Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

SIKU YA GRADUATION - 5

 





    Simulizi : Siku Ya Graduation

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Nikamgeukia Pablo aliyekuwa amejikausha kama hakufanya jambo lolote. Nikainama chini na kuunyanyua mguu wake kwa nguvu, nikaichukuwa flash

    Muda huo tayari tulikuwa tumeshafika maeneo ya ‘Roundabout’ ya Msimbazi. Kapteni akatoa amri kwa dereva

    “Zuia gari.” Dereva hakutia neno, akasogeza gari pembeni

    “Kuna nini Boss?”

    “Kuna hali ya hatari.”

    “Nini hasa?”

    “Geuza gari, tunakwenda maeneo ya posta.. Ofisi ndogo za usalama.”

    “NO! Naomba tuheshimu taratibu za kazi, sisi ni askari na humu tuna wahalifu hivyo hatuwezi kuendelea kupoteza muda hapa, Gari inakwenda moja kwa moja kituoni…kituo cha Msimbazi.” Aliongea kwa sauti ya juu mmoja kati ya wale maaskari tuliopanda nao kwenye gari

    “Pumbavu! we unaongea hivyo kama nani? Unanijua mimi wewe?” Kapteni Makala alifoka huku akiwa amemtolea macho yule Askari

    “Sina haja ya kukujua, Gari inakwenda kituoni na si vinginevyo.” Majibu ya askari huyu yalionesha kumkera sana kapteni kiasi kwamba sasa akashindwa kuvumilia, akaingiza mkono mfukoni, akatoa bastola yake!

    Nikapatwa na hofu zaidi, sikujuwa anataka kufanya nini! Lakini kabla hajafanya chochote nikashangaa yule askari mwingine aliyekuwa kimya muda wote wa malumbano anamnyakia Kapteni kama nyani na kumtandika kichwa… kichwa kilimpata sawia maeneo ya kwenye kimpuma juu kidogo ya nyusi zake za jicho la kushoto na mchana. Hakuna nilichokiona kwa haraka zaidi mchirizi wa damu!kitendo bila kuchelewa, yule askari mwingine naye akaanza kurusha makonde mfululizo bila hata ya kuuliza kitu.

    Nini kinaendelea? Nilijiuliza huku nikiwa bado nimetaharuki, hapakuwa na haja ya askari wale kufanya jambo lile kwa kutofautiana tu kapteni Makala.

    Hali ilipozidi kuwa mbaya sasa dereva aliyekuwa akituendesha ambaye ni mwenzie na kapteni Makala ageuke nyuma ili kujaribu kumsaidi mwenziye, Hilo likawa ni kosa! ikatokea gari moja nyekundu kwa mbele ya gari yetu. Ilikuja kwa kasi ya ajabu, ikajipinda kidogo na kutugonga kwa ubavuni upande wa dereva, ilikua ni ajali ya kijuha sana, sikujuwa dereva wa gari ile alidhamiria nini maana sisi tulikuwa tumepaki pembeni kabisa ya barabara.

    Ajali ile ikapelekea mpambano ule wa ndani ya gari yetu usite kidogo, na hapo ndipo nilipowashuhudia vijana kama watano hivi wakishuka kutoka ndani ya ile gari iliyotugonga kisha wakaja kwa kasi mpaka ndani ya gari yetu walipofika hawakuuliza kitu zaidi ya wao kuwasaidia wale askari kwa kumshambulia kapteni Makala. ikawa ni kipigo juu ya kipigo, Kapteni hakuwa na wa kumsaidia kwa sababu tayari dereva wetu alikuwa amepoteza fahamu kutokana na ajali hiyo ambapo gari ile iligonga upande aliokuwa yeye! Uzalendo ukanishinda ikabidi nami sasa niingilie kati. Kila aliyekaa mbele yangu nilivurumishia ngumi za hatari.. ikawa ni vurugu kubwa sana ndani ya gari ile kiasi kwamba baadhi ya wapita njia wakaanza kutaharuki huku wengine wakitaka kujuwa kinachojiri, na wengine wakimbia hovyo!

    Ajali ile ilitupa jibu moja tu, kuwa ni ya kupangwa! Na hawa askari nao pia bila shaka ni wafuasi wa Mwaki. Raiawalianza kuongezeka eneo lile hivyo ikabidi mmoja kati ya wale vijana akaanza kupiga risasi juu ili kuwatawanya watu walioanza sasa kufurika eneo lile. Wakati vurumai ikizidi kushika kasi tayari vijana baadhi walikuwa wameshafanikiwa kumtoa Pablo nje ya gari huku akichechemea mguu mmoja kwa maumivu. wakamuingiza ndani ya gari na baada ya dakika chache vijana waliobaki ndani ya gari yetu pamoja na askari wale wawili wakatoka kwa kasi ndani ya gari yetu na kuingia kwenye gari waliyokuja nayo, wakaitia moto na kutoweka!



    Ilikuwa ni tukio la ajabu!



    Uso wa Kapteni ulikuwa umeenea damu huku mimi pia nikiwa nimeumizwa vibaya kichwani, hata sikujua wamenipiga na kitu gani. haraka tukatoka nje ya gari na kujaribu kuwafukuzia lakini haikuwa kazi rahisi maana tayari walikwishatokomea!

    “Washenzi wakubwa.. Hawa askari nao wamejiingiza matatizoni! nitawapata tu achananao! nimekariri namba za yule mmoja,” aliongea Kapteni Makala huku akihema kwa kasi.

    Tayari raia walishajaa eneo lile. Ndani ya gari yetu walibaki watu watatu tu; Baunsa na dereva wakiwa hawana fahamu, na Ramla!

    Kila mtu kati ya raia waliohudhuria alikuwa akisimulia yake huku wengine wakijaribu kumhoji kapteni, hakuwajibu kitu! Aliendelea kupiga simu zake sehemu alizozijuwa mwenyewe!

    Muda mfupi baadaye zikawasili gari mbili kwa kasi, wakateremka vijana wakiwa wamevaa Suti nyeusi, mmoja pekee akiwa amevalia gwanda za kipolisi. Wakasalimiana na kapteni, kwa mtindo wa salamu zao niligundua kuwa watakuwa ni maofisa wenziye wa Usalama. wakaingia ndani ya ile gari yetu iliyogongwa, wakamtoa Ramla, Baunsa, pamoja na dereva wetu kuwaingiza kwenye moja ya gari zile walizokuja nazo kisha gari ikaondoka.

    Ikabaki ile gari moja ikiwa na dereva na vijana wawili. tukapanda mimi na Kapteni, nayo ikatuondoa kwa kasi eneo lile na kuiacha ile gari iliyogongwa ikiwa imezungukwa na raia

    Ndani ya gari hakukuwa na maongezi yeyote kati ya kapteni na maafisa wenziye, tukiwa ndani ya gari kijana mmoja alitoa vitambaa vyeusi akamfunga machoni Ramla aliyekuwa akilia huku akiniomba msamaha.Haikufaa kitu!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haikuchukua muda tukawa nje ya nyumba, kwa Mhe. Waziri mkuu! kule tulipohifadhiwa mwanzo. Gari ikasimama wakaniteremsha mimi peke yangu na kuniacha pale halafu wao wakaondoka, sikujua wanakwenda wapi!

    Nikaingia ndani nikiwa nimechoka sana akili na mwili, nikajibwaga katika kochi pale Seating room. mawazo yakatawa ubongo wangu, upweke ukanivaa.. kila nilipovuta taswira ya Ramla nguvu ziliniisha!

    “Aaah shit! mkosi gani huu,” Nilijisemea kwa sauti huku nikibubujikwa machozi, Ntahondi aliniliza zaidi. nilishindwa kujizuia machozi yakawa yanazidi kutiririka,

    Mwisho wa Ntahondi umefika, nilijisemea nikiamini kuwa ni lazima wangemuua tu ili kupoteza ushahidi,

    “Amaa kweli Mwaki ana mtandao mkubwa… na atatumaliza tu,” nilizidi kujisemea peke yangu kama mwehu vile,

    Moyo ulivilia maumivu makubwa nikajiona sina tena thamani ya kuendelea kuishi, maana kila hatua ninayotaraji iniletee faraja badala yake inaleta madhara makubwa. Ntahondi ambaye nilitegemea kuwa ndiye angenifuta machozi na kuniliwaza katika kipindi hiki kigumu, Naye kalazimishwa kutoweka

    Baada ya kukaa kwa muda mrefu pale Sebuleni nikaamua kuinuka na kwenda kule chumbani, kwakuwa nilikuwa tayari mwenyeji hivyo sikuhitaji muongozo wa mtu yeyote

    Nilipofika pale mlangoni nikakuta mlango ukiwa umerudishwa tu, haukufungwa kwa funguo, nikakinyonga tu kitasa na kuufungua!

    Nilipoufungua tu.. TOBAA! Nikashtukia nimevutwa mkono kwa nguvu kuelekea kule chumbani. moyo wangu ulipiga kwa kasi sana huku nikitetemeka kwa hofu!

    Nilipoingia tu mle chumbani mlango ukafungwa kwa nguvu, nilipogeuka nimuangalie aliyenivutia mle chumbani na kuufunga mlango ule..



    Mungu wangu!



    Moyo ulinilipuka tena. sikuamni kilichodhihiri mbele ya mboni za macho yangu!



    Alikua ni Ntahondi!



    Naam, ni Ntahondi mwenyewe, na nguo zake zilezile alizokuwa amezivaa wakati tukienda kwenye Graduationa

    Sasa amefikaje huku?

    Nani kamleta? Nilijiuliza bila mwenyewe nikiwa nimeduwaa!

    Cha ajabu Ntahondi alikuwa akicheka tu, mwenye afya tele! Niliendelea kupigwa na butwaa, Sasa ametekwaje na kuletwa huku!

    Ntahondi akanifuata na kunikumbatia kwa furaha

    “Wewe imekuaje upo hapa?” nilimuuliza

    “Na wewe umefikaje hapa? Au ulikuwa na mwanamke mwingine nd’o umemfuata humu?” alinijibu huku akiachia cheko lake maridhawa

    “Hebu acha mzaha bwana, miye hapa siko sawa kabisa niliambiwa kuwa umetekwa na watu wa Mwaki sasa nashangaa uko huku.” Wakati nikiendelea kumuhoji Ntahondi ghafla nikahisi kama mchakato wa nyayo za mtu nyuma yangu.. nikatulia kidogo ili kuthibitishia, ni kweli kulikuwa na sauti ya nyayo tena ikitoke mlemle chumbani maeneo ya nyuma ya kabati kubwa la nguo,

    Au ni kweli alitekwa? Na watekaji wakaja naye huku ili kuninyaka na mimi?Nilijiuliza.

    Nikamwachia Ntahondi na kujitoa karibu yake ili nisogee kuangalia kuna nini kule nyuma ya kabati.



    Hamad!



    Nilipigwa na mshtuko mwingine mkali moyoni, ilikuwa ni siku ya kushangaa na kushtuka tu. macho yangu yakakutana moja kwa moja na huyo mtu aliyekuwa nyuma ya kabati, alikuwa Mwalimu Honde!

    “Nyie mbona siwaelewi?” niliwauliza huku nikirejesha macho yangu kwa Ntahondi aliyekua amesimama palepale nilipomuacha huku akiendelea tabasamu, na hatimaye kucheka kwa sauti! Nikashusha pumzi, nikarudi mpaka kitandani na kujibwaga kama kiroba!

    Ndipo sasa Honde na Ntahondi wakaja mpaka pale kitandani, Wakaketi!

    “Pole Kijana, mkeo yuko salama huyo hapo…hakuna aliyemteka.” aliniambia mwalimu Honde

    “Mnh, sasa ilikuaje? Unajua mpaka sasa sijaelewa kitu!” Niliposema hivyo Honde naye akacheka kisha nd’o akaanza kunipa habari

    “Iko hivi pale uliposimamisha Teksi ukawapakia akina Mama pamoja na Ntahondi ilikua ni Mistake kubwa sana maana maeneo yale kulikuwa na vijana wengine wa Pablo.. wengi kama Nyuki huku wengine wakiwa ni Askari polisi. sasa wakawa tayaritayari kuivamia ile Teksi ili wamteke Ntahondi… bahati nzuri kulikuwa na maofisa wa usalama wa taifa eneo lile wakaugundua mchezo mzima hivyo wakaiwahi ile Teksi, wakawatoa akina Ntahondi pamoja na kina Mama kisha wakawaingiza kwenye gari zao mpaka nyumbani, lakini kwa usalama ikabidi warudi na Ntahondi mpaka huku! ila sasa wakati wanakuja huku pia wakagundua kuwa wale Askari Polisi mlioingia nao kwenye gari yenu nao ni vijana wa Mwaki na wameshapewa maelekezo na mkuu wao wa kazi kuwa wahakikishe wanamwokoa Mwaki ndipo tukampigia simu Kapteni ili abadili muelekeo… nilimsikia akikwambieni kuwa Ntahondi ametekwa, nilicheka sana maana hakuwa amekata simu.. ile ilikuwa ni mbinu tu ya kiusalama ili kuwafanya wale askari wa Mwaki wajue kazi imefanyika.” Nilibaki kinywa wazi, ilikuwa ni habari ya kustaajabisha na kuogofya sana. japo Ntahondi na Honde walikuwa wakionesha sura za bashasha ila mimi bado sikuwa na amani kabisa moyoni, nikamtupia swali Honde

    “Sasa na lile tukio la kule Msimbazi nalo ni la kuunda?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “No lile ni kweli kabisa, na tayari wamefanikiwa kumtorosha Pablo.”

    “Sasa si itakuwa hatari imenza upya hiyo?”

    “Unajua Pablo si mtu mdogo kama unavyomfikiria, anakula na vigogo serikalini Yule.”

    “Kwahiyo tunamwacha atoroke hivi hivi?”

    “Atoroke mara ngapi?”

    “Nd’o kusema umekubali matokeo?”

    “Hapana, kuna vijana wako kazini wanajitahidi kumsaka… atapatikana tu ila sio kirahisi. inahitaji umakini wa hali ya juu vinginevyo atakufa mtu! Ninyi inabidi muendelee kukaa humuhumu katika jela yenu ya hiari kwa usalama wenu maana kwa sasa mmeshakuwa target, mnaweza kuuawa ili ushahidi upotee.” Kwa jinsi Honde alivyokuwa akiongea kwa kujiamini inaonekana anajuwa kila kitu

    “Mnh, Ok. Lakini Honde we unapata wapi hizi Information zote? Au na wewe Usalama mzee?” Swali hili likasababisha wote tuangue kicheko, nikashusha pumzi nzito kuashiria kuwa nimekubali matokeo kuwa mchumba wangu Ntahondi yuko salama, na niko naye tena,

    Pumzi zangu zilikuwa na maana nyingine, maana kubwa zangu,



    Kwamba Aluta continua

    Mapambano yanaendelea!



    Nilizidi kuiogopa nguvu ya Pablo, swali kubwa likiwa ni Je tutampata?

    Je haki itatendeka?

    Je Maisha yangu na Ntahondi yatakuwa Salama endapo hatotiwa nguvuni?,

    Baada ya kimya cha muda mrefu, mwalimu Honde akatuaga kwa madai kuwa anaenda kule chuoni kujua kinachojiri na pia anahitaji kupumzika

    “Kesho kuna jaribio la kumtia nguvuni Pablo, hivyo nahitaji kupumzika ili kujiandaa na zoezi hilo,” aliongea mwalimu Honde akiwa amesimama mlangoni kwa ajili ya kuondoka

    “Oooh! Na wewe utakwenda?”

    “Sio mimi tu, nadhani hata wewe pia utakuwemo.” Baada ya majibu hayo akafungua mlango na kuondoka, nikabaki mimi na kichuna changu, Ntahondi



    ******

    Tulibaki mle ndani Mimi na Ntahondi, japo nilikuwa nimefarijika kiasi lakini sikuwa na amani kabisa maana mara kwa mara kengere ya hatari ilikuwa ikigonga ndani ya kichwa changu, haikuhitaji msaada wa Profesa wa chuo kikuu cha Havard kuja kunithibitishia nguvu za kua Pablo, na kwakuwa ameshafanikiwa kutoroka sasa itakuwa ni mtanange kumpata maana naye siyo mjinga kihivyo lazima atajihami kwa umakini wa hali ya juu sana

    Siku hiyo iliisha kimyakimya tukiwa zetu chumbani tukiendele kupiga stori tu na kucheza kama watoto. hatimaye usiku ukaingia

    Wahudumu wa Mhe waziri mkuu walikuwa makini kwa kila hatua. Walikuwa wakarimu sana, mara kwa mara walikuja kuangalia usalama wetu, na kila muda wa chakula ulipowadia waliwasili.. hakika walikuwa wanakwenda na muda vilivyo

    Baada ya kupata chakula cha usiku, tuliingia kuoga na hatimaye tukarudi kulala tu,

    Ntahondi alionekana kuchoka sana hivyo mapema tu akawa ameshapitiwa na usingizi, lakini hali ilikuwa tofauti kwangu, Usingizi wote uliparama, nikawa nahesabu tu Paa, mpaka saa saba usiku nd’o kwa mbali usingizi ukailainisha mishipa ya kichwa changu

    *****



    Asubuhi na mapema ya siku iliyofuata nilikuwa wakwanza kuamka licha ya kuchelewa kulala, nikaoga harakaharaka, nikamwamsha Ntahondi naye akaenda kujiswafi mwili, akili yangu ilikuwa na wahka wa kutaka kujua hatma ya Pablo hivyo nilikuwa nikisubiri miadi ya Honde kuwa nami nitaenda katika zoezi adhimu la kumkamata Mafia Pablo Mwaki

    Baada ya Ntahondi kupata maji alijumuika nami pale katika meza ndogo kwa ajili ya kupata Stiftahi, Tulipata stiftahi murua tuliyoandaliwa. baada ya hapo tukawa sasa tunamsubiri Honde

    “Na mimi si n’taenda?” aliniuliza Ntahondi

    “No, hakuna haja”

    “kwanini?”

    “Hii imeshakuwa vita mama, kaa tu utulie usije ukatekwa bure ukaniacha pabaya mimi, jana tu nilitaka kuwa chizi niliposikia umetekwa.”

    “Kwahiyo we unavyotaka kwenda huko ukitekwa utakuwa umeniacha mimi pazuri?”

    “Tuachane na hayo… hivi unajua miye simuelewi kabisa huyu Honde! anaonesha dalili za wazi kuwa naye ni shushushu tu wa usalama wa taifa, au we haujashtukia?”

    “Kweli miye tangu jana najiuliza maana ujuwe ni yeye ndiye aliyekuja na hao vijana anaosema ni maofisa mpaka pale kwenye Teksi wakatuteremsha harakaharaka, na wakati nashuka kwenye teksi nikaangusha simu chini sasa Honde alipoinama kuiniokotea nikaona ana mguu wa kuku kiunoni.”

    “Wee, usiniambie!”

    “Sure, jamaa Shushushu huyu, haiwezekani kuwa mdogo wake tu na waziri mkuu nd’o ajue mambo nyeti kiasi hicho chote.”

    “Mnh mama, ya Ngoswe..” Tuliendelea kubadilishana Story mpaka tukachoka lakini Honde hakutokea, nikaanza kupata hofu. nikajaribu kumpigia kwa simu ya Ntahondi lakini hakupokea. tuliendelea kumsubiria bila mafanikio mpaka jioni ikaingia na giza lililoashiria kuingia kwa usiku nalo likatanda, Tukaingia zetu kulala, basi hali ilikuwa hivyo kwa takribani siku nne mfululizoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tuliendelea kuishi mle ndani bila ya kupata mawasiliano ya Kapteni, Honde, wala mtu mwingine yoyote zaidi ya mawasiliano ya simu na baadhi ya ndugu zetu ili kuwatoa hofu juu ya usalama wetu

    Baada ya siku kama tano hivi mbele ndipo Honde alikuja, kama kawaida yetu huwa akifika tunaanza stori za kila aina pia huwa anatupa taarifa zilizopo huko nje kufuatia tukio zima

    “Huko nje habari zimevuja kuwa Ntahondi anaolewa na Naufal.. mko juu..” alitania Honde na kutufanya nasi tucheke

    “Hiyo utakuwa umeitunga wewe maana hakuna aliyewaambia hao watu.” Aliongea Ntahondi,name niatupa swali

    “Kwa hiyo kuna habari gani za Pablo?”

    “Habari za Pablo sio nzuri sana, kuna mawili, inawezekana ameshatoroka na kakimbilia Kenya ambako atajipanga ili apotelee Dubai nasikia ana mijengo kule, pili inawezekana akawa bado yupo humu nchini ila muda wowote atatokemea.”

    “Sasa nanyi maofisa usalama mmeshindwa kumtia nguvuni kweli?”

    “We bwana tafadhali… aliyekwambia mimi ni Afisa usalama ni nani?”

    “Aah, samahani, kwa jinsi unavyopata data najihisi kama niko na mtu wa usalama.”

    “Ok jitihada zinaendelea kumsaka maana kama atafanikiwa kukimbilia ughaibuni huko na kujificha vizuri itakuwa mbinde kumpata, na hapo sasa ataanza msako dhidi yenu ili awaue apoteze ushahidi ili hata akikamatwa kesi isiwe nzito sana kwake.” Maneno hayo ya Honde yalinipagawisha zaidi lakini sikua na cha kufanya,

    “akina Ramla na yule baunsa nao vipi?”

    “Kesho nd’o watapandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza kujibu tuhuma za kushiriki kuteka, kutesa, na kupanga njama za mauaji… Hii hawachomoki wallah, japo namuonea sana huruma Ramla, unajuwa tayari ujauzito wake unazidi kuchomoza sasa nd’o anazidi kuishiwa nguvu.”

    “Nd’o atakoma mshenzi Yule,” alijibu Ntahondi kwa hasira

    “Sasa ninyi asubuhi muwe tayari tayari kwa ajili ya kuhudhuria mahakamani, kisha baada ya kesi mtarudi huku, nadhani mnaweza kuwasiliana na kina mama nao wakaja mkaonana pale mahakamani”

    Tulipigasoga sana ili kuvuta muda. hatimaye Honde akatuaga, akaondoka.

    Tukabaki na sisi tukiendelea kukaa ndani tu kama wafungwa

    *****



    Hatimaye siku ya mahakamani ikawadia

    Kama ilivyo ada tukawa tumeshaamka mapema na tuko tayari kwa kuhudhuria mahakamani, japo tulikuwa na hamu ya kuonana uso kwa uso na Ramla ili tumuoneshee kuwa Mungu ameanza kulipa lakini bado sikuwa na raha kabisa kwa kutopatika Pablo!

    Haikuwa muda mrefu sana ikafika gari nyeusi LandCruiser V8, punde baada ya kuegeshwa akashuka mwalimu Honde akiwa na vijana wengine wawili waliovalia suti nyeusi, bila shaka nao ni kutoka kitengo maalum cha usalama wa taifa(TISS), nilianza kuwaelewa maofisa hawa waliokuwa wakishiriki katika kesi hii kutokana na aina ya suti walizopendelea kuvaa.

    Hatukukaa tena, Wakatuchukuwa na safari ya kwenda mahakamani ikaanza!

    Ndani yadakika kama thelathini za mwendokasi tulikuwa nje ya mahakama kuu, tukateremka kutoka kwenye gari na kuingia ndani ya mahakama huku macho ya wahudhuriaji wengi waliofurika yakitusindikiza,

    Tukiwa tumeketi kwenye viti maalum ndipo muda huohuo macho yangu yakakutana na watu wawili waliodhoofu hali zao, Ramla na Baunsa

    “Karibu Baunsa,” nilimkaribisha Baunsa kwa sauti ya kebehi, aliishia tu kunitupia jicho moja..hakunijibu kitu!

    Kupitia dirisha dogo niliweza kumwona Mama Ntahondi akiwa amesimama na mama yangu mimi! nikampiga ukope Ntahondi naye akawatambua.Pamoja na wazazi wetu niliwatambua watu wengine wengi tu wakiwa nje. tulipokuwa mle ndani akawasili Kapteni Makala, akasalimiana na makarani kisha akaja usawa wetu nasi tukasabahiana naye kwa furaha. baada ya salamu akamsogelea mwalimu Honde aliyekuwa ameketi nyuma yetu, akateta naye jambo akamtoa faragha Mwl Honde, sikujua walichokwenda kuongea kwani baada ya muda akarudi Honde peke yake nikamuwahi kwa swali

    “Kapteni amekwenda wapi?”

    “Inasemekana Pablo yuko njia moja, nd’o anataka kutoroshwa muda huu…So wanamfukuzia.”

    “Kwahiyo sisi hatuendi tena?”

    “Haina haja sana.” Tuliendelea kukaa pale mahakamani kwa muda mrefu bila kesi kusomwa, ikawa ni stori tu baina yetu mpaka nilipochombeza ile habari yangu ya kuokota ile Flash ya Pablo kule ndani ya gari, nilidhani kuwa jambo lile ni la kwaida sana lakinikumbe ilikuwa tofauti sana kwa jinsi Honde alivyoipokea

    “Una uhakika aliiangusha yeye?”

    “Ndio.”

    “Mbona haukusema muda wote huo?”

    “sikudhani kama ni muhimu kiasi hicho, kwani ina nini?”

    “Itakuwa kuna data za muhimu sana mle ambazo huendazikarahisisha zoezi, we have to do something right now.” Honde akatoa simu yake na kuanza kuandika ‘massage’na kituma.. nikiwa bado namwangalia bila ya kujua cha kumjibu, simu yake ikaita…akapokea na kuongea. Mtindo wa mazungumzo unaonesha mjadala ulikuwa ni juu ya flash

    “Eti hiyo Flash iko wapi?” Mwalimu Honde aliniuliza wakati simu yake ikiwa bado ingali sikioni

    “Iko kule tunapolala.” Honde alimfahamisha huyo aliyekuwa akiongea naye, kisha akakata simu

    “Aisee hiyo Flash ni ya muhimu sana na inaweza kutufaa, Inspekta Makala yuko njiani anakuja kutuchukua mimi na wewe twende kuiangalia hiyo flash ila Ntahondi atabaki hapahapa.”



    Inspekta Makala? Sio kapteni tena?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilishtushwa na cheo hiko kipya alichopewa Makala, nilidhani Honde alikosea kutamka lakini sura yake baada ya kutamka cheo kile ilibadilika na kujenga tahayari, inaonesha Makala kweli ni mwanausalama wa taifa nd’o maana haeleweki cheo chake ni kipi hasa, hiyo haikunipa tabu. Ila sasa Honde naye amejuwaje? Na kwanini ameonekana kujutia kauli yake hiyo? Bila shaka naye ni Shushushu tu. Nikampotezea

    Ntahondi alikuwa akitusikiliza muda wote wa majibizano yetu, naye aliafiki bila kipingamizi kuwa atatusubiri palepale mahakani

    Muda mfupi tukaiona gari ile aliyokuja nayo mwanzo Kapteni Makala lakini alikuwemo dereva tu, tukatoka nje haraka na kuingia ndani ya gari. Safari ikaanza, tukarudi kule nyumbani kwa Mhe Waziri. Hatukuchukuwa muda mrefu tukawasili.

    Tuliwakuta vijana watatu wakiwa wamevaa suti, kati yao akiwemo Kapteni Makala ambaye baada tu ya kutuona alituhimiza kwa ishara ili tuwahi kuingia ndani, tukafanya kama alivyotaka. Tuilipofika Sebuleni maofisa wale wote wakatangulia juu ya meza ambako tayari walikuwa na Kompyuta mpakato ikiwa tayari kwa kazi

    Nikaingia ndani kuchukuwa hiyo Flash, nyuma yangu akanifuata Mwalimu Honde mpaka chumbani, nilipoingia chumbani nikaenda moja kwa moja mpaka kitandani, nikaivuta droo ya kitanda ili nichukuwe hiyo flash, Afanaleki! flash haikuwemo. Mikono yangu ikaanza kutetemeka huku ikivuja jasho kwa uoga, nikainuka haraka na kwenda kwenye pochi ya Ntahondi aliyoining’iniza juu kiti kidogo kilichomo mule chumbani, nikafungua zipu ya katikati kwa kihoro huku nikiomba Mungu niipate…haikuwemo. Sasa nd’o nilizidi kuchanganyikiwa

    “Vipi wewe? Acha upuuzi wako,” alifoka mwalimu Honde huku ile sura yake yenye dalili za urafiki ikitoweka

    “Honde siioni flash na niliiweka humu kwenye droo ya Kitanda.”

    “Ooh shit! Naufal unataka kujiletea tabu, watu wote huko wanaisubiri flash hiyo kama roho..unadhani utaelewekaje?” Sikumjibu kituniliendelea kuitafuta kimyakimya, Nikajaribu kufungua katika zipu ya pembeni ya pochi…haikuwemo! nikawa kama kichaa

    Nani kaichukua? Au mtandao wa Pablo?Nilijiuliza kimoyomoyo, nikafungua zipu ya upande wa kulia, nikashusha pumzi, nikaingiza mkono na kuitoa flash, bila shaka itakuwa ni Ntahondi ndiye aliihifadhi humu, Honde akanisogelea na kutaka kuichukua huku akiwa haamini kama tumeipata

    “Nini sasa?” nilimuliza kama nilyekuwa sikumwona tangu awali

    “Lete haraka twende na muda.”

    “Nilete nini?”

    “Si hiyo flash jamani!”

    “Nikupe wewe kama nani? We sio polisi wala afisa usalama wa taifa, au nawe ni mmoja wao?” Hakunijibu, nikamuachia tabasamu la mamba kisha kama maskhara nikaachana naye na kutoka zangu mpaka sebuleni, nikamkabidhi Kapteni Makala, akaipokea na kuichomeka kwenye ‘laptop’ na kuanza kuperuzi

    Sikujuwa kilichoonekana ndani ya flash kupitia kompyuta ile ila tu nilihisi kuna jambo zito kwa jinsi Kapteni alivyokuwa hatulii kitini, inaonekana alikuwa akiona mambo makubwa na ya ajabu, akiwa amekaza macho yake kwenye komputa akamwita Honde huku akimwonesha kitu katika Kompyuta, haraka Honde akasogea na kuchungulia, naye akashindwa kujizuia! Sekunde kadhaa alizotumia kukichungulia kioo cha kompyuta zilimtosha kutahayari. akapayuka kwa sauti ya mshanga

    “Mheshimiwa Kigwaza?! Hii sasa balaa.” nilishtuka kusikia jina lile maana nilimjuwa aliyetajwa. Mhe Andrew Kigwaza, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa

    Amefanyaje? Sikupata jibu

    Nikiwa sijaelewa kinachoendelea ndani ya ‘Laptop’ ile tena likatajwa jina jingine lililozidi kunipa hamu na kiu ya kutaka kujua kilichomo

    “Jamila Kijukuu.” nililijuwa vema jina hili kwani lilikuwa ni jina la Jaji aliyepangwa kusimamia kesi yetu, na mpaka muda ule tunaondoka mahakamani alikuwa hajaingia

    Sasa kama naye ameonekana kuwa ni mmoja kati ya wana mtandao wa Pablo sijui itakuajenilijisemea peke yanguhuku nikiwa nimewatumbulia macho.

    Ghafla Kapteni akasimama na kupiga meza kwa nguvu

    “Pasword yake hii hapa alikuwa ameificha huku mshenzi huyu” akaingiza mkono mfukoni akatoa Modem ya Internet, akaipachika kwenye Kompyuta na kuanza kuunganisha mtandao palepale, Nilitamani kujuwa kinachoendelea ila sikuwa na mamlaka hayo hivyo nikatulia

    Baada ya muda wa kuperuzi na kudadisi Kapteni alishtuka tena, bila shaka alipata jambo jingine kubwa zaidi, akasimama tena pale kwenye kiti na kusema

    “Mungu wangu tutwahi kweli?!”

    “Wapi?” aliuliza kijana mmoja kati ya wale waliotinga suti

    “Airport, huyu mshenzi anaondoka asubuhi hii kwenda Kenya na ndege ya Shirika la Kenya AirWays, MHZ 6453 naona hapa alikuwa akijibizana kwa barua pepena huyo Jamila.”

    “Kwahiyo tunafanyaje?”

    “Haraka tuondokeni tujaribu kuwawahi.” aliposema tu hivyo haraka tukatoka nje na kuingia kwenye magari…tukaondoka kwa kasi ya ajabu kuelekea Airport

    Tukiwa njiani nilimsikia Kapteni akimwambia Honde apige simu ofisi kuu kuomba nguvu ya ziada pale uwanjani, sikujuwa ofisi kuu nd’o wapi. Tulitembea mwendo wa kasi…mwendo wa farasi, dakika chache mbele tuliwasili katika viunga vya ‘Mwalimu Julius Nyerere Intanational Airport’, gari ziliposimama tu tukashuka haraka, nikamwona Kapteni akiikimbilia ndege moja iliyokuwa nd’o kwanza inaiacha ardhi na kulakiwa na anga. wote tukamkimbilia mpaka pale alipo…haikusaidia kitu! MHZ6453 Ilikuwa ikipotelea angani,

    Abiria wengi walitaharuki na kuanza kukimbia hovyo, nadhani walihisi kuwa sisi ni majambazi au magaidi, hatukujali!

    Tukarudi mpaka pembeni kidogo kulikuwa na abiria wa kike kama watano hivi wakiwa wamesimama na Jeneza lao pembeni huku wakilia, bila shaka walikuwa wakisafirisha maiti, Walikuwa wakiongea kwa lugha ya kingereza kitu kilichonifanya nijuwwe kua hawakuwa watanzani. Na hata nilipoangalia Jeneza lao walikuwa wamelifunika kwa bendera ya Ghana,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Jamaa katukimbia.” Sauti ya Kapteni ilipenya sawia katika masikio yangu, hakika nililainika.. ghafla nikamwona Kapteni akinisogelea na kuniambia nitangulie ndani ya gari, sikujuwa kwanini anitangulize kwenye gari ilihali wao wakibaki pale nje. sikuhoji, haraka nikawahi kwenye gari

    Nikiwa ndani ya gari nilishangazwa na nilichokiona kikitokea nje, ni kama sinema ya bure, ni kama maigizo. Kapteni na vijana wake walikuwa wakinong’ona na kupeana ishara fulani, kisha ghafla waliwavamia wale wafiwa waliokwa na jeneza lilifunikwa kwa bendera ya Ghana na kuanza kutembeza kichapo cha nguvu ghafla! Sikujuwa sababu ila nilishangazwa tu jinsi kile kipondo kilivyokuwa cha haja, nilianza kuwatazama kwa jicho la tahadhari vijana hawa wa kapteni maana walikuwa wakiwaadhibu akina mama waleutadhani wanapigana nawanaume. Baada ya kichapo wakalipitia lile jeneza wakaja nalo kwa kasi mpaka kwenye gari yetu, wakaliingiza huku nao wakipanda haraka kisha dereva kwa kasi ya ajabu akaondoa gari

    Lilikuwa ni tukio la jabu sana kwa abiria na hata kwangu pia, sikujuwa kilichofanya Kapteni na vijana wakewafanye jambo lile, basi tukashika kasi barabarani tukijaribu kutoweka. haikua kazi rahisi maana tayari askari wa pale uwanjani walikuwa wakitufukuzia kwa kasi huku wakiturushia risasi isingekuwa uwezo wa gari zetu kutoruhusu risasi kupenya bila shaka zingetudhuru

    Mji mzima ulichafuka kwa mashambulio yale, mkimbizano wa magari na milio ya risasi iliwatisha wengi na kufanya mji kuwa kama uwanja wa vita. Tuliendelea kukimbia kwa tabu mpaka hatimaye tukaingia katika viwanja vya mahakama kuu. Tukateremka haraka na hapohapo vijana wa kapteni wakaliteremsha lile jeneza, halaiki ya watu nje ya mahakama ikatupokea kwa hofu na mashaka!

    Hapakuwa na maelezo mengi, Kapteni akaanza kutembea kuelekea ndani ya mahakama akifuatiwa na vijana wake wakiwa na jeneza lao mikononi, name nikafuata kwa nyuma. Muda huo tayari askari waliokuwa wakitukimbiza nao walikwishafika mahakamani…hawakutu shughulisha!

    Ndani ya mahakama kulikuwa shwari, kimya cha haja kikizizima. tayari Ramla, Baunsa na baadhi ya viongozi wa jeshi la Polisi wakiwa wamesimamishwa kizimbani mbele ya jaji Jamila Kijukuu. Mahakama nzima ikatuangalia tulivyoingia.. tukiwa tumesimama na jeneza letu mara na wale askari waliokuwa wakitufukuzia nao wakaingia mpaka ndani.

    “Kuna nini?” aliuliza mmoja katika wazee fulani waliokuwa wameketi chini ya Jaji Kijukuu. Hakuna aliyewajibu, Kapteni akaenda mpaka kwenye Jeneza hilo na kulifungua



    Tobaa!



    Ndani ya Jeneza hapakuwa na maiti bali palikuwa na mtu aliye hai, kilichonifanya kugundua kuwa mtu Yule aliyevikwa suti alikuwa hai nipale alipokohoa kwa sauti baada ya kufunuliwa, sikumjuwa kwa haraka.

    Mahakama nzima ikaingiwa na taharuki, baadhi ya majasiri wakasogea karibu ya Jeneza ili kumtambua maiti aliyekohoa, nami nikajongea…Loosalale ni Pablo Mwaki

    “Alikuwa akijaribu kutoroka.. tumemkuta akiwa Airport katika hali hii ya kujifanya ni maiti. tumemkamata kwa ushirikiano wa maofisa wa Polisi wa pale uwanjani japo baadhi ya maaskari wakiwemo hawa walioingia humu hawakutambua chochote.” aliongea kwa kujiamini sana Kapteni Makala. Hapo ndipo nilipomvulia kofia Kapteni,

    Sikuamini tukio lile kama naliona kweli au niko ndotoni, nilijiuliza mara mbilimbili kuwa aliugunduaje mchezo ule

    Mahakama nzima ilizizima, haraka Mwaki akainuliwa, yeye mwenyewe hakuamini alichokiona, alikuwa akihema kwa mshangao na fedheha. Akajumishwa na wenziye kisha sote tukaamriwa tuketi kwa utulivu. Kesi ikatajwa kwa mara ya kwanza bila ya mtuhumiwa yeyote kujibu, baada ya hapo Mhe Jaji akataja tarehe nyingine ya kuja kuanza mtiririko wa kesi hii nzito, japo tulikwishajua kuwa hata yeye Mhe. Jaji ni katika wafuasi wa mtandao wa mwaki lakini hatukuonesha hisia zetu dhidi yake, tulimvutia tu pumzi kwa ajili ya kujipanga kimapambano,

    Watuhumiwa wote wakakabidhiwa kwa Askari magereza na msafara wa kwenda Keko ukaanza huku wahudhuriaji wakitawanyika kwa mshangao na gumzo waliloliona mahakamani, Nasi tukarudi kwenye gari zetu maalumu kwa ajili ya kurejea mafichoni kwetu bila hata ya kupata afasi ya kuzungumzana familia zetu



    ******



    Tarehe iliyopangwa ikafika, tukahudhuria na baada ya washitakiwa kusomewa mashitaka yao, waliyakana yote..hata kututambua sisi pia walikana. Ikapangwa sasa tarehe nyingine ambapo mashahidi walitakiwa kuwasilishwa mahakamani. Tukatawanyika tena! Ilipofika siku hiyo kama kawaida tuliwasili mahakamani na kutoa ushahidi hatua kwa hatu huku tukisaidiwa na akina mzee Banzi na wenzao wa kule kijijini walioletwa kama sehemu ya ushahidi. Baada ya malumbano ya haja kutoka kwa mawakili wa pande zote mwishowe mahakama ikakamilisha kazi yake…tukatawanyika tena, sasa tukiisubiri hukumu

    Hatimaye ikafika siku iliyokuwa ikisubiriwa na wengi, Siku ya kumaliza utatana kuukata mzizi wa fitna. Siku ya hukumu

    Mji mzima ulijawa na shauku ya kutaka kujua kitakachojiri siku hiyo, Kesi nzito hii ilikuwa imeshawakalia pabaya Pablo Mwaki na washirika wake ambaye ni Ramla, Baunsa, na baadhi ya watumishi wa serikalini wakiwemo maaskari ambao hawakuwa waadilifu. Kesi kubwa ni Kuteka, kutesa, kupanga njama za mauaji dhidi yangu mimi na Ntahondi, Kutekeleza mauaji ya yule dereva teksi, Pia kulikuwa na kesi nyingine nyingi sana zilizokuwa zikimkabili Pablo ikiwemo ile ya kumwua yule mfanyabiashara ambaye inasemekana ndiyo msingi wa utajiri wake, pia tuhuma za kujishughulisha na uuzaji wa madawa ya kulevya nchini. Kwa maelezo niliyodokezwa na Mwalimu Honde ni kwamba tayari Naibu waziri wa ulinzi ameshakamatwa na mpaka sasa yuko chini ya ulinzi kwa kutumia nafasi yake kama kiongozi wa serikali kujihusisha na vitendo viovu vya kutumia baadhi ya maafisa wa jeshi lake kuwadhuru watu, na pia kujihusisha na uuzaj wa madawa ya kulevya, Ushahidi wa kina umeshatimia baada ya kupatikana nyaraka kadhaa kwenye ile flash zikionesha ushiriki wao na mtandao wao mzima

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tuliendelea kishi nyumbani kwa Mhe. Waziri mkuu tukisubiri kumalizika kwa mkasa ule, mipango yetu ya kufunga ndoa iliendelea vizuri tu, na sasa ilihama kutoka kuwa yetu pekee na kuwa ya kifamilia, kupitia kwa mwalimu Honde na kaka yangu Jarufu habari ziliwafikia wazazi, nao wakaafiki kwa furaha…Siku zikakatika hatimaye mwezi ukamalizika!



    *****

    Kupitia kwenye upenyo wa dirisha dogo lililopo pale sebuleni niliweza kuona gari nyeusi aina ya Landcruiser ikiingia kupitia geti kuu kisha ikaenda kuegesha mbele ya mlango wa kuingilia ndani, punde wakashuka watu wanne wakiwa wamevalia Suti zao nyeusi. kati yao alikuwepo Kapteni Makala ambaye hatukuwatumeonana naye kwa kitambo hivi, bila shaka hao wengine nao na vijana wake wa kazi kutoka katika kitengo chake ndani ya idara ya usalama wa Taifa, lakini hawakuwa katika waleniliozowea kuwaona

    Kwakua tayari nilikuwa nimeshapewa taarifa na mwalimu Honde kuwa wangekuja maofisa hao kwa ajili ya kutuchukuwa na kutupeleka mahakamani, nikainuka haraka kutokea pale sebuleni nikakimbilia Chumbani kumwita Ntahondi ili tuondoke. muda wote huo Ntahondi alikuwa kwenye Kioo tu akijremba na kujipodoa, wakati nimesimama Mlangoni nikimwita Ntahondi tayari Kapteni alikwishaingia sebuleni

    “Hey..” alinishtua

    “Yes Sir,” nilijibu kwa mbwembwe pia

    “Najuwa taarifa za ujio wetu mlikuwa nazo, are you ready?” Kabla sijamjibu chochote hapo hapo Ntahondi alitoka chumbani akawa amesimama karibu yangu pale katika mlango wa chumbani, hilo likawa ni jibu murua kwa Kapteni kuwa tupo tayari. Kapteni alimtupia Jicho Ntahondi, kisha akapepesea macho kwangu halafu akaachia tabasam maridhawa, tabasamu lile lilibeba maana kubwa, maana ya kwamba hakika tulipendeza vilivyo!

    Tukaanza kuongozana na kutoka nje kabisa ilipo gari, tukasalimiana na maofisa wale tuliowakuta pale nje kisha tukaingia ndani ya gari kwa ajili ya kuanza msafara wetu

    Ndani ya gari, siti ya mbele aliketi mkuu wa msafara Kapteni John Makala akiwa na dereva wake ambaye bila shaka naye ni mtu wa usalama pia, Siti tatu za katikati aliketi mmoja kati ya vijana hawa wa Makala akifuatiwa na Ntahondi halafu Mimi. na siti tatu za nyuma kama zilivyo zilikaliwa na vijana wawili waliosalia

    Gari ikatoka nje taratibu kisha ilipofika barabarani ikachukua kasi yake. huyu kijana aliyekaa karibu na Ntahondi upande wake wa kushoto alikuwa akimwangalia sana Ntahondi, na nilipomchunguza niligunduwa kuwa alikuwa akimwangalia kwa macho ya tama na ufedhuli ndani yake…niliendelea kumtazama kwa tahadhari, Nikajikuta tu namchukia ghafla..wivu!

    Kapteni alionekana kujawa na furaha sana tofauti na ilivyo kawaida yake, yaani alishindwa kabisa kuzificha hisia zake, hisia za furaha, hisia za raha naamani. Mwishowe akaamua kuidhirisha furaha yake kwa kuanza kuongea tukiwa tunaendelea na dafari ya mahakamani

    “Thanks to God, Arobain za huyu mshenzi zimetimia.”

    “Nadhani leo Nchi itazizima baada ya hukumu,” nami nikajibukwa furaha huku nikimtupia jicho la uchokozi Ntahondi, lakini ghafla nilishtushwa na jibu liliotoka kwa kijana aliyeketi katika siti ya nyuma

    “Ni upumbavu na uhayawani kuamini hivyo.” Nadhani hata Kapteni naye alishangazwa na jibu la kijana wake huyo. tukajikuta sote kwa pamoja tumegeuka nyuma kumwangalia. Hapo tena tukapatwa na mshangao mwingine mkubwa zaidi!

    Sikuamini macho yangu, ilikuwa ni kama ndoto vile, yaani tulivyogeuka tu tulikutanisha macho yetu na mitutu miwili ya bunduki kutoka kwa vijana hawa huku sura zao zikiwa zimeshabadilika kutoka katika ile hali waliyokuwa nayo mwanzo ya kistaarabu na kuwa kama waliokunywa damu ya binaadamu…wanyama!

    Nikarejesha macho yangu mbele na kumwangalia Kapteni, lakini naye alikuwa ameshangaa sana hali ile na alionekana kujawa na hasira na woga pia

    “Giggs nini tena mbona siwaelewi?” alisaili Kapteni

    “Shutup Bitch.. Arobain za mwaki bado sana ila leo ni arobaini zenu ninyi,” alijibu kwa dharau kijana Yule ambaye sidhani kama itakuwa halali nikimwita kijana wa Makala tena…bali ni kijana wa Pablo

    “Giggs… am i a bitch to you now?” Kapteni makala alisaili kwa kimombo huku sura yake ikiwa imebadilika kabisa

    “Funga bakuli lako tafadhali takumiminia njugu sasa hivi, Mchezo wowote wa kipuuzi utakaothubutu kuufanya itakuwa ndiyo tiketi yako ya kwenda kuzimu… kumbuka nakujuwa vizuri sana Makala.” Kijana huyu aliendelea kutamba kwa maneno ya kebehi yaliyojaa dharau ya hali ya juu.Hakika vijana hawa walikuwa hawatanii, walionekana kumaanisha wanachosema! Wakati tukio lile likiendelea ghafla na huyu kijana mwingine aliyekaa karibu na Ntahaondi naye akatoa bastola yake na kumuelekezea Kapteni huku akitoa maelekezo kwa dereva

    “Geuza gari fasta tunaelekea Mwenge sasa hivi, ujanja wowote utakaothubutu kuufanya utapelekea mwili wako kuwa kama chandarua jinsi nitakavyo utoboatoboa kwa risasi…sure i’ll blow your fu**n headoff” Gari ikageuza uelekeo na sasa tukaianza safari mpya ya kwenda Mwenge. Uso wa kapteni ulipwaya na sasa hakuwa na ujanja tena maana amegeukwa na vijana wake mwenyewe!

    Vijana wenye kujuwa mbinu hatari za mashambulizi!

    “Shika barabara ya Mwenge kisha moja kwa moja Bagamoyo.” niliposikia tu Bagamoyo moyo wangu ukafanya ‘samasoti’ nikamwona Ntahondi naye akibubujikwa na machozi, bila shaka alikumbuka kuwa huko ndipo ilipo ile kambi ya Pablo ambako tuliteswa na kuponea chupuchupu kuuawa na sasa ndiko tunakorejeshwa

    Nilijua kuwa sasa tumefikia tamati!

    Lazima tuuwawe tu ili kupoteza ushahidi



    Amaa kweli niliamini maneno niliyoambiwa kuwa Pablo Mwaki ni moto wa kuotea mbali,



    Yaani ana mtandao mpaka kwa maafisa wa usalama wa taifa! Nilijisemea mwenyewe

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati gari ikiwa imeshabadilisha uelekeo nikamwona yule kijana aliyekuwa akimuangalia sana Ntahondi akiingiza mkono katika mfuko wa koti lake na kutoa vitambaa vyeusi. akamsogelea Kapteni kwa umakini wa hali ya juu kisha akamfunga kitambaa kimoja usoni! alipomaliza akahamia kwa Ntahondi naye akamfunga, halikadhalika nami akanifunga. wakati huo wale waliopo nyuma yetu wakiwa bado wametuelekezea bastola zao, Sasa tukawa hatuoni tena mbele wala hatuoni muelekeo wetu, hii ikanikumbusha siku niliyokuwa nikipelekwa huko porini..

    Gari ilikuwa ikikimbia kwa kasi sana mpaka tunayumba. Kimya kilitanda ndani ya gari!

    Hapakuwa na sauti yoyote zaidi ya kilio hafifu kutoka kwa Ntahondi. Kilio kilichozuliwa na karipio kali kutoka kwa huyu kijana aliyekuwa anamwangalia kwa uchu

    “KELELE WE MALAYA!! Unamlilia nani humu? Kama una hamu ya kulia subiri tufike utalia mpaka utachoka! Leo tukifika usiku mzima utalala na mimi ukinistarehesha, na kesho ikifika utalala kuzimu.” Maneno haya yalizidi kuuchoma mtima wangu, na sasa nikapoteza kabisa bima ya matumaini!

    Baada ya mwendo kasi wa takribani saa moja hatimaye gari ilisimama, nikasikia tu mlango ukifunguliwa akashuka mtu sikujua ni nani. tuliendelea kutulia ndani ya gari ile karibu dakika kumi nzima kabla ya kusikia sauti nyingine ikituamuru

    “SHUKENI NYIE NGURUWE PORI, karibuni sana kwenye himaya tukufu ya ya PABLO MWAKI.” Ubaridiukapenya mpaka kwenye mifupa yangu..hofu!

    Hapohapo nikasikia tu nimevutwa mkono na kuteremshwa kwenye gari, hakika nilishushwa kibabe na kuanza kupelekwa kusikojulikana huku nikiwa na kitambaa changu usoni. kwa nyuma yangu nilisikia sauti ya Ntahondi akitonga na kutweta, roho iliniuma sana lakini sikuwa na cha kufanya

    Baada ya hatua kadhaa nilisimamishwa kidogo halafu nikasika sauti ya mlango ukifunguliwa taratibu, mara nikaamriwa niingie ndani, nikaingia bila ya kujua nimeingizwa wapi, nikaongozwa mpaka sehemu fulani nikaambiwa nisimame, Nikasimama! kisha Ntahondi nae alikuja mpaka ubavuni mwangu akasimamishwa jirani yangu. nilimjua tu kwa harufu ya marashi na utuli aliyojinyunyuzia.

    Ilikuwa ni sehemu tulivu sana iliyotawaliwa na ukimya wa kuogofya mno, kwa juu usawa wa kichwani nilisikia mlio wa feni kubwa zikipepea, nikajuwa tu ni zile za ‘panga boi’ .Baada ya kusimama kwa dakika kadhaa, nilisikia mtu akinishika maeneo ya kisogoni, nikajua kuwa alikua akinifungua kitambaa, lakini kabla hajafanya hivyo nilisikia sauti kali, tena ya nguvu, ilionekana ikitokea kwenye Spika kubwa zilizomo mle ndani



    “SAPRAAAAAAAAAIZ.” Sauti hiyo ilifuatiwa na sauti kali za watu wakishagalia na kupiga kelele kwa wingi na hapo hapo nikafunguliwa kitambaa changu usoni



    “Oooh my God,” nilijisemea mwenyewe kwa sauti, Sikuamini wala kuelewa nilichokuwa nikikiona mle ndani, hakika nilistaajabu!

    Kulikuwa na umati mkubwa wa watu wakiwa na furaha kubwa, nilipomgeukia Ntahondi naye alikuwa ameshafunguliwa kitambaa, alionekana kuwa haamini pia, kwa kifupi tulikua kama mazuzu tusiojuwa kinachoendelea. Cha ajabu Kapteni makala hakuwa pamoja nasi. Nilipowageukia wale maofisa usalama niliwaona wote wakiwa wamesimama pembeni huku nao wakicheka kwa huku wakipiga makofi.

    Ghafla nikamwona mama yangu mzazi Bi Shammy akija kwangu na kunikumbatia huku akilia kwa furaha

    Huku nako namwona Ntahondi naye akikumbatiwa na mama yake kwa furaha kubwa, watu waliofurika ukumbini mle walikua wakiendelea kushangilia tu bila kutulia na kwa mbali Dj aliachia wimbo laini



    Amaa kweli hii ni ‘SURPRISE’



    Sasa nilianza kupata picha kuwa hatukuwa tumetekwa bali ilikuwa ni mpango maalum wa kutuleta huku kwa mtindo wa kutushtukiza maana sasa nilianza kuwaona watu wengi niliowajua, nilimwona Mwalimu Honde akiwa ameshika kipaza sauti nadhani ni yeye ndiye aliyesema lile neno ‘Surprise’, nikawaona baadhi ya rafiki zake na Ntahondi kutoka chuoni kwao, kwa mbali nikwaona wazee fulani hivi na ndani ya dakika kadhaa nikawakumbuka, walikuwa ni wale wazee wa kule kijijini walikotuokoa na kumpigia simu Oscar, ukumbi ulijaa ndugu, jamaa, na marafiki. Sasa furaha ilianza kutamalaki usoni mwangu, nikajishangaa nikishindwa kujizuia na ghafla machozi yakawa yanitiririka mashavuni, Mama yangu akawa ananifuta huku akinibembeleza

    Ndipo sasa Mc Honde akautuliza ukumbi uliokuwa bado umelipuka kwa shangwe, baada ya ukumbi kutulia akaanza kuongea!

    “Mabibi na Mabwana, ndugu waalikwa wote, sasa huu nd’o muda maalum tuliokuwa tukiusubiri kwa hamu na tayari vijana wenu wameshawasili ukumbini. Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kwamba Naufal na Ntahondi ni vijana waliojitengenezea historia ya kipekee katika maisha yao kufuatia mkasa wa kusikitisha na kuumiza sana uliowakumba, japo waliumizwa nafsi na miili yao kwa kuteswa na kutwezwa lakini kwa ujasiri na jitihada walizozitumia kupambana na kujiokoa Mungu aliwasaidia na kuwaonesha nja na hatimaye leo tupo nao hapa, Hakika wameweza kuishinda nguvu kubwa ya fedhuli na nduli aitwaye Pablo Mwaki. Kwa mliohudhuria juzi mahakamani mlipata wakati mzuri kusikiliza mwenendo wa kesi ulivyokuwa, mlipata kujua uhalifu mkubwa uliokuwa ukifanywa na Mwaki kwa ushirikiano na baadhi ya viongiozi serikalini ambao nao walitiwa nguvuni na kuhukumiwa pamoja…mlipata wasaa mzuri wa kushuhudia Pablo akihukumiwa adhabu ya kifo, na baadhi ya wapambe wake wakihukumiwa vifungo vya maisha jela. Pia mlishuhudia Ramla akihukumiwa miaka Tisini jela pamoja na kazi ngumu kutokana na kushiriki na kupanga njama chafu akiwa na Bwana wake Pablo ambaye baadae iligundulika kumbe alikuwa ni baba yake mzazi. najua kuna mengi ya kujifunza kwenye tukio hili kwa kila mwenye akili timamu, hivyo tumekutana hapa kwa pamoja kuwapa pole vijana hawa na kuwapongeza kwa ujasiri wao tangu mwanzo wa kesi mpaka iliposhia, sina haja ya kuirejea tena hapa kwa kuwa nilishaisimulia hapo awali.” Baada ya maneno hayo tena kwa mara nyingine ukumbi ulilipuka kwa nderemo na vifijo huku tukiwa tumekumbatiwa na wazazi wetu, sasa nilipata picha kuwa kumbe hukumu ilikua juzi yake, japo sikujua kwa nini hatukupelekwa mahakamani.

    Nikiwa bado natafakari, utadhani Honde alizisoma fikra zangu akaendelea kufungukuaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “…Juzi haikuwa rahisi kuwaleta vijana hawa mahakamani kwa sababu walikuwa wakiwindwa ili wauawe kupoteza ushahidi lakini kwa kuwa ushahidi ulikuwa umekamilika hivyo hiyo haikuweza kuathiri mwenendo wa kesi na hatimaye hukumu kutolewa, sasa tukiwa tunajiandaa kuachia muziki laini huku mkipata vinywaji na maakuli napenda kutumia fursa hii kuwasemea jambo moja Naufal na Ntahondi..” Ukumbi mzima ulitulia kimya kujua ni nini hasa tunataka kusemewa! “…Ndani ya muda waliokuwa pamoka katika tabu hatimaye vijana hawa wameamua kuwa pamoja zaidi na zaidi, milele na milele.. kwa maana ya kuwa Mke na Mume, hivyo siku yaleo watajitambulisha kwenu kama wachumba! watavishana pete za uchumba hapahapa, na kwa kuwa jambo hili wameliridhia wenyewe kuwa wana nia ya kufunga ndoa hivyo basi Mhe Waziri Mkuu ambaye ni kaka yangu mimi ametoa gharama zote za kumaliza shughuli ya ndoa yote hii ambayo tumepanga ifanyike Kesho katika ukumbi wa Seflava.” Ukumbi mzima ulilipuka kwa makelele ya kupongeza, nikamuona mama yangu anamsogelea mama yake na Ntahondi akamkumbatia, hapo hapo nasi huku tukakumbatiana huku waalikwa wakiserebuka muziki mzuri uliowekwa na Dj



    TAMATI



    Maundu Mwingizi, 2014

0 comments:

Post a Comment

Blog