Simulizi : Biashara Ya Kifo
Sehemu Ya Tatu (3)
Afande Frank aliongea huku sura yake ikiwa imetamalaki hofu, woga na wasiwasi " Ndio afande. Kuna njama na njama hiyo inaongozwa na Afande Ghalib"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Njama kuhusu nini? Kwanini kuwe na njama? Inafanyikaje hiyo njama? Kwa lengo gani? Kwa faida ya nani?" Maswali mfululizo yalimtoka Inspekta John.
"Unasikia afande, wakati naingia shift jana, afande Ghalib aliniita pembeni, kule nyuma ya mwembe. Akanambia kwamba atamleta mtu ambaye nimuingize selo kwa muda kisha nimtoe. Mimi nilikataa kwa kuwa haukuwa utaratibu wa jeshi la Polisi kumuingiza mtu selo bila kosa. Nilikataa katakata kuruhusu raia aingizwe selo bila ya kuwa na kosa. Afande Ghalib aliondoka kwa hasira. Neno lake la mwisho nililolisikia ni 'Utaona'"
Afande Frank aliendelea " Baada ya dakika zisizozidi kumi na tatu afande Ghalib alirejea tena kituoni. Safari hii akiwa na mtu, ambaye yeye alidai ni mhalifu. Tulibishana na mimi kwa utaratibu akiotaka kuutumia. Alikuwa anataka kumuweka selo yule mtu bila kuandika maelezo yoyote katika kitabu. Ndipo huku akiwa na hasira aliandika kuwa yule jamaa alikuwa katoa lugha chafu mtaani, alimkuta anamtukana mwenzie, lakini cha ajabu hakuwepo huyo aliyedaiwa kutukanwa ama mlalamikaji"
Afande Frank alimeza funda la mate kisha aliendelea " Mimi nilikuwa na wasiwasi mwingi moyoni mwangu. Nikijua kuna kitu kati yake na yule mtu" Aliangalia juu na kusema kwa sauti ndogondogo " Yule jamaa bila shaka ndiye aliyemuua yule mzee mle selo, kamchinja vibaya sana!"
"Unasemaje afande? Una hakika yule jamaa mpiga makelele ndo muuaji?"
"Hakika afande na nilimuona kwa macho yangu akimkaba yule mzee..."
Alimkatisha "Sasa katumia silaha gani mpaka kumchinja mtu namna ile na selo hamna silaha?"
"Afande Ghalib hakumpekua. Alimuingiza vivyo hivyo. Jamaa aliingia na kisu selo. Nilimuona alivyokuwa akimkatakata mithili ya nyama buchani"
"Ngoja, ngoja niwafatilie. Tusipoteze muda kuongea hapa" Inspekta John alisema huku akinyanyuka kitini.
Harakaharaka Inspekta John aliitoa bastola yake, aliishika imara mkononi na kuelekea ule upande wa selo. Akimwacha afande Frank kapigwa na butwaa juu ya kiti.
Inspekta John alifika mle selo. Lakini hakukuwa na mtu. Kuanzia mapokezi hadi ndani ya selo hakukuwa na mtu yeyote yule. Hakuna raia, hakuna askari. Kwa mwendo wa haraka alienda kuchungulia mle ndani ya selo. Hata maiti ya mzee Mwamaja haikuwepo!
Alizungusha macho yake mle ndani ya selo. Aliangalia kila kona ya selo. Sehemu zote kulikokuwa na viungo vya mwili Wa mzee Mwamaja. Hakukuwa na kiungo hata kimoja.
Na la zaidi, hakukuwa hata tone la damu.
Alikumbuka "Au wasafishaji washakuja kusafisha. Inawezekana kweli kwa muda mfupi kama huu ikawa washafanya nilichowaagiza?"
Alitoka nje mkuu mkuu na bastola yake mkononi. Katikati ya baraza ya Polisi alikutana na mwili wa askari mmoja ukiwa hauna uhai.
Alibabaika sana. Alikosa uelekeo maalum wa kwenda, alibaki amesimama tu.
Harakaharaka alitoa simu yake ya mkononi. Alibofyabofya kidogo, kisha akaiweka sikioni.
Alianza kuongea "Inspekta John hapa naongea .." Akatulia kusikikiliza.
Aliongea tena "Hii kesi imekuwa maji marefu sana, nataka niongee na mkuu akujumuishe katika timu, tuifanye wote..kesi ina utata mwingi sana" Alitulia kusikiliza tena simu.
"Ngumu ngumu..hapa nilipo yaani nimezungukwa na maiti. Halafu nahisi askari wangu mmoja ametoroka na mhalifu wa hii kesi"
Baada ya kutulia na kusikiliza aliongea tena "Basi ngoja niongee na mkuu, Inspekta Jasmine nakuhitaji sana uje kutatua utata, jioni nitakupigia nikwambie tumefikia wapi"
Simu ikakatwa.
Ilivyokatika simu ya Inspekta Jasmine, simu nyingine iliingia katika simu ya Inspekta John. Safari hii alipigiwa yeye.
Hakuongea yeye alikuwa msikilizaji tu baada ya kuipokea simu hiyo simu iliongea
"Msamaria mwema hapa, kuna maiti ya askari imeokotwa katika uwanja wa shule ya msingi Njombe"
"Wewe nani?" Inspekta John aliuliza.
"Nimekwambia Msamaria mwema! Umekuwa kiziwi afande" Jamaa alijibu kwa ukali.
Simu ilikatwa.
****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********
*************
Inspekta Jasmine alivyofika tu Mbozi. Hakulaza damu. Aliingia kazini moja kwa moja. Shabaha yake ya kwanza ilikuwa ni kwenda katika kumbi za starehe. Alijua katika kumbi za starehe kuna mengi. Mara nyingi watu wema huenda katika kumbi za starehe. Watu wabaya hukutana katika kumbi za starehe. Watu wema kuufurahia wema wao. Watu wabaya kujipoza na mambo yao mabaya.
Inspekta Jasmine kila siku alibadilisha kiwanja cha kujirusha. Leo hapa, kesho kule. Ilipita wiki bado hakupiga hatua yoyote katika upelelezi wake. Labda angekutana na Inspekta John kabla angepata ABC za mkasa huu wa kitata.
Ni wiki mbili zilikuwa zimepita tangu msako wa kuwasaka wauaji uanze chini ya Inspekta John. Lakini bado askari polisi wala wapelelezi hawakupata bahati ya kukaribiana na wauaji. Tangu tukio lile la mauaji hawakuuwa tena. Ilikuwa kama wauaji wametokomea kabisa Mbozi. Hali ilikuwa shwari. Watu walianza kutembea usiku kama kawaida. Bila uwoga, bila hofu yoyote. Walihisi wauaji wamekimbia ndani ya Mbozi.
Ilikuwa siku ya ijumaa usiku. Siku ya 'weekend' ambayo huwakutanisha watu mbalimbali katika kumbi za starehe.
Ijumaa hiyo ilimkuta Inspekta Jasmine katika baa ya Mbozi Night. Alikuwa katika mavazi ambayo hakuna jicho lililomhusisha yeye na askari Polisi.
Alikuwa amevaa suruali fupi aina ya jeans nyeupe. Jeans iliyomkaa vyema sana katika mwili wake. Juu alikuwa amevaa blauzi fupi nyeupe. Blauzi isiyoruhusu kufunika hata tumbo lake. Umbo lake, rangi yake vilifanya awe mwanamke mrembo sana katika baa hiyo. Macho ya wanaume wakware yalikuwa yanapishana katika meza aliyokuwa amekaa Inspekta Jasmine. Meza iliyokaliwa na mtu mmoja tu, Inspekta Jasmine peke yake.
Inspekta Jasmine alivyofika tu Mbozi. Hakulaza damu. Aliingia kazini moja kwa moja. Shabaha yake ya kwanza ilikuwa ni kwenda katika kumbi za starehe. Alijua katika kumbi za starehe kuna mengi. Mara nyingi watu wema huenda katika kumbi za starehe. Watu wabaya hukutana katika kumbi za starehe. Watu wema kuufurahia wema wao. Watu wabaya kujipoza na mambo yao mabaya.
Inspekta Jasmine kila siku alibadilisha kiwanja cha kujirusha. Leo hapa, kesho kule. Ilipita wiki bado hakupiga hatua yoyote katika upelelezi wake. Labda angekutana na Inspekta John kabla angepata ABC za mkasa huu wa kitata.
Ni wiki mbili zilikuwa zimepita tangu msako wa kuwasaka wauaji uanze chini ya Inspekta John. Lakini bado askari polisi wala wapelelezi hawakupata bahati ya kukaribiana na wauaji. Tangu tukio lile la mauaji hawakuuwa tena. Ilikuwa kama wauaji wametokomea kabisa Mbozi. Hali ilikuwa shwari. Watu walianza kutembea usiku kama kawaida. Bila uwoga, bila hofu yoyote. Walihisi wauaji wamekimbia ndani ya Mbozi.
Ilikuwa siku ya ijumaa usiku. Siku ya 'weekend' ambayo huwakutanisha watu mbalimbali katika kumbi za starehe.
Ijumaa hiyo ilimkuta Inspekta Jasmine katika baa ya Mbozi Night. Alikuwa katika mavazi ambayo hakuna jicho lililomhusisha yeye na askari Polisi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuwa amevaa suruali fupi aina ya jeans nyeupe. Jeans iliyomkaa vyema sana katika mwili wake. Juu alikuwa amevaa blauzi fupi nyeupe. Blauzi isiyoruhusu kufunika hata tumbo lake. Umbo lake, rangi yake vilifanya awe mwanamke mrembo sana katika baa hiyo. Macho ya wanaume wakware yalikuwa yanapishana katika meza aliyokuwa amekaa Inspekta Jasmine. Meza iliyokaliwa na mtu mmoja tu, Inspekta Jasmine peke yake.
Jasmine alikuwa ametulia tuli katika kiti cha plastiki cha ile baa, huku juu ya meza yake kukiwa na chupa ya soda aina ya spirite ambapo soda ilikuwa ipo nusu. Macho yake ya kiaskari yakiwa hayatulii. Yalikuwa yanaangalia huku na kule. Kuona kama kuna lolote lile la kujazia katika upelelezi wake.
Pamoja kwamba zilikuwa zimepita siku kadhaa bila ya kutokea mauaji mengine ya namna ile pale Mbozi. Lakini Inspekta Jasmine aliamini mji wa Mbozi ndio utakaomsogeza karibu na wauaji. Hata kama wamekimbia, lakini Mbozi ndio patakuwa mahala sahihi ya kuwajua wauaji. Aliamua kuweka kambi Mbozi.
Wakati Inspekta Jasmine akiwa anapiga funda la soda yake, ndipo alipopokea ugeni katika meza yake. Alikuwa ni mwanaume mrefu, mweusi. Aliyekuwa amevaa suruali ya kitambaa nyeusi na shati jeupe lenye ufito wa rangi nyekundu katika kola yake. Jamaa alivuta kiti kimadaha na kukaa katika kiti mbele ya Inspekta Jasmine bila ya kukaribishwa.
Inspekta Jasmine alimwangalia yule jamaa kwa macho ya mshangao. Iweje aje kukaa tu kwenye meza yake bila ya kuomba, bila ya kukaribishwa na mwenyeji wake. Alitokea kuuhusudu ujasiri wa yule mwanaume. Ni wanaume wachache wenye ujasiri wa aina ile.
"Naitwa Malolo, Abdalah Malolo" Jamaa alijitambulisha tena bila kuulizwa kwa sauti nzito, sauti ya kiume ya kujiamini. Alijitambulisha kwa jina lake sahihi.
Inspekta Jasmine alimwangalia tu yule jamaa bila ya kuongea lolote.
"Habari yako Dada" Malolo aliamua kubadilisha namna ya kujitambulisha. Safari hii alisalimia.
"Safi tu" Inspekta Jasmine alijibu huku akitabasamu.
"Mbona unanicheka sasa?" Malolo aliuliza huku naye akitabasamu.
"Hapana sikucheki. Umenifurahisha tu" Inspekta Jasmine alijibu huku akielekea kupendezwa na ujio wa yule jamaa.
"Samahani kwa kukuvamia katika meza yako. Nilikuona upo alone nikaona nije nikupe kampani au una miadi na mtu?" Malolo alichokoza.
"Hapana sina miadi na mtu, nipo mwenyewe tu" Jasmine alijibu kwa sauti ya kudeka.
"Bila shaka unaitwa Juliana?" Malolo alibahatisha.
"We kakwambia nani naitwa Juliana?" Inspekta Jasmine alijibu akiwa na tabasamu tele.
"Nimebahatisha tu. Maana una urembo wa kufanana na jina hilo"
"Hapana siitwi Juliana"
"Unaitwa nani sasa?"
"Naitwa Jasmine" Inspekta Jasmine nae alijitambulisha kwa jina lake sahihi.
"Kumbe waitwa Jasmine, mimi nilisema Juliana...lakini majina yote mazuri tu, majina ya kirembo yanayostahili kuvikwa warembo, warembo kama wewe..." Malolo alisema huku akitabasamu. Tabasamu ndio lilikuwa silaha yake kubwa Malolo kwa watoto wa kike.
"Kaka una maneno wewe..." Inspekta Jasmine alisema kwa kudeka. Alionekana kuvurugwa na tabasamu la Malolo.
Maongezi yao yaliendelea. Walizungumzia kuhusu maisha, changamoto mbalimbali za maisha. Walizungumzia kuhusu siasa za nchi, hawakusahau pia kuzungumzia kuhusu muziki, walizungumza kuhusu filamu za kibongo. Walizumgumzia kuhusu riwaya za Tanzania. Walibishana hapa na pale, walikubaliana mara kadhaa. Wote walionesha umahiri mkubwa katika kujua mambo mbalimbali ya dunia. Walijikuta wameendana sana. Walielewana kupita kiasi. Na zaidi walianza kupendana kiukweliukweli. Kupendana kwa moyo wote, ile hali ya kutotamani mmoja aondoke iliwavaa ghafla. Walitamani kuwa pamoja tu muda wote. Kila mmoja asikie sauti ya mwenziwe ikirindima katika masikio yake, amguse mwenzie inapobidi. Ampigepige begani, amkonyeze kwa hisia.
Hali ilivyo sasa hata mtu mgeni asingeamini angeambiwa kama watu wale walikuwa hawajuani hapo kabla, walijuana siku ileile. Ilikuwa ngumu sana kuamini, maana walikuwa wameendana kama chanda na pete.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Cha ajabu na cha kushangaza, macho ya kihalifu ya Malolo. Macho hatari sana kwa kutambua hatari yalishindwa kumtambua Inspekta Jasmine kama askari. Kutambua kama mtu aliyekuwepo mbele yake ni hatari kwake. Pia macho ya kiaskari ya Inspekta Jasmine, macho yaliyofundishwa kumjua mhalifu kwa kumuona tu yalishindwa kumtambua Malolo kama alikuwa Mhalifu. Tena ni miongoni mwa wahalifu aliokwenda kuwatafuta Mbozi kwa udi na uvumba. Saikolojia zao zilishindwa kufanya kazi dhidi ya mapenzi. Mapenzi yaliziteka nyoyo zao.
Maana sasa walipendana kweli.
Katikati ya maongezi yao ilitokea Malolo akauliza.
"Hivi haujanambia unafanya kazi gani mrembo wangu Jasmine?"
"Mimi ni mfanyakazi wa benki ya NMB pale tawi la Kabwe, Mbeya mjini, ni mhasibu, ila kwasasa nipo likizo" Hapo ndipo kwa mara ya kwanza Inspekta Jasmine alimdanganya Malolo.
"Na wewe" Inspekta Jasmine nae alitaka jibu la swali lilelile aliloulizwa yeye.
"Ni mfanyabiashara wa madini huko Geita, namekuja Mbozi kuwasalimia wazee wangu, baba na mama yangu wanaishi huku.." Malolo nae alidanganya.
Waliendelea kunywa bia hadi saa sita usiku.
"Naona muda umekwenda sana, nataka kwenda home" Jasmine alisema huku akimwangalia Malolo kwa jicho la huba.
"Nikusindikize?" Malolo aliuliza kimtego.
"Kama haitokusumbua" Jasmine alinasa katika mtego.
"Siwezi kusumbuka kumsindikiza mwanamke mrembo kama wewe" Malolo aliongea wakati akiwa katika jitihada za kunyanyuka.
Jasmine alicheka huku nae akinyanyuka.
Walitoka nje.
Kwa kutumia gari ya Inspekta Jasmine waliondoka katika ile baa ya Mbozi by Night. Malolo ndiye alikuwa dereva, alikuwa ametulia tuli katika usukani.
"Hivi sitopigwa kweli huko nyumbani kwako?" Malolo alimchokoza Jasmine wakiwa njiani.
"Malolo bwana sa upigwe na nani, am single lady" Jasmine alisema huku akicheka.
"Mwanamke mrembo kama wewe uko single kweli, usiwe mtego wa panya?" Malolo alitania.
"Si tunaenda home, utaamini"
Kikapita kimya kidogo.
"Hivi hatokuuliza kweli?" Inspekta Jasmine safari hii yeye ndiye alichokoza.
"Kuniuliza nani? Aniulize nini?" Malolo aliuliza kujifanya hajaiwelewa dhamira ya Jasmine, wakati alikuwa kashamuelewa.
"Si wifi yangu"
"Ajiulize mwenyewe sasa?"
"Sijakuelewa Malolo" Jasmine alisema huku akimgeukia Malolo.
"Wifi yako nipo nae ndani ya gari" Malolo alisema huku akijifanya yuko bize na kuendesha gari.
"Mmmh umeanza utani wako Malolo" Jasmine alisema kwa kudeka.
"Au hutaki nishuke?"
Jasmine hakujibu.
Kama utani kuanzia usiku ule Malolo na Inspekta Jasmine waliingia katika uhusiano wa kimapenzi. Walilala pamoja siku ile na baadhi ya siku zilizofuata walizoamua wenyewe. Kila mmoja alikuwa makini sana. Hakutaka kuweka wazi vitu walivyoamua kuvificha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wiki moja baada ya uhusiano huo ndipo lilitokea pigo ndani ya Mbozi. Wanafunzi wa shule ya sekondari Tegeta walioenda katika ziara ya kimasomo Mbozi walipotea. Walienda kuangalia mahali kilipoanguka kimondo. Lori lililokuwa na wanafunzi wasiopungua hamsini halikujulikana lilipoelekea.
Hofu na woga zilirejea tena Mbozi. Kila mmoja alikuwa anasubiri habari mbaya juu ya wanafunzi hao.
Siku ya tatu baada ya kupotea lori hilo ndipo majibu ya wanambozi yalijibiwa. Maiti za wanafunzi zilikutwa zimelazwa katika soko la Mbozi. Maiti hamsini za wanafunzi zikiwa hazina ngozi. Maiti zililetwa na nani? Maiti zililetwa saa ngapi? Kwanini maiti zililetwa sokoni? Hakuna mtu aliyekuwa na majibu juu ya maswali hayo...
Baada ya tukio hilo Inspekta Jasmine aliingia kazini. Aliingia mtaani kuwasaka wauaji walioonekana kufanya kazi yao kwa kuvizia. Walikuwa wanafanya matukio kwa kustukiza. Inspekta Jasmine kwa siri kubwa sana alikuwa anapeleleza, bila kujua kwamba miongoni mwa wahusika wa mauaji hayo alikuwa analala nae kitanda kimoja, anajifunika nae shuka.
Upande wa kina Malkia na kundi lake walikuwa na furaha tele. Don Genge alikuwa anawapongeza kila sekunde, alikuwa na furaha kila dakika . Walikuwa wamepiga pigo muja'rabu, na bado walikuwa salama. Mikono ya Polisi ilikuwa mbali sana na wao. Lakini pamoja yote hayo walikuwa hawajui kwamba mmoja wa mshirika wao alikuwa analala kitanda kimoja na mpelelezi mahiri wa kike nchini Tanzania.
Jioni iliyofuata baada ya kutupwa maiti za wanafunzi wa shule ya Sekondari sokoni Mbozi ilimkuta Inspekta Jasmine akiwa mbele ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya. Kamanda alikuwa anamfokea Inspekta Jasmine kwa kushindwa kupiga hatua yoyote zaidi ya mwezi katika kutatua tatizo hili. Na mbaya zaidi mauaji yalikuwa yanaendelea kutokea.
" Afande Jasmine umekuja kazini ama umekuja kustarehe huku Mbozi?" Mkuu wa Polisi alikuwa anamuuliza Inspekta Jasmine bila ya kumuangalia usoni. Alikuwa yuko bize anachambua mafaili yaliyokuwa mezani.
"Nimekuja kazini afande"Inspekta Jasmine alijibu kwa kunyenyekea.
" Kazi ya kuhakikisha mauaji ya kinyama yanaendelea hapa Mbozi?" Mkuu wa Polisi alimuuliza safari hii akinyanyua sura yake kumuangalia Inspekta Jasmine.
"Hapana afande. Kuhakikisha mauaji yanakoma. Na wauaji wanapelekwa mbele ya vyombo vya dola, wakahukumiwe"
"Nikisema umeishindwa hiyo kazi uliyoisema nitakuwa nakosea?"
"Sijashindwa kazi afande"
"Sasa nataka nikupe timeframe, no nataka ujipe timeframe, sema mwenyewe utaifanya hii kazi kwa siku ngapi? Na kuikamilisha kabisa!"
"Nipe wiki mbili afande"
"Nakuongeza wiki mbili zingine, itakuwa wiki nne..hakikisha unawaleta wauaji mbele ya meza yangu hapa. Nakupa mwezi huu, mmoja"
"Punguza hizo mbili Mkuu. Nakuletea wauaji hapa ndani ya wiki mbili tu"
"Inspekta neno langu ni amri!"
"Sawa afande" Inspekta Jasmine alisema kwa kunyenyekea.
Waliagana.
Inspekta Jasmine alitoka ndani ya ofisi ya RPC akiwa na lengo la kumuonesha yeye ni nani? Alipanga kuhakikisha anawakamata wauaji hatari, wauaji wanaoondoka na ngozi za binadamu ndani ya wiki mbili.
Alivyotoka nje ya ofisi ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya. Inspekta Jasmine alipanda pikipiki yake na kuelekea nyumbani kwake. Alipofika alimkuta Malolo akiwa bado amelala kitandani. Inspekta Jasmine nae alikaa kitandani, akimwangalia mpenzi wake aliyetokea kumpenda kwa muda mfupi sana, tena kumpenda pasi na kifano.
Baada ya kumwangalia kama dakika tatu. Alimwinamia. Alimpiga busu katika papi za midomo ya Malolo huku akitamka kwa sauti ndogo sana "Nakupenda sana Malolo"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alinyanyuka kitandani, alilisogelea kabati lake kubwa lililokuwepo ukutani karibu na dirisha. Alifungua kabati na kuchukua vitu kadhaa. Vitu vya kazi. Aliviweka kwenye begi lake dogo. Alirudi tena kitandani. Alikaa na kumwangalia tena mpenzi wake Malolo. Alikuwa anawaza amuage ama asimuage. Amuamshe ama asimuamshe. Sauti ya ndani ya moyo wake ilimwambia asimuamshe. Inspekta Jasmine alifungua mlango na kwenda kazini. Na alidhamiria kuwa kazini mpaka ahakikishe anawatia mikononi wauaji.
Kitu ambacho Inspekta Jasmine alikuwa hakijui, Malolo alikuwa hajalala hata kidogo. Kwa jicho la wizi alishuhudia kilakitu alichokuwa anakifanya Jasmine. Alizidi kumpenda pale alipopigwa busu shavuni. Alisisimka alipoisikia sauti ya Jasmine ikimwambia inampenda akiwa usingizini. Aliamini mwanamke yule kweli alikuwa anampenda kwa dhati. Alimuona Jasmine alipoenda mbele ya kabati, na kutoa vitu kadhaa kabatini na kuviweka katika begi yake, ingawa hakujua ni vitu gani alivyovichukua mpenzi wake. Kwa macho yake yote mawili alimuona Jasmine wakati anatoka nje bila kumuaga. Ghafla...Hisia za wivu zikamvaa. Hisia za kusalitiwa zikaunasa moyo wake
"Jasmine anakwenda kunisaliti" Alijisema kimoyomoyo.
Sekunde hiyohiyo alikurupuka toka kitandani na kuvaa nguo zake harakaharaka. Aliamua kumfatilia kwa siri mahali alikokuwa anaenda mpenzi wake, Jasmine wake. Na kichwani mwake lilimjia neno moja tu 'fumanizi'
Pikipiki ya Inspekta Jasmine ilikuwa mbele. Gari ya Malolo ilikuwa nyuma ikipitwa na kama magari mawili kuifikia pale ilipokuwa pikipiki ya Jasmine. Inspekta Jasmine alikuwa anaenda kazini. Malolo alikuwa anaenda kumfumania mpenzi wake...
Safari ya Inspekta Jasmine ilikomea katika gesti moja ndogo sana iliyopo katika mitaa ya uswahili katika mji wa Mbozi. Jina la kibao cha guest lenye rangi ya bluu, huku maandishi yakiwa yameandikwa kwa rangi nyeusi yalisomeka 'Uchochoroni Guest House'
Baada ya dakika kumi, ya kuongea na msichana aliyemkuta katika dirisha dogo ambaye ndiye alikuwa mhudumu katika gesti ya Uchochoroni, Inspekta Jasmine alikuwa ndani ya chumba chake kidogo cha nyumba hiyo ya kulala wageni ya uswahili. Alikuwa amekaa katika kitanda kidogo, mbele yake alikuwa anatazama na samani pekee iliyokuwepo katika chumba kile ukitoa kitanda, kilikuwa kisturi kidogo kilichochakaa, aliliweka begi lake juu ya ile sturi.
Malolo nae alipaki gari yake mbele kidogo ya nyumba ileile ya kulala wageni ya Uchochoroni. Baada ya kuli'lock' gari lake na kuhakikisha lipo sehemu salama alirudi kwa miguu hadi katika gesti aliyomuona anaingia mpenzi wake Jasmine, nae alipanga chumba katika guest ileile. Nae alikaa katika kitanda kidogo mithili ya kile alichokuwa amekaa Jasmine, kichwani kwake, alikuwa akipanga vizuri fumanizi lake.
Malolo alihakikisha Jasmine atoki nje bila ya yeye kumuona. Huku akiwa makini pia kuhakikisha anamuona mtu yeyote atakayeingia katika kile chumba alichokuwemo Jasmine.
Baada ya kusubiri na kusubiri, kusubiri sana alihisi labda mwanaume wa Jasmine atakuwa ndiye aliyeanza kuingia mle chumbani kabla ya Jasmine.
Saa tatu usiku Malolo alitoka chumbani kwake, alifunga kwa nje mlango wa chumba chake na kuelekea katika chumba alichokuwa amepanga Jasmine...
Alipanga kwenda kufanya kitu alichokuwa anakiwaza kichwani mwake.
Na alipania kweli!
Malolo alifika hadi pale mlangoni. Katika chumba ambacho Jasmine alikuwa ndani yake.
Aligonga.
Kilipita kimya.
Akagonga tena.
Kikapita kimya kingine.
Hakuna aliyeenda kufungua.
Aligonga kwa mara ya tatu, safari hii kwa nguvu zaidi tofauti ni zile mara mbili za awali.
Bado ilikuwa kimya.
Alifikiria harakaharaka nini cha kufanya, hakutaka kuamini kabisa kwamba hakukuwa na mtu mle chumbani. Aliamini mpenzi wake alikuwepo mle ndani. Alimuona tena kwa macho yake Jasmine wake akiingia mle chumbani, na hakumuona Jasmine kutoka. Hisia za wivu zilizidi kuutafuna moyo wake, hisia za kusalitiwa zilimkaba kohoni. Alihisi kutetemeka kwa wivu.
"Lazima atakuwa humu ndani" Alijisemea kimoyomoyo.
"Tena bila shaka atakuwa na mwanaume" Alipowaza hivyo hisia za wivu zilizidi kumvaa.
Wivu wa kuibiwa mwanamke anayempenda kwa moyo wake wote. Mwanamke anayempenda kuliko kitu chochote kile. Alijihisi vibaya sana. Alihisi kusalitiwa, alihisi kudharauliwa.
Kwa mara ya kwanza katika maisha yake Malolo aliteswa na mapenzi, aliumizwa na mapenzi. Hakuweza kuvumilia chozi la wivu lisimtoke katika macho yake. Malolo alilia akiwa katikati ya mlango wa guest. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake Malolo alilizwa na mapenzi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa kama sio kunisaliti kwanini aje kujifungia katika gest hii dhaifu?" Alijiuliza mwenyewe, lakini hakupata jibu. Hakukuwa na wakumjibu.
"Navunja huu mlango!" Aliamua.
Aliuangalia ule mlango wa guest. Ulikuwa dhaifu sana. Alijua hauwezi kuhimili kabisa nguvu ya mguu wake hata wa kushoto. Alirudi nyuma hatua tatu. Alijipanga vizuri. Alienda kwa kasi akiutanguliza mguu wake wa kulia mbele. Mlango haukuweza kuhimili nguvu ya mguu wa Malolo. Ulikuwa mguu wa kiume, mguu wa nguvu. Malolo alijikuta yupo katikati ya chumba alichopanga mpenzi wake. Aliangalia kulia, akaangalia kushoto, kisha akaangalia mbele...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment