Simulizi : Jinamizi
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Gari aina ya suzuki iliegeshwa katika ghorofa moja
lililopo maeneo ya Ilala mtaa wa Lindi katika wilaya
ya Ilala, milango yake ilifunguliwa kisha miguu ya
watumiaji wa gari hiyo ikifuata kugusa ardhi ya maegesho
iliyisakafiwa kwa ruva ndogondogo jirani na ghorofa
hilo. Hawakuwa wengine bali ni Norbert na Hilda na
sasa walikuwa wanaingia ndani ya ghorofa hilo
linalojulikana kama hoteli. Baada ya kufunga milango
ya gari hilo, walipitia mapokezi kisha wakapanda lifti
ambayo haitumiki na watu wa kawaida isipokuwa
wakubwa wa hoteli hiyo. Lifti hiyo ilishuka chini kwa
mwendo wa wastani kwa umbali wa takribani
ghorofa mbili kama ingekuwa inaelekea juu,
milango ilifunguka baada ya kufika mwisho wa safari
na taa zikawa zinawalaki. Norbert alitoka ndani ya
lifti hiyo na kufuata ukumbi mrefu wa sehemu hiyo
akiwa sambamba na Hilda, walitembea hadi kwenye
mlango uliopo mwisho wa ukumbi huo kisha
Norbert akaweka kidole gumba kwenye duara dogo
lililopo pembeni ya mlango. Mlio wa kengele
ulisikika kisha ikasikika sauti ikisema "welcome
N001(karibu N001)" kisha mlango ukajifungua
wenyewe, waliingia ndani moja kwa moja huku
mlango ukijifunga. Walitembea na kupita vyumba
mbalimbali huku wakipishana na watu mbalimbali
hadi kwenye mlango wenye maandishi yaliandikwa
CE, hapo walifungua mlango huo kisha wakaingia
ndani hadi kwa katibu mukhtasi aliyepo katika
chumba hicho.
"we mwanamke hicho kibabu kipo humo ndani"
aliongea Norbert kumwambia katibu Mukhtasi wa
ofisi hiyo huku akimpiga kibao cha uchokozi
"naona leo ndio unanikumbuka we dungadunga
ukiwa na bibi yako wa maigizo, yupo humo ndani
tena anawangoja nyinyi" aliongea Katibu mukhtasi
"we mke mwenzangu nikitoka huko
ninakuja kwako, jiandae kwani nina yako mazito, jiandae bibi"
aliongea Hilda na kupelekea Katibu mukhtasi wa
ofisi acheke kicheko kikubwa.
"bibu wewe tena nakungoja kwa hamu hapa ingia
huko kwa kibabu chako" aliongea Katibu mukhtasi
akiwa anacheka.
"nyie wanawake hebu kaeni kimya, hamjui kama
mume wenu hapa alaa sihitaji kelele" aliongea
Norbert na kusababisha Hilda ampige kibao cha
mgongo huiu akimwambia "looh kazi uhuni tu, una
mke hapa?". Norbert hakutilia maanani swali Hilda
ambalo lipokiutani zaidi, alifungua mlango wa ofisi
uliopo mbele yake huku akimwambia katibu
mukhtasi, " Norene jiandae mama nikitoka huko
maana nina hamu na wewe" kisha akingia ndani
akifutiwa na Hilda.
"ketini kwenye viti tafadhali" ilisikika sauti kutoka
kwenye kiti cha kuzunguka kilichokuwa kimegeuziwa
upande wenye kabati lenye makabrasha mengi.
Norbert na Hilda waliketi katika viti viwili vyenye
kutazama kisha wote kwa pamoja wakasema "ndiyo
mkuu", kauli yao ilisababisha kile kiti cha
kizungushwe na mtu aliyekuwa amekikalia
na kupelekea kiwe kimeelekea usawa wa mlango wa
kutokea. Mzee wa takribani miaka sabini mwenye
mwili mkakamavu ndiye aliyekuwa amekalia kiti
hicho, akiwa ni mwenye uso uliojaa umakini
aliwuliza, " kwanza nilitaka kujua ni wapi mmefikia
katika kaz yenu?". Baada ya kusikia swali hilo
Norbert na Hilda walitazamana kisha Hilda akasema,
"mkuu tumefanikiwa kupiga hatua katika kazi hii
ingawa kuna vikwazo vingi sana kutoka kwa kundi
lisilojulikana".
Mzee huyo ambaye ndiye CE
alimkatisha Hilda kisha akasema "najua wewe HI002
ni mwanamke shupavu na makini na wewe N001 ni
kijana mwenye uwezo wa hali ya juu, sasa
mnatakiwa mnisikilize kwa umakini maana hili suala
lina sura tofauti ndio maana nikawaita sasa
kutokana na taarifa niliyoipokea kutoka kwa Al005
wa Burundi. Huyu ni mpelelezi makini sana wa tawi
letu ambalo lipo Buruni ambaye yupo Tanzania kwa
siri , kijana huyu ameweza kubaini ujio wa wafuasi
wawili wa mr Eagle wa Marekani hivi karibuni
pamoja na uwepo wa mmoja wa wafuasi hao kwa
kipindi cha miaka mitatu hadi sasa. Pia amebaini
uhusiano uliopo kati ya vigogo wa nchini na Mr
Eagle wa marekani" CE alimeza mate kidogo kisha
akawasisitizia "inabidi muwe makini sana vinginevyo
tutawapoteza maana hawa wafuasi wa Eagle
wameshafahamu ujio wenu kwa mujibu wa
mwanausalama wetu tuliyempandikiza katika kikosi
cha usalama wa taifa".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sawa mkuu tumekuelewa, lakini nilikuwa nina ombi
moja tu kama itawezekana" aliongea Norbert na
kupelekea CE amtazame kwa umakini kisha
akamuashiria aseme.
"mkuu ningependa kama inawezekana tuwajue
AL005 na huyo aliyepo usalama wa taifa ili tuweze
kuwa nao pamoja katika kazi hii" Norbert alitoa rai
kwa CE kulingana mawazo yake .
"hapana huu si muda wake muafaka wa kuwa
pamoja, fanyeni kazi nyinyi kama nyinyi halafu
tutawajumuisha pamoja baadaye ikiwa makao
makuu watatoa amri" aliongea CE kupingana na rai
ya Noebrt kisha akamaliza kwa kuwaambia
"maelezo mengine mtayapata kwa Norene ikiwa
pamoja na vitendea kazi , sasa mnaweza mkaenda".
Norbert na Hilda waliinuka kwenye viti kisha kisha
wakasema "sawa mkuu" halafu wakaelekea ulipo
mlango wa kutokea, walifungua wakatoka kuelekea
kwa katibh mukhtasi.
Norbert na Hilda ni wapeleleziwa kampuni ya EASA
(East Africa Security Agency) yenye makao makuu
yake jijini Nairobi nchini Kenya na Dodoma nchini
Tanzania, walikutana kwa mara ya kwanza katika
chuo cha uninja jijini Yokohama nchini Japan
walipopelekwa kwa ajili ya kuchukua mafunzo ya
uninja. Wamefanya kazi mbalimbali pamoja katika
nchi za Afrika ya mashariki na kuipa sifa kampuni
hiyo iliyoanzishwa na viongozi wa nchi za ukanda
huu miaka kumi iliyopita, wapelelezi hawa kwa
kushirikiana na Moses Gawaza wa usalama wa taifa
waliweza kumkamata gaidi aitwae Brian miaka minne
iliyopita. Ukaribu wao umesababisha waonekane
wapenzi ingawa walikuwa kikazi zaidi kwa muda
mrefu hadi mwaka ulipita walipojikuta wakivunja
amri ya sita kutokana na utundu wa Norbert kwa
wasichana. Kijana huyu mwenye mvuto kwa
wasichana na mwenye uhusiano na wasichana
mbalimbali alimuwinda binti huyu na hatimaye
akamnasa, hadi hapo hawakuwa wapenzi rasmi
ingawa wamevunja amri ya sita kwa nyingi sana.
Walipoingia ofisini kwa katibu mukhtasi walimkuta
akiwa anaendelea kufanya kazi kwa kutumia
Tarakilishi iliyo mezani, Norbert alizunguka hadi
nyuma yake kisha akampiga busu la shavu lenye
kila aina ya ucbokozi katika mwili wa binti huyo.
Alimuachia kisha akavuta kitu kilicho jirani halafu
akakaa, Hilda aliendelea kusimama huku
akimtazama Norbert kwa jicho la husuda kisha
akasema, " we mwanaume sikuwezi kabisa".
"mama tulia kidogo basi vumilia tu" Norbert
aliongea kwa masihara kisha akashika kiuno cha
Norene kwa uchokozi na kupelekea Norene ampige
kibao kisichoumiza kisha akakisukuma kiti cha Norbert nyuma.
"yaani hapo umemuweza kweli maana anajifanya
kidume cha mbuzi sana, muone vile" Hilda aliongea
huku akimtazama Norbert kwa jicho la kumsuta.
Norene aliinuka kwenye kiti alichokuwa amekalia
kisha akawaambia "nifuateni", aliingia katika mlango
mmoja ulio pembeni ya ofisi yake huku Norbert na
Hilda wakiwa wapo nyuma yake mithili ya mkia kwa
mnyama. Ukumbi mpana wenye ubao tambarare wenye rangi nyeupe
ndio uliowakaribisha humo ndani, vifaa vya
kiupelelezi vya kila aina pamoja na silaha za kisasa
nazo ziliwalaki. Norene aliwasha tarakilishi
iliyounganishwa na kifaa maaluma cha kurushia
picha katika ubao maalum unaofanana na ule uliopo
katika kumbi za sinema. Tarakilishi hiyo iliwaka
baada ya muda mfupi tu kutokana na uwezo wake kuwa
mkubwa, kisha Norene akawa anafungua vikunja
mafaili vya Tarakilishi hiyo na kupelekea zionekane
picha zilizo ndani ya mafaili hayo. Aliifungua moja
ya picha hizo na kupelekea ionekane kwa ukubwa
wa kutosha katika ubao unaopokea mwanga kutoka
kwenye kirusha picha.
"Jim ndio jina lake na anajulikana kama muwekezaji
binafsi ndani ya nchi hii, ni muuaji wa kuaminika wa
kundi la Three devil na anatafutwa na shirika la
upelelzi la KGB la jijini Moscow nchini Urusi kwa
tuhuma za mauaji ya bilianea wa nchini humo. Kwa
mujibu wa taarifa tulizipata kutoka kampuni ya
kipelelezi ya Mossad ya dola ya Israel, huyu mtu
tayari alishawatoroka na kusababisha maafa makubwa
huko Yerusalemu. Sasa umakini katika kazi hii
inahitajika kwani sio mtu wa kawaida" Norene alisita
kwa muda akiwa mbele ya ubao mkubwa kisha
akawazama wasikilizaji wake kama wapo pamoja
nae, wote walitikisa vichwa kuashiria wamemuelewa
kisha Norene akafungua picha ya pili.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Anaitwa Michael na kibaraka wa Mr Eagle
aliyepandikizwa katika shirika la upelelezi M16 la
nchini Uingereza, huyu ni mtu hatari sana kwa
ulengaji wa shabaha pindi awapo na silaha pia ni
mkufunzi wa mafunzo ya mapigano ya nchini China.
Kijana huyu kwa sasa yupo hapa nchini kwa mujibu
wa mtu wetu aliyepo kitengo cha kamera katika
uwanja wa mwalimu Nyerere baada ya kunasa picha
zake , sasa basi pia umakini wenu unahitajika kwa
usalama wenu nadhani tupo pamoja" alisita kuongea
kwa mara ya pili kisha akawataza tena na kupelekea
hadhira yake imuashirie kuwa imemuelewa,
alifungua tena picha nyingine kisha akaanza kutoa
maelezo.
"huyu ndio wa tatu kati ya hawa vijana wanaounda
kundi la Three devil, Morris ndio jina lake na ndio
anavyojulikana. Huyu pia ni kibaraka wa Mr Eagle
katika shirika la FBI la nchini Marekani, uwezo wake
wa kupigana na kutumia visu ndio umefanya shirika
hilo la kijasusi lumuamini na kumpa nafasi wakijua
atakuwa msaada kwao kumbe ni kinyume chake.
Sasa basi hivi sasa yupo nchini na ushahidi
tumeupata kupitia kamera za ulinzi zilizopo uwanja
wa ndege wa mwalimu Nyerere. Pia napenda mjue
kuwa watu hawa wanafadhiliwa na vigogo wawili
wakubwa hapa Tanzania, mmoja akiwa ni tajiri
mkubwa hapa nchini na mwingine akiwa ni kiongozi
katika nchi hii" Norene aliwaeleza akiwa makini sana
na huo muda tayari alishaweka fimbo chini aliyoitumia
kuwaelekeza kisha akawaambia "kuwajua hao vigogo
ambao wanajiita FI na KL ni jukumu lenu kuanzia
sasa, pia kuhakikisha hao watu wanatiwa nguvuni ni
jambo la muhimu. Inahitajika wapatikane wakiwa
wazima au wawe maiti pia ni lazima, kwa msaada
zaidi mtaupata kwa Moses Gawaza na vitendea kazi
vipo ofisini kwangu nadhani mmenielewa. Alizima
Tarakilishi kisha akazima kirushapicha ukutani
halafu akatoka kuelekea nje, Norbert na Hilda nao
walimfuata kama ilivyokuwa awali. Norene alienda
hadi ofisini kwake kisha akainama chini ya meza
akawa anavuta kitu kilichokuwa hakionekani na
wenzake, alipotoa begi kubwa la kuburuza lenye
rangi nyeusi ambalo limetengenezwa kwa plastiki
ngumu kisha akawaambia "vitendea kazi ni hivi
hapa kwa ajili ya kazi yenu, nadhani nimemaliza na
sina la ziada". Norbert alilipokea begi hilo huku
akitikisa kichwa kuashiria yupo pamoja naye huku
Hilda akisema, "shosti sasa ukitoka hapa nitafute
nikupe mchapo".
"khaa yaani mshaanza umbea wenu hapahapa"
aliongea Norbert huku akivuta begi hilo kuelekea
ulipo mlango wa kutokea katika ofisi ya Katibh
mukhtasi.
"huyu mwanume naye kwa kudandia, lione kwanza"
aliongea Norene kumuumbua Norbert ambaye
alikuwa anafungua mlango ili atoke nje
"Hil utanikuta ofisini" Norbert alisema kisha akatoka
nje na kuufunga mlango pasipo kusikiliza jibu
kutoka kwa Hilda ambaye alikuwa amezama katika
maongezi na Norene.
*********************************************
**********************
Muda huo huo FI na KL walikuwa wapo ndani ya
kambi yao ya siri wakijadiliana na kijana na wao wa
kuaminika aitwae Kitoza, meza ya plastiki pamoja na
viti vitatu ndiyo vitu pekee vilivyokuwa vipo humo
ndani katika ofisi ya Kitoza.
"vipi Kitoza mmefikia wapi katika mambo yenu?"
aliuliza FI
"bosi mipango inakwenda vizuri hadi sasa ingawa
bado kuna mmoja wa mbwa wako muhimu si
msikivu na yuoo upande wa EASA " Kitoza aliongea
kwa kujiamini
"Bado hamjafanikiwa kumjua huyo mbwa wakati
wewe ndio msimamizi wa hao mbwa wote, hapo
inakuwaje?" aliongea KL akionesha kutomuelewa
Kitoza.
"mkuu nahisi huyo si mbwa wa kawaida maana
hajajulikana zaidi ya kupata taarifa kutoka kwa
kibaraka wetu aliyeko EASA tawi kuu la Dodoma"
alisema Kitoza
"hebu elezea vizuri tukuelewe" aliongea KL
" bosi katika EASA tawi la Dodoma tulimpandikiza
kibaraka wetu pasipo wao wenyewe kujua ambaye
ndiye anyetupatia taarifa zote za zinazoingia zikifika
katika usawa wake, pia huyu jamaa ametueleza kuna
mbwa mmoja ndani ya banda si muaminifu baada
ya baadhi ya taarifa zenu kufika ofisini kwao" Kitoza
alitoa maelezo kwa wakubwa zake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sasa napenda nikupatie kazi ya kumtafuta mpaka
umjue la si hivyo mambo yataharibika" aliongea FI
kumpa wajibu mwingine
"sawa bosi nitafanya kila niwezalo huyu mbwa
apatikane" Kitoza alikubali wajibu mpya
aliokabidhiwa.
KL na FI waliinuka kwenye viti walivyokuwa
wamekalia kisha wakatoka ndani ya ofisi hiyo
wakimuacha Kitoza akiendelea na kazi zake
nyingine.
*********************************************
***************
Baada ya kumaliza kuelekezana kila kitu katika kazi
yao waliamua kuchukua begi lenye vitendea kazi na
kuondoka nalo, Norbert na Hilda waliamua kutumia
mlango maalum wa kutokea uliopo sehemu nyingine
tofauti na ule walioutumia kuingilia. Mlango huo
uliwapeleka hadi ilipo lifti nyingine tofauti na ile
waliyoitumia wakati wanashuka chini, walipanda lifti
hiyo kisha Hilda akabonyeza kitufe chenye herufi G
baada ya kuingia humo ndani. Lifti hiyo ilianza
kupanda juu hadi ilipo alama ya G kisha ikapiga
kengele na kufunguka, walishuka humo ndani
wakatokea katika lifti nyingine iliyo jirani na
mapokezi kisha wakatoka nje kuelekea kwenye
maegesho magari. Walipofika wakaingia ndani ya
gari yao waliyoitumia wakati wanakuja kisha
wakaondoka eneo hilo. Muda huo Hilda alikuwa
ndiyo dereva wa gari hiyo na Norbert akiwa
ameamua kujilaza katika kiti kilicho pembeni mwa
Hilda.
Hilda alitoka akifuata njia ya iendayo karia kotoka mtaa
aliokuwepo katika. eneo hilo la Ilala, allipofika kariakoo
alishika barabara iendayo yalipo makutano ya
barabara ya kariakoo gerezani jirani na kituo cha
mafuta kwa upande wa kulia. Mataa ya eneo hilo
yalikuwa yamewaka rangi nyekundu katika upande
aliokuwepo kuashiria magari na vyombo vingine vya
barabarani visimame, hapo alisubiri hadi taa zilipowaka
kijani kisha akafuata barabara iendayo makutano ya
barabara yanayotenganisha njia iendayo kariakoo na
iendayo maeneo ya posta. Hapo akafuata barabara
iendayo bandari hadi katika mzunguko uliopo
mwanzoni mwa barabara ya kilwa, aliingia katika
barabara ya Kilwa kwa
mwendo wa kasi kuelekea upande wa kusini hadi
maeneo ya Mtoni kwa Aziz Ali kisha akakata kona
kuelekea upande wa kushoto . Alienda hadi kwenye
nyumba yenye geti kubwa la rangi nyekundu iliyopo
mtaa wa Bank club kurasini, hapo alipiga honi na
kupelekea geti dogo lifunguliwe kisha kijana wa
makamo akatoka humo ndani na kuja hadi kwenye gari lao. Hapo
Norbert alishuka kisha akaelekea mlango wa nyuma
wa gari hiyo na kuufungua, alitoa begi jeusi lenye vitendea na
kumpatia huyo kijana kisha akarudi ndani ya gari katika
sehemu aliyokuwa amekaa awali. Waliagana na yule
kijana kisha Hilda akaondoa gari hilo kuelekea
nyumbani wanapoishi.
***-*****************************************
**************
Mnamo saa kumi na moja alfajiri hali ilikuwa shwari
sana katikati ya jiji la Dar es salaam, mtu mwenye
mavazi meusi alionekana maeneo ya jirani na ofisi za
WAHANGA. Mtu huyu alionekana kuangalia kila
upande wa eneo hilo kwa zaidi ya mara nne kama
aliyekuwa anayemtafuta mtu, aliporidhika na ukimya
wa eneo hilo alizunguka nyuma ya jengo lenye ofisi
za WAHANGA. Alivaa glovu ngumu mkononi ambazo
hutumiwa kupanda ukuta kisha akapanda ukuta
huo mithili ya mtu anayekwea mti hadi ghorofa ya
kwanza ya jengo hilo. Alitembea kwenye kingo za
ghorofa hadi jirani na dirisha la vioo, alitoa kifaa cha
kukatia vioo kisha akakata kipande kidogo cha kioo.
Alipohakikisha sehemu aliyokata inamfaa
alitumbukiza mkono ndani kisha akafungua dirisha
hilo, dirisha lilipotii amri ya kufunguka yeye aliingia
ndani kisha akalirudishia. Eneo lenye makabati ya
kuhifadhia mafaili ndio lilimlaki, meza za ofisi
zipatazo tatu ndizo zilishuhudia ujio wa kijana huyo
pamoja na kushuhudiwa na yeye pia kama wenyeji
aliowakuta. Alipita katika kila meza huku akishika
pembeni mwa kila meza na kupelekea aibuke na
vinasa sauti vitatu, alienda hadi sehemu iliyofungwa
kiyoyozi ofisini hapo kisha akachomoa kamera
ndogo iliyochomekwa kwa ustadi wa hali ya juu.
Baada ya kuchukua vitu hivyo alikuwa anatafuta kitu
kimoja ambacho alikijua yeye na nafsi yake,
alifungua makabati tofauti ya ofisini humo pasipo
kuonesha dalili zozote za kukipata akitafutacho. Mtu
huyu alisimama kisha akajifikiria kisha akasogelea
kabati kubwa lililopo ofisini humo ambalo
hakulifungua, pasipo hofu ya aina yoyote akashika
kishikizo cha kabati hilo na kukivuta. Kabati
lilifunguka na ukaribisho wa aina yake aliupokea
kutoka ndani ya kabati hilo, hakika ni ngumi nzito
asiyoitarajia ilimpata puani. Akiwa hajakaa sawa
alipokea kichwa kikali kisha ngumi mfululizo
zikauvamia uso wake, mtu huyo alianguka chini
huku damu ikimvuja puani. Kijana mwenye mwili wa
kimazoezi na mwenye kimo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
cha wastani akiwa amevaa suti ndiye mtu pekee
aliweza kumuona akiwa amesimama mbele yake,
hakika ni pigo ambalo lilimpata pasipo yeye
mwenyewe kutarajia. Alijizoa pale chini alipoanguka
kisha akasimama kiukakamavu huku pua zake
zikiwa zinavuja damu, alikuja na mapigo mawili ya
karate ambayo yaliishia hewani pasipo kumpata
aliyemkusudia baada ya yule kijana kuyakwepa yote.
Hasira zilimzidi maradufu baada ya lengo
lake la kumpiga kijana huyo kutotimia, alileta mateke
matatu mfululizo ambayo mawili yalipanguliwa na
moja likampata yule kijana la kifua na kusababisha
arudi nyuma, hapo alitabasamu kisha akakaa sawa
kumsubiri mpinzani. Yule kijana aliifuta suti yake
iliyochafuka kwa teke lililompata kisha akajiweka
sawa halafu akamfuata mpinzani wake na mapigo
mfululizo ambayo yalimsambaratisha adui yake hadi
sakafuni.
"you can call me AI005(unaweza kuniita AI005)"
aliongea yule kijana akamuongeza yule mtu teke la
kifua na kumfanya aishie kutoa mguno wa
maumivu.
AI005 alimpiga yule mtu teke la kisogoni na
kusababisha apoteze fahamu kisha akambeba yule mtu na kumuweka katika bega lake la kulia. Alielekea ulipo mlango wa kutokea nje, alipofika alitoa funguo
mfukoni na
kuufungua mlango huo. Alimtoa yule mtu hadi nje
kisha akaufunga mlango wa ofisi hiya ufunguo,
alimshusha na kukokota hadi kando ya barabara kwenye gari
ndogo iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa
barabara, hapo alifungua mlango na kumuweka yule
mtu ndani ya gari kisha na yeye akaingia.
"kazi imeisha tuondoke" alimwambia dereva.
Dereva akaliondoa gari kwa mwendo wa kasi.
*********************************************
******************
Asubuhi iliyofuata Kitoza alijawa na wasiwasi juu ya
kutorudi kijana wake aliyemtuma kukusanya vitu
vyao walivyovitega katika jengo la wahanga, hadi
jua linachomoza alikuwa tayari ameshakata tamaa
ya kurudi kwa kijana huyo.
"huenda ameingia kwenye mtego bila ya kujujia"
alijisemea huku akinyanyua mkonga wa simu yake
iliyopo mezani katika ofisi yake kisha akauweka
sikioni mwake.
"Briton njoo mara moja ofisini kwangu" kisha
akashusha mkonga wa simu hiyo mahala pake.
Hazikupita dakika tano mlango wa ofisini kwake
ukafunguliwa kisha kijana mwenye kimo kirefu na mwili
uliojengeka kimazoezi akaingia humo ndani.
"mkuu" aliongea kijana huyo
"keti tafadhali" Kitoza
alimwambia kijana huyo kisha
akaendelea baada ya kijana huyo kuketi kwenye kiti,
"Briton napenda nikupatie wajibu wa kuutekeleza
maana naona kuna mtu anatuzunguka hadi muda
huu, saa nane usiku ya jana nilimtuma Tasu
akachukue vifaa vyetu katika ofisi ya wale wambea"
alisita kwa muda huku akimtazama Briton kuona
umakini katika jambo analomweleza.
"sas basi hadi muda huu Tasu hajarejea na si
kawaida hii, hivyo nakupa kazi ya kuwafuatilia hawa
wambea maana nina wasiwasi huenda wakawa sio
watu wa kawaida kama tunavyowachukulia" Kitoza
aliendelea kuongea tena akasisitiza "nataka ujue
hadi mahali wanapoishi na ikiwezekana tumtie
nguvuni mmoja wao na ikiwezekana tuwapoteze".
"sawa mkuu" aliitikia Briton
huku akijiweka sawa
katika kiti alichokikalia.
"kuanzia sasa hakikisha hajui mtu kuhusu kazi hii
hasa huyo swaiba wako ambaye anajifanya
mzalendo, unaweza ukaenda sina la ziada zaidi ya
hilo" Kitoza alimaliza na kupelekea Briton
anyanyuke kwenye kiti chake na kuondoka ofisini
hapo baada ya kupokea maagizo hayo.
*******************************************************
Baada ya siku tano toka ajali iliyoondoa maisha ya
waziri wa maliasili na utalii kutokea, mwili wa waziri
huyo ulikuwa umeshasafirishwa kulekea mkoani
Tanga alipozaliwa katika wilaya ya Korogwe kwa ajili
ya maziko. Hadi muda huo umati wa watu ulikuwa
umefurika katika shamba lililopo jirani na nyumba
ya kisasa katika kijiji cha Mazinde wilayani Korogwe.
Kundi kubwa la wanaume walikuwa wakihudhuria maziko hayo huku wanawake wakiwa wamebaki ndani
ya nyumba iliyo jirani na eneo, hadi muda huo
tayari turubai kubwa lilikuwa limefungwa kuzunguka
eneo la maziko na shimo la kaburi lilikuwa
limechimbwa. Jeneza lenye mwili lilikuwa pembeni
likiwa limefunikwa shuka nyeupe, taratibu za
kuushusha mwili wa marehemu zilianza baada ya
watu watano kuingia ndani ya kaburi na shuka jeupe
kufunika juu yao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"leta dongo" ilisikika sauti kutoka ndani ya kaburi
baada ya taratibu za kuushusha mwili kutoka ndani
ya jeneza kukamilika. Baada ya muda ubao
uliagizwa kisha majani yafuata ili kukamilisha
taratibu za kumfunika marehemu katika
mwanandani, utupaji wa udongo katika kaburi
ulifuatia kwa kuanza viongozi mbalimbali wa serikali
waliokuwepo eneo hilo wakiongozwa na makamu wa
rais Dk Ismail Hafidh. Baada ya hapo kaburi
lilimaliza kufukiwa kisha sheikh mkuu wa Tanzania
Muft Juma Shehoza akatoa nasaha kwa ufupi kisha
akaongoza dua ya kumuombea marehemu ili
kukamilisha maziko. Baada ya hapo watu wote
walitawanyika huku Norbert akiwa ni mmojawapo wa
watu walioshuhudia maziko hayo akiwa mwandishi
wa habari wa kawaida, hadi muda huo ilikuwa ni saa
nane za mchana . Norbert hakutaka kupoteza muda baada ya maziko kukamilika, alikodi
pikipiki iliyompeleka hadi Korogwe mjini kisha
akapanda basi la linaloenda Tanga mjini, alikaa
ndani ya basi kusubiri safari ianze huku akiwa
anawaangalia watu waliomo humo ndani ya gari
mmoja baada ya mmoja kwa ajili ya kujihadhari.
Baada ya muda safari ilianza akiwa hana wasiwasi
wowote baada ya kuhakikisha mazngira yapo
salama.
*********************************************
***********************.
Hadi maziko yanaisha Briton alikuwa ameshamuona
Norbert akiwa katikati ya kundi la waandishi wa
habari akipiga picha mbalimbali, baada ya mazishi
kuisha aliamua kumfuatilia kila anapoelekea bila
kugunduliwa na mtu yoyote. Norbert alipopanda
pikipiki yeye alikuwa anamfuatilia kwa kutumia gari
yake aina ya Nissan xtrail ya rangi nyeusi, Norbert
alipofika Korogwe mjini yeye alimfuatilia vilevile.
Baada ya Norbert kupanda basi liondalo Tanga yeye
alitoa simu yake kisha akaiweka sikioni,
"Luxury
express inayotoka Arusha inaelekea Tanga mjini
ndiyo asusa yetu ilipo, sasa ikifika hapo nyinyi
fanyeni kazi yenu" aliongea baada ya simu
kupokelewa kisha akakata bila kuusikiliza upande wa
pili wa mtu aliyempigia simu. Aliondoa gari kwa
mwendo wa kasi kueleka njia
iendayo Tanga baada ya basi la Luxury express
kuondoka, alilipita basi hilo kwa mwendo wa
kasi usio wa kawaida. Safari yake iliishia mwanzoni
mwa mji mdogo wa Segera kwenye pori lisilo rasmi,
hapo aliingiza gari kando kisha kisha akaifunuka majani,
alikaa sehemu ambayo barabara inaonekana vizuri.
Baada ya muda basi la Luxury ilikuwa inaonekana
vizuri likija kwa mwendo wa kasi sana, hapo Briton
alinyanyua kidole chake juu huku simu ikiwa
sikioni mwake kisha akasema, "shoot".
Sauti ya kupasuka matairi ilisikika kisha basi la
Luxury express likapinduka mara saba kuelekea
katika bonde lililopo jirani, Briton alitoka kwa kasi
kuelekea bondeni kuliangalia basi hilo. Alipofika
bondeni alikuta basi hilo likiwa limepondeka vibaya
sana na damu zikiwa zimetapakaa katika mabati ya
gari hilo, hali hiyo ilimfanya aachie tabasamu la
kifedhuli kisha akapiga mbinja kwa nguvu na
kupelekea mwenzake aje eneo hilo .
"shabaha nzuri kabisa hiyo" Briton alimwambia
mwenzake.
Alimpigapiga mgongoni kwa kumpongeza huku
akitabasamu kisha akamwambia "hakika shabaha
yako umeitumia ipasavyo.
"lakini si kuitumia kwa malengo bali ni nje ya
malengo" ilisikika sauti kutoka nyuma yao
iliwashtua sana. Briton alipogeuka alisalimiana na
soli ngumu ya kiatu huku mwenzake akikumbana
ngumi ya kisogo iliyosababisha apoteze fahamu
Soli hiyo ya kiatu ilimpata mdomoni na puani na damu ianze
kumtoka puani huku akiwa amepagawa kwa pigo
hilo, hadi muda huo alikuwa yupo chini akijianda
kuinuka. Alijiinua kwa namna ya kifyatuka mithili ya
mtego wa panya wa springi kisha akafyatua teke la
kuzunguka lililomkosa adui yake , hadi muda huo
tayari Briton alitambua anapigana na Norbert Kaila
mwandishi pasipo kutambua kuwa anapigana na
mtu mwenye uwezo wa juu. Norbert aliamua kuja na
ngumi mfululizo ambazo zilitolewa na kisha
akapigwa teke zito la kifua hadi akahisi kitu
kikivunjika kifuani mwake, Norbert hakujali mvunjiko
huo zaidi ya kukaa kimapigano zaidi. Briton alipiga
teke jingine la kuzunguka na kupelekea ajikute
akipigiza mgongo wake chini baada ya kuzolewa
mguu aliosimamia na Norbert, Norbert alimfuata ili
amshindilie na kiatu chake lakini alisita baada ya
kusikia ving'ora vya gati la polisi katika éneo hilo,
hapo akahisi kuna jambo litatokea iwapo atakaa
eneo hilo. Hakutaka jambo analohisi litokee kwake
ndani ya muda huo, hivyo aliamua kukimbia eneo
haraka sana kabla polisi hawajafika na kumkuta.
Baada ya Norbert kuondoka Briton alijiinua kivivu
kisha akaanza kuelekea lilipo gari la polisi ambalo
lilikuwa limeshawasili hadi muda huo, akiwa
anakaribia lilipo gari la polisi aligeuka nyuma kwa
lengo la kumuangalia mwenzake aliyezirai na
kupelekea aone miale ya jua ikigonga kwenye kitu
kidogo chenye umbo la mstatili. Briton alisitisha
safari yake kisha akarudi nyuma hadi kwenye kitu
alichokiona halafu akainamana kukiokota, hakika
kilikuwa kitambulisho cha Norbert ambacho
kilidondoka pasipo mwenyewe kujua.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Norbert Kailaaa umekwisha" alikiweka mfukoni
kitambulisho hicho kisha akageuka nyuma ili
aondoke.
"tulia hivyo hivyo" ilisikika sauti ya mmoja wa
maaskri polisi waliomnyooshea bunduki aina ya
SMG baada ya Briton kugeuka, Briton aliwatazama kwa dharau kisha akaachia
tabasamu la kifedhuli halafu akanyoosha mikono
yake. Mmoja wa maaskari alikuja kumpekua
mifukoni mwake huku wengine wakimnyooshea
bunduki zao kwa tahdhari, askari aliyempekua alitoa
pochi ya Briton ya mfukoni akiwa na macho ya
tamaa. Aliifungua kwa papara akijua kuna pesa
baada ya pochi hiyo kuonekana imetuna, kitu
alichokutanaa nacho katika pochi hiyo kilimfanya
atoe saluti kwa Briton. Hakika hazikuwa pesa
zilizomfanya atoe saluti bali ni kitambulisho cha
usalama wa taifa kilichokuwa ndani ya pochi,
kitambulisho hicho kilimtambulisha Briton kuwa ni
usalama wa taifa.
"sajenti Kilanto kutoka kituo cha polisi Segera"
alionge askari huyohuki akimpatia Briton pochi yake
kisha
"iteni gari la wagonjwa upesi sana ili muweze
kuokoa majeruhi kama wapo humo kwenye basi, pia
mnaweza kuendelea taratibu zingine" aliongea
Briton huku akimnyanyua mwenzake aliyepoteza
fahamu . Briton aliondoka eneo la tukio hadi
alipoificha gari yake kisha akamuingiza mwennzake
kwenye gari baada ya kufungua mlango wa ulio
nyuma ya kiti cha dereva, aliondoa miti
iliyolizunguka gari lake kisha akaingia ndani na
kutekenya ufunguona kupelekea gari liwake. Aliingia
barabarani taratibu kisha akaongeza mwendo
kuelekea Segera.
******************************
*************************
MUDA MFUPI ULIOITA
Baada ya Norbert kupanda basi la Luxury alikuwa
yupo kiamani sana, amani yake ilikuja kutoweka
baada ya kukaribia pori lililopo jirani na mji wa
Segera . Kila akijaribu kuituliza nafsi yake alishindwa na kumpelekea afanye uamuzi wa haraka. Alijifanya amechafukwa na tumbo la
kuendesha wakati akiwa amekaa kwenye kiti chake,
hali hii ilipelekea dereva wa basi asimamaishe basi
eneo lisilo rasmi ili abiria wake aweze kujisaidia.
Hapo Norbert alienda hadi mlangoni kisha
akawaomba radhi abiria wote halafu akaanza
kuteremka, aliteremka ndani ya gari akiwa na begi
lake dogo alilowekea kamera . Aliteremka kwa
mwendo wa kasi hadi maporini kisha akatulia
kwenye kichaka bila hata kuonesha dalili ya
kujisaidia, hapo alitoa simu kisha akabonyeza
baadhi ya namba halafu akaongea "nyie nendeni tu
mimi suruali imeharibikiwa, nimeshampigia simu
ndugu aliyepo segera"
"mkubwa tutakuachaje porini peke yako" ilisikika
ikimuuliza
"usiwe na shaka konda mimi nitakuwa salama na ni
ndani ya dakika ishirini tu ndugu yangu anakuja
kunifuata hapa" aliwafafanulia kisha akakata simu na kupelekea mlio wa
basi hilo usikike kuashiria linaanza safari. Muda mfupi baada ya
hapo Norbert alishtuka simu yake ikitoa kitetemeshi
mfukoni mwake kuashiria kuna simu inaingia,
alipoitoa simu yake aliangalia jina la mpigaji lakini
aliambulia patupu.
"Gawaza hapa, hilo basi ulilopanda jua linaandaliwa
ajali na mtu aliyetumwa na mkuu Kitoza. Sasa fanya
haraka iwezekanavyo ushuke ili usalimike na usiwe
katika mikono yao iwapo utapona katika ajali hiyo"
ilisikika sauti ikimsisitiza baada ya kuipokea simu
hiyo.
"nimeteremka tayari" alijibu na kupelekea simu
ikatwe.
Alianza kukimbia kwa kasi kuelekea barabarani
alipokuwa awali kisha akabonyeza namba kwenye
simu yake halafu akaiweka simu sikioni.
"John nipo jirani na segera katika pori baada ya
kushuka kwenye basi, njoo haraka unifuate
maana.." alishindwa kuendelea baada ya kusikia
kishindo kikubwa cha gari kuanguka, alianza
kukimbia kuelekea mahali aliposikia kishindo hiko
pasipo kujua umbali wake. Alikimbia umbali mfupi
kisha akasimama baada ya kusikia mlio wa pikipiki
ikija upande wa nyuma yake, aliisimamisha bila ya
kujali kama ya abiria au siyo ya abiria.
"twende nitakuambia ninaposhuka" alimwambia
dereva kisha akapanda pikipiki hiyo baada ya
kusimama alipoisimaisha. Dereva naye alikubali
akijua ni mteja kama wateja wengine, aliondoa
pikipiki kwa mwendo mkali kwa umbali wa nusu
kilomita wakafanikiwa kumuona mtu akivuka
barabara kwa kasi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"simama hapo" aliongea na kupelekea dereva
aponguze mwendo kisha akasimama, alimpa noti ya
shilingi elfu kumi huku akimwambia "unaweza
kuendelea na itakayobaki chukua". Dereva wa
pikipiki aliondoka kisha Norbert akaingia kwa kasi
katika kichaka kilicho jirani yake kama ameshtuka
jambo na anatazama barabarani, hapo alimuona mtu
wa awali aliyevuka akirudi upande wa barabani
akiangalia upande aliopo Norbert baada ya pikipiki
kuondoka. Yule mtu alirudi alipokuwa ameenda
mwanzo baada ya kuvuka barabarani, muda huohuo
ikasikika mbinja kisha mtu mwingine akaonekana
akivuka barabara kuelekea upande alioenda
mwenzake. Norbert alisubiria kwa muda kisha
akatoka kuelekea upande wale watu wameelekea kwa
mwendo wa tahadhari, alienda kwa mwendo
kukazana usiomshtua mtu kuwafuata watu hao.
Baada ya mwendo mfupi aliwakuta wakiwa
wanapongezana huku basi la Luxury likiwa lipo
mbele yao katika bonde likiwa limepondeka vibaya.
Hapo ndipo alipotamka kauli iliwastua kisha
akawaletea mapigo mawili ya kushtukiza na
kupelekea mmojawapo apoteze fahamu, alipigana na
yule wa pili kwa muda mfupi kisha akakimbia baada
ya kusikia king'ora cha polisi. Alielekea bondeni
kwa umbali mrefu kisha akaingia kwenye vichaka
akiwa katika mwendo wa kasi Mbio zake zote
zilikwama kwenye mti mdogo wenye
kivuli mbali kidogo na barabara, hapo alianza
kujipekua kwa papara kuashiria amepoteza kitu
chake. Alitoa vitu vyote muhimu kwenye kazi ya
uandishi ikiwemo kamera ndogo ya kupigia picha,
alitoa na pochi yake ya kutunzia pesa pamoja na
kitambulisho cha EASA lakini aliambulia patupu.
Aliendea kujipekua sehemu mbalimbali za mwili
wake kisha akasita huku akivuta kumbukumbu kisha
akajisemea "nilikuwa nimekivaa shingoni katika
kamba yake", hapo alijitazama shingoni akaona
kamba tupu kitambulisho hakuna. Kila alipoitazama
ile kamba ilionesha kuna kipande cha plastiki
kilikuwa kimevunjika na ndicho kinachoshikilia
kitambulisho.
"nimejikaanga mwenyewe na mpira unanigeukia
mimi kama wanacho kitambulisho, aah ku.....!"
aliishia kuwatukania mam zao wale watu kwa hasira
kisha akatoa simu yake iliyokuwa inaita kwa muda
huo.
"upo wapi mimi nipo eneo la ajali sasa?" Ilisikika
sauti ikilamika.
"John hapo kimenuka tayari na siwezi kutokea hapo,
kama vipi wewe vuka eneo hilo kama unaelekea Segera na
mimi nitapandisha huko barabarani nikifikia eneo
hilo ulilosimama" aliongea Norbert kisha akakata
simu halafu akaanza kukimbia kuelekea maporini ,
huku akichukua usawa barabara ya Lami hadi
alipohakikisha ameliacha eneo la ajali kwa umbali
mrefu. Hapo alianza kupandisha juu ilipo barabara
kwa mbio sana kutokana na mteremko, barabarani
aliiona gari aina ya toyota hiace nyeusi yenye vioo
vya giza ikiwa imeegeshwa pembezoni mwa
barabara. Alienda hadi ulipo mlango wa gari hiyo halafu
akaufungua kisha akaingia ndani.
"tuondoke haraka maana hapafai" aliamuamuru
dereva wa gari hiyo.
"Nor kuna nini mbona hivyo?" aliuliza yule dereva
"huu si muda wa maswali John tuondoke eneo hili na
tusifikie kwako Segera bali nyoosha Tanga moja
kwa moja" aliongea Norbert huku akitoa kitambaa
cha kufutia jasho. John aliweka gia kisha akanyaga
kikanyagio cha mwendo na kupelekea gari liondoke
kwa kasi eneo hilo, safari yao ilienda hadi walipofika
Segera jirani na makutano ya barabara iendayo
mkoa wa pwani na iendayo Tanga. Barabara ya
eneo hilo ilikuwa imewekwa kizuizi na magari yote
yalikuwa yakipekuliwa na ilionekana ilikuwa ni
msako mkali, gari alilokuwemo Norbert nalo
likapewa ishara ya kusimama na kupelekea John
apunguze mwendo kisha akakanyaga breki na
kusimamisha gari.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"jilaze kwenye kiti na utulie kwani hatujajua ni nani
anaetafutwa" John alimwambia Norbert baada ya
kusimamisha gari. Mbele ya gari lao kulikuwa na
Briton pamoja na baadhi ya maaskari wakiwa
wameshika picha kubwa ambayo haikuonekana
dhahiri, mmoja wa wale maaskari alisogea hadi
katika mlango wa dereva kisha akagonga kioo na
kupelekea John ashushe kioo chake nusu.
"vipi kuna tatizo koplo" John aliuliza na kupelekea
yule askari atoe saluti ya heshima huku akisema,
"mkuu tunapekua magari yote yanayopita hapa
kwani kuna mhalifu amepiga risasi matairi ya basi la
Luxury na kupelekea ajali ambayo imeua wengi, pia
amesababisha mmoja wa wanausalama apoteze
fahamu kwa kumpiga kisha akamjeruhi
mwanausalama mwingine ambaye ni yule pale".
John alipoyasikia maelezo hayo aliafiki kwa kichwa
kisha akauliza , "je una mashaka na mimi na
unataka kupekua gari yangu?"
"aah hapana mkuu unaweza ukaendelea na safari" alijibu
yule askari huku akiwa amenyooka kiheshima.
"hebu leta niiangalie hiyo picha ya huyo mhalifu"
John alimwambia yule askari na kupelekea askari
ampe picha ya mhalifu anaetafutwa.
"mmh si mwandishi wa habari huyu"
"ndiyo ni mwandishi wa habari na mhalifu
aliyesababisha ajali"
"mbona nimepishana akiwepakizwa kwenye pikipiki anaelekea Korogwe wakati
nakuja huku, inamaana hamjamuona na wenzenu
waliopo eneo la ajali hawana taarifa juu ya hili"
"bado hatujawapa taarifa mkuu"
"pumbavu nyinyi yaani mnaweka kizuizi sehemu
moja" aliongea John kisha akafungua mlango wa
gari huku akipandisha kioo. Askari wengine wa eneo
hilo walipomuona John
walitoa saluti huku wakisema "jambo afande".
"sihitaji jambo yenu hivi kwanini mnakuwa wazembe
namna hii hadi mnafikia hatua ya kuweka kizuizi
sehemu moja, mmeona sasa mhalifu keshakimbia.
Sasa nahitaji muwasiliane na wenzenu wa Same na
Korogwe wafunge barabara kwa kizuizi ili wamuwahi
na wamkamate tunaelewana?!" alifoka John kwa
hasira za maigizo.
"ndio afande" askri wote waliitikia
Hadi muda huo Briton alikuwa amesogea karibu na
eneo alilopo John huku akimsikiliza.
"Briton Massawe kutoka usalama wa taifa,
mwenzangu nani" Briton alimuuliza John ambaye
amevaa kiraia.
"Asp John kutoka kituo cha polisi cha mkwakwani"
alijibu John huku akielekea katika gari lake.
"nimekuja kuangalia utendaji wenu wa kazi hapa na
inaonekana ni wazembe sana, sasa ninaenda ofisini
nimeitwa mara moja na nikirudi nimkute" John
aliongea kwa hasira kisha mlango wa gari halafu
akaingia sehemu ya dereva, aliwasha gari kisha
akaondoka eneo hilo.
John Faustin ndiyo jina lake, ni askari polisi kutoka
Tanga na jasusi wa siri wa EASA aliyewekwa jijini
Tanga . Asp huyu wa polisi aliamua kuja katika moja
ya nyumba zake iliyopo Segera, akiwa ndani ya
nyumba yake hiyo ndipo Norbert alimpigia simu na
kumuomba amfuate Segera. Asp John alimfuata
Norbert na kumkomboa katika balaa hilo na sasa
yupo njiani akirudi jijini Tanga.
*******************************************************
Huku nyuma Briton alikuwa ameuma meno yake
kwa hasira kisha akaingia kwenye gari yake halafu
akafuata barabara iendayo Korogwe, aliendesha gari
kwa mwendo wa kas akiwa ana shauku ya kumpata
kwa kuwatumia polisi.
"mwandishi aliyejifunza ngumi ni cha mtoto tu kwa
polisi hawa" alijisemea huku mkono mmoja
ukichezea kitufe cha breki ya mkononi baada ya gari
kuonekana zito kwake.
Aliongeza mwendo hadi akafika mwendo wa kilomita mia
ishirini kwa saa ili awahi kufika, akiwa anakaribia
korogwe aliona kundi la maaskari likiwa limeweka
kizuizi njiani. Hapo alisimamisha gari na kupelekea
askari mmoja aje kwenye gari lake huku wengine
wanne wakiwa wapo nyuma yake, Briton alitoa
kitambulisho na kumuonesha askari huyo kisha
akamuuliza,"mkuu wenu yup wapi?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ametoka sasa hivi na hakusema anaelekea wapi baada
ya kutuachia maagizo"alifafanua askari huyona
kupelekea Briton aingie kwenye gari kisha
akaliondoa kuelekea Korogwe, alialitumia dakika
chache akawa amefika kituo kikuu cha polisi
Korogwe. Alipofika kituoni hapo alipitiliza moja kwa
moja hadi ulipo mlango wa chumba cha mkuu wa
kituo akiwa amewapita maaskari waliopo eneo
la mapokezi maarufu kama kaunta, askari wa kituo
hicho ambao walikuwa mapokezi waliamua
waliamua wamfuate hadi hapo mlangoni kutokana
na dharau alioionesha.
"aloo wewe hata chooni kuna utaratibu ndiyo kituoni
napo pako hivyohivyo, ukija siku nyingine uje
kiadabu sio kukimbilia mlangoni kwa mkuu wa kituo
wakati sisi tupo hii ni dharau" aliongea mmoja wa
maaskari huku akiwa amekamata nguo ya Briton ili amvute
amtoa nje baada ya Briton kuwapita bila salamu.
"ni sheria gani inakuruhusu wewe kama askari
unikunje nguo yangu" Briton aliuliza huku akiwa
amekunja sura yake kwa ghadhabu.
"kimya wewe si usijifanye mjuaji hapa" aliongea
askari mwingine mwenye mwili mkubwa kwa lafudhi
ya kisambaa baada ya kumchapa kibao Briton.
Kibao hicho kilizua tafrani hapo baada ya Briton
kupandwa na hasira, aliwapa kipigo kikali maaskari
hadi huku akiwaambia "naona nidhamu yenu imefika
ukingoni sasa". Hadi muda huo alikuwa tayari
amemkamata askari aliyempiga kibao akimburuza
kumpeleka nje ya kituo huku akimwamuru yule
mwingine amfuate, alipofika nje alichuma bakora
kisha akawachapa kama watoto na kupelekea watu
wa kawaida wawe wengi eneo hilo.
"mkuu wa kituo yupo wapi?" aliwauliza
"ametoka kidogo, tusamehe baba " alijibu askari
aliyempiga huku akihema kwa nguvu kutokana na
kipigo alichokipata. Hadi mkuu wa kituo anawasili
kituoni hapo aliwakuta askari wake wamechafuka
nguo zao huku wakiwa wameweka miguu ukutani
kisha mikono wamepiga ngumi ardhini.
"kuna nini hapa" aliuliza mkuu wa kituo kwa
mshangao
"waulize askari wako wasio na adabu wala heshima
watakujibu" Briton alijibu kwa dharau yenye
mchanganyiko wa hasira.
"wewe kama nani uwafanye hivi hawa askari?" mkuu
wa kituo aliuliza kwa jazba
"Briton kutoka usalama wa taifa" alijibu huku akitoa
kitambulisho na kupelekea jazba za mkuu huyo wa
kituo ziishe ghafla.
"sawa wasamehe tukaongee ofisini tuyamalize"
mkuu wa kituo aliongea kwa sauti ya upole tofauti na
awali na kupelekea Briton awaamrishe askari hao
warudi huku akiwa na hasira. Hakika hasira za
kupigwa na Norbeet hadi akavuja damu puani na hasira za
kumkosa ndizo zilizosababisha awaangushia
kichapo hao maaskari baada ya mmojawapo
kumpiga kibao.
"ndiyo mr Briton" aliongea mkuu wa kituo huku
akimkiribisha Briton kwenye kiti.
"sina muda wa kuketi kwa sasa nilitaka nijue
mlipofikia katika kumtafuta mhalifu aliyesababisha
ajali ya basi la Luxury" Briton aliongea akiwa
amesimama wima na mikono yake akiwa
ameifumbata kifuani mwake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"baada ya kupokea taarifa niliamuru kundi la
maaskri liende huko kuweka kizuizi huku kituoni
nikiwaacha wawili tu, hadi mimi nimetoka huko
kwenye kizuizi sasa hivi na hakuna dalili zozote za
kuonekana mtu huyo ingawa pikipiki zote pamoja na
magari yamepekuliwa kabla hayajafika korogwe
mjini" alifafanua mkuu wa kituo juu ya jambo hilo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment