Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

MWANAHARAMU WA KISIASA - 4

 







    Simulizi : Mwanaharamu Wa Kisiasa

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Umesema huyu rafiki yako anaitwa nani?” ilisikika sauti ya Rais Labad akiuliza.

    “Chris Massawe.”

    “Hebu picha yake?”

    “Hii hapa!”

    Rais Labad akaichukua picha hiyo na kuanza kuiangalia. Mtu aliyekuwa akimuona alimfahamu kabisa, alimkumbuka japokuwa kwa kipindi hicho alikuwa akionekana kukua sana.

    Akayauma meno yake kwa hasira, Sedika alibaki akishangaa, hakujua ni kitu gani kilimfanya baba yake kubadilika namna hiyo, alikunja sura na alionekana kabisa kuchanganyikiwa.

    “Ni lazima auawe,” alisema bila kujali kama mtoto wake alisikia au la.

    “Auawe?” aliuliza Sedika huku akionekana kushtuka. Rais Labad hakujibu chochote kile, haraka sana akachukua simu yake na kupiga sehemu.

    ****

    Sedika hakuelewa sababu iliyomfanya baba yake kuuliza mara mbilimbili kuhusu Chris, alihisi kulikuwa na tatizo sehemu, alitaka kufahamu ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.

    Alimuuliza baba yake mara mbilimbili, alitaka kufahamu kila kitu lakini hakumwambia zaidi ya kuwapigia simu watu wengine na kuwapa taarifa kuhusu Chris ambayee alitakiwa kuuawa haraka iwezekanavyo vinginevyo mwanaume huyo angeweza kumfanyia kitu cha hatari sana.

    Sedika hakumuuliza Chris, alibaki kimya lakini moyo wake ulikuwa na mawazo kupita kawaida, kuna kipindi aliamua kujipanga kwa ajili ya kumuuliza lakini alisita, hakutaka kumuuliza kwani alihisi kama kungekuwa na kitu kingeharibika.



    Aliendelea kuishi kwenye dukuduku lake kila siku, walipokuwa wakiwasiliana, walitumiana picha na mpaka kufikia hatua wenyewe wakapendana na kuwa wapenzi.

    Siku ziliendelea kwenda mbele kama kawaida, nchini MArekani, Chris alikuwa akichukua mazoezi kama kawaida. Alifundishwa mambo mengi, kuhusu kompyuta, kutumia silaha na kutengeneza mabomu.

    Alikuwa na uwezo mkubwa, hakuacha kuwashangaza watu wengine waliokuwa katika kituo hicho cha mafunzo. Hukohuko Marekani ndipo alipoamua kutumia muda wake mwingi katika kutumia kompyuta, kuwa na uwezo mkubwa wa kuingia katika simu za maadui zao.

    Waliweza kuingia kwenye simu za Waarabu ambao walikuwa tishio duniani kwa kipindi hicho. Walitumia muda wao mwingi, hakukuwa na mtu aliyejua kitu chochote kile, hawakujua kama simu zao zilikuwa zikiingiliwa na watu hao.

    Walikuwa na uwezo mkubwa, waliendelea kusoma, CIA ikawaamini kwa kuona kwamba watu hao wangeweza kuwasaidia kupambana na magaidi ambao kwa kipindi hicho walikuwa wakisumbua kupita kawaida.

    Chris aliendelea kukomaa, akawa mtu mwenye uwezo mkubwa, hakuacha kuwasiliana na msichana Sedika, kila siku alihakikisha anawasiliana naye kwa ujumbe au hata kwa kuzungumza kwenye simu.

    Moyo wake ulimpenda mno msichana huyo lakini kilichokuwa kikimuumiza kilikuwa ni baba yake. Hakumpenda, alimchukia na ilikuwa ni lazima amuue kama njia ya kulipa kisasi kwa kile alichokuwa amekifanya kwa wazazi wake.

    Hakumwambia Sedika kuhusu uovu wa baba yake, alifanya siri, hakujua kama tayari msichana huyo aligundua kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.

    Aliendelea na maisha yake kama kawaida, baada ya kumaliza miezi minne, msichana huyo akamwambia kwamba kulikuwa na jambo walitakiwa kulizungumza wawili.

    “Jambo gani?” aliuliza Chris.

    “Ni jambo la muhumu sana. Nakuja hukohuko!” alisema msichana huyo.

    “Huwezi kuuliza kwenye simu?”

    “Hapana! Nitakuja kuongea nawe ana kwa ana.”

    Hilo halikuwa tatizo hata mara moja lakini mwanaume huyo alionekana kuwa na mawazo lukuki, hakujua Sedika alitaka kuzungumza jambo gani pamoja naye. Alimsubiri, baada ya siku tatu, msichana huyo akafika nchini Marekani ambapo moja kwa moja wakaonana na kuanza kuzungumza.

    “Nini kinaendelea?” aliuliza Sedika.

    “Wapi?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kati yako wewe na baba!”

    “Hakuna kinachoendelea. Kwani kuna nini?” aliuliza Chris huku akionekana kutokujua kitu chochote kile.

    Sedika akaanza kumuhadithia kilichokuwa kimeendelea, jinsi baba yake alivyoonekana kuwa na hasira mno kila alipokuwa akiambiwa kuhusu Chris. Mwanaume huyo akajifanya kutokujua kitu chochote kile, akajifanya kwamba hakujua kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.

    “Chris…naomba usinifiche!”

    “Siwezi kukuficha kitu chochote kile. Wewe ni msichana wangu! Laiti kama kungekuwa na kitu ningekwambia!” alisema Chris, kwa kumwangalia machoni alionekana kusema ukweli lakini ukweli kutoka moyoni alikuwa akidanganya.

    “Sawa.”

    Sedika hakutaka kuendelea kukaa nchini MArekani, siku mbili mbele akarudi zake Matapatapa huku akionekana kuwa na mawazo tele. Moyo wake haukukubaliana na Chris, aliamini kwamba mwanaume huyo alikuwa akimdanganya kwa kile alichokuwa amemwambia, alihisi kwamba kulikuwa na kitu nyuma yake, kwani alimfahamu baba yake, alikuwa mtu mwenye hasira, aliye radhi kumuua mtu yeyote yule kuufurahisha moyo wake.

    Miezi ikakatika, ulipofika mwaka, Chris akahitimu masomo yake na kupewa medali ya kuwa mlenga shabaha mahili katika kituo hicho. HAkutaka kuendelea kubaki nchini MArekani bali alichokifanya ni kuondoka kurudi nchini Matapatapa.

    Hakukuwa na mtu aliyemzuia kwani tangu alipokuwa akifika mahali hapo, viongozi walijua alikwenda kufanya nini hivyo kumpa ruhusa na kumwambia kwamba kama kuna siku yoyote angetaka kufanya kazi nao, alikuwa akikaribishwa huko.

    Ndani ya ndege, aliwasiliana na Sedika, alimwambia kwamba alikuwa njiani kuelekea Matapatapa. Msichana huyo alikuwa na furaha tele kwani baada ya kipindi kirefu kupita, hatimaye wangekutana wote, angalau wangepata nafasi ya kulala pamoja kitu ambacho hawakuwahi kukifanya tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi.

    “Nitakuja kukupokea! Nilizungumza na baba jana na kumwambia kwamba unakuja,” alisema Sedika huku akionekana kuwa na furaha.

    “Ulizungumza na baba yako?”

    “Ndiyo!”

    “Na ukamwambia kwamba nakuja leo?”

    “Ndiyo mpenzi!”

    “Sawa. Ni vizuri kumpa taarifa. Nakupenda Sedika!”

    “Nakupenda pia!”

    Akakata simu, moyo wake ulikuwa na hofu nzito, aliiona hatari iliyokuwa mbele yake, kama kweli msichana huyo alimwambia baba yake juu ya ujio wake ilimaanisha kwamba hapo uwanja wa ndege hakukuwa sehemu salama tena.

    Alimfahamu Rais Labad, alikuwa mwanaume mwenye hasira sana ambaye alitaka kukamilisha kila kitu alichokuwa amejiwekea, kitendo cha kuambiwa kwamba alikuwa akiingia nchini hapo siku hiyo ilikuwa ni lazima awaandae vijana wake kwa ajili ya kumteka hapo uwanja wa ndege na kuondoka naye.

    “Haiwezekani! Hawawezi kuniteka,” alisema Chris wakati ndege ikiachia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi na kuelekea Matapatapa.

    ***

    Rais Labad alisubiri kwa kipindi kirefu, kitu alichokuwa akikihitaji kwa wakati huo kilikuwa ni kumuua Chris ambaye kwake alionekana kuwa mtu hatari sana. Hakutaka kumuona mwanaume huyo akiendelea kuishi.

    Katika miaka yote alipotea na kuja kumuona katika kipindi alichokuwa na miaka ishirini, hakutaka kumuacha, kama alivyowaua wazazi wake, ilikuwa ni lazima amuue pia.

    Akawaandaa vijana kwa ajili ya kufanya kazi hiyo na Chris alipokuwa akirudi, akapewa taarifa na Sedika. Msichana huyo hakuwa na nia mbaya, alimwambia baba yake kwa kuwa aliona kwamba kulikuwa na uhitaji wa mzazi wake kumuona mwanaume huyo.

    Siku hiyo ambayo Sedika alitakiwa kwenda uwanja wa ndege kumpokea menzi wake ndiyo siku ambayo baba yake aliwatuma wanaume watatu kwa ajili ya kufanya mauaji hayo.

    Hawakuwa wao peke yao, kwa kuwa hata polisi walikuwa chini yake, akawatumia kwa ajili ya kukamilisha kile kilichotakiwa kufanyi siku hiyo. Sedika hakujua chochote kile, moyo wake ulikuwa na furaha tele, kitendo cha mpenzi wake kuwa njiani na kufika mahali hapo siku hiyo kilimfurahisha kupita kawaida.

    “Ndege inatua!” alisema jamaa mmoja.

    “Yeah! Hapa ni kufanya kazi moja tu! Tumteke!” alisema jamaa mwingine.

    “Ni vizuri sana. Maofisa wa uwanja huu si wanajua kila kitu?”

    “Ndiyo! Hata polisi washaambiwa. Kama sisi tutamkosa, basi watamuua wao,” alisema jamaa mwingine.

    “Safi sana!”

    Wakati ndege inatua, Sedika alikuwa kwenye presha kubwa, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa nguvu, hakuamini kama mpenzi wake ndiye aliyekuwa akiingia mahali hapo.

    Alijisogeza karibu karibu na sehemu iliyokuwa na kioo kikubwa ghorofani kwa ajili ya kumuona mpenzi wake wakati anatua ndani ya ndege. Wakati yey akimsubiria kwa kumwangalia pale, tayari wanaume wale watatu nao wakajiandaa, bastola zilikuwa viunoni mwao, walichokitaka ni kumuua tu, hata kama wangekamatwa, kwa msaada wa Rais Labad wangetoka tena.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hakikisheni haingii garini,” alisema Rais Labad.

    “Kwa hiyo tumuue hapahapa?”

    “Ndiyo!”

    “Sawa mkuu!”



    Walikuwa wamejiandaa vilivyo, walijua tu kwamba mwanaume huyo angefika mahali hapo kwani hakukuwa na sehemu nyingine ya kupita zaidi ya hiyo hapo. Waliendelea kusubiri huku kwa mbali, pembeni karibu kabisa na dirisha wakimuona Sedika ambaye alikuwa kimya akifuatilia kila kitu.

    Muda ulikwenda, abiria wa ndege ile wakaanza kutoka na kwenda katika jumba lile, waliendelea kusubiri, dakika zilikwenda na kwenda lakini hawakufanikiwa kumuona Chris akitokea mahali hapo.

    “JAmani! Hivi ni kweli amekuja na ndege hii?” aliuliza mwanaume mmoja.

    “Ndiyo! Kwa maelezo ya baba yake amesema ni kweli alikuja na ndege hii,” alisema jamaa mwingine.

    Wakati wakiendelea kuulizana, wakamwangalia Sedika alipokuwa amesimama, mahali pale dirishani, mara wakamuona mwanamke mmoja aliyevalia baibui jeusi huku akiwa nikabu iliyoyaacha macho yake wazi.

    Akapiga hatua mpaka pale alipokuwa Sedika na kuanza kuongea. Walizungumza kwa sekunde kama ishirini, wakakaa katika viti vilivyokuwa mahali hapo na kuendelea na maongezi yao huku kila mmoja akicheka kupita kawaida.

    Walichanganyikiwa, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, dakika ziliendelea kwenda mbele lakini bado hawakuweza kumuona Chris mahali hapo kitu kilichowafanya kuchanganyikiwa.

    “Mkuu!” aliita jamaa mmoja baada ya kumpigia simu Rais Labad.

    “Ndiyo!”

    “Tunahisi hajaingia kwa ndege hii!”

    “Kwa nini?”

    “Mpaka sasa hivi bado hajaonekana!”

    “Haiwezekani Sedika anidanganye. Yeye mwenyewe yupo hapo?” aliuliza rais.

    “Ndiyo! Anaongea na shoga yake. Ila kiukweli huyo Chris hajaonekana mahali hapa,” alisema kijana aliyepiga simu.

    “Basi subiri nimpigie simu Sedika aniambie!”

    Wakaendelea kusubiri mahali hapo. Baada ya sekunde kadhaa wakamuona msichana huyo akichukua simu yake iliyokuwa ikiita na kuanza kuongea. Walijua kwamba Rais Labad ndiye aliyempigia simu binti9 huyo na kusikilizia ni kitu gani angeambiwa. Baada ya kumaliza mazungumzo naye, akawapigia.

    “Sasa sikilizeni!” alisema Rais Labad.

    “Ndiyo mkuu!”

    “Anaingia saa kumi kwa ndege ya KLM,” alisema Rais Labad.

    “Kwa hiyo?”

    “Inabidi muendelee kumsubiri, ni saa mbili tu ndiyo zimebaki,” alisema rais huyo.

    Hawakuondoka, waliendelea kumsubiri mwanaume huyo mahali hapo. Sedika hakuwa na tatizo lolote lile, alibaki mahali hapo huku akiendelea kupiga stori na rafiki yake aliyevalia Kiislamu mpaka walipomaliza na kuondoka mahali hapo.

    Walisubiri na kusubiri lakini Chris hakutokea mahali hapo, hata hiyo saa kumi inaingia, hakuonekana, saa kumi na mbili mpaka saa mbili usiku mwanaume huyo hakuonekana kitu kilichowafanya wote kuwa na wasiwasi kwamba mwanaume huyo hakufika mahali hapo hivyo kumwambia Rais Labad kile kilichokuwa kimetokea.

    “Nimezungumza na Sedika. Ameniambia kwamba ameahirisha, anaingia kesho kwani alipofika Uingereza aliamua kupumzika,” alisema Rais Labad.

    “Basi sawa. Tutafika kesho asubuhi na mapema!”

    “Haina shida. Kapumzikeni.”

    ***

    Ndege iliacha Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta na kuanza kuelekea nchini Matapatapa. Akilini mwake alikuwa akimfikiria Rais Labad tu, alijua kwamba ilikuwa ni lazima kwa mwanaume huyo kuwatuma watu uwanja wa ndege kwa ajili ya kumteka au kumuua kabisa.

    Hakumuamini Sedika, alimpenda lakini alijua ni lazima msichana huyo angemwambia baba yake kwamba alikuwa akiingia nchini Matapatapa muda ule uliopangwa, hakutaka kumzuia msichana huyo kumwambia hivyo baba yake kwa kuwa hakuwa akijua kama kulikuwa na historia ndefu iliyokuwa imejificha nyuma yao.

    Hakutaka kuona hilo likitokea, ilikuwa ni lazima aingie salama na kuondoka salama uwanjani hapo. Ndege iliendelea kukata mawingu, zailipobaki dakika hamsini kabla ya kufika Matapatapa, akapata wazo kwamba ni lazima afanye jambo kwa ajili ya kujiokoa katika mikono ya watu ambao alikuwa na uhakika kwamba walikuwa wakimsubiri.

    Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na abiria wengi ambao walipandia ndege nchini Saudi Arabia. Walikuwa wametoka kuhij Maka na walikuwa wakirudi majumbani mwao. Hapohapo akapata wazo la kuvaa baibui kubwa ili kumficha asiweze kugundulika na mtu yeyote yule.

    Akamuona mwanamke mmoja wa Kipemba akiwa amekaa pembeni kabisa, alivalia baibui kubwa huku akiwa amevaa nikabu na kuyafanya macho yake tu kuonekana, akaona kwamba mwanamke huyo angemsaidia kutoka ndani ya uwanja wa ndege salama, hivyo akamfuata na kuanza kuongea naye.

    “Samahani! Ningependa kuzungumza na wewe,” alisema Chris huku akimwangalia mwanamke huyo aliyeonekana kushangaa kidogo.

    “Usijali!”

    “Naomba unisaidie kitu kimoja,” alisema Chris.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kitu gani?”

    “Naitwa Ismail Rajabu, nimetoka kuhij Maka na nipo safarini kurudi nchini Tanzania. Nimefanya ujinga mmoja mkubwa sana,” alisema Chris huku akimwangalia mwanamke huyo kwa macho ya kujiamini.

    “Ujinga gani tena?”

    “Mke wangu aliniagiza nimpelekee baibui kama zawadi lakini shetwani alivyokuwa na nguvu, alinisahaulisha kabisa. Sasa hivi yupo uwanja wa ndege akinisubiri, nahisi kama nitaonana naye na kumwambia kwamba nilisahau kumnunulia juba kutoka Maka, atajisikia vibaya sana, na shetwani anaweza kumuingia hata unyumba akaninyima,” alisema Chris huku akiubadilisha uso wake kuwa kwenye majonzi kiasi kwamba mwanamke yule hakugundua kama alikuwa akidanganywa.

    “Pole sana baba! Ndiyo kazi ya shetwani hiyo! Sasa juba ninayo, tena mengi tu mimi mwenyewe nakwenda kuyauza Tanzania!” alijibu mwanamke huyo.

    “Nitalipia mara mbili zaidi ya gharama ya kawaida ili nimfurahishe mke wangu!” alisema Chris.

    “Sawa.”

    Biashara ikafanyika humohumo. Akachomoa dola tatu za mia moja na kumgawia mwanamke huyo ambaye akafungua kibegi chake na kutoa juba moja na nikabu, mbali na majuba mengine zaidi ya ishirini yaliyokuwa katika begi lake kubwa. Chris akashukuru sana, akachukua na kisha kurudi katika kiti chake.

    Ilikuwa ni lazima aondoke mahali hapo salama kabisa. Kazi kubwa iliyokuwa mbele yake ilikuwa ni kutoka ndani ya uwanja wa ndege. Wakati ndege ikiwa imebakiza dakika tano kabla ya kutua, abiria wakaambiwa wafunge mikanda yao, na ndiyo muda huohuo, tena kwa haraka sana akasimama na kuanza kuelekea chooni.

    “Hey! You have to sit down and fasten your belt,” (Hey! Unatakiwa kukaa chini na kufunga mkanda wako) alisema dada.

    Chris hakutaka kuelewa, akaendelea na safari yake ya kuelekea chooni huku akiwa na lile juba lililokuwa kwenye mfuko mkononi mwake. Alipofika chooni, akaufunga mlango na kutulia humo.

    Baada ya dakika tatu, ndege ikaanza kutua, alishikilia imara chooni mule mpaka ilipotua na baada ya muda akasikia abiria wakianza kutoka, hapohapo akalivaa juba lile na nikabu kisha kuanza kutoka ndani ya choo kile.

    Alibadilika kabisa, kulikuwa na abiria wachache waliokuwa wakimalizia kuteremka na yeye kuungana nao. Akatoka ndani ya ndege na kuanza kuelekea katika jengo la uwanja ule ambapo alipofika, akachukua begi lake na kisha kuangalia huku na kule, alipomuona Sedika akamfuata.

    “Samahani!” alisema huku akimshika Sedika begani, msichana huyo akageuka.

    “Bila samahani!”

    “Sedika! Unachotakia kufanya ni kutulia. Hii sehemu si salama kabisa…” alisema Chris.

    “Christopher!”

    “Shiiiiii! Kaa chini. Njoo tuzungumze kidogo kabla ya kuondoka!” alisema Chris.

    “Mbona umevaa hivyo?”

    “Unawaona watu wale kule?” alisema huku akiwaonyeshea wanaume waliokuwa wamesimama wakiangalia watu waliokuwa wakiingia ndani ya jumba hilo.

    “Ndiyo!”

    “Wapo hapa kwa ajili yangu! Tupige stori kisha tuondoke, tucheke ili wasijue kitu chochote kile,” alisema Chris.

    Hakugundulika hata kidogo, kila wanaume wale walipokuwa wakimwangalia, walihisi kwamba alikuwa rafiki yake wa kike aliyefika mahali hapo kwa ajili ya kuzungumza naye.

    Waliongea huku wakicheka na hata Rais Labad alipopiga simu, Chris alimwambia amwambie kwamba aliingia kwenye ndege nyingine hivyo angechelewa kufika, alitakiwa kusubiri mpaka saa kumi jioni ndipo ndege ya KLM ingeingia mahali hapo.

    Aliaminika, hawakukaa sana, wakaondoka huku wakiwaacha wale wanaume wakiendelea kusubiri mahali pale tena huku wakiwa na bastola tayari kwa kumuua mwanaume huyo.



    Japokuwa Rais Labad aliambiwa na binti yake kwamba Chris aliahirisha safari yake ya kuja Matapatapa lakini hakuliamini hilo, upande mmoja wa moyo wake ulikuwa na uhakika kwamba binti yake alimdanganya na kuna uwezekano kabisa kwamba Chris aliingia nchini japokuwa alimficha ukweli.

    Hakutaka kuliamini hilo, usiku huohuo akampigia simu Sedika na kumuuliza tena kuhusu Chris lakini msichana huyo aliendelea kusisitiza kwamba Chris aliahirisha safari yake na angekwenda Matapatapa siku inayofuata.

    “Una uhakika?”

    “Siwezi kukudanganya. Ila kuna nini kinaendelea kati yenu?” aliuliza msichana huyo.

    “Hakuna kitu!”

    “Haiwezekani! Kama kuna kitu niambie naweza kukusaidia!”

    “Hakuna kitu. Alikuwa rafiki yangu tu!”

    “Kwa hiyo sasa hivi si rafiki yako?”

    “Ni rafiki yangu pia,” alijibu Rais Labad.

    Kama alivyoambiwa na baba yake ndivyo alivyoambiwa na mpenzi wake pia kwamba hakukuwa na kitu chochote kilichokuwa kikiendelea kati yao.

    Sedika alichanganyikiwa, alijua kabisa kwamba kulikuwa na kitu lakini wote wawili hawakuwa radhi kulizungumzia hilo. Akaachana nalo na kuendelea na maisha yake.

    Kwa Chris, kichwa chake kilikuwa kikifikiria kisasi tu, alikumbuka vilivyo jinsi wazazi wake walivyouawa, moyo wake ulimuuma mno, aliwapenda kupita kawaida lakini mtu huyo, kwa kupitia urais aliokuwa nao akaamua kuwamaliza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakutaka kukubali, alijipanga, akaagana na Sedika na kumwambia kwamba wangeonana siku nyingine. ALichokifanya ni kwenda msituni kuonana na Ibrahim Kashindi.

    “Umerudi hatimaye!” alisema Kashindi huku akiwa haamini kama kweli Chris alikuwa amerudi kwani alisubiriwa kwa hamu kubwa kwa ajili ya kupambana na rais huyo na hatimaye kumtoa madarakani.

    “Nimekuja kwa ajili ya kufanya kazi inayonipasa kufanya,” alisema Chris.

    Walipanga mipango yao kabambe juu ya jinsi gani wangeweza kumtoa Rais Labad madarakani. Hawakuwa na hofu, kitendo cha Chris kurudi kutoka katika Kituo cha CIA nchini Marekani waliamini kwamba mwanaume huyo angeweza kufanya kitu chochote kilichotakiwa lakini lazima wafanikiwe.

    Hawakujua namna ya kumtoa mtu huyo madarakani, walijadili suala hilo kwamba ingekuwa vizuri sana kama wangevamia Motown na kisha kuiteka ikulu na kushinikiza tangazo litangazwe kwamba nchi hiyo imepinduliwa.

    “Hilo haliwezekani! Ni jambo gumu! Inatupasa tufanye jambo jepesi ambalo litamfanya kila mtu kumchukia halafu tunamtoa,” alisema Chris.

    “Tufanye nini?” aliuliza Ndezi.

    “Nimepata taarifa kwamba wiki ijayo rais atakwenda Uingereza!” alisema Chris.

    “Kufanya nini?”

    “Sijajua lakini atakwenda huko. Njia rahisi ya kumchezea mchezo ni hukohuko Uingereza,” alisema Chris.

    “kivipi?”

    “Tumeteke!”

    “Halafu?”

    “Mnitengeneze mimi kama yeye!”

    “Kivipi hapo?” aliuliza Kashindi.

    Hawakuelewa kile alichokimaanisha, Chris akatumia muda huo kuwafafanulia mchezo mzima jinsi ulivyotakiwa kuwa. Kila mmoja alifurahia kwa kuona kwamba kweli wangefanikiwa kumtoa rais huyo madarakani.

    Ulikuwa mpango kabambe ambao ungemfanya rais huyo kutoka mwenyewe madarakani. Mpango huo ukaandaliwa na kupewa jina la Mwanaharamu wa Kisiasa ambaye alitakiwa kufanya vitu ambavyo visingeweza kufanywa na mtu mwenye akili timamu. Mtu ambaye alitakiwa kufanya hayo yote alikuwa Chris.

    Mtu ambaye walitakiwa kuzungumza naye alikuwa Xin Chong, mwanamke mtu mzima aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kumtengeneza mtu na kuwa vyovyote vile alivyotaka.

    Xin ndiye aliyekuwa akiwatengenezea watu sura za bandia na kuwatengeneza katika muonekano waliotaka kuwa nao. Mwanamke huyo alihitajika na hivyo kuanza kuitafuta namba yake.

    Kuipata halikuwa jambo gumu, walipoipata wakampigia na kumwambia kwamba walitaka kukutana naye jijini London kwa kuwa kulikuwa na kazi kubwa ya kufanya.

    “Nitoke Beijing mpaka London?”

    “Ndiyo! Tunaomba tuonane huko. Tunataka kufanya na wewe kazi,” alisema Chris.

    “Kazi ipi?”

    “Kama unayoifanya!”

    “Haina shida. Andaa dola elfu kumi.”

    “Ila si sura tu, mpaka umbo!”

    “Basi andaa dola laki moja.”

    “Haina shida.”

    Chris akawaambia kuhusu kile mwanamke huyo alichokuwa akikihitaji. Hilo halikuwa tatizo, kundi hilo la waasi lilikuwa likiongozwa na Wazungu ambao miaka yote walitaka kuona Rais Labad akiondoka madarakani.

    Kiasi hicho cha fedha kikatumwa katika akaunti ya mwanamke huyo na Chris na wenzake watatu kutakiwa kujiandaa kwani walitakiwa kufika nchini Uingereza hata kabla rais huyo hajafika huko.

    ****

    Rais Labad aliitawala Matapatapa alivyotaka, hakukuwa na upenod mioyoni mwa wananchi dhidi yake, watu walimchukia kwa kuwa tu hakuwa mtu aliyewajali wengine, katika maisha yake aliwajali sana viongozi wa chama chake kuliko hata wananchi wake.

    Kila mtu alimchukia, hakupendwa, nchi ilikuwa masikini sana, kwa wale waliokuwa matajiri walijikuta wakiwa na kesi mbalimbali zilizotafuna pesa zaodo na kuona kabisa kwamba walikuwa wakienda kuanguka.

    Kila kitu kilibadilika, kipindi cha nyuma kila mmoja alimuona kuwa mtu mwema, aliyependa watu lakini baada ya kuingia madarakani, kila kitu kilibadilika na watu kuanza kumchukia.

    Kila kona, wananchi walikuwa wakilalamika, nchi ilikuwa na utajiri mkubwa lakini ndiyo ilikuwa nchi masikini kuliko zote katika Ukanda wa Afrika Mashariki ukiachana na Tanzania ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa ikikua kwa kasi.

    Wazungu waliingia na kutoka, walichukua mchanga wa dhahabu, walichukua kila kitu walichokuwa wakikihitaji na hakukuwa na mtu yeyote aliyewazuia kutokana na mikataba mirefu waliyokuwa wameiingia na serikali ya nchi hiyo.

    Shuleni hakukuwa na walimu wa kutosha, vitabu havikutosha lakini hakukuwa na mtu aliyejali, kwa kipindi hicho kila mmoja aliliangalia tumbo lake na familia yake.

    Viongozi hasa mawazili hawakufanya kile kilichotakiwa kufanywa, kwa kuwa rais aliliangalia zaidi tumbo lake, hata nao pia waliyaangalia matumbo yao, hawakuwa tayari kuona wakiwatumikia wananchi kwa asilimia mia moja, walifanya walichokitaka na kila siku kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwakandamiza wananchi wasifanye kile kinachotakiwa kufanywa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kazi yake kubwa ilikuwa ni kusafiri kuelekea nchi za Ulaya kwa ajili ya kufanya mambo yake na katika kipindi hicho alitakiwa kwenda kuonana na waziri mkuu wa Uingereza, Bwana O’Brain kwa ajili ya kuzungumza naye namna ya kuuendeleza urafiki mkubwa waliokuwa nao.

    Hakujua kama huko alikuwa akisubiriwa na mbaya wake, hakujua kwamba kulikuwa na watu waliojipanga kwa ajili yake. Huku nyuma aliwaambia vijana wake kwamba wafanye kila linalowezekana kumtafuta Chris, hakujua kama mtu huyohuyo alikuwa akimsubiri nchini Uingereza.

    Akaagana na familia yake na kuelekea nchini Uingereza, ndani ya ndege, kichwa chake kilimuuma mno, hakuamini kama kweli alimkosa Chris ambaye kwake alikuwa mtu muhimu kupatikana kuliko mtu yeyote yule.

    “Nitampata tu! Hata akijificha wapi! Nitampata tu!” alisema huku macho yake yakiangalia mawingu



    Xin-Chong, mwanamke kutoka nchini China alikuwa tayari kufanya kazi aliyokuwa amepewa. Alikuwa mwanamke hatari aliyekuwa na uwezo wa kutengeneza sura za bandia na hata muonekano wa mwili.

    Aliifanyia kazi serikali ya China, alikuwa msumbufu, aliyezisumbua nchi nyingine pasipo kumfahamu. Huyo ndiye aliyesababisha Hong Kong kujitenga na kuwa nchi huru baada ya kutengeneza sura ya bandia na kumpa mwanaume ambaye alisimama imara kuutetea Mji wa Hong Kong na mwisho wa siku kuwa nchi.

    Alipopewa taarifa kwamba alitakiwa kuonana na Chris nchini Uingereza, hakutaka kubaki nchini China, malipo aliyokuwa amepewa yalikuwa makubwa na kwake lilikuwa jambo gumu sana kuachana na dili hilo kubwa.

    Alichukuliwa chumba katika Hoteli ya Queen Elizabeth ambayo haikuwa mbali kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow, jijini London nchini humo na ndiyo hoteli ambayo Rais Labad aliwekewa oda ya kufikia hapo. Alipofika, akachukua chumba ambacho aliambiwa kukaa na kuambiwa kwamba mgeni wake angefika hotelini hapo siku inayofuata.

    Upande wa pili, Chris na wenzake waliondoka nchini Matapatapa. Ilikuwa vigumu kuwagundua kwa kuwatazama, walivalia kanzu ndefu na kujifanya kama watu waliokuwa wakienda kuhij maka nchini Saudi Arabia.

    Wakafanikiwa kupata ndege na kuanza kuelekea nchini Uingereza ambapo baada ya kufika Dubai, wakateremka, wakabadilisha ndege na kuanza kuelekea Uingereza.

    Walikuwa na uhakika kwamba kazi ingefanyika kwa haraka sana, ilikuwa ni lazima kukamilisha mchakato wa kumteka Rais Labad na kufanya kile walichotaka kukifanya.

    Walichukua saa kadhaa mpaka kufika nchini Uingereza ambapo wakateremka na kuelekea katika Hoteli ya Queen Elizabeth ambapo waliahidiana na Xin-Chong kuonana huko.

    Walipofika, wakachukua vyumba na kutulia humo ambapo baada ya saa moja wakaonana katika chumba kimoja kwa ajili ya kupanga jinsi ya kuonana na mwanamke huyo kutoka China.

    Ndani ya nusu saa tayari walikuwa na mwanamke huyo ndani ya chumba chao, wakaanza kuzungumza namna ya kumtengeneza Chris kuwa na muonekano wa kufanana na Rais Labad, ili kila mtu ambaye angemwangalia, basi asiwe na hofu kwamba mtu huyo ndiye alikuwa rais wa nchi hiyo.

    Wakampa picha za Rais Labad, mwanamke huyo akaziangalia, aliangalia jinsi rais huyo alivyokuwa, muonekano wake kimwili na hata sura yake. Haikuonekana kuwa kazi ngumu, kwake, kumbadilisha mtu na kuwa na muonekano huyo ulikuwa kazi nyepesi mo hivyo akawaambia mahitaji ya vifaa alivyotakiwa kuwa navyo.

    “Hakuna shida. Tutavitafuta na ndani ya dakika kadhaa tutakuwa navyo!” alisema Chris.

    Ilikuwa ni lazima kukamilisha kila kitu ndani ya muda mfupi, wakatoka na kwenda kutafuta vifaa vyote ambavyo vilihitajika, wala hakukuwa na tatizo lolote lile, ndani ya saa mbili, kila kitu wakawa nacho.

    Hakukuwa na sehemu nyingine ya kuifanya kazi hiyo zaidi ya hotelini humu. Wakampa vifaa vyote na mwanamke huyo kuanza kumtengeneza Chris kuwa na muonekano wa rais huyo.

    Hakuwa mnene, hivyo hakukuwa na tatizo lolote lile, alimuwekea ndevu za bandia, akamfanyia make up kubwa na kuanza kuutafuta muonekano wa rais huyo.

    Haikuwa kazi ndogo, ilikuwa kazi kubwa iliyochukua saa kumi, alimtengeneza na kumbadilisha kadiri alivyotakiwa kuwa, alipomaliza na kuumwangalia, alipoonekana bado, alimtibua na kumtengeneza tena kwa kufuata zile picha alizokuwa akionyeshewa.

    Zilipotumia saa kumi, Chris alikamilika, alikuwa na muonekano kama wa Rais Labad na ilikuwa vigumu kumwangalia na kugundua kwamba mtu huyo hakuwa rais huyo.

    “Hapo safi! Hebu kajiangalie kwenye kioo,” alisema jamaa mmoja na Chris kufanya hivyo.

    Yeye mwenyewe hakuamini, alijiangalia vizuri, muonekano wake, haukuwa wake tena, ni kama Rais Labad alisimama mbele yake na kuanza kuangaliana. Walifanana kwa kila kitu, kuanzia kipara kichwani, ndefu nyingi, chunusi za usoni na kila kitu, muonekano wake wote ulikuwa ni kama Rais Labad.

    “Hapa safi! Kazi imekamilika!” alisema Chris na kuanza kujipiga picha kisha kumtumia Kashindi ambaye hata yeye mwenyewe alipozipokea, alishangaa.

    “Ni wewe huyu?”

    “Ndiyo! Unaonaje Mchina alivyoifanya kazi kwa umakini?” aliuliza Chris.

    “Hakika huwezi kujua!” alisema Kashindi, alifurahishwa na kazi nzuri iliyofanyika.

    ****

    Ndege ikatua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow hapo London nchini Uingereza. Waziri mkuu wa nchi hiyo, Bwana Raphael Gordon na mkewe walikuwa uwanjani hapo kwa ajili ya kumpokea Rais Labad ambaye alikuwa na ziara ya siku mbili nchini humo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipoteremka, kitu cha kwanza ni kupewa heshima zote alizostahili kisha kuingia ndani ya gari na kuanza kuelekea katika Hoteli ya Queen Elizabeth ambayo haikuwa mbali sana kutoka uwanjani hapo.

    Walipofika, akaingia ndani ya hoteli hiyo na kupumzika. Hakujua kama tayari kulikuwa na mtu mwingine ndani ya hoteli hiyo aliyekuwa na muonekano kama wake. Alilala hotelini huku akisubiri asubuhi ya siku inayofuata ambapo angetakiwa kuelekea katika ofisi ya waziri mkuu, Bwana Gordon na kuzungumza naye kuhusu mambo ya kitaifa.

    Japokuwa alikuwa nchini Uingereza lakini kichwa chake hakikuacha kumfikiria Chris, alikiumiza kichwa chake na muda wote alikosa raha, akakosa amani kabisa kiasi kwamba wakati mwingine alitamani sana arudi Matapatapa kwa ajili ya kumalizana na mwanaume huyo.

    Alikaa mpaka pale alipolala kabisa. Ilipofika majira ya saa tisa usiku, akashtukia mlango ukifunguliwa na mwanaume mmoja kuingia ndani. Mara ya kwanza alihisi kwamba alikuwa mlinzi wake lakini baada ya mwanaume huyo kuwasha taa, akapigwa na mshtuko, hakuamini kile alichokuwa akikiona, mwanaume aliyesimama mbele yake hakujua kama alikuwa yeye mwenyewe au la.

    “Mungu wangu!” alijikuta akisema kwa mshtuko mkubwa.

    Mwanaume yule ambaye alionekana kuwa kama pacha wake akamsogelea pale alipokuwa, alipomfikia, akamuonyeshea bastola na kumtaka anyamaze.

    “Nyamazaaaaa…” alisema mwanaume huyo, cha kushangaza, hata sauti ilifanana na yake. Akapigwa na mshtuko zaidi, alichohisi ni kama alivamiwa na jini.

    ****

    Chris na wenzake walikuwa chumbani, usiku huo ilikuwa ni kupanga ni kwa namna gani wangeweza kufanikiwa kile walichokuwa wakikitaka. Tayari aliandaliwa, alikuwa na sura ya bandia iliyokuwa na muonekano wa Rais Labad, mbali na sura yake, hata muonekano na urefu alilingana naye kitu kilichowapa uhakika kwamba wangefanikiwa kwa kile walichopanga kukifanya mahali hapo.

    Kulikuwa na kazi moja tu ambayo ndiyo ilikuwa imebaki, kuingia katika chumba alichokuwa rais huyo. Hakukuwa na urahisi wa kuingia humo kwa sababu katika korido, kulikuwa na walinzi wawili waliokuwa wakilinda kwa zamu na wenzao ambao muda huo walikuwa wamelala.

    Ilikuwa ni lazima kuwaondoa walinzi mahali hapo, hawakujua ni kwa namna gani wangeweza kuwaondoa ila alichokifanya Chris ni kuchukua laptop yake kwa ajili ya kufanya kazi fulani.

    “Unataka kufanya nini?” aliuliza jamaa mmoja.

    “Kuingia katika simu ya Rais Labad. Ni lazima nifanye jambo moja kubwa,” alisema Chris.

    Kila mmoja akatulia, walimwamini mwanaume huyo, alikuwa mtu hatari, aliyesomea mambo ya kompyuta alipokuwa akisomea ujasusi nchini MArekani. Hilo, kwake halikuwa gumu, ndani ya dakika chache tu akafanikiwa kuingia katika simu hiyo.

    Kitu cha kwanza kabisa akaanza kupitia simu zote zilizokuwa zimepigwa na kuingia. Alipofika hapo, akaanza kuangalia simu za walinzi, alipozipata, akampigia mmoja.

    “Ndiyo mkuu!”

    “Ni usiku sana! Kuna msichana anakuja, anaitwa Amanda Kitula,” alisema Chris.

    “Ndiyo mkuu! Huyu muigizaji?”

    “Ndiyo! Sasa amefika mapokezi, anakuja huku. Ni msichana aliyejaa aibu sana, hatakiwi kumkuta mtu hapo nje, tafuteni sehemu mkae kwa muda mpaka atakapoingia,” alisema Chris.

    “Lakini mheshim…” alisema jamaa, kabla hayamaliza, akaingilia.

    “Ilikuwa ni kama ombi ila sasa hivi ni amri! Mnatakiwa kuondoka na kurudi ndani ya dakika tano. Mnataka nimkose kisa nyie? Huyu si kama Upendo, huyu si kama Amina, si kama Gladness, huyu ni Amanda, binti mwenye pozi asiyependa skendo,” alisema Chris.

    Vijana hao hawakutaka kuondoka lakini kwa kuwa waliambiwa kwamba ni amri, hawakuwa na jinsi, wakaambiana na kisha kuondoka mahali hapo.

    Chris na wenzake walikuwa makini, wakachungulia kwenye korido, wakawaona vijana hao wakiondoka zao kuelekea mapokezi. Wakati wakiwa wameondoka, Chris akatoka chumbani mule na kuelekea katika chumba alichokuwa Rais Labad. Akaingia ndani.

    “Wewe ni nani? Mzimu?” aliuliza rais huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Nimekwambia nyamaza.”

    Akamchukua na kisha kumpeleka chooni, huko akamfunga mikono kwa nyuma na kumfunga kamba na kumziba mdomo. Muda wote huyo rais huyo alikuwa akishangaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.

    Mtu yule aliyekuwa ameingia chumbani alimshangaza kupita kawaida, hakuelewa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea kwani kwa jinsi alivyokuwa, alifanana naye kwa kiasi kikubwa sana mpaka kuogopa.

    Kule chooni hakuweza kupiga kelele, mdomo wake ulizibwa kwa kitambaa, hakuweza kusogeza kiungo chake chochote kile kwa kuwa alikuwa amefungwa kamba mikono na miguu yake.

    Chris akaelekea kitandani na kutulia. Moyo wake ukafarijika kwani aliamini kwamba kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angegundua kwamba hakuwa Rais LAbad.

    Alikaa chumbani humo mpaka ilipofika asubuhi ambapo akaoga, akachukua simu ya Rais Labad kwa lengo la kuitumia. Asubuhi hiyohiyo akapigiwa simu na kuambiwa kwamba ulikuwa muda sahihi wa yeye kutoka na kwenda kuonana na waziri mkuu wa nchi hiyo kwa ajili ya kupanga mipango yao.

    Hilo halikuwa tatizo, hata walinzi walipomuona akitoka ndani ya chumba kile, hawakuhisi kitu chochote kile, alionekana kuwa Rais Labad na kila mmoja aliamini kwamba alikuwa yeye.

    Akatoka mpaka nje ya hoteli ile, walinzi walikuwa wamemzunguka, gari likaletwa, akaingia na kuondoka mahali hapo huku akitoa maagizo kwamba hakutakiwa kuingia mtu yeyote ndani ya chumba chake.

    “Mwanaharamu wa Kisiasa,” alijikuta akijisemea wakati gari likielekea katika Hoteli ya Momentum Palace Hill iliyokuwa hapohapo London.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hawakutumia muda mrefu wakafika huko. Waandishi wa habari walikuwa wengi mahali hapo, siku hiyo ilikuwa ni siku ya kuweka mkataba baina ya serikali mbili kuingia makubaliano ya kufanya biashara ya kubadilishana baadhi ya vitu.

    Aliyeanza kuzungumza alikuwa waziri mkuu wa Uingereza, Bwana O’Brain. Alimkaribisha Rais Labad pasipo kugundua kwamba huyo hakuwa mtu aliyekwenda kumpokea siku iliyopita. Alizungumza kwa dakika tano, alipomaliza, Chris mwenye muonekano wa rais Labad akasimama.

    “Ninashukuru sana! Nilitaka kuzungumza kitu kimoja tu kwamba hatuwezi kusaini mkataba wa kufanya biashara. Matapatapa ni nchi yangu! Huu mkataba hautufai, hatuwezi kuingia mkataba na wakoloni ambao walitunyanyasa na kututesa sana,” alisema Chris.

    Watu wote waliokuwa mahali hapo wakashtuka, hawakujua ni kitu gani kilimkumba rais huyo. Alitoka nchini Matapatapa mpaka Uingereza huku akiwa anajua kabisa kwamba ni kitu gani alikuwa akienda kuzungumza na rais huyo.

    Siku iliyopita, walikubaliana uwanja wa ndege lakini ghafla tu alibadilika na kukataa kusaini mkataba wa kufanya biashara na nchi hiyo, mkataba ambao ungeineemesha nchi yake.

    Minong’ono ikaanza kusikika mahali hapo, Chris hakujali, huku akionekana kutokupendezwa kuwa mahali hapo, akawaambia walinzi wake kwamba ni lazima waondoke kurudi nyumbani kwani kule hakukuwa sehemu sahihi ya kukaa kwa siku hiyo.

    Simu ikapigwa mpaka kwa rubani na kuambiwa aandae ndege waliyokuja nayo, alishangaa lakini hakuwa na jinsi. Chris hakutaka kurudi hotelini, aliwaambia kwamba alitakiwa kuunganisha kurudi nchini Matapatapa, sehemu ambayo aliamini kwamba Mungu aliiumba kwa ajili yake.

    Ndani ya ndege alikuwa kimya, moyo wake ulifurahi mno, huo ndiyo ulikuwa mpango wake, alitaka kuharibu kila kitu, watu wote duniani wamchukie Rais Labad, wamuone kuwa si kitu chochote kile.

    “Mkuu.” aliita msaidizi wake.

    “Unasemaje?”

    “Nini kinaendelea?”

    “Hakuna kitu! Wazungu hawawezi kutunyanyasa halafu leo tuingie kwenye makubaliano,” alisema Chris.

    “Lakini si ulikubaliana nao?”

    “Si tatizo! Makubaliano yanaweza kuvunjika pia.”

    Watu walishangaa, tukio hilo liliporushwa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, kila mmoja alibaki akimshangaa rais huyo. Halikuwa jambo la kawaida kwa rais yeyote wa Afrika kukataa kusaini mkataba kama ule na serikali ya Uingereza, yeye hakujali, alitaka kuharibu kila kitu na ndiyo maana aliamua kufanya jambo hilo.

    Mijadala ikawa kila kona, na hata alipofika nchini Matapatapa, wananchi walitaka kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea kichwani mwa rais huyo.

    Waliamini kwamba kusainiana mkataba na kuingia katika biashara ya mabadilishano ingekuwa nafuu kwao, kusingekuwa na maisha mabovu tena, waliamini kwamba wangepata dawa hospitalini, wangepata ajira na hata miundombinu ingetengenezwa lakini kitu kilichowauam zaidi ni kwamba Rais Labad alikataa kusaini mkataba.

    “Imekuwaje tena? Inamaana rais anafurahia hali tuliyokuwa nayo? Dunia inatuonaje sasa hivi? Kweli kwa ajili ya ujinga wake hata maisha bora hatupati tena?” alihoji jamaa mmoja, kwa kumwangalia tu ingekuwa rahisi kugundua kwamba jamaa alikuwa na hasira sana.

    Hakukuwa na mtu aliyejali, Chris alitaka kuharibu kila kitu, alitaka rais huyo aonekane mbaya, achukiwe na kila mtu, alichokifanya baada ya kuingia Tanzania ni kuwataarifu wananchi kwamba alitaka kuitengeneza Matapatapa mpya, aligundua kwamba kulikuwa na mambo mengi maovu yaliyokuwa yakiendelea, na kwa kuanzia tu, alitaka kuhakikisha madaktari na walimu kukatwa mishahara yao kwani kiasi walichokuwa wakilipwa kilikuwa kikubwa mno.

    “Amesemaje?”

    “Eti sisi walimu na madaktari tukatwe mishahara, na tupokee nusu,” alijibu jamaa mmoja.

    “Ndivyo alivyosema?”

    “Ndiyo! Hebu tusubiri! Tutamsikia kesho!”



    Usiku mzima mwanamke wa Kichina, Xi-Chong alikuwa akihangaika kutengeneza sura nyingine ya bandia kwa ajili ya kumvisha Rais Labad ili waweze kutoka naye ndani ya hoteli ile.

    Kazi ilikuwa kubwa lakini haikuwa na ukubwa sana kama ilivyokuwa ile kazi aliyofanyiwa Chris. Alitulia, aliifanya kazi kwa umakini mkubwa na baada ya saa kadhaa akafanikiwa kuikamilisha.

    Ilikuwa ni sura ya mwanaume mzee aliyekuwa na ndevu nyingi ambaye kwa kuiangalia tu, ilionekana dhahiri kuwa sura ya mtu aliyekuwa na maumivu makali, mgonjwa aliyetakiwa kuwa hospitali muda huo.

    Walipomaliza, wakati Chris amepiga simu na kuwaambia kwamba alikuwa akiondoka kuelekea Matapatapa kwa hiyo ilikuwa ni lazima kufanya jambo kwa Rais Labad ambaye alikuwa ndani ya choo cha chumba alichokuwa amechukua.

    Hilo halikuwa tatizo, wanaume wawili wakatoka ndani ya chumba kile huku wakiwa na sura ile waliyopewa na Xi kisha kuelekea chumbani mule. Hawakuwa na tatizo kwenye kuufungua mlango na kuingia ndani. Moja kwa moja wakaelekea chooni ambapo wakamkuta Rais Labad akiwa chini huku amefungwa kamba mikono na miguu yake na mdomoni akiwa amewekwa gundi ya plastiki.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Safi sana,” alisema jamaa mmoja na hapohapo kuichukua sura ile na kumvalisha usoni.

    Wakaondoka naye ndani ya chumba kile na kwenda kwenye chumba chao, kule, wakamchoma sindano ya uchovu ambayo ingemfanya kuhisi uchovu mwingi mwilini mwake na dawa ilipoanza kufanya kazi, wakapiga simu mapokezi na kuhitaji msaada wa dharura kwa ajili ya gari la kumpeleka hospitali.

    Ndani ya dakika moja tu, tayari wanaume wawili waliokuwa na makoti yaliyochorwa msalaba mwekundu kufika katika ghorofa hiyo na kumchukua Rais Labad na kumteremsha chini.

    Vijana wale hawakutaka kuwaacha peke yao, nao wakaungana nao ambapo walipofika chini akaingizwa ndani ya gari la wagonjwa na safari ya kuelekea hospitalini kuanza.

    ****

    Kila mtu alishangaa kile kilichotokea, hakukuwa na mtu aliyeamini kama Rais Labad angeamua kuwakata mishahara walimu na madaktari. Waliufahamu uwezo wake mdogo wa kuongoza lakini hilo halikuwapelekea kuhisi kwamba kuna siku rais huyo angeamua kufanya uamuzi kama huo.

    ZIlionekana kuwa kama tetesi hivi kwenye mitandao ya kijamii na kutoka kwa watu wengine mbalimbali lakini baada ya kuwaita waandishi wa habari ikulu na kuwaambia kwamba kile walichokisikia ndicho kilikuwa chenyewe, kila mmoja akashtuka.

    “Ninapunguza mishahara hiyo kwa asilimia hamsini kwani nilichogundua ni kwamba hakuna wagonjwa wengi hapa nchini na hata shuleni kuna walimu wa kutosha ambao wapo radhi kufanya kazi kwa mishahara ambayo imepangwa, asiyetaka basi anaweza kuacha kazi,” alisema Chris huku kila mmoja akijua kwamba huyo alikuwa Rais Labad.

    Hiyo ndiyo ilikuwa habari iliyotikisa kila kona, hakukuwa na mtu aliyeamini kama rais huyo angeweza kufanya kitu kama hicho. Lawama nyingi za wananchi zikahamia kwa washauri wa rais kwa kuamini kwamba rais huyo hakuwa akifanya uamuzi wowote ule pasipo kushauriwa na watu wake lakini cha ajabu kabisa washauri wakasema kwamba walijaribu kumshauri lakini rais huyo hakushaurika hata kidogo.

    Nchini Matapatapa, kila kona watu walikuwa wakilalamika, kile kilichokuwa kimetokea kilimsikitisha kila mmoja. Madaktari, walimu wakakosa nguvu ya kufanya kazi, badala ya kupewa motisha kwa ajili ya kufanya kazi kwa bidii ndiyo kwanza rais huyo aliamua kuwaambia ukweli kwamba hawakuwa na kazi kubwa hivyo mishahara yao ilitakiwa kukatwa.

    Huo ulikuwa mwanzo wa kuiharibu nchi hiyo, hakuishia hapo, alitaka kuhakikisha kwamba kila mtu anamchukia. Hakutaka kulala na mke wa rais huyo, alikataa na aliamua kupanga katika hoteli kubwa ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano ya Princess na kukaa huko.

    Mkewe alishangaa, katika miaka yote ambayo aliishi na mume wake hakuwahi kuona kitu kama hicho. Alihisi kulikuwa na kitu, alikuwa na uhakika kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kwa mumewe huyo kwani maamuzi aliyokuwa akiyafanya yalikuwa ya kushangaza kupita kawaida.

    “Nahisi kuna tatizo,” Bi Linda alimwambia binti yake, Sedika.

    “Tatizo gani?”

    “Kwa baba yako! Tangu atoke Uingereza, hajalala nyumbani hapa na amekuwa si mtu wa kuzungumza nami kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma,” alisema Bi Linda huku akionekana kuwa na unyonge usio wa kawaida.

    “Yaani hakuwahi kulala nyumbani?”

    “Ndiyo!”

    “Haiwezekani!” alisema Sedika.

    Alichokifanya msichana huyo ni kumpigia simu baba yake kwa lengo la kutaka kujua ukweli juu ya kile kilichokuwa kikiendelea. Kitendo cha Chris kuona simu ya Sedika ikiita kwenye simu yake, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa nguvu, hakujua binti huyo angemwambia nini, alimuomba Mungu asijichanganye na kusahau kwamba yeye hakuwa Chris bali ni Rais Labad.

    “Kuna tatizo gani baba?” aliuliza Sedika.

    “Hakuna tatizo binti yangu,” alijibu Chris.

    “Nimezungumza na mama, ameniambia kwamba hujalala ndani tangu urudi kutoka Uingereza!” alisema Sedika.

    “Ni kweli!”

    “Kwa nini sasa?”

    “Nimeamua binti yangu! Nimelala na mama yako kwa zaidi ya miaka ishirini na tano, yaani kutokulala naye kwa siku mbili tu ndiyo achukie?” alisema Chris na kujifanya kushangaa.

    “Baba!”

    “Sedika!”

    “Hukuwahi kuniita jina langu! Imekuwaje leo? Kuna nini baba?” aliuliza Sedika, kidogo Chris akashtuka, hakujua jina ambalo Rais Labad alipenda kulitumia kumuita binti yake.

    “Jina gani?”

    “Yaani hujui? Yaani umesahau?”

    “Sedika binti yangu!”

    “Baba!”

    “Sedika kipenzi changu!”

    “Ndiyo umelikumbuka sasa hivi! Kwa nini unatufanyia hivi baba? Kwa nini lakini?” aliuliza msichana huyo.

    “Naomba unisamehe kipenzi changu! Naomba unipe nafasi moja tu ya kuufurahisha moyo wako,” alisema Chris.

    “Nafasi gani?”

    “Nitahakikisha naandaa harusi kubwa na ya gharama sana kati yako na Chris,” alisema Rais Labad.

    “Kweli baba?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niamini! Anza kuwasiliana naye, pangeni mipango harusi yenu iwe vipi,” alisema Chris.

    “Nashukuru baba! Nashukuru! Nakupenda sana.”

    “Nakupenda pia!” akakata simu na kushusha pumzi ndefu.

    ***

    Moyo wa Sedika ulikuwa na furaha tele, hakuamini kama baba yake alikubaliana naye kuoana na Chris, mwanaume pekee aliyetokea kumpenda kupita kawaida.

    Hakutaka kutulia, ilikuwa ni lazima kuwasiliana na mwanaume huyo na kumwambia kuhusu uamuzi alioufanya baba yake. Akampigia simu lakini simu haikuwa ikipatikana. Moyoni akawa na mshawasha mkubwa wa kuongea naye, hakupiga mara moja, alipiga zaidi ya mara saba na majibu yalikuwa yaleyale kwamba simu haikuwa ikipatikana.

    Moyoni akanyong’onyea, akakosa raha na kila alipokaa, akili yake ilikuwa ikimfikiria mpenzi wake, Chris ambaye mpaka muda huo hakujua mahali alipokuwa japokuwa alikuwa na uhakika kwamba alikuwa hapohapo Matapatapa.

    “Na kwake sipafahamu! Mungu wangu! Hivi ninaishi vipi na huyu mwanaume?” alijiuliza.

    Wakati hayo yakiendelea, bado nchi ya Matapatapa ilikuwa na sintofahamu, maamuzi aliyokuwa akiyafanya mtu waliyehisi ni rais wao, Labad yaliwachanganya mno. Walimu na madaktari wakaamua kuweka mikakati ya kuandama kwani hawakutaka kushuhudia mishahara yao ikikatwa pasipo sababu yoyote ya msingi.

    Wakaanza kuambiana mitaani kwamba ilikuwa ni lazima waandamane, wakajikusanya, wakapigiana simu na kuambiana kwamba kama wangefanya maandamano, Rais Labad angeachana na wazo lake la kutaka kuwakata mishahara yao.

    Hilo likafanyika kwa haraka sana, japokuwa kila mtu alilalamika ikiwemo watu wa nchi jirani lakini hakujali, kile alichokuwa amekipanga ndicho ambacho kilitakiwa kufanywa. Ilikuwa ni maumivu kwa walimu na madaktari, wengi wakataka kuacha kazi kwani kilichokuwa kimetokea kiliwaumiza.

    Walilalamika sana na mwisho wa siku kupanga kukutana kwa ajili ya kupanga mikakati ya kugoma kama tu rais asingebadili msimamo wake. Wakazungumza na uongozi, wakaandika barua kwamba endapo rais angeendelea na msimamo wake basi kungekuwa na mgomo wa madakari na walimu nchi nzima.

    “Eti mtagoma! Hivi mnanijua mnanisikia!” alisema Chris kwa muonekano wa Rais Labad, tena alikuwa akiyazungumza hayo mbele ya waandishi wa habari.

    “Kwa hiyoo tuwaambie nini?”

    “Waambieni kwamba yeyote atakayeandamana, jeshi langu halitokuwa na msalie mtume, ni kuvunjana na kuuana kama kawaida,” alisema Rais Labad na kumfanya kila mtu kushangaa.

    Alionekana kumaanisha alichokizungumza, hakutaka kuwapa nafasi watu waandamane, ilikuwa ni lazima kuhakikisha kila mmoja anamchukia rais huyo kwa kile alichokuwa amepanga kukifanya.

    Kitu cha kwanza kabisa, viongozi wa walimu na madaktari wakakamatwa kimyakimya. Mipango waliyokuwa wakiipanga ikavurugika na kwa makusudi Chris akawatuma watu kusambaza tetesi kwamba yeye ndiye aliyetuma watu wawateke viongozi hao kwa makusudi yake.

    Wananchi walipolisikia hilo, hasira kali zikaingia mioyoni mwao, walimchukia zaidi Rais Labad na kumuona kuwa mtu mwenye roho mbaya. Mwenyewe hakutaka kujali, siku ya bunge, akaingia bungeni na kutangaza kwamba anafanya mabadiliko ya kumtoa waziri mkuu na kumuweka mke wake.

    “Anasemaje huyu?” aliuliza jamaa mmoja.

    “Eti anamtoa uwaziri mkuu Misenju na kumuweka mkewe, jamani! Hii ni kweli au tetesi?” aliuliza jamaa mmoja huku akionekana kushangaa.

    “Ni kweli kabisa. Yaani huyu rais sasa hivi kawa wa hovyo sana,” alisema jamaa mmoja.

    “Siyo sasa hivi! Huyu hajawahi kuwa rais mzuri hata siku moja,” aliongezea jamaa mwingine.

    Hicho ndicho alichokifanya, siku iliyofuata akawaita waandishi wa habari na kuwaambia kwamba uamuzi aliokuwa ameuweka bungeni ndiyo ambao ulitakiwa kujulikana kwamba kuanzia kipindi hicho waziri mkuu wa nchi hiyo alikuwa mke wake na si Mzee Misenju ambaye alionekana kuwa kipenzi cha watu wengi.

    Nchi ikapoteza muelekeo, kila mmoja alibaki akimshangaa, wale waliomzoea, walijua kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wa utawala wake na alitaka kuvuruga kila kitu na kukimbia zake. Hakuacha kufanya mambo ya aibu, akajiingiza katika mitandao ya ajabu, alikuwa mmoja wa wanachama katika mtandao wa Porn Videos kwa ajili ya kuangalia filamu za ngono pasipo gharama zozote zile.

    Gazeti la Udaku la Udakuzi ndiyo lililokuwa la kwanza kuzinyaka taarifa hizo, wakawasiliana na msemaji wa ikulu na kuthibitisha kwamba ni kweli Rais Bokasa aliamua kufanya hivyo kwa kuwa alikuwa mwanaume.

    Majibu hayo yalishangaza, wengi hawakuamini kama rais huyo alimtuma msemaje wa ikulu kutoa majibu hayo, alipoona kwamba haaminiki, akahitaji kuzungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya kulizungumzia jambo hilo.

    “Ni kweli! Hakuna uongo. Halafu jamani! Hivi mimi kujiingiza kwenye mitandao hiyo kuna la ajabu? Si ndiyo naonekana kwamba mwanaume rijali! Hivi mnajisikiaje kama mngesikia rais wenu ni shoga?” aliuliza Chris aliyekuwa na muonekano wa Rais Labad.

    “Lakini mheshimiwa!”

    “Hakuna cha lakini! Nimeamua kuingia kwenye mtandao huo. Urais ni cheo tu ila tabia na mambo mengine yatabaki palepale. Kesho nitahitaji mikopo yote ya vyuo isimame kwa muda usiohesabika. Nchi haina fedha!” alisema Chris na kisha kuondoka mahali hapo.

    “Sikumsikia vizuri! Hivi amesema kusimamishwa kwa mikopo au nimesikia vibaya?” aliuliza mwandishi mmoja.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hujasikia vibaya! Amesema hivyohivyo!”

    “Mmh! Basi kazi tunayo! Ila ninavyowajua wanafunzi! Kesho utasikia kitanuka!” alisema mwandishi mmoja.

    “Wataweza?”

    “Wewe subiri! Yetu macho!”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog