Simulizi
: Kombora Kiotani
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
Kilua alikuwa na kikao cha siri pamoja na moja ya
wanajeshi wake.Kikao hiki kilikuwa mahsusi kikiongozwa na Kilua pamoja na Kanali
Pasua,”Nataka nifanye jambo la hatari sana.”
“Kuna meli ipo
bandarini na kwa muda sasa haijafanyiwa clearance.Mara kadhaa wametaka kupata
kibali kutoka ikulu.Meli hii siyo nzuri kwa uupande wetu.Kuna watu
wanashikiana na wamiliki wa meli hii kunifanyia hujuma lakini binafsi ninampango
wa kuwakomesha.Nataka meli hii ilipuliwe.”
Ilikuwa kauli nzito sana
kwa rais KIlua kuitoa.
Wote walibaki kutumbua macho.
“Kwani mheshimiwa hakuna namna nyingine ya kushghulika na jambo hili hadi
ifikie hatua ya kutumia nguvu kiasi hiki?”
“Watu hawa wamejidai wana
nguvu sana kiasi cha kutaka hata kunitikisa mimi binafsi.Ninawachukia kutoka
moyoni na lazima nitume ujumbe kwamba na mimi najeuri.”
“Kwani
mheshimiwa hii meli ina nini?”
“Kilichomo ni mitambo ya kuchimbia
mafuta inayokuja kutumika nchini kwetu.Hadi sasa hakuna maelezo yoyote yaani
wanafanya jambo hili kimyakimya kana kwamba nchi hiii ni ya mama
zao.”
“Huoni jambo hili ukifuata utaratibu wa kisiasa utaweza
kuwadhibiti.”
“Kabla halijafika huko nataka kuwatikisa.Nataka bomu
litegwe lilipue meli nzima na kila kilichomo kiwe majivu.”
“Lengo
hasa ni nini?”
“Natuma ujumbe kwao kwamba nipo macho.”
“Tukiilipua meli ikiwa pale bandarini tutegemee maafa makubwa sana kwa bandari
na meli zilizoegeshwa jirani.Pia kutaonesha bandari yetu si salama ikiwa
milipuko tena ya mabomu inatokea.Hiii ni ishara mbaya sana.”
“Kwa
vyovyote watu hawa wamejipanga kulinda kilichomo kwenye meli yao.Lazima watajua
tu kwamba meli yao imelipuliwa kwa bomu.”alishuri Dedani.
“Mnafikiri
tufanyeje?”aliuliza Kilua.Kilua ni mbabe kiasili alitaka kuwatia hasara kwa
kuharibu meli yao.Hadi sasa binti yake anasota mikononi mwa hao
afriti.
“Tukiichukulia hatua kwamba meli yao haina vibali au
tuifukuze binti yangu atakuwa mashakani.Lakini tukiipiga kimyakimya pia waatajua
ni mimi na bila shaka watamchukilia hatua kama kisasi.”
“Nitaomba
wote muende mkafikirie mkirudi nataka jibu la maana hapa
mezani.”
Walipitia ajenda nyingine katika kushughulika na jambo hilo
kisha kikao kikaisha na watu kutawanyika.Wakati wanaondoka Kilua alipokea ujumbe
wa simu ulioambatana na picha ya binti yake akiwa kwenye huzuni kali sana.Ujumbe
ulisomeka hivi,”TURUDISHIE MUMEO LA SIVYO MWANAO TUTAMSHUGHULIKIA.UNA MASAA 24
KUAMUA.”
Kilua alihisi moyo kwenda mbio sana.Dedani alimshika mkono
mkewe kisha akampeleka hadi pembezoni nakuamua kumsaili.
“Una tatizo
gani?”alisema Dedani akimuangalia mkewe kwa umakini wa hali ya juu.
Kabla Dedani hajajibu na yeye akasikia ujumbe kwenye simu.Aliufungua kwa haraka
alichokutana nacho kilikuwa cha kutisha.Alikutana na ujumbe mfupi ulioambatana
na video fupi akaifungua nakuona ni tukio lile akiwa faragha na Shunie.Mwili
wote ulipika mkambi halafu kuna ujumbe unasomeka hivi wa maneno,”TWALIPO NDO
MAKAMU WA RAIS VINGINEVYO VIDEO ITAFIKA KWA MKEO.”
Dedani aliduwaa
nakhisi mwili wote kufa ganzi hakutaka kumfedhehesha mkewe kwa video ile wala
kuitia aibu familia yake.Ni kitu kilichomkera sana.Kumleta mtu huyo kwenye
serikali ya Kilua ni kuleta tena kundi lililofisadika.
***CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shunie aliwekwa
kati huko ukweni tayari amekwisha semwa kwamba amekuwa mbali na mchumba wake
bwana Pablo ambaye ana majeraha makubwa sana.
“Tangu mwenzako awe
mgonjwa hujaenda kumuuguza kwanini?”
“Kazi hata mimi nilikuwa kwenye
matatizo makubwa na tangu nitoke huko sijapata muda wa kuwa huru kila mara
nimekuwa nikiitwa na rais kupeleka ripoti.”
“Hata kama lakini simu
hujapiga wala kuuliza chochote.Familia ilikwisha kaa kikao tukapanga Pablo
akitoka hospitali harusi yenu ifanyike ndani ya mwezi.Hebu ingieni kwenye ndoa
haraka mpate watoto.”alisema baba Pablo.
Shunie alikwisha poteza
ndoto ya kuolewa kabisa.Hakuwa na taarifa kama Pablo alikwisha toka hospitali na
sasa anaugulia nyumbani.Hata kwenye kikao hiki hakuwa na habari kwamba Pablo
alikuwepo nyumbani .
“Lakini baba sioni umuhimu wakuifikiwahi
kufunga harusi wakati bado tuna majukumu mengi ya taifa.”
“Unajua
kuna maswali kama familia tunajiuliza sana ni kwanini wewe haupo karibu na
mchumba wako.Imekuwa kama nii yeye analazimisha ndoa hii.”
Shunie
alihisi kubanwa ukweni.
“Hapana baba.Nina operesheni maalum kwasasa
sitakuwa na nafasi maalum ya kushughulika na ndoa.”Shunie alitoa kauli hiyio
wasiwasi ukimshika nakumtafuna ini na moyo ukweli hakuweza
kuikabili.
“Msichana mbona kama hatukuelewi?”
Akasikia
mtu anaguna kwa nyuma.Ile anageuka kutizama akakutana na Pablo akiwa kwenye kiti
cha magurudumu.Pablo alisikia kauli ya Shunie kuipeleka harusi mbele.Uso wake
ulivaa huzuni sana kitendo kile kilimpiga fedheha.
Shunie alijikaza
kisha akasema,”Sorry sipo tayari kuendelea na ndoa kwa sasa.”
Pablo
alitizama tu bila kusema chochote huku machozi yakimtoka.Shunie aliwaza kunywa
sumu saikolojia yake ilikuwa imeharibika.
Alipiga
hatua kutoka pale katika uwepo wa Pablo.Nyuma alihisi kutizamwa kwa macho
makali na wake zake.Shunie alijua ametengeneza vita kubwa sana kati yake na
Pablo na kama ikija kugundulika bila sababu za yeye za yeye kukwepa harusi hata
kuwa na msalia mtume.Hata anaweza akaleta mengine magumu yatakayozidi kumdhibiti
kw asana.Shunie alikubali jambo moja moyoni mwake kwamba ni kweli amejikuta
akimpenda mume wa rais Kilua bwana Dedani.Amempenda sana kiasi cha kushindwa
kujidhibiti na hata akahisi kama kweli akiolewa na Pablo ni kuisaliti nafsi yake
hasa kwa kipindi hiki upendo wake kwa Dedani ukiwa bado mchanga wenye joto na
nguvu za kutaka kuthibitisha kwamba ni kweli anampenda Dedani kiukweli na kuwa
na mtu mwingine kujilisha upepo.Penzi hilo ni batili.Alimpenda kwa penzi lililo
jenga ukuta wa kuamini kwamba moyo wake una milikiwa na Dedani nasio mtu
mwingine hata kufikia hatua ya kusitisha harusi yake kwa kisingizio cha
kazi.
“Shunie mpenzi wangu unaniambiaje?”aliuliza Pablo kwa sauti
iliyo na mawimbi ya kekefu za kilio.
“Sihitaji ndoa kwa
sasa.”alijikaza na neno kumtoka huku akikwepesha macho kumkabili
Pablo.
“Unasemaje?”aliuliza Pablo kwa mshangao!
“Samahani sana najua nitakuwa nimewakera sana.Baba mkwe pamoja na ndugu wote
mlio hapa.Kweli nilipenda kuwa sehemu ya famiilia kwa njia ya ndoa.Nilitamani
sana kuwa mke wa Pablo nakukubaliana na ahadi hiyo lakini mambo yamebadilika na
kwa jinsi hali ilivyo sioni kama nitaweza kutimiza ndoto hii.Kwasasa mimi sio
mke wa kumfaa Pablo.Sioni maisha yangu yakiwa na Pablo.Naomba mnisamehe kwa
kuwakwaza.Najua uamuzi wangu utawadhoofisha wengi sana lakini ndo hivyo naomba
mniwie radhi kwa hatua hii.”Shunie alisema maneno hayo akitizama
chini.Alimsogelea Pablo nakupiga magoti mbele zake.Alimtizama usoni akijitahidi
kuwa na ujasiri.
“Pablo nakuomba…ndani ya uvungu wa moyo wako
unielewe kwamba Shunie kwa sasa hawezi kuwa mkeo.Tafadhali kwa heshma uliyonipa
naomba kwa heshma hiyohiyo unipe nafasi hii ya mimi kujitenga na taratibu za
ndoa.Sipo tayari kuolewa na wewe.”ulikuwa ujumbe mzito sana kwa Pablo kuusikia
hata akaanza kuhisi maumivu tena ya risasi kwenye mwili wake na sasa alihisi ni
kama risasi zilipigwa kwenye moyo wake.Alihisi maumivu ya kisaikolojia tena
makali sana katika kusitishwa nafasi ya kumpata Shunie kama mkewe.Alimwangalia
usoni na uzuri wake na macho mazuri lakini sasa yametiwa huzuni.Pabli hakuwa na
mpango wa kumpoteza Shunie hata iweje.Alikumbuka penzi lake lilivyo tamu na
joto la mwili wake picha zote zilipita kichwani mwake kama mkanda nakujua kweli
alimpenda sana mchumba wake.Kitu kilimwambia kichwani kwamba mwanamke huyu
kapata mtu mwingine.Au kutakuwa na operesheni zao lakini hiyo siyo
suluhu.Makubaliano yao hayakuwathiriwa na kazi zao.
“Shunie usiseme
hivyo.Unauchoma moyo wangu.Tafadhali sana naomba nafasi tutarekebisha kama kuna
tatizo.Pamoja tutapata suluhu ya jaambo hili.”Pabli alijikuta akiropoka bila
kujua hasa anategemea kueleweka au la!Jazba ilimpanda na alikuwa tayari kusema
na kufanya lolote ili mwanamke huyu amuelewe.
“Pablo Pablito please
naomba usiufanye uamuzi wangu kuwa mgumu zaidi.Naomba uelewe.You are
strong.Agent please understand what I need.”alisema Shunie akimhimiza kwa
kumhini Pablo.
“Shunie haiwezekani.Nina malengo na wewe.”alisisitiza
bwana Pablo.
“Asante kwa wema wako lakini siwezi.Kufanya hvi ni
kuisaliti nafsi yangu.Naomba tuachane na utaratibu wa ndoa.Pia nasitisha uchumba
kati yangu na wewe kwa sasa.We need some space a lot of things took place we
need time to think.”ulikuwa ujumbe mzito sana.
“Hivi Shunie una moyo
kweli?”
“Ninao lakini haiwezekani kabisa kwa sasa mimi na wewe kuwa
mke na mume.”
Shunie alihuzunika lilikuwa jambo gumu sana kwa yeye
kulifanya.Alimuona Pablo akiwa ameumia sana.
Shunie aliinuka
nakuanza kusimama.Alipeleka mkono nakuvua Pete ya uchumba kati yake na Pablo
akampa.Ndugu za kina Pablo walishindwa kuvumilia,dada wa Pablo alikuja kwa
haraka akamshika Shunie nakumvuta akimtoa,”Ondoka hapa hatukutaki!Toka!”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shunie alijua
kimenuka akaanza kujitoa kwenye fujo zile akitaka kukimbia aondoke.Alitamani
ardhi ipasuke atumbukie nakufukiwa kabisa.
“Dada Manka tulia acha
hasira.”aliomba Pablo.
“Huyu mbwa ana nini hadi anitesee mdogo wangu
kwani yeye ni nani?Aondoke Malaya mkubwaa!Na wewe Pablo achana na huyu kahaba
asiye na shukrani!Mtu imebaki mwezi harusi ifungwe yeye anatuletea season zake
za kifilipino eti nyoko siwezi kuolewa I need some space!Atoe pumba zake
hapa.Shunie potea kabisa sitaki kukuona tena karibu na mdogo wangu.Shenzi
kabisa!”dada Manka alikuwa amekasirika sana.Ilibidi wazee waingilie kati
kutuliza ghasia.
“Mdogo wangu usijali wanawake wapo wengi achana na
huyu kahaba!Watu tunaangaika kuandaa shughuli tunatumia gharama na heshma zetu
halafu pumbavu nyingine inakuja hapa kutuletea isidingo.Aondoke hapa!”Dada wa
Pablo alizidi kukaripia nakutukana hadi matusi ya nguoni.Shunie aliumia zaidi
moyoni mwake.Aliona hapa ataumbuka.Alitumia utaalamu wake wa kijasusi nakupotea
eneo lile.
***
Dedani alimtizama mkewe kwa makini
sana.Hakutaka kumwambia hofu yake ni nini?Aliona atamzidishia hofu
zaidi.
Kilua naye hakutaka kabisa kuonesha ni kitu gani
amepokea.Anatakiwa amtoe mumewe sadaka ilikumnusuru mwanae.Alifikiria
sana.
“Kwani mke wangu imekuwaje?”
“Hapana nimepokea
ujumbe ni kuhusu mtumishi Fulani wa serikali yangu amepatwa na tatizo.”alisema
Kilua.Alijaribu kupotezea na kweli Dedani alinunua uongo huo
nakuamini.Wasichokijua wote walipokea vitisho.Dedani alipokea kitisho cha
kushawishi bwana Twalipo ateuliwe kuwa makamu wa rais.
“Usijali mke
wangu uwe imara.”alishauri Dedani huku akiwa na kibarua kigumu.Walielekea
ofisini kwa rais Kilua alikuwa na mkutano na balozi wa China aliyekuja
kumtembelea.Dedani aliitwa ofisini kwa Serambovu.Hakupenda lakini alienda
kuonana na bwana huyo.Japo hakumpenda ilibidi aende maana kwa sasa imeshaonekana
Dedani kuwa karibu sana na mkewe kiasi kila mtu anahitaji kuonana naye
kiushauri.
Aliachana na mkewe yeye alikatiza korido za ikulu hadi
kumfikia bwana Serambovu.
Walitizamana kwa hasira
sana,”Unasemaje?”
“Naona umekuwa na sauti sana katika kuunda
serikali ya rais Kilua.Kila mtu anamtaja Dedani.”alizungumza bwana Serambovu kwa
kejeli akimpa sifa hewa mtu huyu.
“Kwa hiyo unasemaje.”
“Hapana sina maana mbaya ila kama chifu wa staffu wa ikulu lazima niwe
nawasiliana na wewe hasa nipatapo jambo lolote.Kwa sasa tupo kwenye mchakato wa
kuunda serikali hivyo kila mtu anatakiwa kuriopoti kwako.”
“So
what?”
“Kuna ujumbe nimepokea kuna mtu anahitaji muonane kujadili
kuhusu mchakato huu.Hakunipa maelezo sana ingawa natamani kujua kuna jambo
gani.Ni vile Serambovu hapendi kuingilia vya watu.”
Dedani kidogo
amrukie lakini akajidhibiti,”Kuwa makini na kauli zako.”
“Kwa vyote
umesikia hii ya kuwa siingilii vya watu?Mtu wa aajabu.Kwa taarifa tu mkeo namjua
kiundani.Nilikuwa wa kwanza kwake na hata ufanyeje bado nitakuwa mwanaume wa
kwanza maishani mwake.Mimi ndiye niliyeondoa usichana wake.Put this in your
thick head I was the first na daima utakula makombo!”yalikuwa maneno makali
sana.Ilionekana dhahiri Serambovu hawezi kuudhibiti ulimi wake.Cha msingi ni
kuendelea kukoleza chuki kwa Dedani.
“Serambovu chunga ulimi
wako!”alionya Dedani.
“Hahaha!”alicheka kicheko cha dharau,kisha
akaendelea,”Ohh!Dedani hujui ni kiasi gani zile nyakati aligugumia kwa Ohh!Papa
Sera unanifikisha!My name she will always remember.”
Dhihaka ilivuka
mipaka sasa.Dedani alikuwa amefika kikomo ila akajikaza kwa heshma ya
mkewe.Alijikuta mikono ikimtetemeka nay eye kutamani kumshughulikia vizuri bwana
huyu lakini alijirudi.
“Nipe ujumbe.”
“Mtu anaitwa Twalipo
kaomba kuonana nawe.Mkutane Chemchem Hotel aanakusubiri fanya juhudi
umfikie.”
Dedani alikuwa amekasirika sana lakini ile kkutajiwa mtu
anaitwa Twalipo kulimgutusha nakumfanya asisimke mwili mzima kwamba mtu huyu ni
nani?Iweje aombe nafasi yakuzungumza naye?Ana ajenda gani hadi aweze kutuma
ujumbe huo wakuomba kikao kupitia Serambovu?Huu ulikuwa mzizi mwingine wenye
kichefuchefu!
Dedani alijikuta akiduwaa!
***
Kilua baada ya mkutano na
balozi wa uchina alitoka nakuelekea sehemu nyingine ya ikulu.Akiwa katika
bustani za ikulu alipokea tena ujumbe.
“TUNAMTAKA DEDANI NDIPO
TUMUACHIE MWANAO.HATUTAKI AHUSIKE NA MCHAKATO WA KUUNDA SERIKALI
YAKO.”
Kilua alishtuka sana!Ina maana tayari wameshajua uwepo wa
Dedani katika uundaji wa serikali?Moyo ulipiga paa!Aligutuka kutoka alipokuwa
nakupiga simu kwa mumewe?
“Uko wapi?”aliuliza Kilua baada ya mumewe
kupokea simu ile.
“Naelekea Chemchem Hotel.”
“Unaenda na
nani?”
“Nitakuwa mwenyewe.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ok chukua gari
lenye namba za ikulu.Na waambie wakupe level F bodyguard mmoja.”alisema Kilua
akijua fika anamuandaa mumewe kwa jambo bay asana.Alikata simu kisha Kilua
alituma ujumbe kuijibu ile namba iiliyompigia awali.
***
Zee Kavu aliitengeneza tai yake vizuri baada ya kusoma
ujumbe ulioingia kwenye simu yake.
“Kasemaje?”
“Kasema
mumewe yupo Chemchem Hotel.Tutume vijana wetu.”
“Siatakuwa na ulinzi
mkali sana.”
“Hapana alipunguza kiwango cha ulinzi kampa mlinzi
level F tena mmoja.Huyu tutaweza kumdhibiti..”alisema Kavu sasa alinyoosha
mikono ya koti lake huku uso wenye ukavu ukiachia kwa tabasamu la
ushindi.
“Timu ipo tayari?”
“Yes.The president has just
offered her husband tumbadilishe kwa binti yake.”alisema Zee Kavu.Aligeuka na
kumwangalia Bwana Tufe wote walitabasamu vizuri.
“Dedani ni problem
hatuna imani kama ataweza kumuingiza bwana Twalipo.Watu kama Dedani ni wajanja
sana anaweza hata kumuua Twalipo akiwa tayari ni makamu wa
rais.”
“Hivyo tumfanyeje?”
“Ni simple tu Dedani afutiliwe
mbali.Yeye atakuwa mfano kwamba Kilua hana ubavu kwetu
sisi.”
“Ni simple tu Dedani afutiliwe mbali.Yeye
atakuwa mfano kwamba Kilua hana ubavu kwetu sisi.”
“Dedani ni
tatizo sana kwa upande wetu.”
“Tudhibiti hili jambo just make sure
tuna best team ndo itamshughulikia.”
Makubaliano yalikuwa
yamefikiwa na sasa ilikuwa ni hatari kubwa sana.Walionekana vijana wa kazi
wakiondoka kuelekea Chemchem hotel kumshughulikia Dedan katika mkutano
wake.Lakini kulikuwa na maswali kama Dedani anaenda kutekwa kwanini wampe
mkutano na Twalipo?Ikiwa Dedani ni mshauri mkuu wa Kilua ambaye anategemewa
kuonekana kama na sauti kwanini wamteke?Ushauri wake utakuwa na maana gani kama
akiwa mikononi mwao kuliko akiwa kwa Kilua?
Jua lilikuwa utosini.Mji
ukiwa na pilikapilika na tayari kamata kamata ilianza kwa wale walioshukiwa kwa
namna moja au nyingine kushiriki kummaliza rais Kisusi na serikali yake.Hii
kamata kamata ilienda kimya kimya huku watu wakijishtukia wakipotea bila kuwa na
maelezo wala nyayo za kufuata.Taharuki ilikwisha pita kila pembe na kila mwenye
ndugu aliyepotezwa alikuwa na mkururo wa maswali ya sintofahamu kuhusu mwenzake
aliyepotea.
Japo serikali ya Kilua ilijua vyema jambo hili litaleta
mushkeli na umma ungetegemea majibu ya kuridhisha.Lakini aliona vyema yeye
binafsi kukamata mnyororo wa hawa wahusika wa chini ilikuondoa uozo huo
kotekote.Japo alijua kwa njia hii wakubwa wa ule mtandao watajitahidi kubadili
mbinu na njia ilikudhorotesha hatua zake.Ila alijipa moyo kwa njia ile
angefanikiwa tu japo kwa mbine na hata kama asingefika anapotaka lakini atakuwa
amefanikiwa kutikisa nyavu zilizoonekana ni chuma!
Katika hotel ya
Chem chem lilikuja gari lenye namba za ikulu nakusimama mbele ya hoteli hiyo
kisha alishuka bwana Dedani.Kwa kuwa alijua umuhimu wa mkutano huo aliona ni
vyema angeenda peke yake kukutana na Bwana Twalipo ili kuwe na uhuru wa kutosha
wakumfanya yeye binafsi aweze kumpeleleza bwana huyu.Alihisi uwepo wa mlinzi
ungemwondolea ujasiri wa yeye kuzungumza na Twalipo.Pengine mazungumzo
yangebebwa na mlinzi japo walinzi hawa walikuwa wamekula viapo kutotoa siri za
wanaowalinda lakini kwa jinsi alivyoona mkewe kazungukwa na wasaliti allijikuta
akikosa imani na hata walinzi waliohodari kutunza siri.
Dedani
alimuelekeza mlinzi kulinda gari na yeye kuingia ndani.Alielekea moja kwa moja
hadi mapokezi.Alijitambulisha nakuuliza kama kuna ujumbe wowote uanohusiana na
jina lake.Msichana wa mapokezi aliangalia kwenye kumbukumbu nakukuta bwana
Dedani kawekwa kwenye miadi na tayari kuna meza ilishatengwa maalum na muhusika
anamsubiri.Msichana wa mapokezi alimwita mhudumu wa pale hotelini kisha
akamwelekeza amuoneshe bwana Dedani wapi pa kwenda.Hotel ilikuwa tulivu
wakionekana watu waliostaarabika wenye ukwasi wakipata huduma katika hotel
hiyo.Dedani alfikishwa kwenye meza iliyoandaliwa.Alimkuta bwana mmoja hivi
ameketi.Alikuwa mtu mzima mwenye mvi za busara.Dedani alikaribishwa na mtu
yule kisha yeye binafsi akaketi.
Walisalimiana kwa bashasha.Japo
bashasha la Dedani lilikuwa batli.Moyoni alikereka akijua watu hawa wamekuwa
mwiba kwenye familia yake na badala ya mkewe kulitumikia taifa bila wasiwasi
watu hawa wamekuwa wasiwasi kwa mkeo!
“Bwana Dedani mimi ndo Mr
Twalipo.”alisema Mzee huyo akionesha tabasamu lake.Kisha alitoa makadabrasha
yake akaweka mezani.
“Hili ni faili langu unaweza kuliangalia kwa
muda wako kupata maelezo kunihusu mimi.Rekodi yangu ni nzuri isiyo na dosari.Ni
naamini nina uwezo wa kulitumikia taifa letu kama naibu rais wa taifa
letu.”alisema mzee huyo kisha akampa Dedani faili lake.
Dedani
alichukua mafaili ya bwana yule.
“Lakini bwana Twalipo siunajua
utaratibu wa kumteua naibu rais lazima uchunguzwe na usalama wa
taifa?”
Hilo kidogo lilionekana kumlemea bwana Twalipo kiasi
alijikohoza kidogo kurekebisha koo lake.
“Ningependa usalama wa taifa
wasifanye upelelezi kunihusu.Nina rekodi safi kitaifa na hata ndani ya chama
chetu tawala wanalijua hilo.Hakuna aliyeomba hadi sasa kupewa nafasi.Najua rais
ndiyo anapendekeza ni nani wa kumteua.Ila mimi nimeamua kujitokeza mwenyewe
nitoe ombi langu ili jina langu lipigiwe debe kisha niteuliwe na rais kuwa
makamu wake.”alishauri bwana Twalipo.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dedani alifikiri
kidogo kisha akasema,”Kuna wakati inabidi tuache utani.Hivi unanichezea
ngonjera wakati unajua wewe ni kibaraka unayetaka kupandikizwa kwa serikali
ya Kilua ili mje kulinda maslahi yenu?”
“Bosi lakini siumeshapewa
maelezio?”
“Tuache kuigiza!”alisema Dedani kwa sauti iliyopanda
kidogo.
Twalipo alinywea kiasi akitizama kwa mshangao.Ni dhahiri Uso
wa Dedani ulibeba hasira ambayo haikujificha hata kidogo.
“Hatuigizi
mkuu.”alijitetea bwana Twallipo.
“Huu upuuzi wa kunipa mafaili
yako ni ujinga tu.Mimi ninajua kabisa kwanini hutaki kuchunguzwa.Yawezekana
wewe ni msafi huna dosari ila shida moja ni kuwa wewe ni kibaraka ni hicho
ndicho unachokiogopa sana.They will brand you as a traitor to the nation and
people like you are to be eliminated from authority!”alitamka kwa hasira
sana.
“Lakini bosi hatuna haja ya kufika huko.”
“Nisikilize kwa umakini sana wewe ni mpuuzi!Tena hufikirii.Unajua hali halisi
ilivyo kwa sasa kwenye taifa hili?Makamu wa rais sio mtu wa mchezomchezo
tu.Unaleta utani.Mimi siwezi kupendekeza jina lako liwepo kirahisirahisi
tu.”
“Dedani inabidi ukubali.Unajua kama mkiniweka kwenye wadhfa huo
na wahakikishia kabisa mtoto wenu mtampata akiwa salama.Endapo mtaenda kinyume
na hilo tusije laumiana.”alisema bwana Twalipo.
“Hahaha wewe unaleta
utani ndugu.”
“Hapana sitanii kwa kweli.”
“Kwanza nataka
nikuhakikishie endapo mwanangu atadhurika zaidi ya vile mlivyomfanya.”alisema
Dedan kwa sauti iliyobebwa na hisia,kisha akaongeza,”Nitakuua kwa mikono
yangu!”
“Unanitishia?”aliuliza bwana Twalipo
“Sikutishii
bali ni onyo nakupa dhidi ya hatua zako!”Dedani alishikwa na hasira.Urais wa
mkewe ulikuwa kama mwiba hvi hadi sasa familia yake haieleweki.
“Kwa
hiyo nataka nikwambie jina langu linatakiwa kugeuka Vice-president Twalipo!Naona
hapa hatuelewani tutaelewana kibabe zaidi.”alisema bwana Twalipo.
Dedani alikereka sana na matisho hayo kiasi cha kuchefukwa kabisa na maelezo
hayo.Huyu wa mtu alioneka kuwadhibiti na sasa aliona kabisa kwamba wapo kwenye
kizuizi.
“Utahakikisha jina langu linapita nategemea kuapishwa ndani
ya muda mfupi sana maana kuna ofisi nyingi sana zipo bure.
Dedani
alivuta pumzi ndefu na kuzishusha alitamani kwenda msalani kwanza anawe uso
kuondoa jinamizi lililompata.Dedani aliinuka nakuelekea moja kwa moja hadi
mlani.Alinawa uso kisha akajifuta kisha alitizama kioo mbele yake akijitahidi
kujidhibiti alitamani amtungue yule bwana kwa ngumi kadhaa lakini
akashindwa.
Akiwa pale alishtukia mlango ukifunguliwa kisha akaingia
yule bwana.Dedani aliona huu ndo mwanya wake wa kumshughulikia bwana
huyu.Alichofanya nikumrukia nakuanza kumshushia kipigo.Alimkwida na kwenda
kumpigiza kwenye karo la kunawia.Alimpigiza mara kadhaa kwenye paji la usoo!Kwa
kila pigizo lilimfanya bwana Twalipo kuhisi kishindo kizito kikipiga na kichwa
kumtikisika hadi ubongo wa ndani hali iliyofanya kuona taswira ya kuona ikififia
na kupoteza kabisa ufahamu wake.Damu zilianza kutota kwenye paji la uso na
tayari alikuwa amempasua sehemu kubwa.Dedani alimuachia bwana huyo.Alijua huyu
mtu hata aamka.Alichofanya alinawa mikono kisha akatoka nje.Alikatiza korido
kadhaa akaja kutokea ukumbi wa hoteli kwenye mgahawa kisha akanyoosha kutoka
nje.Ile alikatiza hapo nakuelekea mahali gari lilipo.Wakati analiona kwa mbali
alishangaa kuona kuna watu wanamfuata kwa nyuma ile kugeuka aliona mabwana
wawili waliovalia suti nyeusi wakimjia.Dedani alijifanya kutowapatiliza kisha
akaenda kwenye gari lake.Alipotaka kuufungua alihisi kusimamiwa na wale watu
wawili.
“Samahni bwana tunaomba mazungumzo na wewe.”alisema mmoja
wao.Dedani alishtuka sana na nywele kumsimama.
“Kuna
nini?”
“Tunaomba usiondoke.”wa pili alijibu.
“Nina
haraka na wahi kwenye shughuli zangu muhimu.”alijitetea.
“Hili lina
umuhimu sana na bila shaka unapaswa kuwa mtaratibu.Tunaamini wewe ni mtu
mstaarabu.”
Dedani hakuona kheri kwenye hizo kauli na kwa namna moja
au nyingine machale yalimcheza na kama angebweteka basi angepoteza.Hawa wanataka
nini.Lakini kuna jambo lilimshtua,alimuona mlinzi wake akiwa kwenye usukani
ameketi kwa kuwa alivalia mawani meusi bila kujigusa Dedani alihisi huyu bwana
atakuwa amelala.Na kama angekuwa maccho bila shaka angesaidia kukabiliana na
hawa watu.
Dedani alivuta pumzi ndefu
nakuzishusha.
“Ok.Natakiwa niwasubiri kwa hapa au
wapi?”
“Ingekuwa vyema kama ungekuja ofisini kwetu.”
Dedani alitikisa kichwa kukubali kisha alisogea hadi kwenye gari kumtaarifu
mlinzi wake.Alienda upande wa pili wa dereva.Kioo kilikuwa kimeshushwa alimgusa
bega lakini mlinzi hakushtuka!Alipotizama maeneo ya tumbo aliona michirizi ya
damu ambayo bado ilikuwa ikitoka tena bado mbichi kuonesha tukio hio limetokea
mida hiyo!Dedani alichichimkwa!Ilibidi awageukie wale watu wawili.Hakutaka
kuwaonesha kama kuna dosari kwenye gari lake.
Walianza kuelekea
kurudi hotelini.
“Tukio ulilofanya chooni tumeliona lote.Tutakuweka
chini ya ulinzi.Polisi wanakuja!”
Dedani alihisi nywele
kumsimama!Hilo lilikuwa tatizo kubwa sana.Dedani alisita kwanza kupiga hatua
alipsoikia jambo hilo.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hawezi kwenda ndani
polisi wa mkamate hata iweje.Huku nikuleta skendo nyingine ambayo ingemtafuna
maana hadi sasa ana operesheni ngumu sana na kkitendo cha kumzimisha bwana
Twalipo ni hatua kuchafuka.Jambo hili halikutakiwa lijulikane.
“Tulikuona kupitia kamera zilizofungwa.Tupo makini sana katika usalama wa hoteli
yetu.Tunaoushahidi kwamba umemuua mtu hapa hotelini.”
Dedani alitaka
kumpigia mkewe kusuluhisha jambo hilo lakini hakuona umuhimu.Kichwa kilichemka
huku akijiuliza a,liyemuua mlinzi wake ni nani?Wakati anawaza hayo huku
akisitasita alishtukia gari ikija kwa kasi nakureeshwa mbele yao.Walishuka
vijana wenye silaha kwa haraka sana nakumvamia Dedani huku wakiwadhibti wale
walinzi wawili wa hoteli.Walinzi walitaka kujibu mashambulizi lakini wakazidiwa
kete na vijana hao.Dedani akadakwa nakuingizwa kwenye gari.Kikaletwa kitambaa
cheusi.Tukio lilikuwa la haraka sana ni kama watu hawa walijipanga wakijua hatua
zote zitakavyotumika hadi kufikia kumkamata bwana Dedani.Tayari alikuwa chini
yao.Kitambaa cheusi kikafungwa usoni mwake.Kisha gari ikatiwa gia nakuanza
kuondoka kwa kasi ya ajabu.
Dedani alifuurukuta alihisi fika hawa
waliomfuata hapa wamejipanga na itakuwa walijua uwepo wake eneo hilo.Hawahawa
ndo wamemdunga kisu mlinzi wake na bila shaka hawa ni timu ya Twalipo nambari
moja na bila shaka kwa kuwa wamemkamata na kama wamejua Twalipo kazimishwa naye
basi hawana budi kummaliza na Dedani.Gari ilikamata barabara nakuanza kuondoka
eneo lile.
Wakati gari lile linatoka kwenye geti ndipo gari la
polisi nalo linaingia kwa kasi ya ajabu.Wakawa wamepishana.Dedani akawa hatarini
zaidi ni bora hata polisi wangemtia nguvuni kuliko watu hawa.Sasa alikuwa kwenye
mikono mibaya sana.
Gari lilikata barabara za mji huo.Dereva wa gari
alijitahidi kuondoka katika eneo la mjini kuepuka shari na wanausalama.Lakini
wakati akitoka mjini alishtuka kuona kupitia kioo ccha pembeni gari likimfuata
kwa nyuma kwa mwendo Fulani ambao ulitilia shaka.Dereva alijihadhari nakujaribu
kucheza karata zake amzubaishe huyo anayemfuatilia.Ishara ya mtu kumfuatilia
ilikuwa mbaya sana kwa dereva huyu kiasi alihisi kama mipango yao sasa haitakuwa
vyema na inahitajika nguvu ya ziada kudhibiti ufuatiliaji wowote
unaojitokeza.Dereva aliwapa ishara vijana wake.
“Hiyo gari nyeusi
naona inatufuatilia.”alisema kwa hofu.Vijana wenzake wazee wakazi walitizama
kisha wote kwa pamoja walianza kuchukua silaha zao nakuzikoki!Tayari kwa lolote
na kama vita na iwe vita!Vichwani mlikuwa na maswali lukuki kwamba endapo
watashindwa itakuaje?Wanakumbuka walipewa onyo kutoshiriki kutumia nguvu endapo
watakuwa katikati ya jiji.Hapo ingewalazimu wanausalama kuingilia kati!Na kama
ingetokea hivyo bila shaka operesheni ile ingechukua nafasi nyingine
kabisa.Tayari walikwisha muweka Kilua kwenye kikaango cha kumfanya atekeleze
wanavyotaka ikiwemo kuweka wepesi wa mumewe kutekwa tena.Hiyo pekee kama
ingesikika kwa vyombo vya usalama ingekuwa hatari zaidi na pengine wangetumia
mbinu zote kulidhibiti kundi hili.Haikuwa hali nzuri kujulikana kwamba rais
kawekwa mtu kati na tayari wanampa vitisho vya hapa na
pale.
Walikatiza barabara kadhaa nakufanikiwa kutoka nje ya mji bila
kusababisha vurugu yoyote.Walipoanza kukamata barabara iliyotoka nje ya mji
walishika kasi nakuzidisha mwendo wao wakijitahidi kupotelea mbali.Lakini sasa
waligundua fika wanafuatiliwa na gari iliyokuja kwa kasi.
Kitendo
hicho kikawa kengele ya hatari masikioni na bila shaka walitakiwa kushughulika
vilivyo la sivyo yangetokea wasiyotegemea.Mwendo wa dakika kama tano gari
lililokuwa nyumba lilikuja kwa kasi nakupita mbele yao nakuzidisha mwendo
zaidi.Mita chache mbeleni walishtukia lile gari likigeuka kwa haraka nakuanza
kuwafuata!Lengo likiwa kugongana au ishara ya kwamba mmoja wao anapaswa
kusimama.Nao pia hakuwakutaka kuonekana mabwege walikaza mwendo bila kuonesha
dalili ya kusimama!Kiburi kwa kiburi.Lakini dereva watekaji aligundua jambo
endapo angegongesha gari kungetokea madhara na kama angeshinda wasingekuwa na
mwanya wakuondoka bila shaka gari litakuwa na uharibifu mkubwa sana.Ilibidi
afikiri mara mbili kati ya kugonga na kukwepa au hata asimame aone shari ya adui
ni nini?
Lakini tofauti na mategemeo gari ile ilikuja nakuwagonga
huku ikiwasukuma!Mtikisiko mkubwa ulisikika!Mkwaruzano ukatokea baina ya gari
mbili hadi cheche zikaonekana.Dereva aliyumba kiasi akajikuta akiachia
usukani!Dedani ajigandisha kwenye kiti kukwepa mtikisiko wa gari.
Ndani ya muda mfupi gari la watekaji lilikuwa limepoteza mwelekeo nakuingizwa
kando ya barabara likajipigiza kwenye mti mkubwa!Kitendo cha ghafla
sana!
Gari lililowagonga lilishika breki kali.Kisha mlango
ukafunguliwa ndani akatoka Shunie akiwa bastola.Kwa kasi ya ajabu aliwafuata
nakuwafikia.Alifika kwenye kioo nakumuona dereva akijitahidi kutoka akamuwekea
bastola kichwani!Shunie akamuamuru atoke nje kimya kimya na wenzake kisha wamtoe
Dedani.Zile purukushani zilifanya waangushe silaha zao.Wakatoka huku wakiwa
wameumia kiasi kufuatia kugongwa kwa gari lao.Walisimama nje ya
gari.
“Hamuwezi shindana na serikali hata siku moja!Huo upuuzi wenu
unaishia hapa mbwa nyie!”alisema Shunie akiwa amevaa sura ya kazi.Aliwafyetulia
risasi za paji la uso wote!Kisha alimfuata Dedani akamchukua akiwa bado
amefungwa.Alimuelekeza kwenye gari lake wakapanda nakuondoka kwa kasi ya
ajabu.
***
Mvua ilikuwa inanyesha kubwa
sana.Ilikuwa nzito iliyoshuka kuinywesha ardhi kame.Pengine ilikuja kwa
furaha!Shunie alikwisha mfikisha Dedani kwenye eneo ficho ambalo hakuna kidudu
mtu angewafikia.Huko aliweza kumtoa kitambaa cha usoni pamoja na kamba alizokuwa
kafungwa nazo.Dedani alihisi kichwa kizito sana.Aliishtuka kuona ni Shunie ndo
kamuokoa.Dedani alihisi fedheha kwa jinsi msichana huyu alivyomtolea maneno
machafu.Alihisi hastahili kabisa kusaidiwa naye.Lakini sasa Shunie kawa mkombozi
wake.Katokea wapi?Alijuaje Dedani yupo matatani?Ilikuwa siri kuu.
“Shunie how?...”
Shunie aliweka kidole kwenye mdomo wa Dedani
akimuashiria anyamaze.Pengine hakuna haja ya kuongea sana.
“Shsss!Cha muhimu you are safe with me.”alisema Shunie.Alienda akachukua mvinyo
mkali nakumimina kwenye glasi mbili kisha alikuja nakumkabidhi Dedani glasi
moja.Ulikuwa ni muda wakusheherekea operesheni maalum.
“Sipendi
kutumia pombe mara kwa mara.”alisema Dedani.
Shunie alitabasamu
kisha akasema,”Nimeanza tangu uliponifokea.”
Dedani alitizama chini
kwa aibu.Hakuona neno lakutumia kulikuwa na msongo na hali ilikuwa
imechemka.Walikuwa peke yao.
“Kwani hapa tupo wapi?”
“Hapa tupo balcksite.Siwezi kukwambia ni wapi?Hakuna anayejua ulipo isipokuwa
mimi.”
“Ilikuwaje ukajua nimevamiwa?”
Shunie alifikiri
kidogo kisha akatabasamu,”Hiyo ni top secret samahani mkuu siwezi kukwambia.Just
know you are safe with me.”
Dedani aliheshimu jambo hilo.Akakumbuka
waziwazi kwamba alimshambulia bwana Twalipo na tayari ushahidi upo.Mwili wake
ulihofu kama mkewe akijua na kama mahasidi wa mkewe watatumia jambo hilo
kumuadhibu.
“Shunie.”
“Bee?”
“Nimemshambulia
Twalipo.”
“Ndo nani?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilibidi Dedani
amweleze ukweli tangu apate vitisho vya bwana huyo hadi sasa.Hilo lilikuwa
tishio kubwa sana na tayari limemtia doa kubwa sana.
“Ungeniambia
tangu mwanzo wala usingechafua mikono yako kwa hao masaliti wa
taifa.”
“Kwa aajili ya rais ilibidi nifanye hivyo.Nachukia sana
wanavyomhangaisha mke wangu.Mambo yalianza kuwa mazuri lakini sasa naona kama
doa linguine linajitokeza.”Dedani alikamata ile glasi nakunywa.
“Una uhakika ulimuua?”
“Ndiyo.Na ndo maana wale walinzi walisema
wameona nikimshambulia kupitia kamera zao za cctv.Ushahidi wanao.”
Shunie alifikiri kidogo.
‘Kama ushaidi huo haujafika polisi au kama
wanao kuna namna yakuufutilia mbali.Lakini ikiwa habari itavuja kwa umma
tujiandae maana adui wa familia yako watatumia kama fimbo ya
adhabu.”
Dedani alionekana kuwa na mawazo mazito sana kiasi
aliogopa.Lakini uoga usingekuwa suluhu ya kutatua jambo hilo.
“Shunie nipo tayari kukupa chochote kile ila naomba unisaidie kuondoa ushahidi
huo?”alisema Dedani akiwa amedhamiria.Shunie alikumbuka maneno makali
aliyotolewa na bwana huyu.Hasira ilimpanda sana kiasi alitamani kumfanya Dedani
amlipe kwa gharama kubwa sana.
Shunie alifikiri kisha akadhibiti
hasira zake,”Dedani huhitaji kuomba.Just ask for it I will be there for
you.”ilikuwa kauli iliyotoka moyoni mwa Shunie.Kitu kikachipuka moyoni mwa
Dedani akajikuta akimsogeelea Shunie akamkamata nakumvuta kwa pupa.Shunie
alilegea sana na pumzi kutoka kwa pupa alikuwa amesalimu amri.Kile alichoona ni
muhali kutokea kilikuwa kinaenda kutokea.
Ilikuwa muda wa
mahaba.Shunie akili ilihama akajikuta machozi yakimtoka sana.
“Tatizo nini?”
“Naogopa sana Dedani!”alisema akiuficha uso wake kwa
mikono.
“Usiogope huenda unachohisi kikawa upande wa pili
pia.”ilikuwa kauli iliyomuamsha Shunie kutoka kwenye giza.Alitafsiri fika kuwa
labda Dedani anamaanisha na yeye anampenda pia ila mazingira hayakuruhusu.Dedani
ni mume wa rais Kilua.Ni kioo cha jamii kuna mambo anapaswa
kuyakwepa.
Shunie alimkumbatia kwa nguvu zote huku akilia mfululizo
bila kujielewa kama ni furaha au huzuni.
Kilichofuata hapo kilikuwa
siri yao.
Alihisi ngozi yake mkabala naya kwake.Alihisi pumzi zake
na harufu ya mwili wake ilimjia vizuri kwenye pua zake kiasi ikaamsha hisia
fiche za mwiii.Dedani alimsahau mkewe kwa muda.
***
Serambovu alikuwa amejiwa na
mkuu wa polisi katika ofisi yake pale ikulu.Serambovu akiwa amepokea flash disk
alikwisha ipachika kwenye tarakilishi yake na sasa alikuwa akitizama video
iliyokuwa ikicheza.Serambovu alitabasamu kumuona adui yake akifanya shambulizi
kali sana lililopelekea mtu kufariki dunia.
Serambovu
akatabasamu.
“Unakopi ngapi?”alimuuliza mkuu Yule wa polisi jimbo la
Capital.
“Ninazo mbili hiyo niliyokupa na moja imebaki kwaajili ya
usalama wa polisi.”
“Ulitaka kufanyaje na ushahidi huu?”Serambovu
alimuuliza.
“Hii ni familia ya rais.”
“Rais Kilua
anafuata sheria sana sidhani kama atalegeza jambo hilo.Jiandae na upelelezi na
popote Dedani atakapoonekana akamatwe haya ni maagizo kutoka ikulu.Sheria ni
sheria tu.”alitoa kauli hiyo bwana Serambovu akijiandaa kwa
bomu.
“Lakini huoni kwamba tutamuathiri rais
Kilua?”
“Mimi ndo chifu wa ikulu kauli ya rais inapitia kinywani
mwangu nakuagiza popote atakapoonekana Dedani kamateni yeye.”alisisitiza
Serambovu.Ilibidi mkuu wa polisi aondoke huku akiacha maswali lukuki
itakuwaje?Serambovu alifungua microsoftword tayari kuandika makala ndefu inayo
husu kuhusika kwa mume wa rais Kilua kwenye mauaji Hotel ya Chemchem!IUlikuwa
mtihani mwingine mzito sana!
Ushahidi ulioangukia
mikononi mwa Serambovu ulikuwa tosha kumpa kiburi cha kumdhibiti Dedani na
hakika asingefanya lolote mbele yake ikiwa yeye Serambovu anamiliki ushahidi
mkubwa wa mauaji yaliyotekelezwa na mume wa rais Kilua.Hili lingekuwa pigo
linguine kubwa sana kwa familia ya rais Kilua ambalo
lingemsambaratisha.Serambovu alitabasamu vizuri sana kuona neema ya kibabe
imeangukia upande wake kwa mara nyingine tena na sasa yeye ndo mcheza karat
azote.
Serambovu alikwisha agana na polisi aliyemletea ushahidi
ule.Kisha alichukua simu yake na kupiga namba Fulani akaweka simu masikioni.Simu
iliita kwa muda huku akisubiri kwa shauku kubw.Alikuwa hatua nzuri kwa mipango
yake.
“Ndiyo chifu unaendeleaje?”
“Kwema mkuu.Nimepata
jambo jema nahakika litakuwa mwiba kwa madam president safari hii lazima abwage
manyanga.”
“Jambo gani hilo?”
“Ninao ushahidi ukionesha
akishiriki mauaji.”
“Ushahidi gani?”
“Kuna mtu anaitwa
Twalipo ndo ameuawa na mume wa rais.”alisema Serambovu.
“Very
good.”sauti ya upande wa pili iliitikia kwa ukavu.Serambovu akatabasamu
nakufurahia kwa jambo hilo akijua sasa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mambo yalianza
kuiva katika uandaaji wa mipango yake.Serambovu alifungua droo nakutoa picha
yake akiwa na rais Kilua katika moja ya makongamano makubwa.Alijuafika
wanatakiwa kuwa pamoja lakini sio Dedani awepo.Kilua alikuwa mali
yake.Amethibitisha hilo mara kadhaa na hata kufikia hatua yakujiona yeye mungu
mtu kwa Kilua.Kila nyakati alikuwepo hata alipopewa madaraka ghafla bado
alikuwepo yeye kwa wakati ule akisimama upande wake.
“You are mine
alone and we shall keep this power together.”alijisemea Serambovu.Akiwa pale
alishangaa kuona Kilua akiingia ghafla ofisini kwake.
Serambovu
akainuka akimtizama.
“Shani ni mwanao.”alisema Rais Kilua
akimwangalia SErambovu usoni kwa umakini wa hali ya juu.
Serambovu
akashtuka sana.Hii ni mara ya pili Kilua anarudia msemo huu ila tofauti kwa sasa
ni tofauti na kipindi kile.Wakati ule ilikuwa kama fumbo na sasa ni waziwazi ana
mwambia usoni.Serambovu aliratibu mipango ya kutekwa kwa Dedani na mwanae akijua
anamkomoa kumbe anaikomoa damu yake.
“Chochote unachokifanya mfikirie
huyo mtoto.”ulikuwa ujumbe mzito sana kwa yeye kuupokea na hakutegemea kabiisa
kama ingetokea kwa jambo kama hilo.Japo alihisi nakukiri kuna uwezekano wa Shani
kuwa mwanae lakini hakuwa na uhakika asilimia mia moja.Kilua alikuwa amemuweka
mumewe kiganjani pamoja nakushiriki kuihujumu ndoa yake lakini Serambovu
hakuwana uhakika kama kweli Shani anaweza kuwa mwanae.Alijua kwa vyovyote Kilua
alikuwa anamrubuni mumewe lakini angezaa naye kwa namna moja au
nyingine.
Serambovu alisogea akamkumbatia Kilua.
“Najua
mimi nawewe tunashea damu.Nilihisi lakini sikuwa na uhakika kama kweli mtoto
huyu ni wa kwangu.Nakuahidi kushirikiana nanyi katika kumrudisha mikononi
mwetu.”
“Ila naomba jambo moja kutoka kwako.”alisema Kilua akijitoa
mwilini mwa Serambovu.
“Anything for you madam
president.”alisisitiza Serambovu akijiamini.
“Don’t tell Dedan
anything.”alisema Kilua.
“Anapaswa ajue.”
“Nyinyi wote
mna nafasi katika maisha yangu.Wewe ulikuwa mwanaume wangu wa kwanza.The
greatest love of my life.The first of my youth and womanhood.Young mighty love
in the sun.”alisema Kilua akisisitiza maneno yake.
Kisha Serambovu
akauliza,”Vipi kuhusu huyo bwege aliyeshindwa kukupa hata mimba.Kazi kulea
watoto wa watu.”
“Usimdharau.Yeye ndo wa mwisho kwangu.Ndo mume
wangu ndo mwanaume wa kuishi naye and I know I have found reasons to love him
more.He won’t betray me.”alisema Kilua akijiamini.
Serambovu
alifikiri kidogo kisha akasema<”Sawa madam president tutaona.Asante kwa
kunizalia mwana.”
Kilua hakusema kitu kuna wakati alijutia jambo
hilo.Lakini ilikwisha tokea.Na sasa anaujauzito mwingine wa Serambovu.Kumbe
wakati wanaongea maneno yale tayari Dedani alikwishafika ikulu na Shunie na
walikuwa wanaelekea ofisini kwa Serambovu.Dedani alifungua mlango bila hodi
nakuwafanya watu hawa washtuke sana.Kisha Dedani alienda hadi ilipomeza ya
Serambovu akachukua kidude Fulani cha kurekodia sauti kisha akakiwasha.Lilikuwa
tukio la ghafla sana kiasi cha kumfanya Kilua na Serambovu watetemeke.Shunie
alikuwa kasimama nyuma ya Serambovu.Leo patachimbika hapa!
Kilua
aliwahi nakukishika kidude kile kisha akakitupa chini nakukikanyaga
nakukikvunjavunja.Serambovu roho kidogo imsimame.Kuwahi kwa rais Kilua ilikuwa
pona yake.Kitendo cha Dedani kuingia ghafla nakuelekea moja kwa moja kwenye meza
kisha akachomoa kifaa hicho kwa lengo lakusikiliza hayo mazungumzo ni dhahiri
alikuwa ameweka huo mtego kwa mida mrefu sana na siajabu kuna mengi
ameshayasikia lakini inakuwaje aweze achilia mbali wazo la kutegesha mtego
hulo?
“Mme wangu ni nini unafanya sasa?”aliuliza Kilua.
“You can’t stop me!”alisema Dedan kwa hasira.
“Kunitegeshea vinasa
sauti faida yake nini?”
“Shida yangu ni huyu afriti nambari
moja!”alisema Dedani akisahau kama mwanamke huyu ni rais.
“Ananifanyia ushushushu mimi?”Serambovu akainguilia kati kwa jazba maana
alijiuliza maswali kadhaa Dedani alitumia muda gani kuwasikiliza na je ni kweli
anajua walichozungumza au amekuja akahisi rais Kilua atakuwepo ofisini kwa
Serambovu.
Kilua alimshika Dedani mkono nakumuondoa pale kwa
haraka sana wakaelea eneo linguine la ikulu.Kilua alipiga hatua kadhaa na moja
kwa moja alimpeleka chumbani kwake kisha akaufunga mlango..
“We need
to talk.”alisema Kilua akimwangalia mume wake huku moyo ukimuenda mbio
mfululizo.
Dedani aliketi kwenye sofa pembeni.Walikwisha wasili
ikulu wakiwa na Shunie ambaye sasa alihisi wivu mkubwa kila akimuona Dedani
karibu na Kilua.
“No more lies nataka nijue ulikuwa unafanya nini
ofisini kwa Serambovu?”
Kilua alisogea kwenye sofa lile akaweka
mkono wake mmoja kwenye kifua cha Dedani.
“Mimi rais wa taif hili na
makazi yangu ni ikulu ninaweza kuingia popote kwa muda wowote ule.”
“Hata kama lakini sio kwa uhuru huu?Serambovu ni hatari kwa mke wangu!”alisema
Dedani kwa jazba.
“Unataka kuujua ukweli?”aliuliza rais Kilua.Kitu
alichotaka kukisema kwa miaka mingi ilifika muda alitakiwa kukisema.Kitendo cha
kugundua mumewe amekuwa akiweka vinasa sauti kilimtisha na ile kukuta kwamba
anaweza kuja kushtukiwa siku moja na ikawa fedheha alihisi ni mwiba mkubwa
sana.Aliona bora aivujishe siri ile mwenyewe kuondoa mzizi wa fitina.Lakini
alitaka iwe maalum pengine angemchukua Dedani nakuandaa mlo jioni maalum kama
familia ili aweze kuchuja nakupembua siri zote kwamba amekuwa akimla mgongo siku
hadi siku.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mke wangu ni
bora tukawekana wazi maisha yakuhisiana ubaya hayana mema.Mimi sipendi kuishi
kwa mashaka nimechoka sana mama watoto ingekuwa vyema tuwekane sawa.Kwanini
Serambovu ana sauti sana kwenye maisha yako?Ukimuondoa utapungukiwa na jambo
gani?”
Kilua alifikiri akapiga picha nakuona ni jinsi gani Dedani
atachukulia jambo hilo?Aliona kama Dedani akiwa amepanda na jazba nap engine
kumletea fujo!
“Kwa muda mrefu nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na
Serambovu.Nilidhani ningeacha lakini imekuwa tatizo kwangu nakujikuta
nikiendelea kukusaliti mara kwa mara hali ambayo ni mbaya.Kibaya zaidi..”alisita
kusema.
Dedani alihisi mwili wote ukifa ganzi.Yale maneno
aliyoambiwa bwana Kavu kuwaa Serambovu analalia kifua cha mkewe ni ukweli mtupu
na sasa amethibitisha mkewe mwenyewe.
Dedani akajikaza
kisabuni.Aliutaka ukweli na sasa anaenda kuusikia nakujifunza namna ya kuishi
nao.
“Sema.”
“Nilipata mimba…”kigugumizi kikamshika mama
Shani kisha akaendelea,”Shani si mwanao.Ni mtoto wa Serambovu.”alisema rais
kiLUA akimwambia Dedani aliyehisi sofa lile lina misumari.Picha ilimjia
kichwani siku alipoambiwa mkewe ni mjamzito.Anakumbuka alivyojitahidi kumlea
mkewe akiwa mjamzito.alinunua vitabu vingi akijifunza namna ya kumtunza mama
kijacho wake halafu leo anaambiwa huyo mtoto si wakwake?Anakumbuka tarehe ya
mtoto kuzaliwa na kilio cha kwanza cha Shani!Alikumbuka vyote DEDANI alikumbuka
hadi alipombeba Shani nakumlea tena alionesha upendo mkubwa sana kwa binti yake
huyo kuliko maelezo.Halafu mama wa mtoto anasema si wa kwake?
“Noo!”alisema Dedani akiwa amechanganyikiwa.
“She is your daughter
legally but biologically Shani is not your blood.!”alisema Kilua
akihuzunika.Lililkuwa jambo zito sana kulitamka.
“Muongo!Muongo!Muongoo!She is my daughter!Shani ni wangu peke yangu!”alisema
Dedani machozi yakimtoka mfululizo.Ulikuwa mwiba mkubwa sana kwenye maisha
yangu.Alikumbuka kalivyokuwa kadogo tena kachanga akikabeba hadi alipokuwa
mkubwa.Mawimbi ya upendo kwa mtoto wake wa kike yalikuwa yenye nguvu bila
kutikiswa na leo anaambiwa huyu mtoto si wa kwake?Amempa hadi jina lake lakini
leo hii anaambiwa sio damu yake?Alitekwa naye nakujitahidi kufanya kila awezalo
lakini leo aanaambiwa ni mtoto wa adui yake nambari moja?
“Tasha na
John pia sio wa kwako!”KIlua akazidi kueleza zaidi.Hao ni wadogo zake
Shani.Kilua aliwaficha mbali baada ya kuona familia yake
inafuatiliwa.
Dedani akamshika mkewe shingo akitaka kuikunja kwa
nguvu.Walinzi walikuwa nje wasingeona walijua tu rais Kilua alihitaji faragha na
mume.
“Hata sasa nina ujauzito wa Serambovu.”alisema
Kilua.
Dedani alitumbua macho,”Ina maana mtoto wa kwanza ni wa
nje?”
“Ndiyo.”
“Wa pili nje?”
“Ndiyo.”
“Watatu nje|?”
“Ndiyo.”
“Na hiyo
mimba ni ya nje?”
Kilua alitikisa kichwa.Dedani alijikuta akimuachia
shingo nakumtwanga ngumi ya tumbo paa!Ilikuwa na hasira tu.
:”Utaniua
mme wangu!”alipiga kelele KILUA nakufanya walinzi wafungue mlango nakuingia kwa
haraka.Wakamkuta Kilua ameshika tumbo akigaragara!Walinzi walimuwahi rais maana
alikuwa na hali mbaya!Dedani alikuwa amemjeruhi mkewe tumboni na mbaya zaidi
alikuwa mjamzito hazikupita dakika mbili Kilua alianza kuvuja damu!
“Mwite daktarii!”alisema moja ya walinzi.
“Alert all units red
code!”walinzi walianza kupashana habari.Hali ya mkuu ilikuwa mbaya.Kilua
aliondolewa chumbani kwake nakupelekwa kwenye hospitali ya ikulu ikiwa na kila
kitu madaktari walimpokea maana huwa tayari muda wote endapo itatokea
dharula.Habari ile ilifanywa kimyakimya isijulikane.
Walinzi
walimkamata Dedani!
Ilikuwa hatari kwake.Hatari
iliyomtisha na kumdhoofisha na akashindwa kujua anajisaidiaje.Walinzi wa rais
walimweka chini ya ulinzi mkali sana na tayari walikuwa mbioni kumuadabisha nap
engine wangemuua palepale.
Dedani akajua amewekwa sehemu mbaya na
wanausalama hawa.Alikuwa amemjeruhi vibaya sana mke wake.Napengine angepoteza
maisha au hata angempoteza mtoto.Kwa sasa Dedani alikuwa adui wa taifa kwa
kuhatarisha maisha ya rais Kilua.Lilikuwa pigo kubwa sana lililohitaji kukemewa
na kudhibitiwa.Alijua amejitakia kifo.
“Nahitaji kumuona mke
wangu?”Dedani aling’ang’ania.
“Hatuna imani na wewe.”alisema moja ya
walinzi.
“Ni mke wangu!”alijitetea bwana Dedani akijaribu kuweka
mambo sawa pengine wangemuelewa.
“Tunajua ni mkeo.Lakini kwetu sisi
Kilua ni rais wa Kiota.Ni amiri jeshi mkuu ndo mwenye dhamana pamoja ya
taifa.Hatua yako ya kumpiga ni tishio na wewe ni hatari kwa usalama wa
rais.Hatuhitaji uwepo wako karibu naye.Tafadhali tunaomba utulie.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dedani alijua
amelikoroga pengine haukuwa mpango lakini imetokea tu kwamba amempiga mkewe
tumboni na sasa kamsababishia maumivu makali sana hali inayoleta sintofahamu kwa
upande wake na usalama wake.Itakuwaje kwa mwanamke huyu kuwa kaibu naye.Hata
aseme ilikuwa bahati mbaya bado wasingemwelewa.Ukelele ulisikika wa rais Kilua
akilia kwamba mume wake atamuaa.Ukelele ulioashiria kwamba kulikuwa na ugomvi na
bila shaka walinzi walikuwa nje ya ofisi hivyo walimsikia vilivyo.Wameingia
wamemkuta rais akiugulia mauvimu isitoshe anavuja damu kuashiria kwamba
amepigwa.
Rais Kilua alikuwa ameweka hali yake ya ujauzito siri na
walinzi hawakujua zaidi yake na daktari wake tu.Siri hii ilikuwa mahsusi kuficha
jambo hilo ili lisitumike kama njia ya kumwadabisha rais KIlua kuhusiana na
tandabelua inayomuandama.Hakupanga kuvujisha siri hii lakini imebidi siri
ivuje.
CHUMBA CHA MATIBABU
Madaktari wakiwa chini ya
usimamizi wa ulinzi wa rais walifanikiwa kumshughulikia rais Kilua.Mitambo ya
upumuaji alikuwa imepachikwa kwenye pua.Alifungwa mitambo mingine mahsusi kwa
aajili ya matibabu.Daktari aligundua jambo moja kuwa mimba ya rais Kilua ilikuwa
imeharibika baada ya kupokea pigo zito sana kutoka kwa mumewe.
“We
have to save her first!”alisema daktari akifanya upasuaji wa kuondoa kijusi.Timu
ya madaktari wengine walikuwa kwenye chumba kile wakimshughulikia bimkubwa hali
ilikuwa tete na sasa mambo yamebadilika sana.Kilua alikuwa chini ya mikono
salama.Tayari walikwisha pasua tumbo na sasa walikuwa wakifanya kazi ya kuondoa
kijusi kile.Ni fedheha kwa mwanamke kupoteza mtoto!
“The baby is
gone!”
Mashine za chumba cha upasuaji zilisikika zikitoa milio
kuonesha shughuli ilikuwa pevu.Hali ilikuwa kwenye hatari ya ponya niponye.Wapo
waliotoka jasho palepale maana rais wan chi alikuwa matatani.Upepo ulikuwa
unabadilika sasa.
***
Taarifa za rais Kilua kuingizwa
chumba cha upasuaji zilipenya hadi kwa Serambovu.Alipata kupitia pandikizi wake
katika ulinzi wa rais alimtumia ujumbe.Kwa Serambovu huo ulikuwa ushindi mkubwa
sana na aliamua kuutumia kwa nafasi iliyo bora ili mambo asije
kuyabananga!Alichokifanya aliwasiliana na timu yake ya THE BIG BOYS kuwapa
taarifa.
“Wakuu kama nilivyosema mheshimiwa yupo hoi.”
“Ni vizuri tunaweza kutumia nafasi hii kuchukua nchi.”
“Hayo ni
mapinduzi siwezi kujihusisha na uhaini.Nimeshatengeneza jina siwezi kuwa rais
aliyempindua mwenzake.No kwa hilo naomba mniwie radhi wakuu.”alijitetea bwana
Serambovu akijitahidi kujitetea.
“Hii ni nafasi yako itumie
vizuri.”
“Kumbukeni rais Kilua hana baraza la mawaziri kwa nafasi
kama hii hatuwezi kumuondoa madarakani.”
“Akiwaa na baraza bila
shaka wewe hautakuwa na nafasi ya kushika wadhfa wake.Tumia mwanya akiwa
hapohapo hospitali wa wewe kutwaa madaraka.Kill her then we take
power.”
Serambovu alijikuta akiwaza sana japo alikuwa tayari kufanya
makubaliano lakini isingekuwa kwa namna ile.Bado Kilua alikuwa mzazi mwenza na
asingekuwa tayari kumuondoa madarakani kwa mtindo ule.Tayari alikuwa ameandika
makala iliyomhusu Dedani na tayari amekwisha isambaza kwenye mitandao ya kijamii
pamoja na vyombo vya habari.Ilikuwa nafasi ngumu sana kwa yeye kumzimisha
Kilua.Upepo ulikuwa umebadilika baadaa ya Dedani kumjeruhi mkewe hadi akapoteza
ujauzito na sasa Serambovu alikuwa anashauriwa kuchukua madaraka.Ilikuwa hatua
ngumu sana kwake.
“Kwanini mmeamua hivi?”
“Tumegundua
Kilua ni imara kila siku anakuwa imara zaidi na tusipo muondoa maapema
tutaambulia hasara.Anatakiwa aondolewe kwa gharama yoyote.Unatakiwa kuchukua
madaraka kwa nguvu.Tuna watu wetu kwenye jeshi watakutetea.They will appoint you
as president.”
“Kwanini tusingoje apone?”
“Kama akipona
jiandae kubeba msalaba wa wewe kuitwa msaliti.Tutathibitisha ulisuka mipango ya
kumteka mumewe na mwanae.Automatically hautapona!”sauti ya upande wa pili
ilijibu.
“Lakini sioni umuhimu wa kutwaa madaraka kimapinduzi taifa
litayumba.”
“Serambovu sisi tumewekeza pakubwa kupata mafuta ya
taifa lenu.Hatupo tayari kukubali hasara hiyo itokee.Uongozi wa rais Kilua ni
mwiba na mpaka sasa ameonesha nia kwamba anatujua na yupo tayari kukamata wote
waliohusika na mauaji ya rais Kisusi.Upembuzi wetu umethibitisha kwamba kuna
uwezekano rais Kilua alipata file nambari 13:14 nakujua vyote vilivyomo.Hadi
sasa kuna mpango wa mashushushu kuja kukagua eneo lile.Hakuishia hapo ameshajua
nyendo zetu na kibaya zaidi anaanza kupachika mizizi yake .Ameshasambaza upupu
watu wenye uaminifu kwake wanaanza kuingizwa na mumewe.We must eliminate her
haraka.”ilisema sauti kavu upande wa pili.Habari ya kwamba Kilua yumo kwenye
chumba cha upasuaji ilikuwa heri kwake na sasa wangesogea kwenye hatua ya pili
kutikisa taifa.
Mtiririko ulikuwa umebadilika sasa na rais Kilua
alionekana kama kizuizi.Wameteka familia yake lakini wapi?Sasa ni bora
kumfutilia mbali.
“Jamani tuwe makini katika hatua hii?”
“Uzembe hauwezi kutokea.Tutafanya usumbufu kidogo wakati nchi ikiwa kwenye
ghasia tutaweza kuondoa lile kontena letu la vifaa pale bandarini nakulipeleka
kwenye visima vyetu vya mafuta.”
“Nani atakuwa rais?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wewe!”ilijibu
sauti ile ikimaanisha hali ikamfanya Serambovu kujiandaa kisaikolojia kwa
mabadiliko mapya yanayokuja.Lakini kichwani mwake aliona ni vyema amfanye Kilua
aondoke nchini.Punde akipewa akipokonya madaraka bila shaka atamfukuza badala
ya kumfutilia mbali hapo ataanzisha uhasama kati yake na Kilua kwa kumpokonya
madaraka kisha atamfukuza kwa lengo lakuyasalimisha maisha yake.Vilevile kama
akifanikiwa kumfukuza nchini atakuwa ameingia mgogoro na mabwana wa THE BIGI
BOYS kwani atakuwa amekaidi agizo la kumfutilia mbali Kilua.Serambovu alikuwa
kwenye wakati mgumu sana.
Serambovu alihisi kichwa kuwa kizito kiasi
akaona upepo ulivyobadilika ni hatari kwake na hatari sana kwa taifa
lake.Hatimaye mkataba wa 13:14 ulikuwa umefikia wakati mwingine.Ni kama upepo
ulikuwa ukibadilika na wahusika walikuwa katika kasi ya haraka kuhakikisha upepo
unabadilika.Kila anayehusika alihitajika kulishwa sumu.Serambovu alikuwa
amewekwa mtu kati kalishwa na sasa aliona pia umuhimu wa kumuua Kilua.Hilo
lilikuwa wazo pia.
Upepo hupima nguvu mti.Kiota ilikuwa majaribuni
tena.Rais wao mpendwa yumo chumba cha upasuaji akishughulikiwa kuondoa mimba
iliyoharibika baada ya kupigwa na mumewe huku nako Serambovu amelishwa sumu
mahsusi yakumuondoa Kilua madarakani haraka iwezekanavyo!Dedani kitanzini kwa
kumjeruhi mkewe!Shunie tayari amekwisha angukia katika penzi zito lisilo na
maelezo kwa kumpenda mume wa rais Kilua.Yalikuwa ni maswali lukuki yasiyo na
majibu maswali yasiyo na hitimisho kwamba nafsi hizi zitafanikiwaje?
Serambovu alikata simu kisha akaenda hadi ofisini mwa rais Kilua.Alifungua
mlango bila kugonga hasa akijua yeye ndo chifu wa ikulu.Akakutana na jenerali
Lupogo akiwa amesimama.Jenerali Lupogo akamuangalia Serambovu kwa
umakini.
“Jenerali?”aliita Serambovu akiogopa maana alitakiwa
kumuamrisha jenerali Lupogo aingize vikosi vya usalama barabarani.Wazo hilo
likawa linaonekana kama mvuke.Ujasiri wake ni kama mshumaa uwakao kwenye upepo
mkali kiasi akahisi yeye mwenyewe hajiamini.
“Ndiyo mkuu.Tupo tayari kuchukua oda kutoka kwako.”alitamka maneno hayo jenerali
Lupogo.
“Kwanza nataka kutangaza hali ya hatari
before anything.”alisema Serambovu akimtizama jenerali Lupogo aliyesimama hatua
chache kutoka pale.Jenerali alimsikiliza.
“Ungetangaza kwamba
umechukua nchi kisha utangaze hali ya hatari.Ni safari ngumu nap engine utegemee
ugumu kutoka mataifa mengine.Kamata kituo cha taifa cha utangazaji.Majeshi yapo
tayari ni wewe tu uingie kilingeni kwa amri!”
“Nafikiri tuandae
matangazo ya mimi kulishika taifa.”
“Vikosi vipo tayari kwaajili
yako.”
“Tuelekee huko kwa haraaka japo nilipenda kutolea maamuzi
nikiwa hapa ikulu.”
“No bado una nafasi salama.”
“Jenerali?”
“Mr President?”
“Unafikiri ni hatua sahihi
tunayochukua?”
“Wote tuna nafasi ya kufanya maamuzi nasio kila uamuzi
utampendeza kila mtu ila mwisho wa siku inabidi tuufuate njia tuliyochagua.Kila
uamuzi una matokeo na lazima tujifunze kuishi kwa matokeo yenyewe.”ulikuwa
ujumbe mzito sana toka kwa jenerali Lupogo.
Serambovu alijiandaa
kisaikolojia kwa upepo mpya na uzembe wowote ule ungefikia pabaya sana ikiwa
hajajipanga.
“Ok Jenerali tunaanza daraja la kwanza.Ikulu ipo
salama?”
“Ndiyo ipo salama ni wewe tu ila kwa muda mfupi kuna
walinzi wa rais wanatakiwa kufutiliwa mbali wale waliopo kwenye chumba cha
upasauaji.”alisema jenerali.
“Kikosi kazi kipo tayari kukabiliana
nao?”aliuliza bwana Serambovu.
“Ndiyo.Utawadhibiti kwanza wao kisha
tutaikamata handaki la silaha hadi hapo tutakuwa salama kuiteka ikulu.Vikosi
kadhaa vimepewa maelezo kuwa katika hali ya hatari it will take time kabla wajue
wewe ndo unaendesha nchi ila lazima tujiandae kwa lolote.”alisema Jeneral
Lupogo.
“Kwanini tusimlazimishe Kilua ajiuzulu kuliko kuingia kwa
rabsha namna hii?”
“Mkuu wote tuna mategemeo sio kila uamuzi
nikuchukua.She won’t resign!”alihakikisha bwana jenerali.
Serambovu
aivuta hisia kali akijiandaa kisaikolojia kupambana na mtiririko huo
mpya.Alijiahakikishia kwa hatua anayoenda kuichukua bila shaka atakuwa na
uhakika wa kum,uondoa bi Kilua madarakani kwa haraka sanaa.
“Ok.Give
the order tuanze kazi!”alisema Serambovu ambapo muda uleule tu jenerali
alikamata redio call yake kisha akaanza kutoa maelekezo kwa vijana wake wa
kazi.Ikulu ilikuwa si salama tena kwa rais Kilua na ndani ya dakika vilionekana
vikosi vilivyovalia tofauti na wanajeshi vikiingia ikulu.Walikuwa na silaha
zilizo tayari kwaajili ya shughuli hiyo maalum.Walipofika ujio wao uliwafanya
walinzi wa ikulu kushtuka nakuanza kujibishana nao hali iliyoleta mapigano
mazito.Dakika tano mbele vikaingia vifaru viwili vya kijeshi pamoja na magari
kadhaa yakiwa tayari kuendeleza mapambano.Tofauti na walinzi walivyo dhani kwani
baada ya vikosi vile kuingia tu vilitulia bila kufanya lolote wakiacha wale
jamaa waliovalia mavazi tofauti na sare za jeshi la Kiota.
Ilikuwa
mitutu mizito sana kwa wakati ule na bila shaka hali haikuwa sawa.Wala
kuridhisha.Ikulu ilingiia katika mhanga mkubwa sana.
***CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Umbali Fulani
kutoka ikulu mlikuwa na jengo kubwa.Katika ofisi ya juu kabisa walikuwepo
vibosile kadhaa wakiangalia usawa wa ikulu kwenye vioo wadunguaji wao walikuwa
na silaha zao wakilenga shabaha ikulu.
“Sniper in position?”aliuliza
mzungu mmoja aliyekuwa hatua chache na pale wadunguaji walipo.
“Eye
eye sir!”
“Alpha team send the drones.”alisema mzungu Yule akiwa
kavalia suti nyeusi.Hiki kilikuwa kikosi cha siri mahsusi kuondoa utawala wa
Kilua.Hakikumilikiwa na serikali yoyote.
“Drones in
position.”
“Shoot on my command!”alisema Mzungu
Yule.
Mzungu Yule alimgeukia mtu aliyekuwa pembeni na tarakilishi
mpakato.Alimuangalia kwa umakini kisha akamwambia,”Ingilia mawasiliano ya vikosi
vya ulinzi vya rais.”
“Eye eye sir!”alisema bwana Yule akaendelea
kubofya tarakilishi yake kisha kupitia kifaa chake cha kupokea nakutuma sauti
akasema,”All team in Redcode condition submit to omega king as your identity
whosoever doesn’t possess the code is unworthy!”
“Umehakikisha
imeenda kwa kundi tofauti?”
“Ndiyo mkuu.”
Mzungu
alirudisha macho kwenye kioo.
Drone vifaa maalum vya kupaa hewani
vikiwa vimebeba silaha vilikuwa hewani kuelekea ikulu tayari kwa mashambulizi
ikiwa tu anayeviongoza atafanikiwa kubofya vitufe vya kulipulia.Rais Kilua
alikuwa matatani na bila shaka alikuwa mbioni kufurushwa na
wavamizi.
Drones kwa kuwa zilikuwa hewani ilikuwa rahisi kuona
vikosi vya ulinzi vya ikulu na kwa haraka vikaanza kurusha makombora kuwalipua
walinzi wa ikulu.Walinzi wengi waliuawa kwa haraka wakati mapigano
yamezuka.Ilikuwa jino kwa jino!Vita kuu!Hadi hapo haikujulikana ni kiasi gani
sserikali ilikuwa imesalitika.Mpango wao kumtikisa Kilua ulikuwa umewadia.Na
sasa hali ilikuwa tete!
***
Zee Kavu alimtoa Shani kule alipokua kwenye chumba.Alimleta
hadi nje kisha kulikuwa na kamera ambazo zilikuwa zikichukua tukio zima linavyo
tokea.Zee huyu alichukua kisu nakukielekeza kwenye shingo ya mtoto.Uoga ulikuwa
umemtafuna Shani kiasi cha kumnyima imani yake.Japo mzee huyu alikwisha tia
najisi utu wake na kumnyima dhamana ya imani yake.Kulikuwa bado na woga kwenye
mwili wake.Woga uliobebwa kwenye kingo za moyo wake.
Shani pamoja na
uoga lakini hakutoa sauti!Mikono ya zee Kavu kwenye mwili wake ilitosha
kumuangamiza.Picha ya zee lile kiuononi mwake ilimnyima imani ya kuishi
pia.
“Shani tunaenda kuangamiza familia yako.Nilimwambia mama ako
kwamba ipo siku hata iona sura yako tena nafikiri ni leo.”alisema zee lile kwa
sauti yake kavu huku uso wake ukibeba mashaka ya moyo wake.
Shingo
aliikamata huku Shani akikodoa macho bila kufanza lolote ulikuwa umewadia muda
wake.Zee Kavu alipitisha ulimi kwenye papi za mido yake tayari kummaliza mwana
wa Kilua.Alichofanya ni unyama uliopitiliza alimdunga kisu mgongoni badala ya
kumchinja kama alivyodhamiria.Alikishindilia kwa umakini mkubwa kisha
akakichomoa.Shani alihisi nguvu kumuishia akatua chini!Zee Kavu aligeuka na
kuwapa ishara vijana wake.
Waliuchukua mwili wa Shani kisha
wakauweka kwenye gunia nakuondoka nao kwenye gari.
***
“Ina maana
hamsikii milio ya risasi?”aliuliza Dedani.Ofisa usalama aliyepo pembeni yake
alimuangalia kwa umakini.
“Tunaisikia response team ipo
kazini.”alijibu bwana Yule.Lakini wakiwa pale wakaingia wanausalama wengine wa
rais.
“Identify yourself?”
“Una maanisha
nini?”
“Give me the new code?Walinzi wote wa rais tumepewa code
mpya nataka unitajie?”alisema mwana usalama Yule.Palepale kile kikosi
kilichokuwa kinamlinda Dedani wakashtukia wakichomolewa bastola na
wenzao.
“Code ipi?Code iliyopo Eagle fly Redcode condition.”alijibu
bwana Yule.
Wanausalama wenzao wakaangaliana nakupeana ishara kuwa
hawa wasio na code ndo wavamizi na wale walio nacode wakaonekana kama wao ndo
wenye makosi.Punde sipunde walianza kurushiana risasi huku wengine wakiingia
kwenye mapigano mazito sana.Dedani alichopoka kwa haraka kisha akajibiringisha
chini.Akainuka wakati wanausalama wakikabiliana.Dedan aliinuka kwa ustadi wa
ajabu.Alisimama akatoka nje.Dedani alipita kwenye korido za ikulu nakukuta watu
wakikimbia huku na kule.Walinzi wa rais walikuwa wakirushiana risasi na wengine
wakitwangana makonde mazito.Ndani ya muda mfupi hakuna mlinzi aliyemuamini
mwenzake.Lengo lakuwachanganya lilifanikiwa baaada ya kuchanganywa na kikosi
haramu kilichovamia ikulu ya rais Kilua.
Dedani alitoa simu yake
mfukoni ili anataka kupiga alishtushwa na risasi iliyopita nakumchubua
sikio.Wakati anaweweseka alishangaa mtu kumsukuma wakaangikia mlango nakuingia
chumba kingine.Kwa kasi ya ajabu aliyemsukuma aliwahi mlangoni na bastola yake
akiwa amechutama akafyatua risasi mbili nakufanikiwa kummaliza aliyemfyatulia
Dedani.
Ile Dedani anageuka anakutana na sura ya Shunie.Shunie
alimkimbilia Dedani nakumkumbatia kwa nguvu zote huku
akimbusu.
“Uwe makini ikulu imevamiwa.Wanataka
kumuondoa Kilua madarakani.Hadi sasa nahisi kuna uzembe mkubwa sana umefanyika
hadi kufikia hatua hii.Tulijua kuna hatari kwa utawala wa Kilua lakini sio kwa
namna hii.Hakuna aliyetegemea.Kwa upembuzi nimegundua hata walinzi
wamechanganywa.Kuna mtu anatoa amri za uongo.Ana wa-confuse ndo maaana
wanapigana.”alisema Shunie.
Dedani,”Mke wangu
siwatamuua?”
“Kuna uwezekano huo.Nimeshangaa kumuona jenerali yupo
hapa.Kuna vikosi tofauti vimeingia hapa.Kimoja kimeanza kushambulia
walinzi.Kingine kimekuja na vifaru viwili cha ajabu hawaonekani kama wanatoa
msaada.Huu ni uvamizi mbaya sana.”
“Shunie nakuomba jambo moja
tena.”
“Ndiyo.”
‘Utakubali nimsaidie Kilua kwa mara ya
mwisho?”
“Dedani kwanini tusitumie mwanya huu kuondoka kabisa eneo
hili?Twende tuanze maisha mapya mimi na wewe.Penzi changa juani?”alisisitiza
Shunie.
“Tafadhali tumsaidie.”
“Dedani ushahidi gani
tena unataka umeshaambiwa na zee Kavu kwamba mkeo ni msaliti tena nini unataka
kwake?Hao wanaovamia watahakikisha wanakumaliza na wewe.”
“No she is
still my wife pia tunarudisha heshma ya taifa letu hakuna wakulichezea.”alisema
Dedani kisha akashika simu yake.Akafya namba Fulani akaweka simu
masikioni.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“This is special
team commandor am activating the silent hunter for the glory of our
nation.100911 We are going in full attack!”alitamka maneno yale bwana Dedani.Na
palepale kikosi cha SILENT HUNTER mahususi kwa ukombozi wa taifa kilipata ujumbe
ule.Kikosi hiki kiliundwa kwa wazalendo wan chi na mashujaa ambao maisha yao
yote hawakujulikana hovyo.Walikuwa wasiri sana.Na leo ilikuwa siku yao maalum
kuingia kazini.Kikosi cha Destruction Control Unit kilikuwa macho kwa matukio
yaliyokuwa yakiendelea.
“So it is true?”aliuliza Shunie akimwangalia
Dedani machoni.
“Kuhusu nini?”
“Kwamba SILENT HUNTER ni
kikosi kilichopo nilidhani DCU ndo vikosi vya mwisho?”
Dedani
akatabasamu,”Ni heshma kuwepo ila tunaruhusiwa kuingia kazini ikiwa tukio
limetokea kama mmoja wetu ameshuhudia mbali na hapo we remain silent
forever.Hata baada ya uamuzi huu nitatakiwa kutoa majibu.”
Dedani na
Shunie walingia kazini Shunie,”Chukua silaha.”
“SILENT HUNTER
hawatumii silaha.Sisi wenyewe ni silaha.Sisi ni wananchi wa kawaida
sana.”alisema Dedani kisha kwa haraka ya ajabu alitoka mbio nakumuwahi moja vile
vikosi vilivyovamia ikulu.Dedani alikuwa na ukomavu wa mafunzo na mwenye uimara
wa ajabu namna alivyodhibti kwa mapigano mazito ilimfanya Shunie aduwae!Dedani
alwashangaza wale kwa haraka alienda moja kwa moja hadi kilipo chumba cha rais
Kilua alipokuwa akitibiwa.Alikuta madaktari wakiwa wamemaliza shughuli
yao.Ilibidi wamfanyie operesheni maana pigo l;a Dedani lilileta hitilafu kubwa
kwenye tumbo lake la uzazi.Upasuaji ulifanikiwa kurekebisha madhara
yaliyojitokeza.s
Kufika pale aliupiga teke mlango akaingia nao
nakukutana walinzi wa rais Kilua pamoja na timu ya madaktari.Walinzi walitaka
kumkabili Dedani lakini kwa kasi ya ajabu Dedani alifanikiwa kuwadhibiti na
kumnyang’anya mmoja silaha kisha akaiweka kwenye kichwa cha rais KIlua ambapo
alitoa amri walinzi wengine washushe silaha zao la sivyo angeondoa ubongo wa
Kilua.Ilibidi wazishushe lakini wakichukizwa maana Dedani aliwashtukiza na
hawakuwa na jeuri ya kupiga risasi mgonjwa hakutakiwa kelele.
“Nisikilizeni ikulu imevamiwa na simuamini mtu mbele ya mke wangu.Wenzenu huko
nje wanapigana na nyie mlioingia kwenye chumba cha upasuaji ndo
mmesalimika.Nataka nimuondoe mke wangu hapa.”
“Una
uhakika?”
“Ndiyo.Kwanini ni danganya.I Just need my family hii kazi
inaleta shida.”
“Kwanza tuambie wewe ulipata wapi mafunzo
haya?”aliuliza bwana Dittu mkuu wa ulinzi wa rais.
“Hilo halina maana
kwa sasa.Mtu lazima ajiandae kulinda familia yake.”alisema Dedani
akiwaangalia.Kisha alitoa bastola akawarudishia.Lilikuwa kosa kubwa sana.Kwani
walinzi hakukoma hapo waliziokota zao na kwa kasi ya ajabu wakamshambulia Dedani
kwa risasi nyingi!
“NOOO!”alipiga kelele Shunie ambaye aliwahiwa kwa
kupigwa teke la kuruka likatua kwenye paji la uso!Shunie alianguka kifuani kwa
Dedani!Dittu aliamuru rais Kilua aondolewe paleKilua hakuwa anaelewa ni kitu
gani kinaendelea hadi muda yeye.Alikuwa usingizi maana dawa za usingizi
zilimsafirisha mbali sana!Wakasukuma kitanda chenye magurudumu wakamuingiza
kwenye lifti kisha ikashuka hadi chini ya handaki la ikulu.
Ndani ya
muda mfupi walikuwa kwenye njia iliyochimbwa chini tayari kumtorosha rais
Kilua.
“Tuna hitaji vikosi zaidi.”alisema moja ya walinzi
wake.
“Hapana simuamini mtu tena!Ulinzi wa rais umeingia doa.Yeyote
anayefanya hivi katushtukiza.”
“Tunaenda wapi
mkuu?”
“Tunamuondoa rais Kilua katika ardhi ya Kiota.”alisema bwana
Dittu.Lakini ghafla akawafyetulia walinzi wenzake risasi pamoja na
madaktari.Dittu aliwaua wote na sasa alikuwa amebadilika na kudhihirisha yeye ni
nan?Mbele yake walittokea watu wamevalia nguo kama za jeshi.Walimsaidia kusukuma
kitanda wakarudi nacho kwenye ile lifti nakukiweka kisha wakapanda pamoja
wakarudi juu.Walimpitisha rais Kilua njia za siri wakamuondoa rais Kilua eneo la
ikulu.Kiota haikuwa salama tena tayari ilikuwa mikononi mwa ghasia na mchanganyo
usioisha.
Wakiwa kwenye magari yao walitengeneza msafara wa
rais.Ikujulikana kwamba Kilua yumo ndani ya moja ya magari yale.Mwendo ulikuwa
mkali sana.Wapo waliokuwa katika msafara ule lakini hawakujua kwamba ule ni
mtego mbaya sana kuwahi kutokea.
***
“Mkuu msafara wa rais Kilua unaelekea sehemu salama.”aliambiwa
Serambovu aliyekuwa katika ofisi ya rais Kilua.
“Hakikisheni
anatoroshwa nchini.Pia kila nyumba ya mbunge nahitaji vikosi vya usalama vivamie
huko.Kila ofisi ya kiongozi wa serikali nataka kuwe na watu wetu.”
“Kila kitu kitapangwa kama kilivyo.”
Lakini ghafla Serambovu anapokea
simu.Aliipokea,”Ndiyo Zee Kavu.”
“Sikiliza kwa makini kijana!Huo
msafara unatunguliwa na mabomu.Kilua hatakiwi kupumua ulikuwa na nafasi ya
kummaliza lakini naona unarembesha.Huyu akiomba msaada kutoka ummoja wa mataifa
hakika hatutatoboa.Tayari kontena letu limeondolewa
bandarini.”
“NO!Niachine Kilua mimi?”
“Seramboviu Kilua
hana umuhimu mwanae tumeshamuua maiti yake tutaitupa popote pale au tuichome kwa
aside!Huna haja umeshakula sana huyo Malaya.Yatosha
sasa!”
“Etiii?”Serambovu alihisi tai kumkaba akawa
anailegeza.
“Shani tumemuua!”
Serambovu kichwa kikawaka
moto.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ile ni damu
yangu jamani mnasemaje mmeua?Acha utani!”
“Kuna gharama kwa kila
jambo.Huyu angekuja kutusumbua huko mbeleni.Tunafuta na ukoo wake wote!”Ulikuwa
ujumbe mzito sana kwa wao kuupokea.
“Nchi ni ya kwako.”
Simu ikakatwa muda uleule.
Serambovu alijua amekabidhiwa madaraka
mazito kwa ncha ya upanga.Kilua hakuwepo tena na sasa Kiota ipo mikononi
mwake!Serambovu aliduwaa.
“What have I done?”
***
“Target acquired?”
“Eye eye
sir!”
“Release the missile destroy the president’s
convoy!”
Mshambuliaji akiwa kwenye tarakilishi yake alikuwa
akiongoza drine kifaa kisichotumia rubani.Alikuwa anaona msafara wa rais Kilua
ambao ulikuwa unaelekea sehemu salamu ambapo angepanda ndege kisha wamuondoe
eneo lile.Huu sasa ulikuwa wakati mgumu sana kuliko vile walivyodhani.Walikuwa
mbioni kumuondoa uhai rais Kilua.
“Goodbye madam
president.BOOM!”Alisema nakubofya.Kisha kombora likaachiwa kutoka kwenye drone
likaenda kwa kasi nakudungua msafara wa rais Kilua.BOOOM!KOMBORA
KIOTANI.
MAWIMBI
Serambovu alikuwa amejishika kichwa
asijue afanye nini?Alikuwa amezungukwa na wanajeshi.Simu zilikuwa zinaita kila
sekunde akawa hapokei.Msafara wa rais Kilua ulikuwa umedunguliwa.Wote
walimuangalia wakisubiri kauli yake kuondoa utata uliokuwemo.Serambovu hakuelewa
hatua ya kuchukua.
“Acha kushika kichwa.Upepo umebadilika.Kiota
imetikiswa ni wakati wako.Hatukutegemea ila imetokea sasa kubaliana na hali
halisi.Hotuba yako isome kuhusu hatma ya Kilua.Kuna mengi ya kufanya kudhibiti
utawala wako.”
Serambovu aliinua kichwa akaona karatasi nyeupe ikiw
na maandishi pengine hayo maandishi hayakuwepo kwa jinsi msongo wa mawazo
ulivyokuwa umemtafuna.Aliinua nakuhisi ni nzito.Mkutano na waandishi wa habari
ulikuwa umewadia kwa yeye kutoa hotuba yake kwamba Kilua hayupo.Yeye kama chifu
wa ikulu kaamua kutwaa madaraka mwenyewe.Kayashika kwa mikono yake na sasa yupo
tayari kuiongoza Kiota.Kuna mataifa ya nje ambayo yangetakiwa kumsikia.Je,ni
wangapi wangekuwa tayari kumuunga mkono?Alijiuliza bila kupata majibu.Ataweza
kuwatuliza wananchi wake?Nchi imetoka katika vuguvugu la kuuawa kwa serikali ya
rais Kisusi.Sasa hata ya Kilua imeondolewa na mnadhimu mkuu wa ikulu.Huu ulikuwa
usaliti wa hali ya juu kuliko wote uliowahi kutokea!Alitakiwa kuyatuliza majeshi
yote na kila sekta ya serikali ya Kiota ijifunze kumtii yeye!Bwana Serambovu
alihisi ubovu alioingia nao.Mlango wa ofisi ukafunguka wakaingia watu Fulani
wamevalia suti nadhifu.Wote walionesha umakini.Walikuwa wane.Wazungu wa tatu na
mtu mweusi mmoja.
“Ni heshma kubwa kukuona
mheshimiwa rais Serambovu.Umefanya kazi nzuri.Kutana na THE BIG BOYS.”alitamka
mmoja wao.
Serambovu aliwatizama ulimi ukawa mzito kwa upande
wake.
“Kuna machache lazima utakuwa huyajui.Tumeamua kujitokeza
kabla hujatoa hotuba.Sisi ni kundi maalum tunashiriki biashara kubwa dunian za
uuzaji mafuta.Tuna mpango wa kusambaza mafuta duniani kote kwa takribani miaka
50 hijayo.Taifa lanu lina mtaji huu.Ndo maana tumewekeza fedha nyingi
sana.Unachotakiwa kufanya nikuishikilia serikali yako vilivyo nchi yenu
inatakiwa iwe kwenye kamtikisiko wa kisiasa ili wazawa wasiwe na muda kuangalia
rasilimali.Nakuhakikishia kuna mengi tutayatekeleza nchini mwako ila uwe makini
sana.Tutakupa back up ya kutosha.Kuna kipindi kigumu utapitia lakini
tutakusaidia kuwatambua wasumbufu na kuwanyamazisha.”alisema bwana Yule akiwa
kavalia mawani ya macho.
“Tulitengeneza visa vyote kwa kushiriikiana
nanyi mliweza kufanikisha ghasia nchi haikupoa na sasa tumefanikiwa tena
kumuondoa Kilua.Hii ni zamu yako.Pesa usiiwaze ipo ya kutosha kwaajili
yako.Utaendesha nchi kawaida ila tu maslahi yetu uyachunge kwa kutukingia
kifua.”aliongeza mwingine.
“Naweza kuyajua majina yenu?”
“Sisi ni big boys team.Hata kufanikiwa kuiona sura yetu ni bahati kubwa sana
kwako.Unasimama mbele ya timu mahiri sana ya wafanyabiashara.”mwingine
alitamka.
“Lakini mabwana mtanihakikishia vipi usalama
wangu?”
“Tuna vikosi vya kutosha.Pesa ipo tunachoangalia ni mwanya
wa sisi kupata hayo mafuta.”
Serambovu alihisi ujasiri
ukimwingia,”Mlifanikisha haya mapinduzi?”
“Sema tulifanikisha wote
maana una husika.Sura yako ndo itakuwa inaulizwa sana.Kuna viapo utatakiwa kula
katika muungano huu pamoja nasi.Kumbuka unapoingia hakuna kutoka.”alisema Yule
bwana.Kisha akawageukia waliokuwepo kuwapa ishara watoke.Wameingia hadi ikulu
kumaanisha walikuwa na uwezo wa kuingia nakutoka.Sasa ilibaki jambo moja tu
kumsimika Serambovu kuwa rais mpya wa taifa hilo.
Walipishwa halafu
wakaingia wengine wawili wakiwa na mkoba.Waliuweka kwenye meza.Kisha
wakamsogelea Serambovu.Mmoja alimpa ishara ya kumpa mkono.Serambovu alitii
nakumpa mkono.
“Mpango wetu no kundi chache kuwaongoza wengi na wewe
utasimikwa leo kuwaongoza wenzako.Kiapo hiki ni cha damu.Binadamu wote tuna
asili ya kuamini kitu kwa kula yamini.Kiapo unachokula leo kitakuwa imani yako
ingawa utahitajika kufanya mambo mazito lakini na hakika kwa kiapo hiki utakuwa
jasiri sana na utaweza kutusaidia sisi.”alisema moja ya watu wale.Serambovu
alitikisa kchwa.Yule aliyemshika mkono alichomoa kisu anakumkata kwenye ncha ya
kidole kidogo kisha akashika kidole kile nakukata kuanzia kwenye ukucha.Aakata
chote nakuelekezwa asipige kelele.Damu zilipokuwa zinavuja walizikinga kwenye
kikombe Fulani hivi.Kilionekana kikombe cha miaka mingi chenye rangi ya
dhahabu.
“Damu yako imetiririka katika kikombe hiki ishara yaw ewe
kujiunga nasi.Kidole chako hakipo chote kumaanisha sehemu ya mwili wako ipo
nasi.Sisi wote tulikatwa.Inatakiwa uyavumilie maumivu hayo yatapoa.Kila
utakapoona kidole chake kimekatwa utakumbuka kiapo hiki.Sasa utasoma maneno haya
kwenye karatasi kimoyomoyo.”
Serambovu alikuwa akiugulia maumivu huku
akiwatukana watu wale kimoyomoyo akiwatukania mama zao.Alisoma maneno yale
kimoyomoyo nakula yamini akawa amejifumba rasmi katika kifungo cha The big
boys.Sasa alikuwa mshirika tayari aliyeiweka nchi yake rehani.Kumbe kule
kutikiswa kote akajua mpango ulikuwa rasilimali za taifa hasa hayo mafuta.Alijua
katika bara lake kuna utajiri mkubwa lakini watu wamekuwa wakiteseka sana katika
kuudhibitisha utajiri huo.Sasa kibarua kilikuwa kikubwa kwake.
“Hatimaye umekuwa mmoja wetu.Karibu katika timu.Hakikisha huwataji wenzako
hovyo.Usifanye makosa na kila uamuzi lazima upitie kwetu.”walimwambia.Serambovu
aliitikia kwa kutikisa kichwa maumivu yalikuwa makali.Alipewa kitambaa kufunika
kidonda chake.
“Pumzika kidogo usije ukaenda kusoma hotuba ya
kutangaza Kilua kafa huku una maumivu.Nenda pale ukiwa
soba.”walimwambia.
“Kontena mshechukua?”
“Ndiyo.Vijana
wetu kwa sasa wanatafuta wafuasi wa Kilua nakuwanyamazisha ni hatua ngumu lakini
tutafanikiwa.Baada ya muda utasikia watu wamepotea hovyo na wengine wamekutwa
wamekufa.”alisema mwingine.
Serambovu alihisia maumvi kisha akabeba
karatasi ya hotuba nakutoka ofisini kwa rais Kilua.Walinzi walimpokeaa.Wale watu
wane waliondoka pamoja naye.Serambovu alitoka hadi kwenye ukumbi wa
ikulu.Waandishi wa habari walikuwepo.Akatoa karatsi yake nakuanza kulihutubia
taifa lake.Kiota ilikuwa mikononi mwake sasa kibarua ni kuwajuza
wananchi.
***CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kulikuwa na
maandamano makubwa taifa zima baada ya Serambovu kujitwalia madaraka akidai rais
Kilua amefariki dunia kwenye ajali.Ajali ya raisi Kilua kuna ambao walirekodi
kisadfa na tayari video kadhaa zilikuwa zimesambaa kila pembe kutaka kujua nini
kimeeendelea.Ilikuwaje Serambovu ajiamulie kuwa rais?Vikosi vya usalama vilikuwa
kila kona kutuliza maandamano hayo.Watu waliuawa ilimradi kuusimika utawala mpya
wa Serambovu ambao hadi muda huo haukuwa na uhalali kisheria kama kweli atawale
au la!Kibarua kilikuwa kigumu sana.Alijaribu kuwatuliza lakini hali ikawa
tete.Simu mbalimbali zilipigwa ikulu zikitaka kujua yu wapi rais Kilua.Mwili
wake upo wapi?Serambovu alijitahidi kutoa muongozo lakini hali ikawa
tete.Maandamano yalisheheni kila kona.
Wafanyakazi wa sekta
mbalimbali waligoma kufanya shughuli zozote hadi pale watakapojua hatma ya rais
Kilua.Kulikuwa na taarifa ya mume wa rais Kilua kumuua mtu aliyeitwa Twalipo
muda mfupi baada ya taarifa ile ikafuatia taarifa ya Kilua kupatwa na ajali
akiwa kwenye msafara wake.Mgongano wa matukio hayo ulikosa majibu kabisa kwamba
ni kitu gani kimefanyika.
TAMATI
0 comments:
Post a Comment