Simulizi : Uchu
Sehemu Ya Pli (2)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa saa kumi na mbili alfajiri simu ya JKS ilipolia na kumwamsha usingizini.
"Hallo, nani?", JKS aliuliza huku amebanwa na usingizi.
"Phillipe".
"Ehe, sema", alijibu kwa shauku.
"Matanga hayatakuwepo, mtu wetu hakulala pale, na hata hajulikani kalala wapi, alionekana akiingia lakini hakuna aliyemuona wakati akitoka. Funguo za chumba kaziacha chumbani, Kavurugavuruga kitanda lakini hakukilalia. Tumefanya utafiti katika hoteli na nyumba zote za kulala wageni Arusha nzima,hayupo. Mtu wako ni mjuzi, naamini maneno yako", Phillipe alimalizia.
"Haya asante, kazi imeanza". JKS alikata simu baada ya kusema.
IV
Baada ya kutelemka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, akitokea Arusha alikwenda kwenye ofisi za Tanzaniar za pale uwanjani na kwa bahati alimkuta meneja hajaondoka, hivyo akafanya mipango ya kukodi ndege yao kesho yake alfajiri ili impeleke Kigali. Ingawa ndege zao zilikuwa na kazi nyingi kesho yake, lakini kwa vile ile biashara ya kwenda Kigali ilikuwa nzuri, meneja alimkubalia ila akaomba Willy asaidie kupata ruhusa ya kutuwa kwenye uwanja wa ndege wa Kavihanda wa mjini Kigali. Willy alilipa na kuahidi kuwa angejitahidi kupata hiyo ruhusa. Alipewa kila kitu ambacho kingehitajika kule Kigali ili kibali kipatikane.
Willy alifika nyumbani yapata saa mbili usiku baada ya kupokelewa uwanja wa ndege na kuletwa moja kwa moja nyumbani na Ismail, dereva wa AVIS. Alitoa shilingi elfu tano akampa Ismail kama bakshishi.
"Asante sana mzee, gharama zitawekwa kwenye akaunti yako", Ismail alijibu.
"Kama kawaida. Asante kwa kuja kunipokea na kwa heri", Willy alijibu na kutelemka kwenye gari.
"Kwa heri mzee", Ismail alimwaga.
Pepe alikuwa jikoni akipika wakati Willy alipoingia ndani. Mara alipomwona alitoka jikoni akamkimbilia sebuleni huku akiwa ameshikilia kipande cha nyama.
"Karibu nyumbani bwana wee", kabla Willy hajajibu, Pepe alimkumbatia na kumbusu. Tumbo la Pepe lilipoligusa la Willy, akahisi mtoto akicheza tumboni.
Kitu ambacho kilimwongeza furaha. Willy, bila kujua akadondosha mkoba wake, na kuendelea kumbusu Pepe. Mara Pepe akamsukuma kidogo na kuangalia jikoni asije akaunguza, na kumwekea Willy kile kipande cha nyama alichokuwa ameshikilia mdomoni, kisha alitabasamu na kukimbilia tena jikoni ambako Willy naye alimfuata.
"Siku nyingine utafanya moyo wangu usimame kwa raha unazonipa", Willy alisema akiwa amemshikilia Pepe begani, huku Pepe akikaangiza nyama kwenye chungu.
"Sasa nimpe nani raha kama si wewe mume wangu", Pepe alijibu.
"Kuoa kutamu", Willy alijibu.
"Kutamu sana, kama ukioa ama kuolewa na akupendaye ki-kwelikweli", Pepe alijibu huku akimtupia jicho la mahaba.
Willy alimgeuza na kuanza kumbusu tena.
"Inatosha kwa sasa. Ngoja kwanza nikakuwekee maji uoge, halafu utakuta chakula tayari ndipo unieleze kwanini umechelewa kuja nyumbani", Pepe alieleza.
"Nakwambia kuoa kutamu, najisikia kama mtoto wa miaka mitatu, nilivyokuwa nafanyiwa na Mama Willy", Willy alijibu kwa dhati kabisa kwani kila aliporudi nyumbani Pepe alimfanya ajisikie kama mtoto, na hivyo kusikia raha isiyo kifani.
Baada ya kuoga na kula, huku wakizungumza mambo yao ya kawaida Willy alifikiria jinsi ya kuanza kumweleza Pepe juu ya safari yake.
Ni mpaka walipokwenda kulala ndipo Pepe alipotoa wasiwasi wake. Wakiwa wameingia kitandani na kujifunika shuka, Pepe alijilaza juu ya kifua cha Willy na kuuliza.
"Chifu keshanieleza huenda ukasafiri kesho, mbona husemi?".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mara moja Willy alimfikiria Chifu ambavyo alijaribu kumsaidia ili asipate tatizo lolote kuhusu masuala ya nyumbani.
"Nilikuwa najishauri nitaanzaje kukueleza".
"Unaenda kesho lakini", Pepe aliuliza kwa sauti kali kidogo.
"Ndio alfajiri", Willy alijibu kwa unyonge.
"Sawa", Pepe alijibu.
"Sawa ya ukweli au ya hasira?".
"Sawa ya kikwelikweli, naelewa. Naelewa ya kwamba mpaka umekubali kuondoka uniache, kweli ni lazima uende, nami yafaa nikubaliane nawe. Willy nataka uelewa kitu kimoja, najuwa unavyonipenda, na unajuwa ninavyokupenda kwa hiyo uamzi wako ndio uamzi wangu, najuwa lingekuwa jambo la hivihivi tu usingekubali na Chifu asingejaribu kama alivyojaribu kunisihi nikueleze. Nimeelewa. Willy, nakupenda Willy, nakupenda sana", Pepe alisema na kuanza kububujikwa na machozi ambayo yalianguka kifuani kwa Willy.
Kwa mara ya kwanza maishani mwake, Willy naye machozi ya mapenzi yalimtoka. Mara mtoto tumboni kwa Pepe alicheza na mara hii kwa fujo sana, na kwa vile walikuwa wamekumbatiana ndani ya shuka Willy naye alimhisi.
Kitendo hiki cha mtoto kiliwatoa kwenye haya mawazo yao ya majonzi ya kuachana kwa muda na kuwarudisha katika hali yao ya furaha ya kawaida".
"Mtoto hataki tuwe na majonzi", Willy alimnong'oneza mkewe.
"Haswa", Pepe alijibu na kumkumbatia kwa kujibana kabisa kwenye mwili wa mumewe na kuweka mguu wake juu ya mapaja yake.
KAZI IMEANZA
Baada ya kuzungumza na Phillipe JKS alimpigia simu ofisa mmoja wa usalama aliyekuwa anashughulikia maswala ya uchukuzi wa abiria. JKS ndiye aliyemsaidia sana ofisa huyu kupanda hadi kufikia ofisa usalama mwandamizi.
"Mulamba", JKS aliita baada ya simu kupokelewa.
"Ndiyo, nani mwenzangu?".
"Pole kwa kukuamsha, naona ulikuwa bado umelala, huyu ni JKS".
Mulamba mara moja usingizi ulimtoka na kuinuka kabisa kitandani na kuketi kwenye ncha ya kitanda.
"Ndiyo mzee, hapana nilikuwa nimeamka ila bado nilikuwa najinyooshanyoosha tu kwani jana nilichelewa kulala", alimjibu kwa woga. Ile sauti ya woga ilimfurahisha JKS maana alipenda na kufurahia kutetemekewa.
"Hamna neno, sasa sikiliza, hii ni amri toka juu kuliko hata mimi. Si unamjuwa Willy Gamba?".
"Ndiyo mzee, nani asiyemjua katika fani yetu hii", Mulamba alijibu.
"Amepewa kazi toka ngazi za juu, na jana alienda Arusha na ndege za Shirika la Ndege Tanzania. Kwa vile sasa hayuko tena kwenye ajira ya serikali, hii kazi amepewa nje ya mipango ya kiserikali maana ni kazi nyeti na serikali haitaki itambulike kuwa inahusika. Ila alitakiwa ajulikane yuko wapi kila wakati, lakini toka jana jioni hajulikani aliko. Sasa imeamriwa tutumie ofisi yako tujuwe yuko wapi na ripoti hiyo isiende kwa mtu yeyote ila mimi", JKS alimaliza.
"Hilo nitalifanya sasa hivi mzee, ila nataka kujua alikuwa anatarajia kwenda wapi baada ya kutoka Arusha?", Mulamba aliuliza.
"Baada ya kutoka Arusha alitakiwa kurudi hapa Dar es Salaam, halafu anende Kigali. Kuna ndege ya asubuhi sana ya ATC toka Kilimanjaro ambayo itaondoka saa moja, kama yumo nipe habari, kama hayumo tafiti ujuwe anakuja Dar es Salaam na usafiri gani, nipate habari haraka. Angalia usafiri wote mabasi, malori na kadhalika.
"Usiwe na wasiwasi mzee, nitakujulisha baada ya saa chache, tutampata tu. Tukimpata tumfanyeje?".
"Usifanye chochote, wewe eleza tu yuko wapi".
"Haya, asante".
"Kwa heri", JKS alikata simu.
Baada ya kukata simu ya Mulamba, JKS alipiga simu Paris kwa Jean na kumweleza mambo yaliyotokea Arusha na hadhari aliyokuwa amechukuwa tayari. Jean, akiwa bado na usingizi kwani Paris ilikuwa yapata saa kumi na nusu za asubuhi, tulikuwa tunapishana saa mbili.
"Nataka utakaponipigia tena simu unieleze kuwa tayari keshauawa, vinginevyo usinipigie simu mpaka utakapofanikiwa kazi hiyo. Natuma pesa leo asubuhi kupitia kwa yule rafiki yangu mwenye kampuni ya kitalii ya Concord Tours zikusaidie kukamilisha kazi. Vilevile nitawapigia simu na marafiki zangu wengine huko Afrika Mashariki wakupe msaada wowote utakaohitaji", Jean alimalizia na kukata simu bila bila kumsubiri JKS ajibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mara ya kwanza katika maisha yake JKS alisikia woga. Alizijua nguvu za Jean na akajuwa itabidi atimize hii kazi, vinginevyo mambo yangeweza kumgeukia. Alifikiria jinsi Jean alivyokuwa amemwahidi kumsaidia kuunyakuwa urais wa Tanzania na alikuwa anaujuwa uwezo wa Jean kuifanikisha azma yake hiyo. Na dhamira ya JKS kuwa Rais ilizidi vitu vingine vyote, lakini leo huyu Willy Gamba angeweza kumfanya akose nafasi hii. Asubuhi hii alisikia jasho la baridi likimtiririka mgongoni na kujisemea kwa sauti. "Kwa kila hali lazima aondoke".
Bila kujua amesema kwa sauti kubwa mke wake aliyekuwa amelala bado alishtuka na kuuliza. "Unasemaje?".
"Hapana, sijasema kitu", JKS alijibu.
Mke wake alimjua sana. Hivyo, akanyamaza lakini alijuwa mzee alikuwa anasumbuliwa na kitu fulani.
Willy alitua kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza mnamo saa mbili na nusu za asubuhi. Asubuhi kabla hajaondoka nyumbani alimpigia simu rafiki yake mmoja ambaye alikuwa na wadhifa wa juu ndani ya Chama cha Msalaba Mwekundu na kumwomba msaada kati ya ndege zao zilizokuwa Mwanza moja impeleke Kigali. Willy aliwahi kukisaidia sana Chama hiki, na huyu rafiki yake aliona bahati sana kupata fursa kama hii ili nae alipe angalau fadhila kidogo za Willy kwa yote aliyowahi kuwatendea.
"Bila shaka Willy, sasa hivi nitapiga simu Mwanza na hiyo saa mbili na nusu unayotegemea kufika Mwanza utakuta ndege ndogo ya injini mbili aina ya Cessina yenye namba MMT 3 ikikusubiri. Sisi tunaruhusiwa bila matatizo kutua Kigali kutokana na hali ilivyo Wilayani Ngara. Hivyo, huna haja ya kuhangaika kupata kibali cha kutua, hicho sisi tunacho na utakuta maofisa wetu pale Mwanza wameshawasiliana na Kigali", yule rafiki yake Willy alieleza.
"Nitafurahi sana, na kama vilevile mtawaeleza kuwa mimi ni afisa wenu", Willy aliongezea.
"Bila shaka", rafiki yake alijibu huku akicheka maana alijua Willy haendi Kigali bure.
Kwa hiyo, Willy alipotelemka ndani ya ndege ya kukodi ya Tanzanair alikuta ndege ya Chama cha Msalana Mwekundu iko tayari.
"Ina maana mimi sasa nitarudia hapa?", rubani wa Tanzanair alimuulizia alipomwona anashuka na mfuko wake.
"Ngoja kidogo", Willy alimjibu.
Willy alikwenda mpaka kwenye ile ndege na kumkuta rubani na ofisa mmoja wa Msalaba Mwekundu wakimsubiri Willy.
"Karibu mzee", wote wawili walitamka kwa pamoja Willy akawapa mikono kuwasalimia.
"Asanteni sana", alijibu.
"Sisi tuko tayari, ila tu tunaomba uende na ndugu yetu mmoja ambaye anaenda huko vilevile kikazi", yule afisa alimwambia willy.
Willy alimwangalia yule jamaa, na kumwona ni wa makamu yake na wa umbo lake.
"Sawa, lakini ningeomba aje na ile ndege ndogo ambayo nimekuja nayo ili rubani awe na mtu wa kuzungumza nae, maana hiyo nayo inakuja Kigali, ila kwa sababu lazima ijaze mafuta na kukaguliwa kidogo ndio sababu imebidi mimi nikifika tu hapa nipate ndege nyingine kwa vile nina miadi maalumu ya kiserikali pale uwanja wa Kigali na mtu ambaye ataondoka saa moja kuanzia sasa", Willy alieleza.
"Basi, vizuri sana. Je, ndege yako ina vibali vyote vya kutua?", yule ofisa aliuliza maana alijua jinsi hali ilivyokuwa uwanjani pale Kigali.
"Hamna taabu, kila kitu kipo", Willy alijibu, kisha akaenda kwa rubani wa ndege yake.
"Sasa ukishajaza mafuta utakuja na yule bwana pale, naye anakuja Kigali. Ukishamshusha tu basi wewe urudi", Willy alimweleza.
Yule rubani alishangaa kwanini wasitumie ndege moja badala ya ndege mbili. Lakini kwa vile haikuwa shughuli yake na kwa vile alikuwa ameagizwa kwenda mpaka Kigali aliamua kubaki ameshangaa lakini atekeleze wajibu wake.
"Sawa mzee", yule rubani alimjibu huku sauti ikionyesha mshangao. Willy alitoa dola mia za kimarekani, akampa.
Tabasamu safi likaonekana usoni mwa rubani.
"Asante sana mzee", alijibu tena na kupeana mikono ya kuagana. Willy alikwenda kwenye ndege, na rubani wa Chama cha Msalaba Mwekundu akaiondoa ndege kuelekea Kigali ikiwa yapata saa tatu kasoro robo. saa za asubuhi.
Ilikuwa saa tatu na dakika kama tano hivi, Mulamba alipompigia simu JKS. JKS alikuwa tayari amefika ofisini.
Simu ya moja kwa moja kwa JKS ililia na haraka akainua. "Nani", aliuliza kwa shauku.
"Mulamba, mzee".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Haya vipi mmempata?".
"Mzee huyu mtu tumeweza kupata nyendo zake zote, ila hatukuweza kumpata yeye kabisa maana alikuwa hatua moja mbele kila tulipokuwa karibu kumpata".
"Una maana gani, hebu sema mambo ya kueleweka", JKS aliuliza kwa ukali.
"Ndio nilitaka nikupe ripoti kamili mzee. Kutokana na taarifa za uchunguzi wetu, aliondoka Arusha jana kwa ndege ya kukodi ya Tanzanair, hivyo hakulala Arusha ila alilala hapa Dar es Salaam. Leo asubuhi ameondoka Dar es Salaam kwa ndege hiyo hiyo ya kukodi ya Tanzaniair na anaelekea Kigali. Habari za watu wangu nilizozipata hivi punde ni kwamba ameondoka Mwanza mnamo saa tatu kamili kuelekea Kigali. Hali ndivyo ilivyo mzee. Sijui tukusaidie nini tena?", Mulamba aliuliza.
"Ndege hiyo ya Tanzaniar ni namba ngapi?", JKS aliuliza.
"Namba zake ni MHZT 12".
"Sawa basi asante, nikikuhitaji nitakutafuta".
"Haya, asante mzee", Mulamba alijibu huku akipumua kwani alikuwa amejawa na wasiwasi angetakiwa kufanya nini tena kwani hakutaka kazi yoyote ya kuhusiana na Willy Gamba, maana mtu huyu alikuwa ni moto wa kuotea mbali. Alibaki anashangaa tu hasa ni nini kilikuwa kinatokea kati ya serikali na Willy Gamba.
JKS alijishika kichwa na kujua kazi imekuwa ngumu na yeye peke yake asingeiweza. Huyu Willy Gamba alikuwa kweli kabisa mtu wa hatari na hakika kuwapo kwake Rwanda kungezua balaa, lazima kila njia ifanyike kabla hajaleta madhara. Hakukuwa na njia nyingine ila kurudi kwa Jean maana yeye alikuwa na uwezo mkubwa kufanya mambo Rwanda kuliko yeye. Uwezo wa JKS uliishia ndani ya mipaka ya Tanzania, isipokuwa tu propagada ya kisiasa ndio angeweza kusaidia kokote ulimwenguni kwani alikubalika sana duniani kote kisiasa. Ingawaje Jean alikuwa amemwamru ampigie simu ikiwa Willy ameshauawa, lakini JKS alionelea afadhali atukanwe kuliko kunyamaza. Aliinua simu akampigia Jean kwenye simu yake ya kutembea nayo (Mobile).
"Hallo", Jean alijibu baada ya kupokea.
"JKS hapa".
"Ehe, mambo mazuri?", Jean aliuliza kwa shauku.
"Hapana, mambo yanazidi kuwa magumu", JKS alijibu na akamweleza jinsi sasa Willy Gamba alivyokuwa anaelekea Kigali.
"Mbona mtu huyu nitampenda", Jean alijibu kwa kejeli.
JKS alinyamaza. Hakuwa na la kusema.
"Hapa kweli tunashughulika na mtu mjuzi, huyo anatakiwa apambane na watu wenye ujuzi kama yeye. Basi niachie huyo mtu kwa sasa. Nitarudi kwako baadae, nipe hiyo namba ya ndege na maelezo mengine yote kuhusu hiyo ndege na huyo mtu wako", Jean alimalizia.
JKS alimpa maelezo yote huku akifurahi kuwa Jean ameelewa na hakuweza kumkasirikia. Baada ya kumpa maelezo JKS alikata simu na kuinuka kitini na kwenda kusimama dirishani mwa ofisi yake na kuwaangalia ndege aina ya tausi waliokuwa wakicheza nje tu ya dirisha lake.
Mara mawazo yake yakarudi kwa Willy Gamba. Kuuawa kwa Willy ndio kupata kwake Urais, maana huyu mtu asipouawa anaweza kuchokonoa ukweli wa mambo na kuleta kashifa ambayo ingeweza kumgusa hata yeye kwani JKS alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanahusika na swala zima la Rwanda, tokea maswala ya kisiasa mpaka kufikia mauaji. Na serikali ya Tanzania ilikuwa imeweka mambo yote yahusuyo Rwanda chini yake na ofisi yake kwa vile aliaminika kuwa ni kiongozi mwadilifu.
Baada ya kukata simu ya JKS, Jean alipiga simu Rwanda kwa rafiki yake alikuwa ndani ya Jeshi la RPF. Baada ya RPF kushika madaraka Rwanda, Col. Gatabazi alikuwa wa kwanza kupata simu iliyofanya kazi. Hii yote ilikuwa kwa hisani ya Jean ambaye alikuwa na uhusiano wa karibu na mkuu wa jeshi la Ufaransa lililokuwa Rwanda pamoja na mkuu wa Idara ya Usalama wa Nje wa Ufaransa (DGSE). Inasemekana kuwa Jean ndiye aliyewasaidia hata kupata vyeo hivi kutokana na kuwa kwake karibu na uongozi wa juu wa serikali ya Ufaransa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jean alikuwa kama ndiye mshauri mkuu wa serikali ya Ufaransa kuhusu maswala ya Rwanda. Kutokana na kuwa kwake karibu na Rais pamoja na watu wote muhimu ndani na nje ya serikali ya Rwanda. Kwa hiyo baada ya Kigali kuangukia mikononi mwa RPF tu na maofisa wa jeshi hilo kujinyakulia nyumba za kukaa zilizokimbiwa na maofisa wa serikali ya MNRD. Col. Gatabazi ambaye siku zote alijulikana kama mkereketwa mkubwa wa RPF, hakuwa mkereketwa ila msaliti na ndiye aliyekuwa akitoa siri zote za RPF kwa Jean, na Jean akazitoa kwa rafiki zake wa serikali ya MNRD. Kwa hiyo, baada ya kupata nyumba tu Jean alihakikisha kuwa Col. Gatabazi anapata simu ili kila kilichokuwa kinaendelea ndani ya RPF kimfikie.
Kutokana na huo uhaini wake Col. Gatabazi alijipenyeza na kujiweka karibu kabisa na kiongozi wa RPF na akaaminika sana. Inasemekana alikuwa Mhutu, lakini mama yake alikuwa Mtutsi. Baba yake alifariki akiwa na umri wa miaka miwili na akakulia kwa mjomba wake na kwa vile alikuwa amechukuwa umbo la mama yake alitambuliwa kama Mtutsi tu. Ila yeye alijuwa ni Mhutu na inasemekana aliwahi kuambiwa kuwa baba yake aliuawa na wajomba zake kwa vile hawakutaka dada yao aolewe na Mhutu. Hivi kinyongo alikuwa nacho moyoni na ndio sababu alipopata nafasi ya kuwasaliti Watutsi alifanya hivyo kwa moyo mmoja.
Baada ya serikali ya MNRD kuanguka na RPF kuingia, Jean alimhakikishia Col. Gatabazi kuwa serikali hiyo isingeweza kukaa madarakani kwa muda mrefu kwani ingepinduliwa na yeye angeiongoza serikali inayofuata. Jean alimhakikishia kuwa serikali ya Ufaransa isingeiruhusu serikali ya RPF ikae madarakani kwani viongozi wake walikuwa na mwelekeo wa Kiingereza kwa kukaa kwao Uganda na hivyo wangeathiri nguvu (influence) ya Ufaransa ndani ya Rwanda kitu ambacho Ufaransa isingekiruhusu kabisa. Kwa hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya MNRD waliokimbia na watu wengine walio ndani kama Col. Gatabazi kwa msaada wa serikali ya Ufaransa. Jean alikuwa anatayarisha jeshi la kuivamia tena Rwanda na kuchukua madaraka toka kwa RPF. Kwa hiyo, Col. Gatabazi alikuwa anajitayarisha kuwaggeuka wenzake mara wakati wa kufanya hivyo utakapofika.
Col. Gatabazi alikuwa anataka kutoka nyumbani kwenda ofisini kwake, Merridian Hotel, ambako ndiko ofisi zake zilikuwa kwani ndiye aliyekuwa anashughulikia uratibu wa shughuli zote za vikosi mbalimbali vya jeshi la RPF na kuripoti kwa mkuu wa majeshi.
Simu ililia. Hallo Col. Gatabazi?".
"Jean".
"Mbona leo unanipigia simu saa hizi? Saa zetu unazijuwa", Col. Gatabazi aliuliza.
"Kuna dharura", Jean alijibu na kumweleza juu ya Willy Gamba na athari za kuwa kwake Kigali.
"Hivyo ni vizuri hiyo ndege yake ingetunguliwa ikiwa hewani iwe mwisho wa tatizo la huyu mtu maana toka jana anatusumbua, nafikiri hiyo ndio njia rahisi", Jean alimalizia.
"Si Tanzania italalamika sana na kwa sasa hivi serikali ya RPF inataka sana kueleweka vizuri, hasa kwa serikali kama ya Tanzania", Col. Gatabazi alijibu kwa njia ya kuuliza swali.
"Usijali, Tanzania inaunga mkono kwa kusema hiyo ndege iliruka anga zetu bila ruhusa hata haikutoa habari huko Tanzania kama ilikuwa inakuja Kigali. Hilo niachie mimi na wewe utasikia itakavyokuwa maana utacheka", Jean alijibu.
"Basi ngoja niwahi kwani watatua kwenye dakika thelathini zijazo kutokana na maelezo yako ya saa walizoondoka mjini Mwanza".
"Asante, kwa heri, ila nipigie simu baada ya tukio".
"Sawa", Col. Gatabazi alijibu.
Ndege ya Chama Cha Msalaba Mwekundu ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Kayibanda mjini Kigali yapata saa nne kamili. Willy Gamba alichukua mkoba wake na kutelemka.
"Asante", Willy alimshukuru rubani na kumpa dola mia za kimarekani.
"Asante sana mzee", yule rubani alishukuru na kufunga mlango tayari kwa kuruka tena.
Willy alikwenda moja kwa moja kwenye jengo la uwanja wa ndege na kuelekea Uhamiaji. Ulinzi uwanjani ulikuwa bado mkali lakini kwa sababu alikuja kwa ndege ya Chama Cha Msalaba Mwekundu na alikuwa amefanyiwa mpango na rafiki yake Dar es Salaam aje apokelewe na mmoja wa maafisa wa Msalaba Mwekundu walioko Kigali, yeye akiwa kama Afisa wa habari wa Msalaba Mwekundu kimataifa na ndivyo Chifu alivyomtayarishia pasipoti aliyoikuta nyumbani, taratibu zake pale uwanja wa ndege zilikwenda haraka bila kipingamizi chochote.
Katika pasipoti yake hii jina lake lilikuwa George Mambo.
Alipojitokeza tu nje, alimkuta mwenyeji wake aliyekuwa amevaa beji ya Msalaba Mwekundu na kwa vile na yeye toka alipotua tu aliweka beji aliyokuwa amepewa na Msalaba Mwekundu wakatambuana mara moja.
"Bwana George Mambo natumai", yule mwenyeji wake alisema huku akitoa mkono wa salamu.
"Ndio mimi. Habari zako", Willy alijibu na kusalimu.
"Nzuri, mimi naitwa Vicent Nyemazi, ni afisa wa habari hapa, na mimi ni Mhutu ila mimi siyo Mhutu mwenye siasa kali", Vicent alijibu huku akitabasamu.
"Vizuri sana na pole kwa yote yaliyotokea hapa nchini kwenu".
"Asante sana, ndio hali ya dunia. Gari nimeegesha hapo mbele", Vicent alieleza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mkahawa wa hapa umefunguliwa?", Willy aliuliza.
"Ndio, uko wazi".
"Unajuwa nimeondoka asubuhi sana, sijanywa hata chai na ndege zetu kama unavyojuwa si kama ndege za abiria, hamna chochote hata kikombe cha chai", Willy alijibu huku akiangalia saa yake.
"Sawa, twende hapa kuna mkahawa mzuri, na hali imeanza kurudi kama zamani, hivyo vitu vingi vinaendelea kama kawaida.
Walipanda juu kwenye mkahawa na willy aliagiza kahawa na kipande cha mkate na Vicent akaagiza kahawa peke yake. Willy aliangalia saa yake kwa chati kabisa, akajuwa ile ndege ya Tanzanair ilikuwa karibu kutua, na alitaka tu kuona kama kungeweza kuwa na fununu za kuja kwake. Hii ilikuwa hadhari tu kwani aliamini hakuna mtu ambaye angeweza kujua kuwa anakuja kwa jinsi alivyokuwa ameondoka Dar es Salaam kisirisiri.
"Ah, vipi hali ya huko Ngara, nasikia hali ya wakimbizi ni mbaya sana, yaani chakula, maji na madawa ni taabu", Vicent aliuliza.
"Ni kweli hali ni mbaya, jumuiya ya kimataifa inajaribu kusaidia lakini wakimbizi ni wengi mno. Fikiria watu kama wa mji huu mnamo wiki moja watengeneze mji mwingine ambao haukuwepo kabisa, ambako ni porini tu hakuna huduma za kijamii za aina...". Kabla Willy hajamaliza kueleza mlio mkubwa ulitokea na mara ukatokea mlipuko. Willy na Vicent walikimbilia dirishani kuangalia kwenye uwanja wa ndege ambako ndiko mlipuko ulikotokea. Kwenye barabara zinakoondokea na kutua ndege wakaona vipande vya ndege vimesambaa na kuwaka moto.
"Kazi imeanza", Willy alisema na kumvuta Vicent mkono. Wakakimbilia chini kuangalia kwani vishindo vya kukimbia uwanjani vilisikika kutoka kila pahala.
Walipofika chini na kuelekea uwanjani walikuta magari ya jeshi aina ya Landrover yakiwa yamejaa askari yakielekea pale mabaki ya ndege yalipoangukia na wengine wakija huku kwenye jengo la uwanja ili kuzuia watu wasiende kule uwanjani.
Vicent na Willy walionyesha beji zao za Msalaba Mwekundu wakiomba wafike kwenye tukio lakini walikataliwa na askari ambao kwa sasa walikuwa wamechachamaa. Willy aligundua kuwa kumbe walishajua atafika na maskini yule rubani na afisa wa Msalaba Mwekundu waliuawa kwa kufikiri ni yeye. Willy alimshukuru Mungu kwa kumfanya afikiri na kufanya kama alivyofanya.
Kweli kama Msoke alivyosema, kazi hii tayari ilionyesha kuwa ni ya hatari. Ila kilichomshangaza Willy ni jinsi yule mtu aliyeshambulia ndege ya Tanzanair alivyojuwa kuwa yeye angekuwemo mle ndani ya ile ndege. Hii ilionyesha kuwa kati ya wale maafisa wa PAM miongoni mwao kulikuwa na msaliti, lakini kwa sasa hakukuwa na haja ya kufikiria hicho ila kufanya kilichomleta Kigali. Huyu msaliti angetafutwa baadaye. Jinsi ile ndege ilivyokuwa imepigwa na kombora. Willy alijua kabisa kuwa hakuna mabaki ya binadamu ambayo yangeweza kutambuliwa, kwani kombora lililotumika lilikuwa kubwa wakati ndege yenyewe ilikuwa ndogo.
"Twende zetu, nipeleke hotelini, acha wanajeshi wafanye kazi yao", Willy alimvuta Vicent wakaondoka huku wakisesera kuelekea kwenye gari la Vicent.
"Kwanini wameipiga ile ndege?", Vicent aliuliza huku akifungua mlango wa gari.
"Huenda ilikuwa na hatari, bado unajuwa mambo hayajatengamaa hapa", Willy alijibu.
"Unafikia hoteli gani?".
"Nafikiri jaribu Meridian Hotel kama kuna nafasi", Willy alijibu na kuikacha Hotel Des Mille Collines aliyokuwa amepangiwa na rafiki za Musoke, kwani sasa hakukuwa tena na kumwamini mtu yeyote kwa vile hakujuwa nani alikuwa ametoa amri ya kupigwa kombora ndege aliyopaswa kuwemo na huyo mtu alikuwa anajuwa habari kiasi gani kumhusu yeye Willy.
"Sawa, pale hotelini wanatua na watu wetu kutoka mataifa ya nje wako pale. Na vilevile pana usalama maana ofisi zingine za jeshi ziko pale, na maafisa wengine wa jeshi wanakaa pale", Vicent alimweleza Willy. Wakati wakielekea Meridian Hotel walikutana na magari madogo ya jeshi, kama matatu, yakielekea uwanja wa ndege. Willy aliona wengi walikuwa maofisa wa vyeo vya juu na akahisi walikuwa wanakwenda kutathimini tukio lililotokea.
Walipofika Meridian walikuwa watu wako vikundi vikundi wakizungumza, bila saka walikuwa wamepata habari za tukio la uwanja wa ndege. Vicent likwenda mapokezi na kuzungumza na mmoja wa wafanyakazi wa pale ambaye alionekana kumfahamu sana, na baada ya muda kidogo Willy aliitwa kujaza fomu za kupatiwa chumba. Baada ya kupewa funguo alichukua mkoba wake na vicent akamweleza kuwa atamsubiri kwenye mkahawa wa hoteli.
"Si utataka twende ofisini?", Vicent aliuliza.
"Bila shaka", Willy alijibu.
"Basi utanikuta hapo kwenye mkahawa".
"Asante", Willy alijibu na kuelekea kwenye ngazi kwani alikuwa ameelezwa lifti zilikuwa hazifanyi kazi. Alikuwa amepewa chumba namba 412, ghorofa ya nne.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
V
Baada ya Col. Gatabazi kuhakikisha kuwa hakuna kitu kilichobaki ndani ya ndege na ndege yenyewe, alielekea nyumbani kwake ili akampashe habari Jean. Alipompata Jean alimweleza. "Kazi tayari, mtu wako hata mfupa haukuonekana, kawa hewa".
"Safi sana, hakika mimi hupenda mtu wa vitendo na siyo maneno", Jean alijibu.
"Lililobaki ni la kujieleza kwanini tumeipiga hiyo ndege, lakini tayari mkuu nimemwandikia taarifa safi ambayo hawezi kuwa na mashaka nayo. Wasiwasi wangu Tanzania tu", Col. Gatabazi alieleza.
"Nilikwambia Tanzania niachie mimi. Tuongee jioni. Kama kawaida mzigo mwingine unatua leo, na ni shehena kubwa", Jean alijibu na kabla Col. Gatabazi hajajibu alikata simu.
Baada ya kukata simu ya Col. Gatabazi. Jean alimpigia simu JKS, Dar es Salaam. JKS, aliyekuwa na wasiwasi mkubwa aliipokea simu haraka ilipolia. "Nani".
"Jean hapa. Kigali Bingo!!, mambo safi".
MIGUU YA NYOKA
Willy alipowasili kwa Col. Thomas Rwivanga, alimkuta anamsubiri. willy alikuwa amemweleza kuwa angekuwa anaendesha gari la Msalaba Mwekundu na angekuja peke yake bila Vicent. Col. Rwivanga alikuwa amemweleza njia ya kupita mpaka huko nyumbani kwake, Kimihurura.
Col. Rwivanga aliposikia mwungurumo wa gari alitoka nje na kwenda kumpokea Willy.
"Habari yako?", Col. Rwivanga alimsalimia Willy huku akimpa mkono.
"Safi, na wewe?", Willy alimjibu.
"Safi kabisa, nafurahi sana kuonana na wewe, Mzee Musoke amenieleza habari zako, nami nilikuwa na shauku kubwa ya kukutana nawe. Karibu ndani", Col. Rwivanga alimkaribisha Willy.
"Asante sana, nimekaribia", Willy alijibu huku akiingia ndani na kuketi.
"Nikupe kinywaji gani?|".
"Klabu soda inatosha", Willy alijibu.
Col. Rwivanga alileta Klabu soda mbili na kuzifungua, wakaanza kunywa.
"Ehee, habari ya maisha?", Col. Rwivanga aliuliza.
"Safi, naamini Mzee Musoke amekueleza kwanini niko hapa".
"Ndio amenieleza".
"Imebidi nikuone mapema maana kuna jambo lililotokea ambalo linaonyesha kuwa katika uongozi wenu kuna mtu aliyejuwa kuwa mimi nimo ndeani ya ile ndege iliyotunguliwa leo asubuhi, akiwa na nia ya kuniua, bahati nzuri sikuwemo ila nilitakiwa kuwemo kwenye ndege hiyo. Na ninafikiri yeyote yule aliyeagiza hiyo ndege itunguliwe anaamini kuwa mimi sasa ni marehemu", Willy alimweleza Col. Rwivanga ambaye wakati huo alikuwa akimwangalia kwa mshangao mkubwa.
"Hivi swala unaloijia hapa ni nyeti kiasi hicho, mpaka wanataka kukuua! Mimi Mzee Musoke aliponieleza, sikutegemea kama kunaweza kuwa na hatari yoyote, maana wewe unakuja kutathimini tu hali ya mambo yalivyotokea mpaka kufikia watu wengi namna ile kuuawa. Lakini sasa inaonekana kuja kwako kumetia watu wasiwasi na wameamua kukumaliza kabisa hata hujaanza huo uchunguzi. Ndugu Gamba hii inaonekana kuna jambo kubwa ambalo hata sisi hatulifahamu. Hii ni hatari na ni hatari kubwa", Col. Rwivanga alijibu.
"Je, unaweza kujuwa ni nani au ni vipi ile ndege ilitunguliwa?, Huenda tukaanzia hapo ndipo tutajuwa hasa ni nani anahusika na kwa sababu gani?", willy aliuliza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Taarifa niliyopata kuhusu tukio hilo kwenye kikao cha makamanda wa jeshi, ambayo imetolewa na Col. Gatabazi, ambaye ndiye mkuu wa utawala jeshini, inasema ndege hiyo ilipoitwa kwenye rada ijitambulishe haikufanya hivyo. Kwa hiyo Luteni Silasi Biniga, ambaye ndiye anaongoza wanajeshi wanaolinda uwanja alimtaarifu Meja Juvenal Mukama, Mkuu wa Kikosi cha Mizinga kinacholinda mji huu, ambaye alitoa amri kuwa kama inakaribia kutua na bado haitoi taarifa yoyote itunguliwe. Na ndivyo ilivyofanyika. Baada ya kujuwa kuwa ilikuwa ndege ya kukodi ya kampuni ya kukodisha ndege ya Kitanzania, habari zilipelekwa Dar es Salaam, na habari tulizopata toka Wizara ya mambo ya Nje ya Tanzania ni kwamba ndege hiyo ilikuwa imekodiwa na mtu mmoja kwa jina la Juma Omari aliyejitambulisha kama mwandishi wa habari na masuala yote ya kupata vibali vya kutua alifanya mwenyewe. Hivyo, serikali ya Tanzania inaunga mkono kutunguliwa kwa ndege hiyo ambayo imeingia anga ya watu bila kibali wala kujitambulisha na huku rubani na kampuni hiyo ikijuwa hali ya hatari iliyomo nchini Rwanda. Taarifa hiyo tumeipata jioni hii na serikali ya Tanzania imezidi kusema itaichukulia hatua kampuni hiyo ya ndege kwani inaweza kuwa inatumiwa na maadui wa Rwanda na kuweza kuleta uhusiano mbaya kati ya nchi zetu rafiki", Col. Rwivanga alieleza na ukawa ni wakati wa Willy kushangazwa na maelezo hayo.
"Rafiki yangu, hapa kuna jambo kubwa maana sababu ya kutunguliwa ndege hii ni moja tu, ambayo ni kutaka kuniua mimi. Lakini sasa maelezo ya makamanda wenu. Col. Gatabazi na maelezo kutoka Dar es Salaam, yamenichanganya kabisa na nahisi kuna kitu kikubwa tusichokijua", Willy alijibu.
"Sasa tufanye nini?", Col. Rwivanga alimwuliza.
"Kwanza, nataka aliyetaka kuniua aendelee kufikiri kwamba ameniua. Pili, huenda huyu Lt. Silasi Biniga anaweza akawa na habari zinazoweza kutusaidia kufumbua hiki kitendawili hivyo anafaa kuonwa na kuulizwa", Willy alijibu.
"Basi niache huyu mimi nitamwuliza", Col. Rwivanga alijibu.
"Hapana, niachie mimi, swala hili linaweza kuwa vilevile linaugusa uongozi wenu. Mimi nikiwa mtu baki naweza kupata ukweli bila kuleta kasheshe sasa hivi. Ni lazima tujitahidi tujue undani wa jambo hili maana ni zito. Naomba tu unieleze huyu Luteni Biniga anakaa wapi nami nitaenda kumwona", Willy alijibu.
"Inaweza kuwa hatari kwako, unajuwa hawa watu ni wanajeshi safi", Col. Rwivanga alimwasa Willy.
"Usijali, hatari ndio jina la kazi yangu", Willy alijibu.
Wote wakacheka, maana Musoke alikwishampa Col. Rwivanga maelezo kamilifu kuhusu Willy na uwezo wake.
"Sawa, huyu Luteni Biniga anakaa barabara ya tatu tu kutoka hapa kwangu, sehemu hiihii ya Kamihurura". Kisha akamweleza mtaa na nyumba ilipo.
"Sasa hivi naanza kushangaa, wakati wanajeshi wa cheo chake wengi bado wako kambini na wengine wako huko Ndera ambako ndiko kuna nyumba za maofisa wa ngazi ya chini yeye anakaa sehemu ambayo wanakaa maofisa wa ngazi za juu. Sijui huenda ikawa tu bahati yake", Col. Rwivanga alisema kama vile anajisemea mwenyewe.
"Nafikiri nikionana naye nitajua. Naona niende kama saa tatu hivi. Nitaacha gari hapa na kwenda kwa miguu", Willy alisema.
"Uamzi wako. Kwa vile bado kuna muda mpaka saa tatu ngoja nitengeneze chakula kidogo", Col. Rwivanga alieleza.
"Na mimi nitakusaidia kupika, kupika ni moja ya starehe zangu", Willy alieleza huku wakiinuka kuelekea jikoni.
Willy alipofika kwenye nyumba ya Luteni Biniga taa za ndani zilikuwa zikiwaka. Nyumba hii ilikuwa imezungushiwa ua kama alivyokuwa ameelezwa na Col. Rwivanga. Badala ya kubisha hodi langoni aliamua kupita kwenye uchochoro, akapanda ukuta kisha akatumbukia ndani. Alitambaa chini kwa chini mpaka akaufikia ukuta wa nyumba hii. Dirisha la nyuma lilikuwa limefungwa, hivyo aliendelea kuambaa na ukuta. Ndipo aliposikia sauti za watu wakizungumza na kucheka. Alichungulia dirishani na kuwaona watu watatu. Wanaume wawili na mwanamke mmoja. Mazungumzo yao yalikuwa kwa lugha ya Kifaransa, ambayo Willy aliielewa vizuri sana, mazungumzo yao ndiyo yaliyomshitua na kumweka chonjo.
"Kazi mimi nimeifanya kwa ustadi mkubwa. Hiyo pesa kweli iko kwenye akaunti yangu Nairobi?", mmoja wa wale vijana alimwuliza yule mwanamke.
"Siyo wewe tu, nyote kesho pigeni simu kwenye benki zenu. Mambo safi. Nimeelezwa na wakala wa mlipaji kuwa pesa zimetumwa kwa njia ya 'swift' na tayari ziko kwenye akaunti zenu", yule mwanamke alijibu.
"Mimi nilihitaji kulipwa dola laki moja. Ndizo zilizotumwa na kuwekwa kwenye akaunti yangu?", yule mwanaume wa pili aliuliza.
"Ndio. Sasa kwenye akaunti yako kuna dola laki tatu. Zimeingia pamoja na zile za malipo ya kuwatorosha wale makamanda wa Intarahamwe kwenda Zaire", yule mwanamke alijibu.
"Kama kesho nikijuwa pesa yangu yote hiyo iko benki, basi mimi nitatoroka kwenda Kenya. Halafu Afrika Kusini. Sitaki kukaa hapa tena, tusije tukabainika kuwa tuko kwenye upinzani", mwanaume wa pili alisema.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapa Willy aliamini kuwa wakati wa kukabiliana ana kwa ana na watu hawa ulikuwa umefika kwani walionekana kana kwamba wanataka kuondoka. Mawazo na akili ya Willy yalivutika sana kwa yule mwanamke kuliko hata kwa wale wanaume wawili ambao alihisi ni Luteni Silasi Biniga na Juvinali Mukama. Alipogeuka tu kutaka kwenda kubisha hodi kwenye mlango wa mbele, alijikuta akiuangalia mtutu wa bunduku kubwa aina ya 'Sub Machine Gun'.
"Usisogee hata hatua moja. Hapohapo ulipo weka mikono yako juu, geuka nyuma na utembee kuelekea mlango wa mbele ya nyumba hii", Willy alimrishwa na yule askari na kutii amri kama alivyokuwa ameamriwa.
"Nani huyo tena", Silasi Biniga aliuliza katika hali ya mshangao.
"Nini Ananie", Juvinali naye aliuliza.
"Inkotanyi", Ananie alijibu.
"Bibiane wewe nenda. Sisi ngoja tujuwe huyu mtu ni nani?", Juvenali alimweleza yule mwanamke huku yeye na Luteni Biniga wakichukuwa bastola zao na kutoka nje kwenda kumkabiri mtu huyu aliyekuja kuwapeleleza ili kabla hawajamuua wajuwe ni nani na anajuwa nini kuhusu wao. Wakati Bibiane anatoka ndani alikutana na Willy pamoja na mtu aliyemkamata, wakiwa wamefika mbele ya nyumba, kwenye mlango wa mbele.
"Simama hapo", Ananie alimwamru Willy huku akiwa bado ameweka mikono yake kichwani. Bibiane alipotoka nje alimwangalia Willy. Willy naye akamtazama. Kulikuwa na mwanga wa kutosha kuweza kumtambua mtu. Bibiane alimwemweseka kwa Willy kisha akalekea kwenye lango kubwa la kutokea nje na kutokomea gizani.
"Luteni Biniga..., lazima mtu huyu ni Inkotanyi, amekuja kupeleleza kuhusu tukio la leo", Ananie alimwambia Luteni Biniga walipotoka nje pamoja na Juvinali. Luteni Biniga alimwangalia Willy na kwa sura yake akabaini kuwa mtu huyu hakuwa Mnyarwanda. Bila kuchelewa Luteni Biniga alimpiga Willy kwa kitako cha bastola kwenye paji la uso na Willy akaanguka chini. Alipoanguka Juvinali naye alimpiga teke la tumboni. Willy alipotaka kuinuka alipigwa teke la ubavuni. Ni hapa ambapo mambo yaligeuka. Baada ya Juvinali kutupa teke kali lililompata Willy vilivyo ubavuni. Willy akahisi amevunjika mbavu, kama sumaku.
Willy aliunasa mguu wa Juvinali kabla haujarudi na kuupinda, kisha akauvuta upande wake, haraka sana akamlalia juu. Hii yote ilitokea kwa haraka mno kiasi cha kuwatatanisha Luteni Biniga na Ananie wasijuwe wafanye nini kwani wangefyatua risasi wangemuua Juvinali. Bastola ya Juvinali ilianguka chini karibu yao. Tena kwa kutumia nguvu zote alizokuwa nazo Willy alimrusha Juvinali kwa Ananie aliyekuwa kama hatua mbili kutoka pale walipokuwa. Juvinali akamkumba Ananie, wakaanguka huku bunduki ya Ananie ikitema risasi zilizomwingia Juvinali na kumwua hapohapo.
Wakati Willy alipomrusha Juvinali kwa Ananie. Haraka aliirukia ile bastola na kumpiga risasi kadhaa Luteni Biniga. Kabla hajafyatua bastola yake, risasi zikampata Luteni Biniga kwenye paja la uso na kumwua pale pale. Ananie naye kwa kutumia nguvu zake zote. Alijaribu kuitoa maiti ya Juvinali ili aichukuwe tena bunduki yake. Lakini hakuwahi. Willy alimpiga tena teke la kichwa na kumtoa fahamu. Willy akaivuta maiti ya Juvinali na kuitoa juu ya Ananie na kuanza kumvuta Ananie ili aweze kumuuliza maswali. Mara akasikia mlio kama wa king'ola. Akajuwa ama yule mwanamke ameripoti au ule mlio wa bunduki na bastola umesikika. Hivyo akajuwa angekutwa pale, kwa hasira aliivunja shingo ya Ananie na kumtupa chini. Akakimbilia ukutani. Akauparamia ukuta na kuangukia kwenye uchochoro wa mtaa wa pili; akakimbilia kwa Col. Rwivanga.
Alipoingia nyumba ya Col. Rwivanga. Ndipo Col. Rwivanga alipojuwa kuwa alipokuwa ameumia sana. Col. Rwivanga alikuwa ameusikia mlio wa bunduki lakini kwa Kigali halikuwa jambo la ajabu, ingawa alikuwa na wasiwasi. Lango la ua wake lilipofunguliwa tu alikuwa nje na ndipo alipomwona Willy akiingia huku akipepesuka. Col. Rwivanga alimsaidia wakaingia ndani. Willy alikuwa anatoka damu puani, Col. Rwivanga akajuwa kuwa alikuwa ameumia sana maana alipoonekana kama ana nyuso mbili kwa vile paji lake lilikuwa limevimba vibaya sana.
"Utadhani umekanyagwa na trekta", Col. Rwivanga alisema baada ya kumwona Willy.
"Nakwambia ni zaidi ya trekta. Sijawahi kupigwa teke lenye nguvu kama lile", Willy alijibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dkt. Daniel Robinson alikuwa daktari mkuu wa Hospitali ya King Faisal mjini Kigali na alikuwa rafiki mkubwa wa Col. Rwivanga kabla Dkt. Robinson hajaja Rwanda alikuwa daktari katika Hospitali ya Mulago mjini Kampala, ambako alikuwa akiishi karibu na Col. Rwivanga. Na kwa muda wote walipokuwa Kampala walikuwa marafiki wa karibu sana.
Kwa hivyo wakati RPF walipoingia tu Kigali, Col. Rwivanga ndiye aliyekuwa kiongozi wa kikosi cha kwanza kabisa kilichoongoza mapambano dhidi ya majeshi ya serikali. Na kituo cha kwanza kabisa ni kuwaokoa watu waliokuwa Hospitali ya King Faisal ambako kuliwa na maelfu ya watu wakiwa pamoja na rafiki yake Dkt. Robinson. walikuwa wamejisalimisha ndani ya Hospita, lakini baada ya Intalahamwe kuwa wamewaua watu wengi Hospitali hapo pamoja na wagonjwa.
Baada ya Col. Rwivanga kuingia na kikosi cha kulinda usalama, watu wengi walipona. Siku zilizofuata majeruhi na wengineo aliponea katika Hospitali hiyo, hivyo Col. Rwivanga alimpigia simu Daktari Robinson ambaye ni Mzungu Mwingereza na kumweleza juu ya Willy kujeruhiwa.
"Niko njiani!", Dkt. Robinson alimweleza Col. Rwivangga, wakati walipokuwa wanamsubiri Daktari, Willy alimweleza Col. Rwivanga yote yaliyotokea nyumbani kwa Luteni Silas Biniga.
"Nini maana ya Inkontanyi?, maana waliniita hivyo", Willy aliuliza baada ya kumaliza maelezo yake.
"Inkontanyi huwa ina maana ya RPF. Maana yake hasa ni mpiganaji mkali na maarufu katika Kinyarwanda. Lilikuwa ni jina lililopewa kikosi kimoja cha Mfalme wa Bugiri katika karne ya kumi na tisa hivyo. Walihisi kuwa wewe utakuwa ni mpelelezi wa RPF", Col. Rwivanga alieleza.
"Kwa hiyo. Inamaana wao siyo RPF", Willy aliuliza.
"Bila shaka, kama ulivyosikia na hili limenitia wasiwasi sana kutambua kuwa katika uongozi wa katikati. Na bila shaka wa juu wa RPF tumeingiliwa na wasalti. Kinachoonekana wazi ni kuwa hawa waliopambana nawe nao ni watu wanaofanya hivi vitendo ni wapenda pesa. Sasa mtu au kikundi hatari ni kile kinachotoa pesa hicho ndicho yafaa tukijuwe na kukiangamiza ili Rwanda iweze kurudi hali yake ya amani", Col. Rwivanga alijibu.
"Basi mtafute yule mwanamke niliyesikia wakimwita Bibiane na jibu lako utakuwa umelipata", Willy alijibu huku akionekana kuwa maumivu yalikuwa yamezidi. Mara akasikia honi ya gari.
"Daktari huyo rafiki yangu, ngoja utubiwe usife maana kazi sasa ndiyo imeaanza", Col. Rwivanga alimtia moyo Willy.
Col. Gatabazi alikuwa kati ya watu wa kwanza kufika kwa Luteni Silas Biniga, maana alikuwa akiishi nyumba ya nne tu kutoka pale. Alipofika hakuamini macho na akili yake ilishindwa kukubali. Watu wote hawa waliouawa walikuwa watu makini katika kundi lake, watu ambao alijua ndio wangemsaidia kuchukua madaraka muda utakapofika. Hili jambo lilimshitua sana. Watu wote hawa walikuwa askari shupavu, jasiri na waliojuwa kazi yao vizuri.
Yeyote yule aliyefanya kitendo hicho hakuwa mtu wa kawaida na kama ni kikundi, hakikuwa kikundi cha kawaida. Hawa watu watatu walikuwa na uwezo wa kuangamiza kikosi kizima cha jeshi la maadui lakini leo wameuawa kirahisi na wote kwa pamoja! Suala hili lilimshitua sana Col. Gatabazi, akaingiwa na woga na wasiwasi.
Gari la jeshi lenye king'ola, lilikuwa tayari limefika pale likiwa na askari wa doria wa sehemu zile, askari hao walifika mara baada ya kusikia milio ya risasi.
"Vipi hamjaona au kukutana na mtu au watu wowote waliofanya kitendo hiki?", Col. Gatabazi aliwauliza wale askari wa doria kwa ghadhabu.
"Hapana afande, kote hapa ni shwari", mmoja wapo alijibu.
"Haiwezekani kuwa shwari wakati maafisa wanaotegemewa kama hawa wameuawa hovyohovyo hivi", Col. Gatabazi alieleza tena kwa ukali.
"Huenda wameuana wao wenyewe afande", askari wa pili wa doria alijibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Col. Gatabazi alimwangalia kwa jicho baya mpaka yule askari akarudi hatua moja nyuma.
"Chukueni hizi maiti pelekeni hospitali na poteeni hapa mara moja", Col. Gatabazi aliamrisha mara moja.
Col. Gatabazi alirudi nyumbani kwake ili apige simu Ufaransa. Alipofungua mlango wa mbele aliukuta uko wazi. Alishituka, akatoa bastola yake tayari kukabiliana na lolote ambalo lingetokea mbele yake. Alifungua mlango kwa ghafla huku bastola yake ikiwa tayari tayari.
"Vipi! mbona wasiwasi?", Bibiane alimuuliza huku akiweka mguu mmoja juu ya mwingine pale sebuleni alipokuwa ameketi.
"Hujui kumetokea mauaji mabaya sana usiku huu na vijana wetu watatu wameuawa?", Col. Gatabazi alihoji huku akirejesha bastola yake kwenye mkoba wake na macho yake yakiangalia mapaja ya Bibiane ambayo yalikuwa yameachwa wazi kwa kitendo chake cha kuweka miguu juu ya mwingine na kufanya nguo yake iliyokuwa fupi na ya kubana kuyaacha wazi.
Bibiane Habyarimana alikuwa mtoto wa Kinyarwanda ambaye baba yake alikuwa Mhutu na Mama yake chotara wa Kitutsi na Kifarasa. Alikuwa msichana aliyeumbika kwa sura na mrembo katika warembo. Alikuwa na urefu wa futi tano na inchi nane, hivyo, alikuwa mwanamke na urefu wa kutosha. Alikuwa na nywele ndefu za singa, macho makubwa ya blue, mashavu ya kumimina, pua ya kuchonga, midomo ya tasi, meno meupe yaliyopangika na kuacha mwanya kwenye safu ya juu. Hakika, alikuwa kapendelewa na muumbaji. Mwili wake mzima ulikuwa na muundo wa nyigu, juu mwembamba chini kajaa, akimalizia na miguu minene ivutiayo macho.
Ilimchukua Col. Gatabazi muda mrefu kupata la kusema maana kila alipoonana na msichana huyu alijikuta ulimi wake unakuwa mzito, anashindwa hata kusema. Mara nyingi alipatwa na kigugumizi kwani moyo ulimwenda mbio.
"Aliyewaua mimi nimemwona", Bibiane alieleza bila wasiwasi utafikiri alikuwa anazungumza kitu cha kawaida tu.
"Unasemaje?", Col. Gatabazi alimuuliza kwa mshangao.
"Aliyewaua nimemuona mimi. Nilikuwepo alipofika pale kwa Luteni Biniga", Bibiane alijibu tena kwa utulivu, kisha akasema, "Hamna hata kinywaji humu ndani". Kila wakati Col. Gatabazi alishangazwa na tabia ya huyu binti.
"Kinywaji kipo, huenda kweli tunakihitaji maana sasa wewe unazidi kunichanganya", Col. Gatabazi alisema na kuelekea kwenye kabati la vinywaji akatoa chupa ya whisky na gini, akaleta barafu na glasi mbili.
"Utakunywa nini?".
"Whisky niwekee barafu tu usiiharifu na maji".
"Sawa mama, ehee unamaje eti ulikuwepo kwa Luteni Biniga?", Col. Gatabazi aliuliza kwa shauku ya kutaka kujua.
Bibiane alimweleza kwa kirefu yaliyotokea pale kwa Luteni Biniga na kumalizia, "Watakati natoka ndani walikuwa wakimwuliza maswali pale nje, awaeleze yeye ni nani. Sikuwa na wasiwasi maana nilijuwa yule kaisha. Mbele ya wale wanaume hakuna ambaye angefanya kitu. Niliposikia risasi zinalia ile ya kwanza nilijuwa kauawa, lakini niliposikia milio ya risasi inazidi nikawa na wasiwasi nikarudi haraka kuchungulia na nikaona uliyoyaona, lakini mimi nilikuwa na bahati ya kumwona akiruka ukuta upande ule mwingine, akapotelea gizani. Yule ni mwanaume wa shoka na hapa kazi ipo, sina shaka yule ni Willy Gamba kama Jean alivyomwelezea. Hivyo, umeshindwa mtihani wako wa kwanza huyu mtu hakufa ndani ya ile ndege mliyoitungua. Fanya utafiti, utakuta amekuja na ndege nyingine, kakuzidi maarifa, tayari alishajuwa ni Luteni Silas Biniga aliyeamrisha ile ndege kupigwa. Mtu huyu ni hatari, mbona ni hatari sana! Kazi kwako Gatabazi. Kama unataka Uras kwanza inakubidi huyu mtu ummalize. Hizi habari zitamsikitisha sana Jean, wewe unajua.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Usipommaliza haraka basi ujuwe wewe umekwisha kwani atakuumbua na RPF watakumaliza na utakuwa umewaangamiza Wahutu", Bibiane alimalizia na tabasamu la mauti.
Woga ulimwingia Col. Gatabazi maana naye alihisi kuwa huenda yule alikuwa Willy Gamba. Rwanda hakukuwa na mtu mwenye uwezo kama huo. Jean alimweleza kwa kirefu uwezo wa huyo Willy Gamba na sasa aliudhihilisha. Vilevile, alijuwa Jean angekasirishwa sana kuona huyu mtu amejipenyeza mpaka kuleta maafa makubwa hivi.
Mtu wa kuweza kumsaidia kumweleza Jean mpaka amwelewe na kumsaidia katika mapambano na mtu huyu alikuwa ni Bibiane. Ingawa alikuwa akimtamani sana Bibiane, lakini alikuwa mwangalifu sana asimguse maana alijuwa siku moja angeweza kumtumia.
Bibiane alikuwa karibu sana na Jean alikuwa mpenzi wake lakini vilevile Bibiane alikuwa mhitimu wa fani ya upelelezi na usalama na akiwa amesomeshwa kwa msaada wa Jean. Jean alikuwa akifanya mambo yake kwa ufasaha. Alihitaji kuwa na mtu Afrika Mashariki na Kati ambaye angeangalia mambo yake bila kuhisiwa. Pamoja na kuwa alikuwa ametumbukia katika lindi la mapenzi na Bibiane, lakini kwa upande mkubwa alimtumia Bibiane kufanikisha mambo yake yaliyokuwa yakimletea maslahi.
Sababu hizi ndizo zilizomfanya Jean amugharamie Bibiane mafunzo ya hali ya juu ya upeleelezi na kweli msichana huyu alifuzu vizuri na alikuwa mjuzi. Idara ya upelelezi na usalama ya Ufaransa inayoshughulikia usalama wa nje (DGSE) ilimuongezea ujuzi msichana huyu na mara nyingi walimtumia katika kazi zake.
Ni huyu msichana, kwa kutumwa na DGSE, alikisambaratisha kikundi cha wanajeshi waliotaka kuipindua serikali ya Hassan Gouled wa Djibouti na kufanya wakamatwe, kwani siri zao zote alitoa wa serikali kupitia DGSE mpaka leo haikujulikana jinsi alivyoweza kupata ushahidi huo ambao hata kikundi hicho cha wanajeshi kilibaki kimepigwa na butwaa. Msaada huo wa Bibiane kwa DGSE ulimwongezea Jean uhusiano wa karibu.
Hivyo hata Bibiane alitumia idara hiyo kwa kumsaidia katika mambo yake. Ni Bibiane aliyekuwa kiungo kikubwa kati ya Jean na familia ya Rais. Ingawaje na yeye aliitwa Bibiane Habyarimana hakuwa na uko na Rais kwani familia za Kinyarwanda hutumia jina lake na siyo jina la ukoo kama jamii zingine.
vilevile, msichana huyu ndiye aliyekuwa kiungo kikubwa na wakubwa wengine wa serikali katika Afrika. Kutokana na umbile na sura yake ya kuvutia, ambayo kila siku ilimuonesha kuwa msichana mdogo asiyezidi umri wa miaka kumi na minane, hakuna aliyeweza kumuhisi kama mmoja ya watu hatari waliokuwa kiungo cha uhaini na ugaidi kati ya wakuu wa serikali, wafanyabiashara na magaidi wa Ulaya. Inasemekana wakati wa mkutano wa amani uliofanyika mjini Arusha, Tanzania, Bibiane alikuwapo kama mkalimani.
Baada ya mkutano huo, rais alimpa nafasi aondoke nae kwenye ndege yake, kwani alikuja kama mkalimani wake lakini Bibiane alikataa na kuondoka na Jean kwa barabara kupitia Nairobi, nchini Kenya. Inasemekana alijua nini kingetokea, kwani yeye aliingia kwa ndege ya jeshi la Ufaransa akitokea Nairobi, mara tu baada ya marais kuuawa tarehe 6 aprili Bibiane alisaidia kumchukua mke wa rais na familia yake ya watu kumi na watano na kuwapeleka Ufaransa.
Pia. Inasemekana. Kwa kusaidiana na Jean aliwawezesha Protais Naimana na Feldinand Zigilanyilazo kuwapatia visa ya kusafiria na kuwawezesha kwenda Ulaya. Hivyo. yote hii inaweza kukuonyesha jinsi gani msichana huyu mwenye umri wa miaka ishirini na saba tu alivyoweza kufanya mambo makubwa. Alikuwa msichana hatari sana.
Lazima tumweleze Jean hali halisi", Col. Gatabazo alimweleza Bibiane.
"Piga simu!".
"Sawa. Lakini uzungumze nae kwanza".
"Sawa!", Bibiane alijibu. Alimwangalia Col. Gatabazi. Akaona kuwa ameingiwa na woga. Bibiane aliwaponda sana wanaume walioonekana waoga. Kwa mara ya kwanza alimponda Col. Gatabazi, aliwapenda sana watu jasiri mwanaume yeyote shupavu aliifanya damu yake ichemke na kuchochea tamaa zake za mwili. Lakini mwanaume mwoga hata awe mzuri na sifa aina gani alimtia baridi. Mara hii alihisi baridi na kumchukia Col. Gatabazo mawazo yake yalitembea na kumfikiria Jean. Ile kumfikiria tu alihisi damu yake ikichemka. Kwake Jean ndiye alikuwa mfano wa mwanaume ampendaye, jasiri, shupavu anayepata kile anachokitaka hata iwe kwa gharama gani, hata ikibidi kuhatarisha maisha yake.
Ndivyo Jean alivyokuwa. Bibiane alimpenda Jean kikwelikweli. Ingawa Jean alikuwa mzungu, lakini alikuwa mzungu wa aina yake. Alijuwa kupenda na alijuwa jinsi ya kumfurahisha mwanamke mpaka kumaliza haja zake za kimwili. Lakini zaidi ya yote alimpenda kwa ujasiri na ushupavu wake katika mambo yake. Iwe biashara, iwe siasa yeye alikuwa ndie bingwa wa mchezo.
Alifikiria jinsi watu wenye vyeo vikubwa, wakuu wa nchi, matajiri walivyo yeyuka kama barafu mbele ya Jean kila alipopambana nao. Kila siku ndiye aliyetokea kuwa mshindi. Hata rais alipojaribu kumgeuka na kukabiliana na mambo kinyume na matakwa yake, Jean aliibuka mshindi na rais akapoteza maisha. Hata hali ya sasa ya Rwanda, kuwepo RPF, ilikuwa kata ya mbinu zake. Na Bibiane aliamini kabisa kuwa hii ilikuwa ni mipango yake ili baadae aiondoe serikali ya RPF na kumuweka mtu wake Col. Gatabazi. Mwanzo Bibiane alirudi kwa Col. Gatabazi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alimfikiria na kisha akatambua mtu kama yeye ndiye angewafaa yeye na Jean, mtu mwoga, mtu anaependa fedha, mtu ambaye anafanya kile ambacho angeambiwa. Kiongozi kama viongozi wengine wa Afrika, mtu anayejifikiria yeye na wala sio nchi au watu wake, mtu mbinafsi, kama walivyo watawala wengi wa kiafrika, Col. Gatabazi alifaa sana kutawala Rwanda.
"Njoo Jean yupo kwenye simu," Col. Gatabazi alimshtua Bibiane kutoka kwenye lindi la mawazo.
"Oh asante sana"" alijibu.
"Mpenzi hujambo?" Bibiane alimsalimia Jean.
"Sijambo, pole na matatizo huko," Jean alijibu.
"Col. amekueleza?"
"Amesema wewe ndiye utanipa safi!"
"Una maana sikupagi safi?"
"Wacha masihara huu si wakati wake. Hebu nieleze imekuwaje?"
"Huwenda na mimi ningekuwepo ningekuwa nimekufa," Bibiane alijibu.
"Sawa tu hiyo ingekuwa kifo kazini," Jean alijibu kwa sauti kavu.
Mara Bibiane akasikia damu yake inasisimka kwani alitaka mwanamume kama huyu asiye na huruma. Huyu ndiye aliyekuwa mwanamume wa kiwango chake.
"Yaani ningekufa asingejali."
"Bila shaka nigejali, lakini kama ungekufa katika mstari wa kazi ni vizuri zaidi kuliko kufa kibudu," Jean alijibu na kuendelea, "Hebu nipe imekuwaje".
Bibiane alichukuwa muda kumwelezea jinsi mambo yalivyotokea.
"Yaani huyu Willy Gamba umemuona kwa macho yako?.
"Ndiyo kwanza sikumtilia maanani sana, nilishtuka kuwa ni yeye baada ya kazi aliyokuwa ameifanya. Mwanzoni nilifikiri ni ka-Inyezi kalikopata fununu ambako vijana walikuwa tayari kushughulika," Bibiane alijibu
"Lazma umsaidie Col. Gatabazi kummaliza huyu mtu, Na mimi nitafanya mipango ya kukupeni msaada wa watu wenye ujuzi wa juu wawasaidie kumuondoa huyu funza anayetaka kula nyama yetu," Jean alijibu.
"Ukisema wewe sisi tutatekeleza, tunaomba hua msaada wako haraka maana hata siye tuna wasiwasi ," Bibiane alijibu.
"Usiwe na wasiwasi, unajua watu kama huyo Willy Gamba ndio nawataka mimi,"
"Najua Jean, wewe tena! Bwana nakuwaza, nataka nije huko unikumbatie, najua huwezi kuja huku sasa!. Bibiane alijibu kwa sauti ya mahaba.
"Baada ya kazi hiyo ya Willy Gamba tuonane Nairobi hata mimi nakutamuni sana," Jean alijibu.
"Haya kazi kwanza."
"Halafu kama kazi," Jean alimalizia na kumuomba Col. Gatabazi tena.
"Kwaheri mpenzi!"
"Kwaheri Bibiane. Col. Gatabazi atakupa mipango yote," Jean alimalizia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jean alipozungumza na Col. Gatabazi alimweleza mipango yake ya kummaliza Willy ambayo ilikuwa ikiendelea kichwani mwake.
"Nafikiri mawazo yako ni sahihi tutafanya hivyo. Asubuhi nitawasiliana na wewe," Col. Gatabazi alijibu.
Simu ilipolia ilimshitua sana JKS, maana alikuwa tayari amelala na ilikuwa yapata saa sita za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
"Hallo", JKS aliita.
"Jean".
Mara moja usingizi ulikwisha.
"Ehe, salama huko?", JKS alijibu kwa shauku maana tokea alipopewa taarifa kuwa Willy Gamba alikuwa ameuawa basi roho yake ilikuwa imetulia kabisa.
"Mambo siyo mazuri, rafiki yako hakufa na kaibuka na mambo mapya", kisha akamweleza yote yaliyotokea Kigali.
"Basi huyu ana miguu ya nyuka", JKS alijibu huku sauti yake ikionyesha wasiwasi.
Si wewe mwenyewe ulisema ni mtu hatari, na huu mchezo anaujuwa, sasa basi kazi imefika na inabidi sasa iwe kazi hasa, maana wakati wote tumekuwa tukimchezea", Jean alijibu.
"Sasa mimi nitakusaidia vipi?", JKS aliuliza.
"Utanisaidia mimi au utajisaidia vipi?, unasema kana kwamba wewe haumo kwenye huu mchezo! mchezo huu ni hatari kwako kuliko mimi maana huyu mtu akigundua kuwa wewe umekuwa mmoja wa watu ambao wamekuwa wakiuhujumu mwelekeo wa nchi yako kuhusu suala hili la Rwanda na masuala mengine basi ujuwe umeisha na urais wa Tanzania utauangalia kwenye ndoto zako tu. Kwa hiyo mtu huyu ni hatari kwako kuliko kwangu, hivyo ni kwa faida yako auawe mara moja!!", Jean alimwasa JKS.
"Tufanye nini sasa?", JKS alijibu kwa sauti ya woga.
"Kati ya vijana wetu wazuri na mahiri na wale vijana walioko Arusha ni wazuri sana. Hao ndio saizi ya huyu Gamba kutokana na uzoefu walionao na ujuzi pia ambao wanao. Kwa hiyo. Nataka wote wanne na kiongozi wao, Xavier Nkubana, waende wakaimalize hii kazi. Sasa ninachotaka ufanye ni kuwatafutia pasi mpya za kitanzania waonekane ni Watutsi ambao zamani walikimbilia Tanzania na sasa wanakwenda kuangalia hali ilivyo. Siku zote walikuwa wakifanyakazi yao kwa siri na hakuna atakayewashitukia. Hivyo watafutie hizo pasi na usafiri. Uhakikishe kesho wako Kigali. Wakifika Kigali wawasiliane na Col. Gatabazi atawapa maelekezo ya kufanya. Lazima tusishindwe juu ya jambo hili", Jean alisisitiza.
"Hilo ulilosema hesabu limefanyika, nitatumia nguvu za dola kuhakikisha kesho wako Kigali mapema kabisa. Nkubana amenipigia simu leo na kusema vijana wanasikia kuchoka kukaa tu bila kazi. Hivyo, nikiwaeleza kuwa wanarudi Kigali kwa kazi ngumu, watafurahi sana", JKS alijibu.
"Hiyo safi, basi fanya hivyo na wakishafika nipe taarifa. Hata hivyo, Col. Gatabazi atanipa taarifa, wakiondoka tu mpigie simu Col. Gatabazi", Jean alimalizia na kukata simu.
Saa ileile JKS alipiga simu Arusha ambako ndiko Xavier Nkubana na wenzake walikuwa wakikaa. Tokea kifo cha Rais wa Rwanda, wao walibaki Tanzania kama wakimbizi na JKS aliwafanyia mipango yote. Hakuna mtu hata mmoja aliyewahisi kwa ubaya, walikuwa wakiishi kwa starehe na kifahari, kama kawaida ya wageni katika Tanzania.
Tanzania ni nchi ya namna ya kipekee kwani wageni ndio wanastarehe kuliko wenyeji. Kwa mtu mgeni kuishi kifahari ilikuwa ni sawa, lakini Mtanzania akitokea kuishi hivyo basi watu humhisi kuwa si mtu mwaminifu na husumbuliwa mara kwa mara na vyombo vya dola mpaka imewafikisha watanzania mahala ambapo hata kama wana uwezo huishi kwa kujibana kwa kuogopa kubuguziwa. Lakini mgeni hata akiishi kifahari vipi alionekana ni sawa na hakuna chombo cha dola ambacho kingeweza kumgusa, na vilevile wananchi hubaki kumsifia kwa ufahari wake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hivyo, Nkubana na wenzake waliishi Arusha kwa raha mstarehe wakiwa wameifanya Arusha kama sehemu yao ya kufanyia mipango ya kuihujumu serikali ya RPF. Kusema kweli hawa jamaa walikuwa wauaji katili sana, na si kweli kuwa walikuwa wamebaki Tanzania wakati wa kifo cha Rais, ila walikuwa miongoni mwa watu walioongoza mauaji ya Watutsi. Inasemekana mmoja kati yao, Felician Nzirorera, ndiye aliyekuwa akitangaza na kuchochea watu kwa kutumia radio ya RPLM iliyokuwa ikimilikiwa na Wahutu wenye siasa kali. Radio Televisheni Libre Des Milles Collines (RTLM), iliyokuwa radio ya uchochezi, na mauaji yalipoanza wengi wa watangazaji wake walijiunga katika mauaji na wakubwa wao kukimbilia nje baada ya kuchochea mauaji.
Lakini Nzirorera aliendelea kwa muda mrefu akiwa anatangaza kwa kuhama na stesheni yake ya redio kwenye gari akiwachochea Wahutu kuendelea kuwauwa Watutsi. Na ni mtu huyu pamoja na wenzake aliyekuwa akila starehe hapo mjini Arusha akiendesha magari ya fahari badala ya kuwa amekamatwa kungojea mahakama maalumu ya wauaji hapo Arusha. Kama si JKS kuwasaidia na kuwapa sifa tofauti kuwa wao walikuwa ni maafisa safi wa serikali waliojikuta kwenye mapambano ambayo hawakuwa washiriki, leo hii wangekuwa kati ya watu waliokuwa wakitafutwa na mahakama ya kimataifa ya mauaji ya Rwanda.
Simu ililia chumbani mwa Nkubana, bahati nzuri alikuwa ndio kwanza amerudi toka hoteli Sabasaba kwenye disko ambako alijipatia msichana wa kustarehe naye usiku huo. Simu ilipolia Nkubana alimwacha yule msichana sebuleni na kwenda kuchukua simu chumbani.
"Hello, Xavier".
"JKS".
"Shikamoo, vipi kulikoni".
"Sikiliza kwa makini".
JKS alimweleza yote kuhusu ambavyo yeye na wenzake walikuwa wakitakiwa kwenda Rwanda kumsaidia Bibiane na Col. Gatabazi kummaliza Willy Gamba.
"Hiyo safi sana, tulikuwa tunakaa hapa, tunalewa na kustarehe tu na wanawake maana hatukuwa na kazi. Sisi tuko tayari hata sasa", Nkubana alijibu.
JKS alimweleza mipango yote na jinsi ambavyo wangesafiri mpaka Kigali.
"Hakika mzee, wewe hushindwi kitu. Kweli madaraka ukijuwa kuyatumia ni matamu sana maana kila kitu kinawezekana, sijui bila wewe tungefanya nini. Asante sana. nitawaeleza wenzangu. Hivyo, saa mbili asubuhi tutakuwa tayari. Na hesabu hiyo kazi huko Kigali imeisha maana tuna uchu na damu", Nkubana alijibu kwa majidai.
"Asante na kwa heri".
Nkubana alikuwa amewaacha wenzake kwenye disko. Aliporudi sabuleni alimkuta yule msichana amelala kwenye kiti.
"We, amka turudi kwenye disko".
"Kwanini, mimi nataka kulala, nimechoka".
""Kwani umekuja kulala hapa, kulala ni nyumbani kwako, hapa uko kazini, kazi ya kunistarehesha mimi, kwa vile nasikia nataka kucheza disko tena, utanifuata".
Yule msichana akiwa anashangaa, Nkubana alimuinua na wakaelekea kwenye gari ili kurudi disko sabasaba.
CENTRE CHRISTUS
Ilikuwa yapata saa moja ya usiku wakati Willy alipofika kwenye kituo cha kidini cha Centre Christus. Alikuwa bado anasikia maumivu ya ubavuni yaliyotokana na mapambano ya juzi yake. Hata hivyo, aliamua kuendelea na kazi kwa vile muda ulikuwa hamruhusu kungoja apone kabisa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Langoni mwa kituo hiku alimkuta mtawa mmoja aliyemwuliza jina, na baada ya kujitambulisha mtawa huyu alimchukuwa Willy na kumpeleka kwenye nyumba ya Padri Marcel Karangwa ambaye alimkuta akimsubiri.
"Karibu sana Willy Gamba, karibu Kigali. Kigali inanuka mauti; hata nyumba ya Mungu inanuka mauti", Padri Karangwa alimkaribisha sebuleni mwa nyumba yake.
"Nashukuru sana Padri hasa kwa kukubali mimi nije nikuone mara tu baada ya maafa yaliyotokea kwenye kituo chako hiki, nashukuru sana", Willy alijibu.
"Unakaribishwa sana, Bwana Musoke amenieleza kila kitu, nasi tunafarijika sana kukutana na watu kama nyinyi ambao mnaweza kuleta matumaini ya amani ya nchi kama hii. Kweli, tuko tayari kukupa maelezo yoyote unayohitaji kwa shughuli yako", Padri Karangwa alimweleza Willy.
"Asante Padri, mimi nisingependa nichukuwe muda wako mwingi kwa vile una majukumu makubwa ya kukijenga upya kituo hiki na kurudisha imani ya watu katika nyumba ya Mungu", Willy alijibu wakati mmoja wa watawa akileta chai na kahawa.
"Utakunywa chai au kahawa", Padri Karangwa alimuuliza Willy.
"Chai ya rangi", Willy alijibu na kupewa chai ya rangi na kipande cha mkate na Padri Karangwa akapewa kahawa.
"Bwana Musoke alisema ungependa kujuwa kwa kifupi hasa ni nini kiini cha chuki iliyokithiri kati ya makabila haya ya Kitutsi na Kihutu".
"Sawa kabisa", Willy alijibu.
"Kwanza kabisa mimi ni Mtutsi...". Alipoanza kuongea akaingia Padri mwingine. Padri Karangwa alimkaribisha na kumjulisha kwa Willy Gamba. "Huyu Padri Boniface Sibomana na ni mmoja wa watu waliopona mauaji". Kisha akamjulisha Willy Gamba. "Na huyu ni Willy Gamba, mwandishi wa habari kutoka Tanzania, ambaye pia amekuja kama wengine wengi waliomtangulia kutupa pole na kutaka kuelewa vipi watu wa nchi moja wanaweza kugeukiana na kuuana kikatili namna hii.
Willy na Padri Sibomana walipeana mikono na wakaketi chini kuendelea na mazungumzo.
"Kama nilivyokueleza mimi ni Mtutsi, lakini Padri Sibomana ni Mhutu, sasa sema tofauti yetu sisi kimaumbile ni nini?", Padri Karangwa alimwuliza Willy. Willy aliwaangalia wote wawili. kweli kimaumbile kati ya hawa wawili hasa hakukuwa na tofauti.
"Hakuna", Willy alijibu huku mapadri hawa wawili wakitabasamu.
"Kama hakuna jibu la swala zima la mauaji ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani, basi mauaji haya yalishinikizwa kisiasa na kikundi cha watu wachache wenye madaraka makubwa katika Serikali ya Rwanda. Mara nyingi vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Rwanda ikisingiziwa kuwa ni vita ya kikabila. Hii si kweli na inapotosha ukweli, ila yanapotokea mauaji kama haya ndipo ujenzi wa chuki wa kikabila unajengwa. Wahutu na Watutsi wameishi pamoja kwa karne nyingi na tofauti zao si hizi tunazoziona leo, kwani hakukuwa na chuki kati ya makabila haya. Ni utawala wa kikoloni wa kugawa nitawale na baadaye. Serikali zetu zilizoongozwa na ubinafsi na uchu wa madaraka uliohubiri kuwepo tofauti kati ya wahutu na Watutsi, tofauti ambazo awali hazikuwepo. Kwa kifupi ni kwamba ili mbinu za kisasa za kuyatumia makabila haya mawili ili watawala wabaki kwenye madaraka ambayo yamesababisha mauaji haya ya kikatili ambayo tumeyashuhudia", Padri Karangwa alinyamaza kidogo ili anywe kahawa yake wakati Willy na Padri Sibomana wakimsikiliza kwa makini.
Kisha Padri Karangwa aliendelea. "Kama nilivyosema mwanzo, mauaji ya kikatili Rwanda hayakutokea ghafla tu kiwendawazimu eti kwa sababu kabila moja lilikuwa likilichukia kabila lingine. Mauaji ya Rwanda yalikuwa yamepangwa siku nyingi na kwa ufasaha kabisa na watawala wa nchi yetu. Ili kulielewa hili na ili mtu asisingizie kuwa mauaji haya yametokana na ukabila inabidi kwa kifupi tuangalie historia ya Rwanda kwa maana ya makabila haya mawili ya Watutsi na wahutu", Padri Karangwa alieleza.
"Nafikiri kweli ni vizuri tupate historia fupi ya jinsi chuki ilivyojengeka maana mauaji haya ya Watutsi na Wahutu wenye siasa kali ni ya kinyama yaani binadamu ameweza kuwa mharibifu na mkatili kiasi hiki", Willy alisema kwa kusikitika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Historia ya Rwanda inaonyesha kwamba watu wa kwanza kuishi Rwanda walikuwa wawindaji ambao ni kizazi cha kabila dogo la Watwa. Inasemekana kuwa wakulima, ambao ni Wahutu, ndio waliofuatia na kisha wafugaji ambao ni Watutsi, ndio walikuwa wa mwisho kufika, na wote waliishi pamoja kila ukoo ukiwa na utawala wake wa kichifu. Kusema kuwa Watutsi walikuja kama wavamizi na kutaka kutawala kwa nguvu makabila mengine si kweli, kwani wana historia wengi wameupinga usemi huo, ila kitu ambacho kilitokea ni kwamba karibu vizazi ishirini vilivyopita ukoo mmoja wa Kitutsi ulioitwa Nyinginya ulipata sifa katikati ya Rwanda na kuanzisha utawala wa kifalme ambao ulitawanyika kwenda kusini mwa Rwanda ya sasa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment