Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

JINAMIZI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : HASSAN O MAMBOSASA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Jinamizi

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hekaheka za uchaguzi zilikuwa zimepamba moto

    nchini Tanzania,kampeni zenye majigambo zikiwa

    zimeshika nafasi yake ndani ya ardhi hii yenye

    amani. Vyama tofauti vilikuwa vikihaha huku na

    kule ndani ya nchi hii ili viweze kujizolea kura kwa

    wananchi, wagombea urais,ubunge na udiwani a

    vyama hivyo walijinadi wawezavyo ili kuwashawishi

    wananchi wawapigie kura. Hakika zilikuwa ni

    kampeni za aina yake zilizoleta upinzani katika

    vyama viwili tofauti, kimoja kikiwa ni chama tawala

    na kingine kikiwa ni kikuu cha upinzani

    nchiniTanzania. Upinzani huu ulipelekea hadi wawe

    wanachafuana kupitia vyombo vya habari, huku

    wanachama wake wakiwa katika makundi yenye

    uhasama mkubwa. Hakika hii ilikuwa ni kipato

    tosha kwa wanahabari wenye tamaa ndani ya nchi

    hii, wanahabari hawa walidiriki kuandika habari za

    uongo zilizoleta uhasama baina ya vyama hivi.

    Kampeni ziliendelea kuendeshwa sehemu

    mbalimbali za nchi hii huku serikali ikitoa fungu

    kwa kila chama ili kiweze kujimudu vyema, kampeni

    za vyama vyote zilikuwa za kawaida ila chama

    tawala na chama kikuu cha upinzani kampeni

    zao zilikuwa zimeimarika zaidi ya vyama vyote.

    Chama tawala kilitumia pesa za wanachama wake

    matajiri waliojitolea kukifadhili chama kipindi cha

    kampeni ,huku wapinzani wao wakuu wakiwa

    hawajulikani ni wapi walipopata fedha za nyongeza

    za kuweza kufanya kampeni zenye gharama kuliko

    uwezo wa chama chao. Utata wa chama hiki

    uliwavuta sana waandishi wa kikundi cha

    kujitegemea kutoka nchi za Afrika ya mashariki

    kuingia kazini, walianza kulifuatilia suala hili kwa

    undani sana ili wapate ukweli juu ya chama hiki.

    Chama hiki cha wanandishi kinachojulikana kama

    WAHANGA kiliundwa na waandishi watano wenye

    roho zisizo na hofu na jeuri ya kupuuzia

    vitisho , kiliundwa na watu watano kutokana nchi

    tano za Afrika ya mashariki amboa ni Norbert Kaila

    wa Tanzania,Davis Elius wa Kenya,Joseph Kiiza wa

    Uganda,Hilda Alphonce wa Rwanda na Allison Frank

    kutoka Burundi. Hawa ndio waliojulikana kama

    vichwa ngumu na baadhi ya vigogo, walikuwa

    wakitoa jarida lao lenye kuumbua mambo mengi

    maovu ndani ya Afrika ya mashariki. Hadi muda

    huo wa kampeni walikuwa tayari wameshaingia

    nchini Tanzania kwa siri,bwalifanya uchunguzi wa

    chini kwa chini huku kampeni zikiwa zinanaendelea. Uchunguzi wao ukiwa unaendelea

    ndio uhasama baina ya vyama hivi ukizidi kushika

    hatamu nchini, mauaji ya mgombea ubunge wa

    chama kikuu cha upinzani katika jimbo la Kahama

    yanatokea katika kampeni za chama hicho wilayani

    Kahama mkoani Shinyanga. Mgombea huyu

    aliyeitwa Gerald Geofrey alipigwa risasi ya kichwa

    akiwa jukwaani akijinadi kwa

    wananchi , hali ya sitomfahamu ilitokea baina ya chama

    cha upinzani maarufu kama PTP(people of Tanzania

    party) na chama tawala RPP (revolutionist political

    party) . PTP walikuwa wakiishutumu RPP ndio

    waliohusika na mauaji ya mgombea katika vyombo

    vya habari, hali hii ilipelekea RPP watumie muda

    wao mwingi kujitetea katika kampeni huku wenzao wakijinadi kwa

    wananchi. Hadi uchaguzi unakaribia tayari RPP

    walikuwa wameshapoteza idadi kubwa ya wafuasi

    na PTP walikuwa wameshajipatia wafuasi wengi

    tofauti na ilivyokuwa awali, RPP walijikuta

    wakipigwa kwenye kampeni zao karibu kila mahali.

    Hatimaye uchaguzi ukawadia ukawadia na ikawa ni

    siku ya mapumziko siku hiyo ya uchaguzi ili

    kuwapa fursa wananchi wapige,uchaguzi ulifanyika

    katika hali ya utulivu na amani nchi nzima.

    *********************************************

    ************************

    Waandishi wa WAHANGA nao walikuwa tayari

    wameshafanya uchunguzi na sasa wapo katika

    hata za mwisho kabla hawajalilipeleka

    jarida lao mtamboni ili liweze kuchapishwa na

    hatimaye liingie mitaani, walipolimaliza tayari

    uchaguzi ulikwisha fanyika na ilikuwa yanasubiriwa

    matokeo ya uchaguzi kwa hamu kubwa ili mshindi

    ajulikane. Binti pekee wa WAHANGA Hilda Alphonce

    ndiye aliyechukua jukumu la kupeleka nakala za

    jarida lao ili liweze kuchapishwa,alipeleka kiwanda

    cha EAPL(east africa publishers limited) tawi la Dar

    es salaam. Kutoka ofisini kwao hadi zilipo ofisi za

    kampuni ya EAPL hakukuwa mbali kwa mwendo wa miguu ingawa Hilda aliamua kutumia gari la umoja wao iliCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    awahu kurudi aweze kuendelea na kazi kama

    kawaida,alifanikiwa kufika zilipo ofisi hizo mtaa wa

    Libya jirani na kituo cha mafuta kisha akaenda kwa

    mtu wao maalum anayewachapishia majarida yao

    wakiwa jijini Dar es salaam. Hakuwa na muda wa

    kukaa tena maeneo hayo baada ya kukabidhi vitu

    muhimu kwa ajili ya uchapishaji, aliondoka ofisini

    hapo. Wakati akiwa anatoka nje ya jengo hilo alipishana na

    kijana mwenye suti nyeusi nadhifu akiingia ofisini humo.

    Hakutaka kumtilia shaka yoyote kwa muonekano

    alionao, alimuona kama mteja wa kawaida kama

    alivyo yeye ktika kampuni hiyo.

    *********************************************

    *************.

    Kijana aliyepishana na Hilda aliingia moja kwa moja

    hadi katika ofisi inayohusika na kupokea nakala za

    waandishi , alimkuta mhusika wa upokeaji wa nakala

    hizo akiwa ameegemea kiti huku miguu ikiwa

    mezani. Aliongea pasipo kuketi katika cha wateja

    kilicho jiranj yake, " we Daud huyu malaya kaleta

    nini" Daud alijibu bila ya kumtilia maananu

    anayezungumza naye, "ni nakala za jarida lao

    ambalo linahitajika kuchapishwa". Yule kijana

    aliingiza mkono katika mfuko wa koti la suti

    yake,alipoutoa ulikuwa na burungutu la pesa

    ambalo aliliweka juu ya meza kisha akasema, "hizi

    pesa ni zako zote ikiwa utanipatia hizo nakala kabla

    hazijafika mitamboni". Daud alikaa sawa kisha

    akamtazama yule kijana kwa umakini, alizitazama na pesa pia kwa macho ya tamaa kisha akasema "siwezi

    kuharibu kazi yangu kisa tamaa". Yule kijana akatia

    mkono katika mfuko nyuma wa suruali

    yake,alipoutoa ulikuwa umeshika pochi ya kuwekea

    hela iliyotuna mithili ya nyoka mwenye hasira.

    Aliifungua zipu ya pochi hiyo kwa majivuno kisha

    akatoa noti kadhaa na kuzihesabu, aliporidhika nazo

    aliziweka juu ya meza huku akisema "maisha yako

    unahitaji uyajenge zaidi ya hapa ulipo rafiki,sasa

    wewe jifanye mzalendo ukale dona na dagaa". Daud

    alizipokea pesa zote kwa pupa kisha akaziweka halafu

    akaziweka katika mkoba wake wa kazi,alipofunga

    zipu ya mkoba wake alifungua mtoto wa meza yake

    kwa funguo. Alitoa karatasi zote alizokuja nazo

    Hilda na kumkabidhi yule kijana akiwa

    ametabasamu, "dona na dagaa ni mlo mbaya kwa

    masikini ila kwa Tajiri ni chakula bora" Daud

    aliongea kwa mzaha na kupelekea wote wacheke.

    Waliagana kwa furaha kisha yule kijana akaondoka

    ofisini hapo akiwa na nakala hizo za WAHANGA.

    Mnamo desemba mwaka huohuo matokeo ya uchaguzi

    huo yalitarajiwa kutangazwa katika ukumbi wa tume

    ya taifa ya uchaguzi,tarehe na saa za kutangazwa

    kwa matokeo hayo ilitajwa mapema sana. Hatimaye

    siku ya siku ikawadia na ukumbi huo ukawa

    umejaa wagombea tofauti huku wagombea wa urais

    wa kila chama wakawa wamekaa katika viti vilivyo

    katika safu moja iliyopo mbele karibia na jukwa

    kuu . Ilipotimu saa nne kamili za asubuhi matokeo

    hayo yalitangazwa na mwenyekiti wa tume hiyo

    mhe Ramadhani Gumbo kwa kutaja asilimia za kura

    kwa kila mgombea,hakika ilikuwa ni shangwe kwa

    chama cha upinzani PTP huku chama tawala RPP

    kikipitwa kwa kura nyingi sana. Vyama vingine

    vilivyobakia vilikuwa na upinzani mdogo hivyo

    havikuweza kufua dafu kabisa. Mgombea urais

    aliyeshinda alipeana mikono na wagombea wote

    kwa tabasami kuu,nao wagombea wengine

    waliupokea mkono wake kuonesha hawana

    kinyongo na wamekubaliana na matokeo hayo.

    Mwisho akapeana mkono na mpinzani wake

    mkubwa mheshimiwa Dominic Mtalemwa wa RPP,

    walipeana mikono wakiwa tabasamu kisha

    wakakumbatiana kwa furaha yao ya maigizo.

    Wakiwa wamekumbatiana mhe Filbert Ole ambaye

    ni mshindi aliongea kwa sauti ya chini, "bado ni

    chekechea kwenye siasa usishindane na aliye chuo

    kikuu". Maneno hayo ya dharau hayakusikika na

    mtu yoyote isipokuwa Mtalemwa mwenyewe

    ambaye hakuhisi kama ipo siku atadharauliwa

    namna hiyo. Hata hamu ya kukaa eneo haikuwepo

    ndani ya nafsi

    yake kutokana dharau aliyooneshwa,kwake ilikuwa

    ni kuaibishwa ingawa hakuna mtu aliyeiona. Alitoka

    hadi nje ya ukumbi katika eneo la maegesho akiwa

    na wapambe wake wote,aliingia ndani ya gari

    alilokuja kisha akamuamuru dereva aendeshe kurudi nyumbani kwake.

    *******************************************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ukimya wa kampuni ya uchapishaji ya EAPL katika

    kuchapisha jarida la WAHANGA ulizua hali ya

    sintofahamu miongoni mwa waandishi hao wa

    kimataifa, kuzungushwa na mtu aliyepokea nakala

    zao kuliwashangaza sana kwani haikuwa kawaida

    kwa jambo kama hilo kutokea.

    "nashauri tuifuatilie nakala yetu" alishauri Norbert

    katika kilichowekwa juu ya suala hilo.

    "hata mimi naona tufanye hivyo" Davis alimuunga

    mkono Norbert

    "hapana tusifanye hivyo " Joseph alitoa rai ya

    kupingana na mawazo ya Norbeert na Davis kisha

    akawaambia "hili suala halijakaa kama

    mnavyofikiria nyinyi jamani, kumbukeni tulimchezea

    simba sharubu akiwa amesinzia na sasa

    amezinduka lakini ametutisha tu pasipo

    kutung'ata". Kauli hiyo ilimuacha kila mmoja njia

    panda, hali hiyo Joseph aliibaini haraka sana na

    ikamlazimu kuwafafanulia "namaanisha hivi kama

    jarida lingetoka tungekuwa tumechokonoa mahali

    pabaya,bsasa ili kutuonesha mhusika anaweza

    kufanikiwa kufanya lolote ndio amezuia kazi yetu".

    Wote waliafiki kwa kutikisa kichwa kuashiria

    wamekubaliana na hoja ya Joseph.



    "jambo ulilolisema Mr Kiiza nakubaliana na wewe

    kwa asilimia mia moja na sasa inatubidi tusitishe

    kazi ya kuchunguza tukubali kazi yetu imepotea tu"

    aliongea Allison kwa mara ya kwanza baada ya

    kuwasikiliza wenzake. Akaendelea kuwaambia "cha

    msingi ni kuangalia kazi nyingine baada ya hapa,

    ila kwa sasa tukubali tumeshindwa kuwazindua

    wanachi usingizini".

    Baada ya wote kutoa mawazo yao walikaa kimya na

    kumtazama Hilda, "hakuna kilichoharibika jamanu

    katika suala hilo mimi nahisi tuwaache wasahau

    kisha tuwaumbue" Hilda kwa mara ya kwanza

    aliongea baada ya kuona anatazamwa na kila mmoja.

    "unamaanisha nini kusema hivyo?" .Alphonce

    alimuuliza kwa pupa. Hilda alianza kuifafanua kauli

    yake kwa kusema "baada ya kukamilisha uchunguzi

    nakala zile nilivutiwa sana nazo,hivyo nilitoa vivuli

    vyake kisha picha za ushahidi nikazihamisha

    kwenye santuri nikavihifadhi mahali ili ziwe kumbukumbu kwangu". Wote walitoa

    tabasamu na kufufua tumauni jipya mioyoni mwao....



    "aisee we mwanamke sijui una...." Norbert

    hakumalizia kauli yake hiyo ya kimasihara baada ya

    kicheko cha ghafla kumshika, hali hiyo ilikuwa kwa

    wenzake pia waliopo eneo hilo kwa kitendo

    alichokifanya Hilda. "sasa nimekuwa kikatuni

    jamani, maana mnavyonicheka " aliongea Hilda

    baada ya kuona vicheko vimezidi. Vicheko vya

    wote vilipotulia Joseph alisema "aisee sikutegemea

    kabisa kama utafanya hivi, hivi ulioteshwa nini kama

    kuna tatizo litatokea?". "labda mzimu wa kitusi

    ulimfungulia njia" Allison naye alidakia na

    kusababisha wenzake wote wacheke.

    "khaa jamani kuwa mtusi nayo imekuwa mada "

    Hilda aliongea kwa mshangao baada ya kusikia

    utani uliotunbukizwa na Allison. Mjadala uliikatika

    kwa muda na utani ukachukua nafasi yake dhidi ya

    Hilda, binti wa kitusi aliyeishi Tanzania kwa muda

    mrefu ingawa makazi yake ni Rwanda. Utani huu

    ulidumu kwa muda kisha Davis akawarejesha

    kwenye kwa kusema "sasa jamani suala limeisha

    au sio?"

    "hata mimi nadhani hivyo" Norbert naye akaafiki

    kauli ya Davis. Wote kwa pamoja

    wakakubaliana wasubiri joto la siasa litulie kisha

    waitoe kazi yao kwa mara ya pili kwa kutumia

    kampuni nyingine na sio ile ya awali. Wakitawaliwa

    nyuso zenye tabasamu baada ya kufufuka tumaini

    jipya la kazi yao, waliamua wapumzike siku hiyo ili

    wakaitulize furaha yao.



    *******************************************************

    Januari mwaka uliofuata rais mpya wa jamhuri ya

    muungano wa Tanzania mheshimiwa Filbert Ole

    aliapishwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es

    salaam, hafla hiyo ya kuapishwa rais Ole

    ilihudhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu

    mbalimbali za jijj la Dar es salaam huku wachache

    wakitoka mikoani kuja kushuhudia hafla hiyo.

    Wanadiplomasia mbalimbali pamoja na viongozi

    nao walialikwa katika sherehe hizo, viongozi wa

    mataifa mbalimbali barani Afrika nao hawakuwa

    nyuma katika uhudhuriaji wa sherehe hizo. Hadi

    muda wa kuanza sheria hizo unakribia tayari

    uwanja mzima ulishafurika watu walioalikwa huku wasioalikwa wakiwa nje ya geti, hali hiu

    iliwalazimu watu wasioalikwa kukaa nje ya uwanja

    huo kutokana na kutokana na ulinzi ulio ndani ya

    uwanja. Ulinzi wa wanausalama nao haukuwa wa

    kulegalega, ulinzi huu ulikuwa imara sana na

    wenye kuridhisha sana kwa viongozi wa eneo hilo.

    Muda mfupi kabla ya sherehe kuanza rais

    anayemaliza muda wake Prof Athumani Kisiga

    aliingia uwanjani akiwa katika gari la wazi kisha

    akauzunguka uwanja huku akipungia mkono watu,

    baada ya hapo alienda kusimama katika jukwa la

    kiapo kisha mizinga ishirini na moja ikafuata. Rais

    mstaafu alishuka kukagua gwaride la majeshi

    yote, alipomaliza alipanda jukwaa na kuketi mahala

    pake huku bendera ya rais ikishushwa kuashiria

    kuisha kwa utawala wake. Hatimaye shughuli ya

    kuapishwa kwa rais Ole ilianza mnamo saa tano za

    asubuhi, rais mtarajiwa alipanda katika jukwaa la

    kiapo baada ya rais mstaafu kupanda tayari wakiwa

    pamoja na jaji mkuu. Shughuli za kuapishwa

    ziliannza na kufuatiwa na kuapishwa kwa makamu

    wa rais Dk. Hilary Jamadin, ukaguzi wa gwaride

    maalum ulifuata kuhitiimisha shughuli hizo. Ratiba

    nyingine zilifuata baada ya shughuli hiyo

    kukamilika.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******************************************************

    Muda huo huo sherehe zikiwa zinaendelea kwenye

    mitaa ya jiji la Dar es salaam watu walikuwa

    wakishuhudia kupitia kwenye luninga tofauti,

    vikundi mbalimbali vya watu vilikuwa vikiijadili

    sherehe hiyo ya kitaifa. Mijadala hiyo ilijadiliwa

    katika makundi tofauti ndani ya mitaa ya

    jiji , wengine walikuwa wamekaa majumbani mwao

    wakiendesha mijadala hiyo. Hali hiyo pia ilikuwa imo

    ndani ya nyumba moja ya kisasa maeneo ya

    mikocheni. Huzuni ya watu humo ndani ilishaanza

    kusahaulika

    kwa watu wote isipokuwa mama mwenye nyumba

    hiyo ambaye ni mjane, watoto wake wakiwa

    wanafurahia kuangalia rais wao mpya waliyempigia

    kura yeye alikuwa amezama katika dimbwi zito la

    mawazo. Hakuwa mwingine bali ni mke wa

    aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la kahama

    bwana Gerald Geofrey aliyeuawa kwa kupigwa

    risasi, mwanamama huyu alionekana ana dukuduku

    zito moyoni wake na kila akiangalia sherehe hizo

    za kumuapisha rais zilikuwa zinamchefua.

    Hakuweza kustahimili kuziangalia sherehe hizo

    tena kwani machozi yalishaanza kumtoka, akaingia

    chumbani akilia kwa uchungu. Hali hiyo

    iliwashangaza sana watoto wake ingawa

    hawakuthubutu kumuuliza chochote, walimuacha

    kama alivyo hadi atakapokuwa sawa.

    *******************************************************

    Baada ya sherehe za kuapishwa kuisha na hatimaye

    rais Ole kukabidhiwa majukumu ya urais na rais

    mstaafu, shughuli za kimaendeleo ziliendelea kama

    kawaida. Rais huyu aliooingia madarakani aliteua

    baraza lake la mawaziri ndani ya muda mfupi tu,

    baraza hili la mawaziri lilikuwa na mchanganyiko

    wa mawaziri wapya na wa awamu iliyopita. Baada

    ya mwaka mmoja tu toka rais Ole aingie

    madarakani tayari nchi ilisheheni miundombinu ya

    kila aina, pia huduma za kijamii zikaimarishwa

    ndani ya muda huo. Hii ilisababisha wananchi

    wazidi kumpenda na kumuamini sana rais wao,

    hata wale waliokuwa sio wanachama wa chama

    chake walianza kuwa na imani nae. Wizara zote

    zilionekana zikifanya kazi ipasavyo na kupelekea

    awamu hii ya urais iwe ya kipekee.

    Ndani ya mwaka huohuo utafiti wa madini ulifanyika

    wilayani kondoa katika mji kuu wa nchi hii, kiwango

    kikubwa cha madini aina ya almasi kiligunduliwa

    ndani ya eneo la kijiji cha Chambalo, madini hayo

    yenye thamani kubwa yaligunduliwa ndani ya eneo

    hilo na ripoti ikapelekwa kwa waziri wa maliasili na

    utalii Dk. Jumanne Mdoe. Habari hizo pia

    zilisambaa kwa wananchi wa kawaida ndani ya nchi

    nzima, wengi wa wananchi kupitia vyombo vya

    habari walitaka mgodi huo utumike kwa manufaa ya

    nchi yao tu. Baada ya siku mbili waziri wa maliasili

    na utalii alieleza uamuzi uliochukuliwa na wizara

    yake juu ya madini. "hakika hii ni bahati ambayo

    Tanzania imetuangukia na tunapaswa tuitumie

    kama bahati ndani ya nchi yetu. Kumbukeni bahati

    haiji mara ya mbili na tunapaswa tusiipoteze bahati

    hii bali tuitumie kwa manufaa ya Tanzania yetu,

    hivyo mimi na wizara nzima ya maliasili na utalii

    tutaitumia bahati hii kwa ajili ya manufaa ya

    watanzania na si vinginevyo. Hivyo watanzaniwa

    watarajie mazuri kutokana na bahati hii na wawe

    na imani ya kupata matunda bora ya bahati hii"

    hayo ndiyo maneno ya waziri wa maliasili na utalii

    juu ya matumizi ya hayo madini. Maneno hayo

    yalimfurahisha kila raia aliyeyasikiliza kupitia

    kwenye vyombo vya habari na ikawa ni kama

    bahati kuwa na kiongozi kama yeye, watu walikuwa

    wanangojea kwa hamu hayo matunda ya maliasili

    iliyogunduliwa nchini mwao. Baada ya mwezi mmoja kupita toka hotuba ya

    waziri huyo katika mkutano wake na waandishi wa

    habari , ajali kubwa ilitokea maeneo ya

    msata baada ya gari ndogo aina ya Land cruiser

    kugongana uso kwa uso na Fuso lililobeba mkaa

    likitokea mkoani Tanga kuja jijini Dar es salaam.

    Dereva wa land cruiser alifariki papo hapo huku bosi

    wake akiwa ni majeruhi hivyo kulazimika

    kukimbizwa hospitali iliyo jirani kwa ajili ya

    matibabu, askari wa usalama barabarani walifika

    eneo la tukio mapema na kupima ajali. Upande wa

    fuso lililobebe mkaa dereva wake hakufahamika

    alipo hadi muda huo, ilikuwa ni mshangao mkubwa

    sana kwa maaskari hao na walipoangalia gari aina

    ya land cruiser ndio walipopata mshango zaidi.

    "aisee hii si gari ya mheshimiwa" aliuliza mmoja

    wa maaskari hao mwenye V moja begani. "kostebo

    una uhakika maana hata majeruhi aliyekutwa

    haujamtambua kutokanana majereha yaliyopo usoni

    mwake" mwenzake alimwambia huku akitazama namba

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    za gari hilo pamoja na stika za gari hiyo. "aisee ni

    lenyewe na nahisi hata majeruhi aliye kwenye hilo

    gari ni yeye maana leo alikuwa anasafiri kuelekea

    Tanga kuangalia hifadhi ya mkomazi" aliongea tena

    yule askari baada ya kukagua namba za gari lile

    kwa umakini. Walipomliza waliamua waliamua

    kuwasiliana na wenzao waliongozana na gari la

    wagonjwa la hospitali ya tumbi lililofika hapo kwa

    ajili ya kuchukua majeruhi na mwili wa dereva

    kwenda kuihufadhi.

    *******************************************************

    Joseph Kiiza wa WAHANGA akiwa safarini akitokea

    mkoani Kilimanjaro alikuta ajali kubwa iliyotokea

    maeno ya Msata mkoani pwani, akiwa kama

    mwanishi wa habari mwenye vifaa vyote

    alisimamisha gari ya ofisi yake aina ya toyota

    harrier na kuanza kuanza kuelekea eneo la ajali.

    Hadi muda huo tayari utepe ulikuwa

    ushazungushiwa eneo na askari walikuwa wamefika

    wengi sana, alipojaribu kuuvuka utepe huo alizuiwa

    na askari hali iliyomlazimu atie kitambulisho chake

    na kuwaonesha maaskari hao. Maaskari

    walimruhusu apite eneo hilo lenye utepe,

    alipouvuka huo utepe alianza kupiga picha

    mbalimbali kisha akafanya mahojiano na baadhi ya

    maaskari wa eneo hilo. Akiwa anaendelea kupiga

    picha mbalimbali za ajali hiyo kamba ya kiatu

    ilimfunguka na kumlazimu ainame ili aifunge akiwa

    jirani na fuso lililopata ajali, alipoinama tu alisikia

    mlio wa bati la fuso ukitobolewa eneo ambalo

    kichwa chake kilipokuwa wakati amesimama.

    Hakuhitaji elimu ya ziada kutambua kuwa alikuwa

    amelengwa na risasi ambayo ilimkosa baada ya

    kuinama na kufunga kamba za viatu. Alijibiringisha

    chini toka pale alioo kuelekea pembeni huku

    maaskari wakiwa tayari wameelekeza silaha zao

    ilipotokea risasi hiyo.



    Hawakuweza kuambulia chochote zaidi ya vichaka

    vilivyopo eneo hilo, baadhi ya askari waliamua

    kuelekea ilipotoka risasi hiyo wakiwa wameweka

    silaha zao kwa namna ya tahadhari. Joseph naye aliinua

    kwa tahadhari pale chini alipokuwa amelala baada

    ya kujibiringisha pembeni, alikimbia kwa haraka

    hadi alipoliacha gari lake kisha akaingia na akakilaza kiti

    chake pamoja na yeye kulala akiwa anahema mfululizo kwa tukio

    lililomkuta. Hakutaka tena kutoka nje kwa kuhofia

    usalama wake, akiwa amejilaza hapo alisikia mlio wa

    pikipiki aina ya bajah ukitokea barabara ya vumbi

    iliyo jirani na eneo hilo. Pikipiki hiyo ilifuata njia iendayo

    Chalinze kwa mwendo wa kasi, mwendo wa pikipiki

    hiyo pamoja na makelele yake ulimvuta Joseph na

    kumfanya ainue kichwa na kuitazama. Aliiona ikiwa

    ina mchoro wa chui katika bango lililokuwa

    linaning'inia nyuma, aliipuuzia kisha akarudi na

    kujilaza kwenye kiti cha gari yake. Baada ya muda

    wale maaskri walirudi pasipo kuambulia chochote

    cha ushahidi zaidi ya bunduki aina ya sniper rifle

    iliyotelekezwa, Joseph aliinua kiti kisha akaiwasha

    gari yake. Maaskari hawakushughulika naye kabisa

    hata alipowaambia anaondoka wao walimruhusu

    aende, Joseph alifuata barabara iendayo chalinze

    kwa mwendo wa wastani kisha akaongeza mwendo

    ili awahi aendapo. Alifanikiwa kufika Chalinze ndani

    ya muda mfupi tu kutokana na kutumia mwendo

    mkali, alifuata njia iendayo Dar es salaam kwa

    mwendo ule hadi kibaha . Hapo alifuata barabara iliyo upande wenye kibao

    kilichoelekeza mahali ilipo hospitali ya tumbi toka

    barabara ya morogoro katika eneo ambalo zamani

    lilijulikana kama Tamko. Baada ya kuingia barabara hiyo alienda mwendo mfupi tu

    alipishana na ile pikipiki aina ya baja ikitokea mahali

    anapoelekea, sasa alimuona dereva wa pikipiki hiyo

    alivyo ingawa alikuwa amevaa kofia ya kujikinga

    kichwani. Alikuwa ni mtu mrefu na mwembamba

    mwenye mavazi yaliyomkaa vilivyo na mikononi

    alivaa glovu za kuendeshea pikipiki, kumuona hapo

    kwa mara ya pili hakukumshtua Joseph zaidi ya

    kuvutika kuuangalia jinsi alivyo. Alipofika hospitali ya tumbi alipitiliza

    hadi mapokezi , alijitambulisha kisha akumuulizia

    majeruhiwa ajali aliyefukishwa hospitalini hapo.

    Joseph alipelekwa kwa mganga mkuu wa hospitali

    hiyo kwani manesi na madaktari wengine

    hawakutakiwa watoe taarifa yoyote juu ya majeruhi

    huyo, alipofika alijieleza kwa mganga huyo shida

    yake iliyomleta kisha akaomba ushirikiano katika

    jambo hilo.



    "kusema ukweli muda si mrefu tumepokea majeruhi

    wa ajali ambaye alikuwa ni mheshimiwa, ninasikitika

    kukutaarifu kuwa hatunaye tena duniani hadi sasa"

    aliongea mganga mkuu Joseph akinakili maelezo

    hayo, alimsaili mganga huyo kwa maswali

    machache kisha akaondoka eneo hilo baada ya

    kuwaaga wenyeji wake.

    ******************************

    *************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taarifa za kifo cha waziri wa maliasili na utalii

    zilisambaa kama moto wa kifuu, karibu sehemu

    zote za jiji la Dar es salaam na majiji mengine

    yalishazipata taarifa hizo kabla hata vyombo vya

    habari havijaitangaza. Maelfu ya wananchi

    walihuzunika na kifo cha mtumishi wa umma

    mwenye kuijali kazi yake, taarifa hizo zilipofika ikulu

    zilipokelewa kinamna nyingine ingawa rais Ole alitoa

    salamu za rambirambi kwa familia ya waziri wake.

    Ilikuwa ni huzuni isiyoelezeka kwa familia ya

    marehemu, hata watu wa karibu waliomjua vizuri

    waziri huyo. Siku iliyofuata mwili wake uliletwa jijini

    Dar es salaam kisha ukaenda kuhifadhiwa katika

    hospitali ya taifa ya Muhimbili, hadi mwili

    unaingizwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti

    tayari hospitali hiyo ilifurika waandishi wa habari

    waliokuwa wakisaka habari na utbibitisho juu ya hilo

    suala. Joseph na Nobert wakiwa miongoni mwa

    waandishi hao, walitumia taaluma yao vizuri jambo

    lililowawezesha wapate picha za uthibitisho wa tukio

    hilo. Waliporidhika waliondoka hadi walipoacha gari

    ya kikundi chao aina ya toyota Noah ya rangi nyeupe, walipanda

    wote huku Norbert akiketi nyuma ya usukani kisha

    wakaondoka hospitalini hapo. Walifuata njia iendayo

    kituo cha zimamoto, wakiwa wanamalizia kona ya jengo la Swiss kuingia

    katika barabara ya umoja wa mataifa Joseph aliangalia

    nyuma kupitia kioo cha pembeni kilicho upande

    wake. Hapo ndipo alipoingiwa wasiwasi kwa kile

    alichokiona aliiona pikipiki aina ya baja ikiwa nyuma

    yao baada ya magari mawili, alipomtazama dereva

    wa ile pikipiki alikuwa mrefu na mwembamba kama

    aliyekutana nae jana msata na hospitali.



    "Norb huyo jamaa mwenye pikipiki huko nyuma sina

    imani nae" alimwambia Norbert



    "yupi? huyo kwenye baja au boxer maana wapo

    wawili huko nyuma na wote wamevaa suti nyeusi"

    alisema Norbert na kumfanya Joseph ageuke

    aangalie vizuri, alipoangalia aliona pikipiki ya tatu

    ain ya suzuki ikija kwa kasi kisha ikaungana na wale

    wawili hali iliyofanya waonekane wapo watatu

    kiidadi. Alipowatazama vizuri aliona wote ni

    wembamba na warefu tena wamevaa mavazi

    yanayofanana.



    "wapo watatu Norb inabidi tufanye kitu aisee ili

    tuwakwepe" aliongea Joseph.



    "punguza uoga Jose" aliongea Norbert.



    "Norb niliwaambia jana nimekoswa na risasi kisha

    nikaiona pikipiki aina ya baja ikiendeshwa na mtu

    mwembamba na mrefu baada ya kukoswa na risasi

    na nilipokuwa naenda hospitali ya Tumbi, sasa mimi

    sina imanu nae huyo" alifafanua Joseph na

    kumfanya Norbert aifuate barabara ya morogoro kwa

    mwendo wa kasi punde tu alipofika katika makutano

    ya barabara yaliyo jirani na kituo cha zimamoto

    maarufu kama fire, aliifuata barabara hiyo kwa

    mwendo wa kasi huku akiangalia nyuma. Zile

    pikipiki tatu nazo bado zilikuwa zinawafuatilia kwa

    mwendo wa kasi lakini hazikuwapita wao, hali hiyo

    ilimsababisha Norbert aifuate barabara iendayo Ilala

    baada ya kufika makutano ya barabara yaliyo jirani

    na msikiti wa kichangani maeneo ya magomeni

    mapipa. Akiwa katika mwendo uleule huku akiyapita

    baadhi ya magari, aliifuata barabara hiyo hadi

    mzunguko wa kigogo kisha akafuata barabara ya

    mkato iendayo ubungo kupitia kigogo. Hadi muda

    huo tayari ilikuwa ni muda wa saa saba muda huo

    watu walikuwa wakiswali swala ya

    adhuhuri katika misikiti. Norbert alifuata njia hiyo ya

    mkato iendayo ubungo kisha akaingia katika

    maegesho ya magari ya msikiti mmoja wa ghorofa

    uliopo upande wa kulia mkabala na dhule ya msingi ,maegesho hayo ya msikiti yalikuwa

    yana magari ya waumini wachache. Kulikuwa kuna

    gari aina ya Noah zenye kufanana na gari la akina

    Noerbert, hakika huo ulikuwa mwanya kwa akina

    Norbert kwani nao waliegesha gari kisha wakalaza

    siti walizokalia. Baada ya muda walisikia milio ya

    pikipiki tatu tofauti huku makelele ya pikipiki aina ya

    baja ikiwa inavuma zaidi, pikipiki hizo zilisimama

    kwa muda mfupi kisha zikaondoka kuendelea mbele.

    ******************************

    *************************



    Vijana watatu wa kundi hatari la three devils kutoka

    Marekani walikuwa wapo maeneo ya hospitali ya

    taifa ya muhimbili, walikuwa hapo kuhakikisha kama

    mwili ulioingizwa hapo ni wa mheshimiwa waziri

    aliyepata ajali siku iliyopita. Wakiwa na vitambulisho

    feki vya usalama wa taifa, waliweza kuiona maiti

    baada ya kujitambulisha wao ni usalama wa taifa na

    walikuwa kwenye uchunguzi. Walipotoka mmoja wao

    alipiga simu na kuongea, "ni yeye bosi" kisha

    akakata simu na kuwaashiria wenzake waondoke.

    Wakiwa wanatoka waliwaona Norbert na Joseph

    wakiwa pamoja, walipotaka kuondoka kuondoka

    mmoja wao akawaambia wenzake wawili, "ni

    sehemu ya kazi yetu, au mmesahau". Walitazamana

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kisha wakaenda kuziegemea pikipiki zao huku

    wakiwasubiri wakina Norbert, baada ya muda

    Norbert na Joseph waliingia ndani ya gari lao na

    kuondoka hospitalini. Three devils nao waliingia

    kwenye pikipiki zao na kuanza kuwafuatilia wakiwa

    katika namna ya kufuatana katika mstari ulionyooka,

    mwenye pikipiki aina ya bajah akiwa mbele kisha

    akafuata mwenye pikipiki aina ya boxer na mwisho

    akaja mwenye pikipiki aina ya suzuki. Kwa

    walivyopangana ilikuwa ni vigumu sana mtu kujua

    kama wapo watatu kwa muonekano wa mbele,

    walitembea hivyohivyo hadi walipofika jirani na

    makutani ya kituo cha kuzimia moto jirani na shule

    ya jangwani. Hapo mwenye boxer alitoka pembeni

    kisha mwenye suzuki akafuata na kukaa nyuma ya

    mwenye bajah kwa upande wa kushoto na kulia.

    Hapo ndipo gari ya akina Norbert iliongeza mwendo

    kuifuata barabara iendayo magomeni,



    "wamegundua

    hawa,tuwafuate hivihivi hakuna kuwaacha" aliongea

    mwenye bajah kuwataarifu wenzake kupitia simu zao

    ndogo zilizokuwa ndani ya sikio. Waliwafuata

    wakiwa na mwendo wa wastani ili kuwaondoa hofu

    wakina Norbert, walipofika magomeni walifuata njia

    iendayo Ilala kisha wakapunguza mwendo ili

    kuwapumbaza wakina Norbert na kuhakikisha

    hawawapotezi. Hadi wakina Norbert wanaingia

    mzunguko wa kigogo na kuelekea upande wa kulia wao walikuwa

    wamewaona ila walikuwa mbali kidogo, hapo ndipo

    walipokuja kupigwa chenga ya mwili na Norbert

    baada ya Norbert kuegesha gari jirani na msikiti

    kwenye magari yanayofanana na gari lao. Three

    devils walipofika hapo kwenye kona yenye barabara

    inayopita msikitini hapo, walisimama kwa muda

    kisha wakayaangalia magari hayo kwa umakini

    halafu wakaondoka.





    Walienda hadi ilipo shule ya sekondari ya Loyola

    kwa mwendo wa kasi, hapi ndipo walibaini

    wamepigwa chenga ya mwili. Baada ya kubaini

    wamepigwa chenga ya mwili, waligeuza pikipiki zao

    kisha wakatazamana kila mmoja halafu wakarudi

    kule walipotokea. Walipofika kigogo kwenye msikiti

    mkabala na shule ya msingi, walikuta bado watu

    hawajamaliza kuswali swala ya adhuhuri na moja ya

    magari haikuwepo eneo lile. Hali hiyo iliwafanya

    wamuite kijana mmoja muuza maji aliyepo jirani,



    "hey njoo mara moja!" alipaza sauti mwenye pikipiki

    aina ya bajah. Kijana huyo alifika mara moja akiwa

    na deli lake la kuuzia maji baada ya kusikia wito

    huo, "mambo vipi?" alimsabahi huku akitoa noti ya

    shilingi elfu moja kisha akampatia yule kijana. "safi

    braza unataka ya shilingi ngapi?" muuza maji

    aliitikia salamu kisha akamuuliza maji anayoyataka.



    "nipe ya mia saba, halafu samahani naomba

    nikuulize" aliongea huku akiweka stendi ya pikipiki

    halafu akashuka.



    "usihofu braza uliza tu" aliongea muuza maji huku

    akimpatia maji.



    "eti hujaona gari yoyote aina ya Noah ikija kuegesha

    hapa msikitini wakati watu wanaswali".



    "nimeiona braza sema imeondoka kitambo kidogo bila

    hata kutoka mtu".



    "poa poa kaka ngoja sisi tuwahi" aliongea huku

    akiuma meno yake kwa hasira. Alichukua maji hayo

    pasipo kuyanywa kisha akaenda kwenye pikipiki

    yake, alipofika akaiwasha kisha akawaashiria

    wenzake waondoke, alitia gia kisha akaondoa

    pikipiki hiyo huku mkono mmoja akiwa ameshika

    maji aliyoyanunua. Alienda hadi kwenye mzunguko

    wa kigogo kisha akayatupa maji hayo kwenye mtaro

    halafu akavuta mafuta kuelekea njia iendayo Ilala.

    Jim ndio jina lake na ndio anavyotambulika hata

    kwa wenzake, ni mmarekani aliyeingia Tanzani

    miaka miatu iliyopita kwa agizo maalumu la mkuu

    wake anayejulikana kwa jina la Eagle kutoka Miami

    jijini Marekani. Kijana huyu ni muuaji wa hatari na

    wakuaminika wa kundi la Three devil , yupo nchini

    Tanzania kwa miaka hiyo ili aweze kutimiza lengo

    maalumh aliloamriwa kulitimiza. Jim ameingia

    Tanzania kama mfanyabiashara aliyeamia Tanzania

    kwa ajili ya kuwekeza, akiwa nchini kwa muda wote

    huo amefanikiwa kujifunza lugha ya kiswahili kama

    inavyozungumzwa na makundi tofauti ya watu

    nchini kulingana na umri na kazi zao. Hadi mwaka

    wa tatu ndipo alipoongezewa wenzake wawili wa

    kundi lake wakiwa tayari wameshajifunza kiswahili,

    sasa wapo kazini na wameshafanikisha sehemu ya

    kazi waliyotumwa. Akiwa peke yake amefanikisha

    mauaji ya waziri kwa kutengeneza ajali dhidi yake,

    pia alijaribu kumuua mwandishi wa habari ingawa

    mpango huo ulifeli. Michael na Morris ndio

    wamarekani wengine wanaounda kundi la Three

    devil wakiwa chini ya Mr Eagle wa Marekani.

    Mpango wao wa kwanza toka waanze kufanya kazi

    pamoja umefeli baada ya kupigwa chenga ya mwili

    na Norbert, sasa wana hasira na wanaelekea yalipo

    maskani yao kujipanga upya.

    *********************************************

    *******************

    Norbert aliinua kiti cha gari kisha akawasha gari

    baada ya zile pikipiki kupita na milio kufifia, alirudi

    hadi kwenye mzunguko wa kigogo kisha akafuata

    barabara iendayo ilala. Alipofika mataa ya Ilala boma

    alikuta taa za upande wake zikiwa zimeruhusu na

    kumlazimu kunyoosha moja kwa moja hadi yalipo

    mataa ya keko, hapo napo ikawa ni kama bahati

    baada ya kukuta askari wa usalama barabarani

    akiwa ameruhusu magari ya upande wake. Alikata

    kona kuingia barabara ya mwalimu nyerere iendayo

    Tazara halafu akaongeza mwendokasi wa gari,

    walipofika yalipo mataa ya makutano ya barabara

    maarufu kama Tazara aliamua kufuata barabara ya

    Mandela iendayo vetenari. Alitumia dakika takribani

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    tatu akawa ameshavuka vetenari na sasa alikuwa

    anakata kona kuingia upande wa kulia kufuata

    barabara iendayo mtoni kwa azizi ally kupitia

    temeke. Hapo alienda kwa mwendo wa kasi

    kutokana na uchache wa magari hadi usalama kisha

    akaingia upande wa kulia kwenye barabara ya vumbi

    ipitayo shule ya msingi Muungano eneo la temeke,

    aliendelea hadi alipoivuka shule ya msingi

    muungano kuingia

    kushoto kisha akaenda moja kwa moja hadi katika

    nyumba moja yenye geti kubwa jeusi kisha akapiga

    honi. Ndani ya dakika moja geti lilifunguliwa kisha

    akaingiza gari hafi kwenye maegesho ya nyumba

    hiyo, alikanyaga breki kisha akazima gari halafu

    wote wakashuka kwa haraka huku wakihema kama

    wamekimbia mbio ndefu. Wakiwa na mwendo wenye

    papara kama wamekuja kwa shari, waliingia ndani

    ya nyumba hiyo kupitia mlango wa uani hadi katika

    ukumbi wa nyumba hiyo unaopendeza kuutazama.

    Waliwakuta wakina Hilda, Davis na Allison wakiwa

    wapo kwenye meza ya inayotumika kwa chakula

    iliyopo katika ukumbi wa pili jirani na ukumbi wa

    sebule wa nyumba hiyo, Joseph alijitupa kwenye

    kochi huku akihema mfululizo na Norbert alibaki

    kasimama huku mikono yake ikiwa imeshika kiuno

    chake na kichwa akiwa anakitikisa kwa masikitiko.



    "nyie wanaume vipi kwema?" aliuliza Hilda baada ya

    kuwaona wakiwa katika hali hiyo.



    "ni kinyume cha kwema" alijibu Norberr huku

    akintoa kitambaa mfuko wa nyuma wa suruali yake

    kisha akajifuta jasho katika uso wake.



    "kulikoni" aliuliza Hilda huku akigeuza kiti

    kuwatazama Norbert na Joseph.



    "yule jamaa niliyemuona msata na kibaha

    tumuona tena muhimbili leo akiwa na wenzake

    wawili" aliongea Joseph halafu akajiweka sawa

    kwenye huku

    akihema kisha akasema ,"walikuwa wanatufatilia

    pasipo sisi kujua, na hata tulipojua Nor aliongeza

    mwendo wa gari na wao wakaongeza mwendo wa

    pikipiki zao kutufualia hadi sehemu moja yenye

    msikiti wa ghorofa. Hapo ndipo Nor akawapiga

    chenga wakapotea".



    "pongezi kwako mr Transporter kwa kucheza na

    usukani kama unamkimbia aduo kuu" aliongea Allison kumfananisha Norbert na

    muigizaji Jason Statham wa Uingereza aliyeigiza

    filamu ya The transporter. Wote walicheka humo

    ndani kasoro Joseph.



    "yaani nyie sisi tumekimbia umauti mnatucheka, na

    wewe Nor unacheka wakati ulikuwa unawindwa"

    alipngea Joseph huku akijigeuza kwenye kochi kisha

    akalala chali kuangalia dari la nyumba hiyo.



    "Jose na wewe umezidi uoga" Davis alisema huku

    akicheka



    "ndugu kifo kitu kingine kabisa msilete mzaha"

    Joseph alisema akiwa anajiinua kivivu kwenye kochi

    huku wenzake wakicheka, aliposimama wima alienda

    moja kwa moja hadi kwenye jokofu lililopo jirani na

    meza ya chakula. Alitoa pombe kali kisha

    akaifungua halafu akaipeleka kichwani, alikunywa

    funda moja halafu akawatizama wenzake na

    kuwaambia "mimi leo wacheni nipumzike mpaka

    kesho, mnaweza mkaendelea". Joseph alifuata

    ukumbi mwembamba

    unaotenganisha vyumba vya humo ndani kisha

    akfungua mlango mmoja wa vyumba halafu akaingia

    ndani na kuufunga. Huku katika ukumbi wa

    unaotumika kama sehemu ya chakula Norbert

    alivuta kiti kilicho jirani na Hilda kisha akakaa karibu

    ya Hilda, "mahaba niue hao wapo pamoja" aliongea

    Davis kuwatania Norbert na Hilda.



    "we ulitaka tuwe mbalimbali kwani?" Hilda alisema

    akiwa

    ameweka mkono wake katika bega la Norbert.

    Waliendea kuongea huku wakitaniana kwa muda

    mfupi kisha ukimya ukatawala huku Norbert na Hilda

    wakiwa wanakumbatiana na kupigana na mabusu

    hapo mezani.



    "ngoja tuwapishe nyie mahaba niue"

    aliongea Davis akivuta kiti nyuma kisha akasimama

    halafu akaondoka eneo hilo, Allison naye alisimama

    akaondoka kumfuata Davis. Wakiwa wamebaki

    wenyewe hapo ukumbini Hilda alinyanyuka katika

    kiti chake kisha akaenda kukaa katika mapaja ya

    Norbert miguu yake akiipitisha kiunoni mwa kijana

    huyo. Hapo waligusanisha mapaji yao uso wakawa

    wanatazamana kwa ukaribu, hakika walionekana ni

    watu waliozama kwenye mapenzi mazito sana kwa

    mkao huo waliokaa.



    "kuna simu leo kutoka kwa CE imeingia leo

    asubuhi" aliongea Hilda kwa sauti ya chini

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "mh! huyo kibabu anasemaje?" aliuliza Norbert kwa

    sauti ya chini.



    "anataka kuongea na wewe, amesema ukirudi

    nimpigie"



    "mh! Kuna jipya limezuka nini?" Norbert aliuliza

    swali hilo kisha akamnyonya ndimi Hilda huku

    akimpapasa mgongo baada ya

    Joseph kutokea eneo hilo.



    "wa mahaba subirini kwanza nichukue kinywaji ndio

    muendele"

    Joseph aliwaambia kwa sauti iliyochangamshwa na

    pombe halafu akafungua jokofu, alitoa

    pombe kali ya pili kisha akaondoka..



    Hapo Norbert aliacha kunyonya ndimi ya Hilda huku

    akiwa amegusanisha paji la uso kama alivyokuwa,

    alihema kwa nguvu kisha akasema, "hizi kazi hizi

    aisee ni tabu kila siku kama wacheza filamu". Kauli

    hiyo ilimfanya Hilda acheke kwa sautu ya chini

    akiwa tayari ameshaingiwa na aibu zake za kike.



    "Nor inabidi umpigie CE leo hii maana unamjua yule

    mzee akisema ujue kuna jambo" Hilda aliongea

    huku ameelekeza macho yake pembeni kwa aibu.

    Norbert alimshika kidevu halafu na kumfanya Hilda

    amuangalie kwa macho malegezo. Walitazamana

    kwa muda mfupi kisha Norbert akambusu Hilda

    mdomoni jambo lililosababisha binti huyo afumbe

    macho kwa hisia.



    "Nor bwana ushaniweka katika wakati mgumu

    mwenzio kumbuka tupo kikazi acha tafadhali" sauti

    ya kudeka na yenye kubembeleza ilitoka kinywani

    mwa Hilda, muda huo tayari Hilda alikuwa ameibana

    miguu yake kwa nguvu katika kiuno cha Norbert.



    "najua mama ila hapa imebidi tuwe hivi" aliongea

    Norbert huku akinyanyuka na Hilda pamoja akiwa

    amembeba kama anampeleka mtoto aliyelala

    kitandani. Hilda naye alikuwa amepitisha miguu

    kiunoni mwa Norbert na mikono ikiwa shingoni kwa

    Norbert huku vifua vyao vikiwa vimegusana. Norbert

    alitembea kuufuata ukumbi mwembamba

    unaotenganisha vyumba vya kulala katika nyumba

    hiyo, alipofika katika mlango wa chumba ulio

    mkabala na chumba alichoingia Joseph alinyonga

    kitasa huku mlango ikikaidi amri ya kufunga na

    ukatii amri ya kufunguka. Alimuingiza binti huyo

    ndani kama anaenda kumlaza mtoto, alienda hadi

    kwenye kitanda kisha akamuachia kitandani ili arudi

    kufunga. Hadi muda huo Hilda alikuwa yupo

    amelazwa kitandani ila hataki kutoa miguu kiunoni

    mwa Norbert wala mikono shingoni.



    "no Hil wacha nifunge mlango kwanza" aliongea

    Norberr na kupelekea Hilda amuachie, Norbert alienda

    kufunga mlango kisha akarejea kitandani hapo

    alipomuacha Hilda. Muda huo tayari Hilda alikuwa

    amelala chali akiwa amejiweka huru kabisa, Norbert

    alipanda juu ya kifua chake kisha wakagusanisha

    ndimi na kupelekea wote waingie kwenye

    ulimwengu mwingine tofauti na sayari hii ya dunia.

    Hakika kila mmoja alionesha kumuhitaji mwenzake

    na hakuna aliyekuwa kumuacha mwenzake kwa

    muda huo, kazi yao waliiweka pembeni kwa muda ili

    kuhitimisha kazi hiyo isiyo rasmi. Baada ya masaa

    mawili walikuwa wameshakamilisha kazi yao na

    sasa wamepitiwa na usingizi mzito wakiwa

    wamejifunika shuka moja, ilipotimu saa kumi na

    moja jioni usingizi wao ulikatika baada ya simu ya

    mkononi inayotumiwa kwa ajili ya kazi kuita.

    Norbert aliinuka kivivu huku akiangalia mpigaji wa

    simu hiyo akiwa na uchovu mwingi, jina la mpigaji

    lilimuondoa uchovu kisha akaipokea simu hiyo kwa

    pupa kisha akaongea ,"N001 hapa naongea".



    "njoo ofisini haraka ukiwa na HI002" ilisikika sauti

    ya mpigaji ikitoa amri kisha simh ikakatwa. Norbert

    akaiweka simu kwenye mtoto wa mtanda kisha

    akampiga Hilda kibao katika kalio lake halafu

    akamwambia, "CE katuita sasa hivi, jiandae twende

    ofisini kwake", kisha akaokota kaptula yake

    aliyoitupa wakati wanaanza kasheshe na kuivaa

    mwilini. Hilda naye alishaamka na alikuwa

    anajinyoosha akiwa hana nguo yoyote mwilini.



    "aisee kama siyo kazi tungekesha leo, maana

    nikikutazama mh!" aliongea Norbert na kusababisha

    Hilda amtizame jicho la upande kisha akasema

    "looh! Lionee". Hilda alijifunga taulo kisha

    akamshika Norbert mkono, alimuongoza hadi bafuni

    pasipo Norbert kuleta pingamizi lolote. Huko

    walioga kisha wakatoka baada ya kumaliza,

    walijiandaa kisha wakatoka humo chumbani hadi

    sebuleni wakiwa wameshikana mikono kiupendo. Sebuleni waliwakuta Allison na Davis wakiangalia luninga na kuwaaga kisha wakatoka hadi nje kwenye banda la

    gari lililopo jirani maegesho ya gari ndani ya

    nyumba hiyo, walifungua milango ya banda hilo

    halafu wakaingia ndani kulifuata gari aina ya suzuki

    ya rangi nyekundu. Waliingia wote kwa pamoja huku

    Norbert akiwa ndio dereva wa gari hilo, mlio wa

    kuwashwa kwa gari hilo ulisikika kisha matairi yake

    yakaanza kujongea taratibu na kusababisha gari

    litoke kwenye banda la gari na kufuata uelekeo wa

    getini. Geti lilifunguliwa na mlinzi kuruhusu gari hilo

    litokee nje ya nyumba hiyo kwa mwendo wa

    taratibu, mwendo uliongezwa baada ya kuingia

    katika barabara ya vumbi inayopita shule ya msingi

    muungano kuelekea usalama kwenye barabara ya

    lami.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *********************************************

    ********************



    Ndani ya nyumba ya ghorofa iliyopo maeneo ya

    msasani kwenye moja ya mitaa ya msasani ambayo

    huwa wanaishi watu wenye kipato cha juu, kulikuwa

    na kikao cha dharura katika moja ya chumba cha

    mikutano cha nyumba hiyo na wahudhuriaji wake

    walionekana ni watu wenye kujiweza kiuchumi na wenye kauli.

    Mmoja akiwa ni kigogo maarufu wa Tanzania

    anayetumia jina KL akiwa sehemu kama hizo,

    mwingine akiwa ni kiongozi maarufu anayejiita FI na

    wengine ni vijana wa kundi la Three devils. Suala

    lililokuwa linajadiliwa katika mkutano huo ni kuhusu mpango

    wao madhubuti wa kupunguza vikwazo katika

    mambo yao. Hadi muda huo wote walishapeana

    salamu na sasa walikuwa ndio wanaanza kujadili,



    "wakuu napenda mjue kuwa tushapunguza moja ya

    magugu katika kubakikisha shamba letu

    linastawisha mazao yetu" Jim aliongea kwa kutumia

    lugha ya mafumbo kutokana na uwepo wa

    wafanyakazi waliokuwa wakiwahudumia wahudhuriaji

    wa mkutano huo.



    "vizuri Jim sasa naona kuna gugu jingine nitaliweka

    katika anga zenu ili muliondoe upesi kama

    ilivyokuwa kwa gugu la kwanza mtindo ni uleule"

    aliongea FI kumpongeza Jim kisha akampa kazi

    nyingine hapohapo.



    "pia ningependa ningependa wale kenge watano

    waondolewe haraka maana ni hatari sana" KL alitoa

    wazo hilo kwa kutumia lugha ya isiyo ya mafumbo

    baada ya wafanyakazi wote kutoka katika chumba

    cha mkutano.



    "hao ni kiporo kwanza kwa sasa tushughulikena

    hawa wenye kauli huku tukifunga midomo kupitia

    kwa wachapishaji" aliongea Michael kwa mara ya

    kwanza.



    "wazo zuri hilo Michael sasa baada ya huzuni

    kutulia nitaweka gugu jingine jirani na jembe ili

    liweze kulimwa haraka" FI aliongea kisha akavuta

    bilauri yenye kinywaji iliyopo halafu akapiga funda

    moja.



    "sasa huko tumemaliza ila kwa sasa inabidi tufanye

    juu chini tuwajue wanausalama wa kampuni ya upelelezi

    ya EASA walioingia nchini kwa kazi maalum ambayo

    bado hatujaijua mpaka saea , yaani siba imani nao kabisa" KL alibainisha jambo geni

    ambalo halijukani kwa wenzake waliopo haoi kwenye

    mkutano.



    "KL hiyo ni habari nyingine ila hawa vijana nina

    uhakika wataimaliza,sasa mimi na KL tunawahi

    sehemu mra moja. Tutakuja siku nyingine kuwapa

    maelekezo kama yakihitajika" FI aliongea baada ya

    simu yake kuita kisha akanyanyuka akiwa na KL

    ambaye alishanyanyuka tayari. Walitoka ndani ya

    chumba hicho cha mkutanina kuwaacha Jim,Michael

    na Morris wakiwa wanajadiliana mamboyao

    mengine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *********************************************

    ******************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog