi.....sawa" Baada ya hapo alikata simu kisha akawatazama wenzake ambao walikuwa wametulia kimya wote kutokana na yeye kuongea na simu hiyo.



    "Jamani kuna jipya limezuka huko nilipompigia simu Mheshimiwa, inabidi tuwe makini sana na huyu kijana kuanzia hivi sasa" Aliongea kwa utulivu mkubwa



    "Come on! Nyoosha maelezo wewe mbona hatukuelewi" Bwana Mushi aliongea kwa jazba baada ya kuona anazungushwa sana hasa ilipotolewa hiyo kauli mpya



    "Norbert Kaila kwa mujibu wa maelezo ya Mheshimiwa huu uandishi wa habari ni zuga yake tu, ila huyu kijana na Agent hatari wa EASA nafikiri unawajua hawa watu ni bora hata ukavaane na makomandoo" Kamishna alieleza, wote walipigwa na mishtuko kutokana na taarifa hiyo.



    "Are you serious?" Bi Kishimba aliuliza akiwa asiyemini kutokana na muonekano wa Norbeet ulivyo



    "Toka lini nikawa nipo kwenye utani kwenye masuala kama haya, hapa, huu ndiyo ukweli" Kamishna alilijibu swali la Bi Kishimba ambaye aliingiwa na uog upya baada ya kusikia suala hilo.



    "Kwahiyo ndiyo huo mtego kauruka au vipi?" Bwan Msuhi naye aliuliza



    "Hajauruka jamani mwanamke ni zaidi ya ukosefu wa kiungo cha mwili atakuja mwenyewe, ila Meshimiwa katuambia tuwe naye makini sana ana akili nyingi sana" Kamishna alieleza



    "Yaani mimi sida yngu huyu mtu asipumue tu huenda kashaunasa ushahidi wote uliokuwa ukihitajika na hata ile ripoti ipo mkononi mwake" Bwana Mushi aliongea



    "Yaani atatuvurugia kabisa mipango yetu, mkumbuke mimi nataka nigombee Ubunge kwetu uchaguzi ujao sasa yeye ataharibu kila kitu" Bi Kishimba aliongea



    "Hilo msihofu jamani hata mimi nina akili vilevile tutakutana huko" Kamishna aliongea kwa kujiaminiCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Kamishna tusijiamini hivyo umakini utapungua kwenye kiumbe hatari kama huyu, cha msingi ni kuwa makini tu." Bwana Mushi aliongea na kisha akanyanyuka kwenye kiti na akasema,"jamani wacha niwaache kuna bibie leo ananisubiri mida hii"



    "Hay msalimie sana najua ni mtoto wa chuo huyo damu changa kabisa" Bi Kishimba alitia utani na kupelelekea wote wacheke sana.



    "Yaani kama ulikuwa vile huyo mwenzetu ni wa mali mpya" Kamishna naye alitia utani



    "Maisha yao ya shida wacha tuzitumie shida zao tu kwa tunakivuna wewe" Bi Mushi aliongea huku akimalizia kutoka nje na kuwafanya wote waliokuwa humo ndani waendelee kucheka.



    ****





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog