Simulizi
: Kombora Kiotani
Sehemu Ya Pili
(2)
Simu ilisisitiza sauti ya rais
inahitajika kuwepo hewani.Baada ya mabishano sana wafanyakazi wa ikulu wa idara
ya mawasiliano walikubaliana simu hiyo ipokelewe na rais
mwenyewe.
“Rais apewe kama mpigaji anavyosisitiza.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Lakini hajatuambia
yeye ni nani kwa sasa rais ina kikao na watu muhimu wa taifa sasa umpe simu
nikumuondoa kwenye umakini wa kazi.”
“Kumbuka mpigaji
alivyosema.”wakati wanabishana simu ikapigwa tena.Ilibidi ipokelewe na moja
walio ikulu.
“Halo Ikulu hapa?”
“Nimesema nataka kuongea na
rais haraka iwezekananvyo mpe simu niongee naye.”sauti ya upande wa pili ilisema
kwa kujiamini.Ndiyo wakati kama ule wangepokea na wameshapokea simu kadhaa
lakini hii ilikuwa ya kipekee na katika zote walikuwa wamepewa maagizo
wayafikishe kwa ngazi husika ila hii ilihitajika kumpa mheshimiwa mwenyewe
apokee simu.
“Ndugu rais kwa sasa hawezi kupokea simu yoyote anakikao
muhimu.”alisema wakala Yule wa ikulu.
“Hicho kikao hakina umuhimu
wowote kama ujumbe nilio nao kwa sasa.’’sauti ya upande wa pili
ilisema.
“Unaweza kuniachia ujumbe nitaufikisha ndugu kwa
mheshimiwa.”
“Wewe ulivaa tai ya samawati nakwambia mpe simu bosi wako
sasa hivi!”sauti ilikuwa kavu ya kujiamini.Wakala wa ikulu akasisimka
alipotajiwa rangi ya tai aliyovaa.Ina maana huyu mtu anamuona kila anachofanya
kutoka huko alipo?Jamaa akaogopa sana.Na kama anamuona si huyu mtu atakuwa yumo
hapahapa.Alijaribu kupepesa macho huku na kule lakini kila mtu alionekana yupo
bize na shughuli zake.Wakala Matibwa alichanganyikiwa.
“Kwani
unaniona?”wakala akauliza.
“Umevaa miwani ya macho!”alipotajiwa hilo
akashtuka au ni mtu wa usalama nini?Lakini wao huwa na mtandao maalum
kupiga.Lakini inakuwaje anamuona!
“Halafu mwanao yupo Green Academy
leo hajaenda shule kwa sababu ya sherehe za uhuru!Anavaa sare ya kahawia.Leo
asubuhi ulimgombeza kwa kuwa alikuwa anaangalia runinga badala ya kufanya
mazoezi ya hesabu ulizompa!”sauti ya upande wa pili ikaongeza tena.Mpaka hapo
Matibwa akajisalimisha.Huyu anayepiga atakuwa mkubwa Fulani.
“Sawa
mkuu namwambia sasa hivi.”
“Jambo hakikisha rais anapokea simu
mwenyewe.”
Matibwa aliamka kwanza akaunganisha simu ile na simu
iliyopo mezani kule rais alipo.Halafu akainuka mwenyewe.Alienda moja kwa moja
hadi ofisi ya rais akafungua mlango.Hakujali waliomshangaa mana kikao kama kile
hakihitaji mtu kuvamia kwa ghafla.Alinyoosha hadi alipo
rais.
“Mheshimiwa naomba kuongea na wewe.”alisema kwa ustaarabu lakini
ukimwona uso utajua fika hakuja kwa mzaha kulikuwa na jambo la umakini
sana.
“Kijana unaona tupo kwenye kikao muhimu unaingia tu!Nani kakupa
ruhusa?”Serambovu alianza kushambulia.Watu wote kwenye meza hawakupendezwa na
namna Serambovu alivyomshambulia kijana Yule.
“Samahani mkuu lakini
imebidi kuna jambo la dharula.”alijitetea
“Kwa hiyo tunachofanya hapa
ni upuuzi?”
“Hapana mkuu.Nisingekuja hivihivi naomba niongee na
rais.”
“Hapana wewe huna adabu unadhani mamako ndo mwenye ofisi watu
tupo kwenye ajenda za taifa wewe unaleta ujuaji?”Serambovu akawa
anashambulia.
Kilua alimhurumia Yule kijana.Ilibidi aingilie,”Hebu
muacheni niongee naye.Kijana unaweza sema jambo lako.”Kilua alijibu kwa
upole.Watu wakanyamaza.Kijana alisogea karibu na Kilua kisha akainama kuonesha
jambo lake lilikuwa la siri sana.
“Kuna simu nimeonganisha naomba
upokee.Ni dharula tafadhali madam nakuomba.”alikuwa kama anabembeleza kiasi
huwezi kumkatalia.Ilibidi Kilua amdadisi kisha akatoa uamuzi.
“Ok sawa
nitapokea naomba uendelee na shughuli zako.”maneno ya rais yalikuwa ya utulivu
hali iliyomlainisha Yule kijana kutokana na kugombezwa na Serambovu.Kijana
alitoka mle ndani kwa hesma.Japo Serambovu alitaka kumshambulia tena lakini
Kilua alimpa ishara ya kutuliza mmunkari.
Kilua aliwaangalia watu wote
kisha akasema,”Maelekezo yangu ni haya.Kamati ya msiba iandaliwe haraka
iwezekanavyo.Najua sote tuna hofu lakini hiyo haisaidii.Nataka kamati ya msiba
huu.Ila kila familia iulizwe ikiwa wanataka msiba wa pamoja au kila mmoja
anataka msiba ufanyike kwa mapenzi yao.”
“Hapana!Ninaweka pingamizi
amri iwe moja msiba uwe wa pamoja!”alianza Mambosasa.
“Una hoja ya
kueleza?”Serambovu alidakia.
“Ndiyo sikubaliani na wazo la kufanya
misiba kila mtu kivyake bora ifanyike kwa pamoja.”
“Ndugu mheshimiwa
hakumaanisha kwamba itakuwa hivyo ni wazo tu alitoa.”
Watu wote
wakabaki wanatizamana.Kuna ambao walijua mbio za Mambosasa nikutaka kumpanga
mheshimiwa anavyotaka yeye.Tayari wapingaji kama Mambosasa walianza kujitokeza
waziwazi tayari kumpelekesha Kilua hili lilikuwa swala la msiba lakini bado kuna
ambao wanaona uamuzi wake kama haufai.
“Hata kama kumbuka hawa ni
viongozi wataifa lazima wapewe heshma yao nchi ijue kuwa ni kina
nani?”
“Hilo jambo halikuwa na mjadala kamati itaandaliwa.Na tena
napendekeza wewe bwana uwe mwenyekiti.”alisema Kilua nakumkata kauli yoyote
yakipinzani.
“Sawa mheshimiwa.”alijibu kwa adabu Mambosasa kuona
ameanza kuonekana na mheshimiwa!
“Hilo jambo la msiba tumemaliza
kamati iatapanga kila kitu.Ila ikulu itakuwa na jukumu la kupokea wageni kutoka
nje watakao kuja kuhudhuria msiba.Viongozi wengi watakuja hapa
kutupokea.Tafadhali tuwe tayari.Naomba tuamie kwenye ishu nyingine.”alisema
Mambosasa.
Wote walikuwa wakiandika vitu kwenye mafaili yao.Mkutano
ulikuwa na hali ngumu sana.Kilua alikuwa anaangaika kukabiliana na mabwana
wale.
Lakini akakumbuka kuna simu aliambiwa apokee Kilua akachukua ile
simu mezania.
“Halo?”
“Sikiliza mheshimiwa najua
umevaa…”sauti ilisema na ikimtajia aina ya mavazi aliyovaa na kiti alichokaa
kisha ikamtajia majina ya watu wote waliopo pale mezani.Kilua
akasisimka.
“Mheshimiwa najua kila kitu hata ukitema mate hapo ikulu
najua.Nikiasi cha kubofya tu kitufe then nakufuta.Kuna kitu nataka kutoka
kwako.”
“Kitu gani?”Kilua akauliza kwa woga.
“File na
13:14.”sauti ilisema kwa kujiamini.
“Sijui hilo faili linahusu
nini?”Kilua alisema.
“Nimesema file 13:14.Wewe ni rais lazima utajua
hilo file.Kingine usimwambie kila mtu chagua watu unaowaamini ndo uwaulize
kuhusu hilo file!”sauti ilisema nakukata simu!Kilua akaduwaa!Ni faili gani
hilo?Kilua aliangalia meza nzima akiwa hajui aanzie kwa nani.Huyu bwana kampigia
simu kamtajia mavazi aliyovaa kamtajia hadi majina ya watu wote waliopo hapo
mezani kumaanisha anajua kila hatua.Kingine kuambiwa kwamba lazima achague mtu
wakumuuliza kuhusu faili hilo ilikuwa tishio tosha kwa upande
wake!Akashtuka!
“Mheshimiwa?”Serambovu aliita baada yakuona Kilua
amemaliza kuzungumza na simu lakini akili yake haipo kawaida kabisa alikuwa
mbali kimawazo.
“Naam?”
“Kuna swali hapa tunataka kujua
kiwango cha utayari wa usalama!Hebu kuwa toa tamko lako.”
“Tunaenda
rangi gani?”
“Kwani hiyo ndo nini?”akauliza Kilua.Viongozi waliopo
pale wakacheka kimoyomoyo yaani hajui hata viwango vya usalama alikuwa gavana
wawapi?Angejua hata kimoja tu.Bure kabisa!Kutokujua jambo hilo ni kama dhihaka
kwa kiongozi tena wa taifa kama huyu.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni viwango vya
usalama vipo vitano.Yaani Defensive Readiness Condition kuna moja mpaka
tano.Tukianzia ya tano kurudi mpaka moja.Ya tano ni utayari wa kawaida.Lakini
ukifika moja hapo huwa ni hatari zaid.Kwa sasa tunaweza kwenda ya
kwanza.”alishauri Mambosasa.
“No ya kwanza tuna vibali gani?Kwanza
hatujawahi kufikia kiwango hicho tangu uhuru.”alisema moja ya waliopale kwenye
mkutano.
“Tunapaswa kufikia hiyo kwani tayari majeshi ya Savanna Lands
yamerusha ndege zao kuja mpakani mwetu tukichelewa kidogo tu tutapigwa mchana
kweupe!”
“Hapana kumbuka kuna viongozi wa mataifa watakuja kuhudhuria
msiba sasa tukipeleka viwango vya usalama Defcon 1 my friends hakuna kiongozi
wanje atakayetia mguu wake hapa!”alishauri mwingine.Wakati mabishano yanaendelea
rais alikuwa ameshapokea vitisho vya aina mbili.Moja alitaka kuuawa muda mfupi
baada ya kuapishwa.Pili anapigiwa simu nakuambiwa maelezo kumhusu yeye ina maana
tayari kuna mtu anamuona pale ofisini.Jengo la ikulu si salama tena kwake maana
kila hatua inaonekana hata akitema mate!Hiyo ni hatari kubwa
sana!
“Defcon1 bado sijaridhika nayo.Na lazima
kiongozi yeyote atakayekuja ajue tupo katika hali gani ya kiusalama.Hii
inathibitisha kwamba eneo letu si salama kiusalama maana tutakuwa vitani!Msiba
huu ni sehemu ya kuimarisha uhusiano wetu kidiplomasia.Wageni watakuja
wengi.Hatuwezi kuwa na viwango vya Defcon 1 no sishauri hilo.”mwingine
akasema.
“Lakini cha muhimu ni nini kulinda nchi yetu au?Mheshimiwa
ukidanganya umma kwamba nchi ipo salama halafu hao maadui wakaja nakuhakikishia
vita ikitokea utakuwa hatiani kwa uzembe uliochukua wa viwango vya
usalama.”Mambosasa hachelewi kila pembe yeye huwepo.Na lazima hoja zake ziwe
na mashiko nakuongoza.Swala la msiba bado lilileta utata.Mambo kadhaa yapo
mezani yanahitaji uamuzi wa rais lakini tayari mabishano yamechukua nafasi
yake.
“Jamani mimi sioni umuhimu wa kuhatarisha usalama wa taifa
letu.Marehemu wanahitaji kuzikwa kwa heshma.Hawa ni viongozi wa taifa wapewe
heshma yao.”
“Lakini bado kamati ya msiba haijaundwa na itakapoundwa
majibu yatahitajika kuhusiana na viwango vya usalama!”alisema Serambovu kuokoa
jahazi.Ilishaanza kuonekana kwamba watu hapa mezani hawakubaliani na mamlaka
aliyopewa Kilua.Na walimtafuta kila kwenye uamuzi wake kuingiza propaganda zao
ilimradi wa mmalize kabisa!
Kilua muda mwingi alikuwa kimya
akisikiliza hoja zao.Bado alikuwa kwenye mshtuko.Alitamani siku ile
iishe.Kichwani alikumbuka file namba 13:14.Lilikuwa jambo zito mpaka amepigiwa
simu ilitakiwa aliangalie.Lakini nchi ilihitaji umakini wa rais kwa wakati
ule.
Kilua akapiga mkono mezani kuonesha anataka kuongea.Wote
wakamgeukia huku kila mmoja akitaka kujua kauli yake wakijiandaa
kumpingaa!
“Nahitaji viongozi wa kijeshi haraka sana.The situation
in Kibatari needs more attention.Kuongeza viwango vya usalama ni priority number
moja kwa upande wangu.Kabla hatujaweka uamuzi wa haraka natoa amri we are moving
not to any level of defcon condition until futher notice.Then nataka kuongea
na rais wa Savanna Lands pili namtaka balozi ikulu ndani ya nusu saa.Majeshi
yetu yote yawe tayari lakini hakuna wakuinua mkono kumpiga mtu.Walinde mipaka
yetu kama wanavyofanya siku zote.Nimemaliza next ajenda ije mezani!”Kilua
aliongea kwa ukali kidogo.Bado hali yake haikushawishi alitamani kuondoka pale
aende kupumzika.Kauli hiyo iliwashtua kidogo wajumbe wale
wakashangaa.
Kwa namna alivyotoa kauli waliona mwanga kidogo lakini
wapo waliobeza kauli zake.Hawakumpatiliza alikuwa mwanamke atawafanza
nini?Walijiambia wenyewe kwenye vichwa vyao.
“Lakini
mheshimiwa…unajua hili ja…”alikuwa Mambosasa.
“Bwana Mambosasa
nadhani nimetoka kwenye hilo.Nimeshamalizana na hilo nataka twende kwenye ajenda
nyingine hatuwezi kalia kitu kimoja kuna mambo mengine yanahitaji macho
yetu.”alikuwa Kilua.
“Ndiyo mheshimiwa gavana…ooh sorry mheshimiwa
rais.Nilikuwa na maanisha issue kuu ni huo ulinzi wa taifa…”alijisahau kiasi cha
kuwafanya wenzake wacheke kidogo.Kilua akamwangalia alishaanza kuona
ukimbelembele wake.Ila kwenye uongozi lazima ukutane na mambo kama
hayo.
“Tafadhali bwana Mambosasa naomba twende ajenda
nyingine.”
Ilibidi Mambosasa amuweke rais kiporo kwa hilo.Hakuwa
ameridhika kabisa na uamuzi rais aliouchukua.
Wakati bado wanajadili
pale Kilua aliona simu yake ikiita.Hakuwa tayari kuipokea lakini alipokumbuka
kuna mtu alizungumza naye aliamua kufanya jambo moja.
Alimwita mpambe
wake nakumwambia,”Mwambie wakala wa mawasiliano wai-track hii namba sasa hivi
nataka majibu.”mpambe hakuwa na ruhusa yakuwa mbali na rais alimpa maelekezo
mlinzi mwingine aliyeenda hadi chumba cha mawasiliano akawapa taarifa kwamba
namba ile ifuatiliwe.Kilua aliamua kupokea wakati akimzubaisha
mpigaji.
“Ndiyo bwana.Rais Kilua anaongea.”
“Nimesema
nataka file namba 13:14 naona upoupo tu ajenda zangu huzifuatilii?”sauti ilisema
upande wa pili Kilua akaitambua ni ya nani?
“Nimesema sijui kuhusu
hicho kitu.”
“You are the president you have the power to get
anything I need file number 13:14 now or else?”sauti ilikuwa ya ukali
kidogo.Haikuwa na masihara.
“Utafanya nini?”Kilua aliuliza.Aliongea
kwa mtindo ambao hakuna aliyehisi ni simu mbaya lakini muda wote huo Serambovu
alikuwa anamkazia macho.
“Nadhani ni muda muafaka uonje joto ya
jiwe!Unajua mahali mumeo na mwanao walipo?”sauti ilisema kwa ukali
tena.
Kilua moyo ulimwenda mbio.Alihisi kichwa kutaka
kumpasuka!
“Unasemaje?”aliuliza kwa sauti ya juu kidogo lakini
akakumbuka masharti watu wengi hawatakiwi kujua mazungumzo hayo.Kilua akajikoki
ili wote wasigundua ni kama wawili ndo walimwangalia.Wakajua kuwa rais lazima
uwe na mengi.
“Mumeo yumo mahali namuona alivyo na mawazo
mengi.Mwanao mrembo katoto kamevaa gauni la zambarau.Nywele zake tena rasta hizi
alisukwa saluni ya Manka Fwaa!...”
Kilua aliijikuta akiinuka kwa
haraka!
“Halo?...Halo…?”Kilua alihofu!Sasa alijua simu hii si ya
mchezo na yeye ndo alifanya mchezo dhidi ya simu hii.Alipoinuka aliwashtua
waliokuwa kwenye kikao.
“Mheshimiwa kuna nini?”
“Sijisikii
vizuri naombeni nipumue kidogo.”alijitetea.
“Lakini mheshimiwa
tunakuhitaji hapa.Kiota inakuhitaji hapa siokupumzika
kwako.”
“Sikubaliani na mapumziko yako au kazi ngumu?”Mambosasa
aliropoka.
Kilua alimwangalia tu bila kumpatia ufumbuzi!Aliona
ataanzisha mengine.Tayari kesha thibitishiwa kuwa mumewe na mwanaye
wanaonekana kwa macho ya sauti ile.Bila shaka hili ni tishio kubwa la kumuweka
sawa.
“This meeting shall continue without me.”’alisema Kilua
akijiandaa kuondoka.Alihisi presha ikimpanda na alijua akizidisha ataanguka
chini.
“Ha!Ha!Ha!”alicheka Mambosasa,halafu akasema,”Tuendelee na
kikao cha usalama wa taifa bila rais?Hiki ni kituko.Hebu kaa hapa madam
tushughulikie nchi.”kauli ya Mambosasa ikawashtua ilikuwa kama mzaha flani.Na
huyo ndo Mambosasa hakopeshi kauli anakurarua mara moja.Ilikuwa mzaha wa
kumshtua tu.
Wengine waliomjua walimzoea.
Kilua alimeza
hilo lakini alichotaka kujua ni usalama wa famlilia yake kwanza!Ni usiku wake
wa kwanza akiwa ikulu zimwi la matatizo limemuandama.Alijikaza kwa
kweli.
“Muda simrefu nataka kuongea na balozi wa Savanna Lands na
baada ya hapo nitaongea na rais wao.Naombeni mniache kwanza pia nitahitajiika
kusema na taifa punde kamati ya msiba itakaapokuwa tayari.”alisema bimkubwa wan
chi.
Mara mlango ukafunguliwa akaingia wakala wa taarifa,”Mheshimiwa
rais kuna taarifa kutoka ubalozi wa Savanna Lands!”wote waka
taharuki.
“Balozi wa Savanna Lands yupo wapi?”
“Hakuwepo ubalozini.Watu wote wa Savanna Lands waliokuwepo ubalozini wa hapo
hawapo.Yaani the embassy is empty!”wakal a alitoa taarifa.Kilua akaduwaa.Hiyo
ilikuwa na maana nzito.
Bila shaka rais alihitajika mezani.Kuna file
namba 13:14,kuna tishio la kumfuta Kilua halafu kuna taarifa ya uwepo wa familia
yake matatani.Hii ya kutoweka kwa balozi wa Savanna Lands na watumishi wote wa
ubalozini ilikuwa hatari kubwa sana!Ukilinganisha mambo utajua fika taifa la
Savanna lilikuwa limeondoa watu wake ubalozini.
“Ni kwamba hawapo
wote.Tuna jaribu kuangalia rekodi ya ndege lakini inaonekana hakupanda ndege
yeyote.Tumecheki mipakani bado hakuna data za uwepo wa balozi wa Savanna Lands
katika ardhi ya Kiota!”wakala aliwasilisha.Kilua akatumbua
macho.
“Simu zake hazijafanyiwa tracking?”
“Kama ubalozini
hayupo una dhani simu zake atakuwa ameziacha wapi?
“Nipigieni simu
Savanna Lands sasa hivi!”alisema Kilua.Muda uleule simu ilipigwa kuelekea
Savanna Lands Kilua alizidi kuwa na hali mbaya.Alichanganyikiwa zaidi.Gavana wa
Savanna Lands hajulikani alipo.Hiyo ilikuwa tafsiri mbaya sana kwake.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya
mawasiliano kuungwanishwa Kilua alichukua simu,”Huyu ni rais
Kilua.”
“Ndiyo bi Kilua naskia umechukua nchi.Hongera.”ilikuwa sauti
ya rais wa Savanna Lands.
“Asante mheshimiwa.Naomba kujua kama
unataarifa zozote za balozi wako?”
“Hapana niliongea naye
mchana.Nikamtumia salamu za rambirambi kwako.”
“Nashkuru kwa
salamu.Ila balozi wako katoweka ubalozini hayupo sehemu yeyote.Tumejaribu
kupitia kona zote za usafiri lakini hayupo!”
“Mheshimiwa Rais Kilua
kwa heshma zote namtaka balozi wangu akiwa hai!”rais wa Savanna Lands alitoa
kauli ya vitisho. “Sifahamu alipo balozi.Kwanza majeshi yako yameanza kutilia
macho anga langu.Nina taarifa za kiintelijensia kwamba wanajiandaa baada ya
kusikia taifa letu limepatwa na msiba!Amri inatoka kwa
nani?”
“Kivipi?”
“Mazungumzo yote hatuwezi kutrace hiyo namba.Anatumia secured line!”
“Ina maana hakuna IT anayeweza kuidhibiti hiyo namba?Simu itaingiaje
ikulu bila kutrace huo ni upuuzi!”Kilua akawa mkali sana.
“Mheshimiwa hawa watu wanajificha sana.Yaani hata rekodi ya mazungumzo hatuwezi
kuipata!”
“What?”Kilua akashtuka zaidi.Kabla hajafanya
mengi akaingia mtumishi mwingine akaleta bahasha kwa mheshimiwa rais.Ile bahasha
Kilua aliipokea nakuifungua akakutana na picha iliyomtisha sana!Mumewe alikuwa
kafungwa kamba pamoja na mwanaye!Kilua alihis kupotea akili!
Walinzi wake waliona jambo lile wote waka taharuki familia ya rais ilikuwa
imetekwa!Walinzi walikuwa na wakati mgumu kwani punde tu Kilua alipoapishwa kuna
kikosi kilitumwa mahususi kuwalinda familia yake lakini mpaka sasa hawajapata
mrejesho ni vile hawakuwa wameuliza.Huo ulikuwa uzembe kwa sheria zao!Kila mmoja
alijiandaa kukabiliana na lawama.
“Mheshimiwa tutawatafuta popote
walipo watapatikana.”alijaribu moja ya walinzi wale.
“Kwanza sitaki
mtu yeyote ajue kwamba familia yangu imetekwa hicho sitaki kijulikane
kabisa.Kufanya hivyo ni kuwahatarisha.”alisema akijikaza asiangushe
machozi.
“Mheshimiwa lak…”
“Hakuna wakujua kama mume
wangu na mwanangu katekwa.Hiyo ni oda!”alisema mheshimiwa rais.
“Lakini.”alitaka kusema kitu Yule wakala wa mawasiliano.
“Hii ni
binafsi nisingependa litumike kama ajenda kwa taifa.Tayari tuna matatizo mengi
hili litagusa pabaya.”
“Ok mheshimiwa tuambie unachojua kuhusu
utekaji huu.Maana wewe pekee ndo umeongea na mtekaji.”aliuliza kiongozi wa
ulinzi.
“Siwezi kusema lolote lakini maelezo yote nitatoa
mwenyewe.Yoyote anayechezea familia yangu anajua anachokifanya ni kama ameniweka
kiganjani.Siamini yeyote.Jana tu ananitajia hadi majina ya watu niliokaa nao
mkutanoni!Hadi nguo nilizovaa!”Kilua ni kama alitaka kulia lakini akajikaza
tu!Walinzi wakagundua mwanamke huyu anapitia kipindi kigumu sana.Umepewa nchi
ghafla unakutana na hali ngumu bado familia yako imetekwa.Hakika ilihitaji
ujasiri wa hali ya juu.
“Mheshimiwa tutampata huyu asidi.Wameigusa
familia ya kwanza.”walijaribu kumhakikishia uimara wao katika kushughulika na
hali kama zile.
“No.Msifanye chochote familia yangu ipo hatarini
hata siamini kama ikulu ni sehemu salama kwa upande wangu.”
Walinzi
walibaki kimya.Lilikuwa tukio la kufedhehesha na lazima hatua zichukuliwe haraka
iwezekanavyo.
“Narudia tena nawapa amri hakuna wakujua habari hii
zaid yenu.Nahitaji kujua adui aliyepo ikulu ni nani?”Kilua alisema akijikaza
kulia.Ina maana nyendo zake zilikuwa zinakaguliwa kw asana.Walinzi
walimwelewa.
“Nahitaji mpelelezi makini aweze kujua ni nani
aliyefanikisha mume wangu na mtoto wa tekwe.”alisema Kilua akiwa anamaanisha kwa
umakini.Walinzi walisikitika kila mmoja akipandisha hasira nakuapa wakimkamata
huyo aliyeiteka familia ya rais basi hatakuwa na msalia mtume nikumfutilia
mbali.Lazima baadae watajadiliana maana wao ndo watakaoulizwa kuhusu tukio ilo
la kutekwa kwa familia ya rais.
“Mheshimiwa tumepokea agizo lake
tutalifanyia kazi tutakagua kila eneo hadi tujue.Lakini kama huamini vikosi vya
taifa basi tutaomba sisi wenyewe tufuatilie jambo hili tutawatuma watu wafanye
ukaguzi na kweli tutampata mumeo.We are the best on this issue.”alisema chifu
Ditu kiongozi wa ulinzi wa rais.
“Naomba usiri katika
hili.”
“Hapana mheshimiwa hutakiwi kutuomba umeshatoa oda na sisi
tunafuata oda tu.”Ditu alisisitiza.Kabla hajatoka akasema.
“Kuna
file nalitaka.”
“Kama ni mambo ya siri kuna mtu wa kushughulika
nalo.”alisema Dittu.
“Nani?”
“Katibu mkuu.”
“Namtaka ofisini kwangu haraka iwezekanavyo.”
“Alikufa kwenye tukio
la jana.”sekretari alisema.Kilua akasugua kichwa.Palepale akamgeukia
sekretari.Uzuri Serambovu hakuwepo hapo alikuwa ametangulia chumba cha
mkutano.
“Nani anaweza kunipa hilo file?”
“Mimi nina uwezo
huo.”alisema sekretari Sada.
Kilua aliwapa ishara walinzi wake
wampishe.Walitii nakutoka nje,Kilua akabaki na Sada mule ndani,”Nataka file
namba 13:14”
Sada alishtuka sana!Alibadilika ndani yamuda mfupi
nakuonesha hofu ambayo hata Kilua aliweza kuiona,”Kuna nini Sada?”
Sada alizunguka pale ofisini huku akiwa kwenye mawazo mazito sana.Kitu hicho
hakutaka aulizwe kabisa au kiangukie kwenye uamuzi wake kwamba kipo
wapi.Alitamani katibu mkuu angekuwepo pale ajibu hayo mambo lakini sio
yeye.
“Sada kuna kitu gani ambacho unaogopa kunitajia hilo file
nimeomba nipewe kwani kuna ugumu gani?”
“Mheshimiwa naomba niache
kazi tafadhali sana.”alisema Sada akiwa na wasiwasi sana.
Kilua
akazidi kupatwa na hofu,”Uache kazi wakati nafikiria kukuteua kuwa katibu
mkuu?”
“Hapana hilo file limeteketeza watu.Kila aliyetaka kuingilia
amekuwa akiishia pabaya.Makatibu takribani watatu walipoteza nafasi zao kisa
hilo file!”
“Hebu niambie vizuri?”habari ilimteka Kilua kusikia
kwamba file nambari 13:14 lina kiza kinene.
“Ilianza awamu
zilizopita kila aliyetaka kugusa hilo file alidhibitiwa sana.Hata rais Kisusi
jambo hilo lilimpa wakati mgumu sana.Wakati alipotaka kuingilia ndo ikaja
taarifa kauawa kwenye maonesho ya uhuru.”
Kilua akawa anameza yale
maelezo,”Kwani hilo file lina nini hadi rais asiweze kuliingilia?”aliuliza
Kilua.Huku akijaribu kukumbuka vitisho vya Yule bwana aliyemwambia anajua hadi
watu aliokaa nao mezani.
“Hilo file sijabahatika kuliona.Kulipata
linahitaji password ya katibu mkuu au sekretari halafu ifuate ya rais.Lakini
Theory inayolizunguka siielewi yasemekana uongozi uliopita ndo wenye hiyo
password na mpaka uombe hiyo password ndo uweze kulifungua.Theory pekee
ninayoiamini ni ya kwamba viongozi wa awamu Fulani ndo walianzisha hilo file na
ajenda halisi ya file hilo tatizo ni kwamba wao wenyewe hakutaka kabisa file
hilo liguswe na uongozi ujao.Hivyo likawekewa password na jina pekee
linalotambulika kuhusu file hilo ni hiyo namba 13:14.”aliendelea kuchuja
nakupembua mwana Sada.
“Linaweza kuwa nini?”
“Ni kama
mkataba wa kitu Fulani cha siri sana.Mara kadhaa nilimsikia rais Kisusi
akizungumza hilo jambo.Lilimsumbua sana na kila alipotaka kutupia jicho alipata
vizuizi vingi!”
“Mhh.”aliguna Kilua tafakari ikiwa ngumu
kuelewa.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwani
mheshimiwa imekuwaje?Nilifarijika sana nilipojua unachukua madaraka nikajua
hakuna atakayekuja na ajenda ya hili file na mambo yataenda kawaida.Lakini siku
ya kwanza tu ofisini umeanza kuulizia hili file.Au ndo maana familia yako
imetekwa?”aliuliza Mwana Sada.Kilua alitikisa kichwa haikujulikana kama alisema
ndio au hapana.Lakini tayari kapokea maelezo mazito kuhusu file nambari
13:14.Sasa ameanza kuunganisha doti zote hadi ajue hilo file lina umuhimu gani
kiasi cha kusababisha familia yake iingie kwenye majaribu makubwa sana.Wakati
anawaza hilo simu tena ya ofisini kwake.Akaipokea.
“Ni rais wa
Savanna Lands natumai una majibu ya wapi balozi wangu yupo?”
“Mheshimiwa sina jibu la kuridhisha kuhusu balozi wako.Kupotea kwake sijui kitu
chochote kile.Wewe ndo mwenye majibu sahihi.”Kilua alizungumza kwa ukali
kidogo.Habari ya file lile ilimnyima hadi amani yake akiwaza mwanae na mumewe na
tayari kuna tishio kubwa la ndani.
“Mheshimiwa kwa heshma zote
nataka balozi apatikane la sivyo nitachukua hatua ikiwezekana majeshi yangu yaje
kwako yamtafute balozi wangu!”alisema kwa ukali rais wa Savanna Lands.Kilua
alikosa jibu ilibidi akate simu palepale!
Kabla hajafikiria simu
yake ya mkononi ikaita tena bila kujishauri sana akaipokea,”Halo?”
“Tuma majeshi yako katika jimbo la Kibatari.Halafu ambia kikosi cha anga kuna
ndege ya jeshi la Savanna LANDS imeruka hadi kwenye anga letu hiyo ndege itungue
sasa hivi!”ilikuwa sauti ile ya mtu asiyemjua.Ina maana huyu mtu anaintelijensia
gani kujua haya mambo?Alijua anaongea na rais wa Savanna Lands.
“Kwanini nifanye hivyo?”
“Wewe ni rahisi na sasa hivi huna mkuu wa
majeshi wewe ndo amiri unauwezo wa kuongozi amri hiyo.”
Kilua
akavuta pumzi ndefu nakuzishusha,”Lakini nina uhakika gani?”
“Unataka mumeo na mwanao wapate mlo wa leo?”sauti ikauliza.
Ina
maana familia yake inanyimwa hata chakula?Roho ikamuuma sana!Bila hata
kuwaza.Akamgeukia sekretari,”Nataka simu ya kambi ya jeshi ya Kibatari?”bila
hata kujishauri kwa mara nyingine akajikuta akicheza ngoma hiyo.
“Kuna simu maalum inayotumiwa na amiri jeshi pekee.Ngoja nikuunganishe.”alisema
Sada akasogea kwenye meza a rais akaingia kwenye droo kuna simu flani hivi kubwa
akaitoa halafu akampa na Kilua.
Kisha akatoa
kijitabu Fulani akafungua kurasa akamwambia asome maneno yale punde simu
itakapopokelewa.Kisha sekretari akapiga simu kuelekea makao ya kijeshi
Kibatari.Mtandao ukawa umeunganishwa.
“Halo!”alianza rais
Kilua.
“Yes CIC!”sauti upande wa pili ikaitikia kwa
ukakamavu.
“This is C-I-C 1 1 order to shoot enemy trespassing in
our airspace scan the air take them down immediately!”alitamka kwa kujiamini
Kilua.
“Roger that cic 1 1!”sauti iliitikia upande wa
pili.
Kilua akashusha simu ile,”Madam unajua
ulichofanya?”aliuliza Sada.
Kilua alimwangalia bila kumwambia
chochote huku mikono ikivuja jasho.Mambo yameivaa!
“You have just
issued an order to kill someone.”alisema Sada kwa huzuni,Kilua akashtuka.Lakini
ndo shughuli ilipompeleka…
Kilua akavuta pumzi ndefu
nakuzishusha.Alihitajika muda ule kuwa sehemu maalum maana ametoa amri
kushambuliwa kwa ndege ya Kibatari iliyopo kwenye eneo lake.Jambo hilo
lilitakiwa kufanywa kwa umakini wa hali ya juu.Tayari keshatoa mari na matokeo
yake lazima ataulizwa ilikuwaje akakubali kutoa amri.Je,vyombo vyake vya
intelijensia vinajua jambo kiasi cha kushauri nini kifanyike?Hilo lilikuwa kama
mtego Fulani uliotakiwa majibu ya hali ya juu.Uzembe wowote lazima utamgharimu
kwa maamuzi yake.
“Najua nilichofanya.”alisema Kilua baada ya
ukimya wa sekunde chache.Alipitisha mkono kwenye paji la uso kama anajifuta
jasho jepesi lililokuwa likifuka kutoka kwenye ngozi yake.Ilikuwa ni kuchemka
haswaa.Mambo yamezua mambo na mkuu kawekwa kiti moto.
Wakiwa pale
ndani mlango wa kile chumba ulifunguliwa akaingia Serambovu akiwa na umakini
kidogo kwenye uso wake.
“Mheshimiwa unahitajika kwenye
mkutano.”alisema Serambovu kwa heshma.Kilua alimwangalia tu bila kusema kitu
huyu ndo mtu aliyepo karibu kwa wakati ule.Alifikiria sana.Palepale machozi
yakaanza kumtoka mfululizo.Serambovu alimsogelea nakumshika mikono akijaribu
kumtuliza.Kuna wakati Kilua alitaka kusema ukweli kwamba familia yake imetekwa
lakini alikumbuka kwamba Serambovu ni hawara wake wa siri hivyo kumwambia jambo
lile lingekuwa mtaji kwa Serambovu kwamba bwana wa Kilua katekwa nayeye
angeutumia muda ule vizuri kumshawishi Kilua awe mbali naye.Hilo siyo la msingi
kwa wakati ule kumwambia bwana huyu.Alifiha tu.Lakini akawaza kuhusu wanawe
wengine wawili.Hao walipaswa kulindwa kwa gharama zozote ilikuwaepusha na hatari
hiyo.
“Usijali kila kitu kitakuwa sawa.”alisema Serambovu
akimpigampiga mgongo kwa kumpa bembelezi.Serambovu alikuwa ameteka viuno vya
mwanamke huyo.
Kilua akajikaza nakuacha kuangua kilio.Kisha
alijifuta machozi.Sada alitoa kwenye mkoba wake vifaa vya urembo nakumtengeneza
rais vizuri kisha wakaondoka na kwenda kwenye kikao.Ndani ya muda mfupi walikuwa
kwenye ukumbi wa vikao.Kilua lipoingia walisimama wote hadi alipowaruhusu
kukaa.
“Ajenda kuu leo tunaomba tuangalie swala lililopelekea ajali
ile iliyoua viongozi wote wa serikali.”alisema Kilua akisoma muongozo uliopo
mezani mwake.
Mbele yake walikuwepo kamati ya ulinzi.Kuna msururu wa
kamati nyingi unaotakiwa kuonana naye.Kazi ile ilikuwa na mambo mengi sana kiasi
ilimchanganya Kilua katika kufanya maamuzi sahihi.Michango mbalimbali ilitolewa
pale mezani kila mmoja akieleza kwa upande wake.
“Tunasubiri ripoti
toka kwa vyombo vyetu vya usalama.Lakini kwa mtazamo wa kwanza kuna tetesi
kwamba jambo hili halikuwa ajali tu.Rubani Kaptein Kipilipili alikuwa sawa
kabisa siku ile na hata alikuwa amefanya mazoezi ya kutosha kwaajili ya zoezi
lile.Lakini cha ajabu nikule kutokea ajali ikiwa anajuafika pale kulikuwa na
umma mkubwa.”
“Inawezekana kuna hitilafu za kiufundi.”
“Isingekuwa rahisi kuangusha ndege eneo lile.”
“Kwani
tunachoangalia hapa ni kitu gani kuhusiana na tukio hili?Was it normal
accident?”mwingine akauliza.
“Hapana.”alitamka kiongozi wa DCU wote
wakamtizama kwa mkupuo.
“Unajua tukio zima lilikuwa la ghafla
natumejaribu kuangalia tangu jana sekta zote kwa ule uchunguzi wa mwanzo ndege
isingeanguka kirahisi.Pili kuanguka kwa ndege…ukiangalia ndege yenyewe
haikutakiwa kutoa mlipuko mkubwa kiasi kile.Kumaanisha kulikuwa na milipuko
zaidi ya mmoja!Kwa ukaguzi ndege ile ilivyoundwa hata kama ingetokea ianguke
inauwezo wakujidhibiti isitoe mlipuko mkubwa kiasi kile!Pili ilipoanguka
inaonekana fika muongoza ndege aliyekuwepo control tower alikuwa akimpa
maelekezo vizuri sana rubani isingekuwa rahisi asijue kama ndege ina
hitilafu.Upembuzi zaidi unaonesha rubani hakutoa taarifa kwamba alikuwa na
tatizo katika udhibiti wa ndege ile.Ina maana aliipeleka moja kwa moja akijua
anachoenda kukifanya!”director alikuwa anatoa ripoti aliyopokea kutoka kwa timu
yake iliyofanya uchunguzi hii ilijumuisha DCU 1 na DCU 2
Watu
wakaduwaa!Ilikuwa habari nzito sana kutolewa.Lakini kwa kuwa chombo hicho
kilijulikana kwa kuwa na weledi wa hali ya juu wasingeweza kukwepa ripoti yao
iliyoenda zaidi ya vile kila mmoja alivyotazamia.
“Una maanisha nini
director Masha?”aliuliza rais kwa mshtuko.
“It was a suicide mission
perfomed by Captain Pilipili!”alisema kwa sauti yenye ukavu kidogo huku macho
yake yakithibitisha ukakamavu Fulani wa kijasiri!CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Una maanisha
mwanajeshi wetu mwenyewe aliamua kuangusha ndege maksudi jukwaa walimoketi
viongozi wa serikali?”
Director aliwaangalia kwa jicho Fulani kila
mmoja abebe ugunduzi huo mpya!Hilo lilikuwa na maana nzito sana kwani nikupeleka
lawama jeshini.Viongozi wa kijeshi waliokuwa pale wote walionesha mshtuko wa
hali ya juu.
“Kama ni mwanajeshi ina maana yalikuwa
mapinduzi?”aliuliza mwingine bila kuonesha dhumuni la kauli yake.Aliijibu kwa
njia ya swali!
“Ndiyo yalikuwa tukisema ni mwanajeshi wetu
alishiriki kuua serikali nzima itafasiriwa kama mapinduzi ya kijeshi na hilo
halitaiweka nchi yetu pazuri ni hatari kubwa sana!Wageni tunaotegemea kuja
watakuwa katika sintofahamu kama Kiota ni paradise tena.”alishauri
mwingine.
“Sasa…”alikwama Kilua akikosa cha kusema.
“Nina uhakika haikuwa ajali hiki kitu kilipangwa!Tayari tumekuta kuna ushahidi
wa bomu kulipuka eneo lile muda uleule ambao ndege ilianguka.Pia makombora ya
ndege yalilipuka pamoja.Vitu vitatu.Mlipuko mdogo wa ndege,pili mlipuko wa
makombora yaliyokuwepo kwenye ndege na tatu mlipuko wa bomu la kutegwa hapa sina
shaka.Ni ukweli bomu lilitegwa kabla ya shughuli kuanza.Ina maana muda wote
wakiwa kwenye shughuli bomu lilikuwa chini yao!”
“Nashauri taarifa
hii istolewe kwa umma bado kuna shida kubwa.Rais anatakiwa atoe hotuba muda
simrefu watu wanangoja kumsikia kiongozi wao!Lazima aende na majibu kwa wananchi
wake.Majibu ya matumaini nasio jibu la jeshi kuhusika katika kumuondoa rais
Kisusi na serikali yake madarakani!”alishauri mwingine.
Kilua
alionekana kuogopa kwa upande Fulani.Yeye mwenyewe kuna vitisho
vinamuandama.
“Kama ni mwanajeshi alifanya tukio hili basi hatuna
budi kuchukua hatua za haraka kulinda nchi na utawala wa rais Kilua.Uchunguzi
ndani ya jeshi ufanyike wa haraka na wote walioshiriki wawekwe vizuizini kwa
uhaini!”alisema Serambovu.
“Utawala wa rais Kilua lazima utunzwe kwa
gharama zote.Japo ni mwanajeshi mmoja hatuwezi sema ni jeshi zima.”moja ya
maafisa wa jeshi alitamka hilo.Jambo hilo likapingwa vikali.
“No!Hata kama ni mmoja lazima kuwe na mnyororo wa watu waliopanga jambo
hilo.Hatua lazima zichukuliwe kwa haraka sana.”mjumbe mwingine aliingilia
kati.
“Ok.Natoa oda.Nataka uchunguzi ufanyike kwa siri sana na mtu
yeyote asitumie jambo hili kumwingiza mtu kwenye conspiracy hii bila kuwa na
uhakika.Najua inapotokea hali kama hii kuna wanaotokea kuingiza wasio na hatia
ndani ya muda mfupi nchi yetu itakuwa na wageni wengi.Lazima tuwe imara
wakulinda amani yetu.Sitapenda kuona tukiigeuza nchi jangwa.”alisema Kilua
ambapo wenzake walitii amri.
“Kikao nakiharisha nahitaji kuongea na
taifa kwanza.”alisema Kilua ambapo aliinuka muda ule.Wote wakasimama nakumpa
heshma zake kisha akaondoka kwa haraka.Mwili wake ulitetemeka.
Kila
alipomuwaza mwanaye na mumewe alikosa amani.
Waandishi wa habari
walikuwa tayari wakingoja tamko la rais wao.Kamera zilikuwa zimfungwa mahsusi
kwa hotuba hiyo ya kwanza kabisa Kilua kuitoa.Nchi na dunia ilikuwa tayari
kumsikiliza rais Kilua.Aliomba akae kwenye meza.Aliketi pale kisha akaendelea
kutoa hotuba yake.
“Tukio hili laweza kuwa limetafuna misingi ya
jukwaa walimoketi viongozi wetu nakutujaza huzuni.Lakini haliweza kutikisa
uimara wa imani yetu katika kusimamisha taifa letu hata kama tumeguswa
pabaya.Tumesimama.Tutasimama kuliinua taifa letu.Kiota iliyokumbwa na huzuni
itasimama.Hata waliotutangulia hawapendezwi na sisi kujikunyata kwa huzuni
tukiliacha taifa letu lianguke.Wangependa tuwaenzi kwa kulisimamia imara!Nchi ni
wewe.Tusikubali kushika tama.Kama rais wenu nawahidi kuilinda nchi yetu kwa
gharama zote kuhakikisha usalama wa taifa letu unakuwa wa kwanza.Hakuna
mwanadamu aliyepanga mimi kuwa rais wenu bali matendo Mungu anayopanga leo ni
mtumishi wenu katika kiti cha urais.Nitalitumikia taifa langu kwa kipindi chote
nitakachokuwa madarakani nakuhakikisha nchi inazidi kusonga mbele.Temepanga na
kuaandaa maandalizi ya msiba wa taifa ambao utakuwa wa pamoja…”
Aliendelea kutoa hotuba yake.Watu walimsikiliza lakini kukawa na tatizo!Rais wa
Savanna lands alikuwa mbioni kujibu mashambulizi baada ya ndege yakle ya kivita
kutunguliwa na majeshi ya Kiota!
Ilibidi
aharakishe mazungumzo yale maana kulikuwa na tatizo kubwa linaenda
kutokea.
Watumishi waikulu walimfuata rais mmoja wao alimwambia
anahitajika haraka chumba cha hali ya dharula.Rais ilibidi afupishe maelezo
nakumuachia msemaji wa ikulu aendelee na mazungumzo.Kilua alitoka kwa haraka
nakuongozana na walinzi wake kuelekea chumba cha dharula.Kule alikutana na timu
ya wajumbe wakiwa tayari kwenye meza ya kikao.Walisimama walipomuona rais
wao.
Kilua aliketi chini nakuwapa ishara wa keti.
“Kuna
nini?”aliuliza.
“Tumepokea taarifa kwamba jeshi letu limetungua
ndege ya kijeshi ya Savanna Lands muda mchache uliopita.Na taarifa zaidi
zinasema serikali ya Savanna Lands imetuma vikosi vyake vya kiusalama kwenye
ubalozi wetu uliopo kwao.Kuenda kwa vikosi hivyo siyo ishara nzuri!”
“Ilikuwaje ndege ikatunguliwa?Who gave the order?”walijuliza pale mezani.Kilua
aliwatizama alichokiamua kimetoa matokeo na kweli hakuwaambia kama angefikia
uamuzi huo.
“Mimi nilitoa amri hiyo!”ilisikika sauti ya rais
Kilua,kitu ambacho kiliwashtua wengi.Hawakujua kama alikuwa na jeuri
hiyo.Kiongozi aliyeonekana dhaifu kapewa madaraka wakaujua angefeli lakini cha
kushangaza siku ya kwanza tu ofisini hata masaa 24 hayajaisha tangu aapishwe
katoa amri kutungua ndege ya taifa lingine!Hilo halikuwa jambo la kawaida
kabisa!Ni tishio kwamba rais anaelekea kuanzisha vita na taifa
jirani!
“Mheshimiwa?Ilikuwaje ukatoa amri hiyo?”
“Ilinibidi nifanye hivyo walikuwa wanachezea anga letu.Nimeshapokea vitisho
kutoka kwao so I had to act incase they pla with us!”alijitetea Kilua.Kila mtu
alijishika kichwa kwa wakati ule.Ilikuwa taarifa mbaya sana kuipokea hasa kwa
siku kama ile.Tayari walikuwa na mambo mengi mbeleni yakushughulikia tena lina
jiri hili katika wakati mgumu kama ule.NI wazi kwamba utawala wa Kilua ulikuwa
katika wakati mgumu baada yay eye kutoa amri kushambuliwa kwa ndege ya kivita
iliyokuwa ikipita kwenye anga lake.
“Mheshimiwa tukio ulilofanya ni
hatari sana!Umeua mwanajeshi wa Savanna Lands they will seek
revenge!Tunategemea wageni hapa kwenye msiba huu wa taifa itakuwaje wakijua
kwamba leo umetoa oda kutungua ndege ya jirani yetu?”moja ya wajumbe
alihoji.
Kilua alikosa jibu akikumbuka alifanya vile kwa shinikizo
la mwanaye na mumewe wapewe chakula alijihisi kuwa kiongozi dhaifu anayefuata
hisia binafsi bila kuweka utaifa mbele.Ni kweli ndege ya Savanna Lands ilipita
kwenye anga lao na bila shaka walitakiwa kujibu japo yeye aliwahi kutoa
maamuzi.Kusema alipotoa taarifa ile lilikuwa jambo zito sana!
“Tupo
katika hali ngumu ya kidiplomasia na nchi ya Savanna Lands bila shaka tujiandae
kwa lolote.”
***
Kulikuwa na kikao cha siri sehemu Fulani kando ya mji
mkuu wa taifa la Kiota.Kikao kilifanyika pembezoni mwa bahari.Mawimbi yalipiga
nakuja na harufu ya chumvi ya bahari.Tetemo la upepo uliokinzana kwa pambio za
mawimbi ulitengeneza mandhari tulivu iliyoshiba.Kulikuwa na vibosile wane wakiwa
kwenye viti vyao.Wameshiba maisha yao.Njaa haikuwa taabu kwao labda tu mwenendo
wa mambo.Suti zenye uzito wa ukwasi zilikaa vyema kwenye miili yenye vitambi vya
utajiri kwa nakshi za rangi mbalimbali.
“Tayari ameshaingizwa
kiongozi mpya.Lazima tufanye hatua inayostahili.”mmoja wa mabosi wale
alizungumza kwa sauti yenye ukavu.
“Ndiyo tunatakiwa kuharakisha
kuweka mizizi yetu kabla wengine hawajaanza kushika serikali vizuri.Pia lazima
kila sekta tuweke watu wetu angalau tuwe na asilimia ya uhakika wa
kulindwa.”mwingine alijibu akiwa ameshika glasi ya kinywaji akapiga funda
mbili.
“Mnaonaje tukitoa mchango wa viti katika msiba huu kama njia
yakuanza kupenyeza mizizi yetu?”mwingine aliongeza hoja kwenye kikao
hiki.
Walitikisa vichwa kuonesha kufurahishwa na hoja hiyo.Walikuwa
na ajenda zao.Haya ndo mambo yaliyokuwepo katika taifa hili kwa wakati huo wenye
shaka kuu.Kila mmoja alijipanga kivyake hasa kwa kujua utawala mpya umeapishwa
kwa hivyo lazima wajichimbie mizizi yao.
“Lakini ajenda yetu ile ya
Kibatari ibaki kama ilivyo.Wakubwa wameshasema wataanza ile ajenda na
watahakikisha hakuna wakuingilia chochote.Tayari vitendea kazi vina karibia
kuingizwa nchini muda simrefu lakini kwa taarifa nilizopata jana kikaoni ikulu
rais hakuwa ameongeza viwango vya usalama hivyo shaka haipo.Bahari ipo shwari na
hata bandarini hakuna taabu.Mzigo utaingia kwa haraka sana.”alisema bwana
Tufe.Wote walimgeukia.Walikatizwa kidogo na binti aliyekuja na sinia la vinywaji
alivitenga pale mezani kwa ustaadi mzuri.Alivalia nguo nadhifu suruale nyeusi na
shati la pinki pamoja na kizibao cha rangi nyeusi.Uso wake ulijaa
ushaufu,alijikwatua kwa tarabizuna zenye utuli wa kushawishi kiasi mabosi wote
waliokuwepo pale walijikuta wakiivuta utuli wake.Kila mmoja aliwaza lake.Halafu
binti aliwapa tabasamu la kiasili la ukaribishwaji.Kisha aliondoka na ndani ya
dakika moja alirudi na sinia lingine la nyama choma.Aliweka vitu hivyo mezani
kwa heshma zote.
“Karibuni.”aliwapa tabasamu.Vibosile wetu
walitamanika na ukaribisho huo.Huku uchu wa mate ukiwachachua midomoni
mwao.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati binti
akiinuka kuondoka alipigwa kikofi cha kalio akaruka kidogo,”Aah!”alitoa mlio
wenye mbwembwe.Bwana Tufe alimkonyonyeza huku msichana akitabasamu.Halafu alimpa
ishara waonane baadae.Ishara ilieleweka.
Wakiwa pale walikamata
minofu ya nyama nakuanza kushughulikia kwa utamu wake.Walioguguna mifupa
walipata wasaa kushughulika kama jamvi kwenye shughuli.Mlo uliwaweza wakishushia
na vinywaji vyao vizito.Walimalizia kwa mazungumzo ya kawaida.Ni kwamba watu
hawa watalala katika hoteli hii kwa siku ile.Baada ya milo na mazungumzo ya hapa
na pale bwana Tufe aliinuka kuelekea kilipo chumba chake wenzake walicheka
walijua anachokifuata ni Yule msichana.Alisugua kitambi chake nakuondoka kwa
haraka hadi kilipo chumba alichokodi.Alifika nakukifungua maana tayari kulikuwa
na mtu ndani.Bwana huyu alimuona Yule msichana akiwa kajifunga khanga akjilaza
juu kitanda kikiwa kimetandazwa asumini.Msichana alitabasamu alipomuona mzee
wake.Akiwa kapatwa na pombe kidogo kuchwani alichapuka baada ya kufunga mlango
akamshukia binti Yule pale kitandani.Kwa mbwembwe alianza kumpapasa.Msichana
alikutana na harufu ya nyama pamoja na pombe japo hakuipenda harufu ya pombe
ilibidi tu acheze ngoma hiyo isiyo yake.
Mzee aliparamia huku binti
akimvua koti.Alimpindua mzee kwa haraka kwa ustaadi wa hali yajuu.Mzee akawa
chini na msichana akawa juu yake.Msichana alianza alifanikiwa kuondoa koti
lile.Akaikamata tai nakuifungua kisha akafungua vifungo vya shati ya mzee.Mzee
alikuwa na uchu uliochungulia kwenye kichwa ukiumuka kwa joto la hawaa.Msichana
alijua fika jambo moja tu lingemsaidia kwa wakati ule ni kumpa huyu mzee
anachotaka!Wakati anaiendea suruale yake alishtushwa na mlio wa simu uliokuwa
kwenye mfuko wa suruale yam zee Yule.Msichana alimsaidia mzee kuitoa ile simu
nakumpa.Mzee aliipokea kwa kuangalia pembeni.Alipokea maelezo Fulani kisha uso
ukabadilika!
“Habibi kuna nini?”msichana aliuliza kwa
kujali.
“Siunajua tena mambo yamebadilika mzigo wetu unaoingia
utakwama.”mzee alisema akiwa ameshika kiuono cha msichana Yule.
“Kwani vipi.”msichana aliuliza.Mzee alichukua simu yake tena aakaandika ujumbe
Fulani kisha akautuma kwa watu kadhaa. Wakati alibaki kimya iliasipoteze
pointi.
“Naskia rais alitoa oda ndege ya Savanna Lands
kutunguliwa.”
Msichana akashika mdomo kwa
mshangao,”Mtumee!”
“Bila shaka viwango vya usalama vitapandishwa na
kila kona kutakuwa na ulinzi mkali.Hii itatuletea shida kwa mzigo wetu kupita
bandarini.”alisema mzee akiendelea kupapasa kiuno kibichi cha msichana
Yule.
“Pole habibi wangu sasa itakuwaje?”
“Ndo
nimewaambia wenzangu wajue kabla hatujachukua hatua nyingine.”
Msichana alishika kifua cha mzee akapapasa kisha akamata chuchu nakuziminya
ukapita mshtuko wa shoti ya umeme.Mzee alifumba macho nakujibana.Tayari binti
alikuwa anamtawala.
“Kwani ni mzigo gani huo habibi?”aliuliza kwa
deko za kike.Mzee alikuwa amefumba macho akisikilizia utamu wake.Binti
aliziminya tena chuchu za mzee kama ana finya hivi hadi mzee wawatu akajikuta
akikaza makalio!
“Kuna mambo mazito nitakwambia
utakapokuja.”
Msichana aliendelea na zoezi lake akizidisha utundu
na njonjo za hapa na pale ilimradi bwana Tufe ajihisi yupo peponi.Alipoona
msichana anazidi kumfanyia shere alimkamata kiuono nakumuinua juu kidogo.Alimpa
ishara amfungue zipu ambapo binti alitii nakutekeleza agizo la bwana Tufe.Ndani
ya sekunde chache walikuwa dunia yao.
***
Shuni alikuwa alikuwa anakatiza njia
kutoka mtaa wao.Kwisha muacha bwana Tufe kule kwenye ngome yao.Shuni alienda
moja kwa moja hadfi kwenye moja ya majengo yao ya kazi.Alifika kwenye jingo
nakuingia ndani.Alikutana na bosi wake aliyekuwa amejimwaga kwenye kiti. Shuni
alipomuona bosi alipewa ishara ya kuketi.
“Agent
unaendelea?”
“Tupo pazuri lakini kwa sasa naona wamechanganyikiwa
baada ya rais kutoa amri kutungua ndege ya Savanna Lands.”alitoa taarifa
Shuni.
“Kwanini inavyoonekana mzigo wao ni shehena
kubwa.”
Bwana Toti alikunja ndita kwa umakini,”Shuni good job kama
ameweza kudokezea kwako basi anaelekea kukuamini.”
“Bosi nimefanya
kila namna naelekea kupata ukweli.Huyu Tufe ni msiri sana.Nahisi itakuwa ni
shehena la madawa ya kulevya.”
Toti alizidi kupagawa,”Tukikamata
ishu hii lazima turudishe heshma kwenye idara yetu ya usalama wa taifa
KISS.Nakuhakikishia jambo hilo.
“Ndiyo hilo
litampa mheshimiwa Kilua uwajibikaji wetu na lazima atutambue.”alisema bwana
Toti.
‘Kwa maelezo ya Tufe ni kwamba shehena inaingia leo usiku
ingawa wana mashaka na ujio wa usalama.Hivyo tutafanya ushushushu kujua kuna
nini kwenye shehena hilo usiku wa leo.”alishauri Shuni,shushushu hatari sana
katika ardhi ya Kiota.Ukimuona ni binti mlaini asiye na makuu mpenda
mpole.Lakini alikuwa ni mtambo unaoweza kusavaivu popote pale.
“Ok
tutaandaa kikosi cha uhakika muende kwenye eneo husika nashauri muwe
makini.”
“Bosi naomba Pablo asiwepo kwenye hiki kikosi!”aliomba
Shuni kwa bosi wake.
“Kwanini?”
“Amekuwa akipinga sana
mimi kushiriki kwenye operesheni hii?”
“Nilisema msiwe na personal
issues kwenye kazi.Unakumbuka mafunzo yako yanasemaje?”
“Ndiyo
bosi.”aliitikia Shuni.
“Mkiwa hapa hakuna cha mambo ya binafsi.Hapa
ni kazi tu.”alisisitiza bosi Toti.Shuni alimuelewa bosi wake.Shuni aliinuka
kwenye kiti nakwenda chumba cha silaha.Alitoa kifaa chake cha mawasiliano
akaandika namba kadhaa kisha akafanya mawasiliano nakuita wakala kadhaa ambao
wangeshiriki pamoja katika operesheni kabambee anayokwenda kuifanya.Aliwapa
muhtasari kuhusiana na shughuli hiyo.Wote walikuwa na weledi wakutosha katika
kufanya operesheni hiyo.
***
Ikulu
“Napandisha kiwango cha
usalama hadi defcon 3 majeshi yetu yote yapewe taarifa hiyo.Savanna Lands
wakiwa tayari tutakabiliana nao muda wowote meanwhile nataka majina ya viongozi
wote wa jeshi nataka kuteua jenerali.”alisema Kilua akiwaambia viongozi wa jeshi
waliokuwa kwenye kikao.Ilikuwa ni tamko lake.Alikuwa na kibarua kizito sana
kukabiliana na vyombo vya habari pamoja na simu kutoka matifa mengine wakihoji
hatua yake yakutungua ndege ya Savanna Lands.Tayari taifa la Savanna Lands
lilianza kutoa malalamiko kuhusiana na hatua ya Kiota kutungua ndege
yao.
Presha ilipanda kila kona na yote ilihitajika majibu ya rais
Kilua aliyekuwa na wakati mgumu sana kuelezea.Muda mwingi alikuwa akishughulikia
mambo mengine huku wasaidizi wakijitahidi kujibu maswali ibuka dhidi ya serikali
hiyo.Utata ni kwamba jana taifa hilo limepatwa na msiba mzito wakufiwa kwa
viongozi wa serikali baada ya ndege ya kijeshi kuangukia kwenye jukwaa
walimoketi viongozi wa serikali leo jeshi hilohilo linatungua ndege ya jeshi la
nchi jirani.Swali lilikuwa kubwa je,ni Savanna Lands waliosababisha ajali ya
jana?Kamati ilikubaliana kutokuleta habari kuhusiana na serikali kushuku ajali
iliyotokea kuwa ni mkono wa mtu!Sasa tayari maswali yameanza kuzuka.
Kilua alikuwa kwenye kipindi kigumu sana!Ni siku nyingine lakini tayari ugumu
unazidi.Alitamani kuachia madaraka!Lakini alijikaza.Nafasi pekee yakuokoa
familia yake ni kubaki madarakani.Majina yaliletwa mbele yake aliyapitia pamoja
na wasifu wa watu hao akitaka kumteua mkuu wa majeshi haraka iwezekanavyo maana
hali ilikuwa tete kwa wakati ule.Alihitaji mkuu wa majeshi tena
wakuaminika.Ndani ya muda mfupi anaenda upekua jeshi pande zote apate majibu ya
kwanini mwanajeshi aliangusha ndege nakuua serikali nzima!Kuna usaliti katika
taifa.
Kilua alielekea kwenye ofisi yake walinzi
wakimsindikiza.Aliingia nakuachwa mwenyewe huku akipitia orodha ile.Lakini ndani
ya muda mfupi aliingia Serambovu nakuichungulia orodha kisha
akatabasamu.
“Kanali Lupogo anafaa kwa kazi hii.”alisema
Serambovu.
“Amefikia viwango vyote vya kuwa jenerali?”
“Wewe ni amiri jeshi unampa yeyote tafadhali mteue.”wakati huo Serambovu
alishampigia simu kanali Lupogo aje ikulu kwaajili yakupokea madaraka.Na tayari
alikuwa amefika hapo.
“Nataka nimteue haraka sana sitaki tuchelewe
Kiota inahitaji kusimama.”alisisitiza Kilua hasa akijielewa hana kauli kwa bwana
huyu.
“Kanali anakusubiri kupewa madaraka.”alisema Serambovu.Kilua
alimwangalia nakushukuru maana Serambovu anajua kupeleka mambo haraka hivyo
anatua mzigo.Aliinuka nakuongozana naye hadi eneo maalum la kumuapishia kanali
Lupogo.Kwa jinsi mambo yalivyofanyika hali ilikuwa tete.Ndani dakika kama
thelathini ikulu ilitulia kushuhudia kanali Lupogo akiapishwa kuwa mkuu wa
majeshi ya Kiota.Zoezi lilisimamiwa na rais Kilua mwenyewe.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimeamua
kumwapisha kanali lupogo kuwa jenerali wa majeshi yetu pia hafla hii itafuatia
kwa mimi kumteua Bi Sada kuwa katibu mkuu wa serikali.Hivyo tushirikiane katika
zoezi hili.Kiota ina hitaji uongozi na mambo lazima yaende.Najua bunge
lingetakiwa kupitia wateule hawa kabla ya kuwapa mamlaka lakini huo muda ni
mchache natunahitaji watendaji.”
Chumba kilikuwa kimya wakati rais
Kilua akizungumza.Zoezi lilianza mara moja.Kiota ilikuwa imepata mkuu mpya wa
majeshi pamoja na katibu mkuu mpya.Cheo cha ukatibu mkuu ilikuwa kidogo Sada
akatae maana alijua angeandamwa na faili namba 13:14
***
Mlio wa boti ulikoma punde
walipofika usawa waliotaka wa bahari.Walivalia mavazi yakupigia mbizi pamoja na
vifaa vya kupumulia.Giza lilikuwa la kiasi litandazwa na mwanga hafifu wa
mbalamwezi angani.Uwepo wa nyota ni kiasi tu.Bahari ilikuwa shwari kwa usiku ule
wenye utulivu.Injini ya boti ilikimya na kuacha sauti ya maji ambayo kutokana na
utulivu wa bahari ilikuwa kiasi ya kuliwaza.Shuni na kikosi chake wakiwa na
mavazi yao maalum kwaajili ya uchunguzi walivalia vifaa vyote nakurukia kwenye
maji!Chubwi!Waliingia huku mavazi yao yakitota kukutana na maji ya
bahari.Walianza kupiga mbizi.
Walikuwa na uhodari wa kuogelea kwa
mwendo mrefu bila kukata tamaa na hivi walikuwa na vifaa vya kupumulia kazi
ilikuwa rahisi kwa upande wao.Waliendelea kuogelea kwa umbali Fulani.Masikioni
walikuwa na vifaa vya mawasiliano maalum.Pamoja na vifaa vya kufuatilia vya
satellite vilivyoonesha usawa waliopo kwenye uso wa dunia.Baada ya muda mfupi
walikuwa usawa husika ambapo kulikuwa na meli inaelekea bandarini.Waliogelea kwa
kasi kidogo hadi walipoifikia meli yenyewe.Walifanikiwa kupanda kwenye meli hiyo
bila kujulikana na yeyote kwa usiri wa hali ya juu na ustadi mkubwa.
Walitegemea kukutana na upinzani mkali ambao ungehatarisha usalama
wao.Walifanikiwa kuvua vifaa vyao vya usafiri kwenye hasa vipumulio wakaviweka
mahali ambapo mmoja wao alibaki anavichunga.Ilikuwa operesheni ngumu hasaa
ukizingatia hawajui ni meli aina gani inakuja.Walikuta ni meli kubwa sana
iliyobeba shehena kubwa ya makontena!Shuli alikuwa na kamera maalum iliyokuwa
imehifadhiwa kwenye vifaa maalum kukwepa kuloana.Alianza kuchukua picha za mnato
pamoja na maeneo kadhaa ya ile meli.Waliingia hadi ndani nakuchukua picha nyingi
za mnato.Waliona watenda kazi wa meli wakiwa bize na shughuli nyingine
wakijiandaa kutia nanga.Mpango wa Shuni ulikuwa kuchukua ushahidi wa kutosha
kabla meli haijatia nanga.Zilikuwa zimebaki umbali mchache meli ifike bandarini
walichokifanya wao kina Shuni walishukia mbali na bandari kisha wakaiwahi meli
nakuizamia kabla haijafika bandarini.Walishukuru hawajaonekana hadi kuingia sasa
ilibaki kazi moja tu kuchukua ushahidi wa kutosha.
Moja ya kontena
walikuta lina kauwazi kidogo.Shuni alijizamisha humo nakuchukua picha za kutosha
mlikuwa na vifaa vingi vikubwa vikiwemo mabomba makubwamakubwa!Shuni alikuwa
mwepesi katika kuchukua picha zile kwa haraka!Wakiwa pale walisikia vishindo
nyuma yao!
“Nyie kina nani?”sauti kavu iliuliza!Shuni aliuma meno
kwa hasira alipogeuka walikutana na mtu mwenye miraba mine akiwa
anawaangalia!Palepale bila ajizi walianza kumshambulia maana ikitokea huyu mtu
akapiga kelele watakuwa wamekwisha.Wakati haya yanaendelea Toti alikuwa
akisikia hatua zote kupitia vifaa vya kupitishia sauti!Mapigano mazito yalifanya
kazi kwa takribani dakika tatu hadi wakafanikiwa kumzidi bwana Yule
nakumuangusha chini walimpiga akazimia!
Shuni alitegemea kupata
shehena kubwa la madawa ya kulevya lakini tofauti alikutana tu na vyuma vikiwa
vimepakiwa!Kwa kuvitambua aliona vifaa kama drill line,drawa-works,stand
pipe,crown block.Kwa akili ya haraka alijua fika hivi ni vifaa mahsusi kwaajili
ya kuchimbia mafuta!Baada yakuona hakuna umuhimu aliwapa ishara wenzake waondoke
eneo lile.Zile picha alichukua memory kadi kutoka kwenye kamera akaiweka kwenye
simu yake kisha akazinyonya picha zote halafu akazituma kwenye barua pepe
yake.Tayari ameshatoa kopi za kutosha.Walianza kutoka kwa uangalifu warudi
majini.Walipofika eneo walipomuacha mwenzao aliyekuwa analinda vifaa vyao vya
kupumulia majini walimkuta kaanguka chini akiwa katoa macho huku kwenye kifua
kukiwa damu!Kitu chenye ncha kali kilikuwa kimepenya kisawasawa!Wote
wakataharuki!Walikuwa wamegundulika!Wakati Shuni anataka kuegeuka watafute njia
nyingine alishtukia kitu chenye ugumu wa chuma kikimpiga kwenye kisogo akahisi
kupoteza fahamuAlijikuta akilewa kwa ustadi mkuu aliitupa simu yake
baharini!Akaanguka chini nakuwa kimya!
Waliomtwanga waliwapiga na
wenzake!Wote walikuwa kimya!
Hatua nzito zikasikika akatoea mtu
mzima mmoja mzungu!Alikuwa kavalia miwani ya macho!
“Ni kina
nani?”aliuliza akiwa amekunja uso.Hakupendezwa na ujio wa watu hao kwenye meli
yao!
“Bado hatujajua wameingiaje lakini kwa mavazi walikuwa
wanaogelea.Hawa sio watu wakawaida hadi wavamie meli yetu usawa huu!Walikuwa na
nyambizi nini?”aliuliza mmoja ya walinzi.
“Nadhani tutawaua wote
halafu tumbakize mmoja tu.Huyu mwanamke ndo atajibu kila kitu wamewezaje kuingia
humu ndani.Ila nataka tuongee na informer wetu wa ikulu aweke mambo
sawa.”alisema Yule mzungu.
“Bosi hii imeshakuwa mbaya kwa sisi
kuvamiwa na wazawa kwenye meli yetu.Ni nani kafanya uzembe huu hadi watu hawa
wajue kwamba meli yetu inakuja usiku huu?”aliuliza moja ya walinzi.
“Ndo maana nasema hadi niwe na majibu na informer wetu wa ikulu.Lazima tujue
anayevujisha hizi habari.Au labda hawa wawe maharamia ndo mnishawishi!”mzungu
alijibu vile.
Palepale mzungu aliondoka akiwaacha walinzi
wanaowachukua mateka wao nakwenda nao hadi ndani nakuwafunga kwenye
chumba!
Mzungu aliingia kwenye chumba cha kuongoza meli.Alichukua
simu ya mkononi nakubofya namba Fulani.Kulikuwa na maelekezo mazito anaenda
kuyatoa!Ni nani anayepigiwa simu ikulu!
Aliinua
mkono uliokuwa umefunikwa na blanketi lenye uzito.Aliupeleka hadi kwenye meza
ilikuwa pembeni kisha akaichukua simu iliyokuwa na mtetemesho wenye kuashiria
kwamba ilikuwa inaita.Aliipokea nakusikia sauti ya upande wa pili kulikuwa na
maelekezo Fulani ambayo yalimzindua fahamu za mwili zilizokuwa bado na wingu la
usingizi nay eye kuamka kabisa.Sasa alihisi mwili wa mwanamke aliyekuwa pembeni
yake huku joto la mwili wake ukimfariji.Harufu ya mwili wa mwanamke huyu
aliyejikwatua kwa tarabizuna ilisababisha utuli wenye kufariji!Hata habari
aliyopokea ilizidi kumtatiza sana!
“No hakuna yeyote zaidi ya mduara
wetu…Impossible kuwe na inspection…No!Listen Mr Zungu nakuhakikishia hakuna
yeyote…just finish her…”alitoa maelezo bwana huyu kisha simu akaikata bila shaka
aliyekuwa anaongea naye hakumpa nafasi yay eye kutamka chochote alimdhibiti
kimaelezo!
Alirudia kuvuta harufu ya mwanamke aliyepembeni yake
nakuupapasa mgongo wake ulikuwa wazi kiasi cha kutuma msisimko kwa mwanamke huyo
unaoshtua!Yule mwanamke alizinduka kutoka usingizini nakujikuta akitamka
neno,”Oh Dedani?”
“Shss!Ni Serambovu siyo Dedani.”alijitambulisha
mwanaume Yule.Kilua alimkumbatia kwa nguvu mwanaume Yule nakujilaza kifuani
mwake huku akivuta hisia kwa nguvu lakini ombwe kubwa liliukumba moyo wake
akahisi kama anasaliti kitu katika maisha yake alijikuta akimuachia mwanaume
Yule kwa haraka.
“Bado unaweweseka na njozi za familia
yako?”
“Ndiyo naziona sura zao kila nikifumba macho nahisi
wananitazama nakunililia moyoni mwao.”
“Kwani
imekuwaje?”
“Tangu atufumanie sijamtia machoni!”
Serambovu alihisi moyo ukienda mbio kwa muda kidogo lakini akakosa
jibu.
“Najua wametekwa.”
“What?”Kilua
akashtuka.
“Ndiyo najua ametekwa.”
“How did you know
that?”
“Najua tu!”
Kilua alihisi kitu iweje Serambovu
ajue ishu ya familia yake kutekwa wakati muda huo wote ni yeye na walinzi wake
na sio rahisi siri ile ivuje hata kwa dawa!Hapana kuna kitu kizito nyuma ya
pazia!Hili jambo kalijuaje?Wakati akiwaza hayo aliamka muda ule ilikuwa saa tisa
usiku.Alienda moja kwa moja hadi bafuni akafungulia maji nakuanza
kuoga.Alijiandaa kwa muda wa dakika 30 za uhakika kisha alivaa.Alitoka nje ya
chumba bila kumsemesha Serambovu kitu chochote kile.Alikutana na walinzi wake
wenye zamu ya usiku.Aliongozana nao hadi ofisini kwake.Walinzi walianza
kugutusha watendaji wengine wa mkuu wajue yupo macho.Aliingia ofisini akachukua
mafaili kadhaa.Leo kazi ilikuwa ngumu kweli kujua atakabiliana vipi na tishio la
kuingia vita na Savanna Lands hapohapo anatakiwa kuhakikisha usalama
unapatikana.Bila shaka amejua mpaka sasa kwamba serikali ya Kisusi iliondolewa
kwa mauaji ya nguvu na bila shaka kuna mikono ya watu.Idara zote zimekuwa katika
kizungumkuti kikubwa sana!
Alimfikiria sana mkuu wa idara ya usalama
wa taifa.Alifikiria pia hatua za kuchukua kama rais.Hakupendelea kuanza kukamata
watu nakuwasweka ndani hasa katikam kipindi kile japo wengi walihitaji majibu ya
haraka kuona kama kuna mkono wa mtu basi waadhibiwe.Alihitaji kukamilisha msiba
mkubwa wa taif kwa kuwapumzisha marehemu wote.
Akiwa pale alisikia
mlango wake ukigongwa kisha mgongaji akaona bora afungue tu.Akaingia ndani
nakumkuta Bi Kilua amejaa tele ka pishi la mchele kwenye shughuli.
Alikuwa ni Director Masha,”Habari Mheshimiwa.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Salama.”
“Nimekuja nataka msaada wako.”
“Upi
tena.”
“Nataka tumuingize mkuu wa idara ya usalama katika uchunguzi
huu.”alisema bwana Masha.
“Kuna nini?”
“Kuna majibu
atatupa.”
“Ni sawa ila kuna jambo nahitaji msaada wako.Hadi
tunavyoongea sijui hatma ya familia yangu.”alisema Kilua akiwa na masikitiko
makubwa.
“Ni vipi kwani?”
Kilua alifikiri kidogo kabla
hajajibu mlango ulifunguliwa akaingia mjakazi wa ikulu akaingia nakuleta kahawa
akawapa wote wawili.Alipomaliza kuwatengea aliwakaribisha kisha akaondoka.Kilua
alimwangalia director Masha kisha akasema,”Some people think I am
weak.”
“Hapana mheshimiwa wewe sio dhaifu tena nimegundua hakuna
rais jasiri kama wewe.Kuchukua nchi katika hali kama hii sio kitu rahisi.Wakati
mwingine hali ndizo zinazoamua maamuzi yetu.Ninaamini unaweza prove them wrong
and lead the country madam President.”
“Hiki kiti kimekuwa mzigo
kwangu wengine wanaona nimepata bahati lakini imekuwa kama mkosi but I will play
their game!Nitawafuata kulekule wanapotaka twende.”
Kilua alikunywa
kahawa iliyopenyeza joto kwenye mwili wake kisha akaendelea,”Wameiteka familia
yangu na wanataka kitu ambacho siwezi kupata.”
“What?”
“Nahitaji usiri wako chunguza jambo hili nataka usalama wa familia yangu
simuamini mtu yeyote katika hili.Naomba usiri wako.”
“Ilitokeaje?”
“Siku ileile niliyoapishwa ndo familia yangu
ilitekwa.”
“Wanataka nini?”
“Nitakwambia muda ukifika
but first nahitaji usiri.Hawa watu wanajua kila ninachofanya hata ikulu.Siajabu
hata ninavyokushirikisha itakuwa wanajua hili jambo.”
“Niamini
mheshimiwa siwezi kukuangusha.”
“Hatua ya kwanza nataka mumfanyie
Serambovu upelelezi wa siri.Dukua mawasiliano yake na kila baada ya muda
nahitaji taarifa ujue anaongea na nani na kipi wanachoongea.”alitamka Kilua
akiwa anajiamini.Masha alikuwa makini kuhusu maagizo haya.
“Unadhani
adui atakuwa humu ikulu?”
“Ndiyo adui yangu anaweza kuwa anatumia
watu.”
“Pili nataka upeleleze kuhusu file namba 13:14.”
Masha akashtuka sana kusikia faili hilo.Mshtuko wake ukamgusa bi Kilua,”Mbona
umeshtuka.”
“Hilo faili liliwapa idara ya usalama taabu sana.Kuna
viongozi walitimuliwa kazi kisa hili file.”
Kilua alitikisa kichwa
kumuelewa nakuona anatakiwa alivalie njunga swala lile.Bila kuenda na umakini
wakiakili inawezekana akapoteza vita ile.Kwa sasa alitakiwa kuwa kama rais wan
chi na si ule udhaifu wa kuonesha alipewa madaraka ghafla bin vuu bila kujiandaa
kwa lolote.Alitakiwa awe makini sana bila kupepesa huku wala kule.Tayari kesha
mwambia director Masha kwamba familia yake imetekwa.
“Ni file lenye
mambo mazito sana na hadi kujua hili jambo inahitajika nguvu ya ziada.Wanahusika
na jambo hili wapo ndani ya serikali kila sekta ni rahisi kujua yeyote anayetaka
kutafuta nyaraka hizo.”
Kilua alikunywa kahawa yake
tena.
“Kwa majibu machache nimeskia hizo nyaraka ni kuhusu mkataba
Fulani wa kitu ambaol ulipita serikali zilizopita na haupaswi kuingiliwa na
yeyote.Lakini sasa nalazimishwa kufanya upekuzi maana…”alikwama
kidogo.
“Wataidhuru familia yako kama hutawapa nyaraka hizo ambazo
hata wewe hauna!”alijibu director Masha akiwa na umakini wa hali ya juu.Hatua
hiyo ikatihibitisha kile ambacho Kilua hakuwa tayari kukisema kwa wakati
huo.Familia yake imetekwa.Kisha anatakiwa kuwasilisha nyaraka za faili namba
13:14 au familia yake idhuriwe.Ilibidi aeleze kila kitu kilivyo tangu alipoingia
madarakani ni vitisho alivyopokea kwa director Masha ambaye alipandwa na hasira
kuona rais wake anatishiwa aliapa kutumia ujuzi wake wote kudhibiti kila kitu
hadi atakapo dhibiti jambo hilo.
“Ndiyo hivyo
ilivyotokea.”
“Usijali nitahakikisha tunadhibiti uzandiki huu
nakuufutilia mbali.Ila najua tutapitia vikwazo lakini nakuahidi nitadhibiti hili
swala.”alisema director Masha.Makubaliano ilikuwa kuanza kupeleleza dhidi ya
faili namba 13:14 pamoja na familia ya rais.
“Pia nataka kufanyike
upembuzi wa mikataba yote iliyoingiwa awamu zilizopita nakuwe na vigezo ilikujua
ni mkataba gani huo uliopo kwenye hizo nyaraka.”alishauri rais Kilua akimalizia
kikombe cha kahawa.
“Tupo pamoja.”
Masha aliondoka
kutoka kwa rais.Sasa alijua fika kupata wepesi wakupitia mikataba hiyo ni lazima
aende kwa mkuu wa idara ya usalama wa taifa huyo anaweza akajua ni mikataba ipi
itakayozua utata hadi aweze kuoanisha nyaraka zile muhimu zinazomnyima usingizi
rais Kilua.Akiwa anatoka ikulu kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake alipotizama
alikuta ni kutoka kwa mhariri ambaye ni mchapaji wa gazeti la Alfajiri.Gazeti
pendwa kwa habari nyeti tena nzito na zile zenye udaku ndani yake unaokaribiana
na ukweli.Mida ilikuwa saa kumi na moja alfajiri.Aliamua kuelekea moja kwa moja
hadi ofisi za gazeti hilo maana ujumbe ulimtaka aweze kufika kwa siku ile.Mwendo
ulikuwa wa dakika kama 40.Hadi inafika saa kumi na moja asubuhi tayari alikuwa
alikuwa viunga vya mjini akiifuata ofisi ya gazeti la Alfajiri.Aliingia hadi
ofisini kwa mhariri nakukutana nakala moja iliyochapishwa ikiwa na kichwa cha
habari kizito chenye kumtisha hata mwendawazimu.RAIS KILUA NA MCHEPUKO WAKE!Hilo
lilitosha kabisa kuona hizi si habari njema kwa rais Kilua nizakumpaka
doa!
Director Masha alipigwa na butwa pamoja na
bumbuwazi lenye kukereketa ini na moyo.Kichwa kile kilizidi kumtisha hasa baada
ya kuwa na hakikisho kwamba mume wa rais Kilua yupo mateka.Sasa linapokuja swala
lakumuandika rais kuwa anamchepuko lilizidi kumtishia na kudhaifisha ustaarabu
wa rais Kilua.Ni kweli rais huyo anapitia kipindi kigumu na wakati sio wa kuja
na habari kama hizi zenye kumkashifu nakuitia doa heshma yake.Alipitia habari
ile inayomshtumu Kilua kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine
amabaye siyo mume wake.Pia habari hiyo inahoji uwepo wa mume wa rais Kilua maana
haonekani ilihali rais anahusishwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine
ambaye ni stafu wake!
Hilo lingeilazimu stafu nzima ya ikulu iwe
matatani hasa kwa kipindi kama kile chenye wingi wa mashaka na huzuni.Iwe kweli
au uongo habari ile ilihitajika kudhibitiwa sana.
“Inachapishwa leo
hii habari?”
“Ndiyo leo inahitajika iwe sokoni.Magazeti yamechelewa
kisa hii habari niliokuwa nakutafuta sana tangu jana ukawa bize.Nilitaka uijue
kwanza kabla habari haijaenda hewani gharama za magazeti yote ni kwa kila nakala
ni milioni 40!”alisema mhariri wa habari ile bwana Sudi.
“Una
maanisha nilazima habari idhibitiwe kwa pesa?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo la sivyo
hatuna bahati.Your President will get it from me.”
Masha alitaka
kuchomoa bastola yake lakini akakumbuka sheria hairuhusu hawa ni waandishi wa
habari wana uhuru wao.Muda ule haitakiwi kabisa kuingiza ubabe japo habari
yenyewe imekuja wakati mbaya.Alivuta pumzi ndefu na kuzishusha.Hili lilikuwa
jambo zito na lazima lidhibitiwe kwa nguvu zote anazojua.
“Nipe kopi
ya hilo gazeti naenda ikulu mara moja naomba usisambaze gazeti hili hadi hapo
nitakapokujulisha.”alisema Masha akiwa anasisitiza ujumbe wake.Sudi alionesha
kumwelewa.Sudi alikuwa na tabia kama hiyo yakutoa vitisho katika kutishia habari
nyeti zisitoke au matakwa yake yatimizwe lasivyo atausambaza.
Ilibidi Masha arudi ikulu muda ule japo alikuwa na miadi yakumtafuta mkuu wa
idara ya usalama lakini wazo hilo likafa kibudu kwa muda hadi pale habari mbaya
kumhusisha rais zikapodhibitiwa nakufukiwa katika kaburi la sahau.Alikamata
usukani wa gari nakwenda mbio kuwahi ikulu.Dakika zilipokatika alikuwa keshafika
ikulu asubuhi ile mida ya saa kumi na mbili.Aliomba nafasi ya kuonana na
rais.Kwa kuwa alikuwa na kibali maalum hakuchelewa kupata wasaa wakumuona rais
wake.
“Kuna nini tena Mr Masha?”aliuliza Kilua maana alijua kama huyu
mtu karudi basi bila shaka kutakuwa na jambo gumu.Wameongea muda mchache
uliopita.
Masha aliweka lile gazeti juu ya meza paap!Kilua alilipokea
nakulitizama moyo ukapiga mkambi.Ilikuwa habari mbaya kwake.Ilikuwaje ikavuja
jambo hilo.
Rais Kilua aliwaza nakuhisi kichwa kuwa kizito kwa
msongo wa mawazo.Habarii ile ni kweli.Yawezekana kweli ikawa imevuja lakini
kutoka kwa nani?Aliyujua kwamba alicheza karata hizo kwa usiri lakini sio kwa
namna ambayo kuna kiumbe angekuwa na thubutu ya kujaribu kuandika habari hiyo
kwenye kurasa za gazeti tena kuitoa ukurasa wa mbele.Nchi ilikuwa kwenye wakati
mgumu na sio kupokea kitu kama kile.Pale ingemlazimu kusema familia yake ilipo
bila shaka mumewe angetafutwa kuthibitisha habari ile au kuikana.Lilikuwa tukio
lisilo na urafiki wowote kwa upande wake!
Pia maadui zake wakisiasa
wangeweza kutumia habari ile kumuadabisha yeye sasa na huko mbeleni kadri siku
zitakavyokuwa.Nilazima jambo hili lidhitiwe kwa hali zote.
“Wanataka
milioni arobaini la sivyo habari hiyo itaingia sokoni muda si mrefu.”alisema
Masha.
“Unaamini habari hizi?”aliuliza Kilua.
“Hapana.Ninachojua wewe ni rais wangu na mishale ni mingi inaelekezwa
kwako.Jukumu langu nikukulinda.Unaweza muita mhariri Yule ukampiga marufuku
kuitoa habari.Lakini tupo katika wakati mgumu hatua yoyote ina matokeo.”alisema
bwana Masha akionesha kumpa ushirikiano rais Kilua.
“Ngoja ni mwite
chifu wangu wa ushauri.”alisema Kilua kisha alichukua simu yake na kumpigia simu
Serambovu ambaye alikuja muda uleule.Aliingia ndani ya ofisi kisha akapewa lile
gazeti na Kilua.Aliliangalia kisha akainua macho kumwangalia Masha.
“Huyu mhariri kesha toa hii habari?”
“Anatishia kuitoa tayari
imechapishwa lakini bado nakala hazijasambazwa na kama zikisambazwa ni mauzo ya
milioni arobaini.Anataka hizo fedha alipwe yaani tulipie gharama za nakala zote
tuzichukue sisi ili umma usizione.”
Serambovu alihamaki kisha
akasema,”Hadi muda huu bado huyu fala anapumua?”
Masha alitegemea
jibu kama hili kutoka kwa rais lakini badala yake akaona kama mwenye kauli ni
Serambovu.
“Unamaanisha afutiliwe mbali?”
“Ndiyo huu sio
muda wakupokea habari kama hii!Ni muda wakumfutilia mbali kabisa.”
Kilua aliinua kikombe cha kahawa alikunywa tena kuchangamsha ubongo.Lakini
alihisi kama kuumwaumwa.
“Sihitaji mauti lakini nahitaji huyo mtu
anyamaze na habari hii isitoke mbele ya umma.”alisema Kilua akihisi kutapika
alikimbilia bafuni kwa haraka kwenda kutapika.Ofisi yake ilikuwa na bafu alienda
huko nakutapika asubuhi ile.Alihisi kama kuumwaumwa asubuhi ile.Mwili wake
haukuwa wa kawaida.Alinawa nakupiga mswaki kisha akarudi ofisini kwake.Aliwakuta
Masha na Serambovu wakimsubiri.
“Upo sawa?”aliuliza Masha.Kilua
alitikisa kichwa kuonesha yupo imara lakini sio kivile.
“Nataka
habari hii isitoke kama ni pesa apewe lakini nakala zote ziteketezwe!”alisema
Kilua.
Serambovu aliomba apewe nafasi yakushughulika na jambo
hilo.Alipewa maelezo na Masha kisha akaanza hatua za kuidhibiti habari ile
isitoke.
***
Masha aliondoka moja kwa
moja hadi makao ya usalama wa taifa.Alifika nakukaribishwa asubuhi ile ambayo
nimbichi.Alikuta kuna kama taharuki akiomba kuonana na mkuu wa idara
ile.
Kwa kuwa alikuwa na kibali maalum kutoka kwa rais alipita mara
moja hadi ofisini kwake.Alimkuta mkuu Yule akiwa mwingi wa mawazo na
wasiwasi.
“Vipi bwana mbona kama haupo sawa?”
“Kuna
tatizo kubwa limetokea.”
“Tatizo gani?”
“Tulikuwa kwenye
oparesheni ya undercover bahati mbaya mashushushu wetu wamekamatwa.Tunashindwa
kuvamia nakuwatoa maana tutaharibu operesheni nzima.”alisema bwana Toti akiwa
ameshika kichwa.Siku ile alikuwa na wakati mgumu sana.Operesheni ya jana
imeshaondoa uhai wa watumishi kadhaa wa idara hiyo na leo hali imekuwa
tete.
“Nikawaida kwa kazi zetu lakini naimani vijana wako wana
mafunzo ya kutosha na watasalimika inshallah!”
Toti alitikisa kichwa
kuonesha kukubali jambo lile.Palepale Masha alitoa kibali chenye muhuri wa rais
kuonesha kwamba amepewa nguvu ya kuvuka mipaka yote kukamilisha uchunguzi
wake.
‘Nikusaidieje bwana Masha.”
“Nataka kujua kuhusu
mikataba iliyoingiwa hapa nchini.”
Toti alikaza ndita kidogo kuwa
makini kwa swala la Masha,”Kuna mikataba mingi sana taifa letu iliyoingia
pengine uwe specific na swali lako ni mkataba upi?”
“Kuna mkataba
mmoja ambao umekuwa wa siri sana na umetesa serikali iliyopita nahii iliyopo.Huu
mkataba uana dira umekuwa gumzo kila anayeutaka anaishia kati ya kuwa chizi au
kufa.Ninaamini taasisi hii ina ufahamu wa mkataba huo.”
Toti
alitetemeka kwa wasiwasi sana.Alishangaa kugusishwa kwa jambo kama hilo kwamba
huo ni mkataba gani?Kichwa chake alikihamisha kutoka kwenye zimwi la kutekwa kwa
vijana wake akajileta kwa Masha amsikilize.
“Kuna mikataba ndiyo
iliingiwa kwa nguvu na kuwanyamazisha watu Fulani.Sasa sijajua unataka kujua ipi
naweza kupitia kaukaguzi kidogo halafu nitakuletea mikataba hiyo yenye kutishia
maisha.”
Masha alitoa shajaa yake akaandika namba 13:14 kisha akampa
bwana Toti,”Naomba uangalie hii namba halafu ukipata faili lenye utambulisho huu
nitahitaji kujua nila nani?”alisisitiza bwana Masha.Toti alimwangalia kisha
akafungua tarakilishi yake nakufungua faili Fulani alianza kupitia wakati huo
Masha alikuwa akibofya simu yake akisoma kitu.Ilimchukua bwana Toti dakika tano
kupata faili hilo lenye jina nywila (CODE NAME 13:14)Alimuonesha bwana Masha
faili hilo.Kilichomshtua zaidi waliamua kuliangalia pamoja kisha waligeukiana
kwa pamoja.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tutalikagua hapa
kwa muda kisha tumpelekee rais taarifa ya nyaraka hizi.Pia nitampa kijana
ninayemuamini anifanyie upekuzi kuona kitu gani kinashabihiana.”ilikuwa kazi
iliyohitaji mambo mengi sana na majibu kadhaa.
***
Shuni alizinduka
nakujikuta akiwa kafungwa kwa kamba nzito juu ya meza.Pembeni alisimama Yule
mzungu.Macho yakiwa makali na ukavu wa ukatili ulijichora kwenye wajihi
wake.Alipojaribu kuinua shingo yake alihisi imefungwa kwa kitu kama mkanda
iliyomshikilia kwa nguvu kwenye meza ile.Ungesema kapigiliwa
misumari!
Watesi wake walichukua kitambaa wakamfunika usoni kisha
likaletwa jagi lililojaa maji wakalimimina kwenye uso wake.Maji mengine
yaliingia kwenye pua na mengine yalinyeshea paji la uso!Aina ya fedheha
aliyopatwa nayo bi Shuni ingebaki daima rohoni mwake.Yalikuwa mateso makubwa
sana alijikuta akifurukuta nakuachia kelele nyingi zilizotoka kwenye moyo
wake!
Walifanya vile kumfedhehesha mwanamke Yule!Kisha wakaacha
nakufunua kile kitambaa.Shuni alizitafuta pumzi kwa hali na
mali
Gari iliingia viunga vya ikulu kwa haraka
sana nakuegeshwa eneo husika.Walishuka bwana Masha pamoja na Toti wakaelekea
moja kwa moja hadi kwenye eneo la mapokezi.Walitoa maelezo yao kwamba walihitaji
kuonana na rais Kilua kwa dharula.Kwa kutumia kibali kilekile alichokuwa nacho
Masha aliweza kwenda kumuona rais Kilua ambaye alikuwa na kikao na kamati ya
diplomasia wakijaribu kudhibiti mzozo wake na taifa la Savanna lands.Kilua
aliposikia ujio wa watu hawa alikuwa na shauku kubwa kuonana nao ajue wamefikia
wapi kwa wakati ule.
Alihakikisha watu wote waliopo karibu yake
wameondolewa ilikuwapa nafasi yenye uhuru kusikia walichokigundua baada ya
kufanya upekuzi wa awali.Hali ilikuwa tete kwa upande wa Kilua.
“Mheshimiwa tumefanya ukaguzi kama ulivyo nituma nikishirikiana na
mwenzangu.”
Kilua alitulia akimsikiliza kwa umakini wa hali ya
juu.Alisikilizia mapigo yake ya moyo yalivyo enda.
“Tumepata faili
linaloshabihiana na lile ulilotaja.Hili nalo lina hiyo tarakimu ya
13:14.Tulichogundua hiki hapa.”Alisema Masha akifungua kompyuta mpakato yake.
Kioo kikaonesha mafaili kadhaa wakachagua lile wanataka kisha
likaonekana.Ilikuwa ramani!Moyo ukawapiga mkambi.Ilikuwa ramani ya taifa la
Kiota.Halafu kuna ramani ya jimbo la Kibatari nakuna eneo limewekewa alama
maalum na kuna kodi 13:14.Eneo hilo.Kukagua maelezo zaidi yalihusu utafiti wa
kitu.Waliendelea kuangalia kwa umakini kila kitu walichokiona.Lakini hakuna
maelezo kusema ni utafiti wa aina gani uliokuwa unafanywa eneo hilo.
“Kuna utafiti unafanyika hapa lakini hakuna data base yoyote inayosema eneo hili
linafanyiwa utafiti wa kitu gani?Temejaribu kila tunapojua kuna data za siri but
hakuna inayohusisha na eneo hili kuwa na utafiti wa aina yoyote.”
“Je,tukifanya upelelezi wa eneo hili kujua kuna jambo gani linafanyika
hapo?”
“Ni jambo jema lakini nisingeshauri eneo hili lichunguzwe kwa
haraka.Tutumie mbinu kwanza kujua kuna vitu gani vina safirishwa na vitu gani
vinaingia nchini.Kila shughuli inayoelezwa kuhusiana na utafiti wowote basi
tujue ni vifaa gani wanatumia vinaingiaje nani wapi vinatumika na kwa matumizi
gani?”alishauri bwana Toti.
“Lakini inaweza kuwa nini?”
“Kuna kitu eneo hili.Nakumbuka watangulizi wangu kwenye idara hawakutushauri
tufanye ushushushu mwingi eneo la Kibatari kwa kuwa mheshimiwa ulikuwa gavana wa
eneo hilo ni kweli haujui utafiti wowote uliokwa unafanyika eneo
hilo?”
Kilua alionesha kushtuka akivuta kumbukumbu.Kweli Kibatari
aliifahamu kama kiganja cha mkono wake lakini hakuna utafiti wowote uliokuwa
unafanyika eneo hilo.Ni eneo lililotwaliwa kutoka taifa jirani na mara nyingi
jeshi limekuwa na nguvu sana eneo lile kiasi huwezi tilia shaka usalama wa
Kibatari kwa namna yoyote.Shughuli nyingi za uchumi hazikuhusisha uchimbaji wa
rasilimali yoyote zaid ya kuwa ni shughuli za kawaida na hiyo ilihusishwa na
kudhibiti eneo lile lisipanuke kiuchumi ilikuondoa makundi yenye ukwasi.Wakwasi
wengi walitoka majimbo mengine nakuwekweza huko,Kibatari walikuja tu kutumia
ukwasi waliovuna kutoka maeneo mengine ya nchi.
“Hapana ningejua tu
kama kuna shughuli ya utafiti maana lazima zipitie ofisi yangu.”
“Yawezekana hukujua.Kwa jinsi faili 13:14 lilivyotesa wengi labda kuna
uwezekano kwenye ramani hii kulikuwa na utafiti wa kitu ambacho hata wewe
hakupewa nafasi ya kujua.Ndo maana gavana wa Kibatari hakuwa anachaguliwa kwa
kura bali ni uteuzi wa rais tu.Kuna sababu nyingi zinazofanya wewe usielewe na
kwa idara yangu tuliliangalia jambo hilo.Gavana wa Kibatari huwa toothless
dog!Lakini ni simba aliyelala maana kuna kitu muhimu amekalia katika jimbo
hilo.Katika top secret za serikali gavana wa kibatari huongozwa kutoka ikulu
bila hata yayeye kujua.’’alisema bwana Toti akimpa maelezo rais Kilua.Toti
alikuwa mwepesi wa kuchambua mambo na kuyapeleka anapotaka.
“Ina
maana sikupaswa kujua kama kuna utafiti eneo langu la Kibatari?”
“Ndiyo mkuu.Hukupaswa ila kuna watu walipanga mambo haya ilikupata kitu
Fulani.Nakumbuka mambo mengi sasa baada ya kusikia tena faili namba 13:14 kutoka
kinywani mwako.Mambo yalivyo kuna watu wa kuwa uliza ilikupata jibu.Mmoja wao
nataka tumpate aliyekuwa mpambe wa rais wa awamu iliyompa Kisusi.That guy knows
a lot anaweza kutusaidia.”
“Ndugu Pangabutu?”
“Ndiyo.Lakini sialifariki maana alikuwepo uwanjani?’’
“Basi tufanye
upekuzi nyumbani kwake naweza pata kitu.Au hata tukimhoji mkewe.”alishauri bwana
Toti.
“Ni wazo zuri naomba lifanyiwe kazi haraka sana.Ila natoa
oda.Punde mkimpata mkewe au yeyote basi nataka ahamishwe nakupelekwa mahala
salama sitaki kuhatarisha usalama wake.”
Toti aliamua kutumia wasaa
huo kujimwaga kwenye jamvi nakuleta sera zake.
“Lakini mheshimiwa
naomba niwaingize vijana wangu ninao waamini sana.”
“Nataka niwajue
hao vijana wapate direct order from me.”alisisitiza Kilua.Toti alijua kama
angempata Shuni halafu awe na Pablo mambo yangeenda anavyotaka vizuri ila kwa
sasa Pablo yupo lakini Shuni amekamatwa katika operesheni.Atamueleza vipi rais
lakini alijua angeweza kumpata Shuni.Ila dhumuni lake kumpata Pablo katika
upelelezi huu ni kumuweka bize iliaondokane na mawazo ya kumchunguza Shunie
ambaye anajua wana mahusiano nje ya kazi.Pia ni namna ya
kuwadhibiti.
“Usijali mheshiwa hawa ni vijana ninao waamini kabisa
wanaweza fanya kazi nzuri sana.”
“Ok nategemea mazuri lakini kuna
misheni nyingine nataka timu maalum kwenda Savanna Lands kuokoa watu wetu
walioko katika ubalozi wetu uliopo taifa hilo.Kuna uwezekano wakawekewa vikwazo
na rais wa taifa hilo I need to be ready incase things go astray!”alisema
Kilua.
“Tukipata fumbo hili tutaweza kupata kisio la nani anaweza
kuwa ameiteka familia yako.”alisema Masha.
Toti na Masha waliondoka
kwenye uwepo wa rais.
***
Masha akishirikiana na Toti
walifanya ziara ya kushtukiza nyumbani kwa Pangabutu.Waliegesha usafiri wao
umbali Fulani.Kisha wakataka kutoka ,lakini kabla hajaenda mbali kuna kitu
alikiona Toti kilichomfanya ashtuka.Kuna gari aliiona imeegeshwa mita chache
kutoka nyumba anayo ishi bwana Pangabutu.Gari lile lilikuwa kama teksi lakini si
teksi.Kuna alama ambayo aliweza kuitambua kitu ambacho kilimfanya Toti kushika
mkono bwana Masha nakumrudisha kwenye gari lao.
“Kuna nini bwana
Toti?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Lile gari pale
nalitilia mashaka!”alisema wakati huo akijaribu kuchukua simu yake ya mkononi
kisha aliwasha kamera ya simu nakuanza kuzuum picha ya gari lile akichukua picha
za mnato hasa akilenga shabaha namba za gari lile pamoja na nembo
aliyoona.Alifanikiwa kupata picha zile kisha akaanza kuzikagua.
“Kwanini unatilia shaka gari lile?”
“Sio gari la kawaida mkuu.Lile
gari ni la usalama wa taifa.”kwanini wawepo eneo hili.Tunapoweka magari yetu
maeneo kama yale lazima kuna kitu kinaendelea.Kuna mtu mkubwa anachungwa
pale.”alisema bwana Toti.Kisha aligeuza gari lake nakuondoka kwa kasi ya ajabu
sana.Toti alikuwa ni kiongozi wa idara hiyo ya usalama.Alikuwa mwenye mafunzo ya
hali ya juu kiasi hakuhitaji kutembea akiwa na walinzi maana yeye mwenyewe ni
mashine kubwa.Ni mara chache ungemkuta akiwa na ulinzi labda kukiwa na shughuli
maalum za kitaifa ambazo angehitajika kuwepo.Jambo hili la rais Kilua aliamua
kulisimamia mwenyewe.
“Atakuwa ni nani?”
“Ngoja
nikifika ofisini nitakuwa na jibu lakutoa.”alisema Toti wakielekea ofisini kwake
ambapo alitakiwa kufanya upekuzi ajue ni kwanini gari la idara yake lipo
pale.Kuna maeneo mengi sana wana misheni za kulinda watu na hawezi kuyajua yote
kwa wakati mmoja.Mengine hufanywa siri maalum.Ndani ya muda mfupi walikuwa
tayari wamo ofisini kwake.Aliweka kupitia mafaili kadhaa nakujua ni gari gani
lilikuwa mitaa ile na kwa nini kulikuwa na operesheni.Alichogundua nikuwa idara
hiyo ilipokea amri ya kumuweka kizuizi cha ndani Pangabutu aliyekuwa mpambe/ADC
wa rais wa awamu zilizopita.Alitafuta sababu maalum kwanini hauona kama
iliwekwa.Jambo hilo lilimtia shaka hasa ni kwanini bwana huyo aliwekwa kizuizini
tena cha ndani?Viongozi waliopita wa idara hiyo ilionesha kwenye mafaili ya siri
kwamba walikuwa wakimlinda Pangabutu kama mfungwa wa ndani lakini wengi
hawakuuliza sababu yake.Ila aliwekwa kama mtu hatari kwa usalama wa taifa
hilo.Jambo hilo lilimnyima kabisa nguvu.Lakini ripoti ilisema kwama Pangabutu
alifariki dunia kwenye tukio lile la mlipuko siku ya sherehe za uhuru.Na hadi
sasa wanasubiri msiba ufanyike.Lakini mbona eneo lile hakuona dalili za kuwepo
msiba wowote?Palikuwa pa kawaida na bila shaka shughuli za kawaida ziliendelea
hilo lilitosha kuweka fikra pevu zaidi.
Alimueleza bwana Masha
kuhusu alichokigundua.Alichofanya alitafuta namna ya kujua ni kiongozi yupi
alianza kuweka kizuizi cha ndani kwa bwana Masha katika idara hiyo.Alisaka
majina nakuliona alilotaka.Alijuafika mtu huyo anapaswa kuhojiwa.Alimuita Pablo
kijana wake wa kazi.
Pablo aliingia ofisini kwa bosi wake,”Ndiyo
mkuu.”
“Nataka uende kwa Kiongozi mstaafu wa idara hii bwana
Pasha.Nataka aletwe hapa.Then nataka vijana wawili waende eneo la area b mtaa
was aba nyumba namba 14.Wasiweke mzingo wa ulinzi bali wafanye ushushushu nyumba
ya bwana Pangabutu kuna gari letu lipo pale nataka waangalie mwenendo tu.Any
movement waripoti kwangu.”
Pablo aliitikia amri.
“Lakini
vipi kuhusu Shuni?”
“Naahidi kumleta akiwa hai.”alisisitiza bosi wa
idara ya usalama wa taifa wa Kiota bwana Toti!Pablo aliondoka na kikosi cha
watu wawili walipanda gari nakuelekea nyumbani kwa bwana Pasha huku yeye Pablo
akiwaacha vijana hao wawili mtaa wa saba area b.Kufika.Mambo yalionekana kuwa
mazito sana maana tayari wameona Pangabutu yumo katika kizuizi kizito ambacho
hatua yoyote ya moja kwa moja inge hatarisha uchunguzi mzima wa faili namba
13:14.Yoyote aliyeonekan kuwa karibu alikuwa
kifungoni
Pablo aliwasili makazi ya Bwana
Pasha.Alifika moja kwa moja hadi mlangoni.Alikuta kuna mlinzi yumo pale.Aliongea
naye kwamba anataka kumuona bwana Pasha.
Alikutana na upinzani mkubwa
wa yeye kuingia ndani lakini alitumia busara hadi akakubaliwa kuingia.Alikutana
na sebule nadhifu kisha akaenda kuketi kwenye kochi akisubiri bwana Pasha
aletwe.Ndani ya dakika chache bwana huyo aliifikishwa mbele yake.
“Habari bwana Pasha.”
“Umefuata nini hapa?”bwana Pasha aliuliza kwa
ukali kidogo.Pablo alipomtizama miguuni aliona kafungiwa kitu Fulani.Alijua ni
kifaa kinachotumika katika idara hiyo hasa wanapowawekea watu ambao wanahisi ni
hatari kwa usalama wa taifa lao.Kile kifaa huwa kinarekodi nyendo nzima za
mhusika aliyefungiwa.Huonesha mahali alipo.Pia hurekodi sauti na kila
anachokizungumza.Vilevile hupima hali joto ya mwili wa mtu na kama hayupo sawa
kinahisi nakutoa taarifa.Hicho huwa kwa mtu ambaye hakupangwa kufa bali anawekwa
kizuizini tu hadi hapo mamlaka husika itakaporidhika nakuamua kumuachia au
vinginevyo.Wakati mwingine anayewekewa huwekewa hadi siku atakapo
kufa!Kifaa!
Pablo alijua vyema hawezi kumhoji kuhusu operesheni
yao.
“Unahitajika mara moja ofisini kwetu.”
“Hamjaridhika
kwa mlichonifanya bado mnanifuatafuata tu?”alifoka.
“Mzee hayo
mengine siyajui ninataka tu uongozane nami.”
“Hahaha!Kijana
nimeshausoma uso wako wala usijidai hakuna unachotaka kwangu.”aliachia kicheko
cha dharau Fulani.Kwa Pablo alishangazwa sana kwanini bwana huyu yumo kizuizini
tena cha ndani nyumbani mwake.
“Mzee kwa heshma naomba
twende.”alisisitiza kwa nidhamu Fulani pengine angeeleweka.
“Siruhusiwi kutoka nje.Sasa unaponiambia unataka nitoke nje
unanishangaza.Siruhusiwi hata kuangalia televisheni,kusikiliza redio wala kusoma
gazeti.Kiufupi sijui kinachoendelea duniani.”alisema kwa huzuni.
Palepale Pablo alichomoa bastola yake nakuelekeza mlangoni akafyatua nakumlima
mlinzi aliyekuwepo pale risasi ya bega kisha akafyetua ya pili iliyoenda
shingoni!Kulikuwa na jibu moja tu!Lazima amtoroshe bwana huyu maana tayari kila
kinachotokea pale kinasikika na bila shaka kuna kamera zinaonesha.Alikuwa tayari
kuanzisha timbwili la mapigano mazito!CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akamshika mzee
nakumwelekeza watoke nje.Kwa haraka ya ajabu walifanikiwa kutoka nje.Hata hakuna
mazungumzo marefu walienda moja kwa moja kwenye gari walilokuja nalo.Wakapanda
kwenye hilo gari nakuliondoa fasta.Mpaka hapo kulikuwa na shaka kubwa dhidi ya
tukio la Pablo kufyetua risasi.Pablo alijua amejiingiza kwenye mambo mapya.Japo
uamuzi wa kumtoa bwana Yule kwa fujo ulikuwa waharaka usiona uchambuzi wa kina
lakini ilibidi afanze vile kulingana na hali halisi.Mambo yalikuwa mazito sana
kwa haraka waliyokuwa nayo lazima lolote lingejiri.Kweli kaja kumchukua huyu
bwana lakini anashangazwa nakumkuta akiwa kizuizi cha ndani.Hilo lilitosha
kuweka maswali mengi yasiyo na majibu nakuona kuna mashaka makubwa sana.Tayari
kesha gusiwa na bosi wake kuhusu operesheni yakujua faili nambari 13:14
limeasisiwa na nani na kwa madhumuni gani na kwanini kila anayeonekana anaweza
kuwa anajua kitu anajikuta akiwa kwenye
matatizo?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment