Search This Blog

Friday, 20 May 2022

BIASHARA YA KIFO - 4

 







    Simulizi : Biashara Ya Kifo

    Sehemu Ya Nne (4)



    Hakukuwa na mtu mle ndani. Alikuwa peke yake ndani ya chumba cha guest ya Uchochoroni. Aligeuka nyuma harakaharaka, bado hakukuwa na mtu, alikuwa anatazamana na sehemu ulipokuwa mlango hapo awali. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa mara ya kwanza katika maisha yake Malolo hakuyaamini macho yake. Hakuyaamini kabisa, alihisi yanamdanganya.



    "Jasmine kaenda wapi? Na kama kweli katoka, katoka saa ngapi?"



    Ghafla, alisikia sauti za miguu ya watu zikielekea upande kilipokuwa chumba alichokuwemo. Bila shaka walisikia kishindo cha teke la Malolo wakati akivunja mlango. Sauti za watu waliokuwa wanaenda zilitokea mbele ya guest ile, kwa kasi ya haraka, yeye alitoka mle chumbani, alivyofika katika korido ya nyumba ile ya kulala wageni alikimbia mbio kuelekea upande wa nyuma wa guest ile, mahali kulikuwa na bafu na choo cha nje.

    Alipishana na wale jamaa kwa sekunde chache sana, la sivyo wangekutana pale kwenye korido.



    Watu waliokuwa wanaenda kule chumbani, walikuwa watu watatu. Wahudumu wawili na mmiliki wa ile guest ya Uchochoroni. Walipofika mle chumbani, wote walishangaa jinsi mlango ulivyovunjwa kibabe, bila kujua lengo la mtu aliyevunja mlango ule.



    "Nani alipanga katika chumba hiki?" Mzee mmoja mfupi mweusi, ambaye ndiye alikuwa mmiliki wa ile guest aliuliza.



    "Dada mmoja hivi, mweupe" Yule mhudumu aliyekuwa mapokezi alijibu.



    "Ulimuona anatoka huyo dada?" Mmiliki wa ile guest aliuliza tena.



    "Mmh sidhani, maana hakuniaga kama anatoka, na wala hajakabidhi funguo kama kweli alitoka"



    "Kwahiyo bila shaka atakuwa humuhumu ndani?" Mhudumu mwengine wa kiume alidakia.



    "Bila shaka, inawezekana kaenda chooni" Yule dada wa mapokezi alijibu.



    Dakika kumi baadae watu walijaa katika chumba kile kilichovunjwa mlango. Miongoni mwa watu hao alikuwepo Malolo. Naye akijifanya kushangaa uwezo wa mtu aliyevunja ule mlango. Malolo alikuwa anaushangaa uwezo wake mwenyewe.

    Alikaa pale dakika zipatazo mbili, hakupata alichokitaka, akaondoka zake kimyakimya. Huku akiwa haelewi Jasmine alitoka vipi ndani ya guest ile.



    Malolo alienda mahali alikopaki gari yake na moja kwa moja alirejea nyumbani kwa Jasmine.

    Aliingia ndani, aliiona runinga ikionesha sawa na alivyoiacha, hakuizima. Alielekea chumbani huku akiwa kichwa kakiinamisha chini, na mawazo lukuki ya kusalitiwa yakikiandama kichwa chake. Alipofika chumbani, ndipo alipomuona...

    Alimuona Jasmine akiwa katika nguo za kulalia kalala kifudifudi kitandani. Akiwa hana habari kabisa na yanayotendeka duniani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Malolo alisimama wima pembeni ya kitandani. Kwa mara ya pili sasa katika maisha yake alikuwa hayaamini macho yako. Mpenzi wake mwenyewe Jasmine alimchanganya, hakika alimchanganya sana.



    Baada ya dakika kama nne za kushangaa, kumshanga Jasmine alikuwa ametopea katika usingizi nzito, Malolo alirudi tena sebuleni, alikaa katika sofa kubwa akiwa amechoka kimawazo, amechoka kiakili.

    Hisia za wivu zilikuwa zinamuandamana. Hisia za kuibiwa mpenzi wake zilikuwa zinamsulubu vibaya sana. Hisia za kusalitiwa Jasmine wake zilimchimba moyoni mwake. Alikaa sofani akiwa kashika tama, mikono yake yote miwili imeyashika mashavu yake. Alikuwa hajielewi kabisa. Alikuwa anatazama ilipokuwa runinga lakini alikuwa haoni chochote kile. Pale ulikuwa mwili tu, yeye alikuwa mbali sana kimawazo.



    Jasmine alikuwa ametulia kitandani. Yeye alikuwa hamuwazi Malolo hata kidogo, alikuwa anawaza jinsi ya kazi ya kuwakamata wahalifu wachuna ngozi ilivyokuwa ngumu. Aliikumbuka ahadi yake aliyoiweka kwa RPC wa Mbeya...Lakini alikuwa na imani anaenda kuimaliza.



    Siku ile Inspekta Jasmine alikuwa amepiga hatua. Hatua kubwa tangu ainze kazi hii. Katika matembezi yake ya usiku kule katika guest ya uchochoroni alikutana na mtu aitwaye Peter Kissali. Ilikuwa kama bahati tu..



    Inspekta Jasmine baada ya kuingia tu mle chumbani katika ile guest hakukaa. Kwa usiri mkubwa sana alienda hadi uwani wa ile guest. Alikuwa anataka kutoka mle ndani bila ya kuonwa na jicho la mtu yeyote. Bila ya kuhisiwa na mtu yeyote. Alipanda ukuta dhaifu wa ile guest. Akiwa juu ya ukuta anataka kurukia kwa nje.



    Hapo ndipo alipomuona...







    Inspekta Jasmine alimuona mtu akiwa kamkaba mtu.

    Ilikuwa gizani lakini alimuona. Kwa macho yake alimshuhudia Jamaa mrefu akiwa amevaa koti jeusi kamkaba mtu mfupi aliyevaa suruali nyeusi na shati jeupe.

    Muda uleule Inspekta Jasmine aliamua kuingia kazini. Aliamua kufanya kazi aipendayo. Alishuka taratibu juu ya ukuta na kuanza kuwasogelea wale watu wawili bila kujua sababu ya watu wale kukabana.



    Yule jamaa mrefu ndiye alikuwa wa kwanza kuhisi kama wananyatiwa. Ghafla! Alitimua mbio huku akimuacha mtu mfupi amesimama palepale. Akiwa ameduwaa, haelewi amenusurika vipi kuuwawa kwa ile kabali muja'rabu.



    Baada ya kuelewa sababu ya yule mtu mrefu kukimbia kuwa ni ujio wa askari yule wa kike, mtu fupi ndiye aliyemueleza Inspekta Jasmine dhumuni la yule mtu mrefu.



    "Wale ndio wachuna ngozi!" Alisema akiwa amechanganyikiwa.



    "Umejuaje" Inspekta Jasmine aliuliza kwa wahka mkubwa.



    "Nimehisi tu" Mtu mfupi akasita, kuongea kidogo, kisha akaendelea".. Lakini bila shaka ni kweli alikuwa anataka kunichuna ngozi"



    "Sio atakuwa kibaka tu?" Inspekta Jasmine aliuliza.



    "Hapana, yule hakutaka kitu chochote toka kwangu, zaidi ya ngozi yangu" Mtu mfupi alijibu.



    "Aiseee"



    "Lakini wakati ananikaba nilifanikiwa kuingiza mkono katika koti, nimechukua hiki" Mtu mfupi alisema huku akimkabidhi kitu Inspekta Jasmine.



    Inspekta Jasmine alikipokea. Kilikuwa kitambulisho. Harakaharaka macho ya Inspekta Jasmine yalitua sehemu lilipoandikwa jina la mmiliki wa kitambulisho hiko ..........alikuwa anaitwa Peter Kissali!



    Patamu hapo.



    Sasa Inspekta Jasmine alikuwa na jina la mmoja ya watu wachuna ngozi kama alivyoaminishwa na mtu mfupi.



    Na muda uleule aliamua kurudi nyumbani kwake, huku akipanga kesho aanze kumsaka mtu aitwaye Peter Kissali. Alijipongeza kwa hatua yake ya kwenda kule kwenye guest ya Uchororoni, huku akiwa hana habari kabisa na mambo yaliyotokea katika chumba alichopanga.



    "Peter Kissali, kesho nina kazi ya kumtafuta binadamu mwenye jina hilo na kabla ya saa nne asubuhi natakiwa kumtia mkononi!" Inspekta Jasmine aliongea wakati akienda ukumbini, kwa mpenzi wake ampendae kwa dhati Malolo.



    Alikuwa anaenda kimya kimya, alipita katika korido ndefu ya nyumba ile aliyopewa na jeshi la Polisi kwa muda. Aliushika mlango wa kuingia katika mlango wa kuingia sebuleni. Alisita baada ya kumsikia mtu akiongea na simu. Alipatwa na hamu ya kusikiliza kilichokuwa kinaongelewa na Malolo usiku ule. Hisia za wivu nae zilimnasa. Alitulia tuli akisikiliza. Kwa sauti ndogo ikiyopenya pale kwenye uwazi mdogo wa mlango alisikia.



    ".....kwa hiyo ilikuwa nusra ukamatwe Peter?"

    Malolo alitulia kidogo akisikiliza.



    Akasema "Sasa kwanini uliamua kufanya hii kazi out of our plan, halafu uko alone master, ni hatari sana"



    Malolo alikaa kimya. Alikuwa anasikiliza tena.



    Baada ya muda kidogo aliongea "Kwahiyo jamaa alikutoa baru kabisa, vipi hujaacha ushahidi wowote?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Kama hujaacha ushahidi ni vizuri, ila take care Peter"



    Baada ya maongezi kidogo simu ilikatwa.



    Na ndipo Inspekta Jasmine alipofungua mlango kwa pupa na kuingia sebuleni.



    Inspekta Jasmine aliingia na swali sebuleni "Who is Peter, Malolo?"



    Malolo aligeuka kumwangalia Jasmine huku akiwa ametahayari.



    "Peter?" Malolo nae alijifanya kuuliza.



    "Ulikuwa unaongea na nani? Saa nane ya usiku hii, unaongea na nani?, na mnaongelea nini?, kwanini?" Jasmine alibadilisha aina ya maswali.



    "Ulienda wapi Jasmine?" Malolo nae aliuliza swali.



    "Swali halijibiwi kwa swali Malolo"



    "Nilikuwa naongea na Peter Ki.." Hakumaliza kutamka,



    Mara simu yake ya mkononi iliita. Juu ya kioo cha simu ya Malolo lilionekana jina la Peter.

    Kivumbi.

    Malolo Aliiangalia simu yake kama kitu cha kushangaza sana. Alikuwa anatamani kuipokea lakini alikuwa anamhofia mpenzi wake Jasmine. Walikuwa na mtafaruku kuhusu Peter na sasa Peter alikuwa anapiga tena simu.



    "Pokea simu yako!" Jasmine alisema kwa hasira.



    "Nitapokea tuongee kwanza mpenzi wangu" Malolo alijitetea.



    "If its true you love me pokea simu Malolo..." Sasa Jasmine aliongea kwa sauti ya kulalamika.



    Malolo alinasa. Hana aliamualo.



    "Pick up your phone my love" Jasmine alisisitiza kwa kiingereza.



    Malolo aliingalia simu, akamwangalia Jasmine. Hakuwa na maamuzi sahihi.

    Na simu ikakata.



    Saa nane ya usiku uhusiano huu wa mapenzi uliingia katika kashikashi kubwa sana. Hisia za wivu zikiwatawala wapenzi hawa. Hisia za kusalitiana. Hisia mbaya sana katika uhusiano. Kila mmoja alikuwa hamuamini mwenzie.



    Mara simu ya Malolo ilitoa mlio, mlio ambao Jasmine aliufahamu vyema, ulikuwa ujumbe kuashiria kwamba kuna ujumbe wa maandishi umeingia katika simu ile.

    Na ilikuwa hivyo kweli.

    Ujumbe mfupi uliingia katika simu ya Peter.

    Macho manne yalitua pale mezani ilipokuwa simu ya Malolo. Kila mmoja akitamani kuusoma ujumbe ulioingia katika simu ile. Wakati Malolo akipeleka mkono wake kulia pale mezani kuichukua simu, na Jasmine alipeleka mkono wake wa kushoto palepale mezani kuichukua simu. Sasa wote walikuwa wameishika simu. Wakinyang'anyana.



    Malolo hakuwa tayari kabisa kuiachia simu. Alijua bila shaka meseji itakuwa imetoka kwa Peter, na kwa vyovyote vile ujumbe ule utakuwa unahusu juu ya ule uvamizi uliotokea kule katika guest ya uchochoroni. Taarifa ambazo katu hakutaka Jasmine azifahamu, kivyovyote vile hakuwa tayari. Zilikuwa ni taarifa za siri, na Jasmine hakuruhusiwa kabisa kuijua siri hiyo...



    "Achia simu Malolo!" Jasmine alisema kwa jazba.



    Malolo alikaa kimya. Akijitahidi kwa nguvu kuitoa ile simu mikononi mwa Jasmine. Jasmine nae alikuwa kaishika bara'bara! Kaishika kwa nguvu zake zote!



    "Kumbe Malolo hunipendi?" Jasmine alisema kwa ukali huku bado akiwa kaing'anga'ania simu.



    "Nakupenda sana" Malolo alijibu kifupi.



    "Basi naomba aachia hii simu kama kweli unanipenda" Jasmine alitupa karata yake.



    "Simu siachii!" Malolo nae akajibu kiume.



    "Utaachia!" Jasmine akasema kiaskari.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Tutaona" Malolo akajibu kijambazi sugu.



    Jasmine alikuwa ameishika ile simu kwa mkono wa kushoto. Mkono wake wa kulia aliupeleka shingoni kwa Malolo, akamkaba, akamkaba kwa nguvu! Malolo nae aliutumia ule mkono wa kushoto usio na kitu kuukamata ule mkono wa kulia wa Jasmine. Zilitumika nguvu, na miguno ya hapa na pale.



    Malolo alirudisha kichwa chake nyuma, na kumpiga Jasmine kichwa cha nguvu katika ya paji lake la uso. Jasmine alikuwa kastukizwa na kile kichwa, kichwa kikampata.



    Nae alijibu mapigo.



    Kwa kasi aliacha kumkaba Malolo na kuurudisha tena kwa nguvu, pigo lililompata Malolo kifuani. Lilikuwa pigo la nguvu ambalo Malolo hakutegemea kutoka kwa Jasmine, yeye alimchukulia kama mwanamke mwengine, atakayempiga makofi ya kike ya mgongoni.



    Pigo lile lilimfanya mkono wa kulia wa Malolo kuachia simu. Sasa simu yote ilikuwa imeshikwa na Jasmine kwa mkono wa kushoto. Malolo alipandwa na hasira. Hakuwa tayari kudhalilishwa na mwanamke namna ile. Akajipanga vizuri, alimrukia mzimamzima, akamvaa, waliangukia sofani. Simu ya Malolo ilitoka mkononi mwa Jasmine.



    Simu ilianguka chini!



    Jasmine alikuwa chini, Malolo alikuwa juu. Nguo ya kulalia ya Jasmine ilipanda juu. Mapaja yake meupe yalikuwa hadharani. Macho ya kiume ya Malolo yalitua katika yake mapaja. Kwa kutumia mkono wa kulia alimkandamiza Jasmine kifuani, mkono wa kushoto aliupeleka katika paja la mguu wa kulia wa Jasmine. Jasmine alitoa mguno wa maumivu, maumivu ya kubanwa na ule mkono wa Malolo kifuani. Kisha alitoa mguno wa raha, raha ya kupapaswa pajani.

    Waliangaliana, macho yao yalihitaji.

    Hakukuwa na walichokuwa wanagombania tena, kama simu haikuwepo mkononi mwa Jasmine. Walitabasamu. Jasmine alimpapasa mgongoni Malolo. Akajaribu kulivua shati la Malolo, lilivuka, sasa alikuwa tumbowazi.



    Baada ya dakika saba. Nguo ya kulalia ya Jasmine na Nguo za Malolo zilikuwa mezani, wao walikuwa katika dunia nyingine. Dunia ya raha, na walikuwa wanapeana raha.



    Ugomvi ule mkubwa kati ya Jasmine na Malolo ulimalizwa kwa kufanya mapenzi. Mapenzi haswaa. Walifanya mapenzi hadi wakatosheka. Walipomaliza, walibebana. Jasmine alibebwa mgongoni na Malolo hadi bafuni. Walipofika bafuni waliingia katika beseni kubwa. Walianza kuchezeana tena, walijikuta wanafanya tena mapenzi ndani ya beseni la maji. Walipomaliza, safari hii Jasmine ndiye aliyembeba Malolo. Wakiwa watupu. Moja kwa moja alienda kumtupia kitandani. Hakuna aliyeongea, viliongea vitendo, walishikanashikana, wakajisikia tena kufanya. Walirudia mchezo uleule kwa mara ya tatu. Walipomaliza, ndipo wakalala usingizi mzito.



    Haukuwa usingizi, walikuwa wanadanganyana. Jasmine alikuwa anamdanganya Malolo, Malolo alikuwa anamdanganya Jasmine. Walikuwa wanategeana. Ingawa ugomvi wao ulikuwa umekwisha kwa kufanya mapenzi, lakini pale kitandani kulikuwa na viwiliwili tu, akili zao, fikra zao, zilikuwa sebuleni.



    Kwenye simu!



    Kila mmoja alikuwa anaiwaza simu. Malolo alikuwa anaiwaza simu yake sebuleni. Bila shaka Peter atakuwa amempigia mara kadhaa na bila shaka alikuwa hapatikani. Hali hiyo lazima itampa shaka Peter na kampani yao kwa ujumla.



    "Lakini kabla simu haijadondoka bila shaka iliingia meseji, meseji kutoka kwa Peter, sijui meseji hiyo itakuwa inahusu nini? Ngoja huyu mwanamke alale ili niende nikaiangalie"



    Upande wa Jasmine nao ulikuwa vivyo hivyo. Alikuwa na hamu ya kumjua Peter aliyekuwa anaongea na Malolo. Alikuwa ana shauku ya kutaka kujua ujumbe uliongia katika simu ya Malolo wakati wa purukushani zao, ujumbe ulikuwa unahusu nini. Alikuwa anasubiri tu Malolo alale ili aende sebuleni akaitafute simu. Hisia za kiaskari zilimwambia katika simu ile kuna kitu ambacho sio chema. Lakini kwa bahati mbaya kabisa hisia za Jasmine hazikuhusianisha hisia zake na ile habari ya Peter Kissali kule katika guest ya Uchochoroni..





    Ilikuwa ni vichekesho juu ya kitanda, vichekesho vya Joti na Mpoki. Mtu na mpenzi wake walikuwa wanaviziana. Huyu akigeuka huku, yule anageuka kule. Huyu akimpapasa mwenzie ajue kama amelala na mwenzie anarejesha mpapaso kuonesha kama yuko macho. Huyu akikohoa, yule anaguna, na mara kadhaa wote walijifanya kukoroma, eti wamelala usingizi mnono.



    Hadi saa kumi na moja asubuhi hakuna aliyeenda sebuleni. Hakuna aliyelala usingizi. Wote walibaki kitandani macho wakisubiriana.

    Na walisubiri kweli.



    Saa mbili asubuhi Jasmine na Malolo waliamka kwa pamoja, au tunaweza sema waliinuka kitandani kwa pamoja, walikokotana hadi bafuni. Wote wakiwa wamechoka kwa mambo waliyofanya jana. Wote walikuwa wamechoka kwa kutokulala kabisa. Wote walikuwa wamechoka kwa kuviziana. Safari hii walioga bila ya kufanya chochote, hawakufanya kama jana. Walioga kimyakimya, mawazo ya kila mmoja yakiwa sebuleni.



    Walivyotoka bafuni moja kwa moja walirudi tena chumbani. Kila mmoja alivaa alichokipenda. Na walienda wote sebuleni wakiwa wameshikana mkono. Walienda katika sofa kila mmoja walikaa, kila mmoja alianza kuitafuta simu kwa macho.

    Lakini simu hawakuiona kwa kuitafuta kwa namna ile.



    Dakika kumi na tano baadae kila mmoja alikuwa anatafuta simu kikwelikweli. Huyu katafuta hapa, yule katafuta pale. Waliinyanyua hiki na kile lakini simu ya Malolo haikupatikana. Walilinyanyua hadi sofa lakini ambalo walikuwa na uhakika ndipo simu ilipodondokea, lakini simu haikuwepo.

    Walichanganyikiwa.



    "Simu imeenda wapi?" Ni Jasmine ndiye aliyeuanzisha mjadala.



    "Hata mimi nashangaa"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Si iliangukia huku?"



    "Ndio nashangaa sasa haipo"



    "Hebu jaribu kuipiga"



    Jasmine aliichukua simu yake na kuanza kuipiga simu ya Malolo. Kilikuwa ni kitendo cha kubahatisha tu, maana wote walikuwa na uhakika kwamba simu ilivyoanguka jana kila kitu kilikuwa kwake, bila shaka mfuniko ulifunga na betri kutoka.



    Lakini cha ajabu simu ya Malolo iliita.



    Simu ilikuwa inaita, lakini pale sebuleni hawakuusikia mlio wa simu. Ilikuwa shara kwamba simu haikuwepo pale ukumbini.



    "Sasa simu imekwenda wapi?" Jasmine aliuliza kwa nguvu.



    Malolo hakujibu kitu, yeye alikuwa amechanganyikiwa. Amechanganyikiwa isivyo kawaida. Alikuwa na uhakika wa zaidi ya asilimia mia moja kuwa Jasmine hakwenda ukumbini usiku ule, alikaa macho usiku kucha kuhakikisha hilo halitokei. Alikuwa na uhakika yeye mwenyewe hakwenda ukumbini, hakuhitaji shahidi juu ya hilo, alikuwa ni yeye mwenyewe, na aliamini kwamba hakwenda kuichukua simu pale ukumbini. Moyoni mwake, alikuwa na uhakika simu yake ilikuwa ipo pale ukumbini. Uhakika usio na shaka.



    "Sasa imekwenda wapi?" Malolo nae alijiuliza kimoyomoyo.



    Malolo alienda hadi katika mlango wa sebule kutokea nje. Aligusa kitasa cha mlango. Alipigwa na butwaa! Mlango wa kutokea nje ulikuwa wazi.



    "Nani jana alikuwa wa mwisho kuingia?" Malolo aliuliza.



    "Ni wewe" Jasmine alijibu.



    "Na niliufunga mlango" Malolo alimalizia.



    "Sasa nani itakuwa kaufungua?" Jasmine ilikuwa zamu ya Jasmine sasa kuuliza.



    "Ina maana kuna mtu aliingia baada yako?" Jasmine aliuliza tena.



    "Sidhani" Malolo alijibu kwa sauti ndogo.



    Malolo aliuvuta mlango kwa ndani. Alitoka nje. Alipoangalia tu chini, macho yake yalikutana na kitu cha ajabu sana. Kulikuwa na mwili wa mtu umelala katikati ya mlango.



    "Jasmine!" Malolo aliita kwa sauti kubwa.



    "Kuna nini tena?" Jasmine alisema huku akitoka nje.



    "Njoo uone!" Malolo alisema kwa nguvu.



    Jasmine alienda harakaharaka, alikutana na kitu kilekile alichokiona Malolo. Kulikuwa na mwili wa mtu ukiwa hauna uhai!



    Macho ya Jasmine yalitua katika sura ya yule mtu, alimfahamu.





    Sura aliyokuwa anaitazama pale chini ilikuwa ni sura sawa na sura iliyokuwepo katika pochi yake, katika kitambulisho alichopewa jana usiku.

    Naam! Mbele yake kulikuwa na maiti ya Peter Kissali.



    Malolo alikuwa anataharuki haijawahi kutokea hapa duniani. Alikuwa na humwehumwe ndani ya moyo wake. Miguu ilikuwa inamtetemeka.

    Alikuwa amemtambua patna wake katika Operesheni mbalimbali, alikuwa amemtambua Peter Kissali lakini hakutaka kabisa kumuonesha Jasmine kwamba alikuwa anamjua yule mtu. Ilikuwa hivyo kwa Malolo, ilikuwa hivyo kwa Jasmine pia. Wote walijifanya hawamtambui Peter Kissali ilihali kila mmoja alikuwa anataka sana kufahamu zaidi nini kimetokea.



    "Huyu ni nani?" Jasmine alifunua mdomo wake kuuliza.



    "Hata simfahamu" Malolo alijibu huku akiwa anaangalia pembeni.



    "Ni yeye atakayekuwa ndiye aliyechukua simu nini?" Jasmine aliuliza.



    "Sasa kwanini afe?" Malolo nae aliuliza.



    Utata!



    Jasmine alirudi ndani, akabeba 'gloves' nyeupe. Akazivaa. Alianza kuikagua maiti ya Peter Kissali, hayo yote yalikuwa yanatazamwa na macho yote mawili ya Malolo.



    Katika mifuko ya Peter hakukuwa na kitu chochote kile.



    "Itakuwa amesachiwa huyu" Jasmine alisema.



    "Na nani?" Malolo aliuliza.



    "Ni jukumu letu kumjua huyo mtu na bila shaka huyo mtu aliyemsachi ndiye kachukua simu yako"



    "Tutaanzaje kumjua, bila shaka huyu kauwawa muda mrefu"



    "Lazima tuungane pamoja tupeleleze"



    "Daaa sasa hii maiti itakuwaje?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Najua mimi cha kufanya, wewe nenda kavae tuingie kazini"



    "Wewe vipi huvai?"



    Malolo na Jasmine wote waliingia ndani ya nyumba. Kuvaa ili wamtafute mtu aliyemuuwa mtu waliyejifanya hawamfahamu. Walikuwa wanadanganyana lakini kila mmoja akijua akifanyacho.



    Dakika tano baadae baada ya kuvaa walitoka tena nje. Walikutana tena na maajabu, maajabu mapya, mwili wa Peter haukuwepo pale katikati ya mlango.



    Mwili ulikuwa umetoweka!



    "E bwana weee, mwili wa Peter umeenda wapi?" Malolo alijikuta anaropoka jina la yule jamaa wakati alijifanya hamtambui awali.



    "Kumbe unamjua yule jamaa mpenzi, ndio uliyeongea nae usiku eeeh" Inspekta Jasmine alimuuliza huku akiwa anacheka.



    "Unacheka! Huu sio muda wa kucheka, tukimbie hapa sio mahali salama"



    "Tukimbie twende wapi? Lakini sawa tutaondoka hapa ukinambia kidogo kuhusu Peter, Peter Kissali, ni nani yule? Una uhusiano nae gani?"



    Malolo macho yalimtoka pima! Alikuwa anamwangalia Jasmine usoni akiwa na maswali mengi sana kichwani mwake.



    "Jasmine unamjua Peter, umemjuaje, kumbe alikuwa bwana wako eeeh?" Malolo alimrushia mpira Jasmine.



    "Kwahiyo unataka kunambia natembea na wanaume wawili wanaofanya kazi pamoja bila kujuana?" Jasmine nae alirusha swali.



    Malolo aliendelea kupatwa na mshangao, hakuyaelewa kabisa maneno yakiyoongelewa na mpenzi wake, Jasmine.



    "Kwani mimi na Peter tunafanya kazi pamoja? Kazi gani?" Naye aliuliza kwa sauti isiyo na nguvu.



    "Hilo la kwanza ni jibu. La pili ni swali lakini unatakiwa wewe ndio unijibu. Mnafanya kazi gani wewe na Peter?" Jasmine alikuwa anamsogelea Malolo sasa.



    "Unajua sikuelewi Jasmine?"



    "Utanielewa tu leo"



    "Unataka ufanye kazi yako kwangu, kumbuka mimi ni mpenzi wako?"



    "Kazi gani?" Mshangao sasa ulimgeukia Jasmine.



    "Unadhani mimi siijui kazi yako?" Malolo aliuliza.



    "Malolo hivi unaelewa unachokiongelea" Jasmine alipoa kidogo.



    "Najua unanielewa, ila unajifanya tu hunielewa. Ila jua najua kila kitu kuhusu wewe"



    "Nami jua najua kila kitu kuhusu wewe na Peter Kissali, Mwendawazimu"



    Sasa wapenzi wale wawili walikuwa wanaangaliana kwa hasira. Kila mmoja akitamani kumvamia mwenziwe. Ilikuwa hali mbaya sana kuwahi kutokea kwa wapenzi hawa wawili, ngumu kuliko ile ya jana usiku...





    Ilikuwa ni kitendo bila kuchelewa. Jasmine alimvaa Malolo na kumkaba shingoni kwa nguvu. Jasmine aliona mambo yameshaharibika. Hakuwa na jinsi, aliamua kutumia nguvu kumdhibiti Malolo. Na Malolo nae alikuwa anafikiria kitu kilekile. Namna pekee ya kumziba mdomo Jasmine ni kumuua!



    Kuvamiwa na Jasmine kulimstua sana Malolo. Alijua yeye ndiye atakayekuwa wa kwanza kumvamia Jasmine, lakini alikuja kugundua kwamba wote walikuwa wanawaza fikra sawa. Hakuwa na jinsi nae ilimpasa kujitoa kwa nguvu katika roba ile toka kwa askari yule wa kike.

    Nae alipeleka mikono kwa kasi pale shingoni kujaribu kuitoa ile roba. Ilikuwa patashika.

    Alikutana na mikono imara na migumu ya Jasmine, sio ile laini aliyozoea kuishika siku zote wakiwa kitandani. Malolo alikuwa mbele, Inspekta Jasmine alikuwa nyuma.



    "Niachie!" Malolo alisema kwa ghadhabu.



    Jasmine alikuwa kama hamsikii vile, au labda alisikia kinyume chake, yeye aliendelea kukandamiza mikono yake shingoni kwa Malolo.



    "Inspekta Jasmine!" Malolo alijikuta amelitamka jina la Jasmine na cheo chake.



    Hapo ndipo alijua kwamba Malolo alikuwa anajua kila kitu kuhusu yeye. Kumbe walikuwa wanaishi kila mmoja akiwa anajua kazi ya mwenzie. Kumbe yale hayakuwa mapenzi. Wote walikuwa kazini, wote walikuwa katika upelelezi. Wakati Inspekta Jasmine akiwa karibu na Malolo ili kujua undani ya wale wauaji, Malolo alikuwa karibu na Inspekta Jasmine ili kujua mipango ya Polisi walivyokuwa wanaipanga, na wao kuipangua. Na wote walikuwa wanajuana kiundani, wanajuana nje, wanajuana ndani.



    Kwa nukta ile walisahau habari ya kutoweka kwa maiti ya Peter, sasa walikuwa wanataka kuoneshana ubabe.



    "Nakuua Jasmine!"



    Malolo alisema huku akikirudisha kichwa chake kwa nyuma kwa nguvu. Kisogo chake kilikutana na mwamba wa pua wa Inspekta Jasmine. Kilimpata bara'bara, Inspekta Jasmine damu zilikuwa zinamtiririka. Lakini bado mikono yake ilikuwa imara katika shingo ya Malolo. Hataki kuiachia ile shingo ya Malolo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kimbembe.



    Malolo alirudia tena mtindo uleule, lakini safari hii kichwa chake kilipiga hewa. Safari hii Inspekta Jasmine alikikwepa kisogo cha Malolo kwa ustadi mkubwa sana, huku mikono yake ikijiimarisha vizuri katika shingo ya Malolo.



    Ilikuwa patashika!



    Mate yalikuwa hayapiti hata kidogo kohoni kwa Malolo, Malolo alikuwa anaelekea kuishiwa nguvu kutokana na kubanwa na roba. Kiutaniutani roba ile ya Inspekta Jasmine ilikuwa inataka kumtoa roho Malolo. Na Malolo nae hakuwa tayari kuuwawa kimtindo ule. Hakuwa tayari kuuliwa na mpenzi wake.



    Alinyanyua mguu wake wa kulia juu na kuurudisha kwa nguvu juu ya mguu wa kulia wa Inspekta Jasmine!

    Hiyo ilikuwa nia yake, na alitenda kweli, lakini alikanyaga ardhi tupu, Jasmine alitoa kwa haraka mguu wake wa kulia na kuurudisha nyuma. Huku mguu wake wa kushoto akimpiga kifuti cha nguvu katikati ya mgongo wa Malolo. Bado roba takatifu ilikuwa imetulia palepale, shingoni kwa Malolo.



    Safari hii Malolo alifanikiwa kutoa ukelele, ukelele wa maumivu kutokana na kifuti kile cha haja toka kwa Jasmine. Sasa alikuwa anaelekea kuzidiwa nguvu na Jasmine. Nguvu za miguuni zilikuwa zinamwishia. Taratibu miguu yake ilishindwa kusimama imara kuweza kuuhimili mwili wake. Pumzi zilimuishia. Taratibu alikuwa anafumba macho, akili zake zililala kama macho yake. Malolo alizimia katika mikono imara ya Inspekta Jasmine.



    Inspekta Jasmine aliuona mwili wa Malolo umezidi uzito, akajua tayari kashaua, akauachia chini mithili ya mzigo. Ulivyotua chini tu, alimuona mtu mbele yake, mwanamke, alikuwa Malikia....



    Malkia na Jasmine walikuwa wanaangaliana. Wote wanaangaliana kwa macho yaliyojaa hasira. Macho ya chuki, walikuwa wanachukiana hasa.



    "Inspekta Jasmine nilikuwa nakutafuta sana mwanamke wewe, utanitambua leo" Malkia alikuwa anaongea kwa hasira huku akimsogelea Jasmine.



    Jasmine hakuongea kitu, aliukanyaga kwa nguvu mwili uliolala chini wa Malolo usoni na kushukia upande wa pili. Kilikuwa ni kitendo kilichomchukiza zaidi Malkia, kuufanya mwili wa patna wake ngazi.



    "Nakuua wewe mar'huni"



    Malkia alikwenda na hasira zake, aliruka juu na miguu yote miwili ilitua katika kifua cha Inspekta Jasmine, Inspekta alipepesuka vibaya sana, lakini hakuanguka. Malkia alikuwa amesimama imara, akimwangalia Malkia jinsi alivyokuwa anajidhibiti ili asianguke.



    Malkia alienda tena hewani na kumfuata Inspekta Jasmine kwa mtindo uleule wa awali, lakini safari hii alimkuta Jasmine yupo imara. Alijisogeza kidogo tu, Malkia alipita jumla. Sasa wanawake wale wawili wote walikuwa wamesimama imara. Wakiwa wamepeana mgongo. Wote waligeuka kwa pamoja, waliangaliana.

    Sasa ilikuwa zamu ya Inspekta Jasmine, alimfata Malkia kwa kasi huku akiwa ameitanguliza ngumi ya mkono wake wa kulia. Malkia aliviona vyote kwa pamoja, Inspekta Jasmine pamoja na ile ngumi. Na alivikwepa vyote kwa pamoja. Na safari hii wote waligeuka kwa pamoja tena



    Waliangaliana.



    "Kumbe ni wewe ndiye uliyeitorosha maiti ya Peter?" Inspekta Jasmine aliuliza kwa jazba.



    Hakukuwa na wa kumjibu.



    Malkia alikuwa kimya, akitafuta nafasi ya kumdhibiti yule askari wa kike, hakuwa na muda wa kumjibu kabisa maswali yake.



    Alimsogelea Inspekta Jasmine kwa mwendo wa kawaida, sasa walikuwa wamekaribiana kabisa, macho ya kila mmoja yakiwa hayatulii sehemu moja. Yalikuwa sekunde hii yakiangalia hapa, sekunde ile yanaangalia pale. Kila mmoja alikuwa anam'timing mwenziwe ili amuoneshe.



    Ni Malkia ndiye aliyepaona pa kupapiga katika mwili wa Inspekta Jasmine. Alirusha teke kwa mguu wake wa kulia kuelekea shingoni kwa Inspekta Jasmine, lakini mguu haukufika shingoni, Inspekta aliukamata ule mguu kabla haujafika shingoni mwake, kwa kasi aliupinda ule mguu kwa kutumia mikono yote miwili. Malkia alistuka, naye alijizungusha kwa kasi upande uleule uliokuwa unazungushwa mguu. Na hiyo ndio ilikuwa nusra yake ya kuvunjwa mguu.



    Pamoja na kujigeuza pamoja na mguu wake, lakini bado Inspekta Jasmine alikuwa kaung'ang'ania ule mguu vilevile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Malkia alirusha kwa nguvu mguu wake wa kushoto ili kuuokoa ule mguu wa kulia. Inspekta Jasmine aliudaka tena ule mguu mwengine.

    Sasa miguu yote ya Malkia ilikuwa mikononi mwa Inspekta Jasmine, imekamatwa bara'bara. Malkia alikuwa kichwa chini miguu juu, huku mikono yake ikiwa imeishika sakafu ya pale chini.

    Inspekta Jasmine alirusha teke lililotua katikati ya tumbo la Malkia. Teke lilimpata bara'bara Malkia, alitoa mguno wa maumivu.

    Inspekta Jasmine alirusha teke lengine, nalo lilimpata sawasawa Malkia tumboni, aliguna tena kwa maumivu.

    Malkia akaona amepatikana. Bila kufanya chochote alikuwa anaenda kufa!

    Alijivuta kwa kasi na kwenda kuishika miguu ya Malkia. Sasa kila mmoja alikuwa ameishika miguu ya mwenzake. Ilikuwa mithili ya mzungu katika karata....





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog