Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

MWANAHARAMU WA KISIASA - 3

 







    Simulizi : Mwanaharamu Wa Kisiasa

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Walikuwa wakiwaona Chris na Ndezi na kujaribu kuwapiga risasi lakini kitu cha ajabu risasi hazikuwa zikitoka kitu kilichowafanya kuwa na hasira sana. Bastola zile ziliingia maji hivyo kusababisha kutokufanya kazi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walibaki pale walipokuwa, walipiga maji kwa hasira, chini kulikuwa na tope jingi hata kabla hawajapiga hatua zaidi wakashtukia wakiguswa na vitu miguuni, walikuwa mamba.

    Walijitahidi kupiga mbizi kutoka majini lakini hawakuweza, wakazingirwa na mamba, walipiga kelele kuomba msaada lakini hakukuwa na mtu aliyetokea zaidi ya Chris na Ndezi ambao walisimama na kuanza kuwaangalia polisi wale jinsi walivyokuwa wakipelekwa huku na kule na mamba waliokuwa mtoni.

    “Tusepe,” alisema Ndezi.

    Hicho ndicho walichokifanya, wakaondoka mahali hapo, bado walikuwa porini na walitembea sana mpaka walipokutana na barabara kubwa ambapo hapo wakasimama na kuanza kusubiri usafiri wa kuelekea Tanga Mjini.

    Walisubiri hapo kwa dakika thelathini ndipo daladala ikatokea ambapo wakaingia ndani na kuanza kuelekea Tanga. Ndani ya gari kila mtu alikuwa akiwashangaa, walionekana kuwa wachafu mno kutokana na maji machafu ya mto waliokuwa wameuvuka.

    Kutoka hapo mpaka Tanga Mjini walichukua saa moja na nusu na kuteremka. Mioyo yao ikajisikia nafuu, wakaona kwamba hatimaye walifanikiwa kufika Tanga ambapo hakukuwa mbali sana mpaka Dar es Salaam ambapo huko ndipo kungekuwa na usalama wa maisha yao.

    Ni stori za kifo cha Bilionea Massawe ndizo zilikuwa zimetawala kipindi hicho, hakukuwa na mtu aliyejua kwamba watoto wawili walioonekana kuwa wa mitaani, mmoja alikuwa Chris ambaye alikuwa akitafutwa sana kipindi hicho.

    Walizururazurura Tanga Mjini na ilipofika usiku, wakalala katika kituo cha mabasi kwani asubuhi ya siku inayofuata walitakiwa kuondoka kuelekea Dar es Salaam na mifukoni hawakuwa na fedha za kutosha, ilibaki nauli tu.

    “Tukifika Dar si tutapata pesa?” aliuliza Ndezi.

    “Ndiyo! Kwanza tufike huko!”

    “Sawa.”

    Hivyo ndivyo walivyokubaliana, asubuhi ya siku iliyofuata wakachukua basi na kuanza kurudi Dar es Salaam. Kila mmoja aliamini kwamba huko ndipo ambapo wangepata nafuu kwani kama wangekutana na ndugu wa Chris waliamini kwamba wangepata msaada.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari hiyo iliwachukua saa sita ndipo wakafika jijini Dar es Salaam ambapo moja kwa moja wakaondoka mpaka nyumbani kwao walipokuwa wakiishi. Walipofika huko, nyumba ilikuwa kimya na mtu waliyemkuta alikuwa mlinzi ambaye mara baada ya kumuona Chris, alishtuka sana.

    “Chris!” aliita mlinzi huku akionekana kutokuamini alichokuwa amekiona.

    “Kaka…” akasema Chris, akamfuata mlinzi na kumkumbatia.

    “Nini kimetokea? Kwa nini baba alimuua mama na dada?” aliuliza mlinzi huku akimwangalia Chris kama mtu aliyekuwa akimchunguza.

    Badala ya kujibu swali hilo, Chris akaanza kulia, moyo wake ulimuuma mno kwani alijua kwamba kila mtu alijazwa uongo kwamba baba yake aliiua familia yake na yeye kujiua kitu ambacho hakikuwa kweli kabisa.

    Mlinzi akawa na kazi kubwa ya kumfariji Chris, alijua ni kwa jinsi gani aliuumiza moyo wa Chris. Ilimchukua dakika ishirini mpaka kunyamaza, hapo ndipo akamwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea nchini Matapatapa.

    “Pole sana!”

    “Nataka niende kwa anko!”

    “Anko hayupo. Amekwenda Moshi kuzika ila atarudi,” asema mlinzi.

    Sehemu hiyo haikuwa salama tena, ilikuwa ni lazima Chris aondoke kwani alihisi kwamba inawezekana Rais Labad angetuma watu kwa ajili ya kumfuata kule alipokuwa na kumuua kama alivyoua wazazi wake.

    Alichokifanya mlinzi ni kumpigia simu mjomba wake Chris aliyeitwa kwa jina la Gabriel Malamba na kumwambia kwamba Chris alifika Dar es Salaam na alikuwa naye.

    Malamba hakuamini, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kutaka kuzungumza na Chris, akapewa simu na kuisikia sauti yake. Kule Moshi hakukukalika, ndugu wakaambiana na hivyo Malamba, siku hiyohiyo kupanda ndege kwa ajili ya kurudi Dar es Salaam kuonana na mtoto huyo ambaye ndiye alikuwa kila kitu kwa wakati huo.

    Baada ya saa kadhaa, akafika Dar es Salaam ambapo moja kwa moja akaelekea nyumbani kwa Bilionea Massawe ambapo akamkuta Chris akiwa na Ndezi na kuwachukua wote wawili.

    Alipouliza kuhusu Ndezi, Chris alimwambia ukweli kwamba kijana huyo ndiye aliyekuwa amemsaidia mpaka kuwa hai kipindi hicho kwani bila hivyo hata na yeye angeuawa.

    “Ni kweli baba yako aliua?” aliuliza Malamba.

    “Hapana! Aliyeua ni Rais Labad, yeye ndiye aliyewatuma watu kwa ajili ya kutuua!” alijibu Chris huku akimwangalia mjomba wake.

    “Na kwa nini alifanya hivyo?”

    “Sijui!”

    “Na wewe ulikuwa wapi?”

    Chris hakutaka kuficha kitu, alisimulia kila kitu kilichokuwa kimetokea nchini Matapatapa, jinsi alivyonusurika kuuawa mpaka alipofika hapo Dar es Salaam.

    Ilikuwa ni simulizi ya kuhuzunisha sana, iliyomgusa na kumtoa machozi Malamba kwani hakujua ni kitu gani kilikuwa nyuma ya pazia mpaka rais huyo kuamua kuiangamiza familia hiyo bila huruma yoyote ile.

    Malamba akawachukua na kuwapeleka chumbani na kuwaonyeshea kwamba maisha yao yangeanzia mahali hapo kwanza walitakiwa kufanya kila linalowezekana taarifa zipelekwe kituo cha polisi na kuwaambia ukweli juu ya kile kilichokuwa kimetokea.

    ****

    Rais Labad alipelekewa taarifa na kuambiwa kwamba Chris hakuwa amepatikana na vijana ambao walimfuatilia yeye na mwenzake ambao walikuwa kwenye harakati za kuelekea nchini Tanzania waliliwa na mamba na hivyo kumkosa.

    Hizo zilikuwa taarifa zenye maumivu makubwa kwa rais huyo, hakuamini kama kweli vijana wake wangeweza kumkosa mtu kama Chris ambaye hakuwa na mafunzo ya kijeshi, alikuwa mtoto wa kawaida ambaye hakuwa na mafunzo yoyote yale sasa ilikuwaje mpaka polisi na vijana wake wa usalama wa taifa washindwe kumpata?

    Ilimuumiza sana moyoni mwake, siku hiyohiyo baada ya kupokea taarifa akawaita vijana wake na kuwaweka kikaoni na kutaka kuwaambia ni kitu gani alitakiwa kufanya kwani iwe isiwe ilikuwa ni lazima huyo Chris apatikane.

    “Huyu mtu asipopatikana nitakuwa kwenye matatizo. Mopasa, wapange vijana wako waende Tanzania kumtafuta. Fanyeni kila linalowezekana apatikane na auawe haraka iwezekanavyo,” alisema Rais Labad huku akiwaangalia vijana wote aliokutana nao.

    “Sawa mkuu!” aliitikia Mopasa.

    “Tena hakikisheni mnammaliza kabisa. Tukikutana tena ndani ya chumba hiki ni kushangilia tu! Mmenielewa?” aliuliza.

    “Ndiyo mkuu!”

    “Basi nendani. Mtakapokwamba kifedha, niambieni,” alisema na vijana hao kuondoka. Iwe isiwe ilikuwa ni lazima kumtafuta Chris nchini Tanzania na kumuua kama ambavyo maagizo waliyopewa yalivyosema.

    ****

    Edson akaanza kuangalia huku na kule, chumba kilikuwa shaghalabhaghala, hakukuwa na mpangilio wowote mzuri, kwa jinsi kilivyoonekana, ilitosha kabisa kuonyesha kwamba kulikuwa na tukio la mauaji lililokuwa limetokea.

    Hakujua sababu ya chumba hicho kuachwa hivyo mpaka muda huo, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alichokifanya ni kupiga picha, aliangalia vitu vyote alivyotaka kuangalia kwa ajili ya kuhakikisha kazi aliyopewa inakamilika.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikaa ndani ya chumba kile kwa dakika kumi, alipomaliza, akapanda juu ya dari na kurudi katika chumba chake huku akiwa ameuacha mlango wa dari ule alioutengeneza ili kuona kama kesho yake angerudi tena. Kazi hiyo aliimaliza na kulikuwa na kazi moja ambayo ilibaki, kujua mahali alipokuwa Chris.

    Aliambiwa kwamba alikimbia, hakujua alikimbilia wapi lakini kama angemtumia Joker, angemwambia mahali alipokuwa huyo mtoto hivyo kutaka kuzungumza naye.

    Usiku wa siku hiyo akakutana na Joker na kitu cha kwanza kabisa kumuuliza ni kuhusu huyo mtoto. Joker hakujua kitu chochote kile lakini aliamini kwamba hapo hotelini kulikuwa na watu waliofahamu kwani huo haukuwa mchezo wa mtu mmoja, kulikuwa na mnyororo mkubwa uliowaunganisha watu wengi.

    “Nitakwambia!” alijibu Joker.

    “Sawa. Nashukuru sana!”

    “Ila kwa nini unamtaka huyu dogo?” aliuliza.

    “Ni kwa sababu lazima tukimalize kizazi cha huyu mbwa, vinginevyo atatusumbua sana baadaye,” alijibu Edson huku akimwangalia Joker machoni kama ishara ya kumuaminisha kile alichokuwa akikizungumza.

    Joker hakutaka kuchelewa, aliwajua watu ambao alikuwa na uhakika kwamba walikuwa wakifahamu mambo mengi, akawafuata na kuwauliza kuhusu Chris, kila mmoja alishtuka baada ya kugundua kwamba kumbe ndani ya hoteli ile kulikuwa na mtu aliyekuja kwa ajili ya kumuua mtoto huyo.

    Hilo liliwashangaza sana, walichokifanya ni kutaka kumfahamu mtu huyo, walipokwenda kumuona, wakagundua kwamba ni yule Mnigeria, kumbe alikuja hapo kwa ajili ya kazi hiyo.

    Vijana hao hawakunyamaza, wakamuahidi Joker kwamba wangemwambia alipoelekea kumbe upande wa pili walitaka kuwasiliana na Rais Labad na kumwambia kilichokuwa kikiendelea.

    Simu ikapigwa na kumpa taarifa. Labad alishtuka, hakuamini kama kweli mpaka Wanigeria walikuwa kwenye mpango mkali wa kumuua Massawe na familia yake, na ilionyesha kabisa kwamba kama asingemuua, basi huyo Mnigeria angemuua.

    “Ni nani?”

    “Kama nilivyokwambia mkuu! Ni Mnigeria.”

    “Sawa. Sasa fanyeni kitu kimoja!”

    “Kipi mkuu!”

    “Ni kwamba Chris amekimbilia Tanzania, kuna vijana wanakwenda kumuua hukohuko, ila huyo Mnigeria muueni na mwili wake mkauzike msituni,” aliagiza Rais Labad.

    “Hakuna shida mkuu!”

    “Fanyeni hivyo haraka sana kwani vinginevyo hii siri haitokuwa siri!” alisisitiza.

    “Sawa mkuu!”

    Hayo yalikuwa maagizo ambayo walitakiwa kuyafanya, hawakutaka kumshirikisha Joker, vijana watatu waliokuwa na bastola wakajipanga kwa ajili ya kummaliza Edson ambaye hakuwa akijua kama tayari kulikuwa na watu walioagizwa kwa ajili ya kumuua.

    “Wamesemaje?”

    “Ndiyo nasubiri majibu! Nitakwambia,” alisema Joker.

    “Nashukuru sana.”

    Akarudi chumbani kwake, akatulia na kuanza kuifikiria safari yake. Katika kazi yake ya upelelezi alikumbuka maneno aliyoambiwa kwamba hakutakiwa kumuamini mtu yeyote, hata yule rafiki yake ambaye alikuwa karibu naye muda wowote ule angabadilika na kuwa mbaya wake.

    Wakati akijifikiria hayo, akakumbuka kwamba kulikuwa na umuhimu wa kurudi darini kwa ajili ya kuufunga mlango ule kwani aligundua kwamba hakukuwa na umuhimu wa kurudi kule kwa sababu Joker angempa majibu yote ya maswali aliyokuwa nayo.

    Saa 6:02 akazima taa, akapanda darini na kuanza kuelekea kule alipolikata dari na kuufanya mlango wa kuingilia ndani ya chumba kile. Alipofika, akaufunga na kuanza kurudi. Alipoukaribia mlango ule wa dari wa kuingia chumbani kwake, akasikia kitasa cha mlango wake kikianza kutekenywa.

    Akashtuka, hakujua alikuwa nani, alitaka kuteremka lakini akatulia kulekule huku akiufunga mlango wa dari, alitaka kujua ni nani alikuwa akikitekenya kitasa cha mlango wake.

    Akiwa kule, akaona mlango wake ukifunguliwa kwa kutumia ufunguo ambao alikuwa na uhakika watu hao waliupata mapokezi, wanaume watatu waliokuwa na bastola wakaingia na kuanza kuangalia huku na kule.

    “Joker amenisaliti! Atakuwa amejua kilichotokea,” alijisemea lakini hata kabla hajajua ni kitu gani alitakiwa kufanya, mara simu yake ikaanza kuita kwa sauti ya juu! Wanaume wote wakatupia macho yao kule darini alipokuwepo.

    “Yupo juu! Yupo juu!” alisema mwanaume mmoja kwa sauti kubwa.

    “Shiiiit!” alisema Edson.



    Vijana wanne wa Rais Labad wakafika jijini Dar es Salaam kwa lengo moja la kumuua Chris, hawakujua mahali alipokuwa ila waliamini kwamba kama wangekwenda nyumbani kwao basi wangeweza kupata taarifa juu ya mahali alipo kwa kipindi hicho.

    Wakaulizia mahali alipokuwa akiishi Bilionea Ma v ssawe, kupajua hakukuwa kazi kwani kila mtu alikuwa akimfahamu kutokana na fedha alizokuwa nazo, tena kwa kipindi hicho ambacho bado kila mtu alikuwa na maswali mengi kutokana na kifo chake.

    Watu hao wakaelekezwa Masaki alipokuwa akiishi na kuelekea huko, kwa msaada wa kuulizia ulizia, wakafika ambapo wakakutana na mlinzi akilinda. Waliongea kwa upole kama wachungaji, walimwambia mlinzi kwamba walisikia kuwa alifariki dunia na ni mtoto wake tu ndiye aliyekuwa amebaki.

    Mlinzi hakuonekana kuwa na hofu na watu hao, kwanza jinsi walivyovaa, suti zilimuogopesha na kuhisi kwamba watu hao walikuwa salama na hawakuwa hatari kama ambavyo angeweza kuhisi.

    Kwa kujiamini sana akaanza kuwaelekea mahali alipokuwa akiishi mjomba wake Chris ambapo huko ndipo alipokuwa huyo mtoto na hivyo kuanza kuelekea huko. Kazi kubwa ambayo walihisi kwamba wangekuwa nayo ikabadilika na kuwa nyepesi sana kama kumsukuma mlevi mlimani.

    Walipofika, hawakuwa na presha ya kuingia, walitaka kufanya mauaji ambayo yangemfanya kila mtu kuhisi kwamba ni ajali ndiyo iliyotokea, kusiwe na mtu yeyote ambaye angehisi kwamba kulikuwa na mtu aliyefanya mauaji kutokana na kipindi chenyewe kilivyo.

    “Tuwaue kwa staili gani?” aliuliza kijana mmoja.

    “Tuichome nyumba moto!”

    “Wazo zuri sana. Na kama ikiwezekana leo hiihii!” alisema jamaa mwingine.

    Hicho ndicho walichotaka kukifanya. Usiku wakawa mahali hapo huku wakiwa na madumu ya mafuta ya petroli. Kabla ya kufanya hivyo, wakataka kuuzima umeme wa nyumba hiyo ili kusiwe na mtu yeyote ambaye angegundua kama nyumba hiyo imechomwa moto, wahisi kwamba kulikuwa na shoti ya umeme.

    Wanaume wawili wakaelekea ndani ya nyumba hiyo, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuwateka, wakafanya hivyo kwa kuwanyooshea bastola walizokuwa nazo mikononi.

    Kila mmoja alishangaa, hawakujua sababu ya watu hao kuwateka na wakati hawakuwa wamefanya kitu chochote kile. Ndezi alipowaangalia watu hao na kusikiliza lafudhi yao akagundua kwamba walikuwa Wamatapatapa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wamekuja kutuua…” alisema Ndezi huku akimwangalia Chris.

    “Unawajua?”

    “Wametoka Matapatapa. Bila shaka wametumwa na rais,” alisema Ndezi.

    “Nyie nguchiro mnaongea nini? Nyamazeniiiii..” alisema mwanaume mmoja na kufanya hivyo.

    Mmoja akaelekea nje huku akiwa na kifaa cha kukatia nyaya, akapanda juu ya bati ambapo huko akakata ule waya uliokuwa ukipeleka umeme kutoka katika nguzo na kuingia ndani, hapohapo umeme ukakatika na kurudi ndani.

    Akawaambia wenzake kwamba kila kitu kilikuwa tayari hivyo wakaanza kumwaga mafuta ya petroli humo ndani.

    “Jamani kuna nini? Mbona mnataka kutuua?” aliuliza mjomba wake Chris huku akimkumbatia mke wake aliyekuwa akilia kama mtoto.

    “Shiiiiiiiiii….” alisema mwanaume mmoja na kumzaba kibao kimoja kitakatifu.

    Walipomaliza, wakatoka ndani na kuelekea nje, wakafunga milango kwa ufunguo na kuzichukua kisha kuwasha kiberiti na kuichoma moto nyumba hiyo ambapo moto ukasafiri kutoka nje na kuelekea ndani, nyumba ikaanza kuteketea, wakaanza kusikia watu wakipiga kelele, hawakutaka kubaki hapo, wakaondoka huku nyumba ikiendelea kuteketea kitu kilichowafanya watu wengi kukusanyika mahali hapo huku wakishangaa ni kitu gani kilisababisha moto huo mkubwa.

    ****

    Wote walikuwa ndani ya nyumba, mioyo yao ilijaza hofu tele kwa kuona kwamba hio ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yao. Waliwaangalia wanaume wale, hawakuonekana kuwa watu wa mchezo, waliposema kwamba walitaka kuwaua kwa kuwachoma moto, walimaanisha kwani walikuwa na vidumu vya petroli mikononi mwao.

    Japokuwa walikuwa wakiomba msamaha lakini hakukuwa na mtu aliyewaelewa, ndiyo kwanza waliwadhihaki Chris na Ndezi kwamba waliwakimbia lakini mwisho wa siku waliwakamata na walitaka kuwaua kisha kuondoka zao.

    Hawakutaka kuchelewa, kijana mmoja akamwaga maji ndani ya nyumba ile, alimwaga katika kila kona, kwenye makochi na sehemu nyingine ambazo zingekuwa rahisi kushika moto, wakachukua funguo na kisha kutoka na kuiwasha petroli ile.

    “Chris...tunakufa…” alisema Ndezi huku moto ukianza kuwaka kwa nguvu.

    Chris akaufuata mlango na kujaribu kuufungua, haukufunguka, hakuishia hapo, alikwenda mpaka jikoni, kote huko watu hao walifunga milango, hawakutaka kuwaona watu hao wakinusurika.

    Sehemu ambayo ilimjia kichwani ilikuwa moja tu, chooni ambapo huko kulikuwa na kidirisha kidogo, akawaambia wenzake kwamba walitakiwa kwenda huko na kujaribu kutoka ndani kupitia dirishani kwani bila kufanya hivyo, wangeweza kufa.

    Wakaelekea huko, kila kitu walichokuwa wakikifanya kwa wakati huio walikifanya kwa haraka sana, hawakutaka kuchelewa, walipofika, wakakiona kidirisha kidogo kilichokuwa na kioo cha aluminium tu na hivyo kupasua kioo hicho.

    “Tupiteni hapa,” alisema Chris.

    Kwa kasi ya ajabu Ndezi akaweka ndoo iliyokuwa pembeni na kupanda mpaka pale dirishani, moto ulikuwa ukija kwa kasi hivyo hakutaka kupoteza muda mahali hapo, kwa haraka sana, akarukia upande wa pili.

    “Shangazi! Ruka…” alisema Chris.

    “Siwezi!”

    “Kwa nini?”

    Chris alipomwangalia shangazi yake, akagundua kwamba asingeweza kupita katika kidirisha kile, si yeye tu bali hata mjomba wake asingeweza kupita kwa sababu walikuwa wanene sana na kidirisha kilikuwa kidogo.

    “Hapana! Siwezi kuwaacha,” alisema Chris huku akianza kulia.

    “Chris! Ruka uondoke, acha tufe,” alisema mjomba wake huku akimwangalia.

    Hakutaka kuondoka, hakutaka kuwaacha watu hao peke yao mahali hapo, alikuwa tayari kufa lakini si kuwapoteza. Baada ya kufariki kwa wazazi wake, hakuwa na ndugu wa karibu sana ambao alibaki nao zaidi ya hao wawili, ingekuwaje kama wangekufa? Angekuwa mgeni wa nani?

    “Hapana! Siwezi,” alisema Chris.

    Alimaanisha alichokuwa akikizungumza, hakutaka kuondoka mahali hapo, hakuwa radhi hata kidogo, alikuwa tayari kufa lakini si kuwaacha watu ambao walichukua nafasi kubwa katika maisha yake zaidi ya mtu yeyote yule.

    Walimbembeleza aondoke, alikataa, lakini walimbembeleza zaidi na mwisho wa siku akakubaliana nao na kuondoka kwa kupitia katika kidirisha kile ambapo akaungangana na Ndezi kisha kuondoka mahali hapo huku machozi yakimtoka.

    Kutokana na nyumba ile kuteketea kwa moto, majirani wakajazana mahali hapo, walibaki wakishangaa kilichokuwa kikiendelea, hakukuwa na nyumba iliyowahi kuteketea kwa moto katika mtaa huo, walikuwa makini kwa utumiaji wa vifaa vya umeme, sasa ilikuwaje mpaka nyumba hiyo kuteketea?

    “Imekuwaje? Au shoti ya umeme?” aliuliza jamaa mmoja huku akionekana kushangaa.

    “Hata mimi nashangaa! Vipi tena? Jamani! Kweli inaweza kuwa umeme hii?” aliuliza jamaa mwingine, kila mmoja aliyakataa mawazo yake kuonyesha kwamba kile kilichokuwa kimeiteketeza nyumba ile kilikuwa ni shoti ya umeme.

    Simu ilikuwa imekwishapigwa katika kitengo cha zimamoto ambao walifika mahali hapo wakiwa na gari lao kisha kuanza kuuzima moto huo. Haikuwa kazi ndogo, ilikuwa kubwa kwani moto ule uliteketeza vitu vingi mule ndani na mbaya zaidi, kwa jinsi ulivyokuwa mkali, watu wakaona kwamba huo haukuwa umeme, inawezekana ilikuwa petroli.

    “Huu si umeme! Hii ni petroli,” alisema jamaa mmoja huku akionekana kushangaa.

    “Kweli! Si unasikia hata harufu ya petroli!” alisema jamaa mwingine huku akiziba pua yake.

    Moto ukazimwa, kila kitu kilichokuwa ndani kilikuwa kimeteketezwa kwa moto. Watu walihuzunika, hawakuamini kama kweli umeme ndiyo ulikuwa chanzo cha moto huo mkubwa.

    Baada ya kupoa, watu wakaingia ndani ili kuona kama kulikuwa na mtu yeyote, walipokwenda chooni, wakaikuta miili ya watu wawili ikiwa imeteketezwa vibaya kwa moto.

    Kila aliyeiona, alishika kichwa, alisikitika, wakaichukua na kuipeleka nje huku baadhi ya viungo vikitoka kwa ajili ya kuungua na kulainika sana. Walipotolewa nje, kila mtu alipowaangalia, alikuwa na uhakika kwamba wale watu wawili walikuwa mjomba wake Chris na shangazi yake.

    “Kuna miili miwili tu?” alisikika jamaa mmoja akiuliza, alikuwa mmoja wa wale vijana.

    “Ndiyo!” alijibu muokoaji.

    “Hapana! Haiwezekani kuwa wawili!”

    “Kwa nini? Unajua lolote?”

    “Hapana!” jamaa huyo alijibu harakaharaka, baada ya dakika mbili, hakuonekana mahali hapo.

    Vijana wale wakachukuana na kupelekana pembeni, hawakuamini kile kilichokuwa kimetokea, waliuliza vizuri juu ya miili iliyokuwa imeteketezwa kwa moto ndani ya nyumba ile, waliambiwa kwamba ilikuwa miili miwili tu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hilo liliwachanganya, walikuwa na uhakika kwamba walipochoma nyumba kulikuwa na watu wanne ndani ya nyumba, sasa iweje miili ipatikane miwili, je Chris na Ndezi walikuwa wapi?

    “Kuna kitu! Inawezekana walijificha chini ya vitanda, halafu wakateketezwa hukohuko bila watu hawa kuwaona,” alisema jamaa mmoja.

    “Hata mimi nahisi hivyo! Haiwezekani mtu apone, hebu tusubirini mpaka mwisho,” aliongezea jamaa mwingine.

    Hawakutaka kumpa taarifa rais Labad, walitaka kuona mpaka mwisho ili wajue kwamba ni watu wangapi walikuwa wamekufa ndani ya nyumba hiyo. Walihisi kwamba idadi ingebadilika lakini kitu cha ajabu kabisa, idadi ilikuwa ileile kwamba waliokufa ndani ya nyumba ile walikuwa watu wawili tu, mtu na mkewe.

    “Wapo wapi? Kama walitoka, walitokaje?” aliuliza jamaa mmoja, alionekana kuchanganyikiwa hasa.

    Wakati wakiwa wanajiuliza, mara simu ya mmoja ikaanza kuita. Harakaharaka akaichukua na kukiangalia kioo, akashtuka, mtu aliyekuwa akipiga simu alikuwa Rais Labad ambaye alitaka kujua ni kitu gani kiliendelea huko.

    Hata kupokea alishindwa, akabaki akiiangalia simu tu.



    Rais Labad alitulia chumbani kwake, alikuwa akisubiri kusikia kitu kilichokuwa kikiendelea nchini Tanzania, mke wake alimshangaa, katika siku za karibuni alimuona mumewe akiwa kwenye hali ya tofauti sana, hakuwa na furaha kama kipindi cha nyuma, muda mwingi alikuwa na mawazo huku akionekana kuwa na kitu kilichokuwa kikimtatiza kichwani mwake.

    Hakumuuliza kwani kila alipofanya hivyo, hakupewa majibu yoyote yale. Chumbani hapo hakukukalika, akasimama na kuelekea sebuleni, napo huko akaona kabisa hakuna dalili kumpa furaha.

    Alitaka kufahamu kama Chris alikuwa amekufa au la! Kila alipotaka kuwapigia simu, alivumilia kwa kuona kwamba angepigiwa yeye, alisubiri na kusubiri mpaka ikafika kipindi akakata tamaa, akapiga yeye.

    “Wameshindwa? Wanashindwaje? Hebu niwasikie,” alisema Rais Labad, alionekana kuwa na dukuduku la kutaka kusikia ni kitu gani kilikuwa kimetokea huko.

    Simu ikaanza kuita.

    ****

    Edson hakutaka kutulia kule juu, aligundulika kama alikuwa huko hivyo alichokifanya ni kurukia ndani ya chumba kile. Ilionekana kuwa bahati kwake kwani kitendo cha kutua, hakukuwa na mtu aliyekuwa ameiandaa bunduki yake hivyo kufanikiwa kupambana nao.

    Haikuwa kazi ndogo, walikuwa watu waliokuwa na miili mikubwa, alipambana nao kwa nguvu zote, alizidiwa lakini alipokumbuka kwamba alikuwa kwenye nchi ya kigeni, akapata nguvu ya kupambana zaidi na kufanikiwa kuwapiga wote.

    Hakutaka kuchukua bunduki, alijua kwamba tayari mahali hapo hakukuwa salama kwa ajili ya maisha yake, hivyo alichokifanya ni kuondoka ndani ya chumba hicho.

    Alipofika nje, akaliona gari moja likiwa limepakiwa, akajua kwamba hilo lilikuwa gari la wale jamaa, hivyo akaanza kulisogelea, alipoufikia mlango, akagundua kwamba ndani kulikuwa na mtu.

    “Puu…puu..puu…” alikigonga kioo cha mlango, jamaa huyo aliyekuwa amelala, akamgeukia na kushusha kioo.

    Hilo lilikuwa kosa kubwa, kwani kwa nguvu sana Edson akapitisha mkono na kumshika jamaa kwenye koromeo na kuanza kumshindilia ngumi za uhakika kiasi kwamba akawa hoi na kuugulia kwa maumivu makali.

    “Sogea huko mpuuzi wewe,” alisema Edson, akamtoa jamaa kwenye usukani na kukaa yeye.

    Akandoka mahali hapo. Alipofika njiani, huku gari likiwa kwenye mwendo akaufungua mlango wa upande mwingine na kumrusha jamaa yule chini, akafunga mlango na kuendelea na safari yake.

    Lengo lake lilikuwa ni kufika Motown, hilo halikuwa tatizo kwani baada ya saa kadhaa, akafanikiwa kufika ambapo akachukua chumba na kuwapigia simu wakuu wake na kuwaambia kwamba alifanikiwa kugundua kuwa Chris alikimbia na kukimbilia nchini Tanzania, hivyo ilikuwa ni lazima wamtafute hukohuko.

    “Wewe rudi! Huyu tutamtafuta hukuhuku,” alisikika mkuu wake kwenye simu.

    “Sawa mkuu!” aliitikia. Asubuhi ya siku iliyofuata akapanda ndege kwa ajili ya kurudi nchini Tanzania.

    ****

    Movement of 40 People au M40P lilikuwa kundi kubwa la waasi nchini Matapatapa ambalo lilikuwa likiongozwa na mwanaume mwenye roho mbaya, ambaye alikuwa na uchu wa madaraka, Ibrahim Kashindi.

    Lilikuwa kundi kubwa ambalo lilianza na watu arobaini ambao maisha yao yalikuwa ni katika msitu mkubwa wa Mapupu uliokuwa nchini Matapatapa. Watu wengi walikuwa wakililalamikia kundi hilo, lilifanya mauaji ya kikatili nchini humo yakiwa na mlengo wa kumtaka rais Labad aachie madaraka kwani kwa kipindi alichokuwa ametawala, kwa miaka zaidi ya kumi, ilikuwa imetosha kabisa.

    Rais Labad hakutaka kuachia madaraka, wananchi wake walikuwa wakiuawa huku wengine wakitekwa na kuingizwa katika kundi hilo la waasi la M40P. Kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo mauaji yalivyokuwa yakiendelea kutokea nchini Matapatapa.

    Nchi nyingi duniani ziliomba Rais Labad akae chini na M40P wazungumze na kuweka makubaliano lakini rais huyo hakutaka kukubali, alichokiangalia ni maisha yake, kuingia mikataba hewa na Wazungu na kujipatia kiasi kikubwa cha fedha.

    Siku zikaendelea kukatika, Kashindi hakutaka kukubali, alichokihitaji ni kuwa rais wa nchi hiyo hivyo alichokifanya ni kuwaandaa vijana wake watatu na kuwataka kwenda mjini na kupeleleza kilichokuwa kikiendelea huko.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hilo halikuwa tatizo, vijana hao wakaondoka huku wakiwa na utambulisho wa majina yao kuwa ni 1, 2 na 3. Walipofika, wakakaa huko, walikuwa ni wataalamu wa kompyuta ambao waliweza kuingia katika simu ya rais huyo na kufuatilia mawasiliano yake yote.

    Walijua mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea, walijua kila kitu, mpaka mipango ya rais huyo ya kutaka kumuua bilionea Massawe, na kila kitu walichokuwa wakikipata waliwasiliana na Kashindi na kumwambia.

    “Kesho ndiyo mauaji yanatokea,” alisema 3 kwenye simu.

    “Nendeni kwenye hiyo hoteli,” alisema Kashindi.

    “Lakini mkuu! Ni kweli tunahitaji kufuatilia tukio hilo?” aliuliza 3.

    “Nyie nendeni, kuna kitu nitahitaji kifanyike, mtanipa kile kitakachotokea,” alisema Kashindi na kukata simu.

    Vijana hao wakaondoka Motown na kuelekea katika mbufga ya wanyama ambapo ndipo mauaji yalipotakiwa kutokea. Walipofika huko, wakachukua chumba katika hoteli ambayo bilionea Massawe angefikia na familia yake.

    Kila kitu baada ya hapo walijua kwamba kilikuwa ni mipango ya Rais Labad, familia hiyo ikauawa isipokuwa mtu mmoja, mtoto Chris ambaye alikimbilia porini.

    Wakampa taarifa Rais Labad kile kilichokuwa kimetokea kwamba mauaji yalifanyika kama yalivyopangwa ila kulikuwa na mtu mmoja alinusurika, alikuwa mtoto aliyekimbilia porini.

    “I want that kid,” (namtaka huyo mtoto) alisema Kashindi.

    Hilo halikuwa tatizo, walichokifanya ni kuendelea kufuatilia mawasiliano ya simu ya rais huyo. Waliweza kugundua kila kitu na mpaka baada ya siku mbili wakapata taarifa kwamba mtoto huyo alikuwa ameingia nchini Tanzania.

    Nao wakaelekea huko, ilikuwa ni lazima kuhakikisha mtoto huyo anapatikana kwa gharama yoyote ile. Walifanikiwa kufika mpaka Dar es Salaam, kilichokuwa kikiwaongoza ni mawasiliano ya simu ya rais huyo na vijana wake, kila hatua waliyokuwa wakifikia, walimpa taarifa ambazo ziliendelea kuwasaidia watu hao.

    Kufuatilia kwao, walifuatilia mpaka nyumba ilipoanza kuteketea, waliisimama pande tatu za nyumba hiyo, 2 alipomuona Chris na Ndezi wakikimbia, akawaita wenzake na kuwaambia mahali walipokuwa wamekimbilia watoto hao.

    Hawakutaka kuchelewa, hakukuwa na sababu ya kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kuelekea kule ambapo watoto hao walikuwa wamekimbilia.

    Waliwafuatilia, kila hatua waliyokuwa wakipiga, walikuwa wakiwaona, walikwenda mpaka kwenye barabara ya lami kwa lengo la kupanda daladala na kuelekea Ubungo kutokea Tabata walipokuwa. Wakiwa barabarani, 2 na 3 wakatokea mahali hapo na wao kukaa kituoni hapo.

    “Nyie watoto mnakwenda wapi?” aliuliza 2 huku akiwaangalia watoto hao.

    Hawakujibu swali hilo, walibaki kimya, mioyo yao ilikuwa na hofu nzito kwa kuhisi kwamba inawezekana watu hao walikuwa miongoni mwa watu wale waliokuwa wakiwatafuta, hivyo wakasogea pembeni kabisa.

    “Msiogope! Chris, hutakiwi kuogopa, tupo hapa kwa ajili ya kukusaidia,” alisema 2 huku akimwangalia Chris.

    Wakashtuka, hawakujua watu hao walikuwa wakina nani na kwa nini walikuwa wakiwafahamu namna hiyo. Chris alibaki akitetemeka, aliwaangalia watu hao, hakuwaelewa.

    “Tunaomba msituue,” alisema Chris.

    “Hatuwezi kuwaua! Ila sisi tunataka tukusaidie umuue rais Labad ambaye aliiua familia yako,” alisema 3.

    “Mmh!”

    “Tutakusaidia tu! Tufuateni!”

    Walionekana kuwa watu wema japokuwa bado vichwa vyao vilikuwa vikijiuliza sana kuhusu watu hao, hawakujua walikuwa wakina nani lakini kwa kuwa walionekana kama watu waliodhamiria kuwasaidia, wakaungana nao na kuondoka mahali hapo.

    Safari yao iliishia katika gari moja aina ya Noah walilokuwa wamelikodi, wakaingia ndani na kisha kuondoka mahali hapo. Vichwa vyao havikuacha kuwa na maswali mengi, wakati mwingine walijiona kama walijikamatisha kwa watu hao lakini wakati mwingine waliwaamini kwamba walikuwa watu wazuri ambao walikuwa na lengo la kuwasaidia.

    Gari hilo likaishia katika gesti bubu iliyokuwa Mwananyamala, wakateremka na kuingia ndani. Watu hao walijiamini, walipofika ndani, wakawaambia wakae chini na kuanza kuwaambia kila kitu kilichokuwa kimetokea, kwamba wao walikuwa wakina nani na kwa nini waliwachukua.

    “Kundi la waasi?” aliuliza Ndezi.

    “Ndiyo! Tunataka tuungane kwa ajili ya kupambana na huyu mtu anayeididimiza nchi yetu,” alisema 1 huku akiwaangalia watoto hao.

    “Sawa. Nitakuwa pamoja nayi. Au siyo Chris?”

    “Haina shida! Nitapambana kuhakikisha anatoka madarakani, na nitamuua kama alivyowaua wazazi wangu na dada yangu,” alisema Chris huku akionekana kuwa na jasira moyoni mwake.



    “Imekuwaje mmeshindwa kumuua?” aliuliza rais Labad huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Mkuu! Tuliichoma nyumba moto!”

    “Ikawaje?”

    “Wote tunaamini wamekufa, ila cha ajabu, miili ilipotolewa, miili yao hatukuiona,” alisema kijana aliyepiga simu.

    “Mtakuwa mnatania! Hebu endeleeni kusibiri zaidi,” alisema Rais Labad.

    “Sawa mkuu!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikasirika, moyo wake ulikuwa na chuki kubwa, hakuamini kile alichokisikia kwamba vijana wake hawakufanya kile walichotakiwa kufanya. Walimwambia kwamba waliichoma nyumba moto na kuwaua watu wote waliokuwa humo ndani lakini kitu cha ajabu kabisa, mwili wa Chris haukuwa umepatikana.

    Hakutulia, kichwa chake kilikuwa na mawazo lukuki, wakati mwingine alikuwa akipiga mikono yake kwa hasira kwani kwake, kazi ya kumuua Chris ilionekana kuwa nyepesi kabisa lakini kitu cha ajabu, vijana wake walishindwa kulitekeleza hilo.

    Baada ya dakika thelathini, akawapigia simu vijana wake na kuwauliza kama miili yote ilitolewa, walimwambia kwamba ileile iliyokuwa imepelekwa nje ndiyo ambayo ilipatikana kitu ambacho hata wao wenyewe walikishangaa.

    “Hebu ingieni ndani mkaangalie,” alisema Rais Labad.

    “Tushaningia mkuU! Hakuna kitu!”

    “Chini ya vitanda?”

    “Kweupe!”

    “Kwenye dari?”

    “Huko napo peupe kwani dari lote limeteketezwa kwa moto,” alijibu kijana aliyekuwa akizungumza naye.

    Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kumuona Chris, hakupata tena taarifa zake, hakujua mahali alipokuwa kijana huyo, wakati mwingine alihisi kwamba alikufa katika moto ule lakini baada ya polisi kugundua, hawakutaka kutangaza kitu chochote kile.

    Moyo wake ukaanza kuwa na amani, akajisikia kufurahia kwani hilo lingemfanya kitendo chake cha kulipiza kisasi kifikie tamati. Akatulia, kazi moja kubwa iliyokuwa mbele yake ni ile ya kuhakikisha waasi wote wa Kundi la M40P wanauawa na wale ambao wananusurika basi ni lazima wafikishwe katika mahakama na kuhukumiwa kifo.

    “Kazi iliyobaki ni moja tu, kuhakikisha naliteketeza kundi lote la M40P,” alijisemea, hiyo, kwake haikuwa kazi kubwa sana, aliiona kuwa ndogo ingawa kwa miaka mingi ilikuwa imemshinda.

    ***

    Siku mbili baadaye, Chris, Ndezi na wanaume wale watatu wakaingia ndani ya kambi hiyo. Kila mtu aliyewaona, alifurahia kwani walijua kwamba Mtanzania huyo ndiye ambaye angewapa nafasi wa kuichukua nafasi ambayo waliihangaikia kwa kipindi kirefu bila mafanikio yoyote yale.

    Kashindi aliwaamini Watanzania kwamba walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na akili, waliojua kuzungumza na pia walikuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile, alitaka kumtumia Chris kupata vitu alivyokuwa akivihitaji katika maisha yake.

    Moyo wake ukatokea kumpenda Chris na kabla hajazungumza naye kitu chochote kile akaagiza wote wawili wapewe chakula kwa ajili ya kula na kufanya mambo mengine.

    Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza kwa Chris kuwa ndani ya kambi hiyo. Hakukuwa na maisha magumu kama zilivyokuwa kambi nyingine, walijitengenezea kijiji chao japokuwa walikuwa msituni, walikula na kufanya mambo mengine, kila kitu kilichokuwa kikiendelea huko, hakukuwa na watu waliokuwa wakifahamu.

    Watoto waliendelea kutekwa na kupelekwa katika kambi hiyo na kupewa mafunzo ya kijeshi na kutumia bunduki. Walitengenezwa kisaikolojia, wakaingiziwa chuki na kumuona mbaya mtu yeyote ambaye alikuwa mbele yao.

    Haikuishia hapo bali waliendelea kuingizwa chuki na kuanza kumchukia Rais Labad, kila siku kulikuwa na picha yake iliyowekwa mbele kabisa na watoto kuambiwa kuilenga kwa risasi kwani alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakichukiwa sana katika kambi hiyo.

    Hayo yalikuwa maisha mapya kwa Chris, aliendelea kukua huko huku akiwa na Ndezi aliyeonekana kuwa na hamu kubwa ya kutumia risasi. Japokuwa kambini kulikuwa na watoto wengi lakini moyo wa Kashindi ulikuwa kwa Chris, kwake, huyo alionekana kuwa mtu ambaye angeweza kumuondoa msituni na kumpeleka ikulu.

    Aliagiza apewe mafunzo maalumu ya kijeshi, alitumia bunduki, alitega mabomu, kila alipokuwa akiamka, kitu cha kwanza kabisa kabla ya kufanya kitu chochote kile ilikuwa ni kufanya mazoezi magumu.

    Akili na mwili wake vikazidi kukua, chuki dhidi ya Rais Labad haikutoka, alimchukia na kila siku kitu alichokuwa akikihitaji ni kumuua tu.

    Siku zikakatika, miezi ikasonga mbele na mwaka wa kwanza mpaka miaka sita kukatika. Maisha yake yote tangu alipokuwa na miaka kumi na tano mpaka miaka ishirini alikuwa ndani ya kambi hiyo tu.

    Alikuwa na mwili mkubwa, kiasi kwamba ilikuwa vigumu kuamini kama alikuwa na miaka ishirini. Mwili wake ulijazia, alikuwa akifanya mazoezi kila siku kiasi kwamba akawa fiti kabisa, kila mtu aliyemwangalia, aliamini kwamba mazoezi yalimkubali.

    Baada ya kukatika miezi kadhaa, akaambiwa kwamba alikuwa akiitwa na Kashindi ambaye alikuwa na mazungumzo naye. Hilo halikuwa tatizo, akaelekea ndani ya ofisi hiyo kwa ajili ya kuzungumza naye.

    Hakujua mwanaume huyo alitaka kumwambia jambo gani, alipofika, akamkaribisha na kumwambia akae kitini. Hakuanza kuzungumza kitu chochote kile, Kashindi akachukua glasi ya maji na kuanza kunywa, akakaa kitini na kumwangalia Chris.

    “Nimekuwa baba yako kwa kipindi kirefu sana, nimekuwa nikikutunza, kukuthamini kwa sababu moja tu,” alisema Kashindi huku akimwangalia Chris.

    “Ndiyo baba!”

    “Huu ni mwanzo wa safari nyingine ndefu. Utatakiwa kuondoka mahali hapa na kuelekea nchini marekani, huko, kutakuwa na kazi moja, utakwenda kusomea ujasusi kwa ajili ya kufanikisha kitu tunachotaka ukifanye,” alisema Kashindi, kidogo Chris akashtuka.

    “Kusomea ujasusi?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo! Nimezungumza na Brian Mc Kendon, amenikubalia kufanya kazi na mimi kwa kuwa wao wenyewe wanahitaji sana niwe rais wa nchi hii! Kwa hiyo, utaondoka hapa keshokutwa na kuelekea Marekani katika FairFax katika Jiji la Virginia,” alisema Kashindi.

    “Sawa mkuu!”

    “Huko! Utaishi kwa miaka mitano, utakuwa ukirudi katika likizo, tutakuwa tukionana. Ila kumbuka kwamba sababu kubwa ya kwenda huko ni kulipiza kisasi cha kifo cha wazazi wako na mdogo wako, ila cha zaidi ni kumuondoa Labad katika nafasi aliyokuwa nayo,” alisema Kashindi.

    “Sawa mkuu! Nitapambana mpaka tufanikiwe.”

    “Ninashukuru sana. Jiandae. Keshokutwa utaanza safari!”

    “Sawa.”

    Moyo wa Chris ulifurahia, alijisikia fahari kupita kawaida, hakuamini kama kweli aliipata nafasi hiyo. Japokuwa kulikuwa na miaka mingi ilipita lakini bado moyo wake ulibeba kisasi kikubwa, kila alipokuwa akiwakumbuka wazazi wake na dada yake moyo wake ulimuuma mno.

    Ulikuwa na jeraha kubwa ambalo hakutegemea kama kuna mtu mwingine ambaye alikuwa ameumia moyo kama ilivyokuwa kwake. Usiku wa siku hiyo ulikuwa ni wa mawazo tele, alikuwa akimfikiria Rais Labad, jinsi atakavyomuua na kuuletea moyo wake furaha kubwa.

    Hakutaka kumficha Ndezi, siku hiyo alizungumza naye mengi, alimwambia kila kitu alichoambiwa na Kashindi kwamba ilikuwa ni lazima aondoke na kuelekea nchini Marekani.

    “Daah! Nitakumisi sana Chris,” alisema Ndezi, rafiki wake wa muda mrefu.

    “Nitakumis pia. Ila tukirudi, tutakwenda kuishi Motown kwa kuwa naamini Kashindi atachukua nchi,” alisema Chris.

    “Kweli kabisa. Ni lazima tupambane tumtoe yule dikteta,” alisema Ndezi na kumpa mkono Chris kwamba ilikuwa ni lazima wahakikishe rais huyo anatoka madarakani.

    Siku ya safari ilipofika, akaondoka kambini na kuelekea Motown ambapo akapanda ndege na kuanza kuelekea nchini Marekani. Alipoingia ndani ya ndege, akatulia kwenye kiti ambapo baada ya dakika kadhaa, msichana mmoja, mrembo akaelekea palepale alipokaa na kukaa naye.

    Kwa kumwangalia msichana huyo, alikuwa na sura nzuri, sura ya kitoto, mwanya huku mashavuni akiwa na vishimo viwili vilivyokuwa vikionekana kila alipokuwa akicheka au kutabasamu.

    “Karibu sana mrembo,” alimkaribisha huku akiachia tabasamu pana.

    “Nashukuru sana.”

    “Naitwa Christopher Massawe!” alisema Chris huku akimpa mkono.

    “Naitwa Sedika Labad!”

    “Mmh!”

    “Nini tena?” aliuliza Sedika huku akiachia tabasamu lililoufanya uzuri wake kuonekana maradufu.

    “Labad huyu mtoto wa rais?”

    “Shiiiiiiii…”

    “Ooh! Nashukuru kukufahamu!” alisema Chris huku naye akiachia tabasamu pana.

    “Nashukuru pia.”

    “Unaishia Marekani au njiani?”

    “Nitaishia Uingereza!”

    “Sawa,” alisema Chris na kuendelea na mazungumzo mengine. Kila alipomwangalia msichana yule, alionekana kuwa mrembo mno, ila tatizo lilikuwa moja tu, kuwa mtoto wa Rais Labad, ila pamoja na yote hayo, bado kisasi chake kiliendelea kumsumbua moyoni.

    “Nikishindwa kumuua, nitamuua hata huyu mtoto wake,” alijisemea moyoni wakati ndege ikiachia ardhi ya Motown.



    Ndani ya ndege kila mmoja alikuwa mchangamfu, Sedika ndiye aliyekuwa akiongoza kwa kuzungumza, hakutaka kumuona Chris akiwa kimya, kila wakati alimuongelesha pasipo kujua kwamba mtu huyo alikuwa adui mkubwa wa baba yake.

    Kichwa cha Chris kilikuwa na mawazo lukuki, alikuwa akifikiria ni kwa namna gani angeweza kufanya mauaji kwa msichana huyo mrembo. Ni kweli alihisi kitu cha tofauti kikiingia moyoni mwake lakini hakutaka kujali lolote lile, ilikuwa ni lazima afanye kazi aliyotaka kuifanya.

    Sedika alitamani kujua mambo mengi kuhusu mwanaume huyo, kila wakati alikuwa akimuuliza maswali ya kiundani kabisa, alitaka kujua maisha yake kabla ya kukutana naye humo ndani ya ndege, alitaka kujua mahali alipokuwa akiishi huku akihisi kwamba mwanaume huyo alikuwa tajiri au mtoto wa tajiri kwani kitendo cha kwenda Marekani, tena kupanda ndege katika daraja la biashara lilionyesha kabisa hakuwa mtu wa mchezo.

    “Wazazi wako?” aliuliza Sedika.

    “Walikufa miaka mingi iliyopita,” alijibu Chris.

    “Pole sana jamani! Huku unakwenda kufanya nini?’ aliuliza Sedika huku akimwangalia mwanaume huyo.

    “Kutembea tu!”

    “Mmh!”

    “Ndiyo hivyo! Nakwenda kutembea kisha nitarudi kuendelea na shughuli zangu,” alisema Chris huku akionekana kutokuwa na wasiwasi hata kidogo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Chris hakutaka kumwambia ukweli Sedika, alimficha kwa kila kitu. Msichana huyo alilijua hilo lakini hakutaka kumuuliza ukweli kwani alijua kwamba halikuwa jambo jema kuambiwa kila kitu ndani ya siku moja, ulihitajika ukaribu baina yao ili mwanaume huyo aweze kuwa muwazi.

    Walizungumza mambo mengi, walilala na walipoamka, ndege ilikuwa ikiingia nchini Uholanzi ambapo wakateremka, wakabadilisha ndege na kuanza kuelekea Ufaransa kabla ya kuingia nchini Uingereza.

    Walichoka, walizungumza mpaka wote kuishiwa maneno na kutulia. Baada ya saa kadhaa kutoka hapo Uholanzi wakaingia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow nchini Uingereza.

    Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa safari ya Sedika, akateremka kutoka kwenye ndege, kwa kuwa walikuwa na dakika arobaini za kupumzika, Chris akatoka na msichana huyo mpaka sehemu iliyokuwa na viti, wakabadilishana namba za simu na kisha kuagana huku kila mmoja akiwa na hamu ya mwenzake.

    Baada ya dakika kusogea sana, Chris akarudi ndani ya ndege na kuanza safari ya kuelekea nchini Marekani. Njiani, alikuwa mnyonge, upweke ulimjaa kwani msichana aliyekutana naye, alikuwa mtoto wa mbaya wake lakini moyo wake ulianza kumuingiza, mapenzi yakaanza kuchipua.

    “Haiwezekani mimi kumpenda mtoto wa adui yangu,” alijisemea, alitamani kumtoa msichana huyo kichwani mwake lakini ilishindikana kabisa.

    Baada ya saa kumi na mbili ndege ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK uliokuwa jijini New York nchini Marekani. Alichoka, akateremka kwani walitakiwa kupanda ndege nyingine ndogo ambayo ingewapeleka mpaka katika Jiji la FairFax huko Virginia.

    Baada ya dakika kadhaa, wakachukua ndege nyingine ambayo iliwapeleka mpaka katika Jiji la FairFax ambapo wakateremka katika Uwanja wa Ndege wa Dulles na kutoka ndani ya uwanja huo.

    Nje, macho yake yakatua kwa wanaume watatu waliokuwa wamevalia suti ambapo mmoja wao alishika bango lililokuwa na jina lake. Akawasogelea na kuwasalimia, wakamchukua na kuelekea ndani ya gari.

    Hakuwa mzungumzaji, alibaki akiwaangalia watu hao, walionekana kuwa wakakamavu, wenye umakini mkubwa ambapo hapo ndani tu, hawakutaka kuzungumza neno lolote lile.

    Hawakuchukua muda mrefu wakafika sehemu moja iliyokuwa na ukuta mkubwa na haikuwa rahisi kuangalia na kuliona jengo lolote lile. Geti kubwa lililoandikwa kwa maandishi makubwa yaliyosomeka CIA Training Centre yaliandikwa katika geti kubwa ambalo likafunguliwa na gari kuingia ndani.

    Alibaki akishangaa, alipoangalia, hakuona jengo lolote lile, gari liliendelea mbele mpaka baada ya dakika tano ndipo macho yake yakatua katika majengo kadhaa ambapo baada ya muda mchache, wakafika sehemu husika.

    Ilikuwa sehemu nzuri ambayo iliyavutia macho yake, pembeni, kulikuwa na sehemu mbalimbali za kufanyia mazoezi, kulikuwa na msitu wa kutengenezwa, mto, milima na mabonde, kila kitu kilichoonekana mahali hapo kilionyesha kwamba sehemu hiyo haikuwa ya masihara, hiyo ilikuwa ni sehemu ya kujifunza ukakamavu tu.

    Masomo yake yakaanza ndani ya chuo hicho, alionekana kuwa kijana mwerevu aliyejua kushika bunduki, kutegua mabomu na hata kutumia silaha nyingine.

    Watu wengi walishangaa, kwani alikuwa mwanafunzi aliyeanza masomo kipindi hicho lakini alionekana kuwa moto wa kuotea mbali, kila mmoja alimshangaa, wengi walihoji kwani hakukuwa na mwanafunzi mpya aliyekuwa akijua mambo mengi kama alivyokuwa Chris.

    Chuoni hapo akatengeneza marafiki wengi, wa kike na kiume, akawafundisha mambo mengi na hata kwenye kutumia kompyuta hakuwa mtu wa masihara, alijua kutumia kompyuta kwa kuingia katika programu mbalimbali.

    MAwasiliano yake na Sedika hayakusimama, walikuwa wakiwasiliana kwenye kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Alimwambia msichana huyo kwamba alikuwa kwenye matembezi yake nchini MArekani na asingerudi katika kipindi hicho.

    “Kwani hapa mafunzo ni kwa muda gani?” aliuliza Chris.

    “Huwa ni mwaka mmoja!”

    “Mwaka mmoja?”

    “Ndiyo! Mbona unashangaa?”

    “Niliambiwa kwamba ni miaka mitano!”

    “Hakuna! Wanaotakiwa kusomea miaka mitano ni wale ambao wanaochaguliwa kwa ajili ya kujiunga na maofisa ambao watafanya kazi ya kumlinda rais,” alisema jamaa mmoja.

    “Wanachaguliwa?”

    “Ndiyo! Ila kwa sisi wengine, ni mwaka mmoja na unakuwa umewiva kweli,” alisema jamaa huyo.

    Moyo wake ulikuwa na hamu ya kufanikiwa katika kila jambo alilokuwa akilitaka kutimia, alikuwa mtu wa kumfikiri sana Rais Labad, aliyakumbuka maisha aliyopitia, tukio lile la kuuawa kwa wazazi wake, mara kwa mara lilikuwa likijirudia kichwani mwake kama mkanda wa filamu.

    Mazoezi yalikuwa magumu, kila siku walikuwa wakiamka asubuhi kabisa na kwenda kufanya mazoezi ambayo hayakutofautiana sana na wanajeshi waliokwenda kusomea ukomandoo.

    Alikuwa hodari kufanya mazoezi na kituoni hapo alijulikana zaidi kutokana na ulengaji wake shabaha aliokuwa nao. Kila mmoja alimshangaa, japokuwa kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakipiga risasi kwa ufasaha, kwa kulenga sana lakini kwa Chris ilikuwa ni hatari kiasi kwamba watu walimtaka kuwa mdunguaji katika jeshi la Marekani.

    “Haiwezekani!” alisema alipoitwa ofisini kwa mkuu wa kituo hicho.

    “Kwa nini?”

    “Nina kazi kubwa sana ya kufanya. Ni lazima niikamilishe kwanza na ndipo nifanye mambo mengine,” alisema Chris.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mambo gani unayotaka kukamilisha?”

    “Ni mambo binafsi. Bado kuna safari ndefu mbele yangu!”

    Walimuhitaji, ilikuwa ni vigumu katika kituo kama hicho kukutana na mtu aliyekuwa na shabaha kama alivyokuwa Chris. Waliwafundisha watu wengi kituoni hapo, wadunguaji mbalimbali lakini kwa mtu huyo alionekana kuwa wa tofauti kabisa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog