Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

JINAMIZI - 5

 







    Simulizi : Jinamizi

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wapelelezi wa kimataifa wa EASA wameamua kuianza kazi yao kwa namna ya kipekee ili wapate mwanga katika kuianza kazi yao, waliianza kwa kufanya mahojiano na teka wao mmoja ambaye anaonekana anajua vitu ambavyo vingeweza kuwasaidia katika upelelezi wao. Mahojiano hayo yaliongozwa na mtaalamu wa kufanya mahojiano na wahalifu ambaye ni mmoja wa wapelelezi wa SECRET SERVICE ndani ya EASA, Norbert ndiye mtaalamu wa mahojiano ya namna hiyo kwa wahalifu sugu ambaye anaaminika na haijawahi kutokea mhalifu aliyepita katika mahojiano yake aligoma kutoa ushirikiano. Ndani ya chumba cha mateka aliingia na meza kubwa ya magurudumu iliyofunikwa kitambaa kikubwa kilichoinuka juu kuashiria kuna vitu vimefunikwa, Hilda naye aliingia na vifaa vya kitabibu na akiwa amevaa koti jeupe la kitabibu. Allison aliingia mikono mitupu akiwa ni muangaliaji tu wa muangaliaji wa mahojiano hayo, viti vitatu vilikuwa vimeingizwa humo ndani ambavyo viwili vilikaliwa na Allison na Hilda. Norbety yeye alipendelea kusimama tu ili afanye kazi yake kiufasaha kwani kukaa aliona kutamtia uvivu, alipotaka kufanya mahojiano naye alivaa koti la kitabibu kama Hilda halafu akamtoa Tasi pale anaponing'inia hadi kwenye kiti cha mateso kikichopo karibu ambacho mwanzo alifungiwa Koplo Uyomo.



    "sasa mjamaa unakumbuka ulijaribu kunipiga kichwa, sasa zamu yake ya kuwa mpole imefika. Hil fanya kazi yako kwanza" Norbert alimwambia Tasi baada ya kumfunga kwenye kiti halafu akamgeukia Hilda akamuamuru afanye kazi yake, Hilda alisogea hadi mbele kisha akampima vipimo vya kitabibu hadi akamaliza.



    "hana tatizo lolote la kiafya,Nor unaweza ukaendelea" Hilda alimuambia Norbert kisha akarudi kwenye kiti alichokuwa amekaa awali na Norbert alisogea hadi kwenye ukuta uliopo jirani na kiti cha mateso alichomfunga Tasi kisha akabonyeza swichi iliyopo ukutani. Kiti cha mateso kiliinuka juu kidogo hadi usawa wa magoti ya Norbert, meza ya magurudumu iliyofunikwa shuka nayo ilikuwa tayari ipo mbele ya kiti cha mateso kwa umbali wa mita mbili. Norbert alifunua shuka iliyoifunikwa juu ya meza ya magurudumu kwa taratibu huku akipiga uruzi kuimba nyimbo ya tanzania, vifaa mbalimbali vya mateso vilionekana kwenye meza hiyo pamoja na mipira ya kuvaa mikononi. Norbert alichukua mipira ya mikononi kisha akaivaa huku usoni amepambwa na tabasamu. Alichukua pasi ya umeme nzito kisha akaichomeka kwenye swichi halafu akawasha, alimtazama Tasi akiwa na tabasamu pana usoni mwake.



    "unaweza kuniambia kilichokuleta ofisini kwetu hadi ukakamatwa?" Norbert alimuuliza Tasi ambaye alionesha kutojali swali aliloulizwa na akaishia kutema mate ambayo hayamkumfikia Norbert.



    "ohoo unahitaji kuzimuliwa kidogo tu" Norbert aliongea kisha akachukua pasi ya umeme aliyoichomeka kwenye swichi halafu akamvua shati Tasi, alimbandika pasi hiyo kifuani kisha akaishikilia kwa nguvu. Tasi alipiga kelele sana hadi machozi yakawa yanamtoka kutokana na pasi hiyo kuunguza halafu ilikuwa ina hitilafu iliyopelekea sehemu ya kupigia pasi iwe na shoti ikigusa mwili wa mtu. Norbert alipoitoa pasi hiyo alimtazama Tasi kisha akamuuliza, "upo tayari kusema au unataka tukufanye useme". Tasi hakujibu swali hilo zaidi ya kujiinamia huku akihema nguvu, alipoinama aliacha mgongo wazi na hapo Norbert alimbandika pasi ya mgongo kisha akaishikilia kwa nguvu. Makelele ya maumivu yalimtoka Tasi huku jasho jingi likimvuja, alimsihi Norbert aitoe na atasema na Norbert alipoitoa aliishia kutukana matusi ya nguoni pamoja na kumtukania mzazi Norbert. Hiyo ilimfanya Norbert atabasamu kisha akarudisha mahala pasi pake halafu akatoa kisu kikali kilicjopo katika meza ya mateso, aliikata suruali ya Tasi ikawa kama kaptula fupi iliyoweka mapaja ya Tasi wazi ambayo yamejaa vinyweleo.



    "naona unajua kutukana sana sasa sikuulizi swali tena na majibu utayatoa mwenyewe kenge we" Norbert aliongea huku akirudisha kisu kwenye meza ya mateso halafu akaichukua pasi ya umeme tena. Alimbandika Tasi kwenye ugoko wake wa mguu wa kushoto na kupelekea vinyweleo vyote viungue huku pasi hiyo ikitoa mvuke kutokana na kuiunguza ngozi ya Tasi, makelele ya maumivu yalimtoka Tasi lakini hakutaka kuzungumza chochote huku Norbett akizidi kumtesa tena safari hii akiiweka pasi hiyo kwenye paja la Tasi alipoitoa ugokoni. Tasi aliendelea kupiga kelele lakini Norbert hakumuachuia na hakuwa na huruma nae na huruma yake ingekuwa kuongea alichoulizwa tu, Norbert alimfungua kifungo cha suruali Tasi na kupelekea nguo yake ya ndani ionekane kwa wote hapo ndani.



    "sasa naona umekuwa mgumu kuongea nilichokuuliza sasa ngoja niibandike hii pasi kwenye hiyo dunguso yako labda utasema na usiposema jua naipeleka kwenye korodani zako" Norbert aliongea huku akiitanua nguo ya ndani ya Tasi hadi sehemu za siri zikawa zinaonekana, aliishusha pasi hiyo taratibu kwenye maungo ya siri ya Tasi na alipokaribia vinyweleo vilivyopo humo ndani tayari joto la pasi lilikuwa likiingia kwenye maungo hayo.



    "nasemaa! Nasemaa! Nasemaa!" Tasi aliongea kwa nguvu huku akihema kwa woga kutokana tukio lililokuwa linaanza kufanywa na Norbert.



    "si mgumu wewe wacha niiguse hiyo dunguso na pasi kidogo halafu" Norbert aliitoa kauli huku akiwa anasogeza pasi zaidi hadi Tasi akajikuta akimwaga haja ndogo hapo hapo huku kijasho cha uoga kikimtoka. Hapo Norbert aliitoa pasi kisha akamwambia, "sirudii swali mara ya pili sasa nahitaji jibu tu".



    "nilitumwa kutoa vinasa sauti na kamera nilizozitegesha" Tasi aliongeakwa uoga.



    "ulitumwa na nani ni kwa ajili gani" Norbert aliuliza.



    "nilitumwa na mkuu kwa ajili ya kuangalia nyendo zenu zote ili msiharibu mikakati ya mheshimiwa" Tasi aliongea kwa uoga na akajikuta akipoteza umakini wote katika kujibu maswali na kutoa yote ya ndani iliyofuatia.



    "mheshimiwa yupi ana mikakati gani?" Norbert aliuliza.



    " Mheshimiwa Ole ana mikakati ya kumpatia mfadhili wake kutoka Marekani mgodi wa almasi wa Kondoa ikiwa atashinda urais, ili ashinde kwa namna yoyote alitumia njia ya mkato ya kuzuia vikwazo vyake vyote na kujipatia kura kwa wanachi kwa namna ya kijanja" Tasi aliongea huku akiugulia maumivu ya vidonda alivyounguzwa na pasi.



    " sasa ueleze kwa urefu hayo maneno yako uliyoyaongea umesikiaa!?" Norbert alimwambia Tasi ambaye alijifanya hajamsikia, Norbert alimbandika pasi kwenye kidonda cha pajani huku akimtazama usoni.

    "aaaaargh! Nimesikia" Tasi alitoa ukelele wa maumivu kisha akatii kwamba amesikia halafu akasema, "wakati uchaguzi unakaribia na kampeni zinaanza Rais Ole alikuwa anaona dalili za kushindwa na mgombea mwenzake wa chama tawala RPP hivyo alitumia kila njia kuhakikisha anashinda. Sera zake akizojinadi hazikueleweka hivyo ikambidi aombe msaada kwa mfadhili wake bwana Eagle kutoka marekani ambaye alimtumia vijana watatu wenye ujuzi mkubwa katika kufanya mauaji, siku walipowasili watu wale alipanga mbinu haramu na uongozi wa juu wa PTP. Mbinu hiyo ilipingwa vikali na mgombea ubunge wa jimbo la Kahama marehemu Gerald Godfrey akiita uhaini kisha akaondoka bila ya kutambua kuwa kuondoka kwake kulikuwa ni mwanya kwa mpango mwingine kusukwa, kwenye kikao hicho wahudhuriaji kutoka usalama wa taifa tulikuwa mimi, Briton na mkuu Kitoza na hapo ndipo nilipopewa jukumu la kufuatilia nyendo zenu kwani mlijulikana kama mmeingia nchini kwa ajili ya kuchunguza juu ya ufadhili wa chama cha PTP na chanzo cha kupata kuwa na fedha nyingi katika kampeni zilizozidi uwezo wa chama kifedha kwa mujibu wa takwimu kabla uchaguzi haujakaribia. Nilianza kuwafuatilia kila hatua yenu na hata mlipoandaa jarida baada ya uchunguzi wenu kukamilika na Hilda alipolipeleka kampuni ya EAPL kuchapishwa ni mimi ndiye niliyezuia lisichapishwe nilipomuhonga Daud ambaye ndiye mpokeaji wa miswada ya kichapishwa vitabu na majarida." Tasi alitoa mambo ambayo yalikuwa ya siri.



    "je ni nani aliyemuua Gerald Godfrey katika kampeni kule Kahama?" Norbert alimuuliza.



    "Jim kijana ambaye alitumwa na Eagle ndiye aliyemuua ikiwa ni mbinu ya kujipatia kura kirahisi kwa wanachi" Tasi alijibu.



    "mbinu ipi hiyo?" Norbert alimuuliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "wakati Mgombea Gerald anawashutumu rais Ole na wenzake ni wahaini katika mkutano wa siri ndiyo ilikuwa tiketi ya wao kuingia ikulu, kwani walimtuma Jim amuue kisha tuhuma za kuuliwa kwake zikapelekwa kwa chama tawala RPP. Hii ilisababisha Mgombea wa RPP ndugu Mtalemwa awe anatumia muda mwingi wa kampeni kujitetea kuliko kunadi sera zake huku rais Ole akiwakandamiza pamoja na kuwamwagia ahadi kedekede wananchi. Mwisho rais Ole akageuka kipenzi cha wananchi wote". Maneno hayo yalisababisha Norbert awatazame Hilda na Allison kisha akamuangalia tena Tasi halafu akamuuliza, "je hilo eneo lenye madini ameshapewa huyo mfadhili wake?".



    "hapana bado hajapewa" Tasi alijibu.



    "hao vijana wa marekani wamefanya kazi ngapi ukitoa mauaji ya Gerald" Norbert aliuliza.



    "wamefanya kazi kibao ikiwemo mauaji wa waziri wa nishati na madini" Tasi alijibu.



    *****



    KAMBI YA USALAMA WA TAIFA

    CHANGANYIKENI



    Kitoza na Eagle walikuwa wapo ofisini kwa ofisini ndogo ya Kitoza iliyopo ndani ya kambi hiyo wakinywa na kujipongeza kwa kazi nzuri ya kuua makomandoo tisa wa kijeshi, hadi muda huo bado walikuwa hawatambui kama mcheozo ulikuwa umewageukia wao. Waliendelea kufurahia ushindi wao katika ofisi hiyo ya kisasa yenye hadhi ya kutumiwa na mtu kama Kitoza na kupokelewa mgeni kama Eagle.



    "aisee Don wewe ni mtu wa kazi nimekubali" Kitoza aliongea kumuambia Eagle.



    "huu ni mwanzo tu kazi yenyewe inaanza leo usiku kwa kummaliza Jenerali Kulika nyumbani kwake maana nina uhakika vijana niliowaacha huko msituni wameshamshika huyo komandoo wa kike na wamemmaliza. Kazi ikiisha Ole natumaini atanipa ninachotaka kwani nimemsaidia sana kwenye mpango wake" Eagle aliongea.



    "lazima akupatie wewe mtu wake wa karibu na mfadhili wake, ila Don mtu unayemfuata leo umakini unahitajika. Nadhani si umesikia balaa lake lilivyo" Kitoza alimwambia.



    "huyo ni mtu mdogo tu na hana uwezo mbele yangu, kumbuka mimi ni ninja na ni komandoo aliyeasi amri ya jeshi sasa na............pokea kwanza hiyo simu" Eagle aliongea kujisifia halafu akasita baada ya simu ya mezani isiyo na waya ilipoita na akamtaka Kitoza apokee. Kitoza aliminya kitufe cha kupokea na kupelekea simu iwe na sauti ya kusikika na mtu aliyepo karibu.



    "Reginald Kitoza naongea na nani?" Kitoza aliongea.



    "Augustin Kulika hapa"sauti ilisikika kwenye spika kubwa ya simu.



    "ohoo! General nakusikiliza" Kitoza aliongea baada ya kumtambua aliyempigia simu.



    "nadhani nimepishana na kundi la vijana wako wakiwa na wazungu wawili maeneo ya Tegeta, vipi kuna tatizo la kiusalama" sauti ya jenerali Kulika ilimuuliza.



    "usalama upo General niliwatuma tu waende msitu wa Pande kwenda kuchukua vifaa vyetu" Kitoza alidanganya akijua Jenerali Kulika hajui chochote.



    "ahaaa! Kumbe ndio wewe umewatuma wawaue vijana wangu, sasa njoo uifuate mizoga yao pamoja na hiyo ya wazungu wawili. Pia uje na melezo ya sababu za kuwaua na aliyewatuma na si vinginevyo" Sauti ya Jenerali Kulika iliongea kwa ukali kisha simu ikakatika. Kitoza na Eagle walibaki wamechoka bila kufanya kazi yoyote ambayo ni nzito.



    "kumeharibika" Kitoza aliongea akiwa amegwaya kwa taarifa aliyopewa na Jenerali Kulika.



    "Shit! Huyu mshenzi sasa usiku huu namuua kifo cha kikatili ili aipate" Eagle aliongea huku akiwa amekaza meno yake kwa hasira halafu akaondoka ofisini kwa Kitoza.



    ****



    Maneno aliyoyaongea Tasi katika mahojiano yao yalikuwa ni mwanga tosha kwa Norbert na Hilda kufanya kazi yao, waliamua kufanya mikakati ya kazi ambayo ilitakiwa imalizike mara moja. Wakiwa wanafanya majadiliano ya kuianza kazi yao simu ya mkononi ya Norbert iliita na jina la Gawaza ndio lilionekana kwenye kioo cha simu yake, simu hiyo iliashiria kuna jambo linaendelea ambalo halijui kwani mpigaji huwa hapigi kwa ajili ya kusalimia bali ni kwa ajili ya kazi. Norbert aliipokea kisha akaiweka sauti ya spika nje.



    "Eagle mhalifu kimataifa amewasili Tanzania na ameshaua makomandoo tisa wa kijeshi akishirikiana na vijana wa usalama wa taifa, usiku wa leo anaenda kummaliza Jerali Kulika nyumbani kwake. Kazi ya kumuokoa ipo juu yako maana huyu ni mtu wa hatari kama na komandoo kama Jenerali Kulika" sauti ya Moses ilisikika kisha simu ikakatika baada ya maelezo kuisha.



    "Jamani nadhani mmesikia, sasa nianze na hii ngoma" Norbert aliwaambia wenzake.



    "hamna shida twende wote kama vipi" Allison aliongea.



    "poa ila huyu mhalifu ni asusa yangu" Norbert aliongea huku akinyanyuka kwenye kiti kisha akasema, "muda unakaribia tujiandaeni kama vipi".



    Hisia za kujiwa na hatari ndiyo zilizokuwa zipo

    kichwani mwa Jenerali Kulika tangu alipowasili

    nyumbani kwake majira ya saa kumi na moja jioni,

    hisia zake zilipelekea aihamishe familia yake katika

    nyumba yake nyingine bila yeyote kujua. Nyumbani

    alibaki yeye mwenyewe bila kuwa na mlinzi wa

    zaada zaidi ya mfungua geti tu, saa moja jioni

    ilipowadia kiza kilianza kuingia taratibu na

    kuifukuza nuru iliyokuwepo. Upweke wa nyumba

    yake ndiyo ulliompa wasaa wa kujihami ikiwa

    kutatokea hatari yoyote, hadi muda huo hakuwa

    amevua sare zake za jeshini zaidi ya kofia tu.

    Kukaa peke yake kulimfanya achukue kinywaji

    katika jokofu hapo nyumbani ili awe anakunywa

    taratibu kutuliza akili zake, kawaida Jenerali Kulika

    hutumia pombe kali maalumu akiwa na jambo la

    hatari lililopo kwenye hisia zake. Hata alipovamiwa

    Marekani alipokuwa masomoni alihisi hatari ipoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mbioni na alitumia pombe ya aina hiyo hiyo muda

    mfupi tu kabla hajapambana na wahalifu

    waliomvamia hadi kuwaua wote. Majira ya saa

    mbili kasoro alisikia mlango mkubwa wa kuingia

    sebuleni ukigongwa, akiwa yupo mkabala na

    mlango katika moja ya kochi lililopo sebuleni hapo

    aliamua kuruhusu mgongaji apite ndani akidhani ni

    mtu wa getini tu.

    "Washoki pita mlango upo wazi" Jenerali Kulika

    alimwambia mgongaji mlango akijua ni mtu wake

    wa getini, mlango mkubwa wa kuingia sebuleni

    hapo ulifunguliwa kisha mshale uliolenga kifua cha

    Jenerali Kulika ukaingia kwa kasi kuelekea eneo

    alipo mlengwa. Jambo hilo lilionekana na na

    Jenerali Kulika kabla hata mlengaji hajauachia

    mshale na alipouachia mshale tayari Jenerali

    Kulika alikuwa amehama kwenye kochi kwa

    sarakasi iliyompeleka kochi la pili. Kisu kikali

    kilirushwa katika kochi la pili ambacho kiliambulia

    patupu baada ya Jenerali Kulika kukikwepa halafu

    akarusha chupa ya pombe aliyokuwa akiinywa

    katika taa ya umeme. Taa hiyo ilipasuka kisha giza

    lifatuata kiasi cha kutoonana sebuleni hapo,

    Jenerali Kulika aliitumia nafasi hiyo kwenda

    kuzima swichi kuu iliyopo hapo sebuleni kisha

    akawa anamtafuta adui yake katika giza la sebuleni

    hapo. Mtafutano na adui yake ulikuwa wa

    kiumakini kuliko kawaida ili asiingie mikononi mwa

    adui yake kijinga, alitembea taratibu kwa umakini

    katika pembe zote za sebule hiyo. Jenerali Kulika

    aliamua kutoa pumzi kwa umakini kwa kuhofia

    kutoa na kuingiza pumzi kwa nguvu jambo ambalo

    lingemfanya ajulikane na adui yake mahali alipo,

    kukabiliana na adui yake kulianza baada ya

    kugongana migongo wakati akirudi nyuma

    kutafuata uelekeo wa adui yake na adui yake

    akirudi nyuma kutafuta uelekeo wa Jenerali Kulika.

    Hapo mapigano ya gizani yalianza kwa namna ya

    kipekee na Jenerali Kulika alikuwa akimpiga adui

    yake kwa mapigo mbalimbali kutokana na adui

    huyo kuvaa koti la mikono la mirefu, kila adui

    aliporusha ngumi impate Jenerali Kulika

    ilipanguliwa kutokana na koti hilo alilovaa kutoa

    sauti kila anaporusha ngumi. Hiyo ndiyo ilikuwa

    nafasi nzuri kwa Jenerali Kulika ambayo aliitumia

    vizuri kwa kumshambulia adui yake kwa nguvu,

    adui yake alipozidiwa alijirusha kwenye dirisha la

    kioo hadi nje kwenye mwanga wa mbalamwezi ili

    aweze kumuona vizuri mtu anayekabiliana naye.

    Jenerali Kulika naye alimfuata adui yake huyo

    akidhani anamkimbia baada ya kuzidiwa na

    mapigano, aliruka dirishani akijua yake

    ameshaanza kukimbia ili amuwahi kabla hajafika

    mbali. Hakutambua kama ni hila ya adui yake ya

    kumvuta nje kwenye mwanga ili apambane naye

    vizuri, Jenerali Kulika alipotua nje baada ya kuruka

    dirishani alihisi sindanl ikipenya shingoni mwake.

    "hiyo sindano niliyokuchoma ina madawa ya kukupunguza nguvu, sasa jiandae kukikabili kifo

    chako ukiwa huna hata uwezo wa kupigana na

    mimi" Eagle ndiye aliyemwambia maneni hayo

    akiwa kasimama mkabala naye, Jenerali Kulika

    alianza kujihisi kichwa kimekuwa kizito na akawa

    haoni vizuri kutokana na dawa iliyomo katika

    sindano aliyochomwa ilikuwa ikifanya kazi mwilini

    mwake. Sindano hiyo ilifanya hata mwili wake

    usiwe na nguvu kabisa ingawa alihimili hata

    kusimama, alijua kapatikana tayari ingawa

    hakuhitaji kufa kizembe kama kondoo kwenye

    mdomo wa fisi wakati wa usiku. Alijitahidi

    kuonesha ukakamavu wake wa kijeshi

    uliomuwezesha kusimama kikamilifu akiwa

    amejizuia asiyumbe, nuru ya macho yake ilianza

    kupotea taratibu na akawa anamuona Eagle kwa

    mbali mithili ya mtumiaji wa miwani asiyeweza

    kuona bila kuvaa miwani. Eagle naye alipoona

    Jenerali Kulika amesimama huku akionekana

    ameishiwa alileta mapigo ya nguvu ya judo

    yaliyompata Jenerali ambaye alijaribu kuyazuia

    lakini hakuwa na nguvu hiyo, mapigo hayo

    yalimpeleka Jenerali Kulika chini huku akiwa

    ameumia baadhi ya sehemu za mwili wake.

    "sasa ukomandoo wako tuuone leo we kunguru,

    umeniulia vijana wangu pamoja na vijana wa

    mshirika wangu. Leo ndiyo kifo chako" Eagle

    aliongea kisha akajiandaa kuachia pigo la mwisho

    la kummaliza Jenerali Kulika, alitoka kwa kasi

    kisha akaachia mateke ya miguu miwili ambayo

    alilenga kifua cha Jenerali Kulika. Mateke hayo ya

    Eagle hayakumpata mlengwa na Eagle akajikuta

    akirudishwa na pigo takatifu la mtu ambaye

    aliongezeka katika mpambano huo, Eagle alianguka

    chini kwa nguvu hadi akahisi maumivu makali

    upande alioangukia. Alipoangaza mbele yake aliona

    watu watatu wameingia ndani ya eneo lake la

    pambano, wanaume wawili pamoja na mwanamke

    mmoja ndiyo waliyoingia ndani ya eneo hilo.

    "Eagle hatimaye tumeonana nadhani ulikuwa

    unanisikia, Kaila ndiyo nipo mbele yako sasa"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Norbert aliongea huku akikunja sweta la mikono

    mirefu alilovaa na pigo alilopigwa Eagle ni yeye

    ndiye aliloliachia. Eagle alipobaini ndiye mtu

    anayeamini alimuulia vijana wa three devil ndiye

    ambaye yupo mbele yake na tena kampiga pigo la

    nguvu ambalo lingeharibu kazi yake.

    "mtoeni General pembeni ili nishughulile na huyu

    mtu" Norbert aliongea huku akikunja ngumi

    ajiandae kupambana na Eagle ambaye alikuwa

    yupo chini hadi muda huo, alimuashiria Eagle

    ainuke ili apambane. Eagle naye alijiinua kwa

    namna kipekee kisha akarusha vitu mfano wa miiba

    kumlenga Norbert, Norbert alivikwepa vitu hivyo

    kisha akawa anamfuata Eagle kwa mateke mawili

    ya juu juu ambayo yalimpata Eagle sawia hadi

    akaachia mguno wa maumivu huku akiyumba

    wakati akijizuia asianguke.

    "ninja" Eagle alijisemea moyoni baada ya kuona

    silaha zake za kininja zikikosa lengo baada ya

    Norbert kuzikwepa, alijipapasa kiunoni akakuta ana

    kisu chake cha kininja kipo. Alimtazama Norbert

    aliyesimama mbele yake kisha akajifanya

    anajirusha teke halafu akakirusha kisu kumlenga

    Norbert kwa utalaamu wa hali ya juu, jambo hilo

    lilionekana na Norbert kwa haraka sana na kisu

    hicho kikaishia mikononi mwa Norbert kisha

    kikaridishwa tena kwake. Eagle alijikuta akiachia

    ukelele wa maumivu baada ya kisu hicho kuzama

    katika bega lake la kushoto, jinsi akivyochomwa

    hicho kisu alikiri anapambana na mtu kama yeye

    na hapo alikuwa keshampunguza nguvu kwa

    kumchoma kisu hicho. Jambo moja tu ndiyo

    lilibaki kichwani mwake alitaka ahakikushe

    linatimia ili aweze kupona, aliamua kurudi nyuma

    hadi jirani na uzio huku Norbert akimfuata taratibu.

    Eagle hakutaka kufanya makosa pale alipokaribia

    uzio wa nyumba hiyo na alitaka kufanya jambo hilo

    kwa manufaa yake, alipiga sarakasi moja kuuruka

    uzio wa nyumba hiyo akimuacha Norbert ndani ya

    uzio. Kukimbia ndiyo aliona suluhu ya

    kumuwezesha kuwa hai na si kupambana na mtu

    aliyempunguza nguvu kwa kumchoma kisu begani

    katika bega la mkono anaoutumia kwa kila kitu.

    "Nor achana naye si tuondoke na General tukampe

    tiba maana hii dawa akicheleweshwa hali yake

    itakuwa mbaya kwani inapunguza nguvu pia ni

    sumu inaua ikiwa mgonjwa hakutibiwa ndani ya

    siku nne" Hilda alimwambia Norbert ambaye

    alikuwa anataka kuruka ukuta.

    "hiyo ni sumu gani Hil?" Norbert aliuliza.

    "ni sumu ya kininja inayoua taratibu" Hilda alijibu.

    "poa tuondokeni" Norbert alisema huku akimsaidia

    Allison kumuinua Jenerali Kulika ambaye alikuwa

    tayari hajitambui hadi muda huo.



    ****



    SIKU ILIYOFUATA

    ASUBUHI



    KITUO CHA POLISI KILWA ROAD

    DAR ES SALAAM

    Askari aliyetumwa kupeleleza kifo cha Michael

    alipeleka ripoti yake ofisini kwa Inspekta Haroub,

    ripoti hiyo iliyomshangaza sana Inspekta Haroub

    ilikuwa na mashaka ya kifo hicho kuwa usalama

    wa taifa wanahusika.

    "staff sajenti hebu nieleze vizuri nikuelewe kuhusu

    hiyo ripoti ya upelelezi wako" Inspekta Haroub

    alihitaji ufafanuzi.

    "afande katika upelelezi wangu na kikosi

    nilichoingia kule South beach baada ya tukio

    nimeweza kubaini mambo mengi ikiwemo uhusikaji

    wa usalama wa taifa katika tukio lile, kwanza kabisa

    chumba kile kilichotokea tukio lile kilikuwa ni

    kimekodishwa na mkurugenzi wa Usalama wa taifa

    ndugu Reginald Kitoza na ushahidi juu yake ni huu

    mkanda wa kamera ya ulinzi wa siku hiyo

    uliyomrekodi wakati anaandikisha chumba hicho

    kwa jina la uongo. Pia uoo mkanda mwingine wa

    siku hiyo hiyo ukimuonesha akiingia ndani ya

    chumba kilichotokea mauaji siku aliyokodisha.

    Upande wa mwili tulioukuta mule ndani tumejaribu

    kutafuta taarifa zinazomuhusu yeye na tumezijua,

    kwanza si mtanzania bali ni raia wa Marekani na

    tulipotafuta taarifa zake kupitia mtaalamu wetu

    ndipo tulipobaki njia panda zaidi" Staff sajenti

    ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa maaskari

    waliokuwa wanaofanya uchunguzi wa mauaji

    yaliyotokea Hoteli ya South Beach alifafanua.

    Maelezo hayo yalimfanya Inspekta Haroub abaki

    anashangaa zaidi na akamuuliza, "Staff sajenti

    hebu eleza hizo taarifa zake zinahusu nini?".

    "mwili uliokutwa umeuawa ni mmojawapo wa

    wahalifu hatari wa kimataifa anayeunda kundi la

    Three devils walio chini ya jambazi na mhalifu

    aitwae Eagle, kundi hili limebainika kuingia

    Tanzania bila ya vyombo vya Usalama kutambuaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    na tumekuja kutambua baada ya huyu Michael

    kuuawa na wenzake asubuhi ya kuamkia leo

    wamekutwa wakiwa maiti katika ufukwe wa bahari

    maeneo ya Coco beach. Afande kutokana na

    umakini mdogo ndani ya nchi hii serikli imefanya

    kazi na mhalifu wa kimataifa wa Three devils

    ambaye ni Jim akiwa kama muwekezaji ambaye

    ameishi Tanzania kwa miaka mitatu hadi anakuta

    maiti ufukweni Coco beach" Staff sajenti aliongea.

    "Staff sajenti tusileweke wazi suala hili kwa

    usalama wa taifa hebu tumtaarifu IGP halafu

    tumuite mkurugenzi wa usalama wa taifa halafu

    tumuambie atoe maelezo jinsi anavyojua yeye

    halafu maneno yake ndiyo yatakayotupa mwanga

    wa tukio hili. Tumelewana?!" Inspekta Haroub

    aliongea.

    "ndiyo afande" Staff sajenti alijibu

    "ok subiri sasa niongee naye" Inspekta Haroub

    aliongea huku akinyanyua mkonga wa simu

    akauweka sikioni huku akibonyeza baadhi ya

    namba. Alisubiri baada ya muda mfupi kisha

    akaongea, "Jambo afande......afande ripoti ya

    upelelezi wa kifo cha mtu aliyekutwa amekufa

    imekamilika ingawa imejaa utata na mtatuzi wa

    utata huo ni wewe ikiwa tutakuja ofisini kwako

    sasa.........sawa afande tunakuja sasa hivi".

    Inspekta Haroub alipomaliza kuongea na simu

    alichukua kofia yake ya kipolisi iliyopo mezani

    ofisini kisha akaivaa halafu akasimama kwenye kiti

    halafu akasema, "Staff sajenti twende haraka sana

    IGP anatusubiri". Wote kwa pamoja walitoka hadi

    kwenye gari ya Inspekta Haroub kisha wakaingia

    na safari ya kuelekea ofisini kwa IGP ikaanza.



    ****



    WIZARA YA MAMBO YA NDANI

    MAKAO MAKUU JESHI LA POLISI

    DAR ES SALAAM



    Maelezo yaliyotolewa kwa Inspekta Haroub

    yalirudiwa tena mbele ya IGP Chulanga hatua kwa

    hatua hadi yakaisha, IGP Chulanga aliyasikiliza

    maelezo hayo kwa umakini hadi yalipomalizika.

    Uso wa mshangao ndiyo uliomtoka kwa maelezo

    aliyoyatoa Staff sajenti, uchunguzi uliofanyika ndiyo

    na ulimpa furaha ya kuwa na kijana mwenye

    umakini katika kazi.

    "kwanza napenda nikupongeze Staff sajenti kwa

    kazi nzuri uliyoifanya, sasa hapo mmesema utatuzi

    wa jambo hilo ni mimi kivipi" IGP Chulanga

    aliuliza.

    "mkuu tunahitaji Mkurugenzi wa usalama wa taifa

    anahusika vipi na kama inawezekana aje hapa

    ofisini kwa kumuita" Inspekta Haroub aliongea

    "ok" IGP Chulanga alikubali kisha akachukua simu

    yake ya mkononi halafu akabonyeza baadhi ya

    namba halafu akaiweka sauti baada ya simu

    kuanza kuita.

    "Kitoza upo wapi?" IGP aliuliza baafs ya simu

    kupokelewa.

    "nipo Obama avenue sasa hivi" Upande wa pili

    Kitoza alijibu.

    "ok unaweza kupitia ofisini kwangu mara moja

    kuna jambo la muhimu sana" IGP Chulanga

    alimwambia.

    "sawa nipe dakika kama kumi hivi nitakuwepo

    hapo" Kitoza alijibu kisha simu ikakatika.

    "tumsubirini" IGP Chulanga aliwaambia Inspekta

    Haroub na Staff sajent huku akiwaonesha ishara ya

    dole gumba kuashiria kuwa mpango wao

    umefanikiwa. Baada ya dakika kumi Kitoza alikuwa

    yupo ndani ya ofisi ya IGP Chulanga, hapo

    hakumkuta yeyote zaidi ya IGP mwenyewe.

    Alisalimiana na IGP Chulanga kisha wakaleta utani

    wa hapa na pale kama ilivyo kawaida yao.

    "Naam Chulanga vipi kuna habari gani?" Kitoza

    aliuliza.

    "habari iliyokuwepo hapa ni kuhusu mauaji

    yaliyotokea South beach, kwa mujibu wa upelelezi

    uliofanywa na vijana wangu imebainika kuwa kile

    chumba ni chako ulichopangisha toka muda mrefu.

    Je ofisi au wewe mwenyewe unahusika vipi?" IGP

    Chulanga aliuliza.

    "kuhusika kwa ofisi yangu ni hivi ule ulikuwa ni

    mpango ambao uliamriwa na mheshimiwa rais ili

    tuweze kumtia hatiani Kaila kwa kushirikiana na

    kachero wa FBI kutoka marekani ili tuweze

    kumkamata na matokeo yake ni kifo cha kachero

    huyo pamoja na kutekwa kwa Koplo Uyomo na

    Jackline ambaye ni kijana wangu" Kitoza alieleza.

    "ok inamaana uhalifu wa Kaila ni mkubwa hadi FBI

    aletwe nchini?" IGP Chulanga aliuliza.

    "ndiyo maana yake, kwa mujibu wa ripoti wa

    maelezo ya FBI mtu huyu ni gaidi hatari na wa

    kimataifa na anatumia uandishi wa habari kama

    mwamvuli wa kuficha uovu wake" Kitoza alizidi

    kuongea uongo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ok ni hayo tu, nadhani tungefahamishana kama

    na nyinyi mpo katika suala hili ili uchunguzi uwe

    mmoja" IGP Chulanga aliongea huku akimpa

    mkono Kitoza.

    "Sawa Chulanga, wacha mimi niwahi ofisini maana

    kuna kikao" Kitoza aliongea akiwa tayari

    ameshainuka kwenye kiti.

    "hamna shida" IGP Chulanga aliitikia na Kitoza

    ofisini hapo kisha akaondoka, Inspekta Haroub na

    Staff sajenti walirejea ofisini kwa IGP muda mfupi

    baada ya Kitoza kuondoka. Waliketi kwenye viti

    baada ya kutoa saluti kwa mara ya pili.

    "nadhani mmesikia maelezo ya Kitoza kupitia

    kamera ya ulinzi na kinasa sauti wakati mkiwa

    chumba cha kuongozea kamera?" IGP Chulanga

    aliwauliza.

    "Ndiyo afande na sasa naweza nikasema ana

    mahusiano na hawa wahalifu ingawa ushahidi

    sijaupata" Staff sajenti aliongea.

    "kivipi Staff sajenti?" IGP Chulanga aliuliza.

    "kwanza jambo kama hilo ubalozi wa Marekani

    nchini lazima wawe na taarifa ya ujio huu na hata

    wizara ya mambo ya ndani lazima wawe na taarifa

    juu ya ujio wa makachero, taarifa ikifika wizara ya

    mambo ya ndani lazima ikufikie kwasababu ni ya

    kiusalama. Kama taarifa hamna na ubalozi wa

    Marekani wamekana hao sio watu wa FBI unafikiri

    kuna nini hapa kama sio mchezo mchafu" Staff

    sajenti alieleza.

    "Staff sajenti ni sahihi uyasemayo maana

    haiwezekani wanausalama kutoka Marekani

    waingie nchini halafu ubalozi wa Marekani usiwe

    na taarifa. Tovuti ya FBI,NSA na CIA zinaonesha

    kuwa watu wale ni mojawapo ya wahalifu

    wanaotafutwa. Pia shirika la M16 la Uingereza na

    KGB la Urusi nayo yanatambua watu hawa ni

    watuhiwa" Inspekta Haroub aliongezea huku IGP

    akitikisa kichwa kukubaliana na maelezo yao

    "hadi sasa sina imani na idara ya usalama wa taifa

    nafikiri msaada tuombe kwa EASA hawa

    watatusaidia na simuamini tena Kitoza" IGP

    Chulanga aliongea kuwaambia vijana

    wakiofanikisha macho yake yakafunguka na akajua

    asivyovijua, hakika, aliona kuna namna

    inayoendelea ambayo yeye haijui.

    "vijana suala limefika kwangu na nitahitaji kuonana

    na CE wa EASA leo ili atusaidie katika hili,

    mnaweza mkaenda" IGP Chulanga aliwaambia

    vijana ambao waliinuka kwenye viti kisha wakatoa

    saluti halafu wakatoka nje ya ofisi hiyo.



    MGAHAWA WA CITY GARDEN

    DAR ES SALAAM



    Baada ya masaa kadhaa toka IGP Chulanga alipoongea na vijana wake, alikuwa tayari ameshampigia simu kiongozi wa EASA kanda ya Dar es salaam na sasa wapo wote ndani ya mgahawa wa City garden uliopo katikati ya jiji. CE ambaye ni kiongozi wa Norbert, Hilda na Allison ndiye aliyekuwa aliyehitajika na IGP Chulanga. Eneo lililo tulivu ndiyo lilichaguliwa kwa ajili ya mazungumzo yao na ukosefu wa raia wa kawaida karibu walilopo, ndiyo kulitoa uhuru mzuri kwa ajili ya mazungumzo yao. Vyakula vinavyopendelewa na kila mmoja ndiyo vilikuwa juu ya meza zao, kinywaji kinachopendelewa na kila mmoja ndiyo kilikuwa pembeni ya meza hizo. Maelezo ya dhumuni la kukutana hapa yalikuwa tayari yameshatolewa na IGP Chulanga kwa kirefu zaidi, CE naye alikuwa tayari ameshayasikiliza maelezo hayo kwa umakini na sasa alikuwa akitafakari juu ya maelezo hayo pamoja na kuisoma akili ya IGP Chulanga kupitia hayo maelezo hayo. CE ambaye umri unaonekana kumtupa mkono na mwili wake bado unaonekana ni kijana kutokana na mazoezi makali anayofanya, aliamua kutumia akili yake ya kijasusi katika kumtazama mtu usoni katika baadhi ya milango ya fahamu ili amuone kama anababaika katika maelezo yake au ni miongoni mwa waongo. Aliporidhika na ukweli wa maneno ya IGP Chulanga aliamua kumuuliza, "je suala hilo limeshikana kabisa katika ofisi zako?"



    "ndiyo CE na nimeomba msaada huku kwako kwani usalama wa Taifa sina imani nao kabisa" IGP Chulanga aliongea.



    "ok...napenda utambue kuwa vijana wangu wapo kazini siku nyingi na hata taarifa za ujio wa hao wanarekani pamoja na bosi wao ninazo" CE aliongea kisha akaweka kituo huku mkono mmoja ukishikilia bilauri yenye shurubati yake aliyoiagiza, alikunywa funda moja kisha akaendelea "vifo vyao vyote ni kazi ya vijana wangu, pia napenda utambue kuwa kijana wako aliyesadakika ametekwa tayari yupo kwenye mikono salama ya vijana wangu ambao kwako wanafahamika vilivyo ingawa sitaweza kukutajia majina yao".



    "inamaana jambo hili nalitambua siku nyingi sana? IGP Chulanga aliuliza, CE aliposikia swali hilo aliingiza mkono katika mfuko wa koti la alilolivaa kisha akatoa picha ambayo alimpatia IGP Chulanga.



    "ndiyo natambua, hivi huyo mtu unamtambua?" CE alimuuliza IGP Chulanga kuhusu mtu aliyepo kwenye picha



    "anaitwa Hilton Roy raia wa kimarekani ambaye ni tajiri mkubwa sana katika jiji la Miami, pia juzi amewasili nchini kufanya ziara ya utalii" IGP Chulanga alitoa ufafanuzi.



    "je huna unachokijua juu yake zaidi ya utambulisho huo?" CE aliuliza.



    "sina zaidi ya utambulisho huo niliokwambia" IGP Chulanga alijibu.



    "huyu mtu anaitwa Hilton Roy alimaarufu kama Eagle the don ni mmoja wa mafia wa wahalifu ndani ya dunia hii, napenda utambue yupo nchini kwa ajili ya kukamilisha kazi iliyomleta na si vinginevyo" CE alitoa maelezo hayo yaliyomshtua sana IGP Chulanga.



    "inamaana nchini kwetu tunafuga wahalifu bila kujijua" IGP Chulanga aliongea kwa mshangao.



    "Chulanga hii ishu ni nyingine kabisa na vijana wako hawaiwezi, hivyo tuachie sisi na wewe unatakiwa upate kile kibali kitakachokuwezesha kumkamata kiongozi yoyote wa nchi" CE aliongea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "kwahiyo anashirikiana na kiongozi ndani ya serikali yetu" IGP Chulanga aliuliza.



    "Chulanga hayo maelezo mengine siwezi kukupatia kwa sasa, fanya kama nilivyokuambia na maongezi yetu mimi na wewe yasifike kwa yoyote......narudia tena yasifike kwa yeyote ikiwa unataka suala hili lipatiwe ufumbuzi mzuri kutoka kwa vijana wangu. Hata mkuu wa nchi unayemuheshimu kama mkubwa wako hatakiwi kupewa maelezo haya" CE aliongea kwa msisitizo.



    "sawa nimekuelewa" IGP Chulsnga alitii agizo hilo.



    "pia vijana wako wasiliingilie suala hili kabisa isipokuwa mpelelezi wangu wa siri aliyepo katika jeshi lako na mwingine aliyepo usalama wa taifa ambao hata wewe huwatambui" CE alitoa agizo.



    "sawa nimekuelewa, majukumu yote nawapa nyinyi" IGP Chulanga aliongea.



    "umefanya uamuzi mzuri sana kunishirikisha katika jambo hili, pia umefanya uamuzi mzuri sana kutokuwa na imani na usalama wa taifa" CE alimpongeza IGP Chulanga kisha akasema, "wacha niwahi ofisini mara moja".



    "Hamna shida, tutaonana siku nyingine" IGP Chulanga aliongea huku akimpatia mkono wa kuagana CE.

    "ok, jioni njema iwe nawe" CE alijibu huku akiondoka ndani ya eneo la Mgahawa huo.



    ****





    SAFE HOUSE

    JIJINI DAR ES SALAAM



    Ndani ya nyumba hii ambayo huwekwa watu kisiri kwa sababu za kiusalama na yenye ulinzi kila kona yake, kulikuwa kuna watu wawili ambao walikuwa wakiongea katika chumba cha matibabu cha nyumba hiyo. Rais Ole pamoja na Eagle ndiyo watu waliokuwa wakiongea ndani ya chumba hicho, Eagle alikuwa kazungushiwa bendeji kubwa yenye dawa katika kidonda chake akiwa kifua wazi. Rais Ole alikuwa ameleta jambo ambalo lingewasaidia katika kushinda vita yao na ingahitajika atumie mbinu ya ziada, ameamua kumshirikisha Eagle ili suala liishe kimya kimya.



    "kesho kutwa ni siku ya mimi kuwa na mkutano wa chama changu ambacho ni chama cha nchi kwa sasa hivyo kuhutubia kwangu katika mkutano huo ndiyo siku nitakayokukabidhi ardhi yenye madini ya almasi ya kule Kondoa, hivyo kabla mkutano hsujafika haya magugu yaliyobaki yanahitaji jembe yang'olewe na makwanja yameshindwa hivyo nimekupa wewe jembe ushirikiane nayo" Rais Ole aliongea.



    "Hilo usiwe na hofu nalo na usiku wa kuamkia siku hiyo itakuwa siku ya kulipa kisasi kwa huyu Kaila kwani nitakuwa nimejiandaa vizuri, pia nahitaji kikosi cha vijana wa kazi kwani hayupo peke yake" Eagle aliongea baada ya kusikiliza maneno ya rais Ole.



    "hivi huyu Kaila ni mtu wa aina gani? Si mwandishi wa kawaida tu sasa mbona ana uwezo wa kufanya haya mambo?" rais Ole aliuliza.



    "Ole ukae ukijua Kaila si mtu wa kawaida bali nilikuwa napambana na ninja mwenzangu na ameniwahi, sasa kesho ndiyo itakuwa kiama chake kwani nitakuwa nimejiandaa" Eagle aliongea maneno yaliyomfanya rais Ole ashangae.



    "hivi kwanza mwandishi wa habari atakuwa ana mafunzo ya kininja kivipi, sio mwanausalama huyu" Rais Ole aliongea kwa mshangao.



    "kwani hapa Tanzania kuna wanausalama wa siri zaidi ya hawa wa Idara ya usalama wa taifa" Eagle aliuliza.



    "ndiyo wapo tena hao ni hatari zaidi na sidhani kama wamejua kinachoendelea" Rais Ole aliongea.



    "una uhakika gani Ole?" Eagle alimuuliza.



    "habari zao zota tunazipata kupitia kwa kibaraka wetu aliyepo makao makuu yao ya Dodoma" rais Ole aliongea.



    "ok sasa kazi inaisha kesho nina uhakika huo na hawa wanausalama wa usalama wa taifa inabidi wachunguzwe wote kabla kazi haijaanza. Nahisi kuna mtu ana mawasiliano na Kaila na ndiye anayevujisha siri zetu, haiwezekani mpango wa kumuua Kulika uwe unajulikana na Kaila wakati siku ile tulipanga kwa siri bila hata kumshirikisha Gawaza" Eagle aliongea.



    "ni kweli uyasemayo inabidi uchunguzi ufanywe tena uongozwe na Gawaza maana yeye ndiye mwaminifu kati ya wanausalama hawa, nafikiri atatusaidia" Rais Ole aliongea jambo lililoafikiwa na Eagle moja kwa moja.



    "sawa nimekuelewa" Eagle aliitikia.



    "tuna siku moja ya kukamilisha kazi hii ili tuwe na amani, nayo ni usiku wa kesho tu. Sasa na hadi usiku unaingia utatakiwa kupumzika ili hilo jeraha la kisu likauke kidogo" Rais Ole alimwambia Eagle huku akitoka nje ya chumba cha matibabu.



    ****



    Jioni ilipowadia tayari Jenerali Kulika alisharejewa na fahamu ingawa hakuwa na nguvu, alipoangalia pembeni yake alikuta dripu ya dawa ikitiririka katika mshipa wake wa damu, pembeni yake kulikuwa kuna binti aliyevaa koti la kitabibu akiwa amempa mgongo akisoma faili alilolishika mkononi. Mazingira ya chumba hicho yalikuwa yanafanana na hospitali kwa kiasi kikubwa ingawa haikuwa haikujulikana ni hospitali ipi. Jenerali Kulika alipofungua jambo la kwanza kulifanya ilikuwa ni kuangalia nembo ya shuka iliyokuwa imemfunika ili ajua kama yupo hospitali au yupo sehemu nyingine, alitegemea katika shuka lililopo kitandani hapo litakuwa na maandishi ya MSD yakimaanisha kifupi cha bohari kuu ya dawa lakini haikuwa hivyo, nembo ya EASA ndiyo ilikuwa kwenye ikimaanisha yupo katika mikono ya wapelelezi, Jenerali Kulika alipoona hivyo alitaka kujiinua kitandani hapo kwa kujilazimisha lakini akashindwa na kubaki akihema tu.



    "General inabidi upumzike kwanza ili dawa iliyopo kwenye dripu iishe na nguvu ndiyo itarudi mwilini" Sauti ya binti aliyevaa koti la kitabibu ilimwambia kisha binti mwenyewe akageuka, hakuwa mwingine bali ni Hilda akiwa amevaa miwani.



    "nimefikaje hapa? Ni wapi hapa?" Jenerali Kulika aliuliza maswali mawili kwa haraka.



    "hapa ni ndani ya nyumba ya EASA na umefika hapa baada ya jana kuokolewa katika kuuawa na mhalifu wa kimataifa" Hilda alimjibu, jibu hilo lilisababisha kumbukumbu za Jeneralu Kulika zimrudishe siku ya iliyopita alipovamiwa hadi alipoishia kukumbuka. Ujio wa watu watatu ambao hakuwa anawaona vizuri kutokana na sindano aliyochomwa ndiyo aliukumbuka, wawili kati ya watu hao walipokuwa wanatazama hali yake huku mmoja wao akipambana na adui yake pia alikumbuka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sisi ndiyo tumekuokoa ili usiuawe na Eagle usiku uliyopita, nadhani unanifahamu kwa jina la Hilda. Nafahamika kama AL002 ndani ya EASA" Hilda aluongea huku akimuonesha Jenerali Kulika kitambulisho chake, Jenerali Kulika alitikisa kichwa kukubaliana na maneno ya Hilda.



    "kwa sasa unahitajika upumzike na tutakuja baadaye tukiwa pamoja ili kukupa maelezo zaidi" Hilda aliongea huku akitoka nje ya chumba alicholazwa Jenerali Kulika. Hilda alitokea kwenye korido ya nyumba ya kampuni yao anayoishi pamoja wenzake wa WAHANGA na polisi waliyemuokoa katika mdomo wa mamba ambaye ni Koplo Uyomo. Alienda hadi sebuleni ambapo aliwakuta Norbert, Allison, Davis, Joseph na Koplo Uyomo wakiongea huku wakicheka, Hilda alipofika hapo alienda kukaa kwenye paja ya Norbert makusudi.



    "oyaaa ndiyo unaturusha roho sio" Allison aliongea kumuambia Hilda ambaye aliishia kucheka.



    "Dah! Mahaba niue hao kwa visa hawajambo" Davis naye alidakia.



    "Mr and Mrs Smith wa Afrika hao" Koplo Uyomo naye alidakia.



    "Koplo Chauchu nawe wa kwako yupo basement nadhani unamkumbuka yule mama Mawowowo" Norbert alimtania Koplo Uyomo huku akiwa ameshika kiuno cha Hilda.



    "Dah! Yule ni demu au jike dume maana sielewi, kwani kifinyo alichonipa sina hamu nae " Koplo Uyomo aliongea na kusababisha wenzake wote wacheke.



    "jamaa alipoona zigo la Jackline akadata....Koplooo uliona umepata kumbe umepatikana. Uyomo sikia nikuambie, ukitaka kuoa chagua mwenye mzigo maana ndiyo unakudatisha" Allison aliongea.



    "Uyomo hivi uzuri wa mwanamke ni nini?" Hilda alitumbukuza swali walipokuwa katikati ya maongezi.



    "uzuri wa mwanamke ni tabia" Koplo Uyomo alijibu.



    "kama uzuri ni tabia kama unavyodai, mbona we unadata na fungashio au ndiyo tabia ilipo huko" Hilda aliuliza kimasihara.



    "we Mtusi ya Ngoswe muachie Ngoswe usitake kujua kwanini aliitwa Ngoswe" Joseph naye aliongea kumuambia Hilda.



    "khaa! Kuwa mtusi imekuwa nongwaeh?!" Hilda aliuliza kwa mshangso.



    "na Uyomo kupenda mawowowo imekuwa nongwaeh?!" Davis naye alidakia



    "mtoto wa kike mie nyie siwawezi bora nikae kimya tu" Hilda aliongea.



    "kwanza vipi huko General ameamka?" Norbert aliuliza kuipoteza mada iliyokuwa inazungumzwa.



    "tayari ameshaamka" Hilda alijibu huku akiwa ameweka mkono shingoni mwa Norbert.



    "oyaa Allison andaa vitu tukamfumbue macho na yeye aijue nchi yake na maovu yaliyopo" Norbert alimwambia Allison huku akimuinua Hilda kutoka pale alipokaa kisha akamuashiria kwa mkono Allison na Hilda wamfuate.



    *****



    SAA NNE USIKU

    Baada ya Jenerali Kulika kurudiwa na nguvu alioneshwa mikanda ya video yote iliyorekodiwa ikimuonesha rais Ole na wenzake wakipanga mikakati mbalimbali ya siri, kikao cha wanausalama wapatao sita kiliitishwa ndani ya chumba cha mkutano katika nyumba ya EASA. Jenerali Kulika, Brigadia Belinda, Norbert, Allison Moses na Hilda ndiyo wahudhuriaji wa mkutano huo. Ajenda ya mkutano huo ilikuwa ni kujadili ukombozi wa taifa la Tanzania pamoja kuondoa utawala wa kidhalimu uliopo, mikanda ya video ya matukio ya kupanga mikakati mbalimbali ya maovu iliyorekodiwa bila rais Ole na watu wake kujua ndiyo ilikuwepo eneo hilo. Ilikuwa ni jambo linalosikitisha kwa watanzania kuweka imani zao kwa mbwa mwitu aliyejivika ngozi ya kondoo, kufanyiwa hujuma kwa mgombea urais wa RPP ndugu Mtalemwa pamoja na kupandikiziwa chuki chama chake ni kitu ambacho wanausalama hawa wahisi watanzania wamemkosea sana Mtalemwa.



    "jamani nadhani mnatambua jinsi hali ilivyo katika uwanja huu na itahitajika tufanye jambo ili kuinusuru nchi hii. Nadhani tumsikilize kwanza ndugu Moses Gawaza kutoka usalama wa taifa atuambie juu ya hali inavyoendelea" Jenerali Kulika aliongea.



    "Asanteni ndugu wazalendo wa taifa hili pamoja na wa Afrika ya mashariki kwa ujumla kwa kunipa nafasi ya kuongea. Kifupi ni kwamba usiku wa kesho ndiyo kumepangwa kuangamiza vikwazo vya rais Ole vyote wakianza na waziri wa mambo ya nje mheshimiwa Zuber Ameir, pia usiku huo wa kesho ndiyo siku ya kuhakikisha kuwa ardhi yenye madini mengi ya Kondoa ndani ya taifa hili iliyopo Kondoa inaenda katika mikono ya Hilton Roy maaarufu kama Eagle. Hadi kuamkia kesho kutwa kama hayo mambo yatakuwa yametimia basi rais Ole ataendelea kuinyonya nchi hii na baada ya mkutano wake wa chama unaofanyika keshokutwa katika viwanja vya jangwani ndiyo Eagle atapanda ndege kurudi Marekani. Ni hayo tu" Moses alimaliza kisha akaketi akimuacha Jenerali Kulika akiwa amesimama tena.



    "Nadhani mmemsikia Gawaza sasa ni muda wa sisi kupanga mikakati ya kuhakikisha tunawaokoa mawaziri wa chama RPP, kuhakikisha kambi ya usalama wa taifa yote inaangamizwa, viongozi wa chama cha PTP wote wanatiwa mbaroni. Yote haya yanatakiwa yafanyike usiku wa kesho na yakamilike usiku huohuo. Pia kesho kutwa viwanja vya jangwani kwenye mkutano wa PTP inatakiwa kila raia ajue uovu wa rais wao Filbert Ole. Sasa basi mipango yote ya jinsi ya kuifanya kazi ipo kwa Brigadia Belinda...... Brigadia Belinda karibu tafadhali" Jenerali Kulika aliongea kisha akatoa ukaribisho kwa Belinda. Belinda alisimama kikamavu kisha akatoa saluti kwa Jenerali Kulika halafu akawasalimia wote waliomo humo ndani.



    "katika kuifanya operesheni hii inayoitwa UFAGIO WA CHUMA tumegawanya katika makundi yafuatayo. Kundi A hili litashughulika kwenda kuwakomboa mawaziri wa RPP pale Serena hotel ambapo wana kikao kesho usiku, kundi hili litaongozwa na Norbert Kaila na Hilda Alphonce kwa kushirikiana na wanajeshi kadhaa wa kikosi cha ardhi. Kundi B hili litashughulika na kuiteketeza kambi yote ya usalama wa taifa hili pamoja na kuwatia mbaroni viongozi wote wa PTP kasoro rais na kundi hili litaongozwa na Allison na pamoja na mimi mwenyewe pamoja na kikosi cha jeshi la ardhi. Kundi la mwisho ni C ambalo litashughulika na kuwafumbua macho watanzania katika viwanja vya jangwani kwenye huo mkutano ambao utaangaliwa na raia karibia nchi nzima kwenye televisheni pamoja na kusikilizwa na kwenye redio, kundi hilo litaongozwa na Jenerali mwenyewe akishirikiana na Moses Gawaza wa usalama wa taifa pamoja na kikosi cha maluteni wa idara ya mawasiliano wa kikosi cha Kambi kuu ya jeshi. Ni hayo tu" Belinda alitoa mpango mzima wa operesheni ya UFAGIO WA CHUMA itakavyofagia kisha akaketi chini baada ya kutoa saluti kwa mara ya pili. Jenerali Kulika alisimama tena kisha akasema, "kuna mwenye la ziada?". Wu wote walikaa kimya kuashiria hakuna la ziada.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "kuanzia hivi sasa hadi kesho ndiyo itakuwa muda kupumzika kwani kesho usiku UFAGIO WA CHUMA unapita hivyo kulala hakuna. UFAGIO WA CHUMAA!"Jenerali Kulika aliongea huiu akiwapa ari wote kwa kutamka kauli mbiu ya operesheni hiyo.



    "FAGIAAA!" wote kwa pamoja walimalizia kauli mbiu ya operesheni hiyo wakiwa wamesimama huku wakinyoosha mkono mbele kwa pamoja, mkutano uliishia hapo na kila mmoja akiwa kajua majukumu yake ya kufanya.



    Hatimaye siku mpya ikaanza kwa kuonesha nuru ya asubuhi iliyotukuka na viumbe wenye kuikaribisha siku mpya nao wakaimba kuikaribisha siku hiyo, muda huu ulikuwa ni muda wa kupumzika kwa wanausalama wote wenye kuendesha operesheni FAGIO LA CHUMA. Vitanda walivithamini kuliko kitu chochote kwa asubuhu hiyo kutokana na kazi nzito wanayotarajia kuifanya usiku wa siku hiyo, mchana ulipoingia kwao ndio waliona ni asubuhi na walikuwa wakifanya mazoezi mbalimbali kuweka miili yao sawa ili waweze kuiendesha operesheni yao vizuri. Jioni ilipowadia wote walikutana kambi ya jeshi la anga iliyopo jirani na uwanja wa ndege. Mavazi maalumu ya kazi hiyo ndiyo waliyokuwa wameyavaa, wote kwa pamoja walivaa gwanda kijeshi pamoja na kofia nyekundu nyekundu kichwani, si wanausalama wa EASA wala jeshini wote walivaa gwanda hizo na mifukoni walisheheni silaha za aina mbalimbali. Sikioni kwa kila mmoja kulikuwa kuna simu ndogo isiyojulkana kwa urahisi ikiwa imewekwa ndani ya ustadi mkubwa, hakika walijiandaa operesheni kuitekeleza.



    "sasa ni muda wa kazi na inabidi tufanye kazi, FAGIO LA CHUMAAA" Jenerali Kulika aliongea.



    "FAGIAAAA", wote kwa pamoja waliitikia kwa kunyoosha mikono yao iliyobeba silaha juu. Kikosi hicho kilijigawa kisha kikaingia kazini mara moja kwa kutangulia vikosi viwili huku kimoja chenye kazi asubuhi inayofuata kikisalia hapo kambini ili kuwapa mawasiliano na mwongozo wenzao.



    ****



    KAMBI YA USALAMA WA TAIFA

    DAR ES SALAAM



    Muda huo huo wakati watu wa operesheni ya FAGIO LA CHUMA wakajiandaa kwa ajili ya kuingia kazini, tayari vijana wa usalama wa taifa wapatao kumi wakiwa pamoja na Eagle na Kitoza walishajianda na sasa ndiyo wapo njiani kuelekea Serena hotel kwenye mkutano wa mawaziri wa chama RPP ukiongozwa na waziri Zuber Ameir. Wote kwa pamoja walikuwa wamevaa suti safi zenye kuvutia na walikuwa wamebeba silaha zao kwa kuzificha, magari mawili ya kifahari ndiyo yalitumika katika msafara wao katika kuelekea katika hoteli hiyo ya kifahari. Kimuonekano walikuwa ni watu wenye pesa zao waliokuwa wakienda kwenye hafla usiku huo au sherehe waliyoalikwa, magari waliyopakia yote yaliashiria wao ni watu wenye pesa zao.



    ****



    SERENA HOTEL

    DAR ES SALAAM



    Chumba cha mkutano kilicho na hadhi ya kukaliwa na watu wazito wa serikalini kilikuwa na mkutano mkubwa wa mawaziri wapatao sita pamoja na wanachama wengine wa juu wa chama cha RPP, wote kwa pamoja waliketi katika meza moja yenye viti kadhaa vilivyokuwa vikitazamwa na kiti kimoja kilichokaliwa na mzungumzaji mkuuwa mkutano huo ambaye ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na pia ni katibu mkuu wa chama cha RPP. Zuber Ameir ndiye msemaji mkuu wa mkutano huo

    na wengine walikuwa ni wasikilizaji.



    "jamani kama mnavyotambua juu ya mstakabali wa taifa hili, hali ni mbaya sana kwani hadi sasa tumeshampoteza mwenzetu Shehoza aliyetaka kutumia rasilimali zetu kwa maslahi ya watanzania. Ikiwa sisi ni wazalendo tupo tayari kwa lolote, kwanini tusitafute njia mbadala ya kupambana na hali hii. Haiwezekani Tanzania yetu yenye rasilimali nyingi ziwe zinaingia katika mikono ya wati wengine wasiohusiana na nchi hii, wazalendo wenzangu inabidi tuhakikishe suala hili linafikiwa ufumbuzi kabla mambo hayajawa mabaya" Zuber Ameir aliongea katika mkutano huo baada ya kuwasalimia wenzake wote waliomo humo ndani.



    "najua chama chetu kimepandikiziwa hila za kutaka kisipendwe na wanachi na hilo limefanikiwa, lakini hawawezi kuzuia mimi nisipendwe na wanachi ndiyo maana ninayeangaliwa kumalizwa ni mimi kuliko hao wengine. Shetani ameingia madarakani na alitaka kuniacha lakini mapenzi ya wananchi kwangu bado yatabakia, jamani kesho nadhani mnatambua ndiyo siku ya mkutano wake na chama chake katika viwanja vya jangwani. Inabidi kesho hiyohiyo ndiyo iwe siku ya kumuangusha huyu shetani na si vingine..." Zuber Ameir alishindea kumalizia kauli yake baafa ya mlango mkuu wa kuingilia chumba hicho kupigwa teke, mlangoni walionekana watu wawili wenye suti nadhifu wakiwa wameshika bastola zenye viwambo vya kuzuia sauti. Eagle na Kitoza ndiyo watu walioingia humo ndani wakiwa wamekuja kishari zaidi ingawa nyuso zao zilikuwa zimepambwa na tabasamu.



    "Eti mnajiita wazalendo wakati mmezaliwa kwenye ahida na mmekulia kwenye shida, eti mnatetea haki za wananchi wakati hawana faida yoyote kwenu zaidi ya kuwapigia kura tu. Mlipewa nafasi zenu katika wizara tofauti lakini hamkutambua kama mnapewa umauti. Sasa leo ndiyo mwisho wenu" Kitoza aliongea huku akiichezea bastola aliyoishika.



    "ardhi ni yenu lakini rasilimali aio zenu bal ni za wenye nazo kama sisi, pia kupata rasilimali hizo msahau ni mali ya wageni kama sisi tu" Eagle aliongea.



    "nashangaa mnajiita watetezi wa wananchi na mnapiga kelele kila muwapo bungeni lakini hamna lolote zaidi ya kupendwa na wananchi na juhudi za matunda yenu kwao hayaonekani, mnalipwa pesa na mnakaa pamoja na familia zenu kwa raha na mkiishia kupiga kelele tu zisizo na faida juu ya rasilimali. Rasilimali mnazijua nyinyi badala ya kuungana na mtu kama mheshimiwa ili mle maisha na mambo wananchi wasio na maana kwenu mkaachana nayo" Kitoza aliongea kwa kejeli.



    "yaani hata mwenye nyumba awe mwii kamwe hawezi kung'atwa na mbwa wake hata siku moja, Kitoza wewe ni mbwa na Ole ni mwenye mbwa sasa lazima uwe upande wake siku zote. Pia ishu ya kula vya haramu hatutaki na tutapigana mpaka tufikie mafanikio na kuondoa uongozi wa kidhalimu pamoja na nyinyi mafirauni kufa moja kwa moja" Barnabas Dickson ambaye ni waziri wa mambo ya ndani aliongea.



    "Sasa tuone kati yetu sisi mnaotuita mafirauni na nyinyi, wapi wataokufa" Eagle aliongea huku akisogea karibu na meza hiyo sambamba na Kitoza, alipokaribia alinyoosha bastola yake mbele huku akiruhusu risasi ziende chemba. Alipotaka kufyatua alishtukia amechomwa kisu cha mkono uliokamata bunduki na Kitoza naye hali ilikuwa hivyohivyo, mguno wa maumivu uliwatoka huku kitambaa cha meza kubwa ya mkutano iliyopo hapo ndani kikifunuliwa na wakitokeza watu wawili waliovaa magwanda ya kijeshi wakiwa na kofia nyekundu kichwani. Kitoza, Eagle pamoja na mawaziri hao wote walishangaa na hakuna hata mmoja aliyetambua uwepo wa watu hao chini ya meza, watu hao walikuwa wameinamisha sura zao chini na walipoinua ndipo walipotambulika na watu waliopo eneo hilo. Norbert na Hilda ndiyo waliokuwa wapo mbele yao wakiwa wanawatazama Eagle na Kitoza kwa dharau. Bastola zilizokuwa zipo mikononi mwa Kitoza na Eagle zilikuwa zimeshaanguka chini na zipo umbali wa mita kadha kutoka mahali waliposimama, Kitoza aligeuza jicho kuitazama bastola yake ili aangalie uwezekano wa kuweza kuipata.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Usije ukajaribu kuinua mguu wako kutoka hapo ulipo la si hivyo utakuwa maiti kama wenzenu mliokuja nao na nadhani umeona kiwambo cha sauti hiki, hatasikia yoyote nje ya humu" Hilda aliongea huku akimelekezea bastola Kitoza ambayo tayari alishaichomoa kiunoni mwake. Hilda alienda kufunga mlango kisha akawaambia, "nyie wanawake leo hatitumii silaha yaani mikono tu", kisha akapiga risasi ukutani hadi bastola ikaisha risasi. Maneno hayo yalimuudhi sana Kitoza na akajikuta anamfuata Hilda kwa mapigo tofauti ya karate yaliyopanguliwa huku kichapo kizito kikimshukia, kila alipojaribu kutumbukiza pigo lake aliambulia patupu na akajikuta anapigwa hadi anavunjwa miguu. Eagle naye alipoona Norbert anaangalia mpambano wa Kitoza na Hilda, alijaribu kujibinua sarakasi kuelekea pembeni ili aokote bastola yake. Sarakasi hiyo haikusaidia kitu kwani Norbert alikuwa ameshamuona na aliitambua hiyo hila yake. Teke zito la tumbo kutoka kwa Norbert lilitua tumboni mwake alipokuwa yupo juu juu baada ya kupiga sarakasi, Norbert alipompiga teke hilo alikunja miguu haraka kisha akatoa ukelele wa kininja. Eagle alijibetua kutoka pale chini alipo kisha akaanza kuweka ishara ya vidole kama wafanyavyo maninja huku Norbert naye akifanya hivyohivyo. Mpambano baina yao ulianza baina yao kwa kasi na kwa kutumia ujuzi wa kipekee walionao, walipigana kwa nguvu zote huku waliobaki kuwa waangaliaji kutokana na sheria za kininja kutoruhusu kuingilia mpambano baina ya ninja wawili. Eagle alikuwa kapania kumshinda Norbet ndani ya usiku na aliamua kuja na mapigo mfululizo ambayo yalipanguliwa na Norbert na mengine kupiga hewa. Norbert alifanya kazi ya kukwepa mapigo hayo bila hata kushambulia hadi pale Eagle alipoanza kuchoka kutokana na kutumia nguvu wakati anaachia mapigo hayo. Hapo ndipo alipoanza kupata mapigo ya judo mfululizo kutoka kwa Norbert yaliyompata yote hadi akawa anayumba, Eagle alijitahidi kuchanganya hadi mapigo ya kombat katika mpambano huo lakini aliishia kuumia tu kwa mapigo ya Norbert. Eagle aliamua kupiga teke la mauaji la mchezo wa kombat ambalo lingempata Norbert basi angekuwa marehemu, ni teke la hatari alililenga shingoni mwa Norbert lililoambulia patupu baada ya Norbert kulikwepa. Eagle alijikuta akipigwa teke la mchezo hatari wa jeet kune do ambao ni mchezo wa mapigano nambari tatu kwa hatari ambo ulianzishwa na mcheza filamu wa kichina aitwae Bruce Lee ambaye ameacha historia kubwa katika ulimwengu wa mapigano, sauti ya kuvunjika kwa mbavu ilisikika kisha baada ya teke hilo kumpata eneo la mbavu za kushoto jirani na eneo lililopo moyo. Eagle alitoa mguno wa maumivu bsada ya kuhisi moyo wake ukitobolewa na kipande cha mbavu akiwa amepiga magoti baada ya pigo lile kumyumbisha.



    "Eagle umekwisha na hustahili kufa kifo cha heshima ya kininja" Norbert aliongea kisha akampiga Eagle mateke ya kifua ya miguu miwili hadi akaenda chini kisha akajiinua kidogo halafu akaanguka chini, safari ya Eagle duniani ndiyo ikawa imefikia tamati baada ya kuanguka chini kwa mara ya pili.



    "Norbert Kaila au N001 wa EASA, waheshimiwa IGP apigiwe simu na apewe taarifa za kuuawa kwa Eagle na Kitoza pia habari hizi zifike kwa vyombo vya habari hadi kazi itakapokamilika" Norbert aliongea huku akitoa kitambulisho chake cha kazi baada ya utambulisho wake ili awatoe hofu mawaziri pamoja na viongozi wa RPP.



    "Wee mbwa sijafa bado na usinitangaze nimeku.." Kitoza aliongea baada ya kusikia Norbert amemtaja miongoni mwa wafu na alishindwa kumalizia kauli yake baada ya kisu kutua kwenye koo lake kikitokea kwa Norbert.



    "Ushakufa tayari" Norbert aliongea huiu akimwangalia Kitoza halafu akawageukia mawaziri wa RPP halafu akawaambia, "Tanzania bila uhaini na utawala mbovu inawezekana na sote tunapambana kuliondoa hili JINAMIZI ambalo linatujia hata mchana likichukua maisha ya watu wazalendo kama waziri Shehoza pamoja na kunyonya rasilimali zetu. Ukombozi umefikia uongozi mzuri kujipatia, naipenda Tanzania". Maneno hayo aliyamaliza huku akiwa ameweka mkono kifuani mwake, mawaziri wote walifurahi na walitoa matabasamu ya matumaini.



    ****



    Upande napo kundi B lilikuwa lipo kwenye uzio wa kambi ya usalama wa taifa likiwa lipo nusu baada ya kujigawa, wengine walienda kuwakamata viongozi wa PTP waliokuwa na kikao usiku huo kilichoongozwa na katibu mkuu wa chama aliyemuwakilisha Rais Ole ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho. Kundi hilo lilikuwa na wanajeshi watupu pasipo komandoo, waliopo nje ya uzio wa kambi ya usalama wa taifa ndiyo walikuwa na komandoo ambaye ni Belinda pamoja na Allison. Kikosi hiki kilichopo eneo hili kilikuwa ni cha kimya kimya kutokana na eneo walilopo, waliruka ukuta wakiongozwa na Allison na Belinda ambao walikuwa wameng'ata visu kwa meno yao kisha wakaviachia baada ya kuingia ndani ya uzio. Zoezi la kuchinja au kuchoma visu vya shingo kila atakayeingia anga zao ndiyo lilifuata, ndani ya muda mfupi eneo la nje ya majengo ya kambi lilikuwa limeenea maiti za vijana wa usalama wa taifa. Zoezi la kuingia ndani ya kambi ndiyo lilifuata huko nako walimmaliza kila wanayekutana naye, waliingia ndani kabisa hadi sehemu yenye korido yenye njia mbili zilizojigawa. Eneo hilo waligawana kila mtu njia yake ambapo Allison na baadhi ya wanajeshi walipita kulia na Belinda na baadhi ya wanajeshi walipita kushoro. Upande aliopita Belinda ulikuwa una wanausalama wengi wa kawaida ambao walikuwa ni kama magugu tu kwake na aliwafyeka wote. Hadi akaufikia mlango uliandikwa MATRON kisha akaupiga tekw kuufungua mlango huo, aliingia ndani na akajikuta akisalimiana na sakafu baada ya teke kali la kumpata usawa wa kiuno kisha mlango ukafungwa kwa nguvu. Belinda hakuwa amemuona aliyempiga lakini hakutaka afuatwe na pigo jingine akiwa bado yupo chini, alifyatuka toka pale alipoanguka hadi akasimama na miguu miwili. Alikuwa akitazamana uso kwa uso na mwanamke ambaye angeweza hata kumzaa, mwanamke huyo alikuwa yupo ndani ya vazi la suti ya kike yenye suruali.



    "karibu mgeni wangu" yule mwanamke aliongea kwa kejeli huku akivua koti la suti alilolivaa halafu akaliweka juu ya meza iliyopembeni yake, aliamua kumfuata Belinda kwa mateke mawili kwa mpigo ya aina yake ambayo yalionekana na Belinda. Mwanamke huyo alionekana ni mtu mwenye kasi kuliko kawaida na alikuwa analeta mapigo ya nguvu, Belinda hakuwa ametambua mchezo anaocheza yule mwanamke na ikawa ngumu kuanza kushambulia pasipo kujua ajihami namna gani. Njia aliyotumia kumjua ni mtu anayecheza mgeni ni kupiga ngumi ya kudokoa, alipopiga ngumi hiyo alikutana na teke lilikuwa linakuja usawa wa kiuno. Belinda alilikwepa teke hilo huku akijisemea,"SAMBO.

    Sambo ni mchezo wa mapigano.hatari ulianzishwa huko Urusi na ndiyo anaoutumua huyu mwanamke anayepigana na Belinda, kutokana kuujua mchezo wa huyo mwanamke ilimbidi Belinda ajihadhari sana kwani huwa wana mapigo ya kuvunja kiuno wakidaka ngumi ya mtu. Belinda aliamua kutumia mtindo wa ngumi inaofanana na taikwondo ya Thailand katika kupigana na mwanamke huyu ambaye yupo vizuri sana kupigana, mtindo huu ulionekana kumshinda mwanamke huyu na hatimaye Belinda akammaliza kwa pigo goti la shingo ambalo hupenda kutumiwa na wapiganaji wa Thailand.



    Upande aliopita Allison huko alikutana na Briton akiwa ameshajua kama kuna uvamizi uliojitokeza katika kambi yao baada ya kuona miili ya wenzake. Briton alipomuona Allison hakutaka kuuliza huyo ni nani zaidi ya kuanza kumshambulia kwemye korido ambayo ni ina wembamba wa wastani, alimshambulia kwa mapigo ya judo ambayo yalikuwa yakipanguliwa na Allison huku akirudi nyuma kutokana na uzito wa mapigo hayo. Briton alitumia nafasi hiyo kushambulia akiwa hatambui kama Allison ana mahesabu yake jinsi anavyorudi nyuma, alipotupa ngumi alikuta akidakwa mkono kisha akabamizwa chini kwa mtindo wa judo. Briton alisikia maumivu lakini alijikaza akainuka kisha akawa anamfuata Allison kwa teke la mawash gel kisha akapiga yoko gel kwa mguu huohuo, Allison alipangua teke la mawashgel kisha akasogea pembeni kulipisha teke la yoko gel huku akiinama chini. Kutoka pale chini alipoinama aliachia ngumi nzito iliyompata Briton ya korodani hadi akatoa yowe la maumivu. Briton alikuwa ameshalainika kutokana na ngumi hiyo na sasa akawa ametoa mikono na akawa ameshikilia sehemu ya korodani, Allison aliona hiyo ndiyo nafasi adimu na alianza kumshambulia Briton kwa ngumi mfululizo usoni kisha akampga teke liiitwalo maigel lililompata la koo. Briton alianguka chini kama mzigo baada ya kusikika sauti ya mfupa wa koo ukigoka huku macho yakiwa yamemtoka na roho ikiwa imeuacha mwili. Allison alliendelea kutembea mbele hadi mwisho wa jengo la kambi hiyo huku akiwamaliza vijana wa usalama wa taifa anaokutana nao, baada ya dakika thelathini tayari kambi yote ilikuwa tupu na maiti zikiwa zimezagaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "piga simu kambini walete gari kubwa ili muondoe mizoga hii kabla haijafika adubuhi" Belinda alimwambia mwanajeshi mmoja aliyekuwa kwenye operesheni hiyo ambaye alipiga saluti kukubaliana na amri yake. Kazi ya kuondoa miili hiyo ilifanyika baada yagari kuwasili eneo hilo kisha zoezi la kwenda kuizika ndiyo likafuata.



    "AL005 sema" Allison aliongea baada ya kusikia mkoromo katika kifaa chake cha mawasiliano muda mfupi tu toka gari la lililobeba miili kuondoka.



    "operesheni imefanikiwa viongozi wa PTP wote wapo selo maalumu kambini" Ilisikika sauti ikimwambia, Allison alimfuata Belinda kisha akamwambia, "mission completed viongozi wa PTP wapo ndani wote". Belinda aliachia tabasamu pana baada ya kusikia taarifa hiyo kisha akasema,"FAGIO LA CHUMAA".



    "FAGIAAAAA" Allison pamoja na wanajeshi waliosalia walipaza sauti.



    SIKU ILIYOFUATA



    ASUBUHI

    VIWANJA VYA JANGWANI

    DAR ES SALAAM



    Eneo lote la uwanja huo lilikuwa limefurika watu waliokuwa wakiimba kwa sauti kubwa baada ya kusikika kwa king'ora cha msafara wa rais Ole wakati msafara huo ulipokaribia eneo la viwanja hivyo, ndelemo na vifijo vilisikika baada ya msafara wa magari hayo kuingia uwanjani hapo hadi jirani na jukwaa atakalolitumia kukaa kwenye mkutano huo. Pembeni ya jukwaa hilo kulikuwa kumefungwa vioo vikubwa vya televishenj vilivyokuqa vikionesha matukio mbalimbali ya rais Ole akiwa na wananchi wa kawaida na hata kutoa msaada. Wanachi walifarijika sana na matukio hayo na wakamuona rais wao ni kipenzi chao anayewasikiliza watu wao. Karibu na jukwaa hilo kulikuwa kumezungukwa na vijana wakakamavu wenye suti nyeusi wakilinda usalama, muonekano wa vijana hao pamoja na umakini ni kitu kilichomfanya rais Ole ajiamini. Rais Ole alipopanda jukwaani baada ya kusalimiana na wanachama, wananchi wote walishangilia.



    "PTP?!" rais Ole aliongea kutaja kauli mbiu ya chama chake.



    "MAENDELEO KWA UMAAAAA!" Wananchi waliitikia kwa sauti kubwa huku mbinja zikitawala kwa wingi, muda huo mtu aliyebeba katiba ya chama alipanda jukwaani ili ampatie, uso wa mtu huyo ulikuwa umefunikwa na kofia ya chama na kuufanya kutokuonekana. Mtu huyo alimpatia katiba ya chama ili rais Ole aibusu kuonesha sehemu ya heshima aliyonayo kwa chama chake, rais Ole aliibusu ile katiba huku yule mtu akivua kofia ya chama aliyoivaa. Rais Ole alipogeuka kumpatia yule mtu alipigwa na mshangao na hata wananchi wote walipigwa na mshangao walipoiona sura ya huyo mtu, sura ya marehemu Gerald Geofrey aliyepanga njama ya kumuua ndiyo aliyoiona kwa mtu huyo ambaye anajua kabisa ni marehemu.



    "si nimekuua wewe?!" Rais alijikuta akiongea na sauti yake ikachukuliwa kwenye kipaza sauti kilichokuwa kipo mbele yake, hakika alichanganyiiiwa kumuona mtu huyo.



    "Haaaaaaaaaaa!" Wananchi walitoa sauti ya mshangao na muda huohuo vioo vya televisheni vilivyokuwa vipo katika jukwaa kuu vikaanza kuonsha mikutano mbalimbali ya siri ambayo raus Ole aliifanya kupanga maovu mbalimbali. Rais Ole alizidi kuchanganyikiwa na akataka kukimbia lakini mlinzi wake anayetembea naye akamdaka mkono, alipojaribu kujitikisa alijikuta amekamatwa kisawasawa kisha akarudishwa alipokuwa awali. Mlinzi wake huyo alivua kofia kisha akashika nywele zake halafu akazivuta kwa nguvu na kupelekea, sura ya bandia ilionekana ikimvuka mlinzi huyo na kupelekea sura yake halisi ionekane. Rais Ole alidhani anatazamana na mlinzi wake kumbe ni Jenerali Kulika alikuwa amevalia sura ya bandia ya mlinzi wake. Wananchi tayari walishaanza kufanya fujo lakini walipoiona sura ya Jenerali Kulika wote walitulia, muda huo anga lote lilikuwa limezungukwa na helikopta huku pembezoni mwa uwanja huo kukiwa kuna magari ya jeshi mengi.



    "Tanzania itabaki kuongozwa na viongozi waadilifu na sio wahainj kama huyu, kuanzia hivi sasa natangaza kuwa nchi ipo chini ya jeshi hadi pale nitakapomteua raia wa mpito aongoze hadi kipindi cha uchaguzi"Jenerali Kulika aliongea kwa sauti iliyosikiwa na wananchi wote pamoja na kurushwa kwenye vyombo vya habari vyote. Ilikuwa ni aibu ya mwaka kwa rais Ole na hata njama za kukiondoa madarakani chama tawala awamu ilityopia iligundulika na wananchi wote wenye kadi za PTP walizichana siku hiyo. Jenerali Kulika alimtia nguvuni rais Ole huku yule mtu mwenye sura ya Gerald Geofrey ambao watu wote waliamini ni yeye akiivua sura ya bandia aliyoivaa, Moses Gawaza ndiye aliyeonekana mbele yao baada ya kuivua sura hiyo. Rais Ole alishushwa juwaani akiwa kadhalilika huku wananchi wakipaza sauti,

    "AULIWEEE!!". Alipelekewa hadi lilipo gari la kijeshi kisha akaondolewa uwanjani hapo kupelekwa mahabusu ya jeshi akiwa chini ya ulinzi mkali.

    Usiku wa siku hiyo msajili wa vyama vya siasa alitangaza kukifuta chama cha PTP katika orodha ya vyama vya siasa Tanzania na huo ndiyo ukawa mwisho wa chama hicho.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Rais Ole pamoja na viongozi wenzake w PTP walipandishwa mahakamani baada ya siku kadhaa wakisomewa mashtaka ya kuhujumu nchi, kuua watu kwa kukusudia na kutumia madaraka vibaya. Ushahidi uliowasilishwa mahakamani kuu upandewa mashtaka ulitosha kuwatia hatiani na wakafungwa kifungo cha maisha jela pamoja na kazi ngumu.



    Baada ya muda wa mwezi mmoja Zuber Ameir alitangazwa kuwa rais wa mpito katika kipindi cha kusubiri uchaguzi mkuu miaka mitatu ijayo na baada ya miaka mitatu uchaguzi mkuu ulifanyika tena na Zuber Ameir akawa ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kipindi hicho Belinda alishafika cheo cha Brigadia jenerali na Moses Gawaza akawa mkurugenzi wa usalama wa taifa, Norbert aliendelea kubaki Tanzania kama mwandishi wa habari. Hilda alirejea ofisi za EASA Rwanda na Allison akarejea ofisi za EASA Burundi... Tanzania ilijiingizia pesa nyingi ndani ya muda huo kutokana na almasi zilizokuwa zinapatikana Kondoa na miradi mingi ikagunduliwa kwa utafiti na kuifanya nchi ijiingizie pesa nyingi.



    MWISHO!!

0 comments:

Post a Comment

Blog