Simulizi
: Kombora Kiotani
Sehemu Ya Tatu
(3)
***CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shuni aliendelea
kupokea mateso.Hakujua yupo wapi?Kwa siku ya pili hakuwa amekula chochote na
njaa ilizidi kumchimba kwenye kuta za tumbo lake!Kuachwa bila chakula ilikuwa
moja ya adhabu wakijaribu kumshurutisha kuona kama atadhaifika nakutoa siri za
kwanini meli hiyo ilifanyiwa ushushushu hadi wakaingia ndani.
“Hutaki kutueleza kwanini mnaifuatilia meli yetu?”
Kimya!Msichana
bado alizidi kuushona ulimi wake kinywani usiseme chochote zaidi ya kuumia ini
na moyo!Lakini bado watesi wake waliona ni vyema kumbana wakwapue siri
zake.Tayari wenzake waliuawa wakatupwa pembezoni mwa bahari.Maiti zingeokotwa
muda simrefu.Shuni alizinduka akili akijua kuwa kwa vyovyote vile anaweza
asiachiwe akauawa au akashikiliwa kwa kipindi kirefu.Ingetokea mtu angepitia
pitio lile hatma huwa na hasi au chanya!
Uamuzi wa kuwa hai ulikuwa
mgumu sana kwa upande wake.Katika kushikiliwa kule alikutana na watu wenye roho
ngumu katika kuhifadhi siri zao!
“Ukimya wako ndo ndo mateso
yako.”alikuwa Yule bwana Zungu.Uso wake ulikuwa mkavu katika adhabu
yake!
“Unajua msichana ni bora ungeniambia mnaifuatilia meli yetu
kwa madhumuni gani?Pengine naweza kukuonea huruma tukakuajiri ufanye kazi na
sisi kwa mtindo huo utapona.Lakini mpaka sasa hauoneshi ushirikiano wowote hali
inayonifanya ni shawishike kutumia nguvu zaid kukuaadhibu!Kiutaratibu ni makosa
makubwa kwa mtu ambaye sio stafu wetu awepo kwenye meli yetu tena kwa mtindo wa
kuvamia kama mlivyo fanya.Hili ni kosa kubwa.Mmekuja na silaha na hautujui
waliowatuma watachukua hatua gani kuwaokoa.Kwa vyovyote vile lazima niwe tayari
kwa lolote hata kama nikutumia nguvu zaidi.”
Shuni alikuwa anaelewa
kila sentensi.Alijua fika kuna matokeo mabaya ambayo yangejiri muda
unavyoenda.Yeye alikuwa kazini akiifanyia uchunguzi meli hiyo ya mzigo akisadiki
mtakuwa na shehena la dawa za kulevya.Tofauti anakuta ni vifaa vya kuchimbia
mafuta.Ina maana bwana Tufe anahusika na shughuli za uchimbaji mafuta?Anavyojua
hakuna kampuni yoyote aliyoona inaweza kuwa na uhusiano wa uchimbaji mafuta
ikawa na uhusiano na bwana Tufe.Yeye alimtafsiri bwana Yule kama mtu wakucheza
dili kubwa kubwa za hatari zenye pesa za chapchap ambazo ni nyingi.Kucheza ishu
za mafuta kungempa shughuli za kistaarabu wakati Shuni hajaona chembechembe ya
kistaarabu kutoka kwa bwana Tufe.Hilo lilikuwa dhahiri aliumiza sana kichwa
kung’amua vifaa vile vinaenda wapi?Alijaribu kuunganisha doti hasa akikumbuka
nyakati zake akiwana Tufe na mambo aliyoongea ya utata.Ni wazi hofu ilikuwepo
kuhusiana na mzigo huo kuingia bandarini.Je,yawezekana mzigo huo haukuwa na
vibali?Kama hauna vibali inakuwaje uje nchini humo?
Shughuli za
uchimbaji mafuta ni jambo rasmi sio la kufanywa kwa siri kiasi kile.Kumbukumbu
zake zilimthibitishia kuwa hakuna shughuli zozote za uchimbaji mafuta nchini
mwao.Wala hakukumbuka kama kuna kitu kama hicho aliwahi kukisikia?Sasa hawa
wanachimba wapi?Pengine inawezekana kwamba kuna shughuli hiyo.Lakini akikumbuka
idara aliyomo na vile upelelezi wake dhidi ya mafia Tufe hakuona dalili zozote
za kuhusu uchimbaji mafuta!
“Usiwe mnyamavu sana.”alikuwa kama
akimbembeleza.Shuni alizidi kuwaza mbali sana.Aliomba Mungu amlinde iliakitoka
ajue kuna jambo gani hasa lilikuwa linaendelea.Na kama kweli watu hawa hawakuwa
na shughuli isiyotia shaka kwanini wamemuweka kwenye kizuizi?Ni sawa wakilaumu
uwepo wao pale lakini mbona wasichukue hatua za kisheria kuwadhibiti waliovamia
kuliko kujichukulia uamuzi wa kumuweka mateka?
“Ulitumwa na
nani?”aliuliza bwana Zungu ni swali lililojirudia mara kibao.Sasa alikuwa kwenye
wakati mgumu kudhibiti hasira zake.Alitamani kumpa adhabu lakini akagoma.Kama ni
kumpiga alishampiga sana kiasi hakuona umuhimu wakuendelea na adhabu zilizodhidi
kumuharibu msichana huyu mrembo!
“Waliokutuma kwa sasa wanakula raha
wewe unateseka.”alisema Zungu huku akibadili nia nakumuinua Shuni.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tutakusafirisha
kwa moja ya viongozi wetu pale wata shughulika na wewe kikamilifu.”kisha
wakamvalisha kitambaa cheusi usoni kikamfunika kichwa chote!Baada ya pale
walimtoa huku vijana kadhaa wakimsindikiza.Alikuwa eneo
lisilojulikana.Alipakizwa kwenye gari nakuanza kuondoka maeneo yale kwa kasi ya
ajabu.Shuni alijaribu kuvumilia asijue hatma yake itaishia wapi kwa wakati
ule.Mwendo ulikuwa mkali.Hakusikia walichoongea maana kulikuwa na ukimya
Fulani.Dereva alikuwa na kipisi cha sigara alichokishika kwenye vidole vyake
huku akipiga pafu kadhaa nakupuliza moshi ambao ulikuwa kero kwa wengine japo
walivumilia kwa namna Fulani.
Safari yao ilidumu kwa masaa
kadhaa.
***
Gari iliingia kwenye eneo Fulani lilionekana
kama mahame hivi maana kulikuwa na nyasi nyingi zilizoota kwa kushiba mvua.Bila
shaka kwa mfugaji angepata eneo zuri la kulisha mifugo yake.Shuni asingeona
makazi yale maana alikuwa amefumbwa macho!Alifuata maelekezo ashuke kwenye gari
akiwa kashikiliwa na wanaume wawili wenye miili mizito ya mazoezi huku wakivalia
mawani meusi.Wakaelekea ndani ya jumba hilo.Walifunguliwa mlango ambapo kwa
muonekano ilikuwa nyumba safi kwa ndani yenye unadhifu.Ule ukuukuu wa nje ni
geresha la kuzima kinachoendelea mule ndani!
Walienda ndani ambapo
Shuni alifunuliwa uso nakupaona.Kwa haraka alikuwa akipakariri palivo na
muonekano wa ndani.Alipelekwa moja kwa moja hadi kwenye chumba
Fulani.Kilifunguliwa kasha akasokomezwa ndani!Mwili wake ulisisimka baada ya
kukuta kuna motto wa kike ameketi sakafuni kashika tama!Shuni
akashtuka!
Kisha wale watu walimfungua zile kambanakumsukuma
chini.Shuni alipepesuka hadi alipoangukia kwenye sakafu.Alikuwa amechoka sana na
mwili ulikuwa na maumivu makali!Yule motto alimsogelea Shuni akijaribu
kumkagua.Shuni alifumba macho nakulala kwa muda wa lisaa limoja.Fahamu zilirejea
aligeuka nakuona Yule motto yupo kaketi pembeni akimwangalia
Shuni!
Kumuona mtoto kulimfanya Shuni awe na maswali mengi sana.Huyu
mtoto anafanya nini hapa?Huu ulikuwa mtandao wa aina yake!Kulikuwa na vitabu na
madaftari pamoja na kalamu.Pia godoro safi la kulalia liliwekwa pale.Shuni
alijua haya yalikuwa makazi ya mtoto huyu!Karatasi kadhaa zilionesha mtoto Yule
alikuwa anachorachora kwenye zile karatasi pamoja nakuandika vitu
kadhaa.
“Unaitwa nani?”Shuni alimuuliza Yule
mtoto.
“Naitwa Shani.”
“Shani nani?”
“Shani
Dedani Tabaradi.”alijitambulisha Yule mtoto.Shuni alitumbua macho aliposikia
jina la kati na la mwisho!Alijua utambulisho huo ni wa nani.Lakini huyu mtoto
anafanya nini hapa?Ilikuwaje?
“Ulifikaje hapa?”
“Kwani
anti mamangu kakutuma uje unichukue?”mtoto akajibu kwa
swali!
“Mamako ni nani?”
“Mamangu ni
gavana Kilua!”mtoto alijibu kwa shauku.Shuni alishtuka sana.Mtoto akaeleza jinsi
alivyowekwa kwenye gari na watu wasiojulikana kisha wakaondoka naye baadaye
aliona wamefika mahali gari likasimama halafu baba yake akaingizwa kwa nguvu
akifungwa kamba!
“Huwajui watu hawa?”
“Siwajui.Walinzi wa
mama nawajua wote ila hawa siwajui.Walimfunga baba ngu kamba.Hawataki
tuonane.Wananifungiaga huku kila siku wananiambia mama atakuja.Ulipokuja wewe
nikajua labda ni mama.Ila nimekuona najua mamangu kakutuma.”mtoto
alieleza.
Shuni alivuta pumzi ndefu nakuzishusha.Alidadisi
nakung’amua ni kweli mtot wa rais pamoja na mume wa rais Kilua walikuwa
wametekwa.Lakini kwanini habari hizo hazija tangazwa?Ina ni nani hao wenye nguvu
hadi waiteke familia ya Kilua?Mmambo kama hayo husadikika kujiri lakini sio kwa
haraka kama ile ya kutilia shaka!Ina maana rais wao anavyoendelea na shughuli
zake anajua kwamba familia yake imetekwa?
Yalikuwa maswali mengi sana
yakujiuliza bila kupata jibu.
“Mamako hajanituma.Kwani hawa watu
walisema mama kasemaje?”
“Wao walisema kaniambia nikae nao hadi
aje.Ila kuna wakati walisema wataniweka hapa hadi pale mama atakapoamua kufanya
wanavyo taka.”Shani alijieleza.
Shuni alizidi kupigwa na bumbuazi
kukutana na kisanga kama kile.Hapa anakutana na mtoto wa rais Kilua
anayesadikiwa kutekwa.
“Baba yupo wapi?”
“Wamemficha
chumba kingine.Huwa tunawasiliana kwa kugonga ukuta.’’alisema Shani ambapo
alisogelea ukuta nakuanza kuugonga kwa mtindo Fulani.Hali hiyo ilisababisha
kusikika mlio wa kugonga upande wa pili ukiashiria kujibiwa.Wakiwa pale mlango
ulifunguliwa akatolewa Shuni kwa pupa kishaakaletwa nje ya chumba.
“Bosi wetu anataka kuonana na wewe!”aliambiwa Shuni ambapo alipitishwa korido
kadhaa hadi alipofikishwa kwenye chumba Fulani.Akakutana mzee mmoja hivi mwenye
kitambi kavalia suti nadhifu.Mzee alipomuona Shuni alikenua kidogo nakumpa
ishara aketi chini.
“Msichana unaitwa nani?”
“Jina langu
halina maana kwako hata nikikwambia.”kwa mara ya kwanza Shuni alimjibu mzee huyu
kwa nyodo za kike.Alibadili nyuso ya mwanamke kwa haraka!
“Nimesikia
habari zako sana.Nataka kujua wewe ni nani?Lakini usijali.Sihitaji hilo kw
asana.Utambulisho wako nimeshaujua.Wewe ni shushushu.”alisema bwana Yule ambapo
alitoa kamera yake akapiga picha ya mnato kisha akatoa ile memory akaiweka
kwennye kisomeo memory nakuipachika kwenye tarakilishi yake.Aliikopi picha ile
kwenye tarakilishi kisha akaanza kupitia data base aliyoijua kuichambua picha
ile.Ilikuja jina la Shuni kama afisa usalama wa taifa!Mzee alitabasamu katika
wajihi wake wenye makunyanzi ya uzee!
“Shuni.”alisema kisha
akaendelea.
Shuni alishtuka sana kugundulika hadi jina lake.Alijua
mtu huyu ana uwezo wakupata data zozote kwa haraka atakuwa ni nani?
“Kwanza naomba kujua ni nani aliyekutuma uje uipeleleza meli ile ya
mizigo?”
“Sikwambii chochote.”alijibu tena kwa nyodo ambapo mzee
Yule alisogea hadi alipo Shuni akamtizama akapeleka mikono nakushika maziwa yake
kwa nguvu nakuyaminya kama anatomasa!Shuni alisukuma lakini tofauti na matarajio
yake alijikuta akishikwa na mikono kakamavu ya Yule mzee hadi Shuni akaogopa
sana.Alitamani arushe makombora ya mateke iliapigane naye lakini akajua yupo
himaya hatari sana kuwahi kutokea.Alishtukia kasukumwa nakuangukia mezani mzee
alimfuata nakumshika tena kwa nguvu!Bila shaka dalili za kufanyiwa kitu mbaya
zilipiga kengele za hatari kichwani mwake!CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unaweza kuwa
askari mzuri sana.Mateso hayafanyi kazi kwako.Unaadhabu moja tu nakubaka kila
siku hadi ushike mimba.Nitakufanyia kitu kuua ujasiri wake.Weaken your
spirit.Nakufungia hapa.Naaweza kuamrisha vijana wangu wakukufanyia
unyama.Hutakufa maana kama ni chakula tutakulazimisha umeze.Nitakufanya chombo
za haja ya mwili nakukufanyia unyama!You won’t like me yet nitakufanya
usichopenda najua una mchumba wako Pablo!I will make sure siku nakuachia
nitakuwa nimekuharibu sehemu zote utalaani siku uliyozaliwa duniani!”alisema
mzee Yule kwa sauti kavu!
Shuni alisisimka mwili!Hakuona mzaa kwa
maelezo ya mtu huyu na alijua fika mzaamzaa hutumbua usaha!Lakini hilo
lakunajisiwa ndo kitu alichokiogopa sana katika maisha yake!Watu kama hawa
hawana msalia mtume.
“Ni vizuri ufuate masharti yangu la sivyo
nitambaka Yule mtoto uliyekuwa naye chumbani!Tena nitambaka mbele yako!”lilisema
zee lile kwa sauti kavu.Ambapo muda ule ule alionesha ishara kwa kijana wake wa
kazi,”Bring the child here.”
Kijana wa kazi alitoka chapu na baada
ya dakika alirudi na Shani!Mzee alimsogelea Shani akazishika nywele kama
anazipapasa!Shani hakuelewa alimuona kama babu tu anayecheza na mjukuu
wake!Hakuelewa lolote.
“Shani?’’aliita Yule mzee.
“Naam
babu.”mtoto aliitika kwa sauti isiyo na hatia.
“Vua nguo?”alisema
Yule mzee.Hilo lilimfanya Shuni kuhisi kama amemwagiwa maji baridi kwenye
mishipa ya damu!Hakuamini kama mzee huyu na uthubutu wa kinyama kama huu!Mzee
alisogea kwenye meza yake akaifungua nakutoa kitu kama ungaunga kisha akauvuta
mapuani!Alijua fika hayo ni madawa ya kulevya!Shuni aliona hapa kuna uzito
mkubwa sana na hulka za watu kama hawa sio nyepesi.Shani alisita maana alikuwa
na uerevu hawezi kuutoa mavazi mbele za watu!
Wakati akisitasita
alishtukia kofi zito kwenye shavu la Shani lililoacha alama ya mistari
iliyoashiria ukavu wa mkono ule na maumivu!Shani aliangua kilio cha
kwikwi!
“Vua nguo!”alisisitiza mzee!Sasa ulevi wa mihadarati
aliyotumia ulianza kufanya kazi kichwani nakujiona yeye mtambowa
nyuklia!
“Babu nisamehe sivui nguo mbele za watu…”mtoto alilia!Hilo
likazidi kumkera mzee.
“Naitwa Mzee Kavu huwa sina
huruma.Nilikwambia Shuni endapo utabishana na mimi utashuhudia picha mbaya
hujawahi ona maishani mwako!Huyu ni mtoto wa rais Kilua.Nimemteka hapa pamoja
na babake.Hadi sasa wewe ndo mwana usalama pekee uliyebahatika kuona familia ya
rais Kilua.Tangu aapishwe tumeiteka familia yake nay eye mwenyewe anajua na
tunaitumia familia hii kukidhi matakwa yetu.Ikitokea kuna mwanausalama yeyote
kapewa taarifa ya kutekwa kwa familia ya rais nahakika tapanda milima na mabonde
kuiokoa.Wewe ni mmoja pekee umeiona familia hii umepewa nafasi ndogo kuiweka
salama.Nimeomba siri nijue kwanini unaifuatilia meli ile ya mizigo?Nani kakutuma
na kwanini amekutuma.Unakuwa mgumu!Nakuambia the child will pay the price so
save her!”
Shuni alihisi tumbo kukata!Ulimi ukawa mzito hawezi sema
lolote kuhusu operesheni aliyokuwa anaifanya hadi hapo uchunguzi
utakapokamilika.Kiukweli alichezwa na machale kwamba kuna mengi asiyoyajua!Huyu
Mzee Kavu ana ajenda gani hadi aiteke familia ya Kilua.Inawezekana taifa halina
usalama na waliopo kwenye himaya husika hawana namna ya kujinasua bali
kukubaliana na gharama za uchungu!
Palepale simu ikapigwa na Mzee
Kavu,”Helo?”alisema Mzee Kavu kwa sauti yenye ukavu wa mti mkavu.
“Nakusikiliza unataka nini tena?”ilikuwa sauti ya Kilua!
“Commander
in chief give your officer ana order to obey me or else something bad will
happen to your daughter!”alisema Mzee Kavu akiwasiliana na rais
Kilua.
“Ofisa yupi?”aliuliza Kilua akiwa
anatetemeka!
“Ofisa wako wa usalama tumemkamata kuna habari tunataka
kutoka kwake.Lakini hataki kusema.”
“Nipe niongee naye.”alisema
Kilua.
Mzee Kavu alimpa simu Shunie aongee na rais Kilua
mwenyewe.Shuni alihisi kuogopa kwa akili yam zee Yule ilivyo kavu anaweza
kutekeleza unyama wa aina yoyote.
“Halo mheshimiwa.”alisema Shuni
kwa huzuni.
“Unaitwa nani?”
“Shuni.”
“Ilikuwaje ukashikwa?”
“Tulikuwa kwenye
operesheni maalum nikatekwa wanahitaji niwape top secret za operesheni
zetu.Nilikula kiapo!Siwezi toa siri za kazi!”alisema Shuni akijikaza
kulia.
“Mlinde mwanangu.Lakini nakupa direct order protect my
daughter at all cost.Naongea kama mama what will you do for your child?”alisema
Kilua akijikaza kulia.
“Mheshimiwa anaweza akamnajisi
mtoto.’’alizungumza Shunie akitokwa na machozi.
Kilua huko
alipoalitamani aingie kwenye hiyo simu atokee mahali alipo mwanaye lakini
haikuwezekana.
“We don’t sell our secrets do what is right my
dear!”alisema Kilua akiwa amekata tamaa.
“I know madam!”alisema Shuni
nakumgeukia Yule mzee.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee Kavu
alichukua simu yake nakuiweka masikioni,”Nita enjoy mapaja ya mwanao!”kisha
akakata simu.
Shuni alimwangalia Yule mzee kwa hasira sana huku
akijipanga afanye nini.Alijua bila hatua za haraka kuna mtoto atafanyiwa unyama
wa kimataifa!Bila kuchelewa mzee Kavu alijua fika afisa huyu wa usalama atasema
siri za operesheni ile!Mwanzoni ilikuwa operesheni rahisi lakini sasa
imewapeleka walipo mateka wa familia ya kwanza.Mzee Kavu akamshika Shani
nakumrusha juu ya meza akachana kauni la mtoto Yule akashika kocho
nakuichana!Shuni alishikiwa bastola kwenye kichwa hakuna
kujigusa
Nguo ya ndani ya Shani ilikuwa
imechanwa!Mzee alimshika kwa nguvu kwenye kiuno akaipanua miguu ya mtoto Yule
kisha akaanza kufungua zipu yake kwa mkono mmoja!Mzee Kavu!Hilo jina lilisumbua
kichwa cha Shunie sana alitamani kuikamata bastola ile lakini akashindwa walio
pale ni watu wenye nguvu kubwa sana!
Mzee aliyafikia majapa ya mtoto
nakujizamisha ndani!Ukasikika ukulele mkubwa wa kudhalilishwa kwa mtoto
huyo!Ulikuwa ukulele!
“Mamaaa!...”alipiga ukulele mkubwa sana hadi
mahali alipokuwepo Kilua akahisi moyo wake kumshtuka na tumbo kumkata!Shuni
alimlaani Yule mzee kwa laana zote tayari alianza kumnajisi mtoto akijilazimisha
kumbaka!Shuni aliona ni lazima ajitoe sadaka!Alichofanya nikurusha
kisugudi(kipepsi)nakumpiga jamaa aliyekuwa nyuma yake kwenye tumbo kisha
akageuka haraka akashika mkono wake nakuuvunja ule ulioshika bastola.Aliupigiza
kwenye kabati nakuushindilia hadi kigasha cha mkono kilipolia kaa bastola
aliyoishika mtu Yule ikaanguka chini!Alikuwa amemvunja mkono Shuni akimuwahi
mlinzi wa pili kwa teke la sehemu za siri kisha kwa kasi ya haraka akamrukia
Mzee Kavu nakutua mgongoni akapeleka vidole kwenye macho nakuanza
kushindilia!Mzee Kavu aliutoa mkono mmoja!Mkono uliobaki Shuni akashika kwa
nguvu nakutoboa jicho moja nakulipasua!
“AAASH!...”kelele kavu
zilisikika kutoka kwa Mzee Kavu hadi akamuachia Shani aliyekuwa anavuja damu
sehemu za siri.Kwa takribani sekunde thelathini alishuhudia unyama mbaya sana
katika dunia wakunajisiwa!Mtoto alikuwa na analia kwa uchungu wote
alioujua!Ilimkera moyoni nakuhisi mwili wake umefanyiwa kitu kibaya
sana!
“Shiit!”alitapatapa mzee Kavu wakati tayari jicho la upande
mmoja likiwa limetobolewa na Shuni kwa kucha zake ndefu!Alikuwa amemjeruhu
vibaaya.Na kama angepewa nafasi basi Shuni angeukatisha uhai wa mzee
Yule.Ukelele aliopika mzee Yule ulifanya walinzi waje pale kwa haraka wakamshika
Shuni nakumvutia pembeni!Shuni alikuwa kama samba jike aliyegusiwa
mwanaye.Hasira yake ya kumvamia ilitoka moyoni ni hasira ya
mwanamke!
“Aaah!...You bitch you…ooh!Macho yangu!...Shetani
wewe…”alipiga kelele mzee Kavu huku akitapatapa!Shuni alishikiliwa lakini
akachomoka nakumuwahi Shani ambaye aliogopa hata mtu kumgusa!Alilia
sana.
“Shetani wewe huna aibu kwa mtoto!Nitakuua kwa mikono
yangu!Nitakuua!”Shuni alipiga kelele akikaripia.
Walinzi waliokuja
walichomoa bastola zao tayari kuumaliza uhai wa Shuni.
“We mwanamke
ngoja tukuue!”alisema moja ya walinzi akiwa tayari kumuua
Shuni!
“No!Don’t kill her put her kwenye room yao.Their pain has just
began.”alisema Mzee Kavu akiwa ameshika mkono mmoja kwenye jicho lililotobolewa
huku damu zikiendelea kutoka.
Maumivu ya Shuni na Shani yalikuwa
yameanza.Wakachukuliwa kama magunia nakupelekwa kwenye chumba chao.Huko
walipofika tu Shani alinyamaza kimya na uso kuutazamisha chini!Alikuwa
amevurugwa kisaikolojia kwa tukio lile.Aliipoteza utoto wake na bashasha
yake.Shauku yake ilikufa kibudi nakusomeka namba ziro!Mtoto aliona kila kitu
kikifutika na tukio lile kuwa kichwani mwake hakutaka kuguswa na mtu yeyote hata
Shuni!Yeyote aliyemgusa alijikuta akishtuka sana!Bwana Kavu alikuwa alikuwa
ameweka ukavu kwenye maisha yake!
***
Pablo alizidi
kukata barabara akielekea makao ya usalama wa taifa.Alipokuwa anaelekea alihisi
kuna gari inamfuatilia baada ya kuitizama kwenye kioo cha pembeni!Alikanyaga
mafuta nakuongeza mwendo wa haraka kuikwepa gari ile.Sio kitu cha ajabu
kufuatiliwa ni jambo alilotegemea kwamba litatokea tu.Kulingana na mazingira
aliyomchukulia bwana Pasha na alivyomkuta alijua tu lazima kungekuwa na
ufuatiliaji.
Alijiandaa kisaikolojia kwamba endapo yatazuka mapigano
atakuwa tayari kupambana.Bastola ilikuwa tayari.Pasha aliona picha nzima akawa
anakenua tu.
“Kijana nashukuru kwa uanvyojitahidi lakini ninavyojua
kunifuata mimi umeanzisha vita!”
“Mzee mimi nafuata amri tu
niliichagua kazi inabidi tu niifanye.”alisema kwa kujiamini huku akionesha adabu
kwa mzee Yule.Kwa jinsi alivyomtundu wa kucheza na barabara alifanikiwa
kuwakwepa na sasa alikuwa mbioni kufika makao ya ofisi yao.
Kazi
kubwa ya kumchukua bwana Pasha ilikuwa imekamilika.Lakini akiwa njiani
alishangaa akipigiwa simu na bosi akiuliza yupo wapi akasema ndo anaingia
getini.Alifanikiwa kufika salama.Kisha alishuka nakwenda moja kwa moja hadi
ofisi ya bosi wake akijitahidi kukwepa kukutana na watu watakaomfahamu bwana
Pasha.Pasha aliifahamu ofisi nje ndani kiasi alianza kumwelekeza wapi pakupita
bila kushukiwa.Hatimaye wakafika ofisi ya mkuu wa idara ile bwana
Toti.
“Karibu bwana.”alisema Toti akimlaki Pasha pamoja na
Masha.Pasha aliketi chini huku akiangalia vijana wale.Akatikisa kichwa.Halafu
akawaonesha kifaa alichofungiwa mguuni.Toti alijua namna ya kukizima.Alichofanya
aliingia kwenye system yake alitafuta jina la Pasha nakuona kifaa kinachomlinda
kinavyorekodi data alichofanya alikizima kwenye mtandao wake.Hapo hakuna
atakayesikia chochote wanachoongea.
“Sasa naweza kukaribia kwa
amani.”alisema Bwana Pasha kisha akaongeza,”Hata hivyo kwa kuzima kifaa hicho
mmefungulia vita kuu maana wataona signal yangu haipo active.”
“Lakini si only director wa usalama ndo mwenye mamlaka ya kuzima signal.Mimi
nimezima ukisema watajua kina nani?”
Pasha alicheka kicheko cha
ujuaji halafua akachukua paketi ya sigara iliyokuwa mezani akaitoa pisi moja
nakuchukua na kiberiti kisha akawasha nakuanza kuvuta.Moshi mzito ukafuka pale
ndani.Alipiga pafu zake za uhakika.Alioneshafika alikuwa amezikumbuka sana enzi
zake.
“Wazito wanajua kila kitu.Wanadukua mtandao nakupata taarifa
zote kunihusu tupo list tunaochungwa kwa kujua mambo Fulani.Wengine tuliachwa
hai kwa sababu maalum na wengine walipotezwa.”alitoa tamko zito na gumu
sana.
“Najua kuna mengi una fahamu ila nataka kitu kutoka
kwako.”alisema Toti.
“Niulize lakini nataka uhakika wa usalama
wangu.Walitishia familia yangu ikabidi nijitoe sadaka.”kuna mambo
yaliwachanganya Masha na Toti tangu kuletwa hapa kwa bwana Pasha anasisitiza
kuna kundi linalomdhibiti nalimeshadhibiti wengi ni kundi gani?Wao walimwita kwa
mambo Fulani na wala sikuzungumzia sababu zake za kuwekwa kizuizini.Lakini
wangetegemea mambo kama yale.
“Mzee kwa heshma zote.Kuna vitu
tunataka kukuuliza ila please personal issues zako ziweke pembeni.Rais aliyepo
madarakani anataka kufahamu kitu.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kitu gani?Ila
lazima mjue mambo yangu binafsi.Nimechoka nimeshawekwa kizuizini kwa muda mrefu
sasa.Siogopi lolote na kama wangekuwa na nia yakunimaliza wangetekeleza kitambo
ila kwa sasa no!”
Masha alimeza mate kukausha koo.
“Ni
kwanini ulitekeleza amri kumuweka kizuizini ADC Pangabutu?”aliuliza Toti huku
akiwa amekaza macho,”Unataka usalama jibu maswali yangu vizuri.”
“Kwasababu alikuwa anajua mengi.Kumuacha astaafu halafu aendelee kuwa raia wa
kawaida kulimuweka katika hatari ya kusema siri!”
“Siri
gani?”
“Kuhusu mkataba wa 13:14!”alitaja bila chenga wala kupepesa
macho!
“Unahabari kwamba Pangabutu alikufa kwenye mlipuko
juzi?”
“Huo ni uongo!Makubaliano alitakiwa kuwekwa kizuizini na sio
kufa.Kwanza iweje awepo kwenye eneo lenye mlipuko alihali yupo kizuizini?Alitoka
saa ngapi na alitoka na nani?Unless mniambie wanabadili mbinu za 13:14!Ilikuwa
hivi kila anayetaka kujiingiza kwenye 13:14 na wakahisi ataharibu au hastahili
basi hupotezwa au wanabadili kanuni ikiwa nikufuta baadhi ya watu wanaoijua ishu
hiyo vizuri au wanafunika kombe kwa wale wanaojua siri sana wanatengenezewa
vifo.”
Masha na Toti wakatumbua macho.Waliangaliana kwa umakini kisha
wakaendelea,”Faili namba 13:14 linahusiana na nini?”
“Lilikuwa jambo
zito napengine ni kitu chepesi tu ambacho kilibebeshwa ngozi ya chui ili wengine
wasikijue.Kuna sababu tatu pesa,nguvu na mapenzi ukiweza kuvijua vitu hivi basi
utajua kuhusu 13:14.Walitumia sababu hizo kwamba ni pesa,nguvu na mapenzi ndo
siri ya 13:14!Hakuna aliyeruhusiwa kuingilia wengine tulibahatika kujua mambo ya
siri tu.”
“Mzee unatuambia mambo mazito lakini tunataka kujua kwamba
ni jambo gani linafanyika katika faili hilo?”
“Ninachojua kwa upande
wangu ni kitu kama mkataba wa siri sana.Kuna watu walikula viapo katika mkataba
huo.Halafu wakatengeneza hali Fulani ya kuwachanganya wengine ili kila anayetaka
kujua anakutana na kizuizi kikubwa sana.Hii ni Afrika kuna mengi hufanyika kwa
maslahi ya mtu binafsi.”
“Ni madawa ya kulevya?”
“Haiwezi
kuwa madawa.Huu ni mkataba kitu kama rasilimali Fulani za taifa.Ila sijui ni
nini?Kuna rasilimali wanataka kuichuma hapa ila ni kama imeuzwa nje.Rasilimali
hiyo haina sharia iliyotungiwa inawafaidisha wachache.Tangu wapange kuanza
kuichimba hawakufanikiwa kutokana udhibiti kutoka kwa makundi yanayotaka
rasilimali hiyo itumike wanavyotaka wao.Hakuna anayetakiwa kuigusa isipokuwa
kundi la watu walioanzisha mkataba huo.Wananguvu na uwezo wa kutosha.Wako tayari
hata kuharibu nchi ilimradi interest zao zilindwe.”
Masha alimtizama
tena Toti,”Ina maana hata ajali pale uwanjani ilikuwa ni kuhusu huu mkataba wa
13:14?”
“Inawezekana mkiweza kulisaka jambo hili kwa undani mtaweza
kuwapata waliohusika na shambulio lile.Naskia ni mwanajeshi aliyeangusha
ndege.Lakini ukweli hiyo ni impossible!Haiwezekani rubani angushe ndege kwa
namna ile.No!... Never!Ile ni maksudi!Wanabadili mbinu.Muwatafute hadi muwapate
then take them out!Serikali ni moja hatuwezi kuwa na kundi linaloamua tofauti
kwa manufaa yao!”
Rais Kilua akiwa kwenye ofisi
yake anaingia mtu.Alienda moja kwa moja hadi alipoketi kwa heshma zote.Kilua
aliinua macho nakumsikiliza kwa makini bwana huyu.
“Madam kuhusu
kufanyiwa ushushushu kwa bwana Serambovu kwa mawasiliano yake.”alisema wakala
huyo kwa umakini.Kilua alimwangalia huku akipitisha ulimi kwenye papi za midomo
yake kwa haiba ya kike.Urembo wake ulikuwa umesimama dede na kila aliyemuona
alihisi wivu kwa mwanaume aliyemuoa nakuona kama ananyimwa wasaa wa kufurahi na
bibi huyu mwenye wajihi kama hurulaini.
“Mmegundua nini?”aliuliza
Kilua.
“Jukumu hili nilipewa na bosi wangu bwana Masha.Na katika
kupitiapitia nilIpata simu nyingi tu alizokuwa anapata bwana Serambovu kila mara
nilijitahidi kuwa makini.Nanilichukulia kila mawasiliano kuwa ni makini sana
nakuyapatiliza.Ila kuna simu moja ilinitatiza sana.Hii ilitoka hivi karibuni.Hii
ilikuwa na mazungumzo yanayohusu kukamatwa kwa mwanausalama wa KISS.Simu hii
iliuliza kwamba kama kuna oda yoyote kutoka ikulu kuhusu kufanyiwa ushushushu
kwa meli ya mizigo iliyopo bandarini.Nilijaribu kufuatilia mazungumzo na hasa
meli hiyo kwanini ifuatiliwe na kama kweli ilikuwa inafuatiliwa kwanini
mfanyakazi wa ikulu atoe siri kwa wanaofuatiliwa?Nilichojua kupitia njia zangu
meli hiyo inahusika kukamatwa kwa wanausalama waliokuwa katika operesheni
zao.Idara ya usalama hadi sasa haijafanikiwa kuwaokoa watu wake.Hivi ni kwamba
meli hiyo kama ina jeuri ya kuwaweka vizuizini watu wa usalama halafu hapohapo
isifuatiliwe na bado kuna mtu kutoka ikulu anaongea nao inaonesha kuna mazito
kuhusu uhusiano wa meli hii na Serambovu.”
Kilua alitumbua
macho.Palepale alichukua simu nakumpigia Bwana Toti,”Halo bwana
Toti?”
“Ndiyo mheshimiwa.”
“Kuna agent wako anaitwa
Shuni?”
“Ndiyo na ndiye aliyekamatwa kwenye meli ile tulioishuku
kuhusu madawa ya kulevya na hadi sasa bado hatujam-recover”
“Dame
it!Nimeisha jua aliyemkamata ni nani?Njoo ofisini kwangu.”alisema rais Kilua kwa
kujiamini bila kupepesa macho.
Alikata simu nakumuangalia kijana
aliyepembeni yake,”Ulifanya kazi nzuri sana unastahili pongezi sana kijana
wangu.’’
Kijana alishukuru kwa pongezi hizo.Zilikuwa pongezi za
kuridhisha kutoka kwa mkuu wa nchi.Kilua alitilia shaka sana kuhusu Serambovu
kuwa na mawasiliano na meli iliyohusika kuwaweka vizuizini watu wa idara ya
usalama.Hilo lilikuwa kosa kubwa sana kuhusika kwake.Kilua alionganisha matukio
kadhaa pamoja na lile la kupigiwa simu kwa yule mtu anayetaka file namba
13:14.Pia alikumbuka alizungumza naye na akaambiwa kuna wakala wa usalama
amekamatwa na huyo wakala anaitwa Shuni!Aliongea na wakala huyo nakumthibitishia
kwamba yupo mikononi mwao akiwa kwenye operesheni zao akatekwa na adui.Adui
mwenyewe naye anahushwa na utekaji wa familia yake.Ina maana ni kweli Serambovu
alijua watu hawa walimteka mwanaye?Anakumbuka siku fulani akiongea na Serambovu
alimtajia kuhusu kutekwa kwa familia yake.Ni kweli Serambovu anajua.Ila
alijuaje?Kilua hakuwa amemwambia na kwasababu hiyo aliweka ushushushu wa
kuchunguzwa kwa Serambovu hadi sasa anapogundua wanaounganishwa na utekaji wa
familia yake.Waliokuwa kwenye meli na yule anayempigia simu za vitisho kuhusu
kuteka familia yake wanaushirikiano au kwa lugha nyepesi ni timu moja!Kama
waliweza kuongea na chifu wake wa ushauri bila shaka walijua vyema nyendo
zake.Hata walipomwambia wanajua hata akitema mate wanajua basi mvujishaji wa
habari ni Serambovu!Kilua aliuma meno kwa hasira sana.Tena huyu mshenzi aliongea
na watu hao wakiwa kitandani kwake!Kampa kila kitu na penzi lake lakini bado
kafikia hatua ya kumsaliti?
Baada ya muda mfupi Toti na Masha
waliwasili ikulu nakueleza walichogundua kuhusu faili nambari 13:14.Walimueleza
yote waliyoyapata kutoka kwa bwana Pasha.Kilua aliwasikiliza kwa umakini
nakuanza kupata picha kuwa ikulu iliingiliwa na sasa imengiliwa
zaidi!
***CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Gentlemen kama
mlivyoniambia basi na mimi nimegundua moja ya staff wangu alikuwa ana mazungumzo
ya siri na kaptein wa meli hiyo na kwa mujibu wa ripoti niliyopata nikuwa
kapteni wa meli anaitwa Mr Zungu.”
“Mheshimiwa pia kulingana na
uchunguzi wa awali Shuni alikuwa akimpeleleza mtu anaitwa bwana Tufe huyu
alikuwa na data zot kuhusu meli hiyo.”alisema bwana Toti.
“Kama huyo
Tufe anahusika na meli basi anajua vyema alipo binti yangu na mume wangu!Namtaka
huyo mtu atiwe nguvuni haraka sana.Alipo Shuni na familia yangu
ipo.”
Kilua alikwisha waeleza watu hawa jinsi familia yake
ilivyotekwa na watu na hadi Shuni kutekwa na ikatokea sadfa kwamba wote
wamekutana sehemu moja!Hilo lilitosha kuwapa muelekeo kwamba adui alianza
kuonekana ni nani.Kilua hakupenda kumuuza Serambovu kwa haraka kwa namna ile
alitaka kumshtukiza.
“Na huyu stafu wako anatakiwa
akamatwe.”alishauri Masha ambaye alionekana hampendi Serambovu hata
kidogo.”
“Huyu tumuweke kwenye uangalizi wa hali ya juu.Tutamtumia
kama chambo kuwapata hao wengine.Nikimshtukiza sasahivi itakuwa hasara
kwetu.Huyu nitamshughulikia mwenyewe!”alisema Kilua hali iliyofanya Masha kuwaza
mara mbilimbili kama ni kweli Serambovu na Kilua walikuwa na uhusiano wa mapenzi
au la!Maana pozi la Kilua lilikuwa kama kuna uaminifu mkubwa kati yake na
Serambovu hivyo kuwa na imani kwamba kwa uaminifu huo Serambovu atakiri kuhusika
na wabaya wake.Hilo halikutosha kumpa lile jibu la swali gumu!
“Inatakiwa tuwe makini.Tukiweza kudhibiti watu hawa tutajua nani alilipua
serikali nzima!”
“Kesho ni siku ya mazishi kwa mashujaa wetu
waliofia kwenye ile ajali natumai iende vizuri.Kuna ujio wa wageni wengi kutoka
nchi za nje.Naomba muweke vijana wenu ulinzi uwe wakutosha.”
Kilua
aliinuka kuashiria kikao kimeisha.Kisha alienda moja kwa moja kwenye chumba cha
mikutano.Humu kulikuwa na kamati ya ulinzi iliyokuwa inamsubiri kwa hamu kwa
siku ile aseme nao.Waliketi walipomuona.Rais wao kafika.Kilua mwanzoni alikuwa
amepitisha utaratibu wake wa ulinzi ambao ungetumika kwa siku ile.Kilichomleta
pale ni kuhakikisha tu kwamba utaratibu alioupitisha upo sawa.Tofauti na
mategemeo akakuta utaratibu umebadilishwa.
“Nani aliyebadili
utaratibu huu?”
“Ni Serambovu pamoja na jenerali Lupogo.”alisema
moja ya wajumbe wa kamati ya ulinzi.Jambo hilo lilimkera Kilua nakuona kama
anaingiliwa kwenye maamuzi yake.Huo ulikuwa utaratibu ambao kuna maeneo uliacha
mwanya na kama kuna mtu angetumia mwanya huo bila shaka angeingilia mzingo wa
usalama jambo ambalo Kilua hakuwa tayari kulishuhudia hata kwa dawa.Mchoro mpya
uliopitishwa na Serambovu na jenerali Lupogo haukumshibisha Kilua.Na aliupinga
toka mwanzo lakini hawa wamepindua uamuzi wake nakumfanya aonekane kituko.Hicho
kilimpeleka mbali ikiwa kweli Serambovu ndo anayemwendesha au kuna laziada
linalotokea.Kilua alihisi mambo siyo sawa na hisia zake zikazidi kuwa za mashaka
hasa jamaa alivyozidi kukumbwa na sakata la kuhisiwa vibaya.Yote haya yalimuweka
Kilua katika wakati mgumu dhidi ya watendaji wake wawili muhimu sana.Jenerali
Lupogo!
“Kwanini walibadili utaratibu?”
“Walipitia
itifaki upya na kujiridhisha kwamba mchoro huu wa kiusalama ungekuwa mzuri zaidi
kuliko ule tulioupitisha mwanzo na Serambovu alisema atazungumza na wewe kuhusu
jambo hili.”alitaarifiwa.Kilua hakutaka kuonesha mashaka yake dhidi ya jambo
hilo nakuona kweli kuna watu hawajajua sauti yake ni nini?
Kilua
aliondoka katika kikao kile bila kumsemesha mtu.Alirudi hadi eneo jingine la
ikulu.Kisha aliongea na walinzi wake kwamba anataka kudhuru eneo ambalo shughuli
ya msiba wa kitaifa utafanyika.Hapo marehemu watapewa heshma zao za
mwisho.Kulizuka mabishano kwamba asiende pale maana bado hawajafanya uhakiki wa
barabara kwa rais kupita.Lakini alifanikiwa kuwashawishi walinzi wake.Ndani ya
muda mfupi tofauti na utaratibu msafara wa rais uliandaliwa kwa yeye kwenda eneo
lile.Kilua aliondoka na walinzi kadhaa.Magari yalianza mwendo huku Kilua akiwa
amekasirika moyoni kwa jinsi Serambovu alivyomtenda!
Alijua akifika
eneo hilo atamkuta jenerali Lupogo.Ving’ora vya msafara vilizidi kusambaa hivyo
kuyafanya magari mengine kupisha njia.Kilua alikuwa anafikiria mambo sana
ikiwemo hisia kali alizopata dhidi ya bintiye kwamba kuna mtu alitishia kumtenda
unyama na toka wakati ule hadi sasa bado roho ya yake imekosa imani kama kweli
mwanaye ana usalama huko alipo au kuna sintofahamu zinaendelea kati
yao!
Baada ya dakika chache alikuwa amefika eneo lile.Kulizuka
mshtuko mkubwa sana baada ya watu kugundua ujio wake rais Kilua ambao hakuna
aliyemtegemea.Wengi walijua wangemuona siku ijayo atakuja akiwa na msafara wake
kuwaongoza wananchi na wageni katika kutoa heshma za mwisho kwa mashujaa wa
taifa walioaga dunia.Tofauti na vile Kilua ametokea eneo la tukio kwa kushtukiza
sana!
Jenerali Lupogo alishtuliwa na ujio huo sana.Ilibidi awe wa
kwanza kwenda kumlaki mkuu wake wa kazi.Kilua alijikuwa mpole.Aliwapa moyo wote
waliokuwa wanafanyakazi kuandaa uwanja ule kwa shughuli ile maalum.Baada ya hapo
aliomba kuongea na jenerali wake.
“Mheshimiwa nakushukuru sana kwa
ujio wako hapa.Na…”jenerali alikatishwa na Kilua.
“Jenerali nafikiri
tuna sahau mipaka yetu ya kazi?”Kilua alianza kwa jazba.Hilo
halikutegemewa
“Kwanini mheshimiwa?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Inakuwaje
mnabadili protokali niliyopitisha nakuweka mchoro wenu?”Kilua akawa
mkali.
“Mheshimiwa unajua…n…”
“Jeneral nadhani hujui ni
nani mwenye mamlaka?Sasa nasema hivi nakusimamisha kazi na kwaanzia hadi pale
nitakapoamua vinginevyo.Agents mkamateni.”
“Ngoja hawa hawana mamlaka
yakunikamata?”jenerali Lupogo alijitetea huku akibabaika.Lilikuwa jambo baya
sana kwa mkuu wa nchi kukusimamisha kazi halafu anakuweka
kizuizini!
Kilua akasogea hatua chache nakumshika
jenerali,”Am the commander in chief therefore am overiding your duties from now
on you are under arrest!”Kilua alisema kwa ujasiri huku walinzi wake wakiwa
makini na silaha zao maana anayekamatwa ni mkuu wa majeshi!Lilikuwa tukio la
ghafla hakuna aliyetegemea litokee.Eneo lile lilichemka na hali kuwa tete.Rais
anamweka chini ya ulinzi mkuu wa majeshi!
“What are my
charges?”jenerali Lupogo alikuwa mkali kidogo!
“Am detaining you
till further notice general so don’t question my orders!Or do you want me to
charge you for treason?You defied my orders general and that gives me enough
doubt if you are capable of handling your duties?”Kilua alikuwa
mkali.
Walinzi wakamshika jenerali.
“Nipe silaha
yako.”alisema Kilua.Jenerali alisimama wima akijua fika lolote atakalo sema au
kutenda halafu lionekane ni kero mbele ya uso wa rais Kilua bila shaka angekuwa
mashakani!Alisimama kwa nidhamu ya kijeshi kisha alitoa silaha yake akamkabidhi
Kilua.
“Jeneral kuwa makini na mimi!”alipiga mkwara Kilua.Kisha
aliichukua silaha.
“Nitauacha mchoro uliopitisha kwa sasa.Lakini
chochote kikienda kombo tutaongea vizuri.”alisema Kilua kisha akaondoka
lile.Jenerali Lupogo aliondoka na walinzi wa Kilua.Kuna walioona tukio lile
wakastaajabu huku minong’ono ikianza kupita huku na kule kufuatia uamuzi
huo.Kesho kulikuwa na ujio wa ugeni mkubwa sana kiasi haikutakiwa itokee makosa
yoyote ya kiusalama.Kumsimamisha kazi jenerali sio jambo la kawaida kabisa hasa
ukizingatia kuna shughuli kubwa ya kitaifa inaenda kujiri siku inayofuata.Uamuzi
wa Kilua ulimtisha hata jenerali mwenyewe kuona kwamba mwanamke huyu hana utani
na kama walidhani wangempelekesha wanavyotaka basi wamenoa pakubwa sana!Kilua
alikuwa anawashtukiza kwa hatua hiyo siyo na utani.
Kilua akampigia
simu bwana Toti na Masha aliwapa maelekezo mazito.Mchezo ulikuwa
umebadilika!
***
Kikosi maalum cha usalama kiliwasili
nyumbani kwa kapten Pangabutu.Ujio huu ulikuwa wa ghafla kiasi wale waliokuwa
wanaweka ulinzi wa kizuizi wakashtushwa maana hakuna ujio kama huo uliokuwa
unategemewa hata taarifa haikutolewa.Walipotaka kuhoji walipewa vibali maalum
kutoka ikulu kwamba wana amri ya kuingia eneo lile.Walifanikiwa kuingia hadi
ndani nakuanza kufanya upekuzi wanyumba hiyo.Tofauti na vile walivyodhani kwamba
bwana Pangabutu ni marehemu na wangekuta kuna hali ya msiba akiwemo
mkewe.Kulikuwa hakuna dalili ya msiba wala ya watu kujikusanya.Walimkuta
Pangabutu akiwa sebuleni kwake na mkewe!
“Pangabutu?”aliita
Pablo!
Pangabutu alisimama kwa mshtuko.Ujio ule ulimpa ishara
kichwani!
“Kuna nini?”
“Tunakuhitaji.”
“Basi
naenda na mke wangu.”alisema kapten Pangabutu akitetemeka!Walimchukua pamoja na
mkewe.Uwepo wa magari ya usalama eneo lile uliianza kutengeneza picha nzito ya
kushuku eneo lile.Waliwachukua pamoja na walinzi waliokuwa pale wakawekwa chini
ya ulinzi kwa pamoja!
“Tunaenda wapi?”aliuliza kwa wasiwasi moyo
ukimwenda mbio.Akili ilizunguka huku na kule.Kulingana na mazingira ya kazi yake
na jinsi alivyoishi kwa miaka yote hii alijua fika hajajiwa kwa amani.Kuna shari
imejificha!Shari inayomtafuta kwa udi na ambani!
“Tuna oda maalum
kutoka kwa rais Kilua.”alisema Pablo akiwa kama kiongozi wa operesheni ile
pamoja na msemaji wa kila hatua.
Msafara huo uliendelea kwenda kwa
kasi.Njia nzima Pablo alikuwa anataka kitendawili hiki kitatuliwe iliaweze
kumpata mchumba wake.Alijua mzunguko wote huu mwisho wa siku Shuni yumo mikononi
mwa watu hawa.Wote wameunganishwa na matukio ya ajabu ajabu.Familia ya mkuu
kutekwa imeshaingia kwenye dimbwi zito la hofu na mashaka
makubwa.
Kazi ilikuwa kazi kweli na imeshawafikisha kwenye mzingo
mgumu sana.Wakiwa njiani ghafla mlio wa risasi ulisikika kasha ikafuatia risasi
kadhaa kupasua kioo upande alimo keti dereva!Pablo gusa gia Fulani kwenye kiti
kwa haraka nakukifanya kilale nay eye akalala chali.Akampa ishara Pangabutu
ambaye naye alilala upande huohuo.Lakini alichelewa risasi ilipenya kwenye
nakumfyetua mguu mmoja.Kisha zikafuatilia nyingine ambazo zilipiga kwenye
mkono!Jamaa walikuwa wanamimina!
Mke wa Pangabutu alizimia!Risasi
zikaendelea kumiminwa.Kwa haraka Pablo alichomoa bastola yake na kuanza kutafuta
shabaha!Milio ikaanza kujibishana!
Taa!Taaa!Taaa!Milio yaa risasi
ilishtua eneo lile huku raia wakikimbia.Mapigano yakawa rasmi baina ya watu
wasiojulikana na Pablo na kundi lake.Kwa ujuzi wa hali ya juu kikosi cha Pablo
kilianza kujibu!Barabara ilichafuka!Wakati Pablo anatafuta namna ya
kulisimamisha gari risasi ilipigwa kwenye matairi kulifanya gari kupoteza
mwelekeo!Alikamata breki na kusababisha matairi yalipoteza pumzi na kuacha vyuma
visugue lami huku mlio mkali ukisikika!Gari lilienda kando nakujipigiza kwenye
mti!Pablo alijigonga kichwa kwa mbele hali iliyofanya apate jeraha la haraka
nakuanza kuvuja damu!
Pablo alipatwa na maumivu makali lakini
alijikaza.Wakati anaanza kujiandaa kujibu mashambulizi alishtukia wale
waliowashambulia wakielekea upande wao kwa kasi ya ajabu.Walisimamisha gari
nakuwafuata!
Pablo alijikazaa nakuvuta nguvu zote alizokuwa nazo
mithili ya Samson alivyobomoa hekalu!Alielekeza silaha yake upande huo nakuanza
kuwa fyetulia wavamizi hao!Kwa haraka alifanikiwa kuwalenga wane!Wawili kati yao
aliwaondoa uhai palepale!Ghafla kwa kutarajia Pablo alipigwa risasi ya bega
nakumfanya ahangaike kwa pupa!Mwili ukatepetevuka!Damu ikaanza kuvuja bega
upande wa kushoto!Walipofika karibu walimlenga kwa risasi Pangabutu tumboni!Gari
lilikuwa libondeka kwa mbele kwa kule kujipigiza kwenye mti!
Hatari
ilikuwa imewadia!Kisha walimshambulia na mke wa Pangabutu kwa risasi za
kutosha.
“Wamekufa wote!”alisema moja ya watu wale!Wakageuka
nakuchukua maiti za wenzao kisha wakarudi kwenye gari lao.Ile wanataka
kuliwasha,Pablo alizinduka nakulenga shabaha usawa wa tanki la mafuta na
kufyetua risasi kadhaa!Haikuchukua muda mlipuko mzito
ukajiri!BUUM!
Waliomo kwenye gari walikuwa wanateketea!Pablo
akajikokota nakuchukua simu yake akapiga kwa bosi!
“Pablo uko
wapi?”
“Tupo Kisusi Road…tumevamiwa na watu wasiojuliikana.Naomba
msaada wa matibabu!”alizungumza kwa taabu sana!Toti kule alipoalianza kuita timu
ya matibabu pamoja na sekta nyingine kuzitaarifu kwamba vijana wao
wamevamiwa!Ndani ya muda mfupi gari la matibabu pamoja na vikosi vya usalama
vilikuwa njiani kuelekea eneo hilo.
Ving’ora vilisambaa
barabarani.Dharula ilikuwa imejiri kwa wakati ule.Ilichukua muda mfupi sana kwa
timu ya usalama pamoja na polisi kufika pale.Pablo alitolewa kwenye gari pamoja
wenzake.Ni Pablo pamoja na Pangabutu na mkewe Pangabutu waliojeruhiwa kwa
risasi.Hao wengine walikoswakoswa!
Pablo alikuwa amepigwa risasi
kwenye bega!Pangabutu yeye alikuwa amejeruhiwa kwenye tumbo mguuni na mkono
upande mmoja!Mkewe alikwisha fariki kwa kupigwa risasi shingoni!Madaktari
walifanya kazi kwa haraka ilikuweza kuokoa maisha ya watu hawa!Ilitakiwa
wajipange kwa haraka lasivyo mambo yangekuwa mabaya zaidi ya vile
yalivyokuwa.Kwa waliojua mfumo mzima wa operesheni ile walikuwa na mashaka
makubwa!Muda mchache tu baada ya Pangabutu kutolewa kizuizini walikuwa
wamevamiwa na watu wasiojulikana!Iliwapa ishara kwamba uwepo wake mikononi mwa
watu wengine ni ishara tosha kuwa jamaa huyo ni tishio kubwa kwao na kwa usalama
wao hivyo ni bora kumvamia nakumfutilia mbali sana!
Kwanini
Pangabutu awindwe kiasi kile?Kuna kipi anachojua?Kuna siri gani kiasi anakuwa
mikononi mwa mauti.Uhai wake umekuwa kama yai mkononi kwa mtu mwenye njaa!Muda
wowote anaweza futwa au alelewe hadi awe kifaranga lakini bado tu ataliwa kama
kuku!Mwendo ukawa na utata!Idara ilikuwa imesimama nakutatizwa.Imekuwaje
ikajulikana kwa haraka kwamba Pangabutu kafunguliwa?Pia ilikuwaje ikaamuliwa
usalama waende kumchukua?Uamuzi wa kujakumchukua kwa uwazi kwa namna ile
kumeleta uvamizi.Na hata wangemchukua kwa namna ya siri bado siri ingevuja.Idara
ya KISS ilikuwa ya siri sana na kila hatua yake ilipochukuliwa ilikuwa ya
kuaminika lakini inapotokea kwamba usiri huu hauna
iman
i kwamba utasimama basi shaka ipo.Toti
alitamani idara hii ifumuliwe upya kabisa!Maana inaongozwa kwa kila hatua
inayochukuliwa na kutikisa utendaji wao!
Jambo lakuvamiwa sio
dogo!Hadi sasa uhai wa bwana Pangabutu unapumulia gesi!Mkewe kaondolewa na yeye
ameshambuliwa kwa minajili ya kumfutilia mbali kabisa!
Jambo limezua
jambo! Muda utaongea!CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
Serambovu akiwa amekasirika alisimama akimhoji Kilua kwanini amemsimamisha kazi
jenerali Lupogo katika kipindi hicho kigumu sana.
“Uamuzi wako
utatugharimu!Yaani mimi sikuelewi inakuaje unakuwa na maamuzi ya
kukurupuka!Siungengoja hadi kesho ndo utoe hiyo oda?”Serambovu
alilalama!
“Najua ninachokifanya.”
“Hata kama lakini
kwanini ufikie uamuzi huo?Kama hukupendezwa na sisi kuondoa mchoro wako wa
usalama ungetuambia tu!Lakini kumsimamisha kazi kwa wakati huu?”
Kilua alimwangalia nakupandwa na hasira sana!Pozi lile alilijua Serambovu na
yeye hakuchelewa akamwangalia pia,”Siuseme au na mimi unataka kunisimamisha
uniweke ndani?”
“Kama usingekuwa baba wa mwanangu leo hii
ningekufanya kitu…”
Serambovu alitumbua macho kwa mshtuko!Ulikuwa
ujumbe mzito kuliko ujumbe wote aliwahi kuupokea!Huu ujumbe ulimsaga ini na
moyo!Yeye kuitwa baba wa
nani?...
“Unasemaje?”aliuliza Serambovu
akitetemeka!
“Kama ulivyosikia.”Kilua alijibu kike.Kwa Serambovu
Kilua alikuwa hazungumzi kama rais bali alizungumza kama mtu na hawara yake
walioshea mambo mengi ya siri.Kuambiwa kuhusu mtoto kuliifanya akili ya bwana
huyu kuanza kuchuja kila tukio.
“Ina maana unasema mimi ni baba wa
mwanao?”
Kilua hakumjibu kitu akamuacha vilevile kuonesha
amekasirika.Alifanya vile ili kama kweli huyu bwana anahusika na utekaji wa
familia yake basi afikirie mara mbilimbili kwamba huyo Shani anaweza kuwa wa
kwake!Ulikuwa mtego mzuri alioucheza kwenye karata zake.Kalamba dume!Na
anageutumia ipasavyo kudhibiti viwembe hawa!
“Hivi upo sawa au
unanitania?”
“Serambovu get out of my office!Kilichompata jenerali
kinaweza kukupata na wewe.Next time msijaribu kutengua maamuzi yangu lasivyo
nitawageuza vibaya!”
Serambovu alitoka akiwa mwingi wa
maswali.
Kilua alichukua glasi ya maji akanywa huku akivuta pumzi
ndefu nakuzishusha!Tayari alikuwa ameingia kwenye hali ngumu zaidi.Akiwa pale
akapokea simu.
“Ndiyo bwana Toti…Yes…What?”alishtuka Kilua akipokea
taarifa kuhusu kuvamiwa kwa Pangabutu.
Alipopata taarifa ile aliomba
kuletewa jenerali Lupogo haraka sana.Jenerali Lupogo aliletwa ofisini
kwake.
Jenerali Lupogo aliletwa akiwa chini ya ulinzi mkali
sana,”Jeneral kesho utakuwepo kwenye msiba.Kila kitu nimeshakipanga lakini
uwepo wako utakuwepo kwa heshma ya jeshi.Utakuwa chini ya uangalizi wangu any
mistake order ni shoot to kill!”alitamka Kilua.Sauti yake ilikuwa ya amri
Fulani.Aliwatisha sana walinzi wake kiasi walihisi bifu lao na jenerali halikuwa
na utani.
“Mheshimiwa tafadhali naomba usiniweke kwenye utata nina
familia.”jenerali aliomba.
“Jenerali mimi sikuwa na tatizo na
wewe.Nilichukia ulivyochukua uamuzi wa kupindua maagizo yangu pamoja na
Serambovu.Unatakiwa ujue ni nani anakupa mamlaka.Serambovu alinipa jina lako
nikijua kwamba wewe unania njema kwangu kumbe unamsikiliza Serambovu kuliko
mimi!Kesho utakuwepo kwenye shughuli lakini utulie.Any movement
nakupoteza!”
“Nakuelewa mheshimiwa naomba uelewe fika ninaomba
samahani sana kwa hatua nilizochukua na wala sikudhani kama
ningekukwaza!”
“Just know this general.You are taking orders from
me!”
“Sawa mheshimiwa.”alijitetea jenerali.
“Kesho
ukishatokea kwenye hafla hiyo nitakusimamisha tena.”
“Sawa
mheshimiwa.”aliitikia jenerali kwa adabu.Kisha aliondolewa tena chini ya ulinzi
na kuwekwa moja ya vyumba pale ikulu.Kisa kile kilivuja kwa wanajeshi kadhaa
ambao wapo waliounga mkono kwa hatua alizochukua Kilua kumwadabisha jenerali wao
kupindua agizo la rais nakufuata alichodhani ni sawa.Pia wao waliompinga.Kila
mmoja alikuwa na wazo lake.Lakini waliopata habari ile walihakikisha haivuji
kwenye vyombo vya habari!Ingekuwa tishio kubwa kwa wageni wajao.
***
Serambovu alikuwa ameondoka ikulu nakuelekea katika mgahawa
Fulani maarufu hapo mjini.Huko alikuwa kwenye kikao na bwana mmoja hivi
kibosile.Mwenye kitambi na wingi wa majigambo ya kifedha.Alikuwa ameshiba sana
mali.Hakuwa na sura njaa.Alikuwa ni bwana Tufe nakofia yake ya kisasa mtindo wa
kofia za pama!
“Kijana nyumba kuu inaenda tunavyotaka?”
“Hapana mzee.Kuna mushkeli kidogo ila najua nitaukabili.Mama atatulia
tu.”
“Kwani vipi huko?”
“Ni mambo madogo.Nilitaka
kukwambia nataka kesho mshtue kidogo kwenye hafla ya msiba.”
Mr Tufe
alitumbua macho kwa mshangao,”Eti unataka nini?”
“Nataka kesho
mshtue kwenye hiyo hafla.”
Mr Tufe alicheka kicheko cha dharau
ambacho kilimshusha kilo za heshma bwana Serambovu.Alionekana kama mjinga fulani
asiyejua lolote.Akili yake ilionekana kwenda kwa haraka sana kwenye ulimwengu
huu wa ujuaji.Mipango yao ilikuwa inapangwa kiakili na siyo kukurupuka kama vile
alivyodhani.
“Kijana wazo lako mbona lina haraka sana tofauti na
sisi tunavyopanga?”
“Mzee naona kuna haja kuu ya kufanya hivyo.Bila
kumshtua rais ataonekana jasiri na sisi lengo letu ni kuitikisa nchi!”alieleza
Serambovu huku akichukua glasi ya kinywaji chake nakupiga funda moja kwa hadhi
ya kizungu,makali ya kinywaji kile yalimiminika kwenye mfumo wake wa ladha na
kumchechua mdomo!Hoteli ilikuwa ya kitulivu iliyo sheheni watu wazito wenye
majina yao.
“Hapana lazima uwe na subra hatuwezi kukurupuka ghafla
halafu itokee kwamba eneo lile livamiwe.Kumbuka kamati yetu itakuwepo hapo sasa
kwanini tuweke rehani usalama wetu?”
Serambovu alifikiri
kidogo,”Bwana mimi namjua huyu mwanamke zaidi ya nyinyi mnanvyomjua.Kuna mambo
anayoyafanya lazima tumshtukize.”
Tufe alimwangalia kijana huyu
nakuona uchu wa machafuko ukiwa umeweka makao kwenye akili yake na ukitamani
kulipuka muda wowote ule angekuwa hatari ya vile alivyotegemewa.Lakini alijua
fika bila kuwa na nguvu zaa kumdhibiti anaweza kuwa tatizo huko
mbeleni!
“Kijana tunashukuru kwa mchango wako.Nadhani huelewi kwamba
tuna taka kitu gani na kwa minajili gani.Hiyo haraka yako ni mwiba tosha
unaotutishia sisi.Hivi unadhani unavyoamua kutekeleza hatua kama hizo ndo
unajenga?”alisema huku akimwangalia kwa pozi la kuonya kati ya baba na kijana
wake.
“Haujengi!”alisema kwa busara kisha
akaendelea,”Unabomoa.Nidhamu ya kundi letu ndo iliyofanya tufanye mambo haya
bila kuwa na mushkeli.Hatufanyi kwa kukurupuka bali tunafanya kwa akili kubwa
sana.”
“Lakini…”alitaka kusema jambo bwana Serambovu ila alikatishwa
na mzee Tufe.
“Siyo cha lakini.Becareful kwa hatua zako la sivyo
utapoteza.”
“Mimi nilitaka kesho rais apigwe risasi ila siyo ya
kumuua.”alisema Serambovu kwa umakini.Mzee Tufe alimwangalia.
“Nani
awe mrithi wake kama akifa?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hawezi kufa
nataka tu ashambuliwe kwa wakati huyo tutaweza kumuonesha kwamba hatari bado
ipo.”
“Kijana kuwa makini…tutakuachia uicheze karata hii lakini
tunataka Kilua afe.Nataka nione huo mpango wako kama utawezekana.”alisema bwana
Tufe kisha akaamka kwenye kiti alisimama nakulinyoosha kidogo koti lake nadhifu
akaanza kuondoka.Kusimama kwake kulifanya vijana kadhaa waliovalia kinidhamu
kusimama kisha wakaongozana naye.Huo ulikuwa ulinzi wake mkuu.Serambovu alijua
wazo lake limepata baraka nusu na huo ndo mtindo wao wa kutenda mambo huwezi
kukubaliwa kwa asilimia mia moja.Alichukua rununu yake nakubofya namba
fulani.
“Ndiyo bosi.”upande wa pili ukawa umepokea.
“Ule
mpango utafanyika kesho ila nataka ashambuliwe kwelikweli.”alisema Serambovu
akijiamini.
“Sawasawa mkuu.”
Serambovu aliamka pale
nakurudi ikulu akijua mpango umekamilika.Ilikuwa lazima aoneshe makucha yake kwa
wakati ule.Alitaka amuweke rais Kilua kitandani.Hakutaka kabisa mwanamke huyo
awe na kiburi dhidi yake.
Alirudi ikulu.
IKULU
Alipofika viunga vya ikulu alikuta kuna ujumbe wake kuwa rais
Kilua alimuhitaji kwa haraka sana waonane.Serambovu alienda hadi ofisini
kwake.Alimkuta Kilua akimaliza kikao na kamati ya msiba iliyokuwa inasimamiwa na
bwana Mambosasa.
“Nashukuru kwa kazi mliyofanya naomba tushikamane
hivyo hadi kesho kwenye shughuli kamili natumai tutamaliza
salama.Asanteni.”alisema Kilua kikao kikiwa kimeisha.Watu hao
waliinuka.Wakapeana mikono ya kheri kisha wakaanza kuondoka Kilua alimpa ishara
bwana Mambosasa asubiri kidogo kitu ambacho Mambosasa alitii amri
hiyo.
“Ndiyo mheshimiwa.”
“Baada ya shughuli ya kesho
nitakuhitaji ikulu kwa kazi maalum so be ready.”alisema Kilua.
“Nitakuwepo mheshimiwa.”alisema Mambosasa akiachia tabasamu la
ushindi.Akaondoka.
Mlango ulifunguliwa akaingia Serambovu na uso wa
tabasamu alienda nakumbusu Kilua.Kilua alimkumbatia Serambovu kisha akambusu kwa
nguvu kama sekunde kumi akamuachia nakumwangalia usoni aliushika mkono wake
nakuupeleka tumboni.Kulikuwa na ukimya fulani umepita.
“You know I
love you so much.”alisema Kilua kwa utulivu wa hali ya juu.Serambovu alihisi
hatia.
Kilua akaendelea,”Nina mimba!Na hii si mara ya
kwanza.”
Serambovu alihisi mdomo
kumkauka!Lilikuwa jambo zito sana!Hofu aliyokuwa ameibeba sasa imewadia dhahiri
machoni mwake nakupenya kwenye masikio yake!Halikuwa jambo lakufanyia
mzaha!Kilichotokea ni kweli kwamba Kilua ni mjamzito.Hilo hawezi kulikataa na
hivi amekuwa na ukaribu sana kiasi cha kuvuka mipaka kana kwamba mwanamke huyo
wa mtu ni wa kwake.Mchezo huo ungewafikisha hapa bila kupepesa macho wala
nini.Rais Kilua alikuwa ana mimba ya mfanyakazi wake!Rais Kilua alikuwa mke
halali wa bwana Dedani Tabiri ambaye ametekwa.Mwenendo mzima wa rais Kilua na
siri zake na huyu afriti Serambovu zilikuwa na matokeo.
Kwake Kilua
mwendo wake na Serambovu ulikuwa na nguvu ni kama alikuwa mutribu wa nyimbo tamu
za mahaba ambazo asingezikwepa hata iweje na sasa imejiri fika kwamba kuna
hatari kubwa sana imetokea ya kupachikwa mimba na bwana huyu!Ilikuwa kama
dhihaka!
Ilibidi ajitathmini mara mbilimbili maana uzembe wowote
ungepelekea matatizo kuwa makubwa zaidi.
“Una mimba?”aliuliza tena
akiwa na hofu kuu.Mwili wake ukatetemeka.
“Ulitegemea nini?Lazima
jambo hili lingejiri tu iwe isiwe.Imetokea kwamba nimeshika mimba.Tumekuwa
kwenye mapenzi mazito sana kwa muda mrefu na bila shaka lingetokea.Hatukuwahi
kutumia kinga hata siku moja!Unadhani jambo hili lingenipeleka
wapi?’’
“Ni kweli tumekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu.Lakini
mimi sikutegemea kama ingetokea ungepata mimaba.Kwani siyo ya…”alitaka kusema
kitu lakini bi Kilua akamzuia kwa kumuwekea kidole mdomoni
kumnyamazisha.
“No!Hii mimba siyo ya Dedani.Ni yako.”alisisitiza bi
Kilua akiwa na uhakika wa anachokisema.
“Kwanini ukaruhusu?”aliuliza
Kilua.
“No nakupenda wewe.Kwa penzi unalonipa nilikuwa tayari kwa
lolote.Wewe unajua toka mwanzo jinsi wazazi walivyozuia mapenzi yetu hadi
kunileta mikononi mwa Dedani.Alijitahidi sana kunipenda nakunionesha kila hali
kwamba ni yeye ndo anayenifaa!Lakini nisingezuia mapenzi yangu kwako.Ulikuwa
moyoni mwangu nakuhisi penzi lako linatembea kwenye damu yangu.Tafadhali naomba
unienzi mimi nalihitaji penzi lako.Huyu mtoto ni wako angekuwepo Dedani
ningemshikisha huyu mtoto lakini katekwa but I will do anything to bring him
back to me kulinda heshma ya cheo cha urais.Dedani atakuwa ubavuni mwangu kama
mume ana sifa zote.So please usijaribu kusema lolote kuhusu mimba hii.”alisema
vile Kilua,kisha akabofya kidude fulani.Wakaingia maaskari.
Kilua
aliwapa ishara wasonge.Walikuja hadi alipo Serambovu wakamkamata.
“Kilua unamaanisha nini?”aliuliza Serambovu kufuatia hatua hiyo ya kukamatwa na
Kilua.Aiiogopa sana kwa jambo hilo la kuogofya.
“From now on
hutaruhusiwa kuonana na mtu yeyote.Hata kuwasiliana na yeyote yule.Nahitaji
uwakabidhi watu hao simu zako.Nakuhakikishia hakuna ataakayedukua simu yako wala
hakuna atakayegusa mafaili yako.Mambo yako utayakuta kama yalivyo.Kukuacha wewe
siri zangu zitajulikana kama nilivyo kwambia kuhusu zao la siri
yetu.”
“Kilua please usithubutu kufanya hivyo!’’
“Utakuwa
sehemu salamu lakini ya siri no one will know where you are.I promise no harm
will come to you.”alisema Kilua akionesha anasikitika kwa uamuzi huo na kwamba
hakupenda kumuweka Serambovu kizuizini lakini inabidi tu afanye hivyo.Serambovu
alijaribu kuwasukuma watu wale amfikiei Kilua lakini walinzi wakamuwahi
nakumshika kwa nguvu.Kilua alionesha masikitiko yake.Yeye Serambovu alijua Kilua
anamuweka chini ya ulinzi ilikuficha siri yake ya kumpa mimba..Ina maana hadi
sasa haaminiki kwamba anaweza kuficha siri ya ujauzito huo?Mbona kaficha mengi
ikiwemo uhusiano wake na Kilua.Serambovu alidata maana Kilua alikuwa amebadilika
sana tofauti na vile anavyodhani kitu ambacho hakukitegemea kabisa kwamba
kingejiri hata siku moja?Alikuwa na wakati mgumu sana kupinga kauli hiyo maana
angeipinga vipi?Huyu ni rais na alichosema ni mwisho!Ikiwa kaamua kumuweka
kimya!
Alianza kumshikisha adabu jenerali sasa ni Serambovu
mwenyewe.Serambovu aliondolewa kutoka uwepo wa Kilua.Alinyang’anywa simu na kila
kitu akachukuliwa nakupitishwa njia za siri pale ikulu.Alipelekwa hadi kwenye
maegesho ya magari huko aliweza kufunikwa usoni asijue anaenda wapi kisha
alifunikwa mdoni pia asiweze kusema kitu chochote.Kichwani aliwaza sana kama
Kilua ni mjamzito na yeye ni baba wa huo ujauzito hata kiwi kumdhuru
Kilua.Tayari kesha wapa vijana wake ishara ya kumshambulia Kilua hapo kesho.Na
bado hajawapa amri ya kusitisha mpango huo.Bila shaka watatekeleza kazi yao kwa
weledi nakuweza kudhuru rais Kilua.Wakimdhuru wamemdhuru na mtoto aliyepo
tumboni mwake!Hiyo ni hatari kubwa sana kwake kama baba mtarajiwa.Kama kweli
mwanamke huyu amebeba ujauzito wake basi ni kweli ana mapenzi ya dhati kwake nay
eye badala ya kuyarudisha amekuwa akimzunguka.Kilua alikuwa mwanamke wa ndoto
zake.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mabadiliko hayo
ya ghafla yalimfanya ajiulize kama kagundua yeye ana mipangao ya siri na watu
wan je?Kama kagundua basi mambo yake yanaenda kubuma vibaya nay eye atakuwa
uwanja wa kupigia ngumi kwa uzembe sana.Lakini aliamini Kilua hawezi kuwa amejua
kuhusu ajenda zake za siri kwamba anamzunguka na tayari kasha panga mkakati wa
kumfanyia shambulizi ambalo linaweza kumuaa au lisimuue.Hapo alijikuta akikuna
kichwa!
Serambovu alijikuta akikasirika sana kwa jinsi mambo
yalivyobadilika.Kuwekwa mbali na Kilua kulimfanya ajihisi hana nguvu na hatia
ambayo hakuwa tayari kuikubali japo ilizidi kumpenya kwenye mishipa ya
moyo!Kilua aliyeonekana dhaifu alianza kuonekana anachukua hatua kali sana.Kujua
kwamba ana mimba Serambovu angewapigia vijana wake awasimamishe wasijaribu
kufanya shambulizi lolote kwa rais Kilua.Lakini sasa Kilua kamtia mafichoni
kabla hata hajapata muda wa kujitete.Hivyo una baki ukweli kwamba Kilua bila
Serambovu hatakuwa salama!Isitoshe kizuizi anachoweka hata toka maapema kama
anavyodhani bali atafungiwa kwa muda mrefu sana!Muda huo wote atakuwa mafichoni
kwa ukimya way eye kupotea kwa jamii!Ataweza vipi kumuonya
Kilua?
Aliuma meno kwa hasira kuona amefeli vibaya sana!Akakumbuka
kauli kwamba hii siyo mara ya kwanza kwa Kilua kubeba mimba?Ina maana alishabeba
na akazaaa?Ina maana wana mtoto na rais Kilua?Huyo mtoto atakuwa ni
Shani?Alijiuliza sana!Kama ni kweli basi yeye aiyefanikisha familia ya rais
Kilua kutekwa akijua anamkomoa Dedani alikuwa anaiteketeza damu yake
mwenyewe!Serambovu aliona mambo ni mazito sana.
Sasa alijiapiza
moyoni kwamba kama kweli yeye ni baba kwa watoto wa Kilua basi Dedani hakuwa na
haja ya kuwepo kama baba wa familia hiyo.Kwa namna nyingine alitakiwa kumuondoa
asiwepo tena ili yeye aichukue familia hiyo.Alijua akitumia udhaifu wa kupendwa
na Kilua anaweza kumshawishi waoane.Sasa atakuwa na nafasi nzuri kwenye shughuli
za kitaifa na kukamilisha mipango yake.Au anaweza tumia mwanya huu wa Kilua kuwa
rais nay eye aweze kujiingiza kwenye siasa ili msimu ujao aweze kuirithi nchi
kutoka kwake.Angejiimarisha kupitia Kilua.Anayetakiwa kushambuliwa akaona ni
Dedani na si Kilua.Mawazo yake yalimfanya aone mbali zuio lilikuwa hili la Kilua
kumtia nguvuni!
***
Shughuli za kutoa heshma kwa
marehemu waliokufa kwenye mlipuko ule zilikuwa zikiendelea siku hii mpya.Vyombo
vya habari vya mataifa mbalimbali vilikuwa vikitangaza tukio hilo ambalo
liliingia kwenye historia ya nchi hiyo.Historia ambayo ingedumu vizazi kwa
vizazi ikieleza namna wana serikali ya Kisusi ilivyofutiliwa mbali kwa ajali
mbaya.Lilikuwa tukio baya ni kama kombora lilipigwa kwenye kiota.Huzuni
iliyokuwa imeikumba taifa haikuwa na maelezo kwa kweli.Watu walikuwa katika
majonzi mazito sana!Halikuwa jambo dogo.Kulikuwa na ugeni mkubwa sana kutoka
mataifa jirani ndani na nje ya bara kuja kuwapa pole taifa la Kiota kwa kujiriwa
na msiba huo ulivunja mioyo ya watu.Mioyo kugugunwa kwa huzuni iliyoleta kuvuja
kwa mawimbi ya machozi.
Rais wa Savanna Lands pamoja na vuguvugu la
mzozo wa kidiplomasia kujiri kati yake na taifa la Kiota lakini alifanikiwa kuja
katika msiba huo.Ujio wake ulitafsirika kama moja ya hatua za kupunguza makali
ya mzozo wao wa kidiplomasia.Ila walihakikisha anaketi mbali na rais Kilua
ambaye alipowasili kuwalaki wageni mbalimbali hakuweza kumpa mkono rais wa
Savanna Lands.Ugomo huo wa Kilua uliwashtua wanadiplomasia wake kiasi kila mmoja
akawa anafanya juhudi sana marais kutokabiliana mbele za umma.Lakini Kilua
alijitahidi kutulia kwenye kiti chake huku akijaribu kuwaweka wageni wake karibu
kwa kuwatuliza waridihike na uwepo wao katika Kiota.Tayari Kilua alishapitia
protakali za kiulinzi nakuongeza ulinzi ikiwemo kufunga mitambo maalum ya
kudungua makombora yatakayorushwa eneo lile.Vyombo vyote vya ulinzi vilikuwa
makini kuhakikisha shughuli zote zinakwenda sawa.
Kilua alihutubia
mkutano vizuri akiwataka watu wawe wapole nakuwaa wajasiri hasa katika kipindi
hicho kigumu taifa linapita.Aliwapa moyo wananchi wake huku akiwasifu viongozi
waliotangulia mbele za haki ushujaa wao wakulitumikia taifa hilo hadi mauti
yalipowakuta.Aliahidi kuhakikisha taifa linasonga mbele.Hakutaka kusema waziwazi
kama serikali inashuku kuwa ajali ile ilikuwa imepangwa na kuna watu
wanahusika.Japo kila dalili na maneno ya chinichini yalipita kwa wananchi
wakihisi ni kweli kuna mkono wa mtu katika vifo vile na serikali ipo katika
wakati mgumu kudhibiti mikono hiyo ili kurudisha imani kwa wananchi
wake.Shughuli za msiba zilifanyika kwa utu hadi zilipokamilika na kila mtu
kuridhika kabisa kwamba shughuli zimekwenda sawa.
Kilimeta kadhaa
kutoka uwanjani palimokuwa na shughuli za msiba,kulikuwa na kikundi cha watu
fulani wakiwa kwenye gari lao.Watu hao walishuka kwenye gari lao nakutoa mtambo
fulani wakufyetulia kombora.Waliuweka sawa nakuanza kuuseti wakijua fika
watafyatua kombora kutoka pale hadi uwanjani.Walipima viwango vya digrii
wakizingatia vipimo vyote vya mzingo wanaotaka kuulipua.Lengo lilikuwa kufyetua
kombora hadi uwanjani waombolezaji walipo.Leo hawakupanga tu kummaliza Kilua
bali wangevamia na wageni waliokuja kutoa pole.Yaani wangekamilisha msiba juu ya
msiba!
‘’Burkan 2h ballistic missile ndo tutalitumia kulipua kombora
hili.”alisema moja watu wale akiendelea kurekebisha vipimo vya
ulipuaji.
“Mwamba sasa situtamaliza uwanja mzima?”
“Lina
madhara makubwa kama litaanguka eneo hilo.”alijibu Mwamba akiwa amekamilisha
shughuli ya kupima.Kisha wakajiandaa kufyetua.Walihesabu kwa utaratibu wao kisha
wakafyetua kombora lile ambalo ndani ya muda mfupi litakuwa limetua uwanjani
nakusambaratisha kila kiumbe katika kiwanja kile.Kombora la Burkani 2h ballistic
missile lilikuwa hewani huku kwa nyuma likitoa moshi flani ulioashiria kupaa
kwake kwa kasi ya ajabu ukielekea mlimo kuwa uwanja waliopo kina rais
Kilua.Ungekuwa mlipuko wa aina yake ambaye ungeandika historia katika taifa
hilo.
Rada ya kijeshi iliyokuwa macho masaa yote
wakati shughuli za msiba zikiendelea kutoa heshma za mwisho kwa viongozi
waliofariki katika ajali mbaya ya ndege kuangukia jukwaani alimo kuwa ameketi
hayati rais Kisusi na serikali yake.Rada ya jeshi ilipata signal nakuona kuna
kombora linakuja kwa kasi ya ajabu.Aliyekuwa ameketi kwenye mtambo wa kuongozea
rada aliona jambo hilo nakuanza kutoa taarifa.Mlio wa kuashiria kunaswa kwa
mawimbi ya kombora ulisikika!
“Missile detection!”alianza bwana huyo
huku akitoa ripoti kwa wenzake ambao walianza kushughulika kwa haraka ili kuweza
kudhibiti hali hiyo kwa haraka sana.Viti walivyokalia vikawa
moto!
Waliokuwa na shughuli ya kulinda pale uwanjani walikuwa katika
wakati mgumu kudhibiti kombora hilo kwa namna yoyote ile.
“Find the
bearings and get me a theat vector.We will take the missile out and the
threat!.”huyo alikuwa kanali Pasua alipohabarishwa kuna kombora limerushwa na
linakuja katika ardhi ya Kiota.Hapo alikuwa akitoa maelezo wapate vipimo haraka
sana nakulitungua kombora hilo kabla halijafika ardhini kisha watungue na
mahasidi wanaotaka kutungua Kiota.Vijana kwa kasi ya ajabu walipata vipimo na
kasi ya kombora hilo.
“Threat vector localized bearings
098”
“Activate Patriot Missile System to neutralize the threat…take it
out at my order!”alikuwa akitoa maelezo Kanali Pasua ambaye alikuwa mita chache
kutoka uwanjani.Alikuwa makini kabisa akiangalia kioo kikubwa cha mitambo yao
iliyokuwa inaonesha hali ya usalama.Macho yalikuwa makavu yaliyoshiba weledi wa
kazi na ukomavu!
“Target acquired!”alihabarisha kijana aliyekuwa
kwenye mtambo wa kudungua hatari ya kombora.
“Fire!”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwanajeshi
aliyekuwa katika operesheni hiyo alibofya kifyetua kombora la kujihami ambalo
lingekabiliana na kombora lililokuwa likirushwa kuja eneo lile.Mungu mkubwa
alifanikiwa kudhibiti hali hiyo kabla hata halijafika uwanjani.Kombora la
kujihami likatoka kwenye mtambo wake kwa kasi ya haraka nakuingia hewani tayari
kukabiliana na kombora lililokuwa linakuja eneo hilo.Ilikuwa ni sekunde chache
nakulifyetua lile kombora likiwa juu kwa juu!BOOM!Alitabasamu!
Mlipuko
ulisikika!Eneo la mji mkuu wa Kiota watu walishtuka sana kusikika kwa mlipuko
ule.Kwa bahati nzuri mabaki ya makombora yaliangukia kwenye msitu uliokuwa una
mto hivyo kuepusha madhara kwa makazi ya watu.Lakini taharuki kwa waliokuwa
karibu ilikuwa kubwa sana huku waliosikia mlipuko huo kukosa
amani!
“Eagle one what is the status?”
“Incoming Threat
neutralized!”
“Have you found their location?”
“Confirmed
sir location on my eyes.”
“Take them out.”
Yalikuwa ni
mazungumzo kutoka usalama wa jeshi uliokuwa ukilinda shughuli ile.Tayari
walikuwa wamepata shabaha ya eneo kombora lilipotoka.Na sasa walikuwa mbioni
kuliondoa kabisa.
“I want three birds on air now got the location.Send
the missile on my order.Give the birds coordinates.”kanali Pasua alizungumza
akiwa makini wakati ule helikopta zilizokuwa zikishika doria angani zilikuwa
zimepewa amri kuelekea mahali kombora lilipotoka.Helkopta takribani tatu
zilikuwa hewani kufuatilia eneo lile kwa kasi ya ajabu.Wakati huohuo eneo la
usalama lilikuwa tayari kutuma kombora eneo la adui kuwafuta kabisa kwenye uso
wa dunia.
“Target north-east fifty kilometres.Birds you are adviced
clear the way for the missile.”
“One…two..three fire!”alisema Kanali
Pasua ambapo muda uleule kombora likaachiwa kwa kasi ya hatari kuelekea sehemu
ya adui ilikuwa sekunde mbili tu kombora la kumdhibiti adui likawafikia
nakuwalipua pamoja na gari lao.Walimalizwa ndani ya muda mfupi sana.Jeshi la
Kiota lilikuwa makini sana katika kudhibiti tukio hilo.
Helikopta
zilipohakikisha kombora limefanya kazi yake zilishika kasi kuelekea kwenye
mlipuko.
“Vikosi vya ardhini alert move.”
Nchi ilikuwa
makini katika kiwango cha usalama.Kwa kuwa walikuwa namba tatu uwepo wa utayari
hivyo walikuwa makini sana.
“Nendeni msitu wa Shaka mto shaba
muangalie mabaki nataka kujua ni kombora gani walitumia.”kanali Pasua alikuwa
akiongoza mapambano.
“Kitengo cha intelijensia kazini nahitaji majibu
hawa waliorusha kombora Kiota ni kina nani?Mipaka yote umakini
uongezwe.”
Hali ilikuwa imetishia na hawakujua kama kuna jaribio
lingine lingetokea muda gani kwa wakati ule!.
“Kuna utata shughuli ya
msiba inatakiwa iendelee kama ilivyokuwa bila kuleta taharuki yoyote.”alisema
kanali Pasua.Habari zilitakiwa zimfikie Kilua haraka sana la sivyo mambo
yangekuwa hatarini.Wanajeshi walizidisha ukaguzi wa hali ya juu.Ndani ya muda
mfupi kikosi cha ardhini kilifika eneo mabaki ya kombora yalipoangukia nakuanza
kukagua aina ya kombora.Wengine walifika eneo kombora limetoka nakukuta gari
likiwa linaunguwa.
Mwili wa dereva ulikuwa umeharibiwa
vipandevipande!Miili kadhaa ilikuwa imeanguka chini isijitambue.Lakini ipo
miwili iliyokuwa na uhai bado.Hii waliweza kuichukua nakuwakimbiza hospitalini
wangetoa ripoti kuwa wao ni kina nani.Kibati chenye namba za usajili wa gari
kilirushwa wakati kombora lilipotua pale.Kibati kile kilikuwa hatua kadhaa
kutoka na moja ya wanajeshi alifanikiwa kukiona akakichukua nakuwapa timu ya
intelijensia ambao kwa ukaguzi wao gari lilikuwa mali ya ubalozi wa Savanna
Lands.Hali ilitia shaka hasa baada ya kujua kuwa balozi wa Savanna Lands alikuwa
ametoweka pale.Watu wawili waliokuwa hai walikimbizwa hospitalini.Katika zile
purukushani walitambua kati ya wawili wale alikuwepo balozi wa Savanna Lands
katika hali mahututi.
Swali kuu alikuwa anafanya nini eneo lile?Hilo
lilitosha kabisa kuleta uhatari wa hali ya juu!.Wanajeshi walikamata eneo lile
nakuanza kukagua kwa weledi wa hali ya juu.Kazi llikuwa moja tu kuhakikisha
hatari iliyochipuka inadhibitiwa vya kutosha.
“Nataka rais Kilua apewe
taarifa.Balozi wa Savanna Lands aliyetoweka nchini tumemkuta sehemu adui
alipokuwa.”alikuwa ni kanali Pasua akiongea na vijana wake kupitia redio call
zao.Kiota ilikuwa imefanyiwa jaribio la shambulizi kwa mara nyingine tena lakini
jeshi lake makini lilifanikiwa kudhibiti tukio
hilo.
***
Vikosi vya usalama vilizidi kuwa makini
kuhakikisha Kiota ipo salama.Muda ule ulikuwa wakutoa heshma za mwisho.Kilua
alikwishatoa heshma zake kama mkuu wa nchi.Itifaki ilizingatiwa wakawa wanapita
wengine kutoa heshma zao.
Kilua akiwa ameketi kwenye kiti chake
aligutushwa kwa habari.
“Mheshimiwa Kiota inashambuliwa.”aliambiwa na
chifu wake wa ulinzi.
“How?”
“Kuna ripoti kombora lilirushwa
kuja hapa lakini jeshi letu limelitungua likiwa hewani.”
“My
God?”
“Mheshimiwa naomba utulivu wako ilitusiwashtue wageni tuna
subiri amri yako kama shughuli iendelee au tusitishe?”aliuliza chifu wa
ulinzi.Kilua hakumjibu haraka akamgeukia jenerali Lupogo.
“General
Kiota is underattack!”alisema Kilua akimwambia jenerali wake ambaye hadi muda
huo kamuweka chini ya udhibiti mkali kiasi hawezi fanya
lolote.
Jenerali Lupogo alishtuka sana.Nafsi ilimuuma maana mchoro wa
ulinzi walioupitisha yeye na Serambovu ulikuwa umedhibitiwa na adui
wamepenya.Hali ilikuwa tete kwa wakati ule.Sasa alishindwa namna ya kujisaidia
maana lawama zote zitatua kwake.
“Makombora ya kuzuia kombora angamizi
yaliyokuwepo kwenye mchoro wangu mliyaondoa kwenye mchoro wenu kama nisingeamuru
asubuhi kuyaweka sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine!Jenerali fix this
situation la sivyo sitawaelewa wewe na Serambovu!Nataka hatua za haraka
zichukuliwe!”
“Madam unamaanisha nini kwa hatua?”
“General I
am activating your duties right now!”alisema Kilua akiwa amekwazika sana kusikia
Kiota inashambuliwa akiwa madarakani.
Jenerali,”Ok ila naomba
tusitishe shughuli hii?”alisema jenerali akitetemeka.
“Tangu mwanzo
nilihisi mnataka kuniaibisha leo kwenye umati huu wote.Sasa narudia tena
shughuli inaendelea zimebaki dakika chache maana baada ya hapa miili itapelekwa
kuzikwa kwa rais Kisusi na timu nzima ya serikali yake watazikwa kwa
pamoja.Wengine watasafirishwa maeneo yao.”
“Mheshimiwa nashindwa
kuhakikisha kama usalama utakuwepo hadi tuzike naona kuna hatari
bado.”alisisitiza jenerali Lupogo.
“General give the order I need our
commandors to be in the field right now!”alisema Kilua.Jenerali alitii heshima
ile ambapo muda uleule alichukua simu yake maalum kwa shughuli za
kiusalama.Kisha alipiga namba Fulani.
“This is general Lupogo am
activating special force commandors code name 23899kiota alpha team delta tango
full attack!”alipotamka maneno yake vikosi vilivyopewa amri ile walitoka kambini
nakuingia kwenye magari yao.Umbali wa pale na eneo la msiba ingewachukua dakika
kumi tu.Ndani ya muda mfupi vikosi vya komandoo wakiwa na mavazi maalum ya
kijeshi walikuwa kwenye magari yao ya kasi wakija eneo lile huku wengine
wakitumwa eneo lakuzikia makaburi ya dhahabu ambapo huzikwa viongozi wa
Kitaifa.Vifaru vya kijeshi vilikuwa tayari endapo hatari ingetokea basi
inngedhibitiwa kwa weledi wa hali ya juu!Vikosi vilizidi ongezeka ambapo ulinzi
sasa ulikuwa imara.
“General no movement in and out our land seal
everything!”alisema Kilua akifunga mipaka yote ya nchi!
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tayari mipaka ya
Kiota ilikuwa imefungwa kwa muda hadi marehemu watakapozikwa.Wakati shughuli
zikiendelea rais wa Marekani aliyekuwa amekuja pale alipewa taarifa kwa
kinachoendelea.Usalama wa marekani uliomba kumuondoa rais wao haraka sana eneo
lile.
Ilibidi Kilua aongee naye chemba rais marekani bwana
Silver,”Kwa heshma zote rais Kilua itabidi usalama wangu uniondoe
hapa.”
“Mheshimiwa najua unataka kuondoka lakini nakuhakikishia timu
yangu ya usalama ipo kazini hakuna atakayethubutu kuleta shida eneo hili.Naomba
marehemu wetu wapewe heshma zao.”
“Ila hata kama nitabaki basi naomba
wanausalama wangu waungane na wa kwako.”aliomba rais Marekani ambaye mwenyewe
hakuwa na lengo la kutaka kuondoka eneo ingawa hali ya hatari ilikuwa
imeripotiwa muda ule.
“Nashkuru kwa msaada wako ila naliamini jeshi
langu.”
“Najua lakini marekani ina usalama wake.”alihakikisha rais
huyo ambaye alikuwa na nia njema na tayari walikuwa na kaurafiki na rais
Kilua.
“Nitashukuru kama mkilipa jeshi langu uhuru
wake.”
“Sina maana kwamba tunalidharau ila ni msaada wa kirafiki nchi
zetu ni marafiki wakubwa na wakati wa kuonesha urafiki huo ni sasa!”alishauri
rais Silver
“Ni kwa heshma yako tu.”alisema Kilua akimpa mkono rais
huyo!Rais Silver aliongea na vyombo vyake vya usalama ambao waliungana na wenzao
wa Kiota nakuendeleza ulinzi wa hali ya juu!Kilua alijitahidi kutuliza akili
yake hadi shughuli itakapoisha.Heshma za mwisho zilikamilika na msafara
ulielekea kwenye makaburi yaliyoandaliwa.Wanajeshi walikuwa wametapakaa kila
kona kuhakikisha ulinzi unakuwa imara.Viongozi wa kigeni waliokuwa pale walipewa
taarifa kilichokuwa kinaendelea na hatua zilizochukuliwa.Ulinzi uliimarishwa na
wakaondolewa hofu dhidi ya shambulio lolote.Wengi walimuonea Kilua huruma kwa
jinsi alivyokuwa anapitia hali ngumu wapo waliolalamika wakiona ni uzembe ila
wote waliweka usiri wa hali ya juu ili umma usipatwe na woga dhidi ya tishio
lililokuwa likiendelea.Makomandoo wa kikosi maalum walikuwa wameungana na
wanajeshi wenzao hali ikawa shwari ndani ya muda mfupi walichosubiri ni huyo
kidudu mtu atakaye thubutu kuinua kidole dhidi ya taifa
hilo.
Helikopta zilikuwa hewani kushika doria huku ndege za kivita
zikipitia anga lote la Kiota kuhakikisha usalama.Ndege zisizotumia rubani
zilikuwa zikipita angani kupitia usalama.Ndege maalum pia za kudhibiti makombora
ambazo hazitumii rubani nazo zilikuwa tayari kudhibiti jambo lolote ambalo
lingeashiria udhibiti wa kiusalamaa.Anga la Kiota lilikuwa na utayari.Ndege zote
zilizokuwa zikiingia zilizuiwa na hakuna iliyotoka!
Kilua alikuwa
anatamani alipize kisasi kwa dharau za shambulio lile.Yaani watu wamepenya na
silaha nzito wanataka kumuaibisha kwenye shughuli muhimu hii kwake aliona ni
dhihaka!Na hata huyo balozi wa Savanna Lands aliyekutwa eneo la tukio aliapa
kumuangamiza kwa nguvu zote!
Watu walifanya mazishi ya wafu wale kwa
amani.Taratibu zote zilikamilika baada ya masaa kadhaa ambapo shughuli
zilipoisha waombolezaji waliondoka eneo lile.Viongozi wakigeni waliomba kuondoka
pale haraka sana wapo walioruhusiwa na wengi waliondoka pale akiwemo rais wa
marekani.Isipokuwa rais wa Savanna Lands alizuiliwa kuondoka.Ilibidi viongozi
kadhaa waingilie kati mzozo huo na kikao kikaitwa ikulu cha dharula wakiwemo
takribani marais sita pamoja na wamarekani.
“Mheshimiwa huwezi
kumzuia aondoke.”alisema moja ya marais aliyekuwepo kikaoni pale.
“Mimi nashangaa huyu mwanamke tangu apewe kiti amekuwa akiniandama mimi na taifa
langu.Kesha tungua hadi ndege ya jeshi letu na mwanagalia tu!”alikuwa
akizungumza kwa ukali rais wa Savanna Lands.
“Jamani tutumie busara
kwa nini rais Kilua hataki rais wa Savanna Lands aondoke
hapa.”
“Anataka kusema mimi nahusika na hili jaribio la leo!”rais wa
Savanna Lands alikuwa muongeaji hodari wa kulalamika.
”Kumzuia huyu
bwana kutasababisha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya taifa lako na
lake.Pengine muingize vita kabisa!”
“Mimi sihusiki kwa
lolote!’alijitetea.
Kilua alipiga meza kwa hasira wanaume wote
wakamuangalia pale,”Waheshimiwa msidhani nachukua hatua hii kwa kumuonea!Huyu
bwana taifa lake lilianza kuleta majeshi yake mipakani mwetu haitoshi akarusha
ndege ya kivita sikuwa na budi nikaidhibiti!Balozi wake alitoweka hapa
akanitishia sana kwamba nahusika lakini cha kushangaza leo mlipuko ulipotokea
tunamkuta balozi wake.Silaha hizi zimetoka Savanna Lands na ripoti hizi hapa
zinasema kabisa gari lilikuwa la ubalozi na leo hii kamera za mipakani
zimethibitisha kwamba gari hili lilipita huko jana!Halafu linakutwa eneo la
shambulizi mnataka nifikirie nini?”
Hali ilikuwa tete,”Madam Kilua
hadi sasa majeshi yangu yanajua kwamba umenizuia ikulu kwako huu ni utekaji
nakutahadharisha tutaingia vitani!”
“Mheshimiwa kwanza achia watu wa
ubalozi wangu waliopo kwako!”alitamka Kilua kwa ujasiri!Thubutu aliyoifanya
ilionesha hatari sana.Kikawaida mizozo huwepo lakini hatua ya Kilua ilishtua
wote nakuona kwamba mwanamke huyu alikuwa msumeno na kama hawatajifunza
kushirikiana naye kwa nidhamu la sivyo anaweza akafanya tukio la
kuogofya!Alionekana kama dikteta kumshikilia rais wa taifa lingine ni ishara ya
vita.Ilibidi wawahini viongozi wote kuhusu ugomvi wao.
“Nimewasikia
mimi nawahakikishia Savanna Lands haihusiki kwa lolote na shambulio la leo na
kama inahusika basi nitaachia madaraka!Naomba nitoe hilo kama
ahadi.”
“Kabla ya yote watu wangu waliopo ubalozini kwako ambao
umewaweka chini ya ulinzi nataka waachiwe huru.Asiguswe hata kidole.”Rais Kilua
hakuwa na ubembelezo wowote kwa wakati kama ule.
“Nitawaachia ila kwa
sharti moja.”alitamka rais wa Savanna Lands.
“Huna mamlaka ya
kuniwekea masharti kama ulikuwa unamchezea rais Kisusi mimi
hutathubutu!”
“Punguzeni jazba wote tunataka tufikie muafaka ila
wataalamu kutoka nje watachunguza ikibainika serikali ya Savanna Lands ina mkono
katika shambulio hili basi itawajibishwa!”moja ya viongozi wa nje alisihi
kuhusiana na jambo hilo.Alieleweka ikabidi wakubaliane dhidi ya mabishano
yale.Kilua aliogopwa sana.
“Pia tunaomba habari hii isitoke
itachochea fujo kati ya watu wenu.Ibaki kuwa top secret.”alishauri rais mwingine
maana katika kuzuiwa kule ni wachache sana walijua hatua aliyochukua
Kilua.
“Lakini nasema tena ni ukweli rais wa Savanna Lands anataka
kingilia nchi yangu mimi nilisema toka mwanzo na hata mkichunguza mtagundua
hilo.”alisema Kilua akiwa ameanza kupoa .Mazungumzo yalidumu takribani masaa
manne ndipo suluhu ikapatikana usiku na hali ikawa imepoa na hata rais wa
Savanna Lands alikiri baada ya pale hakupenda swala lile lifikie umma.Ilikuwa
aibu kubwa sana ikiwa ingegundulika kwamba alikuwa amezuiwa na mwanamke huyo!Wao
walimuona kama dhaifu tofauti na mategemeo Kilua alikuwa anajua wapi
pagusa.Ndege za jeshi lake zilipogusa anga lake alishambuliwa kwa haraka
sana.Hiyo ilimpa tafsiri kwamba mwisho wa siku Kilua alikuwa mbabe na alijua
anapiga wapi anakumaliza.Kikawaida ni kama juhudi zake za kumuingilia Kilua
badala ya kumdhoofisha walijikuta wakizidi kumuimarisha zaidi maana hatua
alizochukua pengine zilionekana za kibabe zaidi ila ziliondoa tabasamu la
kinafiki kwa maadui zake ambao sasa walikuwa wakilowa woga kwa ubabe
wake.
Kilua hakuonekana tena yai bali mbabe anayesubiri
kuchokonolewa kisha akufumuwe nakukuvua nguo mbele ya kadamnasi na kwa hatua ile
si ajabu mataifa hayo yakizidisha uhasama.Na badala ya Kilua kutafuta amani
ikawa ni zamu ya rais wa Savanna Lands kujiondoa katika shutuma hizo za
Kilua.Hata kama alihusika kwa shambulio lile bila shaka alikuwa amevuliwa nguo
mbele ya viongozi wenzake.Na kisasi cha Kilua kilikuwa cha akili
sana.
“Mshemiwa watu wako wanaweza thubutu kutikisa anga langu kwa
sauti za makombora lakini mimi nimekuanika mbele ya viongozi wengine na
ninakuhakikishia taswira ta taifa lako hadi uje ulioshe itakubidi ujishushe
hasa.Mimi nimepewa hiki kiti nakitumia ipasavyo kulinda taifa
langu.”
“Nalijua hilo na ndo maana nataka mniamini kwamba sikuwa
nania yoyote kuhujumu utawala wako.Najuwa tuna mizozo baina yetu lakini hiyo
siyo lengo la kukutikisa bali ni ushindani wa
kibiashara.”
“Hapana!Wewe ulijileta direct iweje silaha hizi ziingie
kwangu kupitia kwako halafu leo wanafanya jaribio.Kinachonishangaza iweje
urushe kombora mahali unajua kabisa nawewe upo?”Kilua alihoji
hilo.
“Ndo maana nasema siuhusiki kwa jambo hili mheshimiwa.”alikuwa
mpole rais wa Savanna Lands.
“Huku jiuliza kuna mataifa mangapi
viongozi wao walikuwepo hapa?Huku nitishia mimi bali mlitishia na viongozi
wengine.”Kilua aliendelea kumshambulia rais wa Savanna Lands na jinsi mazungumzo
yalivyo ilionesha Kilua alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba shambulio
hilo lilikuwa na baraka kwa taifa hilo.
“Tafadhali naomba uondoe
kauli ya kunishutumu moja kwa moja.Mimi sijui kama balozi wangu alikuwa na mkono
wa jambo hili.Hawa wanafanya mambo kutuchonganisha tu!”
“Mheshimiwa
unakumbuka ulivyonitishia kwenye simu!”
Chumba kikawa kama
kinachemka tena baada ya majibizano magumu baina ya watu hawa wawili!Mambo
yalikuwa yana badilika.
“Ok jamani tuwe na nidhamu tafadhali sisi ni
viongozi wa mataifa na wote tunategemewa naomba tufuate utaratibu kama
tulivyokubaliana.Kwanza raia wa Kiota waliopo kizuizini huko Savanna Lands
tunaomba waachiwe huru.Halafu wachunguzi kutoka nje watafanya uchunguzi dhidi ya
shambulio hili na atakayekutwa na utata basi atawajibishwa.Mabishano haya
yanaonesha fika kwamba nyote hamuelewani na kwa namna hii itatulazimu tulete
majeshi ya umoja wa mataifa yalinde amani ikiwa hamuwezi kutuliza hasira
zenu.”alishauri rais marekani.
“Mimi sina haja ya kwenda vita na
huyu.Ninachotaka ni ukweli ujulikane muhusika wa shambulio hili ni nani.Nianze
vita kwa lipi.Namfuata adui wanajeshi wako wanafuata amri tu.Mimi na mfuata
anayehujumu taifa langu tu!”
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kikao kilifikia
muafaka na rais Kilua alikubali kumuachia rais wa Savanna Lands
aondoke.Ilionekana ndege yenye chapa ya jina AIR SAVANA LANDS ikikatiza angani
kuondoka.Kwa rais wa Savanna Lands alipakwa fedheha kufuatia shutuma alizotoa
Kilua.Haikuwa hatua ya kirahisi kama vile ilivyotokea na ilitakiwa aharakishe
kusimamia uhusiano wa kidiplomasia na taifa la Kiota la sivyo angezidi kuonekana
kituko mbele ya kadamnasi na jamii kwa ujumla.Mambo ilikuwa nzito sana na bila
kuzima moto huu kwa busara alikuwa katika mashaka!Hasira ya mwanamke yule
ilizidi kumshushua kila alipowaza na kweli siku ile ilikuwa ngumu katika
historia ya maisha yake kuzuiwa na rais mwenzake!Akiwa angani alitizama kioo
alihisi hasira na woga ukamwingia hadi akajikuta kichozi kikimtoka kwa jinsi
alivyofedheheshwa.Alikuwa tayari kulipa kisasi lakini ingekuwaje mbele ya
mwanamke huyo mbabe ambaye kesha uwekea utawala wake vitisho na kama hata
imarisha uhusiano wa taifa lake na Kiota bila shaka kutakuwa na vikwazo vingi
kwake kiuchumi!
Alitamanii kisasi kwa hali ya juu lakini alishindwa
maana kwaanzia wakati ule lolote lingetokea dhidi ya Kilua mlaumiwa wa kwanza
angekuwa yeye.Ilibidi ageuke awe mlinzi badala ya mshambuliaji.Tayari alipiga
simu kwake nakusitisha hatua zote za kuidhibiti Kiota kwanza hadi hapo mambo
yatakapokuwa sawa.Ndege yake ilitua salama katika ardhi ya taifa
lake.Alipokelewa na usalama wake kisha alienda hadi ikulu kwake.
***
Shuni
alikuwa amemshika mtoto wa Kilua ambaye bado ukimya wa maonevu ulikuwa
umemtafuna ini na moyo.Alikuwa ameharibika kisaikolojia hasemi la bee wala
tee.Ni uharibifu wa hali ya juu ukimtafuna ini na moyo!Shuni aliweza kuoneshwa
kwa mara ya kwanza bwana Dedani mume halali wa rais Kilua akiwa amefungwa kamba
nzito mikononi na miguuni!Alijikuta kwa siku ya kwanza akimkodolea macho bwana
kana kwamba ameona kitu fulani au aliona zaidi kwenye bilula za macho
yake.Aliona kitu zaidi ya upeo na taswira iliyomfifisha hali ya
sintofahamu!Moyoni alihisi amefeli katika kumuokoa mwana wa rais Kilua lakini
kama mumewe ypo na mwanaye bado wana pumua basi alikuwa na uhakika wa kuisaidia
familia hii kwa udi na ambani.
“Walimfanyaje mwanangu?”aliuliza
Dedani akiona mwana wake akiwa kwenye wingu la huruma lisilo na msalia mtume wa
faraja.Kapotezwa kabisa na hajijui wala kujielewa.Picha ya zee Kavu na fimbo
yake nyama ilikita katika kuta za usichana wake nakumfedhehesha alihisi kupasuka
kwa mashaka ya wasiwasi nakutokujiamini!Shani alikuwa si Shani iliyong’aa na
nuru yenye kumliwaza kila mtu.Sasa alikuwa mwana huzuni mbeba kilio cha shake
akijuaye moyo wenye kiza kinene!
“Walimbaka!”alisema Shunie kwa
huzuni kedekede zenye mchakato uliotindwa hofu!
“Kwanini kwa
mwanangu?”alijiuliza Dedani akiwa haamini kabisa kuhusu tukio hilo lenye dhihaka
kwake.
“Bwana najua wote tuna huzuni kwa unyama aliofanyiwa
Shani.”alianza Shunie akijaribu kutuliza.
“Huu si unyama!Hata
wanyama wana hafadhali!Simba hawezi kubaka kinda!Binadamu huyu ndiyo
mkatili,Unawezaje kumnajisi mwanangu ninaapa nitairudisha familia yangu ikiwa
salama!They hurt my baby girl I will kill them!”aliapa Dedani akizidi kudata na
tukio lile ambalo lilifedhehesha sana moyoni!
Shunie akiwa pale
kaketi akitizama akijaribu kumfariji bwana huyu akili ilifanya kazi mara mbili
kati ya kutoroka pale nakuikoa familia ya rais Kilua.
“Tutashinda
jambo hili.Nakuhakikishia bwana lazima tuondoke hapa hawawezi kutuzidi kete watu
hawa.”
Dedani alidata kwa namna fulani akili ikifa ganzi.Mlango
ulifunguliwa akaja akachukuliwa kisha akatolewa nje yeye pamoja na
Shunie.Hakutaka kuwa mbali na mtoto wake ilibidi wamlazimishe kwa nguvu zote
hadi alipotoka.Waliletwa kwenye chumba kingine.
“Bwana Dedani nina
jambo nataka ulifanye.”alianza mzee Kavu akiwa kashika sigareti kubwa iliyonona
nakukaa vyema kwenye mdomo wake.Moshi mzito ulionekana kufuka kwa mbwembwe za
ukwasi.
“Kazi gani mnataka nifanye?”aliuliza japo alikuwa na hasira
sana na alitamani kumvaa bwana huyu nakumfutilia mbali lakini hakuwa na uwezo
ule kwa wakati ule.
“Nadhani ulipata ujumbe kwamba mkeo na mahusiano
ya siri ya kimapenzi bwana Serambovu.Uhusiano huo ni mkubwa sana hata imefikia
mahali Kilua yupo tayari kuishi na huyu mtu kama mumewe na wewe ndo
tatizo.’alisema bwana Kavu akimwangalia shabaha yake.
“Kwa sasa wapo
wote ikulu na siajabu mkeo anazidi kuliwa na huyu bwana ingawa anajua wewe
umetekwa hata ile heshma kwako haipo.”
Dedani alimeza jambo
hilo.Mzee Kavu aligeuza kioo cha tarakilishi yake ya mpakato.Kulikuwa na video
ikionesha hafla za Kilua akiwa kama rais huku pembeni Serambovu akitanda bila
hiyana!
Dedani alikerwa na jambo hilo.Halafu mlango ulifunguliwa
katika chumba kile akaingizwa binti fulani.
Dedani alimwangalia
msichana yule pasi nakumjua hivyo hakumpatiliza sana.
“Huyu msichana
alikuwa mfanyakazi wa ikulu.Msichana hebu tueleze.”
“Ni kweli
nilikuwa mfanyakazi wa ikulu hivi karibuni niliingia chumbani kwa rais asubuhi
kumuandaa.Ajabu walinzi waliniruhusu niingie kwamba rais bado amelala.Niliingia
nakusikiia kelele za mahaba.They were deep making love and seems they didin’t
notice me.Nilidhani ni mumewe inawa ikulu tulishangazwa kwanini familia ya rais
hadi muda ule haijaja ikulu.Kuja kushuhudia nilimkuta rais Kilua kwa macho yangu
akifanya mapenzi na Serambovu!Habari hii kuna mwandishi alitaka kuichapa lakini
akazuiwa.Mimi nilimkuta Kilua akizini na Serambovu.Niliona haya halafu
nikasikitika kwanini rais anakosa heshma nakutembea na mfanayakazi wake ikiwa
wewe upo?Kwani rais wetu ni kicheche?”alihoji binti yule
akimakinika.
“Dedani act like a man!”
Dedani hakujibu
kitu.Alitulia kimya huku machozi yakimtoka kwenye chemchem ya moyo wake kwa
kasi!Aliujua huu udhaifu wa Kilua kutoka kwa bwana Serambovu ameishi nao
ukimsugua ini na moyo hadi akawa na vidonda vya tumbo.
“Bwana Dedani
mkeo nimsaliti wa ndoa!”
“Nifanyeje?Hili ni swali unatakiwa kulijibu
bwana Dedani.Jibu ni rahisi mimi ninatoa wazo zuri tu.Tutakuachia na useme
kwamba mkeo anakusaliti ndo maana hujaonekana tangu yeye kuwa rais wa nchi.Then
sisi tutakuandaa kisiasa uwe mpinzani wa mkeo.Kwa masharti ya jambo moja hapo
mbeleni kuna kitu tunataka uje utusaidie kukipata.”
“Jambo
gani?”
“Nyaraka namba 13:14.Nahisi mkeo anakaribia kutambua jambo
hilo.Lakini sisi tunaandaa baada yake nani ataurudisha tena?Tunataka uwe
mpinzani wa mkeo.Japo tulitegemea awe dhaifu lakini katushangaza baada ya
kugeuza mwenendo tunahitaji njia mbadala na wewe ndo njia hiyo.Kwa hatia ya
kukusaliti anaweza akakupa kiti ilituweze kumdhibiti!”
“Mnataka
kunitumia mimi kwa faida yenu?”alihoji bwana Dedan akiwa bado amepandwa na
hasira.Alitaka kabisa kulipa kisasi dhidi ya usaliti wa mkewe kwa usaliti wake
uliovuka mipaka.
“Ndiyo tunataka kumchafua mkeo tena sana.Huu ni
wakati wako wakutusaidia sisi kulipa kisasi.Ukiwaanika mbele ya umma lazima
Serambovu aondoke kwa Kilua kulinda heshma ya Kilua!Vilevile wewe utakuwa na
nguvu ya kumdhibiti mkeo!Utadai unataka muwe na suluhu!”
Dedani
alifikiri kiasi lakini hakusema kitu.Ilibidi wamrudishe kwenye chumba kingine
cha kizuizi.Shuni alibaki kwa mzee Kavu.
“Tuna hitaji na wewe jambo
moja toka kwako!”
Shunie alishtuka akimwangalia Mzee Kavu na chongo
lake ambalo Shunie ndo aliyemtoboa jicho hilo.
“Kitu
gani?”
“Mrubuni ulale naye leo.Ukifanikiwa tutawaachia!”
“What?”
“Ulipewa mafunzo kumrubuni mwanaume yeyote yule utashindwaje
kumlaghai huyu?”
Shunie alitumbua macho kwa mshangao wa aina
yake.Atawezaje kufanya jambo hilo na mume wa mtu kweli huyu bwana hana nia njema
na Shunie bali uonevu wa kijinsia.Shunie alihisi mwili wote kufa
ganzi.
“Siwezi kufanya hilo jambo!”Shunie aliweka mgomo.
“Wewe mpe jambo lakumsahau mkewe.That fool anampenda sana mkewe.Anahitaji kujua
ladha nyingine.Ukipita kwake anaweza asihisi sasa ila hapo mbeleni kikatokea
kitu.”
“Mna malengo gani?”aliuliza Shunie.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Just do it
siunataka kuwaokoa?Wewe wafanyie jambo hilo nakuhakikishia inawezekana kabisa
mkatoka huku mkiwa salama pia itaokoa kuondoa hatari ya Shani kuendelea
kudhalilishwa.”alitamka mzee Kavu kisha akaamuru Shunie na Dedan waweke chumba
kimoja.Hilo lilifanyika.
“Bosi unadhani jambo hilo
litafanyika?”aliuliza yule binti.
“Vinywaji watakavyokula na vyakula
vitasaidia kuwashawishi wao wafanye jambo hilo then tuta rekodi tukio
hilo.”
***
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment