Simulizi
: Kombora Kiotani
Sehemu Ya Nne
(4)
Dedani alipapasa
godoro nakujikuta akiwa ameshika mwili wa mtu wenye ulaini wa
hurulaini.Alijihisi mtawala wa dunia na ardhi yote.Hakuhisi huzni bali ujaisiri
wa hali ya juu.Mguso huo wenye mpapaso ulirudishiwa kwa mbwembwe za aina yake
kisha yeye mwenyewe alijikuta akiinuka kwa mtikiso uliopeleka moyo na mzunguko
wa damu kuwa kwa kasi ya ajabu.Alijikuta akimshambulia mwanamke aliyekuwa
kitandani mwake.Ujio wa mwili wake kwa msichana huyo ulipatwa na joto na kila
fahamu ya hisia ya mwili wa mwanamke yule aliutambua uwepo wake nakumpokea kwa
katazo lililokinzana na uhitaji wa miiili yao!Kulikuwa na joto katika kitanda
kile.Pengine nikutokana na akili zao kupoteza kumbukumbu mbaya za mateso
waliokuwa wanapitia zaidi walikuwa wao wawili na akili zilikuwa haziwazi
matatizo bali kiwango cha kilele chenye faraja raha!
Wawili
walikuwa wanafanya mapenzi.Mtu mume na kike.Walikuwaa wamezama kabisa katika
dimbwi walilolijua wao wenyewe nakutopatiliza ulimwengu uliwazunguka.Walijua
wapo mahali hata kuona walipo lakini hawakugundua lolote kwa muda ule wa wingi
wa hawaa na chachu ya penzi lenye uzito wa kijuaji!.Dunia iliwaweka kwenye
kiota cha mapenzi yao wawili wenye miili.Mtu nke alikitia joto kitanda kile na
kuzama kwenye bahari yao isiyo na maelezo.Unyevu wa jasho ulitota kwenye mgongo
wa mwanaume yule aliyekuwa akijitahidi kuzama nakutoka kwenye kisima cha
mwanamke yule.Vidole vya msichana vilikuwa vikishika mgongo wenye utelezo wa
jasho huku kucha zikichomachoma kwenye nyama za mgongo.Yalikuwa mahaba mazito ya
ghafla bila kutarajia kwa hawa viumbe waliozama kwenye bahari yao ya muda
mfupi.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Safari ya mahaba
ilikuwa kwenye kilele kila muda ulivyoenda nakuwafanya wote wazinduke katika
mvuke ule uliowatotesha kwa kuwapika na mfukuto wa hawaa.Dakika zilipokinzana na
haja ya mwili viumbe hawa walijikuta wakiachiana nakuhema kwa pupa pumzi
zikishindana kuingia nakutoka.Usingizi mzitoo ulimchukua mwanaume yule
nakumfanya apotee kwenye kiota cha pumziko.Msichana alimwangalia mwanaume yule
alivyofumba macho nakupotelea kwenye usingizi wa pono.Alimtizama kwa wingi wa
maswali hata asimmalize.Alifikiria mbali sana kiasi usingesema wawili hao
walikuwa pamoja muda ule.Tayari akili ya binti ilianza kurejea kwa umbali
nakujua tukio hili litaanzisha mambo mengine.Hatimaye Shunie katimiza lengo
alilotumwa na mzee Kavu kumhini Dedani afanikiwe kuwa nawe kwa muda.Pengine
tukio hilo lingezaa jambo ambalo lingempa sababu Dedani kuwa na mawazo kinzani
kati ya kuwa naye au la!
Aliupapasa uso wa mwanaume huyo aliyekuwa
ubavuni mwake nakuuangalia.Halafu akajichukia sana kutumika kwa namna ile
nakuhofia hatma yake na nafasi kama mwanamke katika jamii ipoje?Ni sawa
kuendelea kutumika kwa namna ile.Leo kalala na mume wa rais Kilua!Hilo tiyari na
tatizo kubwa sana kwa upande wake akijiuliza kama ataeleweka mbele ya rais siku
akijua kitu hicho!Haijalishi alikuwa katika hali gani hadi jambo hilo likajiri
lakini limejitokeza.Akili yake ilikufa ganzi nakumhofisha sana kama ataendelea
katika hali au la!Dedani yu ubavuni mwake muda ule.Tayari kesha fanya
alichotakiwa sasa angesubiri tu bwana huyu aamke ajue kaama tukio hilo
lilikuwa na maana au ni jaribio hewa.Kinachohitajika nikuhakikisha Dedani
anakuwa mikononi mwake!Lakini kwanini apewe jambo zito kama hilo
alitekeleze?Kwaninii yeye na asipewe mtu mwingine?
Aliogopa wakati
mwingine kwa jambo hilo.Lakini alipiga moyo konde kwamba nitukio la mara moja na
pengine halitajirudia tena na yeye atakuwa imara.Ila picha ya uwepo ubavuni
mwake ilizidi kumshawishi asonge zaidi pengine kwa dakika hizo chache aweze
kulifaidi joto la mwanaume huyo!Alijisogeza nakukilaza kichwa chake katika kifua
cha Dedani.Chakula walichokula kilifanikiwa kumlevya Dedani kuondoa ufahamu wake
kwa kiasi fulani hivyo kutoa mwanya kwa wawili hao kufanya lolote ambalo ufahamu
ungelidhibiti!Shunie alihisi kuridhika na kitu fulani kuchepuka katika moyo wake
huku masikio yake yakihisi mapigo ya moyo ya Dedani aliyelala kwa amani!Shunie
alihisi tofauti katika kulaza kichwa chake juu ya kifua cha Dedani .Ilikuwa
tofauti hata akiwa na Mzee Tufe na Pablo.Kumbukumbu zake zilikoma na akili
kutulia kisha amani fulani ilipita kwenye fahamu zake.Usingizi wa amani ulimjia
na yeye kulala kwa amani.Kwa muda mfupi alijihisi yumo kwenye kiota cha paradiso
na akili kuliwazika kabisa na yeye kujisahau.Alisahaau hata matatizo yote ya
kuwekwa kizuizini na watu wale wenye roho za kutu…
***
Pumzi yenye joto nakaubaridi kidogo ilikuwa
ikipuliza kifuani mwake bwana Dedani.Alizinduka kwa taratibu huku akili
ikijaribu kujua mahali alipo lakini uzito wa kichwa ulimfanya azubae na punde
alipojua kuna mtu mke pembezoni mwako nakuipata harufu maridhawa ya mwanamke
huyu alihisi kama ni Kilua wake kwenye bustani ya maua.Alijikuta akimkumbatia
kwa nguvu nakumgeuza tayari kumkabili lakini pua zake zilimwambia utuli wa
mwanamke huyu laini kama hurulaini hakuwa wa Kilua.Huyu alikuwa mtu tofauti na
mazoea yake.Japo ni kwa muda sasa hajaonana na Kilua wake lakini bado anakumbuka
mazoea yake pindi wakiwa pumziko nyumbani basi angekuwa bustani akipalilia maua
yao.Hizo ni siku njema za uhai wa penzi lao.Hazipo tena zimefika
kifo!Akagundua si Kilua bali ni mtu tofauti kabisa na huyu aliyepo
hapo.Alinukia kama malaika kwa utuli ulio na tarabizuna halisi ya mwili pengine
ni kule kuzoea kutumia tarabizuna fulani ambazo bado ziliacha utuli wake kwenye
mwili.Dedani alichachawa ule utuli.Kwa dakika alimwangalia mwanamke yule
nakugundua ni Shunie!Akili yake ikazinduka muda ule nakujua kilichotokea kati
yao hakikuhitaji ufafanuzi wa manunuzi ya kumbukumbu japo hakuna kumbukumbu ya
lolote lililojiri usiku uliopita lakini hali ilimwambia hakuna usalam na kwa
mara ya kwanza alifanikiwa kumsaliti mkewe!Dedani alimtoa mwananke yule kwa
utaratibu pasi nakumuamsha akamlaza vizuri kisha yeye akaamka nakutoka
kitandani huku ameshika kichwa kwa hofu na majuto!
Dakika tatu
mbele Dedani akiwa amejishika kichwa asijue kinachoendelea alimuona Shunie
akiamka nakumkazia macho!Wote walishindwa kukabiliana machoni.Aibu fulani
ilikuwa imewameza kwa ghafla!Hakuna aliyejua ni wapi waliacha mavazi.Lakini
kichwani kwa pamoja likawajia jina la Shani.
“Shani” walitamka kwa
mkupuo halafu wakajishika vinywa kwa aibu fulani.Ni kweli walikuwwa wamepigwa
na butwaa.Dedani aliona maliwato aliyafuata kwa haraka.
***
Mzee Kavu akiwa kwenye chumba chake cha uongozaji
alikuwa akiangalia kupitia tarakilishi yake yenye kamera zilizofungwa kile
chumba alimokuwa Shunie na Dedani.Alikuwa amerekodi kila tukio.
“Game over.”alisema mzee Kavu akiangalia kishujaa tukio zima kwa
mbwembwe.Nimefanikiwa kumlaghai Dedani mikononi mwa Shunie akijua kwaanzia pale
Dedani na Shunie hawatakuwa kawaida tena.Wataangaliana tofauti na hatia kuwala
kila watakapowaza tukio lile hapo alijua fika hata mambo mengine kwenye
fikra zao yatakosa uungwaji mkono sanasana litakalo chukua nafasi maalum ni
hili lla wao kulala pamoja!
“It was the best romantic scene
ever!Watu wawili wasiojuana wanalala pamoja kwa mahaba mazito huku wwasijue kama
wanapendana au la!Wote wana watu wao wanaowapenda.Hii inaitwa kuwachanganya
kiakili.Na kila uchao watatamani kulizungumzia jambo hili bila ujasiri
hawataweza na kila uchao watakuwa na maswali ilikuwaje?Anachohisi mwenzake na
yeye ndo anachohisi?Kutakuwa na taharuki kubwa sana kwao mtu hizi mbili!”alisema
Mzee Kavu akiangalia matukio yale kwenye tarakilishi.
“Ni mpango wa
ajabu sana.”
“Hawatakuwa na amani kati yao hadi watalkapokuwa tayari
kulizungumzia swala hili.”
“Naona wameshajiandaa chakufanya walete
hapa.”alisema bwana Kavu.Baaada ya muda mfupi Dedani na Shunie walikuwa mbele ya
Pilato zee Kavu lenyewe!
“How was your night?”aliuliza zee Kavuu kwa
tabasamu la kejeli.Shunie na Dedani walichukizwa kwa kauli ile.Aibu ilizidi
kuwatafuna ini na moyo!
“Tambueni ninao ushahidi wa tukio lote
mlilofanya ninachohitaji nikubofya kitufe tu halafu na sambaza video hizo
wapenzi wenu waone kila kitu!Najua hamtapendezwa kabisa na hatua
hiyo.Unachotakiwa kufanya bwana Dedani ni kwenda kwenye mahojiano na kituo cha
habari ambacho tumekiandaa.Huko utatakiwa kumsema rais ambaye ni mkeo kwamba
humuamini katika ndoa yenu na unataka kumrudia kwasababu unampenda.Lengo ni
kuonesha rais haaminiki katika ndoa yake na wewe upo tayari kuonesha umma
udhaifuu wa mkeo.Tutamchafua kabisa nakuharibu taswira yake katika jamii.Natumai
utatupa ushirikiano mzuri.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lilkuwa ombi zito
sana kulifanya japo ni kweli kwa shutuma hizo lakini vipi amuaibishe mkewe kiasi
kile hasa akiwa na wadhfa wa urais wan chi?
“Kama nikikataa?”alihoji
Dedani akitetemeka sana.
“Nani alikwambia una kauli kwa
hili!”alisema zee Kavu kasha akaendelea,”Mkeo alijiletea aibu hii sio ya kwako
wewe tekeleza kile unachoambiwa!”
“Lakini…”
“Unajua
mwanao yupo mikononi mwangu au umesahau?”aliuliza bwana Kavu akiwa na
umakini.Sura yake haikubeba mzaha wowote zaid ya umakini wa kuhukumu!Dedani
alitumbua macho kama vile mjusi amebanwa na mlango!
“Nipe mwanangu
halafu nitafanya unachokitaka.!”
“Mwanao hawezi kutoka hapa hadi
nitakaporidhika na ninachotaka ufanze.”alisema zee Kavu. Maandalizi ya
mahujiano yalikuwa yameandaliwa.Lingekuwa bomu kubwa sana kwa rais Kilua kwa
serikali yake.
“Kuna gari lipo hapo nje utaenda nalo nategemea ndani
ya muda mffupi kutikisa anga za habari kwa skendo ya aina yake.”alisema
Kavu.Dedani alichukuliwa pamoja na Shunie wakavalishwa mavazi nadhifu na pamoja
wakapakizwa kwenye gari tayari kuelekea kituo cha habari kwa mahojiano maalum
ambayo yalikuwa yametangazwa kuhusu mtu muhimu nchini kuhojiwa ila matangazo
hayakusema ni nani.Promosheni iliyofanywa ingemshawishi yeyote kutizama kipindi
kile ingawa hakujulikana muhusika ni nani?
Dedani alikuwa amekunywa
kido go kupandisha stimu tayari kwa vamizi kubwa kwenye habari akimshutumu mkewe
kuwa msaliti na ushahidi anao!
Alifika katika viunga vya kituo cha
televisheni ya Pamekucha katika kipindi maarufu cha NYUMA YA PAZIA.Killikuwa
kipindi maalum chenye wafuasi watiifu hasa vikijikita kwenye stori nzitonzito
za watu wazito kitaifa na kimataifa.Kipindi kilikuwa kikongwe na maalum kujenga
au kubomoa sura za Fulani.Leo wafuasi wa kipindi hicho akiwamo rais Kilua pia
walikuwa mbioni kukitizama kupata hatma ya vitendawili vyao.
Dedani
alikaribishwa kwenyee studio za Pambazuko kwa shwangwe tayari kupanda studio
kwaajili ya mahojiano maalum.Utaratibu ulikamilika nay eye kuketi huku kamera
zikianza kuchukua picha!
Wengi walikuwa na shauku
ya jinsi kipindi kingeenda kwa siku ile na jinsi kingepokewa na umma.Kulikuwa na
stori kubwa iliyongoja kuruka hewani.Kilikuwa kipindi maalum kwa siku ile
yenye mengi ya kushangaza na kushtusha.Pigo kwa rais Kilua kama mambo yangeenda
kama kipindi kinnavyotakiwa kuruka hewani siku zote.Dedani alibeba uhusika wa
aina yake kwa siku ile na jinsi tukio litakavyokuwa.Hakuwa tu analipa kisasi
bali pia likuwa anaweka familia yake kwenye sura mpya yenye wingi wa
sintofahamu.
Kamera zilikuwa tayari kuruka
hewani.Na kama ilivyoada kwenye utawaala wowote ule lazima rais awe na
mashushushu wake waliotapaakaa kila pembe ya ardhi ya Kiota.Ujio wa ghafla wa
mume wa rais Kilua katika studio za televisheni ya pamekucha.Ndani ya muda
mchache aliokuwepo bwana Dedani tayari habari zilianza kusambazwa kama moto
wa nyika katika viungaa vya upashaji habari nyeti wa rais kuwa mumewe
kaonekana.Wapambe wa Masha walikuwa kazini kuhakikisha sura ya Dedani popote
itakapoonekana ilindwe.
Kipindi kilikuwa tayari kuruka .Mtangazaji
maarufu wa kipindi kile alikuwa shauku ya kuhakikisha kwamba habari ile inapata
kipaumbele.Kwa mara ya kwanza tanguu rais Kilua kuingia madarakani familia yake
inapata ipaumbeele kuonekana mbele ya umma.illikuwa nafasi nzuri kwa mtangazaji
Lora kutoa kipindi kile adimu mahojiano rasmi na mume wa rais Kilua ambayo
yangekuwa tunu kkubwa kwake kuwahi kufanya.
Shunie akiwa kwenye gari
alichapuka kwa harakaa nakumrushia teke mlinzi aliyepembeni yake.Alimpiga kwa
kishindo nakufanikiwa kumkwida nakuifyetua shingo hali iliyopelekea mlinzi huyo
kupoteza fahamu na asijue kinachoendelea.Shunie kwa haraka ya ajabu alifanikiwa
kudhibiti vibaraka wengine waliokuwa kwenye gari.Hatua ya kuwashambulia ilikuwa
hatari sana kwani ilionesha ukaidi wa hali ya juu.Ni kwamba alikuwa anaruka
viunzi vya zee Kavuu na kuwa huru.Hatua hiyo bila shaka ingeleta hatari kwa
usalama wwa Shani ambaye alitegemea nidhamu yao la sivyo mambo yangekuwa ndivyo
sivyo.Kama Shunie kafikia hatua hiyo basi hatari ipo waziwazi kuwa msalia mtume
haupo tena na maisha ya mtoto Shani hayatakuwa na salama tena kwani tayari
makubaliano yameingia kombo na kuhatarisha kabisa usalama wake.
Shunie alitoka nje moja kwa moja nakuelekea kwenye ofisi za kituo kile
cha habari kwa lengo la kuzuia isije ikatokea mahojiano yale kupanda
hewani.Ghafla ile ya kuingia kwake ilikuwa kwenye hatari sana.Alipita kama
mtu wa kawaida anayeingia kwenye jengo hilo ila akiwa na ajenda zake za
isiri tayri kwa lolote ambalo lingejitokeza.Alienda hadi zilipo ofisi
husika huku akitafuta chumba cha kurushia matangazo maalum kwa aajili ya
kutekeleza Shambulio lile.Akiwa anakatiza kwenye korido alimuona mlinzi akiwa
katika sare zake nadhifu pamoja na mtutu wa bunduki akiwa ameubeba.Pale
akili ya Shunie ilifanya kazi kwa haraka kwamba amnyang’anye mlinzi
bunduki ile kisha yeye aitumie kufyatua risasi kuleta taharuki na watu
wote kwenye jengo lile wakimbie lakini pia njia hiyo bado ingeonesha
juhudi zake za kutuma ujumbe kwa zee Kavu kuwa ni mkono wa Shunie wenye
jeuri hiyo.Pia kungeweza kuleta vyombo vya ulinzi na usalama jambo
ambalo lingerahisisha kwa Dedani pamoja na yeye kupatikana kwa
urahisi.Lakini pia aliwaza njia nyingine ikiwa ni kufinya kengele ya moto
kuashiria kuna hatari ya moto ili watu wawe na taharuki na yeye kufanikiwa
kusitisha mahojiano kati ya Dedani na watangazaji wa kipindi kile.Lengo
kuzuia kuchafuliwa kwa rais Kilua kwa wakati ule.Njia zote zilikuwa kinzani
kwa namna moja au nyingine na zote zilikuwa na tija hasi na chanya kwamba
Dedani angefanikiwa kutoka mikononi mwa watu hao.Lakin hakusahau kwamba
atakuwa amemuweka mashakani mto to Shani.Ilitakiwa awe na uamuzi wa haraka
la sivyo mambo wangezidi kuyabananga.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ktika
purukushani alijikuta akimuwahi bwana mlinzi kiisha kumkwida kwa haraka
akamnyang’anya silaha yake.Matukio yote yalikuwa kama bahati nasibu ya
tatu mzuka au biko tangu afanikiwe kutoka garini hadi kuingia humu
ndani.Alifyetua risasi juu kwa kishindo.Timbwili la mlio lilirindima kwa fujo
nakuzizima zima.Akarudia tena kufyetua risasi kama nje.Tayari uhatari uliozua
taharuki ulisikika pembe zote za jingo lile.Watu walibaini ulikuwa mlio wa
risasi hata waliokuwa studio ambapo tayari walianza mazungumzo kwa njia ya
kumkaribisha bwana Dedani huku akielewa yupo mubashara na umma mkubwa
ulikuwa unamuangalia.
“Karibu sana bwana Dedani.’’alianza
mtangazaji.
‘’Nashukuru kwa ukaribisho.’’alijitahidi bwana Dedani
kuonesha tabsamu lake hafifu akijua sasa mambo yameiva kwa kiasi
kikubwa.
“Wewe ndo mume halisi wa…”kabla hajahitimisha sentensi
yake muhimu ulisikika mlio wa risasi Paa!Paa!Paa!Mliio huo ulimuogopesha hadi
Dedani mwenyewe akajikuta akitetemeka.Waliokuwa wameshika kamera ilibidi
waziachie chini nakipindi kuondolewa hewani kwa haraka sana.Palepale
mlango wa chumba kile ulifunguliwaa kwa ghafla na Shunie kuvamia.Akiwa
kashika mtutu wa bunduki.Wote waliomuona walijikuta wakitaharuki na
nywele kuwasisimka kwa fujo ya asubuhi ile.Katokea binti nadhifu mrembo
kama yai mwenye mtutu wa bunduki kaingia kwenye chumba cha kurushia
matangazo!
Shunie alimfuata Dedani nakumnyooshea bastola kasha
akamuamuru ainuke.
‘’Inuka mikono juu.’’alitamka akijiamini huku
usso wake ukibeba umakini wa hali ya juuu.Dedani alitii nakuinuka wote
wakatoka kwa pamoja katika chumba kile huku Shunie akiwa anaonekana amemweka
Dedani chini ya ulinzi waandishi kadhaa wa vyombo vya habari walikuwa
wakichukua picha ya tukio lile kwa simu zao wengine wakipiga picha na wengine
wakirekodi video kabisa maalum kwa kusambaza habari ile.Shunie akaonekana
akimshikia bastola mume wa rais Kilua katika jingo la kituo cha habari cha
pambazuko tv.Taswira ya Shunie ikaingia kwenye mtirirko mwingine wa
sintofahamu iweje iwe vile?Hata dakika hazikupita kabla hajafika nje ya
jengo lile tayari wengine walianza kusambaza rekodi ndogo za video kwenye
mitandao ya kijamii.Taarifa ikisema mume wa rais Kilua ashikiwa bastola akiwa
katika chumba cha mahojiano.
Mashushushu wa Kiota waliona taarifa
ile nakuanza kuwasiliana na wenzao waliokaribu na jingo lile na kweli kwa
waliopata taarifa ile hawakuchelewa ndani ya dakika zilezile walianza mara
moja kukagua jengo lile.Wamo mashushushu waliokuwa kama wafanyakazi nao pia
walianza kufuatilia kutaka kumjua aliyemshikia Dedani bastola.Shunie
alionekana kama adui ndani ya mfupi na kwamba hatua zozote zitakazopelekea
yeye kukamatwa asingeonekana kama vile shujaa bali adui wa
taifa.
Hatari ilikuwa imepelea hali kuwa tete na ndani ya muda
usio na kipimo vyombo vya usalama vikaanza kazi.Shunie alitoka hadi nje
na Dedani nakuelekea yalipo maegesho ya magari pamoja nakuwa katika
taharuki ile lakini bado aliweza kujidhibiti yeye kama yeye asiweke mashaka
yoyote yale kwa Dedani.Zile purukushani zilifanya baadhi ya watu kuwa
bize kukimbilia ponya yao.Shunie alishusha bastola chini ikawa haina ulazimu
tena wa yeye kumtishia bwana Dedani.Hakumtishia kwamba anamuweka chini ya
ulinzi bali alifanya vile kumuondoa pale kwenye chumba cha
mahojiano.
Nje hakujua aende wapi.Gari waliloletwa nalo aliona
likiwa palepale alipoliacha.Aliona wale vijana aliowadhibiti kabla
haajavamiwa wakiwa wameerejewa na fahamu huku wakishangazwa jinsi mambo
yalivyokuwa Shunie alitambua fika sasa upepo nao unabidili mwelekeo na
siajabu zee Kavu akichukua hatua kali kwa tukio la yeye kumkwapua
Dedani.Aliona mwanya ule autumie vyema ilikumtorosha Dedani.
“Shunie tunaenda wapi?’’aliuliza Dedani akitweta.
“Nakutorosha
hatuwezi kurudi kwa yule afriti!’’
“Hatma ya mwanangu itakuwaje
ikiiwa Kavu hataniona?Huoni kuwa umeniletea matatizo makubwa sana dhidi ya
jambo hili?Kurudi kwangu kwake ndo pona ya Shani wangu.’’
‘’Turudi
iliazidi kushinda?Niliapa kuirejesha familia ya rais Kilua na sasa
nimefanikiwa kumpata mmoja ya mateka wawili na wewe ndo mmoja wao.”alitamka
Shunie akizidi kujikaza.Dedani alimuwaza mwanaye kwa sana alimfikiria sana
lakini pia alimpenda mkewe hakupaswa kutoa shutuma zile mbele ya umma kulinda
heshma ya kiti cha urais alichopewa na mkewe.
“Sikiliza DEDANI
nimeshughulika na waovu kama hawa najua hawana mipaka hata ukirudi bado tu
mwanao ataendelea kuteswa.Huwezi msaidia mwanao ukiwa mateka.Hicho ni kitu
ambacho hakiwezekani.Najua bwana Kavu atataka akupate tena lakini wewe
usimpe nafasi yeyote yakuweza kukudhibiti.Akikutaka na atataka urejee kwake bila
shaka hapo tutaweza kukufanya chambo cha kumtia mbaroni.Lakini inabidi
tucheze karata zake kwa minajili yakujiokoa kwa jambo hili la sivyo
atatumaliza.Naomba niamini sifanyi haya kwa kuhatarisha maisha ya Shani bali
nafasi kwa sisi kuweza kupata nguvu tukiwa kwenye ngome zetu.Yeye ni mbabe
akiwa ametuweka kwenye himaya yake na sisi lazima tuwe wababe tukiwa kwenye
ngome zetu anachotaka kutumia ni udhaifu wa kumteka mwanao na sisi tutumie
udhaifu kama ubabe kwetu.’’CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dedani alibaki
kumshangaa huyu binti.
Shunie alienda hadi kwenye lile gari
nakumuweka moja ya vijana wale chini ya ulinzi kisha alimnyang’anya simu
nakumpigia mkuu wa idara ya usalama wa taifa bwana Toti.Namba maalum kwa
wafanyakazi wa idara hiyo alizitumia kumpigia bwana Toti nakumueleza
alipo.Ndani ya dakika kumi wakiwa wamejificha lilikuja gari la idara hiyo huku
llikifuatiwa na mengine kama manne yakiwa na wanausalama wao walijikoki kisilaha
wakafanikiwa kumchukua Shunie na Dedani pamoja nakuwaweka vijana wa mzee Kavu
chini ya ulinzi.
Gari nyeusi zilitifua vumbi zikiingia eneo lile
kwa kasi.Walishuka wanausalama na mara moja wakaweka mzingo wa usalama kwa
Dedani.Toti mwenyewe alikuwepo kwenye operesheni ile akimkumbatia Shunie kwa
ujasiri aliouonesha kumuokoa mume wa rais Kilua.Watu wawili muhimu walikuwa
matekani lakini sasa mmoja kafanikiwa kupatikana.Lilikuwa jambo lenye kutia moyo
na hata kuonesha imani kwamba mtoto Shani angepatikana tena.
“Shunie nakupa pole kwa uliyopitia.”alitamka bwana Toti akifarjika kwa kazi
aliyoitekeleza Shunie.
“Nahitaji kumuona rais kwanzaa.” alisema
Shunie akimtizama kwa makini bosi wake huyo.
“Hata yeye
anahitaji kukuona mara moja.”alisema bwana Toti wakiingia kwenye gari huku
Dedani akisisitiza hataki kuwa mbali na Shunie.Toti alipanda nao gari kuelekea
ikulu.Kwa haraka ya ajabu magari yalikuwa yakisugua lami.Safari ya
ikulu.Taarifa ya kumshutumu rais Kilua ilikuwa imefeli na sasa taarifa ni kwa
mume wa rais KiLUA Kuonekana kwenye ofisi za pambazuko tv kisha kutekwa na
mwanamke na baada ya hapo anaonekana akienda ikulu.Kila alitoa tafsiri
yake!
Kilua alikuwa akilipapasa tumbo lake
huku akijiangalia kwenye kioo.Tayari alikuwa ametuma watu wamlete Serambovu
ofisini kwake muda mfupi uliopita.Sasa alipokea taarifa tena kwamba mummewe
kapatikana na yupo njiani kuletwa ikulu.Alikuwa na kibarua kigumu sana kumkabili
mumewe.Japo alipata faraaja nusu kwani bado mwanaye hajapatikana.Ujio wa
Dedani ni jambo lenye kheri isiyo na shari,lakini upande wa pili alikuwa na
kibarua kigumu sana.Kilimshinda akili yake kiasi aliona chungu na joto ya
jiwe.Kulikuwa na wingi wa maswali.
Kioo hakikudanganya mama kwani
alizini na kuzinika akapata ujauzito ambao kwa hakika si wa mume wake bali
ni mtu mwingine kabisa.Kkujieleza halikuwa jambo dogo na pengine angezua
shutuma kubwa zaidi a zile za mwanzo.Kulikuwa na mgogoro wa kidiplomasia kati
yake na rais wa Savanna lands ambao ulionekana utakuwa na mlolongo mrefu
hadi utakapo kamilika na hadi sasa ameshaandaa timu ya wanadiplomasia
kuandaa makubaliano yakuingia baina ya mataifa hayo. Makubaliano kwa manufaa
ya taifa lolote.Hii ingeepusha mzozo kwa vizazi vijavyo.Ilikuwa njia bora
kulinda mengi ambayo yalionekana kuwa na faida hapo usoni.
Kwenye
lindi la mawazo mlango ulifunguliwa. Akaingia moja ya wasaidizi wake.Nywele
zzilicheza kwa kusimama akihisi kuna sintofahamu fulani zilizochimba kuta za
moyo wake huku akijifikiria yeye na mustakabali wake dhidi a jambo
linaenda kujiri.Dakika zile alikuwa amewasili asiemtegemea kama
angekuja.Pengine ujio wake ulionekana kama taswira ngumu kuipata lakini
yametimia mbele zake.
“Mheshimiwa mumeo amewasili ikulu.”kwa
heshma mlinzi yule alitamka kauli ile huku uso wake ukionesha utiifu wa
hali ya juu.Utii usio na shaka wala mashaka yoyote!
Kilua
aliitikia kwa kutikisa kichwa.Ila kabla ya kauli alishtushwa na
msaidizi wa pili kuingia akiwa pamoja na Serambovu huku akiwa chini
ya ulinzi mkali sana.
***
Zee Kavu
alikkuwa ameshika tama usso kuwa umesawijika kwa namna binti Shunie
alivyomchezea karata dume na kumharibia mipango yake kuipanga upya siyo
mzahaa wala kitu cha kuchekelea.Alitakiwa awe imara na kuja na mbinu mpya
kumdhibiti rais Kilua.Kuwepo kwa Dedani mikononi mwake ni hatari kubwa
sana kwa zee Kavu.Japo mtoto wa Kilua yupo kwake lakini siyo dhamana ambao
ingedumu kwa namna moja au nyingine.Kilua atapata ujasiri zaidi hasa akiwa
mumewe yupo pamoja nae.vile baba karudi na nguvu pia ya kumtafuta Kavu
itaongezeka hasa kwakuwa Dedani alikuwa katika ngome ile alijua chungu
zote wala humdanganyi kitu na hilo litaweka kisasi.Pengine Dedani atakuwa
wa kwanza kutumia vyombo vya usalama kumuwinda zee Kavu.Ataipindua ardhi
ya Kiota juu chini ili huyu afriti kibiriti awe chambo.
“Hatua
ya Shunie inatuweka mashakani sisi sote.Huu ni uzembe wa hali ya juu
kuwahi kutokea.”alianza mr Tufe lawama haziepukiki.Kila njia inapofeli
basi yupo wa kuvishwa lawama hizo. Uwanja mzuri wa kumimina kuchuja na
kupembua.
Zee Kavu alimeza shutuma hizo.Alijinasua kwa
kujitetea.
“Jamani mimi sikujua kama binti angefikia hatua
hiyo.”
“Wazo lakutengeza mahojiano kwa lengo la kumchafua
Kilua ni feki tena upumbavu wa hali ya juu sana.”mr.Tufe alizidi kupigilia
msumari wa moto hilo tosha ni mwiba kwake.
“Tumeona hilo japo
lilikuwa wazo zuri lakini lilipangwa kizembe.Kavu huku waandaa mateka wako
vilivyo.Ulitakiwa uongeze bidii kwenye mpango.”
“Yule msichana ni
mjanja ni mjanja tena sana.”
“Na sasa yupo nje.”
“Uhuru wake ni hatari kwetu.”
“Tena kubwa sana.Si ajabu wanajipanga
na sasa Kilua atakuwa hatari zaidi siri zetu zinagundulika kwa uzembe
huu.”
Ni wazi timu nzima iliona mambo sio rahisi
tena.
“Tena the big boys Tumepakwa Tope kwa jeuri yake.”mwingine
aliongeza.
Chumba kilitokota kwa kutota lawama ambazo zilionesha
ni kweli the big boys wamekubali kudharauliwa na bibie Shunie jeuri.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kulaumiana haita
mrudisha bwana Dedani mikononi mwetu wala kuondoa mistake iliyotokea bali
ni kujilisha sumu ya majuto.Ni kheri tujipange kwanza inatakiwa
tumshurutishe rais Kilua afanye tunachotaka sisi la sivyo tutamzimisha mwanae
tena kwa mateso makubwaa sana.’’ Alishauri bwana Tufe.
Hoja hio
ilipokelewa kwa hisia mseto.Kuna walioiona kama ni njia bora kuzidisha
urefu wa makucha yao na wengine waliona kama kujipeleka kijinga itaonekana
fika kwamba wanashindana nae.Mashindano ambayo hayaeleweki kabisa kwamba
dhamira kuu ni nini?
“Kufanya hivo sioni mantiki husika hasa ni
nini?Tayari tunamdhibiti vya kutosha…”
“Kilua hatuja mdhibiti
nyota yake ina ng’ara sana.”
“Kumuacha aipate familia yake ni
sisii kujilisha upepo.”Kavu alisisitiza.
“Bila uzembe wako
haya yasingejiri.”
Akameza dabali moja ya shutuma tena.Kavu hasira
zilijipanga kwenye lindi lake la lawama huku akijiapiza kulipiza kisasi cha
uhakika kwa uchafu wa dharau Shunie aliomuonesha ubabe wa
kimataifa
Akakumbuka zile picha za video alizozirekodi wakati
binti huyo akiwa faragha na Dedani.Hizo ni salaha bora kwake
kuzitumia.
“Niachieni Shunie nitamdhibiti mwenyewe.”
Wote wakabaki wakimshangaa.Lakini jibu alikuwa nalo mwenyewe.
“Ok
tunakupa nafasi yamwisho dhibiti huyo malaya.”alisema bwana Tufe ambaye
alishajua Shunie wanaemzungumzia hapa ni msichana ambae ni mchepuko wake
wa muda mrefu na kama akikiri hilo bila shaka itaonekanaa amekuwa akiuza
siri zao kwa kutembea na mtendaji wwa usalama wa taifa.Ina maana Shunie
amekuwa akimfanyia ushushushu wa muda mrefu sana na siajabu kuna siri
nyingi sana zinajulikana dhidi yake.
Inamaana hata meli yao
ilipovamiwa na wale maafisa usalama hadi Shunie kukutwa ni kupitia yeye
ndo siri ikajulikana haata maongezi mengi ya simu amekuwa akiyafanya mbele
za mlimbwende huyo.Ni wazi sasa wamekuwa wakifuatiliwa na serikali bila
wao kujua.Bwana Tufe alitamani kuwaambia wenzake hofu yake lakini akaona
akifanza hivyo nikujionesha jinsi alivyo mzembe kiasi cha kuuza siri kwa
nduli wake.Pengine big boys watamchukulia hatua kali za kinidhamu.Tayari
Kavu kesha ondolewa jicho moja na Shunie sio mchezo tena kwamba Shunie
aanaacha makovu.Kaacha kovu kwa zee Kavu kwa kumtia chongo la maisha pia mr
Tufe kawekwa kovu kubwa la kufanyiwa ushushushu wa muda mrefu.Makovu hayaa
ni hasara tupu.
“Nitamshughulikia vilivyo.”alihakikisha zee
Kavu.
“Namtaka balozi wa Savanna Lands anyamazishwe yeye pamoja
na Serambovu wametupaka tope kwa shambulio la kizembe sana.Serikali
iemedhibiti na tayari balozi yupo mikononi mwa serikali.Serambovu naskia
kawekwa kizuiizini ni kwamba Kilua ameshtukia mipango yetu.”
“Lengo
la shambulio wanadai ni kutikisa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Savanna lands
na Kiota.Kweli wamefanikiwa kwa namna moja au nyingine na hii ni mbinu ya
kumshtua rais wa Savana lands alionekana aking’ang’ana kudhibiti ishu
13:14.Alitaka kuingilia na ndo maana Serambovu na balozi wa Savanna lands
waliamua kutekeleza jambo hilo kupitia balozi wa Savanna lands japo Serambovu
hakuwa na uhakika wa dhamira lakini wakubwa walichonga huo mpango.Tena naskia
hali imekuwa mbaya sana kwa rais wa wa Savanna lands.”
“Kwani
hakujua shambulio hili?”aliuliza mr Zungu.
“Iwe alijua au hakujua
alikuwa sehemu ya big boys lazima akutwe na kadhia hii.Iwe fundisho kwa wote
ukileta kidomo utamalizwaa naskia hata alizuiwa kuondoka Kiota na sasa mataifa
yanampeleleza.Wakati aangaika kujisafisha sisi tutakuwa hatua nyingine kabisa
kimipango.”
Ilidhihirika kuwa shambulio la kwenye msiba lilikuwa la
kupangwa na wakubwa wanaojiita Big boys.Wazee wezito wampango wa faili nambari
13:14.Sasa hali ilikuwa tete kwao kumbe unaeza ukageuka kwa tukio kuundwa illi
na wewe uchafuliwe pamoja.Rais wa Savanna lands walimtengenezea zengwe la
shambulio akiwa katika ardhi ya Kitoa kwa kumhusisha balozi wake huku silaha
zilizotumika zilionekana kutokea taifa lake kuja Kiota.Sasa alikuwa katika
hatia kubwa zaidi ya vile alivyodhani.Kuhusishwa kwake na shambulio ni
muunganiko wa doti za lawama na kweli wamefaniikiwa pakubwa kwa hilo kiasi
cha mzimisha kabisa.Big boys wamemtuliza bwana huyu.Mr Tufe aling’ata meno
kwa dhihaka ile.
“Ukijidai unajua unazimishwa.”
Wote
waliwaza sana dhidi ya tukio lile.Uchonganishi mkubwa sana ulikuwa
unafanyika baina kundi la Big boys na vibaraka wao.Kundi hili lilifanikiwa
hata kuleta mgogoro wa kidiplomsia kati ya taifa la Kiota na Savana
lands.Kundi hili ndo chachu ya yote.
** *
Katika chumba cha hospitali alimolazwa
balozi wa Savanna lands anaonekana nesi akiingia chumba hicho.Mashine za
kupumulia zikiwa zimefungwa vizuri puani mwake.Nesi alifika akiwa ni chano cha
madawa safi na nadhifu.Aliviweka kando huku akichukua sindano nakuvuta dawa
fulani kwenye kchupa kisha akaiminya kidogo dawa iliruka kidogo.Akamshika
mgonjwa mkono akautafuta mfupa halafu kwa umakini akamdunga sindano.Ndani ya
dakika kumi mgonjwa alianza kutapatapa huku ngozi ikibadilika nakutoka vitu
kama majibu huku vikitumbuka halafu akatikiisika kisha alijipigiza kwenye
godoro lake kichefuchefu na tumbo kusokota vilipelekea balozi kuapika damu
ambayo ilifurika kwenye kifaa cha kupumulia kikaajaa top!
Mashine
ya kukagua mapigo ya moyo ilitoa mlio wa ulalamishi na ghafla ikazimwa na
yule muuguzi.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Balozi alikwisha
kaata roho!Hangaiko la kutetea uhai wake lilikwisha nguvu na sasa aliona na
kuhisi wepesi ulioambatana na usingizi mzito sana vikimjia kwa pupa na
hatimae uhai wake ulififia na roho iliponyoka kifua chake pamoja na nafsi
vikaenda katika ulimwengu wa roho.Balozi hakuwa hai tena alikuwa amefariki
dunia!
***
Kilua alimsogelea mumewe aliyekuwa akimngoja katika moja ya
vyumba binafsi mule ikulu.Alimuacha Serambovu upande mwingine huku akiwa
ametoa amri afunguliwe pingu.
Kilua alikuwa na shauku kubwa
kuonana nae baada ya muda mrefu sana kuwa nae mbali na sasa alikuwa
amerudi hakujielewa kama alimpenda au ni ule ukaribu kwa sababu ni mume
hayo yalikuwa mawazo gongana na majibu kinaya.Pengine hakujua lolote.Kwa
dakika kama tano alijikuta akimtizama mumewe bila kusema kitu huku biwi la
machozi llikicheza ngoma kwenye mafiga ya machozi.Machozi yalimtoka akajikuta
akimkimbilia mumewe nakumrukia akamkumbatia kwa nguvu mwilini mwake.Dedani
aliipata tena harufu ya manukato ya mkewe.
Alinukia kama malaika
kwa utuli wa kupendeza pua.Utuli wa mwanamke wake!Mke aliyemkumbatia sasa
alikuwa mbele yake.Ohh ni jinsi gani Dedani alimpenda Kilua kuliko vile
alivyodhani.Alimpenda sana!Anamkubali moyoni mwake.Mama wa watoto wake.Mke wa
ujana wake na nguvu zake.
Kwa dakika kama tano alikuwa amemkumbatia
mkewe asimuachie na alitaka hivyo.
“Dedani wangu nifuate.”alisema
Kilua akimshika mkono mumewe.Wakaenda pamoja hadi chumbani mwake walinzi
waliombwa faragha na rais Kilua aliyekuwa na mumewe.
“Dedani
unaendeleaje?”aliuliza Kilua akimshika mumewe usoni akimkagua aliona makovu
kadhaa aliyopigwa alijua babie wana alikuwa katika maumivu makali sana kiasi
hakuwa kawaida.Kilua alirudia tena kumkumbatia mumewe kama mkewe.Hungedhani
alikuwa akichepuka na Serambovu bila breki.
“Binti yetu.Shani wetu
anateseka Yule mwendawazimu anamharibu mtoto.’’alitoa habari bwana Dedani
japo hakutaka lakini Kilua ni mamake Shani anapaswa kujua madhila ya mwana
wake.Kitendo cha mwana wao kubakwa kilimuumiza sana Dedani nikumbukumbu mba6a
sana kuwahi kutokea.Ni kweli binti yao katumbukizwa kwenye giza nene la
unajisi.
Kilua alijikuta machozi yakimtoka sasa alijua fika ajali
ya kifo iliyoondoa serikali ya Kisusi ilikuwa ni mpango na walijua yeye ndo
raisi ajae hivyo mwanae kutekwa ulikuwa ni mpango wwa kuja kumtumia kama
chambo.
“Tell me what happened?”aliuliza Kilua akiwa na shauku
kuu.
“Nilipokufumania na Serambovu,ilikuwa siku mbaaya sana maishani
mwangu na wala sikutegemekama ingekuwa vile kwa kweli.Nilikuwa na msongo wa
mawazo na akili kufa kabisa.Ajabu nikaenda bustani ya mjini hapo ndo
nilitekwa hawa watu wanajua mengi kukuhusu na hata mimi.Walianza kwa kunitumia
meseji za ajabuajabu hapo walikuwa wananivutia niingie kwenye gari
lao.”alieleza tukio zima llilivojiri hadi walipompeleka na sasa walikuwa
wawili yeye na mkewe wawili tu kama ilivyo paswa kuwa tangu enzi ya ndoa
yao.
Kilua kila akisikia usaliti wake na Dedani alihisi kama upanga
unapita kwenye nafsi yake ukimsuta.Ni saw mume kuwa na hasira nae kwa jinsi
alivyomtenda hata aliona hadhi ya kiti chake imeshuka mbele ya
mumewe.
Dedani alitamani sana kumvutia mkewe dhidi ya shutuma
za fumanizi lakini alijua huuyu ni mama kumletea shutuma zile na hivi
ni rais ni kuzidi kumsumbua kichwa lakini vipi kuhusu yeye.Rais lazima ajue
mipaka yake na sikuonea watu kijinga.Kabla yakuwa rais Kilua alikuwa mwanamke
wake na hakupaswa kabisa kuingiza cheo kwenye mambo yao
binafsi.
Lakini kifua kikawa kizito kwa dedani
kubeba mambo hayo.
“Pole sana mume wangu.”alisema Kilua
akijihisi hatia kwamba kazi yake imeleta kombora katika ndoa yao na sasa
imesambaratisha kiota cha mapenzi yao.Ni kama hakumjua mumewe tena na penzi
lao lilififia shauku penzi ni kama haikuwepo kuja kwake Dedani kahisi kitu
kipya.Pengine hatia ndo inamla.Kilua alihitaji mtuu wa kuzungumza nae na
kumueleza anachojiskia.
Lakini alihisi mtu huyo si Dedani.Aliona
haya kumueleza au kuzungumzia hatma ya ndoa yao.
“Namuwaza
Shani wetu najihisi vibaya sana kuwa mbali nae sijui zee Kavu atamenda
nini?”alisema Dedani akiwa na wasiwasi mwingi sana.Wote wawili walikuwa na
dukuduku moyoni kila mmoja alitaka kumwambia mwenzake anachojiskia lakini
walikuwa na kigugumizi
“Kama mama kuna wakati naumia sana sijui
kama amekula sijui wamemtenda nini ulichoniambia kwangu ni mateso makubwa
nahisi utendaji kazi wangu utaathirika kwa namna moja au
ninyingine.Lakini najitahidi kuna vita kubwa napigwa na hawa
wanaharamu.Wanataka kuniangamiza na kuiangamiza nchi.Tayari nina mgogoro na
rais wa Savanna Lands.Ohh!mme wangu nipo katika wakati mgumu sana hadi
nahisi kuchanganyikiwa.”alisema Kilua akimsogelea Dedani ambae alijilaza
kifuani mwake.Alijua kwa Dedani kuna upendo hasa wa faraja.Siku zote mwanaume
huyyu alikuwa mkarimu kwake.Haijalishi ni mara ngapi mwanaume huyu
kamsaliti lakini bado Dedani alimpenda mkewe.Alikuwa miongoni mwa watu
waliojua kutia moyo.Tumezoea kumuona Kilua kama mwanamke msaliti wa ndoa
yake lakini hatujamuona na mumewe wapoje upande wa pili.Walikuwa ndege
njiwa wawili sare kama tu mwanamke huyu angeibeba kauli ya kuwa muaminifu
kwa mumewe ila mambo aliyabananga muda mrefu.
“Shani anapitia
mambo magumu natumai Mungu atamlinda kwa hili.Our daughter may never be the
same again.:”sauti Ililowa kukata tamaa nakuhisi mambo magumu.Kupitia kipindi
kile kilikuwa kigumu sana kwenye ndoa yao kiasi walihisi ugumu huo ni
kama pigo fulani.Sahani ya urais ilikuja ni mtihani mgumu sana walikosa
amani kwa namna fulani kuhusu mwana wa uzao wao.Kuna wakati ajihisi uanaume
wake unapitia mgogoro kama kweli yeye ni mwanaume aliye mfaa Kilua au
alikuwa hamtoshelezi vilivyo.Lakini bado Dedani alkuwa kichwa cha
familia.Alikumbuka jinsi alivyoelezwa kwamba hata baada ya kutekwa bado
mkewe alikutwa na mahusiano na hasimu wake namba moja yote ilionesha
kidudu mtu katika ndoa yao alikuwa ni Serambovu mwenyewe.Nii kweli
Kilua alikuwa na heshma kwake au ni maigizo tu.Kikawaida kama
alimfumania basi alitegemea Kilua angeachana na Serambovu lakini tofauti
ni kuwa sasa Serambovu yupo karibu sana na Kilua na tena ni chifu wa
stafu nzima wa ikulu.Ni mtu muhimu sana kiserikali ni nafasi iliyomoja kwa
moja na ushauri mkuu wa rais.Kumuondoa halikuwa jambo la mzaha!
“Dedani wangu promise me one thing?”alisema Kilua akihema alimuhitaji mume
wake kwa sana .Alihitaji familia yake kuliko kitu chochote
kile.
“Unahitaji nini?”
“Ukweli wako.”alisema Kiluwa
kwa sauti yenye hamasa na ushawishi wa kike kabisa.Dedani kwa wakati ule
alitamani mzibue makofi lakini alimeza ghadhabu moyoni mwake.Hivi huyu
anataka ukweli gani kutoka kwake.
“Ukweli upi?”aliuliza Dedani
kama vile hajui.Lakini alijua bila shaka mwanamke huyu anamgeuzia gia
angani.Anabadili lengo na halisi ya taizo katika ndoa yao.Tatizo la
ndoa yao ni usaliti ambao Kilua mwenyewe aliubariki.
“Unanipenda?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lilikuwa swali
jepesi ila mazingira na hali halisi likawa gumu kama mwamba kulipatia
jibu muaafaka.
DEdani alikuwa mzito huku kichwa kikiwa na
maumivu makali sana ni vile aliheshimu madaraka ya mkewe pamoja na
kiti chake.Anajua fika Serambovu amekuwa akila hii kitu na sasa amepoteza
sifa za kumthamini mwanamke huyu tena.
“Nimekuuuliza swali
nahitaji majibu.”
“Wewe mwenyewe unajua majibu ambayo
ningekupa.Sioni umuhimu wa kukupa jibu unalolijua.”
“Then make
love to me right now?”alijiamini kwa kauli ile.Kukiwa na msongo na mkazo wa
mawazo Dedani angetamani kuwa kifuani kwa mmkewe wakijiliwaza pengine
mkazo ungepungua na vile salama ya binti yao ipo sehemu mbaya.Dedani
alihisi mwili wote kumsisimka ni muda tangu mkewe aoneshe kuwa na hamu
nay eye kiasi cha kujielezea hisia zake mbele.Ilikuwa Dedani ndo
mbembelezaji wa penzi la Kilua.Alihis anafakamia makombo yalioachwa na
Serambovu.
“Mbona hunijibu.Make love to me now make me your woman
just for this moment.Pengine itapunguza msongo wa mawazo hasa kwa sasa
mwanetu katekwa.”ilikuwa sauti mkewe ambayo hakuitegemea kabisa kama ipo
siku angetoa kauli kama ile kwa nyakati na hali kama zile.DEdani aliona
mkewe amechanganyikiwa alijiuliza kama kweli Kilua anakumbuka mara ya
mwisho alimkuta mazingira gani.
Bado hawakutatua mzozo wao
halafu leo huyu mwanamke anategemea amwingilie kirahisirahisi.Dedani
allipinga jambo ilo.
“Am sorry but najihisi mchovu sana
sidhani kama nitaweza kushiriki.i have been through a lot.”alisema
Dedani.Kauli yake ilimuumiza sana rais |Kilua japo ni mumewe na haki nae
lakini hakutegemea kama angetamka vile.
“Kuna jambo baba
naomba unieleze lakini usininyime haki yangu.”alisema Kilua kwa kudeka
huku akijaribu kuiranda roho ya mumewe kwa mabusu ya shingo akilisaka
penzi lake.
Dedani alimuwaza Shunie aliyemjia kichwani kwa
ghafla palepale hakuhisi kufanya chochote na mkewe.aliona kufanya vile ni
kuisaliti nafsi yake iliyoanza kupotea.Alikumbuka walivyofanya mapenzi
mazito hisia zilikuwa kasi sana alipomfikiria hamu ilimshuka mauongoni na
akatamani kumuona kwa wakati ule.Akili ya mtu ikifunuliwa unawezaa ona
mambo ya ajabu ni vile zimehifadhiwa kwenye taswira ya ndani.
Dedani alijikuta akimgeukia mkeewe na kwa kasi ya ajabu alimwinua nakuanza
kumbusu kwa nguvu kitu ambacho Kilua aliunga mkono huku machozi yakimtoka
asijue ni ya furha au huzuni au alijutia nafsi yake kwa lengo lake la
kumshikisha DEdani mimba ya mtu mwingine.KWa mara ya kwanza mtu na mkewe
walikuwa katika fujo ya kukutana kimwili baada ya muda mrefu wa usaliti na
upweke wa kukosaana kwa kutekwa.Dedani alifanya vile kuondoa mawazo ya
kiumbe aitwae Shunie huku Kilua akiona ni nafasi nzuri kumshikisha mtu
mimba.Ghafla mlango ukafunguliwa akaingia SErambovu bila
hodi!
Kiota cha mapenzi kati ya Dedani na mkewe
kilichukuliwa kwa muda kidogo na utamu pamoja na hisia kochokocho zenye fukuto
la mahaba kwa muda kidogo hakuna aliyeona sababu maalum ya kumbania
mwenzake.Ilikuwa hisia kali sana kwa Dedani na kwa mara moja Dedani alitambua
fika kulikuwa na penzi zito kati yake na Kilua lakini kwa sasa mgawanyo na picha
iliyojijenga kichwani mwake kati yake na Shunie ilikuwa kubwa sana nakuonesha
mfadhaiko wa saikolojia baina ya kufanya maamuzi nakutoa jambo lenye faida na
hasara kwa mkupukuo.Hii picha mpya ya Shunie kwenye ramani hii ilionesha wazi
kushuku msimamo wake kwa mkewe kama kweli alimpenda na nia yenye udhati wa asili
ilikuwa na uwezo wa kukabiliana naye kwamba saikolojia imeingia mdudu
mpya.Alipambana na mdudu huyuu mpya na hata kumpuuzia akiamini fika katika kuta
za nafsi zake kulikuwa na mwanamke mmoja tu ambaye ni Kilua.
Busu la
kati ya mke na mume lilikuwa katika uzito wa mahaba na wao walikuwa kidogo
mbali.Mlio wa mlango kufunguka pengine hawakuusikia au waliusikia na kuupuzia
maana ilikuwa ni wakati wao na Kilua hakutaka mtu kuingia pale alitaka faragha
hiyo na mumewe bila kidudu mtu kuingilia eneo lile huyu punguani anayeingia ana
ajenda gani?Alikasirika sana.Kilua pamoja na Dedani walikuta mtu
kawasimamia.
Wawili katika kumbatio la upendo wao waligeuza shingo
zao nakumtizama mfunguaji wa mlango ambaye alisimama huku akitumbua macho
asiamini alichoona ni kitu gani?Kilua alishtuka kumkuta ni Serambovu!Moyo
ukampiga mkambi na yeye kutweta kwa wasiwasi uliomkubwa sana!Ni kama dunia
ilisimama kwa sekunde kadhaa huku maasimu na wapenzi walikuwa mbele ya uwepo
wao.Mara ya mwisho Dedani anakumbuka bwana huyu alimfumania ofisini kwa mkewe
wakiwa katika mazingira hatarishi sana.Alikuwakuta mubashara wakizini na
mkewe.Na tangu wakati huo hadi leo Dedani hakuwa na nafasi ya kumhoji mkewe na
pengine kumshutumu kwa jambo lolote au hata kuwa na wasaa wakujua ilikuwaje
Kilua na Dedani!Ujio wa Dedani ulichipua hasira kali sana kwa Dedani na kwa mara
moja alijtamani kumshambulia huyu bwana kwa nguvu zote aweze kumdhibiti
kabisa!Hasira!
Dedani aliona kama Serambovu anamtukana kwa
kujitokeza mbele zao.Anajua fika mkewe alitoa angalizo kwa kuhitaji faragha na
mumewe.Hata walinzi wa mkewe walihakikisha hilo sasa iweje huyu fala anakuja
hadi hapa?Dedani alihisi kichefuchefu kikimpanda nakujiapiza kichwani mwake
kwamba angemshughulikia huyu mwendawazimu kwa kuthubutu kumlia mkewe.Na
angemshughulikia vilivyo alihitaji nafasi tu!
Kilua alitumia mwanya
huyo kumuonesha Serambovu kwamba mumewe yupo kwenye ngome yake na yeye
alihitaji faragha ya kutosha kwa mumewe bila kidudu mtu kuleta
propaganda.Lakini pia hatia ilimla maana chumba hikihiki Kilua amekuwa akikitia
najisi hasa alikitumia mara kadhaa kuchepuka na bwana Serambovu leo tena yupo na
mumewe.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unafanya nini
hapa?"alihoji Dedani kwa hasira akimtizama Serambovu.Ni wazi chuki kati yao
ilikuwa dhahiri shairi bila kuificha.
"Samahani bwana Dedani sijajua
upo hapa.Nilitaka tu kuongea na mheshimiwa."alijitetea Serambovu maana mbali na
uadui wa kuibiana mke wawili hawa wana historia fulani huko nyuma ya
kaurafiki.Dedani aliwahi kuwa msaada mkubwa sana kwa Serambovu nyakati
fulani.Na hicho ndicho kitu kilimfanya Serambovu akikutana na Dedani uso kwa
uso alikuwa hajielewi japo alidhamiria fika kumuangamiza kabisa na kumfuta
kwenye ramani ya uso wa dunia.
"Hukujua huoni kwamba nipo sehemu
maalum na mke wangu?"alihoji Dedani kibabe.Serambovu alinywea kwa tishio
lile.Ni hatari sana Dedani kuwa karibu na Kilua.Hilo lilionesha ulinzi wa hali
ya juu kwa familia ya Kilua.Ni sio siri Serambovu anamjua fika Dedani si
mkurupukaji huonekana kama mtaratibu na asiyekurupuka lakini ni mtambo unaojua
namna ya kupangilia na kama kweli Dedani amejua kutekwa kwake kuna mkono wa
Serambovu bila shaka sasa hivi Serambovu angekuwa ameshamfutilia mbali au kuna
mbinu kali sana ambayo Dedani atakuwa anataka kuitumia kumdhibiti.Alimuibia mke
na sasa kamtia mimba mkewe nani anajua atafanya nini jingine?Nani anajua kisasi
cha Dedani kwa Serambovu?
Serambovu hakutaka kabisa Kilua na Dedani
wawe katika halli ileilionesha kuna uwezekano Kilua anairudisha ndoa yake.Lazima
Kilua airudishe ilikutuliza maswali yaliyozuka kwamba rais hana mume na familia
yake haijulikani ilipo?Anakumbuka sharti kubwa lilikuwa kuhakikisha siri ya
kutekwa familia yake isivuje katika jamii na hocho Kilua alifanikiwa kukidhibiti
akitumia wanausalama wachache kufanya operesheni ya kuirudisha familia yake
lakini sadfa Shunie aliweza kumkomboa mumewe jambo ambalo lilionekana laajabu na
halikutegemewa kabisa.
Dedani akamuachia mkewe nakumfuata
Serambovu,"Unajua sijui ni kwanini upo hapa?Nasijui ni kwanini unaendelea
kuifuata familia yangu?"
Serambovu alijikuta akishikwa na
kigugumizi!Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo!
Kabla hajatafuta neno
la kusema ilikuwa ghafla sana Dedani alimkunja shati Serambovu nakumvuta karibu
na uso na kwa kasi ya ajabu Dedani alimpiga kichwa kitakatifu kama kondoo
anavyomshambulia mwenzake!Pigo lilitua kwenye pua ya Serambovu nakumtikisa mfupa
ulio puani kisawasawa!Hali iliyopelekea damu kumvuja puani kwa haraka.Dedani
hakumuachia aliendelea kumkunja shati nakumshindilia tena vichwa
kadhaa.Akamuachia mkono mmoja na kumshushia pigo lingine takatifu la ngumi
kwenye mdomo!Kuu!Alimfumua kwa kishindo tena na tena na ngumi kadhaa za
harakaharaka zilikuwa zimeshauharibu uso wa Serambovu pamoja na kuutotesha
michirizi ya damu!Dedani alihakikisha anampiga kwa haraka kabla walinzi
hawajaingilia kati jambo hilo.
KIlua aliogopa sana.Alijua Dedani
alikuwa bado na hasira na alitegemea hilo.Alipanga nyuma kwamba angehakikisha
wawili hao hawakutani lakini alifanya kosa kubwa sana kuwaruhusu walinzi
wamuachie Serambovu aranderande ikulu bila kumdhibiti na hilo alilimeza na
matokeo yake.Ni nini anafanya sasa!
Ilibidi aingilie kati kwa haraka
ajaribu kuwaachanisha.
"Stop it you two!"alisema Kilua akimshika
mumewe bega nakumvuta pembeni huku akipitisha mikono kiunoni mwa mumewe na
kutokeza tumboni akamshika vizuri nakuulaza uso wake mgongoni mwake.
"Mme wangu nakuomba upunguze hasira!"alimhini mumewe.
Serambovu
aliyumbayumba nakuanguka chini huku akiugulia maumivu.Mke wa mtu ni sumu maziwa
ya Serambovu yalimtokea puani!HII ilikuwa ishara mbaya sana kufanyika ikulu na
habari hii ilitakiwa isifike hata mlangoni.
"Huyu mbwa atokee hapa
nitamuharibu!Nitakuua!"Dedani aliwaka!kilua hakujua kama mumewe alikuwa mbogo
kwa namna hii.Alikuwa amekasirika sana bwana Dedani na pengine angefanya jambo
baya kama hata dhibitiwa maapema kabisa.
"Dedani please control
yourself!"alisema Kilua huku akijihisi hatia sana moyoni mwake.Dedani hakuonesha
ishara ya maelewano kati yake na huyu afriti.
"Sielewi!Kafuata
nini?"
"Unaona anavyonishambulia?Dedani nitakushtaki kwa
kunishambulia nikiwa ikulu!"aliropoka Serambovu!
"Unaona bado
unaoubinafsi hadi leo hujajifunza!"alisema Dedani akiwa na hasira
sana!
"Hebu tulieni mtakabiliana hivi hadi lini?"Kilua alijaribu
kutuliza kidogo.
"Hadi mmoja wetu akubali kukaa mbali na
wewe!"aliropoka Dedani hasira ikimzidia nakujikuta akishindwa
kujidhibiti
Kilua aliona wakati mgumu kuwadhibiti.Manukato ya ikulu
yalikuwa mazuri sana.Hadhi ya jumba lile liliwafanya wote wajihisi ni kama
hawakupaswa kuwa pale na ni kosa kubwa sana kufanya ugomvi ule pale.Lakini
hasira zilimzidi bwana Dedani.
"Dedani unanionea bure."alijitetea
Serambovu.
"Nyie wawili mmekuwa mkinila mgongo nyuma yangu!"alisema
Dedani akizidi kughadhabika sana.
"Dedani tafadhali hebu come down
kwanza."alijaribu KIlua.
"You brought your lover here then utegemee
nimchekee?"aling'aka Dedani akipumua kwa hasira zisizo shuka.Kijacho chembamba
kilipita usoni kuonesha mwili unachemka kwa hasira na sasa zimetota!
"Dedani chunga kauli zako!Mimi na Kilua tuna historia hata kabla wewe hujaja
kwenye maisha yake sisi tulikuwa na dunia yetu!"alisema Serambovu akiamua
kulipua bomu!Mambo yalikuwa yameiva sasa na Serambovu alipeleka mtanange kule
alipotakiwa kuukwepesha.
"Unasemaje wewe hayawani?"alihoji Dedani
akikosa stahamala ya uvumilivu nakuona kama nafsi yake inasalitika kwa mashtaka
ya hawa wawili.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndiyo kwani
uongo!Mimi na Kilua tunapendana wewe ndo tatizo!"
Kilua alilaani
hatua hiyo ya Serambovu ilikuwa yenye makali sana!
"Serambovu
unavuka mipaka!"aling'aka binti Kilua mwana wa nyumba kubwa! Aliona ndoa yake
inaeelekea kubaya sana shutuma za Serambovu na kama hawatamdhibiti siajabu
akawaumbua.
"Mipaka gani wakati ndo ukweli?"ilikuwa kauli nzito
sana
"Serambovu behave yourself!"alifoka Kilua akimwangalia kwa
macho yaliyoomba ustaarabu!
"Ohh what?Utaniweka kizuizini
tena?"alihoji Serambovu kwa kiburi.Akili yake ilibadilika kwa ghafla na kile
kitendo cha Dedani kumpiga kilikuwa kichocheo na njia pekee ni kumshutumu Kilua
hadharani mbele ya mumewe!
Kilua akaona huyu atampanda kichwani na
amani aliyoweza kuijenga kwa muda mfupi ilikuwa inapukutia sasa!Serambovu
anazidi kumtia matatizoni.Ni wazi SeraMBOVU anaenda kumharibia sana mwana mama
huyu kuliko siku zote zile na bila kudhibitiwa atalipua bomu.
Kilua
akamuachia Dedani aliwatizama wote wawili macho yalionesha hatia sana kwa
kitendo alichokifanya.
"Kilua!"aliita Dedani!Lakini mabishano yale
yaliwafanya walinzi wasikie nakuingia kwa kasi ya ajabu pale ndani.
Kilua akawapa ishara inatakiwa Dedani na Serambovu wawekwe vyumba tofauti muda
uleule.Jambo lile likafanyika kwa haraka.Kilua akamfuata Dedani.Alimkabili japo
wasiwasi ulikuwa mkubwa sana!
"Dedani wewe ni wangu peke yangu sipo
tayari kukupoteza kwa lolote.Nitafanya lolote uwe ubavuni mwangu.You are my
husband."alisema Kilua akimwambia Dedani aliyekuwa amewekwa chumba kingine akiwa
amesimama karibu na dirisha huku mwanga wa jua ukipenya nammulika.Pazia
lilichezacheza kwa ujio wa upepo mwanana uliopambwa na manddhari ya ikulu.Dedani
alikuwa amechukizwa sana na kitendo cha Serambovu kuwa karibu na mkewe kiasi
kile.Anakumbuka habari alizopewa na zee Kavu.
Kilua alimsogelea
Dedani nakumbusu shavuni kwa lazima.
Dedani alimgeukia mkewe,"Kama
unataka kuiokoa ndoa hii basi mfutilie mbali Serambovu.Ikiwezekana
auawe!"alisema Dedani akimaanisha!Hilo la kuuawa lilimtisha sana Kilua.Amuue
mwanaume aliyempenda sana wakati fulani?Amuue baba wa...hapana?Ataanzaje kwanza
kumuua.Iistoshe ilionekana fika Serambovu anamnyororo wa yeye Kilua kumpata
binti yake pamoja na kuwadaka watu walio na mtandao wa nyaraka za jalada za
13;14.Kwa vingine inatakiwa Serambovu awe karibu ili Kilua aweze kumdhibiti
akiwa mbali atafanya mabaya zaidi ya yale ya mwanzo lakini akiwa karibu
Serambovu na genge lake watakuwa bize kutaka kumdhibiti bi Kilua kwa kumsoma
hatua anazochukua kuongoza nchi na mwenendo wa faili nambari 13;14.Hapo watakuwa
na kasi ya polepole kupanga vikwazo kuliko Serambovu akiwa mbali.Ulikuwa wakati
mgumu sana kwa Kilua!
"Tutajadili jambo hili.Ondoa hofu."ilibidi
amtulize Dedani ingawa moyoni ilikuwa vigumu sana.Aliondoka mule ndani
nakumfuata Serambovu aliyekuwa amewekwa kwenye chumba kingine.Kilua alionekana
kuelemewa sasa huku mumewe anataka jambo gumu sana ingawa alikuwa tayari kwa
lolote ila hilo.
Serambovu alipomuona Kilua alipamba moto.Aliinuka
alipokuwa ameketi,"Kilua naomba umkanye mumeo!Unaona alichonifanya?Hajui nafasi
yangu kwako?"
"Serambovu control yourself.Yule ni mume wangu sio
takataka!"Kilua akawa mkali.
"Tangu lini Dedani akawa muhimu?Mimi
nina nafasi kubwa kwako.Mimi ni chifu wako wa staffu najua mengi ya utawala
wako."
"Narudia tena jishushe!"
"No!No!No!...Mimi ni
mwanaume wa maisha yako unanipenda kuliko huyo fala.Tena nakutahadharisha
mheshimiwa usipomdhibiti mumeo nitasema ukweli kwamba una mimba yangu!Isitoshe
Shani ni mwanangu ile ni damu yangu ni Serambovu blood!"
Lilikuwa
tishio kubwa sana kuwahi kulipata!
"Sitaki kumuona Dedani hapa
ikulu!"alisema Serambovu kwa sauti kavu kisha akaendelea,"Ninauwezo wa kuichafua
image yako vibaya sana.Kilua mimi nakupenda wewe nipo tayari kwa lolote hata
kama nikuua kwaajili nitaua.Nataka kitu kimoja tu.Sihitaji uwepo wa Dedani hapa
ikulu mrudishe jimbo la Kibatari kwa sasa."
“Unasemaje?”aliuliza Kilua
akiiwa anamshangaa Serambovu kwa kauli zake za matisho.Ilikuwa fedheha sana kwa
upande wake na hakutegemea kama watu hawa watafikia hatua ya kumtishia kwa namna
moja au nyingine.Serambovu alikuwa amevuka mipaka sasa.Ilionekana kwamba ana
sauti kuliko vile Kilua alifiikiria na ilikuwa ni lazima Kilua ameze kiburi hiki
lasivyo operesheni muhimu za kubaini watekaji wa mwanae zingefika tamati bila
yeye muhusika kumaizi hasa ni nani muhusika mkuu kwenye mtandao huo.Kilua
alikereka lakini akajikuta akiigiza kwenye maigizo hayo.
“Nimesema
simtaki Dedani hapa ikulu!”aliurudia tena bwana Serambovu na sasa ilikuwa ni
amri nasio ombi kama vile ilivyoonekana.
“Siwezi kufanya hivyo.Huyu
ni mume wangu ningehitaji utulivu wenu.Nipo katika wakati mgumu sana kwa sasa
iweje na wewe uwe problem?”Kilua alijaribu kumdhibiti bwana Serambovu
kistaarabu pengine angemtuliza bila kuwa na hisia zozote.
“Hapana
mimi simtaki.Kumbuka tuna mtoto!Dedani hapaswi kuwa na hiyo familia ni yangu
mimi!Mimi ndo mtu wako tena damu kabisa tunashea kwa kuzaa!”
“Tumedumu sasa kwa kipindi kirefu na tume-survive bila kuachana.Sitegemei kwa
sasa ukate tamaa kiasi cha kunidhalilisha na kuniweka katika wakati mgumu kiasi
hiki?”alisema Kilua kwa upole.
“ Siyo kukuweka katika wakati mgumu
bali napigania penzi langu kwako na hilo ndo la muhimu.Mimi ni mwanaume
anayeithamini damu yake kuachwa bila kupigania ni kitu cha kizembe nahisi
kuwa mbogo!”alijitetea Serambovu akiwa amedhamiria kuonesha nia
yake.Angejidhibiti lakini hasira zilimzidi kiasi akajisahau kabisa kwamba
kulikuwa na nini mbele yake.Hilo lilikuwa pigo kubwa sana kwake na kwa upande
wake na kwa upande wa Kilua.Huku kujiachia kizembe anakokuachia kuna jenga
picha ya jinsi gani alivyo na uhitaji wa kummiliki Kilua ambaye kwa sasa
amempata mume wake.Uhitaji huu una hatarisha usalama wa Kilua.Pia nafasi ya
Dedani anaitia mashakani.Kwa sasa Kilua alimuhitaji baba wa watoto.Pia angekuwa
mbioni kuonekana katika hafla mbalimbali za kitaifa pamoja na familia
yake.Kumtenga na mumewe ni kitu ambacho hakikuleta maana.Kulinda heshma na
penzi lake kulimgharimu sana bwana Serambovu na kumdhooisha kifikra.Ilionekana
ni ngumu.Pamoja nakuwa alipachikwa ikulu kama shushushu wa wanyonyaji lakini
alitakiwa acheze karata zake kiakili au angezidi kupoteza.Hisia zake zilimzidi
akasahau kwa kuteleza katika mipango yake.Na kama wakubwa wake wangelijiua
hivyo bila shaka angekuwa katika wakati mgumu sana.
“Serambovu
please behave well don’t be one of my problems.”alisisitiza Kilua akiwa na
umakini huku akizidi kumpatiliza.
“Nakupenda Kilua?”alimjibu kwa
kujiamini.Lakini haukuwa wakati wake kwa rais kumtilia maanani na sasa Serambovu
kaonekana king’ang’anizi na kama mdudu aliyeingia sikioni huku akikera sana kwa
hatua zake.Alishaharibu na sasa umimi unazidi kumpotezea imani kama mtu
aliyeaminika sana na Kilua.
Kulikuwa na mengi ya taabu.Bila kuchelewa
Serambovu alimvutia Kilua kwake kwa nguvu nakulazimisha busu la nguvu lakini
aliona kwa mara ya kwanza Kilua akimkwepa kutoka moyoni hiyo ilikuwa ishara
mbaya kwake!Alijichukia sana na kuhisi kasalitika kwa ujio wa Dedani hata zile
busu za kuiba tangu enzi zao ni kama leo zimefika tamati!Hakuweza kusadiki
jambo hilo hata kidogo na kutoka moyoni alichukizwa sana na kitu
hicho.Serambovu alijikuta akilazimishwa kumuachia Kilua.
“Busu na
pambaja zangu zimekuwa kama miiba?”alihoji pointi huku akimkazia Kilua macho kwa
umakini wenye wingi wa huzuni.Kwa mara ya kwanza alihisi moyo wake
kusagikasagika kama unga!Dedani heri usingetoka huko ulipokuwa.Alilaani sana
kwa hatua hizo.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Zimekosa mpapaso
na ulaini wa Hariri.”alisema Kilua akijikaza.
“Mapenzi yana
wenyewe.”alijibu Serambovu kwa kusikitika sana.
Ukimya ulipapasa na
kuzuia ndimi zao kusema na kutenda kwa muda huku sakafu za mioyo zikipashwa na
joto.Hapa Serambovu alihisi mengi sana huku akisaka maneno yenye rutuba
kupunguza sintofahamu zilizoikumba dunia yao.Kiota alichohisi kukimiliki
kilikuwa kimetwaliwa himayani mwake na sio riziki dhiki iliyomkumba alisawijika
nafsini.
Kilua alipiga hatua kuondoka huku akijisemea,”Penzi langu
kwa hawa wawili ni kama chungu na sufuria.Moja penzi lake linapata moto polepole
kama chungu.Mwingine ni sufuria kutia kwenye moto linawaka kwa
haraka.”alijiwazia akizungumza mwenyewe.Fumbo hilo likabaki mtimani.
Alielekea moja kwa moja hadi kwa mumewe.Alimtizama akijua fika bado ana hasira
sana nay eye.Alimsogelea nakuketi karibu naye.Ukimya ukatawala ila palepale
mlango ulifunguliwa wakaingia kina Masha pamoja na Toti wakiongozana na
Shunie.
Wote walimpa salamu rais kwa mpigo kisha wakaomba faragha ya
mazungumzo naye lakini Kilua aliomba waseme naye palepale.
“Mheshemiwa hili ni jambo la usalama wa taifa tunaweza zungumza faragha na
simbele ya mtu mwingine.”alipendekeza bwana Toti.
“Hapana mnaweza
zungumza mbele ya mume wangu.Ninavyojua anahusika sana katika zangu hadi sasa
alikoswakoswa kupoteza maisha dhidi yangu.Anapaswa kushiriki katika
hili.”
Toti walitizamana pamoja na Masha wakaona ni vyema
kumshirikisha bwana Dedani.Pia rais Kilua alihitaji ushirikiano na mumewe hasa
kwa jinsi alivyokuwa anapitia vipindi vigumu sana kiutawala.
“Mheshimiwa tuna ripoti kuhusiana na kuuawa kwa balozi wa Savanna Lands katika
ardhi yetu.Ripoti za uchunguzi wa kina zinaonesha ni kifo cha kuuawa.Na muuaji
alijua anachofanya na alikuwa mfanyakazi wa palepale hivi tunavyozungumza kikosi
chetu kiliweza kumtia nguvuni.Kutokana na ulinzi uliokuwemo ilikuwa ni rahisi
kujua mtekelezaji wa jambo.Pamoja na kumhoji sana mhusika hajaonesha nia ya
kusema ukweli.Tumemweka kizuizini kwanza.”
“Hii italeta mzozo na
Savanna Lands tena mkubwa sana.”alisema Kilua akiwatizama wasaidizi
wake.
“Tunalitegemea hilo na hata majeshi yetu yapo makini sana kwa
sasa pamoja na vyombo vya usalama.Kwa hatua tuliyofikia tangu wakati ule
tunangoja timu ya wanadiplomasia wasimamie mazungumzo haya japo sidhani kama
mauaji haya yatapita bila kuwa na maswali.Wanaweza sema sis indo tumemmaliza na
hatujamlinda hata kumfikisha mahakamani.”alishauri Masha kwa
msisitizo.
“Tunatakiwa kuwa na kauli ya kuridhisha jambo hili lisije
kutumika kama fimbo kwa rais wa Savanna Lands atalitumia kuniandama
kimataifa.”
“Mheshimiwa nadhani tunajuafika huu sio mkono wa
serikali wala vyombo vyetu.Hii ni mipango ya huu mtandao naweza uita wa kigaidi
kwa namna nyingine.”alisema Shunie.Macho ya Dedani yalikuwa yakimwangalia kwa
namna Fulani huku yeye mwenyewe akikabiliana na mtizamo huo.
“Huu
mtandao ndio ulioteka familia yako kwa sasa tunahitaji maelezo kwa
Pangabutu.”
“Pangabutu anaendeleaje?”aliuliza rais
Kilua.
“Kidogo anahafadhali.”alijibu bwana Toti.
Kilua
alifikiri kidogo kisha akasema,”Nataka kwenda kumuona sasa hivi.”alisema Kilua
huku akichukua simu nakuongea na mkuu wake wa usalama kumueleza kwamba
anahitajika kwenda hospitali kumuona mtu.Ndani ya muda mfupi ikulu ilishughulika
kwa ziara ya Kilua kwenda hospitali kumjulia hali bwana Pangabutu.
“Toti nataka tuwe pamoja tunakwenda hospitali kuna kitu ataniambia akiniona
mwenyewe.”alisema Kilua.Wote walitikisa kichwa kwa hatua hiyo kuonesha
inakubalika sana.Kilua pia alimgeukia mumewe,”Please my love be with me
today.First public appearance.”alisema Kilua akimshika mumewe mikono huku
akimtizama machoni.Dedani hakutaka kuwaonesha watu kama kuna mgomo baridi kati
yake na mumewe.Alichofanya alijibu kwa kuitikia kama kumpa ushirikiano
mkewe.
Baada ya muda msafara wa gari ulianza kuelekea hospitali
alimolazwa kapten Pangabutu na vile alikuwa mtu muhimu kwa taifa ilimlazimu mkuu
wa majeshi kuungana nao katika hafla hiyo.Pikipiki zilitangulia mbele kusafisha
barabara isiwepo gari lolote lile wakati rais KIlua akipita eneo hilo.Ukaja
msafara wa gari za polisi ambazo zilikuwa tayari kwa gari lolote kama lingetokea
kuleta fujo basi lingeshughulikiwa vilivyo.Magari ya usalama yalisheheni kwa
wingi huku kikosi maalum cha udunguaji kikiwepo katika msafara huo.Kikosi maalum
kilitangulia kwanza hospitali na kuchukua wadhfa wa usalama ikiwemo kuwaweka
tayari wadunguaji sehemu fiche za siri wakikagua usalama kwa rais Kilua kuzuru
hospitali hiyo.
Wanausalama waliovalia kijeshi pia walikuwepo wakiwa
na silaha zilizotayari kama tu ingetokea hatari yoyote kwa Kilua.Dedani sasa
alionja joto ya nguvu iliyopo kwa mkewe.Kilua alikuwa rais wan chi anayelindwa
kama mboni ya jicho.Usalama wake ulikuwa muhimu sana wa kutilia maanani.Mtu
hutafuta pesa,penzi na nguvu.Kilua alipata pesa na penzi kwa Dedani na
Serambovu sasa alipata nguvu!Nguvu ya kutawala na kutumikiwa na
kusikilizwa.Dedani alihisi hata kumuogopa mkewe kwa ulinzi aliokuwa nao sio wa
kawaida.Hii ilikuwa nguvu kuu!Muda huo wote Kilua alimshika mumewe mkono huku
akifanya kama kuiminyaminya kwa upendo.Alijua moyoni alimuhitaji mumewe lakini
hakujielewa alihisi kwa upande Fulani Serambovu aliutawala moyo wake.Ila alijua
moyo wake kwa mara ya kwanza tangu aingie kuwa rais umekuwa na mabadiliko
makubwa sana hasa akiwa ameonja joto ya jiwe kwenye kidonda.Sasa aliona mambo
kwa mtizamo tofauti.Alikuwa na nguvu.
“Power is everything in life
once you have it you control things.”alijiwazia na kwa kiburi hicho cha nguvu
angefanikiwa kumdhibiti Dedani pamoja na Serambovu!Baada ya muda mfupi walifika
hospitalini hapo.Msafara uligesha magari yao kisha wakashuka wanausalama na
kutengeneza mzingo maalum kwaajili ya rais.
“Secure the perimeter
CIC CLEOPATRA is on the move.”alisema mkuu wa usalama bwana Ditto kupitia kifaa
cha masikioni na kila mwanauslama alipata taarifa hiyo.CIC CLEOPATRA ndo jina la
siri la utambuzi wa Kilua kwa siku ile.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“CIC CLEOPATRA
cleared ALFHA TEAM SNIPER SHOOT ON TARGET!VULTURE TEAM SECURE THE ENTRENCE
ZONE.MOTHER TEAM EYES ON AIR BIRDS 1 2 3 CLEAR THE SKY.THE AREA IS SAFE!”Ditto
alizidi kupasha taarifa kwa lugha ambayo wanausalama pekee
waliieelewa.
Kilua alishuka wakishikana mikono na mumewe wakaelekea
hospitali ndanI.Ilikuwa mara ya kwanza kwa Kilua kuonekana na Dedani katika
sehemu ya umma.Hata waasaidizi wa Kilua walifurahi sana kwa jambo hilo wapo
waliojua Serambovu alikuwa na mchezo Fulani lakini kwa ujio wa Dedani wakawa na
imani kwa tabia ya Kilua kubadilika.
“Asante mme wangu kwa kuja na
mimi hapa.”alisema Kilua akiubinya mkono wa Dedani kwa hamu.Dedani alionesha
tabasamu kwa mkewe jambo ambalo lilizidi kumtatiza Kilua.Alijua hasira ya Dedani
ilikuwa inamtafuna kimyakimya lile tabasamu halikuwa halisi bali maumivu
makuu.
“Tuko pamoja.”alisema Dedani kuhakikisha.Walienda hadi alipo
Pangabutu.Walimkuta akiwa chini ya uangalizi mkali sana.Kilua alimpa salamu
pamoja na mkuu wa majeshi.Walimpa pole akiwemo katibu mkuu bi Saada.Pangabutu
alifarijika sana kwa ujio wa rais Kilua.Huu ulikuwa ushindi kwake ingawa
alijuafika kuna hatari itazidi kummendea.
“Tunakupa pole pia
tunakuombea kwa Mungu upone haraka.”alisema Kilua akijaribu kumpa
tabasamu.Tabasamu lilikuwa la moto hata wanaume waliokuwa pale walikubali kwamba
KIlua ni chuma.
“Nashkuru mheshimiwa aasante sana.Mungu
akubariki…Nimefarijika sana kwa ujio wako hapa.”alisema Pangabutu hadi akahisi
kububujikwa na machozi.Kilua alimfariji kwa kumshika bega.
“Naomba
uwe na amani taifa lipo kwaajili yako.Mimi nipo kwaajili yako.Nakuhakikishia
usalama!”
“Ila mheshimiwa naomba faragha na wewe wabaki Masha na
Toti.”aliomba Pangabutu.Alijiandaa kumwaga mpunga!Kilua aliwapa ishara watu
wengine hadi mkuu wa majeshi hakupaswa kuwepo pale jambo ambalo lilimuogopesha
sana jenerali Lupogo akijua bado yupo kwenye karata za Kilua.
Chumba
kikawa salama kwa Kilua kuzungumza.Dedani alitoka akawa anaenda huku akizunguka
alijiskia kwenda msalani alienda huko moja kwa moja.Kweli kichwa chake kilikuwa
kizito sana kiasi hakuangalia alikuwa anaingia maliwato gani alijikuta akiingia
maliwato moja nakugongana na mwanamke kifuani!Kuja kutahamaki alikuwa ni
Shunie.Walijikuta wakitizama kwa hisia kali sana.Huku midomo ikichezacheza na
kama kaupepo Fulani kakipuliza na nywele za Shunie kumchezacheza huku macho yake
ya kike yenye ulegevu Fulani yakimtizama Dedani.Shunie aliijua saikolojia ya
Dedani nay eye mwenyewe alijijua tayari moyo wake umeshakuwa mtama na sasa
nafsi inasukumwa kama chapatti kwa uwepo wake na Dedani.Lilikuwa kosa kubwa
sana kwa wawili hao kukutana katika mazingira yale.
Leo walikutana
sehemu hii iliyo na ulinzi mkali sana hasa kwa uwepo rais.
Shunie
ulimi ukawa mzito!Akimuona Dedani tangu tukio lile amekuwa hajielewi kabisa kuna
lugha ambayo ilizungumza kihisia kati yao nahakuna aliyetayari kukiri jambo
hilo.
“Mhh samahani sikujua kama…”mlimi wa Dedani ukawa mzito
sana.Alitaka kupiga hatua na alijikaza kweli akapiga hatua kutoka nje ile
anafika mlango alijikuta dhamira ikibadilia nia.Akamfuata Shunie kwa kasi
nakumsogelea.Pengine yangesikika mashairi ya THE SONG OF LAWINO.Au tungesikia
maneno matakatifu kutoka kitabu cha Suleimani WIMBO ULIO BORA.Au taratibu ala za
kilatino,kifilipino na hao kina India.Msukumo mzito wa kisaikolojia ulimkumba
Shunie!Alijikuta mikononi mwa Dedani bila kutarajia!Yakapita maneno kichwani mwa
Shunie na Dedani.
HATA JUA LIPUNGE,NA VIVULI
VIKIMBIE
NITAKWENDA KWENYE MLIMA WA MANEMANE,
NA KWENYE
KILIMA CHA UBANI,
BIBI ARUSI,MIDOMO YAKO YADONDOZA ASALI,ASALI NA
MAZIWA VI CHINI YA ULIMI WAKO:
Dedani alijikuta akifuata papi za
midomo ya Kilua kwa msukumo wa hisia zilizobubujika kama kijito.Lilikuwa busu la
hiyari…
Katika kumbatio hilo na busu la ghafla
Shunie alikuwa amefumbwa mbali sana kiasi cha kushindwa kukabiliana na hisia
zake ambazo sasa zilimezwa na mwanaume huyu!Mume wa rais Kilua na kumfunika
katika mahaba mazito sana.Msukumo uliomjia ghafla kwa kweli haukuwa na maelezo
au ufafanuzi.Kwa wanasaikolojia huwezi kuitafsiri hali hii kama msongo wa hisia
kali sana dhidi ya mtu wa jinsia tofauti.Mtu anashindwa kujizuia awapo naye na
hukuta hata maelewano hakuna lakini wengi huishia katika anguko la penzi zito
ambalo kila waonanapo ni wao pekee ndo wenye falsafa yao.
Kaupepo kadogo kalipuliza na kumpepea Shunie ambaye sasa alikuwa ameupokea
ulimi wa Dedani huku manukato yake yakimfikia Dedani ambaye aliyapokea
nakumsababishia pumzi zake kumpandisha kwa fujo kwa hawaa.Shunie aliivuta vizuri
harufu manukato ya Dedani japo kulikuwa na mchanganyo wa manukato ambayo
aliyasikia kutoka kwa KIlua lakini haya aliweza kuyapata kwa Dedani na
mchanganyo wa manukato binafsi.Shunie asingeweza kujizuia.Alimuhitaji mtu huyu
kwa hisia kali sana napengine kiherehere cha roho kingetulia punde kama bwana
Dedani angefikia hatua ya kuishia ubavuni mwake.Lakini hakujielewa alikuta
akisahau mengi ikiwemo mtu wake aliyemposa bwana Pablo na sasa hatma ya moyo
wake ilikuwa kwa Dedani mume wa rais Kilua.Hupendi mtu kwa kumchagua mazingira
na nyakati na hali ndizo huipeleka moyo kwenye kiota chake.
Kwa
dakika kama mbili hawakuutambua uwepo wa eneo lile.Walikuwa watu wawili tu
katika kumbatio zito la mahaba lilikuwa busu la kuvutana na kila mmoja akitaka
kuwa zaidi ya mwingine na bila shaka waling’ang’aniana.Shunie alihisi
anamuhitaji Dedani nay eye Dedani alihisi anamuhitaji Shunie pengine ule
mshawasha wa kumuwaza nakumfikiria hata wakati akiwa na mkewe alihisi anakuuiona
na kuhisi manukato ya mwanamke huyu kiasi akajishuku kwamba bibi huyu anasambaa
kwenye fikra zake.
Vivyo kwa Shunie alijua bwana huyu katawala fikra
zake na kujitandaza kiasi cha kuziba kama
Utando wa buibui kwenye
ubongo wake.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Chozi
likamponyoka Shunie,”Mheshimiwa tafadhali.”alisema Shunie akijiondoa kwenye
himaya yenye joto.
“Sorry Shunie please forgive me.”alisema Dedani
kwa pupa huku akizidiwa kwa kuhema kwa fujo.Wote walihema roho zikiwaenda
mbio.Kila mmoja aliutamani uwepo wa mwenzake lakini uhalisia haukuwa
ruhusu.Pengine hakuna aliyejua kwamba kwenye mioyo wamekwisha salitika.Walikuwa
wameivana.Lilikuwa penzi la ghafla ambalo halikuwa na ufafanuzi nap engine wao
wenyewe hawakujua kama kweli walikuwa wanapendana au ni tama tu ya ngono ilikuwa
imewapa mshawasha usio na kipimo.Kila mmoja alijaribu kudhibiti lile wazo
aliloliogopa la kwamba alikuwa anamuingilia mwenzake mwenye familia yake.Alikuwa
anaingilia penzi la mtu.
Wakati Dedani anataka kuondoka Shunie
alimshika mkono,”Ngoja.”
Dedani alisita nakusimama.Huku moyo
ukimwenda mbio bado alizihisi sakafu za midomo ya Shunie ikiwaa kwenye midomo
yake ikimsugua.
“Kuna nyakati nawaza sana.”alisema Shunie huku aibu
za kike pamoja na huzuni kwamba kinachotokea hakielewi kabisa.
“Unawaza nini?”
“Kwamba nakuhitaji.OOhh!Dedani nni jambo gani
linanitokea?Sijawahi muwaza mume wa mtu tangu nizaliwe lakini wewe umekuwa
udhaifu wangu Dedani?”Shunie alisema akilia machozi.Alikuwa anaugua
moyoni.
“Unahisi kitu gani?”Dedani alimuuliza Shunie huku akimkazia
macho.
“Mimi ni mtu mzima.Najua ninapoona akili yangu inabadilika
inakuwa inakuwa kama ya motto mdogo.Dedani I think am deeply inlove with
you!”aalisema Shunie kitu ambacho kilikuwa mwiko.Ole wake Kilua
amsikie.
Dedani hakumjibu kitu alijikuta akizibua kofi paa!Lilikuwa
kofi la mpenzi halikuuma.Kilichomuuma ni kule kuhisi anakataliwa!Labda
hakutegemea kukubaliwa lakini hakuhitaji pia kukataliwa.Kilikuwa ni kitu
ambacho hakiwezekani.
“Unadhani nitembee na mwanamke kama wewe
unayejirahisisha kwangu?Wewe kahaba?Hivi unadhani kukushikashika ndo kwamba
nakuhitaji?”Dedani akawa mkali tofauti na sifa alizopata alijikuta amebadilika
sana kiasi hata yeye hakujielewa kilichombadilisha.
“Dedani usiseme
hivyo?...Mheshimiwa wewe ndo uliyenibusu…siyo…”
“Na
ukakubali?Ulijuaje kama nakupima?Mimi mke wangu ni rais wan chi usifikiri
kuniokoa na kujirahisisha kwangu ndo kutanifanya ni kuhonge hela?”
“Mheshimiwa?Usiseme hivyo mimi siko hivyo…”Shunie alihuzunika sana.Hakutegemea
kabisa alijuta kumpa mwanya bwana huyu lilikuwa kosa kubwa sana ambalo alijutia
mwenyewe.Kilichotokea walikijua wao wenyewe.
“Unataka ni mwambie mke
wangu?”alisema Dedani alitishia.Alifanya vile kuondoa jambo ambalo lingewaweka
kwenye wakati mgumu.
“Nakubali adhabu yoyote utakayonipa.Mimi ni
mtu mzima nitavumilia lakini sio kuniweka katika vita na mkuu anaweza
kunifutilia mbali lakini kama hiyo ndo njia pekee basi sina budi kuibeba adhabu
hii!”
Dedani alishtuka sana na hata hakujua alikuwa anasema na
hakujua madhara ya maneno yake!Alichokifanya aliondoka katika uwepo wa
mwanausalama Yule aakimwacha akiwa hampatilizi bali akihofia kauli
zake.
***
Utulivu wa hospitali ulizinduliwa na
uwepo wa mkuu na msafra wake kiasi chakufanya kila mmoja awe katika
harakati.Leo Kilua alikuwa katika mazungumzo mazito kati yake na kaptein
Pangabutu.
“Mheshimiwa nadhani ni wakati wa kujua
kinachoendelea.”alisema bwana Kaptein kwa sauti iliyoamua kumwaga mboga
zote.Sasa makadabrasha ya 13:14 yanaenda kujulikana waziwazi.
“Nakusikiliza.”
“Siruhusiwi kusema jambo hili lakini inabidi
niliseme.Nilikuwa mpambe wa rais awamu Fulani.Kuna mkataba wa siri uliingiwa
miaka Fulani.Taifa la Kiota liligundulika kuwa na utajiri mkubwa wa
mafuta.Matajri wakubwa waliona fursa hivyo ikawapasa kuchangamkia tenda
hii.Lakini ilibidi wawe na mnyororo utakaowazubaisha waafrika kwa minajili ya
wao kutimiza adhma yao.Mnyororo huu ulikuwa na vitengo ambavyo vinashikilia
mkataba.Hawakutaka taifa linufaike kwa jambo hili.Walitaka wakamate uchumi wa
mafuta na njia pekee nikuingilia muundo wa serikali yetu.Walishawishi rais wa
kipindi nilipokuwa mpambe wake.Alitaka kuingia lakini masharti hakupaswa kuwa na
hisa kwenye mradi yeye alitakiwa tu awe mwezeshaji wa mpango huo.Alilipwa fedha
nyingi sana.Shughuli za uchimbaji zilitakiwa zipelekwe bungeni iundwe sharia
lakini kwa mujibu wa wakubwa wa mpango huo hawakutaka sheria yoyote iwekwe maana
Kiota ilikwisha kumbwa na demokrasia yenye nguvu na watu walikuwa werevu kiasi
ingeleta ugumu.”alisema maneno hayo huku Kilua akirekodi kupitia simu
yake.
“Kwanini waogope sheria kutungwa?”
“Ingewadhibiti
kupata asilimia 100% za rasilimali zetu.SO ilitakiwa wasuke mnyororo na huo ni
special kwa kutumia njia za panya.Faili nambari 13:14 ndo mnyororo wenyewe
uliosuka ni dhana inayofukuta kuwahujumu wanaoingia.Baada ya kuusuka wakawekwa
watu wakuutekeleza.Aliyeingia alikula kiapo cha siri no turning back.Mnyororo
huu umekuwa na masharti magumu na kila aliyediriki kwenda kinyume alifutiliwa
mbali na wengine kuingizwa.Simple mistake they finish you!Viongozi waliokuwa
tawala zilizopita wale waliouawa kwenye ajali pamoja na serikali ya Kisusi wapo
waliofanya uzembe kwenye mnyororo na The Big boys wakatoa amri wafutiliwe
mbali.Rais Kisusi alitishiwa kuondolewa madarakani ndani ya muda mfupi.Alikuwa
na wasiwasi sana hata alipokuwa ikulu kila hatua ilikuwa inaonekana na alihisiwa
hatarini maana na yeye alianza kusuka mpango wa kudhibiti mnyororo huo lakini
ulikwisha anza kuzama.”alisema bwana Pangabutu nakumfanya Kilua kuhisi kijasho
chembamba kikimtoka alijaribu kuunganisha matukio akajuafika kila kitu kilikuwa
ni mpango maalum.
“Kisusi alijuafika siku zake zinahesabika japo
mkuu wake wa majeshi alimuhakikishia usalama but The big boys walikuwa hatua
nyingi mbele.Wakaaamua kumzima kabisa.Rais awamu iliyoanzisha mnyororo
alijuafika kalisaliti taifa na alijua Kisusi angeemuumbua hivyo alipanga
kuonana nae siku ile ya sherehe za uhuru na baada ya pale angemwaga mchele
wote.Aliwaambia baadhi ya waliokuwa kwenye mnyororo ambao yeye aliingia nao
akijua ni watiifu.Lakini siri ilivuja kabla.”alisema hivyo akaomba maji
anywe.Ilikuwa kama picha simulizi ya kutisha alikuwa
anahadithiwa.
“Ikawaje?”
“Ndo ukapangwa mnyororo kuvunjwa
lakini kabla ya sherehe za uhuru miezi sita nyuma waliamua kubadili
mzunguko.Ikiwemo namna taifa litakavyokuwa huko mbeleni baada ya Kisusi
kuondolewa madarakani.Kuna mabadiliko ya kikatiba yalifanyika katika uongozi
kuhusiana na mtiririko wa kurithi madaraka ulivyo.Mtiririko huu kwa mara ya
kwanza ulimpa mtu mwenye cheo cha ugavana wa jimbo kushika nafasi ya urais
endapo waliopo kwenye mtiririko hawapo.Walimtaka gavana dhaifu asiye na
makucha.Jimbo la Kibatari lilikuwa sehemu nzuri kwani gavana wake hana nguvu
ya Umma maana huteuliwa na rais na sio uchaguzi wa wananchi.Huyu waliona
ingekuwa rais kumpelekesha.Wewe ulikuwa shabaha.Kwa muda Kibatari huonekana
kama ugenini hasa tukijua eneo hili lilichukuliwa kutoka taifa la Savanna landa
miaka mingi iliyopita wakati wa vita.Inasemekana wakazi wengi wa Kibatari ni
asili ya Savanna Lands na tayari rais wa Savanna Lands alikuwa kwenye
mnyororo.Yeye angetumika kama chambo kukushawishi lakini uliwashtua nakuwa na
nguvu sana kiasi ikabidi waweke uadui mkubwa kati yenu.”
Kilua
aliduwaa mambo yalikuwa mazi.
“Kwanini watuchonganishe?”
“Alitaka ubwana wakati alikuwa kitwana.”
“Duh?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa wewe mbona
hawakukufuata siku zote.”
“Niliwekwa mahususi kuja kuvumbua haya
namuamini sana Mungu na hakika kanilinda kuja kusema ukweli ni jinsi gani mambo
yantendeka katika bara jeusi!Ukitaka kuwamaliza watu watengenezee theory
Fulani wahangaike kupambana nayo huku wao wakiwa tayari wamepigaa hatua
ndefu.”
“Agent Shunie alikuwa amepiga picha meli Fulani na kwa
mujibu wa upelelezi wake vilikuwa vifaa vya kuchumbia mafuta.”alisema rais
Kilua.
“Sishangai na sasa wamefikia hatua yakuleta vifaa huo ni
ubabe mkubwa sana.”
“Vifaa hivi bado vipo bandarini na hadi sasa
meli yao haijafanyiwa clearance japo kwa mujibu wa taarifa hazioneshi ni nani
kaziagiza na mara kadhaa wametaka kutumia muhuri wa ikulu.”
“Ndo
hatua zenyewe.”alisema kisha akanywa maji.
“Unashauri nini
kifanyike.”
“Kuna watu wengi wakuwekwa kizuizini kitendo tu cha
kusababisha ajali ile ni sawa nakuondoa serikali madarakani ni kosa na
wanahitaji kusakwa kuleta maafa kwa taifa.Unatakiwa uanze mabadiliko ya hali ya
juu najua bado hujaunda baraza la mawaziri hivyo ni bora kulitengeneza
kwanza.Ila uwalinde siajabu wakauawa hata kabla hawajaapishwa.”
***
Shunie
akiwa hajielewi kitendo cha kutishiwa kusemwa tu alihisi dunia inambadilikia
bila kufikiri alienda hadi kwenye roshani tayari kujitupa aangukie kichwa
apasuke afutike duniani hapo moyo hautaumwa.Kulikoni kuwekwa nguvuni na rais
Kilua bora ajiondoe kabisa uhai!Shunie alianza kujihesabia hatua namna
atakavyoruka!Alijisogeza hadi ukingoni mwa roshani akapanda zile chuma tayari
kujirusha!Mapenzi yalimharibu Shunie.
Katika
kumbatio hilo na busu la ghafla Shunie alikuwa amefumbwa mbali sana kiasi cha
kushindwa kukabiliana na hisia zake ambazo sasa zilimezwa na mwanaume huyu!Mume
wa rais Kilua na kumfunika katika mahaba mazito sana.Msukumo uliomjia ghafla kwa
kweli haukuwa na maelezo au ufafanuzi.Kwa wanasaikolojia huwezi kuitafsiri hali
hii kama msongo wa hisia kali sana dhidi ya mtu wa jinsia tofauti.Mtu
anashindwa kujizuia awapo naye na hukuta hata maelewano hakuna lakini wengi
huishia katika anguko la penzi zito ambalo kila waonanapo ni wao pekee ndo
wenye falsafa yao.
Kaupepo kadogo kalipuliza na kumpepea Shunie
ambaye sasa alikuwa ameupokea ulimi wa Dedani huku manukato yake yakimfikia
Dedani ambaye aliyapokea nakumsababishia pumzi zake kumpandisha kwa fujo kwa
hawaa.Shunie aliivuta vizuri harufu manukato ya Dedani japo kulikuwa na
mchanganyo wa manukato ambayo aliyasikia kutoka kwa KIlua lakini haya aliweza
kuyapata kwa Dedani na mchanganyo wa manukato binafsi.Shunie asingeweza
kujizuia.Alimuhitaji mtu huyu kwa hisia kali sana napengine kiherehere cha roho
kingetulia punde kama bwana Dedani angefikia hatua ya kuishia ubavuni
mwake.Lakini hakujielewa alikuta akisahau mengi ikiwemo mtu wake aliyemposa
bwana Pablo na sasa hatma ya moyo wake ilikuwa kwa Dedani mume wa rais
Kilua.Hupendi mtu kwa kumchagua mazingira na nyakati na hali ndizo huipeleka
moyo kwenye kiota chake.
Kwa dakika kama mbili hawakuutambua uwepo
wa eneo lile.Walikuwa watu wawili tu katika kumbatio zito la mahaba lilikuwa
busu la kuvutana na kila mmoja akitaka kuwa zaidi ya mwingine na bila shaka
waling’ang’aniana.Shunie alihisi anamuhitaji Dedani nay eye Dedani alihisi
anamuhitaji Shunie pengine ule mshawasha wa kumuwaza nakumfikiria hata wakati
akiwa na mkewe alihisi anakuuiona na kuhisi manukato ya mwanamke huyu kiasi
akajishuku kwamba bibi huyu anasambaa kwenye fikra zake.
Vivyo kwa
Shunie alijua bwana huyu katawala fikra zake na kujitandaza kiasi cha kuziba
kama
Utando wa buibui kwenye ubongo wake.
Chozi
likamponyoka Shunie,”Mheshimiwa tafadhali.”alisema Shunie akijiondoa kwenye
himaya yenye joto.
“Sorry Shunie please forgive me.”alisema Dedani
kwa pupa huku akizidiwa kwa kuhema kwa fujo.Wote walihema roho zikiwaenda
mbio.Kila mmoja aliutamani uwepo wa mwenzake lakini uhalisia haukuwa
ruhusu.Pengine hakuna aliyejua kwamba kwenye mioyo wamekwisha salitika.Walikuwa
wameivana.Lilikuwa penzi la ghafla ambalo halikuwa na ufafanuzi nap engine wao
wenyewe hawakujua kama kweli walikuwa wanapendana au ni tama tu ya ngono ilikuwa
imewapa mshawasha usio na kipimo.Kila mmoja alijaribu kudhibiti lile wazo
aliloliogopa la kwamba alikuwa anamuingilia mwenzake mwenye familia yake.Alikuwa
anaingilia penzi la mtu.
Wakati Dedani anataka kuondoka Shunie
alimshika mkono,”Ngoja.”
Dedani alisita nakusimama.Huku moyo
ukimwenda mbio bado alizihisi sakafu za midomo ya Shunie ikiwaa kwenye midomo
yake ikimsugua.
“Kuna nyakati nawaza sana.”alisema Shunie huku aibu
za kike pamoja na huzuni kwamba kinachotokea hakielewi kabisa.
“Unawaza nini?”
“Kwamba nakuhitaji.OOhh!Dedani nni jambo gani
linanitokea?Sijawahi muwaza mume wa mtu tangu nizaliwe lakini wewe umekuwa
udhaifu wangu Dedani?”Shunie alisema akilia machozi.Alikuwa anaugua
moyoni.
“Unahisi kitu gani?”Dedani alimuuliza Shunie huku akimkazia
macho.
“Mimi ni mtu mzima.Najua ninapoona akili yangu inabadilika
inakuwa inakuwa kama ya motto mdogo.Dedani I think am deeply inlove with
you!”aalisema Shunie kitu ambacho kilikuwa mwiko.Ole wake Kilua
amsikie.
Dedani hakumjibu kitu alijikuta akizibua kofi paa!Lilikuwa
kofi la mpenzi halikuuma.Kilichomuuma ni kule kuhisi anakataliwa!Labda
hakutegemea kukubaliwa lakini hakuhitaji pia kukataliwa.Kilikuwa ni kitu
ambacho hakiwezekani.
“Unadhani nitembee na mwanamke kama wewe
unayejirahisisha kwangu?Wewe kahaba?Hivi unadhani kukushikashika ndo kwamba
nakuhitaji?”Dedani akawa mkali tofauti na sifa alizopata alijikuta amebadilika
sana kiasi hata yeye hakujielewa kilichombadilisha.
“Dedani usiseme
hivyo?...Mheshimiwa wewe ndo uliyenibusu…siyo…”
“Na
ukakubali?Ulijuaje kama nakupima?Mimi mke wangu ni rais wan chi usifikiri
kuniokoa na kujirahisisha kwangu ndo kutanifanya ni kuhonge hela?”
“Mheshimiwa?Usiseme hivyo mimi siko hivyo…”Shunie alihuzunika sana.Hakutegemea
kabisa alijuta kumpa mwanya bwana huyu lilikuwa kosa kubwa sana ambalo alijutia
mwenyewe.Kilichotokea walikijua wao wenyewe.
“Unataka ni mwambie mke
wangu?”alisema Dedani alitishia.Alifanya vile kuondoa jambo ambalo lingewaweka
kwenye wakati mgumu.
“Nakubali adhabu yoyote utakayonipa.Mimi ni
mtu mzima nitavumilia lakini sio kuniweka katika vita na mkuu anaweza
kunifutilia mbali lakini kama hiyo ndo njia pekee basi sina budi kuibeba adhabu
hii!”
Dedani alishtuka sana na hata hakujua alikuwa anasema na
hakujua madhara ya maneno yake!Alichokifanya aliondoka katika uwepo wa
mwanausalama Yule aakimwacha akiwa hampatilizi bali akihofia kauli
zake.
***
Utulivu wa hospitali ulizinduliwa na
uwepo wa mkuu na msafra wake kiasi chakufanya kila mmoja awe katika
harakati.Leo Kilua alikuwa katika mazungumzo mazito kati yake na kaptein
Pangabutu.
“Mheshimiwa nadhani ni wakati wa kujua
kinachoendelea.”alisema bwana Kaptein kwa sauti iliyoamua kumwaga mboga
zote.Sasa makadabrasha ya 13:14 yanaenda kujulikana waziwazi.
“Nakusikiliza.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Siruhusiwi
kusema jambo hili lakini inabidi niliseme.Nilikuwa mpambe wa rais awamu
Fulani.Kuna mkataba wa siri uliingiwa miaka Fulani.Taifa la Kiota liligundulika
kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta.Matajri wakubwa waliona fursa hivyo
ikawapasa kuchangamkia tenda hii.Lakini ilibidi wawe na mnyororo
utakaowazubaisha waafrika kwa minajili ya wao kutimiza adhma yao.Mnyororo huu
ulikuwa na vitengo ambavyo vinashikilia mkataba.Hawakutaka taifa linufaike kwa
jambo hili.Walitaka wakamate uchumi wa mafuta na njia pekee nikuingilia muundo
wa serikali yetu.Walishawishi rais wa kipindi nilipokuwa mpambe wake.Alitaka
kuingia lakini masharti hakupaswa kuwa na hisa kwenye mradi yeye alitakiwa tu
awe mwezeshaji wa mpango huo.Alilipwa fedha nyingi sana.Shughuli za uchimbaji
zilitakiwa zipelekwe bungeni iundwe sharia lakini kwa mujibu wa wakubwa wa
mpango huo hawakutaka sheria yoyote iwekwe maana Kiota ilikwisha kumbwa na
demokrasia yenye nguvu na watu walikuwa werevu kiasi ingeleta ugumu.”alisema
maneno hayo huku Kilua akirekodi kupitia simu yake.
“Kwanini waogope
sheria kutungwa?”
“Ingewadhibiti kupata asilimia 100% za rasilimali
zetu.SO ilitakiwa wasuke mnyororo na huo ni special kwa kutumia njia za
panya.Faili nambari 13:14 ndo mnyororo wenyewe uliosuka ni dhana inayofukuta
kuwahujumu wanaoingia.Baada ya kuusuka wakawekwa watu wakuutekeleza.Aliyeingia
alikula kiapo cha siri no turning back.Mnyororo huu umekuwa na masharti magumu
na kila aliyediriki kwenda kinyume alifutiliwa mbali na wengine kuingizwa.Simple
mistake they finish you!Viongozi waliokuwa tawala zilizopita wale waliouawa
kwenye ajali pamoja na serikali ya Kisusi wapo waliofanya uzembe kwenye mnyororo
na The Big boys wakatoa amri wafutiliwe mbali.Rais Kisusi alitishiwa kuondolewa
madarakani ndani ya muda mfupi.Alikuwa na wasiwasi sana hata alipokuwa ikulu
kila hatua ilikuwa inaonekana na alihisiwa hatarini maana na yeye alianza kusuka
mpango wa kudhibiti mnyororo huo lakini ulikwisha anza kuzama.”alisema bwana
Pangabutu nakumfanya Kilua kuhisi kijasho chembamba kikimtoka alijaribu
kuunganisha matukio akajuafika kila kitu kilikuwa ni mpango maalum.
“Kisusi alijuafika siku zake zinahesabika japo mkuu wake wa majeshi
alimuhakikishia usalama but The big boys walikuwa hatua nyingi mbele.Wakaaamua
kumzima kabisa.Rais awamu iliyoanzisha mnyororo alijuafika kalisaliti taifa
na alijua Kisusi angeemuumbua hivyo alipanga kuonana nae siku ile ya sherehe
za uhuru na baada ya pale angemwaga mchele wote.Aliwaambia baadhi ya waliokuwa
kwenye mnyororo ambao yeye aliingia nao akijua ni watiifu.Lakini siri ilivuja
kabla.”alisema hivyo akaomba maji anywe.Ilikuwa kama picha simulizi ya kutisha
alikuwa anahadithiwa.
“Ikawaje?”
“Ndo ukapangwa mnyororo
kuvunjwa lakini kabla ya sherehe za uhuru miezi sita nyuma waliamua kubadili
mzunguko.Ikiwemo namna taifa litakavyokuwa huko mbeleni baada ya Kisusi
kuondolewa madarakani.Kuna mabadiliko ya kikatiba yalifanyika katika uongozi
kuhusiana na mtiririko wa kurithi madaraka ulivyo.Mtiririko huu kwa mara ya
kwanza ulimpa mtu mwenye cheo cha ugavana wa jimbo kushika nafasi ya urais
endapo waliopo kwenye mtiririko hawapo.Walimtaka gavana dhaifu asiye na
makucha.Jimbo la Kibatari lilikuwa sehemu nzuri kwani gavana wake hana nguvu
ya Umma maana huteuliwa na rais na sio uchaguzi wa wananchi.Huyu waliona
ingekuwa rais kumpelekesha.Wewe ulikuwa shabaha.Kwa muda Kibatari huonekana
kama ugenini hasa tukijua eneo hili lilichukuliwa kutoka taifa la Savanna landa
miaka mingi iliyopita wakati wa vita.Inasemekana wakazi wengi wa Kibatari ni
asili ya Savanna Lands na tayari rais wa Savanna Lands alikuwa kwenye
mnyororo.Yeye angetumika kama chambo kukushawishi lakini uliwashtua nakuwa na
nguvu sana kiasi ikabidi waweke uadui mkubwa kati yenu.”
Kilua
aliduwaa mambo yalikuwa mazi.
“Kwanini watuchonganishe?”
“Alitaka ubwana wakati alikuwa kitwana.”
“Duh?”
“Sasa
wewe mbona hawakukufuata siku zote.”
“Niliwekwa mahususi kuja
kuvumbua haya namuamini sana Mungu na hakika kanilinda kuja kusema ukweli ni
jinsi gani mambo yantendeka katika bara jeusi!Ukitaka kuwamaliza watu
watengenezee theory Fulani wahangaike kupambana nayo huku wao wakiwa tayari
wamepigaa hatua ndefu.”
“Agent Shunie alikuwa amepiga picha meli
Fulani na kwa mujibu wa upelelezi wake vilikuwa vifaa vya kuchumbia
mafuta.”alisema rais Kilua.
“Sishangai na sasa wamefikia hatua
yakuleta vifaa huo ni ubabe mkubwa sana.”
“Vifaa hivi bado vipo
bandarini na hadi sasa meli yao haijafanyiwa clearance japo kwa mujibu wa
taarifa hazioneshi ni nani kaziagiza na mara kadhaa wametaka kutumia muhuri wa
ikulu.”
“Ndo hatua zenyewe.”alisema kisha akanywa maji.
“Unashauri nini kifanyike.”
“Kuna watu wengi wakuwekwa kizuizini
kitendo tu cha kusababisha ajali ile ni sawa nakuondoa serikali madarakani ni
kosa na wanahitaji kusakwa kuleta maafa kwa taifa.Unatakiwa uanze mabadiliko ya
hali ya juu najua bado hujaunda baraza la mawaziri hivyo ni bora kulitengeneza
kwanza.Ila uwalinde siajabu wakauawa hata kabla hawajaapishwa.”
***
Shunie
akiwa hajielewi kitendo cha kutishiwa kusemwa tu alihisi dunia inambadilikia
bila kufikiri alienda hadi kwenye roshani tayari kujitupa aangukie kichwa
apasuke afutike duniani hapo moyo hautaumwa.Kulikoni kuwekwa nguvuni na rais
Kilua bora ajiondoe kabisa uhai!Shunie alianza kujihesabia hatua namna
atakavyoruka!Alijisogeza hadi ukingoni mwa roshani akapanda zile chuma tayari
kujirusha!Mapenzi yalimharibu Shunie.
Tulipoishia
Kilua agundua maadui wa taifa lake na wahujumu rasilimali za taifa.Atafanyaje
kuwajua nakuwadhibiti.Je,ataweza kuwa fahamu wote waliohusika kusuka mpango wa
kuisambaratisha serikali ya Kisusi?Upande mwingine tunamuona Shunie akiwa katika
wakati mgumu akieleza hisia zake za mapenzi kwa mume wa rais Kilua ambaye
anamkataa nakutishia kumshtaki kwa mkewe hali inayomfanya Shunie kuogopa hasira
ya rais Kilua dhidi yake.Shunie anaamua kujitupa kutoka ghorofani.Je,nini
kitaendelea?Tuwe pamoja.
Pambana nayo…
Shunie
alipulizwa na upepo akiwa kwenye kingo za roshani ya ghorofa ya hospitali
ile.Alitizama chini nakuona urefu uliomfaa ikiwa anaweza kujirusha hadi chini
atafanikiwa kuumaliza uhai wake au aumie vibaya sana.Dhamira ilikuwa kuukatisha
uhai au kujiweka katika hatma itakayoondoa maumivu yanayomtesa moyo.Kumpenda
kwake mume wa rais Kilua ilikuwaa ghafla sana na hawezi kujidhibiti kiasi
hakujielewa kabisa ilitokeaje?Yeye alkkuwa mkombozi nasio mpendaji lakini hii
inaitwa ajali kazini alishajiapiza kupambana na hisia hizo lakini zimeonekana
kumshinda nguvu kiasi anajikuta akizidiwa.Alijihisi mpweke sana na alijua kwa
namna anajisikia hata utendaji wake wa kazi unaweza kuathirika kwa namna moja au
nyingine.Aliona muhimu ni kuidhibiti hali hii kabla mambo hayajawa magumu
zaidi.
Shunie alijitupa kutoka kwenye roshani wakati anajiachia tu
alijikuta mkono wake ukishikwa na mtu!Ilikuwa ghafla sana mwenyewe hakutegemea
kama mtu huyo angetokea kuudaka mkono wake kwa namna ile.Ukweli ulikuwa dhahiri
kwamba kuna mtu alikuwa ameushikilia mkono wake wakti yeye akijiachia kutoka
kwenye roshani!Mkono ulimkamata kama wa mkombozi kwa uimara na hakuwa tayari
kumuachia.Alijua akadakwa leo!Aligeuza shingo kumkabili aliyeshika na kweli
alikutana na Dedani akiwa amemdaka!Kumbe Dedani alimuona Shunie akiwa anaelekea
eneo hilo na alijikuta nay eye akimfuata kwa kunyatanyata.Huzuni ya Shunie
ilikuwa kwenye uso wake na yeyote angeusoma huzuni iliyojipaka katika wajihi
wake.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shunie alibaki
kutumbua macho akimuona Dedani kama mkombozi wake aliyekuja kumfuata.Dedani
alimvuta kwa haraka na kumuondoa katika hiyo hatari hiyo.Shunie alihisi moyo
wake ukibubujika nakuzidi kumiminika.Kama vile ndoto ya kila mwanamke kuwepo kwa
mwanaume Fulani amjie akiwa juu ya farasi katika mwanga akimpa mkono nakumshika
waapande pamoja.Kuwa na Yule mtu ajaye kama mkombozi wake amsimamie siku ya
uhitaji wake.Aje siku ya huzuni yake nakumpa uhakika wa kutabasamu basi Shunie
aliona nyotanyota nakuhisi kumbimbi zikimcheza mauongoni.Shunie hadi anatolewa
kwenye roshani nakusimama sakafuni alibaki kumpa Dedani nuru ya macho yake
yaliyomuangalia bila kupepesa wala kumkwepa alimuangalia kwa macho ya kike yenye
tumaini nakujaribu kuona kilichomo kwa Dedani kimejificha wapi?
“Unataka kujiua?”alimuuliza kwa ukali kidogo huku moyo ukimwenda
mbio.
“Bora nife kuliko kushtakiwa kwa mkuu wa majeshi!”alisema
Shunie mwenyewe alijua jinsi gani ilivyo vigumu kupambana na mkuu wan
chi.Hakujielewa kama anataka kumpindua Kilua au la!
“Kifo ndo suluhu
kwa akili zako za kipumbavu?”aliuliza Dedani kwa
hasira?
“Ndiyo!”alijibu kwa kukata tama.
“Usiwe mjinga
sasa unanipa sababu za kukushtaki!”alisema Dedani akifoka kwa hasira
sana.Hakutegemea kukataliwa.
“Dedani kwanini
unanichukia?”
“Sikiliza wewe mwanamke.Mimi kwasasa nipo na mke wangu
chochote kilichotokea kati yangu na wewe kilisababishwa na Kavu sio riddhaa
yangu na si ya kwako.”
Dedani aliondoka nakumuacha Shunie katika
sintofahamu huku akifoka kwa uukali kidogo,”Sitegemei utaondoa uhai wako kisa
huo ujinga wako.”alisema akikatiza korido.
Penzi la moyo wake
likaitwa ujinga!Kukataliwa kulimshusha imani na mwanaume huyo.Wakati anataka
kupiga hatua kuna ujumbe wa simu uliingia kwake.Alishtuka sana kiasi akajikuta
akitetemeka.Ujumbe ulitokea ukweni kwake akihitajika kwa haraka sana.Alipanga
watakapotoka kwenye ziara ile bila shaka angeenda.
Alirudi katika
msafara wa rais.Kilua alikuwa anamaliza mazungumzo na kapteni.
“Tengeneza baraza imara la mawaziri unakipindi cha miaka kama mine hivi.Pamoja
nakuwa haukuandaliwa lakini inabidi ujiimarishe kwa kipindi hiki uhakikishe
hakuna kidudu mtu wa kushusha.”
Kilua alifikiria kidogo kisha
akatikisa kichwa kumuelewa.
“Pitia usalama wa taifa ufanye uchambuzi
yakinifu uweze kupata watendaji wazuri ambao hawadanganyiki nakuhakikishia
ukipata timu nzuri nchi itakuwa salama.”alisema bwana Pangabutu.Rais Kilua
alikubaliana na ushauri wake.
“Ongea na mumeo akusaidie ushauri ni
mtu mwerevu sana hasa linapokuja swala la kudeal na serikali iliyofisadika
anajua namna ya kuisuka.”
“Dedani mbona ni mtu wa kawaida
tu?”alisema Kilua asijue jambo nyuma ya pazia kuhusu mume wake.
“Hahaha.”mgonjwa alicheka Pangabutu kisha akaendelea,”Hujajua uwezo wake ila tu
nakuambia mtumie huyu atasaidia kutoa ushauri mzuri.Dedani ni ngao chache za
taifa na mistake kwa the big boys kumuachia ndo maana walimteka
kwanza.”
Ufahamu mpya kuhusu mumewe ulimshangaza sana Kilua kwanini
mumewe ajulikane na Pangabutu.
“Ina maana Dedani ni
nani?”
“Dedani ni miongoni mwa watu wachache wanaochaguliwa kuwa ngao
lala za taifa ni kama kikosi maalum ambacho hukuwa-active endapo mambo
yanaonekana mabovu.Ila hakikisha ulinzi wake unakuwa mkubwa sana.Mpe usalama wa
taifa umlinde.”alisema mgonjwa.
“Nashukuru bwana Pangabutu umekuwa
na ushauri mzuri sana kwangu.”Kilua alittamka maneno hayo nakumpa mkono mtu
huyo.Ulikuwa umefika wakati way eye kuondoka.Waliagana kisha Kilua aliungana na
mumewe safari ikaanza kundoka eneo lile la pale hospitali.Muda mwingi Kilua
alikuwa ameushika mkono wa mumewe.Alijiegeza ubavuni mwake.Dedani alikuwa mbali
sana kimawazo.
“Leo nimegundua mambo mengi sana.”alisema
Kilua.
“Nadhani umeelewa nchi inapoelekea.”alisema
Dedani.
“Naomba ushauri ni jambo gani nifanye.Nahisi
kuzidiwa.”
“Kwasasa tengeneza baraza la mawaziri kwanza.Pia teua
makamu wa rais pamoja na waziri mkuu.Tunatakiwa tuone nani anapaswa kuwa makamu
kwa sasa nafasi hizi zimeonekana kuwa wazi kwa kipindi kirefu.Inatakiwa
wawekwe kwa haraka.Pia kuna maeneo yanahitajika kufanya uchaguzi hasa kwa wale
waliopoteza viongozi wao.Tuarudi kwenye mtandao wa
utawala.”
“Kweli umesema kitu ambacho sijawahi
kukifikiria.”
“Pia kumbuka lazima ujiimarishe kwenye chama chako cha
kisiasa.Sio kwamba chama kinaridhika na wewe.Lazima na wao wanajipanga
kivyao.Je,utawala wako unakomea miaka mine hii ya urithi kabla hujagombea au una
mpango wakuachia madaraka punde utakapo fikia mwisho wa muda?Umejua siri nyingi
za nchi kwa namna yoyote yapo ambayo yatahitajika wewe binafsi kuyasimamia na
kushughulikia.Kwasasa huna wa kumjibia maana umepewa lakini jipange kuudhibiti
utawala.”
Dedani alikuwa anamfundisha mkewe kutawala nchi na hatua
za kuchukua.Ikulu itakuwa bize sana kutoka sasa hasa anapoandaa baraza la
mawaziri pamoja na makamu wa rais akiongeza na waziri mkuu.Ni wazi kwa hatua
hiyo atafanikiwa kutengeneza mtandao wa kiutawala utakaokuwa imara.Ilikuwa kazi
ngumu lakini yenye manufaa.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Dedani nataka
usimamie jambo hili.”
“Nikiweka makucha yangu sana watasema unaleta
ufamilia kwenye uongozi.”
“Wewe ndo ninayekuamini hakuna
mwingine.”alihakikisha rais Kilua.Muda ule walifika ikulu.Kilua aliitisha kikao
kuhusiana na hatua anayotaka kuichukua.Kutakuwa na mabadiliko makubwa sana
kiutawala kuna mengi yanaenda kubadilishwa ili kuusimamisha utawala
wake.Aliihitaji kwanza kuanza na hawa wa juu ikiwemo makamu wa urais.Majina
kadhaa yalianza kupita Dedani alikuwa makini katika hilo akihakikisha
atalishughulikia jambo hilo ila yeye alijiweka kama kivuli.Serambovu alijua hii
ni fursa ya wao kupandikiza watu wao katika utawala wa Kilua.Japo Kilua hakuwa
na maono yakuendelea na kazi hiyo lakini sasa aliona kuna haja ya kuendelea na
kazi hiyo na tena aifanye kwa umakini wa hali ya juu kuliko hata mwanzo.Kulikuwa
na uozo mkubwa sana.Kilua alijiapiza kama mabaradhuli hawa walifanikiwa kuigusa
familia yake ilitakiwa alipize kisasi maalum na njia pekee ni kuwadhibiti
katika utawala wake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment