Simulizi : Uchu
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini historia inaonyesha kwa bunge lao la wakati huo lilikuwa linaitwa 'abini', nalo liliwashirikisha Wahutu na Watutsi pamoja. Na kwa vile utawala wa Wanyinginya ulikuwa na nguvu, machifu wa Kihutu katikati ya kusini mwa Rwanda walimezwa na kukubalika kama Wanyinginya. Hapa ndipo swala la ukabila wa Kihutu na Kitutsi ulipotambuliwa, si kutokana na ukoo wa Kihutu au Kitutsi bali kwa kutokana na hadhi mtu aliyokuwa nayo. Ukiwa mtawala, hata ukiwa Mhutu uliitwa Mtutsi. Kama huna mali uliitwa Mhutu, na hivyo hii hali iliashiria kuoana kwingi kati ya Wahutu na Watutsi. Ndiyo sababu hata wewe umeshindwa kututoa tofauti," Padri Karangwa alinena.
"Kama si vitambulisho hivi mara nyingi kweli huwezi kujua Mhutu ni yupi na Mtutsi ni yupi maana vile vile tunazungumza lugha moja, tofauti na nyinyi," Padri Sibomana alidakia.
"Huko ndiko ninakokwenda," Padri Karangwa alisema na kisha kuendelea, "Kusema kweli tofauti halisi ambayo ilibaki ilikuwa kwa wahutu wa kaskazini ambao waliendelea na utawala wao mpaka hapo wakoloni walipofika. Pamoja na kwamba utawala wa Wahutu wa kaskazini haukumezwa na utawala wa ukoo wa Nyiginya, bado wahutu hawa na watutsi waliishi bila matatizo."
"Matatizo yalianza lini? Willy aliuliza.
"Usiwe na haraka, mimi taaluma yangu ni ualimu nakupeleka taratibu uelewe na huko tutafika," Padri Karangwa alimjibu na kisha kuendelea, "Tatizo hasa lilianza wakati wakoloni walipofika Rwanda mwishoni mwa karne ya kumi na tisa. Wamisionari wa Kijerumani na kisha askari wa Kijerumani walipofika Rwanda walikuta utawala uliojengeka wa ukoo wa Nyinginya ambao kama nilivyosema ulikuwa ukoo wa Kitutsi. Kama walivyokuwa wakoloni wote walitumia tawala walizozikuta kuwasaidia kutawala. Hivyo, Wajerumani na kisha Wabelgiji baada ya kukuta utawala wenye nguvu ulikuwa wa kitutsi wakaamua kuutumia huu utawala na kuubadilisha uwe wa kinyanyasaji ili ile sera yao ya gawa utawale iweze kufanikiwa. Kwa kusaidiwa na wakoloni sasa watutsi walifuta nafasi yoyote waliyokuwa nayo wahutu kabla ya wakoloni na kuwanyang'anya mali na madaraka, na hii yote ilichochewa na wakoloni ili kuwagawa watu wa nchi hii. Na, kwa vile ilikuwa vigumu kuwatofautisha wahutu na watutsi kwa urahisi mnamo mwaka wa 1933-34 vitambulisho vilianzishwa na wakoloni kwa wananchi wote wa Rwanda vikiwatambulisha kikabila yaani Wahutu, Watutsi au Watwa na vitambulisho hivi hivi ndivyo vilivyotumika katika mauaji haya na mengine mengi yaliyokwisha tokea.
"Kwa kutumia vitambulisho hivi basi maendeleo ya Wahutu na Watwa yalizimwa kabisa?", Willy aliuliza.
"Ndiyo, yalizimwa na hata shule nafasi zote zilitolewa kwa Watutsi, kanisani nako baada ya Omwami kubatizwa kuwa mkatoliki hata kanisa liliwabagua Wahutu. Kanisa Katoliki wakati huo ndilo lilikuwa linamiliki karibu shule zote katika Rwanda. Hivyo liliwasomesha Watutsi na kuhakikisha Wahutu hawapati nafasi ya kusoma ila walibaki na haki ya kuhubiriwa tu", Padri Karangwa alijibu.
"Kwa hiyo vitambulisho vilikuwa moja ya mambo yaliyojenga ukabila ndani ya Rwanda?", Willy aliuliza tena.
"Ndiyo, kabla ya vitambulisho ilikuwa vigumu kujuwa huyu ni kabila gani na vitambulisho kama nilivyosema hapo mwanzo, vilianzishwa na wakoloni wa Kibelgiji ili kujenga ukabila ili wautumie huu ukabila kuwagawa Wanyarwanda kwa faida yao ili iwe rahisi kuwatawala. Baada ya kupewa vitambulisho watu wote waliotambuliwa kama Wahutu walinyanyaswa na kunyimwa hazi zozote na elimu na vilevile mali na hata Wahutu wa Kaskazini ambao walikuwa wakijitawala wenyewe, wakoloni mnamo mwaka 1912 walimshinikiza na kumsaidia Omwami atwae madaraka katika sehemu hizi. Kutwaa madaraka Kaskazini mwa Rwanda kwa Watutsi kulikataliwa na Wahutu wa sehemu hii na mapigano makali yalitokea yakiongozwa na Mhutu aitwae Ndugutse. Kwa vile Watutsi walikuwa wakisaidiana na wakoloni, Wahutu walishindwa na wakatawaliwa na Watutsi. Wahutu wengi waliuawa na huo ndio ukawa mwanza wa uhasama na chuki kati ya Wahutu wa Kaskazini na Watutsi. Sasa, ukiangalia mwanzo mwa hii vita ulikuwa umechochewa na wakoloni maana, kama nilivyosema hapo mwanzo, wakoloni walipofika walikuta makabila haya yakiishi kwa amani", Padri Karangwa alijibu.
"Ilikuwaje sasa baadaye Wahutu kuja kutawala Rwanda", Willy aliuliza.
"Baada ya vita kuu vya pili Watutsi walianza kuomba uhuru kama ilivyokuwa katika nchi zingine za kiafrika. Wakoloni wa Kibelgiji kuona hivi, na jinsi Watutsi walivyokuwa na nguvu na walivyokuwa wamesoma, wakaingiwa na wasiwasi, wakajuwa Watutsi wasingewahitaji iwapo watapata uhuru. Hivyo Wakoloni wa Kibalgiji wakaamua kuwageuka na kuwasaidia Wahutu kuwaunga mkono. Viongozi wa Kihutu walikuwa wachache na wote walikuwa na kisomo kidogo walichopata kwa Wamisionari. Hivyo, kwa vile hawakuwa na nguvu zozote za kiutawala, walipoanza siasa, siasa yao ikawa ya kikabila. Hivyo mwaka 1957 chama cha kupigania haki za Wahutu, kikiongozwa na Gregoire Kayibanda, kilianzishwa kikiitwa Permehutu. Na Wakoloni wa Kibelgiji, wakiwa sasa wamewageuka Watutsi, walianza kukisaidia chama cha Permehutu, huku wakikitafutia nafasi ya kuuangusha utawala wa Watutsi. Nia yao ikiwa kuwaingia kwenye madaraka Wahutu ambao hawakuwa na nguvu ili waendelee kuwategemea kama wangepata uhuru. Hii ingewasaidia wakoloni kuendeleza maslahi yao kwani Wahutu wangewategemea sana kuwalinda dhidi ya Watutsi waliokuwa na nguvu za kijeshi na utawala. Kwa hiyo wakoloni ndio wangeendelea kutawala kiaina kwani watawala wa Kihutu wangekuwepo kama mfano tu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Je, viongozi wa Kitutsi hawakushituka?", Willy aliuliza.
"Walianza kushituka lakini mambo yalitokea kwa ghafla sana wakati Omwami Rudahigwa alipofariki kiajabu mjini Bujumbwe mwaka 1959. Jeshi la Ubelgiji lilisimamia kuangushwa kwa utawala wa Kitutsi ambao ulikuwa na umwagaji wa damu vibaya sana. Jeshi la Ubelgiji lililowasaidia Watutsi kuanzia mwaka 1912 sasa liliwasaidia Wahutu na ile chuki ya mwaka 1912 ya Wahutu wa kaskazini ilijitokeza na inasadikiwa kuwa Watutsi wapatao elfu kumi waliuawa na wengi wao wakakimbilia nchi jirani. Hivyo, Wahutu ndio wakawa watawala chini ya Kayibanda baada ya kusaidiwa na wakoloni wa Kibalgiji kuwaweka madarakani", Padri Karangwa alieleza.
"Kwa nini baada ya hapo vitambulisho viliendelea, si Wahutu wangeachana navyo sasa maana vilikuwa vinawabagua?", Willy alitaka kujua.
"Hapana, mambo sasa yaligeuka; Wahutu sasa ndio walikuwa watawala. Hivyo, wakaanza kuwanyanyasa Watutsi. Na vitambulisho hivyo hivyo vilivyowasaidia Wahutu kuwatambua Watutsi na kuwabagua, hata Watutsi wengine wakabadili vitambulisho vyao na kujiita Wahutu maana sasa kibao kilikuwa kimewageukia. Ingawaje Watutsi ndio waliokuwa wamesoma lakini sasa walibaguliwa na Wahutu waliokuwa hawana kisomo maana ndio waliochukua madaraka serikalini. Elimju yote sasa ilitolewa kwa wahutu na Watutsi wakabaki kuangaika na kunyanyaswa. Wengi wao wakaanza kukimbia. Kwa vile jeshi asilimia kubwa lilibaki la Kibelgiji hivyo hakuna kitu ambacho Watutsi wangefanya. Ingawaje Watutsi waliokimbia walijaribu kuishambulia Rwanda kwa kuunda jeshi la msituni lakini hawakufua dafu. Jeshi zaidi la kuongeza nguvu liliitwa mara moja toka Ubelgiji kuja kutokomeza maasi mara uvamizi wa kitutsi ulipoanza. Kwa hiyo, katika miaka yote ya sitini hali iliendelea kuwa ya wasiwasi nchini Rwanda huku watutsi wakiendelea kuuwawa na kunyanyaswa",
"Ilikuwaje Habyarimana akafanya mapinduzi, maana yeye ni Mhutu na utawala ulikuwa Wakihutu? " Willy aliuliza.
"Swali zuri," Padri Karangwa alijibu na kisha akaendelea, "Serikali ya Kayibanda ilianza kuishiwa mbinu na Wabelgiji wakaanza kuichoka maana sasa ilikuwa inakuwepo kwa sababu ya ukabila tu. Mnamo mwaka 1973 Kayibanda akafanya makosa. Kwa vile Watutsi walikuwa wamenyimwa nafasi yoyote katika serikali, kibiashara na sehemu zingine zozote, sehemu waloyokimbilia ilikuwa ni ndani ya kanisa. Hivyo, Seminari nyingi zilijaa Watutsi pamoja na vyuo vikuu ambavyo viliitwa vyuo vya Watutsi. Kwa hiyo, mwaka 1973 ili kuwaondoa Watutsi katika vyombo vyote vya elimu, serikali ilianza kushambulia seminari, shule na vyuo vikuu. Kwa vile vyombo vyote vya elimu vilikuwa mikononi mwa kanisa katoliki Askofun wa kanisa katoliki akaanza kupiga makelele na kulaani serikali. Hata hivyo, huyu Kayibanda kabla ya kushika madaraka alikuwa katibu wa Askofu huyu na alikuwa akiwaunga mkono wahutu. Hapo ndipo Wabelgiji tena wakapata nafasi na kumtumia Meja Generali Habyarimana kufanya mapinduzi na kumtoa rais Kayibanda.Haybarimana alikuwa Mhutu wa kaskazini na Kayibanda wa kusini. Utawala wake ulipokelewa kwa shangwa na Watutsi na Wahutu ukifikiriwa utakuwa utawala wa haki na usawa lakini hali haikuwa hivyo, badala ya kuwa na mgawanyiko wa Watutsi na Wahutu mambo yalizidi. Sasa kukawa na upendeleo kwa Wahutu wa kaskazini na kuwabagua Watutsi na Wahutu wa kati na kusini. Ndiyo sababu Wahutu wenye siasa ya wastani waliuawa katika mauaji ya aprili wakiwamo wanasiasa, wafanyakazi wa serikali na wafanyabiashara, wote walikuwa wa kusini. hivyo, kufika wakati wa sasa sera ya gawa nitawale iliendelea katika Rwanda."
"Maelezo yako toka mwanzo yameonyesha kuwa Wahutu na Watutsi kama watu hawakuwa na tatizo kati yao. Wamekuwa wakitumiwa na watawala wa kikoloni na watawala wa kizalendo ambao wamekuwa wakiwachonganisha ili wakosane na kwa kukosana kwao wao wafaidike," Willy alieleza.
"Haswa, ndiyo sababu nimeeleza yote haya uweze kulielewa tatizo la Rwanda. Tatizo letu si ukabila, tatizo letu ni uongozi."
"Sasa nini kilifanya hali ifikie mauaji, kama ni tatizo la uongozi nchi nyingi za Kiafrika zina tatizo hilo. Na kama ni kutumiwa na mataifa ya nje nchi nyingi zinatumiwa hivyohivyo, mauaji kama haya ni ya pekee katika dunia, hayana mfano," Willy alimuuliza Padri Sibomana ambaye alikuwa akisikiliza kwa muda mrefu bila kusema kitu.
"Nafikiri hilo swali lako ndilo kila mtu anajiuliza, maana mauaji haya tuliyo yashuudia hayana mfano, hata ya Hitler yalichukua muda mrefu maana vita vilipiganwa kwa miaka, lakini mauaji haya yanashinda fikra kwani yalianza dakika chache tu baada ya kufa Rais na kusambaa nchi nzima utafikiri moto wa petroli," Padri Sibomana alisema.
"Wakati wa Habyarimana kulijitokeza kikundi kidogo cha watu kilichomzunguka ambacho ndicho kilichokuwa kinafaidika na utawala wake. Kikundi hiki kilikuwa cha watu wa kaskazini kutoka sehemu za Gisenyi na Ruhengeri nacho kilijulikana kwa jina la Akazu. Kikundi hiki kilijilimbikizia mali na madaraka, kilijenga ngome ya kukizunguka na hakuna kikundi kingine kilichoweza kupenya ngome hiyo. Hivyo, ili Rais na kikundi hiki waweze kuendelea kujilimbikizia mali na madaraka kilihakikisha kuwa hakuna biashara wala nafasi ya uongozi inayoweza kupatikana mahali popote bila kikundi hicho kutoa ruksa. Kikundi hiki kilikuwa cha Wahutu. Hivyo, uhalali wa serikali ulipoanza kushitukiwa, kwa vile kikundi hiki cha Akazu kilikuwa kimejilimbikizia mali nyingi, kilianza kuitumia mali hii na ya serikali kujenga jeshi lake, redio yake, magazeti na kutumia vyombo hivi kuwachochea Wahutu, ambao ndio wengi, wawachukie Watutsi ambao sasa walikuwa wanausaili uhalali wa serikali hii wakiwemo Wahutu wapendao amani na usawa ambao waliitwa Wahutu wenye msimamo wa wastani. Kufikia mwaka 1990 kulikuwa hakuna Mtutsi mwenye madaraka katika serikali, kwa mfano kati ya wakuu wa mikoa kumi na moja hakukuwa na Mtutsi hata mmoja; kati ya vyeo 143 vya juu serikalini hakukuwa na Mtutsi hata mmoja; kati ya mabalozi wote walioteuliwa kwenda nje Mtutsi alikuwa mmoja tu. Na kati ya wabunge sabini, ni watutsi wawili tu waliokuwa wabunge. Katika jeshi walihakikisha hakuna Mtutsi na hasa jeshi la kumlinda Rais lote lilikuwa na Wahutu na Wahutu hao vilevile walikuwa ni ama ndugu za Rais au wa mkewe", Padri Karangwa alieleza.
"Sijaelewa vizuri jinsi hali hii ilivyoashiria kufikia mauaiji yaliyotokea", Willy alisema huku akionyesha sasa kuwa makini zaidi.
"Huku ndiko ninakokwenda. Hawa Akazu pamoja na familia ya Rais walifikia kujiita miungu wadogo. Walifanya kila walichotaka. Kuna habari za kuaminika kuwa kuna Mzungu mmoja rafiki yake sana na Rais ambaye alikuwa anawatengenezea fedha kwa maana ya kuchapisha na wao wanamlipa mazao kama kahawa kwa bei yake, na mazao mengine yoyote aliyohitaji; na pia kuna tetesi kuwa hata bangi ililimwa na watu hawa na kusambazwa na huyu Mzungu. Kusema kweli, hawa watu walitajirika kuzidi kiasi na wakajisahau kabisa. Ili kubaki katika hali hii kama nilivyosema mwanzo, ilibidi sasa wachochee ukabila. Walikuwa wameshafilisika kisiasa, uhali wa utawala ulikuwa hauna msimamo tena. Hivyo, kimbilio lilikuwa ni ukabila na kuhakikisha Wahutu wananufaika na utawala, na ilikuwa ni rahisi sana kuwachochea na kufanya lolote ambalo viongozi wao wa Kihutu walitaka wafanye. Uchochezi wa Wahutu ulizidi kuanzia mwaka 1988 baada ya kongamano la Watutsi lililofanyika Washington D.C Marekani na kuamua kuiondoa serikali tawala madarakani. Mkutano huo pia ulihuhudhuliwa na Wahutu ambao walikuwa wakipinga mwenendo wa serikali tawala. Haja ya wakimbizi wa Kitutsi kurudi nyumbani kwa njia yoyote ile ndiyo ilikuwa msukumo wa kongamano hili huku Marekani, kwani Rais alikuwa akieleza kuwa wakimbizi hawana haki tena ya kurudi Rwanda kwa kuwa nchi ilikuwa ndogo mno na isingeweza kuwapokea tena". Padri Karangwa alinyamaza kidogo na kuchukua glasi ya maji.
Padri Sibomana akatumia wakati huu kumkata kauli kidogo. akasema, "Padri alilisahau swala la wakimbizi wa Kibanyarwanda Uganda, maana hili lina uhusiano mkubwa mno na hali hii yote anayoieleza".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Bila shaka Padri Sibomana, nilikuwa bado niendelee huko ila kwanza nilitaka kuonyesha mshikamano wa Wahutu ulikuwaje", Padri Karangwa alijibu.
"Sawa Padri, endelea", Padri Sibomana aliafiki.
"Kama alivyo kumbusha Padri Sibomana, wakimbizi wengi walijiunga na jeshi la NRA la Uganda katika miaka ya themanini. Hao walimsaidia Rais wa sasa wa Uganda kuchukua madaraka. Kwa kawaida, wakimbizi mara kwa mara hujiingiza kiurahisi jeshini kuliko kukaa bure na hii vile vile huwapa tamaa ya kutafuta njia za kijeshi kurudi kwao. Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa wakimbizi wa Kibanyarwanda waliokuwa Uganda, wengi wao wakiwa Watutsi na Wahutu wachache. Makamanda wengi wan NRA walikuwa wakimbizi wa Kibanyarwanda. Baada ya kushika madaraka Uganda ubaguzi ulianza wa wakimbizi wa Kinyarwanda Uganda. Waliwapinga hasa waliokuwa wapinzani wa serikali na raia wa kawaida wa Kiganda waliona hawa wakimbizi kama wanaokuja kuwanyang`anya haki zao kwa vile walikuwa wakishika vyeo vya juu katika jeshi la NRA ambali sasa ndilo lililokuwa likitawala Uganda. Ilikuwa ni hali hii na nia ya kurudi kwao kwa hali yoyote sasa, iliyo ashiria kuzaliwa kwa RPF. Hivyo makamanda wa Kinyarwanda walikuwa NRA sasa waliamia RPF.
"Inasemekana Rais wa Uganda, ili asiwe na matatizo nyumbani kwake kwa sababu nilizozisema hapo juu, alikuwa msukumo mkubwa wa kuisaidia RPF ili wakimbizi hawa walazimishe kurudi kwao kwa kutumia nguvu za kijeshi. Kutokana na hali hii mnamo tarehe 1 oktoba 1990 watoto wa wakimbizi wa Kinyarwanda, ambao walikuwa wapiganaji wa NRA, walikusanyika kusini- magharibi mwa Uganda na siku hiyo ya tarehe moja wakaivamia Rwanda. Ingawa hawakufanikiwa, lakini nguvu yao ilifahamika na kusababisha kiwewe kwa utawala wa Rwanda, na hapa ndipo mipigano ya kuwaangamiza Watutsi wote na Wahutu waliokuwa wanaunga mkono jitihada za Watutsi ilipoanza kupangwa na Akazu. Kama nilivyosema hapo mwanzo ili uchochezi kwa Wahutu dhidi ya Watutsi upate kufanikiwa, kundi lililokuwa linafaidika na utawala huu liliunda jeshi lake lililoitwa Interahamwe. Interahamwe maana yake ni "wale wanaovamia na kupigana pamoja". Jeshi hili liliundwa toka sehemu mbali mbali nchi nzima na kufundishwa na kikosi maalumu cha Rais kataka kambi za Gabiro na Bigongwe, na wote waliochaguliwa walikuwa Wahutu isipokuwa kamanda wao alikuwa Mtutsi ambaye baba yake alikuwa amechukua kitambulisho cha Kihutu. Wengi wa Interahamwe walikuwa ni vijana ambao walikuwa hawana kazi, Wakipewa vinywaji na pesa wakifundishwa kuwachukia Watutsi na kufanya maasi ya aina yoyote ile tokea kubaka, kunyang`anya mpaka kuua. Wizara ya ulinzi ndiyo iliyotoa silaha na kutoa sehemu za kufanyia mafunzo ingawa Interahamwe ilibaki mali ya Akazu na cha tawala. Vilevile wakimbizi wa Kirundi nao walichukuliwa na kuingizwa katika jeshi hili Iterahamwe. Inasemekana kuwa hawa wakimbizi wa Kirundi, ambao ni Wahutu, walikuwa wakatili zaidi kuliko hata wenzao wa Rwanda. Wakuu wa Interahamwe hawakuishia hapo tu bali walienda mpaka Goma, Zaire, ambako nako walichukua askari wa kujiunga na Interahamwe. Wazaire waliochukuliwa ni wale wenye asili ya Kihutu lakini Wazaire wanye asili ya kitutsi kwa jina la Wabanyamulenge, wao walikataa kwani wao walikuwa wanaunga mkono harakati za RPF.
"Hawa Interahamwe walikuwa wengi kiasi gani?" Willy aliuliza.
"Hata kufikia tarehe 6 aprili na baada ya kifo cha Rais na mauaji kuanza inasemekana kwamba kila Mhutu sasa alikuwa Interahamwe, lakini Interahamwe waliochukua mafunzo haswa walikuwa wamefikia kiasi cha elfu kumi."
"Inasemekana yalifanyika mauaji mengi kwa silaha hafifu kama rungu, panga na kadhalika.Hii ni kwasababu haya marungu yaliweza kutengenezwa kienyeji na kwa urahisi au vipi?" Willy aliuliza.
"Hapana, marungu na mapanga haya yaliagizwa na kundi la Akazu kutoka China. marungu haya yalipendekezwa na Akazu kwani kila yalipotumiwa yalitoa maumivu ya ajabu kwa adui. Na inasemekana kuwa watu wengi walitoa pesa kununua kuuawa na risasi kuliko kustaimili kifo cha rungu. Marungu haya, kwa mfano yalianza kuingia Rwanda tokea januari 1993 yakipakuliwa toka Mombasa kupitia Nairobi na kuhifadhiwa kwenye maghala Kigali na Kibungo. Lakini, pamoja na marungu haya serikali ya Rwanda, kati ya mwaka 1992 na 1994, iliagiza silaha kubwa kubwa toka Ufaransa. Vile vile silaha zingine zilitoka Ulaya ya mashariki kupitia Zaire. Ufaransa, hata hivyo, ndiyo iliyokuwa mfadhili mkubwa wa siliha kwa serikali ya Rwanda. Inasemekana yule mzungu rafiki wa Rais na Akazu ndiye alipanga mipango yote ya uuzaji wa silaha kati ya Ufaransa na Rwanda. Inasemekanaq kuwa Mfaransa huyu ambaye pia alikuwa na uhusiano wa karibu na Ikulu ya Ufaransa alifikia kuwa mshauri mkuu wa Rais na ndiye aliyekuwa anamshauri Rais afanye nini, aseme nini na hata mauaji mengi inasemekana yalitokana na ushauri wake. Na kwa vile Rais na watu wake walitaka kutawala maisha, huyu mtu ambaye alikuwa akiwapa silaha za hali ya juu ili RPF isiweze kufurukuta, walimwonja kama Mungu, hata ndege ya Rais inasemekana ilitolewa kama zawadi nja mtu maarufu wa huko Ufaransa kwa mipango ya huyu mtu," Padri Karangwa alieleza.
"Kwa hiyo mauaji haya ya Rwanda yalipangwa, na siyo kwamba yalitokea tu kwa bahati mbaya, kwa kuchukizwa na kifo cha Rais?" Willy aliendelea kumdadisi Padri.
"Bila shaka. Hili kundi la Akazu lilikuwa na vyombo vya propaganda vingi ambavyo vilisaidia kuingiza chuki kati ya Wahutu na Watutsi ili iwe rahisi kuwatumia Wahutu katika mpango wao wa kuwamaliza Watutsi ili waweze kutawala milele. Magazeti kama Kangura na Stesheni ya Redio ya RTLM vilikuwa vinamilikiwa na kundi hili. Gazeti hili lilianzishwa katikati ya mwaka 1990 na liliungwa mkono na chama tawala pamoja na Rais na familia yake huku likiongozwa na rafiki wa Rais. Vilevile lilikuwa likifadhiliwa na huyo Mfaransa. Kazi kubwa, kama nilivyo sema hapo awali , ilikuwa ni kuchochea chuki kati ya Wahutu na Watutsi, huku radio hiyo na gazeti hilo vikiwahamasisha Wahutu wajiweke tayari kuwashambulia na kuwavamia Watutsi ambao kila wakati liliwasema kuwa wanataka kurudisha utawala wao wa kifalme, kila Mhutu amwue Mtutsi aliye karibu nae. Maneno makali kama haya ambayo yaliyotokea kila siku katika vyombo hivi yalikuwa ni chanzo kikubwa kwa mambo yaliyotokea kwanzia tarehe 6 Aprili alipouawa Rais," Padri Karangwa alieleza.
"Naona saa zimeenda, tumezungumza sana maana sasa yapata saa tatu na nusu usiku. Lakini kabla hatujamaliza Padri hasa nani alimuua Rais?" Willy aliuliza.
Sura ya Padri alibadilika na kisha akauliza, "Unataka maoni yangu binafsi?"
"Ndiyo kwani kwa maoni yako kutokana na ulivyonieleza unaweza kuhisi, na hisia zako zinaweza kuwa sahihi,willy alijibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Maoni yangu binafsi ni kwamba Rais aliuawa na Akazu. Ilipoonekana kuwa Rais alikuwa ameamua kutia sahihi ya makubaliano ya Arusha, hiki kikundi chake cha Akazu kikajua huu ndio utakuwa mwisho wao kufaidika. Hivyo wakaamua kumuua Rais ili katika machafuko hayo, waweze kupanga serikali mpya na kusimika utawala wao mpya ambao ungewahakikishia kuendelea kufaidi. Ukweli kuwa watu wake ndio waliomuua kwa kuogopa utawala wa kidemokrasia ambao ungefuata baada kutia saini makubaliano ya Arusha, ulijitokeza katika gazeti lao la Kangura, katika gazeti hilo ilitabiriwa kuwa Rais angeuawa na askari wa jeshi la Rwanda mnamo mwezi wa machi 1994 kufuatia kukubali kwake kusaini makubaliano ya Arusha. Gazeti hilo ambalo lilichapishwa mnamo mwezi wa Januari 1994 liliendelea kusema kuwa atakayemwua Rais atakuwa ni Mhutu. Na likasema kuwa waandishi wa gazeti hilo na rafiki zake na Rais huyo walimuasa asiweke saini makubaliano ya Arusha lakini ilionekana kuwa Rais alikuwa amebanwa sana na serikali zilizokuwa zikisuluisha mgogoro kiasi kuwa alikuwa hana msimamo. Hivyo, gazeti hilo katika toleo hilo, lilisema kuwa Rais atauawa na hapo ndipo vitatokea vita na damu nyingi itamwagika na jeshi la UNAMIR lisingeweza kufanya kitu. Lilizidi kumshauri Rais akatae kutia saini makubaliano hayo vinginevyo kifo chake hakitaepukika. Na yote yaliyoandikwa kwenye toleo hilo ndiyo yaliyotokea. Rais alipokubali tu kutia sahihi makubaliano ya Arusha basi hawa watu wake wakatimizi ahadi yao kwani wao ndio walioshika hatamu zote za serikali kuanzia utawala mpaka jeshini. Kwa hiyo, baada ya kusikia amekubali makubaliano ya Arusha basi walikiamurisha kikosi cha mizinga cha Kanombe, na ndege ya Rais ilipokuwa inakaribia kutua makombora matatu yalipigwa, mawili yakaipiga ndege; Rais na watu wote waliokuwemo, ikiwa pamoja na Rais wa Burundi, wakauawa. Akazu walipanga kuwa baada tu ya Rais kuuawa basi jeshi lao la Interahamwa lingeanza mauaji mara moja ya kuakikisha kuwa Watutsi wote pamoja na yeyote aliyekuwa anawaunga mkono anauawa. Mbinu hii ilikuwan ni kutaka RPF kukosa watu wa kuwaunga mkono ndani ya nchi hiyo na hivyo kushindwa vita. Lakina ya mungu mengi, mambo hayakwenda moja kwa moja kama walivyotarajia," Padri Karangwa alieleza na kuchukua glasi ya maji na kunywa.
"Lo maelezo yako yameniingia vizuri na nafkiri kutokana na ulivyoeleza kweli Rais aliuawa na mfumo wake mwenyewe wa kung`ang`ania madaraka kwani hata wakati alipokuwa amefikia kubadili mawazo yake, mfumo wake aliokuwa ameuweka haukumpa nafasi. Hivyo, ilibidi ummalize ili ubinafsi wa watu wake waliomzunguka uendelee,"m Willy alisema huku akiwa kama anajisemea mwenyewe.
"Watu ka nyinyi basi ndio mnaotakiwa mueneze habari hizi ili viongozi wengine wajue kuwa utawala wa mabavu, na wakung`ang`ania madaraka ili wewe tu ndio ufaidike una mwisho wake, na mwisho wake ni mbaya ata ufanyeje,"Padri Sibomana alidakia.
"Tutajitahidi kueleza ukweli huu," Willy alijibu.
"Nafikiri itakuwa vizuri kesho kama ukipata nafasi uje nikuonyeshe mauaji yalivyo fanyika, uone ukatili usio kifani,"Padri karangwa alimweleza Willy.
"Nitajitahidi, lakini kwa vile nina shughuli nyingi inabidi nirudi haraka Arusha. Kama sitaweza kufika maelezo yako yanatosha. Na kabla basi sijaondoka nikuulize swali."
"Uliza usiwe na wasiwasi, sisi tumefurahi kuwa nawe hapa wala hatuoni kama muda unaenda" Padri Karangwa alijibu.
"Unafikiri baada ya RPF kuchukua madaraka kutakuwa na maana na uelewano Rwanda? au niulize tena vingine baada ya haya mauaji ya kikatili dhidi ya Watutsi yalivyofanywa na Wahutu, unafikiri kutakuwa na uelewano kati ya makabila haya hata kama RPF itaweka utawala wa demokrasia?"
"Hilo swali gumu lakini nafikiri ndilo swali lenye maana kubwa sana. Uelewano kwa sasa utakuwa mgumu. Vidonda vya mauaji ya ndugu zao Kitutsi bado vibichi na kama binadamu lazima kutakuwa na kisasi, kwa hili tusijidanganye. Pili, baada ya RPF kuchukua madaraka maelfu ya Wahutu wamekimbia ni wakimbizi huko Tanzania, Zaire, na nchi zinginezo. Kati ya hawa waliokimbia na hasa waliokimbilia Zaire, ni wale Interahamwe na wanajeshi wa serikali ya zamani. Kwa vyovyote, hawa nao wataanza kujikusanya na kuunda tena jeshi la kuja kuvamia tena Rwanda, na Serikali ya sasa haita kubali. Hivyo, vita vitaendelea na itaendelea kwa muda mrefu kama jumuiya ya kimataifa itaendelea kulipa kisogo swala hili la Rwanda. Tatu, miongoni mwa wakimbizi wanaoumia ni wanawake na watoto, na watoto hawa taabu watakazozipata huko watakuwa wanaelezwa kuwa ni sababu ya Watutsi ambao wamewafukuza nchini mwao na hivyo kujenga chuki tena. Watoto wa Kitutsi vilevile watakuwa wanaelezwa ndugu yako fulani aliuawa na Wahutu; na kwa vile kila familia iliathirika chuki hii itazidi kujengeka maradufu. Mimi maoni yangu ni kwa serikali ya RPF isilipize kisasi. Wakimbizi wote warudishwe nyumbani. Wale ambao wanajulikana kabisa ndio waliusika na kuongoza mauaji haya ya kikatili, wakamatwe kokote duniani waliko na wafikishwe maakamani. Kama dunia hii isivyokuwa na usawa, wale wote walioongoza mauaji haya kwa vile wana pesa tayari wapo nchi za nje wanakula starehe. Wanaohangaika sasa ni wanawake na watoto; hii si sawa. Lazima hawa watu wakamatwe hasa kundi la Akazu, wote wakamatwe wafikishwe maakamani,"Padri Karangwa alimalizia huku sasa machozi yakimlengalenga.
"Kwa kweli, hali ya nchi yetu hii itayumba kwa muda mrefu. Wote wanachotegemea sasa ni serikali ya RPF iweze kuwahamasisha wananchi waweze kusameheana ili tujenge taifa jipya. Nakubaliana na Padri Karangwa kuwa ili tukio kama hili lisitokee tena, wote waliohusika na kitendo hiki wafikishwe mbele ya maakama wahukumiwe na adhabu kali itolewe ili kitu kama hiki kisitokee tena popote duniani, maana ni kitu cha kutisha ambacho kinafanya akili isikubali kuwa binadamu anaweza kuwa katili na mharibifu namna hii kama ilivyotutokea sisi hapa. Hapa Willy, dunia isinyamaze mpaka hapo wote waliohusika wameadhibiwa," Padri Sibomana alitoa maoni yake.
Huku akiinuka, Willy alishukuru na kusema, "kusema kweli sina maneno ya kuweza kueleza jinsi ninavyo shukuru kwani naweza kurudi Arusha kesho maana yote nimepata niliyotaka kujua kwenu na nimejifunza mengi, asante sana. Nipatapo nafasi nitawatembelea tena. Nikishindwa kuja kesho mara nyingine nitakuja kwa mapumziko. Asanteni sana, tena sana."
"Nasi tunashukuru sana kwani kuja kwako kumetufariji kumbe kuwa huko duniani kuna watu wanaoyajali matatizo yetu yaliyotupata. Asante sana," Padri Karangwa alimalizia, kisha wakamsindikiza Willy mpaka kwenye gari lake; akaondoka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
BIBIANE
Ilikuwa yapata saa nne usiku wakati Willy Gamba alipokuwa akielekea nyumbani kwa Col. Rwivanga, akitokea Centre Christus. Walikuwa wamekubaliana na Col. Rwivanga kuonana baada tu ya Willy kutoka kwa Mapadri. Wakati anakaribia kukata kona kuingia Barabara inayoingia sehemu ya Kimihurura ili aelekee nyumbani kwa Col. Rwivanga alipitwa na gari nyingine aina ya Landrover 110, lililokuwa likienda kasi sana na kama asingekuwa makini katika uendeshaji wangeweza kumgonga maana pamoja na kuonyesha ishara ya taa kuwa anahitaji kuingia kushoto lakini gari hilo lilipita kasi bila kujali ishara ya taa.
"Hawa wanajeshi ndio sababu hupata ajali mara kwa mara, uendeshaji wao ni wa ovyo sana", Willy alijisemea moyoni na kisha akakata kushoto kuelekea nyumbani kwa Col. Rwivanga.
"Endesha kwa tahadhali Felician, tungeweza kumgonga yule mtu ikaleta balaa hata kabla hatujaanza kazi. Kazi yetu ni kummaliza Willy Gamba na wala si kugonga magari ya watu ovyo", Xavier Nkubana alikaripia Felician.
Nkubana na wenzake waliwasili jioni ile mjini Kigali kwa ndege ya serikali ya Tanzania ambayo iliwasili na ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliofika kuchunguza tukio la kulipuliwa kwa ndege ya Tanzania iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni ya ndege ya Tanzaiar. Ndege hii iliwaleta maafisa kutoka idara ya usalama wa anga, mambo ya nje, polisi na waandishi wa habari. Nkubana na wenzake walifanyiwa mpango na kupanda ndege hii kama wafanyabiashara wa kinyarwanda waishio Tanzania walikuwa wakirudi nyumbani Rwanda kuangalia hali ya nchi ilivyo kwa wakati huu ili kama ikiwezekana waanzishe biashara tena kati ya Tanzania na Rwanda. Waliingia Rwanda bila tatizo lolote na kupokelewa vizuri na viongozi wa serikali ya Rwanda na kupelekwa kwenye Hoteli ya Des Mills Collines. Kwa vile walijulikana kama wafanyabiashara, baada ya kufikishwa hotelini waliachwa ili waendelee na mambo yao, na wale maofisa wa serikali ya Tanzania wakaanza kushugulikiwa na wenzao kuhusu mambo ya hotelina mambo mengine ya kiusalama.
Baada ya kuchukuwa vyumba na kuoga. Nkubana aliondoka na kuelekea nyumbani kwa Co. Gatabazi na kuwaacha wenzake wakipumzika, kwani ratiba yao ya kazi ilikuwa usiku ule ule. Ilikuwa yapata saa moja hivi Nkubana alipowasili nyumbani kwa Col. Gatabazi aliyekuwa akimsubiri.
"Karibu sana", Col. Gatabazi alimkumbatia Nkubana kwani walikuwa hawajaonana kwa muda mrefu.
"Asante, naona mambo mazuri", Nkubana alijibu.
"Mambo mazuri gani haya! Mambo yatakuwa mazuri baada ya sisi wenyewe kuchukuwa madaraka ya nchi hii. Kila siku nasikia uchungu moyoni kuona 'Inyenzi' inazidi kujiimalisha hapa. Lazima mambo yafanyike haraka kabla hawajajizatiti sawasawa, karibu ndani", Col. Gatabazi alijibu huku akiwa ameushikilia mkono wa Nkubana kisha akamwongoza kuelekea sebuleni.
"Utakunywa nini?", Col. Gatabazi alimuuliza.
"Nipe chai kama ipo".
"Tena na mimi sasa hivi nilikuwa nakunywa chai", Col. Gatabazi alijibu na kwenda kuchukuwa chupa ya chai na vikombe viwili vya chai, wakakaa mezani pale sebuleni.
"Karibu".
"Asante sana". Nkubana alichukua kikombe chenye chai na kuanza kunywa.
"Ehee, hamkupata tatizo lolote?".
"Wewe unacheza na mipango ya JKS nini?, atakapokuwa Rais wa Tanzania na wewe hapa mbona tutakula kuku mpaka tuchoke! Tumekuja kwa heshima zote na kupokelewa na 'Inyenzi', na kutupeleka mpaka hotelini. Wangeweza hata kutulipia hoteli lakini sisi tumekataa maana tumekuja kama wafanyabiashara hivyo ni vizuri kujitegemea", Nkubana alijibu.
"Vijana wako katika hali nzuri?".
"Wako na moto kama nini, maana wanataka kumaliza kazi usiku huuhuu, na baada ya hapa tunaelekea Bukavu tukasaidie kupanga mapambano dhidi ya 'Inyenzi', JKS ametueleza mipango yote nasi tumeafiki".
"Hiyo safi, lakini kwanza mambo ya hapa. Huyu Willy Gamba ni mtu hatari kabisa. Inabidi tumfanyie mkakati mzuri. Siyo mtu wa kawaida", Col. Gatabazi alieleza lakini kabla hajajendelea Nkubana alimkata kauli.
"Yaani huna maana sisi watu watano ambao ni sawa na jeshi zima la askari shupavu, bado una wasiwasi? Hivi umesahau kuwa sisi ni makomandoo, tupe mipango tujuwe yuko wapi, kazi ingine tuachie sisi wenyewe", Nkubana alijigamba.
"Imebidi nikutahadharishe kwanza, msije mkamwendea kwa pupa. Ni lazima tupange mipango mathubuti. Inabidi kwanza kueleza nyendo zake kutokana na upelelezi niliofanya toka mambo yaliyotokea juzi usiku", Col. Gatabazi alijibu.
"Sawa endele", Nkubana alijibu huku akionyesha kuwa Col. Gatabazi alikuwa anazidi kupoteza muda kwani anaamini hakuna mtu. Hata awe wa uwezo wa aaina gani asingeweza kutamba mbele ya kikosi chake.
Nkubana alikuwa kati ya askari waliopatiwa mafunzo ya kijeshi na kijasusi kwa pamoja. Alikuwa na cheo cha Meja Jeshini lakini aliingia hata katika kambi za RPF huko Uganda na kuchukuwa habari na ndiye ambaye mara nyingi aliifanya RPF isifanikiwe katika mashambulizi yake kwani yalijulikana mapema. Inasemekana mauaji yote yaliyofanywa kwa watu na wanajeshi waliokuwa wakitoa habari kwa RPF yalifanywa na yeye. Alikuwa jasiri na shupavu lakini uso wake kila siku utadhani wa padri hata namna yake ya kusema akiwa na watu wa kawaida. Pia inasemekana kuwa 'Akazu' walimchagua kufuatilia maofisa ambao baadaye waliwafundisha Intarahamwe, na kuwapa amri kumi ili wazieneze kwa Wahutu. Mhutu yeyote ambaye asingezifuata na kuzitekeleza basi auawe hapohapo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na hizi amri kumi za Wahutu zilikuwa kama ifuatavyo.
1. Kila Mhutu ajue kuwa mwanamke wa Kitutsi kokote aliko, yuko kwa manufaa ya watutsi. Kwa hiyo mtu yeyote atakayeoa, kufanya urafiki au kumwajiri mwanamke wa Kitutsi kama mfanyakazi wake au mkewe basi Mhutu huyo ni msaliti, lazima auawe.
2. Kila Mhutu ajue kuwa ni mwanamke wa Kihutu tu anjayefaa kama mke, kama rafiki na kama mfanyakazi wake ofisini.
3. Wanawake wote wa Kihutu lazima wewe imara na wawahamasishe waume zao, kaka zao na watoto wao wa kiume kumchukia Mtutsi.
4. Kila Mhutu lazima ajue kuwa Mtutsi yeyote si mwaminifu katika biashara. Hivyo, Mhutu anayefanya biashara na Mtutsi, anayewekeza fedha zake au za serikali katika kampuni za Kitutsi, anayekopesha ama kukopa kwa Mtutsi, anayewasaidia wafanyabiashara wa Kitutsi ni msaliti, anatakiwa kuuawa.
5. Kazi zote za juu katika siasa, utawala, uchumi, jeshi na usalama lazima wapewe Wahutu.
6. Katika sekta ya elimu (walimu, watoto wa shule na nguo), lazima wengi wawe Wahutu.
7. Jjeshi la Rwanda liwe kwa Wahutu tu. Na mwanajeshi haruhusiwi kuona Mtutsi.
8. Wahutu waache kuwaonea huruma Watutsi, unyama unyama tu dhidi ya Watutsi.
9. Wahutu popote walipo duniani lazima wawe na umoja kwa kila njia na wajaribu kuzima propaganda za Watutsi na kuungana katika kuwaangamiza Watutsi.
10. Mapinduzi ya kijani ya mwaka 1959 na itikadi za Kihutu lazima zifundishwe kwa kila Mhutu. Na Mhutu yeyote anayemwonea Mhutu mwenzake kwa kueneza itikadi hizi basi huyo Mhutu auawe, maana ni msaliti.
Kwa kutumia askari wa vikosi alivyovifundisha Nkubana alihakikisha kuwa amri hizi zinatekelezwa na zinachochea chuki ya Wahutu dhidi ya Watutsi kama alivyoagizwa na Akazu.
Huyu ndiye Nkubana, mtu jasiri, aliyehitimu katika shule mbalimbali za kijeshi, kijasusi na kikomandoo ulimwenguni, lakini mafunzo yake yote yalikuwa ya dhamira moja tu, ya kuhakikisha kuwa utawala wa Kihutu uliokuwa madarakani unaendelea kutawala milele na milele kwa njia moja tu kuhakikisha Watutsi wote wanafyekwa ili wasiwepo tena duniani. Hivyo, kwake mtu yeyote aliyemuunga mkono Mtutsi lazima afe na yeyote aliyesaidia Mhutu basi yeye Nkubana alimsaidia kwa lolote. Hivyo ndivyo walivyoweza kuelewana na kundi la Jean kwani lilikuwa upande wa Akazu. Na habari za Willy Gamba kuwa alikuwa anajaribu kuharibu mipango ya Wahutu kurudi madarakani, zilimuudhi sana na kusikia hasira isiyo kifani dhidi ya Willy Gamba.
"Lazima usiku huu huu afe", Nkubana alijishitukia amesema kwa hasira hata Col. Gatabazi aliyekuwa ameanza kueleza mipango akashituka. Akashtuka.
"Haya sasa endelea, huyu mtu ameniudhi sanasana, tayari hukumu yake ya kifo imeshapita".
Col. Gatabazi ilibidi aanze upya kumpa mipango ya usiku ule kama walivyokuwa wamepanga na Jean na JKS.
Willy Gamba alimkuta Col. Rwivanga anakula chakula. Alipomuona Willy alionekana kufurahia "Nimekusubiri sana mpaka nikaamua bora niendelee na chakula maana ni zaidi ya saa nne sasa na unajuwa mimi nakula mara moja tu kwa siku, njaa ilikuwa inauma sana", Col. Rwivanga alijitetea.
"Usijali Kamanda", Willy alijibu huku akielekea jikoni kuchukua sahani na kisha akaketi kwenye meza pamoja na Col. Rwivanga na kupakuwa chakula.
"Hiki chote kilikuwa chako peke yako", Willy alimkejeli Col. Rwivanga.
"Hapana, nilijuwa tu utanikuta nakula", Col. Rwivanga alijibu huku akicheka. Willy alichota kijiko cha kwanza na kukitia mdomoni, chakula kilikuwa wali na mchemsho wa nyama.
"Lo, mpishi ni wewe?".
"Kwani vipi?".
"Kitamu sana chakula hiki", Willy alijibu.
"Wapi, na wewe una njaa vilevile, upishi wangu mimi ni mchemsho tu".
"Hapana si njaa ila wali umepikwa vizuri na nyama ya mchemsho, napenda sana mimi", Willy alieleza.
"Ehe vipi huko, umewakuta?".
"Bwana nimewakuta wale mapadri na nimewekwa shule hasa, na sasa hivi naijua historia ya utawala wa nchi vizuri sana kuanzia kabla ya ukoloni".
"Wacha bwana".
"Nakuambia wale mapadri wanaijua nchi hii kuliko viganja vya mikono yao", Willy alimweleza Col. Rwivanga, kisha akamgusia kwa muhtsari mambo muhimu aliyoelezwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kumbe hili swala la Akazu hata hawa wazee wanalifahamu sana?", Col. Rwivanga aliuliza baada ya maelezo ya Willy.
"Sana, na wamesema bila hawa watu kukamatwa hakuwezi kuwa na amani katika nchi hii".
"Hilo ni kweli kabisa na sisi tunalijua na ninafikiri ndio walio nyuma ya hili swala la kutaka kukuua maana hawa watu wana mahusiano dunia nzima na pesa nyingi. Hivyo, tunajua wanajipanga kuja kutuhujumu, hilo tunajua. Ila hatujui kwa sasa hivi wanafanya shughuli zao kutoka wapi. Nia yetu imekuwa ni kuimarisha serikali yetu, halafu ndipo tuangalie habari yao", Col. Rwivanga alieleza.
"Ni sawa, lakini mimi nafikiri jambo hili mgelishughulikia sasa hivi wakati bado nao wamechanganyikiwa, lakini mkisubiri watakusanya nguvu halafu itakuwa shida tena", Willy alishauri.
"Kutokana na matokeo ya siku hizi mbili nasi tumeshituka sana, maana inaonekana hawa watu bado wana watu ndani ya serikali yetu na wameanza kutuhujumu. Kama unavyosema, nasi tumeamua kulishughulikia mara moja swala hili na tutakuwa na mkutano na makamanda wote wa jeshi pamoja na baraza la mawaziri kesho saa moja na nusu asubuhi", Col. Rwivanga alieleza.
"Hivyo itakuwa vizuri. Ingawaje mimi kazi iliyonileta haikuwa ya mapambano, lakini kwa sababu wao ndio wamenianza na mimi naomba ruksa yako unilinde mbele ya wakubwa wako, kwani nataka nami kwa kiasi fulani nijuwe habari ya watu hawa na vipi wameamua kutaka kuniangamiza. La maana hasa nataka nijuwe nani hasa anahusika na kutaka kuniua mimi. Hilo Col. Rwivanga ningependa sana unipe hiyo nafasi nifanye kazi yangu", Willy alijieleza.
"Ni sawa lakini tungeomba na sisi utufahamishe kila hatua unachofanya ili tuweze kukusaidia itakapobidi kwani ukweli ni kuwa kazi hii ni yetu na wala si yako", Col. Rwivanga alijibu.
"Asante Col. Rwivanga. Vipi yule msichana wa jana usiku, Bibiane umepata habari zake?".
"Ahaa, ndio nilikuwa nakusubiri nikueleze. Hivi usingewahi ungenikuta nimeshaenda kumfuata. Huyu msichana inasemekana ni mkalimani, anajuwa lugha kama nane hivi na amekuwa akifanya kazi serikalini kama mkalimani hivyo, alikuwa akisafiri na Rais au mawaziri ama maafisa wakubwa wa serikali wanaposafiri nje ya nchi na vilevile ndiye aliyekuwa mkalimani wa serikali kama wageni wasiojuwa kifaransa wakija nchini hapa. Inasemekana wakati wa mauaji yeye hakuwepo. Alikuwa Nairobi, lakini ni kati ya watu wa kwanza kabisa kurudi na amekaa katika nyumba yake aliyokuwa akiishi toka zamani mtaa uleule wa Silas Biniga, lakini nyumba ya nne mbele kwenye kona watu wamekuwa hawana wasiwasi nae kwani inasemekana ana asili ya Kitutsi ingawa ni chotara na uzuri wake watu wengi wameuchukulia tu kuwa huenda ni chakula ya wazee. Kwa hivyo hakuna ambaye amediliki kumgusa. Hivyo nataka nikajuwe habari zake", Col. Rwivanga alieleza.
"Hapana, usiende wewe, maana wewe ni afisa wa ngazi za juu na unajulikana hapa la pili wewe ni mwanajeshi. Kazi hii ni ya mpelelezi kama mimi. Tatu, nina kisasi naye. Naomba uniachie, usiku huu lazima nitapambana naye kama bado yuko hapa mjini na nitakujulisha habari zake baadae".
"Sawa Willy, kazi kwako, mzee naye alinieleza ndio zako hizo ikibidi msichana au mrembo".
"Zamani siyo sasa, sasa nimestaafu maana nimeoa lakini kwa msichana kama yule ambaye hatishiki na mtu kuuawa, nataka mimi mwenyewe nijuwe habari zake. Habari ulizonazo ni kwamba bado yuko mjini?".
"Jioni hii ameonekana akiendesha gari lake aina ya MB 190E. Na hilo ni gari lake hata kabla ya mauaji na kabla sisi hatujaingia hapa. La ajabu si sisi wala si Intarahamwe aliyegusa gari lake, ni jambo la kushangaza na limefanya nitaka kujuwa huyu binti vipi mambo yake".
"Basi niachie maMBO yake utayapata. Si bure huyU binti ni mtu hatari, na hatari sana".
Baada ya Col. Gatabazi kumwelezea mipango yote kama walivyokuwa wamepanga na Jean, Nkubana aliomba gari ili akawachukuwe wenzake na kuanza kazi ya kumsaka Willy. Col. Gatabazi aliwapa gari aina ya Landrover 110 ya Jeshi ambayo hutumika kwa ajili ya wageni wa Serikali. Kwa sababu ya kazi maalum iliyokuwa ikiwakabili, kutokana na unyeti wa kazi hiyo, Col. Gatabazi aliwaachia gari hilo waendeshe wenyewe. Nkubana alikwenda, moja kwa moja akawaamsha wenzake, baada ya mazoezi makali, walioga na kupata chakula pale hotelini, kisha wakaanza kazi ya kupeleleza habari za Willy Gamba.
Kutokana na maelezo waliyokuwa wamepewa na Col. Gatabazi, mara moja walijua kuwa Willy yuko Meridien Hoteli, mara baada ya kupata namba ya chumba chake cha kulala waliamua kwanza wakafanye shughuli nyingine ili wasubiri wakati mzuri wa kupambana na Willy Gamba ambaye pia walikuwa wakimhofia kwa kiasi fulani.
Baada ya kupanga vyema mipango yao ya kuhakikisha wanamuua Willy Gamba usiku huo. Walirudi hotelini wakapata kinywaji kidogo kwa ajili ya kujiweka safi. Ilipotimia saa nne hivi usiku wakaamua kwenda kwa wote kwa Col. Gatabazi kwa ajili ya mikakati ya ziada. Ni wakati huo walipokuwa wakielekea kwa Col. Gatabazi ndipo walipokaribia kuligonga gari la Willy Gamba bila wao kujuwa kuwa ndiye mtu anayepanga kumuangamiza usiku huo.
Kwa kasi ileile, gari hilo liliingia nyumbani kwa Col. Gatabazi, aliyekuwa nje ya nyumba yake akitafakari jinsi Willy alivyokuwa akiwanyima usingizi. alipowaona akawapokea kwa tabasamu kisha akawaongoza hadi kwenye sebule ya nyumba yake.
"Vipi mmepata habari zozote kuhusu Willy Gamba?", Col. Gatabazi aliwauliza baada tu ya kuketi kwenye makochi.
"Habari za Willy zote tunazo, huyo tutaanza biashara yake, atakuwa marehemu baada ya saa sita usiku", Nkubana alijibu kwa majidai na kujiamini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nasema tena lazima muwe makini sana, huyo mtu ni hatari sana, na amri ni kwamba mara hii isishindikane, akionekana tu ua mara moja", Col. Gatabazi alisisitiza.
"Col. tafadhali usitutishe na huyo mtu wako, atakuwa hatari gari mbele yetu! Vipi una matatizo nini Col. Gatabazi?", Nkubana alijibu kwa mshangao huku vijana wake wote wanne wakicheka kwa dharau.
"Acha wasiwasi mzee, kazi ya Willy hesabu imeisha, amezoea kucheza na wafanzi leo atakutana na waalimu wa kazi", Felician alimhakikishia Col. Gatabazi.
"Ehe, Bibiane umemtaarifu kuwa tutakwenda nyumbani kwake leo?", Nkubana aliuliza.
"Bibiane ana taarifa zenu, na wakati ndio huu, twendeni basi mara moja, hiyo gari acheni hapa maana anakaa ileile nyumba yake", Col. Gatabazi alijibu.
"Ahaa, kweli gari tuache tu hapa, tutalipitia wakati wa kwenda mjini", Felician alijibu.
"Haya twendeni anatusubiri, lakini mjuwe kutokana na mipango ilivyo mimi nitawaacha pale nyinyi mtaendelea nae", Col. Gatabazi aliwaelza.
"Sawa hamna tabu", wote walijibu kwa pamoja na kuondoka kuelekea kwa Bibiane.
Wakati Willy anafika nyumbani kwa Bibiane. Col. Gatabazi alikuwa akifunguliwa lango la mbele nyumba hiyo akatoka na kuondoka akihofia matatizo aliyokumbana nayo kwa Luteni Biniga. Willy alichukuwa hadhari kubwa sana maana alichukuwa vifaa vya kazi si mchezo. Kwa vile nyumba ya Bibiane ilikuwa kwenye kona ya barabara mbili, Willy alibana kwenye kona moja na kuchungulia mbele ya nyumba na kuona lango likifunguliwa. Alimuona mtu mmoja akitoka na kukatisha barabara na kuelekea kwenye uchochoro na kutokomea. Willy alirudi nyuma kidogo na kuhisi kuwa sehemu ile ndiyo ilikuwa nyuma ya nyumba hii. Kwa hadhari sana alikwea ukuta uliozungishiwa vyuma vilivyochongoka juu. Kwa vile Col. Rwivanga alimweleza kuhusu hilo. Willy alikuwa amejitayarisha vizuri kabisa kwa lolote. Alikwea na kuchungulia ndani, baada ya kuangaza vizuri macho yake aliweza kuona kivuli cha mtu amebana kwenye ukuta wa nyumba hii karibu na upande wa pale alipokuwa yeye. Mtu huyu alikuwa amebeba bunduki kubwa. Hivyo, Willy alihisi ni mlinzi wa pale nyumbani.
Baada ya muda kidogo, Willy alimuona mtu mwingine anakuja akitokea upande wa mbele kuja upande huu ambao huyu mwingine alikuwa amebana. Willy alijining'iniza juu ya ukuta kwa nje ili asionekane huku macho yake yakiwa usawa wa ukuta. Yule mtu alikuja moja kwa moja mpaka usawa wa yule mwingine alipokuwa amesimama.
"Unataka sigara?", yule aliyekuja eneo hilo alimuuliza mwenzake.
"Sitaki, hao jamaa ndani si wamalize mambo yao haraka ili waondoke na sisi twende zetu, maana hapa tunapoteza muda na huku kazi yenyewe bado", yule wa pili ajibu.
"Mbona kama una wasiwasi, vipi unaogopa?".
"Kwanini nisiogope, mimi si binadamu bwana?".
"Acha woga wewe, wajuwa Kaisari alisema watu waoga mara nyingi hufa kabla ya tarehe ya vifo vyao kufika, komaa mtoto wa kiume", mwenzake alisema kwa kujiamini.
"Bwana, hebu nenda kalinde sehemu yako na umwambie huyo Nkubana aharakishe kutoka sehemu hii".
Baada ya kuelezwa, yule mtu aliyekuja sehemu hii kutoka mbele aliondoka kimyakimya kurudi kule alikotoka huku mwenzake akimsindikiza. Willy akatumia nafasi hiyo. Kama tumbili aliukwea ule ukuta haraka sana. Kufumba na kufumbua akaruka juu ya vile vyuma na kujitosa ndani bila hata kusababisha kishindo na kujibanza kwenye ukuta. Kwa vile Willy alikuwa amevaa nguo nyeusi pale alipokuwa amejibanza ilibidi umsogelee karibu sana ndipo uweze kumtambua maana upande huu wa nyumba hapakuwa na mwanga. Mara akamsikia yule mlinzi akirudi upande wake, kutokana na mazungumzo aliyokuwa ameyasikia alihisi hawa nao bila shaka walikuwa kundi lilelile kama alilopambana nalo kwa Luteni Biniga. Bila shaka walikuwa wamekuja kwa malipo kwa huyu mwanamke. Willy alijitayarisha na kujibanza kwenye ukuta utafikiri buibui. Yule mtu alikuja akinyata taratibu utafikiri alikuwa amehisi kitu. Willy alikuwa amebana kwenye kona kabisa ya upande wa pili wa nyumba. Huyu mtu alipofika hapo tu, kama Simba anapomrukia Swala, Willy alimtia kabali kwa nguvu zake zote. Yule mtu hakuweza hata kuguna maana kabali ile ilikuwa kali, na huku akitumia utaalam kumuua kimyakimya kwa kumnyonga, Willy alimuua yule mtu. Kisha, alimvuta mpaka kwenye ua wa nyumba na kumvua shati, akavua lake na kuvaa la yule mtu kwani ukubwa wa mwili na urefu walikuwa wanalingana. Akatwaa silaha yake ya AK 47 'Machinegun' ya Kirusi na kuelekea mbele.
Alipofika kwenye kona ya mbele, Willy alimuona yule mtu mwingine akichungulia dirishani, si mbali na aliposimama Willy. Willy alikohoa kidogo na yule mtu akageuka kuangalia. Alionyesha ishala ya kumwita. Na yule, akijuwa fika kuwa alikuwa mwenzake, alikuja haraka bila hadhari. Alipokaribia, na kwa ajili ya giza aliamini ni yule mwenzake, alianza kusema, "Huko ndani naona mambo yanaa...", kabla hajamalizia sentesi yake, Willy alimrukia na kumpiga karate ya shingo na kumuua palepale. Alianguka chini kwa kishindo, na Willy alipomrukia pale chini akammaliza. Baada ya Willy kumkagua alimkuta na Bastola mbili, moja yenye kiwambo cha sauti na nyingine ya kawaida. Vilevile alimkuta na kisu ambacho ukikibonyeza kinachomoka na kutoka urefu wa nchi tisa. Kile kisu kilikuwa silaha hatari sana ikitokea watu wanapigana huku mmeshikana. Willy alijihisi mtu mwenye bahati kwani silaha kama hii kama ingebidi kumenyana bila kujuwa kuwa mtu anayo anakuondoa duniani haraka sana.
Sasa Willy alikimbia mbele kuangalia kama kulikuwa na mtu mwingine, lakini hakukuwa na kitu. Alipozunguka upande mwingine tena hakuna kitu. Kisha akachukua dakika chache kuhakikisha kuwa hakuna hatari nyingine, na alipohakikisha ndipo alipokwenda pale dirishani alipokuwa anachungulia yule mtu wa pili. Dirisha lile lilikuwa sebuleni na lilikuwa wazi kidiogo. Pazia la dirisha lilikuwa limerudishiwa kidogo kiasi kwamba ungeweza kuona ndani na kusikia maneno yote yaliyokuwa yanazungumzwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Willy alishangazwa kuwaona wanaume watatu na mwanamke mmoja ambaye mara moja alimtambua kwani alikuwa Bibiane. Hawa wanaume wote walikuwa wametoa Bastola zao wakizungumza na yule mwanamke. Wawili walikuwa wamesimama na mmoja ameketi kwenye kiti kilichokuwa kinaangaliana uso kwa uso na alichoketi Bibiane.
"Nakwambia hivi, sisi tumetumwa kuja kukuua na huyo huyo bwanako Jean. Faida yako kwake imesisha sasa wewe ni mzigo na yeye hataki kubeba mzigo", yule aliyeketi alimweleza yule mwanamke huku akionyesha kwenye sura yake maudhi na usongo wa ajabu.
"Wewe unatania. Jean! hawezi kusema hivyo. Kwa yote niliyomtendea na jinsi tunavyopendana, Xavier sema jingine kama wewe na Col. Gatabazi mmeamua kuniua basi niuweni, msimsingizie Jean, Jean ni wangu wa kufa na kuzikana", Bibiane alijibu huku akionyesha sura ya hofu maana aliwajuwa hawa jamaa ni wauaji.
"Wanawake ni watu wa ajabu. Epa", yule mtu ambaye Bibiane alimwita Xavier alimwita mmoja wa wale waliosimama.
"Eee", yule mtu alijibu kwa woga vilevile.
"Siku zote nakwambia wanawake ni wajinga, wewe huamini. Huyu anafikiri eti Jean alikuwa anampenda, Jean alikuwa anamtumia tu kama chombo. Kwanza alikuwa anakutumia kwa mambo yake ya kazi zake za kumwingizia pesa na pili, anapokuwa huku Afrika alikuwa akijisaidia kutimiza haja zake za kimwili; hata siku moja hajawahi kukupenda. Pale tu wewe na Col. Gatabazi mlipomweleza kuwa wewe umemwona Willy Gamba na Willy Gamba kukuona mara moja alijuwa Willy Gamba atakutafuta na akikupata utatoa siri, na ukitoa siri si ndiyo mambo yetu yameisha! kwa hiyo, mara moja ametoa hukumu ya kifo kwako na sisi tumekuja kutekeleza amri. Kwa kweli ni uhalibifu kwa kiumbe kizuri kama wewe kuuawa, lakini wewe sasa ni mzigo kwetu nasi hatubebi mzigo," Xavier alieleza.
Kwa maelezo haya Bibiane alijua kweli hukumu imetoka kwa Jean na huo ndio ulikuwa mwisho wake. Pamoja na ujuzi wake wote wa kupigana hakuthubutu mbele ya Xavier na wenzake kwani aliwajuwa vizuri, walikuwa wabaya mara kumi yake, na alijuwa kuwa hao hawabembelezeki hivyo, alikata tamaa na hasira zikampanda dhidi na Jean na machozi yakaanza kumtoka.
"Ukionana naye mwambie atakufa kifo kibaya sana. Nami naamini kuwa huyo Willy Gamba anayemuogopa kweli ndiye atakayenilipia kisasi", Bibiane alisema huku akitetemeka kwa hasira.
Xavier alisimama na kurudisha kiti chake nyuma. Bibiane naye akataka kusimama. "Hapana, kaa hapohapo, usilete ujanja hapa. Huyo Willy baada ya muda si mrefu mtaonana ahera, nasikia huko watu huonana tena. Hamtapishana zaidi ya masaa mawili na yeye atakuwa marehemu kama wewe".
Willy, ambaye alikuwa anasikia na kuona yote haya akiwa dirishani, alipoangalia usoni mwa yule aliyeitwa Epa, akajuwa huyu ndiye akayemuua Bibiane. Aliangalia nafasi aliyokuwa, akajuwa angeweza kumpiga risasi Epa na yule mwingine, lakini si Xavier. Kwa vyovyote Xavier angemmaliza Bibiane, lakini hakukuwa na njia. Hawa walikuwa ni wauaji wataalam, tena huenda wa kulipwa. Hivyo, ilikuwa ni afadhali kwake kupambana na mmoja kuliko watatu na kwa maajabu ya Mungu angeweza kumponyesha Bibiane ambaye akili yake ilimweleza kuwa angeweza kuwa mtu muhimu kwake.
Xavier alimkonyeza Epa. Yeye akavuta kiti na kuanza kugeuka. Bibiane akafumba macho, lakini kabla Epa hajafyatua risasi, palepale Willy akiwa dirishani na mikono yake yote ikiwa na Bastola, alimpiga risasi ya kichwa Epa na yule mwingine kifuani, na Bibiane akajirusha nyuma ya kiti, Nkubana kama umeme akamimina risasi dirishani. Lakini Willy alikuwa tayari amejitupa chini na kujiviringisha na kisha kuchukua AK 47 akamimina risasi kama hamsini hivi kumtia kiwewe Nkubana. Haya mambo yote yalitokea haraka sana kama kufumba na kufumbua. Nkubana alipoangalia akajuwa Epa na Karekezi walikuwa wamekufa na hakujuwa wamezungukwa na watu wangapi. Alijirusha kwenye dirisha upande wa pili ambalo lilikuwa la kioo kitupu na kuangukia nje na kisha kujiviringisha tena. Bibiane alichukua Bastola iliyodondoka kutoka kwa Epa na kujaribu kumpata Xavier lakini naye alijitosa nje akaurukia ukuta wa mbele kwa nanma ya ajabu na kuangukia uapnde wa barabarani. Willy alipokimbia upande ule wa pili ili kumuwahi Nkubana alikuwa amechelewa, Xavier naye alikuwa ndio anaishia baada ya kuruka ule ukuta.
Bibiane alipoinuka pale alipokuwa amejitupa kumfuata Xaviar akajikuta anaangalia kwenye mdomo wa AK 47.
"Tupa silaha yako mama, uko chini ya ulinzi", Willy alimweleza Bibiane.
"Aheri ya Musa kuliko ya Firauni, Bila shaka wewe ni Willy Gamba".
"Naamini wewe ni Bibiane".
Willy alimshika mkono Bibiane na bila hata kumwelezana wanaelekea wapi, wakakimbia kwa tahadhari kuwa kutoka eneo hilo kabla askari na watu wengine hawajafika kuangalia kilichotokea hapo kwani mlio wa risasi za Ak 47 ulikuwa umetikisa eneo hilo na kusikika vibaya sana wakati huo wa usiku
NGUVU YA RUSHWA
Nkubana, huku damu zikimtoka, alikimbia moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Col. Gatabazi. Alipolisukuma lango la mbele alikuta likiwa wazi. Akaingia ndani, moja kwa moja kwenye mlango wa mbele ambao ulikuwa umefungwa. Aligonga kwa nguvu mpaka Col. Gatabazi aliyekuwa anaoga, alitoka haraka huku akiwa amejifunga taulo na bastola mkononi. "Nini", aliuliza kwa shauku baada ya kuona hali aliyokuwanayo Nkubana.
"Vaa tuondoke hapa, mambo yameharibika.
"Nini?", Col. Gatabazi aliuliza tena.
"Nakwambia vaa twende, mambo yameharibika", Nkubana alimjibu huku akielekea sebuleni, akafungua friji akatoa maji baridi na kunywa huku Col. Gatabazi akimwangalia kwa mshangao.
"Huyu mtu wako ni mchawi. Kawaua vijana wangu wote na sasa yuko na Bibiane. Kwa kuwa ilikuwa tumuue Bibiane, sasa atakuwa upande wa Willy Gamba. Hivyo, lazima tayari mambo yako yataelezwa, na Jeshi la RPF litakuwa hapa sasa hivi. Lililopo tuondoke hapa tufuate majeshi yetu Kihumba".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hebu nieleze vizuri imekuwaje, maana siamini kabisa mtu mmoja kufanya kazi kubwa namna hiyo, tena kwa watu wenye uwezo mkubwa kama wewe?", Col. Gatabazi aliuliza kwa hofu huku akielekea chumbani kujitayarisha kwa ajili ya kuondoka eneo hilo. Nkubana alimweleza kila jambo lilivyotokea kwa Bibiane na jinsi alivyopoteza vijana wake.
Willy Gamba akifuatana na Bibiane usiku huo, huku mkononi mwake ameshika bunduki kubwa aina ya AK 47, walitembea kwa tahadhari kubwa kuelekea nyumbani kwa Col. Rwivanga. Walipofika hawakumkuta na nyumba yake ikiwa imefungwa. Kwa vile Willy alikuwa amepewa ufunguo wa ziada, walikuwa wameamua kwa ajili ya swala la kiusalama Willy awe analala pale, Alifungua mlango na kumvuta Bibiane ndani. Aliwasha taa ya sebuleni na kumsukumia Bibiane kwenye kochi.
Kwa mara ya kwanza ndipo Willy alipomwangalia Bibiane vizuri. Alistaajabu kuona kiumbe kizuri kama hiki kilivyojiingiza kwenye vitendo vya ugaidi wa ajabu. Hakika huyu msichana alikuwa mzuri. Ukisikia mrembo, urembo hio huu. Willy katika maisha yake alishawaona wasichana warembo lakini huyu alikuwa msichana mrembo kwelikweli.
"Asante kwa kuniokoa", Bibiane alimshukuru Willy Gamba huku akiwa amelegeza macho yake na kuonyesha tabasamu la aina yake mbele ya Willy ambaye alikaa kimya akimwangalia bila kujibu.
"Sasa niko upande wako, usipate taabu kunilinda, kwa jinsi ulivyookoa maisha yangu sasa nifanye vyovyote upendavyo", Willy kwa kumwangalia Bibiane machoni aliamini kuwa anasema ukweli.
"Nenda kaoge", Willy alimweleza Bibiane huku akielekea kwenye chumba alichokuwa akilala. Bibiane aliinuka taratibu na kumfuata Willy. Chumba alichokuwa akilala kilikuwa na maliwato ya ndani. Hivyo, alimuonyesha ishara Bibiane alifungua mlango na kuingia ndani.
Wakati Bibiane anaoga, Willy aliingia jikoni na kutayarisha kahawa. Alipoangalia saa yake ilikuwa yapata usiku wa manane. Alishangaa kwa nini Col. Rwivanga alikuwa hajarejea, akajiuliza ameelekea wapi wakati huo.
Simu ilipoita Jean alikuwa amelala. JKS alikuwa amemweleza kuwa vijana walikuwa wamefika salama na kazi ya kumsaka na kumuua Willy Gamba ilikuwa ifanyike usiku ule. Alikuwa amefikiria jinsi Bibiane angeshangaa sana baada ya kuelezwa kuwa Jean ndiye aliyetoa amri ya yeye kumuua. Jean alikuwa mtu aliyefurahia uovu, alikuwa mtu katili afadhali ya mnyama. Alifurahi kusikia mtu akipata maumivu, na hapo ndipo roho yake ilipopata faraja. Pamoja na miaka yoye sita aliyokaa na Bibiane, utafikiri walikuwa mtu na mke wake, yaani mume na mke, bado alipomweleza Col. Gatabazi kuwa lazima Bibiane auawe moyoni mwake hakusikia masikitiko. Kilichomfurahisha na kumridhisha ilikuwa ni pesa na nguvu ya pesa, na si mapenzi. Jean aliabudu pesa kwani aliamini kuwa pesa ndizo zilizompatia uwezo alionao duniani.
Kwa kutumia pesa, Jean aliweza kuwakamata wakuu wa nchi nyingi duniani, hasa katika Afrika na Asia, lakini vilevile viongozi wa ngazi za juu katika serikali za nchi za Ulaya. Alipata kila alichokitaka kwa kutumia pesa. Hivyo, simu ilipolia alijua analetewa habari njema za kuuawa kwa Bibiane na Willy Gamba maana alikuwa amesema alikuwa amesema wakishauawa aelezwe. Kila alipopewa taarifa ya kuuawa kwa mtu alipata faraja ndani ya moyo wake, Ndio sababu maelfu ya Watutsi walipouawa alisikia raha isiyo kifani. Hakika mtu huyu alikuwa mgonjwa, tena mgonjwa sana!.
"Jean", aliitikia kwenye simu.
"Col. Gatabazi hapa".
"Sema Col. Gatabazi".
"Kazi imeharibika".
"Nini?".
"Kazi imeharibika. Vijana wote wameuawa. Bibiane yuko hai na ameokolewa na Willy Gamba. mimi na Nkubana tunaondoka kwenda Kibunda, hatuna muda maana wakati wowote wataanza kutusaka, afadhari tuyaandae majeshi yetu tayari kwa vita", Col. Gatabazi alimwambia Jean.
"Ilikuwaje", Jean aliuliza kwa sauti ya kukata tamaa. Col. Gatabazi alimweleza kwa ufupi kama Nkubazi alivyomweleza.
"Basi tuonane kesho Goma, saa tisa mchana nitakuwa huko, natarajiwa kuja na ndege yangu, lakini nitampitia rafiki yetu Kinshasa", Jean alieleza na kukata simu kabla hata Col. Gatabazi hajajibu kitu.
Jean alipokata simu ya Col. Gatabazi, alitumia muda huo kupiga simu Zambia, Zaire, Afrika Kusini, Angola, Kenya na kumalizia Tanzania.
"Umenipata JKS?", Jean alimuuliza JKS baada ya kumweleza yote yaliyotokea na maelekezo mengine huku JKS akipatwa na shinikizo la damu.
"Nimekupata", JKS alijibu kwa sauti ya kutetemeka.
Bibiane alipomaliza kuoga alimkuta Willy amemtengea kikombe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kahawa au chai?"
"Kahawa."
Willy alimmiminia kahawa na alipotaka kumwekea sukari Bibiane alikataa.
"Bila sukari," alisema.
Kwa mara ya kwanza vilevile Bibiane alimuangalia Willy vizuri na kumuona mwanaume mzuri sana, na alipofikiria namna alivyowasambaratisha akina Xavier na kundi lao, mwili wake mara moja ulisisimuka. Halafu, palepale akamfikiria Jean na jinsi alivyompenda na kumfanyia kila kitu lakini akaamua kumuua. Hasira ilimpanda sana, na akaapa kiroho kuwa kwa vile yupo hai atalipiza kisasi.
"Unafikiri nini?" Willy alimwuliza Bibiane.
"Ahera."
"Umeshapona sasa?".
"Xavier alisema mimi na wewe tutaonana ahera baada ya masaa machache, akili yangu inafikiri huenda tupo ahera." wote walicheka.
"Uko tayari kuzungumza lolote," Willy alimuuliza Bibiane huku sauti yake ikiwa imebadilika ghafla na kuwa sauti yenye uzito fulani.
"Niko tayari, nimekuambia kila unachotaka," Bibiane alijibu kwa sauti ya mahaba.
"Wewe ni nani?" Willy alimwuliza.
"Mimi naitwa Bibiane Habyarimana, ni Mnyarwanda, na wewe?".
Willy alishtuka namna alivyo mjibu na kuzidi kuimarisha hisia zake kuwa huyu msichana vilevile alikuwa si mtu wa hivihivi ila alikuwa mtaalamu katika nyanja kama yake. Mara ya kwanza alipohisi, ilikuwa jinsi alivyojirusha nyuma ya kochi pale nyumbani kwake baada ya yeye kuwapiga risasi wale watu wawili, na alivyochupa dirishani kumfuata Xavier. Kwanza alifikiri alikuwa na mafunzo ya kijeshi tu, lakini kutokana na jinsi ya majibizano yao aligundua alikuwa na utaalamu zaidi.
"Willy Gamba, Mtanzania," alijibu na wote wakaangaliana kama wanapimana saizi. "Ningependa nijue historia yako nzima, na usinifiche kitu, mpaka kufikia uhusiano wako na hawa wauaji na hasa huyu aliyekuhukumu kifo bwana Jean", Willy alimwambia Bibiane.
"Nimeshatoa kauli yangu kuwa nitakueleza kila kitu unachotaka niseme. Hivyo, usiwe na wasiwasi nitakueleza, ila itabidi uwe na subira maana ni hadithi ndefu", Bibiane alijibu.
Bibiane alimweleza Willy kwa kirefu maisha yake ya utoto, maisha ya shule, juu ya baba yake na mama yake na akaendelea, "Mwaka nilipoanza kazi baada ya kuhitimu digirii ya kwanza ya lugha katika Chuo Kikuu cha Kigali, wazazi wangu wote wawili walikufa kwa ajali. Nilikuwa nimeanza kazi Wizara ya Mambo ya Nje kama mkalimani.
"Inasemekana kuwa wazazi wangu hawakufa kwa ajali ya kawaida ila waliuawa na vikaragosi vya Watutsi ambao walifikiri kuwa baba yangu alikuwa ndugu yake na Rais. Hivyo waliwaua wazazi wangu ili kumkomoa Rais. Kitendo hicho kiliniuma sana nikawachukia sana Watutsi", Bibiane alieleza.
"Pole sana", Willy alisema kwa sauti ya huruma.
"Kwa kunisikitikia kutokana na yaliyowakuta wazazi wangu, serikali ikanihamishia ofisi ya Rais, huko ndiko nilipokutana na Jean Yves Francois, yeye ni Mfaransa anaishi Paris lakini alikuwa rafiki kipenzi na Rais. Tulionana naye nyumbani kwa Rais ambako alikaribishwa na tulianza urafiki siku hiyohiyo", Bibiane alieleza Willy huku akimwangalia kwa jicho la kuiba.
"Huyu Jean Yves Francois ndiye aliyekufundisha ujasusi?", Willy alimuuliza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Umejuaje?".
"Nimehisi".
"Jean ni mfanyabiashara na alikuwa akifanya biashara na kundi la marafiki wa Rais pamoja na familia ya Rais, wakati mimi nafahamiana naye serikali ilikuwa imeanza kuwa na matatizo kwani Watutsi waliokuwa humu ndani na nje, nchini kwenu na Uganda walikuwa wakipigana ili waiangushe serikali. Jean ndiye aliyekuwa akimsaidia Rais kwa kumjenga kijeshi, kiusalama na kiutawala. Huyu Jean ana utajiri usio kifani, kwani ndiye anayezifadhili serikali na wakuu wengi wa nchi za Afrika. Kwa vile mimi pia nilikuwa kwenye himaya yake alinipeleka kwenye mafunzo ya kiusalama sehemu mbalimbali duniani".
"Na ukahitimu vizuri", Willy alidakia.
"Vizuri sana".
"Ehee, endelea".
"Si ni wewe unanikatisha".
"Huu utajiri aliupataje?", Willy aliuliza.
"Sijui mwenyewe ameupataje, ila anashughulika na mambo ya silaha. Hapa alikuwa analeta silaha, halafu anachukua chai yote na kahawa inayolimwa katika nchi. Hili suala ni moja ya malalamiko mengi ya wananchi maana Jean ndiye aliyekuwa akipanga bei anayotaka, na hakukuwa na mtu wa kusema kitu, maana alikuwa akifanya biashara na Rais na kundi lake, lililokuwa likiitwa Akazu. Kusema kweli Jean na hilo kundi la Akazu ndio waliokuwa wanatawala na si baraza la mawaziri au Bunge", Bibiane aliendelea huku sasa Willy akimsikiliza kwa makini zaidi.
"Huoni kuwa hiyo haikuwa sawa?", Willy aliuliza.
"Mimi ningefanya nini, nilibaki kufanya kila nilichoagizwa kama ilivyokuwa kwa wengine wengi maana sasa hii ndio ilikuwa namna ya maisha. Ama uko na Akazu, vinginevyo hupati kitu cha aina yoyote, iwe mali, elimu au kazi ya aina yoyote Rwanda".
"Kwa hiyo rushwa ndio ilitawala utawala uliopita?", Willy aliuliza.
"Inategemea unavyotafasiri rushwa", Bibiane alijibu huku akiwa kama haelewi anasema nini.
"Rushwa ni pale vyombo vya serikali vinaposhindwa kufanya kazi zake, kwa sababu hiyo kushindwa kutoa haki kwa wananchi wake, na kuwafanya wananchi wengi wapoteze imani, utu, uhuru na maadili kwa serikali yao kwani wote sasa huishi kama wanyama ambapo mwenye nguvu na pesa ndiye anayepata anachohitaji", Bibiane alisema.
"Hivyo ndivyo, maana nchi inakosa maendeleo kwani mapato yote ya nchi badala ya kuendeleza watu wote huingia kwenye mifuko ya watu wachache. Na kama ulivyosema uhalali wa serikali kama chombo cha watu unakwisha, badala yale wale wanaofaidika ndio wanakuwa na nguvu zaidi ya serikali yenyewe", Willy alitafasiri rushwa.
"Kwa tafasiri hiyo nakubali kuwa rushwa ndiyo imetawala. Na sasa Watutsi na Wahutu walipoanza kudai demokrasia isingewezekana maana Jean na Akazu hawakutaka kusikia kitu kama hicho kwa vile kingeweza kuingila maslahi yao. Na ndio sababu Watutsi walipokazana na kusikia eti wako tayari hata kupigana na Akazu, kwa kufadhiliwa na Jean, walianza kulifundisha jeshi la wahutu lililoitwa Intarahamwe ili liweze kuwadhibiti Watutsi wa ndani na nje ya Rwanda".
"Kwa hiyo huyu bwanako Jean ndiye alikuwa Rais hapa?".
"Si hapa tu, mimi najuwa nchi nyingi ambako amewakamata wakuu wa nchi na viongozi wa ngazi za juu serikalini na anawajaza mapesa kila wakati".
"Huoni kuwa yeye ndiye ananufaika zaidi, maana anajaza mapesa watu wachache lakini yeye anachukuwa mali za wananchi wengi", Willy alijaribu kumwelimisha Bibiane.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Najuwa, maana hata huko kwenu Tanzania pia amewakamata wakubwa, ndio sababu nchi yenu imekuwa ikisita juu ya suala hili la Rwanda".
Willy alisitushwa na taarifa hii lakini hakutaka kujionyesha maana kweli msimamo wa serikali ya Tanzania ulikuwa unalegalega kabla na hata baada ya mauaji.
"Ina maana maamzi yoyote ilikuwa lazima Jean akubaliane nao?".
"Ndiyo, na mapesa yalitembea sana kuhusu swala hili na viongozi wengi wamenufaika. Unafikiri kama swala hili lingefanyiwa maamuzi mapema mauaji yangetokea!", Bibiane alimwambia Willy kwa njia ya kushangaza.
"Kwa hiyo huyu Jean ndiye aliamru mauaji haya?".
"Baada ya Rais kuonekana kwamba angekubali mkataba wa Arusha. Jean na Akazu walikasirika sana maana hawakutaka, kama nilivyosema mwanzo, kugawana madaraka na mtu mwingine. Hii ingegusa maslahi yao. Kwa hiyo, kwanza ndio waliamru Rais auawe na pili tayari walikuwa wamewatayarisha na kuwahamasisha Wahutu kuwamaliza Watutsi wote asibaki mtu ili wajihakikishie uwezo wa kutawala milele. Mpango ulikuwa kwamba hata kama jeshi la RPF la Watutsi lingeshinda jeshi lao lazima baada ya kuchukuwa nchi wangeshindwa kutawala maana wangemtawala nani huku Watutsi wote wakiwa wameshauawa, waliobaki ni Wahutu watupu ambao hawawaungi mkono. Hivyo, ingewachukuwa siku chache kuuangusha na kuutokomeza kabisa utawala wa RPF. Hii ingebaki nchi ya Wahutu chini ya utawala wa Jean na Akazu.
Bibiane alipofika hapa ndipo Willy alipoanza kuelewa kwa undani mambo yalivyokuwa. Kumbe mauaji yote haya yalitokana na watu wachache kutaka kulinda maslahi yao ya kunyonya mali ya wananchi, na kutumia hiyo mali kuweza kuwachochea wananchi kuuana!.
Kwa mara ya kwanza Willy aliona jinsi ambavyo nchi zote za Afrika zilivyo hatarini kutokana na rushwa. Kwa vile viongozi wa nchi hizi kuabudu rushwa, hivyo Willy akaamini kuwa tukio kama la Rwanda kumbe linaweza kutokea mahali pengine katika Afrika!.
"Baada ya RPF kushinda na mipango ya Jean kushindwa, wana mikakati gani sasa?", Willy alihoji.
"Kama nilivyosema hawajashindwa. Wewe ndiye umeingilia ndani ya mipango yao, kuna mpango kabambe wa kuisambaratisha serikali ya RPF kutokea jimbo la Kivu, Zaire. Akazu wamekuwa wakiliimarisha jeshi lao katika makambi ya wakimbizi kule Goma na Bukavu, Zaire, huku Jean akiwatumia rafiki zake kutoka Afrika Kusini hasa waliowahi kuwa katika idara ya ujasusi ya makaburu, alikokuwa akinunua silaha na kuzipitishia Angola ya UNITA, Zaire na Zambia kwa kutumia viongozi wa ngazi za juu za serikali za nchi hizo ambao wako kwenye orodha ya malipo kutoka kwa Jean. Kwa hiyo mambo bdo sana Willy, vita ndio sasa karibu vitaanza".
"yaani dunia inafikiri kuwa kambi zilizoko Zaire ni za wakimbizi kumbe ni kambi za jeshi".
"Ni kambi za jeshi na serikali ya Zaire inajua na ndio inayosaidia hata mafunzo. Hata katika kambi zilizoko kwenu Tanzania kuna wanajeshi wa jeshi la zamani na Intarahamwe, na kuna watu wazito katika serikali yenu ambao wanalipwa na huyu Jean ili kuwasaidia hawa watu, kwa hiyo hili si dogo. Kama ulivyosema pesa ni kitu kibaya sana, watu hawaoni tena madhara ya mauaji yaliyotokea bali wanaona pesa tu".
"Swala la rushwa ni swala linalohujumu haki za binadamu, yapaswa lichukuliwe hatua kimataifa katika uzito huo wa haki za binadamu", Willy alijibu kwa hasira.
Bibiane alikaa kimya bila kujibu kitu.
"Wewe ulikuwa uwasaidie vipi Jean na Akazu katika kutekeleza huu mpango wao wa kuivamia tena Rwanda", Willy aliuliza.
"Usije ukanipeleka kwenye mahakama ya mauaji ya Arusha maana mauaji yale sikuyajuwa pia sikushiriki, nilikuwa Nairobi nikitokea kwenye mkutano Arusha. Ila juu ya hili la sasa Jean amekuwa akinituma kupashana habari kati ya kambi za wakimbizi ambazo ni kambi za jeshi lao huko Zaire, yeye na Akazu. Vilevile kuna wanajeshi na viongozi wa RPF ambao tayari wamenunuliwa na wako upande wa Akazu, mmoja wao ndiye anayetarajiwa kuchukua madaraka mara tu jeshi la Akazu litakapotwaa madaraka tena".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Willy hakuamini masikio yake kuwa tayari hata ndani ya RPF kuna wasaliti.
Mara moja Willy alielewa jinsi alivyotaka kuuawa na akagudua kuwa kweli kama anavyosema Bibiane kuna kiongozi wa juu na karibu sana katika serikali ya Tanzania amabye anamtumikia Jean na kundi la Akazu.
"Utasaidia kunipa majina ya watu wote unaowajuwa kuwa wanahusika, maana hiyo ndio njia pekee tunaweza kulikosha jina lako", Willy alimuasa Bibiane.
"Swala la Jean kunisaliti mimi, na kunihukumu kifo, bila kujali yote niliyomtendea kwa hali na mali ikiwa pamoja na kumpa mwili wangu auchezee atakavyo, na jinsi nilivyojitoa kumstarehesha. Willy mimi niko upande wako, kama uko tayari kupambana nao nihesabu na mimi. Jean akishaambiwa kuwa umenichukua ninavyomjua atataka apambane na wewe yeye mwenyewe, ikifika hapo niachie mimi. Majina na mipango yao yote ni juu yako na uongozi wa RPF mjuwe la kufanya kwani jeshi la Akazu, likisaidiwa na viongozi wa nchi kadhaa ambao ni marafiki na Jean watakuwa tayari kuingilia kati. Ni lazima liwahiwe mapema kabla halijajiimarisha sawasawa", Bibiane alieleza.
"Nafikiri swala la vita si letu, ni la serikali ya Rwanda na RPF, mimi nipe hayo majina na kutokea hapo ndipo nitajua kama kazi yangu imeisha au ndio kwanza inaanza", Willy alieleza taratibu.
Bila kuwa ameandika mahali popote, Bibiane alitoa kichwani jina hadi jina akianza na kundi la Akazu mpaka viongozi wa nchi mbalimbali wanaolipwa na Jean huku Willy akiyaandika chini kwa mshangao mkubwa, kwani watu waliokuwa wanatarajiwa wengi wao ni viongozi wanaoheshimika Afrika na kote duniani. Alishangaa zaidi Bibiane alipotaja jina la yule waliyekuwa wakimwita JKS wa Tanzania.
"JKS, hii imenishangaza sana, maana huyu ndiye anayetegemewa kugombea urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu unaokuja," Willy alimweleza Bibiane.
"Najua kabisa, na tayari Jean ameshamtengea mamilioni ya dola za Kimarekani zitakazo msaidia katika kampeni hiyo ya uchaguzi kuusaka urais. Nia ya Jean ni kuwa na marais vibaraka kote Afrika ili yeye na wenzake huko Ulaya, waweze kufanya vile wanavyotaka katika nchi hizi. Jean anaongoza kundi la wafanyabiashara wakubwa wanaomiliki makampuni makubwa ya kimataifa. Na nia yao ni kuhakikisha kuwa Afrika inakuwa soko lao tu, na hata siku moja Afrika isisimame kiuchumi. Ingawaje nchi zao zinapigia kelele rushwa, lakini nchi hizohizo ndizo zinazoyasaidia makampuni makubwa kwa madogo kutoa rushwa kwa nchi zinazoendelea, maana makampuni hayo yakitoa hongo, hongo hii huchukuliwa kama gharama na kutolewa kwenye kodi ya mapato. Hii yote inaonyesha unafiki wa nchi za magharibi, na kila wakati Jean alikuwa akinieleza kuwa kelele zote hizi kuhusu rushwa, demokrasia na soko huria ni kelele za kinafiki tu, lakini huku nyuma katika vikao vya viongozi wa nchi za magharibi ni kuchochea rushwa. Wanajuwa kuwa rushwa ikiisha Afrika basi demokrasia na soko huria vitashamiri na hivyo uchumi wa nchi hizo utakua haraka sana, kitu ambacho hawataki kitokee. Jean anasema, rushwa ndiyo sera inayotumiwa kuendeleza umaskini katika nchi za Afrika ili nchi zilizo endelea ziendelee kuitawala Afrika kiuchumi. Kwa hiyo, iwapo JKS ataitawala Tanzania rushwa itazidi mara dufu, na kutokana na fedha alizotengewa na Jean lazima atashinda, kwani kila walipoweka mtu wao hajawahi kushindwa uchaguzi", Bibiane alieleza.
Sasa Willy alikuwa na picha kamili namna JKS alivyokuwa anahusika na swala zima la Rwanda. na sababu za Tanzania kutokuwa na msimamo dhabiti juu ya swala hili na kuweza kuyumbisha mikutano kule Arusha kiasi cha kutofikia maamzi kwa muda mrefu maana swala hili la Rwanda kwa muda mrefu lilikuwa chini ya Tanzania kwa muda mrefu na JKS alikuwa mmojawapo wa viongozi walioonyesha kuchoshwa na mauaji ya Rwanda. Na alifanya hivyo kwa shinikizo la Jean aliyekuwa akimlipa pesa nyingi na uchu wake wa kutaka madaraka kwa njia ya ruswa ili aweze kuyatumia kwa faida yake na kujinifaisha yeye na rafiki zake. Na ni hii rushwa iliyowanyima Wanyarwanda haki yao mpaka kufikia hatua ya kuuawa vibaya namna ile kweli ni aibu! Aibu sana kwa Afrika nzima.
"Vizazi vijavyo vitakapoyasoma na kuyaelewa matukio haya, hakika hawataamini, watajuwa sisi wote tulikuwa wendawazimu kabisa, kwani ni sisi wote ndio tulioachia hali hii ikafikia hapo ilipo, kwa kuwapa walarushwa madaraka kwa gharama ndogo ya kuuza kura zetu na wao kutumia madaraka tuliyowapa kwa malipo ya fedha kidogo, lazima wayatumie kutuangamiza", Willy alisema kwa uchungu huku akikuna kichwa chake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara moja Willy alimkumbuka Malisa wa Arusha, aliyekuwa mshauri wa JKS katika masuala ya uhusiano wa Kimataifa kabla hajarudi Chuo Kikuu. Hivyo basi, alijuwa Malisa ndiye aliyemweleza JKS kuhusu msimamo na mipango ya PAM na kuteuliwa kwa Willy kufuatilia jambo hili. Willy aliamini kuwa JKS ndiye aliyetoa taarifa za safari ya Rwanda kwa Jean na kundi lake na ndi sababu ndege aliyopanda ikapigwa kabla ya kutua uwanja wa ndege wa Kigali.
"Kwa hiyo JKS ndiye aliyotoa habari zangu zote kwa Jean?", Willy aliuliza kwa shauku.
"Ndio, na ndio sababu Col. Gatabazi aliamru ndege hiyo ipigwe kabla ya kutua uwanja wa ndege, lakini kwa bahati na umahiri wako ukawaponyoka", Bibiane alijibu huku akimwemwesa. Mara mlango wa mbele ukafunguliwa na Col. Gatabazi akaingia ndani.
Willy alipoangalia saa yake ilikuwa yapata saa tisa usiku. Wote walisimama, na Willy akawatambulisha.
"Pole Kanali, leo tumepata mgeni na anaitwa Bibiane, na Bibiane huyu ndiye mwenyeji wetu. Col. Rwivanga, kiongozi katika serikali mpya ya RPF".
"Nashukuru kumfahamu", Col. Rwivanga alijibu.
"Nami nimefurahi kukuona leo, nimekuwa nikisikia sifa zako nyingi kwa muda mrefu, toka kwa Col. Gatabazi kuwa wewe ni mpiganaji hodari, hongera", Bibiane alijibu kwa tabasamu akimwangalia Col. Rwivanga.
"Asante kwa sifa hizo zilizotoka katika kinywa cha msichana mrembo kama wewe", Col. Rwivanga alijibu akaendelea, "Ehe, imekuwaje Willy, hebu nipe habari kamili, maana kazi tumeiona kwa Bibiane, sasa halafu ikawaje hivi", Col. Rwivanga alionekana kuwa wasiwasi na Bibiane.
"Mimi naomba nikalale ili mzungumze vizuri, nionyeshe chumba cha kulala", Bibiane aliomba.
Willy na Col. Rwivanga aliangaliana na Willy ndiye alikuwa wa kwanza kujibu, "Kwa vile nyumba hii ina vyumba viwili tu vya kulala, basi kalale chumbani kwangu, maana tayari hata kuoga umeoga huko. Mimi nitalala hapa sebuleni kwenye kochi hamna taabu".
"Asante", Bibiane aliwaaga na kuelekea chumbani huku wote wakimwangalia. Kisha wakatazamana na kutabasamu.
"Ehe, hebu nipe mambo".
Willy alichukua muda mrefu kumweleza mambo yalivyotokea na mambo mengine yote aliyoelezwa na Bibiane. Col. Rwivanga akasimama na kumshika mkono Willy kwa hatua aliyofikia haraka na kwa umakini mkubwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Simu ilipoita Jean alikuwa amelala. JKS alikuwa amemweleza kuwa vijana walikuwa wamefika salama na kazi ya kumsaka na kumuua Willy Gamba ilikuwa ifanyike usiku ule. Alikuwa amefikiria jinsi Bibiane angeshangaa sana baada ya kuelezwa kuwa Jean ndiye aliyetoa amri ya yeye kumuua. Jean alikuwa mtu aliyefurahia uovu, alikuwa mtu katili afadhali ya mnyama. Alifurahi kusikia mtu akipata maumivu, na hapo ndipo roho yake ilipopata faraja. Pamoja na miaka yoye sita aliyokaa na Bibiane, utafikiri walikuwa mtu na mke wake, yaani mume na mke, bado alipomweleza Col. Gatabazi kuwa lazima Bibiane auawe moyoni mwake hakusikia masikitiko. Kilichomfurahisha na kumridhisha ilikuwa ni pesa na nguvu ya pesa, na si mapenzi. Jean aliabudu pesa kwani aliamini kuwa pesa ndizo zilizompatia uwezo alionao duniani.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment