Simulizi : Jinamizi
Sehemu Ya Nne (4)
"Nor ujue tumeonekana tayari" Mwanahawa alisema akiwa na aibu usoni mwake.
"wasiwasi wako nini sasa?" Norbert alimuuliza akionekana kupuuzia hilo jambo.
"ujue humu ndani kuna kamera ya ulinzi moja iliyounganishwa na makao makuu" Mwanahawa alimuelezea
"punguza hofu mama wale hawana ne..." Norbert alishindwa kumalizia kauli yake baada ya kusikia sauti ya kifunguka kwa dari la nyumba hiyo kisha kishindo cha kutua mtu kikafuata. Alimsukuma Mwanahawa na miguu yake na kupelekea binti huyo aruke sarakasi hadi nyuma ya kochi kisha akajificha, Norbert naye alijirusha hadi usawa wa dirisha kisha akakamata vyuma vya kuchomeka pazia kwa mikono yake na mguu ikawa imedaka sehemu ya juu ya feni lililopo sebuleni hapo hivyo akawa amenasa kama mjusi huku macho yake yakiwa chini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ha! Ha! Ha! Ha! dah mna spidi hatari, kwenye tukio la ghafla kama hili" alikuwa ni Asp John ndiye aliyevamia kwa ghafla kuwajaribu wenzake. Baada ya kumjua aliyevamia Mwanahawa alijifyatua kutoka nyuma ya kochi hadi katika sehemu ya kukalia katika kochi hilo akawa amekaa, Norbert alijiachia kutoka kule juu kwa sarakasi hadi chini kisha akaketi kwenye kochi.
"sasa ndio nini kutujaribu hivi" Norbert alimuuliza Asp John.
"nilitaka niwaone mna kasi kiasi gani" Asp John alijibu
"sasa kama ningekuwa na kisu si ungekuwa umeisha sasa hivi" Mwanahawa alimwambia.
"aah! Wapi hamna kitu kama hicho maana nilijua hamjajiandaa, ujue nimewasoma muda mrefu toka mnaanza hayo mahaba yenu ya kuku" Asp John aliwaambia.
"Loh! Inamaana ulikuwa unakula deo dirishani. Yaani wewe ulitakiwa uwe mwandishi wa habari maana umbea umezidi" Mwanahawa aliongea akiwa ameinamisha macho chini.
"kwanza kwema,maana umevamia usiku kinyume cha kawaida yako" Norbert aliuliza.
"aisee unatakiwa uende bagamoyo usiku huu, ni amri imetoka makao makuu Dodoma kwa mkurugenzi mwenyewe. Tena kasema upunguze huo ukijogoo wako maana utaingia matatanu" Asp John alileta taarifa iliyomleta hapo na kupelekea Norbert aduwae kwa sekunde kadhaa.
"bibie mimi ninakuacha, nadhani umeisikia taarifa hiyo" Norbert alimwambia Mwanahawa ambaye hadi muda huo alikuwa kanywea kwa taarifa hiyo, Norbert aliamua kumfuata kisha akambusu halafu akamkumbatia na kupelekea Mwanahawa amwambie, "kuwa mwangalifu maana nimetokea kukupenda".
"usijali mama" Norbert alimwambia kisha akaingia ndani kwake kujiandaa na baada ya dakika kadhaa alirejea akiwa yupo tayari.
"Utatumia hiyo Prado nyeusi" Asp John alimwambia huku akimrushia funguo ya gari kisha akanyanyuka halafu akafungua mlango wa kutokea nje na akatoka nje. Norbert naye alimfuata akiwa yupo sambamba na Mwanahawa, walienda hadi kwenye maegesho ya magari ndani ya nyumba hiyo. Norbert alifungua mlango wa dereva wa gari hiyo kisha akaingia halafu akaliwasha gari hilo, Mwanahawa alimuonesha ishara ya busu kwa kumuaga. ASP John naye aliingia ndani ya gari kisha akatangulia nje na Norbert akafuata, Norbert alielekea barabara ya pangani na Asp John alirudi nyumbani kwake maeneo ya Usagara
***************************************
USIKU WA MANANE
MAKAO MAKUU YA USALAMA WA TAIFA
JIJINI DAR ES SALAAM
Ndani ya ofisi nzito za usalama ambayo hata wana usalama wa kawaida ni ngumu kwao kuingia ndani ya ofisi hii, kulikuwa kuna kikao kizito kinawahusisha watu wazito ndani ya nchi hii. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Filbert Ole, mfanyabiashara maaraufu Tanzania Kaimuzi Liwale,vijana wa kundi la Three devils na mkurugenzi wa usalama wa Taifa Reginald Kitoza, kutokana na uzito wa mjadala uliokuwepo mule ndani kamera zote iliamriwa zizimwe na jukumu la uzimaji kamera hizo alipewa Moses Gawaza kutokana na kuaminiwa kwake. Mlinzi wa rais pamoja na wapambe wa Liwale walibaki nje ya ofisi hiyo ya kutokana na usiri wa kikso hicho.
"jamani nimewaita hapa wote ili kujipanga tena upya maana naona mambo yanaenda vibaya katika baadhi ya sehemu, kwanza tukio la kuonekana kwa Morris wakati anatega bomu kisha kukaririwa kwa namva za usajili ya pikipiki yake. Jambo hili limefanywa na koplo Uyomo wa kituo cha kati. Pili upoteaji wa Tasu alipoenda kuchukua vinasa sauti na kamera zilizotegeshwa ofisini kwa wahanga. Jamani haya ni majanga na inabidi yatatuliwe kabla mambo hayajaharibika, nadhani ni hayo kwa ufupi" aliongea rais Ole kwa mikhtasari.
"nadhani nyote mmelewa alivyosema FI sasa inabidi haya matatizo yatatiliwe na tuweze kumlipa fadhila Mr Eagle kwa kutuletea vijana wake hodari kwa kazi" Liwale aliongea kisha akakaa kwenye kiti chake.
"kwanza kabisa wakuu ningependa huyo koplo Uyomo siku ya kesho kutwa asilione jua yaani kesho tu nataka aitwe marehemu" Jim alianza kutoa mchango wake.
"hilo ni jambo jema sasa inabidi aandaliwe mtu wa kwenda kummaliza" Rais alikubaliana na ushauri wa Jim.
"wakuu nafikiri huyu polisi aliyeniona auawe na mtu mwingine tofauti na sisi" Morris alisema na kupelekea Kitoza asimame juu halafu akasema ,"suala la huyo koplo Uyomo nadhani tutamuangamiza kwa mtindo wa kijinga tu kwani jamaa udhaifu wake mkubwa ni wanawake wenye makalio makubwa, sasa hapa imebidi nimtumie Jackline ambaye ni mmoja wa vijana wangu wa kuaminika. Nitahitaji mmoja wa vijana wa Three devil na pikipiki moja ili awe dereva wa huyu bibie".
"nadhani hilo ni jukumu la Michael maana ndiye hodari wa kuendesha pikipiki kuliko wenzake" Liwale aliongea na kupelekea wenzake wakubaliane nae kwa kutikisa vichwa.
****************************************
Wakiwa wanaendelea na mazungumzo Moses Gawaza alikuwa yupo katika chumba cha kamera za ulinzi akiangalia kikao chote kupitia tarakilishi yake ya mapajani aliyoiunganisha bila wao kujua. Tarakilishi ambayo iliunganishwa moja kwa moja na Tarakilishi nyingine ambayo ilikuwa nje ya makao makuu hayo kwa mwanausalama aliyekuwa akiwasiliana na Moses kwa siri. Haukuwa mkutano wa siri kama walivyodhani wahusika wa mkutano kwani ulikuwa wa wazi miongoni mwa wanausalama wa siri na wazalendo.
Mipango hiyo iliyokuwa inajadiliwa ilimfikia mwanausalama wa kimataifa mwenye kutetea maslahi ya kampuni yake inayoshughulika na mambo ya ndani ya ukanda wa Afrika ya mashariki.
**************************************
"pia nataka mtambue kuwa Mr Eagle yupo pamoja nasi kwa ahadi ya kumpatia eneo lililogunduliwa madini katika kijiji cha Chambalo kule Kondoa, kutokana na mchango wake kwetu. Eneo ambalo linajulikana na watu wetu hata kabla hawa watafiti hawajalijua, tulipanga tumpatie kimyakimya pasipo mtu yoyote kujua na tulizima pumzi za Mdoe kutokana na kiherehere chake cha kujifanya mzalendo ndani ya nchi hii ya kimasikini" Rais Ole aliendelea kuongea baada ya mpango wa kumuua Koplo Uyomo kukamilika na alizidi kueleza, "sasa basi eneo hilo lote ni mali ya Mr Eagle na inabidi apatiwe kwa namna ambayo haitajulikana baada ya kuondoa vikwazo vinavyotukabili"
"Nadhani mmemsikia FI alivyosema sasa basi kuna baadhi ya vikwazo ambavyo vitakwamisha mambo yetu, kwanza tuanze na mkuu wa majeshi na makomandoo wake kumi wenye uwezo wa kupigana majini, nchi kavu na angani. Pili tufuate hawa EASA maana kuna wapelelezi wao wapo kazini, hivyo inabidi watafutwe na wauawe mara moja na mwisho tumalizie kwa hawa waandishi wa WAHANGA waliobakia ambao ni Kaila na Hilda" Liwale alito ufafanuzi.
"wakuu mpango alioupanga bosi KL up vizuri sana na inahitajika utekelezwe kwa ushirikiano wa pamoja kati yetu na hawa vijana wa usalama wa taifa" Michael aliongea.
"ushirikiano ndio unaanza leo kwa kumshirikiana katika kumuua Koplo Uyomo mlafi wa wanawake" Kitoza aliongea
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kuwaua hao makomandoo wa mkuu wa majeshi ndio itakuwa kazi inayofuata kwa kuungana pamoja, cha msingi ni kupata orodha ya majina yao na mitaa wanayoishi kisha tunammaliza mkuu wa majeshi mwenyewe" Jim aliongea.
"kuna jambo nataka niwaambie kuhusu huyo mkuu wa majeshi jenerali Augustin Kulika, huyu ni mtu mzima kiumri ingawa ana nguvu kama kijana. Mkae mkijua mnapambana na mtu ambaye ana uwezo wa kipekee kutokana na historia yake ya kipindi cha nyuma, aliwahi kupambana na majasusi kumi wa mtandao wa wauza unga miaka minne iliyopita alipokuwa masomoni Urusi. Pia naomba mtambue kuwa mnapambana na komandoo wa Tanzania aliyepata mafunzo Urusi na Cuba. Umakini utahitajika hapo la si hivyo mtarudi maiti nyote kwani rais aliyemaliza muda wake hakukosea kumteua kuwa mkuu wa majeshi" Rais Ole aliwaonya vijana wake.
"basi ni hivyo inabidi tumuue kifo kisichoacha maswali na wala isingundulike kama kuna mkono wa mtu maana itapelekea wanajeshi nao waingie kazini kwa haraka na hapo mipango yetu itakwama" Morris naye alitoa mchango wake.
"wazo zuri sana Morris, inabidi tumuue kwa ajali ya kutengeneza tu au kwa kifo cha kimyakimya" Kitoza alishauri.
"sasa hapo inabidi wewe Kitoza uteue watu wako wenye uwezo wa juu na wenye vifua vya kutunza mambo na nyinyi wakina Jim muungane na vijana wa kazi wa Kitoza. Pia hakikisha unamuingiza Gawaza katika mpango maana yeye ni mmoja wa makomandoo wa usalama wa taifa, aingizwe bila ya kujua kama anashiriki huu mchezo usiomuhusu" Rais Ole alimwambia Kitoza kisha akaendelea kutoa ufafanuzi, "yaani umlaghai kwa kumuambia tuhuma za uongo juu ya mkuu wa majeshi na kikosi chake ili apate hamasa ya kutetea taifa lake na mwisho wake awe ameshiriki mpango wetu bila kujijua".
"hapo umetoa mpango mzuri na kilichobaki na kuufanyia kazi mkuu, nadhani ikulu yako ituongezee bajeti katika suala hili ili mpango uende sawa" Kitoza aliongea.
"mimi ndio rais na hayo mambo yapo ndani ya uwezo wangu, hivyo kuhusu hilo msijali" Rais Ole aliwaeleza kisha akainuka halafu akasema, "nadhani mpango upo sawa maelekezo yafuate, sisi hatuna la ziada zaidi ya kuwatakiwa kazi njema". Baada ya kumaliza kuongea hayo maneno Rais Ole aliinuka na wengine wakainuka , alipeana mikono na kila mmoja kisha akatoka ndani ya chumba hicho cha ofisi ya siri. Liwale nae alipeana mikono na vijana wote wa kazi kisha akawaambia, "kazi njema" halafu akatoka nje ya ofisi hiyo kisha akaondoka ndani ya makao makuu hayo akiwa na msafara mithili ya kiongozi wa nchi. Pesa inatesa na mwenye pesa siku zote hutesa na asiyekuwa na pesa jua hatotesa, yaani mwenye pesa siku zote hufanya kila alitakalo bila kuingiliwa. Ndio maana hata Liwale anatumia pikipiki za polisi katika msafara wake kwasababu ana pesa na hakuna mwenye kauli mbele ya pesa.
***************************************
Koplo Daniel Uyomo ni askari mwaminifu kutoka kituo cha kati jijini, askari huyu amepachikwa jina la 'Mdaku' na askari wenzake kutokana na tabia yake ya kupenda kufuatilia kila jambo analolitilia shaka. Pia ni mwepesi wa kukariri ushahidi anaouona kwa kichwa chake ikiwa ametililia wasiwasi tukio lolote, uhodari wake huu ulimfanya ahamishiwe kituo cha kati na wakubwa zake wa kazi pia akapandishwa cheo baada ya kuongezewa V ya pili katika bega lake na kumfanya aache kuitwa kostebo na akaitwa koplo ili kuendana na daraja la cheo alilokuwepo. Koplo Uyomo huyu pamoja na kuwa mwaminifu pia ni mdhaifu sana kwa wanawake wenye makalio makubwa wenye umbo lililojengeka, udhaifu huu unamfanya kupenda kila mwanamke mwenye umbo la namna hiyo atakayepita mbele yake. Asubuhi akiwa anakuja kazini akiwa na gari yake ndogo aina ya toyota carina, alichubuana na gari aina ya toyota Rav 4 katika foleni iliyopo katika barabara ipitayo mtaa wa bandari jijini Dar es salam. Gari hiyo ya rav 4 ilikuwa ikitokea barabara ya mafuta ipitayo pembeni ya kituo cha mafuta cha Puma ambacho zamani kilikuwa kinaitwa BP. Ukubwa wa foleni wa siku hiyo uliwalazimu baadhi ya watu kupita njia ya mafuta iliwawahi kufika mbele, gari ya Koplo Uyomo siku hiyo ilikuwa barabarani na na rav 4 ilikuwa ikiingia barabarani, kitendo cha kubana gari hiyo isiingie ndiyo sababu pekee iliyosababisha gari hiyo ichubuane na yake. Baada ya kutokea kwa tukio hilo Koplo Uyomo alishuka garini mwake akiwa na hasira ya kuharibiwa gari yake kisha akaenda hadi ilipo gari hiyo, aligonga kioo kwa fujo na kupelekea kioo cha gari hiyo kishushwe.
"afande samahani ni bahati mbaya" sauti ya kike laini ilimuomba radhi koplo Uyomo kisha sura ya mrembo aliyeumbwa kwa namna ya kipekee ikaonekana baada ya kioo cha gari kushushwa hadi mwisho.
"weka gari pembeni" Koplo Uyomo alimuambia mrembo huyo kisha na yeye akarudi hadi kwenye gari halafu akaingia kisha akaitoa barabarani na kuliweka gari pembeni ili kuepuka foleni isiyo ya lazima. Alienda hadi ilipo gari ya mrembo kisha akamwambia ,"shuka garini". Mrembo huyo alitii amri kisha akatoka garini na kufanya aonekane sawia katika macho ya Koplo Uyomo. Alikuwa kavaa sketi fupi yenye kuifanya mapaja yake yaliyojazia yaonekane vizuri, sketi nyeusi na blauzi nyekundu aliyovaa chini kiatu kirefu cha rangi nyeusi kilimfanya apendeze sana. Umbo lake ndio uliokuwa utata mtupu kwa mtu mkware kama Koplo Uyomo, mzigo ulifungashika chini ya kiuno cha binti huyo nao ulimfanya askari huyu aingiwe na ganzi yenye msisimko baina ya mapaja yake mawili. Huo ndiyo udhaifu wake kwa wanawake haswa, uzalendo ulishamshinda ingawa aliamua kujikaza kisabuni.
"afande narudia kukuomba radhi kwa kilichotokea" Binti huyo alimuomba radhi koplo Uyomo kwa mara ya pili
"aah! usi...jali kuhusu hili ingawa gari yangu imechubuka kidogo" Koplo Uyomo alimeza funda la mate kwa uchu kisha akaongea kwa kubabaika.
"kuhusu hilo usijali nitagharamia" Binti huyo alitoa kadi ya mawasiliano akampatia Koplo Uyomo kisha akamwambia "nitakupa pesa ya matengenezo leo leo we wasiliana na mimi tu".
"hamna shida" Koplo Uyomo alikubali huku moyo akishukuru mungu kwa kuahidiwa kurekebishiwa gari. Aliagana na msichana huyo kisha akaelekea kazini huku akijiapiza lazima amtie mkononi.
**************************************
Jackline Fortunatus ni mmoja wa vijana wa vijana waliopo chini ya mkurugenzi Reginald Kitoza wa usalama wa taifa, binti mwenye umbo matata la kumvuta macho ya mwanaume yoyote aendelee kumtazama. Usiku uliopita alikabidhiwa kazi na Kitoza baada ya wakuu wao kuondoka, alikabidhiwa na funguo ya chumba katika hoteli ya South beach iwe kama chambo kwa ajili ya kumuua Koplo Uyomo. Mpango wote ulisukwa ndani ya chumba hicho cha siri wakiwa pamoja na vijana wa three devils. Binti huyu anatambulika kama mfanyakazi wa benki ya CRDB ingawa ni mpelelezi hatari, asubuhi iliyofuata ni yeye ndiye aliyechubua gari ya Koplo Uyomo kwa makusudi ili amnase katika anga zake. Alifanikiwa kwa asilimia zote na aliwasiliana naye kisha wakapanga wakutane South beach alipofikia, binti huyu alimdanganya Koplo Uyomo kama yupo hotelini hapo kwa ajili ya kazi na atalala hotelini hiyo katika vyumba vya juu. Koplo Uyomo pasipo kutambua kuwa anajipeleka kwenye mdomo wa mamba aliamua kwenda moja kwa moja hotelini hapo baada ya muda wa kazi kuisha akiwa amevaa kiraia, alitajiwa namba ya chumba anachopatikana Jackline kupitia ujumbe mfupi wa maneno. Kwa kutumia gari yake alifanikiwa kufika hotelini hapo kisha akaenda hadi chumba alichoelekezwa, aligonga katika mlango wa chumba hicho kisha akaingia baada ya kufunguliwa mlango na Jackline. Jackline muda huo aliamua kuvaa suruali laini ya rangi ya bluu iliyomkaa sawasawa na blauzi ya rangi ya nyeupe iliyombana kiasi cha kuonsha kifua chake kilichobeba embe sindano mbivu zilisimama barabara, hakika alifanikiwa kuiteka akili ya Koplo Uyomo kutokana muonekano huo.
"keti kwenye kiti tafadhali " Jackline alimwambia.
"asante" alijibu kisha akaketi kwenye kochi.
"unatumia kinywaji gani?" Jackline alimuuliza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"grand malt ya baridi" alijibu na kupelekea Jackline aende kwenye jokofu lilipo mkabala na kochi alilokaa Koplo Uyono, alipofika alifungua jokofu kisha akatoa grand malt halafu akafunga kisha akachukua kifungulio kilichopo juu ya jokofu kivivu. Jackline alikishika kifungulio hiko kivivu hadi kikaanguka na ikamlazimu akiokote, hivyo akainama kihasara na kupelekea fungashio la nyuma lionekane vizuri kwa Koplo Uyomo. Hadi hapo uzalendo ulimshinda Koplo Uyomo na akajikuta akimsogelea Jackline hadi alipoinama, alimshika kiuno kwa namna ya kama anakamua jipu na kupelekea binti huyo ainuke akiwa na msisimko bandia kisha akafanya tukio la kujibinua kiuno na hadi Koplo Uyomo akajikuta akishika kifua kichanga cha binti huyo huku akihema kwa nguvu. Koplo Uyomo akiwa kapagawa baada ya Jackline kuanza kuzungusha kiuno chake taratibu, kupagawa huko kulimuisha baada ya kujikuta akipokea kichwa kizito cha mdomoni kutoka kwa Jackline aliyempiga kwa kutumia kisogo. Teke zito la kutumia kisigino ndio lilifuata likampeleka hadi kwenye kochi alilokaa awali huku akiwa anatoa mguno wa maumivu baada ya kupigwa kifuani.
"afande umeingia pabaya leo" Jackline alimwambia kwa dharau akiwa amesimama mbele yake umbaliwa mita kadhaa.
"wewe ni nani?" Koplo Uyomo aliuliza kwa uwoga kisha akasimama huku akiwa amekaa tayari kupambana na Jackline. Uoga wake ulishadhihirika kwa binti huyo na hata aliporusha ngumi alikutana na mapigo matatu ya karate yalimpeleka hadi kwenye kabati akawa amejigonga mgongo wake katika milango ya kabati hilo, akiwa ameegemea milango ya kabati hilo akiugulia maumivu ya kipigo alichopata. Hapo alipoegemea napo palikuwa hapakaliki kama kule alipokuwa awali kwani alijikuta akisukumwa kwa nguvu na milango ya kabati iliyofunguka ghafla hadi akayumba
"mambo vipi Koplo" ilisikika sauti kutoka nyuma yake ikitoka nyuma yake, alipogeuka kuangalia aliyemsabahi alikutana na ngumi nzito ya paji la uso hadi akaanguka chini. Hakuwa mwingine ila ni Michael wa three devils akiwa amevaa nguo nyeusi za mazoezi akitokea ndani ya kabati.
"nadhani nipige pigo la kukuaga Koplo" Michael aliongea huku akiunyanyua mguu wake ili apige pigo linaloitwa 'yokogel (ni teke ambalo hupigwa kwa kutumia sehemu ya pembeni ya unyayo)' katika shingo ya Koplo Uyomo. Pigo hilo halikufanikiwa baada ya dari la chumba hicho kufunguka ghafla na ukatokea ujio wa kiumbe aliyempiga Michael teke la koo hadi akaingia safari ya kuzimu muda huo, Jackline aliingia katika anga za kiumbe huyu na akajikuta akipewa pigo lililoenda kumbamiza ukutani.
"mama mawowowo tulia hivyohivyo sio picha ya kihindi hii ujifanye wewe Akshey Kumar" Kiumbe huyo ambaye ni binadamu wa kawaida alimwambia Jackline kwa kumuita jina kutokana na ukubwa wa makalio yake, muda huo Jackline alikuwa anajiinua ili apambane tena.
"kumbe unapenda hii ngoma, haya njoo tucheze umfuate mwenzako kuzimu" alimwambia Jackline kwa dharau kisha akasimama kimadharau.
Jackline alijisukuma kwa kuweka mikononi ukutani kisha akafyatuka kama mshale kumfuata mtu aliyempiga baada ya kumtambua mtu huyo, alikuja na mateke mawili ya nguvu ili kumsambaratisha huyo akijua ni mtu wa kawaida tu. Mateke hayo yalikosa malengo yote baada ya mlengwa kuondoka eneo alilokuwepo kisha akaachia pigo moja lililompata Jackline la mgongo, pigo hilo lilisababisha Jackline atoe mguno wa maumivu pasipo kugusa sehemu aliyoumia. Maumivu ya sehemu hiyo ya mgongo yalikuwa makali sana na hata kushika sehemu akawa anatamani, kanuni ya mapigano ya mwalimu wake aliyemfundisha kupigana ndiyo iliyomfanya ashindwe kushika sehemu aliumia.
"ukipigwa sehemu yoyote ya mwili ukaumia na ukawa una maumivu makali, ni vyema kutokuonesha kana umeumia sehemu hiyo ili kuepusha adui yako asijue akakupiga sehemu ileile" maneno ya mwalimu wake yalimjia kichwani mwake na akajikaza kikakamavu halafu akajiweka sawa kupigana tena na mpinzani wake. Jackline alitumia mbinu nyingine ya mapigano ili kumuhadaa mpinzani wake aingie kwenye anga zake, alipiga teke la kuzunguka ambalo mpinzani wake alilikwepa kisha akapiga teke la miguu miwili kwa mpigo ambalo lilimpata mpinzani wake kifuani. Hapo ndipo Jackline alitoa tabasamu lake kisha akamuonesha ishara ya dole gumba kikiwa kimeangalia chini.
"ohoo! Nadhani nilikuwa nacheza kwaito pasipo kutambua kuwa huu ni mziki wa rege na kila mtu anacheza kivyake, sasa ngoja nikuchanganyie mitindo ya rege na sebene maana mama mawowowo unaleta dharau sasa" Yule mtu aliongea kisha akaja na mapigo mfululizo ya karate ambayo hayakutarajiwa na Jackline, mapigo hayo karibia yote yalimpata Jackline na kumfanya aanguke chini kama mzigo. Yule mtu alitoa kitu mfukoni mfano wa bastola chenya sindano nene kisha akamchoma Jackline shingoni, kifaa hicho chenye kifyatulio kama bastola kiliingia shingoni mwake kisha yule akaminya kifyatulio chake na kupelekea Jackline apige kelele kwa maumivu.
"sasa mama Mawowowo sikiliza kwa umakini, nimekuweka kifaa kidogo mithili ya punje ya ngano katika shingo yako. Kifaa hicho ni bomu la kisasa maana nilikwambia usijifanye Akshay Kumar picha za kidosi ukawa husikii, hapa mkononi nina saa hii ambayo ndiyo kiongozi cha hilo bomu. Sasa ukitaka uwe salama naomba uongozane na mimi" Yule mtu aliongea kisha akamgeukia Koplo Uyomo ambaye alikuwa pembeni kama mtazamaji kisha akamwambia "wewe mlafi wa mawowowo nifuafe pia na sihitaji maswali zaidi, pia inabidi uwe makini na kazi yako baada ya ngoma hii kuisha". Hadi muda huo Jackline ujanja ulimuisha na akabaki amegwaya tu na asijue la kufanya, alitambua kwamba leo amepatikana na hana ujanja tena, yule mtu alimgeukia Jackline kisha akampiga kibao cha makalio halafu akamwambia," geuka ulipo usawa wa mlango " kisha akamgeukia Koplo Uyomo halafu akamwambia " na wewe fuata nyuma yake". Wote kwa pamoja walitoka wakiuacha mwili wa Michael ukiwa umebakia humo ndani, walienda hadi kwenye maegesho ya magari ambapo kulikuwa na gari aina ya toyota landcruiser nyeupe yenye mkonga. Yule mtu alimpatia Koplo Uyomo ufunguo wa gari halafu akamshika Jackline kiuno kwa makusudi kisha akazunguka naye hadi milango ya nyuma halafu akamfungulia mlango. Wote waliingia ndani ya gari huku Koplo Uyomo akiwa ndiye dereva wa gari hilo, aliamriwa aondoe gari kwa kufuata maelekezo anayopewa.
**************************************
Mnamo saa sita za usiku Norbert akikuwa ameshawasili Bagamoyo na sasa alikuwa anaelekea kwenye nyumba ya kampuni yao ambayo ipo jirani na ufukwe wa bahari ya Hindi, baada ya dakika kumi alikuwa ameshafika kwenye geti la nyumba moja ya kizamani lenye nakshi za mapambo ya asili. Aliminya kitufe cha kilichomo ndani ya gari na kupelekea geti hilo lifunguke kwa kuzama ardhini, aliingiza gari ndani kisha akabobyeza tena kitufe kilekile na sauti ya kujifunga kwa geti ikasikika. Alizima gari kisha akashuka kuelekea mahali ulipo mlango wa kuingilia ndani ya nyumba wenye mapambo ya kizamani ya ngome za waarabu, hapo aligusa moja ya nakshi zilizopo mlangoni kisha akaiminya ndani nakshi hiyo. Kilikuwa ni kitufe kilichofichwa kwa namna ya kipekee na kimuonekano kilikuwa kama nakshi ya dhahabu iliyopo mlangoni hapo, mlango ujifungua wenyewe baada ya mlio wa kengele ndogo kusikika. Norbert aliingia ndani kwenye ukumbi mpana uliopo ndani ya nyumba hiyo iliyopambwa kiasili zaidi, alienda hadi ulipo katikati ya ukumbi huo kwenye zulia dogo la duara lililopo katikati ya makochi kisha akasimama katikati yake. Alikanyaga katikati ya zulia kwenye kitufe ambacho kimekaa kama pambo katika zulia hilo, mlio wa kengele ulisikika kisha zulia hilo likaanza kudidimia kuingia chini ya ardhi hadi eneo lenye ukumbi mpana wa sebule. Nobert alitembea katika ukumbi huo hadi katika chumba kilichopo pembeni ya ukumbi huo, mlango mwa chumba hicho kulikuwa na sehemu ya kuweka kiganja cha mkono ili kufungua mlango wa chumba hicho. Norbert aliweka kiganja chake hapo na kupelekea isikike sauti ikisema "karibu N001" kisha mlango ukafunguka. Aliingia ndani ya chumba hicho ambacho ni mahususi kwa ajili ya kulala kutokana na uwepo wa kitanda cha kisasa kilicholaliwa na binti mmoja mrembo aliyelala kifudifudi huku sehemu kubwa ya mapaja yake ikiwa wazi kutokana na gaunj fupi la kulalia alilovaa. Kitendo cha kumuona binti huyo Norbert alitabasamu kisha akasogea hadi kitandani, akili yake ilimpa wazo la kumgusa binti huyo mwenye mapaja yenye ngozi nyororo. Alipeleka ili amguse na akajikuta amevutwa mkono na binti huyo kwa ghafla akawa anakifuata kisu kikali kilicholengwa tumboni mwake, tendo hilo alishaliona kwa haraka na ikambidi apige sarakasi kwa haraka sana hadi kwenye kitanda pembeni ya binti huyo aliyefunikwa uso na nywele za wigi alilolivaa.
"bibie tulia basi" Norbert alimwambia binti huyo ambaye aliweka nywele za bandia za hilo wigi na kuifanya sura yake ionekane vizuri, hakuwa mwingine bali ni Hilda.
"chunga sana" Hilda alimwambia Norbert ambaye alikuwa amemshika kiuno kwa muda huo akiwa amelala pembeni yake. Norbert alimsogeza karibu binti huyu kisha akabadilishana naye shurubati iliyopo ndani ya kinywa chake kwa sekunde kadhaa kisha akamwachia.
"vua viatu kwanza" Hilda alimwambia Norbert kwa sauti iliyotoka puani, Norbert alivua viatu kisha akavua nguo akawa amebakiwa na bukta kisha akapanda kitandani.
"nimevua na za nyongeza kabisaa" alimwambia Hilda kisha akamvuta na kukumbatiana naye, alivuta shuka lote na kujifunika mwili mzima kisha yeye na Hilda kisha akaanza vituko vyake asivyoviacha kwa binti yoyote aliyevutika naye.
***************************************
Taarifa za kukutwa kwa mtu aliyefariki katika hoteli ya South beach ndio habari iliyoenea jijini Dar es salaam mapambazuko yalipochukua nafasi, waandishi wa habari tayari walishafurika hotelini hapo kutokana umaarufu wa hoteli hiyo. Hadi inatimu saa nne ya asubuhi tayari hoteli hiyo ilikuwa imewekewa utepe mwekundu katika eneo lililokaribu na ulipokutwa mwili huo, uchunguzi juu ya tukio hilo ulichukua nafasi kwa kuanza na kamera za ulinzi za hoteli hiyo. Askari wenye mavazi ya kiofisi na wasio na mavazi ya kiofisi waliingia ndani ya chumba uongozi wa kamera ya ulinzi kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumnasa mhusika kwa kupitia kamera za ulinzi zilizopo kwenye korido ya vyumba katika hoteli hiyo, chumba hicho kilikutwa kitupu tofauti na kuliko kawaida huku vioo vidogo vilivyo na umbo la televisheni vikiwa vinaonesha mandhari ya sehemu mbalimbali katika hoteli hiyo. Hali hii iliwashangwza sana askari hao na ikawabidi waende kwa meneja wa hoteli kumpa taarifa ya kutokuwepo mtu katika chumba cha uongozi wa camers ndani ya hoteli hiyo, taarifa hiyo ilipokekewa kwa mshangao na meneja huyo pia na ikambidi aongozane nao hadi katika chumba hicho.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"inamaana hawa vijana wamekwenda wapi maana muda wao wa kumaliza zamu ni bado kwani wanamaliza saa tano" Meneja wa hoteli hiyo akiongea kisha akafungua milango iliyomo ndani ya chumba hicho ili kukagua. Muundo wa chumba hicho cha kuongozea kamera ulikuwa umejengwa kwa kuwekwa vyumba vitatu, kimoja kilichokaa kama ukumbi ndipo palikuwa na mitambo yote ya kuongozea kamera hizo , kingine kilikuwa kinatumika kuwekwa nguo za wasimamizi wa chumba hicho wakiwa wanaondoka na cha mwisho kilikuwa kunatumika kutunzia mikanda mbalimbali iliyotumika kurekodi matukio ndani ya hoteli hiyo. Meneja wa hoteli hiyo alikagua chumba cha kuhifadhi mikanda na hakukuta mtu, akipoenda chumba cha kuhifadhia nguo alikikuta kikiwa kitupu na kabati la kuhidhia nguo likiwa limefungwa kuashiria wenye zamu wameondoka. Meneja aliridhika kuwa hakukuwa na mtu ndani ya chumba na akageuka ili aondoke, alipiga hatua tatu kisha akarudi hadi kwenye kabati hilo baada ya kusikia miguno ya mtu kwa mbali. Alijaribu kukifungua kabati baada ya kulifikia lakini halikufunguka.
"naombeni funguo zilizopo jirani na mlango wa kutokea" aliwaambia maaskari ambao walikuwa nyuma yake na kupelekea maaskari hao watazamane kisha mmoja wao akakimbia kwa haraka hadi alipoagizwa, alirejea na funguo kisha akampatia meneja wa hoteli hiyo. Kitendo kilichofuata ilikuwa ni kutumbukiza funguo katika tundu ka ufunguo kisha kuunyonga kuelekea kushoto ili kufungua mlango huo, meneja huyu alifanya kitendo hicho kisha akaufungua mlango wa kabati hilo. Watu wawili waliofungwa mikono na miguu kwa kamba ngumu na mdomoni wakiwa wamebandikwa gundi ndio walionekana.
"wenye zamu ni hawa na sijui kimewapata nini?" Meneja aliongea kwa sauti yenye kuashiria kuchanganyikiwa kisha akawaangalia maaskari waliopo humo ndani.
"wengine watoeni hao na mliobaki mkaangalie ushahidi katika kamera za ulinzi" kiongozi wa maaskari hao aliongea huku maaskari wakitii na kufuata maelekezo waliyopewa, askari huyu aliyevaa kiraia alimgeukia Meneja wa hoteli hiyo kisha akamwambia, "usijali wacha tifanya kazi yetu kisha tutaenda kuwahoji hawa".
"sawa afande nimekuelewa ila hii ni balaa katika hoteli yangu na nina wasiwasi wa kupungua kwa wateja kutokana na tukio hili na itakuwa hasara kwetu" Meneja wa hoteli hiyo aliongea kiunyonge.
"hamna kitu kama hicho meneja, cha msingi ni kuchukulia kama changamoto tu" Askari huyo alimfariji Meneja wa hoteli hiyo kisha akwambia, "hebu twende chumba cha kutunzia mikanda iliyorekodiwa nikaangalie kitachoweza kutufaa katika uchunguzi wetu". Waliondoka kwa pamoja hadi katika chumva hicho chenye mikanda mingi ya kamera za ulinzi iliyopangwa kwa tarehe iliyorekodiwa.
"mikanda ya siku ya jana ipo wapi?" Askari alimuuliza meneja
"nadhani ndiyo hiyo inayorekodiwa katika mashine, maana humu bado haijawekwa" Meneja alijibu hivyo kutojana na ukosefu wa mikanda hiyo humo ndani. Wakiwa wamesimama hivyo askari mmoja mwenye nguo za kazi aliingia na kupelekea kiongozi wake aliyesimama na meneja amuulize "kuna tatizo?"
"ndiyo afande tatizo lipo, katika mashine zile hakuna hata mkanda mmoja wa kurekodi tukio na vioo vile vinaonesha tu picha kutoka kwenye kamera lakini hakuna kinachorekodiwa" Askari mwenyr nguo za kazi alijieleza.
"nini?!" Kiongozi wake alihamaki na meneja akajihisi kuchoka kwa taarifa hiyo.
"Shit! Tumechezewa akili hapa" Kiongozi wa maaskari alisema huku akikuna kichwa chake kulitafakari tukio hilo.
"unasemaje wewe?!" Meneja wa hoteli aliuliza jambo alilolisikia kutokana na kuchanganyikiwa na taarifa hiyo.
"ndugu Meneja jua hapa tunacheza na mtu mwenye uwezo usio wa kawaida" Kiongozi wa maaskari alimueleza.
"unamaanisha nini?" Meneja aliuliza.
"huyu muuaji anajua anachokifanya ndio maana anapoteza kila alama ambayo inaweza kumkamatisha" Kiongozi wa maaskari aliongea kisha akameza funda moja la mate halafu akamwambia Meneja "nadhani msaada kwetu sasa hivi umebaki kwa hawa walinzi wako waliofungwa ndani ya kabati, wao ndio tutakaowahoji ili tuweze kupata mwanga katika kuanza upelelezi wa suala hili".
"Kulinda uhuru wa wateja katika hoteli nao umesababisha tukose ushahidi muhimu katika kesi hii, hatuna jinsi zaidi ya kutegemea mahojiano yatakayoendeshwa kwa hawa wasimamizi wa hichi chumba" aliendelea kuongea kiongozi wa maaskari.
Mtuhumiwa waliyekuwa wanamtafuta alikuwa amefuta kila alama itakayomuonesha uwepo wake katika eneo la tukio. Maaskari hao walikuwa wamegwaya wote na wakaona uwezekano wa kumkosa mtuhumiwa ndio unafuata, hawakuwa na uhakika wa kupata mwanga wa kuanzia kutokana na tukio lenyewe lilivyo. Hakika ilikuwa ni utata mtupu kwa maaskari hao na walijaribu kutumia kila aina ya uwezo lakini ikashindikana, kiongozi wa maaskari alijifikiria na mwisho akaamua atumie njia mbadala ambayo ni ndefu ingawa inatoa jibu zuri na lenye kuridhisha.
"hebu twende mapokezi mara moja" Kiongozi wa maaskari alimwambia Meneja huku akipiga hatua kuelekea nje ya chumba cha kuongozea kamera za ulinzi akifuatiwa na Meneja. Walienda hadi mapokezi ambapo walimkuta msichana aliyevaa sare za wafanyakazi wa hoteli hiyo, msichana huyo aliwasabahi wote kisha akawa anawatazama kwa namna ya kusikiliza jambo atakaloambiwa.
"chumba kilichofanyiwa mauaji kimechukuliwa siku gani na ni nani aliyekichukua?" Kiongozi wa wale maaskari alimuuliza.
"ngoja niangalie kitabu cha rekodi" Binti huyo alisema huku akiinama chini ya meza yake kisha akatoa kitabu kikubwa halafu akafungua baadhi ya kurasa.
"ni miezi miwili iliyopita chumba hicho kililipiwa na mfanyabiashara anayeitwa Haruna Ngoleba kutoka Shinyanga" Binti wa mapokezi alijibu.
"je huwa anakuja kulala hapa kila siku kabla ya tukio kutokea" Kiongozi wa maaskari aliuliza.
"hapana, huwa anakuja mara chache sana" Binti wa mapokezi alijibu.
"kwa mujibu wa maelezo yake aliwaambiaje kuhusu hicho chumba?" Kiongozi wa maaskari alimuuliza tena tena .
"amesema yeye ni mfanyabiashara na huwa anakuja jijini Dar es salaam kibiashara, hicho chumba kasema atakilipia hata siku ambayo hatakuwepo". Binti wa mapokezi alijibu.
"unaweza kunionesha tarehe yake aliyokuja kwa mara ya kwanza kuchukua hicho chumba?" Kiongozi wa wa maaskari alimuuliza.
"ndiyo naweza, tarehe ni hii hapa" Binti huyo alijibu huku akimuonesha kwa kidole tarehe iliyohitajika, kiongozi wa maaskari alitoa kitabu kidogo mfukoni mwake kisha akanakili tarehe hiyo.
"ok, jana kabla ya tukio alifika?" Kiongozi wa maaskari alimuuliza.
"taarifa hizo sina kwani ndio naingia zamu sasa labda mkamuulize Stella aliyekuwepo jana usiku" Binti huyo aliwaambia.
Wakati Kiongozi wa maaskari akijianda kumuuliza swali jingine alikatishwa na sauti ya Meneja iliyokuwa ikisema, "Stella njoo haraka sana". Alipogeuka alimuona binti wa miaka takribani ishirini na mbili akiwa na mavazi ya kawaida na mkononi kashika pochi ya kike yenye rangi ya hadhurungi.
"abee Bosi" Stella aliitikia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"unatoka sasa hivi" Meneja alimuuliza.
"ndiyo bosi" Stella alijibu.
"ok..tunakuomba mara moja, nafikiri ofisa hapa atakuwa na shida na wewe" Meneja alimuambia Stella huku akimgisa begani Kiongozi wa maaskari.
"hutachelewa binti ni dakika zisizopungua kumi" Kiongozi wa maaskari alimuambia Stella.
"hamna shida" Stella alijibu.
Kiongozi wa maaskari alimgeukia Binti wa mapokezi kisha akamuambia, "asante sana kwa ushirikiano wako dada...".
"Mirian" Binti wa mapokezi aliongea.
"ok jina zuri sana, nikihitaji msaada zaidi nitakutafuta" Kiongozi wa maaskari alimuambia binti wa mapokezi ambaye aliishia kutabasamu tu kisha akawaashiria Meneja na Stella wamfuate. Kiongozi huyu wa maaskari katika uchunguzi ndani ya hoteli hiyo aliwaongoza Stella na Meneja hadi kwenye ofisi ya meneja.
"nadhani hili ndio eneo zuri la kumuuliza baadhi ya maswali" Kiongozi wa maaskari alisema huku akikaa kwenye makochi ya kisasa yaliyopo humo ofisini , Meneja na Stella nao wakakaa wakiwa mkabala nae kutokana na mbinu za kiaskari ambazo kiongozi wa maaskari alizoamua kuzitumia. Hakutaka Meneja na Stella wakae mkabala wakitazamana kwa kuhofia kupotezwa kwa ushahidi kama Meneja akiwa ni mhusika wa hili tukio, hakuwa na uhakika na mawazo yake lakini hakutaka kumuamini Meneja kwa asilimia mia. Ndio maana alimuweka pembeni ya Stella kwa umbali ambao asingeweza kutoa ishara yoyote kwa binti huyo ikiwa anahusika na tukio.
"Stella najua una habari zote za tukio lililotokea" Kiongozi wa maaskari alimuuliza Stella.
"ndiyo ninayo habari ya tukio lilitokea" Stella alijibu.
"unaweza kunieleza ni nani alikuja kuchukua funguo ya chumba namba 109 jana?" Kiongozi wa maaskari alimuuliza.
"ni binti mmoja ambaye nilipewa maelekezo na mwenye chumba nimpatie funguo" Stella alijibu.
"je alikuja na mtu mwingine yoyote"
"kwa muda huo aliowasili hakuja na mtu mwingine yoyote, ila baadaye aliingia mtu mwingine kabisa akaulizia namba ya chumbo hicho hicho".
"alivyokuuliza wewe ulichukua hatua gani?"
"nilipiga simu chumbani kisha nikamueleza huyo binti juu ya kuuliziwa chumba hicho"
"alikuambiaje baada ya kumpa taarifa hiyo"
"aliniuliza jina la huyo anayemuulizia"
"ulimjibu vipi?"
"nimuambia ni Uyo....mo kitu kama hicho"
"ok...ni hayo tu sina la ziada, nikikuhitaji tena nitakutafuta. Unaweza ukaenda" Kiongozi wa maaskari alimuambia kisha akampa mkono wa shukrani kwa kutoa ushirikiano,Stella aliinuka kwenye kisha akaondoka baada ya kusikia ruhusa ya kuondoka ikitoka.
"Meneja nadhani twende chumba cha kuongozea kamera" alimgeukia Meneja kisha akamuambia baada ya Stella kuondoka. Wote kwa pamoja walirudi chumba cha kuongozea kamera walipowaacha maaskari walio chini yake kicheo.
**************************************
MAKAO MAKUU USALAMA WA TAIFA
DAR ES SALAAM
Taarifa ya kifo cha Michael ilikuwa imeshafika ndani ya ofisi za Usalama wa taifa, kupotea kwa Jackline na asusa yao waliyokuwa wanataka waikate kauli nayo ilikuwa ni taarifa iliyopo ofisini hapo toka vyombo vya habari vinatangaza taarifa hiyo. Ilikuwa ni taarifa iliyowachanganya sana vijana waliosalia wa kundi la Three devils, kumpoteza mwenzao waliyeshirikiana naye katika mambo mbalimbali ilikuwa ni pigo jingine. Vijana hawa ambao waliishi kama ndugu waliichukulia ni kama kumpoteza kaka yao wa damu waliyempenda, hasira juu ya tukio hilo zilizidi na kisasi kilichukua nafasi katika mioyo yao. Kikao cha dharura kiliitishwa ndani ya chumba cha ofisi ya siri na safari hii Moses Gawaza alihusishwa katika kikao hicho, Kitoza ndiye aliyechukua uongozi wa kikao hicho akiwa kama mkuu wa usalama wa taifa. Wahudhuriaji wake walikuwa ni Morris,Jim na Moses, wakubwa zao hawakuwepo hivyo waliamua kuitisha kikao ili uamuzi wa haraka utolewe juu ya kikao hicho.
"jamani najua mna fahamu juu ya tukio lililotokea pale South beach kwenye chumba nilichokichukua kwa ajili ya kazi zangu, na kama kuna baadhi yenu hajui inabidi sasa niwaelezee. Usiku wa kuamkia leo tulipanga kumnasa gaidi wa kimataifa aliyeingia katika anga za Jackline lakini tulimkosa na matokeo yake tukampoteza kachero wa FBI aliyeingia hapa Tanzania kumsaka gaidi huyo na utekwaji wa Jackline na Koplo Uyomo aliyehusika katika mpango huo" Kitoza aliongea huku akitumia uongo mwingi katika baadhi ya maelezo yake kutokana na uwepo wa Moses ofisini hapo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Moses napenda utambue kuwa wewe upo kwa kulinda na kutetea taifa hili na tumeamua tukuhusishe katika mpango huu kutokana na uaminifu na ushujaa wako katika mambo mbalimbali uliyofanya. Sasa hapa ukae ukijua kuwa gaidi aitwae Norbert Kaila ndiye aliyetenda unyama huu kwa maofisa waliotumwa kumkamata na pia ndiye anayewashikilia Koplo Uyomo na Jackline kwa sasa" Kitoza alizidi kumuongopea Moses ili waweze kumhusisha katika michezo yao haramu pasipo yeye kujua.
"sasa basi nakupa kazi ya kumtafuta huyu mtu pia wanausalama waliopo mikononi mwake wapatikane, Jim na Morris kutoka shirika la FBI wapo pamoja nawe katika jambo hili na wanahitaji ushirikiano" Kitoza alizidi kumuongepea Moses tena safari hii akitumia utambulisho wa uongo kwa Jim na Morris. Kumuhusisha Mosea katika mpango huo ni muhimu kutokana na kazi yake nzuri aliyoifanya ya kuzuia uachiwaji wa virusi hatari vilivyotengenezwa na baba yake, kisa hicho kilichompatia jina la SHUJAA ndiyo kisa kilichomfanya Kitoza ampatie kazi hiyo kutokana na ujasiri wa asili pamoja akili za kufikiri alizonazo. Kitoza mwenyewe alipata kusikia habari zake kipindi akiwa mwanausalama wa kawaida, sasa akiwa mkurugenzi anampatia kazi mwanausalama anayejua uovu wake wote.
"nadhani tumeelewana sasa kazi hii nawapa siku kumi tu nataka huyu Kaila awe mikononi mwenu, sina la ziada kazi ianze mara moja" Kitoza alihitimisha maelezo yake kisha akatoka nje ya chumba hicho akiwaacha watu aliowapa kazi wakijadili mambo yanayohusu kazi yao.
************************************
Ndani ya chumba chenye giza totoro na kisicho na madirisha zaidi ya mabomba ya hewa yaliyomo humo, muonekano wa chumba hicho ulijidhihirisha wazi kama kipo chini ya ardhi katika eneo lisilojulikana. Kulikuwa na mateka watatu ndani ya chumba hicho, miongoni mwa mateka wawili waliopo humo hawakuwa wanajua walipo huku mmoja akiwa anajua eneo walilopo. Jackline na Tasu aliyenaswa na mpelelezi AL005 katika ofisi za WAHANGA ndiyo mateka wasiotambua eneo walilopo, na Koplo Uyomo ndiyo teka anayetambua eneo walilokuwepo kutokana na kuwa dereva wa gari wakati wanakuja eneo hilo. Jackline na Tasu walikuwa wamefungwa mikono kwa kamba ngumu iliyofungwa katika chuma zito lililopo juu ya chumba hicho na chini walikuwa wamefungwa kwa minyororo iliyounganishwa na vyuma vilivyosakafiwa ardhini, Koplo Uyomo alifungwa kwenye kiti kizito cha chuma kwa kamba ngumu. Giza liliopo humo ndani lilisababisha wasitambuane zaidi ya kila mmoja kusikia miguno ya mwenzake. Mlango wa chumba hicho ulifunguliwa kisha taa zikawaka na kufanya mateka waliopo humo ndani watambuane, aliingia mtu tofauti na aliyewakamata Jackline na Koplo Uyomo siku iliyopita. Mtu huyo aliyefungua mlango alienda kumfungulia Koplo Uuomo halafu akamwambia, "nifuate". Alitoka ndani ya chumba hicho akiwa ameongozana na Koplo Uyomo kisha akaufunga mlango, korido ndefu yenye mataa zenye mwanga mkali ndio waliyokutana nayo. Yule mtu alimpeleka Koplo Uyomo hadi mwisho wa korido ile kwenye ngazi zinazoelekea iuu, kisha akapanda huku akiwa pamoja nae. Walitokea kwenye Korido nyingine yenye vyumba vingi. Muda huo Koplo Uyomo alikuwa kimya akijua hayupo salama na hakutakiwa kutia neno lolote kwa ajili ya usalama wake, alifuata kila anachoambiwa kwa muda huo kutokana na kutokuwepo uwezekano wa kutoroka. Yule mtu alimpeleka katika mlango wa mwisho wa korido kisha akamfungulia mlango halafu akamwambia, "ingia ndani". Koplo Uyomo aliingia ndani akimuacha yule mtu pale mlangoni.
"Koplo Chauchu karibu sana" ilisikika sauti ikimkaribisha Koplo Uyomo na alipotazama mbele vizuri aliwaona watu ambao hakutarajia kuwaona pale.
"hapana sio nyinyi, haiwezekani" aliishia kusema huku akuwa anatetemeka.
Koplo Uyomo alidhani macho yake yameona vibaya kwa aliowaona mbele yake, alifikicha macho yake akijua ataona tofauti lakini aliona vilevile. Davis na Joseph waliosadikika walikufa kwa mlipuko wa bomu ndio waliokuwa wapo mbele yake, Allison ambaye hakuonekana katika msako wao kule Temeke naye alikuwa pembeni yao na ndiye aliyemkaribisha. Juu ya ukuta ndani ya chumba hicho kulikuwa kuna nembo ya shirika la upelelezi la Afrika ya mashariki (EASA).
"unashangaa kwa kipi? Hawa kuwa hai sio" Allison alimuuliza Koplo Uyomo akiwa hana hata chembe ya mzaha usoni, Koplo Uyomo alibaki kimya pasipo kujibu swali aliloulizwa.
"hivi kati yetu sisi watatu hapa, kuna mtanzania yeyote?" Allison
alimuongeza swali lingine huku akiwa amekunja sura, Koplo Uyomo aliishia kutikisa kichwa kuashiria kukataa.
"kama hamna Mtanzania naomba uniambie ni kwanini sisi wageni ndio tushughulike na kuikomboa nchi yenu halafu nyinyi wazawa tena wanausalama wa jeshi la polisi mpo kimya? Mshafanya uchunguzi wa sakata lolote au mnaishia kukamata watu wasio na hatia" Allison alizidi kumsema .
"sijakuekewa?" Koplo Uyomo alisema.
"utanielewa tu" Allison alisema kisha akabonyeza kitufe ukutani na kupelekea nembo ya EASA iliyopo ukutani igawanyike mara ya mbili baada ya sehemu hiyo ya ukuta kufunguka, kioo bapa kikubwa cha tarakilishi kisicho na kisogo ndio kilionekana. Alibonyeza kitufe kilichopo katika kioo hiko na kupelekea matukio ya picha mithili ya filamu yaonekane katika kioo hicho, mkutano wa siri wa siri wa chama tawala na mipango mbalimbali ya siri ya watu walioheshimika ndio iliyoonekana.
"sasa nikikuambia wewe ni mmojawapo kati ya wanaofuga simba ambaye alikaribia kukung'ata wewe mwenyewe utakataa?" Allison alizidi kumsema.
"nini?" Koplo Uyomo alionesha ishara ya kutokuelewa kwa Allison.
"hujaelewa sio, hebu angalia picha hizo hapo na uniambie umeelewa nini, pia ni kwanini nyinyi wanausalama mpo kimya hata kwa shetani anayewapa amri" Allison alimwambia. Picha iliyofuata katika kioo hicho ndio ilimfanya Koplo Uyomo abaki ameduwaa, alishuhudia mpango mzima ulioandaliwa kwa ajili ya kumuua uliorekodiwa. Kitoza ,rais, mfanyabiashara maarufu na vijana wa Three devils ndio waliohusika na mchezo huo wa kutaka kumuondoa duniani.
"je unaweza kuniambia ni nani unayemfahamu kati ya hao watu? ukitoa Kitoza firauni Liwale na firaun Ole" Allison alimuuliza.
"wote ninawafahamu, kuna Jim ambaye ni muwekezaji mkubwa Tanzania, Hao wawili siwafahamu majina ila mmoja nilimwona kituo cha polisi cha kati akiweka kitu chini ya gari katika gari lililolipuka na mwingine ulimuua jana kule hotelini" Koplo Uyomo alijibu.
"kwa mujibu wa hayo matukio, unaweza kuniambia ni nani mhalifu kati yetu na hao" Allison alimuuliza.
"kwanza wewe ni nani hasa?" Koplo Uyomo aliuliza swali bila kujibu swali aliloulizwa
"naitwa Allison Frank au AL005 kutoka EASA kitengo cha huduma za siri" Allison alijitambulisha kisha akawageukia Joseph na Davis halafu akawaambia, "nadhani mlitaka mnijue kiundani nadhani mmenijua sasa".
"Koplo na wewe inabidi ubaki hapa kama unajipenda uwe hai, hii ngoma ni nzito hutaiweza. Kwanj inabidi niongezewe wenzangu wanaotambulika kama N001 na HI002 ambao wamesimamishwa kazi kwa muda, nchi yenu imeuzwa tayari inabidi tuirudishe mikononi mwenu" Allison alimwambia Koplo Uyomo. Maneno ya Allison yalimfanya Koplo Uyomo aondokwe na hofu yote iliyopo moyoni mwake juu ya waandishi wa WAHANGA na akawa na matumaini mapya ya kuwa kwenye mikono salama ya kachero wa siri wa EASA na ukombozi wa Tanzania kutoka mikononi mwa watu wenye nguvu ya kila namna, ulianza kuonekana kwa mujibu wa mtazamo wake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***************************************
Operesheni ya vijana wa kazi ilianza rasmi nchini na msako wa dhidi ya Norbert ukawa umeshika hatamu, Moses,Jim na Morris walikuwa tayari wameingia kazini kwa kupekua kila maeneo ambayo yalihisiwa kuwepo kwake kwa siku nzima. Hawakuweza kupata alama yoyote ya uwepo wake hadi kiza kinaingia, Jim na Morris hawakuweza kutambua kama wanajihusisha na adui yao na ajuaye eneo alilopo Norbert. Majira ya saa mbili usiku wakiwa wapo ndani ya nyumba ya Moses maeneo ya Tegeta ndipo walipoweza kutambua eneo alilopo Norbert kupitia tarakilishi ya Moses, kitendo cha wao kujua eneo tayari ilikuwa ni ushindi kwao. Ndani ya muda huohuo Jim na Morris walihitaji kutekeleza kazi ya kulipa kisasi kwa Norbert, walipanda pikipiki tatu walizozitumia kufanya msako kuelekea Bagamoyo eneo walilolinasa kwa tarakilishi. Baada ya saa moja walikuwa wapo nje ya nyumba yenye ya kizamani yenye uzio mrefu, kifaa alichokuwa nacho Moses kilitetemeka kuashiria ndio eneo walilokuwa wanalisaka. Mpango waliokuwa nao ni kuvamia ndani ya nyumba hiyo kwa kuruka ukuta kisha wamvamie Norbert na ili wamtie nguvuni kwa pamoja.
"nyinyi anzeni mimi naangalia usalama maana nyumba hii aliyopo mtuhumiwa huenda inalindwa" Moses aliwaambia huku akiangalia kila upande, Jim na Morris walikubaliana na wazo la Moses kisha wakaruka ukuta kwa haraka. Walitua ndani ya nyumba hiyo yenye muonekano wa kizamani wakiwa wamejeruhiwa wote, mapigo ya judo yaliyowapata kwenye mbavu yaliwafanya wasiweze hata kusimama na wakaishia kuegemea ukuta walioruka. Walipoangalia mbele yao waliwaona Norbert na Hilda wakiwa wamesimama wakiwa wamevaa mavazi ya kulalia.
"karibuni wageni wetu, tulipata taarifa ya ujio wenu na ikatubidi tuandae mapokezi ya kiukarimu kwenu kama tulivyowapatia" Norbert aliongea kwa dharau.
"nadhani mgeni mmoja bado hajaja Nor hebu muite akaribishwe nae" Hilda aliongea huku uso wake ukiwa na tabasamu mwanana. Norbert alipiga mbinja moja yenye sauti ya wastani na kishindo cha mtu kikasikika jirani na eneo walilopo, Moses ndiye aliyetua jirani na wakina Norbert baada ya kuruka ukuta. Kilichofuata hapo ilibaki kuwa mshangao kwa Jim na Morris baada ya kushuhudia Moses aligongesha ngumi na Norbert kwa ishara ya salamu ya vijana.
"you son of bitch! You traped us( wewe mtoto wa mbwa umetulengesha)" Jim aliongea kwa hasira
"Ha! Ha! Ha! Ha! Unapojenga urafiki na adui wako unategemea nini, Jim ndio mwisho wako leo" Moses alimwambia Jim kisha akamgeukia Norbert halafu akamwambia, "maliza mchezo wote".
"and you bitch count your fucking death when I succeeded to get out of here(na wewe Kahaba hesabu kifo chako ikiwa nitafanikiwa kutoka hapa)" Jim alimwambia Hilda huku akiugulia maumivu ya pigo lilimvunja baadhi ya mbavu.
"He! He! Heee! We mmarekani uliokuwa unajifanya unajua kiswahili kwa sana utanifanya nini? Mose hebu mshikeni huyo shoga mwenzake halafu tuone atanifanya nini" Hilda aliongea kwa dharau na akawatusi wote kwa pamoja ili ampandishe hasira Jim, Moses alimkamata Morris kisha akamuacha Jim.
"haya bwana shoga bibie huyo hapo kama vipi dhibitisha kama sio shoga" Moses alimwambia Jim huku akicheka, maneno hayo yalimsababisha Jim awe na hasira na hata maumivu ya kuvunjika mbavu chache aliyasahau na akasimama tayari kumkabili Hilda ambaye alionekana ni mwanamke wa kujipodoa tu. Hilda alikuwa amejitenga peke yake na akiwa amesimama kivivu kama asiyejua chochote katika mapigano huku akimuonesha Jim kidole cha kati na kupelekea Jim aje kqa hasira kama mbogo huku akiachia mapigo mfululizo, mapigo hayo yaliishambulia hewa na mlengwa alikuwa ameshatoka eneo hilo.
"we Shoga mbona unapiga hewa tu nipige basi" Hilda alimwambia Jim.
Kauli hiyo ya Hilda ilimfanya Jim amfuate kwa mapigo mfululizo smbayo yote yalipiga hewa baada ya Hilda kuyakwepa.
"Shogaaa yaani umelegea hadi huwezi kupigana, ama kweli ushoga mbaya" Hilda aliendelea kuongea maneno ya kumpandisha hasira Jim huku Norbert na Moses wakicheka sana.
Jim alizidi kupandwa na hasira na akajikuta anapiga mapigo ovyovyo pasipo kuangalia, mapigo yote yaliishia hewani na akajikuta anatoa ukelele wa maumivu baada ya Hilda kupiga sehemu ya mbavu iliyovunjika. Akiwa anasikilizia maumivu aliongezwa teke la kifua na akajikuta ameenda kusalimiana na ardhi, Hilda alipoona mpinzani wake ameishiwa aliuliza, "nyumba yenyewe inashoti tupu, je nikate umeme kuondoa hitilafu zaidi?"
"kata" Moses alijibu swali la Hilda, Hilda alimkanyaga Jim shingoni hadi akaiaga dunia papo hapo.
"kata umeme na nyumba hii kuzuia hitilafu zaidi" Moses alimwambia Hilda huku akimsukuma Morris upande aliopo Hilda na kupelekea apokee judo ya koromeo hadi akaiacha ardhi ya viumbe hai na akaingia katika ardhi ya viumbe wasio hai. Wote kwa pamoja walipongezana kugongesha ngumi zao na wakawa wanafuraha kwa kuwaondoa viumbe wasiohitajika.
"GRIII! GRIIII GRIII! GRIII!" sauti ya simu ya mkononi ilisikika katika miili ya vijana wa Three devils na kupelekea wote watizamane kisha Norbert akaenda kuipekua maiti ya Jim, aliitoa simu ya mkononi kisha akaitazama jina la mpigaji kwenye kioo cha simu hiyo. 'DON EAGLE' ndiyo jina aliloliona kisha akapokea simu hiyo halafu akaongea, "ukisikia sauti hii jua umesikia taarifa ya vifo vya mbwa wako waliotaka kumuangamiza Kaila, nadhani hadi sasa ushatambua Kaila ni mtu wa namna gani. Mchezo umeanza". Alipomaliza alikata simu kisha akatoa kadi ya simu halafu akavunja, aliitaka kurusha simu yenyewe lakini Moses akamzuia huku aiimuambia "haina haja maana itajulikana ipo hapa eneo la Bagamoyo, we ingiza hizo pikipiki tulizokuja nazo humu ndani ya lori la kampuni kisha unipe hiyo simu nikaitupe baharini". Norbert alitii kama alivyoambiwa na ndani ya dakika kadhaa akawa ameishaziweka pikipiki ndani ya lori pamoja na maiti zote.
*******************************
JIJINI MIAMI
NCHINI MAREKANI
Eagle alitaka kujua jinsi kazi inavyoenda kwa vijana wake aliowatuma nchini Tanzania, mchana wa siku hiyo alimpigia simu Jim na majibu aliyoyapata yalimhuzunisha baada ya kusikia taarifa ya kifo cha Michael. Pia alifurahishwa na hatua ya kumuingiza Moses katika mchezo huo ili aweze kuwasaidia pasipo yeye kujijua, usiku alipompigia simu Jim aliambiwa wanaenda kumaliza mchezo na wapo njiani hivyo apige baadaye. Baada ya saa moja kupita alikuwa amezungukwa na wanawake waliovaa nusu utupu katika kitandani chake cha thamani kilichopo chumbani mwake, aliamua kupiga simu na sauti ya Norbert ndiyo ilisikika katika simu ya Jim. Taarifa aliyopewa ilimfanya awasukume wasichana waliokuwa wakimkanda kisha akaelekea akatoka chumbanj kwake, alienda hadi ukumbini kisha akapiga simu akiwa amechanganyikiwa.
"Ole mbona sielewi kinachoendelea huko?! Hivi huyu Kaila ni nani hasa mpaka animalizie vijana wangu?.........huelewi nini inamaana hujui kama Jim na Morris ni maiti sasa.......sasa kazi iliyobaki nakuja kuimaliza mwenyewe" Eagle aliongea kwa hasira baada ya simu kupokewa na mtu aliyekuwa anampigia, alikata simu alipomaliza kuongea kisha akapaza sauti ,"boys!!". Vijana waliovalia suti za kisasa wapatao sita waliingia kwa haraka.
"nahitaji maandalizi ya safari ya kwenda kuivaa vita, vifaa vyangu vyote navihitaji upesi" Eagle aliwaambia kwa jazba.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Vijana wa Eagle walifanya kama walivyoagizwa na ndani ya dakika kumi tu walikuwa wamekamilisha kila walichoagizwa, mkoba mdogo wa kufungwa kwa namba tayari ulikuwa upo mbele ya Eagle ukiwa na zana zote alizozihitaji kwa ajili ya kazi anayoenda kuifanya. Ndani ya dakika kumi tu tayari Eagle alikuwa yupo ndani ya mavazi yenye kumpendeza, shati la rangi ya kijani lenye kuonyesha umbile lake la kimazoezi na suruali nyeupe na kiatu navyo vilizidi kumpa haki yake ya kupendeza. Mikufu ya almasi iliyoning'inia shingoni nayo ilionesha uwezo wa fedha alionao.
"nitatumia Jaguar kuendea uwanja wa ndege pia hakikisheni ndege yangu imetayarishwa kwa ajili ya safari, sihitaji uwepo wa askari yoyote atakayekuwa na kiburi cha kupekua mizigo yangu" Eagle alitoa maelekezo kwa mmoja wa wapambe wake ambaye alikimbia upesi kwenda kutekeleza jambo aliloagizwa. Baada ya dakika kumi yule mpambe alirejea kwa Eagle halafu akamwambia, "kila kitu tayari". Eagle alitoka ndani ya nyumba yake ya kifahari akiwa na wapambe wake wawili wa kuaminika hadi kwenye maegesho ya magari, gari aina ya Jaguar ndiyo ilikuwa ipo mbele ya macho yake na wapambe wengine zaidi ya kumi walikuwa wapo wamesimama kulizunguka gari hilo. Wapambe wake wawili wa kuaminika walimfungulia mlango wa gari kwa heshima kisha wakaingia katika milango ya kushoto na kulia na kupeleke kumuweka Eagle katikati walipoingia ndani ya gari hiyo aina ya Jaguar. Msafara wa magari matatu ulitoka katika makazi ya Eagle mtaa wa NW 8th kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Miami, ulitumia dakika kumi ukawa umefika katika uwanja huo kutokana na mwendo wa kasi waliokuwa wakiutumia. Wapambe wote wa kawaida waliishia uwanjani hapo na wale wawili waliingia naye ndani ya uwanja upande wa ndege binafsi, walipitiliza moja kwa moja ndani ya ndege hiyo na safari ikaanza ndani ya muda huo.
******
Allison ndani ya usiku huo aliomba msaada wa kuongezewa nguvu kutoka kwa wapelelezi wenzake wa siri, ombi lake hilo liliidhinishwa moja kwa moja na CE na akaahidiwa wangewasili asubuhi itakayofuata. Asubuhi na mapema katika nyumba ya maficho aliyopo, gari aina ya landcruiser prado yenye vioo vya giza iliwasili katika geti la nyumba hiyo. Muda huohuo pia simu ya mkononi ya Allison iliita na alipoangalia namba ya mpigaji hakuiona zaidi ya maandishi ya yaliyosomeka N001, aliipokea baada ya kujua ni mmoja kati ya mpelelezi aliomba aongezewe katika operesheni nzito iliyopo mbele yake.
"nipo getini" Sauti ilisikika ikimwambia baada ya kupokea simu.
"ok" Allison alimwambia mtu aliyempigia kisha akanyanyua simu ya upepo halafu akaongea, "fungua geti gari iingie". Geti la nyumba hiyo lilifunguliwa baada ya amri hiyo kutoka kisha gari iliyokuwa getini iliingia, Allison alienda kuwapokea wapelelezi ambao hakuwahi kufanya nao kazi na ilikuwa ni mara ya kwanza kuwaona kutokana na kitengo walichopo ndani ya shirika hilo. Wapelelezi wa EASA wamegawanyika makundi mawili ambayo ni NORMAL SERVICE na SECRET SERVICE, Normal service siku zote hujulikana na wafanyakazi wa shirika hilo na hata watu wa Secret service wanawatambua wote na ndio wao wanaowapatia majukumu kutoka kwa wakubwa. Normal service ni kama Norene, Moses Gawaza na Asp John ambao ni wapelelezi wa kawaida. Wapelelezi wa Secret service siku zote huwa hawajuani kama hawajawahi kukutana kwa ajili ya kazi au sehemu nyingine, wapelelezi hawa ni wa siri sana na ikitokea wamekutana basi ni kwa ajili ya kazi au kwenye mafunzo ya kazi. Daraja hili la upelelezi wanalo Norbert, Hilda na Allison na wengine ambao hawajulikani, kutokana na usiri wa daraja walilopo walikuwa hawatambuani na kama wakitambuana basi hawazidi watatu na hata walipoitwa kwa ajili ya kupewa kazi waliitwa kwa muda tofauti kiasi cha kuwafanya wasionane. Norbert na Hilda peke yao ndiyo waliyoweza kuitwa pamoja kutokana kutambuana na kazi yao ni moja, pia ufanyaji wa kazi pamoja ambayo ilimpa Moses jina la SHUJAA ndiyo iliwafanya wawe pamoja.
Allison alibaki ameduwaa baada ya kuwaona wenzake ni watu anaowafahamu, Hilda na Norbert ambao ndiyo watu aliopewa taarifa na mkuu nao walishangaa kujua Allison nj mpelelezi mwenzao kutoka secret service.
"mahaba niue karibuni" Allison aliwatania kisha akawaambia "yaani hii kazi ama kweli ni fumbo, tupo ofisi moja na tupo shirika moja lakini hatujuani".
"yaani we acha tu, vipi umefikia wapi karika ngoma hii" Norbert alimwambia kisha akamuuliza.
"nimefikia mbali kidogo naweza nikawaonesha ila si kwa maelezo matupu pekee" Allison alimjibu.
"twende basi ukatuoneshe ili tujue pa kuanzia" Hilda aliongea kumuambia Allison, wote kwa pamoja waliingia ndani halafu wakaelekea kwenye chumba kilicho mwanzoni mwa ukumbi wa nyumba hiyo. Allison alifungua mlango wa chumba hicho kisha akaingia ndani, Norbert na Hilda nao waliingia ndani kwenye chumba hicho ambacho ndicho chumba cha kulala cha Joseph, Davis na Koplo Uyomo aliyetolewa chumba cha mateka. Muda huo wahusika wa chumba hicho walikuwa wamelala wote wasio na habari na ujio wa wapelelezi wengine ndani ya chumba hicho.
"hawa nimefanikiwa kuwaokoa katika majanga tofauti ambayo yangeugharimu uhai wao" Allison aliwaelezea Norbert na Hilda.
"ni vizuri maana taifa bado linawahitaji waandishi kama hawa na bado askari shahidi kama huyu anahitajika kwa jeshi lake" Norbert alimpongeza Allison. Walitoka humo ndani wakaelekea chini ya ardhi kwenye vyumba vya mateka, walishuka ngazi hadi kwenye chumba chenye mateka kisha wakafungua mlango halafu wakaingia ndani.
"hawa ni watu waliopo upande wa adui pia ndio kikwazo cha kazi yetu, kwani huyu jamaa nilimkamata ofisini kwetu. Huyu demu huyu ni mtu akiyetumwa kwenda kumuangamiza koplo Uyomo na nilimtia nguvuni kisha nikammaliza mmarekani aliyekuja naye yule wa Three devils" Allison aliwaeleza.
"nadhani hao wamarekani wapo watatu ambao wengine waliosalia tuliwamaliza usiku uliopita" Hilda aliongea maneno ambao yalififisha nuru ya matumaini ya kutoka kwa Jackline na Tasi waliofungwa ndani ya chumba hicho, Norberr alitembea hadi alipofungwa Tasi kisha akamshika kidevu halafu akamwambia "mpira upo kwenu sasa waficha maovu mtajua mcheze rede au hspohapo". Maneno hayo yalimuudhi sana Tasi na akajikuta ameachia kichwa ili ampige Norbert, kichwa hicho kilipiga hewa baada ya Norbert kukikwepa.
"ohoo unajifanya mkali sio sasa subiri nikianza kufanya kazi yangu utakuwa mpole mwenyewe na utasaidia kazi yetu" Norbert alimwambia Tasi kisha akaenda kwa Jackline aliyefungwa pembeni kidogo ya Tasi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Allison umemuona huyu binti uliyemkamata ambaye anaitwa Jackline, ni mmoja kati ya wasichana niliowahi kuwa nao katika mahusiano kipindi cha nyuma kabla sijakutana na bibie Hilda na niliachana naye baada ya kuona simuelewi" Norbert alimwambia Allison kisha akamtekenya Jackline kwa makusudi halafu akamwambia, "bibie hujakumbuka enzi zetu mpaka hivj sasa". Norbert alifanya uchokozi mbalimbali kwenye mwili ya Jackline huku akicheka, uchokozi huo ulimsababisha Hilda ajihisi wivu.
"Nor acha" Hilda alisema kwa ukali na kupelekea Norbert aache kumchezea Jackline baada ya kuona dalili za wivu kwa Hilda.
"haya mama nimeacha, sasa twendeni tukapange mikakati mingine kutokana na ulipoishia" Norbert alikubaliana na kauli ya Hilda kisha akamwambia Allison huku akitoka ndani ya chumba cha mateka, Hilda na Allison nao walimfuata.
*****
KAMBI YA NGOME
UPANGA
JIJINI DAR ES SALAAM
Kamanda msaidizi wa kambi hii ambayo ndiyo makao makuu ya majeshi ya Tanzania alipokea simu kutoka kwa Jenerali akimtaka awapeleke makomandoo kumi katika msitu wa hifadhi wa Mabwepande uliopo nje kidogo ya jiji la Dares salaam. Kamanda msaidizi wa kambi hiyo aliwapakia makomandoo kumi katika busi dogo la jeshi, alimpa maelekezo dereva wa basi hilo kwa mujibu wa maneno ya Jenerali mwenyewe. Basi hilo lilitoka kwa kasi kambini huku Kamanda msaidizi akiwa na uhakika kuwa amekamilisha maelezo ya mkuu wake, baada ya saa moja toka basi hilo liondoke Jenerali Kulika aliingia kambini kisha akaelekea ofisini kwake moja kwa moja. Kamanda msaidizi naye alimfuata ofisini kwake, alipiga saluti alipofika mbele ya Jenerali Kulika alipiga saluti.
"Sema Marwa kuna tatizo lolote?" Jenerali Kulika alimuuliza Msaidizi wake.
"mkuu nilitaka nikujulishe kuwa wale vijana ulioagizwa wapelekwe Mabwepande wameshapelekwa" Kamanda Msaidizi aliongea.
"Marwa unajua unanichanganya kabisa, nimekuambia uwepeleke hao vijana saa ngapi?" Jenerali Kulika aliuliza.
"mkuu si umepiga simu muda mfupi ukinitaka nipeleke makomandoo msitu wa Mabwepande" Marwa aliongea.
"Kwahiyo umewapeleka tayari, khaa kuna mtu anachezea namba yangu basi, wasiliana na dereva wa gari upesi sana ili awarudishe, mimi sijatoa amri hiyo Marwa" Jenerali aliongea. Marwa ambaye ni meja jenerali kicheo alikuwa amepagawa hadi muda huo, maagizo aliyopewa na mkuu wake ndiyo aliyafanya lakini mawasiliano yalikuwa hamna baina yake na dereva . Hapo ndipo akapagawa zaidi na ikambidi aifikishe taarifa kwa jenerali Kulika, taarifa hiyo ilipokelewa kwa mshangao na Jenerali Kulika. Uamuzi aliouchukua ni kwenda mwenyewe katika pori hilo ili ajue kinachoendelea, hakuwa na muda wa kupoteza tena kwani angechelewa basi ingeonekana amefanya uzembe mkubwa. Jenerali Kulika aliingia kwenye gari lake la kazi na akaendesha mwenyewe kuelekea ulipo msitu wa Mabwepande kwa mwendo wa kasi, hakuja na yoyote kama ilivyozoeleka akiwa anaenda sehemu kunakuwa na msafara wake. Njiani ndipo simu yake ilipoita na mpigaji alikuwa nj mmoja wa makomandoo kumi ambaye ni mwanamke.
"Belinda kuna nini huko?" Jenerali Kulika alimuuliza komandoo wake huku akizidi kuongeza mwendo wa gari yake.
"mkuu wenzangu wote wameuawa na hivi ninavyoongea ni mimi tu ndio nipo hai" sauti ya komandoo wake ilimwambia.
"upo wapi kwa sasa?" Jenerali Kulika alimuuliza Komandoo wake.
"nipo Tegeta sasa hivi baada ya kufanikiwa kutoroka" Komandoo wake alijibu.
"sawa nakuja sasa hivi ulipo,hakikisha unakaa sehemu ambayo barabara unaiona ili unipigie tu ukiona gari langu" Jenerali Kulika alimwambia Komandoo wake kisha akakata simu na akazidi kuongeza mwendo wa gari ili awahi kufika.
****
Eagle na wapambe wake wa kuaminika ambao ni wazungu waliwasili Tanzania asubuhi sana katika uwanja wa ndege wa siri uliopo katika kambi ya siri ya usalama wa taifa maeneo ya Changanyikeni, asubuhi ya siku hiyo walianza kazi iliyowaleta mara moja kwa kuinasa simu ya Jenerali kisha wakaitumia namba hiyo kumpigia kamanda msaidizi wa kambi ya Ngome Meja jenerali Marwa baada ya kupata taarifa ya kutokuwepo kwa Jenerali ofisini. Walimtumia kijana wa usalama wa taifa mwenye uwezo wa kuigiza sauti za watu kuigiza sauti ya Jenerali katika kumpa amri msaidizi wa kambi, mpango huo ulifanikiwa kisha wakaenda msitu wa Mabwepande kuwasubiri makomandoo hao ili wawamalize. Basi la jeshi lililobeba makomandoo lilipowasili tayari lilikuwa kwenye anga zao na mahesabu juu yake yalikuwa yamewekwa, makomandoo waliposhuka waliwashambulia kwa bundukii za wadunguaji wakawamaliza. Dereva wa basi la jeshi alipoona kuna hatari ipo mbele yake aliamua kuondoa basi hilo kwa kasi ili aokoe maisha yake lakini hakufika mbali naye alikuwa maiti baada ya busi hilo kulipuliwa. Eagle alijitokeza mafichoni akiwa na wapambe wake pamoja na vijana wa usalama wa taifa, walijipa pongezi kwa kazi nzuri waliyoifanya, kisha wakaiburuza miili hiyo kuitoa eneo la barabarani hadi katikati ya pori.
"mbona wapo tisa hawa, mmoja yupo wapi? au katoroka" Eagle aliwauliza vijana wa kazi alionao.
"Don sidhani kama anaweza kutoroka labda hajaja" Kijana mmojawapo kutoka usalama wa taifa alisema kisha akaweka kituo kwenye maelezo yake halafu "Brigadia Belinda ndio haonekani hapa".
"halafu wakati tunawapiga bunduki hawa nilisikia sauti ta kuvunjika kioo kwenye lile basi, hebu nendeni upande wa pili wa barabara kule juu halafu mumtafute huyu malaya ili naye awafuate wenzake kuzimu" Eagle alitoa amri na vijana wake wakaelekea alipowaagiza.
****
Jenerali Kulika alipofika Tegeta simu yake iliita na alipoangalia mpigaji aliona ni Belinda, aliamua kuegesha gari pembeni ya barabara kisha akatulia. Mlango wa kiti cha pembeni ya dereva ulifunguliwa kisha binti mrembo aliyevalia magwanda ya jeshi aliingia, Brigadia Belinda ndiyo jina la huyu binti na ni komandoo wa kuaminika wa JWTZ.
"Belinda kuna nini kimetokea huko" Jenerali Kulika aliuliza.
"mkuu tulipewa amri yako ya kuja Mabwepande na ndipo yametokea haya" Belinda alieleza.
"mimi sikutoa amri hiyo na hata Marwa anasema nilimpigia simu wakati simu yangu ilikiwa inasumbua mtandao na kioo kinaandika 'NO SERVICE'. Hebu nieleze mkasa mzima wa kilichotokea huko" Jenerali Kulika aliongea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"wakati tunaambiwa tuelekee msitu wa Mabwepande mimi nafsi iliingia na wasiwasi wa ghafla, hivyo nikaamua kukaa kukaa kiti cha mwisho upande wa kulia katika basi hilo. Hadi tunafika na kushuka mimi nilikaa nyuma kama tahadhari, wenzangu wote waliposhuka niliona wakidondoka mmoja mmoja. Nilipoona hivyo nilivunja vioo vya dirisha upande mwingine kisha nikatokomea maporini, nilikuja kutokea barabarani kwa upande mwingine baada ya kusikia sauti ya gari la mchanga ambalo nililidandia hadi nakaribia" Belinda alieleza kilichompata.
"ok, sasa ngoja tukafanye kazi askari wangu" Jenerali Kulika aliongea huku akiweka gia, aliingiza gari barabarani kuelekea msitu wa Mabwepande.
Walipokaribia eneo la msitu huo Jenerali Kulika alisimamisha gari kisha akaliingiza kwenye kichaka halafu akalificha, alishuka kwenye gari huku Belinda naye alishuka pasipo kusubiri lolote. Jenerali Kulika alikuwa yupo katika vazi lake la ofisini lenye shati ya rangi ya kijani inayopauka na suruali ya kijani kibichi huku mabega yake yakiwa yamechafuka kwa vyeo.
"nadhani huo moshi ninaouona angani ni eneo la karibu na huko ulipotoka?" Jenerali Kulika alimuuliza Belinda baada ya kuuona moshi wa basi la jeshi lililolipuliwa.
"ndiyo mkuu" Belinda alijibu.
"vua kofia na uiweke ndani ya gari" Jenerali Kulika alimwambia Belinda huku akivua kofia ya kijani aliyoivaa kisha akafungua mlango wa gari akaitupa ndani. Belinda naye alifanya hivyohivyo kisha akamtazama Jenerali ambaye alimuashiria wasogee eneo hilo, walitembea hadi jirani walilouliwa makomandoo tisa. Hapo Jenerali Kulika alimpa ishara Belinda azunguke upande wa pili baada ya kuwa wamekaribia katika kundi la watu wapatao kumi na nne waliokuwa wanachimba shimo, eneo hilo kulikuwa na wazungu wawili ambao ndiyo wapambe wa Eagle pamoja na vijana wa usalama wa taifa wapatao kumi na mbili. Jenerali Kulika alipohakikisha Belinda ameshazunguka aliamua kutikisa tawi la mti mfupi kisha akapiga sarakasi akajibanza kwenye mti uliopo jirani.
"mbona naona majani pale mbele yanacheza, hebu kaangalieni kuna nini?" Mmoja wa wapambe wa Eagle aliongea na kupelekea vijana wawili wa Usalama wa taifa waende wakiwa wana silaha mkononi. Jambo hilo lilitarajiwa na Jenerali Kulika kama litafanywa na vijana hao, aliposikia vishindo vyao aliukwea ule mti aliouegemea kwa haraka kisha akajibana kwenye tawi kubwa lililomficha, wale vijana walipofika hawakuwa wameona chochote.
"labda wanyama wadogo hamna mtu" Mmoja wa wale vijana alizungumza kisha akaielekeza silaha yake chini na mwenzake akafanya hivyohivyo, vijana hawa ambao muda huo hawakutambua kama walikuwa wapo chini ya Komandoo wa kuogopeka na mkuu wa majeshi. Kitendo cha wao kuzielekeza silaha zao chini ndiyo kosa walilolifanya bila ya wao kujijua na balaa la kimyakimya likawashukia, Jenerali Kulika aliwapigia hesabu ya harakaharaka kisha akajiachia kutoka juu ya mti akiwa amekunja miguu magoti yakiwa yanaangalia chini hadi kwenye vichwa vya vijana hao. Pigo hilo liliwapata katika utosi na kusababisha wote waende chini bila hata kutoa sauti, Jenerali Kulika alipowapa pigo hilo hao vijana alijiwahi kwa sarakasi ili asije akatua akaleta kishindo kitachowashtua wengine. Alipokaa sawa aljwavuta vijana hao pembeni kisha akachukua silaha zao, alijibanza alipokuwa awali huku macho yote yakiwa pale. Ukelele wa mwanamke anayeomba msaada ulisikika na kupelekea wale wapambe wa Eagle watoe amri kwa vijana wa usalama wa taifa.
"inawezekana kuna watu wapo karibu na hili eneo, wamalizeni wote ili wasije wakawa kikwazo baadaye " Mpambe mmoja wa Eagle aliongea kisha vijana wapatao saba wenye silaha wakaenda upande huo.
****
Belinda alipozunguka upande wa pili alitulia katika eneo lenye miti mingi iliyobanana kisha akavua buti moja alilolivaa, aliivuta soli ya buti hilo hadi ikafunguka taratibu na katikati yake kulikuwa kuna visu vyembamba viwili vyenye kung'aa. Alitoa lailoni lililopo ndani ya boti ambalo hutumika kwa ajili ya kukinga soksi isichafuke, laoloni hilo ambalo lilitoka kipande llikuwa na misumari iliyochoma kwenye soli ya kiatu. Belinda aliingiza kiganja chake ndani ya lailoni hilo lililoonekana lina nafasi kama sehemu ya kutumbukiza mguu kwenye soksi, malailoni hayo aliyavaa mikono huku ile misumari ya malailoni hayo ikiwa ipo juu kuanzia kwenye nundu za vidole vyake hadi mwanzoni mwa kiganja. Misumari ambayo ipo ndani ya lailoni ngumu alizovaa zilikuwa ina sumu ya kumlaza mtu papo hapo ikiwa atamchona, alivaa buti lake kisha akavichomeka visu alivyovitoa kwenye soli ya buti lake kijeshi kiunoni kisha akafanya hila ya kuwaingiza wapinzani wake katika anga zake. Belinda alilegeza sauti mithili ya mwanamke aliyechoka kisha akapiga yowe la kuomba msaada mithili ya mtu aliyekuwa yupo katika tabu, alipohakikisha yowe lake limesikuwa na wapinzani wake aliamua kurudi nyuma kwa mitaa kadhaa kisha akajibana kwenye shina la mti. Sauti ya nyayo za watu waliokuwa wakitembea kwa tahadhari ilisikika katika masikio shupavu ya Belinda yenye uwezo kutambua utembeaji wa mtu anayenyata kwenye majani yaliyopo msituni. Utembeaji wa maadui zake ulikuwa wa kitahadhari na siyo rahisi kugundulika na mtu wa kawaida ambaye siye mwenye mafunzo, sauti za nyayo hizo zilipokaribia sehemu aliyopo Belinda walijikuta wakiangalia pembeni na silaha zao wakielekeza pembeni baada ya kusikia sauti ya kitu kikitikisa majani. Vijana hawa wa usalama wa taifa hawakuwa wametambua kuwa ni hila ya Belinda aliyerusha jiwe kwenye majani liliwafanya wazubae, Belinda alitumia mwanya huo kuwavamia kwa kushtukiza kisha akawachoma vijana watatu misumari hiyo ya lailoni alizozivaa kwa haraka halafu akaruka juu akaachia mateke yaliyowapata watatu wengine ambao walienda chini na kusababisha silaha zao zianguke. Mmoja aliyebakia alitaka kuielekeza silaha alipo Belinda lakini alijikuta akikutana na kisu kilochorushwa, kisu hicho kilimpata katika mkono alioshikilia silaha hadi akaiachia ikaanguka. Kisu hicho kilirushwa na Belinda aliyekuwa yupo chini muda huo baada ya kuwapiga wale watu watatu mateke, Belinda alijifyatua kutoka pale chini kisha akamuwahi yule aliyemchoma kisu kwa pigo moja ngumi ambalo lilimlaza mtu huyo baada ya misumari kumchoma. Wale watatu waliopigwa mateke nao waliamka kumfuata ili wammalize Belinda aliyesimama hatua kadha kutoka waliposimama, walimfuata kwa mapigo ya karate ya aina tofauti ambayo yalimkosa mlengwa baada ya kupanguliwa yote kwa mpigo kisha mmoja wao akajikuta akipigwa ngumi ya kifua iliyomlaza kutokana na sumu zilizopo kwenye misumari aliyoivaa Belinda kwenye mikono. Belinda alichomoa kisu kingine kisha akamchoma mmoja cha shingo halafu akamuwahi akamuwahi aliyebaki kwa teke la nguvu la koo, hapo aliwamaliza wote wakawa wamelazwa chini na mmoja akawa ni maiti tayari.
****
Baada ya watu saba kuelekea upande waliosikia ukelele wa mwanamke akiomba msaada, walibaki watu watano tu ambao wawili walikuwa ni wapambe wa Eagle na watatu walikuwa ni vijana wa usalama wa taifa. Jenerali Kulika bado alikuwa kajibana katika eneo ambalo alikuwa awali huku akipiga hesabu kwa kutumia ubongo wake kwa sekunde kadhaa kisha akavua suruali yake aliyovaa, mapajani alikuwa amejifunga fito nyeusi ambazo hutumiwa na wakubwa wa polisi na hata jeshi kutembea nazo au kama kifimbo cha Baba wa taifa . Alizitoa vifo hizo kisha akavaa suruali yake kama awali, fito hizo zilikuwa na kitufe cha kubonyeza ambavyo alivibonyeza na kupelekea visu virefu vichomoze. Jenerali Kulika alitaka kuwavamia lakini akasita kisha akarudi hadi pale alipoiacha miili ya vijana aliowapiga magoti ya utosi, aliwapekua akawakuta na visu ambavyo alivichukua.
"Nyie hebu kaangalieni kuna nini kule mbele maana wenzenu hawajarudi toka walipoenda kuangalia lilipotikisika tawi la mti" Mpambe wa Eagle aliongea na kupelekea vijana watatu wa usalama waliosalia wapige hatua kuelekea upande aliopo Jenerali Kulika. Vijana hawa hawakufika mbali kwani wawili walipiga yowe la maumivu kisha wakaanguka, shingoni walionekana na visu vilizama kabisa. Tukio hili lilisababidha wote waliobaki wapige risasi upande vilivyotoka visu hivyo kwa kwa muda mrefu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"hakikisheni huyo mtu anayefanya hivi hatoki mzii........aaaaargh!" Mpambe mmoja wa Eagle alishindwa kumalizia kauli yake baada ya kuchomwa na chuma kidogo cha duara chenye meno shingoni mwake kutoka upande mwingine tofauti na waliochomwa visu wale vijana wa usalama wa taifa, alidondoka chini moja kwa moja huku Mpambe mwenzake pamoja na kijana mmoja wa usalama wa taifa aliyebaki wakiwa wamepagawa. Waliamua kuegemeana migongo huku wakizunguka kila upande ili wamuone adui yao, mbinu hiyo nayo ilikuwa haifai kwao kwani kijana wa usalama wa taifa aliyebaki alitoa yule la maumivu kisha akamuegemea Mpambe wa Eagle aliyesalia. Kifuani alionekana amechomwa na fito yenye kisu ambazo ni mojawapo ya fito aliyokuwa nayo Jenerali Kulika. Mpambe wa Eagle ndiye aliyebaki peke yake huku akiwa amechanganyikiwa kwa kutomuona adui yake, alinyoosha bunduki yake mbele kisha akamininina risasi kwa fujo.
"jitokeze kama wewe unajiamini na ukijificha basi wewe hujiami..." Mpambe wa Eagle alishindwa kumalizia kauli hiyo baada ya fito nyingine yenye kisu ilipotua kwenye mkono wake huku silaha yake ikimdondoka, akiwa amepagawa na tendo la kuchomwa na kisu cha fito ya Jenerali Kulika alijikuta anapokea mateke mawili ya ghafla hadi akaenda chini.
"sasa nimejitokeza kukuonesha najiamini" Jenerali Kulika aliongea kwa kujiamini akiwa kasimama mbele ya Mpambe huyo, alimuashiria mpambe huyo asimame kisha akakunja ngumi kumkabili. Mpambe huyu naye alipomuona Jenerali Kulika alisimama kimakabiliano kisha naye alisimama kisha akaanza kurusha mateke mfululizo, mateke hayo yalipiga hewa baada ya Jenerali Kulika kuyakwepa kisha akaachia pigo la kombati lililompata Mpambe huyo kwenye mbavu hadi akatoa yowe la maumivu akaanguka chini. Aliposimama kuangalia mahali alipokuwa Jenerali Kulika wakati anampiga hakumuona, alipogeuka nyuma alijikuta akipokea pigo jingine hadi akayumba kiasi cha kutaka kudondoka. Mpambe wa Eagle hadi hapo alitambua kuwa anapambana na mtu mwenye uwezo usio wa kawaida na ambaye kamzidi uwezo, upande aliosimama kwa mufa huo ulikuwa ni sehemu ambayo wenzake saba walikimbia kufuata uilipotokea sauti ya yowe la mwanamke akiomba msaada. Fikra iliyomjia kichwani mwake ni kukimbia na aliamua kukimbia kuelekea upande huo akijua anaweza kuwakuta wenzake waliokwenda huko, uwezo wa kupambana na Jenerali Kulikana hakuwa nao na kukimbia aliona ndio njia ya kuokoka kutoka kwenye mdomo wa Simba mwenye ghadhabu. Mpambe huyu hakutambua kuwa kule anapokimbilia hakuna tofauti na alipotoka, hakujua alikuwa anamkimbia Simba mwenye hasira na sasa anaenda kwa Mamba mwenye njaa. Mbio zake hizo hazikufika mbali kutoka pale alipo kwani upande anaoelekea ndipo Belinda yupo, huko alikutana na kipigo kilichomchanganya hadi akajikuta anarudi upande aliotoka bila kujijua. Alikimbia hadi kwa Jenerali Kulika akiwa hajajijua kama anarudi alipotoka, akili zake zilimrudi sawasawa baada ya Jenerali Kulika kuikamata shingo yake kwa nguvu alipomfikia. Hapo alianza kuingiwa na hofu na akabaki anatetemeka na baadaye alibaki kimya akiwa ameduwaa kauli ikawa imekatika ukiambatana na mlio wa kuvunjika shingo yake, Jenerali Kulika alikuwa amevunja shingo yake kwa kuinyonga.
"wapekue hawa wengine uwaaangalia vizuri maana wale wa mwanzo wana vitambulisho sikupata muda wa kuvisoma" Jenerali Kulika alimwambia Belinda ambaye alikuwa amewasili eneo alilopo muda huo, zoezi la kuwapekua vijana lilianza na hapo ambapo kila mmoja alikutwa na kitambulisho kilichowapa mshangao Jenerali Kulika na Belinda.
"Usalama wa taifa!! Kuna mchezo mchafu hapa unaendelea"Jenerali aliongea kwa mshangao.
"mkuu hapa mbivu na mbichi itajulikana na wenzao ndiyo watakaotueleza" Belinda aliongea.
"kivipi wakati tumewakata kauli wote?" Jenerali Kulika aliuliza.
"wengine nimewachoma misumari yenye sumu inayolaza mtu kwa masaa matano" Belinda alifafanua.
"vizuri sana, sasa basi piga simu katika kikosi cha anga watuletee Helikopta itakayowabeba hawa mbuzi pamoja na miili ya makomandoo. Hakikisha hili tukio la kuuawa kwa makomandoo halifiki katika vyombo vya habari maana litazua mengine" Jenerali Kulika aliongea.
"sawa mkuu" Belinda alijibu huku akitoa saluti.
****
MIKOCHENI
DAR ES SALAAM
Msafara wa rais Ole uliingia kwenye nyumba moja ya kifahari yenye eneo kubwa la maegesho ya magari, rais Ole alishuka kisha akaingia ndani ya nyumba akiwa na mlinzi wake mkuu. Nyumba nzima iliwekwa kwenye ulinzi baada ya rais kuingia ndani.
"kijana hujambo" Rais Ole alimsabahi kijana aliyemkuta sebuleni.
"sijambo, shikamoo mheshimiwa" Kojana huyo alijibu.
"marhaba, mama yako yupo?" Rais Ole alijibu kisha akamuulizia mama wa huyo Kijana.
"ndiyo yupo, ngoja nikamuite. Karibuni mketi" Kijana huyo alijibu kisha akaelekea upande wenye vyumba vya kulala katika nyumba hiyo. Kijana huyo alirejea na mwanamke wa makamo hadi alipo rais Ole.
"karibu" Mwanamke huyo alimkaribisha rais Ole kwa uchangamfu kisha akamgeukia yule kijana aliyemuita akamwambia, "Allen nenda chumbani kwako".
"sawa mama" Allen ambaye ndiye kihana aliyewakaribisha aliitikia kwa utiifu agizo la mama yake.
"ehe! Leo ndio umetukumbuka sio, haya sema shida yako uende" Mwanamke huyo aliongea kwa ukali.
"Bibi Flora tatizo nini? ,kumbuka wewe ni mke wa aliyekuwa mwanachama mwenzetu ambaye kwa sasa ni marehemu kwa hila za watu wachache tu wasiopenda uzalendo wake" Rais Ole aliongea kwa upole.
"wasiopenda uzalendo wake au msiopenda uzalendo wake, yaani mmeona njia pekee ya kumuondoa mume wangu katika mikakati yenu ni kumpatia nafasi ya kugombea ubunge wa kwao Kahama halafu mkamlenga na risasi kama mnawinda mnyama pori. Sasa hivi umerudi tena, unataka na roho yangu pia......niambie nijue unataka na maisha yangu?!........yachukue kama unayataka basi ili uridhike na moyo wako wa kishetani" Mwanamke huyo aliongea kwa uchungu huku machozi yakimtoka, maneno hayo yalimfanya rais Ole ajawe na hasira moyoni mwake ingawa alifanikiwa kuiongoza na akawa anaonekana kawaida tu usoni.
"si hivyo Bibi Flora, unajua wazi hiyo ilikuwa ni njama ya chama tawala katika awamu iliyopita" Rais Ole aliongea kwa upole.
"Njama! Yaani unadhani mimi ni mpumbavu kama wengine na kwa taarifa yako mume wangu alinieleza yaliyotokea katika mkutano wenu wa chama ambao mliufanya kwa siri kabla hamjamuua. Tukio la kuuawa kwa mume wangu umelifanya ndio njia yako kupata kura za kuingia ikulu, nakuchukia sana na ningekuwa na uwezo wa kukuua ningeshakuua siku nyingi. Pia naomba utambue kuwa sihitaji maongezi na mashetani watu, mlango ulioingia nao ndio huo uutumie kutokea...toka nyumbani kwangu" Mwanamke huyu kwa hasira huku machozi yakiwa yanamtoka, hakuwa mwingine bali ni mjane wa aliyekuwa akigombea ubunge jimbo la Kahama mjini ambaye alipigwa risasi kwenye kampeni. Rais Ole aliinuka kwenye kisha akamtazama Bibi Flora halafu akaondoka huku Mlinzi wake akimfuata kwa nyuma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rais Ole alikuwa kakasirishwa sana na maneno ya Bibi Flora ingawa yalijaa ukweli, binadamu siku zote huambiwa uongo akachukulia kawaida ila ukweli huwa unauma na ndio maana rais Ole aliumia kwa kuambiwa ukweli. Unafiki wake kwa Bibi Flora ulikuwa umegonga mwamba, hakutarajia kama atakuwa kama huyu mjane atakuwa anajua hila zake. Rais Ole aliondoka kwa hasira hadi ndani ya gari yake inayomsibiri, aliingia ndani ya gari kisha akauamuru msafara uondoke mahali hapo. Msafara huo ulitoka nyumbani hapo kimya kimya kisha ukaanza kupiga king'ora baada ya kuingia katika barabara iliyopo mbele ya nyumba hiyo.
****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment