Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

JINAMIZI - 3

 







    Simulizi : Jinamizi

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "sina la ziada naenda Same kwenye kwenye kizuzi

    nikaangalia, pia uwafundishe askari wako adabu na

    heshima kwa mtu wasiyemjua akija hapa kituoni"

    aliongea Briton kisha akafungua wa chumba cha

    mkuu wa kituo na kutoka nje. Aliingia kwenye gari

    yake kisha akaliwasha halafu akaweka gia, taratibu

    aliachia breki kisha akakanyaga mwendo kwa nguvu

    na kupelekea gari liondoke eneo la kituoni hapo kwa

    nguvu.



    *********************************************

    **********



    Baada ya kukivuka kizuizi cha Segera Asp John

    aliongeza mwendo wa gari na Norbert alijiinua katika

    alichojilaza halafu akaketi, hadi muda tayari

    walishavuka daraja la mto Pangani liliopo Hale

    wakiwa wanauhakika wamewakwepa polisi kwa

    asilimia zote za mawazoni mwao.



    "hivi pale imekuwaje maana mimi nimekuokoa tu

    bila ya kujua kilichokuwa kinaendelea" aliuliza John

    huku macho yakiwa makini kuangalia mbele

    kutokana na mwendo anaoutumia kwenye gari hiyo.



    "majamaa wamenigeuzia mpira mimi" alijibu Norbert



    "kivipi? Hebu fafanua" John alihitaji ufafanuzi iutika

    kwa Nobert.



    "ile ajali wameisababisha wao kwa kupiga risasi

    matairi ya mbele kwa lengo la kuniangamiza mimi

    wakijua mimi nipo ndani ya basi jambo ambalo

    lilikua ni kinyume chake, mimi nilifika eneo la ajali

    nikawakuta wanapongezana kwa ushenzi huo

    walioufanya"



    "halafu ikawaje?"



    "mzee nimewachezeshea sebene nikaangusha

    kitambulisho cha uandishi wa habari"



    "aisee sasa hapo umefanya kosa kubwa sana inabidi

    utulie mafichoni na ukijitokeza gereza linakuhusu"



    "haina jinsi tu zaidi ya kujificha huku nikiendelea na

    upelelezi wangu wa siri"



    "halafu ile picha yako wameipetaje"



    "ebwanaeh! Yote ni kitambulisho ndio kilisababisha

    kwani wameichapisha wale baada ya kukipata".



    Baada ya muda walikuwa wameshafika Muheza na

    sasa walikuwa wanaiacha wakizidi kuelekea mbele

    kwa mwendo wa kasi na kupeleka wachukua muda mfupi tu

    wakawa wamefika Pongwe. Hapo Asp John

    alisimamisha gari kisha akaiegesha pembeni

    halafuakatoka kuelekea kwenye duka moja lililopo

    jirani na barabara, wakati akiwa dukani akinunua

    baadhi ya vitu na hapo ndipo Norbert alikumbuka jambo

    ambalo alitakiwa alifanye upesi sana. Hapo

    alipoamua kulifanya ili mambo yasiharibike zaidi na

    kupelekea kazi iwe mbaya, alitoa simu yake ya

    kiganjani kisha akatafuta baadhi ya majina

    yaliyohifadhiwa kwenye simu hiyo hadi alipolipata

    jina analolihitaji. Hapo aliweka simu yake sikioni

    kisha akasubiri simu ipokelewe baada ya kubonyeza

    kitufe cha kupiga simu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "bibie potea haraka eneo la nyumbani hapo na hata

    hao wachovu wasijue.....................hakuna muda

    wa maswali mengi mama jua mambo

    yameharibika......................siwezi kukueleza sasa

    nitakueleza tukionana lakini sasa hivi wewe nenda

    kajichimbie kwenye nyumba ya ofisi kule kurasini

    tena hakikisha huachi chochote kitakachoiweka

    pabaya shirika zima maana hawa wajinga watafanya

    upelelezi kwenu ili kunipata mimi.........sawa hivyo"

    Norbert alimaliza kuongea kisha akamtazama Asp

    John ambaye tayari alikuwa amerejea akiwa na

    mfuko mkubwa mweusi.



    "nimemtonya Hilda maana hawa wajinga

    hawachelewi kufikisha Taarifa Dar kisha wawatie

    nguvuni wenzangu ili wanipate mimi" Norbert

    alimwambia Asp John kisha alijiinua kidogo kisha

    akaiweka simu katika mfuko wa suruali. Asp John

    aliweka gia na kupelekea gari liingie barabarani

    halafu akamwambia, "umefanya la maana sana".

    Aliondoa gari kwa mwendo wa taratibu kisha

    akongeza mwendo baada ya kuingia kulivuka eneo

    alilokuwa ameegesha gari.



    *********************************************

    ****************



    Baada ya Hilda kupokea simu yenye kumpa

    tahadhari kutoka kwa Norbert aliamua kukusanya

    vitu vyote vya muhimu vilivyopo kwenye chumba

    wanacholala kisha akavitia kwenye mkoba mdogo,

    alichukua funguo za gari kisha akatoka hadi

    sebuleni ambapo aliwakuta wenzake wakiwa

    wanajadiliana jambo kuhusu kazi yao ya uandishi.



    "jamani natoka kidogo nitarejea baadaye baadaye" aliwaambia

    kisha akatoka hadi uani kwenye maegesho ya gari

    halafu akailekea kwenye banda la gari, alifungua

    mageti ya banda hilo kisha akaingia ndani ya hadi

    kwenye gari ya Norbert iliegeshwa. Aliingia ndani ya

    gari hiyo kisha akaiwasha halafu akaitoa kuelekea

    getini ili aweze kuondoka, alitoka nje ya geti kisha

    akaliondoa gari kwa mwendo wa wastani kuelekea

    kwenye njia ya vumbi ipitayo katika shule ya msingi

    Muungano kutoka hapo nyumbani. Ndani ya dakika

    moja alifanikiwa kufika kwenye barabara hiyo ya

    vumbi, akakata kona kulia kuelekea usalama kisha

    akakanyaga breki kwa nguvu baada ya kuona hatari

    ya kugongana na magari ya polisi yaliyokuwa

    yanakuja kwa kasi yakiwa yameenea njia nzima.

    Akiwa katika mshangao aliona polisi mmoja

    aliyesimama katika mojawapo ya landcruiser nne za

    kipolisi akimuamuru aweke gari pembeni, Hilda

    aliweka gari pembeni akijua ameshaingia pabaya na

    akijua anafuatwa yeye . Magari ya polisi yalipita kwa

    kasi yakielekea upande aliotokea, hapo Hilda

    akaingiza gari barabarani kisha akaliondoa kwa kasi

    kueleka usalama ambapo alifika baada ya muda

    mfupi.



    "wamenikosa tayari" alijisemea huku akikata kona

    kuingia barabara ya Temeke akielekea kwa mtoni

    kwa Azizi Ally kwa mwendo wa kasi.



    *********************************************************



    Baada ya muda takribani dakika moja toka Hilda

    aondoke akiwaacha Allison,Davis na Joseph wakiwa

    majadiliano, simu ya kiganjani ya Allison iliita na kupelekea wote

    wamtazame yeye. Allison aliitoa kisha akatazama

    jina la mpigaji halafu akainuka kuelekea nje huku

    akiwaambia, "shemeji yenu huyo ngoja narudi sasa

    hivi". Alitoka nje huku akipokea simu kisha akawa

    anasikiliza. Davis na Joseph walimsubiri ili waweze

    kuendelea na mjadala wao wakiongea mambo yao

    mengine.



    "dah Allison siku hizi naye amekuwa mtu wa

    wasichana sana" aliongea Davis

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "umeonaeh! Yaani siku ile hawa mahaba niue

    walipotoka jioni na yeye alitoka usiku akimfuate

    bibie wake" aliongea Joseph.



    "dah! bado sisi tu tupate watoto ndani ya Tanzania

    ili tulale nao hadi asubuhi kama jamaa siku ile

    alivyotoka maana alirudi asubuhi" aliongea Davis

    huku akitabasamu.



    "kweli kabisa inabidi na sisi tu........" kauli ya

    Joseph alishindwa kuimalizia baada ya kusikia sauti

    ya kioo kikivunjika kisha kopo kama la dawa ya

    mbu lilidondoka walipo na kupelekea moshi

    mzito wa rangi ya kijanj usambae kwa kasi. Davis na

    Joseph walijirusha kutoka mezani walipo kisha waka

    kimbia kuelekea ulipo mlango kutokea Walifanikiwa

    ulipo mlango wa kutokea kisha

    wakufungua ili waweze kukimbia wakijua

    wamevamiwa baada ya kuona bomu la machozi

    likirushwa ndani, walifanikiwa kutoka nje ya nyumba

    lakini hawakufanikiwa kutoroka baada ya kukuta

    kundi kubwa la maaskari waliovaa kofia nzito kichwani wakiwa wwmewanyooshea

    bunduki nyingi aina ya SMG.



    "mpo chini ya ulinzi kuanzia sasa hivi" aliongea

    mmoja wa maaskari aliyekuwa yupo nyuma ya

    maaskari waliokuwa wamewanyooshea bunduki

    Davis na Joseph ambao muda huo walikuwa

    wameweka mikono kichwani wakiwa wameingiwa na

    uoga.



    "wengine ingieni ndani muwatafute wenzao hawa watu" alisema

    tena yule askari aliyetoa amri ya kuwaweka Davis na

    Joseph chini ya ulinzi. Baadhi ya askari waliingia

    ndani kwenda kuwatafuta wengine waliobakia

    wakidhani wapo ndani wapo, Joseph na Davis

    waliamriwa walale chini watulie kwa usalama wao ili

    wasije wakapata matatizo. Baada ya muda askari

    walioingia ndani walirejea wakiwa kama

    walivyoenda, "afande hakuna mtu mwingine humu

    ndani" mmoja wa maaskari alimwambia askari

    aliyewatuma ambaye alionekana ni mkubwa kuliko

    wao.



    "nyie wenzenu wapo wapi?" aliwauliza wakina Davis

    ambao walikuwa kimya kama mabubu.



    "wafungeni pingu na kisha twende nao wataenda

    kusema kituoni, sajenti Sele utabaki hapa na watu wachache

    kwa usalama wa nyumba na jamaa kama wakirudi ili

    muwakamate. Tumeelewana?!" yule askari ambaye

    ndiye kiongozi wa msafara alitoa amri ambayo

    ilitekelezwa mara moja. Davis na Joseph walifungwa

    pingu kisha wakapelekwa hadi nje yalipoegeshwa

    magari ya polisi, walipakiwa ndani ya gari halafu

    wakawekwa kwenye bodi la moja ya magari ya polisi

    kisha kundi la maaskari likapanda kuwalinda

    kuwalinda wasitoroke. Msafara wa magari ya polisi

    uliondoka eneo hilo kwa mwendo ukishuhudiwa na

    kundi kubwa la watu wa maeneo hayo

    waliojikusanya baada ya muda mfupi tu.



    Msafara wa magari ya polisi ulitoka eneo la

    Temeke ulipitia barabara ya Mandela baada ya

    kuyapita mataa ya Chang'ombe hadi uhasibu kisha

    ukakata kushoto kuingia barabara ya Kilwa,

    msafara huu ulisonga moja kwa moja hadi katika

    kituo cha polisi cha barabara ya Kilwa. Joseph na

    Davis walishushwa punde tu baada ya msafara huo

    kuingia katika kituo hiko.



    "wawekeni ndani kwanza sasa hivi muda umeenda,

    kesho asubuhi tutaanza mahojiano na hakikisheni

    mnawaweka katika chumba cha mateso mpaka

    wawataje wenzao walipo" aliongea mkuu wa

    msafara ule.



    "sawa afande" askari wote waliitikia kisha zoezi la

    kuteremshwa Davis na Joseph likaanza mara moja.

    Waliteremshwa mithili ya magunia ya mkaa huku

    wakipigwa na baadhi ya maaskari wenye

    kuhukumu papo hapo bila hakimu kusoma hukumu.

    Walipelekwa hadi mapokezi kisha wakavuliwa

    mikanda,saa na viatu halafu wakatupwa ndani ya

    selo kama mizigo.



    *******************************************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mnamo saa mbili usiku vituo vyote vilitangaza

    habari ya ajali ya basi la Luxury na kutafutwa kwa

    mshukiwa wa tukio hilo ambaye ni Norbert Kaila,

    msemaji wa jeshi la polisi kuhusu tukio hilo

    alibainisha wazi utafutwaji wa mwandishi huyo.

    Norbert aligeuka mtuhumiwa anayetafutwa na polisi

    kwa udi na uvumba ili aje kujibu tuhuma hizo

    zinazomkabili kwa muda huo, hadi siku inayofuata

    tayari nguzo za umeme na kuta za sehemu

    mbalimbali za Tanzania zilikuwa zimebandikwa

    picha ya Norbert yenye maandishi ya kuonesha

    kutafutwa na polisi. Ahadi ya donge nono ilitolewa

    iwapo tu kama ufanikishwaji wa kupatikana kwa

    mtuhumiwa huyo kutawezekana.

    Hadi muda huo Norbert alikuwa amejichimbia

    katika nyumba ya siri ya EASA iliyopo maeneo ya

    Raskazone jijini Tanga, alikuwa ni kama mwali

    anayesubiri kuolewa kwa jinsi alivyojifungia ndani huku

    akihakikisha hajulikani.Taarifa za kutafutwa kwake

    zilishafika makao makuu ya EASA na ofisa wa siri

    anayeshughulika katika kumpatia ajira alliwasiliana

    na CE akitaka kujua kinachoendelea, CE naye

    alimuunganisha Norbert na ofisa huyo kupitia

    mawasiliano ya tarakilishi yanayowezesha mtu

    kumuona anayewasiliana naye.



    "N001 kuna nini kilichotokea hapa mbona sielewi"

    Ofisa aliongea na Norbert kupitia tarakilishi

    inayoonesha mtu anayezungumza naye.



    "mkuu huo mchezo upo kama firigisi yaani nyama

    nje ngozi ndani" Norbert alijibu kifumbo



    "fafanua we mtoto wa kahaba sihitaji mafumbo"

    Ofisa huyo alikuja juu baada ya kujibiwa

    kimafumbo.



    "ni hivi, hilo basi nilitakiwa niuliwe mimi kwa ajali

    ya kutengeneza lakini nikajulishwa na Gawaza

    mapema. Hivyo nilishuka njiani kwa hila zangu,

    basi ilipopata ajali nikaenda eneo la tukio

    nikakuta waliosababisha ndio wanapongezana.

    Mkuu kosa nililofanya ni kupambana nao hadi

    nikadondosha kitamvulisho ambacho ndicho

    kinachonifanya nieonekana mtuhumiwa"



    "sasa wewe Malaya wa kiume nisikilize, kazi ya

    huko Dar mwachie AL005 na wewe ujiandae kwa

    mengine"



    "sawa mkuu"



    "sasa ulete kimbelembele kama ashiki za punda jike uone,

    pia huyo malaya mwenzako mwambie aende

    nyumba salama ya kampuni iliyopo Bagamoyo"



    "sawa mkuu"

    Norbert alimaliza kuongea na ofisa wa EASA

    anayehusika na ugawaji wa kazi kwa wapelelezi,

    matusi kwa mkuu wake huyu ilikuwa ni kama

    chakula na alishazoea kutukanwa na bosi wake

    huyo. Asubuhi hiyo alimpigia simu Hilda kisha

    akampa taarifa ya aliyopewa na Ofisa mpanga

    mambo ya upelelzi wa makao makuu.



    ******************************************************



    Mnamo saa nne za asubuhi Allison alikuwa anapita

    mitaani katika eneo la Temeke akiwa

    amevaa sweta yenye kofia kubwa iwezayo kufunika

    uso na kumfanya asitambulike kwa

    urahisi, alipita katika mitaa tofauti akiwa kama

    asiyekuwa na muelekeo maalum hadi

    mwisho wa mtaa wa Lusende wenye nyumba

    aliyofikia. Aliamua kupita kwenye

    kichochoro kimoja kirefu ambacho kimepakana

    uzio wa nyumba hiyo, alipofika katikati

    ya kichochoro aliangalia klia na kushoto kisha

    akapanda ukuta mithili ya mjusi hadi

    ndani. Alitua sehemu yenye bustani ya maua kisha

    akajilaza katikati ya maua marefu

    baada ya kuona nyumba hiyo ina maaskari

    wakilinda.



    "kostebo hebu kaangalie kwenye bustani ya maua

    nimesikia kama kishindo kwa mbali"

    sauti ilisikika na kupelekea askari mmoja aje

    kwenye bustani ya maua ya nyumba hiyo.

    Allisn alijilaza chali kwenye maua marefu

    wakati askari huyo akipekua

    kwenye maua ya nyuma yaliyo mbali na eneo

    alilopo Norbert.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "afande hakuna kitu huku zaidi ya ndoo ya

    maua iliyoanguka" askari huyo alipaza sauti .



    "hebu fungua maua hayo marefu yaliyobanana

    uangalie vizuri" ilisikika sauti ikimwambia

    na kupelekea askari huyo aende eneo alilojificha

    Allison. Askari huyo alisogea karibu kisha akafungua

    majani marefu ya maua hayo bila uangalifu wowote

    na kupelekea apewe ukaribisho wa

    aina yake kutoka kwa Allison, hakika ni soli ya

    kiatu ndiyo aliyosalimiana nayo kwenye pua

    yake kisha teke zito la kifua likafuata na

    kusababisha atoe mguno kwa nguvu

    uliowashtua maaskari wenzake. Allison alidandia

    juu ya paa la nyumba ya gari lililo jirani

    yake kwa haraka baada ya kusikia sauti ya

    vishindo vikija alipo, askari wenzake wawili

    walifika eneo hilo huku bunduki zao zikiwa tayari

    kwa lolote. Hakika walichelewa kufika

    na kupelekea wasiambulie lolote zaidi ya mwenzao

    anayevuja damu mdomoni akiwa

    amepoteza fahamu, walizunguka kila kona lakini

    hawakupata mtu yoyote aliyefanya vile

    kisha wakarudi walipomuacha mwenzo

    aliyejeruhiwa. Waliweka bunduki zao mgongoni ili

    wambebe wakijua hakuna mtu aliyefanya tukio hilo,

    hakika walitenda kosa kubwa pasipo

    kujua kama ni kosa kuweka silaha mgongoni.

    Walishtuka wamepigwa mateke ya kifua

    ghafla hadi wakaenda chini na kupigiza visogo

    vyao na kupelekea wazirai, hiyo

    haikuwa kazi ya mtu mwingine bali ni Allison

    aliyejiachia kutoka kwenye paa la banda la

    kulazia magari kisha akawapiga mateke kwa

    mtindo wa msamba kila mmoja.

    Aliwaburuza kila mmoja hadi kwenye maua marefu

    kisha akawafunika vizuri na maua,

    alipomaliza aliingia ndani ya nyumba kwa uangalifu

    hadi chumbani kwake kisha

    akachukua mkoba wenye kipakatishi halafu

    akaondoka humo kuelekea nje . Aliruka uzio

    aliopitia kama alivyoingia kisha akaondoka pasipo

    kujulikana na mtu.



    ***********************************

    *******************************



    Majira ya saa tano asubuhi kituo cha polisi cha

    barabara ya Kilwa kulikuwa kuna mahojiano

    mazito,

    askari polisi wenye uwezo wa hali ya juu katika

    kubana watu walikuwa kwenye chumba wakiwahoji

    watubumiwa wao Davis na Joseph ndiyo watu

    waliokuwa wakihojiwa juu ya kukosekana kwa

    Hilda

    na Allison, waliingizwa kwa zamu katika chumba

    cha mahojiano kwa kutangulia kwa Joseph.

    Joseph alifungwa katika kiti cha chuma chenye

    mikanda iliyomfunga mikononi na miguuni.



    "naitwa Inspekta Haroub, mmi ndiye mpelelezi wa

    kesi hii na ndiye nitakayekuwa msaada kwako

    ikiwa

    utakuwa mkweli. Tunaelewana?!" aliongea Inspekta

    Haroub ambaye ndiye aliyeongoza kikosi cha

    kuwakamata. Joseph aliitikia kwa kishwa na

    kupeleka askari aliyekuwa pembeni yake ampige

    kibao kwa nguvu huku akimwambia,"itikia we huna

    mdomo au vipi?"



    "Staff sajent Mosha ni nani alokwambia umpige

    kibao haya sasa tokeni nje nyote" Inspekta Haroub

    alimfokea askari aliyempiga kibao Joseph kisha

    akawafukuza maaskari wote kwa hasira.



    "sasa ndugu Joseph Kiiza unatambua juu ya tukio

    lililofanywa na Norbert Kaila huko Tanga" Inspekta

    Haroub aliuliza



    "hapana sitambui juu ya tukio alilofanya" Joseph

    alijibu



    "ok kwani mara ya mwisho alikwambia anaenda

    wap?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "aliniambia anaenda kuhudhuria mazishi ya waziri

    akiwa kama mwandishi wa habari"



    "kwahiyo unataka uniambie huwa anahudhuria

    matukio makubwa mengine akiwa tofauti na

    mwandishi wa habari"



    "hapana"



    "sasa hiyo kama inamaanisha ni mfano usiolingana

    na uhalisia je huwa ana kazi nyingine"



    "hapana yeye ni mwandishi wa habari tu"



    "sasa unaposema kama mwandishi wa habari si

    unamaanisha huwa alijifanya ni mwandishiwa

    habari.

    Je huwa anafanya kazi gani?"

    Swali hilo lilimfanya Joseph abaki kimya baada ya

    kushindwa kulijibu na kupelekea Inspekta Haroub

    atoke ndani ya chumba cha mahojinano bila ya

    kusema chochote. Baada ya muda alirudi akiwa

    ameongozana na askari mwenye mwili wa

    mazoezi.



    "sasa bwana Joseph swali uliloshindwa kulijibu

    utalijibu kwa msaada wa rafiki hapa, sasa nataka

    uniambie ni wapi walipo Hilda na Allison" Insepktat

    Haroub aliongea kwa utaratibu sana.



    "afande kusema kweli Hilda aliondoka muda mfupi

    tu toka muingie pale nyumbani na Allison alikuwa

    ametoka nje kuongea na simu na hakurejea na

    hadi

    pale mnatuvamia tulikuwa tunamsubiri yeye" John

    alijitetea.



    "uongo unaofanana na ukweli huo" Inspekta

    Haroub

    alisema kisha akamgeukia askari aliyekuja nae

    halafu akamwambia "nafikiri ni muda wako wa

    kufanya kazi".

    Yule askari alimsogelea Joseph kisha akamuuliza

    kwa upole "je uongo na ukweli upi ni wa muhimu

    kuusema?".



    Joseph akajibu, "ukweli .



    "ok kama ukweli ni wa muhimu mbona

    hukuusema?" alimuuliza tena



    "nimeusema afande" Joseph alijitetea.



    "kama uliusema ni kwanini swali la afande

    lilikushinda kujibu" aliulizwa tena.

    Josepb alikosa cha kujibu kisha akainamisha

    kichwa chini na kupelekea apigwe kofi zito lilimtoa

    damu mdomoni.



    "hapo umekalia kiti cha mateso je unajua? na

    uongo

    wako utakuumiza mwenyewe"aliongea yule askari

    kisha akafungua mkebe uliopo mezani, alitoa koleo

    dogo kisha akavaa glovu za mipira halafu akauliza

    "kama Norbert ni mwandishi wa habari na ni

    mwenzenu, je bunduki aliyopiga risasi matairi ya

    basi na kupelekea kutokea kwa ajali aliitoa wapi?"

    Joseph alibaki kimya na kupelekea yule askari

    ang'oe kucha yake moja kwa koleo huku

    akimwambia, "WAHANGA nyinyi hamfichani

    wenyewe kwa wenyewe hii inajulikana, halafu

    husemi huku unajifanya hujui". Joseph alitoa

    miguno ya maumivu baada ya kucha yake

    kutolewa

    huku akisema "sijui chochote afande".

    Askari huyo aliendelea kung'oa kucha zote za

    mkono wa kulia hadi akazimaliza.



    "je nyinyi si mnasema hamfichani sasa itakuwaje

    jambo la mwenzenu msilijue" Askari yule aliuliza

    huku akisogeza mkebe wa plastiki uliokuwa

    pembeni kisha akaufunua halafu akamwambia "hii

    ni

    chumvi na ipo hapa kwa ajili yako tu ikiwa

    hutosema, kwani vidole vyako vinavyovuja damu

    nitaviweka humu ili chumvi iingie. Je upo tayari

    kusema ukweli?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " afande mnanionea tu ki sijui lolote kuhusu hilo"

    Joseh alijitetea huku akiugulia maumivu ya

    kutolewa kucha kwa koleo



    "inamana hutaki kusema sio?"



    "afande nikuambie nini la ziada wakati hilo ndio

    ninalojua.



    "sasa unaenda kupumzika na ukirudi mara ya pili

    utaje la si hivyo utakuwa kibogoyo" aliongea Askari

    huyo kisha akasema "aletwe mwenzake hapa ".

    Waliingia maaskari wawili humo ndani ambao

    walimfungua Joseph kisha wakamchukua na

    kumrudisha selo, kisha wakamchukua Davis

    wakampeleka chumba mahojiano.



    ********************************************************



    SAA MOJA ILIYOPITA



    MIKOCHENI

    Kikao baina ya kundi la Three devils na wakubwa

    wao kilikuwa kimeitishwa kwa mara ya pili ndani

    ya nyumba wanayoishi wauaji hao, taarifa za

    kupatikana kwa waandishi wa habari wawili wa

    kundi la WAHANGA zilikuwa zimeshawafikia wauaji

    hao hatari. FI na KL walikuwa ndio wafikishaji wa

    taarifa hiyo.



    "sasa wakuu mi naona kazi imeisha cha msingi

    tuwakate kauli kimyakimya" Morris aliwaambia FI na

    KL



    "sasa mtawakata vipi wakati wapo chini ya

    uangalizi wa polisi" KL aliuliza.



    "ni mchezo wa kitoto tu, cha msingi itolewe amri

    ya kuwapeleka mahabusu kisha sisi tutawamaliza

    njiani" Jim alifafanua .



    "sawa kama ni hivyo nahitaji jua la kesho

    wasilione yaani leoleo wanaenda mahabusu" FI

    alitoa amri.



    "haina haja tena ya kujadili wacha Morris

    akamalize mchezo" Jim aliongea na kupelekea

    kikao kiishe kisha wakuu wao waliowapa kazi

    wakaondoka nyumbani hapo. Morris alinyanyuka

    kwenye kiti huku akisema"ni mchezo mdogo tu

    unahitajika wa kuwawekea C4 kwenye gari

    wanalopelekwa mahabusu kisha kazi itakuwa

    imekwisha". C4 ni bomu hatari lenye kutegeshwa

    kwa muda ambalo lina saa ndogo kisha lina

    kibunda kilichofungwa baruti kwenye vitu maalumu

    vinavyofanana na karoti.

    Morris aliondoka nyumbani hapo kwenda kufanya

    kazi aliyopewa baada ya kukamilisha vitendea kazi

    vyake.



    *******************************************************



    KITUO CHA POLISI CHA BARABARA YA KILWA

    Wakati maaskari wakijiandaa kumuhoji Davis

    Inspekta Haroub alipigiwa simu na namba binafsi

    iliyojiandika IGP pasipo kuinesha namba za

    mpigaji, aliwaamuru maaskari hao wasitishe zoezi

    na watulie kimya kish akapokea simu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ndio mkuu.......... lakini afande............sawa

    nimekuelewa" aliongea kisha akawageukia wenzke

    baada ya simu kukatwa halafu akawaambia, " IGP

    katoa amri ya kuwapeleka mahabusu hawa andaeni

    gari upesi" Alipomaliza kuwapa maagizo alitoka

    nje ya chumba hicho akiwaacha askari wakiandaa

    mpango wa kuwapeleka washukiwa wao mahabusu



    Gari la kuwapeleka mahabusu liliandaliwa ndani ya

    muda huo kwa haraka sana kutokana na amri

    iliyotoka, zikiwa zimebaki dakika tano tu ili safari

    ianze Inspekta Haroub alipokea simu tena kutoka

    kwa IGP iliyomwarifu washukiwa wavikwe kitambaa

    kichwa kizima ili kuwafanya wasijue wanapoelekea,

    jambo hili halikuwa kawaida kwa mahabusu wa

    kawaida kufunikwa kama wanaopelekwa kunyingwa.

    Inspekta Haroub aliamua kutii kwasababu ni amri

    kutoka kwa mkuu wake. Alituma watu kwenda kuwa

    makostebo wawili wanaoshughulika na kukaa na

    funguo za selo, makostebo hao ambao huwa

    wanafuga masharub na waliofanana kimaumbo

    walifika ofisini kwa Inspekta Haroub kisha

    wakapokea maagizo ambayo walitakiwa kuyafanya

    kwa muda huo kutoka kwa Inspekta Haroub. Baada

    ya kumaliza kutoa maelezo Inspekta Haroub

    alipokea simu nyingine kutoka kwa kwa IGP, simu

    hii ilimueleza juu ya gari maalum ambayo ingefika

    kituoni hapo kwa ajili ya kuwapeleka watu hao

    mahabusu. Jambo hili nalo lilimshangaza sana

    Inspekta Haroub ingawa alitii kwasababu ni amri

    kutoka kwa mkuu wake. Gari maalum ya rangi ya

    bluu ambayo mara chache hutumika kwa

    watuhumiwa wa ugaidi iliwasili kituoni hapo ikiwa

    ina dereve maalum aliyetumwa kulileta, polisi

    walikabidhiwa gari hilo kwa masharti ya kulirudisha

    kituo cha kati wakishawapeleka washukiwa

    mahabusu, Inspekta Haroub aliwaachia askari wenye

    cheo kidogo wafanya kazi hiyo ya kuwapeleka watu

    hao kisha yeye akaenda ofisini kuendele na kazi

    zake, watuhumiwa walipakiwa kwenye gari maalum

    huku sura zao zikiwa zimezibwa ili kuwafanya

    wasijue wanapoelekea. Baada ya kila kitu kukamilika

    msafara magari matatu ulitoka kituoni hapo kwa kwa

    mwendo wa taratibu kuelekea barabara ya Kilwa

    upande wa kusini, uliongeza mwendo baada ya

    kuingia barabara hiyo. Gari lililobeba watuhumiwa

    lilikuwa lipo katikati huku magari mawili ya polisi

    waliobeba silaha yakiwa yapo mbele na nyuma.

    Msafara huo uliokuwa unaelekea gereza la keko

    haukufika mwisho wa safari yake baada ya tukio

    geni kutokea wakiwa wapo mzunguko ulio jirani na

    shule ya jeshi ya Jitegemee iliyopo katika kambi ya

    JKT ya mgulani, ulikuwa ni mlipuko mkubwa wa

    bomu uliopelekea gari maalum lililotumika

    kuwabeba mahabusu liruke juu likiwa linateketea na

    moto. Magari mawili ya polisi nayo yalipatwa na

    mshtuko huo wa bomu yakapoteza muelekeo

    hadi yakagonga kituo cha daladala kilichopo jirani.

    Hakika lilikuwa ni tukio ambalo halikuwahi kutokea

    katika nchi hii yenye amani ya kimtazamo, kikundi

    cha wanajeshi kutoka kambi ya jeshi ya Mgulani

    kilitoka ndani ya kambi hiyo kikiwa na silaha zao

    tayari kwa lolote. Gari la wagonjwa nalo lilitoka huko

    kambini ili kuokoa majeruhi wa ajali hiyo. Mlipuko

    huo nao ulisikika hadi kituo cha polisi cha barabara

    ya kilwa kutokana na ukaribu uliopo, polisi kutoka

    kituo cha barabara ya kilwa walitoka kwa haraka

    wakiwa na silaha kamili ili kujihami. Ndani ya dakika

    kumi tayari gari la zimamoto lilishafika na askari

    polisi walikuwa wameshazungusha utepe katika

    eneo la tukio, hadi muda huo haikufahamika na wala

    kuenakana dalili za uhai ndani ya gari lililobeba

    watuhumiwa waliokuwa wanapelekwa mahabusu .

    Barabara ya kilwa ilifungwa kuanzia muda huo na

    kupelekea magari yazunguke kupitia barabara ya

    Bandari kuja kutokea uhasibu ili yaendelee na safari,

    kundi kubwa la waandishi wa habari lilishawasili

    ndani ya eneo hilo wakichukua picha ya tukio zima.

    Hadi muda huo hakuna mtu aliyetoka ndani ya gari

    hilo wakiwa hai, miili minne ilitolewa ndani ya gari

    hilo ikiwa imeungua vibaya baada ya moto

    kuzimwa. Wawili walitambulika kama watuhumiwa

    kutokana minyororo mizito iliyokuwa ipo shingoni

    mwao, wengine walitambulika kama maaskari

    kutokana na kutokuwepo kwa alama inayowaonesha

    kama ni watuhumiwa.



    *******************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MUDA MFUPI ULIOPITA

    Gari aina ya Toyota diffender ya polisi yenye vioo

    vya giza iliwasili kituoni hapo ndani ya dakika kumi

    na tano toka amri ya kuwapeleka wakina Davis

    mahabusu kutolewa. Askari polisi mwenye mwili wa

    wastani na kimo kirefu pamoja na nyota tatu mabegani alishuka ndani ya gari hilo

    akiwa na mkoba kisha akaelekea zilipo selo ndani

    ya kituo hicho cha polisi. Muda huo ndio Inspekta

    Haroub alitoa amri ya amri kwa makostebo wawili

    wa polisi wenye sharubu, askari huyu ambaye ni

    mgeni katika kituo aliingia hadi zilipo selo.

    Aliwakuta makostebo wawili wakiwa wanawaanda

    Davis na Joseph ili wawapakize kwenye gari ambalo

    lilitarajiwa kufika ndani ya muda mfupi tu.



    "jambo afande" maaskari hao walitoa saluti kisha

    wakaendelea na zoezi la kuwafunga minyororo

    Davis na Johnson.



    "jamboo, njooni mara moja" askari huyo aliwaambia

    kisha akasogea kwa hatua moja, makostebo hawa

    waliacha kuwa minyonyoro kisha wakasogea hadi

    alipo askari huyo kisha wakasema "ndio afande".



    "mnajua.." Askari huyu alikatisha maneno yake

    kisha akatoa ngumi kwa mikono yake miwili

    zilizowapata makostebo hawa kwenye pua zao hadi

    wakawaangukia wakina Davis.



    "haina kuremba nyinyi wapeni mambo ila msiwaue"

    Askari huyu aliwaambia wakina Davis kwa sauti na tofauti na aliyoitumia

    ya awali ambayo inafahamika kwao, Davis na Joseph waliwakaba makostebo

    wao hadi wakaishiwa nguvu halafu wakaishiwa

    nguvu kabisa.



    "wavueni nguo zao halafu mvae nyinyi" Askari huyo

    aliwaambiwa tena wakina Davis ambao waliwavua

    nguo maaskari hao kisha wakazivaa wao. Askari

    huyo alifungua mkoba wake ambao ulikuwa na sura

    mbili za bandia zinazofanana na za maaskari hao

    halafu akawaambia "vaeni hizi". Joseph na Davis

    walizivaa kwa haraka kisha wakawavalisha maaskari

    hao nguo zao walizozivua.



    "wafingeni gundi mdomoni na muwavalishe sura

    hizi" Askari huyo aliwapa maelekezo wakina Joseph

    huku akiwapatia sura za bandia zinazofanana na

    sura zao. Waliwavalisha sura hizo kisha

    wakawafunga minyororo halafu wakawavisha

    vitambaa vyeusi vikubwa kama kofia, Askari huyo

    alipomaliza kuwaelekeza alimng'oa kostebo

    aliyevishwa sura ya bandia ya Joseph kucha zote za

    mkono wa kulia kisha akafunga mkoba wake.



    "wapelekeni hadi hapo nje mtakuta kuna maaskari

    wanawasubiri, Jose hakikisha unauficha mkono

    wako uliong'olewa kucha ili wasiuone" aliwaambia

    wakina Joseph kisha akatoka huku akiwaambia,

    "nawasubiri kwenye diffender ya bluu isiyo na bodi

    iliyokuwa maegesho".

    Joseph na Davis waliwapeleka maaskari hao hadi

    nje kisha wakawabidhi kwa maaskri walioteuliwa

    kuwapeleka mahabusu kisha wakaelekea

    eneo la maegesho, hapo waliikuta gari

    waliyoelekezwa na yule askari, hapo walifungua milango

    ya viti vya nyuma kisha wakaingia kila mtu upande

    wake. Walimkuta yule askari akiwa amekaa kwenye

    kiti cha dereva akiwa tayari ameshafunga mkanda

    wa gari.



    "mshamaliza mchezo?" yule askari aliwauliza



    "tayari kila kitu sasa tuondoke" Davis aliongea

    Yule askari aliwasha gari kisha akaweka gia halafu

    akakanyaga sehemu ya mwendo na kupelekea gari

    itoke kuelelekea getini, baada ya kutoka getini aliingia katika barabara ya

    waendayo kwa miguu hadi katika mzunguko wa

    Mgulani kisha akaifuata barabara iendayo uhasibu.



    *******************************



    MIKOCHENI

    DAR ES SALAAM

    Baada ya kutega bomu ambalo lilipuka Morris

    aliamua kurudi hadi walipo wenzake akiwa na furaha

    ya kufanikisha kazi yale, aliwakuta wakiwa wapo

    chumba cha mazoezi wakiwa wanapasha miili yao.



    "vipi mzee kazi imeisha maana naona unatabasamu

    tu" Jim alimuuliza



    "imeisha tena kwa mchezo wa kitoto tu" Morris

    alijibuCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "tupe data zote za mchezo huo" Michael

    akamwambia



    "aisee ni mchezo mdogo tu nilioufanya baada ya

    kutajiwa namba za gari ambayo ingewapeleka wale

    mbuzi mahabusu, nilienda hadi kituo cha kati

    nikalikuta lile gari likiwa limetoka kufanyiwa

    marekebisho likisubiri safari ya kwenda kuwachukua

    wale mbuzi. Sasa hapo nilopomaliza mchezo kwa

    kuibandika C4 kwenye uvungu bila kujulikana"

    Morris alielezea.



    "poa karibu upashe mwili" Jim alimkaribisha, Morris

    alijumuika nao katika mazoezi akiwa na furaha ya

    kutoa roho za watu. Three devils ni binadamu wa

    tofauti na wengine wa kawaida, binadamu wa

    kawaida siku zote husikitika sana akisikia roho ya

    mtu asiye na hatia imetolewa kwa namna ya kikatili.

    Jambo hili lilikuwa kinyume kwa vijana hawa wa

    kimarekani wenye roho za paka mwenye hasira,

    kwao kutolewa wa mtu ilikuwa ni firaha sana.

    Kitendo cha wenzao kufanikiwa kulipua gari hilo

    ilikuwa ni kama wimbo uburudishao masikioni

    mwao, waliendelea kufanya mazoezi huku

    wakipanga mikakato yao mingine.



    *********************************



    Safari yao iliishia kurasini mtaa wa Bank club

    kwenye nyumba yenye uzio mrefu, walifika kwenye geti kisha wakaingia ndani ya nyumba hiyo baada

    kufunguliwa geti na mtunzaji wa hiyo nyumba.

    Waliingia hadi ndani kisha wakavua sura walizozivaa

    kila mmoja, yule askari alipoivu sura yake

    alitambulika kuwa ni Allison.



    "hivi we mwanga mbona michezo yako siielewi"

    Davis alimmuliza Allison wakiwa ndani ya nyumba

    hiyo.



    "hakuna muda wa kukusimulia kila kitu ila cha

    msingi ni kuwaeleza kwa ufupi jinsi

    nilivyowakomboa, kabla hamjakamtwa siku ile mimi

    nilitambua ujio wa polisi baada ya kupigiwa simu

    wakati tunajadiliana pale nyumbani " Allison aliwaeleza



    "ndiyo nakumbuka sasa uliondokaje maana

    ulipotoka wewe nje tulivamiwa na polisi ambao

    walikutafuta wakakukosa?" Joseph aliuliza



    "nilifanya mchezo wa nyani tu, yaani nilidandia

    ukuta nikatokea nje kisha nikajichanganya mitaani"

    Allison alijibu kisha akaendelea kuwaeleza



    "asubuhi ya leo nilirudi kisha nikachukua tarakilishi yangu

    halafu nikaamua kuja huku nilipomaliza kuchukua

    hivyo. Hapo ndipo nilipopata simu kutoka kwa mtu

    wangu ambaye yupo kituo cha polisi

    mlichohifadhiwa, niliupanga mchezo mzima kisha

    nikamfahamisha. Huyu askari alinitumia picha za

    maaskari ambao wanawalinda kwa kutumia mtandao

    wa whatsapp ilikukamilisha mchezo, hapo ndio na

    mimi nikachonga sura nne za bandia kwa kutumia

    mashine iliyomo humu ndani. Nilivaa sura ya bandia

    ambayo ipo humu ndani kisha nikaja kuwaokoa kwa

    njia hiyo".



    "ujue maelezo yako yananitisha, kwanza wewe ni

    nani hasa mpaka umiliki mashine ya kuchonga sura

    za bandia" Joseph alimuuliza akiwa ana sura ya

    mashaka.



    "mimi ni Allison kama mnavyonijua, utambulisho

    wangu mwingine mtakuja kuujua baadae. Kwa sasa

    inabidi mkae humu ndani na asitoke mtu kwa

    usalama wenu na kama mkitoka jua mnajichimbia

    kaburi. Joseph na Davis

    naombeni hii ngoma ya shetani na malaika

    msiivamie hata kidogo kama mnapenda muwe

    mnavuta pumzi ila kama hamupendi basi ivamieni ili

    tuwafukie"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sijakuelewa kabisa hebu nieleweshe" Joseph

    alihitaji ufafanuzi zaidi.



    "inabidi mkae hapa kama mnajitaka, sina ufafanuzi

    zaidi ya huo nadhani tunaelewana" Allison

    aliwaambia kisha akaelekea nje akiwaacha wenzake

    wakiwa na maswali zaidi, hakutaka kuwatolea

    ufafanuzi zaidi kutokana na kuhofia kuharibu kazi.



    ********************************



    Tukio la ulipukaji wa bomu katika gari la maalum la

    maabusu wanaoshughulika na ugaidi lilikuwa ndio

    habari kuu kuanzia muda huo nchi nzima, mkuu wa

    jeshi la polisi IGP Rashid Chulanga alizungumzia

    tukio hilo kama la kigaidi. Aliwataja Davis na

    Johnson waandishi wa habari kutoka Kenya na

    Uganda ndio ni miongoni mwa watu wakiopoteza

    maisha, pia alieleza hatua ya jeshi la polisi juu ya

    utafutwaji wa watuhumiwa wa bomu hilo. Hakika

    ilikuwa ni mkutano kati ya waandishi wa na mkuu

    huyo wa polisi na waandishi wa habari katika makao

    makuu ya polisi yaliyopo katika ofisi za wizara ya

    mambo ya ndani. Kikao kilipoisha IGP Chulanga

    aliagana na waandishi wa habari kisha akarejea

    katika ofisi yake, tukio hilo la kulipuka kwa bomu

    lilimchanganya sana.



    "huenda tumevamiwa na magaidi" alijisemea akiwa

    amekaa katika kiti chake akilifikiri hilo tukio kwa

    undani.



    "GRIII! GRIII! GRII!" mlio wa simu ya kiganjani

    ulisikika ndani ya koti lake, aliitoa kisha akabonyeza

    kitufe cha kupokea halafu akaiweza sikioni



    "ndiyo mheshimiwa" IGP Chulanga aliongea.



    "Chulanga hivi inakuaje watu ambao wangefanikiwa

    kumpata mtuhumiwa wanauliwa? hivi ulifuata yale

    maelekezo niliyokupa?!" ilisikika sauti ya mtu

    anayelalamika katika simu ya IGP Chulanga.



    "nimefuata kama ulivyoniambia mheshimiwa, ila

    naona kuna mkono wa mtu" IGP Chulanga alijitetea



    "hakuna cha mkono wa mtu wewe huyo huenda ni

    Kaila aliyesababisha ajali jana".



    "tusidhanie kitu ambacho hatuna uhakika nacho

    mheshimiwa wacha uchunguzi upite" IGP Chulanga

    alishauri.



    "sasa sikiliza hii ni amri na sio ombi, hakikisha

    Kaila anakamatwa haraka iwezekanavyo, sitaki

    kusikia mambo ya dhana".



    "sawa mheshimiwa" IGP Chulanga alikubali amri ya

    mkubwa wake kwa utiifu, baada ya kumaliza

    kuongea na simu hiyo simu ya mezani isiyo na

    waya iliita kwa fujo. Aliipokea simu hiyo kisha

    akasema , "IGP".



    "Regnald Kitoza mkurugenzi wa usalama wa taifa,

    nahitaji tuonane sasa hivi kama itawezekana" sauti

    kwenye simu hiyo ambayo ilikuwa imewekwa sauti

    ya spika nje ilisikika.



    "sawa Kitoza tukutanie wapi?" IGP aliuliza



    "nitakuja ofisini kwako muda si mrefu"



    "sawa utanikuta" IGP alijibu kisha akakata simu

    pasipo mpigaji kukata.



    Baada ya dakika takribani kumi Kitoza alifika ofisini kwa IGP Chulanga akiwa ndani ya vazi nadhifu la suti, alimkuta IGP Chulanga akiwa yupo ofisini .



    "naona nimekuweka sana?" KItoza aliuliza.



    "aah! hapana, vipi habari za muda huu?" IGP Chulanga alimsabahi KItoza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "si nzuri sana aisee ndio maana nikaja hapa kwako" Kitoza alisema



    "kulikoni au ni ile ishu ya Kaila" IGP Chulanga alikisia juu ya jambo linalomsumbua Kitoza



    "hakuna jingine isipokuwa hilohilo tu" Kitoza alisema.



    "ok, hebu lieleze kwa unavyoijua wewe"



    "Chulanga jua tunamtafuta mtu hatari na mwenye kufanya mambo ya hatari, yaani mtu huyu amefikia hatua ya kumjeruhi mwanausalama mwenye kuaminika katika mapigano. Nadhani unamtambua Briton alivyo na uwezo wa juu ila amejeruhiwa na Kaila".



    "Kitoza huyu mimi naona alivizia sio mtu wa kushindana na Briton kabisa"



    "Chulanga punguza kudhani, yaani mtu afikie hatua ya kusababisha ajali ya basi na haitoshi akasababisha mlipuko wa bomu halafu unasema sio wa kushindana".



    "suala la kulipua gari la mahabusu sio la kumpa Kaila maana kijana wangu aliyepo kituo cha kati amebaini jambo, iambo hili sikutaka nimueleze mheshimiwa kabla ya kumkamata mhusika".



    "jambo gani hilo?"



    "kuna kijana ameonekana akiweka kitu chini ya gari hilo kisha akaondoka kituoni hapo na pikipiki aina ya suzuki ambayo namba zake za usajili tunazo. Kwa mujibu wa dereva aliyetumwa alipeleke gari hilo kituo cha barabara ya kilwa, aliweza kumuona tena akiwa nyuma ya akimfuatilia na hadi anafika kituoni yule mwenye pikipiki hakuondoka maeneo ya karibu na kituo hadi gari linalipuka".



    "aisee kwahiyo una uhakika huyo sio Kaila"



    "hawezi kuwa Kaila maana kijana huyo ni mwembamba na mrefu kuliko Kaila, kumbuka Kaila ana mwili wa wastani na sio mrefu".



    "ok, ni vizuri sana. Ila suala la Kaila inabidi nalo tuliangalie kwa jicho la tatu"



    "kwanza apatikane huyo kijana mwenye pikipiki aina ya suzuki nyeusi yenye namba za usajili...." IGP alifungua faili lillopo jirani yake halafu akasoma kisha akasema, "T560 DOY" na imesajiliwa ndani ya miezi miwili iliyopita sasa huyo ndiye atakayetutajia wenzake tukimbana".



    "ok. Pongezi kwa maaskari wako waliombaini mtu huyo" Kitoza alimpongeza kwa namna ya kumchimba zaidi ili aongee zaidi, mkurugenzi huyu wa usalama wa taifa alikuwa na lengo tofauti na mwenzake . IGP Chulanga pasipo kujua lolote alijikuta akisema, "si maaskari bali pongezi ziende kwa Koplo Daniel Uyomo aliyeshuhudia tukio la kijana huyo".



    "sasa hapo mpo katika hatua nzuri na mtu huyo akipatikana jua kazi imeisha"



    "hakika kazi itakuwa imeisha na ikishindikana itanibidi nimtumie askari wangu muaminifu katika hili".



    "kwani askari wako wote si waaminifu au unaemuamini zaidi yao"



    "ndiyo yupo na hivi karibuni utamjua"



    "ok mi sina la ziada kuhusu hilo nadhani mmefikia hatua nzuri kuhusu hilo jambo, wacha mimi niwahi sehemu mara moja na ukitaka msaada usisahau kunijulisha".



    "sawa bwana" IGP Chulanga aliitikia huku akipokea mkono wa kuagana kutoka kwa Kitoza. Kitoza alitoka ofisini kwa IGP hadi lilipo gari lake kisha akaingia ndani halafu akaliwasha,aliliondoa kwa mwendo wa wastani huku akiwa na fikra nzito katika suala aliloambiwa.na IGP Chulanga. Hakika alipata taarifa muhimu za kulinda maslahi yao yasijulikane na wengine.



    "inamaana Morris alifanya uzembe namna hii hadi akaonekana, hili suala inabidi nimuambie mheshimiwa" alijkita akiongea peke yake.



    ***************************************



    RASKAZONE

    TANGA



    Upweke wa kukaa ndani kama mwali tayari ulishaanza kumchosha Norbert, tabia ya kupenda kukutana kimwili na mwanamke kila mara nayo ilimchosha na siku hiyo akajikuta akimtamani binti aitwae Mwanahawa ambaye ndiye anayemuhudumia kila kitu. Uzuri wa binti huyu ulianza kumfanya Norbert atoke mate ya uchu kama ilivyo kawaida yake, binti huyu ni nesi aliyeacha kazi kisha akaja kuajiriwa na EASA kama daktari bingwa wa mifupa na misuli baada ya kusomeshwa na shirika hilo. Pia amepitia mafunzo mbalimbali ya kijasusi. Ndani nyumba hiyo aliyofichwa Norbert kuna vyumba vya chini ya ardhi ambavyo hutumiwa kama hospitali ambayo hutibu wapelelezi tofauti wa EASA waliopo ndani ya ukanda huu wa pwani.



    Muda wa jioni ulipowadia ndani ya nyumba hiyo palikuwa hamna mtu yoyote zaidi ya Norbert na Mwanahawa, hakika huo ndio ulikuwa mwanya kwa Norbert baada ya kuwa ameshaanza kuwa na mazoea na jasusi huyo wa kike mwenye taaluma ya udaktari. Aliamua kuongea naye mambo mbalimbali kama ilivyo kawaida na mwishowe akaanza utani ambao yeye huwa anauita sumu, alianza kumtekenya binti huyo kwa namna ambayo isingedhaniwa ni ya kutaka kumpandisha hisia binti huyo. Baada ya muda Mwanahawa alipandwa na hisia zisizo zuilika na kupelelea ajibu mapigo kwa kufanya mambo anayofanyiwa na Norbert, ndani ya robo saa binti huyo alikuwa hajiwezi kwa utundu aliofanyiwa na Norbert.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nor please acha" Mwanahawa alilalamika huku akiukamata mkono wa Norbert ili usiachie kuendelea kupapasa maungo yake, baada ya muda mfupi Norbert na Mwanahawa walianza kunyonyana ndimi kwa fujo. Norbert alimnyanyua binti huyo kisha akampeleka hadi chumbani kwake kisha akamaliza kazi aliyoianza walipokuwa sebuleni, baada ya masaa mawili wote walitimiziana mahitaji kisha wakaenda kuonga halafu wakarejea sebuleni baada ya kubadisha nguo. Norbert alivaa suruali ya mazoezi nyepesi na fulana nyeupe, Mwanahawa alivaa nguo ya kulalia ya kike nyeupe nyepesi na suruali ya kulalia ya kike, wote walienda kuka kwenye kochi moja huku Norbert akiwa amempakata Mwanahawa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog