Simulizi : Biashara Ya Kifo
Sehemu Ya Pili (2)
"Nawasikiliza" Don Genge aliwastua.
"Sisi tumetoka nyuma ya nondo juzi tu. Bado hatujajua kama watu tuliowaacha uraiani wana ubora uleule. Ngoja tufanye uchunguzi tutakupa jibu mkuu" Peter aliwajibia wenzake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Don Genge alikubali kwa kuitikia kwa kichwa.
"Mkuu mimi nina swali" Peter alisema.
Don Genge alimruhusu kwa kumuoneshea mkono.
"Sisi mkuu wetu wewe, wewe mkuu wako ni nani? Yaani nani ndiye country director wa this mission?" Peter aliuliza huku akimwangalia Don usoni moja kwa moja.
"Kifo!" Don Genge alijibu kwa kifupi.
"Kifo?" Wote watatu waliuliza kwa pamoja kwa sauti ya juu.
Don Genge alikaa vizuri kitini. Aliongea huku akimwangalia Peter "Ndio anaitwa Kifo, yeye haoni shida kumuua yeyote anayeenda kinyume na mipango yake. Ameua watu wengi sana. Na hiyo ndiyo sababu ya kupewa jina hilo. Hivi juzi tu alikuwa gerezani, kwenda kuwaua Six killers baada ya kukwamisha mipango yake. Jamaa anaitwa Kifo, na anaua kweli!" Don Genge alisema kwa hisia.
"Kifo? Jina lake halisi ni nani?" Peter aliuliza tena bila ya kubabaika. Kama Don Genge alisema vile kwa lengo la kuwatisha, basi alifeli.
"Peter Genious, utafanya nini baada ya kulijua jina lake halisi?" Don Genge aliuliza.
"Sina kawaida ya kufanya kazi na mtu nisiyemfahamu. Lazima nimjue bosi wako. Kwa maana ya bosi wetu na sisi pia. Ni katika principle zangu tu nilizojiwekea tangu na tangu" Peter alisema kwa kujiamini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ni siri Peter. Kila kitu hakiwezi kuwa wazi kama unavyofikiria. Hizi ni misheni za siri, acha mambo mengine yabaki kuwa siri" Don Genge alisema.
"Mbona mimi wewe unanijua, mbona wewe mimi nakujua. Nakujua kwa sura, nakujua kwa jina. Kwanini bosi wako awe siri? Yeye ana upekee gani? Nitajie jina lake ili tufanye kazi. I repeat its my principle !" Peter alisema kwa sauti kubwa.
Don Genge alikaa kimya. Alitafakari. Aliona utofauti mkubwa sana kati ya vijana wake wa zamani wa Six killers na hawa waliokuwa mbele yake. Six killers walikuwa sio watu wa kuhoji sana. Walikuwa ni watu wa ndio tu. Hawa walikuwa watu wa kujadili, watu wa kudadisi, watu wa kuuliza, kutoa maoni. Na huyu Peter alikuwa anauliza vitu vya ndani kabisa.
Pamoja na yote hayo bado Don Genge hakutaka kumtaja Kifo ni nani?
"Daaah niseme ukweli tu kwa sasa siwezi kukutajia jina lake halisi. Labda nikamuulize mwenyewe kwanza nione kama ataridhia" Don Genge alisema akiwa amenywea.
"Ukamuulize mwenyewe? Ukamuulize wapi? Wakati kikao hiki anasikiliza kila kitu. Na anatuona. Najua hivi sasa anasikia nahitaji nini, naomba akupigie simu tu na kujibu nilicho..." Peter hakumalizia kusema.
Simu ya Don Genge iliita.
Katika kioo cha simu yake lilitokea jina moja tu, Kifo. Don Genge alitetemeka kidogo. Aliipokea simu.
"Nambie mkuu" Don Genge alisema katika hali ya uwoga.
"Naona mnasumbuana na Peter. Huyo jamaa inaonesha ni mtata sana". Kifo alisema simuni.
" Tena zaidi ya sana" Don Genge alijibu.
"Hebu mpe simu niongee nae" Kifo alisema.
Don Genge alinyoosha mkono na kumkabidhi simu Peter.
Bila ajizi Peter aliipokea.
"Mkuu" Peter alisema pindi tu alipoipokea simu.
"Naitwa Kifo!" Sauti simuni ilisema.
Peter alibabaika kidogo. Aliitambua sauti aliyoongea nayo. Aliisikia sana katika masikio yake. Tena mwisho jana tu aliisikia wakati akiangalia taarifa ya habari. Na alimuona pia.
"Nishakutambua" Peter alisema kwa kujiamini.
"Your a Genious Peter!" Kifo alisema kwa hamasa.
Simu ikakatwa.
Macho sita pale mezani yalikuwa yanamuangalia Peter. Macho yakiwa katika mshangao na udadisi.
Baada ya sekunde kadhaa, macho ya Malkia yalisafiri hadi kwa Don Genge.
Kwa mara ya kwanza alimuona Don Genge akitabasamu tangu amfahamu.
Malkia nae alitabasamu. Alijiona ni mwenye bahati sana kujuana na Peter, mwenye bahati kubwa kujuana na Malolo. Wote walikuwa na vipaji vya pekee katika nyanja zao. Hawakuwahi kumuangusha hata sekunde moja.
"Wewe jamaa wewe, kiboko aisee" Don Genge alisema huku akimpa mkono Peter.
Baadae, Don Genge alifunga kikao kwa ajili ya utekelezaji wa biashara yao ya kifo...
Nusu saa baadae Peter, Malolo na Malkia walikuwa chumbani kwa Peter.
Walikuwa wanaweka mipango yao sawa kabla ya kuingia kazini. Peter alikuwa ameshawaambia wenzake juu ya mtu mwenye sauti aliyoisikia.
Waliijadili na kuijadili.
"Hivi mnaonaje tukiwakomesha wale jamaa kabla hatujajikita kwenye hii kazi?" Malolo alichokoza mada nyingine.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Jamaa gani tena hao Malolo?" Peter aliuliza.
"Wale jamaa wa Mkanda wa siri" Malolo alisema.
"Umesema kitu muhimu sana. Wale jamaa walijifanya wajanja sana. Lazima tuwatafute. Lazima tuwaoneshe, lazima tuwaue". Malkia alisema kwa hasira.
"Unajua wale majamaa wana akili sana, lazima nasi tutumie akili kama tuna nia kweli ya kuwaua. Maana kupambana na Martin Hisia yahitaji uwe na zaidi ya akili" Malolo alisema.
"Tufanye hivi, tumwambie Don kwamba kuna zana zetu za kazi inabidi tuzifuate Dar. Atupe private jet moja na sumu kidogo , tukawaoneshe!" Malolo alitoa maoni yake.
"Mmmh anaweza kutupa kweli proxine kwa ajili ya kwenda nazo Dar?" Malolo aliuliza.
"Tumwambie ni kwa ajili ya kujilinda" Malkia alisema.
Saa tatu baadae Malkia, Peter na Malolo walikuwa katika jiji la Dar es salaam. Walipofika Dar walijigawa ili waifanye kazi yao kwa ufanisi.
Usiku ulimkuta Peter Magomeni. Usiku huohuo ulimkuta Malolo Tandika na Malkia Tegeta. Kila mmoja akiwa na sura ya bandia, sauti ya bandia, mwendo wa bandia na jina la bandia.
Malkia alikuwa na sura ya bandia ya msichana mrembo sana. Sauti ya bandia huku akijitambulisha kwa jina la bandia, Sophia.
Na kwa bahati mbaya kabisa Malkia ndiye aliyekutana na Martin Hisia katika baa moja huko Tegeta. Na kwa bahati mbaya tena Sophia hakuwa na sumu. Sumu walikuwa nazo wakina Malolo. Ndipo alipomlaghai Martin ili wakutane Posta. Kilichotokea huko Posta kimemfanya Martin alazwe hospitalini hadi leo. Huku Malolo akikutana na Richard mchana. Kumpasua vibaya kwa kutumia bastola yake
Jioni ya siku ya pili wakina Malkia walirejea Mbozi, Mbeya na ndege yao ya binafsi. Waliridhika kwa kazi waliyoifanya. Waliamini wamemuua Martin. Waliamini wamemuua Richard na walipata taarifa kwamba mzungu Brown alikuwa amerejea kwao Uholanzi. Sasa walikuwa tayari kurudi Mbozi na kwenda kuifanya kazi, kazi ambayo ni biashara, biashara ya kifo.
*****
Wiki moja baadae Mbozi ilikuwa katika kurasa za mbele katika magazeti yote nchini Tanzania. Mbozi ilikuwa katika habari ya kwanza katika kila stesheni ya runinga. TBC iliizungumzia Mbozi, Channel Ten waliijadili Mbozi, Star Tv waliistikia Mbozi. Mbozi iligeuka na kuwa gumzo katika redio zote Tanzania. Si radio one, clouds FM wala Times FM, zote ziliizungumzia Mbozi. Mbozi ilizungumzwa zaidi mitandaoni. Facebook, WhatsApp na Instagram iliizungumzia Mbozi.
Watu ishirini na saba walikutwa wamekufa, wengine walikutwa wamekufa majumbani kwao, wengine walikutwa wamekufa mitaani, wengine walifikwa na umauti katika nyumba za starehe. Kufa watu ishirini na saba haikuwa sababu ya habari hiyo kupewa kipaumbele katika vyombo mbalimbali vya habari, wala katika mitandao ya kijamii. Sababu ya vifo hivyo ndivyo vilivoipa uzito habari hiyo. Maiti zote zilikutwa hazina ngozi! Ilikutwa miili ikiwa nyama tupu, bila ngozi hata chembe!
Hali hiyo ilizua hofu kubwa sana huko Mbozi, pamoja na jiji la zima la Mbeya kwa ujumla.
Vifo vya watu waliochunwa vilileta taharuki kubwa sana. Watu waliogopa pasi na kawaida.
Watu walibadilisha ratiba zao za matembezi. Saa kumi na mbili jioni ikawa ni nadra kumuona akirandaranda hovyo. Walioendelea kuzurura ni kwa wale waliokuwa hawazipendi ngozi zao. Hawaupendi uhai wao. Wamechoka kuishi. Wanapenda kuzikwa wakiwa hawana ngozi.
Kati ya hao wengi wao walikuwa walevi wasioweza kuishi bila kunywa pombe. Wasioweza kulala bila kutia hata tone la pombe. Yaani ni lazima wao waende kilabuni kunywa pombe katika hali yoyote ile.
Jeshi la Polisi nalo liliingia kazini. Polisi walikuwa wanapeleleza nini chanzo cha vifo vya watu ishirini na saba waliochunwa ngozi.
Pamoja na kufanya kazi mchana, pamoja na kufanya kazi usiku, lakini Jeshi la Polisi hawakupiga hatua yoyote ile. Watu waliokuwa wanafanya mauaji hayo ya kikatili walikuwa wanatumia zaidi ya akili. Akili ambazo askari Polisi zilikuwa ni juu ya uwezo wao.
Alikuwa ni kijana mrefu, rangi ya ngozi yake ni maji ya kunde. Siku zote kichwani alikuwa anajua mtindo wa panki uliokuwa unampendeza sana. Alikuwa na kifua cha mazoezi. Mikono ya kupigana. Kichwa cha kufikiria na kuchambua mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu. Alikuwa ana mke mmoja, mwanamke wa kinyiramba toka Singida. Wakati yeye alikuwa Mhaya toka mkoani Kagera. Alijaliwa kupata watoto wawili mapacha, wote wa kike. Alimpenda mkewe, aliwapenda watoto wake. Alikuwa anaitwa John Kashangaki, kabla ya kupanda vyeo mbalimbali katika jeshi la Polisi na kuuvaa uinspekta.
Kwa sasa jina la John Kashangaki lilifutika kabisa katika midomo ya watu na kuzaliwa jina jipya, Inspekta John.
Na huyo.....Inspekta John Kashangaki wa kituo cha Polisi Mbozi ndiye alikuwa na jukumu gumu la kupeleleza juu ya mauaji ya kikatili ya watu waliochunwa ngozi.
Ni zaidi ya siku sita sasa tangu apewe kazi hiyo, lakini hakupiga hatua yoyote ile kujua chanzo cha vifo hivyo. Alipita katika familia zote za wafiwa, lakini hakuna lolote la maana alilolipata ili kumsaidia katika upelelezi wake.
Kitu ambacho alikuwa hakijui Inspekta John kila alikokuwa anapita nyuma yake kulikuwa na mtu. Mtu ambaye walipita wote katika nyumba zote ishirini na saba. Kama Inspekta John alikuwa anapeleleza, basi na yeye alikuwa anapelelezwa, tena anapelelezwa kwa siri kubwa sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
Ilikuwa ni siku ya jumanne asubuhi. Inspekta John alikuwa na miadi ya kukutana na Dokta aliyezipima na kuzichunguza maiti zote ishirini na saba. Alikuwa ni Dokta Chriss wa hospitali ya mkoa wa Mbeya.
Saa mbili kamili asubuhi ilimkuta Inspekta John mbele ya meza ya Dokta Chriss. Akiwa tayari kupokea ripoti muhimu ya daktari ambayo alikuwa na uhakika kwamba itamsogeza mbele ya sura ya muuaji.
Ndani ya hospitali hiyohiyo kulikuwa na mtu aliyekuwa amemfata kwa nyuma Inspekta John toka alivyokuwa ametoka nyumbani kwake. Na sasa alikuwa amekaa katika benchi nje ya ofisi ya Dokta Chriss. Akiwa na 'earphone' zake sikioni ikiyomuwezesha kusikia kila kitu kilichokuwa kinaongelewa ndani ya ofisi ya Dokta Chriss.
"Karibu sana Afande" Dokta Chriss alisema mara tu Inspekta John alivyoingia ndani ya ofisi yake.
"Ahsante sana Dokta. Pole sana kwa majukumu ya kazi" Inspekta John alijibu.
"Nashukuru, tunaendelea vizuri na kazi"
"Dokta, nimekuja hapa kuhusiana na ripoti ya vifo vya watu ishirini na saba"
"Ahaaa wale watu waliokufa vifo vya kitata. Hivi kuna nini kinaendelea hapa mjini Inspekta?" Dokta Chris aliuliza.
"Ndio maana nimekuja kufuata ripoti yako Dokta Chriss. Kwa kutumia ripoti yako na upelelezi nilioufanya ambao siwezi kuuweka bayana kwa sasa tutakuwa tumegundua chanzo vya vifo vile vya kinyama"
"Ripoti ya vifo vyote nitakukabidhi. Ingawa kuna mambo machache nataka tuongee kabla sijakukabidhi"
"Nakusikiliza daktari" Inspekta John alisema akiwa anamsikiliza daktari.
"Kitu kikubwa nilichogundua marehemu wote wamefariki kati ya saa sita usiku na saa saba. Hivyo bila shaka kama mnahitajika kuimarisha ulinzi basi jitahidini sana kuimarisha muda huo".
Inspekta John alikuwa anamwangalia usoni tu daktari. Alihisi kitu kichwani kwa Dokta. Alihisi alichokuwa anaongea sicho alichodhamiria kuongea. Inspekta John alizidi kumkazia macho Dokta Chriss kumsikiliza.
Dokta alipunguza sauti na kuongea "Eneo hili la hospitali sio salama kwa sasa. Kama sio kuna wafanyakazi wenzetu wanatusaliti basi wauaji wamepandikiza watu wao hapa" Dokta Chris aliongea akiwa ametulia.
"Kwanini unasema hivyo Dokta?" Inspekta John aliuliza huku akikaa vizuri kitini.
"Tangu tuletewe miili ya maiti zilizochunwa ngozi, basi kumekuwa na matukio ya ajabu sana. Nahisi kuna kitu hakipo sawa hapa hospitali"
"Kitu gani hiko dokta?" Inspekta John aliuliza akiwa na kimuhemuhe tele.
"Miili yote ya marehemu imeondolewa sehemu za siri!" Dokta alitulia. Akamwangalia inspekta John usoni. Aliipenda taharuki aliyoiacha usoni kwa Inspekta.
Aliendelea "Na mbaya zaidi hizo sehemu za siri zimeondolewa maiti zikiwa hapahapa hospitali!" Dokta Chris aliongea huku akinyanyuka kitini. Alimshika mkono Inspekta John na kutoka nae nje ya ofisi yake.
Inspekta John alitekeleza bila kuuliza.
Walikuwa wanaelekea katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ile.
Na yule jamaa aliyekuwa amekaa pale nje ya ofisi aliwafuata hukohuko.
Waliingia hadi ndani. Kulikuwa na majokofu mengi yaliyopangwa katika mistari miwili, yote yalikuwa karibu na ukuta kila pande.
Dokta Chriss na Inspekta John walitembea taratibu kuingia ndani.
Hakuna aliyekuwa anaongea. Ulikuwa mwendo wa kimyakimya.
Walipofika usawa yalipo majokofu ya kuhifadhia maiti. Dokta Chriss alivuta jokofu moja. Likafunguka. Ndani ya jokofu ulionekana mwili wa binadamu, ukiwa hauna uhai, mwili ukiwa katika hali ya kutisha sana.
Kwa macho ya kawaida yasiyoyozoea kuangalia vitu vya kutisha ilikuwa si rahisi kuiangalia maiti ile. Lakini macho manne yaliyokuwa yanauangalia ule mwili hayakuwa macho ya kawaida.
Inspekta John aliushuhudia mwili wa mtu ukiwa hauna uhai, hauna ngozi, hauna sehemu zake za siri.
"Umeona Afande, na maiti zingine zote zipo katika hali hiyo" Dokta Chriss alisema.
"Kwahiyo hizi maiti hazikuja hapa katika hali hii?" Inspekta John aliuliza katika hali ya kushangaa.
"Maiti zililetwa hazina ngozi lakini zilikuwa na sehemu za siri" Dokta Chriss alijibu.
"Nani mhusika mkuu katika chumba hiki cha kuhifadhia maiti?" Inspekta John aliuliza.
"Yule pale" Dokta Chriss alisema huku akimuonesha kwa kidole jamaa aliyekuwa kasimama mlangoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Inspekta John alimwita kwa mkono. Mzee mmoja mfupi, mnene kidogo alisogea pale mahali waliposimama Inspekta John na Dokta Chriss.
"Wewe ndiye mhusika hapa?" Inspekta John alianza kumuuliza.
"Ndio" Mzee alijibu kwa uwoga.
"Wewe ndiye uliyepokea hizi maiti zote ishirini na saba?" Inspekta John aliuliza tena.
"Ndio ni mimi" mzee alijibu tena kwa sauti yake iliyojaa uwoga.
"Ulizikagua hizi maiti zote kabla ya kuziruhusu ziingizwe humu ndani?"
Mzee alifikiria kidogo kisha akajibu "Ndio nilizikagua"
"Una uhakika?" Inspekta John aliuliza kwa ukali kidogo.
"Nilizikagua baadhi sio zote" Mzee alijibu kwa kubabaika.
"Kwanini zingine hukuzikagua?"
"Nilivyozikagua nusu tu nilijiridhisha zote zitakuwa hivyo"
"Hizo nusu ulizozikagua zilikuwa katika hali gani?" Inspekta John alizidi kumbana mzee kwa maswali.
"Maiti zilikuwa katika hali ya kutisha, zimechunwa ngozi" Mzee alijibu kwa hisia.
"Zilikuwa na sehemu za siri?" Inspekta John aliuliza akiwa anamwangalia usoni mzee Mwamaja.
"Ndio zote zilikuwa nazo"
"Mbona sasa hivi maiti hazina sehemu za siri?"
Mzee alifikiria kidogo kisha akajibu "Hata mimi sifahamu"
"Kuna maiti nyingine ililetwa baada ya kuwekwa maiti hizi ishirini na saba zilizochunwa ngozi?"
Mzee alifikiria kidogo, kisha akajibu "Hapana"
"Hebu kumbuka tena"
"Haikuletwa maiti nyingine" mzee alijibu kwa sauti ya kutojiamini.
"Hebu nipe kitabu cha maiti zilizoingizwa humu wiki hii?"
Mzee Mwamaja alibabaika hasa. Alienda kuchukua kitabu huku miguu ikiwa inamtetemeka vibaya sana.
Baada ya kama dakika moja mzee alirudi na daftari la maiti. Alimpa Inspekta John kwa mikono yenye kutetemeka.
Inspekta John alitumia dakika zipatazo tatu kukikagua kitabu kile. Alimwangalia yule mzee usoni kwa macho makavu.
"Unaitwa mzee nani? Inspekta John alimuuliza akiwa bado anamwangalia usoni.
" Mzee Mwamaja, naitwa Henry Mwamaja" Alijibu.
"Naitwa Inspekta John" Inspekta John alisema huku akimpelekea kitambulisho chake cha kazi usoni.
Aliona vizuri taharuki iliyojengwa katika uso wa mzee Mwamaja.
"Kuna kitu sio cha kawaida" Inspekta John alijisemea kimoyomoyo.
"Kabla ya hizi maiti ishirini na saba zilizochunwa ngozi kulikuwa na maiti ngapi humu?" Inspekta John aliuliza huku akikiweka kitambulisho chake mfukoni.
"Maiti tisa" Mzee Mwamaja alijibu.
"Na baada ya hizi maiti ishirini na saba za watu waliochunwa ngozi kuingia umesema haijaletwa maiti nyingine?" Inspekta John aliuliza tena.
"Ndio" Mzee Mwamaja alijibu.
"Mzee wangu umebahatika kusoma?"
"Ndio nimesoma afande"
"Nataka unihesabie idadi ya maiti zilizopo humu ndani sasahivi"
Mzee Mwamaja alianza kuhesabu. Alitumia dakika moja na nusu tu kuhesabu.
"Zipo maiti thelathini na saba" Alijibu baada ya kumaliza zoezi la kuhesabu.
"Kulikuwa na maiti tisa mwanzoni uliseme" Mzee Mwamaja aliitikia kwa kichwa. Inspekta John aliendelea, "Zikaongezeka maiti ishirini na saba. Tisa jumlisha ishirini na saba ni thelathini na sita. Sasa mbona umehesabu maiti humu ndani na kuzikuta zipo thelathini na saba? Hiyo moja imetoka wapi?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee Mwamaja alihema kwa nguvu.
"Hii maiti moja imetokea wapi?" Inspekta John aliuliza tena.
Mzee Mwamaja aliwaza kidogo, alisema kwa sauti ndogo sana
"Ililetwa maiti moja baada ya hizi maiti zilizochunwa ngozi "
"Ililetwa na nani?" Inspekta John aliuliza kwa ukali.
"Sijui"
"Ulikuwepo wakati maiti inaletwa?"
"Ndio"
"Uliipokea wewe?"
"Ndio"
"Uliikagua wewe?"
"Ndio"
"Kati ya hizi, maiti yenyewe ndo ipi?"
"Ipo mle" Mzee Mwamaja alionesha kwa kidole jokofu la mwisho.
"Twende"
Walifuatana wote watatu kuelekea katika lile jokofu. Walifika.
Inspekta John alimuonesha ishara mzee Mwamaja alifungue.
Huku akiwa anatetemeka mzee Mwamaja alivuta jokofu lile. Lilibaki wazi.
Walichokutana nacho humo wote walibaki mdomo wazi.
Ndani ya jokofu lile, hawakutana na mwili wa binadamu. Bali walikutana na mabaki ya mwili wa binadamu. Mabaki ya mwili ya mwili wa binadamu yakiwa nyang'anyang'a, yalikuwa yanatembewa na mafunza makubwamakubwa.
Mshangao wa haja uliwapata Dokta Chriss na Inspekta John. Hawakuelewa kabisa maana ya kitendo kile. Lakini alikuwepo wa kuwaelewesha.
Alikuwa ni mzee Mwamaja.
"Haya mabaki ya mwili wa binadamu yaliletwa muda gani?" Inspekta John aliuliza huku akiwa amekunja sura.
Mzee Mwamaja alibaki kimya.
Kibao kikali kilitua katika shavu la kushoto la mzee Mwamaja. Inspekta John alipandwa na hasira vibaya sana. Alihisi kuna vitu anafichwa na mzee yule. Na aliamini vitu avifichavyo mzee ni miongoni mwa sababu ya vifo vya uchunwaji watu ngozi. Alijiona anaukaribia mzizi wa kifo baada ya siku kadhaa za mauaji, na hakutaka kufanya mchezo ili kupoteza.
"Haya mabaki ya mwili wa binadamu yaliletwa na nani?" Aliuliza tena.
"Yaliletwa na mzee mmoja hivi" Mzee Mwamaja alijibu kwa woga.
"Anaitwa nani?" Inspekta aliuliza.
"Simjui jina"
"Daktari gani alithibitisha maiti iletwe humu?"
"Hakuna"
"Alipoleta alikukuta wewe?"
"Ndio"
"Uliikagua maiti alivyoileta?"
"Hapana"
"Kwanini?"
Mzee Mwamaja alikaa kimya.
Alijiroga. Kibao kingine cha nguvu kilitua katika shavu lake. Shavu lilelile. Mahali palepale. Kilipotua kibao cha awali. Machozi ya uchungu yalimdondoka mzee Mwamaja.
"Kwanini hukuikagua maiti ya mzee huyo?"
Alikaa tena kimya.
"Dokta namchukua huyu mzee kumpeleka kituoni....na atajuta!".
"Samahani afande. Nitasema ukweli .."
Pamoja na mzee Mwamaja kulia sana. Haikubadilisha kitu chochote kile. Inspekta John alimchukua mzee Mwamaja hadi kituo cha polisi cha Mbozi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walifika kaunta ya Polisi. Ndipo Inspekta John alibombadilikia Mzee Mwamaja sasa alikuwa anaendeshwa kipolisipolisi. Alivuliwa kila kisichostahili kuingia nacho selo. Akaingizwa ndani ya selo mkuumkuu mithili ya jambazi sugu.
Inspekta John aliamua kumuingiza kwanza selo yule mzee mtunza maiti kama njia ya kumtisha, ili atakapomtoa mzee atapike kila kitu.
Laiti angejua?
Nusu saa baada ya mzee Mwamaja kuwekwa selo aliingia mtu mwingine mle selo. Jamaa aliingia akiwa ananuka pombe. Mzee alibahatika kusikia kosa alilolifanya yule kijana katika hasira za askari wakati akimsukumiza mle ndani.
"Unajifanya unajua kutukana sana eeeeh, sasa tukania selo humo!" Askari alimwambia kwa hasira wakati akimsukumiza kwa nguvu yule kijana ndani ya selo.
Saa mbili asubuhi, kesho yake baada ya kukamatwa kwa Mzee Mwamaja. Inspekta John alifika katika kituo cha Polisi. Alikuwa na lengo moja tu, kumhoji kwa kina mzee Mwamaja ili kujua chanzo cha vifo vile vya kikatili na kusikitisha. Alimtuma askari mmoja ili akamtoe mzee Mwamaja, wakati yeye akiwa ofisini kwake. Dakika nne baadae simu ya inspekta John iliita.
"Halooo"
"Afande"
"Nakusikiliza"
"Naomba njoo katika chumba cha selo"
"Kuna nini?"
"Yule mzee amefariki!"
"Unasema?"
"Njoo afande maana na huyu mhalifu mwengine hali yake ni mbaya sana"
"Sikuelewi unajua,!"
"Njoo afande"
Inspekta John alitoka mbiombio kuelekea sehemu iliyokuwepo selo. Aliwakuta askari watatu wakiwa wamesimama katika ya mlango wa selo.
Wote wakiwa katika mshangao mkubwa sana katika sura zao. Sura za askari zilikuwa na hofu! Inspekta John alianza kwenda kwa tahadhari kubwa sana.
Inspekta John alienda kwa mwendo wa taratibu. Huku mapigo ya moyo yakimpiga kwa mbali. Ndani ya moyo wake alihisi kuna jambo la hatari anaenda kukutana nalo. Hatari kubwa. Jambo la hatari ambalo limewafanya askari wenzie wampigie simu yeye ili aende kulishuhudia ama aende kulitatua.
Askari walivyomuona Inspekta John anakwenda pale walipo, wote walisogea nyuma ili kumpisha Inspekta John. Askari mahiri akiyeaminika sana katika kituo cha Polisi Mbozi. Yeye ndio alikuwa tegemeo lao. Alishatatua mara kadhaa kesi za kitata zilizowashinda askari wa Mbozi, na mara nyingine alifanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu kuwashinda hata askari wa mkoani. Ndio maana kesi hii ya mauaji ya kinyama ya watu waliochunwa ngozi alikabidhiwa yeye. Na waliamini atafanikisha kuwakamata wauaji.
Inspekta John alifika hadi mlangoni. Askari mmoja alimkabidhi 'gloves' pale mlangoni. Akajua leo mle ndani kulikuwa kuna mambo mazito. Mambo yasiyohitaji kushikwa kwa mikono mitupu, yalihitaji kushikwa na mipira maalum.
Aliingia ndani taratibu, huku akiwa kazishika 'gloves' mkononi. Hakuzivaa.
Aliponyanyua macho yake mbele, alikutana na kasheshe. Inspekta John alitazamana na hali ya kutisha sana. Ilikuwa ni balaa! Tena zaidi ya Balaa!
Alishuhudia kichwa kitupu cha mzee Mwamaja kikiwa katika kona moja ya selo. Kichwa kikiwa kinavuja damu peke yake. Kichwa bila kiwiliwili. Mguu wa kulia wa mzee Mwamaja ukiwa umetapaa damu, ulikuwa umesimama wima katika kona nyingine ya selo huku ukiwa na damu nyingi mno. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kiwiliwili cha mzee Mwamaja, kiwiliwili kisicho na mguu mmoja, kiwiliwili kisicho na kichwa kilikuwa kimesweka vibaya katika kona nyingine ya selo. Inspekta John aligeuza sura yake kuangalia kona nyingine. Alimuona mhalifu mpya akiwa amejikunyata konani, mwili wake wote ukiwa umetapaa damu.
Inspekta John alirudia tena kutazama kona moja baada ya nyingine ya ile selo. Aliviona vitu vilevile alivyoviona awali. Inspekta alikuwa bado haamini kilichotokea.
"Kumetokea nini humu? Vitu kama hivi vinatokeaje ndani ya kituo cha Polisi? Mauaji ya kinyama kama haya yanawezaje kutokea ndani ya selo, selo ya Polisi?
Polisi walikuwa wapi? Muuaji aliingiaje hadi ndani ya selo? Muuaji alitokaje ndani ya eneo la Polisi?" Inspekta John alijiuliza kimoyomoyo. Lakini hakupata majibu. Hakutaka kujisumbua kujiuliza mwenyewe, alimuona wa kumjibu maswali yake yote, ambaye bila shaka alikuwepo wakati mauaji yale yakifanyika, na yeye alibaki hai. Na aliamua kwenda kumuuliza.
Alianza kumsogelea Mhalifu yule ili amjibu maswali mengi na magumu yakiyokisumbua kichwa chake. Kila alipopiga hatua kuelekea katika kona aliyekuwepo yule mhalifu mpya. Ulitokea utata!
Jamaa alipiga kelele kali kila hatua ya Inspekta John ilivyokuwa inagusa sakafu ya selo.
Ilikuwa kelele! Kelele nyingi! Kelele zisizo na kifano!
Hatua za Inspekta John zilikuwa kama zinamtonesha yule mhalifu katika vidonda vyake...
"Kimetokea nini humu?" Safari hii sauti ya Inspekta John iliweza kutoka nje ya mdomo wake, na kusikiwa na askari wote waliokuwepo pale mlangoni.
Lakini hakuna aliyemjibu.
Inspekta John aliendelea kupiga hatua taratibu kumfata yule mhalifu mtukanaji, mhalifu anayepiga makelele kila hatua ya Inspekta John ilivyokuwa inagusa chini. Safari hii ilikuwa vilevile, kila Inspekta John alivyogusa ardhi ndipo makelele toka kwa yule mhalifu yalivyokuwa yanazidi.
Inspekta John alisimama.
Aligeuka mlangoni, lakini macho yake yalienda moja kwa moja nyuma ya mlango. Aliona kitu! Utumbo wa binadamu ulikuwa umekusanywa hovyo nyuma ya mlango wa selo.
Bila kupenda Inspekta John lilimtoka tusi zito la nguoni. Sasa alijua kwamba mle selo aliingia muuaji katili sana. Muuaji anayejisikia raha kuua. Muuaji aupendao mchezo wa mauaji.
Muda huohuo baada ya kuuona tu ule utumbo ndipo alipoanza kuivuta harufu mbaya mle ndani.
Harufu ya utumbo!
Harufu ya damu!
Damu ya binadamu!
Hakuweza kuivumilia. Alitoka nje harakaharaka.
Aliwakuta askari wakimsubiri kwa nje.
"Kumetokea nini kwani humu ndani?" Inspekta John aliuliza tena swali lilelile.
Askari wale watatu waliangaliana usoni, hakuna aliyemjibu. Waliendelea kukaa kimya. Sura zao zikiwa na hofu.
Inspekta John akauliza swali lengine " Ni nani aliyenipigia simu nilipokuwa ofisini?"
Askari wote walikataa kwa mabega.
"Nyinyi Askari!" Inspekta John aliita kwa nguvu.
Wote walisimama imara! Wakimuangalia Inspekta John kwa sura zenye uwoga.
"Nani aliyenipigia simu?" Inspekta John aliuliza tena.
"Sijui" Wote walijibu kwa pamoja.
"Nani alikuwa zamu hapa usiku?"
Askari wawili walimuonesha askari mwenzao kwa kidole.
"Nakuhitaji ofisini" Inspekta John alisema huku akiongea.
Alitembea kama hatua tatu. Akasimama. Akageuka nyuma, aliongea tena "Mpigieni daktari akishafanya mambo yake pigeni picha kila kitu kilivyo humu ndani. Then muite wahudumu wasafishe, na huyo jamaa mpelekeni hospitali. Kuweni makini lakini"
"Sawa afande" Askari wale wawili waliobaki waliitikia kwa pamoja.
Katika viti viwili vilivyokuwepo ofisini kwa inspekta John vilikuwa vimekaliwa na askari wawili. Kimoja kilikaliwa na Inspekta John mwenyewe na kingine kilikuwa kimekaliwa na askari mrefu mweusi. Alikuwa anajulikana kwa jina la afande Frank. Askari aliyekuwa zamu jana usiku.
Inspekta John alimwangalia kwa muda yule askari aliyekuwa mgeni pale kituoni. Kisha aliongea kwa sauti kavu.
"Nambie nini kilitokea jana usiku?"
Afande Frank alikaa vizuri kitini huku akiongea "Afande mimi hata sielewi"
"Nakuuliza kwa mara ya pili. Kilitokea nini jana usiku?" Inspekta John aliongea huku akielekea kuufunga mlango kwa ndani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijikuta akiropoka kwa sauti yenye kihoro " Afande nahisi kuna njama hapa kituoni"
Inspekta John alikuwa anarudi kitini kutokea kule mlangoni
"Njama? Njama kivipi?" Alimuuliza akiwa anarejea kukaa kitini.
"Nani aliyenipigia simu?" Inspekta John aliuliza tena.
"Sijui" Wote walijibu kwa pamoja.
"Nani alikuwa zamu hapa usiku?"
Askari wawili walimuonesha askari mwenzao kwa kidole.
"Nakuhitaji ofisini" Inspekta John alisema huku akiongea.
Alitembea kama hatua tatu. Akasimama. Akageuka nyuma, aliongea tena "Mpigieni daktari akishafanya mambo yake pigeni picha kila kitu kilivyo humu ndani. Then muite wahudumu wasafishe, na huyo jamaa mpelekeni hospitali. Kuweni makini lakini"
"Sawa afande" Askari wale wawili waliobaki waliitikia kwa pamoja.
Katika viti viwili vilivyokuwepo ofisini kwa inspekta John vilikuwa vimekaliwa na askari wawili. Kimoja kilikaliwa na Inspekta John mwenyewe na kingine kilikuwa kimekaliwa na askari mrefu mweusi. Alikuwa anajulikana kwa jina la afande Frank. Askari aliyekuwa zamu jana usiku.
Inspekta John alimwangalia kwa muda yule askari aliyekuwa mgeni pale kituoni. Kisha aliongea kwa sauti kavu.
"Nambie nini kilitokea jana usiku?"
Afande Frank alikaa vizuri kitini huku akiongea "Afande mimi hata sielewi"
"Nakuuliza kwa mara ya pili. Kilitokea nini jana usiku?" Inspekta John aliongea huku akielekea kuufunga mlango kwa ndani.
Afande Frank aliogopa sana. Alishazisikia sifa za Inspekta John tangu siku ya kwanza tu alipohamia katika kituo cha Polisi Mbozi. Kwamba hapendi utani. Hataki mas'hara katika kazi. Anaweza kukufanya lolote lile ukitaka kumuharibia kazi. Sasa kufungwa kwa mlango ilidhihirisha hali ya hatari kwake.
Alijikuta akiropoka kwa sauti yenye kihoro " Afande nahisi kuna njama hapa kituoni"
Inspekta John alikuwa anarudi kitini kutokea kule mlangoni CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Njama? Njama kivipi?" Alimuuliza akiwa anarejea kitini.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment