Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

KOMBORA KIOTANI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : BONIFACE BIRAGE


    *********************************************************************************


    Simulizi : Kombora Kiotani
    Sehemu Ya Kwanza (1)
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Uwanja ulipambwa kwa tabasamu za wana nchiMagwaride kadhaa yameshapita kutoa heshma zao kwa mkuu wan chi aliyekuwa jukwaa kuu.Mavazi yaliyovaliwa hapa asilimia kubwa yalikuwa yakizalendo hasa kwa rangi zilizopo kwenye bendera ya taifa.Uzalendo ulitukuka baina ya taifa hili linalokumbuka siku ya uhuru wa taifa lao kutoka kwa wakoloni waliowatawala.Kiuhalisi taifa limeshapiga hatua kutoka kwa mkoloni.Kuimarika kiafya,elimu,ulinzi na mengine mengi.Lilikuwa taifa imara na linaendelea kuimarika japo kwa mapungufu kadhaa wa kadhaa.
        Jeshi la taifa la KIOTA kwa sasa katika sherehe za uhuru lilikuwa linafanya mazoezi kuonesha wana nchi wake uimara na ukakamavu wa jeshi.Pia walikuwa wakimuhakikishia mkuu wan chi ulinzi uliotukuka.Vyama mbalimbali vya siasa vilikuwepo katika sherehe hii pamoja na viongozi wa kitaifa.Vilevile kulikuwa na mialiko ya mataifa ya kadhaa japo wengi wao walituma udhuru na kuleta wawakilishi wao katika uwanja wa taifa.Ulinzi ulikuwa umeimarishwa katika jiji kuu la nchi ambapo taifa lilikuwa linashuhudia maadhimisho haya.
       Rais Kisusi akiwa ameketi meza kuu,pembeni yake alikuwepo mkuu wa majeshi upande mmoja na upande mwingine alifuata naibu rais wake na viongozi wengine.Waliteta na mkuu wa majeshi.
      “Kinachofuata ni nini jeneral maana leo sijisikii vizuri sijui kwanini?”aliuliza rais Kisusi.
    “Ni mwite daktari?”aliuliza jenerali Tindikali.
    “Hapana aliniambia sina tatizo.”alijibu rais Kisusi.
    “Itakuwa msongo wa mawazo mkuu.Usijali nchi ipo salama.”
         “Na wasiwasi na uchaguzi ujao.Lakini sio kwa hilo ni kwamba roho inanienda mbio sana.”
    “Kivipi mkuu?”
           Walikuwa maswaiba wakuu tangu shuleni tofauti ni majukumu ya kazi lakini wote ni wazalendo wazawa wa taifa la Kiota walioamua kuitumikia nchi yao.
    “Au ni vile majirani zako hawajaja?”
          “Hapana Tindikali.”
    “Au tuhairishe shughuli?’”
         “No!Leo ni dhifa muhimu sana sidhani kama kuna haja ya mimi kuondoka ghafla.Ngoja niimalize then tutaondoka.Unajua file namba 13.14 linanitatiza sana kiasi nakosa Amani.”alisema rais Kisusi ambapo alipitisha kitambaa kufuta kijasho kilichokuwa kina msumbua.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Lina ufumbuzi hakuna kidudu mtu atakayesumbua.”Alijibu jenerali Tindikali.Waligutushwa na mshereheshaji aliyekuwa akielezea makundi mbalimbali ya ulinzi yaliyokuwa yanafanya mazoezi.
       “Halafu Mkuu kinachofuata ni Maonesho ya ndege mpya za kijeshi tulizo tengeneza.”
    Rais alipitisha ulimi kwenye papi za midomo yake nakuachia tabasamu hafifu.Akaangalia juu kusubiri maonesho ya ndege.
      “Ndege inaendeshwa na Kapteni Pilipili ya kwanza kabisa kufanya onesho lake.Inatoka makao ya Msanda.Mh RAIS unasikia sauti ikizizima uwanja mzima.Haya ni mafanikio chini ya utawala wako.Ni ndege yetu wenyewe MI fighter Jet ian uwezo wa kwenda kilomita mia tatu kwa saa.Ina beba makombora kwa kumshambulia adui.Kwa heshma mh rais Kaptein…”MC alikuwa anahutubia.
       Kaptein Pilipili akiwa angani kuelekea uwanja wa taifa kuonesha ndege mbele ya rais wao.Alianza kuhisi mikono mkimtetemeka.Makao yakuongozea ndege yalikuwa yakiwasiliana naye kumpa maelekezo ya kipi cha kufanya.Lakini ghafla alipoingia kwenye anga la uwanja aliekeza ndege moja kwa moja kwenye meza kuu walimoketi Rais na watu wake.Halafu akabonyeza kitufe cha kuachia kombora lakini hakubonyeza la kuruhusu kombora kutoka bali mlango wa kombora ulibaki wazi.Na kwa kasi atakayoenda nayo mpaka kufika kwenye jukwaa halitakuwa limeanguka kutoka kwenye eneo lakuhifadhi bali kama ndege ikiwaka moto au kulipuka bila shaka kombora lingelipuka.Kasi yake ilikuwa ya sekunde.
       “Mh Rais kaptein Pilipili ndo….”hata kabla hajamaliza tayari ndege ilipigiza kwa kasi kwenye jukwaa.Kishindo kizito kilikuwa kimejiri.Lakini wakati wa butwaa lile likiendelea kuna mlipuko mwingine ulitokea pale uwanjani!Mlipuko mzito.Moto ulipanda juu na moshi mzito kufuka.Kilio kilikuwa kimesikika kikubwa sana tena cha kuogofya kiasi watu walishtuka ambao hawakupatwa na mlipuko ule.Vikosi vya kijeshi vilivyokuwa pale uwanjani nakubahatika kukoswa na mlipuko ule vili taharuki kwa harka maana mshtuko uliotokea ni waaina yake.Vyombo vya habari kadhaa vilipoteza mawasiliano hasa kamera zilizokuwa karibu jukwaaani.Lakini kwa kamera zilizo mbali kidogo hazikupatwa na kadhaia hiyo.Mambo yote yalionekana mubashara kwenye vyombo vya habari.Taharuki iliyokuwepo katika taifa haikuwa na maeleoz!Nchi ya Kiota ilikuwa taabani.Na kwa haraka tu ilikuwa vigumu kujua ni wangapi walikuwa wamekumbwa na kadhia hii!Ilichukua muda kwa vyombo vya habari kuanza kutangaza kinachotokea uwanjani.Waliopo studio waliona kama ni sinema wana tazama lakini ukweli ni kwamba balaa kubwa lilikuwa limetokea.
         Wakati simu zikipigwa maeneo mbalimbali huku vyombo vya ulinzi vikijitahidi kujua ni ktiu ganoi kimetokea hadi ndege ilyokuwa ikirushwa kwa maonesho ikapoteza mwelekeo nakuanguka jukwaa alimokuwamo Rais Kisusi.Jukwaa ambalo serikali nzima ilikuwemo!Ilikuwa maapema mno kubashiri tukio hili ambalo bichi sana!Nchi ya Kiota ilikuwa imesimama hakuna kilichosonga.Waliokuwa karibu na maeneo yale nje ya uwanja walianza kutimua ovyoo.Waliopo ndani walianza kutoka nje msongamano ambao ulisababisha purukushani hadi watu kubanwa chini nawengine kupoteza fahamu.
       Taharuki!Taharuki kuu!
    Taifa limetetemeshwa!Kiota imeanguka chini kwa kishindo!
                                                                         ****
        Makao makuu ya jeshi!TRIANGLE
         Meza kuu yahali ya hatari ilikaliwa na viongozi wa kijeshi waliokuwa wamebaki kambini.Kulikuwa taharuki.Hakuna kilichotulia kila mmoja aliongea lake.Simu ikipigwa huku na kule.
       “Nimesema tuna tuna tangaza hali ya hatari nakuipeleka kwa kiwango cha DEFCON 3.”alisema kanali Rama.
    “Hapana huna mamlaka yakupandisha hiyo amri.DEFCON 3 nikubwa sana wewe huoni ni mwenzetu ndokaangusha ndege.”alijibiwa na Major Kanda.
      “Major huu siwakati wa mzaa Kiota imepigwa hatucheki na mtu vilevile nataka kujua ikulu nani anachukua napia nijue nani anajua hali ya rais na serikali nzima.Tukisubiri mambo yaendee kijinga tutapoteza nchi!Tuamue hapa hapa kufungulia vikosi vya kijeshi kuingia mtaani.Hivi.”
        “wewe ni nani katika nchi uamuru upuuzi huuo!”
    “Huna mamlaka hana mamlaka!”
        “Pumbavu hujui lolote nimekufundisha kazi mimi.”
        Kila mtu alikuwa na wasiwasi na hasira.Hakuna aliyejua ni uamuzi gani wakuchukua kwa wakati huo.Ilihitajika busara na amani ya hali ya juu.Nchi ilikuwa imetikiswa kwa pigo kubwa kuliko yote pona ya watu ilikuwa na wakati mgumu usio na maelezo yakuridhisha.Hali ilikuwa tete.Hakuna aliyemuamini mwingine.Mfumo mzima wa utawala uliingia dosari ya ajabu.Utamwamini nani?Aliyetekeleza mauaji ni nani?Kwa dhamira gani?Na mpango upi?Ni ajali?Lilikuwa swali lililoshibisha meza nzima ya eneo lile.
       “Jamani hebu tutulie natuwe na uvumilivu wa hali ya juu.Nchi nzima inahitaji amani.”alisema moja ya wazee wa jeshi aliye na umri mkubwa.Ni mstaafu lakini mtu mwenye busara alishashinda medani kadhaa kwa juhudi zake jeshini pamoja na ushirikiano mbalimbali alioutoa jeshini.Vyeo Alisha vipata.Pamoja na mambo mengine,alikuwa mzalendo kwa taifa lake huru.Alilipenda.Alilijali nakulithamini kama kwa uzalendo uliotukuka.Mwili wake wenye ngozi iliyozeeka,sharubu zenye uzito halafu nyeupe pamoja na pua yenye mchongo ilimpa sura ya busara.Utuuzima dawa.
     “Ni sawa nchi imepigwa pigo kuu.Hii ni ajali mbaya…”kabla hajamaliza alivamiwa kwa kauli zenye utata.
    “Sio ajali!”
    “Wewe mzee unazeeka vibaya utaitaje tukio hili ajali?Unaona kuna ushawishiwi wa ajali hapo?”
     “Huu ni uvamizi tumepigwa na adui zetu.Haiwezekani rubani wa jeshi ambaye ni mwanajeshi aangushe ndege mahali alipo mkuu wa majeshi na amiri jeshi mkuu ambaye ni rais?Hii ni dharau kubwa sana na haivumiliki kamwe!Lile eneo lilikuwa na umma mkubwa.Kulikuwa na mazoezi ya kutosha yaliyofanyika kabla ya leo.Rubani alijua fika anachopaswa kusema sasa iweje adondoshe ndege hapo?”
      Mzee Gwamaka alivuta pumzi ndefu na kuzishusha kwa muda akiangalia hali ya hewa kwa ujumla.Alifikiria kidogo kitu gani cha kufanya.Alizitafuta busara zake zilizojificha ndani ya mvi zake.Akapitisha ulimi kwenye baraza la mdomo wake kasha akasema,”Najua tukio lililotokea ni zito.Tena ni kubwa sana.Sio tukio la kawaida.Ni la hatari.Tumepata pigo!Kulalamika sio suluhu.Muhimu tumuombe Mungu atupe ujasiri.Hili sio jambo la mzaa kabisa.Ni jambo lenye huzuni isiyo na mipaka.Kupigwa tumepigwa kweli.Ila sio kwamba ni lazima tuanguke chini kwa pigo hili.”
      Wakamsikiliza,wengine walishayaacha makoti yao purazai.


      “Ni kweli serikali nzima imetikiswa hatujui nani kapona nani kafa?Bado ni maapema mno.Pamoja na umaapema wote huu hatuna budi kujipanga nakuwa tayari kukabiliana na lolote litakalo tokea.Tuchunguze kwanza,tujue ni nini halafu hali ya dharura itangazwe.Kila sekta iliyopo pale jukwaani ilikuwa na wawakilishi wake.Wengi wao wakiwa ni viongozi wa sekta hizo.Bila kuficha kuna sekta nyingi zenye pengo hivi tunavyozungumza.Zinahitaji wasimamizi wapya ili nchi iendelee.Inaweza kuwa siyo ajali bali ni kundi la kivamizi kwa lengo lakuiadabisha serikali yetu tukufu.Ndiposa natoa tamko kwamba tufuate protokali.Uchunguzi ufanyike wa haraka sana ila tuwe na bodi maalum yakufanya uchunguzi huu pamoja na shghuli za uokoaji.


    Chumba cha dharura kilifuka moshi wa wasiwasi.Hakuna aliyejua aanzie wapi.Mzee Gwamaka alikuwa akitoa maneno yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Lazima tujue serikali kuu inaendeshwa na nani.Kama rais hayupo hai lazima nchi iwe na kiongozi wa mpito mpaka hapo mambo yatakapokuwa shwari.”
      Ni kama walipitisha maazimio yakufuata wakati wakitaka kujua nchi inasimama upande gani kwa muda.Kwa kweli siku ya ujio wa shari ni vigumu kujua kitu gani chakufanza.Njia kuu huwa matatani na usijue ni wapi hapo uanzie.
       “Sasa tukisimamia kijeshi jambo hili itaonekana ni mapinduzi hivyo bodi maalum ya sheria itashugulika kuangalia kiprotokali ni nani wakuchukua madaraka.”alieleza mzee Gwamaka.
    “Nina swali mzee wangu.Hivi mpaka sasa tukiangalia vizuri ni kitengo gani kitumike kufanya uchunguzi huu?”




      “KIS,Kiota Intelligence Service,hawa watatupa jibu kwa haraka.”
    “Lakiini kwa nini tusiactivate Destruction Control Unit?”aliuliza Meja Kanda.
      “Ndiyo hao DCU wataweza kazi mara moja.Huwa ni kitengo cha siri sana ambacho kiliundwa chini ya amri ya rais mwaka 1969.Kitengo hiki hakijulikani kwa wengi isipokuwa ikitokea hali mbaya kwa taifa.Hiki hakiendani na vitengo vyovyote vya kiusalama.Huwa kimetengwa na hutumika tu endapo kuna usaliti katika taifa.Ila nani anaweza kukipa amri ya kuingia kazini?”alijibu kaptein Utumbo.
      “Kinaweza pokea amri kutoka kwa rais kama yupo.Ila rais anaweza kuamrisha DCU 1,lakini DCU 2 rais hana mamlaka kikatiba kukipa amri.Chenyewe huingia kazini ikiwa hakuna serikali nzima.Hufanya uchunguzi maana ni chombo huru.Na huwa tayari baada ya nusu saa wakati imejulikana serikali hakuna.”alieleza mzee Gwamaka.
    “Tangu tukio litokee imepita muda gani?”


                                                 ****
    BLACK ZONE 2
      Kengele ilikuwa imelia kutoa tahadhara kwa watu waliokuwa wakifanya kazi kwenye eneo hili la siri.Lilikuwa jengo lililojengwa chini ya ardhi.Askari wake wote walikuwa tayari wamejiandaa kwa kazi.Wamekusanyika nakujipanga mstari wakisubiri maagizo.
       “DCU tumekutana hapa.Nadhani mpaka sasa mmejua kuitwa kwenu kuna hali ya hatari.Kilichotokea mmekisikia nakukiona kwenye vyombo vya habari.Kwa upekuzi wetu wa ghafla tumeweka nukta kwamba tukio hili linaweza kuwa limejiri kupitia mianya tofauti.Tumeshapewa taarifa na mashushu wetu waliopo uwanjani na jinsi hali ya tukio ilivyo.Hatujaridhika kabisa na wanaotaka kutikisa taifa letu.Tuliundwa kikatiba na nijukumu letu DCU 2 KUWA ACTIVE endapo tutakuwa na uhakika kwamba hakuna rais.Lengo letu nikuweka mambo sawa.Kusimamia uchunguzi,kusimamisha serikali mpya.Kwa sasa kiongozi wetu anaelekea ikulu kusimamia ni nani anapewa urais.Timu nyingine itasimamia uchunguzi wa pale uwanjani kwa mapana zaidi.Naomba tuwe macho nakuleta ukombozi kwenye taifa letu tukufu tulilopewa na Mungu.DCU 2 inaposimama ina maana vitengo vingine vya kiusalama havipewi mwanya mkubwa wa uchunguzi sisi tutaenda mbali kujua ni nani muhusika.Tutakuwa kama gesi ya gabon monoxide hakuna wakujua tumefikia uchunguzi gani?”
     Watu wa pale walimsikiliza huyu msemaji kwa makini.Kilikuwa kitengo cha siri na hujulikana na wachache na huwa hakiruhusiwi kuingiliwa na taasisi yoyote bali chenyewe huweza kuingia popote.DCU 2 hakikuwa chini ya rais hivyo chenyewe kilikuwa na mamlaka ya upekee.Maelezo ya kushiba yalitolewa kwa hadhira ile.Baada ya muda wahusika waliandamana kuchukua nafasi zao kwa minajili yakuirudisha Kiota katika usawa.Siku huru ilikuwa taabani.Taarifa zilianza kukusanywa kupitia vitengo mbalimbali kujua ni nini kimetokea na kipi wanatarajia kitokee.Vilio vilivyo tanda katika taifa hilo vilikuwa kama moshi wa volcano.
     Nchi imetikiswa.Kujipanga ilihitajika sana.Matukio kama haya yalikuwa yakutisha na kuogofya nakulipeleka taifa kwenye hali ya kutetemesha.
                                       ***
       Mamia ya waokoaji walikuwa uwanja wa taifa.Macho yalikuwa jukwaa kuu.Vifusi vikitolewa pamoja na miili kuokotwa.Zilikuwa maiti zimepandiana nakufinya wengi.Wapo waliokatika mikono wapo waliopasuliwa vichwa.Asilimia kubwa ya miili ilichomwa na moto wa mlipuko.Zilikuwa maiti zilizo tisha na kuogofya kwa sana.Ilihitaji moyo.Taifa zima liliamishia macho eneo lile.Kulikuwa na mvutano wa hali ya juu.
      Maiti zilitolewa nakuwekwa kwenye mifuko yakuhifadhia.Kikosi cha DCU 2 kilikuwa kazini wao walikuwa wakikagua idadi ya viongozi waliopoteza maisha yao.Orodha ilikuwa ina jaa kwa haraka.Kwa kuwa ni watu waliojipanga na wakala waliopitia mafunzo waliifanya kazi ile kitaalamu.Takbribani sekta zote muhimu zilikuwa zimepoteza viongozi wao.Orodha ilizidi kusheheni majina pamoja na picha za waliowatoka ndani ya lisaa limoja walipata uhakika wakile walichokiogopa kuliko vyote.
      “Confirm! Confirm Eagle Sky is down!”huyo alikuwa ni wakala wa DCU 2 akitanabaisha upatikanaji wa Eagle Sky.Habari zikaanza kusambaa kila eneo kuhusiana na taarifa hiyo muhimu.Wakala wa DCU 2 wakaanza kuandaa taarifa nakuzipitisha kwa waliosalimika katika sekta zote za siri na wazi za taifa ili umma uandaliwe kisaikolojia kuhusiana na jambo zito.Sekta zote za kiserikali zilisimama na hakuna kilichoendelea.Vyombo vya habari vilisimamisha matangazo nakutumia muda mchache kutangaza tanzia.
      Wimbo wataifa ulipigwa katika vyombo vyote vya habari.Wananchi wa Kiota walikuwa macho na masikio kupokea taarifa husika.Mioyo yenye majonzi.Habari ilianza kusomwa yenye huzuni.
      “Habari zilizotufikia hivi punde,hivi leo siku ya kusheherekea uhuru wetu,katika uwanja wataifa imetokea ajali mbaya baada ya ndege ya kijeshi iliyokuwa ikifanya maonesho kupoteza mwelekeo nakugonga jukwaa kuu walimokuwamo viongozi wa taifa.Katika tukio hili lenye kutisha tumepoteza mamia ya raia,rafiki,ndugu,wazazi na viongozi wetu wazalendo waliokuwa kazini.Viongozi wote wa serikali wamefariki na majina yao tutayatoa muda simrefu.Makiwa zaidi tunayo kwa kuondokewa na Rais wetu Mh Kisusi pamoja na makamu wake,pamoja na baraza la mawaziri wote…”mtangazaji alitaja sekta karibu zote zilizokuwa na uwakilishi katika jukwaa kuu.Lilikuwa pigo tena makiwa makuu.Kitwea kilichokumba taifa zima kilikuja na upepo mkavu uliopenya kwenye mfipa ya hisia ya nafsi nakupafanya tetemeko lenye ukiwa.Mengi maneno yalipukuchua mbegu za maumivu kuyawakilisha kwenye gunia lenye ujazo wa kihoro.Habari za taifa la kiota zilipita kila pembe ya dunia kuhabarisha masaibu yaliyojiri siku ile ya kiama chao.Rambirambi zilianza kutangazwa pamoja na pole kutoka mataifa mbalimbali yenye ushirikiano na taifa la Kiota.Hayo yalipokelewa ikulu na wafanya kazi waliokuwepo hapo.Bila ajizi walijibu kwa heshima kupokea pole hizo.Ikulu ilikuwa bize kukiwa na malumbano wa hatua gani stahiki kuchukua.Katika mashaka haya mambo yalikuwa na ugumu wake.
     Bashasha iliyokuwepo ikulu ilikuwa imekufa nakuzikwa kaburi la sahau!Familia ya Hayati rais Kisusi ilikuwa kwenye huzuni kwa kuondokewa na baba na mama pamoja na wana wao wawili ambao waliambatana na wazazi kwenye tafrija hiyo.Ukoo wa Kisusi ulikuwa kwenye maumivu makali sana.Tayari vikosi vya usalama vilienda kujumuika nao kwa heshma ya Kisusi aliyetumikia taifa lake kama rais.Tayari kamati maalum ya jeshi iliundwa kushughulikia msiba huo mkuwa.Familia ya makamu wa rais na baraza la mawaziri waliambatana pamoja.Magavana takbribani ishirini na tano waliokuwa katika majimbo yao walisalimika hawa ndo viongozi pekee wakiserikali kisiasa walibaki.Kuna majimbo 30 katika taifa la Kiota.Magavana watano walifariki kwani walikuwemo katika tafrija ya uhuru uwanjani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
        Hawa 25 walikuwa na wakati mgumu kutuliza majimbo yao maana hali ilikuwa tete.Walitakiwa kuwa na ujasiri kuliko wakati mwingine wowote ule.Walitakiwa kujipanga kwa haraka kunusuru taifa lao lililokuwa linateketea.Tayari walianza kuwasiliana kujua hatma ya tukio lote.
                                                                ***
    IKULU  
    DCU 2 walikuwa tayari wapo ikulu.Timu ya wana sheria ikiwa ikiwemo kwa mapitio ya dharura.Kiongozi wa DCU 2,DIRECTOR Masha alikuwemo kwenye chumba cha mikutano.Makaratasi mbalimbali yalikuwa mezani kwake.Walikuwemo walimsikiliza kwa makini wakisubiri kauli yake.
    “Ndugu zangu kama mjuavyo taifa limepigwa pigo takatifu.Tuna hitaji mwelekeo wa haraka kujua tunaenda wapi?Katika katiba yetu inchi haitakiwi kukaa bila rais kwa sababu yoyote.Rais wetu Kisusi hayupo na hakuna wakutekeleza majukumu.Nipo hapa kuhakikisha taifa linasonga mbele tuna hitaji tujue nani anatakiwa kuchukua madaraka.Naomba mwana sheria atuelezee.”alisema bwana Masha.
     Mzee Panda mwanasheria mbobezi wa serikali alitumia fursa hiyo kueleza mambo aliyuoelewa,”Kwa mujibu wa katika yetu,ikiwa rais hawezi kutekeleza majukumu yake kwa njia ugonjwa au kufa au safari basi makamu wake anachukua usukani.Lakini kwa hapa kwentu ya leo kali.Wote waliopo kwenye mnyororo wakupokea madaraka hawapo.Makamu hayupo,waziri mkuu,spika wa bunge, na mawaziri wa wizara zote hakuna aliyepo.Hivyo katiba inaeleza zaidi kwa mabadiliko yaliyofanyika miezi sita iliyopita kwamba kama watakao kaimu kwa muda hawapo basi hakutakuwa na budi itabidi tuwatumie magavana.Katiba inasema wazi kwamba wakwanza kuchukua madaraka miongoni mwa magavana wetu ni magavana wa kwanza watano wanaoongoza majimbo makubwa.Hawa hakuna hata mmoja walikuwepo kwenye tafrija za uhuru.Katiba inaongeza kama hawapo atachukuliwa gavana anayeongoza jimbo dogo kuliko yote.Na hapa namuhitaji gavana wa jimbo la Kibatari.”Mzee  Walii Panda alisema.


     “Hivyo hatuna budi kufuata jambo ili nakumtafuta gavana wa Kibatari haraka sana aletwe ikulu aapishwe.”director Masha alitoa kauli.
    “Inatakiwa ndani ya muda mfupi awe hapa ikulu.”
       “Ndiyo.Hivyo nataka macho yote yawe kwa gavana wa Kibatari,special convoy yenye ulinzi wa kutosha umfuate toka sasa.DCU 2,mtamfuata na baada ya kuapishwa tutaruhusu Presidential Secret Protection kuchukua usalama wake.Tafadhali tuwe makini maana muda kama huu makundi mbalimbali hutumia nafasi hii kuchezea taifa letu.Msifanye mzaa na usalama wa taifa.Tukishakuwa na kiongozi wa taifa nchi itakuwa  na sura ya utambulisho.Tuna hitaji mahali pakupeleka report nakutoa maamuzi.”
    “Ngoja kwanza.”alisema moja ya waliokuwepo pale mezani.Lazima maamuzi yangefikiwa palepale.
      “Mtampaje huyo gavana wa Kibatari jimbo lenye watu wa chache.Isitoshe Gavana wa Kibatari huwa achaguliwi,huteuliwa na rais.Jimbo hilo sioni kama lina umuhimu.Kuna magavana 25 kwanini tusichague hao?”
      Ilikuwa pointi ya maana.Na bila shaka ingeleta mjadala mgumu tena wa haja na lazima maamuzi yatolewe kwa haraka.Mabishano kama haya ni kawaida kwa hali kama hii.Kila mmoja huja na hoja za kupembua dhana kuu ya lengo.Na kila anayeleta hoja huona yak wake ina nguvu kuliko ya mwingine.
      “Isitoshe gavana wa Kibatari hana weledi katika uteuzi kuongoza kundi kubwa.Kumbukeni jimbo hili ni eneo ambalo tulilitwaa kutoka taifa la Savana lands miaka kumi iliyopita.Na kuana mchanganyiko wa asili.Kama mjuavyo asilimia 70% ya wakazi wa hapa sio Kiota ni wa Savana Lands.Tuta ruhusuje hao mahasimu wetu waje watutawale?” John aliponda wazo hilo.Palepale Director wa Masha akajua pende kutakuwa na mzozo wa hali ya juu.Tayari dosari imeonekana.Kwanini hawakuona hilo.
    “Jambo hili ni gumu.Najua.”alisema mzee Panda akipitisha ulimi kwenye papi za midomo yake,”Lilipoletwa bungeni lilikuwa na maana kama ikitokea kitu kama hiki watu wa Kibatari waweze kujihisi ni wana Kiota kiuraia.Wanaweza kuchukua madaraka nakuwaongoza wana Kiota wenzao.Kuwatenga kwa wakati huu kama katiba inavyosema tutaonekana watu waajabu.Tunaweza tumia mwanya huu kuwaingiza kumpa gavana mwingine.Je,mmesahau watazuka watu wa kuhoji uhalali wa gavana huyo kuongoza ambaye sio wa Kibatari aongoze nchi?Jimbo ambalo halijapewa mamlaka ya kumchagua gavana wake bali huteuliwa?Wapo.Na haitakiwi tuache kanuni zetu kisa Fulani sio wa asili.Sheria iliwekwa tufanye tusichopenda bali kutuweka katika mstari wa maadili.Kanuni hii ina maaana kubwa siadhani kama tuna mamlaka ya sisi kuikwepa.”wakamsikiliza akichuja na kupembua maelezo yake.
    “Ni kweli mzee Masha.Sasa tufanyeje?”aliuliza mtu mwingine.
    “Mimi na pinga hatuwezi ongozwa na yule kahaba!”Mambosasa alitupia cha kwake.
      “Tafadhali dhibiti hasira zako.Yule ni gavana wa kuteuliwa ni kiongozi!Ni mtumishi wa umma na siaajabu akawa rais wako.Huwezi kuwa na ubaguzi wa kiasi hicho!”alisisitiza director Masha.
    “Ngoja.”Mambosasa akadakia,”Yule simtaki awe rais wangu nampinga kwa hali na mali.Hawana haki yakutuongoza hao wana Kibatari!Mnataka Savana Lands waje kutumeza wote hapa?”
     “Katiba!Katiba haina unachokisema.”mwingine akadakia.
      “Wewe hujui lolote niongozwe na kibahalula never!”
    “Tafadhali tuwe na uvumilivu.Sio kila kiongozi anapendwa lakini haina budi kumchukua aliyepo.”
     “Awe rais wa nani?Mtu hakuandaliwa kuwa na macho ya taifa.Kapewa kisehemu kidogo chenye idadi ndogo.Hajui uchungu wa siasa.Leo umpe taifa zito.Ajue silaha zetu.Kahaba huyo!Mbona atamaliza ikulu!”
    Chumba kilichemka kwa mabishano ya hapa na pale.Pengine muafaka usingefikiwa kwa kauli kama zile.Chumba kilikuwa kigumu na kila mtu alitafuta busara na mapigano yake.
    Kauli za kueleweka zimefifishwa nakuwa na chuki.Hii ilithibitisha kulikuwa na mgawanyo mkubwa kwa nani achukue madaraka kuliongoza taifa lile.Katika mgwanyo huu lazima aje mtu wakuliunganisha taifa hili.Na haya ni mabishano ya siri ikulu.Je,itakapokuwa hadharani kwa umma wataweza kuendana na mgwanyo huu wenye nuksi?Tena afadhali hapa ni mezani.Lakini mwananchi…mwananchi?Kitendawili kisicho na majibu kilibetua mdomo na kuchopeza meno.
                                                                              ***
        Ukimya ulikuwa umemeza ofisi nzima.Ukimya wa utulivu,ukelele mwembamba ulitoka katika msuguano baina ya watu wawili waliokuwa wamejisahau kabisa ofisini pale.Kitendo cha pambaja kilizaa mabusu yenye uzito.Hata walijisahau kabisa kwamba mlango ulikuwa wazi.Kilikuwa kitendo cha hisia kali kati ya binti Kilua na kijana Serambovu.Mambo yao yalifanyika kwa usiri sana.Katika purukushani za busu zile,tayari Serambovu alimpindua mwana wa nyumba kuu nakumpeleka kando ya kiti.Hisia zilipanda nyuzi joto 100.Alimbana kwenye kiti huku mikono yake ikichakura kupandisha sketi.Iliinuliwa kiasi.Mchakuraji alifikisha usawa alio taka nakugusa kibaraza cha kocho kwa kupapasa na vidole vyake.Akaendelea kusokomeza ulimi wake ndani ya kinywa cha mwanamke huyo huku ukipokelewa kwa mashaka na mbwembwe za kiuoga.Serambovu alijikakamua kutimiza adhma yake iliyo na pupa za wakati ule.Wasiwasi wa tukio lile uliwakumba wote.
      Japo kwenye ufahamu wao walikuwa wamemezwa na mahaba ya kuiba yenye ushawishi mkubwa walijua kwa umbali wapo ofisini.Katika purukushani za kuwahi tayari bwana mkubwa alishaanza kutekeleza dhamira kuu ya kuhujumu haki ya mwanamke huyu.Alimbana kwa kumkandamiza huku hali ya mwili ikichemka kwa pupa za hapa na pale wakishindana nani zaidi ya mwingine. Katika fujo zile ambazo tayari walikwishaanza kuzama ndani kulikuwa na hatia kwa namna Fulani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
      Uwizi huu umekuwa wa ghafla na bila mpangilio.Haukupangwa wala kutarajiwa  kama ungetokea leo.Hawa wana maisha yao ya kawaida.Lakini katika ukawaida wa maisha kuna hali hii yenye utata na ughafla huja ukijitokeza.Kuupokea huwa uamuzi wa mtu na majuto pia huifadhiwa nafsini mwa mtu.Tukio lao liliwabeba nakuwatupa kwenye kichaka ni kama walisahau aibu iliyokuwa inawasimamia kwa wakati ule.
     Uwizi wa mapenzi ulikuwa katika msafara husika ukiiba kwa mashaka.Mawasiliano yao na nje yalienda kombo na miale ya mawasiliano yalififia.Walikuwa bize kuiba yao.Sasa walisahau kabisa katika misuguano ya wizi wenye wingi wa hawaa joto la ghafla lilipanda na kumeza hali ya ubaridi iliyokuwa imetanda hewani.Ulaini uliwatepetevusha huku ngozi ikikandamizwa juu ya mwingine nakutoa unyevu wa jasho uliozidisha ashiki zao.
      Kilua alishikwa shingo na Serambovu ambaye alimtizama usoni!Kilua akampa jicho la ushaufu nakurudisha kinywa chake katika lami za kinywa cha Serambovu.Mwendelezo wa kukurukakara hizi ulizidi kuwazamisha kwenye dimbwi la mahaba wakajisahau kabisa!Tarakilishi ya Kilua ilikuwa inawaka na kwakuwa mtandao ulikuwa umewasha kulikuwa na jumbe nyingi za barua pepe zikiingia japo sauti ndogo ilimwashiria lakini bimkubwa asingesikia chochote kutokana nakuzama katika bahari ya usahaulifu.
      Hata hakusikia kuna mtu kaingia ghafla nakuusogeza mlango!Mtu kuwasimamia ilimchukua takribani sekunde kumi akiona tukio lote!Ilipigwa na bumbuazi lililomranda moyo nakumkosesha majibu ya hapa na pale!Kilua na Serambovu walikuwa katika harakaharaka za ushaufu wao.Kilichowashtua ni ile mtu kumgusa Serambovu bega kwa ghafla.Kweli ndugu Serambovu aligutushwa mguso huo ambao ulipeleka hisia kwenye mishipa ya fahamu nakujakuifikisha kwenye ubongo ambapo tafsiri kuguswa  ilitolewa ubongoni.Akahisi ni mwanamke Yule ndo kafanza jambo hilo akaendeleza mtanange wake tena sasa walifumba macho kuvuta hisia angekuwa tamati punde tu.Waliendelea kwa sekunde kama tano mara kofi zito likatua kwenye shavu la Serambovu!Akagutuka!
      Macho yao yakakutana na mfumanizi wao!Ilikuwa picha ya aina yake!Kilua alitamani kukimbia akashindwa!Alitamani kusema akashindwa!Alitamani kujitetea kagoma!Umeshindwa kusema utajitetea vipi?Kwa shughuli gani?Kweli hakujijua kwa lolote sichochote!Dakika ni kama hazikuenda na hakujua anaanzia wapi wala kumalizia wapi?Leo kashikwa kweupe bila chenga!Aliyemshika ni mume wake wa ndoa!Yule bwana alimeza mate na ghafla kinywa kikawa kikavu.Mirimbi ya kuchanganyikiwa ilijichora kwenye paji la uso!Halafu muhuri wa huzuni ukavaa wajihi wake.Shani iliyokuwepo ikafifia kama moshi.Nimekuja kumuona mke wangu halafu nakutana na janga kama hili?
       Kichwa chake kikasafiri maili na maili!Kweli mwanamuovu hana utu!Kilua alitumbuka macho.Akili ikasimama kwa muda hata hakujua ajishauri kwa jambo gani?Lakini afanye nini?
    “Mme wangu?...”sauti yake ilikuwa na mawimbi!Hofu!Ni kama amepigwa shoti ya umeme wa gredi ya taifa!Akayumbayumba na miguu kulegea.Kitu cha kwanza kwa Serambovu na Kilua ni kukatika kwa hawaa zao!Yaani hata ingekuwaje hakuna mbaye angethubutu kutekeleza chochote.Sikia tu fumanizi kwa mwingine lakini fanya hima lisikupate utachera na dunia.
        Kilua alijifinyanga akajitahidi kurudisha nguo zake vizuri kwa pupa.Nywele zilitibwirika.Ilhitajika muda ajipambe kutokana na kadhia ile iliyomkumba.
      Mikono aliminyaminya asijue aanzie wapi.Maana kama mwanaume huyu angelianzishia hapa bila shaka kusingekalika na leo bosi wa ofisi kubwa angekuwa mashakani kuhusishwa na ugomvi wa kinyumbani wa fumanizi.Tena mbaya zaidi kufumaniwa na mume wake.Lakini hakujua ni kwa namna gani mwanaume huyu kaja hapa.Alipokuwa anatetemeka mpaka mapajani aliona mumewe akisogea mbele hatua tatu kupisha mtu aliyekuwa nyuma yake.Alitamani ardhi ipasuke aingie ndani!Aliyekuwa nyuma ya mumewe alikuwa mamake mzazi!Mwili wote ukazizima kwa wimbi la mshtuko!
      “Maaa!...Deddani!No I can explain?”alijibaraguza kwa mawimbi.
    “Shame on you!”ndo neno lililomtoika mama wa binti huyu.Lilikuwa neno zito kuliko yote!Dedani hakusema kitu zaidi yakugeuza hatua zake kuufuata mlango aende nje.Huku pumzi zikishindana kuingia nakutoka nje.Dedani alikuwa kama amechanganyikiwa na akili kufa ganzi!Nifanyeje?Alijiuliza bila kupata majibu.
      Dedani iliamua kutoka nje nakutokomea kabisa asijue aanaenda wapi?Lilikuwa tukio bay asana.Kilua alitamani katika muda ule aingie ndani ajifungie asionane na mtu.Lilikuwa tukio baya kuliko yote kujiri!


     Akili ya Kilua ilisimama mguu sawa.Haikuenda mbele wala kur


    udi nyuma kulikuwa na mchanganyo wa hali ya juu kuliko wote uliowahi kujitokeza katika maisha yake.Fumaninizi kubwa kuliko yote limejiri katika maisha yake.Mumewe kamkuta akizini na mtu ofisini kwake.Ilikuwa ofisi kubwa tena siyo ya kitoto!Kilikuwa alibaki kuchanganyikiwa akijaribu kuwaza kila neno asijue wapi pakuanzia.Pangekuwa patamu sana kama angepajua.Ilikuwa safari iliyomchanganya.Alijuta kwanini kafumaniwa kizembe hivi!
    “Ni nini hiki umefanya mwanangu?”aliuliza mama baada ya kupata kitu cha kumsemeshea mwanaye.Ni kama Kilua alimwagiwa maji baridi asijue wapi anaanzia.Hivi ni jambo gani natakiwa kufanya.Aliangalia pale mezani nakuona kibao kikiwa kimeandikwa GAVANA KILUA DEDANI TABIRI kwa maandishi ya rangi ya dhahabu.Akajiuliza ni kwanini nimkefanyia jambo hili hapa katika ofisi kubwa kama hii?
      “Nakuuliza wewe?...”mama alizungumza kwa hasira,”Hivi ni mtoto nilizaa au maradhi nilitoa tumboni?”mama Kilua alihoji kwa majuto.Uso wake ulienda sambamba na huzuni iliyojikita moyoni mwake.Tangu kuwa kwake hakutegemea jambo kama hili lingeikumba familia yake kwa namna yoyote.Kilikuwa kitu cha kufikirika tu lakini sio kingetokea kwa mwana wa uzao wake hata iweje?Lilikuwa pigo la kashfa!Hivi huyu mwanaye ajui yeye ni nani katika taifa hili?Anafanyaje upumbavu kama huu?Tena ofisini kwake?Siingeenda hata gesti au sehemu yoyote ile ilimradi tu asilete mambo haya ofisini?
      Kilua ni kama alimwagiwa maji baridi kafifia nakupoetelea mbali kwenye mawazo mazito.
    “Hivi gavana mzima unakuwa na mambo machafukama haya?Je,wafanyakazi wako wakikuona?Halafu mlango upoupo tu?”
        Mama ilibidi arudi kuufunga mlango,”Haya na wewe bwana hebu toka nje!Tokaa!Baradhuli wewe unamuharibia mwanangu ndoa yake!”alifoka kwa hasira sana mama Yule.
        Serambovu alikuwa akiivuta suruale yake akajikaza nakukimbilia nje nakuufungua mlango uliofungwa tayari.Akatoka moja kwa moja hadi kwenye majilisi yake huko ilibidi ajitengenze tena.
     Huku ndani mama Kilua aliendelea kupandisha mori.Maswali yake kadhaa haya ja jibiwa hata moja!
     “Hivi wewe mtoto huoni haya?Ofisi kwako kabisa una diriki kumtenda uzinifu?Hata ujali watu waliopo hapa?Umekunywa nini wewe?Hebu twende nyumbani haraka.”
      Kilua akakosa.Huwa hivi tangu utotoni akikosa hukosa cha kusema nakujikuta akizubaa kwa ukimya wa huzuni.Alienda bafuni kwake nakujitengeneza.Lakini akaona bora aoge kabisa.Pale ofisini maliwato anayotumia yalikuwa na bafu kabisa.Alichofanya alipiga moyo konde huku hatia ikiwa imempanda.Aliondoa mavazi yake moja baada ya lingine kwa hasira.Akashika koki yakufungulia maji ya bomba la mvua nakuyaachia ya baridi yakashuka nakuanza kumnyeshea mwili mzima.Kulikuwa na sabuni yenye marashi akaanza kujiswafi.Maji yalipokuwa yakishuka kwenye ngozi yake nakuondoa kila kilichokuwemo alihisi maumivu makali moyoni.Maumivu aliyoyajua mwenyewe bila mtu yeyote kuelewa.Alijihisi vibaya sana mwili na roho!Akapitisha sabuni yake huku ubaridi wa maji ukizidi kumtafuna ngozi.Alitamani jambo la kumpa adhabu pengine maumivu ya moyo yangeondoka.Kilichokuwa moyoni mwake ni hatia na upweke uliojibebesha lawama.Ghafla akatamani kulia.Akalia nakuangusha machozi mazito kuliko yote.Akalia nakuugua moyo!Akalia sana huku machozi yake yakimezwa na ubaridi wa maji yakuoga.Aliendelea kujitesa na ubaridi wa maji yale akiona hili ndo jambo jema lakufanya napengine lingemuondolea maumivu makali yaliyoutesa moyo wake!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
      Alilia nakuigomea sauti yake isitoke maana hakutaka mama’ke amsikie kwa lolote!Zaidi mama alisikia mlio wa maji.Kilua alishuka mpaka chini akaketi sakafuni kwenye vigae.Maji yaliendelea kumiminikia kwa fujo!Alilia pale chini!Kilio kilichotoka moyoni mwake.Pengine machozi yangemsaidia kuondoa huzuni iliyojikita moyoni mwake.Kwa takribani dakika kumi na tano alikuwa bafuni.Aliporidhika na kilio alioga nakumaliza.Alijifuta.Ni kawaida yake kuoga hapa ofisini hasa ikiwa limetokea jambo kama la leo.Alijifuta maji.Tayari pale bafuni mlikuwa na vipodozi vya dharura.Alivichukua vipodozi vile akataka kujikwatua lakini akasita.Aliona kama hastahili kufanya vile kutokana na tukio lililopita muda simrefu!Lakini akaishia kujikwatua kishingo upande.Akiwa anajiangalia kwenye kioo aliwaza.Hivi yeye ni nani hata asimshukuru Mungu wake kwa yote anayomtendea?Hakupata jibu.
       Akajitizama kwenye kioo kuona uzuri wake.Bado yupo kwenye chati na watoto wake watatu.Na hivi aliwahi kupata watoto maapema mbona asifurahie maisha!Kweli maisha yake yalikuwa na changamoto zake.Alikuwa naya kwake.Gavana Kilua Tabiri miaka 31.Bado mdogo sana!Alikuwa gavana wa jimbo la Kibatari baada ya kuteuliwa na rais Kisusi.Ana elimu nzuri,familia nzuri na mume muaminifu!...Muaminifu…aliwaza.Kazi ya ugavana ilikuja kibahati.Aliteuliwa kulingana nakuwa mwanafunzi bora chuoni wake.Japo umaarufu wake kisiasa haukuwa mkubwa sana lakini kwa wachache waliobahatika kufanya naye kazi walimjua kama binti mtaratibu dhaifu!Yeye alizoea kufuata maagizo nah ta katika kutawala Kibatari amekuwa akifuata maagizo toka ikulu.Hakuwa na haja yakujitanua misuli kuonesha ujzui wake kisiasa.Siasa haikuwepo kwenye kichwa chake.Na hata alipoingia ugavana alikuwa tofauti na magavana wengine.Yeye muda mwingi alifuata maagizo ya ikulu.Hata ukiangalia maendeleo ya jimbo lake yalitegemea kauli za ikulu ndo awapeleke mbele.Hali hiyo ilifanya eneo lake kuwa miongoni mwa eneo dhaifu kimaaendeleo na watu wengi wakawa hawana maendeleo.Wengi waliobahatika kuishi majimbo mengine walifanikiwa kielimu na uchumi maana mazingira yaliboreshwa vizuri zaidi.Jimbo la Kibatari lilikuwa sehemu iliyochukuliwa kijeshi nan chi ya Kiota kutoka taifa la Savanna land.Eneo hili lilikuwa na siri kubwa sana ndio maana jamhuri ya Kiota haikutaka kabisa watu hawa wapewe nafasi ya siasa kwenye sekta muhimu hii nikufuatia usiri wa eneo lenyewe.Hata wabunge na maseneta wa eneo hili walidhibitiwa na serikali kuu.Eneo hili lilikuwa na mambo yake.Hata Kilua alipopewa ugavana alidhibitiwa sana kuhusu eneo hili.Hata yeye alitaka lipewe fursa ya maendeleo kama majimbo mengine lakina hakupewa nafasi.
          Alidhibitiwa kiutawala!
        Alijiangalia tena kwenye kioo lakini ghafla akamkumbuka mamake.Ilibidi afanye marekebisho ya nguo.Akarudi ofisi kwake.Aliona mamake bado anamkazia macho!Akakumbuka bado amevaa nguo alizofanyia uzinzi.Akahisi aibu.Alichofanya nikuifuata pochi yake akaichukua nakurudi bafuni kwake.Akakuta hana nguo yakubadili.Aling’ata meno kwa hasira.Alitoa simu yake kwenye pochi akapiga namba Fulani.
      “Sofi…”
    “Ndiyo gavana?”
    “Niletee ile mambo.”alisema Gavana Kilua.
    Sofi alicheka upande wa pili,”Hahaha!...Haya Gavana wangu.”simu ikakatwa kama kawaida.Baada ya muda mfupi Sofi aliingia ofisini kwa gavana akiwa na nguo zilizonyooshwa vizuri.Hizi ni nguo wanazotumia watu wanaofanyakazi ofisi ya gavana.Huwa suruale nyeusi ya kitambaa shati jeupe na kikotie cheusi hasa kwa safu yay a mabinti.Alikuja na zile nguo hadi bafuni akamkabidhi gavana Kilua aliyezipokea nakufanya mabadiliko ya mavazi.Kama hajabeba nguo zake za kubadili huwa anatumia sare za wafanyakazi wake..Zile za kwake alizikusanya akaomba Sofi azitie kwenye mfuko aende azichome nyumbani kwake.
    Baada ya kuwa sawa kimavazi bimkubwa Gavana Kilua alirudi ofisini kwake akaketi kwenye kiti chake.
      Ukimya ukapita huku mamake akimuangalia mwanaye,”Kwa hiyo ndo tabia zako hizi unatembea na wanaume hovyo hadi huku ndani?Unaoga kupoteza ushahidi.Kumbe unavyokujaga nyumbani na mavazi tofauti unakuwa tayari umeshate,beza?”mama ni kama alikuwa anamsuta mwanaye.Hakuwa na msalia mtume.Alimpembeua na kumchuja.
      “Mama tafadhali naomba uniache kwanza.”
      “Nikuache?...Hivi umona mumeo alivyokuwa?”aliuliza bimkubwa huyo.
    “Ndiyo najua mume wangu kaumia sana.Najuta kwa kosa langu.Natamani nimuangukie miguuni.”alisema Kilua yakitoka moyoni mwake.Lilikuwa tukio la aibu sana.
    “Tangulini jambo hili limekuwa kati yako ni chifu wako wa ushauri?”aliuliza mama Kilua akimkazia macho bintiye.
    Kilua alifikiri kidogo kasha akazungumza,”Ni muda mrefu sasa.”ilimtoka halafu akajikaza tena.
    “Huyu Serambovu ulimtoa wapi?”
    “Ni Yule kijana mliyenikataza nikiwa shule.”alisema Kilua akivuta pumzi ndefu nakuzishusha ni wakati wa aibu bora uimeze.
    “Eti nini?”mama Kilua akavuta pumzi ndefu nakuzishusha akivuta kumbukumbu kuhusu mtu huyu.Ni kweli anamjua lakini hakutaka akumbuke hasa akiambiwa anamjua kwa namna yoyote ile.
      “Ndiyo kwani haumjui Serambovu ndo Yule boyfriend wangu nikiwa kidato cha pili.Yuleyule mliyemtishia wewe na baba kwamba mngemtupa ndani kama hataachana na mimi.”
       Ilibidi mama Kilua ashike kichwa!Hapa kulikuwa na tafsiri ndefu sana.Ikiwa huyu alikuwa mshikaji wake wa zamani na alishakanywa kwa miaka yote walijua kuna kijana lakini hawakubahatika kumuona kw asana kiasi cha kukariri sura.Ingekuwa vigumu kujua kwa ndo huyu hapa.Imepita takribani miaka 17.Kweli mama Kilua alishapuuzia jambo hilo kulingana na walivyolishgulikia lisingeleta taabu tena.Kumbe jambo hili halikufa kama walivyodhani.Kumbe liliendelea kuoza na mpaka sasa limetoa harufu kali ya kunuka inayohatarisha ndoa ya Kilua.
       “Kwani mwanangu ina maana mmeendelea nay ale mahusiano mpaka leo?”
    “Ni stori ndefu mama na kuna mambo nikisema muda huu nita chafua kila kitu.Ni bora tu ni baki kimya.”Kilua alisema kwa sauti ya mawimbi.Bado alikuwa na wasiwasi hajui mume wake yupo wapi?Ghafla mlango ukafunguliwa wakaingia walinzi wake.
    “Gavana kuna hali ya dharula?”alisema kiongozi wa ulinzi.
    “Ni nini kimetokea?”aliuliza Kilua akiwa anatweta.Yule mlinzi wake alikuja moja kwa moja nakuchukua Kitanza mbali nakubofya kuelekea ilipo runinga.Iliwaka nakukutana na habari ya kusisimua!Akaona tukio la ajali mbaya kuliko zote.Palepale akaamka nakuchukua simu akapiga namba Fulani akasikiliza.
      “Ndiyo…what?...Ohh my God!”alisema Kilua akiendelea kupokea habari.Ilibidi ajishike kichwa huku akirudisha macho kwenye runinga nakuendelea kusikia kwenye simu.Alichoambiwa ni ukweli.
    “Mbona hukwenda kuadhimisha sherehe hii kwenye jimbo lako?”mamake akamuuliza.
    “Nilimtuma mwakilishi wangu.”alijitetea Kilua kumbe alikwepa tukio lile ili kuwa na mtu wake faragha lakini jambo moja likamjia kichwani,leo alitakiwa kuwa makao makuu ya nchi kwa sherehe ile ila usiku wa jana chifu wake wa ushauri alimkataza kwa malengo ya kukutana faragha!Moyo ukamwenda mbio!


    Kwanini Serambovu alihimiza Kilua asiende kwenye sherehe za uhuru makao makuu?Alijiuliza na hata akaamshawishi asiende pia kwenye jimbo lake bali atume mwakilishi.Aliambiwa angealikwa na rais lakini angoje barua ya mwaliko barua ambayo hakuipata!Kukosa barua na ushawishi wa Serambovu kukutana faragha kulimpa hitimisho lakuamua kutohudhuria sherehe hizo nakuwa na ajenda kwamba gavana ana shughuli za kitaifa hatopata nafasi ya kwenda kwenye hafla hizo.Lakini bado alitilia mashaka kwanini Serambovu alipinga vikali asiende kule?Alijiuliza bila kupata jibu zaidi ya moja.Lengo la wao kuwa faragha ni kwasababu siku hiyo kusingekuwa na wafanyakazi wengi ofisini.Hivyo kuepuka usumbufu waliamua kwa pamoja baada ya mmoja kushawishi wasiende popote.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Mwanangu huyo mwakilishi atakuwa hai kweli?”aliuliza mamake.
      Kilua alivuta pumzi ndefu nakuzishusha,”Nilituma wawakilishi wawili  katika sherehe za uhuru za Jimbo langu.Mambo yapo sawa wala hakuna mashaka ila naibu Gavana wangu alienda makao makuu ya nchi!Yaani nimechanganyikiwa.”
      Sofi akaingia ndani muda uleule.Hofu ilikuwa imetanda na ilihitajika hatua zaidi kuchukuliwa ilikuweka mambo sawa.Simu mbalimbali zilianza kuingia pale huku Sofi akizipokea.Kilua alikuwa na wakati mgumu sana kiasi alijikuta akizubaa.Ripoti zilianza kuingia kwa haraka mbalimbali.Ndani ya muda mfupi vikasikika ving’ora vya polisi vikiwasili jingo linalobeba ofisi ya gavana.
    “Hali ni mbaya kwakweli.”alisema mama Kilua.Ofisi nzima ikazizima hofu na mashaka baada ya muda mfupi akaingia mkuu wa polisi wa jimbo pamoja na kamamnda mkuu wa jeshi la polisi akifuatiwa na msimamizi wa jeshi kwa jimbo la Kibatari.Walikuja na timu zao.Karibu sekta muhimu ziliwasili makao ya gavana wa Kibatari.Kabla hajaongea nao aliomba Sofi awapeleke chumba cha mkutano.Ilibidi Kiliua ajikaze maana muda ule alihitajika kuwa imara kuliko muda wote alitamani mume wake awe pale na wanawe.
      Kilua alienda bafuni kwanza akanawa uso tayari alielewa serikali nzima imefutwa na ajali hiyo mbaya.Marafiki pamoja na mabosi wake hawakuwa hai!Alihisi kutikiswa ubongo.Ilikuwa siku mbaya kuliko zote na hata hakujua ilikuwaje jambo hilo likatokea.Alinawa uso kasha akelekea chumba cha mikutano.Waliokuwepo waliinuka kwa heshma ya gavana.
      “Ripoti nilizopata nikuwa mpaka sasa serikali nzima imefukuwa na ajali iliyotokea!Hakuna serikali bali ni hizi tu za majimbo.Tupo katika wakati mgumu sana na lazima kama jimbo tuhakikishe watu wetu wanakuwa sa…”hakumalizia akajikuta machozi yana mtoka akikumbuka hao waliokufa.Lilikuwa jambo zito kuliko yote.Hapa ilihitajika ujasiri wa hali ya juu na kama kiongozi hakutakiwa kuonekana mwepesi wa machozi.
    Viongozi wa usalama walijitahidi kumtuliza gavana wao.Alifuta machozi kisha akakohoa kidogo,”Samahani jamani nashindwa kujizuia.Naomba Kamanda wetu wa jeshi kwa hapa jimboni unipe taarifa zaidi.”
      “Ndiyo mh Gavana.Kwanza nitoe pole kwa janga lililotokea.Nikupe pole wewe gavana.Pole kwa wananchi waKiota na hasa jimbo la Kibatari kwa tukio hili baya.Sisi upande wa jeshi tupo imara tuna subiri maelekezo yako tu.”alisema kiogozi huyo aliyeshiba mazoezi.
    “Jeshi la polisi.”alimgeukia mkuu wa polisi jimbo la Kibatari.
    “Gavana wetu nitoe kwa wananchi wetu na pia kwako.Tupo nyuma yako kuhakikisha mambo yanaenda sawa.”hata mkuu wa polisi jimbo la Kibatari hakuwa na mengi ya kusema wengi walikuwa na huzuni nakubaki kama wamepigwa shoti ya umeme.Chumba chote kilikuwa hakifai.Peke yake Kiliua ndo alikuwa mwanamke.Aliona wafanyakazi wa usalama ambao ni wanaume wamenywea sana kiasi aliogopa maana alishindwa huku machozi yakipenya kwenye bilula za macho yake!Atafanyaje?Alijiuliza bila kupata jibu la kuridhisha.Kiota imetikiswa.Wakiwa pale ghafla akaingia Serambovu.Alienda moja kwa moja hadi kando ya Kilua nakumnong’oneza kitu hali iliyomfanya Kilua kujishika kichwa.Wakuu wa usalama wa jimbo la Kibatari walimgeukia bosi wao wakimshangaa.Atakuwa kapokea taarifa nyingine ya kushtua zaidi.
    “Jamani nataka kujiuzulu!”alisema Kilua akiwa kashika kichwa huku ameinamisha kichwa.Wakuu wa usalama waligeukiana.
       Ilibidi Chifu wa utendaji na ushauri bwana Serambovu asimamie onesho,”Tumepokea taarifa za kiintelijinsia kwamba vikosi vya kijeshi vya Savanna Lands wameanza kujiandaa kusogea mpakani mwa Kibatari.Siajabu waanzisha vita muda simrefuu.Wamejua serikali kuu haipo hivyo wana mwanya wakutumia udhaifu wetu kutuandama!Inahitajika ujasiri wa hali ya juu.”
      Kila mtu akaduwaa.Palepale wote kwenye meza kuu wakamgeukia gavana!Hakuna aliyetaka kusikia swala vita!Hilo ni jambo la fedheha kwa wote waliona kama hatari kuu isiyo na mchezo!Kila mtu alihitajia kauli ya gavana wao ambaye mpaka sasa alionesha udhaifu mkubwa kuliko wote.
      “Ndani ya katiba gavana una mamlaka ya kuhakikisha unalinda eneo la jimbo lako na kuhakikisha usalama upo kwa 100%.Tunakuhitaji gavana wakati huu kuliko wowote.Maamuzi yako ndo taswira ya usalama wa eneo hili.”alisema chifu wa utendaji Serambovu.Hungedhani muda mfupi uliopita kulikuwa na fumanizi kati yao.Kilua alitoa mikono kichwani.
      “Naanzia wapi kuongoza vita?Ndo waje wanimalize na mimi?Nataka kujiuzulu.”
       “Kwa taarifa tu gavana hata useme ujihudhuru bado haitasaidia maana naibu gavana wako amefariki kwenye mlipuko.Unadhani ni nani atatuongoza.Nchio ina hitaji viongozi wa chache mliobaki kuipigania.”alishauri kiongozi wa jeshi jimbo la Kibatari.Alikuwa mtu mzima.
      “Kwahiyo ninafanyaje?Hii ni ishu ya kijeshi inahusu serikali kuu siwezi kuingilia mhimili huo.”alisema Kilua kwa uoga.Alitamani kukimbia jambo hilo.
      “Ikiwa serikali hakuna ina maana nchi ipo hatarini na kundi lolote lenye maslahi kinyume na taswira ya nchi litachukua nafasi.Wewe unachotakiwa nikutumia muda huu kuhakikisha Kibatari ipo salama sasas hujapewa nchi umepewa Kibatari tu unataka kukimbia.Gavana kwa heshima zote naomba uwe imara kwa eneo letu.”alisema kiongozi wa jeshi eneo la Kibatari.
      Kilua alifikiria akiwa na mashaka asijue hatua ya kuchukua ghafla mlango ukafunguliwa wakaingia watu waliovalia suti nyeusi na vifaa vya sauti masikioni.Waliokuwepo wakataharuki.
      “Gavana Kilua Tabaradi?”aliita kiongozi wa watu wale wenye suti nyeusi.
      Kidogo Kilua aingie chini ya meza aliogopa sana akahisi hawa sio wapelelezi wa Savanna lands.Ila akajikaza mbele ya kamati yake ya ulinzi akasema hata kama ikitokea akauawa basi asiende kiuoga wamuone jasiri.
     “Ndiyo ni mimi.”aliitika kiunyonge wa hali ya juu.
    Wale jamaaa wakaangaliana huku kiasha mmoja akongea kupitia kifaa chake cha mawasiliano,”Ndiyo yupo hapa.’’
    “Mheshimiwa Gavana tuankuomba uongozane na sisi.”walisema wale watu walikuwa hawacheki wala kuonesha mzaha.Kilua aliwatizama watu wa kamati yake kana kwamba niteteeni jamani.
    “Samahani mabwana huyu ni gavana na mkuu wetu wa ulinzi na usalama tunaomba kujua mnampeleka wapi?’’alisema kiongozi wa jeshi jimbo la Kibatari tena bila kuchelewa aliinuka kwa kasi ya ajabu nakupeleka mkono kiunoni akatoa bastola nakujihami.Wale jamaa bila kuchelewa kwa kuwa walikuwa wengi walimfyatulia kamanda wa jeshi risasi kupitia bastola yao.Ukasikika ukelele mkubwa paaa!
      Kilua  haja ndogo ilimvujanakumezwa na chupi.Alitetemeka kupita maelezo ukisikia kuumbuka ni leo!Alizoea kuona chombo hicho cha moto napengine kutoa amri kwa walioko chini yake kutumia chombo hicho kwaajili ya usalama wa jimbo lake lakini sio kujeruhi mtu.Kweli Kamanda Pasha alijeruhiwa vibaya na risasi ilimpiga kwenye bega upande wa kulia mkono aliokuwa ameshika nao bastola yake!Kwa uzoefu wake hakutaka kushindwa alitaka kufyetua nayeye lakini ghafla waka muwahi nakumfyetulia nyingine kama tatu tumboni!Hali hiyo iliepelekea kamanda Pasha kuyumba nakuanguka chini!
     Wale wenye suti nyeusi walimsogelea Kilua nakumzunguka wawili walisimama mbele yake.Wengine wawili wakawa nyuma yake.Tayari bastola zao zilikuwa mikononi.Ilikuwa hatari ya ghafla.Mmoja wa wale wenye suti nyeusi akatoa maagizo kupitia kifaa cha mawasiliano alichovaa kama saa mkononi.Ndani ya sekunde chache wakaingia wengine wenye suti wakiwa na silaha nzito.
      “Kila mtu akae chini!Chini!Inspekta chini na watu wako.Yoyote asitoe silaha!”aliongea amabaye alionekana kama kiongozi wa kundi lile.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
      ‘’Madam Gavana hiki ni kikosi maalum cha DCU 2,tupo hapa kwaajili yako.Tukio lililotokea muda mfupi uliopita ndo limefanya tuwe hapa.Unahitajika ikulu haraka iwezekanavyo.Lakini kabla ya kwenda ikulu kuna jambo moja unatakiwa ulifanye ukiwa hapa.Naomba wote mliopo msogee pembeni.”alieleza kiongozi Yule.Palepale kamati ya ulinzi iliyokuwa imeamriwa kukaa chini wakainuka nakusimama walijua kinachofuata lakini hawakutegemea kama jambo hili lingetokea kwa gavana wao.Kilua muoga anayetaka kujiuzulu?Hata jimbo anaona kama mzigo mzito?
      Wakiwa wamesimama pale wakaingia watu wengine mmoja akiwa na joho la jaji pamoja wazee wa heshma.Kilua hakuwa ameelewa lolote.Aliyekuwa amevaa joho ni jaji kutoka mahakama kuu.Alisogea hadi mbele ya Kilua.Palepale wengine wakasogea karibu.Wale waliovaa suti nyeusi  wakatoa kamera zao huku wakianza kuchukua piacha za matukio.Kilua alikuwa anaogopa.Hakuelewa kianchofanyika.Pale chini alimuona kamanda Pasha akihangaika.Kuona tu damu mwili wake ukawa na hofu na tayari wenye suyti nyeusi wakaelewa hilo jambo.
    “Vijana hebu mchukueni kamanda amejeruhiwa vibaya.’’ Alitamka kiongozi Yule.Vijana wake wa kazi walikuja kwa haraka wengine kutoka nje wakambeba kamanda Pasha.
    Kilua alitaka kumsogelea akazuiwa,”Tafadhali gavana naomba usimsogelee huyo mtu atakuwa sawa.Tunalotaka kulifanya hapa lina umuhimu mkubwa!.”alisema jaji Polepole.
      Kilua alitumbua macho.Alimwangalia jaji.Ghafla akaona jaji akipewa biblia,kisha akamkabidhi Kilua.
    “Tafadhali inua mkono mmoja na mwingine shika Biblia.Halafu useme maneno yafuatayo.”jaji Polepole alizungumza huku akimwangalia bimkubwa Kilua aliyekuwa kama kondoo tayari kuchinjwa.Kilua alifuata kila alichoambiwa.  “Mimi Kilua Dedani Tabiri naapa yakuitumikia na kuilinda jamhuri ya Kiota kwa nguvu zangu zote na uwezo wangu wote,nitailinda nakuiheshimu katiba ya jamhuri ya Kiota…eeh Mwenyezi Mungu nisaidie.”alimalizia Kilua na palepale akaja Kaptein wa kijeshi nakusimama nyuma yake!


    “Hongera mheshimiwa rais wetu mpya bi Kilua Dedani Tabiri.Kwa mamlaka yaliyopo katiba katiba yetu tukufu umekuwa rais rasmi wa jamhuri ya Kiota.Hivyo shughuli zote za kiofisi ya rais na mamlaka zote za nchi zipo mikononi mwako kwaanzia sasa.!”alisema jaji Polepole.Palepale Kilua akahisi miguu kuwa mizito nakupepesuka kaptein ADC/mpambe wake aliwahi kumdaka.Walinzi wakamsogelea.
    “Mheshimiwa upo sawa unajiskiaje?”aliuliza mpambe wake kaptein.
    Moja ya walinzi alikuja nakuanza kumkagua,”Mweke kwenye kiti.”aliamrisha kiongozi wa kikundi cha DCU 2.
      Kiti kikasogezwa.Wakati hayo yakiendelea viongozi wa kamati ya ulinzi ya jimbo lile wakakosa jibu.Tayari gavana wao amepewa cheo kikubwa kuliko vyote na hakuna aliyetegemea kama kiti hicho kingeangukia kwao.Japo ndiyo kifungu hicho kilikuwepo kwenye katiba yao.Kilikuwa kipengele tu cha kuwatuliza wananchi wa jimbo lile wasione wanatengwa.Hakuna aliyeona jambo hili jambo kama lingetokea!
     Bila hata kuchelewa vililetwa vifaa akaanza kupimwa mapigo ya moyo pamoja na presha.Walikuwa wakimshughulikia kama mboni ya jicho.Jambo lile walijua limemshtua sana.Wewe unashtukizwa tu eti umepewa kuongoza nchi ghafla bila kutarajia.Hakuwa amejipanga wala kukisia jambo hilo.Na ukimtizama vizuri alikuwa kwenye bumbuazi zito.Yaani kitendo cha yeye kuanguka chini kilishtua watu sana.Wakasema kama anashtuka kiasi hiki ataweza kweli kuongoza nchi?Dhaifu!Walijiwazia kichwani!Vipimo vya haraka waligundua ni mshtuko mdogo sana.
    “Ngoja nilete maji.”alisema Sofi akiwahi kuleta maji.Ile kafika na maji yake kumpa Kilua alishangaa kuzuiliwa.
      “Tafadhali binti huruhusiwi kumpa huyu mtu chochote.Kwaanzia sasa yupo mikononi mwa serikali.Haturuhusu kupewa hata maji na mtu yeyote isipokuwa walinzi wake tu.”alisema kiongozi wa kikosi kile nakumpa tabasamu kidogo Sofi iliaelewe somo.Sio kwamba alimnyima bali ni taratibu na kanuni za kumlinda kiongozi wanchi!
      “Mheshimiwa relax tupo kwaajili yako.”moja ya madaktari waliokuwa wanamuangalia alimwambia hukua akiijenga tabasamu kidogo aweze kutengeneza mazingira rafiki na mgonjwa wake.
    “Sawa.”alijibu Kilua kwa uchovu.Kweli alikuwa kwenye mshtuko wa radi.Akili ilizidi kuganda.Hakujielewa kwa lolote lile.
      Uchunguzi uliwathibitishia kwamba mheshimiwa rais Kilua alikuwa na mshtuko mdogo tu na ungetulia baada ya mapumziko.
    “Ni mshtuko mdogo tu ningeomba apumzike.”alishauri daktari Paulo.
    “Kwani hatakiwi kwenda hospitali kwa matibabu zaidi?”aliuliza kiongozi wa kikosi kile.
      “Hapana kinachohitajika apumzike na nina shauri asipelekeshwe kwa sasa.”dk Paulo aliongeza.
    “Lakini nchi inamuhitaji kuna mambo yanayohitaji Presidential Order!”
    “Najua lakini hali yake siyo imara!”alitetea dk Paulo.
       “Dokta Paulo nchi imetikiswa halafu wewe unaniambia rais apumzishwe kidigo?Unajua sheria za nchi yetu ofisi ya rais inatakiwa kuwa active masaa yote.Hakuna wa kumshikia madaraka mpaka awe sawa.Tuna rais tu.Hakuna kiongozi mwingine.Wewe fanya unachojua lakini na muhitaji akiwa imara ndani ya muda mfupi?”alisema kiongozi wa kikundi kile.
      Dk Paulo ilibidi afungue mkoba wake akatoa kikaratasi kisha akaandika aina Fulani ya dawa.Nakumpa kiongozi wa kikundi,”Nahitaji hizo dawa sasa hivi.”
    “Nipeni nikanunue?”alisema Sofi akijaribu kuwa na masaada wa hali na mali kwa bosi wake.
    “Hilo duka alijafanyiwa ukaguzi na timu yetu haturuhusu kununua dawa za matumizi kwa rais hovyo.”moja ya walinzi alishauri.
      “Lakini tutafganyaje na tuna hitaji masadda wa hali na mal;I muda huu!Siyo muda wa mchezo maisha ya rais lazima yawe imara kwa sasa.Tuna taarifa za kiintelijensia kwamba majeshi ya Savanna Lands yanajipanga kuja hapa.Rais yup hapa hatakiwi kuwepo eneo hili kwa namna yoyote ile!”mwingine alidakia.Kulikuwa na mchanganyo mkubwa sana.
    “Dk Paulo Rais anaweza kufikishwa ikulu bila tatizo?”jaji Polepole aliuliza.
    “Ndiyo lakini asisumbuliwe kumuimarisha.”alishauri dk Paulo.
       Ukumbi ulichemka kwa presha iliyopanda ghafla.Watu walichanganyikiwa.Tayari vyombo vya habri vilikuwa vina tangaza kuapishwa kwa rais Kilua huku wengi wakijiuliza uimara wake katika kulivusha taifa kutoka kwenye miiba hiyo.Kwa mujibu wa katiba yao,inapotokea kifo cha mkuu wan chi basi mrithi wake huchukua madaraka hadi muda kamili wa muhula utakapoisha.Hivyo ilimaanisha kwa kipindi hicho cha rais Kisusi cha miaka mitano alikuwa ametumikia miezi kumi na moja,hivyo kulikuwa na kipindi cha miaka 4 na mwezi mmoja mbele.Kilua alikuwa na muda mrefu sana wa kutawala Kiota na kama angependa kuwa mwanasiasa kamili basi angetumia mwaka huo kujiimarisha napengine angeamua kuitisha uchaguzi mpya nakugombea.Lakini kwa jinsi alivyoonekana kila mtu kwenye kile chumba alihisi huyu binti atafeli mtihani ndani ya wiki!
      Kaapishwa tu na kitu cha kwanza kaanguka chini!Walikuwa na mashaka sana na uimara wake.Tayari waliokuwa kwenye kikao cha kamati ya ulinzi ya jimbo la Kibatari walimsikia rais Kilua akitaka kuachia wadhfa wa ugavana kabla hajawa rais dakika chache zilizopita.Hiyo fika iliweka maswali mengi kuhusu uimara wake kama kiongozi wa taifa.Ataweza kweli kusimamia nchi?
    “Nashauri apelekwe airport haraka sana.Ndege yoyote iliyopo airport iwe tayari agent Pawa fanya utaratibu huo.”alisema kiongozi wa kikundi kile.Mawasiliano yakaanza kufanyika wakifanya taratibu za kumuondoa Kilua eneo lile.
      Wakati haya yakifanyika maandalizi yakumuondoa rais Kilua eneo lile.Ofisi nzima ya gavana ilikuwa katika pilikapilika za kushangazwa na madaraka aliyopewa gvana wao kuwa rais wanchi.Wapo walio furahi na wapo walioshangilia kuhusiana na jambo hilo.Kulikuwa na wingi wa mchanganyo wa kihisia kwa ujumla.Lakini yote tisa Kilua alikuwa tayari mkuu wan chi na hilo lisingebadilika.Nchi ilikuwa bado kwenye taharuki kubwa sana.Taarifa zaidi za kiintelijensia zilianza kupenya nakuhabarisha kwamba majeshi ya Savanna Lands yalikuwa mbioni kuanza kusogea kuja mpakani.Hapa ilihitajika diplomasia ya hali ya juu maana muda simrefu ilitakiwa Kilua aingie vitani.Hana jeuri ya kuingiza majeshi vitani.
                                                                         ***
       Dedani alienda moja kwa moja mpaka katikati ya mji akatafuta bustani ya jiji nakuenda kuketi.Muda mfupi uliopita alikuwa amemfumania mke wake wa ndoa akizini na mfanyakazi mwenzake!Lilikuwa tishio katika ndoa yake.Bila shaka alihitajika kufanya maamuzi magumu kujua hatma ya ndoa yake.Kuna wakati alihisi haitaji ndoa tena maana tayari dosari kubwa ilikwisha ingia nakutishia usalama wake kuwepo kwenye ndoa au la!Akiwa na mawazo mengi huku ajui kipi cha kufanya.Alisikia simu ikita.Alijipekua nakuangalia akaona namba ngeni!Alishtuka sana akijiuliza ni nani?Kwa kuwa kulikuwa na migogoro kati yake na mkewe alihisi anaweza mkewe kampigia kwa namba ngeni na hakutaka kabisa kuongea naye na kama angempigia na ile yak wake bila shaka asingepokea.Alichofanya aliiikata ile namba.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
      Wakati akiendelea kuuhisi upepo wa pale bustanini alishtukia mlio mwingine wa simu ya mkononi.Akaufungua nakukutana na ujumbe wa simu.Moyo ulimwenda mbio.
      “UNATAKA KULIPIZA KISASI KWA SERAMBOVU?NJOO TUKUPE NAFASI HIYO.”alishtuka na mwili kuchichimkwa hadi malaika wa mwili wakamsimama.Atakuwa nani?Alijiuliza na vipi wamejua jambo hili?Kwakuwa mkewe ni gavana wanaweza kutumia jambo hili kumdhihaki kama njia yakuikomoa serikali kuu.Dedan akadata!Alitaka kuipotezea lakini mwisho akaijibu ile meseji,”NDIYO.”
      Japo kuna sekunde kadhaa aliona jibu lake kuwa la kifedhuli maana hawajui ni kina nani na dhamira ni nini?Wamejuaje kama ana kisasi na bwana Serambovu hadi wafikie hatua hiyo?Hakupata jibu.Lakini pia ni vizuri amewajibu kwa kuwa bila hivyo hangeweza kupata jibu la kuridhisha.Aliamua kucheza karata hiyo bila hiyana.
      “KUNA GARI IMEEGESHWA UPANDE WA KUSHOTO KWAKO NI AINA YA NOAH JEUSI.IFUATE.”meseji iliingia kwenye simu yake akaisoma.Kisha aligeuka kuangalia upande alielekezwa kweli kuna gari limeegeshwa.Picha ikamjia kichwani namna Serambovu alivyokuwa akiburudika na mkewe kwa mahaba mazito.Roho ikamchefuka akijikuta akifyinza kwa hasira kisha akainuka.Potelea mbali naenda kumuondoa mtu ubongo.Akaelekea lilipo lile gari.
     Kufika lilifunguliwa mlango alishtuka kumuona binti yake akiwa amepakatwa na mtu huku amezibwa mdomo kwa kiganja cha mkono na jitu lile.Mwili ukamsisimka!Wote waliokuwepo ndani hakuwahi kukutana nao.Alishtuka kuona akipewa alama ya kidole akiashiriwa afyate ulimi wake.Wakati aningia kwenye gari alivutwa kwa haraka kisha wanaume wenye nguvu walimkamata wakamfunga mikono na miguu kwa kamba ngumu.Kisha akazibwa mdomo na macho.
      “Nyamaza kimya kama unapenda usalama wako.Neno moja tu na mwanao hana uhai.”ilitoka amri ya kutihsa.Palepale binti yake naye akafumbwa macho nakuzibwa midomo kisha mikono ikatiwa kamba nzito.
      Hali ikawa si shwari.Gari likaanza kwenda kwa kasi ya ajabu.Tayari mume wa rais Kilua alikuwa mikononi mwa watu wasiojulikana.Waliendelea kupotea mbali na mjini.Wakiwa kwenye mwendo kasi walishtushwa na mlio wa simu ya Dedani.Wakaichomoa mfukononi nakuangalia mpigaji.
      “Shit watu wa usalama wanampigia?”alisema moja ya wale jamaa waliomfunga Dedani kamba.
    “Imekuwaje wakawahi hivyo kumpigia?”mwingine akauliza.
    “Ukiona hivyo tayari mkewe kaapishwa kuwa rais hivyo ni kawaida kwa usalama wa taifa kumlinda rais na familia yake.Watafuatilia wajue popote alipo mpaka wa mpate.Hii simu tuizime nakuitupa.”alisema bwana Kiwembe.Aliizima simu ile kisha akafungua dirisha nakuitupa nje.Dereva akaendelea kuchambua barabara!Hatari ilikuwa imeota.
    “Kiwembe kwahiyo tunawafanyeje?”
      “Hakuna atakayetoka salama hapa.Swali ni moja tu.Je,mheshimiwa rais anampenda kiasi gani mume wake na mtoto?Anaweza fanya nini kwaajili yao?Amechukua tu madaraka then kuna mahitaji mengi anatakiwa kukamilisha.How far can she go?”kengele ya hatari ikalia!


    Kuwaokoa watu wake siatatumia majeshi yake yote?”
    “Hata atumie nini sis indo wapangaji wake!”alisema bwana Kiwembe.
    “Kwahiyo mlisubiri wakati huu muiteke familia yake?”
      “Unapokuwa kiongozi wa Kiota unakuwa tayari adui wa kila mtu!”alieleza Kiwembe.
     “Aisee nyie ni shida mnamteka mume wa rais na mtoto wake wakati rais anakula kiapo.”
    “Ndiyo.Tulichotaka ni kutengeneza historia tu nasi kingine.”
      Gari lao liliendelea kukatiza barabara mpaka likafika eneo Fulani nakukatiza barabara ya vumbi nakueanza kupotelea kwenye vumbi hilo.Mwendo wa muda mrefu kiasi uliwafikisha eneo walilotaka.Kulikuwa na nyumba kuukuu hivi.Hata nje majani yalikuwa yameota kwa wingi.Bila shaka ungejua hapa kulikuwa hakuna uangalizi wa mazingira mazuri.Nyasi zilikuwa zimeota kwa wingi na bila shaka kutengenza makao mazuri kwa wadudu watambaao.Hata mende na panya walipata hifadhi ya kuishi.Yalikuwa kama mahame.Kiwembe alishusha mateka wake na kwenda nao moja kwa moja hadi kwenye jumba lile kuukuu.Alizunguka upande wa pili nakuona korido akaanza kuifuataIolibidi kamba walizomfunga Dedani zilegezwe kidogo ili aweze kutembea pamoja na za mtoto.Waliingia hadi mlango ulipo.Kusikia kwa ndani ni kama sakafu safi iliyotengenezwa.Bila shaka kwa ndani ni makazi mazuri.Mlango ukafunguliwa wakaingia ndani.Walipelekwa moja kwa moja kwenye vyumba maalum vilivyoandaliwa kwaajili yao.Hawakuwekwa pamoja jambo ambalo lilizidisha hofu kwa upande wa Dedani kujua hatma ya mwanaye.Vilevile woga ulimwingia mwanaye zaidi asijue kuna nini kinaendlea.Watu hawa walikuja kucmhukua akiwa shuleni.Walimwambia wametumwa na mamake.Huwa ni kawaida kwa mama kutuma madereva kuja kumchukua mwanaye kutoka shuleni.Na hata siku hiyo Shani alijua hao na madereva wa mama.
      Waliwekwa vyumba hivyo ambavyo vilikuwa na magodoro safi ya kulalia.Chumba cha Shani viliwekwa vitabu kadhaa pamoja na makaratasi na kalamu.Hii ilikuwa mahususi kwa yeye kuto’boreka’ pindi awapo pale ndani.Hivyo alifunguliwa mikono.Kuona baba yake pia aliingizwa kwenye gari alijua kuna afueni lakini mazingira yale yakufungwa kamba yalimthibitishia kuwa usalama wake na wa baba ulikuwa hatarini!Mama asingewatuma watu wafanye vile.Akili ya Shani ilimtahadharisha kuwa makini!
      Chumba cha Dedani kilikuwa tu godoro.Hakupewa chochote kile zaidi ya kuchwa peke yake huku kamba zikiwa zimekazwa mikononi na miguuni mwake.
      Dedani alijua aktekwa.Watu wasingekuleta kulipa kisasi huku wamekufunga na pia wamechukua mwanao.Akikumbuka mazungumzo ya wale watu akiwa kwenye gari alijua fika yupo hatarini.Hata wakatishia kwamba hawatatoka salama.Alijikuta akiogopa sana kwa usalama wa mwanaye.Pia ishu ya mkewe kuapishwa urais ilimshtua sana.Ina maana ni majukumu makubwa.Alijua muda simrefu angepata majibua halisi ya kipi kimetokea hadi mkewe kutajwa kama kiongozi.Lile jambo la mkewe kupewa ugavana na rais Kisusi lilizidi kumtafuna moyo maana alijua maisha yao yanabadilika na kuwa na chembe za siasa.Japo kikawaida GAVANA WA Kibatari hakuhesabiwa mwanasiasa kwa kuwa aliteuliwa tofauti na magavana wengine lakini ile hali ya kupokea maagizo kutoka ikulu ilizidi kumuogopesha.Inamaana siasa nzima ilichezwa na watu wa ikulu,mkewe alikuwa bomba lakupitishia mchezo wote.
    Dedani alikuwa fikra nyingi zilizowekwa kapuni kimajibu.Nani ategue kitendawili kilichopo?
                                                                          ***
    Kilua aliamua kutoa kauli maana ubishi umezidi,”Tuondokeni sasa hivi mnapotaka niende twendeni.”ilikuwa kauli ya ghfala ambayo haikutegemewa na yeyote kama ingetoka kwa Kilua.Maana aliona mabishano yamezidi.
      Mawakala waDCU 2 walishtuka.Hiyo ilikuwa ishara nzuri.Walihitaji kiongozi mwenye uimara hasa nyakati kama zile za kuwa na wasiwasi.Taifa lilihitajika kusogea mbele.
      “Well you heard the President!Let’s go!”aliamrisha kiongozi.
    Wakati wanataka kutoka Serambovu aliomba kuongoozana nao.
      “Ningeomba twende pamoja.Mimi ni chifu wake wa ushauri lazima niwepo alipo.”alijitetea Serambovu mzee wa kujitokeza.
    “Lakini huna uhakiki wetu kwamba uwe naye ikulu.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
      “Jamani RaiS Kilua ndo kwanza kaapishwa hamumjui kama mimi ninavyomjua iweje muanze kumpeleka mahali bila  uwepo wa mut wake wa karibu wakumkumpa moyo!Mimi ndo naweza hiyo kazi kwa wakati huu.Nina tajiriba ya kumshauri hadi hapo atakapopata washauri wa serikali.Mnamjua kama mimi ninavyomjua?”Serambovu alijitetea.
      “Lakini…”
    “Samahani hata sijui jina laoko?”alisema Kilua akimuagiza mkuu wa ulinzi.
      “Bila samahani mheshimiwa mimi ni agent Simon.”alijibu kwa unyenyekevu wa hali ya juu.
      “Naomba huyu bwana aongozane na mimi.Ni mtu niliyefanya naye kazi ananijua vizuri.Kwa sasa nitamuhitaji awe ubavuni mwangu.kauli ya mheshimiwa rais ilikuwa ya mwisho hakuna mwenye haki ya kuigusa hata iweje.
    “Sawa mkuu kwa amri yako.”aliitikia wakala Simon.
     Serambovu akawa tayari kando ya rais Kilua kwa mara nyingine ukawa ushindi kwake.Kamdhibiti kimapenzi na sasa atamdhibiti kiutawala.Serambovu alitabasamu.Simon alimuonesha ishara Sofi amfuate pembemeni.Akaenda kumbonyeza kwa ishu,”Hakikisha mambo yanakuwa sawa hapa mpaka utakapopata maelekezo kutoka juu.Ukiongea na mimi vizuri utapata nafasi ya kufanya kazi ikulu mrembo.”
      Sofi aliitikia kwa kichwa.
    Halafu Sera mbovu akaongeza,”Pia hakikisha mama Kilua anakuwa salama.Nitatuma walinzi walinde nyumba yake pamoja nakuwahamisha ndugu zake wote tukiwa Capital City.”
    “Ndiyo mkuu yote yako sawa.Namba zangu zipo hewani.”
       Maandalizi yakakutoka yalianza.Kilua hakujua uzito wa ulinzi wake.Maana ile wanatoka nje ya ofisi yake alikutana nakundi kubwa la polisi na wana jeshi wakiwa na silaha nzito huklu msafara wa magari ukiwa umepangana hapo nje.Mwili ukasisimka!Ulikuwa ulinzi wa hatari hakuwahi kuutegemea kama ungekuwa wa kwake hata kidogo!Alijikuta akipepesuka nakusihiwa nguvu.Ilibidi walinzi wake wamzingire nakumshikilia kwa weledi wa hali ya juu.Picha zilikuwa zikipigwa na waandishi wa habari ambao walikuwa wamepokea taarifa za kuapishwa kwake.Kila mmoja alitaka kuwa na picha moja kwa rais wao mpya hasa kwa wakati ambapo nchi imekuwa kwenye simanzi nzito.
    “Walinzi wote kuwa makini rais yupo mbele za watu.Stay alert!”alitahadharisha Simon kupitia kifaa cha sauti alichovaa kama saa.Kila akiongelea pale basi walinzi walio na vifaa vya kupokelea sauti ile walipata habari kupitia vifaa walivyofaa masikioni.Ilimpasa kila mmoja kuwa na kifaa cha kupekelea sauti masikioni na chakuongelea kilivaliwa kama saa.
      Picha zilipigwa kwa wingi.Kilua alikimbizwa haraka hadi kwenye gari maalum la rais.Kisha msafara ukaondoka kwa kasi ya ajabu.Ving’ora vilisikika huku barabara zikiondolewa magari pamoja na yeyote aliyetaka kupita.Hali ilikuwa imeivaa.Waandishi wa habari waliendelea kuripoti habari mubashara kwenye runinga.
       “Kama muonavyo wapenzi wa tazamaji gavana wa Kibatari kaapishwa bila sherehe kuchukua nafasi ya uraisi iliyoachwa wazi na hayati rais wetu Kisusi.”
      “The events of today will remain down in history after the entire government of president Kisusi was wiped out in a tragical accident.The governor of Kibatari state has been sworn in as the new president of KIOTA Republic.Shortly after the death of Kisusi’s administration,section two of the constitution was activated giving governor Kiluathe succession power to take over since none in the line of presidential succession is available that only leaves madam Kilua as the heir to the throne.”
     Ripoti mbalimbali zilizidikutamngazwa kuhusiana na taifa la Kiota.Mashirika ya makimataifa kama BBC,Aljazeera,CNN, na mengine mengi yalikuwa yakiripoti habari hizo.Tayari wanahabari wao walikuwa barabarani wakichukua picha mbalimbali za msafara wa rais Kilua akipelekwa kiwanja cha ndege.
      “As you can see the heavily guided convoy of president Kilua Tabiri is heading to the airport to take off.The president is needed at the capital to address the nation.”waadishi wa BBC waliendelea kutoa habari kwa lugha mbalimbali.Macho yalikuwa Kiota dunia nzima.Kila kiongozi akituma salamu za rambirambi.Ripoti nyingine zilisema kupepesuka kwa rais.Japo hilo kila mmoja hakuwa na uhakika nalo kwa kuwa walinzi wake walikuwa wamezingira pembe zote.Msafara wa rais Kilua ulianza kuelekea kiwanja cha ndege.Ndege ya dharula iliandaliwa kwaajili yake.Muda huo aliyekuwa ubavuni mwake si mwingine bali ni Serambovu akijitahidi kwa hali na mali kumpa moyo.Kilua alikuwa kimya asijue analotakiwa kufanya.Maana ulinzi uliokuwepo kwaajili yake hakuutegemea.Japo alikuwa kiongozi wa serikali lakini hakujua uzito wa kuwa rais ni nini haswaa?
      Baada ya muda mchache waliwasili kiwanja cha ndege.Kulikuwa na takribani gari arobaini zikiwa zimegawanyika kimakundi mbalimbali ya kiusalama.Lengo likiwa kuhakikisha ulinzi wa rais upo imara.Ikiwa ndo Kilua anashuka kwenye gari tu,ghafla milio ya risasi ilisikika.Walinzi walitaharuki nakukimbilia kumzingira rais wao.
      Kila mlinzi alikuwa akielekeza macho upande wake akitaka kujua ni wapi mlio huo unatokea.Bila shaka aliyekuwa akifyetua risasi alikuwa ni mtaalamu mdunguaji wa uhakika.Maana risasi zilipigwa vituo takribani tatu!Ya nne ikapita kando ya sikio la Kilua.
      “Kila mtu awe makini!”Simon kiongozi wa kikosi alihabarisha akitafuta mahali sauti inapotokea.
    “Mzingireni rais!”alitoa amri.Walinzi tayari walimuweka kati rais wao!Kilua alikuwa na Serambovu aliyemshika mkono pamoja na jaji Polepole.Watumishi wengine wa serikali walikuwa umbali kidogo.


      Walinzi wa raais kikosi cha DCU2,walisimama kwa umakini.Kila mmoja akikumbuka mafunzo .Lilikuwa tukio gumu na lililohitaji ukomavu wa kiakili.Hapa ilikuwa kufa kupona lakini kiti cha urais kisitingishwe dakika chache baada ya rais mpya kuapishwa.Waandishi wa habari waliokuwa wameongozana na msafara walianza kusambaza habari maeneo mbalimbali.Ndani ya muda mfupi ikajulikana kwamba msafara wa rais umevamiwa akiwa tayari kiwanja cha ndege kuelekea mji mkuu!


     Tukio lakuvamiwa kwa msafara wa rais liliwafanya walinzi wawe macho!Kilua alihisi mkojo kutaka kumtoka!Hiki ndo kiapo alichoingia muda mfupi uliopita.Kuilinda nchi wakati kachagua kifo!Iweje wa vamiwe kwa haraka kiasi hiki.
    “Kuna mdunguaji zaidi ya mmoja kila upande ufanyiwe uangalizi.”alisema Simon.Wakiwa wanakagua maeneo yote wakagundua kweli kulikuwa na zaidi ya mdunguaji mmoja.Miguu yao ilikuwa tayari na mikono ikiwa imeshika silaha tayari kurudisha mashambulizi.
    “Weka ngao kwa rais.”alitoa amri agent Simon.Kichwa chake kilifanya kazi mara mbili maana tayari kuna hatari imetokea mbele ya rais wao.Hatari ya maisha yake.Lazima kwanza atulize tatizo hilo halafu pili mkuu wa nchi aondolewe eneo lile.Kupanda ndege ni hatari huwezi jua kama hawa wadunguaji wameweka bomu au nini?Pili lazima atengeneze njia ya rais kuondoka.Hajui kama alipotoka pako salama au la?Hiyo ilionesha wameingia eneo ambalo lilikuwa hatari kwa usalama wa rais.Ina maana hawakufanya maandalizi ya kutosha kwamba angeingilia wapi na angetokea wapi kama kungekuwa na hali ya hatari?Hilo lilikuwa kosa kubwa la kiintelijensia kwa upande wao.Lakini pia hawakujua kama maisha ya Kilua yalikuwa hatarini.
      Hapa walianza kukumbuka mabishano walipokuwa ikulu kuhusiana na nani achukue nchi ina maana chuki zimeanza kuonekana waziwazi kwa Kilua?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
      Paaa!Paaa!Paaa!Risasi zikaanza kumiminika na vile zilikuwa na viwambo vya kuzuilia sauti zilifanikiwa kuwajeruhi walinzi kadhaa!Ndo kwanza Agent Simon akakumbuka hawakuwa wamempa rais Kilua kifaa cha kuzuia risasi!Huo ukawa uzembe mwingine.
    “Nani ana bullet proof?’’aliuliza Simon.Mmoja wa walinzi akaivua ile anampa Simon risasi aliyofyatuliwa na mdunguaji ilikuja moja kwa moja kumpiga kifuani ikawa imemtoboa!Ilimuua palepale!Simon alichanganyikiwa lakini akajikaza akikumbuka mafunzo hata iweje maisha ya rais kwanza.Ilibidi kwa haraka sana ampe Kilua lile vazi lakuzuia risasi alimvalisha mwenyewe.
    “Mheshimiwa vaa hii.”alisema kwa haraka huku akimvalisha.Kilua alisali sala zote alizojua.Baada ya kumvalisha aliendelea kuangalia.Maana wadunguaji wa kimya walikuwa wanategea.Hawakuwa na haraka.Walitaka kuwazubaisha.Simon akajua hatua ya kuondoka ilitakiwa kufikiwa ndani ya muda mfupi ujao.Na kama wangeanza kusonga basi kuna uwezekano wadunguaji wa kimya wakatumia fursa hiyo kuwalenga na risasi.Na hapo situ rais atakuwa hatarini bali walinzi wa zalendo watakuwa hatarini vilevile.
      “Mungu ukinisaidia kutoka hapa naahidi sizini tena na Serambou.Nisamehe eeh Mungu.”Kilua alijiseme kimoyomoyo huku akiukandaamiza mkono wake kwa mkono wa Serambovu.
    “Tumrudishe rais kwenye gari haraka.”wakasogea kwenye gari la rais nakumuingiza pamoja na jaji Polepole na Serambovu kisha wakaliwasha kwa haraka.Magari mengine ya kuongoza madereva wake waliingia nakuanza kuyaondoa.Huku vikosi vya polisi na wanajeshi wakianza mapambano na wadunguaji wale.Milio ya risasi ilisikika kwa wingi.Fujo ikatokea.Tayari rais alikuwa kwenye gari wakaanza kuondoka kutoka eneo lile.Ilikuwa haraka sana!Ndani ya muda mfupi eneo lote lilikuwa limechemka kwa milio ya risasi.Polisi walifyatu risasi hovyo kuwazuga wadunguaji wakati msafara wa rais ukiondoka.Tayari taarifa zilifika kwenye makao ya jeshi ya nchi na ikulu kuhusiana na uvamizi ule.
       “Mheshimiwa nahitaji uwe jasiri.Hii ni vita nina uhakika ajali ya leo iliyoondoa serikali nzima haikuwa ajali ya kawaida.Bado watu wako kazini.Inatakiwa utangaze hali ya hatari.”alishauri bwana Simon.
    “Kwani kuna nini ambachosielewi?”Kilua aliuliza kwa woga.
      “Wewe ndo rais wa Kiota naomba uwe jasiri.Nchi haipo sawa.Sijajua kwanini wavamie masafara wako.”
    “Jamani siwataniua?”Kilua aliuliza kwa hofu.
    “Labda niwe maiti lakini kadri ninavyopumua hakuna kidudu mtu wakukugusa.Wewe ni wetu.”alihakikisha Simon kwa uimara.Tayari vikosi vya kijeshi vilikuwa wima kulinda.
    “Tunaenda wapi?”Kilua akauliza.
      “Tunaelekea kambi ya jeshi.Tukifika huko tutaagiza helkopta ikuondoe hapa.Inaonekana kuna pingamizi la wewe kufika ikulu ukiwa salama.Lakini utafika tu.”
      Wote walipigwa na bumbuazi.Kulikuwa na mabishano huku simu zikipigwa kila kona.Tayari hatari mpya imetangazwa.Lakini wakati wanaendelea na mazungumzo yale akili ya Simon ilishafanya mahesabau mengine kutafuta njia mbadala.Walioandaa uwanja ni kina nani?Alijiuliza?Bila kupata jibu.Lakini ghafla akasema msafara usimame.
    “Simameni.”msafara ulisimama.Simoni akamwambia rais Kilua,”Naomba uniamini rais wangu.Nataka turudi uwanjani.Huko huko tutapanda ndege sina imani na njia hii.”Tutafanya mchezo wasijue kama wewe upo kwenye huu msafara.”
      Kilua alikubali shingo upande.Rais alibadilishwa gari lingine kisha wakaenda moja kwa moja hadi mjini huku dereva wa gari lake akikwepa magari mengine kuliacha la kwake liwe la mwisho halafua wakalifanya kama ni mwananchi wa kawaida gari lake likapita njia za mkato kurudi kiwanja cha ndege.Wakati haya yakitokea ule msafara ulivamiwa tena kwa kutegeshewa misumari barabarani hali iliyosababisha gari kadhaa kupinduka.Ndani ya gari hili alimokuwamo Kilua walikuwa watu wa chache.Ila wakuu ni Rais Kilua,Jaji Polepole na chifu wa ushauri bwana Serambovu!Walirudi kiwanjani kama watu wa kawaida.Kilua alipishwa milango ya siri.Hata uhakiki wa pale mapokezi hawakuufanya.Walienda moja kwa moja hadi ofisi za meneja mkuu wa kiwanja nakujificha humo ndani.Katika msafara uliopoteza mwelekeo taharuki ilizuka baada ya kubaini uwepo wa rais Kilua haukujulikana yupo wapi?
      Taarifa yakutojua alipo rais Kilua zilianza kusambaa kama moto nyikani.Huku ukaguzi wa mwanzo ukiwa sintofahamu.Lakini Simon aliwapa ishara walinzi wake waweke siri uwepo wa rais Kilua.Hivyo waliobaki kwenye msafara ule walijifanya nao hawajui rais yupo wapi?Ikatafsiriwa labda katekwa na katika msafara wakahisiwa kuna wasaliti.Lakini Simon alikuwa tayari sehemu hatari kuliko zote.
                                                                          ***
       Ikulu
      Director Masha alikuwa na wakati mgumu sana.Chumba kilizidi kuchemka baada ya kujulikana msafara wa rais kuvamiwa.Lilikuwa tukio la kuogofya sana.
    “Ndiyo maana tulisema mtupe presidential protection unit kazii hii.Sasa nyie washenzi mnashindwa kumlinda rais hadi anaingia mikononi mwa adui!’’sauti ilitoka kwa bwana Shezadu kamanda wa ukinzi wa rais.Alimtupia lawama bwana Masha.
      “Kamanda kumbuka nina vijana wangu pale wamepoteza maisha.Hakuna aliyejua kama kuna kundi baya.”alijitetea Masha.
      “Hakuna cha what?Wewe umefanya uzembe hamkufanya uhakiki njia zote ambazo angepita rais.”Kamanda Shezadu na mtu wa maneno.
     “Mnampelekaje raise neo la wazi bila kuwa na uhakiki wa kutosha?Ulitakiwa ufanye uhakiki.”
    “Kamanda nakuheshimu niache nifanye kazi yangu vijana wangu watamrudisha.”alijitetea Masha akiwa anatweta kwa wasiwasi.Haijawahi kutokea DCU 2 wakavamiwa.
    “Hivyo nani ana kaimu nafasi yake sasa.Kwanza rais kapotea mpaka sasa.”
                                                                     ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
      Kibatari kiwanja cha ndege
      Chumba cha meneja kilikuwa na ugeni mkubwa wa rais Kilua.Wakati huo Simon alipiga simu nakuita vijana wengine DCU2 waje watoe msaada wao.Kila wanapoitwa hepewa signal maalum kupitia vifaa vyao muhimu ambavyo huwa na namba ambazo inatakiwa mhusika afanye mahesabu Fulani ili aweze kupata jibu.Ndani ya dakika kumi na tano uwanja wa Kibatari ulijawa na mashushushu wa DCU2 kila kona.Wao kazi yao kubwa ilikuwa ikutafuta namna rais atakapotoka.Simon alichukua uamuzi huo akizingatia hana wa kumuamini kabisa.Alitaka kujua usalama wa rais hauchezewi na mtu yeyote.Makamishna wa polisi wa jimbo la Kibatari waliwasili uwanjani hapo na vikosi vingi kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama.Lakini hawakuwa na habari kwamba eneo hilo tayari rais Kilua amerejea na yupo ndani ya ofisi ya meneja wa kiwanja hicho.Meneja aliwekwa chini ya ulinzi wa Simon ilikulinda usiri wa uwepo wa rais Kilua.
    “Simon kwa hiyo nitakuwa hapa mpaka muda gani?”aliuliza rais Kilua.
      “Tutatoka na ndege lakini kabla ya kutoka nataka polisi wa fagie eneo lote kuondoa hatari.Pia mashushushu wetu wanapitia eneo lote.Najua uamuzi wangu utafanya wakubwa wangu wa kazi wanakalie ngumu.Maana mpaka sasa hakuna polisi anayejua kama upo hapa.Ni mimi na watu wa chache sana.Nikisema upo hapa nitavuta attention kubwa kwa watu.Hivyo kupelekea maadui kutaka kuja karibu”
    Rais Kilua alitingisha kichwa kumuelewa,”Ok.”
    Bumbuazi la mshtuko kuwa rais bado halijafutika kichwani mwake.Bado matukio ni mengi sana.Inatakiwa awe ikulu muda ule.
    “Kuwa jasiri Kilua.Pamoja tutashinda hili jambo.”Serambovu alimuhakikishia kumpa moyo.Muda huu yalihitajika mambo mengi yafanyike kwa haraka.Nchi ilihitaji muelekeo.Wakiwa pale kuna ujumbe ukaingia kwenye simu ya Serambovu.Mwili ukasisimka.Kilua aliona mshtuko huo akaona ngoja niulize?
    “Kuna nini?”
     “Kwa data nilizopata nikuwa majeshi ya Savanna yamerusha ndege zao za kivita na tayari zimeanza kupita karibu na anga letu!Hii ni hatari maana hatujui atashambulia sasa hivi au ata shambulia saa ngapi.Tukipigwa lazima tujibu.Halafu jiandae kisaikolojia very soon utatakiwa kuamrisha majeshi ya Kiota kuingia uwanja wa vita!”sauti kavu ya Serambovu ilisema huku akiwa na umakini wa hali ya juu.
      Kilua akameza mate kulainisha koo lake.


      Simon alianza mawasiliano yakutafuta njia yakutoka.Aliomba ndege yakuondoka lakini amri ilitoka kuwa hakuna ndege yeyote itakayo ruhusiwa kuruka kutoka kiwanja hicho.Jaribio la kumvamia rais muda mfupi kabla hajaondoka limefanya anga la Kibatari kufungwa.Makamishna wote waligoma kuruhusu!Jambo hilo likamfanya atumie akili nyingine ambayo hakuitaka na hiyo ilikuwa kuwa taarifu wa  Makamishna wa polisi kuwa rais yupo pale anatakiwa aondoke muda uleule kufika mji wa Capital.


    “Mheshimiwa nahitaji msaada wako.”alisema Simon akimueleza Kilua.
      Kilua hakujua kwamba kuwa rais upo juu ya mengi hata wakati mgumu ambao wewe unalindwa bado utahitajika kutoa maamuzi.Hapa yeye ndo mhitaji wa ulinzi lakini bado anatakiwa kutoa uamuzi magumu.
    “Upi?”alijibu Kilua akiwa haelewi chochote.
       “Nahitaji  uamuru makamishna  wa polisi waruhusu tutumie anga.Wewe pekee ndo unaweza kufungua anga tukalitumia kwa usafiri kwa amri yako.”
    “Kumaanisha?”Kilua alikuwa bado hajaelewa.
    “Ana maanisha toa oda.”Serambovu alihabarisha.Kilua alitikisa kichwa kumuelewa.Serambovu alielewa mshtuko wa Kilua,”Toka sasa maagizo mengi yatatoka kwako.Hatua zote za Taifa zinatoka kwako.Kuwa jasiri ili dira ipatikane kutoka kwako.”
    “Ok.Niitieni huyo kamishna.”alisema Kilua.
       Ilibidi Simon atume watu wake.Makamishna waliokuja pale wakaja mara moja.Wote hawakujua kama Kilua yupo eneo lile.Walikuja nakumkuta chumba cha meneja.Walipomuona nakumtambua pamoja akiwa na jaji mkuu mheshimiwa Polepole walijikuta wakisimama wima.Wengi wao hawakuwa wamekubali huyu msichana kuchukua nchi.Hivyo kuna ambao walitoa heshma feki.
    “Ndiyo mkuu.”moja ya makamishna alitamka kwa ukakamavu.
    “Nataka ndege yakuondoka nayo kwa haraka.”
    Kamishna Lupogo akasema kwa ukakamavu,”Ndiyo mkuu.Ndege ipo.”
    “Vizuri nataka muda huu niwe hewani kuelekea ikulu.”
      “Sawa mkuu.Ndani  ya muda mfupi tutakuwa tumekamilisha kuhakiki eneo lote kiusalama.”alisema Kamishna Lupogo.
      “Hapana nina hitajika kwa sasa.Sina muda wa kungoja.”alisisitiza Kilua.
      “Ila…”alitaka kusema kitu Simon lakini muda ulikuwa umeenda.Alipotezea.Pengine isingekuwa na umuhimu kila mara kutoa wazo Fulani.Bora waondoke wakishatoka eneo husika.
    “Kamishna rais ana hitaji kuondoka sasa hivi.”aliongezea Serambovu.Kama kawaida yake yupo ukurasa wa mbele katika kila jambo.Tayari kesha vamia kama mshauri wa rais.Kitengo ambacho kama hajadhibitiwa maapema utakuja kuwa na msukumo mkubwa sana kwenye maamuzi ya kitaifa.Na yeye  ni mtu aliyetamani sana kucheza kwenye ulimwengu wa siasa.Sasa nafasi ya bosi wake ambaye ni hawara yake imekuwa kubwa kiasi cha kumpa nafasi kucheza ngoma ya kibabe.Na kwa mwanya huu lazima awanyoroshe wote waliombeza.Kulikuwa na hali kadhaa mikononi mwao.Ambazo zili hitaji amri kutoka kwa rais.Lakini mpaka muda huo Kilua hakuwepo ikulu.Na haitakiwi ofisi ile ikae bila mtu wa kuiongoza.
      Ndege ya dharula iliandaliwa kwa mheshimiwa Kilua kuwasili mji mkuu wan chi.Na mpaka muda huo bado Kilua hajajua wapi familia yake ilipo.Hilo lilikuwa mbali hasa ukizingatia kuna ugeni mkubwa sana kati yake na mumewe.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
      Ndege ilikamilika baada ya wana usalama kuridhika na hali ya usalama na kuhakikisha kiwanja cha ndege si hatari japo walifanya kwa haraka lakini pia kulikuwa na hatari ya kuwepo mapigano.Ndani  ya dakika hamsini ndege ilikuwa hewani kuelekea mji wa  Capital.Wakiwa hewani huku zimebaki kama dakika arobaini watua uwanja wa Kisusi International Airport ilibidi ndugu yetu Simon avunje ukimya nakutoa habari uwanja huo kwamba wanamtegemea kiongozi wa taifa aliyeapishwa muda mfupi uliopita na ambaye inasemekana alitaka kuuawa!
        Kisusi international Airport hali ilikuwa ya huzuni  kwa kuondokewa na viongozi wao wakitafuta.Uwanja huu ulikuwa bize kwa maana ndege zilianza kuingia kwa watu mbalimbali wakija kwaajili ya msiba.Baada ya kufanya mawasiliano ya uhakika ilibidi kiwanja kizuiliwe kwa muda na ndege nyingine kugeuziwa mwelekeo ilikuruhu mkuu wan chi bibi Kilua Tabiri atue.Mabadiliko hayo yaliwa shtua wengi.Ila kusikika kuwepo kwake kuna ambao walishukuru rais wao kuwa salama.Wapo ambao hawakumtaka hasa kwa kudharau jimbo hilo.Mchanganyo huo wa kimajimbo haukukwepeka ni kama kansa ilioanza kutafuna fikra za watu.
      Wana usalama wa ulinzi wa kiti cha urais waliandaa msafara mrefu kutoka uwanja wa ndege kwa kumpitisha rais wao mpya.Japo ilitokea mabishano kiasi wengine waligoma kufunga barabara kwaajili yake.Mwisho wakaamua kutofunga barabara hasa kwa viongozi wa usalama waliokuwa na jukumu lakumfungilia njia.
      Ndege ilitua uwanja wa ndege wa Kisusi airport mchana huo.Ulinzi uliimarishwa.Wakati Kilua anafika eneo hilo akitoka kwenye ndege akapokelewa na walinzi wa rais.Hakuona viongozi wa jeshi wakubwa.Lakini hakutilia mkazo bado kichwa hakikuwa sawa.
      Ving’ora vilianza kulia punde tu alipotoka kwenye ndege.Walinzi wapya wa presidential protection unit walimfikia nakumzingira.
     “Mheshimiwa mimi ni Ditu ndo chifu wa ulinzi.Tuko hapa kukuhakikishia usalama wako.Kwaanzia sasa kila kitu kuhusu wewe tutakishughulikia sisi.”
      “Asante bwana Ditu.”Kilua alijitahidi.
      Akaingizwa kwenye gari na safari kwenda ikulu ikaanza katika msafara mkubwa.Barabara zilikuwa bize hivyo ikawalazimu Kilua na timu ya wenzake kuanza kwenda kwa kasi nakuondoa magari iliwapite.Kilua kila alikopita aliona watu wakiwa katika huzuni.Alikuwa na majukumu makubwa sana yanayomkabili.Mwili wake hakuwa sawa bado.Alihisi kama kuna usingizi mzito unaotaka kumuandama na alitamani sana kupumzika.Bado ni kama hajafikiana na wazo la kuchukua madaraka.Aliapa pengine kwakuwa ilibidi afanye hivyo ili asipingane na sheria.
      Msafara ulifika makazi husika ya ikulu huku baadhi ya viongozi wa usalama waliobaki hai wakiwa tayari kumpokea Kilua.Ving’ora vilisikika vikiingia maeneo ya ikulu kwa haraka.Mambo yote yakasimama huku wakimngoja rais mpya.Kuwepo kwa kiongozi hasa wakati ambapo serikali nzima ilifukiwa kwenye ajali mbaya kule uwanja wa uhuru lilikuwa jambo lenye kutoa mwelekeo na tumaini kwamba siyo vyote vimekufa.
      Kufika kwake ikulu ni mwanzo wakuchukua hatua nyingine.Kuna mengi yanahitaji majibu muda hii ili nchi ianze kudili na mabo yaliyojiri siku hii.Kliua alishuka kwenye gari huku makamanda wa usalama wakiwa wima kumpa saluti kiongozi wan chi nafasi ya heshma.
      Kilua hakujua kama madaraka ya heshma japo wapo wapingaji lakini heshma ya madaraka ni kubwa sana.Saluti zikapigwa wakimpa heshma yake.Ilitakiwa wimbo wa taifa upigwe punde atakapoingia lakini jambo hilo wapo waliolipinga hasa wale walio katika mzunguko wa serikali wakiwa hawana imani na mwanamke huyu.Hivyo alijikuta akitikisa kichwa kupokea heshma yao.Kilua akasogea akielekezwa kwenda ndani.
      “Madam twende huku.”alielekeza moja watumishi wa ikulu.Kilua akafuata huku Serambovu akiwa nyuma yake.Alipelekwa moja kwa moja hadi kwenye ofisi yake kwanza.Akiwa pale ndani alikuta kuna baadhi ya watumishi wa serikali wanamngoja.Wote hawakuwa sawa.Walikuwa na mashaka.
      Akaoneshwa kiti akaenda na kuketi.
    “Mheshimiwa unahitajika kutoa amri kwa vikosi vya jeshi kuingia mtaani.”
      “Mheshimiwa unatakiwa kuanzisha tume ya uchunguzi kwa jambo hili?”
    “Mheshimiwa unahitaji kupandisha viwango vya utayari vya usalama haraka sana.”
      “Mheshimiwa unahitajika kuandaa timu ya kushughulika na msiba huu wa taifa!”
      “Mheshimiwa tumepata taarifa za kiintelijensia kwamba majeshi ya Savanna lands yanajiandaa kuja mpakani mwetu.”
      “Mheshimiwa unahitajika kutuma ujumbe kwa balozi zetu zote zilizoko kwenye mataifa huko  duniani.”
    “Mheshiwa familia za waliofiwa zinahitajika kukusanywa.”
    “Mheshimiwa unahitajika kutoa hotuba kwa taifa.”
      Kila mmoja alipeleka malalamiko yake wakimtaka Kilua kutoa majibu.Mahitaji yote yalitegemea majibu yake kwa haraka ili nchi isonge mbele.Bimkubwa alibaki kutumbua macho asijue anaanzia wapi?Meza ilisheheni shida zinazohitaji kauli ya rais.Wakati mabishano yanaendelea Kilua aliamka,”Jamani…jama…”kabla  hajakamilisha kauli alijikuta akipepesuka nakuanguka mpambe wake alimuwahi nakumshika.Wote walioko pale wakaanza kuwa na wasiwasi.Yaani mara ya kwanza tu kuingia ikulu anaanguka ataweza kweli kuongoza nchi?Ilibidi daktari aje haraka iwezekanavyo nakuanza kumshughulikia.
      Kila mtu aliwaza lake.Kuanguka hovyo kwa mheshimiwa walianza kuhofia afya yake na kama ataanza kutoa huduma yake ipasavyo.Daktari  alicheza kete zake Rais akawa sawa.
     Ilibidi Serambovu aingilie kati kutuliza ghasia,”Jamani hatuwezi kusema mambo yote kwa fujo huyu ni binadamu lazima tutumie busara kuzungumza naye.Kila mtu ana mahitaji yake yanayotegemea amri ya rais.Wote tupo katika wakati mgumu.Tusiufanye wakati kuwa mgumu zaidi kwa mheshimiwa.Mpeni uwanja mzuri aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo!Tuwe wastaarabu jamani!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
      Watu wakatulia,”Ok jambo la kwanza la muhimu nikuhakikisha nchi inatulia kwa wakati huu tusiwape wananchi wetu presha.Msiba lazima upangwe.Kamati ya kusimamia misiba yote nitaandaa mimi.Maana kuna watu wengi wamepoteza maisha na wote ni viongozi wa Serikali na waliokuwa pia.Lakini kabla ya yote tunataka ripoti ya waliopoteza maisha majina yao.Halafu familia zote zipewe taratibu ya msiba kwamba serikali itasimamia kila kitu.”alikuwa ni Serambovu akipembua kauli mwelekeo.Ilikuwa kama yeye Serambovu ndo anaendesha kiti kile.Muda huo wote Kilua alikuwa kimya huku akisikilizia matibabu ya daktari!
      Wakati wakiwa pale kuna simu iliingia lakini ilimtaka rais mwenyewe apokee!


    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog