Simulizi : Wito Wa Kuzimu
Sehemu Ya Tatu (3)
"Mheshimiwa yule siyo kiumbe wa kawaida kabisa, hebu fikiria timu yetu ya awali chini ya General Ibrahim aliiangamiza yeye mwenyewe" Josephine alifafanua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ok kama ni hivyo nyinyi kuleni naye sahani moja tu, sisi tunatafuta jinsi ya kuweza kuwageuza watu fikra maana umaarufu wetu umepungua kwa jinsi Kabinuki anavyolivalia njuga suala la ripoti hili kila siku Bungeni" Mheshimiwa aRoho aliongea
"Roho huyu ni dawa ndogo tu yaani tumfanyie ili ajue kama mdomo ndiyo ulimponza Ibilisi akalaanika pia, tumuuzie tufani tu nafikiri itakuwa ni zawadi yake kwa kidomo chake" Mheshimiwa Moyo aliongea
"Yaani hii ndiyo njia sasa ili kuwapunguza akili waweke akili kwake tu, nafikiri ni kumuwekea vitendea kazi vyetu pamoja na vidhibiti matata ndani ya eneo lake tu" Askofu Vldermar aliongea
"Hii ni nzuri kabisa, huyu jamaa kila mwisho wa wiki kama yupo ndani ya jiji hili basi safari yake ni huko Kimanzichana naamini huko ndipo kutaweza kuwafanya waamini kuwa anaropokea unafiki tu bungeni" Mheshimiwa Moyo aliongea suala ambalo lilipitishwa kwa watu wote hapo na mipango ilianza mara moja katika kulitekeleza suala hilo kabla jua halijatua jioni ya siku hiyo, mpango ulipokamilika sasa kilichobakia ilikuwa ni utekelezaji wake tu hakukuwa na jingine ndani ya muda huo.
****
JIONI YA SIKU HIYO
OYSTERBAY
DAR ES SALAAM
Gari ya jeshi la polisi ilionekana ikiingia kwenye nyumba moja ya kifahari sana ambayo ilikuwa na ulinzi mkali sana, muda huo ulikuwa ni muda mbao mwenye nyumba hiyo alikuwa yupo humo ndani. Gari hiyo ilipofika kwenye eneo la maegesho ya Nyumba hiyo watu waliokuwa wamevaa nguo za kiraia walitoka hadi kenye mlango mkubwa wa nyumba hiyo, ujio wao ndani ya nyumba hiyo ulikuwa umeshatambulika dhahiri tangu wapo nje na walipofika tu mlangni milango ilifunguliwa na wakaingia ndani hadi sebuleni ambako walimkuta mzee wa Makamo akiwa amekaa na mke wake.
"Karibuni vijana" Mzee Huyo aliwakaribisha akuiwa ameweka tabsamu usni mwake"
"Asante Mheshimiwa. sisi si wakaaji sana tumekuja kutekeleza agizo la Mheshimiwa" Aliongea mmojwapo.
"Ndiyo nawasikiliza"
"Hichi ni kibali cha kuja kukukamata kimetoka kwa Mheshimiwa mwenyewe, hivi sasa ninavyoongea upo chini ya ulinzi" Yule aliyeitikia ukaribisho aliongea huku akimpatia Mzee huyo karatasi ambayo ilikuwa ni kibali cha kumkamata ikiwa na saini ya Rais Zuber
"Jamani nimefanya nini kwani?"
"Hilo utalijua mbele ya safari kuanzia sasa ongozana na sisi"
Mke wa Mzee huyo alianza kulia hali kadhalika watoto nao walianza kulia bada ya kusikia mama yao akilia wakaja kushuhdia hicho alichookuwa amekiona mama yao, Mzee huyo ambaye alikuwa ni mtu mzito serikalini alikamatwa na wanausalma hao na kisha akapandishwa kwenye gari ambalo walikuwa wamekuja nao. Aliondolewa eneo hilo akiacha familia yake ikiwa inalia kwa uchungu sana, yeye mwenyewe akiwa yupo ndani ya gari ya jeshi la polisi alionekana ni mwenye huzuni sana kwani hakujua kile ambacho alikuwa amekifanya hadi muda huo aliokuwa amewekwa chini ya Ulinzi.
SAA MBILI USIKU
Taarifa ambayo ilikuwa ni kubwa kwenye vyombo vya habari majira hayo ya saa mbii usiku ilikuwa ni kukamatwa kwa Waziri wa nishati na madini Mheshimiwa Kabinuki katika jioni hiyo nyumbani, tuhuma zake kuu ilikuwa ni kuhusika na milipuko yote iliyokuwa imeua maelfu ya watu ndani ya jiji la Dar es salaam. Ilikuwa ni taarifa ambayo iliwashtua wengi kutokana na jinsi Waziri huyo alivyotokea kuwa maarufu ndani ya kipindi kifupi sana cha muda kutokana na kushikiniza sana ripoti iliyokuwa ipo chini ya Mheshimiwa Bai isomwe haraka sana kabla haijaingia dosari. Sasa mabalaa yote hayo yaliyokuwa yamelikumba jiji wanakuja kusikia kuwa yalikuwa yakisababishwa na yeye,, wengi walioishuhudia habari ile walilaani sana juu ya mauaji ambayo alikuwa ameyasababisha.
****
SAFE HOUSE
DAR ES SALAAM
Baada ya kukamatwa ndani ya nyumba yake kituo cha kwazna kuletwa ilikuwa ni ndani ya jengo ambalo lilikuwa likifahamika kama safehouse, ilikuwa ni amri kutoka kwa Rais Zuber ambaye ndiye aliyemarisha kuwa aletwe ndani ya jengo hilo alikuwa akitaka kumuona huyo msaliti ndani ya serikali yake. Kabinuki aliingizwa ndani kabisa akiwa tayari ameshafungwa pingu na kwenda kuwekwa kwenye sebule ya nyumba hiyo, hapo alikutana na Rais Zuber akiwa amefura kwa hasira kwa jinsi alivyiona sura yake. Kabinuki alikuwa ni mwenye upole mwingi kutokana na kutokana na hali hiyo kwani aliamini kabisa mwenye kuweza kumnusuru alikuwa ni Rasi na hakuna mwingine.
"Mheshimiwa sina hatia mimi naonewa" Alijitetea
"Wee tena funga mdomo wake huna hatia hii ni mali ya nani?" Rais Zuber alifoka kwa hasira sana na alimtupia bahasha ambayo ilikuwa imejaa picha, Kabinuki alipozifungua picha hizo alijikuta haamini kabisa kwani alikuta jengo lilipo shambani kwake kwenye picha moja. Picha nyingine ilikuwa na vitu ambavyo vilikutwa ndani ya jengo hilo ambako aliona bahasha mbalimbali, pamoja na mifuko ya kemikali.
"Yaani sisi tunakaa na kuamini kuwa nchi imekumbwa na ugaidi kumbe ni wewe na kikundi chako mnatengeneza Leter bomb na kusambaza" Alifokewa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mheshimiwa sijui chochote kuhusu hili"
"Hiyo ni mali ya nani sasa kama hujui?"
"Ni yangu"
"Kanini hivyo vitendea kazi vya kutengeza hizo silaha viwepo humo ndani, tena orodha ya kuwaua mawaziri wangu. Umemuua Bai wewe kwani kwenye huyo orodha amewekewa X"
"Mheshimiwa hapana sitambui kuhusu hilo"
"Hilo silijui itaenda kuamua mahakama tu"
"Vijana mpelekeni kituo cha Polisi Oysterbay huyu huku mikifanya taratibu za kufungua kesi, kesi ikifunguliwa mahali kwake ni Segerea tu hakuna kwngine" Rais Zuber alitoa amri na vijana hao walitii wakawa wanamtoa humo ndani huyo waziri ambaye alitokea kujijengea heshima kubwa sana nchini Tanzania.
****
[7]
Asubuhi iliyofuata ilikuwa ni siku ya Ijumaa siku hii Norert aliamka ndani ya nyumba ya EASA, ilikuwa ni siku ambayo alikuwa akihitajika kwenda kufanya malipo ya gari lake ambalo alilipeleka kwenye matengenezo. Ndani ya siku alivaa kila kitu cha kujihami ndani ya mwili wake kwani alikuwa akitambua wazi kuwa alikuwa akielekea eneo lenye maadui wake. Alitoka akiwa amepanda pikipiki yake ambyo alikuwa amepewa kwa ajili ya kazi, alikuwa amevaa kofia ngumu ambayo ilikuwa kwa ajili ya usalama wake katika kipindi chote alichokuwa akitumia hiyo pikipiki.
Majira ya saa mbili alikuwa yupo tayari ndani ya Buguruni na alielekea moja kwa moja hadi ndani ya sehemu ya matengenezo, hapo alielekea hadi ndani kabisa ambako kulikuwa kuna matengenezo ya gari lake. Huko alilikuta likiwa tayari na alipokewa na mpenzi wa hiyari ambaye alimchangamkia sana alipomuona, kwakuwa wote walikuwa wapo eneo la kazi ilibidi wapunguze uchangamfu ilii isije ikaweka maswali kwa wakuu wa kazi wa hapo.
Akiwa katika eneo hilo alitajiwa gharama halisi na tayari kitabu cha risiti kilikuwa kimeshakuja mbele yake, alipotaka kulipa alitokea msichana mmoja aliyekuwa amevaia nguo za wafanyakazi wa ofisi za ndani ya jengo hilo ambako ni jirani kabisa na ofisi za mkurugenzi wa humo.
"Samahani kaka unatakiwa ukalipie kwa Mhasibu ndani" Msichana huyo aliongea, wafanyakazi wote walishangazwa na agizo hilo lakini hawakuwa na la kupinga kwani haikuwa mara ya kwanza kutokea jambo kama hilo. Ilimbidi Norbert tu aelekee huko alipokuwa akihitajika kulipa, muda huo aliondoka huku akimpungia mkono Cellina ambaye alimuoneshe ishara ya busu
Norbet alipofika tu ndani ya jengo hilo mfanyakazi huyo alimuongoza hadi eneo ambalo kulikuwa na mlango wa kioo ambao ulikuwa hauoneshi kile ambacho kilikuwa kilichokuwa ndani, hapo alimuonesha ishara kwamba hiyo ndiyo ilikuwa ofisi yenyewe ya Mhasibu aliyokuwa akitakiwa kulipa kisha akaondoka. Alipoondoka Norbert alisimama hapo kwenye kioo na kisha akaanza kufanya utundu kama wafanyao wale wapendao kupendeza kila muda, alijiangalia hapo kwenye mlango wa kioo huku akirekebisha shati lake kama alikuwa akienda kupiga picha ndogo. Baada ya hapo aliingiza mkono kwenye mfuko wake wa suruali na alitoka miwani ambayo ilikuwa ikifanana kila kitu na miwani ya macho , aliivaa miwani hiyo na kisha akawa anajitazama kwenye kioo cha mlango huo pasipo kujali humo ndani walikuwa wakimuona, Baada ya kujiweka sawa akiongezea miwani hiyo ambayo iliongezea kupendeza kwake. Alisukuma mlango huo wa kioo kuingia ndani ya ofisi hiyo aliyokuwa ameelekezwa kuwa ni ya Mhasibu. Aliingia ndani akatokea eneo lenye chumba kikubwa sana cha ofisi ambapo mbele yake kulikuwa na kiti kilichokuwa kikiangalia ukutani, kwenye kiti hicho ambacho kilikuwa ni kirefu kwenda juu kilionekana nywele za mwanamke ambaye alikuwa ameangalia ukutani. Norbert alipoona hivyo kuwa muonekano wa mwanamke huyo ulikuwa ni kama yupo akiendelea na shughuli zingine, ili kumshtua ilimbidi aachie mguno wa nguvu. Alipotoa mguno huo alihisi kunyemelewa, alisogea kando kwa haraka sana baada ya kuhisi kitu kikija kwa nyuma yake.
Kusogea huko pembeni hakukuwa kutupu bali kuliendanana yeye kujizungusha nyuzi tisini na kuudaka mkono uliokuwa na bastola ambao ulikuwa ukitaka kumuwekea kisogoni. Aliuzunguhsa mkono huo kwa kasi sana na kupelekea yule ambaye alikuwa yupo nyuma atoke mguno wa maumivu kwani alimuumiza sana, bastola ambayo ilikuwa ipo mkononi ilimuanguka kutokana kuumizwa vilivyo mkono. Norbert hakutaka kumlazia damu kabisa alichokifanya ni kumvuta mbele kwa nguvu sana, naye alienda mbele na kisha alinyanyuliwa kwa mtindo wa judo na kutulizwa sakafuni ambapo aliangukia mgongo. Akiwa yupo hapo chini Norbert aliushika mguu wake na kuuvuta nyuma na kupelekea yule mtu ambaye muda huo alikuwa amevaa sweta lenye kofia kujifyatua na kisha akapeleka teke, Norbert alilikwepa teka hilo na kisha akautegua mguu wake na kumuacha akiwa na maumivu . Alipomaliza hapo aliiokota bastola yake na kisha akaketi kwenye kiti akimtazama mtu huyo ambaye alikuwa ameegemea sehemu ya kabati humo ndani kofia ikiwa imemvuka, alimuona Spider kwa macho yake mawili ndiyo alikuwa akitaka kumvamia hapo. Hapo alijua kabisa alikuwa amewekewa mtego na watu hao, kwa kuiona sura hiyo.
"Ukimtaja Norbert jua limebeba maana ya mastermind, hivyo usitegmee kabisa kumshika kijinga namna hiyo. Ujanja huo uliokuwa unaufanya ni level ya chekechea kabisa kwenye ujanja wangu Spider" Norbert alimuambia huku akijenga tabasamu lake ambalo ilikuwa ni kawaida sana akiwa tayari amemshinda adui yake katika kupambana.
"Kipindi nasogea kwenye mlango huo wa tinted sikutaka nijiaminishe kijinga namna hiyo kuwa hii ni ofisi salama wakati najua mabosi wake ni maadui zangu, nimejifanya najiangalia kwenye kioo cha tinted kama vile naenda kupiga passport size lakini haikuwa lengo kujiangalia bali ilikuwa nikihadae ili nivae miwani hii ukiona kuwa nilikuwa nikitaka kupendeza zaidi. Miwani hii ndugu hata kwenye tinted naona ndani ndiyo nikakuona na hiyo basola yako ila sikuijua sura yako" Norbert alimuambia kwa mara ya pili na kisha alisimama na kwenda hadi mezani, alichukua kitabu cha risiti na kisha akamtupia hapo alipokuwa amekaa pamoja na kalamu.
"Haya andika risiti mwenyewe" Alimuamrisha, Spider hakuwa na ujanja zaidi ya kuandika risiti stahiki kwa Norbert ambaye alizama mfukoni na kisha akachomoa burungutu la hela ambalo alimrushia. Baada ya hapo alitoa kibeba risasi chote na kisha akachukua risasi zote na akamrushia bastola tupu, muda huo Spider alikuwa akiunguliwa maumivu ya kuteuliwa hadi ngozi ikawa nyekundu.
"Sishindwi kukuua kabisa ila sitaki hao wafanyakazi wa kawaida ambao wengine wananifahamu wajue mimi ni mhalifu wataniweka pabaya" Alimuambia huku akichukua risiti yake na alitoka ndani ya ofisi hiyo akiwa na risiti, alienda hadi alipokuwa yupo Cellina na alimuaga na kisha alipanda pikipiki yake na kuondoka kwenye eneo hilo akiwa amemuachia maumivu makubwa sana Mzungu aliyekuwa akijaribu kupima uwezo wake.
****
MUDA MCHACHE BAADAYE
Ulikuwa ni muda ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu sana kwa Norbert na Khemiri wakutane kwani ulikuwa ndiyo muda muafaka, ilikuwa ni majira ya saa tano asubuhi ambapo kutokana na suala ambalo Norbert alikuwa amelitunga ilibidi wakutane kwenye chumba cha hoteli kwa ajili ya maongezi hayo. Norbert siku hiyo alikuwa amevaa muundo wa nguo zilezile ambazo alikuwa amezivaa siku mbili zilizopita aliokuwa yupo ofisini kwa Khemiri, ndani ya chumba hicho cha kukutana hakikuwa chumba kulala kama ilivyotazamiwa bali ilikuwa ni chumba cha mkutano ambacho kilikuwa kikitumiwa watu wazito sana waliokuwa na mambo nyeti sana ya kuyazngumza. Khemiei siku hiyo alikuwa yupo ndani ya vazi la kanzu kwani ilikuwa ni siku ya ibada na akitoka hapo alikuwa akielekea msikitini moja, alikuwa amepitia eneo hilo kwa ajili ya miadi hiyo ambayo walikuwa wamewekeana.
"Ndiyo Mr Mashishanga nipe details za mzigo wako ili tujue namna ya kuuuvusha pale" Aliongea Khemiri.
"Mimi ni wakala wa waasi kutoka Kongo na walikuwa wamepungukiwa na risasi, hivyo mzigo huo wote uliokuwa upo kwenye matenki ya mafuta ya Semi trela ni risasi tupu ila nisafirishiwe na magari yako ili kuepuka kukaguliwa. Kenye ulinzi ni mkali sana ila hapa kutokana na uwepo wenu natumai hichi kitu kitakuwa kirahisi sana" Norbert alijieleza
"Huo mzigo ni another issue Goverment ipo makini sana, nitajiweka pabaya sana"
"Nitakupa kiasi chochote ilimradi mzigo huo uweze kuvuka bandari ile tu maana ndiyo kikwazo kikubwa sana kwetu"
"Ni hatari sana tuseme wewe una bei gani huo mzigo uweze kupita hapo kwani nishakipata tayari, nikusikilize"
"Nikusikilize wewe maana wewe ndiyo mwenye gharama inabidi utaje halafu nitakuambiwa kama inawezekana aua haiwezekani"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwanza hizo tenki zipo ngapi nijue gharama halisi ya mzigo huo"
"Zipo tenki ishirini"
"Dola elfu kumi kwa kila tenki hapo ni gharama za kila kitu"
"No Mr Khemiri hapo umeanzia mbali ndugu"
"Mashishanga hii ni too dangerous kabisa akijua Rais tumekwisha wote na inabidi agents wetu wapate kidogo kwenye kila kitengo unachopitia ili usikaguliwe ndugu"
"I know butu hiyo si business ndugu bali ni kufukuza mteja"
"Ok Dol Elfu nane kwa kila tenki zinasafirishwa hadi huko DRC"
"Ok no problem nahitaji namba zenu za beki nikadeposit then nawaletea pay in slip, mzigo unaingia kesho usiku hivyo mazingira nahitaji kwenda kuyaona usiku wa leo nina imani tutakuwa wote. Niyaone then niwape information waendane na mchoro wetu"
"Exactly nitakuwepo hapo, namba hizi hapa ni Barclays " Khemiri aliomgea huku akimpatia karatasi ambayo Norbet aliiangalia na kisha akaiweka mfukoni.
"Ok tutakutana bandarini"
"Hamna shida Mr Mashishanga wacha niwahi masjid muda bwana huu"
"Ok hamna tabu"
Huo ndiyo uliokuwa mwisho wa makubaliano baina ya Norbert na Khemiri, wote walitoka kwa pamoja ndani ya chumba hicho na kila mmoja alielekea njia yake. Norbert alizidi kuachia tabasamu la ushindi hasa baada ya kuzidi kuwaksribia mafisadi wa nchi hii, alijiapiza kufanya kitu ambacho kingewafanya walie na kusaga meno. Hakika alikuwa na uchungu sana wa kuona kuwa nchi yake iliyokuwa na utajiri mkubwa sana watu wake wakiishi kwenye mazingira magumu, maneno ya Khemiri kuwa yupo kiongozi mkubwa nyuma ya tukio hili aliyekuwa akisababisha kila kitu kiende hivyo ilimuuma na alijiapiza kufanya kile ambacho kitawafanya wote hao walie na kusaga meno na pia kujuta kwa kuweza kufanya naye makubaliano wakati si mmoja wa wanyonyaji.
****
ADHUHURI
Muda ambao Norbert alikuwa yupo hotelini hakujua kabisa kuwa upande mwngine muwa mtu aliyekuwa ameshika tarakilishi ya mwanausalama mwingine aliyeuawa na Tarakilishi hiyo ilikuwa ipo mikononi mwa Askofu Valermar hadi muda huo, tarakilihi hiyo ilikuwa ni ngumu sana kuliko tarakioishi ambayo walikuwa wameipata hapo awali. Hii ilikuwa imefungwa katika sehemu mbalimbali jambo ambalo ilimuwia vigumu sana katika kufikia nenosiri jingine walilokuwa wanalitaka, hapo walijikuta wakihangaika hadi wakachoka na wakajikuta wakihitaji mtu mwingine ambaye angeweza kuifungua Tarakilishi. Hapo iliwabidi wamsake Mtundu wa tarakilishi ambaye angeweza kuwasaidia katika kuifungua hiyo tarakilishi, muda huo vijana waliokuwa wapo chini ya Askofu huyo waliingia kazini kumtafuta huyo aliyekuwa akihitajika huku wakimuacha yeye mwenyewe akiwa anahangika nayo Tarakilishi huenda atapata bahati ya kuweza kuifungua. Alifika hadi eneo ambalo lilikuwa na faili lenye nenosiri lakini alishindwa kabisa kulifungua kutokana na mfumo wa tarakilishi huo ulivyo, alihangaika sana na mwisho alichoka akaifunga tarakilishi hiyo akisubiri huyo mtaalamu wa tarakilishi aliyetafutwa aweze kufika atatue kitendawili kilichokuwa kikiwasumbua wao kwenye vichwa vyao.
Robo saa baadaye wale vijana waliweza kurudi wakiwa wameongozana na kijana mwenye asili ya kihindi hadi ndani, kijana huyo alielezwa kila kitu juu ya tatizo ambalo lilikuwa likiwatatiza. Aliwatajia kiasi cha pesa ambcho angepata angetatua tatizo hilo, hilo halikuwa tatizo kabisa wao walimpatia kiasi hicho cha pesa na kisha wakamsogezea tarakilishi hiyo aweze kucheza na ngoma ambayo alikuwa na ujuzi nao. Kijana huyu waliyekuwa wamemtafuta hakika alikuwa ni mtundu wa tarakilishi kuliko kawaida kwani ndani ya dakika mbili tu tayari alikuwa ameweza kufungua faili husika lililokuwa likihitajika. Ilikuwa ni furaha sana kwa Askofu Valdermar kwa kuweza kufunguliwa faili hilo na kisha walimruhusu kijana huyo aondoke kwenye eneo hilo kwani kazi yake ilikuwa imeshaisha tayari.
"Jamani haya maneno tuanyoyakuta humu ndani siyaelewi" Askofu Valdermar aliongea kuwaambia vijana wake
"ALEKUWA ALEKUWA UMRA AU HIJA " Aliongea mmoja wa vijana wake wadogo kabisa ukiachana na wale kina Spider
"Umeona sasa, yaani tunahangaika kote halafu neno ni hili tu la kwanza ni BARA JANGWA kwenye laptop ya kwanza mara hii ya nne iwe hivyo. Yaani haieleweki" Alilalamika
"Madam walioandika haya maneno si watu waliokuwa na ukichaa bali walikuwa na akili timamu. Inabidi tutafute hiyo ya mwisho tujue ina maana gani" Mmoja wa vijna wale alishauri.
"Sasa huyu wa mwisho haijulikani kabisa yupo wapi, alipotea katika mazingira ya ajabu sana. Huyu ni Jama na ule mtego ulipamta mke wake tu sijui yeye yupo wapi" Aliongea akionekana kuchoshwa.
"Madam inabidi kuanzia sasa ni tutrap all commnication ndani ya TISS tu huku tukiendesha msako" Alishauriwa
"Wazi zuri hilo na ni kazi yenu hii kuanzia hivi sasa naamini mtaweza tu" Aliwaambia
"Hilo ondoa shaka kabisa linawezekana, tunaanza kazi leo hii kila siku ni kufuatilia hayo mawasiliano yao" Baada ya hapo wote waliruhusiwa kuianza hiyo kazi mpya kutafuta huyo mwenye kujua nenosiri na tafsiri yake iliwaweze kuwanusuru wakubwa zao,
****
Utata wa maneno yaliyokuwa yapo Tarakilishi zile za wanausalama haukuwa ukiwasumbua maadui wa Tanzania tu, bali ulikuwa ulikuwa ukiwasumbua hata wanayoitetea. Ndani ya nyumba ya EASA Norbeet alikuwa yupo na Moses ambaye ndiye mkurugenzi wa TISS. Aliamua kumuita hapo kutokana na utata ambao ulikuwa umemkumba hata yeye kwani maneno hayo hakuwa ameyaelewa kabisa, suala hilo pia lilikuwa ni tata kwake yeye mwenye kiongozi wa hao vijana waliokusanya ripoti hiyo kwani yeye hakuwa amehusika kabisa na uchunguzi huo. Wale wote waliokuwa wamehusika na uchunguzi huo walikuwa tayari wameshatangulia mbele ya haki na alikuwa amebaki mmoja tu ambaye alikuwa hajulikani ni wapi alipo hadi muda huo. Bosi wake mwenyewe hakuwa akijua ni wapi alipo kutokana na Mtu huyo kutotaka kabisa kujiweka wazi hata kwa Bosi kwakuwa hakuwa akiamini mtu kwa suala kama hilo.
"Jama wa Majama ndiyo mtu pekee ambaye anaweza kutatua kitendawili hiki lakini hajulikani ni wapi alipo" Moses aliongea
"Hii nayo ni ishu sana, inaoekana kaijua hali si nzuri kabisa kwenye ngazi za uongozi ndiyo maana hataki kutaja ni wapi alipo" Norbert naye aliongea muda huuo tarakilihi zote mbili zilikuwa zipo mezani.
"Halafu kibaya zaidi Mheshimiwa aliniambia niteua timu ianze kazi ya utafiti na ikusanye ripoti ya madudu yote yalipo kwenye wizara ya fedha na wizara ya uchukuzi, jamaa wamemaliza ripoti wakaiweka kwenye laptop moja tu halafu nyingine zikawekwa maneno ambayo yakiunganishwa na kuchambuliwa basi ndiyo yanafungua hiyo laptop. Ripoti nyingine ikapelekwa kwa Mheshimiwa Bai huku hii nyingine ikabaki kwa tahadhari ikiwa ile itapotea"
"Sasa inaonekana hadi kwenye idara yako kuna nyoka"
"Hili nahisi Jama kalijua ndiyo maana hataki kabisa kuniambia ni wapi alipo. Uwepo wa msaliti nahisi upo kila mahali si humuo tu, haiwezekani na IGP atume CID wawili na wawindwe na wauawe ndani ya siku moja hii inamaanisha walikuwa wamejulikana wameshaingia kazini sasa nani nikatoa hiyo taarifa wakati waliitwa tu na kisha wakachukua jukumu waondoka. Jibu ni msaliti"
"Hata hiyo ripoti ya kwenye laptop zote zile nayo ni msaliti pia"
"Hilo halipingiki yaani, kuna watu wachache wanaotaka kufelisha utawala wa mheshimiwa na ndiyo wanafanya haya. Mmoja ndiyo huyo kakamatwa na mkanda uliomrekodi akiongea kuhusu kuwangamiza wanausalama umepatikana"
"Huyo kwa sasa simuhukumu kama ni msaliti hadi pale hiyo ripoti itakapo kuja"
"Ok tusubiri tuone miujiza itakayomtetea, yaani laiti ile ripoti ningeisoma kabla haijafika huko basi isingekuwa tabu hivi ila kwa masharti ya Mheshimiwa kuwa niwache na uhuru kwenye kazi ndiyo haya"
"Ndiyo ishatokea tena na isitoshe tunapambana na adui mkubwa tusiyemjua ilihali yeye anatujua"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hiyo ni vita mbaya sana lakini katu hatuwezi kuweka silaha chini tunaianza taratibu, wewe leo usiku ukienda bandarini usisahau kamera na sound recorder tuweze kuwanasa tena chukua Kamera ambayo ni waterproof kwa tahadhari"
"Hilo lipo akilini tayari na nikitoka hapa ni kuanza uchunguzi wa kujua wapi alipo Jama na hiyo laptop"
****
ALASIRI
Habari ya kuuawa kwa mtu mwingine aliyekuwa ameshikilia moja ya tarakilishi zenye siri, ilimfikia mzee aliyekuwa yupo kijiji cha Kibewani. Muda huo alikuwa yupo akiwa anacheza bao na wazee wengine wa kijiji hicho katika majira hayo. Alipoisikia habari hiyo ndipo alipata uhakika kabisa kuwa Tarakilishi zote hazikuwa mikononi mwa watunzaji ispokuwa tarakilishi yake pekee, aliendelea kucheza bao huku akili ikiwa inawaza kwingine kabisa. Akili yake ilikuwa ipo ndani ya jiji la maraha na lenye kila aina ujanja, alipoipata na taarifa ya pili juu ya tuhuma ambazo zilikuwa zikimkabii Mheshimiwa Kabinuki aliona kabisa kuwa tayari mpira ulikuwa umegeuzwa kwa mwingine kabisa ambaye alikuwa hahusiki na lolote. Moyoni hakuvilaumu kabisa vyombo vya dola wala maamuzi ya Rais Zuber ya kutoa kibali cha kukamatwa kwa waziri huyo, aliumia sana moyoni kwa kukamatwa kwa waziri mzalendo ndani ya nchi akituhumiwa kwa tuhuma ambayo haikuwa inamuhusu kabisa lakini hakuona kabisa kuwa huo ulikuwa ni muda muafaka kwa yeye kwenda kumkomboa katika balaa hilo kwani alijua wazi alikuwa akitafutwa na wabaya wake kwa udi na uvumba.
"Kabinuki anahitaji mwamvuli wa kumkinga na mvua kwani manyunyu ndiyo haya yameanza kumuangukia, mvua ikiwa kubwa zaidi sitakuwa na jinsi zaidi ya kwenda na mwamvuli" Aljisemea huku mkononi akiwa na kete kadhaa akicheza bao, alikuwa amezungukwa na baadhi ya wazee ambao alikuwa wakitazama mchezo huo.
Huyu Mzee hakuwa mwingine bali alikuwa ni Jama wa Majama ambaye anatafutwa kwa pande tofauti kutokana na kile alichokuwa nacho, alikuwa amejificha kwenye kijiji hiko ikiwa ni siku kadhaa tu tangu mke wake afe kwa bomu la barua lilokuwa likimlenga yeye. Alikuwa akiendesha maisha hayo hapo kijiji akijifanya ni mdogo wa babu yake mzaa mama, alikuwa yupo katika kuonekano wa kizee kabisa ambapo ingekuwa ngumu kabisa kwa mtu yeyote ambaye anamfahamu kuweza kumtambua. Huko kijini alikuwa akiishi kwa amani zaidi kuliko hata huko mjini ambapo kulikuwa na kila aina ya raha, alipaona ni mahali sahihi kwake kuweza kutulia kwa siku hizo akiwa huko hadi pale hali itakapokuwa shwari.
Moyo wa kumsaidia yule ambaye hana hatia aliyekuwa amekumbwa na kadhia, tayari ulikuwa umeshamjia. Alipofikiria maadui waliokuwa wakimngojea, aliona tatizo ataenda kuongezea. Moyo wa subira ulimjia hakika ndiyo alichokuwa akikitakia, Jama Wa Majama aliacha bao kujichezea.
Akili yake ya kiusalama ilikuwa imeshaamka tayari na alikuwa akicheza hilo bao huku kichwani mwake kukiwa na ukinzano mzito sanaa, mawazo yake yalijigawa sehemu mbili na alikuwa akivutwa katika kila upande wa mawazo hayo. Upande mmoja ulikuwa ukitaka aelekea huko na upande mwingine ulikuwa ukitakia naye abaki hapo. Hakika ulikuwa ni ukinzano mzito sana ndani ya kichwa chake uliokuwa umetokea, upande mmoja ulikuwa ukimsihi asiondoke ndani ya kijiji na aendeleea kubaki hapohapo huku upande mwigine ulikuwa ukimsihi aondoke hapo kijiji kwani kulikuwa na yule ambaye alikuwa akiteseka sana ilihali yeye mkombozi alikuwepo. Aliendelea kucheza bao huku ule ukinzano wa mawazo yake ukiwa na mzigo mzito uliokuwa umekielemea kichwa chake, mzigo huo ulimfanya hadi muda huo aliokuwa akicheza bao ajisahau kabisa kuwa alikuwa yupo ndani ya mchezo huo. Ilikuwa ni zamu yake kucheza bao kwani mwenzake aliyekuwa akicheza naye alikuwa keshalala tayari.
"Mwenehu ukafikira mbali" Mzee aliyekuwa akicheza naye alimuambia na kupelekea Jama Wa Majama ndiyo arudi kwenye mchezo huo aliokuwa akiutumia kupoteza muda ndani ya kijiji hiko akiwa na wazee, alitoa tabasamu na kisha aliendelea kucheza kama kawaida.
****
Kesi tayari ilikuwa imeshafungulia hadi kufikia muda huu wa alasiri, Mheshimiwa Kabinuki aliondolewa ndani ya kituo cha polisi alichokuwa amewekwa kwani hakuwa ndani ya umiliki wa Polisi hadi muda huo kutokana na kuwa tayari amefunguliwa kesi. Alikuwa yupo ndani ya umiliki wa jeshi la magereza kwani alikuwa tayari ni mhasbusu hadi inafikia wakati huo. Safari ya kuelekea gerezani ilianza ndani ya muda mfupi, aliwekwa ndani ya gari ya jeshi la polisi ambayo ilikuwa ni ya kawaida tena aliwekwa kwenye sehemu ya nyuma ya gari hiyo ambako kuikuwa kumewekwa kiti. Mbele na nyuma ya gari hiyo kulikuwa kuna magari mawili ya jeshi la polisi ambayo yalikuwa yapo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wake na pia kuhakikisha hawezi kukimbia. Msafara huo ulitokea Kituo cha polisi Oysterbay na ulitumia dakika kumi na tano tu ukawa umefika eneo la Tabata kwenye gereza la Segerea, hapo alishushwa na kuingizwa ndani ya gereza wote. Alifuata taratibu zote za hapo gerezani na kisha moja kwa moja alipatiwa vazi lake, alitupwa kwenye chumba cha Mahabusu huku hadhi yake ikiwa imeangaliwa na akawekwa kwenye chumba cha Mahabusu aliokuwa akiendana nao.
likuwa ni siku ambayo hakuwa akiamini kabisa kuwa ndyo alikuwa amekuwa kumbe dhalili sana, kujitolea kote kule siku hiyo alikuwa haamini kabisa kama ndiyo alikuwa akiishia nyuma ya nondo. Hakika pamoja na kuwa mtu mzima alijikuta akidondosha chozi akiwa humo gerezani kwa yaliyomkuta, heshima yote aliyokuwa nayo matokeo yake alikuwa akiishia namna hiyo. Mheshimiwa Kabinuki alijua kabisa kuwa alikuwa amepata ajali ya kisiasa, hakuona mkombozi wake kwa vidhibiti vilivyokuwa vimeshikwa kwenye mali yake. Aliona kabisa kuwa alikuwa akienda kupatiwa hukumu ndefu sana kwani ilikuwa ikija kumkuta, vifo vya mamia na mamelfu ya wakazi wa jijini vilivyokuwa vimetokea alikuwa amegeuziwa mpira yeye hakuona kabisa uwepo mtetezi wake hasa kwa vidhibiti vilivyokuwa vimekutwa. Jambo jingine ambalo lilikuwa likimfanya ajute zaidi ilikuwa ni kauli ambayo aliitoa mfanyakazi wa shamba lake, huyo ndiye aliyemuweka pabaya zaidi na yeye hakutarajia kabisa kama angekuja kuongea uzushi kama huo aliouongea kwa jeshi la polisi. Mfanyakazi huyo ndiye aliyeenda kutoa taarifa juu ya uwepo wa vitu hivyo huko shambani kabla hata kibali cha kumkamata hakijawekwa sahihi na Rais Zuber.
Jinsi alivyokuwa akimtambua Rais Zuber ni mtu asiyependa masihara kabisa kwenye masuala yanayohusu nchi, aliona kabisa hicho ndiyo kiama chake kwani hata hao waliokuwa wakiendesha shughuli za kimahakama walikuwa wakimuhofia sana. Hofu ya watu hao iliwafanya watende haki kabisa kwenye shughli zote za kimahakama jambo ambalo mwanzo Mheshimiwa Kabinuki aliliona ilikuwa ni jambo zuri sana, muda huo aliliona ni jambo ambalo halikuwa likifaa kabisa kutokana na kuwa ni jambo ambalo lilikuwa likienda kumkumba yeye mwenyewe. Maisha ambayo hakuwahi kuwaza kama atakuja kuishi ndiyo ndani ya siku moja tu alikuwa ameyaanza kuyaishi akiwa hana mtetezi kabisa.
****
USIKU WA SIKU HIYO
Norbert na Khemiri walikutana jirani kabisa na geti la bandari ambalo muda huo lilikuwa limefungwa na halitumiki kwa matumizi ya kawaida,muda huo Norbert alikuwa amevaa kofia kama ilivyo kawaida kuzidi kuvuruga utambulisho wake kwa watu hao kwani walikuwa wakimfahamu vyema jinsi alivyo katika mambo kama hayo. Khemiri mwenyewe alikuwa akimjua kama ni mwandishi ambaye alikuwa akifuatili sana watu waliokuwa wakifuata nyendo zake lakini kwa hapo hakuwa amemjua kutokana na muonekano mpya aliokuwa nao. Mwendo wake ulishindwa kabisa kuonesha kuwa huyo ndiye alikuwa yule Norbert hatari, alikuwa akitembea mwendo wa majigambo sana na muda huo alikuwa ameshika mkongojo wa dhahabu mkononi mwake kuonesha ni mtu ambaye alikuwa ana damu iliyokuwa imechafuka kwa pesa.
Alipokutana naye walipeana salamu na kisha wote wawili waliingia ndani ya geti hilo la bandari baada ya kufunguliwa, ndani walikuta kukiwa na taa zilizokuwa zikiwaka na vijana waliokuwa wameshika silaha wakiwa wamejipanga katika sehemu tofauti. Kawaida ya Jasusi ilikuwa ni kutotuliza macho yake katika sehemu moja hasa kwenye maeneo kama hayo, hivyohivyo Jasusi huyu hakuwa ametuliza macho sehemu moja bali alikuwa akitembea huku akiyazungusha kwa kasi ya ajabu katika kila pande. Shingo yake haikugeuka kabisa katika muda huo aliokuwa akizungusha macho yake, Khemiri hakuwa amejua juu ya kutaliiwa kwa mazingira ya hapo na Norbert yeye alimuona kama alikuwa akitembea kuelekea huko walipotakiwa kufika ndani ya muda huo. Walitembea kwa mwendo mrefu sana kutokana na eneo hiolo kuwa kubwa sana, walienda hadi kwenye sehemu maalum ya kuifadhia mizigo ndani ya bandari ambapo Khemiri alichukua muda huo kumfafanulia juu ya kila kitu.
"Hii ghala ni maalum kwa mizigo ambayo imeshakaguliwa na kulipiwa kodi kila kitu ikisubiri kusafarishwa tu na mmiliki" Khemiri alimuambia na kisha akatazama katika uso wa Norbert ambaye alikuwa ameshusha kofia, alipohakikisha alikuwa yupo pamoja naye baada ya Norbert kumpa ishara aliendelea.
"Pindi mzigo wako uatakaposhuka tu jua utaingizwa ndani ya ghala hii na siku hiyo wahusika wote watakaohusika na kuushuhsa mzigo huu jua wamepangwa na Mheshimiwa" Aliendelea kumueleza na muda huo walitoka wakawa wanaelekea kule ambako kulikuwa sehemu ambayo meli inaegeshwa kwenda kupata maelekezo mengine, walifka hadi eneo hilo ambako kulikuwa na meli ambayo ilikuwa imeegeshwa baada ya kumaliza kupakua mizigo yake. Hapo alipewa na maelekezo muhimu kabisa ambayo alitakiwa kupewa, baada ya hapo walikuwa wakirudi kule ambako walikuwa walipokuwa awali.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda huo waliokuwa wakirudi ndiyo ilijidhihidrisha katika vitu visivyo na staha ndani ya dunia hii si wanadamu pekee hata viumbe visvyo na uhai pia huwa havina staha, kofia ambayo alikuwa ameivaa kichwani Norert ambayo ilikuwa imeegeshwa ilimletea kadhia nyingne ambayo hakutegema kama ingeweza kutokea. Kadhia hiyo ilikuwa imesababishwa na kile ambacho hakikuwa na staha kabisa, kitu hakikuwa kingine bali ulikuwa ni upepo wa eneo la hapo baharini. Upepo huo uliokuwa ukivuma kutoka nchi kavu kuelekea baharini uliikumba kofia yake kwa ghafla sana kupelekea kuanguka, ilipoanguka kofia hiyo ndipo Khemiri alipoweza kubaini kuwa alikuwa akitazamana na mwandishi wa habari hatari. Hapo alijua kabisa kuwa alikuwa amekuja kupelelezwa na mwandishi huyo na hakukuwa na jingine, macho yalitoka pima huku akimtazama Norbert ambaye alikuwa ametulia tu kama alikuwa hajali kitu hicho kilichokuwa kimetokea.
"Wewe!" Alipaza sauti kwa nguvu sana na kisha akapeleka mkono kiunoni mwake na kutaka kutoa bastola, mkono huo haukufika kabisa kwani ulipigwa teka la nguvu sana hadi akapatwa na maumivu. Norbert alipotaka kumfuata amuongeze kipigo kinggine milio ya risasi ilianza kurindima kulenga huko alipokuwa yupo, kiuwepesi zaidi aliamua kujibiringisha kutoka hilo eneo na kisha akaingia eneo lenye makontena mengi. Kundi la vijana wale waliokuwa wakilinda nalo lilikuwa katika eneo hilo mara moja, walielekea kwenye upande ule ambao alikuwa ameelekea muda huo akiwa na silaha zao. Eneo ambalo alikuwa amepitia ambalo lilikuwa na mkontena matupu hawakuweza kabisa kumkuta na wanatembea hadi mwisho wa eneo hilo bado hakuwepo, walijigawa makundi katika kumsaka mtu huyo ambaye alikuwa amempiga bosi wao teke ambalo lilimletea maumivu mkononi.
Vijana hawa hawakujua kabisa kuwa huyo mtu waliokuwa wakimtafuta alikuwa ni ninja na pia komandoo mwenye mafunzo ya hali ya juu sana, walipoyatazama makontena hayo yalivyokuwa na kimo kirefu kwenda kutokana jinsi yalivyojipanga. Hawakuamini kabisa kuwa huyo mtu ambaye walikuwa wanamtafuta alikuwa amepanda kuelekea juu, lakini ukweli utabaki kuwa uleule kuwa alikuwa amepanda kuelekea juu ingawa wao walipuuzia. Uwezo wa kupanda vitu wa Norbert kama ni mnyama ungeweza kumfananisha na nyani kiuwezo huo, kwani muda huo waliokuwa wakimtafuta yeye huko chini hakuwepo. Kasi ya jabu ilikuwa haielezeki kwani alikuwa ameshafika kabisa juu ya makontena na muda huo alikuwa amejilaza kifudifudi akiwa ametulia. Alikaa kwenye eneo hilo kwa sekunde kadhaa na kisha kwa kasi ya ajabu alinyanyuka na akaruka kutoka kontena alilokuwa amekaa hadi jingine, alito kishindo mabcho kilisikiwa na wale walinzi wakaanza kulekea huko alipo. Yeye hakutaka hata kusimama alikuja na kasi nyingine kabisa na aliruka hadi kontena jingine. Hakutaka napo kukaa kwani aliona alikuwa akijichimbia kaburi zaidi ikiwa ataendelea kuwepo hapo, napo kwa kasi ya jabu alirukia kontena jingine ambalo ndiyo lilikuwa upande wa mwisho jirani kabisa na bahari. walinzi waliokuwa wakimfukuza walikuwa wakifuata vishindo hivyo walikuwa wameshachelwa tayari kwani alijiachia kutoka huko juu na kuingia moja kwa moja kwenye maji. Kutokana na eneo la bandari kuwa na kina kirefu sana ilikuwa rahisi kwake kuweza kutoroka hapo, alianza kupiga mbizi akiwa yupo huko ndani ya maji kuelekea upande ambao kulikuwa na soko la feri. Alikuwa tayari ameshapata kitu ambacho kitakuwa ni mwangaza kwake ingawa mambo tayari yalikuwa yameshaharibika, aliwaacha wale waliokuwa wakitaka kummaliza wakiwa amebaki mdomo wazi kutokana na jinsi alivyokuwa amewatoroka.
Alikuja kwenye kutokea soko le feri katika eneo ambalo kulikuwa na Mashua mengi yaliyokuwa yakitumiwa na wavuvi, alitoka akiwa amelowana kuanzia nguo hadi viatu hadi wavuzi waliokuwa wapo eneo hilo wakamshngaa. Hilo yeye hakujali alitembea hadi barabarani na kisha akaanza kushiriki matembezi ya hisani kwa kuchelea kuwa akichukua teksi au pikipiki angeibua maswali mengi sana kwa dereva, alikata mitaa ya kata ya magogoni na hatimaye alikuja kutokea kwenye ofisi yake ambayo ilikuwa ipo katikati ya jiji. Norbert alipoingia ndani ya ofisi hiyo ambayo ilikuwa imejikamilisha kila kitu jambo la kwanza kulifikiri ilikuwa ni kubadili nguo zake, alibadili nguo hizo kwa haraka sana na kisha akahamisha vitendea kazi vyote kwenye nguo mpya alizozivaa. Baada ya hapo ndipo alipotoka kwenye ofisi hiyo akatumia pikipiki yake ya kazi ambayo alikuwa ameiegesha kuondoka ndani ya eneo hilo na kuelekea kwenye makao yake kwa muda akiwa yupo kazini.
****
Muda mfupi baadaye Khemiri alikuwa yupo mbele ya Askofu Valdermar, alikuwa ameshampa taarifa zote juu ya kufika eneo la bandarini akiwa na mtu ambaye alikuwa akijua ni Mteja kumbe alikuwa ni Norbert. Jambo hilo lilimshtua sana Askofu akaona kuwa kazi yao ilikuwa imeingiwa na hatari kubwa sana kwa kuwepo mtu huyo ambaye ameanza kuwanyima usingizi, tuhuma walikuwa wamempatia mwingine walitegemea kuwa huyo angeweza kukaa chini na kutulia akijua kazi imeisha kumbe bado alikuwa yupo kazini. Wote walichanganywa wakachnganyika na taarifa hiyo, muda huo wote walikuwa wapo kwenye sebule wakiwemo kina Josephine. Spider naye alikuwepo akiwa na ogo sehemu ya mkono pamoja na mguuni kutokana kile ambacho kilikuwa kimemkumba mapema sana ndani ya siku hiyo.
"Yaani huyu mtu mmoja anatutesa sana sisi jamani" Akosfu aliongea
"Shaw huyu mwandishi ni hatari sana na sisi tupo pabaya hadi muda huu, inabidi auawe mara moja" Khemiri alionga akiwa hajui kabisa uhalisia wa Norbert, kauli hiyo ilimfanya Askofu aanze kucheka kutokana na muongeaji alivyokuwa akiichukulia kirahisi sana.
"Hivi unafikiri kumuua huyo ni kazi rahisi sana Khemiri, hebu mtazame Spider nafikiri unamtambua kuwa ni mpiganaji hodari lakini kateguliwa mguu na mkono. Yote kazi ya huyo unayesema tumuue" Askofu alimuambia na kupelekea Khemiri abaki kinywa wazi kwani hakutarajia kabisa kuwa mtu huyo angekuwa hatari namna hiyo.
"Ooooh! No" Alijikuta akitamka akiwa haamini
"Khemiri napenda ujue hatushindani na binadamu wa kawaida pale, yule ndiye N001 halisi kabisa wa EASA nafikiri ushasikia habari zake" Aliambiwa.
"Tumekwisha basi ni huyo maana sifa zake nishawahi kusikia, mwanzo nilijua ni hadithi tu kumbe yupo halisi" Khemiri alismea kwa kukata tamaa
"Hakuna kukata tamaa mapema yote hiyo, cha msingi nikumuwekewa mtego, ana udhaifu wa wanawake yule nafikiri tutamuingiza mtegoni tu. Kwanza kalipa huyu hebu angalia akaunti yetu" Josephine aliuiza na kupelekea Khemiri awashe tarakilishi yake kwa haraka sana na kisha alifungua akunti ya benki kwa njia ya mtandao, alichokiona alijikuta akipiga kelele kama mwendawazimu hakuamini kabisa kama angeweza kukuta kitu kama hicho.
Wote wlibaki wakimshangaa sana wakiwa hawajaelewa alikuwa anapiga kelele kwa sababu gani, Khemiri hakutaka kuongea chochote yeye alimpa Tarakilishi Askofu ambaye naye aliingiwa na ubaridi wa ghafla kwenye moyo wake akiwa haamini kabisa kwa alichokiona. Askofu naye aliweka kiganja cha mkono usoni mwake na kisha akampatia Tarakilishi Scorpio ambaye alikuwa yupo pembeni yake, naye alitoa macho pima kama alikuwa ameingiwa na umeme wenye hitilfu kwenye mwili wake. Alimsogezea Josephine ambaye alishtuka sana akiwa haamini kwani walikuwa amehangaika sana, alimpatia Spider ambaye alijikuta akiinamisha uso wake na huku Tarakilishi hiyo akiiweka pembeni.
"Aaaargh! Norbert hii ni too much sasa, naingia mwenyewe kazini haiwezekani tuhangaike kote aje kufagia akaunti yote" Akosfu Valdermar aliongea
Ilkuwa ni suala ambalo lilikuwa likitosha kabisa kumfanya yule mwenye moyo mwepesi kuweza kupoteza fahamu hata kufa kwa mshtuko kwa jinsi lilivyokuwa limetokea, akaunti yao ya benki ambayo walikuwa wakiitumia kwa ajili ya kazi hizo haramu ilikuwa imesafishwa yote. Hakukuwa na hata na senti tano kwenye akunti yao hiyo ambayo walikuwa wameifanyia kazi, ilikuwa na zaidi ya mabilioni lakini yote walikuwa hawayaoni. Waliona kama macho yao yalikuwa yameingia ukungu waisome kwa sasa lakini haikuwa hivyo, jambo walilokuwa wakilishuhudia hapo lilikuwa halisi kabisa. Wote waliumia sana kwani hiyo ndiyo ilikuwa akaunti yao kubwa na sasa ilikuwa imeshasafishwa, wote hawakuwa na kumlaumu juu ya hilo isipokuwa Norbert tu ambaye ametoka kuchukua namba zake tu mchana wa siku hiyo na sasa ilikuwa imesafishwa. Hiyo waliamini ilikuwa ni mbinu hatari ya waliofuzu kwa kiwango kikubwa katika matumizi ya Tarakilishi ingawa hawakujua kabisa aliyefanya hivyo alitumia njia gani, hakika walipatikana ndani ya siku hiyo na walikuwa wakitakiwa kuanza moja katika biashara hiyo.
"Yaani akaunti ikaribie kufika Trilioni ndiyo asafishe kweli nase hivi sikubali" Aksofu Vldermra aliongea
"Nikimshika nitamkata vipande vipande huyu mshenzi hii ni too much" Scorpio naye aliongea kwa hasira huku akiuma meno.
"Yaani sijui nitamfanya kwa jinsi nilivyokuwa na hasira kwani bado ana kisasi changu halafu anazidi kutushusha nguo za ndani maana nguo za juu katuvua huyuu" Josephine naye aliongea kwa hasira sana hadi macho yakawa yanalengwa na machozi, muda huohuo Akosfu Valdermar alinyanyuka na kisha akaingia ndani bila ya kusema chochote. Alikaa kwa takribani dakika moja na alirejea akiwa ameshika mkoba wa namba ambao alimpa Khemiri, mkoba huo ulipokelea kwa mikono miwili na mlengwa huku akiachia tabasamu.
"Huu mzigo unahitajika uutoe ndani humu na kisha uuweke kwenye kasha zile si unaona tumekombewa hapa nahitaji tujiinue tena" Alimuambiana kisha alimtazama usoni kama alikuwa ameelewa, alipoona alikuwa ameelewa alimruhusu kuondoka eneo hilo akimuambia walikuwa na mpango mzito wa kupanga hivyo kazi ilikuwa imeishi hapohapo hakukuwa na jingine jipya. Hapo Mlengwa aliondoka akiwa amebebea mzigo huo muhimu aliokuwa amekabidhiwa na wenzake
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Zilipopita dakika kadhaa tangu aondoke wote waliokuwa wapo chini ya Akosfu waligeuza macho na kumtazama usoni, wote hawakuwa wameelewa kwanini alikuwa amefanya vile kwa mtu ambaye hakuwa adui yao. Walikuwa wakitambua kabisa kuwa mkoba aliokabidhiwa Khemiri ulikuwa ni aina ya nyingine ya bomu ambalo halina tofauti na bomu la barua, bomu hilo ukifunguliwa mkoba na hewa kuingia ndani hata sekunde mbili haifiki hulipuka haohapo. Sasa alikuwa amemkabidhi Khemiri ambaye alikuwa ni mtu waliyefanya naye kazi nyingi san,waliona alikuwa amekosea sana kumkabidhi huo mzigo lakini hawakutaka kumkosoa ndani ya muda huo kabla hajafafanua.
"Madam kwanini unampa sumu ile jamaa wakati ni mtu wetu mkubwa inamaana hana umuhimu tena?" Josephine aliuliza
"Yule ni Kondomu tu ikishatumiika haina maana" Alijibu kimafumbo zaidi.
"Kondomu ikitumika ni kutupwa kwani haitokuwa na ubora ule wa awali, ndiyo kama huyo kwa sasa hana ubora huo ndiyo maana kafanya uzembe mkubwa sana" Aliwajibu zaidi
"Lakini wakuu hawatatuelewa kwenye suala kama hili Madam hebu fikiria" Spider naye alishauri
"Ikiwa ameonekana na Norbert basi jua atamtumia kama daraja ili atufikie sisi,sasa mimi daraja nalivunja ili asifike upande wetu tu maana atakuwa ni hatari sana" Alifafanua
"Hapo sawa tumekupata, umefanya la msingi sana" Josephine aliongea baada ya kuelewa lengo la Askofu kupanga mpango huo wa kumuangamiza Khemiri wakati alikuwa ni mtu wake wa karibu sana.
"Tulikuwa tumepunguza mzigo yeye anatuletea mzigo mwingine, hiyo ndiyo alilostahiki hakuna jingine"
****
Hakuwa akiwaza kabisa kuwa alikuwa amebeba kiama chake mwenyewe, alipotoka tu kule kwenye makao ya washirika wake aliondoa gari haraka sana akiwa analekea nyumbani kwake. Alikuwa akiutupia sana macho ule mzigo aliokuwa ameubebea ambao aliona ulikuwa na uzito mkubwa sana, moyoni alishukuru kabisa kwa suala kama lile ambalo lilikuwa limeharibika kisa yeye wenzake kumuelewa na kulimaliza kwa namna ya kistarabu sana. Hakujua kabisa kuwa hakuwa ameeleweka na alikuwa amebeba adhabu yake ambayo alikuwa akihitaji kupatiwa kutokana na uzembe aliokuwa ameufanya, kuweza kumuamini Norbert kisa kusikia hela nyingi ilikuwa ni uzembe mkubwa sana ambao hakutakiwa kuufanya. Kushindwa hata kumchunguza huyo adui yake hakujua kabisa kuwa alikuwa akijichimbia kaburi wakati anatoa maelezo hayo, sasa alikuwa amebeba tiketi yake ya kuzimu ndani ya gari hiyo akiwa hajielewi kabisa.
Nyumbani kwake kulikuwa ni Mbezi katika kwenda huko alipofika mataa ya mwenge alikuta taa zilkuwa nyekundu, hapo ilimbidi asimame aweze kusubiri magari ya upande mwigine yaweze kusimamishwa na taa hizo ndiyo na yeye avuke. Akiwa kasimishwa ndiyo alijikuta akipata wahka wa kufungua mkoba huo wa namba, kwakuwa namba alikuwa akizijua haikumuwia vigumu kwani mikoba ya umoja wao ilikuwa ikitumia namba za aina moja yote. Aliweka namba hizo na kisha sehemu ya vibanio za kufunga mooba huo zilifyatuka na kumfanya atabasamu, alipovuta kufungua ndipo kilipotokea kizaazaa kwani alijikuta akirushwa juu huku ukiambatana mlipuko mzito sana.
Hilo lilikuwa ni tukio la kushtusha sana kwa watu waliokuwa wapo jirani na gari hilo hasa magari ya jirani, wote walikumbwa na athari za mlipuko ikiwemo kuruka kwa vioo na pia moto kufika kwenye mgari yao na kuanza kuunguza. Nao walijikuta wakikimbia wakaacha magari hayo huku waliojeruhiwa wakibaki ndani ya eneo. Mayowe ya watu waliokuwa na uoga yalisikika kwa nguvu sana kwani hazikuwa hata zimepita siku mbili tangu watu waanze kuawa ndani ya jiji sasa lilikuwa likitokea tukio hilo, hakuna ambaye alikuwa hajipendi kuendelea kukaa eneo hilo wote walikimbia kwani waliona kulikuwa kumevamiwa. Waliliacha gari ambalo yeye mwenyewe alikuwepo humo ndani akitekea kwa moto, ilichukua dakika kadhaa Askari wa jeshi la polisi wakawa wamekifa ndani ya eneo hilo wakiambatana na wenzao wa zimamoto. Moto ulihangaikiwa kuzimwa na ulipozimika ndilo walipohangika katika kuutoa mwili uliokuwa upo ndani ndani ya gari hiyo, baada ya hapo walianza kukagua gari hiyo wakiangalia bati la namba za gari hilo kuweza kutambua mmiliki wa gari hilo kupitia namba zake. Walipozipata namba za gari hilo muda huo vyombo vya habari vilikuwa vimeshafika eneo hilo na walikuwa wakihitaji kwa kina maelezo yao. Walitumia wasaaa huo kuanza kuwaeleza juu ya hali halisi iliyopo hapo hadi kukatokea hayo, pia waliwatajia namba za gari hilo wakiahidi kuwa uchunguzi ulikuwa ukiendelea.
****
Habari hiyo ilikuwa imefika katika muda ambao Moses alikuwa yupo mke wake Beatrice aliyekuwa akinyonyesha mtoto wao, wote wawili walipigwa na mishangao tofauti kutokana na habari hiyo iliyokuwa ikitangazwa. Mshangao wa Beatrce ulikuwa ni juu ya mfululizo wa matukio hayo ambapo aiingiwa na uoga mkubwa sana kuhusu tukio hilo, aliona ile hatari ambayo ilikuwa ikitajwa kuwa ilikuwa imeisha baada ya Mhusika kukamatwa ilikuwa ikiendelea kama kawaida haikupita muda mrefu kupitia vyombo vya habari mwenye gari hiyo aliweza kufahamika wakiwa bado wapo hapohapo. Moses mwanzo alikuwa na mshangao wa juu ya mauaji hayo yalikuwa yakilenga kuharibu ushahidi muhimu, lakini alipopata taarifa za namba za mmiliki wa gari hilo alijikuta akihisi suala hilo lilikuwa likilenga kumuharbia kazi Norbert kwani siku zilikuwa zinayoyoma zaidi. Alikuwa akijua kabisa kuwa Norbert alikuwa ameshamjua kuwa mtu huyo alikuwa ni mmojawappo kati ya watu waliokuwa wapo ndani ya mtandao wa kifisadi na sasa alikuwa ameuawa, hapo alihisi mbio za Norbert kwa hatua moja zilikuwa zimeanza kugundulika.
"Halafu baby hii kesi nimeletewa ujue" Beatrice alimuambia
"Ksi ipi hiyo my wife" Alimuuliza
"Si hii ya kumtetea Mheshimiwa Kabinuki, yaani wameniwekea dau kubwa nimtetee" Moses aliposikia hivyo aliona kuwa mke wake alikuwa akielekea kuingia katika upande mgumu sana ilihali bado alikuwa akimuhjitaji.
"Mke wangu hivi unataka hela au unataka maisha yako?" Alimuuliza
"Maisha yangu ni muhimu zaidi"
"Basi usiingie kwenye kesi hiyo waachie mawakili wengine"
"Kwanini?"
"Mke wangu nchi hii na serikali yake ina mengi sana angalia utajiweka matatani ni mtandao huo"
"Lakini hii ni taaluma pia"
"Hivi kumtetea mtu ambaye anachukiwa na watanzania ili awe huru utaniweka kundi gani mumeo?" Swali hilo lilimfanya Beatrice anyamaze kabisa kwani alikuwa akitambua kabisa heshima iliyokuwa imechafuka baada ya mume wake kupakaziwa jambo ilikuwa imerejea, sasa aliona kweli alikuwa akielekea kuichafua heshima hiyo kwa mara nyingine.
"Sawa mume wangu hapo nimekuelewa sitokubali ofa yao"
"That's my wife"
"Kwasababu nakupenda ndiyo maana, halafu Mzee Kabaita alipiga simu wakati ukiwa bado hujarudi alikuwa na shida na wewe"
"Mh! Ngoja nitaenda kumuona siku ya kesho nyumbani kwake"
"Yaani kakuambia ufanye haraka sana kwani ana jambo la muhimu sana"
Muda huo waliokuwa wakijadili mambo hayo tayri Mzee Kabaita alikuwa ameshajitoa kwenye siasa na alikuwa akifanya mambo yake mengine kabisa mbali na siasa. Hakuwa na mtoto na alikuwa akiishi na mke wake ambaye ndiyo alikuwa ni faraja kwake, alikuwa akiwasiliana na pia kuongea na Moses juu ya mambo mbalimbali kwani walikuwa wakiheshimiana sana kama mtu na mwanae, ndiyo maana taarifa hiyo Moses hakutaka kuipuuzia kabisa aliona ilikuwa na uzito wake ndiyo maana alitaka kwenda huko moja kwa moja.
****
[6]CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi ya siku iliyofuatia zikiwa zimebaki siku sita kwenye kazi ambayo aalikuwa amepewa Norbert, wakili mwingine kabisa alitafutwa kwenda kutetea kesi ya Mheshimiwa Kabinuki baada ya Beatrice kukataa. Ndani ya asubuhi hiyo Mheshimiwa huyu ambaye alikuwa ameshuka thamani yake, alitolewa kwenye gereza la Segerea akiwa yupo chini ya ulinzi mkali sana kwani ilikuwa ni siku ambayo kesi yake ilikuwa ikisikilizwa kwa mara ya kwanza. Nchi nzima ilikuwa ikitambua kabisa kuwa ndiyo ilikuwa ni siku maaluma ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, alipandishwa kwenye gari maalum alilokuwa ameandaliwa kwa usalama wake na msafara ulianza mara moja. Msafara huo wenye ulinzi mkali sana ulipofika eneo la jirani kabisa na Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu walikutana na idadi kubwa ya wanachi wakiwa wamejaa kwenye mahakama hiyo, wananchi wote walikuwa wamebeba mabango yaliyokuwa yakimlaani kabisa Mheshimiwa huyo. Yeye mwenyewe alipoyaona alijikuta akilia kabisa akiona dunia ilikuwa imemuhukumu na hakuwa na hatia yeyote, msafara huo ulipokaribia kuingia kwenye lango la magari la Mahakama hiyo iliyokuwa ipo maeneo ya Upanga, iliwabidi maofisa wa jeshi la polisi wafanye kazi ya ziada ya kurudisha watu nyuma kwani walikuwa wakileta fujo sana huku wakimtukana Mheshimiwa huyo.
Msafara uliingia ndani kabisa ya mahakama na ulienda kwenye sehemu maalum, hapo Mheshimiwa Kabinuki aliteremshwa akiwa amewekewa ulinzi mkali sana. aliingizwa kwenye chumba cha kusubiri kwani muda wa kesi yake haukuwa umefika, baada ya nusu saa muda ulikuwa umefika tayari na alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza ndani ya maisha yake kwa tuhuma ambayo haikuwa yake. Chumba cha mahakama chote kilikuwa kimesheheni waandishi wa habari ambao walikuwa wamekuja kuchukua matukio muhimu yaliyokuwa yakihusu kesi, baada ya muda mfupi Hakimu aliyekuwa na jukumu ndani ya kesi hiyo kwa siku hiyo alikuwa akihitajika kuingia ndani ya chumba cha Mahakama.
"Kooorti" Ilitolewa kauli hiyo muda ambao Hakimu alikuwa akiingia ndani ya chumba cha Mahakama, watu wote walisimama na Hakimu aliyekuwa amevaa vazi lake nadhifu alionekana akiingia ndani ya chumba cha Mahakama. Aliketi kwenye kiti chake mbele kabisa na watu wote ndani ya chumba hicho waliketi nao, baada ya hapo utaratibu ulianza mara moja.
Muendesha Mashtaka alisimama na kuanza kusoma mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Mheshimiwa Kabinuki, kwakuwa mahakama hiyo haikuwa na uwezo kuiendesha kesi hiyo. Mheshimiwa Kabinuki aliamriwa asijibu chochote, kesi hiyo ilitajwa na kisha ikapangiwa tarehe ya kwenda kusikilizwa Mahakama kuu ambayo ilikuwa ina uwezo wa kuendesha kesi hizo. Alirudishwa tena rumande kwani kesi yake kutokana na uzito wake hakuweza kupata dhamana, muda huo kila kitu kilirushwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kesi hiyo ambapo kwa wale waliokuwa hawajui utaratibu wa kisheria waliona kama kesi hiyo ilikuwa ikichelewa kutolewa ukumu kwa jinsi walivyokuwa wakimchukia Mheshimiwa Kabinuki.
****
Muda ambao Mheshimiwa Kabinuki alikuwa akielekea gerezani Norbert alikuwa yupo kwenye tarakilishi yake, alikuwa akisikiliza kile ambacho alikuwa amekitegea mtego katika siku iliyopita pale alipokutana na Khemiri. Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Khemiri na kundi la wahalifu wenzake baada ya yeye kuweza kumtoroka kule bandarini, alikuwa tayari ameshafanya ujanja katika muda ule ambao alikuwa amekutana na Khemiri kabla hata hawajaingia ndani ya Bandari. Kitendo cha Khemiri kupenda kusalimiana na watu kwa kushikana mikono kutokana na kuwa ni Muislamu aliyekuwa akikanyaga msikiti ila hakuacha maovu, alijikuta kiwa amempa nafasi adimu sana Norbert kwani kushikana huko alikuwa akipenda sana kupeana salamu ya kukumbatiana na kwa kugusanisha mabega ambayo mara nyingi husalimiana vijana wa sasa. Pamoja na kukumbatiana huku hakukuwa kupo kwenye sheria za dini yake yeye alipapenda sana kutokana na kuizoea kwenye genge lake , alipomkumbatia namna hiyo Norbert baadaya kushikana naye mikono ndipo alipowekewa kifaa kidogo sana. Kifaa hicho kilikuwa kina uwezo kurekodi eneo ambalo alielekea hadi anatoka na pia kunasa sauti. Sasa Norbert alikuwa ameshafanikiwa kureodi vyote na muda huo alikuwa akiyapitia maongezi hayo yote, aliyaskiliza kwa umakini akiwa amekaa kwenye kiti ndani ya nyumba ya EASA. Baada maongezi hayo kuisha alisikiliza sauti zilizokuwa zikifuata hadi pale Khemiri alipopanda gari yake na kuondoka ndani ya eneo hilo, njiani alipokuwa akiendesha gari aliweza kusikia jinsi alivyokuwa akiongea na watu mbalimbali ka kutumia simu yake ya mkononi. Sauti ilikuja kukatika baada ya kutokea mlipuko ambako alisikia kishindo na kisha sauti ikakata, alipomaliza kusikiliza alijikuta akitabasamu kama ilivyo kawaida yake na kisha akatazama kwenye kioo cha Tarakilishi akifungua faili jingine. Aliweza kuona nyendo zote ambazo alikuwa amezipitia Khemiri tangu alipotoka bandari na hadi anafika kwenye nyumba yenye makao yao, eneo hilo alilikariri pamoja na kuchukua kifaa kingine ambacho alikitia faili hilo. Hicho kilikuwa kifaa ambacho kilikuwa kina uwezo kumuongoza hadi ndani ya eneo husika kwa kutumia rekodi iliyokuwa imechukuliwa hapo awali"
"Kazi kwao" Alisema na kisha akakichukua kifaa hicho na kunyanyuka kitini.
Alitoka hadi nje kwenye maegesho ya vyombo vya moto yaliyokuwa yapo ndani ya nyumba hiyo, hakuwa na chombo kingine cha kuchukua isipokuwa ni pikipiki yake na aliamua kuitia moto kisha akatoka ndani ya nyumba hiyo baada ya geti kufunguliwa. Aliingia barabarani na aliiondoa kwa kasi sana hadi alipofika eneo la Mtoni kwa Aziz Ally akitokea huko Kurasini. Aliingia kwenye barabara ya Kilwa kwa mwendo wa wastani akiwa upande ilipo barabra iliyokuwa ikielekea Mtoni Mtongani, aliongeza mwendo huo baada ya kuufikia Mlima mdogo uliokuwa upo eneo la Mtoni Madafu na kisha aliendela na mwendo huo huo huku akiyapita baadhi ya magari ambayo yalikuwa yapo kwenye mwendo mdogo sana kuliko yeye. Baada ya dakika takribani kumi alikuwa yupo ndani ya eneo la Mbagala rangi tatu lakini napo hakukaa aliendelea mbele, dakika tano baadaye alikuwa ameshafika Kongowe mwisho na aliingia kwenye barabara iliyokuwa ikielekea Kigamboni. Norbert alipoingia kwenye barabara hiyo hasa kwenye eneo la jirani kabisa na kituo cha Daladala kinachotumiwa na daladala ziendazo Kigamboni, alipunguza mwendo kidogo wa pikipiki hiyo kutokana na kuwepo gari nyingi katika eneo hilo zenye ukubwa tofauti ambazo zilikuwa zikitembea kwa mwendo wa taratibu sana. Hali hii iliyokuwa ikisababishwa na daladala zilizokuwa zikichukua abiria njiani ilimkera sana, lakini na hakuwa na kitu cha kufanya kabisa kwani upande mwingine ulikuwa magari mengi ya mchanga pamoja ya mizigo yaliyokuwa yakipita hivyo ulikuwa si salama kwake. Sifa ya barabara hii ni magari kwenda mbio haikujalishi lilikuwa gari la dogo au kubwa, hiyo ilimfanya asubiri kwenye eneo hilo ambapo alipoteza dakika tano hapo hadi pale daladala zilipoanza kusogea.
Baada ya hapo alikuwa kama amefunguliwa kwenye kifungo kwa jinsi alivyovuta mwendo kwenye pikipiki hiyo, alianza kuyapita magari hayo kwa kasi alipofika kwenye eneo ambalo magari yalikuwa yameachana mabalimbali. Pikipiki hiyo ya kisasa nayo ilijua haswa kuzitii amri zake alizokuwa akiipa, kila alipotoa gia hii na kuweka nyingine nayo ilitii na kupelekea awe kwenye mwendo mkali sana. Alikuwa akipunguza mwendo kwenye maeneo ambayo yalikuwa na Matuta tu au kwenye eneo jirani na makazi ya watu na alipotoka maeneo hayo alikuwa akivuta mafuta sana. Utumiaji wa mwendo mkubwa namna hiyo haikumuwia vigumu kabisa kuweza kufika Kibada mapema, alifika eneo hilo na kupitia kile kifaa ambacho hadi muda huo alikuwa amekipachika kwenye pikipiki. Alifika sehemu ambako kulikuwa kuna kona ambayo aliikata kuendana na kifaa hicho kilivyokuwa kikisema, alitembea kwa mwendo mfupi tu na alifika kwenye nyumba ya kifahari sana iliyokuwa ipo miongoni mwa majengo ya kifahari yaliyokuwa yapo mtaa huo. Kifaa kile kilimuonesha kuwa eneo alilokuwa akielekea lilikuwa ni hilo na hapo Norbert ilimbidi apunguze mwendo na kisha akatafuta eneo zuri la kuegesha pikipiki yake. Alienda hadi kwenye eneo ambalo kulikuwa kuna duka moja kubwa ambalo lilikuwa limeambatana na sehemu ya kunywea vinywaji, hapo aliaingiza Pikipiki yake na kisha akiweka eneo la maegesho ya sehemu hiyo. Alimpungia mkono Mlinzi aliyekuwa eneo hilo ambaye naye alimpungia mkono, hapo alishuka kwenye pikipiki yake na kisha akavua kofia mabyo aliipeleka moja kwa moja kwa Mlinzi huyo.
"Kaka mali hii naingia ndani mara moja nikitoka nitapitia" Alimuambia huku akimkabidhi
"Hamna shida kaka" Mlinzi huyo aliongea huku akiipokea kofia hiyo ya pikipiki ya kisasa kabisa ambayo hakuwani kuziona moja kwa moja katika maisha yake zaidi ya kuziona kwenye luninga tu. Baada ya hapo Norbert alizama ndani ya eneo hilo ambako alitokea kwenye eneo lililokuwa na viti vingi sana, hakutaka kukaa kwnye eneo hilo yeye alizinguka hadi uani ambako kulikuwa na vyoo. Huko aliingia ndani ya choo hiko ambacho kilikuwa na sehemu ambayo ina ukumbi mrefu uliokuwa ukielekeda ndani. Kwenye ukumbi huo hakukuwa na paa kwa juu na hiyo ilimuwia kwa urahisi sana kuuruka ukuta wake na kisha akatokea nje, hapo alichnganya mitaa akiwa amekishika kifaa kile mkononi hadi sehemu ya nyuma ya nyumba ambayo alikuwa amekusudia kwenda. Alipofika hapo alikitazama kifaa hiko ambacho kilinesha ramani ya nyumba hiyo, aliuruka ukuta wa nyumba hiyo na akatokea sehemu yenye maua mengi sana. Hapo alitembea kwa uangalifu sana hadi karibia mwanzo wa kibaraza cha nyumba hiyo. Alijibana kwenye eneo moja na kisha macho akayatupa kwenye lango kuu la kuingilia kwenye nyumba hiyo, aliweza eneo ambalo alikuwa akikaa Mlinzi hakuwepo muda huo na hiyo ikampa nafasi nzuri ya kuweza kutawala kazi yake. Akiwa na mwendo wa kukazana aliingia kwenye baraza la nyumba hiyo na kisha akaelekea ulipo mlango mkubwa, taratbiu alinyonga kitasa ambacho kilitoa mlio wa kukubali kufungua mlango huo.
Aliingia ndani ya sebule pana ambapo muziki ulikuwa ukisikika kwa sauti ya chini sana, hapo alimkuta Spider akiwa amelala kwenye kochi akiwa hana habari yeyote kutokana na ujio huo wa kimyakimya. Norbert alipoingia humo ndani aliona bastola ikiwa ipo kwenye stuli ndogo iliyokuwa ipo jirani na Spider, bilauri yenye mvinyo uliokuwa umeshanyweka ilikuwa nayo ipo pembeni ya batola hiyo. Hapo alichokifanya alienda kuichukua bastola hiyo na kisha akachukua rimoti ya deki ya humo ndani ambayo ilikuwa ikicheza santuri, aliongeza sauti ikawa kubwa zaidi ambayo ilimfanya Spider aamke kutoka kwenye usingizi wake. Spider alipoamka tu alimkuta Norbert kiwa amesimama na mkono akiwa ameweka nyuma, akili yake ilimjia ni kuangalia kwenye stuli iliyokuwa ipo mbele yake akijua silaha yake itakuwa ipo palepale. Alikuta silaha yake ikiwa haipo kabisa ndaniya eneo hilo ambako akiingiwa na ubaridi moyoni mwake.
Muda huohuo Norbert alitoa mikono aliyokuwa ameificha nyuma na alimuonesha bastola hiyo kwani alikuwa ameshajua kuwa alikuwa akiitafuta, alitoa tabasamu na kisha akamfuata hadi jirani yake. Norbert hakuona muda wa kuanza kumsemesha mzungu huyo kwani alikuwa yupo kwenye kazi iliyokuwa na uharaka zaidi, alianza kumshushia kipigo huku akiwa ameongeza hiyo sauti ikawa haisikiki nje. Alimpiga hadi akammuumiza na kisha akammaliza kwa kuvunja shingo yake, baada ya hapo alianza kupekua chumba kimoja baada ya kingine kwani kwani ndaniya nyumba kulikuwa hakuna mtu ndani ya siku hiyo. Alifanikiwa kuzipata zile Tarakilishi mbili ambazo alitoka nazo kupitia mlango wa nyuma ambao aliokuwa ameuona, baada ya hapo aliuendea uzio na kisha aliuruka na kutokea mahala hapo. Alirudi hadi kule alipotokea ambako aliruka tena ukuta wa choo na kisha akaingia ndani akiwa na mkoba wake, alitoka humo chooni na alienda hadi kwenye meza kuu ya kuagiza vinywaji na kisha akaketi kwenye kiti kirefu jirani kabisa eneo ambalo alikuwa amekaa binti mmoja mweupe sana na mrembo aliyekuwa amevaa mavazi maaluma ya wafsnyazi wa eneo hilo.
"Karibu" Alikaribishwa
"Nishakaribia" Aliongea huku akiuweka mkoba wake vizuri mabegani
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nikusadie nini handsome"
"Kile ambacho husaidia wengine wakashindwa kuacha kukiomba tena" Alipomaliza kuongea kauli hiyo aliachia tabsamu lake ambalo ni sumu sana kwa warembo hukua akikaza macho kwenye uso wa msichana huyo
"Una tabasamu zuri haya niambie kitu kipi hicho?"
"Kilichotukuka kuliko voyote kilichokufanya uonekane lulu"
"Halafu we mkaka hayo mambo yako"
"yana nini?"
"Tuache tu, haya nakusikiliza"
"Nilichokuwa nikikihitaji kile kilichokufanya uonekane lulu, upendeze na uzidi kutamaniwa, ni hicho hapo juu kwenye shelf kilichopewa jina la bia kwani kukiuza kwake ndiyo kumekupa pato ukajipatia vya kujikwatua ukazidi kuonekana lulu" Aliongea kimakusudi maneno ambayo yalikuwa ni nje ya mada ambayo ilikuwa imejengeka kichwani kwa mrembo huyo, maneno hayo yalimfanya mrembo huyo acheke kwani alikuwa amewaza jingine kabisa.
"Mmmh! Haya hii hapa"
"Ok ile kuna jingine"
"Lipi hilo?"
"Kaa mkao wa kula ninarudi" Norbeet alipoongea hivyo alichukua kinywaji alichoagiza na kisha akalipia kabisa hela ya chupa, alipomaliza alimuaga Msichana huyo huku akimbania jicho moja na kutoka ndani ya eneo hilo. Hakutaka kabisa kuanza mambo ya kuchombeza wakati alikuwa ametoka kufanya tukio muda si mrefu kwenye eneo ambalo hakukuwa karibu kabisa na maficho yake, aliamua kuondoka hadi kwa Mlinzi ambapo hakuongea chochote zaidi ya kumpatia pesa na kisha akachukua kofia yake. Aliiendea pikipiki yake akaitia moto na kutokomea kwenye eneo hilo kwani hakuwa na muda kupoteza kwenye eneo hilo ambalo lilikuwa lipo jirani kabisa na eneo la maadui zake.
Kanuni mojawapo ya kazi yake ilikuwa ni kutoonesha umaridadi ikiwa tayari umeshapata ushindi kwani umairdadi huondoa ufanisi, kukaa kwenye eneo hilo ilikuwa ni kuonesha umaridadi wake kuwa alikuwa ametoka kufanya tukio na sasa anakaa jirani na maadui zake na hawawezi kumfanya chochote. Hilo hakutaka kulifanya kwa maadui hao ambao hawakujua walikuwa idadi gani kwa ukamilifu, aliamua kuondoka kwa haraka eneo hilo.
****
Wakati Norbert akiwa ameshasabaisha tukio na kuondoka ndani ya eneo la Kibada, Moses alikuwa yupo nyumbani kwa Mzee Kabaita kwenye eneo la uani akiwa amekaa naye. Wote wawili walikuwa na bilauri zao mkononi, muda huo alikuwa amekuja kuitikia wito ambao aliyokuwa ameitwa na Mzee huyo ambaye alikuwa akimuheshimu sana kama Baba yake mzazi. Mke wa mzee Kabaita alikuwa yupo ndani ya nyumba kwa muda huo akiwapisha waongee kwani suala hilo alikuwa hatakiwi kabisa kuwepo wakati wakilizungumza.
"Moses hivi hili suala hili la Kabinuki unalichukulia vipi" Mzee Kabaita alimuuliza
"Ni suala ambalo limekaa vibaya sana baba kiupande wake kwani vithibiti vyote vipo" Alijibu
"Kuwa na vithibiti haimaainishi kuwa ndiyo mtuhumiwa mwanangu, wanasiasa wa nchi hii nawajua fika walivyo"
"Tatizo ni kwamba Kondoo kaibiwa na mifupa yake imekutwa kwa Mbwa unafikiri nani hapo atahisiwa ni mwizi? Halafu ukiangalia kabisa Mheshimiwa naye ndiyo katoa kibali cha kukamatwa kwake anasema Mahakama ifanye kazi haraka"
"Unajua tatizo la Zuber ni moja nafikiri hamumuelewi na pia mimi simlaumu kabisa, hataki afelishwe kwenye uongozi kwa sababu ya mmoja tu. Hivyo akisikia kuwa kuna uozo ni moja kwa moja hatua tu kama ushahidi ukifika kwake"
"Ndiyo hivyo sasa kwenye masuala kama haya huwezi kumuambia kitu"
"Sasa sikia mwanangu mimi naomba ufanye kitu hiki kwa ajili yangu kama unaniheshimu, naomba hili suala la Kabinuki ulifuatilie kwa karibu sana na ikiwezekana umuokoe kwenye hii kadhia"
"Baba hulo suala ni gumu sana kwani kesi yake pia ushahidi mwingine upo kwenye ripoti ambayo ipo kwa Jama na hajulikani yupo wapi"
"Nimefanya nao kazi Kabinuki pamoja na wabunge na mwaziri wengi kabla sijastaafu hii siasa, ninachokuomba ni kumsaidia kwani kuna kitendawili kigumu sana hapo hii ni siasa mwanangu. Mwenye usafi hupakwa uchafu ili aonekane mchafu na mwenye uchafu hujiondoa uchafu aonekane msafi"
"Sawa baba nimekuelewa"
"Jama Wa Majama huyu mtu namfahamu fika ni makamo yanayokaribia na wadogo zangu na kuwa mimi kwenye suala la kuweza kukuleta wewe idara hiyo nimepata bahati ya kujuana naye. Huwa hapendi ambaye hana hatia akose haki yake nafikiri ongea naye utaweza kumfanya aje kumuokoa Kabinuki maana siamini kama ana hatia kwenye suala hili"
"Sawa nimekuelewa Baba"
"Sina la ziada kuhusu hili, vipi mkwe wangu na mjukuu hawajmbo?"
"Wajambo na wazima wa afya kabisa"
"waambie waje siku moja wanisalimu naona imepita muda sana hawajaja"
"Hilo tu usihofu kabisa tena inabidi Baba uniandalie silaha maana watamuiba mjukuu wako kazidi urembo"
"Sasa inabidi uwe mkali hapo tu mimi sihusiki"
"Haa! Baba yaani mjukuu wako yue usimlinde"
Maongezi yalitokuwa yametawaliwa na utani ndiyo yalifuata baina yao baada ya kuweza kumaliza suala lao lililokuwa limefanya wakutane hapo, ulikuwa ni utani ambao ulikuwa ukiendela kila wanapokutana kwani walikuwa wakipendana sana kama mtu na mzazi wa damu kweli.
****
MCHANA
Majira ya saa sita mchana gari ambalo maarufu sana kwa wakazi wa jiji la Tanga pamoja wale waliokuwa wakisafiri kuelekea ndani ya jiji hilo, lilionekana likikata kona kuingia kwenye kituo cha mabasi Ubungo baada ya kufika kwenye jiji la Dar es salaam likitokea Tanga. Abiria walishuka mmoja baada ya moja baada ya bsi hilo kufika kwenye eneo lake la maegesho ndani ya kituo hicho,Jama Wa Majama naye alikuwa mmojawapo kati ya watu waliokuwa wameshuka ndani ya basi hilo akiwa na muonekano wake ueule wa kizee, alikuwa ameamua kabisa kuja kumsaidia Kabinuki baada mkinzano wa mawazo yake kuzidi upande huo.
Aliposhuka ndani ya basi hilo akiwa amebeba begi lililokuwa limechoka aliangaza maeneo ya hapo kituoni kama alikuwa ndiyo anaingia kwa mara ya kwanza. Alijifikira sana na kisha akanyanyua begi lake ambalo lilikuwa limechoka sana, muonekano wake ulikuwa hauna tofauti kabisa na Mzee wa kutoka shamba kwa jinsi alivyo. Alipoangaza sana muda huo wale vijana wajanja wa mji walikuwa wameshaanza kumchangamkia ili waweze kummuingiza mjini, Jama hakutaka kuongea na yeyote yeye alianza kupiga hatua kuelekea nje ya kituo hicho kwani alikuwa akipajua vyema eneo hilo kulivyokuwa kukisifika kwa wizi. Akiwa na mfuko wake ambao kimtazamo kabisa ulikuwa umejazwa mizigo ambayo haikuwa imepangwa vizuri kabisa, alifanikiwa kutoka akawa anatembea kwa mwendo wa kujikongoja hadi zilipo Teksi ndani ya eneo hilo la jirani na kituo cha mabasi. Alienda hadi kwenye mojawapo ya teski na kisha akasogea jirani kwa Dereva wake, alikaribishwa kwa kuchangamkiwa sana kisha akasema mahali alipokuwa akienda. Alitajiwa bei akajikuta ameshtuka sana kwani ilikuwa ni bei ya juu sana kwake, aliomba kupungiziwa huku akiweka uso wa huruma hadi Dereva huyo alikubali na kisha alipanda na mzigo wake kwenye gari na safari ikaanza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wauzaji wa kesi safari hii wameuza hivyo wamempa kesi asiye mnunuaji lazima irudi kwao tu" Aljiseme mwenyewe huku akikumbatia mzigo wake akiwa amekaa kiti cha nyuma na si cha mbele, hiyo ilikuwa ni dalli tosha kwa Dereva huyo kuwa alikuwa amempandisha mshamba aliyezidi kiwango kwenye gari lake hadi yeye mwenyewe alijikuta kibanwa na kicheko.
Macho ya dereva huyu katika muda mbao alikuwa akiendehs agri yalikuwa hayaishi kumtazama Mzee huyu kwa umakini sana kwenye mfuko huo ambao alikuwa amebeba, ukumbatiaji wa namna ile wa mfuko huo ulianza kumfanya ahisi kuwa alikuwa amebeba mali hivyo alikuwa akiilinda. Alienda kuendesha gari huku roho ya tamaa ikiwa imemungia akiutzama tu ule mzigo, hakika tamaa ilimzidi kiwango kuliko kitu chochote. Muda aliokuwa akiendesha gari alipokuwa yupo kwenye barabara ya Mandela alitoa simu yake na kupiga mahali na kisha alizungumza kwa lughz ya kikabila na akakata, walipofika jirani na eneo la Tabata relini aliweka gari kando na watu watatu waliingia kwenye gari hiyo. Wawili kati yao walikaa nyuma katika kile upande na kumuweka Jama kati na mmoja alipanda mbele.
Haikufika mbali ile gari ikiwa inakaribia eneo lenye njia ya kwenda Tabata, vioo voyte vilipandishwa na kiyoyozi ndani ya gari kikachukua nafsi yake. Muda huo Jama alikuwa ameshatambua kabisa kuwa alikuwa amepanda gari moja na wajanja wa maji waliokuwa wanajua yeye ni mshamba, alitulia kimya kama alikuwa ni mjinga vile kwa kitu ambacho kilikuwa kipo vichwani mwa hao watu. Huo ulikuwa ni mpango wa Dereva Teksi kama ilivyo madereva wengine ambao walikuwa wakishiriki vitendo vya uhalifu maeneo ya vituo vikuu vya mabasi. Madereva hawa ndiyo waliokuwa wakichangia kuibiwa kwa wale waliokuwa wakitafua riziki kihalali kabisa, walikuwa wameshawafanya abiria wajenge picha ya ujambazi kila akiona magari yao eneo hilo la kituo kikuu hasa majira ya usiku. Huyu aliamua kuwaleta wenzake katika majira hayo ya mchana akijua huyo aliyekuwa amembeba alikuwa ni mshamba wa jiji, hawakujua kuwa walikuwa wamembeba mtu ambaye ni hatari sana kwenye anga za kutumia silaha na hata kupigana ana kwa ana.
Kutokana na Jama kumtajia kuwa alikuwa akielekea kuwa alikuwa akielekea Kajiungeni, aliamua kuingia njia iendayo Tabata baada ya kufika kwenye njia hiyo na kisha akaongeza mwendo. Muda huohuo wale Watu waliokuwa wamekaa nyuma mmojawapo alitoa bastola lakini kabla hata haijafika kichwani mwa Jama ambapo alitaka kumuwekea alipigwa karate mkono wake silaha ikaanguka chini ya kiti. Alipotazama kule ambako ilikuwa imeanguka silaha hiyo alipigwa ngumi nzito ya shingo hadi akaenda kujigongwa kwenye eneo ambalo lipo pembeni ya kioo. Wa pembeni yake naye alitaka kumkaba alidakwa mkono wake ukavunjwa , muda huohuo mtu wa mbele alileta panga kwa kasi ya ajabu sana akitaka kumchoma lakini halikufika lengo kwani Jama tayari alijosogeza pembeni kwa ustadi mkubwa kisha akaubana kwa miguu mkono wake uliokuwa umeshikilia panga. Kilichofuata hapo ilikuwa ni kuizungusha miguu yake kidogo akaugosha mkono huo hadi panga likamponyoka na kisha akampiga teka jingine la nguvu sana lilipelekea arudi huko mbele kwa kasi sana hadi akaenda kujigonga kwenye eneo lenye makabati madogo ya kuweka nyaraka muhimu. Yule aliyekuwa amejeruhiwa mkono huko nyuma alijaribu tena kurusha ngumi lakini kutokana na ushupavu wa macho aliokuwa nao Jama Wa Majama aliikwepa hiyo ngumi ikapita, alipopita na ngumi alikuwa amesogeza kichw chake jirani kabisa na adui ambapo alipigwa kiwiko cha sehemu ya kisogoni hadi akazira papo hapo. Mwingine kule nyuma alijaribu kuinama chini aweze kuifikia silaha yake lakini kabla hata hajaigusa alipigwa goti la kichwa lililoachiwa na Jama ambalo lilienda kumpigiza kwenye mlango wa gari hilo, akiwa hata hajakaa sawa alipewa ngumi ya kichwa ambayo ilikuwa ni nzito sana ambayo ilimfanya aende kujipigiza kwa mara ya pili. Aliumia sana huyo Jambazi kutokana na ngumi nzito aliyokuwa amepigwa kwani hakutarajia kabisa mtu ambaye walikuwa wakimdhania ni Mzee angeweza kutoa ngumi nzito namna hiyo akiwa anaendelea kuuguliwa maumivu yule aliyekuwa kiti cha mbele alijiweka sawa baada ya maumivu kumuisha na kisha akajaribu kuleta konde kwa mkono mwingine ambao haukuwa umevuunjika. Konde hilo lilikosa lengo kutokana na yeye kuvaa koti la kuteleza ambalo lilikuwa likitoa tahadhari kwa Jama kila akirusha ngumi kwa mlio wake, alikuta Mlengwa alikuwa ameshahama kando na kabla hajakaa sawa alipewa ngumi aina ya uppercut(hii ngumi ambayo hupigwa kwa kuchimbua kidevuni). Hapo alirudi hukohuko alipotoka na akawa ametoa nafasi nzuri sana kwa adui yake waliyemuona mchovu kuingiza mguu chini ya kiti na kutoka akiwa na akiwa na silaha ambayo alikuwa ameibana kwa vidole vya miguu, alimuongezea pigo jingine yule Jambazi wa nyuma kisha akaichukua silaha hiyo kwa mikono yake na akaanza kutabasamu.
"Mmmekuwa mkiwafanya abiria wa kituoni kuwa mitaji wa shughuli zenu haramu siyo sasa leo mtakuwa mfano" Aliongea huku akiwa ameikamta ile bastola mkononi mwake, alipomaliza kuongea aliunyanyua mkono huo uliokuwa na bastola na kuutuliza kwenye kichwa cha Jambazi mwengine ambaye alikuwa amekaa nyuma kusababaisha kumuharibu fahamu zake zote kutokana na ugumu wa kitako hicho. Baada ya hapo alinyoosha bastola mbele na kisha akatulia kama alikuwa hajavamiwa, yule Jambazi aliyekuwa amekaa mbele ujanja ulimuisha kwani aliyekuwa na silaha ya moto alikuwa ni mmoja pekee na ndiyo huyo alikuwa ameshalazwa usingizi.
****
Tarakilishi zote nne kwa muda huo zilikuwa zipo ndani ya nyumba ya EASA kwenye ofisi maalum, nenosiri lote kwa ujumla lilikuwa limeshapatikana na limeungwa kutokana namba za Tarakilishi hizo zilivyo. Lilikuwa ni neno ambalo halikuwa na maana kabisa kwa jinsi lilivyokuwa limeandikwa ingawa aliambiwa kuwa lilikuwa na maana kubwa sana kwa jinsi lilivyokuwa limeandikwa kimafumbo. BARA JANGWA NA USTARABU LIWE NA MAHAJAJI ALEKUWA UMRA UA HIJA, ndiyo lilikuwa ni neno ambalo halikuwa limeandikwa kisarufi zaidi na pia halikuwa na maana ilinyooka mbele ya Norbert. Utaalamu wote wa kuchambua maneno ambayo yalikuwa yana mafumbo kwenye neno hilo alijikuta akishindwa kwani lilikuwa limefumbika zaidi kwa jinsi lilivyokuwa limeandikwa, aliona kabisa kulikuwa kuna umuhimu wa kuweza kumtaufuta Jama ambaye muda huo hakuwa anajua alikuwa amejichimbia wapi kutokana na kupoteza kwenye mazingira ya kawaida. Hapo aliamua tu kuzivunga tarkilishi hizo na kisha akawa anajifikiria jinsi wa kuweza kumpata Jama Wa Majama kwani ndiyo alikuwa ni msaada mkubwa sana, ilikuwa ni muda ambao akiwa anajifikiria hili alijikuta pia akiikumbuka familia yake aliyokuwa ameiacha nyumbani hasa mtoto wake ambaye alikuwa amemdanganya na kumtoroka. Aliona kuwa kazi ndiyo mchawi wa kila kitu lakini hakuwa na jinsi kabisa kwani alikuwa ameshayavulia maji na ilimbidi ayaoge tu, wingi wa mawazo ndiyo ulifanya wazo hio kuchipuka tena ambalo alilifanya moyo wake uingiwe na hisia nyingine kabisa. Hisia hizo hakutaka kabisa kuviweka kichwani mwake yeye aliamua kuziondoa na kisha akawa anafikiri zaidi kuhusu kazi, aliamua kuingia tena kazini kwani hakuwa na muda wa kupumzika kabisa kutokana na siku ambazo alikuwa amepewa za kumaliza kazi hiyo na kisha wahusika waliokuwa wamesabaisha mauaji ya wenzake waliyokuwa wapo nchini Kenya kuweza kubainika na kuweza kutiwa nguvuni.
****
Upande wa kina Askofu hali ilikuwa mbaya kwani hadi kufikia muda huo aliwakuwa wamshabaini kuwa mwenzao mmoja alikuwa ameuawa, ilikuwa ni pigo jingine kwao kwani huyo alikuwa ni mmoja kati ya vijana tegemezi sana kwenye kazi hiyo hivyo alikuwa akihitajika sana. Kitendo cha Askofu kutoka ndani ya siku hiyo akimuacha huyo hapo ndani kutokana na kuuguza majeraha yake ya kuteguliwa, aliona alikuwa amefanya uzembe mkubwa sana kwani ndiyo alikuwa tayari ameuawa kwa kuvunjwa shingo. Akili yake kwa haraka sana alijua kuwa aliyekuwa amefanya tukio hilo alikuwa ni Norbert moja kwa moja ila hakujua kabisa alikuwa kafika vipi ndani ya nyumba hiyo aliyokuwa ameamua kukaa katika eneo hilo lililokuwa limejificha sana. Uhatari wake ulizidi kabisa tofauti na alivyokuwa kiufikiria hapo awali, hii ilimfanya awe na tahadhari zaidi kwani alikuwa ameshatambua kuwa alikuwa akipambana na mtu ambaye alikuwa ni wa ajabu sana kwa jinsi alivyokuwa akiingia eneo lolote na kufanya tukio na kisha kutokomoea bila hata kujulikana kama alikuwa ameingia. Vijana wake tegemezi had muda huo walikuwa wamebaki wawili tu na mwingine alikuwa yupo ndani ya kituo cha polisi kwani alikuwa amekamatwa vilevile kwa kuingia kwenye mtego wa huyo mtu ambaye alikuwa akiwapa homa kila kukicha. Hakika alichanganyikiwa sana kwani hakutarajia kabisa kuwa ndani ya nchi hii kutakuwa na watu hatari zaidi, alikuwa amejenga dharau kabisa mbele ya watu weusi waliokuwa wapo nchi hii na sasa aliamini kuwa lisemwalo lipo. Kwani aliweza kuona uhatari aliokuwa amefanyiwa, muda huo alikuwa ameagiza kijana mwingine aende kushughulika na kupoteza ushahidi na sasa yanatoke mengine ya kutokea ambayo ambayo hakutarajia kama yatatokea, alikuwa ametoka kufanya mpango wa kuichezea arafu serikali pasipo kutambua kuwa na yeye alikuwa amefanyiwa mpango wa kuchezewa rafu. Sasa alikuwa akiumia kwa kitu hicho alichokuwa akifanyiwa pasipo kujali kuwa kulikuwa na wengine nao walikuwa wanaumia kwa kuharibiwa kazi na mipango yake kama alivyofanyiwa, ama kweli mkuki kwa Nguruwe tu kwa binadamu mchungu. Kuumia aumie yeye wala hakujali kuwa kulikuwa a wengine ambao walikuwa wakiumia kama yeye kwa mambo aliyokuwa akiyafanya, alizoea kuona sherehe sana kwa wengine kuumia lakini sasa alikuwa ameumia yeye na anaona huo ni msiba mkubwa sana zaidi hata ya kifo cha mkuu wa nchi. Hakika alijiona alikuwa amewaweza wengine kumbe na yeye alikuwa amewezwa vilevile kwa jambo hilo alilokuwa amefanyiwa na mjanja kiakili zaidi yake, upinzani aliozea kuukuta kwa vyombo vya usalama vya magharibi anaukuta ukiwa upo ndani ya vyombo vya usalama vya ndani ya Afrika tena kwenye ukanda wa Afrika ya mashariki. Hakika alidharau sana udogo wa sindano bila ya kutambua udogo huo ilikuwa ikifanya mambo makubwa, udogo wa kudharauliwa ilikuwa ikishona koti zito kabisa hilo alikuwa amesahau na sasa ilikua imemdhihirishia kuwa ilikuwa na uwezo kuliko kawaida.
****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda huo Askofu alikuwa ametoka kusuka mpango na Josepine wa kuzidi kuwaumiza wengine waliokuwa wapo kazini kama yeye, alikuwa ametoka kusuka mpango wa kwenda kumuangamiza mwenzao aliyekuwa yupo kwenye mikono ya polisi kituo cha Oysterbay baada ya kukamatwa nyumbani kwa Kaboneka alipotumwa. Alikuwa amefeli kwenye kazi yake kwa namna ambayo yeye aliita ni namna ya kijinga sana sasa alitakiwa kuangamizwa mara moja akiwa yupo kwenye mikono ya polisi kutokana na uzembe huo aliokuwa ameufanya. Aliposuka mpango huo na Josephine na kisha kaondoka alimuacha Mwanamke huyo aliyekuwa amempa kazi hiyo akiwa yupo katika maandalizi ya kwenda kuitekeleza kazi hiyo.
Josephine alitoka ilipo ofisi yake akiwa na muonekano mwingine kabisa, alikuwa ameweka nywele kwenye mtindo mpya kabisa na usoni alikuwa na miwani ambayo ilimfanya aonekane kama mwanamke ambaye alikuwa mtafutaji na wala siyo golikipa. Aliingia kwenye gari nyingine ambayo ilikuwa ni ya gharama sana akiwa anaelekea huko kituoni kwani ilikuwa imepigwa simu hapo na aliongea na huyo mwanzao aliyekuwa amekamatwa hapo kituni, alikuwa akija hapo akiwa na muonekano wa wakili aliyekuwa akija kumtetea hyo kijana.
Muonekano wake pamoja na kitambulisho cha kufoji alichokuwa amekibebea haukupingwa kabisa na maaskari wa kituo pindi alipofika na kujitambulisha na kisha kutaka kuonana na Mteja wake. Alipewa nafasi hiyo ya kuongea na Mteja wake kabla hata hajaaza kuhojiwa,alipoipata nafasi hiyo ndiyo aliona ilikuwa ni nafasi pekee ya kuweza kutumiza adhma hiyo wakiwa wapo wawili tu.
"Kwanini unakuwa mzembe hivyo?" Alimuuizaa pindi alipoachiwa nafasi ya kuongea naye
"Si uzembe ila ndani ya nyumba ile kulikuwa na yule mwandishi wa habari"
"Nani Norbert?"
"Huyo huyo alikuwa amekaa nyuma ya mlango katika muda ambao mimi nilikuwa nikiingia ndani ya nyumba hiyo ndiyo maana akaniwahi"
"Sasa wewe kweli ulikuwa unaingia ndani ya nyumba ya mtu ambaye humjui vizuri na wala hupajui palivyo kama kondoo vile"
"Nilikuwa tayari nimeshautuliza ulinzi wa nyumba uliokuwa upo chini ya mlinzi mmoja hivyo sikuwa na wasiwasi kabisaa"
"Kwahiyo ndiyo ukadhania kuwa mlinzi ndani ya nyumba hiyo yupo mmoja tu?"
"Ndiyo"
"Damn! Umefanya kosa kubwa sana ila hatuna budi kukusadia kwani kiongozi amesema utolewe mara moja" Josephine alimueleza kwa sauti ya chini sana na kisha akamtazama yule kijana ambaye alikuw akimsikiliza kwa umakini, alipopewa ishara ya kukubali kutolewa huko aliamua kupanga hila yake. Alimuambia, "Unahojiwa ukiwa upo mbele yangu kama wakili wake hivyo usiwe na hofu kil kitu nilikuwa nimekipanga kama kilivyo".
Hapo walipeana mikono wote kwa pamoja na kisha wakaeleka kwenye chumba cha mahojiano kwani walikuwa wameomba kuongea muda mfupi tu, huko walikuta maafisa ambao walikuwa wakiwasubiri ambapo mahojiano yalianza mara moja. Kutokana na kuwepo kwa Josephine wakijua kuwa alikuwa ni wakili wake mahojiano hayo yalifanyika kwa taratibu na kistarabu sana, maaskari walikuwa wakihofia kuwekwa hatiani na Wakili kwani ilikuwa ikitambulika kabisa walikuwa hawatakiwi kuwapiga watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi. Laiti wangenyanyua mkono na kumpiga basi walikuwa wakizidi kumuweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kujiteteta huko Mahakamani hata kama angekubali kuwa alikuwa akihusika kwenye tuhuma hiyo aliyokuwa amekamatwa nayo
Walihofia huyo waliyekuwa wanamuona ni wakili angeweza hata kuwageuzia kibao Mahakamani akawaambia kuwa walitumia nguvu kumlazimisha na Mteja wake alikiri kutokana na hofu aliyokuwa nayo baada ya kutumika nguvu nyingi katika kumfanya akiri. Hizo zilikuwa ni mojawapo wa hila ambazo walikuwa wakizitumia mawakili katika kumtetea Mteja wake hivyo waliogopa kabisa zisije kutumika kwao kwani zingeweza kuwaweka pabaya kwa kuvunja sheria na pia kuhariu ushahidi muhimu sana kwenye kesi pindi itakapofunguliwa.
Mahojiano yalipomalizika Mtuhumiwa alirudishwa kwenye chumba cha selo alichokuwa amehifadhiwa na kisha jalada lilifunguliwa ili asiweze kukaa ndani ya kituo hicho, ulikuwa ukisubiriwa muda mzuri wakuweza kumpeleka rumande tu wakti akiwa anaendelea na kesi yake. Muda huo Josephine aliondoka kwenye eneo hilo la kituo cha polisi kwani kazi yake iliyomleta hapo ilikuwa imeshakamilika na hakuwa na la ziada. Alikuwa amewaachia kisanga maasakari wenyewe kwa kijana huyo, jambo ambalo halikuwa limejulikana na maofisa hao wa jeshi la polisi ilikuwa ni kwamba Josephine alikuwa amemuwekeawsumu ambayo ilikuwa ikiingia ndani ya ngozi yule mwenzake. Pale waliposhikana mikono baada ya kuongea kwa pamoja ndiyo alimtilia sumu hiyo na kisha yeye mwenyewe aliingiza mkono ndani ya mkoba wake na kugusa dawa ya maji ambayo ilikuwa ni kinga kisha akaelekea kwenye mahojiano hayo.
Ulipofika muda wa kumpeleka rumande ndiyo kuliibuka kwa kizaazaa kwa Maasakri hao wakaona kuwa walikuwa na balaa lililokuwa likiwangojea, walipoenda kumtoa yule Kijana kule selo walikuwa akiwa amelala na mwili ake ukiwa umebadilika rangi kabisa na kuwa mweusi. Wote kwa pamoja walishtuka sana na walienda kutoa taarifa kwa wakubwa zao ambao nao walipatwa na mshtuko sana, waliona walikua na hatari kubwa ya kujibu kesi nyingine kwani yule waliyekuwa wanamdhania ni wakili alikuwa akioneakana kabisa alikuwa yupo makini sana na kazi yake. Hawakutaka kabisa kuugusa mwili wake na walichoamua ni kuita Askari aliyekuwa na taaluma ya udaktari waweze kumuangalia, baada ya robo saa alifika Askari huyo akiwa na nguo za kiraia ambako kutokana na ukubwa wake kicheo baadhi ya maaskari walimpa heshima yake na kisha aliingia ndani ya chumba hicho cha selo. Alipouona tu huo mwili alijikuta akiweka mkono kidevuni mwake na akaanza kukuna kidevu chake kilichokuwa hakina ndevu kutokana na kuzinyoa mara kwa mara, alipoacha kukuna aligeuza macho na kumtazama Askari ambaye alikuwa akikaribiana naye kicheo.
"Rangi hii ya ngozi ni dalili tosha ya kuwa aliuawa kwa sumu, sasa inabidi tuchunguze ili kuhakikisha hilo" Aliongea huku akivaa mipira ya mikono.
Alipomalza kuvaa mipira yake ya mikononi alivaa mpira mwingine wa kufunika pua na mdomo na kisha aliusogelea mwili ule, aliutazama ule mwili kwa umakini sana katika kila sehemu na kisha akawageuka wale maaskari ambao walikuwa wamemuita hapo.
"Nahitaji huu mwili upelekwe kwenye eneo la uchunguzi ili niufanyie utafiti kuna zaidi ya jambo, huko ndiyo tutapata majibu yote jinsi sumu hii ilivyoingia mwilini ulikuwa ni muda gani na akatokwa na uhai muda gani" Maaskari wadogo walitii kiutiifu waliposikia kauli hiyo kisha wakajongea hadi ulipo ule mwili, walivaa mipira nao kisha wakaubeba huo wili kwani gari la kuuchukua lilikuwa limeshafika tayari kuuchukua mwili huo.
****
Wale majambazi waliokuwa wakijaribu bahati yao ya kufanya uhalifu mbele ya Jama Wa Majama walijikuta wakiwa hawana ujanja tena, dereva wagari hilo ndiyo tamaa kabisa illimfanya abaki na majuto muda huo. Ama kweli tamaa mbele mauti nyuma na hii ilikuwa imejidhihidrisha kwani hayo ndiyo yalikuwa matokeo ya tamaa yake aliyokuwa ameileta kwa kumuona Mzee tu akiwa amekumbatia Mzigo wake. Muda huo alikuwa ameishaingia kwenye eneo la Pugu sasa likakata kona kwenye njia iliyokuwa ikipita karibu na kanisa la Pugu Kajiungeni, alifuata maelekezo ya Jamba ambaye alikuwa ameshika silaha mkononi mwake na kisha gari hiyo iliingia kwenye nyumba moja ya kifahari ambayo walipoisogelea tu lango lko lilifunguka mara moja. Gari hilo lilingia ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa na njia ya kuingiza magari iliyokuwa ikielekea hadi chini, walifika kenye eneo la chini ya ardhi kabisa ya nyumba hiyo na kisha aliamriwa kuegesha gari kwenye eneo ambalo kulikuwa na kijana mwenye mwili mkakamavu alikuwa amesimama akisubiria kwa hamu sana waweze kusimama. Baada ya wao kusimamisha gari tu yule kijana alifungua mlango na kuwatoa mmoja baada ya mmoja akiwa amewawekea silaha.
Jama mwenyewe alishuka kwenye mlango akiwa mzigo wake na kisha aliwavuta wale waliokuwa wamepoteza fahamu hadi nje ya gari hiyo, dereva pamoja na yule jambazi ambaye alikuwa amebakia walikuwa wakitetemeka sana kwa uoga kutokana na kumvamia mtu ambaye walikuwa hawamjui. Waliwaku wakimuona ni Mzee aliyekuwa amechoka lakini aliposhuka ndani ya gari hilo alionekana yupo imara kabisa na hakuwa na dalili ya kuwa mtu aliyechoka. Walishngaa sana na hapo wakaona kuwa walikuwa wameingia kwenye anga ambazo hazikuwa zao kabisa, wote walibaki wakimtazama Mzee yule kwa huruma sana wakitamani hata awasamehe kutokana na jambo hilo walilokuwa wakitaka kumfanyia.
"Huruma yenu mimi haiwezi kunibadilisha niwaaachie, inaonekana mchezo huu mshauzoea nyinyi sasa nataka mkitoka hapa mkawasimulie wenzenu kilichowapata kutokana na kufanya ujambazi wenu. Nyote mna nguvu za kufanya kazi nyinyi lakini hamkuona njia za kufanya kazi zaidi ya kuchukua mali zisizo zenu siyo sasa ngoja muipate dawa mmeingia pabaya hapa"Jama aliwaambiwa kisha akampa ishara yule mtu ambaye alionekana yupo chini yake kwa utiifu aliokuwa akiuonesha, wote waliingizwa kwenye chumba kimojawapo ndani ya nyumba hiyo ambayo walikuwa wamejiiingiza wenyewe kwa kuendekeza tamaa zao.
****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment