Simulizi : Siku Ya Graduation
Sehemu Ya Nne (4)
*****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi ya siku iliyofuata tuliamshwa wote mapema sana na Manyampara, tukahesabiwa wote kabla ya wafungwa kuanza kutoka kwa ajili ya kwenda kwenye magenge yao ya kazi huko nje, Nilimshukuru Mungu kwa kuniamsha salama, sikupata usumbufu wowote kutoka kwa wababe wa jela, sasa nikaanza kupambana na hisia za machungu kichwani mwangu huku nikiihesabu siku ya pili nikiwa jela, nilijuwa sasa kuwa bila shaka siku hiyo huenda ningeanza kupata mateso kutoka kwa askari ili niseme wanachotaka wao nikiseme.. hakuna wazo hata moja lililopita kichwani mwangu nikalipatia ufumbuzi zaidi ya kuishia kulia tu kama Mtoto wa kike chambilecho cha yule Mfungwa alinikaripia jana yake
Ukafika muda wa kula, wote tukasimama foleni kwenda kuchukuwa chakula, foleni ilikuwa ndefu huku ikijongea taratibu kama chatu alievimbiwa, tuliendelea tu kusogea mbele.. nilipokuwa nimekaribia kufika sehemu ya meza ya chakula, muda huo geti likafunguliwa wakawa wanaingizwa wafungwa na mahabusu wapya na waliokua wamepelekwa mahakamni, nikawa najaribu kuwatazama kama ningemjua hata mmoja ili nipate kampani.. Naam nilimwona mmoja, kijana hatari, kijana mnyama ambaye sikutegemea kumwona kamwe, moyo wangu ulipiga mpaka nikahisi umeachia nyufa kwa ndani. nilijaribu kujitoa wasiwasi na kujikaza lakini ilishindikana mpaka nikashtuliwa na kijana aliyekuwa nyuma yangu ili nisogee mbele nichukuwe chakula, nikasogea mpaka pale sehemu ya chakula, nikapewa ugali kidogo na maharage. chakula hakikuwa na mvuto hata kidogo lakini haikunishughulisha sana zaidi ya kurudisha macho kwa kijana Yule ambaye sasa naye alikuwa akinitazama huku akimuonesha mwenziye aliyeingia naye mle ndani, Wakaniangalia!
Alikuwa ni Yule baunsa niliyepambana naye kule godauni, kijana wa Pablo Mwaki, nilijiuliza amekuja kwa kesi gani? Au alikamatwa? Sasa mbona ananiangalia mimi tu tangu aingie humu, Au amekuja maalum kwa ajili yangu?
Sikupata jibu, nikaenda mpaka upande kushoto wa selo yetu nikawa nimekaa na mabakuli yangu ya chakula, wakati naanza tu kula huku akili ikinizunguka, nikawaona nao wanakuja kule nilipokaa mimi, Nikajikaza!!
Walipofika tu karibu yangu, Baunsa akaanza kusema na mimi
“Milima haikutani binaadamu hukutana, huwezi kuukimbia mkono wa Pablo Mwaki kijana.” Sikumjibu kitu zaidi ya kumtazama tu. na nikaendelea kula japo chakula sasa kikawa hakipiti kooni. nikachukua mabakuli yangu nikasimama ili niondoke niwaache peke yao, hapohapo yule mwenziye na Baunsa akaniwahi kunishika mkono “Not so fast amigo! Utatukimbia mpaka saa ngapi wakati usiku tunalala na wewe! Kaa tuongee ya mwisho maana asubuhi utaamka jina tu.” Maneno hayo yalizidi kuniumiza. nikajua kuwa naelekea ukingoni, niliamini usiku nitauawa tu! nikajikwapua kutoka katika kiganja kipana cha mkono wa huyo jamaa aliynishika, nikaondoka na kuhamia upande wa pili nikiwa sasa nimeishiwa hamu yote ya kula,
Baada ya chakula tukaingia tena ndani, na sasa nikamwona Mnyampaa akiwaleta wale vijana wa Mwaki katika Selo niliyopo mimi, ikazidi kunidhihirikia wazi kuwa ule ni mpango maalum wa kunimaliza. walipoingia nao wakakaa pembeni kidogo ya nilipokuwa mimi, mawazo yalinijaa kichwani, sikujua nikimbiilie wapi, dunia niliiona kama yai jinsi ilivyonibana
‘Basi sasa namuachia Mungu’ nilijisemea mwenyewe, Nilikaa mle selo mpaka jioni ikaanza kuingia, kadri nilipoona giza linaanza kwa mbali, nilijisikia uchungu mkubwa, nilijuwa sasa ninakwisha.. sikujuwa kule katika selo ya wanawake hali ikoje kwa Ntahondi
“NAUFAL BAKSHI” Nilisikia nikiitwa kwa nguvu na askari jela mmoja nje ya geti kuu, nikaitika na kwenda haraka mpaka pale, wale vijana wa Mwaki nao walishtuka na kushangaa kidogo,
Nilipofika askari akanifungulia mlango nikatoka kisha akufunga. akanikabidhisha kwa askari mwingine ambaye sikumjuwa, wazo likaniijia kuwa sasa huenda nd’o naenda kupewa adhabu nilizoahidiwa na Sajent Gululi,
Afande yule aliyenichukuwa aliniambi nimfuate, nami bila ajizi nikaanza kumfuata huku nikiwa kichwa chini mikono nyuma. nikamfuata mpaka ofisini mwake, nilipoingia tu nilipigwa na mshangao nilipomuona Ntahondi naye akiwa ameshaingizwa mle ofisini, nilipogeuka upande wa pili nikwaona wameketi Mwl Honde na kijana mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi, sikumtambua kwa haraka, nilipofika tu afande Yule akanipa viatu vyangu na mkanda wa suruali walivyovichukua wakati naingizwa selo, nikavipokea na kuvaa,
“Inspekta nadhani vijana wak wapo salama bin salimin,” Aliongea Yule askari magereza
“Nakushukuru kiongozi” akajibu Yule jamaa aliyekuwa ameketi na Honde, bila shaka ndiye Inspekta
“Karibu tena.” Honde na Inspekta wakainuka na kutuambia tuondoke zetu, sikuamini kusikia hivyo, yaani naondoka jela nikiwaacha maharamia ndani. ilikuwa ni kama Nyota ya Jaha imeniangukia,
‘Amaa kweli Mungu mkubwa’ nilijisemea kimoyomoyo, nikatoka nao mpaka nje na sasa tukaingia kwenye gari, tukaanza kuondoka, japo sikujua tunakwenda wapi, mawazo ya maumivu yalinitawala kicwani japo yalopozwa na tukio lile lilionitokea kama ndoto, sikumuuliza Honde kuwa ni kwanini yule askari aliamua kutufanyie vile, nilihisi wameshajua kila kitu ndo maana wapo pale kuniokoa, safari yetu ikawa inaelekea maeneo ya Msasani,
Baada ya magurudumu ya Gari kuzunguka kwa kasi nzuri hatimaye breki zilipigwa mbele ya Nyumba moja kubwa, Nzuri, na ya kifakhari iliyo zungushiwa Fensi kubwa iliyonakshiwa kwa kila aina ya mapambo, baada ya kusimama pale akateremka Mwalimu Honde na kwenda moja kwa moja Getini kuongea na Walinzi waliokuwa pale Mlangoni, baada ya mazungumzo yao mafupi walifungu geti gari yetu ikaingizwa ndani, tulipofika ndani ya geti hili kubwa Tukapokelewa na kijana mmoja Mrefu, maji ya kunde, aliyeonekana kujazia vizuri misuli yake licha ya Suti aliyokua ameivaa lakini bado alionekana vema kuwa ni mwana mazoezi, akatupokea na kutuongoza ndani kabisa ya Mjengo uleCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulitembea katika korido ndefu mpaka katikati ambako wote tulisimama, kisha kijana huyo mwenye Suti nyeusi akagonga Kengele maalum. wakati huu sasa tulikuwaa wanne tu; Mimi, Ntahondi, Mwalimu Honde, na huyu kijana aliyevaa suti nyeusi, baada ya kama dakika mbili mlango ukafunguka tukaingia ndani,
Tulipofika ndani tukapokelewa na watu waliokuwa mle ndani, kwa harakaharaka niliweza kuwatambua wawili tu kwa kuwa nilikuwa nikiwaona mara kadhaa kwenye vyombo vya habari, wakwanza alikuwa ni Mhe. Abraham Honde Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania, na wapili ailikuwa ni Mhe Stanley Kalokola Waziri wa Mambo ya ndani, watatu sikumtambua kwa haraka.
Baada ya mapokezi hayo tukaketi, Waheshimiwa hawa walionekana kuumizwa na kusononeshwa sana na mwonekano wetu uliotokana na kuteswa kikatili hapo. tulikuwa tumepauka vuu kama nyani huku michiirizi ya damu ikiwa imegandana mwilini, mimi nikiwa na jeraha kubwa kichwa nillolipata wakati ule tunakirikishana na Yule Baunsa kule godauni, Ntahondi akiwa kaumia zaidi miguuni kutokana na kukanyaga visiki vikavu vya miti wakati tunakimbia kule Porini, ukijumlisha na adha ya jela ya jana yake ndio kabisa tulikuwa hatutamaniki.
Baada ya kuketi tu kijana Yule aliyetinga suti nyeusi alianza kututambulisha kwa waheshimiwa hawa, na hapo ndipo nikamjua huyu mtu wa tatu, aliitwa Mhe Florent Samwel Madoli ambaye ndiye Mkurugenzi mkuu wa idara ya Usalama wa taifa.. baada ya utambulisho ule naye akajitambulisha kwetu kuwa ni Kapteni John Makala, kilichonishangaza kijana huyu alionekana kutujua vizuri maana alipomaliza kutupa utambulisho wao sasa akatutambulisha sisi kwa Mhe Waziri kwa kututaja majina mpaka na ubini, alianza kwa kunitaja mimi kua ni Naufal Mpodobakshi kisha akafuatia kwa Ntahondi Salum, nilihisi tu kuwa amekuwa akiifuatilia kwa karibu zaidi kesi ile kiasi cha kutujua vizuri, pia niliona mkononi ameshika faili kama lile alilokuwa nalo tukimtolea Sajenti Gululi
Baada ya hapo akamuachia nafasi ya kuongea Mhe Waziri Mkuu ambaye aliongea kwa utulivu mkubwa “…Kwanza poleni sana kwa matatizo yaliyowakuta, hizo ni changamoto katika maisha ya kila mwanadamu na ili mkabiliane nazo inabidi kwanza mzikubali, mkubali kuwa mmefikwa na matatizo. Matatizo yaliyowakuta ninyi pia yametusaidia hata sisi kuzidi kumpeleleza sana huyo anayedhaniwa kuhusuika na matatizo haya na sasa tuna vitu vingi sana tumevipata kama ushahidi wa uharamia wa huyu mtu.. ila kabla hatujafika mbali zaidi hebu tuambieni ilikuwaje huko mlikotekwa maana Naufal huku pia una kesi nyingine ya ajabu sana kuhusu tuhuma za kukutwa na mwili wa Yule dereva teksi aliyeuwa.“ Nikaanza mimi kuelezea Stori nzima jinsi ilivyokuwa, kwakweli hadithi ilikuwa ni ndefu ya kuumiza na kusisimua nilielezea kwa ufasaha bila kuruka hata nukta moja, stori hii ilionekana kumuingia sana Mhe Waziri wa Mambo ya ndani nikaona anaingiza mokono mfukoni na kutoa Leso kisha akawa anafuta machozi, Nikaendelea kusimulia mpaka mwisho.. Nikamaliza!
Ikafika zamu ya Ntahondi ambaye aliongea mengi sana mpaka siku aliyokamatwa na kuteswa kinyama.. hakuweza kufika mbali akaanza kulia, ikabidi Waziri Mkuu ambembeleze kwa kumsihi sana mpaka akanyamaza.. Alipotulia ndipo sasa akaanza kongea Waziri wa mambo ya ndani “..Huyu Pablo ni mtu hatari sana.. ana pesa chafu nyingi zisizojulikana hata amezipata wapi, ana mtandao mkubwa ambao anautumia katika uovu… kwa uchunguzi wa kina tulioufanya tumegundua kuwa huyu bwana mwaka 1998 alifungwa jela kwa kosa la mauaji ya Muuza Madini kutoka mererani, inasemekana alimwua na kumdhulumu pesa nyingi sana, lakini mwaka 2000 alikata rufaa na kushinda kesi yake ambayo inasemekana alihonga pesa nyingi sana kwa baadhi ya mahakimu wasio waadilifu, sasa baada ya kurudi huku uraiani akawa anajihusisha sana na Biashara ambapo baadaye akabobea katika biashara za wizi wa magari pamoja na uuzaji wa dawa ya kulevya... mtu huyu ni hatari sana, amewanunua watu wengi sana katika vitengo tofauti na kuwafanya vibaraka wake.. kuna mapolisi, waandishi wa habari, mahakimu, nk. kesi zote za mauaji aliyoyafanya tayari tuna ushahidi wote juu ya meza, sasa na hiyo ya kumuua huyo dereva nayo tunaiingiza kwenye List” Mhe Waziri alikuwa akiongea kwa hasira iliyotamalaki usoni mwake “Habari tulizo nazo ni kwamba zimebaki wiki mbili tu ifanyike hiyo Graduation ambapo Pablo anataka kumvisha pete ya Uchumba huyo binti… Ramla, naye anapaswa kukamatwa kwa kushiriki katika utekaji nyara uliopelekea mauwaji na utesaji mkubwa. Mipango kabambe inasukwa, tunakusudia kuwatia nguvuni siku hiyo ya Graduation na kuwapeleka mbele ya vyombo vya Sheria. tutakua na ulinzi mkali sana eneo hilo la chuo kwa sababu ya usalama.. mipango yote inatakiwa ifanyike kwa uangalifu na usiri mkubwa, hata ndugu zenu hawapaswi kujua kuwa mko hapa mpaka tutakapo hitimisha mpango huu.” Akamiliza kuongea,
Nilimuelewa vizuri Mhe Waziri na niliielewa vyema habari ile aliyotudokeza, nilitamani hata hiyo siku ya Graduation ifike kesho yake tu tukamalizane, Niliamini itakuwa ni kama kumkamata kuku, hakika sikumjuwa kabisa Pablo Mwaki
Baada ya mazungumzo haya Waziri mkuu akamwambia mdogo wake ambaye ni Mwalimu Honde atupeleke vyumbani tukaoge na kubadili nguo kisha tupewe chakula halafu tupumzike na kwamba yeye angerudi pale kesho yake, Laikini kabla hatujatoka tukaombwa tupige Picha kama ushahidi wa kila tukio linaloendelea. tukapiga picha tukiwa tuko vilevile wachafu! Tulipomaliza tukatoka kwenda vyumbani tulikopelekwa na Honde. baada ya kuoga, kubadili Nguo, na kupata chakula cha nguvu tulikaa pamoja Seating Room tukiwa watatu; Mimi, Ntahondi na Honde ambaye alijaribu kutufurahisha na kututoa hofu kabisa kuwa tupo sehemu yenye usalama mkubwa na kwamba hakuna yeyote atakayeweza kuja kutudhuru mahala pale. Kwakweli tulifarijika na kurejewa na furaha kiasi
Saa mbili mbele mwalimu Honde akatuaga na kuondoka zake. Tukabaki wawili tu..
Tuliishi mle ndani kwa Raha mustarehe, tukiwa na amani na furaha, huku tukiisubiri kwa hamu Siku ya Graduation, siku ambayo tutaustaajabisha umma kwa kuwatia nguvuni Pablo mwaki, Ramla, na wapambe wao wote,
Hali ilikuwa tofauti huko nje ambako Graduation hii ilionekana kusubiriwa kwa hamu na watu wengi wakiwamo wanafunzi, waalimu, na watu wengine ili kushuhudia tukio lilosisimua wengi la kitenda cha Pablo Mwaki kumvisha pete ya uchumba Ramla
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Amaa kweli pesa ilipasua mlima!
Nasikia tayari mwaki amewaandaa baadhi ya waandishi wa habari kutoka katika vyombo kahaa vya habari kwa ajili ya kuripoti tukio hilo
Siku ziliyoyoma tukiwa mle ndani, mara kwa mara Ntahondi alikuwa akilalamika kuwa asingeweza kuendelea kuishi peke yake kule Chumbani kwake kwani kila ikifika usiku mkubwa alikuwa akishtuka na kuogopa sana, sikuwa na jinsi nikamwambia awe anakuja kulala kwangu, haikuwa tabu kabisa na hivi vyumba vyetu vilikuwa jiranijirani, Kulala chumba kimoja haikuwa mara yetu ya kwanza japo mazingira ya kwanza na haya ya pili ni tofauti, kwa sasa miili imeshaanza kujengeka na kupendeza huku virutubisho vya vyakula vikifanya kazi yake.. tukawa tunalala chumba kimoja
Tuliendelea kuishi na kulala pamoja, tukazoeana kupita kiasi, tukawa tunacheka pamoja, kula pamoja huku tukitaniana, mara wazo la ajabu likawa linaniijia kichwani kila mara.. Sijui nimwambie? Kila nilipotaka kumwambia nilijizuwia
Niliendelea kujizuia nisimwambie, lakini akili ilizidiwa na mwili, Uzalendo ukanishinda
“Ntahondi, kuna jambo nataka kukuambia,“ Nilivunja ukimya siku moja tukiwa tumeketi pamoja
“Niambie tu Naufal.“
“Unajuwa tumeteseka sana, na tumeumizwa sana, mkasa huu hauwezi kukamilika kama utamtoa mmoja wetu, huu ni mkasa wetu sote.. naamini Mungu alikuwa na agenda yake kutukutanisha na kutufanya kuwa karibu zaidi..”
“Yeah ni kweli kabisa.“
“Sababu ya mateso yote haya ni mapenzi.. Mapenzi yamepelekea tupate taabu lakini pamoja na hayo huu sio mwisho wa kupenda wala sio mwisho wakuufungua moyo..“
“Ni kweli, na miye nakuombea kwa Mungu umpate mwingine mwenye mapenzi ya dhati akufute machozi ya kila kilichokikumba.“
“Miye nahisi tayari nimeshampata mwenye mapenzi ya dhati, atakayenifuta machozi nami nimfute jasho na kumliwaza..“ Tukaangaliana kwa pamoja kisha tukajikuta tumecheka
“Nani tena huyo mwenzetu aliyepata bahati hiyo?“ Aliuliza Ntahondi huku akiwa bado ametabasamu
“Ni Ntahondi.“ nilijikuta nikiropoka bila kizuwizi, Ntahondi akabaki ananiangalia kamaambaye hakutegemea kusikia kitu hicho kutoka kwangu. Sikutaka kumpa nafasi yakujifikiria zaidi, nikaendelea “..Ntahondi naamini kuna kitu cha ziada mpaka Mungu kutukutanisha ki mtindo huu, tafadhali tusiache historia yetu ipotee.. naomba unikubalie! na kama utaniridhia na kunipokea nataka tukimaliza tu zoezi la kumtia nguvuni Mwaki na muuaji mwenzie Ramla nikuvishe Pete ya Uchumba.. ili tujiandae rasmi kwa ajili ya Ndoa.“ Ntahondi alionesha wasiwasi mkubwa wa kukubali jambo hili,akawa anaweka vipingamizi kadhaa, ila baada ya maongezi marefu tulifikia muafaka na kukubaliana
*******
Siku zilizidi kuyoyoma kuelekea kwenye Graduation, siku inayosubiriwa kwa hamu na watu wengi kila mmoja kwa namna yake, huku kwetu mimi na Ntahondi huba lilizidi kukolea na sasa ikawa kila siku ni mipango yetu ya Ndoa tu kama tutalimaliza salama zoezi hili,
Mara kwa mara Mwl Honde alikuja kupiga Stori nasi, Tulicheka na kufurahi pamoja. Siku moja Ntahondi akiwa amejilaza chumbani Honde akawasili, baada ya salamu na michapo ya hapa na pale akanishauri jambo
“..Sikia Naufal,unajua umeteseka sana kaka kwa ajili ya yule kahaba… waswahili wanasema Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa ujenzi..”
“Una maanisha nini?”
“..Ntahondi yuko mikononi mwako Kamata Fursa hiyo kaka”
“Miye nilifikiri una jambo kubwa kumbe mambo yenyewe nd’o hayo.. embu acha zako bwana, miye bado nina stress zangu, hapa naisubiri kwa hamu Graduation..”
“Au kaka bado ka-moyo kapo kwa Ramla?” Swali hili sasa lilinipa hasira japo nilijikaza ili asielewe, Sikutaka kabisa kusikia habari za Ramla kuwa eti bado nina haja naye. Akaendelea kunipa somo ambalo yeye hakujuwa kuwa nimeshalitekeleza kimyakimya
“Wazungu wana msemowao ‘Some people stick with you only because they have no one to stick with, but when they found someone else they will just leave you’wakiwa na maana kwamba Kuna baadhi ya watu wanakuwa pamoja nawe kwakuwa tu hawana mtu mwingine wakuwa naye karibu, na endapo siku wakipata mtu mwingine wewe watakutelekeza tu!” nilimuelewa vyema Mwalimu Honde kuwa amemgusa Ramla ambaye alikuwa na mimi kwa kuwa tu alitaka kupata msaada ambao kwa wakati ule hakuwa na mtu mwingine wa kumpa, kwa sasa kampata nd’o maana kanifanyia yote yale, Honde akaendelea “…Kama utakuwa na Ntahondi hakika itavuta hisia za wengi, na kutengeneza historia ya kipekee hata kwa vizazi vyenu.”
Alijaribu kunishawishi kila siku
Nakumbuka Siku moja ikiwa zimebaki siku mbili tu kufikia siku ya Gaduation, Nikiwa na Ntahondi tumeketi sebuleni tukipiga soga za hapa na pale, aliingia Mwl Honde akiwa na yule kijana aliyetupokea siku ile tulipowasili, Kapteni John Makala.
Walipofika tukawapokea kwa furaha, baada ya salamu na mazungumzo mafupi ikaanza mipango ya maandalizi ya kuvamia ukumbi katika siku hiyo ya Graduation, Kapteni Makalaalitwambia kuwa yeye ndiye atakaye kuwa Kiongozi wa hiyo Oparation nzima, na tayari kuna vijana wao wa usalama wa taifa wanaosoma pale Chuoni wameshajiweka tayari kwa tukio hilo
Tukapewa Ramani nzima ya jinsi zoezi litakavyokuwa, Kapteni akasema kuwa ikifika siku hiyo wao watatangulia mapema ukumbini kuandaa mazingira, na watakuwa hukohuko mpaka wakati wa shughuli yenyewe, kisha sisi tutatakiwa kwenda mpaka nje na gari yetu bila mtu mwingine yeyote kutambuwa.. tukifika tutatulia tu tukisubiri kuitwa tuCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa sasa mtapaswa kutulia hivyohivyo, na hata siku hiyo ikifika mtakua ndani ya gari tu kabla ya kushuka maana hamtakiwi kuonekana mapema hasa wewe Naufal si unajuwa unatafutwa na polisi kwa tuhuma za mauaji! sasa kama utajitokeza mapema utakamatwa na kusababisha zoezi hili kuvurugika, kwa sasa Polisi hawajajua chochote kuhusiana na kinachoendelea.. hii nisiri ya maofisa wa usalama wa taifa tu.” Maneno hayo yalinichoma tena upya na kunitonesha jeraha langu moyoni kuona pamoja na kutekwa, kuteswa, na kuumizwa vibaya lakini bado Pablo Kanichafua na kwenye vyombo vya habari kwa tuhuma za uongo kuwa nilihusika na mauaji.. nilisononekana sana lakini niliyakumbuka maneno ya kifaransa yaliyopatwa kutamkwa na Mwanamuziki mkongwe Afrika Kofii Olomide ‘Lokuta eyaka na ascenseur, kasi verite eyei na Lokuta escalier mpe ekomi’ akiwa na maana kwamba Uongo hutumia ‘lift’ kupanda Ghorofa(Hivyo unawahi sana kufika), wakatihuo Ukweli hutumia ngazi kupanda ghorofa(Hivyo utachelewa kufika). Japo ukweli utachelewa ila utafika tu, na siku zote ukweli ukifika uongo hujitenga.
Baada ya mazungumzo marefu kutoka kwa Kapteni Makala, akatoka na kuondoka zake na kutuacha tukiwa na Mwl Honde,
Mwalimu Honde akaendelea kutupa hali ilivyo huko nje,
“Nimeongea na kaka yako, Jarufu ameniambia kuwa mama yako anaingia leo kutoka Tabora na Lengo lake kuu ni kuja kuhudhuria hiyo Graduation ili apate nafasi ya kumkabili huyo Pablo a hapohapo amuanzishie vurugu ya hatari.. Jarufu kaka yako amejaribu kumkanya lakini amegoma kau, amesema siku hiyo nd’o Pablo atamuonesha ilipo maiti ya mwanaye kipenzi..” Tukacheka wote kwa kwa pamoja kusikia kuwa Mama alikuwa akijua tayari nitakuwa nimeshauawa.. Japo niliwahurumia sana mama yangu na kaka jinsi wanavyohangaika kwa ajili yangu wakiwa hawajui nilipo ila niliamini ni kweli wananijali, Honde Akaendelea kuongea huku akiwa amejilaza kiubavu kwenye sofa “..Mbaya zaidi sasa Mama’ake Ramla naye nasikia amekatiwa tiketiya Ndege na Pablo aje kuhudhuria tukio hilohilo, nakwambia ni vioja huko” tulikuwa tukisikiliza maneno ya Mwl Honde huku tukicheka.. Honde akaendelea kutiririka “..Huku nako Mama Ntahondi naye kaenda kumtukana Mkuu wa kituo na kumtuhumu kuwa anajua kila kitu kuhusu sakata la kutekwa kwa mwanaye halafu hataki kumkamata mtuhumiwa, almanusura awekwe ndani.. naye kasema atakuja siku hiyo Graduation hapo chuo Kumnanga Pablo Mwaki hadharani..”
Stori ilikuwa tamu sana hasa unapoona watu wako wakipambana kwa ajili yako.. nasi tuliendelea kujidhadhatiti hasa kufuatia taarifa tunazopewa kua Pablo ni mtu hatari hivyo zoezi la kumkamata si la lele mama, Baada ya Mazungumzo marefu Honde akatuaga na kuondoka zake na kutuacha tukiwa tumepumzika pale Sebuleni.
Hatimaye siku ya Tukio ikawadia
Siku ya kipekee kwetu!
Siku nzito!
Siku ya Graduation!
Tuliamka mapema sana siku hiyo kuliko siku zote, tukajiandaa kwa kuoga na na kupiga pamba kali, Ama kwa hakika siku hii tulipendeza,
Ntahondi alikua anang’aa kama Noti mpya ya elfu kumi mpaka nikatamani kuwa hii nd’o ingekuwa siku yetu ya kuvishana pete,
Tukaenda zetu juu yea meza kuu kupata kifungua kinywa kizito kwa ajili ya kujiweka fiti kimapambano. baada ya kupata kifungua kinywa tulirudi kuketi juu ya makochi huku tukiendelea kuangaliana kwa macho ya ushindi.. Haikuchukuwa muda mrefu, ikiwa ni majira ya saa moja asubuhi ziliwasili Gari mbili Nyeusi, Moja walishuka wale askari wawili waliokuja kule kijijini kutuijia wakiwa na kapteni Makala, gari ya pili walishuka Mhe Waziri Mkuu AbrahamHonde, Mhe Stanley Kalokola, na Mhe Florent Samwel, wakajumuika nasi Seating room,
Baada ya Salamu na Mazungumzo Kapteni Makala Akitoa maelekez ya utaratibu wa utekelezaji wa mpango kazi wetu, kisha tukapewa baraka zote na viongozi hawa ambao hawakukaa sana wakaondoka.
Tukabaki ndani sisi na mashushushu hawa tukiendelea kushibishana mbinu na utaratibu wa zoezi zima na baada ya kuelewana vyema Sasa ikawa ni mawasiliano tu yakiendelea kati ya Mwl Honde na Kapteni Makala kuhusu hali ya sherehe kule chuoni, na baada ya kupokea taarifa za awali kuwa Sherehe inafanyikia katika ukumbi wa nje kutokana na kupata wahudhuriaji wengi sana, ikabidi wale Askari wawili waanze kuondoka haraka ili wawahi nafasi muhimu pamoja na kuyaelewa mazingira, sisi tukabaki na Kapteni na ilipofika majira ya saa tatu nasi tukatoka nje na kuingia kwenye gari moja sikumbuki ni aina gani ilikuwa kama Pajero hivi,
Mimi na Ntahondi tukakaa siti za nyuma, huku Kapteni Makala akakaa Siti ya mbele
Safari ikaanza!
Hapo sasa kila mtu akawa kimya akilifikiria tukio la huko tuendako, Tulipokaribia kuingia barabara ile inayotokea moja kwa moja Chuoni ambako ndiko sherehe hizi zinakofanyikiwa ghafla kwa mbele ya Ukumbi wa makumbusho ya taifa ambalo ni jengo lililokaribu kabisa na chuo hiki nikaona gari nyekundu imesimama pembeni ya barabara, nilipozidi kukaza macho nje ya gari hiyo nikawaona vijana watatu wamesimama huku wameegamia gari hiyo.
Mmoja nilimjua vyema, alikuwa yule Baunsa mweupe wa kule godauni tuliyepambana naye na kutoroka, nikamgeukia Ntahondi ili nimuoneshe bahati nzuri alikwishamwona Tukamweleza Kapteni, naye akamuangalia kwa makini kisha hakusema kitu, tulipoipita ile Kapteni akatoa simu yake na kumpigia mmoja wa vijana wake wa kazi na kumwambia awe karibu na watu wale, akakata simu, na muda huo gari yetu ikaingia kwenye viunga vya Chuoni hapa inakofanyikia sherehe hii
Watu walikuwa ni wengi sana, wakionesha kuwa na furaha kubwa! Spika kubwa na za kisasa ziliendelea kutetemesha ardhi kwa kuachia mziki mnene, ilitubidi tushushe kidogo vioo ili tupate kusikia kila kilichokuwa kikijiri!
Shughuli ilikwishaanza!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Gari hatukuiegesha mbali, dereva aliisogeza upande wa jukwaa kuu lilipambwa utadhani anayehutubia ni malkia. Muda huo vioo vyote vikiwa vimepandishwa na kuruhusu hewa safi iliyopozwa kwa mashine maalum ikiendelea kutuliwazi. kwa kuwa vioo vilikuwa ni vya giza/Tinted hivyo tulikuwa huru kuangalia kila kitu kinachoendelea bila ya hofu ya kuonekana
Kapteni Makala akateremka na kwenda kuchukua nafasi kulekule meza kuu!
Tayari wale askari waliotangulia kuja huku walikuwa wameketi meza kuuwakiwa wamevalia kinadhifu. Wengine suti na wengine mashati yao yenye kila ishara ya ughali wakiwa wameyachomekea kwenye suruali zao za jinzi. tukiwa ndani ya gari sasa niliweza kumwona vizuri Ramla aliyeonekana kushauka kisawasawa kuliko hata wenziye, na kile kijitumbo chake kilichoanza kuchomoza basi mimi kama nitapike vile kwa kichefuchefu!
Lazima ashauke! Sherehe imedhaminiwa na mchumba wake, yeye mwenyewe tayari yu mjamzito, anahitimi masomo, navishwa pete ya uchumba tena mbele ya mama yake huku akiamini kuwa boya wake nimetekwa.. Acha afurahi tu maana muda wa kulia umewadia
Wakati tukiendelea kuwaEnjoy wahudhuriaji waliokuwa tayari ukumbini na walioendelea kuingia ndipo ghafla tukamwona Mama yake na Ntahondi akipokelewa na vijana nadhifu walioandaliwa kwa kazi hiyo, akapewa nafasi nzuri tu karibu na meza kuu! Kweli moyoni mwa mtu ni mbali, laity wangeijua dhamira yake wangemweka mbali.
Ratiba ilikuwa ikiendelea kwa mbwembwe huku mshehereshaji Akizikonga nyoyo za wahudhuriaji kwa maneno yake matamu yenye kuvutia. Hakika shughuli ilipendeza!
Shangwe za waalikwa zilikuwa zikilipuka wakati msanii mmoja wa muziki wa Bongo Flavour akikata mauono yake Stejini ndipo ikaingia Gari moja nzuri sana aina ya Hummer na kisha ikaenda kuegesha.. wakashuka watu watatu, sikuwajua wote japo niliwakazia macho kwa makini! nikamwona Ntahondi akinigeuzia shingo na kuniangalia kasha akarejesha tena macho yake kwa wale watu watatu walioteremka kwenye ile Hummer
“Ulisema humjui Pablo Mwaki… haya sasa huyo hapo wa katikati mwenye kipara kama papai.”
Nilihisi kusisimkwa mwili mzima, Nywele zikijizoa na vinyweleo vkijitutumua. Sijui ni hasira au uwoga tu!
Walipokelewa kwa utii wa hali ya juu, ndani ya muda mfupi walionekana vivutia mbele ya macho ya waalikwa! Sikujuwa ni kwa sababu ya umaarufu na utajiri ama ni kwa ughali wa suti walizotinga! Walichukuliwa mpaka meza kuu ambako watu walijikuta wakisimama kwa heshima bila ya kushurutishwa na kuanza kumpa mikono. Wakapewa nafasi huku Pamblo akiwa karibu ya Kapten Makala.
Shughuli ikaendelea kwa kila aina ya burudani huku waalikwa wakipewa sharubati na vitafunwa
Wakati ratiba ikiendelea ghafla jicho langu likatua kwa Bi Shammy, Mama yangu mzazi! naye akiwa ameketi vizuri upande wa wazazi sikujua hata ameingia saa ngapi! nilishtuka sana nikawa najiuliza hivi akina Jarufu wameshindwa kweli kumzuiwa mpaka akaja huku wakati waliijuwa vema dhamira yake! nilijijihisi majonzi na furaha kwa pamoja maana yote haya anayafanya kutokana na mapenzi ya dhati kwangu! nikamwonesha Ntahondi, naye akafurahi kumwona.
Hafla ikaendelea bila tatizo!
Ikafika zamu sasa ya kupokea vyeti sanjari na zawadi! Hapo sasa tukawa tayari kushuhudia Ramla akipewa zawadi ya gari pamoja na kuvishwa pete ya uchumba na Pablo ili nasi tufanye yetu. Zoezi liliratibiwa na kutekelezwa vizuri kwa wahitimu kuitwa majina yao kwa kuzingatia Alphabet.. ukishaitwa jina unakwenda kupokea cheti chako huku ukipata picha kadhaa za ukumbusho, na baada ya hapo unapewa fursa ya kupokea zawadi mbili tu ukiwa pale mbele ila kama utakuwa na zawadi nyingi itakubidi ukazaipokelee pembeni ili kuwapisha wahitimu wengine waendelee.. kubwa zaidi likiwa ni muda!
Wakati zoezi likiendelea ghafla ikaingia gari ikiwa na watu wawili, nadhani walikuwa na hofu ya kuchelewa kwa jinsi walivyoshuka harakaharaka. Nilipotuliza macho nikamgunduwa wa kwanza alikuwa mke wa Mr Jimmy ambaye ni mama yake mdogo na Ramla, wapili nayenikamjuwa ni Mama Ramla mwenyewe akionekana kuzidiwa na na furaha, lakini ile angalia yake ilionesha kitu cha ziada.. kwamba anaonekana kuwashwa shari mwili mzima maana fununu kuwa mama yangu na mama Ntahondi watafanya vurugu ilikwishazagaa. naye akapokelewa na kupewa nafasi upande wa pili wa meza kuu walikokuwa wameketi wazazi pia.
Shughuli ikaendelea!
Hatimaye alphabet sasa zikafikia herufi za “R”
Nikamsikia mshehereshaji kwa mbwembwe na madaha akilitaja jina la Ramla huku akifuatiwa na keleleza za shangwe… Bila shaka huyo mshehereshaji alipangwa maalum,
Wanamshangilia msaliti na muuaji?
Kuna ishara niliiona kwa baadhi ya wahitimu waliokuwa pale ukumbini kutokumshangilia kabisa Ramla, sikushangaa sana kwa kuwa tulikuwa tumeshadokezwa na Mwalimu Honde kuwa fununu zimeshaanza kuongelewa pale Chunio kuwa Ramla ndiye aliyeusuka mpango wa kutekwa kwetu.. wengine itakuwa walimwonea gere tu!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ramla akaenda mpaka pale Mbele kwa mwendo wa mbwembwe kabisa, akakatiza kwenye zulia jekundu na kwenda moja kwa moja meza kuu kupokea vyeti vyake, huku upande wa kulia tayari wageni wake wakiwa wameshasimama kumpa zawadi, Pablo akiwa kwa nyuma yao huku mkoni ameshika boksi lililonakshiwa kwa mapambo ya kuvutia.
Akapokea vyeti vyake na kushangiliwa huku akivikwa mataji ya maua kama ishara ya upendo na pongezi kutoka kwa watu wake!
Wakati tukio hilo likiendelea nikamwona mama Ramla naye akisogea na Boksi lake la zawadi akisindikizwa na wapambe.. mara ‘Mc’ akaanza kutema cheche, ni cheche kweli zilizoanza kuuchoma msitu!
“Mabibi na mabwana baada ya kumpa zawadi motto wenu, rafiki yenu, shemeji yenu na wengine m’baya wenu mlimbwende Ramla sasa kuna zawadi yake maalum kutoka kwa mtarajiwa wake, kipenzi na asali ya moyo wake.. tumedokezwa hapa kwamba pamoja na zawadi kibao kutoka kwa mchumba wake huyo pia atakabidhiwa funguo ya gari ya kifakhari sanjari na kumvisha pete ya uchumba... Karibu sana Mr Mwaki.” Baada ya mshehereshaji kumaliza akafuatiwa na shangwe kutoka kwa wahudhuruaji kisha tukamwona sasa Pablo akijongea mbele ya umati huku mlinzi wake akiwa na boksi dogo ambalo nadhani ndani yake nd’o kuna hiyo pete na funguo ya gari!
Ramla akajisogeza mbele ya Pablo, wapambe nao wakajazana..
Ghafla!
Ikasikika sauti ya mwanamama akipiga kelele za uchungu huku akikataza jambo “NOOOO, HAIWEZEKANI.” Watu wote wakageuka wakiwa wamekumbwana mshangao wa haja! Pablo na Ramla nao walishtuka na kumgeukia huyo aliyepiga kelele zile.
“Nimesema haiwezekani hata kidogo” Alikuwa ni mama Ramla aliyekuwa akiongea kwa mfadhaiko, na mara akaanza kulia kwa sauti. Hakuna aliyeelewa kwanini alilia na kutoa maneno yale, au hakutaka Ramla avikwe pete? Lakini si alikwishapewa taarifa ya matukio yote ya siku hiyo?. Ramla akamkimbilia mama yake na kumwuliza kwa mshangao
“Mama! Nini sasa?”
“Ramla, huyo nd’o mchumba wako?” aliuliza mama Ramlahuku akimsonta Pablo
“Ndiyo mama, kwani vipi?” alijibu Ramla huku akimwangalia usoni Pablo ambaye alionekana kuelewa jambo, uso wake ulitahayari!
“Aibu gani hii jamani.. MAMA WEE!” Mama Ramla aliendelea kubwabwaja maneno huku akilia, watu wote walionekana kuduwaa,
Tukiwa ndani ya Gari yetu tukamuona sasa Kapteni Makala akisogea karibu ya Mwaki huku naye akionesha kushangazwa na kitendo cha mama huyu kulalamika kiasi kile, pia tukawaona Mama Ntahondi na mama yangu mimi nao wakiwa wamesimama eneo la tukio bila shaka walikuwa tayari kuanzisha varangati lakini nao wakashangazwa na hsintofahamu ile
Ghafla mama Ramla akamrukia Pablo Mwaki kwa hasira na kumkwida suti yake huku akilia kwa uchungu, Cha ajabu Pablo Mwaki hakuleta upinzani wowote, ni kama hakutegemea kumwona bi mkubwa Yule
Wakati zogo likiendelea kufukuta miongoni mwa wahudhuriaji ndipo mkuu wa chuo akasogea haraka pale eneo la tukio na kumshikilia Mama Ramla
“Kwani tatizo nini mama? Na kwanini unafanya hivi hasa?”
“Huyu mwanaume mshenzi sana tena MBWA, Hakika amenitia aibu leo..”
“Amefanya nini? Kwani we ni nani hasa?” aliendelea kusaili mkuu wa chuo
“Mimu ni mama yake mzazi na Ramla, naitwa Ayman Gamba.. na huyu fedhuli anaitwa Alex Mwakimsu namfahamu vizuri… ndiye Baba yake mzazi na Ramla.” Ukumbi mzima ukazizima huku kila mmoja akisema lakekwa mshangao.. hata mkuu wa chuo naye alishangaa hasa!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Namjuwa vizuri sana wala sijamfananisha! Ndiye huyuhuyu… sikujuwa kama mwanangu leo ameniita kushuhudia laana hii, miye nimekuja kushuhudia graduation ya mwanangu, akaniambia kuwa pia leo atavishwa pete ya uchumba na mumewe mtarajiwa ambaye ni mfanyabiashara maarufu aitwaye Pablo, sikujua kama ni huyu Shetani..” muda wote huo mama Ramla alikuwa akiongea huku akilia ikabidi tena Mkuu wa chuo ajaribu kumbembeleza ili aendelee kusimulia, baakwa uchungu.. akaendelea kuropoka mama huyu aliyevurugwa “Sikujuwa kama Pablo Mwaki nd’o huyu, mimi namjua kwa jina lake halisi la tangu utotoni, Alex Mwakimbusu… kumbe wamemfupisha na na kumwita mwaki”
“Mama ujuwe tuhuma unazotoa ni nzito sana, unaweza hata kushitakiwa ukishindwa kuzithibitisha... hebu tulia na utueleze vizuri jinsi ulivyojuana na huyu bwana,” Aliongea kwa utulivu Mkuu wa chuo
“Namjuwa sana huyu, nilikutana naye Tabora mwaka 1989 tukapendana sana… sikumjua alipotokea lakini nilitokea kumpenda sana, baada ya muda mfupi wa mahusiano yetu akanipa ujauzito, nilichanganyikiwa sana maana baada ya Baba yangu kugundua kuwa nina ujauzito alinifukuza nyumbani nikawa sina ujanja ikabidi niende mpaka alipokuwa amepanga, akanipokea na kuahidi kuwa ataitunza mimba ile nikawa naishi naye kwake kama mke na mume. baada ya muda tukahama Tabora na kwenda Songea tulipofika huko akanishawishi nibadili dini ili anioe… nikakubali kwakuwa nilimpenda na sikuwa na pakukimbilia lakini kila siku visa vikawa vinazidi mara anipige, mara anilaze njaa, ikawa ni shida juu ya shida! baadaye nikaletewa taarifa kuwa Mwaki ana mahusiano na mwanamke fulani mfanyabiashara kutoka Bukoba ambaye alikuwa akisadikiwa ni muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi… hapo sasa nikashindwa kuvumilia nikaamuwa kuondoka. Mwakimbusu akajaribu kunibembeleza nikakataa, alinibembeleza sana mpaka nikakubali lakini kwa sharti moja tu kuwa tukapime kwanza afya nd’o tuweze kuendelea na mahusiano, akakubali! tukaenda kupima afya.. matokeo yakawa mazuri na mabaya, mazuri kwangu na mabaya kwa Mwakimbusu ambaye alikutwa ameathirika! hapo nd’o ikawa mwisho wetu, nikarudi kwetu kuwaomba msamaha wazazi nao wakanielewa na kunipokea tena.” muda wote wakati mama huyu akiendelea kuongea huku analia kwa uchungu watu wote walikuwa kimya wakimsikiliza.. hata mama yangu aliyejipanga kuanzisha vurugu alikuwa bado kama haamini kinachoendelea, hata huku nasi Mimi na Ntahondi tulikuwa kama vile tunaangalia movie, Mama Ramla akaendelea kusimulia huku akilia kwa kwikwi “..Nikamzaa mwanagu ambaye ndiye huyu Ramla mwaka 1990 na nikamlea peke yangu bila ya kujua hata alipokimbilia huyu mwanaume, sikujuwa anaishi wapi tena na baadaye nikasikia alifungwa kifungo cha maisha jela kwa kesi ya mauaji hivyo mpaka leo nilikuwa nikijuwa bado yuko jela… Sasa mwanangu Ramla ameniita leo jushuhudia tukio hili. kumbe ana mahusiano na baba yake mzazi, tena ameshampa na ujauzito.”
Aibu!
“Amaa kweli malipo ni duniani akhera inakwenda hesabu tu, kwa jinsi ulivyofurahia kitendo cha mwanao kushirikiana na huyu Ibilisi wako kumteka mwanangu ili waoane sasa Mungu kakufedhehesha leo, uso umekushuka kama mbuzi.” Mama yangu alimpasulia maneno mama Ramla baada ya kumsogelea.. ghafla akasogea Mama yake na Ntahondi, yeye hakutaka mengi zaidi ya kumkwida Mzee Mwakimbusu almaarufu kama Pablo Mwaki na kumwambia “…Na mimi leo utanionesha ulipompeleka mwanangu… habari zako zote ninazo jambazi mkubwa we.”
Tafrani!
Wapo waliozomea, wapo walioshangilia huku watu wazima hasa akina mama baadhi yaowakifuta machozi kutokana na fedheha ile iliyomkumba mwanamke mwenzao!
Wakati mama Ntahondi akiwa kamkwida Pablo Mwaki ghafla Ramla aliyekuwa kabaki mdomo wazi muda wote akaanguka chini kama mzigo wa maembe na kupoteza fahamu papo hapo!
Sherehe ikageuka kilio na fedheha!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ghafla macho yangu yakatua kwa Yule baunsa aliyetutesa kule msituni, akamsukuma mama Ntahondi kisha akamwambia Pablo waondoke haraka, ni kama aliyekuwa anaombea Mungu atokee mtu wa kumnusuru haraka Pablo akaanza kuondoka huku nikimsikia huyo baunsa akitoa maneno machafu “…Watoto wenu makahaba, na wengine majambazi wanatekana huko halafu mnataka kuwasingizia watu.” Aliongea baunsa huku akifuata nyuma ya Mwaki.. kabla hajamaliza kusema tu akasukumwa kwa teke madhubuti kutoka kwa Kapteni Makala lililomtupa chini, Kapteni akamsogelea mpaka pale chini, akatoa kitambulisho chake cha kazi na kujitambulisha kua ni afisa wa jeshi, kisha akamgeukia Pablo na kusema “..Wewe Pablo na huyu Mbwa wako ndiyo mliowateka vijana wa watu, Naufal na Nyahondi! mkawapeleka msituni huko na kuwatesa kinyama, na kama haitoshi mkamwua yule dereva teksi ili asije kutoa siri huku mjini.. halafu we unatoa maneno machafu hadharani kama hii Nchi ya baba yako. angalia sasa Laana iliyokukumba kumbe mpenzi mwenyewe ni mwanao wa kumzaa. Kuanzia sasa wote mko chini ya ulinzi.“ watu wakawa wanazidi kutaharuki kufuatia tukio hilo, ikawa ni kimuhemuhe.. Kapteni akaendelea “…Na kwa taarifa yako vijana uliowateka tayari tumeshawaokoa na tunao.” Nikamwona mama yangu akipagawa kwa taarifa ile, huku mama Ntahondi na baadhi a waliotufahamu na kuifahamu kadhia yetu nao wakishituka. baada maelezo hayo Kapteni akageuka na kuangalia usawa wa gari yetu, akatupa Ishara kama alivyotuelekeza,
Tukateremka kutoka ndani ya gari! Dereva alibaki tukateremka mimi na Ntahondi tu, tukiwa smart na wenye kuvutia! Tulipoteremka tukaanza kutembea kusogea eneo la tukio!
Ilikuwa ni tukio la kipekee!
Tukio la ajabu!
Wapo walioshangilia na wapo waliokuwa wakilia. Macho ya baunsa akiwa amekamatwa vilivyo yakakutana na ya kwangu, nikamwoneshea tabasamu la dharau! Hakuamini, nikamwacha na kumgeukia mama yangu ambaye muda wote huo hakujua hata afanyeje, huku nako Mama Ntahondi naye alikuwa ameduwaa.
Tulipofika karibu ya Kapteni Makala, nikamwona mama yangu akija kwa kasi na kunikumbatia huku akitokwa na machozi ya furaha.. uzalendo ulimshinda! huku nako nikamona Ntahondi akiwa amekumbatiwa na mama yake. Nilipotuma macho nyuma ya spika nilifurahi sana kuwaona kaka yangu Jarufu akiwa amesimama na Mwalimu Honde ambao nao walikuwa wakiufutilia mkasa mzima kwa ukaribu wa hali ya juu
Tukiwa bado tumeshikana na wapendwa wetu huku kukiwa na hali ya fujo na kelele za wanafunzi wa chuo wengine wakitaka kumvamia Pablo na kuanza kumpiga, wengine wakitaka kukumbatiana na mwanafunzi mwenzao Ntahondi aliyekua ametekwa kumbe tayari Ramla alikuwa amezinduka na anaangalia kila kitu. Akaanza kulia kwa uchungu sana.. hakika hakuamini wala hakutegemea kuadhirika katika siku ambayo aliamini ni ya furaha.. kila akifikiria kuwa alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na baba yake mzazi ambaye ni muathirika wa ugonjwa hatari wa Ukimwi yaani lilikuwa pigo kubwa sana.. hakika Mungu anajuwa kufedhehesha! Ramla akaanza kutambaa na kuja kunishika miguu yangu huku akiniomba msamaha.. Mama yangu akamsukuma na mguu wake wa kulia na kuanza kumtolea maneno machafu
“Toa mikosi yako hapa, leo nd’o unamwona ni mtu, angekufa huko ungemwona hapa?“
“Mama naomba mnisamehe, sio kosa langu nilishawishiwa tu mimi jamani.“
“Mimi sio mama yako, mama yako huyo huko mke mwenziio.“ wakati mama akimpasha Ramla ndipo ghafla ikazuka tafrani mpya!
Kundi kubwa la vijana wa Pablo walivamia kumwokoa Bosi wao!, Ukumbi ulichaafuka na kubadilika ghafla.. ni vita kama kimbunga! Patashika ya nguo kuchanika
******
Hapo ndipo nilipojuwa kwanini John Makala ni Kapteni.. hakika alistahili kuongoza vita vyovyote vya msituni.. ni zaidi ya umeme kwa kasi, na ni zaidi tishu kwa wepesi.. aliruka sarakasi kama mchina huku akiachia mapigo ya kuangamiza kwa vijana wa Mwaki, ngumi zilipigwa kwa kiwango cha kwenye luninga, Mapambano yakachukuwa sura mpya baada ya milio ya Bunduki kuzagaa kila kona ya chuo, kumbe wafuasi wa Mwaki walikuwa wameshaitana kwa ajili ya kumwokoa mtu wao.. Maofisa wa usalama nao wakawa ndani ya mchezo.. ilikuwa ni kichapo kwa kwenda mbele!
Ndani ya dakika chache tu tulijikuta tuko vumbi japo hatukupambana na yeyot, sasa Je hao waliokuwa wakipimana nguvu? Yule baunsa alikwishainuka, na sasa kajitia kupima msuli na Kapteni Makala, wakati huo nikamwona Pablo akiwa ameshaponyoka, na muda huo akipanda harakaharaka kwenye gari ndogo nyekundu ili atoweke. nikapiga kelele huku nikimonesha Kapteni juu tukio hilo
Haraka kapteni hapo akatoka bastola yake kiunoni na kufyatua risasi, alikwishachelewa! Pablo akatoweka.
Mara kutokea kwa nyuma baunsa akamrukia Kapteni na kumshushia pigo kali, wakaenda mpaka chini, walipotua wakaanza kukikirishana kwa nguvu
Akatoke kijana mwingine wa usalama akiwa na bastola yake mkononi.. akaikimbilia gari iliyombeba Mwaki huku akiishambulia kwa risasi.. hatimaye akafanikiwa kuyapasua matairi. lakini dereva alikuwa mbishi sana akaendelea kuendesha kwa kasi akiwa tayari kaishaingia barabara kuu, haraka vijana wa usalama nao wakaingia kwenye gari yao na kuanza kuwafukuza,
huku nako mapambano yaliendelea kati ya Kapteni na baunsa. ndani ya dakika chache tu kapteni akaonesha umahiri wake kwa kumbinua yule baunsa aliyekuwa kwa juu na kumuweka chini, kisha akam’minya kwenye koromeo kwa dakika kadhaa bila kumwachia, baunsa kapapatika kama kuku anayechinjwa mpaka mwishowe akatulia, kimya! Kapteni akainuka na kujifuta vumbi kwenye suti yake! Akamwita kijana wake wa usalama ambaye nd’o alikuwa amewasili muda ule na gari, akamkabidhi Yule baunsa.. hatukujua kama kapoteza fahamu ama amekufa,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bila kuchelewa kapteni akaingia kwenye gari ile tuliyokuja nayo mwanzo na kuanza kufuata uelekeo wa kule walipokimbilia akina Pablo
Nami harakaharaka nikawachukua Mama yangu, mama Ntahondi na Ntahondi mwenyewe mpaka barabarani nikasimamisha Teksi, nikamlipa dereva, nikamuambia awapeleke Nyumbani. Walipoondoka tu name nikachukuwa bodaboda na kuanza kuwafukuzia akina kapteni Makala, Sikuwaona kabisa ila mtafaruu na taharuki za wananchi nd’o nijuwe muelekeo wao.. nikaenda mpaka karibu ya mnazi mmoja nikakuta vurugu imepamba moto, tayari Pablo akiwa chini ya mikono ya vijana wa usalama wa taifa… muda huo akiwa anavuja damu mguuni, nilipofuatilia kwa karibu nikagundua kuwa alikuwa amepigwa Risasi,
Muda houhuo yule kijana wa usalama wa taifa naye akafika mahala pale, ndani ya gari yake akiwa amembeba yule Baunsa akiwa bado amezimia, pamoja na Ramla. Alipofika tu haraka wakamchukua Pablo naye akaingizwa katika gari hiyo, na maofisa kadhaa wakaingia.. tukaianza safari
Nilishusha pumzi na kumshukuru Mungu kwa hatua ile muhimu. Nilikuwa nikiamini kuwa sasa tumemshinda Pablo. kilichokuwa kikifuata ni kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma za kupanga njama ya kututeka, kututesa, na kutuuwa. pia Mwaki alikuwa akikabliwa na kesi zingine nyingi ambazo nazo ushahidi wake uko tayari kwa mujibu wa Mhe Waziri mkuu, Japo sikua nikiamini kwa asilimia zote kama zoezi nd’o limeishia hapo kwa maana nimekuwa nikisikia Mwaki ana mtandao mpana wenye wafuasi mpaka humohumo serikalini hivyo kama atazicheza vizuri karata zake huenda mambo yakaharibika.
Nilijipa moyo!
*****
Ndani ya gari tulikuwa watu kama wanane hivi kiasi kwamba tukawa tumebanana kisawasawa japo gari haikuwa ndogo sana!
Siti ya mbele karibu na ile ya dereva aliketi Kapteni Makala, huku kwenye siti za nyuma tuliketi Mimi, Pablo, Ramla, Baunsa akiwa hajarejewa na fahamu na wale Askari polisi wawili ambao walitokea pale maeneo ya mnazi mmoja.
Wote tulikuwa kimya tukitazamana kwa kuwindana, hapakuwa na sauti yoyote zaidi ya ile Pablo Mwaki ambaye muda wote alikuwa akigumia kwa chinichini kutokana na maumivu makali katika mguu wake uliopigwa risasi katika jaribio lake la kutoroka. Moyoni niliendelea kujifariji kuwa sasa tuko kileleni mwa ushindi wetu dhidi ya Pablo.
Sasa tulikuwa tumeshika barabara ya Uhuru inayokatisha maeneo ya Kariakoo na kuendelea moja kwa moja Buguruni, ndipo simu ya Kapteni Makala ilipoita
“Hallo mkuu.” Akapokea simu Kapteni, hatukujua alikuwa akiongea na nani lakini kadri alivyozidi kuongea ndivyo sura yake ilivyozidi kubadilika, bila shaka alikuwa akipata taarifa zisizokuwa nzuri. tayari moyo wangu ukaingiwa hofu, Alipomaliza kuongea akajipiga kichwani na kuropoka kwa sauti
“Shit! Mambo yameshaharibika huko.”
“Nini tena kaka?” aliuliza yule afisa usalama aliyekuwa akiendesha gari, hakupewa jibu lolote.
“Kina Ntahondi wako wapi?” alinitupia swali kapteni baada ya kunigeukia
“Nimewachukulia Teksi imewapeleka nyumbani.”
“Umeharibu kila kitu, na kosa hilo hilo linaweza kugharimu maisha ya watu.”
“Kwanini kapteni?” nilijikuta nikitokwa na swali hilo
“Teksi waliyopanda imevamiwa… na tayari wamefanikiwa kumteka Ntahondi na wamefanikiwa kuondoka naye. Lazima wamuue ili wafute ushahidi.” Moyo wangu ulipiga kwa nguvu. Nikawa nahemakwa kasi kama punda, akili iliniruka kabisa!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikamwangalia Pablo mwaki kwa hasira huku nikiwa sijui cha kufanya
“Pamoja na haya yote bado tu unaendelea kuwatuma vijana wako wateke watu, Si ndio?” Kaptain alimwulioza swali la kebehi Pablo, hakujibiwa.Kaptain akamnyooshea mkono kumnyang’anya simu yake.
Wakati anamnyang’anya ile simu kikadondoka na kitu kingine kidogo hivi kutoka kwa Pablo, baadaye nikagundua kuwa ilikuwa ni Flash. Kilichonimakinisha ni kitendo cha Pablo kuikanyaga ile flashili isionekane
Nikamwangalia Kapteni kama ameusoma ule mchezo, hakuonesha kugundua chochote.
0 comments:
Post a Comment